You are on page 1of 24

LENT SONGS

UNIONDOLEE DHAMBI NITAKASE

Uniondolee dhambi, nitakase,

Unioshe niwe mweupe pe *2

1.Nakiri makosa yangu, naziona dhambi zangu

Unioshe niwe mweupe pe

2.Mimi kweli mkosefu, tangu kuzaliwa kwangu

Mwenye dhambi tangu tumboni mwa mama yangu

3.Hivyo unafanya vyema, wewe unaponihukumi

Una haki unaponiadhibu

4.Wewe wataka unyofu, ule unyofu wa ndani

Nifundishe hekima moyoni

5.Niumbie moyo safi, na uweke ndani yangu,

WATUMISHI WAKE BABA

1.Watumishi wake Baba wangapi waliopo

Wanakula na kusaza chakula chake Baba

Nami - Nami nataabika hapa

Nashi - Nashiriki na nguruwe


Chaku - Chakula kisichofaa, yanipasa kurudi

Nita - Nitarudi na kusema

Baba - Baba yangu nisamehe

Nime - Nimekosa kwake Mungu, na mbele yako Baba

2.Baba kamwona yu mbali kashikwa na huruma

Akakimbia kumlaki kamkumbata na busu

3.Baba sistahili tena kuitwa mwana wako

Unifanye kama mmoja wa watumishi wako

4.Baba yangu nimekosa ninaomba huruma

Unisamehe nirudi nikakutumikie

5.Wanikaribisha mimi kwenye karamu yako

Meza imeandaliwa inaningoja mimi

6.Nasogea ninakuja ninakukimbilia

Mimi ni mtoto mpotevu Baba unipokee

MWANZI ULIOPONDEKA

Utambi mchafu wa Moshi mzito

Hatauzima, kadhalika mwanzi, uliopondeka kamwe hatauvunja

(Hatanitupa), Bwana Yesu, (milele yote)atanipigania


(Hataniacha) Bwana Yesu,. (niangamie)atanipigania

2. Najua mtetezi wangu ni mwema, mwenye huruma, mwingi wa rehema,


asiyeyahesabu maovu ya watu.

3. Nakiri Mimi mdhaifu kabisa, nimeanguka, kulitii neno, lakini nitamuangukia


mwenyezi.

4. Nanyi ndugu zangu kweli, natubu. Niliyofanya, sikuwapendeza, nisameheni


nichukulieni pia.

CHA KUTUMAINI SINA

1. Cha kutumaini sina Ila damu yake Yesu

Sina wema wa kutosha dhambi zangu kuziosha.

Kwake Yesu nasimama, ndiye mwamba ni salama,

Kwake Yesu nasimama, ndiye mwamba ni salama

2. Njia yangu iwe ndefu yeye hunipa wokovu

Mawimbi Yakinipiga nguvu zake ndizo nanga.

3. Damu yake na sadaka nategemea daima

Yote chini yakiisha mwokozi atanitosha.


4. Nikiitwa Hukumuni Moyoni nina amani

Nikivikwa haki yake Sina hofu mbele zake

BWANA U SEHEMU YANGU

1.Bwana u sehemu yangu,

Rafiki yangu, wewe,

Katika safari yangu,

Tatembea na wewe.

Pamoja na wewe,

Pamoja na wewe,

Katika safari yangu,

Tatembea na wewe.

2.Mali hapa sikutaka,

Ili niheshimiwe,

Na yanikute mashaka,

Sawasawa na wewe.

Pamoja na wewe,
Pamoja na wewe,

Heri nikute mashaka,

Sawasawa na wewe.

3.Niongoze safarini,

Mbele unichukue,

Mlangoni mwa mbinguni,

Niingie na wewe.

Pamoja na wewe,

Pamoja na wewe,

Mlangoni mwa mbinguni,

Niingie na wewe.

FATHER, WE ADORE

1.Father, We adore You.

Lay our lives before You.

How we love You.

2.Jesus, We adore You.


Lay our lives before You.

How we love You.

3.Spirit, We adore You.

Lay our lives before You.

How we love You.

NIRUDIENI MIMI

{Lakini hata sasa, asema Bwana

Nirudieni mimi, kwa mioyo yenu yote } *2

1.Fanyeni mabadiliko mioyoni mwenu

Kwa kufunga na kwa kulia na kwa kuomboleza

Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote

2.Pigeni tarumbeta huko Sayuni

Wambieni watu wote ili wafunge

Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote

3.Kusanyeni watu wote waleteni kwangu


Waleteni na watoto hata na wazee

Nirudieni Mimi kwa mioyo yenu yote

4.Mpingeni yule mwovu atawakimbia

Nikaribieni nami nitawakaribia

Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote

5.Takaseni mikono yenu iliyojaa dhambi

Safisheni mioyo yenu yenye nia mbili

Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote

YATOSHA SASA

Yatosha sasa mahangaiko haya, yatosha, mapigo ni mengi mno. Yatosha sasa
mateso makali haya, yatosha kabisa, yatosha mno.

1. Ee Mungu tazama chozi langu, sikiliza kilio changu. Narudi kwako mara
nyingine, kulilia huruma yako.

2. Natamani nami nipumzike, Ee Mungu chukua hatua. Kwa nini unanyamaza


kimya, naita mpaka nazimia?

3. Siwezi, siwezi ee Mungu; Mizigo yanielemea.

4. Upendo wako Mungu, nitautumainia bila kuchoka.

5. Huruma yako Mungu, ni huruma ya milele. Huruma yako Mungu, nitakufa


nikiitumainia.
NCHI INAZIZIMA

Yuda akarudi, chukua fedha zenu huyu ni mwema,

Pilato akakiri hana kosa lakini kamuueni,

Kainuliwa mtupu na kajeruhiwa sana,

Amekata roho, nchi inazizima kwa huzuni mkuu.

1.Ona damu, mwili umelowana

Ona nyama, madonda mwili mzima

2.Moyo wake, nao umetoboka.

Mate yao, yamemfunika uso.

3.Meno yake, kang'ata kwa uchungu.

Nafsi yangu, imemjeruhi Yesu

4.Dhambi zangu, zikamchomoa roho

Mungu wangu, nionjeshe uchungu

5.Ili nife, pamoja naye Kristu

Mwisho nije, nikafufuke naye

PASIPO MAKOSA

1.Pasipo makosa Mkombozi wetu,

Katika baraza la wakosefu

Na wote walia asulibiwe,


Aachwe Baraba na Yesu afe

Aachwe Baraba na Yesu afe

2.Ee Yesu washika msalaba wako,

Na unakubali kufa juu yake

Ee Yesu useme sababu gani,

Ya nini mateso makali hayo?

Ya nini mateso makali hayo?

3."Ni pendo kwa Baba wa uwinguni,

Ni huruma yangu kwa wakosefu.

Ewe mkristu kumbuka mateso yangu,

Uache makosa, uache dhambi

Uache makosa, uache dhambi"

MSALABANI YESU ALILIA

Msalabani yesu alilia

Mungu wangu mbona waniacha*2

Makuhani walifurahi

Bwana yesu alipokufa

Watu wengi walisema

Maneno mengi yasiyofaa


Dunia yote ilitetemeka

Bwana yesu alipokufa

Watu wengi walishtuka

Kweli huyu ni mwana wa mungu

Ilipofika alasiri

Dunia yote ikawa giza

Papo hapo pazia la hekalu

Likapasuka vipande viwili

Ndugu na dada siku ya leo

Msiwe kama yuke thomaso

Amini leo na kutubu dhambi

Mtasamehewa na bwana yesu

BWANA KAMA WEWE UNGEHESABU MAOVU YETU

(NANI ANGESIMAMA)

Bwana kama wewe ungehesabu maovu yetu,

Nani angesimama, nani angesimama


Nani angesimama mbele yako

1.Lakini kwako kuna msamaha, ili wewe uogopwe,

Nimemungoja Bwana, Roho yangu,

Na neno lake nimelitumaini

2.Nafsi yangu inamngoja Bwana, kuliko walinzi

Walinzi waingojavyo asubuhi

Naam walinzi wangojavyo asubuhi

3.Ee Bwana toka vilindini, nimekulilia

Bwana sauti yangu usikie

Masikio yako yasikie dua zangu

NAWAPA AMRI

Nawapa amri - amri pendaneni (asema Bwana )

{ Kama vile mimi nilivyowapenda nyinyi

(Nanyi) Nanyi pia mpendaneni } *2

1.Wapenzi na tupendane, neno latoka kwa Mungu

Na pia apendaye amezaliwa na Mungu,

(Naye) Naye anamjua Mungu, tupendane

2.Yule asiye na pendo, hakumjua Mungu wetu


Kwa maana Mungu ni mwenye upendo kamili

(Naye) Naye ametuamuru, tupendane

3.Mungu apenda dunia kwa mapendo yake kwetu

Akamtuma mwanaye mwana wake wa pekee

(Hapa) Hapa kwetu duniani, tupendane

4.Kila amkiriye Yesu, kuwa ni mwana wa Mungu

Ndipo Mungu anakaa, ndani yake mtu yule

(Naye) Naye ndani yake Mungu, tupendane

TUKIPENDA WENZETU

Tukipenda wezetu, kati yetu Mungu yupo *2

1.Aliyetufanya tuwe ndugu ndiye Yesu ndugu yetu

Chuki yote na hasira, kati yetu ziondoe

2.Tukimpenda Mungu wetu, tuwaze na nduguze

Audhiye mmoja wao, mapendoye si ya kweli

3.Tuwe moyo mmoja, roho moja, tuwe pia kundi moja

Tupendane kama vile Yesu alivyotuvyotupenda

4..Furahini nyote binadamu, mwimbieni Mungu wenu


Amri yake ni nyepesi, neno lake kupendana

5.Kati ya ugomvi na fitina, na katika kisirani

Mungu wetu hapapendi, Mungu wetu wa amani

6.Yesu Kiongozi wetu, kweli nenole twalijua

Jaza nyoyo za wakristu wapendane siku zote

YESU KANIKUTA JANGWANI

1.Yesu kanikuta jangwani, akaniambia, nenda huko Yerusaleme

Yesu kanikuta gizani, akasema, kimbilia Yerusaleme

Mimi ni kipofu ni mauti (mimi ni mauti)

Mimi ni kipofu sioni (mimi sioni)

{ Kulikuwa giza, kukapambazuka

Nikamwona Bwana Bwana wangu }*2

2.Natamani mji ule, Yerusaleme kuna nuru kuna raha

Dhambi zangu matendo yangu, ni maovu, tazameni msalabani

Upindo wa nguo (nguo yako safi)

Upindo wa nguo (nguo yako nzuri)

{ Uniguse moyo, moyoni mwangu


Nitaimba sifa sifa zako } *2

3.Watakatifu wa moyo, tumsifuni, Bwana mwenye nchi na mbingu

Twende huko nchi ya mbali, ya Kanaani ndiko tutaishi milele

{ Fimbo yake Musa ilituokoa

Fimbo yake Musa, ilituongoza

{ Nchi ile ya Misri (nchi ya farao)

Tulimwona Bwana mwenye enzi } }*2

AMIN AMIN NAWAAMBIA

1.Amin, amin, nawaambia, ninawaambia

Amin, amin, mmoja wenu, atanisaliti

Nitampiga mchungaji wa kondoo oo

Na kondoo wa kundi lake watatawanyika*2

2.Mwana wa Adamu aenda zake, ilivyoandikwa

Ole ni wake mtu yule, amsalitiye

Ole wangu, ole wako, umsalitiye Bwana


Ingekuwa heri kwetu tusingelizaliwa *2

3.Twaeni mle mwili wangu, uwe ukumbusho

Twaeni mnywe damu yangu, iwe ukumbusho

Nitampiga mchungaji wa kondoo oo

Na kondoo wa kundi lake watatawanyika*2

4.Amini, amini na kutubu, enyi mataifa

Amini, amini na kutubu, turudi kwa Bwana

Ole wangu, ole wako, umsalitiye Bwana

Ingekuwa heri kwetu tusingelizaliwa *2

KUTESWA KWAKE BWANA

1.Kuteswa kwake Bwana kulinipa wokovu

Siachi kumuimbia pote niendapo *2

(Aliyeniokoa ni Yesu aliyevumilia mateso

aliyemwaga damu mtini ndiye Bwana wangu *2)

2.Na kwa kunipenda mimi, aliuawa akafa

Ni pendo la ajabu kunifia *2


3.Rohoni nimeoshwa kwa damu ya thamani

Makosa yameoshwa naye Mwokozi *2

RARUENI MIOYO

Rarueni mioyo mioyo yenu wala si mavazi yenu*2

Mrudieni mungu, mungu mwenyezi

amejaa huruma,huruma na neema

rarueni mioyo yenu

Mwenyezi mungu hachukii upesi,

mwingi wa fadhili tayari kusamehe,

rarueni mioyo yenu

Huko sayuni pigeni tarubeta

waamuruni watu,wote wafunge,

rarueni mioyo yenu

Wakusanye watoto hata wanaonyonya,

na maharusi toka vyumbani mwao,

rarueni mioyo yenu


Mlango wa hekalu mpaka madhabahuni,

makuhani walie na kumwomba,

rarueni mioyo yenu

Ndipo mwenyezi ataipenda nchi,

atawahurumia hawa watu wake,

rarueni mioyo yenu

BWANA NI NGOME NA

MWAMBA WANGU.

(Bwana ni ngome na mwamba wangu ninaye

mkimbilia, naye ni amani yangu moyo wangu

watulia wake) *2

1.Bwana wangu kanitoa,kwenye maji mengi m–no,

kwa kuwa a–nanipenda.

2.Nami nampenda bwana, kwa kuwa ndiye nguvu

yangu, na wimbo wa-ngu milele.


3.Njia zake bwana mungu, ni amini na adili,

ni-tazifwata milele.

BWANA ASEMA NJOONI

KWANGU.

(Bwana asema, njooni kwangu nyote msumbukao,

na kulemewa nakulemewa na mizigo, nami

nitawapumzisha)*2 (mjitwike nira yangu,

nakujifunza kwangu, mimi ni mpole na

mnyenyekevu wa moyo)*2

1.Kwa maana nira yangu, ni laini, na mzigo wangu,

ni mwepesi.

2.Mimi ndiye njia kweli, na uzima, anifwataye,

hatapotea.

3.Mimi ndiye mkate kweli, wa uzima, anipokeaye,

ataishi.
YESU NAKUHITAJI

1.{(S)Yesu nina(ALL)Kuhitaji katika Maisha yangu}*2

{(Tsol)Usiniache(ALL)Usiniache mwokozi

(Tsol)Ninavyo(ALL)Ninavyo kukasirisha

(Tsol)Wewe(ALL)Wewe ndiwe(B){Peke}Bwana wangu.}*2

2.{(S)Nijalie (ALL)Kuwajua marafiki wa uongo}*2

{(Tsol)Nizijue(ALL)Nizijue hila zao

(Tsol)Na udanganyifu(ALL)Na udanganyifu wao

(Tsol)Yesu (ALL)Yesu Bwana(B){Wangu}niokoe.}*2

3.{(S)Ninaomba(ALL)Nifariji huzunini na magonjwa}*2


{(Tsol)Usiniache(ALL)Usiniache mwokozi

(Tsol)Katika(ALL)Katika taabu na vifo

(Tsol)Unishike(ALL)Unishike(B){Bwana}mkono wangu.}*2

4.{(S)Mimi pekee(ALL)Sina nguvu za kushinda majaribu}*2

{(Tsol)Ndipo (ALL)Ndipo Bwana nakuita

(Tsol)Bwana (ALL)Bwana wa wokovu wangu

(Tsol)Wewe (ALL)Wewe ndiwe(B){Bwana} mponya wangu.}*2

SHERIA YAKO BWANA.

(Sheria yako bwana, naipenda ,


naipenda ajabu sheria ya – ko)*2

1.Bwana ndiye aliye fungu langu, nimesema

kwamba nitayati-i nitayatii maneno ya-ke (S/A)

2.Sheria ya kinywa ya kinywa chako, ni njema

kwangu kuliko maelfu maelfu ya dha-ha-bu na

fedha (S/A)

3. Nakuomba fadhili zako zo-te, ziwe faraja

kwangu sawasawa na ahadi ya mtumishi

wa-ko (S/A)

KWA MAFUMBO HAYA @ALL SAINTS CHOIR

MERU

ALL/:Kwa mafumbo ya mkate na divai twasherehekea

kifo nakutukuza ufufuko (mpaka uje)*2


1.(S)Siku ya alhamisi kuu aliandaa meza

(ALL)(ya ukumbusho na wokovu)*2

2.(S)Huu kweli ni mwili wangu twaeni wote mkale

(ALL)(fanyeni hivi kwa kunikumbuka.)*2

3.(S)Hii nayo ni damu yangu kunyweni mkaokoke

(ALL)(fanyeni hivi kwa kunikumbuka.)*2

WEWE BWANA WAVIPENDA VITU VYOTE

(ALL){Ee Bwana wewe wavipenda vitu vyote vilivyopo}*2


{(A)Wala(ALL)Hukichukii kitu hukichukii kitu,

(T)Wala(ALL)Wala Hukichukii kitu chochote ulichokiumba}*2

1.(S)Unawasemehe watu dhambi zao na kuwahurumia

(ALL){Kwa kuwa wewe ndiwe Bwana wa vyote}*2

2.(S)Unawakusanya waliopotea na kuwaleta kwako

(ALL){Na kuwa kumbatia kwa huruma yako}*2

3.(S)Unatukumbusha kuziacha dhambi na kutenda mema

(ALL){Kwa kuwa watupenda sisi wana wako}*2

You might also like