You are on page 1of 5

AKILI NA ROHO (SEHEMU~2)

Na Mwl Mbwaga Joshua

Bwana Yesu apewe sifa!

Karibu katika muendelezo wa somo letu la AKILI NA ROHO.

Sehemu ya kwanza tuliishia katika kuchambua aina mbali mbali za roho, tukazitaja kwamba kuna Roho
wa Mungu/Roho mtakatifu, Roho ya/za Mungu, roho ya mwanadamu na roho za kishetani;

Roho mtakatifu alituongoza na kutufundisha kuhusu Roho mtakitifu na ujio wake tofauti, kwa njia ya
uvuvio na ujazo. Fuatilia sehemu ya kwanza ya utaona.

Leo tunaendele kuchambua roho; aina ya pili roho za Mungu;

2: ROHO “ZA/YA" MUNGU

Wengi tunachanganya kati ya Roho “ya” Mungu na Roho “wa” Mungu, tofauti ipo nayo ni hii Roho WA
Mungu ni nafsi ya Mungu, kumbuka Mungu ana nafsi tatu Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho
mtakatifu.

Hii ina maana unapozungumzia Roho wa Mungu unamzungumzia Mungu mwenyewe katika udhihirisho
wa Roho.

Ndio maana Roho wa Mungu ananena, anazungumza tunamsikia, anafundisha, anatuombea kwa kuugua

Roho ya Mungu ni nini?

Roho ya Mungu ni nguvu ya Mungu, uwezo, upako, mafuta anayoachilia Mungu juu ya mtu. Ukisoma
Isaya 61:1 utaona

Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu
habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao
waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.

Isaya anasema Roho ya Bwana i juu yangu lakini hakuishia hapo anaeleza ni kivipi Roho i juu yake
anatuambia kwa maana Bwana ametia mafuta ili niwahubiri hapa tunagundua kwamba Roho ya Bwana
ni mafuta au nguvu au anayotiwa mtu ili aweze kuifanya kazi ya Bwana.

Tuendelee mbele utaelewa vizuri.


Roho ambaye Yesu alimtaja pale katika Luka 4:18 ni tofauti na ile Roho aliyoitaja Isaya.
Yesu alisema “ Roho wa Bwana yu juu yangu” Isaya alisema “Roho ya Bwana Mungu i juu yangu”.

Hapa tunagundua kuwa Yesu alikuwa anamzungumzia Roho mtakatifu yule aliyemjilia kama hua wakati
alipokuwa akibatizwa na Yohana Mbatizajia Mathayo 3:16

Upande wa pili Isaya alimzungumzia Roho ya Mungu sio Roho mtakatifu/Roho ya Mungu. Pia hili
linathibitika katika sentensi ya pili;

Yesu alisema “kwa maana amenitia mafuta… (because he hath anoint me….)” anamaanisha Roho wa
Bwana aliemtaja katika sentensi ya kwanza.

Isaya alisema “ kwa maana Bwana amenitia mafuta kuwahubiri… (Because the LORD hath anointed
me…)” Hapa Isaya amemtaja Bwana. Roho aliekuwa juu ya Yesu ndiye aliemtia mafuta Yesu lakini Roho
iliyokuwa juu ya Isaya ilikuwa ni uweza/mafuta ambayo Isaya alitiwa na Bwana.

Pia Roho ya Mungu ni kibali au Ruhusa ya kuifanya kazi ya Bwana biblia ya Kiswahili cha kisasa inaandika
“amenichagua” badala ya neno “amenitia Mafuta.”

Sawa sawa na andiko linalotuambia mtu akihudumu ahudumu kwa nguvu alizojaliwa na Mungu Petro
4:11. Hivyo huruhusiwi kuhudumu pasipo Roho ya Bwana.

Roho ya/za Mungu ni zao au matunda ya Roho mtakatifu, ukisoma Matendo 1:8 anasema "Lakini
mtapokea nguvu Roho akishawajilia juu yenu". Roho mtakatifu hushuka na nguvu zake naye huleta roho
za Mungu na nguvu ama upako.

Huwezi kuzipokea Roho za Mungu pasipo kujazwa Roho mtakatifu, maana Roho mtakatifu ndiye
anayetujaza Roho za Mungu katika nguvu zake.

Roho za Bwana huja katika namna nyingi

Soma Kutoka 31
Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 2 Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri,
mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda; 3 nami nimemjaza roho ya Mungu,
KATIKA HEKIMA, NA MAARIFA, NA UJUZI, na mambo ya kazi ya kila aina ,
Ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba, 5 na kukata vito kwa kutiwa
mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote.

Sehemu ya kwanza tuligusia kidogo akili za kiungu akili hizi pia ni Roho ya Mungu ndani ya mtu katika
HEKIMA NA UFAHAMU.

3: ROHO ZA KISHETANI
Hizi ni roho zinazoachiliwa na Shetani kwa mwanadamu ili kumfanya mateka katika ufalme wa giza.
Mfano wa hizi roho ni roho ya mauti, magonjwa, uasherati, kiburi na matendo yote mabaya ya mwili.

Roho hizi huachiliwa na shetani kwa mwanadamu na kuambatana na nafsi/mwili wa mtu huyo, matunda
yake yanadhihirishwa katika matendo ya mwili yametajwa katika wagalatia 5;20,21 ambayo ni uasherati,
uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi,wivu, hasira, fitina ,faraka, uzushi, husuda,
ulevi, ulafi na mambo yanayofanana na hayo.

Lengo la roho hizi ni kumfarakanisha mwanadamu na Mungu. Neno la Mungu linasema Mwivi haji ila
aibe na kuchinja na kuharibu. Yohana 10:10

Njia ya kuziweza hizi roho hizi ni neno la mungu Daudi anasema katika zaburi 169; moyoni mwangu
nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda dhambi.

Pia Neno la Mungu katika Waebrania 4:12 linasema; Neno la Mungu lachoma hata kuzigawa nafsi na
roho.
Hivyo Neno la Mungu linauwezo wa kuitenganisha nafsi ya mwanadamu na roho za kishetani kama
uchawi, uzinzi, fitina n.k.

Lakini pia mwimba zaburi anasema; (Bwana) Hilituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika
maangamizi.
Hivyo Neno la Mungu lina uwezo wa kututoa katika maangamizi yatokanayo na roho za shetani mfano
roho ya mauti.

4: ROHO YA MWANADAMU

Tuligusia katika sehemu ya Kwanza tulipokuwa tunazungumzia maana ya Roho.


Kwa kifupi roho ya mwanadamu ni uhai katika nafsi yake, tulisema roho ni nafsi hai inayoifanya nafsi kua
hai. Hii inamaanisha roho ya mwanadamu ni kiungo muhimu katika uhai wa nafsi.

NB; Ukiona neno kwenye Biblia limeandikwa “Roho” peke yake kwa kuanza na herufi kubwa ujue
anaezungumziwa hapo ni Roho mtakatifu. Ukiona neno “roho” peke yake limeanza na herufi ndogo ujue
inayozungumziwa ni roho ya mwanadamu au roho ya kishetani (inategemea na mazingira)

Moyoni vs Rohoni

Moyoni ni ndani ya nafsi ya mtu,


Moyoni ni ndani au sirini mahali ambapo kila kitu kinachofanyika nje kinaweza kufanyika lakini katika
usiri ambapo Mungu tu ndiye anayeweza kuona naye huweza kuwafunulia watumishi wake.

Mungu anasema Yeye anauchunguza moyo Yeremia 17:9


Mambo yote tuanyofanya katika mwili tunaweza kuyafanya katika moyo, yawe mema au mabaya;
Mathayo 5:28 Yesu anasema mtu amatazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naya
moyoni naye moyoni mwake.

Moyoni unaweza kuzini,kuiba kuchukia na mengine yanayofanana na hayo lakini mtu mwingine asijue.

Wengi watahukumiwa kutokana na moyo, wapo waliovaa vazi la wema lakini moyoni mwao wamejawa
chuki ni nani awajuae? wapo wanaohesabiwa haki na wanadamu lakini Mungu achunguzaye mioyo
amewakataa, huwezi kufanya ushirika na Mungu ikiwa moyo wako hauko sawa.

Neno la Mungu linasema atazamavyo Mungu si kama wanadamu tutazamavyo. Wanadamu tunatazama
nje lakini Bwana anatazama ndani.Samweli 16:17

Watu hulitumia neno hili kujihesabia haki kwa matendo yao mabaya ya mwili, utakuta mdada amevaa
mavazi ya kikahaba kanisani ukimfuata uatasikia anakuambia “Bwana anatazama moyo”.
Asijue ya kuwa kunauhusiano mkubwa kati ya moyo na matendo ya mwili. Huwezi ukawa mchafu
mwilini moyoni ukawa safi. Mtumishi mmoja wa Mungu alisema ulivyo nje ni matokeo ya ulivyo ndani.

Rohoni ni katika ulimwengu wa Roho.

Mtu anaposema yuko rohoni ina maana yuko katika ulimwengu wa roho, Kumbuka kuna ulimwengu wa
mwili na ulimwengu wa Roho. Soma Waefeso 1:3 Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo
aliyetubariki kwa Baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho,…

Katika ulimwengu huu si wote wawezao kuingia au kuyajua mambo yake, mambo ya ulimwengu huu

1wakorintho 2:14,15; basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana
kwake huyo ni upuuzi, wala hawezi kuyafahamu kwa kuwa YANATAMBULIKA KWA JINSI YA ROHONI, 15
Lakini MTU WA ROHONI HUYATAMBUA YOTE wala yeye hatambuliwi na mtu.

Kwa hiyo mambo ya rohoni yanahitaji expert/mjuzi wa mambo ya kiroho, Mtu anaeingia katika
ulimwengu wa roho ndiye anayeweza kuyatambua mambo ya rohoni. Huyu ndiye anayeitwa MTU WA
ROHONI.

Tunapaswa kuwa watu wa rohoni ili tuzijue siri nyingi za ulimwengu wa roho pia ili tuweze kumwabudu
muumba wetu.

Kumbuka Mungu ni Roho nao wamwabudio imewapasa kumwabudu katika roho na kweli Yohana 4:24.
Kama Mungu ni roho tunahitaji masikio ya rohoni ili tuweze kumsikia pia tunahitaji macho ya rohoni ili
tuweze kuijua mipango yake mizuri juu yetu.
Mtumishi wa Elisha aliliona jeshi jeshi la watu na magari na farasi akaogopa lakini hakuliona Jeshi la
Mungu kwa sababu macho yake yalikuwa yamefungwa 2wafalme 6:15.

Macho ya rohoni na masikio ya rohoni ni milango ya fahamu ya rohoni muhimu sana . Marko 8:18 Neno
linasema mna Macho, lakini hamuoni ; mna masikio, hamsikii? Wala hamkumbuki?
Ili uwe mtu wa rohoni inakupasa kuyatafakari mambo kwa namna ya rohoni.

Kutafakari mambo kwa jinsi ya rohoni ni kuyahusianisha na neno la Mungu.


Kwa hivyo ukitaka kuwa mtu wa rohoni lazima ulisome Neno la Mungu, ulishike, ulitafakari na kulitumia
katika maisha ya kawaida.

Biblia inamtambulisha mtu asiyeyatambua mambo ya rohoni kama MWANADAMU WA MAMBO YA


ASILI.
Huyu hayaelewi mambo ya rohoni hivyo hawezi kuyapokea huyapuuza.

NB: Katika ulimwengu wa roho pia kuna ufalme wa Mungu na ufalme wa shetani.
Hivyo ukiwa mtu wa rohoni utaijua mitego yote ya shetani na hila zake zisizoonekana katika ulimwengu
wa mwili.

MUOMBE MUNGU AKUSAIDIE KUWA EXPERT WA MAMBO YA ROHONI YAANI KUWA MTU WA ROHONI.

KILA MTU ANAEMCHA MUNGU ANAPASWA AWE MTU WA ROHONI.


NI LAZIMA UWE MTU WA ROHONI. ILI UYAJUE MAPENZI YA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO NA UJUE
MITEGO YOTE YA SHETANI ISIYOONEKANA KWA JINSI YA MWILINI.

You might also like