You are on page 1of 4

SOMO: KUYAJUA MAONO YA MAHALI UNAPOABUDU.

(ABC GLOBAL)
MHUDUMU: MCH JOSEPH MAKINDI
30-07-2023
Lk 4:16-18, 20-21
"Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama
ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua
chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia
mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa
kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Akakifunga chuo,
akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia
macho. Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu."
Huduma ya Yesu inaanza na shauku ya kuvuna roho za watu na anawaita wanafunzi wake.
Anaanza kuwapa maono ya mwito wake, "Nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu"
Yesu akawaambia, Njoni mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.
Marko 1:17
Badala ya kuua ndipo wavue, kama ilivyo desturi ya uvuaji wa samaki, hawa walipaswa kwenda
kuvua watu na kuwahuisha.
"Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni
roho yenye kuhuisha."
1 Wakorintho 15:45
Yesu aliwaondoa watu kwenye kuvua samaki, kushughulikia chakula au faida binafsi na kuwa
watu wanaovua watu kwa uzima wa Milele na faida ya Mungu.
"Mnifuate" Yesu alimaanisha;
1. Mwe wanafunzi wangu (1Kor 11:1)
2. Muende na maono yangu
3. Muende kila ninakokwenda.
"Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe. Yesu akasema,
Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au
mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili, ila atapewa mara
mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na
mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele."
Mk 10:28-30
Kila mtu anayeamua kumtumikia Mungu
1.Anapata ulinzi
Isaya 54:17
"Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika
hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao
inayotoka kwangu mimi, asema BWANA."
2.Anapata baraka na Mungu anaondoa magonjwa katikati yako.
"Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako;
nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye
tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza."
Kut 23:25-26 SUV
#Kwanini uambatane na huduma /Mchungaji mwenye maono?
Yoh 1.
Mtu yeyote aliyeamua kuambatana na Yesu aliyekuwa na maono makubwa aliishia kuwa na
hatima kubwa.
"Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu,
aichukuaye dhambi ya ulimwengu! Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu
nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. Tena siku ya
pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake. Akamtazama
Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu! Yesu aligeuka, akawaona
wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu),
unakaa wapi?"
Yn 1:29-30, 35-36, 38
Yohana alikuwa na huduma ya kumuandalia njia Yesu. Lakini Yesu alikuwa na maono ya
kuchukua dhambi ya ulimwengu.
Yohana alikuwa na maono ya ubatizo wa maji, Yesu alikuwa na maono ya ubatizo wa Roho
Mtakatifu na moto.
Yohana alikuja na ujumbe kama sauti ya mtu aliaye nyikani kuitengeneza njia ya Bwana, Yesu
alikuja na ujumbe wa ufalme wa Mungu umekaribia watu wote watubu na kuiamini injili.
Hakikisha huduma unayoifuata inaongelewa vizuri. Yohana aliiongelea vizuri huduma ya Yesu
ndiyo maana wanafunzi wake wakamwacha wakaambatana na Yesu.
Lazima huduma iwe Ina uwezo wa kuona ulichonacho na kukijenga. Yesu alipomwona Petro
alimwambia Yeye ni nani na atakauwa nani....Petro utaitwa Kefa maana yake Jiwe.
Hakikisha huduma iliyopo Ina uwezo wa kukujenga kwenye maeneo yote ili uwe vile Mungu
alikusudia uwe kabla hujaja ulimwenguni.
Hakikisha huduma uliyopo Ina uwezo wa kuwatambulisha wengine na kuwaongelea vizuri kama
alivyofanya Yohana Mbatizaji.
Hakikisha mchungaji mwenye maono unayemfuata awe ni mtu mwenye roho ya Mungu ndani
yake.
Hakikisha Mchungaji unayemfuata ni mtu mwenye neema na kweli.
MAONO YA ABC GLOBAL
Maono ni kuwa kama baba alivyo.
"Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa
kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao."
Ebr 13:7
1.Kumdhihirisha Yesu katika uhalisia wake.
Kupitia tabia na mwenendo wako.
"Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa
kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo
ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa
tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa."
2 Pet 1:3-4 SUV
Kwa ishara na ajabu.
"Angalieni, mimi na watoto hawa niliopewa na BWANA tu ishara na ajabu katika Israeli,
zitokazo kwa BWANA wa majeshi, yeye akaaye katika mlima Sayuni."
Isa 8:18 SUV
Watu walitaka ishara kutoka kwa Yesu.
"Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona
ishara kwako. Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zinaa chatafuta ishara, wala
hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona."
Mt 12:38-39
Ishara ni vithibitisho kwamba Yesu ni yeye yule jana na leo na hata milele. Vile vitu alivyofanya
anaweza kufanya leo.
"Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha
mpya;"
Marko 16:17
Kwa upendo.
"Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu."
Wakolosai 3:14
2.Kumtengenezea Mungu watu kwenye kila eneo la maisha.
Huduma yoyote ya kiroho ina kazi mbili,
1.Kuwasaidia watu kutoka dhambini na
2. kuwafanya watu wa mataifa yote kuwa wanafunzi.
Mt28:19
"Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na
Mwana, na Roho Mtakatifu;"
Watu wa Mataifa;
Ni watu wa nchi zote zote
Ni watu wasiomjua Mungu
Baadhi ya milima ya ushawishi ambayo Mungu anataka kuinuliwa watu ni
Mlima wa Elimu
Mlima wa wahubiri wa Injili
Mlima wa Afya
Mlima wa Sanaa na michezo
Mlima wa Biashara
Mlima wa Siasa
3. Kuwaandaa watu kwa ajili ya ujio wa pili wa Yesu na uzima wa Milele.
Kwa njia ya kuhubiri injili.
Kushuhudia watu, mmoja mmoja. Nyumba kwa nyumba ,kwenye mikutano ya Injili, kwenye
magari nk
Dunia imepotea kwa sababu ya udanganyifu wa shetani hivyo kupelekea watu;
• Kupoteza mahusiano na Mungu
• Kutumia kazi, fedha kwa ajili ya ufalme wa giza na kupromote kazi na matendo ya kiovu.
"Anayeijua njia ni Mungu pekeyake.
Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama."
Zab 32:8
Wanafunzi wa Yesu walimuuliza ili kujua ujio wa pili wa Yesu na ili kujua mwisho wa dunia hii
ni lini.
"Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa
faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na
ya mwisho wa dunia?"
Mt 24:3
Mara zote kabla ya Mungu kuangamiza,huwa linatangulia onyo. Na Mungu huwa ana chombo
maalumu kwa ajili ya watu wake.
Wakati wa Nuhu aliandaa safina
Wakati wa Sodoma aliandaa malaika
Wakati wa sasa analiandaa Kanisa, kila atakayekubali kuwa sehemu ya mwili wa Kristo atakuwa
salama.

You might also like