You are on page 1of 1

TANZANIA TANZANIA TANZANIA

MIAKA MIWILI KAMILI IJAYO BILA KUONGEZA SIKU HATA MOJA (MIEZI 24
KAMILI TU TOKA LEO 01.08.2023 YAANI 01.08.2025), MUNGU ATAKUWA
AMEFANYA JAMBO LA AJABU MNO MNO MNO LISILOTARAJIWA,
LISILODHANIWA KABISA, AMBALO LITAFANYA MACHOZI YA WATU WA UFALME
WA MUNGU YATOKE KWA FURAHA NA KICHEKO, HUKU WALIODHANIWA KUWA
WALAJI WAKILIWA WAZIWAZI! SHINA LITACHIPUKA KATIKA TANZANIA,
AMBALO ROHO WA MUNGU ANAKAA JUU YAKE, LITAKALOONGOZA SIMBA,
MAJOKA, WANYAMA WAKALI NA KUPELEKEA SWALA, PAA, NYATI, NA
WANYONGE KUIFURAHIA TENA NCHI YAO NA ASALI YAKE...
ITAKUWA KAMA NDOTO
ZABURI 126:1-3
ITAKUWA KWA GHAFLA SANA KUZALIWA HUKU KWA TAIFA NDANI YA SIKU
MOJA KUTAKAKOZAA VICHEKO, SHANGWE NA FURAHA ISIYOELEZEKA KWA
WANYONGE KATIKA NCHI....
Isaya 66:8-13
[8]Ni nani aliyesikia neno kama hili?
Ni nani aliyeona mambo kama haya?
Je! Nchi yaweza kuzaliwa siku moja?
Taifa laweza kuzaliwa mara?
Maana Sayuni, mara alipoona utungu,
Alizaa watoto wake.
[9]Je! Mimi nilete wana karibu na kuzaliwa, nisizalishe? Asema BWANA; mimi nizalishaye, je!
Nilifunge tumbo? Asema Mungu wako.
[10]Furahini pamoja na Yerusalemu, shangilieni kwa ajili yake, ninyi nyote mmpendao; furahini
pamoja naye kwa furaha, ninyi nyote mliao kwa ajili yake;
[11]mpate kunyonya, na kushibishwa kwa maziwa ya faraja zake, mpate kukama, na kufurahiwa
kwa wingi wa utukufu wake.
[12]Maana BWANA asema hivi, Tazama, nitamwelekezea amani kama mto, na utukufu wa
mataifa kama kijito kifurikacho, nanyi mtapata kunyonya; mtabebwa; na juu ya magoti
mtabembelezwa.
[13]Mfano wa mtu ambaye mama yake amfariji, ndivyo nitakavyowafariji ninyi; nanyi
mtafarijiwa katika Yerusalemu.
UTUNGU UNAOENDELEA USIKUPUMBAZE WALA KUKUCHANGANYA, MARA
ZOTE MAMA AKIKARIBIA KUZAA LAZIMA KUWE NA VURUGU NYINGI NA KILIO
NA MSHIKE MSHIKE...
Yohana 16:21-22
[21]Mwanamke azaapo, yuna huzuni kwa kuwa saa yake imefika; lakini akiisha kuzaa mwana,
haikumbuki tena ile dhiki, kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtu ulimwenguni.
[22]Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na
furaha yenu hakuna awaondoleaye.

You might also like