You are on page 1of 9

MANENO YA NYIMBO ZA DOMINIKA MWAKA (A) WA KANISA

DOMINIKA YA 2 MWAKA A
MWANZO Ee Mungu, nchi yote itakusujudia na kukuimbia, naam, italiimbia
jina lako, wewe Mtukufu
KATIKATI Ndipo niliposema, Tazama nimekuja, kuyafanya mapenzi yako
SHANGILIO Wakasema ndiye mbarikiwa Mfalme ajaye kwa jina la Bwana,
Amani mbinguni na Utukufu huko juu.
KOMUNYO Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi na kuliamini

DOMINIKA YA 3 MWAKA A
MWANZO Mwimbieni Bwana wimbo mpya, mwimbieni Bwana, nchi yote.
Heshima na adhama ziko mbele zake, nguvu na uzuri zimo katika
Patakatifu pake.
KATIKATI Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu.
SHANGILIO Kristo alihubiri Habari njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na
udhaifu wa kila namna katika watu.
KOMUNYO Bwana asema: Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye
hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.

DOMINIKA YA 4 MWAKA A
MWANZO Ee Bwana Mungu wetu, utuokoe, utukusanye kwa kututoa katika
mataifa, tulishukuru jina lako takatifu, tuzifanyie shangwe sifa
zako.
KATIKATI Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
SHANGILIO Thomaso akamwambia Bwana, Sisi hatujui uendako, nasi twaijuaje
njia?
KOMUNYO Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Heri wenye upole; maana watairithi nchi.

DOMINIKA YA 5 MWAKA A
MWANZO Njoni, tuabudu, tusujudu, tupige magoti mbele za Bwana
aliyetuumba; kwa maana ndiye Mungu wetu.
KATIKATI Nuru huwazukia wenye adili gizani.
SHANGILIO Mwanamke mmoja, jina lake Lidya, mwenye kuuza rangi ya
zambarau, mwenyeji wa Thiatira, mcha Mungu, atakusikiliza,
ambaye moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno
yaliyonenwa na Paulo.
KOMUNYO Heri wenye huzuni; maana hao watafarijika. Heri wenye njaa na kiu
ya haki; maana hao watashibishwa.

Kwaya Mt. Francisco Dumila Moro Page 1


MANENO YA NYIMBO ZA DOMINIKA MWAKA (A) WA KANISA

DOMINIKA YA 6 MWAKA A
MWANZO Uwe kwangu mwamba wa nguvu, nyumba yenye maboma ya
kuniokoa. Ndiwe genge langu na ngome yangu; kwa ajili ya jina lako
uniongoze, unichunge.
KATIKATI Heri waendao katika sheria ya Bwana.
SHANGILIO Mimi ndimi Njia, na Ukweli, na Uzima, asema Bwana; Mtu haji kwa
Baba, ila kwa njia ya mimi.
KOMUNYO Jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe wa
pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa
milele.

DOMINIKA YA 7 MWAKA A
MWANZO Nami nimezitumania fadhili zako; moyo wangu na uufurahie
wokovu wako. Naam, nimwimbie Bwana, kwa kuwa amenitendea
kwa ukarimu.
KATIKATI Bwana amejaa huruma na Neema.
SHANGILIO Mtu akinipenda, atalishika neno langu, na Baba yangu atampenda
nasi tutakuja kwake.
KOMUNYO Bwana mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristu, Mwana wa
Mungu, Yule ajaye ulimwenguni.

DOMINIKA YA 8 MWAKA A
MWANZO Bwana alikuwa tegemeo langu, akanitoa akanipeleka panapo nafasi,
akaniponya kwa kuwa alipendezwa nami.
KATIKATI Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa kimya.
SHANGILIO Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa
cha Mungu.
KOMUNYO Tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa
dahari.

DOMINIKA YA 9 MWAKA A
MWANZO Uniangalie na kunifadhili, ee Bwana, maana mimi ni mkiwa na
mteswa. Utazame teso langu na taabu yangu, unisamehe dhambi
zangu zote, ee Mungu wangu.
KATIKATI Uwe kwangu mwamba wa nguvu, Ee Bwana.
SHANGILIO Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana
wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia
kwa Baba yangu nimewaarifu.
KOMUNYO Bwana asema; Amin, nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali,
aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
Kwaya Mt. Francisco Dumila Moro Page 2
MANENO YA NYIMBO ZA DOMINIKA MWAKA (A) WA KANISA

DOMINIKA YA 10 MWAKA A
MWANZO Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, nimwogope nani? Bwana
ni ngome ya uzima wangu nimhofu nani? Watesi wangu na adui
zangu, walijikwaa wakaangua
KATIKATI Naye autengenezaye mwenendo wake. Nitamwonyesha wokovu wa
Mungu.
SHANGILIO Kondoo wangu waisikia sauti yangu, asema Bwana; Nami nawajua,
nao wanifuata.
KOMUNYO Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya
Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.

DOMINIKA YA 11 MWAKA A
MWANZO Ee Bwana, usikie, kwa sauti yangu ninalia. Umekuwa msaada
wangu, usinitupe, wala usiniache, ee Mungu wa wokovu wangu.
KATIKATI Tu watu wake, na Kondoo wa malisho yake.
SHANGILIO Ninyi nimewaita rafiki, kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba
yangu nimewaarifu
KOMUNYO Bwana asema, Baba Mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde
hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.

DOMINIKA YA 12 MWAKA A
MWANZO Bwana ni nguvu za watu wake, naye ni ngome ya wokovu kwa
Kristo wake. Uwaokoe watu wako, uwabariki urithi wako,
uwachunge, uwachunge milele.
KATIKATI Kwa wingi wa fadhili zako unijibu.
SHANGILIO Fungua mioyo yetu, ee Bwana, Ili tuyatunze maneno ya mwanao.
KOMUNYO Bwana asema; mimi ndimi mchungaji mwema, nami nautoa uhai
wangu kwa ajili ya Kondoo wangu.

DOMINIKA YA 13 MWAKA A
MWANZO Enyi watu wote, pigeni makofi, mpigieni Mungu kelele kwa sauti ya
shangwe.
KATIKATI Fadhili za Bwana nitaziimba milele.
SHANGILIO Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo
haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto
wachanga.
KOMUNYO Baba, ninawaombea hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate
kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.

Kwaya Mt. Francisco Dumila Moro Page 3


MANENO YA NYIMBO ZA DOMINIKA MWAKA (A) WA KANISA

DOMINIKA YA 14 MWAKA A
MWANZO Tumezitafakari fadhili zako, ee Mungu, katikati ya hekalu lako.
Kama lilivyo jina lako, ee Mungu, ndivyo na sifa yako hata miisho
ya dunia. Mkono wako wa kuume umejaa haki.
KATIKATI Nitalihimidi jina lako milele na milele.
SHANGILIO Nena, Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikia; Wewe unayo
maneno ya uzima wa milele.
KOMUNYO Bwana asema: Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye
kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

DOMINIKA YA 15 MWAKA A
MWANZO Mimi nikutazame uso wako katika haki, niamkapo nishibishwe kwa
sura yako.
KATIKATI Mbegu nyingine zilianguka penye udongo mzuri, zikamea zikazaa.
SHANGILIO Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Ayatie nuru macho ya mioyo
yetu, Ili tujue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo.
KOMUNYO Bwana asema: Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa
ndani yangu, nami hukaa ndani yake.

DOMINIKA YA 16 MWAKA A
Tazama Mungu ndiye anayenisaidia, Bwana ndiye
anayenitegemeza nafsi yangu. Kwa ukunjufu wa Moyo
MWANZO
nitakutolea dhabihu ee Bwana nitalishukuru jina lako maana ni
jema.
KATIKATI Kwa maana wewe, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe.
SHANGILIO Neno lako ndiyo kweli, Ee Bwana; Ututakase sisi kwa ile kweli.
Bwana asema: Tazama nasimama mlangoni, nabisha; mtu
KOMUNYO akisikia sauti yangu, nakuufungua mlango, nitaingia kwake,
nami nitakula pamoja naye , na yeye pamoja nami.

DOMINIKA YA 17 MWAKA A
Mungu yu katika lake takatifu. Mungu huwakalisha wapweke
MWANZO
nyumbani.Yeye huwapa watu wangu nguvu na uwezo.
KATIKATI Sheria yako naipenda mno ajabu.
Ewe Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Uyatie nuru macho ya
SHANGILIO
mioyo yetu, Ili tujue tumaini la mwito wako jinsi lilivyo.
Heri wenye rehema; maana hao watapata rehema. Heri wenye
KOMUNYO
moyo safi, maana hao watamwona Mungu.

Kwaya Mt. Francisco Dumila Moro Page 4


MANENO YA NYIMBO ZA DOMINIKA MWAKA (A) WA KANISA

DOMINIKA YA 18 MWAKA A
Ee Mungu uniokoe, ee Bwana unisaidie hima. Ndiwe msaada
MWANZO
wangu na mwokozi wangu, ee Bwana, usikawie.
Waufumbua Mkono wako, Wakishibisha kila kilicho hai
KATIKATI
matakwa yake.
Kondoo wangu waisikia sauti yangu, asema Bwana; Nami
SHANGILIO
nawajua nao wanifuata.
Bwana asema: Mimi ndimi mkate wa uzima; Yeye ajaye kwangu
KOMUNYO
hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.

DOMINIKA YA 19 MWAKA A
Ee Bwana ulitafakari agano, usiusahau milele uhai wa watu
MWANZO wako walioonewa. Ee Mungu usimame, ujitetee mwenyewe,
usiisahau sauti ya watesi wako.
KATIKATI Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako, Utupe wokovu wako
Abarikiwe Mfalme ajaye kwa jina la Bwana; Amani mbinguni,
SHANGILIO
na Utukufu huko juu.
Bwana asema; Mkate nitakaotoa mimi ni mwili wangu kwaajili
KOMUNYO
ya uzima wa ulimwengu.

DOMINIKA YA 20 MWAKA A
Ee Mungu ngao yetu, uangalie, umtazame uso Kristo wako.
MWANZO
Hakika siku moja katika nyua zako ni bora kuliko siku elfu.
KATIKATI Watu na wakushukuru, Ee Mungu, watu wote na wakushukuru.
Fungua mioyo yetu, Ee Bwana, Ili tuyatunze maneno ya
SHANGILIO
mwanao.
Bwana asema; mimi ndimi mkate wenye uzima ulioshuka kutoka
KOMUNYO
mbinguni; mtu akila mkate huu, ataishi milele.

DOMINIKA YA 21 MWAKA A
Ee Bwana utege sikio lako unijibu. Wewe uliye Mungu wangu,
MWANZO umwokoe mtumishi wako anayekutumaini. Wewe, Bwana,
unifadhili maana nakulilia wewe mchana kutwa.
Ee Bwana, fadhili zako ni za milele Usiziache kazi za mikono
KATIKATI
yako.
Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa
SHANGILIO mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia
watoto wachanga.
Bwana asema; Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu
KOMUNYO
anaouzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

Kwaya Mt. Francisco Dumila Moro Page 5


MANENO YA NYIMBO ZA DOMINIKA MWAKA (A) WA KANISA

DOMINIKA YA 22 MWAKA A
Ee Bwana, unifadhili, maana nakulilia wewe mchana kutwa.
MWANZO Kwa maana wewe Bwana u mwema, umekuwa tayari kusamehe,
na mwingi wa fadhili kwa watu wote wakuitao.
KATIKATI Ee Bwana, Mungu wangu, Nafsi yangu inakuonea kiu.
Kesheni ninyi kila wakati, ili mpate kuokoka Na kusimama
SHANGILIO
mbele ya Mwana wa Adamu.
Heri wapatanishi; maana hao wataitwa wana wa Mungu. Heri
KOMUNYO wenye kuudhiwa kwaajili ya haki; maana ufalme wa mbinguni ni
wao.

DOMINIKA YA 23 MWAKA A
Ee Bwana wewe ndiwe mwenye haki, na hukumu zako ni za adili.
MWANZO
Kama zilivyo rehema zako umtendendee mtumishi.
Ingekuwa heri leo tusikie sauti yake! Tusifanye migumu mioyo
KATIKATI
yetu.
Mtu akinipenda, atalishika neno langu; Na Baba yangu
SHANGILIO
atampenda; Nasi tutakuja kwake.
Bwana asema: Mimi ndimi nuru ya uzima ya ulimwengu ; yeye
KOMUNYO anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya
uzima.

DOMINIKA YA 24 MWAKA A
Ee Bwana uwape amani wakungojao ili watu wawasadiki
MWANZO manabii wako; usikilize sala ya mtumwa wako, na ya taifa lako
Israeli.
Bwana amejaa huruma na neema, Si mwepesi wa hasira, ni
KATIKATI
mwingi wa fadhili.
Bwana, maneno yako ni roho tena ni uzima; Wewe unayo
SHANGILIO
maneno ya uzima wa milele.
Kikombe kile cha Baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu
KOMUNYO
ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Bwana?

DOMINIKA YA 25 MWAKA A
Bwana asema; Mimi ni wokovu wa watu wakinililia katika taabu
MWANZO
yoyote nami nitawasikiliza. Nami nitakuwa Bwana wao milele.
KATIKATI Bwana yu karibu na wote wamwitao.
Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; Wote waliompokea
SHANGILIO
aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu.
Bwana asema: Mimi ndimi mchungaji mwema; nawajua Kondoo
KOMUNYO
wangu nao wanijua mimi.
Kwaya Mt. Francisco Dumila Moro Page 6
MANENO YA NYIMBO ZA DOMINIKA MWAKA (A) WA KANISA

DOMINIKA YA 26 MWAKA A
Ee Bwana, yote uliyotutendea umeyatenda kwa haki, kwa kuwa
MWANZO sisi tumetenda dhambi, wala hatukuzitii amri zako. Ulitukuze
jina lako na kututendea sawasawa na wingi wa huruma zako.
KATIKATI Kumbuka rehema zako, Ee Bwana
Ninyi nimewaita rafiki, kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba
SHANGILIO
yangu nimewaarifu.
Katika hili tumelifahamu pendo la Mungu, kwa kuwa yeye
KOMUNYO aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai
wetu kwa ajili ya hao ndugu.

DOMINIKA YA 27 MWAKA A
Ee Bwana ulimwengu wote u katika uwezo wako. Wala hakuna
awezaye kukupinga ukipenda.Wewe umeumba yote mbingu na
MWANZO
nchi, na vitu vyote vya ajabu vilivyomo chini ya mbingu, ndiwe
Bwana wa yote.
KATIKATI Shamba la mizabibu la Bwana ndilo shamba la Israeli.
Kondoo wangu waisikia sauti yangu, asema Bwana; Nami
SHANGILIO
nawajua, nao wanifuata
Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja:
KOMUNYO Kwa maana sisi sote twashiriki mkate mmoja na kikombe
kimoja.

DOMINIKA YA 28 MWAKA A
Bwana kama wewe ungehesabu maovu yetu, Ee Bwana nani
MWANZO angesimama? Lakini kwako kuna msamaha, ee Mungu wa
Israeli.
KATIKATI Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.
Mimi ndimi Njia, na Ukweli, na Uzima, asema Bwana; Mtu haji
SHANGILIO
kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Bwana atakapodhihirishwa, tutafanana naye kwa maana
KOMUNYO
tutamwona kama alivyo

Kwaya Mt. Francisco Dumila Moro Page 7


MANENO YA NYIMBO ZA DOMINIKA MWAKA (A) WA KANISA

DOMINIKA YA 29 MWAKA A
Ee Mungu nimekuita, kwa maana utaitika utege sikio lako
MWANZO ulisikie neno langu. Ee Bwana wangu unilinde kama mboni ya
jicho, unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako.
KATIKATI Mpeni Bwana Utukufu na nguvu.
Ninyi nimewaita rafiki, kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba
SHANGILIO
yangu nimewaarifu.
Mwana wa mtu amekuja apate kutoa nafasi yake iwe fidia ya
KOMUNYO
wengi.

DOMINIKA YA 30 MWAKA A
Ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana. Mtakeni Bwana na
MWANZO
nguvu zake, utafuteni uso wake siku zote
KATIKATI Wewe, Bwana, nguvu yangu, nakupenda sana.
Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; Wote waliompokea
SHANGILIO
aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu.
Kristo ametupenda, akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu
KOMUNYO
kwa Mungu, kwa harufu ya manukato.

DOMINIKA YA 31 MWAKA A
Wewe Bwana usiniache, Mungu wangu usijitenge nami, ufanye
MWANZO
haraka kunisaidia ee Bwana, wokovu wangu.
KATIKATI Ee Bwana, uilinde nafsi yangu katika amani yako.
Bwana, maneno yako ni roho tena ni uzima; Wewe unayo
SHANGILIO
maneno ya uzima wa milele.
Bwana asema: Kwa vile Baba aliye hai anavyonituma mimi,
KOMUNYO name ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa
hai kwa mimi.

DOMINIKA YA 32 MWAKA A
Maombi yangu yafike mbele zako, uutegee ukulele wangu sikio
MWANZO
lako, ee Bwana.
KATIKATI Ee Mungu, Mungu wangu, Nafsi yangu inakuonea kiu.
Mtu akinipenda, atalishika neno langu; Na Baba yangu
SHANGILIO
atampenda; Nasi tutakuja kwake.
KOMUNYO Wafuasi walimtambua Bwana Yesu katika kuumega mkate.

Kwaya Mt. Francisco Dumila Moro Page 8


MANENO YA NYIMBO ZA DOMINIKA MWAKA (A) WA KANISA

DOMINIKA YA 33 MWAKA A
Bwana asema: Mawazo ninayowawazia ninyi ni mawazo ya
amani wala si ya mabaya. Nanyi mtaniita name nitawasikiliza
MWANZO
name nitawarudisha kutoka mahali pote watu wenu
waliofungwa.
KATIKATI Taabu ya mikono yako Hakika utaila.
Kesheni basi na kujiweka tayari, Kwa maana hamjui saa
SHANGILIO
atakayokuja, Mwana wa Adamu.
Bwana asema: amin, nawaambia, yoyote myaombayo mkisali,
KOMUNYO
aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.

DOMINIKA YA YESU KRISTO MFALME MWAKA A


Astahili mwanakondoo aliyechinjwa kuupokea uweza na utajiri
MWANZO na hekima na nguvu na heshima. Utukufu na ukuu una yeye hata
milele na milele.
KATIKATI Bwana ndiye mchungaji wangu sitapungukiwa na kitu.
Abarikiwe Yeye ajaye kwa jina la Bwana: Ubarikiwe na Ufalme
SHANGILIO
ujao, wa Baba yetu Daudi.
Bwana Mfalme ameketi milele, Bwana atawabariki watu wake
KOMUNYO
kwa amani.

Kwaya Mt. Francisco Dumila Moro Page 9

You might also like