You are on page 1of 4

1 Petro 1:2-5

 kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata
mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na
ziongezwe kwenu.
 Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake
nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake
Yesu Kristo katika wafu;
 tupate na urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni
kwa ajili yenu.
 Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio
tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.

Sefania 3:19
 Tazama, wakati huo nitawapatiliza watu wote wanaokutesa; nami nitamponya
yeye achechemeaye, nami nitamkusanya yeye aliyefukuzwa; nami nitawafanya
kuwa sifa na jina, hao ambao fedheha yao ilikuwa katika dunia yote.

Yoeli 2:23
 Furahini, basi, enyi wana wa Sayuni, mkamfurahie Bwana, Mungu wenu; kwa
kuwa yeye huwapa ninyi mvua ya masika, kwa kipimo cha haki, naye
huwanyeshea mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli, kama kwanza.

Isaya 24:15
 Basi, mtukuzeni Bwana katika mashariki, litukuzeni jina la Bwana, Mungu wa
Israeli, katika visiwa vya bahari.

Isaya 43:5
 Usiogope; maana mimi ni pamoja nawe; nitaleta wazao wako toka mashariki,
nitakukusanya toka magharibi;

Hagai 2:9
 Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa
kwanza, asema Bwana wa majeshi; na katika mahali hapa nitawapa amani,
asema Bwana wa majeshi.

Yeremia 32:27
 Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo
lote nisiloliweza?

Yeremia 29:11-13
 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya
amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.
 Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.
 Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.

Isaya 55:6-13
 Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu;
 Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na
amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye
atamsamehe kabisa.
 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema
Bwana.
 Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi
juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
 Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi
huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye
mbegu, na mtu alaye chakula;
 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia
bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale
niliyolituma.
 Maana mtatoka kwa furaha, Mtaongozwa kwa amani; Mbele yenu milima na
vilima vitatoa nyimbo; Na miti yote ya kondeni itapiga makofi.
 Badala ya michongoma utamea msunobari, Na badala ya mibigili, mhadesi;
Jambo hili litakuwa la kumpatia Bwana jina, Litakuwa ishara ya milele
isiyokatiliwa mbali.

2 Samweli 7:26
 Jina lako na litukuzwe milele, kusema, Bwana wa majeshi ndiye Mungu juu ya
Israeli; na nyumba ya mtumwa wako, Daudi, itakuwa imara mbele zako.

Mathayo 6:9
 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako
uje,

Isaya 25:1
 Ee Bwana, wewe u Mungu wangu; Nitakutukuza na kulihimidi jina lako; Kwa
kuwa umetenda mambo ya ajabu, Mashauri ya kale, kwa uaminifu na kweli.

Mathayo 11:28-30
 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami
nitawapumzisha.
 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu
wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
Yohana 15:10-16
 Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika
amri za Baba yangu na kukaa katika Pendo Lake.
 Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu
itimizwe.
 Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi.
 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya
rafiki zake.
 Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.
 Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini
ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.
 Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka
mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote
mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.

Mathayo 6:31-33
 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni
anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

Waamuzi 6:11-17
 Malaika wa Bwana akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra,
uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta
ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani.
 Malaika wa Bwana akamtokea, akamwambia, Bwana yu pamoja nawe, Ee
shujaa.
 Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa Bwana yu pamoja nasi, mbona
mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu,
waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye Bwana, aliyetuleta huku kutoka
Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani.
 Bwana akamtazama, akasema, Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe
Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma?
 Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama, jamaa
zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye mdogo katika
nyumba ya baba yangu.
 Bwana akamwambia, Hakika nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga
Wamidiani kama mtu mmoja.
 Naye akamwambia, Kama nimepata kibali mbele za macho yako, basi
unionyeshe ishara, ya kuwa ndiwe wewe unayesema nami.

Matendo ya Mitume 17:24-28


 Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni
Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono;
 wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho
chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.
 Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya
uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani,
na mipaka ya makazi yao;
 ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone,
ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.
 Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu.
Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu
wazao wake.

TUMWABUDU MUNGU WETU


51: Yesu Ndiye Kiongozi Wangu
TABIBU WA KARIBU

Isaiah 6:3
 And they were calling to one another: “Holy, holy, holy is the LORD Almighty; the
whole earth is full of his glory.”

Habakkuk 3:3-4
 God came from Teman, the Holy One from Mount Paran.His glory covered the
heavens and his praise filled the earth. 4 His splendor was like the sunrise; rays
flashed from his hand, where his power was hidden.

Zechariah 2:11
 “Many nations will be joined with the LORD in that day and will become my
people. I will live among you and you will know that the LORD Almighty has sent
me to you.

Psalm 19:1
 The heavens declare the glory of God; the skies proclaim the work of his hands.

You might also like