You are on page 1of 2

SOMO: MAMBO ANAYOFANYA ROHO MTAKATIFU KWENYE MAISHA YA MTU ILI

KUMPA MATOKEO YANAYODUMU


MNENAJI: PASTOR IBRAHIMU AMASI
04.08.2023
Roho Mtakatifu anaweka msukumo ndani mtu akae kwenye nafasi yake.
Kwenye maisha kila kitu ni marudio, Yoeli 2:7. Kwenye mbio za maisha tunategemeana.
Jibu la pamoja ni pamoja siyo moja. (The answer of unit is unit)
Roho Mtakatifu anaweka kitu cha kutambua watu wa mbele yako na wa nyuma yako. Mfano
kwenye maisha kuna watu sio wa kuita 'brother' hata kama umezaliwa nao tumbo moja.
Hii tunaiona kwa Yakobo na Yuda ndugu wa kuzaliwa wa Yesu Kristo hawakumwita Kaka,
brother, ila 'Bwana'
Yakobo 1:1
Yakobo, mtumwa wa Mungu, na wa Bwana Yesu Kristo, kwa kabila kumi na mbili
waliotawanyika; salamu.
Yakobo aliona kitu ndani ya Bwana Yesu ambacho kilimfanya asimwite Kaka ila Bwana.
Yuda aliyekuwa ndugu kwa Yesu na kwa Yakobo, alimwita Yesu Bwana na Yakobo ndugu.
"Yuda, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, kwa hao walioitwa, waliopendwa katika
Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo."
Yud 1:1 SUV
Kwenye maisha lazima ujue kuna watu wana nguvu kuliko wewe, na ukijua usitafute kushindana
nao ila kufaidika nao.
Mathayo 3:11.
"Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu
kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu
na kwa moto."
Hatushindani na safu zetu,ila tunatunza safu zetu.
Dathani na Kora walipopambana na Musa waliteremka kuzimu wakiwa wamesimama.
"Musa akasema, Kwa jambo hili mtajua ya kwamba BWANA amenituma, ili nifanye kazi hizi
zote; kwa kuwa mimi sikuzifanya kwa akili zangu mwenyewe. Kama watu hawa wakifa kifo cha
sikuzote, kama watu wote wafavyo, au kama wakipatilizwa kwa mapatilizo ya watu wote; hapo
basi BWANA hakunituma mimi. Lakini BWANA akiumba kitu kipya, na hiyo nchi ikifunua
kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, nao washukia shimoni wali hai; ndipo
mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau BWANA"
Hes 16:28-30
Hatupaswi kupigana na Neema ila kufaidika na neema.
"kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema
wa neema mbalimbali za Mungu."
1 Pet 4:10
Katika ufalme wa Mungu sisi sio wamiliki ila ni mawakili. Hatumiliki neema, hatumiliki karama
,wala vipawa. Ukiwa mmiliki hakuna wa kukuuliza, ukiwa wakili utatoa hesabu.
2petro 3:15
Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi
Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;
Ukipoteza safu yako unawasababisha na wengine waache kutazama safu zao.
"Hupiga mbio kama mashujaa; huupanda ukuta kama watu wa vita; nao huendelea mbele kila
mmoja katika njia zake, wala hawapotoshi safu zao."
Yoeli 2:7
Sauli alikuwa mfalme hakuwa kuhani. Alikosea kwa kuwa Samweli alichelewa ibadani, kuja
kutoa dhabihu. Watu walimsukuma kutoa dhabihu na akatoa. Akatoka lwenye safu ya ufalme
akaingia safu ya ukuhani na Mungu akamuondolea ufalme siku ileile akanza kumuandaa jirani.
IV. Unyenyekevu.
Roho Mtakatifu ndiye ambaye huleta Unyenyekevu ndani ya mtu.
Mungu hana biashara ya kufanya na mtu mwenye kiburi,majivuno na kujikweza.
.....Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye
mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu
cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa
ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza
akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba."
Flp 2:5-8
Mithali 16:18.
Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.
Mithali 18:12.
Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia
unyenyekevu.
Kuna level tatu;
• All self,None God
• Half self,Half God
• None self, All God
Na tunatakikana kuchukua level ya tatu, hakuna chetu, hakuna wewe ila Mungu pekee.
Mungu hana shida ya kukupeleka juu ila tabia yako ndiyo ana wasiwasi nayo namna utakavyo-
behave ukifika juu.
Shule ya unyenyekevu ya Roho Mtakatifu itakusaidia na kukujenga;
1. ufurahie matokeo ya wengine na kujua kuwa Mungu ndiye anayefanya kazi ndani yao.
2. Kuwa na umoja na wengine.
3.Kusikia ushauri wa watu sahihi wenye moyo mzuri.
4.Kuwapenda wengine kwa moyo .
3. Kubali kuwa mtumwa wa watu wengine ili kufikia kuwa mtu Mkuu.
"Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake
iwe fidia ya wengi."
Marko 10:45
-------------‐--------‐‐‐--------‐-------‐--

You might also like