You are on page 1of 4

"UTUKUFU WA MUNGU NI NINI?

"

Musa; Akasema, Nakusihi unionyeshe "Utukufu wako".


~Kutoka33:18

"Yesu akamwambia, mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?"


~Yohana11:40

"Basi ilikuwa, hapo huo mkutano ulipokuwa umekutanika kinyume cha Musa, na kinyume cha Haruni,
wakaangalia upande wa hema ya kukutania; na tazama, hilo wingu likaifunika hema, na utukufu wa
BWANA ukaonekana."
~Hesabu16:42

Nitaelezea kiundani kidogo Leo hususani ya maneno haya "Utukufu wa Mungu"- kabla ya yote nataka
kutoa kwanza maana ya Neno 'Utukufu' ili unapotamka neno "Utukufu wa Mungu" au "Utukufu wa
Bwana" unaelewa ni kitu gani unamaanisha.

Unaweza ukawa ni mara nyingi umekuwa ukiyatumia maneno haya "nimeuona Utukufu wa Mungu", au
"mahali hapa pana Utukufu wa Mungu" au "mtu huyu amevikwa Utukufu wa Mungu/ Ukutufu wa
Mungu umemfunika".

Basi tuchambue kwanza Neno "UTUKUFU" Maana yake ni nini?


Neno 'Utukufu', linalotumiwa katika lugha ya Kiswahili linatafsiriwa katika lugha ya kiingereza kama
“Glory” neno hili katika kamusi limehusianishwa (synonym) na maneno kama RADIANCE:- yenye
kutafsiriwa katika Kiswahili kumaanisha “ang’avu/enye kudhihirisha wazi upendo/furaha”,

MAGNIFICENCE:- ambalo katika Kiswahili limetafsiriwa kumaanisha “adhimu/enye adhama/enye uzuri


kabisa.”

SPLENDOR:- ambalo linamaanisha “fahari/ubora wa hali ya juu”

WONDER:- hii ikimaanisha ajabu/enye kustaajabisha,

BRILIANCE:- ikimaanisha enye akili sana/enye pande nyingi,

CREDIT:- ikimaanisha heshima/Muamana/sifa njema,

FAME:- ikimaanisha umaarufu/kufahamika/kujulikana/sifa njema,

LAURELS:- ikimaanisha ufahamu/ujuzi wa namna ya kuwashinda washindani/mafanikio aliyopata


mtu/heshima au sifa inayochungwa sana,
STARDOM:- ikimaanisha kuwa kinara au nyota
Kwa tafsiri rahisi kabisa tunaweza kusema kwamba manemo yote haya kwa ujumla wake yanawakilisha
mawanda (Scope) ya kile kinachoitwa utukufu.

Tunapoyatafakari maneno yaliyoainishwa na kuyahusisha na Mungu hasa kwa habari ya kutafakari


utukufu alionao Mungu, ni muhimu kuweka wazi kwamba Mungu ni wa milele, kina chake ni cha milele,
itatugharimu milele kupata kumwelewa Mungu katika ukuu wake.

Maneno haya hayatoshi kueleza maana ya utukufu wa Mungu, ila yanatuwekea msingi wa kutambua
wigo wa utukufu wa Mungu; hivyo kwa kwa maneno haya utukufu wa Mungu unaweza tafsiriwa kuwa
jumla ya;
.
Mng’ao au udhihirisho (Radiance) wa wazi kabisa wa Upendo, Furaha na Amani ya Mungu katika
Kristo Yesu mahali watoto wa Mungu walipo.

Ni kudhihirika kwa uzuri/wema wa Mungu unaovuta watu kumrudia Mungu na kushuhudiwa na kila
mtu anayekuwa kwenye uwepo wa Mungu

Ni kudhihirika kwa Fahari/Ubora unaoambatana na uwepo wa Mungu kila mahali anapopita. Mungu
ni Mfalme wa dunia yote, uwepo wake huendana na fahari/ubora na ule ukuu wa kifalme unaodhihirika
katikati ya watoto wake.

Ni kudhihirika kwa akili au maarifa ya Mungu/Pande tofauti za maarifa ya Mungu zinazoudhihirisha


uweza wa Mungu katikati ya watoto wake.

Ni kudhihirika kwa ajabu za Mungu au matendo ya kustaajabisha yanayoambatana na uwepo wa


Mungu miongoni mwa watoto wake.

Ni kudhihirika kwa Heshima/sifa njema na Imani inayoambatana na uwepo wa Mungu ambayo huwa
ni muamana kwa watu wote waliopo uweponi mwa Mungu.

Ni kudhihirika kwa ukuu wa Mungu kunakomfanya Mungu ajitofautishe na kila kiumbe na kujionesha
kuwa ni wa pekee hivyo kuwa kinara, kuinuliwa na kutukuzwa ba watu wote waliopo uweponi mwake
ambao hushuhudia kuwa yanayotokea ni matendo makuu ya Mungu na si vinginevyo.

Ni udhihiriso wa hekima, maarifa na ujuzi alionao Mungu unaompatia ushindi wakati wote dhidi ya
falme na mamlaka za giza. Ni kudhihirika kwa shangwe za ushindi anaojipatia Mungu dhidi ya shetani na
kazi zake.

sasa ninatarajia umeshaelewa maana ya neno 'Utukufu'. Basi tuchambue kwa undani Utukufu wa
MUNGU.
Utukufu wa Mungu ni kitu kinachotembea na Mungu popote aendapo, utukufu wa Mungu huudhihirisha
uwepo wa Mungu. Utukufu wa Mungu ni suala la ufunuo, ni matokeo ya kusudi la Mungu kutaka
kujifunua kwa watoto wake ili wapate kumjua zaidi na kuzielewa njia zake.

Mtu anapofanikiwa kuuona utukufu wa Mungu anapata neema ya kumjua Mungu zaidi na kuzielewa njia
zake.

Katika kitabu cha Kutoka 33:13 na 18 tunaona ukweli wa jambo hili katika maombi ya Musa akimwomba
Mungu na kusema;
“Basi, sasa nakuomba, ikiwa nimepata neema mbele zako, unionyeshe njia zako, nipate kukujua, ili
nipate neema mbele zako; ukakumbuke ya kuwa taifa hilo ndilo watu wako.”

Tamanio la Musa ilikuwa ni kumjua zaidi Mungu, apate kujua jinsi ya kutunza uwepo wa Mungu ili apate
neema mbele za Mungu ya kumfanikisha kuwaongoza wana wa Israel. Anaomba zaidi katika mstari wa
18 akisema “Nakusihi unionyeshe utukufu wako.” Mungu anamjibu Musa katika Kutoka 33:19-22 kama
ilivyoandikwa;
…Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la Bwana mbele yako; nami
nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu.

Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi. Bwana akasema,
Tazama, hapa pana mahali karibu nami, nawe utasimama juu ya mwamba; kisha itakuwa wakati
unapopita utukufu wangu, nitakutia katika ufa wa ule mwamba, na kukufunika kwa mkono wangu hata
nitakapokuwa nimekwisha kupita"
Katika habari hii kuna mambo kadhaa ya msingi ya kujifunza kama ifuatavyo;

>>Mwanadamu wa kawaida aaliye chini ya laana ya dhambi na mauti, hawezi akamwona Mungu akaishi,
Mungu ni mtakatifu sana na macho yake hayawezi kuitazama dhambi asiiadhibu.

Ni kwa sababu hii Mungu anapokuja katikati ya wanadamu hajidhihirishi jinsi alivyo kwa kujionesha
katika ulimwengu wa Mwili damu na nyama, bali yeye hudhihirisha sifa zake (attributes) kama wema,
Rehema, fadhili ambazo ni sehemu ya utukufu wake ili watu wapate kumjua na kutambua uwepo wake.

Kudhihirika kwa sifa za Mungu ni dalili inayoonesha Mungu yupo mahali fulani kwa kuwa
attributes/sifa za Mungu haziwezi kutengwa na Mungu, ni sehemu kamili ya utukufu wa Mungu
inayokwenda naye kila alipo.

sifa za Mungu ndicho kitu pekee tunachohitaji kukiona katika ulimwengu huu ili tupate kuutambua
uwepo wa Mungu, kumjua zaidi Mungu na kupokea neema mbele zake. Utukufu wa Mungu ni jumla ya
sifa zote (attributes) za Mungu zinazomfunua Mungu jinsi alivyo na kuwawezesha wanadamu kuzijua
njia za Mungu.
Kudhihirika kwa attributes (sifa) za Mungu ni alama kuu ya Rehema za Mungu kwa watu wake,
inaashiria jitihada ya Mungu kuwarehemu watu wake wasiangamie uweponi mwake kwa dhambi zao.

Sifa kuu ya kwanza inayodhihirika kama sehemu ya utukufu wa Mungu akishuka mahali ni Rehema zake
kama ilivyokuwa kwa Musa (Kutoka 34:5 -7 imeandikwa; “Bwana akashuka ndani ya lile wingu,
akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina la Bwana. Bwana akapita mbele yake, akatangaza,
Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema
na kweli; mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi;
wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu
wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.”)

Ni vigumu kwa mtu kuweza kuona utukufu wa Mungu asipofunuliwa na Roho wa Mungu, Inahitaji
akili iliyohuishwa kwa neno la Mungu kuweza kupokea ufunuo wa utukufu wa Mungu kama
unavyodhihirishwa na sifa (attributes) za mungu zinazoonekana pale Mungu alipo.

You might also like