Professional Documents
Culture Documents
BAVUGUBUSA
USIKIKOSE KITABU HIKI, PATA NAKALA YAKO LEO ILI UIFAHAMU IMANI HII
ILIYOTUKUKA
Mwandishi Frater Simon Liberio J.BAVUGUBUSA
Segerea Seminari Kuu, Kitivo Cha Teolojia Dar es Salaam, Tanzania
Mlezi na Mhadhiri wa Mafundisho Msingi ya Imani ya Kanisa Katoliki, Segerea Seminari Kuu
ya Teolojia, Dar es Salaam, Tanzania
1
YALIYOMO
SURA YA KWANZA
ROHO MTAKATIFU
2
I. MAANA NA UFAFANUZI WA ROHO MTAKATIFU ……………………………….. 25
II. UTAMBULISHO WA ROHO MTAKATIFU KIBIBLIA…………………………………. 26
III.ROHO MTAKATIFU NI MUNGU,NI NAFSI YA TATU YA MUNGU(USHAHIDI … 28
1. Agano la Kale………………………………………………………………………………. 32
2. Utatu Mtakatifu uliofunuliwa na Agano Jipya …………………………… 33
3. Agano Jipya , Injili Nne zinavyomshuhudia Roho Mtakatifu ….…. .. 36
4. Pentekoste na Roho Mtakatifu ……………………………………………… 39
5. Barua za Mtume Paulo zinavyomwelezea Roho Mtakatifu …… 45
6. Mitaguso mbalimbali ilivyofundisha juu ya Roho Mtakatifu ……… 47
7. Roho Mtakatifu anatoka kwa Baba na Mwana (Filioque) ……………… 49
8.Ushahidi wa Biblia juu ya Fundisho la Kwamba Roho Mtakatifu anatoka kwa
Baba na Mwana (Filioque)….................................................................. 50
SURA YA PILI
SURA YA TATU
I. FUMBO LA UTATU MTAKATIFU ………….
3
1. Maana na Ufafanuzi wa Fumbo la Utatu Mtakatifu wa Mungu na Maana ya Fumbo la
Imani ………………………………………………………………………………………….. 103
2. Nini maana ya Fumbo la Imani……………………………………………………………... 103
3. Fumbo lipi Kuu ni kiini cha imani na Maisha ya Kikristo ? …………………… 106
4. Ishara ya Msalaba ina ufunua Utatu Mtakatifu wa Mungu ……………………… 106
5. Fundisho la Msingi la Imani Katoliki juu ya Utatu Mtakatifu wa Mungu … 107
6. Tunautaja na kuusifu Utatu Mtakatifu wa Mungu katika Sala ya Atukuzwe Baba na
Mwana na Roho Mtakatifu ………………………………………………………………… 108
7. Imani ya Kanisa Katoliki inavyofundisha juu ya Utatu Mtakatifu wa
Mungu………………………………………………………………………………………………………… 110
8. Kanuni ya Imani ya Athanasi (Quicunque vult) …………………………………… 111
9. Kanuni ya Imani ya Nikea …………………………………………………………………… 114
10. Kanuni ya Imani (NASADIKI) ya Nikea Konstantinopoli …………………… 114
11. Biblia Takatifu inautaja Utatu Mtakatifu wa Mungu …………………………… 115
12. Agano la Kale linavyoonesha Utatu Mtakatifu …………………………………… 115
13. Agano Jipya linavyoonesha Utatu Mtakatifu ………………………………………… 120
14.Mtume Paulo anavyoonesha Utatu Mtakatifu wa Mungu …………………….. 125
16. Nafsi Tatu za Mungu zinafanya kazi kwa Namna gani?................................. 134
4
26. Mtakatifu Ignasius wa Antioki ………………............................................... 146
Baba yangu Mzee Liberio Bahanza Joseph Bavugubusa na wote wenye kumtafuta Mungu kwa
Moyo wa Ibada na Kweli.
NA
5
NENO LA JOPO LA WAHAKIKI NA WATATHIMINI WA KITABU HIKI
6
DIBAJI
7
Kitabu hiki kina utajiri mwingi sana wa Mafundisho ya Imani ya Kanisa Katoliki juu ya
Roho Mtakatifu na Utatu Mtakatifu na kazi zake katika historia ya ukombozi wa
Mwanadamu uliofanywa na Yesu Kristo,aliyezaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kwa
kupitia Mama yetu Bikira Maria (Rejea Mt 1:18 -25).Hivyo basi ,Bikira Maria ni Mama wa
Mungu kwani Yesu ni Mungu tena Mungu Mwana.Mungu aliyetaka aonekane kwa watu kwa
kuzaliwa miongoni mwa watu,akaishi kama sisi isipokuwa dhambi haikuwa na nafasi kwake
(Rejea Ebr 4:14- 15) .Yesu hakutenda dhambi kwa sababu yeye ni Mungu Mtu.
Roho Mtakatifu hutufariji pale tunapoumia, hutupatia nguvu pale tunapoelekea kupoteza
matumaini, hutulinda dhidi ya mwovu shetani.Hutufunza namna ya kusali kwani saa
nyingine hatufanikiwi katika sala zetu kwa kuwa hatujui namna ya kusali. Kwa kuyafahamu
hayo na ukawa mtu wa sala na kwa majitoleo yako, ukayaweka kwa imani kwa Mungu na
Kanisa utakuwa umepiga mbio na hatua kubwa sana katika kuelekea utakatifu.
8
Heko zangu kwako Frater Simon Liberio J.Bavugubusa kwa kuandika Kitabu hiki,ni chakula
cha kukuza roho za Wakristo katika kumfahamu Mungu wetu tunayemwamini aliye Mmoja
katika Utatu Mtakatifu usiogawanyika. Sasa nakukaribisha upate fursa ya kusoma Kitabu
hiki Mwandishi alichokiita ROHO MTAKATIFU NA FUMBO LA UTATU MTAKATIFU upate
kufumbuka na kuelewa Kanisa Katoliki linasemaje juu ya Roho Mtakatifu na Fumbo la Utatu
Mtakatifu
SHUKRANI
9
na Msaada kwa wale wamwitao kwa unyenyekevu bila kuchoka. Kweli Utukuzwe na kusifiwa
Milele Ee Utatu Mtakatifu wa Mungu na Umoja usiogawanyika.
Shukrani zangu za dhati pia ni kwa ndugu zangu wa damu Kaka na dada zangu,Joseph
Liberio na familia yake, Amos Liberio na familia yake,Justine Baraka Liberio na familia yake,
Luteni Moses Liberio Bahanza ( JWTZ), Bertha (Seng ’ Imana) Liberio,Israela(Hatung
’Imana) Liberio,Yusufu Liberio na familia yake,Harun Liberio,Dorka Liberio na Yerusalemu
Liberio.
Napenda kuangazisha shukrani zangu kwa Babu yangu Mzee Yosefu Bavugubusa na
Mama mdogo Asteria Christopher Ntaherezo, Wote wamekuwa pamoja nami katika
kunitakia maisha mema siku zote.Nawashukuru kila siku bila kuchoka.Napenda
kuwashukuru sana, Mapadre wa Shirika la Wamisionari Waafrika kwa kutuletea Injili ya
Kristo kwetu katika ardhi ya Buha(Mkoa wa Kigoma).Kwa namna ya pekee sitausahau
mchango wao katika historia ya Maisha yangu hapa chini ya jua, ni kwa ufadhili wao na
miongozo yao,ninaweza kuonekana hivi nilivyo sasa;Ni kwako Padre Hans
Peters(Henriko),Padre Hans Gulle (John), Padre Walter Gehr na Padre Moris Charles
P, michango yenu mpaka leo imeweka alama moyoni mwangu.
Kwa namna ya pekee namshukuru sana Mwalimu wangu Mwalimu Beatrice SAVYANWA
(apumzike kwa amani), aliyenifundisha kusoma na kuandika, shule ya Msingi Mabamba
darasa la kwanza.Walimu wangu wote wa Shule ya Msingi Mabamba Wilayani
Kibondo.Walimu wa Seminari ndogo ya Mtakatifu Yosefu Ujiji(Kigoma) kwa sasa ikiwa
imehamishiwa Iterambogo - Kidahwe Kigoma ,Seminari ndogo ya Mtakatifu Karoli
Borromeo Itaga(Tabora), Nyumba ya Malezi Iterambongo Kidahwe(Kigoma) kwako Padre
Charles RUFYIRIZA,Padre Matheo NTAMABOKO, Padre Alistacus BARAZEDUKA, Padre
Engelbert NYANDWI kwa malezi na mifano yenu mizuri.
10
Karoli Lwanga Segerea (Dar es Salaam).Nawashukuru sana kwa kunionesha njia njema ya
kuifuata katika Masomo yangu na Malezi yaliyotukuka ya Upadre.
Pia shukrani zangu za dhati ziwaendee Mapadre wa Parokia ya Muhinda kwa upendo
wao wa dhati na michango yao ya hali na mali ni kwako Padre Emil Bwanduruko na Padre
Thomas Muti (Paroko).Asanteni sana.
Kwa namna ya pekee namshukuru mara dufu Frater Josaphat Swai Jimbo Kuu
Katoliki Arusha aliyetoa jasho lake jingi akisoma kwa makini kurasa hizi na wingi wake kwa
11
kurudia mara kadhaa; Nawe Frt.Honest Amani wa Jimbo Katoliki Moshi ninakushukuru
kwa kutumia muda wako ukiusoma mswaada wa Kitabu hiki na kuuweka uwe katika
mtazamo wa kuvutia katika masuala mazima ya kutumia Kitarakishi(kupanga kazi vema kwa
Kitarakishi (computer) asanteni sana . Pia napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Frt.
Benedict Kweyamba Jimbo Katoliki la Bukoba kwa kunisaidia kuchapa baadhi ya kurasa
za Kitabu hiki.
Pacha wangu katika masomo ya Upadre, Frt. Baraka Ruvakule wa Jimbo Katoliki
Kigoma akiwa Masomoni Kipalapala Seminari Kuu ya Teolojia (Tabora).Nakushukuru kwa
matashi mema katika uandishi wa Kitabu hiki, matashi mema yanayolenga ile nyota ya mbali
japo ya matumaini siku moja kwa kudra za Mwenyezi Mungu tuwe watumishi katika Kanisa
hili linalosafiri kama Mapadre wa Jimbo Katoliki Kigoma.Nitakuwa mchoyo wa fadhira
nisipowashukuru Mafrateri wa Jimbo Katoliki la Kigoma,kwa kunitakia mema katika
kukamilisha kitabu hiki,hususani kwako Frt. Liberatus NTATURO na Frt.Albert
LUTUMULA wakiwa hapa Masomoni Segerea Seminari Kuu .
12
Padre Siegnfried Rusimbya NTARE, Mlezi naMuhadhiri wa Masomo ya Nguzi Imani,
MAFUNDISHO MSINGI YA IMANI YA KANISA KATOLIKI (DOGMATIC THEOLOGY)
Napenda kwa moyo wa shukrani nimushukuru Baba Askofu…………… kwa kuruhusu Kitabu
changu kiweze kuchapwa,kwa kukipatia RUHUSA ‘’NA KICHAPWE ’’ ( Imprimatur ) baada ya
kuona kinafaa kwa Kuelimisha Wakristo Wakatoliki na Wote wenye Mapenzi mema.
Nawashukuru sana ndugu,Jamaa,Marafiki na Wafadhili wote wa nje na ndani ya
Tanzania kwa michango yenu ya hali na Mali . Mkaona ni vema kuchangia jasho nililotoa
wakati naandaa kitabu hiki ili jasho langu lisipotee bure hadi tumeweza kuchapa Kitabu hiki
kwa nakshi mbalimbali.
Shukrani zangu ziwaendee wote walionisaidia kifedha Kaka zangu Amos Liberio, na
Justine Baraka Liberio. Pia, Dada Lilian Mallya, Mbopera,Raymond Geofrey, Liberatus
Bigirimana Ntilema,Semeni Samson, Jeremia Ntiboneka, Senorine Libena,Deogratias
Mashimbi, Stanslaus Butungo kwa namna mbalimbali mpaka Muswada wa Kitabu hiki
kuwa katika hali ya Kitabu hiki ; Kinatamanika baada ya Kukichapisha ili kisomwe kiweze
kuelimisha wengi juu ya Roho Mtakatifu na Fumbo la Utatu Mtakatifu.
‘’ Kama sijakutaja Kitabuni, basi nimekuandika moyoni mwangu kwa wino mzito, ama kweli
sitosahau fadhira zenu kwa yale mliyonisaidia’’.
(MATEMBEZINI) Jijini BUJUMBURA; Katika Kikanisa Kidogo Cha Mapokezi kwa Wageni
Jijini Bujumbura, 08-09-2012,
13
VIFUPISHO
1 Thes 1Thes
2 Thes 2Thesalonike
1Fal 1Wafalme
2Fal 2Wafalme
1Kor 1Wakorintho
2Kor 2 Wakorintho
1Pet 1Petro
2Pet 2Petro
1Sam 1Samweli
1Tim 1Timotheo
2Tim 2Timotheo
Tit Tito
1Yoh 1Yohane
2Yoh 2Yohane
2 Thes 2 Thesalonike
2Fal 2Wafalme
2Pet 2Petro
2Sam 2 Samweli
2Tim 2 Timotheo
1Yoh 1Yohane
2Yoh 2 Yohane
14
Amo Amosi
Amu Waamuzi
Ayu Ayubu
Bar Baruku
Dan Danieli
Ebr Waebrania
Efe Wafalme
Eze Ezekieli
Ezr Ezra
Gal Wagalatia
Hes Hesabu
Ibid Ibidem (Maana yake wazo limenukuliwa katika ukurasa ule ule)
Is Isaya
Kol Wakolosai
Kut Kutoka
Lk Luka
15
Mdo Matendo ya Mitume
Mk Marko
Mt Mathayo
Mwa Mwanzo, Kitabu cha kwanza katika orodha ya vitabu vya Biblia.
Na. Namba
Rum Warumi
Ufu Ufunuo
Uk Ukurasa, Kurasa
Yer Yeremia
Yoe Yoeli
Yoh Yohane
Yos Yoshua
Zab Zaburi
16
UTANGULIZI
Hii ndiyo hamu ya Moyo wangu kuandika Kitabu hiki kinachoelezea tunu nyingi za Roho
Mtakatifu na Fumbo la Utatu Mtakatifu. Nimeandika Kitabu hiki kulingana na Mafundisho
ya Mama Kanisa Katoliki. Ilikuwa ni baada ya kuona hitaji kubwa sana kwa waamini wa
Yesu Kristo Mnazareti jinsi gani watapata Kitabu chenye Utajiri wa maelezo na ufafanuzi
mwepesi juu ya Roho Mtakatifu na Fumbo la Utatu Mtakatifu ambapo kwa karne nyingi
tumekuwa na hamu ya kupata Kitabu kitachokuwa Msaada mkubwa kwa kila mkristo, ndipo
nilipolifanyia kazi wazo hilo na kuliweka katika uhalisia kwa kuandika Kitabu hiki ikiwa ni
kitabu changu cha kwanza kabisa katika tasnia hii ya Uandishi wa Vitabu, ni matumaini
yangu makubwa sana kuwa Kitabu hiki kinafungua njia na milango ya vitabu vijavyo
nitakavyoviandika katika maisha yangu ya hapa duniani. Nimekipatia jina Kitabu hiki ROHO
MTAKATIFU NA FUMBO LA UTATU MTAKATIFU.
Nimeanza kuandika katika Sura ya Kwanza ya Kitabu hiki juu ya Roho Mtakatifu kama
mada pekee inayojitegemea kwa kuonesha vyanzo vya Kibiblia,Mapokeo ya Kanisa Katoliki
,Mamlaka funzi ya Kanisa na kuonesha ushahidi unaodhihirisha kuwa Roho Mtakatifu ni
nafsi ya tatu ya Mungu,ni Mungu, ni Roho ya Mungu.
Lakini kwa sababu hauwezi kuzungumzia Fumbo Kuu la Utatu Mtakatifu bila kuwagusa
Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu kwa pamoja, hivyo basi katika Sura ya Pili ya
Kitabu hiki nimeandika mada juu ya Yesu Kristo aliye Nafsi ya Pili ya Mungu katika Utatu
Mtakatifu wa Mungu inayojitegemea :Ambapo nimeweza kuandika kwa kina Kanisa
linasemaje juu ya Yesu Kristo katika Umungu na Ubinadamu wake na pia nimeonesha
Machimbuko ya ushahidi wa hayo tunayoyaamini na kuyafundisha juu ya Yesu Kristo.
Sura ya Tatu ya kitabu hiki ime………….
17
Roho Mtakatifu ndiye chanzo cha hekima, kwani tunaona jinsi Mwenyezi Mungu ameyafanya
mambo yote kwa hekima (Rejea Zab 104:29), Tukiishi kwa msaada wa Roho Mtakatifu, na
tuufate mwongozo wake, Basi tusijivune, tusichokozane wala kuoneana wivu (Rejea Gal
5:25).Ndugu msomaji wangu tunaalikwa tumtegemee Roho Mtakatifu katika karama
anazotujalia, au unataka tutukanwe kama Wagalatia walivyotukanwa na Mtume Paulo
alivyowaita Wagalatia kuwa ni Wajinga? Je na wewe unataka kuwa mjinga katika
kukumbatia ubinafsi na kujishikamanisha na tamaduni zisizo na tunu za KiKristo? (Rejea Gal
3:1-5). Roho Mtakatifu hukaa ndani yetu kwa Sakramenti ya Ubatizo na miili yetu kufanyika
Hekalu la Roho Mtakatifu (Rejea 1Kor 3:16), Kwa Sakramenti ya Kipaimara tunaimarishwa
na Roho Mtakatifu na kuwa ‘’mabingwa’’ Imara katika kushuhudia na kutetea Imani yetu ya
Kikristo Katoliki, ‘’ Kufa ikiwa lazima Imani ibaki salama’’ (Rejea Mt 3:13-17, Lk 4:16-22, Mdo
1:8, 2:38,8:14 -19, 10:38, 45-46). Roho Mtakatifu ni faraja katika dhiki hutufariji katika
mahangaiko na huzuni zetu kama wakati wa mahangaiko ya Waisraeli wakiongozwa na
Nabii Musa Mtumishi wa Mungu wakati wa kuvuka bahari ya Shamu (Rejea Is 63:11 - 14).
Roho Mtakatifu anatusaidia katika udhaifu wetu. Roho Mtakatifu ni Mwalimu wetu
anayetufundisha kusali, Maana hatujui inavyotupasa kuomba, lakini Roho mwenyewe
anatuombea kwa Mungu kwa mlio wa huzuni usioelezeka. Hivyo basi tumkimbilie Roho
Mtakatifu aweze kuwasha moto wa mapendo katika mioyo yetu, tuweze kujua namna njema
ya kumwabudu Mwenyezi Mungu katika sala zetu, dua na maombi yetu (Rejea Rum 8:26).
‘’ Mungu Baba amemzaa Mwana. Mwana amezaliwa kutoka kwa Baba. Roho
Mtakatifu anatoka kwa Baba na kwa Mwana’’. (Hili ni Fundisho la Msingi la Imani
ya Kanisa Katoliki juu ya Utatu Mtakatifu wa Mungu)
Roho Mtakatifu hutufunza namna njema ya kumwabudu Mungu Baba na Mwana katika
Roho na Kweli na katika uchaji wa Mungu (Rejea Yoh 14:26). Hutuimarisha katika tumaini
lisilofifia kumwomba Mungu bila kuchoka. Roho Mtakatifu ni taa ya kutuelekeza kumjua
Mungu katika paji lake la Akili, Roho Mtakatifu huaangaza akili hata za mwanadamu
‘’aliyepinda’’ na ‘’kuchoka’’ aweze kunyooka na kumfuata Mungu. Roho Mtakatifu
huaangazisha akili zetu katika kutambua ukweli na kuwa tayari kumsikiliza Roho huyo wa
Mungu (Rejea Lk 11:13; Yn 14:16 na mstari 26).
18
Roho Mtakatifu ni Mshauri nambari ‘’wani’’ katika wasiwasi wetu na katika maswali
tusiyopata majibu haraka, yeye hutushauri, hutupatia mwanga wa kujikwamua katika
dimbwi hilo la ‘’sintofahamu’’ (Rejea Is 9:6-7). Hushauri mema tu, kwani Roho huyo Mtakatifu
ni mwema milele, ni Mungu hadanganyi wala hana dhiki ya kudanganya .Hapa mfikirie
Bwana wetu Yesu Kristo anavyotabiriwa na Nabii Isaya, anasema; Maana mtoto amezaliwa
kwa ajili yetu, tumepewa mtoto wa kiume. Naye atapewa mamlaka ya kutawala. Ataitwa
‘’Mshauri wa ajabu’’, ‘’Mungu mwenye nguvu’’, ‘’Baba wa Milele’’, ‘’Mfalme wa
Amani’’,utawala wake utastawi daima, amani ya ufalme wake hautakoma… atatawala milele
(Is 7:14).
Roho Mtakatifu aliye mwalimu wetu, siku zote hutufundisha kumwomba vema Mwenyezi
Mungu katika maisha yetu ya kila siku. Na kwa vile tumefanywa kuwa wenye uhusiano
mwema na Mungu kwa imani, basi tunayo amani naye kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.
Kwa imani yeye ametuweka katika hali ya neema ya Mungu ambayo sasa tunaiishi. Vipaji
vya Kiroho ni vya namna nyingi, lakini Roho avitoaye hivyo ni mmoja. Kuna namna nyingi za
kutumikia, lakini Bwana anayetumikiwa ni mmoja. Kuna namna mbalimbali za kufanya kazi
ya huduma, lakini Mungu ni mmoja, anayewezesha kazi zote katika wote (Rejea 1Kor 12:4-
6).
Hapa, Mtume Paulo anatuasa kutumia vipaji vyetu kwa faida ya wote, tusiving’ang’anie
‘’kwapani’’ kwa kuvificha.Vyote ni zawadi kutoka kwa Roho Mtakatifu anayetuwezesha
kuvumiliana na kuchukuliana kwa busara na saburi(uvumilivu) na wenzetu tunaoishi nao.
Roho Mtakatifu ndiye mgawaji wa vipaji vyote,hivyo basi ni mwito wa kila Mkristo
kumnufaisha mwenzake kwa karama alizojaliwa. Mmepewa bure toeni bure.
Basi, tunajivunia tumaini tulilo nalo la kushiriki utukufu wa Mungu. Tumaini hilo haliwezi
kutuhadaa, maana Mungu amekwisha miminia mioyoni mwetu mapendo yake kwa njia ya
Roho Mtakatifu aliyetujalia (Rejea Rum 5:1-2, 5). Hivyo basi Roho Mtakatifu aliye chanzo cha
uzima wetu, hatuachi tubaki ‘’tunawaya waya’’ anazidi kutusimamia na kutumarishia
mapendo yetu kwa Mwenyezi Mungu na Kanisa lake la kweli lisilodanganya wala
kudanganyika, ndilo hilo Moja, Takatifu, Katoliki la Mitume.
Ama kweli, Upendo wa Mwenyezi Mungu hauna mipaka, Mungu mwenyewe ndiye
mwenye kutuimarisha sisi na ninyi pia katika Kristo, na ndiye anayetuweka wakfu; ndiye
aliyetutia muhuri wa kuwa mali yake yeye, na kutujalia Roho mioyoni mwetu kama dhamana
ya mambo yote ambayo ametuwekea (Rejea 2Kor 1:21 -22). Hivyo basi ndugu Msomaji
wangu hauna haja ya ‘’ kuhaha ’’ kutangatanga kwa kubadilisha madhehebu kama vile mtu
anayebadili nguo. Watu wanabadili madhehebu wengi wao kwenda kusaka miujiza.
19
Haujui kwamba Bwana wetu Yesu Kristo alikiita kizazi cha zinaa kinachosaka ishara
kinachotaka ishara miujiza ‘’uchwara’’ ,na mwisho unajichanganya mwenyewe,alaumiwe
nani? Wewe mwenyewe! Badala ya kubaki na Roho Mtakatifu halisi aliye sawa na Baba na
Mwana. Unajikuta unabaki na roho za fujo,majivuno, chuki, dharau na kujiona wewe ni bora
kuliko wengine. Mbona maandiko yakowazi yanatusuta pale tunapojiona tuko bora kuliko
wengine? Kwamba, anayefikiri amesimama aangalie asianguke ‘’ na asemaye hana dhambi
huyo anajidanganya na kweli haimo ndani mwake (Rejea 1Yoh 1:8).
Hivyo basi tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu ninyi ndugu, ninyi
mnaopependwa na Bwana. Kwa maana amewateua tangu mwanzo mpate kuokolewa kwa
nguvu ya Roho Mtakatifu, mfanywe watu wake watakatifu kwa imani yenu katika ukweli.
Mungu aliwaitieni jambo hili kwa njia ya Habari Njema tuliyowahubirieni, aliwaiteni mpate
kupokea sehemu yenu katika utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristu (Rejea 2Tes 2:13-14).
Hapa mtume Paulo anawaonesha Wakristo wa Thesalonike namna wanavyopaswa
kumwabudu Mungu aliye Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Na kujiwekea tumaini jema kwa
Mungu ,kwani Mungu anazidi kufungua mlango kwa yeyote anayeweka tumaini kwake.Hata
kama ajapokufa hatapotea kamwe bali atakuwa na uzima wa milele(Rejea maneno Yesu
aliyomwambia Martha wakati alipomkuta Lazaro amekufa (Yoh 11:20 - 22 ,Yoh 11:25 -27 na
11: 43- 44). Hii inaonesha jinsi gani Martha aliutambua na kuuamini Umungu wa Yesu Kristo
hata wa kurudisha uhai wa mtu aliyekufa tena takribani siku nne. Martha anahisi kaka yake
Lazaro ameshaanza kuoza na kutoa harufu.Lakini hakuna lisilowezekana kwa Mungu.
Mtume Paulo anaonya, kwamba, maneno mabaya yasisikike miongoni mwetu, kila mara
maneno yetu yawe ya kufaa ,na ambayo hujenga na kuwasaidia wengine ili yawaneemeshe
wasikilizaji wetu.Tunaaswa kwamba tusimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu, maana
Roho huyo ni alama ya Mungu kwetu kwamba sisi (wabatizwa wote) ni watu wake, na
thibitisho kwamba siku itakuja ambapo Mungu tutamwona jinsi alivyo. Basi, achaneni na
uhasama, chuki, hasira, kelele, matusi! Achaneni na kila uovu! Muwe na Moyo mwema na
wenye kuhurumiana, kila mmoja na amsamehe mwenzake, kama naye Mungu
alivyowasamehe ninyi kwa njia ya Kristo.Tunayo sababu ya kumwomba Mwenyezi Mungu
waMilele aliyewapeleke mitume Roho Mtakatifu. Roho huyo wa upendo anatufanya tuwe
imara na tudumu katika ule ukweli tuliofundishwa tukaukubali kabisa, ili tuweze
kumshuhudia kiaminifu Mungu wetu mbele ya watu (Rejea 2Tim 3:14). Na tusije tukaona
haya hata siku moja katika kumshuhudia Bwana wetu (Rejea 2Tim 1:8).
Tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu anayetumulika kwa Mwanga wa Neno lake hata
kwa wale wasiomjua. Atuimarishe katika imani mioyoni mwetu tumtangaze bila aibu
yoyote;ili majaribu yasiuzime moto uliowashwa na Roho Mtakatifu ndani yetu. ‘’
Atakapokuja Mtetezi,nitakayemtuma kwenu kutoka kwa Baba ndiye Roho wa ukweli
atokaye kwa Baba,huyo atanishuhudia ( Rejea Yoh 15:26 )
NAWATAKIA USOMAJI MWEMA.
20
‘’ Siyo sisi Ee Mungu, Siyo Sisi bali wewe Peke yako Utukuzwe kwa ajili ya Upendo
wako mkuu na uaminifu wako’’ (Zab 115:1)
FRATER SIMON LIBERIO J.BAVUGUBUSA wa Jimbo Katoliki Kigoma, Tanzania, Seminari Kuu
Segerea, Chuo Cha Upadre, Jijini Dar es salaam, Tanzania (salijo2007@yahoo.com) , 15,Juni
2012 Dar es Salaam, Tanzania
21
SURA YA KWANZA
Katika Sura hii ya kwanza ya Kitabu hiki tutaona Maana ya Roho Mtakatifu, Utambulisho wa
Roho Mtakatifu kibiblia; katika Agano la Kale na Agano Jipya.Pia, ni katika sura hii ya kwanza
tutaona uhusiano baina ya Roho Mtakatifu na tukio zima la Pentekoste.Ni Sura hii,
inayoonesha namna Mitaguso mbalimbali ilivyofundisha juu ya Roho Mtakatifu.Fundisho
msingi la Kanisa la Filioque yaani kwamba Roho Mtakatifu anatoka kwa Baba na kwa Mwana
litajadiriwa katika sura hii ya kwanza na kuonesha chimbuko la fundisho hilo toka kwenye
Maandiko Matakatifu.Na hapo ndipo tutakapoona mgawanyiko wa Kanisa Katoliki na wale
Waothodoksi. Sura ya kwanza itaendelea kueleza namna Mababa wa Kanisa wanavyofundisha
juu ya Roho Mtakatifu.Pia, ndugu msomaji tutaona juu ya Utume wa Roho Mtakatifu katika
Kanisa hili linalo safiri..Sura ya pili itamfafanua Yesu Kristo ambaye ni Nafsi ya Pili ya Mungu.
Na Sura ya Tatu itajadili kwa undani na kwa kina sana juu ya Fumbo zima la Utatu Mtakatifu
wa Mungu. Karibu sasa,uanze kuifaidi Elimu dini juu ya Roho Mtakatifu ndiyo mada
itakayotawala katika Sura hii ya Kwanza.
Roho Mtakatifu ni nafsi ya Tatu ya Mungu, ni Mungu halisi sawa na Baba na Mwana. Lakini
nafsi hizi tatu si miungu watatu, bali ni Mungu mmoja tu, maana UMuungu wao ni mmoja na
tabia ni moja. Kumsadiki Roho Mtakatifu ni kukiri Nafsi ya tatu ya Utatu Mtakatifu, atokaye
kwa Baba na Mwana na ‘’anayeabudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana ‘’ Roho
alitumwa ‘’mioyoni mwetu’’ ( Gal 4:6), ili tupokee uzima mpya wa wana wa Mungu. 1 Roho
Mtakatifu ni Roho wa Maisha ndiye chanzo cha uhai wetu (Rejea Ayu 33:4) .Katika maandiko
Matakatifu Roho Mtakatifu anatambulika kama ruah neno ambalo asili yake ni lugha
Kiebrania lenye kuashiria au kumaanisha ROHO NI MAISHA ,(Rejea Zab 104:29 na Ayu 33:4 )
Hivyo basi Roho wa Bwana (Roho wa Mungu) ni nguvu halisi, ni nguvu ‘’jengefu’’
inayojenga. Kwa kazi ya Bwana, mbingu zilifanyika na makazi yake yote kwa pumzi ya kinywa
chake (Ayu 33:4, Zab 33:6,).Hatupaswi kutamba kifua mbele,kwa kuishi kana kwamba
Mwenyezi Mungu ‘’ tumemfungia kabatini ’’,kwani chanzo cha maisha yetu ni Mungu,ambaye
ameumba vyote vinavyoonekana na visivyo onekana.Roho Mtakatifu ndiye asili ya Uhai wetu
yaani ‘’Ruah’’ kama nilivyotangulia kusema kuwa Ruah ni neno la Kiebrania maana yake kwa
Kiswahili ni Maisha.
22
1Katekisimu ya Kanisa Katoliki, Ufupisho Makini Na. 136,Tafsiri Baraza la Maaskofu Katoliki
Tanzania,Chapa Don Bosco, Makuyu, Kenya, 2008,Uk. 53.
23
Tunazidi kupata tafakuri fundisho kutoka kwenye Katekisimu ya Kanisa Katoliki,
inaendelea kusema; Katika Utatu usiogawanyika, Mwana na Roho ni Nafsi tofauti lakini
hawatenganiki. Tangu mwanzo hadi mwisho wa nyakati, Baba anapomtuma Mwanae,
anamtuma pia Roho wake anayetuunganisha na Kristo kwa imani, ili tukiwa tumefanywa
wana, tuweze kumwita Mungu ‘’Baba’’ (Rum 8:15). Roho haonekani, lakini tunamfahamu
kwa kazi yake, anapotufunulia Neno na anapotenda ndani ya Kanisa. 2
Ni nafsi ya tatu ya Utatu Mtakatifu.Ni Mungu, aliye Mmoja sawa na Baba na Mwana.
Yesu ‘’anatoka kwa Baba’’ (Rejea Yoh 15:26), ambaye akiwa mwanzo usio na mwanzo, ndiye
asili ya uhai wa wote wa Utatu. Anatoka pia kwa Mwana (filioque), kwa njia ya paji la milele
ambalo Baba anampa Mwana. Kwa kutumwa na Baba na Mwana aliyefanyika mwili, Roho
Mtakatifu analiongoza Kanisa alitie ‘’kwenye kweli yote’’(Rejea Yoh 16:13).3
Roho Mtakatifu iliyo nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu wa Mungu alitumwa na Baba na
Mwana (Filioque) ,ili aliimarishe, alitakase na kulitia uzima Kanisa. Kanisa humwita
Kisima chenye uzima.
Katekisimu ya Kanisa Katoliki inazidi kutupatia mwanga mimi na wewe msomaji wangu,
kwamba ‘’Roho Mtakatifu’’ ndilo jina maalumu la Nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu. Yesu
alimwita pia : Roho Parakleto maana yake Mfariji, Mtetezi na Roho wa Ukweli. Agano jipya
linamwita pia :Roho wa Kristo, Roho wa Bwana, Roho wa Mungu, Roho wa Utukufu, Roho wa
Ahadi.4
Ni jambo jema tufahamu Maana ya Fundisho la Kiimani linaposema ‘’alinena kwa vinywa
vya manabii ‘’, nini maana yake? Neno ‘’manabii ’’ linamaanisha wale waliovuviwa na Roho
Mtakatifu waseme kwa jina la Mungu. Roho alitimiza kikamilifu utabiri wa agano la kale
katika Kristo, akifunua fumbo lake katika Agano Jipya.6
24
2 Ibid , Uk. 54
25
Asili ya Milele ya Roho Mtakatifu imefunuliwa kwa kutumwa kwake katika nyakati.
Roho Mtakatifu alipelekwa kwa mitume na kwa Kanisa pia, kutoka kwa Baba kwa jina la
Mwana, sawa kama kutoka kwa Mwana kama nafsi, aliporudi kwa Baba 7(Rejea Yoh 14:26,
15:26, 16:14 ,pia, Kanuni ya Imani)
Kupelekwa nafsi ya Roho baada ya kutukuzwa kwa Yesu,8 (Rejea Yoh 7:39) kunafunua
utimilifu wa fumbo la Utatu Mtakatifu.‘’ Roho Mtakatifu, alitumwa siku ya Pentekoste akae
daima na Kanisa kwa kulisaidia katika kazi yake. Yeye anafanya Kanisa liwe takatifu kwani ni
Roho Mleta uzima (Yoh 4:14, 7:38), ni mwalimu wa Ukweli wote (Yoh 16:13). Yeye anaongoza
Kanisa kwa mapaji yake mbalimbali; Yeye analeta umoja kati ya Wakristo. Hivyo Kanisa
linang’ara kama taifa teule la Mungu katika umoja wa Baba na Mwana na Roho
Mtakatifu.’’(Hati ya Mwanga wa Mataifa namba 4 ya Mtaguso wa II wa Vatikano).
Biblia Takatifu inamwonesha Roho Mtakatifu kuwa ni Mungu na Nafsi (Nafsi ya Mungu), na
hayo tunayakuta pia katika Kanuni ya Imani yetu ya KiKristo Katoliki. Roho huyo Mtakatifu
yupo anafanya kazi duniani na ‘’Kanisani.’’ Roho Mtakatifu ni mgawaji wa mapaji yake Saba.
Ni nafsi ya tatu ya Utatu Mtakatifu.Tuangalie sasa BibliaTakatifu inamzungumziaje Roho
Mtakatifu. Biblia kwa yenyewe inamtambulisha Mungu mmoja, na inamtambulisha Mungu
huyo katika Nafsi Tatu katika uasili wake, Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
Tatu, Roho Mtakatifu yaani Roho wa Bwana ni Mungu, kama tunavyosoma katika tukio la
Anania na Safira Mume na Mke waliouza shamba lao kisha wakadanganya kwa mitume;
mapato mengine ya fedha ile wakajiwekea ‘’kibindoni’’ (hazina binafsi/mafichoni, Rejea
Mdo 5:3-11) ‘’ Petro akamuuliza, ‘’ Anania, mbona shetani amekujaza moyo hata
ukamwambia uongo Roho Mtakatifu kwa kujiwekea sehemu ya fedha ulizopata kutokana na
lile shamba?... Hukumdanganya mtu umemdanganya Mungu! Anania aliposikia hayo
akaanguka chini akafa… Kwa mkewe Anania yaani Safira aliulizwa na Mtume Petro hivi ‘’
Mbona mmekula njama kumjaribu Roho wa Bwana? Naye Safira kwa kujikanyaga kwa
kusema uongo naye akafa vijana wakamzika karibu na mume wake.Hofu kubwa ikalikumba
Kanisa lote na wote waliosikia habari za tukio hilo.
Ndugu msomaji unaweza sasa ukaona namna gani Mtume Petro anavyomwelezea Roho wa
Bwana yaani Roho Mtakatifu kuwa ni Mungu japo si moja kwa moja .Yaani tukio la kusema
uongo kitendo hicho kilicho mkasirisha Roho Mtakatifu ambaye ni Roho wa Bwana ndivyo
hivyo hivyo linavyomkasirisha Mungu. Kumbe sasa Roho Mtakatifu aliye Roho wa Bwana ni
Mungu yuleyule.Kwa hiyo basi Roho Mtakatifu ni Mungu (Nafsi ya Tatu ya Mungu).
Nne, Mtume Paulo naye anamuunga mkono Mtume Petro kwa kusisitiza kuwa Roho
Mtakatifu ni Mungu; soma 1Kor 3:16 anasema ‘’ Je hamjui ya kuwa ninyi ni hekalu la
Mungu,na Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
Maana yake hapa Mtume Paulo anataka kutuambia kuwa Roho Mtakatifu anapokaa ndani
yetu sisi wanadamu maana yake ni Mungu anayekuwa ameweka makazi yake kwetu.Hivyo
basi Roho Mtakatifu hukaa ndani yetu ndiye Mungu mwenyewe anayekaa ndani mwetu.Kwa
mantiki hiyo Roho Mtakatifu ni Mungu.
Tano, Ninakuarika ndugu msomaji wangu, usome 1Kor 6:19 inasomeka hivi ‘’Au hamjui
yakuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu?. Mwili mmepewa na Mungu
! Kwa hiyo si miili yenu’’.
27
Kumbe sasa, tukitambua kuwa Mungu ndiye aliyetuumba ndiye aliyetupatia miili hii na
akatupulizia uzima tukawa viumbe vyenye uzima (Rejea Mwa 1:27, Mwa 2:7; Ayu 33:4).Kwa
tendo hilo la pumzi ya Mungu kuingia ndani mwetu ni sawa kabisa na kusema Mwenyezi
Mungu aliingia ndani mwetu Yeye aliye chanzo cha uzima wote, ili atushirikishe uzima wake
kwa kuishi kwetu. Roho Mtakatifu aliyemo ndani mwetu ni sawa nakusema kuwa Mungu
yumo ndani mwetu. ‘’ Hii ni Teolojia ya hali ya juu na ya ajabu kweli ndugu msomaji wangu
kwa akili za kibinadamu ’’.
Sita , Roho Mtakatifu anaoneshwa kuwa yuko sawa na Mungu Baba na Mungu Mwana
wenye Umungu Mmoja wa kweli,usawa huo unajionesha pia katika fomula (kanuni) ya
ubatizo inayokuwa katika Utatu Mtakatifu wa Mungu (Rejea Mt 28:19) .Tena Roho Mtakatifu
ana sifa za Kimungu hivyo basi Roho Mtakatifu ni Mungu kwani anajua kila kitu katika
ukamilifu wake (Rejea, Hek 1: 7-8). Roho Mtakatifu anafundisha ukweli wote, Pia Roho
Mtakatifu anakazi ya kutahadharisha mambo ya mbele,ya wakati ujao: Kama tunavyosoma
hapa:
Saba, Pia, katika ushahidi wa kuonesha kuwa Roho Mtakatifu ni Mungu; Mtume Paulo
anaonesha kuwa Roho Mtakatifu anafunua siri za Mungu anachunguza kila kitu hata mambo
ya ndani ya Mungu kabisa,na Mtume Paulo anaendelea kwa kuuliza kuwa nani awezaye
kujua mambo ya ndani ya mtu isipokuwa Roho ya mtu huyo. Hali kadharika,hakuna ajuaye
mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu. Mtume Paulo anaongezea kusema kuwa ;Basi
,sisi twafundisha,si kwa maneno tuliyofundishwa na hekima ya binadamu,bali kwa maneno
tuliyofundishwa na Roho,tukifafanua mambo ya kiroho kwa walio na huyo Roho(Rejea 1Kor
2:10 -13).
Nane, Ni Roho Mtakatifu aliyewavuvia Manabii katika Agano la Kale,kwa ufupi tunarudi
kwenye Kanuni ya Imani yetu Wakristo Wakatoliki ya Nikea -Konstantinopole tunayoitumia
kila jumapili katika Adhimisho la Misa Takatifu katika sehenu isemayo ‘’ Nasadiki kwa Roho
Mtakatifu,Bwana mleta uzima atokaye kwa Baba na Mwana.Anayeabudiwa na kutukuzwa
pamoja na Baba na Mwana:aliyenena kwa vinywa vya manabii’’. . Ndugu msomaji wangu!
Ama kweli Roho Mtakatifu ni Mungu , kwani anakidhi sifa za Mungu ,hakuna ubishi hapa
Biblia Takatifu inashuhudia wazi wazi.
28
atokaye kwa Baba na kwa Mwana .Anayeabudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana.
Aliyenena kwa vinywa vya manabii. Sasa, kama Roho Mtakatifu ni Bwana tena mleta uzima
na anayeabudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba , na Mwana ,kwanini asiwe Mungu?. Roho
Mtakatifu ni Mungu kama Imani yetu Wakristo inavyoshuhudia, kufundisha na kuishi.
Kwani twajua kuwa Nafsi Tatu za Mungu zina Umungu sawa,asili sawa, umilele sawa ,
uwamo sawa. Tahadhari hapa ndugu msomaji wangu, kama tutadiriki kutenganisha Nafsi
za Mungu kama mafungu ya nyanya tutaitwa wazushi kama Ariusi alivyoeneza uzushi na
Kanisa likamtenga,alidai kuwa Nafsi hizi za Mungu zinazidiana ukubwa.Hilo si kweli ni
uzushi na atakayelishikilia hilo ni Mzushi ,hatufai kubaki Kanisa Katoliki ,Kanisa litamtenga.
Nafsi ya Baba ni Mungu, Nafsi ya Mwana(Yesu Kristo) ni Mungu na Roho Mtakatifu,Roho wa
Mungu ni Mungu.Kwa kuogezea, Katika Tukio la Pentekoste ,Bwana Yesu Kristo
anawaahidi wanafunzi wake kuwatumia ‘’ahadi’’ ya Baba yake yaani Roho Mtakatifu
(Rejea Lk 24:49; Mdo 2:2-4 )
29
mwanzi ulokunjika,hatazima utambi unaozimika;Bali atajulisha hukumu kwa
ukweli.Hatazimia wala hatakata tamaa, mpaka atakapoweka hukumu duniani,na nchi za
pwani zitangojea mafundisho yake’’.
Ni Roho Mtakatifu, aliyebadiri nyika na kwamba hali itaendelea kuwa hivyo mpaka
tumiminiwe roho ya Mungu kutoka juu. Hapo jangwa litakuwa shamba la rutuba tena na
mashamba ya rutuba yatakuwa msitu. Haki itadumu katika nchi iliyokuwa nyika, uadilifu
utatawala katika mashamba ya rutuba, Kutokana na uadilifu watu watapata amani, utulivu
na usalama utadumu milele. Watu wangu watakaa katika makao ya amani, katika maskani
salama na mazingira matulivu.(Rejea Is 32:15 -18).
Ndugu msomaji wangu Biblia Takatifu inadhihirisha kwamba Roho Mtakatifu ndiye chanzo
cha mabadiliko ya ndani kwani, mioyo yetu hata kama imekuwa ‘’sugu’’, imebobea katika
dhambi yaweza kubadilishwa na kuwa katika njia adilifu.Vile vile penye utawala wa Roho
Mtakatifu Amani, Utulivu na Usalama vinatawala milele kama tulivyosoma hapo juu. Zaidi ya
yote Roho Mtakatifu ndiye chanzo cha uhai wote (Soma Ayu 33:4), Ardhi inazaa mahitaji ya
Wanadamu kwani ni Roho wa Mungu anayetujalia makao ya amani, katika maskani salama
na mazingira matulivu.
Ni Mungu tu aliye Mwumbaji wa uhai au uzima ,na hapa hakuna tofauti kati ya Mungu na
Roho Mtakatifu(Soma tena Ayu 33:4).Ndio maana Katekimu ya Kanisa inatuambia, Kuna
Mungu mmoja katika nafsi tatu za Mungu zisizogawanyika sawa katika kazi tendaji
zisizopingana.Roho Mtakatifu ni nafsi ya Mungu, ni Mungu.Mungu ndiye anayepaswa
kuabudiwa,kuabudiwa katika Roho na Kweli maaana yake ni mwito wetu Wakristo kufanya
Ibada za kumpendeza Mungu,kumwabudu Mungu wa kweli na siyo kujikita na kukimbilia
kwa wagaga wa jadi au kienyeji akina Mahoka au Nyamuragura kwa ajili ya kwenda kupiga
ramuli.Wakristo tuachane na maisha kama ya chura anayeishi maisha ya ajabu kweli ndani
ya maji na nchi kavu .Maisha ya Mkristo asiyesimama imara katika imani Katoliki; mguu
mmoja kwa Mungu yaani Kanisani na mguu mwingine kwa shetani ndio kujikita katika
ushirikina,uchawi wa namna mbalimbali .
30
kutumia pato lako kama upendavyo? Mbona, basi, ulinuia moyoni mwako kufanya
jambo hili?
Roho Mtakatifu anamshukia Mama Bikira Maria na kuweza kupata mimba kwa uwezo wa
huyo huyo Roho Mtakatifu (Rejea Mt 1:18 -25; Lk 2:1-7).Hivyo basi Bwana wetu Yesu Kristo
alizaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kwa mwanamwali Bikira Maria.Mama Bikira Maria
hakumjua Mwanaume (Soma Mt 1:18 , Lk 2:1-7;).
Mwinjili Yohane anamwonesha Roho Mtakatifu, yuko pamoja na Yesu Kristo, anafanya kazi
na Yesu Kristo (Rejea Yoh 1:32-33). Yohane Mbatizaji ndiye aliyemtangaza Yesu Kristo
kwamba, Kristo atabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto (Rejea Lk 3:16). Na wakati Yesu
anabatizwa Roho Mtakatifu alimshukia Yesu Kristo kwa mfano wa njiwa na kutua juu yake
(Rejea Mt 3:16; Mk 1:9-11; Lk 3:21 -22)
Kumbe sasa, Yesu Kristo ana nguvu ya Mungu , nguvu ya Roho Mtakatifu (Rejea Yoh 1:26).
Yesu Kristo anawaahidi Mitume wake juu ya ujio wa Msaidizi ambaye ni Roho Mtakatifu
ndiye Roho wa Kweli atakayetoka kwa Baba na kushuhudia kazi za Yesu Kristo (Rejea Yoh
15:26).Hivyo basi Roho Mtakatifu anakuja kwetu duniani kutukumbusha siku zote yale
Kristo mwenyewe aliyotufundisha,Kwani Kristo ndio Njia, Ukweli na Uzima wa milele na
hakuna awezaye kwenda kwa Mungu Baba bila kupitia kwa Yesu Kristo (Rejea Yoh 14:6 - 7).
Pia, tunasoma Nimewaambieni mambo haya nikiwa bado pamoja nanyi, lakini Msaidizi
wenu ambaye Baba atamtuma kwa jina langu,atawafundisheni kila kitu na
kuwakumbusheni yote niliyowaambieni (Rejea Yoh 14:26)
Roho Mtakatifu ni Roho wa Kweli kama tunavyosoma (Yoh 14:17, Yoh 15:26, Yoh
16:13).Tunahakikishiwa na Kristo kuwa anayempokea Roho Mtakatifu anakuwa mkamilifu
katika maisha ya kiroho ,hivyo basi anapaswa kujibidiisha siku hadi siku katika kuushi
31
ukristo kwa kusali sana na kujifungamanisha na maisha ya Sakramenti za Kanisa na kutenda
Matendo mema kwa jirani zake.
Tukumbuke kuwa Roho Mtakatifu haji kutufundisha mambo yake mapya, bali anakuja
kutufundisha,kutukumbusha,kutufafanulia maneno ya Kristo yaliyo uzima wa milele (Rejea
Yoh 6:68 ).Na hivyo hakuna jina jingine liwezalo kutuokoa sisi wanadamu tofauti na Yesu
Kristo Mnazareti kwani Yeye ndiye Njia, Ukweli na Uzima wa milele (Rejea Yoh
14:6).Tunakumbushwa pia, Kila anayeongea maneno ya Roho wa Mungu yuko na Mungu
;Kwani maneno ya Roho wa Kweli ni Maneno ya Mungu maana Mungu humjalia mtu huyo
Roho wake bila kipimo (Rejea Yoh 3:34).
Huyo ndiye Roho Mtakatifu, Roho wa Kristo kama Mtume Paulo anavyomtaja.Kristo ambaye
aliteswa na siku ya tatu alifufuka ni lazima ahubiriwe na kwa njia yake mataifa yote kuanzia
Yerusalemu, yahubiriwe kwamba watu wanapaswa kutubu na kusamehewa dhambi.
Kwa upande mwingine, Mwinjili Luka hasa (Lk 11:13), Roho Mtakatifu anaoneshwa kuwa ni
zawadi kutoka kwa Mungu.Kwa kumpokea Roho Mtakatifu tunajazwa na nguvu itokayo juu
Mbinguni (Rejea Lk 24:48).
Kuna wakati mwingine katika Agano Jipya,Nafsi mbili au Tatu za Utatu Mtakatifu
wa Mungu zinatajwa katika muungano wao.
32
Mt 3:16-17 ‘’ Baada ya kubatizwa, Yesu akatoka mara majini.Na tazama mbingu
zikamfungukia .Akamwona Roho wa Mungu akimshukia kwa mfano wa njiwa .Tazama pale
pale sauti ikatokea mbinguni ikisema, ‘’Huyu ni Mwanangu mpendwa, anipendezaye.’’ Mtume
Paulo anatoa maelezo yanayozitaja Nafsi tatu za Utatu Mtakatifu wa Mungu. 2Kor 13:13
‘’Neema ya Bwana Yesu Kristo, na upendo wa Mungu Baba, na ushirika wa Roho Mtakatifu
viwe nanyi nyote.’’
Katika Kitabu kilichoandikwa na Baba Mtakatifu Papa Benedicto XVI ‘’ Nasadiki kwa Mungu
Mmoja’’ Ukurasa wa 81 (I BELIEVE IN ONE GOD) anafundisha juu ya Pentekoste hivi:
‘’ Tukio la Pentekoste ndilo linazaa Kanisa Moja, Takatifu, Katoliki na la Kitume.Tukio hilo
linafungua mlango wa wokovu kwa wote ndio maana ni Katoliki,Kanisa ambalo lipo kwa ajili
ya wokovu wa wote.Tukio la Pentekoste linaunda jumuiya mpya ya Wakristo inayoongea
Lugha zote na kuwaunganisha watu wote kuwa watu wamoja,familia moja ya Mungu; ishara
hii inakuwa uhalisia kwamba; wokovu umewafikia watu wote. Na hili linakamilisha utume
wa Mtakatifu Paulo, aliyefahamu kuwa ni mtume wa Yesu Kristo miongoni mwa watu wa
9
CANTALAMESA Ranielo, The Mysteries of Pentecost,The Order of St.Beedict, Inc.
Collegeville, Minnesota,2001,Published in India,Liturgical Press,St. John’s, Abbey,
Collegeville, Minnesota 56321, U.S.A, p.48
33
mataifa. Mtume Paulo aliendelea akifanya kazi ya kueneza Neno la Mungu kama mtumishi
wa Yesu Kristo kwa watu wa mataifa ili watu wa Mataifa waweze kutoa sadaka Safi na za
kumpendeza Mungu, zilizowekwa wakfu na Roho Mtakatifu’’. (Rum 15:16).
Tukio la Pentekoste linaleta Kanisa ‘’katoliki ‘’,yaani Kanisa lisilokuwa na ubaguzi wala
mipaka ambalo halijari utaifa, rangi,sura,ukabila,koo,maumbile na kadha wa kadha.Kumbe
basi ni Kanisa lililowazi kwa yeyote anayetaka kupata wokovu,na anapokelewa kwa kufuata
Sakramenti mbalimbali za Kanisa ili aweze kujitakatifuza.Kumbe sasa Sakramenti za Kanisa
Kristo alizozianzisha ni kwa ajili ya kujitakatifuza.Nazo ni Sakramenti ya Ubatizo,Ekaristi
Takatifu,Kipaimara, Ndoa, Daraja Takatifu la Upadre (Upadrisho), Kitubio(Upatanisho),
Ndoa Takatifu, Mpako wa Wagonjwa.Yesu Kristo yuko pamoja na Kanisa lake akililinda kwa
njia ya Roho Mtakatifu, ndio maana anatufariji kwa kutuambia kuwa hatatuacha kamwe
yatima atakuja kwetu mara,mioyo yetu itajaa furaha ya kumwona. Pia anatuambia
atatuagizia mfariji na msaidizi wetu ili Injili yake Yesu Kristo iendelee kusonga mbele (Rejea
Yoh 16:4- 15 na Yoh 16:22-33).10
10 Ibid,p.12
34
dhambi,kwani yeye ni Mungu kwa asili.Dhambi kwake zitoke wapi? Kiteolojia,Yesu Krsto
alivyobatizwa Mtoni Yordani ,alitaka kuzindua rasmi tukio la Ubatizo(Sakramenti ya
Ubatizo) kwa kuyatakasa Maji na vijito vyake kwa ajili ya wa Wanadamu wote,kazi ni kwako
sasa kuupokea au kutoupokea.
Pili, Kristo alitaka kutuonesha moyo wa unyenyekevu kwa kujishusha hata akabatizwa na
Mwanadamu Yohane Mbatizaji.Yohane Mbatizaji mwenyewe aliogopa hata akasema wazi
kuwa ‘’ yuaja mtu ambaye sistahili hata kulegeza ukanda wa viatu vyake Yesu Kristo (Rejea
Yoh 1: 27-28; Mt 3:13-16, Lk 3:15- 16).Tukio la Pentekoste haliwezi likatenganishwa na Yesu
Kristo.Kwani tunasadiki siku zote kwa Roho Mtakatifu atokaye kwa Baba na Mwana (
filioque).
Ni katika Roho Moja sote tulibatizwa katika Kristo,na Roho Mtakatifu , anabaki kuwa mlinzi
wetu na kanisa siku zote za maisha yetu ya ukristo.Tunasoma ‘’Siku ya Pentekoste
ilipowadia, wote walikuwapo mahali pamoja’’(Rejea Mdo2:1, 1:8 , 2:12-14, 4:31).
Kuna makuu mengi yanayofanywa na Roho Mtakatifu katika maisha yetu na
Sakramenti.Katika kazi za Unabii zinahitaji nguvu kutoka Roho kwa Mtakatifu ndiye
anayejalia uwezo wa kukemea kwa ukali,kufikisha ujumbe hata ikiwa ni kwa njia
ngumu.Nabii hapaswi kuwa na woga wakukemea maovu katka jamii ;kama Ufisadi ambao
kwa Tanzania yetu umepanda ‘’chati’’,wizi wa rasilimali za Kitanzania,Rushwa uzijuazo za
aina mbalimbali na hata kwa namna moja au nyingine kupeana fadhira,kurudishiana wema
maofisini kwa kupandishana vyeo bila kuangalia ueledi na vigezo.
Kwa ufupi,tunaweza kusema, Roho Mtakatifu alimtokea Bwana wetu Yesu Kristo wakati wa
ubatizo wake huko Yordani.Akamtokea pia huko Nazareti na akampaka mafuta rejea(Maana
aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu,kwa maana Mungu anampa Roho pasipo
na kipimo( Rejea Yoh 3:34-35)
35
Eneo lenyewe ni jengo lililoko juu karibu na dari au paa, japo Biblia ya Kiafrika inataja eneo
hilo kama ghorofa ambapo mitume walikuwa wamejikusanya wakiendelea kusali kwa moyo
mmoja,pamoja nao wakiwemo wanawake, na Maria, Mama wa Yesu, na ndugu zake(Rejea
Mdo 1:13).
Tukio la siku ya Pentekoste liliendana na miujiza kwani Roho Mtakatifu alikuwa juu yao,
wakaelewana lugha za Waparthi,Wamedia,Waelami,Wamesopotamia,watu wa Yudea..
mpaka huko Libya,kwa mantiki hiyo hata kiarabu nacho kilitundikwa katka kumtukuza
Mungu Baba,Mwana, na Roho Mtakatifu.Na Roho Mtakatifu aliwashukia kwa umbo la ndimi
za moto, wakapatwa na butwaa na kuanza kushangaana mambo makuu ya Mungu.Kwenye
msafara wa mamba na kenge wamo, pamoja na makuu hayo ya Mungu,yaliyotokea .Kuna
baadhi ya watu waliwakejeri (kuwadhihaki) mitume na waliokuwa nao,kwamba
wamekunywa divai mpya hivyo wamelewa.
‘’ Basi, wote walishtuka na kuhangaika wakiulizana, ‘’Maana yake nini mambo haya? ‘’
Wengine waliwadhihaki na kusema ‘’Wamelewa divai mpya’’ (Rejea Mdo 2:12- 13)’’.
Mosi, Kwa kunena lugha mpya, ni ishara ya kujidhihirisha kwa ‘’ kuumbwa moyo mpya ’’ :
Ulioumbwa ndani mwao.Ni kwa tukio la Pentekoste , Roho Mtakatifu amevunja uzio
uliokuwa unawatenga jamii ya Kiyahudi na Watu wa Mataifa. Kwa kuondoa uzio wa
kutoelewana na kuweka mambo yote yaeleweke bayana;ndilo jawabu la Wana mnara wa
Babeli waliotaka kujenga mnara ili wamfikie Mwenyezi Mungu (Rejea Mwa 11:1-9) ‘’Haya
tushuke tukavuruge lugha yao,wasipate tena kusikilizana wao kwa wao’’(Rejea Mwa
11:7).Bwana Mungu akawatawanya toka huku waenee dunia, nao wakaacha kujenga mji
ule.Kwa sababu hiyo ukaitwa Babeli kwa kuwa hapo ndipo Bwana alipovuruga lugha ya watu
wote wa dunia,na kutoka huko akawatawanya waenee dunia nzima.(Rejea Mwa 11:1-9)
Mungu akawavuruga hawakuelewana,wakaambulia patupu. Pentekoste inakuja kuponya
jeraha lile la Wahanga wa Mnara wa Babeli kuanzia hapo wanaelewana kama awali, kwani
dunia nzima ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja (Rejea Mwa 11:1) .
Katika tukio zima la Pentekoste pamoja kwamba walizungumza katika Lugha ngeni watu
kutoka kabila mbali mbali waliweza kuelewana kwa kila mmoja kulingana na lugha yake
asili.12
36
Tukumbuke kuwa hata jamii ya Kiyahudi ilikumbatia matabaka,kulikuwa na Wayahudi,
Wasamaria na kadha wa kadha.Mungu anafanya maagano mapya kwa mwanadamu.Tukio la
Pentekoste linakuja kuwaunganisha na kuamsha uhusiano mpya wa makabila; baina ya
jamii ya Kiyahudi na Watu wa Mataifa (wasiokuwa Wayahudi). 13 Kwani Wayahudi mpaka
leo tunawafahamu kwa ngebe zao za kukumbatia tamaduni zao,Dini yao ya Kiyahudi na hata
kufikiri wao ni bora kuliko mtu mwingine aliyeko chini ya jua hili.
Ni kweli kwamba ni Taifa teule ambalo Mwenyezi Mungu alijifunua kwao kupitia
Abrahamu Babu yetu wa Imani, Isaka ,Yakobo .Na akawatumia Musa
na Yoshua katika safari ya kwenda nchi ya ahadi ambayo, Musa alikufa bila kufika nchi hiyo
aliyoitamani kufika kwa muda mrefu (Kut 40:35).Kwa matukio mengi hata yakivita Waisraeli
waliweza kushinda.Kwani Mungu alikuwa upande wao. Na kwa mantiki hii Wayahudi
walimchukulia Mungu kama Mungu wao,walitaka kama ‘’kumbinafsisha’’ Mwenyezi Mungu,
kwa kufikiri kwamba Mwenyezi Mungu anawasikiliza wao tu. Baadaye, baada ya Waisraeli
kukengeuka, Mwenyezi Mungu naye akawapa kisogo, wakatupwa ndani ya dimbwi la
utumwa, tangu utumwa wa Misri na Babel.Hata hivyo Mwenyezi Mungu hakuwaacha
,hakuwatupa.Aliwakumbatia kama vile Kuku akumbatiavo vifaranga vyake. Ndio maana kwa
ngebe nyingi wanauliza ni Nani aliye Mungu mkuu kama Mungu wetu? Mungu wa Israeli?.
Pili, Roho Mtakatifu anakuja kuunda jamii mpya .Kwa kunena Lugha Mpya ilikuwa ni
ishara ya kuwaleta pamoja jamii ya Wakristo waweze kuishi Roho moja na moyo mmoja
katika Kristo.14
Tatu Ni kwa tukio hili la Pentekoste milango inafunguliwa kwa Injili kupenya mpaka miisho
ya dunia, toka Yudea, Samaria, mpaka vijiji vya mbali kama Mabamba (Kibondo) na hata
miisho ya pande zote za dunia. Kristo anatawala kwa mataifa yote.Anatupenda na mwenye
huruma. Hana upendeleo ila ni mwenye haki siku zote.
13 Ibid, p.17
14 Ibid, p.13
37
Jioni ya siku ya kwanza ya juma,Yesu Mfufuka aliwatokea wanafunzi wake akawavuvia na
kuwaambia: ‘’Pokeeni Roho Mtakatifu. Wowote mtakaowaondolea dhambi wameondolewa,
na wowote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa(Soma Yoh 20:19 -23).
Hata hivyo,Yesu baada ya kufufuka kwake aliendelea kuwatokea wafuasi wake kwa siku
arobaini kabla ya kupaa kwake (Rejea Mdo 1:3).Katika kipindi hiki baada ya ufufuko wake
Kristo aliwapa ahadi ya kuwaletea huyo Roho Mtakatifu.
‘’Na tazama,nitawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humo mjini, hata mvikwe
uwezo utokao juu’’(Rejea Lk 24:49).
‘’Hata alipokuwa amekutana nao aliwaambia wasitoke Yerusalemu,bali waingojee ahadi ya
Baba,ambayo mlisikia habari zake kwangu; ya kwamba Yohane alibatiza kwa maji, bali ninyi
mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku chache (Rejea Mdo 1: 4-5).
Mtume Paulo anamzungumzia Roho Mtakatifu kwa undani kabisa katika nyaraka zake
mbalimbali .Kiini cha ujumbe wa Kiteolojia kadiri ya Mtume Paulo ni ‘’Kwa uwezo wa Roho
Mtakatifu Yesu Kristo aliyetumwa na Mungu Baba katika ubinadamu kuvunja nguvu
za kuzimu, aliteswa, akafa na akafufuliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Moja, Mtume Paulo anaelezea uwezekano wa kuwa na maisha mapya yanayoongoza mwili
na Roho Mtakatifu; Anasema: Maana sheria ya Roho iletayo uhai kwa kuungana na Kristo
Yesu imenikomboa kutoka katika sheria ya dhambi na kifo (Rejea Rum 8:2).
Mbili, Kwa upande mwingine Roho Mtakatifu anafanya kazi ya kumpa nguvu muamini
kumshuhudia Yesu Kristo kuwa ni Bwana ambapo Mtume Paulo anasema Basi jueni kwamba
mtu yeyote anayeongozwa na Roho wa Mungu hawezi kusema : ‘’Yesu alaaniwe ! ‘’ Hali
kadharika, mtu yeyote hawezi kusema: ‘’ Yesu ni Bwana,’’ asipoongozwa na Roho Mtakatifu
(Rejea 1Kor 12:3 )
Tatu, Mtume Paulo anatuonesha kuwa hatuwezi kuishi bila msaada wa Roho Mtakatifu
katika maisha yetu ya Ukristo ; Kwani tunapaswa kuishi maisha kulingana na matakwa ya
Roho na si ya mwili kama anavyosema: Lakini ninyi hamuishi kufuatana na matakwa ya
mwili, bali kufuatana na matakwa ya Roho, ikiwa Roho wa Mungu anaishi ndani yenu.Yeyote
asiye na Roho wa Kristo,huyo si wake Kristo.Lakini kama Kristo yumo ndani yenu,ingawa miili
yenu imekufa kwa sababu ya dhambi, kwenu Roho ndiye uhai kwa sababu mmefanywa kuwa
waadilifu.Ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Kristo kutoka wafu ataipa miili yenu ya kufa;
ataifanya hivyo kwa njia ya Roho wake akaaye ndani yenu(Rejea Rum 8:9 – 11)
38
Nne, Mtume Paulo anatuambia kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni watoto
wa Mungu (Rejea Rum 8:14).Na ni kwa Roho huyo huyo , sisi tunamwita Mungu ‘’Abba ‘’ yaani
‘’Baba! (Rum 8: 15). Naye Roho Mtakatifu anathibitisha na Roho zetu kwamba sisi ni watoto
wa Mungu (Rum 8:16).Mtume Paulo anamalizia kwa kusema Basi ,kwa vile sisi ni watoto wa
Mungu,tutapokea baraka zote Mungu alizowawekea watu wake, na tutashiriki urithi huo
pamoja na Kristo; maana ,tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia utukufu
wake(Rejea Rum 8:17)
Tano, Roho Mtakatifu anafahamika kwa Mtume Paulo kama Roho wa Yesu Kristo anayetoa
nguvu ya msaada kwa ukombozi; anasema Tena nitaendelea kufurahi,Kwani najua kwamba
kwa sala zenu na kwa msaada wa Roho wa Yesu Kristo,nitakombolewa (Rejea Filip 1:18- 19).
Pia Roho Mtakatifu anaoneshwa na Mtume Paulo kuwa Roho Mtakatifu ni Roho wa Kristo,
kwa kusema yeyote yule asiyekuwa na Roho wa Kristo si wake Kristo (Soma Rum 8:9)
Sita, Roho Mtakatifu ni Roho wa Mwana (Yesu Kristo) Soma Gal 4:6; 1Kor 6:11; Rum 15:16;
1Kor 1:2).
Saba, Mtume Paulo pia anaonesha kuwa,Maisha mapya tunayopokea katika Yesu Kristo
ndiyo maisha katika Roho. Hivyo basi kwa Mtume Paulo Maisha Katika Kristo ndiyo hayo
hayo maisha ya Roho.Roho Mtakatifu ni na Roho wa Kristo ambaye ni Mungu ni ‘’mamoja’’
yaani ni ‘’ sawa’’. Hivyo basi, Roho Mtakatifu ni Mungu kwani anayempokea Roho Mtakatifu
katika maisha ya ufuasi wa Kristo hapo anampokea Mungu.
Nane, Mtume Paulo anaendelea kuonesha kuwa Roho Mtakatifu ndiye Roho anayewaongoza
watu kuielekea imani.Roho Mtakatifu anawasaidia jamii ya waamini Wakristo
kuwaangazisha watu katika kuamini na kuyafuata maongozi yake Mwenyezi Mungu.Ndio
kusema kuwa Mtume Paulo, anaonesha kuwa Roho Mtakatifu anawaongoza Wakristo
kuielekea imani na Roho Mtakatifu tena anasaidia wakristo waishi maisha ya kiroho zaidi.
39
6. MITAGUSO MBALIMBALI ILIVYOFUNDISHA NA KUFAFANUA MAFUNDISHO
JUU YA ROHO MTAKATIFU
40
Roho Mtakatifu anatoka kwa Baba na kwa Mwana.Na maandiko Matakatifu yanashuhudia
ukweli huo.Tunasoma ‘’Atakapokuja huyo Msaidizi nitakayemtuma kwenu kutoka kwa
Baba, huyo Roho wa kweli, atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi (Rejea Yoh
15:26).
Kumbe sasa, Tunakumbushwa na Mtaguso wa Efeso (431 AD) unaotukumbusha kuwa hakuna
mtu mwenye mamlaka ya kuongeza au kupunguza chochote kwenye Mafundisho Msingi ya
Imani ya Kanisa Katoliki.
7. FILIOQUE
ROHO MTAKATIFU ANATOKA KWA BABA NA KWA MWANA (FILIOQUE)
Katika Mtaguso wa Kwanza wa Konstantinopoli fundisho juu ya Filioque lilifafanuliwa vizuri
na kufundishwa katika Kanuni ya Imani(Nasadiki) ya Nikea - Konstantinopoli kwamba
Roho Mtakatifu anatoka kwa Baba na kwa Mwana( kwa kilatini Filioque).Roho Mtakatifu ana
Umungu sawa na Baba na Mwana na Mwenye kuabudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na
Mwana.Ni Fundisho Msingi la Imani Katoliki,kwamba Roho Mtakatifu anatoka kwa Baba na
Mwana likawa limepinga makosa yanayoshikiliwa na Kanisa la Mashariki wao wanaamini
kwamba Roho Mtakatifu anatoka kwa Baba tu, na sio kwa Baba na kwa Mwana.Hilo ni kosa
na ni moja ya sababu zilizosababisha mgawanyiko wa Kanisa Katoliki la Mashariki hususani
Waorthodoksi na Magharibi( Kilalatini –Roma).
Hivyo basi Kanisa Katoliki lilifundisha na linafundisha kwa kusisitiza kwamba :Roho
Mtakatifu anatoka kwa Baba na kwa Mwana.Na maandiko Matakatifu yanashuhudia ukweli
huo. Tunasoma ‘’Atakapokuja huyo Msaidizi nitakayemtuma kwenu kutoka kwa Baba,
huyo Roho wa kweli, atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi (Rejea Yoh 15:26).
41
Ndugu msomaji ni wazi kabisa lengo la Fundisho juu ya Filioque lilikuwa ni katika kusisitizia
kwa kufundisha kwamba Yesu na Mungu Baba wana Umungu sawa na kwamba Roho
Mtakatifu si wa Baba tu bali wa Mwana pia. Mtaguso wa Nne wa Laterano uliweza kutoa
Fundisho juu ya Imani kwamba Roho Mtakatifu anatoka kwa Baba na kwa Mwana . Hivyo
basi Fundisho Msingi la Imani kwamba Roho Mtakatifu anatoka kwa Baba na Mwana
(yaani Filioque kwa Kilatini) lilitangazwa rasmi na Kanisa Katoliki kama Fundisho la Msingi
la Imani ya Kanisa Katoliki mnamo mwaka 1215 AD.
Mitaguso mingine iliyoendelea kulienzi Fundisho hili la Filioque kwa kulifundisha ilikuwa ni
Mtaguso Mkuu wa Pili wa Lioni (Lyons,1277 AD) , Mtaguso wa Florensi (Florence,
1438 -1445) na Kanuni ya imani inayotokana na Mtaguso wa Kumi na moja wa
Toledo(447 AD, Ds19) Rejea Kanuni ya Imani ya Mtaguso wa Toledo wa mwaka
447(DS 19), Kanuni ya Imani ya Athanasi (DS 39), Kanuni ya imani ya Mtaguso wa
Kumi na Moja wa Toledo wa mwaka 675 AD (DS 277), Mtaguso wa Florensi wa mwaka
(DS 691, 703 na kuendelea). Pia fanya rejea ya Kanuni ya Imani ya Mtaguso wa Nikea
Konstantinopoli iliongeza ‘’et filio’’ yaani na Mwana ambapo kimsingi ni Mtaguso wa
Tatu wa Toledo ndio uliingiza ‘’et filio’’ yaani na Mwana kwa mara ya kwanza kabisa
mnamo mwaka 589.15
Mitaguso yote hapo juu inaendelea kufundisha kuwa Roho Mtakatifu anatoka kwa Baba
na Mwana, mwenye Umungu sawa na Baba na Mwana na kuabudiwa na kutukuzwa
pamoja na Baba na Mwana.
15Ott, Ludwig, Fundamentals of Catholic Dogma,The Procession of the Holy Spirit from
the Father and the Son by way of spiration p.62
42
Waandishi wa Maandiko Matakatifu waliovuviwa na Roho Mtakatifu wanamwita Roho
Mtakatifu ‘’Roho wa Mwana’’ (Rejea Gal 4:6).
Pia walimwita Roho Mtakatifu kuwa ni ‘’Roho wa Kristo’’ (Rejea Gal 8:9).
Roho Mtakatifu anajulikana kama ‘’ Roho wa Yesu Kristo’’ (Rejea Filip 1:19).
Roho Mtakatifu anatajwa kama ‘’Roho wa Baba ‘’ (Rejea Mt 10:20)
Roho Mtakatifu anatajwa kama ‘’Roho wa Mungu’’ (Rejea 1Kor 2:11).
Hivyo basi Roho Mtakatifu anaoneshwa kuwa na uhusiano sawa na Mwana na Baba pia.
Tena kulingana na Maaandiko Matakatifu tunaona kuwa Mwana(Yesu Kristo Mnazareti)
anamtuma Roho Mtakatifu(Rejea Lk 24:49; Yoh 15:26, Yoh 16:7, Yoh 20:22; Mdo 2:33; Tit
3:6; Rum 3:3)16
Yeye katika Mafundisho yake juu ya Roho Mtakatifu anasema: Roho Mtakatifu ni Roho ya
Kristo,Roho ya Mwana au ni Roho aliyetumwa na Yesu kwa ajili ya kutakatifuza wanadamu.
Anaendelea kusema kuwa Roho Mtakatifu ni Mungu.Hivyo basi anasisitiza Umungu wa Roho
Mtakatifu. Imani yake thabiti katika Roho Mtakatifu kumwamini kuwa ni Mungu anabaki
amesimamia hapo hapo; na hivyo kubaki kwenye Utatu mtakatifu usioonekana wala
kugawanyika.(Rejea Nyaraka ya Mt. Athanas I, 2) .
Mtakatifu Basilio
Mtakatifu Basilio anaonesha kuwa,Roho Mtakatifu anachukua nafasi anahusika na
Muumba,hivyo anafundisha kuwa Roho Mtakatifu ni Muumbaji.Anashiriki na Muumbaji
katika kuumba.Hivyo basi kwake anamalizia kusema kuwa Roho Mtakatifu ni Bwana na
Mtakatifu(Mungu).
Tertullian
Yeye anampa nafasi Roho Mtakatifu katika fumbo zima la Ukombozi,anaona umoja wa Roho
Mtakatifu katika Umungu wa Baba na Mwana.Zaidi ya yote Tertulian anaonesha kwamba,
Roho Mtakatifu ni Nafsi ya kweli ya Mungu na ukweli.Anafundisha kwa kukemea mafundisho
potofu ya (Praxan).
Origen
Anasisitiza kuwa Roho Mtakatifu ni ukamilifu wa Ukristo,anaelezea kuhusu Roho Mtakatifu
katika kazi yake De Principiis (kilatini),Maana yake Msingi au Mwanzo(Kitu kinachotangulia
vingine).Anasema kuwa Roho Mtakatifu yupo na ni muhimu sana katika Teolojia
(Tauhidi).Hususani katika elimu ya Mungu katika Utatu Mtakatifu.Hauwezi kuutaja utatu
Mtakatifu kama haujataja Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
Origen anazidi kusema kuwa Roho Mtakatifu anajidhihirisha katika Maandiko Matakatifu na
anaoneshwa kuwa Nafsi muhimu sana katika Utatu Mtakatifu katika Ubatizo halari.Ubatizo
unaadhimishwa katika jina la Utatu Mtakatifu yaani Mungu Baba , Mwana na Roho Mtakatifu.
Kanuni ya Ubatizo halari ni … ‘’ (fulani/ unataja jina analopenda kubatizwa na
linalopokeleka na Kanisa ) Nakubatiza kwa jina la Baba na Mwana na la Roho Mtakatifu
,Amina.’’Lazima Nafsi tatu za Mungu zote Baba, ,Mwana na Roho Mtakatifu zihusishwe kwani
huyo ndiye Mungu mmoja katika Nafsi Tatu. Anazidi kutoa mafundisho yake kuwa, Roho
Mtakatifu ndiye anayetakatifuza.Baba anaumba, Mwana(Neno wa Mungu) anamfunua Baba
na Roho Mtakatifu anatakatifuza. Kulingana na Mafundisho ya Origen juu ya Roho
Mtakatifu,anasema kwamba ;Roho Mtakatifu anafanya kazi anawasaidia wale waliokwisha
mpokea Yesu Kristo ili waweze kuishi katika njia njema kama Yesu Kristo mwenyewe.
Mtakatifu Augustino.
Mtakatifu Agustino,ambaye anajulikana kuwa Baba wa fundisho hili imani la Msingi juu ya
Roho Mtakatifu.Ni muhimu katika maendeleo ya Teolojia ya Roho Mtakatifu.Anajikita katika
ukweli wa Ukombozi hususani ,ukombozi wa mwanadamu unaofanywa na Yesu Kristo
anapenda kututafakarisha kwa (Rum 5:5) inayosema ‘’Lakini matumaini hayadanganyi,kwa
maana upendo wa Mungu umeenezwa mioyoni mwetu na Roho Mtakatifu
tuliyempokea.’’(Rejea Rum 5:5).
Mt. Augustino Katika kazi yake ‘’ De Trinitate”’ (kilatini) yaani ‘’Utatu’’,Utatu Mtakatifu wa
Mungu.Anaelezea juu ya Roho Mtakatifu na uhusiano katika Utatu Mtakatifu akikwepa kosa
la kuziwekea nafsi Tatu za Mungu daraja au kipimo ,cha kuonesha kuwa Nafsi moja ni kubwa
kuliko nyingine, na nyingine ni ndogo ambacho kitendo hicho kingeingiza uzushi ( Heresy of
Subordination).
Anaonesha kuwa Nafsi zote Tatu za Mungu zina lingana.Ni katika kuzielezea tu maelezo
yanaweza kutofautiana katika maelezo.Kwa zenyewe hazizidiani ukubwa wala
44
umuhimu.Nafsi zote tatu za Mungu ni muhimu na ni sawa katika Umungu Mmoja.
Anaendelea kueleza kuwa Roho Mtakatifu ni zawadi ya Baba na Mwana katika umoja na Baba
na Mwana. Pamoja kwamba Roho Mtakatifu ni zawadi kutoka kwa Baba na Mwana hata
hivyo,Roho Mtakatifu ni (sawa) mmoja na Baba na Mwana( De Trinitate V, 10 $ 11). Wazo
linalosema kuwa Roho Mtakatifu ni zawadi kutoka kwa Baba na Mwana halina maana
kwamba hapa Roho Mtakatifu ni mdogo kuliko Nafsi nyingine za Utatu Mtakatifu wa
Mungu.Hapana. Kulingana na Mt.Agustino anasema Roho Mtakatifu ni zawadi ikiwa ni
matokeo ya upendo wa Utatu Mtakatifu wa Mungu. 17
10. Kuhusu Utume wa Roho Mtakatifu kwa Kanisa linalosafiri
45
SURA YA PILI
46
NENO WA MUNGU,YAANI YESU ; AKATWAA MWILI AKAKAA KWETU AKAWA
MWANADAMU
Nasadiki kwa Bwana Mmoja Yesu Kristo, Mwana wa pekee wa Mungu.Aliyezaliwa kwa Baba
tangu milele yote…. Mungu aliyetoka kwa Mungu, Mwanga kwa Mwanga, Mungu kweli kwa
Mungu kweli.Aliyezaliwa bila kuumbwa, mwenye umungu mmoja na Baba ambaye vitu vyote
vimeumbwa naye…
Jina ‘’Yesu’’ lilitumika hata wakati wa Agano la Kale (Soma Kitabu cha Ezra 2:2 na
Yoshua 1:1) ,likitumika kama Yehoshua (Yoshua) maana yake Mungu anaokoa,Kumbe sasa
jina Yesu ni kifupisho cha jina Yehoshua ambalo ni Neno la Kiebrania likimaanisha ‘’Mungu
anaokoa’’.
47
Ni yeye, katika Yesu Mwanawe wa milele aliyefanyika Mtu ‘’atakayewaokoa watu wake
na dhambi zao (Rejea Mt 1:21; 2:17).Hivyo katika Yesu, kwa faida ya wanadamu, Mungu
anajumlisha historia yote. 19
Mungu Baba alitaka Mwanae azaliwe duniani kama watoto wengine,kupitia katika
familia .Kama Mtume Paulo anavyoandika Waraka wake kwa Wagalatia akisema Lakini
wakati ulipowadia, Mungu alimtuma Mwana wake aliyezaliwa na mwanamke,aliyezaliwa
chini ya sheria ili awakomboe waliokuwa chini ya sheria,tuweze kufanywa wana (Rejea Gal
4:4).
Mtume Paulo anaendelea kusema, Basi kwa kuwa ninyi mu wana, Mungu amempeleka Roho
wa Mwana wake mioyoni mwenu aliaye ‘’Abba, Baba,Kwa hiyo umeacha kuwa mtumwa, bali u
mwana,na ukiwa mwana,u pia mrithi kwa tendo la Mungu.
Naye Mwana (Yesu) alitaka kuwa kama sisi katika mambo yote ,isipokuwa dhambi (Rejea
Ebr 4:15). Kwa sababu hiyo,akajifanya mtu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu,akazaliwa na
Bikira Maria.Malaika akamwambia : Usiogope Maria ,kwa maana Mungu amekujalia neema
Utachukua mimba na utamzaa mtoto wa kiume, hali nawe utampa jina Yesu… Maria akajibu,
yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?
Malaika akamjibu: Roho Mtakatifu atakushukia ,na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama
kivuli ,kwa sababu hiyo mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu ( Lk. 1:30
-35), Yosefu,Mwana wa Daudi ,usiogope kumchukua Maria awe mke wako,maana amekuwa
mja mzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu (Lk 1:20) .
Kutangazwa kwa kuzaliwa kwa Yesu Kristo kulizindua “ wakati ule maalum’’ wa kutimizwa
ile ahadi na matayarisho ya Mungu katika historia ya ukombozi wa wanadamu,Yesu ndiye
Immanueli yaani Mungu pamoja nasi (Rejea Is 7:14) Na Utabiri wa Mateso ya Yesu (Is 43 )
huo ndio Wimbo wa kwanza wa Mtumishi wa Bwana katika Kitabu cha Nabii Isaya ).
Wimbo huu wa Mtumishi wa Bwana wa Nabii Isaya unakuja kutimilika katika sura nzima ya
Mateso, Kifo na Ufufuko wa Yesu Kristo Bwana na Mkombozi wetu.Tukikumbuka kabla ya
hapo wakati Yesu anabatizwa mtoni Yordani ,tunasoma: ‘’ Baada ya watu wote kubatizwa
na Yesu pia kubatizwa,alipokuwa katika kusali,mbingu zilifunguka na Roho Mtakatifu
akamshukia katika umbo la kiwiliwili mfano wa njiwa tena sauti ikatokea mbinguni ikinena,
‘’ Wewe ndiwe Mwanangu mpendwa ,unipendezaye(Rejea Lk 3:21-22)
Msomaji wangu, hapa Bwana wetu Yesu Kristo anabatizwa katika Mto Yordani ili abariki
vijito vyote vya maji kwa faida ya wokovu wetu kwa njia ya Sakramenti ya Ubatizo. Hakuwa
Ubatizo ndiyo ‘’tiketi’’ na kibali chetu wanadamu kuingizwa rasmi Kanisani kuungana na
jamii ya Wakristo na kuwa Mtoto wa Mungu.Na hapo unakuwa umeungana na Kristo na
Kanisa lake.
Hivyo basi, Ubatizo ni Sakramenti muhimu na sababu ya mtu kupata wokovu,hapa ni kwa
ubatizo halisi, au kwa kutamani kubatizwa (Sheria ya Kanisa Na. 849) .Wakatekumeni
wanapofariki huku bado wanatamani kupata Sakramenti ya Ubatizo,huzikwa Kikristo na
Kanisa, hapa Kanisa linaamini kuwa watu hao au huyo Mkatekumeni,amefariki akiwa na
ubatizo wa Tamaa. (Rejea Sheria ya Kanisa 849 na Katekisimu ya Kanisa Katoliki namba
1259,inasema hivi;Wakatekumeni wanaokufa kabla ya ubatizo,tama yao wazi ya kuupokea
ikiungana na toba ya dhambi zao, na upendo, huwahakikishia wokovu wao ambao
hawakuweza kuupata kwa njia ya Sakramenti). Sakramenti ya Ubatizo inafungulia mlango
kwa sakramenti nyingine kama,Kipaimara,Ekaristi Takatifu, Kitubio,Daraja Takatifu la
Upadre, Mpako wa Wagonjwa, na Sakramenti Takatifu ya Ndoa.Maria aliteuliwa na Mungu
tangu milele ili awe Mama wa Yeye (Yesu Kristo) ambaye ndani yake muna ukamilifu wote.
Mwana wa Mungu alitwaa mwili tumboni mwa Bikira Maria kwa uwezo wa Roho Mtakatifu,
kwa ajili yetu sisi wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu, yaani kusudi atupatanishe sisi
wakosefu na Mungu atujulishe upendo wake usio na mipaka, awe kielelezo cha Utakatifu
kwetu na atushirikishe ‘’ tabia ya UMungu’’ (2Pt 1:4). Ama kweli huyo ndiye Yesu Kristo, jiwe
waliolikataa waashi likawa jiwe la msingi, na jambo hilo linabaki ni la ajabu machoni petu,
toka kwa Kabila la Kiyahudi mpaka kwa Waha na Wandengereko, ( Rejea Zab 118).Licha ya
kwamba Yesu ni Mungu kamili,Yesu ni Mtu pia.Kwa ufupi tunasema kuwa Yesu ni Mungu
kamili na Mtu kamili.Hivyo basi Yesu ni Mungu Mtu,Wakristo Wakatoliki tunaamini ‘’kweli
hiyo’’bila mashaka yoyote kabisa. Na muungano huo wa Umungu na Utu wake, muungano
huo haukuubadilisha Umungu wake. Alibaki kuwa Mungu na ni Mungu milele yote.Kwanza
tufahamu nini lengo la ujio wa Yesu Kristo. Yesu Kristo amekuja duniani kwa ajili ya
49
kutukomboa,kwa kuishi kama sisi wanadamu isipokuwa hakuwa na dhambi (Rejea Ebr 4:14-
15).Ujio wake hapa duniani kama mtu,ulitanguliwa na upendo wa Mungu kwa mwanadamu.
‘’Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe wa pekee,ili kila
amsadikiye asipotee, bali awe na uzima wa milele’’(Rejea Yoh 3:16, Yoh 1:14; Mt 3:17, Rum
8:32).Na anakuja kutoa maisha yake kwa fidia ya dhambi zetu;ambazo kwa anguko la wazazi
wetu wa kwanza Adamu na Eva nasi tumebaki wahanga wa dhambi (Rejea anguko la Adamu
na Eva katika Kitabu cha Mwanzo 3) .
Tukijua na kuamini kuwa Mungu aweza yote na hakuna kisichowezekana kwa
Mungu.Mungu angeweza kutukomboa hata kwa kusema tu mara moja .Pia Mungu
angetaka ingewezekana kwa Mungu, tukakombolewa hata bila mateso ya Kristo,ila
kwa mateso,kifo na ufufuko wa Yesu Kristo; fumbo hili la Pasaka linakuwa ndiyo njia
inayofaa zaidi ,kwani hakuna utukufu bila usumbufu,hakuna msalaba bila
mateso.Hakuna Pasaka bila Ijumaa Kuu.Mungu alitaka amkumbushe na kumshirikisha
mwanadamu maisha ya msalaba,kama tulivyorithi dhambi kwa wazazi wetu Adamu na Eva.
Hivyo basi matokeo ya dhambi hiyo inabaki inatunga’nga’nia kizazi hata kizazi.
Na ili tukombolewe ilimbidi Yesu azaliwe Bethlehemu kwa Bikira Maria kwa uwezo wa
Roho Mtakatifu; katika Yudea wakati wa Mfalme Herode (RejeaSimulizi juu ya Mama Jusi wa
Mashariki waliokwenda kumwabudu Mtoto Yesu Mfalme wa Amani wakapiga magoti,
wakamsujudia.Kisha wakafungua hazina zao,wakampa zawadi: dhahabu, ubani, na
manemane ( Soma, Mt 2:1-12,) aliishi na wanadamu,aliishi kama wao,alijidhihirisha bila
kujificha,alijifunua wamwone kwa macho ya kibinadamu,aliwasikiliza taabu na mahangaiko
yao moja kwa moja.Alionja moja kwa moja maisha ya kibinadamu,ndiyo maana naye akapata
joto,baridi, kiu, njaa, alitembea, alifanya kazi, alichoka kama vile mimi na wewe tunavyoweza
kuchoka ,akajionea dhoruba baharini,akaonja ukimbizi alivyokoswa koswa kuuawa na
Herode (Rejea Mt 2: 13) .
Ndipo akakimbilia Misri alirudi baada ya kifo chake Herode,na neno la nabii likatimia
,kwamba ‘’Nalimwita mwanangu kutoka Misri ‘’(Rejea Mt 2:14- 15) .Mimi Frater Simon
Liberio ni shahidi wa haya ninayoyaandika ,nikidanganya mnipige mawe hadi kufa,
nimeyasoma kwenye Injili Takatifu zote, zina muhusu Yesu Kristo zikushuhudia maneno na
matendo yake,ninayaamini kwa dhati .
Hawa wanawaalika watu wa nyakati zote za kuingia katika ushirika wao na Kristo:Lile
lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia,tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na
mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima,na uzima huo ulidhihirika, nasi
tumeona,tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele,uliokuwa kwa
Baba,ukadhihirika kwetu, hilo tuliliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia
mpate kushirikiana nasi; na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake
Yesu Kristo. Na haya twayaandika,ili furaha yetu itimizwe 22( Rejea 1Yoh 1: 1-4).
20 Ibid, Na.423
21 Ibid, Na.424
22 Ibid, Na.425
51
I. YESU KRISTO NI MUNGU KWELI NA MWANA WA MUNGU KWELI
Imani ya Kanisa Katoliki katika kuamini Uwana wa Mungu wa Yesu Kristo unaelezwa au
kupatikana katika Kanuni zote za Imani (Nasadiki zote)
‘’ Tunaamini na kukubari kwamba Bwana wetu Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu. Ni Mungu
mtu.Ni Mungu aliyezaliwa kwa hulka ya mama yake(Bikira Maria).Ni Mungu kamili na Mtu
kamili’’(DS 40, 54, 86, 148, 214, 290). Fundisho la Imani ya Kanisa Katoliki (Dogma)
linakubali kuwa Yesu Kristo anamiliki hulka ya Umungu wa Milele na Ukamilifu wote wa
Milele kwa kuwa anatoa mamlaka ya utawala katika enzi zote.
52
II.USHAHIDI WA KIBIBLIA A.Ushahidi kutoka Agano la Kale
Agano la Kale linaonesha ushahidi usiokuwa wa moja kwa moja,japo Ushahidi unabaki
palepale kwamba Yesu Kristo ni Mungu Mwana wa Mungu na Masiha.
~ Unabii wa Kimasiha unatabiri Ujio wa Mkombozi kama Nabii( Kumb 18: 15 -18); Kuhani
(Zab 109:4); Mfalme na Bwana,Masiya na Bwana wa Ulimwengu(Zaburi 2:1-11); Mtumishi
wa Mungu anayeteseka(Isa 53), Isaya anamwonesha wazi wazi hapa kuwa Yesu Kristo ni
Mwana wa Mungu.
~ Isa 7:14; 8:8 na Isa 9:6 : Anazungumzia kuhusu Ukubwa wa EMMANUEL,’’Mungu pamoja
nasi’’. ,yaani heshima ya Kimasiha,Waajabu(Mwenye kushangaza na Kuvutia),Mshauri wa
Ajabu; Mungu Mwenyezi, Mfalme wa Amani n.k.
B.Ushahidi kutoka Injili za Ufanano yaani Mathayo, Marko na Luka:
Mwanzo wa Injili ya Marko inasema hivi; Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo (Mwana wa
Mungu) (Rejea Mk 1:1)
Ushahidi wa Mungu Baba wa Mbinguni akimwita Yesu Mwanae mpendwa wake
anayependezwa naye. Wakati wa Ubatizo wake Yesu: ‘’Huyu ni Mwanangu mpendwa
wangu ninayependezwa naye ‘’(Rejea Mt 3:17, Mk 1:11, Lk 3:22).
~Yesu alipogeuka sura Mlimani Tabor: Wakati anasema maneno hayo, tazama, wingu
angavu likawatandia. Mara sauti ikatoka katika wingu lile likisema ‘’Huyu ni Mwanangu
mpendwa,anipendezaye; msikilizeni yeye’’(Rejea Mt 17:5, Mk 9:7, Lk 9:35)
~Wakati wa Ubatizo , Kristo anaelezewa na kuingizwa rasmi katika Utume wa Kimasiya na
uwana wa Mungu unashuhudiwa kwa njia ya Ufunuo wa kiutukufu wa Yohane Mwinjili. Jina
‘’Mwana wa Mungu’’ limetumika katika Agano la Kale likimtambulisha Kristo pekee.
Kibiblia ,maelezo ya ‘’ Mwana Mpendwa’’ limetumika sawa na kusema ‘’ Mwana wa
Pekee’’(Rejea Mwa 22:2, Mk 12:6)
III.Ushahidi wa Yesu:Ukuu wa Yesu kuliko viumbe vyote.
Yesu Kristo anawapita kwa ukubwa Manabii na Wafalme wa Agano la Kale, Yona ,Solomoni(
Mt 12:41,Lk 11:31; ‘’Hapa yupo aliye mkubwa kuliko Yona’’. Anawapita zaidi Musa na Eliya
(Mt 17:3; Mk 9:4, Lk 9:30).
iv.Ni mkubwa kuliko Daudi (Mt 22:43; Mk 12:36; Lk 20:42).Ni mkubwa kuliko wote,hata
Yohane Mbatizaji waliyemtazamia na kumwona mkubwa mpaka Kristo alivyokuja(Mt
11:11; Lk 7:28).Malaika nao ni watumishi wake( Mt 4:11; Mk 1:13, Lk 4:13). Malaika
wataambatana naye katika ujio wake wa pili (Mt 16:27; Mk 8:38; Lk 9:26).
53
V.Amefanana na Mungu: Yesu anakubali mwenyewe kwamba Yahwe aliyezungumzwa
katika Agano la Kale amelingana naye.Amelingana na Mungu.Anawatuma manabii, watabiri
na wataalamu wa sheria( Mt 23:34; Lk 11:49). Kama Bwana (Mungu) anafanya maagano na
mwanadamu (Mt 26:28; Mk 14:24; Lk 22:20). Kama Israeli ilivyo jamii ya Bwana Mungu,
vivyo hivyo Mitume wake ni jamii Yake (Mt 16:18). Kazi zake: Ushahidi wa kazi zake,yaani
miujiza,nayo inaongeza ushuhuda kwa matendo yake, yanamshuhudia Yesu. Japo miujiza
hiyo haikuwa ushahidi pekee wa kumwonesha kuwa ni Masiha,Mungu. Kulingana na Injili ya
nne ya Mwinjili Yohane,miujiza ni ‘’zawadi’’ iliyoendana na upendo na huruma ya Kristo kwa
mwanadamu.Ambayo Umungu wa’’ Ubwana’’ unapatikana katika Kristo.Nguvu ya Kimungu
na Utukufu vinapatikana kwa Yesu na hivyo Asili ya Umungu wake unadhihirika(Rejea Yoh
2:11; 1140). Hiyo ni miujiza ya harusini Kana na ule mwujiza wa kumurudishia Lazaro baada
ya kuwa amekufa takribani siku nne.
VII. Yesu na utambuzi wa kuwa yeye ni Mwana wa Mungu (Mt 25:34, 26:29; Lk 2:49).
Sala ya Baba yetu hii ni sala kwa wafuasi wake Kristo (Mt 6:9).
X Neno alikuwa na Mungu, Naye akatwaa mwili.Nafsi ya pili (Neno) ni tofauti na Baba
(Yoh 1:18). Neno huyo yu sawa na Mwana aliyezaliwa(Yesu).Neno ni Mungu (Yoh 1:3).Neno
ni Yesu, hivyo basi Yesu ni Mungu.
XI.Yesu alikuwepo tangu enzi hizo za nyakati,Ametoka kwa Mungu( Yoh 5:23,37;
6:38 -44) .Ametoka mbinguni (Yn 3:13).Anatoka kwa Mungu Baba (Yoh 8:42; 16:27).
54
XIII.Baba na Yesu ni wamoja ‘’Umoja’’ wa asili (Yoh 10:22 -39) .Muingiliano wa Mungu
Baba na Mwana unawafanya wabaki wamoja na asili moja ya Umungu, ‘’Aliyeniona Mimi
amemwona Baba’’ ( Yoh 14: 9-11).
XIV. Umungu ndani ya Yesu : Yesu alidhihirisha vigezo vyake na kazi zake kuwa za Mungu.
Yeye ni wa milele(Yoh 8:58).Alikuwepo kabla ya Ibrahimu. Yesu akawaambia, ‘’Amini, amini
nawaambieni,kabla ya kuwako Ibrahimu MIMI NDIYE.’’
55
(Rum 8:3)…. ‘’Mungu amemtuma mwanaye’’, Jisomee Kol 1:13; Gal 4:4) na( Ebr.1:4, 1:5- 14)
( Rum 8:32) ‘’Mungu hakumuhurumia hata mwanaye wa pekee bali alimtoa kwa ajili yetu
sote.’’
Mtakatifu Paulo anamwita Kristo ‘’Theos’’ kwa Kigiriki maana yake Mungu (Rum.
9:5).Endelea kujisomea Gal. 1:5; 2Kor 11:31;Fil. 4:20; Tit. 2:13; 1Tim 6:14).
Waebrania 1:8 Lakini kwa Mwana anasema: ‘’ Kiti chako cha enzi,ee Mungu,kipo daima na
milele na fimbo ya utawala wako ni fimbo ya haki’’
56
Mt. Ireneus wa Liyon(+202) Mwana Teolojia muhimu na mashuhuri katika karne ya pili
alipinga vikali mafundisho potofu ya ‘’ Wagnostiki’’ na wa ‘’marcione’’.Ni kuanzia hapo
Alifundisha kwa nguvu kubwa kuhusu umoja kati ya Mungu mwumbaji na Mungu
mwokozi: Umoja kati ya Neno wa Mungu(Yesu) na Ubinadamu wake halisi. Ireneus Adv.
Haer.III 16,6:18,1). Baada ya karne nyingi imani ya kuwa Yesu ni Mungu iliwekwa na
kujidhihirishia kwenye Kanuni ya Imani (Tazama Kanuni za Imani za Mt.Ireneusi,Adv.
Haer.I, 10, I; Tertulian,Adv. Prax.2) 23
23 Ibid Na.423
57
ya Roho Mtakatifu,na kutufanya tushiriki Uzima wa Utatu Mtakatifu(Rejea Yohane Paulo II,
CT 5).25
Kanisa linatoa mwito kwa wale wanaowafundisha watu juu ya huyu Kristo Mungu na
Mkombozi wetu, kama Katekisimu inavyosema, ‘’ Yule ambaye ameitwa ‘’kumfundisha
Kristo Yesu’’, kupoteza kila kitu’’ Ili ampate Kristo na yeye mwenyewe awe ndani yake’’.
24Kenosis ni Neno la Kigiriki likiashiria Kujishusha kwake Yesu Kristo aliye Mungu kwa
kuwa mwanadamu na kuishi kama sisi isipokuwa hakuwa na dhambi. Yesu alikuwa yu Namna
ya Mungu (Rejea Marko 16:12.Neno la Kigiriki lenye maana ya ‘’namna’’ linamaanisha
uonekano wa nje wa ukweli ulio ndani, ni sura inayoonekana au maumbile yanayoonekana
ya Mungu.Kadiri ya aya 5-8,Kristo aliachilia umbo la Mungu na kuchukua umbo la Mtumishi.
Maana yake ni kuwa Kristo aliendelea kuwa katika hali ya UMungu wakati alipojishusha
mwenyewe, yaani wakati alipoutwaa ubinadamu (aya ya 7).Kwa hiyo ni wazi kwamba
utenzi unaeleza kuwa Yesu ndiye ufunuo wa nje wa uhalisia wa ndani ambao ni Mungu.
Yeye ni Mungu. Kuwa sawa na Mungu maana yake ni kwamba Yesu hakung’ang’ania
kwenye hali au nafasi ya usawa na Mungu.Kwa hiyo hakujifanya mwenyewe kuwa Mungu(
kwani jambo hilo haliwezekani) na hata kuwa sawa na Mungu,bali alijishusha kutoka
kwenye utukufu wa Mungu ambao ulikuwa wake kwa haki na kutoka kwenye kuzitumia
sifa za Kimungu .
Asili yake ya Kimungu ilijificha kwenye mapungufu ya hulka yake ya kibinadamu.
Maneno yote kwetu sisi yanasisitiza maonyo ya Mtume Paulo, juu ya Unyenyekevu
na Huduma kwa wengine, Wataalamu kwa pamoja wanakubali kwamba vifungu
vifuatavyo vina tenzi za Kristo ,aya ya 6-11, Kol 1:15- 20, 2:14-15, Efe 1:10, 1:20 -23,
2:14 -16, 1Tim 3:16, Ebr 1:1-4(labda pia 2:14-15, 17-18, 5:7-9, 12:1) 1Pet 2:22 – 24,
3:18.21, Yn 1:1-3-5, 9:11.14-16.(Imenakiriwa kutoka kwenye Biblia toleo la ‘’Biblia
ya Kiafrika’’ katika kuchimbua Rejea ya Wafilipi 2:6).
Kanisa linatoa mwaliko na wajibu wa Mkristo yeyote mbatizwa, kwamba Kutokana na elimu
hii ya upendo wa Kristo: inazaliwa tamaa ya kutangaza ‘’ kueneza Injili’’ kuwaongoza wengine,
‘’kukubali’’ imani katika Yesu Kristo.Wakati huo huo anaonja hitaji la kujua siku zote vizuri
zaidi imani hii. Kwa lengo hili, tukifuata mpango wa Kanuni ya Imani, kwanza yatawekwa
majina ya msingi yanayomhusu Yesu: ‘’Kristo,’’ Mwana wa Mungu’’ na Bwana.
‘’Akapata Mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kwake yeye Bikira Maria akawa
Mwanadamu’’(Kanuni ya Imani ya Nicea inatufundisha hivyo na tunaamini bila ubishi
wowote) kwa Rejea Mt.1:18
Baada ya kuona Umungu wa Yesu,hebu tulitupilie macho fundisho la Msingi kuwa Yesu pia
ni Mtu kamili.
Licha ya kwamba Yesu ni Mungu kamili,Yesu ni Mtu pia.Kwa ufupi tunasema kuwa Yesu ni
Mungu kamili na Mtu kamili.Hivyo basi Yesu ni Mungu Mtu,Wakristo Wakatoliki tunaamini
’’ kweli hiyo’’ bila mashaka yoyote kabisa.Na muungano huo wa Umungu na Utu
wake;Haukuubadilisha Umungu wake.Alibaki kuwa Mungu na ni Mungu milele yote.Kwanza
tufahamu nini lengo la ujio wa Yesu.
Yesu amekuja duniani kwa ajili ya kutukomboa,kwa kuishi kama sisi wanadamu
isipokuwa hakuwa na dhambi (Rejea Ebr 4:14-15).Ujio wake hapa duniani kama
mtu,ulitanguliwa na upendo wa Mungu kwa mwanadamu. ‘’Kwa maana jinsi hii Mungu
aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe wa pekee,ili kila amsadikiye asipotee, bali
awe na uzima wa milele’’(Rejea Yoh 3:16, Yn 1:14; Mt 3:17, Rum 8:32).Na anakuja kutoa
maisha yake kwa fidia ya dhambi zetu;ambazo kwa anguko la wazazi wetu wa kwanza
Adamu na Eva nasi tumebaki wahanga wa dhambi (Rejea anguko la Adamu na Eva Mwanzo
3) .
Na ili tukombolewe ilimbidi Yesu azaliwe Bethlehemu kwa Bikira Maria kwa uwezo wa Roho
Mtakatifu; katika Yudea wakati wa Mfalme Herode (Rejea Mama Jusi, Mt 2:1-12,) aliishi na
wanadamu,aliishi kama wao,alijidhihirisha bila kujificha,alijifunua wamwone kwa macho ya
kibinadamu,aliwasikiliza taabu na mahangaiko yao moja kwa moja.
Alionja moja kwa moja maisha ya kibinadamu,ndiyo maana naye akapata joto,baridi, kiu,
njaa, alitembea, alifanya kazi, alichoka kama vile mimi na wewe tunavyoweza kuchoka
,akajionea dhoruba baharini,akaonja ukimbizi alivyokoswa koswa kuuawa na Herode (Rejea
Mt 2: 13) .Ndipo akakimbilia Misri alirudi baada ya kifo chake Herode,na neno la nabii
likatimia ,kwamba ‘’Nalimwita mwanangu kutoka Misri’’(Rejea Mt 2:14- 15)
60
Yesu alikuzwa maisha ya kifamilia Yosefu Baba Mlishi wake na Mama Bikira Maria
Mama yake.Alipata mahitaji ya kitoto aliviringishwa kwenye mavazi ya kitoto(Rejea
Mk 2:6-7).Akanyonya maziwa ya mama yake Bikira Maria,kama vile mimi na wewe
tulivyonyonyeshwa na mama zetu.
Wakati wako Yerusalemu kama ilivyo desturi ya Wazazi, kila mwaka walikwenda
Yerusalemu kwa siku kuu ya Pasaka; Mtoto Yesu akiwa na takribani miaka kumi na miwili ,
alijichanganya na watu wakubwa mpaka akaelekea hekaluni akabaki Yerusalemu akiongea
na Walimu akiwasikiliza na kuwauliza maswali bila wazazi wake kufahamu(Rejea Mk 2:41-
51).Akaongezeka katika hekima na umri akimpendeza Mungu na wanadamu(Rejea Mk2:52)
Jamani angalieni unafiki mkubwa wa Pilato baada ya kutoa ‘’kichapo’’ kumpiga Bwana wetu
Yesu Kristo,eti anajisemesha kwamba haoni kosa juu yake (Rejea Yoh 19:4).
61
Aliweza kuhisi kiu, kama mimi na wewe hata akatamka mwenyewe ‘’Naona kiu’’(Rejea
Yoh 19:28-30 ). Wakagawana nguo yake kwa kuipasua na kuipigia kura kwani haikuwa na
mshono.Alivaa mavazi (nguo) kama mimi na wewe mwanadamu.Kwa uchungu moyoni
naye aliweza kulia,mfano,pale alipokaribia zaidi na kuona mji wa Yerusalemu,akaulilia
machozi (Lk 19:41- 44). Aliweza kuwapuuza waliokuwa wanamwuliza maswali kwa
kumtega (Rejea Lk 20:8).
Kama wanadamu wengine Yesu alikua kwa kimo na hekima na kupendwa mbele ya
Mungu na watu na neema ya Mungu ilikuwa juu yake (Rejea Lk 2:40). Vile vile alijipokea
akajikubali kuwa ni Mtu kati ya watu,ni mwanadamu kati ya wanadamu.Akiongea nao
akionesha ananjaa (Rejea Mt 4:2; Lk 4:2), Kiu(Rejea Yn19:28). Alikula na kunywa kama
mimi na wewe tunavyo kula na kunywa (Rejea Mt 11:9; Lk 7:34). Alilala ( Rejea Mt 8:24;
Mk 4:38; Lk 8:23).
Alitembea akachoka sana na kutoka jasho la damu (Rejea Lk 22:44). Yesu alichapwa,
akateswa, akafa msalabani ((Rejea Mt 27:45- 56; Mk 15:33-41; Yoh 19:28-30). Yesu alizikwa
kaburini (Rejea Mk 15:42-47; Lk 23:50 -56; Yoh 19:38 -42)
Kwa vigezo hivi na vingine vinavyomdhihirisa kuwa kweli Yesu alikuwa ana hulka ya
kibinadamu pia.Yesu alikuwa ana uanadamu.Hivyo basi Yesu alikuwa Mungu na mtu
(Rejea Mt 12:40).Kwani aliweza kupata yale Yaliyompata, yale ambayo mwanadamu
aliweza kupata .
Mtume Paulo anamwita Mshenga, mpatanishi ‘’ Mtu Yesu Kristo (Rum 5:15; 1Kor 15:21;
1Tim 2:5 >Inasema, ‘’Kwa maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi baina ya wanadamu ni
mmoja ndiye mwanadamu Kristo Yesu’’. Anaweka bayana asili ya Ubinadamu wa Kristo
(Rum 1:3; 9:5>Inasema ‘’Mababu ni wao, na hata Kristo ametokea kwao kadiri alivyo
mwanadamu, ndiye yeye aliye juu ya yote, Mungu na kutukuzwa milele. Amina ’’.
62
1. MTAGUSO WA KWANZA WA NIKEA (NICEA, 325 AD)
Mtaguso wa kwanza wa Nikea uliitishwa wakati Baba Mtakatifu akiwa Papa Silvesta wa
kwanza.Takribani idadi ya Maaskofu 300 Wakatoliki walihudhuria Mtaguso huo.Kimsingi
Mtaguso huu kuitwa kwake ilikuwa ni baada ya ushawishi wa Mfalme Konstantini aliyekuwa
ameongoka na kuwa Mkristo mnamo mwaka 313 A.D. Na hili lilifanywa ili kupambana na
kupinga uzushi wa Ariusi,aliyeukana Umungu wa Yesu Kristo. Hivyo basi Mtaguso huu
ulifundisha kuwa Yesu ni Mungu kamili na mtu kamili.Fundisho hilo lilikuwa ni katika
kupinga uzushi wa Ariusi.Na hivyo mtaguso huo ulilaani mafundisho ya uongo ya Ariusi
yaliyokuwa yanaukana Umungu wa Yesu.Hivyo basi, Mtaguso wa wa Kwanza wa Nikea
ukamtangaza rasmi Ariusi mzushi na mafundisho yake yakalaniwa kwa uzushi
huo.Hatimaye kwa nguvu zote kabisa Mtaguso ukatangaza Fundisho Msingi Imani ya Kanisa
Katoliki kuwa Yesu ni Mungu kamili na Mtu kamili.
Mtaguso wa Efeso uliitishwa mnamo mwaka 431 AD. Kimsingi Mtaguso huu uliiitishwa kwa
mikakati iliyopangwa na Mfalme Theodosiusi wa Pili. Maaskofu takribani 200 Wakatoliki
walihudhuria Mtaguso huu katika vipindi vikuu vitano vya Mtaguso huu.Wakati huo
aliyekuwa Baba Mtakatifu alikuwa ni Mtakatifu Selestini wa kwanza. Mtakatifu Selestini
aliwakilishwa na baadhi ya Wawakilishi wake katika Mtaguso huu wa Efeso. Mtaguso huu
uliyapinga na kuyalaani Mafundisho ya Nestoriusi. Nestoriusi alikana uwezekano wa
muungano wa hulka ya Kimungu na hulka ya Ubinadamu katika Yesu Kristo.
Mtaguso wa Kalsedoni ulitoa na kuendelea kufafanua kwa kufundisha kuwa Hulka (Natures)
mbili za Yesu Kristo yaani Umungu wa Yesu na Ubinadamu wa Yesu ,hulka mbili hizo za
63
Umungu na Ubinadamu zimeungana na hivyo haziwezi zikagawanyika , wala kuchanganywa
wala kubadilika kwa njia yoyote. Hivyo basi Yesu Kristo Mnazareti ni Mungu na Mtu. Kwa
Kiingereza tunaweza kusema ;(The Doctrine: The two Natures in Christ are united (in a
person) but not confused ,nor changed, nor altered in any way whatsoever. It was against
Eutyches, the Council condemned Monophysticism (Cfr. DS 212 -228)
Takribani Maaskofu 600 waliweza kuhudhuria Mtaguso huu katika vipindi vyake vikuu
17.Mtakatifu Leo wa Kwanza (Leo Mkuu) alikuwa ndiye Papa wakati huo.Mtaguso huu
uliyapinga mafundisho ya kizushi yote yaliyoshikilia kuwa uzushi kwamba Yesu alikuwa ana
hulka moja ya Umungu na kwamba hakuwa na ubinadamu wa kueleweka kwani uzushi huu
uliukana ubinadamu wa Yesu Mnazareti. Huu ni uzushi kabisa uliozushwa na mtu aliyeitwa
Eutyches. Mafundisho haya yakizushi yalipingwa na viongozi wa Kanisa katika Mtaguso wa
Kalsedoni kwa nguvu zote na kuulaani uzushi huo wa Eutyches.
Mtaguso wa Tatu wa Konstantinopoli ulibaki imara kwa kufundisha ukweli ule ule
kwamba Yesu Mnazareti ni Mungu kamili na Mtu kamili. Mtaguso huu uliendelea
kufundisha kuwa Katika Kristo kuna hulka ya Mungu na hulka ya Ubinadamu lakini
bado anabaki kuwa katika Nafsi Moja .Agathonus na Leo wa Pili walikuwa ni Mapapa
(Mababa Watakatifu) waliohusika katika Mtaguso huu wa Kiekumenika nikimaanisha
kwamba ni moja ya Mtaguso unaoshirikisha Maaskofu wote duniani kwa ajili ya
Kuelekeza,Kufundisha ,kujadili miongozo ya ya Utume wa Kanisa Katoliki. Na hivyo pale
Maaskofu Wakatoliki wote duniani wanapokutana pamoja katika muungano na Askofu wa
Roma, ambaye ni Papa kama chombo kimoja.Baba Mtakatifu ndiye mwenye mamlaka ya juu
kabisa miongoni mwa Wakristo kwa kufundisha na kuongoza jamii ya waamini wote
duniani.
64
SURA YA TATU
Sura ya Tatu ya Kitabu hiki inalielezea kwa upana sana Fumbo la Utatu Mtakatifu wa
Mungu.Kwanza kabisa ,inatoa Ufafanuzi wa Fumbo la Utatu Mtakatifu wa Mungu na Maana ya
Fumbo la Utatu Mtakatifu wa Mungu na Maana ya Fumbo la Imani.Sura hii ndiyo
itakayotuambia katika Kanisa ni Fumbo gani kuu la imani na maisha ya Kikristo
…………………………….
‘’Mungu Baba amemzaa Mwana. Mwana amezaliwa kutoka kwa Baba. Roho
Mtakatifu anatoka kwa Baba na kwa Mwana’’. (Hili ni Fundisho la Msingi la Imani
ya Kanisa Katoliki juu ya Utatu Mtakatifu wa Mungu)
Utatu Mtakatifu wa Mungu ni Moja kati ya mafumbo makubwa ya imani ya Kanisa Katoliki.
Hili ni moja kati ya mafumbo ya Imani yanayoonesha tofauti kubwa kati ya Ukristo na
Uislamu au imani ya Kiyahudi.Wakristo wanaamini kuwa Yesu aliwafunulia ukweli kwamba
Mungu ni Mmoja kwa hakika ni Nafsi Tatu; Baba ,Mwana na Roho Mtakatifu: ambazo
tunaweza kuzipambanua lakini siyo kuzitenganisha. Ni Nafsi Tatu za Mungu zisizotenganika
zenye Umungu sawa.Na Nafsi hizo Tatu ni Mungu Mmoja.
Kwanza kabisa kabla hatujadili Utatu Mtakatifu tuone maana ya neno Fumbo la Imani.
Ukweli wa Mungu ambao hatuwezi kuujua kimaumbile ni ule unaopita uwezo wa akili
zetu za kimaumbile.Huo ni ukweli mpitamaumbile, na tunaweza tu kuujua
kipitamaumbile, kwa msaada wa Mungu. Kwa mfano Utatu Mtakatifu, Ufufuko wa
Yesu Kristo, Umwilisho wa Neno, Neema, Maono yenyeheri. Neema ya msaada, Neema
takatifuzi, Uwepo halisi wa Yesu Kristo katika Ekaristi Takatifu. Ukweli wa namna hii
huendelea kuzipita akili zetu za maumbile hata baada ya kufunuliwa,na zafahamika
kwa imani peke yake,au kwa akili inayoangaziwa na imani. 30
30 Ibid, Uk. 6
66
Ukweli huu ni Fumbo la Imani; Wazo hapa ni moja kwamba akili ya kibinadamu huona
vigumu sana kulipokea.Moja kati ya mafumbo makubwa ya imani ya Kanisa Katoliki ni lile
tulilozungumzia hapo juu.Nalo ni fumbo la Utatu Mtakatifu. Hili ni moja kati ya mafumbo ya
Imani yanayoonesha tofauti kubwa kati ya Ukristo na Uislamu au imani ya
Kiyahudi.Wakristo wanaamini kuwa Yesu aliwafunulia ukweli kwamba Mungu mmoja kwa
hakika ni Nafsi Tatu; Baba ,Mwana na Roho Mtakatifu: ambazo tunaweza kuzipambanua
lakini siyo kuzitenganisha.Kwa vyovyote vile hautoshi,lakini tunaweza kuona kitu fulani
ambacho huonekana ni kimoja,lakini pia kinaweza kuwa katika hali yautatu.Mifano
mingine,yote ina mipaka yake,la sivyo ingeweza kutolewa. Lakini,pamoja na juhudi dhahiri
za wana teolojia,Wakristo hawadai kuyaelewa mafumbo hayo ya imani; wao wanachofanya
ni kuyakubali tu31 (De Fide kwa Kilatini) Fundisho la Imani; maana yake Mafundisho haya
yako juu zaidi ya akili zetu,tunapaswa kuipa Imani kipaumbele zaidi kuliko akili zetu zenye
mwisho wa kuelewa mambo ya Mungu, katika kuyatafakari). Kama Wakristo wasingeamini
katika Neno la Kristo na Kanisa lake, basi wangekuwa wajinga kuamini mafundisho ya imani
kama hayo.Lakini imani ni zawadi toka kwa Mungu, na kwa wale wanaopewa,inawafungulia
dunia yenye ukweli wa kiroho ndani kabisa,ambao ni sehemu ya dini yao. 32
Lakini si alama tu,ila pia chombo,yaani,Mungu anatumia Kanisa kama chombo chake kwa
kufanya umoja huu. Hivyo tunafahamu pia Kazi ya Kanisa hapa duniani yaani
kuwaunganisha watu wote katika umoja (Rejea Maelezo ya Hati Kumi na Sita za Mtaguso wa
Vatican ,Lumen Gentium, yaani Mwanga wa Mataifa namba 1).Hayo yote Mtaguso unataka
kuyafasiri katika hali hii.
31 Ibid Uk. 20
32 Ibid Uk. 20
67
Fumbo lililo kiini cha imani na maisha ya Kikristo ni fumbo la Utatu Mtakatifu.Wakristo
wanabatizwa kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu,(Rejea KKK –Ufupisho
Makini namba 44). Utatu Mtakatifu huja kwa namna ya pekee kwa Sakramenti ya Ubatizo.
Sheria ya Kanisa Katoliki namba 849) inasema hivi.
4.Ishara ya Msalaba ina ufunua Utatu Mtakatifu katika Sala zetu za kila siku
Je, unaweza kusema lolote lile juu ya Yesu Kristo bila kuzungumzia Msalaba? Utakuwa
unaleta mzaha,mbona hata watoto wadogo wa shirika la mtoto Yesu watakuzomea.Kwani
Salaamu yao maarufu ni ‘’Imani Katika Msalaba ,unajibu Kristo katika Upendo’’ .Teolojia yake
hapa ni kwamba Imani yetu kwa Yesu Kristo inajikita katika upendo wa Kristo aliyekuwa
tayari kujitoa maisha msalabani kwa fidia ya dhambi zetu sisi wanadamu. Ni mwaliko wangu
kusaidiana katika kukumbushana kuheshimu Misalaba popote pale.Kwani Msalaba siku zote
unasistiza Ukombozi wa Kristo na Utatu Mtakatifu kwa kusali kwa jina la Baba na la Mwana
na la Roho Mtakatifu.Amina.
Wakristo wakatoliki tunahimizwa siku zote tunapoanza kusali au kumaliza sala kwa kuanza
na ishara ya msalaba.Huwa tunafungua na kufungua sala zetu kwa jina la Baba na la Mwana
na la Roho Mtakatifu.Ishara hii inazitaja Nafsi zote tatu:Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
Ni ishara inayotangaza ukombozi uliofanywa na Yesu Mungu na mkombozi wetu kwa
mateso,kifo na Ufufuko.Tunaamini katika Utatu Mtakatifu,na ni katika Utatu Mtakatifu ndimo
unamotoka Msalaba wa Yesu msulubiwa.Ishara ya Msalaba inatumika kwa Waamini
Wakristo,japo kuna madhehebu ya Kikristo yasiyotumia ishara ya Msalaba,eti bado wanajiita
Wakristo .Hawajui kama hawajui ukweli au
68
Japo katika kazi tendaji za kila Nafsi ya Mungu zajidhihirisha katika utofauti,utofauti
huo ni katika Mantiki hii :Kwamba Mungu Baba alimzaa Mwana (Yesu) na Roho Mtakatifu
atoka kwa Baba na Mwana. Na kuanzia hapo tunakutana na Fumbo la Utatu Mtakatifu.
Kielelezo alichokitumia Mtakatifu Patrisi kusaidia watu waelewe kwa kiasi chake uzito wa
Fumbo hili,alisema: Mungu Baba,ni Mwumbaji, Yesu Kristo, Mwana wa Mungu ni
Mkombozi,alitukomboa na Roho Mtakatifu wa Mungu ni Mshauri,Roho wa kweli. Kwa
maelezo mengine tunaweza kusema kuwa Mungu Baba ametuumba, Mungu Mwana
ametukomboa kwa mateso,kifo cha aibu msalabani na ufufuko ukiwa ndiyo ishara ya ushindi
dhidi ya shetani ,aliye baba na asili ya uovu wote.
Na Mtume Paulo anawaandikia Wakristo wa Roma hivi: Kwa yeye (Yesu Kristo)
tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo tunasimama ndani yake… Pendo la
Mungu (Baba) limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi
(Rejea Rum 5:1-5).
Mwinjli Yohane katika (Yoh 16:12-15) Yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli,
atawaongoza awatie kwenye kweli yote Yeye atanitukuza mimi (Yesu) Kwa kuwa atatwaa
katika yaliyo yangu…Yote aliyo nayo Baba ni yangu…
Nafsi Tatu za Mungu zimetajwa kwa uwazi kabisa, japo hazijatajwa kwa jina ‘’Utatu
Mtakatifu’’ hata hivyo zinabaki ni Utatu Mtakatifu.
Kwa upande mwingine, Miongoni Mwetu Wakatoliki tumekuwa tukisali kwa sala ya
Atukuzwe Baba na Mwana na Roho Mtakatifu kwa mazoea bila kutafakari Fumbo hili la
Mungu katika Utatu Mtakatifu.Kwani tunaposali sala hii tunautukuza Utatu Mtakatifu
unaopatikana katika Mungu Mmoja. Sala ya hii tunaweza kuiweka kwa namna nyingine tena
kwa kusali ‘’Utukuzwe daima Ee Utatu Mtakatifu ‘’ .Hivyo basi sala hizi ni fupi lakini zina
uzito wake katika kuutukuza Utatu Mtakatifu.
Huyo ndiye Mungu wetu ,Mungu anayeabudiwa katika Utatu Mtakatifu. Ukristo hauwezi
ukasimama bila kuamini kwamba Mungu yu katika Nafsi Tatu,Mungu Baba,Mwana na Roho
Mtakatifu.Ndio kusema kddwamba Mungu anayeabudiwa na sisi Wakristo ni wa Utatu
Mtakatifu.Ni Mungu anayejidhihirisha katika Utatu Mtakatifu.
69
Kwa Utatu Mtakatifu, yaani Mungu Baba(Mwenyezi,Muumba mbingu na dunia) na
Mwana(Katika Yesu Kristo Mwana wa pekee wa Mungu, Bwana wetu,aliyezaliwa kwa uwezo
wa Roho Mtakatifu… toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu) … na Roho
Mtakatifu,Bwana Mleta uzima, atokaye kwa Baba na Mwana. Nasadiki Kanisa Katoliki(lenye
kuleta ukombozi kwa watu wote,kabila zote,mataifa yote,rangi zote,matajiri kwa
masikini).Kwa mantiki hiyo hivyo, Kanisa Katoliki linatangaza Injili kwa watu wote,ili
wapate kuongoka. Hiyo ndio kazi iliyomleta Kristo huku duniani.
Pia, Imani yetu Wakristo Wakatoliki ,inatuoongoza katika kuamini Ufufuko wa mwili
na uzima wa milele ambao kila mtu ‘’anaumezea mate’’(anautamani) .
Kanuni ya Imani ya Mitume,kwa uhakika inajumlisha ungamo la imani katika Mungu Baba,
Mwana na Roho Mtakatifu,yaani ;Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.Hata hivyo inatoa ‘’amini’’
juu ya Yesu Kristo kwa mfano katika Ufufuko kwa kuonesha mpango mzima wa kazi za Utatu
Mtakatifu.
Pamoja kwamba Nafsi hizi Tatu za Mungu zipo bila kugawanyika na kuwa sawa na
kwamba kila Nafsi ni Mungu;bado Nafsi hizi zinatofautiana, Nafsi Tatu zinazotofautiana
katika mantiki hii, Mungu Baba anamzaa Mwana(Yesu) bila kuumbwa ambaye ni Mungu
milele yote na Roho Mtakatifu antoka kwa Baba na Mwana.33 Ama kweli hili ni Fumbo la
Imani yetu linadai imani,linabaki kuwa fumbo kweli hata baada ya kuwa limefunuliwa na
Bwana wetu Yesu Kristo.Si jepesi ni gumu sana na lapita mafiko ya akili zetu,chakufanya
hapa tunapapasa yale ambayo akili zetu za kibinadamu zaweza kufika na kubaki kuamini bila
shaka lolote.
33
HILL, EDMUND, The Mysteries of Trinity, (Introducing Catholic Theology; 4),
Westminster, 3 July 1985, p.4
70
Kumbe basi Imani ndio ituongoze katika kuamini na akili zatuonesha ufunuo huo kwa
njia ya Kristo.Kwani hakuna aliyemwona Mungu ila yule aliyemwona Mwana(Yesu Kristo)
anayemtambulisha kwetu tunasoma hayo katika ( Yoh 1:18).Kwa neno ,Roho Mtakatifu aliye
sawa na Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.Maana yake kwa kila Nafsi Moja ni Mungu,yaani
Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu.Nafsi Tatu za Mungu zinaufanya
Utatu Mtakatifu wa Mungu mmoja.Bado anabaki kuwa Mungu Mmoja katika Utatu Mtakatifu
wa Mungu tunayemwabudu kwa dhati yote.Hilo ndilo Fumbo la Imani katika Utatu Mtakatifu
.
Hapa cha msingi kabisa ni kwamba tunaamini na kujishikamanisha sisi wenyewe kwa
Mungu na kuishi fumbo hili ‘’ Kwa jina la Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho
Mtakatifu.Mungu mmoja katika Utatu Mtakatifu usiogawanyika. Na hayo tunayaungama
katika kanuni ya Ubatizo yaani ,yule aliyetayari kubatizwa anabatizwa katika Utatu
Mtakatifu, ‘’ Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu’’.
Na hiyo ndiyo Kanuni ya Ubatizo ulio sahihi, halari,na wa Sakramenti ,pale Mtu
anapobatizwa kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.Hatubatizwi kwa jina la
Yesu tu,kama wafanyavyo wengine.Tunabatizwa katika Utatu Mtakatifu wa ,Mungu Baba
,Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu.
Imani ya Kanisa Katoliki ni hii: Tunamwabudu Mungu mmoja katika Utatu,na Utatu katika
Umoja,na si miungu watatu,waliojigawanya. Bali ni Mungu Mmoja.Kwani ni Nafsi Tatu za
Mungu mmoja.Au tusema tunamwabudu Mungu mmoja katika Nafsi tatu.Nafsi ya kwanza ni
ya Baba,nyingine ya Mwana,nyingine ni ya Roho Mtakatifu.Lakini Nafsi hizo Tatu za Mungu
Baba,Mwana na Roho Mtakatifu, pamoja nafsi hizo kuwa tatu bado ni Mungu Mmoja .Nafsi
hizo zote Tatu ni Mungu mmoja.Nafsi zote Tatu zinalingana umilele wao.
71
8. Kanuni ya Imani ya Athanasi (+376) Quicunque Vult
Ukamilifu ulio rasmi wa fundisho juu ya Utatu Mtakatifu, unapatikana katika Kanuni
inayoitwa Kanuni ya Athanasi (Athanasian Creed).Inasadikika kuwa machimbuko yake
yaliandikwa katika Lugha ya Kigiriki,ndiye aliyeingiza neno ‘’Ulingano wa Nafsi Tatu za
Mungu.’’Athanasi alifariki (+376 BK),ni shujaa wa fundisho la Mtaguso wa Nikea ambaye
anabaki kwenye kumbukumbu za vichwa vya Wakristo Wakatoliki na wanahistoria wa
Kanisa hili linalosafiri.
Imani Katoliki ndiyo hii: Tunamwabudu Mungu Mmoja katika Utatu na Utatu katika
Umoja,bila kuchanganya nafsi,wala kutenganisha uwamo:Kwani ni nafsi ya Baba,
nyingine ya Mwana,nyingine ya Roho Mtakatifu,ni umungu mmoja,wa Baba,na wa
Mwana na wa Roho Mtakatifu,utukufu ulio sawa,ukuu wa pamoja wa milele (Kanuni ya
Imani ya Athanasi )
Na katika Nafsi hizi tatu za Mungu hakuna mmoja aliye ‘’bosi’’ wa mwingine na hufanya kazi
bila mtengano.Kupelekwa kwa Roho Mtakatifu,ambaye Baba anamtuma kwa jina la Mwana,
na ambaye Mwana anamtuma ‘’toka kwa Baba’’(Yoh 15:26) kunafunua kwamba Yeye pamoja
nao ni Mungu huyo huyo mmoja. ‘’Anaabudiwa na kutukuzwa pamoja na Baba na Mwana
(Rejea Symbolum Nicaenum –Constantinopolitanum)34 = Nafsi za Mungu hazitengani katika
uwamo,nafsi za Mungu katika mambo yale wanayofanya. Lakini katika kazi moja moja za
Mungu kila nafsi huonesha kile kilicho chake katika Utatu hasa katika Utume wa Mungu wa
Umwilisho wa Mwana na Utume wa Paji la Roho Mtakatifu ( KKK 267).
Baada ya kuona yale tunayoyaamini katika Kanuni ya Imani hususani ya Mitume, Athanasi
,Nikea.Tujiulize kwa nini tunayaamini? Kwa nini tunamsadiki Mungu Mmoja katika Nafsi
Tatu,Mungu Baba,Mwana na Roho Mtakatifu? Majibu yanaweza yakatolewa kwa ufupi
kabisa,Sisi Wakristo Wakatoliki tunamsadiki na kumwabudu Mungu katika Utatu Mtakatifu
kwa sababu yamefunuliwa na Mungu mwenyewe,ili tufanye hivyo.
Swali jingine, tulifunuliwaje imani hii ya Mungu katika Utatu Mtakatifu?Na ilikuwa lini? Jibu
ya maswali haya mawili yanajibiwa kama ifuatavyo;Imani hii ya Utatu Mtakatifu inafunuliwa
wazi wazi katika Nafsi ya Pili ya Mungu yaani Yesu Kristo Bwana na Mkombozi wetu.Wakati
gani, Imani hii japo katika Agano la Kale linadokeza kwa mbali,lakini ni katika Agano Jipya
imani hii ya Utatu Mtakatifu inajifunua wakati Yesu(Nafsi ya pili ya Utatu Mtakatifu) akiishi
,akifundisha,alivyokufa na kufufuka kutoka wafu na kupaa kwake Mbinguni kuume kwa
Baba.35
Kwa ‘’kupekua na kuzisoma Injili za Wainjili wote wane na Nyaraka mbalimbali katika
Bibilia Takatifu(hususani Agano Jipya) humo ndimo kuna tunu za Maisha,Matendo na
Mafundisho ya Yesu Kristo . Tunaweza kuona kwamba ,katika kufunuliwa kwetu Fumbo
hili,Mungu anamtuma Mwana wake wa pekee Yesu Kristo kuja ulimwenguni.
Na ujio wa Yesu Kristo unashuhudia ufunuo huo na kupokelewa na Mitume na Wafuasi wake
Yesu Kristo.Na kazi ya kuufundisha kulingana na mafiko(uwezo) wa akili kibinadamu
ukiangazwa na Roho Mtakatifu unaendelezwa na Kanisa kupitia Watumishi wake Maaskofu,
Mapadre na Mashemasi.
73
Utatu Mtakatifu wa Mungu unafunuliwa na Yesu Kristo kwa Mitume wake kwa kuwaambia
hivi : ‘’Basi nendeni,mkayafanye mataifa yote kuwa wafuasi mkiwabatiza kwa jina la Baba na
la Mwana na la Roho Mtakatifu (Rejea Mt 28:19). Ukiendelea kusoma mstari unaofuata
unasema Mkawafundishe kushika yote niliyowaagiza.Na tazama nipo nanyi siku zote mpaka
mwisho wa dahari. Ilikuwa ni wajibu wa Mitume kufundisha hayo yote Kristo
aliyowaagiza,na Mafundisho haya tunayarithi tangu kizazi cha Wakristo wa jamii ya
Waamini wa kwanza mpaka kwetu sisi ambao bado tunapumua leo hii.
Kwa hiyo,pamoja kwamba,Fundisho Mama la Kanisa juu ya Utatu Mtakatifu,lililofunuliwa
kwa wazi wazi katika Agano Jipya zaidi ya Agano la kale lilivyoufunua.Kanisa Katoliki
limebaki linaamini ukweli huu.Na kwa namna nyingine Ufunuo huo juu ya Utatu
Mtakatifu;hujidhihirisha katika uzoefu wa maisha ya kila siku ya Mkristo na Sakramenti.Ni
kwa hilo nikaweza kukiita kitabu hiki Roho Mtakatifu na Fumbo la Utatu Mtakatifu katika
Maisha ya Mkristo na Sakramenti.Kwani ,Utatu Mtakatifu,Mungu Baba,Mwana na Roho
Mtakatifu hujidhihirisha katika Maisha ya Mkristo na Sakramenti.
74
9.KANUNI YA IMANI YA NIKEA
Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, Mwumba mbingu na dunia. Na kwa Yesu
Kristo, Mwanaye wa pekee, Bwana wetu; Aliyetungwa kwa RohoMtakatifu,
akazaliwana Bikira Maria, akawa mwanadamu. Akasulubiwa kwa ajili yetu sisi,
akateswa kwa mamlaka ya Pontio Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa; akashukia
kuzimu, siku ya tatu akafufuka katika wafu; akapaa mbinguni; amekaa kuume kwa
Mungu Baba Mwenyezi toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu. Nasadiki
kwa Roho Mtakatifu,Kanisa takatifu katoliki,ushirika wa watakatifu,maondoleo ya
dhambi,ufufuko wa miili na uzima wa milele.Amina.
75
Biblia Takatifu inautaja Utatu Mtakatifu, Imani ya kumwabudu Mungu katika Utatu
Mtakatifu.Si jambo la kujitungia,bali lina vyazo na ushahidi wake kutoka katika Maandiko
Matakatifu na Mapokeo ya Kanisa yakiendelea kufafanuliwa na Mamlaka funzi (Barua na
Nyaraka za Mababa watakatifu, Rejea Waraka wa Papa Yohane II, ‘’ Bwana na Mtoa
Uzima’’, kwa kilatini inaitwa Dominum et Vivificantem) .Tuone sasa,namna Biblia
inavyotuonesha Imani hii ya Utatu Mtakatifu wa Mungu.
Utatu Mtakatifu unatajwa katika Agano la Kale japo unatajwa kwa kudokezwa kwa mbali,
Tukijua kwamba Agano la Kale linaandaa Agano Jipya (Rejea Ebr 10:1) .Kumbe katika Agano
la Kale Utatu Mtakatifu haujaelezwa moja kwa moja unakuja kuoneshwa wazi wazi katika
Agano Jipya .Na si Moja kwa Moja kama Unavyotajwa katika Agano Jipya .Kwani hata Katika
Agano Jipya hatutakutana na Neno Utatu Mtakatifu,isipokuwa Nafsi Tatu za Utatu Mtakatifu
wa Mungu ndizo zinazotajwa.Tunakutana na Sehemu mbalimbali za Agano la Kale
zikidokeza viashiria vya Utatu huo Mtakatifu wa Mungu.Tuanze sasa kuitalii Biblia Takatifu
katika Agano la Kale.
Moja, Mungu Mwenyewe siku zote anazungumza katika uwingi,Rejea Mwa 1:26 inayosema
‘’Mungu akasema :Tumfanye mtu kwa mfano wetu,afanane nasi’’ vilevile tufananishe pia
Kitabu cha Kutoka 3:6 ,inasema; ‘’Mungu akasema: Mimi ni Mungu wa baba yako,Mungu wa
Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo’’ Hapa tunamwona jinsi Mungu
anavyojitambulisha katika Namna nyingi,japo ni Mungu yulele Mmoja lakini anajifunua
katika umilikishi mwingi.Anayetenda kazi katika Nyakati zote na (nyingi) kwa watu katika
historia ya karne mbalimbali.
Pili, tunakutana katika Kitabu hicho cha Mwa 11:7;inasema , ‘’Haya, tushuke,tukavuruge
lugha yao’’.Hapa pia tunamwona Mungu akisema katika uwingi,yaani uwingi katika Nafsi
zake za Mungu wa Utatu Mtakatifu.Mababa wa Kanisa walielewa na wakafundisha kuwa
maneno hayo yalitamkwa katika mwanga wa ufunuo wa Agano Jipya,kumaanisha kwamba
Nafsi ya kwanza ya Mungu ilikuwa inaiambia nafsi ya Pili ya Mungu au inaziambia Nafsi mbili
yaani kwa Mwana na kwa Roho Mtakatifu.Mtakatifu Ireneo ameandika katika Maandishi
yake ya Kuwapinga Wazushi (Adversus Ad Haeresis IV 20, I ).Japo uwingi huo katika kusema
Natushuke chini tukawavuruge lugha yao,pengine inaweza kuwa ni ile namna ya Ukuu wa
Kimungu au Umwenyezi (Uweza wa Mungu = ile hali ya Mungu kuweza na kuwa na mamlaka
yote ya kufanya lolote kadiri mapenzi yake) .Ukuu huo wa Mungu unabaki ni Mungu mmoja
katika uweza wote.
Tatu, Malaika wa Bwana katika onekano la Agano la Kale anaitwa Yahweh ,El na Elohim na
anajifunua Mwenyewe kama Elohim na Yahweh.Katika hili inajidhihirisha kuwa kuna Nafsi
76
mbili(zimetajwa Nafsi mbili) ambazo zimejitambulisha kuwa ni Mungu:Ambapo katika Nafsi
hizo mbili zilivyotajwa maana yake Kuna anayetuma na Mwingine Anayetumwa Rejea Mwa
16:17-13; Kut 3:2-14).Mababa wa Kanisa walielewa Is 9:6 ikimaanisha Yahweh inayosema
‘’Uwezo wake utaenea’’ na Kitabu cha Nabii Malaki 3:1, ( Kwa Kilatini tunaita Angelus
Testamenti ) Neno Wa Mungu (Logos) yaani Yesu Kristo inasema ‘’ Tazameni, namtuma
mjumbe wangu,naye ataitengeneza njia mbele yangu’’.Baadaye Mababa na Wataalamu wa
Teolojia waliofuata hususani Mtakatifu Augustino na waliomfuata walifundisha kuwa Neno
wa Mungu yaani Yesu Kristo alijifunua Mwenyewe kwa njia ya Malaika.Kumbe basi kwa
mantiki hiyo Anayetuma ni Mungu Baba na Anayetumwa ni Mungu Mwana (Yesu
Kristo).Hapo zimetamkwa Nafsi Mbili za Mungu na Roho Mtakatifu anasemwa katika undani
wake japo hatajwi moja kwa moja katika kipengele hiki.
Tano, Katika Vitabu vya Mithali na Hekima ya Suleimani vinaonesha hekima ya Kimungu
inayokaa daima na Mungu.Hekima hiyo imetoka kwa Mungu(Kulingana na Mithali 8:24 na
kuendelea, kwa kuzaliwa,) tangu milele yote,anayeshirikiana katika uumbaji wa Ulimwengu
(Rejea tena Mithali 8:22-31; Hekima ya Suleimani 7:22 - 8:1,ambapo anazungumza kuwa
Hekima ni kitu cha Kimungu. Soma pia Hekima ya Suleimani 8:3-8).Katika uelewa au
mwanga tunaoupata katika ufunuo wa Agano Jipya tunaweza tukaunganisha ujumbe na
Yohane 1:1 na kuendelea inayosema ‘’Mwanzoni kulikuwako Neno,naye Neno alikuwa kwa
Mungu (Ndugu msomaji Huyo Neno , ni Yesu Kristo anayezungumziwa hapo,ambaye ni Nafsi
ya Pili ya Mungu).Kumbe sasa nako katika vitabu hivyo kuna madokezo yanayoonesha
uwepo wa Nafsi za Mungu zaidi ya Nafsi Moja (Mungu Baba). Pia Kristo ni mngao wa Mungu
Rejea ( Ebr 1:3) nayo inakubaliana na vitabu hivyo vya Agano la Kale Waraka kwa Waebrania
pamoja kwamba inapatikana katika Agano jipya inakamilsha kilichosemwa Agano la Kale
.Yesu Kristo anatajwa kama mng’aro wa utukufu wake (Mungu Baba) na mfano wa hali yake
77
,na ambaye anauhifadhi ulimwengu wote kwa neno la uwezo wake na baada ya kufuta
dhambi, ameketi mkono wa kulia wa Mtukufu wa mbinguni ’’.
Sita, Agano la Kale mara nyingi linazungumza juu ya ‘’Roho wa Mungu,’’ au Roho Mtakatifu.’’
Kwa hapa haipaswi kueleweka kama Nafsi ya Mungu,bali nguvu inayotoka kwa
Mungu,inayotoa uzima,inayotoa nguvu,inayoangaza inayosukuma kuelekea kutenda mema
( yanasemwa na P.Heinsich ).
Kwa marejeo zaidi jisomee mwenyewe Mwa 1:2, Zab 104:30, 143:10, Is 11:2 ( Juu yake
itatoka Roho ya Bwana, roho ya hekima na ufahamu,roho ya shauri na nguvu,roho ya elimu
na ibada ya Bwana.
Katika Agano la Kale,Mungu aliwapa manabii roho wake(Rejea Isa 11:1; Amu 11:1.Hata hivyo
hapa ni alama kamilifu kwamba waamini wote watapewa roho.Ndoto na maono vilikuwa njia
za kawaida za mawasiliano ya kinabii(Rejea Isa 54:13; Yer 31:31). Siku hiyo watu watafanya
uamuzi mkamilifu: ama kuendelea na mitindo yao ya zamani ya maisha au kuomba kwa jina
la Mungu ,Jambo ambalo linamaanisha kuyasalimisha maisha na matumaini yao kwake na
kutegemea uingiliaji kati wake wa nguvu.36
Katika Kitabu cha Nabii Ezekiel 36:27, ‘’Nitatia Roho yangu ndani yenu na nitawawezesha
mfuate amri zangu,na kushika sheria zangu kwa matendo yenu’’.Hapo ni Mungu anawaahidi
wana wa Israeli kwamba endapo wataacha ‘’kukengeuka’’ kutenda dhambi: Baada ya
kufanya toba ya Kweli na kumrudia Mwenyezi Mungu,Mungu ataingia ndani ya mioyo yao
na maisha yao kiujumla.
78
Hek 1:7-8 Maana Roho ya Bwana imeujaza ulimwengu,nayoinavifungamanisha vitu vyote
in ujuzi wa kila sauti.Kwa hiyo yeyote atamkaye yasiyo ya haki hataweza kufichika,wala haki
yenye kuadhibu haitampitia .
Ndugu msomaji unaona kabisa, jinsi Roho Mtakatifu yaani Nafsi ya Tatu ya Mungu
anavyotajwa katika Agano la Kale na kuwa na sifa zile zile za Nafsi ya Mungu Baba na Mwana;
yaani Roho ya Bwana inaujaza ulimwengu,inaweza kuvifungamanisha viumbe
vyote,Inaujuzi wa kila sauti maana yake Roho ya Bwana yajua kila kitu.Hivi kwamba
yeyote atamkaye yasiyo ya haki hataweza kufichika.Na zaidi ya yote tunaambiwa kuwa
;Roho wa Bwana ana uwezo wa kuhukumu. Na Mungu ndiye Mjua yote kwani ndiye
aliyeumba dunia na mbigu, Mwenye hukumu na haki zote.Sasa kwanini ,tusimwite
Roho wa Bwana kuwa ni Mungu katika Nafsi ya Tatu ya Mungu,kama amekidhi sifa za
Kimungu?
Hayo yanakamilishwa katika Agano Jipya (tusome tuone Mdo 2 :16, ‘’Enyi ndugu,andiko
aliloliagua Roho Mtakatifu kwa kinywa cha Daudi,kuhusu Yuda,lilipaswa kutimia ; Yuda huyo
aliwaongoza wale waliomkamata Yesu’’.Roho ya Bwana inayozungumzwa katika Agano la
Kale,Mababa wa Kanisa na Liturujia kwa Nafsi ya Mungu walifundisha kuwa ndiye Roho
Mtakatifu.
Saba, Iliaminika kwamba Mwenyezi Mungu aliye mmoja alitambulishwa kwa jina lililobeba
au linalo onesha Utatu Mtakatifu katika Mwanga unaofunua Agano Jipya.Tunaona Neno la
Kilatini Trisagion Rejea Is 6:3 ambapo tunakutana na neno ‘’Mtakatifu’’ likitajwa mara tatu,
yaani Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu,wakati Nabii Isaya akiitwa na Mungu.
Naona itafaa pia nikitoa mawazo yangu binafsi nilivyoelewa hapa , kwamba,Mtakatifu
iliyotajwa mara tatu inaelekezwa kwa Nafsi tatu za Mungu; kwa Baba kwa Mwana na kwa
Roho Mtakatifu.Tukikumbuka kwamba Mungu yuko katika Nafsi tatu zisizoweza
kugawanyika,au kutenganishwa.Nafsi Tatu za Mungu zafanya kazi kwa pamoja,zina Umungu
mmoja, umilele mmoja,uwamo mmoja(asili) moja.37
Biblia imefundisha suala la Utatu Mtakatifu kwa ngazi.Katika Agano la kale,Mungu Baba
anajionesha zaidi wakati huo huo kukiwa na vidokezo vya nafsi nyingine mbili ‘’ Mungu
akasema:Tumfanye mtu kwa mfano wetu, afanane nasi ‘’ (Rejea Mwa 1:26) ,
79
Tena tunashuhudia Mungu akizungumza katika wingi wa zaidi ya Nafsi Moja ,anaposema
katika tukio la Mnara wa Babeli pale Wanadamu walipotaka kujenga mnara wakifikiria
watamfikia Mungu alipo huko juu mbinguni tunasoma Mungu akasema ‘’ Haya, tushuke
,tukavuruge lugha yao wasipate tena kusikilizana wao kwa wao(Rejea Mwa 11:7) na wageni
watatu waliomjia Abrahamu,walikuja katika Utatu (Rejea Mwa 18:1-2).
80
Katika Biblia ya Kiafrika ya Kiswahili jopo la Wafasiri na Wahariri wa Biblia hiyo yaani Pd.
Titus AMIGU akiwa Mhariri Mkuu, Pd. Thaddeus Alois MWORIA (apumzike kwa Amani),Pd.
Leander BEI, Pd.William NGOWI na Gabriele Maria BRANDOLIN wameipa jina sura ya
kitabu cha (Mwa 18:1-2) kwa kuandika hivi ‘’Kuwakaribisha wageni ni kumkaribisha Mungu
‘’. Hii ni katika tukio hili,ndugu msomaji usije kufikiri kila mgeni ni ‘’Mungu’’,utachekwa !
Maana inabaki kuwa Mungu yumo katika wahitaji,wenye kutaka msaada,wenye kutaka
kukarimiwa.Vilevile hata mwanzo wa Sura hiyo tunasoma kwamba ‘’Bwana akamtokea
Abrahamu kwenye mwaloni wa mamre.Abraham alikuwa amekaa mlangoni pa hema yake,saa
ya joto la mchana.Akainua macho,akaona watu watatu wamesimama mbele
yake.Alipowaona,alipiga mbio akatoka mlangoni pa hema,akawakaribia,akainama mpaka
chini.
Ndugu msomaji naomba uelewe watu hawa watatu ni lugha ya picha inayopapasa suala
zima la Nafsi Tatu za Mungu,na si akina ‘’Mungu watatu’’ ‘’kwani hakuna Mungu watatu’’ ni
Mungu Mmoja katika Nafsi Tatu.,Ni Mungu anayejidhihirisha katika Utatu Mtakatifu, ndio
maana tumesoma kwamba Bwana(Mungu) akamtokea Abrahamu na si Mabwana
wakamtokea Abrahamu.Na tendo la Abrahamu la kuinama mpaka chini ni ishara ya
kuabudu,kumwabudu Mungu katika Utatu Mtakatifu,alimwabudu Mungu.(Tafakari ya
Mwandishi)
Katika Agano Jipya Nafsi ya Pili ya Mungu,yaani Yesu Kristo Bwana wetu amejionesha zaidi
huku Roho Mtakatifu akidokezwa kwa nguvu kabisa(tazama Yoh 14:16; 26, 16:4-15).Baada
ya Pentekoste,enzi ya Kanisa,ndiyo Nafsi ya Tatu ya Mungu,yaani Roho Mtakatifu
anayejionesha zaidi tazama Yoh 20:22, Mdo 2: 1-13).
Yoh 14:26, tunasoma: Lakini Mtetezi, ndiye Roho Mtakatifu,ambaye Baba atamtuma kwa
jina langu,atawafundisha yote na atawakumbusha yote niliyowaambia mimi.
Yoh 16:4-15, Ndugu msomaji naomba ujisomee mwenyewe utaona Namna Nafsi Tatu
za Mungu zinavyotajwa na hapa utaona kazi ya Roho Mtakatifu pia.
81
Yoh 20:22, tunasoma: Baada ya maneno hayo, akawapulizia, akawaambia ‘’Pokeeni
Roho Mtakatifu’’.
Mdo 2:1-13, Jisomee pia hapa ni juu ya tukio la Pentekoste: Kipaji cha Roho.
Moja, Utatu Mtakatifu unatajwa Wakati Malaika anamwambia Mama Bikira Maria kuwa
atapata Mimba kwa Uwezo wa Roho Mtakatifu;Utatu Mtakatifu unatajwa ‘’ Malaika akamjibu
akisema ‘’Roho Mtakatifu atakushukia, na nguvu ya yule Aliye – juu itakufunika kwa kivuli
chake’’. Kwa hiyo kitakachozaliwa kitaitwa Mwana wa Mungu ’’
Hapa tunaona wazi kabisa Nafsi Tatu za Mungu zimetajwa yaani Mungu Baba ( yule Aliye-
juu), Mwana ( Kwa hiyo Kitakachozaliwa kitaitwa Mwana wa Mungu ) na Roho
Mtakatifu(aliyemshukia
Mama Bikira Maria). Turejee pia Lk 1:32-33, ‘’ Huyo atakuwa mkubwa na kuitwa Mwana wa
Aliye- juu na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake’’ … Utawala wake
hautakuwa na Mwisho’’.
Nafsi Tatu za Mungu zimeitwa : Yeye aliye juu (Mungu Baba) , Mwana wa Aliye- juu (Yesu
Kristo) na Roho Mtakatifu. Tunaweza kulinganisha pia na Mdo 1:4-5, ambapo pia Nafsi Tatu
za Mungu zinatajwa kwa mtindo wake kama ifuatavyo, tunasoma : ‘’ Alipokuwa mezani
pamoja nao,aliwaamuru wasitoke Yerusalemu,bali waingoje ‘’ahadi ya Baba,mliyoisikia
kutoka kwangu’’. Tuone ufafanuzi mfupi, ‘’ Ahadi ya Baba’’ ni Roho Mtakatifu, ‘’ Baba’’ ni
Mungu Baba na neno ‘’Kwangu’’ (ni Yesu Mwenyewe).Nafsi Tatu za Mungu zimetajwa
hapa,yaani Mungu Baba,Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu.
Pili, Utatu Mtakatifu unatajwa wakati wa Ubatizo wa Bwana na Mkombozi wetu Yesu
Kristo: ‘’Baada ya kubatizwa,Yesu akatoka mara majini.Na tazama,mbingu
zikafungukia.Akamwona Roho wa Mungu akimshukia kwa mfano wa njiwa. Tazama,pale
pale sauti ikatokea mbinguni ikisema ‘’Huyu ni Mwanangu mpendwa,anipendezaye ‘’ (Rejea
Mt 3:16- 17; Mk 1:10; Lk 3:22)
82
‘’Huyu ni Mwanangu mpendwa,anipendezaye ‘’ Anayesema maneno hayo ni Mungu Baba,
Yesu ni Mwana wa Mungu,ni Mwana wa pekee wa Mungu.Kibiblia neno ‘’ Mwana
anipendezaye’’ mara zote linamaanisha Mwana wa pekee (Rejea Mwa 22:2.12.16; Hapa
Teolojia ya Mwana mpendwa na Mwana wa pekee ilivyotumika ,nikutaka kuoneha ule upendo
wa Mungu Baba kwa Mwanaye mpendwa Yesu Kristo na ule wa Abrahamu kwa Mwanaye
mpendwa Isaka Rejea Mwa 22:2.12.16 .Jisomee pia, Yoh 1:32 utaona Nafsi ya Baba ,Mwana
na Roho Mtakatifu zinatajwa .
Tatu, Utatu Mtakatifu unatajwa wakati wa Karamu ya Mwisho , Yesu Kristo anaahidi
kumtuma Msaidizi mwingine (Paraclitus msaidizi ,ni kilatini ) ‘’ Nami nitamwomba Baba
naye atawapelekea Mtetezi mwingine ili awepo kwenu hata milele ( Rejea Yoh 14:16).
Pia, Yoh 14:26 tunasoma , ‘’ Lakini Mtetezi ndiye Roho Mtakatifu,ambaye Baba atamtuma
kwa jina langu,atawafundisha yote na atawakumbusha yote niliyowaambia mimi’’
Yoh 15:26 tunasoma ‘’ Atakapokuja Mtetezi,nitakayemtuma kwenu kutoka kwa Baba ndiye
Roho wa ukweli atokaye kwa Baba,huyo atanishuhudia’’.
Hapa ,ndugu msomaji Roho Mtakatifu anayetumwa ni Nafsi ya Tatu ya Mungu ambayo ni
Nafsi inayotofautishwa na Baba na Mwana katika Utendaji, yaani pale kila Nafsi inapofanya
kazi tendaji ya kipekee.Yaani ,Roho Mtakatifu kwa kutambulika kwa jina linguine kama
‘’Paraclitus’’ neno la kilatini ,likihusianishwa na kazi zake Roho Mtakatifu ikiwa ni
Kufundisha,kumshuhudia Kristo, na kutakatifuza ambayo ndiyo kazi yake mahususi..
Nne, Fumbo la Utatu Mtakatifu linaoneshwa wazi kabisa katika maagizo aliyoyatoa
Yesu Kristo kwa Mitume wake alipowaambia waende kubatiza ‘’Basi nendeni mkayafanye
mataifa yote kuwa wafuasi mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho
Mtakatifu(Rejea Mt 28:19) . Katika Agizo hili la Yesu Kristo kwa Mitume wake tunakutana
Nafsi Tatu za Mungu zinazotajwa kwa kutofautishwa yaani ,Kwa jina la ‘’Baba’’ (Mungu
Baba,Nafsi ya kwanza ya Mungu) na la Mwana (Yesu Kristo,Nafsi ya Pili ya Mungu) na Roho
Mtakatifu(Nafsi ya Tatu ya Mungu). Asili ya Umungu wa Nafsi Tatu za Mungu ni mmoja.Ndio
maana Yesu Kristo aliwaambia wabatize ‘’ Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho
Mtakatifu’’ na sio kwa majina ya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu. Wanapaswa kubatiza
kwa ‘’umoja’’ yaani kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu kwa kuonesha Mungu
‘’Ambaye’’ ni Mmoja.Ni Mungu mmoja katika Nafsi Tatu,Ni Utatu Mtakatifu wa Mungu wenye
umoja usiogawanyika.
Ubatizo ni Sakramenti ya mkutano na Nafsi Tatu za Mungu,watakatifu na jumuiya ya
Kanisa.Kwa kupitia ubatizo tunakombolewa hatua kwa hatua kutoka kwenye hali yetu ya
dhambi na zaidi na zaidi tunageuzwa kuwa wana na mabinti wa Mungu( 1Kor 3:21-23;
15:28). Formula hii ya ubatizo,bila shaka,ilikuwa ikitumika katika Kanisa wakati Mathayo
83
alipoiandika Injili yake.Inaelezea ushirika wa Utatu Mtakatifu ambao ni msingi wa maisha ya
ufuasi.38
Basi Biblia imedokeza vya kutosha ukweli wa Utatu Mtakatifu.Kwa vyovyote mambo ya Utatu
yalivyomagumu,Mungu mwenye busara zote asingeweza kuyafunua yote kwa mpigo kama
mwalimu mbaya anavyoweza kufundisha sura kumi za kitabu katika kiipindi kimoja.Yeye kwa
busara aliyafunua mambo hayo magumu pole pole akianzia kwenye Agano la Kale na
kuendelea nayo hadi kwenye Agano Jipya na kuja hadi enzi hizi kama madarasa yake matatu
ya kufundisha mada ya Utatu Mtakatifu.Ni katika enzi kwa mada hii kutatokea mbinguni
wakati ule watu watakapowaona Baba,Mwana na Roho Mtakatifu ana kwa ana. 39
Msomaji hapo natumai kama unaubishi juu ya Utatu Mtakatifu,ubishi wako ukauweke
mfukoni uondoke nao ukautupe porini urudi kwa kutubu na kuiamini injili.Kwani
tumehakikishiwa katika kuwaona mbinguni Baba,Mwana na Roho Mtakatifu ,Mungu mmoja
kama alivyo na tutafananaye.
Kuna uwezekano mkubwa kuwa Mtume Paulo hakumwona Yesu Kristo Mnazareti katika
maisha yake yaani kama Mitume wengine akina Simon Petro,Andrea, Thoma na
wengineo.Hapa nina maanisha kuwa Mtume Paulo hakuambatana wala kumshuhudia Yesu
moja kwa moja katika mazingira kama ya Galilaya, Yudea na kwingineko. Isipokuwa alisikia
habari zake na wafuasi wake.Ndio maana aliweza kufanya madhurumu ya kuwaua Wakristo
kabla ya kuongoka, huo ni ushahidi kwamba alikuwa tayari ana habari za jina Maarufu
Yesu.Kwa mara ya kwanza alikutana na Yesu Mfufuka,Wakati Sauli akielekea Damasko
kuwakusanya wakristo kwa ajili ya kuwaua,wakati huo akitambulika kama Sauli yaani kabla
ya kuongoka na kuitwa Paulo .(Soma Mdo 9:1-19).Hata hivyo aliweza kuuliza u nani wewe
Bwana?
Katika Nyaraka za Mtume Paulo anamtambua kwa majina kama Yesu Kristo, Kristo Bwana
wetu,Kristo Yesu,Kristo na majina mengine (Soma Waraka wa Mtume Paaulo kwa Warumi
ina utajiri wa Majina ya Yesu Kristo ambayo Mtume Paulo alimtambua).
38
Biblia ya Kiafrika(FASIRI YA KISWAHILI);Paulines Publications Nairobi,2000 ,
Maelezo ya Ufafanuzi wa Mt 28:19
Amigu, Titus Kisa Cha Imani (SEHEMU YA KWANZA), DINI ZA MUNGU MMOJA V.MAJIBU MAFUPI YA
39
84
Moja, Mara nyingi Mtume Paulo anavyooanza kuandika nyaraka zake anatoa salaamu zenye
kuutaja Utatu Mtakatifu wa Mungu anasema:
‘’Atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo:Yeye ametubariki katika Kristo kwa
baraka zote za mbinguni zitokazo kwa Roho Mtakatifu (Rejea Efe 1:3). Nafsi Tatu za Mungu
Mmoja zimetajwa na Mtume Paulo katika kuanza Waraka wake kwa Waefeso.
Mbili, Mtume Paulo anatoa salaamu zake kwa Wakristo walioko Korintho kwa kuutaja
Utatu Mtakatifu wa Mungu kwa kishindo, anasalimu hivi: ‘’ Neema ya Bwana Yesu Kristo, na
upendo wa Mungu Baba, na ushirika wa Roho Mtakatifu viwe nanyi nyote ’’ (Rejea 2Kor
13:13). Hapa Mtume Paulo anaonesha Muungano na Ushirika wa Nafsi Tatu za Mungu
Mmoja, Baba , Mwana na Roho Mtakatifu. Huo ndio Umoja wa Nafsi Tatu za Mungu
usiogawanyika.Katika adhimisho la Ibada ya Misa Takatifu katika Liturujia ya Sehemu ya
Mwaliko Padre anaweza kutumia salaamu hiyo katika Mwaliko wa adhimisho la Ibada ya
Misa Takatifu badala ya kusema ‘’Bwana awe nanyi’’.
Tatu, Sehemu nyingine Mtume Paulo anaonesha Nafsi zaidi ya Moja, ‘’ Je ,hamjui ya kuwa
ninyi ni hekalu la Mungu,na Roho wa Mungu anakaa ndani yenu kama mtu akiliharibu hekalu
la Mungu,Mungu atamharibu.Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu,nalo ni ninyi’’ (Rejea
1Kor3:16-17) . Kwa Mtume Paulo hapa anatuonesha wazi kwamba ,Roho Mtakatifu aliye
Roho wa Mungu ,ni Nafsi ya Mungu , .Kumbe kwa Mtume Paulo Roho wa Mungu na Mungu
yanamaanisha kitu kimoja.
Nne, Pia hayo yanajirudia katika Waraka wa Kwanza kwa Wakorintho (1Kor 6:19) ‘’Au
hamjui ya kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu? Mtume Paulo
anamwonesha Roho Mtakatifu kuwa ni Mungu anayekaa ndani mwetu akimwandikia Mtoto
wake wa Kiroho Timotheo ; ‘’ Amana nzuri hiyo uitunze kwa nguvu ya Roho Mtakatifu
anayekaa ndani yetu’’ (Rejea 2Tim 1:14).
Tano, Mtume Paulo katika Waraka wake wa Kwanza kwa Wakorinto (1Kor 8:6); Tunaona
Nafsi za Mungu zikitajwa zaidi ya moja : Hata hivyo, kwetu sisi yuko Mungu mmoja tu; Baba,
Muumba wa vyote, ambaye kwa ajili yake sisi tuko.Pia yuko Bwana mmoja tu, Yesu Kristo,
ambaye kwa njia yake vitu vyote viliumbwa na sisi twaishi kwa njia yake
Sita, Kwa upande mwingine Mtume Paulo anaonesha ukamilifu wa Mungu mmoja bila
kuzitaja Nafsi Tatu za Mungu kama tunavyosoma (Efe 4:6); Kuna Mungu mmoja na Baba wa
wote, ambaye yuko juu ya wote, afanya kazi katika yote na yuko katika yote.Kwa tafakuri ya
usemi huu wa Mtume Paulo tunaweza kusema hapa anakazia fundisho la Mungu
Mmoja,anayejidhihirishs katika Utatu Mtakatifu pamoja kwamba hajautaja Utatu huo
Mtakatifu wa Mungu.
85
Kwa maneno mengine tungesema Kuna Mungu mmoja na Baba wa wote, ambaye yuko juu ya
wote (yaani Mungu Baba) afanya kazi katika yote (yaani Mungu Mwana) na yuko katika yote
(yaani Mungu Roho Mtakatifu).Ndugu msomaji hiyo ni tafsiri yangu binafsi mimi mwandishi wa
Kitabu hiki .Ambayo naona inaufunua Utatu Mtakatifu katika kutaja namna za uwepo wa Nafsi
hizo katika maisha ya mkristo na Sakramenti.
Saba, Teolojia ya Mtume Paulo katika kuutaja Utatu Mtakatifu imewekwa kwa namna
mbalimbali ,kwa mfano 1Timotheo 2:5-6, Hapa Mtume Paulo anasema maana yuko Mungu
mmoja, na pia yuko mmoja anayewapatanisha watu na Mungu, binadamu Kristo Yesu,ambaye
alijitoa mwenyewe kuwakomboa watu wote.Huo ulikuwa uthibitisho ,wakati ufaao
ulipowadia,kwamba Mungu anataka kuwaokoa watu wote. Hapa Mtume Paulo anataja Nafsi
mbili za Mungu yaani Baba na Mwana.Roho Mtakatifu anatajwa kiundani tukijua kuwa Roho
ya Kristo ndiye Roho Mtakatifu.Pia Roho wa Mungu Ni Roho Mtakatifu.
Nane, Mtume Paulo anazungumzia vipaji mbalimbali vya Roho Mtakatifu, ambapo tunaona
namna Utatu Mtakatifu wa Mungu unavyoshiriki katika vipaji hivyo ndani ya maisha ya
Mkristo na Sakramenti.Anasema Vipaji vya kiroho ni vya namna nyingi,lakini Roho avitoaye
ni mmoja.Kuna namna nyingi za kutumikia lakini Bwana anayetumikiwa ni mmoja.Kuna
namna mbalimbali za kufanya kazi ya huduma,lakini Mungu ni mmoja anayewezesha kazi
zote katika wote. Hapa Mungu Baba ndiye anayetumikiwa. Mungu Mwana ndiye
anayewezesha kazi zote katika wote na Mungu Roho Mtakatifu ndiye mtoa vipaji vya kiroho
vya namna nyingi .
Kila mtu hupewa mwangaza wa Roho kwa faida ya wote. Roho humpa mmoja ujumbe wa
hekima na mwingine ujumbe wa elimu,apendavyo Roho huyo huyo. Roho huyo huyo humpa
mmoja imani na kumpa mwingine kipaji cha kuponya,humpa mmoja kipaji cha kufanya
miujiza mwingine kipaji cha kusema ujumbe wa Mungu, mwingine kipaji cha kubainishavipaji
vitokavyo kwa Roho na visivyo vya Roho;humpa mmoja kipaji cha kusema lugha ngeni na ,na
mwingine kipaji cha kuzifafanua.Hizo zote ni kazi za Roho huyohuyo mmoja ambaye humpa
kila mtu kipaji tofauti kama apendavyo mwenyewe (Rejea 1Kor 12:4-11).
Hata hivyo Paulo anashauri hivi , Jitahidini kuwa na upendo vilevile fanyeni bidii ya
kupata vipaji vingine,hasa kipaji cha ufafanuaji,yaani unabii.Mwenye kipaji cha lugha hasemi
na watu,asema na Mungu,maana hakuna aelewaye.Kwani ananena rohoni mambo
yaliyofumbika. Bali mwenye kipaji cha unabii anasema na watu maneno
yakuwainua,kuwaonya, na kuwatuliza.Mwenye kunena lugha za kiroho hujiinua
mwenyewe.Lakini mwenye kutoa unabii analiinua Kanisa. Ningependa ninyi nyote mseme kwa
lugha za kiroho,lakini zaidi,napenda mtoe unabii,kwa maana mwenye kutoa unabii anampita
86
mwenye kusema lugha za kiroho,isipokuwa anaifafanua maana ya maneno yake,ili Kanisa
lipate faida.
Mtume Paulo anaendelea kusema kwa kuuliza, Mnaonaje,ndugu nikija kwenu kusema kwa
lugha ya kiroho tu bila kuwafafanulia wala kuwaeleza neno,bila kuwafumbulia mambo
yajayo wala kuwafundisha mapya,nitawaletea faida gani ? Ni kama kwa vyombo vya
muziki,tuseme filimbi au kinubi. Visipotuwezesha kutofautisha baina ya tuni zake,tutajuaje
wimbo upi unapigwa na filimbi,au upi na kinubi? Maana mlio wa baragumu
usipotambulikana waziwazi nani atakuwa tayari kupigana? Vivyo hivyo,ninyi mkisema kwa
lugha za kiroho bila kutoa maneno wazi wazi,maana ya maneno yenu itajulikanaje? Basi
mtasema hewani tu.Kuna aina nyingi za lugha duniani,na kila moja ina maana yake. Lakini
nisipoijua maana ya lugha yake nitakuwa mjinga pa mwenye kuisema,naye atakuwa mjinga
machoni pangu.Kadhalika ninyi mnaotunuka vipaji vya roho fanyeni bidii kuwainua
wanakanisa mpate kukamilika.
Basi ,anayesema kwa lugha ya kiroho na ajiombee uwezo wa kuifafanua.Maana nikisali kwa
lugha ya kiroho,roho yangu inasali,lakini akili yangu haizai kitu.Hapo nifanyeje? Afadhali
nisali kiroho,na pia nisali kwa ufahamu; nishangilie kwa roho,na nishangilie kwa
ufahamu.Kwa maana ukisema sala ya sifa kwa lugha ya kiroho,mtu asiyejaliwa ataitikiaje
‘’Amina’’ mwisho wa shukrani yako? Maana hajui unayoyasema.Hata ukifanya shukrani
nzuri,mwingine hajengeki. Paulo Mtume,anamalizia kwa kusema hivi ‘’Namshukuru
Mungu,kwa kuwa nasema kwa lugha za kiroho zaidi ya ninyi nyote. Lakini kanisani napenda
zaidi kusema maneno matano kwa akili yangu ili kuwaelimisha wengine kuliko kusema
maneno kumi elfu kwa lugha ya kiroho.
Ni matumaini yangu kuwa , haya maelezo ya Mafundisho ya Paulo Mtume ni ‘’ bakora’’ kwa
wale wanaodhani na kufundisha kuwa Roho Mtakatifu ni masikini wa vipaji; hivi kwamba
eti vipaji vya Roho Mtakatifu ni uponyaji na kunena kwa lugha mpya tu,huo ni uongo. Ndugu
msomaji ,Vipaji vya Roho Mtakatifu ni zaidi ya Kuponya watu katika vifungo vya pepo na
ulimbukeni unaokuja kwa kasi yaani Kunena kwa lugha mpya.
87
Biblia Takatifu inamwonesha Mungu mmoja, Ni mmoja asiyegawanyika kwa asili.Maandiko
Matakatifu kamwe hayaoneshi wala kuruhusu dhana(fikra) ya Mungu zaidi ya mmoja.Agano
la kale linakazia umoja wa Mungu kama msingi wa ukweli wa imani (Rejea Kumb 6:4). Ni
vigumu kwa Agano la Kale kusisitiza sana Utatu Mtakatifu kwani,tunatambua kuwa Mungu
wa Waisraeli walivyomtambua,na kwao Yesu Kristo alikuwa hajajifunua kwao katika
ubinadamu,na kwa mtiririko hata Roho Mtakatifu naye hakuwa vichwani mwao,kwa hiyo
kwa Wayahudi Utatu Mtakatifu kwa agano la Kale ingeonekana kama ongezeko la kina
‘’mungu wadogo wadogo’’ ndio maana hata Yesu ilikuwa vigumu kupokeleka .Hususani pale
alipojiita ni mwana wa Mungu.Wayahudi waliona Yesu ni halali yake kuuawa kwani
amekufuru kwa kusema aweza kubomoa hekalu na kulijenga upya kwa siku tatu(Rejea
26:61) na lile la kujiita Mungu .Adhabu yake ilikuwa si nyingine bali kifo.Huo ndio uelewa wa
Mungu katika mazingira ya Kiyahudi ‘’ Sikiliza, ee Israeli ! Bwana Mungu wetu,ndiye Bwana
pekee yake ! (Kumb 6:4 ) . Sikiliza ,ee Israeli : Maneno ya ufunguzi ya shema ,sala
iliyotumika mara nyingi sana.Hili pia ni ungamo la imani. ‘’ Shema’’ hii (aya.4-9)
inanukuliwa na Yesu kama amri kuu na ya kwanza (Mt 22:37) 40
40BIBLIA YA KIAFRIKA, Paulines Publications Africa, 2010, Dondoo ya Kumb 6:4, Uk.
277
88
Kut 20:3 ‘’ Usiwe na miungu mingine mbele yangu’’
Kumb 4:35 ‘’ Ndiwe uliyeteuliwa kuona hayo yote ili upate kujua kwamba Bwana ni
Mungu wa kweli na kwamba hakuna mwingine.’’
1Kor 8:6 ‘’ Lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja,ndiye Baba,aliye asili ya vitu vyote na
shabaha yetu sisi,tena kuna Bwana mmoja tu,ndiye Yesu Kristo,kwa ujumbe wake vitu vyote
vipo,na sisi pia.’’
Efe 4:3-6 ‘’ Fanyeni bidii kuhifadhi umoja wa Roho kwa kifungo cha amani:Mwili
mmoja na Roho moja,kama mlivyoitwa katika tumaini moja, ndio wito wenu.Kuna Bwana
mmoja,imani moja,ubatizao mmoja,tena Mungu mmoja,ndiye Baba wawote,aliye juu ya yote
na katika yote na ndani yenu nyote.’’
Ndugu msomaji wangu, hatujatoka kwenye mada ya Utatu Mtakatifu isipokuwa hapa
nataka ulijue kwanza Kanisa,sura yake,Mwanzilishi wake aliye Kristo Simba wa
Yuda,Mshindi kwa Mateso, Kifo na Ufufuko wake(Soma Ufunuo 5:5).Ndiye Kichwa cha
Kanisa,aliyekuja kukamilisha Ufunuo,yeye ndiye aliyeweka ‘’kitasa’’ na hivyo milango ya
kuwafungulia manabii wa kisasa ilifungwa ( Soma Ufu 5:1 -10 na Ebr 1:1- 4) .
Tusome Sasa ! ‘’Nyakati zilizopita,mara nyingi na kwa namna nyingi Mungu alisema
na mababu zetu kwa ndimi za manabii.Siku hizi za mwisho amesema na sisi kwa ulimi wa
Mwana aliyemweka kuwa mrithi wa vyote, na kwa nafsi yake aliumba ulimwengu.Huyu ni
mng’ao wa utukufu wake na mfano wa hali yake,na ambaye anauhifadhi ulimwengu wote
kwa neno la uwezo wake.Na baada ya kufuta dhambi,ameketi mkono wa kulia wa Mtukufu
wa mbinguni.Ametukuka kupita Malaika kwa kadiri ya jina alilolirithi linavyopita lao.’’ (Rejea
Ebr 1:1-4).
89
Ndugu msomaji hayo si maneno yangu, ni ushahidi tosha wa Kibiblia,jisomee
mwenyewe , na mtu akibisha kwanini tusimwite kichaa? Usiyumbishwe na ‘’vimbunga vya
Ulokole’’ vinavyokuja na misimamo isiyokuwa tayari kufundishika au kufundishwa
.Wanaolikashifu jina la Nabii na Mitume kwa kujiita wenyewe ‘’Manabii na Mitume.’’
Majina yanayotumiwa katika Maandiko matakatifu kwa kutaja Kanisa husaidia pia kwa
kutambua aina yake.Kanisa ni alama azizi ambalo Kristo ni mlango – ni kundi la kondoo na
Kristo ni mchungaji wake mwema, mwenye kutoa uzima wake kwa ajili yao- ni mzeituni – ni
shamba la Mizabibu – ni jengo lililojengwa na Mungu – ni mama mzazi.
Basi daima Kanisa linatajwa kama kitu kimoja chenye uzima na uhai, chenye kuungana
na Kristo,hulinganishwa naye na kuongozwa naye kama vile viungo vinavyofanya mwili
mmoja na kuongozwa na kichwa(6)Kweli mara kwa mara Mt.Paulo analiita Kanisa ‘’ Mwili
wa Kristo’’ kwani waamini wote wanaishi kwa uzima mmoja ulio uzima wa Kristo.
90
41 Ibid, Na. 5
91
Hivyo waamini wanaungana na Kristo na kati yao pia kama viungo vinaungana na
kufanya mwili mmoja ambao Kristo ni kichwa . Yeye analinda umoja katika mwili
wake,anawaongoza na kuwajalia uzima na uhai katika sakramenti ya Ubatizo na ya Ekaristi
(7).
Hivyo ndivyo Kanisa huwahurumia kwa mapendo yake wote wanaotaabika kwa
udhaifu wa kibinadamu.Mwanzishaji wake alikuwa fukara na mtu wa mateso.Hakika Kanisa
linaona katika maskini na wenye kuteswa mfano wake.Kanisa lililo mhitaji 42 katika nchi ya
ugeni,huendelea mbele katikati ya madhulumu ya malimwengu na faraja ya
Mungu,likitangaza msalaba na mauti ya Bwana hata ajapo(8).
92
42 Ibid , Na. 8
93
Tunapaswa kutambua ujumbe muhimu wa imani ya Kikristo uliomo katika maneno
haya: ‘’Kwamba mtu anayebatizwa anasadiki kwa Mungu mmoja katika Nafsi Tatu ‘’. Agano
la kale huzungumzia jambo hili kwa kiasi kidogo ambalo laweza kutafsiriwa kama maelezo
juu ya Utatu Mtakatifu,hata kama tunaweza kuangalia nyuma kutoka sehemu tuliyosimama
sasa na kuona madokezo ya awali ya ukweli wa ufunuo huu.Lakini Kristo alikuja kutueleza
mengi zaidi juu ya uasili wa Mungu.
Kiini cha ufunuo huu ni ukweli kwamba Kristo mwenyewe ni Mungu mmoja sawa na
Baba, na kwamba anatumia Roho Mtakatifu, mtetezi,ambaye ni mmoja na Baba na
Mwana.Wakati tukishikilia imani kwa uthabiti kwamba Mungu ni mmoja,hatuwezi
kuuachilia na kuukana ufunuo kamili alioutoa Kristo,yaani Mungu ni mmoja na mwenye nafsi
tatu.
Tuliona huko nyuma kwamba haishangazi kuona kuna mafumbo katika dini yetu
ambayo hatuwezi kuyaelewa vyema na lazima kuyapokea kwa imani.Kiini hiki cha imani ya
Wakristo ni moja ya mafumbo hayo.Kuna mengine.Lakini hakuna Fumbo lililo na uzito au
linalosumbua vichwa vya wengi ,waamini Wakristo na Wasio Wakristo zaidi ya fumbo hili
la Utatu Mtakatifu.Hapa sina maana kwamba mafumbo mengine ya Kikristo ni mepesi
kueleweka. Hapana !
Katika Fumbo la Utatu Mtakatifu - Mungu ambaye ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu
– Huyu ni Mungu mmoja, katika Nafsi tatu za Mungu, yaani Nafsi ya Baba, Mwana na Roho
Mtakatifu.
Ndugu msomaji wangu unaweza kuona jinsi mambo ya Mungu yanavyochachafya akili
zetu za kibinadamu zenye ukomo wa kufikiri na kuelewa kwa usahihi mambo ya Mungu na
hata yetu wenyewe wanadamu. Kwani siku zote Mawazo ya Mungu si mawazo ya
Mwanadamu na njia zake si njia zetu(Rejea Is 55:8-11). Kwani Mungu ajua yote na yupo
daima,atushinda mambo yote ,ndiye aliyetufinyanga ,ametuumba yeye, ajua njia zetu, kuketi
kwetu na kuondoka kwetu.Yeye Mungu ajua mambo yetu mawazo yetu tokea mbali(Rejea
Zab 139:1-24).Au ngoja nikurahisishie kazi, tuone Mzaburi anasemaje hapa.
94
Wakristo wanaridhika kuishi na mafumbo,hali wakijua kuwa moja ya furaha za
mbinguni itakuwa ni kufahamu kwa undani kabisa,ingawa siyo kwa ukamilifu,maana ya
mafumbo kama hayo.
43 Ibid, Na.49
95
‘’Imani ya Wakristo wote ni juu ya Utatu.’’44 Wakristo wanabatizwa kwa ‘’ jina’’ (umoja)
la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu na siyo kwa ‘’majina’’(uwingi), kwa sababu Mungu
ni mmoja tu, Baba Mwenyezi na Mwanawe Mmoja tu na Roho Mtakatifu :yaani Utatu
Mtakatifu sana(Rejea Katekisimu ya Kanisa Katoliki namba 233).
Kanisa linazidi kufundisha kuwa ,Fumbo la Utatu Mtakatifu sana ndilo fumbo la Msingi
la imani na la maisha ya Kikristo.Ni fumbo la Mungu ndani yake mwenyewe.Kwa hiyo ni
chanzo cha Mafumbo mengine yote ya Imani,nuru inayoyaangaza.Ni fundisho lililo msingi
zaidi na lazima katika hierarkia (ngazi) ya kweli za imani.
Historia yote ya wokovu siyo kitu kingine ila historia ya njia, na jinsi ambazo Mungu
wa kweli na wa pekee, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu,anavyojifunua
mwenyewe,anavyowapatanisha na kuwaunganisha naye watu waliojitenga naye kwa
dhambi.
Katika Ibara hii ya pili itaelezwa kwa kifupi ni kwa jinsi gani fumbo la Utatu wenye heri
limefunuliwa :
(II)na mwishoni jinsi, Kwa utume wa kiMungu wa Mwana na wa Roho Mtakatifu, Mungu Baba
anavyotekeleza ‘’ Mpango wake mpendevu’’ wa kuumba, wa kukomboa na wa kutakatifuza
17.Kwa nini Kanisa linaonesha imani yake katika Utatu Mtakatifu wa Mungu?
96
Kanisa linaonesha imani yake katika Utatu Mtakatifu wa Mungu kwa kumwungama Mungu
Mmoja katika Nafsi tatu: Baba ,Mwana na Roho Mtakatifu.Yaani Nafsi tatu za Mungu. Mungu
mmoja tu kwa kuwa kila mojawapo ni sawa na ukamilifu wa umungu pekee
usiogawanyika.Nafsi hizi kwa kweli zinatofautiana kweli kwa mahusiano yaliyopo kati yao:
Baba anamzaa Mwana, Mwana anazaliwa na Baba,Roho Mtakatifu anatoka kwa Baba na
Mwana.45
18.MAPOKEO YA KANISA
Vile vile Kanuni ya Imani ya Mitume inalishuhudia Fundisho hili la Msingi la Imani yetu
Wakristo Wakatoliki juu ya Utatu Mtakatifu wa Mungu
97
45Ibid Na. 48
46 Mawazo ya Vipindi vya darasani, Masomo ya Teolojia Mwaka wa Tatu 2013,
yaliyotolewa na Padre Siegnifrid Rusimbya NTARE. (yametumika kwa Ruhusa yake),
Segerea Seminari Kuu ya Teolojia ,Dar es Salaam, Tanzania
98
Na kwa sababu kile kilicho cha Baba,Baba mwenyewe amekitoa kwa Mwana wake wa pekee
kwa kumzaa,isipokuwa kuwa kwake Baba, pia kutoka huku kwa Roho Mtakatifu toka kwa
Mwana,anakotoka milele toka kwa Baba yake aliyemzaa tangu milele(Rejea Mtaguso wa
Florence(1439): DS 1300 -1301.) 47
Matumizi ya Kanuni hiyo ya Imani katika ‘’ Credo’’ ‘’Nasadiki’’ yalipokelewa hatua kwa
hatua katika Liturujia ya Kilatini kati ya karne ya nane na ya kumi na moja.Kuingizwa filioque
katika Kanuni ya imani ya Nikea –Konstantinopoli,kulikofanywa na Liturujia ya Kilatini,
kumekuwa, mpaka leo,sababu ya kutokubaliana na Makanisa ya Mashariki (Kiortodoxi).
Mapokeo ya Mashariki toka mwanzo yanaeleza tabia ya Baba kama chanzo cha kwanza
cha Roho.Kwa kumwungama Roho ‘’atoka ‘’ kwa Baba kwa njia ya Mwana Rejea Yoh 15:26 :
Rejea pia AG .2 ). Mapokeo ya Magharibi yaeleza muungano wa uwamo wa pamoja kati ya
Baba na Mwana kwa kusema kwamba Roho atoka kwa Baba na Mwana( filioque).
Mapokeo haya yanasema ‘’ kwa namna iliyo halali na sawa sawa (Rejea Mtaguso wa Florence
(1439): DS 1302.) kwa sababu mpango wa milele wa nafsi za Mungu katika muungano wa
uwamo wa pamoja,unamaanisha kwamba Baba ni chanzo cha kwanza cha Roho kwa kuwa
‘’chanzo bila chanzo’’,(Rejea Mtaguso wa Florence (1442: DS 1331) lakini pia, kwa vile Baba
wa Mwana wa pekee, ni pamoja naye ‘’chanzo kimoja ambamo Roho Mtakatifu
anatoka’’(Rejea Council of Lyons II,Mtaguso II wa Lyons,Ufaransa (1274):DS 850). Ukamilifu
huo wa halali mradi haukazwi bila kiasi, haudhuru umoja wa imani katika ukweli wa fumbo
hilo linalo ungamwa.
99
19. MITAGUSO ILIVYOFUNDISHA JUU YA UTATU MTAKATIFU
Baadaye, kufuata Mapokeo ya Kitume, mwaka ( 325 B.K), katika Mtaguso wa kwanza wa
Nikea, Kanisa liliungama kwamba Mwana anao ‘’uwamo mmoja’’ kwa kilatini
Consubstantialis na Baba,ndiyo kusema Mungu Mmoja pamoja Naye(the English phrase ‘’ of
one being and one (Rejea Vilevile Symbolum Nicaenum: DS 125.
100
matatu si Kanisa Tatu, bali ni Kanisa moja au kwani wote wanaungana katika Kristo aliye
kichwa chao,wote wana mapendo sawa kwa Mungu na kwa ndugu wote, wanaimba wimbo na
sifa ya Mungu hapa duniani na kule mbinguni. Umoja wao hauvunjiki wanapoaga dunia.Bali
unakazwa zaidi kwani wale wa mbinguni wanazidi kutusaidia wakituombea na kutolea
mastahili yao kwa ajili yetu na hivyo tunapata moyo mkuu katika safari yetu na udhaifu wetu.
Mtaguso wa pili wa Vatikani katika kuonesha kazi ya Nafsi za Mungu katika Utatu Mtakatifu
unaeleza kwa lugha nyepesi naya kueleweka kabisa. Hayo tunayasoma kutoka Hati ya Kazi
za Umisionari Na.2 (Hati hii Kwa kilatini inaitwa Ad Gentes).Inasema Kama vile Mungu Baba
alivyomtuma Mungu Mwana na Roho Mtakatifu hivyo pia Kanisa limetumwa,nalo hufanya kazi
ya misioni kulingana na tabia yake ya kutumwa. Kwa ajili ya pendo analokuwa nalo kwa
binadamu,Mungu Baba anataka watu wote washiriki maisha na utukufu wake kama familia
moja kubwa.Ili kutekeleza mpango huo,alimtuma Mwanaye kuanzisha Kanisa, na Roho
Mtakatifu kulitia uzima.Mtaguso huu, unaendelea katika Na.3 ya Hati hii ya ‘ ’ Kazi za Misioni
’’ Kwa kusema ; Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu hawalihitaji Kanisa katika
kuutekeleza mpango huu wa wokovu, maana pengine Mungu hutumia jitihada za kidini za mtu
binafsi kumwongoza amfikie,au kumtayarisha apate kuielewa Injili.Lakini kwa kufuata sheria
Mungu alikata shauri kwamba wokovu utawafikia binadamu siyo kama mtu mmoja mmoja
bali wakiwa katika kundi ambamo mtu anapaswa kuwamo apate kuokoka .Kwa hiyo Mungu
Baba alimtuma Mwanawe kuleta habari njema za mpango wa Mungu wa wokovu na kuonesha
njia,Mambo yote ambayo Mwana aliyasema na kuyatenda ndiyo mambo ambayo yalipaswa
kutangazwa mpaka yafikie mipaka yote ya ulimwengu na kuleta matunda kwa watu wote.
Enjili inapoenezwa sehemu mbalimbali Roho Mtakatifu huzifungua fikara za wale wasiokuwa
Wakristo wapate kusadiki na kwa hiari yao wenyewe wamgeukie Bwana kwani Yeye ndiye njia,
101
ukweli na uzima(Yoh 14:16).Na hivyo Kanisa Katoliki linakataza kabisa mtu asilazimishwe au
kubembelezwa kwa njia zozote zisizofaa kuingia katika dini,ndiyo kusema mtu asizuiliwe na
wenzake.Na utaratibu wa kumwingiza mtu Kanisani uzingatiwe hii ni kama atakuwa tayari.
Ndugu msomaji wangu hapa ndio uamini kuwa sisi Wakristu Wakatoliki tuna utajiri mwingi
sana wa Machimbuko ya Mafundisho ya Imani yetu. Waache hao Walokole wapige mayowe
na magitaa katika ‘’vijikanisa’’ vyao ya misimu,mitaa na mbaya zaidi iliyowekwa dhamana
kwa familia ya’’ baba mchungaji na mama mchungaji bila kuwabania watoto na ndugu zao ’’
kana kwamba ni kitu cha kumiliki au kumilikishwa, ,tuyaache hayo ! Sio lengo la Kitabu
changu, ‘’tuyapotezee’’ (tuyaache) tu .Au ndugu msomaji wangu ungependa niendelee
kuwarushia mikuki ya maneno? Hapana tuwache nao ni wana wa Abrahamu.
102
Kabla ya Pasaka, Yesu anatangaza kumpeleka ‘’Msaidizi mwingine’’(Mtetezi ndiye
Roho Mtakatifu),Roho Mtakatifu akifanya kazi tangu kuumbwa kwa ulimwen gu ‘’alinena
kwa vinywa vya manabii’’(Kanuni ya imani ya Nikea –Konstantinopoli),sasa atakuwa wa
pamoja na wanafunzi na ndani yao, kuwafundisha na kuwaongoza ‘’kwenye kweli
yote’’(Rejea Mwa 1:2, Kanuni ya Nikea (DS 150), Yoh 14:17, 26, 16:13.50 Hivyo basi, Roho
Mtakatifu amefunuliwa kama nafsi nyingine ya Mungu pamoja na Yesu na Baba.
Asili ya Milele ya Roho Mtakatifu imefunuliwa kwa kutumwa kwake katika nyakati.Roho
Mtakatifu alipelekwa kwa mitume na kwa Kanisa pia,kutoka kwa Baba kwa jina la Mwana,
sawa kama kutoka kwa Mwana kama nafsi,aliporudi kwa Baba 51 (Rejea Yoh 14:26, 15:26,
16:14).Kupelekwa nafsi ya Roho baada ya kutukuzwa kwa Yesu,(Rejea Yoh 7:39) 52
kunafunua utimilifu wa fumbo la Utatu Mtakatifu.
‘’Haya aliyasema juu ya Roho ,watakayempokea wale wamsadikio. Kwa maana Roho
alikuwa hajaja bado,kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa bado (Rejea Yoh 7:39).Unaona
wewe menyewe namna amini hii,inayosema,Nasadiki kwa Roho Mtakatfu Bwana Mleta
uzima,atokaye kwa Ba ba na Mwana.
103
Ukweli uliofunuliwa wa Utatu Mtakatifu umekuwa vyanzo vya mizizi ya imani hai ya
Kanisa,hasa kwa njia ya Ubatizo. Ukweli huu unaelezwa katika sheria ya imani ya
Ubatizo,inayoelezwa katika mahubiri,katika Katekesi na katika Sala ya Kanisa.Maelezo hayo
yapo tayari katika maandishi ya Mitume,kwa mfano salamu hii iliyochukuliwa katika
Liturujia ya Ekaristi: ‘’ Neema ya Bwana wetu Yesu Kristu,na pendo la Mungu na ushirika wa
Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote’’(Rejea 1Kor13:13 ,Rejea 1Kor 12: 4-6 ; Efe 4:4-6).53
Wakati wa karne za kwanza Kanisa lilitafuta namna ya kueleza wazi zaidi yake ya
Utatu Mtakatifu kwa kukuza ujuzi wa imani na kuutetea dhidi ya makosa yaliyokuwa
yanaiharibu.Hii ilikuwa ni kazi ya mitaguso ya zamani,ikisaidiwa na utafiti wa Mababa wa
Kanisa na kutegemezwa na jinsi Taifa la Mungu lilivyoishi imani.Ndugu msomaji
wangu,usichoke kufuatilia kuitembelea Katekisimu ya Kanisa Katoliki, bado tunaendelea
kuchimbuka.Kuhusu uundaji wa mafundisho (Dogma) ya Utatu Mtakatifu, Kanisa lilipaswa
kukuza maneno yake (terminolojia) kwa msaada wa maneno yatokanayo na falsafa
”substantia’’ = ‘’uwamo’’, ‘’ persona’’ = ‘’nafsi’’ au “hypostasis’’ = Muungano wa asili mbili,
ya kiMungu naya Kibinadamu, katika nafsi moja = Kristo Mungu – Mtu. ‘’Relatio’’
Uhusiano,nk. Kwa kufanya hivyo, Kanisa halikuweka imani chini ya hekima ya kibinadamu,
bali lilitoa maana mpya, ambayo haijasikilika.Kuanzia hapa linatumia maneno haya kueleza
fumbo lisiloelezeka,ambalo liko juu sana kuliko akili ya kibinadamu inavyoweza
kuelewa’’(Rejea Paul VI, Sollemnis profession fidei, 9: AAS 60(1968) 437 .54
Fundisho Msingi la Imani juu ya Utatu Mtakatifu (Dogma) Utatu ni Mmoja Sisi
hatuungami miungu watatu, bali Mungu Mmoja tu katika nafsi tatu: ‘’Utatu wa uwamo wa
pamoja’’ (consubstantialis)Rejea Mtaguso wa Konstantinopoli II (553 AD) :DS 421.).Nafsi
kamili ‘’Baba ni vile alivyo Mwana, Mwana ni vile alivyo Baba, Baba na Mwana ni vile alivyo
Roho Mtakatifu, yaani Mungu mmoja kwa asili ’’ (Rejea Mtaguso wa Toledo XI (675): DS
530:26). ‘’ Kila moja ya nafsi hizo tatu ni ukweli huu, yaani uwamo (substantia),uwapo
(essentia) asili ya KiMungu (natura divina)Rejea Mtaguso wa Laterani IV(1215)55
104
Nafsi za Mungu zina tofauti ya kweli kati yao ‘’Mungu ni mmoja,lakini siyo mpweke’’(Rejea
Imani ya Damasi:DS 71) ‘’Baba,’’ ‘’Mwana’’, ‘’ Roho Mtakatifu’’ siyo majina tu yanayoonesha
jinsi ya uwapo wa Mungu,kwani ipo tofauti ya kweli kati yao: Pia Tertullian naye anafundisha
hivyo.Yule aliye Mwana si Baba, Yule aliye Baba si Mwana, wala Roho Mtakatifu si Yule aliye
Baba au Mwana(Mtaguso wa Toledo XI (675): DS 530:25. Zipo tofauti kati yao kwa uhusiano
wao wa asili: Baba ndiye anayezaa, Mwana ndiye aliyezaliwa, Roho Mtakatifu ndiye
anayetoka(Rejea Mtaguso wa Laterani IV(1215): DS 804.).Umoja wa Mungu ni Utatu. 56
Nafsi za Mungu zina Uhusiano moja kwa nyingine.Tofauti ya kweli ya uhusiano ambao
nafsi za Mungu kati yao,kwa vile haigawanyi umoja wa Mungu,ipo tu katika uhusiano ambao
nafsi hizi zinaweka moja kuhusiana na nyingine: ‘’Katika uhusiano wa majina ya nafsi ,Baba
ana uhusiano na Mwana, Mwana na Baba,Roho Mtakatifu na wote wawili. Zinapoitwa nafsi
tatu,kwa mtazamo wa uhusiano wao,tunasadiki hata hivyo katika uwapo mmoja au asili moja
‘’( Rejea Mtaguso wa Toledo XI (675): DS 528).
Kwa kweli, ‘’kila kitu ndani yao ni kimoja pale ambapo hapana tofauti ya uhusiano’’(Rejea
Mtaguso wa Florence(1442): DS1330). ‘’ Kwa sababu ya umoja huu,Baba ni mzima ndani ya
Mwana, Yu mzima katika Roho Mtakatifu; Mwana yu Mzima ndani ya Baba; Yu mzima ndani
ya Roho Mtakatifu, Roho Mtakatifu yu mzima ndani ya Baba, Yu mzima ndani ya
Mwana’’(Rejea Mtaguso wa Florence (1442):DS 1331) 57
Mtaguso wa Florensi ( 1442 A.D ) Ulifundisha ,kwamba: Nafsi Tatu za Mungu zinapatikana moja
ndani ya Nafsi nyingine.Baba yu ndani ya Mwana,Mwana yu ndani ya Baba,na Roho Mtakatifu yu
ndani ya Baba na Mwana.Mtaguso huo wa Florensi ulifikia suala hili la Mwingiliano wa Nafsi Tatu
za Mungu kwa kutoa Fundisho Msingi la Imani kwa kusema Kwa sababu ya umoja huu wa Utatu
Mtakatifu wa Mungu; Baba yumo mzima kabisa katika Mwana na yumo mzima kabisa katika
Roho Mtakatifu; Mwana yumo mzima kabisa katika Baba namzima kabisa pia katika Roho
Mtakatifu; na Roho Mtakatifu yuko mzima kabisa katika Baba na mzima kabisa katika Mwana’’
(Rejea DS 704)
Kazi za Mungu zinafunua Yeye ni nani ndani yake Mwenyewe ; na fumbo la uwapo wake
wa ndani linaipa akili nuru juu ya kazi zake zote. Na hivyo ndivyo ilivyo pia, kwa mfano,hata
kati ya watu.Mtu anajionesha kwa kutenda kwake, na tunamfahamu vizuri zaidi
tunapoyafahamu matendo yake.
106
Anasema ‘’ Muwe wanyenyekevu kwa Askofu na kati yenu kama Yesu Kristo alivyo kwa Baba
kulingana na alivyoutwaa mwili,na Mitume kwa Kristo kwa Baba na kwa Roho.’’
27. Tertulliani
Hapa Tertulliani anamaanisha uwepo wa Nafsi nyingine ya Mungu Mwana na Mungu Roho
Mtakatifu. Kwa maneno mengine tungeweza kueleza hivi ,Nafsi ya Mungu Baba haipo peke
yake bali kuna Nafsi ya Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu.Si miungu watatu. Ni Nafsi
Tatu za Mungu Mmoja .
Neno(Logos ) Yesu au Hekima ni lazima aitwe ‘’umilele ulio sawa’’ na Baba na Roho
Mtakatifu.Neno atoka kwa Mungu kwa kuzaliwa bila kuumbwa (Eternal generation)
,akiwepo milele.Na kwa kuzaliwa kwake bila kuumbwa akawa Mwana.Neno ni Mwana wa
Mungu kwa kuutwaa ubinadamu.Ndugu msomaji kazi za Utatu Mtakatifu hazitenganishwi,
umwilisho unamuhusu moja kwa moja Yesu Kristo, lakini kazi ya umwilisho ilikamilishwa
na Utatu Mtakatifu (Rejea Lk 1:35)
Anapokuwa anaelezea suala la Fundisho la msingi la imani yetu Wakristo (Waakatoliki) juu
ya Utatu Mtakatifu,Orijeni hatofautiani sana na Tertulliani, yeye anasema ‘’Kuna tofauti
baina ya Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.Wanatofautiana namna walivyo na hata mmoja
mmoja kwa Mwingine ni tofauti.Lakini bado ni ,Mungu mmoja katika nafsi Tatu za
Mungu.Anaendelea kusema,Mwana ni mzaliwa kwa uzao wa kiroho (Spiritual
generation)aliye katika umilele.Mwana amezaliwa kutoka uasili mmoja na Baba.
Hivyo basi, Orijeni ,anasema Mwana ni Mungu na pia anamchukulia Roho Mtakatifu
kuwa naye ni Mungu,anayetoka kwa Baba na Mwana.Anayeangazisha Roho,Hekima na Akili.
107
29. MTAKATIFU AUGUSTINO
Mtakatifu Augustino amejitahidi sana kutoa mchango wake mkubwa wa Mafundisho juu ya
Utatu Mtakatifu wa Mungu; Anasema kwamba Mungu ni Mmoja na asiyeweza kugawanyika.
Kwa kweli hapo anatoa mchango wake unaoendana na Fundisho Msingi la Imani ya Kanisa
Katoliki (Dogma) linalofundisha kwamba ‘’Mungu ni Mmoja na asiyeweza kugawanyika’’.
Mungu huyu mmoja asiyegawanyika yupo katika Utatu Mtakatifu milele yote. Umungu wa
Nafsi Tatu ni Mmoja na Asili yake ni Moja kwa Nafsi Tatu.Na kila Nafsi ya Mungu ni Mungu.Na
Mungu anapotenda anatenda katika Utatu Mtakatifu katika mantiki hii kwamba Nafsi Tatu
za Mungu zina asili moja ya Umungu,Utashi na utendaji.Hivyo basi kazi ya uumbaji na
kutakatifuza inahusisha ushirikishwaji wa Baba ,Mwana na Roho Mtakatifu.Kila Nafsi Moja
ya Mungu ina ukamilifu wa Umungu hata Nafsi ya Mungu inapokuwa yenyewe kwa kumtaja
kama Mungu Baba,Mwana na Roho Mtakatifu.
Hata hivyo si miungu watatu, bali ni Mungu Mmoja wa Milele. Kama ilivyo kwamba
Nafsi Tatu za Mungu hazijaumbwa na zisivyokuwa na mwanzo wala mwisho, Nafsi Tatu za
Mungu zinabaki katika Umoja wao wa kutoumbwa wala wa kutokuwa na Mwanzo wala
Mwisho. Vilevile, Mwenyezi ni Baba,Mwenyezi ni Mwana, Mwenyezi ni Roho Mtakatifu. Na
bado Umwenyezi wao ni Mmoja (Mtakatifu, Mtukufu, Muumba mbingu na dunia, Muumba
vyote vinavyoonekana na visivyoonekana, Muweza yote). Umwenyezi wao ulivyo Mmoja na
wala sio umwenyezi wa Nafsi Tatu uliogawanyika.
108
Hivyo basi Baba ni Mungu, Mwana ni Mungu,Roho Mtakatifu ni Mungu. Na bado si miungu
watatu bali Mungu mmoja.
Baba hajaundwa na yeyote, wala kuumbwa, wala kuzaliwa. Mwana anatoka kwa Baba pekee
yake,hajaundwa wala kuumbwa,bali alizaliwa.Roho Mtakatifu anatoka kwa Baba na
Mwana,hajaundwa, wala kuumbwa, wala kuzaliwa bali anatoka( Roho Mtakatifu anatoka
kwa Baba na Mwana ndiyo filioque kwa kilatini).
Hivyo basi, kuna Baba Mmoja, sio akina Baba watatu,Mwana Mmoja,sio Wana watatu,Roho
Mtakatifu Mmoja, sio Roho Watakatifu watatu. Na katika Utatu Mtakatifu huu hakuna
anayekuja kabla au baada ya mwingine,hakuna aliyemkubwa au mdogo kwa mwingine. Bali
Nafsi hizo tatu za Mungu zaishi pamoja kwa umoja ulio wa milele yote, na katika usawa
mmoja kati ya Nafsi Moja na Nyingine. Hayo yamekwisha semwa hapo juu, kwa namna
yoyote Umoja wa Utatu Mtakatifu unapaswa kuheshimiwa katika Utatu na Utatu katika
Umoja.Kwa hiyo Yeyote anayetaka kuokolewa lazima afikirie kwa kina juu ya Utatu
Mtakatifu wa Mungu.58
109
Lengo la Waandishi walioandika juu ya Utatu Mtakatifu,nilioweza kusoma,na kwa
kusoma Neno la Mungu (Biblia Takatifu); Kwa kusoma Agano la Kale na Agano
Jipya,na wale walioandika kabla yangu juu ya Utatu Mtakatifu ambaye ni Mungu
Mmoja.Wamekuwa wanaufundisha kulingana na Biblia Takatifu.Baba na Mwana
na Roho Mtakatifu wenye usawa(ulingano) usioweza kugawanyika,ulio katika
Umoja wa Umungu wao.Kwa hiyo hakuna akina Mungu watatu bali Mungu Mmoja;
Japo kweli Baba amemzaa Mwana,na hivyo, aliye Baba sio Mwana,na Mwana
amezaliwa kwa Baba, kwa hiyo aliye Mwana sio Baba; na Roho Mtakatifu sio Baba
wala Mwana,bali ni Roho wa Baba na Mwana.Yeye(Roho Mtakatifu) ni sawa na
Baba na Mwana na anapatikana katika Umoja huo wa Utatu Mtakatifu
usiogawanyika.
Je, si huu Utatu Mtakatifu ,uliozaliwa na Bikira Maria aliyeteswa na kuzikwa kwa
mamlaka ya Ponsio Pilato,Siku ya Tatu akafufuka ,tena akapaa mbinguni lakini
huyu ni Mwana wa pekee tu.
Au ,Je si ule Utatu Mtakatifu uliomshukia Yesu kwa mfano wa njiwa wakati wa
ubatizo wake,au aliyeshuka siku ya Pentekoste baada ya kupaa kwake
Bwana(Yesu),aliyeshuka kwa kishindo kikubwa kutoka mbinguni na upepo mkali
ulioshuka chini,na kugawanyika katika ndimi za moto,lakini huyu ni Roho
Mtakatifu tu.
Anasema,ni imani yake, kama ilivyo Imani Katoliki.Haya ni maelezo anayoyaita initium fidei
kwa Kilatini,maana yake ‘’ Mwanzo wa Imani’’ kwa kiingereza inaitwa ( Starting point of
faith ). Hapa ndio mwanzo wa Imani ambayo tunaendelea kuielewa na si vinginevyo.
Kukataa kuamini mpaka uelewe kwanza, haya yanakuwa yamo katika msimamo wa
Mtakatifu Augustino usiokuwa si wa kuushikilia . Kwani kuna hatari ya kuingia katika
dimbwi la majivuno na unaweza ukapotoshwa.
Moja ya nukuu aliyoipenda inatoka katika Kitabu cha Isaya 7:9 ambayo kulingana na toleo la
Biblia aliyoitumia LXX, inasema ‘’Msipoamini hamtaelewa.’’
59 Ibid P.6
110
Kwa Biblia ya Kiafrika tunasoma ‘’ Lakini kisha miaka sitini na mitano Efraimu
utapondwa,wala hautakuwa tena taifa .Kama hamna imani imara hamtaweza kukaa
imara! Hapa ni kutaka kuonesha umuhimu wa imani katika Mafundisho ya Kanisa Katoliki
hasa haya yanayoumiza vichwa vyetu tunapotumia akili zetu tu bila imani inayoweza
kutupatia mwanga wa kuyafahamu japo kidogo .Kwani yanapita mafiko ya akili zetu
wanadamu (Rejea Isa 55:8-11).
Na hii ndiyo sababu iliyomvutia Mtakatifu Augustino kuandika kazi zake kubwa juu ya Utatu
Mtakatifu.Alikuwa amekwishaanza kazi ngumu juu ya kumjifunza Mungu na kutaka
kufahamu mengi juu ya Mungu (Baba na Mwana na Roho Mtakatifu).
Sasa hapa tunamuunga mkono Mtakatifu Augustino, nami Frater Simon Liberio J.
Bavugubusa nimeandika Kitabu hiki juu ya Utatu Mtakatifu ili tuzidi kumjifunza
Mungu wetu aliye katika Utatu Mtakatifu yaani Baba na Mwana na Roho Mtakatifu
tuliyemfahamu kupitia wazazi wetu kwa imani ya Kanisa la kweli Katoliki.Lakini
tukikumbuka angalisho kwamba Hakuna aliyemwona Mungu. Mwana wa pekee, Mungu
, aliye kifuani mwa Baba,amemtambulisha kwetu (Rejea Yoh1:18)
Kwa hakika Mungu aliacha alama za uwapo wake wa Utatu katika kazi yake ya kuumba ‘’
Mungu akasema na tumfanye Mtu kwa sura na mfano wetu afanane nasi, ambapo hapo
Mungu anazungumza katika Utatu Mtakatifu (Rejea Mw 1: 26-27) ,na katika Ufunuo wake
katika Agano la Kale. Lakini undani wa uwepo wake kama Utatu Mtakatifu ni fumbo
lisilofahamika kwa akili peke yake na hata kwa imani ya Israeli, kabla ya Umwilisho wa
Mwana wa Mungu, na kabla ya kupelekwa Roho Mtakatifu.(Rejea Katekisimu ya Kanisa
Katoliki namba 237)
Utatu Mtakatifu ni fumbo la imani kwa maana halisi, ‘’ ni moja ya mafumbo yaliyofichika
ndani ya Mungu, yasiyoweza kujulikana bila kufunuliwa kutoka juu.Kwa hakika Mungu
aliacha alama za uwapo wake wa Utatu katika kazi yake ya kuumba ‘’ Mungu akasema na
tumfanye Mtu kwa sura na mfano wetu afanane nasi, ambapo hapo Mungu anazungumza
katika Utatu Mtakatifu (Rejea Mwa 1: 26-27) ,na katika Ufunuo wake katika Agano la Kale.
111
Lakini undani wa uwepo wake kama Utatu Mtakatifu ni fumbo lisilofahamika kwa akili peke
yake na hata kwa imani ya Israeli, kabla ya Umwilisho wa Mwana wa Mungu, na kabla ya
kupelekwa Roho Mtakatifu.(Rejea Katekisimu ya Kanisa Katoliki Na. 237)…
1. KELLY Anthony, The Trinity of Love: A Theology of the Christian God,(New Theology Series
4),Peter C. Phan (ed.),Vol 4, Michael Glazier, Inc, Wilmington, 1989
2.Benedict XVI, I believe in One God:The Creed explained, Librerie Editrice Vaticana 2012
3.Biblia: Habari Njema kwa Watu Wote,Yenye Vitabu vya Deuterokanoni,(Toleo la Pili,2001).
(Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa,Vyama vya Kibiblia, Yenye Imprimatur/ na Ipigwe
Chapa ya C.C. DAVIES, Askofu wa Ngong, Mjumbe wa Umoja wa Maaskofu wa Tanzania na
Kenya)
112
8.DUPUIS Jacques, THE CHRISTIAN FAITH in the Doctrinal Documents of the Catholic Church
(Seventh Revised and Enlarged Edition) ,Theologcal publications in India, St.Peters Seminary
Bangalore,India ( 2nd Reprint) 2008
10.ISRAEL Joseph, Msalaba Unang’ara zaidi ya jua, (Kitabu cha Pili), 2009
11.JOHN PAUL II, Encyclical Dominum et Vivificantem ‘’Lord and Giver of Life’’, May 18, 1986
13. Pope Benedict XVI, Jesus of Nazareth, (Volume 2), Holy Week: from the Entrance into
Jerusalem to the Resurrection
16.LUIGI Anataloni, Hot Points of Catholic Teaching, On the Jesus titles, ‘’King ‘’ (4 th pocket
Edition), Consolata Missionaries, Nairobi -2007
17.MAHUNJA Barnabas, Teolojia kwa Walei (Eklesiolojia) (April 1996), Dar es Salaam,
Tanzania
18.COOK L. Michael , Responses to 101 Questions about Jesus, Question number 100,What will
Jesus’ second coming be like? p. 123
21.Reynolds, R. Ekstrom , The New Consise CATHOLIC DICTIONARY ( 4th print, 2010) on the
term Trinity pg 262
22.Rusimbya, Siegfried NTARE Padre, Jalimu letu la Mafundisho Msingi ya Kanisa Katoliki,
Segerea Seminari Kuu, Dar es Salaam, Tanzania, Mawazo ya Darasani, yaliyotokana vipindi
vyake katika Somo la Dogma (Mafundisho Msingi ya Imani ya Kanisa Katoliki hususani kwa
Mada za Roho Mtakatifu na Utatu Mtakatifu wa Mungu, Mwaka wa Pili 2012 na Mwaka wa
Tatu,Teolojia (2012 na 2013)
26. AMIGU Titus, Kisa Cha Imani: (SEHEMU YA KWANZA), Dini za Mungu Mmoja V.Majibu
Mafupi ya Wakatoliki kwa Makanisa Mengine , III.MAJIBU YA FUNDISHO LA UTATU
MTAKATIFU, Uk.18
114