You are on page 1of 7

Moto wa

Madhabahu,Usizimike
Mambo ya Walawi 6:13
Moto wa Madhabahu Usizimike
Mambo ya Walawi 6:13 Moto utatunzwa uwake juu ya
madhabahu daima; usizimike. Kazi kuu ya huo moto ilikuwa ni
kwa ajili ya kuteketeza sadaka mbalimbali zilizokuwa
zinaletwa na watu kwa ajili ya UPATANISHO yani ondoleo la
dhambi zao (utakaso).
Agizo hilo la kuutunza moto wa madhabahu kwetu sisi leo
limekuwa ni jambo la rohoni, kwani sisi tuliokombolewa kwa
damu ya Yesu hatuenendi tena ktk mwili bali twaenenda ktk
Roho.
Madhabu Yetu – Ni roho Zetu !! Mithali 4:23 Linda sana moyo
wako kuliko yote uyalindayo maana ndiko zitokako
chemichemi za Uzima
Kinachozimisha Moto !!
Kuacha Kumpenda Mungu-Kumb 6:5 Nawe mpende
Bwana ,Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho
yako yote na kwa nguvu zako zote ( Kitu gani
unachopenda Zaidi ya Mungu ! Nini kimechukua nafasi ya
moyo wako , wa roho yako na nguvu zako zote ) Je
unafikiri unampenda Mungu kwa kiwango hiki .
Kulala na Kumpa Ibilisi Nafasi: Mathayo 13:25 Lakini watu
walipolala akaja adui yake na akapanda magugu katikati ya
ngano akaenda zake,Usimpe Ibilisi nafasi ya KUPANDA
MAGUGU , !!
Kuwa na Kitu cha Muharibu Yohana 14:30 Mimi sitasema
nanyi maneno mengi tena ,kwa maan yuaja mkuu wa
ulimwengu huu wala hana kitu kwangu Una nini cha
mharibu ? Ana shitaka gani juu yako?
Namna ya Kufanya Moto Uwake
 Utakaso
 Roho wa Mungu ni moto ulao , Roho mtakatifu hutakasa miyoo yetu ili tutamani mambo
yaliyo juu , tumtamani Yesu Zaidi kuliko chochote kingine Waebrania 12:29 Maana Mungu
Wetu ni Moto
Utakaso ni Muhimu maana
 Hutuwezesha kuenenda kwa roho : Wagalatia 5:16-18 Basi Enendeni kwa roho ,wala
hamtazitimiza kamwe tamaa za Mwili ,Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na
roho, na roho kushindana na mwili ,kwa maana hizi zimepingana hata hamwezi kufanya
manayotaka.Lakini mkiongozwa na roho hampo chini ya
 Roho Mtakatifu asipokuwepo ndani yetu ni rahisi kuchukuliwa na tamaa na matakwa ya
ulimwengu huu
 Huondoa taka zote ndani ya moyo wetu Waebrania 9:14 Basi si Zaidi damu yake kristo
ambaye kwamba kwa roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo
na mawaa , itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu mpate kumwabudu Mungu
aliye hai??
 (Hasira ,Wivu,Uongo Uasherati ,Udanganyfu- kama malango ya uhaibifu kwa mtu binafsi ,
familia na Kanisa)
 Hutufanya kuwa tayari kutumika pamoja na Kristo:2Timotheo 2:20-21 Basi ikiwa mtu
amejitakasa kwa kujitenga na hao , atakuwa chombo cha kupata heshima
,kilichosafishwa,kimfaachap bwana kimetengenezwa kwa kila kazi iliyo njema !
Namna ya Kufanya Moto Uwake
 Omba Bila Kukoma:
 Hakuna Mpiganaji asijifua kwanza na kufanya mazoezi ya kutosha , hakuna awaniaye uongozi
asiyejiandaa na kupiga kampeni mchana na usiku ili ashinde , Vivyo hivyo nasi inatubidi kujenga
misuli ya maombi kwa kuomba kwa bidi maana 2 Kor 10 : 3-4 Maana ingawa tunaenenda
katika mwili hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili ,Maana Silaha za vita vita vyetu si za
mwili ,bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome !
 Ili kuangasha ngome tunahitaji silaha stahiki –Waefeso 6 :11
 Falme na Mamlaka-
 Wakuu wa Giza
 Majeshi ya Pepo wabaya katika Ulimwengu wa roho
Silaha ipi itumike wapi ? Vita ipiganwe namna gani ? Haya hufunuliwa kwa maombi
Kweli Viunoni
Vaa Dirii ya haki Kifuani
Kufungiwa utayari Miguuni –injili ya Amani
Ngao ya Imani –Kuzima mishale yote yenye moto ya yule Mwovu
Chapeo ya Wokovu
Upanga wa Roho –Neno la Mungu
Namna ya Kufanya Moto Uwake
Lishe ya Neno la Mungu Wakolosai 3:16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu
katika hekima yote mkifundishana na kuonyana kwa zaburi na nyimbo na tenzi za
rohoni , huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu
Roho yako inahitaji kulishwa kama vile mwili unavyohitaji kula chakula, kwa namna
moja au ingine , kuna jambo /mambo unayolisha roho yako , Na chakula cha roho ni
neon la Mungu , Usipolisha roho chakula chake utapata utapiamlo , unalisha nini roho
yako ?? Hebu tafakari , Mungu ametuumba na uhitaji wa neon lake .Mathayo 4:4 Naye
akajibu akasema imeandikwa ,Mtu hataishi kwa mkate tu ,ila kwa kila neno
litokalo katika kinywa cha Mungu .
Sikiliza neno la Mungu – Fellowship( Hujenga jeshi la waombaji)
Soma Neno la Mungu – Hamu ya chakula hutengenezwa ( Copy appetite za
wengine – Find a reading partner)
Tafakari neon la Mungu (Meditate) lipenye ndani ya moyo wako maana linaishi
likatengeneze na kungo’a kila uharibifu
Conclusion
 Warumi 12:1-2 Basi ndugu zangu ,nawasihi kwa huruma zake
Mungu ,Itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyohai ,takatifu ya
Kumpendeza Mungu , ndiyo ibada yenu yenye maana.Wala
msiifuatishe namna ya dunia hii , bali mgeuzwe kwa kufanywa
upya nia zenu mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo
mema ya kumpendeza na ukamilifu .
 Waefeso 4: 17 Basi nasema neno hili ,tena nashuhudia katika
Bwana ,tangu sasa msienende kama mataifa waenendavyo
katika ubatili wa nia zao.

You might also like