You are on page 1of 6

KUNA NGUVU KATIKA MAWAZO YETU

(SEHEMU YA 3)

MPANGO WA MUNGU KUHUSU MAWAZO YETU.

Bila mimi hamuwezi

Mawazo yetu ni muhimu sana kwa maisha yetu ya sasa na yale


yajayo. Kwa hiyo, Mungu anayo mengi ya kusema kuyahusu.
Ametuwekea utaratibu na mwongozo wa kuweza kuvuna baraka
zake kwa kupitia kwenye mawazo yetu. Hata hivyo ni muhimu
kukumbuka wakati wote kuwa msaada wetu unatoka kwa Bwana.
(Zaburi 124:8). Pia Yeye anasema: “Mimi ni mzabibu ninyi ni
matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana;
maana pasipo mimi ninyi hamuwezi kufanya neno lolote.”
(Yohana 15:5).

3
Kwa hiyo, hata katika suala la kuwaza au kutafakari, bila msaada
wake, hatuwezi kitu. Kama kuwaza tu kwa namna inayofaa
hatuwezi, sembuse kuyafanya hayo mawazo yetu yatupatie
shauku za mioyo yetu? Agizo la muhimu analotupa Bwana,
tunalopaswa kulizingatia ni kuwa, “Mtumaini Bwana kwa moyo
wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe.” (Mithali
3:5).

Bwana anasema nisizitumainie akili zangu! Hili ni jambo la


kushangaza kabisa. Kuzitumainia akili maana yake ni kufanya
mambo yangu bila kumpa Mungu nafasi. Yaani, nikishawaza
jambo tu, ninalitenda. Tena ninakuwa ninajua tu kuwa yale yote
ninayoyafanya ni ujanja, uwezo na juhudi zangu mwenyewe.

Mungu anatuonya kuhusu kuzitumainia akili, si kuhusukuzitumia.


Tunatumia akili zetu kuchagua wapi pa kutumainia. Biblia
inasema, “Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi.”
(1Wakorintho 15:34)

JINSI YA KUWA NA MAWAZO YENYE NGUVU

Hivi itakuwaje kama nitaweza, kila siku, kuwa na mawazo ya


kushinda, kuweza, kufanikiwa, kupona na mengine ya namna hii
hata kama kwa namna ya kibinadamu mambo yanaonekana kuwa
ni mabaya? Bila shaka maisha yangu yatabadilika kwa haraka
sana kuelekea kwenye ubora. Tunaweza kabisa kuzifunza akili
zetu kuwaza mawazo chanya na si mawazo hasi, yaani tunaweza
kuwa na imani. Na uzuri ni kwamba yupo Bwana upande wetu
ambaye anatusaidia katika kila hatua.

Kutofautisha nia

Ili tuweze kujenga tabia ya kutafakari kwa mafanikio, ni lazima


tuwe na uwezo wa kuchunguza na kutambua nia iliyomo ndani
mwetu kila wakati.

Ndani mwetu kuna nia za aina mbili. Biblia inasema, “Kwa kuwa
nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.”
(Warumi 8:6). Kwa hiyo, kuna nia ya mwili na nia ya roho. Nia ya
mwili ni nia ambayo hujificha sana kiasi kwamba wakati mwingine
ni vigumu kuigundua. Bila shaka umeshawahi kukutana na hali
zifuatazo:

• Unapotaka kulala unaomba ulinzi wa Mungu uzingire nyumba


yako. Lakini, baadaye ukisikia kishindo chochote nje, unaingiwa
na hofu kubwa. Kilichokufanya uombe ni nia ya roho, lakini
kilicholeta hofu ni nia ya mwili. Hii imekufanya usimwamini
Mungu ambaye hapo tu kabla uliomba ulinzi wake.

• Unaposafiri, unalifunika gari kwa damu ya Yesu. Lakini, gari


likiyumba kidogo tu njiani, hukumbuki tena maombi uliyofanya.
Hofu inaletwa na nia ya mwili.
• Unaweza kuomba Bwana akufungulie milango ya mafanikio,
kisha baada ya muda mfupi unaanza kusema hali ni ngumu,
maisha ni magumu. Nia ya roho ilikusukuma kuomba lakini nia ya
mwili ikakufanya ukiri kutowezekana.

• Watumishi wa Mungu wanaposema kuwa Bwana ametupa


mamlaka ya kutoa pepo na kuponya wagonjwa, unashangilia na
kupiga makofi. Lakini ukiangalia, hujawahi kumwombea mgonjwa
yoyote wala kukemea pepo. Nia ya roho ilikufanya upige makofi
ya furaha lakini nia ya mwili inakuzuia kuyatendea kazi mambo
hayo.

Mifano hii michache inatuonyesha kuwa, kumbe kwa nje unaweza


kuonyesha kuwa uko upande wa Mungu, lakini ndani yako ukawa
uko kinyume kabisa. Shida ni kwamba, ile nia ya ndani ambayo
iko kinyume na Mungu ndiyo inakuwa na nguvu, na ndiyo
inayoshinda. Kibaya zaidi ni kuwa, unakuwa hujitambui kwamba
una hali hiyo.

Kuchagua nia sahihi

Ili upate mazao mengi na bora shambani ni lazima ufanye kazi.


Lakini, ili upate magugu mengi na mazao yako yaharibiwe,
unatakiwa ukae tu bila kufanya chochote. Magugu yatakuja
yenyewe tu. Hayahitaji juhudi yoyote. Akili ya mwanadamu ni
kama shamba. Mawazo safi ni mazao bora. Mawazo mabaya ni
magugu. Usipojibidisha kwa lolote kuhusu mawazo yako, ni
lazima utavamiwa na lundo la magugu, yaani mawazo yasiyofaa!
Wakati mwingine unaweza usilitambue hilo.

Dalili zinazoonyesha kuwa akili yako ina magugu hayo ni hizi


zifuatazo: kusonya kila mara, kunung’unika, kulaumu watu
wengine, kukosa raha, kujiinamia, kutikisa kichwa, kushika tama,
kukosa usingizi, n.k.
Ili uwe na mawazo bora yatakayozaa matunda mema maishani,
ni lazima ufanye kazi ya kung’oa magugu wewe mwenyewe, kwa
maana, “Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu.” (Mithali 16:1).

Ni lazima kufanya uchaguzi wa makusudi (conscious selection) wa


mawazo mema kutoka katika Neno la Mungu, na kuyatafakari
hayo muda wote. Kufanya uchaguzi wa makusudi maana yake ni
kuwa, usiache tu mawazo yoyote yaingie na kutoka akilini kama
yapendavyo. Simama katika mlango wa akili yako kukagua kila
wazo linalojitokeza, kisha ruhusu yaingie yaliyo safi na zuia yaliyo
magugu.

Ni lazima kuitambua nia ya mwili kila wakati na kuishinda kabisa


na kubaki na nia moja tu – ya roho. Unaishinda kwa kukiri neno
la Mungu. Kwa mfano, unapoingiwa na hofu, unasema,
“Imeandikwa kuwa Mungu hajanipa roho ya woga bali ya nguvu.”

Kitendo cha wewe kusema hivyo kinadhihirisha kuwa umetambua


kwamba kuna magugu, yaani nia isiyo sahihi. Kwa njia hiyo tu
ndipo utaona nguvu za Mungu zikifanya kazi maishani mwako.
Hili ni jambo la muhimu sana! Endapo hufanyi hivyo, uwezekano
mkubwa ni kuwa uko katika kundi la wale ambao hawajui kuwa
wamevamiwa na wanaendeshwa na hiyo nia ya mwili.

Kumbuka kuwa, mwanzoni hii itakuwa ni vita kubwa. Utapata


upinzani mkubwa. Hili ni jambo la kawaida kabisa. Maana kuhusu
adui zetu, Bwana anasema, “Sitawafukuza mbele yako katika
mwaka mmoja nchi isiwe ukiwa na wanyama wa bara
wakaongezeka kukusumbua. Nitawafukuza kidogo kidogo mbele
yako, hata utakapoongezeka wewe, na kuirithi hiyo nchi.”
(Kutoka 23:29-30).

Kasi ya kushinda kwako inategemea kuongezeka kwako - katika


ufahamu, maarifa na nguvu. Kwa hiyo, Bwana anatutia moyo
akisema, “Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa
ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu
wako, yu pamoja nawe kila uendako.” (Yoshua 1:9).

Ukidumu katika kuyazuia mawazo mabaya kuingia akilini mwako


kwa kutafakari mawazo mema kutoka katika neno la Mungu,
hakika yake, baada ya muda mfupi utaona unabadilika kabisa!
Hakika! Kwa maana, neno hilo ni roho na roho ndiyo itiayo uzima!
(Yohana 6:63).

Kwa mfano, unapoumwa, badala ya kutafakari jinsi mwili


unavyouma na udhaifu ulio nao, tafakari kwamba, “Kwa kupigwa
kwake mimi nimepona; yeye ameyachukua magonjwa yangu.
Mimi ni mzima katika Jina la Yesu.” Unapoishiwa fedha, badala ya
kutafakari jinsi ambavyo shida uliyonayo ni kubwa kuliko fedha
unayopata, tafakari, kwa mfano, “Yote yawezekana kwa imani.
Kwa Jina la Yesu naamuru fedha zije kwa ajili ya hitaji hili
nililonalo.”

Kwa kufanya hivi, utakuwa unatimiza andiko linalosema, “Linda


sana moyo wako maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.”
(Mithali 4:23). Uzima haushii kwenye kupona tu magonjwa. Hata
kupata fedha, chakula na nguo ni sehemu ya uzima. Ndani ya
moyo kuna chemchemi itakayotoa huo uponyaji na hizo fedha
ambayo ni mahitaji yako.

Ukiyawaza yale yaliyo kinyume na neno la Mungu, unakuwa


katika kundi hili: “Asiyetawala roho yake ni mfano wa mji
uliobomolewa, usio na kuta.” (Mithali 25:25). Utaanza tu kukiri
udhaifu na kushindwa. Hatimaye, utavamiwa na roho za kuzimu
za kila namna, maana hauna ulinzi. Na hizo ndizo
zitakazokudidimiza chini zaidi na zaidi ili litimie andiko lisemalo,
“Mauti …. huwa katika uwezo wa ulimi.” (Mithali 18:21).

Chagua mawazo ya kutafakari! Usikubali hata kidogo kuwa


mtumwa wa mawazo. Usitawaliwe na mawazo, bali uwe mtawala
wa mawazo. Yaani, wewe ndiyo uchague nini cha kuwaza na nini
cha kutupa nje. Kasha utaona ahadi za Mungu zikitimia maishani
mwako

You might also like