You are on page 1of 26

DANSI KANISANI.

(BIBLIA IMESEMAJE KUHUSU KUCHEZA KANISANI/IBADANI)

Na,
Ev. Malugu
0763577531/0658626432
SEHEMU YA KWANZA: DANSI KANISANI
DANCE IN THE CHURCH….
• Fungu kuu: Zaburi 150:4
“Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi”
Uimbaji huanzia mbinguni
• Karama ya uimbaji bila shaka ilianzishwa na Mungu mwenyewe. Sefania 3:17
“Bwana, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa; Atakushangilia
kwa furaha kuu, Atakutuliza katika upendo wake, Atakufurahia kwa kuimba. Yeye
hugawa vipaji kwa viumbe vyake”.
• Yesu ambaye ndiye Muumbaji wa vitu vyote (Yohana 1:1-3,14; Wakolosai
1:16,17) akiwa hapa duniani alikuwa anaimba Mathayo 26:30 Nao walipokwisha
kuimba, wakatoka nje kwenda mlima wa Mizeituni.
• Isaya 6:1-8 “1Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana
ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi
lake zikalijaza hekalu. 2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na
mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu
yake, na kwa mawili aliruka. 3 Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema,
Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu
wake. ……” (Ufunuo 4:6-8)
Hawa maserafi wanaosimama mbele ya kiti cha enzi,
• Wanapoimba wimbo wao wa kumtukuza Mungu wanafunika nyuso
zao kwa mbawa zao mbili za kwanza kila mmoja. Nichol
(4SDABC1977:128) anaeleza kuwa hawa maserafi hufanya hivyo
ikiwa ni dalili ya ‘kuonyesha kicho na heshima kuu mbele za Mungu’
aliye Muumbaji na Mfalme wa milele.
• Maserafi wasio na mawaa katika tabia zao, wanasimama kwa
kicho….., jinsi gani wanadamu walioanguka katika dhambi
wanapaswa kuwa na uchaji na heshima mbele za Mungu. Mavazi, n.k.
• Huduma ya nyimbo ni ibada na wote wanaoingia katika huduma hii
wanapaswa kuwa watakatifu na wenye kumwogopa Mungu.
• Tukiguswa na kaa la moto (Roho Mtakatifu) kutoka kwenye
madhabahu ya Mungu ndipo huduma zetu za uimbaji zitafaa mbele za
Mungu.
Kusudi la huduma ya Nyimbo ni nini?
• Bila shaka kusudi la huduma ya nyimbo ni kwamba utakatifu na ukuu
wa Mungu uweze kuingizwa mawazoni mwa watu wanaosikiliza na
mioyo yao ipate kuinuliwa juu kwa Mungu katika kicho na heshima.
Nyimbo zikiimbwa kwa uzuri wa utakatifu wake na vyombo
vikipigwa kwa umahiri wa hali ya juu sana, huwa ni mbaraka wa
pekee kwa waabuduo. Kinyume chake ni laana…..
UIMBAJI AGANO LA KALE
2 Nyakati 5:12 “tena Walawi waimbaji, wote pia, yaani Asafu, na Hemani, na Yeduthuni, na wana
wao, na ndugu zao, hali wamevaa kitani safi, wenye matoazi na vinanda na vinubi, wamesimama
upande wa mashariki wa madhabahu, na pamoja nao makuhani mia na ishirini wakipiga panda;) 13
hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu
na kumshukuru Bwana nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu
Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba
ikajawa na wingu, naam, nyumba ya Bwana,..”
2 Nyakati 7:6 “Wakasimama makuhani sawasawa na malinzi yao; Walawi nao
pamoja na vinanda vya Bwana, alivyovifanya Daudi mfalme, ili kumshukuru
Bwana, kwa maana fadhili zake ni za milele, hapo aliposifu Daudi kwa mikono yao;
nao makuhani wakapiga panda mbele yao; nao Israeli wote wakasimama.”
2 Nyakati 20:18 “Yehoshafati akainama kichwa, kifulifuli; wakaanguka mbele za
Bwana Yuda wote na wakaao Yerusalemu, wakimsujudia Bwana. 19 Na Walawi, wa
wana wa Wakohathi na wa wana wa Wakorahi, wakasimama ili wamsifu Bwana,
Mungu wa Israeli, kwa sauti kuu sana.”
References To Dance, Old Testament
Four out of 28 references to dance in the Bible refer without dispute to religious
dancing but none of these have to do with public worship conducted in the House of
God. (Marejeo manne kati ya 28 ya dansi katika Biblia yanarejelea bila ubishi dansi ya kidini lakini hakuna
hata moja kati ya hizo inayohusiana na ibada ya hadhara inayofanywa katika Nyumba ya Mungu.)
1. Neno la kiebrania chagag limetafsiriwa mara moja kama “dansi” katika 1Samwel
30:16 kuhusiana na kunywa na kucheza kwa waamaleki. Hii sio dansi ya kidini. “Na
hapo alipokuwa amewaongoza chini, tazama, hao walikuwa wametawanyika juu ya nchi yote, wakila
na kunywa, na kufanya karamu, kwa sababu ya hizo nyara kubwa walizochukua katika nchi ya
Wafilisti, na katika nchi ya Yuda”
2. Neno la kiebrania chuwl limetafsiriwa mara mbili kama “dansi”
katika Waamuzi 21:21, 23 21 mkaangalie, kisha tazameni, kwamba hao binti za Shilo
watoka ili wacheze katika hiyo michezo, basi tokeni ninyi mizabibuni, nanyi kila mtu na amshike
mkewe katika hao binti za Shilo, kisha rudini nchi ya Benyamini. 23 Wana wa Benyamini wakafanya
vivyo, wakajitwalia wake, sawasawa na hesabu yao, katika hao waliocheza, wakawachukua
wakaenda nao; kisha wakaenda kuurudia urithi wao, na kuijenga miji na kuikaa.
References To Dances…
3. Neno la kiebrania karar limetafsiriwa mara mbili kama ‘dansi’ katika
2samwel 6:14, 16. “14 Daudi akacheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote;
na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani. 16 Ikawa, sanduku la Bwana
lilipoingia mji wa Daudi Mikali, binti Sauli, akachungulia dirishani, akamwona
mfalme Daudi akiruka-ruka na kucheza mbele za Bwana; akamdharau moyoni
mwake.” maelezo yake tutayaona kwa mbele.
4. Neno la kiebrania Machol (maholi) limetafsiriwa mara sita kama ‘dansi’. Zaburi
30:11 imetumia neno hilo kishairi (poetically). “11 Uligeuza matanga yangu kuwa
machezo; Ulinivua gunia, ukanivika furaha.”
Yeremia 31:4 na 13 “4 Mara ya pili nitakujenga, nawe utajengwa, Ee bikira wa
Israeli mara ya pili utapambwa kwa matari yako, nawe utatokea katika michezo yao
wanaofurahi”.
13 Ndipo bikira atafurahi katika kucheza, na vijana na wazee pamoja; maana nitageuza masikitiko
yao kuwa furaha, nami nitawafariji, na kuwafurahisha waache huzuni zao.
Mafungu haya yanaongelea……..hayahusiani kabisa na kucheza ibadani.
Celebration Dance
• Neno la kiebrania Mecholah limetafsiriwa mara saba kama ‘dansi’.
Mafungu tano kati ya saba (5/7), yanaeleza kucheza kwa wanawake
wanaosherehekea ushindi wa kijeshi (1 Sam 18:6; 21:11; 29:5; Judges
11:34; Exodus 15:20).
• Miriamu na wanawake walicheza kusherehekea ushindi dhidi ya jeshi
la Misri (Kut 15:20).
• Binti wa Yeftha alicheza kufurahia ushindi wa baba yake dhidi ya
Waamoni (Waamuzi 11:34).
• Wanawake walicheza kusherekea/kufurahia ushindi, Daudi alipomwua
Mfilisiti (Goliath) (1 Sam 18:6; 21:11; 29:5)
• Mafungu mawili yaliyobaki yanaelezea Israeli walicheza uchi
kuzunguka ndama ya dhahabu (sanamu) (kutoka 32:19) na binti za
shilo walicheza mizabibuni (Waamuzi 21:21)
• In none of these instances is dance a part of a worship service. Miriam’s dance
may be viewed as religious, but so were the dances performed in conjunction with
the annual festivals. But these dances were not seen as a component of a divine
service. They were social celebrations of religious events. The same thing occurs
today in Catholic countries where people celebrate annual holy days by organizing
carnivals.
• Neno la kiebrania raqad limetafsiriwa mara nne kama ‘dansi/cheza’ (1
Nyakati 15:29; Ayubu 21:11; Isaya 13:21; mhubiri 3:4).
• Moja inaelezea namna watoto hucheza (Ayubu 21:11)
• Lingine ni ‘satyr dancing’ (Isa 13:21), which may refer to a goat or a figure
of speech.
• Katika Mhubiri 3:4 neno kucheza limetumika kishairi kuelezea wakati wa
wakucheza kutofautisha wakati wa kuomboleza.
• Fungu la nne (1 Nyakati 15:29) kumhusu Daudi limeelezwa vizuri mbele..
Dancing in Pagan Worship.
• There is the dancing of the Israelites at the foot of Mount Sinai around
the golden calf (Ex 32:19).
• There is an allusion to the dancing of the Israelites at Shittim when
“the people began to play harlot with the daughter of Moab” (Num
25:1). The strategy used by the Moabites women was to invite Israelite
men “to the sacrifice of their gods” (Num 25:2), which normally
entailed dancing.
• There was shouting and dancing on Mount Carmel by the prophets of
Baal (1 King 18:26). The worship of Baal and other idols commonly
took place on the hill with dancing. Thus, the Lord appeals to Israel
through the prophet Jeremiah: “Return, faithless people; I will cure
you of backsliding. .. . Surely the idolatrous commotion on the hills
and mountains is a deception” (Jer 3:22-23, NIV).
Dansi kanisani!
• Tuangalie ndani ya Maandiko Matakatifu tuone kama kuna dansi au kucheza
ndani ya Biblia. Tuangalie maneno ya kiebrania na tafsiri zake zilizotumika;
➢Kwanza; kutoka 15:20-21 “20 Na Miriamu, nabii mke, ndugu yake Haruni,
akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake,
wenye matari na kucheza. 21 Miriamu akawaitikia,Mwimbieni Bwana ,kwa
maana ametukuka sana;Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.
• Tukio hili lilitokea baada ya Mungu kuwaangamiza wamisri kwa kuwafunika na
maji katika bahari ya shamu wakiwa katika harakati za kuwa fuatia wana wa
Israeli ili kuwarudisha utumwani katia nchi ya misri.
• Neno la kiebrania lililotumika hapa ni ‘mecholah (miholah)’ humaanisha
kutembea (matching) katika mduara. Kufafanua zaidi ‘mecholah (miholah)’
humaanisha kucheza (kutembea) katika mistari miwili, kucheza katika kambi la
jeshi . Jeshi kucheza gwaride haina maana kwamba jeshi linanengua viuno na
kukatika katika viungo vyao. Hucheza gwaride kwa kutembea katika mistari
miwili au zaidi na kwa utaratibu…..
• Jambo jingine ‘hawakuwa kwenye ibada au mkutano wowote wa
mafundisho ya neno la Mungu’. Bali walikuwa safarini kutoka nchi ya
misri Kwenda kaanani.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
• Neno hilohilo ‘mecholah (miholah’) limetumiwa katika 1Samweli
18;6 Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua
yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na
kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda.
• Pia Waamuzi 11:34 Kisha Yeftha akafika Mispa nyumbani kwake, na tazama,
binti yake akamtokea kumlaki, na matari na machezo; naye alikuwa ni mwanawe
pekee; hakuwa na mwingine, mwana wala binti, ila yeye.
• (Limetumiwa wakati binti wa Yeftha alipotoka kumlaki baba yake
alipotoka vitani)
• Kutoka 32:6, 19 “6 Wakaondoka asubuhi na mapema, wakatoa dhabihu,
wakaleta sadaka za amani, watu wakaketi kula na kunywa, wakaondoka
wacheze”. 19 Hata alipoyakaribia marago akaiona ile ndama, na ile michezo.
Hasira ya Musa ikawaka, akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini
ya mlima.
• >>Tukio hili lilitokea baada ya uasi wa maagizo ya Mungu kufanyika.
Ndama ilitengenezwa kinyume na amri ya Mungu…(kutoka 20:4-6).
Neno la kiebrania lililotumika hapa ni ‘tsachaq (sahak)’ ambalo
humaanisha “kucheka, kumcheka mtu Fulani, kudhihaki, kutukana,
kucheza (to play) lakini sio dansi. David (The Analytical Hebrew and
Chalideen Lexicon 1993:643). Hapa dhihaka ilikuwa ni kwa Mungu
kwa maana hawa waasi ilionekana Mungu ameshindwa kuwapeleka
katika nchi ya kanaani na hivyo waliamua kurudi katika nchi ya
misri…..
• 2Samweli 6:5 “sachaq” to laugh, mock, play,.. (not authentic or real, but
without the intention to deceive).
• Pia katika 2Samweli 6:14 “Daudi akacheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote;
na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani”.
Neno la kiebrania lililotumika hapo ni ‘karar’ humaanisha ‘kurukaruka na
kuzungukazunguka (leaping and whirling)’. Daudi alikuwa kwenye msafara wa kulileta
sanduku la Bwana kutoka kwenye nyumba ya Obed-Edom hadi kwenye mji wa Daudi.
Daudi kwa furaha alirukaruka…kama ndama….ni kama mwanafunzi apatapo matokeo
mazuri.
• 1Nyakati 15:29 “Hata ikawa, sanduku la agano la Bwana lilipofika mjini kwa Daudi,
Mikali binti Sauli akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi, akicheza na
kushangilia; akamdharau moyoni mwake.”
• >>> ‘raqad’ humanisha kurukaruka………
Mambo ya kuzingatia.
1. Daudi hakuwa na maandalizi yoyote ya namna ya kucheza. Yeye
alirukaruka……
2. Hakuwa na timu au kikundi cha watu ambacho alifanya nacho maandalizi
kwa ajili ya kucheza.
3. Hakuwa hekaluni au kwenye mkutano wa ibada au mafundisho yoyote ya
neno la Mungu.
4. Daudi hakuwa anacheza kama ni sehemu ya ibada mbele za Mungu. Pia
hatuoni kama alikuwa anaimba wimbo wowote…..
• Tuangalie Zaburi 149:3 “Na walisifu jina lake kwa kucheza, Kwa matari na
kinubi wamwimbie.” Zaburi 150:4 “3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni
kwa kinanda na kinubi; 4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na
filimbi;”
• Kiebrania kimetumia neno ‘maholi’ . Baadhi ya wana-eliungu
(Theologians) huamini kwamba ‘maholi’ hutokana na neno ‘chuwl’ ambalo
humaanisa “fanya uwazi”. Kwa maelezo hayo inawezekana ni chombo cha
muziki chenye uwazi kama vile bomba. Tafsiri hii yaweza kuwa sahihi kwa
sababu tukiangalia kwa makini sana tunaweza kuona kuwa ‘maholi’ ni
chombo cha muziki kwa sababu kuna usambamba (parallelism) wa vyombo
vya muziki.
• ‘The study Bible, tafsiri ya Mfalme James, katika footnote, inatafsiri kuwa neno
‘maholi’ kuwa ni chombo cha Muziki aina ya ‘bomba’ (pipe), KJV (The Study
Bible Presenting The Old and The New Testament in the E.G.White Scripture
comments, 1993:670).
• Jambo jingine katika Zaburi…. Ni lugha ya kitamathali au kisitiari (figurative),
ambayo hairuhusu kutafsiri kihalisia (Literary) kucheza dansi ndani ya nyumba ya
Mungu.
• Morphology ya mafungu haya: Noun, Masculine, Singular (N-MS).
References to Dance, New Testament
• Maneno mawili ya kigiriki/kiyunani yametafsiriwa kama ‘dansi’ katika
Agano Jipya.
1. orcheomai, ambalo limetafsiriwa mara nne kama ‘dansi’ kuhusiana
na kucheza kwa binti yake Herode (Mathayo 14:6; Mark 6:22)
Mathayo 14: 6 “Hata ilipofika sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodia
alicheza mbele ya watu, akampendeza Herode”.
na kucheza kwa Watoto (Mathayo 11:17; Luke 7:32)
Luka 7:32 “Wamefanana na watoto walioketi sokoni na kuitana, wakisema,
Tuliwapigia filimbi wala hamkucheza; tuliomboleza, wala hamkulia.”
NB: The word orcheomai means to dance in a rank-like or regular
motion and is never used to refer to religious dance in the Bible.
2. Choros. Limetumika mara moja tu katika Luka 15:25
25 Basi, yule mwanawe mkubwa alikuwako shamba na alipokuwa akija na
kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na machezo.
• The translation “dancing” is disputed because the Greek chorus occurs
only once in this passage and is used in extra-biblical literature with
the meaning of “choir” or “group of singers.”
• At any rate, this was a family reunion of a secular nature and does not
refer to religious dancing.
• The conclusion that emerges from the above survey of the twenty
eight references to dance is that dance in the Bible was essentially a
social celebration of special events, such as a military victory, a
religious festival, or a family reunion. Dance was done mostly by
women and children. The dances mentioned in the Bible were either
processional, encircling, or ecstatic.
• No biblical references indicate that men and women ever danced
together romantically as couples. As H. Wolf observes, “While the
mode of dancing is not known in detail, it is clear that men and women
did not generally dance together, and there is no real evidence that
they ever did.”
• Furthermore, contrary to popular assumptions, dance in the Bible was
never done as part of the divine worship in the Temple, synagogue, or
early church.
Ishara ya kufungwa kwa mlango wa rehema
• Bwana amenionyesha kuwa mambo ambayo umeyaelezea kuwa yanatokea huko Indiana,
yatatokea muda mfupi kabla ya kufungwa kwa mlango wa rehema. Kila jambo la
kishenzi litafanywa. Kutakuwepo makelele, pamoja na ngoma, muziki na kucheza.
Fahamu za viumbe wenye akili zitachanganywa kiasi kwamba hazitaweza kufanya
maamuzi sahihi. Na hayo yataitwa matendo ya Roho Mtakatifu.
• Roho Mtakatifu kamwe hajidhihirishi kwa njia kama hizo, yaani katika makelele na
zahama kana kwamba ni sauti za vichaa, (bedlam of noise). Huu ni ubunifu wa Shetani ili
kuficha mbinu zake kwaujanja akiwa na lengo la kuharibu nguvu ya ukweli wa wakati
huu ulio safi na wenye
kuinua na kutakasa watu.
• Ni bora zaidi kumwabudu Mungu bila muziki kuliko kutumia ala (vyombo vya
muziki) za muziki kufanya kazi ambayo ilionyeshwa kwangu kuwa ingeletwa katika
mikutano yetu…..nguvu za mashetani hujichanganya na makelele na kuamsha
misisimko….shetani anafanya kazi katikati ya makelele na mchanganyiko wa muziki
kama huo, ambao kama ungeendeshwa vizuri, ungemsifu na kumtukuza Mungu. Shetani
anaufanya muziki kuwa na madhara yanayofanana na sumu ya nyoka mwilini…..
shetani ataufanya muziki kuwa mtego kwa namna utakavyoendeshwa ( Selected
Messages, book 2, Uk. 36, 37, 38)
• Moja ya makongamano kama hayo yalipitishwa mbele yangu, ambapo walikuwa
wamekusanyika wale wanaodai kuuamini ukweli. Mmoja alikuwa amekalia ala
ya muziki, na nyimbo zilizoimbwa ziliwafanya malaika kulia na kutoa
machozi. Kulikuwepo na uchangamfu ulioambatana na kicheko kisichokuwa na
adabu, kulikuwepo na wingi wa misisimko na hamasa ya aina yake; lakini furaha
kama ile ni shetani tu kuileta. Huu ni uchangamfu wa ovyo ambao watu
wanaompenda Mungu hawawezi kujihusisha nao hata kidogo. Unawaandaa
washirika wake kuwaza na hatimaye kutenda matendo machafu (Counsels to
Teachers, Uk. 339)
• Malaika wanavinjari karibu na nyumba ambapo vijana wanakutana.
Kuna mvumo wa sauti za vyombo vya muziki. Wakristo wanakutana
pale, lakini unasikia kitu gani pale? Ni nyimbo za pambio za kipuuzi
tu zizizositahili kuimbwa katika ukumbi wa ibada. Tazama Malaika
watakatifu hukunja mbawa zao karibu nao. Ndipo wale walio
nyumbani hufunikwa na giza. Kisha Malaika huondoka pale, nyuso
zao zikijaa huzuni, wanalia. Haya niliyaona mara nyingi yakitokea
katika makundi ya watunzao Sabato. White (Messages to Young
People, 97, 297 cf. 1T p.506)

Mungu Atusaidie!
SEHEMU YA PILI: KELELE ZA SHANGWE

You might also like