You are on page 1of 9

75.WAIMBA SIKILIZENI .

Verse 1

Waimba sikilizeni,
Malaika mbinguni,
Wimbo wa tamu sana,
Wa pendo zake Bwana,
 
Duniani salama,
Kwa wakosa rehema,
Sisi sote na tuimbe;
Waimba, sikilizeni
Malaika mbinguni.
 
Verse 2

Ndiye Bwana wa mbinguni,


Tangu milele Mungu,
Amezaliwa mwili,
Mwana wa mwanamwali
Ametoka enzini
Kuja ulimwenguni
Mwokozi atufie,
Ili tusipotee,
Waimba, sikilizeni,
Malaika mbinguni.
Verse 3

Mtukufu wa amani.
Ametoka mbinguni,
Jua la haki , ndiye
Atumulikaye,
Amejivua enzi,
Verse 3

Alivyo na mapenzi
Ataka kutuponya,
Kutuzalisha upya,
Waimba sikizeni,
Malaika mbinguni,
Verse 4

Njooni upesi , Bwana


Twakutamani sana;
Kaa nasi mwokozi,
Vita hatuviwezi,
Vunja kichwa cha nyoka ,
Sura zako andika,
Tufanane na wewe
Kwetu sifa upewe,
Waimba sikizeni
Malaika mbinguni.

You might also like