You are on page 1of 2

DINI NA MAHUSIANO

Neno hili, dini, likitajwa, hutaarifu uwepo wa mahusiano baina ya mwanadamu na mamlaka anayoiamini kadri
anavyoishi. Tafsiri ya neno, dini, kwa mujibu wa Kamusi ya kiswahili Sanifu,Toleo la 2004, humaanisha
yafuatayo:1.Imani inayohusianiana na mambo ya kiroho kwamba kuna muumba ulimwengu huu na
kwamba ndiye mtawala wa kila kilichomo.2.Mfumo fulani wa imani hii na njia ya kuabudu/kutii huyo
muumba,k.v.Ukristo, Uislamu au Ubuda.
Kutokana na ongezeko la maneno ya kiswahili, mengine yakiwa ni matokeo ya kutohoa, maana za neno, dini,
zinaweza kuwa zimeongezeka. Somo hili linajadili jinsi ya kudhihirisha kufaa kwa, dini ya kikristo, kama
matokeo ya mfumo wake unavyoelezwa ndani ya Biblia,ilijulikanayo kuwa ni Maandiko Matakatifu
yamtambulishayo Mungu kama Muumbaji wa ulimwengu huu aliye mtawala wa kila kilichomo.

A. YALIYOMO KATIKA MFUMO WA DINI YA KIKRISTO


Mfumo wa imani ya dini ya Kikristo, inahusisha matendo mengi,kukiwemo- kuabudu, kusali, na kuheshimu au
kumtii huyo muumba. Katika Yakobo 1:26,27, kunaelezwa mojawapo ya yatakiwayo kuonyeshwa na kila
mkristo, ambayo ni zaidi ya kuabudu au kusali. Aya inasomeka kama ifuatavyo:
“26Mtu akidhani ta kuwa anayo dini; wala hauzuii wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya
moyo wake, dini yakemtu huyo haifai.27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda
kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa".
Katika kufafanua aya hii, Yakobo sura ya pili, kwa kutumia vielelezo kadhaa, anahitimisha kwa kusema kuwa,
“Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa", (Yako 2:26).

Imani inapotumika, huwa inataarifu uhusiano wa kiibada baina ya mwanadamu na Mungu, (Yoha 4:23,24).
Tendo la kumwabudu Mungu siku zote linahusisha kuufanya mwili wa anayeabudu, utawaliwe na Roho wa
Mungu, kwa mujibu wa Warumi 12:1. Katika kumheshimu na kumtii Mungu, kunahitajika udhihirisho wa
upendo kwa Mungu, kwa njia ya kumwabudu, na hapo hapo upendo kwa wanadamu wengine, kwa njia ya
kuwahudumia majirani wa mtu wanaopitia maisha yenye dhiki. Hapa ndipo imani na matendo vinapokutana
katika kudhihirisha ukamilifu wa ibada kwa Mungu na huduma ya kuonyesha kuwajali walio wahitaji. Huduma
hii ni zaidi ya kuwasaidia walio na dhiki ya mahitaji ya kimwili. Inahusisha pia matumizi ya maneno ya faraja
kwa wanaopitia uzoefu wa msongo wa kiasi au kihisia. Hapa ndipo ulimi hutajwa kuwa, maneno yanenwayo
yasipopangiliwa vizuri ili kuwasadia walio na maumivu ya kiakili, huduma ya kuwapatia mahitaji ya
kimwili,kama vile,chakula au mavazi,au kusaidia kutibiwa maradhi ya kimwili, yote yanaweza
yasitoshe,endapo akili zao zinavurugwa na watoa huduma za kimwili. Ni katika upana huu, tunatakiwa
kujifunza jinsi ya kuoanisha yote mawili.

B. MAHUSIANO YA FAMILIA YAWEZA KUHARIBU NGUVU YA DINI


Yako mambo kadhaa miongoni mwa wanafamilia yanayoweza kuharibu nguvu ya mvuto wa kidini. Ni muhimu
kutafakari yaonekanayo kuvuruga matendo ya imani na matendo ya dini kihuduma.
a. CHOYO NA UCHOYO UHARIBU MAHUSIANO
Choyo na Uchoyo, ni tabia ya kutotaka kutoa kitu kumpa mwingine. Ni sifa ya mtu kutumia vitu alivyo navyo
yeye mwenyewe. Matokeo ya tabia hii ni mtu kujikuta amejikusanyia vitu vingi kwa malengo ya kuvitumia kwa
siku za mbeleni, akilenga kuwa hapungukiwi kitu wakati wowote. Uchoyo huongeza sifa kuwa mbaya zaidi,
kwani uchoyo na mchoyo, ni hali ya kutopenda kutoa kitu hata kama aliyenacho hakihitaji, wala hakimnufaishi.
Kuhusiana tabia hii, Yesu alionya dhidi ya tabia hii, kwa kusema, “Angalieni jilindeni na choyo, maana uzima
wa mtu haumo katika wingi wa vitu alivyo navyo”, (Luka 12:15).
b. MWANAFAMILIA MCHOYO HUDHOOFISHA MAHUSIANO
Choyo na uchoyo hudhoofisha pande zote mbili, yaani ndani ya wanafamilia na nje ya familia. Wanafamilia
wakiwa na kiongozi mmojawapo mwenye choyo na uchoyo, huruhusu vitu viozee au kuharibikia ndani ya
makabati na maghala. Uharibikaji huu hupoteza fedha iliyovinunua, ili kuharibikia bila kazi. Mhitaji, ambaye
kingelimfaa kutumiwa,naye akikiomba anaambiwa hakifai, ijapokuwa yeye alikiona kumfaa. Dhambi hii ni
mbaya.
c. SI RAHISI KUBADILISHA MAWAZO YA UCHOYO
Kila mchoyo hujenga tabia ya choyo kwa kutumia hoja zisizo na msingi kibiblia. Mara nyingi husukumwa na
misemo ya kimila au desturi, au mapokeo. Miongoni mwa hoja hizo ni kusema,*Nakitunza hiki ili kumkumbuka

1
fulani aliyenipatia*, (ijapokuwa yawezekana akawa amefariki). Jingine ni kusema, *Aliyenipa aliniagiza
nisikitoe ili ajapo akione*. Mtoaji wa aina hii naye ametoa kwa masharti ya uchoyo. Hekima, Maarifa na
ufahamu, ambavyo huipatia familia nguvu ya akili ya umoja,(Mithali 24:3-6). Nguvu hizi hukosekana endapo
mmojawapo wa wazazi ni mchoyo. Mzazi wa aina hii hugawa watoto, wengine wawe wachoyo kama yeye, na
watakuwemo wakarimu kama mmoja wa wazazi alivyo.
d. MCHOYO HUSAHAU HATARI ILIYO MBELE YAKE
Mfano wa hatari ya aina hii aliutoa Yesu katika Luka 12:16-20, kisha kumhusu mchoyo kinaishia na kauli hii,
“Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea
tayari vitakuwa vya nani?

C. JITAJIRISHE KWA MUNGU USHINDE NAFSI


Kanuni ya,Kujitajirisha kwa Mungu, imeelezwa na Yesu katika Luka 12:20,21, inayoshinda upumbavu na
kujiwekea nafsi mwenyewe. Hii ni kwa sababu hayupo mwanadamu ajuaye siku roho yake itakapoondolewa
kwa kifo. Tunajitajirishaje kwa Mungu? Hapa ndipo tunaporudi katika kile kinachoelezwa katika Yakobo
1:26,27 pamoja na Math 25:34-40, inayoishia na maneno, “kadri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu
zangu walio wadogo, mlinitendea mimi”. Katika Luka 6:38, wote walio na vitu wameagizwa kuwapa watu vitu,
ili kwa kutoa watoaji wazidi kupewa kiasi cha kujaa na kushindilia na kumwagika; na kwamba tukitoa kidogo
tutapewa pia kidogo kutoka kwa Mungu.

TUTAFAKARI UHALISIA WA MALI ZETU


1. Kwa uzoefu wako,je, wasiokuwa na vitu wasivyovihitaji kimatumizi nyumbani ni wengi au ni
wachache? Kwa nini wanavitunza wakati wahitaji wake wapo?
2. Kuna usemi usemao,"Akiba haiozi". Je,kauli hii inao ukweli kiasi gani na uongo kiasi, kama kutu na nondo
na wanyama na wadudu hula vyakula na nguo zilizotunzwa kwa siku zijazo?
3. Je, unadhani kuwa Mungu ameridhishwa na utoaji unaoutoa, ukilinganishwa na mbaraka wa vitu
alivyokupatia? Kama, unajielewa kuwa una vitu usivyovitumia kwa miaka mingi, ni kwa nini huvitoi ili
kuwapatia wanaoweza kunufaika navyo?
4. Unadhani ni busara kuchoma nguo iliyokubana kwa kuwa hujisikii kumpatia ambaye hana nguo zaidi ya
moja au mbili, kwa hoja haipendezi? Kwa nini kusubiri ikubane kisha itunzwe kusubiri ivaliwe tena
utakapokonda tena?
5. Kwa nini tunaruhusu nafaka zingine ziozee ndani ya vyombo vyetu stooni,wakati wapo wahitaji jirani nasi,
ambao hawajifunui kwetu kwa kuwa hatuna mazoea ya kuwatembelea? Kama hatuna walio majirani,
kutokana na mfumo wa Maisha yalivyo, watakuwepo tunaopakana, ambao pengine siyo rahisi kuingiliana.
Lakini zipo Taasisi za kijamii kama, makanisa, Vituo vya Watoto yatma, au wajane, au wenye mahitaji
maalumu. Ni kwa nini tusiwapelekee hao ambao huwa ni rahisi kuwajua wahitaji?
6. Wanandoa wakiishi, mmojawapo akiwa mkarimu na mpenda kutoa; wakati mwenzake akiwa mgumu wa
kutoa, watoto watajifunzaje ukarimu na kuhudumia yatma na wajane kupitia kwa wazazi wa wasio na
mtizamo mmoja katika utoaji wa walivyo? Je, ni rahisi kwa familia aina hiyo kuwa nuru kwa matendo yao,
kwa walio gizani?
7. Baada ya kusoma somo hili utafanya nini ili kujitajirisha kwa Mungu? Jizoeze kuonyesha kuwa wewe na
familia yako ni nuru inayoangazia wasioujua upendo wa Mungu.Jizoeze kusaidia bila kusubiri kuombwa
maana ujirani hujitangaza kimahitaji au uwezo wao.
Somo hili likieleweka kuwa lina kanuni za kuboresha mahusiano na Mungu na wanadamu wenzako,
washirikishe wengine
(Muhtasari umefanywa na Mch E. Kasika, Mshauri wa Vijana na Wazazi na Viongozi, 0764 151 346)

You might also like