You are on page 1of 9

NJOONI TUMFANYIE SHANGWE MUNGU

Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu,

Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu.

Inukeni wote tuimbe pamoja

Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu.

Kwa miondoko ya raha na kucheza

Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu.

Kwa ngoma safi tamu na za midundiko

Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu.

(Tumpigie) makofi makofi (makofi) x12

Ona ametenda wema wa ajabu

Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu.

Machozi ameyageuza kicheko

Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu.

Tumwimbie leo tumsifu yeye

Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu.

Tukipigapiga vifua kwa maringo

Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu.

Tumpungieni mikono kw madaha

Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu.

Ajue kwamba leo tumefurahi

Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu.

Na shingo zinesenese kwa midundo

Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu.

Mwili uyumbeyumbe kushoto kulia

Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu.


Watoto nao wabebwe juu juu

Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu.

Wajue kwamba Mungu anawapenda

Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu.

Umati wote urukeruke juu

Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu.

Tusisitesite Mungu yu kati yetu

Njooni tumfanyie shangwe Mungu wetu.

MISA: ST. VERONICA


Bwana twakuomba tuhurumie,tuhurumie sisi wakosefu x2
Ee kristu twakuomba tuhurumie,tuhurumie sisi wakosefu x2
Bwana twakuomba tuhurumie,tuhurumie sisi wakosefu x2
UTUKUFU
1.Utukufu kwake mungu na Amani duniani,kwa watu wote wenye mapenzi yale mema x2
Tunakusifu baba pia twakueshimu,
Tunakuabudu baba sisi twakutukuzax2
2.Tunakushukuru mungu kwa utukufu wako,Ee Bwana Mungu ndiwe mfalme wa mbingunix2
3. Mwenye kuziondoa dhambi za dunia,utuhurumie baba kwa rehema zako wewex2
4. Mwanakondoo wa Mungu mwana wake Baba,utuhurumie sisi upokee ombi letu x2
5. Ewe mwenye kuketi kuume kwake Baba,utuhurumie sisi uliye mtakatifu x2
6. Bwana mkuu Yesu Kristu naye Roho mtakatifu,mwenye kushiriki utukufu wa Mungu Baba x2
AMACEA MASS
Sop/alt: Bwana utuhurumie (ee Bwana)
All: Bwana utuhurumie
Ten/bass:Kristu utuhurumie (ee Bwana)
All: Kristu utuhurumie
Sop/alt: Bwana utuhurumie (ee Bwana)
All: Bwana utuhurumie
UTUKUFU KWA MUNGU
1. Utukufu kwa Mungu juu mbinguni
Na amani kote duniani (kwa watu) wenye mapenzi mema:
Tunakusifu Baba tunakuheshimu twakuabudu sisi tunakutukuza x2
2. Twakushukuru Mungu kwa tukufu wako mkuu ewe Mungu
Mfalme (ee Baba)wa mbingu Baba yetu.
3. Bwana wetu mwokozi Yesu Kristu
Mwana wa pekee wake Mungu (uliye) Mwana kondoo wa Mungu
4. Unayeziondoa dhambi zote
Za dunia utuhurumie (pokea) pokea ombi letu
5. Wewe unayeketi kuume
Kwake Baba utuhurumie (sikia)sikia ombi letu
6. Kwani pekee yako ndiwe mfalme
Pekee yako mkuu na mkombozi (pekee) pekee Yesu Kristu
7. Kwa umoja war oho mtakatifu
Ndani yake baba watukuzwa (ee yesu )milele na milele.

MATAKATIFU
Mtakatifu, mtakatifu Bwana,Mungu wa majeshi x2
Mbingu na dunia zimejaa,zimejaa,mbingu na dunia zimejaa utukufu wako
Hosana juu x4 mbinguni x2
Mbarikiwa anayekuja x2 Mbarikiwa, mbarikiwa anayekuja kwa jina, jina lake Bwana
Hosana juu x4 mbinguni x2
MWANA KONDOO
Tenor:Mwana kondoo wa mungu uondoaye dhambi za ulimwengu
Ee mwana utuhurumie
Sop: Mwana kondoo wa mungu uondoaye dhambi za ulimwengu
Ee mwana utuhurumie
Bass: Mwana kondoo wa mungu uondoaye dhambi za ulimwengu
Ee mwana utujalie amani
OUR LADY OF MERCY
Bwana Tuhurumie
Bwana Tuhurumie
Bwana Tuhurumie Sisi wakosefu
Kristu Tuhurumie
Kristu Tuhurumie
Kristu Tuhurumie Sisi wakosefu
Bwana Tuhurumie
Bwana Tuhurumie
Bwana Tuhurumie Sisi wakosefu
Utukufu kwa Mungu mbinguni
Utukufu kwa Mungu mbinguni na amani duniani kwao watu kwao watu,
kwa watu wenye mapenzi mema x2
Tunakusifu,twakuheshimu twakuabudu,twakutuza
Twakushukuru mfalme wa mbingu,mwana
wa pekee mwana wa baba Bwana

Unayeondoa makosa yetu,tuhurumie tusikilize,


Kuume kwa Baba unapoketi, mtakatifu mkuu tuhurumie Bwana

Pamoja na roho mtakatifu,ndani ya baba unatukuzwa


Mungu mmoja anayeishi,yeye mtawala milele yote Bwana.
GOSPEL SONGS
UKIITWA ITIKA {NYABURURU}
1. Nimekuja Bwana kuyafanya aa- mapenzi yako,
Naitika wito kueneza aa-injili yako x2
Ukiitwa itika x3 Sema Bwana ndiox2
2. Milimani mabondeni kote ee-nitume Bwana,
Mito pia nyika nienendee ee-nitume Bwana x2
3. Nijalie Mungu ujasiri ii -nitume Bwana,
Nitangaze neno lake Bwana aa-nitume Bwana x2
4. Nitakwenda kote duniani ii-nitume Bwana,
Nihubiri watu wote waokoke ee-nitume Bwanax2
5. Japopita barabara mbovu uu-nitume Bwana
Niongoze Bwana niwe salama aa- nitume Bwanax2
UMNIITA
1. Nasikia sauti nzuri kama ya malaika, ni sauti toka mbinguni sauti ya Mungu aniita
mimi niende nikamtumikie anitume shambani mwake nikavune yote
Umeniita,nimeitika wito nakuja kwako leo najongea mbele zako bwana
nipokee mimi, niko tayari, nimeacha yote, najikabidhi kwako unitume popote name
nitakwenda haraka x2
2. Ninaenda mimi naenda ninaenda mwenyewe,ninaenda mbele za Bwana sitarudi
nyuma,ndugu zangu na marafiki mniache niende nikafanye kazi ya Bwana
nitakapotumwa.
3. Nilitazama moyo wako moyo wako mwanangu,hata kabla hujazaliwa
nilikutambua,nilikuteuwa mapema kati ya ndugu zako uwe kuhani wangu mimi
kuhani mkuu.
4. Shamba lake Bwana ni kubwa na mavuno ni mengi,wavunaji ndio wachache
nitaenda mimi. Nakuomba sana ee Bwana nipeleke shambani,nikavune mavuno
mema yaliyo tayari.
5. Uwe name siku kwa siku wala usiniache, unikinge na majaribu nilinde daima.
Nipeleke habari njema ulimwenguni mwote ,watu wote wakutambue wakugeukie.

NIMESIKIA BWANA
1. Nimesikia Bwana wewe waniita-Nikatangaze neno lake Bwana x2
Nami nakuja - ninakuja nakuja, nitume mimi-
Nitume mimi Bwana x2
2. Kwa walio wagonjwa unitume mimi-nikatangaze neno lake Bwanax2
3. Kwa walio wafungwa unitume mimi-
4. Wamao huzunika unitume mimi-
5. Walo vunjika nyoyo unitume mimi-
WAKRISTO WOTE TUSIMAME
1. Wakristo wote tusimame-tutangaze, injili yake Bwana yesu iende mbele x2
Iende mbele- injili iende mbele,
Injili ya Yesu-injili iende mbele x2
2. Walimu wote tusimame-
3. Watoto wote tusimame-
4. Mapadri wote tusimame-
5. Watawa wote tusimame-

OFFERTORY
SADAKA YANGU
Sadaka yangu kwako ee Mungu
Ni moyo mnyofu
Na uliopodeka
Tazama wapendeza na kweli ya moyo,nawe wanijulisha hekima kwa siri
Nioshe kabisa na uovu wangu,na kinywa change kitanena sifa zako
1. Maana wewe Bwana hupendezwi na dhabihu za kuteketezwa
ama sivyo mimi ningalikutolea
2. Wapendezwa na dhabihu za haki kuto-ka kwa moyo mnyofu
Zitolewazo juu ya madhabahu yako
3. Ee Mungu wa wokovu wangu,unipe moyo radhi wa utii
Usiniondilee roho wako mtakatifu.

NITAKWENDA MIMI MWENYEWE


Nitakwenda mimi mwenyewe nikatoe sadaka kwa Bwana
(Aliyeniumba mimi,aliyeniumba mimi,aliyeniumba mimi mungu wangu, mungu
wangu,Mungu wangu kwa kuniumba hadi nikapendeza x2
1.Kaniumba kwa mfano wake kuliko viumbe vingine, na sasa nikatoe shukrani
2. Vyote nilivyo navyo ni vyake nimrudishie kwa mapendo,na sasa nikatoe
shukrani.
3.Mema mengi amenijalia ya mbinguni na duniani, na sasa nikatoe shukrani
CHETESO
SALA YANGU IPAE
Sala yangu na ipae mbele yako{na ipae}, kama moshi wa ubani x2
1. Ee Bwana upokee sadaka yetu tunayokutolea kama shukrani yetu ee Bwana
pokea
2. Ee Bwana upokee dhabibu zetu tunazokutolea kutoka mashsmbani ee Bwana
pokea.
3. Ee bwana upokee pia nia zetu tunazokutolea kwa moyo wetu wote ee Bwana
pokea.

AMANI-AKAMBA
Amani ya Bwana Yesu,Amani iwe nawe x2
Ewe mwenzangu pokea-amani Amani –ya Yesu x2

COMMUNION
DO NOT BE AFRAID
Simama imara katika Imani x2usiogope,usiogope,usiogope tula katika
maombi,(do not be afraid)x2,do not be afraid,stand strong in faith.
1. Watesi wako wanapokuzunguka.
Moyo wako usiwe na hofu,umtumaini mwokozi Yesu,ewe mteule
2. Hata shetani abishe kwako mpenzi
Moyo wako usiwe na hofu umtumaini mwokozi Yesu,ewe mteule
2. Uwapo kwenye giza totoro
Moyo wako usiwe na hofu mtumaini mwokozi Yesu,ewe mteule

THANKSGIVING SONG
ASANTE YESU
1. Enyi viumbe vyote…
Twendeni mbele zake Bwana
Kwa moyo wa shukrani…
Twendeni mbele zake bwana

Twakushukuru……
Ee Yesu twakushukuru sana x2.
Kwa zawadi ya maisha ya Baraka ulionikirimia,ni upendo wa ajabu
Ulionipa ewe Mungu wangu nitaimba kukusifu, kwa sauti na alatamu,
Jina lako litukuzwe milele na hata milele.
ASANTE YESU WANGU X4
{Twakushukuru } ee Yesu
Twakushukuru sana.
2. Kwa kinywa change nitakushukuru na kukuimbia,{aee}
Kwa wema wako ulionijalia maishsni mwangu.
{asante} ee Yesu…x4 Asante sana x4
3. Ulionpa ni mengi sana siwezi kuhesabu {aee} kwa wema
Wako ulinijalia mimi mja wako.
{Asante} ee Yesu…x4 asante sana.x4
4. Nakurudishia sifa na utukufu ewe Mungu {aee}
Uhimidiwe milele yote uhimidiwe ee Bwana.
{Asante }ee Yesu …x4 asante sana x4.
KONGOI MISING
Kongoi we kongoi cheptalel kongoi we Baba kongoi missing
Twakushukuru Mungu maana we yu mwema kongoi we Baba kongoi missing
1. Wakati wa machozi wewe ndiwe tulizo,wakati wa hasira wewe ni kitulizo
(hakika)wakati wote baba wewe ni tegemeo
2. Giza likitokea wewe ndiwe mwanga,magonjwa yakijiri wewe ndiwe
tabibu(hakika) wakati wote baba wewe ni tegemeo.
3. Adui wangu woteumwaaibisha japo ni wengi sanakama nywele za kichwa
(hakika) wakati wote baba wewe ni tegemeo.
4. Wakati wa njaa wewe ni msaada,wajane mayatima unawalinda wote
(hakika) wakati wote baba wewe ni tegemeo.
TAZAMENI NYOTA YA ASUBUHI
Tazameni {nyota} ya asubuhi inang’aa {hakika} yapendeza x2
Nyota hiyo {ni} mama Maria, njooni nyote tumshangilie mama x2.
1. Yeye ndiye Bikira amini
Yeye ndiye nyumba ya dhahabu.
2. Yeye ndiye mlango wa mbingu,
Yeye ndiye chombo cha heshima.
3. Yeye ndiye mama mpendelevu
Yeye ndiye asiye na dhambi
4. Yeye ndiye Biukira wa enzi
Yeye ndiye mama wa huruma

MWANZI ULIOPONDEKA
1. Utambi mchafu wa moshi mzito,hata uzima kadhalika mwanzi
Uliopondeka kamwe hatauvunja.
Hatanitupa Bwana yesu,milele yote atanipigania
Hataniacha Bwana Yesu,niangamie atanipigania
2. Najua mtetezi wangu ni mwema
Mwenye huruma mwingi wa rehema
Asiyeyahesabu maovu ya watu
3. Nakiri mimi mdhaifu kabisa,nimeanguka kulitii neno
Lakini nitamuangukia mwenyezi
4. Nanyi ndugu zangu kwenu natubu
Niliyofanya sikuwapendeza nisameheni nichukulieni pia

You might also like