You are on page 1of 113

New Apostolic Church

Himnario
Kwa matumizi katika ibada zote za
Kanisa Jipya la Kimitume
New Apostolic Hymnal
(in Swahili Language)

© 2023 New Apostolic Church International.


Toleo la kwanza 2023

Haki zote zimehifadhiwa.

Kila juhudi imefanywa kuamua na kutafuta wamiliki wa nyenzo zote


zinazoonekana katika kitabu hiki. Mchapishaji anajuta makosa yoyote
au mapungufu na akipokea notisi ya malalamiko,atafanya
masahihisho katika uchapishaji utakaofuata.

Kimechapishwa na
New Apostolic Church
P. O. Box 59041-00200
Nairobi, Kenya Printed in Kenya
Baba yetu Uliye Mbinguni
Jina Lako Litukuzwe.
Ufalme Wako uje,
Mapenzi Yako yatimizwe,
Hapa duniani kama huko Mbinguni,
Utupe leo riziki yetu,
Utusamehe deni zetu,
Kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
Na usitutie majaribuni,
Lakini utuokoe na yule mwovu,
Kwa kuwa Ufalme ni Wako
Na nguvu,
Na utukufu,
Hata milele.
Amina.

(Mathayo 6:9-13)
1. Mungu Baba
Father God (NEH 7)

1. Mungu Baba sifa zote ni Zako.


Baba nainua mikono Kwako,
Maana nguvu na pendo Lako;
Vyanishangaza, ninakuabudu Ee Baba

2. Uliumba mbingu nata dunia.


Na vyote vilivyomo kwa neno tu;
Uweza Wako wanishangaza,
Wastahili sifa Ewe Baba Mungu wangu.

3. Utukufu Wako ni wa ajabu;


Viumbe vyote vyakusujudia,
Huko mbinguni na duniani,
Nakutumaini Ewe Baba Mungu wangu.

2. Mungu kati yetu!


God is in our presence! (NIH 103)

1. Mungu yungalipo! Njooni tumwabudu, njooni Kwake kwa heshima.


Yupo kati yetu nasi twangojea, Mioyo yajiandaa Kwake.
Wanaotambua ni wanyenyekevu, na wana shukrani.

2. Pamba mioyo yetu kwa mwangaza Wako, Nyuso zetu zi tayari!


Kama ua zuri na mwanga wa jua, Huleta harufu nzuri
Amani daima kwenye nuru Yake, itufanye wapya.

3. Utukamilishe tuyaache yote yale ya ulimwengu huu!


Tutakase Bwana tuone dhahiri tushike ukweli Wako.
Twakusifu Bwana kwa hisia zetu, na shauku Kwako.

4. Tufanye makao Yako Ewe Bwana kwa pendo Lako la kweli!


Uje Bwana wetu nasi tukuone, sifa utukufu Kwako.
Popote twendapo uwe nasi Bwana, tuwe Wako kweli.
3. Jinsi Wewe ulivyo mkuu
How great Thou art (NEH 15)

1. Bwana Mungu ninashangaa kabisa, nikitazama jinsi vilivyo.


Nyota, ngurumo, vitu vingi vyote, viumbwavyo kwa uweza Wako.

Chorus
Nafsi yangu na ikuimbie; jinsi Wewe ulivyo Mkuu!
Nafsi yangu na ikuimbie; jinsi Wewe ulivyo Mkuu!

2. Nikitembea duniani kote, ndege huimba nawasikia;


Milima hupendeza macho yangu, upepo nao nafurahia.

3. Nikikumbuka jinsi Wewe Baba, Ulivyo mtuma Yesu kwetu;


Afe azichukue dhambi zetu, kutambua ni vigumu sana.

4. Yesu Mwokozi utakaporudi, kuninyakua kwenda mbinguni.


Nitashukuru na kuimba milele, wote wajue jinsi Ulivyo!

4. Nakuabudu ee Mwenyezi
I worship you, almighty God (NEH 19)

1. Nakuabudu Ee Mwenyezi Mungu wa pekee.


Nakuabudu Ewe Mfalme ndiyo shauku yangu.
Nakusifu Wewe ni mwenye haki.
Nakuabudu Ee Mwenyezi Mungu wa pekee.
5. Mungu msaada wetu
O God, our help in ages past (NEH 22)

1. Mungu ndiye msaada wetu tangu miaka yote,


Ndiye tumaini letu, tazamio letu.

2. Kivuli cha kiti Chako ndiyo ngome yetu,


Mkono Wako unatosha, tunakaa salama.

3. Kabla ya kuumbwa kwa dunia na milima,


Ndiwe Mungu; chini Yako, twakaa salama.

4. Na miaka elfu ni kama siku moja Kwako;


Utatulinda daima, tu wenyeji Wako.

5. Mwanadamu huondoka, mwisho hana kitu,


Kama ndoto hutoweka, ndiyo hali yetu.

6. Twaipenda nyumba hii


We love the place, O God (NEH 28)

1. Ni nyumba ya sala, tunapokutana,


Sisi wanao pamoja Nawe Bwana.
Penye utukufu twahisi upendo,
Twapata neema na baraka Zako.

Chorus
Twaipenda nyumba hii, twakuhisi Wewe
Uwepo Wako wazidi mambo yote!

2. Bwana twaipenda madhabahu Yako,


Hapo kwa imani twakuhisi Wewe.
Tunapenda neno, neno la uzima,
Lenye faraja na furaha daima.

3. Twapenda kuimba kwa rehema Zako,


Shauku yetu ni wimbo wa mbinguni.
Yesu tupe neema tukupende sana,
Tukakuone na wateule wote.
7. Watu wote duniani
All people that on earth do dwell (NEH 33)

1. Watu wote duniani, mwimbieni Bwana sifa,


Kwa furaha na shangwe kuu njooni tumshangilie.

2. Bwana ndiye Mungu kweli, ndiye Aliye tuumba


Analisha kundi Lake na sisi ni kondoo W

3. Ee ingia lango Lake ingieni kwa shangwe kuu,


Sifuni kwa sauti kuu kwa maana imetupasa.

4. Kwa maana Mungu ni mwema na fadhili za milele,


Yeye ni mkweli daima tumtafute kila siku.

8. Wakristo tuimbe
Come, Christians, join to sing (NEH 34)

1. Wakristo tuimbe:

Tuimbe kwa shangwe mbele Zake Bwana,


Utukufu K

2.

Ni Rafiki Yetu Anatuongoza,


Hakomi a!

3.

Tufikapo mbingu tutamuona Yeye,


9. Ushukuru
Give thanks (NEH 38)

1. Ushukuru kwa moyo, mshukuru Mtakatifu


Kwa kumtoa Mwana pekee Yesu Kristo x2.
(Sasa mnyonge kapata nguvu na masikini mali,
Bwana ametenda makuu kwetu)x2. Tumshukuru

10. Uaminifu Wako Baba


Great is Thy faithfulness (NEH 40)

1. Baba uaminifu Wako ni mkubwa,


Kwako hakuna mabadiliko.
Huruma Zako hazishindwi kamwe,
Tangu mwanzo na hata milele.

Chorus
Uaminifu Wako, Uaminifu Wako,
Fadhili Zako ni za milele.
Kila ninacho hitaji napata.
Uaminifu Wako ni mkubwa!

2. Kiangazi, vuli, nayo mavuno,


Jua, mwezi, nyota vyaungana.
Na viumbe vyote vikionyesha
Ukuu Wako pendo na huruma.

3. Tusamehe tupatie amani,


Uwe nasi na Utuongoze.
Tupatie nguvu na tumaini,
Hata baraka Zako kwa wingi!
11. Wema Wake Mungu ni mkubwa
(NIH 227)

1. Wema Wake Mungu ni mkubwa! Ni nani asiye guswa?


Ulimwengu hautambui, ni nani anayepinga?
Pendo Lake halipimiki, wajibu wangu kujua;
Bwana alinipa hazina, sitashindwa kumshukuru.

2. Nitamfananisha na nani? Bwana hana shida nami,


Mvumilivu, mwenye huruma, sikatai neema Yake.
Ndiye anipaye amani, Yeye hunifanya upya
Nani awezanipa yote? Ni mkono wa Mungu pekee.

3. Ee nafsi tazama uzima Bwana kakuandalia,


Utaona kiti cha enzi, kilicho jaa utukufu.
Nina sababu kufurahi, kwa neema nabarikiwa;
Kwa dhabihu ya Bwana Yesu, ndiyo maana namtukuza.

4. Je sipaswi kusimulia wema Wake Mungu Baba?


Je nisimsikilize Bwana kwenye njia hii nyembamba,
Nia Yake i ndani yangu, neno Lake nguvu yangu,
Pendo Lake limeshamiri hata kumpenda jirani.

12. Naimba sifa


I sing praises (NEH 42)

1. Naimba sifa Zako Bwana nasifu jina Lako,


Jina Lako kuu Wastahili sifa.
Naimba sifa Zako Bwana nasifu jina Lako,
Kwa kuwa Wewe Wastahili sifa.

2. Nakutukuza Wewe Bwana nalitukuza jina,


Jina Lako kuu Wastahili sifa.
Nalitukuza jina, Bwana nakutukuza Wewe,
Kwa kuwa Wewe Wastahili sifa.
13. Mtukufu
Majesty (47 NEH)

1. Mtukufu, tumhimidi Yeye. Bwana Yesu sifa, utukufu Kwake.


Mtukufu, mamlaka ni Yake yamiminika juu ya walio Wake.
Inueni, jina tukufu la Yesu. Mtukuzeni Yesu Kristo ndiye Mfalme.
Mtukufu, tumhimidi Yeye. Bwana Yesu ndiye Mfalme wa Wafalme.

14. Manyunyu yenye baraka


Mighty the showers of blessing (NEH 50)

1. "Mungu alituahidi manyunyu ya baraka.


Sasa muda umefika, kama alivyosema.

Chorus
(Ni yenye nguvu!)Sop
(Ni manyunyu yenye nguvu!) Alto, Tenor & Bass
Utukufu na pendo,
Rehema nazo fadhili, baraka kutoka juu.

2. Manyunyu yenye baraka, yatiririka kote,


Yaleta uburudisho, kwa wenye kiu na njaa.

3. Ni mvua za b
Kati ya wana wa Mungu wanapata baraka.

4. Ni mvua za baraka kuu, Baba katuma leo,


Na tumwamini Yeye tu, tufuate njia Yake.
15. Tumshukuru Mungu
Now thank we all our God (NIH 256b)

1. Tumshukuru Mungu kwa mioyo na kwa ndimi.


Kwa matendo Yake duniani furaha.
Tangu tuzaliwe Anatubariki
Kwa vipawa vingi visivyo idadi.

2. Mungu wetu mwema awe nasi daima,


Atumiminie furaha na amani.
Atulinde sisi na kutuongoza
Atuweke huru sasa na daima.

3. Tunakupa sifa Ee Mungu Baba yetu,


Wewe na Mwanao watawala wa mbingu.
Mungu wa utatu Unaabudiwa
Tangu hapo kale sasa na daima.

16. Msifuni Mungu kwa nyimbo


Praise our God with joyful singing (NEH 56)

1. Msifuni Mungu kwa nyimbo, paza sauti Kwake


Zisikike pande zote, zifike juu mbinguni.
Twapata baraka Kwake, tumtumaini Yeye.
Tunakiri jina Lake, Mungu wetu ni mwema,
Mungu wetu ni mwema.

2. Tuko hekaluni Mwake, tunamopata neno.


Twahisi rehema Zake, twaona pendo Lake.
Hutupatia baraka na Hutupa nguvu mpya,
Ili tustahili Kwake, kutenda kazi Yake,
Kutenda kazi Yake.

3. Tutapata furaha kuu ambayo Ameandaa.


Punde Atamtuma Mwana na utukufu Wake.
Ahadi Yake ni kweli, daima tutamsifu:
Msaada Wake ni ushindi, na tutamtumikia,
Na tutamtumikia.
17. Msifu Bwana
Praise thou the Lord (NIH 261)

1. Msifu Bwana leteni sifa Kwake Mwenyezi!


Ni wakati mzuri Ee nafsi, kumsifu Mungu.
Kwa shangwe njoo, kwa vinubi msisite
Mwimbieni Mungu Baba!

2. Msifu Bwana ambaye ni mtawala wa vyote.


Kwenye mbawa Zake kuna usalama tele.
Atakuongoza na utafurahi,
Je wewe huhisi hili?

3. Msifu Bwana aliyetuumba kwa upendo;


Ametupa uzima na Anatuongoza.
Kwa rehema twapata mahitaji
Hifadhi mbawani Mwake.

4. Msifu Bwana Katupatia baraka tele.


Kwa rehema upendo Wake watiririka.
Fikiria uweza Wake Mungu
Aliyetupenda sote!

5. Msifu Bwana kwa vyote ulivyo navyo msifu!


Kila mwenye pumzi amsifu Yeye kwa nyimbo.
Mungu ni nuru nafsi ukumbuke
Tumsifu hata milele!

18. Je sipaswi kumwimbia Mungu


Should I not to God be singing (NIH 259)

1. Je sipaswi kumwimbia Mungu na kumshukuru?


Aliyonitendea yaonesha upendo mkuu.
Kitu kinachogusa Moyo Wake ni upendo,
Kwa uvumilivu Awabariki wamfuatao.
Ya dunia yapita, pendo Lake ladumu!

2. Mungu Kamtoa Mwanawe, kama sadaka pekee.


Kwa mateso makali mimi nilikombolewa.
Ewe chemchemi ya pekee, siwezi kuelewa!
Kwa akili
Ya dunia yapita, pendo Lake ladumu!
3. Roho Mtakatifu Kiongozi na neno langu,
Uwe Kiongozi na Mtawala hata mbinguni,
Nijaze moyo wangu kwa nuru Yako ya kweli,
Unishindie kifo, pepo hata nguvu zake.
Ya dunia yapita, pendo Lake ladumu!

4. Anaiongoza nafsi pia na fikra zangu,


Chochote kinipatacho Yuko upande wangu.
Hekima na nguvu zangu zijapokuwa duni!
Mungu Atanijilia na kuniimarisha.
Ya dunia yapita, pendo Lake ladumu!

5. Bwana ninakutukuza, pendo Lako ni kubwa.


Nanyosha mikono Kwako kwa neema nisikie.
Nipatie rehema Yako Uniimarishe!
Uwe nami daima Uishi nami daima.
Sifa na utukufu, ni Kwako, Bwana Yesu!
19. Twamshukuru Bwana
Thank ye, the Lord (NIH 272)

1. Twamshukuru! Mshukuru Bwana;


Rafiki mwema na Mwenye fadhili za milele,
Fadhili Zake, zinadumu milele.

2. Twamshukuru! Mshukuru Bwana!


Ee nafsi yangu usisahau matendo Yake,
Usisahau matendo Yake Bwana.

3. Ni Muweza! Mungu Muweza!


Kazi Zake zimejaa hekima kuu, nayo neema,
Atujaze neema, Atujaze neema.

4. Mungu ni Mkuu! Kweli


Kwa utakatifu Wake, twajazwa utukufu,
Nchi imejazwa utukufu Wake.

5. Msifu Bwana! Msifuni Bwana!


Kwa unyenyekevu mkubwa, twalitaja jina Lake,
Tunaita jina, jina Lake Bwana.

6. Mwimbieni! Mwimbie Bwana!


Imba kwa shangwe, Yeye Asikia sifa zetu,
Sifa zetu Zake, sifa zetu Zake.

20. Bwana kanitoa mbali


Thus far the Lord God has me brought (NIH 30)

1. Bwana kanitoa mbali sana kwa wema Wake,


Usiku na mchana, Yeye Ananiangazia.
Ananiongoza vema na Ananipa furaha,
Yeye ni Msaada wangu.

2. Shukrani zangu za dhati nakupa, Wewe Bwana.


Kwa uaminifu Wako, kwangu wakati wote.
Moyo wangu wakumbuka wema ulioutenda,
Wewe ni Msaada wangu.

3. Bwana Unisaidie katika masumbuko


Nishindie nakuomba na Unipe hifadhi!
Nikilifikia lengo nitasifu jina Lako;
Ewe Msaada wangu Mkuu.
21. Mungu atukuzwe
To God be the glory (NEH 66)

1. Mungu atukuzwe Katenda makuu!


Kwa upendo Alimtoa Mwanawe,
Kuwa ni dhabihu kwa dhambi zetu,
Na kufungua lango la ushindi.

Chorus
Msifuni, msifuni watu wasikie!
Msifuni, msifuni watu wafurahi!
Njooni kwa Baba kupitia Kristo
Utukufu Kwake Katenda makuu.

2. Ukombozi kwa damu ya thamani,


Ahadi ya Mungu kwa waaminifu;
Hata wenye dhambi wakiamini,
Na kutubu upo msamaha kwao.

3. Ametufundisha mambo ya mbingu,


Tukafurahishwa na Mwana Mungu
Ametuinua, tukae Naye
Atatuongoza hata milele.

22. Twakusifu, Bwana Uliyeshuka


We praise Thee, Lord (NIH 277)

1. Twakusifu, Bwana Uliyeshuka,


Na kuniokoa dhidi ya kifo.
Nitabaki Kwako Bwana Yesu,
Kwa uzima wa milele.

2. Twakusifu, Mtakatifu wa Mungu,


Ulijitoa kwa ajili yetu.
Nitabaki Kwako Bwana Yesu,
Kwa uzima wa milele.

3. Twakusifu, Ulijitoa kwetu,


Fidia ya dhambi nisamehewe.
Wokovu wangu ni Kwako Yesu,
Kwa uzima wa milele.
4. Twakusifu, Wewe mwenye mamlaka,
Niongoze njia kwenda Mbinguni.
Sifa na utukufu kwa Yesu,
Kwa uzima wa milele.

5. Twakusifu, ukate kiu yetu,


Tuwe na watakatifu Mbinguni,
Furaha yangu ni Kwako Yesu,
Kwa uzima wa milele.

23. Kwa Kristo Mwokozi


At the feet of Jesus (NIH 130)

1. Kwa Kristo Mwokozi napata neno,


Fadhili na wema, vyote Anipa,
Nitapata nguvu mpya, na nitakuwa safi.

Chorus
Kwa Kristo Mwokozi, sitaondoka,
Hapa nalipata neno tukufu.

2. Kwa neno la Yesu, nimesafishwa,


Vifungo vya mwovu, havina nguvu.
Na kwa neema ya Mungu, nimejawa furaha.

3. Baraka za Mungu, zisinipite.


Nipate kwa wingi, kila wakati,
Nipatapo naponywa, Kwake nakuwa safi.
24. Ndiyo dhamana
Blessed assurance, Jesus is mine (NEH 75)

1. Ndiyo dhamana, Yesu wangu,


Hunipa furaha za mbingu;
Mrithi wa wokovu Wake,
Nimezawa kwa Roho Yake.

Chorus
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu;
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu.

2. Kumsalimu moyo wangu,


Mara namwona raha yangu;
Aniletea malaika,

3. Sina kinyume, nashukuru,


Mchana kutwa Huja kwangu;
Usiku kucha kuna nuru,
Mwokozi wangu ndimi huru.

25. Ni Wako Bwana


I am Thine, O Lord (NEH 84)

1. Ni Wako Bwana Umeniita, Kwako kuna msamaha


Ninayo hamu moyoni mwangu kuwa karibu Nawe.

Chorus
Uniweke karibu Nawe niwe karibu sana.
Uniweke niwe karibu Nawe,Ufungamane nami.

2. Unitakase na Roho Wako niwe Wako kabisa


Nimekupa kile nipendacho sijapata hasara.

3. Ee ni furaha ya jinsi gani nikijitoa Kwako


Kwa upendo najitoa Kwako, niwe Wako kabisa.

4. Kuna pendo lisilopimika kwa wanao kupenda,


Na furaha ya kweli kwa wale wenye shauku Nawe.
26. Najikabidhi kwa Yesu
I surrender all (NEH 88)

1. Najikabidhi kwa Yesu Najitolea Kwake

Chorus
Najikabidhi, Najikabidhi
Kwako Ee Mwokozi wangu najikabidhi

2. Najikabidhi kwa Yesu na kumsujudia


Vya dunia naviacha ni pokee naomba.

3. Ninajikabidhi Kwako Bwana niwe Wako tu,


Nishushie Roho Wako nijue ni Wako tu.

27. Bwana siachi kukupenda


I will never cease to love You (NEH 90)

1. Kwa Ulivyonitendea Bwana, siachi kukupenda.


Kwa neema Yako ya bure, Bwana siachi kukupenda.

Chorus
Bwana siachi kukupenda, Mwokozi wangu, mtakatifu,
Kamwe siachi kukupenda maana U wangu nami Wako.
Ee Bwana kwa upendo Wako Ulimtuma Yesu kwetu
Kwa huruma kuu aliniweka huru.

2. Wanipa nguvu siku zote Bwana, siachi kukupenda.


Waniongoza njiani Bwana siachi kukupenda.

3. Katika safari yangu Bwana, siachi kukupenda.


Nijapo Kwako mbinguni, Bwana siachi kukupenda.
28. Nitaimba juu ya Mkombozi
I will sing of my Redeemer (NEH 91)

1.
Aliteswa msalabani, ili niwekwe huru.

Chorus

Kwa damu kuniokoa, deni zangu zafutwa.

2. za kuokoka kwangu,
Kwa pendo Lake na neema, Alinifanya huru.

3.
Alishinda hata kifo, dhambi hata mauti.

4.
Amenitoa kifoni niwe mwana wa Mungu.

29. Bwana Wewe ni Mwokozi


Lord, my Saviour and my Shepherd (NIH 370)

1. Bwana Wewe ni Mwokozi, uliyeandaa njia,


Moyo wangu nimekupa, Nitakufuata Wewe.

Chorus
Nilinde katika bonde, nifanye mwangalifu.
Kwenye sherehe mbinguni, Nikufuate kwa shangwe.

2. Wewe ndiwe nuru yangu, Uwe faraja pia,


Nionapo nyayo Zako, Nitakufuata Wewe.

3. Nitakase niwe Wako, Ahadi Yako ije.


Uwe mbele yangu Bwana Nikufuate vyema.
30. Fikra za Mwokozi wangu
May the mind of Christ, my Saviour (NEH 98)

1. Fikra za Mwokozi wangu, zidumu ndani yangu.


Nguvu ya upendo Wake initawale.

2. Neno la Mungu lijae tele moyoni mwangu,


Wote wajue nashinda kwa nguvu Zake.

3. Amani ya Mungu Baba initawale sana;


Nifariji wagonjwa na pia wanyonge.

4. Nijazwe pendo la Yesu kama maji ziwani;


Kuinua jina Lake; huu ni ushindi.

5. Nimkimbilie adui kwa ujasiri wote,


Nimtazame Yesu pekee, nisonge mbele.

6. Nijazwe uzuri Wake; kufuata wapotevu


Waziache njia zao, wamwone Yeye.

31. Twaa uzima wangu


Take my life and let it be (NIH 373)

1. Twaa uzima wangu twaa niweke wakfu, Bwana.


Twaa muda wangu pia, nikutukuze Wewe.
Twaa macho na yaone, mema kutoka Kwako.
Twaa masikio yangu, Nikusikie vyema.

2. Twaa na mikono yangu itende Upendayo.


Twaa nayo miguu yangu, kwenye njia nyembamba
Twaa na sauti yangu, ikuimbie Mfalme.
Twaa na ulimi wangu, Nikusifu milele.

3. Twaa mali yangu yote, itumike Kwako tu.


Twaa nafsi yangu yote, Naikabidhi Kwako.
Utwae moyo wangu, uwe Wako halisi.
Kwako najikabidhi, kwa neema Unipokee
32. Twasogea Kwako Bwana
With great joy and fervent longing (NIH 118a)

1. Twasogea Kwako Bwana kwa shangwe na shauku,

Tusikie neno Lako tusipoteze muda;


Neno tulilosikia lituongoze kweli,
Neno tulilosikia lituongoze kweli.

2. Sema nasi Bwana wetu nasi twakusikia,


Tupatie neno Lako liwe faraja kwetu.
Ee Roho utufundishe tulifikie lengo,
Kupokea taji njema, pumziko na amani,
Kupokea taji njema, pumziko na amani.

3. Bwana tupe Roho Wako atuguse mioyoni,


Tulinde na majaribu, Kwako ndiko salama.
Mizigo na majaribu na masumbuko yote,
Yatakoma nasi tutashiriki wema Wako.
Yatakoma nasi tutashiriki wema Wako.

4. Neno Lako nguvu yetu na nuru kwenye njia


Siku zote na kila saa shauku iko Kwako.
Tufundishe kuthamini yaliyo mema Yako,
Tuwaambie wengine njia Yako ya kweli,
Tuwaambie wengine njia Yako ya kweli.

33. Neno Lako ni maji kwa wenye kiu


Your word, O Lord, is gentle dew (NIH 175)

1. Neno Lako ni maji kwa wenye kiu Ee Bwana.


Mimina upako wa mbinguni wote tupate.
Tuzipatapo nguvu mpya, nayo mioyo yastawi, kuzaa matunda mengi.

2. Neno Lako ni upanga na mshale wa uwezo,


Laweza likapenye miamba, mioyo na mifupa.
Litume duniani liokoe wenye dhambi liwatakase kweli.

3. Neno Lako ni nyota ituongozayo njia,


Latuongoza kwa Kristo kusikia ujumbe.
Mwangaza wa mbinguni angaza mioyo yetu tusibaki vipofu
34. Inuka usisite
Arise and let us hasten (NEH 120)

1. Inuka usisite tufikie lengo,


Tufanye kazi Yake bila ya kuchoka.
Njoo kaka njoo dada njooni kwa mkono wa Yesu,

2. Sifu kazi ya Mungu yenye ukombozi,


Katutoa gizani Ametupa nuru.
Njoo kaka njoo dada njooni tushike bendera
Tubakie rohoni mwa Yesu Mwokozi.

3.
Neema nayo rehema bado vingalipo.
Njoo kaka njoo dada njooni Baba katutuma
Tushiriki pamoja na waliochoka.

4. Tukimaliza kazi itakuwa shangwe,


Tutakapoungana kiroho Sayuni.
Njoo kaka njoo dada njooni siku zimekwisha,
Tufuate neno Lake, Mungu kwa utiifu.

35. Panda asubuhi


Bringing in the sheaves (NEH124)

1. Panda asubuhi mbegu ile njema


Panda adhuhuri,tena jioni,
Tunaingojea siku ya mavuno,
Tutafurahi kuleta mavuno.

Chorus
Leta mavuno, leta mavuno,
Tutafurahi kuleta mavuno;
Leta mavuno, leta mavuno
Tutafurahi kuleta mavuno.

2. Tupande mwangani, tena kivulini


Tusiwe na hofu kwa baridi kuu,
Na mwisho wa kazi kuvuna mavuno,
Tutafurahi kuleta mavuno.

3. Mvunieni Bwana kwa machozi mengi,


Ijapo twaona taabu nyingi;
Mwisho wa kilio tutakaribishwa
Tutafurahi kuleta mavuno.
36. Nipe furaha moyoni mwangu
Give me joy in my heart (NEH 127)

1. Nipe furaha moyoni mwangu, (Bwana-Tenors only)


Nipe furaha naomba,
Nipe furaha moyoni mwangu, (Bwana-Tenors only)
Nikutukuze siku zote.

Kiitikio (Chorus):
Tuimbe hosana, tuimbe hosana,
Tuimbe hosana Kwake Mfalme!X2

2. Nipe amani nao upendo,(Bwana-Tenors only)


Nipe amani naomba,
Nipe amani nao upendo, (Bwana-Tenors only)
Nikupende milele yote.

3. Unipe upendo nitumike, (Bwana-Tenors only)


Nipe upendo naomba,
Unipe upendo nitumike, (Bwana-Tenors only)
Nikatumike siku zote.

37. Mioyo yenu ifurahi


Let your hearts be ever joyful (NEH 136)

1. Mioyo yenu ifurahi ijazwe shukurani,


Kwa wema wa Baba yetu Atuita wanawe.

Kiitikio (Chorus):
Tufurahi, tufurahi, kila siku ni nuru!
Raha kwenye njia tufuatayo; daima tufurahi!

2. Mungu Anatuongoza, na kutupigania.


Huturehemu daima; na kutuimarisha.

3. Tutafunikwa na giza tukishindwa kumfuata.


Tutapotea daima nuru itatoweka.

4. Njia yao wenye haki ni safi kila siku.


Na tumtumikie Yesu dhambi haina nuru.
38. Inua juu
Lift high the cross (NEH 137)

1. Inua juu msalaba, wa Kristo


Watu wote wamwabudu Yeye.
Wakristo njooni tumfuate Yesu,
Mfalme Mwana wa Mungu kashinda.

Chorus
Inua juu msalaba, wa Kristo ,
Watu wote wamwabudu Yeye

2. Inua juu msalaba, wa Kristo


Watu wote wamwabudu Yeye.
Njoo utumike Kwake Mwokozi,
Uwe na mhuri Wake usoni.

3. Inua juu msalaba, wa Kristo


Watu wote wamwabudu Yeye.
Bwana kateswa ili tupone,
Kaleta uzima wa milele.

4. Inua juu msalaba, wa Kristo


Watu wote wamwabudu Yeye.
Na tumwimbie wimbo wa sifa:
Na tumsifu kwa ushindi Wake.

39. Nafsi yangu inuka


Rise, my soul, gird thee with power (NIH 355)

1. Nafsi yangu inuka; ukeshe! Kuomba;


Kabla ya yule mwovu kufanya mawindo,
Kwa wale wasio na bidii kuomba maombi ya dhati.

2.
Tazama kazi Yake ya
Mikono na macho vijitoe Kwake, Yeye ndiye mpaji.

3. mka usilale

Sikia na utii usife dhambini usirudi nyuma.


4. Ukeshapo kuomba, kesha kwa saburi,
Yaepuke mabaya uvishinde vita,
Mwishowe kwa msaada tutakuwa Nae milele daima.

40. Mteteeni Yesu


Stand up for Jesus (NEH 152)

1. Mteteeni Yesu, mlio askari;


Inueni beramu, mkae tayari
Kwenda Naye vitani, sisi hatuchoki
Hata washindwe pia Yeye amiliki.

2. Mteteeni Yesu, na kumtumaini


Nguvu zetu za mwili hazitatufaa;
Silaha za Injili vaeni daima;
Kesheni mkiomba, msirudi nyuma.

3. Mteteeni Yesu, vita vitakoma


Leo hofu ya vita, kisha ni ushindi;
Kwake yule mshindi atavishwa taji
Kutawala milele, pamoja na Mfalme.
41. Nashindania uzima
Striving onward, pressing forward (NEH 153)

1. Nashindania uzima, nakaza mwendo.


Nitajitahidi sana mpaka nifike.
Nitavuka vikwazo nitimize ahadi.

2. Nakimbilia nifike kiti cha enzi.


Nikichelewa nakosa baraka Zake.

Ya ulimwengu hayana faida yote.

3. Yesu ananiongoza, nifike lengo.


Nikitetereka Bwana unipe nguvu.
Ninapojaribiwa, nakimbia aibu.

4. Pasipo Wewe siwezi, nakuhitaji.


Nijaposhindwa napata nguvu toka juu.
Neno Lako uzima Umeniweka huru.
Niingie Yerusalemu mji mtukufu.

42. Leo ni siku ya neema


The time of grace redeems today (NIH 135)

1. Leo ni siku ya neema, ufungue moyo,


Kumbuka safari yako, imejaa baraka.
Ee njoo leo.

2.
Roho Wake ni mwalimu; hutuangazia
Ee njoo leo.

3.
Yesu hutoa msamaha na kukuongoza.
Ee njoo leo.

4. Ee tumfuate kwa imani. Mungu wa amani,


Kwake shida zitakoma, kule ni amani.
Ee njoo leo.
43. Tufanyeni kazi
To the work! To the work! (NEH 162)

1. Tufanyeni kazi! Watumishi Wake!


Tuzifuate njia Zake Mungu wetu.
Ushauri Wake, nguvu yetu sisi,
Kwa nguvu ya mikono yetu tutende.

Chorus
Kwa bidii, kwa bidii, Kwa bidii, kwa bidii;
Mtumaini tukeshe Fanya kazi mpaka mwisho.

2. Tufanyeni kazi! Wenye njaa walishwe;


Nao walochoka waongozwe njia.
Msalaba na bendera yetu tukufu
Tutangaze wokovu Wake ni bure!

3. Tufanyeni kazi! Wote twaalikwa!


Kwakuwa ufalme wagiza takoma
Na jina la Bwana litashangiliwa
Kwa sauti kuu, kwa wimbo wa wokovu!

4. Tufanyeni kazi! Kwa nguvu za Bwana,


Kwa kuwa vazi na taji tutavikwa
Tutaishi pamoja Naye Mwokozi
Tukiimba wimbo kwa wokovu wetu!

44. Fanyeni kazi zenu


Work, for the night is coming (NEH 167)

1. Fanyeni kazi zenu, usiku simbali,


Kama vile umande utowekavyo,
Jua likiangaza tuifanye kazi,
Fanyeni kazi zenu, nuru ingalipo.

2. Fanyeni kazi zenu, jua lingalipo,


Wakati unakuja wa kupumzika,
Weka hazina yako kwa kila dakika,
Fanyeni kazi zenu, nuru ingalipo.

3. Fanyeni kazi zenu, jua linazama,


Wakati wa mchana tusichelewe,
Nuru itowekapo wewe fanya kazi,
Fanyeni kazi zenu, nuru ingalipo.
45. Ujaribiwapo, sifanye dhambi
Yield not to temptation (NEH 168)

1. Ujaribiwapo, sifanye dhambi,


Bali ongeza kumtii Bwana Yesu
Pigana kwa nguvu, ushinde giza,
Bwana Yesu yupo Atakulinda.

Chorus
Na umwombe Mwokozi akupe nguvu Zake
Atakusaidia, Atakulinda

2. Umwepuke mwovu, na mambo yake,


Heshima Kwake Mwenyezi Mungu,
Uwe mwaminifu na moyo mkweli.
Umtazame Yesu Atakulinda.

3.
Tuwe na imani tutayashinda,
Mwokozi wetu Atatushindia
Umtazame Yesu Atakulinda.

46. Jikabidhi kwa Mungu


Commit your way, confiding (NIH 146a)

1. Jikabidhi kwa Mungu ujaribiwapo,


Na mkono Wake ndio huongoza vyote,
Mawingu na dhoruba, kwenye njia Yake,
Je Mungu Hataweza kukuvusha vema?

2. Amini Kwake Bwana, akupaye vyote,


Ijenge kazi yako kwenye neema Yake,
Pekee yako huwezi hata kujilinda
Pale unapomwomba, Ajibu maombi.

3. Njia Yake ya pekee, uweza ni Wake,


Ni kwa neema Yake tu, nasi twashukuru
Hakuna wakupinga kazi Yake Mungu,
Hata wanawe wote wapate uzima.

4. Sahau taabu zako, hofu na huzuni


Utumaini kwamba kesho ni furaha,
Wewe siyo mtawala, bali Mungu Baba.
Yeye pekee ni msaada Anatusikia.
5. Yeye Akuongoze kwa hekima Zake,
Na Atakuongoza ukimpa nafasi,
Upeo Wake ni mkuu kuliko chochote,
Mwisho Ataondoa hofu yako yote.

47. Kumbuka mibaraka Yako


Count your blessings (NEH 177)

1. Unaposongwa nayo majaribu,


Udhanipo umepoteza yote,
Zikumbuke baraka, zake Bwana
Utafurahia matendo Yake.

Chorus
Kumbuka mibaraka Yako;
Hesabu matendo ya Bwana!
Ukumbuke, baraka zako,
Utafurahia matendo Yake.

2. Je umeelemewa na mizigo?
Je msalaba wako ni mzito?
Zikumbuke baraka, mtumai
Na kwa nyimbo umtukuze Yeye tu.

3. Uzionapo mali za wengine,


Kumbuka ahadi za Kristo kwako;
Mali haziwezi kamwe nunua
Ujira wako kule juu mbinguni.

4. Matatizo makubwa kwa madogo,


Usihuzunike Mungu aweza;
Malaika watakuhudumia
Kukufariji safarini mwako.
48. Milele kwa Bwana
Forever with the Lord (NIH 402)

1. Milele kwa Bwana! Najitoa Kwake;


Nyota ambayo ni neno itaniongoza.
Hapa duniani, mimi ni mgeni,
Nahama na hema langu, Bwana, karibia
Karibu, karibu, Bwana karibia.

2. Ingawa sioni, macho yafifia


Nairudia safina, kama njiwa yule,
Wingu layeyuka tufani yakoma
Nuru ile ya amani nifaraja kwangu,
Amani, amani ni faraja kwangu.

3. Natazama mbingu, nauona mji;


Watumishi kwa hekima Wananiongoza.
Kisha huo mji, nitapumzika,
Na kushiriki pendo kuu, kwenye nchi hiyo
Pendo kuu, pendo kuu kwenye nchi hiyo.

4. Nitapumzika, nafsi kuwa huru,


Nitakapo shinda kifo Itakuwa shangwe
Nitakapo paa kutoka kuzimu
Ni uzuri ulioje milele kwa Bwana.
Uzuri, uzuri milele kwa Bwana.

49. Ni salama juu ya Mwamba


Hiding in Thee (NEH 183)

1. Ee ni salama katika Mwamba huu,


Majonzi na migogoro huisha.
Bwana mimi nataka niwe Wako.
Najificha Kwako Mwamba Imara.

Chorus
Najificha, Najificha; Kwenye Mwamba Imara najificha

2. Wewe ni faraja nyakati zote,


Katika majaribu na majonzi;
Magumu yote ninayopitia,
Najificha Kwako Mwamba Imara.
3. Kila nipitiapo majaribu,
Ninakuja Kwako unihifadhi!
Nijapo andamwa na migogoro,
, Ee Mwamba wangu.

50. Tazameni
Hold the fort (NEH 184)

1. Tazameni mawinguni kuna ishara!


Msaada na ushindi vyakaribia!

Chorus

Kwa neema Yako Bwana na iwe

2. Jeshi Lako linasonga, shetani naye:


Wengi wetu miongoni warudi nyuma.

3. Mlio wa baragumu unasikika.


Kwa jina la Bwana wetu tutashinda tu.

4. Vita kali mbele yetu kuna Msaada.


Jemedari amekuja tutashinda tu.
51. Namjua nimwaminiye
I know whom I have believed (NEH 186)

1. Sijui lengo Lake kunionyesha neema


Wala rehema Yake Kristo kunikomboa.

Chorus
Lakini ninamjua Yeye nimwaminiye Atanilinda.
Nitunze ahadi Kwake hata Ajapo tena.

2. Sijui jinsi alivyonipa imani


Wala kumwamini kunavyo nipa amani.

3. Sijui jinsi Roho anavyo tuepusha


Wala amdhirishavyo Kristo mioyoni mwetu

4. Sijui lini hakika Bwana Atarudi

52. Baba Yangu ana mali nyingi


(NEH 189)

1. Baba yangu ana mali nyingi,


Hushika hazina zote mkononi;
Fedha zote na mawe thamani,
Na dhahabu zote ulimwenguni.

Chorus
Ni mwana wa Mfalme, mwana wa Mfalme,
Pamoja na Yesu Ni mwana wa Mfalme.

2. Mwana wa Baba, Mwokozi wangu,


Alitembea humu ulimwengu;
Bali anatuombea sasa,
Ili tuwe watu Wake kabisa.

3. Nilitupwa mbali duniani,


Nikakubali kuwa mwenye dhambi;
Bali sasa nimeokolewa,
Kweli, jina langu limeandikwa.

4. Hema au nyumba, sioni shaka,


Makao mazuri nitayapata;
Nikihamishwa na watu wangu,
Nitafurahi na Mwokozi wangu.
55. Nuru baada ya giza
(Light after darkness NIH 200)

1. Baada ya giza, kuna Nuru,


Na nguvu baada, ya uchofu,
Baada ya taabu, tumaini,
Pumziko baada, ya mateso.

2. Mavuno baada, ya kupanda,


Kuona baada, ya upofu
Furaha baada, ya huzuni,
Pumziko baada, ya dhoruba.

3. Uzima baada, ya Magonjwa,


, ;
Baada ya yote, ni Faraja,
Kutoka Kwake, Yesu Kristo.

4. Karibu baada, ya umbali,


Upendo baada, ya upweke,
Baada ya taabu, ni furaha;
Hii ndiyo njia ya uzima.

56. Bwana upepo wavuma


(Master, the tempest is raging NEH 201)

1. Bwana upepo wavuma! Wimbi lina ghadhabu!


Anga limetanda mawingu, msaada uko mbali.
Huoni twaangamia? Mbona Unalala
Na dhoruba yazidi kutisha je tufie majini?

Chorus
Upepo mawimbi vitanitii, Tulia,tulia!
Iwe ghadhabu ya bahari, ama watu, pepo, na chochote, maji,
Hayatameza meli, ni Bwana wa bahari, mbingu na nchi, hivyo
Vyote vitanitii, tulia, tulia! Hivyo vyote vitanitii utulivu!

2. Nakunyenyekea Bwana, kwa uchungu rohoni.


Moyo wangu unateseka; Amka uniokoe
Dhambi na uchungu mwingi vitanizamisha
Ninakufa, nakufa, Ee Bwana; haraka niokoe!

3. Bwana hofu imekoma, hali imetulia.


Jua laangaza dunia nuru ya mbingu kwangu.
Umekawia Mkombozi, siniache tena.
57. Si ushauri wa mwanadamu
Not human advice (NIH 181)

1. Mwanadamu kwa hekima zake


Hazitamfikisha juu Mbinguni.
Kwa sababu zinakatisha tamaa tena si hakika:
Bwana Mkombozi, Yeye ni njia!

2. Kwake yote yanajulikana.


Amini pokea pendo Lake
Bwana atawapa, yaliyo mema, nasi twaamini:
Bwana Mkombozi, Yeye ni njia!

3. Twapita kwenye njia ya Yesu


Yapatikana kwa Yesu pekee.
Kwenye taabu na katika furaha, tuna uhakika:
Bwana Mkombozi, Yeye ni njia!

58. Tupande mlima Sayuni


On (NEH 205)

1. Tupande mlima Sayuni, enyi waaminifu.


Tupige vita mapema, nuru ingalipo.
Tushambulie adui kwa silaha zetu;
Kwa imani tutaushinda ulimwengu huu.

Chorus
Imani hutuongoza, kuushinda!
Ulimwengu kwa ushindi ule mtukufu!

2. Mfalme anatuongoza, neno Lake ngao.


Twafuata nyayo za watakatifu wa kale.
Nen
Hutupa kushinda vita pendo halikomi.

3. Tokea mlima wa nuru, mioyo ya angaza,


Tutayashinda ya giza kwa jina la Yesu.
Mshindi kuvishwa taji ya Mwanakondoo.
Tuzo kubwa kwa mshindi ni kupumzishwa.
59. Bwana We ni nuru
m looking (NIH 371)

1. Bwana We ni nuru, Mwamba imara.


Na Kiongozi, nikuaminie,
, ni Mkate wangu, pia Chemchemi,
, ni lengo ninalopigania!

2. Nguvu, ujasiri ningepataje?


Bila ya msaada Wako Ee We Bwana?
Siwezi kuishi bila ya Wewe;
U imani, tumaini, na pendo!

3. Kwa ulichonipa nitakufuata


Hata nitakapoitwa nyumbani.
Itakuwa shangwe, na nitasema;
Sina chakukulipa: Ee, We, Bwana!

60. Peleka jina la Yesu


Take the name of Jesus with you (NEH 213)

1. Peleka jina la Yesu kokote uendako;


Litafurahisha moyo, peleka uendako.

Chorus
Thamani, na tamu, Ni jina Lake Yesu;
Thamani, na tamu, Ni jina Lake Yesu.

2. Peleka jina la Yesu liwe silaha zako;


Utakapojaribiwa, lilia jina hilo:

3. Yesu, jina la thamani, limenifurahisha;


Nikiwasili mbinguni, Atanikaribisha:

4. Kwa jina la Bwana Yesu, nimejiinamisha;


Ndiye Mfalme wa wafalme,ni katika maisha:
61. Tusongeni mbele
Toiling bravely onward (NEH 219)

1 Tusongeni mbele kwa ujasiri,


Kwa pendo la Yesu hatuogopi.
Hatupigi vita kufurahisha,
Mapenzi ya watu ila ya Yesu.

Chorus
Hata maadui wakitujia
Mitume wa Bwana, tusonge mbele.

2. Tusongeni mbele lengoni mwetu,


Waache wadhihaki kama kwa Nuhu.
Hata maadui wakitujia,
Kristo amekwisha toa neema.

3. Tusongeni mbele, sasa twajua,


Manabii wa kale walitamani.
Kwa kazi za Yesu twamwona Mungu,
Huongoza wana kwenda kwa Baba.

62. Nafsi yangu mngoje


Wait, my soul, and tarry (NIH 190)

1. Nafsi yangu, mngoje Bwana Mungu!


Hutalemewa na mizigo kamwe.
Je wahofu? Kwapambazuka
Baridi yapita, siku mpya yaja.
Hata dhoruba ikizidi,
Atakubariki, nafsi mngoje.

2. Nafsi yangu, mngoje Bwana Mungu!


Hutalemewa na mizigo kamwe.
Ushindwapo Yeye aweza,
Mungu ndiye msaada hashindwi kitu.
Mwenyezi na Mwokozi wetu
Niokoe Bwana ninaomba.

3. Nafsi yangu, mngoje Bwana Mungu!


Hutalemewa na mizigo kamwe.
Hivi punde tutapumzishwa,
Hofu na mashaka vitakomeshwa.
Nikiyashinda ya dunia
Ni shangwe milele Naye Bwana.
63. Yesu kwetu ni Rafiki
What a Friend we have in Jesus (NIH 237)

1. Yesu kwetu ni Rafiki, hwambiwa haja pia.


Tukiomba kwa Babaye, maombi Asikia!
Lakini twajikosesha, twajitweka vibaya!
Kwamba tungemwomba Mungu, dua Angesikia.

2. Unadhiki na maonjo? Unamashaka pia?


Haifai kufa moyo; dua Atasikia.
Hakuna mwingine mwema wakutuhurumia?
Atujua tudhaifu, maombi Asikia.

3. Je, hunayo hata nguvu, huwezi kuendelea?


Ujapodharauliwa; ujaporushwa pia.
Watu wangekudharau, wapendao dunia.
Hukwambata mikononi, dua Atasikia.

64. Tufani inapovuma


When the storms of life are raging (NEH 228)

1. Tufani inapovuma sana moyoni mwangu,


Naona pa kujificha mkononi Mwake Mungu.

Chorus
Hunificha, hunificha adui hatanipata.
Hunificha, hunificha mkononi Mwake Mungu.

2. Ingawa kuna taabu yanisogeza Kwake;


Naijua si hasira, ni ya mapenzi Yake.

3. Nikiwa majaribuni, adui hunidhuru,


Yesu ataniokoa, naongeza imani.

4. Ingawa kuna tufani na mawimbi makubwa,


Kamwe sitarudi nyuma, nitabaki kwa Yesu.
65. Kwa fimbo ya dhahabu
With a golden staff in hand (NIH 204)

1. Kwa fimbo ya dhahabu, nitafika safari,


Na itaniongoza juu mbinguni kwa Baba.
Fimbo yangu ni imani, hunifanya imara.
Mwili ujapokufa, imani itadumu.

2. Wema Wake Mkombozi, unajidhihirisha,


Hunijaza furaha, hunifunza ukweli.
Upendo wa Mungu Baba tusiuache kamwe.
Kama ndugu wamoja, milele naye Mungu.

3.
Hunijaza furaha na faraja moyoni!
Nimetumaini kwayo, nazo mbingu zafunuka
Kuwaongoza wana mbinguni uzimani.

66. Kaa nami


Abide with me (NEH 232)

1. Kaa nami ni usiku tena; Usiniache gizani Bwana;


Msaada Wako haukomi, Nili peke yangu kaa nami.

2. Siku zetu hazikawii kwisha; sioni la kunifurahisha


Hakuna ambacho hakikomi, Usiye na mwisho, kaa nami.

3. Nina haja Nawe kila saa; sina mwingine wa kunifaa;


Mimi nitaongozwa na nani? Ila Wewe Bwana, kaa nami.

4. Sichi neno uwapo karibu; nipatalo lote si taabu;


Kifo na kaburi haviumi; Nitashinda Kwako, kaa nami.
67. Naleta tunu Kwake Mfalme
(NIH 202)

1. Naleta tunu Kwake Mfalme kwa heshima.


Japo ni ndogo sana, Anafurahia.
Nimejitoa Kwake katika njia hii.
Ili mapenzi Yake yawe ndani yangu.

2. Sitaogopa tena wala sitahofu.


Kwa moyo wa furaha nitamtegemea.
Aliutwaa uhai kwa ajili yangu.
Je hataendelea kulipa mazuri?

3. Huruma Yake Baba, ni kuu kama neema.


Wenye dhambi, maskini, Huwakumbatia.
Upendo Wake Baba hunifanya upya.

4. Bwana unitazame kwa huruma Zako


Natazamia nguvu na rehema Zako.
Unishike mikononi Wewe mwenye nguvu,
Na utaniongoza nyumbani kwa Baba.

68. Ee Yesu mbarikiwa


Blessed Jesus, at Thy word (NIH 95)

1. Ee Yesu, mbarikiwa twaja kusikia neno;


Mioyo yetu iguswe kwa maneno ya uzima,
Kwa mafundisho mazuri umetuvutia Kwako.

2. Maarifa; macho yetu yamefikia ukomo,


Roho Wako wa pekee atufumbue kwa nuru,
Yeye pekee anaweza kutufanya tustahili.

3. Mtukufu Bwana wetu, U nuru toka mbinguni,


Fungua mioyo yetu; tusaidie twaomba,
Sikia kilio chetu pokea maombi yetu.
69. Bwana nimejitoa Kwako
Dear Lord, I give completely (NIH 120)

1. Nafsi na moyo wangu navitoa Kwako;


Wewe ni Kuhani Mkuu niongoze Bwana.

Chorus
Moyoni natamani kuwa Nawe Bwana,
Tazama nakungoja uniangazie.

2. Ee Mwokozi muweza, kimbilio langu;


Nakungojea Bwana kwa uaminifu.

3. Niwezeshe nitende yakupendezayo;


Niwe mtumishi Wako kutimiza neno.

4. Nikitumia vyema muda kwa hekima,


Nitapata makao yenye utukufu.

70. Niongoze Ee Mkombozi


Guide me, O Thou great Redeemer (NEH 242)

1. Niongoze Ee Mkombozi, ninapita jangwani.


Ni mnyonge we ni muweza, kwa mkono unishike
Ewe Mkate wa mbinguni, nilishe siku zote (nilishe)
Nilishe siku zote.

2. Ufungulie chemchemi, chimbuko la uzima;


Na uniongoze kwa nguzo ya moto na wingu.
Umpaji Mkuu, umpaji Mkuu, nguvu na ngao yangu, (na ngao)
Nguvu na ngao yangu.

3. Nipitapo kwenye bonde, uniondoe hofu.


Kifo na mauti yake univushe salama.
(Mkombozi)
Kwako Mkombozi wangu.
71. Na iwe kama Utakavyo
Have Thine own way, Lord (NEH 243)

1. Na iwe kama Utakavyo! U mfinyanzi nami udongo.


Niumbe upendavyo Wewe, Nimejitoa Kwako Bwana.

2. Na iwe kama Utakavyo! Unichunguze leo Bwana!


Na unioshe nitakate, Ninasujudu mbele Zako.

3. Na iwe kama Utakavyo! Nisaidie nimechoka.


Uweza na nguvu ni Zako! Mwokozi wangu uniponye!

4. Na iwe kama Utakavyo! Na unitawale kabisa.


Unijaze na Roho Wako Kristo akae ndani yangu!

72. Moyo wangu ninakupa Ee Mungu


Here is my heart (NIH 107a)

1. Moyo wangu; nakupa Ee Mungu, ulieniumba;

Karama Yangu ya upendo; Bwana itwae itakase.


Moyo wangu, ninakupa.

2. Moyo wangu; uchukue Bwana, japo ni dhaifu.


Ninakupa, kwa pendo la kweli, neema yanitosha,
Dhambi hatia imetanda, mfano wa Giza na aibu.
Moyo wangu wenye dhambi

3. Moyo wangu; wote nampa Kristo pale msalabani,


Nitasema, ulikufa ili nipate kupona,
Kupitia jeraha Zako, napata faraja na pendo,
Moyo wangu mwaminifu.
73. Nina haja Nawe
I need Thee every hour (NIH 199)

1. Nina haja Nawe muda wote,


Hakuna mwingine kama Wewe.

Chorus
Yesu nakuhitaji Wewe kila mara,
Nibariki Mwokozi, nakujia.

2. Nina haja Nawe uwe nami,


Kwenye majaribu nishindie.

3. Nina haja Nawe kila hali,


Na uje upesi sitaweza.

4. Nina haja nawe Nifundishe,


Na ahadi Zako Zitimizwe.

5. Nina haja Nawe Mtakatifu,


Unifanye Wako mbarikiwa.

74. Karibu na Wewe


Nearer, my God, to Thee (NIH 366a)

1 Karibu na Wewe, Mungu wangu;


Karibu zaidi, Bwana wangu.
Siku zote niwe, karibu na Wewe.
Karibu zaidi Mungu wangu.

2. Mimi nasafiri duniani,


Pa kupumzika sipaoni,
Nilalapo niwe karibu na Wewe.
Karibu zaidi Mungu wangu.

3. Njia iwe wazi kuja Kwako;


Vyote Unipavyo kwa rehema,
Malaika Wako wanielekeze;
Karibu zaidi Mungu wangu.

4. Nyumbani kwangu juu, Baba yangu;


Zikikoma hapa siku zangu
Kwa furaha niwe pamoja na Wewe,
Karibu zaidi Mungu wangu.
75. Mwokozi wetu Utuongoze
Saviour, like a shepherd lead us (NEH 259)

1. Mwokozi wetu utuongoze, twakuhitaji,


Malisho Yako utulishe tukae salama,
Bwana Yesu, mbarikiwa, sisi tu mali Zako,
Bwana Yesu, mbarikiwa, sisi tu mali Zako.

2. Tuwe marafiki Zako Uweze kutulinda,


Utuchunge kondoo Wako, tusipotee kamwe,
Bwana Yesu, mbarikiwa, sikia wana Wako,
Bwana Yesu, mbarikiwa, sikia tukiomba.

3. Umeahidi kutupokea tu masikini,


Rehema Zako zatutuliza twapata nguvu,
Bwana Yesu, mbarikiwa, tuje Kwako mapema,
Bwana Yesu, mbarikiwa, tuje Kwako mapema.

4. Tufanye mapenzi Yako, Bwana utuwezeshe,


Mbarikiwa Mwokozi twajazwa pendo Lako.
Bwana Yesu, mbarikiwa, Utupende daima,
Bwana Yesu, mbarikiwa, Utupende daima.

76. Bwana nanyosha mikono


See, I spread my arms in yearning (NIH 131)

1. Bwana nanyosha mikono shauku yangu Kwako;


Kwa sh

2. Unipatie chakula, mimi ni muhitaji.


Pekee yangu sitaweza, nipatie pumziko.

3. Sina cha kukupendeza, sina cha kukulipa,


Unilishe nakuomba Wewe ni nguvu yangu.

4. Najua hutoniacha, mimi ni Wako pekee;


Neno Lako ndilo kweli, Bwana mimi ni Wako.

5. Neema Yako Bwana wetu, na uponyaji Wako,


Je haviwezi kuondoa umaskini wangu?
77. Wakati wangu kuomba
Sweet hour of prayer (NEH 261)

1. Wakati wangu kuomba! Umenialika kusali;


Nimsihi Mungu Mwenyezi, Anitulize kwa mapenzi,
Nyakati za shaka nyingi nimepata ufadhili,
Kwa Wewe nitangojea, Ewe, wakati wa kuomba.

2. Wakati wangu kuomba! Umeniletea furaha,


Pamoja nao wenzangu, nashirikiana na Mungu,
Mahali hapa nikae, uso wangu, nimuone;
Kwako nitakungojea, Ewe, wakati wa kuomba.

3. Wakati wangu kuomba! Mabawa Yako hunishika;


Kwa Yesu Aliye kweli, Aningojea kubariki,
Tangu Alinialika nimwamini kwa hakika,
Kwa Wewe nitangojea, Ewe, wakati wa kuomba.

78. Nishike mkono Bwana


Take Thou my hand and lead me (NIH 194)

1. Nishike mkono Bwana, niongoze


Mpaka mwisho wangu hata milele.
Pekee yangu siwezi, Uwe nami.
Popote uendapo Uwe nami.

2. Rehema Zako Bwana zinikinge,


Niwe na subira nyakati zote.
Nistahirishe Bwana nipumzike,
Nitayaona mema mwisho wangu.

3. Uwe ni nuru yangu kwenye giza,


Uniongoze pekee sitaweza.
Nikifuata kwa uaminifu,
Utaniimarisha kila siku.

4. Japo sizitambui nguvu Zako,


Bwana Waniongoza kwenye lengo,
Wewe Uniongoze nakuomba,
Hata mwisho wangu mpaka milele.
79. Nijulishe mwisho wangu
Teach me the measure of my days (NEH 263)

1. Nijulishe mwisho wangu, Ewe Muumba wangu;


Nijulishe nitambue udhaifu wangu.

2. Maisha yetu mafupi, kama maua;


Hunyauka na kurudi katika mavumbi.

3. Huenda huko na huko, mfano wa kivuli,


Hufanya ghasia sana, asijue mwisho.

4. Sasa nangojea nini hapa duniani?


Ee Bwana matumaini, yangu yako Kwako.

5. Tumaini langu sasa, na shauku yangu;


Nakupa maisha yangu niwe Wako kweli.

80. Wakfu wa Mungu ni wa haki


That which my God ordains is right (NIH 156)

1. Kilicho wekwa na Mungu, ni haki, hakipingwi.


Nami nitaamini kwa vipimo vya kimungu.
Kwa maana Mungu kaniokoa na yule mwovu;
Namwamini Yeye tu!

2. Wakfu wa Mungu ni haki, Yeye uwepo wangu.


Huniepusha na mwovu, sitapingana Nae.
Nitamwamini siku zote, hata pendo Lake
Lidhihirike kwangu.

3. Wakfu wa Mungu ni haki, hapo nimesimama.


Kwenye huzuni na hofu sitasahaulika,
Nimezungukwa na wema, Yeye ananilinda;
Namwamini Yeye tu!
81. Njoo ndani Bwana!
Come in, O Lord, come in (NIH 134)

1. Njoo ndani Ee Bwana! Usikae nje.


Uwe ndani yangu Bwana, niwe Wako kweli.

2. Njoo ndani Ee Bwana! Uniangazie


Kwa mwanga Wako wa kweli, nami niwe mkweli.

3. Njoo ndani Ee Bwana! Umengoja sana.


Hakika sitakawia tena kufungua.

4. Bwana njoo kaa nami, Ee Bwana mtukufu,


Uwe nashirika nami na nipe pumziko.

5. Njoo ndani Ee Bwana! Makao tayari.


Nangojea tuzo Yako; taji ya ushindi.

82. Mwokozi Anaita


Come near, you are invited (NIH 112)

1. Mwokozi anaita; sikia mwaliko.


Aita kwa neema na kwa upendo mkuu!
Mbingu hata nchi vyote Aliviumba.
Sasa Atualika kwenye karamu juu.

2. Nafsi yangu, njoo sasa; Bwana Mwokozi!


Maana dhambi, ni chungu, Mungu ni wa neema.
Yeye ni chemchemi; chakula cha uzima
Kitokacho mbinguni katuandalia!
83. Njoo kwa Mwokozi
Come to the Saviour (NEH 276)

1. Njoo kwa Mwokozi njoo leo hii, neno Lake ulipokee


Yu tayari kukubariki hapa Asema

Chorus
Nifuraha tukikutana, tukishakutakaswa dhambi.
Kuingia Nawe Kanani, wateule njooni!

2. Wanangu mje sikieni, mpeni mioyo kwa shangwe,


Yeye chaguo la mbinguni jiandaeni, njoo!

3. Anasikia sala zenu je, twahisi uwepo Wake?


Kwa neema Atawalipa, wenye dhambi njooni!

84. Njooni karamuni


Come, for the feast is spread (NEH 277)

1. Njooni karamuni, mmeitwa;


Vyakula mezani vimewekwa,
Na Mwake nyumbani mlazwe rahani,
Mwake kifuani, njooni, njooni.

2. Mkate wa kweli, Ametoa;


Wa bure, sighali, utapewa;
Wote Awaita, wengi wamepata,
Nanyi awavuta, njooni, njooni.

3. Njooni kulingana Mungu Bwana;


Mwambieni kila haja tena,
Mtakavyo vyote Hupa siku zote
Neema kwa wote; njooni, njooni.

4. Yesu twaja Kwako; tukubali,


Pia tuwe Wako safi kweli,
Kisha huko juu, penye enzi kuu,
Tutaziimba tu sifa Zako.
85. Ninakuombea rafiki yangu
For you I am praying (NEH 278)

1. Mwokozi wangu Ananiombea.


Kanitosheleza kwa haja zangu.
Sasa kwa upendo aniangalia,
Mwokozi wangu ni Mwokozi Wako.

Chorus
Ninakuombea, ninakuombea,
Ninakuombea rafiki yangu.

2. Baba yangu Amenipa ahadi


Kwa tarajio la kuwa Nae juu.
Punde Ataniita kule mbinguni,
Ee, natamani nawe uwe pale.

3. Nina nguo maridhawa nyeupe,


Inaningojea huko mbinguni.
,
Nitafurahi nawe ukivikwa.

4. Akikupata wambie wengine,


Ya kwamba Mwokozi wangu ni wako.
Omba Awalete wengine zizini,
Maombi yako yatajibiwa tu.

86. Mungu kazi Yako Tukufu


Glorious, glorious is the Work of God (NIH 344)

1. Mungu, kazi Yako tukufu,


Katika Sayuni, watakatifu,
Watamwona Yesu, mfano wa mtumwa,
Bwana wa rehema, Mwenye hekima.

Chorus
Utukufu wa ajabu, wenye dhambi waamini,
Utukufu wa ajabu, twapokea utajiri.

2. Kazi, Yako Umeijenga,


Ndani ya mitume, walitangaze
Neno Lako kwetu, walio Wako
Waipata nguvu na neema Yako.
3. Neno, Lake ni takatifu,
Likubali leo neno tukufu,
Makao ya Bwana, utayaona,
Roho waongoze, mfanane Nae.

87. Sikia! Habari njema


Hark! the gospel bells are ringing (NEH 283)

1. Sikia habari njema; ina sikika kote,


Ni habari ya wokovu kwangu mimi na wewe.
Na tumshukuru Mungu kwa kumtoa Mwanawe
Na wewe ukimwamini utapata uzima

Chorus
Kengele yalia, ya wokovu kwa wote,
Kengele yaita, yenye habari njema.

2. Sikia habari njema, karamuni twaitwa


Kuna msaada kwa wote, na wale wenye dhambi.
Yesu, Mkate wa uzima, kula ewe mwenye njaa
Wale walio na Kristo hawatatetereka.

3. Na niwe kama injili yenye ukweli Kwako,


Mwovu akinijaribu asipate nafasi.
Nivishinde vita vyake Roho aniongoze,
Aliyejazwa uzima na nguvu Yake Yesu.

4. Tutaimba wimbo mpya wenye furaha tele,


Wana wa Mungu njooni tukusanyike sote.
Upesi, Mfalme yuaja, tujiandae sote.
Kuwa waaminifu na tutaishi milele.
88. Una nafasi kwa Yesu?
Have you any room for Jesus? (NEH 285)

1. Una nafasi kwa Yesu? Aliyeondoa dhambi;


Abishapo mlango wako, umkaribishe ndani.

Chorus
Nafasi kwa Mfalme Yesu, neno Lake ulitii;
Ufungue moyo wako, Aingie moyoni.

2. Anasa ina nafasi, bali Yesu hawezi;


Kuingia moyo wako, mbona wewe humpendi?

3. Una nafasi kwa Yesu? Leo Akikuita;


Usimkatae, mwenzangu, ni bora kuitika.

89. Naujua mto mtukufu


I know of a river whose glorious stream (NIH 196)

1. Naujua mto mtukufu kweli salama njiani mwake,


, hakika nani aujua leo?

Chorus
Kijito cha utukufu, Ee njoo nafsi usisite!
Chatiririsha maji mazuri; hayo kwa ajili yako.

2. Pale penye mto huu mioyo ya watu imejazwa furaha.


Mwenye kunywa katika mto huu yunapumziko na amani.

3. Kina cha mto huu kina maji safi yenye burudiko kuu,
Huponya wagonjwa na huondoa hofu na niutakaso.

4. Maji ya kijito hiki ni Yesu katika maisha yetu,


Damu Yake ya thamani hutuosha dhambi na kuwa safi.

5. Mwenye kiu na aje anywe maji Roho asema njoo sasa;


Mtakasike na mtoke katika giza na Atakuwa nanyi!
90. Yesu Anaita
Jesus is calling (NEH 290)

1. Yesu anaita wapotevu, Anaita:


kunako dhambi Rehema Ametoa.

Chorus
Anaita, Anaita Yesu anaita njoo upate neema
(Tenor & Bass)
Yesu, Yesu anaita, Yesu, Yesu anaita,
Yesu anaita, anaita njoo upate neema.

2. Yesu anawapa pumziko wenye dhambi, wenye dhambi,


Sikia wito, lete mizigo je utampokea?

3. Yesu awangoja wenye dhambi njooni leo, awangoja,


Wote tubuni msichelewe wenye dhambi mwaitwa.

4. Yesu anateketeza dhambi msikie wito Wake


Watafurahi waaminio, Mwokozi awaita.

91. Ee njoo kwa Yesu


O come now to Jesus (NEH 295)

1. Ee njoo kwa Yesu Umwamini sasa, na Atakufanya upya.

Chorus)

2.
Kwa nini kupingana na Mwokozi Mwenye kusamehe dhambi?

3. Ee kimbilia kwa Yesu Mwokozi, ndipo utakapo shinda;


Na uwe na imani ya kitoto Anakuhitaji wewe.
92. Ya huruma na wokovu
Of compassion and salvation (NIH 250)

1. Ya huruma na wokovu injili kutoka juu;


Yahubiriwa kwa wote msaada uko karibu.
Wapotevu waongozwa wenye kiu wanyweshwa;
Ni msaada kamili toka kwenye chemchemi hai.

2. Mungu Baba wa huruma hii siri ya kipekee


Kupitia huruma hii wanyonge wanapona.
Kwa wanaosikiliza na kuhisi nguvu mpya,
Waitangaza injili Yake Yesu kwa wote.

3. Watumishi Wake Bwana wahubiri amani,


Wanazo habari njema kwa waliopotea.
Wapotevu waongozwa, wenye kiu wanyweshwa,
Ni msaada kamili toka kwenye chemchemi hai.

93. Yeyote anaenisikia


Whosoever heareth (NEH 308)

1. Yeyote anaenisikia, njoo kwenye chemchemi yenye uzima,


Ndani Yake Yesu hakuna kiu, atakae na aje.

Chorus
Mwenye kiu njoo Yesu akwita kupitia wito wao mitume,
Mlango wa neema umefunguliwa, atakae na aje.

2. Yeyote asikiae neno, alitunze na amebarikiwa,


Kuna neema tele nao wokovu, atakae na aje.

3. Mwenye nia na asichelewe, njoo kwenye toba na neema ilipo,


Sikia neno hai Lake Yesu, atakae na aje.
94. Niimbie kila mara
Wonderful words of life (NEH 310)

1. Niimbie kila mara maneno ya Yesu!


Nipate kuyatambua maneno mazuri.
Maneno mazuri yenye mafundisho.

Chorus
Ni mazuri, ya ajabu, yanao uzima!
Ni mazuri, ya ajabu, yanao uzima!

2. Kristo Yu mwenye kutoa maneno mazuri,


Mwenye dhambi usikie maneno mazuri.
Wenye kulemewa watapumzishwa.

3. Injili inasikika; maneno mazuri,


Msamaha ni kwa wote; maneno mazuri.
Wamfuatao Yesu watapata taji.

95. Kweli neema


Amazing grace (NEH 311)

1. Kweli neema ya ajabu iliniokoa.


Nilipotea dhambini sasa niko huru.

2. Neema iliyo nifunza na kunituliza.


Siku ile ya thamani nilipoamini.

3. Kwa hatari na mateso mimi nimekuja.

4. Mwili huu ujaposhindwa na kifo kukoma,


Nitapewa kila kitu furaha amani.

5. Dunia itayeyuka jua kuangaza;


Mungu Aliyeniumba adumu milele.

6. ,
Tutamsifu kila siku kuliko mwanzoni.
96. Rehema Zake
Endless compassion (NEH 313)

1. Rehema Zake, na upendo.


Rehema Zake zatoka juu.
Wenye dhambi wote, wamkirio Kristo
Wanaishi ndani Yake Bwana.

2. Katuokoa, tuko huru,


Katuokoa kwa rehema.
Katutoa kwenye dhambi na huzuni
Tutakuwa Naye siku zote.

3. Sasa ni Wako siku zote,


Nitakusifu siku zote.
Hata kwenye taabu nitabaki Kwako.
Kwako Bwana Wangu sipotei.

97. Nasikia sauti


I hear Thy welcome voice (NEH 318)

1. Nasikia sauti Yako Ee Bwana


Yaniita nitakaswe kwenye damu Yako.

Chorus
Nakuja Bwana, Nakuja Kwako.
Nioshe kwa damu Yako ya Kalivari

2. Ingawa nina dhambi, Wanipa nguvu.


Udhaifu wangu wote unaondolewa.

3. Wito Wake Yesu Unanifundisha.


Pendo, amani tumaini hapa na mbingu.

4. Yesu atambua kazi Yake kwetu.


Nakuleta neema Yake pale penye dhambi.

5. Yeye ndiye shahidi wa mioyo safi,


Tukiomba kwa imani atatusikia.
98. Nilisimama nje
(NEH 321)

1. Nilisimama nje, mwana mpotevu,


Nilijawa hofu:
Hofu ilizidi, je nitachelewa
Nishindwe ingia? Nikaomba nje,
Nikaomba nje.

2. Sasa natambua rehema za Bwana,


Alinitafuta hata kunifia.
Uchungu wa dhambi umeondolewa,
Yote yamekoma, Yesu niingie
Yesu niingie.

3. Nililia sana Uniweke huru,


Tumaini langu halikuwa bure,
Ukanitakasa na kunisogeza
Nikapata raha, na amani tele,
Na amani tele.

99. Kwa Yesu napata Wokovu


In Jesus I have found salvation (NEH 323)

1. Kwa Yesu napata wokovu na furaha ya mbinguni.


Niko huru kwa neema Yake, shetani kuangamizwa.

Chorus
Wokovu wangu ni kwa Yesu,
Upendo Wake thawabu kwangu.

2. Nasafiri kwenda nyumbani Yesu ndiye kiongozi.


Nitamsifu kwa neema Yake, nitamwabudu kwa mema.
100. Nimeyapata makao
ve found a place I love so well (NIH 128)

1. Kuna mahali napenda palipo na usalama,


Moyo wangu wafurahi, najitenga na dunia.

Chorus
Ee mahali pa amani patakatifu kwangu.
Nitaishi kwa amani, makao ya umilele.

2. Kupitia neno Lake Bwana Mwokozi wa kweli.


Hunitakasa kabisa kwa neema na upendo.

3. Mahali patakatifu na penye amani tele.


Pazuri panisubiri, nchi nzuri; juu mbinguni.

101. Nitwae hivi nilivyo


Just as I am (NEH 330)

1. Nitwae hivi nilivyo kupitia neno Lako,


Unaita wenye mizigo wapate pumziko.

2. Nitwae mimi kipofu vyote nitapata Kwako,


Nakuomba Wewe Bwana Kwako kuna uponyaji.

3. Hivi nilivyo natubu neema Yako Umetupa.


Ninajitoa sadaka kwa upendo Wako mwingi.

4. Nitwae hivi nilivyo nakuomba nisamehe.


Siku zote Uwe nami Kristo Ulinifidia.

5. Pendo Lako lanivuta kupitia neema Yako.


Tawala mawazo yangu yanifikishe mbinguni.
102. Furaha kuu, kuna Wokovu!
O boundless joy, there is salvation! (NEH 331)

1. Furaha kuu kuna wokovu! Kwangu mimi mwenye dhambi.


Niliye kuwa sistahili sasa ninayo nafasi, sasa ninayo nafasi.
Kwa upendo Wake mkubwa kwa mimi mwana mpotevu,
Kwa mimi mwana mpotevu.

2. Nafsi yangu itakusifu milele yote, Ee Bwana.


Kwa huruma Yako Mwokozi, nitakwimbia milele, nitakwimbia milele.
Ee injili takatifu! Kristo alitukomboa, Kristo alitukomboa.

3. Utukufu Wako Ee Bwana hautazimika kamwe.


Hata kwenye mawimbi mengi sitaogopa chochote, sitaogopa chochote.
Nikiwa pamoja Nawe, nitaubeba msalaba, nitaubeba msalaba.

4. Hata mauti ikinitwaa, sitakuwa peke yangu.


Kwako ninalo tumaini nitakuja mbele Zako, nitakuja mbele Zako.
Na kuimba kwa furaha nikikusifu milele, nikikusifu milele.

103. Leo ni siku ya furaha


O happy day (NEH 332)

1. Leo siku ya furaha, ya kumkiri Mwokozi.


Moyo umefurahia, wasimulia kwa wote.

Chorus
Furaha, furaha Yesu kaniosha dhambi,
Amenifunza kuomba, na kufurahi daima,
Furaha, furaha Yesu kaniosha dhambi.

2. Nimeapa kumpenda mwanzilishi wa upendo.


Tuijaze nyumba Yake kwa furaha na kwa nyimbo.

3. Tumekwisha kupatana, mimi Wake Yeye wangu.


Na sasa nitamwandama, nilikiri neno Lake.
104. Usinipite Mwokozi
Pass me not, O gentle Saviour (NEH 333)

1. Usinipite Mwokozi, unisikie;


Unapozuru wengine, usinipite.

Chorus
Yesu, Yesu, unisikie;
Unapozuru wengine, usinipite.

2. Kiti chako cha rehema, nakitazama;


Magoti napiga pale, nisamehewe.

3. Sina wa kutegemea, ila Wewe tu;


Uniponye roho yangu kwa neema Yako.

4. U mfariji wangu pekee; nani mwingine,


Duniani na mbinguni, ila Wewe tu.

105. Tabibu mkuu yu karibu


The great Physician (NEH 335)

1. Tabibu mkuu yu karibu, Yesu mwenye huruma;


Hutuletea furaha, sikia wito Wake.

Chorus
Imbeni malaika, sifa za Yesu Bwana,
Pekee limetukuka, jina Lake Yesu

2. Dhambi pia na hatia, ametuondolea


Twende Kwake kwa amani, hata Kwake mbinguni.

3. Huliona tamu jina, la Yesu Kristo Bwana,


Yuna sifa mwenye kufa, asishindwe na kufa.

4. Tukifika juu mbinguni, kumwona Bwana Yesu,


Tutaimba kwenye kiti, jina tukufu Yesu.
106. Damu imebubujika
There is a fountain (NEH 336)

1. Damu imebubujika, ni ya Imanueli,


Wakioga wenye taka husafishwa kweli.

Chorus
Husafishwa, husafishwa, husafishwa kweli,
Wakioga wenye taka husafishwa kweli.

2. Ilimpa kushukuru mwivi mautini;


Nami nisiye udhuru, yanisafi ndani.

3. Kondoo wa kuuawa, damu ina nguvu,


Wako wote kuokoa, kwa utimilivu.

4. Bwana tangu damu Yako kunisafi kale,


Nimeimba sifa Zako taimba milele.

107. Ndiyo bahari yenye neema


What a sea of grace (NEH 339)

1. Ndiyo bahari yenye neema, ni upendo toka kwa Yesu.


Wanyonge wanapata amani, ni Yeye Ametutakasa!

Chorus

Pendo Lako linitunze mpaka siku ya kufika mbinguni.

2. Kwa kupitia pendo la Yesu, hofu, mashaka vinakoma,


Yeye ni pendo toka kwa Mungu katukomboa, tuko huru.

3. Je, ni neema ya jinsi gani kufarijiwa na Mwokozi,


Anatupatia nguvu nyingi, tunaona upendo Wake.

4. Napata upendo na baraka; ndani ya muda mfupi tu!


Ninaipata amani tele, kwa neema napata vyote.
108. Bwana ututayarishe
Grant us, Lord, due preparation (NEH 341)

1. Bwana ututayarishe, tustahili mezani Pako! Ee njoo Bwana uingie.


Utuwezeshe wanao, tukaribie mbele Zako; tutangazie msamaha.

Chorus
Wewe ndiye Bwana, hatuna mwingine, Amen, Amen.
Sifa Kwako juu mbinguni, tuungane karamuni.

2. Mwaliko Wako mtukufu kwa karamu hii takatifu, kwa wote wakupendao.
Ee njooni mnaosikia, tukubali mwaliko Wake Ee njooni tuimarike.

109. Mfalme mwingi wa rehema


Host and King of grace and riches (NIH 291)

1. Mfalme mwingi wa rehema tuna shauku Nawe.


Na leo tuna
Chakula cha kidunia ijapo ni kitamu
Hakiishibishi nafsi, hii hulishwa na Mungu.

2 Ingawa hatuvioni vikombe vya thamani


Wala shangwe ya kidunia mezani pa Bwana,
Lakini mkate na kikombe hiki vyatolewa,
Penye neno la Mungu lisilo mfano wa kitu.

3. Amani nayo baraka, pendo, fadhili Zake,


Walio wahitaji hushibishwa kwa baraka,
Mateso na huzuni kuu vimesahaulika,
Waihisi mbingu kupitia pendo la Yesu.

4. Bwana ameketi pamoja na walio Wake,


Nae awapa karama za neema na rehema,

Machozi ya shangwe yatiririka kushukuru.


110. Mto watunza malisho
A river keeps the pastures green (NEH 344)

1. Mto watunza malisho wanapolishwa kondoo,


Kuna neno la mitume; wito wa Mchungaji Mwema.

Chorus
Sifa kwa Mwanakondoo, hutupatia neema.
Milki yenye furaha kwenye ushirika wetu,
Ngao ya kundi la kondoo tazama nyumbani kwetu.

2. Msamaha wa dhambi zetu Mwanakondoo kaubeba,


Katupatia wokovu na kututoa gizani.

3. Maneno Yake si bure, Akomboa wenye dhambi,


Mioyo yashuhudia kazi ya Mwanakondoo.

4. Mchungaji Anatuchunga kwa neema na mitume,


Kuwa kundi Lake Yesu furaha isiyo mfano.

111. Wakati mzuri nilipo amini


Beautiful, glorious moment (NIH 300)

1. Wakati mzuri ni pale, nilipo amini,


Kupitia kwa mtumishi nilipata nguvu.

Chorus
Sasa nimesamehewa moyo uko huru.
Katika roho nina Mungu, Amenipa neema.

2. Kwenye mji juu mbinguni ndiko nitaishi,


Huko kumejaa amani,

3. Nitakase vyote Bwana; moyo na akili,


Kwa kukufuata Wewe, nitabarikiwa.
112. Nimejaliwa amani
Blessed is the peace to my heart (NEH 346)

1. Nimejaliwa amani, ibubujikayo kwangu,


Kristo yungali ni mwema, huniweka niwe huru.
Nilikuwa mkosaji, dhambi zilinizidia,
Kweli Yeye ni muweza, damu Yake huniosha.

Chorus
Hunitakasa, hunitakasa.
Kweli Yeye ni muweza, damu Yake huniosha. (Safi)

2. Nimejaliwa amani niliyoisubiria,


Mwokozi kanifidia, kunipatia amani.
Kwenye chemchemi safi, kuna ukombozi kweli,
Siyo kwa matendo yangu, damu Yake huniosha.

3. Nimejaliwa amani, ujira na wema Wake,


Vinanisafisha dhambi najaliwa utukufu.
Amani nyingi moyoni, pendo la Yesu la pekee.
Kwake ninategemea, damu Yake huniosha.

113. Njooni tushiriki


Come, share the Lord (NEH 347)

1. Tumekusanyika hapa, katika jina la Bwana wetu Yesu;


Kupitia Yeye tumeunganishwa:

Njooni tule, njooni tunywe, tushiriki.


Hakuna mgeni hapa, wote tuwenyeji;
Tunapata msamaha, nasi tunasamehe.

2. Anamega mkate nasi, Bwana aliyefufuka yupo hapa;


Twampenda sana, ni mwenyeji wetu:
Njooni tule, njooni tunywe, tushiriki.
Tufamilia moja Yeye ndiye kichwa;
Yuko nasi ingawa, hatuwezi kumwona.

3. Nipunde tutaungana; na kuona utukufu Wake Mfalme;


Sasa tutashiriki karamu hiyo:
Njooni tule, njooni tunywe, tushiriki.
114. Ni chemchemi ya upendo
From J (NEH 348)

1. Ni chemchemi ya upendo, itokayo Kwake Yesu.


Ndiyo maji ya uzima, yanakata kiu yangu.

Chorus
Ee kijito cha neema, kinachotuponya.
Ee kijito cha neema, kinanikomboa.

2. Yabubujika kwa wote, kwa huruma Yake Yesu.


Inasafisha kabisa, inaponya maumivu.

3. Ee neema yabubujika yaniburudisha nafsi,


Inanitakasa dhambi, ili nifae mbinguni.

115. Nitakukumbuka
I will remember Thee (NEH 351)

1. Kwa unyenyekevu Bwana,


Hadi mwisho wa safari, nitakukumbuka.

2. Mwili Wako ulivunjwa, Uwe mkate wangu;


Damu Yako ya agano nitakukumbuka.

3. Natazama msalaba pale Kalivari;


Mwanakondoo kanifia, nitakukumbuka.

4. Nikikumbuka mateso Yako na upendo;


Hakika nakaza mwendo, nitakukumbuka.

5. Nitakapofumba mdomo, akili kukoma,


Ufalme Wako ujapo, Bwana nikumbuke.
116. Yesu kwa damu Yako
(NEH 352)

1. Yesu kwa damu Yako, nimepatanishwa.


Kwenye kijito hiki, nimetakasika,
Kwenye kijito hiki, nimetakasika.

Chorus
Nimepatanishwa kweli, nimepatanishwa kweli.
Ee Mpatanishi mwema, kimbilio langu,
Ee Mpatanishi mwema, kimbilio langu.

2. Yesu kwa damu Yako, nimepatanishwa,


Wewe umeniponya dhidi ya mateso,
Wewe umeniponya dhidi ya mateso.

3. Yesu kwa damu Yako, nimepatanishwa,


Kwako nimepumzika, shida zimekoma
Kwako nimepumzika, shida zimekoma.

4. Yesu kwa damu Yako, sasa niko huru,


Na tumaini langu, kuwa Nawe Bwana,
Na tumaini langu, kuwa Nawe Bwana.

117. Napumzika kwa Yesu


I (NEH 353)

1. Napumzika kwa Yesu, amani tele napata.


Ndilo tumaini pekee, dhambi zangu zasafishwa.

Chorus
Ee Yesu Mwokozi, kuwa Nawe Bwana.
Ninapumzika milele, milele.

2. Sasa naishi kwa Yesu, nguvu Yake tegemeo.


Ya ulimwengu yapita, nitadumu Kwake Bwana.

3. Kwa kupitia mitume, napata amani Yake.


Anatimiza ahadi ya kunipeleka Kwake.

4. Moyo wangu vumilia, mawimbi na shida nyingi.


Nitaikir
118. Nimekombolewa na Yesu
Redeemed, I am blessed in Jesus (NEH 357)

1. Nimekombolewa na Yesu, kwa njia ya damu Yake.


Na kwa huruma ya Kimungu, nina furaha ya kweli!

Chorus
Kombolewa na kombolewa kwa damu,
Kombolewa nina furaha ya kweli.

2. Nimekombolewa na Yesu, nashindwa kuelezea


Uwepo Wake wa ajabu, kwa pendo hunibariki!

3. Kwake mimi nitahudumu, kwa ari na kwa unyofu.


Moyo wangu umtukuze, kinywa changu kimwimbie!

4. Nimalizapo vita vyangu, nitahitimu kwa Bwana,


Nikitunza imani Kwake, nitapewa taji yangu!

119. Furaha kubwa sana


(NEH 360)

1. Furaha kubwa sana, kuokolewa kwa damu Yake Bwana, natakaswa.


Nimekuwa kiumbe kipya sasa. Naimba kwa furaha; Yesu mkweli.

Chorus
Ee asifiwe Bwana kwa upendo Wake,
Asifiwe Yeye ni mkombozi.

2. Furaha kubwa sana, kuokolewa mateso yamekoma, Mungu mwema.


Ameniangazia kwa neema tu. Sina mashaka tena, niko Kwake.

3. Furaha kubwa sana, kuokolewa kwa damu Yake Bwana, inaponya.


Na kisha ni furaha ya milele, majonzi yatakoma, Kwake Yesu.

4. Ee Yesu ninaimba sifa Zako Mwokozi Mungu wangu wa amani.


Kwako nashinda vita Bwana wangu neno Lako baraka, lifanyike.
120. Ndugu kaka na dada
Dear brothers and dear sisters (NIH 342)

1. Ndugu kaka na dada ndani Yake Kristo.


Tu viungo vya mwili Wake Bwana Kristo.
Mioyo yetu yawaka kwa mshikamano huu.

Chorus
Upendo Wake Mungu ni kipimo chetu.

2. Mwenye mizigo mingi, na chuki moyoni.


Hawezi kutambua, upendo wa kweli.
Pasipo na upendo, ni ngumu kufuata.

3. Adui anataka kututenganisha,


Kwa kuzipanda mbegu za kututawanya.
Lakini anashindwa tukishika neno.

121. Kuwa pamoja na Bwana


How blessed and glorious with Jesus (NEH 371)

1. Ni baraka ya jinsi gani, kuwa pamoja na Bwana.


Upendo Wako wa ajabu, sisi tumepewa bure.

Chorus)
Karibu, na Wewe twahisi upendo Wako
Karibu, na Wewe twahisi upendo Wako.

2. Tena huruma Yako Bwana, yatupatanisha sisi,


Ulimwengu hautambui, kupokea ni uzima

3. Tulitangatanga jangwani, tukikutafuta Wewe


Na ulipotuona Bwana, ulitupatia msaada.

4. Kupitia upendo Wake, tumestahili malisho,


Kwa neema na huruma Zake, hakika tumetakaswa.

5. Kwa matendo tutashukuru, kwa kututoa gizani.


Imarisha imani yetu, kwa heshima Yako Baba.
122. Yesu A
I heard the voice of Jesus say (NEH 374)

1. , Anipumzishe

2. Nilikwenda Kwake Yesu nilichoka sana,


Nikapumzika Kwake Akanifariji.

3.
Tena ya uzima bure, unywe uwe hai .

4. Nilikwenda Kwake Yesu, Alinipa maji,


Kiu yangu ikakoma sasa niko Kwake.

5. Yesu Aliniita, joo, Mimi ndiye nuru,


.

6. Nilimtazama Yesu, Yeye Nyota yangu,


Nitatembea nuruni hata mwisho wangu.

123. Ninasifu pendo la Mungu


I (NIH 221)

1. Ninasifu pendo la Mungu kupitia Yesu Kristo,


Siku zote lanivutia, ninasamehewa dhambi.
Nazama kwenye upendo huu kweli pendo Lake latosha.

2. Pendo hili la kirafiki shauku ya moyo wangu


Lanivuta karibu Nawe, kwalo najinyenyekeza.
Pendo la Mungu ni la kweli nimechagua pendo hili.

3. Nakupa moyo wangu wote Mwokozi mwema mkarimu


Ulitoa maisha Yako, sasa nimewekwa huru.
Ulinitoa kwenye dhambi najitoa Kwako daima.

4. Lidumu jina Lako Yesu katika maisha yangu


Pendo Lako Ee Yesu wangu lidumu moyoni mwangu.
Kwa maneno na kwa matendo Bwana uwe pamoja nami

5. Kupitia jina la Yesu Baba anadhihirika


Pendo na amani kwa neema vinatiririka leo.
Wenye dhambi watambuapo huja kwenye pendo hili ku
124. Nakupenda Bwana
Lord, more would I love Thee (NIH 236)

1. Nakupenda Bwana, nisikie,


Ninapokuomba kila siku,

Chorus
Ee Bwana Mwokozi,
Nakupenda, nakupenda.

2. Bila Wewe Bwana, sina raha,


Kwa sasa naona, wema Wako,
Na upendo Wako.

3. Japo ninabeba msalaba


Nitaendelea kukupenda
U chaguo langu.

4. Nitakapokoma duniani,

5. Nitakuwa Nawe kwenye enzi,


Nitavikwa taji ya kifalme,

125. Pendo ambalo ni nuru


O love, the golden sunshine bright (NEH 386)

1. Pendo ambalo ni nuru kwa watu wanyonge.


Linaponiangazia napata amani.
Giza latoweka penye pendo Lake Yesu.
Na wanyonge wanajazwa furaha mioyoni.

Chorus
Ee pendo la Mungu Baba, ni la kweli tangu kale.
Liko kwangu liko kwako linatuvutia Kwake.

2. Pendo toka msalabani liligusa moyo,


Na kunipatia nuru nami nikatubu
Najua Anipendaye mpaka kifo changu.
Moyo wangu Utamfuata tumsifu milele.
3. Nuru inayoondoa hofu na mashaka.
Ni Yesu Imanueli kwa milele yote.

126. Bwana kanipa amani kuu


Peace, O how precious (NIH 290)

1. Bwana kanipa amani kuu,


Kama zawadi Yake kwangu,
Rohoni mwangu amepanda,
Na hii ndio shauku yangu
Amani Yake na idumu.

2. Tangu Anipe amani hii,


Nimepumzika Kwake Bwana,
Mateso yote Alishinda,
Kwa neema kuu tuna amani,
Amani isiyo kipimo.

3. Na Utukuzwe ndani yangu,


Amani Yako iwe nami,
Baba mkarimu na mtoaji,
Tufungue macho tuone,
Amani Yako kila muda.
127. Pendo la Mungu lashinda kifo
The love of God (NEH 396)

1. Pendo la Mungu lashinda kifo.


Napata kupitia Mwanawe.
Pendo hilo limejaa uzima,
Faraja na tumaini kwangu.

Chorus
Pendo la Mungu hushinda kifo,
Nalipata kupitia kwa Yesu.
Pendo hilo limejaa uzima
Na hunipa moyo mnyenyekevu.

2. Wahisio pendo Lake Mungu,


Huvutwa karibu Naye Baba.
Huijaza mioyo Roho Wake,
Na hawaufuati ulimwengu.

3. Heri wenye mioyo ya upendo.


Hao hawatikisiki kamwe.
Heri kwao wenye mioyo safi,
Wanaofuata nyayo za Yesu.

128. Nikiwa na amani naye Baba


When peace with the Father (NIH 295)

1. Nikiwa na amani naye Baba,


Hata nikiwa na shida,
Moyo wangu utafurahia tu,
Ni shwari, ni shwari moyoni.

Chorus
Salama, rohoni
Ni salama, rohoni mwangu.

2. Mwanakondoo kabeba dhambi zangu,


Si sehemu, Bali zote.
Mara ngapi napokea rehema,
Nafsi yangu mtukuze Bwana.
3. Japokuwa mwovu atanitesa,

Yesu akafa pale msalabani,


Alimwaga damu nipone.

4. Ninaishi ndani ya Yesu pekee.


Roho ananiongoza.
Kwake kuna amani na wokovu,
Nafsi yangu umsifu Bwana.

129. Mpendao Bwana


Come ye that love the Lord (NEH 406)

1. Mpendao Bwana, njooni kwa furaha.


Imbeni nyimbo za raha, imbeni nyimbo za raha
Kwenye kiti Chake, kwenye kiti Chake.

Chorus
Twaenda Sayuni, mji mzuri Sayuni!
Na twende kule juu Sayuni, mji mzuri wa Mungu!

2. Mungu Atawala ulimwengu wote,


Amiliki hata anga, amiliki hata anga
Na bahari yatii, na bahari yatii.

3. Sayuni chipua mazao mazuri


Kabla kufika mbinguni, kabla kufika mbinguni
Mji wa dhahabu, mji wa dhahabu.

4. Tutakapomwona masumbuko basi,


Mto Wake wa neema, mto Wake wa neema,
Tutakunywa maji, tutakunywa maji.
130. Moyo wangu hima uende mbinguni
Forth, forth, my heart, to heaven (NIH 395)

1. Ee moyo wangu hima uende mbinguni


Ulimwenguni humu hakuna pumziko.
Mwanakondoo wa Mungu Ameandaa makao
Ya kupumzika Enenda mbinguni.

2. Uwapo kifungoni pambana ushinde,


Mwanakondoo kalipa deni lako lote,
Bendera yapepea alipo roho Wake
Ni penye pumziko Enenda mbinguni.

3. Sayuni yapendeza Nae Mwanakondoo


Ningekuwa na mbawa ningeruka sasa
Kwa shangwe ya ushindi wamkumbatia Bwana
Kwa shangwe na pendo Enenda mbinguni.

4. Shauku yangu iwe ni mapenzi Yako,


Nakupa moyo wangu, ufanye Wako tu,
Nitakusubiria nisikie Useme

131. Rohoni mwangu


I see in spirit (NIH 400)

1. Rohoni mwangu naiona enzi,


Naweza rithi nyumba ya milele!
Kwa furaha kuu najikabidhi
Kwa neema nipokee juu mbinguni!

2.
Jina Lako Ee Bwana litukuzwe.
Shauku yangu ni siku ile
Yakurudi Kwake Yesu Kristo.

3. Shukrani Kwako nimeona enzi;


Raha yaningoja juu mbinguni
Nistahirishe uniruhusu
Kuingia kwenye utukufu!
132. Twangojea ujio Wako Bwana
O Son of God, we wait for Thee (NIH 398)

1. Kwa upendo twangojea ujio Wako Bwana.


Muda utayari japo wengine wamechoka.
Mwenye kuamini kwa furaha atabakia na kumlaki Mwokozi

2. Twangojea kwa saburi hata kwenye mateso.


Ulikufa msalabani kulipa deni zetu.
Kwanini nasi tusibebe misalaba yetu mpaka Bwana ajapo.

3. Twakungojea kwa shauku na tumaini kuu.


Twahisi ukaribu na macho yashuhudia.
Twapenda tupumzishwe kwa amani na furaha maisha ya mbinguni.

133. Mikononi mwa Yesu


Safe in the arms of Jesus (NEH 421)

1. Mikononi mwa Yesu, kifuani Mwake,


Mapenzi yanilinda, nitapumzika.
Sauti za sikika zenye furaha kuu
Walio kombolewa wakimtukuza.

Chorus
Mikononi mwa Yesu, kifuani Mwake
Mapenzi yanilinda nitapumzika.

2. Mikononi mwa Yesu tumesalimika,


Maonjo hayawezi kunidhuru kule.
Kutoka mashakani sasa niko huru
Ni kitambo kidogo machozi yafutwa.

3. Yesu ni kimbilio, Yeye kanifia


Yeye Mwamba wa Kale ntamtumaini.
Nitakusubiria hata pambazuko
Na nitabaki hivyo hata asubuhi.
134. Bi harusi asubiri
The bride has waited, O so long (NIH412a)

1. Bi harusi asubiri ujio Wako Bwana.


Utakuja lini Bwana kutimiza ahadi?
Uwepo Wako, baraka, hakuna kilicho mfano?

2. Twahisi uwepo Wako, wanao twakusifu.


Kupitia neno Lako tustahilishe Bwana.
Usitunyime baraka, kubali tukakuone.

3. Wakati wote tukeshe taa zetu na ziwake


Kwa mafuta Yako Bwana tukimngoja ajae
Tusikie tarumbeta Bwana harusi ajapo.

4. Shauku yetu Ee Bwana kushiriki karamu.


Ee Yesu tunakungoja na mavazi meupe.
Twatazama juu kwa shangwe tena twapaza sauti:

135. Kwa Kristo Bwana uwe mwaminifu


To Christ, the Lord, be faithful (NEH 430)

1. Kwa Kristo Bwana wetu, uwe mwaminifu,


Mpaka Ajapo tena kwao waaminifu,
Yuaja na utukufu mkuu. Kesha na uwe tayari

Chorus
Tunza, tunza itunze imani yako.
Siku ile ya Bwana sasa iko karibu
Twaifanya kazi kama agizo tukashiriki karamu.

2. Walio waaminifu watavikwa taji,


Tena iko tayari kwa uzima wao,
Kando ya mto wa uzima watamwona Mungu wao.

3. Itakuwa furaha kwao waaminifu,


Nao wenye ahadi watafunuliwa.
Uwe mkweli hata mwisho mpaka nchi ya ahadi.
136. Atakuja, Atakuja
When He cometh (NEH 434)

1. Atakuja, Atakuja, vito vikusanywe,


Vito Vyake vya thamani, wapenzi Wake.

Chorus
Kama nyota za mbingu, watangára kwa Mungu;
Wapenzi ni watoto kwa taji Yake.

2. Atachanga, Atachanga vito kwa Ufalme;


Vito vyote vya thamani, wapenzi Wake.

3. Ni watoto, ni watoto, waitwao vito;


Ni vito vya Yesu Kristo, wapenzi Wake.

137. Lini ujio Wako Ee Bwana?


When strikes the hour? (NEH 435)

1. Lini ujio Wako Ee Bwana? Natamani mji ule,

Ulimwengu umejaa taabu, kule nitakuwa na furaha,


Ee natamani kwenda nyumbani kule kwangu mbinguni.

138. Sayuni mji mzuri


Beautiful, glorious Zion (NEH 437)

1. Sayuni mji mzuri na mtakatifu,


Wale waliolemewa wanapumzishwa.

Chorus
Sayuni mji mzuri kwa wabarikiwa
Natamani kufika huko nipate pumziko.

2. Nijazwapo na shauku natazama Kwako


Unipe uvumilivu na nguvu njiani.

3. Kwenye enzi ya Mwokozi nafsi zafurahi


Nyimbo mpya zasikika milele daima.
139.
Beyond, where clouds no more appear (NIH 438)

1. , kule kuna raha; usiku hakuna.


Yameandaliwa sasa makao mbinguni.

Chorus
Nina nyumba mbinguni juu, Mungu kaijenga,
Ndiko makao ya Mungu, nitaishi huko.
(Alt&Tnr: Ishi huko).

2. Kunametameta huko, nuru yatawala


Hata kifo kimeshindwa hakina nafasi.

3. Hatia na dhambi zote vitabaki hapa,


Nataka kuwa na Mungu niishi nyumbani.

140.
I have a home beyond the river (NEH 444)

1. Ah!
Nita

Chorus

, nitaishi Naye Bwana.

2. Muda sasa unakwisha tutangaze injili.


Punde tutanyakuliwa tusimame imara.

3. Itakuwa shangwe kubwa kuwaona wapendwa.


Zaidi itakuwa kumwona Mwokozi wetu.

4. Hata kama shida nyingi duniani tulipo,


Kule mbinguni ni raha hakuna taabu tena.
141. Makao ya Bwana Yesu
I know a realm where Jesus dwells (NEH 445)

1. Makao ya Bwana Yesu ni mazuri kweli.


Malaika wanamtukuza siku zote.

Chorus
njooni wote , wanaimba: njooni wote .
Uzuri wa nyimbo za mbinguni unanivutia.
Nyumbani karibu.Uzuri wa nyimbo za mbinguni unanivutia.

2. Mwokozi Anatuita Kwake tupumzike.


Malaika wanaimba kifuani Pake.

142. Nyumbani kwangu ni mbinguni


O the home of my soul is on high (NIH 435)

1. Nyumbani kwangu ni mbinguni mbali na matatizo yote,


Wale waliokombolewa wanamtukuza Mungu Baba.

Chorus
Kule juu, kule juu; nyumbani kwangu ni mbinguni.
Kule juu, kule juu; nyumbani kwangu ni mbinguni!

2.
Daima pamoja na Bwana Aliyetukomboa sisi.

3. Ee Bwana wangu Ulie juu, Wewe, Ndiwe Mwokozi wangu!


Nivute nikukaribie, na kwa pendo Lako nidumu.
143. Maelfu kwa maelfu
Ten thousand times ten thousand (NEH 453)

1. Maelfu kwa maelfu wenye nguo safi


Waliokombolewa wapanda Sayuni.
Hao ndio washindi wameoshwa dhambi
Milango ifunguke waingie ndani.

Chorus
Haleluya, haleluya, Kristo Katufia.
Haleluya,haleluya, Kwake tuko huru.

2. Mbinguni kwasikika nyimbo za washindi


Milio ya vinumbi kama bahari kuu.
Uzuri ulioje tabu ikiisha,
Na Mungu atawapa ujira washindi.

3. Kwa pendo Lako Bwana na kujitoa Kwako,


Ukatufia sisi dhambi ikafutwa.
Mbinguni wanaimba kitini pa enzi,
Na wote duniani wanapigania.

4. Furaha ilioje tukishaonana


Nao wapendwa wetu na Bwana Mwokozi.
Wajane na yatima hawahofu tena.
Na upweke kukoma, machozi kufutwa.

144. Mfariji Yuaja


The Comforter has come (NEH 477)

1. Habari njema hii ifike kwa wote, wale wenye shida na taabu nyingi;
Wakristo tupaze sauti kwa shangwe Mfariji yuaja.

Chorus

Habari njema hii ifike kwa wote Mfariji yuaja.

2. Usiku wapita sasa alfajiri, yote yale ya kutisha yamenyamaa.


Tazama milima sasa kumekucha. Mfariji yuaja

3. Mfalme yuaja kuziponya nafsi, kuzikomboa zote zilizofungwa.


Wimbo wa ushindi wasikiika kote. Mfariji yuaja.
145. Mwaka uko mwishoni
The year so still is ending (NIH 33)

1. Mwaka uko mwishoni, moyo vumilia.


Mungu ni mwaminifu kwa mapito yetu.
Yeye pekee Ajua tuliyopitia,
Majeraha na taabu pia na huzuni.

2. Kwanini furaha, amani havidumu?


Kwanini hatunao marafiki zetu?
Macho hata midomo yao vimefumba.
Utuponye twaomba; kwa upendo Wako.

3. Tusisahau tena; tukajisahau,


Ulimwenguni hapa hatuna makazi.
Makao yameandaliwa juu Sayuni.
Kwa waliobatizwa, huko ndiko kwetu.

4. Twapanda kwa machozi mbegu duniani,


Kwenye nyumba ya Baba kwatawala shangwe.
Bwana tusaidie safarini mwetu.
Na Uwe nasi Bwana tufike mbinguni.
.

146. Nilimwaga damu Yangu


I gave my life for thee (NEH 493)

1. Nilimwaga damu Yangu ya thamani,


Iwe ni fidia, kwa mauti yako.
Nilimwaga damu Yangu, Umenipa nini?
Nilimwaga damu Yangu, Umenipa nini?

2. Niliacha nuru, nyumbani mwa Baba,


Kuja duniani, hapa kwenye giza.
Niliacha enzi Yangu, Ulinipa nini?
Niliacha enzi Yangu, Ulinipa nini?

3. Niliteswa sana, Siwezi eleza,


Nilivumilia upate kupona.
Nilivumilia yote, Umenipa nini?
Nilivumilia yote, Umenipa nini?

4. Nililetwa hapa, kutoka mbinguni,


Nikuweke huru, kwa toba na pendo.
Ninaleta tunu kwako, Ulinipa nini?
Ninaleta tunu kwako, Ulinipa nini?
147. Yesu kwa imani
My faith looks up to Thee (NEH 495)

1. Yesu kwa imani, nakutumaini peke Yako;


Nisikie sasa, na kunitakasa
Ni Wako kabisa tangu leo.

2. Nipe nguvu pia za kusaidia, moyo wangu;


Ulikufa Wewe wokovu nipewe
Nakupenda Wewe Bwana wangu.

3. Hapa nazunguka katika mashaka na matata;


Palipo na giza Utaniongoza,
Hivi nitaweza kufuata.

4. Nikiwa mzima nivushe salama mautini;


Sina hofu kamwe Ukiwapo nami,
Nami nikwandame siku zote.

148. Alidharauliwa na Aliumizwa


O sacred Head, now wounded (NIH 43)

1. Alidharauliwa na aliumizwa,
Alivikwa taji ya miba kwa dhihaka.
Awali Alipambwa kwa sifa potofu.
Alidhihakiwa na kutukanwa Bwana.

2. Walikutemea mate usoni pako.


Japo mbele Zako hakuna awezaye,
Walififisha rangi Yako hata macho,
Lakini hakuna nuru zaidi Yako.

3. Ee Bwana dhambi zangu zilikudhoofisha


Na kwa mateso Yako, umenisamehe.
Sikustahili Kwako, na Usijifiche,
Ee Mwokozi, U furaha yangu kwa neema.

4. Bwana ninakuomba niwe Wako kweli,


Hata kifo kijapo Uwe nami Bwana,
Hofu ikinisonga moyoni ni taabu,
Kwa unyenyekevu Bwana Unikumbuke.

5. Hata nikitoweka Uwe msaada wangu,


Ee Bwana taswira Yako juu ya msalaba,
Iwe mwongozo wangu katika imani,
Kwako moyo wangu umefungamanishwa.
149. Mwamba wenye imara
Rock of Ages, cleft for me (NEH 498)

1. Mwamba wenye imara, Kwako nitajificha;


Maji hayo na damu, yaliyotoka Kwako,
Hunitakasa dhambi, Hunifanya mshindi.

2. Kwa kazi zote pia, sitimizi sheria,


Nijapofanya bidii, nikilia na kuudhi,
Hayaishi makosa, ndiwe wa kuokoa.

3. Sina cha mkononi, naja msalabani;


Nilitupu, nivike, ni mnyonge nishike;
Nili mchafu naja, Nioshe nisijafa.

4. Nikungojapo chini, nakwenda kaburini,


Nipaapo mbinguni, nakukwona enzini;
Roho yangu na iwe, rahani Mwako Wewe.

150. Kristo amefufuka


Christ the Lord is risen today (NEH 508)

1. Kristo amefufuka, Alleluia!


Mbingu na nchi imba: Alleluia !
Furahia ushindi, Alleluia!
Mbingu na nchi imba: Alleluia !

2. Ukombozi kamili, Alleluia!


Naye kashinda vita, Alleluia!
Mauti imeshindwa Alleluia!
Paradiso i wazi Alleluia!

3. Mfalme wetu yu hai, Alleluia!


Wapi uchungu Wako? Alleluia!
Kifo Chake wokovu, Alleluia!
Wapi kushinda Kwako? Alleluia!

4. Twatamani kumfuata, Alleluia!


Kumfuata Aliye juu, Alleluia!
Tutafufuka Naye, Alleluia!
Kaburi hata mbingu, Alleluia!

5. Bwana wa mbingu na nchi, Alleluia!


Atukuzwe na wote, Alleluia!
Tumshangilie sasa, Alleluia!
Sifuni ufufuo, Alleluia!
151. Mvike taji nyingi
Crown Him with many crowns (NEH 510)

1. Mvike taji nyingi Mwanakondoo wetu,


Sikia nyimbo za mbingu zote zamtukuza,
Nafsi yangu amka mwimbie Mwokozi,
Yeye Aliyetufia ni Mfalme milele.

2. Ni Mwana wa Mungu tangia zamani,


Wote twamfuata mvikeni taji Bwana Yesu,
Yeye azijua shida zetu zote,
Yeye huzibeba shida zao wampendao.

3. Bwana wa amani nguvu Zake ni kuu,


Hizo hutuliza vita, tumsifu kwa sala
Utawala Wake wadumu milele,
Amepambwa kwa maua ya harufu nzuri.

4. Bwana wa uzima, Alishinda kifo


Na Alileta ushindi kwa walio Wake
Sasa twamwimbia Aliyekwenda juu,
Na Alileta uzima kwa mateso Yake.

152. Yesu Kristo yu hai


Jesus Christ is risen today (NEH 513)

1. Yesu Kristo yu hai, Alleluia!


Siku tukufu kwetu, Alleluia!
Kateswa msalabani, Alleluia!
Ili Atukomboe, Alleluia!

2. Tumwimbie tumsifu, Alleluia!


Kristo ni Mfalme wetu, Alleluia!
Ameshinda kaburi, Alleluia!
Ili Atuokoe, Alleluia!

3. Kwa maumivu Yake, Alleluia!


Tulipata neema: Alleluia!
Ndiye Mfalme wa mbingu, Alleluia!
Malaika waimba, Alleluia!

4. Tumwimbie Mungu juu, Alleluia!


Na tumsifu milele, Alleluia!
Enyi jeshi ya mbingu, Alleluia!
Baba, Mwana na Roho, Alleluia!
153. Wakristo sasa twimbe
Sing, all you Christians (NIH 66)

1. Wakristo sasa twimbe kwa shangwe kuu,


Msifu Bwana Katuangazia,
Paza sauti zenu kwa furaha.
Yesu ni mshindi Amefufuka!
Yesu ni mshindi Amefufuka!

2. Amani kwenu maneno mazuri,


Aliyefufuka Awaita.
Na fungueni milango kwa wote,
Njoo kwa Mwokozi kuna amani.
Njoo kwa Mwokozi kuna amani.

3. Tuandae Bwana tuwe washindi,


Twakuamini U mwenye nguvu.
Nguvu za ulimwengu ni dhaifu,
Twapenda tuwe Nawe daima.
Twapenda tuwe Nawe daima.

154. Nitakupokeaje?
O, how shall I receive You? (NIH 3)

1. Nitakupokeaje Ee Bwana Ulivyo?


Mataifa yote yakungoja kwa hamu.
Ee Bwana Mtakatifu Wewe ni taa yangu.
Niongoze kiroho Upendezwe nami.

2. Matawi ya mitende yapamba Sayuni,


Nami nitakuimbia zaburi za sifa.
,
Kwa shangwe nitasifu jina Lako Bwana.

3. Je, Hukuteswa sana kunipa amani?


Mwili na Roho Yako vililia sana.
Nilikuwa gizani Ukanipa nuru,
Mwokozi kwa furaha Ulinikomboa.

4. Hata kwenye kifungo Uliniokoa,


Dhambi nayo hatia Bwana nisamehe.
Na Utanitukuza kwa hazina Yako,
Siyo kama hazina za ulimwengu huu.
155. Ndani ya hori
Away in a manager (NEH 533)

1. Ndani ya hori hakuna malazi,


Mtoto Bwana Yesu kalazwa chini,
Nyota angani zatoa ishara,
Mtoto Bwana Yesu kalazwa chini.

2. ,
Lakini Bwana Yesu hakulia.
Nakupenda Yesu unitazam,
Na Uwe karibu mpaka kuchapo.

3. Kaa nami Bwana Yesu nakuomba,


Kaa nami milele na unipende.
Bariki watoto kwa wema Wako,
Tujaze ya juu tukaishi Nawe.

156. Malaika waimba


Hark! the herald angels sing (NEH 544)

1. Malaika waimba: Mfalme amezaliwa.


Amani na rehema, vimetupatanisha.
Mataifa imbeni pamoja na washindi
Kule Bethlehemu Kristo amezaliwa.
Malaika waimba, Mfalme amezaliwa.

2. Kristo Bwana wa mbingu tangu milele yote,


Hakika kazaliwa na bikira halisi.
Ametoka enzini kuja ulimwenguni
Malaika waimba, Mfalme amezaliwa.
Malaika waimba, Mfalme amezaliwa.

3. Ni Mfalme wa amani ametoka mbinguni


Jua la haki, ndiye atumulikiaye.
Amejivua enzini Alivyo na mapenzi
Apate kutuponya na kutuzaa upya.
Malaika waimba, Mfalme amezaliwa.

4. Njoo Bwana tunaita, kaa mioyoni mwetu


Amsha mbegu bora, zimpinge shetani.
Utu ule wa kale, uweze badilishwa.
Na ule mpya uje, urudishe upendo.
Malaika waimba, Mfalme amezaliwa.
157. Ni usiku wa manane
It came upon the midnight clear (NEH 546)

1. Ni usiku wa manane, wenye utukufu,


Malaika waliimba na kusujudia,

Sauti zilisikika, kutoka mbinguni.

2. Malaika walishuka kuleta amani,


Waliimba nyimbo zao, zakuwafariji,
Waliokosa amani waimba kwa shangwe,
Wasikika pande zote tusikie sifa.

3. Sogea karibu ndugu, mwenye kusumbuka,


Wewe unayeteseka, kwa mapito mengi,
Tazama kwapambazuka, jifiche mbawani,
Pumzika ewe mchovu, sikiliza sifa.

4. Na siku zaenda mbio, manabii wanena,


Tangu kale hata sasa, neema imekuja,
Amani itafunika, ya kale yapita,
Ulimwengu unasifu, sikiliza sifa.

158. Wakristo njooni


O come, all ye faithful (NEH 550)

1. Wakristo njooni njooni kwa furaha,


Ee njooni, Ee njooni Bethlehemu.
Njooni mwone Mfalme kazaliwa.

Chorus
Ee njooni tumwabudu, Ee njooni tumwabudu,
Ee njooni tumwabudu Kristo Bwana.

2. Mungu wa Miungu, Mwanga wa Mianga


Kawa radhi kuzaliwa;
Mungu wa kweli, wala si kiumbe.

3. Malaika imbeni kwa shangwe!


Mbingu zote zijae sifa!
Msifuni Mungu Aliye mbinguni;

4. Twakusalimu Bwana mwema,


Utukufu uwe Kwako;
Neno la Bwana limekuwa mwili;
159. Muda wa shangwe
O thou joyful time (NIH 23)

1. Muda wa shangwe wenye baraka,


Noeli hii takatifu!
(Kristo Mwokozi Amezaliwa.
Njoo wote sasa tumetakaswa!)x2.

2. Muda wa shangwe wenye baraka,


Noeli hii takatifu!
(Kristo ni nuru yenye wokovu.
Njoo wote sasa tumetakaswa!)x2.

3. Muda wa shangwe wenye baraka,


Noeli hii takatifu!
(Msifuni Bwana kwa utukufu.
Njoo wote sasa tumetakaswa!)x2.

160. Usiku tulivu!


Silent night, holy night! (NIH 26)

1. Usiku tulivu! Usiku angavu!


Alipozaliwa Mwana Mtoto Mtakatifu ni Bwana.
Amezungukwa na amani ya mbingu.

2. Usiku tulivu! Wachunga wa hofu;


Walisikia sauti Malaika walipoimba
Kristo kazaliwa Kristo na Mwokozi.

3. Usiku tulivu! Ni Mwana wa Mungu;


Ametuletea nuru ukombozi pia na neema
Yesu kazaliwa Yesu kazaliwa.
161. Wachungaji walikesha
While shepherds watched their flocks (NEH 562)

1. Wachungaji walikesha wakichunga kundi.


Malaika alishuka akawaangazia.

2. ,
Naleta habari njema kwenu watu wote .

3. Kwenye mji wa Daudi leo kazaliwa,


Mwokozi na Kristo Bwana, hii ndiyo ishara;

4. Huyo Mwana wa mbinguni ameonekana.


Am

5. Walipokwisha yanena, malaika hao.


Waliimba wimbo huo wakufurahisha.

6. Utukufu kwa Mungu juu dunia amani.


Kwa aliowaridhia sasa na daima .

162. Tunakuomba Bwana


Lord, with fervence do we pray (NEH 572)

1. Tunakuomba Bwana ubariki ndoa hii.


Maisha yao yote wawe Wako kabisa,
Weka agano lao kwa nguvu toka Kwako,
Na angaza pendo Lako,
Katika mioyoni yao, Wajalie katika maisha yao yote.

2. Bariki kazi zao na mahitaji yao.


Na kwa moyo wa kweli wakikufuata Wewe,
Wawapo wahitaji Uwapatie Bwana
Mahitaji yao yote,
Mwaminifu wa kweli Wajalie faraja na furaha moyoni.

3. Na wawe na umoja kwa matunda ya Roho,


Wawe bega kwa bega kama ulivyo sema
Waongoze salama mpaka wafike mwisho,
Bwana Uwape kukesha
Ni kwa ajili Yako wajaponyakuliwa waje wavae taji.
163. Twaiweka wakfu nyumba
We dedicate, now Lord, to Thee (NEH 581)

1. Sasa twaiweka wakfu nyumba iwe Yako, Bwana, kwetu ni kimbilio.


Humu tutapumzishwa kupitia neno Lako ambayo ni mwongozo.
Utawale, tutakase tukutumikie Wewe; ibariki nyumba hili.

2. Bwana, nyumba ya maombi uiweke wakfu, Kwako ikupendeze Wewe.


Humu tusikie neno na tupate neema Yako, tujazwe na baraka.
Umoja na usafi moyoni iwe lengo letu Ili tupate amani.

164. Ndani ya mioyo hii


Within these hearts (NEH 584)

1. Ndani ya mioyo hii, Bwana, robo karne yapita,


Ndoa yao imejazwa upendo na rehema,
Wanakuletea sifa, wakikushukuru Wewe.
Kwa utukufu Wako Bwana, umewalinda.

2. Wastahili sifa Bwana kwa uongozi Wako,


Kwa moyo wameitunza imani Yako Wewe.
Twakushukuru, Ee Bwana tunaungana na Wewe.
Amani Yako kwao, wakuamini Wewe.

165. Kibarikiwe kifungo


Blest be the tie that binds (NEH 585)

1. Kibarikiwe kifungo, kitufungiacho mioyo,


Ushirika wetu wa fikira zetu kama ule wa mbinguni.

2. Mbele ya enzi ya Baba, dua zetu twaziomba;


Hofu zetu na matumaini yetu, hayo ni pamoja kwetu.

3. Huzuni zetu twashika, na mizigo yetu pia,


Ndani yao yote twashirikiana, hata katika kulia.

4. Tutawanyikapo mbali, hivyo yatufadhaisha;


Lakini tungali pamoja rohoni, hata tutakutanika.
166. Mungu awe nanyi daima
God be with you (NEH 586)

1. Mungu awe nanyi daima; hata tuonane tena,


Awachunge kwa fadhili; Mungu awe nanyi daima.

Chorus
Hata twonane huko juu, hata twonane Kwake kwema.
Hata twonane huko juu, Mungu awe nanyi daima.

2. Mungu awe nanyi daima; ziwafunike mbawaze,


Awalishe awakuze; Mungu awe nanyi daima.

3. Mungu awe nanyi daima; kila wakati wa shari,


Awalinde hifadhini; Mungu awe nanyi daima.

4. Mungu awe nanyi daima; Awabarikie sana,


Awapasulie kina; Mungu awe nanyi daima.

167. Tushikamane muda unapita


(NEH 588)

1. Tushikamane muda unapita,


Hapa twapita na tu wageni.
Furaha yetu sasa imekwisha,
Pumziko letu ni juu mbinguni.

Chorus
Tushikamane kwa Kristo Mkombozi;
Tushikamane mwende salama!

2. Tusonge mbele kwa shauku kubwa,


Tufanye kazi kuliko mwanzo.
Kwa hakika na kwa upendo mkubwa,
Bidii yetu ni kwenda mbinguni.

3. Kristo ni chanzo cha furaha yetu,


Wamtumikiao wako huru.
Katika jina la Yesu Mwokozi,
Ndugu wapendwa mwende salama.
168. Ni Shangwe, Mfalme Yuaja!
O great joy, your King shall come! (NIH 40)

1. ,
Ee nafsi: Mfalme yuaja, tazama, niko tayari.
Bwana ingia ndani, vyote ni vyako Wewe.

2. Njoo na uyaondoe machukizo yote Bwana


Takasa nyumba Yako, kwa dhambi niliiharibu.
Dhabihu Yako Bwana, utakaso wa kweli.

3. Uje kwa ushirika, humo twapata wokovu.


Ishi ndani yetu, na tushiriki mwili Wako.
Bwana uishi nami, yawe makao Yako.

4. Uje katika Roho, ambamo Watufundisha.


Wewe watuongoza, kuja Kwako juu mbinguni.
Katika siku hiyo, nasema joo, Ee Bwana .

169. Mkombozi wangu Yu hai


I know that my Redeemer lives (NIH 69)

1. Mkombozi wangu Yu hai, nafsi imefurahia.


Kwa mwangaza wa pasaka, na usiogope nafsi.
Ni mwangaza wa pasaka, Ee nafsi usiogope.

2. Mkombozi wangu Yu hai, nafsi imefurahia


Alishinda hata giza, Alishinda hata kifo.
Alishinda hata giza, Alishinda hata kifo.

3. Mkombozi wangu Yu hai, nafsi imefurahia


Uwe kimbilio langu, Uwe mkate wa uzima
Uwe kimbilio langu, Uwe mkate wa uzima.

4. Mkombozi wangu Yu hai, nafsi imefurahia.


Moyo Wake uwe wangu,
Moyo Wake uwe wangu,
170. Tumaini langu, Bwana
On Your ascension, Lord, alone (NIH 70)

1. Tumaini langu, Bwana, siku ya kupaa Kwako.


Umeniondolea hofu, pamoja na woga.
Mungu Baba amsubiri, Mwanawe na wateule kuungana pamoja.

2. Bwana Ananiandalia makao mbinguni.


Itakuwa shangwe pamoja juu kwenye Ufalme.
Kwa neema umeniita, Moyo umejawa furaha kwa ujio Wako.

3. Ee Bwana, kwa neema Yako, siku ya kupaa kwangu,


Nionyeshe tunda la Roho lililojaa shangwe,
Siku ya kurudi Kwako, nibadirishwe niungane Nawe juu mbinguni.

171. Penye Roho wa Mungu


(NIH 76)

1. Penye Roho wa Mungu pamebarikiwa,


Akiwa kiongozi ataturehemu.
Roho Wake Mungu, nuru, amani yetu,
Na kwa msaada Wake tutajazwa hekima.

2. Kwenye shida na taabu Atatufariji.


Hatusumbuki tena, katuweka huru.
Anatuongoza na anatuchunguza,
Kwa waliopotea anawarejesha.

3. Na nguvu za upendo na utakatifu,


Katupatia sisi kwa furaha kubwa.
Mungu ni muweza, hutuongoza sisi,
Yeye ni mwenye nguvu Atatufikisha.
172. Roho, Unifundishe
Holy Spirit, teach Thou me (NIH 81)

1. Roho, unifundishe, maarifa pia hekima.


Yesu kwa msaada Wako natambua U Mwokozi.
Wewe pekee unaweza kuniongoza kwa Baba.

2. Unihakikishie, nuru Yako itawale.


Nibaki Kwako pekee, kwenye giza niokoe.
Nitende mapenzi Yako niijue kweli Yako.

3. Nioshe nitakate, uniweke wakfu Kwako.


Kwako kuna amani, hekima pia ukweli.
Ni heri wenye karama zitokazo juu mbinguni.

4. Kwako napata vyote: baraka hata wokovu.


Fanya makao kwangu, nifanye kiumbe kipya.
Umeondoa unyonge sasa ninastahimili.

173. Ewe Roho Mtakatifu


Filled with truth and life, O Spirit (NIH 82)

1. Ewe Roho mtakatifu,


Utuwezeshe tupate kulifikia lengo.
Utupatie amani itokayo juu mbinguni.

2. Tumefunikwa na giza, Roho utuongoze.


Kweli Yako iwe njia kuelekea nuruni.
Roho Mtakatifu tupe nguvu tutangaze neno.

3. Ewe Roho mtakatifu kutoka juu enzini,


Dhihirika ndani yetu tufanane na Yesu.
Utuongoze daima tujazwe baraka Zako.
174.Ee Bwana tutoe dhambini
O Lord, free us from guilt (NIH 93)

1. Ee Bwana tutoe dhambini kwenye giza


Na tushike mkono utuongoze Kwako.

2. Twaamini Kwako japo tuna huzuni


Twaamini neno japo tunayo hofu.

3. Amri Yako Bwana tuwe msaada kwa watu,


Lakini twashinda kuwajali wengine.

4. Ee Bwana tutoe kwa mambo ya dunia,


Tuoneshe njia tuwe msaada kwa watu.

175. Bwana Unifundishe


Lord, my God, enlighten me (NIH 96)

1. Bwana unifundishe nielewe, nikufuate.


Kwenye utumishi huu nitambue; nitumike.
Nijaze hekima Zako nikuabudu daima.

2. Neno Lako ni kweli nifundishe nilishike,


Ndiyo shauku yangu ninayoipigania.
Wokovu wapatikana kwa kutenda wema Wako.

3. Usijitenge nami, neno Lako liwe nami.


Nipe moyo wa haki nizishike njia Zako,
Tusibakie dhambini hata tukakosa neema.

4. Neno Lako, Ee Bwana, linipe msingi thabiti.


Na taji ya ahadi kupitia neno Lako.
Katika nyakati ngumu Uwe tumaini langu.

5. Bwana niimarishe, neno Lako ni mwongozo.


Unihakikishie, nikamilishe mwanao,
Nuru itaniandama nitastaajabu mbinguni.
176. Moyo tua mizigo yako
O burdened heart lay down your worry (NIH 97)

1. Moyo tua mizigo yako, inua macho yako juu.


Ni siku yenye utukufu, Mungu atakuongoza.
Na atakupa pumziko; amekupa siku njema.
Njoo tushikamane lengoni, kumfuata Bwana daima.

2. Sifa zote ni Kwake Mungu, umtukuze na umsifu.


Muonyeshe unyenyekevu, tumikia jina Lake.
Ondoa fikra za dunia zisikuzonge akili.
Uitunze imani yako, kwa Mungu kuna amani.

177. Bwana niangazie


Light of light enlighten me (NIH 99)

1. Bwana niangazie siku, mpya yakaribia,


Wewe nuru ya neema, giza latoweka Kwako.
Furaha ya sabato, kwangu iwe pumziko.

2. Giza linatoweka kwa mwanga na neema Yako.


Wewe ndiye chemchemi ya furaha na amani.
Bariki neno Lako lililojaa upendo.

3. Na kwa jua la neema siku imepambazuka.


Furaha na amani, ni chemchemi ya uzima.
Bariki neno Lako na tunda la upendo.

4. Leo na siku zote, moyo wangu ukuimbie,


Sifa kuu za Ufalme, zitustahilishe Kwako.
Nimeonja jinsi ya kukuabudu mbinguni.
178. Ombeni mjitakase
Pray and sanctify yourself (NIH 106)

1. Ombeni mjitakase kwa mafuta safi,


Mjazwe Roho wa Yesu, Yeye atawale.
Ombeni daima bila ya kukoma, muwe safi kweli.

2. Waaminifu wa Mungu, nao waliomba.


Kwenye kiti cha enzi kujiweka wakfu.
Mwokozi, kashinda, tutakuwa Naye milele daima.

3. Je, moyo Wake Mungu hauwezi guswa.


Na ombi takatifu hata akajibu?
Je, sasa tukiwa wengi tukiomba, maombi yakina!

4. Wamuombao wapata nguvu toka Kwake.


Maombi na faraja kwao wahitaji.
Ushindi unasi, Yesu yuko nasi, ametushindia.

179. Ee njoo Kwangu


O come with me (NIH 111)

1.
Yenye maua ya kuburudisha, wanyonge hufarijika kwayo.

2. Ee njoo kwangu utayapata maji kutoka chemchemi hii ya neema.


Ambayo umesubiri kwa hamu, Mungu ndiye Bwana wa mavuno.

3. Usisite njoo lango liko wazi, hakuna kizuizi chochote


Huzuni zote kwenye moyo wako hapa zitakoma uwe huru.

4. Njooni Paradiso kuna baraka, wenyeji wanawakaribisha


Kupitia Kwake mkombozi wetu, kwa upendo atawakomboa.
180. Kristo, Nuru ya dunia
Christ, the Light, this world befriended (NIH 116)

1. Kristo, Nuru ya dunia, mwangaza wa upendo.


Nyota kutoka kwa Mungu, iliondoa giza.
Sasa ziangazie nafsi za wateule.

2. Ponya wagonjwa na wote waliorudi nyuma,


Uwafunge majeraha, watoe hatiani,
Mapenzi Yako mema na yazae matunda.

3. Ubariki ushuhuda wa watumishi Wako.


Wanaozileta nafsi zinazokusujudu.
Saa ya neema ndiyo hii, punde Bwana yuaja.

4. Mwokozi ninakuomba, nipe macho nione.


Na unipe moyo safi, usio na kiburi.
Niongoze daima na nuru ya mbinguni.

181. Nyumba Yako takatifu


Lord, Thy house is blest and holy (NIH 125)

1. Nyumba Yako takatifu, humo nakuabudu.


Nitajitolea Kwako, nikuonapo Bwana.
Popote niendapo, Roho Wako yu nami,
Japo napata ugumu kwa mambo ya ulimwengu.

2. Nitenge na ya dunia, nijaze utukufu.


Kwako napata amani, nafsi inashibishwa,
Chemchemi za dunia hazina cha kunipa,
Nafsi yangu yataabika kwa mizigo ya dunia.

3. Malaika wanaimba nyimbo za kumsifu juu,


Bwana ninaleta sifa, nipate imarika.
Magonjwa, maumivu umeniondolea,
Umenijaza upendo, kwenye kusanyiko Lako.
182. Kaa nasi, Bwana Yesu!
Abide with us, Lord Jesus! (NIH 144b)

1. Kaa nasi, Bwana Yesu! Neema yatutosha.


Mwovu hatatudhuru kwa ujanja wake.

2. Kaa nasi kwa hakika juu ya neno Lako,


Kwamba imani Yako ikatutawale.

3. Kaa nasi tuangaze, kwa Nuru Yako kuu.


Kweli Yako, Ee Bwana, njia yetu sisi.

4. Kaa nasi Ee Mwokozi, na utuongoze,


Bwana tuimarishe tunapohitaji.

5. Kaa nasi kwa ulinzi, Wewe ni muweza,


Nasi tutajifunza kumshinda shetani.

6. Kaa nasi na baraka Zako ziwe nasi.


Tupe nguvu na neema, tuongeze Bwana

183. Tukimtumainia Mungu akatuongoza


If we allow our God to guide us (NIH 154)

1. Tukimtumainia Mungu akatuongoza njia


Atatuimarisha sana, atatulinda na mwovu
Amtumainiye Mungu hatatikisika kamwe.

2. Wasiwasi, malalamiko yatatufaa nini sisi?


Kila tupatapo magumu kwanini kulalamika?
Lawama zinazidisha uzito wa mzigo wetu.

3. Hebu natunyamaze kimya tujawe na furaha kuu,


Neema Yake Mungu i nasi, Yeye hashindwi na kitu,
Mungu ametuchagua na ajua haja zetu.

4. Wakati wa shangwe na shida Wewe waujua vema,


Na hata kwenye majaribu, Wewe unanishindia,
Kwa pendo Lako Ee Bwana We umenifanya Wako.

5. Nisaidie nipumzike, nikungojee kwa furaha,


Kwa kupokea yale yote, kwa neema niipatayo,
Sawa na mapenzi Yako, Wewe umenichagua.
184. Yesu, Mtawala wa uzima wetu
Jesus, Thou Ruler of life everlasting (NIH 158)

1. Yesu Mtawala wa uzima wetu, tuokoe kwa dhambi Ee Bwana.


Nguvu za kuzimu zinatafuta, kutuangamiza nafsi zetu,
Mwovu anataka atuchanganye kwa kupitia njia zake nyingi.

2. Yesu tusaidie tuyashinde maovu yanapotuzunguka.


Nguvu ya kweli inapoangaza, uovu wote hutukimbia,
Ee Mfalme twakuomba uwe nasi, kwa pendo Lako utuangazie.

3. Yesu tusaidie We wakesha Wewe huchoki wala hulali,


Tufunike Kwenye maombi Yako, na itimize ahadi Yako,
Tuwapo wachovu hata gizani, hakika Yesu utatuhifadhi.

4. Yesu utusaidie wanao tunapoyaona majaribu,


Shauku ya kuomba isishuke, na tushindwapo kwa hofu nyingi,
Mwokozi kwa neema utatubeba kutupeleka nyumbani kwa Baba.

185. Nitakuwa mwaminifu kwa neno Lako


True to Thy word will I be faithful (NIH 186)

1. Nitakuwa mwaminifu kwa neno Lako la kweli,


Kama lilivyonenwa kwamba kuna hazina mbinguni.
Kwa wanyonge na wenye dhambi walio katika giza
Katika ufalme wa mwovu nao watawekwa huru.

2. Nitakuwa mwaminifu juu ya mwamba huu imara,


Neno Lako halipotei leo hii limetimizwa
Lahamisha hata milima, falme nyingi zimepita
Hakuna neno hata moja la Yesu halijakuwa.

3. Nitakuwa mwaminifu ingawa ni neno dogo,


Likitoka kinywani Mwake hilo huniimarisha.
Vyote vinavyoonekana neno Lako liliumba,
Neno limetubadilisha japokuwa tu wagumu.

4. Nitakuwa mwaminifu kupitia neno Lako


Japo wengi hawaamini neno Lako nguzo yangu
Neno Lako ni nuru yangu laongoza njia zangu,
Laniongoza wokovuni nitakapomwona Yesu.
186. Uko nami Ee Bwana
With You, O Lord, united (NIH 189)

1. Uko nami Ee Bwana, sihisi upweke,


Muda wote U nami wanifurahisha.
Nyakati za furaha naleta maombi,
Njia yangu ni Wewe, U maisha yangu.

2. Majeraha makali na misukosuko,


Vyote ni mafundisho juu ya Wewe Bwana.
Hakuna ajuae majeraha yangu,
Ni Wewe peke yake waweza niponya.

3. Naingiwa huruma kwa wasumbukao,


Hofu inapotanda ninawaombea.
Nakuja Kwako Bwana kwa unyenyekevu
Wewe ndiye muweza, sikia naomba.

4. Bwana unanijua pale nishindwapo,


Niongoze naomba, nisitende dhambi.
Nikosapo furaha, hofu ikitanda
Nakutafuta Bwana nikushike mkono.

5.
Kwenye shida na raha U pamoja nami.
Nini cha kuogopa, We wajua yote,
Naleta Kwako vyote kwenye enzi Yako.

187. Matone ya maji


Little drops of water (NIH 235)

1. Matone ya maji pia mchanga


Hufanya bahari pia na nchi.

2. Na hizi dakika zilizopita


Zikihesabika mtu hushanga.

3. Makosa madogo yanapoteza


Toka njia nzuri kwenda dhambini.

4. Matendo ya wema hata maneno


Husogeza mbingu chini tulipo.

5. Mbegu za neema humwagwa nasi


Hubariki watu ulimwenguni.
188. Pendo la Mungu lashinda kifo
The love of God is stronger than is death (NIH 243)

1. Pendo la Mungu lashinda kifo.


Napata kupitia Mwanawe.
Pendo hilo limejaa uzima,
Faraja na tumaini kwangu.

Chorus
Pendo la Mungu hushinda kifo,
Nalipata kupitia Yesu.
Pendo hilo limejaa uzima,
Na hunipa moyo mnyenyekevu.

2. Wahisio pendo Lake Mungu,


Huvutwa karibu Nae Baba.
Huijaza mioyo Roho Wake.
Na hawaufuati ulimwengu.

3. Heri wenye mioyo ya upendo.


Hao hawatikisiki kamwe.
Heri kwao wenye mioyo safi,
Wanaofuata nyayo za Yesu.

189. Nafsi amka! simulia neema


Soul, arise! I must be telling (NIH 253)

1. Nafsi amka! Simulia neema ya Bwana kwangu.


Dhambi ilinitawala, sasa Kwake ni huru.

Chorus
Amka nafsi, kasimulie neema Yake Bwana.
Dhambi zangu zimefutwa,

2. Nikipungukiwa nguvu kwenye safari yangu,


Hakika mkono Wako utaniongoza vema.

3. Karama Zako na nguvu, umenipandikiza.


Umeku
190. Mungu Mkuu Twakusifu!
Mighty God, we praise Thy name! (NIH 255)

1. Mungu Mkuu twakusifu. Ulimwengu wasujudu.


Twakushukuru Bwana. Kazi Yako yakusifu.
Tangu enzi za kale iwe hivyo daima.

2. Bwana Mkuu na Mwenyezi Bwana wa mbingu na nchi.


Na jeshi la mbinguni, Kwako kuna usalama.
Tunakusifu Bwana vyote ni vyako Wewe.

3. Mitume Wako Bwana wanakuabudu Wewe.


Ndio wajumbe Wako wanaimba sifa Zako.
Watoto Wako wote wanakusifu Mfalme.

4. Tuhurumie Bwana, tupatie ukombozi.


Tujalie upendo, timiza ahadi Yako.
Tuwe Wako daima usituache Bwana.

5. Tunakusujudia, tumeleta sifa Kwako.


Na kusanyiko Lako linamtukuza Mwanao.
Na Roho Mtakatifu, mfariji wetu sisi.

191. Njoo nafsi umwimbie!


Dear soul, join in the singing! (NIH 257b)

1. Njoo nafsi umwimbie! Mungu sifa Zake.


Sifa Kwake Mungu na wamtumikiao!
Na Usifiwe Mungu, sifa ninakupa.
Moyo wangu utamsifu ningali hai!

2. Tazama neema Yake Mungu ilivyo kuu,


Wale wamfuatao watakuwa Sayuni,
Kukamilisha lengo, thawabu ya pekee,
Bwana na Mungu wetu Atatupa taji!

3. Ee mimi ni dhaifu juu ya jina Lako,


Yesu ni limbuko, tangaza pendo Lake.
Ijapokuwa tumekuwa wana Wako,
Twakusifu Wewe twaimba sifa Zako.
192. Mimi ni mwanakondoo wa Yesu
(NIH 269)

1. Mimi ni mwanakondoo wa Yesu, nafurahi.


Yeye ni Mchungaji mwema, hutimiza haja zangu,
Kwa majina aita, Anatupenda sote.

2. Aniongoza njia kwenda kwenye malisho,


Neema tele I juu yangu, naongozwa malishoni,
Hunipatia maji, ninapohisi kiu.

3. Je, si jambo la shangwe? Kuitwa mwanakondoo,

Atanitwaa nyumbani, itakuwa shangwe Kuu!

193. Msifu Bwana kwa furaha


Praise ye the Lord (NIH 273)

1. Msifu Bwana kwa furaha na shangwe.


Anasikia sifa zetu zote.
Msifu Bwana, msifu Bwana.

2. Msifu Bwana enyi vijana wote,


Kwa sauti nzuri bila kukoma.
Msifu Bwana, msifu Bwana.

3.
Mpaka enzini japo tu wanyonge,
Zikubali tunaomba.

4. Baba yetu wa mbinguni mtukufu,


Twaimba nyimbo mpya za sifa Kwako,
Na milele yote Bwana.
194. Tulete shukrani kwa shangwe!
Let us bring thanks with joyful anthems! (NIH 274)

1. Tulete shukrani kwa shangwe, tujaze hazina yetu,


Tupaze sauti kwa shangwe, utukufu Kwake Mungu.
Yeye alimtuma Mwana kuokoa ulimwengu.

2. Pendo Lake latufunika, tena atuhurumia,


Dhambi ilitutenga Naye, sasa ametukomboa,
Kupitia kwa Mitume twapata pendo na neema.

3. Uwe nasi tuhudumie neno Lako nalidumu,


Uwe ni kimbilio letu, mwamba na msaada milele,
Mwana wa Mungu u njia, utuongoze mbinguni.

195. Ee Yesu, mwangaza, Umeniangazia


O Jesus, in Thy brightness (NIH 289)

1. Ee Yesu, mwangaza, umeniangazia.


Nikiwa ndani Yako niogope nini?
Sifa na utukufu Kwako juu enzini.
Nikiwa ndani Yako nahisi upendo.

2. Lulu hii, hazina kuliko vitu vyote.


Hakuna mfano Wake, ndicho natafuta.

Yanayotaka kunitenga Nawe Bwana.

3. Kujitenga Nawe, Ee! Ni maisha bure.


Wewe ndiye ni chanzo cha uzima wangu
Siogopi kifo kwa maana Uko nami.
Niliteswa dhambini Ukanisamehe.

4. Hapa duniani ninakuhisi Wewe.


Na huko juu mbinguni hakuna usiku.
Unijalie ujira Wako Ee Bwana,
Uliohifadhiwa kwa watakatifu.
196. Mioyo yenu iungane
Heart with heart in love united (NIH 332)

1. Mioyo yenu iungane ikimtafuta Mungu.


Upendo wenu udumu kwa baraka za Mungu.
uru, sisi miale,
dugu, tu wamoja daima.

2. Ee wana wa Mungu, Njooni kwenye agano jipya.


Na mjitoe Kwake Kristo kwa imani na pendo.
Upendo huu ukiyumba, kukosa uthabiti,
Tuombeni kwa pamoja msaada wetu ni Yesu.

3. Unganisha wateule, Ewe Rafiki mwema.


Mioyo yao ifurahi kwa kukujua Wewe.
Kama Mlivyo na umoja, iwe hivyo na kwao.
Wahudumiane Kwako bila kugawanyika!

197. Bwana Awatambua tangia zamani


The Lord knows all His people (NIH 335)

1. Bwana awatambua tangia zamani,


Wanyonge na wenye nguvu,pwani na bara,
Yeye huwaokoa; hawaachi pekee
Kwa kifo na uzima, ni mali ya Bwana.

2. Wanawe awajua kwa imani yao,


Waamini na kutumaini halisi,
Roho awaongoza kwa neno Lake kuu,
Walisujudu neno, hawatetereki.

3. Bwana awatambua wateule Wake,


Katika hali zote na matendo yao.
Kwa Mungu upo wema na uhuru tele
Kwao wabarikiwa na wavumilivu.

4. Mungu awatambua kwa upendo wao,


Wamtafutao Bwana wao kwa shauku
Na kujali wengine, Mungu awagusa
Awapa mara dufu, kwa upendo Wake.

5. Bwana tuimarishe kwenye kazi Yako


Kisiwepo cha kututenganisha Nawe,
Siku hiyo ijapo tutapokuona,
Tutakuwa na Wewe tena kwa uhuru.
198. Rehema ya Baba yetu
Br (NIH 374)

1. Rehema ya Baba yetu yaangaza nchi Yake;


Lakini Ametuweka tuwe walinzi Wake.

Chorus
Taa zenu na ziwake, nuru zenu tumeni;
Msafiri asizame, mwokoeni majini.

2. Twaona giza la dhambi, mawimbi twasikia;


Wengine wanatafuta nuru za kutulia.

3. Taa zitengenezeni, mwokoeni msafiri;


Aangukaye majini, na asife gizani.

199. Ni Utakatifu wa kipekee


Oh how (NIH 376)

1. Ni utakatifu wa kipekee kuwa Nae Bwana juu mbinguni,


Kustaajabu uzuri wa mbingu, ni heri kwa wanaomfuata.

Chorus)
Nitapata utukufu, nitapata utukufu,

2. Kando ya Yesu nanyenyekea, najazwa amani na faraja,


Nimekuwa kama mwanakondoo na chombo kiteule cha Mungu.

200. Kwa Yesu utumike


Of service be to Jesus (NIH 383)

1. Kwa Yesu utumike kwa uaminifu,


Umtazame Yeye tu, nasimama Kwake.
Mungu aliyaandaa makao mazuri.
Tumpe maisha yetu, tupate furaha.

2. Kristo alitujia kama mwanadamu,


Huduma Yake Bwana ilijaa upendo.
Enenda kwa njia hii, kwa upendo mwingi,
Alikufa tupone na kubarikiwa.

3. Mikono ikishindwa sababu ya kifo,


Mungu kwa mkono Wake Atawabariki.
Na watumishi Wake wanao mwamini.
Anawasaidia taji watapata.
201. Itakuwaje baada ya safari
How will it be (NIH 404)

1. Itakuwaje baada ya safari tukisha ushinda ulimwengu,


Je, tunaweza kama bibi harusi kwenda juu mbinguni kwa Baba?
Tutakapofutwa vumbi la miguu, mwisho jasho letu litafutwa,
Huko tutaona faida za kutabika tukiwa Naye Baba.

2. Itakuwaje tutakapoitwa
Tutakapokuwa Nae enzini, kumwona alivyo? Ee ni neema!
Tutajua kwanini tulilia kwa hofu kuu kuogopa watu.
Kwa pendo Lake atatutuliza na tutajazwa furaha tele.

3. Itakuwaje hakuna kuona, kusikia wala kuelewa,


Tukiungana tutapewa vyote kuingia nchi takatifu
Njoo na tukazane, tuvumilie, tujitahidi, tupiganie!
Uvumilivu utatufikisha kwenye safari yetu mbinguni.

202. Ewe nafsi, hima


To Zion, soul, now hasten (NIH 417a)

1. Ewe nafsi hima na twende Sayuni,


Wakati ingalipo nuru ya neema,
Giza lijapotanda, utahifadhiwa,
Mwisho wa kazi yote utawekwa huru.

2. Ewe nafsi hima, usilalamike,


Kila saa ipitayo nuru i karibu,
Msalaba hata dhiki, punde zitakoma,
Bwana atakuita na kukupumzisha.

3. Nafsi yangu twende, ndilo ombi langu,


Mpaka nikauone utukufu Wake,
Na punde nitaitwa, kwa sauti nzuri,
Njoo leo Bwana Yesu, ninakusubiri.
203. Kwa haraka mambo ya dunia
O how fleeting, O how paltry (NIH 430)

1. Kwa haraka mambo ya dunia yatoweka,


Kama ukungu utokeavyo kisha kupotea,
Pia mtu hubadilika.

2. Kwa haraka mambo ya dunia hayadumu


Kama kijito cha msimu maisha nayo hukoma
Kwa haraka duniani.

3. Vivutio vya dunia vyapita haraka,


Giza, nuru, amani, vita navyo havipatani,
Na dunia itapita.

4. Kwa haraka mambo ya dunia ni mazuri,


Kama ua nzuri lichanuavyo kwenye saa nzuri,
Mwisho uzuri hukoma.

5. Kwa haraka mambo ya dunia ni hazina,


Mali na utajiri, hubadilika kirahisi
Na hata mwisho hukoma.

6. Kwa haraka mambo ya dunia hutuonya,


Yote tunayoyaona yatapita yasirudi,

204. Yesu, ni mlinzi wangu


Jesus Christ, my sure defence (NIH 431)

1. Yesu ni mlinzi wangu, ni mwokozi wa milele,


Nalitambua hili, Kwako pekee najitoa,
Hata kwenye dhoruba, Yesu U mlinzi wangu.

2. Bwana mkombozi wangu, nitasimama imara,


. Je eka?
Nitaogopa nini? Huwezi kuniacha.

3. Ninalo tumaini hutaniacha daima,


Siku ya kufa kwangu nikushike kwa imani,
Kifo kisinitenge Nawe Bwana mkombozi.
205. Nakwenda, nakwenda
Let me go, let me go (NIH 434)

1. Nakwenda, nakwenda, Bwana jidhihirishe.


Moyo wangu watamani kufika Kwako mbinguni,
Huko kuna amani.

2. Ee Bwana, U nuru, mawingu hukimbia!


Nitakuja lini Kwako palipo watakatifu,
Nikaishi nuruni?

3. Waimba, waimba malaika huko juu!


Nafsi yangu yatamani kuruka juu milimani,
Nakufika Sayuni.

4. Furaha yote hii nimepewa hazina?


Macho yangu yamefumba, mpaka Yerusalemu mpya,
Nikaone uzuri!

206. Kama nyota zitowekavyo


Just as the stars disappear in the morning (NIH 437)

1. Kama vile nyota zitowekavyo asubuhi kwa nuru ya jua,


Ndivyo nawe utakavyotoweka, ni kazi yako itakumbukwa.

Chorus
Utakumbukwa, Utakumbukwa, Utakumbukwa kwa kazi yako,
Tabu za dunia utaziacha, ni kazi yako itakumbukwa.

2. Jinsi ulivyotumika kupanda kwa hakika ndivyo utavuna.


Mpanzi daima husahaulika, ni kazi yake itakumbukwa.

3. Kama ulikuwa ni mwaminifu kupigania haki ya Mungu,


Hatokusahau kwenye karamu, kazi yako itastahimili.

4. Baraka za mbinguni; hazikomi watakatifu wazipokea;


Hakuna kinachosahaulika kwa kupitia jina la Yesu.
207. Bwana Yesu ndiye Mwokozi
A wonderful Saviour is Jesus (NEH 363)

1. Bwana Yesu ndiye Mwokozi wangu, ni Mwokozi wa ajabu.


Amenificha kwenye mwamba Wake, katika mito tulivu.

Chorus
Amenificha kwenye mwamba Wake, kwenye kivuli mwanana.
Amenikumbatia kwa upendo (chini ya mabawa Yake.)x2

2. Bwana Yesu ndiye Mwokozi wangu, Amenitua mizigo.


Kanishika mkono sitapotea Amenipatia nguvu.

3. Baraka Zake hazihesabiki, Kanitakasa kabisa,


Nami naimba, atukuzwe Mungu, Bwana

4. Nitang , na kumlaki mawinguni,


Kwa pendo Ameniokoa kweli, nitapaza sauti juu.
Fahirisi Ya Alfabeti Alphabetical Index
A A
Alidharauliwa na aliumizwa ----------- 148 A river keeps the pastures green (NEH 344) ----------- 110
Atakuja, atakuja ----------- 136 Abide with me (NEH 232) ----------- 66
B Abide with us, Lord Jesus! (NIH 144b) ----------- 182
Baba yangu ana mali nyingi ----------- 52 All people that on earth do dwell (NEH 33) ----------- 7
Bi harusi asubiri ----------- 134 Amazing grace (NEH 311) ----------- 95
Bwana awatambua tangia ----------- 197 Arise and let us hasten (NEH 120) ----------- 34
Bwana kanipa amani kuu ----------- 126 At the feet of Jesus (NIH 130) ----------- 23
Bwana kanitoa mbali ----------- 20 Away in a manger (NEH 533) ----------- 155
Bwana nanyosha mikono ----------- 76 A wonderful Saviour is Jesus (NEH 363) ----------- 207
Bwana niangazie ----------- 177 B
Bwana nimejitoa kwako ----------- 69 Beautiful, glorious moment (NIH 300) ----------- 111
Bwana siachi kukupenda ----------- 27 Beautiful, glorious Zion (NEH 437) ----------- 138
Bwana unifundishe ----------- 175 Before my heart's King bowing (NIH 202) ----------- 67
Bwana upepo wavuma ----------- 56 Beyond, where clouds no more appear (NIH 438) ----------- 139
Bwana ututayarishe ----------- 108 Blessed assurance, Jesus is mine (NEH 75) ----------- 24
Bwana we ni nuru ----------- 59 Blessed is the peace to my heart (NEH 346) ----------- 112
Bwana wewe ni mwokozi. ----------- 29 Blessed Jesus, at Thy word (NIH 95) ----------- 68
Bwana Yesu ndiye Mwokozi ----------- 207 Blest be the tie that binds (NEH 585) ----------- 165
D Brightly beams our Father's mercy (NIH 374) ----------- 198
Damu imebubujika ----------- 106 Bringing in the sheaves (NEH 124) ----------- 35
E C
Ee Bwana tutoe dhambini ----------- 174 Christ the Lord is risen today (NEH 508) ----------- 150
Ee njoo kwa Yesu ----------- 91 Christ, the Light, this world befriended (NIH 116) ----------- 180
Ee njoo kwangu ----------- 179 Come in, O Lord, come in! (NIH 134) ----------- 81
Ee Yesu mbarikiwa ----------- 68 Come near, you are invited (NIH 112) ----------- 82
Ee Yesu, kama jua ----------- 195 Come to the Saviour (NEH 276) ----------- 83
Ee,we nafsi hima ----------- 202 Come ye that love the Lord (NEH 406) ----------- 129
Ewe roho mtakatifu ----------- 173 Come, Christians, join to sing (NEH 34) ----------- 8
Come, for the feast is spread (NEH 277) ----------- 84
F Come, share the Lord (NEH 347) ----------- 113
Fanyeni kazi zenu ----------- 44 Commit your way, confiding (NIH 146a) ----------- 46
Fikra za mwokozi wangu ----------- 30 Count your blessings (NEH 177) ----------- 47
Furaha kubwa sana ----------- 119 Crown Him with many crowns (NEH 510) ----------- 151
Furaha kuu, kuna wokovu ----------- 102 D
Dear brothers and dear sisters (NIH 342) ----------- 120
I Dear Lord, I give completely (NIH 120) ----------- 69
Inua juu ----------- 38 Dear soul, join in the singing! (NIH 257b) ----------- 191
Inuka Usisite ----------- 34
Itakuwaje baada ya safari ----------- 201 E
Endless compassion (NEH 313) ----------- 96
J F
Je sipaswi kumwimbia Mungu? ----------- 18 Father God (NEH 7) ----------- 1
Jikabidhi kwa Mungu ----------- 46 Filled with truth and life, O Spirit (NIH 82) ----------- 173
Jinsi wewe ulivyo mkuu ----------- 3 For you I am praying(NEH 278) ----------- 85
Forever with the Lord (NIH 402) ----------- 48
K Forth, forth, my heart, to heaven (NIH 395) ----------- 130
Kaa nami ----------- 66 From Jesus' love, the fountain pure (NEH 348) ----------- 114
Kaa nasi Bwana Yesu! ----------- 182
Kama nyota zitowekavyo ----------- 206 G
Karibu na wewe ----------- 74 Give me joy in my heart (NEH 127) ----------- 36
Kibarikiwe kifungo ----------- 165 Give thanks (NEH 38) ----------- 9
Kristo amefufuka ----------- 150 Glorious, glorious is the Work of God (NIH 344) ----------- 86
Kristo nuru ya dunia ----------- 180 God be with you (NEH 586) ----------- 166
Kumbuka mibaraka yako ----------- 47 God is in our presence (NIH 103) ----------- 2
Kuwa pamoja na Bwana ----------- 121 Grant us, Lord, due preparation (NEH 341) ----------- 108
Kwa fimbo ya dhahabu ----------- 65 Great is Thy faithfulness (NEH 40) ----------- 10
Kwa haraka mambo ya dunia ----------- 203 Guide me, O Thou great Redeemer (NEH 242) ----------- 70
Kwa Kristo Bwana uwe mwaminifu ----------- 135
Kwa Kristo mwokozi ----------- 23 H
Kwa Yesu napata wokovu ----------- 99 Hands let's be joining (NEH 588) ----------- 167
Kwa Yesu utumike ----------- 200 Hark! the gospel bells are ringing (NEH 283) ----------- 87
Kweli neema ----------- 95 Hark! the herald angels sing (NEH 544) ----------- 156
Fahirisi Ya Alfabeti Alphabetical Index
L Have Thine own way, Lord (NEH 243) ----------- 71
Leo ni siku ya furaha ----------- 103 Have you any room for Jesus? (NEH 285) ----------- 88
Leo ni siku ya neema ----------- 42 Heart with heart in love united (NIH 332) ----------- 196
Lini ujio wako ee Bwana ----------- 137 Here is my heart (NIH 107a) ----------- 72
M Hiding in Thee (NEH 183) ----------- 49
Maelfu kwa maelfu ----------- 143 Hold the fort (NEH 184) ----------- 50
Makao ya Bwana Yesu ----------- 141 Holy Spirit, teach Thou me (NIH 81) ----------- 172
Malaika waimba ----------- 156 Host and King of grace and riches (NIH 291) ----------- 109
Manyunyu yenye baraka ----------- 14 How blessed and glorious with Jesus (NEH 371) ----------- 121
Matone ya maji ----------- 187 How great is God's almighty kindness (NIH 227) ----------- 11
Mfalme mwingi wa rehema ----------- 109 How great Thou art (NEH 15) ----------- 3
Mfariji yuaja ----------- 144 How will it be? (NIH 404) ----------- 201
Mikononi mwa Yesu ----------- 133
Milele kwa Bwana ----------- 48 I
Mimi ni mwana kondoo wa Yesu ----------- 192 I am Thine, O Lord (NEH 84) ----------- 25
Mioyo yenu ifurahi ----------- 37 I gave My life for thee (NEH 493) ----------- 146
Mioyo yenu iungane ----------- 196 I have a home beyond the river (NEH 444) ----------- 140
Mkombozi wangu yu hai ----------- 169 I hear Thy welcome voice (NEH 318) ----------- 97
Moyo tua mizigo yako ----------- 176 I heard the voice of Jesus say (NEH 374) ----------- 122
Moyo wangu hima uende mbinguni ----------- 130 I know a realm where Jesus dwells (NEH 445) ----------- 141
Moyo wangu ninakupa ee Mungu ----------- 72 I know of a river (NIH 196) ----------- 89
Mpendao Bwana ----------- 129 I know that my Redeemer lives (NIH 69) ----------- 169
Msifu Bwana ----------- 17 I know whom I have believed (NEH 186) ----------- 51
Msifu Bwana kwa furaha ----------- 193 I need Thee every hour (NIH 199) ----------- 73
Msifuni Mungu kwa nyimbo ----------- 16 I praise God's love in adoration (NIH 221) ----------- 123
Mteteeni Yesu ----------- 40 I see in spirit (NIH 400) ----------- 131
Mto watunza malisho ----------- 110 I sing praises (NEH 42) ----------- 12
Mtukufu ----------- 13 I stood at mercy's gate (NEH 321) ----------- 98
Muda wa shangwe ----------- 159 I surrender all (NEH 88) ----------- 26
Mungu atukuzwe ----------- 21 I will never cease to love You (NEH 90) ----------- 27
Mungu awe nanyi daima ----------- 166 I will remember Thee (NEH 351) ----------- 115
Mungu Baba ----------- 1 I will sing of my Redeemer (NEH 91) ----------- 28
Mungu kati yetu ----------- 2 I worship You, almighty God (NEH 19) ----------- 4
Mungu kazi yako tukufu ----------- 86 If we allow our God to guide us (NIH 154) ----------- 183
Mungu mkuu twakusifu ----------- 190 I'm reconciled by mercy (NEH 352) ----------- 116
Mungu msaada wetu ----------- 5 I'm resting now at Jesus' feet (NEH 353) ----------- 117
Mvike taji nyingi ----------- 151 I'm the child of a King (NEH 189) ----------- 52
Mwaka uko mwishoni ----------- 145 In Jesus I have found salvation (NEH 323) ----------- 99
Mwamba wenye imara ----------- 149 It came upon the midnight clear (NEH 546) ----------- 157
Mwokozi anaita ----------- 82 I've found a place I love so well (NIH 128) ----------- 100
Mwokozi wetu utuongoze ----------- 75 J
N Jesus Christ is risen today (NEH 513) ----------- 152
Na iwe kama utakavyo ----------- 71 Jesus Christ, my sure defence (NIH 431) ----------- 204
Nafsi amka, simulia neema ----------- 189 Jesus is calling (NEH 290) ----------- 90
Nafsi yangu inuka ----------- 39 Jesus, Lover of my soul (NIH 168a) ----------- 53
Nafsi yangu mngoje ----------- 62 Jesus, Saviour, pilot me (NEH 196) ----------- 54
Naimba sifa ----------- 12 Jesus, Thou Ruler of life everlasting (NIH 158) ----------- 184
Najikabidhi kwa Yesu ----------- 26 Just as I am (NEH 330) ----------- 101
Nakuabudu ee mwenyezi ----------- 4 Just as the stars disappear in the morning (NIH 437) ----------- 206
Nakupenda Bwana ----------- 124
Nakwenda, nakwenda ----------- 205 L
Naleta tunu kwake mfalme ----------- 67 Let me go, let me go (NIH 434) ----------- 205
Namjua nimwaminiye ----------- 51 Let us bring thanks with joyful anthems (NIH 274) ----------- 194
Napumzika kwa Yesu ----------- 117 Let your hearts be ever joyful (NEH 136) ----------- 37
Nashindania uzima ----------- 41 Lift high the cross (NEH 137) ----------- 38
Nasikia sauti ----------- 97 Light after darkness (NIH 200) ----------- 55
Naujua mto mtukufu ----------- 89 Light of light enlighten me(NIH 99) ----------- 177
Ndani ya hori ----------- 155 Little drops of water (NIH 235) ----------- 187
Ndani ya mioyo hii ----------- 164 Lord, more would I love Thee (NIH 236) ----------- 124
Ndiyo bahari yenye neema ----------- 107 Lord, my God, enlighten me (NIH 96) ----------- 175
Ndiyo dhamana ----------- 24 Lord, my Saviour and my Shepherd (NIH 370) ----------- 29
Ndugu kaka na dada ----------- 120 Lord, Thy house is blest and holy (NIH 125) ----------- 181
Neno lako ni maji kwa wenye kiu ----------- 33 Lord, with fervence do we pray (NEH 572) ----------- 162
Fahirisi Ya Alfabeti Alphabetical Index
N'gambo kule ----------- 139 M
N'gambo kule nina makao ----------- 140 Majesty (NEH 47) ----------- 13
Ni chemchemi ya upendo ----------- 114 Master, the tempest is raging (NEH 201) ----------- 56
Ni salama juu ya mwamba ----------- 49 May the mind of Christ, my Saviour (NEH 98) ----------- 30
Ni shangwe mfalme yuaja! ----------- 168 Mighty God, we praise Thy name (NIH 255) ----------- 190
Ni usiku wa manane ----------- 157 Mighty the showers of blessing (NEH 50) ----------- 14
Ni utakatifu wa kipekee ----------- 199 My faith looks up to Thee (NEH 495) ----------- 147
Ni wako Bwana ----------- 25 N
Niimbie kila mara ----------- 94 Nearer, my God, to Thee (NIH 366a) ----------- 74
Nijulishe mwisho wangu ----------- 79 Not human advice (NIH 181) ----------- 57
Nikiwa na amani naye baba ----------- 128 Now thank we all our God (NIH 256b) ----------- 15
Nilimwaga damu yangu ----------- 146 O
Nilisimama nje ----------- 98 O boundless joy, there is salvation (NEH 331) ----------- 102
Nimejaliwa amani ----------- 112 O burdened heart lay down your worry (NIH 97) ----------- 176
Nimekombolewa na Yesu ----------- 118 O come now to Jesus (NEH 295) ----------- 91
Nimeyapata makao ----------- 100 O come with me (NIH 111) ----------- 179
Nina haja nawe ----------- 73 O come, all ye faithful(NEH 550) ----------- 158
Ninakuombea rafiki yangu ----------- 85 O God, our help in ages past (NEH 22) ----------- 5
Ninasifu pendo la Mungu ----------- 123 O great joy, your King shall come! (NIH 40) ----------- 168
Niongoze ee Mkombozi ----------- 70 O happy day (NEH 332) ----------- 103
Nipe furaha moyo ni mwangu ----------- 36 O how fleeting, O how paltry (NIH 430) ----------- 203
Nishike mkono Bwana ----------- 78 O how shall I receive You? (NIH 3) ----------- 154
Nitaimba juu ya Mkombozi ----------- 28 O Jesus, in Thy brightness (NIH 289) ----------- 195
Nitakukumbuka ----------- 115 O Lord, free us from guilt (NIH 93) ----------- 174
Nitakupokeaje ----------- 154 O love, the golden sunshine bright (NEH 386) ----------- 125
Nitakuwa mwaminifu kwa neno lako ----------- 185 O sacred Head, now wounded (NIH 43) ----------- 148
Nitwae hivi nilivyo ----------- 101 O Son of God, we wait for Thee (NIH 398) ----------- 132
Njoo kwa mwokozi ----------- 83 O the home of my soul is on high (NIH 435) ----------- 142
Njoo nafsi umwimbie! ----------- 191 O thou joyful time (NIH 23) ----------- 159
Njoo ndani Bwana! ----------- 81 Of compassion and salvation (NIH 250) ----------- 92
Njooni karamuni. ----------- 84 Of service be to Jesus (NIH 383) ----------- 200
Njooni tushiriki ----------- 113 Oh, how divine 'tis with Jesus, my Lord (NIH 376) ----------- 199
Nuru baada ya giza ----------- 55 On Your ascension, Lord, alone (NIH 70) ----------- 170
Nyumba Yako takatifu ----------- 181 On Zion's mount of radiant light (NEH 205) ----------- 58
Nyumbani kwangu ni mbinguni ----------- 142 P
O Pass me not, O gentle Saviour (NEH 333) ----------- 104
Ombeni mjitakase ----------- 178 Peace, O how precious (NIH 290) ----------- 126
P Praise our God with joyful singing (NEH 56) ----------- 16
Panda asubuhi ----------- 35 Praise thou the Lord (NIH 261) ----------- 17
Peleka jina la Yesu ----------- 60 Praise ye the Lord (NIH 273) ----------- 193
Pendo ambalo ni nuru ----------- 125 Pray and sanctify yourself (NIH 106) ----------- 178
Pendo la Mungu ----------- 127 R
Pendo la Mungu lashinda kifo ----------- 188 Redeemed, I am blessed in Jesus (NEH 357) ----------- 118
Penye roho wa Mungu ----------- 171 Rise, my soul, gird thee with power (NIH 355) ----------- 39
R Rock of Ages, cleft for me (NEH 498) ----------- 149
Rehema ya Baba yetu ----------- 198 S
Rehema zake ----------- 96 Safe in the arms of Jesus (NEH 421) ----------- 133
Roho unifundishe ----------- 172 Saviour, like a shepherd lead us (NEH 259) ----------- 75
Rohoni mwangu ----------- 131 See, I spread my arms in yearning (NIH 131) ----------- 76
S Seeing I am Jesus' lamb (NIH 269) ----------- 192
Sayuni mji mzuri ----------- 138 Should I not to God be singing? (NIH 259) ----------- 18
Si ushauri wa mwanadamu ----------- 57 Silent night, holy night! (NIH 26) ----------- 160
Sikia! Habari njema ----------- 87 Sing, all you Christians (NIH 66) ----------- 153
T Soul, arise! I must be telling (NIH 253) ----------- 189
Tabibu mkuu yu karibu ----------- 105 Stand up for Jesus (NEH 152) ----------- 40
Tazameni ----------- 50 Star, to which I'm looking (NIH 371) ----------- 59
Tufani inapovuma ----------- 64 Striving onward, pressing forward (NEH 153) ----------- 41
Tufanyeni kazi ----------- 43 Sweet hour of prayer (NEH 261) ----------- 77
Tukimtumainia Mungu akatuongoza ----------- 183 T
Tulete shukrani kwa shangwe ----------- 194 Take my life and let it be (NIH 373) ----------- 31
Tumaini langu Bwana ----------- 170 Take the name of Jesus with you (NEH 213) ----------- 60
Tumshukuru Mungu ----------- 15 Take Thou my hand and lead me (NIH 194) ----------- 78
Tunakuomba Bwana ----------- 162 Teach me the measure of my days (NEH 263) ----------- 79
Fahirisi Ya Alfabeti Alphabetical Index
Tupande mlima Sayuni ----------- 58 Ten thousand times ten thousand (NEH 453) ----------- 143
Tushikamane muda unapita ----------- 167 Thank ye the Lord (NIH 272) ----------- 19
Tusongeni mbele ----------- 61 That which my God ordains is right (NIH 156) ----------- 80
Twaa uzima wangu ----------- 31 The bride has waited, O so long (NIH 412a) ----------- 134
Twaipenda nyumba hii ----------- 6 The Comforter has come (NEH 477) ----------- 144
Twaiweka wakfu nyumba ----------- 163 The great Physician (NEH 335) ----------- 105
Twakusifu, Bwana ulieshuka ----------- 22 The Lord knows all His people (NIH 335) ----------- 197
Twamshukuru Bwana ----------- 19 The love of God (NEH 396) ----------- 127
Twangojea ujio wako Bwana ----------- 132 The love of God is stronger than is death (NIH 243) ----------- 188
Twasogea kwako Bwana ----------- 32 The time of grace redeem today (NIH 135) ----------- 42
U The year so still is ending (NIH 33) ----------- 145
Uaminifu wako baba ----------- 10 There is a fountain (NEH 336) ----------- 106
Ujaribiwapo, sifanye dhambi ----------- 45 Thus far the Lord God has me brought (NIH 30) ----------- 20
Uko nami ee Bwana ----------- 186 To Christ, the Lord, be faithful (NEH 430) ----------- 135
Una nafasi kwa Yesu? ----------- 88 To God be the glory (NEH 66) ----------- 21
Ushukuru ----------- 9 To the work! To the work! (NEH 162) ----------- 43
Usiku tulivu! ----------- 160 To Zion, soul, now hasten (NIH 417a) ----------- 202
Usinipite mwokozi ----------- 104 Toiling bravely onward (NEH 219) ----------- 61
True to Thy word will I be faithful (NIH 186) ----------- 185
W W
Wachungaji walikesha ----------- 161 Wait, my soul, and tarry (NIH 190) ----------- 62
Wakati mzuri nilipo amini ----------- 111 We dedicate, now Lord, to Thee (NEH 581) ----------- 163
Wakati wangu kuomba ----------- 77 We love the place, O God (NEH 28) ----------- 6
Wakfu wa Mungu ni wa haki ----------- 80 We praise Thee, Lord (NIH 277) ----------- 22
Wakristo njooni ----------- 158 What a Friend we have in Jesus (NIH 237) ----------- 63
Wakristo sasa twimbe ----------- 153 What a sea of grace (NEH 339) ----------- 107
Wakristo tuimbe ----------- 8 What joy 'tis redeemed to be (NEH 360) ----------- 119
Watu wote duniani ----------- 7 When He cometh (NEH 434) ----------- 136
Wema wake Mungu ni mkubwa ----------- 11 When peace with the Father (NIH 295) ----------- 128
When strikes the hour? (NEH 435) ----------- 137
Y When the storms of life are raging (NEH 228) ----------- 64
Ya huruma na wokovu ----------- 92 Where'er God's Spirit reigneth (NIH 76) ----------- 171
Yesu aliniita njoo ----------- 122 While shepherds watched their flocks (NEH 562) ----------- 161
Yesu anaita ----------- 90 Whosoever heareth (NEH 308) ----------- 93
Yesu Kristo yu hai ----------- 152 With a golden staff in hand (NIH 204) ----------- 65
Yesu kwa damu yako ----------- 116 With great joy and fervent longing (NIH 118a) ----------- 32
Yesu kwa imani. ----------- 147 With You, O Lord, united (NIH 189) ----------- 186
Yesu kwetu ni rafiki ----------- 63 Within these hearts (NEH 584) ----------- 164
Yesu mtawala wa uzima wetu ----------- 184 Wonderful words of life (NEH 310) ----------- 94
Yesu ni mlinzi wangu ----------- 204 Work, for the night is coming (NEH 167) ----------- 44
Yesu uniongoze ----------- 54 Y
Yesu unipendaye ----------- 53 Yield not to temptation (NEH 168) ----------- 45
Yeyote anaenisikia ----------- 93 Your word, O Lord, is gentle dew (NIH 175) ----------- 33

You might also like