Professional Documents
Culture Documents
KIKUNDI KIDOGO
—NIA na ROHO MOJA
Musa L. Budodi
Oղe-Souɬ Audience Ӎinistry
Kagongwa, Kahama
+255-784-825-660
KIKUNDI KIDOGO—NIA na ROHO MOJA
UTANGULIZI
MWITO WETU
"Kristo hachagui malaika ambao kamwe hawajaanguka kuwa
wawakilishi wake, bali wanadamu, watu wenye hisia sawa na
zile za hao wanaotafuta kuwaokoa.” E. G. White, Tumaini la
Vizazi Vyote uk. 296.4
“Sote tumefungwa pamoja katika wando mkubwa wa
ubinadamu, na lo lote tunaloweza kufanya kuwanufaisha na
kuwainua wengine kutaakisi mibaraka kwetu wenyewe.
Sheria ya kutegemeana inafunga kila tabaka katika jamii.” E.
G. White, Wazee na Manabii uk. 534.4
—KIKUNDI KIDOGO—
KWA AJILI YA KRISTO NA KWA AJILI YA MAISHA YA
KIMWILI
Kwa kawaida, ili kufikia lengo kwa urahisi kunategemea si idadi kubwa
ya watu bali kikundi kidogo kilichonuia na kuazimia, wanaoweza
kukutana toka katika maeneo walikotawanyika. Mungu ndiye
huanzisha hatua, na kikundi kidogo huwa hai pale Roho Mtakatifu
anapofanya kazi ndani ya kila roho inayowiwa hivyo.
‘Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure.
Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure’ (Zaburi
127:1). ‘Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho
yangu, asema Bwana wa majeshi.’ (Zekaria 4:6).
‘Uundaji wa vikundi vidogo kama msingi wa kuwafikia
wengine umeonyeshwa kwangu na Yule asiyekosea.’—E. G.
White, Testimonies vol. 7, uk. 21, 22
‘Ni muhimu kuwa kazi hii itafanyika kwa shughuli za watu
binafsi. Ndivyo Kristo alivyofanya. Kazi yake kubwa ilifanyika
kwa njia ya mjadala wa ana kwa ana. Aliheshimu sana
mazungumzo yake pekee na mtu mmoja mmoja. Mara nyingi
kupitia kwa huyu mmoja ujumbe ulienezwa kwa maelfu.’ E.
G. White, Vielelezo vya Mafundisho ya Kristo uk. 229.1
JISHUGHULISHE
Mifano ya Maagano
Agano la hakikisho: (pendo lisilo na masharti—Agape); mfano,
‘hakuna chochote kitakachonifanya nikuchukie, naweza nisikubaliane
na matendo yako lakini nitakupenda kama mtu na kufanya yote
niwezayo ili kukunyanyua katika pendo la Kristo.’
Mtazamo wa kikristo
Mitazamo yetu sisi wanadamu iko mbali mno na mtazamo wa
Mungu. Tuna kawaida ya kurekodi kile tukihisicho, tukionacho. Kwa
kutazama au kusikia, badala ya kujenga taswira, wengi ni wepesi
kurekodi kile wakionacho au wakisikiacho pasipo kwanza kujenga
picha mawazoni. Watu hawa ni wepesi kuchora msitari wa hitimisho.
Mkao usiofaa wa akili na mawazo hupelekea mtu kuwa hivyo
Mtu haamini kama anaweza kufanya vitu vikubwa kwa kujiangalia
katika muonekano mmoja tu lakini ni jinsi gani mtu anakuja kuwa mtu
wa tofauti kabisa na vile alivyokuwa hapo awali! Lakini pia watu
wanavyokutazama wanaona kama vile hauwezi kufanya vitu vikubwa,
hauwezi kuwa vile, hauwezi kuwa pale; je, vipi tukiondoa dhana hiyo
ya kujitazama au kumtazama mtu na kuhitimisha kuwa hawezi kitu?
Mtu hapimwi kwa rangi, kabila, kimo, umri, kiwango cha elimu, cheo,
hadhi bali kwa maudhui ya maumbile ya tabia. Akili ndicho kipimo
kwa mtu. Wengi tunaongozwa na uraibu wa matazamio (uraibu wa
hatima—Destination addiction). Kwamba fulani tukimweka hapo
anaweza na fulani hawezi! Ipo mifano ya kushangaza ya wale ambao
waliwahi kutazamwa katika mtazamo uliozoeleka lakini walikuja
kuwa tofauti zaidi ya vile walivyotazamiwa.
Haidhuru watu wakuangalie na kukutazamia kwa namna fulani;
tunavyokuona sisi wanadamu wenzako ni tofauti na anavyokuona
aliyekuumba. Mungu ni Mungu tu. Hajali umri, uzoefu, jinsia au ya
nyuma, haishangazi humbarikia ye yote yule. Mkristo halisi
humtazama kila mtu kama: Sura ya Mungu: Mwanadamu ameumbwa
kwa mfano na sura ya Mungu (Mwanzo 1:26,27; 5:1).
‘Ijapokuwa aina ya watu iwe na hali mbaya kiasi gani na hata
iwapo watu wanawadharau na kuwatenga mbali, hawawezi
kuwa chini kiasi ambacho Mungu hawaangalii kwa upendo.’
E. G. White, Vielelezo vya Mafundisho ya Kristo uk. 225.3
KIKUNDI KIDOGO—NIA na ROHO MOJA
THAMANI YA KUJITAWALA
Unapokuwa kiongozi au mtu mwenye kipawa chako unajiweka katika
nafasi ya kuonekana na wengi, na kujaribiwa ni rahisi mno. Wengi
walio maarufu wanashindwa kujitawala hasira zao, misisimko yao n.k
Soma Yakobo 1:12–16 na 1 korintho 10:13
Kaa chini na fikiria udhaifu wako uko wapi. Kuujua udhaifu wako ni
salama. Ukijijua itakuwa rahisi kwako kuishi na watu. Daima
KIKUNDI KIDOGO—NIA na ROHO MOJA
Suala hili linahitaji maamuzi mazito. Kwa sababu ya uzito wa kazi, sharti
kuna muda mnapaswa kuwa peke yenu ili kuchakata wajibu wenu,
kuhuisha roho zenu, akili na mwili.
“Lakini habari zake zikazidi kuenea, wakakutanika makutano
mengi wamsikilize na kuponywa magonjwa yao. Lakini Yeye
alikuwa akijiepua akaenda mahali pasipokuwa na watu,
akaomba.” Luka 5:15, 16