You are on page 1of 5

NENO LA FARAJA KWA GODWIN ERICK NKELEGO

Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka


kama dhahabu. - [Ayubu 23:10]
Mungu wa milele ndiye makazi yako, Na mikono ya milele i
chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui;
Akasema, Angamiza. - [Kumbukumbu la Torati 33:27]
shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu
kwenu katika Kristo Yesu. [1 Wathesalonike 5:18]
tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama
kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya
Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye; - [Waebrania
12:5]
Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake;
bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake. - [Yohana 9:3]
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu.
Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi
nimeushinda ulimwengu. - [Yohana 16:33]
Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini
na mimi. - [Yohana 14:1]
Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi
pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani,
wale walioitwa kwa kusudi lake. Maana wale aliowajua tangu
asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa
Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa
ndugu wengi. - [Warumi 8:28,29]
Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au
shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kama
ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana
kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.
Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya
kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha
kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala
malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala
yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala
yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza
kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu
Bwana wetu. - [Warumi 8:35-39]
Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika
mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea;
wala mwali wa moto hautakuunguza. - [Isaya 43:2]
Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo,
Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote; atufarijiye katika
dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika
dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na
Mungu. Kwa kuwa kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi
kwetu, vivyo hivyo faraja yetu inazidi kwa njia ya Kristo.
Lakini ikiwa sisi tu katika dhiki, ni kwa ajili ya faraja yenu na
wokovu wenu; au ikiwa twafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja
yenu; ambayo hutenda kazi yake kwa kustahimili mateso yale
yale tuteswayo na sisi. Na tumaini letu kwa ajili yenu ni
imara, tukijua ya kuwa kama vile mlivyo washiriki wa yale
mateso, vivyo hivyo mmekuwa washiriki wa zile faraja.
Maana ndugu, hatupendi, msijue habari ya dhiki ile
iliyotupata katika Asia, ya kwamba tulilemewa mno kuliko
nguvu zetu, hata tukakata tamaa ya kuishi. Naam, sisi
wenyewe tulikuwa na hukumu ya mauti katika nafsi zetu ili
tusijitumainie nafsi zetu, bali tumtumaini Mungu, awafufuaye
wafu, aliyetuokoa sisi katika mauti kuu namna ile; tena
atatuokoa; ambaye tumemtumaini kwamba atazidi kutuokoa;
- [2 Wakorintho 1:3-10]
Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia
katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa
kwa imani yenu huleta saburi. Heri mtu astahimiliye
majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya
uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao. - [Yakobo 1:2,3,12]
Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu,
unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu
kigeni kiwapatacho. Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya
Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi
kwa shangwe. - [1Petro 4:12, 13]
Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali
amtukuze Mungu katika jina hilo. Basi wao wateswao kwa
mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika
kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu. - [1 Petro
4:16,19]
Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti
haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala
maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza
yamekwisha kupita. - [Ufunuo wa Yohana 21:4]
Walilia, naye Bwana akasikia, Akawaponya na taabu zao zote.
Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka
roho huwaokoa. - [Zaburi 34:17,18]
Ajapojikwaa hataanguka chini, Bwana humshika mkono na
kumtegemeza. - [Zaburi 37:24]
Wewe, uliyetuonyesha mateso mengi, mabaya, Utatuhuisha
tena. Utatupandisha juu tena Tokea pande za chini ya nchi.
Laiti ungeniongezea ukuu! Urejee tena na kunifariji moyo.
- [Zaburi 71:20,21]
Hii ndiyo faraja yangu katika taabu yangu, Ya kwamba ahadi
yako imenihuisha. [Zaburi 119:50]
Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha, Utanyosha mkono
juu ya hasira ya adui zangu, Na mkono wako wa kuume
utaniokoa. - [Zaburi 138:7]
Maana umekuwa ngome ya maskini, Ngome ya mhitaji katika
dhiki yake, Mahali pa kukimbilia wakati wa tufani, Kivuli
wakati wa hari; Wakati uvumapo upepo wa watu watishao,
Kama dhoruba ipigayo ukuta. - [Isaya 25:4]
usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa
maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam,
nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa
haki yangu. - [Isaya 41:10]
Maskini na wahitaji wanatafuta maji, wala hapana; ndimi zao
zimekauka kwa kiu; mimi, Bwana, nitawasikia, mimi, Mungu
wa Israeli, sitawaacha. - [Isaya 41:17]
Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. Maana
ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa
huruma zake. Maana moyo wake hapendi kuwatesa
wanadamu. Wala kuwahuzunisha. [Maombolezo 3:31-33]
Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi
njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;
- [Wafilipi 1:6]
Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana
yeye, yeye naye atatukana sisi; Kama sisi hatuamini, yeye
hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana
mwenyewe. - [2 Timotheo 2:12,13]
Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe, Maana Wewe,
Bwana hukuwaacha wakutafutao. - [Zaburi 9:10]
Siku ya mateso yangu nitakuita, Kwa maana utaniitikia.
- [Zaburi 86:7]
Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuziganga jeraha zao.
- [Zaburi 147:3]1

1
By Japhet Munnah

You might also like