You are on page 1of 2

(MILIMA TUANGUKIENI)

"Ulimwengu haujaachwa mikononi mwa wanadamu, Ingawa Mungu anaruhusu hali ya mchafuko na
mvurugano kuchukua nafasi kwa msimu. Nguvu kutoka chini inatenda kazi ili kuleta tukio kuu la mwisho
katika mchezo(drama), -- shetani akija kama Kristo, na akifanya kazi kwa madanganyo yote ya uovu kwa
wale wanaojifungaminisha katika vyama vya siri. Wale wanaojisalimisha katika tamaa kwa
kujifungamanisha wanatenda kazi katika kusudi la adui. Kazi ambayo itafuatiwa na athari."---
Testimonies.Vol.8, uk.27,28. ChS.uk.50.1).Kuna siku inakuja ambapo wale waliomtumikia shetani na
Mapapa watakufa kifo kile kile ambacho waliwaua watu wa Mungu na Papa awaye yote hatawaokoa,
Nayeye atapotea kama wanyama wafao na kutoweka. Hakuna damu ambayo haitalipwa, Kuanzia damu
ya Habili hadi ya mtu wa Mungu itakayomwagika dakika ya mwisho wa pambano kuu italipwa hakika
tena kwa kipimo sahihi cha ukatili aliofanyiwa. Ninawahurumia sana wanaovimba vichwa wakimtumaini
shetani na mifumo yake ya kishetani na huku nikiangalia dakika zao zimeshabaki chache sana. Kama vile
ambavyo Kristo atamwaga chozi la mwisho kwa ajili ya waovu na kusema "Imekwisha" nami katika sura
hii ninaandika kuwa "Kama mtu hatabadili njia zake na apotee kwa ushupavu wake mwenyewe na damu
yake iwe juu ya kichwa chake mwenyewe" Natoa pole kwa watu wa MUNGU waliofiwa na ndugu zao na
kuteswa na nawasihi kwa Jina la Yesu msilipe kisasi bali mpisheni BWANA atalipa hakika. Ufunuo wa
Yohana 6:9-11(KJV) Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa
kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.10 Wakalia kwa sauti kuu,
wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu
kwa hao wakaao juu ya nchi? 11 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa
wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa
vile vile kama wao.Warumi 12:19(KJV) Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu;
maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Isaya 65:6-7(KJV) Tazama,
neno hili limeandikwa mbele zangu. Sitanyamaza, lakini nitalipa, naam, mimi nitawalipa ujira wao vifuani
mwao; 7 maovu yenu na maovu ya baba zenu pamoja, asema Bwana, ninyi mliofukiza uvumba juu ya
milima, na kunitukana juu ya vilima; basi, kwa ajili ya hayo nitawapimia kwanza kazi yao vifuani mwao.
Ufunuo wa Yohana 6:14-17(KJV) Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na
kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na
matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya
miamba ya milima,16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye
aketiye juu ya kiti cha enzi,na hasira ya Mwana-Kondoo. 17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao,
imekuja; naye ni nani awezaye kusimama? Luka 23:29-31(KJV) Kwa maana tazama, siku zitakuja
watakaposema, Heri walio tasa, na matumbo yasiyozaa, na maziwa yasiyonyonyesha. 30 Ndipo
watakapoanza kuiambia milima, Tuangukieni, na vilima, Tufunikeni. 31 Kwa kuwa kama wakitenda
mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu? Ufunuo wa Yohana 16:18-20 KJV) Pakawa na
umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu
ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo. 19 Na mji ule mkuu ukagawanyikana
mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu,
kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake. 20 Kila kisiwa kikakimbia, wala milima
haikuonekana tena.Ghadhabu ya Mungu itaanza na Gaidi Aliyesitirika ndani ya kanisa lake la wanaodai
kutunza amri za Mungu yaani Waadventista wa sabato po pote walipo, kila mmoja aliyeshirikiana na
Gaidi aliyesitirika wa nje atapokea mapigo kuliko hata waliomtuma. Wengi wanatumika na kujidanganya
kuwa watatubu wakikaribia kufa lakini niwaambie kuwa Bwana anasema kuwa; “Nilikumbushwa kwa
nguvu juu ya toba ya mtu akaribiapo kufa kitandani (death-bed repentance). Baadhi wanaojitumikia na
kumtumikia shetani maisha yao yote, kadri ugonjwa unapowalemea, na hofu ya kutokuwa na uhakika
wa maisha kuwa mbele yao, hudhirisha huzuni juu dhambi zao, na kisha husema wako tayari kufa, na
huwafanya marafiki zao wafikiri kuwa wameongoka kweli na kuwa wanastahiri kwa ajili ya Mbingu.
Lakini kama hawa watu wangepona wangeendelea na uasi wao kama siku zote. Nilikumbushwa juu ya
Mithali 1:27,28. Hofu yenu ifikapo kama tufani, Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli, Dhiki na taabu
zitakapowafikia. Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; Watanitafuta kwa bidi, wasinione.” (Life Sketches
of James,80.uk. 241.2). Ni toba chache sana za kipindi mtu anapofariki ambazo zinapokelewa;

You might also like