You are on page 1of 43

MWONGOZO

WA
KARISMATIKI KATOLIKI
TANZANIA

Imeandaliwa na:
TUME YA TEOLOJIA
BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA (TEC)
20 Januari, 2016

1
YALIYOMO

UTANGULIZI

DIBAJI

SURA YA KWANZA
1.0.MAANA YA KARISMATIKI KATOLIKI
1.1.Asili ya neno Karismatiki
1.2. Karismatiki Katoliki ni nini?
1.3. Upyaisho wa Roho Mtakatifu

SURA YA PILI
2.0.HISTORIA YA KARISMATIKI KATOLIKI
2.1. Machimbuko ya Karismatiki Katoliki
2.2. Mchakato Papa Leo XIII
2.3. Mchakato Papa Yohane XXIII
2.4. Mchakato Papa Yohane Paulo VI
2.5. Mchakato Papa Yohane II
2.6. Karismatiki Katoliki Tanzania

SURA YA TATU
3.0.MALENGO YA KARISMATIKI KATOLIKI.
3.1.Tamko Maalumu la kuidhinisha Karismatiki Katoliki
3.2.Wongofu
3.3. Utakaso
3.4.Uadilifu
3.5. Uinjilishaji
3.6.Uchangamanisho
3.7.Uamushaji wa Imani

SURA YA NNE
4.0. MUONEKANO WA KARISMATIKI KATOLIKI
4.1. Kikundi cha Sala
4.2. Malengo ya Kikundi cha Sala
4.3. Aina ya Vikundi vya Sala
4.4. Mkutano wa Sala
4.5. Umuhimu wa Kikundi cha Sala

2
SURA YA TANO
5.0. MAKUZI YA KIROHO
5.1.Sala
5.2.Kujifunza Biblia
5.3. Ushirika (fellowship) (Mdo 2:42-47; 4:32-35)
5.4. Masakramenti
5.5.Matendo ya huruma
5.6. Wajibu wa mkarismatiki katoliki
5.7. Karama za Roho Mtakatifu
5.8.Huduma za Uponyaji
5.9.Huduma ya kuwekwa huru kutoka nguvu za giza
5.10. Baadhi ya Karama za Roho Mtakatifu

SURA YA SITA
6.0. KARISMATIKI LAZIMA MMUHESHIMU BIKIRA MARIA (KKK829)
6.1. Heshima ya majitoleo kwa Bikira Maria
6.2. Kielelezo na Tunu
6.3. Bikira Maria mnyenyekevu
6.4. Bikira Maria Nyota ya Uinjilishaji
6.5. Bikira Maria Mwezeshaji wa Miujiza
6.6. Bikira Maria Mama na MWOMBEZI WETU
6.7. Njia ya kumwendea Bikira Maria

SURA YA SABA
7.0. NAFASI YA MAASKOFU NA MAPADRE
7.1. Uongozi wa Maaskofu
7.2. Huduma ya PADRE KWA Wakarismatiki
7.3. Wajibu wa Padre

SURA YA NANE
8.0. MUUNDO WA UONGOZI
8.1. Kamati Tendaji ya Kikundi Cha Sala
8.2. Kamati Tendaji ya Parokia
8.3. Kamati Tendaji ya Jimbo (KTJ)
8.4. Kamati tendaji ya Taifa ya (KTT)
8.5. Kamati Tendaji ya Taifa ya Huduma (KTH)
8.6. Kamati Tendaji ya Huduma ya Taifa (KHT)
8.7. Askofu Mlezi wa Kitume (AMK)

3
SURA YA TISA
9.0. UCHAGUZI NA MIHULA YA UONGOZI
9.1. Utaratibu wa Uchaguzi
9.2. Sifa za viongozi wa Karismatiki Katoliki

SURA YA KUMI
10.0FAIDA ZA KARISMATIKI KATOLIKI

SURA YA KUMI NA MOJA


11.0. MAPUNGUFU NA CHANGAMOTO ZA KARISMATIKI KATOLIKI
11.1. Mapungu
11.2. Changamoto

SURA YA KUMI NA MBILI


12.0 NINI KIFANYIKE?
12.1 Hatua za Kuchukuliwa
12.2 Mambo ya Kuzingatiwa kwa Wakarismatiki
12.3 Yanayoweza Kuchangia Kusimamishwa kwa wakarismatiki

HITIMISHO

BIBLIOGRAFIA

4
UTANGULIZI

Wapendwa wanafamilia ya Mungu,


“Mungu Baba aliyewateua ninyi kufuatana na kusudi lake, na mmefanywa watakatifu na Roho,
mpate kumtii Yesu Kristo na kusafishwa kwa damu yake. Nawatakieni neema na amani tele” (1
Pet 1:2).

Kwa kipindi kirefu waamini wengi wamesikia, wameshuhudi au wameshiriki katika utume na
huduma za Karismatiki Katoliki. Karismatiki Katoliki ni mkondo unaokua kwa kasi katika kanisa
Katoliki. Hapa kwetu Tanzania waamini wengi wamejiunga na vikundi vya Karismatiki au
wamevutiwa kuijiunga navyo kwa sababu ya mabadiliko wanayoyaona katika maisha yao ya
kiroho yaletwayo na mkondo huu. Kwa upande mwingine, kuna mapungufu na changamoto
kadha wa kadha zinazopelekea mkondo huu kutoeleweka vizuri. Wakati mwingine hujifananisha
na makanisa ya kipendekoste, Kilokole au kisabato na kuweka ukatoliki kando. Hivyo, Maaskofu
wameona ni vyema kutoa mwongozo wa Karismatiki Katoliki Tanzania, ili Majimbo yote
Katoliki yawe na kauli moja ya kuelewa, kuupokea na kuusindikiza mkondo huu.

Karismatiki Katoliki ikiendeshwa katika misingi yake, itakuwa chachu ya uinjilisha ji mpya. Kwa
kifupi Karismatiki Katoliki ni chachu nzuri ya imani na Uamsho mwema wa Mungu na jirani.
Maana kama, Baba Mtakatifi Paulo wa VII alivyowahi kusema mwaka 1975, akizungumzia
Karismatiki Katoliki kwamba, kwa njia ya Roho Mtakatifu Kanisa linakuwa na maajabu ya
Pentekoste ya kudumu.Mmiminiko wa karama za Roho Mtakatifu katika mkondo wa Karismatiki
Katoliki, hufanya Kanisa liwe na ujana wake wote.

Mwongozo huu uwe dira yetu katika kuimarisha imani yetu Katoliki na kustawisha Karismatiki
Katoliki nchini Tanzania. Daima ikumbukwe kwamba Krismatiki siyo mkondo nje ya Kanisa
Katoliki, bali ni Kanisa lenyewe likiwa katika muundo wake wa upyaisho. Hivyo, imani Katoliki
isipindishwe wala kubezwa katika huduma za Kikarismatiki Katoliki.

Nawatakieni nyote muusome kwa makini Mwongozo huu. Pia kila mlezi wa mkondo huu, na kila
Mwanakarismatiki anashauriwa kuusoma kwa kina ili kudumu katika njia salama ya imani
tukiongozwa na tahadhali hii tunayopewa na Mt.Yohane: wapenzi wangu msimsadiki kila mtu
asemaye kwamba ana Roho wa Mungu, bali chunguzeni kwa makini kama huyo mtu anaongozwa
na Roho wa Munguau la, maana manabii wengi wa uongo wamezuka ulimwenguni (1Yoh 4:1).

Napenda niwashukuru Makatibu wangu wa Tume ya Teolojia, Padre Novatus Mrighwa na Padre
Victor Tumaini, kwa kudodosa na kutafiti mkondo wa Karismatiki Katoliki. Ninawashuru Bw.
Eslastus Mtema na Bw. Sebastian Chisunga kwa uzoefu wao wa mkondo wa Karismatiki Katoliki
Tanzania, kwa sadaka zao, kwa ushauri wao na ukaribu wao katika kuaandaa Mwongozo huu. Pia
ninawashururu Pdre Almachius Rwejuna na Sr. Juliana Mathias, STh kwa kuhariri na kuchapa
kazi hii.
5
“Mungu wa matumaini atujaze furahana amani yote katika imani yote, tupate kujaa matumaini
kwa nguvu ya Roho Mtakatifu” (Rum 15:13).

Na ichapwe.

Mhashamu Almachius V.Rweyongeza


Askofu wa Jimbo Katoliki la Kayanga
Mwenyekiti Tume ya Teolojia (TEC)
20 Januari, 2016

6
DIBAJI

Mkondo na mwamko wa Karismatiki Katoliki unakuwa kwa kasi kubwa ndani ya kanisa Katoliki.

Leo hii waamini wengi wanajihusisha na vikundi vya kikarismatiki na kuonja mabadiliko makubwa katika
maisha yao ya kiroho na kimwili.kwa upande wa pili yamejitokeza mapungufu na changamoto
mbalimbali, kuhusiana nauelewa pamoja na utendaji wa mkondo huu wa karismatiki.Baraza la Maaskofu
Katoliki Tanzania wameliona hili na kuiomba tume ya teolojia kuifanyia utafiti wakina, na kutoa
mwongozo,mintarafu Karismatiki Katoliki Tanzania.lengo kuu la kazi hii ni kuelimisha juu yaufahamu wa
maana,historia, faida,vikundi vya sala, vikundi vya sala changamoto na namna ya Kuboresha utendaji wa
mkondo huu kwa nia ya kudumisha imani, mapendo na matumaini, umoja naamani tukiongozwa na
mafundisho sahihi ya imani katoliki.

Karismatiki katiloliki ni mkondo na mwamko mmoja wapo katika kanisa katoliki ambao unakazia suala la
uwazi zaidi kwa uwapo wa Roho Mtakatifu, nguvu nakarama zake, mabadiliko ya kiroho ya mtu binafsi
nakanisa kwa jumla(mdo 1:8; yoh 15:26-27)mkondo huu uko ndani ya kanisa kwa ajili ya kanisa na
mali ya kanisa.

7
SURA YA KWANZA

1.0.MAANA YA KARISMATIKI KATOLIKI.


1.1. Asili ya neno karismatiki
Neno Karismatiki linatokana na neno la kiyunani karis au kilatini charisma linaloashiria karama zawadi
au kipawa kutoka kwa roho mtakatifu.linapotumika kama nomino,neno karismatiki lamuwakilisha mtu
aliyapata nakutumia karama za kiroho za Roho Mtakatifu.kimsingi kila mbatizwa ni Mkarismatiki, kwani
amempokea Roho aliye mtoaji wa karama (1kor 12:28-30)na anazitumia. .kwa ujumla Karismatiki
Katoliki ni mfumo wa neema uliobubujika kutoka mtaguso mkuu wa pili wa vatikano unaowavuta wana
kanisa wote warudi kwenye msingi wa ubatizo wao, na kuonja ukombozi wa binafsi unaoletwa na Kristo
ambaye ni Bwana na mwokozi pekee wa ulimwengu wote.

1.2. Karismatiki Katoliki ni Nini?


Karismatiki Katoliki siyo chama cha kitume,bali ni mkondo mmojawapo katika kanisa na ni mwamko wa
Kanisa zima kwa nguvu ya roho mtakatifu. Mwamuko huu unawajumuisha wanakanisa wote walio
nawasio kwenye vyama mbalimbali vya kitume. Kimsingi kila mbatizwa ana haki ya kuitwa
Mkarismatiki. Mkondo huu unavuviwa na Roho Mtakatifu ambaye ndiye aliyopewa jukumu la
kumshuhudia Kristo kwa kutakatifuza kufundisha kuongeza kukumbusha kuchochea karama kuamsha
nk.kutokana na matumizi mbalimbali katika jumuiya na kanisa kwa ujumla wake ,neno Karismatiki
linatumika katika maana ya upyaisho wa Roho Mtakatifu.

1.3. Upyaisho wa Roho Mtakatifu


Katika ubatizo kila mbatizwa hupokea Roho Mtakatifu.kutokana na sababu mbalimbali unafika wakati
ambapo karama na vipawa mbalimbali tulivyokirimiwa havifanyi kazi au havizai matunda yaliyokusudiwa
hivyo dhana ya uamusho inabeba maana ya kuamsha au kuanza kutenda kazi tena kwa zile karama na
vipawa tulivyopewa wakati wa ubatizo wetu. Jukumu kubwa la Uamsho huu ni kuvifanya viwe hai tena
(Rum12:1; Gal 5:22-23a). Kwa ujumla Karismatiki Katoliki ni mkondowa neema unaobubujika kutoka
mtaguso wa pili wa vatikano unao wavuta manakanisa kurudi kwenye msingi wa ubatizo wao na waonje
tena ukombozi waouliofikiwa kwao kwa njia ya Yesu Kristo ili waendelee kupokea sakramenti
zinazopokewa mara nyingi nakuongeza neema.sakramenti ambazo ni Kitubio,Ekaristi na Mpako wa
wagonjwa. Mkondo huu unavuviwa na Roho Mtakatifu aliye na jukumu la kutakatifuza kuongeza
kufundisha kuamusha na kuchochea karama mbalimbali katika maisha ya wakristo ambao daima
wanaitwa na kumshuhudia Kristo.Mdo 1:8)ni wazi kwamba Kristo ndiyo chanzo cha neema zote.yeye
alifanyika mwili akakaa kwetu na wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu Yoh
1:12,14)tunaweza kusema kwa ufupi kwamba karismatiki Katoliki ni mkondo wa neema, kufanya hai ule
usharika au urafiki wa Roho Mtakatifu unaotuunganisha na Kristo.na hii ni kwa ajili ya waamini wote
katika kanisa bila kujali nafasi zao vyeo vyao na rika zao.

8
SURA YA PILI

2.0. HISTORIA YA KARISMATIKI KATOLIKI.


2.1. Machimbuko ya Karismatiki Katoliki.
Kama itakavyodhihirishwa, historia ya mkondo huu ni ndefu na imepitia hatua mbalimbali. Kwa ufupi
machimbuko ya Karismatiki Katoliki yanajumuisha utume wa b wana wetu yesu kristo, Maandiko
Matakatifu Mapokeo ya Kanisa na mang’amuzi ya Mtaguso wa Pili wa Vatikano.

2.2. Mchakato: Papa Leo XIII.


Kwa ujumla historia hii ilianza siku ya pentekoste,siku ambayo roho mtakatifu aliwashukia mitume na
wafuasi wake kristo(mdo 1:13-14,2:1-4).vinginevyo karismatiki katoliki kama ilivyo,ilianza na sista
hellena Guerra ambaye anajulika kama pia “Mtume wa Roho Mtakatifu”au “Mtakatifu wa upyaisho wa
uso wa nchi.” Baada ya kufunga na kusali kwa ajili ya Kanisa mwaka 1886, Sista Hellena alifunuliwa
kinabii nakuelezwa amwandikie Baba Mtakatifu Leo XIII,kumhimiza achukue hatua madhubuti katika
kulifanya upya Kanisa, kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ndiye roho na moyo wa Kanisa---chimbuko
la kila upyaisho. Kufikia mwaka 1897,Baba Mtakatifu alishapokea barua kumi na mbili na kuliagiza
Kanisa lisali Novena ya Roho Mtakatifu. Agizo hili lilipokelewa kwa shingo upande hasa miongoni mwa
Mapadre. Utata huu ulimsukuma Sista Hellena kuongeza maombi yake kwa Papa,mintarafu nia yake
njema yakukomboa na kuamsha uhai wa Kanisa Katoliki. Katika mkesha wa kuanzia mwaka 1901, Papa
Leo wa XIII alifanya ibada maalumu kumuomba Mungu Roho Mtakatifu alishukie tena upya Kanisa
lake,na amwangazie katika suala hilo zito lililoonekana kuyasumbua mawazo yake kama Kiongozi Mkuu
wa Kanisa. Hata hivyo aliiaga dunia kabla ya kuikamilisha nia yake ya kuikubali rasmi Karismatiki
Katoliki nakuifanya itambulike katika Kanisa.

2.3. Mchakato: Papa Yohane XXIII


Mchakato huu ulionekana kusahaulika kwa muda wa miaka kadhaa, hadi wakati Papa Yohane XXIII,
aliye chaguliwa mwaka 1958. Alichaguliwa wakati kukiwa nautulivu na uelewano kiasi kikubwa
ulimwenguni. Mara tu alipochaguliwa alitahadhalisha kwamba ni lazima madirisha yafunguliwe ili hewa
mpya iingie ndani ya kanisa hapa alikuwa anazungumza kwa mafumbo kumhusu Roho Mtakatifu. Katika
sikukuu ya kuongoka kwa Mtume Paulo, January 25, 1959 Papa Yohane XXIII alitangaza ndoto yake ya
kuitisha Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatikano. Lengo lake kuu lilikuwa kulifanya upya Kanisa kuendana
na mabadiliko mbalimbali na kutathimini utume wake. Katika barua yake ya kuhimiza Mtaguso huo,
alibainisha kuwa Mtaguso utakidhi Epifaniampya iliyongojewa na dunia nzima kwa miaka kadhaa. Katika
sala yake ya kuombea Mtaguso, Papa Yohane XXIII aliomba kuweko na Pentekoste mpya kwa kauli
mbiu: “amsha maajabu ya Pentekoste wakati wetu huu.” Wakati wa Mtaguso, mchakato wa Karismatiki
Katoliki ulizungumziwa kupitia mjadala mzito juu ya karama za Roho Mtakatifu. Matokeo ya hiyo
Pentekoste mpya yalianza kuonekana miaka miwili baada ya Mtaguso wa Pili wa Vatikano.

2.4. Mchakato: Papa Paulo VI


Mara baada ya kuchaguliwa kwake, Papa Paulo VI (1963 – 1978) aliahidi kuendelea mbele na Mtaguso.
Matunda ya Pentekoste mpya, yalianza kuonekana kwa kuanzishwa na kikundi cha kwanza cha
Karismatiki Katoliki, katika Chuo Kikuu cha Duquesne huko Rughsbarg(Marekani), tarehe 18
februari1967. Tukio hili lilitokea katika mafungo ya walimu na wanachuo,ambao walishuhudia kupata
ujazo mpya wa Roho Mtakatifu. Ujao huu ulibadilisha maisha yao ya kale na kuanza maisha mapya ya
kumpendeza Mungu kwa sala na maombi. Kwa muda mfupi sana, vikundi vya namna hiyo,vilienea
sehemu mbalimbali duniani bila kuwa na mwanzilishi maalumu,ingawa vyote vilikuwa na utaratibu wa
kusali unao shabihiana.

9
Mkutano wa kwanza wa viongozi wa mkondo huu wa Karismatiki uliitishwa mwaka 1973. Baba
Mtakatifu alitazama Karismatiki kama jumuijya ya watu wanaovutwa kuwa na sala za kina na tafakari,
wanakazia sala na masifu, wana ukarimu mkubwa wa kutoa huduma, na wana upendo mkubwa kwa
Maandiko Matakatifu na kwa jirani. Kutokana na yote hayo, Baba Mtakatifu alikiri kuwa kuna dhihirisho
kubwa la uwapo wa Roho Mtakatifu. Wakati wa uzinduzi wa Sinodi kule Roma mwaka uliofuata 1974,
Papa Paulo wa sita alizungumzia hadharani juu ya miminiko la karama za Roho mtakatifu,katika mkondo
wa karismatiki katoliki amabazo zinalifanya kanisa liwe na hali ya ujana. Kwamba kwa njia ya Roho
Mtakatifu kanisa linakuwa namaajabu ya pentekoste ya kudumu. Kufika mwaka 1975, Karismatiki
Katoliki ilikuwa imeenea kwa kasi kubwa kubwa duniani. Mwaka huohuo katika mkutano wa pili
waviongozi wakarismatiki katoliki, Papa Paulo wa VI alikazia kuwa Karismatiki Katoliki sio mkondo nje
ya kanisa lenyewe, balia ni kanisa lenyewe likiwa katika mkondo wake wa upyaisho.
2.5. Mchakato: papa Yohane Paulo wa II
Kwa upande wake Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa II aliendeleza masimamo wa mtangulizi wake
mintarafu Karismatiki Katoliki. Alitoa mahimizo mbalimbali kwa nyakati tofauti, kabla ya Baraza la
kipapa la walei kutoka tamko rasmi la Kutambua utumishi wa kuratibisha Karismatiki Katoliki
ulimwenguni tarehe 14 septemba 1993, pamoja na tamko na tamko hilo , Baraza la kipapa pia lilipitisha
mwongozo/kanuni (statutes) (regthen Peter stood up publish year……….uk) za Kutambua Karismatiki
Katoliki pamoja na huduma ya chombo cha kulea mkondo hu. Mwongozo huu umeifanya Karismatiki
Katoliki kuwa na msingi imara, na kutambuliwa na kanisa lote, pamoja nakwamba baadhi ya makanisa
mahalia yameshindwa kuelewa na kuushi; hivyo kuwa chanzo cha migogoro na sitofahamu kaika kanisa.

2.6.Karismatiki Katoliki Tanzania


Ni vigumu kusema kwa uhakika lini hasa mwammko wa Karismatiki uliingia Tanzania na kikundi cha
kwanza cha sala kilianzia wapi. Kuna ushahidi wa kutosha kuwa, hadi kufikia tarehe 7 desemba 1980
tayari kulikuwa na vikundi vinane amabvyo Wakatoliki walijihusisha navyo. (Rejea MWAKANJALA,
historia ya upyaisho wa kikarismatiki katoliki , dar es salam mwaka 2005) vingi kati ya hivi vilikuwa
vikihudhuriwa namapadre na watawa. Kwa kiasi kikubwa kuingia kwake nchini kulirahisishwa zaidi na
wamisionari waliokuwa wakienda likizo katika mataifa yao, kukuta wimbi la mwammko huu wa
kikarismatiki. Baadhi yao baada ya kurudi Tanzania wakaanza kukutana kwa sala za kikarismatiki. Walei
wachache walishiriki katika vikundi hivyo, na sehemu nyingine askofu aliruhusu Mapadre na watawa
wakutane wenyewe. Mifano ya vikundi hivi ipo; Lukuledi (masasi) mifano ya vikundi hivi vilianzishwa
wakati wa kwaresma mwaka 1980, chini ya Padre Roman STAD MUELLER DAREDE (daleda babati)
chini ya watawa wa “medical missionaries of mary”mwishoni mwa mwaka 1978; Mbeya chini ya Padre
Etien Sion, MAFR. Pale Ifakara mwaka 1981 Padre DONAT MULLER alianzisha kikundi cha sala baada
ya kupata ruhusa kutoka kwa Askofu wake. Dar es salam miaka ya 1980 pale chuo kikuu, kikundi cha sala
kikiwahusha pia Wapentekoste/kati ya wakatoliki waliojihusisha walikuwepo pia watawa wa kike wawili
kwa sababu hiyo. Parokia ya Upanga Padre Teo van schayck na Padre Agustino Felinandes walianzisha
kikundi cha sala mwaka 1983. Baadaye akina mama Chilambo Luis Bulemela na Teresia Ngaiza
walitokea hapo walianzisha kikundi cha sala katika Paroikia ya Mtakatifu Petro mwaka 1985. Kufikia
mwaka 2011 tayari kulikuwa nawanakarismatiki zaidi ya elfu kumi walitapakaa au kusambaa katika
Majimbo ishirini na mawili (Rejea Karismatiki Katoliki tumaini la kanisa millennia ya tatu, uk 15).
Mkondo huu wa Karismatiki umejikita zaidi katika Majimbo ya Dar es salam, Arusha, Iringa, Mshi,
Ifakara, Mwanza, Dodoma, Morogogro, Mbeya, Mbinga, Songea, Bukoba, Kigoma, Tanga, Njombe, na
Same. Utafiti umeonyeshwa kwamba Majimbo yote hayo yana Padre mlezi wa Karismatiki Kijimbo
pamoja na kamati ya huduma ya kijimbo kwa ngazi ya Kitaifa kuna kamati ya taifa ya huduma na kamati
tendaji ya Taifa.
Mkutano kwanza wa Kitaifa ulifanyika pale Mzumbe Morogoro 1981, baada ya Padre Etien sion, MAFR,
wa jimbo la Mbeya kuandika barua kwa kila Parokia Tanzani kuwaomba iwapo kuna vikundi vya
Karismatiki kuhudhuria mkutano pale Mzumbe. Na Baba askofu Adrian Mkoba aliridhia mkuno huo wa
siku……. ufanyike katika jimbo lake.
10
SURA YA TATU

3.0. MALENGO YA KARISMATIKI KATOLIKI

3.1. Tamako maalumu la kuinisha Karismatiki Katoliki


Malengo hayo, yamefafanuliwa vizuri katika hati maalumu ya Baraza la Kipapa la Walei, “The pontifical
council for the laity”, inayotambua “Huduma za Upyaisho za Karismatiki Katoliki Kimataifa”, kwa
Kiingereza The intenatinal Catholic Charismatic Renewal Services (ICCRS)”, kama chombo cha
kuendeleza Karismatiki Katoliki kwa kadri ya sheria ya Kanisa, namba 116. Hati hiyo ilitolewa kwa mara
ya kwanza na mwadhama Eduardo Kardinali Pironio (Rais wa Baraza la kipapa la walei) na mhashamu
askofu Paulo J. Cordes (MAKAMU WA RAIS tarehe 14 septemba 1993, kama tamko la kisheria (decree
lenye kumbukmbu na. 15665/93/AIC-73.

Aidha, hati hii ilifanyiwa marekebisho mwaka 2004iliidhinishwa na mhashamu Askofu Stanslaw Rylko
RAIS WA Baraza la kipapa la walei na Joseph Cremence (katibu wa Baraza) kwa tamko lenye
kumbukumbu na. 863/05/Aic/73 La Tarehe 9 Mei 2005 Vatcano

Tamko hili la kuidhinisha Karismatiki Katoliki ulimwenguni pote na kanuni/ statutes za chombo hiki
zabainisha wazi kuwa Malengo ya Karismatiki Katoliki ni yale yale ya kanisa lenyewe yaani:

3.2. Uongofu
Kustawisha mahusiano binafsi ya kina, makomavu na uendelevu baina ya mtu naYesu Kristo Bwana na
mwokozi. Kuwasaidia wakatoliki kuonja ubatizo katika Roho Mtakatifu. Yaani, kuonja kwa namna ya
binafsi upendo wa Mungu kwa kupokea wokovu unaopitia kwa njia ya mwane wa pekee Yesu Kristo aliye
peke yake Bwana na mwokozi wetu.

3.3. Utakaso
Kukuza na kustawisha upokeaji binafsi wa nafsi, uwapo na nguvu ya Roho Mtakatifu katika namna
inayobadilisha maisha. Neema hizo hupati kung’amuliwa kwa pamoja katika kile kinachoitwa sehemu
mbambali za Dunia, ubatizo katika roho mtakatifu, ujazo au upyaisho wa roho mtakatifu tukio hili
lieleweke kama kupokea binafsi zile neema tupazo katika sakramenti za kumwingiza mtu ktika Ukristo
yaani ubatizo, kipaimara, sakaramenti za kupokea nguvu katika huduma kwa ajili. Kuwasaidia wakatoliki
kuwa wazi, kupokea na kutumia karama za roho mtakatifu. Karama hizi zilisha pokelewa kwa njia ya
ubatizo na kipaimara, na kuwa kama zimelala. Ubatizo katika roho mtakatifu huziamsha na kumwezesha
muhusika kuwa hai katika kuzitumia.

3.4. Uadilifu
Kukuza na kustawisha matumizi ya karama za Roho Mtakatifu (carismata) siyo tu ndani ya karismatiki
katoliki bali pia ndani kanisa lote kwa ujumla. Karama hizi mbambali huonekana kwa wingi miongoni
mwa walei watawa na wakleri. Mkondo huu huamsha ari ya sala za kumshukuru, kusifu na kuabudu na
kujikabidhi kwa maongozi yake Mungu. Karama hizi zikieleweka na kutumika vizuri bila mgongano na
mambo mengine katika maisha ya kanisa, ni chimbuko la nguvu kwa wakristo katika safari yao ya
kuelekea utakatifu na kwa utekelezaji wa utume wao.

3.5. Uinjilishaji
Kukuza kazi ya uinjilishaji kwa nguvu ya roho mtakatifu, kuwainjilisha upya wakristo waliorudi nyuma,
kuwaiimarisha na kuwatia bidii wakristo wakristo wanaendelea na imani, kuwainjilisha walio nje na
kanisa na kuinjilisha tamaduni na mihimili ya miundo ya kijamii. Upyaisho huu hasa unakuza na
kuchochoe ushiriki wa utume wa kanisa kwa kutangaza injili kwa maneno na matendo, kwa kumshuhudia
11
yesu kristo kwa ushuhuda binafsi kwa njia ya kazi za imani na za haki, kama kila mmoja wetu alivyoitwa.
Karismatiki Katoliki inakazia uinjilishaji mpya uliojawa naujasili mpya mbinu mpya na namana mpya
zinazoambatana na mijiza ya kulithibitisha neno linalohubiriwa.
3.6. Uchangamanisho
Kustawisha ukuaji endelevu wa utakatifu kwa njia ya muunganiko sahihi wa msisitizo hii ya kikarismatiki
na maisha kamili ya Kanisa. Hili linatizwa kwa kushirika maisha kamili ya kisakramenti na kiliturujia na
katika kuenzi utajiri wa mapokeo ya kanisa katoliki katika sala maisha ya kiroho na malezi endelevu
katika mafundisho ya imani katoliki kwa kuongozwa na mamalaka ifundishayo ya kanisa (church
magsterium) na kwa kushiriki katika mpango wa kichungaji wa kanisa.

3.7. Uamshaji wa imani


Kuamsha upya imani iliyofifia miongoni mwa waamini kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya katika
maisha yao na maisha ya kanisa kwa ujumla

12
SURA YA NNE

4.0.MWONEKANO WA KARISMATIKI KATOLIKI


4.1.Kikundi cha sala

Mara nyingi mkondo huu huonekana katika sura ya kikundi cha sala. Kikundi cha sala cha kikarismatiki ni
ushirika huria wa wakatoliki unawapa fursa ya kushirikiana mtindo wa maisha na sala za kikarismatiki.
Mtu anahesabiwa kuwa mkarismatiki baada ya kushiriki semina ya maisha ya kiroho (SMK) kwa
takribani miezi mitatu.

4.1.1 Neema tupatazo kwa ubatizo katika roho mtakatifu (Yohane 1:33,Mdo 1:5, au ujazo wa roho
mtakatifu (Mdo 2:17, 33; 10:45 hutumika kwa Kusaidiana katika kushirikiana na wengine. Kila
atakaye kuishi maisha haya mapya hana budi kujiunga na kikundi cha sala na watu wengine
wanaoishi maisha haya.
4.1.2 Katika karismatiki, Mkutano wa sala hufanyika mara moja au mara mbili kadiri ya uhitaji mahalia
kwa wiki; kwa wale wanaojitahidi kuishi maisha ya kikristo, maadilifu nja ya kina katika
ulimwengu wa le. Kusudi la Awali na msingi katika mkutano huo wa sala, ni kumsifu na kumwadu
mungu katika “roho na kweli” (Yoh 4:24;Efeso 5:18…), kwa shangwe na furaha kwa nyimbo
(zaburi 95:1) karama ya kunena kwa lugha (rum 8:26), sala, kupiga makofi (Zab 47:1), kucheza (2
Sam 6:14), kuinua mikono (Zab 63:4; 134:2) na kutumia kila aina ya vyombo vya mziki (Zab
98:5-6; 150:3-5)
4.1.3 Vipindi vya ukimya na tafakari (kwa ibada) ni lazima viwepo ( Zab 46:10;Papa Benedicti XVI:
neno la Bwana, Verbum domini 66).

4.2.1. Malengo ya Kikundi cha sala

1)Kufanya upya na kustawisha maisha ya Kikristo kadri ya Injili, kama ilivyokuwa katika kanisa la
mwanzo

(Mdo 2:42-47; 4:32-35)

2) Kuwa chombo cha kutia uhai katika kanisa mahalia

3) Kuendesha mikutano ya sala ya kikarismatiki

4) Kufanya semina za maisha ya kiroho na semina za makuzi

5) Kufanya uinjilishaji katika parokia, wiki za neema, uinjilishaji kwenye jumuiya, uinjilisha nyumba
kwa nyumba, makaongamano n.k.

4.3. Aina ya vikundi vya sala


Hapa kwetu Tanzania aina ya kwaida ni ya vikundi vya Parokia au kigango, lakini zipo aina za vikundi
hivi kwa mfano Mosi; vikundi vyevye taasisi/ vyuo, mashule, hospitali, nyumba za watawa n.k.

Pili; vikundi vya mitaani kwa ruhusa ya paroko.

13
4.3.1 Mkutano wa sala

Tukio kubwa katika uhai wa karismatiki katoliki ni mkutano wa kikundi cha sala. Nijumuiiko la
wakatoliki wakishiriki sala ya vikundi vya mtindo wa kikarismatiki. Mkutano wa sala wa kikarismatiki
hujumuisha;

1.Kumsifu na Kumwabudu Mungu kwa shangwe na furaha (Zab 149:3, 47:1, 66:1-4)

2. Kushirikishana neno la Mungu (Kol 3:16)

3. Kushirikishana ushuhuda na maombezi (mambo ambayo Mungu anawatendea)

4. Kuchochoa na kutumia karama za roho mtakatifu kama vile kunena kwa lugha unabii, uponyaji n.k.
(1Wak 12 na 14).

Mkutano wa sala huishia na muda wamaombi/ maombezi na kuwawekea mikono kwa kuwahudumia
walio a shida mabalimbali. Katika kutekeleza hayo yote ni mhimu kuangalia kuwa uendesha ji wa kikundi
cha sala usikinzane wala utendaji wa roho mtakatifu usingiliwe (1Tim 5:19). Mwisho wa yote mambo
hayo lazima yafanywe kwa utaratifu unaofaa (1Wak 14:26-33, 40)

4.4.0. Umuhimu wa kuhudhuria kikundi cha sala

4.4.1. Kila mkarismatiki shariti awe mshika wa kikundi cha sala ambako atalelewa na kuwajibika.

4.4.2. Kila mhudumu lazima awe na mahudhurio mazuri kwenye kikundi chake sala. Yeyote asiyekuwa na
mahudhurio mazuri apaswi kuhudumu popote

4.4.3 Kila mhudumu atakapo Jimbo moja kwenda Jimbo lingine atapaswa kuwa na barua ya askofu wake
wa Jimbo lake, baada ya mhudumu huyo kupata uthibitisho kutoka kwa mratibu wa Jimbo atokako.

4.4.4. Kila muhudumu afikapo katika Jimbo alikotumwa, anapaswa kujitambulisha au kutambulishwa kwa
Askofu mahalia kabla ya kuanza huduma.

4.4.5.Ieleweke kuwa kikundi cha sala ndio msingi na utimilifu wa utume wa kikarismatiki
katoliki.uongozi uliopo katika ngazi zote(vigango ,parokia ,jimbo,taifa,kimataifa)upo kwa ajili ya
kikundi cha sala.

4.4.6. Kutakuwapo pia jumuiya agano za kiinjili za kikarismatiki (yaani jamii ya wakarismatiki wanaoishi
pamoja kijumuiya kama vile agape center nk.)kadiri ya karismatiki katoliki jumuiya hizi
zitawajibika kwa uongozi wa Karismatiki jimbo chini ya askofu mahalia.ni muhimu hapa
ieleweke kuwa viongozi wa jumuiya za agano za kiinjili za kikarismatiki,wana haki ya
kuchaguliwa katika uongozi wa kikundi cha sala wanapoishi.

4.4.7. Kutakuwapo na umoja wa jumuiya za agano za kiinjili za kikarismatiki nchini, ambazo zitakuwa na

uwakilishi katika kamati ya taifa ya huduma.

14
SURA YA TANO

5.0.MAKUZI YA KIROHO

Ubatizo Katika Roho mtakatifu, au ujzo wa Roho Mtakatifu,ni mwanzo tu wa safari binafsi kuelekea
majitoleo ya kina ya maisha ya Kikristo.hali hii haifikiwi mara moja ,bali inahusisha mwenendo wa
majitoleo binafsi na ukuaji hata mkristoafikie ukaribu mkamilifu baina yake na Mungu na jirani (Mk
12:28-30;17-19)

Mafundisho yanahitajika kuhusu jinsi ya kukua kiroho na kimaadili. Katekesi itazingatia mafundisho ya
kanisa Katoliki kama yanavyopatikana katika Biblia, Katekisimu ya kanisa Katoliki, Mtaguso wa pili wa
Vatcano, mapaokeo ya Matakatifu (Nyaraka na mafundisho toka kwa Mapapa na Maaskofu, ili
kuwawezesha wanakikundi wakue kwa namana bora zaidi katika imani Katoliki. Uwapo wa Roho
Mtakatifu na nguvu zake hazina budi kudhihirika kwa ishara na miujiza, lakini pia kwa kjifia nafsi. Ni
mhimu kuwa mafundisho haya yawasaidie wanakikundi kila mmoja kuubeba msalaba wake (Luk 9:23,
RUM 8;9-14).

5.1. Sala

Sala ndio msingi wa kuimarisha na kudumisha mahusiano binafsi ya kina yna ya upendo kwa Mungu,
jirani na nafsi yako yako mwenyewe. Maisha yenye mafanikio yanahitaji ‘kutenga muda wa ukimya kila
siku’(MUKS kwa wakati unaofaa na kadhalika muda wasala na ibada za jumuiya (misa takatifu, kuabudu
Yesu wa Ekarisiti, sala ya familia na pia pamoja na wengine).

Majitoleo kwa Bikira Maria mbarikiwa na kwa Watakatifu ni sehemu muhimu ya imani ya mkatoliki na
chombo cha sala chenye nguvu.

5.2 Kujifunza biblia

Kila Mkristo anahitaji kumjua Mungu na kumwelewa yeye na njia zake. Kuijifunza Biblia ni zoezi la
makusudi linalolenga kuzoeza akili. Kimsingi hapa si kwa maana ya kisomi ya kumtafuta kupata shahada
au nembo nyingine za jinsi hiyo, bali kwa mapana yake katika mwendelezo wa kumtafuta kujua mamabo
ya Mungu zaidi, ili tuweze kumpenda vizuri na kumtumikia zaidi. Kuijinza bibilia kwatuwezesha
Kutambua ‘Mungu nji nani, anafanya nini na nini anataka tufanye’ (1 Tim 3:17). Kwa sababu hiyo ni
muhimu kwetu sisi kama wakatoliki kusoma na kujinza bibilia kama inavyohimizwa na mtaguso wa pili
wa Vatcano (DV 26).

5.2.1 Katika neno la Mungu upo uwez na nguvu nyingi kiasi kwamba neno hilo huwa egemeo na nguvu
kwa kanisa na pia uthabiti wa imani na chakula cha kiroho na chemichemi safi na maisha ya kiroho kwa
watoto wa kanisa (DV 21).

5.3 Ushirika (fellowship) (Mdo 2:42-47, 4:32-35).

Ushirika wa neno ambalo linarejeza karibu kila kitu ambacho wakristo Wanafanya pamoja kama
mwili wa kristo. Ni uthibitisho wa uharisia wa kiroho kwamba tu kina kaka na akina dada wa
familia moja. Katika upweke hatuwezi kuwa wakristo kamaili. Ili tuweze kuonja utimilifu wa

15
maisha ya kikristo inatupasa kuungama na wakristo wengine. Twahitaji utegemezo wa wenzetu,
twahitaji hekima zao na nguvu.

5.3.1 Baadhi ya njia zitusaidiazo kuonja Ushirika wa Kikristo ni;

1.Ibada za kilitrujia

2. Mikutano ya sala

3. Makongamano, wiki za neema, mikutano ya injili (fire conferences

4. Kukutanika kwa kafundisho na majiundo (formation)

5. Kutumika pamoja, kama katika timu za huduma.

6. Sala za pamoja katika jumuiya ndogondogo za kikristo.

7.Mahusiano na uwajibikaji wa kila mmoja kwa mwingine.

5.4. Masakramenti
Kadiri ya mapokeo ya kikatoliki, chombo muhimu zaidi katika makuzi ya kiroho, ni masakramenti. ‘
Kanisa limeweka shariti kwamba kwa waamini kushiriki ibada ya misa takatifu siku za jumapili na
sikukuu zilizoamriwa, na wakiwa wamejiaanda kwa sakramenti ya upatanisho, kanisa linawahimiza sana
waamini wake wapokee Ekaristi takatifu kila siku’, ikiwezekana (Can.1389) kwa sababu hiyo
wakarismatiki, wanahimizwa kupokea sakramenti ya upatanisho mara nyingi, na kushiriki komunio
wakiwa na usafi wa moyo ikiwezekana kila siku (1 Wak 11:23-33)

5.5 Matendo ya huruma


“Huruma ndio msingi thabiti wa uhai wa kanisa…umahili wa kanisa unaonekana kwa namna
linavyoonyesha huruma na upendo, kanisa lina hamu isiyo na kikomo kwa kuonyesha huruma” (Uso wa
huruma Misericordiae vultus na 10) matendo ya huruma ni yale ya kiupendo ambayo twajitoa kumfanyia
hisani jirani katika uhitaji wake kimwili na kiroho.

5.5.1 Matendo ya huruma ya kimwili ni saba yaani;

1.Kuwalisha wenye njaa

2. Kuwanywesha wenye kiu

3. Kuwavika wasio na nguo

4. Kuwakaribisha wasio na makazi

5. Kuwaponya wagonjwa

6. Kuwatembelea wafungwa

7. Kuwazika wafu

5.5.2. Matendo ya huruma ya kiroho nayo ni saba;

16
1. Kuwashauri wenye mashaka

2. Kuwafundisha wasiojua

3. Kuwafariji wenye huzuni

4. Kuwaonya wakosefu

5. Kusamehe makosa

6. Kuwavumilia wasumbufu

7. Kuwaombe wazima na wafu

Wakristo wa mwanzo walijaliana, walihurumiana na Kusaidiana sana katika jumuiya zao za Awali (Mdo
2:43-47,4:32-37)

5.6 Wajibu wa mkarismatiki mkatoliki hai;


5.6.1. Zipo wajibu mbalimbali ambazo zinapaswa kumsaidia Mkarismatiki Mkatoliki akue kiroho.
Wajibu hizi ni pamoja na;

1. Awe na nia, ari na juhudi za kukua kiroho, amepokea sakramenti za kumuzamisha katika imani,
ubatizo,
Ekaristi na kipaimara, (awe na hati ya ubatizo) kwa matendo anasali kila jumapili na siku za amri, na
kila inapowezekana misa za kila siku, na kupokea ekaristi takatifu kulingana na utaratifu wa kanisa
mahalia.

2. Ajitakase na kujiboresha kiroho, kwa kupokea sakramenti za uponyaji, ndio sakramenti ya


upatanisho
(kitubio) na sakramenti ya mpako wa wagonjwa inapohitajika (Yak 5:13-16) anayetoa huduma hii ni
Padre.

3. Awe hai katika chama kimojawapo cha kitume (Rejio Maria, Moyo Mtakatifu wa Yesu, Utawa wa
tatu wa
Wafransikani, Virafra, Mtakatifu ana, Wawata, Uwaka, n.k. (angalau kimoja na kushiriki katika
jumuia ndogondo za kikristo. Ampende Bikira Maria na kusali Rozali na kufanya hija kwa vituo vya
hija vilivyojengwa kwa heshima ya Bikira Maria pale penye uwekano.
4. Asiwe na fikra za kulogwa na hataki aingize mwingine katika fikra hizo za ushirikina na uchawi,
kwani Yesu Kristo ana nguvu kuliko uchawi.

5.Asipige lamli, ni Mwenye upendo mnyenyekevu na wal hawadharao wasio wakarismatiki.

6. Awe mtu Mwenye utii kwa viongozi na Hiarakia (viongozi wa kanisa) na viongozi wa kikundi chake
cha sala.
7. Awe nia au ari ya kukua katika upendo, na katika matumizi ya karama za Roho Mtakatifu kwa ajili ya
utukufu wa Mungu Baba na kwa manufaa ya wengine.

8. Awe mtu mwema aliyejaa imani, hekima na Roho mtakatifu (Mdo 6:3)

17
5.7.Karama za Roho Mtakatifu
5.7.1. Wakristo wengi waliotoa wengi waliotoa maisha yao kwa Yesu Kristo, kumfanya Bwana na
mwokozi wamaisha yao binafsi, na kujiunga na vikundi vya sala vya Ki-karismatiki, hushuhudia
mabadiliko mkubwa na ya msingi katika maisha yao. Mabadiliko hayo ya maisha hutokanan na toba ya
kweli, uamuzi wao thabiti wa kumgeukia Bwana Yesu Kristo, na kukubali Kujazwa nguvu za Roho
Mtakatifu. Tukio hilo la Kujazwa nguvu za Roho Mtakatifu huitwa ubatizo wa Roho Mtakatifu. Pato moja
la kubatizwa Roho Mtakatifu ni kupokea karama zake, kwa mfano unabii, uponyaji, miujiza, kunena kwa
lugha mpya n.k. (1 Wak 12; Rum 12;6-8). Hivi ndivyo utendaji wa Roho Mtakatifu umejionyesha kwa
nguvu nyingitangu kanisa la Awali. Tunawajibika kuwa na shukrani kwa Mungu kwa kutumwagia kwa
kutumwagia siku hizi karama na neema zilezile zilizolibariki kanisa tangu siku zake za mwanzokabisa
(taz. Sala ya misa ya pentekoste.).

5.7.2 Jambo la kukumbukwa ni zawadi inayotolewa na Roho Mtakatifu ili Kujenga Kanisa (1Wak 14;12).
“Roho ni mmoja agawiae Karama zake mbalimbali kwa ajili ya manufaa ya kanisa, kadri ya utajiri wake
mwenyewe na hitaji la huduma (LG.7). Kwa karama hizo Roho anawawezesha waamini kwa “… kwa
kuwafanya wafae na kuwa tayari kazi na huduma mbalimbali zenye kuleta manufaa kwa ajili ya
matengenezo ya kanisa na maongezo yake (LG.12)

5.7.3 Miongoni mwa karama hizo ambazo zinaonekana kuwa ngeni kwa watu wengi japo ni za muhimu
na zina msingi dhahiri katika maandiko matakatifu na mapokeo. Karama hizo ni pamoja na:-

1). Karama ya kunena kwa lugha


Karama hii huonekana zaidi katika vikundi vya sala vya Karismatiki kwa namana ya kumsifu na
kumwomba Mungu kwa lugha isiyoeleweka kibinadamu (Rum 8:26; 1Kor 14:2)

2) Karama ya unabii
Karama hii inajidhihirisha katika vikundi vya sala wakati baadhi ya wanakikundi wanapokea ujumbe wa
Mungu kwa ajili ya kuwajenga, kuwatia moyo na kuwafariji wenzao (1Kor 14:3-5). Kila unabii
upokelewe kwa shukrani, lakini lazima upimwe bila kumzimisha Roho Mtakatifu (1 Thes 5:19-21; 1KOR
14:29; 1YOH 4:1)

3. Karama za uponyaji
Katika kanisa karama hizi zimeendelea kuonekana kwa njia ya sakramenti ya mpako wa wagonjwa,
maombezi ya watakatifu na mahali pengi pa matokeo ya pekee kama vile Lurd-Ufaranza na Fatima –
Uureno. Katika Karismatiki Katoliki, karama hizi zinadhihirika kwa njia ya sala ya imani ya Waumini
kama alivyosema Bwana Yesu kabla ya kupaa kwake (Mk 16:17-18). Kutokana na hitaji kubwa la
uponyaji katika jamii, karama hii imetumika sana hata imekuwa huduma kamili ya uponyaji ndani ya
Karismatiki Katoliki. Kwa sababu hiyo, mwongozo huu unatoa maelezo ya kina kuhusu huduma hii.

5.8. Huduma za uponyaji


5.8.1 Mungu hutuponya kwa njia mbili: Njia ya sala na njia ya matibabu hospitalini (Ybs 38:1-15).
Injili takatifu inaonyesha wazi kabisa kuwa kuponya wagonjwa kwa njia ya sala ilikuwa sehemu muhimu
ya huduma ya kazi za Yesu za kukomboa watu. Naye alilipa kanisa maagizo maagizo maalumu;
kutangaza ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa (Lk 9:2; 1,9) uwezo wa Mungu ni mpana zaidi kuliko
kuponya mwili tu, Mungu huponya roho, mwili mawazo (kisaikolojia) au hayo yote kwa pamoja.
Uponyaji pia unajumuisha kumbukumbu haribifu (traumaticexeperiences). Majeraha haya humzua mtu
asijisikie huru kamili na kukua kiroho ipasavyo. Tangu mwanzo kanisa lilitambua karama za uponyaji na
hizo zilikuwa kama ishara kuwa ufalme wa Mungu umesimikwa duniani ( Mark 16:15 – 20, Lk 11: 20)
huduma za uponyaji zina uwezo wa kuwavutia watu wengi, kwa hiyo zinaweza kutumika katika kuhubiri
injili. Hata hivyo yapo mambo ya kuangalia kwa makini katika kutoa huduma hizi:

18
5.8.1.1. Zisifanywe kuwa sehemu ya kujipatia fedha: “Mmepewa bure toeni bure” (Mt 10:8).

5.8.1.2. Zisiwe njia ya kujipatia njia ya kujipatia sifa au Umaarufu. Sifa na utukufu wote uwe kwa
Mungu mponyaji. Ili kuepuka hali ya mtu binafsi kujichukulia utukufu, maombezi ya wagonjwa yafanywe
na timu ya wanakikundi kadhaa kila iwezekanapo.

5.8.1.3. Uponyaji hupatikana kwa imani, lakini kamwe isifikiriwe kutokufaulu kupona kwa mtu fulani
inaonekana upungufu wa imani tu au hali ya dhambi ya muhusika.

5.8.1.4. Wahudumu wa uponyaji wapatiwe mafunzo ya kutosha.

5.9 Huduma Ya Kuwekwa Huru Kutoka Nguvu Za Giza

5.9.1.Hekima ya kichungaji ituongoze (Yoh 4:1-6)

Katika Biblia huduma hii ni sehemu ya huduma za uponyaji (Mk 16:17-18). Maandi zaidi yanathibitisha
mpango wa Bwana juu ya kutoa pepo; “Yesu aliwaita wale thenashara, akawapa uwezo na mamalaka juu
ya pepo wote na kuponya maradhi” (Lk 9:1; 17-19) Ifahamike kuwa kuponywa kwa ndani au kiroho ni
sehemu ya huduma za uponyaji. Mara nyingie wakati sala za kuponya zinapotolewa yawezekana sala za
kuwinga pepo zikatakiwa. Hapo mambo mawili lazima yazingatiwe: Hekima ya kichungaji na karama ya
kupapambanua roho (1 Yoh 4:1-6; 1 Kor 12:10). Lazima kutofautisha kati ya sala ya kuwekwa huru
kutoka nguvu za giza (derivarence) na sala ya kuwinga shetani (exorcism).

5.9.2. Sala ya kuwekwa huru

Mtu anaposhindwa kujitawala katika jambo fulani maishani mwake, anahitaji sala ya kuwekwa huru.
Jambo hili ni zaidi ya kishawishi cha kawaida na pungufu ya hali ya kutawaliwa kabisa na shetani. Sara
hii inaweza kutolewa na Mkristo mwenye karama ya kufungua na kuweka huru. Lakini huduma hii
ifanyike na kikundi kinachotambuliwa na uongozi uongozi husika wa kanisa. Ieleweke kwamba siyo kila
ni mapepo isipokuwa kila kitu kinahitaji kupambanuliwa.

5.9.3. Kuwinga Shetani (Exorcism)

Kuwinga Pepo ni sala rasmi ya Kanisa ambapo “Kanisa linaomba wazi kwa mamalaka ya Jina la Yesu
Kristo kuwa mtu au kina fulani kilindwe dhidi ya yule mwovu na kuondolewa kutoka wake (KKK 1673).
Exorcism “ huelekezwa katika ufukuzaji wa mapepo au kufunguliwa kutoka hodhi ya kipepe kwa njia ya
mamalaka ya kiroho ambayo Yesu alilikasmia Kanisa lake” (KKK 1673).

Kutokana na asili na ugumu wa huduma ya exorcism, “hapana hata mtu mmoja ambaye kisheria aweza
kumwinga mtu pepo bila ruhusa maalumu na halisi toka kwa Askofu Mahalia” (Can. 1172 par 1).

Ruhusu ya kuwinga pepo hutolewa na Askofu Mahalia kwa au mtu yeyote aliyejaliwa uchaji, maarifa,
busala na msimo thabiti wa maisha “. Kwa sababu hiyo kabla mtu hajawinga pepo “ ni muhimu
Kuhakikisha kuwa kuna uwapo wa pepo wala si ugonjwa pekee” (KKK 1673).

Ikiwa ni suala la kutawaliwa kabisa na shetani, suala ambalo hujitokeza mara chache, huduma ya kuwinga
shetani inahitajika. Huduma hii hufanywa na Askofu au Padre aliyeidhinishwa naye.

19
5.10. Baadhi ya Karama za Roho Mtakatifu

5.10.1. Karama ni nini?


Karama ni zawadi ya kiroho anayopewa mtu kwa manufaa ya Kanisa. Zawadi hizi ni uthibitisho wa nguvu na
uwepo wa Mungu, hutolewa bure kwa ajili ya heshima na utukufu wa Mungu, na kwa ajili ya kuwahudumia
wengine, nazo zimekuwamo na kubaki ndani ya Kanisa katika mafundisho na utendaji wake ( Msgr. Vincent Walsh,
A Key to Charismatic Renewal In The Catholic Church).
Baadhi ya karama hizi ni Kuhubiri, imani, uponyaji, miujiza, unabii, kupambanua roho, ndimi, na tafsiri ya ndimi (
1Kor 12:4-11; Efe 4:7-8, 11:12; Rum 12:6-8). Mt. Paulo anawahimiza wakristo kutaka sana kupata karama iliyo
bora zaidi, ambayo ni Upendo ( 1Kor 13).

5.10.2. Hekima
Hii ni karama ambayo Roho Mtakatifu huitumia kumwongoza mtu kufanya maamuzi sahihi au kuchagua vema na
kuishi maisha ya kweli ya Kikristo. Utambuzi wa fumbo la Kristo kama katika mifano aliyoitoa Yesu, kadharika
mafunuo mengi aliyoyapata Mtakatifu Paulo kuhusu mpango wa Mungu wa Wokovu; ni mifano halisi ya karama
hii. Leo hii Wakatoliki wengi na wote wanaofanya kazi ya kufundisha imani, au wanaoshauri katika nasaha za
Kikristo, wanakiri na pia wanaiona kuwa na thamani maalum, na kwa hivyo huiomba daima. Hekima hii ni ile
itokayo juu mbinguni
(Yak 3:13-18)

5.10.3. Maarifa
Kwa karama hii Roho Mtakatifu humpa mtu uelewa wa kina juu ya fumbo la Imani, au humjuvya kuhusu hakika ya
jambo ambalo asingeweza kulijua ila Mungu Mwenyewe Amelifunua. Karama hii huonekana na kudhihirika katika
maisha ya baadhi ya Watakatifu. Kwa mfano, Yesu alidhihirisha karama pale alipomfunulia yule mwanamke
Msamaria katika kisima cha Yakobo kuwa alishakuwa na waume watano( Yoh 4:18). Mtakatifu Yohane Vianey, pia
Padre Pio walitumia karama hii wakati wa maungamo kuongoza mamia ya waamini wafikie toba ya kweli na
kuanza maisha mapya. Lakini pia yafaa katika huduma ya uponyaji kwa kututambulisha chimbuko la ugonjwa ili
kuomba ipasavyo ( 1Kor 12:6-11).
5.10.4 Imani.
Karama hii humwongoza mtu kuomba kwa uhakika, akitumaini kuwa kile aombacho kitatokea.
Katika Marko 11:23, Yesu alisema, “amin, nawambieni, yeyoteatakayeuambia mlima huu, ng’oka ukatupwe
baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Imani
ya jinsi hii humsukuma mtu katika kutenda, kama pale Mtakatifu Petro alipomwambia yule kiwete akisema” kwa
jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende” (Mdo 3:6-10). Imani huonekana kwa kuvumilia mateso kwa ajili ya
Mungu ( Ebr 11) pia Imani huonekana katika matendo ( Yak 2:14-26).

5.10.5. Miujiza.
Kwa karama hii Mungu hufanya tendo la” Uweza Wake”. Ni tendo lisilowezekana kibinadamu, kwa kumtumia mtu
Fulani, kama chombo chake cha kudhihirishia” kazi zake za nguvu na uweza”, kama alivyomtumia Petro na Paulo
na pia baadhi ya watakatifu. Muujiza mkubwa zaidi ni ule wa uponyaji war oho na mwili kwa sakramenti za
uponyaji yaani mpako wa wagonjwa ( Yak 5: 14-15). Pia kushiriki Sakrament zinazotupa nguvu hasa Ekaristi
Takatifu.

5.10.6 Unabii
Hii ni karama ambayo kwa Mungu kwa kumtumia mtu Fulani hunena neno au kutoa ujumbe kwa mtu binafsi au
kwa jumuia nzima ya Kikristo. Ni Mungu, anamtumia mtu Fulani kuwaambia watu mawazo yake kuhusu hali
iliyopo au kusudi lake ni nini kuhusu mustakabali wa hali ijayo, au ni kipi Mungu anafikiria watu wake wanahitaji
kujua, au kujilinda kwacho kwa wakati huo. Si lazima ujumbe uandamane na utabiri wa mambo yatakayotokea
baadaye, ingawa hilo laweza kutokea na litokeapo lahitaji upambanuzi wa kikundi cha watu hasa viongozi ili
kuthibitisha ujumbe huo. Katika waraka wa Kwanza wa Mt. Paulo kwa Wakorintho, Mtakatifu Paulo anasema, “
Bali yeye ahutubuye ( atoaye unabii) asema na watu maneno ya kuwajenga, na kuwafariji na kuwatia moyo” ( 1Kor
20
14:3), Kwa hiyo, unabii wa kweli utaleta upendo, furaha, amani, wongofu n.k. “ Msimzimishe Roho, msitweze
unabii, jaribuni mambo yote, lishikeni lililo jema, jitengeni na ubaya wa kila namna” ( 1Thes 5:19-22).

5.10.7. Ndimi
Hii ni karama ambayo kwayo mtu hutamka maneno au sauti kwa lugha ambayo yeye mwenyewe haifahamu ( 1Kor
14). Katika UKK hutumika wakati wa masifu – kumuimbia Mungu sifa, Kuabudu, kuombea watu au hali Fulani. Ni
lugha ibubujikayo toka moyoni, hali ambapo Roho wa Mungu ndani ya mtu huendelea kuomba na hasa pale
muhusika anapokuwa hajui cha kusema ( Rum 8:26-27).

Aina tatu za Karama hii:

1. Ni aina ya ndimi za kimiujiza, ambapo mtu anenapo wasikiaji humsikia katika lugha zao, kama katika (
Mdo 2:6-11). Aina hii ya ndimi hutokea kwa nadra sana na inakusudiwa kuwa ishara kwa wasioamini (
1Kor 14:22).

2. Ni aina ya ndimi inayo lenga kutoa ujumbe kwao waaminio. Hata hivyo yanayotamkwa ni lugha ambayo
yenyewe kama yenyewe haieleweki (yanayotamkwa si lugha yakueleweka na mtu yeyote). Ili ieleweke
yahitajika karama nyingine ya kiroho, ni ile ambayo Mt. Paulo anayosisitiza ya kafasiri (1Kor 14:13,26,27).

3. Hatimaye ni aina ya tatu. Kimsingi aina hii ya ndimi, ni sala halisi. Ni aina inayoonekana zaidi katika UKK,
na ina sifa mbili: Ni sala ya sauti ( haijakusudiwa kuwa ya ukimya), na tena yenyewe kama yenyewe
haieleweki kwa wanaosikia ( haitumii maneno ya kawaida). Pamoja na hayo, Maandiko Matakatifu
yatuhakikishia kuwa ni sala, maana yaongozwa na Mungu, inaeleweka na Mungu na inavuviwa na Roho wa
Mungu, ili kuwasaidia waamini katika udhaifu wao, kwa maana aghalabu hatujui kuomba ipasavyo;”
Lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa” ( 1Kor 14:2; Rom 8:26). Faida ya
sala hii ya ndimi, humjenga anayesali (1Kor 14:4).

4. Mtakatifu Paulo anawahimiza Wakristo kuomba kwa namna zote mbili. Kwa Roho, yaani bila matunda ya
akili, na kwa akili (1Kor 14:14)……).

Angalizo: Karama hii inahitaji hekima na busara katika matumizi yake. Lazima kuangalia wakati, mahali ulipo, na
watu wanaokuzunguka. Kwani karama haikulengwa kutumika kwa majivuno
( Mt 4:1-11; Mt 27:39-44).

5.10.8. Uponyaji
Ni kipawa anachopewa mtu kwa ajili ya kuponya magojwa na shida mbalimbali kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
Kwa binadamu kupata maumivu ya kimwili, kisaikolojia au ya kiroho ni sehemu ya maisha yetu. Mara nyingine
mateso tupatayo huunganishwa na dhambi ( Mwa 3:1-19; Kumb 28:21-22, 27-29), lakini pia mateso huweza
kuwapata wenye haki, kama majaribu kwa waadilifu kitabu cha Ayubu, Mateso saba ya Bikira Maria; kwaajili ya
ukombozi wetu:
1) Unabii wa Simeoni ( Lk 2:34-35).
2) Kukimbilia Misri ( Mt 2:13-15).
3) Kumpoteza Mtoto yesu Hekaluni ( Lk 2:43-49).
4) Kukutana Yesu na Maria kwenye Njia ya Msalaba ( Yoh 19:25-27).
5) Kusulibiwa kwa Yesu ( Mt 27:32-44; Mk 15:21-32; Lk 23:26-43; Yoh 19:16-27).
6) Kushushwa mwili wa Yesu toka Msalabani ( Yoh 19:38-40).
7) Kuzikwa kwa Yesu ( Mt 27:57-61; Yoh 19:41-42).
Kwa njia ya mateso yake kristo ya hiari, na matakatifu, binadamu ameponywa na kukombolewa ( rej. 1Pet 2:19-25).
Kwa Mt. Paulo Mtume kuteseka ni faida, “sasa nayafurahia mateso niliyonayo kwa ajili yenu; tena nayatimiliza
21
katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, Kanisa lake” ( Kol
1:24). Katika kipindi chote cha historia ya Wokovu, Mungu alidhamiria kuondoa mateso. Yesu aliwapa mamlaka
mitume wake kuponya wagonjwa na kufukuza pepo (Mt 10:7-8)

Kanisa daima limehudumia wagonjwa (Taasisis za Afya: Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali, Vituo vya
Walemavu, Vituo vya kulelea Yatima, Nyuma za wazee n.k), huduma ya kichungaji (ushauri nasaha, maongozi ya
kiroho, n.k) na huduma ya kiroho ( sala na Baraka, Sakramenti ya Upatanisho, Mpako wa Wagonjwa na Ekaristi
Takatifu).

Katika sala yoyote ya uponyaji uangalifu unatakiwa katika kupambanua na kuthibitisha uponyaji:

Kama unahitaji kwanza vipimo na tiba ya hospitali au ushauri nasaha au kumuona daktari wa magonjwa ya akili; na
baadaye sala na maombi.

5.10.9. Uponyaji wa Ndani


Ni aina ya huduma ya upendo, ambapo mtu huongozwa kutubu na kusamehe wale waliomuumiza
( rej. Mt 5:43-48), kasha humwelekea Yesu kwa kuponya kumbukumbu ya maumivu aliyonayo
( rej. Mt 11:25-30).

22
SURA YA SITA

6.0. KARISMATIKI LAZIMA IMUHESHIMU BIKIRA MARIA (KKK 829)

6.1. Heshima na Majitoleo kwa Bikira Maria

6.1.1. Tangu enzi za kale kabisa Kanisa limekuwa likimheshimu Mbarikiwa Bikira Maria ( KKK,

496 - 498, 500), Mama wa Mungu ( Lk 1:43), aliyetungwa mamba kwa uwezo wa Roho

Mtakatifu ( Lk 1: 34-35). Alijazwa na Roho Mtakatifu akakingiwa dhambi ya asili, naye

aliishi bila dhambi maisha yake yote ( Pius IX, Ineffabilis Deus, 1854). Mwishoni mwa uhai

wake alipalizwa mbinguni mwili na roho ( Papa Pius XII, Magnificantissimus Deus, 1950).

6.1.2. Kwa kuwa yu Mama wa Mungu na Mama wa Kanisa (Yoh 19:25-27), tunamtambua kuwa Mstahiwa, nasi
tunamheshimu (Lk 1:48). Mama Maria ni kielelezo cha imani na upendo wa kweli, mfano wa kuigwa wa
Kanisa ambalo waamini wake wanatambua kuwa waweza kukimbilia ulinzi wake wakati wa hatari na
uhitaji kwa njia ya kusali Rosari, na kwenda kuhiji katika makanisa na vituo vilivyojengwa kwa heshima
yake.

6.1.3. Majitoleo halisi kwa Mama Maria ni zawado adhimu ya Roho kwa kila Mkristo. Yeye alimpokea Roho
Mtakatifu alipopashwa Habari ( Lk 1:35), alijazwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste ( Mdo 2:1-4).

6.1.4. Roho Mtakatifu huvuvia majitoleo halisi kwa Maria, na majitoleo hailisi kwa Maria huchochea utii, usikivu
na welekevu kwa Roho Mtakatifu. Yeye ni muombaji ( Yoh 2:1-12). Tuombe maombezi yake
tunaposherekea sikukuu zake, tusalipo rozari, litania zake, na sala nyingine. Na tufuatishe mema yote
aliyonayo ya imani thabiti nay a kipekee, tumaini, upendo na ujasiri wa utayari wazi wa kupokea na
kutimiza mapenzi ya Mungu.

6.2. Kielelezo na Tunu

Bikira Maria Msikivu, Mjitoa Sadaka, Mpole na Mnyenyekevu Jasiri – Lk 1:34-35. Mama Maria aliyemsikiliza
Malaika wa Bwana, pale alipomwambia juu ya huo wito, akauliza swali kwa upole na unyenyekevu mkubwa,
akitaka kujua mambo magumu katika maneno aliyoelezwa na Malaika wa Bwana, “Litakuwaje Neno hilo maana
sijui mume” ( Lk 1:34-35). Alipopewa majibu na Malaika wa Bwana, japo pia yalikuwa magumu akawa mtii,
akapokea wito huo moja kwa moja, bila kuuliza uliza na kujiuliza uliza, wala kutaka muda wa kutafakari maana
tayari alikuwa na mpango mwingine wa maisha yake, ambao ulikuwa kinyume kabisa na mpango anaoelezwa na
malaika wa Bwana, akajibu na kueleza “Tazama mimi ni mjakazi wa Bwana na iwe kwangu kama ulivyosema” ( Lk
1:38).

6.3. Bikira Maria Mnyenyekevu – Lk 1:28-31; 45-49.

Malaika akaingia nyumbani mwake akasema, “Salamu uliyepewa Neema Bwana yu pamoja nawe” Maria
akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, salamu hii ni ya namna gain? Ili bidi Malaika
amtulize “ Usiogope Maria, maana neema kwa Mungu” salamu hii aliiona ni kubwa kwake.

Maria alipokwisha kuelezwa na Elizabeti aliyejaa Roho Mtakatifu “ Heri aliyesadiki kwa maana yatatimizwa
aliyoambiwa na Bwana”. Maria akaanza kumshukuru Mungu kwa wimbo/Magnificant akisema “ Moyo wangu
wamwadhimisha Bwana, na roho yangu imemfurahia Mungu mwokozi wangu kwa kuwa ameutazama unyonge wa
mjakazi wake” ( Lk 1:45-48: 1Sam 2:7-8).
23
6. 4. Bikira Maria Nyota ya Uinjilishaji

“Mwishoni mwa Barua yake ya Kitume, Evangelii Nuntiandi, Papa Paulo VI anatoa cheo “ nyota ya uinjilishaji kwa
Mama wa Mungu: ‘Katika asubuhi ya Pentekoste aliangalia kwa sasa zake mwanzo wa uinjilishaji uliochochewa na
Roho Mtakatifu: tunaomba awe Nyota ya uinjilishaji unaofanywa upya daima na ambao Kanisa, likitii amri ya
Bwana wake, ni lazima liendeleze na kukamilisha, hasa katika nyakati hizi ambazo ni ngumu, lakini zilizojaa
matumaini’ ( EN 82). Kwa hiyo, Maria ni njia ya uhakika ya kumpata Kristo. Uchaji wa kweli kwa Mama wa
Bwana daima unatuhamasisha kuelekeza maisha yetu kufuatana na Roho Mtakatifu na tunu za Injili” (rej. Ecclesia
in America 22-1-1999, no.11).

6.5. Bikira Maria mwezeshaji wa Miujiza

Bikira Maria daima amekuwa mwezeshaji wa jiujiza kwa maombezi yake kwa mwanae, pale tunapomwomba
atuombee. Mara nyingi, Bikira Maria hutuombea hata pale ambapo hatukumwomba atuombee. Anapoona tu,
tunahangaika na tuna shida Fulani, Maria hasubiri kumwambia Mwanae Yesu Kristo, kama tunavyoona katika
habari ya harusi ya Kana ya Galilaya. Mara tu divai ilipowatindikia hata wakati ambapo Yesu alisema saa yake
haijafika bado, Bikira Maria alimwomba Yesu, na Yesu akafanya sawasawa na ombi lake (Yoh 2:1-12).

Bikira Maria kwa kumtokea Mt. Bernadeta kule Urdi, kwa uwepo wake, amewezesha miujiza mingi. Watu wenye
shida mbalimbali duniani kote huenda huko kwa maombezi ya shida zao, hasa za miujiza, aidha ya uponyaji au
shida mbalimbali nyinginezo, na wengi kila mwaka hupata majibu chanya ya sala na maombi yao.

6.6. Bikira Maria Mama na Mwombezi wetu

Bikira Maria ni mama yetu kwa sababu Yesu Kristo, Bwana na mwokozi wetu ni kaka yetu. Ni mzaliwa wa kwanza
wetu, (Rum 8:29; Kol 1:15, 18) naye anamwita Mungu, Baba, ndiye Baba yetu pia. Hivyo, Mama yake ni Mama
yetu, na amelidhihirisha hilo na kulithibitisha pale msalabani alipomkabidhi Yohane kwa niaba yetu, alimwambia
Mama yake “Mama tazama mwanao” kisha akamwambia Yohane “ Tazama Mama yako”. Na tangu saa ile Yohane
alimchukua Bikira Maria nyumbani kwake ( rej. Yoh 19:25-27).

Hata baada ya Bwana wetu Kristo Kufufuka na kupaa mbinguni, Bikira Maria alikuwa bado kitovu cha mitume
akiwapa malezi ya kimama, kwani hakuna aliyemjua Yesu kati yao kuliko Bikira Maria, maana alikuwa ameungana
na Yesu katika mwili na roho. Maria alikuwa na mitume wakti wa Pentekoste, ( Mdo1:14) na hata baada ya
Pentekoste, akiwasaidia kwa sala, ushauri wake, na hasa kwa uwapo wake kwa muda mchache – muda wa siku
kumi tu, - walimpokea Roho Mtakatifu siku ile ya Pentekoste. Tangu hapo Injili ikaanza kuhubiriwa kwa nguvu za
ajabu. Bado hata sasa Bikira Maria amekuwa si kielelezo tu, bali pia amekuwa mwombezi wetu kwa Mwanae
mpaka hivi leo. Hivyo, tusisahau wala tusisite au kuchelewa kumwendea pale tunapokuwa na haja mbalimbali.

6.7. Njia za Kumwendea Bikira Maria

6.7.1. Kusali Litania ya Bikira Maria

6.7.2. Kusali Rozari Takatifu.

1) Kila siku: Matendo ya Furaha (J’tatu na J’mosi), Matendo ya Uchungu ( J’nne na Ijumaa), Matendo ya
Utukufu ( J’tano na Jumapili), Matendo ya Mwanga ( Alhamisi).
2) Miezi ya Rozari ( Mei na Oktoba)
3) Novena za siku tisa

6.7.3. Kusali au kuhudhuria na kushiriki Misa Takatifu kwa siku; Sikukuu na Sherehe zifuatazo:
24
1) Jumamosi za Bikira Maria
2) Sikukuu na Sherehe mbalimbali za Bikira Maria kama ifuatavyo:
 Januari 01, - Bikira Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu (Sherehe).
 Februari 11, - Bikira Maria wa Lurdi: Sikukuu ya kuombea Wagonjwa.
 Machi 25, - Kupashwa habari Bikira Maria.
 Mei 31, - Bikira Maria kwenda kumwamkia Elizabeti.
 Agosti 15, - Bikira Maria kupalizwa Mbinguni (Sherehe).
 Septemba 15, - Bikira Maria wa Mateso.
 Oktoba 07, - Bikira Maria wa Rozari Takatifu.
 Novemba 21, - Kutolewa Bikira Maria Hekaluni
 Desemba 08, - Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili ( Sherehe)

6.7.4. Kuhiji kwenye vituo vilivyojengwa kwa heshima yake Bikira Maria, Mfano

 Lurdi huko Ufaransa


 Fatima huko Ureno
 Medjurje huko Bosnia – Herzegovisa
 Nyakijoga Mugana huko Bukoba
 Lurd – Bugene, huko Kayanga / Karagwe – Kagera
 Vituo vilivyoidhinishwa na Maaskofu kwa heshima ya Bikira Maria katika
majimbo mbalimbali.

25
SURA YA SABA

7.0. NAFASI YA MAASKOFU NA MAPADRE


7.1. Uongozi wa Maaskofu

Uongozi wa Maaskofu ni muhimu katika kuiwezesha Karismatiki Katoliki kukua na kustawi katika ushirika na
utume wa Kanisa. Huduma ya Karismatiki Katoliki katika Jimbo lolote lazima ipate baraka na kibali cha Askofu wa
Jimbo mahalia. Papa Yohane Paulo wa II alipozungumza na viongozi wa Karismatiki Katoliki ulimwenguni, alisifu
juhudi zinazofanywa na Maaskofu za kutia moyo Karismatiki, kuipa maelekezo na kusaidia jumuiya ya Kikristo
kuelewa vizuri zaidi nafasi ya mkondo huu ndani ya Kanisa. Yote haya wamekuwa wakiyafanya ili kuwezesha
mwamko huu kuwa wazi zaidi kwa tunu mbalimbali za upendo wa Mungu zilizomo ndani ya Kanisa. Pia alisema,
“hata kama Maaskofu hawavutiwi na mitindo ya sala ya Kikarismatiki ambayo ninyi mmeona inajeng,
watakubaliana kwa dhati na matamanio yenu ya kufanywa upya kiroho kwenu wenyewe na kwa Kanisa kwa
ujumla. Hivyo watawapeni maongozi yapasayo bila pingamizi kwani huo ndio wajibu waliopewa na Kanisa.” ( Mei
7, 1981. Taz. Pia Christifideles Laici no. 31).

Maaskofu waupe mkondo huu Mapadre walezi, wawasindikize na kuwashauri.

7.2. Huduma ya Padre kwa Wakarismatiki

Kuhusu Mapadre, Papa Yohane Paulo wa II alisema hivi: “Padre hataweza kutoa huduma kwa Wakarismatiki
asipoukubali na kuukaribisha mkondo huu katika mawazo ya moyo wake. Awe na hamu ya kukua katika vipaji vya
Roho Mtakatifu na moyo wa kushirikiana na kila mkristo katika kukuza vipaji hivyo.” ( Mei 7, 1981. Taz. Pia
Christifideles Laici no. 31). Hivyo Padre anawajibu wa kutia moyo na kutoa ushauri wa kichungaji hata kama yeye
binafsi si Mkarismatiki.

7.3. Wajibu wa Padre

Kadili ya Mtaguso Mkuu, Maelezo ya Hati 16 za Vatikano II; TMP Book Department, Taborauk. 212-213; uk 187
na 25, wajibu wa Padre ni:

1) Padre ni Baba na mwalimu, ni kuhani na mchungaji

2) Padre anapaswa kuwashauri walei na utume wao katika Kanisa bila kuwakatisha tama, na anapaswa
kuwasaidia, kuyasikiliza mashauri yao, kutambua ujuzi wao na ufundi wao katika mahitaji ya Kanisa la siku
hizi.

3) Mara kwa mara Padre ashiriki katika ibada zao, mikutano yao ili kuwasaidia kwa kuwapatia Sakramenti
mbalimbali kwa mfano: Kitubio, Ekaristi, Mpako wa Wagonjwa, kutoa mafundisho na kuwatia moyo.

4) Wote wafurahi wanapoona vipawa vyao kutoka kwa Mungu na hamu yao ya maisha ya roho na kulitumikia
Kanisa inatimia.

26
SURA YA NANE

8.0. MUUNDO WA UONGOZI


8.1. Kamati Tendaji Kikundi Cha Sala:

8.1.1. Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Kikundi:

1) Mratibu wa Kikundi
2) Mratibu Msaidizi
3) Katibu
4) Katibu Msaidizi
5) Mhazini
6) Mhazini Msaidizi
7) Waratibu wa Kamati za Huduma

8.1.2. Majukumu ya Kamati Tendaji ya Kikundi cha Sala

1) Kusimamia nidhamu na uwajibikaji wa Kikundi cha Sala


2) Kuongoza ibada za Kikundi cha Sala
3) Kutunza uwapo na moto wa Roho Mtakatifu katika ibada.
4) Kuandaa Semina na Mikutano mbalimbali katika Kikundi cha Sala
5) Kuhakiki mafundisho na matumizi ya karama mbalimbali
6) Kuhakikisha kuwa Karismatiki, inakuwa chombo cha kutia uhai katika Kigango na Parokia
7) Kufanya uinjilishaji katika jumuia na nyumba kwa nyumba katika Kigango au Parokia
8) Kutoa taarifa ya mipango, kazi na maendeleo ya Kikundi, kwa viongozi wa Parokia
9) Kutoa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha kwa wanakikundi
10) Kubuni na kupanga mipango ya maendeleo ya kimwili na kiroho kwa wanakikundi.
11) Kujenga uomoja wa wanakikundi na umoja wa Kigango au Parokia.

8.1.3. Huduma katika Kikundi

Huduma zinazoweza kuwapo katika kikundi ni:

1) Liturujia, Kusifu na Kuabudu


2) Sakramenti
3) Uinjilishaji
4) Ualimu
5) Maombezi
6) Uponyaji na Kufunguliwa
7) Wazee
8) Vijana
9) Watoto
10) Ufuatiliaji
11) Wagonjwa
12) Ukarimu
13) Mipango na Fedha
14) Ushauri
15) Ndoa na Malezi ya Familia
16) Makongamano n.k.

27
8.1.4. Uongozi katika Huduma za Kikundi

Kila Kikundi cha Sala kitakuwa na timu mbalimbali za kutoa huduma. Kila timu ya kutoa huduma ( yaani Timu ya
Huduma) itaongozwa na viongozi sita:

1) Mratibu
2) Mratibu Msaidizi
3) Katibu
4) Katibu Msaidizi
5) Mweka Hazina
6) Mweka Hazina Msaidizi

8.1.5. Kamati ya Huduma ya Kikundi

Kamati ya Huduma ya Kikundi itakuwa na wajumbe wafuatao:

1) Wajumbe wote sita wa Kamati Tendaji ya Kikundi cha Sala


2) Wahudumu wa kila Timu ya Huduma iliyopo kwenye Kikundi cha Sala

8.1.6. Mlezi wa Kikundi

1) Paroko ndiye Mlezi wa vikundi vyote Parokiani. Paroko aonapo inafaa anaweza kuteua Mlezi wa
Kumwakilisha.

8.1.7. Vikao

1) Kamati ya Huduma ya Kikundi itakutana mara moja kwa wiki kusali pamoja; kuombeana na kuombea
mambo mbalimbali, kutathmini matukio ya wiki yaliyotangulia, na kupanga matukio ya wiki inayofuata.

2) Kikao cha kutathmini Mkutano wa Sala na kupanga unaofuata, kifanywe siku ya Mkutano kabla na mara
baada ya mkutano. Kikao hiki kihudhuriwe na wajumbe wote wa Kamati Tendaji, wahudumu wa Mkutano
wa Sala wa siku hiyo, na wale wa Mkutano unaofuata ambao wataombewa siku hiyo.

3) Kamati itakutana mara moja kwa mwezi kupanga utaratibu wote wa huduma kwa mwezi mzima.

4) Mkutano Mkuu wa Kikundi utafanyika mara moja kwa mwaka. Mkutano huo utahudhuriwa wa
wanakikundi wote. Katika mkutano huo viongozi watatoa taarifa ya maendeleo, mapato na matumizi na
kupokea maoni na ushauri wa wanakikundi.

5) Viongozi wa kila Timu ya Huduma ya Kikundi, watakutana angalau kila baada ya wiki mbili, kwa ajili ya
kuombea huduma husika, na kila mwezi kutathmini na kupanga mwenendo mzima wa huduma katika
kikundi.

8.1.8. Maujukumu ya Uongozi kila Timu ya Huduma ya Kikundi

Uongozi wa kila Timu ya Huduma ya Kikundi ina majukumu yafuatayo:

1) Kubuni mipango-mikakati na mbinu za kuimarisha na kuboresha matumizi ya karama ya huduma husika


katika mkutano wa sala, kwa Parokia kwa ujumla na kuishirikisha Kamati ya Tendaji ya Kikundi.
28
2) Kutekeleza mipango ya utoaji wa huduma husika kulingana na taratibu zilizowekwa na Kamati ya Tendaji
ya Kikundi.
3) Kusimamia utoaji wa huduma kwenye mikutano ya sala na kwenye shughuli zingine za Kikundi na Parokia.
4) Kutoa uongozi bora kwa Timu ya Huduma ili iweze kutoa huduma nzuri kwa ufanisi na endelevu.
5) Kusali na kufunga katika kuombea huduma katika mikutano ya sala na shughuli zingine za kikundi na
Parokia.
6) Kushirikiana na uongozi wa timu zingine za huduma katika Kikundi cha Sala
7) Kuandaa bajeti ya mipango na shughuli mbalimbali za huduma husika na kuishirikisha Kamati Tendaji ya
Kikundi cha Sala.
8) Kuweka orodha ya wahuduma na Kumbukumbu muhimu za huduma husika.
9) Kuombea maendeleo ya Parokia ya kiroho nay a kimwili.

8.1.9. Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Kikundi cha Sala

Mkutano Mkuu wa Mwaka una majukumu yafuatayo:

1) Kupokea Taarifa ya Maendeleo ya Kikundi cha Sala kutoka kwa Mratibu


2) Kupokea Taarifa ya Fedha kutoka kwa Mweka Hazina
3) Kupokea mawazo na maoni ya wanakikundi.
4) Kujadili na kupitisha mipango ya mwaka unaofuata kama ilivyoandaliwa na Kamati Tendaji ya Kikundi.

8.2. Kamati Tendaji ya Parokia (KTP )

Parokia zenye zaidi ya Kikundi kimoja cha Sala zitakuwa na Kamati Tendaji ya Parokia – KTP

8.2.1. Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Parokia ( KTP ) ni:-

1) Mratibu wa Parokia
2) Mratibu Msaidizi
3) Katibu
4) Katibi Msaidizi
5) Mhazini
6) Mhazini Msaidizi
7) Waratibu wa Kamati za Huduma

8.2.2. Majukumu ya Kamati Tendaji ya Parokia ( KTP )

1) Kusimamia Vikundi vya Sala


2) Kuongoza ibada za Kikarismatiki Parokiani
3) Kutunza uwapo na moto wa Roho Mtakatifu katika ibada.
4) Kuandaa semina na mikutano mbalimbali katika PArokia
5) Kuhakiki mafundisho na matumizi ya karama mbalimbali
6) Kuhakikisha kuwa Karismatiki inakuwa chombo cha kutia uhai katika Parokia
7) Kufanya uinjilishaji katika jumuia na nyumba kwa nyumba katika Parokia
8) Kutoa taarifa ya mipango, kazi na maendeleo ya Kikundi au Vikundi kwa Paroko na viongozi wa Jimbo.
9) Kutoa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha kwa wanakikundi.
10) Kubuni na kupanga mipango ya maendeleo ya kimwili na kiroho kwa wanakikundi.
11) Kujenga umoja wa wanakikundi na umoja wa Parokia
12) Kuhudhuria mikutano ya Kijimbo.
13) Kuteua waratibu wa Kamati za huduma.

29
8.3. Kamati Tendaji ya Jimbo (KTJ)

8.3.1. Uundaji wa Kamati Tendaji za Jimbo ( KTJ)

1) Katika kila Jimbo ambamo mna vikundi vya sala kuundwe KTJ.
2) Uchaguzi wa Viongozi ufanywe na utambulishwe kwa Askofu Mahalia.
3) Padre Mlezi atateuliwa na Askofu Mahalia.

8.3.2. Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Jimbo ( KTJ) watakuwa ni:-

1) Mratibu wa Jimbo
2) Mratibu Msaidizi wa Jimbo
3) Katibu wa Jimbo
4) Katibu Msaidizi wa Jimbo
5) Mhazini.
6) Mhazini Msaidizi.
7) Waratibu wa Huduma ya Kijimbo
8) Mjumbe / Wajumbe kutoka Jumuiya za Kikarismatiki.

8.3.3. Mujukumu

1) Ni kama yale ya Parokia kwa ngazi ya Jimbo

8.4. Kamati Tendaji ya Taifa ( KTT)

8.4.1. Kiungo Ratibisha cha Juu

KTT ndiyo Kiungo Ritibisha cha Juuu katika Upyaisho Karismatiki Katoriki Tanzania ( UKKT). Utume wake ni
kuendeleza UKKT hata ienee kila pembe ya nchi kwa tendo la Roho Mtakatifu. UKKT iko chini ya uongozi wa
Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC). Kiutendaji Baraza la Maaskofu litateua Askofu kuwa Mlezi wa mkondo huo,
akishirikiana na Kamati Tendaji ya Taifa kuratibisha shughuli zote za Karismatiki nchini.

8.4.2. Wajumbe wa KTT watakuwa ni:-

1) Mratibu wa Taifa
2) Mratibu Msaidizi wa Taifa
3) Katibu Mkuu
4) Katibu Mkuu Msaidizi
5) Mhazini.
6) Mhazini Msaidizi.
7) Waratibu wa Kamati za Huduma.
8) Wajumbe waalikwa

8.4.3. Majukumu ya KTT

1) Kujenga mahusiano ya karibu kati ya mamlaka ya Kanisa ( Maskofu) na UKKT kwa lengo la kushirikisha
kikamilifu ndani ya maisha ya Kanisa.

2) Kuhakikisha kuwa masuala yote ya kichungaji na kiteolojia hayapotoshwi katika vikundi vya sala nchini
kote kwa kushirikiana na Mshauri wa Kitume au Mlezi.

30
3) Kujenga na kuimarisha umoja wa Vikundi vya Sala na Jumiya za Kikarismatiki nchini, kwa njia ya
mikutano, matukio, na huduma mbalimbali.

4) Kuandaa na kusimamia maono kwa ajili ya Upyaisho na kuhakikisha vikundi vya sala na Jumuiya za
Kikarismatiki zinaendelea vyema.

5) Kuwa kiungo cha mawasiliano nchini kote na kwa mamlaka ya Kanisa kutoa taarifa zinazohusu Upyaisho;
kuandaa taarifa za maendeleo kwa ujumla.

6) Kushughulika na mialiko kwa viongozi wa Upyaisho au wawezeshaji kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili
ya kujiimarisha.

7) Itaendesha shughuli zote za siku kwa siku za UKKT ( Upyaisho Karismatiki Katoliki Tanzania) chini ya
uongozi wa Mratibu wa Taifa.

8) Itatayarisha na kupanga kwa niaba ya KTH ( Kamati ya Taifa ya Huduma) mikutano, matukio na ratiba zote
za Kitaifa.

9) Ni kitovu cha mawasiliano cha UKKT na Mataifa ya nje na huduma mbalimbali za Kikristo za ndani na nje
hasa ICCRS ( International Charismatic Renewal Services) iliyoko Vatikano, Roma; AFSCI ( Africa Sub-
Committee of International Charismatic Renewal Services) n.k.

10) Itatunza kumbukumbu mbalimbali na za mahesabu yote ya fedha na mara kwa mara kufanya ukaguzi wa
mahesabu hayo na kuyawasilisha kwa KTH au mamlaka nyingine za Kanisa.

11) Itaandaa mizania ya hesabu, taarifa ya mapato na matumizi ya mwaka na bajeti ya mwaka.

12) Kutoa taarifa za mipango, kazi na maendeleo ya Karismatiki Katoriki kwa Baraza la Maaskofu na KTH.

13) Kuchagua Waratibu wa Kamati za Huduma

14) Itasimamia na kudumisha nidhamu na utii, na kuchukua hatua za kinidhamu kila inapobidi

8.5. Kamati ya Taifa ya Huduma (KTH)

8.5.1. Wajumbe wake ni:-

1) Wajumbe sita wa KTT


2) Waratibu wa Kamati za Huduma za Taifa
3) Mapadre Walezi wa majimbo yote, wapatao nafasi.
4) Kamati Tendaji za Majimbo
5) Mwakilishi wa Jumuiya za Kiinjili za Karismatiki
6) Wajumbe waalikwa, kwa mfano viongozi wa zamani, wazee na wanaoitwa kwa kusudi maalumu.

31
Kamati hii ya Taifa ya Huduma ( KTH) itakutana mara moja kwa mwaka kwa ajili ya Mkutano Mkuu. Na wakati
wowote ikitokea dharura.

8.5.2. Majukumu ya Kamati ya Taifa ya Huduma.

1) Kuchagua na kupendekeza majina matatu kwa Baraza la Maaskofu ili mmoja achaguliwe kuwa Mratibu wa
Taifa
2) Kuchagua Kamati Tendaji ya Taifa kwa nafasi zilizobaki
3) Kupokea taarifa za mipango- kazi mapato na matumizi ya fedha na maendeleo ya majimbo.
4) Kujadili na kutoa maamuzi juu ya ajenda zote zinazotolewa na KTT na wajumbe mbalimbali.
5) Kuiagiza na kuishauri KTT juu mwelekeo na maendeleo ya Karismatiki nchini.

8.6. Kamati za Huduma za Taifa ( KHT)

8.6.1. Wajumbe wake ni:-

1) Mlezi ( atachaguliwa na Kamati Tendaji ya Taifa).


2) Mratibu ( atachaguliwa na Kamati Tendaji ya Taifa)
3) Mratibu Msaidizi ( atachaguliwa na wajumbe wa huduma husika)
4) Katibu ( atachaguliwa na wajumbe wa huduma husika)
5) Katibu Msaidizi ( atachaguliwa na wajumbe wa huduma husika)
6) Mhazini ( atachaguliwa na wajumbe wa huduma husika)
7) Mhazini Msaidizi ( atachaguliwa na wajumbe wa huduma husika)

8.7. Askofu Mlezi wa Kitume (AMK)

8.7.1.Atateuliwa na Baraza la Maaskofu.

8.7.2. Majukumu ya AMK

1) Atakuwa kiungo cha moja kwa moja kati ya Baraza la Maaskofu na UKKT.
2) Atahudhuria Mikutano ya KTT na KTH anapokuwa na nafasi.
3) Atakuwa Mshauri Mkuu wa KTT wakati wote juu ya mambo yote yanayohusu Karismatiki.

32
SURA YA TISA

8.0. UCHAGUZI NA MIHULA YA UONGOZI


9.1. Utaratibu wa Uchaguzi

9.1.1. Uchaguzi katika ngazi mbalimbali za uongozi utakuwa wa kura ya siri.

9.1.2. Muhula wa uongozi ni miaka mitatu na kiongozi anaweza kuchaguliwa kwa mihula mitatu tu.

9.1.3. Kama kuna ulazima mtu anaweza kuchaguliwa tena katika uongozi baada ya kupita mihula

miwili ya uchaguzi, yaani baada ya miaka sita.

9.2. Sifa za Viongozi wa Karismatiki Katoliki

Karismatiki Katoliki inahitajika uongozi kwa lengo la kuratibu na kurahisisha shughuli mbalimbali za kikarismatiki
katika vikundi vya sala. Hii ni pamoja na mikutano ya sala, semina, mafungo, huduma mbalimbali, na kuwakilisha
Karismatiki Katoriki katika mifumo ya Kanisa (ngazi ya Kigango, Parokia, Jimbo na Taifa). Kufanikiwa kwa
Vikundi vya Sala kunategemea sana uongozi imara unaotokana na ujuzi na uaminifu kwa mafundisho sahihi ya
Kanisa na uelewa wa kutosha wa Karismatiki Katoliki. Kutokana na hayo, kiongozi wa kikundi cha sala awe na sifa
anazotaja Mtume Paulo katika barua zake kwa Timotheo na Tito ( 1 Tim 3:13; Tito 1:5-9). Mbali na sifa hizo, pia
awe na sifa zifuatazo:

1) Awe Mkatoliki Hodari:


Aliyekomaa katika imani yake ya Kikatoliki.

Mshiriki halisi wa maisha ya Sakramenti za Kanisa Katoliki; hasa Sakramenti za Uponyaji (

Upatanisho na mpako wa wagonjwa) na Ekaristi Takatifu.

2) Awe Mwamini Mkomavu na Mwenye Sifa Njema


Kiongozi lazima awe amefikia hali ya kukomaa kiroho, mwenye sifa njema katika Kanisa, Jumuiya na mahali
pa kazi. Anayeweza kuongoza kikundi cha sala ni mtu aliyekomaa inavyopasa katika akili, hekima na hisia zake
( emotional balance).

3) Awe Mwajibikaji
Kiongozi lazima ajue namna ya kupanga na kutekeleza wajibu wake. Awe na wakati wa kutosha kuhudumia
familia yake, kazi zake za kila siku na za kikundi chake cha sala na asiwe na shughuli nyingi mno. Kujitoa
katika mambo mengi mno kunamfanya kiongozi kushindwa katika yote, na hivi kusababisha hasara katika
Kanisa.

4) Watambulishwe kwa Paroko


Kiongozi watambulishwe kwa Paroko wake mara baada ya uchaguzi ili kupata Barak na nasaha zake, kabla ya
kuchukua nafasi yake ya uongozi. Amwarifu Paroko jinsi anavyoendelea na mara kwa mara aombe maongozi
yake ya kichungaji.

5) Awe na Roho ya Uongozi wa Pamoja


Kazi ya kuongoza Kikundi cha Karismatiki inapaswa kufanywa na timu ya Viongozi na siyo mtu peke yake.
Kuongoza kikundi kunahitaji ujuzi na karama mbalimbali. Mara chache sana mtu mmoja anaweza akawa navyo
33
vyote. Uongozi wa pamoja utatoa nafasi kwa vipaji mbalimbali walivyo navyo wanakikundi; tena kuna
uwezekano wa kujilinda kuliko uongozi wa mtu mmoja. Kwa ajili hiyo, viongozi wanapaswa kuwa na karama
ya kufanya kazi pamoja kwa upendo bila migongano. Hata hivyo, Mratibu asikilizwe kwa sababu ya dhamana
ya kikundi.

6) Awe na Utayari wa Kutumikia


Uongozi wa ki-kristo ni wa utumishi na si utawala wala heshima inayotolewa kwa kutegemea umri au hadhi
Fulani. Kwa hiyo uongozi ni utumishi unaotolewa kwa ajili ya wengine. Kiongozi wa Karismatiki Katoliki
lazima awe na moyo wa Kristo aliyekuwa mtumishi wa wote ( Lk 22:24-27, Mk 10:41-45, Yoh 13:12-17).

7) Awe na Nidhamu
Moja ya mambo yanayoimarisha Karismatiki Katoliki ni hali ya nidhamu, kuwajibika, heshima na kujali
uongozi uliopo katika Kanisa. Nidhamu inayotakiwa ni ile yenye uwiano kati ya utii kwa upande mmoja na
uhuru na wajibu wa Mkristo kwa upande mwingine.

8) Awe Mkarismatiki Hodari


Kiongozi wa Karismatiki hawezi kuwa kiongozi mzuri, kama yeye mwenyewe si Mkarismatiki wa mstari wa
mbele. Ili kuweza kutimiza sifa hii, kiongozi wa Karismatiki Katoliki anahitaji kujiendeleza, kwa kutumia
nyenzo na fursa mbalimbali: kama vile kujisomea, kuhudhuria semina na warsha zinazoandaliwa ili akomae na
awe na uwezo na utayari wa kutumia na kuchochea karama alizonazo.

34
SURA YA KUMI

10.0. FAIDA ZA KARISMATIKI KATOLIKI.


10.1.Kuna faida kadhaa kutoka katika mkondo huu, zinazoelekea zaidi katika uhai wa Kanisa

Mahalia, na la kiulimwengu kwa ujumla.

10.1.1. Faida hizo ni pamoja na:

1) Kueneza Injili (Unabii, Ukuhani na Ufalme) – kuamsha hamu ya Wakatoliki katika kuielewa imani yao na
kuiishi vizuri zaidi katika maisha yao ya kila siku.

2) Kuamusha na kukuza moyo was ala. Mkondo huu unasaidia kuondoa roho ya uvuguvugu katika maisha ya
kiroho

3) Kutakatifuza malimwengu, uwapo wake unasaidia kukemea maovu yaliyokithiri katika dunia ya leo, kama
utoaji mamba na matumizi ya vithibiti mamba, michepuko, ndoa za jinsia moja, unyanyasaji wa kijinsia,
ulevi sugu na utumiaji wa madawa ya kulevya, rushwa, ufisadi, udanganyifu, na mengineyo.

4) Kuchoche ari ya kupenda kusoma Biblia na kusikiliza Neno la Mungu. Kwa muda mrefu wazo la walei ni
kuwa, kazi ya kulisoma Neno la Mungu ni ya Padre, Katekista au Mtawa.

5) Kuchochea, kulea na kuwezesha miito ya Upadre, Utawa, na maisha ya Ndoa. Hii ni kwa njia ya maisha
yao ya sala (mafundisho) na kutolea mali zao kwa ukarimu

6) Kuyafikia kwa ukaribu zaidi maisha ya maskini na wahitaji wa aina mbalimbali, hasa wagonjwa,
walemavu, wazee, wanyanyapaliwa, wapweke, yatima, wajane na wengineo.

7) Kuchochea ujasiri wa kumshuhudia Kristo katika maisha ya kila siku. Kwa kufanya hivyo wanawavuta
Wakatoliki kutoshawishiwa na makundi mengine na pia kuwarudisha kundini wale walioanguka.

8) Kuchochea moyo wa ukarimu wa kujitolea na kutoa kwa hali na mali, kwa ajili ya maendeleo ya kiroho na
kimwili ya Kanisa na jamii kwa ujumla.

9) Kuwaalika Mapadre kuhubiri kwenye Makongamano au Mikutano mbalimbali ya Injili ili kuwapa jukwaa
la kufundisha kwa mapana zaidi Neno la Mungu.

10) Kuwapa Wakatoliki fursa ya kutambua Karama zao na kuzitumia kwa kulijenga Kanisa lao.

11) Kuwasaidia Wakriso kuwa wakomavu na hivyo kushinda changamoto za maisha ya kuhimili mateso kwa
ajili ya utukufu wa Mungu.

35
SURA YA KUMI NA MOJA.

11.0. MAPUNGUFU NA CHANGAMOTO ZA KARISMATIKI KATOLIKI.


11.1. Mapungufu

11.1.1. Licha ya faida zake mbalimbali na kukubali kwake na Kanisa, mkondo huu unaonekana

kuwa na mapungufu kadhaa. Kuna mambo ambayo yanasababisha mkondo huu

kutoeleweka vizuri. Haya ni pamoja na:-

1) Baadhi ya kutokuwa na uwiano au kiasi, katika misisitizo ya maombi ya miujiza, maajabu, kuponya
wagonjwa na kufukuza mashetani ( badala ya maisha ya upendo ufuasi na utakatifu.

2) Kutokuwa wanyenyekevu kwa kujiona wanajua Maandiko Matakatifu kuliko wengine nap engine
kupotosha tafsiri halisi ya Maandiko Matakatifu.

3) Baadhi yao kuonekana wanatafuta umaarufu kwa kujisifia matendo ambayo wametendewa na Mungu au
yale ambayo Mungu ametenda kwa kuwatumia wao.

4) Baadhi yao kutopenda kufuata mashauri, maagizo au maongozi ya mapadre wao kwa kujiona wakamilifu na
hata kuwa wepesi kuwahukumu mapadre na waamini wengine na kutopenda kuishirikiana nao.

5) Baadhi yao kupuuza mafundisho ya msingi ya mapokeo ya Kanisa, kama vile nafasi ya Mama Bikira Maria,
Watakatifu, Rosari, Sakramenti ya Kitubio matumizi ya sanamu na vielelezo na hata mafundisho kuhusu
Toharani.

6) Baadhi yao kuchanganya ibada za kikatoliki na ulokole hali inayojionesha katika mahubiri, nyimbo,
misamiati na namna ya kusalimiana.

7) Baadhi yao kupotosha ukweli kuwa kuwa pombe ni dhambi, badala ya kulezea madhara ya pombe au
dhammbi ya ulevi ili kuwataka watu wawe na kiasi ( 1 Tim 4:4; Efe 5:23).

8) Baaadhi yao kutokuwa na kiasi katika utoaji wa mali na muda wao, kwa Mungu/ Karismatiki hata
kusababisha matatizo nap engine matengano katika familia na ndoa zao.

9) Kukazia mno mambo ya uponyaji, na kuona mateso lazima yatokane na laana na mapepo, bila ya kutambua
kuwa, mateso pia huwa ni njia ambayo Mungu huitumia kumuongoza mtu katika kufikia utakatifu.

10) Baadhi yao huzingatia zaidi vionjo vya nje vya kiibada kuliko vya ndani, kama vile kunena kwa lugha na
kuomba kwa makelele, kama ushahidi wa mtu kuwa na Roho Mtakatifu.

36
11.2. Changamoto

11.2.1. Mapungufu hapo juu, pamoja na mengineyo, yanatokana na changamoto mbalimbali. Hizi

nia pamoja na:

1) Kukosekana kwa mwongozo toka kwa wachungaji wa Makanisa Mahalia wanaoifahamu vizuri Karismatiki
Katoliki na nafasi yake katika Kanisa.

2) upungufu wa taarifa na mafundisho sahihi, mintarafu Karismatiki Katoliki. Changamoto hii husababisha
uelewa mbovu na upotoshaji.

3) Matumizi ya mamlaka na nguvu kubwa kupita kiasi kwa baadhi ya Mapadre kupambana, kuwatisha, na
kuwakatisha tama Wakarismatiki. Hali hii huweza kusababisha upotoshaji zaidi unaoweza kuleta mpasuko
katika Kanisa Mahalia.

4) Baadhi ya wachungaji kukosa muda wa kuwa karibu na Wakarismatiki, na hivyo kuwa kama kondoo wasio
na mchungaji. Hali hii huwapa nafasi ya kujiamulia mambo kadiri wanavyojisikia kuwa ni sawa. Matokeo
yake wakati mwingine ni mafarakano ( Mk 14:27).

5) Utamaduni wa mtazamo hasi na mila potofu juu ya magonjwa. Mwelekeo wakuyahusisha magonjwa
mbalimbali na ushirikina, laana, na mapepo. Wanasahau kuwa magonjwa yapo ya kisaikolojia, kibailojia
nay a kurithi.

6) Vikundi / kikundi kutokuwa na mlezi / walezi wenye ufahamu mzuri wa mkondo huu wa maisha ya kiroho
kwa ujumla.

7) Mtazamo hasi wa watu kuwa Karismatiki ni mkusanyiko wa watu wenye shida, ambao wanatafuta majibu
ya haraka.

37
SURA YA KUMI NA MBILI

12.0. NINI KIFANYIKE?

12.1. Hatua za Kuchukuliwa

12.1.1. Kutokana na mapungufu na changamoto kadhaa zilizoanishwa hapo juu, hatua kadhaa

zaweza kuchukuliwa. Lengo kubwa likiwa ni kuleta uelewa mzuri na kuboresha huduma za

mkondo huu. Baadhi ya hatua hizo ni:`

1) Mwongozo huu wa Karismatiki Katoliki Kitaifa ufuatwe na uheshimiwe ili utendaji wa mkondo huu
(Karismatiki Katoliki) uendane na mafundisho sahihi ya Imani Katoriki.

2) Mapadre na Makanisa Mahalia wawe karibu na Wakarismatiki. Ukaribu wao utasaidia kujua nini
kinachoendelea na kutoa maelekezo pale taratibu zinapokiukwa.

3) Elimu ya utambuzi wa maana, lengo na mafundisho ya Kikarismatiki chini ya Imani Katoriki.

4) Wahudumu wote, hususani wahubiri, watambulike rasmi na Kanisa. Wawe wamepitia mafunzo maalumu
ya Elimu ya Biblia, Katekisimu ya Kanisa Katoliki, maisha ya Kiroho na Saikolojia katika chuo
kinachotambuliwa na Kanisa Katoliki, kila inapowezekana.

5) Kuwa na msimamo mmoja wa Maaskofu , mintarafu Karismatiki Katoliki kwa kumteua mmoja wao kuwa
Mlezi.

6) Uwepo utaratibu / mwongozo wa namna ya kuendesha shughuli zao, hususani za kiibada na kipaumbele
kipewe kwa adhimisho la Misa Takatifu. Aidha, uwepo ufuatiliaji wa karibu kuhakikisha kuwa utaratibu
unaheshimiwa.

7) Mkazo zaidi uwekwe katika maandalizi na malezi ya Mapadre watarajiwa katika kuwaandaa kukabiliana na
changamoto mbalimbali katika utume wao.

8) Msisitizo katika kuheshimu nafasi ya Mamlaka – funzi, Hierakia, na Baraza la Walei katika Kanisa
Mahalia.

9) Elimu zaidi ya ujumla, mintarafu mafundisho ya Imani Katoliki. Msisitizo katika uelewa wa dhati wa
Katekisimu ya Kanisa Katoliki.

10) Awepo Mlezi Mkuu Kitaifa ( Askofu) au chombo maalumu cha kitaifa kitakachoratibu na kufuatilia
huduma za Kikarismatiki. Aidha, kila jimbo liwe na Mlezi ( Padre) ambaye atafuatilia kwa karibu mkondo
huu kijimbo.

38
11) Semina za malezi endelevu ya ufahamu wa Karismatiki, kijimbo na kiparokia. Hizi zitawasaidia
Wakarismatiki na wale wanaopenda kuwa sehemu ya mkondo huu kutokumbatia mwelekeo wa kilokole na
siasa kali.

12) Wachungaji wafundishwe zaidi kwa njia ya maisha yao na kuwa karibu na mkondo wao, wasikilize
matatizo yao. Umbali na kutojali kwa baadhi ya Mapadre kunawafanya waamini wao kutafuta njia mbadala.

13) Mafundisho na semina za Kikarismatiki vilenge zaidi katika kuwaimarisha waamini, kuwarudisha kundini
Wakatoliki walioanguka na kuwaongoa watu madhehebu mengine.

14) Wanakikundi wapya wapewe mafundisho ya kina mintarafu maana, mwongozo, na utume mzima wa
Karismatiki ndani ya Kanisa Katoliki.

15) Ili kurahisisha ufuatiliaji, ni vema shughuli zote za Kikarismatiki ziwe zinafanyika katika maeneo ya
Parokia.

16) Kuachwa kwa nyimbo na vitendo vinavyowafanya Wakarismatiki wakati mwingine wadhaniwe kuwa
waamini wa madhehebu mengine. Ni muhimu kwao kutambua na kukumbuka daima kuwa wao ni
Wakatoliki, bila kuwachukia au kuwadharau watu wa madhehebu mengine; tukikumbuka kuwa sisi sote ni
watu wa kundi moja chini ya mchungaji mmoja.

17) Waamini waelimishwe kuwa si kila tatizo sugu au ugonjwa usiotibika ni kazi ya shetani / mapepo. Itolewe
Katekesi ya mateso, kifo na ufufuo wake katika muungano wa mateso, kifo na ufufuko wa Kristo.

18) Mkarismatiki aelewe na kuthamini matumizi ya Rozari, Msalaba wenye sanamu ya Yesu na heshima
itolewayo na Kanisa Katoliki kwa Bikira Maria na Watakatifu.

19) Waamini watambue umuhimu wa kuomba na kupokea Baraka kutoka kwa Mapadre wao na siyo wao
kupeana baraka.

12.2. Mambo ya Kuzingatiwa na Karismatiki

1) Kabla ya kuanza mkutano au sala, kiongozi wa Karismatiki awafahamishe waamini hasara na majanga ya
kutaja jina la anayedhaniwa kuwa mbaya wake au mshiriki / mlozi / mchawi wake. Ikitokea akawepo wa
mwelekeo wa kutaja jina la mlozi aondolewe mara moja na kusikilizwa binafsi na Mkarismatiki mwenye
uwezo wa kutunza siri aliyeteuliwa rasmi kushughulikia kesi za aina hiyo.

2) Anayehitaji kuombewa, asali na wanaosali kumwombea, ili pamoja nao nia yake ya uongofu, yaani, kupona
kiroho na kimwili ifanikiwe ( re. Yak 5:13).

3) Nyimbo, Sala, ishara, maneno na vitendo vinavyowafanya waamini wadhaniwe kuwa ni wa madhehebu
mengine viachwe. Nyimbo, Sala (mf. Sala ya Uje Roho Mtakatifu uzieenee nyoyo za waamini wako…..,
Baba yetu…., Salamu Maria….., Atukuzwe Baba….n.k.), ishara ( mf. Ishara ya Msalaba) na matendo mf.
Maadhimisho ya Sakramenti saba na hasa Sakramenti ya Kitubio, Ekaristi na Mpako wa Wagonjwa) ya
Kikatoliki kulingana na maelezo ( Rubrics) ya Liturujia lazima vionekane wazi katika ibada zao. Itumike

39
Biblia Takatifu yenye vitabu vya Deuterokanoni au yenye Imprimatur / “Ichapwe” ikiwa na jina la Askofu
toka Kanisa Katoliki. Biblia zenyewe ni: (1) “BIBLIA TAKATIFU” yenye utangulizi wa Mahashamu
Tarcisiuc J. Ngalalekumtwa, Askofu wa Iringa; (2) “BIBLIA Habari njema kwa Watu Wote yenye
Vitabu vya Deuterokanoni” yenye ikibali ya Mhashamu C.C.Davies, Askofu wa Ngong, Kenye; (3)
“BIBLIA YA KIAFRIKA” yenye ikibali ya Mhashamu Jude Thaddaeus S.Ruwa’ichi OFMcap, Askofu
wa Dodoma; (4) “THE NEW JERUSALEM BIBLE.” Ni muhimu waamini wakati wote kutambua kuwa
wao ni Wakatoliki.

4) Waamini waelimishwe kuwa si kila tatizo lisiloisha au ugonjwa usiotibika chanzo chake ni shetani.
Katekesi ya mateso, kifo na ufufuko wake katika muunganiko na mateso, kifo na Ufufuko wa Kristo,
itolewe ( rejea 7.1.19).

5) Mkarismatiki ajongee daima Sakramenti ya Kitubio / Upatanisho na kuungama dhambi ( rej. 1Yoh 1:8-10)
kwa Padre.

6) Wagonjwa wawaite Mapadre wawaombee na kuwapa Mpako Mtakatifu na Komunyo – pamba ( rej. Yak
5:14-16)

7) Mkarismatiki aelewe na kuthamini matumizi ya Rozari, Msalaba wenye sanamu ya Yesu na heshima
itolewayo na Kanisa Katoliki kwa Bikira Maria ( rejea 7.1.18).

8) Waamini wajue umuhimu wa kuomba na kupewa Baraka kutoka kwa Mapadre wao na si wao kutoleana
baraka
( rejea 7.1.19).

9) Mkarismatiki asichapishe kitabu chochote kuhusu imani Katoliki bila ikibali ya maandishi au ruhusa ya
kuchapwa yaani Imprimatur toka kwa askofu yeyote Mkatoliki.

12.3. Yanayoweza kuchangia Kusimamishwa kwa Baadhi ya Shughuli za Kikarismatiki.

Ili Utume wa Karismatiki uendelee vizuri, kwa ajili ya kuimarisha imani, upendo, umoja, amani na maendeleo ya
kiroho na kimwili katika Majimbo na baina ya Majimbo Katoliki Tanzania, utaratibu huu uzingatiwe:

1) Kila anayetaka kutoa huduma ya Kikarismatiki ya kuwinga mapepo na uponyaji wa kimijiza, lazima
aonyeshe kwa Askofu wa Jimbo husika barua ya Askofu Mkatoliki inayomruhusu kutoa huduma ya namna
hiyo ( kulingana na maelekezo ya Askofu Mahalia).

2) Kiongozi wa Karismatiki asialikwe kuendesha shughuli za Kikarismatiki ndani ya Jimbo lisilo lake bila
barua au kibali cha askofu wa Jimbo husika.

3) Shughuli za Kikarismatiki katika Parokia zisiendeshwe bila Paroko kuwa na ruhusa ya Askofu inayoruhusu
shughuli hizo kufanyika parokiani mwake ( kwa kadiri ya maelekezo ya Askofu Mahalia).

40
HITIMISHO

Kwa ujumla wake, malengo ya uanzishwaji wa mkondo huu ni mazuri. Tatizo kubwa linakuwa ni katika utekelezaji
wake. Inapotumiwa vema, Karismatiki Katoliki ni chachu nzuri ya imani.

Imewasaidia Wakatoliki wengi kubaki katika imani yao, badala ya kukimbilia katika madhehebu mengine. Utafiti
umeonyesha kuwa ni vigumu sana kumshawishi anayeijua vema na kujiunga mkono Karismatiki Katoliki kulipa
kisogo Kanisa na kuukimbilia ulokole au madhehebu mengine! Kinyume chake, mkondo huu umesaidia sana
kuwarudisha na kuwavuta wengi katika Imani Katoliki. Karismatiki Katoliki inasaidia kuboresha na kuipa liturujia
mvuto zaidi. Kwa ujumla, wana karismatiki wamekuwa mstari wa mbele katika suala zima la utamadunisho.

Ukaribu huu watakiwa kukua na kuongezeka siku kwa siku, ukijengwa katika shina na msingi wa upendo; hata
mkristo afikie kipawa cha ‘kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na
kuujua upendo wake Kristo upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, apate kutimilika kwa utimilifu wote wa
Mungu’ Ni mchakato wa ukaribu utakaojengwa katika ulinganifu wa ongezeko la ufahamu na maarifa ya kumjua
Mungu, na kiwango cha imani.

Jambo la msingi ni ukaribu wa wachungaji katika kuwaongoza na kuwasimamia Wakarismatiki.

Utafiti unaonyesha kuwa maeneo ambayo Mapadre wamekuwa karibu nao, Karismatiki Katoliki imefanya vizuri, na
kuwa kweli ‘Upyaisho’ katika Kanisa. Kinyume chake, sehemu ambazo Mapadre wamejitenga nayo na hata kuipiga
vita, madhara yake yamekuwa makubwa katika Kanisa.

Bila shaka, kubwa kuliko yote, ni vurugu na kupelekea mpasuko katika Kanisa (Mk 14:27). Kwa ujumla lengo
msingi la Karismatiki Katoliki ni kuwaelekeza watu waweze kuufikia wokovu. Yote kwa yote, kwa asili Kanisa
zima linategemewa kuwa Karismatiki kwa vile Roho Mtakatifu yu ndani yake, akitenda kazi daima.

41
BIBLIOGHAFIA

1. Centrem Ignatianum Spiritualitatis, Jesuits and the Charismatic Renewal, Vol. XV, Rome 1984.
2. HATI ZA MTAGUSO MKUU WA VATIKANO II
3. KAMATI YA HUDUMA YA KARISMATIKI KATOLIKI TAIFA, Maadili, Dar es Salaam, 2006.
4. Mwongozo wa Karismatiki Katoliki Tanzania, Toleo la Tatu, Dar es Salaam 2006
5. LENGUEJU Alex Victor, Semina za Maisha ya Kiroho: Masomo ya Walimu, Dar es Salaam, 2005.
6. MWAKYANJALA B., Historia ya Upyaisho wa Kikarismatiki Katoliki, Dar es Salaam, 2005
7. NATIONAL CONFERENCE OF CATHOLIC BISHOPS, A Pastoral Statement on the Catholic
Charismatic Renewal, United States Catholic Conference Inc.., Washington, 1985.

42

You might also like