You are on page 1of 3

KUUKULIA WOKOVU

KUJENGA URAFIKI NA YESU


Yohana 15:12-15
12 Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. 13 Hakuna aliye na upendo
mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. 14 Ninyi mmekuwa rafiki
zangu, mkitenda niwaamuruyo. 15Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo
bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu
nimewaarifu.
ͽ Mara nyingi tunapozungumzia kukuwa katika wokovu, tunazungumzia sana kuhusu
kusoma neno, maombi, kumtumikia Mungu, Kukua kiimani, n.k.
ͽ Haya yote yana nafasi yake kubwa.
ͽ Hata hivyo, katika kuukulia wokovu nitaweka msisitizo katika eneo ambalo naamini lina
nafasi kubwa sana katika kuamua ukuaji wa kiroho wa mtu.
ͽ Eneo hilo linahusu Kujenga urafiki na Yesu

Yesu ni mtu, na kama ambavyo mtu yeyote hupenda kuwa na marafiki, hata Yesu anapenda
marafiki.
ͽ Pamoja na kwamba alikuwa na mitume 12 chini yake kwa ajili ya huduma, lakini
aliwafanya mitume hao kuwa ni rafiki zake.
ͽ Pamoja na wanafunzi wake, Yesu alikuwa na rafiki yake mwingine aitwaye Lazaro
o Yohana 11:11 - Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu,
Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha.
o Tunaona mara kadhaa katika maandiko Yesu akimtembelea Lazaro nyumbani
kwake na kushiriki karamu pamoja naye.
ͽ Yesu anapenda urafiki, na kila mmoja wetu ana nafasi ya kujenga urafiki naye.
ͽ Isitoshe, yeye ndiye rafiki awezaye kuwa karibu kuliko hata ndugu
o Mithali 18:24 - Ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa maangamizi yake mwenyewe;
Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.

KUISHI NA UFAHAMU KWAMBA YESU YUMO NDANI YAKO


Maandiko yako wazi kwamba Kristo anaishi ndani ya watu waliomwamini. Amefanya makao
yake ndani yetu, na anaishi na kutenda kazi kutokea ndani yetu.
ͽ Maandiko
o Ufunuo 3:20 - Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu,
na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye
pamoja nami.
o 2Kor 13:5 - Jichunguzeni wenyewe muone kama mmekuwa katika imani;
jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani
yenu? Isipokuwa iwe mmekataliwa.
o Warumi 8:10 - Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya
dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.
o Wagalatia 2:20 - Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi
tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao
katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa
ajili yangu.
o Wagalatia 4:19 - Watoto wangu wadogo, ambao nawaonea uchungu tena mpaka
Kristo aumbike ndani yenu.
o Waefeso 3:17 - Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na
msingi katika upendo;
o Yohana 14:23 - Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno
langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
o Wakolosai 1:26-27 - siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote,
bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake; 27 ambao Mungu alipenda
kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni
Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu.
o Yohana 14:20 - Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu,
nanyi ndani yangu, nami ndani yenu.
ͽ Maandiko haya na mengine mengi yanathibitisha ukweli kwamba Kristo anaishi ndani
yetu.
ͽ Yaani 24/7 tupo na Kristo.
ͽ Lakini je, wangapi tunaishi katika ufahamu huo. Wangapi tunaenenda kila wakati tukiwa
na ufahamu kwamba Kristo yupo ndani yetu. Wangapi tumejenga urafiki wa karibu na
Yesu.
ͽ Inawezekanaje tukaishi na mtu kila siku alafu tushindwe kuwa na urafiki naye?
ͽ Mtazamo kuhusu uwepo wa Yesu au uwepo wa Mungu
o (The reality of God’s presence) Uhalisia wa uwepo wa Mungu – Daima yupo
nawe, kama tulivyosoma kwenye maandiko.
 Ni uwepo ulio halisi, iwe unajisikia au hujisikii, yeye Yupo ndani yako na
yupo nawe.
o (The felt presence of God) Uwepo wa Mungu unaoweza kuuhisi – Ushahidi na
hisia zinazoonyesha kwamba Mungu yupo nawe. Kila mtu anakuwa na hisia
mbalimbali pale uwepo wa Mungu unapodhihirika kwake.
o (The deliberate consciousness of God’s presence) – Kuishi kwa ufahamu/fikra
zako kujua kwamba Mungu yupo nawe.
o The background consciousness of God’s presence – Huu ni uwepo wa Mungu
ambao mara nyingi hatujui kama upo, ila pale unapotuacha ndipo tunapogundua
kuwa kuna kitu kimekosekana.
ͽ Hisia za uwepo wa Mungu si kipimo cha hali ya kiroho ya mtu na wala si kiashiria
kwamba Mungu ana upendeleo kwa baadhi ya watu.

You might also like