Professional Documents
Culture Documents
1
3. SAUTI ZA MALAIKA
KIITIKIO: sauti za malaika, zinaimba mbinguni zinaimba
mbinguni × 2
4. LEO AMEZALIWA
KIITIKIO: leo amezaliwa kwa ajili yetu mwokozi ndiye
Kristu Bwana
2
EPIFANIA
5. FAMILIA TAKATIFU
8. UTUKUFU NA UKUU
KIITIKIO: Utukufu na Ukuu una yeye Bwana, hata milele na milele
×2
1. Ee mwana Kondoo, astahili kupokea enzi na utajiri
2. Ee mwana Kondoo, astahili kupokea pia heshima
3. Ewe Mungu wangu, mpitie mfalme hukumu pia na haki yako
4. Atawaamua, atawaamua watu wako kwa haki
9. AMKA KINANDA
KIITIKIO: Ee Mungu wangu, moyo wangu u thabiti, nitaimba,
nitaimba, nitaimba zaburi × 2
Amka ewe kinanda, amka ewe kinubi, nitaamka alfajiri
nitamuimbia Bwana × 2
1. Ee Mungu nitakushukuru kati ya watu, nitakuimbia zaburi kati ya
mataifa
4
10. BWANA NDIYE MCHUNGAJI WANGU
KIITIKIO: Bwana ndiye mchungaji wangu, Bwana ndiye mchungaji
wangu, sitapungukiwa na kitu, sitapungukiwa na kitu, sitapungukiwa
na kitu × 2
1. Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu, katika malisho
ya majani mabichi hunilaza kando ya maji ya utulivu huniongoza
2. Hunuhuisha nafsi yangu na kuniongoza katika njia za haki kwa ajiri ya
jina lake, nijapopita kati ya bonde la uvuvi wa mauti sitaogopa
mabaya.
3. Waandaa meza mbele yangu, machoni pa watesi wangu, umenipaka
mafuta kichwani pangu na kikombe changu kinafurika.
4. Hakika wema na fadhili zitanifuata siku zote za maisha yangu maisha
yangu, nami nitakaa nyumbani mwa bwana milele
5
12. KARIBU MOYONI MWANGU
KIITIKIO: karibu moyoni mwangu (Bwana) karibu nakukaribisha
(sana), karibu moyoni mwangu karibu karibu Bwana × 2.
1. Karibu moyoni mwangu, karibu uungane nami, karibu moyoni
mwangu karibu karibu Bwana.
2. Unipe uzima wako, inipe tumaini lako, karibu moyoni mwangu
karibu karibu Bwana.
3. Uniimarishe Bwana, katika njia yenye haki, karibu moyoni
mwangu karibu karibu bwana.
6
5. Baraka za Mungu Baba, Baraka za Mungu mwana na za Roho
mtakatifu ziwe nanyi nyote.
7
BIKIRA MARIA:
8
19. NIONGOZE VEMA MARIA MWEMA
1. Nahangaika hapa duniani maisha hayana furaha, najua wazi hapa
si nyumbani bali njia ya kupita.
KIITIKIO: niongoze vema maria mwema, bondeni huku niliko,
nifike kwa usalama, mbinguni kwa Yesu mwanao.
2. Vita na shori vyote vyanisonga, mashaka mengi yanijia mwili na
roho havina kinga hatari imezidia.
3. Mama Maria ndiwe jibu langu hapa safarini unisaidie uniombee
kwa mwanao Yesu anikinge anilinde.
4. Kwa kuwa Yesu ni mwokozi wangu nakusihi Mama, nakusihi
sana, uzifikishe kwake shida zangu anionee huruma.
5. Kumbuka Mama, Yesu alisema, Mama yangu mwema, nawe
yohana huyo ndiye Mama, huyo ndiye Mama yako.
9
3. Ee Mungu wangu nisaidie mimi, ninapofahamu makosa yangu
nami nisamehe
10
2. Njoni tuabudu tusujudu, tupige magoti mbele za Bwana
aliyetuumba. Kwa maana ndiye Mungu wetu, na sisi tu watu wa
malisho yake, na Kondoo za mkono wake.
3. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake, msifanye migumu mioyo
yenu, kama vile huko meriba/kama siku ya masa jangwani, hapo
waliponijaribu Baba zenu, wakanipima wakayaona matendo
yangu.
12
30. BWANA NIMEAMUA MIMI
KIITIKIO: Bwana nimeamua mimi, kufanya kazi yako × 2
Nitaingia shambani, shambani mwako Bwana,
nijalie Bwana nivune mavuno mema × 2
NAMNA YA KUSALI ROZALI YA HURUMA YA MUNGU
Tumia rozari ya kawaida.
Anza “baba yetu.......... salamu maria ............ × 3 “nasadiki ............
Mwisho Sali:
Bwana utuhurumie,
Kristu utuhurumie,
Bwana utuhurumie,
Kristu utusikie,
Kristu utusikilize
13
Baba wa mbinguni Mungu Utuhurumie
15
Mwanakondoo wa Mungu uliyetuonyesha huruma yako kuu katika
kuikomboa Dunia kwa msalaba wako mtakatifu. UTUSAMEHE EE
BWANA
Mwanakondoo wa Mungu unayejitolea kwetu kwa mapendo na huruma
katika kila adhimisho la sadaka ya misa takatifu UTUSIKILIZE
BWANA
Mwanakondoo wa Mungu unayeondoa dhambi za dunia kwa njia ya
huruma yako isiyo na mwisho UTUHURUMIE
V. Bwana utuhurumie
R. Kristu utuhurumie
W.Bwana utuhurumie
V.Huruma anana za Bwana zi juu ya kazi zake zote
R. Huruma za Bwana nitaziimba milele.
TUOMBE
Ee mungu uliye na huruma isiyo na mwisho, na hazina za wema na
upendo wako hazina mipaka. Tunakusihi ututazame sisi watu wako
huku duniani na kutuongezea huruma yako tena na tena, ili itusaidie
tusije tukakata tama hata mara moja, hadhuru tukumbane na majaribu
makubwa kiasi gani, bali tuweze daima kuzielekea na kuzishika amri
zako. Kwa matumaini na kutimiza mapenzi yako matakatifu, ambayo
ndiyo huruma yenyewe. Tunaomba hayo kwa njia ya bwana wetu yestu
kristu mwanao, mfalme wa amani na huruma, aishie na kutawala nawe,
na roho mtakatifu, kwa pamoja mkituonyesha huruma, daima na milele.
AMINA
16
ENYI WATU WOTE PIGENI MAKOFI – Na S. B. Mutta
Enyi watu wote pigeni makofi, enyi watu wote pigeni makofi, mpigieni
bwana mungu wetu, mshangilieni kwa vigelegele × 2
1. Enyi watu pigeni makofi, mpigieni mungu, pigeni kelele kwa sauti
ya shangwe
2. Kwa kuwa bwana aliye juu ni mwenye kuogopwa, ndiye mfalme
mkuu wa dunia yote
3. Bwana atawatiisha watu wote wan chi yetu na mataifa chini ya
miguu yake.
BWANA NI NURU YANGU – Na Deo Mhumbira
Bwana ni nuru yangu, na wokovu wangu, nimwogope nani, bwana
ni ngome ya uzima wangu, nimhofu nani × 2
1. Watesi wangu na adui zangu, walijikwaa wakaanguka, jeshi
lijapokupigana name, moyo wangu, hautaogopa.
2. Vita vijaponitokea, hata hapo, nitatumaini, neon moja nalitoka kwa
bwana, nalo ndilo nitalitafuta.
3. Nikae nyumbani kwa bwana, siku zota, za maisha yangu,
niutazame uzuri wa bwana, na kutafakari, hekaluni mwake.
EE BWANA TWAKUOMBA UPOKEE – Paschal F. Mwarabu
Ee bwana twakuomba upokee vipaji vyetu × 2
Hivyo vyote ni mali yako, tumepata kwa wema wako pokea × 2
1. Mkate divai twakutolea, twakuomba baba upokee.
2. Mawazo pia matendo yetu, twakuomba baba upokee
3. Sadaka zetu uzibariki, pia nasi baba tubariki.
17
AULAYE MWILI WANGU – Na Stan Mujwahuki
Aulaye mwili wangu, na kuinywa damu yangu (asema bwana)
hukaa ndani yangu name hukaa ndani yake × 2
1. Aulaye mwili wangu, na kuinywa damu yangu ana uzima wa
milele.
2. Njoni enyi wenye njaa, njoni enyi wenye kiu, njoni kwangu
niwashibishe.
3. Aniaminiye mimi, na kuyashika nisemayo, nitamfufua siku ya
mwisho.
4. Mlapo chakula hiki, mnywapo kikombe hiki, mwatangaza kifo cha
bwana.
5.
18