You are on page 1of 12

JINSI MUNGU ANAVYOJIBU MAOMBI

UTANGULIZI
1. Maombi ni jambo ambalo limekuwa likisisitizwa
sana na viongozi wa kanisa. Msisitizo kuhusu maombi
ulikuwepo hata katika siku za Yesu ambapo Yesu
aliwahimiza sana wanafunzi wake kuomba.
2. Kwa mkristo jambo la maombi halikupaswa kuwa
jambo la kusisitizwa. Ni sawa na swala la kula, hakuna
mtu mzima kiafya anayesisitizwa kula chakula. Yeye
mwenyewe atapata njaa itakayomsukuma kuhitaji
chakula.
3. Vivyo hivyo hata katika afya ya kiroho ukiona mtu
anasisitizwa kufanya maombi basi kuna hitilafu katika
kiroho chake. Watu hawaombi kwa sababu aidha
hawaamini kuwa maombi hujibiwa au hawajui jinsi
Mungu anavyojibu maombi na hivyo kuwafanya
kutokuwa na imani na maombi.
4. Mkristo hapaswi kudhani kuwa Mungu hatusikii
tunapoomba bali anapaswa kufahamu kuwa kuna namna
nne ambazo Mungu hujibu maombi. Na ndiyo asubuhi ya
leo tumeona ni vyema kujifunza JINSI AMBAVYO
MUNGU ANAVYOJIBU MAOMBI.

1
I. MUNGU KUJIBU NDIYO
Mara nyingi Mungu hujibu ndiyo pale
tunapomwomba. Zaburi 118:5
5
Katika shida yangu nalimwita Bwana; Bwana
akanijibu akaniweka panapo nafasi.
Na pia Zaburi 138:3
3
Siku ile niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji
nafsi kwa kunitia nguvu.
Zipo sababu zinaweza kumfanya Mungu kujibu
ndiyo kwenye maombi yetu. Baadhi ya sababu ni
ifuatavyo:
a. Kumtanguliza Mungu katika maisha yetu.
Mathayo 6:33
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na
33

haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.


Pia na Mithali 3:5 – 10;
5
Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote,
Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
6
Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye
atayanyosha mapito yako. 7 Usiwe mwenye
hekima machoni pako; Mche Bwana,
ukajiepushe na uovu. 8
Itakuwa afya
2
mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako.
9
Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa
malimbuko ya mazao yako yote. 10Ndipo
ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na
mashinikizo yako yatafurika divai mpya.
b. Kuomba sawa na mapenzi ya Mungu. 1
Yohana 5:14 – 15.
14
Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya
kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi
yake, atusikia. 15Na kama tukijua kwamba
atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba
tunazo zile haja tulizomwomba.
c. Pale tunapotimiza mapenzi yake katika
maisha yetu.
na lo lote tuombalo, twalipokea kwake,
22

kwa kuwa twazishika amri zake, na


kuyatenda yapendezayo machoni pake.
Pale Mungu anapojibu ndiyo kwa maombi yetu nafsi
zetu hufurahi. Lakini wakati mwingine tunaweza
kupokea jibu tofauti…..

3
II. MUNGU KUJIBU NDIYO LAKINI SUBIRI
Kuna wakati Mungu husema ndiyo kwa maombi yetu
lakini lazima iendanae na majira yake. Mhubiri 3:1,
11
1
Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati
kwa kila kusudi chini ya mbingu. …….. 11Kila
kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena
ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila
kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua
kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo
hata mwisho.
Hivyo wakati Mungu anasema ndiyo lakini subiri
tunaweza kudhani kuwa Mungu amesema hapana.
Kwa sababu hiyo hatupaswi kukata tamaa tunapaswa
kuendelea kumlilia. Luka 18:7
Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule
7

wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni


mvumilivu kwao?
Pale ambapo Mungu anasema subiri kwa majibu ya
maombi yetu ni muhimu kuzingatia mambo
yafuatayo:
a. Tunapaswa kuwa na uvumilivu. Ebrania
6:10 – 12.

4
Maana Mungu si dhalimu hata aisahau
10

kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha


kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia
watakatifu, na hata hivi sasa mngali
mkiwahudumia. 11Nasi twataka sana kila
mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa
utimilifu wa matumaini hata mwisho; 12ili
msiwe wavivu, bali mkawe wafuasi wa hao
wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu.
b. Tunapaswa kuendelea kuomba, kutafuta,
kubisha hodi. Luka 11: 8 – 10.
8
Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa
haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake,
lakini kwa vile asivyoacha kumwomba,
ataondoka na kumpa kadiri ya haja yake.
9
Nami nawaambia, Ombeni, nanyi
mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni,
nanyi mtafunguliwa. 10Kwa kuwa kila
aombaye hupokea; naye atafutaye huona;
naye abishaye atafunguliwa.
c. Tunapaswa kuendelea kukumbuka ahadi za
Mungu. Rumi 8:24.

24
Kwa maana tuliokolewa kwa taraja;
lakini kitu kilichotarajiwa kikionekana,
5
hakuna taraja tena. Kwa maana ni nani
anayekitarajia kile akionacho?
Pale Mungu anaposema ndiyo lakini subiri ni wakati
tunapaswa kuwa wavumilivu na kutumainia neema
yake. Tunapaswa kutumainia neema ya Mungu hata
pale jibu la Mungu linakuwa vinginevyo:
III. MUNGU KUJIBU NJE YA MATARAJIO
Kuna wakati Mungu hujibu tofauti na kile
tunachotarajia. Tunapaswa kufahamu kuwa mawazo
ya Mungu na njia za Mungu ziko tofauti na zetu.
Isaya 55: 8 – 9:
8
Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala
njia zenu si njia zangu; asema Bwana. 9Kwa
maana kama vile mbingu zilivyo juu sana
kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana
kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko
mawazo yenu.
Kwa mfano unaweza ukamwomba Mungu nguvu na
uvumilivu lakini Mungu akakupitisha kwenye
mapito. Wafilipi 1:29 – 30.
29
Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si
kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake;
30
mkiwa na mashindano yale yale mliyoyaona
kwangu, na kusikia kwamba ninayo hata sasa.
6
Mapito ya majaribu hayo hukujengea nguvu na
uvumilivu ambao ulimwomba Mungu. Rumi 5: 3 – 4.
3
Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki
pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta
saburi; 4na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo;
na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini;
Hatupaswi kumwekea Mungu mipaka kama
tunavyowaza katika mawazo yetu. Hii ni kwa sababu:
a. Mungu ana uwezo wa kufanya zaidi ya
tuwazavyo kama tunavyoweza kusoma katika
Waefeso 3:20
20
Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya
mambo ya ajabu mno kuliko yote
tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya
nguvu itendayo kazi ndani yetu;
b. Lakini pia sisi hatujui kuomba
inavyotakiwa:
26
Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu
wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi
itupasavyo, lakini Roho mwenyewe
hutuombea kwa kuugua kusikoweza
kutamkwa.

7
Kumwekea Mungu mipaka katika kujibu
maombi yetu ni sawa na kujiwekea mipaka ya
majibu yetu. Mfano pale tunapoomba kwa ajili
ya wagonjwa. Je huwa tunaomba Mungu
afanikishe matibabu ya mgonjwa? Kama
tukiomba hivyo tunakuwa tunampangia Mungu
namna ya kufanya ambapo yeye ana njia zaidi ya
tuwazavyo. Ni vizuri kumwomba Mungu
awafanye uponyaji kwa namna atakavyo yeye.
Tunapomwomba Mungu, inatupasa tutumaini kuwa
atafanya katika namna anavyoona inafaa. Hata hivyo
tunapaswa kuendelea kumtumaini Bwana hata
pale…..
IV. MUNGU KUJIBU HAPANA
Kuna wakati Mungu hujibu hapana kwa maombi yetu
Yakobo 4:3
Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu
3

mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.


Tunapaswa kuamini kwamba Mungu anajua vilivyo
bora kwa ajili yetu. Hivyo hutupatia majibu mema
kwa ajili ustawi wetu mzuri. Ebrania 12: 5 – 11.
5
tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo
nanyi kama kusema na wana, Mwanangu,
usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie
8
moyo ukikemewa naye; 6Maana yeye ambaye
Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila
mwana amkubaliye. 7Ni kwa ajili ya kurudiwa
mwastahimili; Mungu awatendea kama wana;
maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?
8
Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako
ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa
haramu ninyi, wala si wana wa halali. 9Na
pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa
mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si
afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho
zetu na kuishi? 10Maana ni hakika, hao kwa
siku chache waliturudi kama walivyoona vema
wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki
utakatifu wake.
Pale Mungu anajibu hapana tunaweza tusimwelewe,
lakini tunapaswa kumtumainia. Habakuki 3: 17 – 19.
Maana mtini hautachanua maua, Wala
17

mizabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya


mzeituni itakuwa bure, Na mashamba
hayatatoa chakula; Zizini hamtakuwa na
kundi, Wala vibandani hamtakuwa na kundi la
ng'ombe; 18Walakini nitamfurahia Bwana
Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu. 19
YEHOVA, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye
huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu,
9
Naye ataniendesha katika mahali pangu
palipoinuka.
Pia 1Koritho 10:13 tunasoma hivi
Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo
13

kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni


mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe
kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu
atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze
kustahimili.
Pale Mungu anapojibu hapana hutupa neema kuishi
pasipo kuwa na kile tulichokiomba. 2 Koritho 12:7 –
9.
7
Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi,
kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba
katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige,
nisije nikajivuna kupita kiasi. 8Kwa ajili ya kitu
hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba
kinitoke. 9Naye akaniambia, Neema yangu
yakutosha; maana uweza wangu hutimilika
katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu
kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae
juu yangu.

10
HITIMISHO
Wapendwa zipo namna mbalimbali ambavyo Mungu
hujibu maombi yetu baadhi namna hizo ni hizi ambazo
tumejikumbusha leo; kwamba hujibu ndiyo, Mungu
hujibu ndiyo lakini subiri, Mungu kujibu nje ya matarajio
yetu na pia Mungu kujibu hapana.
Vyovyote Mungu atakavyojibu maombi yetu tunapaswa
kufahamu kuwa majibu yake kwa ajili ya mema kwetu.
Hivyo basi hatupaswi kukakta tamaa katika kumwomba
Mungu maana yeye ni Mwema na atatupatia mema kwa
ajili ya ustawi wetu. Zaburi 6:6;
9
Bwana ameisikia dua yangu; Bwana
atayatakabali maombi yangu.

Mungu awabariki sana

Mpelenja Bernard Mongella


Mtumwa Asiye na Faida

11
Wimbo:
Unaweza kufanya, Unaweza kutenda, Mambo makubwa
zaidi ya niombavyo x 2
Mambo makubwa zaidi ya niombavyo x 2
Zaidi ya niombavyo, zaidi nitakavyo unaweza kufanya,
unaweza Yesu
Zaidi ya tarajio, zaidi ya niombavyo unaweza kufanya
unaweza Yesu.
Mambo makubwa zaidi ya niombavyo x 2

12

You might also like