You are on page 1of 2

AMA 15 ZA ROHO MTAKATIFU ALAMA ZA ROHO MTAKATIFU Kutokana na utendaji

na madhihirisho ya kazi na huduma za Roho Mtakatifu, imempendeza Baba kwamba Roho


Mtakatifu awe na alama zinazo mwakilisha.Alama hizi tofauti zinaweka wazi asili,tabia na kazi
za Roho,kama vile ilivyo kwa alama za Yesu Kristo ,Mwana wa Mungu. Alama 15 Za Roho
Mtakatifu. ALAMA YA MAJI Alama ya hii ya maji inapotumiwa kwa Roho Mtakatifu
inawakilisha juu ya utoaji wake wa uzima unaotiririka unaoleta uahi mpya,pia inawakilisha kazi
yake ya kuosha na kusafisha na kuzaa matunda. Maji ni alama ya Roho Mtakatifu kwa maana ya
kuwa mito itatoka ndani yetu baaad ya kubatizwa katika Roho Mtakatifu.(Yohana 7:38,39, 4:4,
Zaburi 72:6, 87:7, Isaya 44:3, Kutoka 17:6, I Kor.10:4) 2.ALAMA YA MOTO Alama hii ya
moto inatumika kuonyesha utakatifu wa Mungu ambapo Roho Mtakatifu anahusika kuhukumu
na kusafisha na kutakasa kama moto.Roho anashuhudia , kuhakikisha na kuhukumu dhambi.
Ubatizo wa Roho huambatana na moto wa kiroho .(Mathayo 3:11, Matendo 2:3, Isaya 4:4,
Kutoka 19:18, Malaki 3:2-3, Waebrania 12:29) 3.ALAMA YA UPEPO AU PUMZI. Alama hii
inaashiria utoaji wa uzima wa pumzi ya Mungu katika nguvu yake ya kutoa uhai mpya.Hii
inasisitiza ukweli kwamba Roho Mtakatifu ni Nafsi isiyo onekana lakini bado athari za utendaji
wake zinaweza kuonekana. ( Matendo 2:2, Yohana 3:8;Ezekieli 37:9-10 ,Isaya 40:7) 4. ALAMA
YA UMANDE Alama hii inaashiria kazi ya Roho Mtakatifu ya kulifariji na kulichangamsha
kanisa. kulifanya liwe hai wakati wote.( Zaburi 133:1-3, Hosea 14:5) 5.ALAMA YA MAFUTA
Alama hii ya Roho Mtakatifu inazungumza juu ya mambo haya yafuatayo;kuwekwa wakfu na
Uwezo wa Kimungu wa Roho Mtakatifu,Neema ya upako,Uwepo wake wa Uponyaji, na
Mwangazio wa mafundisho yake.Ni Roho ambaye huwatia mafuta(kuwateua na Kuwasmika)
waamini wa kanisa kwaajili ya kazi za kitumishi. (Luke 4:18, Matendo 10:38, 1 Yohana 2:20,27,
Zaburi 23:5 6. ALAMA YA NJIWA. Alama ya njiwa inatumika kuwakilisha usafi,uzuri,upole,
Amani na asili na tabia za Roho Mtakatifu kwa Ujumla.(Mathayo 3:16, Luka 3:22,Mwanzo 1:2,
Mathayo 10:16) 7.ALAMA YA MHURI. Mhuri ni alama ya umuhimu ya kuonyesha umiliki,na
usalama.Alama hii inasisitiza juu ya kazi ya Roho Mtakatifu ya kututhibitisha mbele za Mungu
kwamba Yeye Anatumiliki,tu wake,na ana mamlaka juu yetu na usalama wetu upo kwake.
(Efeso 1:13,4:30, 2 Kor. 1:22, 2 Timotheo 2:19) 8.ALAMA YA SAUTI NDOGO YA
UTULIVU. Roho ni sauti ya Mungu ndani ya mtu inayoleta ufunuo wa mapenzi ya Mungu
kwake.Mwanzo 3:8, 2 Wafalme 19:11-13 9.ALAMA YA KIDOLE CHA MUNGU. Roho ndiye
anayeonyeshea kidole cha kumshitaki mwenye dhambi ,kumfanya avutwe na kukujisikia
mwenye hatia hata kumpelekea ampokee Yesu Kristo kama mtetezi wake(wakili wake) Luka
11:20, Mathayo 12:28 10.ALAMA YA MALIMBUKO. Malimbuko ilikuwa ni alama ya mavuno
kamili yanayokuja, Alama hii inaonyesha vile kazi ya awali ya Roho Mtakatifu ya kuifanya upya
roho ya mwamini(kuzaliwa mara ya pili) inapelekea kwenye wokovu kamili na kutukuzwa kwa
mwamini mbele za Mungu. Warumi 8:23 11.ALAMA YA DHAMANA Dhamana Ni malipo ya
mwanzo yanayo ashiria malipo kamili yatakayafuatia.Alama hii ni kuonyesha vile Kazi ya Roho
katika wokovu wetu ni sehemu ya mwanzo ya kazi kamili na kuu ya ukombozi utakao
kuja.Alama hii inafanana na ile ya malimbuko. (Efeso 1:13-14, 1Kor. 1:22) 12.ALAMA YA
VAZI AU KUVIKWA Alama hii ya kuvikwa inamaanisha kumvaa Roho Mtakatifu,yaani Roho
kuwa juu ya mtu.Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni kama kuvaa vazi la kiuungu kutoka juu.Ni vazi
la mwamini kwaajili ya huduma mbele za Bwana. (Luka 24:9,Waamuzi 6:34, Isaya 61:10,)
13.ALAMA YA NAMBA SABA. Namba saba inatumika kuhusisha ufunuo wa Roho
Mtakatifu,Ni alama ya ukamilifu,kukamilika ,na kamili,Inawakilisha ukamilifu wa utendaji wa
Roho katka ulimwengu. Taa saba,Macho saba,pembe saba,Roho saba . (Ufunuo 1:3-4,4:5,5:6)
14.ALAMA YA NURU Roho ni Nuru.Taa saba hizi ni alama za Mwangazio,ufunuo,na uvivio
wa Roho Mtakatifu. Macho saba , Macho saba ni alama ya kuona, ufahamu,kupambanua,Akili,
Hii ni ishara wa Roho wa kujua yote, ukamilifu wa kuona na kufahamu yote.( Ufunuo 1:3-
4,4:5,5:6)Tunapozaliwa upya nuru huja ndani ya mtu wa ndani kwasababu Roho wa Mungu
huingia ( 2 Wakorintho 4:6 Zekaria 3:9,4:10) 15.ALAMA YA NGUVU AU UWEZO. Pembe
Saba ni alama ya nguvu na ulinzi, zinawakilisha uwezo wote,Roho ana nguvu zote. (Ufunuo
5:6). Roho Mtakatifu ni alama ya nguvu na uwezo utakao juu ndani ya mwamini. ( Matendo 1:8,
Luka 34:49) Pastor & Teacher Meinrald Anthony Mtitu. at July 19, 2017 Email ThisBlogThis!
Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest No comments: Post a Comment Newer Post
Older Post Home Subscribe to: Post Comments (Atom) KANUNI 21 ZA KIBIBLIA ZA
UTOAJI Kanuni 21 Za Jinsi Ya Kumtolea Mungu Mungu anatutarajia tumtolea katika mali na
mapato yetu( Fedha zetu) anayotubariki,lakini tuna mtolea... ALAMA 15 ZA ROHO
MTAKATIFU ALAMA ZA ROHO MTAKATIFU Kutokana na utendaji na madhihirisho ya
kazi na huduma za Roho Mtakatifu, imempendeza Baba kwamba Roho Mtakat... TABIA KUMI
ZA MTU MVIVU TABIA KUMI (10) ZA MTU MVIVU 1. HUPENDA SANA USINGIZI NA
KULALA KWA MUDA MREFU. MITHALI 19:15- Uvivu huleta usingizi mzito, naye mtu m...
KANUNI 21 ZA KIBIBLIA ZA UTOAJI Kanuni 21 Za Jinsi Ya Kumtolea Mungu Mungu
anatutarajia tumtolea katika mali na mapato yetu( Fedha zetu) anayotubariki,lakini tuna mtolea...
Search This Blog Pages Home ABOUT THIS BLOG My photo Light of Hope Teaching
Ministry-Nuru ya Matumaini Dar-es-Salaam, Dar-es-Salaam, Tanzania It is Christian Blog
which Focuses on motivating people to live the purpose of God in their lives and to live a
transformed through the teachings of The Word of God View my complete profile Blog Archive
▼ 2017 (26) ► September (3) ► August (3) ▼ July (17) JINSI YA KUISHI KAMA NDEGE
WA ANGANI ALAMA 15 ZA ROHO MTAKATIFU UTAPOKUWA TAJIRI KUMBUKA
MAMBO HAYA. KIONGOZI MTUMISHI SHERIA ZA KUPANDA NA KUVUNA-2
SHERIA ZA KUPANDA NA KUVUNA-1 EWE MVIVU, UTALALA MPAKA LINI?
USIKATE TAMAA,MUUJIZA WAKO UPO KARIBU. PAMOJA NA YOTE, USIACHE
KUMTUKUZA MUNGU KUCHELEWA KWA MUNGU KUWA THABITI KAMA
MTENDE Usikate Tamaa,Chagua Kubakia na Matumaini Usikate Tamaa,Mungu Atayafuta
Machozi yako NGUVU YA KUONA MBALI KAMA TAI KUSTAWI

You might also like