You are on page 1of 5

UVUMILIVU

MAANA YA UVUMILIVU
Kulingana na Biblia, uvumilivu unahusisha mengi zaidi ya kustahimili tu majaribu au hali ngumu.
Uvumilivu unahusisha akili na moyo wetu, au namna tunavyotenda tunapokabili hali ngumu. Mtu
anayevumilia anaonyesha sifa ya ujasiri, uimara, na subira. Kitabu kimoja kinasema kwamba uvumilivu ni
‘mtazamo unaomwezesha mtu kustahimili mambo, si kwa sababu tu hana la kufanya bali kwa sababu
ana tumaini thabiti. Ni sifa inayomwezesha mtu kusimama imara huku akiendelea kukabili tatizo fulani.
Ni sifa nzuri inayoweza kufanya jaribu kali sana lionekane kuwa jambo linaloleta utukufu kwa sababu
ingawa kuna maumivu, bado kuna tumaini.’

Upendo ndio huwachochea Wakristo wavumilie. (1 Wakorintho 13:4,7) "Upendo huvumilia, hufadhili;
upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni. Huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote;
hustahimili yote." Kumpenda Mungu kunatuchochea tuvumilie jambo lolote analoruhusu litupate. (Luka
22:41-42) "Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba, akisema, Ee
Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke."
Kuwapenda ndugu zetu kunatusaidia tuvumilie udhaifu wao. (1 Petro 4:8) "Zaidi ya yote iweni na juhudi
nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi." Kumpendaa mwenzi wetu
wa ndoa hutuwezesha kuvumilia “dhiki” ambazo hata wenzi wa ndoa wenye furaha hukabili na
hutusaidia tuimarishe kifungo chetu cha ndoa. (1 Wakorintho 7:28) " Lakini, kama ukioa, huna hatia;
wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu kama hao watakuwa na dhiki katika mwili nami
nataka kuwazuilia hayo."

Tunaishi katika nyakati ambazo tabia ya uvumilivu,subira ni changamoto kubwa,tunaishi maisha


ambayo ni ya mbio mbio,haraka haraka ,hakuna subira.Ulimwengu wetu wa kisasa wenye vitu na
mambo ya kisasa ya haraka,mashine za haraka,huduma za haraka,vyakula vya haraka,usafiri wa haraka
n.k. hii inafanya uvumilivu na subira kuwa hadimu kwa katika maisha yetu. (Wagalatia 5:23-22;
Wakolosai 3:12-17.).

Tunda la Roho ni Tabia ya kristo ndani yetu. kusudi la Mungu ni tufanane na Kristo. Ukomavu wetu wa
kiroho unapimwa na tunda la roho: Msisitizo mkubwa leo katika kanisa umekuwa katika Karama za roho
Kuliko katika tabia,karama ni utendaji wa kristo ndani yetu, ni nguvu za kristo.tunahitaji uwiano wa
vyote. kuwa na madhihirisho ya karama bila Tabia ya Kristo ni janga kubwa la kiroho.
Neno la kiyunani kwaajili ya uvumilivu ni makrothumia ambalo ni muunganiko wa maneno mawili.
Makro (long ) na-Thumos (- temper) “long-tempered” ni knyume cha neno “Short tempered.”Hasira
iliyo mbali,isiyo ya haraka,uwezo wa kuzuia hasira,kutolipuka kwa hasira.Subira /uvumilivu kuna husiana
na kuwa na “Long fuse”, . Ni uwezo wa kukaa nyuma na kusubiri matokeo yanayotarajiwa bila kuwa na
hali ya wasiwasi ,kuhangaika, kufadhaika, au kukataa tamaa.

Ni uwezo wa kuachia hitaji lako ambalo ungeweza kulilikidhi mara au kulitimiza mara na kuwa tayari
kusubiri. Ni tabia ambayo huonyesha kusthahimli wengine juu ya mawazo na fikra zao, pia kuonyesha
huruma,kuwaelewa na kuwakubali wale walio taratibu,au wazito,polepple katika kukomaa kwao,na
kuchukuliana na uwezo tofauti walionao wengine.

Ni uwezo wa kubakia mtulivu katikati ya machafuko na ,misukosuko mbalimbali ya maisha kwa sababu
unajua ya kwamba Mungu yupo anatawala mambo yote.

Kuwa na uwezo wa kufyonza na kunyonya maudhi,kero,masumbufu ya maisha bila kulipuka na


hasira.Uvumilivu-makrothumia unafyonza mambo yana yokukasirisha, kuudhi,kusumbua na kukukera
pasipo kukupoozesha wewe au kukudhoofisha. Ni kama kuwa na “ shock absorbers”

Watu wenye uvumilivu nao pia wanakasirishishwa na kukerwa,kuudhiwa na mambo mbalimbali kama
mtu mwingine yeyote.haamanishi uwe “door mate” kifutia miguu cha mlangoni.

“ Tofauti ya watu wenye uvumilivu na wengine ni kwamba wanajua wakati gani wa kusema,na wakati
gani wa kulikablili jambo moja kwa moja. Lakini mpaka wakati huo ufike, wana napo mahali pa kuweka
kwanza yale yanayo wakasirisha,yanayo wa kera, na kuwaudhi,bila ya kulipuka,bila ya kukosa
kujitawala.”

TABIA NA HISIA ZINAZOAMBATANA NA KUKOSA UVUMILIVU:


Kuwa mtu usiye na subira, kutoridhika,kufadhaishwa(upset) na kuwa na hasira juu yako mwenyewe na
juu ya wengine kwa mambo mbalimbali hasa yasiyo ya msingi na madogo madogo. (makosa ya
kibinadamu)

Kuwa mtu ambaye mara zote huna uwezo wa kujizuia na kulipuka kwa hasira mara kwa mara na
kupelekea kuiharibu siku yako mwenyewe na kuharibu siku ya wengine-kuifanya siku yako kuwa mbaya
na wengine pia.

Kuwa mtu unaye haribu mahusiano na watu wengine,kirahisi iwe ni kanisani, ofisini,shuleni n.k. kwa
kutaka mambo yaende vile tu unavyotaka wewe .

fahamu ukweli huu: “si mara zote katika maisha mambo yatakwenda vile wewe unavyotaka na kwa
haraka wewe unayoitaka.”
MATOKEO YA KUKOSA UVUMILIVU
Hisia utakazo shughulika nazo utapokuwa huna uvumilivu: Kukasirishwa kwa kila kitu au na kila mtu,
Kufadhaishwa/kuhamakishwa na watu walio polepole au wazito katika kufanya mambo Kukata tama –
kwa maisha kwa ujumla, Kuwa na uchungu-kwamba wengine wana yale/vile wewe unavihitaji,
Wasiwasi-juu ya kila wakati katika siku, Kujawa na fadhaa-kwasababu utataka kufanya zaidi, Kuwa na
mfadhaiko-wakati wote upo chini ya msukumo-Kuchanganyikiwa kwamba wengine hawafanyi vya
kutosha na hasira za haraka,mara kwa mara.

FAIDA ZA UVUMILIVU KATIKA MAISHA YETU.


Uvumilivu unaleta nini katika maisha yetu,kwanini tuutafute?una faida gani? Uvumilivu huleta Amani
katika maisha yetu. (Wagalatia5:22), Uvumilivu hutusaidia kustahimili mambo magumu (Yakobo 5:7-
11), Uvumilivu huweka wazi kusudi la maisha yetu kwetu (Zaburi 40:1 War. 8:25), Uvumilivu hutusaidia
kuendeleza mahusiano yatakayodumu kwa muda mrefu. (Zab.15:18), Uvumilivu hushawishwi watu
wengine pia. (Mithali 25:15) na Uvumilivu ni sifa tunayohitaji ilikuweza kukabili hali ngumu .(Yakobo 5:7-
11).

JINSI GANI TUNAWEZA KUTENGENEZA NA KUKUZA UVUMILIVU NDANI YETU.


“UVUMILIVU si rahisi kwetu kwasababu chanzo chake si asili yetu ya mwili, unatoka katika upendo wa
Mungu, ukweli ni kwamba hatujazaliwa na uvumilivu. Upendo ndio ufunguo unaotupelekwa kwenyew
uvumilivu, mahali pa kuanzia ni upendo ili kupata uvumilivu.” Kujijua na kujitambua wenyewe katika
ufahamu wetu na mioyo yetu na kuuona ugonjwa tulionao. kuliona tatizo ndani yetu na kulikubali,
Kufahamu ya kwamba uvumilivu unaweza kuendelezwa na kukuzwa ndani yetu na Roho wa Mungu
pekee . (Wag 5:22-23), Huwezi kudhihirisha tabia ya Kristo kwa nguvu zako mwenyewe. Ni Roho
Mtakatifu peke yake aliye na nguvu za kufanya mabadiliko anayotaka kufanya Mungu katika maisha
yetu. Mungu hukuza tunda la Roho katika maisha yako kwa kukuruhusu upite katika mazingira
ambayo unajaribiwa kutenda kinyume kabisa cha sifa ya tunda la Roho! Kukua kwa tabia daima
kunahusu uchaguzi, na majaribu hutoa nafasi hiyo. Kwa mfano Mungu hutufundisha upendo kwa watu
wasiopendeka karibu yetu. Haihitaji tabia kupenda watu wanaopendeka na pia wanaokupenda.

Mungu hutufundisha furaha halisi katikati ya huzuni tunapomgeukia. Raha (happiness) hutegemea
mazingira ya nje, lakini furaha (joy) hutegemea uhusiano wako na Mungu. Mungu hukuza amani halisi
ndani yetu, siyo kwa kufanya mambo yatendeke kama tulivyopanga, lakini kwa kuruhusu nyakati za
machafuko na vurugu. Mtu anaweza kuwa na amani akitazama machweo ya jua yanayopendeza au
akistarehe mapumzikoni. Tunajifunza amani halisi kwa kuchagua kumwamini Mungu katika mazingira
ambayo tunajaribiwa kuhofu au kuogopa.
Vivyo hivyo, uvumilivu unakuzwa katika mazingira ambayo tunalazimika kusubiri na tunajaribiwa
kukasirika. Wakati mwingine ni watu wa familia yetu wenyewe watatumika kutengeneza uvumilivu
ndani yetu,watu walio karibu ndani yetu na walio wapendwa wetu ndio hasa wata waujaribu na
kuupima uvumilivu wetu..“Basi kwa kuwa mmekuwa kama wateule wa Mungu ,watakatifu
wapendwao,jivikeni… uvumilivu” Wakolosai 3: 12.

Na Evangelist Hosea Kione


Jr Evangelist at T.A.G
hepkstar@gmail.com
Contact: +255787404327
PO BOX 37, KIDATU.

You might also like