You are on page 1of 3

YONA

Utangulizi
Yona maana yake “hua”.Kitabu hiki kifupi kinachomtaja Yona kuwa mwana wa Amitai(1:1), kinaeleza yale yaliyomtukia
yeye kama mjumbe wa Mungu.Yona alikuwa amepewa agizo na Mungu aende akawaonye watu wa Ninawi juu ya hukumu
iliyokuwa inakuja. Akijaribu kumkimbia Mungu aliamua kuelekea Tarshishi, ambako ni upande wa magharibi, alitelemka
mpaka Yafa, akapanda meli iliyokuwa inaelekea huko. Yona alipotupwa baharini alimezwa na nyangumi a ambaye
alimrudisha mpaka pwani ya mashariki ya Bahari ya Kati (Mediterania). Hatimaye alikwenda Ninawi na akawaonya watu
kuhusu hukumu ya Mungu. Alivunjika moyo kwa ajili ya mafanikio yake mwenyewe watu walipotubu na Mungu akaonyesha
rehema Zake kwa kughairi na kuahirisha siku ya hukumu. Yona akajifunza kitu ambacho hakutarajia, kwamba Mungu
angeweza kusamehe na kubadili alilokusudia watu wakijinyenyekeza, wakatubu, wakaacha njia zao mbaya na kumtafuta
Yeye atasamehe na kuponya nchi husika.. Yamkini hii ilikuwa sababu ya Yona kukasirika Mungu alipowasamehe adui yao.
Inawezekana huyu nabii akawa ndiye yule anayetajwa katika 2Wafalme 14:25 kama Yona mwana wa Amitai. Iwapo
ndiye, basi hii inazungumzia huduma yake ya awali. Kipindi hicho alitabiri kuwa Yeroboamu II (793-753) angepanua mpaka
wa kaskazini wa Israeli kwa kuitia hasara Shamu (Syria), ambayo kwenye utawala wa ufalme wake Hazaeli alikuwa
amepokonya eneo kubwa la Israeli.
Ingawa baadhi ya wasomi wanaotumia akili za kibinadamu wamekihesabu kitabu cha Yona kama kisa cha mambo ya
ajabu au hadithi ya kubuniwa, Haifai kusadiki tu nusu ya uthibitisho wake wa kihistoria, kwa sababu majina na sehemu
zinazotajwa kwenye kitabu ni za kihistoria. Zile nukuu Yesu alizofanya kwenye Yona (Mat.12:39,40; na Lk.11:29,30), yote
haya yanaonyesha msingi wa kihistoria kuhusu matukio yaliyoandikwa kwenye kitabu hiki cha Yona. Yona alimtangulia
Amosi na alihudumu wakati wa Mfalme Yeroboamu II, aliyekuwa mfalme mwenye nguvu kuliko wote katika Israeli (793-753
K.K. - angalia 2Wafalme 14:23-25).
Wazo Kuu
Wingi wa rehema za Mungu watu wanaposikia neno wakaamini na kutubu, anavyosamehe na kufuta hukumu iliyokuwa
inawakabili. Mungu hapendi mtu ye yote aangamie, bali afikilie toba. Watu wa Ninawi waliposikia ujumbe wa Yona juu ya
kuangamizwa kwao, walimsadiki Mungu, mfalme akatangaza kufunga, wakajinyenyekeza tangu mkubwa kabisa hadi
mdogo wa wote pamoja na wanyama, wakavaa nguo za magunia, wakatubu. Mungu akasikia toba yao akasamehe. Toba
ya Ninawi ilikuwa ya muda mfupi kwa sababu baadaye iliharibiwa mnamo mwaka 612 K. K. Ashuru ilikuwa adui mkubwa wa
Israeli na iliishinda Israeli mwaka wa 722 B.C
Mwandishi
Yona mwana wa Amitai.
Kusudi
(1)Wito wa Mungu.(2) Ujumbe wa wokovu ni kwa watu wote. (3)Toba ya kweli. (4)Kuonyesha ukubwa wa neema ya
Mungu. (4)Kukasirishwa kwa Yona

Mambo Muhimu
Hiki kitabu ni tofauti na vitabu vingine vya unabii kwa sababu mkazo uko katika kuelezea habari za nabii na sio unabii wake.
Ni sentensi moja tu inayotoa ufupisho wa ujumbe wake kwa watu wa Ninawi (3:4). Kitabu cha Yona kinatoa maelezo ya
kihistoria inatajwa pia na Yesu kama picha ya kifo na kufufuka kwake (Mathayo 12:38-42)

Mahali
Ninawi.

Tarehe
Kama mwaka 760 K.K.

Wahusika Wakuu
Yona, nahodha wa meli na mabaharia, nyangumi, Mfalme wa Ninawi na Waninawi wote.

Mgawanyo
• Yona anamkimbia Mungu. (1:1-17)
• Sala ya Yona na kuokolewa. (2:1-10)
• Yona aenda Ninawi. (3:1-10)
• Yona amkasirikia Mungu kwa sababu ya huruma yake. (4:1-11)

a
Nyangumi ni samaki mkubwa sana. Ona pia 1:17; 2:10
1
YONA
ilivyokupendeza.’’ 15Kisha walimchukua Yona,
Yona Anamkimbia BWANA wakamtupa baharini nayo bahari iliyokuwa
Neno la BWANA lilimjia Yona mwana wa imechafuka ikatulia. 16Katika jambo hili watu
1 Amitai. 2“Nenda katika mji mkubwa wa wakamwogopa BWANA sana, wakamtolea
Ninawi ukahubiri juu yake, kwa sababu uovu BWANA dhabihu na kumwekea nadhiri.
wake umekuja juu mbele zangu.’’ 17Lakini BWANA akamwandaa nyangumi
3Lakini Yona alimkimbia BWANA na kummeza Yona, naye Yona alikuwa ndani ya
kuelekea Tarshishi. Alishuka mpaka Yafa, tumbo la nyangumi kwa siku tatu mchana na
ambapo alikuta meli iliyokuwa imepangwa usiku.
kuelekea bandari ile. Baada ya kulipa nauli,
akapanda melini na kuelekea Tarshishi ili Maombi ya Yona Katika Tumbo la Nyangumi
kumkimbia BWANA. 4Ndipo BWANA akatuma
upepo mkali baharini, nayo dhoruba kali sana 2 Akiwa ndani ya tumbo la nyangumi, Yona
alimwomba BWANA Mungu wake.
ikavuma hata meli ikawa hatarini kuvunjika. 2Akasema :
5Mabaharia wote waliogopa na kila mmoja

akamlilia mungu wake mwenyewe. Nao ‘‘Katika shida yangu nalimwita BWANA,
wakatupa mizigo baharini ili meli ipungue uzito.
Lakini Yona alikuwa ameteremkia chumba naye akanijibu.
cha ndani ya meli, mahali ambapo alilala na Kutoka kina cha kaburi niliomba msaada,
kupatwa na usingizi mzito. 6Nahodha nawe ukasikiliza kilio changu.
akamwendea na kusema, “Wewe unawezaje 3Ulinitupa kwenye kilindi,

kulala? Amka ukamwite mungu wako! Huenda ndani kabisa ya moyo wa bahari,
akatuangalia, tusiangamie.” mikondo ya maji ilinizunguka,
7Kisha mabaharia wakasemezana wao kwa mawimbi yako yote na viwimbi vilipita juu
wao, “Njoni, tupige kura tumtafute anayehusika yangu.
na maafa haya.’’ Wakapiga kura, kura 4Nikasema, ‘Nimefukuziwa mbali na uso wako,

ikamwangukia hata hivyo nitatazama tena kuelekea hekalu


Yona. lako takatifu.
8Kwa hiyo walimuuliza, “Tuambie, ni nani 5Maji yaliyonimeza yalinitisha,

anayehusika kwa kutuletea tatizo hili lote? kilindi kilinizunguka,


Unafanya kazi gani? Umetoka wapi? Nchi yako mwani a ulijisokota kichwani pangu.
ni ipi? Wewe ni kutoka taifa lipi?’’ 6Nilizama chini sana mpaka pande za mwisho
9Akajibu, ‘‘Mimi ni Mwebrania, nami za milima,
namwabudu BWANA, Mungu wa Mbinguni, makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata
aliyeumba bahari na nchi kavu.’’ milele.
10Hili liliwaogopesha nao wakamuuliza, Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni,
“Umefanya nini?’’ (Walijua alikuwa anamkimbia Ee BWANA Mungu wangu.
BWANA, kwa sababu alishawaambia hivyo.)
11Bahari ilikuwa inazidi kuchafuka. Kwa hiyo 7‘‘Wakati
uhai wangu ulipokuwa unatoka,
walimuuliza, “Tukutendee nini ili kufanya bahari nilikukumbuka Wewe, BWANA,
itulie kwa ajili yetu?’’ maombi yangu yalikufikia wewe,
12Akawajibu, ‘‘Niinueni mkanitupe baharini, katika hekalu lako takatifu.
nayo itakuwa shwari. Ninajua mawimbi haya
makubwa yamewatokea kwa ajili ya kosa 8“Wale watu wanaong’ang’ana na sanamu
langu.’’ zisizofaa
13Badala yake, wale watu walijitahidi kupiga hupoteza neema ile ambayo ingekuwa yao.
makasia wawezavyo ili wapate kurudi pwani. 9Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani,

Lakini hawakuweza, kwa kuwa bahari ilizidi nitakutolea dhabihu.


kuchafuka kuliko mwanzo. 14Ndipo wakamlilia Nililowekea nadhiri nitalitimiza.
BWANA, ‘‘Ee BWANA, tafadhali usituue kwa Wokovu watoka kwa BWANA.’’
kuondoa uhai wa mtu huyu. Usituhesabie hatia
kwa kuutoa uhai wa mtu asiyekuwa na hatia, a5 “Mwani” hapa maana yake ni magugu yaotayo kwenye sakafu
kwa kuwa wewe Ee BWANA, umefanya kama ya kilindi cha bahari.

2
YONA
10BasiBWANA akamwamuru yule nyangumi, Hasira ya Yona Kwa Ajili ya Huruma ya
naye akamtapika Yona katika nchi kavu. BWANA.

Yona Aenda Ninawi 4 Lakini Yona alichukizwa sana akakasirika.


2Akamwomba BWANA, “Ee BWANA, hili si

3 Ndipo neno la BWANA likamjia Yona


mara ya pili. 2Ondoka uende katika mji
lile nililolisema nilipokuwa ningali nyumbani? Hii
ndiyo sababu niliharikisha kukimbilia Tarshishi.
mkubwa wa Ninawi, ukautangazie ujumbe Nikifahamu kuwa wewe ni Mungu mwenye
ninaokupa.” neema na huruma, si mwepesi wa hasira na
3Yona akalitii neno la BWANA naye amejaa upendo, ni Mungu ambaye hughairi
akaenda Ninawi. Basi Ninawi ulikuwa mji katika kupeleka maafa. 3Sasa, Ee BWANA,
maarufu sana, ilichukua siku tatu kuuzunguka. niondolee uhai wangu, kwa kuwa ni afadhali
4Siku ya kwanza, Yona aliingia mjini. mimi nife kuliko kuishi.’’ 4Lakini BWANA

Akatangaza: “Baada ya siku arobaini Ninawi akamjibu, “Je unayo haki yo yote kukasirika?’’
utaangamizwa.’’ 5Watu wa Ninawi wakamsadiki 5Yona akatoka nje akaketi mahali upande

Mungu, wakatangaza kufunga, nao watu wote wa mashariki wa mji. Hapo akajitengenezea
kuanzia mkubwa sana hadi yule mdogo kabisa, kibanda, akaketi kwenye kivuli chake na
wakavaa nguo ya gunia. kungojea ni nini kitakachotokea katika mji.
6Habari zilipomfikia mfalme wa Ninawi, 6Ndipo BWANA, Mungu akaweka tayari mzabibu

aliondoka kwenye kiti chake cha enzi, akavua na kuufanya uote, kumpatia Yona kivuli
majoho yake ya kifalme, akajifunika nguo ya kilichomfunika kichwa ili kuondoa taabu yake,
gunia kisha akaketi chini mavumbini. 7Ndipo naye Yona akafurahi sana kwa ajili ya ule
akatoa tangazo katika Ninawi yote: mzabibu. 7Lakini kesho yake asubuhi na
mapema Mungu akaamuru buu, autafune
“Kwa amri ya mfalme na wakuu wake: mzabibu huo nao ukanyauka. 8Wakati jua
lilipochomoza, Mungu akautuma upepo wa hari
Msiruhusu mtu ye yote au mnyama, wa mashariki, nalo jua likawaka juu ya kichwa
makundi ya ng’ombe au wanyama wengine cha Yona mpaka akazimia. Akatamani kufa,
wafugwao, kuonja kitu cho chote, naye akasema, “Ni afadhali mimi nife kuliko
msiwaruhusu kula wala kunywa. 8Bali kuishi.’’
wanadamu na wanyama wafunikwe kwa 9Lakini Mungu alimwambia Yona, “Je, unayo

nguo ya gunia. Kila mmoja afanye hima haki kukasirika kuhusu mzabibu huo?’’
kumwomba Mungu. Waziache njia zao Akasema, “Ndiyo ninayo haki. Nimekasirika
mbaya na udhalimu ulio mikononi mwao. 9Ni kiasi cha kufa.’’
nani ajuaye? Huenda Mungu akaghairi kwa 10Lakini BWANA akamwambia, “Wewe

huruma yake akaacha hasira yake kali ili waona vibaya kwa ajili ya mzabibu huu, nawe
tusiangamie.’’ hukuusababisha kuota wala kuutunza. Uliota
usiku mmoja nao ukafa usiku mmoja. 11Lakini
10Mungu alipoona walivyofanya na jinsi Ninawi ina zaidi ya watu mia moja na ishirini elfu
walivyogeuka kutoka katika njia zao mbaya, ambao hawawezi kupambanua kulia au kushoto
akawa na huruma wala hakuleta maangamizi pamoja na ng’ombe wengi. Je, hainipasi kufikiri
juu yao kama alivyokuwa ameonya. juu ya mji ule mkubwa?’’

You might also like