You are on page 1of 10

MAOMBI ASUBUHI, MCHANA HATA USIKU

Baba umenipa funguo muhimu katika Mathayo 16:19 za kufunga na kufungua. Ninatumia
funguo hizo kufunga na kufungua, kuvunja na kubamiza kila kitu ambacho kinazuia kutimizwa
kwa mipango yako kamili katika maisha yangu. Ninaamuru na kutangaza kwamba kila mnyororo,
kamba, gereza, pingu kwamba zimefunguliwa, zimekatwa, na kuondolewa kutoka kwenye
maisha yangu katika jina la Yesu.

Baba, Bwana Nakushukuru, kwamba wewe pekee ndiye hakimu wa maisha yetu, kwa mujibu wa
Yeremia 17:9-10 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani
awezaye kuujua? Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi
cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.

Baba naomba katika jina la Yesu, kwa mujibu wa Zaburi 22:19 Nawe, Bwana, usiwe mbali, Ee
Nguvu zangu, fanya haraka kunisaidia. Baba naomba kwamba utusaidie, na kutupa uvumilivu
wa kusubiri mapenzi yako kutimizwa.

Baba katika jina la Yesu, neno lako liniasema katika Isa 41:10-12 usiogope, kwa maana mimi ni
pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam,
nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu. Tazama, wote walioona
hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na
kuangamia. Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa
kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako.

Baba, ninakubaliana na neno lako lenye nguvu, uweza, uhakika, na la kujiamini, kwamba
utawalinda watu wako dhidi ya maadui. Umetuambia kwamba kisasi ni chako asema Bwana, na
utawalipa waovu. Bwana Ninakushukuru, kwa ajili ya ulinzi wako, na neno lako la nguvu na la
ukombozi. Katika jina la Yesu.

Baba tunakushukuru kwa neno lako linalosema katika Ayubu 5:12 Yeye huyatangua mashauri ya
wadanganyifu, Mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao. Baba wa Mbinguni, ninachukua
mamlaka ya neno lako kufunga, kufuta na kung’oa mipango yote miovu ya adui, nakuifanya
kuwa utupu, batili, na kuifuta kwa jina la Yesu.

Baba katika jina la Yesu, umesema katika Zaburi 27:2 "Watenda mabaya waliponikaribia, wanile
nyama yangu, watesi wangu na adui zangu, walijikwaa wakaanguka." Asante Bwana kwa ulinzi
wako. Asante Bwana, kwasababu unatalnda. Wakati maadui zetu wanakuja kula nyama yetu,
tunakuwa dhaifu, tumelala kiroho, tumekata tamaa, lakini uwezo wako katika damu umeruhusu
maadui kuanguka ndani ya shimo la kuzimu. Asante Mungu wa huruma na neema, kwa upendo
wako wa milele kwa watu wako.

Baba neno lako linasema nami katika Luka 10:19 kwamba “Tazama, nimewapa amri ya
kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.”
Bwana natumia uwezo wako na mamlaka yako, ili kuvunja, kubamiza, kuponda, kung’oa,
kutawanya vipande vipande, kila mipango ambayo shetani ameandaa dhidi ya maisha yangu,
familia yangu, huduma yangu, nyumba yangu, uhusiano, fedha, na vitu vyote vilivyo vyangu.
Nakushukuru Bwana, na ninadai ushindi kamili katika jina la Yesu.

Baba nasimama sawa sawa na neno lako katika Ayubu 6: 8 linalosema “Laiti ningepewa haja
yangu, Naye Mungu angenipa neno hilo ninalolitamani sana!” Bwana Naomba katika jina la
Yesu kwamba ombi letu utalijibu kulingana na mapenzi yako na kwa wakati, na utatupa vitu
vilivyomo katika mapenzi yako kwa ajili yetu.

Baba katika jina la Yesu kulingana na Wafilipi 4:6 unatuambia “Msijisumbue kwa neno lo lote;
bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na
Mungu.” Bwana nakushukuru, kwamba tunaweza kuja kwako wakati wowote kwa maombi ili
haja zetu zijulikane kwako.

Baba kama ulivyosema katika Zaburi 23:1 Wewe ni mchungaji wangu, sitapungukiwa au kukosa
vitu vyovyote vizuri katika maisha yangu. Wewe ni Mungu ambaye unatupatia mahitaji yetu
yote. Nakiri kama ulivyosema, kwamba huwezi kuzuia mambo yoyote mazuri kwa watoto wako.
Baba nadai faida zako zote za kiroho, na za kimwili. Katika Jina la Yesu.

Baba umetuambia katika neno lako, katika Luka 17:6 kwamba “Bwana akasema, Kama
mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng'oka, ukapandwe
baharini, nao ungewatii.” Baba nachukua mamlaka ya neno lako leo, na kung’oa madeni yote ya
kifedha, kila mapambano, kila misiba, kila ukosefu, uhitaji, na roho zote zinazoshambulia fedha
zetu, afya, ndoa, nyumba, watoto, huduma, kazi zetu, na yote yaliyo yetu. Nazifunga,
nakuzing’oa toka kwenye maisha yetu, na kuzitupa katika bahari. Katika jina la Yesu.

Baba umeniambia katika 2 Tim. 4:18 kwamba “Bwana ataniokoa na kila neno baya, na
kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.”
Baba nakushukuru kwa kuwa umeniokoa na kila matendo maovu ya adui, na kunihifadhi kwa
ajili ya ufalme wako wa mbinguni. Baba ninasimama sawa sawa na neno lako na kuyafunga kila
matendo maovu, yaliyofanywa maishani kwangu, watoto wangu, familia yangu, nyumbani
kwangu, huduma yangu, afya yangu, fedha zangu, mustakabali wangu na vitu vyote
tunavyomiliki. Ninayafunga toka mashariki, magharibi, kaskazini na kusini, mbingu ya pili,
katika maji, kwenye moto, katika hewa, katika ardhi, katika maeneo, katika mazingira, na kila
maeneo chini ya jua, mwezi, nyota, na sehemu nyingine zote za siri yanakojificha. Ninaachilia
neno lako, damu ya Yesu, na jina lako dhidi yao, katika maeneo hayo yote, kwamba yatakuwa
yamefungwa milele na milele amina.

Baba natumia funguo muhimu katika Mathayo 18:18 kwamba “na yo yote mtakayoyafungua
duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.” Ninajifungua, pamoja na kila kitu changu, toka
kila mnyororo, vifungo, pingu, na kamba katika jina la Yesu.
Baba kama ulivyosema katika kitabu cha Hesabu 11:1. Nasimama kwenye mamlaka ya neno
lako, na amrisha moto ushuke kutoka mbinguni na kuharibu kila roho ya kurudi nyuma ambayo
imewekwa na adui katika maisha yetu. Katika jina la Yesu.

Baba, Bwana nasimama sawasawa na neno lako katika Joshua 1:8. Naomba maneno yako
yasindoke vinywani mwetu wala mioyoni mwetu, bali tuyatafakari mchana na usiku, ndipo
tutakapoifanikisha njia yetu.

Bwana ninaomba mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki,
yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote,
ikiwapo sifa nzuri yo yote, niyatafakari hayo sawasawa na neno lako, katika Wafilipi 4: 8.

Baba umeniambia katika 2 Timotheo 1:7 kwamba Mungu hakunipa roho ya woga, bali ya nguvu
na ya upendo na ya moyo wa kiasi. Baba napinga roho ya woga, nakataa kuwa na wasiwasi, au
kukatishwa tamaa. Nautumia nguvu yako na mamlaka juu ya kila mipango na miradi ya adui.
Nadai ushindi kamili juu ya nguvu zote za giza, katika jina la Yesu.

Baba neno lako linasema katika Yer 23:29 " Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na
kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande? Baba katika jina la Yesu, natumia moto wa
Mungu kuteketeza kila uovu dhidi yangu, na wapendwa wangu, toka mashariki, magharibi,
kaskazini na kusini. Natumia nyundo ya neno la Mungu kuvunja kila uovu wa vifungo vya nafsi,
uhusiano wa damu, uchawi na laana zote mababu, uliopitia kwa uzao wetu. Najifunika, pamoja
na kizazi cha pili, cha tatu na cha nne, kwa damu ya Yesu. Naachilia baraka za Bwana juu yetu,
baraka za kizazi hadi kizazi, baraka za Ibrahimu, na baraka zote. Katika jina la Yesu.

Baba katika jina la Yesu. Navaa silaha zote za Mungu, napokea chapeo ya wokovu, navaa dirii
ya haki kifuani, natwaa ngao ya imani, najifunga kweli kiunoni, nafungiwa miguu yangu utayari
niupatao kwa injili ya amani na upanga wa roho ambao ni neno la Mungu kwa sala zote na
maombi nikisali kila wakati katika Roho kwa mujibu wa Efeso 6: 10-18

Baba kwa mujibu wa neno lako katika Yer 30:17 Ulisema “Maana nitakurudishia afya, nami
nitakuponya jeraha zako, asema Bwana.” Nakushukuru kwa kutuponya machungu yetu,
majeraha, makovu, na maumivu. Nakushukuru kwa ajili ya kuturejesha tena. Katika Jina la Yesu.

Baba katika Isa 53: 4-5, Ulisema “Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona." Bwana nakushukuru
kwa neno lako, lina nguvu, linatupatia nguvu, ujasiri, ulinzi, na uponyaji katika jina la Yesu.

Baba nakushukuru, kama ulivyosema katika Zaburi 46:1 kwamba wewe ni kimbilio na nguvu,
msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Nakushukuru kwa kuwa tunaweza kukuita wakati
wa shida.

Baba nasimama sawa sawa na neno lako katika Marko 3:27. Namfunga huyo mtu mwenye
nguvu, nakuvunja kila vizuizi, kamba, vifungo, pingu, minyororo, minyororo ya utumwa, kutoka
katika maisha yangu, wapendwa wangu, na yote yaliyo yangu. Ninaamrisha mali za mwenye
nguvu kuharibiwa, sasa na hata milele. Katika jina la Yesu.

Baba nakushukuru kwa ulinzi wako, ulisema katika neno lako katika Kutoka 23:27 " Nitatuma
utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami
nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao na kukimbia. Namshukuru wewe
Bwana, kwa nguvu iliyopo katika neno lako ambayo husababisha maadui kuonyesha maungo
yao na kukimbia. Katika jina la Yesu.

Baba katika jina la Yesu ninafungua machafuko na upofu wa mungu wa dunia hii, kutoka
kwenye akili zetu, ambazo zinatuzuia kuona mwanga wa injili ya Kristo. Ninaita kila neno la
Mungu linaloingia kwenye akili zetu, na moyo liinuke kwa nguvu ndani yetu.

Baba wa Mbinguni, asante ninakushukuru wewe, ninakutukuza wewe, ninakuabudu wewe,


nakushukuru kwa neno lako katika Kumbukumbu 28:7 Bwana atawafanya adui zako wainukao
juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa
njia saba. Asante kwa nguvu yako, ulinzi, na usalama ambao umetoa kwa watoto wako,
tukitumia neno, maadui si tu watakimbia, bali watakimbia kwa njia saba kutoka kwetu, katika
jina la Yesu.

Baba nakushukuru, kwa mikono yako imara, na mkono wako wa haki wa kulia. Umetuambia,
katika 1 Petro 5: 7 Tumtwike yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na
mambo yenu. Bwana nakushukuru kwa kujishughulisha na mambo yetu, nakushukuru kwa kuwa
tayari kwa ajili yetu wakati tunakuhitaji.

Baba katika jina la Yesu ninaliadhimisha jina lako; nakupa heshima na utukufu wote unaotoka
kwenye jina lako takatifu. Neno lako linaniambia katika Joshua 1:5 “Hapatakuwa mtu ye yote
atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na
Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia kamwe wala sitakuacha.” Asante
Bwana kwa ulinzi wako, na baraka.

Baba nakushukuru kwa neno lako katika 3 Yohana 1:2 linasema kwamba mipango yako kwa ajili
yetu ni ya kutufanikisha, na kuwa na afya njema kama vile roho zetu zifanikiwavyo. Natumia
mamlaka ya neno lako, na kudai ustawi, afya, furaha, mafanikio, amani ya akili, baraka, na kila
mambo mema ambayo umepanga tupate, juu ya maisha yangu, wapendwa wangu, mali na vitu
vyote nilivyonavyo, katika jina la Yesu.

Baba wa mbinguni neno lako katika Luke 8:11 linatuambia kwamba neno lako ni mbegu, na
mioyo yetu ni ardhi. Bwana ninakuomba utayarishe mioyo yetu kupokea neno lako na kulificha
katika mioyo yetu, tusitende dhambi dhidi yako, kwa jina la Yesu.
MAOMBI YA KUMTEKETEZA SHETANI "NGUVU ZA GIZA"

Kuna watu wanapitia mateso mengi sana, wengine wamefungwa katika vifungo bila wao
kujijuwa basi chukua muongozo huu utakusaidia au itasaidia familia yako.

Biblia inapozungumza habari ya watu waliofungwa wapate kufunguliwa, hii ina maana ya kuwa
kuna watu wamefungwa chini ya utawala wa nguvu za giza katika ulimwengu wa Roho. Watu
hawa wamefungwa kwenye magereza na Ibilisi.

Tutambue ya kuwa Yesu aliposema amekuja kutuokoa hii inamaanisha kwamba kuna mahali
ambako tusingeweza kujikwamua wenyewe bila nguvu yake yeye mwenywe kuingia kati yetu.

MAOMBI YA KUMTEKETEZA SHETANI:

Baba katika Jina la Yesu:

1. Ninayaharibu na kuyateketeza mamlaka yote aliyopewa shetani na mababu/ mababa, ndugu


zangu katika Jina la Yesu.

2. Nina zilaani na kuziteketeza kwa damu ya Yesu roho zote zinazoendelea kutilia mkazo hayo
maagano katika maisha yangu na naziteketeza na kuzivunavunja kwa Jina la Yesu.

3. Kitu chochote kilichoingizwa kwenye maisha yangu,kwa mkono wa kipepo, au majini


ninakiamuru kiachie kwa JIna la Yesu.

4. Kila aina ya sumu iliyopenyezwa kwenye maisha yangu nina iamuru itoke nje sasa, katika jina
la Yesu, nina sukuma nje kwa damu ya Yesu.

5. Ee Bwana Yesu, shusha moto juu ya kila roho ya mauti na kuzimu, iliyoandaliwa kwa ajili
yangu, katika jina la Yesu

6. Nina ponda kichwa na kukanyaga kila mkia wa majoka ya kiroho, katika jina la Yesu

7. Upanga wa moto, na uanze kukata kila kifungo walichokifunga wazazi, katika jina la Yesu

8. Ee Bwana, nifunulie agano lolote la siri ambalo shetani amefunga na nafsi yangu au anataka
kufunga na nafsi yangu, katika jina la Yesu.

9. Kila pando,ambalo baba yangu wa mbinguni hakulipanda katika maisha yangu, nina kungo’a
katika jina la Yesu.

10. Baba nina pitisha umeme katika ardhi ya mahali hapa sasa na kila agano na miguu yangu
lianze kuvunjika sasa katika jina la Yesu.

11. Agano lolote la siri ambalo ni la uovu, ninakuvunja katika jina la Yesu
12. Nina nyunyiza damu ya Yesu kuvunja laana zote

13. [Imba wimbo huu kama unaweza, kama huwezi usilazimshe: Kuna nguvu ya ajabu, damuni
mwa Yesu ]

14. Nina nyunyiza damu ya Yesu kuvunja laana zote za dhambi za wazazi wangu

15. Ee Bwana, badili laana zote zilizoelekezwa kwangu kuwa Baraka

16. Kila nguvu ya uovu iliyoelekezwa kwangu, ninakuamuru kurudi moja kwa moja, kwa
mtumaji katika jina la Yesu.

17. Ee Bwana Mungu, ninaomba kila alichosema adui kwamba hakitawezekana katika maisha
yangu, kikawezekane sasa kwa jina la Yesu.

18. Nina jiondoa na kujitenganisha katika kambi yoyote ya mateka inayomilikiwa na adui,katika
jina la Yesu.

19. Nina jifungua na kujiondoa kutoka kwenye kila kifungo cha kurithi ,katika jina la Yesu.

20. Ee Bwana,tuma shoka lako la moto kwenye misingi ya maisha yangu na uharibu/ulikate kila
pando ambalo amelipanda adui katika jina la Yesu.

21. Nina ipitisha Damu ya Yesu, katika mifumo yote ya mwili wangu [mfumo wa damu, wa
fahamu, wa chakula, wa upumuaji, wa takamwili n.k] na kuisafisha mabaki yote ya urithi wa vitu
viovu katika jina la Yesu.

22. Damu ya Yesu na moto wa Roho mtakatifu,unisafishe kila kiungo cha mwili wangu [Figo,
moyo, mapafu, macho, masikio, n.k] katika jina la Yesu

23. Nina vunja mikataba yote ya kiukoo na kikabila inayonihusisha mimi katika jina la Yesu.

24. Nina jiondo/ninajivua/vunja laana zote za kikabila na kiukoo katika jina la Yesu

25. Nina tapika chakula chochote cha uovu nilicholishwa katika maisha yangu, katika jina la
Yesu

26. Mapepo, majini, mizimu na wachawi manao fuatilia maisha yangu,na mpararaizi[mpooze]
sasa katika jina la Yesu.

27. Shambulio lolote lilopangwa juu ya familia yangu, ninalibatilisha kwa ajili yangu katika jina
la Yesu

28. Nina vunja matoke mabaya yote kwa ajili ya jina la kiuovu, lilipachikwa kwenye nafsi yangu
katika jina la Yesu
29. Nina batilisha laana zote, mikosi, majanga, ajali, maradhi yote yaliyoelekezwa kwenye
maisha yangu katika jina la Yesu.

30. Muombe Mungu aondoe laana zote alizo ziachilia kwenye maisha yako kwa sababu ya
kutotii neon lake[kumb 28:]

31. Pepo lolote lililo jipachika kwenye laana yoyote inayonihusu mimi, toka, katika jina la Yesu

32. Laana zote katika maisha yangu, badilika na kuwa Baraka, katika jina la Yesu

33. Utakapokuwa unataja laana zilizoorodheshwa hapo chini, sema kwa kumaanisha “vunjika,
vunjika, vunjika” katika jina la Yesu. Nina jitenganisha na nyinyi katika jina la Yesu.

• Laana zote za udhaifu wa kiakili na kimwili

• Laana zote za kushidwa katika kila ninalofanya

• Laana zote za umaskini

• Laana zote za kuvunjika kwa familia

• Laana zote za kuonewa na kudharauliwa

• Laana zote za Uharibifu wa mtu binafsi,kama vile kujinyonga n.k

• Laana zote za magonjwa sugu

• Laana zote za kishirikina

• Laana zote za kuharibikiwa mambo ya uzazi na viungo vya uzazi

• Laana zote za kufanya kazi kwa bidii pasipo kuiona faida

• Laana zote za kulowea mambo ya uovu kama vile zinaa, pombe, sigara n.k

34. Jitamkie maneno ya Baraka wewe mwenyewe, kwa mfano kwa kusema “hakutakuwa na
umaskini tena, magonjwa tena n.k katika maisha yangu katika jina la Yesu.

35. Nina jifungua na kujitenganisha na vifungo vya madhabahu zote za giza katika jina la
Yesu.Sema mara kadhaa ukifuatiwa na maneno yafuatayo “nina jitenganisha” katika jina la
Yesu.Tumia muda kidogo kwenye hilo.

36. Nina tapika sumu zote za mashetani nilizozimeza katika jina la Yesu.

37.[Weka mikono yako juu ya kichwa chako] Nina vunja kila mamlaka za giza katika maisha
yangu, katika jina la Yesu.Rudia “nina vunja katika jina la Yesu.

38. Taja mambo yafuatayo kwa mamlaka na sema “vunjika kwa jina la Yesu.
• Mamlaka zote za mizimu na miungu ya familia, ukoo, na kabila

• Mamlaka zote za roho za kichawi zilzopo ndani ya familia, ukoo, kabila

• Mamalaka zote zilizoshika rimoti za kudhibiti familia, ukoo, kabila

• Mamlaka zote ovu ndani ya Familia, ukoo, kabila nk

39. Kila mmiliki wa mzigo niliobebeshwa beba mzigo wako katika jina la Yesu[Mzigo unaweza
kuwa ugonjwa,mikosi wabebeshe wamilki]

40. Nina zipoodhesha/nina zipararaizi madhabahu zote za giza katika jina la Yesu

41. Nina zilaani madhabahu zote za uovu zilizoelekezwa zidi yangu katika jina la Yesu

42. Nina agiza nyundo ya Mungu aliyeumba mbingu na nchi,iponde kila madhabahu ya giza
zilizoelekezwa kwenye maisha yangu katika jina la Yesu.

43. Ee Bwana tuma moto wako na uteketeze madhabahu zote za giza zinazoinuka dhidi ya
maisha yangu,

44. Makuhani wote wa madhabahu zote za giza wanaocheza na maisha yangu,wakutane na


upanga wa roho mtakatifu. Katika jina la Yesu.

45. Mkono wowote unaotaka kunikamata na kuniteka kwa ajili ya Maombi haya ninayoomba
kauka katika jina la Yesu.

46. Nina waamuru makuhani wa madhabahu za giza kunyweni damu wenyewe katika jina la
Yesu

47. Nina rudisha urithi wangu ulioibiwa na madhabahu za giza katika jina la Yesu.

48. Ninafuta/ninaliondoa jina langu kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu

49. [Weka mkono wako mmoja kifuani] Ninaziondoa Baraka zangu kwenye madhabahu za giza
katika jina la Yesu

50. [Weka mkono mmoja kifuani na mwingine kichwani] Ninaondoa kitu chochote kile
kinachoniwakilisha mimi [kama vile nguo] kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu.

51. [Taja kiungo chochote katika mwili wako ambacho akifanyi kazi ipasavyo au kama ni mwili
wote taja mwili] na useme maneno yafuatayo “nina kuondoa kwenye madhabahu za giza” katika
jina la Yesu. Tamka hivyo mara saba.

52. Nina jitenganisha kutoka kwenye maagano yote ya damu na nguvu za giza katika jina la
Yesu
53. Damu ya Yesu na unene kwa ajili yangu dhidi ya maagano yote na nguvu za giza

54. Nina tamka Uharibifu dhidi ya roho chafu zote katika maisha yangu.Katika Jina la Yesu.

55. Nina jitenganisha na laana zote za maagano katika jina la Yesu

56. Nina jitenganisha mimi na familia yangu kutoka katika kila agano la damu katika jina la
Yesu.

57. Ninajitenganisha na kila agano la damu la kurithi katika jina la Yesu.

58. Nina iondoa damu yangu kwenye madhabahu za giza katika jina la Yesu

59. Nina iondoa damu yangu kutoka kwenye benki za damu kwenye ulimwengu wa giza katika
jina la Yesu

60. Nina vunja kila agano la damu la kutokukusudia kwa jina la Yesu

61.Ee bwana, damu ya mnyama yeyote iliyomwagika kwa niaba yangu, Naipoteze nguvu ya
agano sasa, kwa jina la Yesu

62. Kila tone la damu linalotamka mabaya dhidi yangu, na ikae kimya sasa, kwa damu ya Yesu

63. Ninajifungua na kujiondoa kutoka kwenye kila agano la damu la kifamila, kiukoo, kabila
katika jina la Yesu.

64. Nina jitenganisha na kila agano la damu nililoingia kwa kujua au kutojua kwa jina la Yesu

65. Ee Bwana kila agano la damuna nguvu za giza lipoteze nguvu na uhalali wake juu yangu
katika jina la Yesu.

66. Damu ya agano jipya la Bwana na Mwokozi wangu Yesu Kristo, naiikemee damu ya agano
na nguvu za giza ilijipanga kinyume name. Kwa jina la Yesu

67. Nimepewa mamlaka ya kubatilisha haki zote zilizopo kwenye maagano yote ya damu na
nguvu za giza . kwa jina la Yesu.

68.Agano lolote la damu na nguvu za giza lililofungwa kwenye kiungo chochote kwenye mwili
wangu, nalivunjike sasa.Kwa jina la Yesu

69. Ninapokea vitu vyote vilivyoibiwa au kuchukuliwa na adui kupitia maagano na nguvu za
giza. Kwa jina la Yesu.

70. Nina vunja agano lolote la damu na nguvu za giza kwenye damu yangu . Kwa jina la Yesu
AMEN.
BAADA YA KUFANYA HAYO MAOMBI, SASA ENDELEA KUSOMA UJUMBE WA
MUNGU KWAKO:

Mtegemee Roho Mtakatifu kwa maana atakufundisha mengi ikiwemo kuomba na maagizo ya
Yesu. Na kwa kufuata maagizo ya Yesu na kuenenda kwa roho hivyo vifungo vya nafsi
vitakwisha. Soma Wagalatia 5:16-25, Luka 22:40-46. Kudumu katika maombi, kuenenda kiroho
na kuepuka uovu ni muhimu kwa sababu kwa kufuata misingi hiyo ndipo unafunguliwa vifungo
kwa kuombewa ama kwa nguvu inayotenda kazi ndani yako kupitioa roho mtakatifu. Lakini pia
ni muhimu kujua ya kwamba sala ya toba pekee haitoshi kumfungua mtu kama ana vifungo na
sio imani tu bali na juhudi binafsi ya mtu itasaidia katika kumuweka huru. Wapo watu
wanaotaka kupokea miujiza bila ya kuwa na mabadiliko yoyote, ama bila kusoma neno la
Mungu na kukua kiroho ama bila kuomba. Wao husubiria siku za maombi, ama mikesha ama
makongamano ya maombi ili waombewe kisha baada ya hapo hawajishughulishi katika kukua
kiimani.

Kuwa hodari katika Bwana ili upate ulinzi wa Mungu. Waefeso 6:10-11 Hatimaye, mzidi kuwa
hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza
kuzipinga hila za shetani”

Maana ya kuwa hodari katika Bwana ni kukaa kwenye maombi, kusoma na kulishika neno lake
liwe ndani yako, na kutaka kumjua yeye zaidi. Sikuzote Sali kwa bidii katika kupambana na
muovu shetani ndo mana tunaambiwa vaeni silaha zote za Mungu ili kuweza kupingana na hila
za muovu shetani.

You might also like