You are on page 1of 1

SALA ZA KUVUNJA LAANA

KWA JINA LA YESU


Katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth , Baba wa mbinguni
ninakuinulia mkono wangu wa
kuume,mimi……………………………………… (taja jina lako).
Nitazame Bwana maana nguvu na uwezo wote unatoka kwenye kiti
chako cha enzi.kama ilivyo andikwa katika Zaburi ya 62:11-12 “Mara
moja amenena Mungu, mara mbili nimeyasikia haya ya kwamba nguvu
zina Mungu. Na fadhila ziko kwako ee Bwana, maana ndiwe umlipaye
mtu sawa sawa na haki yake”
Baba wa mbinguni, ninapokea nguvu kutoka kwako sasa kwa jina la
Yesu. Ninatumia nguvu hizi kufuta, kuvunja,kuharibu na kujitenga
mwenyewe kutoka kwenye laana zote za maagano yaliyofanywa dhidi
yangu.Nina amuru  laana zote pamoja na mapatano na mazindiko yaliyo
jificha popote dhidi ya maisha yangu kujidhihilisha sasa katika jina la
Yesu. Nina amuru moto wa Roho Mtakatifu na damu ya Yesu kuwa
dhihilishia wote. Nina ziharibu nguvu zenu wote kwa jina la Yesu.
 

Amina.
 

Salamu Maria x10


Atukuzwe Baba x 3

You might also like