You are on page 1of 18

SOMO 13: FUNGUO YA NYAKATI ZA MWISHO

Katika kitabu cha Daniel sura ya pili na sura ya saba inatoa picha ya falme kuu zitakazo tawala
dunia yote zitakazotokea hadi mwisho wa wakati. Katika Daniel sura ya pili ametumia kielelezo
cha sanamu na katika Daniel sura ya saba anatumia kielelezo cha wanyama. Na kwa mkristo
yeyote yule anayetamani kwenda mbinguni ni lazima afahamu unabii huu katika maisha yake.
Na kabla hujaendelea na somo hili ni vyema usome Daniel sura ya pili yote na saba yote ili
kuelewa vizuri somo hili vyema.

Katika kitabu cha ufunuo Ufunuo 1:3 imeandikwa Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya
unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu. Kwa hiyo ni
wajibu wa kila mmoja wetu kusoma na kufahamu unabii huu. Hebu tuangalie mafungu kadhaa
katika biblia takaifu juu ya swala hili muhimu sana katika wokovu wetu.

Daniel 2:31-35
31 Wewe, Ee Mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana. Sanamu hii, iliyokuwa kubwa
sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa lenye
kutisha. 32 Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono
yake ni ya fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba; 33 miguu yake ni ya chuma; na nyayo
za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo. 34 Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa
bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na
udongo, likaivunja vipande vipande. 35 Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile
fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya
kupepetea wakati wa hari; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe
lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.

Daniel 7:2-10
2 Danieli akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo
nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa. 3 Ndipo wanyama wakubwa wanne
wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali. 4 Wa kwanza alikuwa kama simba, naye
alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa
katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa
kibinadamu. 5 Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande
mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake;
wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele. 6 Kisha nikatazama, na kumbe!
Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya
ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka. 7 Baadaye nikaona katika
njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo
mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande,
na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa
kwanza, naye alikuwa na pembe kumi. 8 Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe
nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za
kwanza zikang'olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya
mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu. 9 Nikatazama hata viti vya enzi
vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji,
na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na
gurudumu zake moto uwakao.
10 Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi
mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.

Ni nini maana ya wanyama hawa?


Katika Daniel mbili na danieli saba inatuonyesha falme kuu nne zitakazotokea duniani ambazo
zitakuwa na uwezo wa kuitawala dunia yote. Na baada ya falme hizi hazitatokea tena falme
zenye uwezo mkubwa kama falme hizi. Hebu tuchukue muda kuziangalia moja baada ya moja.
Kitabu cha Daniel, ni kitabu ambacho kinashughulikia unabii, kuanzia karne ya sita kabla
hajazaliwa Yesu hadi wakati wa leo. Kutafsiri mfano katika Biblia hautegemei ujuzi wa mtu.
Unabii ni historia iliyoandikwa kabla ya mambo kutendeka. Biblia yenyewe inatupatia
mwelekeo na ufahamu.
2 Pet. 1:20-21
20 Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama
apendavyo mtu fulani tu. 21 Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu;
bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

N: B. Mnyama katika unabii anawakilisha mfalme au ufalme.


Dan. 7:17, 23:
17 Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani. 23 Akanena
hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme
zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande.

Bahari au maji huwakilisha jamaa na makutano na mataifa na lugha.


Ufunuo 17:15
15 Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na
mataifa na lugha.

Isaya 8:7
7 basi sasa angalia; Bwana aleta juu yao maji ya huo Mto, yenye nguvu, mengi sana, nayo ni
mfalme wa Ashuru na utukufu wake wote; naye atakuja, na kupita juu ya mifereji yake yote,
atafurika juu ya kingo zake zote;

Katika Daniel 7 nabii anaziona falme za dunia zikiwakilishwa na Wanyama Maelezo sawa na
hayo tunayapata katika Dan. 2:27-45 ambapo kila kiungo kinaeleza mwelekeo wa mwanadamu
katika siku za usoni.

Hebu tujifunze wanyama hawa na hizi sehemu za sanamu na maana yake.

1. SIMBA (608-538 K.K)

Wa kwanza alikuwa kama simba... Dan. 7:4 na Dan.


2:37-38. Simba anawakilisha ufalme wa Babeli uliotawala
dunia miaka ya 608-538 kabla Yesu kuzaliwa, utawala wa
pekee siku za Danieli. Sanamu ya Simba mwenye mabawa
imehifadhiwa katika jumba la hifadhi la Pergamon mjini
Berlin, Ujerumani.

2. DUBU
Daniel 7:5 Na tazama, mnyama mwingine, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja,
na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake;
wakamwambia mnyama huyu hivi; inuka ule nyama tele.
Mnyama huyu ni sawa na maelezo ya mikono na kifua cha shaba cha Dan. 2:32-39. Mnyama
huyu anawakilisha falme mbili za waamedi na waajemi waliotawala baada ya Babeli miaka ya
538-331 kabla ya kuzaliwa Yesu. Waamedi ndio
waliotangulia kutawala kisha badaaye Waajemi. Mikono
miwili katika Daniel 2 huwakilisha umedi na uajemi na
mkono mmoja kuwa juu ya mwingine ni kuonyesha kuwa
ufame mmoja ulikuwa na nguvu kuliko mwingine na
kuinuliwa mguu wa upande mmoja juu katika Daniel 7.
Upande mmoja ulikuwa na nguvu kuliko mwingine.
Mbavu tatu zinawakilisha mataifa matatu ya Babeli, Lydia
na Misri yaliyopigwa na Waamedi na Waajemi.

3. CHUI

Danieli 7:6 Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama


mwingine, kama Chui, naye juu ya mgongo wake
alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo
alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka. Mnyama
huyu ni sawa na yule wa Danieli 2:32- 39. Ulikuwa ufalme
wa Wayunani ukiongozwa na Alexander
uliowaangusha Waajemi na kutawala miaka ya 331-168
kabla ya Yesu kuzaliwa. Alexander alifariki June 13, 323
B.C, ufalme wake uligawanyika katika sehemu nne (Falme
za Diadoki) zinazowakilishwa na vichwa vinne.
Sehemu hizi zilikuwa kama ifuatavyo:-

a) Ufalme wa Ptolemy- ulitawala (Misri, Palestina na Shamu ya kusini)-KUSINI


b) Ufalme wa Lysimichas ulitawala (Thrakia na sehemu ya Asia ndogo)-KASKAZINI
c) Ufalme wa Cassander- ulitawala (Makedonia na U giriki)-MAGHARIBI
d) Ufalme wa Seleucus-ulitawala (Asia, Ashuru, Shamu hata India)-MASHARIKI

4. MNYAMA WA NNE

Daniel 7:7 Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na


tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye
nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno
ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande
vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na
umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza,
naye alikuwa na pembe kumi. Mnyama huyu ni sawa
na yule wa Daniel. 2:33.
Ufalme huu wa nne uliokuja baada wa ule wa wayunani
ni ufalme wa Rumi uliotawala kuanzia mwaka wa 168
kabla ya kuzaliwa Yesu, hadi 476 baada ya kuzaliwa Yesu. Mnyama huyu alikuwa tofauti sana na
wale waliomtangulia hivi kwamba Danieli alishindwa kueleza mfano wake. Baada ya ufalme
huu wa nne wataondoka wafalme kumi ni katika Daniel 7 wanawakilishwa na zile pembe
kumi na katika Daniel 2 wanawakilishwa na vidole kumi. Katika Daniel 7:7,24 Biblia inasema
7 Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha,
mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana;
alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake
lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi, 24 Na habari za zile
pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya
hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.
Tangu Rumi ilipoangushwa mwaka 476 baada ya Yesu kuzaliwa yalitokea mataifa kumi
yaliyokuwa yanayowakilishwa na vidole kumi katika Daniel 2 na pembe kumi katika Daniel 7 na
haya mataifa ni mataifa kumi ni ya ulaya ya leo. Mataifa haya ni:-
a) Ujerumani-Alaman
b) Ufaransa-Frank
c) Uingereza-Anglo saxon
d) Uswizi-Burgadian
e) Uispania-Visigoth
f) Ureno-Suev
g) Utaliano-Lombard
h) Heruli
i) Vandals
j) Ostrogoths.

P EMBE NDOGO
Katika Danieli 7:8 inatueleza
tena kitu cha kushangaza
kinachohusiana na huyu
mnyama wa nne.
Nikaziangalia sana pembe
zake, na tazama, pembe
nyingine ikazuka kati yao,
nayo ilikuwa ndogo, ambayo
mbele yake pembe tatu
katika zile za kwanza
zikangolewa kabisa; na
tazama, katika pembe hiyo
mlikuwa na macho kama ya
mwanadamu, na kinywa
kilichokuwa kikinena
maneno makuu.
Alama tofauti za
kuitambua pembe hii
ndogo:
1. Ilizuka kati ya zile pembe (falme) kumi, na wakati alipoinuka kutawala, pembe tatu
zilingolewa na akachukua nafasi yao. Yaani mataifa yaliyo ngolewa ni Heruli, Vandals
na Ostrogoths.
2. Katika Dan. 7:24 tunaambiwa pembe ndogo inazuka baada ya zile kumi. Katika historia
yote ni ufalme mmoja tu unaotimiza masharti haya katika Rumi yenyewe mwaka wa 476
baada ya kuzaliwa Yesu. Upapa, serikali ilioongozwa na mtu mmoja chini ya kanisa
katoliki; ulisimamishwa/ulianzishwa. Katika kuinuliwa kwake, falme tatu za Haruli,
Vandals na Ostrogoths ziliangushwa. Taifa la Heruli liliondolewa kwa njia ya vita na
upapa mwaka 493 kwa sababu ya kutokukubaliana na matakwa yake. Mwaka 534 taifa la
Vandals lilipigwa na kusambalatishwa kabisa na upapa na mpaka hivi leo halipo tena na
ndipo mwaka 538 Ostrogoths ilingolewa kabisa. Na ndipo unabii wa kungoa pembe tatu
ulikamilika na upapa ukamiliki.

Kwa amri ya Justinian (Codex Justinianus), mfalme wa Rumi ya mashariki, katika


mwaka wa 533 K.K, Askofu wa Roma alifanywa kuwa kiongozi wa makanisa yote ya
ukristo na Ostrogoths ni taifa lililokuwa wapinzani wa mwisho kungolewa kabisa
mwaka wa 538 na kufukuzwa kutoka Rumi na Jemerali Balisarius. Mwaka huo ndipo
Rumi ya upapa ilithibitishwa kuwa serikali kwa wakati uliotabiriwa.

3. Katika Dan. 7:25 tunasoma naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu, maana
yake ni mateso makubwa ya wakristo. Yeyote aliye na ufahamu katika historia,
atafahamu ya kwamba maelezo haya yanaulenga Upapa. Mateso makali dhidi ya wakristo
wakati wa zama za giza (Kuwahoji watu kuhusu imani yao, kuwachoma wazushi, vita
vya kidini) haya yote yanajulikana na yamo katika kurasa za historia.

4. Tunazidi kusoma: ataazimu kubadili majira na sheria... Ni dhahiri ya kwamba


Upapa umebadilisha amri kumi za Mungu. Katika Katakisimu ya Katoliki, utawala wa
Upapa umebadilisha sheria ya pili inayopiga marufuku uabudu sanamu. Pia, Upapa
umebadilisha sheria ya nne, ya utunzaji wa Sabato, iliyo sheria ya pekee kuhusu
Wakati, kwa kuifanya Jumapili siku ya kwanza ya juma, kuwa siku ya kupumzika
badala ya siku ya saba ya juma
2 Wathesalonike 2:3-4
3 Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule
ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; 4 yule mpingamizi,
ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe
kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.

Zaburi 94:20
20 Je! Kiti cha udhalimu kishirikiane nawe, Kitungacho madhara kwa njia ya sheria?

Walibadilisha wakati wa kuabudu. Wakaanzisha siku ya kuabudu isiyo ya kweli;


badala ya siku ya Saba ya juma yaani jumamosi, Sabato isiyobadilika tangu mwanzo
ilyotunzwa na Kristo, Mitume na kizazi chote kilichotangulia, ambayo pia ni miongoni
mwa amri kumi za Mungu wetu aliye hai. Hebu tuchunguze kidogo.
Kutoka 31:13, 16-17
13 Kisha, nena wewe na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika Sabato
zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate
kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana niwatakasaye ninyi. 14 Basi mtaishika hiyo Sabato;
kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa
kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.
15 Kazi itafanywa siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, takatifu
kwa Bwana; kila mtu atakayefanya kazi yo yote katika siku ya Sabato, hakika yake
atauawa. 16 Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika Sabato, kuiangalia sana hiyo
Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele. 17 Ni ishara kati ya mimi na wana
wa Israeli milele; kwani kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa
siku ya saba na kupumzika. 18 Hapo Bwana alipokuwa amekwisha zungumza na Musa
katika mlima wa Sinai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe,
zilizoandikwa kwa chanda cha Mungu.

Kutoka 20:8-11
8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10
lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote,
wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako,
wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11 Maana,
kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe
siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa

Ezekiel 20:12, 19-20


12 Tena naliwapa sabato zangu, ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa
mimi, Bwana, ndimi niwatakasaye.19 Mimi ni Bwana, Mungu wenu; endeni katika amri
zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzitenda; 20 zitakaseni sabato zangu; zitakuwa
ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.

Isaya 56:2-3, 6-7


2 Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye sabato asizivunje,
auzuiaye mkono wake usifanye uovu wo wote. 3 Wala mgeni, aambatanaye na Bwana,
asiseme hivi, Hakika yake Bwana atanitenga na watu wake; wala towashi asiseme, Mimi
ni mti mkavu. 4 Kwa maana Bwana awaambia hivi matowashi, wanaozishika sabato
zangu, na kuyachagua mambo yanipendezayo, na kulishika sana agano langu; 5
Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo
jema kuliko kuwa na wana na binti; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali. 6
Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana,
kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu;

Isaya 66:23
23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote
watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.

Waebrania 4:1-11
1 Basi, ikiwa ikaliko ahadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije
akaonekana ameikosa. 2 Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile
kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika
na imani ndani yao waliosikia. 3 Maana sisi tulioamini tunaingia katika raha ile; kama
vile alivyosema, Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu: 4
Kwa maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba,
akaziacha kazi zake zote; 5 na hapa napo, Hawataingia rahani mwangu. 6 Basi, kwa
kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa
habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao, 7 aweka tena siku fulani,
akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo; kama ilivyonenwa tangu
zamani, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu. 8 Maana kama
Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadaye. 9 Basi, imesalia raha ya
sabato kwa watu wa Mungu. 10 Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe
mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake. 11 Basi,
na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa
mfano uo huo wa kuasi.

Zaburi 89:35
35 Neno moja nimeliapa kwa utakatifu wangu, Hakika sitamwambia Daudi uongo,

Yakobo 2:10
10 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja,
amekosa juu ya yote.

Luka 4:14-16
14 Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi
zote za kandokando. 15 Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na
watu wote. 16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika
sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.

Mathayo 24:20
20 Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.

Matendo 13:42
42 Na walipokuwa wakitoka, wakawasihi waambiwe maneno haya sabato ya pili.

Siku ya kwanza ya juma (siku ya Jua), siku ya kuabudu jua, ikaanzishwa, kinyume
kabisa na amri ya Mungu. Mungu tayari alikuwa amewaonya watu wake wasije
wakaikubali hii siku bandia ya ibaada

Ufunuo 14:9-11
9 Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote
akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso
wake, au katika mkono wake,
10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo
kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na
kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo. 11 Na moshi wa
maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku,
hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake.
Ufunuo 16:2
2 Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na jipu baya,
bovu, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia
sanamu yake.

Ufunuo 19:20
20 Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya
hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile
chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa
wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;

Ezekieli 8:16-18
16 Akanileta mpaka ua wa ndani wa nyumba ya Bwana, na tazama, mlangoni pa hekalu
la Bwana, kati ya ukumbi na madhabahu, walikuwako watu kama ishirini na watano,
wamelipa kisogo hekalu la Bwana, na nyuso zao zimeelekea upande wa mashariki, nao
wanaliabudu jua, kwa kuuelekea upande wa mashariki. 17 Basi, akaniambia, Umeyaona
haya, Ee mwanadamu? Je! Ni jambo dogo sana kwa nyumba ya Yuda, wayafanye
machukizo wanayoyafanya hapa? Kwa maana wameijaza nchi hii udhalimu, tena
wamerejea nyuma ili kunikasirisha; na, tazama, wanaliweka tawi puani. 18 Kwa sababu
hiyo mimi nami nitatenda kwa ghadhabu; jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma,
na wajapolia masikioni mwangu kwa sauti kuu, sitawasikiliza.

5. Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu ya makufuru. Akafunua


kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana Jina Lake, na maskani yake, nao
wakaao mbinguni.

Ufunuo 13:5-6
5 Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa
kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili. 6 Akafunua kinywa chake amtukane Mungu,
na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.

Daniel 7:8, 25
8 Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo
ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe 25 Naye atanena maneno kinyume chake
Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili
majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu
wakati.

Daniel 8:25
25 Na kwa mashauri yake atafanikisha hila mkononi mwake; naye atajitukuza nafsi yake
moyoni mwake; naye atawaangamiza wengi katika hali yao ya salama; naye atasimama
kushindana naye aliye Mkuu wa wakuu; lakini atavunjika, bila kazi ya mikono.

2 Wathesalonike 2:3-4
3 Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule
ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; 4 yule mpingamizi,
ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe
kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.

Je, makufuru yanatafsiriwa vipi katika Biblia? Wakati mmoja Yesu Kristo akitafutiwa
makosa, wayahudi walisema ya kwamba amekufuru,

Yohona 10:33
33 Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa
kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu.

Luka 5:21
21 Basi, wale waandishi na Mafarisayo wakaanza kuhojiana wakisema, Ni nani huyu
asemaye maneno ya kukufuru? N'nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu
peke yake?

Aina haya ya makufuru mawili yanalenga upapa


Hapa duniani tunashikilia nafasi ya Mungu Mwenyezi, Encyc. Papa Leo wa kumi
na tatu tarehe, 20-6-1894).

Mara kwa mara papa huitwa Baba Mtakatifu Licha ya Yesu kukataa.
Mathayo 23:9
9 Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni.

Yohona 17:11
11 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja
kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama
sisi tulivyo.

6. Muda wa kutawala ufalme huu ni miaka 1260 na baadaye tena utainuka


Daniel 7:25
25 Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu
wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake
kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.

Ufunuo 12:14
14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake
nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati,
mbali na nyoka huyo.
Daniel 12:7
7 Nami nikamsikia yule mtu aliyevikwa nguo za kitani, aliyekuwa juu ya maji ya mto,
hapo alipoinua mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto kuelekea mbinguni;
akaapa kwa yeye aliye hai milele na milele, ya kwamba itakuwa wakati, na nyakati mbili,
na nusu wakati; tena watakapokuwa wamekwisha kuvunja nguvu za hao watu watakatifu,
ndipo mambo hayo yote yatakapotimizwa.
Kutawala kwa upapa kunatafsiriwa kuwa nyakati tatu na nusu wakati
Ufunuo 11:2
2 Na behewa iliyo nje ya hekalu uiache nje wala usiipime, kwa maana Mataifa
wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini na miwili. 3 Nami
nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na
sitini, hali wamevikwa magunia.

Ufunuo 13:5
5 Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa
kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.

Ufunuo 12:6
6 Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu,
ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.

Tafsiri ya Biblia inayoeleza siku moja = mwaka mmoja


Ezekiel 4:6
6 Tena utakapozitimiza hizo, utalala kwa ubavu wako wa kuume, nawe utauchukua uovu
wa nyumba ya Yuda; siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagizia.

Hesabu 14:34
34 Kwa hesabu ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arobaini kila siku
kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arobaini, nanyi mtakujua
kufarikana kwangu.

Ni dhahiri ya kwamba mafungu haya yote yanamaanisha miaka 1260 ambayo ndiye
muda wa utawala wa huu ufalme kabla hujapata jeraha. Wakati mmoja ni sawa na mwaka
mmoja. Mwezi halisi wa kiblia una siku 30 yaani mwaka una siku 360.
Mwanzo 7:11, 24
Mwanzo 8:4
Kuna siku 150 ambazo ni sawa na miezi 3 x miezi 12 = miezi 42, na miezi 42 x siku 30
ni sawa na siku 1260, au miaka halisi 1260 katika historia.

Tunafahamu kwamba muda uliyotabiriwa ulitimizwa kwa usahihi katika historia ya


upapa. Kuharibiwa kabisa kwa Ostrogoths mashariki mwa ufalme wa kirumi mwaka wa
538 B.K ambao waliokuwa wa mwisho kupinga utawala wa Kirumi, unaeleweka kuwa
ndio mwanzo wa utawala wa Upapa. Tukianza kuhesabu miaka 1260 kwanzia 538,
tunafika mwaka wa 1798.
Katika mwaka huu, Pope Pius VI alichukuliwa mateka na mfaranza Jenerali Berthier
baada ya vita vikuu vya Ufaransa. Ukatimia unabii wa: Mtu akichukua mateka,
atachukuliwa mateka Ufunuo 13:10. Tangu mwaka huo, upapa haujawahi kupata nguvu
sawa na zile za awali. Katiba ya kidemokrasia iliwekwa, na Rumi ikawa nchi huru, nguvu
za kisiasa za Rumi zikafika mwisho, ikatimia miaka 1260 sawa na ilivyotabiriwa katika
Biblia.
Katika Ufunuo 13:1-10 historia inaeleza jinsi nguvu za Upapa zilipoanza kutoka katika
ufalme wa Rumi ya kishenzi, jinzi ulivyotawala miaka 1260, na jinzi ulivyopata jeraha la
mauti. Katika Ufunuo 13:3 tunasoma: Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba
kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia
mnyama yule. Hii ni dhahiri kwamba utawala huu utakuwepo hadi Kristo atakaporudi
Daniel 7:21-22 inasema 21 Nikatazama, na pembe iyo hiyo ilifanya vita na watakatifu,
ikawashinda; 22 hata akaja huyo mzee wa siku, nao watakatifu wake Aliye juu wakapewa
hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme.

7. Wakati wa jeraha la mauti na kurejeshewa nguvu zake, mnyama mwingine


anatokea: Ufunuo 13:11-12
11 Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na
pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka. 12 Naye atumia uwezo
wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao
ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.13
Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi
mbele ya wanadamu. 14 Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile
alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia
sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi. 15 Akapewa kutia
pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya
hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. 16 Naye awafanya wote, wadogo
kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa
katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; 17 tena kwamba mtu
awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama
yule, au hesabu ya jina lake. 18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na
aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni
mia sita, sitini na sita.

Je, ni utawala upi unaoelezwa?


Ni taifa moja duniani linalotimiza masharti haya Marekani, mataifa mbali mbali
yalishikana na kuwa taifa moja miaka ya 1763-1800. Katika Ufunuo 13:11-18, anaanza
akiwa mpole lakini anamalizia kutawala dunia yote. Imetabiriwa kwamba Marekani
itamfanyia mnyama sanamu ambayo itawafanya wanadamu wote Kumsujudia yule
mnyama ambaye jeraha lake lilipona.

Daniel 3:5, 10-11, 14, 18, 28


5 wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na
zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu,
mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha.
10 Wewe, Ee mfalme, ulitoa amri ya kwamba kila mtu atakapoisikia sauti ya panda, na
filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, ni lazima
aanguke na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu; 11 na kila mtu asiyeanguka na kuabudu
atatupwa katika tanuru ya moto uwakao. 12 Wako Wayahudi kadha wa kadha
uliowaweka juu ya mambo ya wilaya ya Babeli, yaani, Shadraka, na Meshaki, na
Abednego; watu hawa, Ee mfalme, hawakukujali wewe; hawaitumikii miungu yako, wala
kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.14 Nebukadreza akajibu, akawaambia,
Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, je! Ni kwa makusudi hata hammtumikii
mungu wangu wala kuisujudia sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha? 18 Bali kama si
hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala
kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha. 28 Nebukadreza akanena, akasema,
Na ahimidiwe Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego; aliyemtuma malaika
wake, akawaokoa watumishi wake waliomtumaini, wakaligeuza neno la mfalme, na
kujitoa miili yao ili wasimtumikie mungu mwingine, wala kumwabudu, ila Mungu wao
wenyewe.

Ni vizuri kama utasoma kitabu cha Daniel sura yote ya tatu (Daniel 3:1-30)

Tunajifunza kuwa ibaada ya sanamu za watu na aina zingine sawa na hizo, ni kuabudu
sanamu kinyume na amri ya Pili ya Mwenyezi Mungu.

Kutoka 20:4-6
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni,
wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 5 Usivisujudie wala
kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu;
nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

Ibaada ya Jumapili ni ishara ya nguvu, alama ya mamlaka ya upapa, kujiwekea sheria


zao wenyewe (wao wenyewe wanakiri ya kuwa sheria hizi ni zao wala si za Mungu!).
Unabii unaeleza kwamba Marekani itaweka sheria ya kuabudu Jumapili, (alama ya
mnyama) kwa kusimamisha sanamu. Sanamu hii ni Uprotestanti ulioasi, mku-
sanyiko wa makanisa, utakaoshirikiana na serikali kuweka sheria za kidini. Dunia
yote tayari inatambua kuwa Jumapili siku ya kwanza ndio siku ya kupumzika ya siku ya
Ibada. Ni ujeuri wa Upapa kudhani ya kuwa wanaweza kubadilisha sheria kumi, amri za
Mungu. Hili ndilo litakalo kuwa swala la muhimu hivi karibuni, uamuzi wa kufa na
kupona

Ufunuo 13:14-15
14 Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya
mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule
mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi. 15 Akapewa kutia pumzi katika ile
sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote
wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.

Je atakubali kumtii Mungu au utakubali kushikiria mapokea ya watu (amri za watu)


Malaki 3:18-4:1
18 Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, na kati ya
yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.4:1 Kwa maana, angalieni, siku ile
inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu,
watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema Bwana wa majeshi; hata
haitawaachia shina wala tawi.

Ufunuo 16:2
2 Akaenda huyo wa kwanza, akakimimina kitasa chake juu ya nchi; pakawa na jipu baya,
bovu, juu ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia
sanamu yake.

Upapa unadai kwamba tendo la kuibadilisha Sabato hadi siku ya kwanza ya juma
ni lao na ni alama ya mamlaka yake katika mambo ya kidini (Daniel 7:25 25 Naye
atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye
juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati,
na nyakati mbili, na nusu wakati.)

Jumapili ilianzishwa na wakatoliki na unaweza kutetea utakatifu wake kwa misingi ya


kikatoliki pekee... Katika Biblia kwanzia Mwanzo hadi Ufunuo, hakuna fungu hata moja
linaloidhinisha kubadilishwa kwa Sabato kutoka siku ya saba ya juma hadi siku ya
kwanza. Catholic Press, Sidney, mnamo tarehe 25-8-1900

Tunaidhinisha Jumapili badala ya Jumamosi kwa sababu kanisa la katoliki lilitoa


utakatifu kutoka Jumamosi hadi Jumapili katika mkutano wa Laodekia mnamo
mwaka wa 364 AD. The Converts Catechism of Catholic Doctrine kutoka kwa P.
Geiermann, kazi ya Papa Pius wa kumi, tarehe 25-1-1910

Kanisa la Mungu lilifurahia kubadilisha sherehe kutoka siku ya Sabato hadi siku ya
Jumapili. Chapisho la katekisimu ya Roma Kurasa wa 247 baada ya uamuzi wa
kusanyiko la Trent kwa amri ya Papa Pius wa Tano.

Sabato, ambayo ni siku ya saba ya juma ilitunzwa na Kristo na mitume na


ilisherehekewa na wakristo wa zama hizo na ilisalia vivyo hivyo hadi ilipobadilishwa
katika Mkutano wa Laodekia. Kwanza kabisa, mkutano huu ulijadili swala la siku ya
Bwana kisha baadaye wakawazuia watu wasipumzike katika siku ya saba ya Juma, na
kwamba atakayefanya hivyo atalaaniwa. William Prynne, Mkufunzi maarufu
Mwingreza wa mambo ya kidini kutoka kwa kazi yake ya Dissertation on Lords Day,
ukurasa wa 32

Sabato, siku inayojulikana katika amri, ilibadilishwa na kuitwa siku ya Bwana. Neno
hili halijabadilika kwa mujibu wa maneno ya Yesu (Kwa sababu anasema mwenyewe
kuwa hakuja kubadilisha sheria, bali kuitimiza) bali kwa ajili ya mamlaka ya kanisa,
sheria hii imebadilika. Askofu Mkuu wa Rheggio, mahubiri ya tarehe 18-1-1562,
Mansi XXIII, ukurasa wa 526

Ni kanisa katoliki lililobadilisha siku ya kupumzika kutoka Jumamosi hadi


Jumapili siku ya kwanza ya Juma... Je, dunia yote inatii mamlaka ya kanisa lipi?
Waprotestanti wanadai ya kwamba wanatii Biblia ilhali kwa kuitunza siku ya Jumapili,
wanatii sheria ya kanisa Katoliki. Biblia inasema, Ikumbuke siku ya Sabato uitakase,
lakini kanisa katoliki linasema, La, uitunze na kuitakasa siku ya kwanza ya Juma na
dunia yote inatii mamlaka ya kikatoliki! Papa Enright tarehe 15-12-1889.

Ni dhahiri kuwa kanisa katoliki linadai kuwa ni wao waliofanya [kutoka Jumamosi
hadi Jumapili] mabadiliko... na kwamba kitendo hicho ni alama ya mamlaka yao ya
kidini. H.F. Thomas, Katibu Mkuu wa Kadinali Gibbons, mnamo tarehe 2-10-1895.

8. Hesabu ya mnyama, ambayo ni hesabu ya kibinadamu ambayo ni ishara nyingine ya


kumtambua huyu mnyama ni nani katika zama hizi ili tujiepushe naye.
Ufunuo 13:17-18
17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile,
yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. 18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye
aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na
hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
Mojawapo wa majina rasmi ya papa ni Vicarius Filii Dei. Tafsiri yake ni,
Mwakilishi wa Mwana wa Mungu. Katika kuwajibu maswali wasomaji wa jarida la
kikatoliki liitwalo Our Sunday Visitor, la tarehe 18-4-1915, tunasoma: Majina yaliopo
katika kofia ya Papa ni haya, Vicarius Filli Dei.

Jina hili ambalo ni makufuru, kwa sababu linajiinua juu ya Roho Mtakatifu

Yohana 14:26
26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina
langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

Yohana 16:12-15
12 Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa.
13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli
yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia
atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. 14 Yeye atanitukuza mimi, kwa
kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. 15 Na yote aliyo nayo Baba ni
yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni
habari.

Warumi 8:26
26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi
itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

Kwa mujibu wa Biblia mwakilishi wa Yesu hapa duniani ni Roho Mtakatifu

Katika kitabu cha ufunuo kimetuambia jina la huyu mnyama (upapa) ni nambari 666.
Katika kilatini baadhi ya herufi zinaweza kuhesabika. Huu ndiyo unabii unaotuonyesha ni
nani Mpinga Kristo (linganisha 2 Wathes. 2:3-12, 1 Yoh. 4:3, 2 Yoh. 7, Warumi 8:3).
Katika lugha ya Kigiriki, neno Mpinga Kristo linamaanisha mtu ajiwekaye katika
nafasi ya Masihi wa Bwana (anti = badala ya, na crio = kutiwa mafuta).
Kwa hivyo Mpinga Kristo ndiye anayedai kuwa mwakilishi wa Kristo hivi ndivyo
anavyodai Papa! Ikiwa Papa angelijitambulisha katika lugha ya agano jipya angalisema
hivi: Mimi ndimi Mpinga Kristo!

Yesu Kristo ndiye pekee yake kuhani Mkuu wa kweli katika hekalu la mbinguni baada
ya kupaa mbinguni. Waebrania 8:1-2 inasema 1 Basi, katika hayo tunayosema, neno
lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa
kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, 2 mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli,
ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu. Hapa Kristo hutuonyesha kila siku, jinsi
ya kufikia kiti cha neema cha Baba kupitia kwa damu yake. Yohana 14:6, 13-14 inasema
6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa
njia ya mimi. 13 Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba
atukuzwe ndani ya Mwana. 14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.

Na Warumi 8:34 inasema 34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye


aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume
wa Mungu; tena ndiye anayetuombea. Yesu Kristo aliye Kuhani wetu mkuu ndiye pekee
ambaye tunaweza kumwendea wakati wowote kwa njia ya maombi, pasipo kumwendea
mtu mwingine yeyote, bali kwa imani na tumaini katika damu ya Kristo.

Waebrania 4:14 inasema 14 Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu,
Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. 15 Kwa kuwa hamna
kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye
alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. 16 Basi na
tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia
wakati wa mahitaji.
Waebrania 5:1-10,
1 Maana kila kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wanadamu amewekwa kwa ajili ya
wanadamu katika mambo yamhusuyo Mungu, ili atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya
dhambi; 2 awezaye kuwachukulia kwa upole wao wasiojua na wenye kupotea, kwa kuwa
yeye mwenyewe yu katika hali ya udhaifu; 3 na kwa sababu hiyo imempasa, kama kwa
ajili ya watu, vivyo hivyo kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, kutoa dhabihu kwa ajili ya
dhambi. 4 Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na
Mungu, kama vile Haruni. 5 Vivyo hivyo Kristo naye hakujitukuza nafsi yake kufanywa
kuhani mkuu, lakini yeye aliyemwambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. 6
kama asemavyo mahali pengine, Ndiwe kuhani wa milele Kwa mfano wa Melkizedeki. 7
Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika
mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi
alivyokuwa mcha Mungu; 8 na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo
yaliyompata; 9 naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa
watu wote wanaomtii; 10 kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa
Melkizedeki.

Waebrania 7:25 inasema 25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao
wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.

Mathayo 6:6-15 inasema 6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na
ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako
aonaye sirini atakujazi. 7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa
mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa
mengi. 8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi
hamjamwomba. 9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe,
Ufalme wako uje, 10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. 11
Utupe leo riziki yetu. 12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni
wetu. 13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. Kwa kuwa ufalme ni
wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.

Hitimisho
Mafundisho kuwa twaweza kumwendea Kristo kupitia mtu fulani au kupitia kwa
watakatifu waliolala, yanawakilisha makufuru ya mnyama kinyume na Mungu na hekalu
lake.

You might also like