You are on page 1of 10

UKIRI WA KUYAFUKUZA MAGONJWA MBALI NA HEMA YAKO

1. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, amejitwika

huzuni zetu… Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu,
alichubuliwa kwa maovu yetu; adhabu ya Amani yetu
ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
Isaya 53:4 – 5.
2. Hata ilipokuwa jioni, wakamletea wengine wenye pepo;
akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote
waliokuwa hawawezi, ili litimie lile neno lililonenwa na
nabii Isaya, akisema, mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, na
kuyachukua magonjwa yetu. Mathayo 8: 16 – 17.

Page 1 of 10
Amini tu na yale unayoyakiri yatakuwa yako. Kiri hata mara elfu mpaka nafsi yako isikie
na kukubaliana na vile Mungu asemavyo.
UKIRI WA KUYAFUKUZA MAGONJWA MBALI NA HEMA YAKO

3. Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu juu ya mti, ili,

tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo
ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa. 1Petro 2: 24.
4. Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa
alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa,
amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; Wagalatia 3:13
Kulingana na Kumbukumbu la torati 28: 15 – 22, 27 – 29, 35 – 61
magonjwa yote na maradhi ni laana ya torati. Lakini, kulingana
na wagalatia 3:13, Kristo alitukomboa katika laana ya torati!!
5. “……. Kwa maana mimi ni BWANA nikuponyaye”
Kutoka 15: 26

Page 2 of 10
Amini tu na yale unayoyakiri yatakuwa yako. Kiri hata mara elfu mpaka nafsi yako isikie
na kukubaliana na vile Mungu asemavyo.
UKIRI WA KUYAFUKUZA MAGONJWA MBALI NA HEMA YAKO

6. “Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye

atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami
nitakuondolea ugonjwa kati yako. Hapatakuwa na mwenye
kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na
hesabu ya miaka ya siku zako nitaitimiza” Kutoka 23:25 – 26.
7. “Kwa maana macho ya BWANA hukimbia kimbia
duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya
hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake…” 2Nyakati 16:9
8. “Mabaya hayatakupata wewe, wala tauni haitakaribia
hema yako. Kwa siku nyingi nitamshibisha, nami
nitamwonyesha wokovu wangu.” Zaburi 91: 10, 16.
Page 3 of 10
Amini tu na yale unayoyakiri yatakuwa yako. Kiri hata mara elfu mpaka nafsi yako isikie
na kukubaliana na vile Mungu asemavyo.
UKIRI WA KUYAFUKUZA MAGONJWA MBALI NA HEMA YAKO

9. Ee nafsi yangu, Mhimidi Bwana, wala usizisahau fadhili

zake zote; Akusamehe maovu yako yote, Akuponya
magonjwa yako yote. Zaburi 103:2-3
10. “Hulituma neno lake, huwaponya na kuwatoa katika
maangamizi yao…” Zaburi 107: 20
11. “Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika
kinywa changu; Halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi
yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.”
Isaya 55:11
12. “Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto
wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye
mbinguni atawapa mema wao wamwombao?” Mathayo 7:11
Page 4 of 10
Amini tu na yale unayoyakiri yatakuwa yako. Kiri hata mara elfu mpaka nafsi yako isikie
na kukubaliana na vile Mungu asemavyo.
UKIRI WA KUYAFUKUZA MAGONJWA MBALI NA HEMA YAKO

13. “Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho

kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake
hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka geuka”. Yakobo
1:17
14. “Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia,
akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa. Yesu
akanyosha mkono, akamgusa, akisema, Nataka; takasika.
Na mara ukoma wake ukatakasika.” Mathayo 8: 2- 3.
Yesu alisema mwenyewe, “Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka
mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake
aliyenipeleka” (Yohana 6:38). Kila kitu Yesu alichokifanya
alipokuwa akitembea hapa duniani, yalikuwa ni mapenzi ya
Page 5 of 10
Amini tu na yale unayoyakiri yatakuwa yako. Kiri hata mara elfu mpaka nafsi yako isikie
na kukubaliana na vile Mungu asemavyo.
UKIRI WA KUYAFUKUZA MAGONJWA MBALI NA HEMA YAKO

Baba yake. Alikuwa mapenzi ya Mungu katika matendo. Ikiwa

wataka kujua mapenzi ya Baba mtazame YESU.
15. “Jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na
nguvu; naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi
njema na kuponya wote walioonewa na ibilisi …” Matendo
10:38
Ni jambo la muhimu kushika kwenye moyo wako kuwa Kristo
ni mponyaji na shetani ndiye mtesi.
16. “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi
nalikuja (Yesu) ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”
Yohana 10:10

Page 6 of 10
Amini tu na yale unayoyakiri yatakuwa yako. Kiri hata mara elfu mpaka nafsi yako isikie
na kukubaliana na vile Mungu asemavyo.
UKIRI WA KUYAFUKUZA MAGONJWA MBALI NA HEMA YAKO

17. “Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji,

akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari
njema ya Ufalme, na kuponya magonjwa yote na udhaifu
wa kila aina.” Mathayo 9:35
18. “Wakamwendea makutano mengi wakimletea viwete,
vipofu, mabubu, vilema, na wengine wengi, wakawaweka
miguuni pake; akawaponya: Hata ule mkutano
wakastaajabu, walipowaona mabubu wanasema, vilema
wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na vipofu
wanaona; wakamtukuza Mungu wa Israeli.” Mathayo 15: 30 – 31.

Page 7 of 10
Amini tu na yale unayoyakiri yatakuwa yako. Kiri hata mara elfu mpaka nafsi yako isikie
na kukubaliana na vile Mungu asemavyo.
UKIRI WA KUYAFUKUZA MAGONJWA MBALI NA HEMA YAKO

19. “Yesu Kristo ni yeye Yule, jana na leo na hata milele”

Waebrani 13:8
20. “Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo
mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa
yenu.” Marko 11:24
21. “Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu; nanyi
mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni MKUU
kuliko yeye aliye katika dunia.” 1Yohana 4:4
22. “Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu,
Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni

Page 8 of 10
Amini tu na yale unayoyakiri yatakuwa yako. Kiri hata mara elfu mpaka nafsi yako isikie
na kukubaliana na vile Mungu asemavyo.
UKIRI WA KUYAFUKUZA MAGONJWA MBALI NA HEMA YAKO

mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia,

yatakuwa yake.” Marko 11:23.
23. “Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako,
uzisikie kauli zangu. Zisiondoke machoni pako; Uzihifadhi
ndani ya moyo wako. Maana ni UHAI kwa wale wazipatao,
Na AFYA ya mwili wao wote. Mithali 4: 20 – 22.
24. “Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye

naye vivyo hivyo alishiriki hayo, ili kwa njia ya mauti

amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,
awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa
hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa. (Ebrania 2:14)
Page 9 of 10
Amini tu na yale unayoyakiri yatakuwa yako. Kiri hata mara elfu mpaka nafsi yako isikie
na kukubaliana na vile Mungu asemavyo.
UKIRI WA KUYAFUKUZA MAGONJWA MBALI NA HEMA YAKO

25. ……“Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa,

ili azivunje kazi za Ibilisi. 1Yohana3: 8b

Page 10 of 10
Amini tu na yale unayoyakiri yatakuwa yako. Kiri hata mara elfu mpaka nafsi yako isikie
na kukubaliana na vile Mungu asemavyo.

You might also like