You are on page 1of 3

ANZA SIKU NA BWANA.

#0004

SOMO: NYUMBA YA MUNGU

(sehemu ya kwanza)

Mungu aliumba Mwanadamu ana vitu vitatu ambavyo vinamfanya awe tofauti na wa kipekee katika
viumbe vyote ulimweguni.Vitu hivi ni mwili, roho na nafsi. Roho ya mwanadamu inaishi ndani ya mwili
wa mwanadamu akiwa hai. Biblia inasema kwamba roho ya mwanadamu ni pumzi ya Mungu Mwenye
Nguvu na ilimpulizwa kwa mwanadamu mwanzoni mwa uumbaji wa Mungu: "Mungu akalifanya anga,
akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo" (Mwanzo 2:7).
Ni roho ya kibinadamu ambayo inatupa ufahamu wa nafsi na mambo mengine ya ajabu, ingawa ni finyu,
sifa "za Mungu". Roho ya binadamu inajumuisha akili zetu, hisia, hofu, tamaa, na ubunifu. Ni roho hii
inatupa uwezo wa pekee wa kuwaza na kuelewa (Ayubu 32: 8, 18).

Msomaji wangu leo somo letu ni “Nyumba ya Mungu”. Mungu aliumba mwili wa mwanadamu uwe
nyumba yake. Shetani alipoona kwamba mwanadamu amependelewa kuliko viumbe vyote alifanya
juhudi zote za kumwagusha mwanadamu wa kwanza. Mwili wa mwanadamu ni nyumba ya Roho.
Shetani hafurahishwi na hili jambo.

1 PETRO 2:5 “Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani
mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.

Mungu haishi kwenye nyumba ambazo zimejegwa na mikono ya mwanadamu.

Matendo 7:48-49 “Ila Yeye aliye juu hakai katika nyumba zilizofanywa kwa mikono, kama vile
asemavyo nabii, Mbingu ni kiti changu cha enzi, Na nchi ni pa kuwekea miguu yangu; Ni nyumba gani
mtakayonijengea? Asema Bwana,”

Mwanadamu ni nyumba ya Mungu, na Roho wa Mungu anapaswa kuishi ndani yake.

Msomaji wangu ni muhimu sana kutambua kwamba mwili wako ni nyumba ya Mungu. Mtume Paulo
kwa uwezo mkuu wa Roho Mtakatifu anasema; 1 WAKORINTHO 3:16 “Hamjui ya kuwa ninyi
mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?”

Shetani yeye yuko kazini kila kukicha kuhakikisha kwamba ana chafua mwili wa Mwanadamu. Kuna
watu kutoka tumboni mwa mama zao shetani amefanya juhudi zote kuona kwamba Roho ya Mungu
haikaai ndani yao. Kazi moja yapo kuu ya shetani nikufanya mwili wa mwanadamu uwe najisi na kutia
uchafu ya aina zote. Mwili wa mwadamu ukisha kuwa mchafu na najisi Roho wa Mungu hawezi kukaa
ndani yake. Leo hii watu wengi wamefungwa kwasababu shetani amefanya miili yao kuwa kituo chake.
Kumbuka kila nyuma ya matatizo uliyo nayo kuna roho mbaya ya shetani nyuma yake.
Matatizo na vifungo hii vyote vimefanya watu wengi wakose kupata na kuishi na Roho wa Mungu.

Itaendelea……………….

Ni mimi ndugu yako;Kuhani na Mwl. Harrison Humphrey Mushenyera.


Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa maoni, ushauri na msaada zaidi
whatsap +255 768522999.
harrisonhumphrey25@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba unisaidie kuishare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la Mungu

SOMO: NYUMBA YA MUNGU

#0004

(sehemu ya pili)

Shetani akisha haribu mwili wa mwanadamu, mambo yafuatayo yanatokea;

-Utukufu wa Mungu unatoweka

-Shetani anaondoa ulinzi wa Kimungu

-Shetani anaondoa kibali cha Mungu.

-Shetani anakuwa ametuweka kama sumaku ya matatizo yote ya kimwili na kiroho.

-Shetani anaondoa uwepo wa Mungu aliye hai.

Uwepo wa Mungu aliye hai ukiondoka, mapepo na roho chafu zote zina pata mpenyo wa kuingia mwili
wa mwanadamu na kukutesa.

Kukaa/kuishi/kutembea na Roho wa Mungu lazima uwe na Neema ya Mungu. Kama huna neema ya
Mungu Roho wa Mungu hawezi kukaa ndani yako. Roho wa Mungu kuishi ndani yako sio jambo rahisi
kama vile watu wanafikiria. Huwezi kuongozwa sala ya toba au uokovu jinsi watu wengini wanafikiria
hapo hapo upokea Roho Mtakatifu, ni ngumu sana. Mitume wa Bwana Yesu alipofufuka alikaa na
mitume yake siku 40 anawafundisha kuhusu Roho Mtakatifu, baada ya hapo waalika siku 10 ndipo Roho
mtakatifu alipo wajia na kunena kwa lugha. Hii inaonyesha kwamba lazima uandae mazingira ya Roho
Mtakatifu. Lazima mazingira yake yawe masafi.

Tuna muona Bwana Yesu Kristo akingia Yerusalemu na kungia hekaluni nakukuta wamegeuza nyumba
ya Mungu kuwa nyumba ya biashara na pango la wanyang’anyi.
Nyumba ya Mungu ni nyumba ya sala. Miili ya watu wengi imeshauzwa.

Mungu aliye hai anategemea kuiona miili yetu inatumika vizuri kwa ajili ya utukufu wake. Mungu
anataka miili yetu imtumikie yeye maana ni nyumba yake. Baadhi yetu tumeigeuza miili yetu kuwa
mapango makuu ya wanyang’anyi. Miili yetu imetumika kuwa visima vya matusi. Miili yetu imetumika
kuwa vyungu vya ufisadi na ufitini na majungu makanisani. Wengine wameigeuza kuwa mapango ya
uasherati. Mtume Paulo anasema ‘Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae
viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! Kama Kristo anakaa ndani yetu iweje miili
yetu tuitumikishe kwenye uzinzi na uasherati?

Mungu ndiye muumbaji wa miili yetu. Imeandikwa katika Zaburi 139:14 "Nita kushukuru kwa kuwa
nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu na nafsi yangu yajua sana. Lazima
tuilinde miili yetu kama kafara takatifu. Warumi 12:1 "Basi ndugu zangu nawasihi kwa huruma zake
Mungu itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai takatifu ya kumpendeza Mungu ndiyo ibada yenyu yenye
maana." AMINA.

Ni mimi ndugu yako;Kuhani na Mwl. Harrison Humphrey Mushenyera.


Kiungo katika mwili wa kristo.
Kwa maoni, ushauri na msaada zaidi
whatsap +255 768522999.
harrisonhumphrey25@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba unisaidie kuishare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la Mungu

You might also like