You are on page 1of 7

IBADA YA KUSIMIKA

NENO LA MUNGU
WAKATI WA IBADA YA MISA
JUMAPILI YA NENO LA MUNGU

prepared by the Daughters of St Paul


sources: The Pontifical Council for Promoting New Evangelisation
Sunday of the Word of God Liturgical- Pastoral Resources- 2022
Ibada ya Kusimika Neno la Mungu
wakati wa Ibada ya Misa
Jumapili ya Neno la Mungu

1. UTANGULIZI
Baada ya kuanza ibada ya misa kama ilivyo kawaida, Kiongozi wa ibada anawaeleza
waamini maana ya sherehe ya leo kama ifuatavyo:

“Leo, andiko hili limetimia masikioni mwenu” – hayo ni maneno ya Bwana


kwa watu wa Nazareti. Kwa njia hii, Yesu anatukumbusha ya kuwa Neno la Mungu
lina nguvu. Biblia sio kitabu, kisomwacho na baadaye kufungwa na kusahaulika, ila
Neno la Mungu li hai. Ni uwepo wa Mungu kati yetu kwani linauwezo wa kuyageu-
za na kuyatakasa maisha yetu. Kufungua Biblia kuna tuwezesha kukutana na Mun-
gu anayetuita binafsi na kujifunua ndani ya Maisha yetu.
Leo Mama Kanisa inasherehekea Jumapili ya Neno la Mungu: hivyo sisi sote
tunaalikwa kufungua mioyo yetu kwa Mungu anayejifunua kwetu kupitia kwa Neno
lake na anapenda kuishi kati yetu. Hivyo basi, ili tuweze kumwalika kati yetu katika
adhimisho hili, tukiri dhambi zetu na tuombe msamaha.

2. TENDO LA TOBA
Kiongozi wa ibada anaweza kutumia tendo la toba kama ifuatavyo:

K: Bwana wetu Yesu, anayetualika kwenye meza ya Neno lake na Ekaristia anatu-
ita tuongoke, hivyo basi tukiri sisi ni wakosefu na kwa imani tuombe huruma ya
Mungu.
K: Bwana Yesu, wewe ni Neno la Mungu aliyefanyika mwili, Bwana utuhurumie.
W: Bwana Utuhumie.
K: Bwana Yesu, uliwaponya vipofu kwa nguvu ya Neno lako, Kristu utuhurumie.
W: Kristu utuhurumie
K: Bwana Yesu, unatukomboa kutoka dhambini, Bwana utuhurumie.
W: Bwana utuhurumie.
K: Mungu mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu, atufikishe kwenye uzi-
ma wa milele.
W: Amina.

Wimbo wa utukufu.
3. LITANIA YA NENO LA MUNGU
Baada ya msafara wa Neno la Mungu, Kiongozi wa ibada anawaalika waumini wote ku-
likaribisha Neno la Mungu kati yao kwa kuinama, ishara ya heshima. Bado akiwa anaonye-
sha Biblia kwa waumini; Waumini wanaimba Litania ifuatayo:

Kiongozi: Baada ya kila sala tutajibu:

Wote: Bwana tumwendee nani? Wewe una maneno ya uzima wa milele.

Mwimbaji: Bwana wetu Yesu Kristu, wewe ni Neno la Baba.


Mwimbaji: Umekuwa mmoja nasi kutueleza upendo wa Baba.
Mwimbaji: Wewe ni mwanga unaye angaza kwenye giza.
Mwimbaji: Unatuokoa kutoka uoga na kuvunja minyororo
ya dhambi na mauti.
Mwimbaji: Unakuja kuongoza miguu yetu na kutuongoza kwa Mungu.
Mwimbaji: Wewe ndiwe Neno la uzima wa milele.
Mwimbaji: Unatujaza kwa Roho Mtakatifu.

Baada ya Litania Padre anaisimika Biblia Mahali palipo andaliwa.

4. KUBARIKI WASOMAJI KABLA YA MASOMO


Padre anasali sala ifutayo kuwabariki wasomaji:

Mungu aliyekuita kutangaza Neno lake, awe moyoni na kinywani mwako.


† Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu.

Msomaji (Wasomaji) wanajibu: Amina.

5. WAJIBU WETU KWA NENO LA MUNGU


(Kabla ya Homilia)

Padre:
Ndugu wapendwa nawalikeni nyote mnyoshe mkono wa kulia kuelekea
kwenye Biblia. Hii ni Ishara ya uwajibikaji wetu binafsi kutafuta uzima
katika Neno la Mungu.
Padre: Tuombe:
Tumeyasikia maneno yako, Yesu.
Yanatupa furaha na kuleta mwanga na ukweli katika maisha yetu.
Uwepo wako unaleta amani katika ulimwengu
unaosumbuka na uliogawanyika.
Twaomba Neno lako litie katika mioyo yetu upendo wako mkubwa.
Kaa mioyoni mwetu katika familia zetu, jumuiya na nchi yetu.
Tujalie Roho Mtakatifu atusaidie kuelewa Neno lako.
Tunalikaribisha Neno lako lililo miongoni mwetu.
Lifanye liwe kiini cha maisha yetu.
Twaomba Neno lako liangaze yale yote tunayofikiri,
tunayosema na tunayofanya.
Tunaomba lituunganishe wote na pamoja nawe, leo na milele yote.

Wote: Amina.

6. KUKIRI IMANI YETU KATIKA NENO LA MUNGU


(Baada ya Kanuni ya Imani)

Padre: Je, unasadiki Mungu Muumba wa ulimwengu, alinena na watu wa kale wa


Israeli kwa ukombozi wa mataifa yote?
Wote: Ndio Nasadiki.
Padre: Je, unasadiki Neno la Mungu aliyefanyika mwili na anaendelea kuishi kati
yetu ni Habari njema kwa wote?
Wote: Ndio Nasadiki.
Padre: Je, unasadiki Mungu alimtuma Roho Mtakatifu kati yetu kutuongoza katika
ukweli na kuelewa Neno lake?

Wote: Ndio Nasadiki.


7. SALA YA WAAMINI
K: Ndugu zangu, katika Bwana wetu Yesu Kristo, maandiko matakatifu yanatimiz-
wa na maisha yetu yanakamilishwa. Tuyalete mahitaji yetu mbele ya Mungu
Baba yetu, ili tuweze kuishi kwa ukamilifu Neno lake Takatifu.

Kiitikio: Tunaomba, Ee Baba, Neno lako litimizwe ndani yetu.

1. “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenipaka mafuta.” Tuombe


kwa ajili ya Baba Mtakatifu, maaskofu, mapadre na mashemasi ili waweze
kwa ujasiri kuwasaidia wote wanaoishi katika utumwa wa kiroho na kimwili.
Tunaomba…

2. “Roho wa Bwana yu juu yangu… niwahubirie maskini Habari njema.” Tuombe


ili wote waliobatizwa kwa neema ya Roho Mtakatifu waweze kuwa watanga-
zaji Hodari wa Habari Njema, kwa wote, hasa walio na mahitaji mbali
mbali. Tunaomba…

3. “Roho wa Bwana yu juu yangu, amenituma kutangazia wafungwa kufungu-


liwa.” Tuwaombee wasomaji, makatekista na wale wote wanaotangaza Neno
la Mungu katika jumuiya zetu, juhudi yao isaidie kuimarisha imani, matu-
maini na mapendo haswa kwa walio wapweke, wasio na matumaini, wangon-
jwa na waliolemewa na uzito wa Maisha. Tunaomba…

4. “Roho wa Bwana yu juu yangu, kuwatangazia vipofu kuona tena.” Tuombe ili
kila mmoja wetu aweze kuufungua moyo wake kwa Mungu, anayetuangaza
na Neno lake, na kutongoza kwenye chemichemi ya uzima. Tunaomba…

K: Mungu Baba mwenyezi, tunakushukuru kwa kumtuma Mwanao kati yetu.


Tujalie kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, tumkaribishe miyoni mwetu,
Unayeishi na kutawala daima na milele.

W: Amina
8. AHADI YA FAMILIA KWA NENO LA MUNGU
(Baada komunyo Padre anawaalika waumini, kuweka ahadi ya kuheshimu,
kusoma na kutafakari Neno la Mungu. Wote wanarudia baada ya Padre):

Tunaahidi kuheshimu Neno la Mungu miongoni mwetu.


Tutalisoma na kulitafakari kama familia ya Mungu.
Tutaongozwa nalo tunapofanya maamuzi yetu.
Litakua nguvu katika kazi zetu na kitulizo wakati wa masubuko.
Yesu, tusaidie tuwe waadilifu kwa ahadi yetu,
wewe unayeishi daima na milele. Amina.

9. BARAKA YA MWISHO WA IBADA YA MISA


K: Mungu mwenyezi awabariki na baraka za mbinguni, awatakase na kuwafanya
watakatifu machoni pake, awamiminie utajiri wa utukufu wake, awafundishe
kwa Neno la kweli, awaangaze na Injili ya wokovu, na awajaze furaha ya upen-
do wa kindugu.
W: Amina
K: Na Baraka yake Mungu Mwenyezi, Baba X na Mwana na Roho Mtkatifu
iwashukie na kukaa nanyi daima.
W: Amina

You might also like