You are on page 1of 14

Somo:

UKUMU YA WATAKATIFU NA TAJI ZAO


Maana ya Maneno

Ukumu

Taji Utukufu, nuru

Watakatifu - ni watu wote waliompokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa


maisha yao, na kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.
Maana ya Maneno
Ukumu
1. Hukumu ni uamuzi wa mwisho kabisa unaotolewa
na mahakama juu ya suala linalobishaniwa baina
ya mlalamikaji na mlalamikiwa. Uamuzi huo
ndio unaotoa kauli ya mwisho na kutamka ni nani
mwenye haki katika suala linalobishaniwa na ni
nini wajibu wa yule aliyekosa ushindi.
2. ni ile hali ya kutendewa au kupewa ujila wako kulingana na kazi yako.
MAANDIKO
Ufunuo 20:11-12 "Nikawaona wafu wakubwa kwa wadogo, wamesimama
mbele ya hicho kiti cha enzi na vitabu vikafunguliwa na kitabu kingine
kikafunguliwa ambacho ni cha enzi na hao wafu wakahukumiwa katika
mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu sawa sawa na matendo yao."
Addition: Matendo 17:31,
VITU VITAKAVYO ZINGATIWA
Watu watahukumiwa kwa matendo yao.
Mathayo 16:27 27 "Kwa sababu mwana wa adamu atakuja katika utukufu wa
baba yake pamoja na malaika zake ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya
matendo yake."
Kila mtu atahukumiwa na kanuni ya sheria za Mungu.
Yakobo 2:10 -12 "Maana mtu awaye yote ila akajikwa katika neno moja
amekosa juu ya yote kwa maana yeye aliye sama usizini pia alisema usiue. basi
ijapokuwa hukizini lakini umeua umekuwa mvunja shria semeni ninyi na
kusema kamawatu wakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru."
VITU VITAKAVYO ZINGATIWA
Hukumu ya Mungu itakuwa ya haki.
Matendo ya mitume 17:31 "Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu
walimwengu kwa haki kwa yule mtu aliyemchagua naya amewapa watu wote
udhabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu."
Hakuna atakaye epuka hukumu.
2Wakorintho 5:10 "Kwa maana imedhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha
Kristo ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili kadiri
alivyotenda kwamba ni mema aumabaya."
VITU VITAKAVYO ZINGATIWA

Hakuna jabo lolote litakalo fishwa katika kiti cha hukumu.


Mhubiri 12:14 "Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi pamoja na kila
neno la siri likiwa jema au likiwa baya."

Picha ya hukumu itakuwaje: Danieli 7:9-10


Yesu ndiye wakili wetu katika hukumu.: 1Yohana 2:1, Ufunuo 3:5
MAMBO YA HATARI
1. Tabia ya kujichukulia Utukufu.
2. Udhaifu wa kiroho. Mf kutokufunga, kuchelewa kanisani,
3. Migawanyiko ndani ya makanisa. Gal 3:18 due to Elimu, Ukabila, Uchumi
n.k
4. Uaminifu katika huduma unayo itumikia.
5. Utoaji wa Sadaka ndani ya kanisa.
KUJARIBIWA KWA KAZI YA KILA MTU.

Wakati wa BEMA kazi ya kila mtu aliyeokoka aliyoifanya katika kumtumikia


Mungu itajaribiwa kwa moto ili ipate kufahamika dhawabu ipi atakayopata (
1WAKORINTHO 3:12-15 ). Moto huu ni Mungu mwenyewe, Yesu Kristo (
KUTOKA 24:17; ISAYA33:14; WAEBRANIA 12:29 ). Kazi ya kila mtu
itajaribiwa kwa kulinganisha na jinsi ambavyo Yesu Kristo mwenyewe
angeifanya kazi hiyo kwa karama hizohizo alizopewa mtu yule.
TAJI/UTUKUFU(nuru,mngao)
AINA ZA TAJIZITAKAZO TOLEWA
KWA WATAKATIFU 3. Taji ya Haki. ( CROWN OF RIGHTEOUSNESS )
2Timotheo 4:8, Ufu 22:17
Daniel 12:3
A. Walio jitunza katika maisha ya
1. Taji ya Ushindi. 1Wak 9:25-27 wokovu(Utakatifu)
Watu walio mtumikia Mungu kwenye Mazingira
magumu. B. Taji hii pia ni kwa wale wote
waliowatendea mema ADUI ZAO (
2. Taji ya Uzima.(CROWN OF LIFE ) Yakobo1:12, LUKA 6:34-36 )
Ufun 2:10. mfano wanaokoka na kufukuzwa
kwako, Uchuimi mgumu but hawakumwacha 4. Taji ya Fulaha. Wafilipi 4:1-2
Yesu. Watapokea wale wakristo wanaofulahia mafaniko
ufunuo 12:11; mathayo 5:11-12; waebrania 11:24- ya wenzao.mf kuwaombea
26; zaburi 129:2 .
5. TAJI ISIYOHARIBIKA ( INCORRUPTIBLE CROWN ).
1wakorintho 9:23-25; 2timotheo 2:4-6 ,
Taji hii watapewa watakatifu ambao walifanya mambo yote kwa ajili ya injili ili
kuishiriki pamoja na wengine. Walijizuia yote katika utoaji wao kwa ajili ya injili,
walijizuia katika maombi yao pia walitumia vyote walivyonavyo, muda, ujuzi,
vipawa, cheo chao, uwezo wao wote n.k; ili kuishiriki injili pamoja na wengine
6. TAJI YA KUJIONEA FAHARI ( CROWN OF REJOICING ).
1wathesalonike 2:19; danieli 12:3,
Taji hii inaitwa taji ya kujionea fahari kwa sababu watakaoipata taji hii watangara kama
nyota tofauti na wengine watakavyongara. Fahari yao itakuwa kubwa kuliko ya
wengine. Mngao wao wa utukufu utakuwa mkubwa kuliko wengine. Taji hii watapewa
wale waliowaleta WATU WENGI kwa Kristo kutokana na kushuhudia kwao au
kuhubiri injili. Washuhudiaji wale waliozaa watoto wengi katika injili yao ya mtu kwa
mtu au vinginevyo na wakawaongoza mahali ambapo watakuzwa kwa mafundisho na
kuwa watenda haki.
7. Taji ya Utukufu. ( CROWN OF GLORY ).
Watapokea wachungaji na watumishi wote walio ACTIVE wanaomtumikia Mungu ndani ya kanisa.
1 petro 5:2-4; matahyo 10:41-42.
( a ). Taji hii watapewa wachungaji, walimu, au watumishi wa Mungu wanaojitaabisha kuwafundisha
wengine na kuwalea kwa njia zozote-Kuwafundisha kanisani na kuwapa huduma za kichungaji,
kuandika vitabu au tracts au mandishi yoyote yanayowasaidia watu wengine kiroho.
( b ). Taji hii watapewa wale ambao wanachukua muda wao kuwafundisha watoto wachanga wengi
wa kiroho mpaka wanakua. Namna yoyote ya kumsaidia mtu kujifunza, itapata dhawabu hii-
Kumwazima au kumpa vitabu au kaseti ( kanda ) za mafundisho mwenzio, kumpa nauli aende
kwenye mafundisho, kazi ya kuhudumia kanisani- Kubeba watoto au kufanya lolote ili watu wawe na
raha ya kujifunza n.k.
( c ). Taji hii watapewa wale ambao wanawahudumia mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na
walimu ili wapate urahisi wa kuzifanya kazi zao
JINSI YA KUJIWEKA TAYARI KUYASHIRIKI HAYA YOTE.

( a ). Kuwa miongoni mwa watakatifu ( WAEBRANIA 12:14 ).

( b ). Kuifanya kazi ya Mungu kwa bidii na nguvu zote ( MHUBIRI 9:10;

YOHANA 4:34-36; WARUMI 12:11; YOHANA 9:4; 1WAKORINTHO

7:29-35; 9:17 ).

You might also like