You are on page 1of 78

4

SOMO LA

SHULE YA BIBLIA TANZANIA


KANISA LA KRISTO

“………...juu ya mwamba
huu nitalijenga kanisa
langu: wala milango ya
kuzimu haitalishinda"

(Mathayo 16:18)

KANISA LA AGANO JIPYA


SHULE YA BIBLIA TANZANIA

Tujifunze Biblia

Shule ya Biblia Tanzania


Kanisa la Kristo Magomeni
P.O. Box 67632
Dar es salaam,
Tanzania

Pepe: info.tbs@magomeni-coc.or.tz
Tovuti: www.magomeni-coc.or.tz

Simu: +255 22 2171532


Faxi: +000 00 0000
Yaliyomo:-
Kanisa ni nini?................................................................................................................ 1
Biblia inavyoongea kuhusu kanisa ................................................................................. 1
Tuchunguze mafundisho hayo ....................................................................................... 2
Kanisa na ufalme ........................................................................................................... 5
Kanisa katika maandalio ................................................................................................ 9
Kuanzishwa kwa kanisa ............................................................................................... 10
Kanisa na madhehebu ................................................................................................. 13
Ibada katika kanisa ...................................................................................................... 25
Kazi za kanisa .............................................................................................................. 34
Utawala wa kanisa ....................................................................................................... 40
Kanisa na wahubiri....................................................................................................... 46
Kanisa na wamiishenari ............................................................................................... 50
Wanawake katika kanisa ............................................................................................. 56
Matatizo katika kanisa.................................................................................................. 57
Wajibu wa kanisa ......................................................................................................... 63
Kuhusu ndoa ................................................................................................................ 64

Jaribio .......................................................................................................................... 73
4
SOMO LA
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

Kanisa la Agano Jipya


Yesu alisema, ". . . juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu: wala milango ya kuzimu haitalishinda"
(Mt. 16:18). Mstari huu ni mahali pa kwanza katika Agano Jipya panapoongea kuhusu kanisa la Kristo.

Ukiwauliza watu swali "Kanisa ni nini?" unaweza kupata majibu mbalimbali. Lakini jibu la watu wengi ni
kwamba kanisa ni jengo ambamo Wakristo hukusanyika wakifanya ibada zao. Je! Kwa maneno hayo
hapo juu Yesu aliahidi kujenga jengo la kusalia? Ebu! tuone jinsi Biblia inavyofundisha kuhusu swali hili.

KANISA NI NINI?
KANISA SIO JENGO – Tunaposoma (1Kor. 1:1, 2), tunaona Mtume Paulo akiliandika barua kwa
kanisa lililokuwapo Korintho, Ni dhahiri kuwa hakuandika barua kwa jengo bali kwa watu. Wakristo ndio
kanisa (Mdo. 8:1:12:5; 14:27; n.k.).

Neno kanisa katika Kiyunani ni neno (ekkleisia). Maana ya neno hili ni "mkusanyiko wa watu
walioitwa watoke mahali fulani". Kwa mfano, Wayahudi wale walioongozwa na Musa kutoka Misri,
waliitwa "kanisa jangwani" (Mdo. 7:38).

Basi, kanisa si jengo au nyumba ambayo inajengwa na wanadamu. Kanisa ni kundi la watu
waliookolewa na Yesu kutoka katika nguvu za giza za Shetani. Isitoshe, kanisa ni ufalme wa kiroho wa
Yesu Kristo. Twasoma:

"Naye (Mungu) alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuinaiza katika ufalme wa Mwana
wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi" (Kol. 1:13.14).
"Bwana akalizisisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa" (Mdo. 2:47).

Mistari hii yaonyesha kuwa kanisa la Kristo ni ufalme wa Kristo. Maana, kanisa ni kundi la watu
wanaookolewa watoke katika ufalme wa Shetani na kuingizwa katika ufalme wa Yesu. (Tutathibitisha
jambo hili katika Somo la Pili.)

Katika Agano Jipya, Wakristo (kanisa) wanafananishwa na vitu fulani vya kimwili. Ebu, tuone.

BIBLIA INAVYOONGEA KUHUSU KANISA


Katika Biblia, kanisa linaitwa kwa majina yafuatayo:

1) Limeitwa kundi la Murigu.

1
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

2) Limeitwa nyumba ya Mungu.

3) Limeitwa hekalu la Mungu.

4) Limeitwa mwili wa Kristo.

5) Limeitwa kanisa la wazaliwa wa kwanza

6) Limeitwa bibi arusi wa Kristo

7) Limeitwa kanisa la Kristo.

8) Limeitwa kanisa la Mungu.

9) Limeitwa ufalme wa Mungu. ufalirne wa Yesu,


na ufalme wa mbinguni.

TUCHUNGUZE MAFUNDISHO HAYO YA BIBLIA

A. KANISA NI KUNDI LA MUNGU

ƒ Wakristo wamefananishwa na kondoo wapotevu, naye Yesu ni mchungaji mkuu awaokoaye


(Yn. 10:14.15; 1 Pet. 5:1-5). Yesu anataka Wakristo tuwe kundi moja tu (Yn. 10:16).
Tutaongea zaidi kuhusu umoja baadaye.

B. KANISA NI NYUMBA YA MUNGU

a) Kanisa laweza kuitwa nyumba au jamii ya Mungu. Manerio hayo yaonyesha uhusiano uliopo
kati ya Mungu na Wakristo (1Tim. 3:14.15; Efe. 2:19).

b) Katika nyumba ya Mungu (kanisa), Baba ndiye Mungu (Efe. 3:14; 4:6; Mt. 23:9; 1 Kor. 8:6).
Kristo ndiye Mwarna. juu ya nyumba ya Mungu (Ebr. 3:6). Kwa njia ya Yesu, Wakristo nao ni
Watoto wa Mungu (Gal. 3:26; 4:4-7; Rum. 8:14-17).

c) Wakristo wamezaliwa upya kiroho wawe wana wa Mungu, Yesu amesema kuwa mtu hawezi
kuingia katika ufalme wa Mungu (yaani, nyumba yake) bila kuzaliwa kwa maji na kwa Roho
(Yn. 3:3-5). Kuzaliwa kwa maji maana yake ni kubatizwa katika maji. Twasoma, "Kwa kuwa
ninyi nyote mmekuwa kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Maana ninyi nyote mliobatizwa
katika Kristo, mmemvaa Kristo” (Gal. 3:26, 27).

d) Yesu alisema, "Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na
kubatizwa ataokoka: asiyeamini, atahukumiwa" (Mk. 16:15,16).

e) Petro naye amesema, "Tubtini mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate
ondoleo la dhambi zenu, nanyi matapokea kipawa cha Roho Mtakatifu" (Mdo. 2:38).

2
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

C. KANISA NI HEKALU LA MUNGU

ƒ Sasa hivi, tumejifunza kuwa, tunapobatizwa katika maji, ndipo tunapozaliwa kwa maji na kwa
Roho ili tuwe wana wa Mungu. Ndipo tunapopewa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu awe
thibitisho ya kuwa sisi ni watoto wa Mungu (Gal. 4:6). Kwa hiyo, kanisa linaitwa hekalu la
Mungu, maana Roho anakaa katika miili ya Wakristo (1 Kor. 3:9,16,17; 6:19, 20; 2 Kor. 6:16).
Wakrisito ni Kama "mawe ya kiroho" yanayojengwa pamoja kuwa hekalu la kiroho la Mungu (1
Pet. 2:5; Efe. 2:20-22).

D. KANISA NI MWILI WA KRISTO

a) Mwili na kanisa ni mamoja (Kol. 1:24; Efe.1:22, 23).

i. Kanisa laitwa mwili wa Kristo kwa sababu kanisa ni watu waliomvaa Yesu kwa njia ya
ubatizo (Gal. 3:27; Rum. 6:3).

ii. Kanisa laitwa mwili wa Kristo kwa sababu Wakristo wamefananishwa na viungo
mbalimbali vya mwili (1 Kor. 12:12-31; Rum. 12:4, 5). Yesu amefarianishwa na kichwa
kinachoongoza vile viungo vya mwili (Kol. 1:18; Efe. 5:23, 24).

iii. Kanisa linaitwa mwili wa Kristo kwa sababu Roho wa Kristo anakaa ndani ya Wakristo
(Rum. 8:9).

b) Je! Yesu ana miili (makanisa) mingapi?

ƒ Biblia inasema upo mwili mmoja tu (Efe. 4:4; 1 Kor.12:12,13, 20). Kwa kule kusema kuna
mwili mmoja tu, tunatambua kwamba Kristo ana kanisa moja tu; kwani, mwili na kanisa ni
mamoja!

c) Kuna umuhimu gani mtu kuwamo katika mwili ule mmoja wa Kristo (yaani, kanisa)?

ƒ Wapo watu wasemao kuwa kanisa si muhimu bali imani tu. Lakini, Biblia inaonyesha kuwa
kanisa ni muhumu sana. Ebu, tuone:

i. Mtu hawezi kuokolewa nje ya kanisa ambalo ni mwili wa Kristo. Yesu alisema, "Mimi ndimi
njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi" (Yn 14:6). Tena
twasoma, "Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha
Kanisa; naye ni mwokoziwa mwili" (Efe. 5:23). Watu wote wanaookolewa wamo katika
kanisa (Mdo. 2:47: Efe. 5:25-27.29.30).

ii. Tunapatanishwa na Mungu kwa njia ya mwili wa Kristo (Efe. 2:15,16; Kol. 1:19-22).

iii. Hekima ya Mungu inajulikana kwa njia ya kanisa (Efe. 3:10).

iv. Katika mwili wa Kristo (kanisa) twamtukuza Mungu (Efe. 3:20, 21).

v. Katika mwili wa Kristo tu, tunapata baraka zote za rohoni (Efe. 1:3).

3
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

E. KANISA LA WAZALIWA WA KWANZA

ƒ Yesu ni mzaliwa wa kwanza wa Mungu (Rum. 8:29; Kol. 1:18; Ebr. 1:6-8). Lakini, tumeona
kuwa Wakristo ni "mwili wa Yesu" na "watoto wa Mungu" kwa njia ya Yesu. Kwa hiyo, Wakristo
wanaweza kuitwa "kanisa la wazaliwa wa kwanza" (Ebr. 12:23).

F. KANISA NI BIBI ARUSI WA KRISTO

ƒ Uhusiano uliopo kati ya Wakristo na Yesu ni kama ule uliopo kati ya mtu na mkewe. Kwa hiyo,
Wakristo wampende Yesu na kumtii kama vile mke amtiivyo mumewe (2 Kor. 11:2; Efe. 5:25-
27; Ufu. 21:1.2).

G. KANISA LA KRISTO

ƒ Kanisa linailwa kanisa la Kristo kwa sababu ni mali yake.

i. Yesu anaitwa "Kristo" kwa sababu ameteuliwa na Mungu kuwa mfalme. Kanisa ni ufalme
wake. Kwa hiyo, Wakristo wanaitwa "kanisa la Kristo" au "ufalme wa Kristo".

ii. Katika (Mt. 16:18). Kristo Yesu alisema "nitalijenga kanisa langu". Kwa hiyo, kanisa ni lake
yeye aliyelijenga. Yaani, ni kanisa la Kristo.

iii. Kristo alilinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe (Mdo. 20:28). Hivyo, kanisa linaitwa
kanisa la Kristo kwa sababu ni mali yake (Rum 16:16).

iv. Kanisa ni bibi arusi wa Kristo (Efe. 5:25-29). Kama vile mke anavyochukua jina la mumewe,
vivyo hivyo kanisa linaitwa kanisa la Kristo.

v. Kanisa linaitwa kanisa la Kristo kwa sababu ni mwili wa kiroho wa Kristo.

vi. Kanisa linaitwa kanisa la Kristo kwa sababu yeye ni mchungaji na kanisa ni kundi lake
(Yn. 10:14-16)

vii. Kanisa linaitwa kanisa la Kristo kwa sababu hakuna wokovu katika jina jingine Iolote (Mdo.
4:10-12). Isitoshe, turneamriwa tumtukuze Mungu katika jina hilo la Kristo (1 Pet. 4:15.16).

H. KANISA LA MUNGU

ƒ Yesu ni Mungu. Kwa hiyo kanisa la Kristo linaitwa ni kanisa la Mungu pia (1 Kor. 1:2; 1 Tim.
3:15; Mdo. 20:28; Kol. 2:2; 1Tim. 3:16).

I. KANISA NI UFALME WA MUNGU

ƒ Kwa sababu somo hili ni muhimu sana, tutaliongea kirefu katika somo la lifuatalo.

i. Je! wewe ni mshiriki wa kundi limaloitwa kwa majina hayo tisa? (1 Kor. 1:10-13).

4
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

KANISA NA UFALME WA MUNGU


A. Wapo baadhi ya watu wanaosema kuwa Mungu alitaka kuusimamisha ufalme katika siku za
Mitume, walakini alishindwa kwa sababu Wayahudi walimwua Yesu.

B. Wanasema kuwa Mungu alisimamisha kanisa badala ya ufalme. Mafundisho hayo si kweli kwa
kuwa Mungu hawezi kushindwa na wanadamu! Isitoshe, tangu mwanzo, ilikuwa mpango wa
Mungu kwamba Yesu angeuwawa. Ndivyo ilivyotakiwa; maana Wakristo tumeokolewa kwa njia ya
mauti yake (Rum. 5:6-10).

C. Kwa kuwa amezichukua dhambi zetu msialabani ndiyo maana tumeingizwa katika ufalme wake.
Twasoma, "Naye (Mungu) alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha..na kutuingiza katika
ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani. msamaha wa
dhambi" (Kol. 1:13,14).

D. Hali tumeingizwa katika ufalme, basi haikosi kuwa ufalme umekwisha kuja! Ufalme ndio kanisa.
Hebu, tuthibitishe ukweli huo:-

i. Mungu alitabiri kuwa atauleta ufalme wake katika siku za wafalme wa Rumi. (Dan. 2:44).

ii. Yesu alizaliwa duniani, katika siku za wafalme wa Rurni, kusudi awe mfalme (Lk. 1:30-33; Mt.
2:2).

iii. Yohana Mbatizaji alisema Kwamba ufalme ulikuwa karibu kufika katika siku zake (Mt. 3:1).

iv. Somo kubwa alilolihubiri Yesu lilikuwa ufalme wa Mungu umekaribia. (Mk .1:14, 15; Mt. 4:23:
Mk. 4:26; 9:1; Lk. 8:10; 9:2; 13:18, 20; Mdo. 1:3; n.k.).

v. Yesu aliahidi kuwa ufalme ungekuja kabla mitume hawajakufa wote (Mk. 9:1). Iwapo ufalme
haujaja bado, basi twamfanya Yesu kuwa ni mwongo, maana mitume wote wakwishakufa!

vi. Yesu alipoahidi mitume kuwa atalijenga kanisa lake, papo hapo alisema kuwa Petro atakuwa
na funguo za ufalme (Mt. 16:18, 19). Maneno hayo yanaonyesha kuwa kanisa na ufalme ni
mamoja. Ebu, tuthibitishe kuwa kanisa na ufalme ni mamoja.

ƒ Yesu aliongea na Nikodemo kuhusu ufalme akitumia maneno ya mafumbo; akamweleza


kuwa ni lazima azaliwe kwa maji kusudi aingie katika ufalme (Yn. 3:3-7).

ƒ Lakini, Petro, aliyepewa funguo za ufalme. hakutumia mafumbo siku ya Pentekoste, bali
alisema peupe kuwa ni lazima kwa watu wabatizwe kusudi wapate ondoleo la dhambi
(Mdo. 2:38). Kubatizwa katika maji ndiyo kuzaliwa kwa maji na kwa roho (Gal. 3:26.27).
Watu wale waliobatizwa siku ya Pentekoste walipata ondoleo la dhambi zao, nao
waliongezwa katika kanisa (Mdo. 2:47). Hivyo, kanisa lilianzishwa siku ya Pentekoste
wakati Petro alipotumia funguo za ufalme!

ƒ Kumbuka, Yesu aliserna kwamba mtu ataingia katika ufalme kwa njia ya kuzaliwa kwa
maji (yaani, kubatizwa). Ndiyo maana, (Kol. 1:13,14) panasema kwamba watu ambao
wamepata ukombozi (yaani, msamaha wa dhambi), wamo katika ufalme. Basi, watu
waliaobatizwa wamo katika kanisa ambalo ndilo ufalme. Kanisa na ufalme ni mamoja!

5
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

E. Yesu aliahidi kuwa Wakristo watakula na kunywa pamoja naye katika ufalme wake (Lk. 22:29, 30).
Tena, alisema kuwa "walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo
katikati yao" (Mt. 18:20). Wakristo wanakula chakula cha Bwana katika. mikusanyiko ya kanisa. (1
Kor. 11:23-34). Hivyo twatambua kwamba kanisa na ufalme ni mamoja.

F. MAJINA YA UFALME.

ƒ Katika Biblia, ufalme umeitwa kuwa ni "Ufalme wa Kristo", "Ufalme wa Mungu", na "Ufalme
wa mbinguni"

ƒ Tuone ni kwa nini.

a) UFALME WA KRISTO - Unaitwa ufalme wa Kristo kwa sababu yeye ndiye mfalme
anayeutawala. (Kol.1:13; Efe. 5:5).

i. Siku ya Pentekoste, Petro alisema, "Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulubisha kuwa
Bwana na Kristo" (Mdo. 2:36).

ii. "KRISTO" maana yake ni mtu aliyeteuliwa na kutiwa mafuta awe mfalme. Tazama maelezo
yaliyoandikwa sehemu ya chini katika ukurasa wa 282 katika Bibla.) Kwa hiyo, tangu Yesu
alipopaa kwa Mungu, amekuwa mfalme (Dan. 7:13,14; Ufu. 1:4-6; 5:9,10).

b) UFALME WA MUNGU

i. Yesu aliongea kuhusu ufalme wake na ufalme wa Mungu. Lakini, falme hizo ni mamoja.
Yesu ameuita kuwa ni ufalme wake kwa sababu amepewa na Mungu. Pia, ameuita kuwa
ni ufalme wa Mungu kwa sababu ataurudisha kwake (1 Kor. 15:24-26). Tazama, mistari hii
inaonyesha kuwa Yesu ni Mfalme tayari na kwamba ataendelea kutawala mpaka ufufuo wa
wafu!

ii. Baadhi ya watu wamedhani kuwa ufalme haujaja bado kwa sababu ya maneno ya Yesu
katika (Mt. 6:9) ambapo aliomba akissema, "Ufalme wako uje." Lakini, tunaona Yesu
aliomba hivyo kabla hajapaa kwenda mbinguni ili apewe ufalme wake. Sasa ufalme
umekwisha kuja (Kol. 1:13). Kwa hiyo, Wakristo wakiomba wakisema "Ufalme wako uje",
watakuwa wanakosea, Maana kuomba hivyo kutaonyesha kuwa hawajaelewa kuwa ufalme
ni nini Isitoshe,kwa nini tumwombe Mungu atupe kitu ambacho tumekwisha kupewa? Je,
isingekuwa tunamwudhi Mungu? Yesu alisema, "Nanyi mkiwa katika kusali,
msipayukepayuke" (Mt. 6:7). Kupayuka payuka ni kurudia rudia maneno, Basi, tusiombe
kwa kule tulichopewa tayari!

c) UFALME WA MBINGUNI

i. Yesu alisema, "Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu" (Yn. 18:36). Maana ya Yesu ni
kwamba ufalme wake ni wa kiroho wala si wa kimwili (Lk. 17:20-21).

ii. Tunaona makao makuu ya ufalme wake ni mbinguni; napo ndipo alipokwenda kutuandalia
makao (Yn. 14:1-4). Wakristo wamo katika ufalme wa Mungu tayari, walakini, tunasubiri
kuingia katika makao yetu Mbinguni.

6
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

iii. Basi, ndiyo maana kuna baadhi ya misitari katika Biblia inayoongea kana kwamba
hatujaingia bado katika ufalme (2 Pet. 1:11; 1 The. 2:12).

G. SEHEMU ZA UFALME

A. Kimsingi ili ufalme ukamilike na uwe imara ni lazima uwe na mambo manne muhimu, hebu
tuyaone mambo hayo na tujue kama tunayo yote katika kanisa (ufalme).

1) Mfalme - Kimsingi haiwezekani ufalme kuwapo mahali pasipo na mfalme. Yesu ni mfalme wetu
(Yn. 13:33-37; Mdo. 2:36; Kol. 1:13; Ufu. 1:4-6).

2) Raia – Tunaona pia haiwezekani kuwako ufalme usio na raia. Paulo amesema kwamba Wakristo
wameingizwa katika ufalme (Kol. 1:13). Kwa hiyo, wote walokubali wito wa Yesu ni raia katika
ufalme wake Yesu (Lk.19:11-27; Mt.11:28-30).

ƒ Kusudi mtu awe raia wa ufalme huu, Yesu amesema kwamba ni lazima azaliwe mara ya pili
(Yn. 3-7).

ƒ Basi Kama tulivyojifunza, kuzaliwa mara ya pili maana yake ni kubatizwa kwa kutoswa katika
maji (Rum. 6:3-6; Kol. 2:12; 2 Kor. 5:17; Mdo. 2:38).

3) Sheria – Tunaona hakuna mfalme anayeweza kutawala watu wake pasipo sheria. Wakristo
wanayo sheria gani?

ƒ Katika Biblia, kuna sheria za Agano la Kale (Torati) na sheria za Kristo za Agano Jipya (1Kor.
9:21).

ƒ Sheria za Musa (Torati) zilitolewa Sinai na sheria za Kristo zimetoka mlima Sayuni (yaani,
Yerusalemu) (Kut. 19:1-6; 20:1-26; Isa. 2:2.3; Mik. 4:1, 2; Mt. 28:16-19; Mdo. 1:4, 5, 8).

ƒ Maandiko yanasema kuwa hatupo chini ya sheria za Agano la Kale. Torati imeondolewa (Yer.
31:31-37; Rum. 7:6; 6:14; Gal. 3:10-12 16-24).

ƒ Paulo amesema kwamba kuna sheria Fulani iliyomweka huru (Rum. 8:1-2; Yak. 1:25). Basi,
Wakristo wapo chini ya ssheria za Yesu (Yn. 1:17; Ebr. 1:1.2; Yn. 14:15; 15:10-14; Mk. 12:28-
31; Mdo. 10:48).

4) Nchi - Hakuna ufalme usiokuwa na nchi. Hapo nyuma tumeona kuwa ufalme wa Yesu sio wa
ulimwengu huu (Yn. 18:36). Maana yake, ufalme wa Yesu si wa kimwili, bali Yesu anatawala
kiroho katika mioyo ya mataifa yote wanaomtii (Mt. 28:18-20).

ƒ Yesu alikwenda kutuandalia makao huko mbinguni (Yn. 14:1-4). Basi, kwa sasa tunaishi
duniani kama wapita njia tu, bali tutakwenda aliko mfalme wetu Yesu Kristo (1 Pet. 2:11; Flp.
3:20.21: 2 Pet. 3:7.1 3).

ƒ Basi, twaona kuwa kanisa ndilo ufalme; maana kanisa lina Mfalme, Raia, Sheria, na Nchi.

7
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

H. UFALME (KANISA) Nl MPANGO WA MUNGU KUMWOKOA MWANADAMU.

B. Kama tulivyojifunza, baadhi ya watu husema kwamba haikuwa mpango wa Mungu kuleta kanisa
duniani, bali alitaka kuleta ufalme. Lakini, tumekwisha kuthibitisha kuwa kanisa na ufalme ni
mamoja. Isitoshe, ilikuwa "kusudi la milele" la Mungu kuleta kanisa duniani ili, kwa njia ya kanisa,
mpango wa wokovu wa Mungu upate kujulikana (Efe. 3:1 1). Ebu, tuone mpango wake huo.

a) Dhambi ilipoingia duniani, mara Mungu alifanya mpango wa kuwaokoa wanadamu.


Alimwahidi Hawa kuwa uzao wake (Yesu) utamshinda nyoka (Shetani) kwa kumponda
kichwa (Mwa. 3:15) Hivyo alitabiri habari za Yesu ambaye ameutimiliza mpango huo wa
Mungu katika kanisa.

b) Ibrahimu naye alipewa ahadi ya kwamba mataifa yote watabarikiwa katika uzao wake (Mwa.
12:3; 22:18). Uzao wake huo ni Yesu ambaye anawabariki mataifa yote katika kanisa (Gal.
3:16; Efe. 1:3-5).

c) Mungu alimwahidi Musa kwamba, baada ya kufa kwake, angemwinua nabii mwingine kwa
mfano wake, ambaye Waisraeli wangemsikiliza kwa wokovu (Kum. 18:15). Yesu Kristo
ndiye nabii yule, Ebu, tutoe mfano. Safari moja, Mungu alimwambia Musa amwinue
nyoka wa shaba jangwani kusudi kila atazamaye nyoka aishi (Hes. 21:8-9). Maneno hayo
yalikuwa utabiri kuhusu Yesu aliyeinuliwa msalabani kusudi kila amtazamaye kwa wokovu
apate kuishi (Yn. 3:14-16; Mk. 16:15,16). Wokovu huu umo katika kanisa (Efe. 5:23; Mdo.
2:47).

d) Manabii mbalimbali walipewa ahadi kuwa utakuja ufalme usio na mwisho (Dan. 2:44; 4:17;
Isa. 2:2, 3; 9:6, 7; Mik. 4:1, 2). Wakati huo wote, Bwana alikuwa akiandaa ufalme (kanisa)
uletao wokovu kwa watu wenye kusikia sauti ya Bwana. Agano Jipya linatueleza kwamba
tangu awali kanisa limekuwa mpango wa Mungu kumwokoa mwanadamu (Efa 3:10, 11;
1 Pet. 1:19-23; Efe. 1:3-6; Ufu. 5: 9,10; 2 Tim. 1:9.10).

I. UMUHIMU WA KUWAMO KATIKA UFALME (KANISA)

A. Biblia inatueleza kuwa kuna falme mbili;

1) Ufalme wa Shetani (1 Yoh. 5:19; Efe. 2:1-3; 6:11, 12; Lk. 4:6, 7; Mt. 12:25-28).

2) Ufalme wa Kristo (Kol. 1:13).

B. Tena, kuna njia mbili;

1) Njia nyembamba iendayo uzimani, na

2) Njia pana iendayo upotevuni (Mt. 7:13, 14).

C. Wote wanaoishi katika dhambi hufuata lie njia pana iendayo upotevuni. Hao huingia katika
ufalme wa Shetani, na mwisho wao ni kilio katika ziwa la moto (Ufu. 20:10-15).

8
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

D. Wote waendao katika njia nyembamba ndio wana wa ufalme wa Kristo. Mwisho wa taabu zao
ni furaha, uzima, na amani (Yn. 5:24-29; Mt. 25:31-46; Ufu. 14:13). Wote walio katika ufalme
wa Yesu wanakula na kunywa pamoja naye katika ufalme wake (kanisa) (Lk. 22:29, 30; Mt.
26:26, 29; 1Kor.10:21).

E. Yesu alisema, "Mtu asiye pamoia nami yu kinyumi change, na mtu asiyekusanya pamoja name
hutapanya" (Mt.12:30). Ni uamuzi wa kila mwanadamu kuchagua aufuate ufalme gani (Yos.
24:14-25).

KANISA KATIKA MAANDALIO


Kabla ya kuanzisha kanisa, Mungu alituma watu mbalimbali kuandaa kwa ajili yake.

A. MANABII WALIANDAA UFALME: (Kanisa)

1) Yakobo alitabiri kwamba mfalme atazaliwa katika kabila la Yuda (Mwa. 49:10).

2) Mungu alimwahidi Daudi kwamba hatakosa kuwa na mzao wake atakayetawala (2 Sam.
7:16).

3) Danieli, Yoeli, Isaya, Mika na wengine walitabiri kuja kwa ufalme (Dan. 2:44; nk)

B. YOHANA MBATIZAJI ALIANDAA UFALME (Kanisa)

ƒ Yohana alikuja kutengeneza au kunyosha njia ya ufalme (Kanisa).

i. Yohana Mbatizaji alikuwa ndiye Eliya aliyetabiriwa kuwa atakuja kabla ya Kristo (Mal. 4:5, 6;
Mt. 11:9-1:1). (Yaani, alikuwa na roho aliyemwongoza Eliya.)

ii. Yohana Mbatizaji ndiye aliyekuwa sauti ya mtu aliaye nyikani. (Isa. 40:3; Yn. 1:23).

iii. Yohana Mbatizaji alitumwa ili atengeneze njia ya Bwana, yaani Yesu (Mal. 3:1).

iv. Alisema, "Tubuni; kwa rnaana ufalme wa mbinguni umekaribia " (Mal. 3:1, 2).

v. Kazi ya Yohana Mbatizaji haikuwa ya kudumu bali ilikuwa maandalio tu (Yn. 3:26-30).

ƒ Baadhi ya watu husema Yohana ndiye aliyeanzisha kanisa. Mawazo hayo si kweli kwa sababu
zifuatazo:

i. Yesu alipoahidi kuwa atalijenga kanisa lake, Yohana alikuwa tayari amefariki. (Mt.14:1-12;
16:18).

ii. Yesu alilinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe (Mdo. 20:28). Kwa hiyo, kanisa
lilijengwa baada ya Yesu kufufuka na kupaa na Yohana alikufa kabla ya Yesu. Hivyo,
haikuwezekana Yohana kuanzisha kanisa!

9
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

iii. Yohana alikuwa mkuu kuliko wote waliomtangulia. Lakini alikuwa mdogo kulko wale
waliomo katika ufalme wa mbinguni (Mt. 11:11) Kwa hiyo, Yohana hakuwamo katika
kanisa!

C. YESU KRISTO ALIANDAA UFALME (Kanisa)

1) Kazi ya Yesu ilikuwa kuuandaa ufalme atakaoujenga. Maana alihubiri akisema, "Wakati
umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini injili" (Mk. 1:14.15).

2) Alipokuwa ulimwenguni, Yesu aliahidi kujenga kanisa lake (ufalme wake) (Mt. 16:18)

3) Ili Yesu ajenge Kanisa lake, ilimbidi afe, afufuke na kupaa mbinguni (Dan. 7:13,14; Lk. 24:44-
47; Mdo.1 :6-8). Kwani, damu yake ndiyo iliyonunua kanisa lake (Mdo. 20:28; Ufu. 5:9, 10;
1Pet. 1:18, 19).

4) Yesu aliahidi kuwa pamoja nasi katika ufalme baada ya kufufuka kwake (Mt. 28:18-20; 26:29).
Kanisa ni ufalme ambao ndani yake Yesu anashirikiana nasi katika uzao wa mzabibu (yaani,
chakula cha Bwana). Maana Yesu alisema, "Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika
kwajina langu, nami nipo papo hapo katikati yao" (Mt. 18:20)

D. MITUME KUMI NA WAWILI WALIANDAA UFALME (KANISA)

1) Mitume walimsaidiaYesu katika kuuandaa ufalme. Maana aliwatuma watangaze habari ya


ufalme kabla hajafa (Lk. 9:2).

2) Yesu aliwaambia mitume kwamba ufalme wake utaanzishwa wakati baadhi yao wakiwa bado
hai (Mk. 9:1).

3) Baada ya kuanzisha kanisa, mitume wakawa mashahidi wa Yesu na ufalme wake katika
mataifa yote (Mdo. 1:8).

KUANZISHWA KWA KANISA


A. MJENZI WA KANISA

1) Tusome kwa makini maneno ya Yesu ili tufahamu kuwa mjenzi wa kanisa ni nani. "Nami
nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu" (Mt. 16:18).
Kwa maneno hayo ni dhahiri ya kuwa mjenzi wa kanisa ni Yesu mwenyewe. (Mdo 20:28).

2) Tangu zamani za kale wamekuwapo watu wanaodaiwa kuwa wao ni wajenzi au waanzilishi wa
makanisa mbalimbali. Hata wafuasi wao wanathubutu kujiita kwa majina yao. Lakini ni kosa
mbele ya Mungu; maana maandiko matakatifu yanatukataza tusijiite kwa majina ya wanadamu
(1Kor. 1:10-13; 3:3-9; 4:6; Kol. 3:17). Kutokana maonyo haya tunathibitisha ya kuwa kama
litakuwapo kanisa linalojiita kwa jina la mwanadamu anayeishi au aliyekwisha kufa, basi, hilo
sio kanisa la Kristo!

10
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

B. UTIMILIFU WA AHADI YA KUJEENGA KANISA

1) Ilitabiriwa kuwa Yesu atakufa kusudi itimilike ahadi yake ya kulijenga kanisa (Ebr 9:16-22).
Yesu alinunua kanisa kwa damu yake (Mdo. 20:28).

2) Yesu aliahidi kulijenga kanisa kabla mitume hawajafa wote (Mt. 16:28).

3) Ilitabiriwa kuwa ufalme (kanisa) utasimamishwa Yeruselemu katika siku za mwisho (Isa. 2:2.3;
Mik. 4:2; Lk. 24:46-49). Mitume walikuwa wakisubiri kupokea ahadi ya Yesu huko
Yerusalemu. Siku ya Pentekoste, Mtume Petro alisema kuwa siku za mwisho zimefika (Mdo.
2:15-21).

4) Ilitabiriwa kuwa ufalme utakuja kwa nguvu (Mk. 9:1). Yesu aliwaagiza mitume wakae
Yerusalemu impaka watakapopokea nguvu (Lk. 24:49; Mdo. 1:4.6). Walipokea nguvu siku ya
Pentekoste (Mdo 2:14). Siku hiyo, zaidi ya watu 3,000 waliingia katika ufalme, yaani kanisa.
Kwa hiyo, kanisa lilianzishwa Pentekoste.

5) Ilitabiriwa kuwa mataifa mbalimbali watakusanywa katika ufalme wake (Isa. 2:2-4). Na ndivyo
ilivyokuwa (Mdo. 2:5.39; Efe. 2:16-18).

C. MSINGI WA KANISA

1) Je, Petro alikuwa msingi wa kanisa? (1Kor. 10:4), Je alikuwa mkuu kuliko wengine? Hebu
tuone:

a) Yesu alikataa kumfanya mtume mmoja awe mkuu kuliko wengine (Mk.10:35-44).

b) Maandiko yanatuonyesha kuwa Petro alikuwa sawa na watu wengine, hata katika hali ya
udhaifu (Mt. 16:23; 26:69-75; Gal. 2:11-14).

c) Petro hakuwa mkuu kuliko Paulo (2 Kor. 12:11; Gal. 2:6-9, 11-14).

d) Mitume wote walipewa kazi ya kufunga na kufungua (Mt. 16:19; 18:18).

e) Wazee wa kanisa ni wachungaji sawa na Petro (Yn. 21:15-17; 1 Pet. 5:1-4).

2) Kanisa halikujengwa juu ya Petro bali juu ya msingi uliowekwa na mitume na manabii!
Twasoma: ''Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii naye Kristo Yesu mwenyewe ni
jiwe kuu la pembeni" (Efe. 2:20)

ƒ Mitume na manabii hawakuwa ndio msingi wa kanisa, bali kazi yao ilikuwa kuuweka
msingi. Mtume Paulo alisema, "Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama
mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi. (1Kor. 3:10). Msingi waliouweka
ulikuwa Yesu mwenyewe aliye jiwe kuu.

3) Yesu alisema, "Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga
kanisa langu" (Mt. 16:18). Kufuatana na usemi huo wa Yesu, baadhi ya watu wamedhani
kuwa kanisa limejengwa juu ya Petro. Lakini siyo kweli. Ebu, tuthibitishe.

11
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

a) Jina la Petro maana yake ni "jiwe" wala sio "mwamba". Twasoma, "Naye Yesu
akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri
yake Petro, au Jiwe)" (Yn. 1:42). Kwa hiyo, tukifuata maana halisi ya jina Petro utagundua,
Yesu akimwambia Petro "ndiwe jiwe na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu";
maana jiwe ni mwingine na mwamba ni mwingine.

b) Chunguza katika (Mt. 16:13, 18) kusudi uone kuwa mwamba ni nani. Katika mistari hii,
Yesu aliwauliza mitume kuwa "mimi ni nani?" Petro alimjibu kuwa "wewe ni Mwana wa
Mungu". Ndipo Yesu aliposema kuwa atalijenga kanisa lake juu ya mwamba. (Hatuoni
sehemu yeyote Petro kuitwa kuwa ni mwamba, bali Yesu katika (1 Kor. 10:4). Kwa hiyo,
Yesu mwenyewe ndive mwamba na msingi wa Kanisa.

D. YESU NI MSINGI PEKEE WA KANISA.

1) Sikiliza tena maneno ya mtume Paulo. "Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi,
kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi. na mtu mwingine anajenga juu
yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake. Maana msingi mwingine hakuna
mtu awezaye kuuweka. isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani. Yesu Kristo" (1 Kor.
3:10-11).

2) Basi mpaka hapa tumepata kushuhudia ya kwamba Petro hakuwa msingi wa kanisa bali ni
Yesu mwenyewe ndiye msingi pekee!

E. FUNGUO ZA UFALME (KANISA)

1) Baadhi ya watu wanadhani kuwa Petro alikuwa mkuu kwa sababu Yesu alimwambia, " Nami
nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni” (Mt. 16:19). Walakini, tunaposoma (Mt. 18:18)
tunagundua funguo hizo hazikutolewa kwa Petro tu, bali hata kwa mitume wengine pia.

ƒ Funguo hizo za ufalme ni za namna gani? Mitume hawakupewa funguo za chuma


Kama wanavyodhani wengi; bali funguo walizopewa ni kutumia maneno ya Yesu ili watu
wapate njia ya kuingia katika ufalme (kanisa).

ƒ Funguo hizo zilitumika siku gani? Petro na mitume walianza kutumia funguo hizo siku
ya Pentekoste (Mdo. 2:1-4.14)

ƒ Siku hiyo, Petro aliufungua ufalme na watu 3,000 wakaingia katika kanisa (ufalme) (Mdo.
2:36, 41, 47; Kol. 1:13, 14).

ƒ Watu wa kale walifungwa chini ya sheria za Torati (Gal. 3:23). Yesu alikuja kutufungulia
katika Torati (Gal. 4:4.5; Rum. 7:6).

ƒ Si kwamba tumefunguliwa tu katika Torati, bali sasa tumefungwa chini ya sheria za Yesu.
(Mt. 28:18-20; 5:21-48; Yn. 12:48).

12
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

2) Mitume wengine nao walitumia funguo za ufalme walipohubiri neno la Bwana (Mdo. 4:33;
5:12-14).

3) Mitume walimaliza kazi yote ya kufunga na kufungua na kwa hiyo, hakuna mwanadamu
mwenye funguo hizo tena! Tunaweza kulithibitisha jannbo hili kwa kusoma. (Gal. 1:8-9; 2
Yoh. 1:9; Ufu. 22:18.19: 2 Tim. 3:16-17; 1 Pet 1:16-21)

KANISA NA MADHEHEBU
A. KANISA LA KRISTO SIYO MADHEHEBU

1) Tukisoma kwenye kamusi ya Kiswahili, tunaona kuwa maana ya neno "Madhehebu" - ni


desturi au mazoea ya jamii ya watu wafuatao dini ya namna Fulani.

2) Lakini, Biblia inatuambia kuwa kanisa halifuati desturi za wanadamu. Yesu aliwakemea baadhi
ya viongozi wa dini akisema, "Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya
mapokeo yenu?" (Mt. 15:3). Kwa sababu ya kuingiza mazoea au desturi za wanadamu, hivyo
viongozi fulani wamefanya matengano yaitwayo madhehebu.

3) Madhehebu ni watu wanaofuata Biblia kwa upande tu. Paulo alimwonya Timotheo kuhusu
madhehebu akisema, "lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia,
kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. Maana utakuja wakati watakapoyakataa
mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi
makundi. kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli. na
kuzigeukia hadithi za uonao" (2 Tim 4:2-3)

4) Madhehebu si kanisa la Kristo bali yameanzishwa na watu waliojitenga na kanisa la kweli.

ƒ Twasoma: "Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo
yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya
kuwa ni wakati wa mwisho. Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama
wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi, Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si
wote walio wa kwetu" (1 Yoh. 2:18,19).

ƒ Kanisa la Kristo si madhehebu!

B. YESU HAKUTAKA MADHEHEBU YAWEPO

1) Yesu aliwaombea watu wote wanaomwamini akisema, "Wala si hao tu ninaowaombea: lakini
na wale watakaoamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja kama wewe, Baba,
ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya
kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja
kama sisi tulivyo umoja. Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika
umoja: ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda
mimi" (Yn. 17:20-23)

13
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

2) Yesu anataka liwepo kundi (kanisa) moja tu (Yn. 10:15, 16).

3) Ili tuwe na umoja, ni lazima tufuate amri za Mungu wala siyo uongozi wa kibinadamu (Mt. 15:1-
9). Yesu ametuonya akisema, "Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang'olewa.
Waacheni; hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu wenzake,
watatumbukia shimoni wote wawili" (Mt. 15:13-14).

C. UPANDAJI WA KANISA LA KRISTO

1) Hapo mwanzoni, Mungu aliumba mimea, wanyama, na wanadanu, Walakini Mungu hakuendelea
kuumba bali alifanya taratibu kwamba kila kiumbe kizaliwe kutokana na mbegu ya namna yake.
Vivyo hivyo, Yesu alilianzisha kanisa lake kwa nguvu ya Roho Mtakatifu (Mk. 9:1; Mdo. 1:8).
Tokea hapo, kanisa linaendelea kupanda mbegu.

a) Neno la Mungu ndiyo mbegu inayozaa kanisa. Soma mfano aliotoa Yesu katika (Mt. 13:24-
30.36-42). Katika kufafanua mfano huo, Yesu alisema kwamba mbegu alizokuwa akipanda yule
mpanzi ni neno la Mungu. Magugu yaliyopandwa na adui ni mafundisho ya uwongo. Akaeleza
kwamba konde ni ulimwengu. (yaani watu). Mbegu mzuri (yaani, neno la Mungu) ikazaa: wana
wa ufalme (yaani, Wakristo) na mbegu mbaya ikazaa magugu (yaani, wana wa Shetani) (Mt.
13:38).

b) Hakuna mtu anayetegemea kuvuna ngano mahali ambapo hapakupandwa ngano. Vivyo hivyo,
hatuwezi kupata Ukristo bila ya kupanda Injili ya Kristo (Gal. 1:6-9). Ikiwa neno la Injili
litahubiriwa bila kuchanganywa na magugu (uongo) litatokea kanisa la Kristo. Lakini,
likichanganywa na uongo, matokeo yake ni madhehebu (Mt.15:13, 14:7; 21-23).

D. MIFANO YA UPANDAJI WA KANISA LA KRISTO

1) Yesu aliwatuma wanafunzi wake wapande mbegu (yaani, wahubiri Injili) duniani pote (Mt. 28:18-
20; Mdo. 1:8).

a) YERUSALEMU - Kanisa la Yerusalemu lilikuwa matokeo ya mahubiri ya Roho Mtakatifu kwa


kinywa cha Mtume Petro (Mdo. 2:1-47). Kanisa hili halikuitwa "kanisa la Mtakatifu Petro"
wala Wakristo hawakujiita kwa jina la Petro. Waliitwa "wanafunzi" wa Yesu.

b) SAMARIA - Kanisa katika Samaria ni matokeo ya mahubiri ya Roho Mtakatifu kwa kinywa cha
mhubiri Filipo (Mdo. 8:5, 13-25). Filipo hakuhubiri yaliyo yake bali yaliyotoka kwa Mungu.

ƒ Katika kuwabatiza walioamini, hakuwaambia wasorne kwanza katekisimu, wala


hakuwapangia siku fulani ya ubatizo. La, hasha! bali walibatizwa saa ile ile walipomkiri
Yesu.

ƒ Filipo hakuwanyunyizia watu maji bali aliingia nao majini na kupanda nao kutoka majini
(Mdo. 8:34-40). Waamini hawakuitwa "Wafilipo", wala kanisa halikuitwa "kanisa la
Mtakatifu Filipo"!

14
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

c) ANTIONKIA YA SIRIA - Baada ya adha kutokea katika kanisa huko Yerusalernu, waamini
walitawanyika huko na huko (Mdo. 8:1). Baadhi yao walifika Antiokia ya Siria wakahubiri neno
(Mdo. 11:20, 21) Waliobatizwa waliitwa "Wakristo" (Mdo.11:26).

d) FILIPI - Twasoma mwanzo wa kanisa hili katika (Mdo. 16:13-15, 29-34). Paulo na wenzake
waliutii wito wa mtu waliyemwona katika maono. Walipofika kwake wakawahubiri wengi.
Wengine wao wakaamini na kubatizwa siku ile ile walipoamini.

ƒ Paulo alimhubiri mlinzi wa gereza naye akabatizwa usiku ule ule alipoamini watu wa Filipi
hawakuitwa "Wapaulo" wala kanisa halikuitwa "kanisa la Mtakatifu Paulo".

ƒ Wakristo ni jamii ya Mungu. Kwa hiyo, wakaitwa "ndugu." (Flp. 1:12; 2:15; 3:1,17; 4:1, 8;
1:14-18)

e) KORINTHO - Twasoma mwanzo wa kanisa hili katika (Mdo. 18:1-8). Watu waliokwenda
kuhubiri neno kule Korintho, walihubiri Injili (yaani, habari njema) ya Kristo tu (1 Kor.15:1-4).
Wale walioamini waliitwa "wana wa Mungu" (1Kor. 1:2).

2) Katika mifano hiyo tumeona kuwa makundi ya kanisa la Kristo yalianzishwa katika miji mbali mbali
kwa njia ya kuhubiri nero lake Kristo. Tena, tumeona wafuasi wa Yesu wakiitwa "wanafunzi", au
"Wakristo", au "Ndugu", au "Wana wa Mungu". Hawakuwahi kuitwa kwa majina ya wanadamu.

3) Baadhi ya waamini katika Korintho walianza kujiita kwa majina ya wanadamu, lakini Paulo
aliwakemea akisema:

ƒ "Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja;
wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja. Kwa maana,
ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba
iko fitina kwenu. Basi, maana yangu ni hii, ya kwamba kila mtu wa kwenu husema,
Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa (Petro), na, Mimi ni wa
Kristo. Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulibiwa kwa ajili yenu? Au je! mlibatizwa
kwa jina la Paulo? . . .Basi, ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na
Apolo kwa ajlli yenu, ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale
yaliyoandikwa; ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe. Maana
ni nani anayekupambanua na mwinglne?" (1 Kor.1:10-13; 4:6, 7).

E. MADHEHEBU YAMETOKA WAPI?

¾ Madhehebu ni matokeo ya mafundisho ya uongo ya watu wasioridhika na neno la Mungu.

a) Petro alionya akisema, "Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile
kwenu waalimu, wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata
Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia. Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa
hao njia ya kwali itatukanwa. Na katika kutamani wataiipatia faida kwenu kwa maneno
yaliyotungwa: ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii" (2 Pet.
2:1-3).

15
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

b) Tukumbuke pia maonyo yaliyotolewa kwa maaskofu (wazee) wa kanisa lililokuwako Efeso.
Mtume Paulo ailiwaambia:

ƒ "Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa
waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake
mwenyewe. Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa mwitu wakali
wataingia kwenu wasilihurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe watainuka watu.
wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao, Kwa hiyo kesheni,
mkikumbuka ya kwamba miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya kila mtu kwa
machozi" (Mdo. 20:28-31).

c) Mtume alisema,

ƒ "Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga imani,
wakisikliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu
wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; wakiwazuia watu wasioe, na
kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na
walio na imani wenya kuijua hiyo kweli" (1Tim. 4:1-3).

d) Yohana alisema,

ƒ "Waliotoka kwetu lakini hawa kuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu.
wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu "
(1.Yoh. 2:18, 19)

e) Basi madhehebu yametohana na wanadamu wala si kwa Mungu. Twasoma,

ƒ "Bali ninyi, wapenzi, yakumbukeni maneno yaliyonenwa zamani na mitume wa Bwana wetu
Yesu Kristo, ya kwamba waliwaambia ya kuwa, Wakati wa mwisho watakuwako watu
wenye kudhihaki, wakizifuata tama zao wenyewe za upotevu. Watu hao ndio waletao
matengano watu wa dunia hii tu, wasio wa Roho” (Yud. 1:17-19)

F. MWISHO WA MADHEHEBU

a) Ibada ya madhehebu haia faida. Yesu alisema:-

ƒ "Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure,
wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu" (Mt. 15:8, 9).

b) Watu wanaobadili Injili ya Yesu wanatembea gizani (2 Kor. 4:3, 4). Watu hawa hawana Mungu
(2 Yoh. 1:9). Mwisho wao watalaaniwa (Gal. 1:6-9; 2 The. 2:10-12).

c) Yesu alisema, "Kila pando asilolipanda Baba yangu wa mbinguni litang'olewa' (Mt. 15:13).
Madhehebu yote yatang'olewa!

d) Kwa hiyo, tumeonywa tusifanye ushirika na watu wa madhedhbu (Mt. 15:14; 2 Yoh. 1:10, 11;
2 The. 3:6).

16
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

G. KUNA TOFAUTI GANI KATI YA KANISA LA KRISTO NA MADHEHEBU?

¾ Kwa kusoma Biblia twaweza kutambua tofauti iliyopo. Tukiwaona watu wanaotenda kinyume cha
neno la Yesu, twaweza kutambua kuwa wao ni madhehebu. Ebu, tuchunguze baadhi ya mambo
wanavyofanya madhehebu.

1. KUFUATA HEKIMA YA KIBINADAMU

a) Wanadamu wanaweza kubuni marnbo mengi yanayofurahisha wenzao sana katika


madhehebu. Walakini, hekima ya kibinadamu haiwezi kuokoa wanadamu. Twasoma,
"Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana. Kwa
maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko
njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu" (Isa. 55:8, 9). "Iko njia ionekenayo kuwa
sawa machoni pa mtu; lakini mwisho wake ni njia za mauti" (Mit. 16:25).

b) Tunaweza kutambua kanisa la kweli kwa jinsi linavyofuata maandiko ya Mungu badala ya
hekima ya wanadamu (Kol. 2:20-23; 1 Kor.1:21; Mt. 7:21; 2Tim 3:16-17).

2. KUFUATA UONGOZI WA KIBINADAMU

a) Biblia yatuambia kuwa Yesu ndiye kichwa cha kanisa alilolijenga (Kol. 1:18). Lakini kwa
desturi, kila madhehebu yanao viongozi wa kidunia. Mfano ni Papa ambaye ni kichwa na
kiongozi wa madhehebu ya Romani Katoliki.

ƒ Vivyo hivyo, mahehebu ya Kilutheri yana Rais wa kanisa ambaye ni kiongozi wao.

b) Madhehebu mengi yana vikao au mikutano ya viongozi wao. Mikutano hii inadai kuwa ina
uwezo wa kutunga sheria yo yote hata kinyurni cha Biblia na kuifunga kwa kanisa. Mshiriki
akikataa kutii sheria zao, basi hutengwa na madhehebu hayo. Vikao kama hivi vimesahau
kuwa Biblia inakataza kuongeza au kupunguza neno nje ya yale yaliyoandikwa katika Biblia.

ƒ Twasoma maneno ya Mtume Paulo akisema, "Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha


upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine.
Wala si nyingine: lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza Injili ya Kristo.
Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa
hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena,
mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe"
(Gal. 1:6-9. Soma pia, Kum. 4:2; 12:32; Mt.15:6, 9; 2 Yoh.1:9,10; Ufu. 22:18,19).

3. KUTUMIA MAJINA YA KIDUNIA

a) Wengi kati ya madhehebu wanadai kuwa jina silo imihimu katika wokovu wa wanadamu.
Kwa hiyo, watu hawa wamejiita kwa majina ya watu fulani ambao walikuwa maarufu katika
madhehebu yao. Lakini Paulo aliwakemea Wakristo wa Korintho kwa ajili ya jambo hilo hilo
akisema linaleta faraka na fitina! Soma kwa makini (1Kor. 1:10-13; 3:3-9).

17
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

4. KANISA LIITWE KWA JINA LA KRISTO

a) Biblia yasema kuwa hakuna wokovu katika jina lolote lingine isipokuwa jina la Kristo (Mdo.
4:10, 12:11, 26). Tumekwisha kujifunza kuwa kanisa ni kundi la watu waliookolewa na
Kristo. Kwa hiyo, washirika wa kanisa la Kristo wanaitwa Wakristo. Tumeamriwa tufanye
mambo yote katika jina lake (Kol. 3:17) Yesu anatukuzwa tunapoliita kanisa kwa jina lake,
yaani kanisa la Kristo (1Pet. 4:15, 16; Fil. 2:9, 10). Kuilita kanisa kwa jina la kibinadamu ni
kumdhanau Kristo na kumnyima heshima yake!

b) Tumejifunza kuwa kanisa ni "mke wa Kristo" (2 Kor. 11:2) Je! mke wa mtu achukue jina la
mtu mwingine? La, hasha! Vivyo hivyo kanisa lisiitwe kamwe kwa jina la mwanadamu!
Kanisa liitwe kwa jina la mumewe; yaani Kristo (kanisa la Kristo) (Rum. 16:16).

c) Yesu Kristo alilinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe (Mdo. 20:28). Je! kanisa liitwe
kwa jina la mtu asiyelinunua? La! bali ni kanisa la Kristo.

d) Walakini, jina halitoshi kumwokoa mtu. Wengine wanaweza kuitwa kwa jina lililo sahihi
lakini, ikiwa matendo yao ni kinyume cha Biblia, hao wanahesabiwa kuwa bado ni
madhehebu (Mt. 7:15-21)

5. MAIKAO MAKUU YA KIDUNIA

a) Watu wengi huuliza "Makao makuu ya kanisa la Kristo yako wapi?" Kufuatana na
mazingira ya ulimwengu, watu wanapoongea habari za makao makuu, wana maana pale
anapokaa mkubwa wa lile jambo Kwa mfano, makao makuu ya serikali ni pale anapokaa
mkuu wa serekali ile.

b) Huko nyuma tumejifuriza kuwa kanisa la Kristo halina mkuu wa kimwili kutawala kanisa.
(Mt. 28:18; Efe. 5:23; Kol. 2:10)

c) Yesu alikataza watu wasiitwe viongozi. Alisema tunaye kiongozi mmoja tu ambaye ni yeye
Yesu mwenyewe. (Mt. 23:8-10).

d) Yesu alipokuwa karibu kufa aliwaita wanafunzi wake aliwafahamisha ni wapi yeye
atakakokwenda (Yn. 14:1-3). Hapo panaonyesha kwamba Yesu amekwenda mbinguni.
Hivvo makao makuu yapo mbinguni alipo Yesu.

e) Yesu analiongoza kanisa lake mpaka sasa kutoka mbinguni (Mt. 28:20) Kanisa
linaongozwa naye kwa njia ya maandiko aliyotuachia (Lk. 21:33; Yn.12:48; 2 Tim. 3:16,
17) Kanisa la Kristo halina makao makuu ya kidunia wala kiongozi duniani.

H. MIFANO YA UPANDAJI WA MADHEHEBU

1. ROMANI KATOLIKI - Romani Katoliki ni madhehebu zee sana. Walakini, si kanisa la asiii, Maana,
kanisa alilolijenga Yesu lilikuwa tofauti sana na kanisa Katoliki, Hebu tuthibitishe hili kwa mifano
michache hapo chini:-.

18
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

a) Kwa mfano, Yesu alikataza tusimwite mtu baba duniani katika (Mt. 23:9) lakini Madhehebu
haya wanafanya hivyo.

b) Yesu alikataza Wakristo wasimweke mtu awe mkuu wao katika (Mt. 20:20-28). Walakini,
baada ya mitume kufa, baadhi ya watu katika madhehebu haya hawakujali maandiko.
wakaanza kuwateua watu wawe wakuu wao na kuwaita kwa majina ya "Papa" na "Padri"
(majina ambayo maana yake ni "baba"), hivyo wakidharau amri ya Yesu na kufuata
uongozi wa kibinadamu, waliendelea kubadili mambo jinsi walivyotaka wakibuni cheo
cha "Kadinali" , n.k.

c) Tunaona walindelea kurekebisha mambo kwa kubadili taratibu ya ubatizo. Walianza


kuwanyunyiza watu maji kichwani badala ya kuwabatiza watu ubatizo ulio halali
wakuzamisha.

d) Waliendelea kwa kusema kuwa watoto wachanga nao wabatizwe.

e) Wakachonga sanamu na kuwaambia watu wasali rozari, n.k. wakilisahau neno la Mungu
katika (2 Yoh. 1:8-11) linalotukataza kuvuka yale yaliyo andikwa.

2. Baada ya muda, kugombania cheo kulisababisha utengano katika madhehebu ya hayo ya Romani
Katoliki; na tokeo lake ni madhehebu yanayoitwa Greek Orthodox. Kusingekuwapo na
madhehebu yo yote kama watu wangejali maandiko.

3. MADHEHEBU YA MATENGENEZO - Baada ya kuona mabadiliko makubwa, baadhi ya watu


walitaka kusahihisha makosa ya madhehebu ya Romani Katoliki. Hata ingawa watu hao
waliweza kurekebisha baadhi ya makosa, walakini hawakuleta umoja. Bali kinyume chake
walianzislia madhehebu mengine mengi.

a) Martin Luther - aliongoza kikundi kirnojawapo cha matengenezo. Alisahihisha baadhi ya


makosa bali si yote na baada ya hapo tunaona naye hakuridhika na Biblia, aliandika kredo au
katekisimu, Luther aliwakataza wafuasi wake wasijiite kwa jina lake. Walakini, waamini wa
madhehebu yake wanaitwa Walutheri mpaka leo.

b) John Calvin - naye, katika kutafuta njia ya matengenezo, hakusahihisha makosa yote. Tokeo
lake ni kwamba akaanzisha madhehebu mengine yaitwayo Presbyterian.

c) Baadaye yalizidi kupachuka madhehebu mengi bila idadi, yote yakidai kusahihisha au
kutengeneza yale ambayo madhehebu mengine yamekosa. Ni vigumu sasa kuongea kwa
kirefu mafundisho ya kila madhehebu. Tutajifunza zaidi baadaye katika SOMO LA 7 katika
mtiririko wetu masomo, somo liitwalo "Mafundisho ya Madhehebu"

I. NAMNA YA KUWA MSHIRIKI KATIKA KANISA

¾ Mshiriki katika kanisa ni yule aliyeokoka (Kol. 1:13-14; Mdo. 2:47). Kwa hiyo, tukijifunza jinsi ya
kuokolewa, basi tutafahamu jinsi ya kuwa mshiriki katika kanisa la Kristo.

19
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

1. MAMBO YA LAZIMA KWA WOKOVU

a) Lazima mtu amtafute Mungu. Mtu akimtafuta Mungu kwa moyo wake wote ataweza
kuokolewa (Yer. 29:13; Mt. 7:7). Hekima ya mtu binafsi na ya ulimwengu huu haiwezi
kumwokoa mwanadamu.

ƒ Twasoma: "Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mleta hoja wa
zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu? Kwa maana
katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu
alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa" (1Kor. 1:20, 21).

ƒ Mungu atawashibisha walio na njaa ya kumtafuta (Mt. 5:6; Zab. 25:9, 14). Mtu anayetaka
kuokolewa ni lazima ayajue mapenzi ya Mungu (Yn. 6:44, 45; 7:17).

b) Lazima mtu atamani kuokolewa kutoka dhambini. Kutokana na mifano mingi katika Agano
Jipya, twaona kuwa wote waliookolewa ni wale waliotamani wokovu.

ƒ Kuna sababu tatu zinazofanya wanadamu wamtafute Mungu, Tuone sababu hizo:-

i. Hofu ya adhabu - Mtu akisikia habari ya adhabu itakiayowapata watu wenye dhambi
anaiweza kumjali Mungu. (Mit 1:7; Ebr. 10:31; 2 Kor. 5:1 1; 2 The. 1:6-9)

ii. Matokeo ya dhambi - Dhambi huleta kifo na humtenga mtu na Mungu (Rum. 6:23;
Efe. 2:1: Kol. 1:21; Isa. 59:2). Dhambi humfanya mtu awe najisi mbele ya Mungu
(Mk. 7:20-23). Mwisho wake mwenye dhambi ni kutupwa motoni (Ufu. 21:8).
Kutambua matokeo ya dhambi kunaweza kumfanya mtu atamani wokovu (Ebr.
10:30,31; 2 Kor. 5:11)

- Mwenye dhambi ni nani? - Mtu hawezi kutamani wokovu asipojithibitisha kuwa


yeye ni mwenye dhambi (Rum. 2:12,13; 3:9-12).

- Tumaini la kupewa thawabu - Tukiairnini kwamba Mungu yupo na kwamba


huwapa thawabu wale wamtafutao, basi tutajitahidi kutafuta wokovu wake (Ebr.
11:6). Yesu mwenyewe alivumilia mateso kwa sababu ya tumaini la kufuluka na
kukaa na Mungu (Ebr. 12:2). Katika (Ebr. 11) tunaweza kusoma habari ya watu
wengi waliomtii Mungu kwa sababu ya tumaini la kupata thawabu

iii. Upendo kwa Mungu na tamaa ya kumpendeza Mungu - Yesu alisema, "Mpende
Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa skill zako zote"
(Mt. 22: 37). Mtu hawezi kumfahamu Mungu kikamilifu ikiwa harnpendi. Mtu
akimpenda Mungu atatamani kuishi naye. Katika kuhubiri kwao, Mitume walieleza
wema wa Mungu na jinsi alivyomtoa mwanawe kwa ajili ya wenye dhambi (Yn. 3:15,
16). Tunampenda Mungu kwa sababu Yeye ametanguilia kutupenda sisi (1 Yoh.
4:19). Mwana ampendaye mzazi wake atajitahidi kumpendeza. Vivyo hivyo, mtu
akimpenda Mungu atashika amri zake (Yn. 14:15; 15:10). Basi, mtu ashikaye amri za
Mungu kwa sababu amempenda, hatakuwa na sababu ya kumwogopa (1 Yoh. 4:18).

c) Awe na Uamuzi Kamili - Mwanadamu atakaye kuokolewa, ajitoe kikamilifu. Mungu


ametuonya akisema, "Nawapenda wato wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii
wataniona" (Mit. 8:17).

20
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

"Nanyi mtanitafuta, na kaniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote" (Yer. 29:13).
Kule kuamua kumtii ni ngazi ya mwisho kwa mtu ili aupate wokovu.

d) Soma (Mt.19:16-22). Tajiri alitaka kuokoka lakini hakufanya uamuzi kamili. Hivyo
alipoambiwa yampasayo kutenda, alishindwa kuitimiza. Bila uamuzi kamili, twaweza
kushindwa. Uarnuzi kamili unatuwezesha kufanya Ip lote iirialotakiwa, hata kama ni gumu
kiasi gani (Mt. 16:24).

e) Mwingine anaweza kuacha kufanya jambo fulani, eti! kwa sababu ni ndogo na haoni faida
yake. Lakini yatupasa kumtii Mungu katika yote asemayo. Kwa mfano:-

ƒ Ibrahimu asingeona sababu ya kumchinja mwanawe, lakini alikuwa tayari kutii kwa
sababu Mungu alimwamuru (Mwa. 22:1-14).

ƒ Yoshua naye asingeona sababu ya kuzunguka Yeriko mara 13, bali alifanya hivyo kwa
sababu alifahamu wazi kuwa Mungu anajua lililo bora kwake (Yos. 6:1-20).

f) Yatulazimu kufanya uamuzi kamili kabisa. Hivyo, twaweza kufanya amri zote bila woga wala
huzuni. Yesu alisema, "Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa
ufalme wa Mungu" (Lk. 9:62).

2. NJIA YA KUPATA WOKOVU - Yaani, kuwa mtoto wa Mungu.

A. Mtoto hawezi kuzaliwa mpaka mbegu ipandwe. Neno la Mungu ni mbegu inayopandwa
moyoni kusudi mtoto wa Mungu azaliwe (Lk. 8:11; 1 Pet. 1:22-23; Yak. 1:18.21; Yn. 1:12-14;
Rum. 10:13-17).

B. Kupanda mbegu hakutoshi. Mbegu ya mmea haiweza kuzaa pasipo mahitaji fulani kama
ardhi, maji, jua, mbolea, na kadhalika. Vivyo hivyo, kusudi neno la Mungu ili liweze kuzaa
watoto wa Mungu, lazima yawepo yafuatayo:-

i. Imani - Lazima mtu aliamini lile neno lililopandwa moyoni mwake (Ebr. 11:6; Gal. 3:26:
Yn. 1:12)

ƒ Wokovu kwa neema -- Mungu huwaokoa watu kwa njia ya neema yake (Rum. 4:4, 5,
16). Kwa matendo ya sheria za Musa, hakuna mtu atakayeokolewa (Rum. 3:20;
GaL. 3:11). Neema hufanya kazi kwa njia ya imani. Walakini, neema haimsaidii lo
lote mtu asiyeamini (Efe. 2:8, 9).

ƒ Imani na matendo ya utii – Mwanadamu haokolewi kwa imani pekee. Kuamini bila
matendo ya utii ni bure (Yak. 2:14, 26; Lk. 6:46; Mt. 7:21). Isitoshe, matendo yasiyo
na imani hayafai nayo. Basi, ni lazima vitu hivi vyote viwepo pamoja kusudi
mwanadamu aokolewe. (Gal. 5:6)

ii. Kutubu - Lazima mtu aache kutenda dhambi. (Mdo. 2:38; 11:18; 17:30; Yak. 1:21-25).

21
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

iii. Kumkiri Yesu - Lazima amkiri Yesu kuwa ni Mwana wa Mungu. (Mt.10:32, 33; Rum
10:9-10; Mdo. 8:36, 37)

iv. Kubatizwa - Lazima abatizwe ili apate ondoleo la dhamb zake (Mk.16:15, 16; Mdo. 2:38;
22:16). Hivyo atakuwa amezaliwa upya katika jamii ya Mungu. (Yn. 3:3-7; Gal. 3:26.27;
Rum. 6:3-7; 1 Pet. 1:22, 23)

3. MAANA NA NJIA YA UBATIZO

a) Neno ubatizo ni neno la Kiyunani ambalo limeingizwa katika Kiswahili bila kufasiriwa. Maana
ya neno "Ubatizo" katika lugha hii ya Kiyunani ni "Kutoswa Majini".

i. Tunaona hata viongozi wa kanisa la Rumi wametambua ukweli huu, maana katika
ukurasa 1032 wa biblia yao ya Kirumi wamesema, "Watu wa zamani hubatizwa kwa
kutoswa majini, na maana ya neno la ubatizo kwa Wayunani ni kutoswa majini."

ii. Ubatizo unahitaji maji mengi, Twasoma: Yobana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni,
karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele: na watu wakamwendea,
wakabatizwa" (Yn. 3:23).

iii. Isitoshe, watu walikuwa wakitelemka na kupanda kutoka katika maji ya ubatizo.
Twasoma, "Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili
abatizwe . . . Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini. na
tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu
yake" (Mt. 3:13,16)

iv. Filipo alimfundisha towashi habari za Yesu. Kisha twasoma: "Akaamuru lile gari lisimame;
waka-telemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza. Kisha,
walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi
asimwone tena', basi alikwenda zake akifurahi" (Mdo. 8:38, 39).

b) Katika mistari hiyo tumeona kwamba kubatizwa kunahitaji maji mengi. Tena, katika ubatizo,
yule anayetaka kubatizwa pamoja na mwenye kumbatiza huingia majini wote wawili.

ƒ Kwa nini watu walijisumbua kufanya mambo hayo? Jibu linapatikana katika mistari
ifuatayo: "Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye,
kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu " (Kol. 2:12).

ƒ Huwezekani kumzika mtu kwa kumpaka maji kichwani.

ƒ Kunyunyiza na kubatiza ni matendo mawili tofauti. Katika Kiyunani, neno kunyunyiza


hutamkwa (Rantizdo) bali kutoswa hutamkwa (Baptidzo)

ƒ Yesu siye mjinga asiyejua tofauti kati ya maneno hayo, bali alituamuru kubatizwa (yaani,
kutoswa) katika maji kwa sababu kutoswa ni mfano wa kuzikwa na kufufuka kwake.

22
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

ƒ Twasoma: "Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi
kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi
tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama tulivyounganika naye katika mfano wa
mauti yake kadhalika tutaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake" (Rum. 6:4-5).

ƒ Paulo anatukumbusha kwamba, kuna ubatizo mmoja tu unaokubaliwa na Mungu (Efe.


4:5) na kwamba ubatizo ule ni kuzikwa majini. Tena, alisema: "Nastaajabu kwa kuwa
mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya
namna nyingine. Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza
injili ya Kristo. Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injiti yo yote
isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe" (Gal. 1:6-8).

ƒ Yesu amezidi kutuonyesha njia ya kubatizwa katika (Yohana 3:3, 5). Tukumbuke tena
kwamba mwenye dhambi ni mtoto wa Shetani (1 Yoh. 3:8-10). Lakini, mtu anapobatizwa
katika maji, dhambi zake zinaondolewa ili awe mtoto wa Mungu (Gal. 3:26-27).

ƒ "Yesu akajibu, akamwambia (Nikodemo), Amin, arnin, nakuambia, Mtu asipozallwa mara
ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu
kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozafiwa kwa maji na kwa Roho. hawezi
kuuingia ufalme wa Mungu. Kilicnozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni
roho. Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili" (Yah. 3:3-7).

c) Kutia maji kichwani si mfano wa mtoto kuzaliwa. Lakini, kutoka majini baada ya kutoswa mwili
wote ni mfano wa mtoto kuzaliwa kutoka tumboni mwa mamaye. Mpendwa, ikiwa hujabatizwa
kwa kutoswa mwili wako wote majini, basi hujamtii Yesu! Tunakusihi uyakumbuke maneno
yake yafuatayo:

ƒ "Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo?" (Lk. 6:46). "Si
kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye
afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni" (Mt. 7:21).

d) Yesu aliwashitaki viongozi wa dini ya kiyahudi wa siku zake akisema: "Ole wenu waandishi na
Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe
hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie" (Mt. 23:13).

e) Kumbe! hata siku zetu viongozi wa madhehebu huwazuia watu wasiuingie katika ufalme
wakiwafundisha kunyunyiziwa maji badala ya kuzaliwa kwa maji, Watu hawa hudhani kwamba
wataokolewa kwa imani yao bila kufanya mapenzi ya Mungu. Lakini, twasoma:

ƒ "Iko njia ionekanayo kuwa sawa machonipa mtu, lakini mwisho wake ni njia za mauti"
(Mit. 14:12).

ƒ "Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; ili wahukumiwe wote
ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu" (2 The.
2:11,12).

ƒ "Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja,
amekosa juu ya yote . . . Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni
dhambi" (Yak 2:10; 4:17). Kuzaliwa tu hakutoshi, bali mtoto wa Mungu awe mwaminifu-

23
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

Mpaka kufa. (Ufu. 2:10; Ebr.10; 38; Mt. 7:24-27; Yak. 1:2, 1-2, 5).

f) Ukiisha kuwa mtoto wa Mungu, atakulinda sana (1 Pet. 1:3-5; 2 The. 3:3; Rum. 8:31-39; 1
Kor. 10:13; Mt. 6:24-34; 7:7-11). Hata ingawa hakuna nguvu wala mtu awezaye kututenga na
Mungu, lakini tunaweza kujitenga wenyewe (Isa. 59:1, 2; 2 Pet. 2:20-22; 1 Kor. 9:27) Kwa
hiyo, ni lazima turudiwe naye na kushiriki mateso (Ebr.12:7-11; 2 Tim. 3:12; Rum. 8 16, 17;
1Pet. 4:1,1 5, 16, 19; 5:10).

J. MFANO YA WATU WALIOOKOKA NA KUFANYWA WASHIRIKI WA KANISA

¾ Kusudi mtu aokoke ni lazima: (1) asikie Injili, (2) aamini Injili, (3) atubu dhambi zake, (4) amkiri
Yesu kuwa ni mwana wa Mungu, na (5) abatizwe (yaani, atoswe). Tuone mifano miwili ya watu
waliookolewa.

a) Watu wa siku ya Pentekoste - Hawa walikuwa Wayaiuidi waliomfahamu Mungu na walikuwa


wakimwabudu kwa sheria za Musa, Waliamini kwamba atakuja masihi (Kristo).

ƒ Walimwona Yesu, ila kwa kutokumtambua kuwa ndiye Kristo, wakamsulubisha.

ƒ Siku ya Pentekoste, waliona ishara ya Roho Mtakatifu (Mdo. 2:14-21) Kisha walipata
kusikia habari za kufufuka kwake! Yesu. (Mdo. 2:22-47)

b) Twasikia watu hawa walipitia taratibu ile ile, hebu tuthibitishe yafuatayo:

i. Walisikia Neno la Yesu (Injili) - Walimsikia Petro akisema kwamba walifanya dhambi
walipo-msulubisha Yesu (Mdo. 2:36, 37; Rum. 10:17).

ii. Waliamini Injili - Waliposikia mahubiri waliuliza "tufanye nini?" Hili swali laonyesha wazi
kwamba waliiamini injili. (Mdo. 2:44)

iii. Walitubu - Petro alijibu swali lao walilo uliza "Tufanyeje?" akiwaambia "Tubunl,
mkabatizwe" (Mdo. 2:38). Wasingalibatzwa bila ya kutubu.

iv. Walibatizwa kwa ondoleo la dhambi – Petro aliwaambia "tubuni, mkabatizwe kila mmoja
kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu.

- " Soma kwa makini katika (Mdo. 2:38-44). Hii yaonyesha kwamba kila mtu hubatizwa
kwa ajili ya dhambi zake wala sio za wazazi wake au za Adamu. Watoto hawarithi
dhambi.

- Soma kwa makini (Eze. 18:4, 20; Kum. 24:16). Kwa hiyo, watoto wadogo hawahitaji
kubatizwa maana hawana dhambi.

v. Waliingizwa katika maji - Wote waliobatizwa wiliokoewa na kufanywa washiriki wa kanisa


(Mdo. 2:42)

24
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

c) Mlinzi wa gereza - Huyo mlinzi wa gereza ailishi mahali ambako neno la Mungu
halikufahamika sana. Wayahudi wa pale walikuwa hawana hata sinagogi (Mdo.16:13).
Kutokana na (Mdo. 16:9-12). twatambua wazi kwamba injili ya Yesu ilikuwa bado haijahubiriwa
sehernu zile. Lakini mtu mgeni katika mambo ya Mungu alipata kuwa mshiriki wa kanisa
akifanya mambo yafuatayo:

i. Alimwamini Yesu - Yule mlinzi wa gereza alipotambua hatari ya dhambi, aliuliza afanye
nini ili aokoke. Jibu alilopewa ni kumwamini Yesu Kristo.

ƒ Pengine ingekuwa shida kwake kumwamini mtu ambaye hajarnuona wala kumsikia
(Yn. 9:36). Kusudi apate kumwamini Yesu, Paulo alihubiri habari za Yesu Kristo
(Mdo. 16:32). Kwa kuwa imani huja kwa kusikia neno la Kristo, hivyo mlinzi aliposikia
alimwamini Yesu (Rum. 10:17).

ii. Kutubu Dhambi - Habari za toba hazikutajwa hapa. Lakini twatambua wazi kuwa mtu yule
alitubu. Kwani, kutubu ni kubadili matendo ya kale (2 Kor. 7:10; Lk. 3:8-14). Yule mlinzi wa
gereza alionyesha matunda ya toba alipoosha mapigo ya Paulo na Sila.

iii. Kubatizwa Katika Maji - Katika (Mdo. 16:19-34), mwandishi anatufahamisha kuwa yule
mlinzi wa gereza alibatizwa baada ya kujua habari za Yesu. Wengine wa nyumba yake
waliomsikia Paulo akihubiri walibatizwa nao.

ƒ Baadhi ya watu wanadai kuwa hata watoto wadogo nao walibatizwa. Lakini si kweii.
Maana, mtu hawezi kubatizwa bila kusikia na kuamini (Mk. 16:15-16).

ƒ Watu wote wa nyumbani mwa mlinzi walikuwa watu wazima maana waliweza kusikia
maneno nao wote walikuwa wakifurahi baada ya kubatizwa. Twasoma:
"Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake.
Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, kisha akabatizwa, yeye na
watu wake wote wakati huo huo. Akawaleta juu nyumbani kwake, akawaandalia
chakula, akafurahi sana, yeye na nyumba yake yote. maana amekwisha kumwa mini
Mungu" (Mdo. 16: 32-34)

ƒ Kulingana na mifano hiyo, tunaweza kujiuliza Je! watoto wadogo wanaweza kusikia,
kuamini, na kufurahia ubatizo?

IBADA KATIKA KANISA


A. MUNGU ANAKUBALI AABUDIWE NA MTU WA NAMNA GANI?

1. Neno la Mungu linatushuhudia katika (Zab. 15:1-5) ya kuwa ni wale walio na uhusiano kamili
naye Twasoma: "Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana: bali maombi ya mtu mnyofu ni
furaha yake" (Mit 15:8). Wote wasiozaliwa na Mungu ni watoto wa Shetani na, kwa hiyo hawezi
kuikubali ibada yao (1 Yoh. 3:10; Mt. 7:21).

a) Mtu lazima awe mtoto wa Mungu. Mungu huzikubali ibada zinazofanyika na watoto wake
tu. Katika ulimwengu huu, kuna watu wa aina mbili tu; (1) watoto wa Mungu (1 Yon. 5:18-
19; Rum. 8:14-17), na (2) Watoto wa ulimwengu (Shetani) (Yn. 8: 44; 1Yoh. 3:10). Hivyo-

25
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

basi wale wote wasio watoto wake, ibada zao hazikubaliwi na Mungu.

b) Mtu awe katika Yesu Kristo ili Mungu amsikilize ombi lake (2 Kor. 5:17-19; Gal. 3:27-29)

c) Awe katika kanisa (nyumba ya Mungu) (1 Tim. 3:14,15). Kila jamii inazo desturi zake
ambazo wote wa nyumba ile huziifuata. Vivyo hivyo katika nyumba ya Mungu (kanisa)
wanaoweza kufuata desturi za nyumba ile ni wale waliomo katika nyumba ile.
Waliobatizwa siku ya Pentekoste walikuwa na miambo fulani ya kuyafanya kijamii (Mdo.
2:41-47; 4:32). Mtu akimtaka Mungu amsikilize, basi na awe katika jamii Mungu (kanisa)
yake.

d) Awe chini ya kuhanii mkuu na uongozi wake - Yesu Kristo ndiye kuhani mkuu katika
nyumba ya Mungu (yaani katika kanisa lake) (Ebr. 4:14; 10:21; 1Tim. 3:15).

ƒ Biblia imetuonya wazi kwamba yule apitaye uongozi wa Kristo hana Mungu (2 Yoh. 1:9),
Basi ikiwa ni hivyo, ibada zetu ni lazima zikubaliwe na huyo kuhani mkuu (Yn.14:6; Kol.
3:17; Ebr. 13:15). Tutajifunza zaidi jinsi itupasavyo kuabudu hapo mbele kidogo katika
kifungu C.

B. WALIO NA MIKONO ILIYOTAKATA (Zab. 24:3, 4).

1. Wengi wamedhani kuwa Mungu atakubali ibada ya kila mtu anayeimba na kuomba. Lakini
tunaona hata ibada ya Mkristo inaweza kukataliwa na Mungu asipoifanya kwa "mikono
iliyotakata". Mikono iliyotakata maana yake ni mikono ya wale waliotubu na kusamehewa
dhambi zao (Zab. 24:3-4; 1Tim. 2:8; Zab. 26:6).

2. Tunaona mfano wa kimwili, Mwanadamu aendapo kuonana na mfalme au rais wan chi ni
lazima ajihakikishe kwamba yu safi. Yesu naye anataka tunapokwenda kuonana na Mungu
katika ibada, sisi nasi tuwe na mioyo safi (Mt. 5:21-26).

3. Maandiko yatueleza kulinda mioyo zaidi kuliko vyote (Mit 4:23) Yesu alisema kwamba mambo
yale yamtiayo mtu unajisi, yatoka moyoni mwake (Mk. 7:20-23). Tumeamriwa kuiziuia mioyo
yetu isitamani (Yak. 1:13-15; Mt. 5:28; 1 Yoh. 3:15; Gal. 5:19-21) .

4. Njia ya kulinda mioyo ni kuijaza mambo ya Mungu (Fil. 4:8; Rum. 12:1, 2). Mtu mwenye moyo
safi atakuwa na "mikono safi". Hatuwezi kuwa na mioyo safi ikiwa hatufuati maneno yake.

ƒ "Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, hata sala yakeni chukizo " (Mit. 28:9). Soma
pia (Isa. 1:13-17). "Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami.
Nao waniabudu bure. Mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu”

ƒ "Sadaka ya wasio haki ni chukizo kwa Bwana: si zaidi sana ailetapo mwenye nia mbaya!"
(Mit. 21:27).

C. NAMNA YA KUABUDU (Kut 34:14)

1. Katika Roho na Kweli - Yesu ametuamuru tuabudu katika roho na kweli (Yn. 4:19-26). Kuna
ibada isiyo ya roho na kweli.

26
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

a) Katika roho - Kuabudu katika roho maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba
aabuduye atoe mawazo yake yote kwa Mungu kwa ajili ya ile ibada (Mk. 12:30).

ƒ Kama ni kuimba, uimbe kwa moyo wako wote na usiimbe bila kuyachunguza maneno
yasemavyo.

ƒ Kama ni kula chakula cha Bwana, alaye ni lazima aweke mawazo yake yote kwa ajili ya
kile chakula, akikumbuka Yesu alivyoteswa kwa ajili ya dhambi zake(1 Kor. 11:24-25,
29).

ƒ Kama ni kusali, iwe ni sala itokayo ndani na kama ni mwingine anaiongoza hakikisha
unasikia na kuyaelewa ayasemayo kabla ya kukiri "amina" (yaani naiwe hivyo) (1 Kor.
14:16).

ƒ Waisraeli wengi hawakumpendeza Mungu na ibada zao hata ingawa walitoa sadaka
zile alizoamuru (Mal. 1:6-14; Isa. 1:12-17; Mik. 6:7, 8), Ingawa wakristo hatutoi
sadaka bali changizo, lakini hata kutoa kwetu ni lazima kuwe sawa na mapenzi ya
Mungu (1 Kor. 16:1-2; 2 Kor. 9:6-11)

b) Katika kweli - Kuabudu katika kweli maana yake nini na kweli ni nini? Kweli ni neno la
Mungu (Yn. 17:17). Hivyo maana yake ni kuabudu kwa kulifuata neno la Mungu pasipo
kulibadilisha.

ƒ Watu wanaomwabudu Mungu kwa kuzifuata nia zao wenyewe wanamwabudu Mungu
bure. (Mat. 15:8.9).

ƒ Hebu tuone mifano ya watu wasidabudu katika roho na kweli.

i. Kaini alipomtolea Mungu sadaka, ibada yake haikuwa katika kweli Ndio maana
haikupokelewa (Mwa.4:3-7; Ebr. 9:22). Tutaongea zaidi kuhusu Kaini baadaye
kidogo.

ii. Nadabu na Abihu walikuwa wana wa Haruni na makuhani wa Mungu, Viongozi


hawa wa dini walithubutu kubadili ibada waliopewa na Mungu. Kwa hiyo,
waliteketezwe. moto kutoka kwa Mungu. (Law. 10:1.2).

iii. Mfalme Sauli alifuata mawazo yake mwenyewe katika kumwabudu Mungu. Kwa
hiyo, Mungu aliondoa ufalme kwake na kumpa Daudi (1 Sam. 13:5-14; 15:1-3, 9,
17-23).

2. Kuenenda kwa imani - Paulo amesema "Maana twaenenda kwa imani si kwa kuona" (2 Kor.
5:7). Huu ndio msingi wa ibada zetu. Lakini, imani huja kwa njia ya kusikia neno la Mungu
(Rum. 10:17). Ili tutambue maana ya kuenenda kwa imani, hebu! tuone baadhi ya mifano:-

i. Nuhu alijenga safina kwa imani (Ebr. 11:7). Biblia inasema, "Ndiyo alivyofanya Nuhu,
sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya" (Mwa. 6:22; 7:5).
Kutokana na maneno haya, twajifunza kwamba kusutii mtu aonekane amefanya kwa imani,
ni lazima atende sawasawa na alivyoamriwa. Kama Nuhu angelijenga safina yenye dari
(ghorofa) tano badala ya tatu au kuweka milango mitatu badala ya mmoja, angalikuwa
haenendi sawa na neno la Mungu na Biblia isingesema kwamba Nuhu alijenga safina kwa
Imani.

27
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

ii. Kaini na Habili ni mifano mizuri kwetu kuonyesha umuhimu wa kufanya jambo kwa imani.

a) Habili alitoa sadaka yake bora kwa imani (Ebr. 11:4; Rum. 10:17).

b) Kaini alitoa sadaka yake kwa jinsi alivyotaka mwenyewe. Bila shaka Kaini naye
aliamini kwamba Mungu yupo na kwamba imempasa amtolee sadaka. Walakini,
hakumtolea Mungu sadaka aliyoitaka. Mungu alitaka sadaka yenye damu (Ebr. 9:22).

ƒ Katika (Mwa. 4:3-7) twasoma, "Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi,
sadaka kwa Bwana. Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na
sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake: bali
Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake
ukakunjamana. Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? na kwa nini
uso wako umekunjamana? Kama_ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda
vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa
uishinde,"

ƒ Tunaona matendo ya Kaini yalikuwa mabaya, maana hakutoa sadaka yenye damu
(1Yon. 3:11, 12). Kwa hiyo, Mbesabjwa....kuwa. hana imani: maana katika (Yak.
2:17) twasoma, "imani. isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake".

ƒ Tunaona, imani yetu haifai kitu tusipomtii Mungu katika kila jambo! Kumbuka,
Nadabu, Abihu, na Sauli wote walisikia neno la Mungu ila hawakumtii. Kwa hiyo,
Mungu aliwapa adhabu.

¾ Kama tulivyotangulia kusema awali, katika siku zetu hatutoi sadaka za wanyama wa
kuteketezwa, kwa sababu taratibu hii ni ya ibada za agano la kale lililowahusu waisrael,
Wakristo hatujaamriwa kufanya hivyo katika taratibu yetu ya ibada. Ibada ya kweli ya
Wakristo ni ile iliyoamriwa na Mungu katika Agano Jipya.

3. Ibada ambayo watu walikuwa nayo katika Torati ilikuwa tofauti sana na ibada ya Yesu katika
Agano Jipya.

- Wakristo hatufuati ibada ya Agano la Kale kwa sababu Torati imeondolewa (Rum. 7:6; Gal.
2:16; 3:10-13; 5:2-6).

- Katika Agano Jipya, Yesu ametupa sheria zake ambazo ni tofauti na zile za Agano la Kale.
(Tutajifunza kirefu kuhusu kuondolewa kwa Agano la Kale na Torati katika Somo la 6
liitwalo "SHERIA na INJILI)

- Hivyo tukiyafanya yale yaliyoamriwa katika Agano Jipya tutakuwa tumefanya kwa imani.
Lakini tukifanya kinyume cha hayo, tutakuwa tumefananishwa na Kaini aliyetoa sadaka kwa
jinsi alivyotaka mwenyewe.

- Basi, imani pasipo kutenda yale tuliyoamriwa na Yesu inafanya ibada yetu itakuwa ya bure
(Mt. 15:8-9; Yak. 2:19).

28
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

4. Matendo ya ibada ya siku zote – Kuna matendo ya ibada ya kila siku ambayo wakristo
wameamriwa wayafanye, hebu tuone yafuatayo:

a) Kuomba na kumshukuru Mungu bila kukoma (Flp. 4:6; 1The. 5:17, 18). Tutaongea zaidi
kuhusu kuomba hapo chini.

b) Tumwimbie Mungu popote tulipo. (Mdo. 16:25). Yakobo alisema, "Mtu wa kwenu
amepatikana na mabaya? na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? na aimbe zaburi"
(Yak. 5:13).

c) Tujitoe miili yetu kwa kazi yake Mungu (Rum. 12:1, 2; 6:12, 13)

d) Tutende mema na kushirikiana tukimsifu Mungu. (Ebr. 13:15, 16)

e) Tuwasaidie Yatima na Wajane na kujilinda na Dunia. (Yak. 1:27)

f) Tuangaliane (wakristo) na kuhimizana. (Ebr. 10:24; Gal. 6:1, 2)

5. Matendo ya ibada Kanisani (Tukusanyikapo) - Tumeamriwa tusiiache kukusanyika pamoja


(Ebr. 10:25-27).

¾ Karisa linakusanyika pamoja siku ya kwanza ya juma (Jumapili) ili tupate chakula cha Bwana
(Mdo. 20:7; 1Kor. 11:17-34) Tena, tunakusanyika kusudi tujengane (1Kor. 14:26; Kol. 3:16).
Ebu, tuone ibada za pamoja:-

I. CHAKULA CHA BWANA – ni moja ya tendo la ibada linalowkusanya wakristo, Tunasoma:


"Nao walipokuwa wakila, Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi
wake, akasema, Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu. Akakitwaa kikombe, akashukuru,
akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano,
imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. Lakini nawaambieni, Sitakunywa
kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi
katika ufalme wa Baba yangu." (Mt. 26:26-29).

a) Kushiriki chakula cha Bwana ni tendo muhimu sana; tena, ni kwa lazima. Yesu alisema,
"Usipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake. hamna uzima ndani
yenu.

ƒ Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua
siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni
kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu,
nami hukaa ndani yake" (Yn. 6:53-56).

b) Yesu aliwaambia wanafunzi kwamba atakula chakula chake nao mpya katika ufalme
(yaani kanisa) (Mt. 26:29; Lk. 22:29-30), Tunathibitisha hayo kwa kule kusema: "Kwa
kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati
yao" (Mt. 18:20).

29
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

c) Katika Biblia, tunaona Wakristo hawakushiriki chakula cha Bwana mara moja tu kwa
mwezi au miezi. La! Bali Wakristo walikuwa wakikusanyika katika jina la Yesu kila siku ya
kwanza ya juma (Jumapili) ili wale chakula cha Bwana (Mdo. 20:7; 1 Kor. 11:23-26.33).
Wakristo walipewa siku ya kwanza ya juma kwa sababu ndiyo siku ambayo Yesu
alifufuka katika wafu. Wakristo hukusanyika siku ya kwanza ya kila juma kusudi
wamkumbuke na kutangaza kifo chake kwa njia ya chakula cha Bwana hata
atakapokuja. Ndivyo tunavyoambiwa tufanye katika (1 Kor. 11:26; Ebr 10:25).

d) Kupata chakula cha Bwana kila Jumapili siyo kukila kwa mazoea; bali ni kufuata
mafundisho ya Mungu mwenyewe katika Biblia. Tena, ndiyo njia ya kusisitiza umuhimu
wake! Watu wasiopata chakula cha Bwana kila Jumapili ndio wenye kulichezea neno la
Mungu kwa kuamua kufuata taratibu yao!

e) Wako watu wanaotoa mkate tu wasitoe na mvinyo. Hawa wanasema kwamba mkate
unatosha, kwani mkate ni mfano wa mwili na mwili haukosi kuwa na damu. Lakini, Yesu
ametuamuru tupata mkate na mvinyo pia: kwani alisema damu yake haitakaa katika mwili
wake! Soma tena maneno yake. Alisema, "Nyweni nyote katika hiki; kwa maana hii ndiyo
damu yangu ya agano, imwagikayo kwa wengi Awa ondoleo la dhambi. Usipoula mwili
wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake hamna uzima ndani yenu" (Mt. 26:27,
28; Yn. 6:53). Basi, watu wasiotumia kikombe cha Bwana huwana uzima!

f) Wako watu wanaoweka madhabahu kanisani. Hawa wanadhani kwamba mkate na


mvinyo hugeuzwa kule madhabahuni kuwa ndiyo mwili na damu halisi. Kufuatana na
mawazo wao, Yesu hurudiarudia kufa kila wakitoa chakula cha Bwana. Mawazo hayo si
ya kweli. Biblia inasema kwamba Yesu alikufa mara moja tu (Ebr. 9:25-28).

ƒ Yesu alisema tule chakula chake kwa kumbukumbu tu. Sikiliza maneno yake. "Naye
akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajiii yenu;
fanyeni hivi kwa ukurnbusho wangu Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe,
akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo.
kwa ukumbusho wangu" (1 Kor. 11:24-25).

ƒ Madhabahu yetu ni mbinguni alipokwenda Yesu, kuhani mkuu wetu (Ebr. 13:10-14;
8:3-5). Wanaoweka madhabahu kanisani wanaongeza kitu kisichokuwapo katika
Agano Jipya! Kumbuka, tumekatazwa tusiongeze wala kupunguzia neno la Mungu!

II. KUIMBA - Kuimba ni sehemu moja katika ibada zetu.

a) Tufundishane na tujengane hali tukiimba kwa akili neno la Kristo. Biblia inasema, "Neno la
Kristo na kae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa
zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni: huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni
mwenu" (Kol. 3:16). Tena inasema, "Msilewe kwa mvinyo, amhamo mna ufisadi; bali
mjazwe roho; mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni huku mkiimba na
kumshangilia Bwana mtoyoni mwenu” (Efe. 5:18,19). "Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa
roho, tena nitaomba kwa akili pia; ni'taimba kwa roho, tens nitaimba kwa akili pia (1 Kor.
14:15)

30
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

b) Kuhusu kutumia vyombo vya muziki ibadani - Katika Agano Jipya hatuwezi kusikia
sehemu yeyote ambayo Mungu alituagiza au Mkristo ye yote aliyetumia vyombo vya muziki,
zingatia yafuatayo:-

ƒ Tusisahau Tumeonywa tusiiongeze wala kubadili yaliyoandikwa (2 Yoh. 1:9; Ufu.


22:18-19: 1 Kor. 4:6).

ƒ Tukumbuke tuiriejifunza muda sio mrefu kwamba lengo la kuimba kanisani ni kuonyana
na kufundishana. Kusudi tufanye hivyo tumeamriwa tutumie neno la Kristo na kuimba
kwa akili zetu.

ƒ Vyombo vya muziki haviwezi kufundisha wa kuonywa mtu kwa neno la Kristo bali mara
nyingi vyombo hivi humfanya mtu aburudike na kutokusikia na kuelewa maneno ya
nyimbo inayoimbwa (1 Kor. 14:6-9.).

ƒ Kwa hiyo, Yesu hakuturuhusu kuvitumia. Tusiwe kama Kaini, Nadabu, Abihu, na
Mfalme Sauli waliojaribu kuabudu kwa jinsi walivyotaka wenyewe, wakakataliwa na
Mungu!

ƒ Ikiwa Mungu angalitaka kanisa litumie vyombo vya muziki angalituamibia, nasi
tungaliona katika Agano Jipya habari ya Wakristo wakivitumia.

ƒ Twajua kwamba kuimba pasipo vyombo vya muziki kanisani si kosa (Mt. 26:30 n.k.).
Lakini, kuimba pamoja na vyombo vya muziki kanisani ni tendo la mashaka kwa kuwa
Mungu hakuliruhusu wala kulikataza katika Agano Jipya na, kwa hiyo, tumekatazwa
tusilifanye tulicho na mashaka nacho. Twasoma; "Lakini aliye na shaka, kama akila,
amehudumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotokana
na imani ni dhambi. (Rum. 14:23)

ƒ Kwa sababu imani huja kwa kusikia neno la Kristo, na kwa sababu neno la Kristo
halijaturuhusu kuvitumia vyombo vya muziki, basi ni kosa kuvitumia!

c) Kwaya – Kwaya nayo haimo katika Biblia. Kwaya ni kundi dogo la watu wanaoimba katika
mikusanyiko ya madhehebu hali wengine wanawasikiliza tu. Tumesoma tayari kwamba tuli-
amriwa kufundishana na kuonyana katika nyimbo zetu.

ƒ Biblia haisemi "tufundishwe na kwaya" bali Wakristo wote wameamriwa "kufundishana"


wao kwa wao kwa njia ya nyimbo. Basi, Kila Mkristo anatakiwa aimbe kanisani!

III. KUOMBA

a) Umuhimu wa kuomba - "Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi,
na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka,
tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri, nalo
lakubalika mbele za Mungu mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na
kupata kujua yaliyo kweli" (1Tim. 2:1-4)

31
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

ƒ Yesu alifundisha kwamba imetupasa kumwomba Mungu siku zote. Soma maneno yake
katika (Lk. 18:1-8).

ƒ Biblia inasema, "Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii" (Yak.
5:16).

b) Tumnyenyekea sana Mungu katika kusali. - "Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye
mbinguni, Jina lako litukuzwe" (Mt. 6:9). Soma pia (1 Pet. 5:6, 7; Yak. 4:10; Isa. 66:2; Lk.
13:9-14).

c) Tusali katika jina la Kristo - (Yn. 14:13-14; Efe. 2:18; 1 Pet. 2:5).

d) Tusitafute matakwa yetu bali mapenzi yake Mungu - (Mt. 6:10; 1 Yoh. 5:14; Mt. 26:39).

e) Tusiombe vibaya - (Yak. 4:2, 3).

f) Tuombe tukiwa na imani kwamba Mungu anatusikia - (Yak. 1:6-8)

g) Tuombe! tukiungama dhambi zeti - (1 Yoh. 1:9; Zab. 34:14).

h) Tuombe hali tumewasamehe waliotukosea sisi - (Mt. 6:12, 15)

i) Tuombe pamoja na kumshukuru Mungu. - "Msijisumbue kwa neno lo tote, bali katika kila
neno kwa kusaii na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu" (Fil.
4:6). Soma tena (1 Tim. 2:1).

j) Tusitumie maneno mengi sana katika kusali - "Nanyi mkiwa katika kusaii, msipayuke-
pavuke. kama watu wa mataifa, maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya
maneno yao kuwa mengi" (Mt. 6:7).

k) Tusitumie rozari – Wanadamu wamebuni rozari na kuiingiza katika madhehebu yao, Mara
nyingi washiriki wao wanaiabudu rozari. Tukumbuke Mungu ametukataza tusitengeneze
cho chote cha kuabudu. Alisema "Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu
cho chote kilicho juu mbinguni wala kilicho chini duniani wala kilicho majini chini ya dunia.
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye
wivu" (Kut. 20:4-5).

ƒ Wanaotumia rozari wanafikiri kwamba Mungu atawasikia kwa kuomba kwao kwingi,
wanarudiarudia maneno yale yale hata zaidi ya mara hamsini!

ƒ Kumbuka, Yesu anakataza maombi kama hayo akisema, "Nanyi mkiwa katika kusali, m
sipayuke-payuke, kama watu wa mataifa: maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa
sababu ya maneno yao kuwa mengi. Basi msifanane na hao" (Mt. 6:7-8) .

ƒ Katika Biblia hatuwezi kuona mtu ye yote aliyetumia rozari. Basi, tumeonywa tusiongeze
neno lo lote katika maneno ya Mungu (Kum. 4:2; Mit. 30:5-6; Ufu. 22:18-19).

ƒ Mapokeo ya wanadamu hufanya ibada yao kuwa ni bure (Mt. 15:8, 9)

32
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

l) Tosisali kusudi tupate sifa za wanadamu - Yesu alisema, "Tena msalipo, msiwe kama wana-
fiki, kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za
njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao" (Mt. 6:5).

m) Kanisani tusali kwa sauti itoshayo kusikika na kwa maneno yanayoeleweka (1 Kor. 14:14-17).

n) Wanaume na wasalishe kanisani. Wanawake hawaruhusiwi (1Tim. 2:8-13; 1 Kor.14:34-35).

o) Kama tunaongozwa sala, tuisiseme "amina" (yaani na iwe hivyo) isipokuwa tumesikia na
kukubali maneno yake yule anayesalisha (1 Kor. 14:16; Zab. 106:48).

IV. KUTOA CHANGIZO.

a) Madhehebu wanafanya makadilio na kuwalazirnisia washiriki wao watoe. Wasipotoa


wananyirnwa huduma mbalimbali za kanisa, Lakini, si ndivyo tunavyoamriwa katika Biblia.

b) Tumepewa amri ya kutoa kila siku ya kwanza ya juma (1 Kor. 16:1-2).

c) Tumeamriwa kutoa kwa ukarimu na kwa moyo (2 Kor. 9:6-7).

d) Kanisa haliruhusiwi kumpimia mtu kiwango na kumlazinnisha atoe. Biblia inatufundisha kutoa
kwa hiari na kwa kadiri ya kufanikiwa kwetu (1 Kor. 16:1-2).

e) Watu wasiotoa kwa moyo na kwa jinsi walivyofanikiwa hawatimizi mapenzi ya Mungu.

f) Kazi za changizo zetu ni kupata mahitaji ya kanisa na kupeleka watu kuhubiri Injili. (1 Kor.16:1;
Rum. 10:15). Tutaongea zaidi huhusu changizo huko mbeleni.

V. KULIHUBIRI NENO LA MUNGU.

a) Kulihubiri nenoni mpango wa Mungu kuwaokoa wanadamu na kuwakamilisha (1Kor. 1:21;


Rum. 10:13-15; 2Tim. 3:15-17).

b) Neno la Mungu ni chakula cha kiroho cha Mkristo. Tunahitaji chakula hiki kila mara (Ebr. 5:12-
14; Mdo. 2:42; Mt. 28:20).

c) Bila ya kufundishana neno la Mungu, watu hawataweza kutambua tofauti kati ya mafundisho ya
wanadamu na ukweli wa Mungu (1Tim. 4:16; Yn 8:32; 17:17).

d) Watabaki kuwa watoto wachanga na roho zao zinaweza kufa na njaa kwa kukosa chakula cha
kiroho (Ebr. 5:12-14; 1Kor. 3:1-3; Efe. 4:14-15)

33
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

KAZI ZA KANISA
¾ Mtu anapojiandikisha katika ajira hapo sipo mwisho wa kazi, bali inamlazimu ahudhurie kila siku
kazini; na hata hivyo hawezi kupata mshahara mpaka afanye kazi ipasavyo. Mambo hayo ni mfano
kwa Mkristo. Ingawaje amefanya kazi ya kusikia neno, kuliamini, kutubu dhambi, kumkiri Kristo na
kubatizwa; hayo yote ni sawa na mtu aliyejiandikisha katika ajira. Baada ya ubatizo kuna kazi ya
kuifanya.

1. KUHUBIRI KWA WALIOPOTEA

- "Lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa
uvumilivu wote na mafundisho" (2 Tim. 4:2).

a) KUHUBIRI MAANA YAKIE NINI? Ni kutangaza kitu au neno waziwazi. Hasa kwa Mkristo, ina
maana ya kumtangaza Yesu Kristo kuwa ni Mwana wa Mungu na Mwokozi wa ulimwengu.
Hivyo basi imempasa mtu aliyebatizwa aende kuwatangazia wengine habari ya Yesu na
kuwaita waje kwake (Mk. 16:15,16; Mt. 28:18-20; Rum. 1:15,16).

b) UHIMIZO WA KUHUBIRI (Kuwapenda waliopotea) - ili tupate kuhubiri Injili kwa waliopotea,
basi kwanza ni lazima tuwapende.

i. Kuwapenda wenye dhambi kutatusukuma sisi tuwahubirie (Yn. 3:16; 1 Yoh. 4:7-11.)

ƒ Paulo, kwa kuwapenda Wayahudi wale waliopotea, alithubutu kusema kwamba


angalikuwa tayari kupoteza nafsi yake kwa ajili yao iwapo ingaliwaokoa (Rum. 9:1-5).

ƒ Upendo mkubwa kama huo ukamfanya atembee hapa na pale katika shida na matatizo
mengi ili ahubiri Injili. Isitoshe, alifahamu waziwazi kuwa wangeweza kumwua (2 Kor.
11:23-33).

ƒ Upendo kama huo haupatikani kwa juma moja au mwezi, bali unakuja baada ya
kutambua hatari walionayo na kuwaonea huruma. Na kama leo Wakristo wangejisikia
hivyo tungewavuta wengi wawe Wakristo!

ii. Kulinganisha kati ya waliopotea na Wakristo - Mtu akitaka kujua kiasi cha kazi iliyobaikia
mbele yake, ni lazima alinganishe alikotoka, alipo, na anakokwenda. Kwa njia hiyo
anaweza kutambua muda anaohitaji kumaliza kazi yake. Kwa mfano:-

ƒ Mkulima mwenye eka moja ya shamba naye amemaliza 1/4 eka, anatambua wazi
kuwa kazi iliyobaki ni kubwa mno kuliko kazi aliyofanya. Hivyo itamlazimu kuzidisha
juhudi mara dufu. Basi, katika kazi yetu ya kuhubiri, twaona kwamba idadi ya waliopotea
ni kubwa mno ikilinganishwa na waliookolewa. Kwa hiyo twafahamu wazi kuwa kazi
yetu ya kuhubiri bado sana.

ƒ Yesu katika kuzunguka akihubiri aliwaona makutano na kuwahurumia kwa


sababu walikuwa kama hawana mchungaji. Ndiyo sababu akawaeleza wanafunzi wake
kwamba mavuno ni mengi nayo yanahitaji wavunaji wengi (Mt. 9:35-38)

34
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

ƒ Lakini sisi mara nyingi tunawaza kwamba bado tunao muda wa kutosha na kwa sababu
hiyo hatufanyi kwa nguvu. Yesu alijua kuwa anao wakati mfupi wa kumaliza kazi yake,
na hivyo alishindwa kula hata chakula (Yn. 4:34-35). Kwa jinsi tuchelewavyo kuhubiri
neno ndivyo wengi wanavyozidi kufa katika dhambi zao!

c) KANISA NI CHOMBO CHA MUNGU KUTANGAZA NENO LAKE (Efe. 3:10).

1) Juhudi ya kanisa kwa jumla - Katika kanisa la Antiokia kulikuwamo manabii na waalimu.
Walakini, Wakristo hawakuwaachia hawa kazi yote. Kanisa likawaturna watu kwenda kuhubiri
Injili mahali ambapo haijasikika. Kwa uongozi wa Roho Mtakatifu, wakawatuma Paulo na
Barnaba (Mdo. 13:1-5). Na hawa waliotumwa, baadaye walileta matokeo ya kazi yao huko
walikokwenda (Mdo. 14:26-27) - Huu ni mfano mmojawapo wa kuhubiri kwa kanisa zima. Kazi
ya kanisa kwa ujumla ni kule kuwatuma watu sehemu mbalimbali kwenda kuhubiri neno.
Walakini, hii haizuii juhudi ya binafsi ya kila Mkristo.

2) Juhudi ya kila mmoja - Si lazima Mkristo asubiri mpaka kanisa litume watu kuhubiri, bali kila
Mkristo alitamgaze neno la Mungu kwa uwezo wake wote. Biblia inaongea sana kuhusu
kuhubiri kwa mtu mmoja mmoja. Wakati kanisa la Yerusalemu lilipokuwa katika adha kuu ya
kutawanyika, Wakristo wali kwenda huko na huko wakihubiri neno (Mdo. 8:1-4). Twasoma

ƒ Filipo akitelemka Samaria (Mdo. 8:5, 8). Hivyo kanisa la Samaria lilianzishwa kwa juhudi ya
mtu mmoja tu.

ƒ Tena twasikia katika adha ile ile, wengine walikwenda mpaka Antiokia ya Siria. Twasoma
kuwa habari ikaletwa masikioni mwa mitume kule Yerusalemu juu ya kazi ya sehemu zile
(Mdo.11:21, 22). Hii inaonyesha umuhimu wa kazi ya kila mmoja.

d) SHAMBA LA KUHUBIRIWA

ƒ Yesu alisema "shamba ni ulimwengu" (Mt. 13:38). Maneno haya yamaonyesha wazi
kwamba kazi ya kuhubiri si ya mahali pamoja tu, bali ni ya ulimwenguni pote.

ƒ Yesu aliwaambia wanafunzi wake, "Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila
kiumbe" (Mk. 16:15). Soma pia (Mt. 28:18-19). Tena aliwaagiza wamshuhudie hata mwisho
wa nchi (Mdo 1:6).

e) NJIA ZA KUHUBIRI

1. Mbele ya mikutano - Yesu mwenyewe aliweza ku hubin katika mikutano ya hadhara.


Kuhubiri mbele ya mikutano ni njia mojawapo ya kuwavuta watu wengi kwa Bwaria.
Walakini inapaswa kuwa makini wakati mwingine unaweza kukuta katika mikutano wapo
watu wabishi wenye nia ya kuvuruga mambo.

2. Kwa njia ya radio - Kwa njia hii tunaweza kuhubiri watu wengi zaidi kuliko kwa kusimama
mbele ya mkutano. Kwani radio ni chombo cha kawaida katika nchi nyingi kinachosikilizwa
na wengi.

35
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

3. Kwa video na kaseti - Hata ingawai si wote walio na uwezo wa kununua vyombo vya video
na kaseti, walakini ni njia zinazovuta watu wengi kutaka kusikiliza mafundisho ya Biblia.

4. Kwa masomo yaliyochapwa - Msomo yaliyochapwa katika karatasi yanaweza


kuwafundisha wengi kwa gharama ndogo kuliko kumtuma mhubiri. Katika kuhubiri, somo
husikiwa, lakini kuna hatari ya kusahauliwa hata kabla ya saa 24 kupita. Lakini, masomo ya
kuchapishwa hubaki na mwanafunzi, naye anaweza kuyasoma kila apendapo.

¾ Mengine yaweza kumfanya msomaji hata afunge radio yake ili asome vizuri. Isitoshe,
anaweza kuwapa watu wengine ili wasome nao Ni kweli kwamba baadhi yake
yatapuuzwa na kutupwa. Lakini imetokea mara nyingi kwamba wengine wameokota
yale yaliyotupwa na kuyasoma! Hivyo basi, hii ni njia njema sana ya kuhubiri Injili
ulimwenguni.

5. Kuwa karibisha watu wahudhurie masomo ya Biblia kanisani - Mara nyingi wageni
hufika kanisani kusali baada ya kukaribishwa na rafiki zao walio wakristo. Kule kanisani
wanaweza kufanya marafiki wengi na kusoma Biblia nao. Hivyo, huvutwa sana na ushirika
wa kanisa.

¾ Viongozi wa madhehebu ya Kibatisti wanasifu njia hiyo sana kuwa ndivyo wanavyopata
idadi kubwa ya watu wanaoongezeka katika madhehebu yao.

6. Kwa kutembea nyumba kwa nyumba – Kuhubiri nyumba kwa nyumba ni njia iliyo nzuri
zaidi, huenda kuliko nyingine. Wakati wa kuhubiri katika makundi, wanaweza kuwapo
wapinzani wenye kuvunja mioyo ya wengine (Mdo. 13:6-12). Katika nyumba, watu
wanaweza kusikiliza kwa moyo (Mdo. 20:20). Isitoshe, mwalimu anaweza kuongea kuhusu
somo linalomhusu mwenye nyumba kwa undani sana na kuyajibu maswali yake. Akiwa
na masomo ya karatasi au ya kaseti anaweza kuyaacha kwa mwenye nyumba yawe
kumbukumbu la mafundisho yake. Katika kuhubiri nyumba kwa nyumba, kunakuwapo
matatizo madogo madogo. (Kwa mfano, kusumbuliwa na watoto wadogo au fujo la
majirani.) Lakini faida yake ni kubwa sana, kwani idadi kubwa ya watu wanaoamua
kumfuata Yesu ni wale wanaovutwa na majirani (Rum. 10:13-15).

2. KUJENGA NA KUWAIMARISHA WAKRISTO - ni kazi nyingine ya kanisa

a) Kazi ya pili ya kanisa ambayo ni muhimu sana ni kujenga waliobatizwa. Ni kweli kwamba Yesu
alituamuru kuhubiri Injili kwa kila kiumbe. Walakini, hakuacha pale bali aliendelea kusema “na
kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi" (Mt. 28:20). Wakristo wanafananishwa
na watoto wadogo waliozaliwa karibuni. Hawa wanahitaji chakula na malazi bora. Kama vile
watoto wanavyohitaji chakula kila wakati kusudi wakue na wawe na afya, vivyo hivyo Wakristo
wachanga wanahitaji chakula cha roho zao kila wakati (1Kor 3:2; 1Pet. 2:2; Ebr. 5:12-14).

¾ Kanisa ni chombo cha Mungu kuwalisha na kuwajenga Wakristo.

i. Juhudi ya kila mmoja - Kila Mkristo anahitaji kujenga wengine (Rum. 14:17; 15:2; 1The.
5:11; Ebr. 10:24).

36
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

ii. Juhudi ya kanisa kwa ujumla - Paulo alitoa maelezo machache kwa kanisa la Korintho
kuhusu kujengana (1 Kor. 14:4-5, 12; Efe. 4:16). Kanisa linahitaji kutiana nguvu, kila kiungo
na mwenzake. Kama vile paa la nyumba haliwezi kusimama bila ukuta na ukuta hausimami
bila msingi, vivyo hivyo kila Mkristo humtegemea mkristo mwenziye.

3. NGUVU YA KUJENGA MWILI - (Kanisa)

a) Mungu ili aujenge mwili wake (kanisa lake) aliweka watu mbali mbali katika kanisa (Efe. 4:11-
12). Na hawa wafuatao ndio nguvu ya kulijenga kanisa:-

ƒ "NABII" huyu alikuwa ni "mjumbe" aliyetangaza neno la Mungu.

ƒ "MTUME" - maana yake ni mtu aliyepelekwa afanye kazi ile aliyopewa na Yule
aliyempeleka.

b) Kazi ya manabii na mitume wa Yesu ilikuwa kuuweka msingi wa kanisa kwa njia ya mafundisho
yao (Efe. 2:20-22).

c) Katika Agano la Kale manabii walitabiri mambo yaliyohusu kanisa hata ingawa hawakujua ni lini
mambo haya yangetimilika (1 Pet. 1:10-12).

d) Mitume nao walifundisha kwa njia nyingi kuhusu kanisa na mwenendo wake. Walimailiza kazi
yao ya kuuweka msingi wa kanisa (1 Kor 3:10-11).

e) Mitume na Manabii wote wlikufa na tunashudia umaliza kazi yao ya kuuweka msingi, msingi
umekwishawekwa na hakuna msingi mwingine (1Kor. 3:11) Kwa maana hiyo, hakuna manabii
wala mitumie wa Yesu wanaoishi duniani leo. - Hebu tuhakikishe jambo hili!

1. Kazi ya mitume wa Yesu hasa ilikuwa kumshuhudia kuwa amekufa na kufufuka. Mitume
walikuwa mashahidi wa kufufuka kwake (Mdo. 1:1-3, 8; 2:32; 3:15; 10:39-43). Mtu
hakuweza kuwa mtume wa Yesu isipokuwa ametimiza daraja zifuatazo:-

a) Awe mtu aliyefuatana nao wanafunzi wa Yesu alipokuwa akitoka na kuingia kwao
(Mdo. 1:21).

b) Awe ameshuhudlia ubatizo wa Yohana Mbatizaji (Mdo 1:22).

c) Awe ameshuhudia kufufuka kwake Yesu kutoka wafu (Mdo. 1:2-3, 22; Gal. 1:11-17;
2:8).

d) Achaguliwe na Yesu mwenyewe (Mdo. 1:24).

2. Yesu alimchagua na kumtokea Paulo (Sauli) kusudi awe shahidi na mtume (Mdo. 26:14-
18; 9:15, 17; 22:14, 15). Hata ingawa Sauli hakumwamini Yesu kuwa ni Mwana wa Mungu
hapo mwanzoni, walakini angaliweza kumwona huku Uyahudi alipokuwa akizunguka huku
na huku akihubiri.

37
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

3. Hakuna mitume wa Yesu sasa kwa sababu hakuna awezaye kutimiza masharti yaliyotajwa
hapo juu Isitoshe, hatuwahitaji mitume wengine leo kwa sababu wale wale wa kwanza
wamemaliza kazi zote.

4. Kazi waliyofanya hawa inatujenga sisi mpaka leo kwa njia ya maandiko yao. (2 Tim. 3:16-
17).

5. 'Manabii walihitajika mwanzoni mwa kanisa, Katika siku za kwanza za kanisa mafundisho
ya Yesu yalikuwa hayajakwisha kuandikwa. Wakristo hawakuwa na vitabu vyote vya
Agano Jipya ili wasome maneno yote ya Yesu. Kwa hiyo Mungu aliweka manabii katika miji
mbalimbali akiwaongoza kwa Roho Mtakatifu ili wakumbuke maneno yote ya Yesu na
kuwafundisha watu wa miji ile (1 Kor.14:26-33). Isitoshe, waliwezeshwa kufanya ishara
(yaani, miujiza) kusudi watu wajue kwamba maneno yao yalitoka kwa Mungu (Yn. 14:26;
15:26, 27; Mk.16:20).

4. MUNGU AUTUAMBIA UNABII UTAKOMA

a) Pamoja na ishara zake wakati ijapo ili iliyo kamili (1 Kor. 13:8-10). "Iliyo kamili" maana yake ni
sheria ya Yesu (Agano Jipya) ambayo sasa imeandikwa kwa ukamilifu kusudi watu wote
wasome wenyewe (Yak. 1:25; 2 Tim. 3:14-17; Yn. 20:30-31).

b) Hatuhitaji manabii wala mitume wa Yesu (wala ishara zao) siku hizi (Lk. 16: 31; Yn. 20:30-31).

c) Biblia ni bora kuliko manabii. Manabii walijua mambo kwa sehemu sehemu tu (1 Kor. 13:9) bali
sasa katika Biblia sisi tunayo maneno yote (yaani iliyo kamili) ya Yesu aliyotaka tuwe nayo
(2 Tim. 3:16-17; Gal. 1:8-9; Efe. 2:20; Yud. 1:3; Mt.12:38-40; Lk. 16:19)

5. WAMISHENARI

a) Tumekwisha kuona kuwa maana ya neno "MTUME" ni mtu aliyepelekwa afanye kazi fulani.
Katika Biblia walikuwapo watu waliokuwa MITUME WA KANISA (2 Kor. 8:23; Rum. 16:7).
Watu hawa walikuwa tofauti na mitume wa Yesu.

b) Kama tulivyoona, mitume wa Yesu walichaguliwa naye wawe mashahidi wake. Yesu alikuwa
na mitume 13 tu!)

c) Katika (Mdo. 14:14) kuna mtu aitwaye Barnaba, naye aliitwa kuwa ni mitume walakini Barnaba
hakuwa mtume wa Yesu bali mtume wa kanisa, maana alitumwa Antiokia ili ahubiri na, halafu,
alitumwa aende na Paulo ili wapeleke msaada kwa kanisa Uyahudi (Mdo. 11:22-30).

d) Katika Kiingereza mtu anayepelekwa na kanisa anaweza kuitwa MISSIONARY. Katika siku
zetu mara nyingi hutumika neno "mmishenari" badala ya "mtume wa kanisa" kwa kusudi la
kuwasaidia watu wasielewe vibaya wakidhani wapo mitume wa Yesu leo. Basi, katika kanisa
tunao wamishenari (mitume wa kanisa) hata leo. Watu hawa hupeleka Injili po pote
wanapotumwa na kundi la kanisa linalowachagua. Wako chini ya wazee wa lile kundi nao
wanawajibika kutimiliza kazi walizopewa nao. Mara nyingi wamishenari wanatumwa –

38
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

waanzishe kanisa mahali lisilokuwapo. Baada ya kulianzisha kanisa, kazi yao ni kuliimarisha
kiroho mpaka liweze kujitegemea.

6. WAINJILISTI (Wahubiri)

a) Mungu amependelea kuwaokoa watu kwa njia ya kulihubiri neno lake (1 Kor. 1:21; Rum. 1:16;
10:13-15).

b) Kazi ya mhubiri zaidi ya kuokoa waliopotea, bali pia ana jukumu la kuimarisha wale
aliowahubiri, yaani azidi kuwajenga katika neno la Bwana (1Tim. 1:3-7). Tutaongea zaidi
kuhusu mhubiri mbele kadri tunavyoendelea.

7. WALIMU

a) Yesu alisema, "enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwajina !a
Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyl"
(Mt. 28: 19-20).

b) Basi waalimu wamewekwa kwa kusudi hilo, wawafundishe watu kuyashika yote ili waimarike
katika Bwana (1Kor. 12:28). Twasorna, "Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya
mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine"
(2 Tim. 2:2). Wakristo wote wanatakiwa wajifunze kuwafundisha wengine (Ebr. 5:12).

8. WACHUNGAJI WA KANISA

¾ Hawa ni watu wanaotunza kundi la kanisa lililopo kwao wakiongozwa na Kristo Yesu kwa njia
ya maandiko matakatifu. Kazi yao muhimu ni kuwalisha na kuwajenga Wakristo wakihakikisha
kwamba wanapata chakula cha kiroho kinachowafaa (Mdo. 20:20-28; 1 Pet. 5:1-2). Tutajifunza
zaidi kuhusu wachungaji Mbeleni.

9. MAKUHANI

a) Katika Agano la Kale makuhani walikuwa watu wachache waliochaguliwa wawe watakatifu ili
wasimame kati ya Mungu na Waisraeli wengine. Walakini, katika kanisa kila Mkristo ni Kuhani
wa Mungu (Pet. 2:5, 9; Ufu. 1:6).

b) Kazi za kuhani zilikuwa:-

i. kulijua neno la Mungu,

ii. kupambanua kati ya mema na mabaya,

iii. kuwafundisha watu wengine neno la Mungu, na

iv. kutoa sadaka na dhabihu kwa Mungu.

39
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

c) Kwa kuwa kila kristo ni kuhani wa Mungu, basi vivyo hivyo, ni kazi ya kilia Mkristo ajifunze na
awafundishe watu neno la Mungu na kupambanua kati ya mema na mabaya. (1 Pet.3:15; Ebr.
5:12-14). Kila Mkristo anawajibika kutoa sadaka na dhabihu za kiroho (Rum. 12:1; Ebr. 13:15-
16). Kila Mkristo awe mtakatifu (Ebr. 12:14).

d) Mtakatifu maana yake ni mtu aliyejitenga na dhambi, Mkristo hahitaji kuungama dhambi kwa
kiongozi wa kanisa kusudi amwombee, bali kila Mkristo anaweza kujiombea kwa Mungu
(1 Tim.2:5; Efe. 2:18; 3:12)

UTAWALA WA KANISA
1. Tumethibitisha ya kuwa Yesu peke yake ni mkuu wa kanisa. Yeye ni kichwa chake na mfalme
wake. Walakini, huko juu, tuliona jinsi Yesu alivyowaweka kanisani watumishi mbalimbali wenye
kazi ya kulitunza na kuliimarisha. Hebu sasa tuone mpango Yesu kwa kanisa.

A. WAZEE WA KANISA

a) Mtu hawezi kuitwa "mzee wa kanisa" kwa sababu amezeeka tu, bali kuna sifa zinazompasa
kuwa nazo.

b) Katika kanisa wale wanaoitwa WAZEE ndio MAASKOFU wa kanisa.

c) Maana ya neno "ASKOFU" ni "MWANGALIZI" wa kanisa. Askofu ni mzee ambaye ni


mwangalizi mwenye jukumu la kuwachunga Wakristo.

d) Kwa hiyo, Askofu anaitwa pia MCHUNGAJI.

e) Neno "MCHUNGAJI" likitafasiriwa katika lugha ya kingereza, hutamkwa "PASTER", hivyo


majina haya yana maana moja tu! (Soma 1 Pet. 5:1-4; Tit. 1:5-9; Mdo. 20:17-18, 28)
Maandiko hayo yanatuonyesha wazi kwamba kila mzee wa kanisa ni askofu (yaani,
mwangalizi) na ni mchungafi (yaani. Paster) pia: maana kazi ya kila mzee ni kuangalia, na
kuchunga, na kutunza, na kulisha kanisa.

2. Si halali mhubiri aitwe mchungaji paster, au askofu isipokuwa kwanza amezitimiza sifa zifuatazo
kama zilivyoainishwa katika biblia:-

¾ Tusisahau neno la Mungu linasema "Kila. apitaye cheo. wala asidurnu katika mafundisho ya
Kristo. yeye hana Mungu" (2 Yoh. 1:9).

B. SIFA ZA ASKOFU (MZEE)

¾ Tangu awali Mungu hajampa mtu kazi isipokuwa kwanza ametimiza sifa zilizotakiwa ili aifanye
vema kazi hiyo (Kut. 18:12-26; Hes. 16:1-50). Vivyo hivyo ni lazima wazee au wachungaji wa
kanisa wachaguliwe kwa mpango wa Mungu. Hapa chini ni ngazi au daraja za kumchagua
askofu. Sifa hizo zinapatikana katika (1 Tim. 3:1-16; Tit. 1:1-16; Yud. 1:5-16; 1 Pet. 5:1-11).
Hebu uzione sifa zifuataazo:-

40
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

1) Aipende kazi - aitake kazi hiyo kwa moyo wake, sio kulazimishwa (1 Pet. 5:2; 1Tim. 3:1;
Yn. 10:11-18).

2) Asiwe mtu wa kulaumika - asisemwe vibaya na watu (Tit. 1:6).

3) Mume wa mke mmoja - lazima awe ameoa ila awe na mke mmoja tu (maana Mkristo
haruhusiwi kuoa wake wengi) (1 Tim. 3:2; Tit. 1:6).

4) Mwenye kiasi - asizidishe chakula na kadhalika bali ajizuie katika mambo ya kimwili (1Tim.
3:2).

5) Mwenye busara - awe na hekima ya kutunza kundi (1Tim. 3:2; 1Fal. 3:16-27).

6) Mtu wa utaratibu - atende mambo yake kwa taratibu ili awe na heshima (1Tim. 3:2).

7) Mkaribishaji - awe mkarimu wa watu mwenye kuwatendea mema (Tit. 1:8; Mwa. 18:1-8).

8) Ajuaye kufundisha - awe na uwezo wa kufundisha neno kwa haki (2 Tim. 4:2).

9) Sio mzoelea ulevi - asiwe mlevi (Tit. 1:7; 1Tim. 3:3). Maana Wakristo wamekatazwa
wasilewe kamwe (Gal. 5:21; Efe. 5:18; 1 Kor. 5:11; 6:9-10).

10) Asiwe mipiga watu - asiwe mgomvi na watu (1Tim. 3:3).

11) Awe mpole - asiwe mkatili, lakini asiwe na upole wa kijinga (1Tim. 3:3). (tukumbuke sifa ya
nne inamtaka awe na kiasi katika kila jambo)

12) Asiwe mtu wa kujadiliana - asipende mazungumzo yaletayo ugomvi (1 Tim. 3:3).

13) Asiwe mpenda fedha - asipende fedha kuliko kazi ya Mungu (Ebr. 13:5, 6; 1 Tim. 6:10;
Lk. 8:14).

14) Ajuaye kusimamia nyumba yake – ajuaye kuitiisha nyumba yake katika adabu na kicho
cha Bwana (1Tim. 5:8).

15) Asiwe aliyeongoka karibuni – asiwe mtu aliyebatizwa karibuni wala asiwe mtoto katika
imani (1Tim. 3:6; Mit. 16:18).

16) Ashuhudiwe mema na watu wa nje – wasio Wakristo wamwone kuwa mwerna na wa
haki (1Tim. 3:7; Lk. 6:26)

17) Awe na watoto waaminio - awe na watoto, nao wawe Wakristo waaminifu (Tit. 1:6; 1Tim.
3:4).

18) Asijipendeze nafsi yake - aonyeshe upendo kwa watu atangulize wenzake (Tit 1:7; Flp.
2:3-4).

19) Asiwe mwepesi wa hasiira - asikasirike haraka kabla ya kuchunguza jambo (Tit. 1:7; Yak.
1:19-20).

41
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

20) Apende wema - ashkamane na wanaopenda na kutenda mema (Tit. 1:8).

21) Awe mwenye haki - afuate neno la Mungu katika matendo yake na maneno yake, naye
aamue mambo ya watu bila upendeleo (Tit. 1:8).

22) Awe mtakatifu - ajitenge na dhambi (Tit. 1:8; 1Kor. 7:9)

23) Mwenye kudhibiti nafsi yake - ajitawale nafsi yake (Tit. 1:8)

24) Mwenye kushika imani - asimame katika imani ya Irijili (Tit. 1:9; Yud. 1:3).

25) Awe na uwezo wa kuonya na kuwashinda waalimu wa uongo - maana ni wajibu wa


wazee kulilinda kundi la Mungu dhidi ya mbwa-mwitu (Tit. 1:9; Mdo. 20:29-30).

26) Awe na uwezo wa kudhibiti wapindua imani - Ajitahidi kuziba vinywa vya wapindua imani
ya kundi lake (Tit. 1:10-11).

27) Mkewe awe mwaminifu – awe na mke mwaminifu katika yote (1 Tim. 3:11)

C. ANGALIZO

a) Wengine wanasema si iazima kwa askofu awe amehitimu ngazi hizi. Maneno yao yanaonekana
kuwa ni kweli kwa mawazo yao. Lakini tujue kwamba iwapo ingekuwa hivyo Roho Mtakatifu
asingekuwa na sababu ya kumworigoza Paulo kuiagiza amri hii.

b) Wengine wamesema ni vigumu kumpata mtu anayeweza kuhitimu mambo hayo. Hii ni kweli
kwa upande, lakini inaionyesha umuhimu na uzito wa kazi ya askofu. Mungu hatoi amri ambazo
wanadamu hawawezi kuzitii. ikurnbukwe pia kwamba kila Mkristo anapaswa awe na tabia hizo
wala si askofu tu.)

c) Wazee wa kanisa wa mahali fulani ni waangalizi wa kundi lile moja tu. Kwa mfano, wazee wa
kanisa lililopo Temeke hawawezi kutambuliwa kama ni wazee kule Arusha iwapo
wangelitembelea kanisa la Arusha.

D. KAZI ZA MAASKOFU

1) Kuamigalia - "Askofu" maana yake ni "mwangalizi" Kazi ya maaskofu ni kuangalia mahitaji,


usalama, afya, na maendeleo ya kiroho ya kanisa. Wanahakikisha kuwa mambo yote
yatendeke kwa utaratibu (1 Kor. 14:40). Si wajibu wa maaskofu wafanye kazi zote wao
wenyewe tu, bali wanawapangia mashemasi, wahubiri, na Wakristo wengine kazi zao na
kuwaangalia.

2) Kulilisha Kanisa - Neno la Mungu ni chakula safi cha kiroho cha Wakristo. Chakula hiki kisi-
changanywe na cho chote kingine. Baadhi ya Wakristo ni wachanga nao wanahitaji maziwa
tu. Wengine ni watu wazima nao wanahitaji chakula kigumu (Ebr. 5:12-13). Ni kazi ya
maaskofu kuhakikisha kwamba kila Mkristo katika kundi lake apate chakula kile kinachotakiwa
ili akue (Mdo. 20:2, 6). Maaskofu ni waalimu wa neno (1 Tim. 3:2). Wialakini, haina maana
tuwaachie kazi hiyo maaskofu tu, bali wao wawe kama waangalizi wenye kuhakikisha kwamba-

42
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

kundi linapata mafundisho sahihi ya kutosha. Watu wengine wanaweza kusaidiana nao. Kwa
mfano, mhubiri, waalimu, na mashemasi (Efe. 4:11; 1 Pet. 2:1-3; 1 Kor. 12:28; Yak. 3:11).

3) Kuchunga kanisa - Mchungaji anawajibu kuwalinda na kuwatunza kondoo wake. Vivyo hivyo,
maaskofu ni wachungaji wa kundi lao (1 Pet. 5:1-2). Wachungaji wa kanisa wawe tayari kutoa
maisha yao kwa ajili ya kanisa wapigane na waalimu wa uongo na nguvu za Ibilisi (Efe. 4:14;
Mdo. 20:29-30; Tito 1:9-11).

4) Kulitiisha kanisa na kukesha kwa ajili ya roho za washiriki - Maaskofu sio watoa sheria.
bali watambue mahitaji ya kanisa kwa ujumla wakiangalia sana sheria ya Yesu jinsi isemavyo
(1. Tim. 5:17; 1 Pet. 5:2-3; Rum. 16:17; 1Thes. 5:14; 2 Thes. 3:6, 1, 1). Yesu pekee ni kichwa
cha kanisa. Kazi ya maaskofu ni nzito. Wanaweyibika kutoa hesabu kwa roho za kundi lao!
Lazima wamjue kila Mkristo na kushirikiana naye kiroho. (Ebr. 13:17).

E. WAJIBU WA WAKRISTO KWA MAASKOFU

¾ “Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu,
kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana
isingewafaa ninyi” (Ebr. 13:17).

1) Kuwatii wazee - Hii haimaanishi kwamba Mkristo anatakiwa atii kila aamriwacho na
mwanadamu, hasha! bali atii kufuatana na yale yasemwayo katika Biblia. (1Pet. 5:1-3; 1 Kor.
11:1).

2) "Lakini, ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia
ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni; mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao.
Iweni na amani ninyi kwa ninyi" (1 Thes. 5:12-13).

3) Kumbuka jinsi Mungu alivyowakasirikia sana Waisraeli akatoa adhabu kwao hapo
waliposhindwa kumtii Musa (Hes. 16:1-35).

4) Kuwanyenyekea - Inatupasa kuangalia sana hapa. Watu wengine, kwa kukosa kuelewa,
wameanza kuwapigia wazee (maaskofu) magoti. Petro alikataa jambo hili (Mdo. 10:25-26).
Paulo naye alikataa kuabudiwa (Mdo 14:8-18). Hatutaki wazee waabudiwe kama Mungu.
Bali maana yetu ni kuwatambua kuwa ni wazee wetu na kuwaonyesha heshima katika
Bwana. Tusingewadharau (1 Tim. 5:1; Tito 3:1; 1Tim. 5:17-19)

5) Mashemasi wako chini ya uwangalizi wa wazee waifanye kazi ya utumishi wa kanisa.

6) Wahubiri na Wamishenari nao wanawajibika kuwasikiliza wazee wa kanisa!

F. UCHAGUZI WA WAZEE

a) Lazima wawepo watu wawili au zaidi waliohitimu ngazi za askofu kabla ya kuwaweka maaskofu
katikakanisa. Maana, kanisa haliwezi kuwa na askofu mmoja tu (Tit. 1:5).

b) Watu wote ambao wametimiza ngazi zile za askofu wangewekwa wawe maaskofu. Wingi wa
maaskofu ni baraka kwa kanisa (Mit. 11:14).

43
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

c) Nani achague wazee wa kanisa? Katika maandiko hatujaelezwa ni nani awachague. Ingawaje
katika (Tito. 1:5) Paulo alimwagiza Tito kuweka wazee kila mji. Si kwamba alimwambia
awachague bali kuwaweka katika kanisa.

d) Katika (Mdo. 6:2-3) tunaona masherrasi wanavyochaguliwa na kanisa. Maaskofu nao


wangechaguliwa kwa njia hiyo pia (Mdo. 14:23). Maaskofu wasichaguliwe kwa sababu ya
kabila zao na kadhalika. Wote ambao wamehitirnu ngazi za uaskofu wanahitajika kuwa
maaskofu. Kazi ya kanisa ni kuwatambua na kuwaweka kanisani.

G. KANISA NA MASHEMASI

ƒ MAANA YA NEMO SHEMASI.

1) Neno SHEMASI maana yake ni MTUMISHI (1 Tim. 3:8-13)

2) Neno hili limetumika katika njia mbalimbali lakini kila mara linapotumiwa huonyesha kuwa
mtumishi ni mtu anayejishugulisha kwa faida ya mtu mwingine.

3) Katika (Mt. 22:13; Yn. 2:5) neno hili limetumika kwa ajili ya watumishi wa nyumbani. Wapo
watumislhi wa serikali vile vile (Rum.13:4). Pia kuna watumishi wa Shetani (2 Kor. 11:15) , na
yeyote atakayetumika chini ya mwingine ni shemasi.

4) Mashemasi wa kanisa ni watumishi wanaosaidia Wakristo wenzao (Mdo. 6:1-7). Lakini


shemasi hawezi kushika kazi hii mpaka atimize sifa au ngazi ya kazi yake.

H. SIFA ZA MTU KUSHIKA KAZI YA SHEMASI – (Soma 1Tim. 3:8-1 3; Mdo. 6:3).

1) Awe mstahivu - mwenye heshima ya kujiheshimu mwenyewe pamoja na wengine.

2) Asiwe mwenye kauli mbili - Asiwe kigeugeu. Leo asene hili kesho lile.

3) Asiwe mwenye kutamani fedha - Asipende fedha kuliko kazi yake (Mdo. 20:33-35; 1 Tim.
6:10).

4) Asiwe mwenye kutumia mvinyo sana - Asiwe mlevi.

5) Awe mwenye dhamiri (njema) safi - Yaani mwenye nia au mawazo mema juu ya nafsi yake
na anaowatumikia.

6) Awe amejaribiwa kwanza - Hii haina maana kwamba apewe mtihani wa kujibu. Bali aonekane
kama kweli anazo sifa zote za shemasi.

ƒ Ni nani mwenye kumjaribu? - Kanisa kwa ujumla ndilo liwajaribu (Mdo. 6:2-3). Kanisa
liliwachague kutokana na sifa zao.

7) Mume wa mke mmoja - Shemasi awe ni mume wa mke mmoja.

44
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

8) Awe mwenye kusimamia nyumba yake vema - yaani kuiweka nyumba yake katika heshima
na kicho cha Bwana (Tito 1:6; Efe. 6:1-4).

9) Awe mwenye sifa njema

10) Awe amejawa na Roho Mtakatifu (GaL 5:22-23).

11) Wake za mashemasi nao wanahitajika kuwa na sifa:

- Wawe wastahivu.

- Wasiwe wasengenyaji,

- Wenye kiasi.

- Wawe waaminifu katika mambo yote.

I. MASHEMASI WA KIKE?

a) Fibi aliitwa kuwa "mhudumu" wa kanisa katika Kenkrea (Rum. 16:1). Wengine wamefikiri
kwamba mwanamke anaweza kuwa shemasi wa kanisa.

ƒ Lakini (1Tim. 3:12) panasema kwamba shemasi lazima awe na mke mmoja na awe
mwenye kusimamia nyumba yake vema. Hivyo kwa maneno hayo tunapata kuthibitisha ya
kuwa mashemasi wa kanisa ni wanaume.

b) Kila Mkristo anatakiwa awe mhudumu wa kanisa akitumia uwezo wake wote (Rum. 16:3, 6, 12;
Flp. 4:2, 3). Walakini, Mkristo asiitwe "shemasi wa kanisa" isipokuwa amehitimu ngazi za
shemasi. Fibi aiijitoa kusaidia kanisa walakini hakupewa cheo cha "ushemasi" kama wale
wanaotajwa katika (1 Tim. 3.8-13).

J. KAZI YA SHEMASI KATIKA KANISA

1) Uhusiano wao na wazee

a) Utumishi wa askofu ni mkubwa na mzito kuliko wa shemasi. Hivyo basi kwa kawaida
mashemasi huwa chini ya wazee. Katika Biblia hatusikii habari ya kuwapo kwa mashemasi
isipokuwa wamekuwapo wazee pia (Fil. 1:1)

b) Wazee wakilisha kanisa kiroho, mashemasi wanalilisha kimwili, yaani kuliangalia kundi katika
mahitaji ya kimwili. Kwa njia hii wazee na mashemasi lazima washirikiane katika kuangalia
kundi waone jinsi gani wanaweza kuwasaidia wahitaji (Mdo. 11:27-30).

c) Kuhusu wajibu wao katika kanisa tumeona mfano wa kanisa la kwanza pale Yerusalemu (Mdo.
6:1-7).

45
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

2) Utumishi wao kwa kanisa

a) Kuwasaidia wajane wa kanisa (Mdo. 6:1-7) Lakini, si kila mjane ambaye anaweza kupewa
msaada wa kanisa (1 Tim. 5:3-16; 2:8-15).

b) Kuwasaidia Wakristo wengine wenye shida ya kimwili (Mdo. 4:32-37; 11:27-30).

c) Mara nyingi mashemasi husaidia kuangalia usafi wa jengo, hununua vifaa (karna mvinyo, fagio,
n.k.) na huangalia mambo mengine ya kimwili ya kanisa.

d) Mashemasi hufanya kazi zote za kawaida za Wakristo pia; kama kuhubiri, kufundisha na
kadhaiika. Stefano na Filipo waliochaguliwa kuwa mashemasi na waliendelea kuhubiri pia
(Mdo. 6:8-10; 8:5, 6).

3) Mashemasi wamsaidie nani fedha ya kanisa?

a) Ni amri ya Mungu kwa kila Mkristo kutoa changizo kila siku ya kwanza ya juma (1 Kor. 16:1-2).
changizo hii hutolewa kwa madhumuni mbalimbali.

i. Kusaidia wenye shida mbalimbali kwa mfano: wenye njaa, wajane, na maafa mbalimbali ya
kimwili (Yak. 1:27; 1Tim. 5:1-16).

ii. Kufanya kazi ya kuhubiri Injili sehemu mbalimbali (Mdo. 11:1-16; 1 Kor. 9:7-18).

ƒ Tutaongea zaidi kuhusu fedha ya kanisa mbeleni.

b) Watumishi (mashemasi) waangalie sana jinsi ya kutumia au kugawa fedha hii kwa wahitaji.

c) Wasiitoe kwa kila mtu anayeomba (2 The. 3:6-14; 1The. 4:11-12; 1Tim. 5:16).

d) Wasiitoe kwa upendeleo. Kanisa linaweza kusaidia mtu yeyote, hata mtu asiye Mkristo
maadamu ionekane kuwa kweli anastahili msaada (Gal. 6:10)

KANISA NA WAHUBIRI
A. KUMFATA MHUBIRI

a) Tunaona mpango wa Mungu wa kuokoa na kuwajenga watu ni kwa njia ya kuhubiri neno lake
(1 Kor. 1:21: Rum. 1:16; 10:13-15).

ƒ Ni wajibu wa kanisa kuwafundisha na kuwasaidia Wakristo ili waweze kuhubiri (2 Tim. 2:2).

ƒ Kila Mkristo ana wajibu wa kuwafundisha wengine (Mt. 28:18-20; Ebr. 5:12).

b) Kwa kuwa uwezo na mafanikio ya kueneza injili yanatofautiana kati ya mtu na mtu, watu
wanaofaulu sana katika kueneza Injili wangehimizwa wajitoe zaidi katika kazi hiyo.

46
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

c) Kuhubiri kwa zamu - Wakristo wanaweza kuhubiri kanisani kwa zamu, tunaona mpango huu
una faida zake na upungufu wake.

ƒ Faida moja ni kwamba unasaidia kuwapa nafasi watu wengi wapate kujizoeza kazi ya
kutunga na kuhubiri.

ƒ Faida nyingine ni kwamba unasaidi kanisa kutambua uwezo wa wahubiri wake katika
kutunga na kuhubiri.

e) Walakini, kuna hasara pia.

ƒ Hasara moja wapo ni kwamba hutokea hao wanaohubiri kutofuata taratibu maalum. Hivyo,
wanahubiri zaidi mambo mawili matatu tu kila mara na kuyaacha mengi yanayohitajiwa na
kundi. Kama vile wanadamu wanavyohitaji chakula cha aina mbalimbali kusudi wawe na
afya, vivyo hivyo roho zao zinahitaji kulishwa vyakula mbalimbali vya kiroho (Mdo. 20:26-
27).

- Basi, ikiwa kanisa litafuata mpango huo wa kuwatumia watu wengi, wazee wa kanisa
(au wanaume wa kanisa lile lisilo na wazee) wangekuwa na taratibu kuhakikisha
kwamba maneno yote ya Mungu yahubiriwe. Isitoshe! wasingekubali mtu ahubiri
ambaye anafundisha uongo au ambaye anashindwa kuhubiri somo linaloeleweka.

- Twasoma "... msipotoa kwa ulimi neno lililo dhahiri, neno lile linenwalo litajulikanaje?
Maana mtakuwa mkinena hewani tu ... katika kanisa napenda kunena maneno matano
kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, zaidi ya kunena kumi elfu kwa lugha" (1
Kor. 14:9, 19)

- Kazi ya kuhubiri si kwamba mtu aonekane mbele ya watu tu. Kazi yake ni kuwalisha na
kuwajenga kiroho. Ikiwa hawezi kufanya hivyo, basi asingesimama mbele ya kundi!

- Hata wageni wanaohudhuria kanisani wanaweza kujikwaa wakimwona mtu akisirnama


kuhubiri ambaye hana uwezo wa kazi.

f) Mara nyingi, ni bora kwa kanisa limtafute Mkristo mmoja ambaye ana uwezo zaidi awe mhubiri
wao. Mhubiri huyo ataweza kufanya taratibu kuhakikisha kwamba kila neno la Mungu
litahubiriwa wakati wake. Pia, atajishugulisha sana na washiriki ili afahamu vizuri zaidi mahitaji
yao ya kiroho. Hivyo, ataweza kuwalisha chakula kinachotakiwa wakati unaowafaa.

g) Lakini, mhubiri huyo naye awe chini ya wazee (au wanaume) wa kanisa. Asijione kuwa ni
mkuu. Awasikilize waliomchagua katika mambo yote mema. Walakini, asijipendekeze machoni
pao kwa kuhubiri mambo wanayotaka yakiwa ni kinyume cha neno la Mungu!

h) Kanisa linapomtafuta mtu atakayefaa awe mhubiri lisisahau kumchunguza mke wake pia.

ƒ Mke wake asipokuwa Mkristo mwaminifu, basi anaweza kuvuruga kazi zake nyingi.

i) Mhubiri na jamii yake wanalisimamia kanisa machoni pa watu, hasa walio nje. Kwa hiyo,
wangekuwa kielelezo katika kila hali ya kiroho na kimwili pia.

47
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

B. KUMWANGALIA MHUBIRI.

a) Ni wajibu wa kanisa kumwangalia mhubiri. Pengine, mhubiri anaweza kujitegemea mwenyewe


kama vile Paulo alivyofanya (1 Kor. 4:12). Walakini, mara nyingine atahitaji msaada wa
chakula na kadhalika kusudi ajitoe zaidi katika kazi ya Mungu (1 Kor. 9:14).

b) Kanisa limwangalie yule anayestahili kupata riziki kwa kanisa! Ikiwa kanisa halina uwezo wa
kumpa riziki yote, basi kabla hajaanza kazi wangeelewana naye kwamba ataishije. Huenda
watapatena kwamba anaweza kuwa na shamba au kazi nyingine za kimwili. Kama ni hivyo,
wangekubaliana kwamba anaweza kutumia muda gani katika kazi hizo. Isiwe anapata msaada
wa kanisa bila kufanya kazi ya kanisa! (2 The. 3:10).

c) Iwapo kanisa lina mali fulani (kwa mfano: gari, baisikeli, vitabu, nyumba, n.k.) ambayo
linamkabidhi mhubiri huyu, basi lihakikishe kwamba ameelewa masharti ya matumizi yake.
Baadhi ya wahubiri wanafanya mali ya kanisa kuwa kama ni mali yao binafsi. Wanajiona huru
kuiuza au kuiharibu jinsi wanavyotaka. Basi mhubiri akumbushwe kuwa yeye ni wakili wa
mali ile na kwamba wajibu wake ni kuitunza na kuilinda vyema (1 Kor. 4:2).

d) Wakristo wasiwaze kwamba, kwa sababu mhubiri anapata riziki kutoka kwa kanisa, basi ni
wajibu wake kumpokea na kumwagaiia kila mgeni wa kanisa. Huu ni mzigo mkubwa mno kwa
mhubiri. Mara nyingi atakuwa hana uwezo wa kuwakaribisha wageni wote.

e) Kanisa likitaka mhubiri awakaribishe wageni, basi na limpe fungu la kutosha kazi hiyo! Isitoshe,
mara nyingi ni Wakristo wenyewe wanaomjia saa ya kula chakula kusudi walishwa naye!
Tendo hili ni la aibu! Wakristo wakiwa na shida basi, waliambie kanisa ili lipate kuwasaidia
iwapo Iitaona wanastahili. Maana ndiyo sababu mojawapo kwamba changizo inatolewa.
Tusifanye kazi ile iliyo ya kanisa zima kuwa ni kazi ya mhubiri tu, Mikono mingi hufanya kazi
kuwa rahisi. Lakini kumwisha mtu (mhubiri) mmoja tu kazi zote, atalemewa.

f) Wakristo wasisahau kumjenga mhubiri wao kwa maneno na materido pia. Walakini
wasingezoea kumtembelea mhubiri kila mara bila sababu. Kumbuka kwamba kazi yake muda
mwingi itakuwa ni kusoma Biblia, kuandaa masomo mbali mbali, kuwafundisha na kuwajenga
watu, na kadhalika. Basi, hataweza kutimiza wajibu wake ikiwa Wakristo watakuwa
wanapoteza muda wake.

g) Wakristo wamhimize mhubiri awe msomaji wa neno siku zote. Anapolegea kusoma neno
akijivuna kwamba hana haja kusoma huyo hafai kuwa mhubiri. Maana atawezaje kuwalisha
wengine ikiwa hajilishi mwenyewe? Anapasa awe kielelezo katika kusoma!

h) Wakristo wamhimize mhubiri awe safi katika mambo ya kiroho na kimwili pia. Mhubiri
analisimamia kanisa machoni pa watu. Anaweza kuharibu heshima ya kanisa zima kwa kukosa
usafi (1Tim 4:12; 2 Kor. 7:1-2)

i) Wakristo wamhimize mhubiri asiwe mtu atumiaye siasa katika kanisa kusudi watu wafanye
anavyotaka yeye. Akumbushwe kazi yake ni kuhubiri neno la Mungu na kuwahimiza Wakristo
wafanye yaliyo haki. Akifanya hivyo, hatokuwa na sababu ya kutumia siasa.

48
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

j) Wakristo wasimsengenye mhubiri. Iwapo amekosa, basi wamwonye wakifuata taratibu wa Yesu
jinsi alivyosema:-

ƒ “Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia,
umempata nduguyo. La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wnwili, ili
kwa viywa vya mashahidi wawili au watalu kila neno lithibitike. Na asipowasikiliza wao,
liambie kanisa, na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza
ushuru" (Mt 18:15-17).

C. KUMWONDOA MHUBIRI KATIKA HUDUMA

a) Mhubiri ni mtumishi wa kanisa. Kazi yake ni kuwajenga Wakristo na kuokoa roho za watu kwa
kulifundisha neno Ia Mungu

b) Mhubiri anayeshindwa kutimiza wajibu wake ahimizwe sana na Wakristo kwa upendo mwingi.
Walakini akiendelea katika makosa yake, basi na aoodolewe katika huduma kabla hajaliharibu
kanisa!

c) Mhubiri mlegevu na mvivu ni hatari kubwa sana kwa kanisa.

d) Maana mara nyingi mhubiri anapaswa awe sauti ya kutosha na muonekano wa kiungwana zaidi
kuliko wengine katika kanisa. Ni vigumu sana Wakristo wawe wakamilifu ikiwa mhubiri
mwenyewe hatimizi wajibu wake.

e) Kumwondoa mhubiri katika huduma kunatakiwa iwapo ameshindwa kufanya kazi zake kama
inavyotakiwa au akithibitika kuanguaka katika dhambi naye hataki kutubu. Hata hivyo,
asitendewe kama ni adui bali kama ndugu mpendwa kusudi asipotee roho yake!

f) Ni wajibu wa nani kumwondoa mhubiri katika huduma? - Katika kanisa linalokuwa na wazee
(maaskofu) ni wajibu wa wale wazee kumwondoa. Walakini, mikusanyiko mingi haina wazee
(kwa sababu mbali mbali, ikiwemo kukosekana kwa mtu mwe sifa katika huduma hiyo). Basi,
katika makanisa hayo itakuwa wajibu wa wanaume wa kanisa kukaa kikao na kujadili katika
upendo umuhimu wa kumwondoa na taratibu ya kufuata.

D. NAMNA YA KUMWONDOA MHUBIRI KATIKA HUDUMA

a) Jambo lililo muhimu zaidi ni kukumbuka kwamba mhubiri ni ndugu mpendwa, hivyo,
tusimfanyie jambo lolote kwa jazba au moyo mbaya, asije akaanguka kabisa na kurudi nyuma.

ƒ Anaweza kuondolewa katika huduma, lakini aokolewe roho yake! Kwa maana ya kufanya
aweze kutambua kosa lake na kutubu.

b) Kwa wastani, asingeondolewa bila kuonywa kwanza makosa yake na kupewa nafasi ya
kujirekebisha na ikiwa atashindwa kujirekebisha baada ya muda wa kutosha, basi na
aondolewe kwa faida ya kanisa.

49
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

c) Jitihada katika kutokumkwaza zaidi, walakini asiogope kuondolewa iwapo analiharibu kanisa.
Ni bora ajikwae mmoja kuliko kuliharibu kanisa zima!

d) Upendo kwake ni jambo la msingi pia. Pengine atahitaji muda fulani wa kutafuta shughuli
nyingine ya kujipatia kipato ikiwa alilitegema kanisa hapo mwanzo. Kanisa linaweza kuendelea
kumsaidia kwa muda wakati akiendelea kutafuta namna nyingine ya kujipatia kipato.

E. ANGALIZO

a) Mhubiri aliyeondolewa katika hudauma asiendelee kusimama mbele ya kanisa kuhubiri.

ƒ Kuna uwezekanao akaanguka katika dhambi ya kujaribu kulipiza kisasi kwa kuhubiri
yasiyofaa mbele ya kundi na kulikwaza kundi.

ƒ Lakini ni hatari pia kwa wageni watakaokuwa wametembelea kanisa kwa siku hiyo,
tukumbuke mhubiri huchua dhamana ya kanisa lote, lolote alifanyalo liwe zuri au baya
hurudisha sifa kwa kanisa

ƒ Kwa kutumia ujuzi wa neno anaweza kujaribu kuwavuta watu wengine waandarnane nae
kusudi waliharibu kanisa.

b) Ikiwa mhubiri hapati msaada kutoka kwa kundi lile analolihubiri, basi washiriki wasiseme
kwamba hawawezi kumwondoa. Wajibu wao ni kumwonyesha makosa yake na kumhirniza
ajirekebishe. Asipowasikiliza, basi wawaambie wale wanaotoa msaada au udhamini wa
mhubiri huyo na kuwashauri maamuzi yaliyofikiwa ya kumtoa katika huduma na kwamba
hastahili kupata pato lolote kutokana na huduma aliyokuwa akiifanya.

F. AGIZO KWA MHUBIRI ANAYEACHA HUDUMA

a) Mhubiri akiombwa na kanisa aache huduma yake, basi aonyeshe moyo wa upole na upendo.
Hata ikiwa ataondolewa katika huduma isivyostahili kwa ujanja wa watu wabaya, lakini
asikasirike na kutaka kulipiza kisasi.

ƒ Mhubiri na akumbuke ni kazi ya Mungu kulipiza kisasi wala si kazi yetu (Ebr. 10:30)!
Akumbuke kwamba akifanya lolote kuliharibu kanisa au mali yake, basi amemtendea hivyo
Yesu mwenyewe! (Mt. 25:41-46; Mdo. 9:5).

b) Mhubiri akumbuke hata katika kuondoka kwake katika huduma, anapaswa awe kielelezo kwa
watu wote kutenda mema ! Akifanya hivyo, bila shaka atampendeza Mungu!

KANISA NA WAMISHENARI
A. WAMISHENARI NI WAKINA NANI?

ƒ "Mmishenari" ni neno linalopatikana kutoka neno "missionary" katika lugha ya Kiingereza


ambalo maana yake ni mtu aliyepelekwa atimize shughuli fulani.

50
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

a) Katika kanisa wamishenari ni watu waliotumwa na kundi fulani la kanisa wafanye kazi maalumu
iliyokusudiwa na lile kundi. Katika Biblia watu hawa waliitwa "mitume wa kanisa" (2 Kor 8:23;
Rum. 16:7; Mdo. 14:14). Lakini, kwa wastani, tunawaita watu hawa "wamishenari" kusudi watu
wasielewe vibaya wakidhani kwamba tunao mitume wa Yesu leo. (Kumbuka tuliongea kuhusu
mitume wa Yesu katika somo la 3 liitwalo Matendo ya Mitume)

b) Hata ingawa tumezoea kuwaona wamishenari wengi wazungu, walakini mmishenari anaweza
kuwa mtu wa kabila lo lote. Ingefaa kila kundi la kanisa lenye uwezo limtume mmishenari
ahubiri (Mt. 28:18-20; Rum. 10:13-15)

c) Basi, mara nyingi kanisa linaweza kuarnua kumtuma mtu imahali pasipokuwa na kanisa kusudi
ahubiri na kulianzisha kanisa huko.

d) Baada ya kuanzisha kanisa, matatizo yanaweza kutokea kwa sababu wenyeji hawaelewi
uhusiano uliopo kati yao na mmishenari. Mara nyingi wanakosa kuelewana hasa kuhusu
mamlaka ya mmishenari na misaada ya kanisa.

B. MAMLAKA YA MMISHINARI

1) Katika mambo ya kiroho, mmishenari hana mamlaka isipokuwa kufundisha neno la Mungu tu.

ƒ Kwa wastani, mmishenari ni Mkristo ambaye amelisoma na kulielewa neno la Mungu vizuri
kusudi aweze kuwafundisha watu wengine. Walakini, mmishenari ni mwanadamu tu naye
anaweza kukosa katika maneno yake na matendo yake pia.

ƒ Kwa hiyo, ni wajibu wa watu vvanaomsikiliza mmishenari wahakikishe kila neno


analolisema kwa kusoma Biblia (Mdo. 17:11; Mt. 15:14; Yn. 8:32; 17:17)

2) Mmishenari ana wajibu mkubwa sana awe kielelezo katika mambo yote kwa sababu, katika
mawazo ya watu wengi, amesimama badala ya Yesu mwenyewe.

3) Walakini Wakristo wakumbuka daima kwamba mmishenari si mwokozi bali ni mwanadamu


mkosefu sawasawa na wao wenyewe na kwa hiyo imani yao iwe katika Bwana Yesu, wala si
katika mwanadamu awaye yote.

ƒ Hata ikiwa mmishenari atapatikana katika dhambi kubwa, wasipoteze imani yao na roho
zao kwa sababu yake.

4) Katika mambo ya kimwili, huenda mmishenari anaweza kuwa na mamlaka fulani, Kwa mfano,
iwapo kanisa lililomtuma wamemkabidhi fedha au mali ili afanye kazi maalum, basi yeye ni
wakili wao. Ni wajibu wake kuangalia matumizi ya fedha au mali ile kusudi itumike walivyotaka
wenye kumkabidhi.

5) Kwa mfano, mmishenari akitumwa ajenge jengo la kanisa, basi ni wajibu wake kutunza na
kutumia kwa haki fedha na vifaa vyote.

ƒ Katika hilo tunaona ni wazi atakuwa na mamlaka (kama wakili) kufanya lolote analoliona
kuwa ni vyema akikumbuka kwamba lazima atoe wajibu kwa waliomtuma.

51
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

6) Bahati mbaya, mara nyingine wakristo ambao wanajengewa jengo, wanajiona kuwa wana
mamlaka juu ya fedha, vifaa, na kazi. Wanaweza kunung'unika na kumhangaisha mmishenari
sana.

ƒ Wanapaswa kumbuka kuwa, hata ingawa jengo linajengwa kwa ajili yao, walakini
halitakuwa mali yao mpaka watakapokabidhiwa na wale wanaolijenga.

ƒ Kwa kweli, ni jambo la busara kwa mmishenari ikiwezekana awasikilize mawazo wa


Wakristo wenyeji. Maana, wanaweza kuwa na shauri nzuri linalofaa sana. Hata hivyo,
wajibu wake ni kwa wale waliomtuma!

7) Ikitokea wenyeji wakiwa na mashaka kwamba fedha haitumiki kihalali, basi wanaweza kuandika
kwa kanisa linalotoa msaada kuwaeleza mashaka yao. Ndipo itakuwa wajibu wa kanisa lile
kumwuliza mmishenari wao atoe jibu kwao. (Kwa wastani, kanisa lilitomtuma litakuwa
limekwisha kujua mengi. Maana, kwa kawaida, mmishenari atakuwa akitoa hesabu ya
matuimizi ya fedha kila mwezi kusudi wajue analolifanya.)

8) Wakristo wanaotoa msaada wa jengo wasingependa kusikia baadaye kwamba wale


wanaosali mle wameiacha imani ile waliyofundishwa na wenye kulijenga jengo. Kwa hiyo,
wanaweza kuweka masharti kwamba wanalikabidhi lile jengo litumiwe mradi au maadam
Wakristo watakuwa waaminifu kufuata Biblia. Inawezekana watampa mmishenari wajibu wa
kuliangalia jengo kuhakikisha kwamba litatumiwa kwa kazi ya Mungu tu na kwamba Wakristo
wasingeanza kufundisha uongo.

9) Msaada kwa wahubiri wenyeji ukiwapo, huenda mmishenari atakuwa wakili wa kuhakikisha
kuwa wanapokea msaada na kwamba wanastahili kuupata.

10) Misaada ya hospitali, dawa, na kadhalika ikiwapo, mmishenari anaweza kuwa na mamlaka
kuongoza kazi hizo zote mpaka watoaji misaada watakapoamua kuwakabidhi wenyeji uongozi
wa kazi.

11) Mara nyingi mmishenari anaweza kukabidhiwa gari limsaidie katika kazi zake. Basi, anakuwa
na mamlaka kulitumia gari kwa jinsi alivyopatana na walionunua gari. Hata anapomaliza kazi
yake, kabla ya kurudi kwao anaweza kuliuza gari kusudi awarudishie fedha au kusudi itumiwe
kwa kazi nyingine kwa jinsi walivyomwagiza.

C. MISAADA NA WAMISHENARI

1) Mara nyingi kuna kutokuelewana kuhusu misaada inayotoewa na wamishenari.

2) Kanisa la Kristo ni tofauti sana na madhehebu ya watu. Madhehebu wanafanya makadirio na


kuwa-lazimisha washiriki wao watoe.

3) Tena, wanawalazimisha watoe fedha kusudi Padri awabatize, afungishe ndoa, amzike
aliyekufa, awaombee wao au marehemu wao, na kadhalika.

4) Hivyo madhehebu yanapata fedha nyingi. Wakuu wao wanapanga matumizi ya fedha yote ya
madhehebu.

52
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

5) Kusudi wapate washiriki wengi wamezoea kutuma wamishenari wajenge mashule, na hospitali,
na misheni mahali pengi.

6) Wananchi huvutwa sana na mambo hayo kwa kuwa ni huduma zinazowagusa moja kwa moja.
Walakini, wanaambiwa kuwa hawawezi kupata msaada isipokuvva wawe washiriki wa
madhehebu yao. Basi, wengi hujiunga nao kusudi wapate misaada bure, kumbe si bure,
Maana, baada ya kujiunga nao wanalazimishwa watoe fedha ili wapate huduma zile zote
tulizozitaja hapa juu! Wasipotoa, basi hunyimwa msaada wa kanisa.

7) Sivyo ilivyo kanisa la Kristo tumekwisha kujifunza hapo awali jinsi Biblia inavyotufundisha
kuhusu kutoa changizo. (Tutajifunza zaidi kuhusu tatizo la fedha hapo mbele)

8) Kanisa la Kristo haliwalazimishi watu kutoe wala hatuwanunui kwa kuwapa ahadi ya msaada
ikiwa watajiunga na kanisa.

9) Kanisa halina mkuu wa ki-duniani anayepanga matumizi ya fedha na kuwatuma wamishenari ili
wajenge misheni, shule, na hospitali. Bali kila kundi Ia kanisa liko huru kufanya kwa uwezo
wake lile linalompendeza Mungu.

10) Basi, tunawapataje wamishenari na misaada? A. Kwa wastani, wamishenari wanapatikana


kama ifuatavyo:-

a) Kwanza, Mkristo fulani anaguswa na neno la Mungu akisikia hamu ya kupeleka Injili mahali
ambapo halijafika. Anajitoa kujifunza zaidi neno la Mungu na kujiandaa kuondoka kwao.

b) Kisha, akiwa na uwezo wa kujitegemea mwenyewe, atawaaga wenzake na kuondoka


kwao. (Wamishenari wengi wa kanisa la kristo hawapati msaada wa kanisa bali
wanajitegernea wenyewe.) Lakini, ikiwa hana uweizo, basi atawaeleza Wakristo wengine
wanaomfahamu wamsaidie ili aende kuhubiri, wakimwamini kuwa ni Mkristo mwaminifu
huenda watajitoa kumsaidia. Msaada wenyewe hutegemea mahitaji yake na uwezo wao
wanaomsaidia.

c) Wakiona kwarnba kazi yake itahitaji fedha nyingi, na wakiwa na uwezo, huenda watampa
fungu la fedha kwa ajili ya mambo maalumu. (Kwa mfano, kwa ajili ya kuchapa masomo
ya Biblia, au kununua stampu za kutuma masomo kwa njia ya posta, kujenga jingo na
kadhalika).

d) Kwa wastani, misaada ikiwapo, basi inatolewa kwa sababu wamemfahamu na kumwamini
yeye na
kutaka kumsadia katika kuifanya kazi za Mungu. Ikumbukwe kuwa hawajawafahamu bado
watu wale atakaokuwa akiwafundisha. Kwa hiyo, misaada yote itakabidhiwa kwa
mmishenari wanayemfahamu.

e) Mmishenari huyu atakuwa wakili wao na atawajibika kuwafahamisha matumizi ya fedha.


wasiporidhika na matumizi yake, basi wataamua la kufanya. (Ni kawaida kwa
mmishenari ambaye amekabidhiwa misaada kwa ajili ya kazi kwamba atoe hesabu ya
matumizi yake kila mwezi.)

53
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

f) Kwa wastani, akiondoka mmishenari basi msaada unakoma pia. Ikiwa msaada ulikuwapo kwa
sababu yeye aliomba kwa wale waliomfahamu, basi huenda msaada utamfuata huko
astakapokwenda au pengine utakoma. (Si mara nyingi kwamba wanaotoa msaada watamtafuta
mmishenari mwengine ashike kazi ya Yule aliyeondoka.)

g) Pengine kanisa lenyewe litaamua kujitoa kusaidia nchi fulani au mji fulani badala ya kumsaidia
mmishenari tu. Kanisa hili linaweza kutoa msaada wa kudurnu zaidi. Kwani, mmishenari mmoja
akiondoka kazini, basi kanisa litamtafuta mwingine kuchukua nafasi yake. Hivyo msaada
haukomi kwa sababu eti, ameondoka mtu fulani.

h) Tanzania Bible School imeendelea kwa miaka mengi sasa kwa sababu kuasnyiko moja la
Kanisa limejitoa kutafuta fedha na wamishenari ili huduma hii muhimu iendelee.

i) Vivyo hivyo Hospitali ya Chimala inaendetea kwa sababu kusanyikofulani la kanisa limejitoa
kwa ajili yake. Kwa kweli, mpango huu unafaa zaidi. Walakini hatuwezi kulazirnisha
makusanyiko yote ya kanisa yafanye hivyo. Kila kundi liko huru kuamua la kufanya.

j) Kwa kawaida misaada ni ya muda tu. Mzazi yuko radhi kutoa msiaada kwa mtoto wake akiwa
mdogo. Walakini, akisha kuwa mtu mzima, inampasa ajitegemee. Vivyo hivyo, makusanyiko
mengi yako tayari kutoa msaada wa muda kwa kundi la kanisa lililo changa. Walakini, kila kundi
la kanisa lingejitahidi sana kujitegemea lisiwe mzigo kwa Wakristo wengine. Kwa hiyo, hata
msaada wa Tanzania Bible School unaweza kukoma wakati fulani. Basin a kusanyiko husika
litawajibika kupokea kazi hiyo na kuiendeleza!

D. WAJIBU WA MMISHENAIRI KWA WAKRISTO.

1) Kazi kubwa ya mmisheriari ni kuhubiri neno la Mungu ili watu waokolewe. Kwa hiyo, anapaswa
awe kielelezo kwao katika maisha ya utauwa.

2) Atapaswa ajitahidi kujifunza desturi za wenyeji ili asiwakwaze (Rum. 14:14-18; 1 Kor. 9:21-23).

3) Mmishenari asijifanye kuwa mkuu, apaswa amtukuze Yesu na kufundisha neno lake Mungu
akiwahimiza watu walifuate. Ikiwezekana awashirikishe wakristo kazi zote.

4) Ni jambo la busara kwa mmiishenari kusikiliza mawazo na mashauri ya wenyeji. Wanaweza


kumfundisha mengi na kurnsaidia katika kazi zake.

E. WAJIBU WA WAKRISTO KWA MMISHENARI.

1) Wajaribu kuelewa matatizo yanayompata mmishenari.

2) Mmishenari akiwa na gari na nyumba, watu wanaweza kufikiri kwamba ni mali yake
mwenyewe na kwamba anaishi kwa furaha sana.

3) Walakini Wakristo wanapaswa kutambua kwamba yawezekama maisha yake ni ya taabu sana
na pengine gari na nyumba si mali yake ila amekabidhiwa tu kwa muda.

54
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

4) Ikiwa mmishenari ni mzungu, huenda atakuwa akijisumbua sana kujifunza na kuzoea lugha
mpya, sheria na desturi tofauti, chakula tofauti, nyumba tofauti, hali ya hewa tofauti, na
kadhalika.

5) Inawezekana akawa katika hali ya kusikia ukiwa na hamu ya kukumbuka kwake.

6) Pengine anaweza kusumbuliwa na mke wake au watoto wake ambao wamepata ugonjwa
ambao unawalazimu kurudi kwao.

7) Ameacha wazee, ndugu, marafiki, kazi, nyumba, mazingira, desturi, na maisha ya furaha
kusudi awashirikishe watu baraka za Mungu.

8) Haitokuwa jambo la busara kama wale ambao amejitoa kuwasaidia hawamwonyeshi upendo
na kinyume chake kumshitaki kuwa ni mchoyo au kwamba anakula fedha ambazo wanadhani
zimetolewa kwa ajili yao bila kujua ni watu wangapi wanaokuja mara kwa mara kuomba
msaada kwake.

9) Ni fikra potofu kufikiri mmishenari amepewa fungu la fedha kwa ajili yao na si kazi ya Mungu!
Kwa hali hiyo, mmishenari anaweza kusikia huzuni na uchungu kwa sababu hapendi kuitwa
mchoyo wala hapendi kuwanyima watu msaada; walakini hana uwezo kuwasaidia wote.

10) Isitoshe, hata ikiwa angekuwa na fedha kutosha, asingependa kazi ile ya kumhoji sana kila
mtu
anayeomba msaada kusudi ahakikishe kuwa kweli anastahili kupata msaada wake.

11) Ni lazima wakristo watambue hii ni kazi nzitomno inayomchosha sana na kutia aibu kwa
mmishenari na kwa yule ndugu anayeomba pia.

12) Wakristo wanawajibu wa kumsaidia kwa uvumilivu na upendo. Mmishenari anahitaji


kufundishwa na wenyeji desturi zao na taratibu ya jumuiya, hasa akiwa ni mgeni kabisa. Mara
nyingine hutoke kutokuelewana kunatokea kwa sababu mmishenari hakufahamu kuwa neno
fulani alilolitumia lilieleweka vibaya. Kumbe! yeye hana habari kwamba amewaudhi watu. Basi
inawapasa wakristo kumuelekeza kwa upole na upendo.

13) Inawezekana mkristo akaomba msaada kwa mmishenari na mmishenari akamjibu "Nitajaribu
kutoa msaada" ni vizuri ieleweke kuwa mtu asemapo nitajaribu si ahadi ya kwamba atatoa
msaada bali maana yake ni kuonyesha kujali kwake na kwamba msaada wake utategemea
uwezo wake. Na kama akikosa uwezo, basi hatatoa msaada.

14) Ni vuzuri wakristo wakafahamu ya kuwa mmshenari huyu si mdeni kwao bali amejitoa kwa
upendo wake tu. Si jambo jema kwa Wakristo kumdai misaada kana kwamba yeye ni mdeni
kwao. Wanaweza kufikiri kwamba akiwa na gari, basi ni lazima alitumie kama wanavyotaka
wao. Na Pengine mmishenari amelinunua gari kwa fedha zake mwenyewe. Lakini, hata ikiwa
limenunuliwa kwa fedha ya waliomtuma, haina maana kwamba ni lazima apoteze muda wake
na petroli yake kuwapeleka watu huko na huko. Ni vuziri ifahamike ya kwa hawezi kumsaidia
kila mtu katika kusanyiko! Basi, Mkristo akiwa na tatizo na aombe msaada walakini asijikwae
akikataliwa.

55
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

15) Si jambo jema kusengenya, bali wamwonye ikiwa amekosa. Yesu alisema, "Na ndugu yako
akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu akikusikia, umempata nduguyo.
La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya
mashahidi wawili au watatu kila neno lithihitike. Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa, na
asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru" (Mt. 18:15-
17).

16) Mmishenari ni Mkristo tu na angetendewa sawasawa na wengine. Ni dhambi kwa Mkristo


kumsengenya au kumchongea mtu ye yote. Inaharibu sifa za Yesu na kanisa lake kwa mtu
kumaziri mzee, mhubiri, mnishenari, au Mkristo ye yote anayelisimamia kanisa. Soma kwa
makiini sana (1 Kor. 6: 1-8).

WANAWAKE KATIKA KANISA


A. THAMANI YA WANAWAKE

1) Kimsingi roho ya mwanamke ina thamani sawasawa na roho ya mwanamume. "Maana ninyi
nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana
mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja
katika Kristo Yesu" (Gal. 3:27-28).

2) Mke mwema ana thamani kuliko marijani (Mit. 31:10-31).

B. KAZI YA WANAWAKE KATIKA KANISA

1) Hata ingawa roho ya mwanamke ina thamani sawasawa na mwanamume, walakini kazi ya
mwanamke katika kanisa ni tofauti na kazi ya mwanamume. Haina maana kwamba Mungu
ana upendeleo. La! bali kuna ngazi au sifa fulani zinazotakiwa mtu awe nazo kusudi aweze
kufanya kazi mbalimbali za Mungu.

2) Mwanamke hawezi kuwa askofu wala shemasi kwa sababu hawezi kuhitimu sifa za kazi hizo
(1Tim. 3-13; Tit. 1:5-9). Walakini, si wanawake tu bali hata wanaume wengi nao hawawezi
kuhitimu sifa za shemasi wala askofu.

3) Mwanamke hawezi kuwa mhubiri kanisani.

ƒ "Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena; bali watii, kama
vile inenavyo torati nayo. Nao wakitaka kujifunza neno lolote, na wawaulize waume zao
wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa" (1 Kor. 14:34-
35).

ƒ "Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. Simpi mwanamke ruhusa ya
kufundisha wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu" (1 Tim. 2:11-12).

4) Mwanamke anaweza kufundisha wanawake wenzake. Twasoma:-

56
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

ƒ "Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji,


wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema; ili wawatie wanawake vijana
akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao; na kuwa wenye kiasi, kuwa safi,
kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu
lisitukanwe" (Tit. 2:3-5).

5) Mwanamke anaweza kuwafundisha watoto (2 Tim. 1:4-5; 3:14-15).

6) Mwanamke anaweza kumsaidia mume we kufundisha watu wazima wa kike na wa kiume


(Mdo. 18:26; Rum. 16:3-4).

7) Mwanamke anaweza kulihudumia kanisa (Mdo. 9:36-39; Rum. 16:1-21)

8) Mafundisho mengine kuhusu wanawake kanisani yanapatikana katika (1Tim. 2:9-15; 1Pet.
3:1-6; 1Tim 5:3-16; Efe. 5:22-24; 1Tim. 3:11).

MATATIZO KATIKA KANISA


A. TATIZO LIHUSULO FEDHA

a) Mawazo ya kimadhehehu - Wakristo wengi wamezoea matendo ya madhehebu na, kwa hiyo,
hawaelewi mpango wa Mungu kwa kanisa kuhusu kupata na kutumia fedha.

1) Madhehebu yana fedha nyingi kwa sababu mbalimbali. Kwa mfano: (1) wanafanya
makeidilio na kuwalazimisha washiriki wao watoe kiasi fulani; (2) tena, wanawalazimisha
watoe fedha ili wawape huduma kama kubatizwa, kufunga ndoa, kumzika aliye kufa,
waombewe msamaha wa dhambi, n.k.;

2) (3) wanaweka maduka na mashamba ya kanisa; (4) wanatumia michezo ya fedha, n.k.
Mambo hayo yote ni kinyume cha mafundisho ya Biblia. Kwa sababu madhehebu
yamekuwa na fedha nyingi yamejenga mashule na mahospital kwa kusudi la kuwavuta
wawavute watu. Watu ambao wamezoea mambo hayo wanaweza kudhani kwamba ni
wajibu wa kanisa liwe nayo. Wanauiiza kwamba "Ni kanisa gani lisilo na misaada?"

3) Walakini, tunaona kazi ya kwanza ya kanisa ni kuhubiri neno la Mungu ili watu waokoke.
Yesu mwenyewe hakuwasaidia wagonjwa wote (Lk. 4:23-30).

4) Katika Agano Jipya hatuwezi kusoma habari ya shule au hospitali ya kanisa, ingawa, kanisa
linaweza kutoa misaada ya tiba na elimu au dawakwa jamii likiwa na uwezo, walakini, si
wajibu wake!

5) Wakristo wasifuate dini kwa ajili ya misaada ya kimwili tu ( Yn. 6:26-27)! Tutafute ukweli!

b) Ukosefu wa fedha - Kazi nyingi za Mungu haziwezi kuendelea pasipo fedha. Yesu na
wanafunzi wake walikuwa na mfuko wa fedha (Yn.12:3-6). Mafundisho zaidi yanatakiwa
kuhusu changizo kusudi tumpendeze Mungu na kuitimiliza kazi yake.

57
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

1) Mara nyingi kuna ukosefu wa fedha kwa sababu watu wameelewa vibaya maneno ya Mungu
katika (2 Kor. 9:7). Hapo twasoma, "Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si
kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa
ukunjufu".

2) Bahati mbaya, baadhi ya Wakristo hudhani maneno hayo yaana maana kwamba si lazima
kutoa. Kwa hiyo, watu wenye choyo hawatoi kama inavyowapasa. Ebu, tuone kwamba
Mungu aliweza kuwa na maana gani alipossema mtu asitoe kwa lazima.

ƒ "Si kwa lazima" maana yake nini? Mkristo atoe kwa moyo safi Mungu hakubali kupokea
kitolewacho na mtu mwenye choyo (Mal 1:6-14). Kwa hiyo, mtu akitoa kwa sababu
amelazimishwa tu wala si kwa moyo, basi haimsaidii kitu. Kutoa kunatakiwa, ila tutoe kwa
moyo!

ƒ Tusifanye kama madhehebu wanavyofanya - Madhehebu wanafanya makadirio ya


mwaka na kuwalazimisha washiriki wao watoe. Sivyo, basi wanawanyima huduma za mbali
mbali. Kanisa halipaswi kumlazimisha mtu atoe hivyo.

3) Ni lazima Mkristo atoe – hebu tuone sababu mbali mbali.

i. Upendo unatulazimisha tutoe - Ukimpenda mtu itakuwa vigumu kumnyima. Tu-


napokumbuka upendo wa Yesu kwetu, twatambua kuwa kile tunachokitoa sisi hakilingani
na yale aliyotutendea. Hebu! Jaribu waza Yesu annefanya nini kwa ajili yako, Alijifanya
mtumishi wa wanadamu (Mt. 20:28; 2 Kor. 8:9). Ametoa maisha yake (Yn. 3:16). Je!
tumnyime yeye aliyetupenda hivyo?

ii. Tafakari ni wa ngapi wamepotea dhambini kwa kukosa mhubiri (Rum. 10:13-16). Kama
kweli tuna upendo kwa wengine, ni wajibu wangu na wako tutoe ili tutume watu waende
kuhubiri huko na huko. Tafakari pia ni wajane wangapi na maskini, wafungwa, wagonjwa,
n.k. ambao wamekosa huduma zetu kwa sababu hatujatoa (Mt. 25:31-46).

iii. Tumeamriwa kutoa kwa moyo (upendo) (2 Kor. 9:7). Kutoa kwa moyo nizaidi ya hiiyari.
Tusitoe eti! kwa sababu ya kuogopa kwenda Jehanamu, au eti! kwa sababu mwinjilisti wetu
ametuhimiza sana kutoa, au kwa sababu ndugu wengine wataniona mimi kuwa sikutoa.
Nitoe kwa jinsi moyo wangu unavyonituma kwa kadri nampenda Yesu na wahitaji.

iv. Tunaposoma (Mt. 5:20) tunaonaambiwa lazima haki ya Mkristo izidi haki ya Mafarisayo
(Wayahudi)

ƒ Mafarisayo walitoa zaka (sehernu ya kumi) ya pato lao lote (Kum. 14:22-27; 12:17;
Hes. 18:21-29).

v. Mbali na zaka (sehemu ya kumi) ya pato, Wayahudi walitoa mazao ya kwanza (Kut. 23:16,
19). na matoleo mengine mengi, hebu tuyaone:-

ƒ Matoleo ya nadhiri na sadaka za hiari (Law. 22:18),

ƒ Sadaka za dhambi (Law. 4:1-35).

ƒ Sadaka ya unga (Law. 2:1-16).

58
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

ƒ Sadaka za amani (Law. 3:1-17),

ƒ Sadaka za hatia (Law. 5:1-19)

ƒ Pamoja na hizo, waliamriwa wawaachie maskini na mgeni mazao ya pembe za


mashamba yao na matunda yaliyopukutika (Law. 19:9-10).

vi. Kwa mifano hiyo tumeona, Myahudi halisi alikuwa akitoa zaidi ya sehemu ya kumi ya wala
si sehemu ya 10 tu!

vii. Basi ikiwa haki ya mkristo inapaswa izidi ya mafarisayo (wayahudi) (Mt. 5:20), Mkristo
anatatakiwa atoae zaidi ya sehemu ya 10 ya pato lake ili haki yake izidi ile ya Mafarisayo.

viii. Soma kwa makini (2 Kor. 9:6-15)

ƒ Mkristo akitaka kuvuna kwa ukarimu baraka za Mungu lazima atoe kwa ukarimu
(2 Kor. 9:6).

ƒ Mkristo akitaka Mungu ampende lazima atoe kwa moyo wa ukunjufu (2 Kor. 9:7)

ƒ Mkristo akitaka utajiri kwa Mungu lazima awe mkarimu (2 Kor. 9:11). Soma pia (2 Kor.
9:13-15).

ix. Ni lazima kila Mkristo atoe kwa jinsi alivyofanikiwa na Mungu (1 Kor. 16:2)

ƒ MAONYO:

1) Mungu anasema tunamwibia tusipotoa kwa jinsi tulivyofanikiwa (Mal. 3:8-10).

2) Mungu aliwaua Wakristo wawili waliotaka kudanganya katika kutoa changizo. (Mdo. 5:1-11)

3) Tutoe lini? - Katika (1Kor. 16:1-2) tunaambiwa tutoe "siku ya kwanza ya juma." Kutokana na
neno la Kiyunani lililotumika hapia wakati wa uandishi, tunaiona linamaanisha kwamba "kiia ijapo
siku hiyo"' ya kwanza ya juma mtu awe na kiitu cha kutoa Kama changizo yake.

4) Tukumbuke pato la kanisa litatoka na changizo ya siku ya kwanza ya juma na kwa mkristo mmoja
mmoja na si vinginevyo. (1 Kor. 16:1-2; 2 Kor. 9:5-15)

5) Hebu tuone njia zisizo halali kwa kanisa kujipatia pato lake:-

6) Tunaona madhenebu hutafuta fedha kwa njia nyingi sana ambazo si mapango wa Mungu; kwa
mifano:

ƒ Kuweka biashara kama duka au shamba la kanisa,

ƒ Kufanya michezo na kujipatia pato kutokana na hilo,

ƒ Kunyima watu huduma fulani ya kanisa kwa sababu hawakutoa, na kadhalika.

59
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

7) Njia pekee ya kibiblia ya kupata fedha ni kwa njia ya michango ya hiari. (1 Kor. 16:1-2; 2 Kor.
9:5-15)

ƒ MATUMIZI MAZURI YA FEDHA YA KANISA

1) Wapo watu wanaostahili msaada wa kanisa, hebu tuwaone:-

i. Wanaokosa riziki - Yesu alisema, "maskini mnao sikuzote pamoja nanyi" (Yn, 12:8).
Tusiwanyime wenye shida wanaostahili msaada (Yak. 2:15-16; 2 Kor. 9:12).

ii. Wahubiri - Kanisa linaweza kumsaidia mhubiri riziki yake ikiwa ameshindwa kujisaidia kwa
sababu anatumia wakati wake katika kazi za Mungu (1 Kor. 9:14)

ƒ Kanisa lisimpunje mhubiri anayestahiliye riziki kwa kuwa Mungu ameruhusu wahubiri
wapate riziki yao kwa hiyo injili (1 Kor. 9:9-11, 14)

ƒ Msaada utolewe kwa upendo na ukarimu. (Mt. 22:39)

ƒ Mhubiri asilete manung’uniko wala ugomvi juu ya msaada wao unaotolewa na kanisa
(1 Tim. 6:8). Anatakiwa akumbuke kwamba kazi anayo fanya ni ya Mungu na kwamba
Mungu atamlipa (Mt. 10:42)

ƒ Iwapo mhubiri anajiona amenyimwa msaada, yambidi awaze mambo mawili:

a) Huenda mhubiri hajawafundisha Wakristo vizuri habari ya kutoa na kazi ya changizo.


Wasingemnyima ikiwa wangefundishwa upendo na wajibu wao wa kutoa.

b) Huenda Wakristo wametambua kuwa mhubiri hastahili msaada!

iii. Mhubiri akiwa anapata msaada wa kanisa, basi na atimize wajibu wake katika kanisa.
Asijiingize katika kazi za kimwili na kulipunja kanisa.

ƒ Ikiwa kanisa halina fedha ya kumtosha kumpa riziki, basi aelewane na Wakristo kwamba
anaruhusiwa kutumia muda gani katika kazi za binafsi. Wakikosa kuelewana, ni bora
akajiondoa katika jukumu hilo.

ƒ Anaweza kuhubiri akijitegemea Kama Paulo alivyofanya. Tusi-liharibu kanisa kwa ajili ya
chakula!

iv. Mhubiri aliye na uwezo wa kujitegemea asilemee Kanisa. Ole! wake yule anayehubiri ili apate
mshahara tu! Atakuwa amekwisha kupata thawabu yake!

ƒ Paulo alihubiri kwa bidii kuliko watu wote. Hata hivyo, alifanya kazi kwa mikono yake
ajilishe mwenyewe na wenzake! Hakutaka awe mzigo kwa kanisa (1 The. 2:9; 2 The. 3:7-
10; 1 Kor. 4:11-12; 9:18; 2 Kor. 12:14-18).

60
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

v. Baadhi ya wazee (maaskofu) - Baadhi ya wazee wa kanisa wanajitoa sana katika kazi za
kanisa kama kazi ile ya kuhubiri. Maandiko yasema wanaweza kupewa riziki wapo wanahitaji
msaada ill waendefee katika kazi ya Mungu (1 Tim. 5:17-18).

ƒ MATUMIZI MABAYA YA FEDHA YA KANISA.

a) Kukopesha - Hatuwezi kusoma mahali po pote katika Biblia panapoturuhusu kumkopesha mtu
fedha ya kanisa au kuona mfano wowote wa kusanyiko lililowahi kufanya hivyo. Mtu akistahili
msaada, basi na apewe tu! Kumkopesha fedha mara nyingi kunaleta matatizo mengi, hebu
tuone baadhi:-

i. Kwa kuwa changizo za wakristo ni kwa ajili ya kundeleza kazi ya Mungu na kusaidia
wasiojiweza, inapokopesha huleta ukosefu wa fedha kwa kazi hizo zilizo muhimu..

ii. Kunapoteza wakati mwingi katika kujadiliana kwamba nani apate mkopo na nani asipate
katika kuandika mahesabu mpaka arudhishe fedha zote.

iii. Kunaweza kuleta dhambi kwa watu kuwa na ugomvi kwa ye yote atakayenyimwa mkopo.
Tena kunaweza kuletei ugomnvi hata kwa yule aliyepata mkopo hasa anaposhidwa
kuurudisha kwa wakati au anaweza kudai kuwa amerudisha fedha hali bado.

iv. Mara nyingi yule anayeshindwa kurudisha mkopo ataacha kuhudhuria kanisani kwa sababu
ya aibu. Hivyo, mkopo unaweza kumsababisha mtu apoteze roho yake.

b) Kuwapa wale wasiostahili msaada - Si kila mtu (wala kanisa) astahiliye kupata msaada wa
kanisa.

i. Neno la Mungu linatukumbusha Mtu asiyetaka kufanya kazi na asile (2 The. 3:10)

ii. Hata kanisa lisilofanya bidii katika kazi zake za kutoa na kuhubiri halistahili kupata msaada
kutoka kwa kanisa lingine! Kanisa linaweza kuwa na uvivu pia!

iii. Hata baadhi ya wajane hawastahili kupata msaada wa kanisa (1 Tim. 5:3-16; 2:8-15).

c) Kutumia fedha kusudi kanisa litiizamwe na watu - Kanisa ni chombo cha Mungu na kinastahili
heshima kusudi watu waokolewe. Hivyo, wakristo wanapaswa kuhakikisha kiburi chao
kisisababishe watumie fedha ya kanisa kujenga au kununua vitu visivyo vya lazima. Hekima ya
kumpandeza Mungu inapaswa kutumika wala si wanadamu tu.

d) Utunzaji wa fedha - Mtume Paulo alikataa kabisa asishike fedha ya kanisa peke yake.

i. Fedha isikabidhiwe kwa mtu mmoja tu (1 Kor. 16:3-4; 2 Kor. 8:16-24).

ii. Shetani anaweza kumjaribu mtu yule ashikaye fedha (Yn. 12:3-6). Hata asipoiba, lakini
Wakristo wengine wanaweza kumtia shaka.

iii. Basi, wawepo watu waaminifu wakisaidiana katika kuhesabu, kutunza, na kutoa fedha ya
kanisa.

61
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

iv. Ripoti za fedha na matumizi yake zitolewe mara kwa mara kwa kanisa zima ili wakristo
wapate kuelewa na kuona kazi za michango yao.

B. TATIZO LA KUMRUDI AU KUMTENGA ALIYETENDA DHAMBI

1) Katika (Tit. 3:10; Mt. 18:15-17). tunasoma maagizo kwa kanisa ya kumtenga mtu mwovu baada
ya kumuonya. Hili limekuwa tatizo kubwa katika kanisa siku hizi. Kanisa linashindwa kumtenga
Mkristo kwa hofu kuwa kanisa litapungua. Kanisa lazima liwatenge wote wenye dhambi zilizo
dhahiri (zilizojulikana).

ƒ Ni bora kumtenga mtu mmoja kuliko kuwaharibu wengine wengi. Mungu hapendelei wenye
haki kukaa na waovu (Yos. 7:12-26). Tunao usemi wa Kiswahili kuwa "samaki akioza ni
mtungo pia." Kuwa nao watu wasiotaka kutubu kanisani kutawafungia mlango wengine
wanaota.ka kuokoka.

ƒ Maana watashindwa kwa sababu hawaoni utofauti wa Ukristo na wao. Hatuwatengi watu ili
tuwapoteze, bali ni kuwarudi wapate kutambua dhambi na kutubu (1 Kor. 5:1-8; 2 Thes.
3:6,14-15; Rum. 16:17; Ufu. 22:14) .

2) Faidai ya kumtenga mtu:-

i. Kumtia aibu ili apate kutubu (2 Kor. 7:9-l0).

ii. Ni njia ya kumwokoa (1 Kor. 5:5)

iii. Ni njia ya kuliweka kanisa katika hali ya usafi daima (1 Kor. 5:6-7; Efe. 5:25-27; 2 Kor. 11:2).

iv. Kumtenga mwenye dhambi ni njia ya kusaidia ili wengine waoqope kucheza na dhambi (Mdo.
5:11; 1Tim. 5:20-21)

C. TATIZO LA UGOMVI KATI YA WAKRISTO

1) Kutokuelewana kunaweza kutokea hata kati Wakristo (Mdo 15:36-40).

2) Nidhambi kwa Wakristo kushitakiana mbele ya serikali au wasio Wakristo! Soma kwa makini sana
(1Kor. 6:1-8)

ƒ Imewahi kutokea kwamba Wakristo waliotamani fedha ya misheni au ukuu katika kanisa
Wemewapeleka barazani wamishenari! Soma (3 Yoh. 1:9-10 na Mt. 18:15-17).

D. TATIZO LIHUSULO MAZISHI

1) Jambo hili Iimekuwa tatizo kwa baadhi ya watu, hasa madhehebu. Wengine wamejiunga katika
Ukristo kuwa kama ni chama cha kuzikana baada ya kufa. Wanawaza nikifa nitazikwa na nani?
Hata wengine wamegawa viwanja vya kuzikia katika sehemu mbali mbali.

62
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

2) Hebu tuliangalie kwa urefu swali hili:-

a) Viwanja vya kuzikia — Mi vema kuwa na viwanja au maeneo ya kuzikia ili makaburi yasienee
ovyo. Lakini hakuna umuhimu wa kuvigawa katika tabaka. Je! Mkristo aliye mwaminifu akizikwa
katika eneo la waliotengwa atakuwa ametengwa kwa sababu hiyo? Jibu ni hapana.

ƒ Au mpagani akizikwa katika eneo la Wakristo waaminifu atakuwa mwaminifu kwa sababu
hiyo? Jibu ni hapana. Kuna wengine wamekufa bila ya miili yao kupatikana na kuzikwa na
ndugu. Kwa mfano: mtu aliyeliwa na wanyama wakali, au aliyechukuliwa na maji maiti yake
isipatikane. Itakuwaje kwa hao siku ya ufufuo? Soma (Ufu. 14:13:20;13).

b) Kuhubiri makaburini au katika majengo - Wengine wamefikiri mtu akifa ni lazima kuipeleka
maiti ya marehemu mpaka kwenye jengo la kanisa kuisudi aombewe na ionekane amezikwa
Kikristo. Isitoshe! Pale makiaburini napo pawepo wahubiri na watu kutia mchanga kaburini
mara tatu wakisema “U mavumbi nawe mavurnbini utarudi tena."

c) Kuhubiri katika majengo au kaburini hakumsaidii marehernu, bali ni faida yao walio hai ili waone
kifo ni nini na baada ya kifo huwa nini (Ebr. 9:27). Kuhubiri kule au kutokuhubiri hakutaweza
kumwokoa marehemu wala kumpoteza. Iwapo alikuwa mwenye haki, basi atakwenda mbinguni
hata asipozikwa kabisa. Lakini pia hata kama tutahubiri na kuimba usiku kucha, kama alikuwa ni
mwenye dhambi ataenda motoni tu. (Mdo. 5:1-11).

d) Wengine pia wanawaza kuwa mwenye Kuzika ni lazima awe mchungaji, padre au winjilisti.
Walakini Biblia haifundishi hivyo. Yeyote anaweza kuzika.

e) Tunaweza kufuata desturi zatu ili mradi tu zisivunje amri za Mungu. Kwa mfano kuchimba
mwandani haipingi mafundisho ya Mungu (Ufa. 20:11-15). Lakini tusifunge desturi za
wanadamu ziwe amri! (Mt. 15:8-9)

WAJIBU WA KANISA
A. WAJIBU WA KANISA KWA JAMII (FAMILY)

1) Elimu ya namna ya kuijenga jamii – Watu hawafahamu kwa asili au kwa bahati bahati tu
namna ya kujenga jamii. Jamii ya Kikristo ni matokeo ya kuelewa mafundisho ya neno la
Mungu na kuyakubali katika hali ya unyenyekevu hivyo ni jukumu la kanisa kueneza elimu hii.

2) Ni kazi ya kanisa kuwaokoa watu na kuwaita katika kanisa. Lakini pia ni wajibu wa kanisa
kuwaangalia watu hawa katika mahitaji yao kiroho na kimwili.

ƒ Mahitaji ya kiroho (Mt. 28:19-20; Mdo. 2:41-42).

ƒ Mahitaji ya kimwili (1Tim. 5:1-16; Mdo. 4:32-37).

3) Kanisa linalazimika kufundisha kuwa kila Mkristo na kila jamii iliyopo kanisani ni ndugu (Mt.
19:27-30; 1 Kor. 12:12-27). Hivyo inahitajika kupendana jamii kwa jamii na kukuzupendano
ndani ya kanisa (1 The. 5:14-15).

63
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

4) Kanisa lina wajibu wa kufundisha jamii mpango wa Mungu kuhusu ndoa na jamii.

B. WAJIBU WA JAMII KWA KANISA

1) Ni wajibu wa jamii kutii madaraka yote ya kanisa (1 Kor. 4:6; Gal. 6:6; Ebr. 13:7).

2) Ni wajibu wa jamii kulipenda kanisa na ushirikiano uliomo katika kanisa (Ebr. 10:24-25).

3) Jamii inatakiwa kujitoa kwa hali na mali kwa ajili ya kanisa; katika kutangaza Injili na katika
kutoa (1Kor. 9:7-14; 2 Kor. 8:1-14).

KUHUSU NDOA

A. NDOA NI NINI?
1) Ndoa ni mapatano (agano) kati ya mwanamume mmoja na mwanamke mmoia naye Mungu ni
shahidi.

2) Bwana amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana,
angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako" (Malaki 2:4).

3) Mume mmoja na Mke mmoja tu - Tunaona Mungu alimpa Adamu kazi kubwa wa kujaza
ulimwengu na watu.

ƒ "Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume
na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, zaeni, mongezeke,
mkaijaze nchi" (Mwa. 1:27-28).

ƒ Hata ingawa kazi yake hiyo ilikuwa kubwa, Adamu alipewa mke mmoja tu !

ƒ "Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;
na hao wawili watakuwa mwili mmoja?'' (Mathayo 19:4-5)

ƒ "Kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe namke wake mwenyewewe na kila
mwanamke na awe na mume wake mwenyewe." (1 Wakorintho 7:2)

B. MUME NA MKE WASIACHANE.

1) Mume awaache wazazi wake aambatane na rnkewe.

ƒ "... mwanamu atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe. nao
watakuwa mwlli mmoja" (Mwanzo 2:24).

ƒ "Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na
mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini" (Mathayo 5:32).

64
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

ƒ "... Mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana. Maana mimi
nakuchukia kuachana, asema Bwana, Mungu" (Malaki 2:15,16).

2) Baada ya mtu mume na mtu mke kupatana kuoana wasiachane! Hata ikiwa mke hazai mtoto
au ikiwa mume amechoka naye, haruhusiwi kuoa mke mwingine! Isitoshe, mtu asifikiri kwamba
kwa sababu hana cheti cha ndoa anaweza kumwacha mkewe!

ƒ "Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi, kwa maana waasherati na wazinzi
Mungu atawahukumia adhabu" (Waebrania 13:4).

C. ARUSI (Sherehe)

1) Ndoa inaiweza kuwapo pasipo kutoa mahari, pasipo kutanya sherehe (arusi).

2) Pasipo kupata cheti, na

3) Pasipo kibali cha kanisa ama serikali.

ƒ Tunaona Adamu na Hawa walioana pasipo vitu hivi.

ƒ Aliyewaunganisha Adamu na Hawa ni Mungu ambaye mpaka sasa huwaunganisha katika


ndoa.

ƒ Yesu alisema, "Aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe" (Mathayo 19:6)

ƒ Sherehe ya arusi ya kimila inaweza kuwapo mradi isipinge na kuwa kinyume na maneno ya
Mungu. Walakini, tusifunge sheria kuwa lazima iwepo! Hakuna sheria kuhusu sherehe ya
arusi katika Agano Jipya.

D. CHETI CHA NDOA –

1) Hata igawa ndoa haitegemei cheti, walakini kuna sababu ya kukipata kwa kuwa Wakristo
tumeamriwa tutii mamlaka (sheria za seirekali).

ƒ "Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu: na
ile iliyopo imeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la
Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu" (Warumi 13:1-2).

2) Kwa usalama wa ndoa (na hasa usalama wa wanawake na watoto) serikali inatuamuru tupate
cheti cha ndoa. Sheria hii inasaidia kuzuia wanaume wasiwadanganye wanawake na kasha
kuwakimbia. Hivyo hata watu wasiomjali Mungu wansilazimishwa na serekali wafanye mambo
yaliyo halali machoni pa watu.

3) Kwa usalama wa jamii, Wayahudi wa zamani wasiomjali Mungu waliamriwa watoe cheti cha
talaka walipokuwa wakiwaacha wake zao. Maana Wayahudi wengine walikuwa wakiachana
kwa sababu yo yote. Katika desturi zao, mwanarnurne akikasirika kwa sababu mkewe
hakufagia nyurnba, au kwa sababu amechelewa kupika, au kwa sababu yo yote nyingine,
aliweza kumfukuza mkewe kwa kusema mara tatu "Nakuacha"! Basi, kwa usalama wa mke
sheria ya talaka ilitolewa kwa wale wasiomcha Mungu.

65
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

ƒ Yesu alisema, "Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha
wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Nami nawaamhia ninyi, Kila mtu
atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu va uasherati. akaoa mwingine, azini;
naye amwoaye yule aliyeachwa azini" (Mathayo. 19:8-9).

4) Basi, ni serikali inayoruhusu kanisa litoe cheti cha ndoa wala si sheria ya Mungu. Kwa hiyo,
tusingesahau kamwe mtujwia uhuru wa kumwacha mkewe eti. kwa sababu hana cheti au kwa
sababu hakufungisha ndoa kanisani!

5) Hivyo, Wakristo tunatakiwa tupate cheti cha ndoa kwa sababu ni sheria ya serikali.

E. MPANGO WA MUNGU WA NDOA

1) Wanadamu waliumbwa kwa mpango wa Mungu wajaze ulimwengu na watu

ƒ "Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume
na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, zaeni,
mkaonaezeke. mkaijaze nchi. na kuitiisha: mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa
angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi" (Mwa 1:27-28).

2) Adamu hakuweza kujaza ulimwengu peke yake.

ƒ "Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaklizi wa
kufanana naye" (Mwa. 2:18).

3) Watawale ulimwengu

ƒ "Mungu akasema, Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samake wa
baharini, na ncfege wa angani. Na wanyama. na nchi yote pia. na kila chenye kutambaa
kitambaacho juu ya nchi" (Mwa. 1:26).

4) Mungu alimpa Adamu kazi

ƒ "Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na
kuitunza" (Mwa. 2:15).

ƒ Ikumbukwe Mungu alimpa mwanadamu kazi ya kulima shamba! Huenda mwanamke ni


msaidizi katika kazi hiyo, lakini yeye si mtumwa wa mwanamume wala hakuumbwa kusudi
mwanamume astarehe amwachie mke wake kazi ya shambani!

5) Mwanamke hakuumbwa awe mtumishi au mtu-nwa wa mwanamume.

ƒ "Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akautwaa ubavu wake
mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu
akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. Adamu akasema, Sasa huvu ni mfupa
katika mifupa yangu na nyama katika nyama yangu. basi ataitwa mwanamke, kwa maana
ametwaliwa katika mwanamume. Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama
yaka naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja" (Mwa. 2:21-24)

66
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

ƒ "Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao weny ewe.
Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake
popote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa" (Efe. 5:28-29)

F. WAJIBU WA MUME KATIKA JAMII.

1) Mume ampende mke wake;

ƒ "Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajiioa kwa
ajili yake ... Vivyo hivyo imewapasa waurne nao kuwapenda wake zao kama miili yao
wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. Maana hakuna mtu anayeuchukia
mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa"
(Efe. 5:25, 28-29).

2) Amvalishe.

3) Amlishe.

4) Amtunze kama nafsi yake.

5) Atimizie haja ya ndoa.

ƒ "Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. Mke
hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake
bali mkewe. Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali;
mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu" (1 Kor. 7:3-5).

6) Mume ana wajibu wa kuwa kichwa cha nyumba katika mambo ya kiroho na ya kimwili.

7) Ana wajibu wa kumtafuta mchumba atakayekuwa msaidizi mwenye kumfaa kimwili na kiroho
pia.

ƒ "Msifungwe nira pamoia na wasioamini. kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki
gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? Tena pana ulinganifu
gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye
asiyeamini?" (2 Kor. 6:14-15)

ƒ "Hatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke alive nduiiu, kama v/ao mitume wengine, na
ndugu wa Bwana, na Kefa?" (1 Kor 1:4).

ƒ "Mwanamke hufungwa maadamu mumewe yu hai, lakini ikiwa mumewe amefariki, yu huru
kuolewa na mtu ye yote amtakaye; katika Bwana tu" (1 Kor. 7:39)

ƒ "Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.
Moyo wa mumewe humwamini, wala hatakosa kupata mapato. Humtendea mema wala si
mabaya, siku zote za imaisha yake ... Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili, bali
mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa". (Mit. 31:10-12, 30)

67
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

ƒ Hata ingawa Sulemani alikuwa na hekima sana lakini alifanya kosa la kuoa wanawake
wasiomjua Mungu. Wake zake wakamsababisha aabudu sanamu. (1Fal. 11:1-11).

ƒ Mfalme Ahabu naye akamwoa Yezebeli, mwanamke mwovu aliyesababisha hasara nyingi
(1 Fal. 16:31).

ƒ Vivyo hivyo mfalme Yehoramu akakossa akamwoa Athalia, binti mwovu wa Yezebeli (2 Fal.
8:18).

8) Kwa sababu mume ni kichwa cha nyumba, basi ana wajibu awe kielelezo katika imani na katika
matendo yake.

9) Anapaswa ajifunze na afundishe neno la Mungu

ƒ "Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe
watoto wako kwa bidii. na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na
ulalapo, na uondokapo" (Kum. 6:6, 7).

ƒ “Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena; bali watii, kama
vile inenavyo torati nayo. Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao
wenyewe nyumbani mwao" (1Kor. 14:34-35).

10) Mume anaweza kumfundisha na kumwuta mkewe kwa matendo yake pia.

ƒ "... wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo?" (1 Kor. 7:16).

ƒ “Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama
chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba
kwenu kusizuiliwe " (1 Pet. 3:7) .

ƒ "Ninyi waume, wapenaeni wake zenu msiwe na uchungu nao" (Kol. 3:19).

11) Mume ana wajibu wa kuwatunza jamii yake.

ƒ "Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na
kulitunza" (Mwa. 2:15).

ƒ "Kwajasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo
ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi" (Mwa. 3:19).

ƒ "... Ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula" (2 The. 3:10).

ƒ "Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa,
ameikana Imani tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini" (1Tim. 5:8)

ƒ "... imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye
mkewe hujipenda mwenyewe ... hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote, bali
huulisha na kuutunza" (Efe. 5:28-29)

68
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

ƒ "... haiwapasi watoto kuweka akiba kwa wazazi, bali wazazi kwa watoto" (2 Kor. 12:14).

G. WAJIBU WA MKE KATIKA JAMII

1) Mke amtii mumewe.

ƒ "Enye wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni
kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo, vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika
kilajambo" (Efe. 5:22).

2) Mke amtii mumewe katika yote yaliyo haki na mema machoni pa Mungu na watu wote.
Mwanamke aliumbwa awe msaidizi wa mwanamume.

3) Sio vigumu kwa mke kumtii mume aliye Mkristo ikiwa anatambua kwamba mumewe
anampenda na ya kuwa hutafuta faida yao.

4) Mke asimtii mumewe katika dhambi (Mdo. 5:1-10).

5) Mke awe kieielezo cherna kwa mumewe.

ƒ "Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe
kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa
hofu. Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia
dhahabu na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo
yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, Hiyo ya thamani kuu mbele za Mungu,
Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini
Mungu, na kuwatii waume zao" (1 Pet. 3:1-4).

ƒ "Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? au wajuaje, wewe
mwanamume, kama utamwokoa mkeo?"' (1Kor. 7:16).

6) Mke asimpoteze mume wake katika jambo lo lote.

i. Adamu aliongozwa na Hawa katika dharnbi (Mwa. 3:6; 1Tim. 2:13-15).

ii. Wake zake Sulemani walimwongoza katika kuabudu sanamu (1Fal. 11:1-8).

iii. Yezebeli alimwongoza mfalme Ahabu katika dhambi nyingi (1Faf. 21:1-25).

7) Mwanamke awafundishe wanawake vijana.

ƒ "Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji,


wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema; ili wawatie wanawake vijana
akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao; na kuwa wenye kiasi, kuwa safi,
kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe, ili neno la Mungu
lisitukanwe" (Tit. 2:3-5).

69
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

8) Hali ya mwanamke mpumbavu

ƒ "Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; bali aliye mpumbavu hubomoa
kwa mikono yake inwenyewe" (Mit. 14:1).

ƒ "Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, kuliko katika nyumba pana pamoja na
mwanamke mgomvi" (Mt. 21:9).

ƒ "Chakula cha mboga penye mapendano; ni bora kuliko ng'ombe aliyenona pamoja na
kuchukiana. Mtu wa hasira huchochea ugomvi; bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza
mashindano" (Mit. 15:17-18).

9) "Maana midomo ya malaya hudondoza asali, na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; lakini
mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; ni mkali kama upanga wa makali kuwili. Miguu yake
inatelemkia mauti; hatua zake zinashikamana na kuzimu; hata asiweze kuiona njia sawa ya
uzima; njia zake ni za kutangatanga wala hana habari" (Mit. 5:3-6)

10) Sifa za mwanamke mwema (Mit. 31:10-31).

i. Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.
(Mit. 31:10)

ii. Moyo wa mumewe humwamini, wala hatakosa kupata mapato. (Mit. 31:11)

iii. Humtendea mema wala sirnabaya, siku zote za maisha yake. (Mit. 31:12)

iv. Hutafuta sufu na kitani; hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo. (Mit. 31:13)

v. Afanana na merikebu za biashara; huieta chakula chake kutoka mbali. (Mit. 31:14)

vi. Tena huantka, kabla haujaisha usiku; huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; na
wajakazi wake sehemu zao. (Mit. 31:15)

vii. Huangalia shamba, akalinunua; kws mapato ya mikono yake hupanda mizabibu. (Mit.
31:16)

viii. Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; huitia mikono yake nguvu. (Mit. 31:17)

ix. Huona kama bidhaa yake ina /a/da; tea yake haizimiki usiku. (Mit. 31:18)

x. Hutia mikono yake katika kusokota; na mikono yake huishika pia. (Mit. 31:19)

xi. Huwakunjulia maskini mikono yake; naatrt, huwanyoshea wahitaji mikono yake. (Mit. 31:20)

xii. Hawahofi theluji watu wa nyumbani mwake; ma-ana wote wa nyumbani mwake huvikwa
nguo nyekundu. (Mit. 31:21)

xiii. Hujifanyia mazulia ya urembo; mavazi yake ni kitani safi na urujuani. (Mit. 31:22)

70
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

xiv. Mume wake hujulikana malangoni; aketipo pamojs na wazee wa nchi. (Mit. 31:23)

xv. Hufanya nguo za kitani na kuziuza; huwapa wafanya biashara mishipi. (Mit. 31:24)

xvi. Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; anaucheka wakati ujao. (Mit. 31:25)

xvii. Hufumbua kinywa chake kwa hekima, na sheria ya wema i katika ulimi wake. (Mit. 31:26)

xviii. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; wala hali chakula cha uviwu. (Mit.
31:27)

xix. Wanawe huondoka na kumwita heri; mumewe naye humsifu, na kusema, (Mit. 31:28)

xx. Binti za watu wengi wamefanya mema, lakini wewe umewapita wote. (Mit. 31:29)

xxi. Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye
atakayesifiwa, (Mit. 31:30)

xxii. Mpe mapato ya mikono yake, na matendo yake yamsifu malangoni." (Mit. 31:31)

H. WAJIBU WA WATOTO KATIKA JAMII

1) Mtoto afahamu kuwa ana wazazi wa kirnwili na mzazi wa kiroho pia!

a) Wajibu wa mtoto kwa mzazi wa kiroho, yaani Mungu.

ƒ "Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, kabla hazijaja siku zilizo mbaya, wala
haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo" (Mhu. 12:1).

ƒ "Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri
zake, maana kwajumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi,
pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya" (Mhu. 12:13-14).

ƒ Hatujui siku yetu ya kufa. Hata watoto wadogo wanaweza kufa. Basi, tuwe tayari siku zote
kusimama mbele ya Muumba wetu.

2) Angalia vijana waliobarikiwa kwa sababu walijifunza kumpendeza Mungu katika ujana wao.
Kwa mfano:

i. Musa,

ii. Yusufu,

iii. Danieli,

iv. Samweli,

v. Timotheo

71
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

3) Kila jamii inao utaratibu wake. Vivyo hivyo, jamii ya Mungu ina utaratibu wake. Watoto waishi
sawa sawa na maadili ya jamii ya Mungu.

4) Watoto wajifunze neno la Mungu kwa bidii.

ƒ "Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, bali wapumbavu hudharau hekima na adabu"
(Mit. 1:7).

ƒ "Kwa kuwa Bwana huwapa watu hekima; Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu"
(Mt. 2:6).

ƒ "Mwanangu, usiisahau sheria yangu, bali moyo wako uzishike amri zangu. Maana
zitakuongezea wingi wa siku, na miaka ya uzima, na amani. Rehema na kweli zifunge
shingoni mwako; ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Ndivyo utakavyopata kibali na akili
nzuri, mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu. Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote,
wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye
atayanyosha mapito yako Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana, ukajiepushe
na uovu. Itakuwa afya mwilini pako, na mafuta mifupani mwako ... Ndipo utakapokwenda
katika njia yako salama, wala mguu wako hautakwaa. Ulalapo hutaona hofu; naam, utalala
na usingizi wako utekuwa mtamu. Usiogope hofu ya ghafula, wala uharibifu wa waovu
utakapofika. Kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako, naye atakulinda mguu wako usinaswe
" (Mit. 3:1-8, 23-26).

5) Watoto wawe kielelezo na wawafundishe wenzao neno la Mungu.

ƒ "Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwa waaminio, katika usemi na
mwenendo, na katika upendo na imani na usafi ... Jitunze nafsi yako, na mafundisho yako.
Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale
wakusikiao pia" (1Tim. 4:12, 16)

6) Wajibu wa watoto kwa wazazi wao wa kimwili, tunaona tangu mwanzo Mungu alitaka watoto
wawaheshimu.

ƒ "Waheshimu haba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo
na Bwana, Mungu wako" (Kut. 20:12).

7) Kwa nini watoto waheshimu wazazi?

a) Watoto waheshimu wazazi kwa sababu Mungu amewapa wazazi kazi ya kuwatunza na
kuwalea.

b) Wazazi ni baraka kwa watoto.

c) Wazazi wanawapenda watoto wao na kujaribu kuwapatia mahitaji yao yote ya kirnwili na
kiroho pia.

d) Watoto wawatii wazazi kusudi waishi siku nyingi duniani.

72
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

ƒ "Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba
yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri, ukae siku
nyingi katika dunia" (Efe. 6:1-3)

8) Hakuna mzazi anayependa kumwona mtoto wake akiumia. Mara nyingi wazazi wametoa uhai
wao kuwalinda watoto wao.

9) Kwa sababu wazazi wameishi siku nyingi kuliko watoto wao, wanaweza kufahamu mambo
mengi kuliko watoto wao. Mtoto anaweza kulilia moto akidhani moto ni kitu chema. Lakini
mzazi, hali amefahamu hatari ya moto, atazidi kumkataza ili asiumie. Vivyo hivyo, wazazi
wanaweza kujua hatari za pombe, bangi, uasherati, na kadhalika. Wanafahamu matokeo ya
dhambi na uzuri wa kumfuata Mungu. Kwa hiyo, mzazi mwema latajaribu kumzuia mtoto
mwake katika tendo lo lote litakalomletea hasara.

10) Mtoto mwenye busara atatambua kwamba wazazi wake wasingemzuia au kumnyima kitu cho
chote chema. Lakini hata asipowaelewe sababu zao, na awatii.

11) Watoto wajifunze kwa wazazi wao. Mungu amewapa wazazi kazi ya kuwafundisha watoto wao
neno lake (Kum. 6:6-7). Kwa hiyo, mtoto ajitoe kujifunza.

12) Watoto wasichukie marudia au adhabu (Ebr. 12:5-13). Wazazi wanamrudi mtoto kwa sababu
ya upendo wao. Ni amri ya Mungu kwa mzazi kumrudi mtoto mkaidi.

ƒ "Usimnyime mtoto wako mapigo; maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. Utampiga kwa
fimbo, na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu" (Mit. 23:13-14).

JARIBIO
A. JIBU MASWALI YOTE

1) Watu wengi huamini kuwa Kanisa ni jengo ambamo Wakristo hufanya ibada zao. Kanusha
jambo hilo na kueleza ukweli ulivyo kwa kirefu.

2) Baadhi ya majina ya Kanisa katika Biblia ni kama vile; Mwili wa Kristo na Kanisa la Kristo.
Eleza kwanini Kanisa liitwe hivyo.

3) Wapo watu wanaodhani kuwa Kanisa na Ufalme ni vitu viwili tofauti. Fafanua.

4) Je, kwanini ufalme umeitwa kuwa, Ufalme wa Kristo, Ufalme wa Mungu na Ufalme wa
Mbinguni?

5) Ili Ufalme ukamilike lazima uwe na sehemu kuu nne. Zitaje pamoja fafanuzi zake.

6) Je, kuna umuhimu gani wa kuwemo katika Ufalme (kanisa)?

7) Taja wa-andaaji wa Ufalme (Kanisa) na kueleza mwandaaji wa pili ujumbe wake ulikuwa
nini?

73
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

8) Je, utimilifu wa ahadi ya ujenzi wa Kanisa ilitimiaje? Toa maelezo ya kutosha.

9) Wengi huamini kuwa Kanisa limejengwa juu ya Petro. "na juu ya mwamba huu nitalijenga
kanisa langu." (Mt. 16:18b) Fafanua ukweli ulivyo kwa mujibu wa Biblia.

10) Baadhi ya madhehebu huamini kuwa funguo za Ufalme walizopewa Petro na wenzake,
(Mt. 16:19 na Mt. 18:18) kwa sasa viongozi wao wamebaki nazo. Kanusha fundisho hilo kwa
kueleza ukweli ulivyo.

11) Je, nini maana ya neno Madhehebu?

12) " Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Murigu kwa ajili ya mapokeo yenu? " (Mt 15:3) Fafanua,
kwanini Yesu alisema maneno hayc na maana yake nini?

13) Je, kwanini tunaamini kuwa Yesu hakutaka madhehebu yawepo? Toa maelezo ya kutosha.

14) Fafanua juu ya mfano aliotoa Yesu katika (Mt 13:24-30, 36 42) juu ya mbegu njema na
magugu, ambao ni kiashirio cha upandaji wa Kanisa ia Kristo.

15) Eleza mifano miwili ya upandaji wa Kanisa la Kristo.

16) Je, madhehebu yametoka wapi?

17) Je, nini mwisho wa ibada za madhehebu?

18) Tunaweza kuona kwa uwazi tofauti kati ya Kanisa la Kristo na madhehebu, kwa kuangalia
mambo kama marine (4). Yataje

19) Wengi huamini kuwa R.C. ndio kanisa la asili. Kanusha fundisho hilo, kwa mujibu wa Biblia.

20) Je, kwanini makanisa ya rnatengenezo, kama vile Walutheri na Wapresbyterian nao
hujumlishwa katika madhehebu?

21) Taja matendo ya ibada ya siku zote angalau manne (4).

22) Kuimba ni tendo mojawapo katika matendo ya ibada kanisani. Je, kwanini Wakristo wana
shaka kutumla vyombo vya muziki katika kuimba? Toa maelezo ya kutosha.

23) Je, kwanini katika kuomba lazima tuzingatie yafuatayo: (a) Tuombe katika jina la Yesu. (b)
Tusitafute mapenzi yetu (c) Tusitumie maneno mengi (d) Wanaume waongoze sala.

24) Eleza tofauti kati ya sadaka katika Agano la kale na changizo katika Agano jipya. *

25) Toa maelezo juu ya faida kama mbili za kulihubiri neno la Mungu pindi Wakristo wanapokuwa
katika ibada.

26) Je, kuna ubaya gani kutumia rozali katka kusali? Toa maelezo ya kutosha.

74
S H U L E Y A B I B L I A T A N Z A N I A

27) Je, kwa mujibu wa Agano jipya, mzee wa kanisa ni mtu wa aina gani?

28) Fafanua juu ya sifa zifuatazo za mzee wa kanisa:

a) Aipende kazi. (1Tim. 3:l)

b) Mume wa mke mrnoja. (Tit. 1:6)

c) Ajuaye kufundisha. (1Tim. 3:2)

d) Awe na watoto waaminio. (Tit. 1:6)

MUNGU AKUBARIKI SANA; SASA UNAWEZA KUENDELEA NA SOMO LA TANO

Shule ya Biblia Tanzania


Kanisa la Kristo Magomeni
P.O. Box 67632
Dar es salaam,
Tanzania

Pepe: info.tbs@magomeni-coc.or.tz
Tovuti: www.magomeni-coc.or.tz

Simu: +255 22 2171532


Faxi: +000 00 00000

75

You might also like