You are on page 1of 27

SALA ZA KANISA KATOLIKI

Kitabu hiki kimeandaliwa na ALFRED PATRICK


SALA ZA KANISA KUU TAKATIFU KATOLIKI LA MITUME
Sala ya Baba yetu
Baba Yetu uliye mbinguni,
jina lako litukuzwe;
ufalme wako ufike,
utakalo lifanyike
duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku,
utusamehe makosa yetu,
kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.
Usitutie katika kishawishi,
lakini utuopoe maovuni.
Amina

KANUNI YA IMANI YA NICEA.


Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi,
Mwumba mbingu na nchi na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.
Nasadiki kwa Bwana mmoja Yesu Kristu,mwana wa pekee wa Mungu.
Aliyezaliwa kwa Baba tangu milele yote.
Mungu aliyetoka kwa Mungu, Mwanga kwa mwanga, Mungu kweli kwa Mungu kweli.
Aliyezaliwa bila kuumbwa,
Mwenye umungu mmoja na Baba,
Ambaye vitu vyote vimeumbwa naye.
Ameshuka toka mbinguni kwa ajili yetu sisi wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu.
Akapata mwili kwa uwezo wa Roho mtakatifu, kwake yeye Bikira Maria, akawa
mwanadamu.
Akasulibiwa pia kwa ajili yetu sisi,
Akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato,
Akafa akazikwa.
Akafufuka siku ya tatu ilivyoandikwa.
Akapaa mbiguni, amekaa kuume kwa baba

1
Atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu wazima na wafu nao ufalme wake hautakuwa
na mwisho.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Bwana mleta uzima atokaye kwa Baba na Mwana,
anayeabudiwa na kutukuzwa
pamoja na Baba na Mwana, aliyenena kwa vinywa vya manabii.
Nasadiki kwa Kanisa moja, Takatifu, Katoliki la mitume . Naungama ubatizo mmoja
kwa maondoleo ya dhambi.
Nangojea na ufufuko wa wafu.
Na uzima wa milele ijayo.
Amina.
KUOMBA KIFO CHEMA
Enyi Yesu na Maria na Yosefu,nawatolea Moyo, na roho, na uzima wangu. Enyi Yesu
na Maria na Yosefu, mnipokee saa ya kufa kwangu. Enyi Yesu na Maria na Yosefu,
mnijalie nife mikoni mwenu.

SALA YA ASUBUHI.
Kwa jina la Baba…..
Ee Baba yetu Mungu mkuu,umenilinda usiku huu.
Nakushukuru kwa moyo, ee Baba,Mwana na Roho.
Nilinde tena siku hii,niache dhambi nikutii.Naomba sana Baba wee, baraka yako
nipokee.
Bikira safi, Ee Maria nisipotee nisimamie.
Mlinzi mkuu malaika wee kwa Mungu wetu niombee,nitake nitende mema tu na
mwisho nije kwako juu.Amina.
NIA NJEMA.
Kumueshimu Mungu wangu,namtolea roho yangu.
Nifanye kazi nipumzike ,amri zake tu nishike.
Wazo,neno,tendo lote namtolea Mungu pote Roho,Mwili chote changu.
Pendo na uzima wangu.
Mungu wangu nitampenda wala dhambi sitatenda.
Jina lako nasifia,utakalo hutimia kwa utii navumili.
Teso na matata pia,nipe Bwana neema zako, niongeze sifa yako.Amina.

2
SALA YA MATOLEO.
Ee Yesu kwa mikono ya Bikira Maria,na kwa maungano na sadaka yako kuu.
Ninakutolea sala,matendo,masumbuko na furaha zangu zote za leo.
Ee Yesu ufalme wako utufikie.Amina.
BABA YETU.
Baba yetu uliye mbinguni,jina lako litukuzwe.
Ufalme wako ufike.Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku.Utusamehe makosa yetu,kama tunavyo wasamehe
na sisi waliyo tukosea.
Usitutie katika kishawishi,lakini utuopoe maovuni.Amina.
SALAMU MARIA.
Salamu Maria,umejaa neema Bwana yu nawe,umebarikiwa kuliko wanawake wote,na
Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria mtakatifu Mama wa Mungu,utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa
kwetu.Amina.
KANUNI YA IMANI.
Nasadiki kwa Mungu,Baba Mwenyezi,muumba mbingu na dunia.
Na kwa Yesu Kristu Mwanaye wa pekee,Bwana wetu aliyetungwa kwa Roho
Mtakatifu,akazaliwa na Bikira Maria,akateswa kwa mamlaka ya ponsyo
Pilato,akasulibiwa, akafa,akazikwa,akashukia kuzimu siku ya tatu akafufuka katika,
akapaa mbinguni amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi,toka huko atakuja
kuwahukumu wazima na wafu.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu,kanisa takatifu katoliki ushirika wa
Watakatifu,maondoleo ya dhambi,ufufuko wa miili na uzima wa milele.Amina.
AMRI ZA MUNGU.
1.Ndimi Bwana Mungu wako,usiabudu miungu wengine.
2.Usilitaje bure jina la Mungu wako.
3.Shika kitakatifu siku ya Mungu.
4.Waheshimu Baba na Mama upate miaka mingi na heri duniani.
5.Usiue.
6.Usizini.
7.Usiibe.
8.Usiseme uwongo.

3
9.Usitamani mwanamke asiye mke wako.
10.Usitamani mali ya mtu mwingine.
AMRI ZA KANISA.
1.Hudhuria misa takatifu dominica na sikukuu zilizo amuliwa.
2.Funga siku ya jumatano ya majivu,usile nyama siku ya Ijumaa kuu.
3.Ungama dhambi zako walau mara moja kwa mwaka.
4.Pokea Ekarist takatifu hasa wakati wa Pasaka
5.Saidia kanisa katoliki kwa zaka.
6.Shika sheria katoliki za ndoa.
SALA YA IMANI.
Mungu wangu,nasadiki maneno yote linayo sadiki na kufundisha kanisa katoliki la
Roma kwani ndiwe uliye fumbuliwa hayo,wala hudanganyiki na wala
hudanganyi.Amina.
SALA YA MATUMAINI.
Mungu wangu,natumaini kwako nitapewa kwa njia ya Yesu Kristu,neema zako duniani
na utukufu mbinguni.Kwani ndiwe uliyeagana hayo nasi nawe mwamini.Amina.
SALA YA MAPENDO.
Mungu wangu,nakupenda zaidi ya chochote, kwani ndiwe mwema ndiwe mwenye
kupendeza.
Nampenda na jirani yangu kama nafisi yangu kwa ajili yako.Amina.
SALA YA KUTUBU.
Mungu wangu,nimetubu sana dhambi zangu kwani ndiwe mwema,ndiwe mwenye
kupendeza wachukizwa na dhambi.
Basi sitaki kukosa tena nitafanya kitubio,naomba neema yako nipate kurudi.Amina.
SALA KWA MALAIKA MLINZI.
Malaika mlinzi wangu,unilinde katika hatari zote za Roho na za Mwili.Amina.
MALAIKA WA BWANA.
K.Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria.
W.Naye akapata mimba kwa Roho mtakatifu.
Salamu Maria…..

4
K.Ndimi mtumishi wa Bwana.
W.Nitendewe ulivyo nena.
Salamu Maria…..
K. Neno la Mungu akatwaa Mwili.
W. Akakaa kwetu.
Salamu Maria….
K. Utuombee Mzazi Mtakatifu wa Mungu.
W. Tujaliwe ahadi za Kristu.
Tuombe.
Tunakuomba Ee Bwana utie neema yako mioyoni mwetu ili sisi tuliyojuwa kwa
maelezo ya malaika kwamba, Kristu mwanao amejifanya mtu kwa mateso na msalaba
wake.
Tufikishwe kwenye utukufu wa ufufuko.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu.Amina.
ATUKUZWE BABA.
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu,kama mwanzo na sasa na siku zote na
milele.Amina.
K. Moyo Mtakatifu wa Yesu
W.Utuhurumie.
K. Moyo safi wa Bikira Maria.
W. Utuombee.
K. Mtakatifu Yosefu.
W. Utuombee.
K. Watakatifu somo wa majina yetu.
W. Mtuombee.
K.Watakatifu wote wa Mungu.
W.Mtuombee.
Kwa jina la Baba…..✍✍
SALA YA MATUMAINI

5
Mungu wangu, natumaini kwako nitapewa kwa njia ya Yesu Kristu, neema zako
duniani na utukufu mbinguni, kwani ndiwe uliyeagana hayo nasi, nawe mwamini.

SALA YA KUOMBEA AMANI


Ee Bwana, unifanye kuwa chombo cha amani yako:
Palipo na chuki, nilete mapendo,
Palipo na kukoseana, nilete msamaha,
Palipo na utengano, nilete umoja,
Palipo na shaka, nilete Imani,
Palipo na makosa, nilete ukweli,
Palipo na kukata tamaa, nilete matumaini,
Palipo na huzuni, nilete furaha,
Palipo na giza, nilete mwanga,
Ee Bwana unijalie nitamani zaidi:
Kufariji kuliko kufarijiwa,
Kufahamu, kuliko kufahamika,
Kupenda kuliko kupendwa,
Kwa kuwa:
Ni katika kutoa ndipo tunapokea,
Ni katika kusamehe ndipo tunasamehewa;
Ni katika kufa ndipo tunazaliwa katika uzima wa milele.
Amina.

SALA YA USIKU KABLA YA KULALA

6
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
SALA YA KUSHUKURU
Tunakushukuru, ee Mungu, kwa mapaji uliyotujalia leo. Amina.
Baba yetu …
Salamu Maria …
SALA YA IMANI
Mungu wangu, nasadiki maneno yote. Linayosadiki na linayofundisha Kanisa Katoliki
la Roma. Kwani ndiwe uliyetufumbulia hayo. Wala hudanganyiki, wala hudanganyi.
Amina.
SALA YA MATUMAINI
Mungu wangu, natumaini kwako, nitapewa kwa njia ya Yesu Kristo. Neema zako hapa
duniani, na utukufu mbinguni. Kwani ndiwe uliye agana hayo nasi, nawe mwamini.
Amina.
SALA YA MAPENDO
Mungu wangu, nakupenda zaidi ya chochote. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye
kupendeza. Nampenda na jirani yangu, kama nafsi yangu, kwa ajili yako. Amina.
KUTUBU DHAMBI
Tuwaze katika moyo wetu makosa ya leo tuliyomkosea Mungu kwa mawazo, kwa
maneno, kwa vitendo na kwa kutotimiza wajibu. (Husubiri kidogo ).
Nakuungamia Mungu Mwenyezi, nanyi ndugu zangu, kwani nimekosa mno, kwa
mawazo, kwa maneno, kwa vitendo, na kwa kutotimiza wajibu.
Nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana. Ndiyo maana nakuomba Maria
mwenye heri, Bikira daima, Malaika na Watakatifu wote, nanyi ndugu zangu,
niombeeni kwa Bwana Mungu wetu.
Mungu Mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu, atufikishe kwenye uzima wa
milele. Amina.
SALA YA KUWAOMBEA WATU
Ee Mungu, nawaombea watu wa nchi hii, wapate kusikia maneno yako na kukupenda
wewe Bwana Mungu wetu.
SALA KWA MALAIKA MLINZI

7
Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote za roho na za mwili. Amina.
MALAIKA WA BWANA
(kipindi kisicho cha Pasaka)
Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria.
Naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Salamu, Maria,…..
Ndimi mtumishi wa Bwana.
Nitendewe ulivyonena.
Salamu, Maria….
Neno la Mungu akatwaa mwili.
Akakaa kwetu.
Salamu, Maria….
Utuombee, Mzazi mtakatifu wa Mungu.
Tujaliwe ahadi za Kristu.
Tuombe:
Tunakuomba, Ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa
maelezo ya Malaika kwamba Mwanao amejifanya Mtu kwa mateso na msalaba wake
tufikishwe kwenye utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana
wetu. AMINA.
AU;
MALKIA WA MBINGU (kipindi cha Pasaka)
Malkia wa mbingu, furahi, aleluya.
Kwani uliyestahili kumchukua, Aleluya.
Amefufuka alivyosema, Aleluya.
Utuombee kwa Mungu, Aleluya.
Furahi shangilia, ee Bikira Maria, Alaluya.
Kwani hakika Bwana amefufuka Aleluya.
Tuombe.
Ee Mungu, uliyependa kuifurahisha dunia kwa kufufuka kwake Bwana wetu Yesu
Kristu, Mwanao, fanyiza, twakuomba, kwa ajili ya Bikira Maria, tupate nasi furaha za
uzima wa milele. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristu Bwana wetu. Amina.
ATUKUZWE (mara tatu)
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Kama mwanzo na sasa na siku zote na
milele. Amina.

8
KUJIKABIDHI
Enyi Yesu, Maria na Yosefu nawatolea moyo na roho na uzima wangu!
Enyi Yesu, Maria na Yosefu mnijilie saa ya kufa kwangu!
Enyi Yesu, Maria na Yosefu mnijalie nife mikononi mwenu!
(Rehema ya siku 300).
WIMBO:
Kwa heri Yesu mpenzi mwema,
Naenda usiudhike mno.
Nakushukuru, nakupenda,
Kwa hizo nyimbo za mwisho.
Asubuhi nitarudi.
Yesu kwa heri.
Kwa heri Mama mtakatifu,
Sasa napita pumzika.
Asante kwa moyo na nguvu,
Leo umeniombea.
Asubuhi nitarudi.
Mama kwa heri.
Kwa heri Yosefu mnyenyekevu,
Kazi zatimilizika.
Kama mchana, leo usiku,
Nisimamie salama.
Asubuhi nitarudi.
Yosefu kwa heri.
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.
KUOMBA ULINZI WA USIKU
Mungu wangu naenda kulala naomba malaika 14, waende nami, wawili juu, wawili
chini, wawili upande wa kuume, wawili upande wa kushoto, wawili wanifunike, wawili
waniamshe, wawili wanipeleke juu mbinguni. Mimi mtoto mdogo, roho yangu ni
ndogo, haina nafasi kwa mtu yoyote ila kwa Yesu pekee. Amina.
Sala ya Malaika wa Bwana
Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho
Mtakatifu. Salamu Maria,….
9
Ndimi Mtumishi wa Bwana, nitendewe ulivyonena. Salamu Maria, ……
Neno wa Bwana akatwaa Mwili, akakaa kwetu. Salamu Maria, …..
Utuombee, ee Mzazi Mtakatifu wa Mungu, tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe:
Tunakuomba ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo
ya Malaika, kwamba, Kristo Mwanao amejifanya mtu: kwa mateso na Msalaba wake,
utufikishe kwenye utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana
wetu, Amina.

SALA KWA MALAIKA MLINZI


Ee Malaika wangu, uliyewekwa na Mungu mwema unilinde, naomba uniongoze leo,
unitunze, unisimamie, unishauri. Amina.
SALA KWA WENYE KUZIMIA
Ee Yesu mwenye huruma, mpenda roho za watu, nakuomba kwa ajili ya kuzimia kwa
Moyo wako Mtakatifu, na kwa ajili ya Mama Yako asiye na doa, uwatakase kwa damu
yako, watu wote wenye dhambi wanaokufa sasa, na watakaokufa leo.
SALA KWA MT. YOSEFU
Ee Yosef mwenye heri, tunakimbilia kwako, katika masumbuko yetu, na kishaomba
shime ya Mchumba wako Mtakatifu, tunaomba pia kwa matumaini usimamizi wako.
Kwa ajili ya mapendo uliyompenda nayo Bikira Mtakatifu, Mzazi wa Mungu, na kwa
ajili ya tunza ya Baba, uliyomtunza nayo Mtoto Yesu, tunakuomba sana, utuangalie
kwa wema, sisi tuliokuwa fungu lake Yesu Kristo, tuliokombolewa kwa damu yake,
utusimamie katika masumbuko yetu, kwa enzi na shime yako.

SALA KWA MT. YUDA THADEI


(Sala hii inaweza kusaliwa kila siku au kama Novena ya siku tisa mfululizo kuomba
kitu kilekile)
Mtakatifu Yuda Tadei,/ Mtume Mtakatifu,/ Mtumishi mwaminifu na rafiki wa Yesu./
Jina la yule msaliti aliyemwuza Yesu/ limewafanya wengi wakusahau./ Walakini
Kanisa zima linakuheshimu/ na kukuomba kama Msaidizi katika mashaka makubwa,/

10
na katika mambo yasiyo na matumaini tena./
Uniombee mimi mnyonge./ Ninaomba utumie uwezo ule uliojaliwa/ wa kuleta upesi
msaada kwa watu walioukosa./ Unisaidie sasa katika mahitaji yangu,/ ili nipate kitulizo
na msaada wa mbinguni/ katika lazima zangu,/ masumbuko na mateso,/ hasa/ (taja
shida yako)./ Pia ili niweze kumsifu Mungu nawe na wateule wote milele./
Mtakatifu Yuda Tadei,/ utuombee,/ na uwaombee watu wote wanaokuheshimu na
kukuomba msaada./
Baba yetu……. Salamu Maria ……… Atukuzwe ……….
SALA YA KUOMBEA FAMILIA.
Ewe Mungu Mwenyezi, sisi kama familia tunakushukuru kwa zawadi ya Mama Kanisa
Katoliki ambaye siku zote hutupatia malezi bora kwa ajili ya wokovu wetu. Kanisa
halichoki kutuhimiza tutafakari na kuishi utakatifu wa familia ya Nazareti ya Yesu,
Maria na Yosefu. Familia hii iliishi upendo uliojengwa kwa fadhila za imani, uaminifu,
utii, uvumilivu na upole hata wakawa watakatifu. Tunapoadhimisha mwaka wa
Familia, tunaiweka mbele yetu familia ya Nazareti iwe dira, baraka na mfano kwa
familia zetu. Tunakushukuru Baba kwa ajili ya familia zote zinazojitahidi kuishi fadhila
hizo za Familia takatifu na tunakuomba uzidi kuwaimarisha wanandoa ili tupate kwao
mifano mingi na bora ya kuigwa. Ee Bwana, tunaomba Roho Mtakatifu atuangazie
tuweze: kutambua familia kuwa Kanisa la nyumbani na shule ya imani na upendo;
kuimarisha familia kwa sala, sakramenti na tunu za kiinjili na kushirikiana kwa heshima
katika familia kwa usitawi wa roho na wa mwili kwa wanafamilia wote. Tunaziombea
familia zetu na Jumuiya Ndogondogo za Kikristo ziwe bustani bora na salama za
kuchipusha na kulea miito mitakatifu ya Ndoa, Utawa na Upadre. Tunawaombea
vijana na watoto wetu Uchaji wa Mungu ili wawe na bidii ya kujitunza kwa kushika
amri za Mungu na kuishi fadhila za kiinjili, wawe na roho ya kimisionari yaani
walipende Kanisa na kuwa na moyo wa kueneza ufalme wako kwa matendo ya imani.
Baba wa huruma, tunakukabidhi familia zenye misukosuko ya mafarakano, ulevi,
ubinafsi, uregevu-dini, uvivu, ushirikina, hofu, magonjwa sugu na mengineyo yenye
kuleta huzuni; kwa hisani yako uwape neema, mwanga na nguvu za kuanza maisha
mapya yenye amani, waweze kufurahia upatanisho na uponyi wa pendo lako la kibaba
kati yao. Tunaomba toba na msamaha kwa ukatili, manyanyaso na hata mauaji katika
familia zetu na uwaponye wote waliojeruhiwa kwa maneno, matendo na makwazo ya
aina yeyote. Aidha tunakuomba uwe kitulizo na faraja kwa wagonjwa na wazee, pia
tegemeo la yatima na wajane. Wenye matatizo ya kiafya au ya kijamii wasikate tamaa
bali waunganishe hali zao na msalaba wa Mwanao na kukutumaini wewe Mweza yote.
Jamii iwajibike nao kwa kuzijali haki zao na kuwapa misaada wanayohitaji.
Tunakuomba ubariki miradi na kazi zetu ili familia zipate usitawi na maendeleo; na
11
utujalie hekima ya kukushukuru kwa maisha ya haki, amani na ukarimu na mwisho
tukaimbe sifa zako pamoja na familia Takatifu ya Yesu, Maria na Yosefuna jeshi lote la
mbinguni. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina. Baba yetu…
…..Salamu Maria….…Atukuzwe Baba………
SALA YA MEDALI YA MWUJIZA.
Ee Bikira Maria uliyekingiwa dhambi ya asili, utuombee sisi wenye kukimbilia kwako,
uwaombee na wale wasioukimbilia kwako, hasa maadui wa Kanisa Takatifu, na wale
waliokabidhiwa kwako. Amina.

12
SALA KWA YESU KRISTO
NOVENA YA HURUMA YA MUNGU SIKU YA NANE
NOVENA YA HURUMA YA MUNGU SIKU YA NANE, IJUMAA BAADA YA
PASAKA
Novena hii pia inaweza kusaliwa wakati wowote na katika kipindi chochote cha
mwaka lakini inapendekezwa Novena ianzwe katika siku ya Ijumaa.
Tujiandae kusali kwa kuanza na sala za awali kama vile Uje Roho Mtakatifu pamoja na
Sala ya kutubu kisha tuendelee kama inavyoonyeshwa hapa chini:
Maneno ya Mwokozi: “Leo niletee roho za wale WALIOFUNGWA BADO
TOHARANI, na uwazamishe ndani ya Bahari Kuu ya Huruma yangu. Humo,
mafuriko ya Damu yangu, yazimishe miali ya motto mkubwa unaowachoma. Roho
hizi zote hupendwa sana nami. Wako humo toharani kwa ajili ya kulipia Haki yangu
waliyoikosa hapa duniani. Wewe una uwezo wa kuwapatia faraja. Chota rehema zote
za Kanisa langu na uzitolee kwa ajili yao. Ungalijua tu ukali wa mateso yao, loo!
Ungetolea daima sadaka za kiroho kwa ajili yao, na kulipa deni zima la Haki ya
Mungu”.
Kiongozi: Tuwaombee marehemu wa toharani, wanaoilipia Haki ya Mungu, ili
mtiririko wa Huruma wa Damu ya Yesu uweze kupunguza na kufupisha mateso yao.
Wote: Ee Yesu mwenye Huruma uliyesema, “Muwe na Huruma kama Baba yenu wa
mbinguni alivyo na Huruma”. Uzitazame kwa Huruma roho zile zinazoteswa toharani,
kwa kulipia deni la Haki ya Mungu waliyoikosea. Mtiririko ule wa Damu na Maji
uliotoka kwa kasi Moyoni mwako, uzimishe miale ya moto mkali wa toharani, ili huko
pia Huruma yako isifiwe na kuadhimishwa. Amina.
Baba yetu ……. Salamu Maria ……. Atukuzwe ………
Wote: Baba wa Milele, uzitazame kwa wema na huruma, roho zile zinazoteswa
Toharani, wao pia wameingizwa ndani ya Moyo wa Mwanao Mpenzi Yesu, na
uchungu wote ulioelemea Moyo na Roho yake, onyesha Huruma yako kwa roho
zilizotiwa nguvuni na Haki yako. Uwatazame watu hao kwa njia ya Madonda yake

13
Yesu Mwanao Mpenzi, kwa kuwa tunaamini kabisa kuwa wema na Huruma yako
havina mwisho. Amina
Tumia Rozari ya kawaida kusali Rozari ya Huruma ya Mungu kama ifuatavyo:
Baba yetu … Salamu Maria …. X3 Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi …….
Kila penye punje kubwa (Badala ya Baba yetu):
Baba wa Milele, ninakutolea Mwili na Damu, Roho na Umungu, wa Mwanao Mpenzi
sana, Bwana wetu Yesu Kristu, kwa ajili ya malipizi ya dhambi zetu, na dhambi za
dunia nzima.
Kila penye punje ndogo (badala ya Salamu Maria):
Mwanzishaji: Kwa ajili ya mateso makali ya Bwana wetu Yesu Kristu,
Wote huitika: Utuhurumie sisi na dunia nzima.
Mwisho wa Rozari sali mara tatu sala ifuatayo:
Mungu Mtakatifu,
Mtakatifu mwenye Enzi,
Mtakatifu unayeishi milele,
Utuhurumie sisi na dunia nzima (x3).
LITANIA YA HURUMA YA MUNGU
Bwana utuhurumie – Bwana utuhurumie
Kristu utuhurumie – Kristu utuhurumie
Bwana utuhurumie – Bwana utuhurumie
Kristu utusikie – Kristu utusikilize
Baba wa mbinguni Mungu – utuhurumie
Mwana Mkombozi wa dunia Mungu - utuhurumie
Roho Mtakatifu Mungu - utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu mmoja – utuhurumie.
Huruma ya Mungu iliyo sifa kuu ya Muumba wetu - Tunakutumainia (iwe kiitikio)
Huruma ya Mungu iliyo kilele cha ukamilifu wa Mwokozi wetu

14
Huruma ya Mungu iliyo upendo usiopimika wa Roho Mtakasa
Huruma ya Mungu fumbo lisilofahamika la Utatu Mtakatifu
Huruma ya Mungu iliyo ishara ya uwezo mkuu wa Mungu Mwenyezi
Huruma ya Mungu iliyofumbuliwa katika kuziumba Roho za Malaika wa mbinguni
Huruma ya Mungu iliyotuumba na kutuamuru tuwepo bila kutokana na chochote
Huruma ya Mungu inayotujalia maisha ya kutokufa
Huruma ya Mungu inayotukinga na adhabu tunazostahili
Huruma ya Mungu inayotuinua tutoke katika taabu, unyonge na maumivu ya dhambi
zetu
Huruma ya Mungu inayotufanya wenye haki katika Neno aliyejifanya Mtu
Huruma ya Mungu inayofurika kutoka katika majeraha ya Kristu
Huruma ya Mungu inayobubujika kutoka ndani ya Moyo Mtakatifu wa Yesu
Huruma ya Mungu iliyotupatia Bikira Maria Mtukufu awe kwetu Mama wa Huruma
Huruma ya Mungu iliyoonyeshwa katika kuanzishwa Kanisa Katoliki
Huruma ya Mungu inayopatikana katika mafumbo ya Sakramenti Takatifu
Huruma ya Mungu inayotolewa kwa wanadamu wote kwa njia ya Sakramenti ya
Ubatizo na Kitubio
Huruma ya Mungu inayotolewa katika Sakramenti ya Ekaristi na Upadrisho
Huruma ya Mungu inayoonyeshwa kwetu pale inapotuita na kutuingiza katika
kuwatakatifuza wenye haki
Huruma ya Mungu inayotimilika katika ukamilifu wa watu watakatifu
Huruma ya Mungu chemchemi ya afya kwa wagonjwa na wote wanaoteseka
Huruma ya Mungu iliyo faraja ya wote wenye uchungu moyoni
Huruma ya Mungu iliyo tumaini la roho zinazosumbuliwa na mkato wa tamaa
Huruma ya Mungu iliyo mwenzi wa daima na popote wa watu wote
Huruma ya Mungu inayowahi kutuletea neema zake
Huruma ya Mungu iliyo amani yao wanaokufa

15
Huruma ya Mungu iliyo burudisho na faraja yao marehemu wa toharani
Huruma ya Mungu iliyo furaha ya mbinguni kwa watakatifu wote
Huruma ya Mungu iliyo taji la watakatifu wote
Huruma ya Mungu chemchemi ya miujiza isiyokauka
Mwanakondoo wa Mungu uliyetuonyesha huruma yako kuu katika kuikomboa dunia
kwa msalaba wako mtakatifu, - utusamehe ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu unayejitolea kwetu kwa mapendo na huruma katika kila
adhimisho la Sadaka ya Misa Takatifu,- utusikilize ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu anayeondoa dhambi za dunia kwa njia ya huruma yako
isiyo na mwisho,- utuhurumie.
Kiongozi : Bwana utuhurumie –
Wote: Kristu utuhurumie, Bwana utuhurumie.
Kiongozi : Huruma anana za Bwana zi juu ya kazi zake zote –
Wote: Huruma za Bwana nitaziimba milele.
Tuombe: Ee Mungu uliye na huruma isiyo na mwisho, na hazina za wema na upendo
wako hazina mipaka. Tunakusihi ututazame sisi watu wako huku duniani na
kutuongezea huruma yako tena na tena, ili itusaidie tusije tukakata tamaa hata mara
moja, haidhuru tukumbane na majaribu makubwa kiasi gani, bali tuweze daima
kuzielekea na kuzishika amri zako, kwa matumaini na kutimiza mapenzi yako
matakatifu, ambayo ndiyo huruma yenyewe. Tunaomba hayo kwa njia ya Bwana wetu
Yesu Kristu Mwanao, Mfalme wa Amani na Huruma, aishiye na kutawala nawe, na
Roho Mtakatifu, kwa pamoja mkituonyesha huruma, daima na milele. Amina.
NOVENA YA HURUMA YA MUNGU SIKU YA TISA
NOVENA YA HURUMA YA MUNGU SIKU YA TISA, JUMAMOSI BAADA YA
PASAKA
Novena hii pia inaweza kusaliwa wakati wowote na katika kipindi chochote cha
mwaka lakini inapendekezwa Novena ianzwe katika siku ya Ijumaa.
Tujiandae kusali kwa kuanza na sala za awali kama vile Uje Roho Mtakatifu pamoja na
Sala ya kutubu kisha tuendelee kama inavyoonyeshwa hapa chini:

16
Maneno ya Mwokozi: “Leo niletee roho za WALE WALIOKWISHAINGIA HALI
YA UVUGUVUGU, na uwazamishe katika kilindi cha Huruma yangu. Roho hizi
huumiza sana Moyo wangu. Roho yangu iliteseka sana kwa kinyaa cha kutisha kule
bustanini kwa sababu ya roho hizi vuguvugu. Ni wao waliosababisha nilie; Baba ikiwa
ni mapenzi yako uniondolee mbali kikombe hiki nisikinywe. Kwa watu hawa, tumaini
la mwisho lililowabakia ni kuikimbilia Huruma yangu tu basi”.
Kiongozi: Tuwaombee watu walio na hali ya uvuguvugu, hali ya hatari kwa wokovu,
ambao walisababisha mateso makali sana kwa Yesu Kristu kule bustanini mwa
mizeituni.
Wote: Ee Yesu mwenye Huruma nyingi, Wewe u Huruma yenyewe, Uzipokee roho
vuguvugu ndani ya Moyo wako ulio na Huruma bila kiasi. Roho hizi ni kama mizoga
iliyojaa na kunuka uvundo, uziingize katika moto wa upendo wako safi, zitakasike.
Roho hizi zilikutia kinyaa kingi. Sasa uziwashe tena, na kwa Huruma yako, uzipe paji la
Upendo Mtakatifu. Ee Yesu mwenye Huruma Kuu, tumia uwezo wako na uzipatie
roho hizi bidii tena, kwani kwako hakuna kitu kisichowezekana, na kwa njia hii wapate
kuitukuza daima Huruma Yako. Amina.
Baba yetu, Salamu Maria ………..Atukuzwe,
Wote: Baba wa Huruma, uzitazame kwa macho ya Huruma, roho zilizo vuguvugu,
ambazo katika hali yao hiyo, wameingizwa ndani ya Moyo wa Mwanao Yesu, ulio
kilindi cha Huruma. Ee Baba wa Huruma, tunakusihi kwa ajili ya mateso makali ya
Mwanao Mpenzi, Bwana wetu Yesu Kristu, uliyovumilia pale msalabani, kwa masaa
matatu ukiwa katika hali ya umahututi ya uchungu, uziwezeshe hata roho hizi zipupie
utukufu wako. Uijaze mioyo ya watu hawa upendo wa kweli, hivyo kwa Baraka
takatifu, waweze kutenda matendo mengi ya huruma hapa duniani, na huko Mbinguni
wafike kuitukuza Huruma yako Kuu kwa milele yote. Amina.
Tumia Rozari ya kawaida kusali Rozari ya Huruma ya Mungu kama ifuatavyo:
Baba yetu … Salamu Maria …. X3 Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi …….
Kila penye punje kubwa (Badala ya Baba yetu):
Baba wa Milele, ninakutolea Mwili na Damu, Roho na Umungu, wa Mwanao Mpenzi
sana, Bwana wetu Yesu Kristu, kwa ajili ya malipizi ya dhambi zetu, na dhambi za
dunia nzima.
Kila penye punje ndogo (badala ya Salamu Maria):
Mwanzishaji: Kwa ajili ya mateso makali ya Bwana wetu Yesu Kristu,

17
Wote huitika: Utuhurumie sisi na dunia nzima.
Mwisho wa Rozari sali mara tatu sala ifuatayo:
Mungu Mtakatifu,
Mtakatifu mwenye Enzi,
Mtakatifu unayeishi milele,
Utuhurumie sisi na dunia nzima (x3).
LITANIA YA HURUMA YA MUNGU
Bwana utuhurumie – Bwana utuhurumie
Kristu utuhurumie – Kristu utuhurumie
Bwana utuhurumie – Bwana utuhurumie
Kristu utusikie – Kristu utusikilize
Baba wa mbinguni Mungu – utuhurumie
Mwana Mkombozi wa dunia Mungu - utuhurumie
Roho Mtakatifu Mungu - utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu mmoja – utuhurumie.
Huruma ya Mungu iliyo sifa kuu ya Muumba wetu - Tunakutumainia (iwe kiitikio)
Huruma ya Mungu iliyo kilele cha ukamilifu wa Mwokozi wetu
Huruma ya Mungu iliyo upendo usiopimika wa Roho Mtakasa
Huruma ya Mungu fumbo lisilofahamika la Utatu Mtakatifu
Huruma ya Mungu iliyo ishara ya uwezo mkuu wa Mungu Mwenyezi
Huruma ya Mungu iliyofumbuliwa katika kuziumba Roho za Malaika wa mbinguni
Huruma ya Mungu iliyotuumba na kutuamuru tuwepo bila kutokana na chochote
Huruma ya Mungu inayotujalia maisha ya kutokufa
Huruma ya Mungu inayotukinga na adhabu tunazostahili
Huruma ya Mungu inayotuinua tutoke katika taabu, unyonge na maumivu ya dhambi
zetu

18
Huruma ya Mungu inayotufanya wenye haki katika Neno aliyejifanya Mtu
Huruma ya Mungu inayofurika kutoka katika majeraha ya Kristu
Huruma ya Mungu inayobubujika kutoka ndani ya Moyo Mtakatifu wa Yesu
Huruma ya Mungu iliyotupatia Bikira Maria Mtukufu awe kwetu Mama wa Huruma
Huruma ya Mungu iliyoonyeshwa katika kuanzishwa Kanisa Katoliki
Huruma ya Mungu inayopatikana katika mafumbo ya Sakramenti Takatifu
Huruma ya Mungu inayotolewa kwa wanadamu wote kwa njia ya Sakramenti ya
Ubatizo na Kitubio
Huruma ya Mungu inayotolewa katika Sakramenti ya Ekaristi na Upadrisho
Huruma ya Mungu inayoonyeshwa kwetu pale inapotuita na kutuingiza katika
kuwatakatifuza wenye haki
Huruma ya Mungu inayotimilika katika ukamilifu wa watu watakatifu
Huruma ya Mungu chemchemi ya afya kwa wagonjwa na wote wanaoteseka
Huruma ya Mungu iliyo faraja ya wote wenye uchungu moyoni
Huruma ya Mungu iliyo tumaini la roho zinazosumbuliwa na mkato wa tamaa
Huruma ya Mungu iliyo mwenzi wa daima na popote wa watu wote
Huruma ya Mungu inayowahi kutuletea neema zake
Huruma ya Mungu iliyo amani yao wanaokufa
Huruma ya Mungu iliyo burudisho na faraja yao marehemu wa toharani
Huruma ya Mungu iliyo furaha ya mbinguni kwa watakatifu wote
Huruma ya Mungu iliyo taji la watakatifu wote
Huruma ya Mungu chemchemi ya miujiza isiyokauka
Mwanakondoo wa Mungu uliyetuonyesha huruma yako kuu katika kuikomboa dunia
kwa msalaba wako mtakatifu, - utusamehe ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu unayejitolea kwetu kwa mapendo na huruma katika kila
adhimisho la Sadaka ya Misa Takatifu,- utusikilize ee Bwana

19
Mwanakondoo wa Mungu anayeondoa dhambi za dunia kwa njia ya huruma yako
isiyo na mwisho,- utuhurumie.
Kiongozi : Bwana utuhurumie –
Wote: Kristu utuhurumie, Bwana utuhurumie.
Kiongozi : Huruma anana za Bwana zi juu ya kazi zake zote –
Wote: Huruma za Bwana nitaziimba milele.
Tuombe: Ee Mungu uliye na huruma isiyo na mwisho, na hazina za wema na upendo
wako hazina mipaka. Tunakusihi ututazame sisi watu wako huku duniani na
kutuongezea huruma yako tena na tena, ili itusaidie tusije tukakata tamaa hata mara
moja, haidhuru tukumbane na majaribu makubwa kiasi gani, bali tuweze daima
kuzielekea na kuzishika amri zako, kwa matumaini na kutimiza mapenzi yako
matakatifu, ambayo ndiyo huruma yenyewe. Tunaomba hayo kwa njia ya Bwana wetu
Yesu Kristu Mwanao, Mfalme wa Amani na Huruma, aishiye na kutawala nawe, na
Roho Mtakatifu, kwa pamoja mkituonyesha huruma, daima na milele. Amina.
SALA YA KUMWABUDU BWANA YESU KATIKA SAKRAMENTI
TAKATIFU
Ee Yesu Kristu,/ Bwana wangu na Mungu wangu/ ambaye ninasadiki kuwa upo
hapa/ katika Sakramenti Takatifu ya Altare;/ pokea kitendo hiki cha kukuangukia
kifudi fudi/ kama ishara ya tamaa niliyonayo ya kukuabudu Wewe/ bila kuchoka/ na
kukushukuru kwa mapendo yako makubwa/ yasiyo na kipimo/ ambayo Moyo wako
Mtakatifu sana/ unawaka katika Sakramenti Takatifu hii./ Siwezi kukushukuru vizuri
zaidi/ kuliko kama ningetolea kwako/ matendo yangu yote ya kukuabudu/
unyenyekevu wangu/ uvumilivu na mapendo/ ambayo huu Moyo Mwabudiwa
ulifanya,/ bado unafanya/ na utaendelea kufanya katika uzima wa milele mbinguni./
Ninaahidi kupitia Moyo huu,/ nitakupenda,/ nitakutukuza,/ na nitakuabudu kama
nitakavyoweza./ Ninajiunganisha na hii Sadaka Takatifu/ ambayo unatoa kwa Baba
Mungu/ na ninatolea kwako utu wangu./ Ninakuomba kuangamiza ndani yangu/
dhambi zote pamoja na majeraha yake/ na usikubali kunitenga nawe milele./ Amina.
(Na Mt. Margareta Maria Alakoki)
Novena ya Noeli
*Novena ya Noeli (maarufu kama novena ya Mt. Andrea)*

20
Husaliwa kuanzia tar 30 Nov hadi usiku wa Noeli, tar 24 Disemba. Inajulikana kama
novena ya Mt. Andrea kwa sababu novena hii huanza kusaliwa katika siku ya
kumbukumbu ya Mt. Andrea Mtume.
"IHESHIMIWE, NA IBARIKIWE, SAA ILE NA WAKATI ULE, AMBAO
MWANA WA MUNGU, ALIZALIWA NA BIKIRA MBARIKIWA SANA, USIKU
WA MANANE, KULE BETHLEHEM, WAKATI WA BARIDI KALI.
WAKATI HUO, UPENDE E MUNGU WANGU, KUSIKIA MAOMBI YANGU,
NA KUNIJALIA YALE NINAYOYAOMBA KWAKO, KWA NJIA YA
MASTAHILI YA MWOKOZI WETU YESU KRISTO, NA YA MAMA YAKE
MBARIKIWA. AMINA. (Sali mara 15 kwa siku).
Inasadikika kuwa chochote uombacho kwa imani kwa sala hii utakipata mradi kipatane
na mapenzi ya Mungu. Sali na watoto/ familia kuwatafakarisha na kuwaongezea
matazamio juu ya sikukuu ya Noeli.
SALA KWA BIKIRA MARIA
LITANIA YA BIKIRA MARIA
Litani ya Bikira Maria
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utuhurumie
Bwana utuhurumie
Bwana utuhurumie
Kristo utusikie
Kristo utusikilize
Mungu Baba wa Mbinguni,…… Utuhurumie
Mungu Mwana Mkombozi wa dunia ……… Utuhurumie
Mungu Roho Mtakatifu …….. Utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu Mmoja …….. Utuhurumie
Maria Mtakatifu ………. utuombee
Mzazi Mtakatifu wa Mungu …….. utuombee

21
Bikira Mtakatifu Mkuu wa Mabikira …….. utuombee
Mama wa Kristo ……… utuombee
Mama wa Neema ya Mungu ………….. utuombee
Mama Mtakatifu sana ……… utuombee
Mama mwenye usafi wa Moyo ……….. utuombee
Mama mwenye ubikira ……….. utuombee
Mama usiye na doa ……….. utuombee
Mama mpendelevu ………. utuombee
Mama mstajabivu ………. utuombee
Mama wa Muumba ………. utuombee
Mama wa Mkombozi ………….. utuombee
Mama wa Kanisa……….. utuombee
Bikira mwenye utaratibu ………….. utuombee
Bikira mwenye heshima ………….. utuombee
Bikira mwenye sifa ………….. utuombee
Bikira mwenye uwezo ………….. utuombee
Bikra mweye huruma ………….. utuombee
Bikra mwaminifu………….. utuombee
Kioo cha haki ………….. utuombee
Kikao cha hekima ………….. utuombee
Sababu ya furaha yetu ………….. utuombee
Chombo cha neema ………….. utuombee
Chombo cha kuheshimiwa ………….. utuombee
Chombo bora cha ibada ………….. utuombee
Waridi lenye fumbo ………….. utuombee
Mnara wa Daudi ………….. utuombee

22
Mnara wa pembe ………….. utuombee
Nyumba ya dhahabu ………….. utuombee
Sanduku la Agano ………….. utuombee
Mlango wa Mbingu ………….. utuombee
Nyota ya asubuhi ………….. utuombee
Afya ya wagonjwa ………….. utuombee
Kimbilio la wakosefu ………….. utuombee
Mtuliza wenye huzuni ………….. utuombee
Msaada wa waKristo ………….. utuombee
Malkia wa Malaika ………….. utuombee
Malkia wa Mababu ………….. utuombee
Malkia wa Manabii ………….. utuombee
Malkia wa Mitume ………….. utuombee
Malkia wa Mashahidi ………….. utuombee
Malkia wa Waungama dini ………….. utuombee
Malkia wa Mabikira ………….. utuombee
Malkia wa Watakatifu wote ………….. utuombee
Malkia uliyepalizwa Mbinguni ………….. utuombee
Malkia wa Rozari takatifu ………….. utuombee
Malkia wa amani ………….. utuombee

Mwanakodoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utusamehe ee


Bwana.
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utusikilize ee
Bwana
Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za dunia,…………..Utuhurumie.

23
Utuombee, Mzazi Mtakatifu wa Mungu,…………..Tujaliwe ahadi za Kristo.
Tuombe
Ee Bwana Mungu, utujalie sisi watumishi wako afya ya roho na mwili siku zote; na
kwa maombezi matukufu ya Maria Mtakaatifu Bikira daima, tuopolewe na mashaka ya
saa, tupate na furaha za milele. Kwa Kristo Bwana wetu, Amina.
Matendo ya Rozari Takatifu
MATENDO YA FURAHA (Jumatatu na Jumamosi)
Tendo la kwanza; Malaika Gabrieli anampasha habari Maria kuwa atakuwa Mama wa
Mungu. Tumwombe Mungu atujalie unyenyekevu.
Tendo la pili; Maria Mtakatifu anakwenda kumtembelea Elizabeti. Tumwombe Mungu
atujalie mapendo ya jirani.
Tendo la tatu; Yesu anazaliwa Betlehemu. Tumwombe Mungu atujalie moyo wa
ufukara
Tendo la nne; Yesu anatolewa hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie usafi wa moyo.
Tendo la tano; Maria anamkuta Yesu hekaluni. Tumwombe Mungu atujalie kuwatii
wakubwa wetu.
MATENDO YA UCHUNGU (Jumanne na Ijumaa)
Tendo la kwanza; Yesu anatoka jasho la damu kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu
atujalie sikitiko la dhambi.
Tendo la pili; Yesu anapigwa kwa mijeledi kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie
kuacha dhambi za uchafu.
Tendo la tatu; Yesu anatiwa miiba kichwani kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie
kushinda kiburi.
Tendo la nne; Yesu anachukua Msalaba kwa ajili yetu. Tumwombe Mungu atujalie
kuvumilia taabu.
Tendo la tano; Yesu anakufa Msalabani. Tumwombe Mungu atujalie kuwapenda Yesu
na Maria.
MATENDO YA UTUKUFU (Jumatano na Jumapili)

24
Tendo la kwanza; Yesu anafufuka. Tumwombe Mungu atujalie kugeuka watakatifu.
Tendo la pili; Yesu anapaa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kwenda mbinguni.
Tendo la tatu; Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Tumwombe Mungu atujalie bidii
katika dini yetu.
Tendo la nne; Bikira Maria anapalizwa mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie kufa
vizuri.
Tendo la tano; Bikira Maria anawekwa Malkia mbinguni. Tumwombe Mungu atujalie
kudumu katika njia njema.
MATENDO YA MWANGA (Alhamisi)
Tendo la kwanza; Yesu anabatizwa Mto Jordani. Tumwombe Mungu atujalie uaminifu
kwa ahadi zetu za ubatizo.
Tendo la pili; Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana. Tumwombe Mungu atujalie
kuukoleza ulimwengu kwa chachu ya enjili.
Tendo la tatu; Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. Tumwombe Mungu atujalie
kupokea Ufalme wake kwa toba ya kweli.
Tendo la nne; Yesu anageuka sura. Tumwombe Mungu atujalie neema ya kuung’arisha
ulimwengu kwa uso wa Yesu.
Tendo la tano; Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristia. Tumwombe Mungu atujalie
neema ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wengine.

SALA KWA BIKIRA MARIA KATIKA UKIWA WAKE


Nakusikitikia sana Mama Mtakatifu Maria kwa sababu ya ukiwa wako mkuu. Uchungu
wako ulikuwa mkubwa sana ulipotazama mateso na kifo cha Mwana wako mpenzi.
Muda ule uliweza kutuliz kidogo kwa sababu ya kumwona angali hai. Lakini je, baada
ya kufa na kumzika? Sasa wewe ni mkiwa mkubwa mno! Uh, ukiwa wa pekee,
uniombee mimi ninayempoteza mara nyingi kwa dhambi zangu. Unijalie nisimpoteze
tena Yesu wangu kwa ubaya wa uvivu wangu, bali nimtumikie kiaminifu duniani hapa
ili nimwone na kumfurahia milele mbinguni. Amina.

25
Kuomba kifo chema
Enyi Yesu na Maria na Yosefu,nawatolea Moyo, na roho, na uzima wangu. Enyi Yesu
na Maria na Yosefu, mnipokee saa ya kufa kwangu. Enyi Yesu na Maria na Yosefu,
mnijalie nife mikoni mwenu.
amina
Majitoleo
Ee Yesu, kupitia mikono safi ya Bikira Maria, na kwa maungano na sadaka yako kuu,
ninakutolea sala, matendo, kazi, masumbuko, na furaha zangu zote za siku hii ya leo,
kwa ajili ya nia za Moyo wako Mtakatifu, Ee Yesu ufalme wako utufikie!
Baba Yetu….
Salamu Maria, …..
Nasadiki …….
Amri za Mungu ……
Amri za Kanisa …

26

You might also like