You are on page 1of 7

[Type here]

“KUKABILIANA NA YANAYOWEZEKANA (An Encounter of Possibilities)”


HUDUMA WEZESHI YA KIADVENTISTA (Adventist Possibility Ministries)
HUBIRI LA SABATO YA TAREHE 20 APRILI 2024
By Pastor Julio Cesar Ribeiro1

Utangulizi
Huduma ya Wezeshi ya Kiadventista ni harakati ya kiutume ambapo
ujumuishaji na uthamini wa watu wenye ulemavu ni vipaumbele na
nguzo za msingi. "Wote ni wenye vipawa, wanahitajika na
wanathaminiwa!" Leo, juu ya Huduma Wezeshi ya Sabato ya 2024,
tutachunguza hadithi ya Yakobo na kukutana kwake na Mungu.
Tutachunguza mapambano yake ya kiroho na Kristo. Hatupati tu
mfano wenye nguvu wa mabadiliko ya kiroho lakini pia ujumbe wa
kina juu ya umuhimu na kusudi la watu wenye ulemavu katika historia
ya kibiblia na maisha yetu leo. Wakati huu wa kihistoria katika Agano
la Kale unatualika kutafakari juu ya kina cha neema ya Mungu na
kuingizwa. Tunapochunguza mabadiliko matatu katika maisha ya
Yakobo - tabia yake, jina lake, na hali yake ya kimwili - tuna
changamoto ya kufikiria upya uelewa wetu wenyewe wa heshima na
kusudi la watu wenye ulemavu. Tutaona jinsi kila kipengele cha
maisha ya Yakobo kinavyoonyesha kazi ya Mungu inayojumuisha
katika safari yetu kiduniani.

1. Kukutana katika Mto Yaboki (Mwanzo 32:22-32)


Wakati wa kushangaza zaidi katika maisha ya Yakobo hutokea
wakati anapigana na mtu wa ajabu wakati wa usiku. Mtu huyu,
baadaye alitambuliwa kama Malaika wa Bwana (Kristo Mwenyewe
katika umbile la mtu), anampa changamoto Yakobo katika vita vya
1Mchungaji Julio Cesar Ribeiro ni Mtu mwenye Ulemavu na Mshauri wa Kujitolea kwa eneo la ulemavu wa kimwili
na / au kupunguzwa kwa uhamaji kwa Huduma za Uwezekano wa Waadventista wa Divisheni ya Amerika Kusini.
Kwa sasa anahudumu kama Mchungaji wa Wanafunzi katika Chuo cha Waadventista cha Limeira (katika Konferensi
ya Paulista ya Kati / Union ya Brazil ya Kati). Hapo awali alifanya kazi kama Mkurugenzi Msaidizi katika Chuo cha
Theolojia cha UNASP na kama Msaidizi katika Kituo cha Utafiti cha Ellen G. White, pamoja na Mwalimu wa Elimu ya
Kidini katika kozi mbalimbali za shahada ya kwanza katika UNASP Engenheiro Coelho. Yeye pia ni Profesa katika Kozi
ya Ukalimani wa Kibiblia katika Chuo Kikuu cha MissioNow cha Konferensi ya Paulista ya Kati. Anachukua shahada
ya Udaktari katika Theolojia ya Biblia ya Agano la Kale katika Chuo Kikuu cha Waadventista cha River Plate (UAP),
Argentina, akitafiti eneo la ulemavu katika Biblia. Ana shahada ya Uzamili katika Theolojia ya Kikristo kutoka Chuo
Kikuu cha Kipapa cha Katoliki cha São Paulo (PUC-SP), shahada ya Uzamili katika Theolojia ya Kibiblia kutoka
Seminari ya Theolojia ya Waadventista wa Amerika ya Kusini (SALT), na ni Mtaalamu katika Theolojia ya Kibiblia na
Shahada ya Theolojia kutoka Kituo cha Chuo Kikuu cha Waadventista wa São Paulo (UNASP).
IMETAFSIRIWA NA PR. FILBERT J. MWAGNA, APM DIRECTOR – STU 1
[Type here]

kimwili na kiroho. Yakobo anaibuka kutoka kwa mapambano haya


akiwa na utambulisho mpya na kusudi jipya. Anapokea jina jipya,
Israeli, ambalo linamaanisha "mtu anayeshindana na Mungu."
Mabadiliko haya ya jina hayaonyeshi tu mabadiliko katika
utambulisho wa Yakobo lakini pia mabadiliko katika tabia yake na
uhusiano wake na Mungu. Zaidi ya hayo, inafafanua utume ambao
Mungu alikuwa akimpatia na moyo uliohitajika kuubeba huo (utume).

1.1 Safari ya Yakobo: kutoka mdanganyifu hadi Israeli


Hadithi ya Yakobo huanza na yeye kuonyeshwa kama mtu mjanja
(mwenye hila), aliye tayari kudanganya ili kufikia malengo yake. Jina
lake, ambalo linamaanisha "mdanganyifu" au "mtu anayepanda,"
huonyesha asili yake ya awali. Hata hivyo, katika safari yake yote,
Yakobo anakabiliwa na mfululizo wa changamoto na kukutana kwa
Mungu ambayo husababisha mabadiliko makubwa.

1.2 Mabadiliko ya tabia


Yakobo alikuwa mtu aliyetiwa alama na ujanja na ufuatiliaji usio na
kikomo wa maslahi yake. Hakusita kutumia ujanja ujanja kufikia
malengo yake, hata kama ilimaanisha kumdanganya kaka na baba
yake. Hata hivyo, wakati wa kukabiliana na Mungu katika
mapambano makali wakati wa usiku, Yakobo alikabiliwa na sio tu
mpinzani wa kimwili lakini mgogoro wa kiroho ambao ungebadilisha
mtazamo wake na maisha yake milele. Katika hili la kukabiliana na
Mungu, Yakobo alikabiliwa na udhaifu wake na upeo katika uso wa
utakatifu na nguvu za Mungu. Hakuweza tena kutegemea uwezo
wake au mipango yake lakini ilibidi ajisalimishe kabisa kwa neema
ya Mungu na udhibiti wa utawala (wa Mungu). Kama vile Yakobo,
watu wenye ulemavu mara nyingi hutengwa na kudharauliwa na
jamii kutokana na mapungufu yao ya kimwili au kiakili.
Wanakabiliwa na unyanyapaa na ubaguzi. Hata hivyo, ni hakika
(prisicely) katika mapungufu haya kwamba neema ya Mungu
inadhihirika kwa nguvu zaidi. Watu wenye ulemavu hutufundisha
umuhimu wa unyenyekevu, uvumilivu, na kumwamini Mungu.
Wanatupatia changamoto ya kufikiria upya viwango vyetu vya
kujithamini na mafanikio. Tunakumbushwa kwamba maana ya kweli
ya maisha iko katika uhusiano wetu na Mungu na uwezo wetu
IMETAFSIRIWA NA PR. FILBERT J. MWAGNA, APM DIRECTOR – STU 2
[Type here]

unatambua heshima ya utu ikiwa kila mtu atampenda na kutumikia


wengine. Ili kuunga mkono tafakari hii, tunaweza kufikiria maneno ya
Paulo katika 2 Wakorintho 12: 9-10: "Naye akaniambia, Neema yangu
yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia
udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. 10 Kwa
hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili
ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu."

1.3 Mabadiliko ya jina


Baada ya mapambano, Yakobo alipokea jina jipya: Israeli, ambalo
linamaanisha "mtu anayeshindana na Mungu." Mabadiliko haya ya
jina hayakuwa tu ishara ya mabadiliko yake ya kiroho lakini tamko la
kina la utambulisho wake na kusudi lake mbele za Mungu.
Jina Israeli liliashiria kukoma kwa uhakika wa mambo yake ya
zamani ya udanganyifu na ujanja ujanja (manipulation) na
kumtambulisha kwa uhalisia mpya wa baraka na wajibu kama
kiongozi wa watu waliochaguliwa na Mungu. Vivyo hivyo, watu
wenye ulemavu mara nyingi hutambuliwa/kuonekana (labeled) na
kutafsiriwa kwa mapungufu yao ya kimwili au kiakili. Hata hivyo,
machoni pa Mungu, wao ni wa thamani na wamejaliwa kwa kusudi
la Mungu. Mungu anaona uwezo wao! Mungu anaona uwezekano
wa kila mtu! Kama vile Yakobo alivyopokea jina jipya na
utambulisho mpya, Mungu huwawezesha watu wenye ulemavu
kutimiza wito wao na kushiriki kikamilifu katika jumuiya ya Ufalme.
Ushuhuda wao unapinga dhana zetu ndogo za uthamani na
heshima ya utu, kutualika kutambua mfano wa Mungu kwa kila mtu,
bila kujali uwezo au mapungufu yao. Tunaweza kupata msaada
kwa tafakari hii katika Isaya 43:1b: "Usiogope, maana nimekukomboa;
nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu." Maneno haya yanasisitiza
umuhimu wa jina lililotolewa na Mungu na utambulisho wa kipekee
wa kila mtu kabla yake.

1.4 Hali ya kimwili


Wakati wa mapambano, Jacob alijeruhiwa katika kiungo cha
nyonga [uvungu wa paja] na akawa mlemavu. Jeraha hili la kimwili
sio tu liliashiria maisha yake lakini pia liliashiria udhaifu wake wa
kibinadamu na utegemezi kwa Mungu. Licha ya jeraha lake la
IMETAFSIRIWA NA PR. FILBERT J. MWAGNA, APM DIRECTOR – STU 3
[Type here]

kimwili, Yakobo alivumilia mapambano na alikataa kuacha mpaka


apokee baraka za Mungu. Kidonda hiki kiligeuka kuwa alama ya
uzoefu wake na Mungu, ukumbusho wa daima wa hitaji lake
endelevu la nguvu na neema ya Mungu. Vivyo hivyo, watu wenye
ulemavu wanakabiliwa na changamoto za kila siku za kimwili Hii
mara nyingi hueleweka vibaya na jamii. Hata hivyo, ni muhimu
kutambua kwamba udhaifu wa kimwili haupunguzi thamani ya
ndani ya mtu wala utume ambao Mungu anao kwao. Badala yake,
Mungu hutumia hata udhaifu wetu kuonyesha utukufu na nguvu
zake. Watu wenye ulemavu ni Ushahidi ulio hai wa neema ya Mungu
ya ukombozi na tumaini tunalopata katika Kristo. Uwepo wao katika
jamii yetu unatupa changamoto kuwa kanisa linalojumuisha,
ambapo watu wote wanathaminiwa, kuheshimiwa, na kuwezeshwa
kuchangia kulingana na vipawa na uwezo wao. Kifungu kutoka 1
Wakorintho 12: 22-26 kinatukumbusha umuhimu wa kila mshiriki wa
mwili wa Kristo, bila kujali hali yao ya kimwili: "22 Bali zaidi sana vile
viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi. 23 Na
vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa
heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana. 24 Kwa
maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; bali Mungu
ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima zaidi kile kiungo
kilichopungukiwa; 25 ili kusiwe na faraka katika mwili, bali viungo vitunzane kila
kiungo na mwenziwe. 26 Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia
nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho."

2. Kuingilia kati kwa Mungu: umuhimu wa Watu wenye Ulemavu


katika Biblia
Hadithi ya Yakobo sio tu inaonyesha mabadiliko ya mtu binafsi lakini
pia inatoa mwanga juu ya kuingilia kati kwa Mungu katika hadithi ya
kibiblia. Katika Maandiko yote, tunapata hadithi nyingi za watu
wenye ulemavu ambao wana jukumu muhimu katika historia na
Utume wa Mungu. Hapa kuna mifano mitatu ya jinsi Mungu
alivyowaandaa/wawezesha, kuwaita, na kuwajumuisha watu wenye
uwezekano katika uongozi wa misheni/utume!

2.1 Mungu Huwajumuisha Watu Wenye Uwezo katika Uongozi wa


Misheni/Utume

IMETAFSIRIWA NA PR. FILBERT J. MWAGNA, APM DIRECTOR – STU 4


[Type here]

Musa: Ingawa alikuwa na kigugumizi, Musa alichaguliwa na Mungu


kuwaongoza Waisraeli kutoka utumwani Misri. (Kutoka 3:10-12) Musa
alichaguliwa kuwa kiongozi wa watu wa Mungu.

Daudi: Licha ya ujana wake na kuonekana kuwa na kimo duni cha


mwili, Daudi alitiwa mafuta na Mungu kama mfalme wa Israeli na
akawa mmoja wa viongozi wakuu sana wa watu wa Mungu. (1
Samweli 16:11-13) Daudi alichaguliwa na Mungu kwa ajili ya utume
Wake!

Paulo: Hata ingawa alisumbuliwa na "mwiba katika mwili," Paulo


alitumiwa na Mungu kueneza Injili katika ulimwengu wote uliojulikana
(wakati huo). (2 Wakorintho 12:7-10). Paulo alichaguliwa na Mungu
kwa ajili ya utume wake!

2.2 Somo la kuingizwa pamoja katika Kristo


Mbali na mifano iliyotajwa, maisha ya Yesu mwenyewe ni ushuhuda
mkuu wa kuhusishwa pamoja na Uungu. Yesu aliwakaribisha na
kuwaponya watu wenye ulemavu, akituonyesha kwamba kila mtu ni
wa thamani machoni pa Mungu. Alifundisha kwamba katika jumuiya
ya Ufalme, hakuna tofauti kati ya watu wenye ulemavu au wasio na
ulemavu; Wote wanapendwa na kuthaminiwa na Mungu. (Marko
10:46-52). Wote ni wenye vipawa, wanaohitajika, na
wanaothaminiwa! Wote wana mchango muhimu wa kufanya ndani
ya Mwili wa Kristo!

3. Nafasi/Majukumu ya Watu wenye Ulemavu katika jamii ya imani


Hadithi za watu hawa na wengine wengi katika Biblia
zinatukumbusha kwamba Mungu haoni watu wenye ulemavu kuwa
hawana uwezo au hawajitoshelezi. Kinyume chake, Anawajumuisha
katika mpango Wake wa ukombozi na kuwapa majukumu muhimu
katika kazi Yake. Kama jumuiya ya imani, tunaitwa kufuata mfano wa
Mungu na kuthamini kikamilifu na kujumuisha watu wenye ulemavu
katika ibada yetu, huduma, na ushirika.

3.1 Changamoto za ushirikishwaji katika jumuiya ya imani

IMETAFSIRIWA NA PR. FILBERT J. MWAGNA, APM DIRECTOR – STU 5


[Type here]

Ingawa kuingizwa (katika utendaji) kwa Mungu ni mada kuu katika


Biblia, mara nyingi tunakabiliwa na changamoto katika jamii yetu ya
imani. Hii ndiyo sababu Huduma Wezeshi katika Sabato hii ni muhimu
sana! Huduma Wezeshi ina mikakati mitatu ya K 3 au kwa Kiingereza
ya A 3: Kuleta Uelewa (Awareness), Kukubalika (Acceptable), na
Kitendo/Kutenda (Action). Kwanza, tunahitaji kuwa na ufahamu wa
vizuizi vya kimwili, kihisia, na kiroho ambavyo vinaweza kuzuia ushiriki
kamili wa watu wenye ulemavu katika makanisa yetu. Pili, kupitia
neema ya Mungu, tunaweza kuwa na mabadiliko ya moyo na
mawazo ya kufikiri tofauti na kuwa na kukubalika. Kufikiria
uwezekano! Na tatu A ya mkakati wa Huduma Wezeshi ni Vitendo!
Kama wafuasi wa Kristo, tunaitwa kuwa mawakala wa mabadiliko na
kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kuhusishwa na Mungu na fursa sawa
kwa washiriki wote wa jamii yetu, bila kujali uwezo wao wa kimwili au
kiakili.

3.2 Masomo kwa safari yetu ya kiroho


Kama vile Yakobo, sisi sote tunakabiliwa na mapambano na
changamoto katika safari yetu ya kiroho. Ni katika nyakati za ugumu
mkubwa kwamba tumeumbwa na kubadilishwa na neema ya
Mungu. Mabadiliko ya Yakobo yanatukumbusha kwamba, bila kujali
kushindwa kwetu na udhaifu wetu, Mungu daima yuko tayari kutupa
utambulisho mpya na kusudi jipya katika kazi Yake. Safari ya Yakobo
inatufundisha kwamba mabadiliko ya tabia ya kweli huja kupitia
kukutana kwa karibu na Mungu. Lazima daima tutafute uwepo wa
Bwana katika maisha yetu, tukimruhusu Yeye kutubadilisha kutoka
ndani.

Hitimisho:
Kukabiliana kwa Yakobo na Mungu kumesababisha mabadiliko
makubwa ya tabia yake. Anatoka kwa mtu mwenye ubinafsi na
mdanganyifu hadi kiongozi wa kiroho, mtu anayetafuta mapenzi ya
Mungu katika mambo yote. Uzoefu katika Mto Yaboki ulimtengeneza
Yakobo na kumtayarisha kutimiza jukumu ambalo Mungu alimpa
kama baba wa makabila kumi na mawili ya Israeli. Kwa mujibu wa
hadithi ya Yakobo, tunakabiliwa na kuingizwa kwa Mungu katika

IMETAFSIRIWA NA PR. FILBERT J. MWAGNA, APM DIRECTOR – STU 6


[Type here]

ubinadamu wetu uliovunjika. Tufungue mioyo yetu na jamii zetu


kupokea na kuwathamini watu wote, ikiwa ni pamoja na wale wenye
ulemavu. Na tutambue kwamba kila mtu ameumbwa kwa mfano na
mfano wa Mungu na ameitwa kutimiza jukumu muhimu katika Ufalme
Wake. Hebu tuwe mawakala wa upendo, huruma, na haki, kujenga
jumuiya ya imani ya umoja ambapo kila mtu anaweza kustawi na
kuchangia kikamilifu kwa utukufu wa Mungu. Wote ni wenye vipawa,
wanahitajika, na wanathaminiwa! Kama vile Yakobo
alivyobadilishwa na kukutana kwake na Mungu, tunaweza kupata
msukumo na tumaini katika hadithi yake. Na tuwe jamii inayothamini
na kujumuisha watu wenye ulemavu, tukitambua kwamba wao pia
waliumbwa kwa mfano wa Mungu na kuwa na jukumu muhimu katika
mpango Wake wa ukombozi. Mfano wa Yakobo na kuingizwa kwa
Mungu katika Biblia kutuhamasisha kuwa mawakala wa mabadiliko
na upendo katika ulimwengu wetu, kukuza ujumuishaji na hadhi ya
watoto wote wa Mungu.

IMETAFSIRIWA NA PR. FILBERT J. MWAGNA, APM DIRECTOR – STU 7

You might also like