You are on page 1of 11

SEMINA YA MWANZO WA MWAKA NA MWALIMU

MWAKASEGE-2023

SIKU YA KWANZA (1.) YA SEMINA: JUMATANO TAR 11/01/2023


MSG: KUZIOMBEA SAUTI ZILIZOJIPANGA KUVURUGA HATIMA YANGU

MALENGO YA SOMO

1.Ili niweze kutambua uwezo wa sauti juu ya hatma yangu i.e uwezo wa
kujenga
au kubomoa
2. Kuweka angalizo juu ya sauti niisikiayo i.e niwe muangalifu
3. Kunifikishia ujumbe wa Mungu wa majira haya na yajayo.

1. SAUTI ILIYOBEBWA NA MANENO


-Ziko sauti nyingi duniani na kila sauti ina sababu ya kuwepo kwake
1Cor 14:10. Nisiipuuzie sauti,
 Maneno yana uwezo wa kubeba sauti Zab 103:20
 Masikio ya mtu yaliumbwa yakiwa na uwezo wa kusikia maneno
na sauti iliyoko ndani ya maneno, 2Tim 4:3-4- Kati ya uwezo
ulionao masikio ni kufanya utafiti- kufuatilia kitu undani wake kwa
kukichunguza kwa nia ya kutoa tafsiri na nipate uelewa na
hatimaye kutoa uamuzi. Mtu wa nje anasikia maneno, mtu wa
ndani anasikia sauti iliyoko katika maneno Mathayo13:13-14
 Sauti zina roho ndani yake na maneno yana roho ndani yake, kwa
sababu hii sauti inaweza kubeba roho ama roho ikabeba sauti na
maneno yanaweza kubeba roho ama maneno yakabeba roho yoh
6:63,
Mfano wa 1: Mwanzo3:8-11(Aliyesikia movement ya Mungu akiwa
anakuja ni Adamu wa ndani)

Mfano wa 2: Yoh 10:1-6( Ninaweza kukopi maneno na sio roho iliyoko


katika sauti, i.e Roho iliyoko ndani yangu ina uwezo wa kutambua hii ni
sauti ya Mungu au ni ya shetani hata kama wana sauti inayofanana)

Mfano 3 : Mathayo 16:13-23 ( Yesu alitambua roho iliyobeba sauti ya


Petro i.e Shetani i.e Shetani hakuwa na shida na Petro bali mdomo wake.
kwa nje ulisikia sauti ya Petro ila kwa ndani Yesu alisikia sauti ya shetani
ndani ya Petro.)

Mfano wa 4: (Mat 19:16-19-Sio kila roho inayosema kweli inatoka kwa


Bwana. Kijakazi aliwaunga mkono wakina Paulo lakini haikuwa ni sauti
inayotoka kwa Mungu)

Mfano wa 5 : Watumishi wa Mungu, Luka 10:16(Sauti tatu- Nikitaka


kujua Kuwa huyu ni mtumishi wa Mungu au la, nisifuatilie anachokisema
bali sauti iliyoko ndani yake. Sauti imebeba roho)
JE HATMA YANGU NI MATOKEO YA SAUTI IPI?
1Samw 15:22-24(24-22- Sauli hakuogopa maneno bali sauti ya watu
ilikuja na kitisho-Kitu gani kilibadilisha hatma ya Sauli- Ni sauti iliyoko
ndani ya shetani kupitia watu. Ukiangalia ushauri ulikuwa mzuri wa
kwenda kutoa sadaka ila haukutoka katika sauti ya Mungu....Hatima
yangu, mahali nilipo, na ninapo elekea ninatekeleza maneno ya sauti ipi?.

Watu wengi sana hatma zao zimeharibika kutokana na kusikia sauti ya


roho ambazo si ya Mungu. Wameweka Imani katika hizo sauti(imani huja
kwa kusikia)- wameweekea msingi sauti hizo lakini roho yake haitoki kwa
Mungu.

Nisifanye maamuzi ya haraka katika utekelezaji kutokana na sauti


niliyosikia pasipokujua ni roho gani iliyoko nyuma yake. Nimsubiri Mungu
aniweze kujua roho hiyo

Note: Hizi ni siku za mwisho ni msimu mwingine.

SIKU YA PILI (2)- 12/01/2023


UJUMBE:KUZIOMBEA SAUTI ZILIZOJIPANGA KUVURUGA HATMA
YANGU

2. SAUTI ZILIZOMO NDANI YA DAMU/SAUTI ZILIZOBEBWA NA DAMU


--Damu ina uwezo wa kuongea na kwa sababu hio damu inayo sauti.
Hbr12:24, Mwz4:10
Kama sauti ina damu, kila damu ina sauti

-- Damu inaweza kuongea kwa niaba ya mwenye damu husika au kwa


niaba ya mtu mwingine.
Lawi 17:11 (Mungu amezungumza kutoka katika nchi yetu kuna sauti
nyingi sana za damu za wanyama na watu anasikia lakini hasikii sauti ya
Damu ya Yesu)

--Sauti ya Damu na maneno yake ni vya matumizi ya ulimwengu wa Roho,


ingawa matokeo ya matumizi hayo yanaonekana katika ulimwengu wa
kimwili. Lawi 17:11. Uhai ni Damu, Damu ni uhai. Uhai wa Yesu upo katika
Damu yake. Hebr 9:14- Yesu alipokuwa anapeleka Damu yake katika
madhabahu ya mbinguni alipeleka kwa Roho yake. Mungu anapoona
Damu anaona uhai. Tunapoomba toba kwa kutumia damu ya Yesu katika
ulimwengu wa Roho Uhai wa Damu ya Yesu unatokea mbele za Mungu
na kwa niaba yangu na kisha roho yangu inasimama pamoja naye mbele
za Mungu.

--Kazi moja wapo ya Damu ya Yesu ni kushughulikia kiagano, maneno


yanayotoka kwenye damu zingine Hebr 12:24. Damu ya Yesu ni bora
kuliko damu zote za kiagano zilizokuwa zinatumika katika agano la kale.
Damu ya Yesu imechukua mbadala ya Damu zile zote. Kama damu ya
mafahali iliachilia utukufu katika madhabahu katika agano la kale si zaidi
sana damu ya Yesu katika madhabahu katika siku za kwetu.

--Damu ya Yesu inaitwa ya kunyunyizwa ili niweze kuiamini kiagano Hebr


12:24, Hebr 9:19-22. (Rum 3:23-26-- Imani katika Damu ya Yesu-- Vile
nina imani katika Yesu haimaanishi ninaamini damu yake pia). Tofauti ni
aina za Damu ila vitendo vinafanana(Kunyunyiza). Kuamini kiagano
inamaana kuamini ki matumizi. Imani isipokuwa kimatendo imekufa.
Nikiwa na imani katika damu ya Yesu na siitumii imani yangu inakuwa
haina matunda. Imani katika Damu ya Yesu inathibitika katika matumizi
yake. Mf; Kutoka 12: Damu ambayo haijamwagika haina sauti. Kama
wana wa israeli wasingechinja kondoo na kutumia damu yake
wangepigwa. Damu iliyomwagika peke yake ndio iliyokuwa na thamani
na ni damu pekee iliyopakwa katika miimo ya milango ndio iliyoweka
agano. Imani hukamilika baada ya kuweka katika utendani maelekezo
yote ambayo Mungu ameagiza.(kuchinja na kupaka damu ya kondoo
katika miimo ya milango kwa muda husika).
Damu ya kondoo ilifungua malengo mbalimbali kama;
 lango la muda
 lango mzaliwa wa kwanza
 lango la kieneo(mipaka)- Ninaweza kuwa nina utumishi mkuu na
nguvu za Mungu katika huduma lakini malango ya kieneo yakawa
yamefunga nikawa ninashindwa kutoka.
 lango la baraka

NOTE: Vile nimetembea na Yesu miaka mingi haimaniishi ninapiga hatua.


Hatua zangu zitaonekana pale nitakapochukua hatua ya IMANI katika
kufuatilia maelekezo yake.
SIKU YA TATU (3)- 13/01/2023
UJUMBE:KUZIOMBEA SAUTI ZILIZOJIPANGA KUVURUGA HATMA
YANGU
MAMLAKA YA SAUTI YA DAMU KIAGANO
Waebr 12:24
 Swali alilioambiwa kuniuliza(Mwakasege) na Mungu jana
(12/1/2023) kwa nini watu wake ni wazito kutumia Damu ya Yesu
kama alivyoagiza katika Neno lake la Biblia?

JIBU: Watu wake hawajui MUNGU alivyo iamuru na alichoamuru Damu


ya Yesu kwa ajili yetu Hebr 9:18-22. Ni amri ilyoko kwa Mungu iliweka
sauti au mamlaka katika Damu ya Yesu. Na hio mamlaka iliwekwa katika
ngazi 2 muhimu;
 Kusimama na sisi wanadamu katika ulimwengu wa roho kwa ajili ya
Mungu-sisi tunaosimama na Damu ya Yesu tunasimama kwa ajili ya
Mungu. Wanaosimama na damu zingine wanasimama kwa ajili ya
nguvu nyingine wanazoziabudu
 Kusimama na Mungu katika ulimwengu wa kimwili kwa ajili yetu.
Yesu alisubiri kazi ya msalaba ili aweze kuturejeshea tuliyopoteza
katika ulimwengu wa mwili kupitia Damu yake katika ulimwengu
wa roho.(Kabla ya hapo tulimpa shetani mamlaka ya vitu vyote
tulipoasi)

NOTE: Mungu amemsemesha mtumishi wake kuwa watu ni wepesi


kutumia Jina la Yesu kuliko Damu yake.
 Kuokoka kunampa mtu uhalali wa kutumia mamlaka au sauti
iliyomo katika Damu ya Yesu kwa Imani Ufunuo 5:9-10. Rum 3:23-
26
 Imani inampa mtu na Mungu mamlaka ya kutumia Damu ya agano,
Kutoka 12:13,23. Hebr11:28

Mungu alivyotaka watu wapake Damu alitaka aone imani yao juu ya
Damu ya agano ili kumkumbusha Mungu alichoahidi kiagano ili
kuwafungulia watoke.Kwanini aone Imani yao kabla ya Damu?
Mwz 15:8-16,18-19
Mungu amenipa Damu msalabani nisipoitumia nimemfunga mkono
kutenda. N ninatumia Damu kwa njia ya Imani.

 Aliposema weka kwenye miimo miwili ya mlango( ulikuwa ni


mlango katika ulimwengu wa roho. mlango ulitumika kama ishara-
ishara kazi yake ni kuelekeza mahali.
Kizingiti kilikuwa kinawakilisha (Mbingu) iwe shahidi.

Kwanini amri ya pasaka ilikuwa ni ya milele?


 Damu iliwapa umiliki kwa Mungu kwa maana walikuwa
wanamilikiwa na miungu ya kimisri kutokana na damu zilizokuwa
zinatolewa kwa ajili ya wazaliwa wa kwanza.
 Mungu aliweza kuwaona- kutambua nafasi zao kiagano
kushughulikia haki zao
 Mungu kujilipizia kisasi cha damu kwa damu ili kuondoa kizuiacho
malangoni, Mwz 9:6, Ufunuo 6:9-10. Damu ya Yesu inenayo mema
huingilia kati kumlipa aliyemwagiwa damu yake. Damu ya Yesu
hulipa kisasi.

 Ninapokuwa nimefunikwa chini ya Damu ya kiagano, ninakuwa sio


mimi tena bali Kristo Mwz 26:4. Mungu anamwambia Isaka
hajamfuata kwa sababu yake bali kwa sababu ya Ibrahim kwa
sababu ndani ya agano la Ibrahim Isaka yupo.

NOTE: UJUMBE KATIKA DAMU YESU: NIAMKE NITUMIE DAMU YA


YESU.

SIKU YA TANO (5)- 15/01/2023


UJUMBE:KUZIOMBEA SAUTI ZILIZOJIPANGA KUVURUGA HATMA
YANGU
Huu ni msimu mpya na kuna sauti nyingi sana zimeachiwa ulimwenguni.
Na sauti hizi nyingi ni za kubomoa

3. SAUTI ZA MASHITAKA KWENYE LANGO LA MUDA


1. SHETANI NDIYE MSHITAKI, 1Petro 5:8, Uf 12:10
2. KUNA SAUTI ZA MASHITAKA KWENYE LANGO LA MUDA, ninaweza
kukutana na mashitaka machache ama kidogo. Nisipokutana na
mashitaka ina maana kuwa nilichobeba katika msimu huo sio tishio.
Aina ya mashitaka;
 Shitaka la kumshitaki mtu kwa Mungu
 Shitaka la mtu kwa mtu mwingine Danieli 6:4-5.
 Shitaka la mtu bibafsi 1Yoh3:21
 Shitaka la kumshitaki Mungu kwa mtu. Mwz 3:1
 Shitaka la Mungu kujishitaki mwenyewe Mwz 6:5-8
3.Kuna sababu kwa kila shitaka lile ni la kweli au la uongo. 1Kor 14:10.
Dan 6:4-5.

Kuna mambo mawili ndani ya sababu ya kushitaki


 Sababu ya mshitaki kushitaki- anachopata mshitaki katika shitaka
hilo kwa mshitakiwa.
 Ni kutafuta kitakachofanya mshitakiwa atiwe hatiani.
Kitakachofanya mshitakiwa akubali kutoa kile anachotaka mshitaki.
NOTE: KILA LANGO LA MAISHA YANGU LA KUINGIA KATIKA MSIMU
MPYA KUNAKUWA NA MASHITAKA.
Kama kwenye lango la msimu nina kitu chenye kuleta tishio kwa shetani
ni lazima nitakuta shitaka katika msimu huo mpya.

4. Mashitaka yakiibuka kwenye lango la muda kuna kitu kinatafutwa,


Mwz 3:1---Sababu ya shetani kumshitaki Mungu kwa mtu
 Alimshitaki Mungu kwa mtu ili mwanadamu amhukumu Mungu.
 Alitaka kuondoa heshima ya Neno la Mungu kwa mtu- alishitaki
uaminifu wa Mungu katika kusimamia ahadi zake.

 Mashitaka yakija hayaji peke yake kuna vitu yanakuja nayo


Wakolosai 2:14-Nikiona mashitaka ndani yake yanakuja na
hukumu. Hukumu maana yake ni kutengwa. Ndani ya mashitaka
kuna uadui. 1Petro 5:8. Kummeza maana yake ni kummiliki.
Kumiliki mtu na kitu alichonacho.

NOTE:Nicheki mimi mwenyewe ni mara ngapi nimemshitaki Mungu


kutokana na yale ambayo ninaona hayajafanya kwangu kutokana na
maombi nimemuomba au juhudi nimeweka.

5. Mungu amempa mtu njia kadhaa za kushughulika ma mashitaka


anayokutana nayo kwenye lango la muda

 Nisiwe mwepesi kusema au nisihamaki ninapokutana na mashitaka


Luka 21:14(nidhamirie kukaa kimya)- maana yake nini

 Niende msalabani. Nipeleke mashitaka yangu niliyoshtakiwa kwa


njia ya maombi(toba). Mungu ameweka utaratibu wa mashitaka
kwa watoto wake whether ni ya kweli au si ya kweli, Mungu
anasimama na mtoto wake Warumi 8:33-34. Ninapopata
mashitaka niende msalabani si kwa kujihesabia haki bali kwa njia
ya toba.

 Nisubiri nipewe hekima ya namna ya kufanya juu ya hayo


mashtaka, Luka21:14-15.

 Nisikae upande wa anayemshitaki Mungu kwangu. Nikifanya hivyo


maana yake na mimi ninaweka kiulizo juu ya uamnifu wa Mungu.
Mwz 3:1. Adamu alisikia sauti ya mke wake hivyo akawa upande
wa anayemshitaki Mungu kwake (mke wake) ambaye shetani
alimshitaki Mungu kwake na yeye akapeleka maneno ya
mashitaka kwa mume wake.

 Nilinde imani nyangu juu ya ahadi ya Mungu kwangu ili nilinde


nilichobebeshwa na Mungu 1Petro 5:8-9.
 Ninyunyize damu ya Yesu juu ya mashtaka na hukumu na uadui.

You might also like