You are on page 1of 11

THAWABU ZA UAMINIFU

Somo la 12 kwajili ya
Machi 25, 2023
“Bwana wake
akamwambia,
‘Vema, mtumwa
mwema na
mwaminifu; ulikuwa
mwaminifu ka
machache,
nitakuweka juu ya
mengi; ingia katika
furaha ya bwana
wako’’”
(Mathayo 25:21)
Tunapoupokea wokovu ambao Yesu alishinda msalabani,
tunakuwa “tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo
mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende
nayo” (Ef. 2:10). “Kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe
sawasawa na taabu yake mwenyewe.” (1Kor. 3:8)
Ikiwa “ni Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na
kutenda kwenu, kwa kutimiliza kusudi lake jema” (Fil. 2:13),
kwanini Atupe thawabu? Kwa upande mwingine, kwanini
thawabu itusubiri?
Thawabu:
Thawabu Yake
Uzima wa milele
Kuwa na Yesu
Uaminifu:
kusimamia kwaajili ya Bwana…
…hadi Ajapo
THAWABU
THAWABU
“Tazama, naja upesi, na ujira wangu u
pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake
ilivyo.” (Ufunuo 22:12)
Ni akina nani watapokea thawabu zao kutoka kwa Yesu atakapokuja?

Waliouawa Wale
Waliopanda wanaowapen
watakatifu kwa sababu ya
haki da maadui zao
(Za. 58:11) imani zao
(Mit. 11:18)
(Mt. 5:12) (Lk. 6:35)

Wale wenye Wale Manabii, watakatifu, walichao


ujasiri wanaomtafuta Jina Lake
(Eb. 10:35) (Eb. 11:6) (Uf. 11:18)

Thawabu itakuwa sawa na matendo ya kila mtu (1Kor. 3:8). Je, hiyo
inamanisha tunaokolewa kwa matendo yetu? Hapana kabisa!
Wokovu ni karama ambayo kila mmoja anaweza kuipata bila kujali
matendo yake (Tit. 3:5). Woye waliokombolewa watapokea “taji” zao,
thawabu ya haki (2Tim. 4:8).
UZIMA WA MILELE
“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni
uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.” (Warumi 6:23)

Ni nini hasa tunachostahili? “Ujira” wetu ni nini? Kifo tu. Ni nini


Mungu anachotupatia kama “karama”? Uzima wa milele (Rum. 6:23).

Hii ni thawabu tusiyostahili, hatima tofauti


kabisa na ile tuliyostaili. Kila mmoja
anaweza kuipokea kama ataipokea kwa
imani (Yn. 3:16).
Yesu alisema, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mnamwamini Mungu,
niaminini na Mimi.” (Yn. 14:1)
Kifo na ufufuo wa Yesu ni dhamana ya uzima
wetu wa milele (Ru. 6:3-4), lakini ni lazima
tusubiri hadi Ujio Wake wa Mara ya Pili
kuipokea thawabu hii (Yn. 14:3).
KUWA KAMA YESU
“Nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao.” (Ufunuo 22:4)

Wale walioamini kabla yetu walitarajia Mungu awapatie mji


(Eb. 11:10, 16).
Tuna tumaini kama hilo: kuishi katika Yerusalemu Mpya, mji
kwa ajili ya “mataifa ya wale waliokombolewa” (Uf. 21:24).
Tutapata nini hapo?

Mkono wa Mungu wa upendo utatufuta machozi yetu. Maumivu na


kifo havitakuwepo tena (Uf. 21:4)

Bustani ya Edeni, ambapo tutafika na kula kwenye mti wa uzima (Mwz.


3:22; Uf. 22:2)

Yesu. Tutamwona uso kwa uso (Uf. 22:4)


UAMINIFU
KUSIMAMIA KWA AJILI YA BWANA…
“Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila
mtu kwa kadri ya uwezo wake; akasafiri.” (Mathayo 25:15)

Mfano wa talanta unashughulika na namna


tunavyosimamia kile Mungu alichotupatia, katika
muktadha wa Wakati wa Mwisho (Mt. 25:14-30).
Inatupasa kusimamia talanta zetu za asili, karama
ambazo Roho Mtakatifu ametupatia, na kila kitu
ambacho Mungu ametupatia. Anatupatia kwa kadri
tunavyosimamia.
Kila mmoja anawajibika kwa karama na raslimali
walizopewa, haijalishi ni ngapi. Thawabu ni ya
thamani (Mt. 25:23).
…HADI AJAPO
“Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu kama utukufu
ule utakaofunuliwa kwetu.” (Warumi 8:18)
Paulo alipitia dhiki nyingi sana kwa sababu ya
uaminifu wake kwa Yesu (2Kor. 11:23-28).
Inawezekana tusipitie hayo, lakini
hatujaahidiwa maisha rahisi (2Tim. 3:12).

Inavyoonekana, Paulo hakuishi maisha ya mafanikio. Hata hivyo, Biblia


inasemaje kuhusu kuishi maisha ya furaha na mafanikio (1Tim. 6:6-12)?
Siyo kuwa na mali nyingi
Ni kupata kitu wakati unakihitaji
Ni kung’ang’ania ahadi za Mungu
Ni kumshukuru na kumtumainia Mungu
Pale Yesu atakaporudi, tutapokea thawabu yetu kwa kusimamia kilicho
Chake (2Tim. 4:6-8).
“Je, washiriki wote wa kanisa wanatambua kuwa vyote
walivyonavyo walipewa wavitumie kwa ajili ya utukufu
wa Mungu? Mungu hutunza kumbukumbu ya uaminifu
wake kwa kila mwanadamu ulimwenguni. Na siku ya
kutoa hesabu itakapofika, wakili mwaminifu
hajichukulii sifa mwenyewe […]
Uthibitisho wa Bwana hupokelewa kwa mshangao,
huwa haitarajiwi. Lakini Kristo anamwambia, ‘Vema,
mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu
kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika
furaha ya Bwana wako.’”
E. G. W. (Counsels on Stewardship, cp. 23, p. 111-112)

You might also like