You are on page 1of 6

ANGUKO

UTANGULIZI

Somo hili ni muhimu kwa kuwa ni vizuri kumjua adui yetu kama alivyo. Si kutaka
kumwinua ila ni kumjua na kujua mamlaka yetu dhidi yake. Wengi wetu tunapicha
tofauti za shetani mawazoni mwetu. Wengine tukidhani ni jitu jeusi lenye mkia, wengine
tukidhani ana jicho moja, mrefu sana nk.

LUCIPHER

1. Kabla hajaanguka alikuwa ni mmoja wa Malaika wakuu.


2. Alikuwa Malaika anayeongoza kundi la kumsifu Mungu, kwa hivyo alikuwa mbele
ya uso wa Mungu kila siku.
3. Aliumbwa vizuri sana (aliwekewa madini ya thamani ndani yake)na
4. aliwekewa ndani yake kila chombo kinachohitajika kwa ajili ya muziki –matari,
vinubi, NK.

Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako,
akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti
samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako
ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari. Wewe
ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya
mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. Taz EZE.
28:13, 14

ILIVYOKUWA

 Kutokana na uzuri wake, kiburi kiliota ndani yake.


 Akatamani na yeye awe anaimbiwa na kusifiwa kama Mungu, akatamani awe
kama Mungu na aketi katika kiti cha enzi.
 Mungu aliliona wazo alililokuwa nalo shetani ndani yake kwa hivyo akaamuru
afukuzwe.
Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu
ulipoonekana ndani yako. Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza
udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa
nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza,
Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto. Moyo wako uliinuka
kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza
wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.
Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi
patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza,
nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote
wakutazamao. (EZE. 28:15-18 SUV)

ALIVYOANGUKA.

Hapa tunaiona dhambi yake ya kutaka kuwa kama Mungu.

Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi
ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! Nawe ulisema moyoni mwako,
Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami
nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita
vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. Lakini utashushwa mpaka kuzimu;
Mpaka pande za mwisho za shimo. (ISA. 14:12-15

Dhambi hii hii ndiyo aliyoiingiza kwa binadamu pale alipomuambia Eva kuwa akila
tunda atakuwa kama Mungu.

ALIVYOTUPWA

 Hakukubali kirahisi kutoka mbinguni, kwa hivyo alianzisha vita.


 Kutokana na kutokuwa na uzoefu wa kivita (kumbuka alikuwa ni Malaika wa sifa
na ilihali michaeli alikuwa Malaika wa vita) alitupwa na mahali pake
pakaondolewa mbinguni.
 Alitupwa pamoja na Malaika wake waliojaribu kumtetea (theluthi moja ya
Malaika)

Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka
naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao
hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani,
aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na
malaika zake wakatupwa pamoja naye. (UFU. 12:7-9 SUV)

KISASI

 Alijipanga kulipiza kisasi kwa Mungu kwa kupitia watu wake aliowapenda.
 Mungu aliruhusu kwa kuwa anajua kuwa una uwezo wa kumshinda katika
jina la Yesu.

Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule
aliyemzaa mtoto mwanamume. Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake
afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na
ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari. (UFU. 12:13, 17
SUV)

Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya


kila kabila na jamaa na lugha na taifa. (UFU. 13:7 SUV)

Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA
Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda
ya miti yote ya bustani? Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa
maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa
macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. (MWA. 3:1, 4, 5 SUV)

Amepanga mikakati ya kumuangusha binadamu.

Kutokana na mikakati yake na pia Kutokana na aina ya Malaika alioanguka nao,


amewagawa katika makundi Tisa.

I. Kerubi
II. Serafi
III. Wenye enzi
IV. Wenye nguvu
V. Falme… Dan 10
VI. Watawala
VII. Wenye mamlaka…
VIII. Wakuu wa giza…
IX. Majeshi ya pepo wabaya

Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme
na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika
ulimwengu wa roho. (EFE. 6:12 SUV)

MWISHO WAKE

Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, Na sauti ya vinanda vyako; Funza


wametandazwa chini yako, Na vidudu vinakufunika. (ISA. 14:11 SUV)

Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu
ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate
kukutazama. Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia
unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza,
nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao.
(EZE. 28:17-18 SUV)

Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo
yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na
milele. (UFU. 20:10 SUV)

Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye
kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza,
asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi. Nanyi mtawakanyaga
waovu; maana watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu; katika siku ile
niifanyayo, asema BWANA wa majeshi. (MAL. 4:1, 3)

MILANGO MIKUBWA.

1. Mti wa Ukoo/Familia
2. Maumivu ya Ndani
3. Kutokusamehe
4. Hofu
5. Dhambi za Mazoea.
6. Uongo tunaouamini/ MINDSET/UFAHAMU

MWISHO.

Sisi wote tulio katika Kristo Yesu ni washindi hata kabla ya kupigana.

Tunatakiwa kuzingatia yafuatayo.

A. Kudumu katika wokovu wetu na mahusiano yetu na Bwana Yesu

Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni


mwaminifu; (EBR. 10:23 SUV)

B. Kubadilisha na kutawala Fikira/Nia/Ufahamu.

“Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana
silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha
ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu
ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;” 2 Kor 10:3-5 SUV

“Do not be conformed to this world (this age), [fashioned after and adapted to
its external, superficial customs], but be transformed (changed) by the [entire]
renewal of your mind [by its new ideals and its new attitude], so that you may
prove [for yourselves] what is the good and acceptable and perfect will of
God, even the thing which is good and acceptable and perfect [in His sight for
you].” Romans 12:2 AMPC

C. Kuvaa silaha za Mungu kwa kusoma Neno la Mungu na kuliishi Neno.

Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya
uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni, hali mmejifunga kweli
viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya
amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima
mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na
upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila
wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu
wote; (EFE. 6:13-18

A. Tumia AMRI na mamlaka uliyopewa ili kumkanyaga na kumpinga shetani

Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala
hakuna kitu kitakachowadhuru.

Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu
yameandikwa mbinguni. (LK. 10:19, 20 SUV)

Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye
aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. (1 YOH. 4:4

Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana
wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. [Amina.] (RUM. 16:20

Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao;


ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. (UFU. 12:11

Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja


mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme; na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi, na
yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunja-vunja gari la vita, na yeye
achukuliwaye ndani yake; na kwa wewe nitawavunja-vunja mwanamume na
mwanamke; na kwa wewe nitawavunja-vunja mzee na mtoto; na kwa wewe
nitawavunja-vunja kijana mwanamume na kijana mwanamke; na kwa wewe
nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe nitamvunja-vunja
mkulima na jozi yake ya ng’ombe; na kwa wewe nitawavunja-vunja maliwali na
maakida. (YER. 51:20-23.

You might also like