You are on page 1of 4

28 MACHI 2024

ALHAMISI
KATIKA KARAMU YA BWANA

SOMO LA KWANZA Kutoka 12:1-8, 11-14

Somo katika kitabu cha Kutoka.


Siku zile: Bwana alisema na Musa na Haruni katika nchi ya Misri,
akiwaambia: “Mwezi huu utakuwa kwenu mwanzo wa miezi:
mtaufanya kuwa mwezi wa kwanza wa mwaka. Semeni na mkutano
wote wa Israeli, mkawaambie: Siku ya kumi ya mwezi huu, kila mtu
atwae mwanakondoo jamaa kwa jamaa: mwanakondoo mmoja kwa
kila nyumba moja. Kama jamaa ina watu wachache wasioweza
kummaliza mwanakondoo, mtu ashirikiane na jirani yake aliye karibu
na nyumba yake, kwa kadiri ya hesabu ya watu. Mtapima kadiri
awezayo kula kila mtu kwa kujua hesabu ya watu wataokula
mwanakondoo. Mnyama atakuwa asiye na kilema, dume, wa mwaka
mmoja. Mtamchagua kati ya kondoo au mbuzi. Mtamweka mpaka
siku ya kumi na nne ya mwezi huu; hapo watu wote wa mkutano wa
Israeli watamchinja saa za jioni. Watachukua damu yake na kupaka
juu ya miimo miwili na kizingiti cha mlango wa nyumba
watakamomlia. Usiku huo huo italiwa nyama hiyo imeokwa kwa
moto; italiwa pamoja na mikate isiyotiwa chachu, na mboga chungu.
Mtamla hivi: viuno vyema vimefungwa, mmevaa viatu vyenu
miguuni, fimbo zenu mkononi. Mtakula kwa haraka: hiyo ndiyo
Pasaka ya Bwana. Usiku huo, mimi nitapita katika nchi ya Misri, na
kuwaua wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa
wanadamu na wa wanyama. Tena miungu yote ya Misri nitaiadhibu,
mimi ndimi Bwana! Na ile damu itawasaidia kutambulisha nyumba
mnamokaa. Nitakapoiona damu hiyo, nitawapita, nanyi hamtapatwa
na pigo la kuangamiza, nitakapoipiga nchi ya Misri. Siku hiyo
mtaifanya kuwa siku ya ukumbusho, nanyi mtaiadhimisha kama
sikukuu kwa heshima ya Bwana. Katika vizazi vyenu vyote, mtaifanya
iwe sikukuu milele.”
Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.

ZABURI YA KUITIKIZANA Zaburi 116


K. Kikombe tunachokibariki ni ushirika
katika damu ya Kristo.
Nimrudishie Bwana nini
kwa ukarimu wake wote alionitendea?
Nitakiinua kikombe cha wokovu,
na kuliita jina la Bwana. K.

Kina thamani kubwa machoni pa Bwana


kifo cha watakatifu wake.
Mimi ni mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako;
umevifungua vifungo vyangu. K.

Nitakutolea dhabihu ya shukrani,


na kuliita jina la Bwana.
Nitamtimizia Bwana nadhiri zangu
mbele ya watu wake wote. K.

2
SOMO LA PILI 1 Wakorintho 11:23-26

Somo katika barua ya kwanza ya Mtakatifu Paulo kwa Wakorintho.


Ndugu zangu: Niliyowakabidhi ninyi ndiyo niliyoyapokea mimi kwa
Bwana, yaani usiku ule alipotolewa, Yesu alitwaa mkate, akashukuru,
akaumega, akasema, “Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili
yenu: fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” Kadhalika akatwaa
kikombe baada ya kula, akasema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika
damu yangu. Fanyeni hivi, kila mnapokinywa, kwa ukumbusho
wangu.” Maana kila mnapoula mkate huu na kunywa kikombe hiki,
mnatangaia kifo cha Bwana hata atakapokuja.
Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO LA INJILI
K. Sifa na utukufu kwako, ee Kristo.
W. Sifa na utukufu kwako, ee Kristo.
K. Amri mpya nawapeni, asema Bwana.
Kama mimi nilivyowapenda, nanyi pia mpendane.
W. Sifa na utukufu kwako, ee Kristo.

3
INJILI Yohane 13:1-15

Somo la Injili takatifu ilivyoandikwa na Yohane.


Ilikuwa kabla ya Sikukuu ya Pasaka, Yesu alijua ya kuwa saa yake
imewadia ya kuondoka ulimwenguni hapa kwenda kwa Baba. Naye
kwa kuwa aliwapenda watu wake waliopo ulimwenguni, aliwapenda
mpaka mwisho.
Hata wakati wa chakula cha jioni, naye Shetani amekwisha kumtia
Yuda mwana wa Simoni Iskariote nia ya kumsaliti, Yesu hali akijua ya
kuwa Baba ameweka vyote mikononi mwake, na ya kuwa ametoka
kwa Mungu, na anakwenda kwa Mungu, aliinuka kutoka mezani,
akaweka kanzu yake kando, akachukua kitambaa cha kitani,
akajifunga kiunoni. Kisha akatia maji katika chombo, akaanza kuiosha
miguu ya wafuasi na kuifuta kwa kitambaa alichojifunga.
Aiipokuja kwa Simoni Petro, huyo akamwambia, “Bwana, wewe
wataka kuniosha mimi miguu?” Yesu akajibu, akamwambia, “Sasa
huelewi nifanyalo, lakini baadaye utalifahamu.” Petro akamwambia,
“Wewe hutaniosha miguu mimi, hata kidogo.” Yesu akamjibu,
“Nisipokuosha, huna shirika nami.” Simoni Petro akamwambia,
“Bwana, si miguu yangu tu, hata na mikono na kichwa.” Yesu
akamwambia, “Aliyekwishaoga hana haja ya kunawa isipokuwa
miguu, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote.”
Kwa maana alimjua atakayemsaliti; ndiyo maana, alisema, “Si nyote
mlio safi.”
Baada ya kuwaosha miguu, alivaa tena nguo zake, akaketi mezani.
Akawaambia, “Je, mmeelewa hayo niliyowatendea? Mwaniita
‘mwalimu’ na ‘bwana,’ tena kwa haki, maana ni hivyo. Basi, kama
mimi niliye bwana na mwalimu nimewaosha miguu, imewapasa
ninyi pia kuoshana miguu. Kwa maana nimewapa mfano, ili nanyi
mtende kama mimi nilivyowatendea.”
Injili ya Bwana... Sifa kwako Ee Kristu.

You might also like