You are on page 1of 12

JILINDE NA

CHOYO

Somo la 9 kwa ajili ya Machi 4, 2023


“Akawaambia, Angalieni, jilindeni na
choyo, maana uzima wa mtu haumo
katika wingi wa vitu vyake alivyo
navyo”
(Luka 12:15)
Kutamani ni kutaka sana kitu fulani.
You
Amri ya kumi inaonya juu ya kutamani vitu visivyo shall not
vyetu. Paulo alisema tamaa ni ibada ya sanamu, kwa covet
hiyo watu wenye choyo wanavunja amri ya pili vilevile
(Kol. 3:5).
Hebu tujifunze namna choyo ilivyoanza na visa vya
watu walioshikiliwa nayo na kujifunza namna ya
kuishinda.

Chanzo cha Tamaa


Mifano ya tamaa:
Akani
Yuda
Anania and Sapphira
Namna ya kushinda tamaa
CHANZ
O CHA
TAMA
A
“Nawe ulisema moyoni mwako: ‘Nitapanda mpaka mbinguni. Nitakiinua kiti change juu
kuliko nyota za Mungu. Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, katika pande za mwisho
kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu. Nitafanana na yeye Aliye juu.’” (Isaya 14:13-
14)

Mungu alivipa viumbe vyake kila vilichohitaji ili


kuwa na furaha. Hata hivyo, hitaji la kuinuliwa juu
ya Mungu lilikua kwa namna isiyoelezeka katika
moyo wa Lusifa.
Lusifa alitamani ibada ambayo ni Muumbaji
pekee anaweza kupewa. Hata alitamani enzi ya
Mungu (Isa. 14:12-14).

Baadaye, alimdanganya Hawa kutenda dhambi ile


ile, na kutamani kile Mungu alichokataza: mti wa
ujuzi wa mema na mabaya (Mwa. 3:6).
Hivi ndivyo tamaa ilikuja kuwa sehemu ya hali yetu
ya dhambi.
MIFAN
O YA T
AM AA
“Nilipoona katika nyara joho nzuri ya Babeli, na
shekeli mia mbili za fedha, na kabari ya dhahabu

AKANI
nikavitamani nikavitwaa […]” (Yoshua 7:21)

Neno la Kiebrania châmad au chemdâh (kutamani)


halionyeshi kitu kibaya. Linaweza kutafsiriwa kama,
kizuri, chema, bora, kikarimu, kipendwacho,
kifurahishacho na kitamanishwacho.
Neno hili lilitumiwa kumtambulisha Danieli kama
“aliyependwa sana” (Dan. 9:23) au Yesu kama
“Kinachotamaniwa ” (Hag. 2:7).
Shida ni kutamani kisichokuwa chetu, kama Akani
alivyofanya.
Tamaa ya Akani ilikuwa uharibufu wake mwenyewe,
na likaidhuru familia yake yote. Watu 36 walikufa
(Yos. 7:5, 10-11, 15, 24-26).
“akasema, ‘Ni nini mtakachonipa,

YUDA nami nitamsaliti kwenu?’


Wakampimia vipande thelathini vya
fedha.” (Matthayo 26:15)

Yuda alitamani kitu kilichokuwa chema: kuwa karibu na Yesu,


kuwa kama Yeye, kuhubiri habari njema ya wokovu…

Hata hivyo, kamwe hakuweza kuishinda choyo.


Choyo kilimpelekea kuiba, kusaliti, na kujiua
(Yoh. 12:6; Mat. 26:15; 27:5).

Tamaa yake ilimpelekea kuvunja Amri zingine tatu


kwa uchache: Ibada ya sanamu/choyo [pili], Kuua
[sita], na kuiba [nane].
Yuda hakustahili mwisho wake. Kama sisi, angaliweza kuikubali
nguvu ya Yesu ambayo ingeweza kubadilisha moyo wake. Kisa
chake kingalikuwa tofauti.
ANANIA NA SAFIRA
“akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe
naye akijua haya,akaleta fung moja akaliweka
miguuni pa mitume.” (Matendo 5:2)

Anania na Safiira walitiwa moyo na mfano wa Barbana


(Matendo 4:36-37), kwa hiyo waliahidi kuuza ardhi yao
na kumpa Mungu kiasi chote.
Hicho kilikuwa kitu kizuri, lakini kila kitu kilibadilika
baada ya kupokea fedha. Wakafikiri kuwa kiasi kile
kilikuwa kikubwa mno kukitoa, wakaamua kubakisha
sehemu ya mauzo. Walifikiri kwamba hakuna atakayejua
kiasi halisi walichopata, na wangaliheshimiwa vilevile
kama Barnaba.
Dhambi hufunika mafikara yetu. Mungu angalijuwa kiasi
walichokipata. Hakuna anayeweza kumwibia Mungu na
kutoadhibiwa. Tamaa yao ilikuwa ndio uangamivu wao.
KUISH
I NDA T
AMAA
/CHO
YO
“Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa. Kwa maana hatukuja
na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu. Ila tukiwa na chakula na nguo
tutaridhika na vitu hivyo.” (1 Timotheo 6:6-8)

Je tunaweza kufanya nini tunapojisikia kujaribiwa na dhambi ya kutamani?

Omba ili Mungu


Kumbuka Mungu yu
abadilishe mawazo na
aweza kutuweka huru ili
hisia zetu, ili tusijaribiwe
tusijaribiwe
navyo (Luk. 11:4; 2Pet.
(1Kor. 10:13)
2:9)

Kumbuka ushauri Mungu


Amua kumwamini Mungu aliotupa katika Neno
na kuridhika na kila lake: “Neno lako
Alichotupatia nimelihifadhi moyoni
(1Tim. 6:6-8; Mith. 30:7- mwangu,ili nisikutende
9) dhambi.”
(Zab. 119:11)
“Ikiwa tutaruhusu mawazo kudumu katika
Kristo na ulimwengu wa mbinguni, tunaweza
kupata msukumo wa nguvu na kusaidia
katika kupigana vita za Bwana. Kiburi na
upendo wa dunia vitapoteza nguvu
tunavyotafakari utukufu wa ile nchi nzuri
itakayo kuwa nyumbani hivi punde. Kando ya
uzuri wa Kristo, vivutiavyo hapa duniani
vitaonekana kuwa na thamni kidogo.”
E. G. W. (Shuhuda kwa Kanisa, sura. 6, p. 57)

You might also like