You are on page 1of 402

Pambano Kuu

Ellen G. White

1
Pambano Kuu
Kati ya Kristo na Shetani

"Pambano la Vizazi"
The Great Controversy (GC) 1911

Na
E. G. White

Tafsiri ya Kiswahili Imefanywa na:


Onesmo Emmanuel
2015

2
KUHUSU TOLEO HILI LA KISWAHILI

Pambano Kuu (The Great Controversy) ni kitabu chenye ujumbe muhimu kwa wanadamu wa
vizazi hivi. Kimepata kutafsiriwa kwa Kiswahili katika matoleo kadha wa kadha ambayo, hata
hivyo, kwa kiasi kikubwa hayakuwasilisha ujumbe wote wa kitabu husika. Kwa kutambua
umuhimu wa mafundisho yaliyo katika kitabu hiki, mtafsiri amekitafsiri kutoka Kingereza
kwenda Kiswahili kwa ajili ya matumizi ya familia yake na marafiki.

Kitabu hiki kimetafsiriwa kwa mtindo wa neno kwa neno. Kwa hiyo kinazo sura zote na aya zote
za kitabu cha asili cha lugha ya Kingereza cha mwaka 1911. Kurasa rasmi kwa ajili ya marejeleo
zimewekwa katika mabano kwa wino uliokolezwa, nazo ndizo zimetumika katika kuonyesha
Yaliyomo. Maelezo ya mwishoni ambayo hayatoki kwa mwandishi yamewekwa kwa ufupi na
uchache tu kutegemea umuhimu wake. Maelezo ya ziada ya mwenye kutafsiri yameongezwa
kwa kusudi la kufafanua maneno mageni kwa msomaji.

Msomaji azingatie kwamba majina ya watu na ya mahali yameachwa vile vile yalivyoandikwa
kwa lugha ya Kingereza ili kusalisha maana na mwonekano wa asili, isipokuwa yale tu ambayo
yako katika Kiswahili ambacho kimezoeleka sana kwa watumiaji wa Kiswahili. Pia katika kazi
hii neno “onyesha” limependelewa kutumiwa badala ya “onesha” ambalo limeibuka kuwa
maarufu kwa watumiaji wengi wa Kiswahili rasmi.

3
YALIYOMO
Utangulizi v
1 Kuharibiwa kwa Yerusalemu 17
2 Mateso Mnamo Karne za Kwanza 39
3 Kipindi cha Giza la Kiroho 49
4 Wawaldensi 61
5 John Wycliffe 79
6 Huss na Jerome 97
7 Luther Ajitenga na Roma 120
8 Luther Mbele ya Baraza 145
9 Mwanamatengenezo wa Uswisi 171
10 Matengenezo Yasonga Mbele Ujerumani 185
11 Upinzani wa Wakuu 197
12 Matengenezo Ufaransa 211
13 Huko Uholanzi na Skandinavia 237
14 Mwanamatengenezo wa Uingereza 245
15 Biblia na Mapinduzi ya Ufaransa 265
16 Safari ya Mababa Kuvuka Ng’ambo 289
17 Dalili za Mapambazuko 299
18 Mwanamatengenezo wa Amerika 317
19 Nuru Yapenya Gizani 343
20 Mwamko Mkuu wa Kidini 355
21 Onyo Lakataliwa 375
22 Unabii Watimizwa 391
23 Patakatifu ni Nini? 409
24 Katika Patakatifu pa Patakatifu 423
25 Sheria ya Mungu Isiyobadilika 433
26 Kazi ya Matengenezo 451
27 Uamsho wa Kisasa 461
28 Mbele ya Kumbukumbu za Maisha 479
29 Asili ya Uovu 492
30 Uadui kati ya Mwanadamu na Shetani 505
31 Nguvu za Roho Waovu 511
32 Mitego ya Shetani 518
33 Udanganyifu Mkuu wa Kwanza 531
34 Wafu wetu wanaweza Kusema Nasi? 551
35 Uhuru wa Dhamiri Watishwa 563
36 Vita Inayokaribia 582
37 Maandiko Kinga Salama 593
38 Onyo la Mwisho 603
39 Wakati wa Taabu 613
40 Watu wa Mungu Waokolewa 635
41 Dunia Kufanywa Ukiwa 653
42 Pambano Likiisha 662

4
UTANGULIZI

Kabla ya kuingia kwa dhambi, Adamu alifurahia ushirika wa wazi na Muumba wake; lakini tangu
mwanadamu alipojitenga na Mungu kwa kuasi, jamii ya mwanadamu imetengwa na baraka hiyo. Hata
hivyo, kupitia mpango wa wokovu, njia imefunguliwa ili wakazi wa dunia waendelee kuunganishwa na
mbingu. Mungu amewasiliana na wanadamu kupitia kwa Roho wake, na nuru yake imeingizwa
ulimwenguni kwa njia ya ufunuo kwa watumishi wake waliochaguliwa. Watakatifu wake “walinena
yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu." 2 Petro 1:21.
Katika kipindi cha miaka 2500 ya kwanza ya historia ya mwanadamu, hakukuwa na mafunuo yaliyo
katika maandishi. Wale waliokuwa wamefundishwa kuhusu Mungu walirithisha elimu hiyo kutoka kizazi
hata kizazi, na ilikuwa ni kutoka kwa baba kwenda kwa mwana. Maandalizi ya maneno yaliyo katika
maandishi yalianza wakati wa Musa. Ndipo mafunuo yenye uvuvio yalipowekwa katika kitabu. Kazi hii
iliendelea kwa kipindi kirefu cha miaka 1600 – kutoka kwa Musa, aliyetoa historia ya uumbaji na torati,
hadi kwa Yohana, mwandishi wa kweli za injili zenye mguso mkuu.
Biblia inaelekeza kwamba Mungu ndiye mtunzi wake; lakini iliandikwa na mikono ya wanadamu; na
katika mitindo tofauti-tofauti ya vitabu vyake, inawakilisha sifa za waandishi wake walio tofauti. Ukweli
wote uliofunuliwa humo umevuviwa na "pumzi ya Mungu" (2 Timotheo 3:16); lakini umewekwa katika
maneno ya wanadamu. Yeye Aliye wa Milele ameangaza nuru yake katika akili na mioyo ya watumishi
wake kwa njia ya Roho wake Mtakatifu. Amewapa ndoto na maono, mifano na ishara; na wale ambao
wamefunuliwa ukweli huo waliuweka katika lugha ya wanadamu.
Amri Kumi zilitamkwa na Mungu mwenyewe, na ziliandikwa na mkono wake mwenyewe. Zimetungwa na
Mungu mwenyewe, (vi) wala si ufahamu wa mwanadamu. Lakini Biblia, pamoja na kweli zake zilizotoka
kwa Mungu zikawekwa katika lugha ya wanadamu, inaonyesha mwunganiko wa uungu na uanadamu.
Mwunganiko huo ulikuwepo katika Yesu, aliyekuwa Mwana wa Mungu na Mwana wa mtu. Vivyo hivyo ni
hakika kwa Biblia, kama ilivyokuwa kwa Kristo, kwamba "Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni
mwetu." Yohana 1:14.
Vitabu vya Biblia viko katika mitindo tofauti-tofauti ya uandishi na ujumbe wake, kwa kuwa
vimeandikwa katika vipindi tofauti, na kuandikwa na watu waliotofautiana sana katika hadhi na kazi
zao, na wenye vipaji tofauti vya kiakili na kiroho. Mitindo tofauti ya kueleza imetumiwa. Mara nyingi
ujumbe ule ule umesisitizwa na mwandishi mmoja kuliko mwingine. Na kadiri waandishi kadhaa
wanavyoongelea mada moja katika mtazamo na mahusiano tofauti, inaweza kutokea kwa msomaji wa
juu juu tu, asiye makini, au mwenye ushupavu, kuona kwamba Biblia iko katika vipande-vipande
visivyoshabihiana au vinavyopingana vyenyewe kwa vyenyewe; lakini msomaji anayejifunza kwa
umakini, anayetafakari na mwenye mtazamo wa dhati, anabaini kwamba sehemu za Biblia zina
mwunganiko na mapatano murua na ya kwamba zinakamilishana.
Kama ulivyotolewa kupitia watu tofauti-tofauti, ukweli uliletwa kwa mitazamo inayotofautiana pia.
Mwandishi mmoja anavutwa katika eneo moja la mafundisho; mawazo yake yanaelekea katika eneo
linaloendana na uzoefu wake au uwezo wake wa kuelewa na kutambua; mwingine anaelekea katika
eneo jingine; na kila mmoja, akiwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, anawasilisha kile kinachogusa
zaidi mawazo yake – kila mmoja akiwa na mtazamo tofauti-tofauti, lakini yote yakiwa katika hali ya
5
kushabihiana na yenye ukamilifu. Na ukweli uliofunuliwa hivyo unaunganika na kufanya kitu kimoja
kilichokamilika, kilicholetwa ili kukidhi mahitaji ya wanadamu katika mazingira na uzoefu wa maisha
yao.
Imempendeza Mungu kuwasilisha ukweli wake kwa ulimwengu kupitia mawakala walio wanadamu, na
yeye mwenyewe, kupitia Roho wake Mtakatifu, aliwastahilisha watu hao na kuwawezesha kufanya kazi
hii. Aliongoza akili zao katika kuchagua kipi cha kunena na kipi cha kuandika. Hazina ilidhaminiwa
katika vyombo vya kidunia, lakini ilitoka Mbinguni. Ushuhuda (vii) umepitishwa katika lugha ya
mwanadamu isiyo na ukamilifu, lakini bado ni ushuhuda wa Mungu; na mtoto wa Mungu mwenye kutii na
kuamini anakuta ndani yake utukufu wa uweza wa Mungu, uliojaa neema na kweli.
Katika neno lake, Mungu amekabidhi kwa wanadamu elimu muhimu kwa ajili ya wokovu. Hebu Maandiko
Matakatifu yapokelewe kama ufunuo wa mapenzi ya Mungu ulio na mamlaka na usiokosea. Ni kiwango
cha maisha, ufunuo wa mafundisho, na kipimo cha uzoefu. "Kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa
mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema." 2 Timotheo 3:16, 17.
Hata hivyo, ukweli kwamba Mungu amefunua mapenzi yake kwa wanadamu kupitia neno lake hauondoi
uhitaji wa kuendelea kuwepo kwa Roho Mtakatifu na uongozi wake. Roho aliahidiwa na Mwokozi wetu ili
kuifunua kweli kwa watumishi wake, kumulika na kufanyia kazi mafundisho yake. Na kwa kuwa ni Roho
wa Mungu aliyeivuvia Biblia, haiwezekani mafundisho ya Roho huyo kuwa kinyume cha neno la Mungu.
Roho hakutolewa – wala hawezi kutolewa – ili kuwa mbadala wa Biblia; kwa maana Maandiko yanasema
wazi wazi kwamba neno la Mungu ni kiwango ambacho ni lazima kitumike kupima mafundisho yote na
uzoefu wote. Mtume Yohana anasema, "Msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho kwamba zimetokana
na Mungu; kwa maana manabii wengi wa uongo wametokea duniani." 1 Yohana 4:1. Isaya naye
anatangaza, "Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka
kwa hao hapana asubuhi." Isaya 8:20.
Lawama kubwa imeelekezwa kwa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu ya makosa ya kundi la watu
ambao, wakidai kuangaziwa nuru, wanadai kutokuwa na haja tena ya kuongozwa na neno la Mungu.
Wanatawaliwa na maono ya hisia za uongo wanayodhani kuwa ni sauti ya Mungu ya rohoni. Lakini roho
inayowaongoza siyo Roho wa Mungu. Huku kufuata (viii) maono ya uongo, na kupuuza Maandiko,
kunaweza kuwaongoza watu katika kuchanganyikiwa, kudanganyika na kuharibika. Hali hii inasaidia tu
kuendeleza mipango ya mwovu. Kwa kuwa huduma ya Roho Mtakatifu ina umuhimu wa pekee kwa
Kanisa la Kristo; ni nyenzo mojawapo ambayo Shetani, kupitia kwa makosa ya watu wenye itikadi kali na
ushupavu, anaitumia kuhafifisha kazi ya Roho na kuwafanya watu wapuuze chanzo hiki cha nguvu
ambacho Bwana wetu mwenyewe ametoa.
Roho wa Mungu, katika kukubaliana na neno la Mungu, alikuwa wa kuendelea na kazi yake katika muda
wote wa kuitangaza injili. Katika vizazi, wakati ambapo Maandiko yote ya Agano la Kale na Jipya
yalikuwa yanatolewa, Roho Mtakatifu hakukoma kupeleka nuru katika akili za watu, licha ya kuwepo
kwa ufunuo uliopaswa kuingizwa katika kitabu kitakatifu. Biblia yenyewe inaonyesha namna ambavyo,
kupitia kwa Roho Mtakatifu, watu walipokea maonyo, mashauri na mafundisho katika mambo ambayo
hayako katika Biblia. Manabii wa vizazi tofauti-tofauti ambao maneno yao hayakuandikwa wametajwa.
Vivyo hivyo, hata baada ya kukamilika kwa Maandiko Matakatifu, Roho Mtakatifu aliendelea na kazi
yake, kuwaangazia nuru, kuwaonya na kuwafariji watoto wa Mungu.
Yesu aliwaahidi wanafunzi wake akisema, "Huyo msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba
atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia." "Yeye
6
atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote: . . . na mambo yajayo
atawapasha habari yake." Yohana 14:26; 16:13. Maandiko yanafundisha wazi kwamba ahadi hizi, pamoja
na kwamba zilikuwa za siku za mitume, zinaendelea katika kanisa la Kristo katika vizazi vyote. Mwokozi
anawahakikishia wafuasi wake akisema, "Mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari."
Mathayo 28:20. Na Paulo anasema kwamba karama za Roho na udhihirisho wake viliwekwa kanisani
“kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe:
hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu
mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo." Waefeso 4:12, 13.
Kwa ajili ya waamini wa Efeso, mtume aliomba, "Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu,
awape ninyi roho ya hekima na ufunuo katika kumjua yeye; macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue
tumaini la mwili wenu jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;
na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo." Waefeso 1:17-19. Huduma ya roho
wa Mungu katika kuangazia ufahamu na kufungua akilini mambo ya kina ya neno takatifu la Mungu,
ulikuwa mbaraka ambao Paulo alikuwa akiomba kwa ajili ya kanisa la Efeso.
Baada ya kumwagwa kwa ajabu kwa Roho Mtakatifu Siku ya Pentekoste, Petro aliwaasa watu watubu na
kubatizwa kwa jina la Kristo kwa ajili ya ondoleo la dhambi; na akasema: "Mtapokea kipawa cha Roho
Mtakatifu. Kwa maana ahadi hii ni yenu, na ya watoto wenu, na kwa wote walio mbali, hata kwa wale
ambao Bwana Mungu wetu atawaita." Matendo 2:38, 39.
Kwa kuunganishwa na matukio ya siku kuu ya Mungu, Bwana kupitia kwa nabii Yoeli ameahidi
udhihirisho wa Roho wake, Yoeli 2:28. Sehemu ya unabii huu ilipata kutimizwa katika tukio la
kumwagwa kwa Roho Mtakatifu Siku ya Pentekoste; lakini itafikia upeo wake wa ukamilifu katika uwepo
wa uthihirisho wa neema ya Mungu katika kipindi cha kuifunga kazi ya injili.
Pambano kuu kati ya wema na uovu litazidi kuongezeka kadiri tunavyoelekea mwisho wa wakati. Hasira
ya Shetani dhidi ya kanisa la Kristo imedhihirishwa katika zama zote; na Mungu ametoa zawadi ya
neema na Roho wake kwa watu wake ili kuwatia nguvu na kuwawezesha kusimama dhidi ya nguvu za
yule mwovu. Wakati mitume wa Kristo walipotakiwa kuibeba kazi ya injili kwenda kwa ulimwengu wote
na kuiandika kwa ajili ya kumbukumbu kwa vizazi vyote vijavyo, walijaliwa nuru ya pekee ya Roho.
Lakini kadiri (x) kanisa linavyokaribia ukombozi wake, shetani atafanya kazi kwa nguvu zaidi. Anashuka
"akiwa na ghadhabu nyingi, kwa maana anajua kwamba anao wakati mchache tu." Ufunuo 12:12.
Atafanya kazi “kwa nguvu zote na ishara na maajabu." 2 Wathesalonike 2:9.
Kwa muda wa miaka elfu sita, yule mwanamipango ambaye wakati fulani alikuwa juu kabisa miongoni
mwa malaika wa Mungu ameelekea katika kazi ya udanganyifu na uharibifu. Na ujuzi na werevu wote
wa kishetani uliopata kujulikana, ukatili wote uliokuzwa, wakati wa mapambano haya ya vizazi,
utaletwa pamoja na kutwishwa juu ya watu wa Mungu katika pambano la mwisho. Na katika wakati huu
wa hatari kubwa, wafuasi wa Kristo wataupelekea ulimwengu ujumbe wa onyo kuhusu kurudi kwa
Bwana mara ya pili; na watu wataandaliwa ili wakati ajapo wasimame pasipo “mawaa wala aibu mbele
yake." 2 Petro 3:14. Wakati huu, kipawa maalum cha neema na nguvu za Mungu hakitahitajika kanisani
kwa kiasi kidogo kuliko kipindi cha wakati wa mitume.
Kwa njia ya nuru ya Roho Mtakatifu, matukio ya pambano la muda mrefu kati ya wema na uovu
yamefunuliwa kwa mwandishi wa kurasa hizi. Kwa nyakati mbalimbali nimeruhusiwa kuona kazi za
pambano hili kati ya Kristo, aliye Mfalme wa uzima na mwanzilishi wa wokovu wetu, na Shetani, aliye
mfalme wa uovu, mwanzilishi wa dhambi, muasi wa kwanza wa sheria takatifu ya Mungu. Uadui wa
Shetani dhidi ya Kristo umeelekezwa kwa wafuasi wake. Chuki ile ile dhidi ya kanuni za sheria ya
7
Mungu, sera ile ile ya udanganyifu, ambayo kwayo uongo unafanywa kuwa kama ukweli, sheria za
wanadamu zinachukua nafasi ya sheria ya Mungu, na watu wanaongozwa katika kuabudu viumbe badala
ya Muumba, vinaonekana katika historia yote iliyopita. Jitihada za Shetani katika kuonyesha tabia ya
Mungu kwa uongo, kuwafanya watu wawe na mawazo yasiyo sahihi kuhusu Muumba, na hivyo kumwona
Mungu kama kitu kinacholeta woga na chuki badala ya upendo; mikakati yake ya kuweka kando sheria
ya Mungu, kuwaongoza watu kudhani kwamba wako huru nje ya matakwa ya sheria; na mateso yake kwa
wale wanaopinga madanganyo yake, vimetekelezwa kwa nguvu sana katika zama zote. Haya yanaweza
kuonekana (xi) katika historia ya wazee wa zamani, manabii, na mitume, wafia-dini na
wanamatengenezo.
Katika pambano kuu la mwisho, Shetani atatumia mbinu zile zile, ataidhihirisha roho ile ile, na atafanya
kazi kwa kusudi lile lile kama ilivyokuwa kwa vizazi vilivyopita. Kile ambacho kimekuwa, kitakuwa,
isipokuwa tu kwamba pambano lijalo litakuwa la kutisha kiasi ambacho ulimwengu haujapata
kushuhudia. Madanganyo ya Shetani yatakuwa ya ujanja na werevu zaidi, mashambulizi yake yatakuwa
ya kudhamiria zaidi, kama ingewezekana, awapotoshe hata walio wateule, Marko 13:22.
Kama Roho wa Mungu alivyofunua ukweli mkuu wa neno lake katika akili yangu, na matukio yaliyopita
na yajayo, nimetakiwa kuwajulisha wengine ukweli uliofunuliwa – kujifunza historia ya pambano katika
zama zilizopita, na hasa ili kutoa nuru kwa ajili ya pambano linalokuja haraka. Katika kutekeleza
jukumu hilo, nimechagua na kuweka pamoja matukio katika historia ya kanisa kwa namna ambayo
inaweza kufunua ukweli mkuu wa kipimo, ambao umetolewa kwa ulimwengu katika vipindi tofauti,
ambao umeamsha hasira za Shetani, na uadui wa kanisa linalopenda ulimwengu, na ule ambao
umedumishwa na shahidi wa wale ambao “hawakupenda maisha yao mpaka kufa.”
Katika maandishi haya tunaweza kuona utabiri wa pambano lililo mbele yetu. Kwa mwanga wa neno la
Mungu, na nuru ya Roho wake, tunaweza kuona wazi zana za yule mwovu, na hatari ambazo wale
watakaokutwa “bila hatia” mbele za Bwana wakati ajapo lazima wajikinge nazo.
Matukio makubwa yanayoonyesha maendeleo ya matengenezo katika zama zilizopita ni mambo ya
historia, yanafahamika sana na yanatambulika katika ulimwengu wote wa Kiprotestanti; ni ukweli
ambao hakuna anayeweza kuupinga. Nimeieleza kwa muhtasari historia hiyo, kulingana na muktadha wa
kitabu hiki, na ufupi ambao ni lazima uzingatiwe, ukweli wa matukio hayo ukiwa umefupishwa katika
nafasi ndogo kadiri ilivyoonekana inaleta mfuatano mzuri na (xii) kuleta uelewa mzuri na uwezekano
thabiti wa kuyafanyia kazi. Katika maeneo mengine ambapo mwanahistoria amekusanya pamoja
matukio, kwa ufupi, au ameeleza mambo ya kina kwa muhtasari kwa namna iliyo muafaka, maneno
yake yamenukuliwa; lakini katika maeneo mengine hakutambuliwa rasmi kwani nukuu hazikufanywa
kwa nia ya kumtambua mwandishi, ila kwa kuwa maneno yake yameonekana kwamba yanarahisisha
uwasilishaji wa fundisho husika. Katika kusimulia uzoefu na mawazo ya wale wanaopeleka mbele kazi ya
matengenezo katika wakati wetu huu, matumizi kama hayo yamefanyika kuhusu machapisho yao.
Kusudi kubwa la kitabu hiki si kueleza sana ukweli mpya kuhusu mapambano ya nyakati zilizopita, bali
kufunua mambo na kanuni zinazoelekeza kwa matukio yajayo. Hata hivyo, yakionekana kama sehemu ya
pambano kati ya nguvu za nuru na za giza, maandishi haya yanayohusu mambo yaliyopita yanaonekana
kuwa na umuhimu mpya; na kupitia hayo nuru inaangaza kwa ajili ya wakati ujao, ikiwaangazia njia
wale ambao, kama ilivyokuwa kwa wanamatengenezo wa vizazi vilivyopita, wataitwa, hata kwa
gharama ya kuachana na mazuri ya kidunia, kushuhudia “kwa ajili ya neno la Mungu, na ushuhuda wa
Yesu.”

8
Kusudi la kitabu hiki ni kufungua pazia la matukio ya pambano kuu kati ya ukweli na uongo; kufichua
mbinu za Shetani, na njia zinazoweza kusaidia kumpinga; kuleta suluhisho la kutosheleza kutatua tatizo
kuu la uovu; kumlika chanzo cha dhambi na hatima yake kama kudhihirisha wazi haki na wema wa
Mungu katika kushughulika na viumbe wake; na kuonyesha sheria yake takatifu isiyobadilika. Kwamba
kupitia ushawishi huu roho ziokolewe toka katika nguvu za giza, na kufanywa kuwa “washirika wa urithi
wa watakatifu katika nuru,” kwa sifa zake yeye aliyetupenda, na akajitoa mwenyewe kwa ajili yetu,
ndilo ombi la dhati la mwandishi.
E.G.W.

9
Sura ya 1
KUHARIBIWA KWA YERUSALEMU

"Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. Kwa
kuwa siku zinakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke, watakuzingira na kukuhusuru
pande zote; watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa
sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako." Luka 19:42-44.
Kutoka kwenye kilele cha Mlima wa Mizeituni, Yesu aliuangalia mji wa Yerusalemu. Mwonekano
uliokuwa mbele yake ulikuwa wa shwari na amani. Huu ulikuwa msimu wa Pasaka, na wana wa Yakobo
walikuwa wamekusanyika kutoka pande mbalimbali za nchi ili kusherehekea sikukuu hii ya kitaifa.
Katika bustani na shamba la mizabibu, na mitelemko ya kijani iliyojazwa na mahema ya mahujaji hao,
kiliinuka kilima chenye mitelemko yenye matuta ya ngazi, jumba la kifalme na kuta nene za ngome ya
mji mkuu wa Israeli. Binti Sayuni alionekana katika kiburi chake akisema, “Nimeketi malkia wala sitaona
huzuni, kama mpendwa wa wakati huo, akijiona mwenyewe kuwa salama na katika upendeleo wa
Mungu, kama alivyoimba mwimba zaburi katika vizazi vilivyopita: "Ni mzuri katika kuinuka kwake juu
sana, furaha ya dunia yote. Kama vilele vya juu sana vya mlima Sayuni, ndio mji wa Mfalme Mkuu."
Zaburi 48:2. Jengo la kupendeza la hekalu la kifahari lilionekana katika mwonekano kamili. Mionzi ya
jua linalotua ilimulika katika kuta zake za marumaru na za rangi nyeupe kama theluji na kulifanya jengo
ling’ae hata lango lake la dhahabu na minara yake. "Ukamilifu wa (18) uzuri wake” vilisababisha kiburi
kwa taifa la Kiyahudi. Ni mwana wa Israeli yupi ambaye angeangalia mandhari hii asipate raha na
kustaajabu! Lakini kwa mbali Yesu alijawa na mawazo tofauti. "Alipofika karibu, aliuona mji, akaulilia."
Luka 19:41.
Katikati ya shangwe za furaha wakati wa kuingia kwa shangwe, wakati matawi ya mitende
yakipeperushwa, wakati mwangwi wa nyimbo za hosana ukitoka kila upande vilimani, na sauti za maelfu
zikimtaja kama mfalme, ghafla Mwokozi wa ulimwengu alikuwa amegubikwa na huzuni ya ajabu. Yeye
aliye Mwana wa Mungu, aliye Ahadi kwa Israeli, ambaye nguvu zake zilishinda kifo na kuwaita mateka
kutoka makaburini, alikuwa katika machozi, siyo ya maumivu ya kawaida, bali ya huzuni nzito na
maumivu makubwa.
Machozi yake hayakuwa kwa ajili yake mwenyewe, ingawa alijua mahali miguu yake ilikokuwa
inaelekea. Mbele yake kulikuwa na Gethsemani, mahali pa mateso yake. Mlango wa kondoo pia ulikuwa
wazi machoni pake, mahali ambapo kondoo wa kafara waliokuwa wanasonda kidole kwake yeye aliye
“mwanakondoo apelekwaye machinjoni" (Isaya 53:7), hapa walikuwa wamepitishwa kwa karne nyingi.
Mahali ambapo si mbali ulionekana mlima wa Kalvari, mahali pa yeye kusulibishiwa. Hapa ilikuwepo njia
ambayo Yesu angepita muda si mrefu, mahali ambapo pangetokea tukio la giza wakati fulani
anapoifanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi. Lakini si mawazo ya mambo haya yaliyomtia
Yesu uvuli wa simanzi katika wakati huu ambao shamra-shamra na shangwe zilikuwa zimemzunguka.
Alilia kwa ajili ya maelfu ya watu wa Yerusalemu – kwa sababu ya upofu na kutotubu kwa wale aliokuja
kuwabariki na kuwaokoa.

10
Historia ya zaidi ya miaka 1000 ya upendeleo na uongozi maalum wa Mungu kwa wateule wake, na
kujidhihirisha kwake kwao, ilikuwa wazi machoni pa Yesu. Kulikuwa na Mlima Moria pale, mahali
ambapo mwana wa ahadi, asiye na upinzani, alifungwa kwenye madhabahu – kama alama ya sadaka ya
Mwana wa Mungu. Pale ndipo agano la baraka, ahadi tukufu ya Masihi, ilikuwa imethibitishwa kwa baba
wa imani (Mwanzo 22:9, 16-18). Pale ndipo miale ya moto ya kafara iliyopanda mbinguni kutoka katika
kiwanja cha kupuria cha Arauna (Ornani) ilipogeuza (19) upanga wa malaika mwenye kuharibu (1
Nyakati 21) – ikiwa alama ya kafara ya Mwokozi na upatanisho kwa wanadamu wenye hatia. Yerusalemu
ulikuwa umeinuliwa na Mungu juu zaidi kuliko dunia. Bwana alikuwa “ameichagua Sayuni," alikuwa
“ametamani yawe makao yake." Zaburi 132:13.
Kwa vizazi vingi, manabii watakatifu walikuwa wametangaza ujumbe wa onyo. Makuhani walikuwa
wameinua chetezo, na wingu la ubani, pamoja na maombi ya waabuduo, na vilikuwa vimepanda juu
mbele za Mungu. Kila siku damu ya wanakondoo waliochinjwa ilikuwa imetolewa, ikielekeza kwa
Mwanakondoo wa Mungu. Pale Yehova alidhihirisha uwepo wake katika wingu la utukufu lililokuwa juu
ya kiti cha rehema. Pale ndipo iliposimama ile ngazi inayoiunganisha nchi na mbingu (Mwanzo 28:12;
Yohana 1:51) – ngazi ile ambayo kupitia kwake malaika wa Mungu walishuka na kupanda, tena ambayo
iliufungulia ulimwengu njia ya kwenda katika patakatifu sana. Ikiwa taifa la Israeli lingehifadhi agano
lake kwa mbingu, Yerusalemu ungekuwepo milele, kama mteule wa Mungu (Yeremia 17:21-25). Badala
yake historia ya watu hawa waliopendelewa ilijazwa na matukio ya kurudi nyuma na kuasi. Walikuwa
wamepinga neema ya mbinguni, wakatumia vibaya upendeleo waliopewa, na wakachezea nafasi.
Ingawa Israeli walikuwa “wamewadhihaki wajumbe wa Mungu, wamedharau maneno yake, na
kuwacheka manabii wake" (2 Nyakati 36:16), alikuwa bado akijidhihirisha kwao kama "Bwana Mungu,
mwenye rehema na utukufu, mvumilivu, na mwenye wingi wa wema na kweli" (Kutoka 34:6). Hata kama
walikuwa wakirudia-rudia kumkataa, rehema yake ilikuwa imeendelea kuwasihi. Zaidi ya upendo wa
baba ulivyo kwa mwana wake, Mungu alikuwa ametuma kwao wajumbe wake; kwa sababu aliguswa sana
na watu wake, na mahali pa makao yake." 2 Nyakati 36:15. Hata waliposhindwa kumrudia, Mungu
aliwapelekea zawadi kubwa kuliko zote kutoka mbinguni; naam, aliimimina mbingu yote katika zawadi
hiyo moja.
Mwana wa Mungu mwenyewe alitumwa kuja kuusihi mji ule ulioasi. Alikuwa Kristo aliyekuwa amemleta
Israeli kama mzabibu mwema kutoka Misri (Zaburi 80:8). Mkono wake mwenyewe ulikuwa umeyapiga
(20) mataifa ya kipagani mbele yake. Alikuwa amempandikiza Israeli "katika kilima chenye rutuba."
Utunzaji wake ulikuwa wa hakika pande zote. Watumishi wake walikuwa wametumwa kwake ili
kumtunza. Alisema, "Ni nini zaidi ambacho ningefanya kwa mzabibu wangu ambacho sijafanya?" Isaya
5:1-4. Tazama alipoangalia kama ungezaa zabibu, ulikuwa umezaaa zabibu mwitu. Kwa kutumaini
kwamba utazaa matunda alikuja yeye mwenyewe kwa mzabibu wake, labda ungeokoka kuharibiwa.
Aliupalilia mzabibu wake; aliupogolea na kuupenda. Alikuwa na bidii bila kuchoka katika kuuokoa
mzabibu huu alioupanda yeye mwenyewe.
Kwa muda wa miaka mitatu Bwana wa nuru na utukufu alikuwa ametembea katikati ya watu wake.
Aliishi “akitenda mema, na kuponya wote walioonewa na ibilisi,” akiwahuisha waliovunjika moyo,
akiwaweka huru wafungwa, akiwarejeshea kuona waliokuwa vipofu, akiwafanya viwete kutembea na
viziwi kusikia, akiwatakasa wenye ukoma, akifufua waliokufa, na akifundisha injili kwa maskini
(Matendo 10:38; Luka 4:18; Mathayo 11:5). Kwa matabaka yote alitoa wito wa neema akisema: "Njooni
kwangu ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo mizito, nami nitawapumzisha" (Mathayo 11:28).

11
Ingawa alilipwa maovu kwa mema, na chuki kwa upendo wake (Zaburi 109:5), alikuwa amedumu
kutekeleza utume wake wa rehema. Si wale waliochukizwa naye waliopokea neema yake. Yeye asiye na
makazi, wa kulaumiwa, wa kukataliwa na aliye maskini, aliishi akiwahudumia wenye shida na kufungua
vifungo vya watu, akiwasihi wapokee zawadi ya uzima. Mawimbi ya rehema, yaliyosukumwa na wale
wenye mioyo ya usumbufu, yalirejeshwa naye kwa msukumo wa nguvu na upendo usioelezeka. Lakini
Israeli aligeukia mbali kutoka kwa Rafiki yake na Msaada wake mkubwa. Kusihi kwake kwa upendo
kulikuwa kumepuuzwa, mashauri yake yamekataliwa, na maonyo yake yamedhihakiwa.
Saa ya tumaini na msamaha ilikuwa inapita haraka; kikombe cha hasira ya Mungu kilichokuwa
kimekawizwa kilikuwa karibu kujaa. Wingu lililokuwa limejikusanya kupitia vizazi vya upotovu na kuasi,
sasa likiwa limekuwa jeusi kwa ghadhabu, lilikuwa linakaribia kuwalipukia watu walioasi; (21) na yeye
pekee ambaye angewaokoa na uangamivu amedharauliwa, kutukanwa na kukataliwa, na baada ya
kitambo kidogo alikuwa asulibiwe. Wakati Yesu anapoangikwa msalabani Kalvari, ndipo mwisho wa
Israeli kuwa taifa lililochaguliwa na kubarikiwa na Mungu ungekuwa umefika. Kupotea kwa roho hata
moja ni balaa kubwa linalozidi utajiri na mali za dunia; lakini Yesu alipoiangalia Yerusalemu,
maangamizi ya mji wote, taifa lote, yalikuwa mbele yake – mji ule, taifa lile ambalo hapo kabla
lilichaguliwa na Mungu kuwa hazina yake ya pekee.
Manabii walikuwa wamelia juu ya uasi wa Israeli na maangamizi ya kutisha ambayo yangeletwa na
dhambi zake. Yeremia alikuwa ametamani kwamba macho yake yangekuwa chemchemi ya machozi, ili
aweze kulia usiku na mchana kwa habari ya kuchinjwa kwa binti wa watu wake, kwa ajili ya kundi la
Bwana lililochukuliwa utumwani (Yeremiah 9:1; 13:17). Je, yalikuwa maumivu kiasi gani kwake yeye
ambaye manabii walimwangalia, si kwa miaka, bali vizazi na vizazi! Aliona malaika mwenye kuharibu
akiwa na upanga ulioinuliwa juu ya mji ambao kwa muda mrefu ulikuwa ni mahali pa makao ya Yehova.
Kutoka kwenye kilima cha Mizeituni, mahali ambapo baadaye palivamiwa na Tito na jeshi lake,
aliangalia na kuona bonde la eneo takatifu, na kwa macho yanayolengalenga machozi aliona kuta
zilizozingirwa na majeshi ya adui. Alisikia vishindo vya miguu vya majeshi ya adui yaendayo vitani.
Alisikia sauti za akina mama na watoto wakililia mkate katika mji ambao umehusuriwa. Aliona hekalu
lake zuri na takatifu, kumbi zake na minara yake, vikiwashwa moto, na mahali pake kubaki na rundo la
vifusi vinavyofuka moshi wa moto unaoharibu.
Akiangalia mbele ya nyakati, aliwaona watu waliokuwa wa agano lake wakiwa wametawanyika huku na
huko, "kama vipande vya chombo kilichovunjika-vunjika katika kingo za jangwa." Kwa uharibifu wa awali
ambao ungewapata watoto wake, aliona mwanzo tu wa hasira itakayomwagwa katika hukumu ya
mwisho. Huruma ya uungu, kiu ya upendo vilitamkwa katika maneno ya kuomboleza: "Ee Yerusalemu,
Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga mawe wale wanaotumwa kwako! ni mara ngapi nimetaka
(22) kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo viranga vyake chini ya mabawa
yake, lakini hukutaka!" Ewe taifa uliyependelewa kuliko mengine yote, laiti ungejua muda wa kujiliwa
kwako, na mambo yanayokupasa wakati wa amani! Nimekaa kama malaika wa haki, nimekusihi utubu,
lakini haukufanya hivyo. Si tu kwamba umewakataa watumishi na manabii waliotumwa kwako, bali pia
hata Aliye Mtakatifu wa Israeli, Mkombozi wako. Ikiwa utaharibiwa, ni kwa sababu yako mwenyewe.
"Wala hamkutaka kuja kwangu mpate kuwa na uzima." Mathayo 23:37; Yohana 5:40.
Katika Yerusalemu, Kristo aliona alama ya ulimwengu uliogubikwa na roho ya kutokuamini na uasi,
ukifanya haraka kwenda kukutana na hukumu ya Mungu. Taabu ya mwanadamu aliyeanguka,
iliyokandamiza nafsi yake Yesu, ilitoka katika midomo yake ikiwa ni zaidi ya kilio cha uchungu. Aliona
kumbukumbu iliyojaa dhambi katika taabu, machozi na damu; moyo wake ulivutwa na huruma kwa
wadhambi wanaoteseka duniani; alitamani kuwaokoa wote. Lakini hata mkono wake usingeweza
12
kurudisha nyuma msukumo wa taabu za mwanadamu; wachache ndio wangetafuta msaada kwake yeye
aliye chanzo cha msaada. Alikuwa tayari kuimimina roho yake hata kufa, ili kuuleta wokovu mahali
ambapo wanaweza kuufikia; lakini wachache ndio wangekuja ili wawe na uzima.
Mfalme wa mbingu analia machozi! Mwana wa Mungu aliye hai anasumbuka moyoni na kuinama chini
kwa huzuni! Tukio hili liliijaza mbingu yote mshangao. Ni tukio linalotuonyesha namna dhambi ilivyo;
linatuonyesha namna ilivyo ngumu, hata kwa nguvu ya mbingu, kumwokoa mdhambi kutoka katika
matokeo ya hatia ya kukiuka sheria ya Mungu. Yesu, akiangalia mbali katika kizazi cha mwisho, aliuona
ulimwengu ukiwa katika upotofu kama ule ule uliosababisha uharibifu wa Yerusalemu. Dhambi kubwa ya
Wayahudi ilikuwa ni kumkataa Kristo; dhambi kubwa ya ulimwengu wa Kikristo ingekuwa kuikataa sheria
ya Mungu, msingi wa serikali yake mbinguni na duniani. Mafundisho ya Yehova yangepuuzwa na
kuonekana si kitu. Mamilioni walio katika vifungo vya dhambi, watumwa wa Shetani, wanaosubiri
kukumbwa na mauti ya pili, (23) wangekataa kusikiliza maneno ya kweli katika siku za kujiliwa kwao.
Upofu wa kutisha! Kupenda dunia kusiko na maana!
Siku mbili kabla ya Pasaka, Yesu alipokuwa ameondoka mara ya mwisho hekaluni, baada ya kukemea
unafiki wa viongozi wa Wayahudi, alitoka akaenda tena na wanafunzi wake kwenye Mlima wa Mizeituni
na akakaa nao kwenye majani yaliyo katika mtelemko unaoikabili Yerusalemu. Mara tena alizitazama
kuta zake na minara yake. Na mara nyingine tena alilitazama hekalu katika mng’ao na uzuri wake
ulioupendezesha mlima mtakatifu.
Miaka elfu moja iliyopita, mwimba zaburi alikuwa ameutukuza upendeleo wa Mungu kwa Israeli kwa
kuifanya nyumba yake takatifu ya Israeli kuwa makazi yake: "Hema lake liko Salemu, makao yake katika
Sayuni." Lakini alilichagua kabila la Yuda, Mlima Sayuni, ambao aliupenda. Alijenga mahali patakatifu
pake kama vilele, kama dunia ambayo aliiimarisha milele" (Zaburi 76:2; 78:68, 69). Hekalu la kwanza
lilikuwa limejengwa katika kipindi ambacho Israeli ilikuwa katika mafanikio kuliko kipindi kingine
chochote katika historia yake. Hazina ya kutosha kwa lengo la kazi hii ilikuwa imekusanywa na Mfalme
Daudi, na mipango ya ujenzi wa hekalu hili ilifanywa kwa uvuvio wa Mungu (1 Nyakati 28:12, 19).
Sulemani, mwenye hekima kuliko wafalme wote wa Israeli, alikuwa ameikamilisha kazi hiyo. Hekalu hili
lilikuwa zuri kuliko yote ambayo ulimwengu ulikuwa umepata kuona. Lakini Bwana alikuwa amenena
kupitia Nabii Hagai, kuhusu hekalu la pili: "Utukufu wa hekalu hili jingine utakuwa mkubwa kuliko huo
wa hekalu la awali." "Nitayatikisa mataifa yote, na Tumaini la mataifa yote litakuja; na nitaijaza
nyumba hii utukufu, asema Bwana wa Majeshi" (Hagai 2:9, 7).
Baada ya hekalu kuharibiwa na Nebukadnezar lilijengwa tena karibu miaka 500 kabla ya Kristo kuzaliwa.
Lilijengwa na watu ambao walikuwa wamekaa utumwani kwa muda mrefu wa maisha yao na walikuwa
wamerejea katika nchi iliyoharibiwa na kuachwa ukiwa. Walikuwemo miongoni mwao wazee ambao
waliona utukufu wa hekalu la Sulemani, ambao walilia panapo msingi wa jengo hili jipya la hekalu,
kwamba huenda hili likawa hafifu kuliko lile la awali. Hisia iliyokuwepo inaelezwa hapa na nabii: "Nani
amesalia miongoni mwenu aliyeona nyumba hii katika utukufu wake wa kwanza? Na je mnaionaje sasa?
Je machoni mwenu si mnaiona kama si kitu?" Hagai 2:3; Ezra 3:12. Hatimaye, ilitolewa ahadi kwamba
utukufu wa nyumba hii ungekuwa mkubwa kuliko ule wa ile ya kwanza.
Lakini hekalu la pili halikuwa na uzuri kama ule wa lile la kwanza; wala halikudhihirishwa na
mwonekano wa kuwepo kwa Mungu kama ilivyokuwa katika hekalu la kwanza. Hakukuwa na udhihirisho
wa nguvu na uweza ulioashiria kuwekwa wakfu kwake. Hakukuwa na wingu la utukufu lililojaza
patakatifu. Hakuna moto ulioshuka madhabahuni kutoka mbinguni ili kuteketeza dhabihu. Hakukuwa na
Shekina katikati ya makerubi katika patakatifu pa patakatifu; sanduku, kiti cha rehema, na meza za

13
ushuhuda zisingeonekana mle ndani. Hakuna sauti iliyotoka mbinguni kuwajulisha makuhani mapenzi ya
Yehova.
Kwa karne nyingi Wayahudi walikuwa wametafuta pasipo mafanikio kuonyesha ikiwa ahadi ya Mungu
aliyotoa kupitia Hagai ilikuwa imetimia; lakini kiburi na kutokuamini vilipofusha mawazo yao wasielewe
maana halisi ya maneno ya nabii. Hekalu la pili halikujazwa na utukufu wa Yehova, isipokuwa kwa
uwepo wake yeye aliye na ujazo wote wa Uungu – aliyekuwa Mungu mwenyewe akijidhihirisha katika
mwili. Yeye aliye “Tumaini la mataifa yote” alikuwa amekuja katika hekalu lake wakati Mnazareti
alipofundisha na kuponya. Katika uwepo wa Kristo, na katika huu tu, ndipo hekalu la pili lilipolizidi la
kwanza kwa utukufu. Lakini Israeli alikuwa ameachana na zawadi hii muhimu ya mbinguni. Utukufu wa
hekalu uliondoka pamoja na Mwalimu huyu mnyenyekevu aliyeondoka hekaluni kupitia lango lake la
dhahabu siku ile. Hapo maneno ya Mwokozi yalikuwa yametimia: “Nyumba yenu mmeachiwa hali ya
ukiwa" (Mathayo 23:38).
Wanafunzi walikuwa wamejawa na mshangao wakati Kristo alipotabiri kuhusu uharibifu wa hekalu, na
walitamani kuelewa vizuri maana ya maneno yake. Mali, kazi na ujuzi wa kusanifu majengo ulikuwa
umetumika kwa miaka zaidi ya 40 kukamilisha uzuri wake. Herode (25) Mkuu alikuwa ametoa mali za
Roma na hazina ya Wayahudi, hata na mtawala wa ulimwengu alikuwa ameliongezea mali zake. Mawe
makubwa ya marumaru, yalitoka Roma kwa ajili ya kazi ya jengo hili, na yakafanya sehemu ya
mwonekano wa jengo. Ni mawe hayo ambayo kwayo wanafunzi wanavuta hisia za Bwana wao,
wakisema: "Tazama, yalivyo mawe na majengo haya!" Marko 13:1.
Kwa maneno hayo waliyosema, Yesu alijibu kwa masikitiko na mshangao: "Amin, nawaambia, Halitasalia
jiwe juu ya jiwe hapa, ambalo halitabomoshwa." Mathayo 24:2.
Wanafunzi walihusianisha utabiri wa kuharibiwa kwa Yerusalemu na ujio wa muda wa Kristo katika
mwili kutawala, kuwaadhibu Wayahudi wakorofi, na kuvunjavunja kongwa la Warumi. Bwana alikuwa
amewaambia kwamba atakuja tena mara ya pili. Kwa hiyo kwa kutaja hukumu juu ya Yerusalemu,
mawazo yao yalielekea katika ujio ule, na walipokuwa wamekusanyika na Mwokozi kwenye Mlima wa
Mizeituni, waliuliza: “Mambo hayo yatakuwa lini? Na ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa
dunia?” Fungu la 3.
Wakati ujao ulifunikwa na rehema zake na kufichwa machoni pa wanafunzi. Ikiwa wangeelewa kwa
ukamilifu wakati ule ule matukio mawili – mateso ya Mkombozi na kifo chake, na kuharibiwa kwa mji
wao na hekalu - wangejawa na hofu. Kristo aliwaeleza kwa ufupi matukio ambayo yangetukia kabla ya
kufungwa kwa wakati. Maneno yake yalikuwa bado hayajaeleweka vizuri; lakini maana yake
ingefunguliwa kadiri watu watakavyohitaji mafundisho yake yaliyomo humo. Unabii uliosemwa ulikuwa
na maana mbili: wakati ukiwa unaelekeza katika uharibifu wa Yerusalemu, ulikuwa ukiwakilisha pia
utisho wa siku kuu ya mwisho.
Yesu aliwaambia wanafunzi waliokuwa wakimsikiliza hukumu ambazo zingeanguka juu ya Israeli iliyoasi,
na hasa adhabu ambayo ingekuja juu yake kwa sababu ya kumkataa na kumsulibisha Masihi. Dalili zisizo
na makosa zingetangulia kabla ya mwisho wa tukio. Saa ya kutisha ingekuja (26) ghafla na haraka.
Mwokozi aliwaonya wafuasi wake: “Basi mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii
Danieli, limesimama patakatifu, (asomaye na afahamu); ndipo yeye aliye Uyahudi akimbilie milimani."
Mathayo 24:15, 16; Luke 21:20, 21. Wakati viwango vya uasherati wa Warumi vitakaposimamishwa
katika mahali patakatifu, ambapo palifika mpaka nje ya kuta za mji, ndipo wafuasi wa Kristo
wangetafuta salama yao kwa kukimbia. Dalili ya onyo itakapoonekana, lazima wale wa kuokoka wasiwe
na muda wa kuchelewa. Katika nchi yote ya Uyahudi, na Yerusalemu yenyewe, ishara ya kukimbia
14
lazima itiiwe. Yeye ambaye alijikuta juu ya nyumba asirudi tena ndani ya nyumba yake, hata kama ni
kuokoa vitu vyake vya thamani kubwa. Wale waliokuwa wanafanya kazi katika shamba wasitumie muda
zaidi kurudi kuchukua nguo zao walizoweka pembezoni mwa shamba wakati wa kazi. Wasiwe na muda
wa kukawia hata kidogo, la sivyo watapitiwa na uharibifu.
Katika utawala wa Herode, Yerusalemu haikuwa tu imetengenezwa vizuri sana, bali pia kuinuliwa kwa
kuta, minara na maboma viliongeza uzuri wake wa asili, na kuongeza uimara na usalama wake. Yeye
ambaye wakati huo angetabiri hadharani kuhusu kuharibiwa kwa mji huu angeonekana mpiga-mbiu
aliyerukwa na akili, kama ilivyokuwa kwa Nuhu wakati wa kipindi chake. Lakini Kristo alikuwa amesema:
“Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita" (Mathayo 24:35). Kwa sababu ya dhambi
zake, hasira imetangazwa dhidi ya Yerusalemu, na kutokuamini kwake kulikuwa kumefanya uangamivu
wake kuwa hakika.
Bwana amesema kupitia nabii Mika: "Sikieni hili, enyi viongozi wa nyumba ya Yakobo, enyi watawala wa
nyumba ya Israeli, mnaodharau haki na kupotosha kila lililo sawa, mnaojenga Sayuni kwa kumwaga
damu na Yerusalemu kwa uovu. Viongozi wake wanahukumu kwa rushwa, makuhani wake wanafundisha
kwa malipo na manabii wake wanatabiri kwa fedha. Hata hivyo wanamwegemea BWANA na kusema,
“Je, BWANA si yumo miongoni mwetu? Hakuna maafa yatakayotupata." Mika 3:9-11. (27)
Kwa uaminifu kabisa, maneno haya yalielezea kuhusu upotofu na kujihesabia haki kwa wakazi wa
Yerusalemu. Wakijigamba kwamba wanashika mafundisho ya sheria ya Mungu, walikuwa wakikiuka
kanuni zake zote. Walimchukia Kristo kwa sababu usafi na utakatifu wake ulifunua maovu yao; na
walimshtaki kwamba yeye ndiye sababu ya matatizo yaliyowapata kama matokeo ya dhambi zao.
Ingawa walifahamu kwamba yeye hana dhambi, walikuwa wametangaza kwamba kifo chake kilikuwa
muhimu kwa ajili ya usalama wao kama taifa. “Kama tukimwacha huru, watu wote watamwamini,”
walisema viongozi wa Wayahudi; “na Warumi watakuja na watatuondolea mahali petu na taifa letu.”
Yohana 11:48. Waliona kwamba kama Yesu angetolewa kafara, wangerejea tena kuwa na nguvu na
umoja. Kwa hiyo walitoa hoja na kukubaliana na uamuzi wa makuhani, kwamba ni vema mtu mmoja afe
kuliko taifa zima kuangamia.
Kwa hiyo viongozi wa Wayahudi walikuwa wameijenga “Sayuni kwa damu, na Yerusalemu kwa uovu”
(Mika 3:10). Hata hivyo, wakati walimchinja Mwokozi wao kwa sababu alikemea dhambi zao, hiyo
ilikuwa ni kujihesabia haki wao wenyewe kama walivyojiona wenyewe kwamba ni taifa lililopendwa na
Mungu na wakimtegemea Bwana awaokoe na adui zao. "Kwa hiyo," nabii aliendelea kusema, "Sayuni
italimwa kama shamba, Yerusalemu itakuwa rundo la kokoto na kilima cha hekalu kuwa kama kichuguu
kilichofunikwa na vichaka." Fungu la 12.
Kwa karibu miaka 40 baada ya uangamivu juu ya Yerusalemu kutangazwa na Kristo mwenyewe, Bwana
alikawiza hukumu zake juu ya mji na taifa hili. Uvumilivu wa Bwana ulikuwa wa ajabu sana kwa watu
hawa waliokataa injili yake na wauaji wa Mwana wake. Mfano wa mti usiozaa matunda uliwakilisha
namna Mungu alivyochukuliana na taifa la Wayahudi. Amri imetolewa, "Ukate; mbona hata nchi
unaiharibu?" (Luka 13:7) lakini rehema za Mungu zimeiacha tena kwa muda. Bado walikuwepo wengi
miongoni mwa Wayahudi ambao hawakujua tabia na kazi ya Kristo. Na watoto hawakuwa wamepata
fursa au (28) nafasi ya kupokea mwanga ambao wazazi wao walikuwa wameupuuza. Kwa njia ya
mahubiri ya mitume na washirika wao, Mungu angesababisha wao kuangaziwa nuru; wangeruhusiwa
kuona jinsi unabii unavyotimia, si tu katika kuzaliwa na maisha ya Kristo, lakini pia katika kifo na
kufufuka kwake. Watoto hawakuhukumiwa kwa dhambi za wazazi wao; lakini kwa kukataa nuru

15
iliyotolewa kwao kama ziada ya ile waliyopata toka kwa wazazi wao, walikuwa wameshiriki dhambi za
wazazi, na kukijaza kipimo cha uovu wao.
Uvumilivu wa Mungu kwa Yerusalemu uliishia tu kwa wao kudhihirisha utovu wa toba. Kwa chuki na
ukatili wao kwa wanafunzi wa Yesu walikataa nafasi ya mwisho ya rehema. Ndipo Mungu aliondoa ulinzi
na nguvu yake imzuiayo Shetani na malaika zake, na taifa likaachwa katika udhibiti wa kiongozi ambaye
lilikuwa limemchagua. Watoto wake walikuwa wamekataa neema ya Kristo, ambayo ingewawezesha
kutawala tamaa zao za uovu, na hivyo zikawashinda. Shetani akainua mateso makali ya kutisha kwa
nafsi zao. Watu hawakufikiri vema; walikuwa mbali na fikra sahihi – wakiongozwa na tamaa na hasira.
Walikuwa na ushetani katika ukatili wao. Katika jamaa na katika taifa, katika matabaka ya juu na ya
chini, kulikuwa na mashaka, husuda, chuki, ugomvi, uasi na mauaji. Hakukuwa na usalama mahali
popote. Marafiki na ndugu walisalitiana wao kwa wao. Wazazi walichinja watoto wao na watoto
walichinja wazazi wao. Watawala wa watu walishindwa kujitawala wenyewe. Mateso yasiyo na udhibiti
yaliwafanya kuwa watu wasio na mipaka. Wayahudi walikuwa wamekubali ushahidi wa uongo katika
kumhukumu Mwana wa Mungu asiye na kosa. Sasa mashtaka yao yasiyo sahihi yalifanya maisha yao
yasiwe na uhakika. Kwa matendo yao walikuwa wamesema: "Mkomesheni Mtakatifu wa Israeli mbele
yetu." Isaya 30:11. Sasa nia yao ilitekelezwa. Ile hofu ya Mungu haikuwepo tena kuwasumbua. Shetani
(29) alikuwa akiliongoza taifa, na mamlaka ya juu ya kiraia na kidini ilikuwa chini yake.
Viongozi wa makundi pinzani waliungana kuvamia na kuwatesa watu, halafu waligeukiana na kuchinjana
bila huruma. Hata utakatifu wa hekalu haukustahimili ukatili wao wa kutisha. Waabuduo hekaluni
walipigwa mbele ya madhabahu, na patakatifu palichafuliwa na miili ya watu waliochinjwa. Lakini bado
katika upofu wao na kukufuru watu hawa waliendelea kusema kwamba hawana hofu na kuharibiwa kwa
Yerusalemu, maana ulikuwa mji wa Mungu. Kudhihirisha nguvu zaidi, walihonga manabii wa uongo ili
watoe unabii wa uongo, hata majeshi ya Kirumi yalipokuwa yakilikabili hekalu, kwamba watu walipaswa
kusubiri wokovu toka kwa Mungu. Mwisho, makutano waliendelea kuamini kwamba Aliye Juu angeingilia
kati na kufanya adui kushindwa. Lakini Israeli alikuwa amekataa ulinzi wa Mungu, na sasa hakuwa na
kinga. Yerusalemu isiyo na furaha! Kwa uasi wake ikilipa damu ya watoto wake waliochinjwa na mikono
yao wenyewe, wakati majeshi ya adui yakiwapiga na kuwaua watu wake wa vita!
Utabiri wote wa Kristo juu ya uharibifu wa Yerusalemu ulikuwa unatimia. Wayahudi walipatwa na
ukweli wa maneno yake ya onyo: "Kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa." Mathayo 7:2.
Ishara na maajabu vilitokea, majanga na uangamivu. Wakati wa usiku wa manane, mwanga usio wa
kawaida ulimulika juu ya hekalu na madhabahu. Wakati wa kutua kwa jua, mawingu yalionyesha picha
za wapanda farasi na watu waendao vitani wakijikusanya kwa vita. Makuhani wanaohudumu patakatifu
usiku waliogofywa na sauti za ajabu; dunia ikatetemeka, na sauti za mkusanyiko zikasikika zikilia: "Na
tuondoke sasa." Lango kuu la mashariki, lililokuwa zito sana kiasi kwamba watu wachache wasingeweza
kulifunga, na ambalo lilikuwa limeimarishwa kwa (30) nguzo za chuma zilizochimbiwa katika mwamba,
lilifunguka wakati wa usiku, pasipo kufunguliwa na kitu kinachoonekana. 1
Kwa muda wa miaka saba mtu mmoja alizunguka katika mitaa ya Yerusalemu, akitangaza ole zilizokuwa
zinaujia mji. Usiku na mchana aliendelea na wimbo wake wa kilio: "Sauti kutoka mashariki! Sauti kutoka
magharibi! Sauti kutoka katika pepo nne! Sauti dhidi ya Yerusalemu na dhidi ya hekalu! Sauti dhidi ya
mabwana arusi na mabibi arusi! Sauti dhidi ya watu wote!." 2 Kiumbe huyu wa ajabu alitiwa gerezani na
kupigwa, lakini hakuna malalamiko yaliyotoka midomoni mwake. Katika matukano na kutendewa jeuri

1
Milman, The History of the Jews, book 13
2
Milman, The History of the Jews, book 13
16
kote yeye alijibu akisema: "Ole, ole kwa Yerusalemu!" "Ole, ole kwa wakazi walio ndani yake!" Kilio
chake cha onyo hakikukoma hadi alipouawa wakati wa maangamizi aliyokuwa ameyatabiri.
Hakuna Mkristo hata mmoja aliyepotea katika kuharibiwa kwa Yerusalemu. Yesu alikuwa amewapa
wanafunzi wake onyo, na wote walioamini maneno yake walikuwa macho juu ya ishara iliyoahidiwa.
Yesu alisema: "Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya
kwamba uharibifu wake umekaribia. Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio
katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie." Luka 21:20, 21. Baada ya Warumi
kuuzunguka mji wakiongozwa na Cestius, pasipo kutarajiwa waliacha kuushambulia mji wakati nafasi na
uwezekano wote viliruhusu wao kuushambulia upesi. Waliokuwa wanavamiwa, hawakuwa na matumaini
ya kupinga mashambulizi, walikuwa wamefikia hatua ya kusalimu amri; huo ndio wakati ambapo
Jemadari wa majeshi ya Kirumi alirudisha majeshi yake nyuma pasipo na sababu yoyote. Kumbe rehema
ya Mungu ilikuwa inatolewa kwa watu wake. Ishara ya ahadi ilikuwa imetolewa kwa Wakristo
waliosubiri, na kwa hiyo nafasi ilitolewa kwa wote waliokuwa tayari kutii onyo la Mwokozi. Matukio yote
yalikuwa yanaratibiwa kiasi kwamba Wakristo hawakuzuiliwa na Wayahudi wala Warumi kukimbia.
Cestius aliporudi nyuma, Wayahudi waliuacha mji na kuwafuata nyuma ili kuwakabili; na wakati
mapambano yakiwa yamepamba moto, Wakristo walipata nafasi ya kuukimbia mji. Wakati huu nchi pia
(31) haikuwa na adui wa kuwazuia watu wa Mungu kukimbia. Wakati wa uharibifu, Wayahudi walikuwa
wamekusanyika Yerusalemu kwa ajili ya Sikukuu ya Vibanda, kwa hiyo Wakristo wote waliweza kutoroka
kwa urahisi. Pasipo kuchelewa walikimbilia mahali pa salama – katika mji wa Pela, katika nchi ya Perea,
ng’ambo ya Yordani.
Majeshi ya Kiyahudi, yakimfuata Cestius na majeshi yake, yaliwainukia kwa upande wa nyuma na kutaka
kuwaangamiza. Warumi walifanikiwa kuwarudisha nyuma kwa shida sana. Karibu pasipo hasara yeyote,
Wayahudi walirudi Yerusalemu na nyara za vita wakishangilia ushindi. Hata hivyo, mafanikio hayo
yaliwaletea mabaya makubwa. Yalichochea upinzani na ukaidi kutoka kwa Warumi, vitu ambavyo
viliwaletea ole na maangamizi yasiyosemeka.
Maafa makubwa yaliuangukia Yerusalemu wakati uvamizi ulipofanywa kwa mara nyingine ukiongozwa na
Tito. Mji ulizingirwa wakati wa kipindi cha Pasaka, wakati ambapo mamilioni ya Wayahudi walikuwa
wamekusanyika ndani ya kuta zake. Maghala ya vyakula, ambavyo kama vingehifadhiwa kwa uangalifu
vingeweza kuwa chakula cha wakazi kwa miaka, vilikuwa vimeharibiwa na adui waliokuwa wanalipiza
kisasi, na kwa hiyo janga la njaa lilikuwa lao. Kipimo cha ngano kiliuzwa kwa talanta. Njaa ilikuwa kali
kiasi kwamba watu walikula ngozi za mikanda, ndala na mikoba yao. Watu wengi walitoka usiku kwa
kificho ili kukusanya mimea ya mwitu iliyoota nje ya kuta za mji. Wengi wao walitekwa na kuuawa
kikatili sana, na mara nyingi wale waliofanikiwa kurudi walinyang’anywa na wenzao hata kile
walichopata kwa hatari na shida kubwa. Mateso mengi ya kikatili yalifanywa na wale wenye madaraka,
kuwanyang’anya wale wasio nacho hata kile kidogo walichobaki nacho. Ukatili kama huu haukuwa wa
kawaida kufanywa na watu ambao wametosheka, tena wale ambao walikuwa watunzaji wa chakula
katika ghala kwa ajili ya siku za usoni. (32)
Maelfu ya watu walikufa kwa njaa na maradhi. Upendo wa asili ulipotea miongoni mwa watu. Wanaume
waliwaibia wake zao, na wake wakawaibia waume zao. Watoto wangeonekana wakikwapua chakula
kutoka mdomoni mwa wazazi wao waliokuwa wazee. Swali la nabii, "Je mama aweza kumsahau mtoto
wake anayenyonya?" lilipata jibu ndani ya kuta za mji huu uliokuwa ukiangamia: "Mikono ya wanawake
ikawageukia watoto wao; walikuwa nyama yao wakati wa uharibifu wa binti wa watu wangu." Isaya
49:15; Maomboleza 4:10. Pia ulitimia unabii wa onyo uliotolewa karne 14 kabla: "Mwanamke ambaye ni
mwungwana sana na makini miongoni mwako, yaani, ambaye ni makini sana na muungwana kiasi
17
kwamba asingethubutu kugusa ardhi kwa wayo wa mguu wake, yeye atakuwa mchoyo kwa mume
ampendaye na mwanawe mwenyewe au binti yake … na watoto anaowazaa, kwa kuwa anakusudia
kuwala kwa siri wakati wa kuzingirwa na katika taabu zile ambazo adui yako atazileta juu yako na miji
yako." Kumbukumbu la Torati 28:56, 57.
Viongozi wa Warumi walidhamiria kuwapiga Wayahudi kwa kipigo kile ambacho kingewafanya kusalimu
amri. Wale mateka walioleta upinzani wakati wa kuchukuliwa walipigwa, kuteswa na kutundikwa katika
misalaba mbele ya ukuta wa mji. Mamia ya watu waliuawa kwa namna hii kila siku, na kazi hii ya
kutisha iliendelea kiasi kwamba, katika bonde la Yehoshafati na kwenye mlima wa Kalvari, misalaba
iliinuliwa kwa wingi sana kiasi kwamba ilikuwa vigumu kupata njia ya kupita katikati yake. Kwa hiyo
yakatimia maneno yaliyotamkwa mbele ya kiti cha hukumu cha Pilato: "Damu yake na iwe juu yetu, na
juu ya watoto wetu." Mathayo 27:25.
Jemadari Tito alitamani kusitisha tukio hili la kutisha ili kuiponya Yerusalemu na ujazo wa kipimo cha
maangamizi. Alijawa na hofu alipoona mirundikano ya miili ya waliouawa bondeni. Kama aliyevutwa na
mawazo, alilitazama hekalu tukufu na la fahari kutoka katika kilele cha Mlima wa Mizeituni, akatoa
amri kwamba hata jiwe moja la jengo hilo lisiguswe. Kabla hajaifikia ngome hii ya hekalu, (33) aliwasihi
viongozi wa Wayahudi wasimlazimishe kunajisi mahali patakatifu kwa damu. Laiti kama wangetoka na
kuja kupigania katika eneo jingine, hakuna Mrumi ambaye angeharibu utakatifu wa hekalu. Josephus
mwenyewe aliwasihi sana kwamba wasalimu amri, ili wajiokoe, waokoe mji wao, na mahali pao pa
ibada. Lakini maneno yake yalijibiwa kwa matukano na kulaani sana. Alishambuliwa, wakati akisimama
kuwasihi kama mpatanishi wao wa kibinadamu wa mwisho. Wayahudi walikuwa wamekataa wito wa
Mwana wa Mungu, na sasa wito huu uliwafanya tu wapinge kwa nguvu mpaka mwisho. Juhudi za Tito
kuliokoa hekalu zilikuwa kazi bure; Mkuu kuliko yeye alikuwa ameshasema kuwa jiwe lisingesalia juu ya
jiwe.
Ugumu na upofu wa viongozi wa Wayahudi, na uhalifu uliokuwa ukifanywa katika mji uliozingirwa,
ulihamasisha hasira ya uharibifu ya Warumi, na Tito hatimaye aliazimia kuliteka hekalu kwa nguvu.
Aliazimia hata hivyo kwamba, kama ingewezekana, lisiharibiwe. Lakini maagizo yake hayakuzingatiwa.
Wakati alipokwenda kupumzika katika hema lake, Wayahudi walitoka katika hekalu na kuwavamia watu
wa vita waliokuwa nje. Katika mapambano, askari mmoja aliingiza moto ndani ya hekalu kupitia
mwanya wa kibaraza cha hekalu, na tazama sehemu za ndani za patakatifu zikaanza kuwaka moto. Tito
alikimbilia mahali pa tukio, akifuatiwa na makamanda na viongozi wa majeshi, na kuamrisha askari
wauzime moto. Maneno yake hayakutiiwa. Kwa hasira askari waliendelea kusambaza moto katika
vyumba vingine, halafu wakawaua kwa upanga watu wengi waliokuwa wamejificha humo hekaluni.
Damu ilitiririka katika ngazi za hekalu kama maji. Maelfu kwa maelfu ya Wayahudi waliangamia.
Ukiacha sauti ya vita vyenyewe, sauti nyingine zilizosikika ni zile zilizopiga kelele zikisema: "Ichabod!" –
utukufu umetoweka.
"Tito alishindwa kudhibiti hasira ya askari wake; aliingia na maafisa wake, na kukagua vyumba vya ndani
ya patakatifu. Uzuri wake uliwashangaza sana; na kwa kuwa moto ulikuwa haujapenya hadi mahali
patakatifu, (34) alifanya jitihada yake ya mwisho kupaokoa, akiwataka askari wasiendelee na uharibifu.
Kiongozi huyu alitaka kulazimisha utii wa maafisa wake lakini hakuweza kuzuia hasira ya wapiganaji
hawa dhidi ya Wayahudi. Askari waliona vitu vyote vilivyokuwa karibu yao viking’aa kwa dhahabu,
vikimetameta kwa mwanga wa moto; wakaona kwamba utajiri usiopimika ulikuwa umetumika katika
kujenga patakatifu hapa. Askari asiyejulikana, aliwasha kijinga chake cha moto kupitia katikati ya
mlango: na tazama jengo lote lilionekana likiwaka moto. Moto na moshi mzito ulisababisha maofisa
waliokuwa wakizuia kushindwa, na jengo lote likaachwa katika hatima yake lenyewe.
18
"Ilikuwa kama jambo la tamasha na maonyesho kwa Warumi – Ilikuwa jambo la kutisha jinsi gani kwa
Wayahudi? Kilele chote cha mlima ambao mji uko juu yake kiliwaka kama volkano. Nyumba moja baada
ya nyingine zilianguka, kwa kishindo, na kumezwa pamoja. Mapaa ya nyumba na minara ya malango
yalikuwa yanawaka moto, yakipandisha juu miale ya moto na moshi. Vilima vilivyokuwa jirani viliwaka
pia, na makundi ya watu walionekana wakiangalia kwa mshangao na hofu kazi hii ya uharibifu. Kelele za
majeshi ya Roma waliokuwa wakikimbia huku na huko, na kelele za yowe kutoka kwa wale waliokuwa
wanaangamia katika moto, zilichanganyika na sauti za milipuko na vishindo vya mbao zilizokuwa
zikidondoka. Mwangwi kutoka milimani ulirudisha sauti, zilizopokelewa na kuta, na sauti za wale
waliokuwa na njaa wakilia kwa nguvu ndogo waliyokuwa wamesalia nayo. (35)
"Mauaji yaliyokuwa ndani yalikuwa ya kutisha kuliko kile kilichoonekana kwa nje. Wanaume kwa
wanawake, wazee kwa vijana, watu wa kawaida na makuhani, wapiganaji na watu wa kawaida
waliostahili huruma, waliangamizwa kwa pamoja. Idadi ya waliouawa ilizidi ile ya wauaji. Ilibidi
wapiganaji wapande vilima vya mirundikano ya miili ya waliokufa wakati wa kuendelea kuimaliza kazi
yao." 3
Baada ya uharibifu wa hekalu, mji wote ulikuwa mikononi mwa Warumi. Viongozi wa Wayahudi waliacha
ngome zao, na Tito alizikuta tupu. Alizunguka-zunguka humo akiangalia uzuri wake, na akasema
kwamba Mungu ndiye amezitia mikononi mwake; maana hakuna mitambo ambayo ina nguvu za kuweza
kupenya ngome hizo. Mji na hekalu vilivunjwa vyote tangu misingi yake, na mahali ambapo nyumba
takatifu ilikuwa palikuwa “kama shamba lilimwavyo." Yeremia 26:18. Katika uvamizi na mauaji haya ya
pili, zaidi ya watu milioni moja waliangamia; walionusurika walichukuliwa mateka, wengine waliuzwa
kama watumwa, wengine walikokotwa hadi Roma kusherehesha ushindi, wengine walitupwa kwa
wanyama-mwitu wakali katika maonyesho ya hadhara, na wengine walitawanyika katika nchi bila ya
makazi.
Wayahudi walikuwa wametengeneza hatima yao wenyewe; walikuwa wamekijaza kikombe chao cha
kisasi. Katika uharibifu uliolikumba taifa lao, na katika ole iliyowafuata katika kutawanyika kwao,
walikuwa wakivuna matokeo ya kazi ya pando la mikono yao. Nabii anasema: "Ee Israeli, umejiangamiza
mwenyewe;" "kwa maana umeanguka kwa sababu ya maovu yako." Hosea 13:9; 14:1. Mateso yao
yanaonekana kuwa adhabu iliyoletwa kwao na tamko la Mungu. Ni kama vile mdanganyifu mkuu
anakanusha kazi yake mwenyewe. Kwa kukataa upendo na rehema za Mungu, Wayahaudi walikuwa
wamesababisha kuondolewa kwa ulinzi wa Mungu kutoka kwao, na Shetani alikuwa ameruhusiwa
kutawala juu yao kulingana na matakwa yake. Ukatili wa kutisha wakati wa (36) uharibifu wa
Yerusalemu ni udhihirisho wa nguvu ziangamizazo za Shetani juu ya wale anaowatawala.
Hatuwezi kujua ni kiasi gani tunawiwa na Kristo kwa ajili ya amani na ulinzi wake kwetu. Ni uwezo wa
Mungu unaozuia mwanadamu asipite katika udhibiti kamili wa Shetani. Wasiotii na wasio na shukrani
wanayo sababu ya kushukuru kwa huruma na uvumilivu wa Mungu kwa kudhibiti na kuzuia ukatili wa
yule mwovu. Lakini wanadamu wanapozidi kipimo cha uvumilivu wa Mungu, kinga inaondolewa. Mungu
hamwadhibu mdhambi; bali anamwacha mdhambi kuvuna matokeo ya kile anachopanda. Kila mwale wa
nuru uliokataliwa, kila onyo lililopuuzwa au kutosikilizwa, kila uvunjaji wa sheria ya Mungu, ni mbegu
iliyopandwa na inayotoa mavuno. Roho wa Mungu, anapopingwa kwa muda mrefu, hatimaye
anaondolewa kwa mdhambi, kwa hiyo anaachwa bila uwezo wa kudhibiti maovu, na hakuna ulinzi dhidi
ya mabaya na uadui wa Shetani. Uharibifu wa Yerusalemu ni onyo kwa wale wote wanaocheza-cheza na

3
Milman, The History of the Jews, book 16

19
zawadi ya Mungu na kupingana na rehema. Hakukupata kutolewa ushuhuda zaidi ya huo wa jinsi Mungu
anavyochukia dhambi na kuhusu adhabu itakayompata mwenye hatia.
Unabii wa Mwokozi kuhusu Yerusalemu kujiliwa na hukumu utakuwa na utimilifu mwingine, ambao
kwake uharibifu ule ulikuwa ni kivuli hafifu tu. Katika hatima ya mji mteule tunaweza kutazama
uangamivu wa ulimwengu uliokataa rehema yake na kuikanyaga sheria yake. Kumbukumbu ambazo
dunia imeshuhudia, kuhusu shida za mwanadamu katika karne nyingi za uhalifu, ni za giza. Moyo
unashtuka, na mawazo yananyong’onyea yanapotafakari kumbukumbu hizo. Matokeo ya kukataa
mamlaka ya mbinguni huwa ya kutisha. Lakini tukio la giza zaidi bado linafunuliwa kwa ajili ya wakati
ujao. Kumbukumbu ya yaliyopita – mtiririko wa ghasia, (37) vurugu, na mapinduzi ya “mapigano na
wapiganaji … na fujo, na mavazi yaliyochovywa katika damu" (Isaiah 9:5), - ni nini, ukilinganisha na
majanga ya siku ile ambapo Roho wa Mungu azuiaye ataondolewa kabisa kutoka kwa waovu, na hakuna
kitakachozuia mlipuko wa uovu wa mwanadamu na gadhabu ya kishetani! Ulimwengu utashuhudia
matokeo ya utawala wa Shetani kwa namna ambayo haijapata kutokea.
Lakini katika siku ile, kama ilivyokuwa wakati wa kuharibiwa kwa Yerusalemu, watu wa Mungu
wataokolewa, kila atakayekuwa ameandikwa miongoni mwa walio hai. Isaya 4:3. Yesu ametamka
kwamba atakuja tena mara ya pili kuwachukua waaminifu wake kwake: "Ndipo makabila yote
yatakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni na uweza na
utukufu mwingi. Naye atawatuma malaika zake na sauti kubwa ya tarumbeta, nao watawakusanya
wateule wake kutoka katika pepo nne, kutoka mwisho mmoja hadi mwingine." Mathayo 24:30, 31. Ndipo
wale wasioitii injili watakapomezwa na roho ya kinywa chake na kuharibiwa na utukufu wa kuja kwake.
2 Wathesalonike 2:8. Kama Israeli ya zamani waovu walijiangamiza wenyewe; wanaanguka kwa uovu
wao. Kwa maisha ya dhambi, wamejiweka nje pasipo kuelekeana na Mungu, tabia zao zimekuwa za
uovu, kudhihirishwa kwa utukufu wake kwao ni moto ulao.
Hebu watu wajihadhari wasipuuze mafundisho yaliyotolewa na Kristo kwao. Kama alivyowaonya
wanafunzi wake kuhusu uharibifu wa Yerusalemu, akiwapa ishara ya uangamivu uliokuwa karibu, kusudi
wapate kuokoka; vivyo hivyo ameuonya ulimwengu kuhusu siku ya uharibifu wa mwisho na amewapa
vidokeza vya kuja kwa siku hiyo, ili wote watakao waikimbie gadhabu ijayo. Yesu alisema: "Kutakuwa na
ishara katika jua, na katika mwezi, na katika nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa." Luka 21:25;
Mathayo 24:29; Marko 13:24-26; Ufunuo 6:12-17. Wale waonao viashiria hivi vya kuja kwake “wajue
kwamba yuko karibu, (38) tena mlangoni." Mathayo 24:33. "Kesheni basi," ni maneno yake. Marko 13:35.
Wale watakaozingatia maonyo yake hawataachwa gizani, hata siku ile iwakute bila kujua. Lakini kwa
wale wasiokesha, "siku ya Bwana yaja kama mwivi usiku" (1 Wathesalonike 5:2-5).
Ulimwengu hauko tayari kujali ujumbe kwa ajili ya wakati huu zaidi ya vile walivyokuwa Wayahudi
katika kupokea maonyo ya Mwokozi kuhusu Yerusalemu. Vyovyote iwavyo, siku ya Mungu itakuja kama
mwivi kwa wasio wake. Maisha yatakapokuwa yanaendelea katika mzunguko wake wa kawaida; wakati
ambapo watu watakuwa wamemezwa katika raha za dunia, katika shughuli, katika safari za huku na
huko, katika kutafuta pesa; wakati viongozi wa dini wanapotukuza maendeleo na ujuzi wa kidunia, na
watu wakipumbazwa katika usalama wa bandia – ndipo, kama mwizi aibavyo usiku wa manane katika
nyumba isiyo na ulinzi, uharibifu utakuja ghafla juu yao wasiojali na wasiomcha Mungu, "wala hakika
hawataokolewa." (1 Wathesalonike 5:3).

20
Sura ya 2
MATESO MNAMO KARNE ZA KWANZA

Wakati Yesu alipowafunulia wanafunzi wake hatima ya Yerusalemu na matukio ya kurudi kwake,
alitabiri pia uzoefu ambao wanafunzi wake watapitia tangu wakati ambao angechukuliwa kutoka kwao
mpaka wakati wa kurudi kwake katika uweza na utukufu ili kuwaokoa. Kutoka Mlima wa Mizeituni,
Mwokozi aliona dhoruba ambayo ingeliliangukia kanisa la mitume, na jicho lake lilipenya mbali mpaka
siku za mbele na kuona tufani kali ambayo ingewapiga wafuasi wake katika kipindi kijacho cha mateso
na giza. Katika maneno muhimu machache na mafupi, alitabiri kuhusu namna ambavyo watawala wa
dunia wangeligawa kanisa la Mungu. Mathayo 24:9, 21, 22. Lazima wafuasi wa Kristo wapite katika njia
ile ile aliyoipita Bwana wao, njia ya kudharauliwa, kulaumiwa na kusumbuliwa. Chuki ile iliyolipuka
dhidi ya Mkombozi wa ulimwengu ingedhihirishwa tena dhidi ya wote ambao wangeliamini jina lake.
Historia ya kanisa la awali inaonyesha kwamba maneno ya Mwokozi yalitimia. Mamlaka za dunia na za
kuzimu ziliungana dhidi ya Kristo akiwa katika miili ya wafuasi wake. Upagani uliona kwa mbali kwamba
hekalu na madhabahu zake vitafutiliwa mbali ikiwa injili ingefanikiwa; kwa hiyo uliamrisha majeshi
yake kuharibu Ukristo. Mioto ya mateso iliwashwa. Wakristo walinyang’anywa mali zao na kufukuzwa
kutoka majumbani mwao. Walistahimili mashindano makubwa ya maumivu. Waebrania 10:32.
"Walijaribiwa (40) kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa vifungo na kutiwa gerezani" (Waebrania 11:36).
Idadi kubwa ya watu waliutia muhuri ushuhuda kwa damu yao. Mabwana na watumwa, matajiri kwa
maskini, wenye elimu na wasio na elimu, waliuawa bila huruma.
Mateso haya, yakianza chini ya utawala wa Nero katika nyakati za kifo cha kufia imani cha Paulo,
yaliendelea yakiongezeka na kupungua kwa karne kadhaa. Wakristo walishtakiwa kwa uongo kwamba
wao ndio waliokuwa wanasababisha uhalifu mkubwa na majanga – njaa, magonjwa, na matetemeko.
Kadiri walivyokuwa wahanga wa kuchukiwa na umma wa watu wengi, watoa habari walijiweka tayari
kuwasaliti watu hawa wasio na hatia kwa lengo la kujinufaisha. Walishtakiwa kwamba ni waasi kwa
serikali, na kwa dini, hivyo wasiohitajika katika jamii. Idadi kubwa ya watu hawa walitupwa kwa
wanyama-mwitu wakali au kuchomwa moto wakiwa hai mbele ya halaiki. Wengine waliangikwa mitini;
wengine walivalishwa ngozi za wanyama-mwitu na kuwekwa mbele ya mbwa wengi ili wararuliwe.
Adhabu zao mara nyingi zilitumika katika kuburudisha watu wakati wa maadhimisho au sherehe za
halaiki. Makutano ya watu yalikusanyika ili kuangalia na kufurahisha macho, na wengi walitoa salamu za
dhihaka na kejeli kwa watu hawa waliokuwa wanateseka.
Kila walipotafuta hifadhi, wafuasi wa Kristo waliwindwa kama wanyama wawindwao. Walilazimika
kutafuta maficho mahali pa upweke. "Walikuwa wahitaji, wakiteswa, wakitendewa mabaya; (watu
ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao) walikuwa wakizunguka-zunguka katika nyika, na milima, na
katika mapango na mashimo ya nchi." Sura ya 37 na 38. Misururu ya mahandaki ilihifadhi maelfu ya
watu. Chini ya vilima nje ya Roma, mahandaki marefu yalikuwa yamechimbwa chini ya ardhi na
miamba, mtandao wa njia za chini zenye giza ulifika maili nyingi hadi nje ya kuta za mji. Katika
maficho haya ya chini ya ardhi wafuasi wa Kristo walizika wafu wao; hapa pia wengi waliogundulika
waliishia humo. Wakati Yeye Aletaye uhai atakapowaamsha wote waliopigana vita vizuri, wengi
waliokufa kishujaa kwa ajili ya Kristo watatoka katika mapango haya. (41)

21
Mashahidi hawa wa Yesu waliitetea imani yao katika mateso makali. Ingawa walikuwa
wamenyang’anywa kila aina ya faraja, wakifungiwa mbali na nuru ya jua, wakifanya makao yao katika
giza, hawakutamka neno lolote la kulaumu. Kwa maneno ya imani, uvumilivu na tumaini, walitiana
moyo wakivumilia mateso. Kuondolewa kwa kila aina ya mema ya dunia hakukuweza kuwafanya
waikane imani yao katika Kristo. Majaribu na mateso yalikuwa kama hatua tu za kuwaleta karibu zaidi
na pumziko lao na thawabu yao.
Kama watumishi wa zamani wa Mungu, wengi “waliteswa, wasikubali ukombozi; ili wapate ufufuo ulio
bora zaidi." Fungu la 35. Walitafakari maneno ya Bwana wao, kwamba wanapoteswa kwa ajili ya Kristo,
walipaswa wafurahi, kwa sababu thawabu yao ni kubwa mbinguni; kwa maana manabii nao waliteswa
vivyo hivyo kabla yao. Walifurahi kwa sababu walihesabiwa kama walioteswa kwa ajili ya ukweli; na
nyimbo za ushindi zilipanda juu kutoka katika moto uwakao. Wakiangalia juu kwa imani, walimwona
Kristo na malaika wakiwachungulia kutoka mbinguni, wakiwaangalia kwa mvuto mkubwa na kukubaliana
na msimamo wao. Sauti iliwashukia kutoka katika kiti cha enzi ikisema: "Uwe mwaminifu mpaka kufa,
nami nitakupa taji ya uzima" (Ufunuo 2:10).
Juhudi za shetani kuliharibu kanisa kwa mabavu zilikuwa kazi bure. Pambano kuu ambalo lilisababisha
wanafunzi wa Yesu kuyatoa maisha yao halikukomea pale. Badala ya kushindwa walikuwa wameshinda.
Watenda-kazi wa Mungu walichinjwa, lakini kazi yake ilisonga mbele. Kazi ya injili iliendelea na idadi ya
walioipokea na kuitii iliongezeka. Injili ilipenya hata katika maeneo ambayo yalikuwa hayafikiki. Mkristo
mmoja alisema wakati akiwapinga watesaji: Mnaweza “kutuua, kututesa na kutuhukumu … Kutofuata
haki kwenu ni ushahidi kwamba sisi hatuna hatia (42) … Wala ukatili wenu hautawafaidi kitu." Ilikuwa tu
kama mwaliko kwa wengine kujiunga katika mateso. "Kadiri tunavyoangushwa chini ndivyo
tunavyoongezeka kwa wingi; damu ya Wakristo ni mbegu." 4
Maelfu walitupwa magerezani na kuuawa, lakini wengine waliinuka na kuchukua nafasi zao. Na wale
waliokufa kishujaa kwa ajili ya imani walikubalika kwa Kristo na kuhesabika kama washindi. Walikuwa
wamepigana vita vizuri, na watapokea taji ya utukufu wakati Kristo anaporudi. Mateso waliyoyapata
Wakristo yaliwaleta karibu wao kwa wao na karibu na Mkombozi wao. Mfano wa maisha yao na ushuhuda
wa vifo vyao vilikuwa ushuhuda wa kudumu wa ukweli; na mahali pengine watumishi wa shetani
waliacha kazi yake na kujiunga na watu waliokuwa wakimwinua Yesu.
Shetani aliweka mipango ya kupigana vita dhidi ya serikali ya Mungu kwa mafanikio zaidi kwa
kupandikiza mambo yake katika kanisa la Kikristo. Kama wafuasi wa Kristo wangedanganyika na
kuongozwa katika kushindwa kumpendeza Mungu, ndipo nguvu, msimamo na uimara wao ungeanguka na
wangekuwa mawindo yake.
Mpinzani mkuu sasa alielekea katika kutafuta kwa njia ya hila kile alichokosa kwa kutumia nguvu.
Mateso yalikoma, na badala yake ililetwa roho ya hatari ya kutukuza mafanikio ya muda na kuipenda
dunia. Waabudu sanamu waliongozwa kupokea kwa sehemu tu imani ya Kikristo, huku wakikataa ukweli
mwingine muhimu. Walikiri kumkubali Yesu kama Mwana wa Mungu na kuamini katika kifo na kufufuka
kwake, lakini wakiwa hawana wongofu wa kweli wa kuchukia dhambi au kuona haja ya toba au badiliko
la moyo. Waliridhia kukubali baadhi ya mambo ya Wakristo, na kuwashawishi Wakristo nao kukubali
baadhi ya mambo yao, kusudi wote waungane katika jukwaa la imani ya Yesu.

4
Tertullian, Apology, paragraph 50

22
Sasa kanisa lilikuwa katika hatari ya kutisha. Gereza, mateso, moto na upanga vilikuwa kama baraka
ukilinganisha na hali hii ya sasa. Baadhi ya Wakristo walisimama imara, wakikataa kufanya (43)
maafikiano. Wengine walipendelea kukubaliana au kurekebisha baadhi ya mambo katika imani yao ili
kuungana na wale waliokuwa wamekubali Ukristo kwa sehemu tu, wakidai kwamba hii ndiyo njia ya
kuwaelekeza katika wongofu kamili. Hiki kilikuwa kipindi cha maumivu makali kwa wafuasi wa Kristo.
Akiwa katika vazi la Ukristo la bandia, Shetani alikuwa akijiimarisha katika kanisa, kuchafua imani yao
na kugeuza mawazo yao kutoka katika neno la kweli.
Hatimaye wengi wa Wakristo walikubali kushusha viwango vyao vya imani, na muungano ukafanyika kati
ya Ukristo na upagani. Ingawa waabuduo sanamu walidai wameongoka, na kuungana na kanisa,
waliendelea kung’ang’ania miungu yao, wakiibadili tu kwa kuifanya sanamu za Yesu, za Maria na za
watakatifu. Uchafu wa chachu ya ibada ya sanamu ulioletwa kanisani uliendelea na kazi yake ya ajabu.
Mafundisho yasiyo sahihi, dini za kishirikina, na sikukuu za ibada ya sanamu ziliingizwa katika imani ya
kanisa na ibada. Kadiri wafuasi wa Kristo walivyoungana na waabudu sanamu, dini ya Kikristo ilipotoka,
na kanisa likapoteza usafi na nguvu. Hata hivyo, walikuwepo baadhi ambao hawakupotoshwa na
madanganyo haya. Waliendelea kudumisha msimamo wao kwake Yeye aliye asili ya ukweli, na
wakamwabudu Mungu peke yake.
Daima kumekuwepo makundi mawili miongoni mwa watu wanaodai kuwa wafuasi wa Kristo. Wakati
kundi moja linajifunza maisha ya Mwokozi na kwa kicho wanatafuta kusahihisha mapungufu yao ili kuwa
katika mpango wake, kundi jingine linakataa ukweli wa wazi na bayana unaomulika makosa yao. Hata
katika kipindi ambacho lilikuwa katika hali yake bora zaidi, kanisa halikuwa na watu wa kweli na wasafi
tu. Mwokozi wetu alifundisha kwamba wale ambao watadumu katika dhambi kwa makusudi
wasipokelewe kanisani; ila aliwaunganisha naye wale waliokuwa wadhambi, na kuwapa nafasi ya
kupokea mafundisho yake na mfano wa maisha yake ili waweze kuona makosa yao na kuyasahihisha.
Miongoni mwa mitume kumi na wawili mmoja alikuwa msaliti. Yuda aliunganishwa (44) na wanafunzi wa
Yesu ili, kupitia mafundisho na kielelezo cha Yesu, ajifunze tabia ya Kikristo, na hivyo aongozwe kuona
mapungufu yake, atubu, na kwa neema ya Mungu, asafishe nafsi yake “katika kutii ile kweli.” Lakini
Yuda hakutembea katika nuru iliyoruhusiwa kumulika mbele yake. Kwa kuchezacheza na dhambi
alikaribisha majaribu ya shetani. Tabia yake ya uovu ikatawala maisha yake. Alielekeza mawazo yake
katika utawala wa giza, alikuwa mwenye hasira wakati alipoonywa kuhusu madhaifu yake, na kwa hiyo
aliongozwa kutenda uhalifu wa kuogofya wa kumsaliti Bwana wake. Hivyo ndivyo wanavyofanya wote
wanaoendelea na uovu wakidai kwamba ndio utauwa, huku wakichukia wale wanaowasumbua kwa
kuhukumu mienendo yao mibaya ya dhambi. Watu hawa wakipata nafasi muafaka, kama alivyofanya
Yuda, watawasaliti wale ambao wamekuwa wakijitaabisha kutafuta kuwaonya kwa ajili ya hatima yao
njema.
Mitume walikumbana na wale ambao walijiona kuwa watu wa Mungu huku wakiendelea na dhambi kwa
siri. Anania na Safira walitenda kwa nafasi ya udanganyifu, wakijifanya kwamba wametoa vyote kwa
Mungu, wakati walikuwa wamezuia sehemu kwa ajili yao. Roho wa kweli aliwafunulia mitume tabia
halisi iliyofichika ya watu hawa, na hukumu za Mungu zikalisafisha kanisa kutoka katika uchafu huo.
Uwepo huu wa Roho ya Kristo ulikuwa ni mwiba mkali kwa wanafiki na watenda maovu. Wasingeendelea
kuwa katika mwunganiko na wale ambao, kwa tabia na mwonekano, walidumu kumwakilisha Kristo; na
kadiri majaribu na mateso yalivyokuja kwa wanafunzi wake, wale tu waliokuwa tayari kuacha vyote kwa
ajili ya ukweli ndio walioendelea kuwa wanafunzi wake. Kwa hiyo, kadiri mateso yalivyoendelea, kanisa
liliendelea kuwa safi. Lakini yalipokoma, waongofu ambao hawakuwa waongofu waliojitoa kweli kweli
waliongezeka, na njia ilikuwa wazi kwa shetani kupata mahali pa kutegemeza mguu wake.

23
(45) Hata hivyo hakuna ushirika kati ya Mfalme wa nuru na mfalme wa giza, na haiwezekani kuwa na
muungano kati ya wafuasi wa hao. Pindi Wakristo walipokubali kuungana na wale walioongoka kwa nusu
tu kutoka upaganini, waliingia katika njia iliyowapeleka mbali zaidi kutoka katika kweli. Shetani
alijiinua kwamba amefanikiwa kudanganya idadi kubwa ya wafuasi wa Kristo. Ndipo alipoleta nguvu
yake kamili juu yao, akawaongoza kuwatesa wale waliobaki wakiishika kweli ya Mungu. Hakuna
aliyekuwa mashuhuri katika kuipinga kweli ya Kristo kama wale waliopata kuitetea hapo kabla; na
Wakristo hawa walioasi, wakiwa wameungana na wenzao waliokuwa nusu-wapagani walielekeza vita yao
dhidi ya viini vya mafundisho muhimu ya Kristo.
Kusimama imara kwa wale ambao wangekuwa waaminifu dhidi ya madanganyo na machukizo
yaliyoingizwa kanisani yakiwa yamefichwa katika mavazi ya kikasisi kulihitaji mapambano magumu.
Biblia ilikuwa haikubaliki kama kiwango cha imani. Fundisho la uhuru wa dini lilichukuliwa kama uasi, na
wale waliolitetea walichukiwa na kupigwa marufuku.
Baada ya mapambano makali ya muda mrefu, wale wachache wenye imani waliamua kuachana na
ushirika wa aina zote katika kanisa lililoasi ikiwa lingeendelea kushindwa kuachana na mafundisho ya
uongo na ibada ya sanamu. Waliona kwamba kujitenga kulikuwa ni jambo muhimu lisilokwepeka ili
kuendelea kutii neno la Mungu. Hawakudiriki kuendelea kuvumilia makosa ambayo yangehatarisha nafsi
zao, na kuwa mfano mbaya ambao ungehatarisha imani ya watoto wao na watoto wa watoto wao.
Walikuwa tayari kufanya kila jambo lisilokuwa kinyume na imani yao kwa Mungu ili kupata amani na
umoja; lakini walihisi kwamba ingefikia hatua ambayo hata amani ingependwa sana na kuhitaji
kupatikana kwa gharama ya kuiacha kanuni. Ikiwa hakuna namna ya kupata umoja isipokuwa tu kwa
kuiacha ile kweli na haki basi heri tofauti iwepo, na hata vita.
(46) Ingekuwa vyema kwa kanisa na kwa ulimwengu ikiwa kanuni zile zilizowaimarisha watu
waliosimama imara zingehuishwa katika mioyo ya wacha Mungu. Kuna hali ya kutofautiana katika
mafundisho yanayounda nguzo za imani ya Kikristo. Mtazamo unaozidi kupata nguvu miongoni mwa watu
ni kwamba, kwa vyovyote vile, mafundisho ya namna hiyo hayana maana sana. Mawazo haya potofu
yanaimarisha mikono ya mawakala wa Shetani, kiasi kwamba dhana zisizo kweli na madanganyo ambayo
waaminifu wa zama zilizopita walihatarisha maisha yao wakiyapinga kwa muda mrefu, sasa
yanaonekana yakikubalika machoni pa maelfu ya watu wanaodai kuwa wafuasi wa Kristo.
Wakristo wa awali walikuwa watu wa pekee kweli kweli. Maisha yao yasiyolaumiwa kitu na imani yao
isiyoyumbishwa viliendelea kuwa onyo linalosumbua amani ya wadhambi. Ingawa walikuwa wachache
kwa idadi, wakiwa hawana mali, nafasi, wala vyeo vya heshima, walikuwa mwiba kwa watenda maovu
kila mahali mafundisho yao na tabia zao vilipojulikana. Kwa hiyo walichukiwa na wenye dhambi, kama
vile Habili alivyochukiwa na Kaini aliyekuwa hamchi Mungu. Kwa sababu kama ile ile iliyomfanya Kaini
kumuua Habili, ndivyo walivyofanya hawa waliomwacha Roho Mtakatifu azuiaye. Waliwaua watu wa
Mungu. Ilikuwa ni kwa sababu kama ile ile iliyosababisha Wayahudi kumkataa na kumuua Mwokozi – kwa
sababu usafi na utakatifu wa tabia yake vilikuwa ni kemeo la kudumu kwa ubinafsi na upotovu wao.
Tangu siku za Kristo mpaka sasa, wanafunzi wake waaminifu wamekuwa wakikumbana na chuki na
upinzani kutoka kwa wale wanaopenda na kufuata njia za dhambi.
Inawezekanaje sasa injili iitwe ujumbe wa amani? Isaya alipotabiri kuzaliwa kwa Masihi, alimpa jina,
“Mfalme wa Amani." Wakati malaika walipotangaza kwa wachungaji kwamba Kristo amezaliwa,
waliimba juu ya uwanda wa Bethlehemu wakisema: "Atukuzwe Mungu juu mbinguni, na duniani iwe
amani, kwa watu aliowaridhia" (Luka 2:14). Kunaonekana kuwa na tofauti kati ya matamko haya ya
unabii na maneno ya Kristo: "Sikuja kuleta amani, bali upanga" (Mathayo 10:34). Lakini, haya

24
yakieleweka kwa usahihi, (47) yanakubaliana kabisa. Injili ni ujumbe wa amani. Ukristo ni mfumo
ambao, ukipokelewa na kutiiwa, unaeneza amani, utulivu, na furaha dunia nzima. Dini ya Kristo
itawaunganisha na kuwafanya ndugu wote wanaokubali mafundisho yake. Ilikuwa kusudi la Yesu
kuwapatanisha wanadamu na Mungu, na hivyo mtu na mtu. Lakini sehemu kubwa ya walimwengu iko
chini ya udhibiti wa Shetani, mpinzani mkubwa wa Kristo. Injili inawaletea kanuni takatifu za maisha
ambazo zote ziko mbali sana na tabia zao na nia zao, kwa hiyo wanainuka na kuzipinga. Wanachukia
usafi wa maisha unaofunua na kuhukumu dhambi zao, wao wanawatesa na kuwaharibu wale
wanaowashawishi na kuwataka wawe wenye haki na watakatifu. Kwa mtazamo huu – kwa sababu ukweli
ukiinuliwa juu unasababisha chuki na vurugu – injili inaitwa upanga.
Siri ya ajabu iliyo ndani ya ruhusa ya wenye haki kuteswa mikononi mwa waovu imekuwa sababu ya
watu wenye imani dhaifu kuvunjika moyo. Wengine wako katika nafasi ya kupoteza ujasiri wao kwa
Mungu kwa sababu anawafanikisha watu wabaya, wakati wenye haki na wasafi wanahangaishwa na
kushambuliwa. Watu hawa wanauliza: inakuwaje kwa Yeye aliye wa haki na huruma, tena mwenye
uweza wote, avumilie kuonewa na kukandamizwa kwa watu wake? Hili ni swali ambalo hatuna jambo la
kufanya kuhusiana nalo. Mungu ametupatia uthibitisho wa kutosha kuhusu upendo wake, na tusiwe na
mashaka juu ya wema wake kwa sababu hatuwezi kujua kazi zake. Mwokozi alisema kwa wanafunzi
wake, akiona mashaka ambayo yangejaza nafsi zao katika siku za majaribu na giza: "Likumbukeni lile
neno nililowaambia, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake. Ikiwa wameniudhi mimi, watawaudhi ninyi
pia" (Yohana 15:20). Yesu aliteseka kwa ajili yetu kuliko vyovyote vile ambavyo mwanafunzi wake
yeyote anaweza kuteseka chini ya ukatili wa wanadamu wenye dhambi. Wale wanaoitwa kustahimili
mateso na kifo kwa ajili ya imani wanafuata tu nyayo za Mwana mpendwa wa Mungu. (48)
"Bwana hakawii kutimiza ahadi zake." 2 Petro 3:9. Hasahau wala hapuuzi watoto wake; lakini
anawaruhusu wenye dhambi kufunua tabia yao halisi, ili asiwepo yeye apendaye kufanya mapenzi yake
anayedanganywa nao. Pia, wenye haki wanawekwa katika tanuru la mateso, ili kwamba wao wenyewe
wasafishwe; kusudi mfano wao uwavute wengine katika uhalisi wa imani na ucha-Mungu; na pia ili njia
zao ziwahukumu wasiomcha Mungu na wasioamini.
Mungu anawaruhusu waovu kufanikiwa na kufunua uovu wao dhidi yake, kusudi wakiishajaza kikombe
cha uovu wao wote waione haki yake na rehema yake na kiasi wanachostahili adhabu. Siku ya kisasi
chake inaharakisha, wakati ambapo wote waliovunja sheria yake na kuwaudhi watu wake watapokea
malipo ya matendo yao kwa haki; wakati ambapo kila tendo la kikatili na lisilo haki lililofanywa kwa
watu wa Mungu litaadhibiwa kama vile lilifanywa kwa Kristo mwenyewe.
Kuna swali jingine la muhimu sana kwa ajili ya makanisa ya leo. Mtume Paulo alisema kwamba, wote
watakaoishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa" (2 Timotheo 3:12). Kwa nini sasa mateso
yanaonekana kama kwa kiasi kikubwa yamepoa? Jibu pekee ni kwamba kanisa limeafikiana na viwango
vya ulimwengu na kwa hiyo haliamshi upinzani wowote. Dini iliyopo leo kwetu si ya tabia safi na
takatifu kama ilivyokuwa imani katika siku za Yesu na mitume wake. Ni kwa sababu ya roho ya
kuafikiana na dhambi, kwa sababu ukweli muhimu wa neno la Mungu unaangaliwa kwa namna tofauti-
tofauti, na kwa sababu hakuna utauwa katika kanisa, kiasi kwamba Ukristo ni jambo la kawaida kwa
dunia. Hebu kuwe na mwamko wa imani na nguvu kama ya kanisa la awali, roho ya mateso itaamka na
mioto ya mateso itawashwa.

25
Sura ya 3
KIPINDI CHA GIZA LA KIROHO

Mtume Paulo, katika barua yake ya pili kwa Wathesalonike, alitabiri kuhusu uasi mkuu ambao ungeinuka
wakati wa kuanzisha mamlaka ya upapa. Alisema kwamba siku ya Kristo haitakuja, "usipokuja kwanza
ukengeufu, akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; apingaye na kujiinua juu ya kila
kiitwacho Mungu, au kinachoabudiwa; kiasi kwamba, kama Mungu, anakaa katika hekalu, akijionyesha
kwamba ni Mungu." Zaidi ya hapo, Mtume anaonya akisema "ile siri ya kuasi inatenda kazi tayari." 2
Wathesalonike 2:3, 4, 7. Hata tangu mapema kiasi kile aliona kanisa likinyemelewa na uasi ambao
ungetayarisha njia kwa ajili ya kuinuka kwa upapa.
Kidogo kidogo, kwanza kwa kificho na kimya-kimya, halafu kwa uwazi zaidi kadiri ilivyoongezeka nguvu
na uthibiti wa mawazo ya watu, "ile siri ya kuasi," iliendelea na kazi yake ya madanganyo na makufuru.
Pasipokushtukiwa, desturi za kipagani zilifika kanisani. Kwa muda, roho ya kuridhiana na kuafikiana
ilizuiwa na mateso ambayo kanisa liliyapata chini ya upagani. Lakini mateso yalipokoma, na Ukristo
ukaingia katika majumba ya wafalme, kanisa liliweka kando imani ya Kristo na mitume wake na
kuvutiwa na makasisi na watawala wa kipagani; na mahali pa maagizo ya Mungu, likaweka mafundisho
na mapokeo ya wanadamu. Hicho kiitwacho kuongoka kwa Konstantino (50) mwanzoni mwa karne ya
nne, kilisababisha shangwe; ulimwengu, ukiwa umejivika vazi kama la wenye haki, ulitembea na kuingia
kanisani. Sasa kazi ya upotoshaji iliongezeka kwa haraka. Upagani, huku ukionekana kama vile
umetokomezwa, ndio ulioshinda. Roho ya kipagani ililiongoza kanisa. Mafundisho yake, maadhimisho ya
sikukuu, na imani za umizimu yaliunganishwa katika imani na ibada za wale waliojiita wafuasi wa Kristo
wakati huo.
Haya mafungamano kati ya upagani na Ukristo yalisababisha kuinuka kwa yule "mtu wa kuasi"
aliyetabiriwa katika unabii kwamba atapinga na kujiinua juu ya Mungu. Mfumo huu mkuu wa dini ya
uongo ni sehemu ya nguvu ya Shetani – jitihada zake za kukaa kwenye kiti cha enzi na kuitawala dunia
apendavyo yeye.
Mnamo wakati fulani Shetani aliazimia kufanya maridhiano na Kristo. Alikuja kwa Mwana wa Mungu
katika jangwa la majaribu, na kumwonyesha milki zote za ulimwengu na utukufu wake, akaahidi
kumpatia vyote ikiwa angeikiri mamlaka ya mfalme wa giza. Kristo alimkemea mjaribu huyu na
kumwamuru aondoke. Lakini sasa Shetani anapata mafanikio makubwa anapoleta majaribu yale yale
kwa mwanadamu. Ili kupata mali za dunia na heshima yake, kanisa lilielekea katika kutafuta kuungwa
mkono na kusaidiwa na wakuu wa dunia; na likiwa limemkataa Kristo kwa namna hiyo, lilijisalimisha
chini ya mamlaka inayomwakilisha Shetani – askofu wa Roma.
Moja ya mafundisho makuu ya Uroma ni kwamba papa ni kichwa kinachoonekana cha kanisa la Kristo la
ulimwengu wote, aliyepewa mamlaka juu ya maaskofu na wachungaji katika sehemu zote za dunia.
Zaidi ya hapo, papa amepewa jina lile la Uungu. Ameitwa "Bwana Mungu Papa (Lord God the Pope"), 5 na
anatajwa kama asiyekosea. 6 Anadai kuwa wa kuheshimiwa na watu wote. Dai lile lile lililofanywa na

5
Angalia maelezo ya nyongeza katika Kiambatanisho
6
Angalia maelezo ya nyongeza katika Kiambatanisho
26
Shetani katika jangwa la majaribu ndilo linalofanywa na huyu kupitia Kanisa la Roma, na idadi kubwa ya
watu iko tayari kujisalimisha kwake kumheshimu. (51)
Lakini wale wanaomcha Mungu wanakutana na kile ambacho Kristo alikutana nacho na kusema:
"Mwabudu Bwana Mungu, na umtumikie yeye peke yake." Luka 4:8. Mungu hajatoa dokezo lolote katika
neno lake kwamba amemteua mwanadamu kuwa mkuu wa kanisa. Mafundisho kuhusu mamlaka ya
upapa yanapingana kabisa na mafundisho ya Maandiko. Papa hawezi kuwa na mamlaka juu ya kanisa la
Kristo isipokuwa kwa njia ya unyang’anyi.
Wale wa dini ya Kiroma wamedumu kuwalaumu Waprotestanti kwamba ni waasi na wameamua
kujitenga na kanisa la kweli. Lakini mashtaka haya yanawastahili wao wenyewe. Ni wao walioshusha
chini bendera ya Yesu na kutanga mbali na "imani ambayo kwanza ilitolewa kwa watakatifu." Yuda 3.
Shetani alijua vema kwamba Maandiko Matakatifu yangewawezesha watu kugundua madanganyo yake
na kumpinga. Ilikuwa ni kwa neno kwamba hata Mwokozi wa ulimwengu alipinga hila za shetani. Kwa
kila hatua ya mashambulizi, Kristo alionyesha kinga ya ukweli wa kudumu, akisema, "Imeandikwa." Kwa
kila shauri lililotolewa na mpinzani, alipinga kwa kutumia hekima na nguvu ya neno. Ili Shetani
aendeleze upotoshaji wake kwa watu, na kuanzisha mamlaka ya upapa kwa nguvu, lazima awaweke
watu mbali na ujuzi wa Maandiko. Alijua kwamba Biblia ingemwinua Mungu na kuwaweka wanadamu
katika nafasi sahihi; kwa hiyo lazima ukweli wake mtakatifu ufichwe na kufutiliwa mbali. Hoja hii
ilichukuliwa na kutekelezwa na Kanisa la Roma. Kwa mamia ya miaka Biblia zilipigwa vita zisionekane.
Watu walizuiwa kusoma Biblia au kuwa nayo nyumbani, na makasisi na maaskofu ndio waliofasiri
mafundisho ya Biblia kwa namna walivyotaka. Kwa hiyo papa alikuwa amekubalika katika ulimwengu
wote kuwa kama mwakilishi wa Mungu aliye duniani, akiwa amepewa mamlaka juu ya kanisa na juu ya
dola.
Sasa king’amuzi cha makosa kikiwa kimeondolewa hivyo, Shetani alifanya kazi yake vile atakavyo.
Unabii ulikuwa umesema kwamba papa “ataazimu kubadili majira na sheria" (Danieli 7:25). (52)
Kutekeleza kazi hii hakukufanyika pole pole. Ili kuwapatia mbadala wa ibada ya sanamu wale waongofu
waliotoka upaganini, na kuhimiza hali yao ya kuupokea Ukristo kwa jina tu, sanamu na ibada za wafu
viliingizwa kanisani. Hatimaye, tamko la baraza kuu 7 lilianzisha rasmi mfumo huu wa ibada ya sanamu.
Kukamilisha kazi hii ya kufuru, Roma iliondoa amri ya pili katika sheria ya Mungu, amri inayokataza
kuabudu sanamu, na kugawanya amri ya kumi, ili kuendelea kuwa na idadi ile ile ya amri kumi.
Roho ya kuafiki upagani ilifungua njia ya kutojali zaidi na zaidi mamlaka ya Mbinguni. Akifanya kazi na
viongozi wa kanisa wasiojitoa kikamilifu, Shetani aliichezea pia amri ya nne, akaazimia kuweka pembeni
Sabato ya tangu zama za kale, siku ambayo Mungu aliibariki na kuitakasa (Mwanzo 2:2, 3), na badala
yake akaanzisha utunzaji wa sikukuu za kipagani za kutukuza “siku ya jua." Kwanza, badiliko hili
halikufanywa wazi wazi. Katika karne za kwanza, Sabato ya kweli ilitunzwa na Wakristo wote. Walikuwa
na wivu wa kumcha Mungu, na wakiamini kwamba sheria yake ni ya milele, walidumu kuitukuza. Lakini
kwa werevu mkubwa, Shetani alifanya kazi na mawakala wake kuingiza mambo yake. Ili kuvuta mawazo
ya watu kuielekea Jumapili, siku hiyo ilifanywa kuwa sikukuu ya kuadhimisha kufufuka kwa Yesu.
Huduma za kidini zilihusianishwa nayo; ila ilichukuliwa kama siku ya burudani, Sabato ikiwa bado
inatunzwa.

7
Angalia maelezo ya nyongeza katika Kiambatanisho

27
Ili kutayarisha njia kwa ajili ya kazi aliyoazimia kukamilisha, Shetani alikuwa amewaongoza Wayahudi,
kabla ya kuja kwa Kristo, kuiwekea Sabato mizigo mingi na kufanya utunzaji wake kuwa mzigo.
Akitumia nuru isiyo sahihi aliyokuwa amesababisha, alielekeza lawama kwa Sabato na kuionyesha kama
maadhimisho ya Kiyahudi. Kadiri Wakristo walivyoendelea kuadhimisha Jumapili kama siku ya kisherehe,
aliwaongoza (53) kuchukia dini ya Kiyahudi na kuifanya Sabato kuwa siku ya huzuni, ya majonzi na ya
kufunga.
Katika kipindi cha mwanzo wa karne ya nne mfalme Konstantino alitoa amri ya kuifanya Jumapili kuwa
sikukuu kote katika Himaya ya Roma. 8 Siku ya jua ilitukuzwa na raia wake wapagani na iliheshimiwa na
Wakristo; sera ya mfalme huyu ilikuwa ni kuwaunganisha wapagani na Wakristo waliokuwa katika tofauti
kubwa. Aliombwa kufanya hivyo na maaskofu wa kanisa, ambao, wakivutwa na uchu wa madaraka,
waliona kwamba ikiwa wapagani na Wakristo wangetunza siku moja ingekuwa rahisi kwa wapagani
kupokea japo kwa bandia Ukristo na kuongeza nguvu na heshima ya kanisa. Lakini wakati Wakristo
wacha-Mungu wengi waliongozwa taratibu kuekea kuiona Jumapili kama ina utakatifu fulani, bado
waliendelea kuishika Sabato kama siku takatifu ya Bwana na waliizingatia kwa kuitii amri ya nne.
Yule mwongo mkuu hakuwa amemaliza kazi yake. Aliamua kukusanya ulimwengu wa Kikristo chini ya
bendera yake na kutekeleza mamlaka yake kupitia kwa makamu wake, askofu mkuu mwenye kiburi
aliyejifanya kuwa mwakilishi wa Kristo. Alikamilisha kusudi lake kupitia kwa wapagani walioongoka
nusu, makasisi, na washiriki wa kanisa wanaoupenda ulimwengu. Vikao vya baraza vilikaa mara kwa
mara, ambamo wawakilishi wa kanisa walitoka ulimwenguni kote. Katika kila kikao, Sabato ambayo
Mungu aliianzisha ilimomonyolewa na kushushwa chini, wakati Jumapili ilikuwa ikiinuliwa. Hatimaye,
sikukuu hii ya kipagani iliheshimiwa kama vile ni ya Mungu, wakati Sabato ya Biblia alitajwa kama
desturi ya dini ya Kiyahudi, na walioitunza walionekana kuwa walio na laana.
Muasi mkuu alikuwa amefanikiwa kujiinua "juu ya kila kiitwacho Mungu, au kinachoabudiwa." 2
Wathesalonike 2:4. Alikuwa amediriki kubadili fundisho pekee la sheria ya Mungu ambalo kwa usahihi
linawaelekeza wanadamu wote kwa Mungu wa kweli aliye hai. Katika amri ya nne, Mungu (54)
anafunuliwa kama Muumba wa mbingu na nchi, na kwa hali hiyo anatofautishwa na miungu ya uongo.
Siku ya saba ilitakaswa kuwa siku ya pumziko kwa mwanadamu ikiwa kama ukumbusho wa kazi ya
uumbaji. Iliazimiwa kuwa siku ya kuweka kumbukumbu katika mawazo ya mwanadamu kwamba Mungu
aliye hai ndiye asili ya vyote na anastahili kuabudiwa. Shetani anapambana kuwaondoa watu kwa Mungu
wao, na kuwatoa katika utii wa sheria yake; kwa hiyo anaelekeza juhudi zake dhidi ya amri ile
inayomdhihirisha Mungu kama Muumba.
Waprotestanti wao wanadai kwamba kufufuka kwa Yesu siku ya Jumapili kuliifanya kuwa Sabato ya
Wakristo. Lakini ushahidi wa Maandiko unakosekana. Hakuna heshima ya namna hiyo iliyotolewa na
Kristo au mitume wake. Kuishika Jumapili kama siku ya ibada ya Wakristo ina asili yake katika ile "siri ya
kuasi" (2 Wathesalonike 2:7) ambayo ilikuwa imeanza kazi hata mnamo siku za Paulo. Ni wapi na lini
ambapo Bwana alimkubali huyu mtoto aliyezaliwa na upapa? Ni sababu gani ya msingi inayoweza
kutolewa kwa badiliko hili ambalo haliungwi mkono na Maandiko?
Katika karne ya sita upapa ulikuwa umeimarika. Kiti chake cha mamlaka kilikuwa kimeimarika katika
mji na himaya yote, na askofu wa Roma alitangazwa kuwa ndiye mkuu wa kanisa lote. Upagani ulikuwa
umezaa upapa. Joka alikuwa amempa yule mnyama “”nguvu zake, na kiti chake, na uwezo mwingi."
Ufunuo 13:2. Ndipo ikaanza miaka 1,260 ya makandamizo yaliyofanywa na upapa yaliyotabiriwa katika

8
Angalia maelezo ya nyongeza katika Kiambatanisho
28
unabii wa Danieli na Ufunuo. Danieli 7:25; Ufunuo 13:5-7. 9 Wakristo walilazimishwa kuchagua ama
kukubali na kuheshimu maadhimisho na ibada za kipapa au kuhatarisha maisha yao kwa kutupwa
gerezani au kukabili kifo. Yakatimizwa maneno ya Yesu: "Mtasalitiwa na wazazi, ndugu, jamaa, rafiki;
na baadhi yenu watawaua. Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu." Luka 21:16, 17.
Mateso yalifunua hasira kubwa ya ulimwengu dhidi ya waaminifu kuliko ilivykuwa kabla, (55) na
ulimwengu ukawa kama uwanja wa vita. Kwa mamia ya miaka kanisa la Kristo lilipata makimbilio katika
maficho ya upweke. Ndiyo maana nabii anasema: "Mwanamke akakimbilia nyikani, mahali ambapo
Mungu amemwandalia, ili atunzwe huko kwa siku elfu moja na mia mbili na sitini." Ufunuo 12:6.
Kuinuka kwa mamlaka ya Kanisa la Roma ndio ulikuwa mwanzo wa Zama za Giza. Kadiri nguvu zake
zilivyoongezeka ndivyo giza lilivyoongezeka uzito. Imani ilihamishwa kutoka kwa Kristo, aliye msingi wa
kweli, kwenda kwa papa wa Roma. Badala ya kumwamini Mwana wa Mungu kwa ajili ya ondoleo la
dhambi na kwa wokovu wa milele, watu walimtumainia papa, na makasisi na mapadri ambao aliwapatia
mamlaka. Walifundishwa kwamba papa ndiye mpatanishi wa duniani na kwamba hakuna ambaye
angemwendea Mungu pasipo kupitia kwake; na zaidi, kwamba yeye alisimama mahali pa Mungu kwao na
kwa hiyo alistahili kutiiwa. Tendo la kuacha kufanya matakwa yake lilikuwa sababu tosha ya kustahili
adhabu kubwa kuliko zote ambazo zingepata kutolewa kwa mhalifu. Kwa hiyo mawazo ya watu
yaliondolewa kwa Mungu na kuelekezwa kwa wanadamu wakatili na wasio wakamilifu, naam, kwa mkuu
wa giza mwenyewe aliyekuwa anatenda kazi kupitia wao. Dhambi ilisitiriwa ndani ya vazi la utakatifu.
Maandiko Matakatifu yanapokuwa yamefutiliwa mbali, na mwanadamu anapokuwa amejiona kuwa ndiye
yuko juu, kinachotarajiwa ni uongo na madanganyo tu. Kuinuliwa kwa sheria na mapokeo ya wanadamu
kunaleta opotokaji unaosababishwa na kuachwa kwa sheria ya Mungu.
Hizo zilikuwa siku za hatari kwa kanisa la Kristo. Waaminifu waliobeba viwango vya imani walikuwa
wachache mno. Ingawa ukweli haukuachwa pasipo ushuhuda, lakini kwa nyakati fulani ilionekana kama
vile uasi na umizimu vilifunika imani yote, na dini ya kweli ilikuwa kama imetoweka duniani. Injili
ilipotea, lakini miundo ya dini iliongezeka na kuzidi.
Si kwamba walifundishwa tu kumwangalia papa kama mpatanishi wao, lakini pia kuamini kwamba
matendo yao yangeleta ondoleo la dhambi zao. Safari ndefu za hija, matendo ya kujionyesha binafsi,
ibada za kuwaheshimu waliokufa, (56) ujenzi wa makanisa makubwa, mahekalu, na madhabahu,
matoleo ya kiasi kikubwa cha fedha kwa kanisa - haya na matendo mengine kama hayo yalitumika kwa
kusudi la kupunguza ghadhabu ya Mungu au kutafuta wema wake; kana kwamba Mungu yuko kama
wanadamu, kiasi cha kuweza kuchukizwa na utoaji wa fedha kidogo, au kuvutiwa na matoleo au
matendo ya kitubio cha malipizi!
Licha ya kwamba uovu huo ulienea, hata miongoni mwa viongozi wa Kanisa la Roma, ushawishi wake
uliendelea kuongezeka kwa nguvu. Karibu na mwisho wa karne ya nane, upapa ulidai kwamba katika
zama za mwanzo za kanisa maaskofu wa Roma walikuwa na mamlaka ya kiroho kama hiyo. Kuanzisha
dai hilo, lazima mbinu zitumike; na hili lilipendekezwa haraka na baba wa uongo. Masifii waligushi
maandishi yaliyoitwa ya zamani za kale. Matamko ya mabaraza ambayo yalikuwa hayajawahi kusikika
yalisemekana kugunduliwa, yakianzisha mamlaka ya upapa tangu nyakati za zamani. Kanisa hili
lililokuwa limekataa ukweli lilikubaliana na uongo huu. 10
Waaminifu wachache waliojenga katika msingi wa kweli (1 Wakorintho 3:10, 11) walidhoofishwa na
kutatanishwa na machafu na kazi ya mafundisho ya uongo. Kama ilivyokuwa kwa wajenzi wa ukuta wa

9
Angalia maelezo ya nyongeza katika Kiambatanisho
10
Angalia maelezo ya nyongeza katika Kiambatanisho
29
mji wa Yerusalemu katika siku za Nehemia, baadhi walikuwa tayari kusema: "Nguvu zao wachukuao
mizigo zimedhoofika, na kifusi tele; hatuwezi kuujenga ukuta." Nehemia 4:10. Wakiwa na hofu ya
mapambano ya muda mrefu dhidi ya mateso yaliyokuwa yanaendelea, uovu na vikwazo vingine vyote
ambavyo Shetani alibuni ili kuwazuia, baadhi ya wale waliokuwa wajenzi waaminifu walianza kuvunjika
moyo; na ili kupata amani na usalama wa mali zao na maisha yao, waligeuka na kuacha msingi wa kweli.
Wengine, pasipo kuogopa upinzani wa adui, walitamka wazi wazi : "Msiwaogope; mkumbukeni Bwana,
yeye aliye mkuu mwenye kuogofya" (fungu la 14); na wakaendelea na kazi, kila mmoja na upanga wake
ubavuni mwake. Waefeso 6:17.
Roho ile ile ya chuki na upinzani dhidi ya kweli imewaongoza adui za Mungu katika vizazi vyote, na
utiifu na (57) imani ile ile vimekuwa vikihitajika miongoni mwa watumishi wake. Maneno ya Yesu
aliyowaambia wanafunzi wake bado yana maana kwa wafuasi wake hadi mwisho wa wakati: "Hilo
niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni." Marko 13:37.
Giza lilionekana kuongezeka uzito. Ibada ya sanamu iligeuka jambo la kawaida zaidi. Mishumaa
iliwashwa mbele ya sanamu, na sala zilifanywa kwa sanamu hizo. Umizimu wa hali ya juu ulikuwa
umeenea. Mawazo ya watu yalikuwa yanaendeshwa na umizimu. Kwa kuwa makasisi na maaskofu wao
walikuwa watu wa kujipendezesha wenyewe na waliopotoka, ilikuwa wazi kwamba watu waliotegemea
uongozi wao wangezama katika ujinga na ufedhuli.
Hatua nyingine katika maendeleo ya upapa ilichukuliwa wakati Papa Gregory VII alipotangaza mnamo
karne ya kumi na moja kwamba Kanisa la Roma ni kamilifu. Miongoni mwa kauli alizotoa ilikuwa ile
inayodai kwamba kanisa halijakosea, wala lisingekosea kamwe, kama vile Maandiko yasemavyo. Lakini
uthibitisho wa Maandiko hauungi mkono madai hayo. Mwenye kujivuna huyu alidai pia kuwa na mamlaka
ya kuondoa watawala wa dola, na akadai kuwa hakuna mtu yeyote anayeweza kugeuza maamuzi yake
kuhusu jambo lolote, lakini yeye alikuwa na mamlaka ya kubadili maamuzi ya wengine wote. 11
Kielelezo halisi cha tabia ya mwenye majivuno huyu kilionekana katika namna alivyomtendea mtawala
wa Ujerumani, Henry VI. Kwa kuonekana kwamba hakujali mamlaka ya papa, mtawala huyu alitishiwa
kutengwa na kuondolewa madarakani. Kwa kuogopa kwamba watumishi katika utawala wake
waliohamasishwa na mamlaka ya papa wasimwasi, Henry aliona haja ya kutafuta amani kati yake na
Roma. Akisindikizwa na mke wake na mtumishi mmoja mwaminifu kwake, alivuka na kupita milima ya
Alps katikati ya majira ya baridi ili kujisalimisha kwa papa. Alipofika katika makao ya papa aliachwa nje
ya kiwanja bila walinzi, akiwa katika baridi kali wakati wa msimu wa baridi, akiwa hakufunika kichwa
wala (58) miguu, na akiwa amevaa mavazi yasiyoendana na hali ya mazingira iliyokuwepo, akiwa
anasubiri ruhusa ya papa kukutana naye. Mpaka zilipoisha siku tatu za kufunga akiomba msamaha ndipo
aliposamehewa na papa. Hata hivyo alisamehewa kwa masharti kwamba alikuwa anasubiri vikwazo
vingine vya kutekelezwa kabla ya kuendelea na utawala wake. Huyu ni Gregory aliyekuwa amechaguliwa
kwa kishindo na akajigamba kwamba anaweza kuwatiisha na kuwashusha wafalme.
Kuna tofauti kubwa kiasi gani kati ya kiburi na kujitukuza kwa askofu huyu wa Roma vinapolinganishwa
na ule upole na unyenyekevu wa Kristo, anayejieleza kama mtu asimamaye akibembeleza mlangoni pa
moyo, akisubiri kufunguliwa, ili alete msamaha na amani, tena aliyewafundisha wanafunzi wake:
"Yeyote atakaye kuwa mkubwa miongoni mwenu, na awe mtumishi." Mathayo 20:27.
Karne zilizoendelea zilishuhudia kuendelea kwa makosa katika mafundisho ya Roma. Hata kabla ya
kuanzishwa kwa upapa mafundisho ya wanafalsafa wapagani yalikuwa yameingizwa na kupokelewa

11
Angalia maelezo ya nyongeza katika Kiambatanisho
30
kanisani. Wengi waliojidai kuongoka walikuwa bado wanashikilia mafundisho ya falsafa za kipagani, na
si kwamba waliendelea tu kujifunza falsafa hizo, bali pia waliwataka na wengine kukubaliana nazo.
Makosa makubwa yaliingizwa katika kanisa. Kubwa kati ya haya ilikuwa ni imani kwamba mwanadamu
hafi. Hili ndilo fundisho ambalo liliweka msingi wa Roma kuanzisha maombi kwa watakatifu na heshima
kwa Bikira Maria.
Bado njia nyingine ilitengenezwa kwa ajili ya kufanya uvumbuzi mwingine wa kipagani wa kitu ambacho
Roma ilikiita pagatori, na ikakitumia kuwatishia na kuwaridhisha watu wengi. Uongo huu ulihusu habari
ya kuwepo kwa mahali pa mateso, ambapo roho za wale wasiotenda yale yaliyoagizwa zinaadhibiwa kwa
sababu ya dhambi zao, (59) na wale wanaotoka humo wakiwa wametakaswa huingia mbinguni. 12
Uongo mwingine ulikuwa bado unahitajika ili kuiwezesha Roma kunufaika na woga na ufuasi wa wale
wanaoitii. Uongo huu ulikuwa katika fundisho la kupenda anasa. Ondoleo kamili la dhambi, ziwe
zilizokuwepo, zilizopo sasa au zitakazokuwepo, na kufunguliwa kutoka katika machungu na adhabu za
dhambi, viliahidiwa kutolewa kwa wote waliojiorodhesha kupigana upande wake katika vita ya kupanua
himaya yake, kuwaadhibu adui zake, au kufutilia mbali wale waliodiriki kukana mamlaka yake ya
kiroho. Watu walifundishwa pia kwamba kwa kutoa fedha kanisani wanapata ondoleo la dhambi na
kuwaondoa katika moto wa mateso wapendwa wao waliokufa. Kwa njia hiyo, Roma ilijaza hazina yake
na kutukuza fahari yake huyu aliyejifanya mwakilishi wa bandia wa Yeye aliyekuwa hana mahali pa
kulaza kichwa chake. 13
Huduma ya meza ya Bwana ya Maandiko ilibadilishwa na kuweka mahali pake ibada ya sanamu. Makasisi
wa kipapa walijifanya kuwa na uwezo wa kubadili mkate na divai kuwa mwili na damu halisi ya Kristo." 14
Kwa namna ya kukufuru, walidai wazi wazi kuwa na uwezo wa kumtengeneza Mungu, Muumba wa vyote.
Wakristo walipaswa kuisimamia imani, hata kwa kufa, katika kipindi hiki ambacho Mbingu ilikuwa
ikitukanwa na uasi. Wengi waliokataa kuafiki walichomwa moto. 15
Mnamo karne ya kumi na tatu, mbinu ya kutisha zaidi kuliko injini zote za upapa ilianzishwa - taasisi ya
kimahakama ya kanisa la Roma. Mfalme wa giza alishirikiana na viongozi wa utawala wa kipapa. Katika
mabaraza ya siri Shetani na malaika zake waliongoza mawazo ya watu waovu, wakati malaika wa Mungu
asiyeonekana alisimama katikati akichukua kumbukumbu ya machukizo yote yaliyofanywa na mabaraza
hayo. "Babeli mkuu" alikuwa "amelevywa na damu ya watakatifu." Mchanganyiko wa sauti za mamilioni
ya (60) walioifia imani walimlilia Mungu kwa ajili ya kisasi kwa mamlaka hii iliyoasi.
Upapa ulikuwa umekuwa nguvu ya ulimwengu. Wafalme na watawala walisujudia matamko ya mkuu wa
Roma. Hatima yote ya wanadamu, iwe ya sasa au ya milele, ilionekana kuwa chini ya udhibiti wake.
Kwa mamia ya miaka mafundisho ya Roma yalikuwa yamepokelewa, matakwa yake yalikuwa
yametendwa, sikukuu zake zilikuwa zimetukuzwa. Watumishi wa kanisa walikuwa wameheshimika na
kutukuzwa. Tofauti na wakati huo, Kanisa la Roma halikupata kuheshimika, kuwa na fahari na nguvu
namna hiyo.

12
Angalia maelezo ya nyongeza katika Kiambatanisho
13
Angalia maelezo ya nyongeza katika Kiambatanisho
14
Cardinal Wiseman, The Real Presence of the Body and Blood of Our Lord Jesus Christ in the Blessed Eucharist, Proved From
Scripture, lecture 8, sec. 3, par. 26
15
Angalia maelezo ya nyongeza katika Kiambatanisho
31
Lakini "mchana huu wa upapa ulikuwa ni usiku wa manane kwa ulimwengu." 16 Maandiko Matakatifu
yalikuwa kwa kiasi kikubwa hayajulikani, si kwa watu tu, bali pia hata kwa makasisi. Kama ilivyokuwa
kwa Mafarisayo wa zamani, viongozi wa upapa waliichukia nuru ambayo ingefunua dhambi zao. Sheria
ya Mungu, kipimo cha haki, ikiwa imeondolewa, walitekeleza mamlaka yao pasipo mipaka. Ubadhilifu,
tamaa ya mali na ufisadi vilishamiri. Watu walijitanibu kutokana na uharifu ambao si kwamba ulikuwa
wa kuwaletea mali au nafasi nzuri. Majumba ya kitawala ya mapapa na mapadri yalijazwa na matukio
ya uovu. Baadhi ya makasisi walifanya hatia kubwa ya uharifu kiasi kwamba watawala wa dunia waliona
hali hiyo haivumiliki. Kwa karne kadhaa Ulaya haikufanya maendeleo yoyote katika elimu, sanaa au
ustaarabu. Kupooza kwa kimaadili na kielimu kulikuwa kumeiangukia.
Hali ya ulimwengu chini ya utawala wa Kirumi ilitimiza kwa namna ya kuogofya na kutisha maneno ya
nabii Hosea: "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa: kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa,
mimi nami nitakukataa wewe: . . . kwa kuona mmesahau sheria ya Mungu wenu, nami pia nitawasahau
watoto wenu." "Hapana kweli, wala fadhila, wala kumjua Mungu katika nchi. Kuapa kwa uongo, na
kuvunja ahadi, na kuua, na kuiba, na kuzini; huruka mpaka, na damu hugusana na damu." Hosea 4:6, 1,
2. Hayo yalikuwa ni matokeo ya kukataa neno la Mungu.

16
J. A. Wylie, The History of Protestantism, b. 1, ch. 4
32
Sura ya 4
WAWALDENSI 17

Katikati ya utusitusi ulioikalia dunia kwa muda mrefu wa utawala wa upapa, nuru ya ukweli
haikumalizwa yote. Katika kila zama kulikuwa na mashahidi wa Mungu–- watu walioshikilia imani katika
Kristo kama mpatanishi pekee kati ya Mungu na mwanadamu, walioshikilia Biblia kama mwongozo pekee
wa maisha yao, na watu walioitunza Sabato ya kweli. Ni kiasi gani ambacho ulimwengu unawiwa na
watu hawa, vizazi vya baada ya pale haviwezi kujua kamwe! Walionekana kama watu waasi, mielekeo
yao ilihafifishwa, utu wao ulipingwa, maandiko yao yaliondoshwa, kuelezwa vibaya na kuharibiwa.
Lakini walisimama imara, na wakaisimamia imani kwa usahihi kutoka kizazi hata kizazi, kama urithi
uliotukuka wa vizazi vijavyo.
Historia ya watu wa Mungu mnamo zama zile za giza zilizofuata baada ya mamlaka ya Roma kuinuka
imeandikwa mbinguni, lakini wana nafasi kidogo tu katika kumbukumbu zilizoandikwa za wanadamu.
Kumbukumbu chache tu za uwepo wao zinaweza kupatikana, isipokuwa katika mashtaka ya watesi wao.
Ilikuwa ni sera ya Roma kufuta kila alama inayoonyesha upinzani kutoka katika mafundisho au maagizo
yake. Iliazimiwa kwamba kila kilichokuwa kinahusu uzushi, iwe wa watu au maandishi, viharibiwe.
Hatua yoyote ya kuonyesha wasiwasi au kuwa na maswali juu ya mamlaka ya papa ilitosha kuondoa
maisha ya tajiri au maskini yeyote, wa hali ya juu au ya chini. Roma iliazimia pia kuharibu kumbukumbu
zote za ukatili iliofanya kwa wote walioipinga. Mabaraza ya kipapa yalitoa matamko kwamba vitabu na
maandishi yote yenye kumbukumbu za namna hiyo (62) vichomwe moto. Kabla ya kuvumbua uchapaji,
vitabu vilikuwa vichache, tena katika muundo ambao hauvutii kuhifadhiwa; kwa hiyo hakukuwa na
kikubwa cha kuwazuia Warumi kutekeleza azma yao.
Hatamu za Warumi hazikuliachia kanisa lolote uhuru wa dini pasipo kusumbuliwa. Pindi tu upapa
ulipokuwa umepata nguvu ulinyosha mkono wake ili kuwaminya wote waliokataa kuutambua, na
makanisa, moja baada ya jingine, yalijisalimisha chini yake.
Huko Uingereza, Ukristo wa kale ulikuwa na mizizi tangu zamani. Injili iliyopokelewa na Waingereza
mnamo karne za kwanza sasa ilikuwa imepotoshwa na uasi wa Kirumi. Mateso yaliyotekelezwa na
watawala wapagani, yaliyoenea mpaka sehemu hizi za ndani mbali na pwani, yalikuwa ndiyo zawadi
pekee ambayo makanisa ya Uingereza yalipokea toka Roma. Wengi wa Wakristo waliokuwa wakikimbia
mateso Uingereza walipata maficho huko Scotland; kutoka huko ukweli ulipelekwa Ireland, na katika
nchi zote hizi ulipokelewa kwa furaha.
Wakati Wasaksoni 18 walipoivamia Uingereza, upagani uliongezeka nguvu. Washindi hawa wa vita
walikataa kufundishwa na watumwa wao hawa, na Wakristo walilazimika kukimbilia milimani na
maporini. Hata hivyo, nuru iliyokuwa imefichwa kwa muda iliendelea kuangaza. Karne moja baadaye,
iliendelea kuwaka ndani ya Scotland, kwa nguvu iliyoenea mpaka maeneo ya mbali. Kutoka Ireland,

17
Wawaldensi (Kingereza Waldenses) ni jamii ya Wakristo wanaosemekana kuwa wenye asili ya kusini mwa Ufaransa, ambao
waliojitenga na Kanisa Katoliki katika karne ya 12 na kukumbwa na mateso makali.
18
Wasaksoni (Saxons), kwa mujibu wa historia, ni watu wa Ujerumani ya Magharibi waliopanuka kuelekea magharibi mpaka
wakaanzisha himaya yao maeneo ya kusini mwa Uingereza mnamo karne ya 7.
33
alikuja mtu wa kiroho Columba na watenda-kazi wenzake, ambao walifanya kituo cha utume katika
Kisiwa cha Iona wakiwa wamewakusanya waamini waliotawanyika huku na huko. Miongoni mwa
Wainjilisti hawa alikuwemo mmoja anayetunza Sabato ya Biblia, na kwa hiyo ukweli huu ulifikishwa kwa
watu hawa. Shule ilianzishwa Iona, mahali ambapo wamishenari walitokea wakienda, si tu Scotland na
Uingereza, bali pia Ujerumani, Uswizi, na Italia.
Lakini Roma ilikuwa imeikodolea macho Uingereza, ikinuia kuileta chini ya mamlaka yake. Katika karne
ya sita, wamishenari wake waliwaongoa Wasaksoni wapagani. (63) Walipokelewa kwa shangwe na
washenzi hawa wenye kiburi, na wakavuta maelfu ya watu kuitangaza imani ya Kiroma. Kadiri kazi hii
ilivyosonga mbele, viongozi wa upapa na waongofu wao waliwakabili Wakristo. Tofauti kubwa
ilionekana. Kundi hili la pili lilikuwa la watu rahisi, wanyenyekevu, na wenye tabia, mafundisho na
mwonekano wa Kimaandiko, wakati kundi lile la kwanza lilikuwa la kishirikina, la kujionyesha na lenye
kiburi cha kipapa. Mawakala wa Roma walidai kwamba makanisa ya Kikristo hayana budi kutambua
mamlaka ya askofu wa Roma. Kwa unyenyekevu Waingereza walijibu kwamba wao waliazimia
kuwapenda watu wote, lakini kwamba papa hakuwa na stahili ya kuwa na mamlaka juu ya kanisa, na
kwamba wangeweza kumpatia tu ile heshima ambayo kila mfuasi wa Kristo alistahili. Majaribio ya
kuwafanya watu hawa wakubali mamlaka ya Roma yalirudiwa-rudiwa, lakini Wakristo hawa
wanyenyekevu, wakishangazwa na kiburi cha mawakala hawa wa Roma, walidumu na msimamo kwamba
hawamjui mkuu mwingine zaidi ya Kristo. Sasa roho halisi ya upapa ilifunuliwa. Kiongozi mmoja wa
Kirumi alisema: "Kama hamtaki kuwapokea ndugu wanaowaletea amani, mtapokea adui wanaowaletea
vita. Kama hamuungani nasi katika kuwaonyesha Waingereza njia ya kuishi, mtapokea kwao pigo la
mauti." 19 Hivi havikuwa vitisho vya bure. Vita na madanganyo vilitumika dhidi ya mashahidi wa imani ya
Biblia, hadi makanisa ya Uingereza yalipoharibiwa, au kujisalimisha chini ya mamlaka ya papa.
Kwa karne nyingi kulikuweko na makundi ya Wakristo walioendelea kuwa huru kabisa mbali na
madanganyo ya upapa; hawa walikuwa nje ya maeneo yaliyokuwa ndani ya utawala wa Roma. Walikuwa
wamezungukwa na upagani na baada ya vizazi kadhaa waliathiriwa na uasi wao; lakini waliendelea
kuiona Biblia kama kiongozi cha imani yao na wakazitii nyingi za kweli zake. Wakristo hawa waliamini
katika kudumu kwa sheria ya Mungu na waliitunza Sabato ya amri ya nne. Makanisa yaliyokuwa
yakidumu katika imani hii na kutenda hivyo yalikuwa katika maeneo ya Afrika ya Kati na miongoni mwa
Waarmenia wa Asia.
(64) Lakini miongoni mwa wale waliopinga kuingia kwa nguvu ya upapa, Wawaldensi walikuwa ni zaidi.
Katika maeneo yao ambapo upapa ulisimika kiti chake, uongo wake na madanganyo yake vilipingwa kwa
nguvu. Kwa karne kadhaa makanisa ya Piedmont yaliendelea kuwa huru; lakini hatimaye muda ulikuja
wakati Roma ilipotaka watu hawa wajisalimishe. Baada ya mapambano dhidi ya utawala huu, viongoza
wa makanisa haya waliitambua bila kupenda mamlaka hii iliyoonekana kuheshimiwa na ulimwengu
wote. Lakini walikuwepo baadhi waliokataa kuonyesha heshima kwa mamlaka ya kipapa. Waliazimia
kuonyesha heshima yao kwa Mungu na kuuhifadhi usafi wa imani yao. Mgawanyiko ulitokea. Wale
walioitii imani yao ya tangu zamani walijitoa; baadhi wakiyaacha maeneo yao ya Alps, walilibeba bango
la ukweli katika maeneo ya ugenini; wengine walijificha katika maeneo ya kimya na katika miamba ya
milimani, na kule wakaendelea kuwa na uhuru wa kumwabudu Mungu.
Imani ambayo ilishikiliwa na kufundishwa na Wawaldensi kwa karne nyingi ilikuwa tofauti kabisa na
mafundisho ya uongo yaliyoletwa na Roma. Imani yao ya kidini ilikuwa na msingi katika neno la Mungu

19
J. H. Merle D'Aubigne, History of the Reformation of the Sixteenth Century, b. 17, ch. 2

34
lililoandikwa, mfumo wa kweli wa Ukristo. Lakini wakulima hawa wanyenyekevu, wakiwa katika maeneo
yaliyojificha mbali na ulimwengu, na wakiwa katika mahangaiko ya kila siku na mifugo na mashamba
yao, hawakuwa wamefika katika ukweli ulio kinyume cha mfumo wa dini ya mazoea na uasi wa kanisa
lililoasi. Imani yao haikuwa imani mpya iliyopokelewa. Imani yao ya dini ilikuwa ni ya urithi wao kutoka
kwa mababa zao. Kwa hiyo walikuwa wanapigania imani ya kanisa la mitume, - "imani waliyokabidhiwa
watakatifu mara moja tu." Yuda 3. "Kanisa lililo jangwani," wala si ule mfumo wa utawala wa msonge
wa kiburi wenye makao yake makuu katika mji mkuu wa ulimwengu, ndilo lililokuwa kanisa la kweli la
Kristo, wakili wa hazina ya ukweli ambao Mungu amewakabidhi watu wake kusudi waufikishie
ulimwengu.
(65) Miongoni mwa sababu kubwa zilizosababisha kujitenga kwa kanisa la kweli kutoka Roma ilikuwa ni
chuki ya Roma dhidi ya Sabato ya Biblia. Kama ilivyotabiriwa na unabii, nguvu ya upapa iliuangusha
chini ukweli. Sheria ya Mungu ilikanyagwa mavumbini, huku mapokeo na desturi za wanadamu
zikiinuliwa juu. Makanisa yaliyokuwa chini ya mamlaka ya upapa yalilazimishwa kuitunza Jumapili kama
siku takatifu. Katika kipindi hiki cha uasi na madanganyo, wengi, hata miongoni mwa watu wa kweli wa
Mungu, walichanganyikiwa kiasi kwamba wakati waliitunza Sabato, waliacha pia kufanya kazi siku ya
Jumapili. Lakini hii haikuwatosheleza watu wa upapa. Hawakudai tu Jumapili itukuzwe, bali pia Sabato
iharamishwe; na waliwakemea kwa lugha kali wale wote walioonyesha kuiheshimu Sabato. Ilikuwa ni
kwa kuukimbia utawala wa Roma tu ndipo yeyote angeweza kuitii sheria ya Mungu kwa amani. 20
Wawaldensi walikuwa miongoni mwa watu wa kwanza wa Ulaya kupata tafsiri ya Maandiko Matakatifu. 21
Mamia ya miaka kabla ya Matengenezo walikuwa na Biblia iliyoandikwa kwa mkono katika lugha yao.
Walikuwa na ukweli usiochafuliwa, na hili liliwaweka katika nafasi ya kuchukiwa na kuingizwa katika
mateso. Walitangaza kwamba Kanisa la Roma ni Babeli iliyoanguka, na kwa gharama ya maisha yao
walisimama wakiupinga upotofu. Wakiwa chini ya mateso ya muda mrefu, baadhi walisalimisha imani
yao, kidogo-kidogo waliacha misingi ya imani, wengine waliendelea kuushikilia ukweli. Kupitia katika
zama za giza na uasi walikuwepo Wawaldensi walioikataa mamlaka ya Roma, waliokataa ibada ya
sanamu, na walioishika Sabato ya kweli. Wakiwa katika uchungu wa upinzani mkali waliishikilia imani.
Ingawa walitobolewa na mkuki na kupigwa, walisimama pasipo kuteteleka kwa ajili ya heshima na neno
la Mungu.
Nyuma ya miinuko ya milima - maficho ya wale wanaoteswa na kukandamizwa kwa vizazi vyote -
Wawaldensi (66) walipata mahali pa kujificha. Mahali hapa nuru ya ukweli iliendelea kuwaka katika giza
la Zama za Kati. Kwa miaka elfu moja, mashahidi wa ile kweli waliitunza imani ya zamani.
Mungu alikuwa amewapa watu wake hekalu la hadhi ya kutisha, kulingana na ukweli mkubwa
waliopatiwa. Kwa waaminifu hawa waliohamia mafichoni mbali, milima ilikuwa ndiyo nembo ya haki
isiyofutika ya Yehova. Waliwaonyesha watoto wao vilele vya milima vilivyokuwa vimesimama juu yao
pasipo kubadilika, wakivitumia kuwaeleza kuhusu yeye asiyebadilika wala asiye kama kivuli kigeukacho,
ambaye neno lake linadumu kusimama kama milima. Mungu amesimamisha milima na akaiwekea misingi
yenye nguvu; hakuna mkono unaoweza kuihamisha kutoka mahali pake, isipokuwa mkono wake wenye
nguvu na uweza. Kwa namna hiyo hiyo aliiweka sheria yake, msingi wa serikali yake mbinguni na
duniani. Mkono wa mwanadamu unaweza kuwafikia wanadamu wenzake na kuondosha maisha yao;
lakini mkono huo ungeweza kung’oa milima kwa urahisi kutoka katika misingi yake na kuisukumia
baharini, kwa kiasi ambacho ungeweza kubadili kipengele kimoja cha sheria ya Yehova, au kuondosha

20
Angalia maelezo ya nyongeza katika Kiambatanisho
21
Angalia maelezo ya nyongeza katika Kiambatanisho
35
moja ya ahadi zake kwao wafanyao mapenzi yake. Lakini kwa kusimama katika sheria yake, lazima
watumishi wa Mungu wasimame imara kama ilivyo milima isiyobadilika.
Milima iliyosimama ikiyafunika mabonde yao ya hali ya chini ilidumu kuwa ushuhuda kwao kuhusu uweza
wa Mungu wa uumbaji, na ahadi ya hakika isiyoshindwa ya ulinzi wake kwao. Wahamaji hawa
walijifunza kupenda ishara za kimya za uwepo wa Yehova. Hawakufadhaishwa na ugumu wa maisha
haya waliyochagua; hawakuwa wapweke katikati ya milima ile. Walimshukuru Mungu kwa kuwa alikuwa
amewapatia hifadhi mahali palipo mbali na ghadhabu na ukatili wa wanadamu. Walifurahia uhuru
waliokuwa nao wa kumwabudu. Mara kwa mara walipokabiliwa na adui zao, nguvu za milima ile
zaliwahakikishia ulinzi wa hakika. Walishangilia na kumsifu Mungu katika majabali ya milima, na wale
adui zao kutoka Roma wasingeweza kunyamazisha nyimbo zao za shukrani.
(67) Usafi, urahisi na umakini ndivyo vilivyotawala maisha ya wafuasi hawa wa Kristo. Walithamini
kanuni za ukweli kuliko nyumba, mashamba, marafiki, na hata maisha yenyewe. Walitafuta kuziweka
kanuni hizi katika mioyo ya vijana wao. Tangu miaka ya awali ya utoto wao vijana walifundishwa
Maandiko na jinsi ya kuheshimu na kutunza maagizo ya sheria ya Mungu. Nakala za Biblia zilikuwa haba;
kwa hiyo maneno yake ya thamani yalitunzwa katika kumbukumbu za kichwani. Wengi waliweza
kukaririri vipande vikubwa vya Agano la Kale na Agano Jipya. Mafikirio kuhusu Mungu yaliandamana na
mwonekano wa viumbe vya asili na mibaraka yake katika maisha ya kila siku. Watoto wadogo
walijifunza kumshukuru Mungu wakimwangalia kama mpaji wa kila lililo jema na kila faraja.
Wazazi hawa wenye moyo wa kupenda waliwapenda watoto wao na kuwafundisha kuwa na moyo wa
kujikana. Mbele yao kulikuwa na maisha magumu ya kujaribiwa, ikiwezekana hata kuyatoa maisha yao.
Walifundishwa kuvumilia matatizo tangu utoto wao, kudhibitika, lakini kufikiri na kutenda kama wao
binafsi. Mapema sana walifundishwa kubeba majukumu yao, kuwa makini katika kuongea, na kuielewa
hekima ya kukaa kimya. Neno moja ambalo lingetamkwa pasipo kutafakari lingeweza kufika masikioni
mwa adui zao na kusababisha athari kwa maisha, si tu ya mtamkaji, bali pia ya mamia ya ndugu zake;
maana kama mbwa-mwitu walio katika mawindo, ndivyo walivyokuwa adui wa ile kweli wakiwakabili
wale walioonyesha kudai uhuru wa imani ya kidini.
Wawaldensi waliyatoa kafara mafanikio yao ya ulimwengu huu kwa ajili ya ukweli, na katika uvumilivu
wa taabu zao walipata mkate wao. Kila sehemu iliyo ndogo milimani ambayo ingewezekana kulimwa
iliendelezwa kwa uangalifu; mabonde na mitelemko ya milima isiyo na rutuba ya kutosha ilitengenezwa
ili iweze kuzalisha. Uchumi na maisha ya kujikana ilikuwa sehemu ya elimu ambayo watoto walipata
kama urithi wao pekee. Walifundishwa kwamba Mungu anayapanga maisha yawe fundisho la nidhamu,
na kwamba mahitaji yao yangetolewa tu kwa njia ya kila mmoja kufanya kazi, kwa akili, uangalifu na
kwa imani. Mchakato huu wa maisha ulikuwa wa kufanya kazi, wa usumbufu, lakini (68) mkamilifu. Kile
ambacho mwanadamu anataka katika hali yake ya kuanguka, ndiyo shule ambayo Mungu ameiweka ili
kumfundisha na kumwendeleza. Wakati watoto walifunzwa kuhangaika na kukabiliana na ugumu, akili
zao hazikuachwa hivi hivi. Walifundishwa kwamba uwezo wao wote ulikuwa mali ya Mungu, na kwamba
ulipaswa uboreshwe na kuendelezwa kwa ajili ya huduma yake.
Makanisa ya Wavaudois (Wawaldensi), kwa habari ya usafi na urahisi, yalifanana na kanisa la kipindi cha
mitume. Waliishikilia Biblia kama mamlaka yao pekee isiyokoma, wakikataa mamlaka ya upapa. Tofauti
na makuhani wa Roma, wachungaji wao walifuata kielelezo cha Bwana wao aliyekuja kuhudumu, wala si
kuhudumiwa. Walilisha kundi la Mungu, wakiliongoza katika majani mabichi na chemchemi ya uzima ya
neno lake takatifu. Watu walikusanyika mbali mahali pasipo na fahari yenye mandhari nzuri ili kusikiliza
neno la kweli kutoka kwa watumishi wa Kristo. Hawakukusanyika katika makanisa mazuri na makubwa

36
ya kifahari, bali chini ya vivuli vya milima, katika mabonde ya Milima ya Alps, au, nyakati za hatari,
chini ya majabali na miamba. Si kwamba wachungaji walihubiri tu injili, bali pia walihudumia watoto,
walirejesha waliopotoka, na walifanya kazi ya kusuluhisha migogoro na kuleta hali ya utulivu na upendo
wa ndugu. Katika nyakati za amani, walitegemezwa na sadaka ya hiari ya watu; lakini, kama Paulo
mtengeneza-mahema, kila mmoja alijifunza ufundi au fani fulani ambayo ingemwezesha kuishi, kama
ingelazimu kufanya hivyo.
Vijana walipata mafundisho kutoka kwa wachungaji wao. Wakati huu ambapo msukumo ulielekezwa
katika migawanyo ya mafundisho, Biblia ilikuwa ndiyo mafundisho makuu. Injili za Mathayo na Yohana
ziliwekwa katika kumbukumbu au kukaririwa, pamoja na nyaraka za mitume za Biblia. Walikuwa na kazi
pia ya kuandika nakala za Biblia. Baadhi ya nakala zilikuwa za Biblia yote, na nyingine sehemu fupi tu
zilizochaguliwa, na wale waliokuwa na mwanga wa Biblia wakayaongezewa maelezo mepesi. Hazina ya
ukweli ambayo kwa muda mrefu ilikuwa (69) imetoweshwa na wale waliotafuta kujiinua juu ya Mungu
ikarejeshwa.
Kwa uvumilivu, pasipo kuchoka, wakati mwingine wakiwa katika mapango marefu ya nchi, wakimulika
kwa mienge, Maandiko matakatifu yaliandikwa, fungu kwa fungu, sura kwa sura. Kazi iliendelea hivyo,
mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa yaking’aa kama dhahabu safi; yalikuwa na nuru kubwa kiasi cha
ajabu, yakiwa na uweza wa nguvu kiasi cha ajabu kwa sababu yalikuwa yamepatikana katika mazingira
ya majaribu ambayo yalijulikana kwa wale tu walioyapitia. Malaika kutoka mbinguni waliwazungukia
watumishi hawa waaminifu.
Shetani alikuwa amewasukuma makasisi wa kipapa na mawakala wao kulifukia neno la kweli chini ya
uchafu wa uongo, uasi na madanganyo; lakini kwa namna ya ajabu sana lilihifadhiwa bila kuchafuliwa
katika kipindi chote cha zama zile za giza. Halikubeba muhuri wa mwanadamu, bali chapa ya Mungu.
Wanadamu wamekuwa wakijitahidi bila kuchoka kuitia giza maana ya Maandiko yaliyo wazi na rahisi
kwa kuyafanya yaonekane yanapingana na ushuhuda uliomo; lakini kama ilivyo safina inayoelea juu ya
vilindi vyenye tufani, neno la Mungu linashinda dhoruba zinazotaka kuliharibu. Kama ilivyo kwa
machimbo na utajiri wa miamba yenye dhahabu na fedha iliyofichika chini ya ardhi, ili wote
watakaogundua hazina iliyomo wachimbe, ndivyo ilivyo kwa Maandiko Matakatifu na hazina ya ukweli
inayofunuliwa tu kwa wote wanaoyatafuta kwa unyenyekevu, kicho na maombi. Mungu aliiweka Biblia
kusudi iwe kitabu cha mafundisho kwa wanadamu wote, katika utoto, ujana na utu uzima, na watu
wajifunze wakati wote. Aliwapa watu neno lake likiwa kama ufunuo wa Yeye mwenyewe. Kila ukweli
mpya unaowekwa wazi humo ni ufunuo mwingine wa tabia ya Mtunzi wake huyo. Kujifunza Maandiko ni
njia iliyowekwa na mbingu ya kuwaleta wanadamu katika mwungano wa karibu na Muumba wao na
kuwapa ufahamu wa wazi zaidi wa mapenzi yake. Ni njia ya mawasiliano kati ya Mungu na mwanadamu.
Wakati Wawaldensi wakikuchukulia kumcha Bwana kama chanzo cha maarifa, hawakuwa na upofu
kuhusu umuhimu wa kujikutanisha na ulimwengu, kufahamu kuhusu watu na (70) kuhusu shughuli za
maisha, ili kupanua akili na kukuza uelewa. Baadhi ya vijana waliotoka katika shule zao milimani
walipelekwa katika taasisi za elimu zilizokuwa katika miji mikubwa ya Ufaransa na Italia, mahali
kulikokuwa na mambo mapana zaidi ya kusoma, ya kutafakari na kuchunguza tofauti na ilivyokuwa kule
kwao katika maeneo ya milima ya Alps. Hawa vijana waliopelekwa kule walikutanishwa na majaribu,
walishuhudia matendo mabaya, walikabiliana na mawakala wa Shetani waliowaletea uasi mkubwa na
madanganyo ya hatari. Lakini elimu yao waliyopata utotoni ilikuwa imewaandaa vema kukabiliana na
yote hayo.

37
Katika shule hizi walikokwenda hawakupaswa kufanya mafungamano yoyote ya kizembe. Mavazi yao
yalikuwa yameandaliwa kwa namna ambayo ingeyafanya yatumike kusitiri hazina yao kubwa – nakala za
Maandiko. Walienda na Maandiko haya, ambayo yalikuwa matunda ya taabu yao ya miezi na miaka, na
kila mahali walipoona hawawezi kuhisiwa vibaya walizisogeza kwa uangalifu baadhi ya sehemu za
Maandiko yale mahali ambapo yangeonwa na wale walioonekana kuwa na moyo wa kupenda kuyapokea.
Tangu wakiwa katika magoti ya mama zao, vijana wa Kiwaldensi walikuwa wamefundishwa kwa kusudi
hili; walifahamu kazi yao na waliifanya kwa uaminifu. Katika taasisi hizi za elimu watu waliiongokea
imani hii mpya, na pole pole kanuni za imani hii zilionekana zikipenya na kuenea katika shule nzima;
pamoja na viongozi wa kipapa kufuatilia kwa karibu, bado hawakuweza kupata chanzo cha kitu hiki
walichokiita uzushi wenye kuharibu.
Roho ya Kristo ni roho ya umishenari. Msukumo wa kwanza kabisa wa moyo uliofanywa upya ni kuwaleta
wengine pia kwa Mwokozi. Hiyo ndiyo iliyokuwa roho ya Wakristo wale wa Vaudois. Waliona kwamba
Mungu alihitaji kwao jambo lililo zaidi ya kuuhifadhi ukweli katika makanisa yao; kwamba jukumu lao
walilopewa hasa lilikuwa ni kuifanya nuru yao iangaze mbele yao waliokuwa gizani; kwa nguvu za neno
la Mungu waliazimia kuzivunja kuta za vifungo ambavyo viliwekwa na Roma. Wahubiri wa Vaudois
walifundishwa kama wamishenari, kila mmoja anayetarajia kuingia katika kazi ya kuhubiri alipaswa
kupata kwanza uzoefu wa uinjilisti. Kila mmoja (71) alipaswa kutumika katika kazi ya utume kwa miaka
mitatu kabla ya kukabidhiwa kazi katika kanisa lake. Huduma hii, iliyohitaji kwanza kujikana nafsi na
maisha ya kujitoa mwanzoni, iliwapa wachungaji mwanzo wa maisha yaliyozijaribu nafsi zao katika siku
hizo. Vijana waliotengwa kuhudumu katika ofisi takatifu hawakutafuta kupata mafanikio ya utajiri na
miliki za dunia, bali waliyaona mbele yao maisha ya masumbufu na hatari, na ikiwezekana kupoteza
maisha. Wamishenari walienda wawili wawili, kama Yesu alivyowatuma wanafunzi wake. Kila kijana
mdogo aliandamana na mwanaume wa makamo mwenye uzoefu, kijana akiwa chini ya uangalizi na
mafunzo aliyostahili. Watenda-kazi hawa wawili hawakuwa pamoja muda wote, lakini mara kwa mara
walikutana kwa maombi na mashauri, kwa namna hiyo wakitiana nguvu katika imani.
Kitendo cha kulifanya kusudi la utume wao kujulikana kingesababisha kushindwa kwao; kwa hiyo
hawakuweka wazi mwenendo wao halisi. Kila mhubiri alikuwa na fani au kazi fulani, na wamishenari
walifanya kazi zao hizi chini ya mwavuli usio katika wito wa mambo ya dini. Mara nyingi walichagua kazi
za biashara. "Walichukua na kupeleka hariri, vito, na vitu vingine ambavyo wakati ule vilikuwa
haviuzikani isipokuwa maeneo ya mbali; na walikaribishwa kama wafanyabiashara mahali ambapo
wangesusiwa ikiwa wangeenda kama wamishenari." 22 Huo ndio wakati mioyo yao ilipoinuliwa kwa Mungu
kwa ajili ya hekima yao ya kuifikisha kwa watu hazina iliyokuwa na thamani kuliko dhahabu au kito cha
thamani. Waliondoka na nakala za Biblia kwa siri, zikiwa kamili au sehemu sehemu; na kila nafasi
ilipopatikana, walivuta mawazo ya wateja wao kuyaelekeza katika maandishi yale. Mara kwa mara
hamu ya kusoma neno la Mungu iliamshwa, na sehemu kadhaa za maandishi yale ziliachwa kwa furaha
mikononi mwa wale waliopenda kuzipokea.
Kazi ya wamishenari hawa ilianzia katika tambarare na mabonde yanayozunguka milima yao wenyewe,
halafu ilipanuka na kwenda mbali nje ya mipaka yao. Wakiwa na miguu isiyo na viatu na mavazi yaliyo
na madoa-madoa ya safarini kama yalivyokuwa yale ya Bwana wao, (72) walipita katika miji mikubwa
na kutokezea katika maeneo ya mbali. Kila mahali walisambaza mbegu ya thamani. Makanisa yaliota
katika njia waliyopita, na damu ya wafia imani ilikuwa ushuhuda wa ukweli. Siku ya Bwana itafunua
mavuno mengi ya roho yaliyopatikana kwa kazi ya watu hawa waaminifu. Pole pole na kimya kimya,

22
Wylie, b. 1, ch. 7

38
neno la Mungu lilikuwa linaingia kwa Wakristo na kupokelewa kwa furaha katika majumba na mioyo ya
watu.
Kwa Wawaldensi Maandiko hayakuwa tu maandishi yanayoonyesha namna Mungu alivyoshughulika na
watu wake mnamo siku zilizopita, na ufunuo wa majukumu na wajibu wa sasa, bali yalikuwa ni ufunguo
wa hatari zijazo na utukufu wa wakati ujao. Waliamini kwamba mwisho wa mambo yote hauko mbali,
na kadiri walivyojifunza Biblia kwa maombi na machozi waliguswa sana na maneno yaliyomo ya ukweli
uokoao wakaona wajibu wao wa kuyafanya yajulikane kwa wengine pia. Waliona mpango wa wokovu
ukiwa umefunuliwa wazi katika kurasa takatifu, wakapata faraja, tumaini na amani katika kumwamini
Yesu. Kadiri nuru ilivyouangazia ufahamu wao na kuleta furaha mioyoni mwao, walifanya kila wawezalo
kuelekeza miale ya nuru hiyo kwa wale waliokuwa katika giza la madanganyo ya upapa.
Waliona kwamba makutano, chini ya uongozi wa papa na makasisi, walikuwa wakijitaabisha kwa kutesa
miili yao ili kupata msamaha wa dhambi za nafsi zao. Wakiwa wamefundishwa kuamini kwamba wokovu
unapatikana kwa njia ya matendo yao, walikuwa wakijiangalia wao wenyewe, akili zao zikizama katika
hali zao za dhambi, wakijiona kwamba wako mbele za hasira ya Mungu, wakitesa miili na nafsi zao,
lakini pasipo kupata faraja. Nafsi za watu hawa zilikuwa zimefungwa katika mafundisho ya Roma.
Maelfu waliacha marafiki na jamaa zao na kwenda kuishi katika vyumba vya watawa. Kwa kufunga mara
kwa mara na kujitendea mateso ya kikatili, kwa kufanya mikesha ya usiku wa manane, kujichosha nje
wakati wa saa za baridi kali, kufanya safari ndefu za hija, kujitesa kwa adhabu za kujidhalilisha, maelfu
walijitahidi kutafuta amani ya dhamiri zao. Wakikandamizwa na hisia ya dhambi, wakisumbuliwa na
hofu ya ghadhabu ya kisasi cha Mungu, (73) wengi waliendelea kupata maumivu, mpaka hali ya
maumbile ya asili ilipochukua nafasi yake, wakazama kaburini bila kupata mwale wowote wa mwanga
au tumaini.
Wawaldensi walikuwa wakifanya kazi ya kuzipatia mkate wa uzima roho hizi zilizokuwa zikiteseka kwa
njaa, kuzifungulia ujumbe wa amani katika ahadi za Mungu, na kuzielekeza kwa Kristo aliye tumaini lao
pekee la wokovu. Mafundisho yaliyoshikiliwa na watu kwamba matendo yao mema yanaweza
kuwaondolea dhambi ya kuiharifu sheria ya Mungu yalijengwa katika uongo. Kutegemea wema wa
kibinadamu kunapingana na upendo wa Kristo usio na kipimo. Yesu alikufa kama kafara kwa ajili ya
mwanadamu kwa sababu wanadamu walioanguka hawawezi kujitafutia kukubalika mbele za Mungu.
Wema wa Mwokozi aliyesulibiwa na kufufuka ndio msingi wa imani ya Mkristo. Kumtegemea Kristo ni
jambo halisi kwa mtu, na kuunganishwa kwa roho ya mtu na Kristo lazima kuwe kwa karibu kama mguu
ulivyo kwa mwili, au tawi lilivyo kwa mzabibu.
Mafundisho ya mapapa na makasisi yaliwaongoza watu kuiona tabia ya Mungu, na hata ya Kristo, kama
isiyo na huruma, isiyovutia, na ya kutisha. Mwokozi alionyeshwa machoni pa watu kama vile
amepungukiwa rehema kwa mwanadamu aliyeanguka kiasi cha kuhitaji upatanisho wa makasisi na
watakatifu. Wale ambao fahamu zao zilimulikiwa na neno la Mungu waliwaelekeza watu kwa Yesu kama
kipenzi na Mwokozi wao, asimamaye akiwa amenyosha mikono yake akiwaalika wote kuja kwake na
mizigo yao ya dhambi, haja na shida zao. Walitafuta kuondolea mbali vizuizi ambavyo Shetani alikuwa
amerundika ili kuwazuia watu wasiione ahadi na kuja moja kwa moja kwa Mungu kutubu dhambi na
kupata msamaha na amani.
Kwa shauku mmishenari wa Vaudois aliufunua ukweli wa thamani wa injili kwa watu waliokuwa
wakiuhitaji. Kwa tahadhari alizitoa sehemu za Maandiko Matakatifu zilizokuwa zimeandikwa kwa
uangalifu. Furaha yake kubwa ilikuwa ni kuwapa tumaini watu waliovunjika moyo, nafsi zilizozongwa na
dhambi, watu waliomwona Mungu kama mwenye kisasi, anayesubiri kumlipa mtu kwa haki. Huku akiwa

39
anatetemeka midomo na macho yake yakiwa na machozi, mara nyingi akiwa ameinamia magoti,
aliwafungulia watu (74) ahadi tamu zinazofunua tumaini pekee la mdhambi. Nuru ya ukweli ikapenya
katika mawazo yao ya giza, ikaondoa wingu la hofu, hadi Jua la Haki likaangazia mioyo yao likiwa na
miale inayoponya. Mara kwa mara baadhi ya sehemu za Maandiko zilisomwa tena na tena, msikilizaji
akitamani zirudiwe-rudiwe, kama aliyetaka kujiridhisha kama kweli alikuwa amesikia kwa usahihi.
Maneno haya ndiyo hasa yaliyopendwa kusikika tena na tena: "Damu yake Yesu, Mwana wake,
yatusafisha dhambi yote." 1 Yohana 1:7. "Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo
hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa: ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye."
Yohana 3:14, 15.
Watu wengi walifunguka toka katika madanganyo ya madai ya Roma. Waliona jinsi upatanisho wa
wanadamu au malaika kwa wadhambi ulivyokuwa bure. Kadiri nuru ya kweli ilivyowazukia katika
fahamu zao waliitikia kwa mshangao wa furaha wakisema: "Kristo ndiye kuhani wangu; damu yake ndiyo
kafara yangu; madhabahu yake ndiyo toba yangu." Walijitoa kikamilifu kwa Yesu, wakirudia maneno
haya, "Pasipo imani haiwezekani kumpendeza." Waebrania 11:6. "Hapana jina jingine chini ya mbingu
walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo." Matendo 4:12.
Uhakika wa upendo wa Mwokozi ulionekana mkubwa sana kwa kutambuliwa na baadhi ya roho hizi
zilizozama katika dhoruba. Ulileta ahueni kubwa sana, mafuriko ya nuru yalimwagwa juu yao, walijiona
kama wanasafirishwa kwenda mbinguni. Mikono yao ilishikiliwa katika mikono ya Kristo; miguu yao
ilisimikwa juu ya Mwamba wa Kale. Hofu yote ya kifo ilitoweka. Sasa walitamani magereza na vifungo
ikiwa hivyo ndivyo ingewalazimu kuliheshimu jina la Mwokozi wao.
Hivyo ndivyo neno la Mungu lilivyoletwa na kusomwa katika maeneo yaliyojificha, wakati mwingine kwa
mtu mmoja, na wakati mwingine kwa kundi dogo la watu waliokuwa wakiitafuta nuru ya ukweli. Mara
nyingi usiku mzima ulitumika kwa kazi kama hii. Mara nyingi mshangao mkubwa na kustaajabu
viliwapata wasikilizaji kiasi kwamba wajumbe wa rehema hii walikuwa wanatakiwa wasikome kuyasoma
maneno (75) mpaka pale akili zao zilipohisi mawimbi ya wokovu. Mara nyingi maneno kama haya
yalisikika yakitamkwa: "Hivi kweli Mungu ataipokea dhabihu yangu? Atatabasamu kwangu? Atanisamehe?"
Jawabu lilisomeka hivi: "Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami
nitawapumzisha." Mathayo 11:28.
Imani iliishikilia ahadi hiyo, na mwitikio wa furaha ulisikika kwamba: "Hakuna haja ya safari za hija
tena; hakuna safari za maumivu tena kwenda katika maeneo matakatifu. Naweza kuja kwa Yesu hivi
hivi nilivyo, mdhambi na nisiye na utakatifu, wala hatakataa ombi langu. 'Umesamehewa dhambi zako.'
Dhambi zangu, naam, hata zangu, zinaweza kusamehewa!"
Wimbi la furaha ya ajabu lilijaza moyo, na jina la Yesu liliinuliwa kwa sifa na shukrani. Roho hizi zenye
furaha zilirudi majumbani kusambaza nuru, kurudia kwa watu wengine uzoefu wao mpya kadiri
walivyoweza; kwamba walikuwa wamepata Njia halisi na ya kweli. Kulikuwa na nguvu ya ajabu katika
maneno yaliyo katika Maandiko ambayo yaliongea moja kwa moja na mioyo ya wale waliokuwa
wanautafuta ukweli. Ilikuwa sauti ya Mungu, na ilikuwa na usadikisho kwa wale walioisikia.
Mjumbe wa ukweli aliondoka zake; lakini mwonekano wake wa unyenyekevu, uaminifu wake, upendo
wake viliendelea kukumbukwa. Kwa muda wote wasikilizaji wake hawakuwa wamemwuliza kuhusu
mahali alikotoka au alikokuwa anakwenda. Walikuwa wametekewa kabisa, mwanzoni kwa sababu ya
mshangao, na baadaye kwa sababu ya furaha na shukurani, kiasi kwamba hawakufikiria kumwuliza
masawali hayo. Walipokuwa wamemwomba aambatane nao majumbani mwao, alikuwa amewajibu

40
kwamba yeye hana budi kuwatembelea kondoo wa kundi waliopotea. Je huenda alikuwa malaika kutoka
mbinguni? ndivyo walivyojiuliza.
Mara nyingi mjumbe wa kweli kama huyu hakuonekana tena. Alikuwa ameelekea katika maeneo
mengine, au maisha yake yalikuwa yanateseka katika gereza fulani lisilojulikana, au huenda mifupa
yake ilikuwa imezagaa katika sehemu alipokuwa ameushuhudia (76) ukweli. Lakini maneno aliyokuwa
ameacha nyuma yake yasingeweza kuharibiwa. Yalikuwa yanafanya kazi yake katika mioyo ya watu;
matokeo yake ya baraka yatajulikana tu wakati wa hukumu.
Wawaldensi wamishenari walikuwa wanauvamia ufalme wa Shetani, na nguvu za giza ziliinuka kwa
hamu. Kila jitihada ya kuendeleza utangazaji wa ukweli iliangaliwa na mfalme wa uovu, na
akahamasisha woga kwa mawakala wake. Viongozi wa upapa wakaona dalili za hatari kwao kutokana na
kazi ya watumishi hawa waendao huku na huko. Ikiwa nuru ya ukweli ingeruhusiwa kuangaza pasipo
vizuizi, ingepeperushia mbali mawingu mazito ya upotofu uliofunika watu. Ingewaelekeza watu kwa
Mungu peke yake na hatimaye ingeharibu mamlaka ya Roma.
Uwepo wa watu hawa wanaoshikilia imani ya kanisa la kwanza ulikuwa ushuhuda kwa uasi wa Roma, na
kwa hiyo hali hii iliamsha chuki na mateso machungu mno. Kukataa kwao kujiweka mbali na Maandiko
kulikuwa pia ni jinai ambayo isingevumiliwa na Roma. Roma iliamua kuwafutilia mbali kutoka usoni pa
nchi. Sasa yakaanza mashambulizi ya kutisha kuliko yote kwa watu wa Mungu katika makazi yao
milimani. Wapelelezi waliwekwa ili kufuatilia njia zao, na tukio la Habili asiye na hatia mbele ya Kaini
mwuaji likawa linarudiwa mara kwa mara hapa.
Tena na tena ardhi yao yenye rutuba iliharibiwa, makazi yao na mahali pao pa kuabudia pakafagiliwa
mbali, kiasi kwamba mahali ambapo kabla palikuwa pamejazwa na mashamba na nyumba za watu wasio
na hatia, wanaojishughulisha kwa bidii katika kazi, pakaachwa pakiwa jangwa. Kama mnyama mkali
mwenye njaa aliye na hamu ya damu, ndivyo ilivyokuwa hasira ya upapa kwao wanaoteswa. Wengi wa
mashahidi hawa wa ukweli walikabiliwa kutoka mlima hadi mlima na kuwindwa mabondeni walikotafuta
maficho, wakiwa wamefunikwa na misitu mizito na majabali makubwa ya miamba.
Hakuna mashtaka yaliyotolewa dhidi ya tabia za watu hawa waliokuwa waadilifu. Hata adui zao walikiri
kwamba hawa watu walikuwa watu wa amani, wakimya na wa dini. Kosa lao kubwa lilikuwa ni kwamba
hawakumwabudu Mungu kulingana na matakwa (77) ya papa. Kwa uhalifu wa aina hii kila fedheha,
matusi, na mateso ambayo watu au waouvu waliweza kubuni yalirundikwa juu yao.
Wakati Roma ilipoazimia kumaliza kikundi cha watu hawa wachukiwao, amri ya tangazo ilitolewa na
papa, ikiwatambua rasmi kama wazushi, kuwatangazia hukumu ya kuchinjwa. 23 Hawakushtakiwa kama
wazururaji wasio na kazi, au watu wasio wakweli, au wasioenda kwa utaratibu; lakini ilikuwa
imetangazwa kwamba wao wanao wema na utakatifu uliowashawishi “kondoo wa zizi la kweli.” Kwa
hiyo papa aliagiza kwamba "hili kundi la kishetani lililo ovu na lenye machukizo," ikiwa "linakataa
kusalimu amri, liteketezwe kama nyoka wenye sumu." 24 Je mtawala huyu mwenye kiburi alitarajia
kukutana na maneno haya tena? Je alijua kwamba yameandikwa katika vitabu vya mbinguni, ili
kumkabili siku ile ya hukumu? Yesu alisema, "Kadiri mlivyomtendea aliye mdogo kati ya hawa,
mlinitendea mimi." Mathayo 25:40.
Tamko hili liliwataka washiriki wote wa kanisa kuungana katika mashambulizi dhidi ya waasi. Kama
kivutio kwa watu kujiunga na kazi hii ya kikatili, "aliwaachilia huru kutoka katika maumivu na adhabu za

23
Angalia maelezo ya nyongeza katika Kiambatanisho
24
-Wylie, b. 16, ch. 1
41
kidini, ya jumla au ya dhahiri; watu waliachiliwa kutoka katika viapo ambavyo vilikuwa vimewafunga;
walihalalishiwa umiliki wa mali ambazo huenda walipata isivyostahili; na waliahidiwa kupunguziwa
dhambi zao zote ikiwa wangemwua muasi yeyote. Marufuku ilipigwa kwa mikataba yote inayonufaisha
Wavaudois, wafanyakazi wao wa ndani waliagizwa kuachana nao, watu wote walizuiliwa kuwapa
msaada wa aina yoyote, na wakawawezesha watu wote kuchukua mali zao." 25 Waraka huu ulidhihirisha
roho iliyokuwa nyuma ya matukio haya. Kinachosikika humo ni mwungurumo halisi wa joka, wala si sauti
ya Kristo.
Viongozi wa kipapa wasingeweza kulinganisha tabia zao na kiwango cha sheria ya Mungu, badala yake
walisimika kiwango chao ili kukidhi mahitaji yao binafsi, na wakaazimia kulazimisha watu wote
kukubaliana nacho kwa sababu tu Roma ilitaka. Msiba mkubwa sana ulitekelezwa. Makasisi na mapapa
waliopotoka na wenye kukufuru walikuwa wanafanya kazi waliyotumwa na Shetani. Huruma (78)
haikuwa na nafasi kwao. Roho ile ile iliyomsulibisha Kristo na kuwaua mitume, ile ile iliyomsukuma Nero
katika kiu ya damu ya waaminifu wakati wake, ilikuwa kazini ikiiendesha dunia dhidi ya wapendwa wa
Mungu.
Kwa muda wa karne nyingi mateso yaliendelea kuwatembelea wacha-Mungu hawa nao wakayavumilia
kama heshima kwa Mkombozi. Licha ya mashambulizi waliyofanyiwa, na namna walivyokuwa
wakichinjwa kama vile siyo binadamu, waliendelea kutuma wamishenari kwenda kuusambaza ukweli.
Waliwindwa na kuuawa; lakini damu yao ni kama ilimwagilia mbegu iliyopandwa, wala haikushindwa
kuzaa matunda. Kwa hiyo Wawaldensi walishuhudia kwa ajili ya Mungu karne kadhaa kabla ya Luther
kuzaliwa. Wakiwa wametawanyika katika sehemu nyingi, walipanda mbegu za Matengenezo zilizoanza
mnamo siku za Wycliffe, zikakua, kupanuka na kuota mizizi mnamo siku za Luther, na zitaendelezwa
mpaka mwisho wa wakati kupitia wale watakaokubali kuacha vyote kwa ajili "neno la Mungu, na kwa
ushuhuda wa Yesu Kristo." Ufunuo 1:9.

25
Wylie, b. 16, ch. 1
42
Sura ya 5
JOHN WYCLIFFE

Kabla ya Matengenezo kulikuwa na nyakati ambapo kulikuwa na nakala chache tu za Biblia, lakini Mungu
hakuwa ameruhusu kwamba neno lake liharibiwe lote. Ukweli uliomo usingeweza kufichwa muda wote.
Angeweza kufungulia maneno ya uzima kutoka katika vifungo kama alivyofungua milango ya gereza na
kufungua komeo za malango ya chuma na kuwaacha watumishi wake huru. Katika nchi tofauti za Ulaya
watu walipata msukumo wa Roho wa Mungu kuutafuta ukweli kama hazina iliyositirika. Wakielekezwa
kwenda kwa Maandiko Matakatifu walijifunza hizo kurasa takatifu kwa moyo wa kupenda. Walikuwa
tayari kuikubali nuru kwa gharama yoyote. Ingawa hawakuona vitu vyote kwa uwazi, waliweza kuona
ukweli mwingi uliozikwa. Kama wajumbe waliotumwa na mbingu, walisonga mbele, wakibaini vifungo
vya madanganyo na upotofu, na kutoa wito kwa wale ambao wamekuwa katika utumwa wa muda mrefu
kuamka na kuchukua uhuru wao.
Isipokuwa kwa Wawaldensi, wakati ule neno la Mungu lilikuwa limefungwa katika lugha zinazoeleweka
kwa wasomi tu; lakini muda ulikuwa umefika wa Maandiko kutafsiriwa na kugawiwa kwa watu wa nchi
na lugha mbalimbali. Ulimwengu ulikuwa umeupita usiku wa manane. Saa za giza zilikuwa zinaisha, na
katika sehemu nyingi zilionekana dalili za mapambazuko.
(80) Katika karne ya kumi na nne “nyota ya asubuhi ya Matengenezo” iliinuka huko Uingereza. John
Wycliffe alikuwa mjumbe wa matengenezo, si tu katika Uingereza, bali kwa ulimwengu wote wa
Kikristo. Upinzani mkubwa aliopewa kuufanya dhidi ya Roma usingenyamazishwa kamwe. Upinzani huo
ulianzisha mapambano ambayo yangesababisha ukombozi wa watu, makanisa na mataifa.
Wycliffe alipata elimu ya kiliberali, na kwake, kumcha Bwana ilikuwa chanzo cha maarifa. Chuoni
alionekana kuwa makini, mwema, mwenye vipaji na makini katika kujifunza. Kiu yake ya ufahamu
ilimsukuma kujifunza karibu kila kitu katika elimu. Alisomea mambo ya taaluma ya falsafa, kanuni au
sheria za kanisa, na sheria ya nchi, hasa ile ya nchi yake. Katika kazi zake baadaye thamani ya mafunzo
haya aliyopata ilikuwa dhahiri. Ufahamu wake katika masuala ya falsafa wakati huo ulimwezesha
kubaini madanganyo; na kwa kuwa alikuwa amesomea sheria ya nchi na ya kanisa alikuwa ameandaliwa
kujihusisha na mapambano ya kupigania uhuru wa kiraia na wa kidini. Huku akiweza kutumia silaha
alizopata kutoka katika neno la Mungu, alikuwa amepata pia maarifa kutoka shuleni, na alielewa mbinu
za kisomi. Nguvu ya vipaji vyake na elimu yake vilimletea heshima kutoka kwa marafiki na maadui.
Wale wanaomuunga mkono waliridhishwa kuona kwamba kiongozi huyu alikuwa miongoni mwa watu
ambao ni tegemeo la taifa; na adui zake walishindwa kutoa lawama kwa kazi ya matengenezo kwamba
inaendeshwa kwa udhaifu au pasipo na elimu.
Akiwa bado chuoni, Wycliffe alijiingiza katika kujifunza Maandiko. Katika siku hizo za awali, Biblia ikiwa
katika lugha za awali, wasomi ndio walioweza kukifikia hiki kisima cha ukweli, ambacho kilikuwa
kimefungiwa mbali na macho ya matabaka ya watu wasio wasomi. Kwa hiyo njia ilikuwa tayari
imeandaliwa kwa ajili ya kazi yake ya baadaye kama Mwanamatengenezo. (81) Wale walio wasomi
walikuwa wamejifunza neno la Mungu na kugundua ukweli mkuu wa neema ya Mungu ya bure
iliyofunuliwa. Katika mafundisho yao walikuwa wametawanya elimu juu ya ukweli huu, na walikuwa
wamewaelekeza wengine kwa Mungu aliye hai.

43
Pindi mawazo ya Wycliffe yalipovutwa na kuelekezwa kwa Maandiko, alianza kuyachunguza kwa umakini
ule ule uliomwezesha kujifunza akiwa shuleni. Alikuwa amehisi kuwiwa kwa namna ambayo elimu
aliyosoma na mafundisho ya kanisa havikutosheleza kiu yake. Alipata katika neno la Mungu kile ambacho
alikuwa anakitafuta pasipo mafanikio. Aliona humo mpango wa wokovu ukiwa umefunuliwa, Kristo
akiwa mtetezi wa mwanadamu. Aliamua kuingia katika huduma ya Kristo na akajitoa kuutangaza ukweli
ule aliogundua.
Kama ilivyokuwa kwa Wanamatengenezo wa baada yake, wakati wa kuanza kazi yake hii, Wycliffe
hakuona mbali mahali kazi hii ilikokuwa inampeleka baadaye. Hakujiweka katika upinzani wa moja kwa
moja na Roma. Lakini kujiunga kwake na ukweli hakukumwepusha na kuingia katika mgogoro dhidi ya
imani za uongo. Kadiri alivyoweka bayana madanganyo ya upapa, ndivyo alivyoweka wazi zaidi
mafundisho ya Biblia. Aliona kwamba Roma ilikuwa imeacha neno la Mungu na kuchukua mapokeo ya
wanadamu; na bila woga alishutumu mfumo wa kipadri ulioondosha Maandiko, akadai kwamba Biblia
irejeshwe kwa watu na mamlaka yake iwe kanisani. Alikuwa mwalimu mwenye uwezo na mhubiri mzuri,
na maisha yake yalikuwa yakidhihirisha ukweli alioufundisha. Uelewa wake wa Maandiko, na nguvu ya
kujenga hoja, usafi wa maisha yake, na msimamo wake usioyumba vilimletea heshima na ujasiri. Watu
walio wengi walionyesha kutoridhishwa na imani yao ya awali kwa kuwa waliona udhalimu uliokuwa
katika Kanisa la Roma, na walipokea kwa furaha isiyofichika ukweli uliofunuliwa na Wycliffe; lakini watu
wa upapa walijawa ghadhabu walipoona kwamba Mwanamatengenezo huyu anapata ushawishi mkubwa
kuliko wao.
(82) Wycliffe alikuwa mtu makini katika kubaini makosa, na alipinga bila woga mabaya mengi
yaliyowekwa na mamlaka ya Roma. Akifanya kazi kama chapleni kwa ajili ya mfalme, alikuwa na
msimamo wake dhidi ya kitendo cha utozaji wa tozo ambapo papa alidai malipo kutoka kwa mtawala wa
Uingereza. Alionyesha kwamba kitendo cha upapa kujipa mamlaka juu ya watawala wasio wa kidini
ilikuwa kinyume cha ufunuo na hali ya kawaida. Matakwa haya ya papa yaliibua kutokuridhika miongoni
mwa watu, na mafundisho ya Wycliffe yalileta ushawishi miongoni mwa watu wanaotegemewa katika
taifa. Mfalme na watawala walio wasaidizi wake waliungana katika kukataa mamlaka ya papa na
vitendo vyake vya kutoza tozo. Kwa hiyo upinzani wa nguvu ulitokea dhidi ya upapa huko Uingereza.
Uovu mwingine ambao Mwanamatengenezo huyu alipambana nao sana na kwa mapambano ya dhati ni
uanzishaji wa mfumo wa watawa ombaomba. Watawa hawa wa kiume waliingia Uingereza kwa wingi na
kutia doa ukuu na mafanikio makubwa ya taifa hilo. Viwanda, elimu, maadili, vyote vilionekana
kuathiriwa. Maisha ya kivivu na ya kuombaomba ya watawa hawa hayakuwa mzigo mkubwa kwa
rasilimali za watu tu, bali pia yalisababisha chuki kwa nguvu kazi hii isiyotumika. Vijana walikatishwa
tamaa na kudanganyika. Kwa kushawishiwa na watawa, wengi walivutwa na kujiunga katika makazi ya
watawa na kuishi maisha ya kitawa, mambo haya yakifanyika pasipo ridhaa ya wazazi wao, na bila wao
wenyewe kuwa na ufahamu au uelewa wa hicho walichokuwa wanafanya. Mmoja wa Mapadri wa awali
wa Kanisa la Roma, akiwa anahamasisha watu, alipata kusema: “Hata kama baba yako atalala mahali pa
mlango wako akilia na kuomboleza, na mama yako hata akivua nguo akaweka wazi mwili uliokuzaa na
maziwa yaliyokunyonyesha, wakanyage wewe usonge mbele kwenda kwa Kristo.” Baadaye Luther
aliieleza hali hiyo kama “utovu wa ubinadamu unaotafuta manufaa ya mbwa-mwitu na ya mdhalimu
badala ya Mkristo au mtu," na ndivyo ilivyokuwa mioyo ya watoto dhidi ya wazazi wao. 26 Hivyo ndivyo
walivyofanya viongozi wa upapa, (83) kama Mafarisayo wa zamani, kufanya amri za Mungu zisiwe na

26
Barnas Sears, The Life of Luther, pages 70, 69

44
maana kwa sababu ya mapokeo yao. Nyumba zilifanywa ukiwa, na wazazi walinyang’anywa hali ya
kujumuika na wana na binti zao.
Hata wanafunzi waliokuwa katika vyuo vikuu walidanganywa na ushawishi wa watawa hawa na kuvutwa
kuungana na jumuiya yao. Baadaye wengi walikiri kupotea, wakaona kwamba wamedanganya maisha
yao na kusababisha huzuni kwa wazazi wao; lakini wakishakuwa katika mitego hiyo ilikuwa vigumu kwao
kupata uhuru. Wazazi wengi walikataa kupeleka watoto wao vyuoni wakiuhofu ushawishi wa watawa.
Mahudhurio ya wanafunzi katika vituo vya kujifunzia yalishuka kwa kiasi kikubwa. Shule zilifungwa,
ujinga ukashamiri.
Papa alikuwa amewapatia watawa hawa mamlaka ya kupokea toba za watu na kutoa msamaha. Hiki
kilikuwa chanzo cha uovu mkuu. Wakijielekeza katika kutafuta manufaa yao ya kimwili, watawa hawa
walikuwa tayari kusamehe wahalifu wa aina zote waliowajia, na, matokeo yake, uhalifu uliongezeka
kwa haraka katika jamii. Wagonjwa na maskini waliachwa wakihangaika, huku sadaka ambazo
zingewahudumia zikipelekwa kwa watawa, ambao walitumia vitisho kudai wapewe matoleo, wakipinga
uchoyo ulioonyeshwa na wale ambao waliacha kuwapatia na kwenda kinyume na maelekezo yao. Licha
ya kuhubiri umaskini, utajiri wa watawa hawa ulikuwa ukiendelea kuongezeka, na majengo yao
makubwa ya kifahari na meza za anasa viliendelea kuongeza umaskini kwa taifa. Wakati wakiendelea na
maisha yao ya anasa na kujifurahisha, waliwatuma badala yao watu wasiojua kitu, ambao waliishia tu
kuwasimulia watu hadithi za kuvutia, na maelezo ya utani ili kuridhisha watu kusudi wawe watulivu
katika madanganyo ya watawa. Watawa waliendelea kushikilia makutano na kuwaongoza kuamini
kwamba wajibu wa kidini uko ndani ya kutambua mamlaka ya papa, kukarimu watakatifu, na kutoa kwa
watawa, na ya kwamba hili lilitosha kuwaandalia mahali pao mbinguni. (84)
Watu wasomi na wakarimu walikuwa wametumika pasipo mafanikio katika kuleta matengenezo katika
mfumo huu wa kitawa; lakini Wycliffe, kwa mtazamo wa wazi, alianzia katika mzizi wa uovu,
akitangaza wazi kwamba mfumo wenyewe haukuwa sahihi na kwa hiyo upigwe marufuku. Mijadala na
maswali yaliamshwa. Kadiri watawa walivyotawanyika katika nchi, wakitoa msamaha wa papa, watu
wengi waliongozwa kuwa na mashaka juu ya uhalali wa kununua msamaha kwa fedha, na walihoji ikiwa
haiwapasi kutafuta msamaha toka kwa Mungu wala si kwa kasisi wa Roma. 27 Si watu wachache
walioamshwa na tabia hizi za watawa, ambao walionekana watu walafi wasiotosheka. Walisema:
"Watawa na makasisi wa Roma wanatutafuna kama saratani. Lazima Mungu atuokoe, la sivyo watu
watakwisha." 28 Kuficha uroho, hawa watawa ombaomba walidai kwamba walikuwa wanafuata mfano wa
Mwokozi, wakitangaza kwamba Yesu na wanafunzi wake walikuwa wakitegemezwa na ukarimu wa watu.
Madai haya yalileta matatizo kwa kazi yao, kwa sababu yalielekeza watu kujifunza ukweli wa Biblia wao
wenyewe – ambapo matokeo yake yalikuwa mambo yasiyoipendeza Roma. Mawazo ya watu yalielekezwa
kwenye kile Chanzo cha ukweli, ambacho ilikuwa ni nia ya Roma kukificha.
Wycliffe alianza kuandika na kuchapisha vipeperushi kupinga watawa, huku akijihadhali asijiingize
katika ugomvi na wao, kwa kuyaelekeza mawazo ya watu katika Biblia na Mtunzi wake. Alitangaza
kwamba mamlaka ya kusamehe au kutenga mtu imewekwa kwa makasisi wa Roma kwa makosa, na ya
kwamba mtu hawezi kutengwa isipokuwa amejiletea yeye mwenyewe hukumu ya Mungu. Hakuweza
kupindua kazi kubwa iliyokuwa imejengwa na upapa katika roho na miili ya mamilioni ya watu walio
utumwani.

27
Angalia ufafanuzi wa nyongeza au rejea mwishoni
28
--D'Aubigne, b. 17, ch. 7.
45
Tena Wycliffe aliitwa ili kutetea haki za Waingereza zilizokuwa zimeingiliwa na Roma; na akiwa
ameteuliwa kama balozi, alikaa Uholanzi kwa miaka miwili, akiwa katika mikutano ya majadiliano na
mabalozi wa papa. Hapa alikutanishwa na (85) viongozi wa dini kutoka Ufaransa, Italia na Hispania, na
alipata nafasi ya kuona na kujua vitu vingi ambavyo vingeendelea kufichwa kwake ikiwa angebaki
Uingereza. Alijifunza mengi ambayo yangemsaidia katika kazi baadaye. Kwa hawa wawakilishi wa papa
alijifunza mfumo halisi wa upapa na makusudi yake. Alirudi Uingereza kurudia mafundisho yake kwa
uwazi zaidi, akitangaza kwamba tama ya mali, kiburi na madanganyo vilikuwa miungu ya Roma.
Akiongolea habari ya papa na wasaidizi wake katika moja ya vitini vyake, Wycliffe alisema: "Wanachota
riziki za watu maskini kutoka katika nchi yetu, na maelfu ya fedha za mfalme, kila mwaka, kwa
sakramenti na mambo ya kiroho, huu ni uasi uliolaaniwa, na unafanya Wakristo wote wafuate uasi huu.
Ufalme wetu ulikuwa na mlima wa dhahabu, na hakuna mtu aliyeichukua ila wasaidizi wanaomkusanyia
kasisi wa ulimwengu huu mwenye kiburi, baada ya muda mlima wote utakuwa umetumika; kwa kuwa
anachukua fedha kutoka katika nchi yetu, na hakuna anachopeleka isipokuwa laana ya Mungu." 29
Muda mfupi baada ya kurudi Uingereza, Wycliffe aliteuliwa na mfalme kuwa kasisi wa Lutterworth. Hili
lilikuwa hakikisho ya kuwa walau mtawala yule hakuwa amechukizwa na maneno yake yale ya wazi
wazi. Ushawishi wa Wycliffe ulionekana katika kuushawishi utawala, na hata kurekebisha imani ya taifa.
Baada ya muda mfupi radi za kipapa zilimwungurumia. Nyaraka za matamko tatu zilipelekwa Uingereza,
- kwa chuo kikuu, kwa mfalme, na kwa maaskofu, - zikiagiza kuchukua hatua za kumnyamazisha mzushi
huyu. 30 31 Hata hivyo, kabla ya maagizo hayo kufika, maaskofu walikuwa wameshamwita Wycliffe kwa
ajili ya kuhojiwa. Lakini wawili miongoni mwa wana wa kifalme wenye nguvu sana katika himaya ile
walimsindikiza mbele ya baraza hili; na watu, wakiwa wamezunguka jengo lile na kuingia mle ndani,
waliwatisha waamuzi wa baraza kwamba (86) kazi ambayo ingefanyika pale imesitishwa kwa muda huo,
na mtuhumiwa aliruhusiwa kwenda zake kwa amani. Muda mfupi baadaye, Edward III, ambaye wakati
huu wa uzee wake alitegemewa na maaskofu kutumia ushawishi wake dhidi ya Mwanamatengenezo
huyu, alikufa, na mtetezi wa Wycliffe akawa ndiye mfalme.
Lakini kufika kwa amri ya papa kulikuwa kama amri isiyopingwa kote Uingereza, kwamba mzushi huyu
akamatwe na kutiwa gerezani. Hatua hizi zililenga mahali penyewe. Ilionekana hakika kwamba ndani ya
muda mfupi Wycliffe atatiwa mikononi mwa nguvu za Roma. Lakini yeye aliyemwambia mtu mmoja wa
zamani kwamba, "Usiogope: . . . Mimi ni ngao yako" (Mwanzo 15:1), alinyoosha mkono wake tena na
kumlinda mtumishi wake. Mauti ilikuja, lakini si kwa Mwanamatengenezo huyu, bali kwa papa
mwenyewe aliyetoa amri ya kuharibu. Gregory XI akafa, na maaskofu waliokuwa wamejikusanya
kumhoji Wycliffe wakatawanyika.
Bado ukuu wa Mungu uliendelea kuyatawala matukio kusudi kazi ya Matengenezo ikue. Kifo cha Gregory
kilifuatiwa na kuchaguliwa kwa mapapa wawili wasiopatana. Watawala hawa wawili wanaopingana
walidai kutiiwa na kuheshimiwa, kila mmoja akijidai kuwa kamili. (Angalia maelezo ya Kiambatanisho
kwa ajili ya ukurasa wa 50 na 86). Kila mmoja alialika watu walio watiifu kwake ili kufanya vita na
mpinzani wake, akilazimisha wamfanyie vurugu mpinzani wake, na kuwaahidi thawabu ya mbinguni
wote wanaomuunga mkono. Tukio hili lilidhoofisha kwa sehemu kubwa nguvu ya upapa. Pande mbili
zinazohitilafiana zilifanya kila linalowezekana kukabiliana, na kwa muda Wycliffe akapumzika. Vurugu
na vitendo vya uhalifu viliendelezwa kutoka kwa papa mmoja kwenda kwa mwingine, na tiririko la damu

29
John Lewis, History of the Life and Sufferings of J. Wiclif, page 37.
30
Augustus Neander, General History of the Christian Religion and Church, period 6, sec. 2, pt. 1, par. 8.
31
Angalia nyongeza mwishoni
46
lilifuatia mapambano yao. Matukio ya uhalifu na kashfa vilifurika katika kanisa. Kimya-kimya, akistaafu
kazi yake katika parishi ya Lutterworth, Mwanamatengenezo yeye aliendelea kuwageuza watu kutoka
kwa mapapa wanaogombana na kuwaelekeza kwa Yesu, Mfalme wa Amani.
Mgawanyiko ule, pamoja na machafuko yote ambayo ulisababisha, viliandaa njia ya Matengenezo kwa
kuwaonyesha watu uhalisia wa upapa. Katika kitini alichochapisha kinachoitwa, On the Schism of the
Popes (Kuhusu Mgawanyiko wa Mapapa), Wycliffe aliwataka (87) watu watafakari ikiwa si ya kweli
maneno yale ambayo makasisi wale walikuwa wakirushiana kila mmoja akimtuhumu mwingine kuwa ni
mpinga-Kristo. Alisema "Mungu hawezi tena kuruhusu mtu mwovu kutawala kama kasisi, lakini . . .
aliweka mgawanyiko kati ya hao wawili, kusudi watu, katika jina la Kristo, wawashinde wote wawili kwa
urahisi." 32
Kama Bwana wake alivyofanya, Wycliffe alihubiri injili kwa maskini. Bila kuridhika na usambazaji wa
nuru majumbani mwa watu katika parishi yake ya Lutterworth, aliazimia kwamba nuru ihubiriwe kote
katika Uingereza. Ili kutekeleza hili, alianzisha kundi la wahubiri walio wepesi, watu waliojitoa,
waliopenda ukweli na ambao hawakutamani kitu kingine zaidi ya kuusambaza. Watu hawa walienda kila
mahali, wakifundisha sokoni, mitaani, katika miji mikubwa, na katika vijiji. Waliwatafuta walio wazee
wa umri, wagonjwa, na kuwafungulia furaha ya neema ya Mungu.
Akiwa profesa wa thiolojia katika chuo kikuu cha Oxford, Wycliffe alihubiri neno la Mungu katika kumbi
za chuo. Kwa uaminifu aliwasilisha ukweli kwa wanafunzi waliokuwa wakifundishwa naye, kiasi kwamba
alipewa jina la "daktari wa injili." Lakini kazi yake kubwa kuliko zote ingekuwa kutafsiri Maandiko katika
lugha ya Kingereza. Katika toleo linaloitwa On the Truth and Meaning of Scripture (Kuhusu Ukweli na
Maana ya Maandiko), alielezea nia yake ya kutafsiri Biblia, kusudi kila mtu katika Uingereza apate
kuyasoma matendo ya ajabu ya Mungu katika lugha yake ya kuzaliwa.
Lakini ghafla, kazi zake zilisitishwa. Ingawa alikuwa hajafikia umri wa miaka sitini, mahangaiko
yasiyokoma, masomo, na usumbufu na mapigo ya wale waliomchukia vilimpunguzia nguvu ya mwili na
kumfanya azeeke kabla ya wakati. Alishikwa na ugonjwa wa hatari. Tatizo hili lilileta furaha kubwa kwa
mapadri. Sasa walidhani atatubia uovu aliolitendea kanisa, na waliharakisha kwenda chumbani kwake ili
kumsikiliza anavyotubu. Wawakilishi kutoka katika mifumo minne ya kitawa ya kanisa lile, na maafisa
wanne wa kiserikali, walikusanyika kwa mtu huyu aliyetarajiwa kufa. Walisema hivi, "Wewe (88)
umebeba kifo midomoni mwako, guswa na uovu wako, sasa futa yote uliyoyasema dhidi yetu."
Mwanamatengenezo yule aliwasikiliza akiwa kimya; halafu alimwomba mtunzaji wake amwinue
kitandani pake, na, akiwakazia macho walipokuwa wamesimama wakimsubiri ayakane maneno yake,
alisema kwa sauti yenye nguvu, ambayo mara kwa mara ilikuwa imewafanya kutetemeka: "Sitakufa, bali
nitaishi; nitayasema tena matendo maovu ya watawa." 33 Wakiwa wameshangazwa na kutahayari, wale
mabradha watawa walitoweka haraka kutoka chumbani.
Maneno ya Wycliffe yalitimia. Aliishi na kuweka mikononi mwa watu wa nchi yake silaha zote za nguvu
za kupambana na Roma – kwa kuwapa Biblia, nyenzo aliyeteuliwa na Mbingu ili kuwakomboa,
kuwaangazia nuru na kuwainjilisha watu. Kulikuwa na vikwazo vingi katika kuikamilisha kazi hii. Uzito
Wycliffe alielemewa na maradhi; alijua kwamba bado ana miaka michache tu ya kufanya kazi; aliuona
upinzani uliokuwa mbele yake; lakini alitiwa moyo na ahadi za neno la Mungu, akasonga mbele bila
kuogopa. Kwa msukumo na nguvu ya usomi wake, akiwa na uzoefu tele, alikuwa ameandaliwa na Mungu
kwa ajili ya wakati kama huu, ndiyo kazi yake kubwa kuliko zote. Wakati huu ambapo Ukristo wote

32
R. Vaughan, Life and Opinions of John de Wycliffe, vol. 2, p. 6
33
D'Aubigne, b. 17, ch. 7
47
ulikuwa katika mfadhaiko, Mwanamatengenezo, akiwa katika jumba la ukasisi la Lutterworth, pasipo
kuogopa hasira ya dhoruba, aliingia katika shughuli yake.
Hatimaye kazi ilikamilika – tafsiri ya kwanza ya Biblia ilitolewa kwa Kingereza. Neno la Mungu
lilifunguliwa ndani ya nchi ya Uingereza. Mwanamatengenezo huyu hakuogopa tena vifungo wala
mateso. Alikuwa ameiweka mikononi mwa Waingereza nuru ambayo isingezimika. Kwa kuwapa watu wa
nchi yake Biblia, alikuwa amejitahidi kuzikata pingu za ujinga na madanganyo, ili kuikomboa nchi yake
na kuipandisha juu, kwa namna ya kuzidi juhudi zote na ushindi uliokuwa umepatikana kabla.
Sanaa ya uchapishaji ikiwa haijajulikana bado, kuzalisha nakala za Biblia ilikuwa kazi ya taratibu na ya
muda mrefu. Kupata kitabu hicho lilikuwa jambo la kuvutia kiasi kwamba (89) watu wengi walijisikia
kushiriki katika kazi ya kuinakili, lakini ilikuwa vigumu kwa wenye kunakili kuweza kutimiza mahitaji ya
watu. Baadhi ya watu waliokuwa na uwezo wa kununua walihitaji Biblia nzima. Wengine walinunua
sehemu tu. Katika hali fulani fulani jamaa ziliungana na kununua nakala moja. Hatimaye Biblia ya
Wycliffe ikapata njia ya kufika majumbani mwa watu.
Nguvu ya neno la Mungu iliyaondoa mawazo ya watu katika mfumo wa imani ya upapa. Sasa Wycliffe
alifundisha mafundisho yenyewe ya Uprotestanti – wokovu kwa imani katika Kristo, na hali ya
kutokukosea kwa Maandiko. Wahubiri aliokuwa amewatuma waliisambaza Biblia, ikiwa ni pamoja na
maandishi mengine ya Mwanamatengenezo huyu, na kwa hiyo mafanikio yakawa makubwa kiasi kwamba
imani hii mpya ilipokelewa na karibu nusu ya watu wote wa Uingereza.
Kupatika kwa Maandiko kulileta mfadhaiko kwa mamlaka za kanisa. Sasa zilikuwa zikabiliane na nguvu
kubwa zaidi kuliko Wycliffe – nguvu ambayo silaha zao zingeleta mafanikio kidogo sana. Wakati huu
Uingereza hakukuwa na sheria inayokataza watu kuwa na Biblia, kwa kuwa Biblia ilikuwa haijawahi
kuchapishwa katika lugha ya watu wale. Sheria kama hizo zilitungwa baadaye na kutekelezwa kwa
nguvu. Lakini kwa wakati huu, licha ya juhudi zote za makasisi kuleta upinzani, kulikuwa na fursa ya
kulisambaza neno la Mungu.
Watu wa upapa waliazimia tena kuinyamazisha sauti ya Mwanamatengenezo. Katika mabaraza matatu
aliitwa na kuhojiwa, pasipo mafanikio. Kwanza mkutano wa maaskofu ulitoa azimio la kutangaza
kwamba maandishi yake ni ya kiuzushi, na wakamvutia upande wao mfalme kijana, Richard II, kutoa
tamko la kiutawala kwamba mtu yeyote atakayekutwa na mafundisho yaliyozuiliwa atatupwa gerezani.
Wycliffe alikata rufaa kutoka kwa sinodi kwenda kwa Bunge; bila hofu aliushtaki mfumo wa kanisa kwa
baraza hili la taifa akihitaji marekebisho yafanyike kuhusu mashinikizo ya kanisa. Kwa ushawishi na
mvuto wa hoja alibainisha ubaya na madanganyo ya upapa. Adui zake walichanganyikiwa. Marafiki zake
na wale wanaomuunga mkono walikuwa wamelazimishwa kumwacha, na kulikuwa (90) na matarajio ya
uhakika kwamba Mwanamatengenezo huyu, katika uzee wake, akiwa peke yake pasipo rafiki yeyote,
angeheshimu na kukubaliana na mamlaka ya muungano wa kofia ya kifalme na ile ya kiaskofu. Lakini
badala ya kuwa hivyo, mawakala wa papa walijikuta wameshindwa wao. Bunge liliungana na wito wa
Wycliffe, likasitisha amri ya kutesa watu, na Mwanamatengenezo huyu akawa huru tena.
Kwa mara ya tatu aliletwa tena kuhojiwa, wakati huu katika baraza la juu la kanisa katika ufame wote.
Mahali hapa huwa hakuna huruma kwa mzushi. Hapa ndipo mahali ambapo hatimaye Roma ingeshinda,
na kazi ya Mwanamatengenezo huyu kukomeshwa. Hivyo ndivyo mawakala wa upapa walivyodhani.
Ikiwa wangetekeleza tu azma yao, Wycliffe angelazimika kuyakana na kuachana na mafundisho yake, au
angetoka mbele ya baraza lile kuelekea katika ndimi za moto.

48
Lakini Wycliffe hakusalimu amri. Aliendelea na msimamo wa mafundisho yake pasipo woga na akapinga
mashtaka ya washtaki wake. Akiwa amejisahau, akisahau nafasi yake, na tukio lenyewe, alijikuta
akiwapeleka wasikilizaji wake katika mahakama ya mbinguni, kuyapima madanganyo yao kwa
kulinganisha na ukweli wa milele. Nguvu ya Roho Mtakatifu ilionekana katika chumba cha baraza.
Hukumu kutoka kwa Mungu ilikuwa juu ya wasikilizaji wale. Walionekana kukosa nguvu za kuondoka
pale. Kama mishale kutoka katika mvumo wa sauti ya Bwana, maneno ya Mwanamatengenezo huyu
yaliwachoma mioyo. Kwa nguvu yake ya ushawishi, alirudisha kwao wenyewe mashtaka ya uasi
waliyokuwa wamemshtaki. Alilalamika kwamba, ni kwa nini walisambaza udanganyifu wao? Kwa nini
wajitafutie faida kwa kufanya biashara ya neema ya Mungu?
Mwisho alisema "Mnafikiri mnapingana na nani? Na mzee tu anayeelekea kaburini? La! Mnapingana na
ukweli – Ukweli ulio na nguvu kuliko ninyi wenyewe, nao utawashinda." 34 Kwa kusema hayo, akatoka
katika mkutano, na hakuna hata mmoja wa wapinzani wake aliyediriki kumzuia.
Kazi ya Wycliffe ilikuwa kama imefanyika tayari; bendera ya ukweli ambayo alikuwa ameibeba kwa
muda mrefu ilikuwa inakaribia kushuka kutoka mkononi mwake; lakini mara nyingine zaidi alikuwa
aubebe ushuhuda wa injili. (91) Ukweli ulihitaji kutamkwa kuanzia katika ngome yenyewe ya ufalme wa
uasi. Wycliffe aliitwa kuhojiwa na baraza la papa huko Roma, ambako damu nyingi za watakatifu
zilikuwa zimemwagwa. Hakuwa kipofu kuhusu hatari zilizokuwa zikimkabili mbele yake, lakini angeitikia
wito wa kwenda barazani ikiwa mshtuko wa kupooza ubongo usingempata na kushindwa kusafiri. Hata
hivyo, ingawa sauti yake isingesikika Roma, angeweza kuongea kwa barua, na aliazimia kufanya hivyo.
Kutoka katika jumba lake la kitawa, Mwanamatengenezo huyu aliandika barua kwa papa, ambayo, kwa
maneno ya heshima na roho ya Kikristo, ilikuwa ni onyo makini la kuikemea hali ya kujionyesha na kiburi
ya taasisi ya upapa.
Alisema "Hakika ninayo furaha kufunua na kutangaza kwa kila mtu imani niliyo nayo, na hasa kwa askofu
wa Roma: imani ambayo ni sahihi na ya kweli, naye atapendezwa kuithibitisha imani yangu hiyo, la
kama ina makosa, airekebishe.
"Kwanza, naelewa kwamba injili ya Kristo ni sheria yote ya Mungu. . . . Namjua askofu wa Roma, kadiri
alivyo makamu wa Kristo hapa duniani, kwamba naye anategemewa keheshimu sheria ya injili, kama
watu wengine. Kwa kuwa ukubwa miongoni mwa wanafunzi wa Kristo haukuendana na kujikweza na
heshima, bali kule kuwa karibu na Kristo na kumfuata katika maisha na tabia yake.... Wakati akitembea
hapa duniani, Kristo alikuwa maskini kuliko wote, akipuuza na kuacha mamlaka na heshima za
ulimwengu. . . .
"Hakuna mtu mwaminifu anayelazimishwa kumfuata papa au mtakatifu yeyote, isipokuwa katika mambo
ambayo anamfuata Bwana Yesu Kristo; kwa kuwa Petro na wana wa Zebedayo, kwa kutamani heshima
ya ulimwengu badala ya kufuata hatua za Kristo, walikosea, na katika makosa yao yale hawastahili
kufuatwa. . . .
"Ilimpasa papa kuacha mamlaka na utawala kwa tawala zisizo za kidini, na hivyo kuacha kukandamiza
watumishi wa kanisa; maana ndivyo alivyofanya Kristo, hata mitume wake. Kwa hiyo kama nimeasi kwa
mambo haya, nitakuwa tayari kusahihishwa, (92) hata kwa kifo, kama italazimu hivyo; na kama
ningefanya kazi kwa mapenzi yangu mwenyewe na nafsi yangu, ningejisalimisha kwa askofu wa Roma;
lakini tofauti na hivyo Bwana amenitembelea kwa namna nyingine, amenifundisha kumtii Mungu kuliko
wanadamu."

34
Wylie, b. 2, ch. 13
49
Alifunga barua yake kwa kusema: "Hebu tumwombe Mungu wetu ili awashe moto ndani ya Papa Urban
VI, kama alivyokwisha kuanza, ili kwamba yeye na watumishi wa kanisa wamfuate Bwana Yesu Kristo
kwa maisha na tabia; na ya kwamba wawafundishe watu pia kuwafuata katika mambo hayo." 35
Wycliffe aliwasilisha unyenyekevu wa Kristo kwa papa na makadinali wake, akidhihirisha, si kwao tu bali
kwa Wakristo wote pia, tofauti iliyopo kati yao na Bwana ambaye walidai kuwa wawakilishi wake.
Wycliffe alijua fika kwamba uhai wake ndio ungekuwa gharama ya msimamo wake huu. Mfalme, papa
na maaskofu walikuwa wameungana ili kukamilisha kifo chake, na ilionekana dhahiri kwamba kazi ya
kumfikisha hapo, kama itachukua muda mrefu, ni miezi michache tu. Lakini ujasiri wake ulikuwa ule
usiotikiswa. Alisema, "Kwa nini unaitafuta taji ya kuwa mfia-dini mbali? Ihubiri injili ya Kristo
uwachukize makasisi, hadhi ya ufia dini haitakukosa. Nini hii! Niishi nikiwa kimya? . . . Kamwe! Kipigo
na kije, nasubiri kuja kwake." 36
Lakini ulinzi wa Mungu uliendelea kumfunika mtumishi wake. Haikuwezekana mtu ambaye amesimama
imara kwa ajili ya ukweli maisha yake yote, katika mahangaiko yake ya kila siku, aangukie katika
matokeo mabaya ya kuchukiwa na watu. Wycliffe hakuwahi kujitahidi kujilinda yeye mwenyewe, lakini
Bwana alikuwa mlinzi wake wakati wote; na sasa, adui zake walipokuwa na hakika kwamba yeye
alikuwa mawindo yao, mkono wa Mungu ulimpeleka mbali zaidi kuliko mahali ambapo wangeweza
kumfikia. Katika kanisa lake la Lutterworth, alipokuwa anataka kuhudumia katika komuniyo, alianguka
chini kwa sababu ya kupooza, na baada ya muda mfupi uhai ukamtoka.
Mungu alikuwa amemteua Wycliffe kwa kazi yake. Alikuwa ameweka (93) neno la kweli midomoni
mwake, na aliweka ulinzi kwake kusudi neno lake liwafikie watu. Maisha yake yalilindwa, na kazi zake
zilirefushwa, mpaka msingi mkuu wa Matengenezo ulipowekwa.
Wycliffe aliibuka katika utusitusi wa Zama za Giza. Hakuna waliotangulia kabla yake ambao wangeweka
mwelekeo wa mfumo wake wa matengenezo. Akiibuka kama ilivyokuwa kwa Yohana Mbatizaji kwa ajili
ya kuitekeleza kazi maalum, alikuwa ni nyota ya zama mpya. Lakini katika mfumo wa ukweli
aliofundisha kulikuwa na mwunganiko na ukamilifu ambao haukupitwa na Wanamatengenezo
waliomfuata, tena wengine hawakuufikia kabisa, hata kwa miaka mia moja baadaye. Msingi alioweka
ulikuwa mpana na wa kina, mfumo wake ulikuwa imara na wa kweli, kiasi kwamba haukuhitaji
kujengwa tena na wale waliofuata baada yake.
Harakati kubwa aliyozindua Wycliffe, iliyolenga kukomboa dhamira na akili, na kuyafanya huru mataifa
yaliyokuwa katika kifungo cha Roma iliyokuwa na nguvu, ilibubujikoa kutoka katika Biblia. Hiki ndicho
kilichokuwa chanzo cha kijito kile cha baraka, ambacho, kama maji ya uzima, kimetiririka katika vizazi
tangu karne ya kumi na nne. Wycliffe aliyakubali Maandiko Matakatifu kwa imani yake kama uvuvio wa
ufunuo wa mapenzi ya Mungu, kiongozi tosha cha imani na matendo. Alikuwa ameelimishwa kuheshimu
Kanisa la Roma kama mamlaka kamilifu kutoka mbinguni, na kupokea pasipo kuhoji mafundisho na
desturi zake zilizojengwa kwa maelfu ya miaka; lakini aligeukia mbali na haya na kuamua kusikiliza
neno takatifu la Mungu. Hii ndiyo mamlaka ambayo aliwaalika watu waipokee. Badala ya kanisa
lililonena kupitia papa, alitangaza kwamba mamlaka ya kweli ni sauti ya Mungu inayoongea kupitia neno
lake. Na hakufundisha tu kwamba Biblia ni ufunuo mkamilifu wa mapenzi ya Mungu, bali pia kwamba
Roho Mtakatifu ndiye mtafsiri pekee wa Biblia, na kwamba kila mmoja anajifunza wajibu wake yeye

35
John Foxe, Acts and Monuments, vol. 3, pp. 49, 50
36
D'Aubigne, b. 17, ch. 8

50
mwenyewe kwa kujifunza mafundisho ya Biblia. Kwa hiyo aligeuza mawazo ya watu kutoka kwa papa na
Kanisa la Roma kuyapeleka kwa neno la Mungu.
(94) Wycliffe alikuwa mmoja wa Wanamatengenezo wakubwa. Kwa upana wa akili yake, kwa mawazo
yake ya wazi, katika msimamo wake wa kuusimamia na kuulinda ukweli, aliweza kulinganishwa na
wachache waliokuja baada yake. Usafi wa maisha, umakini wake katika kujifunza na kufanya kazi,
uadilifu wake, na upendo wake wa Kikristo, na uaminifu katika huduma yake, vilikuwa sifa ya
Wanamatengenezo wa kwanza. Haya yote yaliwezekana licha ya giza la kiakili na upotovu wa kimaadili
uliokuwepo katika zama zake.
Tabia ya Wycliffe ni ushuhuda wa nguvu za Maandiko Matakatiffu zinazoelimisha na kubadili maisha.
Biblia ndiyo ilimfanya kuwa vile alivyokuwa. Juhudi za kuelewa ukweli mkuu uliofunuliwa zilileta upya
wa maisha na nguvu katika maeneo yote. Kujifunza Biblia kunapanua akili, kunanoa mitazamo kuhusu
mambo, na kunakuza uwezo wa maamuzi. Kunaboresha kila fikra, hisia na nia kiasi ambacho kitu
kingine chochote cha kujifunza hakiwezi. Kunatoa msimamo katika malengo, subira, ujasiri, na nguvu;
kunaosha tabia na kutakasa roho. Ujifunzaji wa Maandiko kwa moyo na unyenyekevu unakutanisha
mawazo ya mtu na umilele, na ungetoa kwa ulimwengu watu wenye upeo mkubwa wa akili kuliko vile
mafunzo ya falsafa za wanadamu yatoavyo. Mwimba Zaburi anasema, "Kufafanusha maneno yako kwatia
nuru, na kumfahamisha mjinga." Zaburi 119:130.
Mafundisho yaliyokuwa yamefundishwa na Wycliffe yaliendelea kusambaa kwa muda; wafuasi wake,
waliojulikana kama Wycliffites na Lollards, si tu kwamba walitawanyika kote Uingereza, bali pia
walitawanyika hata kwingine nje ya Uingereza, wakiipeleka injili. Kwamba kiongozi wao alikuwa
ameondolewa kwao, wahubiri hawa walifanya kazi hata kwa nguvu zaidi kuliko awali, na makutano
wengi walimininika kusikiliza mafundisho yao. Baadhi ya wana wa nyumba ya kifalme, hata mke wa
mfalme mwenyewe, walikuwa miongoni mwa waongofu. Mahali pengi kulikuwa na viashiria vya
matengenezo katika tabia za maisha ya watu, na alama za ibada ya sanamu ziliondolewa makanisani.
Lakini baada ya muda, dhoruba isiyo na mpaka ya mateso ilivuma juu ya wote waliokuwa wameipokea
(95) Biblia kama kiongozi chao. Watawala wadhalimu wa Uingereza, wakiwa na hamu ya kuimarisha
nguvu zao huku wakiungwa mkono na Roma hawakusita kuwatoa kafara Wanamatengenezo. Kwa mara
ya kwanza katika historia ya Uingereza amri ya kuruhhsu nguzo ya mateso ilitolewa dhidi ya wanafunzi
wa injili. Wafia-dini baada ya wafia-dini walifuatana. Wateteao ukweli waliingizwa katika mateso, na
vilio vyao vingesikika kwa Bwana tu. Wakiwindwa kama watu wa balaa kwa kanisa na wasaliti wa jamii
ya waamini, waliendelea kuhubiri katika maeneo ya siri, wakijitahidi kutafuta hifadhi katika nyumba za
maskini, na mara nyingi wakijificha mbali katika mapango na mashimo ya nchi.
Bila kujali janga la mateso, maneno ya upinzani makini wa kimya dhidi ya imani ya dini ya udanganyifu
yaliendelea kutajwa kwa karne nyingi. Wakristo wa kipindi hicho cha kale walikuwa na uelewa wa
ukweli kwa sehemu tu, lakini walikuwa wamejifunza kumpenda na kumtii Mungu, na kwa saburi
walipata mateso kwa sababu yake. Kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa Yesu wa nyakati za mitume,
wengi walitoa kafara ya mali zao kwa ajili ya kazi ya Kristo. Wale walioruhusiwa kuishi katika nyumba
zao walitoa hifadhi kwa furaha kwa ndugu zao waliofukuzwa, na wao pia walipofukuzwa walipokea kwa
tabasamu kipimo hicho hicho cha waliokataliwa. Kweli, maelfu walitishwa na ghadhabu ya watesi wao,
wakaununua uhuru kwa gharama ya kutoa kafara imani yao, na wakatolewa magerezani hali
wamevishwa kanzu maalum ili kuutangazia umma kwamba wameikana imani yao. Lakini idadi haikuwa
ndogo – baadhi wakiwa wa kutoka katika nyumba ya kifalme na wengine wa hali ya kawaida na ya chini –
ya walioubeba ushuhuda katika vyumba vya magereza bila woga, katika “minara ya Lollard," na katikati

51
ya mateso na moto, wakifurahi ya kwamba walihesabiwa kustahili kujua maana ya “kushiriki mateso ya
Bwana wao.”
Watu wa upapa walikuwa wameshindwa kutekeleza azma yao kwa Wycliffe wakati wa uhai wake, na
chuki yao haikuridhishwa kuona mwili wake umepumzishwa hivi hivi kaburini. Kwa amri ya Baraza la
Constance, miaka zaidi ya arobaini baada ya kifo chake, mifupa yake ilifukuliwa ikachomwa moto, na
majivu yakatupwa mtoni. Mwandishi mmoja wa zamani anasema: "Mto huu (96) ulipeleka majivu yake
hadi Avon, Avon hadi Severn, Severn hadi katika bahari nyembamba, halafu katika bahari kuu. Kwa hiyo
majivu ya Wycliffe ni nembo ya mafundisho yake, ambayo sasa yamesambaa ulimwenguni kote." 37 Adui
zake hawakugundua kuhusu matokeo ya kitendo chao kiovu.
Ni kupitia maandishi ya Wycliffe kwamba John Huss, wa Bohemia, aliongozwa kuyakataa makosa mengi
ya Roma na kuingia katika kazi ya matengenezo. Katika karne hizi mbili, mbegu ya ukweli ilipandwa kwa
kusambaa katika mtawanyiko mkubwa. Kutoka Bohemia kazi ilitawanyika mpaka sehemu nyingine.
Mawazo ya watu yaligeuzwa na kuelekezwa kwa neno la Mungu lililosahaulika kwa muda mrefu. Mkono
wa Mungu ulikuwa unaiandaa njia kwa ajili ya Matengenezo Makuu.

37
T. Fuller, Church History of Britain, b. 4, sec. 2, par. 54

52
Sura ya 6
HUSS NA JEROME
Injili ilikuwa imeshapandwa Bohemia hata mapema mnamo karne ya tisa. Biblia ilitafsiriwa katika lugha
za wenyeji, na ibada ya hadhara ilikuwa ikifanyika. Lakini kadiri nguvu ya papa ilivyoongezeka, ndivyo
neno la Mungu lilivyozuiliwa. Gregory VII, aliyekuwa ameelekea katika upande wa kuheshimu kiburi cha
wafalme, hakuwa nyuma kuwafanya watu kuwa watumwa, na kwa hiyo amri ilitolewa ya kupiga
marufuku ibada zote za hadhara katika lugha ya Wabohemia. Papa alitangaza eti "ilimpendeza
Mwenyezi kwamba ibada isherehekewe katika lugha isiyojulikana, na kwamba maovu mengi na uasi
vimekuja kwa sababu ya kuacha kuzingatia kanuni hiyo." 38 Kwa hiyo Roma ilitoa tamko kwamba lazima
nuru ya neno la Mungu izimwe na watu wafungiwe katika giza. Lakini Mbingu ilikuwa imeleta mawakala
wengine ili kulihifadhi kanisa. Wengi wa Wawaldensi na Waalbigensi, waliokimbia mateso kutoka kwao
Ufaransa na Italia, walikuja Bohemia. Ingawa hawakudiriki kufundisha waziwazi, walifanya kazi kwa siri.
Kwa hiyo imani ya kweli ilihifadhiwa kutoka karne hadi karne.
Kabla ya siku za Huss kulikuwa na watu huko Bohemia walioinuka na kupinga waziwazi madanganyo
katika kanisa na ufisadi wa watu. Kazi zao ziliibua hisia za wengi. Hofu ya watawala iliamshwa, na
mateso yalifunguliwa dhidi ya wanafunzi wa injili. (98) Wakiwa wamefukuzwa na kwenda kuabudia
misituni na milimani, waliwindwa na askari, na wengi waliuawa. Baada ya muda iliamriwa kwamba wote
walioachana na ibada ya Kirumi wachomwe moto. Hata kama Wakristo waliyatoa maisha yao hata kufa,
walitazamia ushindi wa kazi yao baadaye. Mmoja wa wale “waliofundisha kwamba wokovu ulikuwa
unapatikana tu kwa njia ya imani katika Mwokozi aliyesulibiwa" alisema hivi wakati akiwa anakufa:
"Hasira ya maadui dhidi ya ukweli inaendelea sasa dhidi yetu, lakini haitakuwa hivyo milele; atainuka
mtu miongoni mwa watu wa kawaida, pasipo upanga wala mamlaka, nao hawatakuwa na uwezo wa
kumshinda." 39 Wakati wa Luther ulikuwa bado uko mbali; lakini tayari mtu mmoja alikuwa anaibuka,
ambaye ushuhuda wake ungeshangaza mataifa.
John Huss alizaliwa katika nyumba ya hali ya chini, na aliachwa yatima mapema baada ya kifo cha baba
yake. Mama yake alikuwa mtu wa dini, na alichukulia elimu na kumcha Mungu kama mali za thamani
kuliko vyote, na hivyo alikuwa na nia ya kuvifanya viwe ndio urithi wa mwanawe. Huss alisoma katika
shule iliyo katika jimbo lake, halafu akaendelea katika chuo kikuu kule Prague, akiwa mwanafunzi
anayefadhiliwa. Alisindikizwa na mama yake kwenda Prague. Huku akiwa mjane na maskini, mama huyu
hakuwa na zawadi zitokanazo na mali za ulimwengu za kumpatia kijana wake, lakini walipoukaribia ule
mji, alipiga magoti pamoja na kijana huyu asiye na baba na kumwombea baraka kutoka kwa Baba wa
mbinguni. Huyu mama alijua kidogo sana kuhusu namna ambavyo ombi lake lile lingejibiwa.
Muda mfupi tu baada ya kufika chuoni, Huss alijipambanua na kuwa tofautisha na wengine kwa kufanya
kazi kwa bidii na kuonyesha maendeleo mazuri, huku maisha yake ya upole yasiyolaumiwa kitu
yakimletea heshima. Alikuwa mtiifu mwaminifu kwa Kanisa la Roma na mtafutaji wa baraka za kiroho
ambazo kanisa lilihubiri kwamba linazitoa. Wakati wa tukio la jubilii alienda kuungama; alilipa sarafu
chache alizokuwa amebaki nazo, akaingia katika utaratibu wa kitubio ili ashiriki baraka hiyo maalum
iliyoahidiwa. Baada ya kumaliza masomo yake chuoni, aliingia katika upadri, na haraka alithibitishwa

38
Wylie, b. 3, ch. 1
39
Ibid., b. 3, ch. 1
53
(99) na kuunganishwa na nyumba ya mfalme. Alifanywa kuwa profesa na baadaye kuwa mwalimu katika
chuo kikuu aliposomea. Baada ya miaka michache mtu huyu aliyesoma kwa hisani tu alikuwa amekuwa
fahari ya nchi yake, na jina lake likavuma kote Ulaya.
Ni katika medani nyingine ambako Huss alianza kazi ya matengenezo. Miaka kadhaa baada ya kupata
upadri aliteuliwa kuwa mhubiri wa kanisa dogo la Bethlehem. Mwanzilishi wa kanisa hili alikuwa
amehimiza kwamba Maandiko yahubiriwe katika lugha ya wenyeji. Licha ya upinzani wa Roma kuhusu
jambo hilo, halikuzuiwa mahali pote huko Bohemia. Lakini kulikuwa na kutojua kukubwa kuhusu Biblia
na madanganyo mengi miongoni mwa watu wa matabaka yote. Haya ni maovu ambayo Huss alipingana
nayo kwa nguvu, akisisitiza umuhimu wa neno la Mungu kama kanuni ya ukweli na usafi.
Jerome alikuwa raia wa Prague aliyetokea kuwa karibu sana na Huss. Alikuwa amerudi kutoka Uingereza
na kuja na matini ya Wycliffe. Malkia wa Uingereza, aliyekuwa mwongofu kwa mafundisho ya Wycliffe,
alikuwa binti wa mfalme wa Bohemia, na kwa ushawishi wake kazi ya Mwanamatengenezo ilisambaa
katika nchi yake. Huss alisoma maandishi hayo kwa hamu; aliamini kwamba mwandishi wa maandiko
hayo ni Mkristo wa kweli, na alivutwa kukubaliana na kile alichohubiri. Ingawa hakujua, tayari Huss
alikuwa ameingia katika njia ambayo ingemwongoza kwenda mbali na Roma.
Wakati huu wageni wawili kutoka Uingereza waliwasili Prague, watu waliojifunza, waliopokea nuru na
sasa wakija kuisambaza katika nchi hii ya mbali. Walianza harakati zao kwa kumshambulia papa wazi
wazi, wakanyamazishwa na mamlaka; lakini kwa lengo la kuacha kupoteza kusudi lao, walitafuta
harakati nyingine. Wakiwa wasanifu na wahubiri, waliendeleza maarifa yao. Walichora picha mbili
katika eneo lililo wazi kwa watu wengi. Picha moja ilionyesha kuingia kwa Yesu Yerusalemu, (100)
akiwa mnyenyekevu, amepanda juu ya mwanapunda (Mathayo 21:5), na wanafunzi wake wakimfuata
wakiwa wamevaa mavazi ya safari na miguu isiyo na viatu. Picha nyingine ilionyesha kasisi na fahari
yake – papa akiwa amevalia kanzu ya thamani kubwa na taji tatu kichwani, akiwa amepanda punda
aliyepambwa kwa ufasaha, akiwa ametanguliwa na wapiga-tarumbeta huku akifuatwa na msafara wa
makadinali na makasisi katika mpangilio wa kifahari.
Hili lilikuwa hubiri lililovuta hisia za watu wa makundi yote. Makutano walikuja kuangalia picha zile.
Hakuna aliyeshindwa kupambanua, na wengi waliguswa sana na tofauti iliyokuwepo kati ya unyenyekevu
na kujishusha kwa Kristo aliye Bwana, na kiburi na kujikweza kwa papa, aliyedai kuwa mtumishi wa
Kristo. Ghasia kubwa iliibuka Prague, na wageni wale wakaona umuhimu wa kuondoka kwa ajili ya
usalama wao. Lakini somo walilofundisha halikusahaulika. Picha zile zilileta mguso katika mawazo ya
Huss na zikamwongoza kujifunza Biblia na maandishi ya Wycliffe kwa karibu zaidi. Ingawa hakuwa tayari
bado kukubaliana na matengenezo yote yaliyofundishwa na Wycliffe, aliona bayana sura halisi ya upapa,
na kwa shauku kubwa akaanza kupinga kiburi, tamaa na madanganyo ya mfumo wa upapa.
Kutoka Bohemia nuru ilitawanyika hadi Ujerumani, kwa maana ghasia zilizokuwa katika chuo kikuu cha
Prague zilisababisha mamia ya wanafunzi kutoka Ujerumani kuacha masomo. Wengi wao walikuwa
wamepokea ujuzi wa Biblia kwa mara ya kwanza kutoka kwa Huss, nao baada ya kurudi katika nchi yao
waliisambaza injili.
Vuguvugu la kazi iliyofanyika Prague ilipelekwa Roma, na baada ya muda mfupi tu Huss aliitwa mbele ya
papa. Kutii wito huu ilikuwa kama kujiingiza katika kifo. Mfalme na malkia wa Bohemia, chuo kikuu,
jamii ya waungwana, na maafisa wa serikali waliungana kumwomba papa kwamba Huss aruhusiwe
kubaki Prague na atoe utetezi wake kupitia makamu wake. Badala ya kutoa ruhusa, papa aliendelea na
shauri lile na kumhukumu Huss, halafu akatangaza kuwa mji wa Prague uko chini ya zuio la kutengwa
kama karipio.
54
(101) Katika zama zile, adhabu hii ilipotajwa ilikuwa ni jambo la kutia hofu na mshtuko. Sherehe
ambazo ziliandamana na jambo hilo zilielekea kukomesha uasi wa watu mahali ambapo papa alionekana
kama mwakilishi wa Mungu mwenyewe, anayeshikilia funguo za mbinguni na za kuzimu, na mwenye
uwezo wa kutoa maamuzi kuhusu jambo lolote, liwe la maisha ya kawaida au ya kiroho. Iliaminiwa
kwamba malango ya mbinguni hufungwa kwa eneo linalokuwa katika karipio la kutengwa; kama
haijampendeza papa kuondoa kifungo alichoweka waliokufa walijulikana kwamba wamefungiwa mbali
na makao ya raha. Katika janga hili, huduma zote za kidini zilisimamishwa katika eneo hilo. Makanisa
yalifungwa. Ndoa zilisherehekewa katika sehemu za makaburi ya kanisa. Waliokufa hawakuzikwa katika
viwanja vitakatifu vya maziko, walizikwa katika makorongo au shambani pasipo na taratibu za ibada.
Kwa hiyo hatua hizi zilichochea fikra, Roma ikijitahidi kutawala dhamiri za watu.
Mji wa Prague ulijawa na fujo. Watu wengi walimlaumu Huss kwamba ndiye sababu ya majanga
yaliyokuwa yanawapata, hivyo wakataka akabiliwe na adhabu ya Roma. Ili kutuliza dhoruba,
Mwanamatengenezo huyo aliondoka na kwenda katika kijiji cha nyumbani kwao. Akiandika kwa rafiki
zake aliowaacha Prague, alisema: "Kama nimeondoka miongoni mwenu, ni kwa ajili ya kufuata amri na
mfano wa Yesu Kristo, ili kutoa nafasi kwa yeye mwenye mawazo maovu kujitwika hukumu ya milele, na
ili nisiwe mcha-Mungu anayesababisha maumivu na mateso. Nimejitenga pia kwa kutambua kwamba
makasisi wasiomcha Mungu wanaweza kuendelea kuzuia kwa muda mrefu kuhubiriwa kwa neno la Mungu
miongoni mwenu; lakini sijatoka kwenu ili kuukana ukweli wa Mungu, ambao kwa ajili yake, kwa
msaada wa Mungu, niko tayari kufa." 40 Huss hakukoma katika kazi yake, bali alisafiri katika maeneo
yanayozunguka sehemu alipo, akihubiri kwa makusanyiko ya watu waliopenda. Kwa hiyo hatua
iliyochukuliwa na papa kuzuia injili ilisababisha kuisambaza zaidi. "Hatuwezi kutenda neno lolote
kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli." 2 Wakorintho 13:8.
(102) "Mawazo ya Huss, katika hatua hii ya utumishi wake, yalionekana kuwa na mgogoro. Ingawa kanisa
lilikuwa linapanga kumtiisha kwa nguvu, hakuliachia mamlaka yote. Kwake, Kanisa la Roma lilikuwa
bado ni mke wa Kristo, na papa alikuwa ni mwakilishi wa Mungu. Kitu ambacho Huss alikuwa
anapambana nacho ni matumizi mabaya ya mamlaka, si mfumo wenyewe. Jambo hili lilileta mgogoro
mkubwa kati ya uhakika wa kile alichoelewa na madai ya dhamiri yake. Ikiwa mamlaka ilikuwa ya haki
na kamilifu, kama alivyoamini, ilikuwaje basi ashawishike kuacha kuitii? Aliona kwamba kutii ni kufanya
dhambi; lakini kwa nini kutii mamlaka kamilifu ya kanisa liwe tatizo? Hili lilikuwa tatizo ambalo
hakuweza kutatua; jambo hili liliendelea kumpa wasiwasi kila wakati. Makadirio ya karibu ya suluhisho
aliloona ni kwamba tatizo la makuhani wa kanisa kutenda maovu na kutumia mamlaka yao halali
kufanya mambo yasiyo halali, kama ilivyokuwa mnamo siku za Mwokozi, lilijitokeza tena. Hili lilimfanya
afuate mwongozo wake mwenyewe, na kuwahubiri wengine kwa ule wa kwao, mafundisho toka katika
Maandiko, ili yaweze kutawala dhamiri; kwa maneno mengine, kwamba Mungu anasema nini katika
Biblia, na siyo kanisa linasema nini kupitia makasisi, huo ndio mwongozo mkamilifu." 41
Baada ya muda, wakati vuguvugu lilipopoa huko Prague, Huss alirudi katika kanisa lake la Bethlehem na
kuendelea kuhubiri neno la Mungu kwa hamu na ujasiri. Adui zake walikuwa bado wameshika hatamu na
wakiwa na nguvu, lakini malkia na wengi wa jamii ya waungwana walikuwa rafiki zake, na idadi kubwa
ya watu walikuwa katika upande wake. Mafundisho yake safi yanayoinua na maisha yake matakatifu
vikilinganishwa na imani za uongo zilizofundishwa na wale wahubirio dini ya Kirumi, na matendo yao ya
uovu na unafiki, viliwaonyesha watu wengi kwamba kuwa katika upande wake ni heshima kubwa.

40
Bonnechose, The Reformers Before the Reformation, vol. 1, p. 87
41
Wylie, b. 3, ch. 2
55
Hapa Huss alikuwa amesimama kazini peke yake; lakini sasa Jerome, ambaye alipokuwa Uingereza
alipokea mafundisho ya Wycliffe, alijiunga katika kazi ya matengenezo. Hawa wawili (103) waliungana
katika maisha, na hata kwa kifo wasingegawanyika. Jerome alikuwa amejaliwa zaidi uwezo mkubwa wa
akili, ushawishi, na wepesi wa kujifunza – vipaji vinavyopendwa sana; lakini katika sifa zinazohusiana na
nguvu halisi za tabia, Huss alikuwa juu. Maamuzi yake ya pole yalisaidia kupoza roho ya maamuzi ya
haraka-haraka ya Jerome, ambaye, kwa unyenyekevu wa kweli alikuwa na mtazamo wa kutegemea
kustahili kwake kama kiongozi cha maamuzi yake. Chini ya muunganiko wa kazi zao matengenezo
yalisambazwa haraka.
Mungu aliruhusu nuru kubwa imulike katika mawazo ya watu hawa waliochaguliwa, akifunua kwao
makosa mengi ya Roma; lakini hawakupokea nuru yote ambayo ingetolewa kwa ulimwengu. Kupitia
watumishi wake hawa, Mungu alikuwa anawaongoza watu wake kutoka katika giza la mafundisho ya
Kirumi; lakini kulikuwa na vikwazo vingi ambavyo wangekumbana navyo; aliwaongoza hatua kwa hatua
kulingana na uwezo wao. Hawakuwa tayari kupokea ujumbe wote kwa wakati mmoja. Kama ilivyo kwa
mwanga wa jua la mchana machoni mwa watu ambao wamekaa gizani kwa muda mrefu, kama
ingetokea, ndivyo ambavyo ingekuwa; ujumbe wote ungewafanya wageuke nyuma na kuukimbia. Kwa
hiyo aliufunua kidogo kidogo kwa viongozi, kadiri ambavyo ingewezekana watu kuupokea. Kutoka karne
hadi karne, watumishi wengine waaminifu wangefuata, kuwaongoza watu katika safari ndefu ya
matengenezo.
Mgawanyiko ndani ya kanisa bado uliendelea. Mapapa watatu walikuwa sasa wanagombania madaraka,
na mapambano yao yaliujaza Ukristo wote vitendo vya uhalifu na vurugu. Pasipo kutosheka na
machukizo hayo yaliyokuwepo, waliamua kutumia silaha. Kila mmoja alisukumwa kununua silaha za vita
na kukusanya askari. Ili kupata fedha ya kununulia vitu hivi, zawadi, vyeo na baraka za kanisa vilitolewa
kwa kulipiwa pesa. 42 Makasisi pia, wakiwaiga wakubwa zao, waliazimia kupigana ili kuwatiisha
wapinzani wao na kuimarisha nguvu zao. Kwa nguvu zilizoongezeka siku hadi siku, Huss aliunguruma
kupinga machukizo yaliyovumiliwa katika mwavuli wa dini; na watu waliwalaumu viongozi wa Roma
wazi wazi kama sababu ya mabaya yaliyokuwa yakiipata jamii ya Wakristo.
(104) Kwa mara nyingine mji wa Prague ulionekana kuwa katika mgogoro wa kumwaga damu. Kama
ilivyokuwa katika zama za zamani, mtumishi wa Mungu huyu alishtakiwa kwamba ndiye "anayetaabisha
Israeli." 1 Wafalme 18:17. Mji ukaangukia tena chini ya karipio la kutengwa, na Huss akakimbilia kijijini
kwake. Ule ushuhuda uliosambazwa kutokea katika kanisa lake pendwa la Bethlehem ulisitishwa.
Alikuwa aitangaze sasa katika hatua pana zaidi, kwa Wakristo wa ulimwengu wote, kabla ya kuyatoa
maisha yake kama shahidi wa ukweli.
Ili kuponya maovu yaliyokuwa yakiitafuna Ulaya, kikao cha baraza kiliitishwa ili kukaa huko Constance.
Kwa matakwa ya mfalme Sigismund, baraza liliitishwa na mmoja wa mapapa watatu wanaogombana,
John XXIII. Madai ya baraza yalikuwa mbali na matarajio ya Papa John, ambaye tabia na sera yake
havikuweza kushawishi upelelezi, hata kwa kufanywa na maaskofu waliokuwa watovu wa maadili kama
walivyokuwa wana-kanisa wa wakati huo. Hata hivyo hakuthubutu kupinga matakwa ya Sigismund. 43
Makusudi makuu ya baraza hili ilikuwa ni kutibu mparanganyiko uliokuwa ndani ya kanisa na kung’oa
mzizi wa uasi. Kwa hiyo mapapa wawili wanaopingana waliitwa kujitetea mbele ya baraza, pamoja pia
na mpandikizi kiongozi wa mawazo mapya, John Huss. Hao wawili wa kwanza, wakionyesha kujali
usalama wao, hawakuhudhuria wao wenyewe, bali waliwakilishwa na wajumbe wao. Akidhaniwa

42
Angalia nyongeza ya maelezo mwishoni
43
Angalia Kiambatanisho
56
kwamba ndiye aliyeitisha baraza, Papa John alikuja barazani akiwa na mashaka mengi, akishuku
kwamba mfalme ana kusudi la siri la kumwondoa madarakani, na akiogopa kuwajibishwa kwa mabaya
yote yaliyogubika kiti cha upapa, pamoja na uhalifu wote uliopo. Lakini aliingia katika mji wa Constance
kwa mandhari kubwa, akiambatana na viongozi wa kanisa wa ngazi za juu sana na wakifuatiwa na
msururu wa watumishi. Watumishi na wenye heshima wote katika mji, pamoja na makutano makubwa
ya raia, walitoka na kwenda kumlaki. Juu ya kichwa chake kulikuwa na mwamvuli wa dhahabu,
ukibebwa na wanne miongoni mwa mahakimu wakuu. Mwenyeji alipelekwa mbele yake, na mavazi ya
kitajiri ya makadinali na waungwana yalifanya onyesho kubwa la adhama.
Muda mfupi tu msafiri mwingine alikuwa anakaribia Constance. Huss alielewa hatari iliyomtisha. (105)
Aliachana na rafiki zake kama vile hatakutana nao tena, na alienda katika safari yake kama vile
inampeleka katika kifo. Licha ya kwamba alikuwa amepata hati ya usalama ya kusafiria toka kwa
mfalme wa Bohemia, na nyingine kutoka kwa mfalme Sigismund, aliweka mipango yote vizuri akijua
huenda akapatwa na kifo.
Katika barua yake aliyowaandikia rafiki zake alisema: "Ndugu zangu, . . . Ninaondoka nikiwa na hati ya
usalama ya kusafiria toka kwa mfalme nikienda kukutana na idadi kubwa ya adui wenye mwili wa kufa. .
. . Namwachia yote Mungu mwenye nguvu zote, katika Mwokozi wangu, naamini kwamba atasikiliza
maombi yenu ya imani, ili kwamba aingize ukweli na hekima yake katika kinywa changu; ili ya kwamba
niwapinge; na aniunganishe na Roho wake Mtakatifu ili aniimarishe katika kweli, nipate kusimama kwa
ujasiri katika majaribu, gereza, na hata ikilazimu, kifo cha kikatili. Yesu Kristo aliteseka kwa ajili ya
wale aliowapenda; kwa nini tushangazwe ya kwamba ametuachia kielelezo, ili sisi nasi tustahimili
mambo yote kwa ajili ya wokovu wetu? Yeye ni Mungu, na sisi ni viumbe wake; Yeye ni Bwana, nasi ni
watumishi wake; Yeye ni Bwana wa ulimwengu, na sisi ni wa kufa tu – lakini bado aliteseka! Kwa nini
nasi pia tusiteseke, hasa pale ambapo mateso ni kwa ajili ya kutusafisha? Kwa hiyo, wapendwa, ikiwa
kifo changu kitachangia katika kumtukuza, ombeni ya kwamba kije haraka, na ya kwamba aniwezeshe
kustahimili yote kwa uaminifu. Lakini ikiwa vema zaidi kwangu kurejea miongoni mwenu, hebu
tumwombe Mungu ya kwamba nirejee bila tatizo – yaani, kwamba nisiache ukweli wa injili hata ulio
mdogo, kusudi niwaachie ndugu zangu kielelezo bora. Kwa hiyo, huenda hamtaniona uso wangu tena
Prague; lakini ikiwa mapenzi ya Mungu mweza wa yote yatanirejesha kwenu, hebu na tusonge mbele
tukiwa na mioyo imara zaidi katika kuijua na kuipenda sheria yake." 44
Katika barua yake nyingine kwa padri aliyekuwa amekuwa mwanafunzi wa injili, Huss aliongea kwa
unyenyekevu wa kina kuhusu makosa yake, akijilaumu mwenyewe kwa kujiingiza katika anasa za (106)
kuvaa mavazi ya kifahari na kupoteza muda mwingi katika sanaa za mchezo-mchezo. Halafu akaongeza
tahadhari hizi zenye mguso: "Hebu utukufu wa Mungu na wokovu wa roho ujaze mawazo yako, na siyo
mali za kifahari. Jihadhari na tabia ya kupamba nyumba yako kuliko roho yako; na, zaidi ya yote,
chunga sana vyumba vya ndani ya roho yako. Uwe mwadilifu na mnyenyekevu kwa maskini, na usitumie
mali yako kwa kufanya karamu. Usipotengeneza maisha yako na kuachana na maisha ya anasa,
ninaogopa kwamba utawajibishwa vikali, kama mimi mwenyewe. . . . Unafahamu mafundisho yangu,
kwa kuwa umepokea mafundisho yangu tangu utoto wako; kwa hiyo haina maana kukuandikia tena
zaidi. Lakini nakusihi sana, kwa rehema za Bwana wetu, usiniige katika lolote kati ya majivuno ambayo

44
Bonnechose, vol. 1, pp. 147, 148

57
umeniona nikianguka kwayo…" Kwenye karatasi aliyofunikia barua yake aliongeza hivi: "Nakusihi sana,
rafiki yangu, usifungue barua hii mpaka utakapopata uhakika kwamba nimekufa." 45
Safarini mwake, kila mahali aliona ushahidi wa kusambaa kwa mafundisho yake na heshima iliyotolewa
kwa kazi zake. Watu walitafuta kukutana naye, na katika baadhi ya miji, mahakimu walikuwa naye
mitaani.
Alipofika Constance, Huss alipewa uhuru wote. Kwenye ile hati ya usalama wa safari aliopewa na
mfalme papa alimwongezea uhakika wa usalama wake binafsi. Lakini, kwa kukiuka maneno yake ya
ahadi ya dhati, Mwanamatengenezo huyu alitiwa nguvuni kwa amri ya papa na makadinali, na kutupwa
katika gereza la chini ya ardhi. Baadaye alihamishwa na kupelekwa katika ngome ng’ambo ya Mto Rhine
ambako alihifadhiwa kama mfungwa. Papa alinufaika kidogo sana na udanganyifu wake, maana na yeye
baadaye alifikishwa katika gereza hilo hilo. 46 Mbele ya baraza, alikuwa amepatikana na hatia ya kuwa
mzizi wa uhalifu, licha ya mauaji na uzinzi, "dhambi ambazo hazifai kutajwa." Baraza lilitamka hivyo, na
yeye akanyang’anywa kofia yake na kutupwa gerezani. Wapinzani wa papa nao pia waliondolewa,
akachaguliwa papa mwingine.
(107) Ingawa papa mwenyewe alikutwa na makosa makubwa kuliko yale ya Huss aliyosema kuhusu
makasisi, madai yake ya kufanya matengenezo, lakini baraza hilo hilo lililomshusha papa ndilo
lililotangulia kumkandamiza Mwanamatengenezo huyu. Kufungwa kwa Huss kulisababisha hasira kubwa
kwa watu wa Bohemia. Jamii ya waungwana wenye ushawishi walionyesha upinzani kwa baraza kuhusu
walivyomtendea Huss kwa hasira. Mfalme, ambaye hakupendezwa na ukiukwaji wa hati ya usalama ya
kusafiria aliyotoa kwa Huss, alipinga mwenendo wa baraza dhidi ya Huss. Lakini adui wa Huss walikuwa
na chuki sana na walikuwa wamedhamiria. Walimtaka mfalme aonyeshe upendeleo, awe na hofu kwa
kanisa. Walileta hoja ndefu za kuthibitisha kwamba "imani haipaswi kuwa pamoja na uasi, wala mtu
anayeshukiwa kuwa muasi, hata kama analindwa na hati za usalama za wafalme." 47 Kwa hiyo
wakashinda.
Akiwa amedhoofishwa na maradhi na kifungo, - kwa kuwa hewa chafu ya gereza la chini ya ardhi
ilimsababishia homa ambayo ilikaribia kukatisha maisha yake, - hatimaye Huss aliletwa mbele ya
baraza. Akiwa amefungwa pingu nzito, alisimama mbele ya mfalme, ambaye heshima na imani yake
vilikuwa vimempa hati ya usalama. Kwa wakati wote mrefu wa kuhojiwa kwake aliusimamia ukweli, na
mbele ya uwepo wa viongozi wa juu wa kanisa na wa serikali alitamka kwa uaminifu akipinga ufisadi wa
kanisa. Alipoulizwa achague moja kukana maneno yake au kufa, alikubali kufa kama shujaa wa imani.
Rehema ya Mungu ilimbidisha. Kwa majuma aliyokuwa gerezani kabla ya hukumu, amani ya mbinguni
ilijaza moyo wake. Akimwandikia rafiki yake alisema: "Naandika barua hii nikiwa gerezani, tena kwa
mkono wangu ambao umefungwa pingu, nikisubiri adhabu yangu ya kifo kesho. . . . Wakati ambapo, kwa
msaada wa Yesu Kristo, tutaonana tena katika maisha yajayo yaliyo matamu na ya amani, utajifunza
jinsi Mungu wa neema alivyojidhihirisha kwangu, na namna ambavyo amenisaidia katika safari ya
kuhojiwa na kujaribiwa." 48 (108)
Katika upweke wa gereza la chini ya ardhi, aliona mbele ushindi wa imani ya kweli. Akirudi kwa ndoto
katika kanisa lake la Prague alikokuwa ameihubiri injili, alimwona papa na makasisi wake wakizifuta

45
Ibid., vol. 1, pp. 148, 149
46
Ibid., vol. 1, p. 247.
47
Jacques Lenfant, History of the Council of Constance, vol. 1, p. 516
48
Bonnechose, vol. 2, p. 67
58
picha za Yesu alizokuwa amechora kwenye kuta za kanisa. "Maono haya yalimshtua sana; lakini siku
iliyofuata aliona wachoraji wengi sana wakizirejesha picha zile tena kwa wingi na kwa rangi zing’aazo
zaidi. Walipokuwa wamemaliza kazi yao, wachoraji hawa, waliokuwa wamezungukwa na makutano
makubwa, walisema, 'Sasa mapapa na makasisi na waje; kamwe hawataweza kuzifuta tena!'"
Mwanamatengenezo akisimulia ndoto yake alisema: "Nashikilia hili kwa hakika, kwamba picha ya Yesu
haitafutika kamwe. Wametamani kuiharibu, lakini itachorwa upya katika mioyo yote, tena kupitia
wahubiri walio bora zaidi kuliko mimi." 49
Huss aliletwa barazani mara ya mwisho. Lilikuwa baraza kubwa na lililokamilika – mfalme, wana wa
mfalme, viongozi wasaidizi wa mfalme, makadinali, makasisi, mapadri, na umati wa watu waliokuja
kushuhudia tukio la siku hiyo. Watu kutoka katika maeneo yote ya Ukristo walikuwa wamekusanyika
kushuhudia kafara kubwa ya kwanza katika safari ndefu ya mapambano ya kutafuta uhuru wa dhamiri.
Akiwa ameitwa kwa ajili ya uamuzi wake wa mwisho, Huss alitangaza kukataa kufuta maneno yake, na
akimwangalia mfalme ambaye ahadi za maneno yake zilikuwa zimekiukwa bila aibu, alisema: "Niliazimia
kufika mbele ya baraza, kwa kuamua mimi mwenyewe, nikiwa nalindwa na umma na imani ya mfalme
ambaye yupo hapa." 50 Mwale wa kina ulifika usoni mwa Sigismund kadiri macho ya wote waliokuwepo
yalivyomwelekea.
Baada ya adhabu yake kutajwa, sherehe ya kumshusha wadhifa na hadhi ilianza. Makasisi walimvisha
vazi la kanzu rasmi kwa tukio hilo, naye alipoipokea ile kanzu, alisema: "Bwana wetu Yesu Kristo
alivalishwa kanzu nyeupe, kwa namna ya (109) dhihaka, wakati Herode alipoamuru apelekwe kwa
Pilato." 51 Alipotakiwa tena kuacha msimamo wake na kuomba radhi, alijibu, huku akiwageukia watu:
"Nitazitazama mbingu kwa uso upi? Nitawatazamaje makutano ambao nimewahubiri injili safi? Hapana;
Najali wokovu wao kuliko mwili huu ulio maskini, ambao sasa umeamuriwa kwa mauti." Mavazi ya
heshima yalianza kuondolewa moja baada ya jingine, kila kasisi akitamka maneno ya laana kadiri
alivyofanya sehemu yake katika sherehe hii. Hatimaye waliweka kichwani pake kofia ya msonge ya
karatasi, ambayo ilikuwa imechorwa michoro mibaya ya mashetani, na neno 'Archheretic' (Mzushi mkuu)
katika upande wa mbele. Yeye alisema, “Kwa furaha nitaivaa taji hii ya aibu kwa ajili yako, Ee Yesu,
ambaye ulivaa taji ya miiba kwa ajili yangu.”
Alipokuwa amekwisha kupambwa hivyo, “viongozi wa kanisa wakatamka, 'Sasa roho yako tunamkabidhi
yule mwovu.' Na John Huss akasema, huku akiinua macho yake mbinguni, 'Naikabidhi roho yangu
mikononi mwako, Ee Yesu Bwana, kwa maana umenikomboa.'" 52
Sasa alipelekwa kwa mamlaka zisizo za dini na akapelekwa mahali pa kutekelezea adhabu yake. Msafara
mkubwa ulifuata, mamia ya watu walio na silaha, mapadri na makasisi wakiwa katika mavazi yao ya
gharama kubwa, pamoja na wakazi wa mji wa Constance. Alipokuwa amefungwa barabara kwenye
nguzo ya kuchomea moto, na kila kitu kikiwa tayari kwa ajili ya moto kuwashwa, mfia-dini huyu
alitakiwa tena kujiponya nafsi kwa kukiri makosa yake. "Makosa gani ambayo natakiwa kukiri?" Huss
alisema, "Mimi sijui kosa lolote. Namwita Mungu ashuhudie kwamba yote niliyoandika na kuhubiri
yalikuwa kwa ajili ya kuokoa roho kutoka dhambini na upotofuni; na, kwa hiyo, kwa furaha nathibitisha
kwa damu yangu ukweli ambao nimeandika na kuuhubiri." 53 Miale ya moto ilipowashwa mwilini mwake,

49
D'Aubigne, b. 1, ch. 6
50
Bonnechose, vol. 2, p. 84
51
Ibid., vol. 2, p. 86
52
Wylie, b. 3, ch. 7
53
Ibid., b. 3, ch. 7
59
alianza kuimba, "Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu," na aliendelea hivyo mpaka sauti yake ilipokoma
milele.
Hata adui zake walishangazwa na ushujaa wake. Mwanaharakati wa upapa aliyekuwa na huruma, alipata
kueleza kifo cha kishujaa cha Huss, na cha (110) Jerome, aliyekufa baadaye, kwa kusema: "Wote
walijitwika mawazo yale yale wakati saa yao ya mwisho ilipokaribia. Walijiandaa kwa ajili ya moto
kama vile walikuwa wanakwenda kwenye karamu ya harusi. Hawakutoa kilio chochote cha maumivu.
Moto ulipowaka kwao walianza kuimba nyimbo; na nguvu ya mwako wa moto haikuzuia nyimbo zao." 54
Pindi mwili wa Huss ulipoteketea wote, majivu yake, pamoja na udongo uliokuwa chini yake,
vilikusanywa na kutupwa katika Mto Rhine, vikatiririshwa mpaka baharini. Watesi wake walijidanganya
kwa kujigamba kwamba kwa kufanya hivyo wameng’oa ukweli alioufundisha. Hawakuweza kuota
kwamba majivu yaliyobebwa siku ile hadi baharini yalikuwa mbegu iliyotawanyika katika sehemu zote
za dunia; kwamba siku moja ingezaa matunda tele kama ushuhuda wa ukweli katika nchi ambayo
ilikuwa haijajulikana. Sauti iliyosikika katika ukumbi wa baraza la Constance iliacha miangwi ambayo
ingesikika katika vizazi vyote ambavyo vingefuata. Huss hakuwepo tena, lakini ukweli aliokufa kwa ajili
yake usingeangamizwa kamwe. Mfano wake wa imani na kusimama imara kungetia moyo watu wengi
kusimama imara kwa ajili ya kweli, mbele ya mateso na kifo. Kuuawa kwake kuliudhihirishia ulimwengu
ukatili wa Roma. Ingawa hawakujua, maadui wa ukweli walikuwa wanazidi kuiendeleza kazi ambayo
walifikiri wanaiharibu.
Bado nguzo nyingine ya kuchomea moto ilikuwa isimamishwe tena Constance. Lazima damu ya shahidi
mwingine iushuhudie ukweli. Jerome, aliyeagana na Husss alipokuwa anakwenda mbele ya baraza,
alikuwa amemtia moyo na nguvu, akimwahidi kwamba ikiwa angeangukia katika shida yoyote yeye
angeruka haraka na kumpa msaada. Aliposikia habari ya kifungo cha Mwanamatengenezo, mwanafunzi
huyu mwaminifu alianza kujiandaa kutimiza ahadi yake. Bila kuwa na hati ya usalama ya kusafiria
aliondoka kwenda Constance, akiwa na rafiki yake mmoja. Alipofika kule alijulishwa kwamba amejileta
mwenyewe katika shida pasipo na uwezekano wa kufanya lolote kumwokoa Huss. Alikimbia kutoka
mjini, lakini alikamatwa akiwa njiani kurudi nyumbani na akarudishwa mjini akiwa amefungwa
minyororo mizito na akilindwa na kundi la askari. Alipotokea mara ya kwanza mbele (111) ya baraza ili
kujibu mashtaka yaliyoelekezwa kwake alikutana na kelele zinazosema, "Motoni kama yule! motoni!" 55
Alitupwa katika gereza la chini ya ardhi, akiwa amefungwa minyororo katika mkao ambao
ulimsababishia maumivu makubwa, na alilishwa mkate na maji. Baada ya miezi michache, ukatili wa
gerezani ulimletea Jerome ugonjwa ambao ulitishia maisha yake, na adui zake wakapunguza ukatili
kwake wakihofia kwamba kifo kinaweza kusababisha awaepuke, ingawa aliendelea kubaki gerezani.
Kifo cha Huss hakikuleta matokeo ambayo watu wa upapa walitarajia. Kukiukwa kwa hati ya usalama ya
kusafiria aliyokuwa nayo kuliibua dhoruba ya hasira, na kwa hiyo baraza liliazimia, badala ya kumchoma
Jerome kwa moto, kumlazimisha, ikiwezekana, kukana na kutengua maneno yake. Aliletwa mbele ya
baraza na kupewa nafasi ya kukiri makosa, la sivyo akabili kifo. Mwanzoni mwa kifungo chake, kifo
kingeonekana nafuu ukilinganisha na mateso ya kutisha aliyopata; lakini sasa, akiwa amedhoofishwa na
ugonjwa, kwa uchovu wa maisha ya gerezani, na mateso ya wasiwasi, akiwa ametengwa na rafiki zake,
huku akiwa amevunjwa moyo na kifo cha Huss, Jerome alikubali kusalimu amri kwa baraza. Aliahidi

54
Ibid., b. 3, ch. 7.
55
Bonnechose, vol. 1, p. 234
60
kutii imani ya Kikatoliki, na alikubali uamuzi wa baraza kulaani mafundisho ya Wycliffe na Huss,
isipokuwa tu, hata hivyo, “ukweli mtakatifu" ambao walifundisha. 56
Kwa njia hii Jerome alikuwa amenyamazisha dhamiri na kukwepa maangamizi. Lakini katika hali yake ya
upweke katika gereza aliona kile alichofanya kwa uwazi zaidi. Alitafakari msimamo na ujasiri wa Huss,
akatafakari tofauti iliyoletwa na usaliti wake wa kuikana kweli. Alifikiri kuhusu Bwana wa uungu
ambaye alikuwa ameazimia kumtumikia, na ambaye alistahimili kifo cha msalaba kwa ajili yake. Kabla
ya kukana, alikuwa amepata faraja, katika maumivu yake yote, katika kuhakikishiwa upendeleo wa
Mungu; lakini sasa majuto na mashaka viliisumbua roho yake. Alijua kwamba kusalimu amri katika
mambo mengine pia kungefuata kabla ya kuifikia amani ya Roma. Njia ambayo (112) alikuwa anaipitia
ingempeleka katika uasi kamili. Alifanya maamuzi: Asingemkana Bwana wake kwa kukwepa mateso ya
muda mfupi.
Baadaye aliletwa mbele ya baraza tena. Kusalimu amri kwake hakukuwaridhisha waamuzi wa baraza.
Kiu yao ya kutaka damu, ikihamasishwa na kifo cha Huss, ilidai wahanga wapya. Ni kwa kusalimu amri
kwa mambo yote tu ambako kungeokoa maisha ya Jerome. Lakini alikuwa ameazimia kurejesha imani
yake na kumfuata ndugu yake shujaa katika moto.
Alikutengua kule kukana na kukiri kwake kwa awali na, kama mtu anayekufa, aliomba nafasi ya
kujitetea. Wakiwa wanaogopa madhara ya maneno yake, makasisi walisisitiza kwamba kinachohitajika
ni kukubali au kukana ukweli wa mashtaka yaliyoletwa kwake. Jerome alipinga ukatili wao na kutotenda
haki. Alisema: "Mmenifunga kwa siku mia tatu na arobaini katika gereza la kutisha, katika uchafu, fujo,
maumivu, na uhitaji wa hali ya juu; halafu mnanileta nje mbele yenu, na kuwapa masikio yenu adui
zangu ambao wana miili ya kufa, mnakataa kunisikiliza … Kama kweli ninyi mna hekima, na ni nuru ya
ulimwengu, jihadharini msitende dhambi ya kukosa kutenda haki. Kwa upande wangu, mimi ni dhaifu
mwenye mwili wa kufa; maisha yangu yana thamani kidogo sana; na ninapowashawishi kuacha kutenda
isivyo haki, siongei sana kwa ajili yangu mwenyewe bali kwa ajili yenu." 57
Hatimaye ombi lake lilikubaliwa. Mbele ya waamuzi wake, Jerome alipiga magoti na kuomba Roho wa
Mungu aongoze mawazo na maneno yake, ili ya kwamba asiseme lolote lililo kinyume cha kweli au
lisilokubalika mbele za Bwana wake. Siku ile ilitimizwa kwake ahadi ya Mungu kwa wanafunzi wake:
"Mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu …. Lakini hapo watakapowapeleka,
msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema." Mathayo 10:18-20.
Maneno ya Jerome yalisababisha mshangao mkubwa, hata kwa adui zake. Kwa mwaka mzima alikuwa
(113) amehangaika gerezani, pasipokuwa na uwezo wa kusoma au hata kuona, katika maumivu
makubwa ya kimwili na ya kiakili. Hata hivyo, hoja zake zilitolewa kwa nguvu na uwazi kama vile
alikuwa amepata nafasi ya kujifunza pasipo bughudha. Aliwaelekeza wasikilizaji wake kwa orodha ndefu
ya watakatifu waliopata kuhukumiwa na waamuzi wasiofuata haki. Karibu kila kizazi kumekuwepo watu
ambao, katika nia yao ya kuinua watu wa wakati wao na kuwaletea wokovu, wamekuwa wakilaumiwa na
kukataliwa, lakini baadaye walionekana watu wanaostahili heshima. Kristo mwenyewe alishtakiwa kuwa
mhalifu katika mahakama zisizo haki.
Katika kukiri kwake kwa awali, Jerome alikuwa amekubali kwamba haki ilitendeka kwa hukumu
iliyompata Huss; sasa alitangaza kuungama kwake na kutoa ushuhuda kwa ajili ya shujaa aliyeitetea
imani hata kufa. Alisema, "Nilimjua tangu utoto wake. Alikuwa mtu mwema sana, mwenye haki na

56
Ibid, vol. 2, p. 141.
57
Ibid., vol. 2, pp. 146, 147
61
mtakatifu; alihukumiwa, licha ya kuwa mtu asiye na kosa … Nami pia – niko tayari kufa: Sitatishwa na
mateso ambayo kwa ajili yangu yameandaliwa na adui zangu na mashahidi wa uongo, ambao
watatakiwa siku moja kutoa hesabu ya matendo yao mbele za Mungu mkuu, ambaye hawezi
kudanganywa na kitu chochote." 58
Katika kueleza jinsi alivyoikana ile kweli, Jerome aliendelea kusema: "Katika dhambi zote nilizopata
kutenda tangu ujana wangu, hakuna iliyo nzito mawazoni mwangu, na kunisababishia majuto yenye
mguso mkubwa, kama hii niliyotenda katika tukio hili, nilipothibitisha hukumu potofu iliyotolewa kwa
Wycliffe, na kwa shujaa mtakatifu wa imani, John Huss, mwalimu wangu na rafiki yangu. Naam! Ninakiri
jambo hilo kutoka moyoni mwangu, nikitangaza kwa nguvu kwamba nilifanya makosa kwa kukana
mafundisho yao, kwa hofu ya kifo. Ninasihi … Mungu Mwenyezi anisamehe dhambi zangu, na hasa
dhambi hii, mbaya kuliko zote." Akigeuka kuwaelekea waamuzi wa baraza, alisema kwa ujasiri:
"Mlimhukumu Wycliffe na John Huss, si kwa sababu walitikisa mafundisho ya kanisa, lakini tu kwa kuwa
walionyesha fedheha ya kashfa iliyoanzia kwa watumishi wa kanisa – kujionyesha kwao, kiburi chao, na
maovu yote ya mapadri na makasisi. (114) Hayo waliyasema na kuyathibitisha, na ni mambo
yasiyopingika, nami pia nafikiri na kutangaza hivyo, kama wao."
Maneno yake yalikatizwa. Makasisi, wakitetemeka kwa ghadhabu, walipiga kelele wakisema: Tuna haja
gani ya kutafuta ushahidi zaidi? Tunatazama kwa macho yetu wenyewe uasi wa makusudi uliopitiliza!"
Bila hofu ya dhoruba iliyokuwa mbele yake, Jerome alihamaki: "Nini! Mnafikiri kwamba ninaogopa kufa?
Mmenishikilia kwa mwaka mzima katika gereza la kutisha, baya kuliko hata kifo chenyewe!
Mmenitendea kwa ukatili mkubwa kuliko Mturuki, Myahudi, au mpagani, na nyama yote ya mwili wangu
imekwisha na kuacha mifupa nikali bado hai; wala silalamiki, kwa kuwa maovu yaletwayo na waovu
huleta moyo mkuu na nguvu; mimi siwezi kushangazwa na ukatili huo kwa Mkristo." 59
Dhoruba ya hasira ililipuka tena, na Jerome akafurushwa haraka kuelekea gerezani. Lakini baadhi ya
wale waliokuwa barazani waliguswa na maneno yake nao wakatafuta kuponya maisha yake.
Alitembelewa na watu maarufu wa kanisa wakimtaka ajisalimishe kwa baraza. Ahadi kubwa na njema
kuliko zote zilitolewa kwake kama zawadi ikiwa angeachana na upinzani wake dhidi ya Roma. Kama vile
Bwana wake alivyofanya alipoahidiwa utukufu wa dunia hii, Jerome aliendelea kusimama imara.
Alisema: "Nihakikishieni kutoka katika Maandiko Matakatifu kwamba niko katika makosa, nami
nitaachana na msimamo huu."
"Maandiko Matakatifu! Kwani kila kitu kinapimwa kwa hayo? Alidai mmoja wa wahukumu wake. “Nani
anayeweza kuyaelewa isipokuwa kanisa limeyatafsiri?"
"Je mapokeo ya wanadamu yana thamani katika imani zaidi ya injili ya Mwokozi wetu?" alijibu Jerome.
"Paulo hakuwaasa wale aliowaandikia kuyasikiliza mapokeo ya wanadamu, bali alisema, “Someni
Maandiko.'"
"Mzushi!" huo ulikuwa mwitikio, "Najuta kuendelea kukusihi. Naona kama vile umetumwa na yule
mwovu." 60
Hukumu ilipitishwa juu yake. Alipelekwa mahali pale pale ambapo (115) Huss aliyatoa maisha yake.
Alienda akiimba njia yote, kustahimili kwake kulileta nuru ya furaha na amani. Macho yake yalielekezwa

58
Bonnechose, vol. 2, p. 151
59
Ibid., vol. 2, pp. 151-153
60
Wylie, b. 3, ch. 10.
62
kwa Kristo muda wote, na kwake kifo kilipoteza utisho. Wakati mtekelezaji wa adhabu alipopita nyuma
yake akiwa tayari kuwasha moto, mfia-dini huyu alisema: "Njoo mbele kwa kujiamini; washa moto
mbele ya uso wangu. Ningekuwa naogopa, nisingekuwa hapa."
Maneno yake ya mwisho, yaliyotamkwa wakati miale ya moto ikimwinukia, yalikuwa ni ombi. Alilia
akisema, "Bwana, Baba Mwenyezi, unirehemu, na unisamehe dhambi; kwa maana unajua kwamba
nimeipenda kweli yako." 61 Sauti yake ilikoma, lakini midomo yake iliendelea na sala. Moto ulipomaliza
kazi yake, majivu ya mfia imani huyu, na udongo uliokuwa chini yake, vilikusanywa, na kama ilivyokuwa
kwa vile vya Huss, vilitupwa katika Mto Rhine.
Hivyo ndivyo walivyoondoshwa waaminifu wa Mungu walioibeba nuru. Lakini nuru ya ukweli
waliyoihubiri – nuru ya mfano wao wa ushujaa – isingewezekana kuzimwa. Ilikuwa kama watu
wanaojaribu kurudisha nyuma jua katika njia yake ili kulizuia kuchwa na kuisha kwa siku ambayo hata
wakati ule ilikuwa imeufunukia ulimwengu.
Alichotendewa Huss kilikuwa kimewasha moto wa hasira na harara Bohemia. Ilihisiwa katika taifa lote
kwamba alifanywa muhanga wa uovu wa makasisi na usaliti wa mfalme. Alitajwa kuwa mwalimu
mwaminifu wa ukweli, na baraza lililoidhinisha kifo chake lililaumiwa kwa kuwa na hatia ya kuua.
Mafundisho yake yalipata umaarufu zaidi kuliko hata kabla. Kwa tamko la papa, ilikuwa imetangazwa
kwamba maandishi ya Wycliffe yachomwe moto. Lakini yale yaliyopona kuchomwa moto yaliletwa sasa
kutoka mafichoni na kujifunzwa yakiunganishwa na Biblia, au vipande vya Biblia vilivyoweza kupatikana,
na watu wengi wakaongozwa kuikubali imani ya matengenezo.
Wauaji wa Huss hawakuweza kukaa kimya tu wakishuhudia ushindi wa kazi ya wapinzani wao. Papa na
mfalme waliungana ili kusambaratisha harakati zile, na majeshi ya Sigismund yakafurika Bohemia. (116)
Lakini mwokoaji aliinuliwa. Ziska, ambaye muda mfupi baada ya kuanza kwa vita alipofuka macho
kabisa, lakini aliyekuwa mmoja wa makamanda wenye uwezo katika kipindi kile, alikuwa kiongozi wa
Wabohemia. Wakimtumaini Mungu na haki ya kazi yao, watu wale walihimili kukabili majeshi yenye
nguvu yaliyokuja dhidi yao. Tena na tena, mfalme aliinua majeshi mapya na kuivamia Bohemia,
yakaishia kurudishwa nyuma kwa fedheha. Wafuasi wa Huss waliinuliwa juu kuliko hofu ya kifo, na
hakuna ambacho kingesimama kuwashinda. Miaka michache baada ya vita kuanza, Ziska akafa; lakini
nafasi yake ilichukuliwa na Procopius, ambaye alikuwa mwerevu na mjuzi vile vile, na katika maeneo
fulani akiwa kiongozi mwenye uwezo zaidi.
Maadui wa Wabohemia, wakijua kwamba mpiganaji kipofu amekufa, waliuona wakati huo kama fursa
yao ya kulipiza kwa ajili ya vyote walivyopoteza. Sasa papa alitangaza mashambulizi kwa Wahusi
(Wafuasi wa Huss), kwa hiyo mvua ya majeshi ikanyesha tena Bohemia, ambako waliambulia kushindwa
vibaya. Shambulio jingine tena lilitangazwa. Katika nchi zote za kipapa za Ulaya, watu, fedha na vifaa
vya vita vilikusanywa. Makutano wengi walijisalimisha katika msimamo wa upapa, wakihakikishiwa
kwamba hatimaye Wahusi wa uasi wangefikishwa mwisho. Yakiwa na ujasiri wa kushinda, majeshi
yaliingia Bohemia. Watu waliungana kuyapinga. Majeshi ya pande mbili yalisogeleana mpaka yalipobaki
yametenganishwa na mto tu. "Wavamizi walikuwa na nguvu sana, lakini badala ya kuvuka mto na
kupambana na Wahusi waliokuwa wamewafuata, walisimama kimya wakiwaangalia." 62 Ndipo hofu ya
kimiujiza ilikuja ghafla. Bila kufanya shambulio, jeshi lile kubwa lilivunjika na kutawanyika kama vile
lilifukuzwa na nguvu isiyoonekana. Idadi kubwa ya watu waliuawa na jeshi la Wahusi, ambalo

61
Bonnechose, vol. 2, p. 168
62
Wylie, b. 3, ch. 17
63
liliwakabili wavamizi waliokuwa wakikimbia, na mali nyingi iliangukia mikononi mwa jeshi lililoshinda,
kiasi kwamba, badala ya vita kuleta umaskini kwa Wabohemia, iliwatajirisha.
Miaka michache baadaye, chini ya papa mpya, shambulio jingine lilipangwa. Kama ilivyokuwa awali,
watu, na mali vilikusanywa (117) kutoka katika nchi zote za kipapa katika Ulaya. Ahadi kubwa za
kushawishi watu kushiriki katika kazi ile zilitolewa. Msamaha kamili kwa uhalifu mkubwa uliofanywa
ulikuwa wa hakika kwa wote walioshiriki katika shambulizi. Wote waliokufa vitani waliahidiwa zawadi
kubwa mbinguni, na wale waliopona vitani walikuwa na nafasi ya kuvuna heshima na utajiri katika
mapambano. Kwa mara nyingine jeshi kubwa lilikusanywa, wakavuka mpaka na kuingia Bohemia.
Majeshi ya Wahusi yalirudi nyuma mbele ya maadui na hivyo kuwavuta wavamizi mbali sana ndani ya
nchi, wakiwapeleka kwenda mahali pa kuwasaidia kuhesabu ushindi ambao walikuwa wameshaupata
tayari. Hatimaye jeshi la Procopius liliweka kituo, na kugeuka kuwakabili wavamizi. Wakiwa
wamegundua kosa lao, sasa wavamizi walibaki katika hema lao wakisubiri mapambano yaanze.
Waliposikia tu sauti za jeshi la Wahusi lililokuwa linakuja, hata kabla halijaonekana, wavamizi
waliingiwa na hofu tena. Wana wa mfalme, makamanda, na askari wa kawaida wa jeshi la wavamizi
walitimua mbio huku na huko na kuacha zana zao. Jitihada za balozi wa papa, aliyekuwa kiongozi wa
uvamizi, hazikufanikiwa kulikusanya jeshi lake lililosambaratika. Pamoja na jitihada zake hizo, hata
yeye mwenyewe alisombwa na wimbi la askari waliokuwa wanakimbia. Kazi ilikuwa imekwisha na mali
nyingi ikaangukia mikononi mwa jeshi lililoshinda tena.
Kwa hiyo, kwa mara ya pili, jeshi lenye nguvu, lililopelekwa na mataifa yenye nguvu sana ya Ulaya,
kitovu cha ujuzi, watu wa vita, waliofundishwa na kuandaliwa kwa vita, walikimbizwa na kushindwa na
walinzi wa taifa dogo. Hapa kulikuwa na udhihirisho wa nguvu ya Mungu. Wavamizi walipigwa na hofu
isiyo ya kawaida. Yeye aliyeyashinda majeshi ya Farao katika Bahari ya Shamu, aliyeyafukuza majeshi ya
Midiani mbele ya Gideoni na askari mia tatu, ambaye alishusha majeshi yenye kiburi ya Siria katika
usiku mmoja, alikuwa tena amenyosha mkono wake kunyausha nguvu ya ukandamizaji. "Hapo waliingiwa
na hofu, mahali pasipokuwapo hofu: maana Mungu ameitawanya mifupa yake aliyekuhusuru: Umewatia
aibu, kwa sababu Mungu amewadharau." Zaburi 53:5.
(118) Hatimaye watu wa upapa, wakiwa wamekata tamaa ya kushinda kwa kutumia nguvu, waliazimia
kutumia diplomasia. Maridhiano yalifanyika, wakati walikubali kutoa uhuru wa dhamiri kwa Wabohemia,
waliwasaliti kwa mamlaka ya Roma. Wabohemia walibainisha mambo mahsusi manne kama masharti ya
amani na Roma: kuhubiri Biblia kwa uhuru; haki ya kanisa zima kwa mkate na divai wakati wa
komuniyo, na matumizi ya lugha ya wenyeji wakati wa ibada; kuwatenganisha watumishi wa kanisa
kutoka katika ofisi za mamlaka ya serikali; na, kwa habari ya uhalifu, mwenendo wa mahakama uwe
sawa kwa wote watumishi wa kanisa na watu wa kawaida. Hatimaye mamlaka ya kipapa "ilikubali
kwamba masharti ya Wahusi yakubaliwe, lakini kwamba haki ya kuyaeleza, yaani kuamua jinsi ya
kuyatekeleza, iwe katika mamlaka ya baraza, kwa maneno mengine, kwa papa na mfalme." 63 Kwa
msingi huu, mkataba uliingiwa, na Roma ikapata kwa njia ya kugeuza kile ilichoshindwa kupata kwa
vita; maana kwa kushinikiza tafsiri yake kuhusu masharti ya Wahusi, kama ilivyokuwa kwa Biblia,
iliweza kukwepesha maana yake kulingana na makusudi yake.
Sehemu kubwa ya watu wa Bohemia, wakiona kwamba wamesaliti uhuru wao, hawakukubali
makubaliano yaliyofikiwa. Upinzani na mgawanyiko viliibuka, vikasababisha fujo na umwagaji wa damu
miongoni mwao wenyewe. Katika mtafaruku huu wafuasi wa Procopius walishindwa, na uhuru wa
Bohemia ukatoweka.

63
Wylie, b. 3, ch. 18
64
Sigismund, msaliti wa Huss na Jerome, sasa alikuwa mfalme wa Bohemia, na licha ya kiapo chake cha
kudumisha haki za Wabohemia, alisonga mbele katika kuanzisha upapa. Lakini alikuwa amepata faida
ndogo tu kwa kunyenyekea kwa Roma. Kwa muda wa miaka ishirini maisha yake yalikuwa yamejawa na
kutumika na mahangaiko. Majeshi yake na hazina zake vilikuwa vimetumika katika mapambano ya muda
mrefu yasiyo na matunda; na sasa, baada ya kutawala kwa mwaka mmoja tu, alikufa, akiacha ufalme
wake katika vita ya wenyewe kwa wenyewe, na kukiachia kizazi kilichofuata jina baya.
Ghasia, vurugu na umwagaji damu viliendelea. Kwa mara nyingine majeshi ya kigeni yaliivamia
Bohemia, na upinzani wa ndani (119) uliendelea kulisumbua taifa. Wale waliosalia kuwa waaminifu kwa
injili walikabiliwa na mateso ya kumwaga damu.
Kama ilivyokuwa kwa ndugu zao wa awali, wakiingia katika mwunganiko na Roma, walikunywa uovu wa
uasi wake, wale walioshikilia imani yao ya zamani walikuwa wameunda kanisa lao tofauti, likiwa na jina
la "United Brethren." Kitendo hiki kiliibua hali ya kulaaniwa na matabaka yote. Lakini msimamo wao
haukuwezekana kutikiswa. Wakiwa wamelazimishwa kukimbilia mistuni na mapangoni, waliendelea
kukutana kusoma neno la Mungu na kuungana katika ibada.
Kupitia kwa wajumbe ambao walitumwa kwa siri katika nchi tofauti, walijifunza kwamba hapa na pale
kulikuwa na "mtawanyiko wa watu walioitii kweli, wachache katika mji huu na wachache mji ule,
wahanga wa mateso kama walivyokuwa wao; na katika milima ya Alps kulikuwa na kanisa la zamani,
lililojengwa juu ya msingi wa Maandiko, likipinga upotofu wa Roma." 64 Taarifa hii ilipokelewa kwa
furaha kubwa, na mawasiliano yalianzishwa kati yao na Wakristo Wawaldensi.
Wakiwa wamesimama imara katika injili, Wabohemia walisubiri katika usiku wa mateso yao, katika saa
ya mwisho waliendelea kugeuza macho yao kwa pambazuko kama watu waisubirio asubuhi. "Kura yao
ilipigwa katika siku za uovu, lakini . . . walikumbuka maneno ambayo kwanza yalitamkwa na Huss, na
kurudiwa na Jerome, kwamba lazima karne ipite kabla ya siku hiyo kuja. Maneno haya kwa Watabori
(Wahusi) yalikuwa kama yale ya Yusufu kwa makabila yaliyokuwa utumwani: `Nakufa, na Mungu
atawajilia kwa hakika, na kuwatoa.'" 65 "Mwisho wa kipindi cha karne ya kumi na tano ulishuhudia
ongezeko la makanisa ya Brethren la polepole lakini la hakika. Ingawa walikuwa mbali, walifurahia
utulivu. Mwanzoni mwa karne ya kumi na sita idadi ya makanisa yao ilifika mia mbili kule Bohemia na
Moravia." 66 "Masalio walipendezwa ambao, kwa kuepuka moto na upanga uharibuo, waliruhusiwa kuona
mapambazuko ya siku ile aliyoitabiri Huss." 67

64
Wylie, b. 3, ch. 19
65
Ibid., b. 3, ch. 19
66
Ezra Hall Gillett, Life and Times of John Huss, vol. 2, p. 570
67
Wylie, b. 3, ch. 19
65
Sura ya 7
LUTHER AJITENGA NA ROMA

Miongoni mwa watu walioitwa kuliongoza kanisa katika nuru ya imani safi kutoka katika giza la upapa,
Martin Luther anasimama juu zaidi. Akiwa na shauku, bidii na kujitoa, akiwa asiyejua woga wowote ila
kumwogopa Mungu, na akiwa hatambui msingi wowote wa imani ya dini isipokuwa Maandiko Matakatifu,
Luther alikuwa shujaa wa wakati wake; kupitia kwake Mungu alikamilisha kazi kubwa kwa ajili ya
matengenezo ya kanisa na ya kuuangazia ulimwengu.
Kama wapiga-mbiu wa injili wa kwanza, Luther alikua kutoka katika tabaka la kimaskini. Aliishi miaka
yake ya awali katika nyumba ya mkulima wa Kijerumani. Baba yake aliweza kumudu kulipa kwa ajili ya
elimu yake kwa kazi ya kila siku ya jasho katika uchimbaji wa madini. Alikusudia mwanawe awe
mwanasheria; lakini Mungu alikusudia kumfanya mjenzi katika hekalu lililokuwa linainuka taratibu kwa
karne kadhaa. Ugumu, uhitaji na nidhamu kali vilikuwa shule ambamo Hekima Kamilifu ilimwandaa
Luther kwa ajili ya utume muhimu wa maisha yake.
Baba yake Luther alikuwa mtu mwenye uelewa mkubwa, na mvuto wa tabia, uaminifu, imara na
asiyeyumbishwa. Alikuwa mkweli kwa kile alichokuwa na hakika nacho, bila kujali kwamba matokeo
yatakuwaje. Sifa yake hiyo ilisababisha autilie mashaka mfumo wa kitawa. Alihuzunishwa sana na hatua
ya Luther, bila ridhaa yake, kuingia katika utawa; na ilikuwa miaka miwili kabla ya baba yake kupatana
naye, lakini bado mtazamo wake uliendelea kuwa ule ule.
(121) Wazazi wa Luther walijali sana elimu na mafunzo ya watoto wao. Waliazimia kuwaelekeza katika
kumfahamu Mungu na matendo ya imani ya Kikristo. Ombi la baba yake lilipanda juu mara kwa mara
likisikika kwa mwanae huyu kwamba mtoto huyu akumbuke jina la Bwana na siku moja afanye sehemu
katika kueneza ukweli wake. Kila fursa ya kimaadili au ufahamu ambayo maisha yao ya mahangaiko
yaliwaruhusu kupata iliboreshwa na wazazi hawa. Juhudi zao zilikuwa thabiti na za uvumilivu kwa ajili
ya kuwaandaa watoto wao kwa maisha mema na yanayofaa. Kwa msimamo wao na nguvu ya tabia zao
wakati mwingine walikuwa wakali sana, lakini Mwanamatengenezo yeye, ingawa kwa kujua kwamba
kiasi fulani walikuwa katika makosa, aliona katika nidhamu yao mambo mengi ya kuenzi zaidi kuliko
yale ya kuhukumu.
Shuleni alikopelekwa wakati wa umri mdogo, Luther alitendewa kwa ukali na mabavu. Umaskini wa
wazazi wake ulikuwa mkubwa kiasi kwamba baada ya kupelekwa shule katika mji mwingine tofauti na
nyumbani alilazimika wakati mwingine kupata chakula kwa kuimba katika mlango wa nyumba moja hadi
nyingine akiombaomba, na mara nyingi alibaki na njaa. Mawazo ya huzuni na upotofu ya dini
yaliyokuwepo wakati huo yalimjaza hofu. Aliweza wakati mwingine kulala usiku akiwa na moyo wa
huzuni, kwa kutetemeka akisubiri giza linalokuja na kwa hofu ya muda wote akiwaza kuhusu Mungu
aliye mkali, anayehukumu, dikteta katili, badala ya Baba wa mbinguni mwenye ukarimu.
Lakini chini ya huku kukata tamaa kwingi na kukubwa Luther aliamua kusonga mbele katika maisha ya
viwango vya juu vya maadili na ufahamu ambavyo vilivutia nafsi yake. Alikuwa na kiu ya elimu, na
uthabiti na mwonekano wa tabia yake vilimwongoza kutaka vitu ambavyo vina matumizi ya kufaa kuliko
vya kujionyesha na vya juu juu.

66
Alipofikia umri wa miaka kumi na nane, aliingia katika Chuo Kikuu cha Erfurt, hali yake ilikuwa njema
kidogo na matarajio yake yalikuwa na mwanga zaidi kuliko miaka ya awali. Uchumi wa wazazi wake
ulikuwa umeongezeka kidogo na hivyo kuweza kumdu kumpatia msaada wa mahitaji yake. Na ushawishi
wa (122) rafiki zake wema ulipunguza kwa kiasi fulani madhara ya huzuni ya mafunzo yake ya awali.
Alijielekeza kusoma kazi za waandishi wazuri, akichota hazina za mawazo yao na kuifanya hekima ya
wenye hekima kuwa yake. Pamoja na malezi magumu aliyofanyiwa na walimu wake wa awali alikuwa
ameshatoa ahadi ya kufanya vizuri sana, na akili yake ilishawishika kuelekea huko. Akili inayokumbuka,
fikra za ubunifu, nguvu ya uwezo wa kufikiri, na utendaji usiochoka vilimweka juu miongoni mwa
wenzake. Nidhamu yake ya uelewa ilifanikisha uelewa wake na kuamsha ubongo unaofanya kazi na
umakini katika mtazamo uliomwandaa kwa ajili ya mapambano katika maisha yake.
Kumcha Bwana kulikaa ndani ya moyo wa Luther, kukimwezesha kuwa na msimamo imara na
kumwongoza katika kujinyenyekeza mbele za Mungu. Muda wote alikuwa na hisia ya kutegemea msaada
wa Mungu, na hakushindwa kuianza kila siku kwa maombi, wakati moyo wake uliomba uongozi na uwezo
kila wakati. Mara nyingi alisema, "Kuomba vema, ni nusu muhimu ya kusoma." 68
Siku moja akiwa anaangalia vitabu katika maktaba ya chuo, Luther aligundua Biblia ya Kilatini. Alikuwa
hajawahi kuona kitabu kama hicho. Wala hakujua hata habari kwamba kimeshapata kuwepo kitabu
kama hicho. Alikuwa ameshasikia kwamba kuna sehemu za injili na nyaraka, ambazo zilisomwa kwa
watu katika mihadhara ya ibada, na yeye alifikiri kwamba zile ndiyo Biblia nzima. Sasa kwa mara ya
kwanza, aliliona neno la Mungu lote. Kwa butwaa na mshangao alifungua kurasa zile takatifu; kwa
haraka haraka na moyo unaoenda mbio alijisomea yeye mwenyewe maneno ya uzima, akipumzika kwa
vituo vidogo na kusema kwa mshangao: "Natamani Mungu angenipatia kitabu kama hiki kwa ajili yangu
mwenyewe!" 69 Malaika wa mbinguni walikuwa naye, na miale ya nuru kutoka katika kiti cha enzi cha
Mungu ilifunua hazina ya ukweli katika ufahamu wake. Muda wote alikuwa ameogopa kumkosea Mungu,
lakini sasa uhalisia wa hali yake ya dhambi ulionekana kuliko kabla wa wakati huu.
(123) Hamu kubwa ya kuwa huru kutoka dhambini na kupata amani kwa Mungu vilimsukuma hatimaye
kuingia katika nyumba ya watawa na kujitoa kwa maisha ya kitawa. Hapa alitakiwa kufanya kazi ngumu
za hadhi ya chini na kuomba kutoka nyumba moja hadi nyingine. Alikuwa wa makamo ambapo heshima
na kutambuliwa vinahitajika sana, na ofisi hizi za hali ya chini zilifedhehesha hisia zake za asili; lakini
alivumilia fedheha hii, akiamini kwamba ilikuwa ya muhimu kwa sababu ya dhambi zake.
Kila muda uliopatikana usio wa kufanya kazi za kila siku aliutumia kujifunza, akijinyima usingizi na
kutumia hata muda mfupi aliopewa kwa ajili ya chakula. Zaidi ya vitu vingine vyote alivutwa na
kujifunza neno la Mungu. Alikuwa ameiona Biblia ikiwa imefungwa mnyororo penye ukuta wa nyumba ya
watawa, na akaifanyia matenganezo. Kadiri alivyohisi dhambi zaidi moyoni mwake, alitafuta kwa
matendo yake kupata msamaha na amani. Aliamua kuishi maisha makini, kwa kufunga, kukesha, na
kujitesa ili kutiisha hali yake, ambayo haikupata nafuu kutokana na maisha ya kitawa. Alijisikia kukosa
kafara ya kumpa usafi wa moyo ambao ungemwezesha kukubalika mbele za Mungu. Baadaye alisema,
"Nilikuwa mtawa mtiifu na kufuata taratibu sana kwa namna ambayo siwezi kueleza. Ikiwa kweli mtawa
angeipata mbingu kwa kazi zake za kitawa, mimi ningekuwa nimeistahili. . . . Kama ingeendelea zaidi,
ningeendelea na udhalilishaji wangu ule hadi kaburini." 70Kama matokeo ya nidhamu hii ya maumivu

68
D'Aubigne, b. 2, ch. 2
69
Ibid., b. 2, ch. 2
70
Ibid., b. 2, ch. 3
67
alipoteza nguvu na kupata matatizo ya mshtuko, kutokana na madhara ambayo hakupona kabisa. Lakini
pamoja na jitihada zote nafsi yake haikupata ahueni. Hatimaye alifika mahali pa kukata tamaa.
Pindi ilipooanekana kana kwamba Luther amepoteza kila kitu, Mungu alimwinulia rafiki aliye msaada.
Staupitz alimfungulia neno la Mungu na kumwongoza katika kuacha kujiangalia yeye mwenyewe,
akimshauri kuacha kuwazia adhabu yake kwa kuvunja sheria ya Mungu, amwangalie Yesu, aliye Mwokozi
anayesamehe dhambi. "Badala ya kujitesa wewe mwenyewe kwa (124) ajili ya dhambi zako, jitupe
mikononi mwa Mkombozi. Mwamini yeye, katika haki ya maisha yake, katika upatanisho wa kifo chake.
... Msikilize Mwana wa Mungu. Yeye alifanyika mwanadamu kusudi akupe uhakika wa upendo wa
Mungu." "Mpende yeye aliyekupenda kwanza." 71 Hivi ndivyo alivyosema mjumbe huyu wa neema.
Maneno yake yalikuwa na mguso wa kina katika mawazo ya Luther. Baada ya kupambana na makosa kwa
muda mrefu, aliwezeshwa kuelewa ukweli, na amani ilimjia katika moyo wake uliokuwa katika
usumbufu.
Luther alitawazwa kuwa padri na akaitwa kutoka katika nyumba ya utawa kwenda kuwa profesa katika
Chuo Kikuu cha Wittenberg. Hapa alijielekeza katika kujifunza Maandiko katika lugha za asili. Alianza
kufundisha Biblia katika chuo; na kitabu cha Zaburi, Injili na Nyaraka vilifunguliwa katika mawazo ya
makutano ya wasikilizaji. Rafiki yake na mkuu wake, Staupitz, alimtaka kupanda mimbarani na
kulihubiri neno la Mungu. Luther alikataa, akihisi kwamba hastahili kunena kwa watu mahali pa Kristo.
Baada ya mapambano marefu ya moyoni, alikubali kufanya matakwa hayo ya rafiki yake. Tayari alikuwa
mzuri katika Maandiko, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake. Maneno yake yaliwafanya wasikilizaji
wake kutekewa, uwazi na nguvu katika kuueleza ukweli vilileta mguso katika fahamu zao, na hisia yake
iligusa mioyo yao.
Bado Luther alikuwa mtoto halisi wa kanisa la kipapa na hakuwa na wazo kwamba angeweza kuwa kitu
kingine tofauti. Kwa uongozi wa Mungu alitembelea Roma. Alisafiri kwa mguu, akilala katika nyumba za
kitawa njiani. Mara alipofika Italia alijawa na mshangao kwa sababu ya utajiri, fahari, na anasa
alivyoshuhudia. Wakiwa wamejaliwa na mapato ya kifalme, watawa waliishi katika vyumba vya fahari,
wakijivika majoho ya kitajiri na gharama kubwa, wakila katika meza za anasa. Kwa maumivu, Luther
aliona tofauti iliyopo kati ya mwonekano huu na maisha yake magumu na ya kujikana. Akili yake ilikuwa
kama vile inachanganyikiwa.
Hatimaye kwa mbali aliuona mji ule uliokuwa juu ya vilima saba. (125) Kwa mguso wa kina aliinama
mpaka chini na kusema kwa mshangao: "Ee Roma Mtakatifu, Nakusalimu!" 72 Aliuingia mji, akatembelea
makanisa, akasikiliza simulizi zilizorudiwa-rudiwa na makasisi na watawa, akatekeleza matendo yote ya
kidini yaliyotakiwa kufanywa. Aliangalia mwonekano wa mahali pale na kila mahali akajawa na
mshangao na hofu. Aliona kwamba uovu upo katika matabaka yote ya watumishi wa kanisa. Alisikia
manung’uniko miongoni mwa mapadri, na alijawa na hofu kwa namna walivyolaani, hata wakati wa
misa. Kadiri alivyojichanganya na watawa na raia alikuta vitendo vya ubadhirifu na ufisadi wa
kupindukia. Akigeuka mahali alipoweza, aliona upotofu mahali pa utakatifu. "Hakuna ambaye
angetarajia dhambi na mambo mabaya yanayofanywa Roma; kuyaamini ni mpaka yaonekane na
kusikika. Kwa hiyo ni kama vile kusema: Kama kuna kuzimu, basi Roma imejengwa juu yake: ni shimo
refu linalotoa kila aina ya dhambi" aliandika.'" 73

71
Ibid., b. 2, ch. 4
72
Ibid., b. 2, ch. 6.
73
Ibid., b. 2, ch. 6
68
Ahadi nzuri zilitolewa na papa kwa wote ambao wangepanda “ngazi za Pilato” kwa kutembelea magoti
ikisemwa kwamba ndipo aliposhuka Mwokozi wetu alipokuwa akiondoka katika ukumbi wa hukumu ya
Kirumi, na ya kwamba zilihamishwa kimiujiza kutoka Yerusalemu hadi Roma. Siku moja Luther alikuwa
akipanda ngazi hizi kama tendo la kidini, wakati ambapo sauti kama radi ilisikika ikimwambia: "Mwenye
haki ataishi kwa imani." Warumi 1:17. Alisimama kwa miguu na kuharakisha kutoka mahali pale kwa
aibu na hofu. Andiko hilo halikupoteza nguvu tena moyoni mwake. Tangu wakati ule aliona kwa uwazi
zaidi kosa la fundisho la kutegemea matendo ya mtu kwa ajili ya wokovu, na hitaji la imani ya kudumu
katika Kristo. Macho yake yalikuwa yamefunguliwa, na yasingefungwa tena, kwa uongo wa upapa.
Alipogeuza uso wake kutoka Roma ndipo alipokuwa amegeuza na moyo wake pia, na kuanzia wakati ule
utengano huo uliendelea kukua, mpaka alipokata mambo yote yanayomuunganisha na kanisa la kipapa.
Baada ya kurudi kutoka Roma, Luther alipata shahada ya elimu ya dini katika Chuo Kikuu cha
Wittenberg. Sasa alikuwa tayari kujitoa zaidi, kuliko awali, kwa ajili ya (126) Maandiko aliyoyapenda.
Alikuwa ameapa kwa dhati kujifunza neno la Mungu, si hadithi za mafundisho ya mapapa, na kulihubiri
kwa ujasiri siku zote za maisha yake. Hakuwa tena mtawa au profesa wa kawaida, bali mjumbe wa
Biblia. Alikuwa ameitwa kama mchungaji wa kondoo kulisha kundi la watu wa Mungu waliokuwa na njaa
na kiu ya ukweli. Alitangaza kwamba Wakristo hawapaswi kupokea mafundisho mengine zaidi ya yale
yaliyojengwa katika mamlaka ya Maandiko Matakatifu. Maneno haya yalipiga mahali penyewe penye
msingi wa upapa. Ni maneno yaliyokuwa na kanuni muhimu ya Matengenezo.
Luther aliona hatari ya kuinua nadharia za wanadamu juu kuliko neno la Mungu. Bila hofu, alipinga
mawazo ya wasomi na kupinga falsafa na thiolojia ambazo zilikuwa zimewaongoza watu kwa muda
mrefu. Alishambulia elimu zile na kuziona kuwa ni za uharibifu, akaazimia kugeuza mawazo ya
wasikilizaji wake kutoka katika maneno ya ghiliba ya wanafalsafa na wanathiolojia na kuyaelekeza
katika ukweli wa milele uliowekwa na manabii na mitume.
Ujumbe aliotoa kwa makutano ulikuwa wa thamani kubwa kwao, nao wakaushika. Kamwe mafundisho
kama yale hayakuwa yamepata kuangukia katika masikio yao. Mawimbi ya furaha ya upendo wa
Mwokozi, uhakika wa msamaha wa dhambi na amani kupitia damu yake ya upatanisho, vilifurahisha
mioyo yao na kuwapa tumaini la milele ndani yao. Pale Wittenberg, nuru ambayo ingesambaa katika
dunia yote iliwashwa, nuru ambayo mwangaza wake ungeongezeka zaidi kadiri mwisho wa wakati
unavyokaribia.
Lakini nuru na giza haviwezi kuwa pamoja. Kuna mapambano kati ya ukweli na uongo. Kushikilia na
kutetea kimoja ni kupinga na kupambana na kingine. Mwokozi wetu mwenyewe alisema: "Sikuja kuleta
amani, bali upanga." Mathayo 10:34. Miaka michache baada ya kuanza kwa Matengenezo, Luther
alisema: "Mungu haniongozi, ananisukuma kwenda. Ananipeleka mbali. Sijisimamii mwenyewe.
Natamani kuishi kwa utulivu; lakini ninaingizwa (127) katika vurugu na mapinduzi." 74 Alikuwa karibu na
kuingia katika hali hiyo.
Kanisa la Kirumi lilikuwa limeifanya neema ya Mungu kuwa biashara. Meza za watu wenye kubadili fedha
(Mathayo 21:12) zilikuwa pembeni ya madhabahu zake, na anga lilijazwa na kelele za wauzaji na
wanunuzi. Katika kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la Mt. Petro la Roma, mali kwa ajili ya
msamaha wa dhambi zilitolewa ili kuuzwa hadharani na mamlaka ya papa. Kwa kutumia malipo ya
uhalifu, hekalu lilikuwa linajengwa kwa ajili ya kumwabudu Mungu – jiwe la msingi likiwa limewekwa
kwa fedha ya udhalimu! Lakini mali hiyo hiyo iliyotumika kwa Roma kujitukuza ilichochea tatizo baya

74
D'Aubigne, b. 5, ch. 2
69
kwa utawala na ukuu wake. Ndiyo iliyoibua adui mkubwa wa upapa kuliko maadui wake wote, na
ikasababisha vita ambayo ilitikisa kiti cha upapa na taji ya kifalme ya papa.
Afisa aliyeteuliwa kukusanya na kuuza mali kule Ujerumani – kwa jina la Tetzel – alikuwa ameshtakiwa
kwa uhalifu katika jamii na dhidi ya sheria ya Mungu; lakini akiwa amekwepa adhabu ya uhalifu wake,
akaajiriwa katika kuendeleza miradi hii isiyokubalika ya papa. Kwa ujasiri mkubwa alirudia mambo
kama yale yale ya kuwadanganya watu wasiojua wala wasio na hatia. Watu hawa wangekuwa na neno la
Mungu wasingedanganywa. Biblia alifichwa kutoka kwao, wakawekwa chini ya udhibiti wa upapa, kusudi
wajaze utajiri wa viongozi wa mamlaka ile. 75
Tetzel alipoingia mjini, mtumishi alitangulia mbele yake, akitangaza: "Neema ya Mungu na ya baba
mtakatifu iko malangoni mwenu." 76 Na watu walimkaribisha mkufuru huyu aliyejifanya Mungu kama vile
ni Mungu Mwenyewe aliyeshuka kwao kutoka mbinguni. Msafara wa kutisha ukaelekea kanisani, na
Tetzel, akipanda (128) mimbarani, alitukuza mali zilizokusanywa kama sadaka ya thamani kubwa kwa
Mungu kuliko zote. Alitangaza kwamba kwa mujibu wa hati zake za msamaha, dhambi ambazo mtoaji
wa mali angefanya baadaye zingesamehewa, na ya kwamba “wala hakukuwa na haja ya kuzitubia
tena." 77 Zaidi ya hapo, aliwahakikishia wasikilizaji wake kwamba matoleo yale yalikuwa na nguvu ya
kuwaokoa walio hai na waliokufa; kwamba mara tu pesa inapolia katika chombo cha matoleo, roho ya
mtu ambaye pesa imetolewa kwa ajili yake inahama kutoka toharani (purgatory) na kuelekea
mbinguni. 78
Wakati Simoni alipotaka kutoa fedha ili kununua uweza wa mitume wa kutenda miujiza, Petro alimjibu:
"Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhani ya kwamba karama ya Mungu
yanunuliwa kwa pesa." Matendo 8:20. Lakini alichotoa Tetzel kiliaminiwa na maelfu ya watu. Dhahabu
na fedha vikamiminika katika hazina yake. Wokovu unaotolewa kwa pesa ulipatikana kwa urahisi kuliko
ule unaopatikana kwa njia ya toba, imani na juhudi ya kupambana na kuishinda dhambi. 79
Mafundisho ya matoleo hayo yalikuwa yamepingwa na watu waliojifunza katika Kanisa la Kirumi, na
walikuwepo wengi ambao hawakuwa na imani ya ubandia. Hakuna mtumishi wa kanisa aliyediriki kutoa
sauti dhidi ya msululu huu; lakini mawazo ya watu yalikuwa yanasumbuka, na wengi waliuliza ikiwa
Mungu asingefanya kazi ya kulisafisha kanisa.
Ingawa Luther aliendelea kuwa katika upapa, hakuridhishwa na makufuru ya kuthamini mali. Wengi wa
waumini wake walikuwa wamenunua hati ya msamaha, na baadaye walianza kuja kwake kama
mchungaji wao, wakitaka msamaha wa dhambi zao, si kwa sababu walitubu na kutaka kufanya
matengenezo, bali kwa kutaka kupitia katika matoleo ya mali. Luther aliwakatalia msamaha, na
akawaonya kwamba ikiwa (129) hawatatubu dhambi na kutengeneza maisha yao, watapotea katika
dhambi zao. Ndipo wakamwendea Tetzel wakilalamika kwamba mtumishi amekataa hati zao; na wengi
wakidai kwamba pesa yao irudishwe kwao. Kusikia hivyo, mtawa huyu alijawa na ghadhabu. Alitamka
maneno ya laana ya kutisha, na kusababisha moto kuwaka miongoni mwa watu,na akatangaza kwamba

75
John C. L. Gieseler, A Compendium of Ecclesiastical History, per. 4, sec. 1, par. 5.
76
D'Aubigne, b. 3, ch. 1
77
Ibid., b. 3, ch. 1.
78
K. R. Hagenbach, History of the Reformation, vol. 1, p. 96
79
Angalia maelezo ya nyongeza katika Kiambatanisho
70
“alikuwa amepata maelekezo kutoka kwa papa kupiga marufuku wazushi wote waliokuwa wanapinga
habari ya matoleo matakatifu." 80
Sasa Luther aliingia katika kazi ya kuisimamia kweli. Sauti yake ilisikika kutoka mimbarani ikisihi na
kuonya. Aliweka wazi tabia ya dhambi na kuwafundisha watu kwamba haiwezekani kwa mtu kujiondolea
hatia yake au adhabu yake kwa matendo yake. Hakuna kinachoweza kumwokoa mdhambi isipokuwa
kuungama mbele za Mungu na kuwa na imani katika Kristo. Neema ya Mungu haiwezi kununuliwa;
inatolewa bure. Aliwashauri watu wasinunue msamaha, bali wamwangalie kwa imani Mkombozi
aliyesulibiwa. Alihadithia uzoefu wake yeye mwenyewe katika kutafuta wokovu kwa kujiumiza na
kujitesa, na kuwahakikishia wasikilizaji wake kwamba aliipata amani na raha kwa kutojiangalia yeye ila
kwa kumwamini Kristo.
Kadiri Tetzel alivyoendelea na msafara na kujidai, Luther aliazimia kupambana zaidi na machafu haya.
Tukio fulani likatoa fursa. Kanisa kuu la Wittenberg lilikuwa na masalia mengi ya kumbukumbu za vitu
vya zamani, ambayo yalikuwa yanaonyeshwa kwa watu mnamo siku kadhaa za sikukuu, na msamaha
kamili wa dhambi ulitolewa kwa wote waliotembelea kanisani na kuungama katika siku hizo. Kwa hiyo,
idadi kubwa ya watu ilikuja kanisani katika siku hizo. Moja ya matukio haya, sikukuu ya Watakatifu
Wote, ilikuwa inakaribia. Siku moja kabla ya siku hiyo, akiwa ameungana na watu waliokuwa
wakielekea kanisani, Luther alibandika mlangoni pa kanisa waraka wenye mapendekezo tisini na tano
yaliyokuwa yakipinga mafundisho ya mfumo uliokuwepo. Alitangaza kwamba alikuwa na nia (130) ya
kuzieleza hoja zake zile chuoni siku inayofuata, dhidi ya wote watakaoamua kuzipinga.
Mapendekezo yake yalivuta hisia za wengi. Yalisomwa na kusomwa tena na tena kutoka katika pande
zote. Taharuki kubwa ilitokea chuoni pale na katika mji wote. Mapendekezo haya yalikuwa na maana
kwamba kumbe hakuna uwezo maalum aliopewa papa au mwanadamu yeyote kutoa msamaha wa
dhambi, wala kuidhinisha adhabu kwa mdhambi. Utaratibu uliokuwepo ulikuwa ni ulaghai - mchezo wa
kukusanya pesa kwa kuwalaghai watu – mbinu ya Shetani kuharibu roho za wote wale wanaoamini
uongo. Ilionyeshwa wazi pia kwamba injili ya Kristo ni hazina ya kanisa ya thamani kubwa, na ya
kwamba neema ya Mungu, iliyodhihirishwa humo, inatolewa kwa wote wanaoitafuta kwa toba na imani.
Mapendekezo ya Luther yaliibua mjadala lakini hakuna mtu aliyekuwa tayari kuhimili changamoto ile.
Mambo aliyopendekeza yalisambaa katika Ujerumani yote, na ndani ya majuma machache yalikuwa
yanasikika katika ulimwengu wote wa Kikristo. Watiifu wengi wa mfumo wa Kirumi, waliokuwa
wameona na kunung’unikia uovu uliokuwa kanisani, lakini hawakujua namna ya kuukomesha, walisoma
mapendekezo ya Luther kwa furaha, wakitambua kwamba yana sauti ya Mungu ndani yake. Walihisi
kwamba Bwana amenyosha mkono wake wenye rehema ili kukomesha wimbi kubwa la udhalimu
uliokuwa katika Roma. Kwa siri, wana wa kifalme na mahakimu walifurahi kuona kwamba mamlaka ile
potovu iliyominya haki ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi yake imepata kudhibitiwa.
Lakini makundi ya wale waliokuwa wapenda-dhambi na udhalimu walitishwa na hali hii iliyotishia
kuondoa mambo waliyoyapenda. Makasisi wa uongo, wakiwa wameingiliwa katika kazi yao ya kuweka
vikwazo dhidi ya uhalifu, huku wakiona kwamba manufaa yao yanahatarishwa, walichukizwa na
wakatafuta jinsi ya kudumisha matakwa yao. Mwanamatengenezo alikuwa na washtaki wengi wa
kukabili. Baadhi walimshtaki kwa uharaka wa kufanya mambo. Wengine walimshtaki kwa kudhania tu,
wakisema kwamba hakuagizwa na Mungu, bali alitenda kwa kiburi na kimbelembele. Alisema, "Nani
(131) hajui kwamba si rahisi kwa mtu kutoa wazo jipya pasipo kuwa na mwonekano fulani wa kiburi, au
kushtakiwa kwa kuleta mgogoro? … . Kwa nini Kristo na mashujaa wa imani wote waliuawa? Kwa sababu

80
D'Aubigne, b. 3, ch. 4
71
walionekana kuwa na kiburi kulingana na ujuzi wa wakati wao, na kwa sababu walihimiza mambo yao
mapya bila kutafuta kwanza mashauri kutoka katika mafundisho yaliyotangulia."
Alisema tena: "Lolote ninalofanya litafanyika, si kwa umakini wa wanadamu, bali kwa mashauri ya
Mungu. Ikiwa kazi ni yake Mungu, ni nani ataisimamisha? Ikiwa siyo ya Mungu, ni nani itaiendeleza? Si
kwa mapenzi yangu, si kwa mapenzi yao, wala si kwa mapenzi yetu; bali mapenzi yako ee Baba
mtakatifu, uliye mbinguni." 81
Ingawa Luther alikuwa amesukumwa na Roho wa Mungu kuanza kazi yake, asingeifanya pasipokuwa na
upinzani mkali. Upinzani kutoka kwa adui zake, upotoshaji wao wa malengo yake, na kumbukumbu zao
zisizo za kweli na zenye chuki kuhusu tabia na mvuto wake, vilielekezwa kwake kama ujazo wa
mafuriko; na hazikupita pasipo madhara. Alikuwa amedhani kwamba viongozi wa watu kanisani na
katika shule wangeungana naye kwa furaha katika jitihada za kuleta mageuzi. Maneno ya kutia moyo
yaliyotoka kwa watu wenye nyadhifa za juu yalikuwa yamempa tumaini na furaha. Tayari alikuwa na
matumaini ya kuona mapambazuko ya siku mpya katika kanisa. Lakini sasa maneno ya kutia moyo
yalikuwa yamegeuka na kuwa upinzani na lawama. Watu wengi mashuhuri, katika kanisa na serikali,
walikuwa wameguswa na ukweli wa mapendekezo yake; lakini baadaye waliona kwamba kuukubali
ukweli ule kulihitaji mabadiliko makubwa. Kimaadili, kuwafumbua macho na kuwageuza watu lingekuwa
tendo la kudhoofisha mamlaka ya Roma, kusitisha maelfu ya vijito vinavyotiririka kuingia katika hazina
yake, na kwa hiyo kuathiri kwa kiasi kukubwa maisha ya anasa na matumizi mabaya ya watu wa upapa.
Zaidi ya hapo, kuwafundisha watu kufikiri na kutenda wao wenyewe, wakimwangalia Kristo pekee kwa
ajili ya wokovu wao, kungesababisha mapinduzi ya enzi ya upapa na hatimaye kuharibu mamlaka yao
wenyewe. Kwa sababu hii walikataa ufahamu waliopewa na Mungu na kujipanga (132) kinyume cha
Kristo na kinyume cha ukweli kwa kumpinga mtu aliyekuwa ametumwa kwao ili kuwapa ufahamu.
Luther aliogopa alipojiangalia mwenyewe – mtu mmoja anayepingana na mamlaka kubwa za dunia.
Wakati mwingine aliona shaka kama ni kweli kwamba alikuwa ameongozwa na Mungu kusimama
kinyume na mamlaka ya kanisa. Aliandika: "Mimi nilikuwa nani kupinga ukuu wa papa, yeye ambaye …
anatetemekewa na wafalme wa dunia na ulimwengu mzima? ... Hakuna awezaye kujua jinsi moyo
wangu ulivyoumia katika kipindi hiki cha miaka miwili ya kwanza, na ni hali ya huzuni kiasi gani, niseme
katika ukiwa kiasi gani, nilizamishwa." 82 Lakini hakuachwa kuvunjika moyo kabisa. Wakati msaada wa
kibinadamu uliposhindwa, alimwangalia Mungu peke yake na akajifunza kwamba angeweza kujifunza
katika usalama kamili akiwa katika mkono ule wenye nguvu zote.
Akimwandikia rafiki yake katika Matengenezo, Luther alisema: "Hatuwezi kuelewa Maandiko kwa usomi
au uwezo wa akili. Jukumu lako ni kuanza na maombi. Msihi Bwana akupatie ufahamu wa kweli wa neno
lake, kwa neema yake kuu. Hakuna mtu mwingine anayeweza kutafsiri neno la Mungu zaidi ya Mtunzi
wa neno hilo, maana yeye mwenyewe amesema, 'Wote watafundishwa juu ya Mungu.' Usitumainie kitu
chochote kutokana na kazi zako mwenyewe, kutoka katika fahamu zako mwenyewe; jenga imani yako
katika Mungu, na katika ushawishi wa Roho wake. Amini haya kutoka kwa neno la mtu ambaye amekuwa
na uzoefu." 83 Hapa kuna somo muhimu la kujifunza kwa wale wanaodhani kwamba Mungu amewaita ili
kuuwasilisha ukweli wa wakati huu kwa watu wengine. Kweli hizi zitachochea uadui wa Shetani na wa
watu wale wapendao hadithi za uongo alizobuni. Katika mapambano dhidi ya nguvu za uovu kuna hitaji
la kitu kikubwa zaidi ya nguvu na akili za hekima ya kibinadamu.

81
Ibid., b. 3, ch. 6
82
Ibid., b. 3, ch. 6
83
Ibid., b. 3, ch. 7
72
Wapinzani walipotegemea mila na desturi, au mafundisho na mamlaka ya papa, Luther alikabiliana nao
kwa Biblia, Biblia peke yake. Hapa kulikuwa na hoja ambazo wasingezijibu; kwa hiyo watumwa hawa wa
itikadi ya mfumo na udhalimu walionekana kuwa na kiu ya damu yake, vile vile kama Wayahudi
walivyokuwa na kiu ya damu ya Kristo. "Ni mzushi," (133) walisema mashabiki hawa wa mfumo wa
Kiroma. "Ni jeuri ya hali ya juu dhidi ya kanisa kiasi kwamba mzushi wa kutisha namna hii hawezi
kuachwa aishi hata kwa saa moja zaidi. Hebu jukwaa la kunyongea liinuliwe haraka kwa ajili yake!" 84
Lakini Luther hakuangukia katika hasira ya mawindo yao. Mungu alikuwa na kazi ya kufanywa naye, na
malaika wa mbinguni walitumwa kumlinda. Hata hivyo, wengi walioipokea nuru kutoka kwa Luther
walikabiliwa na ghadhabu ya Shetani, kwa ajili ya ile kweli wakapita katika mateso makali na vifo
pasipo woga.
Mafundisho ya Luther yalivuta mawazo ya watu wenye fikra njema katika Ujerumani yote. Mahubiri na
maandiko yake yalitoa miali ya mwanga ambao uliwaangazia na kuwaamsha maelfu ya watu. Imani iliyo
hai ilikuwa inachukua nafasi ya itikadi mfu ya mfumo wa dini ya mazoea ambamo kanisa lilikuwa
limewekwa. Watu walikuwa wakipoteza imani na mfumo dhalimu wa Kiroma siku hadi siku. Vipingamizi
vinavyofanywa na mawazo ya kutungwa vilikuwa vinaondoka. Neno la Mungu, ambalo Luther alilitumia
kupimia kila fundisho na kila dai la mtu, lilikuwa kama upanga wenye makali kuwili, ukikata katika
mioyo ya watu. Nia ya uamsho wa hali ya maendeleo kiroho ilionekana kila mahali. Kila mahali kulikuwa
na kitu kama njaa na kiu kwa ajili ya haki kwa namna ambayo haikupata kujulikana kwa zama kadhaa.
Macho ya watu, ambayo yalikuwa yameelekezwa kwa mambo ya dini yaliyoletwa na wanadamu na
wapatanishi wa duniani, yalikuwa yanageuzwa, kwa toba na imani, kumwelekea Kristo.
Kuenea kwa mwamko huu kuliibua zaidi hofu ya mamlaka ya upapa. Luther alipokea wito wa kufika
Roma kujibu mashtaka ya uasi. Amri hii iliwajaza hofu wenzake. Walijua bayana hatari iliyokuwa mbele
yake katika jiji lile la kidhalimu, lililokwisha kulevywa kwa damu ya mashujaa wa imani wa Yesu.
Walipinga kwamba asiende Roma wakaomba ahojiwe akiwa Ujerumani.
Hatimaye mpango huu ulitekelezwa, na balozi wa papa akateuliwa kusikiliza shauri hilo. Katika
maelekezo ya papa yaliyotolewa kwa balozi huyu, ilisemekana kuwa Luther ameshaonekana kama
mzushi. Kwa hiyo mwakilishi huyu wa papa alitakiwa achuke hatua bila (134) kukawia. Kama Luther
ataendelea na msimamo wake, na balozi akashindwa kumtia nguvuni, alipewa kibali "kumpiga marufuku
Luther kuonekana mahali popote katika Ujerumani; na kupiga marufuku, kulaani na kusambaratisha
watu wote waliojifungamanisha naye." 85 Na zaidi, papa alimwelekeza balozi wake kwamba, ili kung’oa
kabisa mzizi wa uasi, watu wote, wa hadhi zote, katika kanisa na serikalini, wazuiwe kuwasiliana na
Luther, isipokuwa mfalme tu, ambaye atampeleka Luther na wafuasi wake Roma kwa ajili ya kupata
adhabu.
Hapa inajionyesha wazi roho ya upapa. Hakuna chembe ya kanuni ya Kikristo, wala hata haki ya kawaida
tu haionekani. Luther alikuwa ametengwa kwa umbali mkubwa kutoka Roma; hakuwa na fursa ya
kueleza au kutetea msimamo wake; lakini hata kabla ya kesi yake kusikilizwa, alikuwa tayari
ameshahukumiwa kama mzushi, na katika siku moja tu, alikuwa ameitishwa, kushtakiwa, kuhukumiwa
na kuadhibiwa; na yote haya yalifanywa na yeye aliyejiita mwenyewe baba mtakatifu, yeye pekee
mwenye mamlaka na uweza katika kanisa na dola!
Katika wakati huu, ambapo Luther alihitaji sana faraja na mashauri ya rafiki wa kweli, ukarimu wa
Mungu ulimleta Melanchthon pale Wittenberg. Melanchthon alikuwa kijana kwa umri, mnyenyekevu na

84
Ibid., b. 3, ch. 9
85
Ibid., b. 4, ch. 2
73
mpole, mwenye maamuzi makini, ufahamu mpana na mwenye mvuto, mwenye tabia safi, na
aliyestaajabisha wengi. Vipaji vyake havikuonekana haraka kuliko unyenyekevu na upole wake. Baada
ya muda mfupi tu alikuwa mwanafunzi wa injili, na rafiki wa karibu sana na msaada wa thamani sana
kwa Luther; upole wake, umakini wake na usahihi wa kazi zake ulikamilisha faraja na nguvu ya Luther.
Muungano wao kazini uliongeza nguvu kwa kazi ya Matengenezo na ikawa chanzo cha ujasiri mkubwa wa
Luther.
Augsburg ulikuwa umewekwa kama sehemu ya mateso, na Mtengenezaji alifunga safari kuelekea huko.
Woga mkubwa ulikuwepo kuhusu safari hii. Vitisho vilikuwa vimeonyeshwa wazi wazi kwamba
angetekwa na kuuawa njiani, na wenzake walimwomba aache jambo hilo. Walimsihi (135) pia aondoke
Wittenberg kwa muda atafute sehemu ya kwenda ambako angepata watu wa kumhakikishia usalama
wake. Lakini asingeacha nafasi ambapo Mungu alimweka! Lazima aendeleze njia ya ukweli, licha ya
dhoruba zilizokuwa zinampiga. Lugha yake ilikuwa: "Mimi ni sawa na Yeremia, mtu wa mapigano na
mashindano; lakini kadiri mikasa inavyozidi, ndivyo furaha inavyozidishwa. . . . Wameshaharibu heshima
na hadhi yangu. Kitu kimoja tu kinabaki; ni mwili wangu huu uharibikao: hebu na wauchukue;
watafupisha maisha yangu kwa saa chache. Lakini kwa habari ya roho yangu, hawawezi kuichukua. Yeye
atakaye kulitangaza neno la Kristo ulimwenguni, lazima atarajie kifo kila wakati." 86
Habari za kufika kwa Luther Augsburg kulimridhisha mwakilishi wa upapa (balozi). Mzushi huyu
msumbufu aliyevuta hisia za ulimwengu wote alionekana kuwa mikononi mwa mamlaka ya Roma, na
mwakilishi huyo wa papa akaazimia kwamba hatapona. Mwanamatengenezo huyu hakuwa amejipatia
hati ya usalama ya safari. Rafiki zake walimwonya asiende mbele za baraza bila hati hiyo, na wakafanya
jitihada ya kuinunua kwa mfalme. Mwakilishi huyo alikusudia kumlazimisha Luther akane msimamo
wake, ikiwezekana, au kama akishindwa, apelekwe Roma ili aende kushiriki katika hatima ya Huss na
Jerome. Kwa hiyo, kupitia mawakala wake, alimshawishi Luther ajitokeze bila kuwa na hati ya usalama
ya kusafiria, akimwaminisha kwamba yuko salama. Mwanamatengenezo huyu alikataa kufanya hivyo.
Hakujitokeza mbele ya balozi wa papa mpaka alipopata waraka uliomhakikishia ulinzi kutoka kwa
mfalme.
Waroma walikuwa wameamua kuingia kwa Luther kwa sura ya upole. Balozi mwenyewe, wakati wa
kumhoji, alionyesha urafiki mkubwa; lakini alidai kwamba Luther ajisalimishe kwa mamlaka ya kanisa,
na akubaliane na kila jambo pasipo kuhoji wala kuuliza. Hakuwa amemchukulia kirahisi mtu aliyekuwa
anashughulika naye. Kwa kujibu, Luther alionyesha mtazamo wake kwa kanisa, hamu yake kwa ajili ya
(136) ukweli, utayari wake wa kujibu upinzani dhidi ya mafundisho yake, na kukabidhi mafundisho yake
yafanyiwe maamuzi na chuo kikuu chochote kilicho mashuhuri. Lakini wakati huo huo alipinga mpango
wa kadinali kumtaka akubali kila jambo bila kumthibitishia makosa yake.
Jibu moja tu lilikuwa ni: "Tangua, tangua!" Mwanamatengenezo alionyesha kwamba msimamo wake
ulikuwa katika Maandiko na akatangaza kwamba kamwe hawezi kuukana ukweli. Akishindwa kujibu hoja
za Luther, balozi alimmwagia lawama, kebehi na dharau, akitumia nukuu za misemo na mapokeo ya
maaskofu, pasipo kumpa Luther nafasi ya kuongea. Kwa kuona kwamba mahojiano yale yanaweza
yasiwe na maana, hatimaye Luther alipata ruhusa ya shingo-upande kuwasilisha majibu yake kwa
maandishi.
"Kwa kufanya hivyo anayekandamizwa hupata faida mara mbili;” alisema akimwandikia rafiki yake.
Kwanza kilichoandikwa chaweza kuwasilishwa kwa watu wengine ili kukipima; na pili, mtu yuko kwenye

86
Ibid., b. 4, ch. 4
74
nafasi nzuri ya kuvuta hofu, kama si dhamili, ya huruma na michanganyo mtu mwenye kiburi anayeweza
kutawala kwa kutumia lugha tu." 87
Katika awamu nyingine ya mahojiano, Luther aliwasilisha msimamo na mawazo yake kwa uwazi, kwa
ufupi, na yakisindikizwa na nukuu za kutosha kutoka katika Maandiko. Waraka huu, baada ya kuusoma
kwa sauti, aliuwasilisha kwa kadinali, ambaye aliutupa pembeni, akidai kuwa umejaa maneno yasiyo na
kitu na nukuu zisizo sahihi. Luther, akiwa na msisimko, alikutana na balozi huyu mwenye kiburi katika
msimamo wake - mapokeo na mafundisho ya kanisa - na akapindua kabisa hoja zake.
Balozi wa papa alipoona ya kwamba hoja ya Luther haikuwa na majibu, alishindwa kujizuia, na kwa
ghadhabu apaza sauti akisema: "Tangua! La sivyo nitakupeleka Roma, kule utasimama mbele ya
waamuzi ambao wamepewa kazi ya kushughulikia tatizo lako. Nitakutenga wewe na washirika wako
wote, na wote (137) watakaokutetea wakati wowote, na nitawafukuzia mbali na kanisa." Na mwisho
akasema, kwa sauti ya hasira na ghadhabu: "Tangua, au uishilie mbali." 88
Haraka Mwanamatengenezo aliwaacha rafiki zake, akitangaza wazi wazi kwamba kutangua hakutarajiwi
kwake. Hali hii ilikuwa kinyume na lengo la kadinali huyu. Alikuwa amejidai kwamba kwa vitisho vyake
angemyumbisha Luther na kumfanya ajisalimishe. Sasa, akiwa ameachwa peke yake na wale
wanaomuunga mkono, alimwangalia mmoja baada ya mwingine kwa fadhaa ya kushindwa kwa mipango
yake.
Jitihada za Luther katika tukio hili hazikuwa bure pasipo matunda. Mkutano mkubwa uliokuwepo ulipata
fursa ya kulinganisha watu wale wawili, na kuamua wao wenyewe juu ya roho iliyodhihirishwa, pamoja
na nguvu na ukweli wa misimamo yao. Waliona tofauti kubwa kiasi gani! Mwanamatengenezo
aliyeonekana kuwa rahisi, mnyenyekevu, na jasiri, alisimama kwa nguvu za Mungu, akiwa na ukweli;
mwakilishi wa papa, akiwa mwenye kujikweza, mwenye kutaka kutawala, mwenye ghadhabu, asiye na
hoja, hakuwa na sababu hata moja kutoka katika Maandiko, lakini aliunguruma kwa vitisho: "Tangua, la
sivyo upelekwe Roma ukapate adhabu yako."
Pamoja na kwamba Luther alikuwa amepata hati ya usalama ya kusafiria, Waromi hawa walikuwa
wanapanga kumkamata na kumtupa gerezani. Rafiki zake walimshauri kwamba haikuwa na maana
kwake kuendelea kukawia pale, inampasa kurudi Wittenberg bila kukawia, na kwamba tahadhari kubwa
ichukuliwe kuficha mpango huo. Hivyo aliondoka Augsburg kabla ya mapambazuko, akiwa amepanda
farasi, akisindikizwa tu na mwongozi wake. Akiwa mwenye hisia mbaya alipita kwa siri katika mitaa ya
mji yenye giza na ukimya. Adui waliojawa na chuki na ukatili walikuwa wanapanga kumharibu. Je
angepona mitego aliyoandaliwa? Hizi zilikuwa nyakati za shida na maombi ya kina. Alifika panapo lango
dogo la mji. Lilifunguliwa kwa ajili yake, yeye na mwongozi wake walipita bila kizuizi. Walipofika nje
salama, waliharakisha na safari, na kabla ya (138) balozi wa papa kufahamu kuhusu kuondoka kwake
alikuwa ameshafika mbali kutoka kwa wabaya wake. Shetani na vibaraka wake walikuwa wameshindwa.
Mtu waliyedhani kuwa yuko mikononi mwao alikuwa ameondoka, alitoroka kama ndege kutoka katika
mtego.
Habari zilipomfikia balozi juu ya kutoroka kwa Luther alishikwa na mshangao na hasira. Alikuwa
ametarajia kupata heshima kwa hekima na msimamo katika kushughulika na msumbufu huyu wa kanisa;
lakini aliishia kufadhaika. Alionyesha hisia yake katika barua aliyomwandikia Frederick, mkuu wa

87
Martyn, The Life and Times of Luther, pages 271, 272
88
D'Aubigne, London ed., b. 4, ch. 8
75
jimbo 89 wa Saksoni, akishusha lawama kwa Luther na kudai kwamba Frederick ampeleke
Mwanamatengenezo Roma au ampige marufuku kule Saksoni.
Katika utetezi wake, Luther alimtaka balozi au papa amwonyeshe makosa yake kutoka katika Maandiko,
na akaahidi kwamba angeachana na mafundisho yake ikiwa yangeonekana yanapingana na neno la
Mungu. Na alionyesha shukrani zake kwa Mungu kwamba alihesabiwa kustahili kuteswa katika kazi hii
takatifu.
Mkuu wa jimbo alikuwa bado na ufahamu mdogo kuhusu mafundisho ya matengenezo, lakini aliguswa
sana na uwazi, nguvu na uelekevu wa maneno ya Luther. Frederick akaazimia kwamba atamlinda Luther
mpaka atakapothibitisha kwamba hayuko sahihi. Akiandika kumjibu balozi wa papa, alisema: "Kwa kuwa
Dokta Martin alisimama mbele yako huko Augsburg, yakupasa utosheke. Hatukutarajia kwamba
ungetaka kumlazimisha atangue maneno yake bila kumwonyesha makosa yake. Hakuna hata mmoja
miongoni mwa wasomi wa himaya yetu ambaye amenipa habari kwamba mafundisho ya Martin ni
potofu, yasiyo ya kikristo au ya kizushi. Zaidi ya hayo, mfalme alikataa kumpeleka Luther Roma, au
kumfukuza katika himaya yake." 90
Kiongozi huyu aliona kwamba kulikuwa na hali ya kuvunjika kwa uadilifu katika jamii. Kazi kubwa ya
marekebisho ilikuwa inahitajika. Mipango ya gharama kubwa ya kuzuia na kuadhibu wahalifu
isingehitajika ikiwa watu wangetambua na kuheshimu maelekezo ya Mungu na uhuru wa dhamiri. Hivyo,
aliona kwamba (139) Luther alikuwa akifanya kazi ya kufikia lengo hilo, na kwa siri alifurahia kwamba
ushawishi huu ulio bora zaidi ulikuwa unaingia kanisani.
Aliona pia kwamba Luther alikuwa amefanikiwa kama profesa katika chuo kikuu. Ni mwaka mmoja tu
ulikuwa umepita tangu Mwanamatengenezo huyu alipobandika mapendekezo yake mbele ya kanisa, hata
hivyo tayari kulikuwa na tatizo la kushuka kwa idadi ya mahujaji wanaotembelea kanisa wakati wa
sikukuu ya Watakatifu Wote. Roma ilikuwa imepoteza waumini na mapato, lakini nafasi yake ilijazwa na
tabaka jingine, ambao sasa walikuja Wittenberg, si kama mahujaji wa kuangalia maonyesho ya kale,
bali kama wanafunzi waliojaza kumbi za kujifunzia. Maandishi ya Luther yaliwasha hamu mpya ya
kujifunza Maandiko Matakatifu. Hii si kwa sehemu zote za Ujerumani tu, bali kutoka katika nchi
nyingine pia wanafunzi walifurika kuingia chuo kikuu. Vijana waliokuwa wamekuja Wittenberg kwa mara
ya kwanza waliinua mikono juu mbinguni, na kumshukuru Mungu kwa kuifanya nuru ya ukweli kuangaza
kutokea katika mji huu, kama kutoka Sayuni mnamo kipindi cha kale, na ikaenea hata maeneo ya
mbali." 91
Luther alikuwa bado hajaongoka kikamilifu kutoka katika makosa ya Roma. Lakini alipolinganisha Biblia
Takatifu na maelekezo na katiba ya papa, alijawa na mshangao. Aliandika: "Ninasoma matamko ya
maskofu, na . . . sijui kama papa ni mpinga-Kristo peke yake, au ni mtume wake, maana Kristo
anawasilishwa vibaya kwa kiwango kikubwa na kusulibishwa ndani yao." 92 Lakini wakati huu Luther
alikuwa bado anaunga mkono Kanisa la Roma, na hakuwa na wazo kwamba angejitenga na ushirika
wake.

89
Mkuu wa jimbo alikuwa kiongozi aliyewakilisha jimbo katika kumchagua mfalme; anaitwa elector

90
D'Aubigne, b. 4, ch. 10
91
Ibid., b. 4, ch. 10
92
Ibid., b. 5, ch. 1
76
Maandishi ya Mtengenezaji na mafundisho yake yalikuwa yanatawanyika katika ulimwengu wote wa
Kikristo. Kazi ile ilisambaa Uswisi na Uholanzi. Nakala za maandishi yake zilienda hadi Ufaransa na
Hispania. Huko Uingereza mafundisho yake yalipokelewa kama neno la uzima. Ubelgiji na Italia nako
ukweli ulifika. Watu kwa maelfu waliamshwa kutoka katika kutokujua kama katika kifo na kuelekezwa
katika raha na tumaini la maisha ya imani.
(140) Roma iliendelea kufadhaishwa na mashambulio ya Luther, na ilitangazwa na baadhi ya wapinzani
wake shupavu, wakiwemo madokta katika vyuo vikuu vya Kikatoliki, kwamba atakayemwua mtawa huyu
aliyeasi atakuwa hana dhambi. Siku moja mgeni, aliyekuwa na bastola iliyofichwa ndani ya kanzu yake,
alimjia Mwanamatengenezo huyu na kutaka kujua sababu ya yeye kushika njia yake peke yake. Luther
akajibu, "Niko mikononi mwa Mungu. Yeye ni nguvu yangu na ngao yangu. Mwanadamu atanitenda
nini?" 93 Aliposikia maneno haya, yule mgeni alilainika na kuondoka pale kama mahali ambapo pana
uwepo wa malaika wa mbinguni.
Roma ilikazania kumkomesha Luther; lakini Mungu alikuwa ulinzi kwake. Mafundisho yake yalisikika kila
mahali--"majumbani na katika jumuiya, . . . katika ngome za mabwana, katika vyuo vikuu, na katika
majumba ya kifalme;" na tabaka la mabwana walikuwa wanainuka na kuunga mkono jitihada zake. 94
Ni katika wakati huu ambapo Luther, kwa kusoma maandishi ya Huss, aliona kwamba ukweli mkuu wa
haki kwa imani, ambao hata yeye alikuwa akiutafuta ili kuushika na kuufundisha, ulikuwa unafuatwa na
Mwanamatengenezo wa Bohemia. Luther akasema: “Sote, Paulo, Augustine na mimi, tumekuwa Wahuss
(wafuasi wa Huss) pasipo kujijua!” “Hakika Mungu ataujilia ulimwengu kwa habari hiyo, kwani ukweli
huo ulihubiriwa kwa ulimwengu karne moja iliyopita, na ukapigwa vita!" 95
Akitoa wito kwa mfalme na mabwana wa Ujerumani kwa niaba ya jamii ya matengenezo ya Kikristo,
Luther aliandika kuhusu papa akisema: Ni jambo la ajabu sana kwa mwanadamu kujifanya makamu wa
Kristo, akijionyesha kwa fahari ambayo hakuna mfalme anayeweza kuifikia. Je kiumbe huyu ni sawa na
Yesu aliyekuwa maskini, au Petro mnyenyekevu? Wanasema kwamba yeye ni bwana wa ulimwengu!
Lakini Kristo, ambaye huyu anadai kuwa makamu wake, amesema, ‘Ufalme wangu si wa ulimwengu
huu.’ Je, fahari ya makamu inaweza kupita ile ya mkuu wake?" 96
Kuhusu vyuo vikuu aliandika hivi: "Naogopa kwamba vyuo vikuu vitathibitika kuwa malango makuu ya
kuzimu, (141) visipojishughulisha na kuyaeleza Maandiko Matakatifu, na kuyaweka katika mioyo ya
vijana. Simshauri mtu yeyote kumpeleka mtoto wake mahali ambapo hapatawaliwi na Maandiko. Kila
taasisi ambamo watu hawajishughulishi na neno la Mungu bila kukoma lazima itapotoka." 97
Wito huu ulisambazwa kwa kasi katika Ujerumani yote na ukawa na ushawishi mkubwa kwa watu. Taifa
lote lilihamasika, na watu wengi walivutwa kufuata viwango vya matengenezo. Wapinzani wa Luther,
wakisukumwa na hamu ya kisasi, walimwomba papa achukue hatua madhubuti dhidi yake. Tamko
likatolewa kwamba mafundisho yake yapigwe marufuku haraka. Siku sitini zilitolewa kwa Mtengenezaji
na wafuasi wake, kwamba zikipita bila wao kukana mafundisho yao, watatengwa na ushirika.

93
Ibid., b. 6, ch. 2
94
Ibid., b. 6, ch. 2
95
Wylie, b. 6. ch. 1
96
D'Aubigne, b. 6, ch. 3
97
Ibid., b. 6, ch. 3

77
Ilikuwa hali ya hatari kwa Matengenezo. Kwa karne kadhaa adhabu ya kutenga na ushirika ilikuwa
imetumiwa na Roma na kuleta hofu kwa watawala; ilikuwa imezifanya himaya zenye nguvu kujazwa ole
na kuachwa ukiwa. Himaya ambazo ziliangukiwa na adhabu hiyo zilitiwa hofu na vitisho; zilitengwa na
kuzuiwa kushirikiana na nyingine na kuonekana kama zisizofaa kitu, zinazostahili kuwindwa na
kutokomezwa. Luther hakuwa kipofu kuona kimbunga kilichokuwa kinataka kumkumba; lakini alisimama
imara, akimwamini Kristo kama tegemeo na ngome yake. Akiwa mwenye imani na ujasiri wa kishujaa
aliandika: "Sijui kinachotaka kutokea, wala sijali kutaka kukijua. . . . Hebu mlipuko utokee mahali
unapotaka, mimi sina hofu. Hakuna kitu zaidi ya jani kiangukacho, bila mapenzi ya Baba yetu. Badala
yake ni kiasi gani yeye anatujali. Ni jambo jepesi kufa kwa ajili ya Neno, maana hata Neno mwenyewe
aliyefanyika mwili alikufa. Ikiwa tunakufa na yeye, tutaishi na yeye; na kupitia mahali alipopitia kabla
yetu tutakuwa mahali alipo na kukaa naye milele." 98
Wakati tamko la papa la kumtenga Luther lilipomfikia, Luther alisema: "Nalidharau na kulipinga, ni
kama haramu, lisilo la kweli. . . . Ni Yesu mwenyewe (142) anayekataliwa ndani ya hilo. . . . Nafurahi
katika hali hii ya kubeba shida kwa ajili ya mafanikio ya njia hii. Tayari nahisi uhuru moyoni mwangu;
maana hatimaye najua kwamba papa ni mpinga-Kristo, na ya kwamba kiti chake cha enzi ni kile cha
Shetani mwenyewe." 99
Lakini tamko la Roma halikukosa madhara. Kifungo, mateso, na upanga vilikuwa silaha zilizotumika
kulazimisha utii. Wale waliokuwa dhaifu na shupavu walitetemekea tamko hilo la papa; na wakati watu
wakimhurumia Luther, wengi walihisi kwamba maisha yalikuwa mazuri kiasi kwamba wasingeyahatarisha
katika barabara ya matengenezo. Kila kitu kilikuwa kinaashiria kwamba kazi ya Mwanamatengenezo
ilikuwa inaenda kukoma.
Lakini Luther alikuwa hana hofu. Roma ilikuwa imevurumisha maguvu yake juu yake, na ulimwengu
haukutazamia jambo jingine isipokuwa kutoweshwa kwake au kulazimishwa kutangua. Lakini kwa nguvu
ya kutisha alimtupia adhabu ya hukumu yeye mwenyewe na akatangaza hadharani kuachana naye.
Mbele ya uwepo wa kundi kubwa la wanafunzi, madaktari wa falsafa, na raia wa hadhi zote, Luther
alipinga amri ya papa, pamoja na sheria za kanisa, na maandishi yote yanayodumisha nguvu za upapa.
Alisema, "Adui zangu wameweza kujeruhi kazi ya ujumbe wa ukweli katika mawazo ya watu wa
kawaida, na kuharibu roho zao, kwa kuzuia vitabu vyangu; kwa sababu hii nimeondosha vitabu vyao.
Shindano kali limeanza. Hapa nimekuwa nikicheza tu na papa. Nilianza kazi hii katika jina la Mungu;
itamalizwa pasipo mimi, ila kwa uweza wake." 100
Kuhusu maneno ya upinzani ya adui zake waliomdhihaki kwamba njia yake ni dhaifu, Luther alijibu:
"Nani ajuaye kwamba Mungu amenichagua na kuniita, na kama hawawezi kuogopa hilo, kwa kunidharau,
wanamdharau Mungu mwenyewe? Musa alikuwa peke yake wakati wa kuanza kutoka Misri; Eliya alikuwa
peke yake wakati wa enzi ya Mfalme Ahabu; Isaya alikuwa peke yake Yerusalemu; Ezekieli alikuwa peke
yake Babeli. . . . Kamwe Mungu hakuchagua kuhani mkuu au mtu mashuhuri kuwa nabii; bali alichagua
watu wa kawaida wa hali ya chini na waliodharauliwa, wakati fulani hata (143) Amosi mchunga kondoo.
Katika kila kizazi, watakatifu wametoa maonyo kwa wakuu, wafalme, wana wa wafalme, makuhani, na
wenye hekima, kwa gharama ya maisha yao. . . . Sisemi kwamba mimi ni nabii; lakini nasema kwamba

98
Ibid., 3d London ed., Walther, 1840, b. 6, ch. 9
99
D'Aubigne, b. 6, ch. 9
100
Ibid., b. 6, ch. 10
78
hawakuwa na budi kuogopa kwa sababu mimi niko peke yangu na wao wako wengi. Nina hakika na hili,
kwamba neno la Mungu liko ndani yangu, na ya kwamba haliko ndani yao." 101
Lakini haikuwa pasipo mashindano makali ndani yake mwenyewe kwamba Luther alijitenga na kanisa. Ni
wakati huu ambapo aliandika: "Kila siku nahisi zaidi na zaidi jinsi ilivyo kazi ngumu kuweka pembeni
mafundisho ambayo mtu amelishwa wakati wa utoto. Lo, imenisababishia maumivu kiasi gani, ingawa
nilikuwa na Maandiko pembeni yangu, kujithibitishia mwenyewe kwamba naweza kudiriki kusimama
peke yangu kinyume cha papa, na kumdhihirisha kwamba ni mpinga-Kristo! Ni taabu kiasi gani moyoni
mwangu ambayo haijawahi kutokea! Ni mara ngapi ambapo sijapata kujiuliza kwa uchungu swali lile
ambalo limekuwa likiulizwa na washirika wa papa mara kwa mara: 'Wewe peke yako ndiye mjuaji?
Wengine wote wamekosea? Itakuwaje ikiwa ni wewe ambaye hauko sahihi, na unayehusisha roho nyingi
katika makosa yako, ambazo hatimaye zitaharibiwa milele?' 'Hivyo ndivyo nilivyopambana na mimi
mwenyewe na Shetani, mpaka Kristo, kwa neno lake kamilifu, alipothibitisha moyo wangu dhidi ya
mashaka haya." 102
Papa alikuwa amemtishia Luther kutengwa kama asingekana msimamo wake, na sasa kitisho hicho
kilitimilizwa. Tamko jipya lilitolewa, likitangaza kwamba Luther ametengwa rasmi na kanisa la Roma,
likimhukumu kama mtu aliyelaaniwa Mbinguni, na kuwahusisha katika hukumu hiyo wote watakaopokea
mafundisho yake. Mapambano makubwa yalikuwa yamefikiwa kwa ukamilifu.
Upinzani ni hali iliyopo dhidi ya wote ambao Mungu huwatumia kuutangaza ukweli maalum wa wakati
wao. Kulikuwa na ukweli wa wakati mnamo siku za Luther, - ukweli wenye umuhimu maalum kwa
wakati ule. Kuna ukweli wa wakati wetu katika kanisa leo.
(144) Yeye afanyaye mambo yote kulingana na mashauri ya mapenzi yake amependezwa kuweka watu
katika hali tofauti na kuwakabidhi majukumu maalum ya wakati wao na mazingira waliyomo. Kama
wangethamini nuru iliyotolewa kwao, upeo mkubwa wa ukweli ungefunuliwa kwao. Lakini ukweli
hautakiwi tena na walio wengi leo kwa namna bora zaidi ya vile ilivyokuwa kwa watu wa upapa na
Luther. Ipo hali ile ile ya kukubali nadharia na mapokeo ya wanadamu badala ya neno la Mungu kama
ilivyokuwa mnamo zama zilizopita. Wale waupelekao ukweli wa wakati huu wasitarajie kupokelewa kwa
kupendwa kuliko ilivyokuwa kwa matengenezo ya awali. Pambano kuu kati ya ukweli na uongo, kati ya
Kristo na Shetani, litaongezeka makali yake kadiri tunavyoelekea katika kufungwa kwa historia ya dunia
hii.
Yesu aliwaambia wanafunzi wake: "Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio
wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua kutoka katika ulimwengu, kwa
sababu hiyo ulimwengu huwachukia. Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko
bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu, watalishika na
lenu." Yohana 15:19, 20. Na kwa upande mwingine Bwana wetu alisema wazi wazi: "Ole wenu ninyi watu
wote watakapowasifu, kwa kuwa baba zao waliwatenda manabii wa uongo mambo kama hayo." Luka
6:26. Roho ya ulimwengu haiikubali tena roho ya Kristo leo zaidi hata ya vile ilivyokuwa zamani, na
wale walihubirio neno la Mungu katika usafi wake watapokelewa pasipo upendo leo zaidi hata kuliko
zama zilizopita. Miundo ya upinzani dhidi ya neno inaweza kubadilika, uadui unaweza kuwa usio wa
wazi kwa sababu ni hafifu; lakini uadui ule ule bado upo na utajidhihirisha kadiri mwisho wa wakati
unavyokaribia.

101
Ibid., b. 6, ch. 10
102
Martyn, pages 372, 373

79
Sura ya 8
LUTHER MBELE YA BARAZA

Mfalme mpya wa dola, Charles V, aliinuka kuitawala Ujerumani, na mawakala wa Roma wakaharakisha
kummwagia salamu za pongezi na kumshawishi kutumia uwezo wake dhidi ya Matengenezo. Kwa upande
mwingine, mkuu wa jimbo 103 wa Saksoni, mwenye nafasi katika kumteua mfalme, ambaye Charles
aliwiwa sana kwa sababu ya taji yake, alimtaka asichukue hatua yoyote dhidi ya Luther mpaka
atakapokuwa amempa nafasi ya kumsikiliza. Kwa hiyo mfalme alikuwa amewekwa katika hali ya
kuchanganyikiwa na kufadhaika. Wale watu wa upapa wasingeridhishwa na kitu chochote kidogo kuliko
mfalme kumhukumu Luther kufa. Mkuu wa jimbo wa Saksoni alikuwa ametamka wazi kwamba "si
mtawala wala mtu mwingine ambaye amepata kuthibitisha kwamba maandishi ya Luther yamebatilika;"
kwa hiyo aliomba kwamba Dakt. Luther apatiwe hati ya usalama ya kusafiria ili asafiri kwenda mbele ya
baraza la mahakimu wasomi, waadilifu, na wasiopendelea upande mmoja." 104
Macho ya watu wote sasa yalikuwa yameelekezwa katika baraza la dola ya Ujerumani lililokutana
Worms muda mfupi tu baada ya Charles kuingia madarakani. Yalikuwepo maswali na hoja za kisiasa za
kuangaliwa na baraza hili la taifa; kwa mara ya kwanza watawala wa Ujerumani walikuwa wanakutana
na mfalme wao mpya katika baraza hili. Watu mashuhuri wa kanisa na serikali walikuwa wamekusanyika
kutoka pande zote za nchi. Wakuu wasio wa kidini, waliozaliwa katika koo za hadhi ya juu, wenye
nguvu, wenye wivu juu ya haki zao za kurithi; viongozi wakuu wa kanisa, (146) walikuja na nguvu zao za
heshima na ukubwa; watu walio mashuhuri wa vita katika jumba la mfalme pamoja na wafuasi wao
wenye silaha; na mabalozi kutoka nchi za kigeni na maeneo ya mbali,- wote walikutanika pale Worms.
Lakini habari kubwa iliyoibua hamu kubwa katika baraza lile kubwa ilikuwa ni kazi ya
Mwanamatengenezo wa Saksoni.
Hapo kabla, Charles alikuwa amemwagiza mkuu wa jimbo wa Saksoni kuja na Luther katika Baraza, 105
akimhakikishia ulinzi, na akaahidi kuruhusu majadiliano yaliyo huru, yanayohusisha wajuzi wa mambo,
kuhusu hoja zile zinazobishaniwa. Luther aliguswa na jambo hili la kujitokeza mbele ya mfalme. Kwa
wakati huu afya yake ilikuwa imeshakuwa na matatizo; lakini bado aliandika kwa mwana wa mfalme
akisema: "Ikiwa sitaweza kwenda Worms nikiwa na afya njema, basi nitabebwa kwenda kule, nikiwa

103
Mkuu wa jimbo alikuwa kiongozi aliyewakilisha jimbo katika kumchagua mfalme; anaitwa elector
104
D’Aubigne, book 6, chapter 11
105
Neno Baraza linaloanza na herufi kubwa humu humaanisha mkutano mkuu wa nchi zote zilizounda himaya takatifu ya Rumi
wakati huo, yaani Diet.
80
mgonjwa hivyo hivyo. Maana kama mfalme ananiita, sina shaka kwamba huo ni wito wa Mungu
mwenyewe. Ikiwa wanatamani kutumia nguvu dhidi yangu, na hilo ni jambo linalowezekana sana
(maana hawakuniita kwenda mbele yao kwa nia ya kujifunza), naweka jambo hili mikononi mwa Bwana.
Yeye aliyewaokoa vijana watatu na tanuru liwakalo moto bado anaishi na kutawala. Kama hataniokoa
basi maisha yangu hayana maana sana. Hebu sisi tuiepushe tu injili isiharibiwe na yule mwovu, na
tuiache damu yetu imwagike kwa ajili ya injili, kwa woga wetu watashinda. Si juu yangu mimi kuamua
kwamba maisha yangu au kifo changu kitatoa mchango mkubwa zaidi kwa wokovu wa wote. . . .
Unaweza kutarajia kila kitu kutoka kwangu. . . ila si kukimbia wala kuikana imani. Kukimbia siwezi, na
bado siwezi kukana kazi yangu." 106
Habari zilipoenezwa pale Worms kwamba Luther angefika mbele ya Baraza, taharuki kubwa ilitokea.
Aleander, yule mwakilishi au balozi wa papa aliyekabidhiwa kushughulikia kesi ya Luther alishtushwa na
kughadhabika. Aliona kwamba matokeo ya jambo lile yangekuwa na hatari kwa upapa. Kuweka
utaratibu wa uchunguzi wa jambo ambalo papa ameshalitamkia hukumu ingekuwa sawa na kupingana na
mamlaka kuu ya papa. Zaidi ya hilo, alikuwa na wasiwasi kwamba ufasaha na nguvu ya hoja ya mtu yule
vingeweza kuwageuza wengi wa watawala na kuwaondoa katika madai ya upapa. Kwa hiyo, kwa namna
kama ya (147) dharura kubwa, aliweka pingamizi kwa Charles akizuia Luther asije Worms. Wakati huu
waraka wa kutangaza kumtenga Luther na kanisa ulikuwa umechapishwa; na hili, likiambatanishwa na
ujumbe wa balozi vilimshawishi mfalme kukubaliana. Alimwandikia yule mkuu wa jimbo la Saksoni
kwamba kama Luther hataki kukiri na kuacha msimamo wake, basi abaki Wittenberg.
Akiwa hajatosheka na ushindi huu, Aleander alifanya kila analoweza kwa nguvu zote na werevu wote
kuhakikisha kwamba Luther anahukumiwa. Kwa juhudi kubwa iliyostahili kutumika kwa kazi njema,
aliomba kwamba jambo lile litazamwe na watawala, maaskofu, na wajumbe wengine wa baraza,
akimshtaki Mwanamatengenezo kwa makosa ya "uchochezi, uzushi, na hamheshimu Mungu na
anakufuru." Lakini ukali na hasira vilivyoonyeshwa na maneno ya balozi huyu vilifunua roho iliyokuwa
inamsukuma. Mwitikio waliotoa kwa habari hii ni: "Anasukumwa na chuki na kisasi zaidi kuliko moyo wa
upendo na uchaji wa Mungu." 107 Wajumbe walio wengi katika baraza walionekana kuvutwa upande wa
Luther kuliko ilivyopata kutokea kabla.
Akiwa mwenye hamu mara dufu, Aleander alimsisitiza mfalme atekeleze tamko lililotangazwa na papa.
Lakini kwa mujibu wa sheria za Ujerumani jambo hili lisingefanyika bila kuungwa mkono na watawala;
na, akiwa ameelemewa na king’ang’anizi cha balozi huyo, Charles alimtaka awasilishe shauri lake
Barazani. "Ilikuwa siku ya fahari sana kwa balozi wa papa. Mkutano ule wa baraza ulikuwa ni kitu
kikubwa: vivyo hivyo kazi ilikuwa kubwa zaidi. Aleander alikuwa aitetee Roma, . . . mama na bibi wa
makanisa yote." Alikuwa athibitishe mbele ya mamlaka za ulimwengu wa Kikristo zilizokusanyika pale
kuhusu ufalme wa Petro. "Alikuwa na kipaji cha ushawishi, na alilisubiri tukio hilo kwa hamu kubwa
sana. Mungu alikuwa ameagiza kwamba Roma ijitokeze na kujieleza kupitia kwa msemaji wake mahiri
mbele ya mahakama ya hadhi ya juu kuliko zote, kabla ya kuhukumiwa kwake." 108 Wengi wa wale
waliopendelea kazi ya Mwanamatengenezo walisubiri matokeo ya hotuba ya Aleander kwa wasiwasi.
Mkuu wa jimbo la Saksoni hakuwepo, lakini kwa maagizo yake baadhi ya wajumbe wa halmashauri yake
walihudhuria ili kuandika muhtasari wa maelezo ya mjumbe wa papa. (148) Kwa nguvu zote za elimu
yake na ushawishi wake, Aleander alijipanga kuipindua kweli. Shutuma juu ya shutuma zilisemwa dhidi

106
Ibid., book 7, chapter 1
107
Ibid., book 7, chapter 1
108
Wylie, b. 6, ch. 4
81
ya Luther kama adui wa kanisa na serikali, adui wa walio hai na waliokufa, wa watumishi wa kanisa na
waumini wa kawaida, wa mabaraza na Wakristo binafsi. "Makosa ya Luther yatosha kuwa sawa na
wazushi mia moja elfu,” alisema kuhalalisha kuchomwa moto.
Katika kuhitimisha, aliazimia kutupa lawama kwa wale waliokubali imani ya matengenezo: "Hawa
Walutheri ni nani? Kundi la walimu mafidhuli, makasisi wapotofu, watawa wapotofu, wanasheria
wasiojua kitu, na wakuu walioanguka, na watu wa kawaida ambao wamedanganywa na kupotoshwa.
Kundi la Wakatoliki linawazidi hawa mbali kiasi gani kwa idadi, uwezo, na nguvu! Tamko la kauli moja
toka kwa wajumbe wa baraza hili litatoa maamzi kwa urahisi, litamwonya asiye na busara, litaamua
kuhusu wasio na msimamo, na litampa nguvu aliye dhaifu." 109
Katika kila kizazi watetezi wa ukweli wameshambuliwa kwa silaha kama hizo. Hoja hizo hizo ndizo
zinazotolewa dhidi ya wote wanaodiriki kusema mafundisho ya wazi na ya moja kwa moja ya Mungu,
kinyume cha upotofu ulioanzishwa na watu. "Nani hawa wanaohubiri mafundisho mageni?" Ndivyo
wasemavyo wale wanaotaka dini ya umaarufu inayopendwa na wengi. "Hawana elimu, ni wachache,
wanatoka katika tabaka maskini. Lakini wanadai kwamba wanayo kweli, na ya kwamba ni watu
walioteuliwa na Mungu. Hawajui kitu na wamedanganyika. Kanisa letu lina ushawishi kiasi gani na lina
watu wengi maarufu kiasi gani! Tuna watu wenye heshima wangapi, tena ambao wamesoma! Upande
wetu una nguvu nyingi kiasi gani!" Hizi ni hoja ambazo zina mvuto kwa ulimwengu; lakini si kwamba
maneno hayo yanayotumika leo zaidi ya vile yalivyotumika wakati wa Mwanamatengenezo huyo.
Matengenezo hayakuisha na Luther, kama wengi wanavyodhani. Yataendelea hadi kufungwa kwa
historia ya dunia hii. Luther alikuwa na kazi kubwa ya kupokea nuru ambayo Mungu aliruhusu
imwangazie na kuielekeza kwa watu wengine; lakini bado hakupokea nuru yote ambayo ilikuwa itolewe
kwa ulimwengu. Tangu wakati ule hadi sasa, nuru mpya imekuwa (149) ikiendelea kuangazia Maandiko,
na ukweli mpya umeendelea kufunuliwa.
Hotuba ya balozi wa papa ililifanya Baraza kutekewa. Luther hakuwa pale, akiwa na ukweli ulio wazi wa
neno la Mungu, ili kumshinda huyu shujaa wa upapa. Hakuna aliyejaribu kumtetea Mwanamatengenezo.
Ulijionyesha msukumo si tu wa kutaka kumshutumu yeye na mafundisho yake, bali pia ikiwezekana
kuung’oa kabisa uzushi. Roma ilikuwa imefurahia fursa nzuri iliyopata kujitokeza na kuitetea njia yake.
Yote ambayo angeweza kuyasema kujithibitisha yalikuwa yamesemwa. Lakini kilichoonekana kuwa
ushindi kwake kilikuwa ishara ya kushindwa. Baada ya hapo tofauti kati ya ukweli na uongo ingeonekana
bayana zaidi, maana mapambano yangekuwa ya mahali pa wazi. Tangu siku ile Roma isingesimama
kamwe kwa usalama kama ilivyokuwa kabla.
Wakati ule ambao wajumbe walio wengi wa Baraza wasingesita kumtoa Luther kwa ajili ya kisasi cha
Roma, wengi wao waliona udhalimu uliokuwa unaendelea katika kanisa, na walitamani kukomeshwa kwa
maovu yalikuwa yanafanywa dhidi ya watu wa Ujerumani kama matokeo ya udhalimu na ulafi wa
mamlaka ya Roma. Balozi alikuwa amewasilisha kanuni ya upapa kwa namna inayoupendelea. Sasa
Bwana alimsukuma mjumbe mmoja wa Baraza kutoa mwelekeo wa kweli wa madhara ya utawala wa
mabavu wa kipapa. Kwa ujasiri wa kiungwana, Duke George wa Saksoni alisimama katika ukumbi wa
Baraza na kuweka bayana ukweli wa kutisha kuhusu udanganyifu na machukizo ya upapa, na matokeo
yake. Wakati wa kuhitimisha alisema hivi:
"Haya ni baadhi ya maovu yanayolia dhidi ya Roma. Imeweka kando aibu zote, na inachotafuta tu ni . . .
pesa, pesa, pesa, . . . kiasi kwamba viongozi wa kiroho ambao wangefundisha ukweli, hawatamki kitu

109
D’Aubigne, book 7, chapter 3
82
bali uongo, na si kwamba wanavumiliwa tu, bali pia wanapewa zawadi, kwa sababu kadiri
wanavyodanganya sana ndivyo wanavyopata zaidi. Kutoka katika chemchemi hii chafu hububujika maji
hayo machafu. Ufisadi hunyosha mkono kuelekea kwenye tamaa ya mali. . . . Lakini, ni kashfa
iliyosababishwa na watumishi wa kanisa wanaozitupa roho nyingi zilizo maskini katika laana ya milele.
Lazima matengenezo ya jumla yafanyike." 110
Upinzani wenye nguvu zaidi dhidi ya (150) upapa usingetolewa na Luther mwenyewe; na ile hali ya
kwamba msemaji huyu alikuwa adui mkubwa wa Mwanamatengenezo iliyapa maneno yake uzito
mkubwa zaidi.
Laiti kama macho ya baraza yangefumbuliwa, wangeona malaika wa Mungu wakiwa katikati yao,
wakiwasha miale ya nuru katikati ya giza la madanganyo na kufungua mawazo na mioyo kwa ajili ya
kuupokea ukweli. Ilikuwa nguvu ya Mungu na hekima yake iliyoendesha hata wapinzani wa
matengenezo, na kwa hiyo ikatayarisha njia kwa ajili ya kazi kubwa iliyokuwa tayari kukamilishwa.
Martin Luther hakuwepo pale; lakini sauti yake Yeye aliye mkuu kuliko Luther ilikuwa imesikika katika
baraza.
Kamati iliundwa na Baraza haraka ili kuandaa orodha ya mambo mabaya ya upapa yaliyofanywa zaidi
kwa Wajerumani. Orodha hii, iliyokuwa na mambo mia moja na moja ya unyanyasaji, yaliwasilishwa
kwa mfalme, pamoja na ombi kwamba achukue hatua za haraka ili kusahihisha maovu hayo. "Ni upotevu
wa roho za Wakristo kiasi gani," walisema waombaji wale, "unyang’anyi ulioje, utozaji wa fedha kwa
mabavu kiasi gani, mambo yanayohusu kashfa zinazomzunguka kiongozi wa kiroho wa jamii ya Wakristo
duniani! Ni jukumu letu kuepusha maangamizi na kufedheheshwa kwa watu wetu. Kwa sababu hii
tunakuomba kwa heshima kubwa, lakini kwa kusisitiza sana, utoe amri marekebisho makubwa
yafanyike, na uyafanye yakamilishwe." 111
Sasa Baraza lilihitaji Mwanamatengenezo aje mbele yao. Licha ya vikwazo, mapingamizi na vitisho vya
Aleander, hatimaye mfalme alikubali, na Luther akaitwa barazani. Pamoja na wito huo, alipewa pia hati
ya usalama ya kusafiria, ikimhakikishia kurejea kwa amani. Vitu hivi vililetwa Wittenberg na mjumbe,
aliyepewa kazi ya kumfikisha Luther Worms.
Rafiki za Luther waliingiwa na hofu na wasiwasi. Wakijua chuki na uadui uliokuwepo dhidi yake,
walihofu kwamba hata hati ya usalama ya kusafiria isingeheshimiwa, na walimuonya kwamba
asihatarishe maisha yake. Luther akajibu akasema: "Watu wa upapa hawapendi mimi niende Worms,
bali wanataka (151) nilaaniwe na kufa. Hayo si kitu. Msiombe kwa ajili yangu, bali kwa ajili ya neno la
Mungu. . . . Kristo atanipa Roho wake nami nitawashinda watumishi wa uongo. Nawadharau maishani
mwangu; nitawashinda kwa kifo changu. Wanashughulika sana ili kunilazimisha nifute mafundisho
yangu; na hivi ndivyo nitakavyokiri: Nilisema kabla kwamba papa alikuwa makamu wa Kristo; sasa
natangaza kwamba ni mpinzani wa Bwana wetu, na mtume wa mwovu." 112
Luther asingeingia katika safari ya hatari peke yake. Licha ya yule mjumbe wa mfalme, kulikuwa na
rafiki zake watatu wenye msimamo mkubwa walioazimu kumsindikiza. Melanchthon alikuwa na hamu ya
kujiunga nao. Moyo wake ulikuwa karibu na ule wa Luther, na alitaka amfuate, kama ikibidi, hata
gerezani au mautini. Lakini hitaji lake hili lilikataliwa. Kama Luther angeangamia, tumaini la
Matengenezo lingebaki kwa kijana huyu mtenda-kazi pamoja naye. Wakati wa kuagana na Melanchthon,

110
Ibid., book 7, chapter 4
111
Ibid., book 7, chapter 4
112
Ibid., book 7, chapter 6
83
Mwanamatengenezo alisema: "Ikiwa sitarudi, adui zangu wakiniua, wewe endelea kufundisha, na
simama imara katika kweli. Fanya kazi mahali pangu. . . . Kama utasalia wewe, kifo changu kitakuwa na
madhara kidogo." 113 Wanafunzi na raia waliokuwa wamekusanyika kushuhudia kuondoka kwa Luther
waliguswa sana. Makutano ambao walikuwa wameguswa na injili, walimtakia safari njema huku
wakitokwa na machozi. Hivyo ndivyo Mwanamatengenezo na wasindikizaji wake walivyoondoka
Wittenberg.
Wakiwa safarini waliona kwamba mawazo ya watu yalijawa na hisia za huzuni. Katika baadhi ya miji
hakuna heshima iliyoonyeshwa kwao. Walipofanya kituo usiku, kasisi mmoja mwenye moyo wa urafiki
alionyesha hofu yake kwa kumwonyesha Luther tukio la kuuawa kwa mfia-dini aliyekuwa
mwanamatengenezo wa Italia. Siku iliyofuata walifahamu kwamba maandishi ya Luther yalikuwa
yamelaaniwa kule Worms. Wajumbe wa mfalme walikuwa wanatangaza amri ya mfalme na kuwataka
watu walete maandiko ya Luther kwa mahakimu. Mpiga-mbiu mmoja, akihofia usalama wa Luther katika
baraza, na akidhani kwamba maamuzi kuhusu yeye yalikuwa yameshafanyika, aliuliza kama bado Luther
alitaka kwenda kule. Luther alijibu: "Ingawa nimetahadharishwa katika kila mji, nitaendelea mbele." 114
(152) Luther alipokelewa kwa heshima kule Erfurt. Akiwa amezungukwa na vikundi vinavyostaajabu,
alipita katika mitaa ambayo alikuwa mara kwa mara ameipita alipokuwa mtawa anayeombaomba wakati
akiwa na mkoba wake. Alitembelea chumba chake katika nyumba ya kitawa, na akatafakari juu ya
mapambano aliyokuwa nayo pindi nuru hii iliyofurika Ujerumani sasa ilipomwagwa kwake. Alisikia
kutakiwa kuhubiri. Alikuwa amezuiliwa kufanya hivyo, lakini mpiga-mbiu alimpa ruhusa, na mtawa huyu
aliyekuwa anatumika kwa kazi za kuchosha zamani, akapanda mimbarani.
Alisema maneno ya Kristo kwa makutano waliokusanyika, "Amani na iwe kwenu." "Wanafalsafa,
madaktari wa falsafa, na waandishi," alisema, "wamejitahidi kuwafundisha watu njia ya kuupata uzima
wa milele, wala hawakufanikiwa. Sasa nitawaeleza ninyi njia hiyo: . . . Mungu amemfufua Mtu mmoja
kutoka katika wafu, Bwana Yesu Kristo, ili ya kwamba aharibu kifo, akomeshe dhambi, na afunge
milango ya kuzimu. Hii ni kazi ya wokovu. . . . Kristo ameshinda! Hizi ndiyo habari njema; nasi
tumeokolewa kwa kazi yake, na si kwa kazi yetu wenyewe. . . . Bwana wetu Yesu Kristo alisema, 'Amani
iwe nanyi; tazameni mikono yangu;' hii ni kusema, Tazama ee mwanadamu! Ni mimi, Mimi peke yangu,
niliyeziondoa dhambi zako, na kukukomboa; na sasa una amani, asema Bwana."
Aliendelea kusema, akionyesha kwamba imani ya kweli itadhihirishwa na maisha matakatifu. "Kwa kuwa
Mungu ametuokoa, na tufanye kazi zetu katika mpango unaokubalika mbele zake. Je wewe ni tajiri?
Hebu mali yako itumike kumhudumia maskini. Je wewe ni maskini? Hebu utumishi wako uwe ule
unaokubalika kwa tajiri. Ikiwa kazi zako ni kwa ajili yako wewe peke yako, huduma unayojidai kuifanya
kwa Mungu ni ya uongo." 115
Watu walimsikiliza kama vile walitamani kuendelea kusikiliza. Mkate ulimegwa kwa ajili ya roho hizi
zilizokuwa na njaa. Kristo aliinuliwa mbele yao juu kuliko mapapa, mabalozi wa papa, watawala wakuu
na wafalme. Luther hakuwarejesha watu katika hatari na shida alizokuwa nazo. Hakutaka kuvutia kwake
mwenyewe mawazo na huruma za watu. Katika kumtafakari Kristo, alipoteza uwezo wa kujitazama
yeye binafsi. Alijificha nyuma ya Mtu wa Kalvari, akitafuta kumwonyesha Yesu kama Mkombozi wa
mdhambi.

113
-- Ibid., book 7, chapter
114
Ibid., book 7, chapter 7
115
Ibid., book 7, chapter 7
84
(153) Kadiri Mtengenezaji alivyoendelea na safari yake, aliangaliwa na watu kwa shauku kubwa. Kundi
kubwa la watu lilimkusanyikia, na kwa lugha ya upendo walimwonya kuhusu nia mbaya ya Warumi.
Wengine walisema, "Watakuchoma moto, na kuuacha mwili wako katika hali ya majivu, kama
walivyofanya kwa John Huss." Luther akajibu na kuwaambia, "Hata wakiwasha moto njia yote tangu
Worms hadi Wittenberg, moto mkubwa unaofika hadi mbinguni, mimi ningetembea ndani ya moto kwa
jina la Bwana; ningefika mbele yao; ningeingia katika taya za mroho huyu, na kuyavunja meno yake,
nikimkiri Bwana Yesu Kristo." 116
Habari ya kukaribia kwake kuingia mjini Worms ilisababisha msukosuko mkubwa. Rafiki zake
walihangaika kwa ajili ya usalama wake; adui zake nao waliogopa kuhusu kufanikiwa kwa mpango wao.
Juhudi zilifanywa kumkatisha tamaa asiingie mjini. Kwa shinikizo la watu wa upapa aliombwa kwenda
katika ngome ya mkuu wa askari wa nyumba ya mfalme, ambaye alikuwa ni mtu mwema, ambako,
ilisemekana kwamba, matatizo yote yangeweza kusuluhishwa kwa amani. Rafiki zake walijaribu
kumwogopesha kwa kumweleza hatari zilizokuwa zinamkabili. Jitihada zao zote zilishindwa. Pasipo
kuyumbishwa, Luther alitangaza kwa nguvu: "Hata kama kungekuwa na mashetani wengi waliojitandaza
mjini Worms kama vigae vilivyo kwenye mapaa ya nyumba, bado mimi ningeingia humo." 117
Alipofika mjini Worms, kusanyiko kubwa lilijitokeza kumkaribisha. Haijawahi kutokea umati mkubwa
kama huo kukusanyika hata kumsalimu mfalme mwenyewe. Taharuki ilikuwa kubwa, na kutoka katikati
ya mkusanyiko ule sauti za huzuni na hisia za maumivu ziliimba wimbo wa msiba kama onyo kwa Luther
kuhusu hatima iliyokuwa inamsubiri. "Mungu atakuwa mlinzi wangu," alisema Luther, huku akishuka
kutoka kwenye gari lake.
Watu wa upapa hawakuamini kama Luther angethubutu kuingia Worms, na kufika kwake kuliwajaza
hofu. Mfalme aliwataka wajumbe wa baraza kuangalia namna ya kushughulikia jambo hilo. Mmoja wa
maaskofu, mtu wa upapa kweli kweli, akasema: "Tumeshughulika na jambo hili kwa muda mrefu sana.
Hebu heshima yako ya kifalme ishughulike na mtu huyu mara moja. Je Sigismund hakufanya John Huss
kuchomwa moto? Hatulazimiki kutoa au (154) kuheshimu hati ya usalama ya kusafiria ya mzushi."
"Hapana," alisema mfalme, "lazima tuheshimu ahadi yetu." 118 Kwa hiyo ikakubalika kwamba
Mwanamatengenezo asikilizwe.
Mji wote ulikuwa na hamu ya kumwona mtu maarufu huyu, na wageni kwa msururu walikuwa tayari
wamejaza nyumba aliyofikia. Luther alikuwa hajapata nafuu ya ugonjwa aliokuwa nao; alikuwa
amechoka na safari, iliyokuwa imechukua majuma mawili kamili; alihitaji kujiandaa kukutana na tukio
kubwa lililokuwa linamsubiri kesho yake, na alihitaji mahali pa utulivu na pa pumziko. Lakini hamu ya
watu kutaka kumwona ilikuwa kubwa kiasi kwamba alipata masaa machache tu ya kupumzika wakati
waheshimiwa, watu wakubwa wa jeshi katika jumba la mfalme, makasisi, na raia walipokusanyika ili
kumwona. Miongoni mwao, walikuwemo wale wakuu ambao walikuwa wamedai kwamba mfalme
aongoze kufanya matengenezo ya kuondoa mambo mabaya ya dini na ambao, kama alivyosema Luther,
"wote walikuwa wamewekwa huru kwa injili yangu." 119 Maadui, pamoja na marafiki, walikuja
kumwangalia mtawa huyu jasiri; lakini yeye aliwapokea kwa upole na uthabiti, akiwajibu wote kwa
ufasaha na hekima. Mwonekano wake ulikuwa wa ujasiri na wa kutia moyo. Uso wake mwembamba,

116
Ibid., b. 7, ch. 7
117
Ibid., book 7, chapter 7
118
Ibid., b. 7, ch. 8
119
Martyn, page 393

85
ukiwa na alama za mahangaiko na maradhi, ulikuwa na mwonekano wa ukarimu na furaha. Maneno yake
ya dhati na ya kina yalimpa uwezo ambao hata adui zake hawakuyastahimili kabisa. Marafiki na maadui
zake wote walijawa na mshangao. Baadhi walishawishika kukubali kwamba nguvu za Mungu
zilimwezesha; wengine walisema, kama Mafarisayo walivyosema kuhusu Yesu: "Ana pepo."
Siku iliyofuata, Luther alipewa wito wa kufika katika Baraza kwa ajili ya shauri lake. Afisa wa mfalme
alipewa kazi ya kumpeleka katika ukumbi mbele ya wajumbe; hata hivyo alifika kule kwa shida. Katika
njia yote kulikuwa na umati mkubwa wa watu waliokusanyika ili kumwona mtawa huyu aliyediriki
kupambana na mamlaka ya papa.
Alipokaribia kuingia mbele ya wahukumu wake, jenerali mmoja mzee, shujaa katika mapigano mengi,
alimwambia kwa upendo: "Maskini mtawa wee, maskini mtawa, sasa unaenda kuonyesha msimamo wako
ulio bora kuliko wangu au vile makapteni wengine walivyopata kuonyesha wakati wa mapigano makali
ya damu. Lakini ikiwa madai yako ni ya haki, na kama una hakika nayo, songa mbele katika jina la
Mungu, na usiogope (155) kitu chochote. Mungu hatakuacha." 120 Luther alisimama mbele ya baraza kwa
mbali. Mfalme akakaa katika kiti chake cha enzi. Alikuwa amezungukwa na watu mashuhuri katika
himaya yake. Kamwe hakupata mtu yeyote kusimama mbele ya baraza lenye hadhi kubwa zaidi ya hili
ambalo Martin Luther alisimama mbele yake ili kuitetea imani yake. "Mwonekano huu peke yake ulikuwa
ni ishara ya ushindi dhidi ya upapa. Papa alikuwa amemlaani mtu huyu, na sasa alikuwa mbele ya
mahakama ambayo, kwa namna lilivyokuwa, lilikuwa juu ya papa. Papa alikuwa amemtenga na kanisa,
na kumtenga mbali na jamii ya wanadamu; lakini bado aliitwa kwa lugha ya heshima, na kupokelewa
katika mahakama ya juu kuliko zote ulimwenguni. Papa alikuwa amemhukumu kwa kumnyamazisha, na
sasa alikuwa azungumze na maelfu ya wasikilizaji wanaosikiliza kwa makini wakiwa wamekusanyika
kutoka maeneo ya mbali katika sehemu zote za ulimwengu wa Wakristo. Mageuzi makubwa yalikuwa
yamefanywa kupitia Luther. Tayari Roma ilikuwa inashuka kutoka katika kiti chake cha enzi, na ilikuwa
sauti ya mtawa huyu iliyosababisha aibu hii." 121
Mbele ya baraza hili lenye nguvu na hadhi kubwa Mtengenezaji huyu aliyezaliwa katika hali ya chini
alionekana kuogopa na kutahayari. Wakuu kadhaa, waliong’amua hisia alizokuwa nazo walimwendea, na
mmoja akamnong’oneza akisema: "Usiwaogope wauao mwili, wasiweze kuiua roho." Mwingine akasema:
"Watakapowapeleka mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, mtapewa saa ile na Roho wa Baba
yenu mtakayosema." Hivyo ndivyo maneno ya Kristo yalivyoletwa na wakuu hawa wa ulimwengu ili
kumtia nguvu mtumishi wake katika saa yake ya kujaribiwa.
Luther aliongozwa kwenda katika sehemu ya mbele kabisa ya kiti cha mfalme. Ukimya mkubwa ulilijaza
baraza lote. Ndipo afisa wa mfalme aliposimama na, akionyesha mkusanyiko wa maandishi ya Luther,
alitaka Mwanamatengenezo ajibu maswali mawili - kama anakubali kwamba ni ya kwake, na kama
alikuwa tayari kukiri na kuyafuta mawazo yaliyomo aliyokuwa anaendeleza. Baada ya majina ya vitabu
vile (156) kusomwa, Luther alijibu kulingana na swali la kwanza, akikubali kwamba vitabu vile ni vyake.
"Kuhusu swali la pili,” Alisema, “kwa kuwa ni swali ambalo linahusu mambo ya imani na wokovu wa roho
za watu, na ndani yake mna maneno ya Mungu, hazina kubwa na ya thamani kuliko zote iwe mbinguni
au duniani, ningetenda pasipo busara ikiwa ningejibu pasipo kutafakari. Ningeweza kukubali kwa hali ya
chini kuliko hali halisi inavyotaka, au nikajibu zaidi ya vile ukweli unavyotaka, na kwa hiyo ikawa
dhambi dhidi ya kile Yesu alichosema: 'Mtu yeyote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana

120
D'Aubigne, book 7, chapter 8
121
Ibid., book 7, chapter 8
86
mbele za Baba yangu aliye mbinguni.' Kwa sababu hii namsihi mwenye taadhima mfalme, kwa
unyenyekevu wote, aruhusu nipewe muda, ili nitoe jibu pasipo kukiuka neno la Mungu. 122
Kwa kutoa ombi hili, Luther alienenda kwa hekima. Njia aliyotumia kufanya jambo hili ililishawishi
baraza kwamba hakutenda kwa dharau wala harara. Utulivu wake na kujitawala, tofauti na mtu
aliyedhaniwa kuwa shupavu na asiyetaka maridhiano, viliongeza nguvu upande wake, na ilimwezesha
baada ya hapo kujibu kwa umakini zaidi, kwa maamuzi, hekima, na ujasiri, kiasi cha kuwashangaza na
kuwafadhaisha adui zake, na kukemea chuki yao na kiburi chao.
Siku iliyofuata alitakiwa kujitokeze ili kutoa jibu lake la mwisho. Kwa muda fulani moyo wake ulizama
ndani yake alipotafakari nguvu zilizokuwa zimeungana kinyume cha kweli. Imani yake ilitishwa; hofu na
kugwaya vilimjia, na woga ulimjaa. Hatari ziliongezeka kwake mara dufu; adui zake walionekana
kushinda, na nguvu za giza zilijiinua. Ilikuwa kama vile mawingu yamemzunguka na kumtenganisha na
Mungu. Alitaka sana kupata hakika kama Bwana wa majeshi angekuwa naye. Katika maumivu ya moyo,
alijitupa chini kifudifudi na kutoa kilio cha kurarua moyo, ambacho hakuna awezaye kukifahamu kwa
ukamilifu isipokuwa Mungu.
Aliomba: "Ee Mwenyezi Mungu wa milele, ulimwengu huu unatisha kama nini! Tazama, unafunua kinywa
chake kunimeza, nami nina imani ndogo kwako. . . . Ikiwa nitaweka imani yangu kwa (157) nguvu ya
ulimwengu huu, yote yamekwisha. . . . Saa yangu ya mwisho imefika, hukumu yangu imekwisha
kutamkwa. . . . Ee Mungu, unisaidie dhidi ya hekima ya ulimwengu. Fanya hili, . . . Wewe peke yako; . .
. maana hii si kazi yangu, bali yako. Sina la kufanya hapa, sina namna ya kupambana na wakuu hawa wa
ulimwengu. . . . Lakini kazi ni yako, . . . na ni kazi ya haki na ya milele. Ee Bwana, nisaidie! Mungu
mwaminifu na usiyebadilika, hakuna mwanadamu aliye tumaini langu. . . . Yote yaliyo ya mwanadamu
hayana hakika, yote yatokayo kwa mwanadamu yanashindwa. . . . Wewe umenichagua kwa kazi hii. . . .
Simama upande wangu, kwa ajili ya Mpendwa wako Yesu Kristo, aliye mlinzi wangu, ngao yangu, na
ngome yangu imara." 123
Yeye aliye mtoaji wa hekima yote alimruhusu Luther apate kutambua hatari kubwa iliyomkabili, ili
asitegemee nguvu zake mwenyewe na kujiingiza haraka na kwa kiburi chake cha makusudi katika hatari
ile. Hata hivyo, kilichomfanya azidiwe na hofu kuu si kuogopa mateso yake binafsi, yaani, hofu ya
mateso, au kifo ambacho kilionekana kimekaribia sana kwake. Alikuwa amefikia kilele cha hatari, naye
alijisikia kuwa hajitoshelezi mwenyewe kuikabili. Kupitia udhaifu wake kazi ya ukweli ingepoteza
uelekeo. Alipigana mwereka na Mungu, si kwa ajili ya usalama wake, bali kwa ajili ya ushindi wa injili.
Kama kwa Israeli, katika mapambano ya usiku ule akiwa mpweke kando ya kijito, haya yalikuwa
mapambano ya nafsi yake. Kama kwa Israel, alishindana na Mungu. Katika maneno yake ya kukosa
msaada imani yake ilifungamanishwa kwa Kristo, yeye aliye Mwokozi mwenye nguvu. Alitiwa nguvu na
kuhakikishiwa kwamba hatakuwa peke yake barazani. Amani ilirudi moyoni mwake, na alifurahi kwamba
aliruhusiwa kuinua juu neno la Mungu mbele ya watawala wa mataifa.
Akiwa ameelekeza mawazo yake kwa Mungu, Luther alijiandaa kwa pambano lililokuwa mbele yake.
Alifikiri kuhusu mpango wake wa kujibu lile swali, akapima aya zilizo katika maandishi yake, na
akachukua uthibitisho wa msimamo wake kutoka katika Maandiko Matakatifu. Halafu, akiwa ameweka
mkono wake wa kushoto juu ya Kitabu Kitakatifu, kilichokuwa kimefunguliwa mbele yake, aliinua mkono

122
D’Aubigne, book 7, chapter 8
123
Ibid., book 7, chapter 8
87
wake wa kulia juu mbinguni na kuapa "kuwa mwaminifu kwa injili, na (158) kuwa radhi kuitetea imani
yake, hata kama ni kwa kutia muhuri ushuhuda kwa damu yake." 124
Wakati alipopelekwa tena mbele ya Baraza, wapinzani wake hawakuona tena kwake dalili za woga wala
aibu. Akiwa mtulivu na mwenye amani, lakini mwenye ujasiri na nguvu, alisimama kama shahidi wa
Mungu katikati ya wakuu wa dunia. Afisa wa mfalme alimtaka aseme kuhusu uamuzi wake kama alitaka
kukiri na kuyafuta mafundisho yake. Luther alitoa jibu lake kwa sauti ya kujishusha na kujinyenyekeza,
bila fujo wala harara. Mwonekano wake ulikuwa wa staha na heshima; lakini alionyesha kujiamini na
furaha kiasi cha kulishangaza baraza.
Luther akasema, "Mwenye taadhima sana mfalme, waheshimiwa mabwana, niko mbele yenu leo hii,
kulingana na agizo nililopewa jana, na kwa neema ya Mungu naomba waheshimiwa mnisikilize kwa
hisani yenu ninapotetea kazi ambayo nimehakikishiwa kwamba ni ya haki na ya kweli. Ikiwa, kwa
sababu ya kutokujua kwangu, nitakiuka taratibu za baraza, naomba mnisamehe; maana sikukulia katika
majumba ya kifalme, bali katika nyumba iliyotengwa ya watawa." 125 Kisha, akiendelea katika swali,
alisema kwamba machapisho yake hayakuwa ya aina moja. Baadhi yanasisitiza imani na matendo mema,
hata adui zake waliyasifu kwa sababu si tu kwamba hayakuwa na madhara bali pia yalikuwa na
manufaa. Kuyakataa haya ni sawa na kuukataa ukweli ambao pande zote zinaukubali. Kundi la pili la
machapisho lina habari zinazohusu udhalimu na matendo mabaya ya upapa. Kukataa kazi hizi ni sawa na
kuimarisha udhalimu wa Roma na kufungua mlango zaidi wa makufuru mengi. Katika kundi la tatu la
vitabu vyake alikuwa amewashambulia watu binafsi waliokuwa wametetea maovu. Kuhusu machapisho
haya aliungama wazi kwamba alikuwa amefanya ukali kuliko ilivyompasa. Hakudai kuwa hana makosa;
lakini hakubatilisha vitabu vile, maana hilo lingewaimarisha maadui wa ile kweli, nao wangetumia tukio
hili kuwapinga watu wa Mungu kwa ukatili mkubwa zaidi.
(159) "Lakini mimi ni mwanadamu tu, na si Mungu," aliendelea kusema; "kwa hiyo mimi nitajitetea
kama Kristo alivyofanya: 'Kama nimesema jambo baya basi muushuhudie ubaya huo.' . . . Kwa neema ya
Mungu, nawasihi, nakusihi mheshimiwa sana mfalme, na ninyi, waheshimiwa watawala, na watu wote
wa makundi yote, kunishuhudia kwa maandiko ya manabii na mitume ya kwamba nimekosea.
Nikishawishika kuhusu hilo, nitakiri kila kosa, tena nitakuwa mtu wa kwanza kushika vitabu vyangu na
kuvitupa motoni.
"Naamini kwamba kile nilichosema wazi wazi kinaonyesha kwamba nimepima na kutathmini kwa umakini
hatari iliyo katika nafasi yangu sasa; lakini mbali zaidi kuliko hofu, nafurahi kuona kwamba injili ni kazi
ya shida na upinzani, kama ilivyokuwa nyakati za zamani. Hiyo ndiyo tabia, na ndiyo hatima ya neno la
Mungu. 'Sikuja kuleta amani duniani, bali upanga,' alisema Yesu. Mungu ni wa ajabu na wa kutisha
katika mashauri yake; jihadharini msije mkalitesa neno la Mungu, mkidhani ya kwamba mnazima
upinzani, kumbe mkajiletea gharika ya hatari, ya majanga ya sasa, na uangamivu wa milele. . . .
Ningeweza kunukuu mifano mingi kutoka katika maneno matakatifu ya Mungu. Ningeweza kusema
habari za Mafarao, wafalme wa Babeli, na wale wa Israeli, ambao kazi zao hazikuwaingiza katika
uharibifu mkubwa zaidi kuliko wakati walipotegemea mashauri ya mabaraza yao, yaliyoonekana kuwa ya
hekima, ya kuimarisha utawala wao. 'Mungu huhamisha milima, wala hawajui" 126

124
Ibid., book 7, chapter 8
125
Ibid., book 7, chapter 8
126
Ibid., book 7, chapter 8
88
Luther alikuwa amezungumza kwa lugha ya Kijerumani; sasa aliombwa kurudia maneno yale yale kwa
lugha ya Kilatini. Ingawa alikuwa amechoshwa na jitihada za awali, alikubali, na akatoa hotuba yake
tena, kwa uwazi ule ule na nguvu kama ya kwanza. Uwezo wa Mungu uliongoza katika jambo hili. Akili
za wengi wa watawala zilipofushwa na upotofu na udhalimu kiasi kwamba hawakuiona nguvu ya hoja ya
Luther awali; kwa hiyo kuirudia hotuba yake kuliwawezesha kuelewa vizuri hoja zilizosemwa.
(160) Wale waliopuuza na kufumba macho yao wasione nuru, na wakaazimia kwamba hawataki
kushawishiwa na ukweli, walighadhabishwa na nguvu ya maneno ya Luther. Alipomaliza kuongea,
msemaji wa Baraza alisema kwa hasira: "Haujajibu swali uliloulizwa. . . . Unatakiwa kutoa jibu lililo
fupi na la wazi. . . . Je unatengua mafundisho yako au la?"
Mwanamatengenezo akajibu na kusema: "Kwa kuwa mheshimiwa sana mfalme na wakuu wote mmetaka
nitoe jibu rahisi na kwa ufupi, basi nitawapa, nalo ni hili: Mimi siwezi kuisalimisha imani yangu kwa
papa wala kwa mabaraza, kwa sababu iko dhahiri kama mchana ulivyo ya kwamba wamekuwa
wakikosea na kupingana wao kwa wao mara kwa mara. Kwa hiyo ikiwa sitashawishiwa vinginevyo na
ushuhuda wa Maandiko au hoja zilizo wazi kabisa, nisiposhawishiwa kwa nukuu nilizotumia, na
wasipoheshimu dhamiri yangu iliyofungamanishwa na neno la Mungu, siwezi na sitaweza kutengua
mafundisho, maana si salama kwa Mkristo kusema kinyume na dhamiri yake. Nasimamia hapo, siwezi
kufanya jambo jingine tofauti; Mungu na anisaidie. Amina." 127
Hivyo ndivyo mtu huyu wa haki alivyosimama juu ya msingi wa hakika wa neno la Mungu. Nuru ya
mbinguni ilimtia nguvu. Uimara wake na usafi wa tabia yake, amani na furaha aliyokuwa nayo,
vilithibitishwa kwa wote wakati alipoishuhudia mamlaka ya makosa na kuidhihirisha imani inayoushinda
ulimwengu.
Kwa muda baraza lote lilikuwa kimya likiwa limeduwazwa. Katika jibu la kwanza Luther alikuwa
ameongea kwa sauti ya chini, kwa heshima na unyenyekevu. Tafsiri ya wana wa Kiromi ilikuwa ni
kwamba hii ni ishara ya kuanza kushindwa kwa ujasiri wake. Walichukulia kwamba ombi lake la
kuchelewesha jibu lilikuwa mwanzo wa kukiri kwake. Charles mwenyewe, akimwona mtawa aliyechoka,
uvaaji wake, na maneno yake mepesi, alisema: "Mtawa huyu hawezi kunifanya mzushi." Ujasiri na
msimamo alioonyesha sasa, pamoja na nguvu na ukweli wa hoja yake, vilisababisha mshangao kwa
makundi yote. (161) Mfalme aliunguruma akisukumwa na mshangao: "Huyu mtawa anaongea kwa moyo
wa ujasiri usioyumbishwa." Wengi wa watawala wa Ujerumani walimwangalia huyu mwakilishi wa taifa
lao kwa fahari kubwa.
Wafuasi wa Roma walikuwa wameshindwa kabisa; madai yao yalionekana yasiyokubalika. Waliazimia
kudumisha mamlaka yao, si kwa kufuata Maandiko, bali kwa vitisho, ndiyo hoja ya Roma isiyoshidwa.
Akasema msemaji wa Baraza hivi: "Kama haukani msimamo, mfalme na serikali za himaya yote
watatafakari namna ya kufanya dhidi ya mzushi asiyerekebishika."
Marafiki zake Luther, waliokuwa wamefuatilia maelezo yake ya utetezi kwa furaha kubwa,
walitetemeshwa na maneno haya; lakini daktari mwenyewe alisema kwa pole: "Mungu na awe msaada
wangu, maana siwezi kukiri lolote." 128
Aliagizwa kuondoka katika Baraza wakati wajumbe wakishauriana jambo la kufanya. Ilihisiwa kwamba
hali ya hatari imekuja. Msimamo wa Luther wa kukataa katakata kukiri ungeathiri historia nzima ya
kanisa kwa vizazi vingi. Iliamriwa kwamba apewe nafasi moja zaidi ya kukiri. Aliletwa barazani kwa

127
Ibid., b. 7, ch. 8
128
Ibid., b. 7, ch. 8
89
mara ya mwisho. Swali liliulizwa tena, likimtaka kusema kama anafuta mafundisho yake. "Sina jibu
jingine tena zaidi ya lile nililotoa," Alisema Luther. Ilikuwa dhahiri kwamba asingeweza kushawishika
kujisalimisha kwa mamlaka ya Roma, iwe ni kwa ahadi au kwa vitisho.
Viongozi wa kipapa waliudhika sana kwamba ile mamlaka yao, iliyowafanya wafalme na wakuu
kutetemeka, inadharauliwa na mtawa yule wa hali duni; wakaazimia kumwonyesha ukali wa ghadhabu
yao kwa kumtesa hadi kumpotezea maisha yake. Lakini Luther, akiwa ameng’amua hatari iliyomkabili,
alikuwa amenena na wote kwa heshima na utulivu wa Kikristo. Maneno yake hayakuwa ya kiburi,
harara, wala yaliyowasilishwa isivyo. Hakujiangalia yeye, wala wakuu wale waliokuwa wamemzunguka
pale, aliona tu kwamba yuko mbele ya Yeye aliye mkuu kuliko mapapa, maaskofu, wafalme, na
watawala. Kristo alikuwa amenena kupitia ushuhuda ule wa Luther, kwa nguvu na kwa utukufu ambao,
kwa muda ule uliwagusa marafiki na wabaya wake na kuwatia hali ya mshangao. Roho wa Mungu
alikuwemo katika baraza lile, akiigusa mioyo ya wakuu wale wa dola. Baadhi ya watawala walikiri
kwamba madai ya Luther yalikuwa ya haki. Wengi waliusadiki ule ukweli; lakini kwa wengine ushawishi
waliopokea mle haukuwa wa kudumu. Kulikuwapo na kundi jingine la watu ambao wakati ule
hawakuonyesha kushawishika, lakini ambao, baada ya wao kuyachunguza Maandiko wao wenyewe siku
zilizofuata, waligeuka na kuwa watu waliounga mkono Matengenezo pasipo woga.
Frederick, yule mkuu, alitazamia kwa shauku kubwa kujitokeza kwa Luther mbele ya Baraza, na
alisikiliza hotuba yake huku akiguswa sana moyoni mwake. Kwa furaha na fahari alishuhudia na kuuona
ujasiri, uthabiti, na kujitawala kwa daktari, akadhamiria kusimama kwa uthabiti zaidi katika kumtetea.
Alizilinganisha pande zile zilizokuwa zinapambana, na kuona kwamba hekima ya mapapa, wafalme, na
maaskofu ilikuwa si kitu mbele ya nguvu ya ukweli. Upapa ulikuwa umeenda katika kushindwa ambako
kungesikika miongoni mwa mataifa yote na katika vizazi vyote.
Kadiri yule balozi wa papa alivyohisi athari za hotuba ya Luther, aliingiwa na hofu kubwa, kiasi ambacho
hajawahi kupata, juu ya usalama wa mamlaka ya Roma, naye akaazimu kutumia kila njia iliyokuwa
katika uwezo wake ili kutimiza mpango wa kumshinda Mwanamatengenezo. Pamoja na uwezo wake
wote wa kuongea kwa ufasaha na mbinu za kidiplomasia ambazo kwazo alikuwa mashuhuri, alimweleza
yule mfalme kijana hatari ya kupoteza urafiki na kuungwa mkono na nguvu za Roma, kwa sababu tu ya
madai ya mtawa asiye na maana.
Maneno yake hayakwenda pasipo madhara. Siku iliyofuata baada ya Luther kutoa jibu lile, Charles
aliagiza kwamba ujumbe uliotangaza nia yake ya kuendelea kuzifuata sera za watangulizi wake za
kudumisha na kulinda dini ya Katoliki upelekwe katika Baraza. Kwa kuwa Luther alikuwa amekataa
kukiri makosa yake, hatua kali sana zilikuwa zichuchukuliwe dhidi yake na uzushi ule aliofundisha.
“Mtawa mmoja, aliyepotoshwa na upumbavu wake, ameinuka na kuipinga imani ya ulimwengu wa
Kikristo. Kuzuia kufuru kama hiyo, mimi nitajitolea mhanga falme zangu, hazina zangu, (163) rafiki
zangu, mwili wangu, damu yangu, nafsi yangu, na uhai wangu. Nakaribia kumfukuza Luther Muagostino,
kumkataza asilete machafuko hata kidogo miongoni mwa watu; kisha nitamshtaki yeye pamoja na
wafuasi wake kuwa ni wazushi, waasi sugu, na kuwatenga na kanisa, kuwapiga marufuku wao pamoja na
ibada zao, na kuwaangamiza kwa gharama yoyote. Natoa wito kwa wajumbe wote wa majimbo
kuenenda kama Wakristo waaminifu.” 129 Hata hivyo, mfalme yule alisema kwamba lazima hati ya
usalama ya kusafiria ya Luther iheshimiwe, na ya kwamba kabla mashtaka haya hayajafunguliwa dhidi
yake lazima aruhusiwe kufika nyumbani kwake salama.

129
Ibid., book 7, chapter 9
90
Mitazamo miwili iliyopingana ilikuwa sasa miongoni mwa wajumbe wa Baraza. Wale wajumbe na
wawakilishi wa papa walidai tena kwamba hati ya usalama ya kusafiria ya Mwanamatengenezo
isiheshimiwe. Walisema; “Mto Rhine uyapokee majivu yake, kama ulivyoyapokea majivu ya John Huss
karne moja iliyopita.” 130 Lakini watawala wa Ujerumani, ingawa wao wenyewe walikuwa wafuasi wa
papa na maadui wa wazi wa Luther, walipinga kuvunja imani ya umma, ingekuwa doa katika heshima ya
taifa. Walionyesha matatizo yaliyofuata baada ya kifo cha Huss, na wakatangaza kwamba wasingependa
marudio ya maovu yale ya kutisha yaanguke juu ya Ujerumani, na juu ya kichwa cha mfalme wao
kijana.
Charles mwenyewe, akitoa jibu lake juu ya pendekezo hilo, alisema: “Ingawa heshima na imani inaweza
kufutiliwa mbali ulimwenguni kote, mambo hayo mawili yangepata mahali pa salama pa kukimbilia
ndani ya mioyo ya watawala wetu.” 131 Alizidi kusisitizwa zaidi na mfuasi wa upapa aliye adui mkubwa
wa Luther kuliko wote ya kwamba amshughulikie Mwanamatengenezo kama vile Sigismund
alivyomshughulikia Huss, amwache mikononi mwa rehema za kanisa; lakini akikumbushia kuhusu tukio
wakati Huss alipoonyesha minyororo yake, katika mkutano ule wa hadhara, na kumkumbuaha mfalme
juu ya ahadi yake aliyoitoa kumpa imani kuwa atamlinda, Charles V alisema hivi: “Nisingependa
kuaibika kama Sigismund.” 132
Hata hivyo, Charles alikuwa amezikataa kwa makusudi zile kweli alizozihubiri Luther. “Mimi kwa
uthabiti nimeazimia kuiga mfano wa watangulizi wangu,” ndivya alivyoandika mfalme. 133 Alikuwa
ameamua kwamba yeye asingeweza kuiacha ile njia ya (164) kufuata desturi, naam, kutembea katika
njia za kweli na haki. Kwa kuwa baba zake walifanya vile, basi, yeye naye angeweza kuutetea upapa,
pamoja na ukatili na ufisadi wake wote. Kwa hiyo alichukua nafasi yake hiyo, akikataa katakata
kuipokea nuru yo yote iliyo juu zaidi ya ile waliyokuwa wamepokea baba zake, au kufanya wajibu
wowote ambao wao hawakuwa wamefanya.
Wapo wengi mnamo siku hizi wanaong’ang’ania desturi na mapokeo ya baba zao. Mungu anapowaletea
nuru ya ziada, wanakataa kuipokea, eti kwa sababu, kwa kule kutotolewa kwa baba zao, haikupokelewa
na baba wale. Sisi hatukuwekwa mahali walipokuwa baba zetu; vivyo hivyo, majukumu yetu na wajibu
wetu si kama wao. Hatutaweza kukubaliwa mbele za Mungu kwa kufuata mfano wa mababa zetu katika
kuamua jukumu letu, badala ya sisi wenyewe kulichunguza lile neno la kweli. Wajibu wetu ni mkubwa
kuliko ulivyokuwa ule wa mababu zetu. Tunawajibika kwa ile nuru waliyoipokea wao, ambayo ilitufikia
kama urithi wetu, na tena tunao wajibu kwa nuru ya ziada inayoongezeka kwetu ikituangazia kutoka
katika neno la Mungu.
Kristo alisema hivi juu ya Wayahudi wasioamini: “Kama nisingalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na
dhambi; lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi zao.” Yohana 15:22. Mamlaka ile ile ya mbinguni
ilikuwa imezungumza na mfalme na watawala wa Ujerumani kupitia kwa Luther. Na nuru ile ilipoangaza
kutoka katika neno la Mungu, Roho wake aliwasihi wengi katika mkutano ule kwa mara ya mwisho.
Kama Pilato, karne nyingi zilizopita, alivyoruhusu kiburi na umaarufu kufunga mlango wa moyo wake
dhidi ya Mkombozi wa ulimwengu; kama Feliki aliyetetemeka alivyomwambia mjumbe yule wa ukweli,
akisema, “Sasa enenda zako, nami nikipata nafasi nitakuita;” na kama alivyokiri yule Agripa mwenye
majivuno, aliposema, “Kwa maneno machache wadhani kunifanya mimi kuwa Mkristo” (Matendo 24:25;

130
Ibid., book 7, chapter 9
131
Ibid., book 7, chapter 9
132
Lenfant, vol. la 1, uk. 422
133
D’Aubigne, book 7, chapter 9
91
26:28), lakini wao wakawa wakiupa kisogo ujumbe ule uliokuwa umetumwa kwao kutoka mbinguni –
hivyo ndivyo alivyofanya Charles V, akitawaliwa na nguvu ya kiburi na sera za ulimwengu, aliamua
kuikataa nuru ya ile kweli.
Tetesi kuhusu njama ile iliyokusudiwa kufanywa dhidi ya Luther zilienezwa sana, na kusababisha mji
wote kutaharuki. Yule (165) Mwanamatengenezo alikuwa amejipatia marafiki wengi, ambao, hali
wakiujua ukatili wa Roma uliojaa hila kwa wale wote waliothubutu kuyafunua maovu yake, wakaazimia
kwamba hatatolewa kafara. Mamia ya watu wenye vyeo wakaahidi kumlinda. Si wachache walioulaumu
waziwazi ujumbe wa mfalme uliodhihirisha udhaifu wake kwa kujisalimisha kwake chini ya udhibiti wa
mamlaka ya Roma. Mabango ya matangazo yaliwekwa kwenye milango mikubwa ya nyumba pamoja na
sehemu zile zinazotembelewa na watu wengi, mengine yakimshutumu Luther, na mengine yakimwunga
mkono. Katika bango moja kati ya yale kuliandikwa maneno ya maana ya mwenye hekima: “Ole wako,
nchi, akiwa mfalme wako kijana.” Mhubiri 10:16. Upendo wa watu wengi kwa Luther katika nchi ya
Ujerumani ulimthibitishia mfalme na Baraza lile kwamba dhuluma yo yote itakayotendwa dhidi yake
ingeweza kuhatirisha amani ya dola zima na hata usalama wenyewe wa kiti cha enzi.
Frederick wa Saksoni aliendelea kuhifadhi kwa werevu, akaficha kwa uangalifu hisia zake halisi
alizokuwa nazo kuhusiana na Mwanamatengenezo yule, na wakati ule ule akamlinda bila kuchoka,
akimwangalia kila alikokwenda na pia akiangalia mienendo ya adui zake. Lakini walikuwepo wengi
ambao hawakujaribu kuficha hisia zao za huruma kwa Luther. Alitembelewa na watawala, wakuu,
wenye nyadhifa za utawala, na watu wengine wenye sifa, watu walio wa kawaida na waliotoka kanisani.
“Chumba cha dokta huyu kilichokuwa kidogo,” kama alivyoandika Spalatini, “hakikuweza kuwatosha
wageni wote waliokuja kumwona.” 134 Watu walimtazama kana kwamba alikuwa zaidi ya binadamu. Hata
wale ambao hawakuwa na imani juu ya mafundisho yake hawakuweza kujizuia bali walistaajabia
msimamo wa hali ya juu wa shujaa aliyekuwa tayari kukabili kifo kuliko kwenda kinyume na dhamiri
yake.
Juhudi kubwa zilifanywa ili kumfanya Luther aridhie kuyafikia maridhiano na Roma. Wenye vyeo na
watawala walimweleza kwamba kama angezidi kung’ang’ania msimamo wake dhidi ya ule wa kanisa na
mabaraza, basi, muda si mrefu angefukuzwa katika dola ile na asingekuwa na ulinzi wo wote. Kwa
jambo hili Luther alijibu: “Injili ya Kristo haiwezi kuhubiriwa bila kuleta chuki…. Kwa nini basi hofu au
kuogopa hatari kunitenganishe na Bwana, na kunitenga na neno la Mungu ambalo peke yake ndilo kweli?
Hapana; mimi (166) ningependelea kujitoa mhanga mwili wangu, damu yangu, na uhai wangu.” 135
Aliombwa kwa mara nyingine kukubali hukumu ya mfalme, na ya kwamba tangu hapo asingekuwa na
kitu chochote cha kuogopa. “Nakubali,” akajibu, “kwa moyo wangu wote, kwamba mfalme, watawala,
na hata Mkristo wa kawaida angezipima na kuzikosoa kazi zangu; lakini kwa sharti moja, kwamba
walichukue neno la Mungu kama kipimo. Wanadamu hawana chaguo jingine isipokuwa kulitii neno tu.
Msiitendee jeuri dhamiri yangu, ambayo imefungwa na kutiwa minyororo kwa Maandiko Matakatifu.” 136
Kuhusu ombi jingine lililotolewa kwake, alisema hivi: “Nakubaliana kuachana na hati yangu ya usalama
ya kusafiri. Naweka utu wangu na uhai wangu mikononi mwa mfalme wa dola, badala ya neno la Mungu
- kamwe!” 137 Akaeleza utayari wake wa kukubali maamuzi ya baraza lile kuu, ila tu kwa sharti kwamba
baraza lile litoe maamuzi yake kwa kufuata Maandiko. Aliongeza hivi: "Katika jambo linalohusu neno la

134
Martyn, vol. la 1, uk. 404
135
D’Aubigne, book 7, chapter 10
136
Ibid., book 7, chapter 10
137
Ibid., book 7, chapter 10
92
Mungu na imani, kila Mkristo ni mwamuzi mzuri kama alivyo papa, ingawa anaungwa mkono na mamiloni
ya mabaraza, yaweza kuwa kwa ajili yake.” 138 Mwisho rafiki zake na adui zake walishawishika kwamba
hata kama juhudi za ziada zingefanywa kusuluhisha jambo hili bado zisingefanikiwa.
Ikiwa Mwanamatengenezo angeshindwa katika neno moja, Shetani na majeshi yake wangekuwa
wamejipatia ushindi. Lakini uthabiti wake usioyumba ulikuwa ndiyo njia ya kulikomboa kanisa, na
kuanzisha zama mpya zilizo bora zaidi. Mvuto wa mtu yule mmoja, ambaye alidiriki kufikiri na kutenda
kwa nafsi yake mwenyewe katika mambo yahusuyo dini, ulikuwa uwe na athari kwa kanisa na
ulimwengu, si kwa wakati wake tu, bali kwa vizazi vyote vya mbele. Msimamo wake na uaminifu wake
ungewatia nguvu wote ambao wangepitia katika uzoefu wa maisha unaofanana na ule wa kwake mpaka
mwisho wa wakati. Uweza na ukuu wa Mungu ulisimama juu ya mashauri ya wanadamu, na juu ya nguvu
za uweza wa Shetani.
Baada ya muda mfupi, Luther aliamriwa na mamlaka ya mfalme kurudi nyumbani, naye alijua kwamba
taarifa ile ingefuatiwa kwa karibu na hukumu yake. Mawingu ya kutisha yalijaza njia yake; lakini wakati
alipokuwa akiondoka kutoka Worms, (167) moyo wake ulijaa furaha na sifa. Akasema: “Ibilisi
mwenyewe, aliilinda ngome ya papa; lakini Kristo ameipasua na kuacha ufa mpana ndani yake, naye
Shetani amelazimika kukiri ya kwamba Bwana ana uwezo kuliko yeye.” 139
Baada ya kuondoka kwake, akiwa bado anatamani kwamba ushupavu wake ule usieleweke kuwa ni uasi,
Luther alimwandikia barua mfalme. “Mungu, ambaye huichunguza mioyo, ni shahidi wangu,” alisema,
“kwamba mimi niko tayari kabisa kukutii wewe mheshimiwa mfalme, katika heshima au katika aibu,
katika uzima au mautini, na bila kizuizi chochote isipokuwa tu katika neno la Mungu, ambalo kwalo
mwanadamu huishi. Katika mambo yote yahusuyo maisha haya, msimamo wangu hautalegalega, maana
kupoteza au kupata hapa hakuleti athari yoyote kwa wokovu. Lakini pale ambapo mambo ya kiroho
yanahusika, Mungu hapendi mwanadamu yeyote ajikabidhi chini ya mwanadamu mwingine. Kwa maana
kujikabidhi kama huko katika mambo ya kiroho ni ibada halisi, ambayo lazima itolewe kwa Muumba
peke yake.” 140
Mapokezi ya Luther alipokuwa njiani kutoka Worms yalikuwa ya kupendeza kuliko wakati ule alipokuwa
anaenda. Viongozi wa kanisa wa kifahari walimkaribisha mtawa huyu aliyetengwa na kanisa, na
watawala wa serikali wakampa heshima mtu huyu ambaye alikuwa ameshutumiwa na mfalme. Aliombwa
kuhubiri, na, bila ya kujali zuio la mfalme, aliingia tena mimbarani. “Kamwe sijatoa ahadi ya kulifunga
minyororo neno la Mungu,” alisema, “wala sitafanya hivyo.” 141
Wakati Luther hajakaa muda mrefu nje ya Worms wafuasi wa papa wakafanikiwa kumshawishi mfalme
kutoa amri dhidi yake. Katika amri ile Luther alishutumiwa kuwa yeye ndiye “Shetani mwenyewe katika
umbile la mwanadamu, liyevaa joho la kitawa.” 142 Iliamriwa kwamba mara tu muda wa hati yake ya
usalama utakapokwisha, hatua zichukuliwe kuikomesha kazi yake. Watu wote walikatazwa kumpa
hifadhi, kumpa chakula au kinywaji, au kwa neno au kwa tendo, hadharani au faraghani, kumsaidia au
kushirikiana naye. Popote ambapo angekuwa angepaswa kukamatwa, na kukabidhiwa kwa wenye
mamlaka. Wafuasi wake pia walipaswa kufungwa gerezani na mali zao kuchukuliwa. Maandiko yake
yalipaswa kuteketezwa, na, hatimaye wale wote ambao wangethubutu kufanya kinyume cha amri ile

138
Martyn, vol. 1, p. 410
139
D’Aubigne, book 7, chapter 11
140
Ibid., book 7, chapter 11
141
Martyn, vol. la 1, uk. 420
142
D’Aubigne, book 7, chapter 11
93
wangejumuishwa katika hukumu ile. (168) Mkuu wa jimbo la Saksoni, pamoja na watawala waliokuwa
marafiki wa Luther walikuwa wameondoka Worms mara tu baada ya kuondoka kwake, na ile amri ya
mfalme ilikuwa imepata kibali cha Baraza. Basi, wafuasi wa Roma wakafurahi na kushangilia. Walidhani
kwamba mwisho wa Matengenezo ulikuwa umetiwa muhuri.
Mungu alikuwa ametoa njia kwa ajili ya mtumishi wake kuokoka katika saa ile ya hatari. Jicho la muda
mrefu lilikuwa limefuatilia mienendo ya Luther, na moyo wake wa ukweli na wema ulikuwa
umethibitika katika kuokoka kwake. Ilikuwa wazi kwamba Roma isingeridhika na kitu cho chote kilicho
pungufu ya kifo cha Luther; ni kwa kificho tu angeweza kuokoka na kinywa cha simba yule. Mungu
alimpatia Frederick wa Saksoni hekima ya kubuni mpango wa kumhifadhi Mwanamatengenezo.
Akisaidiana na rafiki zake wa kweli, kusudi la mtawala yule lilitekelezwa, na Luther akafichwa mbali na
rafiki na adui zake. Alipokuwa njiani kurudi nyumbani alikamatwa, akatengwa na wahudumu wake, na
kuchukuliwa haraka kupitia msituni hadi katika ngome ya Wartburg, ngome iliyoko katika milima
iliyojitenga. Kukamatwa kwake na kufichwa kwake kulikuwa ni kwa siri mno kiasi kwamba hata
Frederick mwenyewe kwa muda mrefu hakujua mahali alikokuwa amepelekwa. Kutokujua huko
hakukuwa bila mpango; kwa kuwa huyu mtawala hakujua lolote kuhusu mahali alipokuwa Luther,
asingeweza kufichua lolote. Alijifariji kwamba Mwanamatengenezo alikuwa salama, naye akatosheka na
ufahamu huo.
Majira ya kuchipua, majira ya joto, na majira ya kipupwe (kupukutisha) yalipita, na majira ya baridi
yakaja, Luther akiwa bado kifungoni. Aleander na wenzake walishangilia sana kwa kuwa nuru ya injili
ilionekana kana kwamba ilikuwa karibu kuzimika. Kumbe, tofauti na hivyo, Mwanamatengenezo alikuwa
anaijaza taa yake mafuta kutoka katika hazina ya ile kweli; na nuru yake ilikuwa karibu kuangaza kote
kwa mwanga mkali zaidi.
Akiwa katika usalama ulio wa kirafiki wa watu wa Wartburg, kwa muda fulani Luther alifurahia hali ya
kufunguliwa kwake kutoka katika moto na msukosuko wa mapambano. Lakini hakuweza kutosheka na
hali ya kukaa kimya na kupumzika kwa muda mrefu. Akiwa amezoea maisha ya kazi na kukabiliana na
mapambano makali, alivumilia kukaa bila shughuli yoyote kwa shida. Katika siku zile za upweke hali ya
kanisa ilionekana mbele yake, naye akalia kwa huzuni: “Oh! hakuna hata mtu mmoja katika siku hizi za
mwisho za hasira Yake, awezaye kusimama kama ukuta mbele za Bwana, na kuiokoa Israeli!” 143 Mara,
mawazo yakamjia tena, akaogopa kuitwa mwoga kwa kujiondoa katika pambano lile. Ndipo akajilaumu
mwenyewe kwa uzembe wake na hali ya kujithamini yeye mwenyewe. Lakini, wakati huo huo alikuwa
akifanya mambo mengi kuliko yale yanayowezekana kufanywa na mtu mmoja. Kamwe kalamu yake
haikukaa hivi hivi tu. Wakati ambapo adui zake walikuwa wakijisifu kwamba alikuwa amenyamazishwa,
walishangazwa na kuchanganyikiwa kwa sababu ya ushahidi wa wazi ulioonyesha kwamba alikuwa bado
kazini. Vijizuu vingi, vilivyoandikwa kwa kalamu yake, vilitawanywa katika Ujerumani yote. Pia alifanya
kazi nyingine muhimu sana kwa ajili ya watu wa nchi yake kwa kutafsiri Agano Jipya katika lugha ya
Kijerumani. Kutoka katika Patmo yake hii yenye miamba aliendelea kwa karibu mwaka mzima
kutangaza injili na kuzikemea dhambi na mafundisho potofu ya wakati ule.
Lakini Mungu hakuwa amemwondoa Luther katika jukwaa la maisha ya kijamii kwa ajili hasa ya
kumlinda mtumishi wake na hasira ya adui zake, wala kwa lengo la kumpatia kipindi cha utulivu kwa
ajili ya kazi za maana alizozifanya. Kulikuwa na matokeo mengine ya thamani zaidi yaliyokuwa
yapatikane. Katika upweke na uficho wa makazi yake ya milimani, Luther aliwekwa mbali na misaada ya

143
Ibid., book 9, chapter 2

94
kidunia na alifungiwa mbali na sifa za wanadamu. Kwa njia hiyo aliwekwa mbali na kiburi na kule
kujitumainia ambavyo mara nyingi husababishwa na mafanikio. Kwa kuteseka na kudhalilishwa vile
alikuwa ametayarishwa ili apate kutembea tena kwa usalama katika vilele vya juu vinavyosababisha
kizunguzungu, mahali ambapo alikuwa ameinuliwa ghafla.
Kadiri watu wanavyofurahia uhuru uletwao na ukweli, wanakuwa na mwelekeo wa kuwasifu wale
wanaotumiwa na Mungu kuivunjilia mbali minyororo ya mafundisho ya uongo pamoja na upotofu.
Shetani hutafuta kuyapindisha mawazo na hisia zao kuviondoa kwa Mungu, na kuvielekeza kwa
mawakala wa kibinadamu; anawaongoza kuheshimu hivi vyombo tu na kuudharau Mkono ule
unaoendesha mambo yote. Mara nyingi viongozi wa dini wanaosifiwa hivyo na kupewa heshima na watu
wanapoteza nguvu ya kumtegemea Mungu, na kuongozwa katika kujitumainia wao wenyewe. (170)
Matokeo yake ni kwamba wanajitahidi kudhibiti mawazo na dhamiri za watu, ambao wamependa
mwelekeo wa kuwategemea viongozi wao kama mwongozo wao badala ya kulitegemea neno la Mungu.
Mara nyingi kazi ya matengenezo inahafifishwa kwa sababu ya roho hii ipandikizwayo na wale
wanaoiunga mkono. Kwa kuachana na hatari hiyo, Mungu angeongoza njia ya Matengenezo. Alitaka kazi
ile ipokee, si chapa ya mwanadamu, bali ile ya Mungu. Macho ya watu yalikuwa yamegeuzwa kwa
Luther kama vile ndiye mwenye uwezo wa kuifafanua ile kweli; aliondolewa kwao ili macho yote yapate
kumwelekea Mtunzi wa milele wa ile kweli.

95
Sura ya 9
MWANAMATENGENEZO WA USWISI

Katika kuchagua vyombo kwa ajili ya kulitengeneza kanisa, unaonekana ukitumika mpango wa Mungu
ule ule uliotumika wakati wa kulisimika kanisa. Mwalimu yule wa Mbinguni aliwapita wakuu wa nchi,
wenye vyeo na matajiri, waliozoeleka kupokea sifa na heshima kama viongozi wa watu. Walikuwa na
kiburi, na kujitumainia wenyewe katika ukuu wao kiasi kwamba wasingekuwa tayari kufinyangwa na
kuweza kuwahudumia wanadamu wenzao na kuwa wafanyakazi pamoja na yule Mtu wa Nazareti
mnyenyekevu. Wito ulitolewa kwa wavuvi wale wa Galilaya waliokuwa katika kazi ngumu, na wasio na
elimu: “Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.” Mathayo 4:19. Wanafunzi wale walikuwa
wanyenyekevu na wa kufundishika. Kadiri walivyokuwa hawajaathiriwa sana na mafundisho ya uongo ya
wakati wao, ndivyo Kristo angeweza kufaulu sana kuwaelekeza na kuwafunza kwa ajili ya huduma yake.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa katika siku zile za Matengenezo. Wanamatengenezo wakuu walikuwa ni watu
kutoka katika hali duni ya maisha - watu waliokuwa hawana kiburi kutokana na cheo na mvuto wa
ujanja wa makasisi. Ni mpango wake Mungu kuvitumia vyombo vilivyo vinyenyekevu ili kuleta matokeo
makubwa. Ndipo utukufu hautatolewa kwa wanadamu, bali kwake Yeye afanyaye kazi kupitia kwao
kupenda na kutenda yaliyo mapenzi yake mema.
Majuma machache baada ya kuzaliwa kwa Luther katika kibanda cha mchimba madini kule Saksoni,
Ulric Zwingli alizaliwa katika kibanda cha mchungaji wa mifugo katika milima ya Alps. Mazingira ya
utoto ya Zwingli, na (172) mafundisho yake ya awali, yalikuwa kama vile kumwandaa kwa ajili ya utume
wake wa baadaye. Akiwa amekulia katika mazingira yale yenye sura ya asili, mazuri, na ya kuvutia,
mawazo yake yaliguswa na hisia ya ukuu, uweza, na utukufu wa Mungu. Historia ya matendo ya kishujaa
yaliyotendwa katika milima ile ya nyumbani iliwasha hamu yake ya wakati wa ujana. Kutoka kwa bibi
yake mcha Mungu alizisikiliza hadithi chache nzuri za Biblia ambazo alikuwa amezikusanya kama urithi
na mapokeo ya kanisa. Kwa hamu kubwa alisikiliza habari za matendo makuu ya wazee na manabii, ya
wachungaji wale waliochunga mifugo yao katika vilima vya Palestina mahali ambako malaika
walizungumza nao, habari za Mtoto yule wa Bethlehemu na yule Mtu wa Kalvari.
Kama alivyokuwa John Luther, baba yake Zwingli alitamani mtoto wake apate elimu, na mtoto yule
aliondolewa mapema katika bonde lile la nyumbani na kupelekwa kupata elimu. Akili yake iliendelea
haraka, na, baada ya muda mfupi, suala lilikuwa ni wapi pa kupata walimu wenye umahiri wa
kumfundisha. Akiwa na umri wa miaka kumi na tatu alienda Bern, mahali ambapo palikuwa na shule
maalum sana kuliko zote katika nchi ya Uswisi. Hata hivyo, mahali hapa palikuwa na hatari iliyotishia
matumaini ya maisha yake. Juhudi kubwa zilifanywa na watawa ili kumvutia katika nyumba ya kitawa.
Watawa wa Kidominika na wale wa Kifransisi walikuwa katika mashindano ya kutafuta kupendwa na
watu walio wengi. Walijitahidi kufikia azma hii kwa kuyapamba kimaonyesho makanisa yao, kuzifanya
sherehe zao kuwa za kifahari, na kuweka vivutio vya mabaki ya watakatifu na miujiza - kazi za sanamu.

96
Wadominika wa kule Bern waliona kuwa kama wangeweza kumpata mwanafunzi yule kijana mwenye
kipaji, basi, wangejipatia faida na heshima. Ujana wake shupavu, uwezo wake wa asili wa kusema na
kuandika, na kipaji chake maalum katika muziki na mashairi, vingewaletea matokeo makubwa kuliko
fahari yao yote na kujionyesha kwao katika kuwavuta watu kuja kwenye ibada zao na kuongeza mapato
ya kikundi chao. Kwa kutumia udanganyifu na kumsifu mno walijitahidi sana kumshawishi Zwingli
kuingia katika nyumba yao ya utawa. Luther, alipokuwa shuleni, alijichimbia katika chumba cha nyumba
ya watawa, na angepotea ulimwenguni ikiwa rehema za Mungu zisingemwokoa. Zwingli hakuachwa
apambane na (173) hatari ya namna ile. Kwa bahati baba yake alipata habari ya mpango wa watawa
wale. Hakuwa na nia ya kumwacha mwana wake afuate maisha ya kivivu na yasiyofaa ya watawa. Aliona
kwamba kuhitajika kwake kwa maisha ya baadaye kulikuwa hatarini, na aliagiza arudi nyumbani pasipo
kukawia.
Agizo lile lilitiiwa; lakini kijana yule hakuweza kuridhika kukaa katika bonde lile la nyumbani kwa muda
mrefu, na mara hiyo akarejea katika masomo yake, akifidia kwa muda, kwenda Basel. Mahali hapa
ndipo Zwingli aliposikia kwanza habari ya injili ya neema ya Mungu itolewayo bure. Wittembach,
mwalimu wa lugha za kale, alikuwa ameongozwa katika Maandiko Matakatifu, alipokuwa anajifunza
Kigiriki na Kiebrania, na kwa njia hiyo miale ya nuru ya Mungu ikayaangazia mawazo ya wanafunzi
waliokuwa chini ya ufundishaji wake. Akawatangazia kwamba kulikuwa na kweli ya zamani zaidi, na ya
thamani ya juu zaidi, kuliko nadharia zile zilizofundishwa na wasomi na wanafalsafa. Ile kweli ya
zamani ilikuwa ya kwamba kifo chake Kristo kilikuwa ndiyo fidia ya pekee kwa mdhambi. Kwa Zwingli
maneno yale yalikuwa kama mshale wa kwanza wa nuru ya mapambazuko.
Baada ya muda mfupi Zwingli aliitwa kutoka Bazel kwenda katika kazi yake ya maisha. Eneo lake la
kwanza la kazi lilikuwa katika parokia ya milima ya Alps, mahali ambapo si mbali sana na bonde la
nyumbani kwao. Akiisha kutengwa rasmi kama padri, “alijitoa mwenyewe na roho yake yote kuitafuta
ile kweli ya Mungu; maana yeye alijua wazi,” anasema Mwanamatengenezo mwenzake, “ni kiasi gani
ilikuwa lazima ajue kwamba kundi la Kristo limekabidhiwa kwa nani.” 144 Kadiri alivyozidi kuyachunguza
Maandiko, ndivyo ilivyoonekana dhahiri tofauti kati ya kweli zake na uzushi wa Roma. Alijisalimisha
mwenyewe kwa Biblia kuwa ndilo neno la Mungu, kanuni ya kutosha na kamilifu isiyokosea. Aliona
kwamba ni lazima ijitafsiri yenyewe. Hakuthubutu kuyafafanua Maandiko ili kuunga mkono nadharia au
mafundisho yaliyobuniwa na watu zamani, bali yeye alishikilia kwamba lilikuwa ni jukumu lake
kujifunza mafundisho yale ya moja kwa moja na dhahiri. Alijitahidi sana kupata kila msaada ili apate
ufahamu kamili na ulio sahihi wa maana yake, na aliomba uongozi wa Roho Mtakatifu, ambaye alisema
angeweza kuyafunua yote kwa wale walioyatafuta kwa unyofu wa moyo na maombi.
(174) Mafundisho ya imani aliyokuwa anafundisha Zwingli hayakutoka kwa Luther. Yalikuwa ni
mafundisho ya Kristo. “Ikiwa Luther anamhubiri Kristo,” alisema yule Mwanamatengenezo Mswisi,
“anafanya kile ninachofanya mimi. Wale aliowaleta kwa Kristo ni wengi sana kuliko wale niliowaleta
mimi. Lakini hilo si kitu. Mimi sitabeba jina jingine lolote isipokuwa jina la Kristo, ambaye mimi ni
askari wake, na ambaye yeye peke yake ndiye Mkuu wangu. Hakuna hata neno moja ambalo
nimemwandikia Luther, au Luther kuniandikia mimi. Na kwa nini? … Ili ipate kudhihirika jinsi Roho wa
Mungu alivyo mmoja, kwa kuwa, sisi wawili, bila kukutana na kukubaliana, tunafundisha fundisho la
Kristo linalokubaliana.” 145

144
Wylie, book 8, chapter 5
145
D’Aubigne, book 8, chapter 9
97
Mnamo mwaka 1516, Zwingli alialikwa kuwa mhubiri katika nyumba ya watawa ya Einsiedeln. Mahali
hapa angejionea mwenyewe kwa karibu zaidi ufisadi wa Roma, tena angeleta athari yenye nguvu kama
Mwanamatengenezo, ambayo ingeweza kufika mbali kupita nchi yake ya Alps alikozaliwa. Miongoni mwa
vivutio vikuu vya Einsiedeln ilikuwa ni sanamu ya Bikira ambayo ilisemekana kwamba ilikuwa na uwezo
wa kufanya miujiza. Juu ya lango kubwa la kuingilia katika nyumba ile ya watawa palikuwa na
maandishi: “Msamaha wa dhambi unaweza (175) kupatikana hapa.” 146 Kwa majira yote wana hija
walikwenda katika sehemu ya Bikira; lakini wakati ule wa sikukuu kubwa ya kila mwaka ya kuitukuza,
watu wengi walikuja pale kutoka katika sehemu zote za nchi ile ya Uswisi, na hata kutoka Ufaransa na
Ujerumani. Akiwa amehuzunishwa sana na hali ile, Zwingli alitumia nafasi ile kuwatangazia wale
watumwa wa ushirikina uhuru unaopatikana kwa njia ya injili.
Alisema, “Msidhani kwamba Mungu yu katika hekalu hili kuliko sehemu nyingine yo yote ya uumbaji
wake. Katika nchi yoyote mnayokaa, Mungu yupo mahali pale na anasikia…. Je, matendo yenu hayo
yasiyo na faida, safari ndefu za kuhiji, sadaka, sanamu, maombi kwa Bikira au kwa watakatifu,
yanaweza kuwapatia ninyi neema ya Mungu?… Maneno yetu mengi ya kuzipamba sala hizi yana faida
gani? Ni manufaa gani yanayopatikana kwa kuvaa kofia ya kitawa, kunyolewa kichwa, na kuvaa kanzu
ndefu inayopepea, au kuvaa sapatu zilizotiwa dhahabu?… Mungu anaangalia moyoni, na mioyo yetu iko
mbali naye.” Akasema, “Kristo, ambaye alitolewa msalabani mara moja, ndiye kafara na mhanga,
aliyetosheleza kwa dhambi za waamini hata milele zote.” 147
Mafundisho haya hayakupokelewa Kwa wasikilizaji wengi waliokuwa pale. Lilikuwa ni jambo la kutia
uchungu na kufadhaisha kuambiwa kwamba safari yao ndefu waliyokuwa wamefanya ilikuwa ni bure.
Hawakuweza kuuelewa msamaha huo utolewao bure kupitia kwa Kristo. Walikuwa wametosheka na njia
ile ya zamani ya kwenda mbinguni ambayo waliwekewa na Roma. Walikataa kujiingiza katika kutafuta
kitu kingine kilicho bora zaidi. Ilikuwa rahisi zaidi kwao kutumainia wokovu wao kupitia kwa makasisi na
papa kuliko kutafuta usafi wa moyo.
Lakini watu wa kundi jingine walipokea kwa furaha habari hii ya ukombozi kupitia Kristo. Kanuni za dini
zilizoletwa na Roma zilikuwa zimeshindwa kuwaletea amani nafsini mwao, na kwa imani wakakubali
damu ya Yesu kama neema kwa ajili yao. Hawa walirudi majumbani kwao na kuwafunulia wengine nuru
hii ya thamani waliyokuwa wamepokea. Ukweli huu ulisambazwa kutoka kijiji hadi kijiji, kutoka mji
hadi mji, na idadi ya mahujaji wanaosafiri kwenda kwenye sehemu ya heshima ya Bikira ilipungua sana.
Kulikuwa na kushuka (176) kwa matoleo ya sadaka, na vivyo hivyo kiasi cha mshahara wa Zwingli,
uliotokana na makusanyo hayo. Lakini jambo hili lilimpatia furaha maana aliona kwamba nguvu za
misimamo potofu zilikuwa zinavunjika.
Mamlaka za kanisa hazikufumbia macho hali hii; lakini kwa wakati huu waliacha kuingilia kati.
Wakitarajia kumrejesha katika njia yao, waliazimia kumpata kwa kujipendekeza kwake; wakati huo
ukweli ukaendelea kuifikia mioyo ya watu.
Kazi ya Zwingli kule Einsiedeln ilikuwa imemwandaa kwa utumishi mpana zaidi, na karibu alikuwa aingie
humo. Baada ya miaka mitatu aliitwa katika cheo cha kuwa mhubiri katika kanisa kuu la jimbo la
Zurich. Huu ulikuwa mji muhimu kuliko yote katika shirikisho la Uswisi, na ushawishi ambao ungetokea
mahali hapa ungesikika kwa mapana. Maaskofu waliokuwa wamempa mwaliko kuja Zurich walikuwa,
hata hivyo, wanazuia maboresho yoyote, na waliendelea kumfundisha majukumu yake kama kawaida.

146
Ibid., book 8, chapter 5
147
Ibid., book 8, chapter 5

98
"Utafanya kila juhudi kukusanya mapato ya mkutano wa mapadri, bila kudharau hata kidogo,” walisema.
“Utawashawishi waaminifu, wote mapadri na wale walio katika maungamo, kulipa zaka zote na matoleo
yote, na kuonyesha kwa njia ya sadaka zao upendo wao kwa kanisa. Uwe jasiri katika kuongeza mapato
yatokanayo na wagonjwa, kutoka kwa waamini, na kwa ujumla kutokana na maagizo ya kanisa."
Wakaongeza kwamba, "Kwa habari ya kuendesha sakramenti, kuhubiri na kulichunga kundi, nayo pia ni
majukumu ya kasisi. Lakini kwa kazi hizi unaweza kumpa mtu mwingine badala yako, na hasa
kufundisha. Usifanye huduma ya sakramenti kwa mtu yeyote isipokuwa aliye na barua, tena pale tu
unapoitwa; hauruhusiwi kufanya huduma hiyo bila kutofautisha watu." 148
Zwingli alisikiliza maelekezo haya kwa ukimya, halafu akajibu, baada ya kutoa shukrani kwa heshima hii
aliyokuwa ametunukiwa ya kuitwa katika kituo hiki muhimu, akieleza njia aliyopendekeza kufuata
(177). Alisema, "Watu wamefichwa maisha ya Yesu kwa muda mrefu. Nitahubiri Injili yote ya Mathayo
Mtakatifu, . . . nitazama na kuchota katika visima vya Maandiko, nikilinganisha aya moja na nyingine,
nikitafuta kuelewa kwa maombi ya bidii mara kwa mara. Kwa utukufu wa Mungu, kwa sifa ya Mwanawe
wa pekee, kwa ajili ya wokovu wa roho za watu, na katika kuwaongoza katika imani ya kweli, nitaweka
wakfu huduma yangu." 149 Ingawa baadhi ya makasisi hawakukubaliana na mpango wake, badala yake
wakaazimia kumkatisha tamaa, Zwingli alisimama imara. Aliweka wazi kwamba yeye hakukusudia
kuanzisha njia mpya, ila ile ya zamani iliyotumiwa na kanisa la awali katika nyakati zake za usafi.
Tayari aliamsha hamasa ya watu kuhusu ukweli wa mafundisho yake; na watu wengi wakafurika kuja
kumsikiliza. Watu wengi ambao walikuwa hawahudhurii ibada kwa muda mrefu walikuwa miongoni mwa
waliokuja kumsikiliza. Alianza huduma yake kwa kusoma Injili na kuwaeleza wasikilizaji wake visa vya
maisha, mafundisho na kifo cha Kristo. Hapa, kama ilivyokuwa kule Einsiedeln, alifundisha neno la
Mungu kama mamlaka pekee iliyo sahihi na kifo cha Kristo kama kafara pekee iliyo kamilifu.
"Ninatumaini kuwaongoza kwa Kristo – kwa Kristo, chanzo cha kweli cha wokovu." 150 Watu waliofurika
kumzunguka mhubiri huyu walitoka madaraja yote, walitoka miongoni mwa watawala, wasomi, mafundi
na wakulima. Walisikiliza maneno yake kwa hamu. Si tu kwamba alitangaza habari ya wokovu wa bure
pasipo malipo, bali pia alikemea maovu na upotofu wa wakati ule. Wengi walirudi kutoka kanisani
wakimsifu Mungu. Walisema, "Mtu huyu ni mhubiri anayehubiri ukweli. Atakuwa Musa wetu,
atakayetuongoza kutoka katika Misri yetu ya giza." 151
Ingawa awali kazi yake ilipokelewa kwa hamu, baada ya muda upinzani uliinuka. Masufii (watawa wa
kiume) walijipanga kukwamisha kazi yake na kupinga mafundisho yake. (178) Wengi walimkebehi na
kumbeza; wengine walimtendea jeuri na vitisho. Lakini Zwingli alivumilia yote, akisema: "Ikiwa
tunataka kuwashinda waovu kwa ajili ya Yesu, lazima tufumbe macho yetu kwa mambo mengi." 152
Wakati huu mtenda kazi mwingine alijitokeza kuendeleza kazi ya matengenezo. Mtu ajulikanaye kama
Lucian alipelekwa Zurich na rafiki wa imani ya matengenezo wa kule Basel, akiwa na baadhi ya
maandiko ya Luther, akiwa na wazo kwamba machapisho yale yangeuzwa huko ili kuisambaza nuru ile
kwa nguvu. Aliandika kwa Zwingli akisema, "Jihakikishie kama mtu huyu ana ujuzi na uangalifu wa
kutosha; kama ndivyo, mruhusu atawanye kazi hizi za Luther miongoni mwa Waswisi, hasa maelezo yake
kuhusu Sala ya Bwana, kutoka mji mmoja hadi mwingine, kutoka kijiji hata kijiji, na hata kutoka

148
Ibid., b. 8, ch. 6
149
Ibid., b. 8, ch. 6
150
Ibid., b. 8, ch. 6
151
Ibid., b. 8, ch. 6
152
Ibid., b. 8, ch. 6.
99
nyumba moja hadi nyingine. Kadiri yajulikanavyo sana ndivyo wanunuzi wake watakavyopatikana." 153
Hivyo ndivyo nuru ilivyopata njia.
Wakati Mungu anapoandaa mpango wa kuzivunjilia mbali pingu za ujinga na upotofu, ndipo Shetani
anapofanya kazi yake kwa nguvu zake zote kuwafunika wanadamu katika giza na kuwafunga pingu zake
kwa kuzikaza zaidi. Kadiri watu walivyojitokeza katika nchi mbalimbali kuhubiri kwa watu msamaha na
kuhesabiwa haki kwa njia ya damu ya Kristo, Roma iliendela kwa nguvu mpya kufungua soko lake katika
Ulimwengu wote wa Kikristo, ikitoa msamaha kwa kubadilishana na fedha.
Kila dhambi ilikuwa na bei ya malipo yake, na watu waliachwa watende uhalifu alimradi hazina ya
kanisa ilikuwa inaendelea kujazwa. Kwa hiyo harakati za namna mbili ziliendelezwa – moja ikitoa
msamaha wa dhambi kwa malipo ya fedha, nyingine msamaha kwa njia ya Kristo, - Roma ikiruhusu
dhambi na kuifanya chanzo chake cha mapato; huku Wanamatengenezo wakiipinga dhambi na
kuwaelekeza watu kwa Kristo aliye kipatanisho na mwokozi.
Kule Ujerumani kazi ya kuuza misamaha ya dhambi ilikabidhiwa kwa watawa wa Kidominika, na
ilisimamiwa na mtu asiye mashuhuri, Tetzel. Katika nchi ya Uswisi shughuli hii ilikabidhiwa mikononi
mwa Wafransisko, chini ya uongozi wa Samsoni, mtawa wa Kiitalia. (179) Samsoni alikuwa amekwisha
kufanya kazi nzuri kwa ajili ya kanisa, akiwa amekusanya fedha nyingi sana kutoka Ujerumani na Uswisi
na kujaza hazina ya papa. Sasa alipita katika Uswisi yote, akiyavuta makundi makubwa ya watu,
akifagia mapato kidogo ya wakulima maskini, na kudai tozo nono kutoka kwa tabaka la wenye mali.
Lakini nguvu ya matengenezo ilikuwa umeshaathiri biashara ile, ingawa haikuweza kuikomesha kabisa.
Zwingli alikuwa bado angali Einsiedeln wakati Samsoni, mara tu alipoingia katika nchi ya Uswisi,
alipowasili na biashara yake katika mji jirani. Akiwa amejulishwa kuhusu utume wake,
Mwanamatengenezo alianza mara kujipanga ili kumpinga. Hao wawili hawakukutana, lakini hayo
yalikuwa ndiyo mafanikio ya Zwingli kuuweka wazi unafiki wa mtawa yule hata akalazimika kuondoka
kwenda mahali pengine.
Kule Zurich, Zwingli alihubiri kwa nguvu dhidi ya wafanya-biashara ya msamaha wa dhambi; na Samsoni
alipokaribia mahali pale, alikutana na mjumbe kutoka kwa baraza aliyempa habari ya kutakiwa kusonga
mbele. Hatimaye aliweza kuingia pale kwa kutumia hila, lakini aliondolewa pale bila kuuza msamaha wa
dhambi hata mmoja, na baada ya muda mfupi aliondoka Uswisi.
Msukumo mkubwa ulitokea kusaidia harakati za matengenezo, kwa kutokea kwa gonjwa, au “mauti
kuu,” lililoikumba nchi yote ya Uswisi mnamo mwaka wa 1519. Watu walipokabiliwa ana kwa ana na
tauni hii ya kuangamiza, ndipo wengi waliona kwamba msamaha wa dhambi waliokuwa wameuziwa
haukuwafaa kitu; nao wakatamani kuupata msingi imara kwa ajili ya imani yao. Akiwa Zurich, Zwingli
alipigwa na ugonjwa ule; alidhoofika sana na kupoteza tumaini la kupona, na taarifa ikaenezwa mahali
pengi kwamba amekufa. Katika saa ile ya kujaribiwa, tumaini lake na ujasiri wake havikutikiswa.
Aliutazama msalaba wa Kalvari kwa imani, akitumainia upatanisho utoshao wa dhambi. Aliporejea toka
katika milango ya mauti, ilikuwa ni kuihubiri injili kwa nguvu zaidi kuliko kabla; na maneno yake
yalikuwa na nguvu isiyo ya kawaida. Watu walimkaribisha mchungaji wao mpendwa kwa furaha, akiwa
amerudi kutoka katika ukingo wa kaburi. Hata wao walikuwa wametoka kushughulika kwa ajili ya
wagonjwa na (180) wale waliokuwa wanakufa, na wakahisi thamani ya injili kuliko ilivyokuwa kabla ya
hapo.

153
Ibid., b. 8, ch. 6.

100
Zwingli alikuwa amefikia hatua ya kuelewa dhahiri zaidi kweli za injili, na alikuwa amepata uzoefu
kamili kupitia yeye mwenyewe jinsi ilivyo na uwezo wa kumfanya mtu kuwa kiumbe kipya. Anguko la
mwanadamu na mpango wa ukombozi yalikuwa ndiyo masomo alimojikita. Alisema, “Katika Adamu, sisi
sote tumekufa, tukiwa tumezama katika ufisadi na laana.” 154 “Kristo … ametununulia sisi ukombozi usio
na kikomo…. Mateso aliyopata ni … dhambihu ya milele, na uwezo wa milele wa kuponya; inaitosheleza
haki ya Mungu milele kwa niaba ya wale wote wanaoitegemea kwa imani thabiti isiyotikisika.” Hata
hivyo, alifundisha wazi kwamba wanadamu, kwa sababu ya neema hiyo ya Kristo, hawako huru
kuendelea katika dhambi. “Popote palipo na imani katika Mungu, Mungu yupo pale; na popote akaapo
Mungu, hapo ndipo ilipo juhudi inayowahimiza na kuwasukuma watu katika matendo mema.” 155
Hilo ndilo lililovutia katika mahubiri ya Zwingli kiasi cha kusababisha ukumbi wa kanisa kujaa na
kufurika kwa makundi ya watu waliokuja kumsikiliza. Kidogo kidogo, kwa kadiri ambavyo wangeweza
kustahimili, aliwafunulia wasikilizaji wake ile kweli. Alikuwa mwangalifu mwanzoni asilete mambo
ambayo yangewashtua sana na kuamsha chuki yao. Kazi yake ilikuwa ni ya kuiongoa mioyo yao kwa
kuipatia mafundisho ya Kristo, kuilainisha kwa pendo la Kristo, na kuweka machoni pao kielelezo cha
Kristo; na wakisha kuzipokea kanuni zile za injili, imani zao potofu na matendo yao vingepinduliwa kwa
namna isiyozuilika.
Hatua kwa hatua Matengenezo yalisonga mbele katika mji wa Zurich. Adui zake waliamka na kufanya
upinzani wa wazi kwa mshtuko wa hofu. Mwaka mmoja kabla, mtawa huyu wa Wittenberg alikuwa
amesema Hapana kwa papa na kwa mfalme wa dola kule Worms, na sasa kila kitu kiliashiria kwamba
mapambano dhidi ya madai ya Papa pale Zurich ni kama yale yale. Mashambulio ya kujirudia-rudia
yalifanywa dhidi ya Zwingli. Mara kwa mara, katika majimbo ya kipapa, wafuasi wa injili waliletwa
kwenye nguzo ya kuchomea watu moto, lakini hilo halikutosha; lazima mwalimu wa uzushi
anyamazishwe. Kutokana na hilo, askofu wa Constance aliwatuma manaibu wake watatu kwenda
kwenye Baraza la Zurich, wamshtaki Zwingli kwa kuwafundisha watu (181) kuasi sheria za kanisa, hivyo
kuhatarisha amani na utulivu wa jamii. Alisisitiza kwamba, ikiwa mamlaka ya kanisa ingewekwa kando,
basi, kungetokea hali ya kutotawalika mahali kote. Zwingli akajibu kwamba kwa muda wa miaka minne
alikuwa akifundisha injili katika mji wa Zurich, “mji ambao ulikuwa shwari na wenye amani kuliko mji
mwingine wowote katika shirikisho.” “Basi, je,” alisema, “Ukristo sio mlinzi bora zaidi wa usalama
wote?” 156
Wale manaibu walikuwa wamewaonya wanabaraza kuendelea kuwa ndani ya kanisa, wakidai kwamba,
nje ya kanisa hakuna wokovu. Zwingli akajibu: “Hebu mashtaka haya yasiwayumbishe. Msingi wa Kanisa
ni Mwamba ule ule, ni Kristo yule yule, yeye aliyempa Petro jina lake kwa sababu alimkiri Kristo kwa
imani. Katika kila taifa, yeyote amwaminiye Bwana kwa moyo wake wote hukubaliwa na Mungu. Hapa,
kwa kweli, ndipo penye kanisa ambalo, nje ya hilo, hakuna awezaye kuokoka.” 157 Matokeo ya mkutano
huu, mmoja wa wale manaibu wa askofu akaipokea imani ya Matengenezo.
Baraza lilikataa kuchukua hatua yo yote dhidi ya Zwingli, ndipo Roma ikajiandaa kufanya shambulio
jipya. Akishakupashwa habari ya njama za maadui zake, Mwanamatengenezo alisema kwa nguvu: “Hebu
waje; mimi nawaogopa kama vile jabali la ukuta wa ukingo wa bahari linavyoogopa mawimbi

154
Wylie, book 8, chapter 9
155
D’Aubigne, book 8, chapter 9.
156
Wylie, book 8, chapter 11
157
D'Aubigne, London ed., b. 8, ch. 11
101
yanayolipiga” 158 Juhudi za viongozi wale wa kanisa zilisaidia tu kuiendeleza kazi ile waliyoazimia
kuisambaratisha. Ukweli uliendelea kuenea. Watiifu wa ile kweli kule Ujerumani, wakiwa
wamehuzunishwa na kutoweka kwa Luther, walitiwa moyo tena, walipoyaona maendeleo ya injili katika
nchi ya Uswisi.
Kadiri Matengenezo yalivyoimarishwa katika mji wa Zurich, matunda yake yalionekana kwa ukamilifu
zaidi katika kuzuia uhalifu na kuendeleza amani na utulivu. “Amani ina maskani yake katika mji wetu,”
aliandika Zwingli; “hakuna magomvi, hakuna unafiki, hakuna wivu, wala migongano. Umoja kama huo
unaweza kutoka wapi kama sio kwa Bwana, na mafundisho yetu ya dini, ambayo hutujaza matunda ya
amani na utauwa?” 159
Ushindi ambao Matengenezo yalipata uliwachochea watawala wa Kanisa la Roma kufanya juhudi zaidi za
kudhamiria kuyaondosha. (182) Walipoona jinsi walivyopata mafanikio kidogo tu katika kutokomeza kazi
ya Luther kwa njia ya mateso katika Ujerumani, waliamua kupambana na matengenezo yale kwa
kutumia silaha za matengenezo yenyewe. Wangefanya majadiliano na Zwingli, na wakisha kupanga
mambo, wangehakikisha kwamba wanapata ushindi kwa kuchagua wenyewe, sio tu mahali pa
kushindania, bali na waamuzi ambao wangewaamua hao wanaopingana. Na kama wangeweza kumtia
Zwingli katika mamlaka yao mara hii moja, basi, wangehakikisha kwamba haponyoki mikononi mwao.
Kiongozi akinyamazishwa, harakati zile zingepondwa-pondwa kwa haraka. Hata hivyo, azima hii
ilitunzwa kuwa siri kwa uangalifu.
Ilipangwa kwamba majadiliano yafanyikie Baden; lakini Zwingli hakuwepo. Baraza la Zurich, likishuku
mipango ya hila ya wafuasi wale wa upapa, na likiwa limeonywa kutokana na marundo ya mioto
iliyowashwa katika majimbo ya upapa kuwachoma wale walioikiri injili, walimkataza mchungaji wao
asijiweke katika hatari ile. Alikuwa tayari kukutana na wajumbe ambao Roma ingetuma kuja pale pale
Zurich; lakini kwenda kule Baden, ambako damu ya wafia-dini kwa ajili ya ile kweli ilikuwa imemwagwa
karibuni, ingekuwa kwenda kwenye kifo kinachojulikana wazi. Oecolampadius na Haller waliteuliwa
kuwakilisha Wanamatengenezo, wakati mtu mashuhuri, Dk. Eck, akisaidiwa na kundi kubwa la
madaktari wasomi na maaskofu, alikuwa ndiye mpambanaji upande wa Roma.
Ingawa Zwingli hakuwepo katika mkutano ule, ushawishi wake ulionekana. Makatibu wote walichaguliwa
na wafuasi wa papa, na watu wengine walikatazwa kuandika, kwa tishio la kifo. Licha ya hayo yote,
Zwingli alipata kila siku taarifa ya kuaminika ya yote yaliyosemwa pale Baden. Kila jioni mwanafunzi
aliyekuwa anahudhuria kwenye mdahalo ule aliandika kumbukumbu ya hoja zilizotolewa siku ile.
Wanafunzi wengine wawili walifanya kazi ya kuzipeleka nyaraka zile kule Zurich kwa Zwingli, pamoja na
barua za kila siku alizoandikiwa na Oecolampadius. Mwanamatengenezo yule alijibu, akitoa ushauri na
mapendekezo yake. Barua zake ziliandikwa usiku, kisha wanafunzi wale walirudi nazo Baden asubuhi.
Katika kukwepa macho ya udadisi ya mlinzi aliyewekwa penye malango ya mji, wajumbe wale walibeba
vichwani mwao vikapu vilivyokuwa na kuku, na waliruhusiwa kupita bila kipingamizi.
(183) Hivyo ndivyo Zwingli alivyofanya mapambano dhidi ya wapinzani wake wenye hila. Yeye “kafanya
kazi kubwa zaidi,” anasema Myconius, “katika maombi, kukesha bila kusinzia usiku, na ushauri wake
aliokuwa akituma kwenda Baden, kuliko vile ambavyo angefanya kama angekuwa anajadiliana ana kwa
ana na adui zake.” 160

158
Wylie, b. 8, ch. 11
159
Ibid., b. 8, ch. 15.
160
D'Aubigne, b. 11, ch. 13
102
Wakiwa wamejawa matumaini ya kupata ushindi, wawakilishi wale wa Roma walikuwa wamekuja Baden
wakiwa wamevalia mavazi ya kitajiri na yakimetameta kwa vito vya thamani. Walikula kwa anasa, meza
zao zikiwa zimejaa vyakula vizuri vya gharama kubwa na mvinyo ya kiwango cha juu sana. Mzigo wa
majukumu yao ya kidini ulifanywa mwepesi kutokana na shamrashamra zao na mandhari iliyokuwepo.
Wanamatengenezo walikuwa katika mwonekano tofauti sana, macho ya watu yakiwaangalia kama watu
waliokuwa punde zaidi kidogo tu ya kundi la ombaomba, na chakula chao kikiwafanya wakae mezani
kwa muda mfupi tu. Mwenye nyumba aliyempangisha Oecolampadius, akipata wasaa fulani
kumchungulia Oecolampadius katika chumba chake, humwona wakati mwingi akijishughulisha na
kusoma au kuomba, na akiwa katika mshangao mkuu, alitaarifu akisema kwamba mzushi yule walau
alikuwa “mcha Mungu sana.”
Katika mkutano, “Eck alipanda kwa madaha kwenye mimbara iliyokuwa imepambwa sana, wakati
mnyenyekevu Oecolampadius, aliyekuwa amevaa nguo za kawaida, alilazimishwa kukalia kiti kidogo
hafifu kilichokuwa mbele ya mpinzani wake.” 161 Sauti ya Eck ya ngurumo na uhakika wake kamwe
havikupata kumwangusha. Ari yake ile ilichochewa na tumaini lake la kupata dhahabu na umaarufu;
maana mtetezi huyu wa imani alikuwa atunukiwe zawadi yake kubwa. Pale ambapo hata hoja nzuri
zaidi zingeshindwa, aliazimu kutumia matusi, na hata kulaani.
Akiwa mtulivu asiyejitumainia, Oecolampadius alikuwa amesinyaa katika pambano hili, na akaingia
katika pambano kwa kiapo thabiti akisema: “Sitambui kanuni nyingine ya kufanya hukumu zaidi ya neno
la Mungu.” 162 Ingawa alikuwa mpole na mwenye adabu katika mwenendo, alijionyesha kuwa anao uwezo
na msimamo thabiti. Wakati wale Waroma, kulingana na desturi zao, waliheshimu mamlaka ya mapokeo
ya kanisa, Mwanamatengenezo yeye alishikilia Maandiko Matakatifu. “Mapokeo,” alisema, “hayana
nguvu katika nchi yetu ya Uswisi, isipokuwa kama yanapatana na katiba; ila, katika mambo ya imani,
Biblia ndiyo katiba yetu.” 163 (184)
Tofauti iliyokuwapo kati ya washindani wale wa pande mbili haikukosa matokeo. Sababu zilizotolewa na
Mwanamatengenezo kwa utulivu na uwazi, ambazo ziliwasilishwa kwa upole na heshima, ziligusa akili za
watu wale ambapo waligeuka na kuchukia maneno ya Eck yaliyotolewa kwa majivuno na dhana hafifu.
Majadiliano yaliendelea kwa siku kumi na nane. Wakati wa kuhitimisha wafuasi wale wa papa kwa
ujasiri walidai kwamba wamepata ushindi. Wengi miongoni mwa manaibu wale walisimama upande wa
Roma, na Baraza likasema kwamba Wanamatengenezo wameshindwa na likatangaza kwamba wao,
pamoja na kiongozi wao Zwingli, walikuwa wametengwa na Kanisa. Lakini matunda ya mkutano ule
yalidhihirisha kwamba ni upande upi ulinufaika. Shindano lile lilileta msukumo wenye nguvu kwa kazi ya
Uprotestanti, na haikuchukua muda mrefu miji ile muhimu ya Bern na Basel ikatangaza kuwa inayaunga
mkono Matengenezo.

161
Ibid., b. 11, ch. 13
162
Ibid., b. 11, ch. 13
163
Ibid., b. 11, ch. 13
103
Sura ya 10
MAENDELEO YA MATENGENEZO UJERUMANI

Kutoweka kwa Luther kimaajabu kuliamsha fadhaa katika Ujerumani yote. Maswali yaliyoulizwa kuhusu
yeye yalisikika kila mahali. Uvumi mkubwa ulienezwa, na wengi wakaamini kwamba alikuwa ameuawa.
Kulikuwa na maombolezo makubwa, sio tu kwa rafiki zake waliojionyesha waziwazi, bali pia maelfu
ambao walikuwa hawajaweka msimamo wao wazi katika Matengenezo. Wengi waliapa kulipiza kisasi
kwa kifo chake.
Viongozi wa Roma waliona hofu kubwa jinsi hisia mbaya ilivyoibuka dhidi yao. Ingawa mwanzoni
walishangilia kudhani kwamba Luther amekufa, lakini mara wakatamani kuficha kutokana na ghadhabu
ya watu. Adui zake hawakutaabishwa sana na matendo yake ya ujasiri wakati alipokuwa miongoni mwao
kama walivyotaabika alipoondolewa kwao. Wale ambao katika ghadhabu yao walikuwa wameazimia
kumwangamiza Mwanamatengenezo huyu hodari sasa walijawa na hofu kwamba alikuwa amekuwa
mateka asiye na msaada wowote. “Njia pekee iliyobaki ya sisi kujiokoa,” alisema mmoja, “ni kuwasha
taa, na kumwinda Luther ulimwenguni kote, ili kumrejesha kwa taifa hili ambalo linamtaka.” 164 Amri ya
mfalme wa dola ilionekana kukosa nguvu kabisa. Mabalozi wa papa waliudhika walipoona kwamba amri
ile haikuzingatiwa sana kama ilivyofanyika kwa hatima ya Luther.
Taarifa zilizosema kwamba Luther alikuwa salama, ingawa mfungwa, zilituliza hofu za watu, wakati
ziliamsha zaidi shauku yao ya kupendelea upande wake. Maandiko yake yalisomwa kwa (186) hamu
kubwa sana kuliko kabla ya hapo. Idadi kubwa ikaendelea kuongezeka katika kujiunga upande wa shujaa
huyu ambaye, katika mazingira yale ya kutisha, alilitetea neno la Mungu. Matengenezo yaliendelea
kupata nguvu zaidi. Mbegu ambayo Luther alikuwa amepanda ilisitawi kila mahali. Kutokuwapo kwake
kulikamilisha kazi ambayo kuwepo kwake kungeshindwa kuifanya. Watendakazi wengine waliona wajibu
wao mpya, kwa vile sasa kiongozi wao alikuwa ameondolewa. Kwa imani na juhudi mpya walisonga
mbele katika kufanya yote yaliyokuwa katika uwezo wao, ili kazi iliyokuwa imeanzishwa vizuri
isikwamishwe.
Lakini Shetani hakukaa bila kazi. Basi akajaribu kufanya kile alichokuwa amefanya katika kila harakati
ya kimatengenezo - kuwadanganya na kuwaangamiza watu kwa kuwatapeli na kuwapa kazi ya bandia
mahali pa ile ya kweli. Kama vile walivyokuwako makristo wa uongo katika karne ile ya kwanza ya
Kanisa la Kikristo, ndivyo walivyojitokeza manabii wa uongo katika karne ya kumi na sita.

164
D'Aubigne, b. 9, ch. 1

104
Watu wachache, wakiwa wameathiriwa sana na msisimko wa ulimwengu wa kidini, wakidhani kwamba
walikuwa wamepokea mafunuo toka Mbinguni, walijifanya kwamba walikuwa wamepewa na Mungu kazi
ya kuyaendeleza katika ukamilifu wake Matengenezo ambayo, walidai, yalikuwa yameanzishwa na
Luther yakiwa na mapungufu. Kiukweli, walikuwa wanaivuruga kazi ile aliyokuwa ameifanya. Waliikataa
ile kanuni kuu iliyokuwa ndio msingi wa Matengenezo - kwamba neno la Mungu ndiyo kiongozi tosha cha
imani na matendo; na mahali pa mwongozo huo usiokosea wakaweka viwango vya hisia na maono yao
wenyewe ambayo hubadilika-badilika na hayana uhakika. Kwa kitendo kile cha kumweka kando
mng’amuzi mkuu wa makosa na uongo, njia ilikuwa imefunguliwa kwa ajili ya Shetani kuitawala mioyo
ya watu jinsi apendavyo.
Mmoja wa manabii hawa alidai kwamba alikuwa ameelekezwa na malaika Gabrieli. Mwanafunzi mmoja
aliyejiunga naye aliacha masomo yake, akidai kwamba alikuwa amejaliwa na Mungu Mwenyewe hekima
ya kulitangaza neno Lake. Wengine waliokuwa na mwelekeo wa ushupavu wa dini walijiunga nao.
Shughuli za mashabiki hawa ziliamsha msisimko ambao haukuwa mdogo. (187) Mahubiri ya Luther
yalikuwa yamewaamsha watu kila mahali kuona umuhimu wa matengenezo, lakini sasa baadhi ya watu
waliokuwa waaminifu kabisa walipotoshwa na ulaghai wa manabii hawa wapya.
Viongozi wa harakati hizo waliendelea hadi Wittenberg na kusisitiza madai yao hayo kwa Melanchthon
na watendakazi wenzake. Walisema: “Tumetumwa na Mungu kuwafundisha watu. Tumefanya
mazungumzo bayana na Bwana; tunajua kitakachotokea; kwa ufupi, sisi ni mitume na manabii, na
tunavutiwa na Luther.” 165
Wanamatengenezo walishangazwa na kupata mkanganyiko. Hili lilikuwa jambo ambalo walikuwa
hawajawahi kukutana nalo kabla, na hawakujua la kufanya. Melancthon alisema: “Hakika kuna roho
zisizo za kawaida ndani ya watu hawa; lakini ni roho gani?… Kwa upande mmoja, hebu na tujihadhari
tusimzimishe Roho wa Mungu, na kwa upande mwingine, tusipotoshwe na roho ya Shetani.” 166
Tunda la mafundisho hayo mapya likaanza kuonekana wazi baada ya muda mfupi. Watu waliongozwa
kuipuuza Biblia au kuiweka kando kabisa. Shule ziliingizwa katika machafuko. Wanafunzi, wakipuuza
makatazo yote, waliacha masomo na kujiondoa chuo kikuu. Walichofanikiwa wale watu waliojidhania
kuwa mahiri kuirejesha na kuiongoza kazi ya Matengenezo ni kuifikisha tu katika ukingo wa uharibifu.
Sasa Waroma wakapata ujasiri zaidi tena na kutangaza kwa shangwe wakisema: “Bado pambano moja la
mwisho, halafu wote watakuwa wetu.” 167
Luther kule Wartburg, aliposikia kuhusu hayo yaliyotokea, alisema kwa kuguswa sana: “Nilitarajia
wakati wote kwamba Shetani angetuletea pigo hilo.” 168 Aliitazama tabia halisi ya wale waliojifanya
manabii na kuiona hatari iliyoikabili kazi ya ile kweli. Upinzani wa papa na mfalme wa dola haukuwa
umemsababishia mfadhaiko mkubwa na maumivu makubwa kama haya aliyopata sasa. Kutoka kwa wale
waliojidai kuwa marafiki wa Matengenezo kuliibuka maadui wabaya sana wa Matengenezo. Kweli zile
zile zilizokuwa zimemletea furaha na (188) faraja kubwa zilikuwa zinatumiwa kuchochea magomvi na
kuleta machafuko ndani ya kanisa.
Katika kazi ile ya Matengenezo, Luther alikuwa amesukumwa na Roho wa Mungu, na alikuwa
amepelekwa katika kiwango kinachopita uwezo wake binafsi. Hakuwa amekusudia kuchukua misimamo

165
Ibid., b. 9, ch. 7
166
Ibid., b. 9, ch. 7
167
Ibid., b. 9, ch. 7
168
Ibid., b. 9, ch. 7
105
kama ile aliyoichukua, au kufanya mabadiliko hayo makubwa. Yeye alikuwa amewekwa tu kama chombo
mkononi mwa Mungu Mwenye Uweza. Lakini, wakati mwingine alitetemeshwa na matokeo ya kazi yake.
Wakati fulani alikuwa amepata kusema: “Laiti ningejua kwamba mafundisho yangu yangeweza
kumdhuru mtu mmoja, mtu mmoja tu, hata awe mnyonge na asiyejulikana, … jambo ambalo hayawezi
kufanya, kwa maana ni injili yenyewe, … ingekuwa heri kwangu mimi kufa mara kumi kuliko kuacha
kuyakana.” 169
Na sasa mji wenyewe wa Wittenberg, kitovu hasa cha Matengenezo, ulikuwa unaanguka kwa kasi chini
ya nguvu ya ushupavu wa kidini na maasi. Hali hii ya kutisha haikutokana na mafundisho ya Luther;
lakini katika Ujerumani yote wapinzani wake walikuwa wanamshutumu yeye kwa hali ile. Kwa uchungu
wa moyo, wakati fulani aliuliza: “Basi, je, huo unaweza kuwa ndio mwisho wa kazi hii kubwa ya
Matengenezo?” 170 Kisha, kadiri alivyoendelea kushindana na Mungu katika maombi, amani ilibubujika
moyoni mwake. “Kazi hii si yangu, bali yako Wewe,” alisema; “Hautaiacha iharibiwe na ushirikina na
ushupavu.” Lakini wazo la yeye kukaa mbali na pambano lile kwa muda zaidi wakati wa hatari ile,
lisingeungwa mkono na yeye. Aliamua kurudi Wittenberg.
Bila kukawia, alishika safari yake ile ya hatari. Alikuwa chini ya amri ya marufuku ya dola. Maadui
walikuwa na uhuru wa kuyachukua maisha yake; rafiki zake walikatazwa kumsaidia wala kumpa hifadhi.
Serikali ya dola ilikuwa inachukua hatua kali sana dhidi ya wafuasi wake. Lakini yeye aliona kwamba
kazi ya injili ilikuwa hatarini, na katika jina la Bwana alitoka bila hofu yoyote ili kupigana kwa ajili ya
ile kweli.
Katika barua aliyoandika kwa mtawala, baada ya kueleza kusudi lake la kuondoka Wartburg, Luther
alisema: “Na ijulikane kwako mheshimiwa ya kwamba ninakwenda Wittenberg chini ya ulinzi wa hali ya
juu kuliko ule wa wakuu na watawala. Sifikirii kupata msaada kutoka kwako mheshimiwa, na mbali
kuliko kutamani ulinzi wako, (189) mimi ndiye ningekulinda wewe. Kama ningejua kwamba wewe
mheshimiwa unaweza au ungependa kunilinda, nisingeenda kabisa kule Wittenberg. Hakuna upanga
wowote unaoweza kuiendeleza kazi hii. Lazima Mungu peke yake ndiye afanye kila kitu, pasipo msaada
wala kibali cha mwanadamu. Yeye aliye na imani kuu kuliko zote ndiye aliye na uwezo mkubwa zaidi wa
kulinda.” 171
Katika barua ya pili, aliyoandika akiwa njiani kuelekea Wittenberg, Luther aliongeza hivi: “Mimi niko
tayari kupata shutuma zako mheshimiwa, na hasira ya ulimwengu mzima. Je! watu wa Wittenberg si
kondoo wangu? Je! Mungu hakuwakabidhi kwangu? Na, je, kama ni lazima, hainipasi kujiweka katika
hatari ya kifo kwa ajili yao? Licha ya hayo, naogopa kuona mlipuko wa kutisha katika Ujerumani, ambao
kwa huo Mungu ataliadhibu taifa letu.” 172
Kwa tahadhari kubwa na unyenyekevu, lakini kwa uamuzi thabiti, aliingia katika kazi yake. “Kwa neno,”
alisema, “lazima tupindue na kuharibu kile kilichosimamishwa kwa mabavu. Sitatumia nguvu dhidi ya
washirikina na wasioamini…. Hakuna mtu wa kushurutishwa. Uhuru ndio kiini hasa cha imani.” 173
Punde ikatangazwa katika mji wote wa Wittenberg kwamba Luther alikuwa amerudi na ya kwamba
ilikuwa ahubiri. Watu wakakusanyika toka pande zote, na kanisa likajaa na kufurika. Akipanda

169
Ibid., b. 9, ch. 7
170
Ibid., b. 9, ch. 7
171
Ibid., b. 9, ch. 8
172
Ibid., b. 9, ch. 7
173
Ibid., b. 9, ch. 8
106
mimbarani, alifundisha, kuonya na kukemea kwa hekima na upole mwingi. Akigusia mwenendo wa
baadhi ya watu walioazimia kutumia njia za mabavu kukomesha misa, alisema:
“Misa ni kitu kibaya; Mungu anapingana nayo; inastahili kukomeshwa; na ningependa kwamba mahali
pake ulimwenguni pote kuwe na chakula cha injili. Lakini mtu yeyote asitenganishwe nayo kwa
kulazimishwa. Yatupasa kuliacha jambo hilo mikononi mwa Mungu. Lazima neno lake litende, sio sisi.
Na kwa nini iwe hivyo? mtauliza. Kwa sababu mimi siichukui mioyo ya watu mkononi mwangu, kama vile
mfinyanzi achukuavyo udongo wa kufinyanga. Tunayo haki ya kusema: hatuna haki ya kutenda. Hebu sisi
tuhubiri; yaliyobaki ni ya Mungu. Maana kama ningetumia nguvu, ingenifaidi nini? Kukunja uso, kufuata
desturi, kuiga maneno na matendo ya wengine, kufuata maagizo ya wanadamu, na unafiki…. Lakini
kusingekuwapo unyofu (190) wa moyo, wala imani, wala wema. Mahali yanapokosekana mambo haya
matatu, mambo yote hukosekana, nami nisingependa matokeo ya namna hiyo…. Mungu hufanya mengi
zaidi kwa neno lake peke yake kuliko vile ambavyo wewe na mimi na ulimwengu wote tungefanya kwa
kuunganisha nguvu zetu wote. Mungu anashikilia moyo; na moyo unapochukuliwa naye, yote yanakuwa
yamepatikana….
“Nitahubiri, nitajadili, na nitaandika; lakini sitamshurutisha mtu ye yote, maana imani ni tendo la hiari.
Angalieni ambavyo nimefanya. Nilisimama kinyume cha papa, hati za msamaha, na wafuasi wa papa, ila
pasipo kutumia mabavu wala fujo. Nilitanguliza neno la Mungu; nilihubiri na kuandika - hayo ndiyo yote
niliyofanya. Na hata nilipokuwa usingizini,… lile neno nililokuwa nimehubiri likaupindua upapa, kiasi
kwamba hakuna mkuu wala mfalme wa dola ambaye amelidhuru sana. Na bado mimi sikufanya lolote;
neno peke yake lilifanya yote. Kama ningeazimu kutenda kwa nguvu, huenda Ujerumani yote ingekuwa
imegharikishwa na damu. Lakini matokeo yake yangekuwa nini? Maangamizi na uharibifu wa vyote viwili
mwili na roho. Kwa hiyo, mimi nilikaa kimya, na kuliacha neno liende peke yake ulimwenguni kote.” 174
Siku kwa siku, kwa juma zima, Luther aliendelea kuhubiri kwa makutano yale yaliyokuwa na hamu.
Neno la Mungu likavunja lile vuguvugu la msisimko wa ushupavu. Nguvu ya injili ikawarudisha katika njia
ya ukweli watu wale waliokuwa wamepotoshwa.
Luther hakuwa na nia ya kupambana na washupavu wale ambao njia yao ilileta maovu makubwa.
Aliwafahamu kuwa walikuwa watu wasiokuwa na maamuzi sahihi na wenye harara, ambao, wakati
wanadai kuwa wamepewa nuru maalum toka mbinguni, wasingestahimili mgongano hata kwa kiwango
kidogo au hata kukosolewa au kushauriwa kwa wema. Wakiwa wamejipa mamlaka ya juu, walitaka kila
mtu, pasipo kuhoji, ayakubali madai yao. Lakini, walipohitaji kuhojiana naye, alikubali kukutana nao;
naye alifanikiwa kuzifichua hila zao hata walaghai wale wakaondoka mara moja Wittenberg.
Ule ushupavu wa dini ulidhibitiwa kwa muda; lakini baada ya miaka kadhaa uliibuka ukiwa na nguvu
nyingi zaidi na matokeo ya kutisha zaidi. Kuhusu viongozi wa harakati hizi, Luther alisema: (191) “Kwao
wao Maandiko Matakatifu yalikuwa ni kama andiko lililokufa tu, na wote walianza kupiga makelele
wakisema, ‘Roho! Roho!’ Lakini kwa hakika kabisa mimi sitafuata kwenda kule roho yao inakowaongoza.
Naomba Mungu wa rehema zake anihifadhi mbali na kanisa ambalo halina watu wengine ila watakatifu.
Natamani kukaa pamoja na wanyenyekevu, walio dhaifu, wagonjwa, wanaojua na kuhisi dhambi zao, na
wale ambao wanaugua mioyoni na kumlilia Mungu daima kutoka katika vina vya mioyo yao ili kupata
faraja na msaada wake.” 175

174
Ibid., b. 9, ch. 8
175
Ibid., b. 10, ch. 10
107
Thomas Munzer, shupavu wa dini maarufu kuliko wote, alikuwa mtu mwenye uwezo mkubwa, ambao,
ungetumika vizuri, ungemwezesha kufanya mema; lakini hakuwa amejifunza kanuni za kwanza za dini
ya kweli. “Alikuwa amejawa na hamasa ya kuufanyia matengenezo ulimwengu mzima, na kusahau,
kama watu wengi wenye ushabiki wafanyavyo, kwamba ilipasa matengenezo yaanzie kwake yeye
mwenyewe.” 176 Alikuwa na tamaa ya kupata nafasi na mvuto, na alikuwa hapendi kuwa wa pili, hata
kwa Luther. Alitangaza kwamba Wanamatengenezo, kwa kuweka mamlaka ya Maandiko mahali pa yale
ya papa, walikuwa wanaanzisha tu mfumo mwingine wa upapa. Alidai kwamba, yeye mwenyewe
alikuwa amepewa utume mtakatifu wa kuanzisha matengenezo ya kweli. “Yeye aliye na roho hii,”
alisema Munzer, “anayo imani ya kweli, hata kama hatayaona kamwe Maandiko katika maisha yake
yote.” 177
Walimu wale wa dini ya ushupavu walijitoa na kutawaliwa na hisia, wakichukulia kila wazo na hisia ya
moyoni kama sauti ya Mungu; matokeo yake, wakapitiliza sana. Wengine walifikia hatua ya kuchoma
moto Biblia zao, wakisema: “Andiko linaua, bali roho inahuisha.” Mafundisho ya Munzer yaliivutia sana
tamaa ya wanadamu ya kutaka makuu, maana yalikidhi kiburi chao kwa kuweka mawazo na maoni ya
kibinadamu juu kuliko neno la Mungu. Mafundisho yake yalipokewa na maelfu. Mara akashutumu
utaratibu wote uliotumika katika ibada ya hadhara, na akatangaza kwamba kuwatii watawala ilikuwa ni
kujaribu kumtii Mungu na Belial.
Yakiwa yameanza kuondokana na kongwa la upapa, mawazo ya watu yalikuwa pia yanaelekea kukosa
uvumilivu wa kuwa chini ya mipaka ya mamlaka ya kiraia. Mafundisho ya kimapinduzi ya Munzerr, (192)
ikidaiwa kwamba yana idhini toka juu, yaliwaongoza kujitenga na udhibiti wote na wakajiachilia
kutawaliwa na maono na hisia zao wenyewe. Hali ya kutisha mno iliyofuata ni kuchochea maasi na
machafuko, na maeneo ya Ujerumani yakalowa damu.
Masumbuko ya moyo ambayo Luther alikuwa ameyapitia kule Erfurt yalimwelemea sasa yakiwa na nguvu
mara mbili alipoona matokeo ya ushupavu wa dini yakihusishwa na Matengenezo. Wakuu wa upapa
walitangaza – na wengi walikuwa tayari kuunga mkono usemi wao - kwamba maasi yale yalikuwa ni
tunda halisi la mafundisho ya Luther. Ingawa shitaka lile halikuwa na msingi hata kidogo, lisingeweza
kufanya kitu isipokuwa kumletea Mwanamatengenezo maumivu makubwa. Kwamba kazi ya ile kweli
ifedheheshwe kwa kuhesabiwa pamoja na ushupavu ule mbaya wa dini, lilionekana kuwa jambo kubwa
kuliko alivyoweza kustahimili. Kwa upande mwingine, viongozi wa maasi yale walimchukia Luther kwa
sababu hakuwa tu ameyapinga mafundisho yao ya dini na kukataa madai yao ya kuwa na uvuvio
mtakatifu, bali pia alikuwa amewatangaza kama waasi dhidi ya serikali ya kiraia. Kwa kulipiza kisasi
wakamshutumu kuwa ndiye mnafiki mkuu. Alionekana kana kwamba amejiletea uadui toka kwa pande
zote mbili wakuu na watu wa kawaida.
Warumi walishangilia, wakitarajia kushuhudia anguko la haraka la Matengenezo; na walimshutumu
Luther, hata kwa makosa yale aliyokuwa amekazana kuyasahihisha. Kikundi kile cha washupavu wa dini,
wakidai kwa uongo kwamba walikuwa wametendewa isivyo haki kabisa, walifanikiwa kupata huruma ya
kundi kubwa la watu, na, kama ilivyo mara nyingi kwa wale wanaosimama upande usio sahihi, walikuja
kuonekana kama mashujaa wafia-dini. Hivyo wale waliokuwa wanatumia kila aina ya nguvu kupinga
Matengenezo walisikitikiwa na kusifiwa kwamba ni wahanga wa ukatili na ukandamizaji. Hii ilikuwa kazi
ya Shetani, ikisukumwa na roho ile ile ya uasi iliyodhihirika kwanza mbinguni.

176
Ibid., b. 9, ch. 8
177
Ibid., b. 10, ch. 10

108
Wakati wote Shetani anatafuta kuwadanganya wanadamu na kuwafanya waiite dhambi kuwa ni haki, na
haki kuwa ndiyo dhambi. Kazi yake hiyo imefanikiwa kiasi gani! Ni mara ngapi lawama na shutuma
zimetupwa kwa watumishi waaminifu wa Mungu kwa sababu wao (193) watasimama bila hofu kuitetea
ile kweli! Wanadamu ambao ni vibaraka tu wa Shetani wanatukuzwa na kusifiwa, na hata kuonwa kama
wafia-dini, wakati wale wanaostahili kuheshimiwa na kutegemezwa kwa uaminifu wao kwa Mungu,
wanaachwa wasimame peke yao, wakilaumiwa na kushutumiwa.
Utakatifu wa bandia, utakaso wa uongo, bado unafanya kazi yake ya udanganyifu. Katika mwonekano
tofauti-tofauti unaonyesha roho ile ile kama ya mnamo siku za Luther, ukigeuza uelekeo wa mioyo ya
watu kwenda mbali na Maandiko na kuwaongoza watu kufuata hisia na maono yao wenyewe badala ya
kufanya utii kwa sheria ya Mungu. Hii ni moja ya mbinu za Shetani zinazofanikiwa sana katika kutoa
shutuma dhidi ya usafi wa maisha na ukweli.
Pasipo hofu Luther aliitetea injili dhidi ya mashambulizi kutoka kila upande. Neno la Mungu
lilijithibitisha kuwa ndiyo silaha yenye nguvu katika kila pambano. Kwa kutumia neno lile alipigana vita
dhidi ya mamlaka ya papa iliyojiinua, na dhidi ya falsafa ya kimantiki ya wasomi, wakati huo huo
akisimama imara kama mwamba dhidi ya ushupavu wa dini ambao ulitafuta kujifungamanisha na
Matengenezo.
Kila kimoja cha vikundi hivi vilivyoleta upinzani kilikuwa kwa namna yake kinayaweka kando Maandiko
Matakatifu na kutukuza hekima ya kibinadamu kama chimbuko la ukweli wa kidini. Nadharia ya mantiki
ikaabudiwa kama kigezo cha mambo ya dini. Uroma, ukidai kuwa na papa mwenye uvuvio ulioshuka
katika mstari usiovunjika toka kwa mitume, na ambao haubadiliki kwa wakati wote, unatoa nafasi ya
kutosha kwa kila aina ya ubadhirifu na udhalimu uliofichwa chini ya utakatifu wa agizo la utume. Uvuvio
ule uliodaiwa na Munzer na wenzake haukutoka kwenye chimbuko lolote lililo juu zaidi ya mawazo ya
kubuni, na msukumo wake ulileta maasi dhidi ya mamlaka yote, ya wanadamu au ya Mungu. Ukristo wa
kweli hupokea neno la Mungu kama jumba kuu la hazina ya ile kweli iliyovuviwa na kama kipimo cha
kujaribia uvuvio wote.
Aliporudi kutoka Wartburg, Luther alikamilisha kazi yake ya kutafsiri Agano Jipya, na baada ya muda
mfupi injili ilitolewa kwa watu wa Ujerumani katika (194) lugha yao. Tafsiri hii ilipokelewa kwa furaha
kubwa na wote walioipenda ile kweli; lakini ilikataliwa kwa dharau na wale waliochagua mapokeo na
amri za wanadamu.
Makasisi waliingiwa na hofu kwa kufikiri kwamba sasa watu wa kawaida wangeweza kujibizana nao juu
ya maagizo ya neno la Mungu, na hivyo ujinga wao ungewekwa wazi. Silaha za kutumia hoja ya akili
zilikuwa hazina nguvu kabisa dhidi ya upanga ule wa Roho. Roma iliitisha mamlaka yake yote kuzuia
kutawanywa kwa Maandiko yale; lakini amri, laana, na mateso, yalikuwa kazi bure kabisa. Kadiri
ilivyozidi kuilaani na kuipiga marufuku Biblia, ndivyo watu walivyozidi kuwa na hamu kubwa ya kutaka
kujua kilichokuwa kinafundishwa humo. Wote waliokuwa wanaweza kusoma walikuwa na hamu ya
kujifunza neno la Mungu wao wenyewe. Waliibeba walikokwenda, na waliisoma na kusoma tena, wala
hawakutosheka mpaka walipokuwa wamekariri sehemu kubwa. Akiona jinsi Agano Jipya lilivyopokelewa
kwa kupendwa, Luther akaanza mara kutafsiri Agano la Kale, na kulichapisha sehemu-sehemu kwa
kadiri zilivyowahi kukamilika katika kutafsiri.
Maandiko ya Luther yalipokelewa kwa namna ile ile mjini na kijijini. Kile ambacho Luther na wenzake
waliandika, kilitawanywa na wengine. Watawa, wakiwa wameshawishika kuhusu kutokuwa halali kwa
masharti ya utawa, wakiwa katika kutamani kubadilisha maisha yao ya muda mrefu katika uvivu na
kuyafanya yawe ya kufanya kazi kwa bidii, lakini wakiwa wajinga wasio na uwezo wa kulitangaza neno
109
la Mungu, walisafiri katika majimbo wakitembelea vijiji na vibanda vya mashambani, ambako waliuza
vitabu vya Luther na wenzake. Muda si muda Ujerumani yote ikafunikwa na wauzaji hawa wa vitabu.” 178
Maandiko haya yalisomwa kwa hamu kubwa na matajiri kwa maskini, wasomi kwa wasiosoma. Usiku
walimu wa shule za vijijini waliyasoma kwa sauti kubwa kwa vikundi vidogo vilivyokusanyika kando ya
moto. Kwa kila jitihada roho kadhaa zingeaminishwa kwa ile kweli na, wakilipokea lile neno kwa furaha,
nao wangerudi na kuwaambia wenzao habari ile njema.
(195) Maneno yale ya uvuvio yalithibitishwa: “Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, na kumfahamisha
mjinga.” Zaburi 119:130. Kujifunza Maandiko kulikuwa kunaleta badiliko kubwa katika akili na mioyo ya
watu. Utawala wa papa ulikuwa umeweka juu ya watu wake kongwa zito la chuma lililowashikilia katika
ujinga na hali ya chini. Kuadhimisha taratibu za dini kulikuwa kumeimarishwa kwa ufundi; lakini moyo
wao na akili vilikuwa na sehemu ndogo katika ibada zao zile. Mahubiri ya Luther, yakiziweka wazi kweli
zile za neno la Mungu, kisha lile neno lenyewe, likiwa limewekwa mikononi mwa watu wa kawaida,
lilikuwa limeamsha uwezo wao uliokuwa umelala, si tu kwamba yalizitakasa na kuziadilisha tabia zao za
kiroho, bali pia yaliingiza nguvu mpya na hamasa katika akili.
Watu wa madaraja yote waliweza kuonekana wakiwa na Biblia mikononi mwao, wakitetea mafundisho
ya Matengenezo. Watu wa upapa waliokuwa wamewaachia makasisi na watawa kazi ya kujifunza
Maandiko, sasa waliwataka wajitokeze mbele yao na kukanusha mafundisho haya mapya. Lakini, wakiwa
na usawa wa ujinga wa Maandiko na uweza wa Mungu, makasisi na watawa wakashindwa kabisa na wale
waliokuwa wamewashutumu kwamba walikuwa si wasomi na kuwa ni wazushi. “Kwa masikitiko,”
alisema mwandishi mmoja wa Kikatoliki, “Luther alikuwa amewashawishi wafuasi wake kuacha kuweka
imani yao katika uongozi mwingine wowote zaidi ya Maandiko Matakatifu.” 179 Makundi yangeweza
kukusanyika kuisikiliza kweli inayotamkwa na watu wenye elimu ndogo, na hata wanapojadiliana na
wasomi na wanathiolojia mahiri. Ujinga wa kufedhehesha wa wakuu wale ulidhihirika wakati hoja zao
zilipojibiwa kwa mafundisho yaliyokuwa rahisi ya neno la Mungu. Vibarua, wanajeshi, wanawake, na
hata watoto walikuwa wanayafahamu zaidi mafundisho ya Biblia kuliko makasisi na madaktari wasomi.
Tofauti iliyokuwapo kati ya wanafunzi wale wa injili na watetezi wale wa ushirikina wa kipapa
haikuonekana ndogo katika safu za wasomi kuliko miongoni mwa watu wa kawaida. “Miongoni mwa
wapinzani wa watu wa utawala wa mfumo wa msonge wa kidini, ambao walikuwa wamepuuza (196)
kusoma lugha na kukuza ufahamu wa fasihi, … walikuwa ni vijana wale wenye akili, waliojitoa
kujifunza, kuyachunguza Maandiko, na kujiweka katika hali ya kuyafahamu maandiko bora yale ya zama
zilizopita. Wakiwa na akili inayofanya kazi, roho iliyoamshwa, na moyo wa kishujaa, vijana wale
walipata kwa muda mfupi ujuzi ule ambao kwa kipindi kirefu kuanzia pale hapakuwa na mtu aliyeweza
kushindana nao…. Kwa hiyo, pindi vijana hawa watetezi wa Matengenezo walipokutana na madaktari
wasomi wa Kirumi katika mkusanyiko wowote, waliwashambulia kwa urahisi na kwa imani kiasi kwamba
watu wale wajinga walibabaika, wakatahayari, na kuangukia katika dharau machoni pa watu wote.” 180
Kadiri makasisi wa Kirumi walipoona waumini wao wanapungua, waliomba msaada wa mahakimu, na
kwa kila njia iliyokuwa katika uwezo wao walijitahidi sana kuwarudisha watu wao. Lakini watu wale
walikuwa wamepata kile kilichokidhi mahitaji ya roho zao katika mafundisho haya mapya, ndipo

178
Ibid., b. 9, ch. 11
179
D'Aubigne, b. 9, ch. 11
180
Ibid., b. 9, ch. 11
110
wakawapa kisogo wale waliokuwa wamewalisha kwa muda mrefu makapi yasiyofaa ya taratibu zao za
ibada na mapokeo ya wanadamu.
Wakati mateso yalipochochewa dhidi ya walimu wa ile kweli, waliyazingatia maneno ya Kristo: “Lakini
watakapowafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine.” Mathayo 10:23. Nuru ilipenya kila mahali.
Wakimbizi wale wangeweza kupata mahali fulani ambapo mlango wa ukarimu ulikuwa umefunguliwa
kwa ajili yao, nao walipokuwa pale, wangeweza kumhubiri Kristo, wakati mwingine kanisani, au,
wakizuiliwa hiyo fursa, walihubiri katika nyumba za watu binafsi au katika sehemu za wazi. Mahali
popote walipoweza kupata wasikilizaji palikuwa ni hekalu lililotengwa kwa kazi hiyo. Ukweli,
uliohubiriwa kwa nguvu na imani kama ile, ulienea kwa nguvu isiyoweza kuzuilika.
Kuwaomba wenye mamlaka ya kanisa na serikali kuufuta uzushi ule ilikuwa kazi bure. Kutumia vifungo
gerezani, mateso, moto, na upanga ilikuwa kazi bure. Maelfu ya waumini walitia muhuri imani yao kwa
damu yao, lakini bado kazi ile ikasonga mbele. Mateso yalisaidia tu kuieneza ile kweli, na ushupavu ule
ambao Shetani alijitahidi kuuunganisha na kazi hii ulileta matokeo yaliyofanya tofauti kati ya kazi ya
Shetani na kazi ya Mungu iwe dhahiri zaidi.

111
Sura ya 11
UPINZANI KUTOKA KWA WAKUU

Ushuhuda mmoja kati ya shuhuda nzuri zilizopata kutajwa kwa ajili ya Matengenezo ni Upinzani wa
Wakristo waliokuwa wakuu wa Ujerumani uliotokea katika Baraza la Spires mwaka 1529. Ujasiri, imani,
na uthabiti wa watu wa Mungu wale uliviletea vizazi vilivyofuata uhuru wao wa mawazo na wa dhamiri.
Upinzani ule ulilipatia kanisa lililokuwa katika matengenezo jina la Protestant; kanuni zake ndizo “kiini
cha Uprotestanti.” 181
Siku ya giza na ya kutisha kwa Matengenezo ilikuwa imekuja. Licha ya lile Tamko la Worms,
lililomtangaza Luther kuwa ni mhalifu na kupiga marufuku kufundisha au kuamini mafundisho yake,
uvumilivu wa kidini ulikuwa bado umedumu katika dola. Majaliwa ya Mungu yalikuwa yamedhibiti nguvu
zilizopinga ukweli. Charles V aliazimu kuukandamiza Uprotestanti, lakini mara nyingi alipoinua mkono
wake kuyapiga alilazimishwa kuahirisha mashambulizi yake. Tena na tena maangamizi ya haraka ya
wale wote waliothubutu kujiweka katika kuipinga Roma yalionekana kuwa hayaepukiki; lakini katika
wakati wenyewe mgumu majeshi ya Waturuki yalijitokeza katika mpaka wa mashariki, au mfalme wa
Ufaransa, au hata papa mwenyewe, wakiwa na wivu dhidi ya ukuu wa mfalme uliokuwa unaongezeka,
walifanya vita dhidi yake; na hivyo, katika misukosuko ya vita na machafuko ya mataifa, Matengenezo
yalikuwa yameachwa katika kuimarika na kuenea.
Hatimaye, hata hivyo, watawala wa kipapa walikuwa wameukomesha ugomvi uliokuwa miongoni mwao,
ili wapambane na Matengenezo kwa nguvu moja. Baraza la Spires la mwaka 1526 lilikuwa limelipatia
kila jimbo uhuru kamili katika mambo ya dini hadi kufikia wakati wa (198) mkutano wa baraza kuu;
lakini muda si muda tangu kupita kwa hatari zile zilizosababisha kutolewa kwa kibali kile, mfalme wa
dola akaitisha baraza la pili likutane Spires mwaka wa 1529 kwa kusudi la kuvunjavunja uzushi. Wakuu
walikuwa washawishiwe, kwa njia za amani kama ingewezekana, ili wapate kuwa upande ulio kinyume
na Matengenezo; lakini kama njia hizi zingeshindwa, Charles alikuwa tayari kutumia upanga.
Watu wa upapa walifurahi sana. Walijitokeza Spires kwa wingi sana, na walionyesha waziwazi chuki yao
dhidi ya Wanamatengenezo na wote waliopenda Wanamatengenezo. Melanchthon alisema: “Sisi ni
takataka na uchafu wa ulimwengu huu; lakini Kristo atawaangalia watu wake maskini walio chini, naye
atawahifadhi.” 182 Wakuu wale wa kiinjilisti waliohudhuria Baraza walikatazwa injili isihubiriwe hata
mahali walipoishi. Lakini watu wale wa Spires walikuwa na kiu ya neno la Mungu, na, licha ya marufuku

181
D'Aubigne, b. 13, ch. 6
182
Ibid., b. 13, ch. 5
112
ile, maelfu walimiminika kwenda kwenye huduma za ibada zilizoendeshwa katika kanisa la mkuu wa
jimbo la Saksoni.
Jambo hili liliharakisha hatari. Ujumbe toka kwa mfalme ulitangazwa kwa Baraza kwamba kwa kuwa
azimio lile lililotoa uhuru wa dhamiri lilikuwa limeleta machafuko makubwa, mfalme wa dola alitaka
libatilishwe. Kitendo hiki cha kidhalimu kiliamsha hasira na hofu ya wale wainjilisti wa Kikristo. Mmoja
wao alisema: “Kristo ameangukia mikononi mwa Kayafa na Pilato kwa mara nyingine.” Waroma wakawa
wakali sana. Mtu wa upapa shupavu alitangaza: “Waturuki ni bora kuliko Walutheri; maana Waturuki
wanaadhimisha siku za kufunga, wakati Walutheri wanazikiuka. Kama ni lazima tuchague kimoja kati ya
Maandiko Matakatifu ya Mungu na makosa ya zamani ya kanisa, yatupasa kukataa hilo la kwanza.”
Melanchthon alisema: “Kila siku, katika mkutano uliojaa watu, Faber anawapiga jiwe jipya
wanainjili.” 183
Uvumilivu wa kidini ulikuwa umewekwa kisheria, na majimbo yale yenye injili yaliazimu kupinga
uingiliwaji wa haki zao. Luther, akiwa bado yuko chini ya marufuku ya Tamko la Worms, hakuruhusiwa
kuhudhuria pale Spires; lakini nafasi yake ilijazwa na watendakazi wenzake na wakuu wa nchi ambao
walikuwa wameinuliwa na Mungu ili kuitetea kazi yake katika dharura hii. Mheshimiwa Frederick wa
Saksoni, (199) mlinzi wa zamani wa Luther, alikuwa ameondolewa kwa kifo; lakini Duke John, ndugu na
mrithi wa utawala wake, alikuwa ameyakaribisha Matengenezo kwa furaha, na akiwa rafiki mpenda
amani, alionyesha juhudi kubwa na ujasiri katika mambo yote yaliyohusiana na matakwa ya imani hii.
Makasisi walidai kwamba majimbo yaliyokubali Matengenezo yajisalimishe kabisa kwa mamlaka ya
Roma. Kwa upande mwingine, Wanamatengenezo walidai uhuru ambao ulikuwa umeruhusiwa kabla.
Wasingeweza kukubali kwamba Roma iyarudishe tena chini ya utawala wake majimbo yale yaliyokuwa
yamelipokea neno la Mungu kwa furaha kubwa.
Hatimaye ilipendekezwa kama maridhiano kwamba mahali ambapo Matengenezo yalikuwa
hayajaanzishwa, Tamko la Worms litekelezwe kwa ufasaha; na ya kwamba “katika maeneo ambako
watu walikuwa wameacha kulifuata, na katika maeneo ambako watu wasingeweza kuliheshimu pasipo
hatari ya maasi, basi watu wasifanye matengenezo mengine yoyote mapya, wasiguse jambo lolote
linalobishaniwa, wasipinge uadhimishaji wa misa, wasimruhusu mfuasi wa Roman Catholic kupokea
imani ya Kilutheri." 184 Hatua hiyo ilipitishwa na Baraza, ikawaridhisha sana wale makasisi wa papa na
maaskofu.
Laiti tamko hili lingetekelezwa, “Matengenezo yasingeweza kuenezwa … mahali ambako yalikuwa bado
hayajajulikana, wala yasingeweza kuimarishwa juu ya misingi imara … kama pale ambapo tayari
yalikuwapo.” 185 Uhuru wa kusema ungekuwa umezuiwa. Hakuna kuongoa ambako kungeruhusiwa. Na
marafiki wa Matengenezo walitakiwa kutekeleza mazuio na makatazo haya mara moja. Matumaini ya
ulimwengu yalionekana kana kwamba yako karibu na kuzimika. “Kuanzishwa tena kwa utawala msonge
wa Roma … kungeyarejesha hakika yale mabaya ya zama zilizokuwa zimepita;” na nafasi ingepatikana
ya “kukamilisha uharibifu wa kazi ile iliyokuwa tayari imetikiswa kwa nguvu” kutokana na ushupavu wa
kidini na mafarakano. 186

183
Ibid., b. 13, ch. 5
184
Ibid., b. 13, ch. 5
185
Ibid., b. 13, ch. 5
186
Ibid., b. 13, ch. 5
113
Pindi kundi la wainjili lilipokutana kwa ajili ya kushauriana, waliangaliana kwa mtazamo wa fadhaa.
Swali lilipita kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine: “Nini la kufanya?” Mambo makubwa ya
kiulimwengu yalikuwa hatarini. “Je! viongozi wa Matengenezo (200) watajisalimisha, na kuikubali amri
hiyo? Ingekuwa rahisi kiasi gani kwa Wanamatengenezo hawa walio katika hatari, ambayo ilikuwa kubwa
kweli kweli, kujihoji kuelekea katika njia isiyo sahihi! Kungekuwa na visingizio vingapi ambavyo
vingetumika kutoa sababu zinazokubalika ili kusalimu amri? Wakuu wa imani ya Kiluther walikuwa
wamepewa uhuru wa kuendelea na dini yao. Upendeleo kama huo ulitolewa kwa wote waliokuwa chini
yao ambao, kabla ya kupitishwa kwa tamko lile, walikuwa wameupokea mtazamo ule wa matengenezo.
Je! Hili lisingewafanya waridhike? Kujisalimisha kungeepusha hatari kiasi gani! Upinzani wao
ungewaingiza katika matatizo na mizozo kiasi gani isiyojulikana bado! Nani ajuaye fursa ambazo
wangepokea mnamo siku za usoni? Hebu tuikumbatie amani; hebu na tulitwae tawi la mzeituni
linaloshikiliwa na Roma, na tuyafunge majeraha ya Ujerumani. Kwa hoja kama hizi Wanamatengenezo
wangeweza kujihalalishia uamuzi wa kukubali njia ile ambayo kwa hakika ingepindua kazi yao katika
muda usiokuwa mrefu.
“Kwa furaha, waliichunguza kanuni ya msingi wa mpango ule, na wakatenda kwa imani. Ilikuwa kanuni
gani ile? Ilikuwa kawaida sahihi ya Roma kulazimisha dhamiri ya mtu kwa nguvu na kudhibiti uhuru wa
mtu kuhoji. Lakini, je, wao wenyewe pamoja na walio chini yao katika Uprotestanti si walifurahia uhuru
wa dini? Ndiyo, walikuwa nao kama upendeleo maalum tu uliowekewa masharti katika mpango ule,
lakini si kama haki. Kwa wote waliokuwa nje ya mpango huu, kanuni hiyo kuu ya mamlaka ile ilitawala;
dhamiri ya mtu ilikuwa nje ya uwezo wa kuhojiwa mahakamani; Roma ilikuwa mwamuzi wa mwisho
asiyekosea, na ilikuwa lazima atiiwe. Kuukubali mpango ule uliopendekezwa ingekuwa ni kukubali
kabisa kwamba uhuru wa dini ungepaswa kuwa ndani ya mipaka ya jimbo la Saksoni lililopokea imani ya
Matengenezo; na kwa ulimwengu mwingine wote wa Kikristo, uhuru wa mtu kuhoji na kuikiri imani ya
Matengenezo ilikuwa ni makosa ya jinai, na lazima yangepatilizwa kwa kifungo cha gereza la chini ya
ardhi na kuchomwa moto kwenye nguzo. Je! wangeafiki kuufanya uhuru wa dini uwe wa eneo fulani tu?
Kuruhusu itangazwe kwamba Matengenezo yalikuwa yameongoa mtu wa mara ya mwisho? Kwamba
yalikuwa yameshindwa kusonga mbele zaidi ya pale palipoonekana kama eneo lake la mwisho kufika? Na
ya kwamba popote Roma ilipotawala katika saa ile, pale ufalme wake ungedumu milele? Je!
Wanamatengenezo wangekuwa wametangaza kwamba hawana hatia ya damu ya mamia na maelfu ya
wale ambao, kwa kutekelezwa kwa mpango ule, wangelazimika kuyatoa (201) mhanga maisha yao
katika nchi yote ya Kipapa? Jambo hilo lingekuwa ni kuisaliti, katika saa ile ngumu, kazi ya injili pamoja
na uhuru wa Ulimwengu wote wa Kikristo.” 187 La sivyo “wangetoa kafara ya kila kitu, hata majimbo yao,
taji zao, na maisha yao.” 188
“Hebu na tukatae amri hii,” wale wakuu walisema. “Katika mambo yanayohusu dhamiri ya mtu walio
wengi hawana mamlaka. Wajumbe wale wakatangaza, wakisema: “Ni kwa amri ile ya mwaka wa 1526
kwamba sisi tunawiwa amani ambayo dola hii inaifurahia: kuipiga marufuku kungeweza kuijaza shida na
migawanyiko nchi ya Ujerumani. Baraza halina uwezo wa kufanya kitu zaidi ya kuhifadhi uhuru wa dini
mpaka hapo halmashauri itakapokutana.” 189 Kulinda uhuru wa dhamiri ya mtu ndilo jukumu la serikali,
na huu ndio mpaka wa mamlaka yake katika masuala ya dini. Kila serikali ya kidunia inayojaribu
kurekebisha au kulazimisha maadhimisho fulani ya kidini kwa kutumia mamlaka ya kidola inakiuka
kanuni ile ile ambayo Mkristo wa kiinjili alipigania vizuri sana.

187
Wylie, b. 9, ch. 15
188
D'Aubigne, b. 13, ch. 5
189
Ibid., b. 13, ch. 5
114
Watu wa upapa walidhamiria kuzima kile walichoita “ukaidi.” Walianza kwa kujaribu kusababisha
mgawanyiko miongoni mwa watu waliounga mkono Matengenezo na kuwatisha sana wote waliokuwa
hawajaonyesha waziwazi kuwa upande wa Matengenezo. Hatimaye wawakilishi wa miji ile iliyokuwa
huru waliitwa mbele ya Baraza na kutakiwa kutangaza iwapo wangekubaliana na yale masharti
yaliyowekwa katika mpango ule. Waliomba subira, hawakufanikiwa. Walipoletwa kuhojiwa, karibu nusu
yao walikuwa upande wa Wanamatengenezo. Wale ambao kwa njia ile walikataa kuachilia mbali uhuru
wa dhamiri na haki ya kila mtu kuamua mambo yake walijua vema kwamba msimamo wao ule
uliwaweka katika nafasi ya kupingwa, kushutumiwa na mateso kwa siku za mbele. Mmoja miongoni mwa
wajumbe wale alisema: “Ni lazima ama tulikane neno la Mungu, au tuchomwe moto.” 190 Mfalme
Ferdinand, aliyekuwa mwakilishi wa mfalme wa dola katika Baraza lile, aliona kwamba amri ile
ingesababisha mgawanyiko mkubwa sana, isipokuwa kama wakuu wale wangeshawishiwa ili kuikubali na
kuiunga mkono. Kwa hiyo, alijaribu kufanya mbinu ya ushawishi, akijua vema kwamba kutumia nguvu
kwa watu kama wale kungewafanya tu kuwa washupavu zaidi. “Aliwaomba wakuu waikubali amri ile,
(202) akiwahakikishia kwamba mfalme wa dola atapendezwa sana nao.” Lakini watu hawa waaminifu
waliikiri mamlaka ile iliyo juu ya zile za watawala wa kidunia, na wakajibu kwa utulivu: “Tutamtii
mfalme katika kila kitu ambacho kingechangia katika kudumisha amani na heshima kwa Mungu.” 191
Mbele ya Baraza lile hatimaye mfalme alitangaza kwa mtawala (mkuu wa jimbo) na rafiki zake kwamba
amri ile “ilikuwa inakaribia kuandikwa kama amri ya dola,” na ya kwamba “njia pekee iliyobaki kwao
ilikuwa ni kukubaliana na walio wengi.” Akiisha kusema hivyo, aliondoka katika mkutano ule, bila
kuwapa Wanamatengenezo nafasi yoyote ya kutafakari au kujibu. “Ilikuwa kama kazi bure walipotuma
ujumbe kwake mfalme wakimsihi arudi.” Aliyajibu maneno yao kwa kusema: “Hilo ni jambo ambalo
limeshaisha; utii ndicho kitu kilichobaki. 192
Watu wa upande wa mfalme wa dola walikuwa wameshawishika kwamba wakuu wale Wakristo
wangefuata Maandiko Matakatifu kama mamlaka ya juu kuliko mafundisho na matakwa ya wanadamu;
tena walijua kwamba popote pale ambapo kanuni hii ingekubalika, hatimaye upapa ungepinduliwa.
Lakini, kama ilivyokuwa kwa maelfu walioishi tangu wakati huo, wakiangalia tu “vitu vile
vinavyoonekana kwa macho,” walijigamba kwamba mfalme na papa walikuwa na nguvu, na
Wanamatengenezo walikuwa dhaifu. Ikiwa Wanamatengenezo wangekuwa wameutegemea msaada wa
wanadamu pekee, wasingekuwa na uwezo wowote kama ilivyodhaniwa na wafuasi wa papa. Lakini
ingawa walikuwa wanyonge kwa idadi yao, na kwa kupingana na Roma, walikuwa na nguvu yao.
Walitafuta rufaa yao “kutoka kwa taarifa ya Baraza lile kwenda kwa neno la Mungu, na kutoka kwa
mfalme Charles kwenda kwa Yesu Kristo, Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.” 193
Kwa vile Ferdinand alikataa kujali maoni yao ya moyoni, wakuu wale waliamua kutojali kule
kutokuwapo kwake, wakaleta Hati yao ya kupinga mbele ya mkutano ule pasipo kukawaia. Azimioo
murua lilitayarishwa na kuwasilishwa kwa Baraza:
“Tunapinga kwa hati hizi, mbele za Mungu, Muumba wetu pekee, Mhifadhi, Mkombozi, na Mwokozi, na
ambaye atakuwa Mhukumu wetu siku moja, pamoja na mbele ya watu wote na viumbe vyote, kwamba
sisi, kwa ajili yetu na watu wetu, hatukubaliani (203) wala hatutii kwa namna yoyote ile amri hiyo

190
Ibid., b. 13, ch. 5.
191
Ibid., b. 13, ch. 5
192
Ibid., b. 13, ch. 5
193
Ibid., b. 13, ch. 6
115
inayopendekezwa, katika jambo lo lote lililo kinyume na Mungu, kinyume na neno lake takatifu,
kinyume na haki ya dhamiri yetu, kinyume na wokovu wa roho zetu.”
“Nini! Tukubaliane na tamko hilo! Tunatangaza kwamba Mungu Mwenyezi anapomwita mtu katika ujuzi
wa kumjua Yeye, mwanadamu yule hapokei ujuzi wa Mungu!” “Hakuna fundisho la dini lililo la hakika
isipokuwa lile linalopatana na neno la Mungu…. Bwana anakataza kuhusu kufundisha fundisho tofauti na
hilo…. Lazima Maandiko Matakatifu yafafanuliwe na aya nyingine zilizo wazi zaidi,…. Kitabu hiki
Kitakatifu ni rahisi, katika mambo yote ambayo ni muhimu kwa Mkristo, kukielewa, tena yamepangiliwa
ili kusambaratisha giza. Tumeazimia, kwa neema ya Mungu, kudumisha kuhubiri neno lake tu lililo safi
na pekee, kama lilivyo katika vitabu vya Biblia vya Agano la Kale na Jipya, pasipo kuongeza kitu
chochote juu yake kilicho kinyume. Neno hili ndiyo kweli peke yake; ni kanuni ya hakika ya kupimia
mafundisho yote ya dini na maisha yote, wala haliwezi kamwe kutukosesha wala kutudanganya. Yule
ajengaye juu ya msingi huu atasimama dhidi ya nguvu zote za kuzimu, wakati ubatili wote wa
kibinadamu uliowekwa kupingana nalo utaanguka chini mbele za uso wa Mungu.”
“Kwa sababu hii, tunalikataa kongwa hilo linalowekwa juu yetu.” “Wakati huo huo tunatarajia kwamba
mtukufu mfalme atatenda machoni petu kama mkuu wa nchi aliye Mkristo anayempenda Mungu zaidi ya
vitu vyote; nasi tunatangaza wenyewe kwamba tuko tayari kumpa yeye, pamoja na ninyi mabwana
waheshimiwa, heshima na utii wetu wote ambavyo ni wajibu wetu wa haki na jukumu letu halali.” 194
Mguso wa kina ulilipata Baraza. Watu wengi walijawa na mshangao na mshtuko kuona ujasiri wa wale
wapingaji. Wakati wao wa mbele ulionekana kuwa wenye dhoruba na usio na uhakika. Ilionekana kama
mfarakano, vurugu, na umwagaji damu haviepukiki. Lakini Wanamatengenezo, wakiwa na uhakika
kwamba njia ni ya haki, na wakiutegemea mkono wa Mwenye Uweza wote, walikuwa “wamejawa na
ujasiri na msimamo thabiti.”
“Kanuni zilizomo ndani ya Upinzani huu … ndizo zinazounda hali yenyewe ya Uprotestanti. Upinzani huu
uko kinyume cha mambo maovu mawili ya mwanadamu katika masuala ya imani: la kwanza ni (204)
kule kujiingiza kwa mahakimu wa serikali, na la pili ni mamlaka ya kulazimisha ya kanisa. Badala ya
maovu haya, Uprotestanti unaweka uwezo wa dhamiri ya mtu juu ya mahakamu, na mamlaka ya neno la
Mungu kuwa juu ya kanisa linaloonekana. Katika sehemu ya kwanza, Uprotestanti unakataa mamlaka ya
kiserikali katika mambo ya Mungu, unaungana na manabii na mitume kusema, ‘Imetupasa kumtii Mungu
kuliko wanadamu.’ Hapa mbele ya taji ya mfalme Charles V, Uprotestanti unainua juu zaidi taji ya Yesu
Kristo. Lakini unaenda mbali zaidi: unaweka kanuni ya kwamba mafundisho yote ya wanadamu
yanatiishwa chini ya maagizo ya Mungu.” 195 Zaidi ya hayo, wapingaji hao walikuwa wameithibitisha haki
yao ya kuitamka kwa uhuru imani yao ya kuikiri ile kweli. Si tu kwamba wangeamini na kutii, bali pia
wangefundisha kile kinachowasilishwa na neno la Mungu, na waliikataa haki ya kasisi au hakimu
kuingilia. Upinzani wa Spire ulikuwa ni ushuhuda mzito dhidi ya ukosefu wa kuvumiliana kidini, na
ulikuwa utangazaji wa haki ya watu wote kumwabudu Mungu kulingana na matakwa ya dhamiri zao
wenyewe.
Azimio lilikuwa limefanyika. Liliandikwa katika kumbukumbu za maelfu ya watu na kuingizwa katika
vitabu vya mbinguni, mahali ambako juhudi yoyote ya mwanadamu haiwezi kulifuta. Ujerumani yote ya
kiinjili ilichukua Upinzani huu kama udhihirisho wa imani yake. Kila mahali watu waliona tumaini la ujio
wa kipindi kipya kilicho bora zaidi. Mmoja wa wale wakuu wa Uprotestanti wa Spire alisema: “Mungu

194
Ibid., b. 13, ch. 6
195
Ibid., b. 13, ch. 6
116
Mwenyezi, aliyewapa neema ya kumkiri kwa nguvu, kwa uhuru, na pasipo woga, na awahifadhi katika
huo msimamo thabiti wa Kikristo mpaka siku ile ya milele.” 196
Ikiwa Matengenezo, baada ya kufikia kiwango hiki cha mafanikio, yangekubali kupoa ili kupata
upendeleo wa ulimwengu, yangekuwa si ya kweli mbele za Mungu na kwake yenyewe, na kwa hiyo
yangejihakikishia uangamivu wake. Uzoefu wa Wanamatengenezo hawa wakuu una somo kwa ajili ya
vizazi vyote vinavyofuata. Namna ya shetani kufanya kazi dhidi ya Mungu na neno lake havijabadilika;
kwa kiasi kama kile kile cha karne ya kumi na sita bado anapingana na Maandiko yaliyowekwa kama
mwongozo wa maisha. Katika wakati wetu huu, tumeacha kwa mbali mafundisho na imani yao; na kwa
hiyo yatupasa kurudi katika (205) kanuni kuu ya Uprotestanti – Biblia, Biblia pekee, ndio mwongozo wa
imani na wajibu. Bado shetani anafanya kazi kwa kila njia anayoweza kudhibiti na kuharibu uhuru wa
dini. Nguvu zilizo kinyume na Ukristo zilizokataliwa na wapingaji wa Spires zina nguvu mpya sasa
zikitafuta kuanzisha tena mamlaka yake iliyopotea. Msimamo ule usioyumba katika kufuata neno la
Mungu uliodhihirika wakati wa hatari ya Matengenezo ndio tumaini pekee la matengenezo leo.
Ishara za hatari zilijitokeza kwa Waprotestanti; kulikuwa na ishara pia kwamba mkono wa Mungu
ulikuwa umenyoshwa kuwalinda waaminifu. Ilikuwa wakati huu ambapo “Melanchthon alimpitisha
haraka rafiki yake Simon Grynaeus katika mitaa ya mji ule wa Spire kuelekea mto Rhine, akimhimiza
avuke. Huyu wa pili alishangaa kuiona haraka ya namna ile. ‘Mtu mmoja mzee, lakini nisiyemjua,’
alisema Melanchthon, ‘alitokea mbele yangu na kuniambia, Katika muda wa dakika moja maafisa wa
sheria watatumwa na Ferdinand kumtia mikononi Grynaeus.’”
Kwa siku ile, wakati wa mahubiri Grynaeus alikuwa amemwudhi Faber, kiongozi wa madokta wa kipapa,
na kumwona ana kashfa; na katika kufunga mahubiri alipingana naye kwa sababu ya kutetea
“mafundisho fulani potofu na ya kuchukiza.” “Faber aliificha hasira yake, lakini ilikuwa mara tu baada
ya kumwendea mfalme, ambaye kutoka kwake alikuwa amepata amri dhidi ya profesa yule wa
Heidelberg mwenye kuudhi. Melanchthon hakuwa na shaka kwamba Mungu alikuwa amemwokoa rafiki
yake kwa kumtuma mmoja wa malaika zake kumwonya kabla.
Pale kwenye kingo za mto Rhine, alisubiri pasipo kutoka mpaka maji ya mto yalipomwokoa Grynaeus
mbali na watesi wake. ‘Hatimaye, hatimaye amepokonywa toka katika taya katili za wale walio na kiu
ya damu isiyo na hatia,’ alipiga kelele Melanchthon alipomwona Grynaeus ng’ambo ya pili. Aliporudi
nyumbani kwake, Melanchthon alipewa habari kwamba maafisa wanaomtafuta Grynaeus wamepekua
nyumba yote tangu juu hadi chini." 197 Matengenezo yalikuwa yanaletwa mahali ambapo yangeweza
kujulikana sana mbele ya wenye nguvu wa dunia. Wale wakuu wainjilisti walikuwa wamenyimwa na
mfalme Ferdinand nafasi ya kusikilizwa; lakini walikuwa wapewe fursa ya kuwasilisha msimamo wao
(206) mbele ya mfalme mkuu wa dola na kusanyiko la viongozi wakuu wa kanisa na serikali. Ili
kunyamazisha mafarakano yaliyoivuruga nchi, Charles V, katika mwaka uliofuata baada ya Upinzani ule
wa Spire, aliitisha mkutano wa Baraza kule Augsburg, na akatangaza kwamba yeye mwenyewe ndiye
atakuwa mwenyekiti wa mkutano. Viongozi wa Uprotestanti waliitwa shaurini katika mkutano huo.
Hatari kubwa ziliyatishia Matengenezo; lakini watetezi wake bado walimtegemea Mungu kwa kazi yao
ile, na kuahidi kwamba watakuwa imara kwa injili. Mtawala yule wa Saksoni (mkuu wa jimbo) aliombwa
na wanahalmashauri wake asijitokeze katika Baraza lile. Walisema kwamba mfalme aliwataka wakuu
wahudhurie ili kuwavuta na kuwaingiza katika mtego. “Je! si kuhatirisha kila kitu mtu kwenda

196
Ibid., b. 13, ch. 6
197
Ibid., b. 13, ch. 6
117
kujifungia mwenyewe ndani ya kuta za mji huku akiwa na adui mwenye nguvu?” Lakini wengine
wakatangaza, wakisema: “Acheni wakuu waende kwa ujasiri, na kazi ya Mungu itaokolewa.” “Mungu ni
mwaminifu; hatatuacha,” alisema Luther.” 198 Mtawala yule (mkuu wa jimbo) akafunga safari, na
msafara wake, kuelekea Augsburg. Wote walizijua hatari zilizomtishia, na wengi walikwenda mbele
wakiwa na uso wenye huzuni na moyo uliojaa fadhaa. Lakini Luther, aliyewasindikiza hadi Coburg,
aliirejesha imani yao iliyokuwa inazama kwa kuimba wimbo, ulioandikwa wakati wa safari ile, uliosema,
“Mungu wetu ndiye mnara imara.” Wasiwasi mwingi uliokuwepo ulitoweka, mioyo mingi iliyokuwa
mizito ikawa myepesi, waliposikia sauti ya wimbo ule wa kutia nguvu.
Wale wakuu watengezaji walikuwa wamedhamiria kuwa na maelezo ya maoni yao katika muundo ulio na
mpangilio mzuri, wakiwa na ushahidi kutoka katika Maandiko, ili kuyatoa mbele ya Baraza lile; na kazi
ya kuyaandaa ilikabidhiwa kwa Luther, Melanchthon, na wenzao. Hati hii ya kukiri ilikubaliwa na
Waprotestanti kama ndiyo maelezo ya imani yao, nao wakajikusanya pamoja ili kuweka majina yao
katika hati hii muhimu. Ulikuwa ni wakati mugumu na wa kujaribiwa sana. Wanamatengenezo wale
walikuwa waangalifu kwamba kazi yao isichanganywe na hoja za kisiasa; waliona kwamba Matengenezo
yasingepaswa kutumia mvuto mwingine wowote zaidi ya ule utokao katika neno la Mungu.
(207) Wakati wakuu wale wa Kikristo wakiendelea kutia sahihi katika tamko lile, Melanchthon
alichomekea maneno kwa kusema: “Ni kwa wanathiolojia na wachungaji kupendekeza mambo haya;
hebu na tuwaachie mambo mengine yahusuyo mamlaka hao wakuu wa nchi wenye nguvu.” “Mungu
aepushie mbali,” alijibu John wa Saksoni, “ya kwamba usinijumuishe mimi. Nimeamua kufanya lililo
haki, bila kuwa na wasiwasi wowote kuhusu taji yangu. Nataka kumkiri Bwana. Kofia yangu ya uteuzi na
vazi zuri la ngozi havina thamani kubwa kwangu kama ulivyo msalaba wa Yesu Kristo.” Akisha kusema
hayo akaorodhesha jina lake katika hati ile. Mwingine miongoni mwa wakuu wale akasema wakati
akichukua kalamu ili kuandika jina lake: “Ikiwa heshima ya Bwana wangu Yesu Kristo inataka hivyo,
basi, mimi niko tayari … kuacha mali zangu na maisha yangu nyuma.” “Heri niwakatae raia zangu na
majimbo yangu, na kuiacha nchi ya baba zangu iliyo mkononi mwangu,” aliendelea kusema, “kuliko
kupokea fundisho jingine lolote zaidi ya lile lililo katika Hati ya tamko hili.” 199 Hiyo ndiyo ilikuwa imani
na ujasiri wa watu wale wa Mungu.
Wakati uliopangwa wa kujitokeza mbele ya mfalme mkuu wa dola uliwadia. Charles V, akiwa ameketi
katika kiti chake cha enzi, na kuzungukwa na watawala na wakuu, akatoa nafasi ya kuwasikiliza
Wanamatengenezo Waprotestanti. Tamko lao la kukiri imani likasomwa. Katika mkutano ule mkubwa wa
Agosti kweli za injili ziliwekwa wazi, na makosa ya kanisa la kipapa yakaonyeshwa. Naam, siku ile
imetajwa vema kuwa ni “siku kuu sana ya Matengenezo, na moja kati ya siku tukufu sana katika historia
ya Ukristo na ya wanadamu.” 200
Lakini miaka michache tu ilikuwa imepita tangu mtawa yule wa Wittenberg alipokuwa amesimama peke
yake pale Worms mbele ya mkutano mkuu wa taifa. Sasa mahali pake walikuwa wamesimama wakuu
wale watukufu na wenye nguvu katika dola. Luther alikuwa amekatazwa kwenda kule Augsburg, lakini
alikuwa amehudhuria kule kwa njia ya maneno na maombi yake. “Nimefurahi kupita kiasi,” aliandika,
“ya kwamba mimi nimeishi mpaka saa hii, ambapo Kristo ametukuzwa hadharani na wale wanaomkiri,

198
Ibid., b. 14, ch. 2
199
Ibid., b. 14, ch. 6
200
Ibid., b. 14, ch. 7
118
na katika mkutano mtukufu mno namna hii.” 201 Kwa njia ile yakatimia maneno ya Maandiko yasemayo:
“Nitazinena shuhuda zako … mbele ya wafalme.” Zaburi 119:46.
(208) Injili ile ya siku za Paulo ambayo kwa ajili yake alifungwa, ililetwa kwa njia kama ile mbele ya
wakuu wa nchi na wenye vyeo waliokuwa katika mji huu wa dola. Kwa hiyo, katika tukio hili, kile
ambacho mfalme wa dola alikuwa amekataza kuhubiriwa kutokea mimbarani kikatangazwa kutokea
katika jumba la kifalme; kile kilichodhaniwa na wengi kwamba hakifai kusikilizwa hata na watumishi
walio wadogo, kwa mshangao kikawa kinasikilizwa na wakubwa na mabwana wa dola. Wafalme na
watawala walikuwa ndio wasikilizaji, wakuu wale ndio walikuwa wahubiri, na hubiri lenyewe lilikuwa ni
ile kweli ya heshima ya Mungu. “Tangu kipindi kile cha Mitume,” alisema mwandishi mmoja,
“hapajapata kuwapo kazi kubwa zaidi au kuikiri imani kuliko kukubwa namna hii.” 202
“Yote ambayo yamesemwa na wafuasi wa Luther ni kweli; hatuwezi kuyakana,” alisema askofu mmoja
wa kipapa. Je, unaweza kuwa na sababu nzuri za kupinga tangazo hili la imani lililotolewa na mjumbe -
mtawala na wenzake?” aliuliza mwingine, wa Dr. Eck. “Kwa kutumia maandiko ya manabii na mitume -
hapana!” hilo ndilo lilikuwa jibu; “lakini kwa kutumia maandiko ya Mababa na ya mabaraza –
inawezekana!” “Nafahamu,” alisema mwulizaji. “Wafuasi wa Luther, kwa mujibu wako, wako katika
Maandiko, na sisi tuko nje.” 203
Baadhi ya watawala wa Ujerumani waliongolewa na imani ya matengenezo. Mfalme wa dola mwenyewe
alikiri kwamba tamko lile halikuwa kitu kingine ila ukweli. Tamko lile la ushuhuda lilitafsiriwa katika
lugha nyingi na kusambazwa katika Ulaya yote, na limekubaliwa na mamilioni ya watu walioishi baada
ya pale kama udhihirisho wa imani.
Watumishi waaminifu wa Mungu walikuwa hawafanyi kazi ile ngumu wakiwa peke yao. Wakati falme na
mamlaka na roho ovu katika nafasi za juu zilipokuwa zimeungana dhidi yao, Bwana hakuwaacha watu
wake. Laiti kama macho yao yangefumbuliwa, wangeuona ushahidi dhahiri wa kuwako kwake Mungu
pamoja na msaada wake kama ilivyoruhusiwa kwa nabii yule wa kale. Mtumishi wa Elisha
alipomwonyesha bwana wake jeshi lile la maadui lililokuwa limewazingira na kuondoa kabisa uwezekano
wa wao kukimbia, nabii aliomba, akasema: “Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona.”
2 Wafalme 6:17. Na, tazama, mlima wote ulikuwa umejaa magari ya vita na farasi wa moto, jeshi la
mbinguni liliweka kituo pale kumlinda mtu wa Mungu. Hivyo ndivyo malaika walivyowalinda
watendakazi wale katika kazi ya Matengenezo.
(209) Moja ya kanuni ambazo zilishikiliwa sana na Luther ni kwamba matengenezo yasitegemezwe na
mamlaka ya kiserikali, wala silaha zisitumike kuyatetea. Alifurahi kwamba wakuu wa dola walikuwa
wameikiri injili; lakini walipopendekeza kuungana ili kushirikiana kuilinda kwa pamoja, alitangaza wazi
kwamba “mafundisho ya injili yanatetewa na Mungu peke yake … . Kadiri mwanadamu anavyopunguza
kuchangamana katika kazi hii, ndivyo Mungu anavyoingilia kati kwa nguvu zaidi kwa ajili ya kazi hiyo.
Zile tahadhari za kisiasa zote zilizopendekezwa zilikuwa, kwa mtazamo wake yeye, zinaelekeza kwa
hofu isiyostahili na mashaka yaletayo dhambi.” 204
Pindi maadui wale wenye nguvu walipokuwa wanaungana ili kuivunjilia mbali imani ya matengenezo, na
maelfu ya sime yalipoonekana kutaka kuchomolewa alani dhidi ya imani hii, Luther aliandika: “Shetani

201
Ibid., b. 14, ch. 7
202
D'Aubigne, b. 14, ch. 7
203
Ibid., b. 14, ch. 8
204
D'Aubigne, London ed., b. 10, ch. 14
119
analeta ghadhabu yake; makuhani wasiomcha Mungu wako katika shauri baya; na tuko katika hatari ya
vita. Waongoze watu kushindana kwa ushujaa mbele ya kiti cha enzi cha Bwana, kwa imani na sala, ili
adui zetu, wakiwa wamepondwa na Roho wa Mungu, waelekezwe katika amani. Hitaji letu kuu, kazi
yetu kubwa, ni maombi; hebu watu wajue kwamba sasa wako katika ncha ya upanga na ghadhabu ya
Shetani, hebu na waombe.” 205
Tena, siku nyingine baadaye, akirejea kwa ushirikiano ule uliofikiriwa na wakuu waliofanya
matengenezo, Luther alibainisha kwamba silaha pekee katika vita hii ni “upanga wa Roho.”
Alimwandikia yule mtawala-mteuzi wa Saksoni, akisema: “Hatuwezi kwa dhamiri yetu kuunga mkono
ushirikiano huo unaopendekezwa. Heri tufe mara kumi kuliko kuona injili yetu ikisababisha tone moja la
damu kumwagika. Sehemu yetu sisi ni kuwa kama mwanakondoo wa kuchinjwa. Lazima msalaba wa
Kristo ubebwe. Hebu mheshimiwa asiwe na hofu. Tutafanya zaidi kwa maombi yetu kuliko wanayofanya
adui zetu kwa kujivuna. Wewe jizuie tu mikono yako isichafuliwe na damu ya ndugu zako. Ikiwa mfalme
wa dola atatutaka tufike katika mabaraza ya hukumu, tuko tayari kujitokeza. Wewe hauwezi kutetea
imani yetu: lazima kila mmoja aamini kwa kubeba gharama ya shida na hatari yeye mwenyewe.” 206
(210)
Kutoka mahali pa faragha pa maombi ulikuja uwezo ulioutikisa ulimwengu mzima katika Matengenezo
Makuu. Wakiwa na utulivu mtakatifu pale, watumishi wa Bwana walisimika miguu yao juu ya mwamba
wa ahadi zake. Katika mapambano yao kule Augsburg, Luther “hakuacha siku ipite bila kutumia walau
saa tatu katika maombi, na zilikuwa ni saa za siku zilizochaguliwa kufaa sana kwa kujifunza.” Katika
faragha ya chumba chake alisikika akiimimina roho yake mbele za Mungu katika maneno “yaliyojaa
kujitoa, kicho, na tumaini, kama kwa mtu anayezungumza na rafiki yake.” “Najua kwamba Wewe ni
Baba yetu na Mungu wetu,” alisema, “na ya kwamba utawasambaratisha watesi wa watoto wako;
maana wewe mwenyewe unahatarishwa pamoja nasi. Jambo lote hili ni lako, na ni kwa kukinga kwako
kwamba sisi tumeweka mikono yetu juu yake. Basi, tulinde, Ee Baba!” 207
Kwa Melanchthon, aliyekuwa amekandamizwa na mzigo mzito wa wasiwasi na hofu, aliandika, akisema:
“Neema na amani katika Kristo – katika Kristo, nasema, wala si katika ulimwengu. Amen. Nachukia kwa
chuki iliyozidi hali ya kujali kwako kulikopitiliza ambako kunakutafuna. Kama kazi hii si ya haki, iache;
kama ni kazi ya haki, kwa nini tupingane na ahadi zake yeye ambaye hutuamuru kulala usingizi pasipo
hofu? … Kristo hatapungukiwa katika kazi hii ya haki na kweli. Yeye yu hai, anatawala; sisi basi tuwe na
hofu gani?” 208
Mungu alisikiliza vilio vya watumishi wake. Aliwapa wale wakuu na watumishi neema na ujasiri wa
kuendelea kushikilia ukweli dhidi ya watawala wa giza wa ulimwengu huu. Bwana anasema: “Tazama,
naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima; na kila amwaminiye hatatahayarika.”
1 Petro 2:6. Wanamatengenezo Waprotestanti walikuwa wamejenga juu ya Kristo, na milango ya kuzima
haikuweza kuwashinda.

205
D'Aubigne, b. 10, ch. 14
206
Ibid., b. 14, ch. 1
207
Ibid., b. 14, ch. 6
208
Ibid., b. 14, ch. 6
120
Sura ya 12
MATENGENEZO UFARANSA

Ule Upinzani wa Spires na Kuikiri imani kwa Augsburg, ambavyo vilionyesha ushindi wa Matengenezo
huko Ujerumani, vilifuatiwa na miaka ya mapambano na giza. Ukiwa umedhoofishwa na migawanyiko
miongoni mwa wale waliouunga mkono, na ukishambuliwa na maadui wenye nguvu, Uprotestanti
ulionekana kana kwamba unaenda kuharibiwa kabisa. Maelfu walitia muhuri ushuhuda wao kwa damu
yao. Vita ya ndani ya nchi ikatokea; kazi ya Kiprotestanti ikasalitiwa na mmoja miongoni mwa waumini
wake waliokuwa viongozi; na wakuu zaidi miongoni mwa wakuu waliokuwa wamepokea matengenezo
wakaangukia mikononi mwa mfalme wa dola na kuburutwa wakiwa mateka toka mji hata mji. Lakini
katika wakati huu wa ushindi wake uliokuwa dhahiri, mfalme yule wa dola alipigwa na kushindwa.
Aliona mawindo yake yakipokonywa kutoka katika milki yake, na hatimaye akalazimika kutoa nafasi ya
uvumilivu kwa mafundisho yale ambayo shauku ya maisha yake ilikuwa ni kuyaharibu. Alikuwa
ameuhatirisha ufalme wake, hazina zake, na maisha yake kwa kusudi la kuuponda-ponda kabisa uzushi.
Sasa aliona majeshi yake yamedhoofishwa na vita, hazina zake zimekaushwa, nchi nyingi alizotawala
zikitishiwa na maasi, wakati kila mahali imani ile aliyokuwa ameitaabisha bure kuizima, ilikuwa ikienea.
Charles V alikuwa anapigana na mamlaka yenye uwezo wote. Mungu alikuwa amesema, “Iwe nuru,”
lakini yule mfalme alikuwa ameazimia kulidumisha giza pasipo kuvunjika. Makusudi yake yalikuwa
yameshindwa; na katika uzee wa mapema, akiwa amedhoofishwa na mapambano ya muda mrefu,
aling’atuka kutoka katika kiti chake cha enzi na kujizika katika nyumba ya watawa.
Kule Uswisi, kama ilivyokuwa kwa Ujerumani, zilikuja siku za giza kwa Matengenezo. Wakati wilaya
nyingi zilipokea (212) imani ya matengenezo, wengine waling’ang’ania kwa upofu mafundisho ya Roma.
Vitendo vyao vya kuwatesa wale waliotaka kuupokea ukweli vilileta hatimaye vita ya wenyewe kwa
wenyewe. Zwingli na wengine wengi waliokuwa wameungana naye katika matengenezo wakaangukia
katika uwanja wa damu wa Cappel. Oecolampadius, akiwa ameshindwa na majanga haya, alikufa
baadaye. Roma ilikuwa inashinda, na katika maeneo mengi ilionekana kurejesha kile ilichokuwa
imepoteza. Lakini Yeye ambaye mashauri yake ni ya milele hakuwa ameiacha kazi yake wala watu
wake. Mkono wake ungeleta wokovu kwa ajili yao. Katika nchi nyingine, alikuwa ameinua watenda-kazi
ili kuendeleza matengenezo.
Kule Ufaransa, kabla jina la Luther halijasikika kama Mwanamatengenezo, siku ilikuwa
imekwishakupazuka. Mmoja wa watu waliokuwa wa kwanza kuikamata nuru alikuwa ni mtu wa umri
mkubwa Lefevre, mtu aliyekuwa msomi mkubwa, profesa katika Chuo Kikuu cha Paris, na muumini

121
mwaminifu na mtiifu wa upapa. Katika utafiti wake wa maandishi ya kale alivutwa kuelekea kwa Biblia,
na akaanzisha ujifunzaji wa Biblia kwa wanafunzi wake.
Lefevre alikuwa muumini anayependa ibada ya watakatifu, na alikuwa ameanza kazi ya kutengeneza
historia ya watakatifu na wafia-dini kama ilivyotolewa katika hadithi za kanisa. Hii ilikuwa kazi ambayo
ilihitaji nguvu nyingi; lakini alikuwa ameshaifanya kwa kiasi fulani, wakati ambapo, akifikiri kwamba
anaweza kupata msaada muhimu kutoka katika Biblia, alianza kujifunza kitabu hicho kwa lengo hilo.
Kweli, hapa alipata watakatifu wakifunuliwa kwake, lakini siyo kama walivyoonyeshwa katika kalenda
ya Kirumi. Mafuriko ya nuru ya Mungu yaliingia akilini mwake. Kwa mshangao na kutopendezwa
aliachana na kazi aliyokuwa amejipa na akajielekeza katika neno la Mungu. Baada ya muda mfupi
alianza kuzifundisha kweli za thamani alizogundua humo.
Mwaka 1512, wakati Luther au Zwingli walipokuwa hawajaanza kazi ya matengenezo, Lefevre aliandika:
“Ni Mungu anayetupatia, kwa neema, haki ile ambayo kwa imani inatuhalalisha kwa ajili ya uzima wa
milele” 209 Akijikita katika siri za ukombozi, alisema kwa mshangao: Oh, ukuu usioelezeka wa
kubadilishana, - Yeye Asiye na dhambi anatiwa hatiani, (213) na yeye aliye na hatia anaachwa huru;
aliye Baraka anabeba laana, na aliyelaaniwa analetwa katika baraka; Aliye hai anakufa, na wafu
wanapewa kuishi; Utukufu unahafifishwa katika giza, na yeye asiyejua lolote isipokuwa uso uliochafuka
anavishwa utukufu." 210
Na wakati akifundisha kwamba utukufu wa wokovu ni wa Mungu hasa, alifundisha pia kwamba wajibu
wa utii ni wa mwanadamu. “Ikiwa wewe ni mshiriki wa kanisa la Kristo, wewe ni mshiriki wa mwili
wake; ikiwa wewe ni wa mwili wake, basi umejaa asili ya uungu. … Oh, laiti watu wangeweza tu kuingia
katika ufahamu wa upendeleo huu, ni kwa kiasi gani wangekuwa safi, wasio na doa na watakatifu, na ni
aibu kiasi gani, wanapolinganishwa na utukufu ulio ndani yao,-- utukufu ule ambao hauonekani kwa
jicho la kimwili,--- wangeona kama vile ni utukufu wote wa ulimwengu huu." 211
Walikuwepo baadhi miongoni mwa wanafunzi wa Lefevre ambao walisikiliza maneno yake kwa shauku,
na ambao, wakati ambapo sauti ya mwalimu huyu ingenyamazishwa, wangeendelea kuitangaza ile
kweli. William Farel alikuwa wa namna hiyo. Mwana wa wazazi wenye dini, aliyeelimishwa kupokea
mafundisho ya kanisa kwa imani, huenda angeweza, pamoja na mtume Paulo, kutangaza kuhusu yeye
mwenyewe: “Nalikuwa Farisayo kwa kulifuata dhehebu la dini yetu iliyo sahihi kabisa.” Matendo 26:5.
Akiwa mtu aliyejitoa kwa dini ya Kirumi, alikuwa na ari ya kuharibu watu wote ambao wangediriki
kulipinga kanisa. Akirejea kwa kipindi hiki cha maisha yake, alisema: “Ningesaga meno yangu kama
mbwa mwitu mwenye gadhabu ikiwa ningemsikia mtu yeyote akisema jambo dhidi ya papa" 212
Hakuchoka kufanya ibada kwa watakatifu, akiwa na Lefevre kuzunguka katika makanisa ya Paris,
wakiabudu kwenye altare, na wakiyapamba maeneo matakatifu kwa sadaka. Lakini maadhimisho yote
haya hayakuleta amani ya moyo. Hatia ya dhambi ilimbana, ambayo haikuweza kuondolewa na malipo
ya kidini aliyofanya. Kama kwa sauti kutoka mbinguni aliyasikiliza maneno ya Mwanamatengenezo:
“Wokovu ni wa neema.” “Yeye Asiye na hatia anatiwa hatiani, na mhalifu anaachiliwa.” Ni msalaba wa
Yesu peke yake unaoweza (214) kufungua malango ya mbinguni, na kuyafunga malango ya kuzimu." 213

209
Wylie, b. 13, ch. 1
210
D'Aubigne, London ed., b. 12, ch. 2
211
Ibid., b. 12, ch. 2
212
Wylie, b. 13, ch. 2
213
Ibid., b. 13, ch. 2
122
Farel aliupokea ukweli kwa furaha. Kwa wongofu kama wa Paulo aligeuka kutoka katika kifungo cha
mapokeo kwenda katika uhuru wa wana wa Mungu. “Badala ya moyo wa kiuaji wa mbwa-mwitu
awindaye akawa kama mwanakondoo mpole na asiye na madhara, akiwa na moyo ambao umeondolewa
kwa papa, na kupelekwa kwa Yesu Kristo." 214
Wakati Lefevre alipokuwa anaendelea kusambaza nuru miongoni mwa wanafunzi wake, Farel, akiwa na
shauku katika kazi ya Kristo kama aliyokuwa nayo kwa kazi ya papa, alisonga mbele kutangaza ukweli
katika hadhara. Baada ya muda mfupi, mtu mwenye cheo kanisani, askofu wa Meaux, aliungana nao.
Walimu wengine waliokuwa katika nafasi za juu kwa uwezo na usomi walijiunga katika kuitangaza injili,
na ikapata waongofu miongoni mwa matabaka yote, kutoka katika nyumba za mafundi stadi na
wakulima hadi katika ukumbi wa mfalme. Dada wa Francis I, mfalme wa wakati huo, aliipokea imani ya
matengenezo. Mfalme mwenyewe, na mama malkia, walionekana wakati fulani kuiunga mkono, na kwa
matumaini makubwa Wanamatengenezo walitarajia kuona wakati ambao Ufaransa ingeongokea injili.
Lakini matarajio yao yasingetimia. Majaribu na mateso yalikuwa yanawasubiri wanafunzi wa Kristo. Hata
hivyo, hili lilifichwa kwa rehema kutoka machoni pao. Wakati wa amani uliendelea, ili wapate nguvu
zaidi kukutana na dhoruba; na Matengenezo yalipata kusonga mbele haraka. Askofu wa Meaux alifanya
kazi kwa bidii katika jimbo lake akiwafundisha wote makasisi na watu wa kawaida. Mapadri wasio na
elimu na wasio waadilifu waliondolewa, kwa kadiri ilivyowezekana, walibadilishwa na wengine wenye
ujuzi na maadili. Askofu aliazimia sana kwamba watu wake waweze kulifikia neno la Mungu wao
wenyewe, na hili baada ya muda lilikamilika. Lefevre alifanya kazi ya kutafsiri Agano Jipya; na wakati
ule ule ambapo Biblia ya Kijerumani ya Luther ilikuwa inatoka kiwandani Wittenberg, Agano Jipya kwa
Kifaransa lilikuwa linachapishwa kule Meaux. Askofu hakukwepa kutumia nguvu wala gharama
kusambaza toleo hili kwa parishi zile, na baada ya muda mfupi (215) wakulima wa Meaux walikuwa na
Maandiko Matakatifu.
Kama vile wasafiri wanaougua kwa kiu wapokeavyo kwa furaha maji ya chemchemi hai, ndivyo roho hizi
zilivyopokea ujumbe huu wa mbinguni. Watenda kazi shambani, wasanifu katika karakana, walifurahia
kazi zao za siku kwa kuongea kuhusu kweli za thamani za Biblia. Wakati wa jioni, badala ya kuvinjari
katika maduka ya vinywaji, walikusanyika katika nyumba za mmoja mmoja miongoni mwao kusoma
neno la Mungu na kujumuika katika maombi na kusifu. Badiliko kubwa lilidhihirika katika jamii hizi.
Ingawa walikuwa wa tabaka la watu wa chini sana, wakulima wafanyao kazi za sulubu na wasio na
elimu, nguvu ya neema ya kimbingu iinuayo, ya matengenezo, ilionekana katika maisha yao. Kwa
unyenyekevu, upendo na utakatifu, walisimama kama mashahidi wa kile kitakachokamilishwa na injili
kwa ajili wale wanaoipokea kwa moyo mkunjufu.
Nuru iliyowashwa Meaux ilipeleka miali ya mwanga hadi mbali. Idadi ya waongofu iliongezeka kila siku.
Ghadhabu ya utawala-msonge ilidhibitiwa kwa muda na mfalme, ambaye alidharau mtazamo finyu wa
watawa; lakini hatimaye watu wa upapa wakashinda. Sasa nguzo ya kuchomea moto ikasimamishwa.
Askofu wa Meaux, akiwa amelazimishwa kuchagua kati ya moto na kukana imani, alichagua njia rahisi;
lakini licha ya kiongozi kushindwa, kundi lake lilibaki imara. Wengi walishuhudia kwa ajili ya ile kweli
wakiwa katika miale ya moto. Kwa ujasiri na uimara wao mahali pa kuchomea moto, Wakristo hawa
wanyenyekevu waliongea kwa maelfu ambao kamwe hawakusikia ushuhuda wao wakati wa siku za
amani.
Hawakuwa watu wa hali ya chini na maskini tu ambao walidiriki kubeba ushuhuda wa Kristo katikati ya
mateso na uchungu. Katika kumbi na ngome za mabwana na jumba la mtawala kulikuwa na nafsi za

214
D'Aubigne, b. 12, ch. 3
123
kifalme ambazo kwazo ukweli ulithaminiwa zaidi ya mali au cheo au hata maisha. Vazi la ngao ya
kifalme lilisitiri roho ya juu sana na iliyo imara zaidi kuliko kanzu na taji ya askofu. Louis de Berquin
alikuwa mzao wa kifalme. Akiwa mwenye busara na mtu mkubwa, alijikita katika kujifunza, akiwa
amejengewa nidhamu, na asiyelaumiwa kwa utovu wa uadilifu. Mwandishi anasema "Alikuwa mfuasi
mkubwa wa mambo ya upapa, na msikilizaji mkubwa wa misa na mahubiri; . . . na alifunika tabia zake
nyingine zote za uadilifu kwa kuchukia Ulutherii (216) kwa namna ya pekee." Lakini, kama wengine
wengi, akiongozwa na uweza ulio juu ya yote kuelekea kwa Biblia, alishangaa kukuta humo,
“mafundisho ambayo si ya Roma, bali mafundisho ya Luther.” 215 Tangu hapo, alijitoa kuingia katika kazi
ya injili.
“Kule kuwa na elimu kubwa sana miongoni mwa watu wa tabaka la juu wa Ufaransa,” kuwa na kipaji na
mvuto, ujasiri na ushujaa mkubwa aliokuwa nao, na ushawishi wake katika maeneo ya kifalme, - maana
alikuwa anapendwa na mfalme, - kulisababisha wengi kumwona kama mtu ambaye ataishia kuwa
Mwanamatengenezo wa nchi yake. Beza alisema: “Berquin angekuwa Luther wa pili, ikiwa angempata
Francis I kuwa mtawala mwingine wa pili.” “Ni mbaya zaidi kuliko Luther,” walisema watu wa upapa. 216
Kweli Waumini wa Roma walimwona tishio sana. Walimtupa gerezani kama mzushi, lakini mfalme
alimfungua na kumwachia huru. Mapambano haya yaliendelea kwa miaka. Francis, akiyumbayumba
katikati ya Roma na Matengenezo, kwa kubadilika-badilika alivumilia na kuzuia hasira kubwa za
watawa. Mamlaka za papa zilimfunga Berquin gerezani mara tatu, akafunguliwa tu na mfalme, ambaye,
kwa kuguswa na uwezo wake mkubwa wa akili na tabia yake ya staha, alikataa kumwacha awe kafara
kwa mamlaka-msonge yenye ghadhabu.
Berquin alionywa mara kwa mara kuhusu tishio la hatari iliyokuwa inamkabili huko Ufaransa, na
akashauriwa kufuata hatua za wale waliokuwa wametafuta usalama wao kwa kwenda uhamishoni kwa
hiari. Erusmus, yule mwoga na kigeugeu, ambaye pamoja na fahari ya usomi wake alikosa kiwango
kikubwa cha uadilifu ambacho kinatambua kwamba maisha na heshima yanatiishwa chini ya ukweli,
aliandika hivi kwa Berquin: "Omba upelekwe katika nchi ya kigeni kama balozi; nenda utembelee
Ujerumani. Unamfahamu Beda na wengine walio kama yeye – yeye ni jitu lenye vichwa elfu, linalopuliza
sumu kila upande. Adui zako wanaitwa legioni (jeshi). Ikiwa kazi yako ni bora kuliko ile ya Yesu Kristo,
hawatakuacha uende mpaka watakapokuangamiza kabisa. Usiamini sana ulinzi toka kwa mfalme. Katika
matukio yote, usinihusianishe na thiolojia." 217
Lakini kadiri hatari zilivyoongezeka, ndivyo ustahimilivu wa Berquin ulivyokuwa wa nguvu zaidi. Tofauti
na kufuata (217) ushauri wa Erasmus wa kisiasa na wa kumnufaisha yeye binafsi, bado aliazimia
kuchukua hatua za msimamo mkubwa zaidi. Asingesimama kuitetea ile kweli tu, bali angeyapinga pia
makosa. Mashtaka ambayo viongozi wa Roma walitaka kuyakaza kwake kwamba ni mzushi angeyageuzia
kwao. Wapinzani wakubwa na wachungu kwake walikuwa ni madokta na watawa wasomi wa idara ya
thiolojia ya Chuo Kikuu cha Paris kilichokuwa maarufu, moja ya mamlaka za juu za kanisa katika jiji lile
na katika taifa. Kutoka katika maandishi ya madokta wasomi hawa, Berquin alipata hoja kumi na mbili,
ambazo alitangaza kwamba ziko “kinyume na Biblia, na ni za kizushi;” na akaomba mfalme awe kama
hakimu katika mapingano haya.

215
Wylie, b. 13, ch. 9
216
Ibid., b. 13, ch. 9
217
Ibid., b. 13, ch. 9
124
Mfalme, akiwa hapendi kuacha kuonyesha ukinzani kati ya mamlaka na viongozi wa upinzani, na
akifurahia fursa hii ya kushusha kiburi cha watawa hawa wenye majivuno, aliwataka viongozi wa Roma
watetee msimamo wao kwa kutumia Biblia. Walijua vema kwamba silaha hii ingewanufaisha kidogo
sana; gereza, mateso, na kuchoma moto ndizo silaha ambazo walijua zaidi namna ya kuzitumia. Sasa
meza ilikuwa imegeuka, na waliona kwamba wanaelekea kuanguka katika shimo ambalo walikuwa
wametaka kumtumbukiza Berquin. Kwa mshangao walitafuta njia ya kuponyokea.
“Wakati ule sanamu ya Bikira iliyokuwa katika kona ya mtaa ilivunjwa.” Kulikuwa na taharuki kubwa
katika mji. Makundi ya watu yalimininika kuja mahali pale, wakiwa na mwonekano wa huzuni na hasira.
Mfalme naye aliguswa pia. Hii ilikuwa nafasi nzuri ya watawa kutumia, na waliharakisha kuhanikiza.
Walisema: “Haya ni matunda ya mafundisho ya Berquin. Muda si mrefu mambo yote yatapinduliwa —
dini, sheria, kiti cha enzi chenyewe — na mpango huu ni wa Ulutherii." 218
Kwa mara nyingine Berquin alishikiliwa. Mfalme aliondoka Paris, na watawa walikuwa wameachwa hivyo
huru kutimiza matakwa yao. Mwanamatengenezo alishtakiwa na akahukumiwa kufa, na ili Francis
asiingilie na kumwokoa, hukumu ile ilitekelezwa siku ile ile ilipotolewa. Wakati wa mchana (218)
Berquin alipelekwa mahali pa kifo. Umati mkubwa sana ulikusanyika kushuhudia tukio hili, na
walikuwepo wengi walioangalia tukio hili kwa mshtuko na wasiwasi kwamba mhanga huyu amechukuliwa
kutoka miongoni mwa watu bora na werevu sana katika jamaa za Ufaransa. Mshangao, uchungu,
udhalilishaji na chuki kubwa vilijaza nyuso za umati ule; lakini katika uso wa mtu mmoja hakukuwa na
giza. Mawazo ya mfia-dini yule hayakuwa katika hekaheka za tukio lile; fahamu zake zilikuwa katika
uwepo wa Bwana tu.
Mkokoteni wa kusikitisha aliopandishwa, nyuso zenye hasira za watesi wake, kifo cha kutisha
kilichokuwa kinamkabili - yeye hakuyajali mambo hayo; Yeye aliye hai alikuwa amekufa, na yuko hai
milele na milele, tena aliye na funguo za mauti na kuzimu, alikuwa kando yake. Mwonekano wa Bequin
uliangaziwa nuru na amani ya mbinguni. Alikuwa amejivika mavazi vizuri, akiwa amevaa joho laini,
jaketi la kubana la hariri na soksi za dhahabu." 219 Alikuwa anaelekea kutoa ushuhuda wa imani yake
mbele ya Mfalme wa wafalme na malimwengu yote yaliyokuwa yanashuhudia, na hakuna ishara yoyote
ya majonzi ambayo ingeweza kuzuia furaha yake.
Kadiri msafara ulivyoendela taratibu kupita katika mitaa iliyojaa umati wa watu, watu walibaini kwa
mshangao mwonekano wake wa furaha ya ushindi na amani isiyogubikwa na wingu. Walisema, "Yuko
kama mtu aketiye hekaluni, na anayetafakari mambo matakatifu." 220
Mahali pa nguzo ya kuchomea moto, Berquine alijaribu kuwahubiria watu kwa maneno machache; lakini
kwa kuhofia matokeo ya jambo hilo, watawa wale walianza kutoa sauti za kelele, nao askari
waligonganisha mikono kwa kupiga makofi, na kishindo cha sauti zao kikameza sauti ya mfia-dini. Hivyo,
mnamo mwaka 1929, mamlaka ya juu ya kanisa ya Paris iliwawekea umma wa watu wa 1793 msingi wa
mfano kwa maneno matakatifu ya yeye aliyekuwa anakufa yaliyokuwa yanatokota kwenye jukwaa la
kunyongea." 221
Berquin alinyongwa, na mwili wake ukateketezwa na moto. Habari za kifo chake zilisababisha huzuni
kwa watu waliokuwa rafiki wa Matengenezo katika Ufaransa. Lakini kielelezo chake (219) hakikupotea.

218
Ibid., b. 13, ch. 9
219
D'Aubigne, History of the Reformation in Europe in the Time of Calvin, b. 2, ch. 16
220
Wylie, b. 13, ch. 9
221
Ibid., b, 13, ch. 9
125
"Sisi pia tuko tayari," walisema mashahidi wa ile kweli, "kukabili kifo kwa furaha, tukielekeza macho
yetu kwa maisha yale yajayo." 222
Wakati wa mateso ya Meaux, walimu wa imani ya matengenezo walifutiwa leseni za kuhubiri, na
walitawanyika kwenda maeneo mengine. Lefevre alishika njia baada ya muda kwenda Ujerumani. Farel
alirudi katika mji wake wa nyumbani kule mashariki mwa Ufaransa, kuineza nuru nyumbani alikokulia.
Taarifa zilikuwa zimeenea tayari kuhusu kilichokuwa kinaendelea kule Meaux, na ukweli, alioufundisha
pasipo woga, ulipata wasikilizaji. Baada ya muda mfupi mamlaka ziliamshwa ili kumnyamazisha, na
akafukuzwa kutoka katika mji ule. Ingawa hakuweza tena kufanya kazi hadharani, alitembelea nyanda
za tambarare na vijiji, akifundisha katika makazi binafsi ya watu na katika mashamba yaliyofichika, na
akijipatia hifadhi ya malazi katika misitu na mapango ya miamba ambayo yalikuwa yamemsumbua
wakati akiwa bado mvulana. Mungu alikuwa anamwandaa kwa ajili ya majaribu makubwa zaidi.
Alisema, "Misalaba, mateso, na hila za Shetani, ambavyo nilitahadharishwa kabla, havikupungua, na
vilikuwa vikali sana zaidi kuliko ambavyo ningeweza kustahimili mimi mwenyewe; lakini Mungu ni Baba
yangu; amenipatia na wakati wote atanipatia nguvu ninazohitaji." 223
Kama ilivyokuwa katika siku za mitume, mateso yalikuwa “zaidi yamewezesha injili kuenea." Wafilipi
1:12. Wakiwa wamefukuzwa Paris na Meaux, "wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri
neno." Matendo 8:4. Na kwa hiyo nuru ilipata njia ya kufika katika maeneo mengi yasiyofikika katika
majimbo ya Ufaransa.
Bado Mungu alikuwa anaandaa watendakazi wake ili kuieneza kazi yake. Katika moja ya shule
zilizokuwa Paris kulikuwa na kijana mmoja mpole, mwelekevu, aliyethibitisha kuwa na fikira pevu ya
kina, asiye na dalili ya kuwa na maisha yenye kulaumika wala kupungukiwa uwezo wa akili au kujitoa
kwa mambo ya dini. Uwezo wake mkubwa wa akili ulimfanya kuwa fahari ya chuo chake baada ya muda
mfupi, na ilitumainiwa pasipo shaka kwamba John Calvin angekuwa (220) mmoja wa watetezi wa kanisa
wenye uwezo na wenye kuheshimiwa. Lakini mwale wa mwanga ulipenya hadi mle katika kuta za
uanazuoni na falsafa za uongo zilizomzunguka Calvin. Alisikia mafundisho mapya kwa mshtuko, wakati
akiwa hana mashaka yoyote kwamba wazushi walistahili kuchomwa moto kama walivyokuwa
wanafanyiwa. Lakini pasipo matarajio yoyote alijikuta amekutanishwa na uzushi uso kwa uso ili
kuzijaribu nguvu za thiolojia ya Roma akiyapigania mafundisho ya Uprotestanti.
Binamu wa Calvin, ambaye alikuwa amejiunga na Wanamatengenezo, alikuwa pale Paris. Hawa ndugu
wawili walikutana mara kwa mara kujadili pamoja kuhusu mambo yaliyokuwa yakisumbua ulimwengu
wa Kikristo. Olivetan, yule Mprotestanti alisema "Kuna dini mbili tu. Kundi moja la dini ni la zile ambazo
zimevumbuliwa na wanadamu, ambamo mtu anajiokoa mwenyewe kwa njia ya sherehe na matendo
mema; nyingine ni dini ile inayofunuliwa katika Biblia, na inayomfundisha mtu kutafuta wokovu kutoka
kwa neema ya Mungu tu itolewayo bure."
"Sitachukua chochote katika mafundisho yako," alisema Calvin; "unadhani kwamba mimi nimeishi katika
makosa kwa siku zangu zote?" 224
Lakini mawazo yalikuwa yamewashwa katika akili yake na hakuweza kuyaondoa. Akiwa peke yake
chumbani kwake alitafakari yale maneno ya binamu yake. Hatia ya dhami ilimbana; alijiona, akiwa hana
mpatanishi, mbele ya Hakimu mtakatifu na wa haki. Kuwatukuza watakatifu, matendo mema, kaida za

222
D'Aubigne, History of the Reformation in Europe in the Time of Calvin, b. 2, ch. 16
223
D'Aubigne, History of the Reformation of the Sixteenth Century, b. 12, ch. 9
224
Wylie, b. 13, ch. 7
126
kanisa, vyote havikuwa na nguvu ya kuondolea dhambi. Hakuona kitu mbele yake ila giza la uharibifu wa
milele. Jitihada za madaktari wasomi wa kanisa kumwondolea huzuni hii zilikuwa bure. Maungamo na
kitubio, vilifanywa lakini vilikuwa bure; havikuweza kuipatanisha nafsi yake na Mungu.
Akiwa bado katika mapambano haya yasiyo na mafanikio, akiwa amepata nafasi ya kutembelea moja ya
maeneo ya hadhara ya kukusanyikia, Calvin alishuhudia mzushi mmoja akichomwa moto. Alijawa na
mshangao kwa sababu ya amani iliyoonekana katika sura ya mfia-dini yule. Katika kifo kile cha kutisha,
na akiwa chini ya hukumu za kutisha sana za kanisa, (221) alidhihirisha imani na ujasiri ambavyo kijana
yule mwanafunzi aliona vikiwa tofauti na giza lake na kukata tamaa, wakati akiishi katika hali ya
kuonyesha utii mkubwa kwa kanisa. Alijua kwamba wafia-dini waliweka imani yao kwenye Biblia.
Aliazimia kuisoma Biblia, na kuigunduasiri ya furaha yao, kama angeweza.
Katika Biblia alimwona Kristo. Akalia: "Ee Baba, kafara yake imepoza hasira yako; damu yake imeosha
uchafu wangu; msalaba wake umebeba laana yangu; kifo chake kimekuwa badala yangu. Tulikuwa
tumebuni kwa ajili yetu mambo yasiyo na msaada, lakini Wewe umeliweka neno lako mbele yangu kama
taa, na umeugusa moyo wangu, ili kwamba niyaone mambo yote kama machukizo isipokuwa yale yaliyo
ya Yesu." 225
Calvin alikuwa amesomeshwa ili kuwa padri. Akiwa bado wa umri wa miaka kumi na mbili alikuwa
ameteuliwa kuwa mwangalizi wa kanisa dogo, na kichwa chake kilikuwa kimenyolewa na askofu
kulingana na matakwa ya kanuni ya kanisa. Hakupata kuwekwa wakfu, wala hakufanya majukumu ya
padri, lakini alikuwa amekuwa mmoja wa makasisi, akiwa na cheo cha ofisi yake, na akilipwa posho
aliyostahili.
Sasa, akihisi kwamba hawezi kuwa padri, alibadili na kuanza kusoma sheria kwa muda, lakini hatimaye
akaachana na nia hii na kuamua kuyaelekeza maisha yake katika injili. Lakini alisita kuwa mwalimu wa
hadhara. Alikuwa na asili ya woga, na alielemewa na hisia ya uzito wa wajibu katika nafasi hiyo, na
aliazimia bado kujifunza. Hata hivyo, hatimaye ushawishi wa wenzake ulimfanya akubali. Akasema: "Ni
ajabu kwamba mtu mwenye chimbuko la watu wa chini apate kuinuliwa mpaka nafasi ya heshima
hivyo." 226
Calvin aliingia katika kazi yake kimya kimya, na maneno yake yalikuwa kama umande unaoshuka
kuiburudisha nchi. Alikuwa ameondoka Paris, na sasa alikuwa katika mji wa jimbo akiwa katika ulinzi wa
binti mfalme Magreth, ambaye, akiwa mpenzi wa injili, alidumisha ulinzi kwa wanafunzi wa injili. Calvin
alikuwa bado kijana, (222) mpole na asiyejionyesha isivyo. Kazi yake ilianza na watu katika majumba
yao. Alisoma Biblia na kuufunua ukweli wa wokovu, akiwa amezungukwa na watu wa jamaa yote. Wale
waliosikia ujumbe walipeleka habari njema kwa wengine, na muda si mrefu mwalimu huyu alifika nje ya
jiji hadi katika miji na vitongoji. Alipata kuingia kote katika majumba ya maboma na katika vijumba
vidogo, na alisonga mbele, akiweka msingi wa makanisa ambayo yangeishuhudia ile kweli pasipo hofu.
Miezi michache ilipita na akawa yuko Paris tena. Kulikuwa na mabishano yasiyo ya kawaida miongoni
mwa wenye elimu na wasomi. Ujifunzaji wa lugha za kale uliwaelekeza watu katika Biblia, na watu
wengi wenye mioyo ambayo haijaguswa na kweli za Biblia waliweza kuzijadili kwa hamu na hata
wakitoa upinzani kwa viongozi wa Roma. Ingawa alikuwa na uwezo wa kupambana katika eneo hili la
mabishano ya kithiolojia, Calvin alikuwa na wito wa juu zaidi wa kukamilisha kuliko huu wa wasomi
hawa wenye fujo. Akili za watu zilikuwa zimevurugwa, na sasa ulikuwa ni wakati muafaka wa

225
Martyn, vol. 3, ch. 13
226
Wylie, b. 13, ch. 9
127
kuwafunulia ukweli. Wakati ambapo kumbi za chuo kikuu zilikuwa zimejawa na fujo za mabishano ya
kithiolojia, Calvin alikuwa akipita nyumba hadi nyumba, akiifungua Biblia kwa watu, na akiwaambia
habari za Kristo aliyesulibiwa.
Kwa majaliwa ya Mungu, Paris ilikuwa ipokee mwaliko mwingine wa kuipokea injili. Wito uliotolewa na
Lefevre na Farel ulikuwa umekataliwa, lakini ujumbe ulikuwa usikike tena kwa matabaka yote katika
mji ule mkubwa. Akiwa katika ushawishi wa kisiasa, mfalme alikuwa hajawa katika upande wa Roma
kikamilifu dhidi ya Matengenezo. Margaret alikuwa bado ana matumaini kwamba Uprotestanti
ungeshinda Ufaransa. Aliazimia kwamba imani ya matengenezo ihubiriwe Paris. Wakati ambao mfalme
hakuwepo, Margaret alimwagiza mhubiri wa Kiprotestanti kuhubiri katika makanisa yaliyo katika jiji.
Kwa kuwa jambo hili lilizuiliwa na wakuu wa upapa, binti wa mfalme huyu alifungua milango ya jumba
la mfalme. Chumba kimoja kilifanywa kuwa kanisa dogo, na ilitangazwa kwamba kila siku, katika saa
maalum, mahubiri yangefanyika, na watu wa hadhi zote na wa kila mahali walialikwa kuhudhuria. (223)
Makutano walimiminika katika huduma hii. Siyo chumba kile tu cha ibada kilichojaa, bali hata vyumba
vya kusubiria na kumbi zilifurika. Maelfu ya watu walikutanika kila siku – mabwana, watawala,
wanasheria, wafanyabiashara na mafundi wa sanaa. Mfalme, badala ya kukataza mikusanyiko hii,
aliagiza kwamba mawili miongoni mwa makanisa ya Paris yafunguliwe. Jiji hili lilikuwa halijawahi kuwa
na mguso wa neno la Mungu kama huu. Ilionekana kama watu wamepuliziwa roho ya uzima kutoka
mbinguni. Maisha ya kiasi, usafi, utaratibu, na bidii ya kazi vilikuwa vinachukua nafasi mahali pa ulevi,
anasa, magomvi, na uvivu.
Lakini mfumo-msonge haukuwa kimya. Mfalme aliendelea kukataa kuingia katika kazi ya kuzuia
kuhubiri, ndipo watu wa msonge wakageuka kwenda kwa wananchi. Hakuna njia iliyoachwa kutumiwa
katika kuamsha hofu, chuki, na ushupavu miongoni mwa watu hawa waliokuwa na ujinga na upotovu.
Ikifuata kwa upofu walimu wake wa uongo, Paris, kama ilivyokuwa kwa Yerusalemu ya zamani, haikujua
majira ya kujiliwa kwake wala mambo yahusuyo amani yake. Neno la Mungu lilihubiriwa katika mji ule
mkuu kwa miaka miwili; lakini, ingawa walikuwapo wengi walioipokea injili, walio wengi miongoni mwa
watu waliikataa. Francis alikuwa amejionyesha kuwa mvumilivu kwa lengo la kutimiza tu makusudi
yake, na watu wa upapa walifanikiwa kujipatia tena nguvu yao. Kwa mara nyingine makanisa
yalifungwa, na nguzo ya kuchomea watu moto ikasimamishwa.
Kalvini alikuwa bado angali Paris, akijiandaa kwa kujifunza, kutafakari, na maombi kwa ajili ya kazi
zake za baadaye, huku akiendelea kuieneza nuru. Hata hivyo, hatimaye, alitiliwa mashaka. Mamlaka
zilidhamiria kumfikisha katika miale ya moto. Akidhani kwamba yuko salama katika mahali pake pa
faragha, hakuwa na wazo kuhusu hatari yoyote, wakati rafiki zake walipokuja kwa haraka katika
chumba chake wakimletea habari kwamba maafisa walikuwa njiani wakija kumkamata. Wakati huo huo
walisikia lango la nje likigongwa kwa sauti kubwa ya kubisha hodi. Hakukuwa na muda wa kupoteza.
Baadhi ya rafiki zake waliwachelewesha maafisa pale langoni, wakati wengine walikuwa wakimsaidia
Mwanamatengenezo kushuka chini kupitia dirishani, na kwa haraka sana akaondoka kupitia viunga vya
mji ule. Akiwa amepata hifadhi katika kibanda cha mfanyakazi mmoja aliyekuwa rafiki wa
matengenezo, alijibadili kwa kuvaa mavazi ya mwenyeji wake, na, (224) akiwa na jembe begani
mwake, akaanza safari yake kutoka pale. Akisafiri kuelekea upande wa kusini, alipata tena hifadhi
katika maeneo ya milki ya Margaret. 227

227
D'Aubigne, History of the Reformation in Europe in the Time of Calvin, b. 2, ch. 30

128
Alibaki mahali hapa kwa miezi michache, akiwa salama katika ulinzi wa rafiki zake wenye nguvu, na
akiendelea kujishughulisha katika kujifunza kama ilivyokuwa kabla. Lakini moyo wake ulikuwa
umekazwa kuhusu kuieneza injili katika nchi ya Ufaransa, na asingeweza kukaa kwa muda mrefu pasipo
kufanya kazi. Muda mfupi baada ya dhoruba kupungua kidogo, alipata eneo jipya la kazi kule Poitiers,
mahali ambako kulikuwa na chuo kikuu, na habari hizi mpya zilikuwa zimepata kupendwa huko. Watu
wa matabaka yote walisikiliza injili kwa furaha. Hakukuwa na mahubiri ya hadhara, ila katika nyumba
ya hakimu mkuu, katika makao yake, na wakati mwingine katika bustani ya umma, Calvin aliyafunua
maneno ya uzima wa milele kwa wale waliopenda kuyasikia. Baada ya muda, kadiri idadi ya wasikilizaji
ilivyozidi kuongezeka, ilionekana kwamba ni salama zaidi kukusanyikia nje ya jiji lile. Pango lililokuwa
kwenye ukingo wa korongo jembamba lenye kina, mahali ambapo miti na miamba inayoning’inia
vilifanya pawe na faragha zaidi iliyokamilika, palichaguliwa kuwa ndipo mahali pa kukutania. Vikundi
vidogo, vilivyokuwa vikiondoka mjini kwa njia tofauti-tofauti, vilikuja mahali hapa. Katika kituo hiki
kilichojitenga Biblia ilisomwa kwa sauti na kufafanuliwa. Meza ya Bwana iliadhimishwa na Waprotestanti
wa Ufaransa kwa mara ya kwanza mahali hapa. Kutoka katika kanisa hili dogo wainjilisti kadhaa
waaminifu walitumwa kwenda nje.
Kwa mara nyingine Calvin alirudi Paris. Bado hakuweza kupoteza tumaini lake kwamba Ufaransa kama
taifa ingeweza kuyapokea Matengenezo. Lakini alikuta karibu kila mlango wa kufanya kazi ukiwa
umefungwa. Kitendo cha kufundisha injili ilikuwa ni njia ya moja kwa moja kuelekea kwenye nguzo ya
kuchomea moto, na ndipo hatimaye akaazimia kuondoka kwenda Ujerumani. Mara tu alipokuwa
ameondoka Ufaransa, dhoruba kali ikafumuka juu ya Waprotestanti, kiasi kwamba, kama angebaki pale,
kwa hakika angejumuishwa katika maangamizi yale.
Wanamatengenezo wa Kifaransa, wakiwa na hamu ya kuiona nchi yao ikipiga hatua sambamba na
Ujerumani na Uswisi, waliazimia kufanya kazi ya kishindo dhidi ya ushirikina wa Roma, kishindo
ambacho kingeliamsha taifa lote. Hivyo, usiku mmoja mabango yanayopinga (225) misa yaliwekwa
katika nchi yote ya Ufaransa. Badala ya kuendeleza matengenezo, jambo hili la ari kubwa lakini ambalo
liliamuliwa vibaya, lilileta maangamizi, sio tu kwa watangazaji wake, bali pia kwa marafiki wa imani ya
matengenezo katika Ufaransa yote. Liliwapa Warumi kile walichokitamani kwa muda mrefu - kisingizio
cha kudai kuangamizwa kwa wazushi ambao ni wapinzani wanaohatarisha utengemano wa kiti cha enzi
na amani ya taifa lote.
Kwa mkono fulani wa siri – iwe ulikuwa wa rafiki mzembe au wa adui mwenye nia mbaya ambaye
hakujulikana – bango moja kati ya yale lilibandikwa kwenye mlango wa chumba binafsi cha mfalme.
Mfalme alijawa na mshtuko. Katika kikaratasi cha bango hili, mkono wa upinzani ulikuwa umeshambulia
ushirikina ulioheshimiwa kwa vizazi na vizazi. Na uthubutu huu usio kifani wa kuyaingiza maneno haya
yaliyo wazi na makavu-makavu katika mahali pa kifalme uliamsha hasira ya mfalme. Kwa mshtuko
alisimama kimya kwa muda huku akitetemeka. Halafu hasira yake ikaonyeshwa katika maneno ya
kutisha: "Wote na wakamatwe bila kutenganisha kwamba ni wepi wanaotuhumiwa kwa Ulutherii huu.
Nitawakatilia mbali wote. 228 Kura ilikuwa imepigwa tayari. Mfalme alikuwa ameazimia kujitupa upande
wa Roma.
Hatua zilichukuliwa mara moja kwa kumkamata kila Mluther aliyekuwa katika Paris. Fundi-msanifu
maskini mmoja, mfuasi wa imani ile ya matengenezo, ambaye alikuwa na mazoea ya kuwaita waumini
kwenda kwenye mikutano yao ya siri, alikamatwa, naye, akiwa chini ya kitisho cha kuchomwa moto
haraka kwenye nguzo, aliamrishwa kumpeleka mpelelezi wa papa kwenye nyumba ya kila Mprotestanti

228
Ibid., b. 4, ch. 10
129
katika mji ule. Alisinyaa kwa hofu dhidi ya matakwa yale, lakini hatimaye hofu ya ndimi za moto
ilimuelemea, akakubali kufanya usaliti kwa ndugu zake. Akitanguliwa na hostia, na kuzungukwa na
msafara wa makasisi, wachukuzi wa chombo cha kufukizia uvumba, watawa, na askari, Morin, mpelelezi
wa mfalme, pamoja na yule msaliti walipita polepole na kimya-kimya katika mitaa ya mji. Maandamano
yale yalikuwa ni kwa fahari ya kuiheshimu “sakramenti ile takatifu,” kitendo cha kulipiza kisasi kwa
matusi yaliyokuwa yametolewa na wapinzani dhidi ya misa. Lakini ndani ya tamasha hili kulikuwa na
kusudi la kufisha (226) lililokuwa limefichwa. Walipofika mkabala na nyumba ya mfuasi wa Ulutheri,
msaliti yule alitoa ishara, lakini bila kutamka neno. Pale maandamano yalisimama, nyumba ile
ikaingiwa, watu wa jamaa ile wakaburutwa nje na kufungwa kwa minyororo, halafu kundi lile la kutisha
likasonga mbele kusaka wahanga wengine. Wao “hawakuacha nyumba yoyote, iwe kubwa au ndogo,
hata katika vyuo vya Chuo Kikuu cha Paris…. Morin aliufanya mji wote kutikisika…. Ulikuwa utawala wa
kutisha.” 229
Wahanga waliokamatwa waliuawa kwa mateso ya kikatili, ikiwa imeamriwa kwa namna ya pekee
kwamba moto upunguzwe nguvu ili kurefusha muda wa wahanga kuumia kabla ya kufa. Lakini walikufa
kama washindi. Msimamo wao thabiti haukutikisika, amani yao haikutiwa giza. Watesi wao, wakiwa
hawana uwezo wa kuondoa msimamo wa wahanga usioyumba, walijiona wameshindwa. “Nguzo za
kuchomea moto watu zilitawanywa sehemu zote za mji wa Paris, na matukio ya kuwachoma watu kwa
moto yakafanyika mfululizo kwa siku zinazofuatana, mpango ukiwa ni kueneza hofu kuu dhidi ya uzushi
ule kwa kueneza kila mahali matukio ya mateso. Lakini, hata hivyo, hatimaye faida ilibaki kuwa upande
wa injili. Mji wote wa Paris uliwezeshwa kujionea wenyewe aina ya watu wanaozalishwa na imani mpya.
Hakukuwa na mimbara ya mahubiri kwao zaidi ya rundo la kuni za kumchomea moto mfia-dini. Furaha
iliyoangaza katika nyuso za watu hawa kadiri walivyotembea wakipita … kwenda mahali pao pa
kutesewa, ushujaa wao waliposimama katikati ya miale michungu ya moto, upole wao wa kuwasamehe
wanaowatia majeraha, viligeuza mara moja si kwa uchache, hasira kuwa huruma, chuki kuwa upendo,
na kuwashawishi watu kwa mvuto usiopingika kuelekea upande wa injili.” 230
Makasisi, wakiwa wamenuia kuendelea kupandisha juu vileleni ghadhabu ya watu, walieneza mashtaka
ya kutisha kuliko yote dhidi ya Waprotestanti. Walishtakiwa kwamba walikuwa wamepanga kuwaua
Wakatoliki, kuipindua serikali, na kumwua mfalme. Hakuna ushahidi hata kidogo uliotolewa kuhusu hoja
hizi. Hata hivyo, utabiri huu wa uovu ilikuwa uwe na utimilifu wake; lakini katika mazingira tofauti
kabisa kwa mbali, na kutokana na sababu zilizo na sura iliyo kinyume cha hayo. Ukatili ule uliofanywa
na Wakatoliki dhidi ya Waprotestanti wasiokuwa na hatia ulijikusanya katika uzito wa kisasi kilichokuja,
na muda baada ya karne kadhaa ulileta maangamizi yale waliyokuwa wametabiri, kumjia mfalme,
serikali yake, na (227) raia wake; lakini yaliletwa na makafiri, na watu wa upapa wenyewe. Si kule
kuuanzisha Uprotestanti, bali ni kule kuusambaratisha Uprotestanti, ambako kulileta maafa ya kutisha
katika nchi ya Ufaransa miaka mia tatu baadaye.
Shuku, tuhuma, na hofu vilighubika watu wa tabaka zote za jamii. Katikati ya taharuki hii ilidhihirika
jinsi mafundisho yale ya Ulutheri yalivyoingia ndani ya mioyo ya watu waliosimama juu katika nafasi za
elimu, uongozi, na katika ubora wa tabia. Vyeo vyenye amana na adhima kubwa vilibaki wazi ghafla.
Mafundi-sanifu, wachapishaji, wasomi, maprofesa katika vyuo vikuu, watunzi wa vitabu na hata
watumishi wa mahakama wakatoweka. Mamia walikimbia toka Paris, wakijipeleka uhamishoni kutoka
katika nchi yao ya kuzaliwa, na kuwa katika mionekano mingi inayoonyesha kwamba walikuwa

229
Ibid., b. 4, ch. 10
230
Wylie, b. 13, ch. 20

130
wanaipenda imani ya matengenezo. Viongozi wa papa waliwatazama kwa mshangao wakiwaona kama
wazushi ambao walikuwa wameweza kuishi miongoni mwao pasipo kutiliwa mashaka. Hasira yao
ilielekezwa kwa makundi ya wahanga wanyonge waliokuwa ndani ya uwezo wao. Kukawa na
msongamano magerezani, na hewa yenyewe ilionekana kama yenye giza kwa moshi uliotoka katika
marundo ya kuni zilizowashwa moto kwa ajili ya watu walioikiri injili.
Francis I alibahatika kuwa kiongozi katika vuguvugu kubwa la mwamko wa elimu ambalo liliweka
mwanzo wa karne ya kumi na sita. Alikuwa amependezwa kuwakusanya katika jumba lake la kifalme
watu wenye elimu kutoka katika kila nchi. Kupenda kwake elimu na kudharau ujinga na ushirikina wa
watawa kulichangia, walau kwa kiwango kidogo, ustahimilivu ule uliotolewa kwa kazi ya matengenezo.
Lakini akisukumwa na ile juhudi yake ya kukomesha uzushi, mlezi huyu wa elimu akatoa amri ya kupiga
marufuku uchapishaji katika nchi yote ya Ufaransa! Francis I anakuwa mfano kati ya mifano mingi iliyo
katika kumbukumbu inayoonyesha kwamba usomi si kinga dhidi ya kukosa kuvumiliana kidini wala dhidi
ya kuwatesa watu.
Kwa kufanya sherehe ya hadhara Ufaransa kwa dhati ilikuwa ijiweke katika azimio la kuangamiza kabisa
Uprotestanti. Makasisi walidai kwamba matusi yaliyotolewa dhidi ya Mbinguni Juu kwa kuishutumu misa
yalipiziwe kisasi cha damu, na ya kwamba mfalme, kwa niaba ya watu wake, atangaze adhabu ya tendo
hilo la kutisha hadharani.
(228) Tarehe 21 Januari, 1535 ilipangwa kwa ajili ya sherehe hiyo mbaya. Hofu za upotofu na chuki
kubwa kupita kiasi zilihamasishwa katika taifa zima. Mji wa Paris ulijawa na msongamano wa watu
waliomiminika kujaza mitaa wakitoka katika maeneo yote ya vijijini yaliyouzunguka. Siku ile ilikuwa
izinduliwe kwa mandamano makubwa ya kifahari. “Nyumba zilizokuwa kando ya njia ya maandamano
zilitundikwa nguo za matanga, na altare zilijitokeza kila baada ya umbali unaolingana.” Mbele ya kila
mlango palikuwa na mwenge uliowashwa kwa heshima ya ile “sakramenti takatifu.” Kabla ya
mapambazuko ya siku ile, msafara uliundwa mahali pa jumba la mfalme. Kwanza yalitangulia mabango
pamoja na misalaba ya parishi kadhaa; nyuma yake walikuwepo raia, wakitembea wawili wawili, na
kushika mienge mikononi.” Makundi manne ya watawa yalifuata, kila moja likiwa na mavazi yake ya
pekee. Kisha ukaja mkusanyo mkubwa wa masalia ya watakatifu waliokufa zamani. Halafu wakaja
viongozi mabwana wa dini wakiwa katika mavazi yao ya rangi ya zambarau na nyekundu na mapambo ya
vito katika mpango wa kupendeza na kumeremeta.
“Hostia ilibebwa na askofu wa Paris chini ya mwamvuli wa kifahari,… akisaidiwa na wana wanne wa
kifalme wa damu…. Nyuma ya hostia ile alikuwepo mfalme. ... Francis I hakuvaa taji ya kifalme siku ile,
wala hakuwa na vazi lake la taifa.” Akiwa na “kichwa kisichofunikwa, macho yake yakiinamishwa chini,
na mkononi mwake akiwa na mshumaa mwembamba sana uliowashwa,” mfalme yule wa Ufaransa
alionekana “katika sura ya mtu mwenye toba.” 231 Katika kila altare aliinama chini kwa unyenyekevu, si
kwa ajili ya uovu ulioinajisi nafsi yake, wala si kwa ajili ya damu isiyokuwa na hatia iliyokuwa katika
mikono yake, bali kwa ajili ya dhambi ya mauti iliyotendwa na raia zake waliodiriki kuipinga misa.
Nyuma yake alifuata malkia na wakuu wa taifa, nao wakitembea wawili wawili, kila mmoja akiwa na
mwenge uliowashwa.
Kama sehemu ya ibada ya siku ile, mfalme mwenyewe alihutubia maafisa wa ngazi za juu wa ufalme
wake katika ukumbi mkubwa wa jumba la askofu. Akiwa na uso uliojaa huzuni, akajitokeza mbele yao,
na kwa maneno yake ya ufasaha yaliyowagusa watu aliomboleza kwa ajili ya “uhalifu, kufuru, siku ya
huzuni na aibu,” ambayo ilikuwa imekuja juu ya taifa. Na akatoa wito kwa kila raia mtiifu kusaidia

231
Ibid., b. 13, ch. 21
131
katika kuukomesha kabisa uzushi ule mbaya sana uliotishia kuangamiza nchi ya Ufaransa. “Kama mimi
kweli, mimi mfalme wenu,” alisema, “kama ningejua kwamba mmoja kati ya (229) miguu yangu
umechafuka au kuambukizwa na uozo huo unaochukiza, basi, ningewapa ili muukate…. Na zaidi ya hayo,
kama ningemwona mmojawapo wa watoto wangu amenajisiwa na hayo, basi, nisingemwacha….
Ningempeleka mimi mwenyewe, ningemtoa kafara kwa Mungu.” Machozi yakazuia hata asiweze
kutamka, na mkutano wote ukaangua kilio, na kwa kauli moja wakasema kwa nguvu: “Tutaishi na kufa
kwa ajili ya dini Katoliki!” 232
Giza la kutisha lilikuwa limelijia taifa lililokuwa limeikataa nuru ya kweli. Neema “iletayo wokovu”
ilikuwa imefunuliwa; lakini Ufaransa, baada ya kuiona nguvu yake na utakatifu wake, baada ya maelfu
kuvutwa na uzuri wake usio na kifani, baada ya miji na vijiji kutiwa nuru kwa mng’ao wake, ilikuwa
imegeuka na kuipa kisogo, ikachagua giza kuliko nuru. Walikuwa wamesukumia mbali ile zawadi ya
mbinguni iliyokuwa imetolewa kwao. Walikuwa wameuita uovu kuwa ni wema, na wema kuwa ni uovu,
mpaka wakawa wamegeuka na kuwa wahanga wa kujidanganya wao wenyewe. Ingawa wangeweza
kuamini kwamba walikuwa wakimfanyia Mungu ibada kwa kuwatesa watu wake, bado kuamini hivyo
mioyoni mwao hakukuwafanya wasiwe na hatia. Nuru ile ambayo ingeweza kuwaokoa kutoka katika
madanganyo, kutoka katika kuzitia waa nafsi zao kwa hatia ya kumwaga damu, walikuwa wameikataa
kwa hiari yao.
Kiapo murua cha kuukomesha kabisa uzushi kilifanyika katika kanisa kuu ambamo, karibu karne tatu
baadaye, mungu wao aitwaye Goddess of Reason angetawazwa kukalia kiti cha enzi cha taifa hili
lililokuwa limemsahau Mungu aliye hai. Msafara ulijipanga tena, na wawakilishi wale wa nchi ya
Ufaransa wakaondoka kwenda kuanza kazi ile waliyokuwa wameapishwa kuifanya. “Majukwaa ya
kunyongea watu yalikuwa yamejengwa kwa umbali mfupi-mfupi, ambayo juu yake Wakristo wa
Kiprotestanti kadhaa wangechomwa moto wakiwa hai, na ilikuwa imepangwa kwamba marundo yale ya
kuni yangewashwa moto wakati ule mfalme atakapokaribia pale, na ya kwamba maandamano yale
yangesimama pale kushuhudia mateso yale.” 233 Maelezo ya kina ya mateso haya waliyostahimili
mashahidi hawa wa Kristo yanatia simanzi moyoni kuyashuhudia; lakini hapakuwa na kuyumba kokote
kwa upande wa wahanga wale. Kwa kushurutishwa kukana imani, mmoja wao alijibu hivi: “Mimi
naamini tu katika yale yaliyohubiriwa na manabii na mitume zamani, pamoja na yale ambayo kundi lote
la (230) watakatifu waliamini. Imani yangu ina ujasiri katika Mungu ambaye atazipinga nguvu zote za
kuzimu.” 234
Tena na tena maandamano yalisimama mahali pale pa mateso. Walipofika mahali pale walipoanzia
katika jumba lile la kifalme, makutano walitawanyika, naye mfalme na maaskofu wakaondoka, wakiwa
wametosheka sana na mambo yaliyofanyika siku ile, huku wakijipongeza wenyewe na kusema kwamba
kazi ile waliyoianza ingeendelea mpaka uzushi ule utakapoteketezwa kabisa.
Injili ya amani ambayo ilikuwa imekataliwa na Ufaransa ilikuwa lazima ing’olewe kwa hakika kabisa, na
matokeo yake yangekuwa ya kuogofya. Tarehe 21 Januari, 1793, miaka mia mbili na hamsini na minane
toka siku ile ya Ufaransa kuazimia kikamilifu kuwatesa Wanamatengenezo, maandamano mengine,
yenye madhumuni tofauti na yale kwa mbali, yalipita katika mitaa ya Paris. “Kwa mara nyingine tena
mfalme akawa mtu muhimu; kukawa tena na machafuko na ghasia; kwa mara nyingine wito wa kutaka
wahanga wengi zaidi waletwe ulisikika; yalikuwapo tena majukwaa meusi ya kunyongea watu; na

232
D’Aubigne, History of the Reformation in Europe in the Time of Calvin, book 4, chapter 12
233
Wylie, book 13, chapter 21
234
D’Aubigne, History of the Reformation in Europe in the Time of Calvin, book 4, chapter 12
132
matukio ya siku ile yakafungwa tena kwa mauaji mabaya sana; Louis XVI, akipambana upande mmoja na
walinzi wake wa gereza na wauaji, aliburutwa na kuletwa kwenye gogo la kukatia vichwa, akashikiliwa
pale kwa nguvu ya jeshi mpaka shoka lilipotua, na kichwa chake kilichotenganishwa kikavingirika juu ya
jukwaa lile la kunyongea.” 235 Wala mfalme hakuwa mhanga peke yake; karibu na mahali pale pale watu
elfu mbili na mia nane waliuawa kwa kukatwa vichwa na mashine katika kipindi hiki cha umwagaji damu
uliofanywa na Utawala wa Kitisho.
Matengenezo yalikuwa yameupatia ulimwengu Biblia iliyo wazi, yamefunua kanuni za sheria ya Mungu,
na kusisitiza madai yake katika dhamiri za watu. Upendo wa Mungu ulikuwa umewafunulia wanadamu
amri na kanuni zile za mbinguni. Mungu alikuwa amesema: “Zishikeni basi, mkazitende, maana hii ndiyo
hekima yenu na akili zenu, machoni pa mataifa watakaozisikia amri hizi zote, nao watasema, Hakika
taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na akili.” Kumbukumbu la Torati 4:6. Pindi Ufaransa ilipoikataa
zawadi ile ya mbinguni, ilikuwa imepanda mbegu za kutotawalika na machafuko; ndipo utendaji ule
usioepukika wa dhana ya sababu na matokeo ukaishia katika Mapinduzi na Utawala wa Kitisho.
(231) Muda mrefu kabla ya mateso yale yaliyokuwa yamechochewa na mabango, Farel yule mtu jasiri
na makini, alikuwa amelazimika kuikimbia nchi yake ya kuzaliwa. Alikwenda Uswisi, na kwa njia ya kazi
yake, akaiunga mkono kazi ile ya Zwingli, akasaidia kuigeuza mizani kuelekea kuyaunga mkono
Matengenezo. Miaka yake ya baadaye ingetumika hapa, lakini aliendelea kutoa mvuto wake mkubwa
katika upande wa Matengenezo ya Ufaransa. Katika miaka yake ya mwanzo ya kuishi kwake uhamishoni,
juhudi zake zilielekezwa hasa katika kuieneza Injili katika nchi yake ya nyumbani. Alitumia wakati wake
mwingi kuhubiri miongoni mwa watu wa nchi yake waliokuwa mpakani, ambako kwa uangalifu na
pasipokuchoka aliliangalia pambano na kusaidia kwa maneno yake ya kutia moyo pamoja na mausia
yake. Kwa msaada wa wakimbizi wengine, maandiko ya Wanamatengenezo wa Ujerumani yalitafsiriwa
katika lugha ya Kifaransa, na, pamoja na Biblia ya Kifaransa, yakazalishwa kwa wingi sana. Kwa njia ya
wauzaji wa vitabu vya kiroho, machapisho yale yakauzwa kwa wingi katika nchi ya Ufaransa. Vilitolewa
kwa wauzaji wale wa vitabu kwa bei ya chini, na kwa njia hiyo faida iliyopatikana kutokana na kazi ile
iliwawezesha kuiendeleza kazi.
Farel alianza kazi yake katika nchi ya Uswisi akiwa katika vazi duni la mwalimu mkuu wa shule. Kwa
kwenda kwenye parokia iliyokuwa imejitenga mbali, aliutumia muda wake mwingi katika kuwafundisha
watoto wadogo. Mbali na kutoa fani za kawaida za elimu, alizipenyeza kweli za Biblia kwa uangalifu
sana, akitumainia kwamba kupitia kwa watoto zingeweza kuwafikia wazazi wao. Baadhi waliamini,
lakini mapadri walikuja kuikomesha kazi ile, na wananchi wale wa shamba waliokuwa wamejaa upotofu
waliinuka kuipinga kazi ile. “Hiyo haiwezi kuwa injili ya Kristo,” alisisitiza padri, “kwa kuwa kuihubiri
hakuleti amani, bali vita.” 236 Kama wale wanafunzi wa kwanza, alipoteswa katika mji mmoja alikimbilia
mji mwingine. Toka kijiji hata kijiji, toka mji hata mji, alikwenda, akitembea kwa miguu, akistahimili
njaa, baridi, na uchovu mwingi, na kila mahali akiyahatirisha maisha yake. Alihubiri sokoni, makanisani,
na wakati mwingine katika mimbara za makanisa makubwa. Wakati mwingine alikuta kanisa likiwa tupu,
bila wasikilizaji; nyakati nyingine mahubiri yake yaliingiliwa kwa makelele na kuchekwa; mara nyingine
aliburutwa kwa nguvu toka mimbarani. Zaidi ya mara moja alishambuliwa na kundi la watu na kupigwa
karibu ya kufa. Hata hivyo, yeye (232) alisonga mbele. Ingawa mara nyingi alifukuzwa, kwa ustahimilivu
wake alirudi tena katika uwanja wa mashambulio; na, aliona miji midogo na mikubwa iliyokuwa ngome
ya upapa, mmoja baada ya mwingine, ikifungua malango yake na kuipokea injili. Parokia ndogo ya

235
Wylie, book 13, chapter 21
236
Wylie, book 14, chapter 3

133
mahali alipokuwa amefanya kazi yake mwanzoni ikaipokea imani ile ya matengenezo. Miji ya Morat na
Neuchatel nayo pia ikaachana na taratibu za dini ya Kirumi na kuziondoa sanamu zilizoabudiwa toka
katika makanisa yao.
Kwa muda mrefu Farel alikuwa ametamani kupandikiza viwango vya Kiprotestanti katika mji wa
Geneva. Ikiwa mji huu ungeongolewa, basi, ungekuwa makao makuu ya Matengenezo ya Kanisa kwa nchi
za Ufaransa, Uswisi, na Italia. Akiwa na lengo hili, alikuwa ameendelea kufanya kazi mpaka miji mingi
na vijiji vingi vilivyouzunguka vilipoongolewa. Kisha akiwa na mwenzake mmoja, aliingia mjini Geneva.
Lakini aliruhusiwa kuhubiri hotuba mbili tu. Makasisi wale, baada ya kushindwa kufanikiwa kutaka
wenye mamlaka wamhukumu na kumwadhibu, walimwita mbele ya baraza la kanisa, ambamo walikuja
wakiwa wameficha silaha zao ndani ya kanzu zao, wakidhamiria kuutoa uhai wake. Nje ya ukumbi ule,
kundi la watu wenye hasira, wakiwa na marungu na mapanga, walijikusanya kuhakikisha kifo chake
endapo angefanikiwa kulitoroka baraza lile. Lakini uwapo wa mahakimu na jeshi lenye silaha
ulimwokoa. Mapema alfajiri iliyofuata aliongozwa, pamoja na yule mwenzake, kuvuka ziwa kwenda
mahali pa usalama. Hivyo ndivyo juhudi yake ya kwanza ya kuihubiri Geneva ilivyokwisha.
Kwa ajili ya jaribu jingine ambalo lingefuata, chombo duni zaidi kilichaguliwa – kijana wa kiume,
mwenye mwonekano wa unyenyekevu sana kiasi kwamba alitendewa kwa hali ya chini hata na wale
waliotambuliwa kuwa rafiki wa matengenezo. Lakini, mtu huyu angefanya nini mahali ambapo Farel
alikuwa amekataliwa?” Mtu huyu mwenye ujasiri mdogo na uzoefu mdogo anawezaje kustahimili tufani
ambayo ilifanya watu wenye nguvu sana na hodari zaidi kulazimika kuikimbia? “Si kwa uwezo, wala si
kwa nguvu, bali ni kwa Roho yangu, asema BWANA wa majeshi.” Zekaria 4:6. “Mungu alivichagua vitu
dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu.” “Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya
wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.” 1 Wakorintho 1:27,25.
Froment alianza kazi yake kama mkuu wa shule. Ukweli aliowafundisha watoto shuleni ulirudiwa na
watoto wale (233) majumbani kwao. Baada ya muda mfupi wazazi walikuja kusikia Biblia
inavyofafanuliwa, mpaka chumba cha shule kikajaa wasikilizaji makini. Agano Jipya na vipeperushi
viligawiwa bure, na viliwafikia wengi ambao hawakudiriki kuja kusikiliza mafundisho mapya wazi wazi.
Baada ya muda mtendakazi huyu naye akalazimishwa kukimbia; lakini ukweli aliofundisha ulikuwa
umeshika akili za watu. Matengenezo yalikuwa yamepandikizwa, nayo yaliendelea kuimarika na
kusambaa. Wahubiri walirejea, na kupitia kazi yao hatimaye ibada ya Kiprotestanti ilianzishwa Geneva.
Mji ule ulikuwa umeshajitangaza kuwa wa Matengenezo wakati Calvin alipoingia katika malango yake
baada ya kutangatanga na kuwa na mikasa kadhaa. Akirudi kutoka katika matembezi yake ya mwisho
kule alikozaliwa, alikuwa njiani kuelekea Basel, wakati alipokuta barabara ya moja kwa moja imekaliwa
na majeshi ya Charles V, akalazimika kushika njia iliyozunguka kupitia Geneva.
Katika ziara hii Farel aligundua mkono wa Mungu. Ingawa Geneva ulikuwa umeipokea imani ya
matengenezo, bado kazi kubwa ilitakiwa kufanyika hapa. Watu humwongokea Mungu kama mtu mmoja
mmoja si kama jumuiya; kazi ya kufanywa upya haina budi kufanyika moyoni na katika dhamiri kwa
uwezo wa Roho Mtakatifu, si kwa maagizo ya mabaraza. Wakati watu wa Geneva walikuwa wameitupilia
mbali mamlaka ya Roma, hawakuwa tayari kuachana na maovu yaliyokuwa yamesitawi chini ya utawala
wake. Kuimarisha kanuni safi za injili mahali hapa na kuwatayarisha watu hawa kujaza nafasi ambayo
Mungu alionekana kuwaita ili waijaze haikuwa kazi nyepesi.
Farel alikuwa na ujasiri kwamba alikuwa amepata katika Calvin mtu ambaye angeweza kuungana naye
katika kazi hii. Katika jina la Mungu alimwapisha kwa dhati mwinjilisti huyu kijana ili apate kubaki na
kufanya kazi hapa. Calvin alirudi nyuma kwa hofu. Akiwa mwoga na mpenda amani, aliogopa kukutana
134
na roho zenye nguvu, huru na zenye mabavu za watu wa Geneva. Udhaifu wa afya yake, pamoja na
mazoea yake ya kujifunza, yalimfanya kutafuta kujitenga. Kwa kuamini kwamba kwa njia ya kalamu
yake angeweza kuisaidia kazi ya matengenezo, aliazimia kutafuta (234) mahali pa faragha, penye
utulivu, pa kujifunzia, na pale, kwa njia ya uchapishaji, apate kuyafundisha na kuyajenga makanisa.
Lakini wito mzito kutoka kwa Farel ulimjia kama mwito toka Mbinguni, naye hakuthubutu kukataa.
Ilionekana kwake kama, alisema mwenyewe, “kwamba mkono wa Mungu ulikuwa umenyoshwa kuja
chini toka mbinguni, ukashikilia juu yake, na bila kupingwaa ukambandika mahali pale alipotaka
kuondoka.” 237
Wakati huu zahama kubwa zilizingira kazi ya Uprotestanti. Maapizo ya laana yaliyotolewa na papa
yaliunguruma dhidi ya Geneva, na mataifa yenye nguvu yaliutishia kuuangamiza. Mji huu mdogo
ungewezaje kuupinga utawala-msonge ambao mara kwa mara umewalazimisha wafalme na watawala
wa dola kusalimu amri? Ungewezaje kusimama dhidi ya majeshi ya washindi mabingwa wa ulimwengu?
Katika Ulimwengu wote wa Kikristo, Uprotestanti ulitishiwa na adui zake wa hatari sana. Roma
iliamrisha majeshi mapya ikitarajia kuangamiza ushindi wa kwanza wa Matengenezo ya nyuma. Wakati
huu mpango wa Jesuits uliundwa, kundi katili sana, ovu mno, na lenye nguvu kuliko watetezi wote wa
upapa. Wakiwa wamefungiwa mbali na uhusiano wowote duniani na hisia za matakwa ya kibinadamu,
wakiwa kama wafu katika mambo ya matakwa ya kuonyesha upendo wa asili, mantiki na dhamiri,
hawakujua sheria wala mafungamano yoyote na watu, isipokuwa yale ya mpango wao, wala hawakujua
wajibu mwingine wo wote isipokuwa wa kueneza mamlaka yake. 238 Injili ya Kristo ilikuwa
imewawezesha wafuasi wake kukabiliana na hatari na kustahimili mateso, kutokatishwa tamaa na
baridi, njaa, uchovu, na umaskini, kuiinua bendera ya ile kweli wakikabili kitanda cha kutesea, gereza
la chini ya ardhi, na nguzo ya kuchomea watu moto. Ili kupambana na nguvu hizi, U-Jesuit uliwaingizia
wafuasi wake ushupavu mbaya uliowawezesha kustahimili hatari kama hizo, na kuwapa silaha zote za
madanganyo ili kuipinga nguvu ya ile kweli. Hakukuwa na uhalifu wowote ulio mkubwa sana kiasi cha
kutoutenda, hakukuwa na madanganyo yoyote yaliyo mabaya mno kwao kiasi cha kutoyafanya,
hapakuwa na hila yoyote ngumu kwao kiasi cha kuacha kuitumia. Wakiwa wameapa kuwa maskini na
watiifu muda wote, lengo lao lililokusudiwa lilikuwa ni kujipatia utajiri na madaraka, kujitoa kwa ajili
ya kupindua Uprotestanti, na kuirejesha tena heshima ya upapa.
(235) Walipojitokeza kama washirika wa mpango wao, walivaa vazi la utakatifu, wakitembelea
magereza na hospitali, wakiwahudumia wagonjwa na maskini, wakitangaza kwamba wao wameikataa
dunia, na ya kwamba wanalichukua jina takatifu la Yesu, aliyekwenda huku na huko akitenda mema.
Lakini ndani ya vazi hili la nje lisilolaumiwa kitu ulifichwa uhalifu mbaya mno na makusudi mabaya ya
kutisha. Kanuni ya mpango wao ya msingi ilikuwa ni kwamba mwisho wa jambo huthibitisha uhalali wa
njia au mchakato. Kwa kanuni hii, uongo, wizi, viapo vya uongo, mauaji, yalikuwa si tu kwamba
yanasameheka bali pia yanaungwa mkono pale yalipotumika kutimiza mambo yaliyopendwa na kanisa.
Kwa mbinu tofauti Jesuits walijiingiza katika ofisi za serikali, wakipanda vyeo hadi kuwa washauri wa
wafalme, na kuirekebisha sera ya mataifa. Walikuwa watumishi ili kufanya kazi ya kuwapeleleza
mabwana wao. Walianzisha vyuo kwa ajili ya wana wa wakuu wa nchi na mabwana, na shule kwa ajili ya
watu wa kawaida; na watoto wa wazazi wa Kiprotestanti walivutwa katika kuziadhimisha taratibu za
ibada ya kipapa. Fahari yote ya nje na maonyesho ya ibada ya Kirumi yalifanywa ili kuwafanya watoto
wale wapate kuchanganyikiwa na kushangaza na kunasa mawazo, na kwa njia hiyo uhuru ambao wazazi

237
D’Aubigne, History of the Reformation in Europe in the Times of Calvin, book 9, chapter 17
238
Angalia maelezo ya nyongeza katika Kiambatanisho
135
wao walisumbukia na kumwaga damu yao ili kuupata, ukasalitiwa na wana wao. Haraka sana Jesuits
wakasambaa Ulaya yote, na kila mahali walikokwenda, palifuatiwa na kurejea kwa upapa.
Ili kuwapa nguvu zaidi, amri ya papa ilitolewa ili kuanzisha tena mahakama ya kanisa. 239 Licha ya
kuchukiwa na watu wengi, hata katika nchi za Kikatoliki, mahakama hii mbaya ilianzishwa tena na
watawala wa kipapa, na ukatili mbaya mno na wa kuogofya sana usioweza kuvumilika kuuona kwenye
nuru ya mchana ulirudiwa tena katika magereza yake ya siri yaliyo chini ya ardhi. Katika nchi nyingi,
maelfu kwa maelfu miongoni mwa watu bora wa taifa, wenye maisha safi sana na waungwana, wenye
akili na wasomi sana, wachungaji wacha Mungu na waliojitoa wakfu, raia wazalendo na wenye bidii
katika kazi, wanazuoni wenye akili sana, wasanii wenye vipaji, mafundi stadi, walichinjwa au
kulazimika kukimbilia katika sehemu nyingine.
Hizo ndizo njia ambazo Roma ilikuwa imetumia kuizima ile nuru ya Matengenezo, kuondoa Biblia kwa
watu, na kuurejesha ujinga na ushirikina wa (236) Zama za Giza. Lakini chini ya mbaraka wa Mungu na
kazi ya watu waadilifu ambao alikuwa amewainua kuchukua nafasi ya Luther, Uprotestanti haukuweza
kupinduliwa. Nguvu zake hazikupatikana kutoka katika kuungwa mkono wala silaha za wakuu wa nchi.
Nchi zile zilizokuwa ndogo sana, mataifa yale yaliyokuwa na unyonge sana na yenye nguvu kidogo mno,
ndiyo yaliyokuwa ngome ya Matengenezo. Ulikuwa ni Geneva mdogo mno katikati ya maadui wenye
nguvu nyingi waliokuwa wanafanya mpango wa kuuangamiza; ilikuwa ni Uholanzi iliyo katika kingo
zenye mchanga za bahari ya kaskazini, ikipigana miereka dhidi ya udikteta wa Hispania, ambao kwa
wakati ule ulikuwa ni ufalme mkuu kupita zote na wenye utajiri mwingi; ilikuwa ni Sweden iliyokuwa
ukiwa na kame, ambazo zilipata ushindi kwa ajili ya Matengenezo.
Kwa karibu miaka thelathini Calvin alifanya kazi Geneva, kwanza akianzisha pale kanisa lenye kufuata
maadili ya Biblia, na halafu kazi kwa ajili ya maendeleo ya Matengenezo kote Ulaya. Mwenendo wake
kama kiongozi wa umma haukukosa kuwa na mapungufu, na mafundisho yake hayakukosa kuwa na
makosa. Lakini alikuwa chombo cha kutangaza zile kweli ambazo zilikuwa na umuhimu wa pekee kwa
wakati wake, katika kudumisha kanuni za Uprotestanti dhidi ya lile wimbi la upapa lililokuwa linakuja
tena upesi, na katika kukuza hali ya maisha mepesi na yaliyo safi katika kanisa, badala ya kiburi na
ufisadi ulioendelezwa chini ya mafundisho Kirumi.
Kutokea Geneva, machapisho na walimu walikwenda nje kueneza mafundisho ya matengenezo. Watu
walioteswa katika nchi zote walitazamia kupata mafundisho, ushauri, na kutiwa moyo katika kituo hiki.
Mji wa Calvin ukawa kimbilio la Wanamatengenezo wa Ulaya ya Magharibi yote waliokuwa wanawindwa.
Wakizikimbia tufani zile zilizoendelea kwa karne nyingi, wakimbizi wale walikuja kwenye malango ya
Geneva. Wakidhoofu kwa njaa, wakiwa wamejeruhiwa, wakiwa wamepoteza miji yao na ndugu zao,
walikaribishwa vizuri na kutunzwa kwa upendo; na wakapata makao yao hapa, waliubariki mji wao wa
kufikia kwa ujuzi wao, elimu yao, na ucha Mungu wao. Wengi waliotafuta kimbilio lao pale walirudi
katika nchi zao na kuendelea kuupinga udikteta wa Roma. John Knox, Mwanamatengenezo hodari wa
Scotland, watu wasiokuwa wachache miongoni mwa Wapyuritani Waingereza, Waprotestanti wa
Uholanzi na wa Hispania, Wahuguenoti wa Ufaransa walichukua mwenge wa ile kweli toka Geneva na
kwenda kuangaza katika giza la nchi zao walikozaliwa.

239
Angalia maelezo ya nyongeza katika Kiambatanisho
136
Sura ya 13
UHOLANZI NA SKANDINAVIA

Katika nchi ya Uholanzi udikteta wa kipapa uliamsha upinzani mapema sana. Miaka mia saba kabla ya
wakati wa Luther, papa wa Roma alishutumiwa bila woga na maaskofu wawili, ambao, wakiwa
wamepelekwa Roma kama mabalozi, walikuwa wamejifunza na kujua tabia halisi ya “mamlaka
takatifu,” wakisema: Mungu “amemfanya malkia wake ambaye ni mke wake, kanisa, kuwa mwangalizi
na mtunzaji wa familia yake, kwa gharama ambayo haikomi wala haiharibiki, na amelipatia taji na
fimbo ya kifalme ya milele;… ambavyo vyote hivi vinakunufaisha wewe kama mwizi aliye mnyang’anyi.
Unajiketisha mwenyewe katika hekalu la Mungu; badala ya kuwa mchungaji, wewe umegeuka kuwa
mbwa-mwitu kwa kondoo;… ungetuaminisha kwamba wewe ni askofu mkuu kuliko wote, lakini
unaonyesha tabia kama za dikteta. … Mahali ambapo ungekuwa mtumishi wa watumishi, kama
unavyojiita mwenyewe, wewe unakazana kuwa bwana wa mabwana. ... Unazidharau amri za Mungu. ...
Roho Mtakatifu ndiye mjenzi wa makanisa yote kote dunia inakofika. … Mji wa Mungu wetu, ambao sisi
ni raia zake, hufika katika maeneo yote ya mbingu; tena wenyewe ni mkubwa kuliko mji huu, ulioitwa
na manabii kuwa ni Babeli, unaojifanya kuwa mtakatifu, unaojikweza wenyewe hata mbinguni, na
kujidai kwamba hekima yake ni ya milele; na mwisho, ingawa pasipo sababu yenye mantiki, husema
kwamba haujakosea kamwe, wala hauwezi kukosea.” 240
(238) Wengine waliinuka toka karne hata karne na kurudia upinzani huu. Na walimu wale wa mwanzo
ambao, wakisafiri katika nchi mbali mbali na kujulikana kwa majina mbalimbali, wakiwa na tabia ya
Wamishonari wa Vaudois, walieneza ufahamu wa injili kila mahali, wakapenya mpaka Uholanzi.
Mafundisho yao yalienea haraka. Walitafsiri Biblia ya lugha ya Wawaldensi katika lugha ya Kidachi aya
kwa aya. Walitangaza “kwamba kulikuwa na faida nyingi mle; haina mizaha, haina hadithi za uongo,
haina upuuzi, haina hadaa, bali ilikuwa ina maneno ya kweli; na ya kwamba kweli hapa na pale
kulikuwa na ganda gumu, lakini kwamba kiini na utamu wa kile kilichokuwa chema na kitakatifu vipate
kugunduliwa kwa urahisi ndani yake.” 241 Hivyo ndivyo walivyoandika marafiki wa imani ya kale katika
karne ya kumi na mbili.
Sasa mateso ya Kirumi yakaanza; lakini katikati ya kuni za moto na mateso waumini walizidi
kuongezeka, pasipo kutetereka wakatangaza kwamba Biblia peke yake ndiyo mamlaka isiyokosea katika
dini, na ya kwamba “hakuna mtu wa kulazimishwa kwa nguvu kuamini, bali aongolewe kwa
mahubiri.” 242

240
Gerard Brandt, History of the Reformation in and About the Low Countries, book 1, page wa 6
241
Ibid., book 1, page wa 14
242
Martyn, vol. la 2, page wa 87
137
Mafundisho ya Luther yalipata udongo wenye rutuba Uholanzi, na watu waminifu na waliojitoa waliinuka
kuihubiri injili. Kutoka katika moja ya majimbo ya Uholanzi alikuja Menno Simons. Akiwa amepata elimu
katika Kanisa Katoliki na akiwa amesimikwa katika upadri, alikuwa hajui kabisa Biblia, wala hakutaka
kuisoma kwa kuogopa kushawishika na kuingia katika uzushi. Mashaka yake kuhusu fundisho kwamba
mkate au divai hugeuka kuwa mwili na damu yalipokuja juu yake kwa nguvu, aliona kuwa ni jaribu
lililotoka kwa Shetani, na kwa sala na toba akatafuta jinsi ya kuepukana na jambo hilo; lakini bila
mafanikio. Kwa kujichangamanisha katika mambo ya ufisadi alijaribu kuinyamazisha sauti ya dhamiri
yake iliyokuwa ikimshtaki ndani; lakini bila mafanikio yoyote. Baada ya kupita muda fulani aliongozwa
kujifunza Agano Jipya, na hili, pamoja na maandishi ya Luther, yalimfanya aipokee imani ya
matengenezo. Muda mfupi baada ya pale alishuhudia katika kijiji jirani kukatwa kichwa kwa mtu mmoja
aliyeuawa kwa sababu alikuwa amebatizwa tena. Jambo lile likamfanya aisome Biblia ili kujifunza juu
ya ubatizo wa watoto wachanga. Hakuweza kupata ushahidi wo wote wa ubatizo huo katika Maandiko,
ila yeye aliona kwamba toba na imani (239) vinatakiwa kila mahali kama sharti la kupokea ubatizo.
Menno alijiondoa katika Kanisa la Roma na kutumia maisha yake yote kwa kuzifundisha zile kweli
alizokuwa amezipokea. Katika nchi za Ujerumani na Uholanzi, tabaka la washupavu potofu wa dini
walikuwa wamejitokeza, wakifundisha mafundisho ya kipuuzi na yenye kuwachochea watu kuiasi
serikali, wakitenda maovu kwa ujeuri na kuvuruga amani na utulivu, na kuchukua hatua za kutumia
nguvu na kufanya maasi. Menno aliona matokeo ya kutisha yasiyoepukika ambayo makundi yale
yangeweza kuwasababishia watu, naye kwa bidii aliyapinga mafundisho yale potofu pamoja na mbinu za
kishenzi zilizojaa hila za washupavu wale. Lakini, walikuwapo wengi waliokuwa wameshapotoshwa na
washupavu wale wa dini, lakini ambao walikuwa wameyakataa mafundisho yao yale potofu; tena
palikuwa bado na wazao wa vizazi vya Wakristo wa zamani, matunda ya mafundisho ya Wawaldensi.
Menno alifanya kazi miongoni mwa makundi haya kwa juhudi kubwa na mafanikio.
Kwa miaka ishirini na mitano alisafiri pamoja na mke na watoto wake, akistahimili shida kubwa na
umaskini, na mara kwa mara, akihatarisha maisha yake. Alitembea katika nchi ya Uholanzi na kaskazini
mwa Ujerumani, akifanya kazi kwa sehemu kubwa miongoni mwa watu wa kawaida, lakini akitoa mvuto
wenye nguvu katika eneo kubwa. Alikuwa msemaji kwa asili, ingawa alikuwa na elimu ya chini alikuwa
mtu mwenye msimamo usioyumba, mwenye roho ya unyenyekevu na tabia ya upole, na mwenye utauwa
wa kweli utokao moyoni, maisha yake yakionyesha mfano wa kanuni zile alizozifundisha, na akajenga
ujasiri wa kuaminika kwa watu. Wafuasi wake walitawanywa na kuteswa. Walipata mateso mengi sana
kwa kuchanganywa pamoja na washupavu potofu wa Munster. Lakini watu wengi waliongolewa kwa kazi
yake.
Hakuna mahali ambako mafundisho ya Matengenezo yalipokewa kwa ujumla zaidi ya Uholanzi. Katika
nchi chache wafuasi wa mafundisho haya walikutana na mateso ya kutisha zaidi. Kule Ujerumani Charles
V alikuwa amepiga marufuku Matengenezo, tena angefurahi sana kuwaleta wafuasi wote wa
Matengenezo kwenye nguzo ya kuchomea watu moto; lakini wale wakuu walisimama kidete kama kizuizi
dhidi ya ukandamizaji wake. Kule Uholanzi mamlaka yake ilikuwa kubwa zaidi, na amri za kutekeleza
mateso zilitolewa mfululizo kwa kufuatana haraka. Kusoma Biblia, kuisikiliza au kuihubiri (240), au hata
kuzungumza kuhusu Biblia, ilikuwa ni kujiletea adhabu ya kifo kwa kuchomwa moto kwenye nguzo.
Kumwomba Mungu faraghani, kuacha kuisujudia sanamu, au kuimba zaburi vilikuwa na adhabu ya kifo
pia. Hata wale ambao wangeyakana makosa yao, kama ni wanaume, walihukumiwa kufa kwa upanga;
kama ni wanawake, walizikwa wakiwa hai. Maelfu waliangamia chini ya utawala wa Charles na Philip II.
Wakati mmoja familia nzima ililetwa mbele ya mashtaka, ikituhumiwa kuwa mbali na misa na kuabudia
nyumbani. Akijibu tuhuma katika mashtaka yale, mtoto wa kiume akasema: “Tunapiga magoti, na
138
kuomba kwamba Mungu atie nuru yake akilini mwetu na kutusamehe dhambi zetu; tunamwombea
mfalme wetu ili utawala wake upate kufanikiwa na maisha yake yapate kuwa ya furaha; tunawaombea
mahakimu wetu ili Mungu apate kuwalinda.” 243 Baadhi ya mahakimu waliguswa sana moyoni mwao,
lakini, hata hivyo, baba na mmojawapo wa watoto wake walihukumiwa kuchomwa moto kwenye nguzo.
Ghadhabu ya watesi ililingana na imani ya wafia-dini. Si wanaume tu, bali hata wanawake dhaifu,
pamoja na wasichana wadogo walionyesha ujasiri wao usiotetereka. “Wake walisimama kando ya mti wa
kuwachomea moto waume zao, na wakati mme alipokuwa akistahimili moto ule waliweza kunong’ona
maneno ya faraja au kuimba nyimbo za kumtia moyo.” “Wasichana wadogo waliweza kulala katika
kaburi lao wakiwa hai kana kwamba walikuwa wanaingia katika kitanda chao kulala usingizi wa usiku, au
walienda kwenye nguzo ya kuchomewa moto, wakiwa wamevalia nguo zao nzuri kuliko zote, kana
kwamba walikuwa wanakwenda katika harusi zao.” 244
Kama katika siku zile wakati upagani ulipojaribu kuiangamiza injili, damu ya Wakristo ilikuwa mbegu. 245
Mateso yale yalifanya kazi ya kuiongeza idadi ya mashahidi wa ile kweli. Mwaka baada ya mwaka
mfalme, akiwa kama mwenye wazimu kwa kuona msimamo usioshindwa wa watu hawa, alitoa wito wa
kuendelea na kazi yake ile ya kikatili; lakini ikawa bure. Chini ya bwana William Orange, hatimaye
Mapinduzi yakaleta uhuru wa kumwabudu Mungu katika Uholanzi.
Katika milima ya Piedmont, katika nyanda tambarare za Ufaransa na pwani za Uholanzi, maendeleo ya
injili (241) yalitiwa alama ya damu ya wafuasi wake. Lakini katika nchi za kaskazini iliingia kwa amani.
Wanafunzi pale Wittenberg, wakiwa wanarudi majumbani kwao, walikwenda na imani ya matengenezo
kule Skandinavia. Uchapishaji wa maandiko ya Luther ulieneza nuru ile pia. Watu wa kawaida wa
kaskazini, wazoefu wa kazi za taabu, wakaachana na ufisadi, fahari, na ushirikina wa Roma,
wakazipokea zile kweli safi, nyepesi, na zenye kuleta uzima kutoka katika Biblia.
Tausen, “Mwanamatengenezo wa Denmark,” alikuwa mwana wa mkulima mdogo. Mvulana yule
alionyesha mapema kuwa na akili ya utendaji; alikuwa na kiu ya elimu; lakini alinyimwa elimu kutokana
na hali ya wazazi wake, na akaingia katika nyumba ya utawa. Usafi wa maisha yake mle pamoja na bidii
yake ya kazi vilimpatia upendeleo kutoka kwa mkuu wake. Kipimo kilionyesha kwamba alikuwa na kipaji
ambacho kingemfanya aweze kulitumikia kanisa vizuri. Iliamuliwa kwamba apatiwe elimu katika
kimojawapo cha vyuo vikuu vilivyoko Ujerumani au Uholanzi. Mwanafunzi yule kijana aliruhusiwa
kujichagulia shule mwenyewe, kwa sharti moja, kwamba ni lazima asiende Wittenberg. Ilikuwa huyu
msomi wa kanisa asihatarishwe na sumu ile ya uzushi. Walisema hivyo watawa.
Tausen alienda Cologne, ambao kwa wakati ule ulikuwa, kama ulivyo sasa, ngome mojawapo ya Uroma.
Muda si mrefu akawa amechukizwa na mafundisho ya kufikirika ya wasomi wa chuo. Karibu na wakati
ule ule aliyapata maandiko ya Luther. Aliyasoma kwa mshangao na furaha, na kutamani sana na
kufurahia kupata mafunzo yake toka kwa Mwanamatengenezo huyu. Lakini kufanya vile ilikuwa ni
kujihatirisha kwani angemchukiza mkuu wake wa watawa na kupoteza msaada anaompa. Alifanya
uamuzi wake upesi, na muda si mrefu baada ya pale akawa amejiandikisha kama mwanafunzi pale
Wittenberg.
Aliporudi Denmark alikwenda tena katika nyumba yake ya watawa. Bado hakuna mtu aliyemtilia
mashaka kuwa anayo imani ya Ulutheri; hakufunua siri yake kuhusu hilo, lakini, pasipo kuamsha chuki

243
Wylie, book 18, chapter 6
244
Ibid., book 18, chapter 6
245
Tertullian, Apology, aya ya 50
139
yao, alijaribu kuwaongoza katika imani safi zaidi na maisha matakatifu zaidi. Aliifungua Biblia na
kueleza maana yake ya kweli, na hatimaye aliwahubiria Kristo kuwa ndiye haki ya mwenye dhambi na
tumaini lake pekee la wokovu. (242) Ghadhabu ilikuwa kali sana toka kwa mkuu wake, ambaye alikuwa
amejenga matumaini makubwa kwake kwamba angekuwa mtetezi hodari wa Roma. Mara moja
aliondolewa katika nyumba yake ya watawa akapelekwa katika nyumba nyingine na kufungiwa katika
chumba kidogo akiwa chini ya usimamizi mkali.
Kwa hofu ya walinzi wake wapya watawa kadhaa wakajitangaza kuwa waongofu wa Uprotestanti.
Kupitia katika nafasi za katikati ya nondo za chumba chake, Tausen alikuwa amewasiliana na wenzake
na kuwapa ufahamu wa ile kweli. Kama wale mababa wa Wadenishi wangekuwa wameujua mpango wa
kanisa wa kushughulikia uzushi, basi, sauti ya Tausen isingeweza kusikika tena; lakini badala ya wao
kumfungia kaburini katika mojawapo ya magereza ya chini ya ardhi, walimfukuza katika nyumba ile ya
watawa. Sasa walikuwa hawana uwezo juu yake. Amri ya mfalme, iliyokuwa imetolewa karibuni, ilitoa
ulinzi kwa walimu wa mafundisho yale mapya. Tausen alianza kuhubiri. Makanisa yakamfungulia
milango, na watu wakasongamana kwenda kumsikiliza. Watu wengine pia walikuwa wanahubiri neno la
Mungu. Ikiwa imetafsiriwa katika lugha ya Kidenishi, Agano Jipya lilisambazwa sehemu nyingi. Juhudi
zilizofanywa na watu wa upapa kutaka kuipindua kazi hii zilileta matokeo ya kuiendeleza, na muda si
mrefu Denmark ikatangaza kuwa imeipokea imani ya matengenezo.
Kule Sweden, pia, vijana wa kiume waliokuwa wamekunywa maji toka katika kisima cha Wittenberg
walichukua maji ya uzima na kuwapelekea watu wa nchi yao. Wawili miongoni mwa viongozi wa
Matengenezo ya Sweden, Olaf na Laurentius Petri, wana wa mhunzi mmoja aliyekaa Orebro, walijifunza
chini ya Luther na Melanchthon, na walikuwa tayari kuzifundisha kweli zile walizojifunza. Kama
alivyofanya yule Mwanamatengenezo mkuu, Olafu aliwaamsha watu kwa bidii na ufasaha wake, ambapo
Laurentius, kama Melanchthon, alikuwa msomi, mwangalifu, na mtulivu. Wote wawili walikuwa wacha
Mungu, waliokuwa wamepata mafunzo ya juu ya thiolojia, na wenye ujasiri usiotetereka katika kazi ya
kuiendeleza ile kweli. Upinzani kutoka kwa watu wa upapa haukukosa kuwepo. Kasisi mmoja wa
Kikatoliki aliwachochea watu wenye ujinga na upotofu. Olaf Petri alishambuliwa na kundi la watu
wabaya mara kwa mara, na katika matukio kadhaa aliponea chupuchupu kupoteza maisha yake. Hata
hivyo, Wanamatengenezo hawa walipata upendeleo na ulinzi kutoka kwa mfalme.
(243) Chini ya utawala wa Kanisa la Roma watu walizamishwa katika lindi la umaskini na kuwekwa chini
ya ukandamizaji. Walikuwa maskini wa Maandiko, na wakiwa na dini ya maonyesho na sherehe tu,
ambayo haikuleta nuru yoyote akilini, walikuwa wanarudia vitendo vya imani za ushirikina na desturi za
kipagani za mababu zao washenzi wa zamani. Taifa liligawanyika katika makundi yanayoshindana,
ambavyo mapigano yao yaliendelea na kuongeza shida kwa wote. Mfalme alidhamiria kuona
matengenezo serikalini na kanisani, naye akawakaribisha wasaidizi wake wenye uwezo katika vita yake
dhidi ya Roma.
Mbele ya mfalme na viongozi wakubwa wa Sweden, Olaf Petro aliyatetea mafundisho ya imani ya
matengenezo kwa uwezo mkubwa dhidi ya watetezi wa Roma. Alitangaza kwamba mafundisho ya
Mababa wa kanisa yanapaswa kupokewa pale tu yanapokuwa yanapatana na Maandiko; kwamba
mafundisho muhimu ya imani yako katika Biblia kwa namna iliyo wazi na rahisi, ili ya kwamba watu
wote waweze kuyaelewa. Kristo alisema, “Mafundisho yangu si yangu mimi, ila ni yake Yeye
aliyenipeleka” (Yohana 7:16); Paulo naye alitangaza kwamba kama angehubiri injili nyingine yoyote
zaidi ya ile aliyokwisha kuipokea, basi, na alaaniwe (Wagalatia 1:8). “Inakuwaje, basi,” alisema
Mwanamatengenezo, “kwamba wengine wanachukua jukumu la kutunga mafundisho ya imani

140
wapendavyo wao, na kuwafanya watu wayafuate kama mambo ya lazima kwa wokovu?” 246 Alionyesha
kwamba amri za kanisa hazina mamlaka yoyote zinapopingana na amri za Mungu, kisha akaitetea ile
kanuni kuu ya Uprotestanti isemayo kwamba “Biblia na Biblia pekee” ndiyo kanuni ya imani na
matendo.
Shindano hili, japokuwa lilifanyika katika jukwaa kama lisiloonekana wazi, linasaidia kutuonyesha sisi
“aina ya watu waliojiunga kuwa askari katika jeshi la Wanamatengenezo. Hawakuwa watu wasio na
elimu, watu wafuatao vikundi vya madhehebu, wabishi wenye makelele - mbali kabisa na hao; wao
walikuwa ni watu waliokuwa wamejifunza neno la Mungu, na kujua kuzitumia vizuri silaha zilizotoka
katika ghala ya silaha ya Biblia. Kwa habari ya ujuzi wao, walikuwa mbele zaidi kuliko hata umri wao.
Tunapopeleka mawazo yetu kwenye vituo angavu vya Wittenberg na Zurich, na katika (244) majina
kielelezo kama Luther na Melanchthon, ya Zwingli na Oecolampadius, ni kama tunaelekea kuambiwa
kwamba hao walikuwa ndio viongozi wa Matengenezo, na lazima tutarajie uwezo mkubwa mno na
mafanikio makubwa ndani yao; lakini waliokuwa chini hawakuwa na uwezo kama wao. Sawa, sasa
tugeukie kwa tukio lisilo wazi la Sweden, na majina ya hali ya chini ya Olaf na Laurentius Petri – kutoka
kuwa mabwana hadi wanafunzi – tunaona nini?… Wasomi na wanathiolojia; watu ambao wamehitimu
kabisa mfumo mzima wa kweli ya injili, na ambao wanapata ushindi kwa urahisi dhidi ya wasomi wa
shule wapotoshaji na viongozi wakuu wa Roma.” 247
Kama matokeo ya mahojiano haya mfalme wa Sweden aliipokea imani ya Kiprotestanti, na muda si
mrefu baada ya hapo bunge nalo likatoa tangazo la kuunga mkono imani ile. Agano Jipya lilikuwa
limetafsiriwa na Olaf Petri katika lugha ya Swedish, na kwa kupenda kwa mfalme wale ndugu wawili
walichukua jukumu la kuitafsiri Biblia yote. Hivyo kwa mara ya kwanza watu wa Sweden wakalipata
neno la Mungu katika lugha yao ya nyumbani. Iliamriwa na Baraza kwamba katika ufalme wote, wahubiri
wayafafanue Maandiko na watoto shuleni wafundishwe kusoma Biblia.
Taratibu na kwa hakika giza la ujinga na ushirikina lilifukuzwa na nuru ya injili. Likiwa limekombolewa
kutoka katika ukandamizaji ule wa Kirumi, taifa lile likajipatia nguvu nyingi na ukuu, mambo ambayo
lilikuwa halijawahi kuyafikia katika siku zake za nyuma. Sweden ikawa moja ya ngome kuu za
Uprotestanti. Karne moja baadaye, katika wakati ule wa hatari kubwa, taifa hili dogo na ambalo mpaka
wakati huu lilikuwa duni - taifa pekee la Ulaya lililothubutu kutoa mkono wa msaada - lilikuja
kuikomboa Ujerumani katika pambano lake kubwa la Vita ya Miaka Thelathini. Ni kama Ulaya ya
Kaskazini yote ilikuwa inaletwa tena chini ya udikteta wa Roma. Yalikuwa ni majeshi ya Sweden
yaliyoiwezesha Ujerumani kuligeuzia mbali wimbi la ushindi wa kipapa, na kuleta hali ya kuvumilia
imani ya Waprotestanti, - Wacalvin na Waluther, - na kurejesha uhuru wa dhamiri katika nchi zilizokuwa
zimepokea Matengenezo.

246
Wylie, book 10, chapter 4
247
Ibid., book10, chapter 4
141
Sura ya 14
WANAMATENGENEZO WA BAADAYE WA UINGEREZA
Wakati Luther alipokuwa anaifungua Biblia iliyokuwa imefungwa kwa watu wa Ujerumani, Tyndale
alisukumwa na Roho wa Mungu kufanya jambo kama hilo katika nchi ya Uingereza. Biblia ya Wycliffe
ilikuwa imetafsiriwa kutoka katika tafsiri ya Kilatini, ambayo ilikuwa na makosa mengi. Ilikuwa
haijapata kuchapishwa kamwe, na bei ya nakala zilizoandikwa kwa mkono ilikuwa kubwa mno kiasi
kwamba wachache tu waliokuwa matajiri na wakuu ndio walioweza kuinunua; tena, isitoshe, kwa kuwa
ilikuwa imepigwa marufuku kali na kanisa, ilikuwa imesambazwa kwa uchache sana. Mnamo mwaka
1516, mwaka mmoja kabla ya kutolewa zile hoja kuu za Luther, Erasmus alikuwa amechapisha toleo
lake la Kiyunani (Kigiriki) na Kilatini la Agano Jipya. Sasa kwa mara ya kwanza neno la Mungu lilikuwa
limechapishwa katika lugha ya asili. Katika kazi hii makosa mengi ya tafsiri zilizotangulia yalisahihishwa,
na maana yake ilitolewa kwa wazi zaidi. Toleo hili liliwafanya wengi miongoni mwa matabaka ya
wasomi kupata ujuzi bora zaidi wa ile kweli, na kuipa nguvu mpya kazi ya Matengenezo. Lakini watu wa
kawaida, kwa sehemu kubwa, walikuwa bado wamezuiwa kulipata neno la Mungu. Ilikuwa Tyndale ndiye
aikamilishe kazi ya Wycliffe ya kuwapatia Biblia wananchi wa nchi yake.
Akiwa mwanafunzi mwenye bidii na mtafutaji mwaminifu wa ile kweli, alikuwa ameipokea injili kutoka
katika Agano Jipya ya Kigiriki ya Erasmus. Aliihubiri imani yake bila hofu, akisisitiza kwamba mafundisho
yote yapimwe kwa Maandiko. Kuhusu madai ya watu wa upapa kwamba kanisa lao ndilo lililokuwa
limewapatia Biblia, na kwamba ni kanisa tu ambalo lingeweza kuifafanua, Tyndale alijibu hivi:
“Mnamfahamu (246) aliyewafundisha tai kutafuta mawindo yao? Naam, Mungu yule yule anawafundisha
watoto wake wenye njaa namna ya kumtafuta Baba yao katika neno lake. Mbali na yeye kutupatia
Maandiko, ni ninyi mlioyaficha kutoka kwetu; ni ninyi mnaowachoma moto wale wanaoyafundisha
Maandiko, na kama mngeweza mngeyachoma moto hata Maandiko yenyewe.” 248
Kuhubiri kwa Tyndale kuliamsha hamu kubwa ya watu; wengi waliupokea ukweli. Lakini makasisi
walikuwa macho, na si muda mrefu tangu alipoondoka katika eneo lile wao walipojaribu kuiharibu ile
kazi kwa kutumia vitisho vyao na visingizio vya uongo. Mara nyingi walifanikiwa. “Nini la kufanya?”
alihamaki. “Mimi ninapopanda mbegu sehemu moja, adui analiharibu shamba lile nikishaondoka. Siwezi
kuwa kila mahali. Oh! Laiti Wakristo wangekuwa na Maandiko Matakatifu katika lugha yao wenyewe,
wangeweza kukabiliana wao wenyewe dhidi ya walimu hawa wa uongo. Bila kuwa na Biblia ni vigumu
kuwahifadhi watu wa kawaida katika ukweli.” 249
Kusudi jipya sasa lilijaza mawazo yake. Alisema, “Ilikuwa ni katika lugha ya Israeli zaburi ziliimbwa
katika hekalu la Yehova; je! injili isiweze kuzungumza miongoni mwetu katika lugha ya Uingereza?… Je!

248
D'Aubigne, History of the Reformation of the Sixteenth Century, b. 18, ch. 4
249
Ibid., book 18, chapter 4
142
kanisa linapaswa kuwa na nuru pungufu wakati wa adhuhuri kuliko wakati wa mapambazuko?… Lazima
Wakristo wasome Agano Jipya katika lugha yao ya kuzaliwa.” Madokta wa falsafa na walimu wa kanisa
hawakukubaliana wao kwa wao. “Mmoja anamwunga mkono dokta huyu, mwingine anaungana na yule….
Sasa kila mmoja miongoni mwa hao waandishi hupingana na mwingine. Tunawezaje basi kutofautisha
kati ya yule asemaye kweli na yeye asemaye uongo?… Namna gani?… Hakika ni kwa neno la Mungu.” 250
Haukupita muda mrefu baadaye pale dokta msomi wa Kikatoliki, aliyekuwa amejiingiza katika
mapambano naye, aliposema ghafla: “Tungekuwa heri kutokuwa na amri za Mungu kuliko kutokuwa na
zile za papa.” Tyndale akajibu: “Namkataa papa pamoja na amri zake zote; na kama Mungu akiniachia
uhai wangu, baada ya miaka mingi kuanzia sasa nitasababisha mvulana anayeongoza jembe la ng’ombe
kuyajua Maandiko vizuri kuliko uyajuavyo wewe.” 251
Kusudi lile alilokuwa ameanza kufanyia kazi, la kuwapatia (247) Maandiko ya Agano Jipya katika lugha
yao, sasa lilithibitishwa, na mara akaanza kuifanya kazi hiyo yeye mwenyewe. Akiwa amefukuzwa
nyumbani kwake kwa sababu ya mateso, alikwenda London, na akaendelea kuifanya kazi yake pale kwa
muda fulani bila bughudha. Lakini kwa mara nyingine ukatili wa watu wa upapa ukamlazimisha
kukimbia. Nchi yote ya Uingereza ilionekana kumkataa, akaazimu kutafuta kimbilio Ujerumani. Mahali
hapa alianza kuchapisha Agano Jipya la Kingereza. Mara mbili kazi ile ilisimamishwa; lakini kila
alipozuiliwa kuchapisha katika mji mmoja, alienda katika mji mwingine. Hatimaye akaenda Worms,
mahali ambako, miaka michache ya nyuma, Luther alikuwa ameitetea injili mbele ya Baraza. Katika mji
ule wa zamani walikuwemo marafiki wengi wa Matengenezo, na Tyndale akaifanya kazi yake bila kizuizi
kingine. Nakala elfu tatu za Agano Jipya zilichapishwa, na toleo jingine likafuata mwaka ule ule.
Kwa moyo mkunjufu na ustahimilivu mkubwa aliendelea na kazi yake. Licha ya wenye mamlaka wa
Uingereza kuzilinda vikali bandari zao na kuwa macho sana, kwa njia mbalimbali neno la Mungu
lilipelekwa kwa siri mpaka London na kutoka pale lilienezwa katika nchi yote. Watu wa upapa walijaribu
kuzuia, lakini ilikuwa kazi bure. Wakati mmoja askofu wa Durham alinunua mzigo wote wa Biblia kutoka
kwa muuzaji wa vitabu aliyekuwa rafiki wa Tyndale, kwa madhumuni ya kuziharibu, akidhani kwamba
jambo hili lingeweza kuirudisha nyuma kwa kiasi kikubwa kazi ile. Lakini, kinyume chake, fedha ile
iliyopatikana, ilinunua vifaa kwa ajili ya kuchapisha toleo jipya na bora zaidi, ambalo, kama isingekuwa
kwa njia hii, lisingechapishwa. Wakati Tyndale alipokamatwa na kuwekwa kifungoni baadaye, aliachiwa
huru kwa sharti kwamba ataje majina ya watu waliomsaidia gharama za kuchapisha Biblia zile. Alijibu
kwamba askofu wa Durham alikuwa amefanya sehemu kubwa kuliko mtu mwingine yeyote; maana kwa
kulipa bei kubwa kwa vitabu vilivyokuwa vimebaki alikuwa amemwezesha kusonga mbele kwa ujasiri
mzuri.
Tyndale alisalitiwa na kutiwa mikononi mwa adui zake, na wakati fulani aliteseka gerezani kwa miezi
mingi. Hatimaye akaishuhudia imani yake kwa kifo cha mfia-dini; lakini silaha alizoandaa
zimewawezesha askari wengine (248) kupigana vita katika karne zote mpaka wakati wetu huu.
Latimer aliendeleza mafundisho mimbarani kwamba Biblia ilipaswa kusomwa katika lugha ya watu.
Mtunzi wa Maandiko Matakatifu, alisema, “ni Mungu mwenyewe;” na Maandiko haya yanashiriki uwezo
na umilele wa Mtunzi wake. “Hakuna mfalme ye yote, wala mkuu wa dola, wala hakimu, wala mtawala
ye yote… wote wanawajibika kutii … neno lake takatifu.” “Hebu na tusipite katika njia za pembeni, bali

250
Ibid., book 18, chapter 4
251
Anderson, Annals of the English Bible, uk. 19

143
tuliruhusu neno la Mungu lituongoze: hebu na tusifuate … mababu zetu wa zamani, wala tusitafute yale
waliyofanya wao, bali yale yaliyowapasa kufanya.” 252
Barnes na Frith, marafiki waaminifu wa Tyndale, waliinuka kuitetea kweli. Akina Ridleys na Cranmer
wakafuata. Viongozi hawa katika Matengenezo ya Uingereza walikuwa wasomi wakubwa, na wengi wao
walikuwa wamepewa heshima ya juu sana kwa juhudi yao na uchaji katika jamii ya Kirumi. Upinzani
wao kwa upapa ulitokana na kung’amua kwao makosa ya “mamlaka takatifu.” Ufahamu wao wa siri za
Babeli uliwapa uwezo mkubwa wa kutoa ushuhuda wao dhidi yake.
“Sasa ningependa kuuliza swali la ajabu,” alisema Latimer. “Ni askofu yupi na kasisi wa ngazi ya juu
yupi mwenye bidii kuliko wote katika nchi yote ya Uingereza?… Nawaona mnasikiliza na kuzidi kusikiliza
kwamba nimtaje…. Nitawaambia: ni yule mwovu…. Kamwe hayuko nje ya dayosisi yake; mwiteni wakati
wowote mnaotaka, yuko nyumbani daima;… yuko shambani mwake daima…. Hamtamkuta bila kazi
kamwe, nawahakikishieni…. Mahali akaapo huyo Ibilisi,… huko mbali na vitabu, bali katika kuinua
mishumaa; mbali na Biblia, bali pa kutukuza rozari; mbali na nuru ya injili, bali karibu na nuru ya
mishumaa, naam, nyakati za mchana;… msalaba wa Kristo unakuwa chini, mfuko wa matoleo kwa ajili
ya walio toharani juu;… mbali na kuwavika walio uchi, maskini, na wasio na uwezo, ila juu katika
kunakshi sanamu, kutia urembo na kung’arisha sanamu za mawe; juu katika mapokeo ya mwanadamu
na amri zake, chini katika mapokeo kutoka kwa Mungu na neno lake takatifu…. Laiti maaskofu wetu
wangekuwa na bidii sana katika kupanda mbegu ya mafundisho mema, kama Shetani alivyo katika
kupanda magugu!” 253
Kanuni kuu iliyosimamiwa na Wanamatengenezo hawa - ile ile iliyoshikiliwa na Wawaldensi, na Wycliffe,
na John Huss, na Luther, Zwingli, na wale waliojiunga nao - ilikuwa ile mamlaka isiyokosea ya Maandiko
Matakatifu ndiyo kiwango cha imani na kazi. Walikana haki ya papa, mabaraza, Mababa, na wafalme
kudhibiti dhamiri katika masuala ya dini. Biblia ilikuwa ndiyo mamlaka yao, na kwa mafundisho yake
walipima mafundisho na madai yote. Imani katika Mungu na neno lake iliwategemeza watu hawa
watakatifu walipoyatoa maisha mahali penye nguzo ya kuchomewa moto. “Uwe na moyo mkuu,”
alisema Latimer akimwambia mfia-dini mwenzake wakati ndimi za moto zinakaribia kuzinyamazisha
sauti zao, “siku ya leo tutawasha mshumaa ambao, kwa neema ya Mungu, katika nchi hii ya Uingereza,
naamini hautaweza kuzimwa kamwe.” 254
Mbegu zilizotawanywa na Columba pamoja na watendakazi wenzake katika nchi ya Scotland zilikuwa
hazijaharibiwa zote. Kwa mamia ya miaka baada ya makanisa ya Uingereza kusalimu amri kwa Roma,
watu wa Scotland waliendelea kudumisha uhuru wao. Lakini, katika karne ya kumi na mbili, upapa
uliotesha mizizi yake hapa, tena hakuna nchi nyingine yoyote ambapo ulishamiri zaidi ya hapa katika
hatamu zake. Hakuna mahali popote ambapo giza lilikuwa zito zaidi ya hapa. Lakini miale ya nuru
ilipenya kiza kile kinene na kuleta matumaini ya mchana uliokuwa unakuja. Waloladi (Lollards), wakija
toka Uingereza na Biblia zao pamoja na mafundisho ya Wycliffe, walifanya mengi kuhifadhi ujuzi wa
injili, na kila karne ilikuwa na mashahidi na wafia-dini wake.
Kufunguliwa kwa Matengenezo Makuu kulikuja pamoja na maandiko ya Luther, na halafu Agano Jipya la
Kiingereza la Tyndale. Pasipokugundulika kwa utawala-msonge, wajumbe wale walipita milimani na
mabondeni kimya kimya, wakiuwasha upya mwenge wa ile kweli ambao uliokuwa umezimwa karibuni

252
Hugh Latimer, "First Sermon Preached Before King Edward VI”
253
Ibid., "Sermon of the Plough”
254
Works of Hugh Latimer, vol. la 1, page wa xiii
144
katika nchi ya Scotland, na kubomoa kazi iliyokuwa imefanywa na Roma kwa karne nne za ukandamizaji
wake.
Ndipo damu ya wafia-dini ilipotia harakati msukumo mpya. Viongozi wale wa kipapa, waking’amua kwa
ghafla hatari iliyokuwa inatishia kazi yao, wakawaleta kwenye nguzo ya kuchomea moto baadhi ya
(250) wana wa kiungwana na waheshimiwa miongoni mwa wana wa Scotland. Waliijenga tu mimbara
ambapo maneno ya mashahidi waliokuwa wanakufa yalisikika katika nchi yote, yakiichochea mioyo ya
watu katika kusudi lisilokufa la kuitupilia mbali minyororo ya Roma.
Hamilton na Wishart, wakiwa wana wa kifalme kwa tabia kama kwa kuzaliwa, wakiwa na mlolongo
mrefu wa wanafunzi wao wanyenyekevu, waliyasalimisha maisha yao kwa kuchomwa moto kwenye
nguzo ya kuchomea. Lakini kutoka katika rundo lile la kuni la Wishart alitokea mmoja ambaye
asingenyamazishwa na ndimi za moto, yeye ambaye kwa uongozi wa Mungu angetoa kipigo cha ishara ya
kifo cha upapa katika nchi ya Scotland.
John Knox alikuwa ameyapa kisogo mapokeo na mafundisho potofu ya kanisa, ili kujilisha kwa zile kweli
za neno la Mungu; na mafundisho ya Wishart yalikuwa yameiimarisha azma yake ya kuachana na
jumuiya ya Roma na kujiunga na Wanamatengenezo waliokuwa wanateswa.
Akiwa ameombwa na wenzake kukalia cheo cha mhubiri, alisinyaa na kutetemeka kuhusiana na
majukumu ya kazi ile, na ilikuwa tu baada ya siku kadhaa za kujitenga faraghani na kuwa na vita ya
maumivu ndani yake ndipo alipokubali. Lakini mara tu alipokuwa amekipokea cheo kile, alisonga mbele
kwa ushujaa usiotetereka na ujasiri usiojua hofu yoyote kadiri alivyoendelea kuishi. Mwanamatengenezo
huyu mwenye moyo mnyofu hakuweza kuuogopa uso wa mtu. Mioto ya wafia-dini, iliyomzunguka kila
upande, ilimfanya tu kuongeza zaidi kasi ya juhudi zake. Pamoja na shoka la dikteta kushikiliwa kwa
namna ya kuogofya juu ya kichwa chake, bado alisimama imara, akipiga upande wa kulia na kushoto ili
kuiharibu ibada ya sanamu.
Alipoletwa mbele ya malkia wa nchi ya Scotland uso kwa uso, ambaye mbele yake moto wa viongozi
wengi wa Waprotestanti ulipoa, John Knox alitoa ushuhuda wake usioyumba kwa ajili ya ile kweli.
Hakuwa mtu wa kushawishika kwa kubembelezwa; hakusinyaa kwa hofu mbele ya vitisho. Malkia yule
akamshtaki kwa uzushi wake. Alikuwa amewafundisha watu kuipokea dini iliyopigwa marufuku na
serikali, akasema, kwa njia ile alikuwa ameivunja amri ya Mungu iliyowaamuru raia kuwatii wakuu wa
nchi. Knox alijibu hivi kwa uthabiti:
“Kama vile ambavyo dini sahihi haikuchukua nguvu za kawaida wala haikuchukua mamlaka toka kwa
wakuu wa nchi wa dunia, bali toka kwa Mungu wa milele peke yake, vivyo hivyo raia hawafungwi
kuiweka dini yao kwa namna inayokidhi matashi ya wakuu wao wa nchi. Kwa maana mara nyingi wakuu
wa nchi ndio wajinga kabisa kuliko wengine wote kuhusu dini ya kweli ya Mungu…. Kama uzao wote wa
Ibrahimu ungekuwa na dini ya Farao, ambaye wao walikuwa ni raia zake kwa muda mrefu, nakusihi
mama, hivi kungekuwa na dini gani ulimwenguni? Au endapo wote katika siku zile za Mitume wangekuwa
na dini ile ya watawala wa dola ya Kirumi, kungekuwa na dini gani juu ya uso wa dunia?… Na kwa hiyo,
mama, wewe unaweza kuelewa ya kwamba raia hawafungwi kufuata dini ya wakuu wao wa nchi, ingawa
wanaamriwa kuwatii.”
Maria alisema: “Mnayatafsiri Maandiko kwa njia moja, na wao (walimu wa Roman Catholic)
wanayatafsiri kwa njia nyingine; nimwamini yupi, na nani atakuwa mwamuzi?”
“Yawapasa mmwamini Mungu, anayesema wazi katika neno lake,” alijibu Mwanamatengenezo; “na
mbali zaidi ya vile neno linavyowafundisha, msimwamini huyu wala mwingine. Neno la Mungu lenyewe

145
liko wazi; na kama kunatokea fumbo lolote katika sehemu moja, Roho Mtakatifu, ambaye kamwe
hajipingi mwenyewe, analieleza jambo hilo kwa uwazi zaidi katika sehemu nyingine, ili ya kwamba
lisibaki shaka lolote isipokuwa tu kwa wale ambao kwa ukaidi wao wanataka kubaki wajinga.” 255
Hizo ndizo kweli ambazo Mwanamatengenezo yule asiyeogopa, aliyehatirisha maisha yake, alisema
katika masikio ya mfalme. Kwa ujasiri ule ule usioogopa aliendelea na kazi yake, akiomba na kupigana
vita za Bwana, mpaka pale nchi ya Scotland ilipokuwa huru na upapa.
Kule Uingereza kuanzishwa kwa Uprotestanti kama dini ya taifa kulipunguza, ingawa hakukuyakomesha
kabisa, mateso. Japokuwa mafundisho mengi ya Roma yalikuwa yamekataliwa, taratibu zake za ibada
zisizokuwa chache ziliendelezwa. Ukuu wa papa ulikataliwa, lakini mahali pake akatawazwa mfalme
kuwa kichwa cha kanisa. Katika ibada za kanisa kulikuwa bado na kwenda mbali na usafi na urahisi wa
injili. Kanuni kuu ya uhuru wa dini ilikuwa bado haijafahamika kwao. Ingawa (252) ukatili wa kuchukiza
ambao Roma iliutumia dhidi ya uzushi ulitumika kwa nadra tu na watawala wale wa Kiprotestanti, hata
hivyo, haki ya kila mtu ya kumwabudu Mungu kulingana na matashi ya dhamiri yake mwenyewe
haikuzingatiwa. Wote walitakiwa kuyakubali mafundisho na kufuata taratibu za ibada zilizokuwa
zimeamriwa na kanisa lililokuwa limeanzishwa. Walioenda kinyume waliteswa, kwa viwango tofaut-
tofauti, kwa mamia ya miaka.
Katika karne ya kumi na saba maelfu ya wachungaji walifukuzwa kutoka katika nafasi zao. Kwa tishio la
kulipa faini kubwa, kufungwa jela, na kufukuzwa katika nchi, watu walikatazwa, kuhudhuria mkutano
wa dini wowote isipokuwa ule uliokuwa umeidhinishwa na kanisa. Watu wale waliokuwa waaminifu
ambao walishindwa kujizuia kukusanyika pamoja kwa ajili ya kumwabudu Mungu, walilazimika kukutana
katika vichochoro vyenye giza, katika vipenu vilivyofichika vya orofani, na wakati wa majira fulani
msituni wakati wa usiku wa manane. Katika maficho yale ya msitu mnene, hekalu la nyumba ya Mungu
mwenyewe, watoto wale wa Bwana waliotawanyika na kuteswa walikusanyika kuzimimina roho zao
katika maombi na sifa. Lakini, japokuwa walichukua tahadhari zote, wengi waliteseka kwa sababu ya
imani yao. Magereza yalijaa. Familia zilisambaratika. Wengi walifukuzwa kwenda katika nchi za kigeni.
Lakini Mungu alikuwa pamoja na watu wake, na mateso hayakuweza kunyamazisha ushuhuda wao.
Wengi walisukumwa kuvuka bahari hadi Amerika mahali ambapo waliweka misingi ya uhuru wa kiraia na
kidini ambayo yamekuwa nguzo na fahari ya nchi hii.
Kwa mara nyingine, kama ilivyokuwa katika siku za mitume, mateso yaligeuka na kuwa njia ya
kuiendeleza injili. Katika gereza la kuudhi la chini ya ardhi lililojazwa na wafisadi na wauaji, John
Bunyan alipumua hewa ya mbinguni; na, mle ndimo alimoandikia kisa kile cha ajabu cha safari ya
msafiri kutoka nchi ya uharibifu kwenda kwenye mji wa mbinguni. Kwa miaka zaidi ya mia mbili sauti ile
toka katika gereza la Bedford imeendelea kunena kwa uwezo wa kusisimua katika mioyo ya watu.
Vitabu vya Bunyan vinavyoitwa, Pilgrims Progress na Grace Abounding to the Chief of Sinners
vimeziongoza nyayo nyingi katika njia ya uzima.
Baxter, Flavel, Alleine, na watu wengine wenye vipaji, elimu, uzoefu mkubwa wa Ukristo walisimama
imara kuitetea (253) imani ambayo ilitolewa kwa watakatifu mara moja. Kazi hii iliyofanywa na watu
hawa, iliyopingwa na kupigwa marufuku kisheria na watawala wa ulimwengu huu, haiwezi kukomeshwa.
Kitabu cha Flavel kinachoitwa Fountain of Life and Method of Grace kimefundisha maelfu namna ya
kuendelea kukabidhi nafsi zao kwa Kristo. Kitabu cha Baxter kinachoitwa Reformed Pastor kimekuwa
mbaraka kwa watu wengi wanaotamani uamsho kwa kazi ya Mungu, na kitabu chake kingine kinachoitwa

255
David Lang, The Collected Works of John Knox, vol. la 2, page wa 281 na 284

146
Saints' Everlasting Rest kimefanya kazi yake katika kuziongoza roho kwenda katika “raha” ambayo
imesalia kwa watu wa Mungu.
Miaka mia moja baadaye, katika siku ya giza kuu la kiroho, Whitefield na Wesleys walijitokeza kama
wabebaji wa nuru kwa ajili ya Mungu. Chini ya utawala wa kanisa lililoanzishwa watu wa Uingereza
walikuwa wamerudia hali ya mmomonyoko wa maadili ya kidini hata ikawa vigumu kuitofautisha dini ile
na ushenzi. Dini ya mambo yaliyopo ndiyo iliyopenda kusomewa na viongozi wa dini, nayo ilichukua
sehemu kubwa sana ya thiolojia yao. Watu wa matabaka ya juu sana walinuna na kujivuna, na walikuwa
na kiburi kwamba wao wako juu ya kile walichokiita ushupavu wa kidini. Wale waliokuwa katika
matabaka ya chini walikuwa wajinga kabisa, tena walitelekezwa katika utovu wa maadili, wakati kanisa
halikuwa na ujasiri tena wala imani ya kuendelea kuisaidia kazi ya ile ya kweli iliyokuwa imeanguka.
Fundisho kuu la kuhesabiwa haki kwa imani, ambalo lilifundishwa kwa uwazi na Luther, lilikuwa karibu
limesahauliwa lote; na ile kanuni ya Kirumi ya kutegemea matendo mema kwa ajili ya wokovu ilikuwa
imechukua mahali pake. Whitefield na Wesleys, ambao walikuwa washiriki wa kanisa lile lililokuwa
limeanzishwa, walikuwa watafutaji waaminifu wa Mungu, na walikuwa wamefundishwa kwamba hali
hiyo inapatikana kwa kuwa na maisha mema na kushika taratibu za dini.
Wakati Charles Wesley alipokuwa mgonjwa wakati fulani, na kuhisi kwamba kifo kilikuwa kinakaribia
kwake, aliulizwa swali kwamba alitegemeza tumaini lake la uzima wa milele juu ya kitu gani. Jibu lake
lilikuwa: “Nimetumia juhudi zangu vizuri kumtumikia Mungu.” Kama vile rafiki yake aliyekuwa
amemwuliza swali lile alionekana kana kwamba hajaridhika na jibu lile, Wesley aliwaza hivi: “Nini!
Kwani juhudi zangu si mahali pa kutosha kujenga tumaini langu? Anataka kunipora juhudi zangu
nilizofanya? Sina kitu kingine cho chote cha kutumainia.” 256 Hilo lilikuwa giza nene (254) lililokuwa
limetanda juu ya kanisa, likificha huduma ya upatanisho, likimpora Kristo utukufu wake, na kuigeuza
mioyo ya watu mbali na tumaini lao pekee la wokovu - damu ya Mkombozi aliyesulibiwa.
Wesley na rafiki zake waliongozwa kuona kwamba dini ya kweli inakaa moyoni, na ya kwamba sheria ya
Mungu inaenda hadi katika mawazo na hadi katika maneno na matendo. Wakiwa wamesadikishwa juu ya
umuhimu wa utakatifu wa moyo, pamoja na usahihi wa mwenendo wa nje, walifanya mwanzo wa dhati
wa maisha mapya. Kwa juhudi za dhati na za maombi waliazimia kushinda uovu wa moyo wa asili.
Waliishi maisha ya kujikana nafsi, ukarimu, na unyenyekevu, wakishika kwa msimamo mkali na kwa
usahihi kila hatua waliyodhani ingeweza kuwasaidia katika kukipata kile walichotamani sana - ule
utakatifu ambao ungeweza kuwapa upendeleo kwa Mungu. Lakini hawakupata kile walichotafuta.
Juhudi zao za kutaka kujiweka huru mbali na hukumu ya dhambi au kuvunjilia nguvu za dhambi vilikuwa
bure. Lilikuwa ni pambano kama lile ambalo Luther alikuwa amelipitia katika chumba chake kidogo
kule Erfurt. Lilikuwa swali lile lile lililokuwa limetesa nafsi yake - “Mtu anakuwaje mwenye haki mbele
za Mungu?” Ayubu 9:2.
Mioto ya ukweli wa mbinguni, ambayo ilikuwa karibu kuzimwa katika madhabahu za Uprotestanti,
ilikuwa iwashwe tena na Wakristo wa Bohemia kutoka katika taa iliyorithishwa kupitia vizazi na vizazi.
Baada ya Matengenezo, Uprotestanti kule Bohemia ulikuwa umekanyagwa chini ya miguu ya genge la
Roma. Wote waliokataa kuukana ukweli walilazimishwa kukimbia. Baadhi ya hawa, wakijipatia mahali
pa kimbilio Saksoni, waliendeleza imani yao ya kale pale. Kutoka kwa wazao wa Wakristo hawa nuru
ilimfikia Wesley na rafiki zake.

256
John Whitefield, Life of the Rev. Charles Wesley, page 102

147
John na Charles Wesley, baada ya kutawazwa katika utumishi wa injili, walitumwa kwenda kupeleka
utume Amerika. Katika meli ile lilikuwamo kundi la Wamoraviani. Walikumbana na dhoruba kali katika
safari ile, na John Wesley, akiwa ameletwa mahali pa uso kwa uso na kifo, alihisi kwamba hakuwa na
hakika ya kuwa na amani kati yake na Mungu. Wajerumani wale, kinyume chake, walionyesha roho ya
utulivu na tumaini, mambo ambayo kwake yalikuwa mageni.
(255) “Nilikuwa nimechunguza kwa muda mrefu tabia yao ya umakini mkubwa,” alisema. Kuhusu
unyenyekevu wao, walikuwa wametoa hakikisho la kutosha, kwa kufanya kazi zile za kitumwa kwa ajili
ya wasafiri wengine ambazo hakuna mtu miongoni mwa Waingereza ambaye angezifanya; ambazo
walipenda kuzifanya na hawakuhitaji malipo, wakisema kwamba ilikuwa ni vema kwa ajili ya mioyo yao
ya kiburi, na ya kwamba Mwokozi wao mwenye pendo alikuwa amefanya zaidi kwa ajili yao. Na kila siku
ilikuwa imewapa nafasi ya kuonyesha unyenyekevu ule ambao usingeweza kuzuiwa na jeraha lolote.
Ikiwa walisukumwa, kupigwa, au kuangushwa chini, waliinuka tena na kwenda zao; lakini hakuna
lalamiko lolote lililopatikana kutoka kinywani mwao. Sasa kulikuwa na nafasi ya kuwapima kuona kama
walikuwa wameokolewa kutokana na roho ya woga, na ya kiburi, hasira, na kisasi. Katikati ya kuimba
zaburi mahali huduma yao ilipoanzia, bahari ilijimwaga, ikapasua tanga lile vipande vipande, na
kuifunika meli, na kumwagika katikati ya sitaha kana kwamba kilindi kilikuwa kimetumeza tayari. Kilio
cha ajabu kilianza kutolewa miongoni mwa Waingereza. Wajerumani waliendelea kuimba kwa utulivu.
Baada ya pale nilimwuliza mmoja wao, ‘Wewe ulikuwa hauogopi?’ Alijibu, ‘La, namshukuru Mungu.’
Nikauliza, ‘Lakini, wanawake wenu na watoto wenu hawakuogopa?’ Akajibu kwa upole, ‘La; wanawake
na watoto wetu hawaogopi kufa.’” 257
Walipofika Savannah, Wesley kwa muda mfupi alikaa na Wamoraviani wale, naye akaguswa sana moyoni
mwake kwa mwenendo wao wa Kikristo. Kuhusu moja ya huduma zao za kidini, iliyokuwa kinyume sana
na dini ya urasimu na maonyesho isiyo hai ya Kanisa la Uingereza, aliandika hivi: “Taratibu zao za ibada
za kawaida sana pamoja na kicho chao kwa Mungu katika ibada yao yote, zilinifanya nisahau miaka elfu
moja na mia saba ya katikati, na kunifanya nihisi kama niko katika moja ya makusanyiko ambayo
haikuwa na muundo rasimu wala dola; lakini Paulo, mtengeneza mahema, au Petro, mvuvi wa samaki,
alikuwa mwenyekiti; lakini kwa maonyesho ya Roho na uwezo.” 258
Aliporudi Uingereza, Wesley, chini ya mafunzo ya mhubiri wa Kimoraviani, alifikia ufahamu ulio wazi wa
imani ya Biblia. Aliaminishwa kwamba ni lazima aachane na kutegemea matendo yake kwa ajili ya
wokovu wake na ya kwamba ni lazima amtumaini (256) tu “Mwana-Kondoo wa Mungu, aichukuaye
dhambi ya ulimwengu.” Katika kusanyiko la jamii ya Wamoraviani mjini London, maneno ya Luther
yalisomwa, yakielezea badiliko ambalo Roho wa Mungu anafanya moyoni mwa mtu aaminiye. Wesley
aliposikiliza, imani iliwashwa moyoni mwake. “Nilijisikia moyo wangu ukipata joto kwa namna ya
ajabu” anasema. “Nilijisikia kweli kwamba mimi nilikuwa nimemwamini Kristo, Kristo pekee, kwa ajili
ya wokovu wangu: na uthibitisho ulitolewa kwangu, kwamba alikuwa ameziondoa dhambi zangu, zangu
mimi, na kuniokoa mimi kutoka katika sheria ya dhambi na mauti.” 259
Katika muda mrefu wa miaka ya mahangaiko yake ya kuchosha na yasiyo na faraja - miaka ya kujikana
nafsi kwa nguvu, kujishutumu na kujitweza - Wesley, kwa uthabiti, alikuwa amelishikilia kusudi lake
moja la kumtafuta Mungu. Sasa akawa amempata; naye akaona kwamba ile neema aliyosumbuka sana

257
Whitefield, Life of the Rev. John Wesley, page wa 10
258
Ibid., page wa 11 na 12
259
Ibid., uk. 52

148
kuitafuta kwa maombi na kufunga, kwa matendo ya matoleo ya sadaka na kujinyima, ilikuwa ni zawadi,
“pasipokulipiwa fedha na bila bei.”
Alipokwisha kuimarishwa katika imani ya Kristo, roho yake yote ikawaka moto kwa hamu ya kueneza
elimu hii ya injili tukufu ya neema ya Mungu ya bure. “Nauangalia ulimwengu wote kama parishi
yangu,” alisema; “katika sehemu yake yoyote nilipo, nafikiri inastahili, ni haki, na wajibu wangu
unaonifunga, kuwatangazia wote walio tayari kusikia habari njema hii ya furaha ya wokovu.” 260
Aliendelea na maisha yake ya kuwa na nidhamu kali na kujinyima, sio kama msingi wa imani kwa sasa,
bali kama matokeo ya imani; sio kama mzizi, bali kama tunda la utakatifu. Neema ya Mungu katika
Kristo ndiyo msingi wa tumaini la Mkristo, na neema hiyo itajidhihirisha katika utii. Maisha ya Wesley
yalitolewa wakfu kwa ajili ya kuzihubiri zile kweli kuu alizokuwa amezipokea - kuhesabiwa haki kwa
imani katika damu ya upatanisho ya Kristo, na uweza wa Roho Mtakatifu ufanyao upya moyo, ukizaa
matunda katika maisha yanayoendana na kielelezo cha Kristo.
Hisia kali ya kutambua hali yao ya kupotea kwa muda mrefu iliwatayarisha Whitefield na Wasleys kwa
kazi yao; na ili kwamba waweze kustahimili kushiriki taabu (257) kama askari wema wa Kristo,
walikuwa wamewekwa chini ya moto wa majaribu wa dharau, dhihaka, na mateso, walipokuwa sehemu
zote mbili chuo kikuu na kuingia katika kazi ya utumishi. Wanafunzi wenzao wasiomcha Mungu
waliwaita wao pamoja na wengine wachache waliowaunga mkono kwa dharau kuwa ni Wamethodisti -
jina ambalo kwa sasa linafikiriwa na mojawapo ya madhehebu makubwa sana katika nchi ya Uingereza
na Amerika kuwa ni jina linalostahili heshima.
Wakiwa washiriki wa Kanisa la Uingereza, walikuwa wamefungamanishwa sana na taratibu zake za
ibada, lakini Bwana akawa ameweka mbele yao katika neno lake kiwango cha juu zaidi. Roho Mtakatifu
aliwabidisha kumhubiri Kristo aliyesulibiwa. Uweza wake Aliye juu ulifuatana na kazi zao. Maelfu
waliguswa na kuongoka kweli kweli. Ilikuwa ni muhimu kwamba kondoo wale walindwe kutokana na
mbwa-mwitu wenye njaa kali. Wesley hakuwa na wazo lolote la kuanzisha dhehebu jipya, lakini
aliwasimamia wakiwa chini ya kile kilichoitwa Muunganisho wa Kimethodisti.
Upinzani ambao wahubiri hawa walikutana nao toka kwa kanisa lililokuwepo ulikuwa wa ajabu na wa
majaribu; lakini, Mungu, katika hekima yake, alikuwa ameyageuza matukio na kusababisha
matengenezo kuanza ndani ya kanisa lenyewe. Kama matengenezo yangekuja yote kutokea nje,
yasingeweza kupenya mpaka mahali yalipokuwa yanahitajika sana. Lakini kwa kuwa wahubiri wale wa
uamsho walikuwa ni wanakanisa, na walifanya kazi yao ndani ya mipaka ya kanisa pale walipopata
nafasi, ile kweli iliweza kuingia mahali ambapo vinginevyo milango ingebaki imefungwa. Baadhi ya
viongozi wa kanisa waliamshwa kutoka katika usingizi mzito wa kimaadili wakawa wahubiri motomoto
katika parishi zao. Makanisa yaliyokuwa yamegubikwa na urasimu wa desturi na taratibu za kanisa
yalihuishwa haraka na kuwa hai.
Mnamo wakati wa Wesley, kama ilivyokuwa katika vizazi vyote vya historia ya kanisa, watu wenye
vipawa mbalimbali walifanya kazi walizopewa kufanya. Hawakuafikiana katika kila jambo linalohusu
mafundisho ya dini, lakini wote waliongozwa na Roho wa Mungu, na kuungana katika lengo moja
linalowavuta pamoja la kuwaleta watu kwa Kristo. Tofauti zilizokuwapo kati ya Whitefield na Wesleys
zilitishia kuleta mfarakano wakati mmoja; (258) lakini walipojifunza upole katika shule ya Kristo,
walipatanishwa na kuvumiliana na upendo wa ukarimu. Hawakuwa na muda wa kupingana, wakati

260
Ibid., page wa 74

149
mafundisho potofu na uovu vilikuwa vinaenea kila mahali, na wenye dhambi wakiwa wanashuka katika
uangamivu.
Watumishi wa Mungu walipita katika njia yenye kuparuza. Watu wenye mvuto na elimu waliutumia
uwezo wao dhidi yao. Baada ya muda, wengi miongoni mwa viongozi wa kanisa walionyesha uadui wao
waziwazi, na milango ya makanisa ikafungwa dhidi ya imani safi na dhidi ya wale walioitangaza. Njia
waliyoitumia viongozi wale kuwalaani watu hawa mimbarani iliamsha chembechembe za giza, ujinga,
na uovu. Tena na tena John Wesley alinusurika kufa kwa mwujiza wa rehema ya Mungu. Ghadhabu ya
kundi la watu wenye ghasia ilipochochewa dhidi yake, tena ilionekana kana kwamba hapakuwa na njia
ya kuponyokea, malaika katika umbo la mwanadamu alikuja na kusimama upande wake, kundi lile lenye
ghasia likarudi kinyumenyume, na mtumishi yule wa Kristo akapita salama mahali pale pa hatari.
Kwa habari za kuokolewa kwake kutokana na kundi lile lenye ghadhabu na ghasia katika moja ya
matukio yale, Wesley alisema: “Wengi walijitahidi sana kuniangusha chini tulipokuwa tunatelemka
kilima kile chenye njia ya utelezi kuelekea mjini; na wakijua kwamba nikishaanguka chini, basi,
ingekuwa vigumu kwangu kuinuka pale. Lakini mimi sikujikwaa hata kidogo ili kuanguka, wala sikuteleza
hata kidogo, mpaka nikaponyoka kabisa kutoka mikononi mwao…. Japokuwa wengi walijaribu sana
kunishika kola yangu au nguo zangu ili kunivuta na kuniangusha chini, ila hawakuweza kabisa kushika
sana: ni mmoja tu aliyeshika sana kipande cha kisibau changu, ambacho kilibaki mkononi mwake;
mwingine akashika mfuko mmoja uliokuwa na noti moja, ukachanwa nusu…. Mtu mmoja mwenye nguvu
aliyekuwa karibu na mgongo wangu, alinipiga mara kadhaa kwa fimbo kubwa; ambayo kama angenipiga
nayo kisogoni mara moja tu ingekuwa imemsaidia kuondoa udhia wake wote. Lakini kila mara
aliponipiga, pigo lilipelekwa kando, sijui ilikuwaje; maana sikukwepa kwenda kulia wala kushoto….
Mwingine akaja mbio kupitia katika msongamano ule wa watu, naye akanyanyua mkono wake juu ili
kunipiga, ghafla akaushusha chini, na kunipangusa tu kichwa changu, akisema, ‘Tazama! ana nywele
laini namna hii!’… Watu wa kwanza kabisa kugeuzwa mioyo walikuwa mashujaa wa mji ule, makapteni
wa watu wale wenye ghasia katika (259) matukio yote, mmoja wao akiwa mpiganaji ngumi aliyepata
tuzo katika bustani za watu wakali….
“Ni kwa hatua za upole jinsi gani Mungu anavyotuandaa kufanya mapenzi yake! Miaka miwili iliyopita,
kipande cha tofali kilichubua mabega yangu. Ilikuwa ni mwaka mmoja baadaye wakati jiwe liliponigonga
katikati ya macho. Mwezi uliopita nilipata kipigo kimoja, na leo jioni viwili, kimoja kabla hatujaingia
katika mji huu, na kimoja tulipokuwa tumetoka katika mji huu; lakini vyote viwili vilikuwa kama si kitu
kwangu: maana ijapokuwa mtu mmoja alinipiga kifuani kwa nguvu zake zote, na mwingine mdomoni
kwa nguvu iliyofanya damu itoke sana, kutokana na kipigo chochote kati ya hivyo sikusikia maumivu
yoyote ambayo ni zaidi ya kuguswa na jani kavu.” 261
Wamethodisti wa siku zile za kale - watu wa kawaida pamoja na viongozi wao wa kiroho - walistahimili
dhihaka na mateso ya aina moja ile ile toka kwa washiriki wa kanisa na kwa wale waliojionyesha
waziwazi kuwa hawapendi dini ambao walikuwa wamekasirishwa kwa kusemwa vibaya. Walishtakiwa
mbele ya mahakama za sheria - zilizoitwa hivyo kwa jina tu, kwa maana haki ilikuwa adimu sana katika
mahakama za wakati ule. Mara nyingi walipata mateso makali sana toka kwa watesi wao. Makundi ya
watu wenye ghasia yalikwenda nyumba kwa nyumba yakiharibu samani na mali, wakipora chochote
walichochagua, na kwa ukatili wakidhalilisha wanaume, wanawake, na watoto. Katika baadhi ya
matukio, matangazo ya hadhara yalibandikwa, yakiwaita wale waliopenda kusaidia kuvunja madirisha

261
John Wesley, Works, vol. la 3, page wa 297 na 298

150
na kupora mali toka katika nyumba za Wamethodisti, kukutana katika muda na mahali fulani. Ukiukaji
huo wa wazi wa sheria za wanadamu na za Mungu uliruhusiwa kupita bila kukemewa. Mateso
yaliyoratibishwa yaliendelea dhidi ya watu ambao kosa lao pekee lilikuwa ni la kuigeuza miguu ya
wenye dhambi kutoka katika njia ya uharibifu kwenda katika njia ya utakatifu.
Akirejea katika mashtaka yaliyotolewa dhidi yake na wenzake, John Wesley alisema: “Baadhi ya watu
wanadai kwamba mafundisho ya watu hawa ni ya uongo, yana makosa, na ya ushabiki; kwamba ni
mapya na hayajapata kusikiwa - hadi siku za karibuni; kwamba ni ya dhehebu la Quakerism, washupavu
na wa upapa. Unafiki wote huu umeshakatwa mpaka mizizi yake, ikiwa imeonyeshwa kwa mapana
kwamba kila tawi la mafundisho haya ni mafundisho ya wazi ya Maandiko (260) yaliyotafsiriwa na kanisa
letu. Kwa hiyo, hayawezi kuwa ya uongo au ya makosa, ikiwa Maandiko yenyewe ni ya kweli.” “Wengine
wanadai kwamba, ‘Mafundisho yao ni makali; yanaifanya njia ya kwenda mbinguni kuwa nyembamba
mno.’ Haya madai kwa kweli ndiyo kipingamizi cha mwanzo, (kwa kuwa ndiyo madai pekee
yaliyokuwapo kwa muda fulani,) na kwa siri ndiyo yako chini ya mengine elfu zaidi, yanayojitokeza
katika sura mbalimbali. Lakini, je! haya yanaifanya njia ya kwenda mbinguni kuwa nyembamba zaidi
kuliko vile Kristo na mitume wake walivyoifanya? Je! mafundisho haya ni makali zaidi kuliko ya Biblia?
Hebu tafakari maandiko haya machache ya wazi: ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na
kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote.’ ‘Kila neno lisilo maana,
watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.’ ‘Basi, mlapo, au mnywapo au
mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.’”
“Ikiwa mafundisho yao yana ukali sana kuliko haya, basi, walaumiwe; lakini ninyi mnajua katika dhamiri
zenu ya kwamba sivyo. Na ni yupi anayeweza kupunguza ukali hata kwa yodi moja pasipo kupotosha
neno la Mungu? Je, mtumishi-mwangalizi wa siri za Mungu aweza kuonekana kuwa mwaminifu ikiwa
anabadili sehemu yoyote ya amana takatifu aliyokabidhiwa? La. Hawezi kupunguza chochote, hawezi
kulainisha; anatakiwa kuwatangazia watu wote kwamba, ‘Siwezi kushusha Maandiko katika kiwango cha
radha mnayotaka ninyi. Lazima ninyi ndio mpande juu kufikia kiwango chake, vinginevyo muangamie
milele.’ Huu ndio msingi halisi wa kelele zile nyingine kuhusu ‘watu hawa hawana huruma.’ Hawana
huruma, ndivyo walivyo? Katika mtazamo upi? Hawawapi chakula wenye njaa na kuwavika nguo walio
uchi? ‘La; jambo lenyewe siyo hilo: hawapungukiwi katika hilo: ila hawana huruma katika kuhukumu!
wanafikiri kwamba hakuna anayeweza kuokolewa isipokuwa wale tu walio katika njia yao.” 262
Kuporomoka kwa hali ya kiroho kule Uingereza muda mfupi tu kabla ya wakati wa Wesley kulikuwa kwa
sehemu kubwa matokeo ya mafundisho ya antinomian (imani kwamba wokovu hupatikana kwa imani na
neema, si kwa sheria). Wengi waliamini kwamba Kristo alikuwa amekomesha sheria ya maadili, na ya
kwamba kwa sababu hiyo Wakristo walikuwa hawawajibiki kuishika; na ya kwamba muamini alikuwa
huru na “kufungwa na matendo mema.” Wengine, ingawa wanakubali (261) kwamba sheria inadumu,
walitangaza kwamba si muhimu wahubiri kuhimiza watu kuzitii, maana wale ambao Mungu alikuwa
amewachagua kwa ajili ya wokovu wangeweza, “kwa msukumo usiozuilika wa neema ya Mungu,
kuongozwa kutenda wema na uadilifu,” wakati wale waliokuwa wameandikiwa laana ya milele
“hawakuna na nguvu ya kuitii sheria ya Mungu.”
Wengine, pia wakishikilia imani kwamba “wateule hawawezi kuanguka kutoka katika neema wala
kupoteza upendeleo wa Mungu,” walifikia katika hitimisho la kuogofya zaidi kwamba “matendo maovu
wanayotenda si dhambi hasa, wala hayapaswi kufikiriwa kama matukio ya uvunjaji wa sheria ya Mungu,
na kwamba, kwa hiyo hakuna mahali pa ama kuungama dhambi zao hizo au kuziondoa kwa njia ya

262
Ibid., vol. la 3, page 152 na 153
151
toba.” 263 Kwa hiyo, wao wakatangaza ya kwamba hata moja miongoni mwa dhambi mbaya sana,
“iliyofikiriwa kwa ujumla kuwa uvunjaji mkubwa wa sheria ya Mungu, si dhambi machoni pa Mungu,”
kama ikitendwa na mmoja wa wateule, “kwa sababu ni moja ya tabia muhimu zinazowatofautisha
wateule, ya kwamba hawawezi kutenda neno lolote ambalo ama linamchukiza Mungu au limekatazwa na
sheria.”
Mafundisho haya ya ajabu kimsingi yanafanana na mafundisho ya baadaye ya wasomi na wanathiolojia
maarufu - kwamba hakuna sheria ya Mungu iliyo kiwango cha haki ambayo haibadiliki, na ya kwamba
kiwango cha maadili kinaonyeshwa na jamii yenyewe, na ya kwamba kimekuwa kikibadilika.’ Mawazo
yote haya yanatiwa msukumo na na roho ile – ile ambayo, hata miongoni mwa wakazi wa mbinguni
wasio na dhambi, ilianza kazi yake ya kutafuta kuvunjilia mbali vifungo vya haki ya sheria ya Mungu.
Fundisho la dini la amri za Mungu, ambazo zinafunga tabia ya wanadamu, limewafanya wengi kuikataa
kabisa sheria ya Mungu. Wesley aliyapinga kwa uthabiti mafundisho potofu ya walimu wa antinomian na
kuonyesha kuwa fundisho hili lililowaingiza watu katika uantinomia lilikuwa linapingana na Maandiko.
“Neema (262) ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa.” “Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele
za Mungu Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. Kwa
sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;
ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote.” Tito 2:11; 1 Timotheo 2:3-6. Roho wa
Mungu hutolewa bure ili kumwezesha kila mtu kuishikilia njia ya wokovu. Hivyo ndivyo alivyo Kristo,
“Nuru halisi,” “amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.” Yohana 1:9. Watu wanakosa wokovu
kwa ukaidi wao wenyewe kwa kuikataa zawadi hiyo ya uzima.
Katika jibu la dai kwamba wakati wa kufa kwa Kristo agizo la Amri Kumi lilikuwa limekomeshwa pamoja
na sheria ya taratibu za ibada, Wesley alisema: “Sheria ile ya maadili ambayo imo katika Amri Kumi, na
ambayo ilihimizwa na manabii, hakuiondoa. Kuja kwake hakukuwa na mpango wa kuondoa sehemu
yoyote ya sheria. Hii ni sheria ambayo haiwezi kamwe kuvunjwa, nayo ‘inasimama imara kama shahidi
mwaminifu wa mbinguni.’… Hiyo ilikuwako tangu mwanzo wa ulimwengu, ikiwa ‘imeandikwa si katika
mbao za mawe,’ bali katika mioyo ya wana wote wa wanadamu, walipotoka mikononi mwa Muumba. Na
japokuwa sasa herufi zile zilizoandikwa kwa kidole cha Mungu, kwa sehemu kubwa, zimeharibiwa na
dhambi, lakini haziwezi kufutwa kabisa, maadam bado tunayo dhamiri ya kujua mema na mabaya.
Lazima kila kipengele cha sheria hii kitekelezwe kwa wanadamu wote, katika vizazi vyote; bila
kutegemea wakati au mahali, au hali nyingine iwayo yote iliyo na mwelekeo wa kubadilika, bali
hutegemea asili ya Mungu, na asili ya mwanadamu, na uhusiano usiobadilika-badilika kati ya mtu na
mwingine.
“‘Sikuja kutangua, bali kutimiliza.’… Bila swali, maana aliyo nayo hapa (ikizingatia yote yaliyotangulia
na yale yanayofuata), - Nimekuja kuiweka katika ukamilifu wake, licha ya wanadamu kuzipamba:
Nimekuja kuweka mwonekano kamili na wa wazi katika kile ambacho kilikuwa na giza au kivuli humo:
Nimekuja kuwatangazia maana ya kweli na kamilifu katika kila kipengele chake. Kuwaonyesha marefu
na mapana, upeo wote wa kila amri iliyomo ndani yake, pamoja na (263) kimo na kina chake, usafi
wake na ubora wake kiroho upitao ufahamu wetu katika nyanja zake zote.” 264
Wesley alitangaza kuhusu mapatano sahihi yaliyopo kati ya sheria na injili. “Basi, kuna uhusiano wa
karibu mno unaoeleweka kati ya sheria na injili. Kwa upande mmoja, sheria daima inaweka njia kwa
ajili ya, na kutuelekeza kwa, injili; kwa upande mwingine, injili inatuongoza daima kwenye utimilizaji

263
McClintock and Strong, Cyclopedia, article “Antinomians”
264
Wesley, hotuba ya 25
152
sahihi wa sheria. Sheria, kwa mfano, inatutaka tumpende Mungu, na kumpenda jirani yetu, kuwa
wapole, wanyenyekevu au watakatifu. Sisi tunahisi kuwa hatuna uwezo wa kuyatenda mambo hayo;
naam, ‘kwa mwanadamu hilo haliwezekani kabisa;’ lakini tunaiona ahadi ya Mungu ya kutupatia upendo
huo, na kutufanya sisi kuwa wanyenyekevu, wapole, na watakatifu; tunaishika injili hiyo, hizo habari
njema; inafanyika hivyo kwetu kwa kadiri ya imani yetu; na ile ‘haki ya sheria inatimizwa ndani yetu,’
kwa njia ya imani iliyo ndani ya Kristo Yesu….
“Katika ngazi ya juu ya maadui wa Injili ya Kristo,” alisema Wesley, “wamo wale ambao kwa waziwazi
na kwa uwazi ‘wanaihukumu sheria’ na ‘wanaisema vibaya sheria;’ ambao wanafundisha watu kuvunja
(kufuta, kulegeza, kuvifungua vifungo vya uwajibikaji kwake) si amri moja tu, iwe ndogo zaidi au kubwa
zaidi, bali amri zote kwa mpigo…. Jambo la kushangaza kuliko hali zote zinazoambatana na uongo huo
ni kwamba wale wanaouchukua wanaamini kweli kweli kwamba wanamheshimu Kristo kwa kuifutilia
mbali sheria yake, na ya kwamba wanaitukuza kazi yake kumbe wakiwa wanaliharibu fundisho lake!
Naam, wanamheshimu kama vile Yuda alivyofanya, wakati aliposema, ‘Salamu, Rabi, akambusu.’ Naye
anaweza kusema kwa haki kwa kila mmoja wa watu hawa, ‘Wamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu?’
Si kitu kingine zaidi ya kumsaliti kwa kumbusu kwa mtu kuzungumza kuhusu damu yake, huku
akimnyang’anya taji yake; kuondosha nuru katika kipengele chochote cha sheria yake kwa unafiki
kwamba tunaiendeleza injili yake. Wala kwa kweli hakuna mtu awaye yote awezaye kukwepa shtaka
hilo, ambaye anahubiri imani kwa namna yoyote inayoweka kando utii iwe moja kwa moja au si moja
kwa moja: ambaye anamhubiri Kristo ili kuondoa, au kuhafifisha kwa namna yoyote, ndogo kabisa
miongoni mwa amri za Mungu.” 265
(264) Kwa wale waliosisitiza kwamba “kuihubiri injili ni kujibu miisho yote ya sheria,” Wesley alijibu
hivi: “Hili tunalikataa kabisa. Halitoi jibu kuhusu ule mwisho wa kwanza wa sheria, yaani, kuwashawishi
watu kuhusu dhambi zao, kuwaamsha wale ambao bado wamelala usingizi wakiwa ukingoni mwa
jehanum.” Mtume Paulo anatangaza kwamba “kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria;”
“tena ni mpaka hapo mtu atakapohakikishiwa kwa habari ya dhambi yake, ndipo anapoona kweli hitaji
lake la damu ya upatanisho ya Kristo…. ‘Wenye afya,’ kama alivyosema Bwana wetu mwenyewe,
‘hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi.’ Kwa hiyo, ni jambo la kushangaza kuwapatia tabibu wale
walio na afya, au walau hata wale wanaojiona kuwa hivyo. Lazima kwanza uwahakikishie kwamba
wanaumwa; la sivyo hawatakushukuru kwa kazi yako. Ni jambo la kushangaza pia kuwapelekea Kristo
watu ambao wana mioyo iliyo mizima, ikiwa haijapata kupondeka.” 266
Kwa hiyo alipokuwa anaihubiri injili hii ya neema ya Mungu, Wesley, kama alivyofanya Bwana wake,
alitafuta “kuitukuza sheria, na kuiadhimisha.’ Kwa uaminifu alifanya kazi ile aliyopewa na Mungu, na
alijaliwa kuyaona matokeo yake matukufu. Mwishoni mwa maisha yake marefu ya zaidi ya miaka
themanini – akiwa ametumia zaidi ya nusu karne katika safari zake za utumishi - wafuasi wake wa wazi
walikuwa wamefikia idadi ya zaidi ya nusu milioni. Lakini idadi ya umati wa watu ambao kwa njia ya
kazi yake walikuwa wameinuliwa kutoka katika uangamivu na utumwa wa dhambi kwenda katika maisha
ya juu na yaliyo safi zaidi, na idadi ya watu ambao kwa mafundisho yake walipata utajiri wa uzoefu wa
kutosha na wa kina, haitajulikana kamwe hadi jamaa yote ya waliokombolewa itakapokusanywa katika
ufalme wa Mungu. Maisha yake yanatoa fundisho la thamani isiyo na bei kwa kila Mkristo. Laiti kama
imani na unyenyekevu, juhudi isiyochoka, kujikana, na kumcha Mungu kwa mtumishi huyu wa Kristo
vingeakisiwa katika makanisa ya leo!

265
Ibid
266
Ibid., Hotuba ya 35
153
Sura ya 15
BIBLIA NA MAPINDUZI YA UFARANSA

Katika karne ya kumi na sita Matengenezo, yakiwapa watu Biblia iliyo wazi, yalikuwa yamepata
kukubalika katika nchi zote za Ulaya. Baadhi ya mataifa yalipokea Matengenezo kwa furaha, kama
mjumbe wa Mbinguni. Katika sehemu nyingine nyingi upapa ulifanikiwa kwa kiwango kikubwa kuyazuia
yasipate kuingia; na nuru ile ya ufahamu wa Biblia, pamoja na mivuto yake inayoinua, ilikuwa kama
imefungiwa nje kabisa. Katika nchi moja, japokuwa nuru ilikuwa imeingia, haikuweza kukubalika kuwa
pamoja na giza lililokuwamo. Kwa karne nyingi, kweli na uongo vikawa katika mapambano ya kutaka
kuongoza. Hatimaye uovu ukashinda, na ile kweli ya Mbinguni ikatupwa nje. “Na hii ndiyo hukumu; ya
kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru.” Yohana 3:19. Taifa hilo
likaachwa livune matokeo ya njia ambayo lilikuwa limechagua. Zuio la Roho wa Mungu liliondolewa kwa
watu wale waliokuwa wamedharau zawadi ya neema yake. Uovu uliruhusiwa kufikia hatua ya kukomaa.
Na ulimwengu wote uliona matunda ya kuikataa nuru kwa makusudi.
Vita dhidi ya Biblia, iliyoendelezwa Ufaransa kwa karne nyingi, iliishia katika matukio ya Mapinduzi.
Tukio hilo la kutisha lilikuwa matokeo halali ya Roma kunyamazisha Maandiko. 267 Lilitoa kielelezo cha
kichapo kiasi ambacho ulimwengu haujashuhudia katika utendaji wa sera za upapa - kielelezo cha
matokeo ya mahali ambako kwa miaka zaidi ya elfu moja (266) mafundisho ya Kanisa la Roma yalikuwa
yakijielekeza.
Unyamazishaji wa Maandiko katika kipindi cha hatamu za upapa ulikuwa umetabiriwa na manabii; na
Mfunuaji wa kitabu cha Ufunuo anasonda kidole kuelekea matokeo ya kutisha ambayo yangetokea hasa
kwa nchi ya Ufaransa kutokana na utawala wa yule “mtu wa kuasi”.
Malaika wa Bwana alisema: “Nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini na miwili. Nami
nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali
wamevikwa magunia…. Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu
atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua. Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu,
uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wao aliposulibishwa…. Nao wakaao juu
ya nchi watafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii
hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi. Na baada ya siku hizo tatu na nusu, roho ya uhai
itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu
waliowatazama.” Ufunuo 11:2-11.
Vipindi vilivyotajwa hapa -“miezi arobaini na miwili,” na “siku elfu na mia mbili na sitini” – ni kitu kile
kile, vyote kwa pamoja vinawakilisha muda ambao kanisa la Kristo lilikuwa lipate mateso kutoka Roma.
Miaka 1260 ya upapa kushika hatamu ilianza mwaka 538 B.K., na kwa hiyo ingekoma mwaka wa 1798. 268
Wakati huo jeshi la Ufaransa liliingia Roma na kumchukua papa kama mateka, na alikufa akiwa
kifungoni. Ingawa papa mpya aliteuliwa muda mfupi baadaye, msonge wa upapa haujapata uwezo wa
kuwa na nguvu kama ulizokuwa nazo kabla ya hapo.

267
Maelezo ya nyongeza yametolewa mwishoni
268
Maelezo ya nyongeza yametolewa mwishoni
154
Mateso ya kanisa hayakuendelea mfululizo kwa kipindi chote cha miaka 1260. Mungu kwa rehema zake
kwa watu wake alikifupiza kipindi kile cha moto wa majaribu. Katika kutabiri kuhusu (267) “dhiki kuu”
ambayo ingeliangukia kanisa lake, Mwokozi alisema: “Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka
mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo.” Mathayo 24:22. Kupitia ushawishi wa
Matengenezo, mateso yalifika mwisho kabla ya mwaka 1798.
Kwa habari ya mashahidi wale wawili, nabii huyo anatangaza zaidi akisema: “Hao ndio ile mizeituni
miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za Bwana wa nchi.” “Neno lako,” alisema Mtunga Zaburi,
“ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu.” Ufunuo 11:4; Zaburi 119:105. Mashahidi wawili
wanawakilisha Maandiko ya Agano la Kale na Agano Jipya. Yote mawili ni ushuhuda muhimu kwa ajili ya
chimbuko na umilele wa sheria ya Mungu. Yote mawili ni mashahidi pia wa mpango wa wokovu. Mifano,
dhabihu, na unabii wa Agano la Kale husonda kidole kwa Mwokozi ajaye. Injili na nyaraka za Agano
Jipya husimulia habari za Mwokozi aliyekuja kwa jinsi ile ile kabisa kama ilivyotabiriwa katika mifano na
unabii ule.
“Nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia.” Katika sehemu kubwa
ya kipindi hiki, mashahidi wa Mungu waliendelea kubaki katika hali ya kufichwa-fichwa tu. Mamlaka ya
kipapa ilijitahidi sana kulificha neno la kweli mbali na watu, na iliweka mbele yao mashahidi wa uongo
ili kuupinga ushuhuda wa lile neno. 269 Biblia ilipopigwa marufuku na mamlaka za kidini na za kiserikali;
wakati ushuhuda wake ulipopotoshwa, na kufanywa kwa juhudi za kila namna ambazo wanadamu na
mashetani waliweza kubuni ili kuyageuza mawazo ya watu mbali na hiyo; wakati ambapo wale
waliothubutu kuzihubiri kweli zake takatifu waliwindwa, wakasalitiwa, kuteswa vibaya, kuzikwa katika
seli ndogo za magereza ya chini ya ardhi, wakiuawa kifo cha wafia-dini kwa ajili ya imani yao, au
kulazimika kukimbilia kwenye ngome zile za milimani, na kwenye mashimo na mapango ya nchi – hapo
mashahidi waaminifu walitoa unabii wao hali wamevikwa magunia. Lakini waliendelea na ushuhuda wao
katika kipindi chote cha miaka 1260. Katika nyakati hizi za giza kubwa walikuwepo watu waaminifu
waliolipenda neno la Mungu na walikuwa na wivu kwa heshima ya Mungu. Watumishi hawa watiifu (268)
walipewa hekima, uwezo, na mamlaka ya kuitangaza kweli yake katika kipindi chote.
“Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka
kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa.” Ufunuo 11:5. Haiwezekani watu walikanyage neno la
Mungu chini ya miguu yao bila kuogopa. Maana ya hukumu hii ya kuogofya imefafanuliwa katika sura ya
kufungia ya kitabu cha Ufunuo: “Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, mtu
ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Na Mtu ye
yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika
ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.”
Ufunuo 22:18,19.
Hayo ndiyo maonyo ambayo Mungu ametoa ili kuwalinda watu wasibadili kwa njia yoyote kile
alichokifunua au kuamru. Hukumu hizi nzito zinawahusu wale wote ambao kwa mvuto wao
wanawaongoza watu kuichukulia kwa wepesi sheria ya Mungu. Lazima ziwasababishie kuogopa na
kutetemeka wale wanaotangaza kwa mzaha kwamba tukitii au kutotii sheria ya Mungu ni jambo lisilo na
madhara makubwa. Wale wote wanaoyatukuza maoni yao wenyewe zaidi ya mafunuo ya Mungu, wale
wote ambao wangegeuza maana iliyo wazi ya Maandiko ili kukidhi matakwa yao wenyewe, au kwa
kutafuta kuafikiana na ulimwengu, wanajitwisha jukumu la kuogopesha. Neno hilo lililoandikwa, sheria

269
Maelezo ya nyongeza yametolewa mwishoni

155
ya Mungu, vitaipima tabia ya kila mtu na kuwahukumu wote ambao kipimo hiki kisichokosea kamwe
kitawatangaza kuwa wamepungua.
“Hata watakapomaliza ushuhuda wao.” Kipindi kile ambacho wale mashahidi wawili wangetoa unabii
wao hali wamevikwa magunia kilikwisha mwaka wa 1798. Walipokuwa wanakaribia kumaliza kazi yao
kwa siri, vita ilikuwa ifanywe dhidi yao ikiletwa na mamlaka inayowakilishwa kama “mnyama atokaye
katika kuzimu.” Katika mengi ya mataifa ya Ulaya mamlaka zilizotawala kanisani na serikalini kwa karne
kadhaa zilikuwa zinaongozwa na Shetani kupitia kwa (269) njia ya upapa. Lakini hapa unaletwa
mwonekano mpya wa nguvu za kishetani.
Ilikuwa ni sera ya Roma, chini ya madai yake kwamba ilikuwa inaiheshimu Biblia, kuifungia katika lugha
isiyojulikana na ikiwa imefichwa mbali na watu. Chini ya utawala wake mashahidi wale walitoa unabii
wao “hali wamevikwa magunia.” Lakini mamlaka nyingine - mnyama toka kuzimu – ilikuwa iinuke na
kufanya vita ya wazi na dhahiri dhidi ya neno la Mungu.
“Mji ule mkuu” ambao katika njia zake mashahidi wale wanauawa, na ambamo miili yao iliyokufa
inakaa, ni Misri “kiroho.” Kati ya mataifa yote yaliyosimuliwa katika historia ya Biblia, Misri ilikana
kuwako kwa Mungu aliye hai kwa nguvu nyingi na kuzipinga amri zake. Hakuna mfalme yeyote aliyediriki
kufanya maasi ya waziwazi na kwa ujeuri dhidi ya mamlaka ya Mbinguni kama alivyofanya mfalme wa
Misri. Ujumbe ulipoletwa na Musa kwake, katika jina la Bwana, Farao kwa kiburi alijibu: “BWANA ni
nani, hata niisikilize sauti yake, na kuwapa Israeli ruhusa waende zao? Mimi simjui BWANA, wala
sitawapa Israeli ruhusa waende zao.” Kutoka 5:2. Huo ni ukafiri, na taifa linalowakilishwa na Misri
lingeweza kutoa sauti ya madai yanayofanana na haya na kukana matakwa ya Mungu aliye hai, tena
lingeonyesha roho hiyo ya kutokuamini na maasi. “Mji ule mkuu” pia unalinganishwa na Sodoma
“kiroho.” Ufisadi wa Sodoma kwa kuvunja sheria ya Mungu ulionekana hasa katika uasherati. Na dhambi
hiyo pia ingekuwa ni tabia iliyokithiri ya taifa lile ambalo lingetimiza maelezo ya andiko hilo.
Kwa mujibu wa maneno ya nabii huyo, kitambo kidogo kabla ya mwaka wa 1798 mamlaka fulani ya
kishetani ingejitokeza na kufanya vita dhidi ya Biblia. Na katika sehemu ambamo ushuhuda wa wale
mashahidi wawili ungeweza kunyamazishwa hivyo, kungejionyesha ukafiri kama ule wa Farao na ufisadi
wa Sodoma.
Unabii huu ulipata ulimilifu wake mkubwa sana na kwa usahihi mkubwa katika historia ya Ufaransa.
Wakati wa Mapinduzi, mwaka 1793, “ulimwengu, kwa mara ya kwanza, ulisikia kusanyiko la watu, (270)
waliozaliwa na kuelimishwa katika ustaarabu, wakijitwalia haki ya kutawala moja ya mataifa bora sana
ya Ulaya, wakipaza sauti zao zilizounganishwa pamoja na kuikana kweli ile takatifu sana ambayo roho
ya mtu huipokea, na kuikataa kwa kauli moja imani na ibada ya Mungu.” 270 “Ufaransa ndilo taifa pekee
ulimwenguni ambalo kumbukumbu zinazolihusu kuhusu haya bado zipo, kwamba kama taifa liliinua
mkono wake katika maasi ya wazi dhidi ya Mwasisi wa ulimwengu huu. Watu wenye kukufuru wengi,
makafiri wengi, wamekuwako, na bado wataendelea kuwako kule Uingereza, Ujerumani, Hispania, na
kwingineko; lakini Ufaransa linasimama peke yake katika historia ya ulimwengu huu kama taifa pekee
ambalo, kwa amri ya Bunge la Taifa, lilitamka kwamba hakuna Mungu, na watu wote waliokuwa katika
mji mkuu, na wengi sana penginepo, wanawake kwa wanaume, wakacheza dansi na kuimba kwa furaha
wakilikubali azimio hilo.” 271

270
Sir Walter Scott, Life of Napoleon, vol. la 1, chapter 17
271
Blackwood’s Magazine, Novemba, 1870
156
Ufaransa ilionyesha pia tabia za pekee zilizoitambulisha Sodoma. Wakati wa Mapinduzi ilijidhihirisha
hali ya ukosefu wa maadili na ufisadi inayofanana na ile iliyosababisha maangamizi ya miji ile ya nyanda
za tambarare. Na mwanahistoria anaeleza habari za kuwako kwa ukafiri na ufisadi katika nchi ya
Ufaransa kama ilivyotabiriwa katika unabii: “Iliyounganishwa sana na amri zilizoathiri dini, ilikuwa ni
amri iliyopunguza muungano wa ndoa - kifungo kile kitakatifu sana ambacho wanadamu wanaweza
kufanya, na ambacho kudumu kwake kunaelekeza kwa nguvu katika kuiimarisha jamii - na kuufanya
muungano huo kuwa mkataba wa mpito tu, ambao watu wowote wawili wanaweza kuufanya na kuacha
wanavyojisikia…. Ikiwa waovu walikuwa wamepania kuingia katika kazi ya kuvumbua njia ya kuharibu
kabisa kitu chochote kinachoheshimika, kizuri, au cha kudumu katika maisha ya nyumbani, na kupata
wakati huo huo uhakika kwamba madhara yale ambayo lilikuwa ni lengo lao kuyasababisha yangeweza
kuendelezwa toka kizazi hadi kizazi kingine, basi, wasingevumbua mpango unaofanikisha zaidi ya ule wa
kushusha hadhi ya ndoa…. Sophie Arnoult, (271) mwigizaji wa kike, maarufu kwa maneno ya busara
aliyosema, aliisema ndoa ile ya kiserikali kama “sakramenti ya uzinzi.'" 272
“Tena ni hapo Bwana wao aliposulibiwa.” Maelezo hayo ya unabii yalitimizwa pia na nchi ya Ufaransa.
Hakuna nchi nyingine yoyote ambayo ndani yake roho ya uadui dhidi ya Kristo ilijidhihirisha kwa namna
ya kustaajabisha sana. Hakuna nchi nyingine yoyote ambayo ndani yake kweli ilikuwa imekabiliana na
upinzani mkali na wa kikatili sana. Katika mateso yale ambayo Ufaransa ilikuwa imewashushia wale
walioikiri injili, ilikuwa imemsulibisha Kristo katika kiwiliwili cha wafuasi wake.
Karne baada ya karne damu ya watakatifu ilikuwa imemwagwa. Wakati Wawaldensi waliyatoa maisha
yao katika milima ya Piedmont kwa ajili ya “neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo,” ushuhuda
kama ule kwa ajili ya ile kweli ulikuwa umebebwa na ndugu zao, Waalbigensi wa Ufaransa. Katika siku
za Matengenezo wafuasi wake waliuawa kwa mateso ya kutisha sana. Wafalme na wakuu, wanawake
waliozaliwa katika koo za hali ya juu pamoja na vijana wanawake wazuri waliyafurahisha macho yao
kwa kuangalia shida za mateso ya wafia-dini mashahidi wa Yesu. Wahuguenot ambao walisifika kwa
busara, wakipigania haki zile ambazo moyo wa kibinadamu unazishikilia kama kitu kitakatifu mno,
walikuwa wamemwaga damu yao katika viwanja vya vita mahali pengi. Waprotestanti hawa
walihesabiwa kama maharamia wasio na sheria, gharama yao ilikuwa imehesabiwa kuwa ni vichwa vyao,
wakawindwa kama wanyama pori.
“Kanisa la Jangwani,” wazao wachache wa Wakristo wa zamani waliokuwa bado wamo katika nchi ya
Ufaransa katika karne ya kumi na nane, wakiwa wanajificha katika milima ya kusini, waliendelea
kuihifadhi imani ya baba zao. Walipojaribu kukutana usiku kando ya milima au kwenye bonde la upweke
nyikani, walifukuzwa na askari wapanda farasi na kuburutwa kwenda kutumika maisha yote kama
watumwa katika majahazi. Watu waliokuwa na maisha safi, waungwana, na wenye akili nyingi miongoni
mwa Wafaransa, walifungwa kwa minyororo, na kupata mateso mabaya, wakihesibiwa miongoni mwa
majambazi na wauaji. 273 Wale waliotendewa kwa huruma zaidi, walipigwa risasi, kama ambao hawana
silaha wala msaada wowote, walipiga magoti katika maombi. Mamia ya wanaume wenye umri mkubwa,
wanawake wasio na ulinzi, pamoja na watoto wasio na hatia yoyote waliachwa wakiwa wamekufa juu ya
nchi mahali pao pa kukutania. Katika kupita-pita kwao kando ya milima au msitu, walikokuwa
wamezoea kukusanyikia, lilikuwa jambo la kawaida kukuta “kila baada ya hatua nne, miili iliyokufa
kwenye majani, na maiti zilizokuwa zinaning’inia zikiwa zimetundikwa kwenye miti.” Nchi yao, ikiwa
imeharibiwa kwa upanga, shoka, na kuni za kuchomea watu moto, “iligeuzwa kuwa nyika kubwa ya

272
Scott, vol. 1, ch. 17
273
Angalia Wylie, book 22, chapter 6
157
giza.” “Ukatili ule ulitendeka … si katika zama za giza, bali katika kipindi adhimu cha Louis XIV. Wakati
huo sayansi ilikuwa imekuzwa, maandishi yalikuwa mengi, wajuzi wa mambo ya Mungu katika
mahakama na katika mji ule mkuu walikuwa ni wasomi sana na watu wenye ufasaha sana ambao
walijifanya kana kwamba wanazo tabia njema za upole na upendo.” 274
Lakini mbaya mno katika orodha ya uhalifu mbaya, uovu wa kutisha kuliko miongoni mwa matendo yote
maovu ya karne zote za uovu, ulikuwa ni ule wa Mauaji ya Kinyama ya Mtakatifu Bartholomayo. Bado
ulimwengu unayakumbuka na kutetemeka na kuchukizwa sana na mandhari za kuwashambulia kwa
ghafla watu wale, kitendo ambacho ni cha uovu na ukatili mkubwa. Mfalme wa Ufaransa, akiwa
ameombwa na mapadri pamoja na maaskofu wa Roma, alitoa kibali chake ili kazi ile ya kinyama ipate
kufanyika. Kengele, ikiendelea kugongwa usiku, ilikuwa ni ishara ya kuanza mauaji. Waprotestanti kwa
maelfu, wakiwa wamelala usingizi katika nyumba zao, wakiitumainia ahadi iliyotolewa kwa heshima ya
mfalme, waliburutwa nje bila kupewa onyo lolote na kuuawa kwa njia ya kikatili sana.
Kama vile Kristo alivyokuwa kiongozi asiyeonekana wa watu wake waliokuwa wanatoka utumwani Misri,
ndivyo Shetani alivyokuwa kiongozi asiyeonekana wa raia zake wale waliofanya kazi hii ya kutisha mno
ya kuzidisha idadi ya wafia-dini. Kwa siku saba mauaji yale ya kinyama yaliendelea mjini Paris, katika
siku zake tatu za kwanza yakifanywa kwa ghadhabu kali mno isiyofikirika. Wala hayakuwa mjini mle
peke yake, bali kwa amri maalum ya mfalme yalienea katika majimbo na miji yote walikokuwa
Waprotestanti. Hawakuheshimu umri wa mtu wala jinsia yake. Hakuachwa mtoto mchanga asiye na
hatia wala mzee mwenye mvi. Muungwana na mkulima, mzee na kijana, mama na mtoto, walikatwa-
katwa pamoja. Katika Ufaransa yote chinja-chinja iliendelea kwa miezi miwili. Watu elfu sabini
miongoni mwa maua yale bora ya taifa waliangamizwa.
“Habari za mauaji yale zilipofika Roma, (273) shangwe kubwa ililipuka miongoni mwa mapadri na
maaskofu. Kadinali Lorraine alimzawadia mleta habari zile fedha zipatazo crown elfu moja; mizinga ya
Mtakatifu Angelo ikaunguruma kutoa heshima ya furaha; na kengele zikalia kutoka kwenye kila mnara;
mioto mikubwa ya kusherehekea tukio lile ikawashwa na kuugeuza usiku kuwa mchana; na Gregori XIII,
akisindikizwa na makadinali na wakuu wengine wa kanisa, akafanya maandamano marefu kwenda
kwenye Kanisa la Mtakatifu Louis, ambako kadinali wa Loreni aliimba wimbo wa Te Deum…. Medali
ikapigiliwa ukutani kuwa ukumbusho wa mauaji yale ya kinyama, na ndani ya Vatikani bado kuna
sanamu tatu za Vasari ukutani, zinazoelezea kuhusu shambulio la manowari, mfalme katika mashauri
akipanga kuhusu mauaji, na mauaji ya kinyama yenyewe. Gregory alimtumia Charles Waridi la Dhahabu;
na miezi minne baada ya mauaji yale ya kinyama,… alisikiliza na kupendezwa sana na hotuba
iliyotolewa na padri mmoja wa Kifaransa,… ambaye aliongelea habari za ‘siku ile iliyojaa furaha nyingi
na nderemo, wakati baba mtakatifu sana alipozipokea habari zile, na kwenda kwa hali ya kicho kutoa
shukrani kwa Mungu na kwa Mtakatifu Louis.’” 275
Roho ile ile iliyosukuma Mauaji makuu ya Mtakatifu Bartholomew ndiyo iliongoza pia katika matukio ya
Mapinduzi. Yesu Kristo alitangazwa kuwa laghai, na kelele zilizopigwa na mkusanyiko ule wa makafiri
wa Kifaransa zilikuwa: “Mponde Fidhuli” wakimaanisha Kristo. Makufuru yale yaliyofanywa kwa
ushupavu dhidi ya Mbingu na uovu wa kuchukiza sana, vilienda sambamba, na watu waovu kupindukia
miongoni mwa wanadamu, watu walioachwa na kuwa viongozi waliokubuhu kwa ukatili, walitukuzwa

274
Ibid., book 22, chapter 7
275
Henry White, The Massacre of St. Bartholomew, chapter 14, aya ya 34

158
zaidi. Katika mambo haya yote, heshima ya juu ilitolewa kwa Shetani; wakati Kristo, katika sifa zake za
ukweli, usafi wa maisha, na upendo usio na ubinafsi, alisulibishwa.
“Yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao naye atawashinda na kuwaua.” Mamlaka ya
kikafiri iliyoitawala Ufaransa katika kipindi cha Mapinduzi na Utawala wa Kitisho, ilifanya vita ile dhidi
ya Mungu na neno lake takatifu kwa namna ambayo ulimwengu haujapata kushuhudia. Ibada ya Mungu
ilipigwa marufuku kwa amri ya Bunge la taifa. Biblia zilikusanywa na kuchomwa moto hadharani na
kuonyesha dharau kubwa dhidi yake kwa kila njia iliyowezekana. Sheria ya Mungu (274) ilikanyagwa
chini. Mambo yaliyowekwa na Biblia ili yatendwe yakapigwa marufuku. Siku ya mapumziko ya kila juma
ikawekwa kando na mahali pake kila siku ya kumi ikatolewa ili ipate kutumika kwa karamu za burudani
na makufuru. Ubatizo na Ushirika Mtakatifu vilipigwa marufuku. Na matangazo yaliyowekwa katika
maeneo ya makaburi yalitangaza kwamba kifo ni usingizi wa milele.
Kumcha Bwana kulisemekana kuwa mbali mno na mwanzo wa hekima kiasi kwamba ilionekana kuwa ni
mwanzo wa upumbavu. Ibada zote za dini zilipigwa marufuku, isipokuwa ile ya uhuru na ya nchi ile.
“Askofu wa Paris aliyewekwa kikatiba aliletwa ili kufanya sehemu yake muhimu katika mchezo wa
dhihaka wa kifidhuli ulioigizwa mbele ya wawakilishi wa taifa…. Aliletwa akiwa katika maandamano
kamili ili kuja kutangaza mbele ya Mkutano ule kwamba dini ile ambayo alikuwa amefundisha kwa
miaka mingi, kwa kila hali, ilikuwa ni ujanja-ujanja wa makasisi, ambao haukuwa na msingi wowote iwe
katika historia au katika ukweli mtakatifu. Alikana, kwa dhati na waziwazi, uwepo wa Mungu, ambaye
yeye mwenyewe alikuwa amewekwa wakfu kwa ajili ya ibada kwake, na kuahidi kuutumia muda wake
wote uliobaki kuheshimu uhuru, usawa, wema, na maadili. Kisha akaweka mezani nishani za uaskofu, na
kupokea kumbatio la kirafiki kutoka kwa rais wa Mkutano. Makasisi waasi kadhaa wakafuata mfano wa
askofu yule.” 276
“Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao,
kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi.” Ufaransa ile ya kikafiri ilikuwa
imeinyamazisha sauti ya onyo ya mashahidi wawili wa Mungu. Neno la kweli lililala likiwa limekufa
katika njia zake, na wale waliokuwa wanachukia makatazo na matakwa ya sheria ya Mungu
walishangilia. Watu wakamdharau hadharani Mfalme wa Mbinguni. Kama wenye dhambi wa zamani
walivyofanya, wakapiga makelele, wakisema: “Mungu ajuaje? Yako maarifa kwake Aliye Juu?” Zaburi
73:11.
Kwa ushupavu wa kukufuru karibu usioweza kusadikika kabisa, mmoja wa mapadre wale wa mpango
mpya wa utawala, alisema hivi: “Mungu, kama uko, basi, lipiza kisasi kwa ajili ya jina lako ambalo sifa
zake zimeharibiwa. Nakutangazia kutotii! Unaendelea kuwa kimya; hauthubutu kuzianzisha ngurumo
zako. Ni nani ambaye baada ya mambo haya (275) ataamini kwamba upo?” 277 Huu ni mwangwi wa madai
ya Farao kiasi gani yaliyosema: “BWANA ni nani, hata niisikilize sauti yake?” “Mimi simjui BWANA!”
“Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu.” Zaburi 14:1. Naye Mungu anatangaza hivi kuwahusu
wale wanaoipotosha kweli yake: “Maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote.” 2 Timotheo
3:9. Baada ya Ufaransa kuikataa katakata ibada ya Mungu aliye hai, “yeye Aliye juu, aliyetukuka,
akaaye milele,” ilichukua muda mfupi tu iliposhuka chini na kuabudu sanamu, kwa kumwabudu mungu
mke aliyeitwa Mungu wa Akili, katika umbile la mwanamke yule kahaba mkuu. Na haya yalitokea ndani
ya mkutano wa uwakilishi wa taifa lile, na yakifanywa na wenye mamlaka ya juu sana serikalini na
katika mamlaka za kutunga sheria! Mwanahistoria anasema: “Mojawapo ya sherehe za wakati huu wa

276
Scott, vol. la 1, chapter 12
277
Lacretelle, History, vol. 11, p. 309; in Sir Archibald Alison, History of Europe, vol. 1, ch. 10
159
wazimu inasimama bila kupinzangwa katika upuuzi wake na kufuru. Milango ya jumba la mkutano
liliachwa wazi ili kikundi cha wanamuziki kiingie, mbele yao wakiwa wamewatangulia wajumbe wa
manispaa, wakaingia kwa maandamano ya heshima, wakiimba wimbo wa kuusifu uhuru, na kumsindikiza
mwanamke yule aliyefunikwa kilemba, ambaye ndiye angekuwa lengo la ibada yao ya siku za usoni,
waliyemwita Mungu wa Akili. Akiwa ameletwa katikati, alivuliwa kilemba kile kwa madaha makubwa,
akawekwa upande wa kuume wa rais, wakati alipotambuliwa kwa ujumla kama msichana anayecheza
dansi katika michezo ya maonyesho…. Mkutano Mkuu wa Taifa la Ufaransa ukatoa heshima zake za ibada
kwa mwanamke yule, akiwa kama mwakilishi sahihi wa yule wa kuabudiwa.
“Onyesho hili la uovu na ujinga lilikuwa na mtindo fulani; na kule kusimikwa kwa Mungu wa Akili
kulirudiwa na kuigwa katika taifa lote, katika sehemu zile ambazo wakazi wake walitaka kujionyesha
kwamba wako sawasawa na vilele vya juu vya Mapinduzi.” 278
Msemaji katika kuzindua ile ibada ya Akili alisema: “Enyi Watunga sheria! Ushupavu wa dini umesalimu
amri kwa Akili. Macho ya msisimko huo yasiyoona vema hayakuweza kustahimili mng’ao mkali wa nuru
hii. Siku hii mkutano mkubwa umekusanyika chini ya matao hayo, ambayo, kwa mara yake ya kwanza,
yametoa mwangwi wa ukweli. Hapa (276) Wafaransa wamesherehekea ibada pekee ya kweli, - ile ya
Uhuru, ya Akili. Pale tumefanya matakwa yetu kwa usitawi wa nguvu za Jamhuri hii. Hapa tumezitupilia
mbali sanamu zisizokuwa na uhai na mahali pake tukapata Akili, kwa sanamu hii iliyo hai, kazi bora ya
asili.” 279
Mungu mke yule alipoletwa katika Mkutano ule, msemaji alimshika mkono, na kuugeukia Mkutano ule,
akisema: “Enyi wanadamu wenye maisha ya kufa, mkome kutetemeka mbele ya ngurumo za Mungu
zisizoweza kitu ambazo zimetengenezwa na hofu zenu wenyewe. Kuanzia sasa msitambue uungu
wowote isipokuwa huyu Akili. Naweka mbele yenu umbo lake zuri na safi sana; kama ni lazima mwe na
sanamu, basi, toeni sadaka zenu kwa sanamu kama hii peke yake…. Anguka chini mbele ya Baraza la
Uhuru mtukufu, ewe, Kilemba cha Akili!”
“Yule mungu mke, baada ya kubusiwa na rais, alipandishwa kwenye gari la kifahari, na kupitishwa
katikati ya kundi kubwa sana la watu, kwenda katika kanisa kuu la Notre Dame, kuchukua mahali pa
Mungu. Alipofika kule alipandishwa juu kwenye altare ndefu, na kupata ibada kutoka kwa wote
waliohudhuria mle.” 280
Jambo hili lilifuatwa, baada ya muda usiokuwa mrefu, na uchomaji wa Biblia hadharani. Katika tukio
moja “Chama Maarufu cha Makumbusho” kiliingia katika ukumbi wa Manispaa kikipiga makelele,
“Adumu Akili!” huku kikibeba juu ya mti masalia ya vitabu vilivyokuwa vimeungua nusu, miongoni
mwake vikiwemo vitabu vya sala za Warumi, vitabu vya misale vya Kirumi, na Agano la Kale na Jipya,
ambavyo “vimelipizwa kisasi katika moto ule mkubwa,” yule rais alisema, “kwa upumbavu wote
vilivyowafanya wanadamu kuutenda.” 281
Upapa ndio uliokuwa umeanzisha kazi ile iliyokuwa inatimizwa na ukafiri ule. Sera ya Roma ilikuwa
imesababisha hali zile zilizokuwapo, kijamii, kisiasa, na kidini, zilizokuwa zinaiharakisha Ufaransa
kwenda kwenye maangamizi yake. Waandishi, wakirejea katika mambo ya kuogofya ya Mapinduzi,

278
Scott, vol. la 1, chapter 17
279
M. A. Thiers, History of the French Revolution, vol. la 2, page wa 370, 371
280
Alison, vol. la 1, chapter 10
281
Journal of Paris, 1793, No. 318. Quoted in Buchez-Roux, Collection of Parliamentary History, vol. 30, pp. 200, 201
160
wanasema kwamba lawama za mabaya haya yaliyopitiliza zielekezwe kwa kiti cha enzi na kwa kanisa. 282
Kwa kufuata haki kabisa lawama zielekezwe kwa kanisa. Upapa ulikuwa umetia sumu (277) fikra za
wafalme dhidi ya Matengenezo, kwamba ni adui wa mfalme, jambo ambalo lingeweza kuhatarisha
amani na utulivu wa taifa. Wenye akili wa Roma ndio waliochochea ukatili wa kutisha na ukandamizaji
uliotoka kwenye kiti cha enzi.
Roho ya uhuru iliondoka pamoja na Biblia. Popote ilipopokewa injili, mawazo ya watu yaliamshwa.
Walianza kutupilia mbali pingu zilizowafunga na kuwafanya watumwa wa ujinga, uovu, na ushirikina.
Walianza kufikiri na kutenda kama watu. Wafalme waliliona jambo lile na kutetemeka kutokana na
udikteta wao.
Roma haikwenda polepole kuzichochea hofu zao zilizojaa wivu. Papa alisema akimwambia mtawala wa
Ufaransa aliyekuwa mahali pa mfalme mwaka 1525: “Ushapavu huu hautasababisha kuchanganyikiwa na
kuharibika kwa dini tu, bali falme zote, wakuu, sheria, na nafasi mbalimbali za utawala.” 283 Miaka
michache baadaye mwakilishi wa papa alimwonya mfalme, akisema: “Bwana, usidanganyike.
Waprotestanti watapindua utaratibu wote wa serikali na wa dini…. Kiti cha enzi kiko hatarini kama
ilivyo kwa altare…. Kuanzishwa kwa dini mpya ni lazima kuanzishe serikali mpya!” 284 Wanathiolojia nao
walitumia chuki ambayo watu walikuwa nayo kwa kutangaza kwamba mafundisho ya dini ya
Kiprotestanti “yanawashawishi watu kwenda mbali kwenye mambo mapya na upumbavu;
yanamnyang’anya mfalme upendo wa raia zake watiifu, na kuliangamiza kanisa pamoja na serikali.”
Hivyo ndivyo Roma ilivyofanikiwa kuipanga Ufaransa kusimama kinyume na Matengenezo. “Ilikuwa ni
kwa lengo la kukitegemeza kiti cha enzi, kuwalinda wakuu wenye vyeo, na kudumisha sheria
zilizokuwapo, kwamba upanga ule wa mateso ulichomolewa kutoka katika ala yake kwa mara ya kwanza
kule Ufaransa.” 285
Watawala wa nchi waliona mbele kidogo tu matokeo ya sera ile mbaya. Mafundisho yale ya Biblia
yangekuwa yamepandikiza katika akili na mioyo ya watu kanuni za kutenda haki, kiasi, ukweli, usawa,
na ukarimu, ambazo ndizo hasa zilizo msingi wa usitawi wa taifa lo lote. “Haki huinua taifa.” Kwa njia
hiyo “kiti cha enzi huthibitika” Mithali 14:34; 16:12.
(278) “Na kazi ya haki itakuwa amani;” na matokeo yatakuwa “ni utulivu na matumaini daima.” Isaya
32:17. Yule anayeitii sheria ya Mungu, ataziheshimu na kuzitii kweli kweli sheria za nchi yake. Yule
anayemcha Mungu atamheshimu mfalme katika utumiaji wa mamlaka yake yote yaliyo ya haki na halali.
Lakini Ufaransa isiyo na furaha, ikaipiga marufuku Biblia na kuwafukuza nchini wafuasi wake. Karne
baada ya karne, watu wanaofuata kanuni na wenye msimamo thabiti, yaani, watu wenye akili sana na
nguvu za kimaadili, waliokuwa na ujasiri wa kuikiri imani yao na kuwa na imani ya kustahimili mateso
kwa ajili ya ile kweli - kwa karne nyingi watu hawa walifanya kazi za sulubu wakiwa watumwa katika
majahazi ya matanga, waliangamizwa kwa kuchomwa moto kwenye nguzo, au kuozea katika seli za
magereza yaliyokuwa chini ya ardhi. Maelfu kwa maelfu walipata usalama wao kwa kukimbia; na hali ile
iliendelea kwa miaka mia mbili na hamsini baada ya kuanzishwa kwa Matengenezo.
Ni kwa uchache sana katika kipindi kile kirefu kupata kizazi cha Wafaransa ambacho hakikushuhudia
wafuasi wa injili wakikimbia mbele ya mtesaji mwenye ghadhabu, wakiondoka na utaalam, ufundi, bidii

282
Maelezo ya nyongeza yametolewa mwishoni
283
G. de Felice, History of the Protestants of France, book 1, chapter 2, aya ya 8
284
D’Aubigne, History of the Reformation in Europe in the Time of Calvin, book 2, chapter 36
285
Wylie, book 13, chapter 4
161
ya kazi, utaratibu, ambavyo, kama kawaida, waliwapita wote, wakaenda kuzitajirisha nchi nyingine
walikopata kimbilio. Na kwa uwiano ule walionufaisha kwa vipaji vyao nchi zile walizokimbilia, ndivyo
walivyopunguza manufaa katika nchi yao. Ikiwa mambo yote yale yaliyofukuziwa mbali yangekuwa
yamebaki katika nchi ya Ufaransa; ikiwa, katika kipindi kile cha miaka mia tatu, ujuzi wa kazi za
wakimbizi wale ungetumika katika kuilima ardhi ya nchi hii; ikiwa, katika miaka ile mia tatu, ufundi
wao wa sanaa ungeendeleza mbele utengenezaji wa vitu viwandani; ikiwa, katika miaka ile mia tatu,
kipaji chao cha pekee cha ubunifu na uwezo wao wa uchambuzi ungekuwa unaboresha fasihi yake na
kuikuza sayansi yake; ikiwa hekima yao ingekuwa inaongoza mashauri yao, ushujaa wao ukitumika
katika kupigana vita zao, ufahamu wao wa mambo ya haki ukitumika katika kutengeneza sheria zao, na
dini ya Biblia ikiitia nguvu akili na kuiongoza dhamiri ya watu wake, ni utukufu ulioje ambao ungeifunika
nchi ya Ufaransa leo! Ni kwa kiasi gani ingekuwa nchi kuu, tajiri, na ya furaha - kielelezo cha kuigwa -
kwa mataifa yote!
(279) “Lakini ushupavu wa upofu usio na uvumilivu ulimfukuza kutoka katika ardhi yake kila mwalimu
aliyewafundisha watu maisha safi, kila mtetezi wa utaratibu, kila mlinzi mwaminifu wa kiti cha enzi;
uliwaambia maneno haya watu wale ambao wangekuwa wameifanya nchi yao kuwa na ‘sifa na utukufu’
katika ulimwengu huu, Chagueni kimoja mnachotaka, kuchomwa moto kwenye nguzo au kuwa wakimbizi
katika nchi nyingine. Hatimaye maangamizi ya taifa lile yakakamilika; haikubaki tena dhamiri zaidi ili
kuishughulikia; hapakuwa na dini zaidi ya kuweza kuburuta wafuasi wake kuwapeleka kwenye nguzo ya
kuchomea moto; hapakusalia wazalendo zaidi wa kufukuzia mbali katika nchi zingine.” 286 Na Mapinduzi
yale, pamoja na vitisho vyake vyote, yalikuwa ndiyo matokeo yake mabaya.
“Kukimbia kwa wale Wahuguenot kuliendana na kushuka kukubwa kulikoikalia nchi ya Ufaransa. Miji
yenye viwanda iliyokuwa inasitawi ilipooza; maeneo yenye rutuba nyingi yaligeuka na kuwa nyika;
kudumaa kwa akili na mmomonyoko wa maadili vilifuata kipindi kile cha maendeleo makubwa yasiyo ya
kawaida. Mji wa Paris ukawa nyumba kubwa ya ombaomba, inakadiriwa kwamba, wakati ule wa kutokea
kwa Mapinduzi, maskini mia mbili elfu walikuwa wanaomba msaada toka kwa mfalme. Majesuit peke
yao ndio walionawiri katika taifa lile lililokuwa linaendelea kuharibika, nao walitawala kwa
ukandamizaji wa kutisha, makanisani na shuleni, magerezani na katika majahazi.”
Injili ingeiletea Ufaransa suluhisho la matatizo yake ya kisiasa na kijamii, ambayo yalifunika ujuzi wa
mapadri na maaskofu wake, mfalme wake, na watunga sheria wake, na hatimaye kulitumbukiza taifa
lile katika maasi yale na maangamizi. Lakini chini ya utawala wa Roma watu walikuwa wamepoteza
mafundisho ya Mwokozi yenye mibaraka juu ya kujitoa mhanga na kuwa na upendo usio na ubinafsi.
Walikuwa wamepotoshwa na kwenda mbali na roho ya kujinyima kwa ajili ya faida ya wengine. Matajiri
hawakupata karipio lolote kwa kuwakandamiza maskini, maskini hawakupata msaada wowote kwa
utumishi wao na kunyanyaswa. Ubinafsi wa wenye mali na wenye mamlaka ulizidi kukua wazi zaidi na
kuwa wa ukandamizaji zaidi. Kwa karne nyingi uchoyo na ufisadi wa mabwana ulikuwa na matokeo ya
kuwadhulumu vibaya sana wakulima wadogo kwa kuwatoza ushuru mkubwa kwa nguvu. Matajiri
waliwaonea maskini, na maskini waliwachukia matajiri.
Katika majimbo mengi mashamba makubwa yalimilikiwa na mabwana, na tabaka la vibarua walikuwa
watwana katika mashamba yale; majaliwa yao yalikuwa kwa (280) mabwana wale na walilazimishwa
kuwatii mabwana zao waliowapangisha mashamba yale, tena walilazimishwa kutekeleza madai yao
mengi. Mzigo wa kulisaidia kanisa na serikali uliliangukia tabaka la kati na la chini, ambao walitozwa

286
Wylie, book 13, chapter 20

162
malipo makubwa na mamlaka ya serikali na mamlaka ya viongozi wa kanisa. “Anasa za matajiri wale
ndizo zilizofikiriwa kuwa sheria kuu kuliko zote; wakulima na wakulima wadogo wangeweza kufa kwa
njaa, kulingana na vile wakandamizaji wao walivyoona…. Kila wakati wananchi wale walilazimika
kushughulikia tu mambo yale yaliyompendeza bwana wao. Maisha ya vibarua wale waliokuwa
wanashughulika na kilimo yalikuwa ni maisha ya kufanya kazi ngumu isiyokwisha na kubeba mzigo wa
umaskini usioisha; malalamiko yao, kama waliweza kudiriki kulalamika, yalishughulikiwa kwa dharau ya
kifidhuli. Mahakama za sheria siku zote ziliweza kumsikiliza tajiri kuliko yule mkulima mdogo; rushwa
ilikuwa inachukuliwa sana na mahakimu; mfumo wa utawala wa serikali ulikuwa na nguvu ndogo sana
kuweza kusimamia sheria mahali ambapo mfumo wa rushwa umekita mizizi. Kwa habari ya zile kodi za
watu wa chini zilizokamuliwa na matajiri walio wakuu wa serikali kwa upande mmoja, na viongozi wa
kanisa kwa upande mwingine, ile iliyoingia katika hazina ya mfalme au katika hazina ya kanisa haikufika
hata nusu; fedha iliyobaki ilitapanywa katika kujifurahisha nafsi zao kwa ufisadi. Na wale watu
waliowafanya wananchi kuwa maskini, wao wenyewe walikuwa wamesamehewa kulipa kodi, tena
walikuwa na haki kisheria au kwa desturi iliyohusu wateuliwa wa serikalini. Tabaka zilizopata upendeleo
ule zilifikia idadi ya watu mia moja na hamsini elfu, na kwa ajili ya kutosheleza mahitaji yao, mamilioni
ya wananchi waliadhibiwa kwa kuwafanya waishi maisha duni kabisa na yasiyo na matumaini.” 287
Makazi ya mfalme yalizama katika anasa na rushwa. Palikuwa na kuaminiana kidogo sana kati ya
wananchi na watawala. Hatua zote zilizochukuliwa na serikali zilitiliwa wasiwasi na kusemwa kwamba
zilikuwa za hila na uchoyo. Kwa zaidi ya nusu karne kabla ya muda wa Mapinduzi kiti cha enzi kilikuwa
kimekaliwa na Louis XV, ambaye, hata katika nyakati zile za uovu, alijulikana kama mfalme mzembe,
mpuuzi, na mwasherati. Wakiwa na watawala wale matajiri waliomomonyoka kimaadili na wakatili,
pamoja na tabaka ile ya chini ya wananchi waliofanywa kuwa maskini na wajinga, dola ilikuwa
imefilisika na kufedheheka, na wananchi wale wakiwa wamechukia sana, kiasi kwamba halikuhitajika
jicho la nabii kuweza kuona mbele maasi ya kutisha yaliyokuwa yanakuja. Kwa maonyo yaliyotolewa
kwake na washauri, mfalme alikuwa na tabia ya kujibu hivi: “Jitahidini (281) kuyafanya mambo yaende
mbele kwa kadiri mimi ninavyoishi; baada ya kufa kwangu, mambo na yawe kama yatakavyokuwa.”
Mabadiliko yalitakiwa yafanywe lakini ilikuwa ni bure. Maovu aliyaona, lakini hakuwa na ujasiri, wala
uwezo wo wote wa kuyakabili. Maangamizi yale yaliyoingojea Ufaransa, picha yake halisi ilijionyesha tu
katika jibu lake hili la kizembe na ubinafsi: “Baada yangu mimi, gharika!”
Ikifanyia kazi wivu wa mfalme na tabaka la watawala, Roma ilikuwa imewaongoza na kuwaweka
wananchi wale katika utumwa, ikijua fika ya kwamba kwa njia ile taifa lile lingeweza kudhoofika,
ikikusudia kwa njia ile kuwafunga watawala na wananchi ili wawe watumwa. Ikiwa na sera yake
inayoona mbali sana, ilitambua kwamba ili kuwafanya wananchi wale wawe watumwa, na kuleta
matokeo yaliyokusudiwa, ilikuwa ni lazima roho zao zifungwe pingu; na ya kwamba njia ya hakika ya
kuwazuia wasiweze kuponyoka katika utumwa wao ule ilikuwa ni kuwafanya wasiweze kuwa na uhuru.
La kutisha sana mara elfu kuliko mateso yale ya mwili, lilikuwa ni yale ya mmomonyoko wa maadili
yaliyokuwa yametokana na sera yake. Wakiwa wamenyimwa Biblia, na kuachwa kupewa mafundisho ya
ushupavu na uchoyo, wananchi wale walikuwa wamefunikwa na ujinga na ushirikina, na kuzama katika
maovu, hata wakawa hawafai kabisa kujitawala wenyewe.
Lakini matokeo ya mambo yote haya yalikuwa tofauti sana na kile ambacho Roma alikuwa amekusudia
kukipata. Badala ya kuwafanya watu wengi kutii mafundisho yake wakiwa kama vipofu, kazi yake ilileta
matokeo ya kutengeneza makafiri na wanamapinduzi. Waliudharau Uroma kama dini ya ujanja-ujanja

287
Maelezo ya nyongeza yametolewa mwisho

163
wa mapadri na maaskofu. Waliwaona watumishi wa kanisa kama chama kinachowakandamiza. Mungu
pekee waliyemjua alikuwa mungu wa Roma; mafundisho yake ndiyo iliyokuwa dini yao pekee. Waliona
uroho na ukatili wake kama tunda halali la Biblia, nao wasingeweza kuwa na jambo tofauti na hiyo.
Roma ilikuwa imewakilisha tabia ya Mungu vibaya na kupotosha matakwa yake, na sasa watu walikataa
vyote viwili, Biblia na Mwasisi wake. Ilikuwa imetaka watu wawe na imani ya upofu ya dogma, chini ya
masharti ya uongo kwamba ni maagizo ya Maandiko. Kama mwitikio wa hayo, Vltaire na washirika wake
walilitupa kando neno la Mungu na kueneza kila mahali sumu hiyo ya ukafiri. Roma ilikuwa
imewakanyaga-kanyaga watu chini ya kisigino chake cha chuma; na sasa watu, ukiwa umenyanyaswa na
kutendewa vibaya, katika kutaharuki kwao kutokana na (282) ukandamizaji huu, walivitupilia mbali
vizuizi vyote. Wakiwa wameudhika sana kutokana na madanganyo waliyofanyiwa ambayo walikuwa
wameusujudia kwa muda mrefu, waliukataa ukweli na uongo kwa pamoja; wakidhani kwamba kujiachia
wafanye lolote watakalo ndio uhuru, watumwa wale wa uovu wakashangilia katika hicho walichodhani
ni uhuru.
Katika ufunguzi wa Mapinduzi, kwa ukubali wa mfalme, wananchi walipewa nafasi kubwa ya uwakilishi
kuliko zile za mabwana na viongozi wa kanisa zikiunganishwa pamoja. Hivyo mizania ya mamlaka
ilikuwa mikononi mwao; lakini hawakuwa wameandaliwa kuitumia vizuri na kwa busara. Wakiwa na
hamu ya kurejesha hali nzuri badala ya maovu waliyotendewa, wakaazimu kufanya mageuzi ya jamii.
Umma huu wenye hasira, ambao akili zao zilikuwa zimejawa na mawazo machungu ya makosa
waliyokuwa wamekuwa nayo kwa muda mrefu, waliazimia kupindua hali ile ya maumivu yasiyovulika
iliyokuwepo na kulipiza kisasi dhidi ya wale waliodhaniwa kwamba ndio waasisi wa mateso yale
waliyokuwa wamepata. Wale waliokuwa wamekandamizwa walipindisha fundisho walilokuwa
wamejifunza chini ya ukandamizaji, wakageuka wao kuwa wakandamizaji wa wale waliokuwa
wamewakandamiza.
Ufaransa isiyo na furaha ikavuna kwa damu mavuno iliyokuwa imeyapanda. Matokeo ya kujisalimisha
kwake kwa utawala wa Roma yalikuwa ya kuogofya sana. Mahali ambapo Ufaransa, chini ya msukumo
wa Roma, ilisimamisha nguzo ya kwanza ya kuchomea watu moto wakati wa kuanza kwa Matengenezo,
ndipo Mapinduzi yalipoweka mashine yake ya kwanza ya kukata vichwa vya watu. Mahali pale pale
walipochomewa moto wafia-dini wa kwanza wa imani ya Kiprotestanti mnamo karne ya kumi na sita,
ndipo hapo wahanga wa kwanza walikatwa vichwa kwa mashine katika karne ya kumi na nane. Katika
kuizuia injili, ambayo ndiyo ingeiletea uponyaji, Ufaransa ikawa imeufungua mlango wa ukafiri na
maangamizi. Wakati makatazo ya sheria ya Mungu yalipotupwa kando, ikaonekana dhahiri ya kwamba
sheria za mwanadamu zilikuwa hazitoshi kuyazuia mawimbi ya hasira za wanadamu; na taifa lile
likaswagwa kuingia katika maasi na machafuko ya kisiasa. Vita dhidi ya Biblia ilizindua kipindi kile
kinachosimama katika historia ya ulimwengu kikiitwa “The Reign of Terror”, yaani utawala wa kitisho.
Amani na furaha vilitoweshwa majumbani na mioyoni mwa watu. Hakuna aliyekuwa salama. Aliyekuwa
mshindi leo alitiliwa mashaka, na kuhukumiwa kesho. Ukatili wa kutumia nguvu ulitawala kabisa bila
kuzuiwa.
(283) Mfalme, viongozi wa kanisa na wakuu walilazimika kusalimu amri kwa ukatili wa wananchi
waliokuwa wamekasirika na kuwa kama wenye wazimu. Kiu yao ya kutaka kulipiza kisasi iliamshwa tu na
kuuawa kwa mfalme; na wale waliokuwa wameamuru kuuawa kwake wakafuata mara kuelekea kwenye
jukwaa la kunyongea. Mauaji ya halaiki kwa wale walioshukiwa kuwa walikuwa wapinzani wa Mapinduzi
yalipangwa. Magereza yalikuwa na msongamano wa watu, wakati mmoja yakiwa na wafungwa zaidi ya
laki mbili. Miji mikubwa ya ufalme ule ilijaa matukio ya kutisha. Kundi moja la wanamapinduzi lilikuwa
likipingana na jingine, na nchi ya Ufaransa ikawa uwanja mpana kwa makundi ya watu kupambana,
164
wakitawaliwa na ghadhabu zao. “Mle Paris msukosuko mmoja ulifuata mwingine, na raia walikuwa
wamegawanyika katika vikundi vya fujo, ambavyo vilionekana kana kwamba vilikuwa havina kusudi
jingine ila kuangamizana vyenyewe kwa vyenyewe.” Na kuongezea juu ya msiba ule, taifa lile lilihusika
katika vita ya muda mrefu na ya maangamizi baina ya mataifa makubwa ya Ulaya. “Nchi ilikuwa karibu
ya kufilisika, na majeshi yalikuwa yakidai kwa nguvu malipo ya malimbikizo ya mishahara. Wakazi wa
Paris walikuwa wanakufa kwa njaa, majimbo yalikuwa yameachwa ukiwa kutokana na maharamia, na
ustaarabu ulikuwa karibu ya kutoweka kabisa kwa maasi yale na uhuru wa mtu kufanya atakalo.”
Roma isiyoachilia kitu sasa ilionja nguvu za kufisha za wale iliokuwa imewafundisha kufurahia vitendo
vya kumwaga damu. "Mfano wa mateso ambayo watumishi wa kanisa wa Ufaransa walikuwa
wameonyesha kwa vizazi vingi, sasa ulielekezwa kwao kwa nguvu. Majukwaa ya kunyongea yaligeuka
mekundu kwa damu ya makasisi. Mahandaki na magereza, yaliyojawa na Wahuguenot wakati fulani,
sasa yalikuwa yamejawa na watesaji wao. Wakiwa wamefungwa minyororo kwenye viti wakisumbuka na
makasia, viongozi wa Roman Catholic walipata uzoefu wa yale mabaya yote ambayo kanisa lao."
Watu wote pia walikuwa wamejifunza vizuri mafunzo ya ukatili na utesaji vile Roma ilivyokuwa
imewafundisha kwa bidii. Mwisho siku ya kupatilizwa ikawa imefika. Sasa si wafuasi wa Yesu waliotupwa
katika magereza ya chini ya ardhi na kuburutwa kwenda kuchomwa moto kwenye nguzo ya kuchomea
moto. Hawa walikuwa wameshaangamizwa zamani au kusukumwa na kukimbilia nchi za kigeni. Roma
sasa inakutana na nguvu ya kufisha ya wale iliokuwa amewafundisha kufurahia matendo ya kumwaga
damu. “Mfano wa mateso ambayo viongozi wa kanisa wa Ufaransa walikuwa wameonyesha kwa vizazi
vingi, sasa yaliwarudia wao kwa nguvu ivumayo. Majukwaa ya kunyongea yakawa mekundu kwa damu ya
wale mapadri. Majahazi ya utumwa na magereza, ambayo zamani yalijawa na msongamano wa
Wahuguenot sasa yakawa yamejaa watesi wao. Wakiwa wamefungwa minyororo kwenye viti na
kusumbuka na kazi ngumu ya makasia, viongozi wa kanisa la Roman Catholic walipata uzoefu wa taabu
ambazo kanisa lao lilikuwa limeyafanya kwa wazushi wanyenyekevu.” 288
(284) “Halafu zilikuja siku za wakati ilipotolewa sheria ya kishenzi kabisa kuliko zote na kutekelezwa na
mahakama ya kishenzi kabisa kuliko zote; wakati ambapo mtu hakuweza kuwasalimu jirani zake au
kusema sala zake … bila kuwa katika hatari ya kutenda kosa kubwa la kifo; wakati wapelelezi
walipotapakaa katika kila kona; wakati ambao mashine ya kukatia watu vichwa ilikuwa katika kazi
kubwa ya muda mrefu kila asubuhi; wakati magereza yalipokuwa yamesongamanisha wafungwa kama
vyumba vya meli ya watumwa; wakati mifereji ilipotiririsha damu kupeleka katika mto Seine…. Wakati
magari ya farasi yaliyojaa wahanga yalipokuwa yanawapeleka katika maangamizi kupitia katika mitaa ya
Paris. Mabalozi, ambao walikuwa wamepelekwa na kamati ya kifalme katika idara mbalimbali,
walifanya karamu kubwa kusherehekea ukatili ule mbaya sana uliokuwa haujapata kujulikana hata
katika mji ule. Kisu cha mashine ile ya kufisha kiliinuka na kushuka taratibu katika kazi yao ya kuchinja.
Misururu mirefu ya wafungwa ilifyekwa kwa risasi za marisau. Matundu yalitobolewa upande wa chini
wa mashua iliyojaa watu. Mji wa Lyons uligeuka jangwa. Kule Arras kwenyewe wafungwa wote
walinyimwa hata ule ukatili wenye huruma wa kuua kwa haraka. Njia yote ya mto Loire, toka Saumur
hadi baharini, makundi makubwa ya kunguru na tai walifanya karamu ya kula maiti zilizokuwa uchi,
zikiwa zimefungwa mbilimbili pamoja kwa kukumbatianishwa kwa namna ya kuchukiza sana. Hakukuwa
na huruma iliyoonyeshwa kwa jinsia wala umri. Idadi ya vijana wa kiume na wasichana wa miaka kumi
na saba waliouawa na serikali ile mbaya inaweza kufikiriwa kwa mamia. Watoto wadogo waliopokonywa
kutoka katika maziwa ya mama zao walirushwarushwa na kuachwa kudondoka kwenye ncha ya mkuki

288
Maelezo ya nyongeza yametolewa mwishoni

165
mmoja baada ya mwingine katika safu za jeshi lile la Wajacobin.” 289 Katika kipindi kile kifupi cha miaka
kumi, makundi ya wanadamu yaliangamizwa.
Yote haya yalitendeka kama Shetani alivyotaka. Haya ndiyo aliyokuwa akiyatafuta katika kazi yake ya
vizazi vingi. Sera yake ni udanganyifu toka mwanzo mpaka mwisho, na kusudi lake thabiti ni kuleta
maafa na taabu kwa wanadamu, kuharibu na kuchafua kazi ya uumbaji ya Mungu, kuharibu makusudi ya
fadhili na upendo wa Mungu, na kwa njia hiyo kusababisha huzuni mbinguni. Kisha kwa mbinu zake za
udanganyifu anawapofusha wanadamu, na kuwafanya waelekeze lawama ya kazi yake kwa Mungu, kama
vile misiba yote hii ilikuwa matokeo ya mpango wa Muumba. Vile vile, pindi (285) wale waliodhalilishwa
na kutendewa mabaya kwa nguvu zake za kikatili wanapopata uhuru, anawasukuma kuzidi kiasi na
kutenda mambo ya kikatili. Halafu picha hiyo ya uhuru uliopitiliza bila kizuizi hunyoshewa kidole na
watawala wa kidikteta na wakandamizaji wakionyesha kuwa ni kielelezo cha matokeo ya uhuru.
Wakati kosa linapogunduliwa katika vazi moja, Shetani analifunika tu kwa vazi jingine tofauti, na watu
wengi hulipokea kwa hamu nyingi sana kama vile walivyofanya mara ya kwanza. Pindi watu
walipogundua kwamba Uroma ulikuwa udanganyifu, na yeye asingeweza tena kupitia kwa wakala huyu
kuwaongoza katika kuivunja sheria ya Mungu, aliwaongoza kuichukulia dini yote kama udanganyifu, na
Biblia kama hadithi tu; nao, wakizitupilia mbali amri za Mungu, walijiingiza katika kufanya maovu bila
kujizuia.
Kosa la kufisha lililoleta msiba ule kwa wakazi wa Ufaransa lilikuwa ni lile la kuipuuzia kweli hii moja
kuu: kwamba uhuru wa kweli uko ndani ya mipaka ya makatazo ya sheria ya Mungu. “Laiti kama
ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi
ya bahari.” “Hapana amani kwa wabaya, asema BWANA.” “Bali kila anisikilizaye atakaa salama, naye
atatulia bila kuogopa mabaya.” Isaya 48:18,22; Mithali 1:33.
Wanaokana uwepo wa Mungu, makafiri, na waasi huipinga na kuishutumu sheria ya Mungu; lakini
matokeo ya mvuto wao huthibitisha kwamba usitawi wa mwanadamu unafungamana na utii wake kwa
amri za Mungu. Wale ambao hawataweza kulisoma fundisho hilo katika kitabu cha Mungu wanaelekezwa
kulisoma kutoka katika historia ya mataifa.
Wakati Shetani alipopindisha mambo kupitia kwa Kanisa la Roma kwa kuwafanya watu waende mbali na
utii, wakala wake huyu alikuwa amefichwa, na kazi yake ilikuwa imejificha sana kiasi kwamba hali ile
duni ya watu, pamoja na misiba iliyowapata haikuonekana kama ni matunda ya kuvunja sheria. Na
nguvu zake zilipunguzwa na utendaji wa Roho wa Mungu kiasi kwamba matunda ya makusudi yake
hayakufikia utimilifu wake wote. Watu hawakufuatilia matokeo tangu katika chanzo chake na
kuligundua chimbuko la misiba yao. Lakini katika (286) Mapinduzi yale sheria ya Mungu iliwekwa kando
na Baraza la Taifa waziwazi. Na katika kipindi kile cha Utawala wa Kitisho kilichofuata, utendaji wa
nadharia ya sababu na matokeo uliweza kuonwa na watu wote.
Wakati Ufaransa ilipomkataa Mungu hadharani na kuiweka kando Biblia, watu waovu na pepo wa giza
waliinuka katika kulifikia lengo walilokuwa wamelitamani kwa muda mrefu - ufalme ulio huru mbali na
makatazo ya sheria ya Mungu. Kwa sababu hukumu dhidi ya tendo baya haikutekelezwa upesi, mioyo ya
wana wa wanadamu ilithibitishwa ndani yao ili kutenda mabaya. Mhubiri 8:11. Lakini lazima uvunjaji wa
sheria adilifu na ya haki uwe na matokeo ya misiba na maangamizi. Ingawa haukupatilizwa kwa hukumu
mara moja, hata hivyo, uovu wa watu haukuwaepushia maangamizi. Karne nyingi za maasi na uhalifu

289
Maelezo ya nyongeza yametolewa mwishoni

166
zilikuwa zinaweka akiba ya ghadhabu kwa siku ile ya kisasi; na maovu yao yalipokijaza kikombe, wale
waliokuwa wanamdharau Mungu walitambua, wakiwa wamechelewa, kwamba ni jambo la kutisha
kuuchokoza uvumilivu wa Mungu. Roho wa Mungu azuiaye, ambaye anazuia uwezo wa kikatili wa
Shetani, alikuwa ameondolewa kwao kwa kiwango kikubwa, na yule ambaye furaha yake pekee ni
kufurahia taabu inayowapata wanadamu, aliruhusiwa kufanya mapenzi yake kwao. Wale waliokuwa
wamechagua kutumikia uasi, wakaachwa kuvuna matunda yake mpaka nchi ikajawa uhalifu wa kuogofya
mno kiasi cha kalamu kushindwa kuyaweka. Kutoka katika majimbo yaliyokuwa yamefanywa ukiwa na
miji ile iliyokuwa imeharibiwa vibaya, kilio cha kutisha kilisikika - kilio cha maumivu makali. Ufaransa
ilitikiswa vibaya sana kana kwamba ni kwa tetemeko la nchi. Dini, sheria, utulivu wa jamii, familia,
serikali, na kanisa - vyote hivi vilipata kipigo kwa mkono wa kikafiri uliokuwa umeinuliwa dhidi ya sheria
ya Mungu. Yule mwenye hekima alisema kweli: “Mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake.” “Ajapokuwa
mwenye dhambi amefanya maovu mara mia, akazidisha siku zake; lakini hata hivyo najua hakika ya
kwamba itakuwa heri kwao wamchao Mungu, wenye kicho mbele zake; walakini haitakuwa heri kwa
mwovu.” Mithali 11:5; Mhubiri 8:12,13. “Kwa kuwa walichukia maarifa, wala hawakuchagua kumcha
BWANA, kwa hiyo watakula matunda ya njia yao, watashiba mashauri yao wenyewe.” Mithali 1:29,31.
(287) Mashahidi waaminifu wa Mungu, waliouawa na mamalaka ile “toka katika kuzimu” yenye
makufuru, hawakupaswa kunyamaza kwa muda mrefu. “Baada ya siku hizo tatu u nusu, roho ya uhai
itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu
waliowatazama.” Ufunuo 11:11. Ilikuwa ni katika mwaka wa 1793 zilipopitishwa na Bunge la Ufaransa
sheria ambazo ziliifutilia mbali dini ya Kikristo na kuiweka Biblia kando. Miaka mitatu u nusu baadaye
azimio lililozitangua sheria zile lilipitishwa na Bunge lile lile likitoa ruhusa ya kuchukuliana na
Maandiko. Ulimwengu ulisimama mdomo wazi ukishangaa kuuona uovu ule mkubwa sana uliotokana na
kuyakataa Mausia Matakatifu, na wanadamu wakatambua umuhimu wa kuwa na imani katika Mungu na
katika neno lake kama msingi wa wema na uadilifu. Bwana asema: “Ni nani uliyemshutumu na
kumtukana? Umeinua sauti yako juu ya nani, na kuinua macho yako juu? Juu ya Mtakatifu wa Israeli,”
Isaya 37:23. “Basi, tazama, nitawajulisha, mkono wangu, na nguvu zangu; nao watajua ya kuwa, jina
langu ni YEHOVA.” Yeremia 16:21.
Kwa habari ya wale mashahidi wawili nabii anatangaza zaidi akisema: “Wakasikia sauti kuu kutoka
mbinguni ikiwaambia, Pandeni hata huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama.”
Ufunuo 11:12. Tangu Ufaransa ilipofanya vita dhidi ya mashahidi wale wawili wa Mungu ndipo
wameheshimiwa kuliko ilivyopata kutokea kabla. Mnamo mwaka 1804 chama cha Biblia kinachoitwa the
British and Foreign Bible Society kilianzishwa. Hiki kilifuatiwa na vyama vingine vya aina hiyo, vikiwa na
matawi mengi, katika bara la Ulaya. Katika mwaka wa 1816 chama cha Biblia kinachoitwa the American
Bible Society kilianzishwa. Chama cha British Society kilipoundwa, Biblia ilikuwa imechapishwa na
kutawanywa ikiwa katika lugha hamsini. Tangu hapo imetafsiriwa katika mamia mengi ya lugha na
lahaja. 290
Kwa miaka hamsini iliyotangulia kabla ya mwaka wa 1792, watu walijali kidogo kazi ya misheni katika
nchi za kigeni. Hakuna vyama vipya vilivyoundwa, tena palikuwa na makanisa machache tu yaliyofanya
(288) juhudi ya aina yoyote kueneza Ukristo katika nchi zile za kishenzi. Lakini kuelekea mwisho wa
karne ya kumi na nane badiliko kubwa lilitokea. Watu hawakuridhishwa na matokeo ya falsafa

290
Maelezo ya nyongeza yametolewa mwishoni
167
inayozingatia mantiki na wakatambua umuhimu wa kuwa na mafunuo ya Mungu na dini iliyo mpya.
Kuanzia wakati huu kazi ya misheni za nchi za kigeni ikakua sana kwa namna isivyopata kutokea. 291
Maendeleo katika kazi ya uchapaji yametoa msukumo kwa kazi ya kusambaza Biblia. Ongezeko la njia za
mawasiliano miongoni mwa nchi mbalimbali, kazi ya kuvibomoa vipingamizi vya zamani vya chuki na
kujibagua kitaifa; na papa wa Roma kupoteza mamlaka ya dunia vimefungua njia ya kuingia kwa neno la
Mungu. Kwa miaka fulani Biblia imeuzwa bila kuwapo kipingamizi chochote katika mitaa ya Roma, na
kwa sasa imepelekwa katika kila sehemu inayokaliwa na watu katika dunia hii.
Voltaire kafiri alipata kujigamba, akisema: “Nimechoka kusikia watu wakisema tena na tena kwamba
watu kumi na wawili walianzisha dini ya Kikristo. Nitawahakikishia kwamba mtu mmoja anatosha
kuipindua.” Vizazi vimepita tangu kufa kwa mtu huyo. Mamilioni wamejiunga katika vita ya kuipinga
Biblia. Lakini iko mbali na kuharibiwa, kiasi kwamba mahali ambapo zilikuwa mia mnamo wakati wa
Voltire, sasa ziko elfu kumi, naam, nakala mia moja elfu za kitabu cha Mungu. Katika maneno ya
Mwanamatengenezo wa awali kuhusu kanisa la Kikristo, alisema: “Biblia ni fuawe ambayo imezichakaza
nyundo nyingi.” Bwana asema: “Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi
utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa
BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.” Isaya 54:17.
“Neno la Mungu wetu litasimama milele.” “Maagizo yake yote ni amini. Yamethibitika milele na milele,
yamefanywa katika kweli na adili.” Isaya 40:8; Zaburi 111:7,8. Kitu chochote kilichojengwa juu ya
mamlaka ya mwanadamu kitapinduliwa; lakini kile kilicho na msingi wake juu ya mwamba wa neno la
Mungu lisilobadilika kitadumu milele.

291
Maelezo ya nyongeza yametolewa mwishoni
168
Sura ya 16
SAFARI YA MABABA KUVUKA NG’AMBO
Wanamatengenezo Waingereza, wakiyakataa mafundisho ya dini ya Kirumi, walikuwa bado wamebaki na
nyingi za desturi zake. Kwa hiyo ingawa mamlaka na itikadi ya Roma vilikataliwa, si chache miongoni
mwa desturi na taratibu zake za ibada zilizoingizwa katika ibada ya Kanisa la Uingereza. Ilidaiwa
kwamba mambo haya hayakuwa masuala ya dhamiri; kwamba, japo yalikuwa hayajaagizwa katika
Maandiko, na kwa hiyo hayakuwa ya muhimu sana, lakini yakiwa hayajakatazwa, haya na uovu ndani
yake. Kule kuyaadhimisha kulikuwa na mwelekeo wa kupunguza pengo lililotenganisha kati ya makanisa
ya Matengenezo na Roma, tena ilisemekana kwamba kuyafanya hayo kungewezesha Warumi kuikubali
imani ya Kiprotestanti.
Kwa wasiopenda mabadiliko na wanaopenda maridhiano, hoja hizo zilionekana kuleta suluhisho. Lakini
palikuwa na kundi jingine ambalo halikuonelea hivyo. Ukweli kwamba desturi zile “zilielekea kujenga
daraja juu ya bonde lililokuwa linatenganisha Roma na Matengenezo,” 292 ulikuwa kwa mawazo yao hoja
hitimishi dhidi ya kuendelea kuwa na desturi zile. Waliziona kama beji za utumwa ambao kutokana nao
walikuwa wamekombolewa na hawakuwa na nia ya kurudi huko. Waliwaza kwamba Mungu alikuwa
ameweka katika neno lake taratibu zinazoongoza ibada yake, na ya kwamba wanadamu hawana uhuru
wa kuongeza au kupunguza chochote katika hizo. Mwanzo wenyewe wa uasi mkuu ilikuwa ni habari ya
kutaka kuongeza mamlaka ya kanisa katika (290) mamlaka ya Mungu. Roma ilianza kwa kuamru
kufanyika mambo ambayo Mungu hakuwa amekataza, na ikaishia kukataza mambo ambayo Mungu
alikuwa ameamru waziwazi.
Wengi walitamani kwa dhati kurudi katika usafi na uarahisi ule uliokuwa tabia ya kanisa lile la kwanza.
Walizichukulia desturi nyingi zilizowekwa na Kanisa la Uingereza kama ibada ya sanamu, na katika
dhamiri zao hawakuungana katika ibada zake. Lakini kanisa, likiungwa mkono na mamlaka ya serikali,
lisingeruhusu kutokukubaliana na taratibu zake. Kuhudhuria katika ibada zake kulitakiwa kwa mujibu wa
sheria ya nchi, na mikusanyiko ya ibada isiyo na kibali ilipigwa marufuku, kwa adhabu ya kifungo,
kufukuzwa nchini, na kifo.
Mwanzoni mwa karne ya kumi na saba mfalme aliyekuwa amepanda kukalia kiti cha enzi cha Uingereza
alitangaza nia yake ya kuwafanya Wapuritan “kutii, au vinginevyo … kuwatesa hadi waikimbie nchi, au
kuwatenda mabaya zaidi.” 293 Wakiwindwa, wakiteswa, na kufungwa, hawakuweza kuona matumaini
yoyote ya siku njema za usoni, na wengi walishawishika kuamini kwamba kwa wale ambao wangetaka
kumtumikia Mungu kulingana na matashi ya dhamiri zao, “Uingereza ilikuwa inakoma daima kuwa
mahali pa kukaa.” 294 Baadhi yao hatimaye waliazimia kutafuta kimbilio Uholanzi. Walikabiliwa na shida,
hasara, na kifungo. Makusudi yao yaliwekewa vipingamizi, na walisalitiwa na kutiwa katika mikono ya
adui zao. Lakini hatimaye subira yao thabiti ilishinda, na wakapata hifadhi katika pwani rafiki za
Jamhuri ya Wadachi.

292
Martyn, volume 5, page 22
293
George Bancroft, History of the United States of America, sehemu ya 1, chapter 12, aya ya 6
294
J. G. Palfrey, History of New England, chapter 3, aya ya 43
169
Katika kuondoka kwao walikuwa wameacha nyumba zao, mali zao, na njia zao za kupatia riziki.
Walikuwa wageni katika nchi ya kigeni, wakiwa miongoni mwa watu wa lugha na desturi tofauti.
Walilazimika kuingia katika kazi mpya ambazo hazijapata kujaribiwa ili kujipatia mkate wao. Wanaume
wa umri wa kati, waliokuwa wameishi maisha yao wakiilima ardhi, iliwalazimu sasa kujifunza kazi za
ufundi. Lakini kwa moyo mkunjufu waliyakubali mazingira yale, na hawakupoteza wakati wao kwa uvivu
wala malalamiko. Ingawa mara nyingi waliteseka kwa umaskini, (291) walimshukuru Mungu kwa
mibaraka ile ambayo walikuwa wanaendelea kupewa na kupata furaha yao katika ushirika wa kiroho
pasipo kusumbuliwa. “Walijua kwamba walikuwa wasafiri, wala hawakutafuta mengi kutoka katika
mambo yale, bali waliyainua macho yao mbinguni, nchi yao waliyoipenda sana, na wakaituliza mioyo
yao.” 295
Katikati ya hali yao ya kuishi uhamishoni na katika shida, upendo na imani yao vilipata nguvu zaidi.
Walizitumainia ahadi za Bwana, naye hakuwapungukia katika wakati wa uhitaji. Malaika zake walikuwa
kando yao, kuwatia moyo na kuwasaidia. Na pindi mkono wa Mungu ulipoonekana kama unawaelekeza
ng’ambo ya bahari, kwenda katika nchi ambako wangeweza kuanzisha serikali yao, na kuwaachia
watoto wao urithi wa thamani wa uhuru wa dini, walisonga mbele, pasipo woga, katika njia
waliyoongozwa na mtoaji wa vyote.
Mungu alikuwa ameruhusu majaribu kuwajia watu wake ili kuwatayarisha kulitimiza kusudi lake jema
kwa ajili yao. Kanisa lilikuwa limeshushwa chini, kusudi lipate kutukuzwa. Mungu alikuwa anataka
kuuonyesha uweza wake kwa niaba ya kanisa, ili kuupa ulimwengu ushahidi mwingine kwamba
hatawaacha wale wanaomtumainia yeye. Alikuwa ametawala matukio kuifanya ghadhabu ya Shetani na
mipango ya hila ya watu waovu ipate kuendeleza utukufu wake na kuwaleta watu wake mahali pa
usalama. Mateso na kufukuzwa kutoka katika nchi yao vilikuwa vikifungua njia ya kuwafikisha kwenye
uhuru.
Walipolazimika kwanza kujitenga na Kanisa la Uingereza, Wapuritan wale walikuwa
wamejifungamanisha kwa agano, wakiwa watu wa Mungu walio huru, “kutembea pamoja katika njia
zote za Mungu ambazo zilifanywa kujulikana kwao au zingefanywa kujulikana kwao.” 296 Hapa ndipo
kulipokuwa na roho ya kweli ya matengenezo, kanuni muhimu ya Uprotestanti. Ni kwa kusudi hilo
kwamba Wasafiri wale waliondoka Uholanzi na kwenda kutafuta makao katika Ulimwengu Mpya. John
Robinson, mchungaji wao, ambaye kwa maongozi ya Mungu alizuiwa asiandamane nao, katika hotuba
yake ya kuagana na wakimbizi wale, alisema hivi:
“Ndugu, sasa tunatengana kwa muda, na Bwana anajua kama nitakuwa hai kuweza kuziona nyuso zenu
tena. Lakini kama Bwana amepanga hivyo au la, (292) nawaagiza, mbele za Mungu na mbele za malaika
zake wabarikiwa, ya kwamba mnifuate mimi kwa kiasi ambacho si zaidi ya vile nilivyomfuata Kristo.
Endapo Mungu atawafunulia jambo lolote kupitia kwa chombo chake kingine, iweni tayari kulipokea
kama vile mlivyokuwa tayari kuipokea kweli yoyote katika huduma yangu; maana nina uhakika kwamba
Bwana anayo kweli na nuru zaidi ambayo itaangaza toka katika neno lake takatifu.” 297
“Kwa upande wangu, siwezi kusikitika kiasi cha kutosha kuhusu hali ya makanisa ya matengenezo,
ambayo yamefika katika kipindi kimoja cha dini, na sasa hayawezi kwenda mbali zaidi kuliko pale
walipofika watumishi walioyaanzisha. Waluther hawawezi kuvutwa kwenda mbali zaidi ya pale alipoona

295
Bancroft, sehemu ya 1, chapter 12, aya ya 15
296
J. Brown, The Pilgrim Fathers, page wa 74
297
Martyn, vol. la 5, page wa 70
170
Luther;… na Wacalvin, mnaona, wanang’ang’ania kwa nguvu mahali pale walipoachwa na yule mtu
mkuu wa Mungu, ambaye alikuwa bado hajayaona mambo yote. Huu ni msiba mkubwa kiasi cha
kuombolezewa; maana, japokuwa wao walikuwa nuru zinazowaka na kuangaza katika wakati wao, bado
hawakupenya na kuingia katika mausia yote ya Mungu, lakini, kama wangekuwa wangali hai sasa,
wangekuwa tayari kuipokea nuru zaidi kama ile waliyopokea kwanza.” 298
“Likumbukeni agano lenu la kanisa, ambamo mlikubali kutembea katika njia zote za Bwana,
zilizofanywa au ambazo zitafanywa kujulikana miongoni mwenu. Ikumbukeni ahadi yenu na agano lenu
kwa Mungu na kwenu ninyi kwa ninyi, kuipokea nuru na kweli yoyote itakayojulishwa kwenu kutoka
katika neno lake lililoandikwa; lakini pamoja na hayo yote, jihadharini, nawasihi, kile mnachokipokea
kama kweli, kilinganisheni na kukipima na maandiko mengine ya ile kweli kabla ya kukikubali; kwa
maana haiwezekani kabisa kwamba ulimwengu wa Kikristo utoke hivi karibuni katika giza nene la
Mpinga Kristo, na ujuzi kamili kupatikana mara moja.” 299
Ilikuwa ni shauku ya kupata uhuru wa dhamiri ambayo iliwasukuma Wasafiri wale kukabiliana na hatari
za safari ndefu ya kuivuka bahari, kustahimili shida na hatari katika nyika, na kwa mibaraka ya Mungu
kuweka, katika pwani ya Amerika, msingi wa taifa lenye nguvu. Lakini wakiwa wanyofu wa moyo na
wacha Mungu (293), Wasafiri wale walikuwa bado hawaielewi vema kanuni kuu ya uhuru wa dini. Uhuru
ule waliojitolea mhanga kuupata kwa ajili yao, na wao vile vile hawakuwa tayari kuutoa kwa wengine.
“Ni wachache sana, hata miongoni mwa watu wenye fikra pevu na watu wa maadili wa karne ya kumi na
saba, waliokuwa na dhana sahihi juu ya kanuni ile kuu, iliyochipuka kutoka katika Agano Jipya,
ikimtambua Mungu kama mhukumu pekee wa imani ya mwanadamu.” 300 Fundisho kwamba Mungu
amelikabidhi kanisa haki ya kuidhibiti dhamiri ya mtu, pamoja na kuamua kuhusu kipi ni uzushi na
adhabu yake, ni moja ya makosa ya upapa yaliyokita mizizi kwa kina. Wakati Wanamatengenezo
walipoyakataa mafundisho ya imani ya Roma, hawakuwa huru kabisa mbali na roho yake ya kutoivumilia
imani nyingine. Giza nene ambamo, kwa muda wa vizazi vingi vya utawala wake, upapa ulikuwa
umeufunika Ulimwengu wa Kikristo, lilikuwa bado halijatoweshwa lote. Mmoja wa viongozi katika koloni
la Ghuba ya Massachusetts alisema: “Roho ya kuvumiliana kiimani ndiyo iliyoufanya ulimwengu kuwa
mpinga-kristo; wala kanisa halikupata madhara kamwe kwa kuwaadhibu wazushi.” 301 Utaratibu ule
ulitumiwa na wakoloni kwamba washiriki wa kanisa tu ndio wawe na sauti katika serikali ya kiraia. Aina
fulani ya kanisa la serikali ilijitokeza, na watu wote wakatakiwa kuchangia kuwategemeza watumishi wa
kanisa na mahakimu waliokuwa wamepewa mamlaka ya kuufutilia mbali uzushi. Hivyo mamlaka ya
serikali ikawa mikononi mwa kanisa. Haikuchukua muda mrefu kabla ya hatua hizi kuleta matokeo
yasiyoepukika - mateso.
Miaka kumi na moja baada ya kupandikiza koloni lile la kwanza, Roger Williams alikuja katika
Ulimwengu Mpya. Kama ilivyokuwa kwa Wasafiri wa awali alikuja kufurahia uhuru wa dini; lakini,
tofauti na wao, aliona - kile ambacho wachache mno mnamo wakati wake walikuwa wamepata kukiona
- kwamba uhuru ule ulikuwa ni haki kwa ajili ya wote isiyoondoleka, kwa imani yao iwayo yote. Alikuwa
mtafutaji mwenye bidii wa ile kweli, akiwa na mwelekeo wa Robinson kwamba haiwezekani nuru yote
toka katika neno la Mungu iwe imekwisha kupokewa. Williams “alikuwa mtu wa kwanza katika
Ulimwengu wa sasa wa Kikristo kuanzisha serikali ya kiraia juu ya msingi wa fundisho la uhuru wa

298
D. Neal, History of the Puritans, vol. la 1, page wa 269
299
Martyn, vol. la 5, uk. 70,71
300
Ibid., vol. la 5, uk. 297
301
Ibid., vol. la 5, uk. 335
171
dhamiri, usawa wa maoni mbele (294) ya sheria ya nchi..” 302 Alitangaza kwamba lilikuwa jukumu la
hakimu kukomesha uhalifu, lakini kamwe asiitawale dhamiri. “Umma au mahakimu wanaweza kuamua,”
alisema, “yampasayo mtu mmoja kwa mwingine, lakini wanapojaribu kumpangia mwanadamu
majukumu yake kwa Mungu, wanakuwa mahali pasipokuwa pao, na hakuwezi kuwa na usalama; maana
ni wazi kwamba kama hakimu anao uwezo, basi, anaweza kuamru namna moja ya maoni au imani leo na
namna nyingine kesho; kama ilivyopata kufanywa na wafalme na malkia mbalimbali kule Uingereza, na
mapapa na mabaraza mbalimbali katika Kanisa la Roma; hivyo imani hiyo ingekuwa rundo la
machafuko.” 303
Mahudhurio katika ibada ya kanisa lililoanzishwa yalikuwa ya lazima chini ya adhabu ya kutozwa faini au
kufungwa. “William aliipinga sheria; amri mbaya zaidi kuliko zote katika sheria za Kiingereza ilikuwa ile
ya kulazimisha mahudhurio katika kanisa la parokiani. Kuwalazimisha watu kuungana na watu wenye
itikadi ya imani tofauti na yake, aliona kuwa ni ukiukaji wa wazi wa haki zao za asili; kuwaburuta hadi
kwenye ibada watu wasio na dini na wasiopenda kwenda, ilionekana tu kama kutaka unafiki…. ‘Hakuna
mtu anayefungwa kuabudu kwa lazima, au,’ aliongeza, ‘kuwa na ibada kinyume cha ridhaa yake
mwenyewe.’ ‘Nini!’ wakasema kwa ghadhabu wapinzani wake, wakishangazwa na itikadi zake, na
kusema ‘mtendakazi hastahili kupata ujira wake?’ ‘Ndiyo,’ yeye alijibu, ‘toka kwa wale
wanaomwajiri.’” 304
Roger Williams aliheshimiwa na kupendwa kama mtumishi mwaminifu, mtu mwenye vipaji visivyokuwa
vya kawaida, mwenye msimamo usiotetereka na mwenye ukarimu wa kweli; lakini uthabiti wake wa
kukana haki ya mahakimu wa serikali kuwa na mamlaka juu ya kanisa, na madai yake ya kutaka kuwepo
uhuru wa dini, hayakuweza kuvumiliwa. Utekelezaji wa fundisho hili jipya, ilisisitizwa, ungeweza
“kupindua msingi wa taifa lile pamoja na serikali ya nchi.” 305 Alihukumiwa kuondoshwa katika makoloni
yale, na, hatimaye, kuepuka kutiwa mbaroni, alilazimika kukimbilia katika msitu mnene, katika hali ya
baridi kali na dhoruba za majira ya baridi.
“Kwa majuma kumi na manne,” anasema, “nilitoswa hasa katika msimu mchungu, nisijue maana ya
mkate wala.” (295) Lakini “kunguru walinilisha katika nyika,” na mara nyingi nilipata hifandhi katika
tundu la mti. 306 Hivyo aliendelea na kukimbia kwake kwa maumivu kupitia katika theluji na msitu
usiokuwa na njia, mpaka alipopata hifadhi katika kabila moja la Wahindi ambao aliweza kuwashawishi
na kupata huruma yao huku akitafuta kuwafundisha kweli za injili.
Hatimaye akijielekeza, baada ya miezi mingi ya kuhamahama na kutangatanga, katika pwani za Ghuba
ya Narragansett, pale aliweka msingi wa jimbo la kwanza miongoni mwa yale ya sasa ambalo kwa
maana kamili lilitambua haki ya uhuru wa dini. Kanuni ya msingi ya koloni la Roger Williams ilikuwa ni
“kwamba kila mtu awe na uhuru wa kumwabudu Mungu kulingana na nuru ya dhamiri yake
mwenyewe.” 307 Jimbo lake hili dogo, Kisiwa cha Rhode, lilikuja kuwa kimbilio la watu walioonewa, na
lilikua na kufanikiwa mpaka kanuni zake za msingi - uhuru wa serikali na uhuru wa dini - zikawa msingi
wa Jamhuri ya Amerika.

302
Bancroft, sehemu ya 1, chapter 15, aya ya 16
303
Martyn, vol. la 5, uk. 340
304
Bancroft, sehemu ya 1, chapter 15, aya ya 2
305
Ibid., pt. 1, ch. 15, par. 10
306
Martyn, vol. la 5, uk. 349,350
307
Ibid., vol. la 5, uk. 354
172
Katika hati ya zamani ambayo mababu zetu waliiweka kama sheria yao ya haki za binadamu - Azimio la
Uhuru – walisema hivi: “Tunazishikilia kweli hizi kuwa ni dhahiri, kwamba watu wote wameumbwa
sawa; kwamba wamepewa na Muumba wao haki fulani zisizoondosheka; kwamba miongoni mwa hizo ni
uhai, uhuru, na kutafuta furaha.” Na Katiba inatoa, kwa maneno yaliyo wazi kabisa kutokukiukika kwa
dhamiri: “Hakuna kipimo chochote cha kidini kitakachotakiwa kama sifa ya kuajiriwa katika kazi ya
umma katika nchi ya Marekani.” “Bunge la Marekani halitatunga sheria yoyote inayoheshimu kuanzishwa
kwa dini fulani, au itakayokataza kuendesha dini.”
“Waundaji wa Katiba ile walitambua kanuni ya daima kwamba uhusiano wa mwanadamu na Mungu wake
uko juu ya sheria za wanadamu, na ya kwamba haki zake za dhamiri haziwezi kuondolewa. Kutumia
hoja ya mantiki hakukuwa muhimu katika kuuweka ukweli huu; tunaujua katika vifua vyetu. Ni dhamiri
hiyo ambayo, kwa kutofautiana na amri za wanadamu, imewaweka wafia-dini wengi katika mateso na
ndimi za moto. Waliona kwamba wajibu wao kwa Mungu ulikuwa juu sana kuliko amri zilizowekwa na
wanadamu, na ya kwamba mwanadamu asingekuwa (296) na mamlaka juu ya dhamiri. Ni kanuni ya
kuzaliwa nayo ambayo hakuna kitu kinachoweza kuiondoa.” 308
Pindi habari zilipoenea katika nchi za Ulaya, kuhusu nchi ambayo ndani yake kila mtu anaweza
kufurahia matunda ya kazi yake na kuitii misukumo ya imani iliyo ndani ya dhamiri yake mwenyewe,
maelfu wakaelekea katika pwani za Ulimwengu Mpya. Makoloni yaliongezeka kwa kasi. Massachusetts,
kwa sheria maalum, ikawakaribisha bure na kuwasaidia, kwa gharama za serikali, Wakristo wa taifa
lolote ambao wangekimbia na kuvuka bahari ya Atlantiki ‘wakikwepa vita au njaa, au mateso kutoka
kwa watesi wao.’ Hivyo ndivyo wakimbizi na waliokandamizwa walivyopokewa, kwa sheria, kuwa
wageni katika nchi ile.” 309 Katika kipindi cha miaka ishirini tangu walipotia nanga mara ya kwanza pale
Plymouth, kiasi cha Wasafiri elfu nyingi walifanya makazi yao pale New England.
Ili kujipatia lengo walilolitafuta, “waliridhika kupata kipato kidogo cha kuwawezesha kuishi maisha kwa
kubana matumizi na kufanya kazi ngumu. Hawakutafuta kitu katika udongo isipokuwa matokeo ya
kawaida ya jasho lao. Hakuna njozi ya dhahabu iliyotupa kivuli cha kuwahadaa katika njia yao….
Walikuwa radhi na maendeleo ya serikali yao ya kijamii ya pole pole lakini ya hakika. Kwa uvumilivu
walistahimili umaskini wa nyika ile, wakiumwagilia mti wa uhuru kwa machozi yao, na kwa jasho la uso
wao, mpaka ulipootesha mzizi wake wa kina katika nchi ile.
Biblia ilishikiliwa kama msingi wa imani, chanzo cha hekima, na hati ya uhuru. Kanuni zake
zilifundishwa kwa bidii nyumbani, shuleni, na kanisani, na matunda yake yalionekana waziwazi katika
kubana matumizi, kuwa na akili, usafi wa maisha, na kiasi. Mtu angeweza kuishi katika makazi ya
Wapuritan kwa miaka mingi, “na asione mtu mlevi, au kusikia kiapo, au kukutana na mtu
ombaomba.” 310 Ilionekana wazi ya kwamba kanuni za Biblia ndizo kinga za hakika za ukuu wa taifa lo
lote. Makoloni yale dhaifu na yaliyokuwa yamejitenga mbali yakakua na kuwa shirikisho la majimbo
yenye nguvu, na ulimwengu ukaangalia kwa mshangao amani na usitawi wa “kanisa lisilokuwa na papa,
na serikali isiyokuwa na mfalme.”
Lakini idadi ya watu ilivyoendelea kuongezeka walivutwa kwenda (297) katika pwani zile za Amerika,
wakisukumwa na makusudi yaliyoachana sana na yale ya Wasafiri wa kwanza. Ingawa imani ile ya
kwanza pamoja na usafi wa maisha ilieneza mvuto wake wenye nguvu na wenye uwezo wa kubadilisha

308
Congressional documents (U.S.A.), serial No. 200, document No. 271
309
Martyn, vol. la 5, uk. 417
310
Bancroft, sehemu ya 1, chapter 19, aya ya 25

173
tabia kwa mapana, bado ushawishi wake ulipungua na kupungua, kadiri idadi ya wale waliokwenda
kutafuta manufaa ya kidunia tu ilivyozidi kuongezeka.
Utaratibu uliotumiwa na wakoloni wa kwanza wa kuwaruhusu washiriki wa kanisa tu kupiga kura au
kuajiriwa katika ofisi ya serikali ya kiraia, ulileta matokeo yenye madhara makubwa sana. Hatua hiyo
ilikuwa imekubaliwa kama njia ya kuhifadhi usafi wa taifa, lakini ikaleta ufisadi ndani ya kanisa. Kukiri
dini kukiwa ndilo sharti la kupewa haki ya kupiga kura kwa wote na kukalia cheo serikalini, wengi,
wakisukumwa tu na makusudi yao ya sera za kidunia, walijiunga na kanisa bila kuwa na badiliko la
moyo. Hivyo makanisa yale yakawa, kwa kiwango kikubwa, na watu ambao hawajaongoka; na hata
katika kazi ya huduma walikuwamo watu ambao si tu kwamba walishikilia mafundisho potofu, bali pia
walikuwa hawaujui uweza wa Roho Mtakatifu uwafanyao watu kuwa viumbe vipya. Hivyo yakaonekana
tena matokeo mabaya, ambayo yamekuwa yakishuhudiwa mara kwa mara katika historia ya kanisa
tangu siku zile za Constantine hadi wakati huu wa sasa, ya kujaribu kulijenga kanisa kwa msaada wa
serikali, ya kuomba msaada wa nguvu za dola kuiunga mkono injili ya yule ambaye alitangaza: “Ufalme
wangu sio wa ulimwengu huu.” Yohana 18:36. Muungano wa kanisa na serikali, hata uwe kwa kiwango
kidogo sana, wakati unaweza kuonekana kama unauleta ulimwengu karibu zaidi na kanisa, lakini kwa
kweli unalileta kanisa karibu zaidi na ulimwengu.
Kanuni kuu iliyotetewa vema kwa bidii na Robinson na Roger Williams, ya kwamba ukweli ni wa
kuendelea, kwamba Wakristo wawe tayari kuipokea nuru yote inayoweza kuangaza toka katika neno
takatifu la Mungu, ilikuwa imesahauliwa na wazao wao. Makanisa ya Kiprotestanti ya Amerika, - na yale
ya Ulaya pia - yaliyopendelewa mno kupokea mibaraka ya Matengenezo, yalishindwa kusonga mbele
katika njia ya Matengenezo. Ingawa watu wachache waaminifu walijitokeza, kwa nyakati tofauti
kutangaza ukweli mpya na kuyafichua makosa yaliyoshikiliwa kwa muda mrefu, watu walio wengi, kama
Wayahudi katika siku za Kristo au watu wa upapa mnamo wakati wa Luther, walitosheka kuamini vile
baba zao walivyokuwa (298) wameamini, na kuishi vile walivyokuwa wameishi wao. Kwa hiyo, dini
ikapotoka tena na kugeuka kuwa dini ya mazoea na desturi; na mafundisho potofu na ushirikina
ambavyo vingekuwa vimetupwa kando ikiwa kanisa lingekuwa limeendelea kutembea katika nuru ya
neno la Mungu, yakaendelea kushikiliwa na kuhifadhiwa. Hivyo roho ile iliyochochewa na Matengenezo
ikafa taratibu, mpaka kukawa na haja kubwa ya kufanya matengenezo ndani ya makanisa ya
Kiprotestanti kama ilivyokuwepo haja ya kufanya vile katika Kanisa la Roma wakati wa Luther. Kulikuwa
na hali kama ile ile ya kufanana na dunia na kuwa na usingizi mzito wa kiroho, hali kama ile ile ya
kuyaheshimu mawazo ya wanadamu, na ubadilishaji wa kuweka nadharia za wanadamu mahali pa neno
la Mungu.
Usambazaji mkubwa wa Biblia katika sehemu ya awali ya karne ya kumi na tisa, na nuru kubwa
iliyomlikwa hivyo ulimwenguni, hakukufuatiwa na ongezeko sawia la kuijua kweli iliyofunuliwa, au
kuiweka dini yao katika matendo. Shetani hakuweza, kama ilivyokuwa kwa vizazi vya kabla, kulizuia
neno la Mungu kuwafikia watu; lilikuwa limewekwa mahali ambapo wote wangeweza kulipata; lakini ili
kuendelea kulitimiza kusudi lake, aliwafanya wengi kulithamini kidogo tu. Watu walipuuza
kuyachunguza Maandiko, na hivyo waliendelea kuzikubali tafsiri za uongo, na kuyashikilia mafundisho
ambayo hayakuwa na msingi katika Biblia.
Kwa kuona juhudi zake za kuifutilia mbali ile kweli kwa kutumia mateso zimeshindwa, Shetani alitumia
tena mpango ule wa kufanya maridhiano ambao ulisababisha uasi mkuu na kuundwa kwa Kanisa la
Roma. Alikuwa amewashawishi Wakristo kuungana, si pamoja na wapagani kwa sasa, bali kuungana na
wale ambao, kwa kujielekeza katika mambo ya ulimwengu huu, walikuwa wamedhihirisha kwamba wao
ni waabudu sanamu sawa na wale waabuduo sanamu za kuchongwa. Na matokeo ya muungano huu
174
hayakuwa na madhara kidogo sasa kuliko zama zilizokuwa zimepita. Kiburi na matumizi makubwa ya
fedha na mali viliendekezwa chini ya mwamvuli wa kinafiki wa dini, na makanisa yaligeuka upotofu.
Shetani aliendelea kupotosha mafundisho ya Biblia, na mapokeo ambayo yangeangamiza mamilioni
yalikuwa yanakita mizizi yake. Kanisa lilikuwa linayashikilia na kuyatetea mapokeo yale, badala ya
kuishindania ile “imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu.” Hivyo zikahafifishwa kanuni zile
ambazo kwa ajili yake Wanamatengenezo walikuwa wamefanya kazi na kupata mateso mengi.

175
Sura ya 17
DALILI ZA MAPAMBAZUKO

Moja ya kweli muhimu na zenye utukufu mno zilizofunuliwa katika Biblia ni ile ya kuja kwa Kristo mara
ya pili kuikamilisha kazi yake ya ukombozi. Kwa watu wa Mungu walio wasafiri, walioachwa kwa muda
mrefu wakikaa katika “nchi na uvuli wa mauti,” tumaini la thamani, linaloamsha furaha ndani yao
limetolewa katika ahadi ya kuja kwake, yeye aliye “huo ufufuo na uzima,” ili apate “kuwaleta
nyumbani kwao tena watu wake waliofukuzwa.” Fundisho la kuja kwa Yesu mara ya pili ndio msingi hasa
wa Maandiko Matakatifu. Tangu siku ile wawili wale walipogeuza hatua zao kwa huzuni kuondoka Edeni,
watoto wa imani wanamngojea Yeye Aliyeahidiwa kuja kuzivunjilia mbali nguvu za yule mharibifu na
kuwarudisha tena katika Paradiso ile iliyopotea. Watakatifu wa kale walitazamia kuja kwake Masihi
katika utukufu wake, kama hitimisho la tumaini lao. Henoko, mtu wa saba kutoka kwao wale walioishi
Edeni, ambaye kwa karne tatu akiwa duniani alitembea na Mungu wake, aliruhusiwa kuona tokea mbali
kuja kwake Mkombozi. “Tazama,” alisema, “Bwana anakuja na watakatifu wake, maelfu maelfu, ili
afanye hukumu juu ya watu wote.” Yuda 14,15. Mzee Ayubu katika usiku ule wa mateso yake alisema
maneno haya kwa nguvu kwa tumaini lisilotikisika: “Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai,
na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi…. katika mwili wangu nitamwona Mungu; nami nitamwona
mimi nafsi yangu, na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine.” Ayubu 19:25-27.
(300) Marejeo yake Kristo kuja kuuanzisha utawala wake wa haki yamechochea maneno ya dhati za
waandishi watakatifu. Waimbaji wa mashairi na manabii wa Biblia wamejikita katika habari zake kwa
maneno yanayowaka kwa moto wa utukufu wa mbinguni. Mwimba zaburi aliimba kuhusu uweza na
utukufu wa Mfalme wa Israeli: “Tokea Sayuni, ukamilifu wa uzuri, Mungu amemulika. Mungu wetu
atakuja wala hatanyamaza…. Ataziita mbingu zilizo juu, na nchi pia awahukumu watu wake.” Zaburi
50:2-4. “Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie … mbele za BWANA, kwa maana anakuja aihukumu nchi.
Atauhukumu ulimwengu kwa haki, na mataifa kwa uaminifu wake. Zaburi 96:11-13.
Nabii Isaya alisema: “Amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama
umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.” “Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka.”
“Atameza mauti hata milele, na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu
wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana BWANA amenena hayo. Katika siku hiyo watasema,
Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, ndiye tuliyemngoja atuokoe; huyu ndiye BWANA tuliyemngoja, na
tushangilie na kuufurahia wokovu wake.” Isaya 26:19; 25:8,9
Naye Habakuki, akiwa amefungwa katika maono matakatifu, aliona kuja kwake. “Mungu alikuja kutoka
Temani, Yeye aliye Mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, nayo dunia
ikajaa sifa yake. Mwangaza wake ulikuwa kama nuru.” “Akasimama, akaitetemesha dunia; akatazama
akawasitusha mataifa; na milima ya zamani ikatawanyika; vilima vya kale vikainama: Miendo yake
ilikuwa kama siku za kale.” “Milima ilikuona, ikaogopa;… Vilindi vikatoa sauti yake, vikainua juu mikono
yake. Jua na mwezi vikasimama (301) makaoni mwao; mbele ya nuru ya mishale yako ilipotapakaa,

176
mbele ya mwangaza wa mkuki wako umeremetao.” “Ukatokea kwa ajili ya wokovu wa watu wako, kwa
ajili ya wokovu wa masihi wako.” Habakuki 3:3,4,6,8,10,11,13.
Wakati Mwokozi alipokuwa anakaribia kutengwa mbali na wanafunzi wake, aliwafariji katika huzuni yao
kwa kuwapa ahadi kwamba angekuja tena: “Msifadhaike mioyoni mwenu…. Nyumbani mwa Baba yangu
mna makao mengi…. Naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja
tena, niwakaribishe kwangu.” Yohana 14:1-3. “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu
wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye.” “Ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na
mataifa yote yatakusanyika mbele zake.” Mathayo 25:31,32.
Malaika waliobaki nyuma pale kwenye Mlima wa Mizeituni, baada ya kupaa kwake Kristo, waliirudia
ahadi ya kuja kwake kwa wanafunzi wale: “Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu
mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.” Matendo 1:11. Naye Mtume
Paulo, akisema kwa njia ya Uvuvio wa Roho, alishuhudia akisema: “Bwana mwenyewe atashuka kutoka
mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu.” 1 Wathesalonike
4:16. Yule nabii wa Patmo anasema: “Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona.” Ufunuo
1:7.
Marejeo yake yanazungukwa na tukufu zile za “zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na
Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.” Matendo 3:21. Halafu
utawala wa muda mrefu wa uovu utavunjwa-vunjwa; “falme za dunia hii” zitakuwa “ufalme wa Bwana
wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.” Ufunuo 11:15. “Na utukufu wa BWANA
utafunuliwa, na wote wenye mwili watauona pamoja.” “Ndivyo Bwana MUNGU atakavyootesha haki na
sifa mbele ya mataifa.” Atakuwa “taji ya fahari, na kilemba cha uzuri, kwa mabaki ya watu wake.”
Isaya 40:5; 61:11; 28:5.
(302) Wakati huo ndipo ufalme wa amani wa Masihi uliotamaniwa kwa muda mrefu utakapoanzishwa
chini ya mbingu yote. “Maana BWANA ataufariji Sayuni; atapafariji mahali pake palipokuwa ukiwa;
atalifanya jangwa lake kuwa kama Bustani ya Edeni, na nyika yake kama Bustani ya BWANA.” “Litapewa
uzuri wa Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni.” “Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako
haitaitwa tena, Ukiwa; bali utaitwa Hefsiba; na nchi yako Beula.” “Kama vile bwana arusi amfurahiavyo
bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.” Isaya 51:3; 35:2; 62:4,5.
Kuja kwa Bwana kumekuwa katika vizazi vyote tumaini la wafuasi wake wa kweli. Ahadi ya Mwokozi
akiondoka katika Mlima wa Mizeituni, kwamba atakuja tena, iliangazia siku za usoni kwa ajili ya
wanafunzi wake, ikiijaza mioyo yao furaha na tumaini ambavyo visingeweza kuzimwa na huzuni, wala
kuhafifishwa na majaribu. Katikati ya maumivu na mateso, “kutokea kwa Mungu mkuu na Mwokozi wetu
Yesu Kristo” lilikuwa ndilo “tumaini lenye baraka” kwao. Wakati Wakristo wa Thesalonike walipokuwa
wamejawa na huzuni kwa kuwazika wapendwa wao, ambao walikuwa wametumainia kuwa hai ili
kushuhudia marejeo yake Bwana, Paulo, mwalimu wao, aliwaonyesha ufufuo ule ambao ungetokea
wakati wa marejeo ya Mwokozi. Ndipo wale waliokufa katika Kristo wangefufuka; na pamoja na wale
walio hai wangenyakuliwa kumlaki Bwana hewani. “Na hivyo,” akasema, “tutakuwa pamoja na Bwana
milele. Basi farijianeni kwa maneno hayo.” 1 Wathesalonike 4:16-17.
Kwenye kisiwa chenye miamba cha Patmo mwanafunzi mpendwa anaisikia ahadi, “Naam, naja upesi,”
na mwitikio wake unatoa sauti ya sala ya kanisa katika safari yake yote, “Amina; na uje, Bwana Yesu.”
Ufunuo 22:20.
Kutoka katika gereza la chini ya ardhi, nguzo ya kuchomea moto, jukwaa la kunyongea, mahali ambapo
watakatifu na wafia-dini walitoa ushuhuda wa ile kweli, yanatiririka kupitia karne na karne maneno ya
177
imani na tumaini lao. Wakiwa “wamethibitishiwa kuhusu ufufuo wake, na hatimaye ule wa kwao wakati
wa kuja kwake, kwa ajili hiyo,” anasema mmoja wa Wakristo hawa, “walikidharau kifo, na walijiona
kuwa juu ya kifo.” 311 (303) Walikuwa tayari kushuka kaburini, ili ya kwamba wapate “kufufuka wakiwa
huru.” 312 Walimtazamia “Bwana kuja kutoka mbinguni katika mawingu kwa utukufu wa Baba yake,”
“akiwaletea wenye haki nyakati za ufalme.” Wawaldensi walikuwa na imani kama hiyo.” 313 Wycliffe
alitazamia kuja kwa Mkombozi kama tumaini la kanisa. 314
Luther alisema wazi: “Najishawishi kuamini, kwamba siku ya hukumu haitakosa kuja katika muda wote
wa miaka mia tatu. Mungu hataweza, hawezi, kuuacha ulimwengu huu ulio mwovu kwa muda mrefu
zaidi.” “Siku ile kuu inakaribia ambayo katika hiyo ufalme huo wa machukizo utapinduliwa.” 315
“Ulimwengu huu uliozeeka hauko mbali na mwisho wake,” alisema hivyo Melanchthon. Calvin anawaasa
Wakristo “wasisite, waitamani kwa shauku kubwa siku ile ya kuja kwake Kristo kama tukio lililo heri
kuliko yote,” na akasema wazi kwamba “jamaa yote ya waaminifu wataiona siku ile.” “Lazima tuhisi
njaa ya kumtaka Kristo, lazima tutafute, na kutafakari,” alisema, “mpaka itakapopambazuka siku ile
kuu, wakati Bwana wetu atakapoudhihirisha utukufu wa ufalme wake.” 316
“Je, Bwana wetu Yesu Kristo hakuupeleka mwili wetu juu mbinguni?” alisema Knox,
Mwanamatengenezo wa Scotland, “na je, hatarudi tena? Tunajua kwamba atarudi, na kwa upesi sana.
Ridley na Latimer, waliolaza chini maisha yao kwa ajili ya ile kweli, walitazamia kurudi kwa Bwana kwa
imani. Ridley aliandika hivi: “Ulimwengu huu pasipo shaka – hili naamini, na kwa hiyo nalisema –
unakaribia mwisho wake. Hebu sisi pamoja na Yohana, mtumishi wa Mungu, na tupige kelele mioyoni
mwetu kumlilia Kristo Mwokozi wetu, tukisema, Na uje, Bwana Yesu, uje.” 317
“Mawazo juu ya kuja kwa Bwana,” Baxter alisema, “ni matamu na ya kufurahisha kuliko mambo yote
kwangu.” 318 “Ni kazi ya imani na tabia ya watakatifu wake kupenda marejeo yake na kulitazamia
tumaini lile lenye baraka.” “Ikiwa mauti ndiye adui wa mwisho kuangamizwa wakati ule wa ufufuo,
basi, sisi tujifunze kwa bidii jinsi waamini wanavyopaswa kutafuta na kuomba kwa ajili ya marejeo ya
Kristo mara ya pili, wakati ambapo (304) ushindi huu kamili na wa mwisho utakapopatikana.” 319 “Hii
ndiyo siku ambayo waamini wote wanapaswa kuitafuta, na kuitumainia, na kuingojea, ikiwa ndio
utimilizo wa kazi yote ya ukombozi wao, na hamu na juhudi zote za roho zao.” “Njoo haraka, Ee Bwana,
kuja kwa siku hiyo iliyo heri!” 320 Hilo lilikuwa ndilo tumaini la kanisa la Mitume, na la “kanisa la
jangwani,” na lile la Wanamatengenezo.
Unabii hautabiri tu jinsi Kristo atakavyokuja na lengo la kuja kwake, bali unaonyesha dalili ambazo
kwazo wanadamu watajua wakati kunapokaribia. Yesu alisema: “Kutakuwa na ishara katika jua, na
mwezi, na nyota.” Luka 21:25. “Jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota za

311
Daniel T. Taylor, The Reign of Christ on Earth: or, The Voice of the Church in All Ages, page wa 33
312
Ibid., page 54
313
Ibid., page 129-132
314
Ibid., page 132-134
315
Ibid., page 158,134
316
Ibid., page 158,134
317
Ibid., page 151, 145
318
Richard Baxter, Works, vol. la 17, page wa 555
319
Ibid., vol. la 17, uk. 500
320
Ibid., vol. la 17, uk. 182,183
178
mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika. Hapo ndipo watakapomwona
Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu.” Marko 13:24-26. Mwandishi wa
Ufunuo anazielezea ishara za kwanza kati ya hizo zitakazotangulia kuja kwake mara ya pili: “Palikuwa
na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu.” Ufunuo
6:12.
Ishara hizi zilishuhudiwa kabla ya mwanzo wa karne ya kumi na tisa. Katika kutimiza unabii huu
palitokea, mnamo mwaka wa 1755, tetemeko la nchi la kutisha kuliko ambayo yamepata kuwekwa
katika kumbukumbu. Ingawa kwa kawaida linajulikana kama Tetemeko la Lisbon, lilienea katika sehemu
kubwa ya Ulaya, Afrika na Amerika. Lilisikika kule Greenland, West Indies, katika kisiwa cha Madeira,
katika nchi ya Norway na Sweden, Uingereza na Ireland. Lilienea katika eneo lisilopungua maili za
mraba milioni nne. Katika Afrika mtikisiko ulikuwa na ukali karibu sawa na ule wa Ulaya. Sehemu kubwa
ya Algiers iliharibiwa; na umbali mfupi tu kutoka Morocco, kijiji kimoja chenye wakazi elfu nane au
kumi hivi kilimezwa. Wimbi kubwa sana liliifagia pwani ya Hispania na Afrika likiyameza majiji na
kusababisha uharibifu mkubwa.
Ni katika nchi za Hispania na Ureno ambako mtikisiko wa ardhi ulijitokeza katika ukali wa juu. Pale
Cadiz wimbi lililoingia katika nchi lilisemekana kuwa na kimo cha futi sitini. Milima, “baadhi ikiwa
milima mikubwa zaidi katika nchi ya Ureno, ilitikiswa kwa nguvu, kama vile, kuanzia chini katika (305)
misingi yake, na baadhi yake ikifumuliwa vilele vyake, ambavyo viligawanywa na kuchanwa kwa namna
ya kushangaza, sehemu kubwa ya milima ile ikirushwa chini katika mabonde yaliyokuwa karibu.
Inasimuliwa kwamba miale ya moto ilionekana ikitoka katika milima hii.” 321
Pale Lisbon “sauti ya radi ilisikika chini ya ardhi, na mara tu kishindo kikubwa chenye nguvu kiliangusha
chini sehemu kubwa ya mji huu. Katika muda wa kama dakika sita watu elfu sitini walikuwa wamekufa.
Bahari ilirudi nyuma kwanza, na kuufanya ukanda mwembamba wa ufukweni kuwa mkavu; halafu
ikarudi, ikiwa imeinuka kwa futi hamsini au zaidi juu ya usawa wake wa kawaida.” “Miongoni mwa
matukio yasiyokuwa ya kawaida yaliyosimuliwa kutokea pale Lisbon wakati wa maafa haya ni lile la
kudidimia kwa gati jipya la kuegeshea meli, likiwa limejengwa lote kwa marumaru, kwa gharama kubwa
sana. Umati mkubwa wa watu ulikuwa umejikusanya pale kutafuta usalama wao, ikiwa sehemu iliyo
mbali na majengo yanayoanguka; lakini ghafla gati lile likazama chini pamoja na watu wote waliokuwa
juu yake, wala hakuna hata mwili mmoja miongoni mwa maiti zao ulioelea juu ya uso wa bahari.” 322
“Kishindo” cha tetemeko lile “kikafuatiwa wakati huo huo na kuanguka kwa kila jengo la kanisa na
nyumba za watawa, karibu majengo yote makubwa ya halaiki, yaani zaidi ya robo moja ya nyumba zote.
Katika muda wa karibu saa mbili hivi baada ya kishindo kile, moto ulitokea katika sehemu mbalimbali,
na kuwaka kwa nguvu nyingi kwa karibu siku tatu hivi, hata mji ule ukawa umeharibiwa vibaya.
Tetemeko lile lilitokea mnamo siku takatifu, wakati makanisa na nyumba za watawa zilipokuwa
zimefurika watu, ambapo wachache wao tu walinusurika kufa.” 323 “Hofu iliyowashika watu ilikuwa
isiyoelezeka. Hakuna aliyelia; ilikuwa imevuka kiwango cha machozi. Walikimbia huku na kule, wakiwa
wamepagawa kwa hofu na mshangao, wakijigonga nyuso na vifua, wakipiga kelele, ‘Misericordia! dunia
imefika mwisho!’ Akina mama walisahau watoto wao, na kukimbia wakiwa wamebebelea sanamu za
msalaba wenye mtu aliyeangikwa. Kwa bahati mbaya, wengi walikimbilia makanisani kutafuta usalama
wao huko; kutoa sakramenti ilikuwa kazi bure; viumbe hawa maskini kuzikumbatia altare ikawa ni kazi

321
Sir Charles Lyell, Principles of Geology, page wa 495
322
Ibid., page wa 495
323
Encyclopedia Americana, art. "Lisbon," note (ed. 1831)
179
bure; sanamu, mapadre, na watu wa kawaida wakazikwa pamoja katika maangamizi ya pamoja.”
Imekisiwa kwamba watu tisini elfu walipoteza maisha katika siku ile ya kufisha.
(306) Miaka ishirini na mitano baadaye ikatokea ishara inayofuata kutajwa katika unabii ule, jua na
mwezi kutiwa giza. Kilichoifanya ishara hii kuwa ya kushangaza zaidi ni ukweli kwamba wakati wa
kutimizwa kwake ulikuwa umeonyeshwa dhahiri. Mwokozi akizungumza na wanafunzi wake kwenye
Mlima wa Mizeituni, baada ya kuwaeleza kuhusu kipindi kile kirefu cha majaribu kwa kanisa, - miaka
1260 ya mateso ya upapa, ambacho alikuwa ameahidi kwamba kingefupizwa, - alitaja hivyo matukio
fulani ambayo yangetangulia kuja kwake, na akaweka wakati dhahiri ambapo la kwanza katika hayo
lingeonekana: “Lakini siku zile, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga
wake.” Marko 13:24. Siku au miaka ile 1260 ilifika mwisho mwaka wa 1798. Robo ya karne kabla,
mateso yalikuwa karibu yamekoma kabisa. Baada ya mateso yale, kulingana na maneno yake Kristo, jua
lilikuwa litiwe giza. Tarehe 19 Mei, 1780, unabii huu ulitimizwa.
“Karibu, kama sio kabisa, siri kubwa mno na kama tukio la aina yake ambalo mpaka sasa halijapatiwa
maelezo, … ni siku ya Mei 19, 1780, - kutiwa giza kusikoelezeka kwa mbingu zote zinazoonekana na
anga katika eneo la New England.” 324
Mtu aliyeshuhudia kwa macho ambaye alikuwa anaishi Massachusetts analieleza tukio hili kama
ifuatavyo: Asubuhi jua lilichomoza pasipo mawingu, lakini mara likafunikwa. Mawingu yakashuka, na
kutoka humo, yakiwa meusi na yenye utisho, umeme ukamulika, ngurumo ya radi ikafuatia, na mvua
nyepesi ikanyesha. Kuelekea saa tatu, mawingu yale yakawa mepesi, tena yakawa na mwonekano kama
wa shaba nyeupe au nyekundu, kisha nchi, miamba, miti, majengo, maji, na watu wakabadilika kwa
nuru ile ngeni, isiyo kawaida duniani. Dakika chache baadaye, wingu zito jeusi likatanda katika anga
yote isipokuwa ukingo mwembamba uliokuwa mbali pembeni katika upeo wa macho, na giza likawa
nene kama inavyokuwa muda wa saa tatu usiku katika majira ya joto….
“Woga, wasiwasi, na hofu vikaijaza mawazo ya watu taratibu. Wanawake walisimama mlangoni,
wakiangalia sura ya nchi nje iliyokuwa imefunikwa na giza; wanaume walirudi kutoka katika kazi zao
mashambani; (307) fundi seremala aliacha zana zake za kazi, mhunzi aliacha karakana yake, mfanya
biashara akaiacha kaunta yake. Wanafunzi mashuleni walitawanywa, na watoto wakakimbilia
majumbani huku wakitetemeka. Wasafiri walitafuta malazi katika nyumba ya shamba iliyokuwa karibu.
‘Nini kinakuja?’ kila mdomo na moyo uliuliza. Ilionekana kana kwamba tufani ilikuwa karibu kuvuma
katika nchi nzima, au kana kwamba siku ya mwisho wa mambo yote imefika.
“Mishumaa ilitumiwa; na mioto ya mekoni ikawaka sana kama wakati wa usiku usio na mbalamwezi
katika majira ya kupukutisha majani…. Kuku walirudi katika mabanda yao na kulala usingizi, ng’ombe
walikusanyika katika ugo wa malisho, vyura walitoa sauti zao, ndege waliimba nyimbo zao za jioni, na
popo wakaruka huku na huko. Lakini wanadamu walijua kwamba usiku haukuwa umekuja….
"Dr. Nathanael Whittaker, mchungaji wa kanisa la Tabernacle kule Salemu, aliendesha ibada katika
nyumba ya kukutania, na kutoa hotuba ambamo alisisitiza kwamba giza lile lilikuwa la nguvu isiyo ya
kawaida. Mikusanyiko ya dini ilifanyika na mahali pengi katika sehemu nyingine. Aya za maandiko
yaliyotumika kwa hotuba za dharura zilikuwa zisizoachana ambazo inaonyesha zilielekeza kwamba giza
lile lililandana na unabii wa Maandiko. … Giza lilikuwa zito zaidi kuliko muda mfupi baada ya saa tano
kamili.” 325 “Katika sehemu nyingi za nchi giza lilikuwa kubwa sana wakati wa mchana, kiasi kwamba

324
R. M. Devens, Our First Century, page wa 89
325
The Essex Antiquarium, Aprili, 1899, vol. la 3, Na. 4, page 53 na 54
180
watu wasingeweza kueleza ni saa ngapi kwa kuangalia saa za mkono au saa kubwa za mezani au
ukutani, hakuna kula, wala kufanya shughuli zao za nyumbani, bila kutumia mwanga wa mishumaa….
“Kiasi cha giza hili kilikuwa kisicho cha kawaida. Giza lilionekana mbali hadi Falmouth. Kuelekea
upande wa magharibi lilifika hadi sehemu ya mbali ya mji wa Connecticut, na hadi Albany. Kuelekea
kusini, lilionekana katika pwani ya bahari; na kuelekea kaskazini lilifika mbali kiasi cha kufikia
yalikofika makazi ya Waamerika.” 326
Giza hili nene la mchana lilifuatiwa, kama saa moja au mbili hivi kabla ya jioni, na anga lililokuwa
mwanga hafifu, na jua likajitokeza, ingawa bado lilikuwa limefunikwa na ukungu mkubwa mweusi.
Baada ya jua kuzama, mawingu yalikuja tena, na (308) ghafla yakawa mazito.” “Wala giza la usiku
halikuwa lisilokuwa la kawaida wala lisilo la kuogofya kuliko la mchana; licha ya kwamba kulikuwa na
mwezi mpevu, hakuna kitu chochote kilichoweza kutambulika, isipokuwa kwa msaada wa nuru ya
kutengeneza, ambayo, ikiwa inaonekana kutoka nyumba zilizo jirani, na mahali penginepo palipokuwa
mbali, ilionekana kama mfano wa giza la Misri lilionekana kana kwamba halipenywi na miale ya
mwanga.” 327 Aliyeshuhudia tukio hili kwa macho yake alisema hivi: “Sikuweza kujizuia kufikiri kwamba,
endapo kila kitu kitoacho mwanga angani kingekuwa kimefunikwa na vivuli visivyopenyeka, au
kingekuwa kimeondolewa kisiwepo kabisa, giza ambalo lingetokea lisingekuwa kamili zaidi ya hili.” 328
Ingawa mnamo saa tatu ya usiku ule mwezi ulijitokeza wote, “haukuwa na madhara hata kidogo ya
kuvifukuzilia mbali vivuli vilivyokuwa mfano wa mauti.” Baada ya usiku wa manane giza lilitoweka, na
mwezi, ulipoonekana kwa mara ya kwanza, ulikuwa kama damu.
Tarehe 19 Mei 1780 inasimama katika historia kama “Siku ya Giza.” Tangu wakati wa Musa hakuna
kumbukumbu ya kipindi ambacho kimeshakuwa na giza lenye uzito, kiasi, na lililodumu kwa muda kama
hili. Maelezo ya tukio hili, kama yalivyotolewa na mashahidi walioona kwa macho, ni mwangwi tu wa
maneno ya Bwana, yaliyoandikwa na nabii Yoeli, miaka elfu mbili na mia tano kabla ya kutimizwa
kwake: “Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya BWANA iliyo kuu na
itishayo.” Yoeli 2:31.
Kristo alikuwa amewaagiza watu wake kuziangalia dalili za kuja kwake na kufurahi watakapoziona
ishara za Mfalme wao ajaye. “Basi mambo hayo yaanzapo kutokea,” alisema, “changamkeni, mkaviinue
vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia.” Aliwaelekeza wanafunzi wake kwa miti
ichanuayo wakati wa majira ya kuchipua, na kuwaambia: “Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na
kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu. Nanyi kadhalika, mwonapo
mambo hayo (309) yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu.” Luka
21:28,30,31.
Lakini kadiri roho ya unyenyekevu na uchaji wa Mungu ndani ya kanisa ilivyokuwa imetoa nafasi ya kuwa
na kiburi na kufuata mazoea, upendo kwa Kristo na imani katika marejeo yake vilipoa. Wakiwa
wamezama katika kuipenda dunia na kutafuta raha, wale waliojiita watu wa Mungu walipofushwa
macho wasiweze kuyatambua maagizo ya Mwokozi kuhusu dalili za kuja kwake. Fundisho la kuja kwake
mara ya pili lilikuwa limepuuzwa; maandiko yanayohusiana nalo yalifichwa chini ya tafsiri potofu,
mpaka likawa, kwa kiasi kikubwa, limepuuzwa na kusahaulika. Jambo hili lilijitokeza hasa katika
makanisa ya Amerika. Uhuru na raha vilivyofurahiwa na watu wa tabaka zote katika jamii, tamaa ya

326
William Gordon, History of the Rise, Progress, and Establishment of the Independence of the U.S.A., vol. la 3, uk. 57
327
Isaiah Thomas, Massachusetts Spy; au, American Oracle of Liberty, vol. la 10, Na. 472 (Mei 25, 1780)
328
Letter by Dr. Samuel Tenney, of Exeter, New Hampshire, December, 1785 (in Massachusetts Historical Society Collections,
1792, 1st series, vol. 1, p. 97)
181
mali na kuishi maisha ya anasa, kujielekeza katika kutafuta pesa, hamu ya kutafuta umaarufu na
mamlaka, vitu vilivyoonekana kuwa katika uwezo wa kufikiwa na wote, viliwafanya watu kukusanya
shauku na matumaini yao kuelekea katika mambo ya maisha haya, na kuiweka mbali wakati ujao siku ile
ya kutisha ambapo mambo ya wakati huu yatakuwa yamepita.
Mwokozi alipowaonyesha wafuasi wake dalili za marejeo yake, alitabiri hali ya kurudi nyuma
itakayokuwako pindi tu kabla ya marejeo yake. Pangekuwepo, kama katika siku za Nuhu, na shughuli na
mwamko wa mambo ya kidunia na kutafuta anasa – kununua, kuuza, kupanda, kujenga, kuoa, na
kuolewa – pamoja na kumsahau Mungu na maisha yajayo. Kwa wale wanaoishi wakati huu, onyo lake
Kristo ni hili: “Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha
haya; siku ile ikawajia ghafla, kama mtego unasavyo.” “Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili
mpate kuokoka katika hayo yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.” Luka
21:34,36.
Hali ya kanisa kwa wakati huu imedokezwa katika maneno ya Mwokozi yaliyo katika kitabu cha Ufunuo:
“Una jina (310) la kuwa hai, nawe umekufa.” Na kwa wale wanaokataa kuamka kutoka katika usalama
wao wa uzembe, onyo hili la kutisha limeelekezwa kwao: “Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi,
wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.” Ufunuo 3:1,3.
Ilihitajika kwamba watu wapate kuamshwa waitambue hatari yao; kwamba wangeamshwa ili wapate
kujiandaa kwa matukio yaambatanayo na kufungwa kwa rehema. Nabii wa Mungu anatangaza: “Siku ya
BWANA ni kuu, yenye kitisho sana; naye ni nani awezaye kuistahimili?” Ni nani atakayesimama ajapo
yule aliye na “macho safi hata asiweze kuangalia uovu,” wala “asiyeweza kutazama ukaidi”? Yoeli 2:11;
Habakuki 1:13. Kwa wale wanaopiga makelele, wakisema, “Mungu wangu! Sisi … tunakujua Wewe,”
lakini wamelivunja agano lake na kumkimbilia upesi mungu mwingine, wakificha uovu mioyoni mwao, na
kuzipenda njia za udhalimu - kwa hao siku ya Bwana ni “giza, wala si nuru, naam, yenye giza sana, wala
haina mwanga.” Hosea 8:2,1; Zaburi 16:4; Amosi 5:20. “Kisha itakuwa wakati ule,” asema Bwana,
“nitauchunguza Yerusalemu kwa taa; nami nitawaadhibu watu walioganda juu ya sira zao; wasemao
katika mioyo yao, BWANA hatatenda mema, wala hatatenda mabaya.” Sefania 1:12. “Nami nitaadhibu
ulimwengu kwa sababu ya uovu wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha
fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali.” Isaya 13:11. “Fedha yao
wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa.” “Na huo utajiri wao utakuwa mateka, na nyumba zao
zitakuwa ukiwa.” Sefania 1:18,13.
Nabii Yeremia, akiutazama kwa mbele wakati huu wa kuogofya, alipiga kelele, akasema: “Naumwa
katika moyo wangu wa ndani…. Siwezi kunyamaza; kwa sababu umesikia, Ee nafsi yangu, sauti ya
tarumbeta, mshindo wa vita. Uangamivu baada ya uangamivu umetangazwa.” Yeremia 4:19,20.
“Siku ile ni siku ya ghadhabu, siku ya ukiwa, siku ya giza na utusitusi, siku ya mawingu na giza kuu, siku
ya tarumbeta na ya kamsa.” Sefania 1:15,16. “Tazama, siku (311) ya BWANA inakuja,… ili iifanye nchi
kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.” Isaya 13:9.
Kuhusu siku ile kuu neno la Mungu, kwa lugha nzito na yenye mguso, linawataka watu wa Mungu kuamka
toka katika usingizi mzito wa kiroho na kuutafuta uso wake kwa toba na unyenyekevu: “Pigeni
tarumbeta katika Sayuni, pigeni kelele katika mlima wangu mtakatifu; wenyeji wote wa nchi na
watetemeke; kwa maana siku ya BWANA inakuja. Kwa sababu inakaribia.” “Takaseni saumu, kusanyeni
kusanyiko kuu; kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko, kusanyeni wazee, kusanyeni watoto,… Bwana arusi
na atoke chumbani mwake, na bibi arusi katika hema yake. Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, na
walie kati ya patakatifu na madhabahu.” “Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na
182
kwa kulia, na kwa kuombolea; rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie BWANA, Mungu
wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa
rehema, naye hughairi mabaya.” Yoeli 2:1,15-17,12,13.
Ili kuwaandaa watu kusimama katika siku ile ya Mungu, kazi kubwa ya matengenezo ilihitaji kufanyika.
Mungu aliona kwamba wengi miongoni mwa wale waliojiita watu wake walikuwa hawajengi kwa ajili ya
umilele, na kwa rehema zake alikuwa karibu kupeleka ujumbe wake wa onyo ili kuwaamsha toka katika
usingizi wao mzito na kuwafanya wajitayarishe kwa marejeo yake Bwana.
Onyo hili linaletwa katika Ufunuo 14. Hapa kuna ujumbe wa aina tatu unaowasilishwa kama unahubiriwa
na viumbe wa mbinguni na kufuatiwa punde tu na kuja kwa Mwana wa Adamu kuvuna “mavuno ya
nchi.” La kwanza katika maonyo haya linatangaza hukumu inayokuja. Nabii huyo aliona malaika akiruka
“katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila
na lugha na jamaa, akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu
yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.” Ufunuo
14;6,7.
(312) Ujumbe huu unatangazwa kuwa ni sehemu ya “injili ya milele.” Kazi ya kuihubiri injili
haikukabidhiwa kwa malaika, bali imekabidhiwa kwa wanadamu. Malaika watakatifu wametumiwa
kuielekeza kazi hii, wana usimamizi wa misukumo kwa ajili ya wokovu wa wanadamu; lakini kutangaza
kwenyewe kwa injili kunafanywa na watumishi wa Kristo walio duniani.
Watu waaminifu, waliokuwa watiifu kwa misukumo ya Roho wa Mungu na mafundisho ya neno lake,
walikuwa hawana budi kulitangaza onyo hili kwa ulimwengu. Walikuwa ni wale waliokuwa
wamelizingatia lile “neno la unabii lililo imara,” ile “taa ing’aayo mahali penye giza, mpaka
kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwao.” 2 Petro 1:19. Walikuwa wakitafuta
kumjua Mungu zaidi kuliko hazina zote zilizositirika, wakihesabu kuwa ni “bora kuliko biashara ya
fedha, na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.” Mithali 3:14. Naye Bwana aliwafunulia mambo
makuu ya ufalme wake. “Siri ya BWANA iko kwao wamchao, naye atawajulisha agano lake.” Zaburi
25:14.
Si wanathiolojia wasomi waliokuwa na ufahamu wa ukweli huu, na kujishughulisha katika kuutangaza.
Ikiwa hao wangekuwa walinzi waaminifu, wakiyachunguza Maandiko kwa bidii na maombi, wangekuwa
wameyajua majira ya usiku; unabii ungekuwa umewafunulia matukio yale yaliyokuwa karibu kutokea.
Lakini hawakuwa katika nafasi hii, na ujumbe ule ukatolewa na watu duni sana. Yesu alisema:
“Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza.” Yohana 12:35. Wale wanaogeuka na
kuipa kisogo nuru ambayo Mungu ameitoa, au ambao wanapuuzia kuitafuta inapokuwa mahali pale
wawezapo kuipata, huachwa gizani. Lakini Mwokozi anatangaza: “Yeye anifuataye hatakwenda gizani
kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.” Yohana 8:12. Yeye aliye na kusudi moja nyofu la kutafuta
kufanya mapenzi ya Mungu, akiizingatia kwa dhati nuru aliyokwishapewa tayari, atapokea nuru kubwa
zaidi; nyota yenye mng’ao wa mbinguni itatumwa kwa mtu huyo ili kumwongoza katika kweli yote.
(313) Wakati ule wa kuja kwa Kristo mara ya kwanza makuhani na waandishi wa Mji Mtakatifu, ambao
walikabidhiwa mausia ya Mungu, wangeweza kuzitambua dalili za nyakati na kukutangaza kuja kwake
Yeye Aliyeahidiwa. Unabii wa Mika ulipataja mahali atakapozaliwa; Danieli alitaja wakati mahsusi wa
kuja kwake. Mika 5:2; Danieli 9:25. Mungu alikabidhi unabii huu kwa viongozi wa Kiyahudi; walikuwa
hawana udhuru kwa kutokujua na kutowatangazia watu kwamba kuja kwake Masihi kulikuwa
kumekaribia. Ujinga wao ulikuwa ni matokeo ya upuuzi katika dhambi. Wayahudi walikuwa wakijenga
kumbukumbu za manabii wa Mungu waliouawa, wakati kwa kujiweka chini ya wakuu wa dunia hii
183
walikuwa wanatoa heshima zao kwa watumishi wa Shetani. Wakiwa wamezama katika tamaa zao za
kutaka nafasi na mamlaka miongoni mwa wanadamu, walikosa kuona heshima za kimbingu
walizokabidhiwa na Mfalme wa mbinguni.
Kwa shauku na hamu ya kicho wazee wa Israeli wangekuwa wamejifunza kuhusu mahali, wakati, na
mazingira, kuhusiana na tukio lile lililo kuu katika historia ya ulimwengu - kuja kwa Mwana wa Mungu
kukamilisha ukombozi wa mwanadamu. Watu wote wangekuwa wamekesha na kungoja ili wawe
miongoni mwa watu wa kwanza kumkaribisha Mkombozi wa ulimwengu. Lakini, tazama, pale
Bethlehemu kulikuwa na wasafiri wawili kutoka katika milima ya Nazareti wakitembea umbali wote
kupitia mitaa finyu ya mji mpaka sehemu ya mwisho kabisa ya mashariki mwa mji, wakitafuta bila
mafanikio mahali pa kupumzikia na pa kujihifadhi usiku ule. Hakuna milango iliyo wazi kuwapokea.
Hatimaye wanapata hifadhi katika kibanda kibaya kilichoandaliwa kwa ajili ya ng’ombe, hapo ndipo
alipozaliwa Mwokozi wa ulimwengu.
Malaika wa mbinguni walikuwa wameuona utukufu aliokuwa nao Mwana wa Mungu akiwa pamoja na
Baba kabla ya ulimwengu kuwako, nao walitazamia kwa hamu kubwa kwamba kule kuonekana kwake
duniani kungekuwa tukio lenye furaha kubwa sana kwa watu wote. Malaika waliwekwa tayari kupeleka
habari njema za kishindo kwa wale waliokuwa tayari kuzipokea na ambao kwa furaha wangewajulisha
wakazi wa ulimwengu. Kristo alikuwa amejishusha na kuchukua asili ya mwanadamu; alikuwa abebe
(314) uzito wa shida usio kipimo katika kuitoa nafsi yake kama sadaka kwa ajili ya dhambi; lakini
malaika walitamani kwamba hata katika kujidhili kwake Mwana wa Aliye Juu apate kuonekana mbele ya
wanadamu katika ukuu na utukufu wake unaolingana na sifa yake. Je, wakuu wa dunia wangeweza
kukusanyika katika mji ule mkuu wa Israeli kumpokea kwa furaha wakati wa kuja kwake? Je, majeshi
mengi ya malaika yangemfikisha kwa kundi lililotarajiwa?
Malaika anaitembelea dunia ili kuona wale walio tayari kumkaribisha Yesu. Lakini hawezi kuona dalili
zilizotarajiwa. Hasikii sauti yoyote ya sifa na shangwe inayoonyesha kwamba kipindi cha kuja kwake
Masihi kimekaribia. Malaika yule anabaki hewani akiruka juu ya mji ule na juu ya hekalu lile ambalo
ndani yake kuwako kwa Mungu kulikuwa kumedhihirishwa kwa vizazi vingi; lakini hata humo anaiona
hali isiyokuwa tofauti. Makuhani wale, katika fahari na kiburi, wanatoa sadaka zilizonajisiwa katika
hekalu. Mafarisayo wanahutubia watu kwa sauti kubwa au wakitoa sala za kujikinai maeneo ya njia-
panda za mitaa. Katika majumba ya kifalme, katika mikusanyiko ya wanafalsafa, katika shule za
marabi, wote kwa namna moja hawana habari na tukio la ajabu ambao limeijaza mbingu yote kwa
furaha na sifa - kwamba Mkombozi wa wanadamu yu karibu kuonekana duniani.
Hakuna ushahidi wowote unaoonyesha kwamba Kristo anatarajiwa, na hakuna maandalizi yoyote kwa
ajili ya huyo Mkuu wa uzima. Kwa mshangao mkubwa yule mjumbe wa mbinguni yu karibu kurudi
mbinguni akiwa na bahari mbaya ya aibu, wakati anapogundua kundi la wachungaji wa kondoo
wanaoichunga mifugo yao usiku, nao, wanapoangaza macho yao katika mbingu zenye nyota,
wanautafakari unabii wa Masihi ajaye, na kutamani kuja kwake Mkombozi yule wa ulimwengu. Hapa
kuna kundi lililo tayari kuupokea ujumbe wa mbinguni. Na ghafla malaika yule wa Bwana anatokea,
akitangaza habari ile ya furaha kuu. Utukufu wa mbinguni unauangaza uwanda wote, kundi la malaika
wasiohesabika linadhirishwa, na kama vile furaha ile ilikuwa kubwa mno kwa malaika mmoja kuileta
kutoka mbinguni, kusanyiko lile la malaika linatoa sauti katika wimbo ambao utaimbwa na mataifa yote
ya waliokombolewa siku moja: “Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu
aliowaridhia.” Luka 2:14.

184
(315) Lo, kuna fundisho kubwa kiasi gani katika kisa cha ajabu kilichotokea Bethlehemu! Ni jinsi gani
kinakemea kutokuamini kwetu, kiburi chetu, na kutosheka kwetu. Ni jinsi gani kinatuonya sisi kuwa
macho, la sivyo kwa kosa letu la kutokuwa tofauti tutashindwa pia kuziona dalili za nyakati, na hivyo
kutojua siku ya kujiliwa kwetu.
Si katika vilima vile vya Yudea tu, si miongoni mwa wachungaji wale waliokuwa duni peke yake, mahali
ambapo malaika walikuwa wamewapata watu wanaokesha kwa ajili ya kuja kwa Masihi. Katika nchi ya
wasiomjua Mungu pia walikuwako watu waliomtazamia kwamba atakuja; walikuwa ni watu wenye
hekima, matajiri na wenye vyeo, wanafalsafa wa Mashariki. Wakijifunza maumbile ya asili, Mamajusi
walikuwa wamemwona Mungu katika kazi za mikono yake. Katika Maandiko ya Kiebrania walikuwa
wamejifunza kuhusu Nyota itakayotokea katika Yakobo na kwa shauku walikungojea kuja kwake yeye
ambaye asingekuwa tu “Faraja ya Israeli,” bali pia “Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa,” na “kuwa
wokovu hata mwisho wa dunia.” Luka 2:25,32; Matendo 13:47. Walikuwa watafutaji wa ile nuru, na
nuru toka kwenye kiti cha enzi cha Mungu ikawaangazia njia ya miguu yao. Wakati makuhani na walimu
wa Yerusalemu wamefunikwa na giza, wateule katika kazi ya ulinzi na ufafanuaji wa ile kweli, walikuwa
wamefunikwa katika giza, nyota iliyotumwa kutoka mbinguni iliwaongoza wageni hao Wamataifa hadi
mahali alipozaliwa Mfalme mpya aliyezaliwa.
Ni kwa hao “wamtazamiao” Kristo “atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, … kwa wokovu” wao.
Waebrania 9:28. Kama ilivyokuwa katika habari za kuzaliwa kwa Mwokozi, ujumbe wa kuja kwake mara
ya pili haukukabidhiwa kwa viongozi wa kidini wanaoongoza watu. Walikuwa wameshindwa kuhifadhi
uhusiano wao na Mungu, na walikuwa wameikataa nuru ile iliyotoka mbinguni; kwa hiyo, wao
hawakuwamo katika hesabu ya wale anaowaeleza mtume Paulo: “Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata
siku ile iwapate kama mwivi. Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi
si wa usiku, wala wa giza.” 1 Wathesalonike 5:4,5.
Walinzi katika kuta za Sayuni wangekuwa wa kwanza kupata habari za kuja kwa Mwokozi, wangekuwa
wa kwanza kupaza sauti zao na kutangaza kwamba yu karibu, wangekuwa wa kwanza kuwaonya watu ili
wajiandae kwa kuja kwake. Lakini walikuwa wametulia tu, (316) wakiota ndoto za amani na salama,
watu wakiwa wamelala usingizi katika dhambi zao. Yesu aliliona kanisa lake, kama mtini usiozaa
matunda, uliojifunika kwa unafiki majani ya udanganyifu, kumbe likiwa halina matunda. Palikuwa na
kujidai kwamba linashika taratibu zote za dini, wakati roho ya unyenyekevu wa kweli, toba, na imani -
mambo pekee ambayo yangeweza kuifanya huduma yao ipate kukubaliwa na Mungu - yalikosekana.
Badala ya neema za Roho kilionekana kiburi, kushikilia desturi za kanisa, kujisifu, ubinafsi,
ukandamizaji. Kanisa lililorudi nyuma lilifumba macho yao wasizione dalili za nyakati. Mungu
hakuwaacha, wala kuruhusu uaminifu wake kushindwa; lakini wao wakamwacha, na kujitenga mbali na
upendo wake. Walipokataa kutekeleza masharti, ahadi zake kwao hazikutimizwa.
Hayo ndiyo matokeo ya hakika ya kupuuza kutambua na kuendeleza nuru na upendeleo utolewao na
Mungu. Ikiwa kanisa halifuati katika maongozi ya Mungu yanayofunuliwa, ili likubali kila mwale wa nuru,
kutekeleza kila jukumu linaloweza kufunuliwa kwake, pasipo kuepuka litashuka hadhi na kuwa tu
maadhimisho ya taratibu za kanisa, na roho ya utauwa halisi itatoweka. Ukweli huu umejionyesha kwa
kujirudia-rudia katika historia ya kanisa. Mungu anataka kwa watu wake matendo ya imani na utii
vinavyolingana na mibaraka na haki zake zilizotolewa. Utii unadai kujitoa kafara na unahusisha
msalaba; na hii ndiyo maana wengi wa wale wanaojiita wafuasi wa Kristo walikataa kuipokea nuru
iliyotoka mbinguni, na, kama ilivyokuwa kwa Wayahudi wa zamani, hawakuyajua majira ya kujiliwa
kwao. Luka 19:44. Kwa sababu ya kiburi chao na kutokuamini kwao Bwana aliwapita na kufunua ukweli

185
wake kwa wale ambao, kama wachungaji wa Bethlehemu na Mamajusi wa Mashariki, walikuwa
wamezingatia nuru yote waliyokuwa wamepokea.

Sura ya 18
MWANAMATENGENEZO WA AMERIKA

Mkulima mmoja mwenye heshima na unyofu wa moyo, aliyekuwa ameongozwa kuwa na mashaka dhidi
ya mamlaka ya kimbingu ya Maandiko, lakini ambaye alitamani kwa dhati kuujua ukweli, alikuwa mtu
aliyechaguliwa na Mungu kwa njia ya pekee ili kuongoza katika kutangaza habari ya kuja kwa Kristo
mara ya pili. Kama ilivyo kwa Wanamatengenezo wengine wengi, William Miller alikuwa amepambana
na umaskini mapema katika maisha yake na hivyo alikuwa amejifunza mafundisho makuu ya kufanya
kazi kwa nguvu na kujinyima. Watu wa nyumbani alimokulia walikuwa na sifa ya kuwa na roho ya
kujitegemea na kupenda kujituma, na kuwa na uwezo wa kustahimili na uzalendo - sifa hizo pia zilikuwa
zimejitokeza katika tabia yake. Baba yake alikuwa kapteni katika jeshi la Mapinduzi, na kujitoa mhanga
kwake alikofanya katika jitihada zake pamoja na mateso yake ya kipindi kile cha dhoruba vinaweza
kuonekana katika mazingira ya dhiki za maisha ya mwanzo ya Miller.
Alikuwa na mwili wenye afya njema, na hata katika utoto wake alionyesha uwezo wa kiakili usio wa
kawaida. Kadiri alivyozidi kukua, hali hiyo ilijionyesha dhahiri. Akili yake ilikuwa inafanya kazi vizuri na
ikawa imeendelea, na alikuwa na kiu ya kutafuta ujuzi wa mambo. Japo hakufaidi kupata manufaa ya
elimu ya chuo, kupenda kwake kujifunza na tabia yake ya kuwa makini katika kutafakari na kule
kudadisi kwake kwa karibu sana vilimfanya awe mtu mwenye maamuzi mazuri na mwenye mtazamo
mzuri. Alikuwa na tabia njema isiyo na lawama na sifa za kutamanika, kwa kawaida alikuwa
anaheshimika kwa unyofu wake, uangalifu wake katika kutumia fedha, na ukarimu wake. Kwa sababu ya
bidii yake na welekevu wake alijipatia (318) ustadi mapema, ingawa mazoea yake ya kujifunza bado
yalidumishwa. Alikalia vyeo mbalimbali vya serikali na jeshi kwa sifa zinazotakiwa, na njia za kuifikia
mali na heshima zilionekana kufunguka wazi kwake.
Mama yake alikuwa mwanamke mcha Mungu sana, na utotoni mwake, Miller alikuwa chini ya mivuto ya
kidini. Hata hivyo, mwanzoni mwa ukubwa wake alitupwa katika jamii ya watu wenye msimamo wa
kuamwamini uwepo wa Mungu kulingana na mantiki (deists), ambao mvuto wao ulikuwa na nguvu nyingi
zaidi kwake kutokana na ukweli kwamba walikuwa raia wema sana na watu wenye tabia ya upole na
ukarimu. Wakiishi, kama walivyokuwa, katikati ya taasisi za Kikristo, tabia zao kwa kiwango fulani
zilirekebishwa kulingana na mazingira yao haya. Kwa uzuri wao uliowapatia heshima na imani kwa watu,
waliwiwa kuongozwa na Biblia; na hata hivyo vipawa vile vizuri vilitumiwa isivyo kiasi cha kuleta mvuto
ulio dhidi ya neno la Mungu. Kwa kushirikiana na watu hawa, Miller alishawishiwa kuchukua mitazamo
yao. Tafsiri za Maandiko wakati huu zilileta matatizo yaliyoonekana kwake kuwa magumu sana; lakini
imani yake mpya, wakati ikiiweka Biblia kando, haikutoa chochote kilicho bora kuzingatia, naye akabaki
kuwa mbali katika kutoridhika. Hata hivyo, aliendelea kuwa na mtazamo huu kwa takribani miaka kumi
na miwili. Lakini katika umri wa miaka thelathini na minne Roho Mtakatifu aliusukuma moyo wake kwa
kumpa hisia ya hali yake ya dhambi. Katika imani yake ya awali hakuona uhakika wa furaha ng’ambo ya
kaburi. Maisha yake yajayo yalikuwa ya giza na utusitusi. Baadaye akirejea kwa hali ya wakati huu,
alisema:

186
“Uharibifu ulikuwa ni fikra isiyovutia na ya kusumbua, na uwajibikaji ulikuwa ni uharibifu wa hakika kwa
wote. Mbingu zilikuwa kama shaba nyeupe juu ya kichwa changu, na nchi kama chuma chini ya miguu
yangu. Umilele –ilikuwa ni nini? Na mauti - kwa nini ilikuwapo? Kadiri nilivyozidi kufikiri na kutafuta
sababu, ndivyo nilivyozidi kwenda mbali katika kukosa uhakika. Kadiri nilivyofikiri zaidi ndivyo
nilivyopata zaidi majibu yaliyotawanyika-tawanyika. Nilijaribu kuacha kufikiri, lakini mawazo yangu
hayakuweza kudhibitiwa, nilihuzunishwa kweli, lakini sikujua sababu. Nilinung’unika na kulalamika,
lakini sikujua nafanya hivyo dhidi ya nani? Nilijua kwamba kulikuwa na jambo ambalo si sahihi, lakini
sikujua namna au mahali pa kupata jambo sahihi. Niliomboleza, lakini pasipo tumaini.”
(319) Aliendelea na hali hii kwa miezi kadhaa. “Ghafla,” anasema, “tabia ya Mwokozi ilionekana wazi
mawazoni mwangu. Ilionekana kana kwamba yamkini alikuwako mmoja aliyekuwa mwema na mwenye
huruma kiasi cha yeye mwenyewe kupatanisha kwa ajili ya dhambi zetu, na kwa njia hiyo kutuokoa sisi
toka katika adhabu ya dhambi. Mara nikahisi jinsi huyo alivyokuwa mwema, tena nikajisikia kwamba
mimi mwenyewe ningeweza kujikabidhi katika mikono, na kutumainia rehema, yake huyo. Lakini swali
liliibuka, Namna gani inawezekana kuthibitisha kwamba mtu wa jinsi hiyo yuko? Kando ya Biblia, niliona
kwamba nisingeweza kupata ushahidi wowote wa kuwako kwa Mwokozi kama huyo, au hata kuwako kwa
hali ya baadaye….
“Niliona kwamba Biblia ilimfunua Mwokozi wa namna ile niliyohitaji; na nilichanganyikiwa kuona jinsi
kitabu kisichokuwa na uvuvio kinavyoweza kuonyesha kanuni za kukidhi kwa ukamilifu mahitaji ya
ulimwengu ulioanguka. Nikalazimika kukubali kwamba lazima Maandiko ni ufunuo unaotoka kwa Mungu.
Hayo yakawa ndiyo furaha yangu; na nikampata rafiki Yesu. Mwokozi alikuwa bora kwangu katika watu
kumi elfu; na Maandiko, ambayo zamani yalikuwa giza kwangu na yaliyokuwa yanajipinga yenyewe, sasa
yakawa taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu. Mawazo yangu yakatulia na kutosheka. Niliona
Bwana Mungu akiwa ni Mwamba katikati ya bahari ya maisha. Biblia sasa ilikuwa ni somo langu kuu la
kujifunza, na naweza kusema kwa kweli kwamba, niliichunguza kwa furaha kubwa. Nikagundua kwamba
nusu yake ilikuwa haijapata kusimuliwa kwangu kamwe. Nilistaajabu kuona kwamba nilikuwa sijapata
kuona uzuri na utukufu wake kabla, na nikashangaa sana kwamba niliweza kuikataa. Niliona kila kitu
kilichotamaniwa na moyo kikiwa kimefunuliwa, na tiba kwa kila ugonjwa wa roho. Nilipoteza hamu yote
ya kusoma maandiko mengine, na kuushughulisha moyo wangu ili kujipatia hekima toka kwa Mungu.” 329
Miller aliikiri hadharani imani yake katika dini aliyokuwa ameidharau. Lakini rafiki zake wasioamini
hawakuchelewa kuleta mbele yake hoja zote ambazo yeye mwenyewe mara nyingi alikuwa amezitoa
dhidi ya mamlaka ya kimbingu ya Maandiko. Wakati ule hakuwa tayari kuzijibu; lakini aliwaza kwamba
ikiwa Biblia ni ufunuo utokao kwa Mungu, ni lazima (320) ionyeshe kutojipinga ndani yake; na ya
kwamba kwa kuwa ilitolewa ili kumpa mwanadamu mafundisho, basi, ni lazima iendane na ufahamu wa
mwanadamu. Aliazimia kujifunza Maandiko yeye mwenyewe, na kujiridhisha kama kila ukinzani
unaoonekana humo umesawazishwa.
Kwa hamu kubwa sana alijifunza vitabu vya Danieli na Ufunuo, akizitumia kanuni za kutafsiri zile zile
alizotumia katika maandiko yale mengine, na akaona, kwa furaha kubwa, kwamba lugha za mifano
katika unabii zinaweza kueleweka. Aliona kwamba unabii, kwa kadiri ulivyokuwa umetimizwa, ulikuwa
umetimizwa kwa maana halisi ya maneno yalivyo; kwamba matumizi mbalimbali ya maneno, sitiari, visa
kwa njia vielelezo, mifano, na kadhalika, yalikuwa yameelezwa kwa maana ya moja kwa moja, au
maana iliyobebwa na maneno ilikuwa imefafanuliwa katika maandiko mengine, na kwa hiyo ielezwapo,
ilikuwa ieleweke kwa maana yake halisi. “Hivyo mimi niliridhika,” anasema, “kwamba Biblia ni mfumo

329
S. Bliss, Memoirs of Wm. Miller, pages 65-67
187
wa kweli zilizofunuliwa, zilizotolewa kwa uwazi na urahisi kiasi kwamba msafiri, japo (321) awe
mjinga, hawezi kuyakosea.” 330 Mwunganiko mmoja baada ya mwingine wa mnyororo wa ile kweli
ulikuwa thawabu ya juhudi zake, kadiri alivyofuatilia mistari mikuu ya unabii. Malaika wa mbinguni
walikuwa wakiyaongoza mawazo yake na kufunua Maandiko katika fahamu zake.
Akizingatia namna unabii ulivyokuwa umetimizwa mnamo siku za nyuma kama kigezo cha kupimia
kutimizwa kwa unabii wa yale yaliyokuwa mbele, alitosheka kwamba maoni ya wengi ya utawala wa
kiroho wa Kristo - milenia ya muda kabla ya mwisho wa ulimwengu huu - hayakuungwa mkono na neno
la Mungu. Fundisho hili, likielekeza kwa kipindi cha miaka elfu moja ya haki na amani kabla ya kuja kwa
Bwana katika mwonekano wake, liliweka mbali utisho wa siku ya Mungu. Lakini, hata liwe la kupendeza
kama lilivyo, liko kinyume na mafundisho ya Kristo na ya mitume wake, waliotangaza kwamba ngano na
magugu vitakua pamoja mpaka wakati wa mavuno, mwisho wa ulimwengu; kwamba “wabaya na
wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu,” kwamba katika “siku za mwisho kutakuwako
nyakati za hatari;” na ya kwamba ufalme wa giza utaendelea kuwako mpaka wakati wa marejeo yake
Bwana na kwamba utaangamizwa kabisa kwa pumzi ya kinywa chake na kuangamizwa kwa ufunuo wa
kuwapo kwake. Mathayo 13:30,38-41; 2 Timotheo 3:13,1; 2 Wathesalonike 2:8.
Fundisho la kuongoka kwa ulimwengu wote na utawala wa kiroho wa Kristo halikushikwa na kanisa la
Mitume. Kwa ujumla halikukubalika miongoni mwa Wakristo mpaka karibu na mwanzo wa karne ya kumi
na nane. Kama ilivyo kwa fundisho jingine lolote la uongo, matokeo yake yalikuwa mabaya.
Liliwafundisha watu kuyaona marejeo ya Bwana mbali siku za mbele na yaliwazuia kuzingatia dalili
zinazotangaza kukaribia kwake. Liliamsha hisia ya kujiamini na kujiona kuwa salama ambayo haikuwa na
msingi mzuri na iliwafanya wengi kupuuzia kufanya maandalizi ambayo ni muhimu ili kukutana na
Bwana wao.
Miller aliona kwamba kuja kwa uhalisia kwa Kristo kulifundishwa waziwazi katika Maandiko. Paulo
anasema: “Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti (322)
ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu.” 1 Wathesalonike 4:16. Na Mwokozi anasema: “Nao
watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.”
“Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo
kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.” Mathayo 24:30,27. Ataandamana na majeshi yote ya
mbinguni. “Atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja
naye.” Mathayo 25:31. “Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao
watawakusanya wateule wake.” Mathayo 24:31.
Wakati ajapo wenye haki waliokufa watafufuliwa, na wenye haki walio hai watabadilishwa. “Hatutalala
sote,” anasema Paulo, “lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa
parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi
tutabadilika. Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.” 1
Wakorintho 15:51-53. Kisha katika waraka wake kwa Wathesalonike, baada ya kuelezea habari za
marejeo ya Bwana, anasema hivi: “Nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio
hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa
pamoja na Bwana milele.” 1 Wathesalonike 4:16,17.
Ni mpaka hapo atakapokuja Kristo mwenyewe ndipo watu wake watakapoupokea ufalme. Mwokozi
alisema: “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote
pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele

330
Bliss, page wa 70
188
zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono
wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono
wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa
ulimwengu.” Mathayo 25:31-34. Tumeona katika Maandiko ambayo yametolewa ya kwamba hapo ajapo
Mwana wa Adamu, wafu wanafufuliwa wasiweze kupatikana na uharibifu tena, na wale walio hai
wanabadilishwa. Kwa badiliko hili kubwa (323) wanaandaliwa kuupokea ufalme; maana Paulo anasema:
“Nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharibika.” 1
Wakorintho 15:50. Mwanadamu katika hali yake ya sasa ana mwili wa kufa, mwenye kuharibika; lakini
ufalme wa Mungu utakuwa usioharibika, ukidumu milele. Kwa hiyo, mwanadamu katika hali yake ya sasa
hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu. Lakini hapo Yesu ajapo, anawapa watu wake mwili usiokufa;
kisha anawaita kuurithi ufalme ule ambao mpaka sasa wamekuwa warithi tu.
Haya pamoja na maandiko mengine yalithibitishia mawazo ya Miller kwamba matukio yaliyokuwa
yakitarajiwa na watu wote kutokea kabla ya marejeo yake Kristo, kama vile utawala wa amani
ulimwenguni pote na usimamishaji wa ufalme wa Mungu duniani, yangefuata baada ya kuja kwake mara
ya pili. Zaidi ya hayo, dalili zote za nyakati na hali ya ulimwengu vililandana na maelezo ya unabii wa
siku za mwisho. Alilazimika kufikia hitimisho, kutokana na kujifunza Maandiko tu, kwamba kipindi
kilichotolewa cha kuendelea kuwako kwa dunia hii katika hali yake ya sasa kilikuwa kinakaribia kufikia
mwisho.
“Aina nyingine ya ushahidi iliyoathiri sana mawazo yangu,” anasema, “ilikuwa mpangilio wa wendo
katika Maandiko…. Nilikuta kwamba matukio yaliyotabiriwa, ambayo yalikuwa yametimizwa katika siku
za nyuma, mara nyingi yalitukia katika muda ule ule uliomuriwa. Miaka mia moja na ishirini kuelekea
kwenye gharika (Mwanzo 6:3); siku saba ambazo zingeitangulia gharika, pamoja na siku arobaini za
mvua iliyotabiriwa kunyesha (Mwanzo 7:4); miaka mia nne ya kukaa ugenini kwa uzao wa Ibrahimu
(Mwanzo 15:13); siku tatu za ndoto ya mnyweshaji na mwokaji (Mwanzo 40:12-20); miaka saba
inayomhusu Farao (Mwanzo 41:28-54); miaka arobaini jangwani (Hesabu 14:34); miaka mitatu na nusu
ya njaa (1 Wafalme 17:1); miaka sabini ya utumwa (Yeremia 25:11); nyakati saba za Nebukadneza
(Danieli 4:13-16); na majuma saba, majuma sitini na mawili, na juma moja, yanayofanya jumla ya
majuma sabini yaliyoamriwa juu ya Wayahudi (Danieli 9:24-27), - matukio hayo yote yaliyowekewa
mipaka ya nyakati yalikuwa wakati mmoja mambo ya unabii tu, nayo yalitimizwa kulingana na utabiri
huo.” 331
(324) Basi, alipogundua, katika kujifunza kwake Biblia, wendo wa vipindi mbalimbali ambavyo, kwa
mujibu wa uelewa wake, vilienda hadi katika marejeo ya Kristo, hakuzichulia vinginevyo isipokuwa
kama zile “nyakati zilizoamriwa mapema,” ambazo Mungu alikuwa amewafunulia watumishi wake.
“Mambo ya siri,” anasema Musa, “ni ya BWANA, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi
na watoto wetu milele;” na Bwana anatangaza kwa njia ya nabii Amosi, kwamba yeye “hatafanya neno
lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.” Kumbukumbu la Torati 29:29; Amosi 3:7.
Wanafunzi wa neno la Mungu, wanaweza sasa kutarajia kwa ujasiri kuliona tukio kuu kuliko yote
kutokea katika historia ya mwanadamu, ambalo limeelezwa waziwazi katika Maandiko ya kweli.
“Kadiri nilivyokuwa nimesadikishwa kikamilifu,” anasema Miller, kwamba “kila andiko, lenye pumzi ya
Mungu, lafaa kwa mafundisho (2 Timotheo 3:16); kwamba halikuja wakati wo wote kwa mapenzi ya
mwanadamu, bali liliandikwa na wanadamu watakatifu, walioongozwa na Roho Mtakatifu (2 Petro 1:21),

331
Bliss, pages 74, 75

189
tena kwamba liliandikwa ‘ili kutufundisha sisi, ili kwa saburi na faraja ya Maandiko tupate kuwa na
tumaini’ (Warumi 15:4), nisingechukulia wendo wa vipindi vya sehemu za Biblia vinginevyo isipokuwa
vile vile kama sehemu za neno la Mungu, na ya kwamba zilikuwa zinakidhi kupata tafakari yetu ya
makini, kama sehemu nyingine yoyote ya Maandiko. Kwa hiyo, nilihisi kwamba katika kujibidisha
kufahamu kile ambacho Mungu kwa rehema zake alikuwa ameona vema kutufunulia, sikuwa na haki ya
kuvipita vipindi vya unabii.” 332
Unabii ulioonekana kwa wazi sana kuufunua wakati wa kuja mara ya pili ulikuwa ni ule wa Danieli 8:14:
“Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu, ndipo patakatifu patakapotakaswa.” Kufuata
kanuni yake ya kuyafanya Maandiko yajitafsiri yenyewe, Miller alijifunza kwamba siku moja katika
mifano ya unabii inawakilisha mwaka mmoja (Hesabu 14:34; Ezekieli 4:6); aliona kwamba kipindi cha
siku 2300 za unabii, ama miaka halisi, kingefika mbali kupita kipindi cha kuachiliwa kwa Wayahudi, kwa
hiyo kisingehusu patakatifu pa kipindi kile. Miller alikubali mtazamo uliopokewa kwa ujumla kwamba
katika kipindi cha Kikristo (325) dunia ni patakatifu, na kwa hiyo, alielewa kwamba kutakaswa kwa
patakatifu kulikotabiriwa katika Danieli 8:14 kuliwakilisha kutakaswa kwa ulimwengu huu kwa moto
wakati wa kuja kwa Kristo mara ya pili. Kwa hiyo, sasa, ikiwa mahali sahihi pa kuanzia siku zile 2300
pangejulikana, alifikia uamuzi kwamba wakati wa kuja kwake mara ya pili hakika ungeweza kujulikana
bila shaka. Hivyo ndivyo ungeweza kujulikana wakati wa mwisho mkuu wa mambo yote, wakati ule
ambapo hali ya mambo ilivyo sasa, pamoja na “kiburi chake chote na mamlaka yake, fahari yake,
vingefikia mwisho wake;” wakati ambapo laana “ingeondolewa duniani, mauti ingeangamizwa, thawabu
ingetolewa kwa watumishi wa Mungu, manabii na watakatifu, pamoja na wale wanaolicha jina lake, na
wale wanaoiharibu nchi kuharibiwa” 333
Kwa juhudi mpya na ya kina, Miller aliendelea kuupima unabii huo, mida yote ya usiku na mchana
ikitumika kujifunza kile kilichoonekana kabisa kwake kuwa kina umuhimu mkubwa wa kushangaza na
cha kuvuta hisia zote. Katika sura ya nane ya Danieli hakuweza kupata kidokezo chochote kuhusu
mwanzo wa siku zile 2300; malaika Gabrieli, ingawa aliagizwa kumfanya Danieli afahamu maono yale,
alimpa maelezo kwa sehemu tu. Kadiri mateso ya kutisha yatakayoliangukia kanisa yalivyofunuliwa
katika maono ya nabii, nguvu zake za mwili zilimwishia. Hakuweza kustahimili tena; na malaika
akamwacha kwa muda. Danieli alizimia “akaugua siku kadha wa kadha.” “Nami naliyastaajabia yale
maono,” anasema, “ila hakuna aliyeyafahamu.”
Lakini Mungu alikuwa amemwagiza mjumbe wake: “Mfahamishe mtu huyu maono haya.” Lazima agizo
hilo litekelezwe. Katika kulitii hilo, malaika, muda fulani baadaye, alirudi kwa Danieli, na kumwambia:
“Nimetokea sasa, ili nikupe akili upate kufahamu;” “basi itafakari habari hii, na kuyafahamu maono
haya.” Danieli 8:27, 16; 9:22, 23, 25-27. Palikuwa na jambo moja la muhimu katika maono ya sura ya
nane ambalo lilikuwa limeachwa bila kufafanuliwa, nalo ni, lile lililohusiana na wakati - kipindi kile cha
siku 2300; kwa hiyo malaika, anaporejea katika maelezo yake, anakita hasa katika somo la wakati:
(326) “Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya Mji wako Mtakatifu…. Basi ujue
na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani
zake Masihi aliye Mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena
pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu. Na baada ya yale majuma sitini na
mawili, Masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu…. Naye atafanya agano thabiti na watu wengi
kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu.”

332
Bliss, page 75
333
Bliss, page 76
190
Malaika alikuwa ametumwa kwa Danieli kwa kusudi maalum la kumweleza jambo ambalo alishindwa
kufahamu katika maono ya sura ya nane, tamko linalohusu wakati - “Hata nyakati za jioni na asubuhi
elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.” Baada ya kumwagiza Danieli “kuitafakari
habari hii, na kuyafahamu maono haya,” maneno ya kwanza kabisa ya malaika yule ni: “Muda wa
majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya Mji wako Mtakatifu.” Neno lililotafsiriwa hapa
“umeamriwa” kwa maana yake halisi linaashiria “kukatwa”. Majuma sabini, yawakilishayo miaka 490,
yanatangazwa na malaika huyo kuwa yametengwa, kuwa yanawahusu hasa Wayahudi. Lakini yalitengwa
kutoka katika kipindi gani? Kwa kuwa siku 2300 ndicho kipindi pekee kilichotajwa katika sura ya 8, basi,
hapana budi hicho ndicho kiwe kipindi ambacho kutokana nacho majuma hayo sabini yalikatwa; kwa
hiyo, majuma hayo sabini ni lazima yawe sehemu ya zile siku 2300, na vipindi hivyo viwili havina budi
kuanza pamoja. Majuma hayo sabini yalitangazwa na malaika kwamba yanahesabiwa kuanzia muda wa
kutolewa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu. Ikiwa tarehe ya amri ile ingeweza
kupatikana, basi, mwanzo wa kipindi hicho kikuu cha siku 2300 ungeweza kupatikana kwa uhakika.
Katika sura ya saba ya Ezra amri hiyo inapatikana. Fungu la 12 hadi la 26. Katika ukamilifu wake wote
ilitolewa na Artashasta, mfalme wa Uajemi, mwaka wa 457 K.K. Lakini katika Ezra 6:14 nyumba ya
Bwana kule Yerusalemu inasemekana kwamba ilikuwa imejengwa “kwa amri ya Koreshi, na Dario, na
Artashasta mfalme wa Uajemi.” Wafalme hao watatu, katika (327) kuianzisha, kuithibitisha tena, na
kuitekeleza amri ile, walifikisha katika ukamilifu wake uliotakiwa na unabii ule kwa kuweka mwanzo wa
miaka ile 2300. Tukiuchukua mwaka wa 457 K.K., wakati tamko lile lilipokamilishwa, kama tarehe ya
amri ile, kila maelezo ya unabii huo unaohusu majuma sabini yanaonekana kuwa yamekamilishwa.
“Tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake Masihi aliye
Mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili” - yaani, majuma sitini na tisa, au
miaka 483. Amri ya Artashasta ilitekelezwa katika majira ya kupukutisha ya mwaka 457 K.K. Kuanzia
mwaka huo ile miaka 483 ilifika hadi majira ya kupukutisha ya mwaka 27 B.K. 334 Unabii huu ulitimizwa
wakati huu. Neno “Masihi” linaashiria “Mtiwa Mafuta.” Mwaka wa 27 B.K. katika kipindi cha kupukutisha
Kristo alibatizwa na Yohana na kutiwa mafuta na Roho Mtakatifu. Mtume Petro anashuhudia kwamba
“Mungu alimtia mafuta Yesu wa Nazareti kwa Roho Mtakatifu na kwa nguvu.” Matendo 10:38. Na
Mwokozi mwenyewe alitangaza, akisema: “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta
kuwahubiri maskini habari njema.” Luka 4:18. Baada ya kubatizwa alikwenda Galilaya, “akiihubiri
habari njema ya ufalme wa Mungu, akisema, Wakati umetimia.” Marko 1:14,15.
“Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja.” “Juma” linaloonekana hapa ni
lile la mwisho katika yale sabini; ni miaka saba ya mwisho iliyokuwa imetengwa mahsusi kwa ajili ya
Wayahudi. Katika kipindi hicho kuanzia mwaka wa 27 B.K. mpaka mwaka wa 34 B.K., Kristo, kwanza
yeye mwenyewe, na baadaye kwa wanafunzi wake, alitoa mwaliko wake wa injili hasa kwa Wayahudi.
Kadiri wanafunzi wake walivyotoka na kwenda kutangaza habari njema za ufalme, agizo la Mwokozi
kwao lilikuwa: “Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie.
Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.” Mathayo 10:5,6.
“Na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu.” Katika mwaka wa 31 B.K., yaani, miaka
mitatu na nusu baada ya ubatizo wake, Bwana wetu alisulibiwa. Kwa kafara ile kuu (328) iliyotolewa
juu ya Kalvari, mfumo wa sadaka ambao kwa miaka elfu nne ulikuwa umesonda kidole kwa Mwana-

334
Maelezo ya nyongeza yametolewa mwishoni

191
Kondoo wa Mungu ukakoma. Kivuli kilikuwa kimekutana na uhalisi wake, na sadaka na dhabihu zote na
huduma za uadhimishaji katika mfumo ule zikakoma pale.
Majuma sabini, au miaka 490, yaliyotengwa mahsusi kwa ajili ya Wayahudi, yaliisha, kama ambavyo
tumeona, katika mwaka wa 34 B.K. Wakati huo, kupitia kazi ya baraza kuu la Kiyahudi la Sanhedrin,
taifa lile lilitia muhuri wake katika kuikataa injili kwa kumwua Stefano na kuwatesa wafuasi wa Kristo.
Ndipo ujumbe wa wokovu, ukiwa haufungiwi tena katika mipaka ya walioteuliwa, ulitolewa kwa
ulimwengu wote. Wanafunzi wake, wakilazimishwa na mateso kukimbia kutoka Yerusalemu, “wakaenda
huko na huko wakilihubiri neno.” “Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria akawahubiri Kristo.”
Petro, akiongozwa na Mungu, akamfunulia injili yule akida wa Kaisaria, yaani, Kornelio aliyekuwa mcha
Mungu; na Paulo aliyekuwa motomoto, ambaye alikuwa ameongolewa katika imani ya Kristo, alipewa
agizo kuipeleka habari njema yenye furaha “mbali kwa watu wa Mataifa.” Matendo 8:4,5; 22:21.
Mpaka hapo kila ainisho la unabii limetimizwa kabisa, na mwanzo wa majuma yale sabini umekazwa
pasipo shaka katika mwaka wa 457 K.K. na mwisho wake ni katika mwaka wa 34 B.K. Kutokana na
taarifa hizi hakuna ugumu wowote katika kutafuta mwisho wa siku zile 2300. Majuma yale sabini - siku
490 - yakiwa yamekatwa kutoka katika siku 2300, kulikuwa na siku 1810 zilizobaki. Baada ya mwisho wa
siku 490, siku 1810 zilikuwa bado kutimia. Kutoka mwaka wa 34 B.K. miaka ile 1810 ilienda hadi mwaka
1844. Kwa kuwa ni hivyo, basi, siku 2300 za Danieli 8:14 zilikoma katika mwaka wa 1844. Mwisho wa
kipindi hiki kikuu cha unabii, kwa mujibu wa ushuhuda wa malaika wa Mungu, “ndipo patakatifu
patakapotakaswa.” Hivyo wakati wa kutakaswa kwa patakatifu – tukio ambalo ni kama lilisadikiwa na
wote kwamba lingetokea wakati wa kuja mara ya pili - ukawa umebainishwa wazi.
Miller na wenzake waliamini kwanza kwamba siku zile 2300 zingekoma katika majira ya vuli ya mwaka
1844, wakati unabii huo (329) unaelekeza katika majira ya kipupwe mwaka huo. 335 Kutokuelewa vema
jambo hilo kulisababisha kukata tamaa na mfadhaiko kwa wale waliokuwa wamejiweka katika nafasi ya
tarehe ya mapema zaidi kuwa ndio wakati wa marejeo ya Bwana. Lakini hilo halikuathiri hata kidogo
nguvu ya hoja ionyeshayo kwamba siku 2300 zilikoma mwaka 1844, na ya kwamba lazima tukio lile kuu
lililowakilishwa na kutakaswa kwa patakatifu litokee wakati ule.
Wakati alipoingia katika kujifunza Maandiko kama alivyokuwa amefanya, ili kuthibitisha kwamba yale
yalikuwa mafunuo kutoka kwa Mungu, mwanzoni, Miller hakuwa na matarajio hata kidogo ya kufikia
hitimisho lile ambalo alikuwa amelifikia sasa. Yeye mwenyewe aliona vigumu sana kuamini matokeo ya
uchunguzi wake. Lakini ushahidi wa Maandiko ulikuwa wazi mno na wenye nguvu kiasi kwamba
usingewekwa kando.
Alikuwa ametumia miaka miwili katika kujifunza Biblia, wakati, mwaka 1818, alipofikia kuthibitisha
kwamba katika kipindi cha miaka ishirini na tano Kristo angetokea kwa ajili ya ukombozi wa watu wake.
“Sina haja ya kusema,” alisema Miller, “habari ya furaha iliyokuwa imeujaza moyo wangu kwa sababu
ya matarajio haya ya kufurahisha, wala shauku ya moyo wangu kuhusu kushiriki katika shangwe ya
waliokombolewa. Kwangu, Biblia ilikuwa kitabu kipya sasa. Kilikuwa hasa karamu ya akili; yote yale
yaliyokuwa giza, siri, au yasiyo wazi kwangu katika mafundisho yaliyomo, yalikuwa yametoweka akilini
mwangu kwa nuru iliyo wazi ambayo sasa iliangaza kutoka katika kurasa zake takatifu; na, tazama, ni
jinsi gani ukweli ulivyo angavu na wenye utukufu! Mambo yote niliyokuwa nimeona awali kama
yanahitilafiana na kupingana katika neno yalikuwa yametoweka; na ingawa kulikuwa na sehemu nyingi
ambazo sikuridhika kwamba nilikuwa na ufahamu kamili, bado nuru kubwa sana ilikuwa imetoka ndani
yake na kuangaza mwanga katika akili yangu iliyokuwa imetiwa giza kabla, hata, katika kujifunza

335
Angalia maelezo ya nyongeza katika Kiambatanisho
192
Maandiko, nikahisi furaha ambayo sikuwa nimetarajia kama inaweza kupatikana kutokana na
mafundisho yale.” 336
“Nikiwa nimesadikishwa kabisa kwamba matukio hayo muhimu yalikuwa yametabiriwa katika Maandiko
kwamba yatimizwe katika muda mfupi namna hiyo, swali lilikuja mawazoni mwangu kwa (330) kishindo
kuhusu wajibu wangu kwa ulimwengu, kuhusu uthibitisho huo uliokuwa umeathiri mawazo yangu.” 337
Alihisi tu kwamba alikuwa na jukumu la kuwajulisha wengine nuru ile aliyokuwa ameipokea. Alitazamia
kukabiliana na upinzani toka kwa watu wasiomcha Mungu, lakini alikuwa na ujasiri kwamba Wakristo
wote wangefurahia katika tumaini la kukutana na Mwokozi ambaye walitangaza kumpenda. Hofu yake
ilikuwa tu kwamba katika furaha yao kubwa ya kutazamia kuokolewa kule kutukufu, ambako
kungetimizwa muda si mrefu, wengi wangelipokea fundisho hili bila kuyapima Maandiko kiasi cha
kutosha ili kuonyesha ukweli huu. Kwa hiyo alisita kutoa fundisho hilo, asije akawa yuko katika makosa
na kuwa njia ya kuwapotosha wengine. Alielekezwa kuupitia upya uthibitisho unaounga mkono hitimisho
alilokuwa amelifikia, na kutafakari kwa makini kila jambo gumu lililokuja lenyewe mawazoni mwake.
Aliona kwamba vipingamizi vilikuwa vimetoweka kwa nuru ya neno la Mungu kama ulivyo ukungu mbele
ya miale ya jua. Miaka mitano iliyotumika hivyo ilimwacha akiwa ameshawishika kuhusu usahihi wa
msimamo wake.
Na sasa jukumu la kuwajulisha wengine kile alichokiamini kuwa kinafundishwa wazi katika Maandiko,
lilijisukumia kwake kwa nguvu. Alisema, “Nilipokuwa katika shughuli zangu, liliendelea kulia masikioni
mwangu, ‘Nenda kauambie ulimwengu habari ya hatari yao.’ Aya hii ilikuwa inanijia kila mara:
‘Nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu mbaya, hakika utakufa, nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo,
aiache njia yake, mtu mbaya huyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi
mwako. Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache; wala yeye asiiache;
atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho yako.’ Ezekieli 33:8,9. Nilihisi kwamba
ikiwa waovu wangeonywa, wengi wao wangetubu; na ya kwamba ikiwa wasingeonywa, damu yao
ingetakiwa mkononi mwangu.” 338
Akaanza kutoa mitazamo yake hii faraghani kwa kadiri alivyoweza kupata nafasi, akiomba kwamba
mhubiri fulani angeweza kuiona nguvu ya mitazamo hii na kujituma katika kuyatangaza. Lakini
hakuweza (332) kufuta ushawishi ndani yake kwamba alikuwa na jukumu yeye mwenyewe la kufanya
katika kutoa onyo. Maneno haya yalikuwa yanajirudia tena na tena mawazoni mwake: “Nenda kauambie
ulimwengu jambo hili; damu yao nitaitaka mkononi mwako.” Alingoja kwa miaka tisa, mzigo huo ukizidi
kuelemea moyo wake, mpaka katika mwaka wa 1831 ambapo kwa mara ya kwanza alitoa hoja za imani
yake hadharani.
Kama vile Elisha alivyoitwa kuachana na kuchunga ng’ombe, ili kulipokea vazi lililowekwa wakfu kwa
kazi ya nabii, ndivyo William Miller alivyoitwa kuachana na plau yake na kuwafunulia watu siri za ufalme
wa Mungu. Akiwa anatetemeka aliingia katika kazi yake, akiwaongoza wasikilizaji wake, hatua kwa
hatua, kupitia katika vipindi vya unabii hadi kwenye marejeo ya Kristo. Kwa kila jitihada aliyoifanya
alipata nguvu na ujasiri kwa kadiri alivyoona hamu iliyoamshwa na maneno yake ikienea.
Ilikuwa kwa kuombwa na ndugu zake, ambao katika maneno yao alisikia wito wa Mungu, Miller alikubali
kutoa mitazamo yake hadharani. Sasa alikuwa na umri wa miaka hamsini, akiwa hana mazoea ya
kuhutubia hadharani, na akiwa amelemewa na hisia ya kujiona kwamba hafai kwa kazi ile iliyokuwa

336
Bliss, pages 76, 77.
337
Ibid., page 81
338
Bliss, page 92
193
mbele yake. Lakini kuanzia mwanzo kazi zake zilibarikiwa kwa namna ya ajabu hata kuweza kuwaongoa
watu. Hotuba yake ya kwanza ilifuatiwa na uamsho wa kidini ambamo familia kumi na tatu nzima
nzima, isipokuwa watu wawili, ziliongolewa. Mara akaombwa kwenda kuzungumza mahali pengine, na
karibu kila mahali kazi yake ilileta matokeo ya uamsho wa kazi ya Mungu. Wenye dhambi waliongolewa,
Wakristo waliamshwa kujitoa wakfu zaidi, na watu wenye imani isiyokubali ufunuo wale wasioamini
wakaongozwa kuikubali kweli ya Biblia na dini ya Kikristo. Ushuhuda wa wale ambao miongoni mwao
alifanya kazi ulikuwa huu: “Kundi la watu linafikiwa naye pasipo ushawishi wa watu wengine.” -Ibid.,
ukurasa wa 138. Mahubiri yake yalikusudiwa kuwaamsha watu ili wapate kutambua mambo makuu ya
dini na kuzuia hali ya kuipenda dunia na anasa vya kizazi kile.
Karibu katika kila mji walipatikana waongofu wengi, katika mingine, mamia, kama matokeo ya mahubiri
yake. Mahali pengi (332) karibu madhehebu yote ya makanisa ya Kiprotestanti yaliacha milango wazi
kwa ajili yake, na mara nyingi mialiko ya kufanya kazi huko ilitoka kwa wachungaji wa makusanyiko
kadhaa. Ilikuwa ni kanuni yake isiyobadilika kutofanya kazi mahali pale alipokuwa hajaalikwa, lakini
mara akajikuta hawezi kutimiza hata nusu ya maombi yaliyomiminika kuja kwake. Wengi ambao
hawakuyakubali maoni yake kuhusu wakati halisi wa kuja kwa Kristo mara ya pili walisadikishwa juu ya
uhakika na ukaribu wa marejeo yake Kristo na kuiona haja yao ya kujiweka tayari. Katika baadhi ya miji
mikubwa kazi yake iliwagusa sana watu. Wauzaji wa vileo waliachana na biashara yao hiyo na
kuyageuza maduka yao ya vinywaji kuwa vyumba vya mikutano; maficho ya kuchezea kamari
yalivunjiliwa mbali; wasioamini, wanaomwamini Mungu bila kukubali mafunuo yake, na wale wale
waumini wa dini inayoaminisha kwamba watu wote wataokolewa, na hata wafisadi sugu walifanyishwa
matengenezo, baadhi yao wakiwa hawajapata kuingia katika nyumba ya ibada kwa miaka mingi.
Mikutano ya maombi ilianzishwa na madhehebu mbalimbali, katika sehemu mbalimbali, karibu kila saa,
wafanya biashara wakikutana mchana adhuhuri kwa maombi na kumsifu Mungu. Hapakuwa na misisimko
iliyozidi kiasi, bali palikuwa na umakini katika ibada ulioenea katika mioyo ya watu. Kazi yake, kama ile
ya Wanamatengenezo wa awali, ilikuwa na mwelekeo wa kushawishi ufahamu na kuamsha dhamiri
kuliko kuzichochea hisia.
Mwaka 1833 Miller alipata leseni ya kuhubiri, kutoka kwa Kanisa la Kibaptisti, ambamo yeye alikuwa
mshiriki. Idadi kubwa ya viongozi wa dhehebu lake pia waliikubali kazi yake, tena aliendelea na kazi
yake kwa idhini yao rasmi. Alisafiri na kuhubiri bila kukoma, ingawa kazi zake kwa kawaida zilikuwa
zimekitwa katika mipaka ya eneo la New England na lile la Middle States. Kwa miaka kadhaa matumizi
yake yote yalitokana na pesa zake mwenyewe, na baadaye hakuweza kupata kiasi cha kutosha kukidhi
matumizi yake ya kusafiri kwenda mahali alikoalikwa. Hivyo kazi zake kwa watu, tofauti sana na
kumletea manufaa ya kifedha, zilikuwa mzigo mzito ulioelemea katika mali zake, ambazo zilipungua
taratibu katika kipindi hiki cha maisha yake. Alikuwa baba wa familia pana, lakini kwa kuwa wote
walikuwa watu wanaobana matumizi na wazalishaji katika kazi, shamba lake lilimudu kuwapatia
mahitaji wao na yeye.
(333) Katika mwaka wa 1833, miaka miwili baada ya Miller kuanza kutoa hadharani ushahidi wa
marejeo ya Kristo, ilitokea dalili ya mwisho kati ya zile zilizoahidiwa na Mwokozi kwamba ni ishara za
kuja kwake mara ya pili. Yesu alisema: “Nyota zitaanguka mbinguni.” Mathayo 24:29. Naye Yohana
katika kitabu cha Ufunuo alisema, alipoona katika maono yake matukio yatakayoashiria siku ya Mungu:
“Na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo
mwingi.” Ufunuo 6:13. Unabii huo ulitimizwa kwa namna ya kustaajabisha na kuvutia sana katika tukio
la kunyesha kwa vimondo vilivyodondoka tarehe 13 Novemba, 1833. Ilikuwa ni hali ya kuanguka kwa
nyota katika mwonekano mkubwa na wa kushangaza ambao haujapata kuwekwa katika kumbukumbu;

194
“anga lote, lililo juu ya nchi yote ya Marekani, wakati ule, kwa masaa, lilionekana kana kwamba liko
katika msukosuko wa mwako wa moto! Hakuna tukio linalohusisha kiumbe cha angani lililopata kutokea
katika nchi hii, tangu ilipokaliwa na watu kwa mara ya kwanza, ambalo lilitazamwa kwa mshangao
mkubwa na kundi moja la watu katika jamii, au kwa hofu na wasiwasi mkubwa kwa kundi jingine.
“Fahari yake na uzuri wake wa kuogofya bado viko katika mawazo ya wengi…. Kamwe mvua haikupata
kunyesha ikiwa kubwa kuliko vile vimwondo vilivyonyesha katika nchi; mashariki, magharibi, kaskazini,
na kusini, mambo yalikuwa ni yale yale. Kwa kifupi, mbingu yote ilionekana kama iko katika mwendo….
Mwonekano ule, kama ulivyoelezwa katika jarida linaloitwa Professor Silliman's Journal, ulionekana
katika Amerika ya Kaskazini yote…. Kuanzia saa nane usiku hadi mchana, mbingu zikiwa zimetulia na
bila mawingu, nuru iliyocheza-cheza mfululizo kutoka kwenye mianga iliyong’aa iliendelea kumulika
katika mbingu yote.” 339
“Hakuna lugha ambayo inaweza kupatikana kuelezea vema mwonekano wa tukio lile kushangaza na
kuvutia;…. hakuna mtu ambaye hakushuhudia mwonekano ule anayeweza kuelewa kwa ukamilifu
utukufu wa mwonekano ule. Ilionekana kama vile mbingu yote iliyojawa na nyota ilikuwa imejikusanya
katika sehemu moja juu karibu na upeo wa anga, na kama vile nyota zikawa zinajivurumisha kwa wakati
mmoja, kwa kasi ya mwako wa radi, kuelekea pande zote za upeo wa macho; wala hazikuisha … maelfu
ya hizo yalifuata katika njia za maelfu yaliyotangulia kana kwamba ni vitu vilivyoumbwa kwa ajili ya
tukio hilo.” 340 (334) “Picha nyingine ya mtini unaopukutisha mapooza yake unapotikiswa na upepo
wenye nguvu, iliyo sahihi zaidi ya hii, isingeweza kuonekana.” Imenukuliwa kutoka katika “The Old
Countryman” katika gazeti linaloitwa Portland Evening Advertiser, Nov. 26, 1833.
Katika gazeti la New York Journal of Commerce la Novemba 14, 1833, kulikuwa na makala ndefu kuhusu
kioja hiki cha ajabu, ikiwa na maneno haya: “Hakuna mwanafalsafa au mwanazuoni ye yote aliyesimulia
au kuandika tukio, nadhani, kama lile la jana asubuhi. Nabii mmoja alitabiri kwa hakika miaka elfu
moja na mia nane iliyopita kuhusu tukio hilo, kama tutapata shida kuelewa kwamba kuanguka kwa
nyota kuna maana ya nyota zinazoanguka,… katika maana yenyewe ambayo hili linaweza kuwa la kweli
kiuhalisia.”
Hivyo ndivyo ilivyoonekana dalili ya mwisho katika dalili za marejeo yake, ambazo kuhusu hizo Yesu
aliwaagiza wanafunzi wake, akisema: “Nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu
mlangoni.” Mathayo 24:33. Baada ya dalili hizo, Yohana aliona, kama tukio kuu lililokuwa linakuja,
mbingu zikipita kama ukurasa, wakati nchi ilitetemeka, milima na visiwa vikawa vinaondolewa mahali
pake, na wale waovu kwa hofu kuu wakitafuta kukimbilia mbali na uwepo wake Mwana wa Adamu.
Ufunuo 6:12-17.
Wengi walioshuhudia kule kuanguka kwa nyota, walikuangalia kama ishara ya hukumu ile ijayo,
“kiashiria cha kuogofya, kitangulizi cha hakika, ishara ya rehema, kuhusu siku ile kuu na ya
kuogofya.” 341 Kwa hiyo usikivu wa watu ulielekezwa kwenye utimilifu wa unabii ule, na wengi
walishawishiwa kuzingatia onyo la marejeo ya Yesu.
Mnamo mwaka 1840 utimilizo mwingine wa ajabu wa unabii uliamsha hamu kubwa mahali pengi. Miaka
miwili kabla, Josiah Litch, mmoja wa wahubiri wakubwa waliohubiri habari za marejeo ya Yesu,
alichapisha maelezo yake ya Ufunuo 9, akitabiri kuanguka kwa Himaya ya Ottoman. Kwa mujibu wa
kukokotoa kwake, dola hili lilikuwa lipinduliwe “katika mwaka wa 1840 B.K., muda fulani katika mwezi

339
R. M. Devens, American Progress; or, The Great Events of the Greatest Century, ch. 28, pars. 1-5
340
F. Reed, katika Christian Advocate and Journal, Des. 13, 1833
341
The Old Countryman," in Portland Evening Advertiser, Nov. 26, 1833
195
Agosti;” na siku chache tu kabla ya kutimizwa kwake, aliandika hivi: “Kwa kukubali kipindi kile cha
kwanza, miaka 150, kuwa kilitimizwa barabara kabla Deacoses hajakalia kiti cha enzi kwa kibali cha
Waturuki, na ya kwamba miaka 391, na siku 15, ilianza mwisho wa kipindi kile cha kwanza, itamalizika
tarehe 11 Agosti, 1840, wakati ambapo mamlaka ya Ottoman (335) katika Contantinople yaweza
kutazamiwa kuvunjika. Na hili, naamini, litaonekana kuwa halisi." 342.
Katika wakati ule ule uliotajwa, Uturuki, kupitia kwa mabalozi wake, ilikubali kuwa chini ya uangalizi
wa mamlaka za ushirikiano za Ulaya, na hivyo ikajiweka yenyewe chini ya udhibiti wa mataifa ya
Kikristo. Tukio hili lilitimiza barabara utabiri ule. 343 Jambo hili lilipojulikana, watu wengi walisadiki
usahihi wa kanuni za kutafsiri unabii zilizotumiwa na Miller na rafiki zake, na msukumo mkubwa wa
watu ulielekezwa kuunga mkono vuguvugu la marejeo ya Yesu (uadventisti). Watu walio wasomi na
wenye vyeo waliungana na Miller, katika kuhubiri na kuchapisha mafundisho yake, na tangu mwaka 1840
hadi 1844 kazi ile ilienea kwa haraka sana.
William Miller alikuwa na nguvu za akili, zenye fikra njema na kujifunza; na aliongeza juu ya hayo
hekima ya mbinguni kwa kujiunganisha na Chanzo cha hekima. Alikuwa mtu anayefaa sana, ambaye
alionekana kuwa mtu anayestahili heshima na kuenziwa mahali po pote ambapo uadilifu na unyofu wa
tabia ulithaminiwa. Akiunganisha wema wa moyo pamoja na unyenyekevu wa Kikristo na uwezo wa
kujitawala, alikuwa msikivu na rafiki kwa wote, akiwa tayari kusikiliza maoni ya wengine na kupima
hoja zao. Bila harara wala msisimko alizipima nadharia na mafundisho yote kwa neno la Mungu, na fikra
yake njema na ujuzi wake makini wa Maandiko vilimwezesha kukataa upotofu na kuufichua uongo.
Lakini hakufanya kazi yake bila kukabiliwa na upinzani mchungu. Kama ilivyokuwa kwa
Wanamatengenezo wa awali, kweli zile alizozihubiri hazikupokewa kwa kupendwa miongoni mwa
walimu wa dini. Kwa kuwa hawa hawakuweza kutetea msimamo wao kwa Maandiko, walilazimika
kutumia misemo na mafundisho ya dini ya wanadamu, kutumia mapokeo ya Mababa. Lakini neno la
Mungu lilikuwa ndio ushuhuda pekee uliokubaliwa na wahubiri wa ukweli wa marejeo. “Biblia, na Biblia
pekee,” lilikuwa ndilo neno lao kuu. Kile kitendo cha wapinzani wao kukosa hoja zilizojengwa katika
Maandiko kilifidiwa kwa dhihaka na dharau zao. Muda, mali na talanta vilitumika katika kuwapinga kwa
kuwaudhi wale ambao (336) kosa lao tu lilikuwa ni kutazamia kwa furaha marejeo ya Bwana wao na
walikuwa wanang’ang’ania kuishi maisha matakatifu na kuwaonya wengine ili nao wapate kujiandaa
kwa marejeo yake.
Kulikuwa na juhudi kubwa katika kuifanya mioyo ya watu igeukie mbali na fundisho la marejeo.
Kujifunza unabii unaohusiana na marejeo na mwisho wa dunia kulifanywa kuonekane kama dhambi,
kama kitu ambacho kingemfanya mtu aonee aibu. Kwa hiyo wahubiri waliokuwa maarufu walihafifisha
imani ya watu katika neno la Mungu. Mafundisho yao yaliwafanya watu kuwa wapotofu, na wengi
wakajiona kuwa huru kufuata tamaa zao zisizohusiana na Mungu. Kisha waasisi wa uovu wakaelekeza
lawama zote kuhusu uovu huo kwa Waadventisti.
Katika majumba yaliyojawa na wasikilizaji makini na wenye akili sana, jina la Miller lilitajwa na
makundi ya kidini kwa nadra isipokuwa kwa dhihaka na kupinga. Watu wasiojali na waovu wakitiwa jeuri
na msimamo wa walimu wa dini, waliazimia kumwudhi kwa kumwita majina ya matusi, kumbeza na
kumsema kwa misemo ya kejeli, katika jitihada zao za kumrundikia matusi ya kumtweza yeye na kazi
yake. Mzee mwenye kichwa chenye mvi aliyeacha nyumba yenye raha na kusafiri kwa gharama zake
mwenyewe toka jiji moja hadi jingine, toka mji mmoja hadi mwingine, akisumbuka bila kukoma

342
Josiah Litch, in Signs of the Times, and Expositor of Prophecy, Aug. 1, 1840
343
Maelezo ya nyongeza yametolewa mwishoni
196
kuupelekea ulimwengu onyo kubwa kuhusu hukumu iliyo karibu, alipingwa kwa dhihaka na kushutumiwa
kwamba ni shupavu wa dini, mwongo, mwoteaji wa kukisia-kisia.
Dhihaka, uongo, na matusi vilivyorundikwa juu yake viliamsha upinzani wenye hasira, hata kutoka kwa
watu wasio wa dini. “Kuichukulia mada iliyo kuu sana na yenye athari za kuogopesha hivyo,” kama kitu
kidogo na kwa mzaha kulionyeshwa na watu wa ulimwengu huu kuwa “si tu kufanya utani na hisia za
watu wanaoitangaza na kuitetea,” bali “ni kufanya mzaha kuhusu siku ya hukumu, kumdhihaki Mungu
Mwenyewe, na kupuuza utisho wa hukumu yake.” 344
Mwanzilishi wa maovu yote alitafuta si tu kuzuia matokeo ya ujumbe wa marejeo, bali pia
kumwangamiza mjumbe mwenyewe. Miller alifanya matumizi ya Maandiko kwa vitendo kuwa ukweli
katika mioyo ya wasikilizaji wake, yakizikemea dhambi zao na (337) kusumbua hali ya kutafuta mapenzi
yao wenyewe, na maneno yake yaliyo ya wazi na yenye kuchoma yaliamsha uadui wao. Upinzani
ulioonyeshwa na washiriki wa kanisa dhidi ya ujumbe wake ulisababisha makundi ya watu kufika mbali
katika huo; na maadui walikula njama kuyaondoa maisha yake wakati atakapokuwa anaondoka mahali
pa mkutano. Lakini malaika watakatifu walikuwa wamekusanyika pale, na mmoja wao, akiwa katika
umbile la mwanadamu, aliushika mkono wa mtumishi huyu wa Bwana na kumwongoza kwa salama bila
kuathiriwa na kundi hili la watu wenye hasira. Kazi yake ilikuwa haijafanyika bado, na Shetani na
mwakala wake walifadhaishwa katika makusudi yao.
Licha ya upinzani wote, hamu ya watu kupenda vuguvugu la harakati za marejeo ilikuwa imezidi
kuongezeka. Kutoka makumi na mamia ya watu, mikusanyiko ilikuwa imekua kiasi cha kufikia maelfu
mengi. Makundi makubwa ya waliochukua msimamo huu yalikuwa yamejitokeza katika makanisa, lakini
baada ya muda, roho ya upinzani ilidhihirishwa hata dhidi ya waongofu hawa, na makanisa yalianza
kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wale waliokuwa wameyapokea mawazo ya Miller. Kitendo hiki
kilishawishi kufanya mwitikio toka kwa kalamu yake, kuwaandikia Wakristo wa madhehebu yote,
akisisitiza kwamba ikiwa mafundisho yake yalikuwa ya uongo, angeonyeshwa kosa lake kutokana na
Maandiko.
“Tumeamini nini,” alisema, “ambacho neno la Mungu halikutuagiza kukiamini, ambalo ninyi wenyewe
mnakiri kwamba ndiyo kanuni, na kanuni pekee ya imani na matendo yetu? Tumefanya kitu gani
ambacho kinawasukuma kutupinga kwa shutuma kali hivi toka mimbarani na katika machapisho, na
kuwapa sababu ya haki ya kututenga (Wanamarejeo) toka katika makanisa yenu na ushirika wenu?”
“Ikiwa tumekosea, salini mtuonyeshe kosa letu. Tuonyesheni toka katika neno la Mungu kwamba
tumekosea; tumedhihakiwa vya kutosha; kiasi kwamba hatuwezi kushawishika kwamba tuko katika
makosa; neno la Mungu pekee linaweza kugeuza mtazamo wetu. Hitimisho la msimamo wa maoni yetu
limefikiwa kwa uangalifu mkubwa sana na kwa maombi, kama sisi tulivyouona ushahidi wa
Maandiko.” 345
Toka kizazi hata kizazi maonyo ambayo Mungu ameyatuma kwa ulimwengu kwa kutumia watumishi
wake yamekuwa yakipokewa kwa mashaka na kutoamini namna hiyo. Wakati uovu wa watu walioishi
kabla ya gharika (338) ulipomsukuma Mungu kuleta gharika ya maji juu ya dunia, aliwajulisha kwanza
njia zake, ili ya kwamba wapate nafasi ya kugeuka kutoka katika njia zao mbaya. Kwa miaka mia na
ishirini onyo la kuwataka watubu lilisikika masikioni mwao, ili ya kwamba ghadhabu ya Mungu isije
ikadhihirishwa na kuwaletea uharibifu. Lakini ujumbe ule ulionekana kwao kama hadithi ya uongo, wala
hawakuuamini. Wakijawa na kiburi katika uovu wao, walimdhihaki mjumbe wa Mungu, wakakuchukulia

344
Bliss, page 183
345
Ibid., pages 250, 252
197
kwa wepesi kule kusihi kwake, hata wakamlaumu kwamba ni mtu mwenye mambo ya kufikirika tu.
Inawezekanaje mtu mmoja adiriki kusimama kinyume cha wakubwa wote wa dunia? Ikiwa ujumbe wa
Nuhu ulikuwa wa kweli, kwa nini ulimwengu wote haukuuona na kuuamini? Yaani madai ya mtu mmoja
dhidi ya hekima ya maelfu ya watu! Hawakuthamini onyo lile, wala hawakutaka kutafuta hifadhi katika
safina.
Wenye dhihaka walisonda kidole kwa mambo ya asili, - kuonyesha majira ya mwaka yanayofuatana bila
kubadilika, kuonyesha mbingu zenye rangi ya bluu ambazo zilikuwa hazijapata kamwe kumwaga mvua,
kuonyesha mashamba ya kijani yaliyonyweshwa na umande laini wa usiku, - kisha wakapiga makelele
wakisema: “Je, huyu hasemi hadithi tu?” Kwa dharau walimtangaza mhubiri huyu wa haki kuwa ni mtu
mwenyea msimamo wa uendawazimu; na wakaendelea kwa hamasa zaidi katika kutafuta anasa zao,
wakinuia kuendelea na njia zao mbaya, kuliko kabla. Lakini kutokuamini kwao hakukuzuia tukio
lililotabiriwa. Mungu alivumilia uovu wao kwa muda mrefu, akiwapa nafasi ya kutosha ili kutubu; lakini
kwa wakati uliokubalika hukumu zake zikawajilia wale walioikataa rehema yake.
Kristo anasema kwamba kutakuwa na kutokuamini kwa namna ile ile katika habari ya kuja kwake mara
ya pili. Kama vile ambavyo watu wa siku za Nuhu “hawakutambua, hata Gharika ikaja, ikawachukua
wote, ndivyo,” katikaa maneno ya Mwokozi wetu, “kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.”
Mathayo 24:39. Wakati wale wanaojiita watu wa Mungu wanapoungana na ulimwengu, wakiishi vile
wanavyoishi, na kuungana nao katika starehe zilizokatazwa; wakati anasa za ulimwengu zinapokuwa
anasa za kanisa; wakati kengele za harusi zinapolia, na wote wanapotazamia kuwa na miaka mingi ya
usitawi wa kiulimwengu - ndipo, ghafla kama vile umeme wa radi umulikavyo kutoka mbinguni, utakuja
mwisho wa njozi zao njema na matumaini yapotoshayo.
Kama vile Mungu alivyomtuma mtumishi wake kuuonya ulimwengu juu ya Gharika iliyokuwa inakuja,
ndivyo alivyowatuma wajumbe wake kufanya kukaribia kwa hukumu ya mwisho kujulikane. Na kama
watu wa wakati wa wa Nuhu walivyocheka na kupuuza utabiri wa mhubiri yule wa haki, ndivyo katika
siku za Miller wengi, hata walio miongoni mwa wale wajiitao watu wa Mungu, walivyoyadharau maneno
ya onyo.
Na ni kwa nini fundisho na mahubiri ya marejeo ya Kristo hayakupokewa hivyo na makanisa? Wakati
marejeo ya Bwana yanaleta ole na maangamizi kwa waovu, kwa wenye haki yamejaa furaha na tumaini.
Ukweli huu mkuu umekuwa faraja kwa waaminifu wa Mungu katika vizazi vyote; mbona ulikuwa
umekuwa, kama alivyo Mwasisi wake, “jiwe la kujikwaza” na “mwamba wa kujikwaa” kwa watu
wanaojiita walio wake? Ni Bwana wetu mwenyewe aliyewaahidi wanafunzi wake: “Basi mimi nikienda
na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu.” Yohana 14:3. Alikuwa Mwokozi mwenye
huruma, ambaye, akitarajia hali ya upweke na huzuni kwa wafuasi wake, aliwaagiza malaika kuwafariji
kwa kuwapa uhakika kwamba angekuja tena kama alivyo, kama vile alivyoenda mbinguni. Kadiri
wanafunzi walivyokaza macho juu kumwona kwa mara yao ya mwisho yeye waliyempenda, usikivu wao
ulivutwa na maneno: “Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu
aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake
mbinguni.” Matendo 1:11. Tumaini likawashwa upya kwa ujumbe wa malaika. Wanafunzi wale
“wakarudi Yerusalemu wenye furaha kuu. Nao walikuwa daima ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu.”
Luka 24:52,53. Hawakuwa na furaha kwa sababu Yesu alikuwa ametengwa mbali nao na wao waliachwa
peke yao kupambana na majaribu na vishawishi vya ulimwengu huu, bali kwa sababu ya uthibitisho wa
malaika wale kwamba angerudi tena.

198
Tangazo la marejeo ya Kristo liwe sasa, kama wakati lilipotolewa na malaika kwa wachungaji wa kondoo
wa Bethlehemu, (340) habari njema za furaha kuu. Watu wale ambao wanampenda Mwokozi kweli
kweli hawawezi kukosa kushangilia kwa furaha tangazo hilo lililojengwa katika neno la Mungu ya
kwamba Yeye ambaye kwake yanaelekea matumaini yao ya uzima wa milele anakuja tena, sio kuja
kutukanwa, kudharauliwa, na kukataliwa, kama wakati alipokuja mara ya kwanza, bali katika uweza na
utukufu kuwakomboa watu wake. Wale wasiompenda Mwokozi ndio ambao wanatamani aendelee kubaki
mbali, na hakuwezi kuwapo ushahidi wa hitimisho zaidi kwamba makanisa yametawanyika mbali na
Mungu kuliko hasira na chuki vinavyochochewa na ujumbe huu uliotumwa kutoka Mbinguni.
Wale waliolipokea fundisho la marejeo ya Kristo waliamshwa kuona umuhimu wa kufanya toba na
kujinyenyekeza mbele zake Mungu. Wengi walikuwa wakihamahama katikati ya Kristo na ulimwengu
kwa muda mrefu; sasa walihisi kwamba ulikuwa wakati wa kuchukua msimamo. “Mambo yale ya milele
yalikuwa kwao kama mambo yenye uhalisia usio kifani. Mbingu ililetwa karibu yao, na wakajisikia
wamba walikuwa na hatia mbele za Mungu.” 346 Wakristo waliharakishwa kwenda katika maisha mapya.
Walipewa kuhisi kwamba muda ulikuwa mfupi, kwamba kile walichopaswa kufanya kwa ajili ya
wanadamu wenzao kilikuwa hakina budi kufanywa haraka. Dunia ilitoweka, umilele ukaonekana kama
unafunguka mbele yao, na roho, pamoja na mambo yote yaliyohusu hatima yake njema au mbaya ya
milele, yalionekana kufunika kila kitu kilicho cha muda tu. Roho wa Mungu alikaa juu yao na kuyapa
nguvu maneno yao waliyotumia kuwasihi ndugu zao, pamoja na wenye dhambi, ili wapate kujiweka
tayari kwa siku ya Mungu. Ushuhuda wa kimya wa maisha yao ya kila siku ukawa ni kemeo la kudumu
kwa washiriki wa kanisa waliozoea kufuata desturi tu na ambao walikuwa hawajajitoa sawasawa. Watu
hawa hawakutaka kusumbuliwa katika makusudi yao ya kutafuta anasa zao, kujielekeza katika kutafuta
fedha, na tamaa yao ya kutafuta kupata heshima ya ulimwenguni. Hivyo uadui na upinzani uliamshwa
dhidi ya imani ya marejeo na dhidi ya wale walioitangaza.
Kadiri hoja zinazotokana na vipindi vya unabii zilivyoonekana kutopingika, wapinzani wakaazimia
kuhafifisha uchunguzaji wa somo lile kwa kufundisha kwamba unabii ule ulikuwa umefungwa. Hivyo
Waprotestanti walifuata nyayo za Warumi. Wakati kanisa la kipapa linaficha Biblia 347 watu wasiwe
nayo, makanisa ya Kiprotestanti nayo yalidai kwamba (341) sehemu muhimu ya Neno Takatifu – yaani
sehemu ile inayozifunua zile kweli zinazohusika sana na wakati wetu – haiwezi kueleweka.
Viongozi wa kiroho na watu wa kawaida walitangaza kwamba unabii wa Danieli na Ufunuo ulikuwa na
mafumbo ya siri. Lakini Kristo aliwaelekeza wanafunzi wake kwenye maneno ya nabii Danieli kuhusu
matukio ambayo yangetokea katika nyakati zao, akisema: “Asomaye na afahamu.” Mathayo 24:15. Na
madai kwamba kitabu cha Ufunuo ni fumbo, yaani, kisichoweza kueleweka, yanapingana na kichwa
chenyewe cha kitabu hicho: “Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake
mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi…. Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya
unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.” Ufunuo 1:1-3.
Nabii anasema: “Heri asomaye” - wako wale ambao hawatasoma; heri hiyo si kwa ajili yao. “Na wao
wasikiao” - wako wengine, pia, wanaokataa kusikiliza kitu cho chote kinachohusiana na unabii; heri hiyo
si kwa ajili ya kundi hili. “Na kuyashika yaliyoandikwa humo” - wengi wanakataa kuzingatia maonyo na
mafundisho yaliyomo katika Ufunuo; hakuna yeyote miongoni mwa hawa awezaye kudai heri
iliyoahidiwa. Wote wanaodhihaki mafundisho hayo ya unabii na kuvifanyia mzaha vielelezo vilivyotolewa

346
Bliss, page 146
347
Angalia maelezo ya nyongeza katika Kiambatanisho
199
thabiti, wote wanaokataa kutengeneza upya maisha yao na kujiandaa kwa ajili ya marejeo ya Mwana wa
Adamu, hawatakuwa heri.
Kuhusu ushuhuda wa Ufunuo, inakuwaje watu wanathubutu kufundisha kwamba kitabu cha Ufunuo ni
siri ambayo haiwezi kufikiwa na ufahamu wa mwanadamu? Ni siri iliyofunuliwa, kitabu kilichofunuliwa.
Kujifunza Ufunuo huyaongoza mawazo kwenye unabii wa Danieli, na vitabu hivi viwili hutoa mafundisho
muhimu zaidi, yaliyotolewa na Mungu kwa wanadamu, yakihusu matukio yatakayotokea wakati wa
kufungwa kwa historia ya dunia.
Yohana alifunuliwa mambo yenye kina na ya kusisimua katika uzoefu wa kanisa. Aliona nafasi, hatari,
mapambano, na ukombozi wa mwisho wa watu wa Mungu. (342) Anaandika ujumbe wa kufungia
utakaoyafanya mavuno ya nchi yakomae, ama kama mavuno safi yatakayowekwa katika ghala ya
mbinguni, ama kama matita ya kuchomwa katika mioto iharibuo. Masomo yenye maana sana
yalifunuliwa kwake, hasa kwa ajili ya kanisa la mwisho, ya kwamba wale watakaoachana na mafundisho
potofu na kuigeukia kweli wapate kupewa mafundisho kuhusu hatari na mapambano yaliyo mbele yao.
Hakuna anayehitaji kuwa gizani kuhusu kile kinachoujia ulimwengu.
Kwa nini, basi, kuna ujinga ulioenea kuhusu sehemu muhimu ya Maandiko Matakatifu? Kwa nini watu
wengi hawapendi kuyachunguza mafundisho yake? Hayo ni matokeo ya juhudi iliyopangiliwa ya yule
mkuu wa giza kutaka kuwaficha wanadamu kile kinachoyaweka wazi madanganyo yake. Kwa sababu
hiyo, Kristo Mfunuaji, aliona kwa mbali vita ambayo ingetokea dhidi ya kujifunza mafundisho ya kitabu
cha Ufunuo, alitamka baraka za heri kwa wote ambao wangesoma, kusikia, na kuyashika maneno ya
unabii huu.

200
Sura ya 19
NURU YAPENYA GIZANI
Kazi ya Mungu duniani inaonyesha, toka kizazi hata kizazi, kufanana kwa namna ya ajabu kwa kila
matengenezo makuu au vuguvugu la mabadiliko ya kidini. Kanuni za Mungu katika kushughulika na
wanadamu ni zile zile daima. Harakati muhimu za sasa zinalandana na zile za wakati uliopita, na uzoefu
wa mambo ya kanisa katika zama zilizopita yana mafundisho ya thamani kuu kwa ajili ya wakati wetu.
Hakuna ukweli unaofundishwa kwa uwazi zaidi katika Biblia kama huu ya kwamba Mungu hasa kwa njia
ya Roho wake Mtakatifu anawaongoza watumishi wake duniani katika harakati kuu za kuisukuma mbele
kazi ya wokovu. Wanadamu ni vyombo mkononi mwa Mungu, ambao wanatumiwa naye kutekeleza
makusudi yake ya neema na rehema. Kila mmoja anayo sehemu yake ya kufanya, kwa kila mmoja
kimetolewa kiasi cha nuru, ambacho hutolewa kukidhi mahitaji ya wakati wake, na ambacho
kinatosheleza kumfanya aweze kutenda kazi ile aliyopewa na Mungu kufanya. Lakini hakuna
mwanadamu yeyote, hata awe ameheshimiwa na mbingu kiasi gani, ambaye amewahi kupata ufahamu
kamili wa mpango mkuu wa ukombozi, au hata kuelewa kwa ukamilifu kusudi la mbingu katika kazi
mnamo wakati wa kipindi chake anachoishi. Wanadamu hawajui kwa ukamilifu kile ambacho Mungu
angeweza kutimiza kupitia kazi anayowapa kufanya; hawawezi kufahamu, katika nyanja zote, ujumbe
ule wanaoutangaza katika jina lake.
“Je! wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu? Waweza kuufikilia upeo wa huyo Mwenyezi?” “Maana
mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema (344) BWANA. Kwa maana kama
vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo
yangu kuliko mawazo yenu.” “Mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi; nitangazaye mwisho tangu
mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado.” Ayubu 11:7; Isaya 55:8,9; 46:9,10.
Hata manabii waliopendelewa kwa kupewa nuru maalum ya Roho hawakufahamu kwa ukamilifu maana
ya mafunuo waliyokabidhiwa. Maana yake ilikusudiwa kufunuliwa toka kizazi hata kizazi kwa kadiri
ambavyo watu wa Mungu wangehitaji mafundisho yaliyokuwa ndani yake.
Petro, akiandika habari ya wokovu uliofunuliwa na injili, anasema: Kwa habari ya wokovu huu “manabii
walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi.
Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao,
ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya
hayo. Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yetu walihudumu katika mambo
hayo.” 1 Petro 1:10-12.
Hata hivyo ingawa manabii wale hawakupewa uwezo wa kuelewa kikamilifu mambo yaliyofunuliwa
kwao, walitafuta kwa dhati kuipata nuru yote ambayo Mungu alipendezwa kuwafunulia. Wao
“walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, “Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani

201
ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao.” Ni fundisho la jinsi gani kwa watu wa Mungu waishio
katika kizazi cha Kikristo, ambao kwa faida yao unabii huu ulitolewa kwa watumishi wake!
“Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yetu walihudumu katika mambo hayo.”
Shuhudia jinsi watu wale watakatifu wa Mungu walivyo“tafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza kwa
bidii” habari ya mafunuo waliyopewa kwa ajili ya vizazi vilivyokuwa havijazaliwa bado. Linganisha kati
ya bidii yao takatifu na kutojali kusiko na idadi ambako kwa huko watu waliopendelewa wa vizazi vya
baada ya pale wanakitendea kipawa cha Mbinguni. Ni kemeo la jinsi gani kwa mpenda starehe, mpenda
ulimwengu asiyejali ambaye anaridhika kutangaza kwamba unabii hauwezi kueleweka!
Ingawa akili finyu za wanadamu hazitoshi kuingia (345) katika mashauri yake Aliye wa Milele, au
kuelewa kikamilifu utendaji wa makusudi yake, hata hivyo mara nyingi ni kwa sababu ya kosa fulani au
kupuuza kwa upande wao kwamba wanaelewa kwa uhafifu sana ujumbe wa Mbinguni. Si mara chache
ambapo mawazo ya wanadamu, na hata ya watumishi wa Mungu, hupofushwa na maoni ya wanadamu,
mapokeo na mafundisho ya uongo ya wanadamu, kiasi kwamba wana uwezo wa kuelewa kwa sehemu
ndogo tu mambo makuu ambayo Mungu ameyafunua katika neno lake. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa
wanafunzi wa Kristo, hata wakati Mwokozi alipokuwa pamoja nao katika mwili. Mawazo yao yalikuwa
yamejazwa na maoni yaliyopendwa na wengi kumhusu Masihi kama mfalme wa muda tu, ambaye
angewainua Israeli katika kiti cha enzi cha himaya yote, na hawakuweza kuelewa maana ya maneno
yake yaliyotabiri habari ya mateso na kifo chake.
Kristo mwenyewe alikuwa amewatuma na ujumbe: “Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia;
tubuni, na kuiamini Injili.” Marko 1:15. Ujumbe ule ulijengwa juu ya msingi wa unabii wa Danieli 9.
Majuma yale sitini na tisa yalitangazwa na yule malaika kufika hata zamani zake “Masihi aliye Mkuu,” na
kwa matumaini makuu na matarajio yaliyojaa furaha wanafunzi wale wakatazamia kuanzishwa kwa
ufalme wa Masihi pale Yerusalemu ili kutawala dunia nzima.
Waliuhubiri ujumbe ule ambao Kristo alikuwa amewakabidhi, ingawa wao wenyewe waliielewa vibaya
maana yake. Wakati tangazo lao lilikuwa na msingi wake katika Danieli 9:25, wao hawakuona, katika
fungu linalofuata la sura ile ile, kwamba Masihi atakatiliwa mbali. Tangu kuzaliwa kwao mioyo yao
ilikuwa imekazwa kwa matarajio ya utukufu wa himaya ya kidunia, na hili lilipofusha ufahamu wao kwa
kiwango kimoja kuhusu maelezo ya unabii na kuhusu maneno ya Kristo.
Walifanya jukumu lao katika kulitangazia taifa la Wayahudi mwaliko wa rehema, na halafu, katika
wakati wenyewe hasa walipotazamia kumwona Bwana wao akipanda kukalia kiti cha enzi cha Daudi,
wakamwona akitiwa nguvuni kama mhalifu, akipigwa vikali, kudhihakiwa, na kuhukumiwa hatia, na
akainuliwa juu katika msalaba wa (346) Kalvari. Ni kukata tamaa na uchungu wa moyo ulioje
vilivyoumiza mioyo ya wanafunzi wale katika siku zile Bwana wao alipokuwa amelala kaburini!
Kristo alikuwa amekuja katika wakati sahihi kabisa na kwa njia iliyotabiriwa na unabii. Ushuhuda wa
Maandiko ulikuwa umetimizwa kwa kila kipengele cha huduma yake. Alikuwa ameuhubiri ujumbe wa
wokovu, na “neno lake lilikuwa na uwezo.” Mioyo ya wasikilizaji wake ilikuwa imeshuhudia kwamba
ulikuwa ujumbe wa mbinguni. Neno na Roho wa Mungu viliushuhudia utume ule wa Mwana wake.
Bado wanafunzi walikuwa wanaushikilia upendo usiokoma kwa Bwana wao mpendwa. Lakini mawazo yao
yalifunikwa na wasiwasi na mashaka. Katika uchungu wao wakati ule hawakuweza kukumbuka maneno
ya Kristo yaliyosonda kidole kwenye mateso na kifo chake. Ikiwa Yesu wa Nazareti alikuwa ndiye Masihi
kweli, inakuwaje wametumbukizwa hivyo katika majonzi na kukata tamaa namna hii? Hili ndilo swali
lililotesa mioyo yao wakati Mwokozi alipokuwa amelala kaburini mwake katika saa zisizo na matumaini
za Sabato zilizokuwa katikati ya kifo chake na kufufuka kwake.
202
Ingawa usiku wa huzuni ulikusanya giza kuwazunguka wafuasi hawa wa Yesu, bado hawakuachwa.
Anasema nabii: “Nikaapo gizani, BWANA atakuwa nuru kwangu…. Atanileta nje kwenye nuru, nami
nitaiona haki yake.” “Giza nalo halikufichi kitu, bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga
kwako ni sawasawa.” Mungu amenena hivi: “Nuru huwazukia wenye adili gizani.” “Nitawaleta vipofu
kwa njia wasiyoijua; katika mapito wasiyoyajua nitawaongoza; nitafanya giza kuwa nuru mbele yao; na
mahali palipopotoka kuwa pamenyoka. Haya nitayatenda, wala sitawaacha.” Mika 7:8,9; Zaburi 139:12;
112:4; Isaya 42:16.
Tangazo la injili lililokuwa limetolewa na wanafunzi wale katika jina la Bwana lilikuwa sahihi kwa kila
hali, na matukio yaliyosondwa kidole na tangazo lile yalikuwa yanatokea hata wakati ule. “Wakati
umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia,” ulikuwa (347) umekuwa ujumbe wao. Mwisho wa “wakati”
- yale majuma sitini na tisa ya Danieli 9, ambayo yalipaswa kufika hadi wakati wa Masihi, “Mpakwa
Mafuta” - Kristo alikuwa amepakwa mafuta na Roho baada ya kubatizwa na Yohana katika Yordani. Na
“ufalme wa Mungu” waliokuwa wameutangaza kwamba umekaribia ulianzishwa na kifo cha Kristo.
Ufalme huu haukuwa, kama walivyokuwa wamefundishwa kuamini, himaya ya kidunia. Wala haukuwa
ufalme ule wa milele wa baadaye ambao utasimamishwa wakati ambapo “ufalme, na mamlaka, na ukuu
wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye Juu;” ule ufalme wa
milele, ambamo “wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.” Danieli 7:27. Kama ulivyotumika
katika Biblia, usemi huu “ufalme wa Mungu” unatumika kuonyesha falme zote mbili, ufalme wa neema
na ufalme wa utukufu. Ufalme wa neema unaonyeshwa na Paulo katika Waraka kwa Waebrania. Baada
ya kumwonyesha Kristo, Mwombezi wetu mwenye huruma, ambaye “anachukuana nasi katika mambo
yetu ya udhaifu,” mtume huyo anasema: “Basi, na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe
rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.” Waebrania 4:15,16. Kiti cha neema
kinawakilisha ufalme wa neema; maana kule kuwako kwa kiti cha enzi kunamaanisha kuwako kwa
ufalme. Katika mifano yake mingi, Kristo anatumia usemi huu “ufalme wa mbinguni” kuonyesha kazi ya
neema ya Mungu katika mioyo ya wanadamu.
Hivyo kiti cha enzi cha utukufu huwakilisha ufalme wa utukufu; na ufalme huo unarejewa katika
maneno ya Mwokozi: “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu
wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika
mbele zake.” Mathayo 25:31,32. Ufalme huo bado uko mbele. Hautasimamishwa mpaka wakati wa kuja
kwa Kristo mara ya pili.
Ufalme wa neema ulianzishwa mara tu baada ya anguko la mwanadamu, wakati mpango ulipobuniwa
kwa ajili ya ukombozi wa jamii yenye hatia. Kisha uliendelea kuwepo katika nia na ahadi ya Mungu; na
kwa njia ya imani, wanadamu wangeweza kuwa raia wa ufalme huo. Hata hivyo, haukuanzishwa rasmi
mpaka kifo cha (348) Kristo. Hata baada ya kuanza utume wake hapa duniani, Mwokozi, akiwa
amechoshwa na usumbufu na utovu wa shukrani wa wanadamu, angeweza kujiondoa na kuachana na
kafara ya Kalvari. Kule Gethsemane kikombe cha huzuni kilitetemeka mkononi mwake. Hata wakati ule
angeweza kupangusa jasho lake la damu kutoka usoni mwake na kuiacha jamii yenye hatia iangamie
katika uovu wake. Ikiwa angefanya hivyo, kusingelikuwa na ukombozi kwa wanadamu walioanguka.
Lakini Mwokozi alipoyatoa maisha yake, na kwa pumzi yake ya mwisho akalia, “Imekwisha,” ndipo
utimilifu wa mpango wa ukombozi ulipodhihirika. Ahadi ya wokovu iliyotolewa kwa watu wawili wenye
dhambi ndani ya Edeni iliidhinishwa. Ufalme wa neema, ambao hapo kwanza ulikuwako kwa ahadi ya
Mungu, ndipo ukawa umeanzishwa.
Hivyo, kifo cha Kristo - tukio lile ambalo wanafunzi wale waliliona kama uharibifu wa mwisho wa
tumaini lao - ndicho kilicholifanya kuwa hakika milele. Wakati kiliwaletea kukata tamaa kwa ukatili,
203
kilikuwa ndicho kilele cha uthibitisho ulioonyesha kwamba imani yao ilikuwa sahihi. Tukio lililokuwa
limewajaza maombolezo na kukata tamaa, ndilo lililoufungua mlango wa matumaini kwa kila mwana wa
Adamu, na ambalo lilikuwa kiini cha maisha ya baadaye na furaha ya milele ya waaminifu wote wa
Mungu katika vizazi vyote.
Makusudi ya rehema isiyo mwisho yalikuwa yanaufikia utimilifu wake, hata kupitia katika kufadhaika
kwa wanafunzi wake. Wakati mioyo yao ilikuwa imeongolewa na neema na uwezo wa mafundisho yake,
yeye ambaye “hajanena kamwe mtu yeyote kama huyu anavyonena,” bado kilichokuwa
kimechanganywa nayo pamoja na dhahabu safi ya upendo wao kwa Yesu, ilikuwa ni kuchanganya kiburi
cha kidunia na mivuto ya ubinafsi. Hata katika chumba kile walicholia Pasaka, katika saa ile ya kutisha
wakati Bwana alipokuwa tayari anaingia katika kivuli cha Gethsemane, palikuwa na “mashindano kati
yao, kwamba ni nani anayehesabiwa kuwa mkubwa.” Luka 22:24. Matarajio yao yalijazwa na kiti cha
enzi, taji ya kifalme, na utukufu, wakati mbele yao palikuwa na aibu na maumivu makali ya bustanini,
ukumbi wa hukumu, msalaba ule wa Kalvari. Ni kiburi kile kilichokuwa ndani ya moyo wao, kiu yao ya
kutaka kuwa na (349) utukufu wa dunia hii, kilichowafanya kuyang’ang’ania sana mafundisho potofu ya
wakati wao, na kutoyazingatia maneno yale aliyosema Mwokozi yanayoonyesha jinsi ufalme wake ulivyo
hasa, na kuwaelekeza mbele kwenye mateso yake na kifo chake. Na makosa haya yaliwaletea majaribu
- makali lakini yanayohitajika - ambayo yaliruhusiwa kwa ajili ya kuwasahihisha. Ingawa wanafunzi wale
walikuwa wamekosea kuelewa maana ya ujumbe wao, na walikuwa wameshindwa kuyapata matarajio
yao, bado walikuwa wamelihubiri onyo walilopewa na Mungu, na Bwana angeweza kuwapa thawabu kwa
imani yao ile na kuheshimu utii wao. Kwao ingekabidhiwa kazi ya kuitangaza kwa mataifa yote injili
tukufu ya Bwana wao aliyefufuka. Ilikuwa ni kwa ajili ya kuwaandaa kwa kazi kwamba uzoefu
ulioonekana kuwa mchungu sana uliruhusiwa kuwapata.
Baada ya kufufuka kwake, Yesu aliwatokea wanafunzi wake wakiwa njiani kwenda Emau, naye “akaanza
kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika Maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.”
Luka 24:27. Mioyo ya wanafunzi wale iliwaka moto ndani yao. Imani iliamshwa. Wakawa wamezaliwa
mara ya pili ili wapate tumaini lenye uzima hata kabla Yesu hajajifunua mwenyewe kwao. Lilikuwa ni
kusudi lake kuwatia nuru katika ufahamu wao na kuikaza imani yao juu ya lile “neno la unabii lililo
imara zaidi.” Alitamani kwamba ukweli upate kuotesha mizizi imara ndani ya mioyo yao, si kwa sababu
tu iliungwa mkono kwa ushuhuda wake mwenyewe alioutoa, bali kwa sababu ya ushahidi usio na
mashaka ulioonyeshwa kwa mifano na vivuli vya sheria ya kafara na kwa njia ya unabii wa Agano la
Kale. Ilikuwapo haja kwa wafuasi wa Kristo kuwa na imani iliyojengwa katika ujuzi, si kwa ajili yao peke
yao, bali ya kwamba waweze kupeleka maarifa ya kumjua Kristo kwa ulimwengu mzima. Na kama hatua
ya kwanza kabisa ya kutoa maarifa, Yesu aliwaelekeza wanafunzi wale kwa “Musa na manabii wote”.
Huo ulikuwa ndio ushuhuda uliotolewa na Mwokozi aliyefufuka kuonyesha thamani na umuhimu wa
Maandiko ya Agano la Kale.
Ni badiliko kubwa jinsi gani lililotokea mioyoni mwa wanafunzi walipoutazama tena uso wa (350) Bwana
wao walioupenda! Luka 24:32. Katika mtazamo wa ukamilifu na usahihi zaidi kuliko kabla walikuwa
“wamemwona yeye ambaye Musa aliandika habari zake katika torati na manabii.” Hali ya mashaka,
uchungu, mfadhaiko viliondoka na mahali pake kukawa na uhakika wenye ukamilifu, imani isiyo na
wingu la giza. Ni ajabu kiasi gani kwamba baada ya kupaa kwake wao “walikuwa daima ndani ya hekalu
wakimsifu Mungu.” Watu, waliokuwa wanajua tu habari za kifo cha Mwokozi cha aibu, waliwaangalia ili
kuona nyusoni mwao dalili za huzuni, kutanzika, na kushindwa; lakini waliona furaha na ushindi.
Wanafunzi walikuwa wamepata maandalizi yaliyoje kwa ajili ya kazi iliyokuwa mbele yao! Walikuwa
wamepita katika jaribio la kina sana ambalo liliwezekana kwao kupata uzoefu, na walikuwa wameona

204
jinsi, wakati mambo yote yanapoonekana kushindwa kwa mtazamo wa mwanadamu, neno la Mungu
lilivyokuwa limetimizwa kwa ushindi. Kuanzia pale na kuendelea ni kitu gani kingeweza kuizima imani
yao au kupoza nguvu ya upendo wao? Wakati wa huzuni ya kiwango cha juu walikuwa wamepata “faraja
iliyo imara,” yaani, tumaini lililokuwa kama “nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu.” Waebrania
6:18,19. Walikuwa wamekuwa mashahidi wa hekima na uweza wa Mungu, nao walikuwa “wamekwisha
kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo,
wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho
chote, hakitaweza kuwatenga mbali na “upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.” “Lakini
katika mambo hayo yote,” walisema, “tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.”
Warumi 8:38, 39, 37. “Bali Neno la Bwana hudumu hata milele.” 1 Petro 1:25. Tena, “Ni nani
anayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu,
naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.” Warumi 8:34.
Asema Bwana: “Watu wangu hawatatahayari kamwe.” Yoeli 2:26. “Huenda kilio kikaendelea usiku
kucha, lakini furaha huja asubuhi.” Zaburi 30:5. Wakati wanafunzi walipokutana na Mwokozi siku ile ya
ufufuko wake, na mioyo yao ilipowaka ndani yao walipokuwa wakiyasikiliza maneno yake; walipotazama
kichwa na mikono na miguu yake iliyokuwa imejeruhiwa kwa ajili yao; wakati Yesu, kabla ya kupaa
kwake, alipowaongoza (351) kwenda mbali mpaka Bethania, na kuinua mikono yake juu kwa baraka,
aliwaagiza, “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili,” akaongeza, “Na tazama, mimi nipo
pamoja nanyi siku zote” (Marko 16:15; Mathayo 28:20); wakati yule Mfariji aliyeahidiwa aliposhuka siku
ya Pentekoste na nguvu kutoka juu ikatolewa kwao na watu wale walioamini walipofurahi sana
kutambua kuwapo kwake Bwana wao aliyekuwa amepaa - wakati ule, hata kama njia yao, kama yake,
iliwapitisha katika kutoa kafara maisha yao na kuuawa kama wafia-dini, je, wangekuwa wamebadilisha
huduma ya injili ya neema yake Bwana, pamoja na “taji ya haki” itakayopokelewa wakati wa kuja
kwake, kwa utukufu wa kiti cha enzi cha duniani, kitu ambacho ndicho kilikuwa tumaini la uanafunzi
wao wa awali? Yeye “awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo”
alikuwa amewapa, pamoja na ushirika wa mateso yake, ushirika wa furaha yake - furaha ile ya
“kuwaleta wana wengi waufikilie utukufu,” “furaha isiyoneneka,” “utukufu wa milele uzidio kuwa
mwingi sana,” ambao Paulo anasema, “dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu,” “haiwezi
kulinganishwa.”
Uzoefu wa wanafunzi walioihubiri “injili ya ufalme” wakati ule wa kuja kwa Kristo mara ya kwanza,
yana mfanano wake katika uzoefu wa wale waliotangaza ujumbe wa kuja kwake mara ya pili. Kama
wanafunzi walivyotoka kwenda kuhubiri, wakisema, “Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu
umekaribia,” ndivyo Miller na wenzake walivyotangaza kwamba kile kipindi kirefu na cha mwisho cha
unabii kilichofunuliwa katika Biblia kilikuwa kinakaribia kufika mwisho, kwamba hukumu ilikuwa
imewadia, na ufalme wa milele ulikuwa karibu kuanza. Mahubiri ya wanafunzi wale kuhusu wakati
yalijengwa kwenye majuma sabini ya Danieli 9. Ujumbe ule uliotolewa na Miller na wenzake ulitangaza
mwisho wa zile siku 2300 za Danieli 8:14, ambazo yale majuma sabini ni sehemu yake. Mahubiri juu ya
kila kipindi kati ya hivyo viwili yalitegemea kutimizwa kwa sehemu tofauti ya kipindi kikuu cha unabii
hicho hicho.
Kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa kwanza, William Miller na wenzake hawakufahamu, wao wenyewe,
kwa ukamilifu maana ya ujumbe ule walioupeleka. Upotofu ambao ulikuwa umeshajengeka (352) katika
kanisa kwa muda mrefu uliwazuia wasiweze kuifikia tafsiri sahihi ya jambo muhimu lililokuwa katika
unabii ule. Kwa hiyo, japo waliutangaza ujumbe ule waliokuwa wamekabidhiwa na Mungu ili kuupeleka

205
kwa ulimwengu, bado kutokana na kuelewa vibaya kuhusu maana yake walipatwa na uchungu wa
kufadhaisha.
Katika kufafanua aya ya Danieli 8:14, “Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo
patakatifu patakapotakaswa,” Miller, kama ilivyoelezwa, alichukua mtazamo uliokuwa umeshikiliwa na
wengi kwamba dunia ndiyo patakatifu, na aliamini kwamba kutakaswa kwa patakatifu kuliwakilisha
kutakaswa kwa dunia hii kwa moto wakati wa kuja kwa Bwana. Kwa hiyo, alipoona kwamba mwisho wa
siku zile 2300 ulikuwa umetabiriwa waziwazi, alihitimisha kwamba tukio hili linadhihirisha wakati wa
kuja mara ya pili. Kosa lake lilitokana na kuukubali mtazamo uliopendwa na watu wengi kuhusu kitu
kinachounda patakatifu.
Katika mfumo wa kafara uliokuwa kiwakilishi, ambao ulikuwa kivuli cha kafara na ukuhani wa Kristo,
kutakaswa kwa patakatifu kulikuwa ni huduma ya mwisho iliyofanywa na kuhani mkuu katika mzunguko
wa huduma ya kila mwaka. Ilikuwa kazi ya kumalizia huduma ya upatanisho - kuondoa au kuweka
dhambi mbali na Israeli. Ilikuwa ni mfano wa kazi ya mwisho katika huduma ya Kuhani wetu Mkuu kule
mbinguni, katika kuziondoa au kuzifuta dhambi za watu wake, ambazo zimeandikwa katika
kumbukumbu zilizoko mbinguni. Huduma hii inahusisha kazi ya upelelezi, kazi ya hukumu; nayo
inatangulia muda mfupi kabla ya marejeo ya Kristo katika mawingu ya mbinguni kwa nguvu na utukufu
mwingi; kwa maana yeye ajapo, kesi ya kila mtu itakuwa imekatwa. Yesu anasema: “Tazama, naja
upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.” Ufunuo 22:12. Ni kazi hii
ya hukumu, ambayo punde tu inatangulia marejeo ya Kristo, ambayo inatangazwa katika Ujumbe wa
Malaika wa Kwanza wa Ufunuo 14:7, usemao: “Mcheni Mungu na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu
yake imekuja.”
Wale waliolitangaza onyo hilo walitoa ujumbe sahihi kwa wakati sahihi. Lakini kama wanafunzi wale wa
kwanza walivyotangaza, “Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia,” (353) wakati
walishindwa kutambua kwamba kifo cha Masihi kilikuwa kimetabiriwa katika maandiko yale yale, hivyo
ndivyo Miller na wenzake walivyoutangaza ujumbe ule uliojengwa katika msingi wa Danieli 8:14 na
Ufunuo 14:7, na kushindwa kuona kwamba kuliwa na ujumbe mwingine mwingi uliofunuliwa katika
Ufunuo 14, ambao nao pia ulipaswa kutolewa kabla ya marejeo ya Bwana. Kama vile wanafunzi
walivyokosea kuhusu ufalme uliotazamiwa kuanzishwa mwishoni mwa majuma yale sabini, ndivyo
Waadventisti wale walivyokosea kuhusu tukio lililotarajiwa kutokea mwishoni mwa siku zile 2300. Katika
hali hizo zote mbili kulikuwa na hali ya kuyakubali, au pengine kuyatii, mafundisho potofu yaliyopendwa
na wengi ambayo yalipofusha akili na kushindwa kuuona ukweli. Makundi yote haya mawili yalitimiza
mapenzi ya Mungu kwa kutangaza ujumbe ule ambao yeye alitaka utolewe, na yote mawili, kwa
kuuelewa vibaya ujumbe wao, yalipatwa na mfadhaiko.
Bado Mungu alitimiza kusudi lake jema kwa kuruhusu onyo la hukumu kutolewa kama ilivyokuwa. Siku
kuu ilikuwa imekaribia, na kwa maongozi yake watu waliletwa katika jaribio la wakati wao halisi, ili
kuwafunulia kile kilichokuwamo ndani ya mioyo yao. Ujumbe ule ulikuwa umekusudiwa kulipima na
kulitakasa kanisa. Walikuwa waongozwe kuona kama mapenzi yao yalikuwa yamejengwa juu ya
ulimwengu huu au juu ya Kristo na mbinguni. Walidai kwamba wanampenda Mwokozi; sasa iliwapasa
kuthibitisha upendo wao. Je, walikuwa tayari kuyatupilia mbali matumaini na matarajio yao ya kidunia,
na kukaribisha marejeo ya Bwana wao kwa furaha? Ujumbe ule ulikusudiwa kuwawezesha kubainisha
hali yao halisi ya kiroho; ulitumwa ukiwa na rehema ili kuwaamsha wapate kumtafuta Bwana wakiwa na
toba na unyenyekevu.

206
Kule kufadhaika, ingawa ni matokeo ya wao kuelewa vibaya ujumbe walioutoa, kungeweza kugeuzwa
pia na kuwa kwa ajili ya jambo jema. Kungepima mioyo ya wale waliodai kulipokea onyo lile. Je, katika
kukabili mfadhaiko ule wangesalimu amri kwa pupa na kuacha uzoefu waliokuwa nao na kutupilia mbali
imani yao katika neno la Mungu? Au wangeweza, katika (354) sala na unyenyekevu, kutafuta kujua
mahali waliposhindwa kufahamu maana muhimu ya unabii ule? Wangapi walikuwa wamesukumwa na
hofu tu, au shauku fulani na msisimko? Ni wangapi walijitoa nusu-nusu na pasipo kuamini? Watu wengi
walikiri kwamba wanakupenda kuja kwa Bwana. Je, wakitakiwa kustahimili dhihaka na shutuma za
ulimwengu, na jaribio la kuchelewa na mfadhaiko, wangeikana imani? Je, kwa kuwa hawakuelewa
wakati ule utendaji wa Mungu kwao, wangezitupa kando kweli zilizothibitishwa na ushuhuda ulio wazi
sana wa neno lake?
Jaribio hili lingeweza kuzidhihirisha nguvu za wale ambao walikuwa wametii kwa imani ya kweli kile
walichokiamini kwamba kilikuwa ni mafundisho ya neno na Roho wa Mungu. Lingeweza kuwafundisha,
vile ambavyo uzoefu huu waliopitia tu ndio ungeweza, hatari ya kupokea nadharia na tafsiri zinazotoka
kwa wanadamu, badala ya kuifanya Biblia ijitafsiri yenyewe. Kwa watoto hawa wa imani, mkanganyiko
na huzuni vitokanavyo na kosa lao vingetenda kazi ya masahihisho yaliyohitajika. Wangeongozwa
kwenda katika kujifunza neno la unabii kwa undani zaidi. Wangefundishwa kuchunguza kwa makini zaidi
msingi wa imani yao, na kukataa kila kitu ambacho, hata kama kinakubalika kwa kiasi kikubwa katika
ulimwengu wa Kikristo, hakikujengwa juu ya msingi wa Maandiko ya kweli.
Kwa waumini hawa, kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wale wa kwanza, kile ambacho wakati wa saa ya
kujaribiwa kwao kilionekana giza katika ufahamu wao kingefanywa kuwa wazi baada ya pale. Wakati
ambapo wangeuona ule “mwisho wa Bwana” wangejua kwamba, licha ya majaribu yale waliyoyapata
kutokana na makosa yao, makusudi yake Bwana ya upendo kwao yalikuwa yakitimizwa kwa uthabiti.
Wangejifunza kutokana na uzoefu wenye heri kwamba Yeye ni “mwingi wa rehema, mwenye huruma”,
na ya kwamba njia zake zote “ni fadhili na kweli, kwao walishikao agano lake na shuhuda zake”

207
Sura ya 20
MWAMKO MKUU WA KIDINI

Mwamko mkuu wa kidini chini ya tangazo la kuja kwa Kristo upesi umetabiriwa katika unabii wa ujumbe
wa malaika wa kwanza wa Ufunuo 14. Malaika anaonekana akiruka “katikati ya mbingu, mwenye injili
ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa.” “Kwa sauti
kuu,” anatangaza ujumbe huu: “Mcheni Mungu na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja.
Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.” Aya ya 6 na 7.
Ukweli kwamba malaika huyo anasemekana kuwa ndiye anayebeba ujumbe wa onyo ni wa muhimu sana.
Kwa usafi, utukufu na uwezo wa mjumbe huyo wa mbinguni, hekima ya kimbingu imependezwa
kuiwakilisha sifa iliyotukuzwa ya kazi itakayokamilishwa na ujumbe na uweza na utukufu
vitakavyokuwepo. Na kuruka kwa malaika “katikati ya mbingu,” ile “sauti kuu” ambayo kwayo onyo hilo
linatolewa, na kutangazwa kwake waziwazi kwa hao wote “wakaao juu ya nchi,” – vinatoa ushahidi wa
utendaji wa haraka na ueneaji wa vuguvugu hilo katika ulimwenguni.
Ujumbe wenyewe unatumlikia mwanga kuhusu wakati wa kutokea kwa vuguvugu la harakati hizi.
Linatajwa kuwa sehemu ya “injili ya milele;” na linatangaza kuanza kwa (356) hukumu. Ujumbe wa
wokovu wenyewe umehubiriwa katika vizazi vyote; lakini ujumbe huu ni sehemu ya injili ambayo
ingeweza kutangazwa tu katika siku za mwisho, maana ni wakati ule tu ambapo ingekuwa kweli kwamba
saa ya hukumu ilikuwa imekuja. Unabii huo unaonyesha mfuatano wa matukio yanayotupeleka katika
mwanzo wa hukumu. Hii ni kweli hasa kuhusu kitabu cha Danieli. Lakini sehemu ile ya unabii wake
iliyohusu siku za mwisho, Danieli aliagizwa kuifunga na kuitia muhuri “hata wakati wa mwisho.” Ujumbe
huo unaohusu hukumu usingetangazwa mpaka hapo tunapoufikia wakati huu, tukijikita katika kutimizwa
kwa unabii huo. Lakini katika wakati wa mwisho, nabii anasema, “wengi wataenda mbio huko na huko,
na maarifa yataongezeka.” Danieli 12:4.
Mtume Paulo alilionya kanisa lisitazamie kuja kwa Kristo katika wakati ule alioishi. Alisema, “Maana
haiji, usipokuja kwanza ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa dhambi.” 2 Wathesalonike 2:3. Ni mpaka
baada ya ule uasi mkuu, na kipindi kirefu cha utawala wa yule “mtu wa dhambi,” ndipo tunaweza
kutazamia marejeo ya Bwana wetu. Yule “mtu wa dhambi,” ambaye pia anaitwa “siri ya kuasi,”
“mwana wa uharibifu,” na “yule asi,” anawakilisha upapa, ambao, kama ulivyotabiriwa katika unabii,
ulipaswa kuendelea kushika hatamu kwa miaka 1260. Kipindi hiki kiliisha mwaka 1798. Marejeo ya Kristo
yasingetokea kabla ya wakati ule. Paulo anakifunika kwa tahadhari hii kipindi chote cha Ukristo
kinachoenda hadi mwaka 1798. Ni upande huu wa wakati ule ambapo ujumbe wa kuja kwa Kristo mara
ya pili kunapaswa kutangazwa.

208
Hakuna ujumbe kama huo uliopata kutolewa katika vizazi vilivyopita. Paulo, kama ambavyo tumeona,
hakuuhubiri ujumbe huo; aliwaelekeza ndugu zake kutazamia kuja kwa Bwana mbali sana na kipindi
chao. Wanamatengenezo hawakuutangaza ujumbe huo. Martin Luther aliiweka hukumu kadiri ya miaka
mia tatu mbele ya wakati wake. Lakini tangu mwaka 1798 kitabu cha Danieli kimefunguliwa, maarifa ya
kuujua unabii yameongezeka, na wengi wameutangaza ujumbe huo murua wa hukumu iliyokaribia.
(357) Kama yalivyokuwa Matengenezo makuu ya karne ya kumi na sita, vuguvugu la uadventisti
lilijitokeza katika nchi mbalimbali za ulimwengu wa Kikristo kwa wakati mmoja. Katika Ulaya na
Amerika watu wenye imani na maombi waliongozwa kujifunza unabii mbalimbali, na, wakifuatilia katika
katika maandishi yenye uvuvio, wakaona ushahidi unaoshawishi kwamba mwisho wa mambo yote
ulikuwa umekaribia. Katika nchi mbalimbali kulikuwa na makundi yaliyojitenga ya Wakristo ambayo,
kwa kujikita katika kujifunza Maandiko, walifikia katika imani kwamba marejeo ya Mwokozi yalikuwa
karibu.
Katika mwaka wa 1821, miaka mitatu baada ya Miller kufikia katika msimamo wake wa unabii tofauti-
tofauti uliokuwa unaelekeza kwenye wakati wa hukumu, Dr. Joseph Wolff, “mmishonari kwa
ulimwengu,” alianza kutangaza habari za kuja kwa Bwana upesi. Wolff alizaliwa katika nchi ya
Ujerumani, akiwa wa uzao wa Waebrania, baba yake akiwa ni rabi wa Kiyahudi. Akiwa mdogo sana
alisadikishwa ukweli wa dini ya Kikristo. Akiwa mwenye akili iliyochemka, akili ya kudadisi, alikuwa
msikivu makini kusikiliza mazungumzo yaliyofanyika katika nyumba ya baba yake pindi Waebrania wa
dhati walipokusanyika kila siku kusimulia matumaini na matarajio ya watu wao, utukufu wa Masihi
ajaye, na urejeshwaji wa Israeli. Siku moja akisikia Yesu wa Nazareti akitajwa, huyu kijana aliuliza
kwamba huyo ni nani. “Myahudi mwenye talanta kubwa sana,” lilikuwa ndilo jibu; “lakini yeye
alipojifanya kuwa Masihi, baraza la Wayahudi likamhukumu kufa.” “Kwa nini,” alidakia mwulizaji,
“Yerusalemu umeangamizwa, na kwa nini tuko utumwani?” “Ole! ole!” alijibu baba yake, “kwa sababu
Wayahudi waliwaua manabii.” Mara moja wazo likamjia yule mtoto: “Huenda Yesu pia alikuwa ni nabii,
na Wayahudi walimwua alipokuwa hana hatia yo yote.” 348 Hisia hiyo ilikuwa na nguvu mno kiasi
kwamba, japo alikatazwa kuingia katika kanisa la Kikristo, mara kwa mara angekaa-kaa nje kusikiliza
mahubiri.
Akiwa na umri wa miaka saba tu alikuwa anajidai kwa jirani yake mzee aliye Mkristo kuhusu ushindi
utarajiwao wa Israeli wakati wa kuja kwa Masihi, wakati yule mwanaume mzee alisema kwa upole:
“Kijana mpendwa, nitakuambia Masihi wa kweli alikuwa nani: Alikuwa ni Yesu (358) wa Nazareti,…
ambaye babu zako wa zamani wamemsulibisha, kama walivyowafanya manabii wa zamani. Nenda
nyumbani ukasome sura ya hamsini na tatu ya Isaya, nawe utasadiki ya kwamba Yesu Kristo ni Mwana
wa Mungu.” 349 Mguso wa moyo ukambana. Alienda nyumbani akasoma yale maandiko, akastaajabu
kuona jinsi yalivyokuwa yametimia kikamilifu ndani ya Yesu wa Nazareti. Je, maneno ya Mkristo yule
yalikuwa ya kweli? Yule kijana alimwuliza baba yake ampe ufafanuzi wa unabii ule, lakini alikutana na
ukimya wa kuogofya kiasi kwamba hakuthubutu tena kurejea katika mada hii. Hali hii, hata hivyo,
ilizidisha tu hamu yake ya kutaka kujua zaidi kuhusu dini ya Kikristo.
Ujuzi aliokuwa akiutafuta ulifichwa sana mbali na yeye katika nyumba ile ya Kiyahudi; lakini, alipokuwa
na miaka kumi na moja tu, aliondoka nyumbani kwa baba yake na kwenda ulimwenguni kujipatia elimu
yake, kujichagulia dini yake, na kazi yake ya maisha. Alipata maskani yake ya muda pamoja na ndugu
zake, lakini alifukuzwa mara moja kutoka kwao kama muasi, akiwa peke yake, na bila fedha yoyote,

348
Travels and Adventures of the Rev. Joseph Wolff, vol. 1, p. 6
349
Ibid., vol. 1, p. 7
209
alilazimika kuishi maisha yake miongoni mwa wageni. Alikwenda toka sehemu moja hadi nyingine,
akisoma masomo yake kwa bidii na kujipatia riziki yake kwa kufundisha Kiebrania. Kwa ushawishi wa
mwalimu wa Katoliki alivutwa kuipokea imani ya Kirumi na kuwa na nia ya kuwa mmishonari kwa watu
wake. Akiwa na kusudi hili, miaka michache baadaye, alikwenda kwa ajili ya masomo katika Chuo cha
Propaganda kule Roma. Tabia yake ya kuwa na mawazo yake binafsi na kusema kwa uwazi kule
yalimletea kutuhumiwa kuwa mzushi. Alishambulia waziwazi matendo mabaya ya kanisa na kusisitiza
umuhimu wa kufanya mabadiliko. Ingawa mwanzoni wakuu wa upapa walimchukulia kwa upendeleo,
baada ya muda fulani aliondolewa na kupelekwa mbali na Roma. Akiwa chini ya uchunguzi wa kanisa,
alienda sehemu moja baada ya nyingine, mpaka ilipodhihirika kwamba asingeweza kuletwa katika hatua
ya kujitiisha katika utumwa wa Uroma. Alitangazwa kuwa mtu asiyeweza kurudiwa na kubadilika na
akaachwa huru kwenda kokote atakako. Sasa alishika njia kwenda Uingereza na, akiwa ameikiri imani
ya Kiprotestanti, aliungana na Kanisa la Uingereza. Baada ya masomo yake ya miaka miwili alienda
kuanza utume mwaka wa 1821.
Wakati Wolff alipokubali ukweli mkuu wa kuja kwa Kristo (359) mara ya kwanza akiwa kama “Mtu wa
huzuni nyingi, ajuaye sikitiko,” aliona ya kwamba unabii unadhihirisha kwa uwazi sawia kuhusu kuja
kwa Kristo mara ya pili akiwa na nguvu na utukufu. Na wakati alitafuta kuwaongoza watu wake kwa
Yesu wa Nazareti kama Yeye Aliyeahidiwa, na kuwaonyesha ujio wake wa mara ya kwanza katika hali ya
kudhalilishwa akiwa kafara kwa dhambi za wanadamu, aliwafundisha pia kuhusu kuja kwake mara ya pili
kama mfalme na mkombozi.
“Yesu wa Nazareti, Masihi wa kweli,” alisema, “ambaye mikono na miguu yake ilitobolewa, ambaye
aliletwa kama mwana-kondoo aendaye machinjoni, aliyekuwa Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko,
ambaye fimbo ya utawala ilipoondolewa katika Yuda na mamlaka yake ya utawala kuondolewa katikati
ya miguu yake, alikuja mara ya kwanza; atakuja mara ya pili katika mawingu ya mbinguni, na kwa
parapanda ya Malaika Mkuu,” 350 “naye atasimama juu ya Mlima wa Mizeituni; hapo ndipo utawala, ule
uliokabidhiwa kwa Adamu juu ya viumbe vyote, na kunyang’anywa kutoka kwake (Mwanzo 1:26; 3:17),
utakapokabidhiwa kwa Yesu. Atakuwa Mfalme juu ya dunia yote. Kuugua na maombolezo ya viumbe
vyote yatakoma; ila nyimbo za sifa na shukrani zitasikika…. Hapo Yesu atakapokuja katika utukufu wa
Baba yake, pamoja na malaika zake watakatifu,… watakatifu waliokufa watafufuliwa kwanza. 1
Wathesalonike 4:16; 1 Wakorintho 15:32. Hiki ndicho kitu ambacho sisi Wakristo tunakiita ufufuo wa
kwanza. Halafu wanyama watabadilika hali yao (Isaya 11:6-9), na kutiishwa kwa Kristo. Zaburi 8. Amani
ya vitu vyote itashamiri kote.” 351 “Bwana ataangalia tena chini duniani, na kusema, ‘Tazama, ni njema
sana.’” 352
Wolff aliamini kuhusu kukaribia kwa kuja kwa Bwana, tafsiri yake ya vipindi vya unabii vinavyouweka
mwisho mkuu miaka michache ndani ya wakati ulioonyeshwa na Miller. Kwa wale waliouliza kutokana na
maandiko kwamba “Habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye,” wakisema kwamba wanadamu
hawapaswi kujua chochote kuhusu kukaribia kwa marejeo yake, Wolff alijibu: “Kwani Bwana wetu
alisema kwamba siku na saa ile haiwezi kujulikana kamwe? Je, Yeye hakutupatia dalili za nyakati, ili
kwamba (360) tuweze kujua ukaribu wa kuja kwake kama mtu anavyojua kukaribia kwa majira ya
mavuno kwa kuuangalia mtini unapotoa majani yake? Mathayo 24:32. Je, hatuwezi kujua kamwe kipindi
kile, wakati Yeye mwenyewe alituhimiza sio tu kusoma kitabu cha nabii Danieli, bali pia kukifahamu? Na

350
Joseph Wolff, Researches and Missionary Labors, page 62
351
Journal of the Rev. Joseph Wolff, pages 378, 379
352
Ibid., page 294
210
katika kitabu hicho hicho cha Danieli, kuna mahali panaposema kwamba maneno yalifungwa mpaka
wakati wa mwisho (hali ambayo ndiyo iliyokuwepo katika wakati wake), na ya kwamba, “wengi
wataenda mbio huko na huko’ (usemi wa Kiebrania unaoonyesha kuchunguza na kutafakari kuhusu
wakati), ‘na maarifa’ (yanayohusishwa na wakati ule) ‘yataongezeka.’ Danieli 12:4. Mbali na haya, kwa
maneno haya, Bwana wetu hakusudii kusema kwamba kukaribia kwa wakati hakutajulikana, bali
kwamba kwa usahihi kabisa ‘siku ile na saa ile hakuna aijuaye.’ Yeye hasemi habari ya kutosha kwamba
itajulikana kwa dalili za nyakati, ili kutuvuta sisi kujiandaa kwa ajili ya marejeo yake, kama Nuhu
alivyoandaa safina.” 353
Kuhusu utaratibu unaopendwa na wengi katika kutafsiri, au kutafsiri vibaya, Maandiko, Wolff aliandika
hivi: “Sehemu kubwa zaidi ya kanisa la Kikristo imechepuka mbali na maana iliyo wazi ya Maandiko, na
wameugeukia mtindo wa kudhania wa Wabudha, ambao wanaamini kwamba furaha ya baadaye ya
wanadamu itahusisha kuhamia hewani, na wanadhani kwamba wanaposoma Wayahudi lazima waelewe
kwamba ni Wamataifa; na wanaposoma Yerusalemu, lazima waelewe kwamba ni kanisa; na inaposemwa
nchi, inamaanisha anga; na kwa habari ya kuja kwa Bwana lazima waelewe kwamba ni maendeleo ya
vyama vya kimishonari; na ya kwamba kupanda kwenda kwenye mlima wa nyumba ya Bwana,
kunaashiria darasa la mkutano mkuu wa Wamethodisti.” 354
Katika kipindi cha miaka ishirini na nne ya kuanzia 1821 hadi 1845, Wolff alisafiri katika maeneo mengi:
katika bara la Afrika, akizuru maeneo ya Misri na Abyssinia; katika Asia, alitembea katika Palestina,
Syria, Uajemi, Bokhara, na India. Aliitembelea Marekani pia, katika safari ya kwenda huko, alihubiri
katika kisiwa cha Saint Helena. Aliwasili New York mwezi Agosti, 1837; na, baada ya kuhutubia katika
mji ule, alihubiri kule Philadelfia na Baltimore, na hatimaye aliendelea na safari kwenda Washington.
Mahali hapa, anasema, “katika hoja iliyoletwa (361) na Rais mstaafu, John Quincy Adams, katika
mojawapo ya vikao vya Bunge la Marekani, Bunge liliniruhusu kwa kauli moja kutumia ukumbi wa Bunge
kutoa hotuba, ambayo niliitoa katika siku ya Jumamosi, nikipewa heshima ya uwepo wa wajumbe wote
wa Bunge, na uwepo wa askofu wa Virginia, na wa wachungaji na maaskofu na wananchi wa kawaida wa
Washington. Heshima kama ile ilitolewa kwangu na wajumbe wa serikali ya New Jersey na Pennsylvania,
ambao katika uwepo wao nilitoa hotuba zilizotokana na utafiti wangu kule Asia, na pia kuhusu utawala
wa Yesu Kristo mwenyewe.” 355
Dk. Wolff alisafiri katika nchi za kipagani zaidi pasipo kupewa ulinzi na mamlaka yoyote ya Ulaya,
akistahimili shida nyingi na akizungukwa na hatari zisizohesabika. Aliadhibiwa kwa kupigwa katika nyayo
zake na kuachwa akiwa na njaa, akauzwa kama mtumwa, na mara tatu alihukumiwa kufa.
Alishambuliwa na wanyang’anyi, na wakati mwingine alikaribia kufa kwa kiu. Wakati mmoja aliporwa
vitu vyote alivyokuwa navyo na kuachwa akitembea kwa miguu mamia ya maili kupitia milimani,
akipigwa na theluji usoni na miguu yake iliyokuwa pekupeku ikifa ganzi katika ardhi iliyoganda kwa
barafu.
Alipoonywa dhidi ya kutembea bila kuwa na silaha miongoni mwa makabila yale katili na mabaya,
alitangaza kuwa yeye “kapewa silaha” - “sala, shauku kwa ajili ya Kristo, na ujasiri katika msaada
utokao kwake.” “Pia mimi,” alisema “nimepewa upendo kwa Mungu na kwa jirani yangu katika moyo

353
Wolf, Researches and Missionary Labors, pages 404, 405
354
Journal of the Rev. Joseph Wolff, page wa 96
355
Ibid., pages 398, 399
211
wangu, na Biblia katika mkono wangu.” 356 Kokote alikokwenda alibeba Biblia katika lugha ya Kiebrania
na Kingereza. Kuhusu moja ya safari zake za mwisho anasema: “Mimi … niliendelea kuwa na Biblia
iliyofunguliwa mkononi mwangu. Nilihisi kwamba nguvu zangu zilikuwa katika Kitabu hicho, na ya
kwamba uweza wake ungeweza kunitegemeza.” 357
Hivyo ndivyo alivyostahimili katika kazi zake mpaka pale ujumbe wa hukumu ulipokuwa umepelekwa
katika sehemu kubwa ya mahali panapokaliwa na watu duniani. Kwa Wayahudi, Waturuki, Waparsee,
Wahindu, na watu wa makundi ya jamii na mataifa mengine mengi alitawanya neno la Mungu katika
lugha hizi mbalimbali na kila
Katika safari zake Bokhara alikuta fundisho la kuja upesi kwa Bwana ambalo lilishikwa na watu wale
waliokaa katika sehemu za upweke na zilizojitenga. (362) Warabu wa Yemeni, anasema, “wanacho
kitabu kinachoitwa Seera, ambacho kinatoa habari za kuja kwa Kristo mara ya pili na utawala wake
katika utukufu; na wanatazamia kwamba matukio makubwa yatatokea mwaka 1840.” 358 “Kule Yemeni,…
nilitumia siku sita nikiwa na watoto wa Rekabu. Hawanywi mvinyo, hawalimi mizabibu, hawapandi
mbegu, na wanaishi katika mahema, na wanamkumbuka yule mzee mwema Yehonadabu, mwana wa
Rekabu; na katika kundi lao niliwakuta wana wa Israeli, wa kabila ya Dani,… ambao wanatazamia,
pamoja na wana wa Rekabu, kuja upesi kwa Masihi katika mawingu ya mbinguni.” 359
Imani ya namna hiyo ilionwa na mmishonari mwingine ambaye angekuwa kule Tatary. Kuhani aliyekuwa
Mtatar aliuliza swali kwa mmishonari kuhusu lini Kristo atakapokuja mara ya pili. Yule mmishonari
alipojibu kwamba hakujua chochote kuhusu habari ile, kuhani alionekana kushangazwa sana kwa ujinga
ule ulio katika mtu aliyejidai kuwa mwalimu wa Biblia, na yeye akaeleza imani yake, iliyojengwa juu ya
unabii, kwamba Kristo angekuja kadiri ya mwaka 1844.
Mapema kiasi cha mwaka wa 1826 ujumbe wa marejeo ulianza kuhubiriwa Uingereza. Harakati hizi za
hapa hazikuwa na utaratibu unaoeleweka kama kule Amerika; wakati halisi wa marejeo ya Kristo
haukufundishwa hasa, lakini ukweli mkuu wa kuja kwa Kristo upesi katika nguvu na utukufu ulitangazwa
mahali pengi. Na hili halikuwa tu miongoni mwa wapinzani wa kanisa au wasiokubali imani na taratibu
za kanisa lililokuwepo. Mourant Brock, mwandishi Mwingereza, anaeleza kwamba viongozi wa kanisa
wapatao mia saba katika Kanisa la Uingereza walijishughulisha katika kuihubiri “injili hii ya ufalme.”
Ujumbe uliolenga mwaka 1844 kama wakati wa kuja kwake Bwana ulitolewa hata katika maeneo yote
ya Uingereza. Machapisho ya marejeo kutoka Amerika vilitawanywa sana. Vitabu na majarida
vilichapishwa tena Uingereza. Na katika mwaka wa 1842, Robert Winter, Mwingereza kwa kuzaliwa,
aliyekuwa amepokea imani ya marejeo kule Amerika, alirudi katika nchi yake ya kuzaliwa kutangaza
marejeo ya Bwana. Wengi waliungana naye katika kazi hii, na ujumbe wa hukumu ulitangazwa katika
sehemu mbalimbali za Uingereza.
(363) Kule Amerika ya Kusini, katikati ya hali ya ushenzi, na ujanja-ujanja wa makasisi, Lacunza,
Mhispania na Mjesuiti, aliyafikia Maandiko na hivyo akapokea ukweli kuhusu kurudi upesi kwa Kristo.
Akisukumwa kutoa onyo hili, lakini akitamani kukwepa mashutumu kutoka Roma, alichapisha maoni
yake kwa jina lisilo lake la “Rabbi Ben-Ezra,” akijionyesha kwamba ni Myahudi aliyeongoka. Lacunza
aliishi mnamo karne ya kumi na nane, lakini ilikuwa kadiri ya mwaka 1825 wakati kitabu chake, kikiwa
kimefika London, kilipotafsiriwa katika lugha ya Kingereza. Kuchapishwa kwa kitabu hiki kulisaidia

356
W. H. D. Adams, In Perils Oft, page 192
357
Ibid., page 201
358
Journal of the Rev. Joseph Wolff, page 377
359
Ibid., page 389
212
kuongeza mwamko wa kupenda mada ya marejeo ya Kristo mara pili ambao ulikuwa imekwishashika kasi
huko Uingereza.
Huko Ujerumani, katika karne ya kumi na nane, fundisho hili lilikuwa limefundishwa na Bengel,
mtumishi wa injili katika Kanisa la Lutheran na msomi na mhakiki wa Biblia aliyekuwa anaipenda.
Alipomaliza elimu yake, Bengel alikuwa “ameutumia muda wake mwingi kujifunza thiolojia, ambayo
kwayo mwelekeo wa akili yake na mvuto wa kidini katika mawazo yake, vikiwa vimeimarishwa kwake
kutokana na mafunzo na nidhamu aliyopata mapema, vilimpa mwelekeo huo. Kama ilivyo kwa vijana
wengine wenye tabia ya kutafakari, tangu pale na kabla ya pale, alipambana na mashaka na ugumu
kuhusu mambo ya dini, na hudokeza, kwa hisia za kina, kuhusu hii ‘mishale mingi iliyouchoma moyo
wake mnyonge, na kuufanya ujana wake kuwa mgumu kuustahimili.’” Alipoingia kuwa mjumbe wa
baraza la makadinali na papa (consistory) la Wurttemberg, alitetea habari ya uhuru wa dini. “Huku
akichunga haki na stahili za kanisa, alikuwa mtetezi kwamba pale penye sababu uhuru utolewe kwa
wale wote waliojisikia kuwa wamefungwa, kwa misingi ya dhamiri, ili wapate kujiondoa katika ushirika
wake.” 360 Matokeo mazuri ya sera hii bado yanaonekana katika jimbo lake.
Ilikuwa wakati alipokuwa anatayarisha hubiri kutoka katika Ufunuo 21 kwa ajili ya Jumapili ya
wanamarejeo ndipo nuru ya kuja kwa Kristo mara ya pili ilipoupenya moyo wa Bengel. Unabii wa Ufunuo
ulifunguliwa katika ufahamu wake kiasi ambacho hakikuwahi kutokea kabla. Akiwa amelemewa na hisia
ya umuhimu mkubwa na utukufu usio na kifani wa mandhari iliyotolewa na nabii, alilazimika kuacha
kwa muda kulitafakari somo lile. Akiwa mimbarani (364) nuru ile ilimjia tena kwa uwazi wake wote na
nguvu. Tangu wakati ule alijielekeza katika kujifunza unabii, hasa ule wa Ufunuo, na mara akaifikia
imani kwamba unabii ule ulikuwa ukielekeza kwamba kuja kwa Kristo kulikuwa kumekaribia. Muda
alioweka kwamba ndio wa marejeo ya mara ya pili ulikuwa miaka michache kuliko ile iliyowekwa na
Miller.
Maandiko ya Bengel yametawanywa katika Ulimwengu wote wa Kikristo. Maoni yake juu ya unabii
yalipokewa na watu wengi sana katika jimbo lake la Wurttemberg, na kwa kiasi fulani katika sehemu
nyingine za Ujerumani. Harakati hiyo iliendelea baada ya kifo chake, na ujumbe wa marejeo ulisikika
Ujerumani kwa wakati ule ule ulipokuwa unavuta usikivu katika nchi nyinginezo. Muda wa mapema
baadhi ya waumini walikwenda Urusi na kuanzisha makundi ya makazi kule, na ujumbe wa kuja upesi
kwa Kristo bado unashikiliwa na makanisa ya Kijerumani ya nchi hiyo mpaka sasa.
Nuru ile iliangaza pia katika nchi ya Ufaransa na Uswisi. Pale Geneva mahali ambapo Farel na Calvin
walikuwa wameeneza ukweli wa Matengenezo, Gaussen alihubiri ujumbe wa kuja kwa Kristo mara ya
pili. Akiwa mwanafunzi shuleni, Gaussen alikuwa amekumbana na ile roho ya falsafa ya kimantiki
iliyoikumba Ulaya yote katika kipindi cha mwisho cha karne ya kumi na nane na mwanzoni mwa karne
ya kumi na tisa; naye alipoingia katika kazi ya utumishi si tu kwamba alikuwa mjinga wa imani ya kweli,
bali pia alikuwa na mwelekeo wenye mashaka. Katika ujana wake alikuwa amekuwa na moyo wa
kupenda kujifunza unabii. Baada ya kusoma kitabu cha Rollin kinachoitwa Ancient History, mawazo
yake yalivutwa kuelekea katika sura ya pili ya Danieli, naye alishtushwa kuona usahihi wa ajabu wa
kutimia kwa unabii ule, kama inavyoonekana katika maandishi ya mwanahistoria huyo. Hapa kulikuwa
na ushahidi wa uvuvio wa Maandiko, jambo ambalo lilikuwa nanga yake katikati ya hatari za baadaye.
Hakuweza kutosheka na mafundisho ya ile falsafa ya kimantiki, na katika kujifunza Biblia na kutafuta
nuru iliyo wazi zaidi, baada ya muda, aliongozwa kuwa na imani yenye mwelekeo chanya.

360
Encyclopedia Britannica, 9th ed., art. “Bengel.”

213
Alipoendelea na uchunguzi wake wa unabii, alifika mahali pa kuamini kwamba kuja kwa Bwana kulikuwa
kumekaribia. Akiwa ameguswa na uzito na umuhimu wa ukweli huu (365) mkuu, alitamani kuuleta
mbele za watu; lakini imani iliyozoeleka miongoni mwa wengi kwamba unabii wa Danieli ulikuwa siri na
kwamba hauwezi kueleweka ilikuwa kipingamizi kikubwa katika njia yake. Hatimaye aliazimia - kama
Farel alivyokuwa amefanya kabla yake katika kuihubiri Injili pale Geneva - kuanza na watoto, ambao
kupitia kwao alitumaini kuwavuta wazazi wao.
“Natamani jambo hili lieleweke,” alisema baadaye, akiongea kuhusu lengo lake katika kazi hii, “si kwa
sababu ya umuhimu wake mdogo, bali kinyume chake kwa sababu ya thamani yake kubwa, kwamba
nilipenda kuutoa katika mtindo huu uliozoeleka, nami nikazungumza na watoto. Nilitamani kusikika,
lakini niliogopa kwamba isingewezekana ikiwa ningejitokeza kuzungumza mbele ya watu wazima
kwanza. “Basi, niliazimu kuwaendea wadogo kabisa. Nakusanya kundi la wasikilizaji walio watoto; ikiwa
kundi hilo linaongezeka ukubwa, ikiwa inaonekana kwamba wanasikiliza, wanapendezwa, wanavutiwa,
kwamba wanaelewa na wanaweza kulielezea somo, nina uhakika wa kuwa na kundi la pili muda si
mrefu, na katika kurudi kwao, watu wazima wataona kwamba inawafaa kwa muda kuketi chini na
kujifunza. Jambo hilo linapofanyika, basi mafanikio yanakuwa yamepatikana.” 361
Jitihada hii ilifanikiwa. Kadiri alivyozungumza na watoto, watu wazima walikuja kusikiliza. Sehemu za
juu za kanisa lake zilijaa watu waliokuwa wakisikiliza kwa makini. Miongoni mwao walikuwa watu vyeo
na wasomi, na wageni na wa watu wa kutoka nchi za nje waliokuwa wanatembelea Geneva; na kwa njia
hiyo ujumbe ule ulipelekwa katika maeneo mengine.
Akiwa ametiwa moyo kwa sababu ya mafanikio hayo, Gaussen akachapisha masomo yake, akitumaini
kukuza moyo wa kujifunza vitabu vya unabii katika makanisa ya watu wazungumzao Kifaransa.
“Kuchapisha mafundisho yaliyotolewa kwa watoto,” anasema Gaussen, “ni kuzungumza na watu
wazima, ambao mara nyingi hupuuza vitabu kama hivyo wakidai kwamba havieleweki, ‘Vinawezaje
kuwa visivyoeleweka, ila watoto wenu wanavielewa?’” “Nilikuwa na shauku kubwa,” anaongeza, “ya
kuyafanya maarifa ya unabii yapate kujulikana sana katika makundi yetu, kama inawezekana.” “Hakuna
kujifunza kunakokidhi mahitaji ya wakati huu.” “Ni kwa kujifunza huku sisi tunatakiwa kujiandaa kwa
ile dhiki iliyo mlangoni, na kukesha na kumngoja Yesu Kristo.”
(366) Ingawa alikuwa mmoja wa wahubiri maarufu sana na wanaopendwa katika lugha ya Kifaransa,
Gaussen alisimamishwa kazi yake ya kuhubiri baada ya muda, kosa lake kuu likiwa kwamba badala ya
kutumia katekisimu ya kanisa, kitabu cha mwongozo kilichokuwa kimeanzishwa kifuatwe, ambacho
kilikuwa kama hakina imani iliyo na mwelekeo chanya, yeye alikuwa ametumia Biblia kuwapatia vijana
mafunzo. Baadaye alikuja kuwa mwalimu katika shule ya thiolojia, wakati siku za Jumapili aliendelea
na kazi yake kama katekista, akizungumza na watoto na kuwafundisha katika Maandiko. Maandiko yake
juu ya unabii yaliamsha pia moyo wa kuvutiwa. Tangu kwenye kiti cha uprofesa, kupitia katika kiwanda
cha uchapishaji, na katika kazi yake aliyoipenda ya mwalimu wa watoto aliendelea kwa miaka mingi
kuleta mvuto ambao ulienea mahali pengi na alikuwa chombo cha kuvuta usikivu wa wengi kuelekea
katika kujifunza unabii ulioonyesha kwamba kuja kwa Bwana kulikuwa karibu.
Katika nchi za Skandinavia nako pia ujumbe wa marejeo ulihubiriwa, na hamu kubwa miongoni mwa
watu wengi iliamshwa. Wengi waligutushwa kutoka katika uzembe wa kujiona kuwa salama hadi
wakaungama na kuziacha dhambi zao, na kutafuta msamaha katika jina la Kristo. Lakini makasisi na
maaskofu wa kanisa la dola walipinga harakati hizi, na kwa kupitia ushawishi wao baadhi ya watu

361
L Gaussen, Daniel the Prophet, vol. 2, Preface

214
waliouhubiri ujumbe huo walitupwa gerezani. Katika maeneo mengi ambapo wahubiri wa habari ya kuja
upesi kwa Bwana walinyamazishwa, Mungu alipendezwa kuupeleka ujumbe ule, kwa njia ya mwujiza,
kupitia watoto wadogo. Kwa kuwa walikuwa chini ya umri uliotambuliwa, sheria ya nchi ile haikuweza
kuwazuia, na wakaruhusiwa kuhubiri bila kubughudhiwa.
Harakati zile zilikuwa hasa miongoni mwa watu wa daraja la chini, na ilikuwa katika makazi duni ya
watu wanaofanya kazi za mikono ambapo watu walikusanyika kulisikia onyo. Wahubiri watoto wao kwa
sehemu kubwa walikuwa wakazi wa vibanda vya kimaskini. Baadhi yao hawakuzidi umri wa miaka sita
au nane; na wakati maisha yao yalithibitisha kwamba walikuwa wanampenda Mwokozi, na kwamba
walikuwa wanajitahidi kuishi kwa kutii matakwa matakatifu ya Mungu, kwa kawaida walionyesha tu akili
na uwezo unaoonekana kwa watoto wa umri ule. Hata hivyo waliposimama mbele ya watu, (367)
ilidhirika kwamba walisukumwa na uwezo uliopita vipawa vyao vya kawaida. Sauti na tabia vilibadilika,
na kwa uwezo mkubwa wakalitoa lile onyo la hukumu, wakitumia maneno yale yale ya Maandiko:
“Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake, imekuja.” Walizikemea dhambi za
watu, sio tu kwa kushutumu uasherati na uovu, bali wakikemea hali ya kupenda ulimwengu na kurudi
nyuma, na kuwaonya wasikilizaji wao kwamba waikimbie haraka ghadhabu ijayo.
Watu walisikiliza kwa kutetemeka. Roho wa Mungu asadikishaye moyo alisema na mioyo yao. Wengi
waliongozwa katika kuchunguza Maandiko kwa moyo mpya na wa kina, wasiojitawala na watovu wa
uadilifu wakatengenezwa upya, wengine wakaachana na vitendo vyao vya udhalimu, na kazi kubwa
inayoonekana ilikuwa imefanyika kiasi kwamba hata watumishi wa kanisa la dola wakalazimika kukiri
kwamba mkono wa Mungu ulikuwa katika harakati zile.
Yalikuwa mapenzi ya Mungu kwamba habari za kuja kwa Mwokozi zipate kutolewa katika nchi za
Skandinavia; na wakati sauti za watumishi wake ziliponyamazishwa, alitia Roho wake juu ya watoto, ili
kazi ipate kufanyika. Wakati Yesu alipoukaribia Yerusalemu akiandamana na makutano wenye shangwe
waliokuwa, kwa kelele za shangwe na kupepea matawi ya mitende, wakimtangaza kama Mwana wa
Daudi, Mafarisayo wenye wivu walimtaka awanyamazishe; lakini Yesu alijibu kwamba yote haya
yalifanyika ili kutimiza unabii, na kama hao wangenyamaza, mawe yenyewe yangepiga kelele. Watu
wale, wakitiwa hofu na vitisho vya makuhani na watawala, waliacha kumtangaza kwa furaha pindi
walipoingia katika malango ya Yerusalemu; lakini watoto waliokuwa katika nyua za hekalu, baadaye
waliupokea ule wimbo, na, wakipepea matawi yao ya mitende, waliimba: “Hosana, Mwana wa Daudi.”
Mathayo 21:8-16. Wakati Mafarisayo, wakiwa wamechukizwa sana, walipomwambia, “Wasikia hawa
wasemavyo?” Yesu alijibu akawaambia, “Naam, hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga
na wanyonyao umewakamilisha sifa?” Kama Mungu alivyofanya kupitia kwa watoto (368) wakati wa kuja
kwa Kristo mara ya kwanza, ndivyo alivyofanya kupitia kwao katika kuutoa ujumbe wa marejeo yake ya
pili. Lazima neno la Mungu litimizwe, kwamba tangazo la kuja kwa Mwokozi linapaswa kutolewa kwa
watu wote, lugha zote, na mataifa yote.
Mila na watendakazi wenzake walipewa kulihubiri onyo Amerika. Nchi hii ikawa kituo kikuu cha harakati
za marejeo. Ni mahali hapa ambapo unabii wa ujumbe wa malaika wa kwanza ulipata utimilifu wa moja
kwa moja kuliko pengine pote. Maandiko ya Miller na wenzake yalipelekwa katika nchi za mbali. Popote
wamishonari walipokuwa wamepenya katika ulimwengu wote zilipelekwa habari njema za kurudi upesi
kwa Kristo. Kwa umbali na kwa mapana ulitawanyika ujumbe wa injili ya milele usemao: “Mcheni
Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja.”
Ushuhuda wa unabii ulioonekana kuelekeza kwamba kuja kwa Kristo kuko katika majira ya vuli ya
mwaka 1844, uligusa kwa kina akili za watu. Kadiri ujumbe ule ulivyosonga mbele kutoka jimbo moja

215
hadi jingine, mwamko wa hamu uliamshwa kila mahali. Wengi walisadiki kwamba hoja zile zilizotoka
katika vipindi vya unabiii zilikuwa sahihi, nao, wakiachana na kiburi cha maoni yao, waliupokea ukweli
kwa furaha. Baadhi ya watumishi wa injili waliweka kando mitazamo na hisia za madhehebu, waliacha
mishahara yao na makanisa yao, wakajiunga katika kutangaza marejeo ya Yesu. Hata hivyo, kwa
ulinganishaji, watumishi walioupokea ujumbe huu walikuwa wachache mno; kwa hiyo, kwa sehemu
kubwa ulikabidhiwa kwa walei wanyenyekevu. Wakulima waliyaacha mashamba yao, makanika waliacha
vifaa vyao, wafanya biashara waliacha bidhaa zao, wataalam waliacha nafasi zao za kazi; lakini bado
idadi ya watendakazi ilikuwa ndogo ikilinganishwa na kazi iliyopaswa kufanywa. Hali ya kanisa
lililokuwepo bila uchaji wa Mungu na ulimwengu uliokuwa katika uovu, viliilemea mioyo ya walinzi wa
kweli, nao kwa hiari yao walistahimili taabu, umaskini, na mateso, ili kwamba wapate kuwaita watu
katika toba na wokovu. Ingawa ilipingwa na Shetani, kazi ilisonga mbele kwa nguvu, na ukweli wa
marejeo ulipokelewa na maelfu mengi ya watu.
(369) Kila mahali ushuhuda unaopenya moyo ulisikika, ukiwaonya wadhambi, wa makundi yote mawili,
yaani, wale wapendao mambo ya dunia hii na wale walio washiriki wa kanisa, ili wapate kuikimbia
ghadhabu ile ijayo. Kama alivyofanya Yohana Mbatizaji, mtangulizi wa Kristo, wahubiri waliweka shoka
penye shina la mti na kuwasihi wote wazae matunda yapasayo toba. Wito wao unaosumbua moyo
ulitofautiana dhahiri na ujumbe unaowahakikishia watu amani na usalama utokao kwenye mimbara
zinazopendwa na wengi; na po pote ujumbe ule ulipotolewa, uligusa watu. Ushuhuda ule wa Maandiko
ulio rahisi na wa moja kwa moja, uliofikishwa mahali pake kwa uweza wa Roho Mtakatifu, ulileta mzigo
wa kusadikisha watu kuhusu hatia yao ambapo wachache tu ndio waliweza kupambana nao. Watu
waliodai kuwa na dini walizinduliwa kutoka katika usalama wao wa uongo. Waliona kurudi nyuma kwao,
kuipenda dunia kwao, na kutoamini kwao, kiburi chao na ubinafsi. Wengi walimtafuta Bwana kwa toba
na kunyenyekea. Mapenzi yao yaliyokuwa yameng’ang’ania vitu vya dunia kwa muda mrefu sana sasa
yalikazwa kuelekea mbinguni. Roho wa Mungu alitulia juu yao, na kwa mioyo iliyolainishwa na kutiishwa
walijiunga katika kutoa sauti isemayo: “Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake
imekuja.”
Wadhambi waliuliza huku wakilia: “Nifanye nini nipate kuokoka?” Wale ambao maisha yao yalikuwa
yametiwa alama ya kukosa uadilifu walikuwa na wasiwasi wakitaka kutoa malipo ya fidia kwa kile
walichochukua kwa udanganyifu. Wote waliopata amani katika Kristo walitafuta kuona kwamba watu
wengine pia wanashiriki mbaraka huu. Mioyo ya wazazi ikawaelekea watoto wao, na mioyo ya watoto
ikawaelekea wazazi wao. Vipingamizi vilivyowekwa na kiburi na ubinafsi vilifagiliwa mbali. Maungamo
ya dhati yalifanywa, na watu waliokuwa katika jamaa moja walifanya kazi kwa ajili ya wokovu wa wale
walioishi karibu zaidi na wale waliokuwa wapendwa zaidi. Mara kwa mara ilisikika sauti ya maombi ya
dhati ya kuombea wengine. Kila mahali kulikuwa na roho zenye uchungu zikimsihi sana Mungu. Wengi
walishindana mwereka wa maombi usiku kucha ili wapate uhakika kwamba dhambi zao zilikuwa
zimesamehewa, au kwa ajili ya kuongoka kwa ndugu zao au majirani zao.
Watu wa matabaka yote walisongamana kuelekea katika mikutano ya Wanamarejeo. Matajiri na
maskini, wenye vyeo na wa hali ya chini, walikuwa, kutoka katika kazi zao mbalimbali, na shauku ya
kulisikia wenyewe fundisho la kuja kwa Kristo mara ya pili. Bwana alizuia roho ya upinzani wakati
watumishi wake (370) walipokuwa wakieleza sababu za imani yao. Wakati mwingine chombo kilikuwa
kinyonge; lakini Roho wa Mungu alitoa uwezo kwa ukweli ulio wake. Uwepo wa malaika watakatifu
ulihisiwa katika mikutano ile, na wengi walikuwa wakiongezeka katika idadi ya waamini kila siku. Kadiri
ushahidi wa kuja upesi kwa Kristo ulivyokuwa unarudiwa tena na tena, makundi makubwa sana ya watu
yalisikiliza maneno yale mazito yakiwa kimya kabisa. Mbingu na Dunia zilionekana kama zinakaribiana.

216
Nguvu za Mungu zilionekana ndani ya wazee na vijana na watu wa umri wa kati. Watu walienda
majumbani kwao wakiwa na sifa midomoni mwao, na sauti ya shangwe ilisikika katika hewa ya usiku
mtulivu. Hakuna mtu aliyehudhuria mikutano ile awezaye kusahau mandhari zile zenye mvuto wa kina
sana.
Kutangazwa kwa wakati halisi wa marejeo ya Kristo kuliamsha upinzani mkubwa toka kwa watu wa
tabaka zote, kuanzia kwa mhubiri aliye mimbarani na kushuka chini mpaka kwa yule mwenye dhambi
asiyejali kabisa, asiyeweza kuithubutu Mbingu. Maneno ya unabii yalitimizwa: “Katika siku za mwisho
watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe, na kusema, Iko wapi
ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo,
tangu mwanzo wa kuumbwa.” 2 Petro 3:3,4. Wengi waliodai kwamba wanampenda Mwokozi
wakatangaza kwamba wao hawakuwa na upinzani wowote dhidi ya fundisho la marejeo ya Kristo; ila
walikuwa na tatizo tu katika kuweka muda halisi. Lakini jicho la Mungu linaloona mambo yote likaisoma
mioyo yao. Hawakutaka kusikia habari ya kuja kwa Kristo kuuhukumu ulimwengu katika haki. Walikuwa
watumishi wasio waaminifu, matendo yao yasingestahimili kuchunguzwa na Mungu achunguzaye moyo,
na waliogopa kukutana na Bwana wao. Kama walivyokuwa Wayahudi wakati wa kuja kwa Kristo mara ya
kwanza hawa hawakuwa wamejiandaa kumpokea Yesu. Si tu kwamba walikataa kuzisikiliza hoja za wazi
kutoka katika Biblia, bali pia waliwadhihaki wale waliokuwa wanamtazamia Bwana. Shetani na malaika
zake walishangilia, na walirusha shutuma zao usoni mwa Kristo na malaika zake watakatifu wakisema
kwamba wale waliojiita watu wake walikuwa na upendo kidogo mno kwa Kristo kiasi kwamba
hawakutamani kuja kwake.
“Hakuna aijuaye siku ile na saa ile” ilikuwa ndiyo hoja iliyoletwa mara kwa mara na wale walioikataa
imani ya marejeo yake Kristo. Maandiko ni haya: “Habari ya siku ile na saa ile hakuna (371) aijuaye,
hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.” Mathayo 24:36. Maelezo yaliyo wazi na
yanayoafikiana na aya hiyo yalitolewa na wale waliokuwa wanamngojea Bwana, na matumizi yake
potofu yaliyofanywa na wapinzani wao yakafichuliwa. Maneno haya yalisemwa na Kristo katika
mazungumzo ya kukumbukwa aliyofanya na wanafunzi wake kwenye mlima wa Mizeituni baada ya
kutoka hekaluni kwa mara yake ya mwisho. Wanafunzi walikuwa wameuliza swali: “Nayo ni nini dalili ya
kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?” Yesu akawapa dalili, kisha akasema: “Nanyi kadhalika, myaonapo
hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, mlangoni.” Fungu la 3 na la 33. Usemi mmoja wa Kristo
usilazimishwe kuharibu mwingine. Ingawa hakuna mtu yeyote ajuaye siku wala saa ya kuja kwake,
tunafundishwa na kutakiwa kujua wakati kutakapokuwa karibu. Tunafundishwa zaidi kwamba kulidharau
onyo lake hili, na kukataa au kupuuza kujua kukaribia kwa kuja kwake, kutaleta ajali ya kufisha kwetu
kama kulivyowaletea wale walioishi katika siku za Nuhu waliokosa kujua wakati wa kuja kwa gharika. Na
mfano huo katika sura hiyo hiyo, unaotofautisha kati ya mtumishi mwaminifu na yule asiye mwaminifu,
na kutangaza ole ya yule aliyesema moyoni mwake, “Bwana wangu anakawia,” huonyesha ni kwa nuru
gani Kristo atawaangalia na kuwapa thawabu wale atakaowakuta wakimngojea, na kufundisha habari ya
marejeo yake, na kwa walewanaoukataa ujumbe huo. “Kesheni basi,” anasema. “Heri mtumwa yule,
ambaye Bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo.” Fungu la 42 na 46. “Walakini usipokesha, nitakuja
kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.” Ufunuo 3:3.
Paulo anazungumza habari ya kundi ambalo marejeo ya Bwana kwao yatakuja bila kujua. “Siku ya
Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku. Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu
uwajiapo kwa ghafla,… wala hakika hawataokolewa.” Lakini anaongeza hivi, kwa wale waliozingatia
onyo la Mwokozi: “Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi. Kwa kuwa ninyi

217
nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.” 1 Wathesalonike
5:2-5.
(372) Hivyo ndivyo ilivyoonyeshwa kwamba Maandiko hayawapi wanadamu kibali cha kuwaruhusu kubaki
katika ujinga kuhusu kukaribia kwa marejeo ya Kristo. Walakini wale waliotamani tu kutoa udhuru wao
kwa kuikataa kweli waliziba masikio yao wasisikie ufafanuzi ule, na maneno “Hakuna aijuaye siku ile na
saa ile” yakaendelea kutoa mwangwi wake kutoka kwa mwenye dhihaka mkubwa na hata kutoka kwa
mhubiri anayesemwa kwamba anamkiri Kristo. Wakati watu walipokuwa wameamshwa, na kuanza
kuuliza kutafuta njia ya wokovu, walimu wa dini waliingia katikati, kati ya watu hao na ukweli,
wakitafuta kuzituliza hofu zao kwa kutafsiri neno la Mungu kwa uongo. Walinzi hawa wasio waaminifu
walijiunga katika kazi ya yule mwongo mkuu, wakiimba, Amani, amani, wakati Mungu alikuwa hajasema
amani. Kama Mafarisayo katika siku zake Kristo, wengi walikataa kuingia katika ufalme wa mbinguni
wao wenyewe, na kuwazuia wale waliokuwa wakitaka kuingia. Damu ya watu wale itatakiwa mikononi
mwao.
Kwa kawaida, watu waliokuwa wanyenyekevu zaidi na wacha Mungu katika makanisa ndio waliokuwa wa
kwanza kupokea ujumbe. Wale waliojifunza Biblia wao wenyewe waliiona sifa isiyo ya kimaandiko
katika maoni yaliyoonekana ya wengi kuhusu unabii; na mahali popote ambapo watu hawakudhibitiwa
na ushawishi wa viongozi wa makanisa, popote ambapo walichunguza neno la Mungu wao wenyewe,
fundisho la marejeo lilihitaji tu kulinganishwa na Maandiko ili kuweza kuthibitisha mamlaka yake ya
kimbingu.
Wengi waliteswa na ndugu zao wasioamini. Ili kulinda vyeo vyao kanisani, wengine walikubali
kunyamaza kimya kuhusu tumaini lao; lakini wengine waliona kwamba uaminifu wao kwa Mungu
uliwakataza kuficha vile ukweli ambao Mungu ameweka amana kwao. Si watu wachache walioondolewa
katika ushirika wa kanisa kwa sababu ambayo si nyingine zaidi ya ile ya kueleza imani yao katika
marejeo ya Kristo. Kwa wale waliostahimili jaribu la imani yao maneno ya nabii yalikuwa ya thamani
sana kwao: “Ndugu zenu wawachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina langu, wamesema, Na
atukuzwe BWANA, tupate kuiona furaha yenu; lakini watatahayarika.” Isaya 66:5.
Malaika wa Mungu walikuwa wakiangalia kwa shauku ya kina sana (373) matokeo ya onyo lile. Wakati
ujumbe ule ulipokataliwa na makanisa kwa ujumla, malaika waligeuka na kwenda zao kwa huzuni.
Lakini palikuwa na watu wengi ambao walikuwa hawajapimwa bado kuhusu ukweli wa marejeo. Wengi
walipotoshwa na waume zao, wake zao, wazazi wao, au watoto wao, na walifanywa kuamini kwamba
ilikuwa ni dhambi hata kusikiliza uzushi ule kama ulivyokuwa ukifundishwa na Wanamarejeo. Malaika
wale walitakiwa kuwalinda kwa uaminifu watu wale, maana nuru nyingine ilikuwa iwaangazie kutoka
katika kiti cha enzi cha Mungu.
Kwa shauku kubwa isiyosemekana wale waliokuwa wameupokea ujumbe ule walikesha wakisubiri kuja
kwa Mwokozi wao. Wakati waliotazamia kumlaki ulikuwa umekaribia. Waliikaribia saa hii kwa kicho cha
utulivu. Walistarehe katika ushirika mtamu na Mungu wao, na kuwa na ari ya kuipata amani ile ambayo
ingekuwa yao katika maisha maangavu ambayo yangefuata. Hakuna mtu aliyepitia uzoefu wa tumaini
hili na imani hii anayeweza kuusahau wakati ule wa saa za thamani za kungoja. Kwa majuma kadhaa
kabla ya wakati ule, shughuli za kidunia, kwa sehemu kubwa sana, zilikuwa zimewekwa kando. Waamini
wale wanyofu wa moyo walichunguza kila wazo na hisia ya mioyo yao kwa makini sana kana kwamba
wako katika vitanda vyao vya mauti katika hali ambayo katika saa chache wangefumba macho yao

218
wasione matukio ya dunia hii tena. Hapakuwa na uandaaji wa “mavazi ya kupaa nayo” 362; lakini wote
walihisi kuhitaji uthibitisho utokao ndani kuonyesha kwamba walikuwa wamejiandaa kumlaki Mwokozi
wao; mavazi yao meupe yalikuwa ni usafi wa moyo - yaani, tabia zolizotakaswa kutoka katika dhambi
kwa damu ya upatanisho ya Kristo. Laiti kama ingekuwa bado ipo miongoni mwa wale wanaodaiwa kuwa
watu wa Mungu roho ile ya kupeleleza moyo, imani ile ya dhati, imani ya kudhamiria. Laiti wangekuwa
wameendelea kujinyenyekeza hivyo mbele za Bwana na kuzipeleka dua zao kwa bidii mbele za kile kiti
cha rehema wangekuwa na utajiri wa uzoefu mkubwa kwa mbali kuliko ule walio nao sasa. Kuna sala
kidogo sana, kusadikishwa halisi kuhusu hatia ya dhambi ni kudogo sana, na kuwa na imani isiyo hai
kunawaacha wengi wakibaki na neema kidogo inayotolewa kwa wingi na Mwokozi wetu.
Mungu alikuwa amekusudia kuthibitisha watu wake. Mkono wake ulifunika kosa katika kuhesabu vipindi
vya unabii. Wanamarejeo (374) hawakugundua kosa lile, wala halikugunduliwa na wasomi wakubwa
sana waliokuwa miongoni mwa wapinzani wao. Hao wa mwisho walisema: “Hesabu zenu za vipindi vile
vya unabii ni sahihi. Tukio moja kubwa sana karibu sana litatokea; ila si lile analolitabiri Miller; ni
kuongoka kwa ulimwengu, wala si marejeo ya Kristo.” 363
Wakati uliotazamiwa ulipita, wala Kristo hakuja kwa ajili ya ukombozi wa watu wake. Wale ambao kwa
imani na upendo wao wa dhati walikuwa wamemngojea Mwokozi wao, walipata uzoefu wa mfadhaiko
mchungu. Lakini makusudi ya Mungu yalikuwa yanatimizwa. Alikuwa anapima mioyo ya wale waliojidai
kuwa wanakungojea kuja kwake. Miongoni mwao walikuwamo wengi ambao walikuwa wamesukumwa na
sababu ambayo si nyingine zaidi ya hofu. Kuikiri kwao imani ile kulikuwa hakujaibadilisha mioyo yao
wala maisha yao. Tukio lile walilotarajia lilipokosa kutokea, watu wale wakatangaza kwamba wao
hawakuwa wamefadhaishwa; hawakupata kamwe kuamini kwamba Kristo angekuja. Walikuwa miongoni
mwa watu wa kwanza kudhihaki huzuni waliyokuwa nayo waamini wa kweli.
Lakini Yesu na jeshi lote la mbinguni waliwatazama kwa upendo na huruma wale watu waliokuwa
wamejaribiwa na waaminifu lakini waliofadhaika. Laiti kama pazia linaloutenga ulimwengu huu
unaoonekana kwa macho lingeondolewa, malaika wangeonekana wakija karibu na watu hawa wenye
msimamo thabiti na kuwakinga wasipigwe na mishale ya Shetani.

362
Angalia maelezo ya nyongeza katika Kiambatanisho
363
Maelezo ya nyongeza yametolewa mwishoni

219
Sura ya 21
ONYO LAKATALIWA

Katika kulihubiri fundisho la marejeo ya Kristo, William Miller na wenzake walikuwa wamefanya kazi
kwa kusudi kuu la kuwaamsha watu ili wapate kujiandaa kwa ajili ya hukumu. Walikuwa wamejitahidi
sana kuwaamsha wale waliojidai kuwa na dini ili wapate kuliona tumaini la kweli la kanisa na hitaji lao
la kuwa na uzoefu wa Kikristo wa kina, na walifanya kazi pia kuwaamsha wale waliokuwa hawajaongoka
kuhusu jukumu lao la kutubu haraka na kumwongokea Mungu. “Hawakujaribu kuwaongoa watu ili
kuwaingiza katika dhehebu lolote wala sehemu fulani katika dini. Hivyo walifanya kazi miongoni mwa
makundi na madhehebu yote, bila kuingilia mambo ya kitaasisi au taratibu za nidhamu.”
Miller alisema, “Katika kazi zangu zote, sikuwa na shauku au wazo la kuanzisha maslahi yoyote mbali na
yale ya madhehebu yaliyokuwepo, au kulinufaisha dhehebu moja kwa gharama ya hasara ya jingine.
Nilifikiria kuyanufaisha yote. Nikidhani kwamba Wakristo wote wangeweza kufurahia katika kutarajia
marejeo ya Kristo, na ya kwamba wale ambao wasingeona kama mimi nilivyoona wasingewapenda kwa
namna ndogo wale ambao wangelipokea fundisho hili, sikuwaza kwamba pangekuwapo na haja yo yote
ya kuwa na mikutano iliyojitenga. Lengo langu zima lilikuwa ni shauku ya kuwaongoa watu kwa Mungu,
kuujulisha ulimwengu habari ya hukumu iliyokuwa inakuja, na kuwashawishi wanadamu wenzangu
kufanya yale maandalizi ya moyo ambayo yangewawezesha kukutana na Mungu wao kwa amani. Watu
wengi sana miongoni mwa wale waliokuwa wameongolewa kwa kazi yangu walijiunga na makanisa
yaliyokuwapo.” 364
(376) Kwa kuwa kazi yake ilikuwa na mwelekeo wa kuyajenga makanisa, kwa kipindi fulani iliangaliwa
kwa upendeleo. Lakini pindi watumishi na viongozi wa dini walipoamua kuyapinga mafundisho ya
marejeo na kutaka kukomesha vuguvugu linalohusu mada hiyo, hawakuyapinga tu kutoka katika
mimbara zao, bali pia waliwanyima washiriki wao haki ya kuhudhuria kwenye mahubiri yanayohusu kuja
kwa Kristo mara ya pili, au hata kule kuongea tu juu ya tumaini lao katika mikutano ya kijamii ya
kanisa. Hivyo waumini wale walijikuta katika majaribu na kuchanganyikiwa. Waliyapenda makanisa yao
na hawakupenda kujitenga nayo; lakini walipoona kwamba ushuhuda wa neno la Mungu unakandamizwa
na haki yao ya kuuchunguza unabii inakataliwa, waliona kwamba utii wao kwa Mungu uliwakataza
kujisalimisha. Wale waliojitahidi kuufungia nje ushuhuda wa neno la Mungu hawakuwaona hawa kama
sehemu ya Kanisa la Kristo, ambalo ni “nguzo na msingi wa kweli.” Kwa hiyo waliona kwamba wanayo
sababu ya kujitenga na miunganiko ya awali. Wakati wa majira ya joto ya mwaka 1844 karibu watu elfu
hamsini walijiengua kutoka katika makanisa yaliyokuwepo.

364
Bliss, page 328

220
Mpaka wakati huu badiliko kubwa lilionekana wazi katika yaliyo mengi ya makanisa ya Marekani. Kwa
miaka mingi palikuwa na hali iliyoendelea taratibu lakini kwa nguvu ya kufanana na mwenendo na
desturi za dunia, na kushuka kwa kiwango cha maisha halisi ya kiroho kwa uwiano ule ule; lakini mwaka
ule palikuwa na ushahidi wa mmomonyoko wa ghafla, ulioonekana waziwazi katika makanisa yote katika
nchi hii. Wakati hakuna mtu aliyeonekana kuweza kupendekeza njia ya kufuata, ukweli wenyewe
ulionekana mahali pengi na kusemwa na wanahabari na wahubiri mimbarani.
Katika mkutano wa viongozi wa kanisa kule Philadelphia, Bwana Barnes, mwandishi wa kitabu cha
ufafanuzi kilichotumika mahali pengi na mchungaji wa mojawapo la makanisa makuu katika mji ule
“alisema kwamba yeye alikuwa katika kazi ya uchungaji kwa miaka ishirini, na ya kwamba mpaka
wakati wa huduma ya meza ya Bwana iliyopita, alikuwa hajapata kamwe kutoa huduma ile bila
kuwapokea kanisani watu wa idadi kadhaa. Lakini sasa hakuna mwamko, hakuna wanaoongolewa,
hakuna ukuaji katika neema wala hakuna anayekuja kuongea naye juu ya wokovu wa roho yake kwenye
chumba chake cha kujifunzia. Pamoja na ongezeko la (377) biashara, na matumaini ya kufurahisha ya
biashara kati ya mataifa na uzalishaji wa bidhaa viwandani, lipo ongezeko la kuipenda dunia. Hivyo
ndivyo hali ya mambo ilivyo kwa madhehebu zote.” 365
Mnamo mwezi Februari mwaka ule ule, Profesa Finney wa Chuo cha Oberlin alisema: “Tulikuwa na hali
hii katika kumbukumbu zetu, kwamba, kwa jumla, Makanisa ya Kiprotestanti katika nchi yetu, kama hivi
yalivyo, ama yalikuwa hayajali, au yana uhasama karibu kwa matengenezo yote ya kimaadili katika
kizazi hiki. Yapo ambayo hayako hivyo kwa sehemu, lakini hizo tofauti hazitoshi kuufanya ukweli huo
kuwa vinginevyo zaidi ya ujumla. Pia tunao ukweli mwingine unaothibitisha: kule kutoweka karibu kote
kwa mvuto wa uamsho katika makanisa. Hali ya kutojali mambo ya kiroho imeenea karibu kote, tena ni
ya kina cha kutisha; hivyo ndivyo magazeti ya dini ya nchi nzima yanavyoshuhudia…. Mahali pengi,
washiriki wa kanisa wamejielekeza katika mitindo, - wanaungana mkono na waovu katika sherehe zao
za anasa, kucheza dansi, na katika tamasha mbalimbali, na kadhalika…. Lakini hatuna haja ya kulipanua
somo hili lililo chungu sana. Yatosha tu kwamba ushahidi unazidi kuwa mwingi sana, nao unatuangukia
juu yetu kama mzigo mzito, kutuonyesha kwamba makanisa kwa jumla yanageuka na kushukakimaadili
kwa namna ya kusikitisha sana. Yamekwenda mbali sana na Bwana, naye amejiondoa kutoka ndani
yake.”
Na mwandishi mmoja katika gazeti la Religious Telescope alishuhudia: “Kamwe hatujapata kushuhudia
kushuka kwa maadili ya dini ambako kunaonekana kila mahali kama hali ya mambo ilivyo kwa wakati
huu wa sasa. Kwa kweli, kanisa linapaswa kuamka na kuchunguza chanzo cha ugonjwa huo; kwa maana
huo ni kama ugonjwa ambao kila aipendaye Sayuni hana budi kuuona hivyo. Tunapokumbuka hali ya
wale wanaongoka kweli kweli ‘jinsi walivyo wachache mno, tena mmoja hapa na mwingine kule,’ na
kuona hali ambayo haiendani kabisa ya wenye dhambi wasiotaka kutubu, tena wagumu mno,
tunashangaa kabisa, bila kujitambua, na kusema, ‘Je! Mungu amesahau kuwa wa neema? Au, je! mlango
wa rehema umefungwa?’”
Hali kama hiyo kamwe haiwezi kuwepo bila kuwa na sababu katika kanisa lenyewe. Giza la kiroho
linalofunika juu ya mataifa, juu ya makanisa, na kwa mtu mmoja mmoja, linatokana na kutoijali au
kuikataa nuru ya Mungu kwa upande wa wanadamu, si kuondolewa kwa msaada wa neema ya Mungu
kwa upande wake. (378) Mfano halisi kabisa wa ukweli huu umetolewa katika historia ya Wayahudi
katika nyakati zile za Kristo. Kwa kuelekeza maisha katika mambo ya ulimwengu na kumsahau Mungu na

365
Congregational Journal, Mei 23, 1844

221
neno lake, ufahamu wao ulikuwa umetiwa giza, mioyo yao ikawa na mwelekeo wa vitu vya dunia na
tamaa. Kwa hiyo walikuwa katika ujinga kwa habari ya kuja kwa Masihi na katika kiburi chao na
kutokuamini kwao wakamkataa Mkombozi. Hata wakati ule Mungu hakuzuilia taifa la Israeli kupata
kujua, au kushiriki, katika mibaraka ya wokovu. Lakini wale waliokataa ukweli walipoteza hamu yote ya
kutamani zawadi ya Mbinguni. Walikuwa wamekuwa “watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya
giza” mpaka nuru iliyokuwa ndani yao ilipogeuka na kuwa giza, na lilikuwa kubwa kiasi gani giza lile!
Ni mbinu ya Shetani kwamba wanadamu washikilie desturi tu za dini wakati roho ya utauwa haipo.
Baada ya kuikataa injili, Wayahudi waliendelea kwa juhudi kubwa kuzishika taratibu zao za ibada za
zamani, walihifadhi kwa bidii ile hali ya kuwa taifa pekee, wakati wao wenyewe walilazimika kukiri
kwamba kuwako kwa Mungu kulikuwa hakuonekani tena miongoni mwao. Unabii wa Danieli ulioonyesha
bila kukosea wakati wa kuja kwa Masihi, na kwa wazi kabisa ulitabiri juu ya kifo chake, kiasi kwamba
wao walikatisha tamaa watu kujifunza unabii ule, na mwishowe marabi walitamka laana kwa wale wote
ambao wangejaribu kufanya mahesabu ya wakati ule. Katika upofu na kutojuta kwao watu wa Israeli
katika kipindi cha karne zilizofuata wamesimama, wakiwa tofauti na neema iletayo wokovu, wakiwa
hawana ufahamu wa baraka za injili, kama onyo dhahiri na la kuogofya la hatari ya kukataa nuru kutoka
mbinguni.
Popote pale panapokuwa na sababu hiyo, matokeo yale yale hufuata. Yeyote anayezuia kwa makusudi
hali za kusadikisha moyoni kuhusu wajibu ati kwa kuwa inaingilia mambo ayapendayo hatimaye
atapoteza uwezo wake wa kupambanua kati ya ukweli na uongo. Ufahamu hutiwa giza, dhamiri hufa
ganzi, moyo wake huwa mgumu, na roho hutengwa mbali na Mungu. Mahali ambapo ukweli wa kimbingu
unapigwa teke au kudharauliwa, kanisa litafunikwa na giza; imani na upendo wao utapoa, (379) na
mafarakano na upinzani vinaingia. Washiriki wa kanisa huelekeza hamu yao katika kutafuta mambo ya
kidunia, na wenye dhambi huwa wagumu katika kutotaka kutubu.
Ujumbe wa malaika wa kwanza wa Ufunuo 14, utangazao saa ya hukumu ya Mungu na kuwaita watu
kumcha Mungu na kumtukuza, ulikuwa umekusudiwa kuwatenga wale waliojiita watu wa Mungu mbali
na mivuto ipotoshayo ya ulimwengu, na kuwaamsha wapate kuiona hali yao halisi ya kuipenda dunia na
kurudi nyuma. Katika ujumbe huu, Mungu ametuma onyo kwa kanisa, ambalo, kama lingepokewa,
lingekuwa limesahihisha maovu yaliyokuwa yanawafungia mbali naye. Laiti kama wangeupokea ujumbe
kutoka mbinguni, wakinyenyekeza mioyo yao mbele za Bwana na kutafuta kwa unyofu wa moyo kufanya
maandalizi ili wapate kusimama mbele zake, Roho na uweza wa Mungu ungekuwa umeonekana wazi
miongoni mwao. Kanisa lingekuwa limefikia tena hali ile nzuri ya umoja, imani, na upendo, iliyokuwepo
katika siku zile za Mitume, wakati ule ambapo waamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja,” na
kulinena neno la Mungu kwa ujasiri, wakati ule “Bwana alipolizidisha kanisa kila siku kwa wale
waliokuwa wakiokolewa.” Matendo 4:32,31; 2:47.
Ikiwa wale wanaojiita watu wa Mungu wangeipokea nuru kama inavyoangaza juu yao kutoka katika neno
lake, wangeweza kuufikia umoja ule ambao kwa ajili ya huo Kristo aliomba, ule ambao mtume
anaueleza, “umoja wa Roho katika kifungo cha amani.” Anasema kuna “Mwili mmoja, na Roho mmoja,
kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.”
Waefeso 4:3-5.
Hayo ndiyo yalikuwa matokeo mema waliyokutana nayo wale walioupokea ujumbe wa marejeo ya
Kristo. Walitoka katika madhehebu tofauti-tofauti; na vizuizi vya kimadhehebu vilitupwa chini; misingi
ya imani ya itikadi za madhehebu iliyosigana ilivunjwa-vunjwa na kuwa kama atomu; tumaini lisilo la
kimaandiko kwamba kuna milenia ya duniani likaachwa kabisa, mtazamo usio sahihi kuhusu marejeo ya

222
mara ya pili ulisahihishwa, kiburi na kuafikiana na dunia vilifagiliwa mbali; makosa yalirekebishwa na
kuwekwa sawa; mioyo iliungana katika ushirika mtamu sana, na upendo na furaha vikatawala. Ikiwa
fundisho hili lilifanya haya (380) kwa wale wachache waliolipokea, lingefanya hivyo hivyo kwa wote
endapo wote wangelipokea.
Lakini makanisa yale kwa jumla hayakulipokea onyo lile. Watumishi wao wa injili, ambao, kama walinzi
“juu ya nyumba ya Israeli,” wangekuwa wa kwanza kuzitambua dalili za kuja kwa Yesu, walikuwa
wameshindwa kuijua ile kweli kutokana na ushuhuda wa manabii au kutokana na dalili za nyakati. Kadiri
matumaini ya kidunia na kutafuta makuu kulivyjaza moyo wao, upendo kwa Mungu na imani katika neno
lake vikawa vimepoa; na pindi fundisho la marejeo lilipotolewa liliamsha tu moyo wa chuki na
kutokuamini. Ile hali ya kwamba ujumbe ule, kwa sehemu kubwa, ulihubiriwa na watu wa kawaida wa
hali ya chini, ulichukuliwa kama zana ya kuupingia. Kama ilivyokuwa kwa ule wa zamani, ushuhuda
murua wa neno la Mungu ulikutana na swali: “Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo?”
Nao walipoona kwamba ilikuwa ni kazi ngumu kuzikanusha hoja zilizotolewa kutokana na vile vipindi vya
unabii, wengi wao waliwakatisha tamaa watu kujifunza unabii ule, wakafundisha kwamba vitabu vile
vya unabii vilikuwa vimefungwa na visingeeleweka. Watu wengi sana, wakiwaamini bila shaka
wachungaji wao, walikataa kulisikia onyo lile; na wengine, ingawa waliguswa na ukweli ule,
hawakuthubutu kuukiri, wasije “wakatengwa na sinagogi.” Ujumbe ule ambao Mungu alipeleka kwa
madhumuni ya kulipima na kulitakasa kanisa lake ulidhihirisha bila shaka jinsi ilivyokuwa kubwa sana
idadi ya wale waliokuwa wameweka mapenzi yao katika ulimwengu huu badala ya kuyaweka kwa Kristo.
Vifungo vilivyokuwa vimewafungamanisha na ulimwengu vilikuwa na nguvu kuliko mivuto ya
kuwaelekeza mbinguni. Walichagua kusikiliza sauti ya hekima ya ulimwengu huu na kuupa kisogo
ujumbe wa ukweli unaopeleleza moyo.
Kwa kulikataa onyo la malaika wa kwanza, walikataa njia iliyokuwa imewekwa na Mbingu kwa ajili ya
kuponywa kwao. Walimpiga teke mjumbe mwema ambaye angeweza kuyasahihisha maovu yao
yaliyowatenga mbali na Mungu, na kwa shauku kubwa zaidi wakageuka kutafuta urafiki kati yao na
ulimwengu. Hapa ndipo kilipokuwa chanzo cha hali ya kuogofya ya kuipenda dunia, kurudi nyuma, na
kifo cha kiroho ambavyo vilikuwa ndani ya makanisa mwaka 1844.
(381) Katika Ufunuo 14 malaika wa kwanza anafuatiwa na yule wa pili anayetangaza: “Umeanguka,
umeanguka Babeli, mji ule mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya
uasherati wake. Ufunuo 14:8. Neno hili “Babeli” limetokana na neno “Babel,” nalo huashiria
machafuko. Linatumika katika Maandiko kuonyesha mifumo ya dini ya uongo au iliyopotoka. Katika
Ufunuo 17 Babeli inaonyeshwa kama mwanamke - mfano unaotumika katika Biblia kama alama ya
kuwakilisha kanisa, mwanamke safi akiwakilisha kanisa safi, mwanamke mwovu akiwakilisha kanisa
lililoasi.
Katika Biblia tabia takatifu na ya muda wote ya uhusiano kati ya Kristo na kanisa lake inawakilishwa na
muungano wa ndoa. Bwana amewaunganisha watu wake na yeye mwenyewe kwa agano thabiti, yeye
akiahidi kuwa Mungu wao, na wao wakiahidi kuwa watu wake na wake yeye peke yake. Anasema: “Nami
nitakuposa uwe wangu kwa milele; naam, nitakuposa kwa haki, na kwa hukumu, na kwa ufadhili, na
kwa rehema.” Hosea 2:19. Na tena, anasema, “Mimi ni mume wenu.” Yeremia 3:14. Paulo naye
anatumia mfano huo huo katika Agano Jipya anaposema: “Naliwaposea mume mmoja, ili nimletee
Kristo bikira safi.” 2 Wakorintho 11:2.
Kutokuwa mwaminifu kwa kanisa dhidi ya Kristo kwa kuruhusu ujasiri na mapenzi yake kugeuziwa mbali
na Kristo, na kuruhusu moyo wake kujazwa na mambo yanayohusiana na kuyapenda mambo ya dunia,

223
kunafananishwa na kuvunja kiapo cha ndoa. Dhambi ya Israeli ya kumwacha Bwana inawakilishwa kwa
mfano huu; na upendo wa ajabu wa Mungu uliodharauliwa nao umeonyeshwa: “Nalikuapia, nikafanya
agano nawe, asema Bwana MUNGU, ukawa wangu.” “Nawe ulikuwa mzuri mno, ukafanikiwa hata
kufikilia hali ya kifalme. Sifa zako zikaenea kati ya mataifa kwa sababu ya uzuri wako; kwa maana
ulikuwa mkamilifu, kwa sababu ya utukufu wangu niliokutia,… Lakini uliutumainia uzuri wako, ukafanya
mambo ya kikahaba kwa sababu ya sifa zako.” “Kama mke wa mtu, (382) aziniye! Akaribishaye wageni
badala ya mumewe!” Ezekieli 16:8,13-15,32; Yeremia 3:20.
Katika Agano Jipya, lugha inayofanana sana na hiyo inasemawa kwa wale wajiitao Wakristo ambao
hutafuta kuwa na urafiki na dunia kwa hali ya juu zaidi ya upendeleo wa Mungu. Mtume Yakobo
anasema: “Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila
atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu”
Yule mwanamke (Babeli) wa Ufunuo 17 anaelezwa kuwa “alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau,
na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha
dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake. Na katika kipaji
cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, Siri, Babeli Mkuu, Mama wa Makahaba.” Nabii anasema:
“Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu.”
Babeli anatangazwa tena kuwa ni “mji ule mkubwa wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi.” Ufunuo
17:4-6,18. Mamlaka iliyodumisha utawala wake wa kidikteta juu ya wafalme wa ulimwengu wa Kikristo
kwa karne nyingi ni Roma. Rangi ya zambarau na nyekundu, dhahabu na kito cha thamani, na lulu,
huonyesha waziwazi hali ya utukufu na fahari ya Roma iliyozidi ya wafalme wa kawaida. Na hakuna
mamlaka nyingine ambayo kwa usahihi ingesemwa kwamba “amelewa kwa damu ya watakatifu,” kama
kanisa hilo ambalo limewatesa wafuasi wa Kristo kwa ukatili mkubwa. Babeli analaumiwa pia kwa
dhambi ya kuungana na “wafalme wa nchi” isivyo halali. Ilikuwa kwa njia ya kujitenga mbali na Bwana,
na kuungana na washenzi, ndipo kanisa la Kiyahudi liligeuka na kuwa kahaba; na Roma, akifanya
uasherati wa namna hiyo hiyo kwa kutafuta kuungwa mkono na mamlaka za kidunia, anapata hukumu
hiyo hiyo.
Babeli anasemekana kuwa ni “mama wa makahaba.” Kule kusema anao binti zake ni lazima kuwe ni
mfano wa makanisa yale yanayoshikilia mafundisho yake pamoja na mapokeo yake, na kufuata mfano
wake katika kuutupilia mbali (383) ukweli pamoja na upendeleo wa Mungu kwa madhumuni ya kufanya
muungano haramu na ulimwengu. Ujumbe wa Ufunuo 14, unaotangaza anguko la Babeli hauna budi
kuzihusu taasisi za kidini ambazo zilikuwa safi na sasa zimekuwa potofu. Kwa kuwa ujumbe huu unakuja
baada ya onyo lile la hukumu, hauna budi kutolewa katika siku za mwisho; kwa hiyo hauwezi kulihusu
kanisa la Roma peke yake, maana kanisa hilo limekuwa katika hali hiyo ya kuanguka kwa karne nyingi.
Zaidi ya hayo, katika sura ya kumi na nane ya Ufunuo, watu wa Mungu wanaitwa ili watoke Babeli. Kwa
mujibu wa andiko hili, lazima watu wa Mungu wengi bado katika Babeli. Na, ni katika taasisi zipi za dini
ambamo sehemu kubwa zaidi ya wafuasi wa Kristo wanapatikana hivi sasa? Bila shaka, ni katika
makanisa mbalimbali yanayokiri imani ya Kiprotestanti. Wakati ule wa kuinuka kwake makanisa haya
yalikuwa na msimamo bora kwa ajili ya Mungu na kweli yake, na mbaraka wake ulikuwa pamoja nao.
Hata ulimwengu usioamini ulibidishwa kukiri matokeo yenye manufaa yaliyoandamana na kuzikubali
kanuni zile za injili. Kwa maneno ya nabii kwa Israeli: “Sifa zako zikaenea kati ya mataifa kwa sababu
ya uzuri wako; kwa maana ulikuwa mkamilifu, kwa sababu ya utukufu wangu niliokutia, asema Bwana
MUNGU.” Lakini walianguka kwa tamaa ile ile ambayo ilikuwa imeleta laana na maangamizi kwa Israeli -
tamaa ya kuiga desturi za watu wasiomcha Mungu na kubembeleza ili kufanya urafiki nao. “Uliutumainia
uzuri wako, ukafanya mambo ya kikahaba kwa sababu ya sifa zako.” Ezekieli 16:14,15.

224
Makanisa mengi ya Kiprotestanti yanafuata mfano wa Roma kwa kujifungamanisha katika udhalimu
pamoja na “wafalme wa nchi” - makanisa ya dola, kwa mahusiano yake na serikali za kidunia; na
madhehebu mengine, kwa kutafuta upendeleo kutoka kwa ulimwengu. Tena neno “Babeli” - machafuko
- linaweza kufaa kutumika kwa mashirika hayo, yote yakidai kwamba yanapata mafundisho yao kutoka
katika Biblia, huku yakiwa yamegawanyika katika vikundi visivyohesabika vya madhehebu, yakiwa na
miongozo ya imani na itikadi zinazopingana-pingana.
Mbali na muungano huo wa dhambi na ulimwengu, makanisa hayo yaliyojitenga kutoka Roma
yanazidhihirisha tabia zake. (384) Kitabu cha Kanisa Katoliki la Roma kinasema kwamba: “Ikiwa Kanisa
la Roma lilipata kuwa na hatia ya kuwa na ibada ya sanamu kuhusiana na watakatifu, basi, binti yake,
Kanisa la Uingereza, anasimama katika hatia ile ile, ambaye ana makanisa kumi yaliyowekwa wakfu kwa
Maria huku wakiwa na moja lililowekwa wakfu kwa Kristo.” 366
Naye Dr. Hopkins katika makala “A Treatise on the Millennium,” anasema: “Hakuna sababu ya
kuchukulia kwamba roho ya mpinga Kristo na kazi zake ziko tu kwa kile kinachoitwa sasa Kanisa la
Roma. Makanisa ya Kiprotestanti yanacho kiwango kikubwa cha roho ya mpinga Kristo ndani yake, nayo
yako mbali sana kutoka katika hali ya kufanyiwa matengenezo kutoka kwa … ufisadi na maovu yake.” 367
Kwa habari ya kujitenga kwa Kanisa la Presbyterian kutoka Roma, Dr. Guthrie anaandika hivi: “Miaka
mia tatu iliyopita, kanisa letu, likiwa na Biblia iliyofunguliwa katika bango lake, na kauli-mbiu yake
isemayo, ‘Chunguza Maandiko,’ katika vitabu vyake, lilitoka nje ya malango ya Roma.” Halafu anauliza
swali muhimu: “Je, walitoka Babeli wakiwa safi?” 368
“Kanisa la Uingereza,” anasema Spurgeon, “linaonekana kana kwamba limeliwa ndani kwa ndani katika
imani za sakramenti; lakini kutokukubaliana na kanisa kunaonekana kuwa kitendawili cha ufidhuli cha
kifalsafa. Wale ambao ni miongoni mwa tuliodhani kwamba wana mambo mazuri zaidi wanageukia
kando mmoja baada ya mwingine kwa kuacha misingi ya imani. Mimi naamini kabisa kwamba moyo
halisi wa Uingereza umetobolewa na ukafiri mbaya sana ambao bado unadiriki hata kwenda mimbarani
na kujiita Ukristo.”
Chimbuko la uasi mkuu lilikuwa nini? Kanisa liliwezaje kujitenga na urahisi wa injili kwa mara ya
kwanza? Kwa kuafikiana na desturi za upagani, kuwezesha wapagani kuupokea Ukristo. Hata katika siku
zake, mtume Paulo alisema, “Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi.” 2 Wathesalonike 2:7.
Mnamo kipindi cha maisha ya mitume kanisa lilibaki safi. Lakini “kuelekea mwishoni mwa karne ya pili,
karibu makanisa yote yalichukua muundo mpya; urahisi wa kwanza (385) ulitoweka; na bila kujali,
kadiri wafuasi wa injili wazee walivyolala makaburini mwao, watoto wao, pamoja na waongofu wapya,…
walikuja na dini yenye muundo mpya.” 369 Kujipatia waongofu, kanuni ya imani ya Kikristo iliyoinuliwa
juu ilishushwa, na matokeo yake “gharika ya wapagani, ikitiririka kuingia kanisani, ilikuja pamoja na
desturi zake, taratibu zake za ibada, na sanamu zake. 370 Kadiri dini ya Kikristo ilipojipatia upendeleo na
kuungwa mkono na watawala wa kidunia, ilipokewa na watu wengi kwa jina tu; lakini japo walikuwa

366
Richard Challoner, The Catholic Christian Instructor, Preface, pages 21, 22
367
Samuel Hopkins, Works, vol. 2, p. 328
368
Thomas Guthrie, The Gospel in Ezekiel, page 237
369
Robert Robinson, Ecclesiastical Researches, ch. 6, par. 17, p. 51
370
Gavazzi, Lectures, page 278
225
Wakristo kwa mwonekano wa nje walikuwa, wengi “walibaki kuwa wapagani kwa ndani, hasa wakiwa
wanaabudu sanamu zao kwa siri.” 371
Je, njia ile ile haijarudiwa tena karibu katika kila kanisa lijiitalo la Kiprotestanti? Kadiri waasisi,
waliokuwa na roho ya kweli ya matengenezo, wanapokufa, watoto wao hujitokeza na “kuunda mfumo
mpya wa kazi.” Wakati wanaposhikilia miongozo ya baba zao kwa upofu wao na kukataa kupokea ukweli
wowote wa kuendeleza zaidi ya ule ulioonwa na wale, watoto wa wanamatengenezo wale huacha kwa
mbali kielelezo chao cha unyenyekevu, kujikana nafsi, na kuachana na ulimwengu huu. Kwa njia hii
“taratibu rahisi za kwanza hutoweka.” Gharika ya kidunia, iingiayo kanisani, huingia “pamoja na desturi
zake, tabia zake, na sanamu zake.”
Tazama, ni wa kuogofya kiasi gani urafiki na dunia ambao ni “uadui na Mungu” unaodumishwa miongoni
mwa wale wanaojidai kuwa wafuasi wa Kristo! Ni kwa mapana kiasi gani makanisa maarufu katika
ulimwengu wa Kikristo yameviacha viwango vya Biblia vya unyenyekevu, kujikana nafsi, urahisi, na
utauwa! John Wesley alisema, akiongelea matumizi mazuri ya fedha: “Msitapanye sehemu yo yote ya
talanta hiyo ya thamani, kwa kukidhi tu tamaa ya macho, kwa mavazi yanayozidi kiasi au ya gharama
kubwa, au kwa mapambo yasiyohitajika. Msitapanye sehemu yoyote ya fedha kwa kuzipamba nyumba
zenu; kwa samani zinazozidi kiasi au ya gharama kubwa; kwa picha za gharama, michoro, kupaka
dhahabu…. Msitoe cho chote ili kukidhi kiburi cha uzima, ili kujitafutia kutambuliwa au kusifiwa na
watu…. ‘Kadiri unavyotenda vyema wewe mwenyewe, ndivyo watu watakavyokusema vizuri.’ Kadiri
unavyovaa ‘vazi la zambarau na kitani safi’ na kufanya ‘anasa zako (386) kila siku,’ bila shaka wengi
watakusifu kwa umaridadi wako, utoaji na ukarimu wako. Lakini usinunue sifa zako hizo kwa gharama
kubwa. Bora utosheke na heshima itokayo kwa Mungu.” 372 Lakini katika makanisa mengi ya wakati wetu
mafundisho ya namna hii hayazingatiwi.
Kuikiri imani ya dini kumekuwa jambo maarufu kwa ulimwengu. Watawala, wanasiasa, wanasheria,
madaktari, wafanya biashara, hujiunga na kanisa kama njia ya kujipatia heshima na kuaminiwa na
jamii, na kuendeleza mambo ya kidunia wayapendayo. Hivyo wanatafuta kufunika miamala isiyo ya haki
chini ya kivuli cha Ukristo. Mashirika mbalimbali ya dini, yanayosukumwa na utajiri na mvuto wa
wapenda-ulimwengu hawa waliobatizwa, yanaendelea kufanya jitihada zaidi za kusaka umaarufu na
uungwaji mkono. Makanisa ya kifahari, yenye uzuri uliosababisha matumizi mabaya ya gharama kubwa
sana, yanainuliwa katika mitaa maarufu. Waabuduo humo hujivika mavazi ya gharama kubwa ya mitindo
ya kisasa. Mshahara mkubwa hulipwa kwa mchungaji mwenye kipaji cha kuburudisha na kuwavuta watu.
Mahubiri yake hayatakiwi kugusa dhambi zinazopendwa na wengi, bali yafanywe laini na ya kuvutia
masikio ya mtindo wa kisasa. Hivyo wenye dhambi za kimtindo wanasajiliwa katika vitabu vya kanisa, na
dhambi zao hizo hufichwa kinafiki kwa kujifanya wacha Mungu.
Likitoa maoni kuhusu mtazamo wa siku hizi wa wale wanaojiita Wakristo kwa ulimwengu, jarida moja
maarufu linasema: “Bila kujitambua kanisa limesalimu amri kwa roho ya kizazi hiki, na limeifanya
mifumo ya ibada zake ziendane na matakwa ya kisasa.” “Mambo yote yanayosaidia kuifanya dini iwe na
mvuto, kanisa linayatumia sasa kama zana zake.” Na mwandishi mmoja katika gazeti la New York
Independent anasema hivi kuhusu Umethodisti kama ulivyo sasa: “Mstari unaowatenga wacha Mungu na
wale wasio wa dini unafifia na kuwa kivuli chepesi, na watu walio motomoto katika pande zote mbili
wanajitahidi kwa bidii kuondoa tofauti yote iliyokuwa katika mitindo yao ya utendaji starehe.”

371
Ibid., page 278
372
Wesley, Works, Sermon 50, "The Use of Money."
226
“Umaarufu wa dini una mwelekeo wa kuongeza idadi ya wale ambao wangependa kujipatia manufaa
yake pasipo kutekeleza majukumu yaliyomo.”
(387) Howard Crosby anasema: “Ni jambo la kuangalia kwa kina kwamba tunaona kanisa la Kristo
likitimiza kwa kiwango kidogo mno mipango ya Bwana wake. Kama vile Wayahudi wa zamani
walivyoruhusu maingiliano ya kirafiki kati yao na mataifa yaliyoabudu sanamu yaibe mioyo yao toka kwa
Mungu,… ndivyo lilivyo sasa kanisa la Yesu, kwa kufanya mashirikiano na ulimwengu usioamini,
likiziacha njia za kimbingu za maisha ya kweli, na kujisalimisha lenyewe chini ya tabia zinazodhuru,
ingawa mara nyingi zinaonekana za kuaminika, za jamii isiyo na Kristo, likitumia hoja na hitimisho
ambazo ni ngeni kwa mtazamo wa mafunuo ya Mungu, na ambazo hazipatani moja kwa moja na ukuaji
katika neema.” 373
Katika wimbi hili la kuwa kama watu wa ulimwengu na kutafuta anasa, kujikana nafsi na kujinyima kwa
ajili ya Kristo ni kama vimetoweka kabisa. “Baadhi ya wanaume na wanawake walio katika maisha ya
utendaji sasa katika makanisa yetu walielimishwa, wakiwa watoto, kujinyima ili kuweza kutoa au
kufanya kitu fulani kwa ajili ya Kristo.” Lakini “ikiwa fedha inatakiwa sasa,… hakuna mtu aliye tayari
kuitwa kutoa. Oh, hakuna! Kuwa na maonyesho ya bidhaa, maonyesho ya picha, michezo ya kuigiza,
chakula cha kumbukumbu ya mambo ya kale, au kitu cha kula - chochote cha kuwaburudisha watu.”
Gavana Washburn wa Wisconsin katika ujumbe wake wa mwaka, Januari 9, 1873, alisema: “Sheria fulani
inaonekana kuhitajika ili kuzivunja shule zinazowafanya watoto kuwa wachezaji wa kamari. Hizo ziko
kila mahali. Hata kanisa (pasipo kujijua, bila shaka) wakati mwingine linakutwa likifanya kazi ya
mwovu. Matamasha ya kutoa, mikutano ya biashara na michezo ya kuhamasisha watu kutoa, wakati
mwingine kwa ajili ya kusaidia kazi za kidini na za matendo ya huruma, lakini mara nyingi kwa malengo
yenye umuhimu kidogo zaidi, michezo ya bahati nasibu, vifurushi vya zawadi, n.k, yote hayo ni mbinu
za kujipatia pesa isiyolingana na thamani ya kitu kilichotolewa. Hakuna kitu kinachovunja moyo na
kulewesha, hasa kwa vijana, kama kupata pesa au mali bila kufanya kazi. Watu wanaoheshimiwa
hujishughulisha katika biashara hizi za bahati nasibu, na kuziridhisha dhamiri zao kwa kuwaza kwamba
fedha hiyo inapelekwa katika kazi njema, si ajabu kwamba vijana wa taifa hili mara kwa mara
huangukia katika tabia zile zinazochochewa na michezo hii yenye kuhatarisha.”
(388) Roho ya maridhiano na ulimwengu inayavamia makanisa katika Ulimwengu wote wa Kikristo.
Robert Atkins, katika hotuba yake ya mahubiri aliyotoa London, anaonyesha picha ya mbaya ya uwepo
wa kushuka kwa hali ya kiroho katika nchi ya Uingereza: “Wenye haki wa kweli wanaisha duniani, wala
hakuna mtu anayeliweka hilo moyoni. Wale wanaojidai kuwa na dini siku hizi, katika kila kanisa, ni
wapenda dunia, watu wanaoafikiana na dunia, wanaopenda raha, tena wanaotamani kuheshimiwa.
Wanaitwa ili kuteswa na Kristo, lakini wanasinyaa hata kwa kulaumiwa tu…. Uasi, uasi, uasi, umetiwa
kwa nakishi mbele hasa ya kila kanisa; na kama wangejua hilo, na kama wangehisi hilo, yumkini
kungekuwa na tumaini; lakini, lo, wanasema, ‘Sisi tu matajiri, tumejitajirisha, wala hatuna haja ya
kitu.” 374
Dhambi kuu anayoshtakiwa kwayo Babeli ni kwamba “aliwanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu
ya uasherati wake.” Kikombe hiki cha kulevya anachoupa ulimwengu mzima kinawakilisha mafundisho
ya uongo ambayo ameyapokea kama matokeo ya kuungana isivyo halali na watu wakuu wa dunia. Urafiki

373
The Healthy Christian: an Appeal to the Church, pages 141, 142
374
Second Advent Library, Tract No. 39

227
wake na ulimwengu unapotosha imani yake, naye kwa upande wake anatoa mvuto potofu kwa dunia
kwa kufundisha mafundisho ya kidini yanayopingana na maneno ya wazi ya Maandiko Matakatifu.
Roma iliificha Biblia mbali na watu na kuwataka watu wote kuyakubali mafundisho yake badala ya yale
ya Biblia. Ilikuwa kazi ya Matengenezo kurejesha kwa watu neno la Mungu; lakini je, si kweli kwamba
katika makanisa ya nyakati zetu hizi watu hufundishwa kuamini matamko ya kanuni ya imani na
mafundisho ya kanisa lao badala ya Maandiko? Charles Beecher alisema, akiongea juu ya makanisa ya
Kiprotestanti: “Wanasinyaa wanaposikia neno kali dhidi ya itikadi za kanisa kwa namna ile ile ambayo
wale mababa watakatifu wangefanya kutokana na neno kali dhidi ya kuongezeka kwa hali ya
kuwatukuza watakatifu na wafia-dini walikokuwa wanakuhimiza…. Madhehebu ya kiinjili ya
Kiprotestanti yameifungamanisha kwa nguvu mikono ya watu na watu, na ya dhehebu lenyewe, kiasi
kwamba kati ya hayo yote, mtu hawezi kuwa mhubiri kabisa, popote, bila kukubali kitabu fulani kando
ya (389) Biblia…. Hakuna jambo la kukisia katika usemi kwamba nguvu ya kanuni na misingi ya imani
iliyowekwa na watu sasa inaanza kuizuia Biblia vile vile kama Roma ilivyofanya, ingawa kwa njia
tofauti.” 375
Pindi walimu waaminifu wanapolifafanua neno la Mungu, hutokea watu wenye elimu, viongozi wa kiroho
wanaojidai kuyafahamu Maandiko, ambao huyashutumu mafundisho na kuyaita ya uzushi, na hivyo
huwageuzia mbali wale wanaouliza wakitafuta kujua ukweli. Ingekuwa kwamba dunia haijalevywa kwa
mvinyo wa Babeli pasipo tumaini, watu wengi sana wangesadikishwa na kuongolewa na ukweli ulio wazi
unaokata-kata wa neno la Mungu. Lakini imani ya dini inaonekana kama vile imechanganyikiwa na kuwa
na utata kiasi kwamba watu hawajui kipi cha kuamini kama ukweli. Dhambi ya kutotubu ya ulimwengu
iko katika mlango wa kanisa.
Ujumbe wa malaika wa pili wa Ufunuo 14 ulihubiriwa kwa mara ya kwanza katika majira ya joto mwaka
1844, na halafu zaidi ulikuwa unahusu moja kwa moja makanisa ya Amerika wakati ule, mahali ambapo
onyo la hukumu lilikuwa limetangazwa karibu mahali pote na kukataliwa karibu kila mahali, na mahali
ambako kushuka kwa hali ya kiroho katika makanisa kulikuwa kwa upesi zaidi. Lakini ujumbe wa
malaika wa pili haukufikia ukamilifu wa kutimizwa kwake mwaka 1844. Wakati ule makanisa yalipitiwa
na uzoefu wa kushuka kwa maadili, kama matokeo ya kuikataa nuru ya ujumbe wa marejeo; lakini
anguko lile halikufikia ukamilifu wake. Kadiri ambavyo yameendelea kuzikataa kweli maalum za wakati
huu yamekuwa yakianguka zaidi na zaidi. Hata hivyo, bado haiwezi kusemwa kwamba “Umeanguka,
umeanguka Babeli,… maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.”
Bado yeye hajayafanya mataifa yote kufanya hivyo. Roho ile ya kuafikiana na dunia na kutojali kweli
zinazopima kwa ajili ya wakati wetu huu ipo na imekuwa ikiongezeka katika makanisa ya imani ya
Kiprotestanti katika ulimwengu wote wa Kikristo; na makanisa haya yanajumuishwa katika suto la
malaika wa pili. Lakini bado kazi ya uasi haijafikia kilele chake.
Biblia inatangaza kwamba kabla ya kuja kwa Bwana, Shetani atafanya kazi “kwa uwezo wote, na ishara
na ajabu za uongo; (390) na katika madanganyo yote ya udhalimu,” na wale ambao “hawakukubali
kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa,” wataachwa wapokee “nguvu ya upotevu, wauamini uongo.” 2
Wathesalonike 2:9-11. Ni mpaka hapo hali hii itakapofikiwa, na muungano wa kanisa na ulimwengu
utakapokamilika kabisa katika ulimwengu wote wa Kikristo, ndipo anguko la Babeli litakuwa
limekamilika. Badiliko hili ni la hatua kwa hatua, na utimilifu kamili wa Ufunuo 14:8 bado uko mbele.

375
Sermon on "The Bible a Sufficient Creed," delivered at Fort Wayne, Indiana, Feb. 22, 1846

228
Licha ya giza la kiroho na hali ya kujitenga mbali na Mungu vilivyokuwa katika makanisa yanayounda
Babeli, kundi kubwa la wafuasi waaminifu wa Kristo bado wanapatikana katika ushirika wa hayo. Wako
wengi miongoni mwao ambao hawajapata kamwe kuziona kweli maalum za wakati huu. Si wachache
ambao hawaridhishwi na hali waliyo nayo humo kwa sasa na wanahangaika kutafuta nuru iliyo wazi
zaidi. Wanatafuta pasipo mafanikio sura ya Kristo ndani ya makanisa hayo waliyomo. Kadiri makanisa
haya yanavyozidi kwenda mbali zaidi na zaidi katika kuiacha ile kweli, na kujishirikisha yenyewe karibu
zaidi na ulimwengu, tofauti kati ya matabaka mawili ya watu makanisani itakuwa pana zaidi, na
hatimaye matokeo yake yatakuwa utengano. Wakati utafika ambapo wale wanaompenda Mungu kweli
hawataweza tena kubaki pamoja na watu kama hao “wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; wenye
mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake.”
Ufunuo 18 unaelekeza katika wakati ambapo, kama matokeo ya kukataa onyo lenye ujumbe wa aina
tatu ulio katika Ufunuo 14:6-12, kanisa litakuwa limeifikia kikamilifu hali ile iliyotabiriwa na malaika wa
pili, na watu wa Mungu ambao watakuwa bado wamo katika Babeli wataitwa ili wajitenge na ushirika
wake. Ujumbe huu ni wa mwisho utakaopata kutolewa kwa ulimwengu; nao utaitimiza kazi yake.
Wakati wale ambao “hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu” (2
Wathesalonike 2:12), watakapoachwa kupokea nguvu ya upotevu na kuuamini uongo, ndipo nuru ya
ukweli itakapowaangazia wote ambao mioyo yao itakuwa imefunguliwa kuupokea, na watoto wote wa
Bwana waliobaki ndani ya Babeli watauitikia wito usemao: “TOKENI KWAKE, ENYI WATU WANGU.”
Ufunuo 18:4.

229
Sura ya 22
UNABII WATIMIZWA

Wakati ulipopita muda ambao Bwana alitazamiwa kuja, - katika majira ya kuchipua ya mwaka wa 1844,
- wale waliokuwa wametazamia kwa imani kuja kwake waliingiwa na mashaka na wasiwasi kwa kipindi
fulani. Wakati ulimwengu uliwaona kama watu waliokuwa wameshindwa vibaya na kuthibitika kuwa ni
watu waliofuata udanganyifu, chanzo chao cha faraja bado kilikuwa ni neno la Mungu. Wengi
waliendelea kuyachunguza Maandiko, wakiuchunguza upya ushahidi wa imani yao na kujifunza unabii
kwa makini ili kupata nuru zaidi. Ushuhuda wa Biblia katika kuunga mkono msimano wao ulionekana
kuwa dhahiri na wenye hitimisho. Dalili ambazo zisingeweza kukosewa zilisonda kidole katika marejeo
ya Kristo kwamba yalikuwa karibu. Mbaraka pekee wa Bwana, katika kuwaongoa wenye dhambi na
kuamsha maisha ya kiroho miongoni mwa Wakristo, ulikuwa umeshuhudia kwamba ujumbe ule ulikuwa
wa Mbinguni. Na ingawa waamini wale hawakuweza kueleza sababu ya mfadhaiko wao, walihisi
kuhakikishiwa kwamba Mungu ndiye aliyekuwa amewaongoza katika uzoefu ule uliowapata.
Mafundisho yaliyokuwa yamechukuliwa kutokana na hali yao ya kutokuwa na hakika na mashaka
yaliyokuwa yamechanganyika katika unabii ambao walikuwa wameuchukulia kuhusiana na wakati wa
marejeo, na walitiwa moyo kusubiri kwa uvumilivu katika imani kwamba kile kilichokuwa giza sasa
katika ufahamu wao kingeweza kufanywa kuwa wazi kwa wakati wake.
(392) Miongoni mwa unabii huo ulikuwa ule wa Habakuki 2:1-4: “Mimi nitasimama katika zamu yangu,
nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya
kulalamika kwangu. BWANA akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili
aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili
kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja,
haitakawia. Tazama, roho yake hujivuna, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa
imani yake.”
Mapema kadiri ya mwaka 1842 maagizo yaliyotolewa katika unabii huo ya “kuiandika njozi na kuifanya
iwe wazi sana katika vibao, ili asomaye apate kuisoma kama maji,” yalikuwa yamependekeza kwa
Charles Fitch matayarisho ya mchoro wa chati ya unabii unaoelezea maono ya Danieli na Ufunuo.
Kuchapishwa kwa mchoro ule kulichukuliwa kwamba ni kutimizwa kwa agizo la Habakuki. Hata hivyo,
hakuna aliyeng’amua kwamba kuchelewa kule kwa dhahiri katika kutimizwa kwa njozi ile - kipindi cha
230
kukawia kwake - kulikuwa kumeelezwa katika unabii ule ule. Baada ya mfadhaiko, andiko hili
lilionekana kwa umuhimu sana: “Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili
kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja,
haitakawia…. Mwenye haki ataishi kwa imani yake.”
Sehemu ya unabii wa Ezekieli pia ilikuwa chanzo cha nguvu na faraja kwa waamini wale: “Neno la
BWANA likanijia, kusema, Mwanadamu, ni mithali gani hii mliyo nayo katika nchi ya Israeli, mkisema,
Siku hizo zinakawia na maono yote hayatimizwi. Basi uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi;… Siku hizo
ni karibu, na utimilizo wa maono yote…. Mimi nitanena, na neno lile nitakalolinena litatimizwa; wala
halitakawilishwa tena.” “Hao wa nyumba ya Israeli husema, Maono hayo ayaonayo ni ya siku nyingi
zijazo, naye anatabiri habari ya nyakati zilizo mbali sana. Basi uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi,
Maneno yangu hayatakawilishwa tena hata moja, bali neno (393) nitakalolinena litatimizwa.” Ezekieli
12:2125,27,28.
Wale waliokuwa wakingojea walifurahi, wakiamini kwamba yeye aujuaye mwisho kutoka mwanzo
alikuwa ametazama kote kupitia vizazi na, akiona mapema mfadhaiko wao, alikuwa amewapa maneno
ya kuwatia moyo na tumaini. Isingekuwa sehemu zile za Maandiko, zilizowaasa kungojea kwa uvumilivu
na kuishikilia kwa nguvu ujasiri katika neno la Mungu, imani yao ingeshindwa katika saa ile ya
kujaribiwa.
Mfano wa wanawali kumi ulio katika Mathayo 25 unafafanua pia uzoefu ule waliopitia na Wanamarejeo
wale. Katika Mathayo 24, katika jibu la swali la wanafunzi wake kuhusu dalili ya kuja kwake na ya
mwisho wa ulimwengu, Kristo alionyesha baadhi ya matukio muhimu katika historia ya ulimwengu huu
na ya kanisa kuanzia wakati wa kuja kwake mara ya kwanza hadi kuja kwake mara ya pili; yaani,
maangamizi yale ya Yerusalemu, dhiki kuu ya kanisa chini ya mateso ya wapagani na mapapa, kutiwa
giza kwa jua na mwezi, na kuanguka kwa nyota mbinguni. Baada ya hayo alisema kuhusu kuja kwake
katika ufalme wake, na alisimulia mfano ulioyaeleza makundi mawili ya watumishi wanaongojea
marejeo yake. Sura ya 25 inaanza kwa maneno haya: “Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na
wanawali kumi.” Hapa linaletwa katika mtazamo kanisa linaloishi katika siku za mwisho, lile lile
lililodokezwa mwishoni mwa sura ya 24. Katika mfano huu uzoefu wa maisha yao unaelezwa kwa
mazingira ya matukio harusi katika nchi za Mashariki.
“Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda
kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. Wale waliokuwa
wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; bali wale wenye busara walitwaa
mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala
usingizi. Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki.”
Kuja kwa Kristo, kama kulivyotangazwa na ujumbe wa malaika wa kwanza, kulionekana kuwakilishwa na
kuja (394) kwa bwana arusi. Matengenezo mapana yaliyofanyika chini ya tangazo la kuja kwake upesi,
yalikuwa ni jibu la hali ile ya kutoka kwa wanawali. Katika mfano huu, kama ilivyo katika ule wa
Mathayo 24, makundi mawili yanawakilishwa. Wote walikuwa wamezitwaa taa zao, Biblia, na kwa nuru
yake walitoka kwenda kumlaki Bwana arusi. Lakini wakati “wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa
zao, wasitwae na mafuta pamoja nao,” “wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao
pamoja na taa zao.” Kundi hili la pili lilikuwa limeipokea neema ya Mungu, nguvu ya Roho Mtakatifu
inayomlika na kuumba upya, ambayo inalifanya neno lake kuwa taa ya miguu na mwanga wa njia. Kwa
kumcha Mungu walikuwa wamejifunza Maandiko ili kuijua ile kweli, na walikuwa wametafuta kwa bidii
usafi wa moyo na maisha. Hawa walikuwa na uzoefu wa maisha, imani kwa Mungu na katika neno lake,

231
uzoefu ambao usingeweza kupinduliwa na mfadhaiko na kukawia kwake. Wengine “walizitwaa taa zao,
wasitwae na mafuta pamoja nao.” Walikuwa wamesukumwa na hisia. Hofu zao zilikuwa zimeamshwa na
ujumbe mzito, lakini wao walikuwa wakitegemea imani ya ndugu zao, wakitosheka kwa kuwaka kwa
nuru ya hisia zao nzuri, bila kuwa na ufahamu sawasawa wa ukweli au kujua kazi halisi ya neema
moyoni. Hawa walikuwa wametoka kwenda kumlaki Bwana, wakiwa wamejawa na tumaini la kupata
thawabu yao mapema kwa wakati ule, lakini hawakuwa wamejiandaa kukabiliana na kukawia na
kufadhaika. Majaribu yalipokuja, imani yao ilishindwa, na nuru yao ikafifia na kuzimika.
“Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.” Kukawia kwa bwana arusi
kunawakilisha kupita kwa wakati ule aliotazamiwa Bwana kuja, ni kufadhaika, na ule mwonekano wa
kukawia. Katika wakati ule wa mashaka, shauku ya wale waliokuwa na imani ya juu juu na wale
walioamini nusu-nusu, ikaanza kuyumba, juhudi zao zikalegea; lakini wale ambao imani yao ilijengwa
juu ya msingi wa ufahamu wao wa Biblia walikuwa na mwamba chini ya miguu yao, mwamba ambao
usingeweza kufagiliwa mbali na mawimbi ya mfadhaiko. “Wote wakasinzia wakalala usingizi;” kundi
moja likiwa halijihusishi tena na limeitupilia mbali imani yake, na kundi jingine likingojea kwa saburi
mpaka nuru iliyo wazi zaidi itolewe. Lakini (395) katika usiku ule wa kujaribiwa, kundi la pili
lilionekana kupoteza, kwa kiasi fulani, juhudi yake na kujitoa kwake. Wale waliojitoa nusu-nusu na
wenye imani ya juu juu hawakuweza kujitegemeza tena katika imani ya ndugu zao hawa. Lazima kila
mmoja asimame au aanguke yeye mwenyewe.
Wakati huu, ushupavu ulianza kujitokeza. Baadhi waliokuwa wamejidai kuwa waumini wa dhati wa
ujumbe ule walilikana neno la Mungu kama kiongozi kisichokosea na, wakidai kuongozwa na Roho,
walijiachia kutawaliwa na hisia, maono, na mawazo ya kubuni. Walikuwapo baadhi walioonyesha juhudi
ya upofu na ujinga, wakiwashutumu wale wote ambao hawakuiunga mkono njia yao. Mawazo yao ya
kishupavu na matendo yao hayakupendwa na sehemu kubwa ya Wanamarejeo; lakini walichangia kuleta
upinzani kwa kazi ya ile kweli.
Shetani alikuwa anatafuta kwa njia hii namna ya kuipinga na kuiharibu kazi ya Mungu. Watu walikuwa
wameamshwa mno na harakati za marejeo, maelfu ya wenye dhambi walikuwa wameongolewa, na watu
waaminifu walikuwa wanajitoa kufanya kazi ya kuitangaza ile kweli, hata katika wakati ule wa kukawia.
Mkuu wa uovu alikuwa anapoteza raia zake; na ili kuleta upinzani kwa kazi ya Mungu, alijitahidi
kuwadanganya baadhi ya wale walioikiri imani na kuwasukuma wafanye mambo kupita kiasi. Kisha
mawakala wake wakajiweka tayari kutafuta kila kosa, kila tendo lisilofaa, na kulionyesha mbele ya watu
katika nuru iliyotiwa chumvi sana, ili kuwafanya Wanamarejeo na imani yao kuchukiwa. Hivyo kadiri
idadi ya wale aliowakusanya ili wadai kuikiri imani ya marejeo wakidhibitiwa na uwezo wake ilivyokuwa
kubwa zaidi, ndivyo ambavyo angenufaika zaidi kwa kuvuta usikivu kwao kwamba ni wawakilishi wa
jamii ya waamini.
Shetani ni “mshitaki wa ndugu zetu,” na ni roho yake inayowachochea watu kuwinda makosa na kasoro
walizo nazo watu wa Bwana, na kuyaonyesha juu ili watu wayaone, wakati matendo yao mazuri
yanaachwa bila kutajwa. Wakati wote yuko kazini wakati Mungu anapotenda kazi kwa ajili ya wokovu
wa watu. Wana wa Mungu wanapokuja kujihudhurisha mbele za Bwana, (396) Shetani anakuja pia
miongoni mwao. Katika kila uamsho yuko tayari kuwaingiza wale ambao mioyo yao haijatakaswa wala
akili zao hazina mtazamo sahihi. Wakati hawa wanapokubali mambo fulani ya ukweli, na kupata nafasi
miongoni mwa waamini, anafanya kazi kupitia kwao kuingiza nadharia zitakazowapotosha wale wasio na
hadhari. Hakuna mtu anayethibitishwa kuwa Mkristo wa kweli kwa sababu tu yeye yuko katika kundi la
wana wa Mungu, hata ndani ya nyumba ya ibada na katika meza ya Bwana. Mara kwa mara Shetani yupo

232
pale katika matukio muhimu sana akiwa katika umbile la wale anaoweza kuwatumia kama mawakala
wake.
Mkuu wa uovu anapigana vita akigombania kila urefu wa inchi ya ardhi ambayo juu yake watu wa Mungu
wanasonga mbele katika safari yao ya kwenda kwenye mji ule wa mbinguni. Katika historia yote ya
kanisa hakuna matengenezo yaliyofanywa bila kukutana na vipingamizi vikali. Hivyo ndivyo ilivyokuwa
katika siku za Paulo. Popote pale alipoinua kanisa, walikuwepo baadhi waliodai kuipokea ile imani,
lakini walioingiza uzushi, ambao, kama ungepokelewa, ungeweza kuuondoa upendo wote wa ukweli.
Luther pia aliteseka na kuwa na mfadhaiko mkubwa na dhiki kutokana na mwenendo wa washupavu wa
dini ambao walidai kwamba Mungu alikuwa amesema nao, na ambao waliyaweka mawazo yao juu zaidi
ya ushuhuda wa ule Maandiko. Wengi waliokuwa na mapungufu katika imani na uzoefu, lakini waliojawa
na kutosheka kwao wenyewe, na ambao walipenda kusikia na kusimulia mambo mapya, walidanganywa
kwa unafiki wa walimu wapya, nao wakajiunga na mawakala wa Shetani katika kazi ya kubomoa kile
ambacho Mungu alikuwa amemtuma Luther kujenga. Na Wawesley, na wengineo walioubariki
ulimwengu kwa mvuto na imani yao, walikumbana katika kila hatua na hila za Shetani katika kuwaletea
watu wenye ushupavu, wasio na ulinganifu wa akili, na waliokuwa hawajatakaswa ambao waliwaingiza
katika tatizo la ushupavu.
William Miller hakuunga mkono mivuto ile iliyoleta ushupavu wa dini. Aliungana na Luther kusema
kwamba lazima kila roho ipimwe kwa neno la Mungu. “Ibilisi ana uwezo mkubwa juu ya mioyo ya baadhi
ya watu katika (397) siku hizi. Tutajuaje kwamba wao ni wa roho ipi? Biblia inajibu: ‘Kwa matunda yao
mtawatambua.’… Kuna roho nyingi zilizokwenda katika ulimwengu wote; na sisi tumeagizwa kuzipima
hizo roho. Roho ile isiyotufanya sisi kuishi kwa kiasi, kwa haki, na kwa utauwa, katika ulimwengu huu
wa sasa, si Roho wa Kristo. Mimi nimeshawishika zaidi na zaidi kuamini kwamba Shetani ana sehemu
kubwa ya kufanya katika harakati hizi za misisimko…. Wengi miongoni mwetu wanaojifanya kutakaswa
kabisa, wanafuata mapokeo ya wanadamu, na kwa dhahiri ni wajinga wa ukweli kama walivyo wengine
wasiojidai hivyo.” 376 “Roho wa uongo atatupeleka mbali na ile kweli; na Roho wa Mungu atatutia katika
ile kweli. Lakini, ninyi mwasema, mtu anaweza kuwa katika makosa, na kufikiri kwamba ana ukweli. Ni
nini basi? Sisi twajibu, Roho na neno huafikiana. Mtu akijihukumu mwenyewe kwa neno la Mungu, naye
anaona kupatana kamili kuliko katika neno lote, basi anapaswa kuamini kwamba anayo ile kweli; ila
kama anaona roho yule anayemwongoza hapatani na utaratibu mzima wa sheria ya Mungu au Kitabu,
basi huyo aende kwa uangalifu, asije akanaswa katika mtego wa Ibilisi.” 377 “Mara nyingi nimeupata
ushahidi zaidi wa utu wa ndani kutoka kwa jicho linalolengalenga, shavu lililolowa, na sauti inayotoka
kwa kigugumizi, kuliko kutoka katika kelele zote za ulimwengu wa Kikristo.” 378
Mnamo siku zile za Matengenezo maadui wake walitupa shutuma za uovu wote wa ushupavu kwa wale
waliokuwa wakijitahidi sana kufanya kazi kwa uaminifu dhidi ya ushupavu huo. Njia hiyo hiyo ilifuatwa
na wapinzani wa harakati za marejeo. Tena wakiwa hawajatosheka na kuwaeleza vibaya na kuyakuza
makosa ya wale waliopita kiasi na washupavu, walieneza taarifa zisizokuwa nzuri ambazo hazikuwa na
chembe yoyote ya ukweli ndani yake. Watu wale walisukumwa na chuki na kisirani. Amani yao
ilisumbuliwa na kutangazwa kule kwamba Kristo alikuwa mlangoni. Walihofu kwamba huenda ikawa ni
kweli, lakini walitumaini kwamba si kweli, na hii ndiyo ilikuwa siri ya vita yao dhidi ya Wanamarejeo na
imani yao.

376
Bliss, pages 236, 237
377
The Advent Herald and Signs of the Times Reporter, vol. 8, No. 23 (Jan. 15, 1845)
378
Bliss, page 282
233
(398) Ukweli kwamba washupavu wachache waliingia katika safu za Wanamarejeo si sababu tena ya
kusema kwamba harakati ile haikuwa ya Mungu zaidi ya vile ambavyo uwepo wa washupavu wa dini na
wadanganyaji katika kanisa mnamo siku za Paulo na za Luther ungekuwa sababu tosha ya kuishutumu
kazi yao. Hebu watu wa Mungu na waamke toka usingizini na kuanza kwa dhati kazi ya kutubu na
kufanya matengenezo; hebu na wayachunguze Maandiko ili kujifunza ukweli kama ulivyo katika Yesu;
hebu na wajitoe kikamilifu kwa Mungu, na ushahidi hautawapungukia kuonyesha kwamba Shetani bado
anafanya kazi yake na yuko macho. Kwa madanganyo yote iwezekanavyo atadhihirisha nguvu zake,
akiita malaika wote walioanguka na walio katika utawala wake kumsaidia.
Kilichosababisha ushupavu wa dini na mafarakano yale si lile tangazo la marejeo ya Kristo. Haya
yalitokea katika majira ya joto ya mwaka 1844, wakati Wanamarejeo walipokuwa katika hali ya
mashaka na kuchanganyikiwa kuhusu msimamo wao halisi. Kuhubiriwa kwa ujumbe wa malaika wa
kwanza na ule wa “kilio cha usiku wa manane” kulikuwa na mwelekeo wa kuzuia ushupavu wa dini na
faraka. Wale walioshiriki katika harakati hizi za dhati walikuwa na hali ya kupatana; mioyo yao ilijazwa
na upendo kwa kila mmoja na kwa Yesu, ambaye walitazamia kumwona upesi. Imani yao moja, tumaini
lao moja, viliwainua juu kuliko udhibiti wa mvuto wowote wa kibinadamu, na viliwathibitika kuwa ngao
imara dhidi ya mashambulizi ya Shetani.
“Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. Lakini usiku wa manane, pakawa na
kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. Mara wakaondoka wanawali wale wote,
wakazitengeneza taa zao.” Mathayo 25:5-7. Katika majira ya joto ya mwaka 1844, katikati ya wakati ule
ambao mwanzoni ilidhaniwa kwamba siku 2300 zingeishia, na majira ya kupukutisha ya mwaka ule ule,
muda ambao baadaye ilionekana kwamba ndio mwisho wa siku zile, ujumbe ule ulitangazwa kwa
maneno yale yale ya Maandiko: “Haya, bwana arusi anakuja!”
Kile kilichowasukuma kufanya harakati hizi kilikuwa ni kule kungundua kwamba amri ya Artashasta kwa
ajili ya kuutengeneza na kuujenga upya mji wa Yerusalemu, ambayo ndiyo iliweka mwanzo wa kipindi
kile cha siku 2300, ilitekelezwa katika majira ya kupukutisha ya mwaka 457 K.K., wala (399) si
mwanzoni mwa mwaka huo, kama ilivyokuwa imeaminika kabla. Kuhesabu tangu majira ya kupukutisha
ya mwaka 457 K.K., miaka 2300 inakoma katika majira ya kupukutisha ya mwaka 1844. 379
Hoja zilizopatikana katika mifano ya kivuli ya Agano la Kale pia zilielekeza katika majira ya kupukutisha
kuwa ndio wakati ambapo tukio linalowakilishwa na “kutakaswa kwa patakatifu” litakapotokea. Jambo
hili liliwekwa wazi kabisa kadiri umakini ulivyowekwa katika kuangalia namna mifano ya vivuli
inayohusiana na marejeo ya Kristo ilivyotimia.
Kuchinjwa kwa mwana-kondoo wa Pasaka kulikuwa mfano wa kivuli wa kifo cha Kristo. Paulo anasema:
“Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo.” 1 Wakorintho 5:7. Mganda ule wa
malimbuko ya kwanza, ambao ulitikiswa mbele za Bwana wakati wa Pasaka, ulikuwa mfano wa kivuli wa
kufufuka kwa Kristo. Paulo anasema, akiongelea juu ya ufufuko wa Bwana na wa watu wake wote:
“Limbuko ni Kristo, baadaye walio wake Kristo, atakapokuja.” 1 Wakorintho 15:23. Kama ulivyokuwa
ule mganda unaotikiswa, ambao ulikuwa ni malimbuko ya kwanza ya nafaka yaliyokusanywa kabla ya
mavuno, Kristo naye ni malimbuko ya mavuno ya uzima wa milele ya waliokombolewa ambao katika
ufufuo ujao watakusanywa katika ghala ya Mungu.

379
Maelezo ya nyongeza yametolewa mwishoni

234
Mifano hii ya vivuli ilitimizwa, si kwa tukio tu; bali hata kwa wakati wake. Mnamo siku ya kumi na nne
ya mwezi wa kwanza wa Kiyahudi, siku ile ile na mwezi ule ule ambao kwa muda mrefu wa karne kumi
na tano mwana-kondoo wa Pasaka alikuwa amekuwa akichinjwa, Kristo, akiisha kuila Pasaka pamoja na
wanafunzi wake, alianzisha karamu ambayo ingeweka kumbukumbu ya kifo chake mwenyewe kama
“Mwana-Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Usiku ule ule alikamatwa kwa mikono
miovu na kusulibiwa na kuuawa. Na kama mfano kivuli wa mganda uliotikiswa Bwana wetu alifufuka
kutoka kwa wafu siku ya tatu, “limbuko lao waliolala,” sampuli ya wenye haki wote watakaofufuliwa,
ambao “mwili wa unyonge” wao utabadilishwa, na “kufanana na mwili wake wa utukufu.” Fungu la 20;
Wafilipi 3:21.
Kwa namna hiyo hiyo lazima mifano ya vivuli vinavyohusiana na kuja kwa Kristo mara ya pili itimizwe
kwa wakati ulioonyeshwa katika (400) huduma ya kivuli. Chini ya mfumo wa kipindi kile cha Musa
kutakaswa kwa patakatifu, au Siku kuu ya Upatanisho, kulitokea katika siku ya kumi ya mwezi wa saba
wa Kiyahudi (Mambo ya Walawi 16:29-34), wakati ambapo kuhani mkuu, akiwa amefanya upatanisho
kwa Israeli wote, na kwa njia hiyo kuziondoa dhambi zao toka patakatifu, alikuja nje na kuwabariki
watu. Hivyo ndivyo ilivyoaminika kwamba Kristo, Kuhani Mkuu wetu, angetokea kuitakasa dunia kwa
kuangamiza dhambi na wenye dhambi, na kuwabariki watu wake kwa kuwapa kutokufa. Siku ya kumi ya
mwezi wa saba, Siku kuu ya Upatanisho, wakati wa kutakaswa kwa patakatifu, ambayo katika mwaka
1844 iliangukia katika tarehe ya 22 Oktoba, ilidhaniwa kwamba ndio wakati wa kuja kwa Bwana. Hilo
lilienda sawa na ushahidi uliokwisha kutolewa kwamba siku 2300 zingekoma katika majira ya
kupukutisha, na hitimisho hilo lilionekana lisilopingika.
Katika mfano ulio katika Mathayo 25 wakati wa kungojea na kusinzia unafuatiwa na kuja kwa Bwana
arusi. Hili lilikuwa linakubaliana na sababu ambazo zimetolewa punde, kutokana vyote viwili: unabii na
mifano ya vivuli. Mambo hayo yalikuwa na ukweli wa kusadikisha; na kile “kilio cha usiku wa manane”
kilitangazwa na maelfu ya waamini.
Kama wimbi kubwa la bahari, vuguvugu la harakati zile lilifagia nchini kote. Kutoka mji hata mji, kijiji
hata kijiji, na hata katika sehemu za nchi zisozofikika lilienda, mpaka watu wa Mungu waliokuwa
wangojeao walipoamshwa kikamilifu. Ushupavu ulitoweka mbele ya tangazo lile kama umande wa
alfajiri kabla ya jua kuchomoza. Waamini waliona mashaka yao na kuchanganyikiwa vikiwa vimetoweka,
na tumaini na ujasiri viliichangamsha mioyo yao. Kazi ilikuwa haina misisimko ile ya kupitiliza ambayo
daima huonekana kunapokuwepo msisimko wa kibinadamu usiotawaliwa na neno na Roho wa Mungu.
Ilikuwa na tabia sawa na zile zilizokuwepo nyakati za kujinyenyekeza na kumrudia Bwana miongoni mwa
Israeli ya zamani zilizofuata baada ya ujumbe wa onyo kutolewa na watumishi wake. Ilibeba sifa
zinazoitambulisha kazi ya Mungu katika kila kizazi. Kulikuwa na furaha ya msisimko kidogo, ila palikuwa
na kujichunguza moyo kwa kina, kuungama dhambi, na kuachana na ulimwengu. (401) Maandalizi ya
kukutana na Bwana yalikuwa mzigo wa roho zile zilizokuwa zikiugua. Palikuwa na maombi ya uvumilivu
na kujitoa kikamilifu kwa Mungu.
Miller alisema hivi katika kuielezea kazi ile: “Hapana mwonekano mkubwa wa furaha: ambayo, kama
vile ilivyokuwa, imezimwa kwa ajili ya tukio lijalo, wakati mbingu yote na dunia vitakaposhangilia
pamoja kwa furaha isiyosemeka na iliyojaa utukufu. Hakuna kushangilia kwa makelele: hilo pia
limehifadhiwa kwa ajili ya kilele zitakazotoka mbinguni. Waimbaji wako kimya: wanangojea kujiunga na
jeshi la malaika, kwaya ya kutoka mbinguni…. Hakuna mgongano wa mawazo: wote wana moyo mmoja
na nia moja.” 380

380
Bliss, pages 270, 271
235
Mwingine aliyeshiriki katika harakati alisema: “Ilileta kila mahali hali ya kujichunguza moyo kwa undani
sana na kujinyenyekeza nafsi mbele za Mungu wa mbinguni juu. Ilisababisha kuondoa mapenzi katika
mambo ya ulimwengu huu, uponyaji wa mabishano na uhasama, kuungama makosa, kupondeka mbele
za Mungu, na kujutia mabaya, kuomba msamaha na kukubaliwa naye. Ilileta kuushusha na
kuunyenyekeza moyo, hali ambayo hatukupata kuishuhudia kamwe. Kama vile Mungu alivyoagiza kupitia
kwa Yoeli, wakati siku ya Bwana itakapokuwa imekaribia, ilileta hali ya kuirarua mioyo wala si mavazi,
na kumgeukia Bwana kwa kufunga na kulia na kuomboleza. Kama Mungu alivyosema kupitia kwa
Zekaria, roho ya neema na kuomba ilimwagwa juu ya watoto wake; nao wakamtazama yeye ambaye
walimchoma, pakawa na maombolezo makuu katika nchi,… tena wale waliokuwa wakitazamia kumwona
Bwana walijitesa nafsi zao mbele zake.” 381
Miongoni mwa harakati zote kuu za kidini tangu siku za mitume, hakuna iliyokuwa huru pasipo udhaifu
wa kibinadamu na hila za Shetani kama ile ya majira ya kupukutisha ya mwaka 1844. Hata sasa, baada
ya miaka mingi kupita, wale wote walioshiriki katika harakati zile na ambao wamesimama imara juu ya
jukwaa la ile kweli bado wanausikia mvuto mtakatifu wa kazi ile yenye heri na wanatoa ushuhuda
kwamba ilikuwa ya Mungu.
(402) Wito ulipotolewa ukisema, “Haya, bwana arusi anakuja; tokeni mwende kumlaki,” wale
waliokuwa wanangojea “wakaondoka … wakazitengeneza taa zao;” walijifunza neno la Mungu kwa bidii
na hamu kubwa ambayo hakupata kujulikana kabla. Malaika walitumwa kutoka mbinguni kuwaamsha
wale waliokuwa wamekata tamaa na kuwatayarisha kuupokea ujumbe. Kazi ile haikuwa katika hekima
na elimu ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu. Si wale wenye vipaji vikubwa waliokuwa wa kwanza
kuusikia na kuutii wito huu, bali wale waliokuwa wanyenyekevu sana na waliojitoa. Wakulima
waliyaacha mazao yao yakiwa yamesimama mashambani mwao, makanika waliziweka chini zana zao, na
kwa machozi na furaha wakatoka kwenda kulitangaza onyo lile. Wale waliokuwa walioongoza kazi kama
hii kabla walikuwa wa mwisho kujiunga na harakati hizi. Makanisa kwa ujumla wake yalifunga milango
kuukataa ujumbe huu, na kundi kubwa la wale walioupokea walijiondoa katika makanisa. Kwa maongozi
ya Mungu tangazo hili liliungana na ujumbe wa malaika wa pili na kazi ile ikawa na nguvu.
Ujumbe usemao, “Haya, bwana arusi anakuja!” haukuwa habari ya kubishaniwa sana, ingawa ushahidi
wa Maandiko ulikuwa dhahiri na usio na ubishi. Ulienda pamoja na nguvu yenye msukumo uliogusa
mioyo. Hapakuwa na mashaka, hapakuwa na maswali. Katika tukio la Kristo la kuingia mjini Yerusalemu
kwa shangwe, watu waliokuwa wamekusanyika kutoka sehemu zote za nchi kuja kusherehekea sikukuu
walikusanyika kuelekea Mlima wa Mizeituni, nao walipojiunga na msafara uliokuwa ukimsindikiza Yesu
walishikwa na msisimko uliokuwepo saa ile na wakasaidia kuzidisha sauti zilizoimba: “Ndiye mbarikiwa,
yeye ajaye kwa jina la Bwana!” Mathayo 21:9. Kwa jinsi hiyo hiyo ndivyo wasioamini waliomiminika
katika mikutano ya Wanamarejeo - baadhi kwa udadisi wao, wengine kwa ajili ya dhihaka tu -
walivyosikia nguvu ya ushawishi ulioambatana na ujumbe ule uliosema: “Haya, bwana arusi anakuja!”
Wakati ule kulikuwa na imani iliyoleta majibu kwa maombi - imani iliyokuwa inatambua thawabu. Kama
manyunyu ya mvua kwenye ardhi yenye kiu, Roho wa neema aliwashukia watafutaji wa kweli wenye
bidii. Wale (403) waliotazamia kusimama ana kwa ana na Mkombozi wao muda si mrefu walipata furaha
kubwa iliyokuwa haisemeki. Uweza wa Roho Mtakatifu ulainishao na kutiisha uliyeyusha moyo kadiri
mbaraka wake ulipotolewa kwa wingi sana juu ya wale waliokuwa waaminifu na wenye imani.
Kwa uangalifu na kwa thati wale walioupokea ujumbe waliufikia wakati ule waliotumainia kukutana na
Bwana wao. Walihisi kwamba kila asubuhi walikuwa na wajibu wa kwanza kujipatia ushahidi wa

381
Bliss, in Advent Shield and Review, vol. I, p. 271 (January, 1845)
236
kukubaliwa kwao na Mungu. Mioyo yao ilikuwa imeunganishwa kwa karibu, na waliomba sana pamoja na
kuombeana. Mara kwa mara walikutana pamoja mahali pa faragha ili kuzungumza na Mungu, na sauti ya
maombi ilipanda juu mbinguni kutoka mashambani na vichakani. Uhakika wa kupata kibali cha Mwokozi
ulikuwa wa muhimu kwao kuliko chakula chao cha kila siku; na ikiwa wingu lilitia giza mawazo yao,
hawakupumzika mpaka lilipofagiliwa mbali. Waliposikia ushuhuda wa neema ile isameheyo, walitamani
sana kumwona yeye ambaye nafsi zao zilimpenda.
Lakini kwa mara nyingine tena wakaishia katika mfadhaiko. Wakati uliotazamiwa ulipita, wala Mwokozi
wao hakutokea. Kwa imani isiyotetereka walikuwa wametazamia kuja kwake, na sasa walijisikia vibaya
kama ilivyokuwa kwa Mariamu wakati alipokuja kwenye kaburi la Mwokozi na kulikuta liko tupu,
alipopiga kelele na kulia: “Wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka.” Yohana 20:13.
Hisia ya mshangao wa hofu, woga kwamba huenda ujumbe ule ni wa kweli, kwa kipindi fulani ilikuwa
kama kizuizi kwa ulimwengu ule uliokuwa hauamini. Baada ya kupita ule wakati hali ile haikutoweka
mara moja; mwanzoni hawakuthubutu kujigamba dhidi ya wale waliopatwa na mfadhaiko; lakini kadiri
walivyoona hakuna ishara zo zote za ghadhabu ya Mungu, waliondokana na hofu zao na kurejea katika
shutuma na dhihaka zao. Kundi kubwa lililokuwa limejidai kwamba linaamini habari ya kuja upesi kwa
Bwana, likaikana imani yao. Baadhi ambao walikuwa na ujasiri mkubwa waliumia vibaya sana katika
kiburi chao kiasi kwamba walitamani kukimbia kutoka ulimwenguni. Kama Yona, walimlalamikia Mungu,
na kuchagua kifo kuliko kuishi.
(404) Wale waliokuwa wamejenga imani yao juu ya maoni ya wengine, wala sio juu ya neno la Mungu,
sasa walikuwa tayari tena kubadili maoni yao. Wenye dhihaka wakawavuta kwao wale waliokuwa dhaifu
na waoga, na wote hao wakaungana pamoja kutangaza kwamba sasa pasingekuwa na hofu tena wala
matazamio mengine zaidi. Wakati ulikuwa umepita, Bwana hakuwa amekuja, na ulimwengu
ungeendelea kubaki vile vile kwa maelfu ya miaka.
Waumini halisi na wa dhati walikuwa wamesalimisha vyote kwa ajili ya Kristo na walishiriki uwepo wake
kuliko walivyopata kufanya kabla. Kama walivyoamini, walikuwa wametoa onyo lao la mwisho kwa
ulimwengu; na, wakitazamia kupokewa punde katika jamii ya Bwana wao na ya malaika wa mbinguni,
kwa kiasi kikubwa, walikuwa wamejitenga na jamii ya wale ambao hawakuupokea ujumbe ule. Kwa
shauku kubwa ya hali ya juu walikuwa wameomba wakisema: “Njoo, Bwana Yesu, njoo upesi.” Lakini
alikuwa hakuja. Na sasa kuchukua tena mzigo mzito wa masumbufu ya maisha haya na mahangaiko, na
kustahimili masuto na kejeli za ulimwengu wenye dhihaka, vilikuwa jaribu la kutisha kwa imani na
uvumilivu.
Lakini bado kufadhaika huku hakukuwa kukubwa kama kule kulikopitiwa na wanafunzi wakati Kristo
alipokuja mara ya kwanza. Yesu alipopanda mwana-punda kuingia kwa shangwe mjini Yerusalemu,
wafuasi wake waliamini kwamba alikuwa karibu kukalia kiti cha enzi cha Daudi na kuwakomboa Israeli
kutoka kwa wakandamizaji wao. Kwa matumaini makubwa na matarajio ya furaha walishindania ukubwa
wao kwa wao kwa kuonyesha heshima yao kwa Mfalme. Wengi walitandika mavazi yao ya nje chini kama
zulia katika njia yake, au kuyapepea matawi ya mitende mbele zake. Katika furaha yao iliyojaa shauku
kubwa waliungana katika shangwe wakisema: “Hosana, Mwana wa Daudi!” Mafarisayo wale, walipokuwa
wamesumbuliwa na kukasirishwa na mlipuko ule wa furaha, walitaka Kristo awakemee wanafunzi wake,
yeye akawajibu, akisema: “Wakinyamaza hawa, mawe yatapiga kelele.” Luka 19:40. Lazima unabii
utimizwe. Wanafunzi wale walikuwa wanakamilisha kusudi la Mungu; lakini walikumbwa na mfadhaiko
mchungu. Lakini siku chache tu zilipita wakashuhudia kifo cha uchungu cha Mwokozi, na akalazwa
kaburini. Matarajio yao (405) hayakutimizwa hata kwa namna moja, na matumaini yao yalikufa pamoja

237
na Yesu. Mpaka alipofufuka akiwa mshindi ndipo waliweza kutambua kwamba yote yale yalikuwa
yametabiriwa katika unabii, na kuelezwa “kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu.”
Matendo 17:13.
Miaka mia tano kabla, Bwana alikuwa ametangaza kupitia kwa nabii Zekaria: “Furahi sana, Ee binti
Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye
ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwana-punda, mtoto wa punda.” Zekaria 9:9.
Ikiwa wanafunzi wale wangekuwa wametambua kwamba Kristo alikuwa anakwenda kuhukumiwa na
kuuawa, wasingeweza kuutimiza unabii ule.
Kwa namna hiyo hiyo Miller na wenzake walitimiza unabii na kutoa ujumbe ambao mafunuo yalikuwa
yametabiri utolewe kwa ulimwengu, lakini ukiwa ujumbe ambao wasingeutoa ikiwa wangeuelewa
kikamilifu unabii ule uliokuwa unaelekeza katika mfadhaiko, na kuleta ujumbe mwingine uliopaswa
kuhubiriwa kwa mataifa yote kabla ya kuja kwa Bwana. Ujumbe wa malaika wa kwanza na wa pili
ulitolewa kwa wakati wake sahihi na ulifanya kazi ambayo Mungu alikusudia ikamilishwe nao.
Ulimwengu ulikuwa ukisubiri, kwa kutatarajia kwamba endapo wakati ule ulipita na Kristo hakuja,
mfumo mzima wa Uadventisti usalimu amri. Lakini wakati wengi, chini ya majaribu ya nguvu, waliiacha
imani yao, walikuwepo wengine waliosimama imara. Matunda ya harakati zile za marejeo, roho ya
unyenyekevu na kujipeleleza moyo, ya kuukataa ulimwengu na kufanya matengenezo ya maisha,
ambavyo viliambatana na kazi ile, vilishuhudia kwamba ilikuwa kazi ya Mungu. Hawakuthubutu kukana
kwamba ulikuwa uweza wa Roho Mtakatifu uliokuwa umeyashuhudia mahubiri ya marejeo ya Kristo, na
hawakuweza kugundua kosa lo lote katika kuhesabu vipindi vya unabii. Watu wenye uwezo mkubwa
miongoni mwa wapinzani wao hawakuwa wamefanikiwa kupindua mfumo wao wa kutafsiri unabii. Bila
ushahidi wa Biblia, hawakuweza kukubali kukana misimano iliyokuwa imefikiwa kwa njia ya
kuyachunguza Maandiko kwa makini na kwa maombi, kwa mawazo yaliyomlikiwa (406) na Roho wa
Mungu na mioyo ikawaka kwa uweza wake ulio hai; misimamo iliyokuwa imehimili ukosoaji wa kina sana
na upinzani mkali kutoka kwa walimu wa dini walio maarufu na wenye hekima wa ulimwengu, na ambao
ulisimama imara dhidi ya nguvu zilizounganishwa za wasomi na wasemaji maarufu, pamoja na kejeli na
matukano kutoka kwa watu waheshimiwa na watu wa kutumainiwa katika jamii.
Kweli, kulikuwa na kushindwa kuhusu tukio lililotazamiwa, lakini hata hilo halikuweza kuitikisa imani
yao katika neno la Mungu. Wakati Yona alipotangaza katika mitaa ya Ninawi kwamba katika muda wa
siku arobaini mji ule ungeangamizwa kabisa, Bwana alikubali kujinyenyekeza kwa watu wa Ninawi, na
kuongeza muda wao kuangaliwa; lakini bado ujumbe ule wa Yona ulitoka kwa Mungu, na Ninawi
ulipimwa kulingana na mapenzi ya Mungu. Wanamarejeo waliamini kwamba kwa njia ile ile Mungu
alikuwa amewaongoza kulitoa onyo la hukumu. Walisema: “Limeipima mioyo ya wote waliolisikia na
kuamsha upendo kwa ajili ya kuja kwa Bwana; au limeibua chuki dhidi dhidi ya kuja kwake,
isiyojulikana, lakini ikijulikana kwa Mungu. Limechora mstari,… ili kwamba wale watakaoipima mioyo
yao, wapate kujua ni upande gani wa mstari huo wangekutwa, ikiwa Bwana angekuwa amekuja - ikiwa
wangeweza kupiga kelele kwa shangwe wakisema, ‘Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, ndiye
tuliyemngoja atuokoe; au ikiwa wangekuwa wameiita miamba na milima ili ipate kuwaangukia na
kuwaficha wasiuone uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na mbele ya hasira ya Mwana Kondoo.
Hivyo Mungu, tunavyoamini, amewapima watu wake, ameijaribu imani yao, amewahakiki, na kuona

238
kama wangesinyaa, katika saa kujaribiwa, na kuacha mahali pale ambapo yeye angependa kuwaweka;
na ikiwa wangeweza kuachana kabisa na ulimwengu huu na kutegemea kabisa katika neno la Mungu.” 382
Hisia za wale waliokuwa bado wanaamini kwamba Mungu alikuwa amewaongoza katika uzoefu uliopita
zimeonyeshwa katika maneno ya William Miller: “Ikiwa ningeishi maisha yangu tena, nikiwa na (407)
ushahidi niliokuwa nao, ili kuwa mwaminifu kwa Mungu na kwa mwanadamu ningefanya yale yale
niliyofanya.” “Natumaini kwamba nimeyatakasa mavazi yangu kutokana na damu ya watu. Nahisi
kwamba, kwa kadiri ya uwezo wangu, nimekuwa huru mbali na hatia yote katika hukumu yao.” Mtu
huyu aliandika akisema, “Ingawa nimefadhaishwa mara mbili sijasononeshwa wala kukatishwa tamaa….
Tumaini langu katika marejeo ya Kristo lina nguvu kama litakavyodumu kuwa. Nimefanya kile tu
ambacho, baada ya miaka mingi ya kutafakari kwa makini, nilijisikia kwamba ni wajibu wangu
kukifanya. Ikiwa nimekosea, imekuwa ni kwa upande wa ukarimu, upendo kwa wanadamu wenzangu, na
usadikishwaji wangu wa wajibu kwa Mungu.” “Jambo moja nilijualo mimi, sikuhubiri kingine ila kile
nilichoamini; na Mungu amekuwa pamoja nami; uweza wake umedhihirika katika kazi, na mambo mengi
mema yamefanywa.” “Watu elfu nyingi, wa aina zote, wamefanywa wajifunze Maandiko kutokana na
mahubiri ya kuhusu wakati; na kwa njia hiyo, kwa imani na kwa kunyunyiziwa damu ya Kristo,
wamepatanishwa na Mungu.” 383 “Sijapata kutafuta kupendwa na wenye kiburi, wala kuwatetemeka
ulimwengu uliponikunjia uso. Sitaweza sasa kununua upendo wao kwangu, wala sitakwenda nje ya
wajibu wangu ili kuibua chuki yao. Kamwe sitatia maisha yangu mikononi mwao, wala kurudi nyuma kwa
kuogopa kuyapoteza, natumaini, ikiwa Mungu kwa mapenzi yake ataamuru iwe hivyo.” 384
Mungu hakuwaacha watu wake; Roho wake bado aliendelea kukaa pamoja na wale ambao hawakuikana
pasipo subira nuru waliyokuwa wamepokea, na kuzishutumu harakati za marejeo. Katika Waraka kwa
Waebrania kuna maneno ya kutia moyo na maonyo kwa wale wanaojaribiwa, wanaongojea katika hatari
hii: “Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu. Maana mnahitaji saburi, ili kwamba
mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi. Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye
atakuja, wala hatakawia. Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisitasita, roho yangu
haina furaha naye. Lakini sisi hatumo miongoni mwao (408) wasitao na kupotea, bali tumo miongoni
mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.” Waebrania 10:35-39.
Maneno haya yanayohusu ukaribu wa kuja kwa Bwana ni ushahidi kwamba mausia haya yametolewa kwa
kanisa la siku za mwisho: “Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia.”
Na imedokezwa kwa uwazi kwamba kutakuwa na mwonekano wa kukawia na ya kwamba Bwana
ataonekana kana kwamba anakawia. Mashauri yaliyotolewa hapa yanafaa hasa kwa uzoefu wa
Wanamarejeo wa wakati huu. Watu wanaohusika hapa walikuwa katika hatari ya kupoteza imani.
Walikuwa wamefanya mapenzi ya Mungu kwa kufuata uongozi wa Roho wake na neno lake; lakini
hawakuweza kuelewa kusudi lake katika uzoefu wao uliopita, wala hawakuweza kutambua kwa uwazi
njia iliyokuwa mbele yao, nao walijaribiwa na kuingiwa na mashaka kuhusu ikiwa ni Mungu kweli
aliyekuwa anawaongoza. Wakati huu maneno haya yalihusika: “Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa
imani.” Kadiri mwangaza mkali wa nuru ya “kilio cha usiku wa manane” ulipokuwa umeangazia njia yao,
na wakawa wameona unabii uliofunuliwa na dalili zilizokuwa zikitimia upesi zikiwaambia kwamba kuja
kwa Kristo kulikuwa kumekaribia, walikuwa wametembea, kama vile mambo yalivyokuwa, katika nuru.
Lakini sasa wakiwa wameinamishwa chini na matumaini yaliyofadhaishwa, wangesimama tu kwa imani

382
The Advent Herald and Signs of the Times Reporter, vol. 8, No. 14 (Nov 13, 1844)
383
Bliss, pages 256, 255, 277, 280, 281
384
J. White, Life of Wm. Miller, page 315
239
kwa Mungu na katika neno lake. Ulimwengu wenye dhihaka ulikuwa unasema: “Mmedanganyika.
Acahaneni na imani yenu, na semeni kwamba harakati za marejeo zilikuwa za Shetani.” Lakini Neno la
Mungu linasema: “Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.”” Kuikana imani yao sasa, na
kuukataa uweza wa Roho Mtakatifu ulioambatana na ujumbe ule, ingekuwa ni kurudi nyuma katika
upotevu. Walitiwa moyo na kuwa thabiti kwa maneno haya ya Paulo: “Basi msiutupe ujasiri wenu,”
“maana mnahitaji saburi,” “kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, yeye ajaye atakuja, wala hatakawia.”
Njia yao pekee ya salama ilikuwa ni kuihifadhi nuru ile waliyokuwa tayari wameipokea kutoka kwa
Mungu, kuzishikilia ahadi zake, na kuendelea kuyachunguza Maandiko, na kungoja na kukesha kwa
saburi ili kupokea nuru nyingine zaidi.

Sura ya 23
PATAKATIFU NI NINI?
Andiko ambalo lilikuwa msingi na nguzo ya imani ya marejeo zaidi ya mengine yote lilikuwa ni tangazo
hili: “Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.”
Danieli 8:14. Haya yalikuwa maneno yaliyofahamika kwa waamini wote walioamini katika kurejea upesi
kwa Bwana kulikokuwa karibu. Kwa vinywa vya maelfu ya watu unabii huo ulirudiwa-rudiwa kama neno
kuu la imani yao. Wote waliona kwamba matarajio yao kung’aa sana na matumaini yao waliyoyapenda
sana yalitegemea juu ya matukio yaliyotabiriwa humo. Ilikuwa imeonyeshwa kwamba siku hizo za unabii
zingekoma katika majira ya kupukutisha ya mwaka 1844. Kama ilivyokuwa kwa watu wengine wa
ulimwengu wa Kikristo, Wanamarejeo wakati ule waliamini kwamba dunia hii, au sehemu yake, ilikuwa
ndiyo patakatifu. Walielewa kwamba kutakaswa kwa patakatifu kulikuwa ni kuitakasa dunia hii kwa
moto wa siku kuu ya mwisho, na ya kwamba jambo hili lingetokea wakati wa kuja mara ya pili. Hilo
ndilo lilikuwa hitimisho kwamba Kristo angerudi duniani mwaka 1844.
Lakini wakati ule uliowekwa ukawa umepita, na Bwana hakuwa ameonekana. Waamini walijua kwamba
neno la Mungu lisingeweza kukosea; lazima tafsiri yao ya unabii iwe na makosa; lakini kosa lile lilikuwa
wapi? Wengi kwa haraka wakarahisisha utata kwa kukana kwamba siku 2300 zilikuwa haziishii katika
mwaka wa 1844. Hakuna sababu iliyotolewa isipokuwa tu kwamba Kristo hakuja kwa wakati
waliomtazamia. Walihoji kwamba kama siku zile za unabii zilikuwa zimeisha katika mwaka wa 1844,
basi, Kristo angekuwa amerudi kuja (410) kupatakasa patakatifu kwa kuitakasa dunia hii kwa moto; na
ya kwamba kwa kuwa alikuwa hakuja, huenda siku zilikuwa hazijafika mwisho.
Kukubali hitimisho hilo ilikuwa ni kuzikana hesabu za awali za vipindi vile vya unabii. Siku 2300 zilikuwa
zimeonekana kwamba zilianza wakati ilipotangazwa amri ya Artashasta ya kuutengeneza na kuujenga
upya Yerusalemu katika majira ya kupukutisha ya mwaka wa 457 K.K. Ikichukuliwa kwamba huo ndio
mwanzo, kulikuwa na mwafaka kamili wa matukio yote yaliyotabiriwa katika maelezo ya kipindi kilicho
katika Danieli 9:25-27. Majuma sitini na tisa, miaka 483 ya kwanza katika miaka 2300, ilikuwa ifike
wakati wa Masihi, Mpakwa Mafuta; na ubatizo wa Kristo na kutiwa mafuta na Roho Mtakatifu katika
mwaka wa 27 B.K., kulitimiza kwa usahihi maelezo hayo. Katikati ya juma la sabini, Masihi alikuwa

240
akatiliwe mbali. Miaka mitatu na nusu baada ya ubatizo wake, Kristo alisulibiwa katika majira ya
kuchipua ya mwaka wa 31 B.K. Majuma yale sabini, au miaka 490, yaliwahusu Wayahudi hasa. Mwishoni
mwa kipindi hiki taifa lile lilitia muhuri wa kumkataa Kristo kwa kuwatesa wanafunzi wake, ndipo
Mitume wale walipowageukia Mataifa, mwaka 34 B.K. Miaka 490 ya kwanza katika ile 2300 ikiwa
imekwisha wakati ule, ingebaki miaka 1810. Tangu mwaka 34 B.K. miaka 1810 ingeenda hadi mwaka wa
1844. “Ndipo patakatifu patakapotakaswa,” Malaika alisema. Vipimo vyote vya matukio ya unabii
vilivyotangulia vilikuwa vimetimizwa kwa wakati wa utimilifu wake bila kuacha shaka lo lote.
Kutokana na mahesabu haya, mambo yote yalikuwa wazi na yaliafikiana, isipokuwa ilionekana kwamba
hapakuwa na tukio lo lote lililokuwa limetokea katika mwaka wa 1844 ambalo lingetoa jibu la
kutosheleza kuhusu kutakaswa kwa patakatifu. Kukataa kwamba siku zile hazikukoma wakati ule ilikuwa
ni kuliweka jambo lote katika utata, na ingekuwa ni kuishutumu misimamo iliyokuwa imewekwa
kutokana na kutimia kwa unabii mara kwa mara bila kukosea.
Lakini Mungu alikuwa amewaongoza watu wake katika harakati zile za marejeo; uweza na utukufu wake
ulikuwa umeambatana na kazi ile, na yeye asingeruhusu kazi ile iishie gizani na katika mfadhaiko,
katika kushutumiwa kwamba ilikuwa ya msisimko wa uongo na wa ushupavu. Asingeweza kuliacha neno
lake liingizwe katika mashaka na kutokuwa na uhakika. (411) Ingawa wengi waliacha njia yao ya awali
ya kuhesabu vipindi vile vya unabii na kukana usahihi wa harakati zilizojengwa juu yake, wengine
hawakuwa tayari kuvikana vipengele vya imani yao na uzoefu waliokuwa wameupata kwa kuungwa
mkono na Maandiko na ushuhuda wa Roho wa Mungu. Walisadiki ya kwamba walikuwa wametumia
kanuni nzuri za kufasiri katika kujifunza unabii ule, na ya kwamba ulikuwa ni wajibu wao kuzishikilia
zile kweli zilizokwishapatikana, na kuendelea na njia ile ya kuichunguza Biblia. Kwa maombi ya dhati
waliupitia upya msimamo wao na kujifunza Maandiko ili kugundua kosa lao. Waliposhindwa kuliona kosa
lo lote katika kuvihesabu vipindi vile unabii, waliongozwa kulichunguza kwa karibu sana somo la
patakatifu.
Katika uchunguzi wao walijifunza kwamba hapakuwa na ushahidi wo wote wa Maandiko unaounga
mkono wazo maarufu kwamba dunia ni patakatifu; lakini waliona katika Biblia maelezo kamili juu ya
somo la patakatifu, jinsi palivyo, mahali palipo, na huduma zake; ushuhuda wa waandishi watakatifu
ukiwa uko wazi na wa kutosha kuweza kuliweka suala hilo mbali na ubishani. Mtume Paulo, katika
Waraka wake kwa Waebrania, anasema: “Basi hata agano la kwanza lilikuwa na kawaida za ibada, na
patakatifu pake, pa kidunia. Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa,
na meza, na mikate ya Wonyesho; ndipo palipoitwa, Patakatifu. Na nyuma ya pazia la pili, ile hema
iitwayo Patakatifu pa patakatifu, yenye chetezo cha dhahabu, na sanduku la agano lililofunikwa kwa
dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni
iliyochipuka, na vile vibao vya agano [Amri Kumi]; na juu yake makerubi ya utukufu, yakikitia kivuli kiti
cha rehema.” Waebrania 9:1-5.
Patakatifu hapa ambapo Paulo anapataja ni ile hema iliyojengwa na Musa kwa amri ya Mungu kama
mahali pa maskani ya kidunia ya yeye Aliye Juu. “Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati
yao” (Kutoka 25:8), yalikuwa ndiyo maagizo aliyopewa Musa alipokuwa katika katika mlima pamoja na
Mungu. Wana wa Israeli walikuwa wakisafiri jangwani, (412) na hema ile ilikuwa imetengenezwa kwa
namna ambayo iliweza kuhamishwa toka mahali hata mahali; lakini ilikuwa na utukufu mwingi. Kuta
zake zilitengenezwa kwa mbao zilizosimama wima ambazo zilifunikwa kwa dhahabu nyingi na kusimikwa
katika matundu ya fedha, wakati paa lake lilitengenezwa kwa mpangilio wa mapazia, au vifuniko, lile la
nje kabisa likiwa la ngozi, la ndani kabisa likiwa la kitani iliyopambwa kwa picha za makerubi. Licha ya
ua wa nje, uliokuwa na madhabahu ya sadaka za kuteketezwa, hema yenyewe ilikuwa na vyumba viwili
241
vilivyoitwa patakatifu na patakatifu pa patakatifu, vikitenganishwa kwa pazia lenye rangi nzuri na
linalopendeza sana, au shela; pazia kama hilo liliufunga mlango wa kuingilia katika chumba cha kwanza.
Ndani ya Patakatifu palikuwa na kinara cha taa, upande wa kusini, chenye taa saba ambacho kilitoa
mwanga wake katika hema ile mchana na usiku; upande wa kaskazini ilisimama meza ya mikate ya
wonyesho; na mbele ya lile pazia lililotenganisha patakatifu na patakatifu pa patakatifu palikuwa na
madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba, mahali ambapo wingu la harufu nzuri, pamoja na maombi
ya Israeli, lilikuwa likipanda juu kila siku mbele za Mungu.
Ndani ya patakatifu pa patakatifu kulikuwa na sanduku la agano, sanduku la mti wa thamani
lililofunikwa kwa dhahabu, hifadhi ya zile mbao mbili za mawe ambazo juu yake Mungu alikuwa
ameandika sheria ya Amri Kumi. Juu ya sanduku la Agano, kikiwa ndicho kifuniko cha sanduku takatifu,
kulikuwa na kiti cha rehema, kazi nzuri sana ya usanii, makerubi wawili wakiwa wamewekwa juu yake,
mmoja mwisho huu na mwingine mwisho huu, wote wawili wakiwa wamefuliwa kwa dhahabu tupu.
Katika chumba hiki uwepo wa Mungu ulidhihirishwa katika wingu la utukufu katikati ya makerubi wale.
Baada ya Waebrania kufanya makazi yao katika nchi ya Kanaani, nafasi ya hema ile ilichukuliwa na
hekalu la Sulemani, ambalo, ingawa lilikuwa jingo la kudumu na kubwa zaidi, lilifuata uwiano ule ule,
na liliwekewa vitu kama vile vile. Katika utaratibu huu patakatifu paliendelea kuwapo – isipokuwa
wakati palipoachwa katika hali ya ukiwa wakati wa Danieli – hadi wakati wa uharibifu wake uliofanywa
na Warumi, mwaka wa 70 B.K.
Hapa ndipo patakatifu pekee palipopata kuwapo hapa duniani, ambapo panahusika na habari zozote za
Biblia. Hapa palitangazwa (413) na Paulo kuwa ni patakatifu pa agano la kwanza. Lakini, je, agano
jipya halina patakatifu pake?
Wakigeukia tena katika kitabu cha Waebrania, watafutaji wa ukweli waliona kwamba kuwako kwa
patakatifu pa agano la pili, au pa agano jipya, palikuwa pamedokezwa katika maneno ya Paulo
yaliyonukuliwa: “Basi hata agano la kwanza lilikuwa na kawaida za ibada, na patakatifu pake, pa
kidunia.” Na matumizi ya neno “hata” huashiria kwamba Paulo tayari ametaja Patakatifu hapo kabla.
Wakirudi nyuma mwanzoni mwa sura iliyotangulia, walisoma maneno haya: “Basi, katika hayo
tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye Kuhani Mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa
kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, Mhudumu wa Patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana
aliiweka wala si mwanadamu.” Waebrania 8:1,2.
Kinachofunuliwa hapa ni patakatifu pa agano jipya. Patakatifu pale pa agano la kwanza paliwekwa na
mwanadamu, palijengwa na Musa; hapa pamejengwa na Bwana, wala si mwanadamu. Katika patakatifu
pale makuhani wa kidunia walifanya huduma yao; katika patakatifu hapa, Kristo, Kuhani Mkuu wetu,
anahudumu akiwa mkono wa kuume wa Mungu. Patakatifu pa kwanza palikuwa hapa duniani, Patakatifu
hapa pengine pako mbinguni.
Zaidi ya hayo, hema ile iliyojengwa na Musa ilitengenezwa kwa kufuata mfano. Bwana alimwagiza:
“Sawasawa na haya yote nikuonyeshayo, mfano wa maskani, na mfano wa vyombo vyake vyote, ndivyo
mtakavyovifanya.” Tena aliamriwa: “Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama mfano wake ulioonyeshwa
mlimani.” Kutoka 25:9,40. Na Paulo anasema kwamba hema ya kwanza ilikuwa “ndiyo mfano wa wakati
huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhabihu zinatolewa;” kwamba vyumba vya patakatifu pake
vilikuwa “nakala za mambo yaliyo mbinguni,” na ya kwamba makuhani waliotoa sadaka kwa mujibu wa
walihudumu kwa “mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni,” na ya kwamba “Kristo hakuingia katika
patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa Patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa,
aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu.” Waebrania 9:9,23; 8:4; 9:24.
242
(414) Patakatifu pa mbinguni, anapohudumu Yesu kwa ajili yetu, ndipo pa asilia pakuu, ambapo
kutokana napo patakatifu palipojengwa na Musa palikuwa ni nakala. Mungu aliweka Roho wake juu ya
wajenzi wa patakatifu pa duniani. Ufundi wa kisanii uliodhihirishwa katika ujenzi wake ulikuwa ni
udhihirisho wa hekima ya mbinguni. Kuta zake zilikuwa na mwonekano wa dhahabu nene, zikiakisi kila
upande nuru ya taa zile saba za vinara vya dhahabu. Meza ya mikate ya wonyesho na madhabahu ya
kufukizia uvumba viling’aa kama dhahabu iliyong’arishwa sana. Pazia kubwa lililounda dari, ambalo
lilichorwa picha za malaika, lenye rangi ya samawi, na ya zambarau, na nyekundu, liliongeza uzuri wa
mandhari ile. Na ndani ya pazia lile la pili palikuwa na Shekina takatifu, mwonekano wa utukufu wa
Mungu, ambao mbele zake hakuna aliyeweza kuingia na kuwa hai, isipokuwa kuhani mkuu peke yake.
Fahari isiyo kifani ya patakatifu pa duniani iliakisi katika muono wa kibinadamu utukufu wa hekalu la
Mbinguni mahali ambapo Kristo mtangulizi wetu anahudumu kwa ajili yetu mbele ya kiti cha enzi cha
Mungu. Mahali akaapo Mfalme wa wafalme, ambapo elfu maelfu wanamtumikia, na kumi elfu mara kumi
elfu husimama mbele zake (Danieli 7:10); hekalu lile, lililojazwa na utukufu wa kiti cha enzi cha milele,
mahali ambapo maserafi, walinzi wake wanaong’aa, wanazifunika nyuso zao kwa kicho, yangeonekana,
katika jengo la kifahari sana lililopata kujengwa kwa mikono ya wanadamu, kuakisiwa kwa uzuri na
utukufu wake ingawa kwa uhafifu tu. Lakini kweli za kuhusu patakatifu pa mbinguni na kazi kuu
inayoendelea kufanyika kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu zilifundishwa kwa njia ya patakatifu pa
duniani pamoja na huduma zake.
Maeneo ya patakatifu pa mbinguni yamewakilishwa na vyumba viwili katika patakatifu duniani. Akiwa
katika maono mtume Yohana alipopewa kuona mwonekano wa hekalu la Mungu mbinguni, aliona mle
“taa saba za moto zikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi.” Ufunuo 4:5. Alimwona malaika “mwenye
chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya
madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi.” Ufunuo 8:3. Hapa nabii aliruhusiwa kuona chumba
cha kwanza (415) cha patakatifu pa mbinguni; naye aliona mle “taa saba za moto” na “madhabahu ya
dhahabu,” iliyowakilishwa na kinara cha dhahabu na madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba katika
patakatifu pa duniani. Tena, “Hekalu la Mungu likafunguliwa” (Ufunuo 11:19), kisha akaangalia ndani ya
pazia lile la ndani, ndani ya patakatifu pa patakatifu. Hapa aliona “sanduku la agano lake,”
lililowakilishwa na sanduku lile takatifu ambalo lilitengenezwa na Musa ili kuihifadhi ndani yake sheria
ya Mungu.
Hivyo ndivyo wale waliokuwa wanalichunguza somo hilo walivyopata ushahidi usiokanushika wa kuwako
kwa patakatifu mbinguni. Musa alitengeneza patakatifu pa duniani kwa mfano ule alioonyeshwa. Paulo
anafundisha kwamba mpangilio ule ulikuwa patakatifu pa kweli pa mbinguni. Na Yohana anashuhudia
kwamba aliuona mbinguni.
Katika Hekalu la mbinguni, makazi ya Mungu, kiti chake cha enzi kimethibitika katika haki na hukumu.
Katika patakatifu pa patakatifu iko sheria yake, ile kanuni kuu ya haki ambayo kwayo wanadamu wote
wanapimwa. Sanduku la agano linalohifadhi mbao zile za sheria limefunikwa na kiti cha rehema, mbele
ya kiti hicho, Kristo anamwombea mwenye dhambi kwa damu yake. Hivyo ndivyo ulivyowakilishwa
muungano wa haki na rehema katika mpango wa ukombozi wa mwanadamu. Ni hekima ya Mungu tu
inayoweza kubuni muungano huu, na ni uweza wa Mungu tu unaoweza kuutekeleza; ni muungano
unaoijaza mbingu yote mshangao na kicho. Wale makerubi wa patakatifu pa duniani, ambao kwa
heshima kuu walikiangalia kiti cha rehema, wanawakilisha shauku kubwa waliyonayo jeshi la mbinguni
katika kuitafakari kazi ya ukombozi. Hii ni siri ya rehema ambayo malaika wanatamani kuiangalia -
kwamba Mungu anaweza kutenda haki na wakati anamhesabia haki mwenye dhambi atubuye na
anarejesha upya mahusiano yake na wanadamu walioanguka; kwamba Kristo alishuka chini ili kuwainua
243
watu wengi wasi na hesabu kutoka katika shimo refu la maangamizi na kuwavika mavazi yasiyo na waa
ya haki yake mwenyewe ili wapate kuungana na malaika ambao hawajaanguka kamwe na wapate kuishi
milele katika uwepo wa Mungu.
Kazi ya Kristo kama mwombezi wa mwanadamu imeelezwa katika unabii ule mzuri wa Zekaria
unaomhusu yeye ambaye “jina lake ni Chipukizi.” Nabii huyo anasema: “Yeye (416) atalijenga hekalu la
BWANA; naye atauchukua huo utukufu; ataketi akimiliki katika kiti chake [Baba] cha enzi; na shauri la
amani litakuwa kati yao hao wawili.” Zekaria 6:12,13.
“Yeye atalijenga hekalu la BWANA.” Kwa kafara yake na upatanishi wake, Kristo ndiye msingi na mjenzi
wa kanisa la Mungu. Mtume Paulo anasonda kidole kwake kuwa ndiye “jiwe kuu la pembeni, katika yeye
jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Katika yeye ninyi
nanyi,” anasema, “mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.” Waefeso 2:20-22.
“Naye atauchukua huo utukufu.” Utukufu wa ukombozi kwa ajili ya wanadamu walioanguka ni wa
Kristo. Katika vizazi vyote milele, wimbo wa wale waliokombolewa utakuwa ni: “Yeye atupendaye na
kutuosha dhambi zetu katika damu yake,… utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele.” Ufunuo
1:5,6.
Yeye “ataketi akimiliki katika kiti chake cha enzi; naye atakuwa kuhani katika kiti chake cha enzi”. Si
sasa ambapo yuko “katika kiti chake cha enzi cha utukufu;” maana ufalme wa utukufu bado
haujaanzishwa sasa. Mungu hatampa “kiti cha enzi cha Daudi, baba yake,” yaani, ufalme ule ambao
utakuwa “hauna mwisho,” mpaka kazi yake kama matanishi itakapokwisha. Luka 1:32,33. Akiwa kama
kuhani, Kristo hivi sasa ameketi pamoja na Baba yake katika kiti chake cha enzi. Ufunuo 3:21. Akiwa
kwenye kiti kile cha enzi pamoja na Yeye wa milele, Yeye aliyekuwako milele “ameyachukua masikitiko
yetu, amejitwika huzuni zetu,” ambaye “alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya
dhambi,” ili “aweze kuwasaidia wao wanaojaribiwa.” “Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi
kwa Baba,” 1 Yohana 2:1. Maombezi yake ni yale ya mwili wake uliochomwa na kuvunjwa, wa maisha
yasiyo na waa. Viganja vyake vilivyojeruhiwa, ubavu wake uliochomwa, miguu yake iliyoumbuliwa,
anamwombea mwanadamu aliyeanguka, ambaye ukombozi wake ulinunuliwa kwa gharama kubwa mno
isiyokadirika.
“Na agano la amani litakuwa kati ya hao wawili.” Upendo wa Baba, ambao si pungufu kuliko ule wa
Mwana, ni chemchemi ya wokovu kwa wanadamu waliopotea. Yesu aliwaambia wanafunzi wake kabla
(417) hajaenda zake: “Siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea kwa Baba; kwa maana Baba
mwenyewe awapenda.” Yohana 16:26,27. Mungu alikuwa ndani ya “Kristo, akiupatanisha ulimwengu na
nafsi yake.” 2 Wakorintho 5:19. Na katika hudumainayoendelea katika patakatifu pa juu, “agano la
amani li kati ya hao wawili.” “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe
pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Yohana 3:16.
Swali linalouliza, Patakatifu ni Kitu Gani? limejibiwa kwa uwazi katika Maandiko. Neno “patakatifu,”
kama lilivyotumika katika Biblia, linahusu, kwanza, ile hema iliyojengwa na Musa, kama mfano wa
mambo yale ya mbinguni; na, pili, linahusu pale “maskani halisi” ya mbinguni, ambako patakatifu pa
duniani palikuwa panawakilisha. Wakati wa kifo cha Kristo huduma ile ya kivuli ilikoma. “Maskani halisi
ya Mungu” ya mbinguni ndipo patakatifu pa agano jipya. Na kwa vile unabii wa Danieli 8:14 umetimizwa
katika kizazi hiki, basi, patakatifu panapotajwa hapana budi kuwa pale pa agano jipya. Mwishoni mwa
siku 2300, mwaka 1844, kulikuwa hakuna patakatifu pa duniani kwa karne nyingi. Hivyo unabii
unaosema “Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa,”
bila shaka husonda kidole kwenye patakatifu pa mbinguni.
244
Lakini swali muhimu kuliko yote bado bado halijajibiwa: Maana ya kutakaswa kwa patakatifu ni nini?
Kwamba kulikuwa na huduma kama hiyo kuhusiana na patakatifu pa duniani inaelezwa katika Maandiko
ya Agano la Kale. Lakini, je, panaweza kuwako kitu cho chote cha kutakaswa kule mbinguni? Katika
Waebrania 9 kutakaswa kwa patakatifu pote pawili, yaani pa duniani na pa mbinguni, kunafundishwa
waziwazi. “Na katika torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna
ondoleo. Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya
mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo” (Waebrania 9:22,23), hata kwa damu
ya thamani ya Kristo.
Kutakaswa, katika huduma zote mbili ya kivuli na ile halisi, ni sharti kufanyike kwa damu: katika ile ya
kwanza, kwa (418) damu ya wanyama; katika ile ya pili, kwa damu ya Kristo. Paulo anaeleza, kama
sababu ya kutakaswa huko sharti kufanyike kwa damu, kwamba pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo
la dhambi. Ondoleo la dhambi, au kuondolewa katika dhambi, ni kazi ya kufanya. Lakini inakuwaje
kuwe na dhambi inayohusishwa na patakatifu, pawe pa mbinguni au pa duniani? Hilo linaweza
kujifunzwa kwa kurejea katika huduma ile ya mfano; kwa maana makuhani wale waliohudumu duniani,
walihudumu kulingana na “mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni.” Waebrania 8:5.
Huduma ya patakatifu pa duniani iligawanyika katika sehemu mbili; makuhani walihudumu kila siku
katika patakatifu, wakati mara moja kwa mwaka kuhani mkuu alifanya kazi ya pekee ya upatanisho
katika patakatifu pa patakatifu. Siku kwa siku mwenye dhambi alileta sadaka yake penye mlango wa
hema na, akiweka mkono wake juu ya kichwa cha mnyama wake wa kafara, aliungama dhambi zake,
hivyo katika mfano alizihamisha kutoka kwake yeye kwenda kwa kafara isiyo na hatia. Kisha mnyama
yule alichinjwa. “Na pasipo kumwaga damu,” asema huyo Mtume, “hakuna ondoleo la dhambi.” “Kwa
kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu.” Mambo ya Walawi 17:11. Sheria ya Mungu iliyovunjwa ilidai
uhai wa mtu aliyeivunja. Damu ile, ikiwakilisha uhai ulioondolewa wa yule mwenye dhambi, ambaye
dhambi yake ilibebwa na yule mnyama wa kafara, ilipelekwa na kuhani mpaka mahali patakatifu na
kunyunyiziwa mbele ya lile pazia, ambalo nyuma yake kulikuwa na sanduku lile la agano lenye Sheria ile
iliyokuwa imekiukwa. Kwa sherehe hii dhambi, kwa njia ya damu, ilihamishiwa patakatifu. Katika
nyakati nyingine damu haikupelekwa patakatifu; lakini baadaye nyama ile ilipaswa kuliwa na kuhani,
kama Musa alivyowaagiza wana wa Haruni, akisema: “Naye amewapa ninyi ili kuuchukua uovu wa
mkutano.” Mambo ya Walawi 10:17. Sherehe zote mbili za ibada ya kafara kwa namna ile ile moja
zilionyesha mfano wa kuihamisha dhambi toka kwa yule atubuye kwenda pale patakatifu.
Hiyo ndiyo kazi iliyoendelea, siku kwa siku, kwa mwaka mzima. Hivyo ndivyo dhambi za Israeli
zilivyohamishiwa patakatifu, na kazi maalum ilihitajika ili kuziondoa. Mungu aliagiza kwamba
upatanisho ufanyike kwa ajili ya kila (419) kimoja cha vyumba vile vitakatifu. “Naye atafanya
upatanisho kwa ajili ya mahali Patakatifu, kwa sababu ya mambo machafu ya wana wa Israeli, na kwa
sababu ya makosa yao, naam, kwa ajili ya dhambi zao zote; naye atafanya vile vile kwa ajili ya hema ya
kukutania, ikaayo pamoja nao katikati ya machafu yao.” Upatanisho ulipaswa kufanywa pia kwa ajili ya
ile madhabahu, ili “kuitakasa, ili machafu yote ya wana wa Israeli yaitoke.” Mambo ya Walawi 16:16,19.
Mara moja kwa mwaka, katika Siku kuu ya Upatanisho, kuhani aliingia katika patakatifu pa patakatifu
kwa ajili ya kupatakasa patakatifu. Kazi iliyofanyika mle ilikamilisha mzunguko wa huduma wa mwaka
mzima. Siku ile ya Upatanisho wana-mbuzi wawili waliletwa kwenye mlango wa hema, kisha kura
zilipigwa juu yao, “kura moja kwa ajili ya BWANA; na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli.” Fungu la 8.
Mbuzi yule aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Bwana ilikuwa anachinjwa kama sadaka ya dhambi kwa
ajili ya watu wote. Kisha kuhani alipaswa kuichukua damu yake mpaka ndani ya pazia na kuinyunyiza

245
juu ya kiti cha rehema na mbele ya kiti cha rehema. Damu ilipaswa pia kunyunyizwa juu ya madhabahu
ya kufukizia uvumba iliyokuwa mbele ya pazia lile.
“Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake
uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa
chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari. Na yule mbuzi
atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo na watu; naye atamwacha mbuzi jangwani.”
Fungu la 21 na 22. Mbuzi yule wa azazeli hakuweza kurudi tena katika kambi ya Israeli, na mtu yule
aliyempeleka kule mbali alitakiwa kujiosha na kuzifua nguo zake kwa maji kabla ya kurudi kambini.
Sherehe yote hii ilikusudiwa kuwafanya Waisraeli kuuona utakatifu wa Mungu na jinsi anavyochukia sana
dhambi; na, zaidi, kuwaonyesha kwamba wasingeweza kugusana na dhambi bila kunajisika. Kila mtu
alitakiwa kujitesa nafsi yake wakati kazi ya upatanisho ilipokuwa ikiendelea. Shughuli zote zilipaswa
kuwekwa kando, na mkutano wote wa Israeli ulipaswa kuitumia siku ile nzima kwa kujinyenyekeza kwa
kicho mbele za Mungu, pamoja na maombi, kufunga, na kujipeleleza moyo.
Ukweli muhimu kuhusu upatanisho unafundishwa kupitia katika huduma hiyo ya mfano wa kivuli. Aliye
mbadala alipokelewa kuchukua mahali pa mwenye dhambi; lakini dhambi yake haikufutwa kwa njia ya
damu ya yule kafara. Hiyo ilikuwa njia iliyowekwa ya kuhamisha dhambi kuzipeleka patakatifu. Kwa
toleo lile la damu mwenye dhambi alitambua mamlaka ya sheria, aliungama hatia yake ya kuivunja
sheria, na alionyesha tumaini lake la kupata msamaha kwa imani katika Mkombozi atakayekuja; lakini
hakuwa ameachiliwa huru moja kwa moja kutoka katika hukumu ya sheria. Mnamo Siku ya Upatanisho
kuhani mkuu, baada ya kuipokea sadaka kutoka kwa mkutano, aliingia patakatifu pa patakatifu akiwa na
damu ya sadaka ile, kisha aliinyunyiza juu ya kiti cha rehema, juu kabisa ya sheria, kuridhisha madai
yake. halafu, akiwa katika sifa ya mpatanishi, alizichukua dhambi zile juu yake mwenyewe na kubeba
kuziondoa patakatifu. Akiwa ameweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi wa Azazeli, aliziungama
dhambi zote zilizokuwa juu yake, hivyo kwa mfano akizihamisha kutoka kwake kwenda kwa yule mbuzi.
Kisha mbuzi yule alizichukua na kwenda nazo mbali, nazo zilihesabiwa kwamba zilikuwa zimetengwa
mbali na watu wale milele.
Hiyo ndiyo huduma iliyofanywa kwa “mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni.” Na kile kilichofanywa
kwa kivuli katika huduma ya patakatifu pa duniani kinafanywa kwa uhalisi wake katika huduma ya
patakatifu pa mbinguni. Baada ya kupaa kwake Mwokozi wetu alianza kazi yake kama kuhani mkuu
wetu. Paulo anasema: “Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa
patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu.” Waebrania
9:24.
Huduma ya kuhani kwa mwaka mzima katika chumba cha kwanza cha patakatifu, “ndani ya pazia”
ambalo lilikuwa ndio mlango uliotenganisha patakatifu na ua wa nje, huwakilisha kazi ya huduma
aliyoianza Kristo baada ya kupaa kwake. Ilikuwa kazi ya kuhani mkuu katika (421) huduma yake ya kila
siku kutoa damu ya sadaka ya dhambi mbele za Mungu, pia uvumba uliopanda juu pamoja na maombi ya
Israeli. Hivyo ndivyo Kristo anawasilisha damu yake mbele za Baba yake kwa ajili ya wenye dhambi, na
kutoa pia mbele zake maombi ya wenye dhambi waliotubu yaliyochanganywa pamoja na harufu nzuri ya
thamani ya haki yake. Hiyo ndiyo kazi iliyofanyika katika huduma ya chumba cha kwanza kule mbinguni.
Imani ya wanafunzi wake Kristo ilimfuata kule wakati alipopaa mbele ya macho yao. Hapa ndipo
matumaini yao yalipowekwa, “matumaini … tuliyo nayo,” alisema Paulo, “kama nanga ya roho, yenye
salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia, alimoingia Yesu kwa ajili yetu,
Mtangulizi wetu, amekuwa Kuhani Mkuu hata milele.” “Wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa
246
damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi milele.”
Waebrania 6:19,20; 9:12.
Kwa karne kumi na nane kazi hii ya huduma iliendelea katika chumba cha kwanza cha patakatifu. Damu
ya Kristo, ikiomba mahali pa waamini waliotubu, ilipata msamaha wao na kibali mbele za Baba, lakini
dhambi zao zilibaki bado katika vitabu vya kumbukumbu. Kama ilivyokuwa katika huduma ya kivuli
palikuwa na kazi ya upatanisho mwishoni mwa mwaka, vivyo hivyo kabla ya kazi ya Kristo ya ukombozi
kumalizika kuna kazi ya upatanisho kwa ajili ya kuiondoa dhambi mahali patakatifu. Hiyo ndiyo huduma
iliyoanza wakati zilipokoma zile siku 2300. Wakati ule, kama ilivyotabiriwa na nabii Danieli, Kuhani
wetu Mkuu aliingia patakatifu pa patakatifu, kufanya sehemu ya mwisho ya kazi yake takatifu -
kupatakasa patakatifu.
Kama zamani dhambi za watu zilivyowekwa kwa imani juu ya sadaka ile ya dhambi na kwa njia ya damu
yake kuhamishwa kwa mfano kwenda katika patakatifu pa duniani, ndivyo katika agano jipya dhambi za
yule aliyetubu zilivyowekwa kwa imani juu ya Kristo na kuhamishwa kwa hakika kwenda patakatifu pa
mbinguni. Na kama vile kutakaswa kwa mfano wa duniani kulivyokamilishwa kwa kuziondoa dhambi
ambazo kwazo palikuwa pamenajisiwa, ndivyo kutakaswa halisi kwa pale pa mbinguni
kutakavyokamilishwa kwa (422) kuziondoa, au kuzifuta, dhambi zilizoandikwa mle. Lakini kabla ya
jambo hilo kufanyika, ni lazima pawe na uchunguzi wa vitabu vile vya kumbukumbu kuona ni nani, kwa
njia ya kutubu dhambi na imani katika Kristo, ana haki ya kupewa manufaa ya upatanisho wake. Kumbe
kutakaswa kwa patakatifu kunajumuisha kazi ya upelelezi - kazi ya hukumu. Lazima kazi hii ifanyike
kabla ya kuja kwa Kristo kuwakomboa watu wake; maana anapokuja, ujira wake u pamoja naye kumlipa
kila mtu kama kazi yake ilivyo. Ufunuo 22:12.
Kwa hiyo wale walioifuatilia nuru ya neno lile la unabii waliona kwamba, badala ya kuja duniani
mwishoni mwa siku zile 2300 mwaka 1844, pale Kristo aliingia ndani ya patakatifu pa patakatifu katika
patakatifu pa mbinguni kwenda kufanya kazi ya mwisho ya upatanisho kama maandalizi ya kuja.
Ilionekana pia kwamba wakati sadaka ya dhambi ilikuwa ikisonda kidole kwa Kristo kama kafara, na
kuhani mkuu aliwakilisha Kristo kama mpatanishi, yule mbuzi wa Azazeli alikuwa mfano wa kivuli wa
Shetani, mwasisi wa dhambi, ambaye dhambi za wale waliotubu kweli kweli hatimaye zitawekwa juu
yake. Wakati kuhani mkuu, kwa mamlaka ya damu ya sadaka ya dhambi, alipoziondoa dhambi toka
patakatifu, aliziweka juu ya mbuzi yule wa azazeli. Wakati Kristo, kwa mamlaka ya damu yake
mwenyewe, anapoziondoa dhambi za watu wake kutoka katika patakatifu pa mbinguni wakati wa
kufunga huduma yake, ataziweka juu ya Shetani, ambaye, katika utekelezaji wa hukumu, lazima abebe
adhabu ya mwisho. Mbuzi wa Azazeli alipelekwa mbali katika nchi isiyokaliwa na watu, ili asiweze
kamwe kurudi tena katika kusanyiko la Israeli. Hivyo ndivyo Shetani atakavyofukuzwa milele kutoka
katika uwepo wa Mungu na wa watu wake, naye atafutiliwa mbali katika maangamizo ya mwisho ya
dhambi na wadhambi na hatakuweko.

247
Sura ya 24
KATIKA PATAKATIFU PA PATAKATIFU

Somo la patakatifu lilikuwa ufunguo ulioifungua siri ya mfadhaiko wa mwaka 1844. Lilifungua wazi
mfumo kamili wa ukweli, ulioungana na kuafikiana, kuonyesha kwamba mkono wa Mungu ulikuwa
umeongoza vuguvugu la harakati za marejeo na kuufunua wajibu wa wakati huu kwa kadiri ulivyoleta
nafasi na kazi ya watu wake katika nuru. Kama vile wanafunzi wa Yesu baada ya usiku ule wa kutisha
uliojaa utungu na kukata tamaa “walivyofurahi walipomwona Bwana,” ndivyo wale waliokuwa
wamengojea kwa imani kuja kwake mara ya pili walivyofurahi. Walikuwa wametarajia kumwona akija
katika utukufu kuwapa thawabu watumishi wake. Matumaini yao yalipovunjika, walikuwa wamekosa
kumwona Yesu, nao pamoja na Maria walilia mahali pa kaburi wakisema: “Wamemwondoa Bwana
wangu, wala mimi sijui walikomweka.” Sasa walimwona tena akiwa patakatifu pa patakatifu,
KuhaniMkuu wao mwenye huruma, ambaye punde atatokea kama Mfalme na Mwokozi wao. Nuru kutoka
patakatifu ikaangazia kipindi kilichopita, kilichopo na kile kijacho. Walijua kwamba Mungu alikuwa
amewaongoza kwa maongozi yasiyokosea. Ingawa wao wenyewe, kama wale wanafunzi wa kwanza,
walikuwa wameshindwa kuuelewa ujumbe ule waliouchukua, hata hivyo, kwa kila hali ulikuwa sahihi.
Kwa kuutangaza walikuwa wamelitimiza kusudi la Mungu, na kazi yao haikuwa bure katika Bwana.
Wakiwa wamezaliwa “mara ya pili katika tumaini lenye uzima,” walifurahi sana “kwa furaha
isiyoneneka, yenye utukufu.”
(424) Unabii wa Danieli 8:14, usemao, “Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo
patakatifu patakapotakaswa,” pamoja na ujumbe wa malaika wa kwanza, usemao, “Mcheni Mungu, na
kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja,” ulisonda kidole kwenye huduma ya Kristo katika
patakatifu pa patakatifu, yaani, kwenye hukumu ya upelelezi, na wala siyo kwenye marejeo ya Kristo
kuja kuwakomboa watu wake na kuwaangamiza waovu. Kosa halikuwa katika kufanya mahesabu ya
vipindi vya unabii, bali lilikuwa katika tukio lililopaswa kutokea mwisho wa siku zile 2300. Kupitia kosa
hili waamini wale wakapatwa na mfadhaiko, lakini bado yale yote yaliyotabiriwa na unabii huo, na yote
yale waliyokuwa na mamlaka ya Maandiko kuyatarajia, yalikuwa yametimizwa. Katika wakati ule ule
walipokuwa wakiomboleza kwa kushindwa kuyapata matumaini yao, tukio lile lililokuwa limetabiriwa
katika ujumbe ule lilikuwa limetokea, tukio ambalo halina budi kutimizwa kabla Bwana hajaweza
kutokea kuwapa thawabu watumishi wake.
Kristo alikuwa amekuja, sio duniani kama walivyotazamia, bali, kama ilivyoonyeshwa katika mfano wa
kivuli, patakatifu pa patakatifu katika hekalu la Mungu lililoko mbinguni. Nabii Danieli anamwonyesha
wakati huu kama anakuja kwa Mzee wa Siku: “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye

248
mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu” - si kuja duniani, bali -“akamkaribia huyo
Mzee wa Siku, wakamleta karibu naye.” Danieli 7:13.
Kuja huku kumetabiriwa pia na nabii Malaki: “Naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafla;
naam, yule Mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema BWANA wa majeshi.” Malaki
3:1. Kuja kwake Bwana katika hekalu lake kulikuwa kwa ghafla, hakukutarajiwa na watu wake.
Hawakumtazamia pale. Walimtazamia kuja duniani, “katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao
wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili.” 2 Wathesalonike 1:8.
Lakini watu walikuwa bado hawajawa tayari kukutana na Bwana wao. Kulikuwa bado na kazi ya
maandalizi iliyohitaji (425) kufanywa nao. Nuru ingetolewa, inayoelekeza mawazo yao kwenye hekalu
la Mungu lililoko mbinguni; nao kama wangemfuata kwa imani Kuhani Mkuu wao katika huduma yake
pale, majukumu mapya yangefunuliwa kwao. Ujumbe mwingine wa onyo na mafundisho ulikuwa
utolewe kwa kanisa.
Nabii anasema: “Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama
atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha na kuitakasa, naye
atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea BWANA dhabihu
katika haki.” Malaki 3:2,3. Wale wanaoishi duniani wakati maombezi ya Kristo yatakapokoma katika
patakatifu huko juu watapaswa kusimama mbele za Mungu Mtakatifu bila kuwa na mpatanishi. Mavazi
yao hayana budi kuwa bila mawaa, tabia zao ni lazima zitakaswe na kuwa mbali na dhambi kwa njia ya
damu ya kunyunyiza. Kwa neema yake Mungu na juhudi yao kubwa wanapaswa kuwa washindi katika
vita yao dhidi ya uovu. Wakati hukumu ya upelelezi inaendelea kule mbinguni, wakati dhambi za
waamini waliotubu zinaondolewa toka Patakatifu, lazima iwepo kazi maalum ya utakaso miongoni mwa
watu wa Mungu walio juu ya uso wa dunia, ya kuziweka mbali dhambi. Kazi hiyo imeelezwa kwa wazi
zaidi katika ujumbe wa Ufunuo 14.
Wakati kazi hii itakapokuwa imekamilika, wafuasi wa Kristo watakuwa tayari kwa kuja kwake. “Wakati
ule ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele za BWANA, kama katika siku za kale,
na kama katika miaka ya zamani.” Malaki 3:4. Hapo ndipo kanisa lile atakalolinyakua wakati wa kuja
kwake litakuwa ni “Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi, wala lo lote kama hayo.” Waefeso 5:27.
Hapo ndipo litakapoonekana “kama alfajiri, zuri kama mwezi, safi kama jua, kutisha kama wenye
endera?” Wimbo Ulio Bora 6:10.
Mbali na kuja kwa Bwana katika hekalu lake, Malaki pia anatabiri kuja kwake mara ya pili, kuja kwake
kutekeleza hukumu, kwa maneno haya: “Nami nitawakaribieni (426) ili kuhukumu; nami nitakuwa
shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao
wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na
kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema BWANA wa majeshi.” Malaki 3:5.
Yuda analitaja tukio lilo hilo anaposema, “Angalia Bwana anakuja namaelfu kumi ya watakatifu wake,
ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwathibitishia wote wasiomcha Mungu miongoni mwao
matendo yao yote maovu waliyoyatenda kwa uovu wao.” Yuda 14,15. Kuja huku, na kuja kwa Bwana
katika hekalu lake, ni matukio mawili tofauti na yaliyotengana.
Kuja kwa Kristo kama kuhani wetu mkuu katika patakatifu pa patakatifu, kwa ajili ya kupatakasa
patakatifu, kunakoonyeshwa katika Danieli 8:14; kuja kwa Mwana wa Adamu kwa Mzee wa Siku, kama
kunavyoonyeshwa katika Danieli 7:13; na kuja kwake Bwana katika hekalu lake, kama alivyotabiri
Malaki, ni maelezo ya tukio lile lile moja; tena tukio hilo ndilo limewakilishwa pia na kuja kwa bwana
arusi arusini kulikoelezwa na Kristo katika mfano wa wanawali kumi, wa Mathayo 25.
249
Katika majira ya joto na ya kupukutisha ya mwaka wa 1844, tangazo hili, “Haya Bwana Arusi yuaja,”
lilitolewa. Makundi yale mawili yaliyowakilishwa na wanawali wenye busara na wapumbavu yalikuwa
yamejitokeza - kundi moja la wale waliotazamia kwa furaha kuja kwa Bwana, na ambao walikuwa
wanajiandaa kwa bidii kukutana naye; na kundi jingine ni lile lililokuwa limetosheka na nadharia ya
ukweli, likishawishiwa na hofu na kutenda kwa msisimko, huku likipungukiwa na neema ya Mungu.
Katika mfano huo, wkati bwana arusi alipokuja, “nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini.”
Kuja kwa Bwana Arusi, kunakoonyeshwa hapa, kunatokea kabla ya arusi. Arusi hiyo inawakilisha hali ya
Kristo akiupokea ufalme wake. Mji Mtakatifu, yaani, Yerusalemu Mpya, ambao ni mji mkuu na
kiwakilishi cha ufalme, unaitwa “bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.” “Akanichukua katika Roho,”
anasema nabii, “akanionyesha ule Mji Mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi
Mungu.” Ufunuo (427) 21:9,10. Ni dhahiri, basi, kwamba Bibi-arusi anawakilisha Mji ule Mtakatifu, na
wanawali wanaotoka kwenda kumlaki Bwana Arusi ni mfano wa kanisa. Katika kitabu cha Ufunuo watu
wa Mungu wanasemekana ya kwamba ni wageni walioalikwa katika karamu ya arusi. Ufunuo 19:9. Kama
ni wageni, basi, hawawezi kuwakilishwa hapo kama bibi-arusi pia. Kristo, kama alivyoeleza Danieli,
atapokea toka kwa yule Mzee wa Siku, “mamlaka, na utukufu, na ufalme,” yaani, ataipokea,
Yerusalemu Mpya, Mji Mkuu wa ufalme wake, ukiwa “umewekwa tayari kama bibi-arusi aliyekwisha
kupambwa kwa mumewe.” Danieli 7:14; Ufunuo 21:2. Baada ya yeye kuupokea ufalme huo, ndipo
atakuja katika utukufu wake kama Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana, kwa madhumuni ya
kuwakomboa watu wake, ambao “wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo” mezani pake
katika ufalme wake (Mathayo 8:11; Luka 22:30), kula karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo.
Tangazo lililosema, “Haya, Bwana-arusi yuaja,” lililotolewa katika majira ya kiangazi ya mwaka 1844,
liliwafanya wengi kutazamia kuja upesi kwa Bwana. Katika wakati uliokubalika Bwana-arusi akaja, si
duniani, kama watu walivyotarajia, bali kwa yule Mzee wa Siku kule mbinguni, kwenye arusi, katika
mapokezi ya ufalme. “Nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.”
Wasingeweza kuwako kule arusini kimwili; maana inafanyika mbinguni, wakati wao wako duniani.
Wafuasi wa Kristo wanatakiwa ku“mngojea Bwana wao, atakaporudi kutoka arusini.” Luka 12:36. Lakini
yawapasa kuijua kazi yake, na kumfuata kwa imani anapoingia mbele za Mungu. Ni kwa maana hii ndipo
wanasemekana kuingia arusini.
Katika mfano huo ilikuwa ni wale waliokuwa na mafuta katika vyombo vyao na taa zao ambao waliingia
pamoja naye arusini. Wale ambao, pamoja na ujuzi wao wa ukweli kutoka katika Maandiko, pia
walikuwa na Roho wa neema ya Mungu, na ambao, katika usiku ule wa uchungu wa maonjo, walikuwa
wamengojea kwa uvumilivu, wakiichunguza Biblia ili kupata nuru iliyo wazi zaidi - hawa waliona ukweli
kuhusu patakatifu pa mbinguni na badiliko katika huduma ya Mwokozi wao, na kwa imani walimfuata
katika kazi yake katika patakatifu pa juu. Na wale wote ambao kupitia shuhuda za Maandiko
wanazikubali (428) kweli hizo hizo, wakimfuata Kristo kwa imani anapoingia mbele za Mungu kufanya
kazi yake ya mwisho ya upatanisho, na mwisho wake kuupokea ufalme wake - wote hao huonyeshwa
kama wanaingia pamoja naye arusini.
Katika mfano ulio katika Mathayo 22 kielelezo kile kile cha arusi kinatolewa, na hukumu ya upelelezi
inaonyeshwa waziwazi kama inafanywa kabla ya arusi. Kabla ya arusi mfalme anaingia kuwaona wageni
wake, kuona kama wote wamevaa vazi la arusi, vazi lisilo na waa la tabia lililoonywa na kufanywa jeupe
katika damu ya Mwana-Kondoo. Mathayo 22:11; Ufunuo 7:14. Yule anayeonekana kupungua anatupwa
nje, lakini wale wote ambao baada ya kukaguliwa wanaonekana kuwa wanalo vazi la arusi
wanakubaliwa na Mungu na kuhesabiwa kuwa wanastahili kushiriki katika ufalme wake na kuwa na kiti
katika kiti chake cha enzi. Kazi hiyo ya kupima tabia, ya kuona kwamba ni wepi wako tayari kuingia

250
katika ufalme huo wa Mungu, ni kazi ya hukumu ya upelelezi, kazi ya kukamilishia huduma katika
patakatifu pa mbinguni.
Pindi kazi ya upelelezi itakapofika mwisho, wakati kesi za wale ambao katika vizazi vyote wamedai
kwamba ni wafuasi wa Kristo zitakapokuwa zimechunguzwa na kukatwa, hapo ndipo, wala si kabla ya
hapo, muda wao wa majaribio utakapofungwa, na mlango wa rehema utafungwa. Hivyo kwa sentensi
moja fupi isemayo, “Nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa,”
tunachukuliwa kupitia huduma ya mwisho ya Mwokozi, kuelekea katika wakati ambapo kazi kuu kwa
ajili ya wokovu wa mwanadamu itakuwa imekamilika.
Katika huduma ya patakatifu pa duniani, ambayo, kama tulivyokwisha kuona, ni mfano wa huduma ya
mbinguni, wakati kuhani mkuu alipoingia patakatifu pa patakatifu mnamo Siku ya Upatanisho, huduma
katika chumba cha kwanza ilikoma. Mungu aliamuru: “Wala hapatakuwa na mtu katika hema ya
kukutania, wakati aingiapo ili kufanya upatanisho katika patakatifu, hata atakapotoka nje.” Mambo ya
Walawi 16:17. Hivyo Kristo alipoingia ndani ya patakatifu pa patakatifu kufanya kazi yake ya mwisho ya
upatanisho, huduma yake katika chumba cha kwanza ilikoma. Lakini wakati huduma yake katika chumba
cha kwanza (429) ilipokoma, huduma katika chumba cha pili ilianza. Wakati katika huduma ile ya mfano
wa kivuli kuhani mkuu alipokuwa ameondoka patakatifu Siku ya Upatanisho, aliingia mbele za Mungu
kutoa damu ya sadaka ya dhambi kwa ajili ya Waisraeli wote waliotubu dhambi zao kweli kweli. Vivyo
hivyo, Kristo alikuwa amemaliza tu sehemu moja ya kazi yake kama Mwombezi wetu, ili aingie katika
sehemu nyingine ya kazi ile, naye aliendelea kulilia damu yake mbele za Baba yake badala ya wenye
dhambi.
Somo hili halikueleweka kwa Wanamarejeo wa mwaka 1844. Baada ya wakati aliotazamiwa Mwokozi
kupita, waliendelea kuamini kwamba kuja kwake kulikuwa karibu; walishikilia kwamba walikuwa
wamekifikia kilele muhimu na ya kwamba kazi ya Kristo kama Mwombezi wa mwanadamu mbele za
Mungu ilikuwa imekoma. Kwao ilionekana kama vile Biblia inafundisha kwamba muda wa kupimwa
mwanadamu ungefungwa muda mfupi tu kabla ya kuja kwake Bwana katika mawingu ya mbinguni. Hilo
lilionekana kama kuwa na ushahidi katika maandiko kuelekeza katika wakati wanadamu
watakapotafuta, watakapobisha hodi, na kulia mbele ya mlango wa rehema, na wala usifunguliwe. Na
kwao ilikuwa ni habari kwamba huenda tarehe waliyokuwa wametazamia kuja kwake Kristo isingeweza
kuwa ni alama ya kuonyesha mwanzo wa kipindi kilichokuwa hakina budi kuja kabla ya kuja kwake.
Wakiwa wamekwisha kutoa onyo la hukumu iliyokuwa karibu, waliona kwamba kazi yao kwa ulimwengu
ilikuwa imekwisha, nao walipoteza mzigo uliokuwa nafsini mwao kwa ajili ya wokovu wa wadhambi,
wakati kiburi na kufuru za dhihaka za wasiomcha Mungu vilionekana kwao kama ushahidi mwingine
kwamba Roho wa Mungu alikuwa ameondolewa kwa wale walioikataa rehema yake. Yote haya
yaliwaimarisha katika imani yao kwamba muda wa kupimwa ulikuwa umekwisha, au, kama walivyosema
wao wakati ule, “mlango wa rehema ulikuwa umefungwa.”
Lakini nuru iliyo wazi zaidi iliwajia walipolichunguza suala la patakatifu. Sasa wakaona kwamba
walikuwa hawajakosea katika kuamini kwao kwamba mwisho wa siku 2300 katika mwaka wa 1844
uliashiria tukio muhimu. Lakini wakati ilikuwa kweli kwamba mlango ule wa tumaini na rehema ambao
kupitia huo kwa karne kumi na nane watu walikuwa wakimwendea Mungu, ulikuwa umefungwa, mlango
mwingine ulifunguliwa (430), na msamaha wa dhambi ulitolewa kwa wanadamu kwa njia ya maombezi
ya Kristo katika patakatifu sana. Sehemu moja ya huduma yake ilikuwa imefungwa, ili tu kutoa nafasi
kwa ajili ya nyingine. Bado palikuwa na “mlango ulio wazi” kuelekea katika patakatifu pa mbinguni,
ambapo Kristo alikuwa anahudumu kwa niaba ya mwenye dhambi.

251
Sasa uhalisia wa maneno ya Kristo katika Ufunuo ulionekana, yakitolewa kwa kanisa la wakati huu:
“Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye
kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.” Ufunuo 3:7,8.
Ni wale wanaomfuata Yesu kwa imani katika kazi ile kuu ya upatanisho wanaopokea manufaa ya kazi
yake ya upatanishi anayofanya kwa ajili yao, wakati wale wanaoikataa nuru ambayo inaweka wazi
kuona kazi hii ya huduma yake hawanufaiki nayo. Wayahudi waliokataa nuru waliyopewa wakati wa kuja
kwa Kristo mara ya kwanza, na wakakataa kumwamini kama Mwokozi wa ulimwengu, hawakupokea
msamaha kupitia kwake. Wakati Yesu alipoingia patakatifu pa mbinguni kwa damu yake wakati wa
kupaa kwake ili kuwapatia wanafunzi wake mibaraka ya upatanishi wake, Wayahudi waliachwa katika
giza nene waendelee na dhabihu na sadaka zao zisizowafaa kitu. Huduma ya mifano na vivuli ilikuwa
imekoma. Mlango ule ambao kupitia huo wanadamu walikuwa wamepata njia ya kumfikia Mungu zamani
haukuwa wazi tena. Wayahudi walikuwa wamekataa kumtafuta kwa njia ile tu ambayo kwayo angeweza
kupatikana kwa wakati ule, kupitia katika huduma yake katika patakatifu pa mbinguni. Kwa hiyo,
hawakupata ushirika pamoja na Mungu. Kwao mlango ulikuwa umefungwa. Hawakumjua Kristo kama
kafara ya kweli na mpatanishi pekee mbele za Mungu; kwa hiyo hawakuweza kupata manufaa ya kazi
yake ya upatanishi.
Hali ya Wayahudi wale wasioamini inaonyesha hali ya wale wasiojali na wasioamini walioko miongoni
mwa wale wanaojiita Wakristo, ambao kwa makusudi yao hawajui kazi ile anayofanya Kuhani Mkuu wetu
mwenye rehema nyingi. Katika huduma ile ya mfano, kuhani mkuu (431) alipoingia patakatifu pa
patakatifu, Waisraeli wote walitakiwa kukusanyika pamoja na kupazunguka patakatifu pale, na kwa
kicho sana kuzinyenyekeza nafsi zao mbele za Mungu, ili wapate kupokea msamaha wa dhambi zao,
wasije wakakatiliwa mbali na mkutano. Tuelewa mengi kiasi gani kutoka katika Siku ya Upatanisho halisi
kwamba tunaelewa kazi ya Kuhani Mkuu wetu na kujua wajibu unaotakiwa kwetu.
Wanadamu hawawezi kuwa huru kukataa onyo ambalo Mungu anawapelekea kwa rehema. Ujumbe
ulitumwa kutoka mbinguni kuja duniani katika siku za Nuhu, na wokovu wao ulitegemea namna
walivyoupokea ujumbe ule. Kwa kuwa walilikataa onyo lile, Roho wa Mungu aliondolewa kutoka wa
wanadamu wenye dhambi, nao wakaangamia katika maji ya Gharika ile. Katika siku za Ibrahimu,
rehema iliacha kuwaombea wakazi wa Sodoma waliokuwa na hatia, na wote, isipokuwa Lutu na mkewe
na binti zake wawili, waliteketezwa kwa moto ulioshuka kutoka mbinguni. Hivyo ndivyo ilivyokuwa
katika siku za Kristo. Mwana wa Mungu aliwatangazia Wayahudi wa kizazi kile wasioamini: “Angalieni,
nyumba yenu mmeachiwa hali ya ukiwa” Mathayo 23:38. Akiangalia mbele hadi siku za mwisho, nguvu
ile ile yenye Uweza Wote inasema kuhusu wale ambao “hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate
kuokolewa,” akisema: “Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; ili wahukumiwe
wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.” 2 Wathesalonike
2:10-12. Kadiri wanavyoyakataa mafundisho yatokayo katika neno lake, Mungu anamwondoa Roho wake
kwao na kuwaacha wapate kudanyanywa na madanganyo yale wayapendayo.
Lakini bado Kristo anafanya maombezi kwa ajili ya mwanadamu, na nuru itatolewa kwa wale
wanaoitafuta. Ingawa jambo hili halikufahamika mwanzoni kwa Wanamarejeo, baadaye liliwekwa wazi
kadiri Maandiko yale yaliyoeleza kazi yao halisi yalivyoanza kufunuliwa machoni pao.
Kupita kwa wakati katika mwaka wa 1844 kulifuatiwa na kipindi cha majaribu makuu kwa wale ambao
bado waliendelea kuishikilia imani ya marejeo. Faraja yao pekee, kwa kadiri inavyothibitishwa na
msimamo wao wa kweli, (432) ilikuwa ni ile nuru iliyopeleka mawazo yao kuelekea patakatifu pa juu.
Baadhi waliiacha imani yao kwa habari ya mahesabu yao ya kabla ya vipindi vya unabii na kuuhesabu

252
mvuto ule wenye nguvu wa Roho Mtakatifu ulioambatana na harakati zile za marejeo kwamba ulitokana
na mawakala wa kibinadamu au wa kishetani. Kundi jingine lilishikilia sana ukweli na kusema kwamba
Bwana alikuwa amewaongoza katika uzoefu waliokuwa wamepitia; na kadiri walivyongoja na kukesha na
kuomba ili wapate kuyajua mapenzi ya Mungu waliona kwamba Kuhani Mkuu wao alikuwa ameingia
katika kazi nyingine ya huduma, na, wakimfuata humo kwa imani, waliongozwa pia kuona kazi ya
ufungaji wa kazi ya kanisa. Waliuelewa vizuri zaidi ujumbe wa malaika wa kwanza na wa malaika wa
pili, na walikuwa tayari kulipokea onyo la kutisha la malaika wa tatu wa Ufunuo 14 na kulitoa kwa
ulimwengu wote.

Sura ya 25
SHERIA YA MUNGU ISIYOBADILIKA

“Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano likaonekana ndani ya
Hekalu lake.” Ufunuo 11:19. Sanduku la agano la Mungu liko ndani ya patakatifu pa patakatifu, chumba
cha pili cha patakatifu. Katika huduma ya hema ya kidunia, ambayo ilikuwa “mfano na kivuli cha
mambo ya mbinguni,” chumba kile kilifunguliwa tu mnamo Siku kuu ya Upatanisho kwa madhumuni ya
kupatakasa patakatifu. Kwa hiyo, tangazo hili lisemalo kwamba Hekalu la Mungu lililoko mbinguni
likafunguliwa, na sanduku la agano likaonekana, huelekeza katika kufunguliwa kwa patakatifu pa
patakatifu ndani ya patakatifu pa mbinguni katika mwaka wa 1844 wakati Kristo alipoingia mle kufanya
kazi yake ya mwisho ya upatanisho. Wale ambao kwa imani walimfuata Kuhani Mkuu wao alipoingia
kufanya huduma yake ndani ya patakatifu pa patakatifu, waliliona sanduku lake la agano. Kwa vile
walikuwa wamejifunza somo la patakatifu walikuwa wamepata kuelewa badiliko la huduma ya Mwokozi,
na waliona kwamba sasa alikuwa akitekeleza huduma yake mbele ya sanduku la agano la Mungu, akidai
msamaha kwa damu yake iliyomwagika kwa ajili ya wenye dhambi.
Sanduku la agano katika hema ya kukutania ya duniani lilikuwa na mbao mbili za mawe, ambazo juu
yake ziliandikwa amri za Mungu. Sanduku la agano lilikuwa chombo tu cha kutunzia mbao zile za sheria
ya Mungu, na uwepo wa amri zile kulilipa sanduku lile thamani yake na utakatifu wake. Wakati hekalu
la Mungu lilipofunguliwa mbinguni, sanduku la agano lake likaonekana kule. (434) Ndani ya patakatifu
pa patakatifu, katika patakatifu pa mbinguni, sheria ya Mungu inahifadhiwa katika utakatifu - sheria
ambayo ilitamkwa na Mungu mwenyewe katikati ya ngurumo za Sinai na kuandikwa kwa kidole chake
mwenyewe juu ya mbao zile za mawe.
Sheria ya Mungu iliyo katika patakatifu pa mbinguni ndiyo ya asili kuu, ambayo kutokana nayo amri zile
zilizoandikwa kwenye mbao za mawe na kuandikwa na Musa katika vitabu Vitabu vitano vya Musa vya
Biblia ilikuwa ni nakala yake halisi isiyo na makosa. Wale waliofika mahali pa kulielewa jambo hili
muhimu waliongozwa kwa njia hiyo kuiona tabia ya sheria ya kimbingu iliyo takatifu na isiyobadilika.
Waliona, vile ambavyo haikupata kutokea kabla, nguvu ya maneno ya Mwokozi: “Mpaka mbingu na nchi
zitakapoondoka, yodi moja au nukta moja ya torati haitaondoka.” Mathayo 5:18. Sheria ya Mungu, ikiwa
ni ufunuo wa mapenzi ya Mungu, chapa ya tabia yake, lazima idumu milele, ikiwa “kama shahidi
mwaminifu mbinguni.” Hakuna hata amri moja iliyofutwa; hakuna hata yodi wala nukta iliyobadilishwa.
Mwimba zaburi anasema: “Ee BWANA, neno lako lasimama imara mbinguni hata milele.” “Maagizo yake
yote ni amini. Yamethibitika milele na milele.” Zaburi 119:89; 111:7,8.
Katikati kabisa ya Sheria ya Amri Kumi kuna amri ya nne, ikiwa kama ilivyotangazwa kwa mara ya
kwanza: “Ikumbuke Siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini Siku

253
ya Saba ni Sabato YA BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako,
wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni
aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita, BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na
vyote vilivyomo, akastarehe Siku ya Saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato, akaitakasa.”
Kutoka 20:8-11.
Roho wa Mungu alisukuma mioyo ya wale wanafunzi wa neno lake. Usadikisho uliletwa kwao kwamba
walikuwa walikuwa wameivunja amri hiyo kwa kule kutoijali siku hiyo ya mapumziko ya Muumba.
Walianza kuchunguza sababu za kutunza siku ya kwanza ya juma badala ya kuitunza siku ile iliyotakaswa
na Mungu. Hawakuweza kupata ushahidi katika (435) Maandiko unaoonyesha kwamba amri ya nne
ilikuwa imefutwa, au kwamba Sabato ilikuwa imebadilishwa; mbaraka ulioitakasa siku ya saba tangu
mwanzo ulikuwa haujapata kuondolewa kamwe. Walikuwa wakitafuta kwa bidii kujua na kufanya
mapenzi ya Mungu; na sasa, kadiri walivyojiona wenyewe kuwa wavunjaji wa sheria ya Mungu, huzuni
iliijaza mioyo yao, nao waliamua kuonyesha utiifu wao kwa Mungu kwa kutunza utakatifu wa Sabato
yake.
Juhudi zilizofanywa kuipindua imani yao zilikuwa nyingi na za kudhamiria. Hakuna aliyeshindwa kuona
kwamba ikiwa patakatifu pa duniani palikuwa ni mfano au kivuli cha pale pa mbinguni, basi ni dhahiri
kwamba sheria iliyowekwa ndani ya sanduku la agano la duniani ilikuwa ni nakala halisi ya sheria iliyo
ndani ya sanduku la agano kule mbinguni; na ya kwamba kuikubali ukweli uliohusu patakatifu pa
mbinguni kulifungamana na kuyakubali madai ya sheria ya Mungu na wajibu kwa masharti ya Sabato ya
amri ya nne. Hapa ndipo kulipokuwa na siri ya upinzani mkali uliodhamiriwa dhidi ya kufunuliwa kwa
Maandiko murua ambako kuliifunua huduma ya Kristo katika patakatifu pa mbinguni. Wanadamu
walijitahidi kufunga mlango ambao Mungu alikuwa amefungua, na kufungua mlango ambao alikuwa
amefunga. Lakini yeye “mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana
afunguaye,” alikuwa ametangaza: “Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao
hapana awezaye kuufunga.” Ufunuo 3:7,8. Kristo alikuwa amefungua mlango wa, au ameanza huduma
yake ya, patakatifu pa patakatifu, nuru ilikuwa inaangaza kutoka katika mlango uliofunguliwa wa
patakatifu pa mbinguni, na amri ya nne ilioonrkana kujumuishwa katika sheria iliyokuwa imehifadhiwa
kule; kile ambacho kimeanzishwa na Mungu, hakuna mwanadamu ambaye angeweza kukipindua.
Wale waliokuwa wameipokea nuru inayohusu upatanishi wa Kristo na kudumu kwa sheria ya Mungu
waligundua kwamba hizo ndizo kweli zilizokuwa zimeelezwa katika Ufunuo 14. Ujumbe wa sura hiyo una
onyo la aina tatu 385 ambalo litaweza kuwaandaa wakazi wa dunia hii ili wawe tayari kwa kuja kwa
Kristo mara ya pili. Tangazo linalosema, “Saa ya hukumu yake imekuja,” linaelekeza katika kazi ya
mwisho ya huduma ya Kristo kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Linatangaza (436) ukweli ambao
lazima uendelee kutangazwa mpaka hapo maombezi ya Mwokozi yatakapokoma na atakaporudi duniani
kuwachukua watu wake kwenda nao kwake. Kazi ya hukumu iliyoanza mwaka 1844 lazima iendelee
mpaka hapo kesi za wote zitakapokuwa zimekatwa, kwa makundi yote mawili ya walio hai na wafu; kwa
hiyo itaendelea mpaka mwisho wa muda wa kupimwa wanadamu. Ili watu wapate kuwa tayari kusimama
katika hukumu hiyo, ujumbe huo unawaamuru “Mcheni Mungu, na kumtukuza,” tena “Msujudieni yeye
aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.” Matokeo ya kukubali ujumbe huo
yametolewa katika neno: “Hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.” Ili kujiweka tayari kwa
hukumu hiyo, ni muhimu kwamba watu waishike sheria ya Mungu. Sheria hiyo itakuwa ndicho kipimo
cha tabia katika hukumu. Mtume Paulo alisema: “Na wote waliokosa wenye sheria, watahukumiwa kwa

385
Maelezo ya nyongeza yametolewa mwishoni

254
sheria,… katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu kwa Kristo Yesu.” Tena anasema:
“Bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki.” Warumi 2:12-16. Imani ni ya lazima ili kuweza
kuishika sheria ya Mungu; maana “pasipo imani haiwezekani kumpendeza.” Tena “kila tendo lisilotoka
katika imani ni dhambi.” Waebrania 11:6; Warumi 14:23.
Kwa njia ya malaika wa kwanza, wanadamu wanaalikwa kwa kuambiwa “Mcheni Mungu, na kumtukuza,”
na kumsujudia yeye kama Muumba wa mbingu na nchi. Ili kuweza kufanya hivyo, ni lazima waitii sheria
yake. Mwenye hekima anasema: “Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo
impasayo mtu.” Mhubiri 12:13. Pasipo kuzitii amri zake hakuna ibada inayoweza kumpendeza Mungu.
“Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake.” “Yeye aligeuzaye sikio lake
asiisikie sheria, hata sala yake ni chukizo.” 1 Yohana 5:3; Mithali 28:9.
Wajibu wa kumwabudu Mungu umejengwa juu ya ukweli kwamba yeye ndiye Muumba na ya kwamba
viumbe vingine vyote vinawiwa naye uhai vilio nao. Na po pote pale, katika Biblia, ambapo yanatolewa
madai yake ya kupewa kicho na kusujudiwa, zaidi ya miungu ya washenzi, (437) unatajwa ushahidi wa
uweza wake wa uumbaji. “Maana miungu yote ya watu si kitu, lakini BWANA ndiye aliyezifanya
mbingu.” Zaburi 96:5. “Mtanifananisha na nani, basi, nipate kuwa sawa naye? Asema yeye aliye
Mtakatifu. Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi.” “Maana BWANA, aliyeziumba
mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya;… Mimi ni BWANA, wala hapana
mwingine.” Isaya 40:25,26; 45:18. Mwimba zaburi anasema: “Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu; ndiye
aliyetuumba, wala hatukujiumba sisi wenyewe.” “Njoni, tuabudu, tusujudu, tupige magoti mbele za
BWANA aliyetuumba.” Zaburi 100:3; 95:6. Na viumbe wale watakatifu wanaomsujudu Mungu katika hali
ya kimbingu, wanatoa maneno haya kama sababu yao ya kumsujudu yeye: “Umestahili wewe, Bwana
wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu
vyote.” Ufunuo 4:11.
Katika Ufunuo 14, wanadamu wanaitwa kumsujudia Muumba; na unabii huo unalifunua wazi kundi
ambalo, kama matokeo ya ujumbe huo wa aina tatu, ni la watu wanaozishika amri za Mungu. Moja ya
amri hizo inaelekeza moja kwa moja kwa Mungu kama Muumba. Amri ya nne inasema: “Siku ya saba ni
Sabato ya BWANA, Mungu wako,… Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na
vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.”
Kutoka 20:10,11. Kuhusu Sabato, Bwana asema zaidi kwamba ni “ishara,… mpate kujua ya kuwa mimi
ndimi BWANA, Mungu wenu.” Na sababu iliyotolewa ni: “Kwani kwa siku sita BWANA alifanya mbingu na
nchi; akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika.” Kutoka 31:17.
“Umuhimu wa Sabato kama kumbukumbu ya uumbaji ni kwamba daima inaendeleza sababu ya kweli ya
kumwabudu Mungu” - kwa sababu yeye ni Muumba, na sisi tu viumbe vyake. “Kwa hiyo, Kwa hiyo Sabato
iko katika msingi wenyewe wa ibada ya Mungu, maana inafundisha ukweli huu mkuu kwa njia ya kuvutia
mno, wala hakuna fundisho jingine linalofanya hivyo. Sababu ya kweli ya kumwabudu Mungu, sio ile tu
inayofanyika mnamo siku ya saba, (438) bali ibada yote, inapatikana katika tofauti iliyopo kati ya
Muumba na viumbe vyake. Ukweli huu mkuu hauwezi kamwe kupitwa na wakati, wala haupaswi
kusahauliwa kamwe.” 386 Lilikuwa kusudi la kuuweka ukweli huu daima katika mawazo ya wanadamu,
kwamba Mungu aliiweka Sabato Edeni; na kadiri ukweli huu kwamba yeye ndiye Muumba wetu
unavyoendelea kuwa sababu inayoonyesha kwa nini sisi tunastahili kumsujudia, ndivyo Sabato
itakavyoendelea kuwa ishara na kumbukumbu ya hilo. Laiti kama Sabato ingalikuwa imeshikwa na watu

386
J. N. Andrews, History of the Sabbath, chapter 27

255
wote, mawazo ya mwanadamu na mapenzi yake yangalikuwa yameelekezwa kwa Muumba wake kama
lengo la kicho na ibada yake, wala kamwe asingekuwepo mwabudu sanamu, mshenzi, wala kafiri.
Kuitunza Sabato ni ishara ya utii wetu kwa Mungu wa kweli, “Yeye aliyezifanya mbingu na nchi na
bahari na chemchemi za maji.” Kinachofuata ni kwamba ujumbe ule unaowaamuru wanadamu
kumsujudia Mungu na kuzishika amri zake utawaalika kuitunza hasa amri ya nne.
Tofauti na wale wazishikao amri za Mungu na kuwa na imani ya Yesu, malaika wa tatu anaelekeza kwa
kundi jingine, ambalo onyo zito na la kutisha linatamkwa dhidi ya makosa yake: “Mtu awaye yote
akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika
mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu.” Ufunuo 14:9,10. Tafsiri
sahihi ya mifano hiyo iliyotumika hapo ni ya lazima ili kuweza kuuelewa ujumbe huo. Ni kitu gani
kinachowakilishwa na mnyama, sanamu, na chapa?
Mkondo wa unabii ambamo alama hizi zinapatikana unaanzia kwa Ufunuo 12, ukianza na yule joka
aliyejaribu kumwangamiza Kristo wakati wa kuzaliwa kwake. Joka huyo anasemekana kuwa Shetani;
yeye ndiye aliyemsukuma Herode kumwua Mwokozi. Lakini wakala mkubwa wa Shetani katika kufanya
vita dhidi ya Kristo na watu wake mnamo karne za kwanza za Kipindi cha Ukristo ilikuwa ni Dola ya
Kirumi, ambamo upagani ulikuwa ndiyo dini iliyokuwepo. Hivyo, wakati joka, kimsingi, anamwakilisha
Shetani, kwa hatua ya pili, yeye ni alama kiwakilishi ya Roma ya Kipagani.
(439) Katika Sura ya 13 (aya za 1-10) anaelezwa mnyama mwingine, aliyekuwa “mfano wa chui,”
ambaye joka alimpa “nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.” Mfano huo, kadiri ambavyo
Waprotestanti wengi wameamini, huwakilisha upapa, ambao ulichukua nguvu na kiti cha enzi na uwezo
uliokuwa umeshikiliwa kabla na dola ya Roma ya kale. Kwa habari ya mnyama huyo mfano wa chui
inasemwa hivi: “Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, na makufuru…. Akafunua kinywa
chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa
kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na
taifa. Unabii huo, ambao unalandana karibu sana na maelezo ya ile pembe ndogo ya Danieli 7, pasipo
swali lolote unaelekeza kwa upapa.
“Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.” Na, anasema nabii, “Nikaona kimoja
cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti.” Na tena asema: “Mtu akichukua mateka,
atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga.” Miezi ile arobaini na miwili ni
sawa na “wakati na nyakati na nusu wakati,” miaka mitatu na nusu, au siku 1260, ya Danieli 7 - kipindi
ambacho mamlaka ya kipapa ingewatesa watu wa Mungu. Kipindi hiki, kama ilivyoelezwa katika sura
zilizotangulia, kilianza na kushika hatamu kwa upapa, katika mwaka wa 538 B.K., na kilikoma mwaka
1798. Wakati huo papa alichukuliwa mateka na jeshi la Kifaransa, mamlaka ya kipapa ikawawa imetiwa
jeraha la mauti, na neno lililotabiriwa likawa limetimizwa, “Mtu akichukua mateka, atachukuliwa
mateka.”
Katika hatua hii alama nyingine ya kiwakilishi inatambulishwa. Nabii anasema: “Kisha nikaona mnyama
mwingine, akipanda juu katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa mwana-kondoo.” Aya ya
11. Mwonekano wa mnyama huyo na jinsi alivyotokea huonyesha kwamba taifa linalowakilishwa naye
halifanani na yale yaliyoelezwa katika mifano iliyotangulia. Falme kuu zilizoutawala ulimwengu huu
zilionyeshwa kwa nabii Danieli kama (440) wanyama wakatili wanaokamata mawindo, waliotokea
wakati zile “pepo nne za mbinguni zilipovuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa.” Danieli 7:2. Katika
Ufunuo 17 malaika alifafanua kwamba maji yanawakilisha “jamaa na makutano na mataifa na lugha.”
Ufunuo 17:15. Pepo ni alama ya vita. Pepo nne za mbinguni zilizovuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa

256
huwakilisha matukio ya kutisha ya ushindi wa vita na mapinduzi ambayo kwayo falme zile zilijitwalia
mamlaka yake.
Lakini mnyama mwenye pembe mbili kama za mwanakondoo alionekana “akipanda juu kutoka katika
nchi.” Badala ya kuipindua mamlaka nyingine ili kujiimarisha, taifa lililowakilishwa hivyo lazima litokee
katika nchi isiyokaliwa na watu na kukua taratibu na kwa amani. Lisingeweza, wakati huo, kuibuka
miongoni mwa mataifa mengi yanapambanayo ya Ulimwengu wa Zamani – ule msukosuko wa bahari wa
“jamaa na makutano na mataifa na lugha.” Lazima litafutwe katika Bara la Magharibi.
Ni taifa gani la Ulimwengu Mpya lililokuwa linatokea na kuwa na mamlaka, likitoa matumaini ya kuwa
na nguvu na ukuu, na kuyavuta mawazo ya ulimwengu mzima? Uelekeo wa alama hii hauna swali lolote.
Taifa moja, moja tu, linatimiza maelezo yote ya unabii huo; unaelekeza kwa Marekani pasipo kukosea.
Tena na tena wazo hilo, karibu kwa kutumia maneno yale yale, la mwandishi mtakatifu limetumiwa bila
kutambua na msimuliaji mwanahistoria akielezea kuibuka na kukua kwa taifa hili. Mnyama yule
alionekana “akipanda juu kutoka katika nchi;” na kwa mujibu wa wafasiri, maneno “kupanda juu”
humaanisha “kukua au kuchipua kama mmea.” Na, kama ambavyo tumeona, lazima taifa hili litokee
katika nchi ambayo haijapata kukaliwa na watu. Mwandishi maarufu, akieleza kuibuka kwa Marekani,
anazungumza juu ya “siri ya kupanda kwake juu kutoka katika ukiwa,” akisema: “Kama mbegu iliyo
kimya tulikua na kuwa dola.” 387 Jarida moja la Ulaya mwaka 1850 liliandika kuhusu Marekani kama dola
ya ajabu, ambayo ilikuwa “inajitokeza,” “katikati ya ukimya wa dunia na kuongezeka nguvu zake kila
siku.” Edward Evarett - katika hotuba (441) yake kuhusu Wasafiri waanzilishi wa taifa hili, alisema: “Je!
walitafuta mahali pa utulivu, pasipochukiza kwa kutojulikana kwake, na palipo salama kwa kuwa
hapafikiki kwa urahisi, mahali ambapo kanisa dogo la Leyden lingeweza kufurahia uhuru wa dhamiri?
Tazama maeneo makubwa ambapo, kwa ushindi wa amani,… wamezibeba bendera za msalaba!” 388
“Naye alikuwa na pembe mbili mfano wa mwana-kondoo.” Pembe mfano wa mwanakondoo zinaonyesha
ujana, kutokuwa na hatia, na upole, mambo ambayo yaliiwakilisha vema tabia ya Marekani
ilipoonyeshwa kwa nabii kama “ikipanda juu” katika mwaka wa 1798. Miongoni mwa wakimbizi wa
Kikristo waliokimbilia Amerika kwa mara ya kwanza na kutafuta kimbilio lao mbali na mateso ya
wafalme na ukosefu wa uvumilivu wa makasisi walikuwemo wengi waliodhamiria kuanzisha serikali juu
ya msingi mpana wa uhuru wa dini na wa kiraia. Mtazamo wao ulipata nafasi katika Azimio la Uhuru,
ambalo linasimika ukweli usemao kwamba “watu wote wameumbwa sawa,” na wamepewa haki
isiyoondoleka ya “kuishi, uhuru, na kutafuta furaha.” Tena Katiba inawahakikishia wananchi haki ya
kujitawala katika serikali yao wenyewe, ikisema kwamba wawakilishi wanaochaguliwa kwa kura ya
wengi watatunga na kusimamia sheria. Uhuru wa imani ya dini ulitolewa pia, kila mtu akiruhusiwa
kumwabudu Mungu kulingana na matashi ya dhamiri yake. Mfumo wa serikali ya kuchaguliwa na
wananchi na Uprotestanti vikawa ndizo nguzo kuu za taifa hilo. Nguzo hizi ndizo siri ya uwezo na usitawi
wan chi hii. Wale waliokandamizwa na kukanyagwa-kanyagwa katika Ulimwengu wote wa Kikristo
wameigeukia nchi hii kwa shauku na matumaini. Mamilioni wametafuta pwani zake, na Marekani
imeibuka na kuwa miongoni mwa mataifa yenye nguvu zaidi duniani.
Lakini yule mnyama mwenye pembe mbili kama za mwana-kondoo “akanna kama joka. Naye atumia
uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake
wamsujudu mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona…. Akiwaambia wale wakaao juu

387
G. A. Townsend, The New World Compared With the Old, page 462
388
Hotuba iliyotolewa Plymouth, Massachusetts, Desemba 22, 1824, uk. 11
257
ya nchi kumfanyia (442) sanamu ya yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la mauti naye akaishi.” Ufunuo
13:11-14.
Pembe zile kama za mwana-kondoo na sauti ile ya joka katika alama hii ya mfano zinaonyesha tofauti
dhahiri iliyopo kati ya maneno yanayosema na matendo yanayofanywa na taifa hilo lililowakilishwa.
Kule “kunena” kwa taifa hilo ni kazi ya mamlaka zake za chombo cha kutunga sheria na mahakama. Kwa
utendaji huo litasema uongo kwa zile kanuni za uhuru na amani ambazo limeziweka kama msingi wa
sera zake. Utabiri kwamba litanena “kama joka” na “kutumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza”
huashiria waziwazi kuhusu kutokea kwa roho ya kukosa uvumilivu na tabia ya kufanya mateso ambavyo
vilidhihirishwa na mataifa yanayowakilishwa na joka na mnyama yule aliye mfano wa chui. Na usemi
kwamba mnyama mwenye pembe mbili “aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama
yule wa kwanza” huonyesha kwamba mamlaka ya taifa hilo itatumika kulazimisha mambo ya
kuadhimisha ambayo ni tendo la heshima ya kuutii upapa.
Kitendo cha namna hiyo moja kwa moja kingekuwa kinyume cha misingi ya serikali hiyo, kinyume cha
upekee wa taasisi zake huru, kinyume na matamko yake mazito na ya moja kwa moja ya Azimio la
Uhuru, na kinyume na Katiba ya nchi. Waasisi wa taifa hili walijitahidi kwa hekima kuweka kinga dhidi
ya matumizi ya mamlaka ya serikali katika mambo ya kanisa, pamoja na matokeo yake yasiyoepukika -
ya kukosa uvumilivu kwa imani ya watu na kufanya mateso. Katiba ya nchi inaweka masharti kwamba
“Bunge la Marekani halitatunga sheria yo yote inayohusu kuanzisha dini, au kuzuia uendeshaji huru wa
dini,” na kwamba “hakuna kipimo cha kidini kitakachotakiwa kuzingatiwa kama sifa ya kupewa cheo
katika kazi ya umma nchini Marekani. Ni kwa kukiuka tu kinga hizi za uhuru wa taifa ndipo maadhimisho
ya kidini yanaweza kulazimishwa na mamlaka ya nchi. Lakini ukiukaji ambao ungefanywa na kitendo hiki
hauendi mbali na alama yenyewe ya mfano inayowakilisha hali hii. Ni mnyama mwenye pembe kama za
mwana-kondoo - kwa maneno yake ni safi, mpole, na asiye na madhara - ambaye ananena kama joka.
“Akiwaambia wakaao juu ya nchi (443) wamfanyie sanamu yule mnyama.” Hapa unawakilishwa
waziwazi mfumo wa serikali ambao mamlaka yake ya kutunga sheria iko mikononi mwa wananchi,
ushahidi ulio dhahiri kabisa kwamba Marekani ndilo taifa linalotajwa katika unabii huu.
Lakini “sanamu ya mnyama” ni nini? na itaundwaje? Sanamu hiyo inaundwa na mnyama mwenye pembe
mbili, na ni sanamu kwa yule mnyama. Pia inaitwa sanamu ya mnyama. Sasa kujua jinsi sanamu hiyo
ilivyo na jinsi itakavyoundwa ni lazima tujifunze sifa za yule mnyama mwenyewe - upapa.
Wakati kanisa la kale lilipopotoka kwa kuacha urahisi wa injili likapokea maadhimisho na desturi za
kishenzi, lilipoteza Roho na uweza wa Mungu; na ili lipate kuzitawala dhamiri za watu, liliomba
kuungwa mkono na mamlaka ya serikali ya kidunia. Matokeo yake yakawa upapa, kanisa lililoendesha
mamlaka ya serikali na kuitumia serikali kutekeleza makusudi yake, hasa yale ya kuadhibu “uzushi.”. Ili
Marekani iunde sanamu ya mnyama, lazima mamlaka ya kidini iendeshe hivyo hivyo serikali ya kiraia
kiasi cha kanisa kutumia mamlaka ya serikali kutimiza makusudi yake.
Wakati wo wote ambapo kanisa limekuwa likipata mamlaka ya kiserikali, limeyatumia mamlaka hayo
kuadhibu wale wasiokubaliana na mafundisho yake. Makanisa ya Kiprotestanti ambayo yamezifuata
nyayo za Roma kwa kufanya ushirikiano na mamlaka za ulimwengu yamedhihirisha shauku hiyo hiyo ya
kuuwekea mipaka uhuru wa dhamiri ya mtu. Mfano wa jambo hili unapatikana katika mateso
yaliyoendelea kwa muda mrefu ambayo yalifanywa na Kanisa la Uingereza kwa wale waliokataa
kukubaliana na mafundisho ya kanisa hilo. Katika karne ya kumi na sita na ya kumi na saba, maelfu ya
wahubiri waliotofautiana na mafundisho ya kanisa walilazimishwa kuyakimbia makanisa yao, na wengi,

258
wote wachungaji na watu wa kawaida, walikabiliwa na adhabu za kutozwa faini, kufungwa jela,
kuteswa kwa ukatili, na kuuawa kwa sababu ya imani.
Uasi ndio ulioongoza kanisa la kale kuomba msaada kutoka kwa serikali ya kiraia, na jambo hili
lilitayarisha njia ya kuzuka kwa upapa - yule mnyama. Paulo alisema: “Utakuja ukengeufu; (444)
akafunuliwa yule mtu wa dhambi.” 2 Wathesalonike 2:3. Kwa hiyo, uasi ndani ya kanisa utatayarisha
njia kwa ajili ya sanamu ya mnyama.
Biblia inatangaza kwamba kabla ya marejeo ya Bwana kutakuwa na hali ya kushuka katika mambo ya
kidini kama ile iliyotokea katika karne zile za kwanza. “Siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi,
wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao, wasiotaka
kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wanaowadharau walio wema, wasaliti, wakaidi,
wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana
nguvu zake.” 2 Timotheo 3:1-5. “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine
watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani.” 1 Timotheo 4:1.
Shetani atatenda kwa “madanganyo yote ya udhalimu.” Ndipo wale wote ambao “hawakukubali
kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa,” wataachwa ili waipokee ile “nguvu ya upotevu, wauamini
uongo.” 2 Wathesalonike 2:9-11. Wakati hali hii ya uovu itakapofikiwa, matokeo yale yale yatafuata
kama yalivyokuwa katika karne zile za mwanzo.
Kuwepo kwa tofauti kubwa ya imani katika makanisa ya Kiprotestanti kunachukuliwa na wengi kama
ndio ushahidi wa msingi kwamba juhudi yo yote ya kupata umoja wa kulazimisha haiwezi kufanywa.
Lakini kwa miaka mingi pamekuwepo, katika makanisa ya imani ya Kiprotestanti, shauku kubwa na
inayoendelea kuongezeka ya kupendelea kuwepo kwa muungano uliojengwa juu ya msingi wa yale
maeneo ya mafundisho yanayokubaliwa na makundi yote. Kufikia muungano huo, lazima ionekane
muhimu kuachana na mjadala unaohusu mafundisho yale ambayo hayakubaliwi na wote - hata yawe
muhimu jinsi gani kwa mtazamo wa Biblia.
Charles Beecher, katika hotuba yake ya mwaka wa 1846, alisema bayana kwamba huduma ya
“madhehebu ya kiinjili ya Kiprotestanti si tu kwamba njia yote hadi mwisho imejengwa kwa shinikizo
kubwa la hofu ya kibinadamu, bali pia watu wake wanaishi, wanakwenda, na kupumua wakiwa katika
mambo ya upotofu kabisa, na kila saa wakiitetea tabia yao mbaya ili kuinyamazisha (445) ile kweli, na
kuipigia magoti mamlaka ya uasi. Je, hivyo sivyo mambo yalivyokuwa kwa Roma? Je, hatuko tunaishi
maisha ya Roma tena? Na je, tunaona nini mbele yetu hivi sasa? Ni baraza kuu jingine! Mkutano wa
ulimwengu! Ushirikiano wa kiinjili, na itikadi ya imani moja kwa wote!” - Hotuba kuhusu "The Bible a
Sufficient Creed," delivered at Fort Wayne, Indiana, Feb. 22, 1846. Jambo hili litakapokuwa limefikiwa,
hapo ndipo, kama jitihada ya kupata mfanano kamili, itakuwa ni hatua tu ya kuelekea katika matumizi
ya nguvu.
Wakati makanisa makubwa ya Marekani, yakiungana katika vipengele vya mafundisho ambavyo yote
yanakubali, yatashawishi dola kuhimiza utekelezaji wa maagizo ya imani yao na kuziwezesha taasisi za
makanisa yao, hapo ndipo Amerika ya Kiprotestanti itakuwa imeunda sanamu ya mfumo wa Roma, na
vitendo vya kuhimiza utoaji wa adhabu kali za serikali kwa wale wasiokubaliana na mafundisho yao
vitakuwa ndiyo matokeo ya hali hiyo yasiyoepukika.
Mnyama mwenye pembe mbili “awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na
walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;
tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la
259
mnyama yule, au hesabu ya jina lake.” Ufunuo 13:16,17. Onyo la malaika wa tatu ni: “Mtu awaye yote
akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika
mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu.” “Mnyama” aliyetajwa katika
ujumbe huu, ambaye kumsujudu huyu kutalazimishwa na mnyama yule mwenye pembe mbili, ni wa
kwanza, au mnyama wa mfano wa chui wa Ufunuo 13 - upapa. “Sanamu ya mnyama” inawakilisha
Uprotestanti ulioasi utakaoibuka wakati ambapo makanisa ya Kiprotestanti yataomba msaada wa
mamlaka ya serikali kwa ajili ya kusukuma mbele utekelezaji wa mafundisho yao ya dini. “Bado alama
ya mnyama haijafafanuliwa.
Baada ya onyo hilo dhidi ya kumsujudu mnyama na sanamu yake unabii unasema: “Hapa ndipo penye
subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.” Kwa kuwa wale wazishikao
amri za Mungu wanawekwa katika tofauti hiyo baina yao na wale wanaomsujudu mnyama na sanamu
yake na kupokea chapa yake, basi inakuwa kwamba kule kuishika sheria ya Mungu, kwa (446) upande
mmoja, na kule kuivunja, kwa upande mwingine, vitafanya tofauti kati ya wale wanaomsujudia Mungu
na wale wanaomsujudia mnyama.
Sifa maalum ya mnyama huyo, na kwa hiyo ya sanamu yake, ni ile ya kuzivunja amri za Mungu. Danieli
anasema, kuhusu pembe ndogo, upapa: “Naye ataazimu kubadili majira na sheria.” Danieli 7:25. Na
Paulo aliipa jina mamlaka hiyo kuwa ni “mtu wa dhambi,” ambaye angejiinua mwenyewe juu ya Mungu.
Unabii mmoja unaukamilisha unabii mwingine. Ni kwa njia ya kuibadili sheria ya Mungu tu upapa
ungeweza kujitukuza wenyewe juu ya Mungu; mtu ye yote ambaye ataitunza sheria hiyo iliyobadilishwa
kwa kujua atakuwa anaipa heshima ya utii mamlaka ambayo ilifanya badiliko hilo. Tendo kama hilo la
kutii sheria za kipapa ingekuwa alama ya utii kwa papa badala ya Mungu.
Upapa umejaribu kubadili sheria ya Mungu. Amri ya pili, inayokataza ibada ya sanamu, imeondolewa
kabisa katika sheria, na amri ya nne imebadilishwa kiasi cha kuidhinisha utunzaji wa siku ya kwanza
badala ya siku ya saba kama Sabato. Lakini watu wa upapa wanadai, kama sababu yao ya kuiondoa amri
ya pili, kwamba si ya lazima, ikiwa imejumishwa ndani ya ile ya kwanza, na ya kwamba wao wanaiweka
sheria sawasawa kabisa na vile Mungu alivyokusudia ieleweke kwa watu. Hili haliwezi kuwa badiliko lile
alilotabiri nabii. Badiliko la makusudi, la kudhamiriwa linaelezwa: “Naye ataazimu kubadili majira na
sheria.” Badiliko katika amri ya nne hutimiza unabii huo kabisa. Kwa hili mamlaka pekee inayodaiwa ni
ya kanisa. Hapa mamlaka ya papa inajiweka yenyewe waziwazi juu ya Mungu.
Wakati wale wanaomsujudia Mungu watatambulika kwa njia ya pekee kwa kuitunza amri ya nne, - kwa
kuwa hiyo ndiyo ishara ya uweza wake wa uumbaji na ushuhuda wa madai yake juu ya mwanadamu
kumcha na kumhshimu yeye, - wale wanaomsujudia mnyama watatambulika kwa juhudi zao za
kuivunjilia mbali kumbukumbu hiyo ya Muumba, kuitukuza kitu kilichoanzishwa na Roma. Ilikuwa ni kwa
ajili ya Jumapili kwamba upapa kwa mara ya kwanza ulitoa (447) madai ya majivuno 389; na azimio lake
kwa mara ya kwanza kutumia mamlaka ya serikali lilikuwa na madhumuni ya kulazimisha kwa nguvu
uadhimishaji wa Jumapili kama “siku ya Bwana.” Lakini Biblia inaelekeza kwa siku ya saba, wala siyo ya
kwanza, kama siku ya Bwana. Kristo alisema: “Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato pia.” Amri
ya nne inasema: “Siku ya saba ni Sabato ya Bwana.” Na kupitia kwa nabii Isaya Bwana anaiita siku hiyo:
“Siku ya utakatifu wangu.” Marko 2:28; Isaya 58:13.
Madai yanayotolewa mara kwa mara kwamba Kristo aliibadili Sabato yanakanushwa na maneno yake
mwenyewe. Katika Hotuba yake aliyoitoa Mlimani alisema hivi: “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua
torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na

389
Maelezo ya nyongeza yametolewa mwishoni
260
nchi zitakapoondoka yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie. Basi mtu ye
yote atakayeivunja amri moja katika hizi zilizo ndogo na kuwafundisha watu hivyo ataitwa mdogo kabisa
katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika
ufalme wa mbinguni.” Mathayo 5:17-19.
Ni ukweli ambao kwa ujumla unakubaliwa na Waprotestanti kwamba Maandiko hayatoi idhini yoyote ya
kuibadili Sabato. Jambo hili limesemwa waziwazi katika vijitabu vilivyotolewa na American Tract
Society na American Sunday School Union. Kimojawapo cha vijitabu hivyo kinakiri kuhusu “ukimya
kabisa wa Agano Jipya kwa habari ya amri iliyo wazi kuhusu Sabato kama hiyo au kuwapo kwa kanuni
zilizo wazi za utunzaji wake.” 390
Kingine kinasema: “Mpaka wakati wa kufa kwa Kristo, hakuna badiliko lolote lililofanyika kwa siku
hiyo;” tena, “kwa kadiri kumbukumbu inavyoonyesha, hawakuwahi … kutoa amri yo yote iliyo dhahiri
inayoamuru kuiacha Sabato ya siku ya saba, na kuitunza Sabato katika siku ya kwanza ya juma.” 391
Watu wa Kanisa Katoliki la Roma wanakiri kwamba badiliko la Sabato lilifanywa na kanisa lao, na
wanasema wazi kwamba Waprotestanti (448) kwa kuiadhimisha Jumapili wanaitambua mamlaka ya
kanisa lao. Katika Katekisimu yao inayoitwa Catholic Catechism of Christian Religion, katika jibu la
swali kuhusu siku inayopaswa kutunzwa kwa kuitii amri ya nne, maelezo haya yametolewa: “Katika
kipindi cha sheria ya kale, Jumamosi ilikuwa ndiyo siku iliyokuwa imetakaswa; lakini kanisa, likiwa
limepewa agizo na Yesu Kristo, na kuongozwa na Roho wa Mungu, limeiweka Jumapili mahali pa
Jumamosi; hivyo sasa tunaitakasa siku ya kwanza, siyo siku ya saba. Jumapili humaanisha, na sasa ni,
siku ya Bwana.”
Kama ishara ya mamlaka ya Kanisa Katoliki, waandishi wengi ambao ni watu wa upapa wananukuu
“tendo lenyewe la kuibadili Sabato kuwa Jumapili, ambalo Waprotestanti wanalikubali;… kwa sababu
kwa kuitunza Jumapili, wanaukubali uwezo wa kanisa wa kutenga rasmi sikukuu, na kuwaamuru wawe
chini ya dhambi.” 392 Maana ya badiliko la Sabato ni nini basi, kama si ishara, au alama, ya mamlaka ya
Kanisa la Roma – “alama ya mnyama”?
Kanisa la Roma halijaachana na dai lake la ukuu; na wakati ulimwengu na makanisa ya Kiprotestanti
wanapokubali sabato iliyowekwa nalo, na kuikataa Sabato ya Biblia, wanalikubali kabisa dai hilo.
Wanaweza kutoa madai yatokayo katika mapokeo na kwa Mababa kwa badiliko hilo; lakini kwa kufanya
hivyo wanaipuuza kanuni yenyewe inayowatenga na Roma - isemayo kwamba, “Biblia, na Biblia pekee,
ndiyo dini ya Waprotestanti.” Mtu wa upapa anaweza kuona kwamba wanajidanganya wenyewe, kwa
makusudi wakifumba macho yao wasiuone ukweli katika hilo. Kadiri harakati za kuhimiza utunzaji wa
Jumapili zinavyozidi kuchukua nafasi, anashangilia, akihisi kuhakikishiwa kwamba hatimaye hali hiyo
itauleta ulimwengu wote wa Kiprotestanti chini ya bendera ya Roma.
Waumini wa Roma wanasema wazi kwamba “utunzaji wa Jumapili unaofanywa na Waprotestanti ni
heshima wanayotoa, licha ya kujipinga wenyewe, kwa mamlaka ya Kanisa.” 393 Kutekeleza utunzaji wa
Jumapili kwa upande wa makanisa ya Kiprostestanti ni kuwalazimisha watu kuusujudia upapa –
kumsujudia mnyama. Wale ambao, hali wakiyaelewa madai ya amri ya (449) nne, wanachagua kutunza
Sabato ya uongo badala ya Sabato ya kweli wanaisujudia kwa njia hiyo mamlaka ile ambayo peke yake

390
George Elliot, The Abiding Sabbath, page. 184
391
A. E. Waffle, The Lord’s Day, pages 186-188
392
Henry Tuberville, An Abridgment of the Christian Doctrine, page 58
393
Mgr. Segur, Plain Talk About the Protestantism of Today, page 213
261
ndiyo imeiamru. Lakini katika tendo lenyewe la kulazimisha wajibu wa kidini kwa kutumia mamlaka ya
serikali ya kidunia, makanisa hayo hayo yangeweza kuunda sanamu ya mnyama; kwa hiyo, kulazimisha
utunzaji wa Jumapili katika nchi ya Marekani kungekuwa ni kulazimisha kumsujudia mnyama na sanamu
yake.
Lakini Wakristo wa vizazi vilivyopita waliitunza Jumapili, wakidhani kwamba kwa kufanya vile walikuwa
wanaitunza Sabato ya Biblia; na hata sasa wamo Wakristo wa kweli katika kila kanisa, bila kusahau
jumuiya ya Wakatoliki, ambao kwa unyofu wa moyo wanaamini kwamba Jumapili ni Sabato ile
iliyowekwa na Mungu. Mungu anaikubali nia ya makusudi yao na unyofu wao wa moyo kwake. Lakini
wakati utunzaji wa Jumapili utakapohimizwa kwa sheria, na ulimwengu wote ukawa umepewa mwanga
kuhusu wajibu wa watu wote kwa Sabato ya kweli, hapo ndipo ye yote yule atakayeivunja amri hiyo ya
Mungu, ili kuitii amri isiyokuwa na mamlaka ya juu kuliko Roma, atakuwa anaiheshimu Roma kuliko
Mungu. Anaiheshimu Roma na mamlaka inayotekeleza taratibu zilizoanzishwa na Roma. Mtu huyo
anamsujudia mnyama na sanamu yake. Kadiri wanadamu wanavyoikataa siku ambayo Mungu ameiweka
iwe ishara ya mamlaka yake, na mahali pake kuiheshimu ile iliyochaguliwa na Roma kama ishara ya
ukuu wake, kwa njia hiyo wataipokea alama ya utii wao kwa Roma - “alama ya mnyama.” Na jambo hilo
halitakuwa mpaka suala hilo litakapokuwa limewekwa mbele ya watu, na wameletwa mahali pa
kuchagua kati ya amri za Mungu na amri za wanadamu, ndipo wale watakaoendelea kukiuka
watakapopokea “alama ya mnyama.
Tishio la kuogofya mno lililopata kunenwa kwa wenye mwili wa kufa linapatikana katika ujumbe wa
malaika wa tatu. Lazima lile ni dhambi ya kuogofya ambayo inashusha toka mbinguni ghadhabu ya
Mungu isiyochanganywa na rehema. Watu hawapaswi kuachwa gizani kuhusu jambo hili muhimu; onyo
dhidi ya dhambi hii linapaswa kutolewa kwa ulimwengu kabla ya kujiliwa na hukumu za Mungu, ili wote
wapate kujua kwa nini watapaswa kuteswa kwa hizo hukumu, na wapate (450) nafasi ya kuziepuka.
Unabii unasema kwamba malaika wa kwanza angetoa tangazo lake kwa “kila taifa na kabila na lugha na
jamaa.” Onyo la malaika wa tatu, ambalo ni sehemu ya ujumbe wa aina tatu, halitatawanywa katika
maeneo madogo kuliko hilo. Linawakilishwa kama linatangazwa kwa sauti kuu na malaika arukaye
katikati ya mbingu; nalo litakuwa na uwezo wa kuyavuta mawazo ya ulimwengu mzima.
Katika habari ya pambano hilo Ulimwengu wote wa Kikristo utagawanyika katika makundi makuu mawili
- wale wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu, na wale wanaomsujudu myama na sanamu yake na
kupokea chapa yake. Ingawa kanisa na serikali vitaunganisha nguvu zao ili kuwalazimisha “wote,
wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru na watumwa” (Ufunuo 13:16) ili wapate
kupokea “chapa ya mnyama,” hata hivyo, watu wa Mungu hawataipokea. Nabii wa Patmo anaona “wale
waliokuwa wamejipatia ushindi wao dhidi ya mnyama, na dhidi ya sanamu yake, na dhidi ya alama
yake, na dhidi ya hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo,
wenye vinubi vya Mungu,” nao wauimba wimbo wa Musa na wimbo wa Mwana-Kondoo. Ufunuo 15:2,3.

262
Sura ya 26
KAZI YA MATENGENEZO

Kazi ya matengenezo ya Sabato ya kukamilishwa mnamo siku za mwisho imetabiriwa katika unabii wa
Isaya: “BWANA asema hivi, Shikeni hukumu, mkatende haki; kwa maana wokovu wangu u karibu kuja,
na haki yangu kufunuliwa. Heri afanyaye haya, na mwanadamu ayashikaye sana; azishikaye Sabato
zangu asizivunje, auzuiaye mkono wake usifanye uovu wo wote.” “Na wageni, walioandamana na
BWANA ili wamhudumu, na kulipenda jina la BWANA, kuwa watumishi wake; kila aishikaye Sabato
asiivunje, na kulishika sana agano langu; Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na
kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala.” Isaya 56:1,2,6,7.
Maneno haya yanahusika na zama za Ukristo, kama yanavyoonyeshwa na muktadha: “Bwana MUNGU,
akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema, Pamoja na hayo nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao
walio wake waliokusanywa. Fungu la 8. Hapa inaonekana mapema ishara ya kukusanywa kwa Mataifa
kwa njia ya injili. Na juu ya wale wanaoiheshimu Sabato, baraka inatamkwa. Hivyo masharti ya amri ya
nne yanakwenda mbele zaidi ya wakati ule wa kusulibiwa, kufufuka, na kupaa kwake Kristo, mpaka
wakati ule watumishi wake watakapolazimika kuhubiri kwa mataifa yote ujumbe huo wa habari njema
ya furaha.
(452) Bwana anaamru kupitia kwa nabii yule yule: “Ufunge huo ushuhuda,ukaitie muhuri sheria kati ya
wanafunzi wangu.” Isaya 8:16. Muhuri wa sheria ya Mungu unapatikana katika amri ya nne. Hii tu,
katika zote kumi, ndiyo huonyesha jina na cheo cha Mtoa-sheria. Inamtaja yeye kuwa Muumba wa
mbingu na dunia, na kwa njia hiyo inayadhihirisha madai yake ya kupewa kicho na kusujudiwa kuliko
wengine wote. Pembeni ya amri hii hakuna kingine chochote katika sheria ya Amri Kumi kinachoonyesha
mamlaka ya mtoaji wa sheria. Sabato ilipobadilishwa na mamlaka ya papa, muhuri uliondolewa katika
sheria. Wanafunzi wa Yesu wanaagizwa kuurejesha muhuri huo kwa njia ya kuiinua Sabato ya amri ya
nne na kuiweka mahali pake sahihi kama kumbukumbu ya Muumba na ishara ya mamlaka yake.
“Na waende kwa sheria na ushuhuda.” Wakati mafundisho yanayogongana na nadharia zinazogongana
vinapoenea, kanuni moja isiyokosea kamwe ni sheria ya Mungu, ambayo kwayo maoni yote, mafundisho
yote, pamoja na nadharia zote lazima vipimwe. Nabii anasema: “Ikiwa hawasemi sawasawa na neno
hili, bila shaka kwao hapana asubuhi.” Isaya 8:20.
Tena, amri inatolewa: “Piga kelele, usiache, paza sauti yako kama tarumbeta; uwahubiri watu wangu
kosa lao, na nyumba ya Yakobo dhambi zao.” Si ulimwengu mwovu unaopaswa kukemewa kwa uasi, bali
ni wale anaowaita Bwana kama “watu wangu.” Anatangaza zaidi: “Walakini wanitafuta kila siku,
hupenda kujua njia zangu; kama vile taifa waliotenda haki, wasioacha sheria ya Mungu wao.” Isaya
58:1,2. Hapa linaonekana kundi la watu wanaojiona kuwa ni wenye haki, nao wanaonekana kana

263
kwamba wanaonyesha ari kubwa katika kazi ya Bwana; lakini kemeo kali na zito la Mchunguzaji wa
mioyo huonyesha kwamba wao wanazikanyaga chini ya miguu yao amri.
Hivyo nabii anaelekeza kwenye amri iliyoachwa: “Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa;
utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka, na, Mwenye
kurejeza njia za kukalia. Kama ukigeuza (453) mguu wako usiihalifu Sabato, usifanye anasa yako siku ya
utakatifu wangu; ukiita Sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya BWANA yenye heshima; ukiitukuza
kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako
mwenyewe; ndipo utakapojifurahisha katika BWANA.” Mafungu ya 12 - 14. Unabii huu pia una kazi
katika wakati wetu. Hali ya kubomolewa ilifanywa katika sheria ya Mungu Sabato ilipobadilishwa na
mamlaka ya Roma. Lakini wakati umewadia wa kurejeshwa mahali pake kwa amri ile iliyowekwa na
Mungu. Mahali pale palipobomoka ni lazima patengenezwe, na lazima msingi wa vizazi vingi uinuliwe.
Ikiwa imetakaswa kwa pumziko na baraka za Muumba, Sabato ilitunzwa na Adamu alipokuwa hana hatia
yo yote katika Edeni takatifu; ilitunzwa na Adamu, aliyeanguka dhambini lakini aliyekuwa na moyo wa
toba, alipofukuzwa katika shamba lake la furaha. Ilitunzwa na wazee wote wa zamani, tangu Habili hadi
kwa Nuhu mwenye haki, hadi kwa Ibrahimu, hadi kwa Yakobo. Wakati wale wateule walipokuwa
utumwani Misri, wengi, wakiwa katikati ya ibada ya sanamu iliyoenea kote, walipoteza ujuzi wao wa
Sheria ya Mungu; lakini Bwana alipowakomboa Israeli alitangaza sheria yake kwa utukufu wa kuogofya
mno kwa kusanyiko la watu wale wengi, ili wapate kuyajua mapenzi yake na kumcha na kumtii yeye
milele.
Tangu siku ile mpaka sasa maarifa ya sheria ya Mungu yamehifadhiwa duniani, na Sabato ya amri ya nne
imekuwa ikitunzwa. Ingawa yule “mtu wa dhambi” alifanikiwa kuikanyaga chini ya miguu yake siku hiyo
takatifu ya Mungu, bado hata wakati wa kipindi cha kushika kwake hatamu za utawala walikuwepo watu
waliokuwa waaminifu wakiiheshimu siku hiyo, wakiwa wamejificha mahali pa siri. Tangu wakati wa
Matengenezo, wamekuwepo baadhi ya watu katika kila kizazi walioendelea kuitunza. Ingawa mara
nyingi walijikuta katikati ya shutuma na mateso, ushuhuda wao umeendelea kutolewa daima kuhusu
kudumu kwa sheria ya Mungu na wajibu mtakatifu wa wanadamu kuitunza Sabato ya uumbaji.
Kweli hizo, kama zilivyoelezwa katika Ufunuo 14 kuhusiana na “injili ya milele,” zitalitambulisha Kanisa
la Kristo wakati wa kuja kwake. Maana kama matokeo ya (454) ujumbe huo wa aina tatu tangazo
linatolewa: “Hao wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu.” Na ujumbe huu ndio wa mwisho
kutolewa kabla ya kuja kwake Bwana. Mara tu baada ya kutangazwa kwa ujumbe huo Mwana wa Adamu
anaonwa na nabii akija katika utukufu kuja kuvuna mavuno ya nchi.
Wale walioipokea nuru inayohusu patakatifu na kutobadilika kwa sheria ya Mungu walijawa na furaha na
mshangao walipouona uzuri na mwafaka wa mfumo wa ile kweli iliyofunuliwa katika ufahamu wao.
Walitamani kwamba kweli ile iliyoonekana kwao kuwa ya thamani mno ingeweza kufundishwa kwa
Wakristo wote; nao waliweza kuamini tu kwamba ingeweza kupokelewa kwa furaha. Lakini kweli zile
ambazo zingewaweka katika kuhitilafiana na ulimwengu hazikupendwa na wengi waliojiita wafuasi wa
Kristo. Utii kwa amri ya nne ulihitaji kujikana jambo ambalo walio wengi walirudi nyuma kwa sababu ya
hilo.
Kadiri masharti ya Sabato yalipotolewa, wengi walitoa sababu za mtazamo wa kupenda ulimwengu.
Walisema: “tumeitunza Jumapili mara zote, baba zetu waliitunza, na watu wengi wema na wacha
Mungu walikufa kwa furaha wakiwa wanaitunza. Kama walikuwa sahihi, nasi vivyo hivyo. Utunzaji wa
Sabato hii mpya ungetufanya tusiendane na ulimwengu, na tusingekuwa na mvuto wo wote juu yao. Lile
kundi dogo linalotunza siku ya saba linaweza kufanya nini dhidi ya ulimwengu mzima unaoendelea
264
kuitunza Jumapili?” Ilikuwa ni kwa hoja kama zile zile ambazo Wayahudi walitumia kuhalalisha
kumkataa Kristo. Baba zao walikuwa wamekubaliwa na Mungu kwa kutoa sadaka zao za wanyama, kwa
nini basi wana wao wasingeweza kuupata wokovu kwa kufuata njia ile ile? Hivyo hivyo, mnamo nyakati
za Luther, watu wa upapa walitoa sababu zao kwamba Wakristo wa kweli walikuwa wamekufa katika
imani ya Kikatoliki, na kwa sababu hiyo dini ile ilikuwa inatosha kwa wokovu. Sababu kama hizo
zitajionyesha kuwa kipingamizi cha kutosha kuzuia maendeleo yote ya imani ya kidini au kazi zake.
Wengi walisisitiza kwamba utunzaji wa Jumapili ulitokana na fundisho lililokuwa limeimarika, na
kwamba ilikuwa ni desturi ya kanisa iliyoenea mahali pote kwa (455) karne nyingi. Kinyume cha hoja hii
ilionyeshwa kwamba Sabato na utunzaji wake ilikuwa ya zamani zaidi na iliyoenea, tena ikiwa na umri
sawa na dunia yenyewe, na ikiwa na msisitizo wa malaika na wa Mungu. Wakati misingi ya dunia
ilipowekwa, nyota zile za asubuhi zilipoimba pamoja, na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa
furaha, ndipo ulipowekwa msingi wa Sabato. Ayubu 38:6,7; Mwanzo 2:1-3. Siku hii inadai kicho chetu;
haikuamriwa na mamlaka yo yote ya kibinadamu, wala haitegemei mapokeo yo yote ya kibinadamu;
iliwekwa na Mzee wa Siku na kuamriwa kwa neno lake la milele.
Kadiri usikivu wa watu ulivyovutwa kuelekea kwenye somo hili la matengenezo ya Sabato, wahubiri
maarufu walilipotoa neno la Mungu, wakiweka tafsiri zao juu ya ushuhuda wa somo hili kwa namna
ambayo ingeonekana vema kuweza kutuliza mawazo ya watu waliokuwa wanataka kuijua. Na wale
ambao hawakuyachunguza Maandiko wao wenyewe waliridhika kupokea mahitimisho yaliyolandana na
tamaa zao. Kwa mahojiano, hoja za hila, mapokeo ya Mababa, na mamlaka ya kanisa, wengi walijitahidi
sana kuipindua kweli ile. Wale walioitetea walisukumiwa katika Biblia zao kutetea uhalali wa amri ile ya
nne. Watu wanyenyekevu, wakiwa wamevalia silaha ya neno la kweli pekee, waliyapinga mashambulio
ya wasomi, ambao, kwa mshangao na hasira, walijikuta ufasaha wao wa kutumia maneno kwa hila
hauna nguvu kabisa dhidi ya sababu rahisi, nyofu za watu wale waliokuwa wana ujuzi wa Maandiko
kuliko kuwa na werevu ule uliofundishwa shuleni.
Kwa kukosa kwa ushahidi wa Biblia unaowaunga mkono, wengi kwa juhudi yao isiyochoka walisema, -
wakisahau jinsi sababu kama hiyo ilivyokuwa imetumiwa dhidi ya Kristo na Mitume wake: “Mbona wakuu
wetu hawaielewi habari hii ya Sabato? Ni wachache tu wanaoamini kama ninyi mnavyoamini.
Haiwezekani kwamba ninyi ndio mko sahihi na watu wote wenye elimu ulimwenguni kote wamekosea.”
Kuzikanusha hoja za namna hiyo kulikuwa na hitaji la kutumia mafundisho ya Maandiko na historia
kuhusu jinsi Bwana alivyochukuliana na watu wake katika vizazi vyote. Mungu anafanya kazi kupitia
(456) kwa wale wanaoisikia na kuitii sauti yake, wale ambao, ikibidi, watasema ukweli mchungu, wale
wasioogopa kukemea dhambi zinazopendwa na watu wengi. Sababu inayomfanya Mungu mara nyingi
asiwachague wenye elimu na wenye vyeo vya juu ni kwamba wao wanategemea itikadi zao za dini,
nadharia zao, na mifumo yao ya thiolojia, wala hawaoni haja ya kufundishwa na Mungu. Ni wale tu
walio na uhusiano binafsi na Chanzo cha hekima wawezao kuelewa au kuyafafanua Maandiko. Watu
wenye elimu ndogo tu ya shuleni wakati mwingine huitwa kuutangaza ukweli, si kwa kuwa hawana
kisomo, bali kwa sababu si watu wa kujitosheleza wenyewe kiasi kwamba wanafundishwa na Mungu.
Wanajifunza katika shule ya Kristo, na unyenyekevu na utii wao huwafanya kuwa wakuu. Katika
kuwakabidhi maarifa ya kweli yake, Mungu anaweka juu yao heshima, ambayo, kwa kuilinganisha,
inaifanya heshima ile ya kidunia na ukuu wa kibinadamu kuzama na kuwa si kitu.
Wanamarejeo walio wengi walizikataa kweli zinazohusu patakatifu na sheria ya Mungu, na wengi pia
waliikana imani yao kuhusu harakati za marejeo na wakafuata mitazamo isiyo sahihi na yenye
migongano unabii uliohusu kazi ile. Wengine waliingizwa katika kosa lile lile la kurudia tena na tena

265
kuweka tarehe maalum ya kuja kwa Kristo. Nuru ambayo ilikuwa inaangaza sasa kwenye somo la
patakatifu ingekuwa imewaonyesha kwamba hakuna kipindi cha unabii kinachofikia kwenye marejeo ya
Kristo; kwamba wakati halisi wa marejeo hayo haujatabiriwa. Lakini, walipoipa kisogo nuru ile,
waliendelea kuweka muda baada ya mwingine wa tarehe ya kuja kwa Bwana, na kama kawaida
walifadhaika.
Wakati kanisa la Thesalonike lilipoyapokea mawazo potofu juu ya kuja kwa Kristo, Mtume Paulo
aliwashauri kupima matumaini na matarajio yao kwa uangalifu kwa kutumia neno la Mungu.
Aliwarejesha katika unabii unaofunua matukio yatakayotokea kabla ya kuja kwa Kristo, na kuonyesha
kwamba hawakuwa na sababu ya kumtazamia katika siku zao. “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia
yo yote” (2 Wathesalonike 2:3), hayo ni maneno yake ya onyo. Kama wangezingatia matarajio ambayo
hayana kibali cha Maandiko, wangeongozwa katika (457) mkondo wa utendaji wenye makosa;
kufadhaika kungewaweka mbele ya kejeli za wasioamini, na wangekuwa katika hatari ya kuvunjika
moyo na wangejaribiwa kuwa na mashaka kuhusu kweli muhimu za wokovu wao. Onyo mtume kwa
Wathesalonike lina fundisho muhimu kwa wale wanaoishi katika siku za mwisho. Wanamarejeo wengi
wameona kwamba wasipoweka imani yao katika muda mahsusi wa kuja kwa Bwana, wasingeweza kuwa
na dhati na bidii katika kujiweka tayari. Lakini matumaini yao yanapoamshwa tena na tena,
yakikumbana na kuvunjika, imani yao inapata mshituko mkubwa kiasi kwamba inakuwa kama
haiwezekani tena kwao kuguswa na kweli kuu za unabii.
Kule kuhubiri wakati mahsusi wa hukumu, katika kuutangaza ujumbe ule wa kwanza, kuliamriwa na
Mungu. Mahesabu ya vipindi vile vya unabii ambavyo ujumbe ule ulijengwa juu yake, ambayo
yalionyesha mwisho wa siku 2300 kuwa majira ya kupukutisha ya mwaka 1844, yanasimama bila
kupingwa. Juhudi ya kujirudia-rudia katika kutafuta tarehe mpya za kuanza na kukoma kwa vipindi
hivyo vya unabii, na sababu zisizoridhisha zinazoonekana muhimu kutetea misimamo hii, si tu kwamba
zinawapeleka watu mbali na ukweli wa leo, bali pia zinatweza juhudi zote za kufafanua unabii. Kadiri
muda wa marejeo unavyowekwa tena na tena, na kadiri unavyofundishwa mahali pengi, ndivyo hali hiyo
inavyofaa zaidi katika kutimiza makusudi ya Shetani. Baada ya tarehe inayowekwa kupita, anachochea
dhihaka na dharau dhidi ya wanaoitetea, na kwa njia hiyo anatupa shutuma juu ya harakati kuu ya
marejeo ya mwaka 1843 na 1844. Wale wanaozidi kuendelea katika kosa hili hatimaye wataweka tarehe
ya kuja kwa Kristo mbali zaidi mbele kuliko muda wenyewe. Kwa hiyo watafanywa kutulia wakiwa
katika hali ya usalama wa uongo, na wengi hawatatoka katika madanganyo mpaka watapokuwa
wamechelewa.
Historia ya Israeli ya zamani ni kielelezo dhahiri cha uzoefu uliopita wa kundi la Wanamarejeo. Mungu
aliwaongoza watu wake waliokuwa katika harakati za marejeo, kama vile alivyowaongoza wana wa
Israeli kutoka Misri. Katika mdhaiko mkuu ule imani yao ilipimwa kama imani ya Waebrania wale
ilivyopimwa wakti walipofika kwenye Bahari ya Shamu. Kama wangekuwa bado wameutegemea mkono
ule uliokuwa umekuwa pamoja nao katika (458) uzoefu uliokuwa umepita, wangekuwa wameuona
wokovu wa Mungu. Ikiwa wote waliokuwa wameshughulika pamoja katika kazi mwaka 1844
wangeupokea ujumbe wa malaika wa tatu na kuutangaza kwa uweza wa Roho Mtakatifu, Bwana
angekuwa ametenda pamoja na juhudi zao kwa uweza mkuu. Gharika ya nuru ingekuwa imeangazwa juu
ya ulimwengu. Katika miaka iliyopita wakazi wa ulimwengu huu wangekuwa wameonywa, kazi ya
kufunga kazi ingekuwa imekamilika, na Kristo angekuwa amekuja kuwakomboa watu wake.
Hayakuwa mapenzi ya Mungu kwamba Israeli wapate kutangatanga jangwani kwa miaka arobaini;
alitamani awaongoze moja kwa moja kwenda katika nchi ya Kanaani na awakalishe humo, wakiwa
watakatifu na wenye furaha. Lakini “hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao.”
266
Waebrania 3:19. Kwa sababu ya kurudi nyuma kwao na uasi wao waliangamia jangwani, na wengine
waliinuliwa ili kuiingia Nchi ya Ahadi. Kwa namna hiyo hiyo, hayakuwa mapenzi ya Mungu kwamba kuja
kwa Kristo kucheleweshwe kwa muda mrefu hivi na watu wake waendelee kubaki kwa miaka mingi kiasi
hiki katika dunia hii yenye dhambi na huzuni. Lakini kutokuamini kuliwatenga mbali na Mungu.
Walipokataa kufanya kazi ile aliyokuwa amewapa kufanya, wengine waliinuliwa ili kutangaza ujumbe
ule. Kwa rehema zake kwa ulimwengu, Yesu anachelewesha kuja kwake, ili kwamba wenye dhambi
wapate fursa ya kulisikia onyo na kupata hifadhi ndani yake kabla ghadhabu ya Mungu haijamwagwa.
Katika wakati huu kama ilivyokuwa katika vizazi vilivyopita, kuuhubiri ukweli unaokemea dhambi na
makosa ya nyakati hizi kutaamsha upinzani. “Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala
haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa.” Yohana 3:20. Kadiri watu wanavyoona kwamba
hawawezi kutetea msimamo wao kwa Maandiko, wengi hudhamiria kuutetea kwa kutumia hatari zote,
na kwa msukumo wa kuwadhuru wengine wanashambulia tabia na mivuto ya wale wanaosimama kutetea
ukweli usiopendwa na wengi. Ni sera hiyo hiyo ambayo imetumika katika vizazi vyote. Eliya alitajwa
kuwa mtaabishaji wa Israeli, Yeremia alionekana msaliti, Paulo kama mtu anayenajisi hekalu. Tangu
wakati ule mpaka sasa, wale wanaokuwa watiifu kwa ile kweli wameshutumiwa kuwa ni wachochezi wa
upinzani au maasi, (459) wazushi, au wenye kutaka mafarakano. Makutano ya watu wengi wasioamini
kabisa kiasi cha kutolikubali neno la hakika la unabii watapokea kwa urahisi bila maswali mashtaka
yatakayotolewa dhidi ya wale wanaothubutu kuzikemea dhambi zile zinazopendwa kwa wakati husika.
Roho ya namna hii itaongezeka zaidi na zaidi. Na Biblia kwa uwazi inafundisha kwamba wakati unakuja
wakati ambapo sheria za nchi zitapingana na sheria ya Mungu kiasi kwamba yeyote ambaye angetii amri
zote za kimbingu lazima akutane na shutuma na adhabu kama mtenda maovu.
Kwa kuangalia haya, wajibu wa mjumbe wa ile kweli ni upi? Je, ataamua kuhitimisha kwamba ukweli
usisemwe, kwa kuwa mara nyingi matokeo yake ni kuchochea watu kukwepa au kupinga matakwa ya
ukweli huo? La; hana sababu nyingine zaidi inayomruhusu kuuzuia ushuhuda wa neno la Mungu, eti kwa
sababu unaamsha upinzani, kuliko ilivyokuwa kwa wanamatengezo wa awali. Kuikiri imani kulikofanywa
na watakatifu na wafia-dini wale kuliandikwa katika kumbukumbu kwa faida ya vizazi vilivyofuata.
Vielelezo hivyo vilivyo hai vya utakatifu na msimamo thabiti vimetufikia ili kuwatia ujasiri wale
wanaoitwa sasa kusimama kama mashahidi wa Mungu. Walipokea neema na ukweli, si kwa ajili yao tu,
bali kwamba, kwa njia yao, maarifa ya kumjua Mungu yapate kuiangaza dunia nzima. Je, Mungu
amewapa nuru watumishi wake katika kizazi hiki? Basi na waiache ipate kuangaza kwa ulimwengu.
Zamani Bwana alimtangazia yule aliyenena kwa jina lake: “Nyumba ya Israeli hawatakusikiliza wewe;
kwa kuwa hawanisikilizi Mimi.” Akaendelea kusema: “Nawe utawaambia maneno yangu, kwamba
watasikia, au kwamba hawataki kusikia.” Ezekieli 3:7; 2:7. Kwa mtumishi wa Mungu wa wakati huu amri
hii inatolewa: “Paza sauti yako kama tarumbeta; uwahubiri watu wangu kosa lao, na nyumba ya Yakobo
dhambi zao.”
Mpaka hapa kadiri fursa inavyoendelea, kila mmoja aliyeipokea nuru ya ukweli yuko chini ya uwajibikaji
huo huo mzito na wa kuogofya kama aliokuwa nao nabii yule wa Israeli, ambaye neno la Bwana lilimjia
likisema: “Mwanadamu nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli; basi ulisikie (460) neno hili
kinywani mwangu, ukawape maonyo yangu. Nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu mbaya, hakika utakufa,
nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo, aiache njia yake, mtu mbaya huyo atakufa katika uovu
wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia
yake, kusudi aiache; wala yeye asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho
yako.” Ezekieli 33:7-9.

267
Kipingamizi kikubwa dhidi ya yote kuupokea na kuutangaza ukweli ni hali halisi ya kwamba inaleta
usumbufu na shutuma. Hiyo ndiyo hoja pekee dhidi ya ukweli ambayo wale wanaoutetea hawajapata
kuikanusha kamwe. Lakini hili haliwazuii wafuasi wa kweli wa Kristo. Wao hawasubiri mpaka ukweli
upendwe na watu wengi. Wakiisha kuthibitishiwa jukumu lao, kwa uthabiti wanaukubali msalaba,
wakihesabu pamoja na Mtume Paulo kwamba “dhiki yetu nyepesi iliyo ya muda wa kitambo tu,
yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana;” na pamoja na mtu yule wa kale, “wakihesabu
ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri.” 2 Wakorintho 4:17;
Waebrania 11:26.
Vyovyote wanavyoweza kujidai, ni wale tu wanaoitumikia dunia hii kwa moyo wao wote ambao
wanatenda kutokana na sera kuliko kufuata kanuni katika mambo ya dini. Yatupasa kuchagua usahihi
kwa sababu ni usahihi, na kuacha matokeo mikononi mwa Mungu. Watu wa kanuni, imani, na ujasiri,
wanadaiwa na ulimwengu matengenezo makubwa. Lazima kazi ya matengenezo kwa wakati huu
iendelezwe na watu wa jinsi hiyo.
Hivi ndivyo asemavyo Bwana: “Nisikilizeni ninyi mjuao haki, watu ambao mioyoni mwenu mna sheria
yangu; msiogope matukano ya watu, wala msifadhaike kwa sababu ya dhihaka zao. Maana nondo itawala
kama vazi, na funza atawala kama sufu; bali haki yangu itakuwa ya milele, na wokovu wangu hata vizazi
vyote.” Isaya 51:7,8.

268
Sura ya 27
UAMSHO WA KISASA

Mahali popote ambapo neno la Mungu limehubiriwa kwa uaminifu, matokeo yanayolithibitisha kwamba
lina chanzo cha kimbingu yamefuata. Roho wa Mungu aliambatana na ujumbe uliotolewa na watumishi
wake, na neno lile lilikuwa na nguvu. Wenye dhambi waliona dhamiri zao zikiamshwa. “Nuru Halisi,
amtiaye nuru kila mtu, ajaye katika ulimwengu” alivimulika vyumba vya siri vya mioyo yao, na mambo
ya giza yaliyofichika yalifunuliwa wazi. Mguso wa kina ulifanyika katika mawazo na mioyo yao.
Walihakikishiwa kuhusu dhambi na haki na hukumu ijayo. Waliielewa haki ya Yehova na waliingiwa na
hofu ya kuonekana kwake, wakiwa katika hatia na uchafu, mbele zake yeye Aichunguzaye mioyo.
Walilia kwa uchungu: “Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?” Kadiri msalaba wa Kalvari
ulivyofunuliwa kwao, pamoja na kafara yake isiyo na kifani iliyotolewa kwa ajili ya dhambi za
wanadamu, waliona kwamba hakuna chochote ambacho kingeweza kutosheleza kulipa fidia kwa ajili ya
dhambi zao isipokuwa wema wa Kristo; hicho tu ndicho kingeweza kuwapatanisha wanadamu na Mungu.
Kwa imani na unyenyekevu walimpokea Mwana-Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu.
Kupitia damu ya Yesu walipata “ondoleo la dhambi zilizotangulia kufanywa.”
Watu hawa walizaa matunda yapasayo toba. Waliamini na kubatizwa, na waliinukia kutembea katika
upya wa maisha - viumbe vipya ndani ya Kristo Yesu; si kwa kujinakshi katika tamaa zao za zamani, bali
kwa imani ya Mwana wa (462) Mungu kufuata katika nyayo zake, kuakisi tabia yake, na kujitakasa
wenyewe kama yeye alivyo mtakatifu. Mambo yale waliyoyachukia zamani sasa waliyapenda, na mambo
waliyoyapenda zamani waliyachukia. Wale wenye kiburi na kujidai waligeuka kuwa wapole na
wanyenyekevu wa moyo. Wenye mizaha na majivuno waligeuka kuwa watu wa dhati na wasiopenda
kujiingiza katika mambo ya wengine. Wenye kukufuru walikuwa na kicho, walevi wakawa hawalewi, na
waasherati wakawa na maisha safi. Mitindo ya ulimwengu isiyokuwa na maana ikawekwa kando.
Wakristo wale hawakutafuta “kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia
mavazi; bali … utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na
utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.’ -1 Petro 3:3,4.
Uamsho ulileta hali ya kujichunguza moyo kwa kina na unyenyekevu. Ulikuwa na sifa ya kuwa na wito
mzito na wa dhati kwa mwenye dhambi, kwa kuwaonea shauku ya huruma wale walionunuliwa kwa
damu ya Kristo. Wanaume na wanawake waliomba na kupambana na Mungu kwa ajili ya wokovu wa roho
za watu. Matunda ya uamsho wa namna hii yalionekana ndani ya watu ambao hawakusinyaa
walipotakiwa kujikana nafsi na kujitoa kafara, bali walifurahi kwamba walihesabiwa kuwa wanastahili
kupatwa na shutuma na majaribu kwa ajili ya Kristo. Watu waliona mabadiliko katika maisha ya wale
waliolikiri jina la Yesu. Jamii ilinufaishwa na mvuto wao. Walikusanya pamoja na Kristo, na walipanda
mbegu kwa Roho, ili kuvuna uzima wa milele.
Ingeweza kusemwa kuwahusu hao: “Mlihuzunishwa, hata mkatubu.” “Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya
Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti. Maana,
angalieni, kuhuzunishwa kuko huko kwa jinsi ya Mungu kulitenda bidii kama nini ndani yenu; naam, na

269
kujitetea, naam, na kukasirika, naam, na hofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi!
Kwa kila njia mmejionyesha wenyewe kuwa safi katika jambo hilo.” 2 Wakorintho 7:9-11.
Haya ndiyo matokeo ya kazi ya Roho wa Mungu. Hakuna ushahidi wo wote wa toba ya kweli isipokuwa
kama kuna matengenezo. (463) Kama akirudisha rehani, akimrudishia mtu mali yake aliyomnyang’anya,
akiziungama dhambi zake, na kumpenda Mungu na wanadamu wenzake, mdhambi anaweze kuwa na
hakika kwamba amepata amani kati yake na Mungu. Hayo ndiyo yalikuwa matokeo yaliyofuata baada ya
vipindi vya uamsho wa kidini. Wakipimwa kwa matunda yao, walijulikana ya kuwa walikuwa
wamebarikiwa na Mungu kwa ajili ya wokovu wa watu pamoja na kuhimiza utu.
Lakini uamsho mwingi wa siku hizi umeonyesha tofauti kubwa kati yake na udhihirisho wa neema ya
kimbingu ambayo ilifuata kazi za watumishi wa Mungu mnamo siku zile za awali. Ni kweli kwamba
shauku ya kupenda mambo ya dini inaamshwa mahali pengi, wengi wanakiri kuwa wameongoka, na watu
wengi wanaingia makanisani; hata hivyo matokeo yake si kama yale yanayoweza kuaminisha kwamba
kumekuwepo na ongezeko linganifu la maisha ya kiroho. Mwanga unaowaka sana kwa muda huzimika,
ukiacha giza zito kuliko lile la kabla.
Uamsho ulio maarufu kwa kiasi kikubwa ni wa kuigiza tu, kwa kuamsha hisia, kwa kuvuta watu kupenda
kusikia mambo mapya na ya kushtusha. Waongofu wanaopatikana kwa njia hiyo wana hamu kidogo ya
kusikiliza ukweli wa Biblia, wana hamu kidogo tu ya ushuhuda wa manabii na mitume. Ikiwa huduma ya
ibada ya kidini haina kitu chenye namna ya kusisimua, hiyo haina mvuto kwao. Ujumbe wowote
unaohitaji kutumia akili zao bila maamuzi ya harara hauna mwitikio. Maonyo dhahiri ya neno la Mungu,
ambayo moja kwa moja yanahusu hamu ya umilele, hayazingatiwi.
Kwa kila mtu ambaye ameongoka kweli kweli, uhusiano wake na Mungu na mambo ya milele utakuwa
ndio mada kuu ya maisha yake. Lakini iko wapi, katika makanisa maarufu ya leo, roho ya kujitoa wakfu
kwa Mungu? Waongofu hawaachani na kiburi na kuupenda ulimwengu. Hawako tayari kujikana nafsi,
kujitwika msalaba, na kumfuata Yesu aliye mpole na mnyenyekevu, zaidi ya vile walivyokuwa kabla ya
kuongoka. Dini imekuwa kitu cha mzaha kwa makafiri na wanafiki kwa sababu wengi wenye jina hilo
hawajui misingi yake. Nguvu ya utauwa imetoweka kabisa katika makanisa yaliyo mengi. Pikniki,
shughuli za maonyesho ya kanisa, (464) minada ya kanisa, majumba mazuri, kujionyesha kwa watu,
vimeondoa mawazo ya kumwelekea Mungu. Ardhi na mali na kazi za kiulimwengu vinashughulisha
mawazo, na mambo ya umilele yanaangaliwa kwa shida sana.
Licha ya kuenea kwa mmomonyoko wa imani na utauwa, wapo wafuasi wa kweli wa Kristo ndani ya
makanisa haya. Kabla hukumu za Mungu hazijapatilizwa duniani kwa mara ya mwisho, kutakuwa na
uamsho wa utauwa wa zamani miongoni mwa watu wa Bwana, ambao haujapata kushuhudiwa tangu
nyakati za mitume. Roho na uweza wa Mungu vitamwagwa juu ya watoto wake. Wakati huo wengi
watajitenga na makanisa hayo ambamo kuupenda ulimwengu huu kumechukua mahali pa upendo wao
kwa Mungu na neno lake. Wengi, makundi yote ya viongozi wa kiroho na watu wa kawaida, kwa furaha
watazipokea kweli hizo kuu ambazo Mungu amefanya zipate kutangazwa kwa wakati huu ili kuwaandaa
watu wake kwa ajili ya kuja kwa Bwana mara ya pili. Adui wa roho za watu anatamani sana kuizuia kazi
hiyo; na kabla ya wakati huo wa harakati hizo kuja, atajitahidi sana kuzizuia kwa kuanzisha za bandia.
Atafanya ionekane kama vile mbaraka maalum wa Mungu umemwagwa katika makanisa yale anayoweza
kuleta chini ya uwezo wake wa madanganyo; ndani ya hayo kutakuwa na udhihirisho wa kitu
kitakachodhaniwa kuwa mwamko mkuu wa mambo ya dini. Makutano watashangilia kwamba Mungu
anawatendea kwa maajabu, wakati kazi hiyo ni ya roho yule mwingine. Akiwa amevalia vazi la kidini,
Shetani atatafuta kuueneza ushawishi wake juu ya ulimwengu wa Kikristo.

270
Katika namna nyingi za uamsho uliotokea katika kipindi cha nusu karne iliyopita, ushawishi huo
umekuwa kazini, kwa viwango tofauti-tofauti, ambao utadhihirika katika zile harakati kubwa zaidi za
wakati ujao. Kuna msisimko wa hisia, kuna mchanganyiko wa ukweli na uongo, ambao umetengenezwa
ili kupotosha. Lakini hakuna haja ya mtu ye yote kudanganyika. Katika nuru ya neno la Mungu si vigumu
kubaini asili ya harakati hizo. Popote watu wanapodharau ushuhuda wa Biblia, wakigeukia mbali
kuziacha kweli hizo zilizo wazi, zinazoipima mioyo, na zinazowataka watu wajikane nafsi na kuachana
na ulimwengu, tunaweza kuwa na hakika kwamba mbaraka wa Mungu haujatolewa hapo. (465) Na kwa
kanuni ile ambayo Kristo mwenyewe ametoa, “Mtawatambua kwa matunda yao” (Mathayo 7:16), ni
dhahiri kwamba harakati hizi si kazi ya Roho wa Mungu.
Katika kweli za neno lake, Mungu amewapa wanadamu ufunuo wa yeye mwenyewe; na kwa wote
wanaozikubali zinakuwa ngao yao dhidi ya madanganyo ya Shetani. Ni kule kuzipuuza kweli hizi
kulikoyafungulia mlango maovu yanayoenea sasa katika ulimwengu wa kidini. Tabia na umuhimu wa
sheria ya Mungu, kwa kiasi kikubwa, havionekani. Dhana potofu kuhusu tabia, kudumu, na umuhimu wa
sheria ya Mungu vimeleta mafundisho potofu kuhusu uongofu na utakaso, na matokeo yake yamekuwa ni
kuishusha chini kanuni hiyo ya utauwa katika kanisa. Hapa ndipo ilipo siri ya kukosekana kwa Roho na
uweza wa Mungu katika uamsho unaotokea katika siku zetu hizi.
Katika madhehebu mbalimbali wamo watu wanaojulikana kwa utauwa wao, watu wanaokiri uwepo wa
hali hii na kuchukizwa nayo. Profesa Edwards A. Parks, akieleza hatari za kidini zilizopo sasa,
anastahimili kusema: “Chanzo kimoja cha hatari ni hali ya viongozi wa kanisa kupuuza sheria ya Mungu.
Katika siku za zamani mimbari ilikuwa mwangwi wa sauti ya dhamiri…. Wahubiri wetu waliokuwa
maarufu, kwa njia ya hotuba zao, walileta utukufu wa ajabu kwa kufuata kielelezo cha Bwana, na kuipa
umuhimu sheria, amri zake, na utisho wake. Walirudiarudia kanuni mbili kuu, kwamba sheria ni nakala
halisi ya ukamilifu wa Mungu, na kwamba mtu asiyeipenda sheria haipendi injili; maana sheria, pamoja
na injili, ni kioo kinachoakisi tabia halisi ya Mungu. Hatari hii inaongoza katika hatari nyingine, nayo ni
ile ya kuhafifisha ubaya wa dhambi, ukubwa wake, na mapungufu yake. Ubaya wa kutotii sheria uko
katika ulinganifu wa uwiano kama wa uhalali wa amri….
“Kilichofungamanishwa na hatari hizo zilizokwisha kutajwa ni hatari ya kukadiria haki ya Mungu kwa
udogo. Mwelekeo wa wahubiri wa kisasa ni kuchuja haki ya Mungu kutoka katika wema wa Mungu,
kuuzamisha wema wake katika hisia badala (466) ya kuuinua juu kama msingi. Prismu mpya ya
kithiolojia inatawanya vile ambavyo Mungu aliunganisha pamoja. Sheria ya Mungu ni njema au mbaya?
Ni njema. Basi haki ni njema; kwa maana ndiyo tabia ya kutekeleza sheria. Kutokana na tabia ya
kushusha hadhi ya sheria ya Mungu na haki, kipimo cha kiasi na mapungufu cha utii, watu wanateleza
kwa urahisi kuingia katika tabia ya kukadiria kwa upungufu neema ambayo imeleta upatanisho wa
dhambi.” Hivyo injili inapoteza thamani na umuhimu katika mawazo ya watu, na punde tu wanakuwa
tayari kuitupa kando hata Biblia yenyewe.
Walimu wengi wa dini wanadai kwamba Kristo aliikoesha sheria kwa kifo chake, na ya kwamba tangu
wakati huo watu wako huru na masharti yake. Wapo baadhi ambao wanaieleza kama kongwa zito, na
kinyume na utumwa katika sheria wanahubiri uhuru katika injili.
Lakini hivyo sivyo manabii na mitume walivyoichukulia sheria takatifu ya Mungu. Daudi alisema: “Nami
nitakwenda panapo nafasi, kwa kuwa nimejifunza mausia yako.” Zaburi 119:45. Mtume Yakobo,
aliyeandika baada ya kifo cha Kristo, anaitaja sheria ya amri kumi kama “sheria ya kifalme” na “sheria
kamilifu iliyo ya uhuru.” Yakobo 2:8; 1:25. Na mwandishi wa kitabu cha Ufunuo, nusu karne baada ya

271
kusulibiwa kwa Kristo, anataja baraka juu ya wale “wazishikao amri zake, wawe na haki kuuendea huo
mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.” Ufunuo 22:14.
Madai kwamba Kristo kwa kifo chake aliifutilia mbali sheria ya Baba yake hayana msingi. Laiti
ingewezakana kwa sheria hiyo kubadilishwa au kuwekwa kando, basi Kristo asingehitaji kufa ili
kumwokoa mwanadamu kutoka katika adhabu ya dhambi. Kifo cha Kristo, mbali kabisa na kuikomesha
sheria, kinathibitisha kwamba haibadiliki. Mwana wa Mungu alikuja “kuitukuza Sheria, na
kuiadhimisha.” Isaya 42:21. Alisema: “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati;” “mpaka mbingu na
nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja haitaondoka.” Mathayo 5:17,18. Tena kumhusu yeye
mwenyewe anasema: “Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu, ndiyo furaha yangu; Naam, Sheria yako imo
moyoni mwangu.” Zaburi 40:8.
(467) Sheria ya Mungu, tangu katika asili yake halisi, haibadiliki. Ni ufunuo wa mapenzi na tabia ya
Mwasisi wake. Mungu ni upendo; na sheria yake ni upendo. Misingi yake mikuu miwili ni upendo kwa
Mungu na upendo kwa mwanadamu. “Pendo ndilo utimilifu wa sheria.” Warumi 13:10. Tabia ya Mungu
ni haki na ukweli; vile vile hiyo ndiyo tabia ya sheria yake. Mwimba zaburi anasema: “Sheria yako ni
kweli;” “Maana maagizo yako yote ni ya haki.” Zaburi 119:142,172. Na mtume Paulo anasema wazi:
“Basi, torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema.” Warumi 7:12. Sheria hiyo, ikiwa
udhihirisho wa mawazo na mapenzi ya Mungu, lazima iwe ya kudumu kama alivyo Mwasisi wake.
Kupatanisha wanadamu na Mungu kwa kuwaleta katika mwafaka kamili na kanuni za sheria yake ni kazi
ya uongofu na utakaso. Hapo mwanzo, mtu aliumbwa kwa sura ya Mungu. Alikuwa katika mpatano
thabiti na asili na sheria ya Mungu; kanuni za haki ziliandikwa moyoni mwake. Lakini dhambi ilimtenga
mbali na Muumba wake. Hakuweza kuakisi tena tabia ya kimbingu. Moyo wake ulikuwa vitani ukipingana
na kanuni za sheria ya Mungu. “Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii
sheria ya Mungu, wala haiwezi kutii.” Warumi 8:7. Lakini, “Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa
Mwanawe pekee,” ili kwamba mwanadamu apate kupatanishwa na Mungu. Kwa njia ya wema wa Kristo
mwanadamu anaweza kurejeshwa katika upatano na Muumba wake. Lazima moyo wake ufanywe kuwa
mpya kwa neema ya Mungu; sharti apate maisha mapya kutoka juu. Badiliko hilo ndiko kuzaliwa upya,
ambapo pasipo huko, Yesu anasema, “hawezi kuuona ufalme wa Mungu.”
Hatua ya kwanza katika kupatanishwa na Mungu ni kusadikishwa kuhusu dhambi. “Dhambi ni uvunjaji
wa sheria.” “Kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.” 1 Yohana 3:4; Warumi 3:20. Ili mdhambi apate
kuona hatia yake, lazima aipime tabia yake kwa kutumia kiwango cha haki cha Mungu. Hicho ndicho
kioo kinachoonyedha ukamilifu wa tabia ya haki na cha kumwezesha mtu kutambua kasoro alizo nazo
katika tabia yake.
Sheria humwonyesha mtu dhambi zake, lakini haileti tiba ya dhambi. (468) Inapoahidi uzima kwa mtu
anayeitii, inatangaza kwamba sehemu ya mkiukaji wa sheria ni mauti. Injili ya Kristo pekee ndiyo
iwezayo kumweka huru kutoka katika hukumu au unajisi wa dhambi. Lazima afanye toba kwa Mungu,
ambaye ndiye mwenye sheria iliyovunjwa; na awe na imani kwa Kristo, ambaye ni kafara ya upatanisho
ya mdhambi. Kwa njia hiyo anapata “msamaha wa dhambi zilizotangulia kufanywa,” kisha anakuwa
mshirika wa tabia ya Mungu. Yeye ni mwana wa Mungu, akiisha kuipokea roho ya kufanywa mwana,
ambapo kwa hiyo analia: “Aba, Baba!”
Je, sasa anao uhuru wa kuvunja sheria ya Mungu? Paulo anasema: “Basi, je! Twaibatilisha sheria kwa
imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.” “Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena
katika dhambi? Naye Yohana anasema: “Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike
amri zake; wala amri zake si nzito.” Warumi 3:31; 6:2; 1 Yohana 5:3. Katika kuzaliwa upya moyo
272
unaletwa katika hali ya kupatana na Mungu, kadiri unavyoletwa katika mwafaka na sheria yake. Badiliko
hili kubwa linapokuwa limetokea ndani ya mwenye dhambi, anakuwa amepita kutoka mautini kwenda
uzimani, kutoka dhambini kwenda katika utakatifu, kutoka katika uvunjaji wa sheria na uasi kwenda
katika utii na uaminifu. Maisha ya zamani ya kutengana na Mungu yamekoma; maisha mapya ya
upatanisho, ya imani na upendo, yameanza. Hapo ndipo ile “haki ya sheria” “itakapotimizwa ndani yetu
sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya Roho.” Warumi 8:4. Na lugha ya mtu
huyo itakuwa ni: “Sheria yako naipenda mno ajabu, ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa.” Zaburi
119:97.
“Sheria ya BWANA ni kamilifu; huiburudisha nafsi.” Zaburi 19:7. Pasipo sheria, watu hawawezi kuwa na
mawazo sahihi kuhusu usafi na utakatifu wa Mungu au kuhusu uchafu wao na dhambi zao wenyewe.
Hawana utambuzi wa kweli kuwathibitishia hatia ya dhambi na hawahisi hitaji la kutubu. Kwa
kushindwa kuona hali yao ya kupotea wakiwa wavunjaji wa sheria ya Mungu, hagundui uhitaji wao wa
damu ya Kristo ya inayopatanisha. Tumaini la wokovu linapokelewa bila kuwa na badiliko muhimu la
moyo au bila matengenezo ya maisha. Kwa njia hiyo uongofu wa juu juu unaenea, na watu wengi
wanajiunga na kanisa pasipo kuunganishwa na Kristo kamwe.
(469) Nadharia potofu za utakaso, pia, zikichipuka kutokana na kupuuza na kukataa sheria ya Mungu,
zina sehemu ya maana sana katika harakati za kidini siku hizi. Nadharia hizo ni za uongo kimafundisho
na ni za hatari zinapotekelezwa; na ukweli kwamba kwa ujumla nadharia hizo zinapendelewa na watu
wengi, hulifanya jambo hilo kuwa la muhimu maradufu kwamba wote wapate kuwa na ufahamu dhahiri
kuhusu kile kinachofundishwa na Maandiko kulihusu.
Utakaso wa kweli ni fundisho la Biblia. Mtume Paulo, katika Waraka wake kwa kanisa la Wathesalonike,
anasema: “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu.” Tena anaomba kwamba: “Mungu
wa amani mwenyewe awatakase kabisa.” 1 Wathesalonike 4:3; 5:23. Biblia inafundisha waziwazi maana
ya utakaso na jinsi unavyoweza kupatikana. Mwokozi aliwaombea wanafunzi wake: “Uwatakase kwa ile
kweli; neno lako ndiyo kweli.” Yohana 17:17,19. Na Paulo anafundisha kwamba waumini wanapaswa
“kutakaswa na Roho Mtakatifu.” Warumi 15:16. Roho Mtakatifu anafanya kazi gani? Yesu aliwaambia
wanafunzi wake: “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli
yote.” Yohana 16:13. Na mwimba zaburi anasema: “Sheria yako ni kweli.” Kwa njia ya neno na Roho wa
Mungu kanuni kuu za haki ambazo zimo ndani ya sheria yake zinafunuliwa kwa watu. Na kwa kuwa
sheria ya Mungu ni “takatifu, na ya haki, na njema,” tena ni nakala ya ukamilifu wa Mungu, kwa hiyo
tabia inayojengwa na utii wa sheria hiyo ni takatifu. Kristo ni kielelezo kikamilifu cha tabia hiyo.
Anasema: “Nimezishika amri za Baba yangu.” “Nafanya sikuzote yale yampendezayo.” Yohana 15:10;
8:29. Yawapasa wafuasi wa Kristo kuwa kama yeye - kwa neema ya Mungu kujenga tabia zinazopatana
na kanuni za sheria yake takatifu. Huo ndio utakaso wa Biblia.
Kazi hii inaweza kukamilishwa tu kwa njia ya imani katika Kristo, kwa nguvu ya Roho wa Mungu
anayekaa ndani. Paulo anawaonya waumini: “Utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na
kutetemeka. Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa
kulitimiza kusudi lake jema.” Wafilipi 2:12,13. Mkristo atahisi hisia za dhambi inayosukuma ndani yake,
lakini ataendelea (470) kupambana nayo daima. Hapa ndipo msaada wa Kristo unapohitajika. Udhaifu
wa mwanadamu unaunganishwa kwa nguvu za uungu, na imani inashangilia: “Mungu na ashukuriwe
atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.” 1 Wakorintho 15:17.
Maandiko yanaonyesha wazi kwamba kazi ya utakaso ni ya kuendelea. Wakati anapokuwa katika
wongofu, mwenye dhambi anapata kwa Mungu kwa njia ya damu ya upatanisho, maisha ya Kikristo

273
ndipo tu yameanza. Sasa ndipo anatakiwa kusonga mbele “hata kuwa mtu mkamilifu;” na kukua “hata
kufika kwenye cheo cha utimilifu wa Kristo.” Mtume Paulo anasema: “Natenda neno moja tu;
nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu
ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.” Wafilipi 4:13,14. Naye Petro anatuwekea hatua ambazo
kwazo utakaso wa Biblia unaweza kufikiwa: “Mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni
wema, na katika wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na
katika saburi yenu utauwa, na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu,
upendo…. Maana mkitenda hayo, hamtajikwaa kamwe.” 2 Petro 1:5-10.
Wale wanaopitia uzoefu wa utakaso wa Biblia wataonyesha moyo wa unyenyekevu. Kama Musa,
wamepata kuona ukuu wenye utisho wa utakatifu, na wanaona kutostahili kwao kunavyotofautiana na
utakatifu na ukamilifu wa hali ya juu alio nao Yeye wa Milele.
Nabii Danieli alikuwa kielelezo cha utakaso wa kweli. Maisha yake marefu yalijawa na hutumishi bora
kwa Bwana wake. Alikuwa “mtu apendwaye sana” (Danieli 10:11) na Mungu. Lakini badala ya kujidai
kuwa msafi na mtakatifu, nabii huyu aliyeheshimiwa alijihesabu pamoja na Israeli wenye dhambi
alipoomba mbele za Mungu kwa ajili ya watu wake: “Hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu,
lakini kwa sababu ya rehema zao nyingi.” “Tumefanya dhambi, tumetenda maovu.” Anasema kwa
mkazo: “Basi hapo nilipokuwa nikisema, na kuomba, na kuiungama dhambi yangu, na dhambi ya watu
wangu.” Baadaye Mwana wa Mungu alipomtokea ili (471) kumpa maagizo fulani, Danieli anasema:
“Uzuri wangu uligeuzwa ndani yangu kuwa uharibifu, wala sikusaziwa nguvu.” Danieli 9:18,15,20; 10:8.
Ayubu aliposikia sauti ya Bwana katika upepo wa kisulisuli, alisema: “Najichukia nafsi yangu, na kutubu
katika mavumbi na majivu.” Ayubu 42:6. Ni wakati Isaya alipouona utukufu wa Bwana, na kuwasikia
makerubi wakisema, “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA wa majeshi,” akalia akisema: “Ole
wangu! Kwa maana nimepotea.” Isaya 6:3,5. Paulo, baada ya kunyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu na
kusikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene, anasema kuhusu yeye mwenyewe
kwamba “ni mdogo wa watakatifu wote.” 2 Wakorintho 12:2-4; Waefeso 3:8. Alikuwa Yohana yule
mpendwa, aliyeegama kifuani pa Yesu na kuuona utukufu wake, ambaye alianguka kama mtu aliyekufa
chini ya miguu ya malaika. Ufunuo 1:17.
Kwenye upande wa wale wanaotembea katika kivuli cha msalaba wa Kalvari, hapawezi kuwa na
kujikweza, wala kuwa na madai ya kujisifu kwamba wako huru mbali na dhambi. Wanajisikia kwamba
dhambi yao ndiyo iliyosababisha mateso yaliyopasua moyo wa Mwana wa Mungu, na wazo hilo
litawafanya wajitweze. Wale wanaoishi karibu sana na Yesu wanauona dhahiri udhaifu na uovu wa
kibinadamu, na tumaini lao pekee li katika wema wa Mwokozi aliyesulibiwa na kufufuka.
Hali ya utakaso unaozidi kutukuzwa sasa katika ulimwengu wa Kikristo ina roho ya kujikweza na
kudharau sheria ya Mungu inayoonyesha kwamba hilo ni jambo geni katika dini ya Biblia. Wanaoitetea
wanafundisha kwamba utakaso ni kazi ya ghafla, ambayo kwa hiyo, kwa njia ya imani peke yake,
wanapata utakatifu kamili. “Amini tu,” wanasema, “na mbaraka huo ni wako.” Hakuna juhudi zaidi
inayohitajika kwa upande wa mpokeaji. Wakati huo huo wanakana mamlaka ya sheria ya Mungu,
wakidai kwamba wamefunguliwa kutoka katika wajibu wa kuzishika amri. Lakini, je, inawezekana kwa
wanadamu kuwa watakatifu, kupatana na mapenzi na tabia ya Mungu, bila ya wao kuja katika hali ya
kupatana na kanuni zile ambazo zinafunua tabia na mapenzi yake?
(472) Tamaa ya kuwa na dini nyepesi isiyowataka watu kujitahidi, isiyo na kujikana nafsi, isiyo na
kuachana na mabaya ya ulimwengu, imefanya fundisho linalosema imani, na imani pekee, kuwa
fundisho maarufu; lakini neno la Mungu linasemaje? Mtume Yakobo anasema: “Ndugu zangu, yafaa nini,
274
mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo. Je, ile imani yaweza kumwokoa?… Lakini
wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai? Je! baba yetu
Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya
madhabahu? Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile
ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale…. Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa
matendo yake; si kwa imani peke yake.” Yakobo 2:14-24
Ushuhuda wa neno la Mungu uko kinyume cha fundisho hilo la mtego unasao kuhusu imani pasipo
matendo. Hiyo si imani inayodai kukubaliwa na Mbingu bila kutimiza masharti yake ambayo kwayo
rehema inatolewa, ni ufidhuli; kwa kuwa imani ya kweli ina msingi wake katika ahadi na masharti ya
Maandiko.
Hebu wasiwepo watu wanaojidanganya kwa kuamini kwamba wanaweza kuwa watakatifu wakati
wanavunja mojawapo ya matakwa ya Mungu kwa makusudi. Kuendekeza kutenda dhambi inayojulikana
kunanyamazisha sauti ya Roho anayetushuhudia na kumtenga mtu mbali na Mungu. “Dhambi ni uvunjaji
wa sheria.” Na “kila atendaye dhambi [avunjaye sheria] hakumwona yeye wala hakumtambua.” 1
Yohana 3:6. Ingawa Yohana katika nyaraka zake anazungumza kwa ukamilifu kuhusu upendo, lakini
hasiti kufunua tabia halisi ya kundi linalodai kwamba limetakaswa wakati linaishi katika uasi na kuvunja
sheria ya Mungu. “Yeye asemaye nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo
ndani yake. Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli.”
1 Yohana 2:4,5. Hapa kipo kipimo cha imani ya kila mtu. Hatuwezi kumhesabia utakatifu mtu yeyote
pasipo kumleta kwanza kwenye kipimo pekee cha Mungu cha utakatifu mbinguni na duniani. Ikiwa watu
hawaoni uzito wa sheria iliyo ya maadili, ikiwa wanaziona amri za Mungu kuwa ndogo na kuzifanya
nyepesi, ikiwa wanavunja moja ya (473) amri zilizo ndogo na kuwafundisha watu hivyo, hawatapata
heshima yoyote mbinguni, na tunaweza kujua kwamba madai yao hayana msingi.
Na madai ya kutokuwa na dhambi yo yote ni ushahidi, ndani yake, kwamba mtu anayetoa madai hayo
yuko mbali na utakatifu. Ni kwa sababu yeye hana uelewa sahihi wa usafi na utakatifu wa Mungu au vile
wanavyopaswa kuwa wale watakaokuwa katika kupatana na tabia yake; kwa sababu hana uelewa sahihi
wa usafi na upendo uliotukuka wa Yesu, na kwa sababu ya ubaya na uovu wa dhambi, kiasi kwamba mtu
anajiona mwenyewe kuwa mtakatifu. Kadiri umbali kati yake na Kristo unavyozidi kuongezeka, na kadiri
anavyozidi kuwa na upungufu wa uelewa kuhusu tabia na matakwa ya Mungu, ndivyo anavyozidi kujiona
kuwa mwenye haki machoni pake mwenyewe.
Utakaso ulioelezwa katika Maandiko unahusu mtu mzima - nafsi, roho, na mwili. Paulo aliwaombea
Wathesalonike kwamba “nafsi na roho na miili wahifadhiwe wawe kamili, bila lawama wakati wa kuja
kwake Bwana wetu Yesu Kristo.” 1 Wathesalonike 5:23. Tena anawaandikia waamini: “Basi, ndugu
zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya
kumpendeza Mungu.” Warumi 12:1. Katika nyakati zile za Israeli ya zamani kila dhabihu iliyoletwa kama
kafara kwa Mungu ilichunguzwa kwa makini. Endapo kasoro yoyote iligunduliwa katika mnyama
aliyeletwa, alikataliwa; kwa maana Mungu alikuwa ameagiza kwamba ni lazima dhabihu iwe “haina ila.”
Hivyo ndivyo Wakristo wanavyoagizwa kuitoa miili yao, iwe “dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza
Mungu.” Ili kufanya hivyo, lazima nguvu zao zote za mwili zihifadhiwe katika hali bora iwezekanavyo.
Kila tendo linalodhoofisha nguvu za mwili au za akili humfanya mtu huyo asiweze kufaa kumtumikia
Muumba wake. Je! Mungu atapendezwa na kitu cho chote kilicho pungufu kuliko kile kilicho bora kabisa
tunachoweza kutoa? Kristo alisema: “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote.” Wale
wanaompenda Mungu kwa moyo wao wote, watatamani kumtumikia vizuri sana katika maisha yao yote,
na daima watajitahidi kuileta kila nguvu ya mwili wao ili ipate kupatana na sheria zile zitakazoukuza
275
uwezo wao wa kufanya mapenzi yake. Hawataweza, kwa tamaa mbaya (474) za chakula au za mwili,
kudhoofisha au kuinajisi dhabihu wanayoitoa kwa Baba yao aliye mbinguni.
Petro anasema: “Ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.” 1 Petro 2:11. Kila tendo la kukidhi
tamaa mbaya huelekea kutia ganzi nguvu za akili na utambuzi wa kiakili na kiroho, kisha neno au Roho
wa Mungu anaweza kuugusa moyo kidogo tu. Paulo anawaandikia Wakorintho: “Basi, wapenzi wangu,
kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza
utakatifu katika kumcha Mungu.” 2 Wakorintho 7:1. Tena pamoja na matunda ya Roho - upendo, furaha,
amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole” – anaweka humo “kiasi.” Wagalatia 5:22,23.
Licha ya mashauri haya yaliyovuviwa, ni wangapi wanaojiita Wakristo wanaozidhoofisha nguvu zao za
mwili kwa kujishughulisha kutafuta faida au kuiabudu mitindo; ni wangapi wanaoshusha hadhi ya utu
wao ulio wa mfano wa Mungu kwa ulafi, kwa kunywa mvinyo, kwa kujifurahisha kwa anasa
zilizokatazwa. Na kanisa, badala ya kuyakemea mambo hayo, mara nyingi huhimiza uovu huo kwa
kuamsha tamaa mbaya ya ulafi, tamaa ya kupata faida au kupenda anasa, ili lipate kujaza mali katika
hazina yake, ambayo kwayo upendo kwa Kristo ni hafifu mno kiasi cha kutoweza kuijaza. Ikiwa Yesu
angeweza kuingia ndani ya makanisa ya siku hizi na kuziangalia sherehe za karamu na biashara haramu
zisizo na utakatifu zinazofanywa humo zikiwa na jina la dini, je! asingewafukuzia nje hao wanaonajisi,
kama alivyowafukuza hekaluni wale waliokuwa wanabadili fedha?
Mtume Yakobo anatangaza ya kwamba hekima itokayo juu “kwanza ni safi.” Laiti kama angekutana na
wale wanaolitaja jina la thamani la Yesu katika vinywa vilivyonajisiwa na tumbaku, wale ambao pumzi
yao na miili yao imechafuliwa kwa harufu, na ambao wanachafua hewa ya mbinguni na kuwalazimisha
wote walio karibu nao kuvuta hewa yenye sumu - laiti kama mtume yule angekutana na tabia hiyo
inayopingana kabisa na usafi wa injili, je, asingeishutumu kuwa ni “ya dunia, ya hisia za tamaa, na ya
kishetani”? Watumwa wa tumbaku, wanaodai kwamba wameupata mbaraka wa utakaso kamili,
wanaongelea tumaini lao la mbinguni; lakini neno la Mungu linasema waziwazi kwamba “Na ndani yake
hakitaingia kamwe cho chote kilicho kichafu.” Ufunuo 21:27.
(475) “Au hamjui kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu?
Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika
miili yenu.” 1 Wakorintho 6:19,20. Yule ambaye mwili wake ni hekalu la Roho Mtakatifu hatakuwa
mtumwa wa tabia iletayo madhara mabaya. Nguvu zake ni mali ya Kristo, ambaye amemnunua kwa
thamani ya damu yake. Mali yake ni ya Bwana. Anawezaje kukosa kuwa na hatia kwa kutapanya amana
ya mtaji uliokabidhiwa kwake? Wale wajiitao Wakristo wanatumia fedha nyingi kila mwaka kukidhi
tamaa zao mbaya zisizokuwa na maana na zenye kuleta madhara, wakati roho zinaangamia kwa kukosa
neno la uzima. Mungu anaibiwa zaka na sadaka, wakati wao wanakula katika madhabahu ya uharibifu
zaidi ya vile wanavyotoa kuwasaidia maskini au kutegemeza kazi ya injili. Ikiwa wote wanaojidai kuwa
wafuasi wa Kristo wangekuwa wametakaswa kweli kweli, mali yao, badala ya kutumika katika mambo
yasiyo muhimu na hata yanayoleta madhara, ingeingizwa katika hazina ya Bwana, na Wakristo
wangeweka kielelezo cha kuwa na kiasi, kujikana nafsi, na kujitoa kama kafara. Hapo wangekuwa nuru
ya ulimwengu.
Ulimwengu umejitosa katika kukidhi tamaa. “Tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima”
vinatawala watu wengi. Lakini wafuasi wa Kristo wana mwito mtakatifu zaidi. “Tokeni kati yao,
mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu. Katika nuru ya neno la Mungu, sisi tunayo
haki ya kutangaza kwamba utakaso hauwezi kuwa wa kweli kama hausababishi kuyakataa hali ya
ulimwengu ya kutafuta mambo ya dhambi na kujifurahisha.

276
Kwa wale wanaotekeleza masharti haya: “Tokeni kati yao, mkatengwe nao,… Msiguse kitu kichafu,”
ahadi ya Mungu ni, “Nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa
kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi.” 2 Wakorintho 6:17,18. Ni heshima na wajibu wa kila
Mkristo kuwa na uzoefu tele katika mambo ya Mungu. “Mimi ndimi Nuru ya (476) ulimwengu,” alisema
Yesu. “Yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.” Yohana 8:12. “Bali
njia ya wenye haki ni kama nuru ing’aayo, ikizidi kung’aa hata mchana mkamilifu.” Mithali 4:18. Kila
hatua ya imani na utii inayochukuliwa humleta mtu katika uhusiano wa karibu zaidi na yeye aliye Nuru
ya ulimwengu, ambaye “giza lo lote hamna ndani yake.” Miale ya mwangaza wa Jua la Haki huangaza
juu ya watumishi wa Mungu, nao ni lazima waiakisi mionzi hiyo. Kama vile nyota zinavyotuambia sisi
kwamba kuna nuru kuu mbinguni ambayo kwa utukufu wake zimefanywa kuangaza, vivyo hivyo Wakristo
wanapaswa kudhihirisha kuwa Mungu yuko katika kiti chake cha enzi cha malimwengu ambaye tabia
yake inastahili kusifiwa na kuigwa. Neema ya Roho wake, usafi na utakatifu wa tabia yake, vitaonekana
wazi katika tabia ya mashahidi wake.
Katika Waraka wake kwa Wakolosai, Paulo anafafanua mibaraka mingi iliyotolewa kwa wana wa Mungu.
Anasema hivi: Sisi “hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi
yake katika hekima yote na ufahamu na rohoni; mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana,
mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;
mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila
namna na uvumilivu pamoja na furaha.” Wakolosai 1:9-11.
Anaandika tena kuhusu shauku yake kwamba ndugu zake wale wa Efeso wapate kuufikia ufahamu wa
kimo cha upendeleo alio nao Mkristo. Anafunua mbele yao, kwa lugha inayoeleweka, uwezo wa ajabu na
maarifa wanavyoweza kuwa navyo kama wana na binti zake yeye Aliye juu sana. Ilikuwa ni fursa yao
“kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake, katika utu wa ndani,” na “kuwa na shina na
msingi katika upendo,” ili wapate “kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu,
na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu.” Lakini sala ya mtume huyo inakifikia
kilele cha upendeleo anapoomba kwamba “mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.” Waefeso
3:16-19.
(477) Hapa vinafunuliwa vimo tunavyoweza kufikia kwa njia ya imani katika ahadi za Baba yetu aliye
mbinguni, tunapotimiza masharti yake. Kwa njia ya sifa zake Kristo, sisi tunayo njia ya kukifikia kiti cha
enzi cha Mungu Mwenyezi. “Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu
sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?” Warumi 8:32. Baba alimtoa Roho wake
bila kipimo kwa Mwanawe, na sisi pia tunaweza kushiriki utimilifu wake. Yesu asema hivi, “Ikiwa ninyi
mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa
Roho Mtakatifu hao wamwombao?” Luka 11:13. “Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.”
“Ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.” Yohana 14:14; 16:24.
Wakati maisha ya Mkristo yanatakiwa kuwa na tabia ya unyenyekevu, hayapaswi kujzwa na huzuni na
kujidhalilisha. Ni fursa ya kila mmoja kuishi kwa namna ambayo Mungu atapendezwa naye na kumbariki.
Si mapenzi ya Baba yetu aliye mbinguni kwamba tuwe chini ya laana na giza daima. Hakuna ushahidi wo
wote wa kuwapo kwa unyenyekevu wa kweli pale mtu anapotembea akiwa ameinamisha kichwa chini na
moyo wake ukiwa umejazwa na mawazo ya kujifikiria yeye mwenyewe. Twaweza kwenda kwa Yesu na
kutakaswa, na kuweza kusimama mbele ya sheria yake bila kutahayari, wala bila kuwa na majuto.
“Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu, nenda kwa kufuata mambo ya
mwili, bali mambo ya Roho. Warumi 8:1.

277
Kupitia Yesu wana wa Adamu walioanguka wanakuwa “wana wa Mungu.” “Maana yeye atakasaye na hao
wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake.” Waebrania
2:11. Maisha ya Mkristo yanapaswa kuwa maisha ya imani, ya ushindi, na yenye furaha katika Mungu.
“Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda
kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.” 1 Yohana 5:4. Mtumishi wa Mungu Nehemia alisema kweli:
“Furaha ya BWANA ni nguvu zenu.” Nehemia 8:10. Na Paulo anasema: “Furahini katika Bwana sikuzote;
ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo (478) ni mapenzi ya Mungu kwenu katika
Kristo Yesu.” Wafilipi 4:4; 1 Wathesalonike 5:16-18.
Hayo ndiyo matunda ya uongofu na utakaso wa Biblia; tena ni kwa sababu kanuni kuu za haki
zilizofafanuliwa katika sheria ya Mungu zinazingatiwa kidogo sana na ulimwengu wa Kikristo kiasi
kwamba matunda haya yanaonekana kwa nadra. Hii ndiyo sababu inaonekana kidogo mno kazi ile yenye
kina, inayoendelea daima ya Roho wa Mungu ambayo ilikuwa katika uamsho katika miaka ya zamani.
Ni kwa kutazama ndipo tunabadilika. Na kadiri zile amri takatifu ambamo Mungu amewafunulia
wanadamu ukamilifu na utakatifu wa tabia yake zinavyopuuzwa, na mawazo ya watu yanavyovutwa
kuyaendea mafundisho ya wanadamu pamoja na nadharia zao potofu, ni ajabu ilioje kwamba kushuka
kwa maisha ya utauwa kumejitokeza ndani ya kanisa. Bwana anasema: “Wameniacha mimi, niliye
chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia mabirika, mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji.”
Yeremia 2:13.
“Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki;… Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, na
sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya vijito vya
maji, uzaao matunda yake kwa majira yake, wala jani lake halinyauki; na kila alitendalo litafanikiwa.”
Zaburi 1:1-3. Ni pale tu sheria ya Mungu inaporejeshwa katika hadhi yake halali ndipo panaweza kuwepo
uamsho wa imani ya kale na utauwa miongoni mwa watu wake. “BWANA asema hivi, Simameni katika
njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia
hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu.” Yeremia 6:16.

278
Sura ya 28
MBELE YA KUMBUKUMBU ZA MAISHA

“Nikatazama,” anasema nabii Danieli, “hata viti vya enzi vikawekwa, na Mmoja aliye Mzee wa Siku
ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti
chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. Mto kama wa moto ukatoka
ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake;
hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.” Danieli 7:9,10
Hivyo ndivyo ilivyoonyeshwa katika maono ya nabii ile siku kuu na ya kutisha wakati tabia na maisha ya
wanadamu yatakapopita katika uchunguzi mbele ya Hakimu wa ulimwengu wote, na kila mtu
atakapolipwa “kama kazi yake ilivyo.” Mzee wa Siku ni Mungu Baba. Mwimba zaburi anasema: “Kabla
haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.” Zaburi 90:2. Ni
yeye, chanzo cha uhai wote, na chemchemi ya sheria yote, ambaye ndiye atakuwa mwenyekiti katika
hukumu. Na malaika watakatifu kama wahudumu na mashahidi, hesabu yao “elfu kumi mara elfu kumi,
na maelfu elfu,” wanahudhuria katika Mahakama hii kuu.
“Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, Mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na
mawingu ya mbingu akamkaribia huyo Mzee wa Siku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa (480)
mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie;
mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo haitapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza
kuangamizwa.” Danieli 7:13,14. Kuja kwa Kristo kulikoelezwa hapo sio kule kuja kwake mara ya pili
katika dunia hii. Anakuja kwa Mzee wa Siku mbinguni kupokea mamlaka yake, na utukufu, na ufalme,
ambao atapewa atakapomaliza kazi yake kama mpatanishi wetu. Ni kuja huku, wala sio kuja kwake
mara ya pili, ambako kulitabiriwa katika unabii kwamba kutatokea zitakapokoma siku zile 2300 katika
mwaka wa 1844. Akiwa ameandamana na malaika wa mbinguni, Kuhani Mkuu wetu anaingia katika
patakatifu pa patakatifu na pale anaonekana mbele za Mungu na kuingia katika kazi zake za mwisho za
huduma yake kwa ajili ya mwanadamu - kufanya kazi ya kukumu ya upelelezi na kufanya upatanisho
kwa wote wanaoonekana kuwa na haki ya kunufaika nao.
Katika huduma ya mfano ya kivuli watu waliokuwa na sehemu katika huduma ya Siku ya Upatanisho ni
wale tu waliokuwa wamekuja mbele za Mungu kwa maungamo na toba, na ambao dhambi zao zilikuwa
zimehamishiwa patakatifu kwa njia ya damu ya sadaka ya dhambi. Vivyo hivyo katika siku kuu ya
upatanisho wa mwisho na hukumu ya upelelezi kesi zitakazofikiriwa ni za watu wale wanaoitwa watu wa
Mungu. Hukumu ya waovu ni kazi iliyotenganishwa na hiyo na iliyo mbali, nayo inafanyika katika kipindi
cha baadaye. “Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza
kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje?” 1 Petro 4:17.
Vitabu vya kumbukumbu vilivyoko mbinguni, ambamo majina na matendo ya wanadamu yameandikwa,
vitaamua kuhusu maamuzi ya hukumu. Nabii Danieli anasema: “Hukumu ikawekwa, na vitabu
vikafunuliwa.” Mwandishi wa Ufunuo, akielezea habari za tukio hilo, anaongeza: “Na kitabu kingine
kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu, wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa
katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.” Ufunuo 20:12.

279
Kitabu cha uzima kina majina ya wote waliopata kuingia katika kazi ya Mungu. Yesu aliwaagiza
wanafunzi wake: “Furahini (481) kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.” Luka 10:20. Paulo
anazungumza kuhusu watenda kazi wenzake waaminifu, “ambao majina yao yamo katika kitabu cha
uzima.” Wafilipi 4:3. Danieli, akiangalia mbali hadi “wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo,”
anatangaza kwamba watu wa Mungu wataokolewa, “kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika
kitabu kile. Na mwandishi wa Ufunuo anasema kwamba watakaoingia katika mji wa Mungu ni wale tu
ambao majina yao “yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.” Danieli 12:1; Ufunuo
21:27.
“Kitabu cha Ukumbusho” kimeandikwa mbele za Mungu, ambamo ndani yake yameandikwa matendo
mema ya “hao waliomcha BWANA, na kulitafakari jina lake.” Malaki 3:16. Maneno yao ya imani,
matendo yao ya upendo, yameandikwa mbinguni. Nehemia anarejea katika habari hiyo anaposema:
“Unikumbukie hayo, Ee Mungu wangu, wala usifute fadhili zangu nilizozitenda kwa ajili ya nyumba ya
Mungu wangu.” Nehemia13:14. Katika kitabu cha Mungu cha ukumbusho kila tendo la haki lililofanywa
linadumishwa. Kila jaribu lililopingwa, kila ovu lililolishindwa, kila neno la huruma lililonenwa,
limeandikwa mle kwa uaminifu. Na kila tendo la kujitoa kafara, kila taabu na huzuni iliyostahimiliwa
kwa ajili ya Kristo, yameandikwa mle. Mwimba zaburi anasema: “Umehesabu kutanga-tanga kwangu;
uyatie machozi yangu katika chupa yako; Je! hayamo katika kitabu chako?” Zaburi 56:8.
Pia kuna maandishi ya kumbukumbu za dhambi za wanadamu. “Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila
kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.” “Kila neno lisilo maana, watakalolinena
wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.” Mwokozi alisema: “Kwa maneno yako
utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.” Mhubiri 12:14; Mathayo 12:36,37. Makusudi na
misukumo ya siri yako katika maandishi pasipo kukosea; kwa maana Mungu “atayamulikisha
yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo.” 1 Wakorintho 4:5. “Tazama, neno hili
limeandikwa mbele zangu…. Maovu yenu na maovu ya baba zenu pamoja, asema BWANA.” Isaya 65:6,7.
(482) Kazi ya kila mtu inachunguzwa mbele za Mungu na inaandikwa kama ya uaminifu au ya kutokuwa
ya uaminifu. Mkabala na kila jina katika vitabu vya mbinguni huandikwa kwa usahihi wa kutisha kila
neno baya, kila tendo la ubinafsi, kila jukumu ambalo halikufanywa, na kila dhambi ya siri, pamoja na
kila udanganyifu wa unafiki uliofanywa kwa werevu. Maonyo na makaripio yaliyotumwa kutoka mbinguni
yakapuuzwa, muda uliopotezwa, fursa ambazo hazikutumiwa vema, mvuto uliotolewa kwa wema au
kwa ubaya, pamoja na matokeo yake yaendeleayo hadi mbali, yote yameandikwa na malaika
anayeandika.
Sheria ya Mungu ndiyo kiwango ambacho kwacho tabia na maisha ya wanadamu yatapimwa katika
hukumu. Mtu mwenye hekima anasema: “Mche Mungu, nawe uzishike amri zake. Maana kwa jumla ndiyo
impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema
au likiwa baya.” Mhubiri 12:13,14. Mtume Yakobo anawaasa ndugu zake: “Semeni ninyi, na kutenda
kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru. Yakobo 2:12.
Katika hukumu hii, wale ambao wanahesabiwa kuwa wamestahili” watakuwa na sehemu yao katika
ufufuo wa wenye haki. Yesu alisema: “Wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na
kufufuka katika wafu … huwa sawasawa na malaika; nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa
ufufuo.” Luka 20:35,36. Na tena alisema kwamba “wale waliofanya mema” watatoka “kwa ufufuo wa
uzima.” Yohana 5:29. Wenye haki waliokufa hawatafufuliwa mpaka baada ya kukumu hii ambapo ndipo
watahesabiwa kuwa wamestahili kuupata huo “ufufuo wa uzima.” Hivyo hawatakuwepo kimwili katika
mahakama wakati kumbukumbu zao zinapochunguzwa na kesi zao kukatwa.

280
Yesu atajitokeza pale kama wakili wao, ili kuwaomba kwa niaba yao mbele za Mungu. “Na kama mtu
akitenda dhambi tunaye mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki.” 1 Yohana 2:1. “Kwa sababu
Kristo hakuingia patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia
mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu.” “Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa
kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.” Waebrania 9:24; 7:25.
(483) Vitabu vya kumbukumbu vinapofunuliwa katika hukumu, maisha ya wote waliomwamini Yesu
yanachunguzwa mbele za Mungu. Kuanzia kwa wale waliotangulia kwanza kuishi duniani, Mtetezi wetu
anawasilisha kesi za kila kizazi kilichofuata, na anamalizia kwa walio hai. Kila jina hutajwa, kila kesi
huchunguzwa kwa makini sana. Majina yanakubaliwa, majina yanakataliwa. Ikiwa wapo wale ambao
bado wana dhambi katika vitabu vya kumbukumbu, dhambi ambazo hazijatubiwa wala kusamehewa,
majina yao yataondolewa katika kitabu cha uzima, na kumbukumbu ya matendo yao mema itafutwa
katika kitabu cha Mungu cha ukumbusho. Mungu alitangaza kwa Musa: “Mtu ye yote aliyenitenda dhambi
ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu.” Kutoka 32:33. Naye nabii Ezekieli anasema: “Bali mwenye
haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu … Katika matendo yake yote ya haki
aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo.” Ezekieli 18:24.
Wale wote waliotubu dhambi zao kweli kweli, na kwa imani walidai damu ya Kristo iwe kafara yao ya
upatanisho, wana msamaha ambao umeandikwa mbele ya majina yao katika vitabu vya mbinguni; kwa
kuwa wamekuwa washirika wa haki ya Kristo, na tabia zao zimeonekana kuwa zinapatana kabisa na
sheria ya Mungu, dhambi zao zitafutwa, na wenyewe watahesabiwa kuwa wanastahili kuupata uzima wa
milele. Bwana anasema kupitia kwa nabii Isaya,: “Mimi, naam, Mimi ndimi niyafutaye makosa yako kwa
ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.” Isaya 43:25. Yesu alisema: “Yeye ashindaye
atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri
jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake.” “Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya
watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya
watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.” Ufunuo 3:5; Mathayo 10:32,33.
Hamu ya kina inayoonekana miongoni mwa wanadamu kuhusu maamuzi ya mahakama za kidunia
huwakilisha kwa uhafifu tu hamu (484) inayoonekana katika mahakama za mbinguni wakati majina
yaliyoingizwa katika kitabu cha uzima yanapoletwa kupitiwa mbele ya Hakimu wa ulimwengu wote.
Mwombezi wetu wa mbinguni anaomba kwamba wale wote walioshinda kwa imani katika damu yake
wasamehewe dhambi zao, kwamba wapate kurejeshwa nyumbani kwao Edeni, na kuvikwa taji kama
warithi pamoja naye wa ile “mamlaka ya kwanza.” Mika 4:8. Shetani katika juhudi yake yote ya
kuidanganya na kuijaribu jamii yetu alikuwa amefikiria kuuvuruga mpango wa Mungu wa kumwumba
mwanadamu; lakini sasa Kristo anaomba kwamba mpango huu utekelezwe sasa kana kwamba
mwanadamu hakupata kuanguka kamwe. Anawaombea watu wake si tu msamaha na kuhesabiwa haki,
timilifu na kamili, bali pia kwamba wapate kushiriki katika utukufu wake na kuketi katika kiti chake cha
enzi.
Wakati Yesu akiwaombea wanufaika wa neema yake, Shetani anawashtaki mbele za Mungu kama waasi.
Mwongo mkuu huyu ametafuta kuwaingiza katika mashaka, kuwafanya wapoteze ujasiri kwa Mungu,
kuwafanya wajitenge mbali na upendo wa Mungu, na kuivunja sheria yake. Sasa anawaelekeza katika
kumbukumbu ya maisha yao, kuwaonyesha kasoro walizo nazo katika tabia zao, kutofanana kwao na
Kristo, jambo ambalo limemfedhehesha Mkombozi wao, akiwaonyesha dhambi zote alizowaongoza
kutenda, na kwa sababu ya haya anadai kwamba wao wako chini ya himaya yake.

281
Yesu haonyeshi udhuru kwa dhambi zao, bali anaonyesha toba na imani yao, na, akiomba msamaha kwa
ajili yao, anainua mikono yake iliyojeruhiwa mbele za Baba yake na mbele ya malaika zake watakatifu,
akisema: “Nawajua kwa jina. Nimewachora katika vitanga vya mikono yangu. “Dhabihu za Mungu ni
roho iliyovunjika; ni moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.” Zaburi 51:17. Na kwa
yule mshtaki wa watu wake anasema: “BWANA na akukemee, Ewe Shetani; naam, BWANA, aliyechagua
Yerusalemu, na akukemee; je! hiki si kinga kilichotolewa motoni?” Zekaria 3:2. Kristo atawavika
waaminifu wake haki yake mwenyewe, ili apate kuwaleta mbele za Baba yake wakiwa “Kanisa tukufu,
lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo.” Waefeso 5:27. Majina yao yanabaki yakiwa
yameandikwa katika kile kitabu cha uzima, na kwa habari yao imeandikwa: “Nao watakwenda pamoja
nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.” Ufunuo 3:4.
(485) Hapo ndipo utakavyofikiwa utimilifu kamili wa ahadi ya agano jipya: “Maana nitausamehe uovu
wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.” “Katika siku hizo na wakati huo, asema BWANA, uovu wa
Israeli utatafutwa, wala uovu hapana; na dhambi za Yuda zitatafutwa, wala hazitaonekana.” Isaya
31:34; 50:20. “Siku hiyo chipukizi la BWANA litakuwa zuri, lenye utukufu na matunda ya nchi yatakuwa
mema sana, na kupendeza, kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka. Tena itakuwa ya kwamba yeye
aliyebaki katika Sayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa mtakatifu; yaani, kila mmoja
aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusalemu.” Isaya 4:2,3.
Kazi ya hukumu ya upelelezi na ufutaji wa dhambi itakoma kabla ya Bwana wetu kuja mara ya pili. Kwa
kuwa wafu wanapaswa kuhukumiwa kutokana na mambo yale yaliyoandikwa katika vitabu vile,
haiwezekani kwamba dhambi za wanadamu zitakuwa zinafutwa hadi baada ya hukumu hiyo ambapo kesi
zao zinachunguzwa. Lakini Mtume Petro anaeleza waziwazi kwamba dhambi za waamini zitafutwa
wakati ule zitakapokuja “nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; apate kumtuma Kristo.”
Matendo 3:19,20. Hukumu ya Upelelezi itakapofungwa, Kristo atakuja, na ujira wake utakuwa pamoja
naye kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
Katika huduma ya mfano-kivuli ya patakatifu pa duniani, kuhani mkuu, baada ya kufanya upatanisho
kwa ajili ya Israeli, alitoka nje na kuwabariki makutano. Kristo naye, mwisho wa kazi yake kama
mpatanishi, atatokea, ‘pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu,’ (Waebrania 9:28),
kuwabariki watu wake wanaomngojea kwa kuwapa uzima wa milele. Kama vile kuhani, katika kuiondoa
dhambi kutoka katika patakatifu, alivyoziungama dhambi juu ya kichwa cha mbuzi wa Azazeli, ndivyo
Kristo naye atakavyoweka dhambi zote juu ya Shetani, mwasisi na mwendelezaji wa dhambi. Yule
mbuzi wa Azazeli, akiwa amebeba dhambi za Israeli, alipelekwa mbali katika nchi “isiyo na watu”
(Mambo ya Walawi 16:22); hivyo ndivyo Shetani naye, akiwa amebeba hatia ya dhambi zote
alizosababisha watu wa Mungu kuzitenda, atakavyofungwa kwa miaka elfu moja katika dunia hii,
ambayo kwa wakati huo itakuwa tupu, haina watu, na hatimaye atapata (486) adhabu kamili ya dhambi
zake katika moto ule utakaowaangamiza waovu wote. Hivyo ndivyo mpango mkuu wa ukombozi
utakavyofikia utimilifu wake wakati wa kuiangamiza dhambi mara ya mwisho na kuwakomboa wale wote
waliopenda kuachana na uovu.
Wakati wa muda uliokubalika kwa ajili ya hukumu - mwisho wa siku 2300, mwaka 1844 - kazi ya
upelelezi na ufutaji wa dhambi ilianza. Lazima wote ambao wamekuwa wakilichukua jina la Kristo
wapitishwe katika uchunguzi. Makundi yote mawili, walio hai na wafu, hawana budi kuhukumiwa
“katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vitabu, sawasawa na matendo yao.”
Dhambi ambazo hazijatubiwa na kuachwa hazitasamehewa wala kufutwa katika vitabu vya
kumbukumbu, bali zitasimama kama ushahidi dhidi ya mwenye dhambi katika siku ile ya Mungu. Mtu

282
aweza kuwa ametenda matendo yake mabaya katika nuru ya mchana au katika giza la usiku; lakini
zilikuwa wazi na dhahiri mbele zake yeye ambaye tunapaswa kutenda pamoja naye. Malaika wa Mungu
walishudia kila dhambi iliyotendwa na waliisajili katika kumbukumbu zisizo na makosa. Dhambi inaweza
kufichwa, kukanwa, kufunikwa ili isionekane kwa baba, mama, mke, watoto, na marafiki; hakuna mtu
wa kuweza kuibaini hata kidogo jambo hilo baya, isipokuwa waliotenda hatia hiyo; lakini iko wazi mbele
ya hekima za mbinguni. Giza la usiku wenye giza nene kuliko zote, usiri wa mbinu zote za udanganyifu,
havitoshi kuficha hata wazo moja lisijulikane kwake aliye wa Milele. Mungu anayo kumbukumbu halisi ya
kila taarifa ya kila taarifa iliyotolewa pasipo haki na kila tendo la lenye kupendelea isivyo sahihi. Yeye
hadanganywi na mwonekano wa nje wa unafiki. Hafanyi kosa lo lote katika kukadiria tabia ya mtu.
Wanadamu wanaweza kudanganywa na wale walio wafisadi moyoni, lakini Mungu anapenya ndani ya
mwonekano wote wa nje na kusoma maisha ya ndani.
Ni wazo zito kiasi gani! Siku baada ya siku, kila siku moja ikipita na kuondoka milele, ina mzigo wa
kumbukumbu zake katika vitabu vya mbinguni. Maneno yaliyopata kutamkwa, matendo yaliyopata
kutendwa, hayawezi kutanguka kamwe. Malaika wameyaandika yote mema na mabaya. Hodari aliye
bingwa wa vita kuliko wote duniani hawezi kuondosha kumbukumbu za siku hata moja. Matendo yetu,
maneno yetu, hata misukumo yetu ya siri sana, yote yana uzito wake katika kuamua hatima yetu kwa
ajili ya umilele au ole. Ingawa yanaweza kuwa yamesahaulika (487) kwetu, yatatoa ushahidi wake
kuleta haki au kuhukumu.
Kama vile sifa za mwonekano wa sura zinavyoonyeshwa na msanii kwenye bamba lililonakishiwa pasipo
kukosea, ndivyo tabia ilivyoonyeshwa kwa uaminifu katika vitabu vilivyoko huko juu. Lakini ni kwa
kiwango kidogo jinsi gani watu wanajali na kuguswa na kumbukumbu ambayo inakwenda kukutana na
macho ya viumbe wa mbinguni! Laiti pazia linalotenganisha ulimwengu unaoonekana na ule usioonekana
lingekunjwa, na wana wa wanadamu wakamwona malaika anayeandika kila neno na kila tendo, ambalo
lazima wakutane nalo tena katika hukumu ile, ni maneno mangapi kati ya yale yanayosemwa kila siku
ambayo yangebakizwa bila kusemwa, ni matendo mangapi ambayo yangeachwa bila kutendwa.
Katika hukumu matumizi ya kila talanta yaliyofanywa yatachunguzwa. Tumeutumiaje mtaji tulioazimwa
na Mbingu? Je, Bwana atakapokuja atajipatia iliyo yake pamoja na faida? Je, tumekuza uwezo
uliokabidhiwa kwetu, katika mkono na moyo na akili, kwa utukufu wa Mungu na kwa kubariki
ulimwengu? Tumetumiaje wakati wetu, kalamu yetu, sauti zetu, fedha zetu, mvuto wetu? Tumefanya
nini kwa ajili ya Kristo, akiwa katika umbo la maskini, wanaoteseka, yatima, au mjane? Mungu
ametufanya kuwa hazina ya neno lake takatifu; tumefanya nini na nuru na ukweli tuliopewa ili
kuwahekimisha watu wafikie wokovu? Hakuna thamani anayohesabiwa mtu kwa kukiri tu kuwa na imani
katika Kristo; kinachohesabika kuwa muhimu ni upendo tu unaoonekana kwa matendo. Bado ni upendo
peke yake ambao hulifanya tendo lolote kuwa la thamani machoni pa Mbingu. Chochote kinachofanywa
kutokana na upendo, hata kionekane kidogo kiasi gani katika makadirio ya wanadamu, kinakubaliwa na
kutolewa thawabu na Mungu.
Ubinafsi wa wanadamu uliofichika uko wazi katika vitabu vya mbinguni. Kuna kumbukumbu ya wajibu
wa watu kwa wanadamu wenzao ambao haukutimizwawa kwa wanadamu wenzao, na kumbukumbu ya
usahaulifu wa matakwa ya Mwokozi. Mle wataona kwamba ni mara ngapi walimpatia Shetani wakati,
mawazo, na nguvu zilizokuwa mali ya Kristo.
Kumbukumbu ambazo malaika wanapeleka mbinguni ni za huzuni. Viumbe wenye akili, wanaojiita
wafuasi wa Kristo, wamezama katika kuchuma mali ya ulimwengu huu au kujifurahisha katika anasa za
ulimwengu. Fedha, muda, na nguvu hutumiwa kwa maonyesho na (488) kujifurahisha binafsi; lakini ni

283
mida michache iliyotolewa kwa maombi, kwa kuyachunguza Maandiko, katika kujinyenyekeza nafsi na
kuungama dhambi.
Shetani anavumbua mipango isiyohesabika ili kujaza shughuli katika mawazo yetu, kusudi yasipate
nafasi ya kujikita katika kazi ambayo tungepaswa kuifahamu zaidi. Mlaghai mkuu huyu anazichukia
kweli kuu zinazowafanya watu waione kafara ya upatanisho na mpatanishi mwenye uweza wote. Anajua
kwamba kwa upande wake kila kitu kinategemea kazi yake ya kuyageuza mawazo ya watu yaelekee
mbali na Yesu na kweli yake.
Hebu wale wanaotaka kushiriki manufaa ya kazi ya Mwokozi ya upatanishi wasiruhusu kitu chochote
kuingilia jukumu lao la kuwa na utakatifu mkamilifu katika kumcha Mungu. Badala ya kutumia saa zao
za thamani kwa mambo ya anasa, kwa mambo ya mapnyesho, au kutafuta faida, yangetumika katika
kujifunza neno la kweli kwa bidii na maombi. Somo la patakatifu na hukumu ya upelelezi linapaswa
lieleweke wazi kwa watu wa Mungu. Wote wanahitaji kujua wao wenyewe kuhusu mahali alipo na kazi
anayofanya Kuhani Mkuu wao. La sivyo itakuwa haiwezekani kwao kuifanyia kazi imani yao ambayo ni ya
muhimu sana kwa wakati huu au haitawezekana kuwa katika nafasi ambayo Mungu amekusudia waijaze.
Kila mtu anayo nafsi ya kuokoa au ya kupoteza. Kila mmoja anayo kesi inayomngoja katika kizimba cha
Mungu. Lazima kila mmoja akutane ana kwa ana na Jaji mkuu. Kwa hiyo ni jambo muhimu kiasi gani
kwamba kila mtu aitafakari mara kwa mara mandhari hiyo ya kutisha wakati hukumu itakapowekwa na
vitabu vitakapofunuliwa, wakati ambapo, kwa kuongeza maneno ya Danieli, kila mtu atasimama katika
kura yake peke yake, mnamo mwisho wa siku zile.
Wote ambao wamepata nuru kuhusu masomo haya wanatakiwa kuwapa watu wengine ushuhuda wa
kweli kuu ambazo Mungu amewakabidhi. Patakatifu pa mbinguni ni kitovu chenyewe cha kazi ya Kristo
kwa ajili ya wanadamu. Pale panamhusu kila mtu anayeishi duniani. Panatufunulia tupate kuuona
mpango wa ukombozi, pakituleta hadi mwisho wa wakati na kutufunulia suala la ushindi wa pambano
kati ya haki na dhambi. Ni jambo la muhimu kupita kiasi kwamba wote wanapaswa kuyachunguza
masomo haya vema na kuwa na uwezo wa kutoa jibu kwa (489) kila mmoja anayewauliza sababu ya
tumaini lililo ndani yao.
Maombezi ya Kristo kwa ajili ya mwanadamu katika patakatifu kule juu ni ya muhimu katika mpango wa
wokovu kama kilivyokuwa kifo chake msalabani. Kwa kifo chake aliianza kazi ile ambayo baada ya
kufufuka kwake alipaa mbinguni kwenda kuikamilisha. Lazima tuingie kwa imani ndani ya pazia,
“alimoingia Yesu kwa ajili yetu mtangulizi wetu.” Waebrania 6:20. Nuru itokayo kwenye msalaba wa
Kalvari inaakisiwa pale. Tunaweza kupata pale uelewa wa wazi zaidi kuhusu siri za ukombozi. Wokovu
wa mwanadamu unatekelezwa kwa gharama kubwa mno kutoka mbinguni; kafara iliyotolewa ni
sawasawa na ukubwa wa madai ya sheria ya Mungu iliyovunjwa. Yesu ameifungua njia ya kwenda
kwenye kiti cha enzi cha Baba, na kwa njia ya maombezi yake shauku ya kweli ya wale wanaokuja
kwake kwa imani inaweza kufikishwa mbele za Mungu.

“Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema” Mithali
28:13. Ikiwa wale wanaoficha makosa yao na kuyatolea udhuru wangeona jinsi Shetani
anavyowashangilia, jinsi anavyomdhihaki Kristo na malaika zake watakatifu na kazi yao, wangefanya
haraka kuungama dhambi zao na kuziacha. Kupitia katika kasoro za tabia, Shetani anafanya kazi ya
kutawala akili yote, na anajua kwamba kasoro hizo zikiendelezwa, atafanikiwa. Kwa hiyo anatafuta
daima kuwadanganya wafuasi wa Kristo, akitumia hila zake za kufisha kiasi kwamba haiwezekani kwao
kuzishinda. Lakini Yesu anaomba mahali pao kwa mikono yake iliyojeruhiwa, mwili wake uliochubuliwa;
na anawatangazia wote ambao wangetaka kumfuata kwamba, “Neema yangu yakutosha.” 2 Wakorintho

284
12:9. “Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpoke na mnyenyekevu wa moyo; nanyi
mtapata raha nafsini mwenu. Kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.” Mathayo
11:29,30. Asiwepo mtu hata mmoja anayedhani kwamba kasoro zake haziponyeki. Mungu ataleta imani
na neema ya kuzishinda.
Sasa tunaishi katika siku kuu ya upatanisho. Katika huduma ya mfano kivuli, wakati ambapo kuhani
mkuu alikuwa akifanya (490) upatanisho kwa ajili ya Israeli, wote walitakiwa kutesa nafsi zao kwa
kutubu dhambi na kujinyenyekeza mbele za Bwana, la sivyo wangekatiliwa mbali na watu. Kwa namna
hiyo hiyo, wale wote wanaotaka majina yao yabaki katika kitabu cha uzima wanatakiwa sasa watese
nafsi zao mbele za Mungu, katika siku chache zilizobaki za muda wa kupimwa kwao, kwa huzuni ya
dhambi na toba ya kweli. Lazima kuwe na kazi ya kujichunguza moyo kwa kina na kwa uaminifu. Roho
ya kupuuza na kudharau inayoonyeshwa na wengi wanaoitwa Wakristo lazima iwekwe mbali. Ipo vita
kali mbele ya watu wote wanaotaka kuzishinda tabia za uovu zinazotafuta kuwatawala. Kazi ya
kujiweka tayari ni ya mtu mwenyewe. Hatuokolewi katika makundi. Usafi wa maisha na kujitoa kwa mtu
mmoja havitafidia kupungua kwa sifa hizo kwa mtu mwingine. Ingawa mataifa yote yatapita mbele za
Mungu kwa ajili ya hukumu, bado Yeye ataichunguza kesi ya kila mtu kwa makini sana kana kwamba
hakuna kiumbe mwingine ye yote duniani. Lazima kila mmoja apimwe na kuonekana kuwa hana waa,
wala kunyanzi, wala kitu cho chote kama hicho.
Mandhari ya matukio yanayohusiana na kufungwa kwa kazi ya upatanisho ni nzito. Mambo yaliyomo ni ya
maana sana. Hukumu inaendelea sasa katika patakatifu huko juu. Kwa miaka mingi kazi hiyo imekuwa
ikiendelea. Hivi punde - hakuna ajuaye ni punde kiasi gani - itafikia kesi za wale walio hai. Katika hali
ya utisho wa kuwepo kwa Mungu maisha yetu yanaletwa katika uchunguzi. Katika wakati huu ni vema
zaidi kuliko mambo mengine yote kwa kila mtu kuzingatia onyo la Mwokozi: “Angalieni, kesheni, kwa
kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo.” Marko 13:33. “Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi,
wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.” Ufunuo 3:3.
Wakati kazi ya hukumu ya upelelezi itakapofungwa, hatima ya watu wote itakuwa imeamuliwa kwa
uzima au mauti. Muda wa kupimwa unakoma muda mfupi kabla ya kutokea kwa Bwana katika mawingu
ya mbinguni. Kristo akiangalia mbele katika wakati ujao, anasema katika kitabu cha Ufunuo: “Mwenye
kudhulumu na azidi kudhulumu; mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi
kufanya haki; na (491) mtakatifu na azidi kutakaswa. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja
nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.” Ufunuo 22:11,12.
Wenye haki na waovu watakuwa bado wanaishi duniani katika hali yao ya kufa - watu watakuwa
wakipanda na kujenga, wakila na kunywa, wote wasijue kwamba hukumu ya mwisho isiyobadilika
imetajwa katika patakatifu kule juu. Kabla ya Gharika, baada ya Nuhu kuingia katika safina, Mungu
alimfungia ndani na kuwafungia waovu nje; lakini kwa siku saba watu, bila kujua ya kwamba
maangamizi yao yalikuwa yamepangwa, waliendelea na maisha yao ya kutojali, ya anasa na walidhihaki
maonyo ya hukumu iliyokuwa ikiwajia. Mwokozi anasema: “Ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana
wa Adamu.” Mathayo 24:39. Kimya-kimya, paipo kujulikana kama mwivi wa usiku wa manane, saa
inayoamua hatima ya kila mtu itakuja, kuondolewa kwa mara ya mwisho kwa msaada wa rehema kwa
wanadamu wenye dhambi.
“Kesheni basi … asije akawasili ghafla akawakuta mmelala.” Marko 13:35,36. Hali ya hatari iko kwa
wale ambao, kwa kuchoka kukesha, wanavigeukia vishawishi vya ulimwengu huu. Wakati ambapo mtu
wa biashara amezama katika kutafuta faida, mtu apendaye anasa anaendelea kutafuta kujifurahisha,
binti apendaye mitindo ya kisasa anaendelea kupanga mapambo yake – inaweza kuwa hiyo ndiyo saa

285
ambapo Hakimu wa dunia yote atatamka hukumu: “Umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa
umepunguka.” Danieli 5:27.

286
Sura ya 29
ASILI YA UOVU

Asili ya uovu na sababu ya kuwepo kwake ni chanzo cha utata mkubwa katika akili ya watu wengi.
Wanaona kazi ya uovu, pamoja na matokeo yake ya kutisha na ya maangamizi, na wanauliza kwamba
haya yote yanawezaje kuwepo chini ya utawala wa Yeye asiye na kikomo katika hekima, uweza, na
upendo. Hapa kuna fumbo ambalo haliwapatii maelezo. Na katika hali yao ya mashaka na kutokuwa na
uhakika wanapigwa upofu wasiweze kuziona kweli zilizofunuliwa waziwazi katika neno la Mungu na
zilizo muhimu kwa wokovu wetu. Wapo wale ambao, katika kutafuta-tafuta sababu ya kuwepo kwa
dhambi; wanajitahidi kutafiti katika kile ambacho Mungu hakufunua kamwe; hivyo hawapati ufumbuzi
wa matatizo yao; na kadiri watu kama hao wanavyosukumwa na mwelekeo wa mashaka na ubishi
wanashikilia jambo hilo kama sababu ya kuyakataa maneno yatokayo katika Maandiko Matakatifu. Lakini
wengine wanashindwa kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu tatizo kubwa la uovu kutokana na uhalisia
kwamba mapokeo na tafsiri zisizo sahihi vimekinga na kufunika mafundisho ya Biblia kuhusu tabia ya
Mungu, jinsi serikali yake ilivyo, na kanuni anazotumia katika kushughulikia dhambi.
Ni jambo lisilowezekana kueleza asili ya dhambi kwa kiasi cha kutoa sababu ya kuwapo kwake. Lakini
habari za kutosha zinaweza kufahamika kuhusu mambo hayo mawili yaani asili ya dhambi na suluhisho
lake la mwisho ili kudhihirisha kwa ukamilifu haki na fadhili za Mungu katika ushughulikiaji wake wote
wa uovu. Hakuna jambo linalofundishwa katika (493) Maandiko kwa wazi zaidi kuliko kwamba Mungu
hakuhusika kwa vyo vyote na kuingia kwa dhambi; kwamba hakukuwa na uamuzi wa kuondoa neema
yake, hakukuwa na kasoro katika serikali ya mbinguni, ambavyo vilitoa nafasi ya kuibuka kwa uasi.
Dhambi ni kitu kigeni kilichojiingiza, sababu ya uwepo wake haiwezi kutolewa kwa kuhusishwa na
uwepo wa yeyote. Ni fumbo, haina maelezo; kuitolea udhuru ni kuitetea. Laiti udhuru wa kuwepo
kwake ungepatikana, au sababu ya kuwepo kwake ingetolewa, ingekoma kuwa dhambi. Dhana pekee
tuliyo nayo ya dhambi ni ile iliyotolewa katika neno la Mungu; ambayo ni, “uvunjaji wa sheria;” ni
utendaji wa kanuni inayopigana vita dhidi ya sheria kuu ya upendo ambayo ni msingi wa serikali ya
mbinguni.
Kabla ya uovu kuingia kulikuwa na amani na furaha katika malimwengu yote. Mambo yote yalikuwa
katika uafikiano mkamilifu na mapenzi ya Mwumbaji. Upendo kwa Mungu ulitawala, upendo wa mmoja
kwa mwenzake haukuwa nusu-nusu. Kristo Neno, Mwana pekee wa Mungu, alikuwa umoja na Baba wa
milele, - umoja katika asili, tabia, na katika makusudi, - ni yeye pekee katika malimwengu yote ambaye
aliweza kuingia katika mashauri na makusudi yote ya Mungu. Kwa njia ya Kristo, Baba aliumba viumbe
vyote vya mbinguni. “Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni … ikiwa ni viti vya
enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka” (Wakolosai 1:16); na kwa Kristo, sawa sawa na vile ilivyokuwa
kwa Baba, mbingu yote ilionyesha utii.
Sheria ya upendo ikiwa ndiyo msingi wa serikali ya Mungu, furaha ya viumbe vyote ilitegemea upatanifu
mkamilifu wao kwa kanuni za haki. Mungu anataka huduma ya upendo toka kwa viumbe vyake vyote -
ibada ile itokanayo na kuithamini tabia yake Mungu. Haufurahii utii unaotolewa kwa kujilazimisha, tena
yeye huwapa wote uhuru wa kufanya wapendavyo, ili waweze kumpa huduma yao ya hiari.
Lakini alikuweko mmoja aliyechagua kupotosha uhuru huu. Dhambi ilianzia ndani yake huyu ambaye,
baada tu ya Kristo, alikuwa amepewa na Mungu heshima kubwa kuliko wote na kusimama katika nafasi

287
ya juu kuliko wakazi wengine wote wa mbinguni. Kabla ya anguko lake, Lusifa alikuwa (494) kerubi wa
kwanza miongoni mwa makerubi wafunikao, akiwa mtakatifu, na asiye na waa. “BWANA Mungu asema
hivi; Wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima, na ukamilifu wa uzuri. Ulikuwa ndani ya Edeni,
bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako.” “Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa
mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na
huko kati ya mawe ya moto. Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu
ulipoonekana ndani yako.” Ezekieli 28:12-15.
Lusifa angeweza kubakia katika kupendwa na Mungu, akipendwa na kuheshimiwa na jeshi lote la
malaika, akitumia uwezo wake mkuu kuwabariki wengine na kumtukuza Muumba wake. Lakini, nabii
anasema, “Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya
mwangaza wako.” Fungu la 17. Kidogo kidogo, Lusifa aliiingiwa na tamaa ya kujikweza. “Umeweka
moyo wako kama moyo wa Mungu.” “Nawe ulisema … Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na
yeye Aliye juu.” Fungu la 6; Isaya 14:13,14. Badala ya kutafuta kumfanya Mungu aonekane mkuu kwa
upendo na heshima miongoni mwa viumbe vyake, Lusifa alijitihadi kuwashawishi wamtumikie na kumtii
yeye. Naye akitamani heshima ambayo Baba wa milele alikuwa ameweka juu ya Mwana wake, huyu
mkuu wa malaika alitaka madaraka ambayo yalikuwa yametolewa kwa Kristo peke yake.
Mbingu yote ilikuwa imefurahia kuakisi utukufu wa Mwumbaji na kuzitangaza sifa zake. Na wakati
Mungu akiheshimiwa hivyo, mambo yote yalikuwa shwari na furaha. Lakini hali ya kutopatana ilivuruga
utulivu wa mbinguni. Kuitumikia na kuiinua nafsi, kinyume cha mpango wa Mwumbaji, kuliamsha hisia
za uovu katika mawazo ya wale ambao miongoni mwao utukufu wa Mungu ulikuwa unatawala. Mabaraza
ya mbinguni yalimsihi Lusifa. Mwana wa Mungu alimwonyesha ukuu wa Mwumbaji, fadhili zake, na haki
yake, na utakatifu na tabia ya sheria yake isiyobadilika. Mungu mwenyewe ndiye aliyeuweka utaratibu
wa mbinguni; (495) na kwa kule kuachana nao, Lusifa angekuwa anamvunjia heshima Mwumbaji wake,
na kujiletea maangamizi. Lakini onyo hili, lililotolewa kwa upendo na rehema isiyo na kifani, liliamsha
tu roho ya upinzani. Lusifa aliruhusu kuwepo kwa wivu dhidi ya Kristo, na akawa shupavu zaidi.
Kiburi katika utukufu wake mwenyewe kilichochea tamaa ya kutaka ukuu wote. Heshima za juu
zilizowekwa kwa Lusifa hazikuthaminiwa kama zawadi ya Mungu na hazikumfanya awe na shukrani kwa
Mwumbaji. Alijitukuza kwa mng’ao wake na kujikweza, na akataka kuwa sawa na Mungu. Alikuwa
anapendwa na kuheshimiwa na jeshi la mbinguni. Malaika walifurahia kutekeleza maagizo yake, na
alikuwa amevikwa hekima na utukufu kuwapita wao wote. Lakini Mwana wa Mungu ndiye aliyekuwa
amekubaliwa kuwa Mfalme wa mbinguni, akiwa na uweza na mamlaka pamoja na Baba. Katika mashauri
yote ya Mungu, Kristo alishiriki, wakati Lusifa alikuwa haruhusiwi hivyo kuingia katika makusudi ya
Mungu. “Kwa nini Kristo awe mkuu?” aliuliza yule malaika mwenye nguvu, “Kwa nini anaheshimiwa
hivyo zaidi ya Lusifa?”
Akiacha mahali pake na kuondoka mbele za Mungu, Lusifa alienda kueneza roho ya manung’uniko
miongoni mwa malaika. Akifanya kazi yake kwa siri kubwa, na kwa kitambo akilificha kusudi lake halisi
chini ya mwonekano wa kumheshimu Mungu, alijitahidi kuchochea hali ya kutoridhishwa na sheria
zilizokuwa zinawatawala viumbe wa mbinguni, akionyesha kwamba ziliweka makatazo yasiyokuwa ya
lazima. Kwa kuwa tabia zao zilikuwa takatifu, alisisitiza kwamba malaika wanapaswa wafuate kuyatii
mapenzi ya nia zao. Alitafuta kupata huruma yao kwake kwa kuonyesha kwamba Mungu hakumtendea
yeye kwa haki kwa kumpatia Kristo heshima ya juu sana. Alidai kwamba katika kutaka mamlaka na
heshima kubwa zaidi hakuwa na lengo la kujikweza mwenyewe, bali alikuwa anatafuta kupata uhuru
kwa ajili ya wakazi wote wa mbinguni, kwamba kwa njia hii wangeweza kupata hali ya juu zaidi ya
maisha.
288
Mungu kwa rehema zake nyingi alimvumilia Lusifa kwa muda mrefu. Hakushushwa haraka kutoka katika
nafasi yake ile ya juu wakati ule ule alipoonyesha roho ya kutoridhika, wala pale (496) alipoanza kutoa
madai yake ya uongo mbele za malaika watiifu. Aliachwa mbinguni kwa muda mrefu. Alipewa msamaha
tena na tena kwa sharti la kutubu na kunyenyekea. Juhudi zile ambazo zingebuniwa tu na yeye aliye na
upendo na hekima visivyokoma zilifanywa ili kumthibitishia kosa lake. Roho ya kutoridhika ilikuwa
haijapata kujulikana mbinguni. Lusifa mwenyewe hakujua mwanzoni kwamba alikuwa anaelekea wapi;
hakuelewa kiini halisi cha hisia zake. Lakini kadiri kutoridhika kwake kulivyothibitika kwamba hakukuwa
na sababu, Lusifa alishawishika kwamba alikuwa katika makosa, kwamba madai ya Mungu yalikuwa ya
haki, na kwamba ilimpasa kukiri hivyo mbele ya mbingu yote. Laiti kama angefanya hivyo, angekuwa
amejiokoa mwenyewe na kuwaokoa malaika wengi. Wakati huu alikuwa bado hajaachana kabisa na utii
wake kwa Mungu. Ingawa alikuwa ameiacha nafasi yake ya kerubi afunikaye, bado kama angehiari
kumrudia Mungu, huku akitambua hekima ya Mwumbaji, na kuridhika kukalia nafasi aliyopangiwa katika
mpango mkuu wa Mungu, angeweza kurejeshwa katika nafasi yake. Lakini kiburi kilimzuia kunyenyekea.
Aliendelea kung’ang’ania kutetea msimamo wake, akiendelea kuona kwamba hakuwa na haja ya
kutubu, na akaingia kikamilifu kuwa, katika pambano kuu, akishindana na Mwumbaji wake.
Uwezo wote wa mipango yake ulielekezwa katika kufanya kazi ya udanganyifu, kutafuta kuvuta hisia za
malaika wote waliokuwa chini ya ushawishi wake. Hata habari ya kwamba Kristo alikuwa amemwonya
na kumshauri ilipotoshwa kutimiza mipango yake ya uasi. Shetani aliwaeleza wale ambao upendo wao
ulikuwa umewafungamanisha sana kwake kwamba alikuwa amehukumiwa pasipo haki, kwamba nafasi
yake haikuheshimiwa, na kwamba uhuru wake ulikuwa unaelekea kukandamizwa. Kutoka katika
kuyaeleza isivyo sahihi maneno ya Kristo alienda mbele katika kutosema ukweli kabisa na kusema uongo
moja kwa moja, akimshutumu Mwana wa Mungu kuwa ana mpango wa kumdhalilisha mbele ya wakazi
wa mbinguni. Pia alitafuta njia ya kujenga tatizo la uongo kati yake na malaika watiifu. Wale wote
ambao hakuweza kuwageuza na kuwaleta upande wake kikamilifu aliwashutumu kwamba walikuwa
wanapingana na masilahi ya wakazi wa mbinguni. Kwa sababu ya kazi ile ile ambayo ilikuwa inafanywa
na yeye mwenyewe aliwashutumu wale (497) waliobaki watiifu kwa Mungu. Na kuendeleza mashtaka
yake ya kwamba Mungu si mwenye haki kwake, alitafuta kueleza isivyo sahihi maneno na matendo ya
Mwumbaji. Sera yake ilikuwa ni kuwatatanisha malaika kwa njia ya hoja zake kuhusu makusudi ya
Mungu. Kila kitu kilichokuwa cha kawaida alikifunika kuwa siri, na kwa ustadi mkubwa wa kupotosha
alitilia mashaka kauli zilizo wazi kabisa za Yehova. Nafasi yake ya juu, katika mwunganiko huo wa
utawala wa Mungu, ilimpa msukumo mkubwa kujieleza hivyo, na wengi wakashawishika kujiunga naye
katika kuasi dhidi ya mamlaka ya Mbingu.
Mungu katika hekima yake alimruhusu Shetani kuendeleza kazi yake, mpaka roho ya chuki ilipokomaa na
kuzaa maasi halisi. Ilikuwa muhimu kwamba mipango yake iendelezwe hadi ikamilike, ili kwamba wote
waone tabia na mwelekeo halisi wa mipango hiyo. Lusifa, akiwa malaika aliyetiwa mafuta, alikuwa
ametukuzwa kwa hali ya juu sana; alikuwa anapendwa sana na viumbe wa mbinguni, na mvuto wake wa
ushawishi kwao ulikuwa na nguvu sana. Serikali ya Mungu haikuwajumuisha tu wakazi wa mbinguni, bali
ilijumuisha na wa malimwengu yote aliyokuwa ameyaumba; na Shetani akadhani kwamba akiwachukua
malaika wa mbinguni pamoja naye katika maasi yale, angeweza pia kuyachukua malimwengu yale
mengine. Alikuwa ameueleza msimamo wake kwa ustadi, akitumia werevu na udanganyifu ili kufikia
malengo yake. Uwezo wake wa kudanganya ulikuwa mkubwa sana, na kwa kujificha katika vazi lile la
uongo alifanikiwa. Hata malaika waaminifu hawakuweza kabisa kugundua tabia yake hiyo wala kule kazi
yake ilikokuwa ikielekeza.

289
Shetani alikuwa amepewa heshima kubwa sana, na kazi zake zote zilikuwa zimefunikwa katika fumbo,
kiasi kwamba ilikuwa vigumu kuwafunulia malaika hali halisi ya kazi yake. Mpaka muda ambapo
ingefikia ukamilifu wake, dhambi isingeonekana kuwa kitu kiovu vile ilivyokuwa. Mpaka wakati huo
dhambi haikuwa na nafasi katika malimwengu ya Mungu, na viumbe watakatifu waliokuwemo hawakuwa
na fikira yoyote kuhusu ilivyo na ubaya wake. Hawakuweza kutambua athari ambazo zingetokana na
kitendo cha kuiweka kando sheria ya Mungu. Mwanzoni Shetani alikuwa ameficha kazi yake chini ya
kujifanya kwamba alikuwa mtiifu kwa Mungu. Alidai kwamba alikuwa anatafuta njia ya kudumisha
heshima kwa Mungu, uthabiti wa Serikali yake, na usitawi wa wakazi wote wa (498) mbinguni. Wakati
akichochea hali ya kutoridhika mawazoni mwa malaika waliokuwa chini yake, kwa hila alikuwa
amefanya ionekane kwamba anatafuta kuondoa tatizo la hali ya kutoridhika miongoni mwao. Wakati
alipotaka mabadiliko yafanyike katika taratibu na sheria za serikali ya Mungu, ilikuwa kwa kisingizio
kwamba mambo hayo yalikuwa ya lazima ili kuhifadhi amani mbinguni.
Katika kushughulika na dhambi, Mungu aliweza kutumia haki na kweli tupu. Shetani aliweza kutumia
kile ambacho Mungu asingeweza kutumia - kujipendekeza na udanganyifu. Alikuwa ametafuta kulifanya
neno la Mungu lionekane la uongo na kuuelezea isivyo sahihi mpango wa serikali yake kwa malaika,
akidai kwamba Mungu hakutenda kwa haki katika kuwawekea wakazi wa mbinguni sheria na kanuni;
kwamba katika kutaka unyenyekevu na utii kutoka kwa kwa viumbe wake, alikuwa anataka tu kujikweza
yeye mwenyewe. Kwa hiyo lazima idhihirike mbele ya wakazi wote wa mbinguni, na kwa wale wa
malimwengu mengine, kwamba serikali ya Mungu ilikuwa ya haki, kuwa sheria yake ni kamilifu. Shetani
alikuwa amefanya ionekane kana kwamba yeye mwenyewe alikuwa anatafuta kuendeleza usitawi wa
malimwengu yote. Tabia halisi ya mnyang’anyi huyu, na makusudi yake hasa, vinapaswa vieleweke
vyote. Lazima awe na muda wa kujidhihirisha mwenyewe kwa matendo yake maovu.
Kwa hali ile ya ukengeufu iliyosababishwa na msimamo wake kule mbinguni, Shetani alitupa lawama
zake kwa sheria na serikali ya Mungu. Alisema kwamba maovu yote yalikuwa ni matokeo ya utawala wa
Mungu. Alidai kwamba lilikuwa ni lengo lake kuziboresha sheria za Yehova. Kwa hiyo ilikuwa muhimu
kwamba aonyeshe sura ya madai yake, na kuonyesha utendaji wa mabadiliko yake aliyokuwa
anapendekeza yafanyike katika sheria ya Mungu. Lazima kazi yake mwenyewe imhukumu. Tangu
mwanzo Shetani alikuwa amedai kwamba hakuwa katika maasi. Lazima malimwengu yote yamwone
mwongo huyo akiwa amefichuliwa wazi.
Hata wakati ilipokuwa imeamuliwa kwamba asingeweza tena kubaki kule mbinguni, Yeye aliye Hekima
yote hakumwangamiza Shetani. Kwa kuwa huduma ya upendo tu ndiyo inayokubaliwa na Mungu, lazima
utiifu wa viumbe vyake utegemee jinsi wanavyoitambua haki yake na fadhili zake. Wakazi wa mbinguni
na wa malimwengu mengine, wakiwa hawako tayari kuelewa tabia au matokeo ya dhambi, kwa wakati
ule wasingekuwa wameona haki na (499) rehema ya Mungu katika kumwangamiza Shetani. Ikiwa
angefutiliwa mbali pale pale, wangekuwa wanamtumikia Mungu kwa hofu kuliko kwa upendo. Mvuto wa
mdanganyifu huyo usingeweza kufutika kabisa, wala roho ya uas isingekuwa imeondoshwa kabisa.
Lazima uovu uachwe mpaka ukomae. Kwa usitawi wa malimwengu yote kwa vizazi visivyokoma, lazima
Shetani adhihirishe kwa ukamilifu zaidi kanuni zake, ili shutuma zake dhidi ya Serikali ya Mungu zipate
kuonekana katika nuru yake halisi mbele ya viumbe vyake vyote, ili haki na rehema ya Mungu na sheria
yake isiyobadilika vipate kuwekwa wazi pasipo shaka milele zote.
Uasi wa Shetani ulipaswa kuwa fundisho kwa malimwengu yote kupitia vizazi vyote vilivyofuatia, ni
ushuhuda wa kudumu wa tabia na matokeo ya kutisha ya dhambi. Utendaji wa utawala wa Shetani,
athari zake kwa wanadamu na malaika, ungeonyesha kile ambacho lazima kiwe ni matokeo ya kuiweka
kando mamlaka ya Mungu. Ungeshuhudia kwamba katika kuweko kwa serikali ya Mungu na sheria yake
290
usitawi wa viumbe vyote alivyovifanya umefungamanishwa. Hivyo historia ya jaribio hili la kutisha la
uasi lingedumu kuwa kinga kwa viumbe vyote vitakatifu, ili kuvizuia visipate kudanganywa kuhusu hali
halisi ya uasi, kuwasaidia wasitende dhambi na kupatwa na adhabu zake.
Mpaka mwisho wenyewe wa pambano hilo kule mbinguni mnyang’anyi huyo mkuu aliendelea kujihesabu
kuwa ana haki. Wakati ilipotangazwa kwamba lazima yeye na washirika wake wote wafukuzwe kutoka
kwenye makao yale ya raha, ndipo muasi kiongozi huyo alipothibitisha kwa uwazi kabisa chuki yake
dhidi ya sheria ya Mwumbaji. Alirudia madai yake kwamba malaika hawakuhitaji kudhibitiwa, bali
kwamba waachwe wafuate utashi wao, ambao daima ungewaongoza kwa usahihi. Alizishutumu amri za
kimbingu kwamba zinazuia uhuru wao na kutangaza kwamba kusudi lake lilikuwa ni kupiga marufuku
sheria; kwamba, wakiisha kuwekwa huru mbali na kizuizi hicho, majeshi ya mbinguni yangeweza kuingia
katika hali ya maisha ya juu zaidi, hali ya utukufu zaidi wa maisha.
Kwa nia moja, Shetani na jeshi lake walitupa lawama ya maasi yao yote kwa Kristo, wakidai kwamba
kama (500) wasingeshutumiwa, wasingeweza kuasi kamwe. Hivyo wakiwa wakaidi na wasiotii,
wakitafuta pasipo mafanikio kuipindua serikali ya Mungu, lakini bado wakidai kwa kukufuru kwamba
wao ni wahanga katika mamlaka ya ukandamizaji wasiokuwa na hatia, hatimaye muasi mkuu pamoja na
walioungana naye walifukuzwa mbinguni.
Roho ile ile iliyochochea uasi kule mbinguni bado inaendelea kuchochea uasi duniani. Shetani
ameendeleza kwa wanadamu sera ile ile aliyotekeleza kwa malaika. Roho yake sasa inatawala miongoni
mwa wana wa kuasi. Kama yeye wanajitahidi sana kuvunja vizuizi vinavyowekwa na sheria ya Mungu na
wanawaahidi watu kwamba watapata uhuru kwa kuvunja kanuni za sheria. Kukemea dhambi bado
kunaamsha roho ya chuki na upinzani. Ujumbe wa Mungu wa onyo unapoletwa nyumbani pake katika
dhamiri zao, Shetani anawaongoza watu kujihesabia haki na kutafuta kuungwa mkono na watu wengine
katika njia yao ambayo ni ya dhambi. Badala ya kuyarekebisha makosa yao, wanachochea chuki dhidi ya
mkemeaji, kana kwamba yeye ndiye msababishaji mkuu wa tatizo. Tangu siku za Habili mwenye haki
hadi wakati wetu huu hiyo ndiyo roho ambayo imekuwa ikionyeshwa kwa wale wanaothubutu kuipinga
dhambi.
Kwa njia ile ile ya kuieleza isivyo tabia ya Mungu kama vile alivyofanya mbinguni, akifanya Mungu
aonekane kuwa mkali na dhalimu, Shetani alimshawishi mwanadamu kutenda dhambi. Na
akishakufanikiwa kiasi hicho, alitangaza kwamba vizuizi vya Mungu ambavyo si vya haki ndivyo
vilisababisha anguko la mwanadamu, kama vile ambavyo vilisababisha uasi wake yeye.
Lakini Yeye Aliye wa Milele mwenyewe anatangaza tabia yake: “BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa
huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; mwenye kuwaonea huruma
watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu
kuwa hana hatia kamwe.” Kutoka 34:6,7.
Katika kumfukuza Shetani kutoka mbinguni, Mungu alitangaza haki yake na kuendeleza heshima ya kiti
chake cha enzi. Lakini mwanadamu alipokosa kwa kuyakubali madanganyo ya roho hii iliyoasi, Mungu
alitoa ushahidi wa upendo wake kwa kumtoa Mwanawe pekee kufa kwa ajili ya jamii ya wanadamu
iliyoanguka. (501) Katika huduma ya upatanisho tabia ya Mungu inadhihirishwa. Hoja kubwa ya msalaba
inaonyesha kwa malimwengu yote kwamba njia ya dhambi iliyochaguliwa na Lusifa haikustahili kwa
vyovyote kuwa na lawama zilizoelekezwa kwa serikali ya Mungu.
Katika pambano kati ya Kristo na Shetani, wakati wa huduma ya Mwokozi duniani, tabia ya mwongo
mkuu huyo ilifichuliwa wazi. Hakuna kitu cho chote ambacho kingeweza kumng’oa Shetani kutoka
katika mapendo ya malaika wa mbinguni na katika malimwengu yote yenye kumtii Mungu kama
291
ilivyofanya vita ile ya kikatili aliyofanya dhidi ya Mkombozi wa ulimwengu. Uthubutu wa kukufuru wa
kudai kwamba Kristo amsujudie, ujasiri wa kiburi katika kumchukua mpaka juu ya kilele cha mlima na
juu ya kinara cha hekalu, kusudi lake ovu lililokataliwa akimtaka ajitupe chini kutoka juu kwa umbali
ule unaosababisha kizunguzungu, uovu usiolala usingizi uliomwinda toka mahali hata mahali, ukichochea
mioyo ya makuhani na watu kulikataa pendo lake, na mwishowe kupiga kelele, “Msulibishe! Msulibishe!”
- yote haya yaliamsha mshangao na uchungu wa malimwengu.
Shetani ndiye aliyeuchochea ulimwengu kumkataa Kristo. Mkuu wa uovu alitumia uwezo wake wote na
mbinu zake zote kumwangamiza Yesu; maana aliona kwamba rehema na upendo wa Mwokozi, huruma
yake na upole wake, vilikuwa vinaudhihirishia ulimwengu tabia ya Mungu. Shetani alipinga kila dai
lilitolewa na Mwana wa Mungu na akawatumia wanadamu kama mawakala wake kufanya maisha ya
Mwokozi yajae mateso na huzuni. Udanganyifu na uongo wake ambao aliutumia kuizuia kazi ya Yesu,
chuki iliyoonyeshwa kupitia kwa wana wa kuasi, mashtaka ya kikatili yaliyotolewa dhidi yake yeye
aliyekuwa na maisha mema yasiyo na mfano, vyote hivyo vilitoka katika vina vya kulipiza kisasi. Mioto
ya wivu na uovu, chuki na kisasi, vilifumuka dhidi ya Mwana wa Mungu pale Kalvari, wakati mbingu yote
ikiliangalia tukio lile katika hali ya ukimya wa mshtuko.
Pindi kafara ile kuu ilipokwishakutolewa, Kristo alipaa juu, akikataa kupokea ibada ya malaika mpaka
alipokuwa ameomba: “Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami po pote nilipo.” Yohana 17:24.
Ndipo (502) kwa upendo usioelezeka na kwa nguvu lilikuja jibu kutoka kwenye kiti cha enzi cha Baba:
“Na wamsujudu malaika wote wa Mungu.” Waebrania 1:6. Hapakuwa na waa lililokuwa kwa Yesu.
Kujinyenyekeza kwake kulikoma, kafara yake ilikuwa imekamilika, alipewa jina lile lipitalo kila jina.
Sasa hatia ya Shetani ilikuwa wazi pasipo udhuru. Alikuwa amedhihirisha tabia yake halisi kuwa ni
mwongo na mwuaji. Ilionekana kwamba roho ile aliyokuwa nayo katika kuwatawala wana wa
wanadamu, ambao walikuwa chini ya himaya yake, angekuwa ameidhihirisha ikiwa angekuwa
ameruhusiwa kutawala wakazi wa mbinguni. Alikuwa amedai kwamba uvunjaji wa sheria ya Mungu
ungeleta uhuru na utukufu; lakini ulionekana kwamba unaleta matokeo ya utumwa na kushusha hadhi ya
maisha.
Mashtaka ya uongo ya Shetani dhidi ya tabia ya Mungu na serikali yake yalionekana katika mwanga wake
halisi. Alikuwa amemshtaki Mungu kuwa anatafuta kujikweza mwenyewe kwa kudai unyenyekevu na utii
toka kwa viumbe wake, na alikuwa ametangaza kwamba, wakati Mwumbaji alilazimisha wengine wote
kujikana nafsi, yeye mwenyewe alikuwa hatekelezi hali ya kujikana nafsi, wala kujitoa. Sasa ilionekana
wazi kwamba kwa ajili ya wokovu wa wanadamu walioanguka na wenye dhambi, Mtawala wa
malimwengu alikuwa ametoa kafara kubwa kuliko zote ambayo ingefanywa na pendo tu; kwa maana
“Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake.” 2 Wakorintho 5:19. Pia
ilionekana wazi kwamba, wakati Lusifa alikuwa amefungua mlango ili dhambi iingie kwa sababu ya
tamaa yake ya kupata heshima na ukuu, Kristo, ili kuiharibu dhambi, alikuwa amejinyenyekeza
mwenyewe na kuwa mtii hata mauti.
Mungu alikuwa amedhihirisha chuki yake dhidi ya kanuni za uasi. Mbingu yote iliona haki yake
ikifunuliwa, pote katika kumhukumu Shetani na katika kumkomboa mwanadamu. Lusifa alikuwa
ametangaza kwamba ikiwa sheria ya Mungu haibadiliki, na adhabu yake haiwezi kutanguliwa, lazima
kila mvunjaji wa sheria azuiwe milele kuwa upande wa Mwumbaji. Alikuwa amedai kwamba jamii yote
ya wadhambi ilikuwa imekwenda mbali kupita kiasi cha kukombolewa na kwa hiyo walikuwa mateka
wake halali. Lakini kifo cha Kristo kilikuwa ni hoja iliyotolewa kwa niaba ya mwanadamu ambayo
isingeweza kupinduliwa. (503) Adhabu ya sheria ilimwangukia yeye aliyekuwa sawa na Mungu, na

292
mwanadamu alikuwa huru kuipokea haki ya Kristo na kwa maisha ya toba na unyenyekevu kupata
ushindi, kama vile Mwana wa Mungu alivyopata ushindi, dhidi ya nguvu ya Shetani. Hivyo Mungu ni
mwenye haki na bado mwenye kuwahesabia haki wote wanaomwamini Yesu.
Lakini kuja kwa Kristo duniani kuteswa na kufa hakukuwa kwa ajili ya kukamilisha ukombozi wa
mwanadamu tu. Alikuja “kuitukuza sheria” na “kuiadhimisha.” Si tu kwamba ili wakazi wa ulimwengu
wapate kuichukulia sheria kama inavyopaswa, bali ilikuwa ni kwa madhumuni ya kuyaonyesha
malimwengu yote kwamba sheria ya Mungu haibadiliki. Ikiwa matakwa ya sheria yangeweza kuwekwa
kando, Mwana wa Mungu asingelazimika kuutoa uhai wake ili kufanya upatanisho kwa ajili ya uvunjaji
wa sheria hiyo. Kifo cha Yesu kinathibitisha kwamba haibadiliki. Na kafara ile ambayo upendo wa milele
ulimsukuma Baba na Mwana kuitoa, ili wenye dhambi wapate kukombolewa, inaonyesha kwa
malimwengu yote - ambapo hakuna kitu kidogo zaidi ya mpango huo wa upatanisho ambacho kingeweza
kutosheleza kazi hiyo - kwamba haki na rehema ni msingi wa sheria na serikali ya Mungu.
Katika utekelezaji wa mwisho wa hukumu itadhihirika kwamba sababu ya kuwepo kwa dhambi haipo.
Wakati Hakimu wa dunia yote atamtaka Shetani ajibu swali, “Kwa nini wewe umeniasi Mimi, na
kuninyang’anya hao raia wa ufalme wangu?” mwasisi wa dhambi hataweza kutoa udhuru. Kila kinywa
kitafumbwa, na majeshi yote ya uasi yatakuwa hayana la kusema.
Msalaba wa Kalvari, wakati unatangaza kwamba sheria haibadiliki, unatangaza kwa malimwengu yote
kwamba mshahara wa dhambi ni mauti. Katika kilio cha mwisho cha Mwokozi, “Imekwisha,” kengele ya
kifo cha Shetani iligongwa. Pambano kuu lililokuwa limeendelea kwa muda mrefu liliamuliwa wakati
huo, na habari ya kufutilia mbali dhambi mara ya mwisho ilifanywa kuwa ya hakika. Mwana wa Mungu
alipitia katika malango ya kaburi, ili “kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti,
yaani, Ibilisi.” Waebrania 2:14. Tamaa ya Lusifa ya kujikweza mwenyewe ilikuwa imemwongoza
kusema: “Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu;… Nitafanana na yeye Aliye juu.” Mungu
anasema: “Nami nitakufanya (504) kuwa majivu juu ya nchi,… wala hutakuwapo tena hata milele.”
Isaya 14:13,14; Ezekieli 28:18,19. “Siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi,
nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa
majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.” Malaki 4:1.
Malimwengu yote yatakuwa yamekuwa mashuhuda wa tabia na athari ya dhambi. Na kule kufutiliwa
mbali kwa dhambi, ambako mwanzoni kungeleta hofu kwa malaika na kumvunjia heshima Mungu, sasa
kutaithibitisha haki ya upendo wake na kuiimarisha heshima yake mbele ya malimwengu yote yaliyo na
viumbe wanaofurahia kuyafanya mapenzi yake, na ambao mioyoni mwao imo sheria yake. Kamwe
dhambi haitaonekana tena. Neno la Mungu linasema, “Mateso hayatainuka mara ya pili.” Nahumu 1:9.
Sheria ya Mungu, ambayo Shetani ameishutumu kwamba ni kongwa la utumwa, itaheshimiwa kama
sheria ya uhuru. Viumbe waliokwisha kujaribiwa na kuthibitishwa hawataweza kamwe kugeuka tena na
kuacha utii wao kwake yeye ambaye tabia yake imedhihirishwa kikamilifu mbele yao kuwa ni ya upendo
wa kina kisichopimika na hekima isiyo na kikomo.

293
Sura ya 30
UADUI KATI YA MWANADAMU NA SHETANI

“Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo
utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.” Mwanzo 3:15. Hukumu ya Mungu iliyotamkwa dhidi
ya Shetani baada ya kuanguka kwa mwanadamu ilikuwa ni unabii pia, unaojumuisha vizazi vyote hadi
mwisho wa wakati, ukiashiria mapigano makuu yatakayohusisha jamii zote za wanadamu watakaopata
kuishi duniani.
Mungu anasema: “Nami nitaweka uadui.” Uadui huo haupokelewi kwa asili. Mwanadamu alipovunja
sheria ya kimbingu, asili yake iligeuka na kuwa ya uovu, na alikuwa katika upatanifu, wala hakuwa
kinyume, na Shetani. Kwa asili hakuna uadui kati ya mwanadamu mwenye dhambi na mwanzilishi wa
dhambi. Wote wawili waligeuka waovu kwa njia ya uasi. Muasi hapumziki kamwe, isipokuwa mpaka
akipata kuungwa mkono na kuwashawishi wengine kufuata mfano wake. Kwa sababu hii malaika
walioanguka na wanadamu waovu huungana katika urafiki mkubwa. Ikiwa Mungu asingekuwa ameingilia
kati kwa namna ya pekee, Shetani na mwanadamu wangekuwa wameingia katika ushirikiano dhidi ya
Mbingu; na badala ya kuwa na uadui dhidi ya Shetani, jamaa yote ya kibinadamu ingekuwa imeungana
kumpinga Mungu.
Shetani alimjaribu mwanadamu kutenda dhambi, kama vile alivyokuwa amewafanya malaika kuasi, ili
kwamba apate ushirikiano wao katika vita yake dhidi ya Mbingu. Hapakuwa na kutofautiana kati yake na
malaika wale walioanguka kwa habari ya chuki yao dhidi ya Kristo; wakati katika mambo yote (506)
mengine walikuwa hawapatani, walikuwa wameungana thabiti katika kuipinga mamlaka ya Mtawala wa
malimwengu. Lakini Shetani aliposikia tangazo kwamba uadui ungekuwapo kati yake na yule
mwanamke, kati ya uzao wake na uzao wa mwanamke, alijua kwamba juhudi zake za kupotosha hali ya
binadamu zingevurugwa; kwamba kwa njia fulani mwanadamu angewezeshwa kuupinga uwezo wake.
Uadui wa Shetani dhidi ya jamii ya kibinadamu unachochewa kwa sababu, kupitia Kristo, wao ni
walengwa wa upendo wa Mungu na rehema yake. Anatamani kuuzuia mpango wa Mungu kwa ajili ya
ukombozi wa mwanadamu, kumvunjia Mungu heshima yake, kwa kuiharibu sura yake ndani yao na
kuichafua kazi ya mikono yake; yeye angesababisha huzuni kubwa mbinguni na kuijaza dunia kwa misiba
na maangamizi. Na yeye husonda kidole kuelekeza kwenye maovu kwamba ni matokeo ya kazi ya Mungu
ya kumwumba mwanadamu.
Neema ambayo Kristo anaipandikiza moyoni ndiyo inayoumba ndani ya mwanadamu uadui dhidi ya
Shetani. Pasipo neema hii inayobadilisha na uweza huu unaoumba upya, mwanadamu angeendelea kuwa
mateka wa Shetani, mtumishi wake aliye tayari daima kufanya kama anavyoamriwa. Lakini msingi mpya
ukiwa moyoni huanzisha vita mahali ambapo panakuwa pamekuwa na amani kabla. Nguvu ambayo
inawekwa ma Yesu inamwezesha mwanadamu kumpinga mtawala huyo dhalimu na mnyang’anyi. Ye
yote aonekanaye kuichukia dhambi badala ya kuipenda, ye yote azipingaye na kuzishinda tamaa za
mwili zilizokuwa zimetawala ndani yake, anadhihirisha utendaji wa kanuni itokayo kwa ujumla
mbinguni.
Uadui uliopo kati ya roho ya Kristo na roho ya Shetani ulidhihirishwa kwa namna ya wazi mno kwa
namna ulimwengu ulivyompokea Yesu. Sababu kubwa iliyofanya Wayahudi waliongozwa kumkataa

294
haikuwa kwamba alitokea bila utajiri wa dunia hii, fahari, au utukufu. Waliona kwamba alikuwa na
uwezo ambao ungefidia zaidi sana upungufu aliokuwa nao katika mambo hayo yaliyo ya manufaa ya nje.
Lakini usafi na utakatifu wa Kristo uliamsha chuki ya waovu dhidi yake. Maisha yake ya kujikana nafsi na
utauwa usio na dhambi vilikuwa ni kemeo la kudumu dhidi ya watu wenye majivuno na waasherati. Ni
jambo hili lililoibua uadui dhidi ya Mwana wa Mungu. Shetani na malaika zake waovu waliungana
pamoja na watu waovu. Nguvu zote za uasi zilipatana kumpinga Mtetezi wa ile kweli.
(507) Uadui ule ule unadhihirishwa dhidi ya wafuasi wa Kristo kama ulivyoonyeshwa dhidi ya Bwana
wao. Yeyote anayeona ubaya wa dhambi, na kwa uwezo utokao juu anayapinga majaribu, kwa hakika
ataamsha ghadhabu ya Shetani na ya raia zake. Chuki kwa kanuni safi za ukweli, na shutuma na mateso
dhidi ya wale wanaoitetea, vitaendelea kuwepo kwa kadiri ambavyo dhambi na wadhambi wanaendelea
kuwepo. Wafuasi wa Kristo na watumishi wa Shetani hawawezi kupatana. Mashambulizi ya msalaba
hayajakoma. “Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.” 2
Timotheo 3:12.
Mawakala wa Shetani wanaendelea kufanya kazi chini ya uongozi wake kuimarisha mamlaka yake na
kuujenga ufalme unaopingana na serikali ya Mungu. Kwa makusudi haya wanajitahidi kudanganya
wafuasi wa Kristo na kuwavuta kwa werevu ili wauache utii wao. Kama kiongozi wao alivyo,
wanayaetafsiri vibaya na kuyapotosha Maandiko ili kutimiza lengo lao. Kama vile Shetani alivyojitahidi
kumtupia lawama Mungu, ndivyo mawakala wake wanavyojitahidi kuwashtaki kwa uongo watu wa
Mungu. Roho ile iliyomwua Kristo ndiyo inayowasukuma waovu kuwaangamiza wafuasi wake. Mambo
haya yote yalitabiriwa katika unabii ule wa kwanza: “Nami nitaweka uadui kati yako na huyo
mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake.” Na hali hii itaendelea hadi mwisho wa wakati.
Shetani hukusanya majeshi yake yote na kutumia nguvu zake zote katika mapambano hayo. Kwa nini
sasa hakabiliwi na upinzani mkubwa? Kwa nini askari wa Kristo wamelala usingizi mzito na kuwa wasio
na upande maalum? Ni kwa sababu wana kiwango kidogo cha mwunganiko wa kweli na Kristo; kwa
sababu wanakosa Roho wake. Kwao dhambi si mbaya wala ya kuchukiza, kama ilivyokuwa kwa Bwana
wao. Hawakutani nayo kwa kudhamiria na kwa upinzani thabiti, kama alivyofanya Kristo. Hawatambui
ubaya wa kupita kiasi na uovu mkubwa wa dhambi, na wamepofushwa macho wasione tabia na nguvu za
mkuu wa giza. Kuna uadui kidogo sana ndani yao dhidi ya Shetani na kazi zake, kwa sababu wana ujinga
mkubwa kuhusu uwezo wake na madhara yake mabaya, na uwanja mpana wa vita yake dhidi ya Kristo
na kanisa lake. Watu wengi wanadanganyika hapa. Hawajui kwamba adui yao ni jenerali hodari wa vita,
anayeongoza mawazo ya malaika waovu, (508) na ya kwamba kwa kutumia mipango iliyokamilika vema
na mienendo yenye mbinu za hali ya juu anapigana na Kristo ili kuzuia wokovu wa watu. Ni kwa nadira
sana kusikia Shetani akitajwa miongoni mwa wale wajiitao Wakristo, na hata miongoni mwa wahubiri
wa injili, isipokuwa labda kwa nasibu tu anapotajwa mimbarani. Wanapuuza ushahidi wa kuendelea kwa
utendaji wake na mafanikio yake; wanapuuza maonyo mengi kuhusu hila zake; wanaonekana kama
kupuuza hata kuhusu uwepo wake.
Wakati wanadamu wanakuwa wasiojua mbinu zake, adui huyu shupavu anavizia katika njia yao wakati
wote. Anaingiza uwepo wake katika kila idara ya nyumbani, katika kila mtaa wa miji yetu, katika
makanisa, katika mabaraza ya taifa, katika mahakama za kutoa haki, akitatanisha mawazo,
akidanganya, akiangamiza nafsi na miili ya wanaume, wanawake, na watoto, akizivunja familia,
akipandikiza chuki, wivu, ugomvi, maasi, na mauaji. Na ulimwengu wa Kikristo unaonekana kama vile
unayachukulia mambo haya kwamba yamekubaliwa na Mungu na kwamba lazima yawepo.

295
Shetani anatafuta muda wote kuwashinda watu wa Mungu kwa kuvivunja vizuizi vinavyowatenganisha na
ulimwengu. Israeli ya zamani walishawishika kuingia katika dhambi wakati walipojiingiza katika
ushirikiano na wapagani uliokatazwa. Kwa njia inayofanana na ile Israeli ya leo wanapotoka. “Mungu wa
dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura
yake Mungu.” 2 Wakorintho 4:4. Wote ambao si wafuasi wa Kristo waliokata shauri ni watumishi wa
Shetani. Katika moyo usiozaliwa upya kuna hali ya kuipenda dhambi na msukumo wa kuifuga na kuitolea
udhuru. Katika moyo uliofanywa upya kuna chuki dhidi ya dhambi na hali ya kuipingana kwa kudhamiria.
Wakati Wakristo wanapochagua kushirikiana na jamii ya wasiomcha Mungu na wasioamini, wanajipeleka
katika majaribu. Shetani hujificha asionekane na kwa pasipo kuonekana anafunika macho yao kwa vazi
la udanganyifu. Hawawezi kuona kwamba ushirikiano na kundi kama hilo umepangiliwa ili kuwaletea
madhara; na wakati muda wote wanazidi kufanana na ulimwengu kwa tabia, maneno, na matendo,
wanapigwa upofu zaidi na zaidi.
(509) Kufuata desturi za ulimwengu kunalifanya kanisa liongolewe na ulimwengu; kamwe hakuuongoi
ulimwengu kwa Kristo. Kufanya mazoea na dhambi kutaleta matokeo yasiyoepukika ya kuifanya
ionekane ya kuchukiza. Yeyote anayechagua kufanya urafiki na watumishi wa Shetani punde atakoma
kumwogopa bwana wao. Wakati tunapoletwa katika kujaribiwa katika namna ya kutimiza wajibu wetu,
kama ilivyokuwa kwa Danieli katika jumba la mfalme, tunaweza kuwa na uhakika kwamba Mungu
atatulinda; lakini ikiwa tunaweka wenyewe katika majaribu tutaanguka muda wowote.
Mara kwa mara mjaribu hufanya kazi kwa mafanikio kupitia kwa wale ambao wanatiliwa shaka kidogo
sana kwamba wako chini ya utawala wake. Watu wenye talanta na elimu wanapendwa na kuheshimiwa,
kana kwamba sifa hizi zingeweza kufidia utovu wao wa uchaji wa Mungu au kuwafanya watu wakubaliwe
naye. Talanta na ujuzi, kwa kuzingatia hayo tu, ni vipawa vya Mungu; lakini hivyo vinapofanywa kuwa
badala ya utauwa, wakati, badala ya kumleta mtu aliye navyo karibu zaidi na Mungu, vinampeleka mbali
na yeye, hapo vinakuwa laana na mtego. Lipo wazo lililoenea kwa wengi kwamba yale yote
yanayoonekana kama adabu au usafi lazima, kwa mtazamo fulani, yanahusiana na Kristo. Kamwe
hapakuwa na kosa kubwa zaidi ya hilo. Sifa hizo zinapaswa kuchangia katika tabia ya kila Mkristo,
maana zingeweza kuleta mvuto wenye nguvu kwa watu kuelekea katika dini ya kweli; lakini lazima
ziwekwe wakfu kwa Mungu, la sivyo vitu hivyo ni nguvu pia kwa ajili ya uovu. Watu wengi waliokuza
akili zao na kuwa na tabia inayopendeza, ambao wasingeweza kupinda kuelekea kwa kitu
kinachofikiriwa kwa ujumla kuwa tendo lisilo la maadili, hao ni chombo tu kilichonakishiwa mikononi
mwa Shetani. Tabia ya uongo na ya kudhuru ya mvuto wa watu hao na kielelezo chao huwafanya kuwa
adui wa hatari kwa kazi ya Kristo kuliko vile walivyo wale ambao hawajui na hawakufunzwa.
Kwa maombi ya bidii na kumtegemea Mungu, Sulemani alijipatia hekima ambayo iliusisimua na
kustaajabisha ulimwengu. Lakini alipogeuka kuacha Chanzo cha nguvu zake, na kusonga mbele
akijitegemea mwenyewe, alianguka majaribuni na kuwa mateka. Halafu nguvu za ajabu zilizotolewa
kwa mtu huyo mwenye hekima kuliko wafalme wote zikamfanya kuwa wakala wa yule adui wa watu.
(510) Wakati Shetani anapojitahidi muda wote kupofusha mawazo yao kuhusu hali halisi, hebu Wakristo
wasisahau kamwe kwamba “wanashindana … si juu ya damu na nyama; bali … juu ya falme na mamlaka,
juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Waefeso 6:12.
Onyo lenye uvuvio linasikika kupitia kupitia karne zote hadi nyakati zetu: “Mwe na kiasi na kukesha;
kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.”
1 Petro 5:8. “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.” Waefeso 6:11.

296
Tangu siku za Adamu mpaka wakati wetu huu, adui yetu mkuu amekuwa akitumia uwezo wake kutesa
na kuharibu. Sasa anajiandaa kwa pambano lake la mwisho dhidi ya kanisa. Wale wote wanaotafuta
kumfuata Yesu wataingizwa katika pambano dhidi ya adui huyo asiyechoka. Kadiri Mkristo anavyoiga
mpangilio wa Mungu kwa karibu, ndivyo atakavyojiwekea alama zaidi inayoshambuliwa na Shetani. Wote
wanaojishughulisha kwa bidii katika kazi ya Mungu, wakitafuta kuyafichua madanganyo ya yule mwovu
na kumhubiri Kristo mbele ya watu, wataweza kujiunga katika ushuhuda wa Paulo, ambamo
anazungumza kuhusu kumtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote wa moyo, kwa machozi na majaribu
mengi.
Shetani alimshambulia Kristo kwa majaribu makali na magumu zaidi, lakini alishindwa katika kila
mapambano. Vita vile vilipiganwa kwa niaba yetu; ushindi wote ule unafanya iwezekane kwetu
kushinda. Kristo atawapatia uwezo wale wote wanaoutafuta. Hakuna mtu ye yote ambaye pasipo
kukubali yeye mwenyewe anaweza kushindwa na Shetani. Mjaribu hana uwezo wa kuitawala nia ya mtu
au kumilazimisha nafsi yake kutenda dhambi. Anaweza kusababisha mateso, lakini hawezi kumtia
uchafu. Anaweza kusababisha maumivu, lakini si unajisi. Ukweli kwamba Kristo ameshinda unapaswa
kuwapa ujasiri wafuasi wake ili wapate kupigana kiume vita dhidi ya dhambi na Shetani.

297
Sura ya 31
NGUVU ZA ROHO WAOVU

Mwunganiko kati ya ulimwengu uonekanao na ule usioonekana, huduma ya malaika wa Mungu, na


uwakala wa roho waovu, yamefunuliwa wazi katika Maandiko, na yamefungamanishwa na historia ya
wanadamu kwa namna isiyotenganishika. Kuna hali ya kuongezeka kwa mwelekeo wa kutoamini uwepo
wa roho waovu, huku malaika watakatifu ambao “huwahudumu wale watakaourithi wokovu” (Waebrania
1:14) wakidhaniwa na wengi kuwa roho za wafu. Lakini Maandiko hayafundishi tu kuhusu kuwako kwa
malaika, wote wema na wabaya, bali pia yanaonyesha ushahidi usiopingika kwamba hao si roho za wafu
zilizovuliwa miili.
Kabla ya kuumbwa kwa mwanadamu, malaika walikuweko; maana wakati misingi ya dunia ilipowekwa,
ndipo “Nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha.”
Ayubu 38:7. Baada ya kuanguka kwa mwanadamu, malaika walitumwa kuulinda mti wa uzima, na
mambo haya yalikuwa kabla mwanadamu hajafa. Kwa asili malaika wana hadhi ya juu kuliko
mwanadamu, maana mwimba zaburi anasema kwamba mtu alifanywa “mdogo punde kuliko malaika.”
Zaburi 8:5.
Tunajulishwa na Maandiko kuhusu idadi, na uwezo na utukufu, wa viumbe hivyo vya mbinguni, kuhusu
uhusiano wao na serikali ya Mungu, na pia kuhusu uhusiano wao na kazi ya ukombozi. “BWANA ameweka
kiti chake cha enzi mbinguni, na ufalme wake unavitawala vitu vyote.” Nabii naye anasema, “Nikasikia
sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi.” Katika chumba kile alimo Mfalme wa wafalme
(512) wanangoja - “malaika zake, walio hodari,” “watumishi wake wafanyao mapenzi yake,”
“wakiisikiliza sauti ya neno lake.” Zaburi 103:19-21; Ufunuo 5:11. Elfu kumi mara elfu kumi na maelfu
elfu, ni watumishi wa mbinguni walioonwa na nabii Danieli. Mtume Paulo alisema kwamba idadi yao ni
“majeshi ya malaika elfu nyingi.” Danieli 7:10; Waebrania 12:22. Wakiwa wajumbe wa Mungu wanatoka
na kwenda, mfano wa “kumulika kwa umeme,” (Ezekieli 1:14), waking’aa kwa utukufu, na kuruka kwao
ni kwa kasi sana. Malaika yule aliyejitokeza penye kaburi la Mwokozi, akiwa na mwonekano “kama
umeme, na mavazi yake meupe kama theluji,” aliwafanya walinzi kutetemeka sana kwa hofu, na “kuwa
kama wafu.” Mathayo 18:3,4. Wakati Senakeribu, Mwashuri mwenye majivuno, alipomtukana na
kumkufuru Mungu, na kutishia kuiangamiza Israeli, “ikawa usiku uo huo malaika wa BWANA alitoka,
akakiingia kituo cha Waashuri, akawapiga watu mia na themanini na tano elfu.” Pale mashujaa wote, na
majemadari, na maakida katika jeshi la Senakeribu walipigwa.” “Basi akarudia nchi yake mwenye haya
ya uso.” 2 Wafalme 19:35; 2 Mambo ya Nyakati 32:21.
Malaika hutumwa kwenda kufanya kazi za rehema kwa wana wa Mungu. Kwa Ibrahimu, kuleta ahadi
nyingi zenye baraka; kwenye malango ya Sodoma, kumwokoa mwenye haki Lutu kutokana na
maangamizi ya moto yaliyoukabili mji ule; kwa Eliya, alipokuwa karibu ya kufa kwa uchovu na njaa
jangwani; kwa Elisha, pamoja na farasi na magari ya moto ili kuuzunguka pande zote mji mdogo adui
zake walikuwa wamemfungia; kwa Danieli, wakati anatafuta hekima ya mbinguni akiwa katika jumba la
kifalme la mfalme mshenzi, au alipoachwa awe chakula cha simba; kwa Petro, akikabiliwa na kifo
katika gereza la chini ya ardhi la Herode; kwa wafungwa kule Filipi; kwa Paulo na wenzake katika usiku
ule wa tufani walipokuwa baharini; kuufungua moyo wa Kornelio ili apate kuipokea injili; kumletea
298
Petro ujumbe wa wokovu kwa mgeni yule aliye mmataifa – kwa hiyo malaika watakatifu wamekuwa,
katika vizazi vyote, wakiwahudumia watu wa Mungu.
Malaika mlinzi ameteuliwa kwa ajili ya kila mfuasi wa Kristo. Walinzi hawa wa mbinguni huwakinga
wenye haki dhidi ya nguvu (513) za yule mwovu. Shetani mwenyewe alilitambua hilo wakati aliposema:
“Je! huyo Ayubu yuamcha BWANA bure? Wewe hukumzingira kwa ukingo pande zote, pamoja na nyumba
yake, na vitu vyote alivyo navyo?” Ayubu 1:9,10. Njia ambayo Mungu anatumia kuwalinda watu wake
imeelezwa kwa maneno mwimba zaburi: “Malaika wa BWANA hufanya kituo, akiwazungukia wamchao na
kuwaokoa.” Zaburi 34:7. Mwokozi alisema haya aliponena kuhusu wale wanaomwamini: “Angalieni
msidharau mmojawapo wa wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku
zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.” Mathayo 18:10. Malaika waliowekwa kuhudumia
watoto wa Mungu wana nafasi ya kufika mbele uwepo wa Mungu wakati wote.
Kwa hiyo watu wa Mungu, wanapokabiliwa na nguvu za udanganyifu za mkuu wa giza na ghadhabu yake
isiyolala usingizi, na wakiwa katika mapambano dhidi ya nguvu zote za uovu, wamehakikishiwa uongozi
usiokoma wa malaika wa mbinguni. Si kwamba uthibitisho huo unatolewa pasipo kuhitajika. Ikiwa Mungu
amewapa watoto wake ahadi ya neema na ulinzi, ni kwa sababu kuna nguvu kubwa za uovu za
kukabiliana nazo – nguvu hizo ni nyingi, zilizodhamiria, na zisizochoka, ambapo hakuna mtu awezaye
kubaki salama ikiwa hajui wala kuzingatia madhara yake na uwezo wake.
Pepo waovu, ambao mwanzo waliumbwa wakiwa hawana dhambi, walikuwa sawa na viumbe watakatifu
ambao ni wajumbe wa Mungu, wakifanana kwa tabia, uwezo, na utukufu. Lakini wakiwa wameanguka
kwa dhambi, wameunganishwa pamoja kwa kusudi la kumfedhehesha Mungu na kuwaangamiza
wanadamu. Wakiwa wamejiunga na Shetani katika uasi wake, na kutupwa pamoja naye kutoka
mbinguni, wameshirikiana naye, katika vizazi vyote, katika vita dhidi ya mamlaka ya Mungu. Katika
Maandiko tunaambiwa kuhusu mwungano wao na serikali yao, kuhusu ngazi mbalimbali za vyeo vyao,
kuhusu uwezo wao wa akili na werevu, na kuhusu mipango yao ya hila dhidi ya amani na furaha ya
wanadamu.
Historia ya Agano la Kale inaonyesha kutajwa mara kwa mara kwa uwepo wao na kazi zao; lakini ilikuwa
wakati Kristo alipokuwa duniani ambapo roho waovu walionyesha uwezo wao kwa namna ya
kustaajabisha. Kristo alikuwa amekuja kuingia (514) kwenye mpango uliobuniwa kwa ajili ya ukombozi
wa mwanadamu, na Shetani alikuwa ameazimia kuitetea haki yake ya kuutawala ulimwengu. Alikuwa
amefanikiwa kuanzisha ibada ya sanamu katika kila sehemu ya dunia hii isipokuwa katika nchi ya
Palestina. Katika nchi ile ambayo ilikuwa haijajisalimisha kikamilifu kutawaliwa na yule mjaribu, Kristo
alikuja kuwaangazia watu nuru ya mbinguni. Mahali hapa nguvu mbili zinazopingana zilidai utawala.
Yesu alikuwa ananyosha mikono yake ya upendo, akiwaalika wote ambao wangependa wapate msamaha
na amani ndani yake. Majeshi ya giza yalitambua kwamba hayakuwa na udhibiti usio na mipaka, na
walielewa kwamba utume wa Kristo ukifanikiwa, utawala wao ungefika mwisho muda si mrefu. Shetani
alighadhabika kama simba aliyefungwa minyororo na kwa ufidhuli wake alionyesha nguvu zake juu ya
miili na nafsi za wanadamu.
Ukweli kwamba watu wamekuwa wakipagawa na mapepo umeelezwa kwa uwazi katika Agano Jipya.
Watu walioteswa hivyo hawakuwa wanateseka kwa magonjwa yenye sababu za kawaida. Kristo alikuwa
na ufahamu kamili wa kile alichokuwa anashughulika nacho, na alitambua uwepo wa moja kwa moja wa
roho waovu na kazi zao.
Mfano halisi wa idadi yao, uwezo, na ghadhabu yao, na pia wa uwezo na rehema za Kristo, umetolewa
katika maelezo ya Maandiko ya kisa cha uponyaji wa watu wenye pepo wachafu katika nchi ya Wagerasi.
299
Wale watu waliochanganyikiwa akili, wakivishinda vifungo vyote walivyofungwa navyo, wakifurukuta na
kugaragara, wakitoa mapovu, wakiwa na hasira, walikuwa wanaijaza hewa kwa vilio, wakijidhuru
wenyewe kwa mabavu, na kuwahatirisha wote ambao wangeweza kuwakaribia. Miili yao iliyokuwa
inatokwa na damu na kuharibika na akili zao zilizokuwa zimevurugika vilifanya tamasha linalompendeza
sana mkuu wa giza. Mmojawapo wa mapepo hayo aliyetawala watu waliokuwa katika kusumbuliwa huko
alisema: “Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi.” Marko 5:9. Katika jeshi la Kirumi legioni iliundwa
na watu kuanzia elfu tatu hadi elfu tano. Majeshi ya Shetani pia yamekusanywa katika vikosi, na kikosi
kimoja kilichokuwa na mapepo yale kilikuwa na idadi isiyopungua legioni moja.
Kwa amri ya Yesu mapepo yaliwatoka wale waathirika, yakiwaacha wakiwa wamekaa kwa amani
miguuni pa Mwokozi, wakiwa wamenyenyekezwa, wenye akili timamu, na wapole. Lakini mapepo (515)
yaliruhusiwa kuliswaga kundi la nguruwe hadi baharini; na kwa wale wenyeji wa nchi ya Wagerasi,
hasara ya wale nguruwe ilikuwa na uzito mkubwa kuliko mibaraka ambayo Kristo alikuwa ameleta, na
Mponyaji yule wa mbinguni alishauriwa aondoke pale. Haya ni matokeo ambayo Shetani alipanga
kuyapata. Kwa kumtupia Yesu lawama ya hasara waliyopata, aliamsha hofu ya ubinafsi wa watu wale na
kuwazuia wasipate kuyasikiliza maneno ya Yesu. Wakati wote Shetani anawashtaki Wakristo kuwa
wanasababisha hasara, misiba, na mateso, badala ya kuiacha shutuma hiyo iangukie mahali inapostahili
- juu yake mwenyewe na mawakala wake.
Lakini makusudi ya Kristo hayakuzuiwa. Aliyaruhusu mapepo yaharibu kundi la nguruwe kama kemeo
kwa Wayahudi wale waliokuwa wanafuga wanyama hawa najisi kwa lengo la kujipatia faida. Kama
Kristo asingeyazuia yale mapepo, yasingetumbukiza baharini nguruwe tu bali pia na wachungaji wa
nguruwe na wawamiliki. Kule kuwahifadhi wachungaji na wamiliki kuliwezekana kwa uweza wake tu,
aliofanywa kwa huruma kwa ajili ya kuokolewa kwao. Zaidi ya hayo, tukio hili liliruhusiwa kutokea ili
wanafunzi wake wapate kushuhudia nguvu ya ukatili wa Shetani kwa mwanadamu na kwa wanyama.
Mwokozi alitaka wafuasi wake wamjue yule adui ambaye wangekabiliana naye, ili wasipate
kudanganyika na kushindwa kwa hila zake. Pia ilikuwa nia yake kwamba watu wa eneo lile waone uwezo
wake wa kuvivunjilia mbali vifungo vya Shetani na kuwaachilia huru wafungwa wake. Na ingawa Yesu
mwenyewe aliondoka pale, watu wale waliokuwa wameokolewa kwa maajabu, walibaki wakitangaza
rehema ya Mfadhili wao.
Matukio mengine yanayofanana na hilo yameandikwa katika Maandiko. Yule binti wa mwanamke
Msirofoinike alikuwa anasumbuliwa sana na mwovu, ambaye aliondolewa na Yesu kwa neno lake. (Marko
7:26-30). “Mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu” (Mathayo 12:22; kijana aliyekuwa na pepo bubu,
ambaye mara nyingi alikuwa “amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize” (Marko 9:17-27);
na mwenye wazimu yule ambaye, akiwa ameteswa na “roho ya pepo mchafu” (Luka 4:33-36), alivuruga
utulivu wa Sabato wa sinagogi kule Kapernaumu - wote hao (516) waliponywa kwa huruma za Mwokosi.
Karibu katika kila tukio, Kristo alimsema pepo kama kiumbe kilicho na akili, akimwamuru kumtoka mtu
aliyekuwa anateswa na asimtese tena. Waabudu waliokuwa Kapernaumu, wakiuona uwezo wake mkuu,
“mshangao ukawashika wote, wakasemezana wakisema, Ni neno gani hili, maana awaamuru pepo
wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka.” Luka 4:36.
Wale wanaopagawa na mapepo kwa kawaida huonekana kama wanateseka sana; hata hivyo kuna hali
tofauti na hiyo. Wengine walizikaribisha nguvu za kishetani kwa lengo la kupata uwezo wa kufanya
miujiza. Hao, kwa kweli, hawakuwa na mgogoro na hao pepo. Katika kundi hili walikuwemo wale
waliokuwa na roho ya uaguzi, - Simoni Mugus, Elima yule mchawi, na yule kijakazi aliyewafuata Paulo
na Sila kule Filipi.

300
Hakuna walio katika hatari kubwa ya kupagawa na mapepo kama wale ambao, licha ya kuwapo ushahidi
wa wazi na na wa kutosha kutoka katika Maandiko, wanakana uwepo na kazi za mwovu na malaika zake.
Kadiri tusivyozijua hila zao, wao wananufaika sana; watu wengi huzingatia mapendekezo yao
wanapodhani kwamba wanafuata maongozi ya hekima yao wenyewe. Hii ndiyo sababu, kadiri
tunavyokaribia mwisho wa wakati, wakati Shetani anapotazamiwa kufanya kazi yake kwa nguvu kubwa
sana kuwadanganya na kuwaangamiza, anaeneza kila mahali imani kwamba yeye hayupo. Ni mbinu yake
kujificha yeye mwenyewe na namna anavyofanya kazi.
Hakuna kitu ambacho mwongo mkuu huyu anaogopa sana kama hali ya sisi kufahamu mbinu zake. Katika
kuificha tabia yake halisi na makusudi yake vema, amewafanya watu wamwonyesha kwa namna ambayo
haiamshi hisia zenye nguvu dhidi yake ndani ya mioyo ya watu zaidi ya kuwafanya wacheke tu au
wazidharau habari zake. Anafurahishwa sana anapochorwa kwa picha za rangi akionyeshwa kama kitu
fulani cha kuchekesha au cha kuchukiza mno, kilichoumbika vibaya, nusu mnyama na nusu mtu.
Anapendezwa kusikia jina lake likitumika katika michezo na mizaha na wale wanaojifikiria kuwa wana
akili nyingi, na wanajua sana mambo.
(517) Ni kwa kuwa amejificha katika kinyago wa ustadi kiasi kwamba swali linaulizwa na wengi: “Je,
kiumbe kama huyo yupo kweli?” Ni ushahidi unaoonyesha mafanikio yake kwamba nadharia zinazosema
uongo dhidi ya ushuhuda ulio wazi wa Maandiko zinapokewa na watu wengi katika ulimwengu wa dini.
Na ni kwa sababu Shetani anaweza kudhibiti mioyo ya wasiojua ushawishi wake, ndiyo maana neno la
Mungu hutupatia mifano mingi ya kazi yake iletayo madhara kwa wanadamu, likifunua kwetu nguvu
zake, na kutufanya kuwa macho na mashambulio yake.
Uwezo na ubaya wa Shetani na jeshi lake ungetutisha ikiwa si kwa kupata hifadhi na wokovu katika
uweza mkuu wa Mkombozi wetu. Tunaimarisha usalama wa nyumba zetu kwa makomeo na makufuli ili
kulinda mali zetu na maisha yetu kutokana na watu waovu; lakini kwa nadira sana tunawafikiria malaika
waovu ambao wakati wote wanajitahidi kutupata, na ambao sisi hatuna njia za kujilinda na
mashambulio yao, kwa nguvu zetu. Wakiruhusiwa, wanaweza kuvuruga akili yetu, wanaleta maradhi na
mateso, wanaharibu mali zetu na uhai wetu. Furaha yao ni kutuletea taabu na maangamizi. Wana hali
ya kuogofya wale wanaopinga matakwa ya Mungu na kusalimu amri chini ya majaribu ya Shetani, mpaka
Mungu anawatoa ili watawaliwe na mapepo. Lakini wale wanaomfuata Kristo wako salama daima chini
ya utunzaji wake. Malaika wenye nguvu kuzidi wanatumwa kutoka mbinguni ili kuwalinda. Ibilisi hawezi
kuivunja ngome ambayo Mungu amewazungushia.

301
Sura ya 32
MITEGO YA SHETANI

Pambano kuu kati ya Kristo na Shetani, ambalo limeendelea kwa takribani miaka elfu sita, punde
litafungwa; na yule mwovu anazidisha jitihada zake maradufu ili kuishinda kazi ya Kristo kwa ajili ya
mwanadamu na kukaza kuwafunga watu katika mitego yake. Lengo analotaka kufikia ni kuwashikilia
watu gizani na kuwafanya wawe na mioyo migumu mpaka kazi ya Mwokozi ya upatanishi iishe, wakati
ambapo hakuna dhabihu tena kwa ajili ya dhambi.
Wakati ambapo hakuna jitihada maalum ya kuzipinga nguvu zake, kunapokuwa na hali ya kutojali ndani
ya kanisa na ulimwenguni, Shetani hashughuliki; maana hayuko katika hatari ya kupoteza wale
anaowashikilia mateka na kuwaendesha apendavyo. Lakini pindi mawazo yanapovutwa katika mambo ya
milele, na watu wanapouliza, “Nifanye nini ili nipate kuokoka?” hapo ndipo anapoingia uwanjani,
akijitahidi kutumia uwezo wake kinyume na uweza wa Kristo na kuupinga ushawishi wa Roho Mtakatifu.
Maandiko yanasema kwamba katika tukio fulani, wakati malaika wa Mungu walipokuja kujihudhurisha
mbele za Bwana, Shetani naye alikuja miongoni mwao (Ayubu 1:6), si kuja kusujudu mbele za Mfalme
wa Milele, bali kuendeleza mipango yake ya hila dhidi ya wenye haki. Kwa lengo hilo hilo anahudhuria
sasa pindi watu wa Mungu wanapokusanyika pamoja kwa ajili ya ibada kwa Mungu. Ingawa amefichika
asionekane kwa macho, anafanya kazi kwa bidii kuongoza mawazo ya watu wanaoabudu. Kama kiongozi
mwerevu wa vita, anaweka mipango kabla. Anapomwona mjumbe wa Bwana akisoma Maandiko,
anang’amua mada (519) itakayohubiriwa kwa watu. Kisha hutumia werevu na ujuzi wake wote kudhibiti
mambo ili ujumbe ule usiwafikie wale ambao amepanga kuwadanganya hapo. Yule ambaye ndiye
mhitaji mkubwa wa onyo la ujumbe huo atatakiwa kuwa katika shughuli fulani za miamala ambayo
inahitaji uwepo wake yeye mwenyewe, au kwa namna nyingine atazuiwa kusikia maneno yale ambayo
yangemhakikishia furaha ya uzima hadi uzima.
Tena, Shetani huwaona watumishi wa Bwana wakiwa wameelemewa na mzigo kwa sababu ya giza la
kiroho linawalofunika watu. Anayasikia maombi yao ya dhati wakihitaji neema ya mbinguni na nguvu ili
kuvunja hali ya kutojali, kutokuwa na uangalifu na uzembe. Ndipo kwa hamu iliyofanywa mpya
anatumia ustadi wake. Anawajaribu watu wajielekeze katika uchu wa kula na kunywa au katika namna
nyingine za kujifurahisha nafsi, na kwa njia hiyo anazitia ganzi fahamu zao hata wanashindwa
kupambanua mambo yale ambayo ndiyo mahitaji yao hasa.
Shetani anajua vema kwamba wale wote anaoweza kuwaongoza kupuuza maombi na kuchunguza
Maandiko, watashindwa katika mashambulio yake. Kwa hiyo anavumbua kila mbinu iwezekanayo
kuyashughulisha mawazo. Wakati wote kumekuwa na kundi la watu wanaodai kuwa wacha Mungu,
ambao, badala ya kufuatilia kuujua ukweli, wanafanya dini yao iwe ya kutafuta mapungufu fulani katika
tabia au dosari katika imani ya wale ambao hawakubaliani nao. Hao ni wasaidizi wa mkono wa kuume
wa Shetani. Washtaki wa ndugu si wachache, na wakati wote wako kazini pale Mungu anapotenda kazi
na watumishi wake wanapompa ibada ya kweli. Watatia rangi ya uongo katika maneno na matendo ya
wale wanaoupenda na kuutii ukweli. Wataonyesha kwamba watumishi wa Kristo wa dhati, wenye bidii,
na waliojikana nafsi ni watu ambao wamedanganyika au wadanganyaji. Kazi yao ni kueleza vibaya

302
mivuto ya kila tendo la kweli na nyoofu, kukuza na kueneza makosa, na kuamsha shuku ndani ya mioyo
ya wale wasiokuwa wakomavu katika mambo. Kwa kila njia inayoweza kufikirika watajaribu kukifanya
kile kilicho safi na cha haki kifikiriwe na watu kuwa ni kichafu na cha uongo.
Lakini hakuna haja ya mtu ye yote kudanganyika kuhusu watu hao. Inaweza kuonekana kwa urahisi
kwamba wao ni watoto wa nani, wanafuata kielelezo cha nani, na wanafanya kazi ya nani.
“Mtawatambua kwa (520) matunda yao.” Mathayo 7:16. Mwenendo wao unafanana na ule wa Shetani,
mharibifu mwenye ghadhabu, “mshtaki wa ndugu zetu.” Ufunuo 12:10.
Mdanganyaji mkuu ana mawakala wengi ambao wako tayari kufundisha upotofu wowote na wa kila aina
ili kunasa watu mtegoni - uzushi ulioandaliwa ili kufaa kukidhi matakwa na uwezo au nafasi za wale
ambao angeangamiza. Ni mpango wake kuingiza kanisani watu ambao si wanyofu na ni watu
wasiofanywa wapya ambao wataleta hali ya mashaka na kutokuamini, na kuwawekea vizuizi wale
wanaotamani kuona kazi ya Mungu ikisonga mbele na wanaotaka kusonga mbele pamoja nayo. Wengi
ambao hawana imani katika Mungu au katika neno lake wanazikubali baadhi ya kanuni za ukweli na
kupita kama Wakristo, hivyo huwezeshwa kuingiza mafundisho yao ya uongo kama vile ni mafundisho ya
Maandiko.
Msimamo kwamba kitu wanachoamini watu hakina madhara ni mmojawapo ya madanganyo ya Shetani
yenye mafanikio sana. Yeye anajua kwamba ukweli, ukipokelewa kwa moyo wa kuupenda, unatakasa
moyo wa yule anayeupokea; kwa hiyo anajitahidi daima kubadilisha na kuweka mahali pake nadharia za
uongo, hadithi za kutunga, injili nyingine. Tangu mwanzo watumishi wa Mungu wamepambana na
walimu wa uongo, si tu kwamba hao ni watu wabaya, bali ni wafundishaji wa uongo ambao una uwezo
wa kuifisha roho. Eliya, Yeremia na Paulo, kwa msimamo bila woga, waliwapinga wale waliokuwa
wanawageuza watu kuwatoa katika neno la Mungu. Ule uhuru unaoihesabu imani sahihi ya dini kuwa
haina umuhimu haukupata kuungwa mkono kabisa na walinzi watakatifu hawa wa ile kweli.
Fafanuzi za Maandiko zisizokuwa wazi na za kufikirika tu, na zile nadharia nyingi zinazogongana kuhusu
imani ya dini, ambazo zinapatikana katika ulimwengu wa Kikristo ni kazi ya adui yetu mkuu anayetaka
kuchanganya akili za watu ili wasipate kuutambua ukweli. Na mpishano na migawanyiko iliyopo
miongoni mwa makanisa katika ulimwengu wa Kikristo inasababishwa kwa sehemu kubwa na desturi
iliyopo ya kupotosha Maandiko ili yaendane na nadharia inayopendwa na watu. Badala ya kujifunza neno
la Mungu kwa makini na moyo wa unyenyekevu ili kupata kujua mapenzi ya Mungu, wengi hutafuta tu
kugundua kitu kisicho cha kawaida au kilicho kipya.
(521) Ili kuendeleza mafundisho ya uongo au desturi zisizokuwa za Kikristo, wengine hushikilia aya za
Maandiko zilizotenganishwa na muktadha wake, pengine wakinukuu nusu ya fungu katika kutoa hoja
yao, wakati sehemu iliyobaki ingeonyesha kwamba maana yake ni kinyume chake kabisa. Kwa werevu
wa nyoka wanajihami wenyewe katika maneno yaliyotenganishwa yanayofafanuliwa ili kukidhi matakwa
yao. Hivyo ndivyo wengi wanavyopotosha neno la Mungu kwa makusudi. Wengine, wanao hodari wa
mawazo ya kubuni, wanafuata lugha ya mifano na ishara ilivyotumika katika Maandiko Matakatifu,
wanatafsiri ili kukidhi mawazo yao, bila kujali sana ushuhuda wa Maandiko unaoonyesha kwamba
yanajitafsiri yenyewe, halafu wanafundisha mawazo yao yasiyo ya kweli kama vile ndiyo mafundisho ya
Biblia.
Wakati mtu anapoingia katika kujifunza Maandiko bila kuwa na roho ya maombi, ya unyenyekevu,
inayofundishika, aya zilizo wazi na nyepesi kabisa pamoja za zile zilizo ngumu sana vinapotoshwa mbali
kutoka katika tafsiri yake ya kweli. Viongozi wa upapa wanachagua zile sehemu za Maandiko zinazokidhi
vizuri kusudi lao, wanazifafanua ili zipate kuwafaa wao wenyewe, halafu wanafundisha watu mambo
303
hayo, wakati wanawanyima nafasi ya kujifunza Biblia na kuelewa kweli zake takatifu wao wenyewe.
Walipaswa kuwapa watu Biblia yote kama inavyosomeka. Ingekuwa heri kwao kutokuwa na mafundisho
yo yote ya Biblia kuliko kuwa na mafundisho ya Maandiko ambayo yamepotoshwa sana hivyo.
Biblia ilikusudiwa kuwa mwongozo kwa wote wanaotaka kuyajua mapenzi ya Muumba wao. Mungu
aliwapa wanadamu neno lake la unabii lililo imara; wale malaika na hata Kristo mwenyewe walikuja
kumjulisha Danieli na Yohana mambo ambayo hayana budi kuwako upesi. Yale mambo muhimu yahusuyo
wokovu wetu hayakuachwa katika hali ya fumbo. Hayakufunuliwa kwa njia ambayo ingeleta utata na
kumpotosha mtu mwaminifu anayetafuta ukweli. Bwana alisema kupitia kwa nabii Habakuki: “Iandike
njozi ukaifanye iwe wazi sana … ili asomaye apate kuisoma kama maji.” Habakuki 2:2. Neno la Mungu
liko wazi kwa wote wanaolisoma kwa (522) moyo wa maombi. Kila mtu aliye mnyofu wa kweli atakuja
kwenye nuru ya kweli. “Nuru imemzukia mwenye haki.” Zaburi 97:11. Wala hakuna kanisa linaloweza
kusonga mbele katika utakatifu isipokuwa kama waumini wake wanaitafuta ile kweli kwa dhati kama
hazina iliyositirika.
Kwa kelele zisemazo, Uhuru, watu wanapofushwa macho wasiweze kuziona hila za adui yao, wakati
yeye anafanya kazi wakati wote ili kulifikia lengo lake. Kadiri anavyofanikiwa kubadilisha na kuweka
maneno ya kufikirika ya wanadamu mahali pa Biblia, sheria ya Mungu huwekwa kando, na makanisa
yanakuwa chini ya utumwa wa dhambi huku yakijidai kuwa yako huru.
Kwa wengi, utafiti wa kisayansi umekuwa laana. Mungu ameruhusu mafriko ya nuru kumwagwa
ulimwenguni kwa njia ya ugunduzi wa kisayansi na sanaa; lakini hata watu wenye akili sana, ikiwa
hawaongozwi na neno la Mungu katika utafiti wao, wanachanganyikiwa katika jitihada zao za
kuchunguza uhusiano uliopo kati ya sayansi na mafunuo ya Mungu.
Maarifa ya mwanadamu kuhusu mambo yaonekanayo na yale ya kiroho ni ya sehemu tu na si makamilifu;
kwa hiyo wengi hawawezi kuhusianisha maoni yao ya sayansi na kauli za Maandiko. Wengi hukubali
nadharia na mambo yao ya kufikirika kwamba ni mambo ya kweli ya kisayansi, na wanadhani kamba
neno la Mungu linastahili lipimwe kwa mafundisho ya “sayansi iitwayo sayansi kwa uongo.” 1 Timotheo
6:20. Mwumbaji na kazi zake viko juu kupita uwezo wao wa kufahamu; na kwa kuwa hawawezi
kuyaeleza mambo haya kwa kutumia sheria za asili, basi historia ya Biblia huonekana kama kitu
ambacho hakiwezi kutumainiwa. Wale wanaoona mashaka kuhusu kuaminika kwa kumbukumbu zilizo
katika Agano la Kale na Agano Jipya mara nyingi wanakwenda hatua moja mbele kwenda katika kutilia
mashaka uwepo wa Mungu na huyapa maumbile ya asili uwezo wa Kimungu. Wakiisha kuachana na
nanga yao hiyo, wanabaki wanajigonga-gonga kwenye miamba ya udanganyifu.
Hivyo ndivyo wengi wanavyokuwa na makosa katika imani na kupotoshwa na mwovu. Wanadamu
wameazimia kuwa na hekima zaidi kuliko Muumba wao; falsafa ya kibinadamu imejitahidi kuchunguza
na kueleza siri ambazo kamwe hazitafunuliwa katika vizazi vyote milele. Ikiwa wanadamu
wangechunguza na kujua tu kile ambacho Mungu amefanya kijulikane kumhusu yeye na makusudi yake,
wangeona picha ya utukufu, ukuu, na uweza wa Yehova kiasi kwamba (523) wangetambua udogo wao
wenyewe na wangeridhika na kile ambacho kimefunuliwa kwa ajili yao na watoto wao.
Ni mbinu ya hali ya juu ya madanganyo ya Shetani kuyaweka mawazo ya wanadamu katika kutafiti na
kukisia kile ambacho Mungu hakufanya kijulikane na ambacho hakusudii kwamba tukijue. Kwa namna
hiyo Lusifa alipoteza mahali pake mbinguni. Hakuridhika kwa sababu hakufunuliwa siri zote za makusudi
ya Mungu, na hakuheshimu vya kutosha kile kilichokuwa kimefunuliwa kwake kuhusu kazi yake
mwenyewe katika wadhifa ule wa juu sana aliokuwa amepewa. Kwa kuamsha hali ile ile ya kutoridhika

304
ndani ya malaika waliokuwa chini mwelekeo wake alisababisha anguko lao. Sasa anajitahidi kuyajaza
mawazo ya wanadamu roho ile ile na kuwaelekeza pia katika wazidharau amri za Mungu zilizo dhahiri.
Wale ambao hawataki kuzikubali kweli za Biblia zilizo wazi, zinazochoma moyo, wanaendelea kutafuta
hadithi za uongo za kuwapendeza ambazo zitanyamazisha dhamiri. Kadiri mafundisho ya dini
yahubiriwayo yanavyozidi kuwa na kiwango cha chini cha mguso wa kiroho, kujikana nafsi, na
kujinyenyekeza, ndivyo yanavyopokelewa kwa upendeleo mkubwa zaidi. Watu hao wanahafifisha nguvu
zao za akili ili wapate kuzitumikia tamaa zao za mwili. Wakiwa wenye hekima katika kiburi chao
wenyewe kuliko kuyachunguza Maandiko kwa toba ya moyo na maombi ya dhati ili wapewe uongozi wa
Mungu, hawana kinga yoyote dhidi ya madanganyo. Shetani yuko tayari kuleta hamu ya moyo, halafu
anaingiza madanganyo yake mahali pa ukweli. Hivyo ndivyo upapa ulivyojipatia mamlaka yake juu ya
mawazo ya watu; na kwa kuukataa ukweli kwa sababu unahusisha msalaba, Waprotestanti wanaifuata
njia ile ile. Wote wanaopuuza neno la Mungu ili kujifunza yale wanayoona yanakubaliana na nafasi yao
na mashauri ya wanadamu, eti ili wasihitilafiane na ulimwengu, wataachwa wapokee uzushi mbaya
badala ya ukweli wa dini. Kila aina ya fundisho la uongo linalofikiriwa litapokelewa na wale ambao
wanakataa ukweli kwa makusudi. Yeye anayehofu kupokea danganyo moja atalipokea jingine kwa
urahisi. Mtume Paulo, akiongea kuhusu kundi la watu, ambao “hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate
kuokolewa” anasema: “Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; ili (524)
wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu.” 2
Wathesalonike 2:10-12. Tukiwa na onyo hilo mbele yetu ni juu yetu kuwa na hadhari kuhusu mafundisho
tunayopokea.
Miongoni mwa mbinu za mwovu zenye mafanikio makubwa zaidi ni mafundisho na maajabu ya uongo ya
umizimu. Akiwa amejifanya kuwa kama malaika wa nuru, anatandaza nyavu zake mahali ambapo
hazitiliwi shaka sana. Ikiwa watu wangejifunza Kitabu cha Mungu kwa maombi ya dhati ili ya kwamba
wakielewe, wasingeachwa gizani kupokea mafundisho ya uongo. Lakini wanapoukataa ukweli wanaishia
kuwa mateka katika madanganyo.
Upotofu mwingine wa hatari ni fundisho linalokana uungu wa Kristo, likidai kwamba yeye hakuwako
kabla ya kuja kwake duniani. Nadharia hii imepokelewa na kupendwa na kundi kubwa la wale wanaodai
kuiamini Biblia; lakini inakinzana moja kwa moja na kauli za wazi alizotoa Mwokozi wetu kuhusu
uhusiano wake na Baba, tabia yake ya uungu, na kuwako kwake kabla. Haiwezi kuzingatiwa bila
kuyapotosha Maandiko kwa namna ambayo hairuhusiwi. Hali hiyo si tu kwamba inashusha ufahamu wa
mwanadamu kuhusu kazi ya ukombozi, bali pia inadhoofisha imani katika Biblia kama mafunuo yatokayo
kwa Mungu. Wakati hali hii inaleta hatari zaidi, inafanya pia iwe vigumu zaidi kukabiliana nayo. Ikiwa
watu wanaukataa ushuhuda wa Maandiko yenye uvuvio kuhusu uungu wa Kristo, basi, ni kazi bure
kuhojiana nao; maana hakuna hoja, hata iwe ya kuhitimisha vizuri, inayoweza kuwashawishi. “Basi
mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala
hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.” 1 Wakorintho 2:14. Hakuna mtu
anayeshikilio fundisho hili la uongo anayeweza kuwa na mawazo sahihi kuhusu tabia au utume wa
Kristo, au kuhusu mpango mkuu wa Mungu kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu.
Bado fundisho jingine la uongo linalosumbua ni imani inayoenea haraka kwamba Shetani si kitu halisi
ambacho kipo, kwamba jina hilo hutumika tu katika Maandiko kuelezea mawazo machafu ya watu na
shauku zao.
(525) Fundisho linalotoa mwangwi sana kutoka katika mimbara zilizo maarufu miongoni mwa watu,
kwamba kuja kwa Kristo mara ya pili ni kuja kwake kwa kila mtu wakati anapokufa, ni mbinu ya

305
kugeuza mawazo ya watu yasielekee katika kuja kwake halsi katika mawingu ya mbinguni. Kwa miaka
mingi Shetani amekuwa akisema, “Tazama, …yumo nyumbani” (Mathayo 24:23-26); na watu wengi
wamepotea kwa kukubali uongo huo.
Tena, hekima ya ulimwengu hufundisha kwamba maombi si ya lazima. Watu wa sayansi wanadai
kwamba haiwezekani kuwa na jibu halisi la maombi; kwamba jambo hilo lingekuwa ni kukiuka sheria ya
asili, ni mwujiza, na kwamba miujiza haipo katika maisha. Katika malimwengu, wanasema wao, vitu
vinatawaliwa na sheria mahsusi zisizobadilika-badilika, na Mungu mwenyewe hafanyi jambo lo lote
kinyume cha sheria hizo. Kwa hiyo wanamwonyesha Mungu kama amefungwa na sheria zake mwenyewe
- kana kwamba utendaji wa sheria za Mungu unaweka mbali uhuru wa Mungu. Fundisho kama hilo
linapingana na ushahidi wa Maandiko. Je, miujiza haikutendwa na Kristo na mitume wake? Mwokozi yule
yule mwenye huruma anaishi leo, na yuko tayari kusikiliza maombi ya imani kama ilivyokuwa wakati ule
alipotembea akionekana miongoni mwa watu. Mambo ya kawaida ya asili yanashirikiana na mambo ya
rohoni yasiyo ya kawaida. Ni sehemu ya mpango wa Mungu kutupatia, kama majibu ya maombi ya imani,
kile ambacho asingeweza kutoa kama tusingekuwa tumeomba hivyo.
Mafundisho yenye makosa na mawazo ya kudhania tu yanayokubalika miongoni mwa makanisa ya
ulimwengu wa Kikristo hayahesabiki. Ni vigumu kabisa kukadiria matokeo maovu ya kuondoa moja ya
mawazo muhimu yaliyowekwa na neno la Mungu. Ni wachache wanaothubutu kufanya hilo wakaishia
kuukataa ukweli mmoja tu. Walio wengi huendelea kuweka kando misingi ya ukweli mmoja baada ya
mwingine, mpaka wanakuwa makafiri hasa.
Mafundisho potofu ya thiolojia maarufu yamesukuma wengi na kuwafanya mtu mwenye imani ya
kushuku, ambaye vinginevyo, angekuwa muumini wa Maandiko. Ni jambo gumu kwake kukubali
mafundisho yanayopita uelewa wake kuhusu haki, rehema, na wema; na kwa kuwa haya yanaonyeshwa
kama mafundisho ya Biblia, anakataa kuipokea Biblia kama neno la Mungu.
(526) Na hili ndilo lengo ambalo Shetani anajitahidi kulifikia. Hakuna kitu anachokitamani sana kama
kuharibu imani ya watu kwa Mungu na katika neno lake. Shetani anasimama mbele ya jeshi kubwa la
wenye mashaka, na anafanya kazi kwa uwezo wake wote kuwadanganya watu waingie katika jeshi lake.
Kuwa na mashaka kumekuwa jambo la mtindo. Kuna kundi kubwa ambalo linaangalia neno la Mungu kwa
mashaka kwa sababu ile ile iliyotumiwa kwa Mwasisi wake - kwa sababu linakemea na kuhukumu
dhambi. Wale wasiotaka kuyatii matakwa yake wanatafuta kupindua mamlaka yake. Wanasoma Biblia,
au kusikiliza mafundisho yake yanayohubiriwa kutoka katika mimbara, ili tu kutafuta kosa katika
Maandiko au katika mahubiri hayo. Si wachache wanaogeuka kuwa makafiri ili kuhalalisha au kutafuta
udhuru wa kupuuza jukumu. Wengine huchukua kanuni za imani ya kushuku kutokana na kiburi na
uzembe. Wakiwa watu wanaopenda raha kiasi kwamba hawawezi kujipambanua kwa kufanya jambo lo
lote linalostahili heshima, linalohitaji juhudi na kujikana, wanaamua kutafuta kujipatia sifa ya kuwa na
hekima kwa kuikosoa Biblia. Yapo mengi ambayo mawazo finyu ya mwanadamu, yasipotiwa nuru kwa
hekima ya mbinguni, hayana uwezo wa kuyafahamu; na kwa njia hiyo wao wanatafuta kuyakosoa. Wapo
wengi wanaoonekana kama wanaona vema kusimama upande wa kutoamini, kushuku, na ukafiri. Lakini
chini ya mwonekano huo wa unyofu itakutwa kwamba watu kama hao wanasukumwa na haki ya
kujitumainia wenyewe na kiburi. Wengi hufurahi katika kupata katika Maandiko kitu fulani cha
kutatanisha mawazo ya wengine. Baadhi wanakosoa na kutoa sababu upande usio sahihi mwanzoni,
kutokana tu na kupenda mabishano. Hawatambui ya kwamba kwa njia hiyo wanajitia katika mtego wa
mwindaji. Lakini wakishakuonyesha kutoamini kwao wazi wazi, wanajisikia kwamba ni lazima
waendeleze msimamo wao huo. Hivyo wanajiunga na waovu na kujifungia malango ya Paradiso.

306
Mungu ametupatia katika neno lake ushahidi wa kutosha kuonyesha kwamba lina tabia takatifu. Kweli
kuu zinazohusu ukombozi wetu zimeelezwa wazi. Kwa msaada wa Roho Mtakatifu, ambaye ameahidiwa
kutolewa kwa wote wanaomtafuta kwa unyofu wa moyo, kila mtu anaweza (527) kuzielewa kweli hizo
yeye mwenyewe. Mungu amewapatia wanadamu msingi imara ambao juu yake wanapaswa kuiweka
imani.
Lakini bado mawazo finyu ya wanadamu hayatoshi kuweza kuelewa kwa ukamilifu mipango na makusudi
ya Mungu asiye na mpaka. Hatuwezi kumwona Mungu kwa kutafiti. Tusijaribu kufunua pazia linalouficha
ukuu wake kwa mikono yenye kiburi. Mtume anasema kwa mshangao: “Hukumu zake hazichunguziki,
wala njia zake hazitafutikani!” Warumi 11:33. Mpaka hapa tunaweza kufahamu matendo yake kwetu, na
makusudi yake yanayomsukuma kututendea hivyo, hata kutuwezesha kutambua upendo wake usio na
mipaka pamoja na rehema zake, mambo ambayo yamefungamana na uweza wake usio na kikomo. Baba
yetu aliye mbinguni anapanga utaratibu wa kila kitu kwa hekima na haki, na sisi hatupaswi kuwa katika
hali ya kutoridhika au kutoamini, bali kupiga magoti kwa kicho na kutii. Yeye atatufunulia wingi wa
makusudi yake kwa kiasi kilicho chema kwetu kufahamu, na zaidi ya hapo lazima tuamini Mkono ule
wenye uweza wote, Moyo ule uliojaa upendo.
Wakati Mungu ametoa ushahidi wa kutosha kwa ajili ya imani, hataondoa kamwe visingizio vyote vya
kutokuamini. Wote wanaotafuta mahali pa kushikiza mashaka yao watapapata. Na wale wanaokataa
kukubali na kutii neno la Mungu mpaka pale kila kikwazo kitakapokuwa kimeondolewa, wakati ambapo
hakuna tena uwezekano wa mashaka, hawatakuja kwenye nuru kamwe.
Kutokumwamini Mungu ni matokeo ya asili ya moyo ambao haujafanywa upya, ambao uko katika uadui
na Mungu. Lakini imani inaletwa na Roho Mtakatifu, na inasitawi tu inapothaminiwa. Hakuna mtu
anayeweza kuwa na imani yenye nguvu pasipo kufanya juhudi ya kudhamiria. Hali ya kutoamini
inaimarika inapoendelezwa, na pale watu wanapojiruhusu kuwa na mashaka na kukosoa pasipo sababu
ya msingi, badala ya kujikita katika vithibitisho ambavyo vimetolewa na Mungu ili kuimarisha imani yao,
watakuta kwamba mashaka yao yanaendelea kukubalika zaidi.
Lakini wale wanaozionea mashaka ahadi za Mungu na kuacha kuamini uthibitisho wa neema yake
wanaonyesha kutomheshimu; na mvuto wao una tabia ya kuwasukuma (528) wengine kwenda mbali na
Kristo, badala ya kuwavuta kwenda kwake. Hao ni miti isiyozaa, ambayo inatandaza matawi yake ya
giza kwa marefu na mapana, yakizuia mwanga wa jua usifikie mimea mingine, na kuifanya idhoofike na
kufa ikiwa chini ya kivuli cha baridi. Kazi ya maisha ya watu hao itajitokeza kama ushahidi usiokoma
dhidi yao. Wanapanda mbegu za kutokusadiki na kushuku ambazo zitazaa mavuno yake ya hakika.
Kuna njia moja tu ya kufuatwa na wale ambao kwa unyofu wao wa moyo wanatamani kuwekwa huru na
mashaka. Badala ya kuhoji na kupinga kile wasichoelewa, hebu na wazingatie nuru ambayo tayari
inawaangazia, halafu watapokea nuru kubwa zaidi. Hebu na wafanye kila jukumu lililowekwa wazi
katika ufahamu wao, nao watawezeshwa kuelewa na kutenda yale ambayo kwa sasa wanayaonea
mashaka.
Shetani anaweza kuonyesha kitu cha bandia kinachofanana sana na ukweli kwa karibu kiasi kwamba
kinawadanganya wale wanaohiari kudanganywa, wanaotamani kukwepa kujikana nafsi na kujitoa
kunakotakiwa na ukweli; lakini haiwezekani kwake kumshikilia katika mamlaka yake mtu anayetamani
kwa dhati kuujua ukweli kwa gharama yoyote ile. Kristo ndiye kweli na ndiye “Nuru … amtiaye nuru kila
mtu, ajaye katika ulimeengu.” Yohana 1:9. Roho wa kweli ametumwa kuwatia watu katika kweli yote.
Na kwa mamlaka ya Mwana wa Mungu tangazo linatolewa: “Tafuteni, nanyi mtaona.” “Mtu akipenda
kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo.” Mathayo 7:7; Yohana 7:17.
307
Wafuasi wa Kristo wanajua kidogo tu mipango mibaya ambayo Shetani na majeshi yake wanaandaa dhidi
yao. Lakini Yeye aketiye mbinguni atazishinda mbinu hizo zote ili kuyatimiza makusudi yake ya kina.
Mungu anaruhusu watu wake kupatwa na moto wa majaribu, si kwa sababu anafurahia maudhi na
mateso yao, bali kwa sababu huo ni mchakato wa muhimu kwa ajili ya ushindi wao wa mwisho.
Kulingana na utukufu wake, asingeweza kuwakinga wasipatwe na majaribu; maana lengo hasa la
majaribu hayo ni kuwatayarisha ili wapate kuvipinga vishawishi vyote vya uovu.
(529) Si wanadamu waovu wala mashetani wawezao kuizuia kazi ya Mungu, au kumzuia Yeye kuwa
pamoja na watu wake, ikiwa wanakiri na kuachana na dhambi zao, kwa mioyo iliyonyenyekezwa na
kupondeka, na kuzidai ahadi zake kwa imani. Kila jaribu, kila ushawishi wa ulio kinyume, iwe kwa wazi
au kwa siri, unaweza kupingwa kwa ufanisi, “Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho yangu,
asema BWANA wa majeshi.” Zekaria 4:6.
“Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake husikiliza maombi yao…. Naye ni nani
atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?” 1 Petro 3:12,13. Wakati Balaamu, akiwa
amevutiwa na ahadi ya kupewa zawadi nono, alipofanya uchawi kwa Israeli, na kwa sadaka zake kwa
Bwana alitafuta kuwalaani watu hawa wa Mungu, Roho wa Mungu alimkataza kutenda uovu ule aliotaka
kuutamka, na Balaamu alilazimishwa kusema: “Nitamlaanije, yeye ambaye Mungu hakumlaani?
Nimshutumuje, yeye ambaye BWANA hakumshutumu?” “Na nife kifo cha mwenye haki, na mwisho
wangu uwe mfano wa mwisho wake!” Wakati sadaka nyingine ilipokuwa imetolewa, nabii huyu mwovu
alitangaza: “Tazama, nimepewa amri kubariki, Yeye amebariki, nami siwezi kulitangua. Hakutazama
uovu katika Yakobo, wala hakuona ukaidi katika Israeli. BWANA, Mungu wake, yu pamoja naye, na sauti
kuu ya mfalme i katikati yao.” “Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, wala hapana uganga juu ya
Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!” Hata hivyo,
kwa mara ya tatu madhabahu zikajengwa, na tena Balaamu akafanya bidii ya kuwalaani. Lakini kutoka
katika midomo isiyotaka ya yule nabii, Roho wa Mungu akatangaza usitawi wa wateule wake, na
kukemea upumbavu na nia mbaya ya kuwadhuru waliyokuwa nayo wale maadui zao: “Na abarikiwe kila
akubarikiye, na alaaniwe kila akulaaniye.” Hesabu 23:8,10,20,21,23; 24:9.
Wakati huo Waisraeli walikuwa watiifu kwa Mungu; na kwa kadiri walivyoendelea kuwa watiifu kwa
sheria yake Mungu, hakuna mamlaka duniani wala kuzimuni ambayo ingefanikiwa dhidi yao. Lakini laana
ile ambayo Balaamu hakuruhusiwa kutamka dhidi ya (530) watu wa Mungu, alifanikiwa hatimaye kuileta
kwa watu wa Mungu wale kwa kuwashawishi kuingia dhambini. Walipozivunja amri za Mungu,
walijitenga mbali naye, na waliachwa waskie nguvu ya mwenye kuharibu.
Shetani anatambua vizuri kwamba mtu mmoja aliye dhaifu kuliko wote ndani ya Kristo ana uwezo zaidi
ya majeshi ya giza, na ya kwamba, kama yeye mwenyewe angejionyesha waziwazi, angekabiliwa kabisa
na kupingwa. Kwa hiyo anajitahidi kuwavuta askari wa msalaba mbali na ngome yao imara, wakati
anavizia akiwa na majeshi yake, tayari kuwaangamiza wote wanaothubutu kuingia katika uwanja wake.
Ni kwa kumtegemea Mungu tu kwa unyenyekevu, na kuzitii amri zake zote, ndipo tunaweza kuwa
salama.
Hakuna mtu yuko salama hata kwa siku moja au kwa saa moja pasipo maombi. Yatupasa kumsihi Bwana
hasa ili atupatie hekima ya kulielewa neno lake. Humo ndimo zimefichuliwa hila za mjaribu na njia
zinazoweza kutumiwa kumpinga. Shetani ni mtaalam katika kunukuu Maandiko, akiweka tafsiri yake
mwenyewe katika aya, ambapo kwa hizo anatumaini kutufanya tujikwae. Lazima tujifunze Biblia kwa
unyenyekevu wa moyo, pasipo kupoteza kamwe kuona umuhimu wa kumtegemea Mungu. Wakati

308
tunatakiwa kuwa macho wakati wote dhidi ya mitego ya Shetani, inatupasa kuomba kwa imani daima
kwamba: “Usitutie majaribuni.”

309
Sura ya 33
UDANGANYIFU MKUU WA KWANZA
Tangu historia ya kale ya mwanadamu, Shetani alianza jitihada zake za kuidanganya jamii yetu ya
wanadamu. Yeye aliyekuwa amechochea maasi mbinguni alitaka kuwafanya wakazi wa dunia hii
waungane naye katika vita yake dhidi ya serikali ya Mungu. Adamu na Hawa walikuwa na furaha kamilifu
katika utii wao kwa sheria ya Mungu, na hali hii ilikuwa ni ushuhuda wa wakati wote dhidi ya madai
ambayo Shetani alikuwa ameyatoa mbinguni, kwamba sheria ya Mungu ilikuwa ya ukandamizaji na
ilipingana na usitawi wa viumbe vyake. Na zaidi, wivu wa Shetani uliamshwa alipotazama makazi mazuri
yaliyokuwa yameandaliwa kwa watu wale wawili wasio na dhambi. Aliazimu kusababisha anguko lao, ili,
akishawatenga mbali na Mungu na kuwaleta chini ya mamlaka yake, apate umiliki wa dunia na
kuanzisha ufalme wake hapa katika kumpinga Aliye Juu.
Ikiwa Shetani angekuwa amejifunua katika tabia yake halisi, angekuwa amekataliwa mara moja, maana
Adamu na Hawa walikuwa wamekwisha kuonywa kuhusu adui huyu wa hatari; lakini alifanyia kazi yake
gizani, akilificha kusudi lake ili kwa ufanisi zaidi apate kutimiza lengo lake. Akimtumia nyoka kama njia
yake, wakati ule nyoka akiwa kiumbe aliyekuwa na mwonekano wa kuvutia sana, alizungumza na Hawa,
akisema: “Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?” Mwanzo 3:1.
Kama Hawa angejizuia asiingie katika majadiliano na mjaribu, angesalimika; lakini yeye aliamua
kujadilianan naye akaanguka na kuwa mhanga wa (532) hila zake. Ni kwa njia kama hiyo wengi bado
wanashindwa. Wanaingiwa na mashaka na kutoa hoja kuhusu matakwa ya Mungu; na badala ya kutii
amri za kimbingu, wanakubali nadharia za wanadamu, ambazo zimeficha tu hila za Shetani.
“Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio
katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia
mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti
huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” Fungu la 2 hadi la
5. Aliwatangazia kwamba wangekuwa kama Mungu wakiwa na hekima nyingi sana kuliko kabla na kuwa
na uwezo wa kuishi maisha ya hali ya juu zaidi. Hawa akaingia katika jaribu lile; na kwa njia ya
ushawishi wake, Adamu aliingizwa dhambini. Waliyakubali maneno ya yule nyoka, kwamba Mungu
hakumaanisha alichokisema; hawakumsadiki Muumba wao na wakadhania kwamba alikuwa anawawekea
mipaka ya uhuru wao na ya kwamba wangepata hekima kubwa na kutukuzwa zaidi kwa kuivunja sheria
yake.
Lakini Adamu, baada ya kutenda dhambi, aligundua kuwa ni nini maana ya maneno, “Kwa maana siku
utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika?” Je, aliona aliona yakiwa na maana, kama Shetani
alivyomshawishi kuamini, kwamba angeingia katika hali ya juu zaidi ya maisha? Kama ndivyo basi
kulikuwa na faida kubwa iliyopatikana kwa kuvunja sheria ya Mungu, na Shetani alithibitishwa kuwa
mfadhili wa wanadamu. Lakini Adamu hakuona kwamba hiyo ndiyo ilikuwa maana ya hukumu ya Mungu.
Mungu alitangaza kwamba, kama adhabu kwa dhambi zake, mwanadamu angepaswa kurudi mavumbini
alikotwaliwa. “Kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.” Fungu la 19. Maneno ya
Shetani kwamba, “mtafumbuliwa macho,” yalionekana kuwa ya kweli kwa maana hii moja tu: baada ya
Adamu na Hawa kumwasi Mungu, macho yao yalifumbuliwa na kutambua upumbavu wao; walijua uovu,
na walionja matokeo machungu ya uasi.
310
Katikati ya Edeni uliota mti wa uzima, ambao matunda yake yalikuwa na uwezo wa kuendeleza uhai.
Kama Adamu angebaki kuwa (533) mtiifu kwa Mungu, angeendelea kufurahia uhuru wa kuufikia mti huu
na angekuwa ameishi milele. Lakini alipotenda dhambi alitengwa mbali asipate kula matunda ya mti wa
uzima, naye akawa mhanga wa mauti. Hukumu ya Mungu, “U mavumbi wewe, na mavumbini utarudi,”
huonyesha kukoma kabisa kwa maisha.
Uhai wa kutokufa, ambao ulikuwa umeahidiwa kwa mwanadamu kwa sharti la utii, ulikuwa umepotezwa
kwa ukiukaji wa maagizo. Adamu asingeweza kurithisha kwa wazao wake kile ambacho hakuwa nacho;
wala pasingekuwapo na tumaini lolote kwa wanadamu walioanguka kama Mungu, kwa kutoa kafara ya
Mwana wake, asingewaletea uzima wa milele karibu yao. Wakati “mauti ilipowafikia watu wote kwa
sababu wote wamefanya dhambi,” Kristo ameufunua “uzima na kutokuharibika, kwa ile injili.” Warumi
5:12; 2 Timotheo 1:10. Tena katika Kristo peke yake uzima wa milele unaweza kupatikana. Yesu
alisema: “Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima.” Yohana
3:36. Kila mtu anaweza kuwa na mbaraka huu usio na bei kama atatimiza masharti. Wote “wale ambao
kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika,” watapewa “uzima
wa milele.” Warumi 2:7.
Mmoja tu aliyemwahidi Adamu uzima katika kutotii ni yule mdanganyaji mkuu. Na tamko la nyoka kwa
Hawa mle Edeni – “Hakika hamtakufa” - lilikuwa hubiri la kwanza kutolewa kuhusu kutokufa kwa nafsi.
Lakini, tangazo hilo, likijengwa juu ya mamlaka ya Shetani, linasikia kutoka katika mimbara za
ulimwengu wa Kikristo, na linapokelewa na watu wengi miongoni mwa wanadamu kwa urahisi kama
lilivyopokelewa na wazazi wetu wa kwanza. Hukumu ya Mungu, “Roho itendayo dhambi, ndiyo
itakayokufa” (Ezekieli 18:20), imefanywa iwe na maana: Roho itendayo dhambi, haitakufa, bali itaishi
milele. Hatuna la kufanya ila kushangaa jinsi kupumbazika akili kwa ajabu kunavyowafanya watu
kuyaamini maneno ya Shetani na kutoamini maneno ya Mungu.
Ikiwa mwanadamu angeruhusiwa kuwa huru kuuendea mti (534) wa uzima baada ya anguko lake,
angekuwa anaishi milele; na kwa njia hiyo dhambi ingefanywa kuwa ya milele. Lakini makerubi na
upanga wa moto uliogeuka huku na huko viliilinda ile “njia ya mti wa uzima” (Mwanzo 3:24), wala
hakuna hata mmoja katika jamaa ya Adamu aliyeruhusiwa kukipita kizuizi kile na kula tunda liletalo
uzima. Kwa hiyo hakuna mwenye dhambi yeyote aishiye milele.
Lakini baada ya Anguko, Shetani aliwaagiza malaika zake kufanya jitihada maalum kuwafundisha
wanadamu imani isemayo kwamba mwanadamu kwa asili yake anao uhai usio na mwisho; na wakisha
kuwashawishi wanadamu kulipokea fundisho hilo la uongo, walitakiwa kuwafanya wanadamu watoe
hitimisho kwamba mwenye dhambi ataishi katika mateso ya milele na milele. Kwa hiyo, mkuu wa giza,
akifanya kazi kupitia kwa mawakala wake, anamwonyesha Mungu kuwa mtawala katili mwenye visasi,
akisema kwamba anawatupa jehanum wale wote wasiompendeza, na kuwafanya wapate kuionja
ghadhabu yake daima; na kwamba wakati wanapoendelea kupata maumivu makali sana yasiyoelezeka
na kugaagaa katika ndimi za moto wa milele, Mwumbaji wao anawachungulia chini waliko kwa
kuridhika.
Hivyo mwovu anatumia sifa za tabia yake mwenyewe kuzivika kwa tabia ya Mwumbaji na Mruzuku wa
wanadamu. Ukatili ni sifa ya kishetani. Mungu ni upendo; na vitu vyote alivyoviumba vilikuwa safi,
vitakatifu, na vyenye upendo, mpaka pale dhambi ilipoingizwa na mwasi huyo mkuu wa kwanza. Shetani
mwenyewe ndiye adui anayemjaribu mwanadamu kutenda dhambi, halafu anamwangamiza akiweza; na
anapohakikisha kwamba amempata mhanga wake, ndipo anaposhangilia sana kwa maangamizi aliyoleta.
Kama angeruhusiwa, angeweza kuswaga wanadamu wote na kuwaingiza katika wavu wake. Isingekuwa

311
ni kule kuingilia kati kwa uweza wa Mungu, hakuna mwana au binti yeyote wa Adamu ambaye angeweza
kuponyoka.
Shetani anatafuta kuwashinda wanadamu leo, kama alivyowashinda wazazi wetu wa kwanza, kwa
kutikisa ujasiri wao kwa Muumba wao na kuwafanya watilie mashaka hekima ya serikali yake na haki ya
sheria zake. Shetani na wajumbe wake humweleza Mungu kuwa ni mbaya hata kuliko wao wenyewe, ili
kuhalalisha nia yao ovu na uasi wao. Mdanganyifu mkuu anajitahidi kuhamisha tabia yake mwenyewe
iliyojaa ukatili wa kutisha kuipeleka kwa Baba yetu wa mbinguni, ili kujifanya aonekane kama ndiye
aliyetendewa vibaya kwa kufukuzwa toka mbinguni kwa sababu ya kushindwa kumtii mtawala dhalimu
namna hiyo. Anaonyesha mbele ya (535) ulimwengu uhuru ambao wangefurahia chini ya utawala wake
usio na ukali, tofauti na utumwa unaoletwa na maagizo makali ya Yehova. Hivyo anafanikiwa
kuwashawishi watu kwenda mbali na utii kwa Mungu.
Linachukiza jinsi gani kwa kila hisia ya upendo na huruma, na hata kwa ufahamu wetu wa haki, fundisho
lisemalo kwamba waovu waliokufa wanateswa kwa moto na kiberiti katika jehanum inayowaka moto
milele na milele; kwamba kwa dhambi za muda mfupi wa maisha yao duniani wanapaswa kuteswa kwa
muda wote kadiri Mungu atakavyoendelea kuwako. Hata hivyo, fundisho hilo limefundishwa katika
maeneo mengi na bado liko miongoni mwa misingi ya imani katika ulimwengu wa Kikristo. Daktari
mmoja msomi wa dini alisema: “Mwonekano wa mateso makali ya kuzimu utaongeza furaha ya
watakatifu milele na milele. Wanapowaona wengine wenye asili moja na wao na waliozaliwa katika hali
kama yao, wakiwa wametupwa katika mateso yale, na wao wakiwa wametenganishwa nao hivyo, jambo
hili litafanya kutambua jinsi walivyo na furaha.” Mwingine alitumia maneno haya: “Wakati amri ya
hukumu inapoendelea kutekelezwa milele na milele juu ya vyombo vya ghadhabu, moshi wa maumivu
yao utakuwa ukipanda juu milele hata milele ukionwa na vyombo vya rehema, ambao, badala ya
kushiriki na wale wanaoteseka, watasema, Amina, Haleluya! Msifuni Bwana!”
Fundisho la namna hiyo linapatikana wapi katika kurasa za neno la Mungu? Je, kule mbinguni
waliokombolewa watakuwa wamepoteza hisia zote za huruma na upendo, hata hisia za ubinadamu wa
kawaida? Je, hizi zitabadilishwa kuwa mtu asiye na hisia kabisa za huzuni wala maumivu au
zitabadilishwa kuwa za ukatili usio na huruma kabisa? Hapana, hapana; hayo si mafundisho ya Kitabu
cha Mungu. Wale wanaofundisha maoni yaliyoelezwa katika dondoo hizo zilizoonyeshwa hapo juu
huenda wakawa ni wasomi sana na hata kuwa watu walio wanyofu wa moyo, lakini wamedanganywa na
hila za Shetani. Anawaongoza kuelewa isivyo maana ya semi zenye nguvu za Maandiko, akiipa lugha
rangi ya uchungu na nia mbaya ambayo ni yake yeye mwenyewe, lakini si ya Mwumbaji wetu. “Kama
mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na
kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa,
Enyi nyumba ya Israeli?” Ezekieli 33:11.
(536) Mungu angepata faida gani ikiwa tungekubali kwamba anafurahia kuona mateso yasiyokoma;
kwamba anaburudishwa na kilio cha maumivu na yowe na kulaani kwa viumbe wanaoteswa ambao
anawashikilia katika ndimi za moto wa kuzimu? Je, sauti hizi zisizopendeza zinaweza kuwa muziki
mtamu katika sikio lake yeye aliye mwenye Pendo la Milele? Inasisitizwa nao kwamba kupatilizwa kwa
mateso yasiyokoma kwa waovu kungeonyesha chuki ya Mungu dhidi ya dhambi kama uovu unaoharibu
amani na utulivu wa malimwengu. Lo! Makufuru ya kutisha! Ni kama vile chuki ya Mungu dhidi ya
dhambi ndiyo sababu ya kuendelezwa kwa mateso. Kwa maana, kulingana na mafundisho ya
wanathiolojia hawa, mwendelezo wa mateso bila kuwapo tumaini la rehema huwatia wazimu wale
wahanga waovu, na wanapomwaga hasira zao kwa kulaani na kukufuru, wanaendelea kuongeza mzigo

312
wao wa hatia milele. Utukufu wa Mungu hauletwi kwa kudumisha hivyo hali ya kuendelea kuiongeza
dhambi kwa vizazi visivyokoma.
Kukadiria uovu ambao umeletwa na uzushi kuhusu mateso ya milele kuko nje ya uwezo wa akili ya
mwanadamu. Dini ya Biblia, iliyojaa upendo na fadhili, na ikiwa na huruma nyingi, inatiwa giza kwa
upotoshaji huo na imevikwa vazi la kitisho. Je, tunapofikiria jinsi ambavyo Shetani ameipaka rangi za
uongo tabia ya Mungu, tunaweza kushangaa kuona Mwumbaji wetu mwenye rehema nyingi
anavyoogopwa, anavyohofiwa sana, na hata kuchukiwa? Mitazamo ya kutisha kuhusu Mungu ambayo
imeenea kote ulimwenguni kutokana na mahubiri yanayotolewa katika mafundisho ya mimbarani
imewafanya maelfu, naam, mamilioni, kuwa na mashaka kuhusu Mungu na kuwa makafiri.
Nadharia ya mateso ya milele ni mojawapo ya mafundisho ya uongo ambayo yana ile mvinyo ya
ghadhabu ya uasherati wa Babeli, ambayo anayafanya mataifa yote kuinywa. Ufunuo 14:8; 17:2.
Kwamba watumishi wa Kristo walipaswa kuupokea uzushi huu na kuutangaza kutoka katika mimbari
takatifu ni fumbo kweli kweli. Walilipokea kutoka Roma, kama vile walivyopokea sabato ya uongo. Ni
kweli kwamba limekuwa likifundishwa na watu wakubwa na wema; lakini nuru juu ya somo hili haikuja
kwao kama ambavyo imekuja kwetu. Waliwajibika tu kwa nuru iliyowaangazia katika nyakati zao; sisi
tunawajibika kwa ile inayotuangazia katika siku zetu. Kama tunaupa kisogo ushuhuda wa neno la Mungu,
na kukubali (537) mafundisho ya uongo kwa sababu baba zetu waliyafundisha, tunaanguka katika
hukumu iliyotamkwa kwa Babeli; tunakunywa katika mvinyo wa uasherati wake.
Watu wengi wanaochukizwa na fundisho la kuteswa milele wanasukumwa kwenda katika kosa lililo
kinyume cha hilo. Wao wanaona kwamba Maandiko yanamwonyesha Mungu kuwa ni mwenye upendo na
huruma, na hawawezi kuamini kwamba atapeleka viumbe wake kuzimu katika moto wa milele. Lakini
wakishikilia imani kwamba roho kwa asili haifi, hawaoni njia mbadala bali kutoa hitimisho kwamba
wanadamu wote wataokolewa hatimaye. Wengi wanachukulia kwamba vitisho vilivyomo katika Biblia
vimebuniwa tu ili kuwatishia wanadamu wapate kutii, na si kwamba yatatimizwa kama yalivyo. Hivyo
mwenye dhambi anaweza kuishi katika anasa za ubinafsi, akidharau matakwa ya Mungu, na bado
akaweza kutazamia hatimaye kupokewa katika upendeleo wa Mungu. Fundisho kama hilo,
linaloaminisha kuhusu rehema ya Mungu, likipuuza haki yake, linaufurahisha moyo wa tamaa na
linawaimarisha waovu katika uovu wao.
Ili kuonyesha jinsi wale wanaoamini katika wokovu wa watu wote wanavyoyapotosha Maandiko ili
kuendeleza mafundisho ya dini zao yanayoangamiza roho za watu, tunahitaji tu kudondoa maneno yao
wenyewe. Wakati wa mazishi ya kijana mmoja asiye mtu wa dini, ambaye alikuwa ameuawa ghafla kwa
ajali, kiongozi wa dini inayoamini wokovu kwa wote alichagua maneno ya Maandiko kuhusu Daudi kama
fungu lake: “Kwa kuwa ametulizwa kwa habari ya Amnoni, kwa maana amekufa.” 2 Samweli 13:39.
“Mara kwa mara naulizwa,” alisema mnenaji huyo, “utakuwaje mwisho wa wale wanaoondoka duniani
wakiwa na dhambi, wakifa, labda, katika hali ya ulevi, wakifa katika madoa mekundu sana ya uhalifu
waliofanya bila mavazi yao kuoshwa, au wakifa kama alivyokufa kijana huyu, pasipo kupata kamwe
kuikiri imani au kufurahia uzoefu wa maisha ya dini. Tumetosheka na Maandiko; jibu litokalo humo
litatatua tatizo hilo linaloogofya. Amnoni alikuwa mwovu aliyepitiliza; hakutubu, alileweshwa, na
wakati alipokuwa amelewa aliuawa. Daudi alikuwa nabii wa Mungu; lazima atakuwa alijua kama
ingekuwa ole au heri kwa Amnoni katika ulimwengu ujao. Maneno yake ya kutoka moyoni yalikuwa yepi?
(538) “Mfalme Daudi akatamani kutoka kumwendea Absalomu kwa kuwa ametulizwa kwa habari ya
Amnoni, kwa maana amekufa.” Fungu la 39.

313
“Basi, hitimisho tunaloweza kupata kutokana na lugha hiyo ni lipi? Si kwamba mateso ya milele
hayakuwa sehemu ya imani yake ya dini? Hivyo ndivyo tuonavyo; na hapo tunagundua hoja iletayo
ushindi katika kutetea hoja ile ya kupendeza zaidi, ya hekima zaidi, na jema zaidi, ambayo inahusu
usafi na amani sawa kwa watu wote. Yeye alitulizwa, alipomwona mwanawe amekufa. Na kwa nini iwe
hivyo? Kwa sababu kwa jicho la nabii aliweza kuangalia mbele katika utukufu wa baadaye na kumwona
mwanawe yule akiwa ameondolewa na kuwekwa mbali na majaribu yote, akiwa amefunguliwa kutoka
kifungoni na kutakaswa uchafu wote wa dhambi, na baada ya kufanywa mtakatifu kwa kiwango cha
kutosha na kutiwa nuru, alipokewa katika kusanyiko la roho zilizopaa zenye furaha. Faraja yake pekee
ilikuwa kwamba, katika kuondolewa kwake kutoka katika hali yake ya sasa ya dhambi na mateso,
mwanawe mpendwa alikuwa amekwenda kule ambako uvuvio wa hali ya juu kabisa wa Roho Mtakatifu
ungeangaza katika roho yake iliyotiwa giza, kule ambako akili yake ingefunguliwa na kuijua hekima ya
mbinguni na nderemo tamu itokanayo na upendo wa milele, na hivyo kutayarishwa kwa kupewa tabia
iliyotakaswa ili apate kufurahia pumziko na kukaa na jamii ya warithi wa mbinguni.
“Katika mawazo haya tungeeleweka kuamini kwamba wokovu wa mbinguni hautegemei kitu chochote
tuwezacho kufanya katika maisha haya, wala kutegemea badiliko la sasa la moyo, wala juu ya imani ya
sasa, au tunavyokiri dini kwa sasa.”
Hivyo ndivyo mtumishi anayedaiwa kuwa wa Kristo anavyorudia kusema uongo ulionenwa na nyoka mle
Edeni: “Hakika hamtakufa.” “Siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi
mtakuwa kama Mungu.” Anasema kwamba mdhambi mbaya – mwuaji, mwizi, na mzinzi – ataandaliwa
baada ya kufa kwake kuingia katika raha ya milele.
Na mpotoaji huyu wa Maandiko analipata wapi hitimisho lake hilo? Ni kutoka katika sentensi moja
inayoeleza kujinyenyekeza kwa Daudi chini ya maongozi ya Mungu. Moyo (539) wake ulitamani “kutoka
kumwendea Absalomu kwa kuwa ametulizwa kwa habari ya Amnoni, kwa maana amekufa.” Uchungu
wake wa majonzi, ukiwa umetulizwa baada ya muda kupita, mawazo yake yaligeuzwa kutoka kwa
kijana aliyekufa kwenda kwa mwanaye aliyekuwa hai, ambaye alikuwa amejifukuza mwenyewe toka
nyumbani kwa hofu ya kuadhibiwa kwa jambo baya alilokuwa amelitenda. Na huu ndio ushahidi
unaotolewa kuonyesha kwamba Amnoni mlevi na aliyezini na ndugu yake alikuwa amekufa na
kusafirishwa mara moja kwenda kwenye makao yale ya raha, kutakaswa akiwa kule, na kuwa tayari
kushirikiana pamoja na malaika wasio na dhambi! Hii ni hadithi ya uongo kweli kweli, inayofanywa ili
kufaa kukidhi moyo wa tamaa! Hili ni fundisho la Shetani mwenyewe, na linafanya kazi yake kwa
ufanisi. Je, kwa mafundisho kama hayo, tunashangaa kuona maovu yakiongezeka?
Njia iliyofuatwa na mwalimu huyu wa uongo ni mfano wa uongo wa wengine wengi. Maneno machache
ya Maandiko yanachukuliwa kwa kutenganishwa na muktadha wake, ambao mara nyingi unaonyesha
kwamba maana ya maneno hayo ni kinyume na tafsiri inayohusianishwa nayo; na vifungu aya
zilizotenganishwa hivyo zinapotoshwa na kutumiwa kama uthibitisho wa mafundisho yao ambayo hayana
msingi katika neno la Mungu. Ushahidi ulionukuliwa ili kuthibitisha kwamba Amnoni mlevi yuko mbinguni
ni hitimisho linalopingwa moja kwa moja na kauli chanya ya wazi ya Maandiko kwamba hakuna mlevi
atakayeurithi ufalme wa Mungu. 1 Wakorintho 6:10. Ni kwa njia kama hiyo wenye mashaka, wasiosadiki,
na wale wanaoshuku wanavyogeuza ukweli kuwa uongo. Na watu wengi wamedanganyika kutokana na
hila hiyo na kubembea katika usingizi wa kitanda cha tamaa mbaya za mwili.
Ingekuwa ni kweli kwamba roho za wanadamu wote zinakwenda moja kwa moja mbinguni katika saa yao
ya kufa, tungetamani sana kufa kuliko kuishi. Wengi kutokana na fundisho hili wameshawishika kusitisha

314
maisha yao wenyewe. Wanapokuwa wamegubikwa na shida, wasiwasi, na kufadhaika, inaonekana jambo
jepesi kwao ni kukata kamba ya uhai wao na kupaa kwenda katika raha ya ulimwengu wa milele.
Mungu ametupatia ushahidi wa hakika katika neno lake kwamba atawaadhibu wavunjaji wote wa sheria
yake. Wale wanaojifurahisha (540) wenyewe kwa kusema kwamba Mungu ni mwenye rehema mno hata
asiweze kutekeleza haki yake dhidi ya mwenye dhambi, wanapaswa tu kutazama msalaba wa Kalvari.
Kifo cha Mwana wa Mungu asiye na waa hushuhudia kwamba “mshahara wa dhambi ni mauti,” kwamba
lazima kila uvunjaji wa sheria ya Mungu upate malipo yake ya haki. Kristo asiye na dhambi, alikuwa
dhambi kwa ajili ya mwanadamu. Alibeba hatia ya dhambi , hata uso wa Baba yake ukafichwa asiuone,
mpaka moyo wake ulipovunjika na maisha yake kupondwa-pondwa na kutoweshwa. Kafara yote hii
ilitolewa ili kwamba wadhambi wapate kukombolewa. Kusingekuwa na njia nyingine ya kumweka
mwanadamu huru mbali na adhabu ya dhambi. Na kila mtu anayekataa kuwa mshirika wa upatanisho
uliotolewa kwa gharama kubwa kiasi hicho lazima abebe katika nafsi yake mwenyewe hatia na adhabu
ya uasi.
Hebu na tutafakari zaidi kile kinachofundishwa na Biblia kuhusu waovu na wale wasiotaka kutubu,
ambao yule mwenye imani ya wokovu kwa watu wote anawaweka mbinguni kwamba ni malaika
watakatifu na wenye furaha.
“Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.” Ufunuo 21:6. Ahadi hiyo ni
kwa wale tu walio na kiu. Hakuna atakayepewa isipokuwa wale tu wanaoona kwamba wana haja ya
kunywa maji ya uzima, na wanayatafuta kwa gharama ya vitu vingine vyote. “Yeye ashindaye atayarithi
haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.” Fungu la 7. Hapa, pia, masharti
yametajwa wazi. Ili kuyarithi yote hayo, lazima tuipinge na kuishinda dhambi.
Bwana anatangaza kupitia kwa nabii Isaya: “Waambieni wenye haki ya kuwa watakuwa heri.” “Ole wake
mtu mbaya; shari itakuwa kwake; kwa maana atapewa ijara ya mikono yake.” Isaya 3:10,11.
“Ajapokuwa mwenye dhambi amefanya maovu mara mia, akazidisha siku zake; lakini hata hivyo najua
hakika ya kwamba itakuwa heri kwao wamchao Mungu, na wenye kicho mbele zake; walakini haitakuwa
heri kwa mwovu.” Mhubiri 8:12,13. Na Paulo naye anashuhudia kwamba mwenye dhambi anajiwekea
mwenyewe akiba ya “hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,
atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake;” “dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu
atendaye uovu.” Warumi 2:5,6.9.
(541) “Hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi
katika ufalme wa Kristo na Mungu.” Waefeso 5:5. “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na
huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao.” Waebrania 12:14. “Heri wale
wazishikao amri zake, wawe na haki ya kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.
Huko nje wako mbwa, na wazinzi, na wauaji, na hao waabudio sanamu, na kila mtu apendaye uongo na
kuufanya.” Ufunuo 22:14,15.
Mungu amewapatia wanadamu maelezo ya tabia yake na ya njia yake atakayotumia kushughulikia
dhambi. “BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa
rehema na kweli; mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na
dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe.” Kutoka 34:6,7. “Na wote
wasio haki atawaangamiza.” “Wakosaji wataangamizwa pamoja, wasio haki mwisho wao wataharibiwa.”
Zaburi 145:20; 37:38. Nguvu na mamlaka ya serikali ya mbinguni itatumika kuyazima maasi hayo; hata
hivyo, udhihirisho wa malipizo yote ya kisasi ya haki utalingana kabisa na unyofu wa tabia ya Mungu
aliye mwenye huruma, asiyekuwa mwepesi wa hasira, na mwenye fadhili.
315
Mungu halazimishi nia ya mtu au maamuzi ya yeyote. Hana furaha katika utii wa utumwa. Anapenda
kwamba viumbe wa mikono yake wampende kwa sababu anastahili kupendwa. Angewependa wamtii
kwa sababu wanayo akili ya kutambua hekima yake, haki yake, na fadhili zake. Na wote ambao wana
mawazo sahihi ya sifa hizi watampenda kwa sababu wanavutwa kwake kwa kutamani tabia zake hizo.
Kanuni za wema, huruma, na upendo, zilizofundishwa na kuonyeshwa na Mwokozi wetu, ni chapa ya
mapenzi na tabia ya Mungu. Kristo alisema kwamba alikuwa hafundishi neno lolote ila lile alilopokea
kwa Baba yake. Kanuni za serikali ya Mungu zinapatana kabisa na amri ya Mwokozi, “Wapendeni adui
zenu.” Mungu (542) anatekeleza haki yake kwa waovu, kwa faida ya malimwengu, na hata kwa faida ya
wale ambao hukumu zake zinapatilizwa kwao. Angeweza kuwafanya wawe na furaha kama angeweza
kufanya hivyo kulingana na sheria za serikali yake na haki ya tabia yake. Anawazungushia ishara za
upendo wake, anawapatia maarifa ya kuijua sheria yake, na anawafuata kwa kuwapa rehema zake;
lakini wao wanaudharau upendo wake, wanaitangua sheria yake, na kuikataa rehema yake. Wakati
wanapokea wakati wote zawadi; hawamheshimu Mpaji huyo; wanamchukia Mungu kwa sababu wanajua
kwamba anazichukia dhambi zao. Bwana anavumilia upotovu wao; lakini saa ya mwisho ya kuamua
mambo hatimaye itafika, ndipo mwisho wao utakapoamuliwa. Je, wakati huo atawafunga minyororo
waasi hawa na kuwaweka upande wake? Je, atawalazimisha kufanya mapenzi yake?
Wale ambao wamemchagua Shetani kama kiongozi wao na wamekuwa wakitawaliwa na nguvu zake
hawako tayari kuingia mbele za Mungu. Kiburi, udanganyifu, uasherati, ukatili, vimebandikwa katika
tabia zao. Wanaweza kuingia mbinguni kuishi milele pamoja na wale waliowadharau na kuwachukia
duniani? Kamwe ukweli hautakubalika kwa aliye mwongo; upole hautaitosheleza hali ya kujisifu na
kiburi; usafi wa maisha haukubaliki mbele ya ufisadi; upendo usiotafuta manufaa hauonekani kuwa na
mvuto kwa mchoyo. Mbingu itapata chanzo kipi cha furaha ya kuwapa wale waliozama katika tamaa za
ubinafsi za dunia?
Ingetokea wale ambao wametumia maisha yao katika kumwasi Mungu wakasafirishwa ghafla hadi
mbinguni na kushuhudia hali kamilifu ya juu na takatifu iliyopo kule wakati wote, - kila mtu akiwa
amejaa upendo, kila uso uking’aa kwa furaha, na muziki wa nyimbo tamu zinazoimbwa kwa heshima ya
Mungu na ya Mwana-kondoo, na mkondo wa nuru unaotiririka bila kukoma juu ya wale waliokombolewa
ukitoka katika uso wake Yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, - je, wale wenye mioyo iliyojazwa na
chuki kwa Mungu, mwenye ukweli na utakatifu, wangechanganyika na halaiki ya mbinguni na kujiunga
katika nyimbo zao za sifa? Wangestahimili utukufu wa Mungu na wa Mwanakondoo? La, la; walipewa
miaka mingi ya muda wao wa majaribio, (543) ili wapate kutengeneza tabia za mbinguni; lakini
hawajapata kamwe kuyazoeza mawazo yao kupenda usafi wa maisha; hawajawahi kamwe kujifunza
lugha ya mbinguni, na sasa wamechelewa. Maisha ya uasi dhidi ya Mungu yamewafanya wasifae kwenda
mbinguni. Usafi wa mbinguni, utakatifu wa kule, na amani ya kule vingekuwa mateso kwao; utukufu wa
Mungu ungekuwa moto ulao. Wangetamani kukimbia kutoka mahali pale patakatifu. Wangeyakaribisha
maangamizi yao, ili wapate kujificha, wasiuone uso wake yeye aliyekufa ili kuwakomboa. Hatima ya
waovu inawekwa na uchaguzi wao wenyewe. Kutengwa kwao na mbingu ni kwa hiari yao wenyewe, na
ni kwa haki na huruma kwa upande wa Mungu.
Kama yalivyokuwa maji ya Gharika mioto ya ile siku kuu hutangaza hukumu ya Mungu ya mwisho
inayoonyesha kwamba waovu hawaponyeki. Hawana mwelekeo wa kuitii mamlaka ya mbinguni. Nia yao
imezoezwa kufanya vurugu; na maisha yanapokwisha, watakuwa wamechelewa kugeuza mkondo wa
mawazo yao ya sasa katika uelekeo ulio kinyume, wamechelewa kubadilisha uasi na kuwa watii, kutoka
katika chuki kuwa na upendo.

316
Kwa kuyaachilia maisha ya Kaini yule mwuaji, Mungu aliupatia ulimwengu mfano wa kile ambacho
kingekuwa matokeo ya kumruhusu mwenye dhambi kuishi ili aendelee kwenda katika njia ya uovu bila
kizuizi. Kupitia katika mvuto wa fundisho na mfano wa Kaini, wazao wake wengi waliongozwa katika
dhambi, mpaka wakati ule “maovu ya mwanadamu yalipokuwa makubwa duniani” na “kila kusudi
analowaza moyoni mwake likawa ni baya tu sikuzote.” “Dunia ikaharibika mbele za Mungu, dunia ikajaa
dhuluma.” Mwanzo 6:5,11.
Kwa kuhurumia ulimwengu, Mungu aliwafutilia mbali wakazi wa dunia waovu katika siku za Nuhu. Kwa
huruma aliwaangamiza wakazi wafisadi wa Sodoma. Kupitia nguvu za udanganyifu za Shetani watendao
maovu huungwa mkono na kusifiwa, na kwa njia hiyo sikuzote wanawaingiza wengine katika maasi.
Ilikuwa hivyo katika siku za Kaini na Nuhu, na katika wakati wa Ibrahimu na Lutu; ni hivyo pia katika
siku zetu hizi. Ni kwa huruma kwa malimwengu kwamba hatimaye Mungu atawaangamiza wale
wanaoikataa neema yake.
(544) “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika
Kristo Yesu Bwana wetu.” Warumi 6:23. Wakati uzima ndio urithi wa wenye haki, mauti ndilo fungu la
waovu. Musa aliwatangazia Israeli: “Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema na mauti na
mabaya.” Kumbukumbu la Torati 30:15. Mauti inayotajwa katika maandiko haya si ile iliyotamkwa kwa
Adamu, kwa maana wanadamu wote wanapatwa na adhabu hiyo iliyotokana na dhambi yake. Hiyo ni
“mauti ya pili” ambayo inatofautishwa na uzima wa milele.
Kama matokeo ya dhambi ya Adamu, mauti ikawafikia wanadamu wote. Wote kwa njia moja wanaingia
kaburini. Na kwa kupitia nafasi ya mpango wa wokovu, wote wanapaswa kuondolewa makaburini mwao.
“Kutakuwa na ufufuo wa wafu, wenye haki na wasio haki pia.” “Kwa kuwa kama katika Adamu wote
wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.” Matendo 24:15; 1 Wakorintho 15:22. Lakini
tofauti dhahiri inawekwa kati ya makundi hayo mawili yanayofufuliwa. “Watu wote waliomo makaburini
wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda
mabaya kwa ufufuo wa hukumu.” Yohana 5:28,29. Wale watakaokuwa “wamehesabiwa kuwa
wanastahili” katika ufufuo wa uzima ndio walio “heri, na mtakatifu.” “Juu ya hao mauti ya pili haina
nguvu.” Ufunuo 20:6. Lakini wale ambao hawakupata msamaha, kwa njia ya toba na imani, lazima
wapokee adhabu ya dhambi zao - huo “mshahara wa dhambi.” Wanapata adhabu inayotofautiana muda
na ukali, “sawasawa na matendo yao,” lakini hatimaye wataishia katika mauti ya pili. Kwa kuwa
haiwezekani kwa Mungu, kulingana na haki yake na rehema zake, kumwokoa mwenye dhambi katika
dhambi zake, anamnyang’anya uhai ambao umepotezwa na uasi wake na ambao yeye mwenyewe
amejionyesha kuwa haustahili kuwa nao. Mwandishi aliyevuviwa anasema: “Maana bado kitambo kidogo
asiye haki hatakuwapo, utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo.” Na mwingine anasema: “Nao
watakuwa kana kwamba (545) hawakuwako kamwe.” Zaburi 37:16; Obadia 16. Wakiwa wamefunikwa
na aibu, wanazama katika hali ya kusahauliwa milele pasipo tumaini.
Hivyo ndivyo mwisho wa dhambi utakavyokuwa, pamoja na misiba na maangamizi yote yaliyosababishwa
nayo. Mwimba zaburi anasema: “Umewakemea mataifa; na kumwangamiza mdhalimu; umelifuta jina
lao milele na milele; adui wamekoma na kuachwa ukiwa milele.” Zaburi 9:5,6. Yohana, katika kitabu
cha Ufunuo, akiangalia mbele kwenye hali ya milele, anasikia wimbo wa kumsifu Mungu kutoka katika
malimwengu yote ukiwa haujaathiriwa na sauti hata moja isiyoendana. Kila kiumbe kilichoko mbinguni
na duniani kilisikika kikimpa Mungu utukufu. Ufunuo 5:13. Wakati ule hakutakuwa na watu waliopotea
wanaomkufuru Mungu, huku wakigaagaa motoni kwa mateso yasiyo na mwisho; hakutakuwa na waovu
kuzimu ambao watatoa sauti zao zinazoingilia nyimbo za waliookolewa.

317
Kwenye msingi wa uongo kwamba mwanadamu ana roho isiyokufa limejengwa fundisho la uongo
lisemalo kwamba waliokufa wana fahamu zao za utambuzi - fundisho, kama la kuteswa milele motoni,
lipinganalo na mafundisho ya Maandiko, kinyume na akili ya kawaida, tena ni kinyume na hisia za
kibinadamu. Kulingana na imani hiyo maarufu, wale waliokombolewa kule mbinguni wanajua kila kitu
kinachotokea hapa duniani, hasa habari za maisha ya rafiki zao walioachwa nyuma. Lakini itakuwa
furaha gani kwa hao wafu kuzijua taabu zinazowapata walio hai, kuziona dhambi zinazotendwa na
wapendwa wao, na kuwaona wakistahimili huzuni zote, kukata tamaa kwao kote, na uchungu wote
unaowapata katika maisha haya? Ni raha ya mbinguni ya kiasi gani ambayo wangeweza kuipata wale
waliokuwa wakiruka juu ya rafiki zao hapa duniani? Tena inachukiza jinsi gani imani kwamba mara tu
pumzi inapotoka mwilini roho ya mtu yule aliyekuwa hataki kutubu inatupwa katika ndimi za moto wa
kuzimu? Ni kina kirefu cha maumivu jinsi gani wanacholazimika kutumbukizwa ndani yake wale
waliokuwa wanawaona rafiki zao wakiingia makaburini mwao bila kujitayarisha, wakiingia katika
umilele kupata taabu kubwa na kusumbuka na dhambi! Wengi wamerukwa na akili kwa kulitafakari sana
wazo hili linalowatia uchungu.
Maandiko yanasema nini kuhusu mambo haya? Daudi anatangaza kwamba mtu anapokufa hawezi kuwa
na ufahamu wa kutambua mambo. “Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, siku hiyo (546) mawazo
yake yapotea.” Zaburi 146:4. Sulemani anatoa ushuhuda huo huo: “Kwa sababu walio hai wanajua ya
kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote.” “Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao,
imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.” “Kwa
kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.” Mhubiri
9:5,6,10.
Wakati maisha ya Hezekia yalipoongezwa, kama jibu la ombi lake, kwa miaka kumi na mitano, mfalme
huyu mwenye shukrani alimpa Mungu sifa kwa rehema zake nyingi. Katika wimbo huu anaeleza sababu
ya kufurahi hivyo: “Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu; mauti haiwezi kukuadhimisha; wale washukao
shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako. Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi
leo.” Isaya 38:18,19. Thiolojia maarufu inawaonyesha wenye haki waliokufa kuwa wako mbinguni,
wameingia katika raha ile na wanamsifu Mungu kwa ulimi usioweza kufa; lakini Hezekia hakuona
matarajio yenye utukufu kama hayo katika mauti. Kwa maneno yake anakubali sshuhuda wa mwimba
zaburi: “Maana mautini hapana kumbukumbu lako; katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?” “Sio wafu
wamsifuo BWANA, wala wo wote washukao kwenye kimya. Zaburi 6:5; 115:17.
Petro katika Siku ya Pentekoste alisema kwamba mzee wa zamani Daudi “alifariki akazikwa, na kaburi
lake liko kwetu hata leo.” “Maana Daudi hakupanda mbinguni.” Matendo 2:29,34. Ukweli kwamba Daudi
angali kaburini mpaka siku ya ufufuo unatuthibitishia kwamba wenye haki wanapokufa hawaendi
mbinguni. Ni kwa njia ya ufufuo tu, na kwa sababu Kristo amefufuka, kwamba Daudi hatimaye ataketi
mkono wa kuume wa Mungu.
Na Paulo alisema: “Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka. Na kama Kristo hakufufuka,
imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu. Na hapo wao nao waliolala katika Kristo
wamepotea.” 1 Wakorintho 15:16-18. Ikiwa kwa miaka elfu nne a moja kwa moja mbinguni
wanapokufa, inakuwaje Paulo aseme kwamba kama hakuna ufufuo, (547) “wao nao waliolala katika
Kristo wamepotea”? Ufufuo usingekuwa wa lazima.
Tyndale yule mfia-dini, akirejea kwa hali ya wafu, alisema: “Nakiri wazi, kwamba sijashawishika
kwamba wao wako katika utukufu kamili ambao Kristo anao, au ule walio nao malaika wateule wa
Mungu. Wala hilo si sehemu ya imani yangu; maana kama ingekuwa hivyo, sioni kitu chochote ila

318
kwamba kuhubiri habari za ufufuo wa mwili kulikuwa jambo lisilo na maana.” - William Tyndale,
William Tyndale, Preface to New Testament (ed. 1534). Ilichapishwa tena katika kiitwacho British
Reformers - Tindal, Frith, Barnes, page 349.
Ni ukweli usiokanushika kwamba tumaini la mbaraka wa kutokufa mtu anapokufa limewafanya watu
wengi kulidharau fundisho la Biblia la ufufuo. Mwelekeo huu uliongelewa na Dk. Adam Clarke, ambaye
alisema: “Fundisho kuhusu ufufuo linaonekana kuwa lilifikiriwa kuwa la matokeo makubwa sana
miongoni mwa Wakristo wa kale kuliko lilivyo sasa! Hili likoje? Mitume walikuwa wanalisisitiza muda
wote, na kuwaamsha wafuasi wa Mungu kuwa na bidii, utii, na furaha kupitia hilo. Na waliorithi kazi yao
katika siku hizi wanalitaja kwa nadra! Mitume walihubiri hivyo, na Wakristo wa kale waliamini hivyo; sisi
tunahubiri hivyo, na ndivyo wasikilizaji wetu wanavyoamini. Hakuna fundisho katika injili ambalo
linatiliwa mkazo zaidi ya hilo; na hakuna fundisho katika mfumo wa mahubiri ya siku hizi ambalo
linapuuzwa zaidi kuliko hilo!” - Commentary, remarks on I Corinthians 15, paragraph 3.
Hali hii imeendelea mpaka utukufu wa ukweli wa ufufuo ni kama umefichika kabisa na kusahauliwa na
ulimwengu wa Kikristo. Mwandishi mkubwa wa mambo ya dini, akitoa maoni kuhusu maneno ya Paulo
katika 1 Wathesalonike 4:13-18, anasema: “Kwa makusudi yote ya kuleta faraja, fundisho juu ya
mbaraka wa kutokufa kwa wenye haki linachukua nafasi ya fundisho lenye mashaka kwetu kuhusu kuja
kwa Bwana mara ya pili. Katika kufa kwetu Bwana anatujia. Hilo ndilo tunalopaswa kungoja na kukesha
kwa ajili yake. Wafu wameingizwa katika utukufu tayari. Wao hawaisubiri parapanda kwa ajili ya
hukumu na mibaraka yao.”
(548) Lakini alipokuwa karibu kuachana na wanafunzi wake, Yesu hakuwaambia kwamba wangekwenda
kwake punde. “Maana naenda kuwaandalia mahali,” alisema. “Basi mimi nikienda na kuwaandalia
mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu.” Yohana 14:2,3. Paulo naye anatupatia maelezo zaidi
kwamba “Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya Malaika Mkuu,
na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia,
tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa na Bwana
milele.” Kisha anaongeza maneno haya: “Basi, farijianeni kwa maneno hayo.” 1 Wathesalonike 4:16-17.
Ni kubwa kiasi gani tofauti iliyopo kati ya maneno hayo ya faraja na yale ya mtumishi yule aaminiye
kuhusu wokovu kwa watu wote ambaye maneno yake tumeyanukuu! Huyu mtumishi aliwafariji rafiki
zake wafiwa kwa kuwapa tumaini kwamba, hata iwe amekuwa mdhambi kiasi gani, marehemu yule
alipokewa miongoni mwa malaika wakati ule alipokata roho. Paulo anawaonyesha ndugu zake katika
wakati ujao wa kuja kwa Bwana, wakati vifungo vya kaburi vitakapovunjwa, na wale “waliokufa katika
Kristo” watakapofufuliwa kwa ajili ya uzima wa milele.
Kabla watu wowote hawajaingia katika makao yale ya wenye heri, lazima kesi zao zichunguzwe, na
tabia zao na matendo yao yapitiwe mbele za Mungu. Wote watahukumiwa sawasawa na mambo yale
yaliyoandikwa katika vitabu vile na kupewa ijara yao sawasawa na matendo yao. Hukumu hii haifanyiki
wakati mtu anapokufa. Zingatia maneno ya Paulo: “Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu
walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya
kwa kumfufua katika wafu.” Matendo 17:31. Hapa mtume alieleza waziwazi kwamba wakati mahsusi,
muda ujao kwa wakati ule, ulikuwa umewekwa kwa hukumu ya walimwengu wote.
Yuda anarejea kwa kipindi hicho hicho: “Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha
makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile
kuu.” Tena, anayanukuu maneno ya Henoko: “Angalia, Bwana anakuja na maelfu kumi ya (549)
watakatifu wake, ili afanye hukumu juu ya watu wote.” Yuda 6,14,15. Yohana anatangaza kwamba

319
aliona “wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu
vikafunguliwa;… na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu.”
Ufunuo 20:12.
Lakini kama wafu wanafurahia raha kule mbinguni au wanaumia katika ndimi za moto wa kuzimu, pana
haja gani tena ya kuwekwa kwa hukumu ijayo? Mafundisho ya neno la Mungu kuhusu mambo haya
muhimu hayakufichika wala hayajipingi; yanaweza kueleweka kwa akili za kawaida. Lakini ni mtu gani
mnyofu wa moyo awezaye kuona busara au haki katika nadharia ya sasa? Je, wenye haki, baada ya kesi
zao kuchunguzwa katika hukumu, watapokea maneno haya ya pongezi, “Vema, mtumwa mwema na
mwaminifu;… ingia katika furaha ya Bwana wako,” wakati tayari wamekuwa wakiishi mahali pale,
huenda kwa muda wa vizazi vingi? Je, waovu wanaitwa kutoka katika mateso ili kupokea hukumu yao
kwa Hakimu wa ulimwengu wote: “Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele”?
Mathayo 25:21,41. Lo, dhihaka kubwa! Ni tuhuma ya aibu kiasi gani dhidi ya hekima na haki ya Mungu!
Nadharia kuhusu roho isiyokufa ilikuwa mojawapo ya mafundisho ya uongo ambayo Roma, ikiyaazima
kutoka kwa wapagani, iliingiza katika dini ya ulimwengu wa Kikristo. Martin Luther aliliweka katika
kundi la “hadithi za uongo wa kutisha zinazojenga rundo la uchafu wa mafundisho ya upapa.” - E.
Petavel, The Problem of Immortality, page 255. Akitoa ufafanuzi wa maneno ya Sulemani katika kitabu
cha Mhubiri yasemayo kwamba wafu hawajui neno lo lote, Mwanamatengenezo huyo anasema: “Mahali
pengine panapothibitisha kwamba wafu hawana … hisia. Hakuna, anasema, kazi yo yote, wala sayansi,
wala maarifa, wala hekima kule. Sulemani anaona kwamba wafu wamelala, na hawahisi kitu cho chote
kabisa. Maana wafu wanalala, wasiweze kuhesabu siku wala miaka, lakini watakapoamshwa, watajiona
kana kwamba wamelala kwa muda usiofika hata dakika moja.” -Martin Luther, Exposition of Solomon’s
Booke Called Ecclesiastes, page 152.
Hakuna mahali katika Maandiko Matakatifu panapopatikana kauli (550) kwamba wenye haki wanaenda
katika thawabu yao au waovu wanaenda katika adhabu yao wakati wanapokufa. Wazee na manabii
hawakuacha uthibitisho kama huo. Kristo na mitume wake hawakutoa dokezo lo lote kuhusu hilo. Biblia
inafundisha waziwazi kwamba wafu hawaendi mbinguni mara wanapokufa. Wanaonyeshwa kwamba
waliolala usingizi mpaka siku ya ufufuo. 1 Wathesalonike 4:14; Ayubu 14:10-12. Katika siku ile ile kamba
ya fedha inapokatika na kuvunjwa bakuli la dhahabu (Mhubiri 12:6), mawazo ya mtu hutoweka. Wale
washukao kaburini wako katika ukimya. Hawajui jambo lolote lifanyikalo chini ya jua. Ayubu 14:21. Ni
pumziko la heri kwa wenye haki waliochoka! Muda, uwe mrefu au mfupi, kwao ni muda mfupi mno.
Wanalala usingizi; wanaamshwa kwa parapanda ya Mungu na kupewa miili mitukufu isiyokufa. “Maana
parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu…. Basi huu uharibikao utakapovaa
kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa,
Mauti imemezwa kwa kushinda.” 1 Wakorintho 15:52-54. Wanapoitwa tu kutoka katika usingizi wao
mzito, wanafikiri kuanzia pale walipoishia wakati wa kufa kwao. Hisia yao ya mwisho ilikuwa ni uchungu
wa mauti; wazo lao la mwisho, lilikuwa ni lile la kuanguka katika nguvu za kaburi. Wanapofufuka kutoka
kaburini, wazo lao la kwanza lenye furaha litatoa mwangwi wake katika sauti ya ushindi: “Ku wapi, Ewe
mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti uchungu wako?” Fungu la 55.

320
Sura ya 34
WAFU WETU WANAWEZA KUSEMA NASI?

Huduma ya malaika watakatifu, kama ilivyoelezwa katika Maandiko, ni ukweli wenye faraja kuu na wa
thamani kwa kila mfuasi wa Kristo. Lakini fundisho la Biblia juu ya jambo hilo limetiwa giza na
kupotoshwa na uongo wa thiolojia maarufu. Fundisho la kutokufa, ambalo liliazimwa kwanza kutoka
katika falsafa ya kipagani, na kuingizwa katika imani ya Kikristo katika giza la kipindi cha uasi mkuu,
limechukua nafasi ya ukweli, unaofundishwa waziwazi katika Maandiko, kwamba “wafu hawajui neno
lolote.” Watu wengi wamekuja kuamini kwamba wale “watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale
watakaourithi wokovu” ni roho za watu waliokufa. Lakini imani hii ni kinyume na ushuhuda wa Maandiko
kuhusu kuwako kwa malaika mbinguni, na uhusiano wao na historia ya mwanadamu, kabla ya kifo cha
mwanadamu.
Fundisho kuhusu mtu kuwa na fahamu akiwa amekufa, hasa ile imani kwamba roho za wafu zinarudi
kuja kuwasaidia walio hai, limetayarisha njia kwa dini ya umizimu ya kisasa. Kama wafu wanapokelewa
mbele za Mungu na mbele za malaika watakatifu, na kujaliwa kupewa ufahamu mkubwa kwa mbali sana
kuliko walivyokuwa kabla, kwa nini wasirudi duniani kuwaelekeza walio hai? Ikiwa, kama
walivyofundisha wanathiolojia, roho za wafu zinaruka zikiwaendea marafiki walio duniani, kwa nini
wasiruhusiwe kuwasiliana nao, kuwaonya dhidi ya uovu, ama kuwafariji (552) katika huzuni?
Itawezekanaje wale wanaoamini kuwepo kwa uhai pindi mtu anapokufa waikatae nuru inayowajia kama
nuru ya mbinguni inayoletwa na roho zilizotukuzwa? Hapa ndipo ilipo njia inayodhaniwa kuwa ni
takatifu, ambayo Shetani anafanya kazi kuipitia hiyo ili kutimiza makusudi yake. Malaika walioanguka
watekelezao kazi zake wanaonekana kama wajumbe wanaotoka katika ulimwengu wa roho. Wakati
mkuu wa uovu akijidai kwamba anawaunganisha walio hai na wafu, anatumia ushawishi wake wa
kichawi katika akili zao.
Anao uwezo wa kuleta mbele ya wanadamu mwonekano wa rafiki zao waliokufa. Mwonekano wa umbile
hilo la bandia ni mkamilifu, katika umbile lile lile linalofahamika, maneno na sauti viko katika usahihi
wa kushangaza. Wengi wanafarijika kwa kuhakikishiwa kwamba ndugu zao wapendwa wanafurahia raha
ya mbinguni, na bila ya kuhisi hatari, wanatega sikio “wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya
mashetani.”
Baada ya kuongozwa kuamini kwamba wafu wanarudi kweli kweli na kuwasiliana nao, Shetani
anasababisha kujitokeza kwa wale walioenda kaburini bila kujiweka tayari. Watadai kwamba wako
mbinguni na tena wako katika nafasi za juu zilizotukuzwa, na kwa hiyo uongo unaenezwa kwa kiasi
kikubwa kwamba hakuna tofauti yoyote kati ya wenye haki na waovu. Wageni hao wa bandia
wanaojionyesha kutoka katika ulimwengu wa roho wakati mwingine wanatamka maneno ya tahadhari na
maonyo ambayo huthibitika kuwa sahihi. Halafu, wakishavuta imani ya watu, wanawasilisha mafundisho
ambayo yanahafifisha moja kwa moja imani ya watu katika Maandiko. Kwa mwonekano wa kupenda
kuona hali njema ya rafiki zao walioko duniani, wanapenyeza kwa hila uongo wa hatari kuliko uongo
wote. Ile hali ya wao kusema ukweli fulani, na uwezo wao wa kubashiri wakati fulani matukio ya
baadaye, hufanya kauli zao kuonekana za kukubalika; na mafundisho yao ya uongo yanapokelewa upesi,
na kuaminika bila shaka, kama vile hayo ndiyo kweli takatifu sana za Biblia. Sheria ya Mungu huwekwa
kando, Roho wa neema hudharauliwa, damu ya agano huhesabiwa kama kitu kisicho na utakatifu. Roho
hizo hukana uungu wa Kristo na hata humweka Mwumbaji kuwa katika nafasi iliyo sawa na roho hizo.

321
Hivyo chini ya uigizaji huu mpya, mwasi mkuu huyu (553) anaendelea kufanya vita dhidi ya Mungu,
ambayo ilianzia mbinguni na kwa karibu miaka elfu sita imeendelezwa hapa duniani.
Wengi huazimu kuona hila hizo za udanganyifu na kiinimacho zinazofanywa kwa mwonekano huo kama
mafunuo ya kiroho. Lakini wakati ni kweli kwamba mara nyingi matokeo hayo ya mbinu za uongo
yameweza kufanywa kuwa kama mwonekano wa ishara za kweli, kumekuwa pia, na hali ya kuonyeshwa
kwa ishara za nguvu zisizo za kawaida. Mvumo na kelele za miujiza ambazo umizimu wa kisasa ulianza
nazo hazikuwa matokeo ya udanganyifu wala hila za mwanadamu, bali ilikuwa kazi ya moja kwa moja
ya wale malaika waovu, ambao kwa njia hiyo walianzisha mojawapo ya madanganyo yaliyofanikiwa sana
kuziangamiza roho za watu. Wengi watanaswa kwa kuamini kwamba umizimu ni uongo wa wanadamu
tu; hapo watakapokutana ana kwa ana na ishara ambazo hakuna jinsi isipokuwa kuziona kama zilizo juu
ya uwezo wa kibinadamu, watadanganyika, na watafanywa wazikubali kwamba ni nguvu za Mungu.
Watu hao hawatilii maanani ushuhuda wa Maandiko kuhusu maajabu hayo yanayofanywa na Shetani na
mawakala zake. Ilikuwa ni msaada wa Shetani uliowafanya wachawi wa Farao kuweza kuigiza kazi ya
Mungu. Paulo anatoa ushuhuda kwamba kabla ya marejeo ya Kristo kutakuwa na ishara kama hizo za
nguvu za Shetani. Kuja kwa Bwana kutatanguliwa na “kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na
ishara na ajabu za uongo; na katika madanganyo yote ya udhalimu..” 2 Wathesalonike 2:9,10. Naye
mtume Yohana, akielezea habari za mamlaka hiyo itendayo miujiza itakayojitokeza katika siku za
mwisho, anasema: “Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya
nchi mbele ya wanadamu. Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa
kuzifanya.” Ufunuo 13:13,14. Hakuna udanganyifu wa kuigiza unaotabiriwa hapa. Wanadamu
wanadanganywa na miujiza ambayo mawakala wa Shetani wana uwezo wa kuifanya, sio ile wanayofanya
kwa kuigiza.
Mfalme wa giza, ambaye kwa muda mrefu amebadilisha mwelekeo wa mamlaka za mipango yake katika
kazi ya udanganyifu, kwa ujuzi mkubwa anaufanya upotoshaji wake uzoeleke kwa watu wa matabaka
yote na hali zote. Kwa watu walioelimika na wajuzi analeta imani ya umizimu katika mtazamo wa
kitaalam na kisomi, na kwa njia hiyo anafanikiwa kuwavuta wengi na kuwanasa katika mtego wake.
Hekima inayoletwa na imani ya umizimu ni ile iliyoelezwa na mtume Yakobo, kuwa “sio ile ishukayo
kutoka mbinguni, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani.” Yakobo 3:15. Jambo hili, hata
hivyo, hufichwa na mdanganyifu mkuu wakati anapoona kuficha kunakidhi makusudi yake. Yeye
aliyeweza kujitokeza kwa Kristo wakati wa majaribu ya nyikani akiwa amevikwa nuru ya maserafi wa
mbinguni, anakuja kwa wanadamu kwa namna ya kuvutia sana kama malaika wa nuru. Anaishawishi akili
kwa kuleta mafundisho yanayoinua; anaamsha furaha ya hali ya juu na yenye mandhari zinazofurahisha;
tena anaivuta akili kwa ufasaha wa kusema uonyeshao upendo na huruma. Anachochea hali ya kujisikia
kupaa juu sana, akiwaongoza wanadamu kujivuna katika hekima yao wenyewe kiasi kwamba katika
mioyo yao wanamdharau Aliye wa Milele. Kiumbe huyu mwenye nguvu aliyeweza kumchukua Mkombozi
wa ulimwengu hadi kwenye kilele cha mlima mrefu kuliko kawaida na kuleta machoni pake falme zote
za dunia na fahari zake, ataleta majaribu yake kwa wanadamu kwa namna ya kuzipotosha fahamu za
wale wote wasiolindwa na nguvu ya kimbingu.
Shetani anadanganya watu leo kama alivyomdanganya Hawa kule Edeni kwa kusifia, kwa kuamsha hamu
ya kupata maarifa yaliyokatazwa, kwa kuamsha tamaa ya kujikweza. Ilikuwa kuendekeza maovu haya
kulikosababisha kuanguka kwake, na kwa kupitia hayo hayo anakusudia kuwazungushia watu
maangamizi. “Mtakuwa kama miungu,” anasema wazi, “mkijua mema na mabaya.” Mwanzo 3:5.
Umizimu unafundisha “kwamba mwanadamu ni kiumbe wa kuendelea; kwamba tangu kuzaliwa kwake
hatima yake ni kuendelea, hata kuufikia umilele, kwenda kwa Uungu.” Na tena: “Kila akili itajiamulia
322
yenyewe wala si nyingine kuiamulia.” “Hukumu hiyo itakuwa ya haki, kwa sababu ni hukumu ya
binafsi…. Kiti cha enzi kiko ndani yako mwenyewe.” Mwalimu wa imani ya umizimu alisema, pindi “hali
ya kiroho” alipowaka ndani yake: “Wanadamu wenzangu, wote walikuwa mungu wadogo.” Na mwingine
anasema: “Kiumbe yeyote mwenye haki na mkamilifu ni Kristo.”
Hivyo, mahali pa haki na ukamilifu wa (555) Mungu wa milele, yeye aliye mlengwa wa kweli wa ibada;
mahali pa haki kamilifu ya sheria yake, kiwango cha kweli mafanikio ya mwanadamu, Shetani ameweka
asili ya mwanadamu ya dhambi na makosa kuwa ndiyo lengo pekee la ibada, kanuni pekee ya hukumu,
au kiwango cha tabia. Hii ni hali ya kuendelea, sio kwenda juu, bali kwenda chini.
Ni sheria ya akili na ya kiroho ambayo kwa kuitazama tunabadilishwa. Akili inabadilika kufuatana na
mambo ambayo kwayo inaruhusiwa kujikita. Inazoea kufanana na kile ambacho imezoezwa kupenda na
kuheshimu. Kamwe mtu hatapanda juu zaidi ya kanuni aliyo nayo ya usafi wa maisha au wema au
ukweli. Kama kujipenda mwenyewe ndicho kipeo chake cha juu sana, hataweza kupata kitu cho chote
kilicho juu zaidi yake. Badala yake, atazidi kuzama na kuzama chini zaidi. Neema ya Mungu pekee ndiyo
ina uwezo wa kumpandisha mwanadamu. Akiachwa peke yake, lazima njia yake iwe ya kwenda chini
kwa hali isiyoepukika.
Kwa wale wanaotafuta kutimiza matakwa yao, wapenda anasa, wenye tamaa ya mwili, umizimu
unajionyesha kwa kificho kidogo sana kuliko kwa wale walioelimika na wenye ujuzi; katika ujumla wa
mifumo yake wanapata kitu kinachoafikiana na mielekeo yao. Shetani anachunguza kila dalili ya dhaifu
wa tabia ya kibinadamu, anabainisha dhambi ambazo kila mmoja anaelekea kuzifanya, kisha
anahakikisha kwamba fursa hazipungui kutosheleza kukidhi hali ya kuelekea katika dhambi.
Anawashawishi watu kuzidisha kiasi katika kile ambacho ni halali, akiwasababishia, kupitia kutokuwa na
kiasi, wadhoofishe nguvu za mwili, za akili, na za kimaadili. Ameharibu na bado anaharibu maelfu ya
watu kwa njia ya kutimiza tamaa zao za mwili, na hivyo kuifanya tabia yote ya mwanadamu kuwa kama
ya hayawani. Na katika kuikamilisha kazi yake, anasema, kupitia kwa mapepo kwamba “ujuzi wa kweli
unamweka mwanadamu juu ya sheria yote;” kwamba “chochote kilichopo, ni halali;” kwamba “Mungu
hahukumu;” na ya kwamba “dhambi zote zinazotendwa hazina hatia.” Watu wanaposhawishika kusadiki
kwamba nia zao ndiyo sheria ya juu kuliko zote, kwamba uhuru ni ruhusa ya kufanya watakavyo, na ya
kwamba mwanadamu anawajibika kwake yeye mwenyewe tu, nani awezaye kushangaa kwamba kila
mahali kumejaa (556) upotovu na ufisadi? Watu wengi wanakubali kwa shauku mafundisho
yanayowaacha katika uhuru wa kufuata mivuto ya moyo wenye tamaa. Hatamu za kujitawala
zimewekwa katika shingo ya tamaa, nguvu za akili na roho zimefanywa kutawaliwa na mwelekeo wa
kihayawani, na Shetani kwa shangwe anawaswaga na kuwaingiza katika wavu wake maelfu ya wale
wanaojidai kuwa wafuasi wa Kristo.
Lakini hakuna haja ya mtu yeyote kudanganywa na madai ya uongo ya umizimu. Mungu amewapatia
walimwengu nuru ya kutosha kuwawezesha kugundua mtego huo. Kama ilivyokwisha kuonyeshwa,
nadharia inayounda msingi wenyewe wa umizimu inapigana vita dhidi ya maneno yaliyo wazi sana ya
Maandiko. Biblia inasema wazi kwamba wafu hawajui neno lolote, kwamba mawazo yao yamepotea;
hawana sehemu tena katika jambo lolote linalofanyika chini ya jua; kwamba hawajui habari yoyote ya
furaha au huzuni ya wale waliokuwa wapendwa wao wakubwa walioko duniani.
Zaidi ya hayo, Mungu amekataza kabisa hayo yote yanaoitwa mawasiliano na roho za waliokufa. Mnamo
siku za Waebrania kulikuwa na kundi la watu ambao walidai kuwa na mawasiliano na wafu, kama
wanavyofanya wenye imani ya umizimu wa leo. Lakini wale “pepo wa utambuzi,” kama walivyoitwa
wageni hawa watokao katika malimwengu mengine, wanatangazwa na Biblia kuwa hao ni “roho za

323
mashetani.” (Linganisha na Hesabu 25:1-3; Zaburi 106:28; 1 Wakorintho 10:20; Ufunuo 16:14.) Kazi ya
kushirikiana na “pepo wa utambuzi” ilitangazwa kuwa chukizo kwa Bwana, na jambo hilo lilikatazwa
sana kwa adhabu ya kifo. Mambo ya Walawi 19:31; 20:27. Jina lile lile la uchawi sasa linabezwa. Madai
kwamba wanadamu wanaweza kushirikiana na pepo waovu yanaonekana kama hadithi za uongo za Zama
za Giza. Lakini imani ya mizimu, ambayo ina idadi ya waongofu inayofika mamia ya maelfu, naam,
mamilioni, ambayo imejipenyeza na kuingia katika nyanja za wanasayansi, ambayo imevamia makanisa,
na imejipatia kupendwa katika vyombo vya kutunga sheria, na hata katika ikulu za wafalme -
udanganyifu huu mkubwa ni urejeshaji tu wa uchawi ule uliolaaniwa na kukatazwa hapo zamani,
unaokuja katika mwonekano mpya uliojificha.
Ingekuwa hakuna ushahidi mwingine wa tabia halisi ya umizimu, ingetosha kwa Mkristo kwamba (557)
roho hizo haziweki tofauti ya haki na dhambi, tofauti kati ya mitume wema sana na watakatifu sana wa
Kristo na watumishi wachafu na wapotofu sana wa Shetani. Kwa kuwaonyesha watu waliokuwa waovu
kupindukia kwamba wako mbinguni, na wakiwa wametukuzwa, Shetani anauambia ulimwengu kwamba:
“Haijalishi wewe ni mwovu kiasi gani, haidhuru kama unamwamini Mungu na Biblia au hauamini. Ishi
upendavyo; mbinguni ni nyumbani kwako.” Walimu wa imani ya umizimu hutangaza hivi: “Kila atendaye
mabaya ni mwema machoni pa BWANA, naye huwafurahishwa nao; au, Yuko wapi Mungu mwenye
kuhukumu?” Malaki 2:17. Neno la Mungu linasema: “Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na
kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza.” Isaya 5:20.
Mitume, kama wanavyoigizwa kujitokeza katika roho hizi zidanganyazo, wanafanywa kusema maneno ya
kupingana na yale waliyoandika wakisukumwa Roho Mtakatifu walipokuwa wanaishi duniani.
Wanakanusha kwamba chimbuko la Biblia ni Mungu, na kwa kufanya hivyo wanabomoa msingi wa
tumaini la Mkristo na kuizima nuru ile inayoonyesha njia ya kwenda mbinguni. Shetani anaufanya
ulimwengu uamini kwamba Biblia ni hadithi za kutunga tu, au kitabu kilichofaa kwa wanadamu wa
awali, lakini kwa sasa hakifai kuzingatiwa sana, au kuwekwa pembeni kama kitu kilichopitwa na wakati.
Anahimiza maonyesho ya mambo ya roho kama mbadala wa neno la Mungu. Hapa kuna ambayo kwa
ujumla iko chini ya udhibiti wake; kwa njia hii anaweza kuufanya ulimwengu uamini anachotaka yeye.
Kitabu kile kinachomhukumu yeye na wafuasi wake kinatupwa na yeye kivulini, pale anapotaka kiwe;
anamfanya Mwokozi wa ulimwengu aonekane kama si zaidi ya mwanadamu wa kawaida tu. Na kama vile
askari wa Kirumi waliolilinda kaburi la Yesu walivyoeneza habari za uongo ambazo makuhani na wazee
waliweka vinywani mwao ili wasithibitishe ufufuo wake, ndivyo hao waumini wa ishara za mapepo
wanavyojaribu kufanya ili ionekane kwamba hakuna lolote la kimwujiza mambo yanayohusu maisha ya
Mwokozi wetu. Baada ya kutafuta kwa jinsi hiyo kumweka Yesu nyuma, wanawataka watu kuiangalia
miujiza yao, wakitangaza kwamba miujiza hii ni zaidi ya ile ya Kristo.
Ni kweli kwamba sasa imani ya umizimu inabadili sura yake na, ikiwa imeficha baadhi ya mambo yake
yenye yanayopingwa, inavaa (558) vazi la Kikristo. Lakini maneno yake yanayotoka jukwaani na katika
machapisho yamewekwa mbele ya watu kwa miaka mingi, na katika hayo tabia yake halisi inasimama
ikiwa wazi. Mafundisho hayo hayawezi kukanwa wala kufichwa.
Hata katika sura yake ya sasa, mbali na hali ya kuweza kustahili kuvumiliwa sasa kuliko zamani,
imekuwa ya hatari zaidi, kwa sababu ni udanganyifu ulio mgumu kuutambua kwa urahisi. Wakati awali
ilimshutumu Kristo na Biblia, sasa inakiri kwamba inayakubali yote hayo mawili. Lakini Biblia
inatafsiriwa kwa namna inayoupendeza moyo usiofanywa mpya, wakti kweli nzito na za maana
zinafanywa kuwa zisizo na athari. Upendo unaongelewa sana kuwa ndiyo tabia kuu ya Mungu, lakini
unashushwa na kugeuka kuwa hali dhaifu ya hisia kali za akili, kukiwa hakuna tofauti kati ya jema na
baya. Haki ya Mungu, kemeo lake la dhambi, matakwa ya sheria yake takatifu, yote hayo yamefanywa
324
yasionekane. Watu wanafundishwa kuziangalia amri kumi kama andiko lililokufa. Hadithi potofu
zinazopendeza watu zinayaamsha mawazo ya watu na kuwafanya waikatae Biblia kama msingi wa imani
yao. Kristo anakataliwa kwa hakika kama ilivyokuwa zamani; lakini Shetani ameyapofusha macho ya
watu kiasi kwamba udanganyifu haugunduliki.
Kuna wachache ambao wana dhana sahihi ya nguvu ya udanganyifu ya umizimu na hatari ya kuingia
chini ya ushawishi wake. Wengi wanachezacheza nayo kwa ajili ya kukidhi udadisi wao. Hawana imani
ya kweli katika huo na wangejawa na hofu kuu wawazapo kuhusu kujisalimisha chini ya utawala wa
mapepo. Lakini wanachezea katika uwanja uliokatazwa, na mharibifu mwenye nguvu anatumia uwezo
wake juu yao kinyume na matakwa yao. Hebu mara moja tu washawishike kuisalimisha mioyo yao
upande wake, waone atakavyowakamata mateka. Haiwezekani, kwa nguvu zao wenyewe, kujinasua na
nguvu ya uchawi yenye ushawishi mkubwa. Hakuna kitu cho chote kinachweza kuwaokoa watu hawa
walionaswa mtegoni, isipokuwa nguvu za Mungu zitolewazo kama majibu ya maombi ya dhati
yanayoombwa kwa imani.
Wote wanaendekeza tabia za dhambi, au kwa kupenda kwao wanaendelea na dhambi wanayoijua,
wanakaribisha majaribu ya Shetani. (559) Wanajitenga wenyewe mbali na Mungu na ulinzi wa malaika
zake; pindi yule mwovu anapoleta madanganyo yake, hawa hawana kinga na wanaanguka kuwa mateka
kwa urahisi. Wale wanaojiweka hivyo katika nguvu zake hawatambui sana mahali njia yao itakakoishia.
Akiisha kuwapindua, mjaribu anawatumia kama mawakala wake ili kuwashawishi wengine kuelekea
katika maangamizi.
Nabii Isaya anasema: “Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa
wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je!
waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai? Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa
hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.” Isaya 8:19,20. Ikiwa watu
wangekuwa tayari kuipokea kweli ile iliyoelezwa wazi katika Maandiko kuhusu asili ya mwanadamu na
hali ya wafu, wangeweza kuona katika madai na udhihirisho wa umizimu kutenda kwake Shetani kwa
uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo. Lakini badala ya kuachana na uhuru unaoafikiana na moyo wa
tamaa, na kuzikataa dhambi wazipendazo, watu wengi wanaifumbia macho nuru na kuipita, bila
kuyajali maonyo, wakati Shetani anatega mitego yake kuwazunguka pande zote, nao wanakuwa
mawindo yake. “Kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa,” kwa hiyo “Mungu
anawaletea nguvu ya upotevu; wauamini uongo.” 2 Wathesalonike 2:10,11.
Wale wanaopinga mafundisho ya umizimu wanasumbua, si wanadamu tu, bali Shetani na malaika zake.
Wameingia katika vita dhidi ya falme, na mamlaka na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa
roho. Shetani hataachia hata inchi moja ya himaya yake isipokuwa kama anarudishwa nyuma na nguvu
ya wajumbe wa mbinguni. Lazima watu wa Mungu wakabiliane naye, kama alivyofanya Mwokozi, kwa
kutumia neno: “Imeandikwa.” Shetani anaweza kunukuu Maandiko sasa kama alivyofanya siku zile za
Kristo, naye ataweza kuyapotoa mafundisho ya Biblia ili apate kuyaendeleza madanganyo yake. Wale
watakaosimama katika siku hizi za mwisho za hatari sana inawapasa kuuelewa ushuhuda wa Maandiko
wao wenyewe.
(560) Wengi watakutanishwa na roho za uovu zikiwa katika maumbile ya ndugu zao wapendwa au
marafiki na kuwatangazia uzushi wa hatari mno. Wageni hawa wataamsha mguso mkubwa wa huruma na
watafanya miujiza ili kuuendeleza uongo wao. Yatupasa kuwa tayari kuwapinga kwa kutumia ukweli wa
Biblia kwamba wafu hawajui neno lolote, na ya kwamba wale wanaojitokeza hivyo ni roho za uovu.

325
Punde mbele yetu ipo “saa ya kujaribiwa iliyo tayari kuujia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya
nchi.” Ufunuo 3:10. Wale ambao imani yao haijajikita kwenye neno la Mungu watadanganyika na
kushindwa. Shetani anafanya kazi yake kwa kutumia “madanganyo yote ya udhalimu” ili kuwatawala
wana wa wanadamu, na madanganyo yake yatazidi kuongezeka. Lakini anaweza kulifikia lengo lake tu
kwa kadiri watu wanavyojisalimisha wenyewe katika majaribu yake. Wale ambao wanatafuta kwa bidii
kuijua kweli na wanajitahidi kuzitakasa roho zao kwa kutii, hivyo wakifanya kila wanaloweza kujiandaa
kwa pambano hilo, watapata ngome imara ndani ya Mungu wa kweli. “Kwa kuwa umelishika neno la
subira yangu, Mimi nami nitakulinda” (Fungu la 10), ni ahadi ya Mwokozi. Yeye angeweza punde kutuma
kila malaika kutoka mbinguni kuwalinda watu wake kuliko kumwacha mtu mmoja anayemtumainia
kushindwa na Shetani.
Nabii Isaya anaufunua udanganyifu wa kuogofya utakaowajia waovu, ukiwafanya wajione kuwa wako
salama kutokana na hukumu za Mungu: “Tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu; pigo
lifurikalo litakapopita, halitatufikia sisi; kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu,
tumejificha chini ya maneno yasiyo kweli.” Isaya 28:15. Katika kundi hili linaloelezwa wamo wale
ambao kwa kiburi chao cha kutotaka kutubu wanajifariji kwa maneno yao wakisema kwamba mwenye
dhambi hataweza kuhukumiwa; kwamba wanadamu wote, haidhuru wawe waovu kiasi gani,
watakwezwa mpaka mbinguni, kwenda kuwa kama malaika wa Mungu. Lakini kwa mkazo zaidi (561)
wapo wale wanaofanya agano na mauti na kufanya mapatano na kuzimu, ambao wanakataa kweli
ambazo zimetolewa na Mbingu kuwa kinga kwa wenye haki katika siku ya taabu, na badala yake
wanakubali kimbilio la uongo uliotolewa na Shetani - madanganyo ya uongo ya umizimu.
Jambo la kushangaza zaidi ya maelezo ni upofu wa watu wa kizazi hiki. Maelfu wanakataa neno la
Mungu kwamba halistahili kuaminiwa na kwa juhudi ya ujasiri wanayapokea madanganyo ya Shetani.
Wenye mashaka na wenye dhihaka wanaushutumu ushupavu wa dini walio nao wale wanaoishindania
imani ya manabii na mitume, na wanapinda na kujielekeza katika kuyadhihaki maneno mazito ya
Maandiko yanayomhusu Kristo na mpango wa wokovu, na kisasi kitakachowajilia wale wanaokataa
ukweli. Wanajifanya kana kwamba wana huruma sana kwa watu hao wanaoonekana wenye mawazo
finyu, duni, na ya ushupavu ambao wanakubali madai ya Mungu na kuyatii matakwa ya sheria yake.
Wanajionyesha wenyewe kama walio na hakika kama vile walikuwa wamefanya agano na mauti na
mapatano na kuzimu - kama vile walikuwa wameweka kizuizi kisichopitika, kisichopenyeka kati yao na
adhabu ya Mungu. Hakuna kitu kinachoweza kuamsha hofu zao. Wamejitoa kikamilifu kwa mjaribu,
wameungana naye kwa karibu sana, na kujazwa na roho yake kabisa, kiasi kwamba hawana wala
mwelekeo wa kujinasua kutoka katika mtego wake.
Kwa muda mrefu Shetani amekua akijitayarisha kufanya jitihada yake ya mwisho ya kuudanganya
ulimwengu. Msingi wa kazi yake uliwekwa kwa uhakika uliotolewa kwa Hawa mle Edeni: “Hakika
hamtakufa.” “Siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama
miungu, mkijua mema na mabaya.” Mwanzo 3:4,5. Kidogo kidogo ametayarisha njia kwa madanganyo
yake ya juu kwa kuendeleza umizimu. Bado hajakifikia ukamilifu wa hila zake anazotaka kukamilisha;
lakini kitafikiwa katika muda wa masalio wa siku za siku za mwisho. Nabii anasema: “Nikaona roho tatu
za uchafu zilizofanana na vyura … Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, (562) zitokazo na
kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.”
Ufunuo 16:13,14. Ulimwengu wote utakumbwa na kuingizwa katika madanganyo hayo, isipokuwa wale
tu wanaolindwa na nguvu za Mungu, kwa njia ya imani yao katika neno lake. Watu wanaliwazwa haraka
katika usingizi wa usalama wa bandia, waje kuamshwa tu na tukio la kumwagwa kwa ghadhabu ya
Mungu.

326
Bwana Mungu anasema: “Nami nitafanya hukumu kuwa ndiyo kanuni, na haki kuwa ndiyo timazi; na
mvua ya mawe itachukulia mbali hilo kimbilio la maneno ya uongo, na maji yatapagharikisha mahali pa
kujisitiri. Na agano lenu mliloagana na mauti, litabatilika, tena mapatano yenu mliyopatana na kuzimu
hayatasimama; pigo lifurikalo litakapopita, ndipo ninyi mtakapokanyagwa nalo.” Isaya 28:17,18.

327
Sura ya 35
UHURU WA DHAMIRI WATISHWA

Hivi sasa Uroma unatazamwa na Waprotestanti kwa namna ya kupendwa kwa mbali sana ukilinganisha
na miaka iliyopita. Katika nchi zile ambako Ukatoliki hauna nguvu sana, na pale ambapo watu wa upapa
wanachukua hatua za maridhiano ili kujiongezea ushawishi, kuna ongezeko la hali ya kutojali
mafundisho yanayotofautisha makanisa ya matengenezo na msonge wa upapa; mtazamo unaozidi
kuenea miongoni mwa Waprotestanti ni kwamba, hata hivyo, hatutofautiani sana katika mambo ya
muhimu kama ilivyodhaniwa, na kwamba kupunguza msimamo kidogo kwa upande wetu kutatuleta
katika maelewano bora zaidi na Roma. Kuna wakati Waprotestanti walithamini sana sana uhuru wa
dhamiri uliokuwa umenunuliwa kwa gharama kubwa. Waliwafundisha watoto wao kuuchukia sana upapa
na kushikilia msimamo kwamba kutafuta maafikiano na Roma kungekuwa ni kumwasi Mungu. Lakini ni
tofauti kubwa kiasi gani iliyopo katika mtazamo unaoonyeshwa sasa!
Watetezi wa upapa wanasema kwamba kanisa hilo limekashifiwa, na Waprotestanti wanaelekea
kukubali kauli hiyo. Wengi wanasema kwamba si haki kulishutumu kanisa la leo kwa machukizo na
makosa yaliyojitokeza katika kipindi cha utawala wake mnamo karne zile za ujinga na giza. Wanatoa
udhuru kwamba ukatili wake wa kutisha ni matokeo ya ushenzi uliokuwako nyakati zile na wanadai
kwamba ushawishi wa ustaarabu wa siku hizi umebadili mtazamo wa kanisa hilo.
(564) Je, watu hawa wamesahau madai ambayo yalitolewa na mamlaka hiyo yenye majivuno kwa miaka
mia nane kwamba kanisa haliwezi kukosea? Badala ya kuyatupilia mbali, madai hayo yalithibitishwa kwa
mkazo mkubwa mnamo karne ya kumi na tisa kwa mbali kuliko kabla. Kama Roma inadai kwamba
“kanisa halikuwahi kukosea kamwe; wala halitakosea, kulingana na Maandiko,” 394 inawezaje kuziacha
kanuni hizo ambazo ziliongoza mwenendo wake katika zama zilizopita?
Kamwe kanisa hilo la kipapa halitaacha madai yake kwamba haliwezi kukosea. Linadai kwamba yote
ambayo limeyafanya katika kuwatesa wale wanaokataa mafundisho yaliyowekwa na kanisa yako sahihi;
na je, haliwezi kurudia matendo yale yale endapo nafasi ingejitokeza? Hebu vipingamizi vinavyowekwa
na serikali za kidunia viondolewe na Roma irejeshwe tena katika utawala wake kama zamani, ndipo kwa
haraka sana ungeamshwa udikteta wake na mateso.
Mwandishi mmoja anayejulikana vema anasema habari ya mtazamo wa utawala msonge wa kipapa
kuhusu uhuru wa dhamiri, na kuhusu hatari hasa zinazoitishia Marekani kutokana na kufanikiwa kwa sera
ya Roma:
“Wapo wengi walio na mwelekeo wa kuonyesha kwamba hofu ya kuuogopa Ukatoliki wa Kirumi katika
nchi ya Marekani ni kukosa uvumilivu au tabia ya kitoto. Watu kama hao hawaoni jambo lolote katika
tabia na mtazamo wa Uroma ambavyo vina uadui kwa taasisi zetu zilizo huru, au hawaoni lolote la
kushtusha katika ukuaji wa Uroma. Hebu, basi, tulinganishe kwanza baadhi ya kanuni za msingi za
serikali yetu na zile za Kanisa Katoliki.

394
John L. von Mosheim, Institutes of Ecclesiastical History, book 3, century II, part 2, chapter 2, section 9, note 17

328
“Katiba ya Marekani inatoa sharti la kuruhusu uhuru wa dhamiri. Hakuna jambo lililo la thamani sana au
la msingi sana kama hilo. Papa Pius wa IX, katika Barua ya Kipapa aliyoandika Agosti 15, 1854, alisema:
‘Mafundisho yasiyofaa na ya uongo au yasiyo maana ya kutetea uhuru wa dhamiri ni kosa baya sana la
kutisha – ni kitu chenye uharibifu, miongoni mwa mengine, ya kuogopwa zaidi katika taifa.’ Papa huyo
huyo, katika Barua ya Kipapa ya Desemba 8, 1864, aliwalaani ‘wale wanaodai uhuru wa dhamiri na wa
ibada (565) ya dini,’ pia ‘wale wote wanaoona kwamba kanisa haliwezi kutumia mabavu.’
“Maneno ya Roma ya kuhimiza amani katika nchi ya Marekani hayamaanishi badiliko la moyo wake.
Anakuwa mvumilivu pale anapokuwa hana la kufanya. Askofu O‘Conner anasema: ‘Uhuru wa dini
unavumiliwa mpaka hapo tu upinzani unapoweza kuendelezwa bila kuuhatirisha ulimwengu wa
Kikatoliki.’… Askofu mkuu wa St. Louis alisema wakati fulani: ‘Uzushi na kutokuamini ni uhalifu; na
katika nchi za Kikristo, kama Italia na Hispania, kwa mfano, ambako watu wote ni Wakatoliki, na
ambako dini ya Kikatoliki ni sehemu muhimu ya sheria za nchi, mambo hayo yanaadhibiwa kama makosa
mengine ya uhalifu.’…
Kila Kadinali, askofu mkuu, na askofu wa kawaida katika Kanisa la Katoliki anakula kiapo kuwa mtiifu
kwa papa, ambapo ndani ya kiapo hicho kuna maneno yafuatayo: ‘Wazushi, watu waletao mgawanyiko,
na waasi dhidi ya yeye aitwaye bwana wetu (papa), au warithi wake waliokwisha tajwa, nitawatesa na
kuwapinga kwa nguvu zangu zote.’” 395
Ni kweli kwamba kuna Wakristo wa kweli katika jamii ya Roman Catholic. Maelfu ya watu katika kanisa
hilo wanamtumikia Mungu kulingana na nuru iliyoonekana kubwa kwao. Hawaruhusiwi kupata neno lake,
na kwa sababu hiyo hawapambanui ukweli. Kamwe hawajapata kuona tofauti iliyopo kati ya huduma
iliyo hai inayofanywa kwa moyo na ile ya desturi za kukariri na maadhimisho. Mungu anawaangalia watu
hawa kwa huruma ya upendo, wakiwa wameelimishwa kama walivyo katika imani ya uongo na
isiyoridhisha. Ataifanya miale ya nuru kupenya giza nene linalowazunguka. Atawafunulia ukweli kama
ulivyo ndani ya Yesu, na wengi watachagua kusimama upande wa watu wa Mungu.
Lakini kwa sasa Uroma kama mfumo hauendani na injili ya Kristo zaidi ya vile ulivyokuwa katika kipindi
chochote cha nyuma katika historia yake. Makanisa ya Kiprotestanti yako katika giza kubwa, la sivyo
wangezitambua dalili za nyakati. Kanisa la Roma limefika mbali sana katika mipango yake na njia za
utendaji wake. Linatumia kila hila kueneza ushawishi wake na kuongeza mamlaka yake katika kujiandaa
kwa pambano (566) kali na la kudhamiria ili kuirudia hali ya kuutawala ulimwengu, kuanzisha mateso
tena, na kubomoa yote ambayo Uprotestanti umefanya. Ukatoliki unajieneza sana kila eneo. Angalia
idadi ya makanisa yake makubwa na madogo yanayozidi kuongezeka katika nchi za Kiprotestanti.
Angalia umaarufu wa vyuo vyake na seminari zake katika nchi ya Amerika, ambavyo vinaungwa mkono
na Waprotestanti. Angalia ukuaji wa taratibu zake za ibada katika nchi ya Uingereza na mara kwa mara
watu wengine kutoroka na kuingia katika safu za Wakatoliki. Mambo haya yangeamsha wasiwasi kwa
wote wanaothamini kanuni safi za injili.
Waprotestanti wanachezea upapa na kuuunga mkono; wamefanya maridhiano na maelewano ambayo
hata watu wa upapa wenyewe wanashangaa kuyaona na wanashindwa kuelewa. Watu wanafumba
macho wasione tabia halisi ya Uroma na hatari zinazojulikana kutokana na hatamu za utawala wake.
Watu wanahitaji kuamshwa ili kupinga kusonga mbele kwa huyu adui wa hatari aliye kinyume na uhuru
wa serikali na uhuru wa dini.

395
Josiah Strong, Our Country, ch. 5, pars. 2-4. (Angalia maelezo mwishoni kuhusu masahihisho ya rejea hii).

329
Waprotestanti wengi wanadhani kwamba dini ya Kikatoliki haivutii na kwamba ibada yake imepooza,
haina maana na ni ya mazoea. Hapo wanakosea. Wakati Uroma umejengwa katika uongo, si udanganyifu
wa hovyo usiopangiliwa. Huduma ya ibada ya Kanisa la Kirumi ni ya utaratibu wenye kuvutia sana. Uzuri
wa taratibu zake za ibada zenye mwonekano wa kicho hupumbaza mawazo na kunyamazisha sauti ya
fikra na dhamiri. Jicho linavutiwa sana. Makanisa makubwa ya kifahari, mpangilio wa kuvutia wa
maandamano, altare za dhahabu, mahali patakatifu palipopambwa kwa vito, rangi zilizopakwa kwa
kuchaguliwa vema, na sanamu za kuchongwa zilizonakshiwa vizuri na kuwa na mwonekano wa
kupendeza, vinavutia macho. Sikio nalo pia hunaswa. Muziki hauna mfano wa kuuzidi. Sauti tamu za
kinanda chenye sauti zilizotulia, zikichanganyika na sauti tamu za kuimba zitokazo kwa watu wengi
waliokaa katika safu za chini na juu ghorofani katika makanisa makubwa yenye nguzo na mapaa marefu
ya mviringo, haviwezi kushindwa kusababisha moyo wenye hofu na kusababisha heshima.
Fahari hii ya nje nje, maonyesho, na maadhimisho, mambo ambayo yanadhihaki mahangaiko ya moyo
unaougua kwa dhambi, ni ushahidi wa upotovu wa ndani. Dini ya Kristo haihitaji vivutio kama hivyo
kuifanya ikubalike. Katika nuru inayoangaza kutoka msalabani, Ukristo wa kweli unajitokeza ukiwa safi
na wa kupendeza kiasi kwamba hakuna (567) mapambo ya nje yanayoweza kuongeza thamani yake ya
kweli. Kilicho cha thamani mbele za Mungu ni uzuri wa utakatifu, roho ya upole na utulivu.
Uzuri wa mtindo si lazima uwe kigezo cha mawazo masafi, na bora. Usanii wa hali ya juu, mvuto
mwororo, mara nyingi huwa katika mioyo inayopenda dunia na tamaa. Mara kwa mara vinatumiwa na
Shetani kuwafanya watu wasahau mambo muhimu ya roho zao, kuwafanya kushindwa kuona mambo
yajayo, ya uzima wa milele, kuwafanya kumpa kisogo Msaidizi wao wa milele, na kuishi kwa ajili ya
ulimwengu huu tu.
Dini ya mambo ya nje inavutia kwa moyo ambao haujaumbwa upya. Maonyesho na maadhimisho ya
ibada za Kikatoliki vina nguvu za kushawishi na kuleta msukumo, vitu ambavyo watu wanadanganywa
navyo; na wanafika mahali pa kuliangalia Kanisa la Kirumi kama mlango wenyewe wa kuingilia
mbinguni. Hakuna wanaoweza kujikinga na ushawishi wake isipokuwa wale waliosimamisha miguu yao
kwa uimara katika msingi wa ukweli, na ambao mioyo yao imefanywa upya na Roho wa Mungu. Maelfu
ambao hawana maarifa ya kumjua Kristo kwa vitendo watapelekwa katika kukubali mfano tu wa utauwa
bila nguvu. Dini kama hiyo ndiyo inayotamaniwa na watu wengi.
Madai ya kanisa kuwa na haki ya kusamehe dhambi humfanya Mrumi kuhisi kuwa huru kutenda dhambi;
na ibada ya kitubio, ambayo bila hiyo msamaha wa dhambi wa kanisa hautolewi, ina tabia ya kutoa
kibali cha watu kufanya uovu. Yeyote apigaye magoti mbele ya mwanadamu aliyeanguka, na kufungua
mawazo ya siri na hisia za moyoni mwake katika maungamo, anadhalilisha utu wake na kufedhesha
hadhi ya msukumo wake wa ndani. Katika kuzifunua dhambi za maisha yake kwa padri, - ambaye ni mtu
anayekosea, mdhambi mwenye maisha ya kufa, na mara nyingi mtu aliyechafuliwa na mvinyo na
uasherati, - kiwango cha tabia ya mtu huyu kinashushwa, na matokeo yake ananajisika. Fikra zake
kuhusu Mungu zinashushwa chini na kumfananisha Mungu na binadamu aliyeanguka, maana yule padri
anasimama kama mwakilishi wa Mungu. Maungamo haya ya mwanadamu kwa mwanadamu yanayoshusha
hadhi ndiyo chemchemi ya siri ambako yametoka maovu mengi yanayonajisi ulimwengu na kuufanya
ufae kwa ajili ya maangamizi ya mwisho. Lakini kwa mtu apendaye kujifurahisha katika tamaa, (568)
inapendeza zaidi kuungama dhambi zake kwa mwanadamu mwenzake kuliko kuufungua moyo wake kwa
Mungu. Ni jambo tamu kwa mwanadamu wa kawaida kuwa tayari kufanya malipizi ya kitubio kuliko
kuacha dhambi; ni rahisi kuutesa mwili kwa kuvaa nguo za magunia na kujimwagia mwasho wa upupu na
kujifunga kwa minyororo iumizayo kuliko kuzisulibisha tamaa za mwili. Kongwa ambalo moyo wa tamaa
unaafiki kubeba ni zito kuliko kuinama na kujitia nira ya Kristo.
330
Kuna mfanano mkubwa kati ya Kanisa la Roma na Kanisa la Wayahudi la wakati Yesu alipokuja mara ya
kwanza. Wakati Wayahudi walikuwa wakikanyaga kwa siri kila kanuni ya sheria ya Mungu, kwa nje
walikuwa wakali katika mambo ya kuzitii amri zile, wakikandamiza kwa madai yao na mapokeo yao
yaliyofanya utii kuwa mchungu na wa mzigo. Kama Wayahudi walivyodai kuiheshimu sheria, ndivyo
Warumi wanavyodai kuuheshimu msalaba. Wanaitukuza alama ya mateso ya Kristo, wakati wakimkana
katika maisha yao yeye ambaye anawakilishwa na msalaba.
Watu wa upapa huweka misalaba kwenye makanisa yao, kwenye altare zao, na kwenye mavazi yao. Kila
mahali huonekana alama ya msalaba. Kila mahali msalaba unaheshimiwa na kutukuzwa kwa mwonekano
wa nje. Lakini mafundisho ya Kristo yanazikwa chini ya mkusanyiko wa mapokeo yasiyo na maana,
tafsiri za uongo, na amri za shuruti. Maneno ya Mwokozi kuhusu Wayahudi waliokuwa shupavu, bado
yanawahusu viongozi wa Kanisa Katoliki la Roma kwa uzito mkubwa zaidi: “Wao hufunga mizigo mizito
na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao.” Mathayo 23:4. Watu
wanaotii maelekezo ya wengine wamewekwa wakati wote katika hali ya hofu wakiogopa ghadhabu ya
Mungu anayechukizwa na maovu, wakati viongozi wakubwa wengi katika kanisa wanaishi maisha ya
anasa na uasherati.
Ibada ya sanamu na masalia ya miili ya watakatifu waliokufa zamani, kuomba watakatifu, na kumtukuza
papa ni mbinu anazotumia Shetani kuivuta mioyo ya watu iondoke kwa Mungu na kwa Mwana wake. Ili
kukamilisha kuangamizwa kwao, anajitahidi kugeuza usikivu wao kwenda mbali na yeye ambaye kupitia
kwake yeye peke yake wanaweza kupata wokovu. Ataelekeza mawazo yao kwenye kitu kingine chochote
kinachoweza kuwekwa mahali pa Yeye aliyesema: “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao (569) na
wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.” Mathayo 11:28.
Ni jitihada ya Shetani wakati wote kueleza vibaya tabia ya Mungu, asili ya dhambi, na masuala muhimu
yenye mguso mkubwa katika pambano kuu. Uongo wake hulegeza wajibu kwa sheria ya Mungu na
kuwapa watu kibali cha kutenda dhambi. Wakati huo huo anawafanya watu wawe na mawazo potofu juu
ya Mungu wakimwangalia kwa hofu na chuki badala ya kumwangalia kwa upendo. Ukatili ambao ni asili
ya tabia yake mwenyewe unawekwa kwa Mwumbaji; unawekwa katika mifumo ya dini na kuonyeshwa
katika taratibu za ibada. Hivyo akili za wanadamu hupofushwa, na Shetani anawachukua na kuwafanya
mawakala wake wapate kufanya vita dhidi ya Mungu. Kwa mawazo yaliyopotoshwa kuhusu sifa za tabia
ya Mungu, mataifa ya kishenzi yalifanywa kuamini kwamba kuwatoa wanadamu kama kafara ilikuwa
muhimu ili kupata upendeleo wa Mungu; na ukatili wa kuogofya umefanywa chini ya mifumo mbalimbali
ya ibada ya sanamu.
Kanisa Katoliki la Roma, likiunganisha mifumo ya upagani na ya Ukristo, tena, kama upagani
ulivyofanya, likiieleza vibaya tabia ya Mungu, limeingia katika vitendo vya kikatili na vya kuchukiza
ambavyo si haba ukilinganisha na vile. Mnamo siku za Roma kushika hatamu kulikuwa na vyombo vya
mateso ili kulazimisha watu wakubali mafundisho yake ya dini. Kulikuwa na nguzo ya kuchomea watu
moto iliyokuwepo kwa ajili ya wale ambao hawakukubali matakwa yake. Kulikuwa na mauaji ya halaiki
kwa kipimo ambacho hakitaweza kufahamika mpaka hapo kitakapofunuliwa katika hukumu. Chini ya
bwana wao Shetani, viongozi wakuu wa kanisa walijifunza kuvumbua njia za kusababisha mateso
makubwa iwezekanavyo lakini yasiondoe uhai wa mtu anayeteswa. Katika matukio mengi, kitendo cha
mateso maovu kilirudiwa-rudiwa mpaka kufikia kilele cha uvumilivu wa mwili wa mwanadamu, kiasi cha
mwili kusalimu amri, na mhanga wa mateso kupokea kifo chake kama furaha ya kufunguliwa kwake
kutoka katika hali ile.

331
Hiyo ilikuwa ndiyo hatima ya watu wanaoipinga Roma. Ili kupata kutiiwa Roma ilikuwa na adhabu ya
kupiga mijeledi, kutesa kwa njaa, na kuutesa mwili wa mtu kwa maumivu makali kwa kila njia
inayofikirika kuweza kuumiza na kuleta maumivu ya moyo. Ili kupata msamaha wa Mungu, wale
waliokuwa wanatubu walizivunja sheria za Mungu kwa kuzivunja sheria za asili za maumbile.
Walifundishwa kuvunja vifungo vya mahusiano ambavyo Mungu aliviweka ili kumbariki na kumpa furaha
mwanadamu katika maisha yake duniani. Uwanja wa makaburi ya kanisa umejaa mamilioni ya (570)
wahanga waliotumia maisha yao yote kwa kujitahidi pasipo mafanikio kuyabana mapenzi yao ya asili,
kukandamiza kila wazo na hisia ya huruma kwa viumbe wenzao, kwamba ni kitu cha kumchukiza Mungu.
Kama tunataka kuelewa ukatili wa Shetani uliodhamiriwa, ulioonyeshwa kwa mamia ya miaka, ukiwa
hauonyweshwi miongoni mwa wale waliokuwa hawajapata kusikia habari za Mungu, bali katikati kabisa
na katika eneo lote la ulimwengu wa Kikristo, tunahitaji kuiangalia historia ya Uroma. Kwa njia ya
mfumo huu mkubwa wa udanganyifu, yule mkuu wa uovu anafikia kusudi lake la kuondoa heshima kwa
Mungu na kumletea mwanadamu huzuni. Na kadiri tunavyomwona jinsi anavyofanikiwa katika kujigeuza-
geuza na kutekeleza kazi yake kupitia kwa viongozi wa kanisa, tunaweza kuelewa zaidi ni kwa nini ana
chuki sana dhidi ya Biblia. Ikiwa kitabu hicho kitasomwa, rehema na upendo wa Mungu utafunuliwa;
itaonekana wazi kwamba Mungu haweki juu ya wanadamu mizigo mizito yoyote katika hii iliyopo. Kwa
ujumla anachokitaka Mungu kwao ni moyo uliovunjika na kupondeka, roho ya unyenyekevu, na ya utii.
Kristo hatoi kielelezo chochote katika maisha yake kinachowafanya wanaume na wanawake kujifungia
katika nyumba za kitawa ili wapate kufaa kwa ajili ya mbingu. Hajawahi kufundisha kwamba upendo na
huruma vinalazimishwa kwa nguvu. Moyo wa Mwokozi ulifurika upendo. Kadiri mwanadamu
anavyokaribia ukamilifu wa kimaadili, ndivyo fahamu zake zinavyozidi kuwa nzuri, ndivyo
anavyoitambua dhambi zaidi, na ndivyo anavyokuwa na kina katika huruma kwa wanaoteswa. Papa
anadai kuwa mwakilishi wa Kristo; lakini, sifa zake zinalinganaje na zile za Mwokozi wetu? Je, Kristo
alipata kujulikana kwamba alifunga watu gerezani au kuwalaza kwenye kitanda cha kutesea kwa sababu
walikuwa wamekataa kumpa heshima kama Mfalme wa mbinguni? Je, sauti yake ilisikika ikitangaza
adhabu ya kifo kwa watu waliomkataa? Wakati alipopuuzwa na watu wa kijiji cha Samaria, mtume
Yohana alijawa na hasira, na akauliza: “Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni,
uwaangamize; kama Eliya naye alivyofanya?” Yesu alimwangalia mwanafunzi wake yule kwa huruma, na
kuikemea roho yake ya ukatili, akisema: “Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali
kuziokoa.” Luka 9:54,56. Ni tofauti iliyoje iliyopo kati (571) ya roho aliyoionyesha Kristo na ile
inayoonyeshwa na yule anayesemwa kuwa ni mwakilishi wake.
Kwa sasa Kanisa la Roma linaonyesha uso wa haki ulimwenguni, likifunika kumbukumbu yake ya ukatili
wa kutisha kwa kuomba radhi. Limejivika mavazi kama ya Kristo; lakini halijabadilika. Kila kanuni ya
upapa iliyokuwako katika vizazi vilivyopita bado ipo hata leo. Mafundisho yake ya dini yaliyotungwa
katika zama zile za giza kubwa bado yanashikiliwa mpaka sasa. Hebu wasiwepo watu wanaojidanganya
wenyewe. Upapa ambao Waprotestanti wako tayari kuuheshimu hivi sasa ni ule ule ulioitawala dunia
katika siku za Matengenezo, wakati watu wa Mungu waliposimama, kwa gharama ya maisha yao, ili
kuufichua uovu wake. Ana kiburi kile kile na madai yake ya kujinyakulia mamlaka juu ya wafalme na
wakuu wa nchi, na alidai kuwa na haki za Mungu. Roho yake haijapungua ukatili na ukandamizaji wake
siku hizi ikilinganishwa na wakati ule alipoupondaponda uhuru wa wanadamu na kuwachinja watakatifu
wake Aliye Juu.
Upapa uko vile vile unabii unavyotangaza kwamba ungekuwa, yaani uasi wa nyakati za mwisho. 2
Wathesalonike 2:3,4. Ni sehemu ya mbinu yake kuchukua tabia itakayomwezesha kutimiza vema kusudi
lake; lakini chini ya mwonekano wake kama wa kinyonga anaficha sumu kali ya nyoka. Anasema, “Imani
332
haipaswi kuwa pamoja na wazushi, wala watu wanaohisiwa kuwa wazushi” (Lenfant, volume 1, page
516). Je, mamlaka hii, ambayo kumbukumbu zake kwa miaka elfu moja zimeandikwa kwa damu ya
watakatifu, inaweza kukubalika sasa kwamba ni sehemu ya Kanisa la Kristo?
Madai yanayotolewa katika nchi za Kiprotestanti kwamba Ukatoliki sasa unatofautiana kidogo sana na
Uprotestanti kuliko ilivyokuwa katika zama zilizopita halitokei bila sababu. Kumekuwa na badiliko;
lakini si badiliko katika upapa. Ni kweli Ukatoliki unafanana na sehemu kubwa ya Uprotestanti uliopo
sasa, kwa sababu Uprotestanti umeshuka kiwango sana tangu siku zile za Wanamatengenezo.
Kadiri ambavyo makanisa ya Kiprotestanti yamekuwa yakitafuta kupendwa na ulimwengu, ukarimu wa
uongo umeyapofusha macho. Hawaoni kitu isipokuwa kuona ni sahihi kuamini kwamba maovu ni mema,
na kama matokeo yake yasiyoepukika hatimaye wataamini kwamba mema ni maovu. (572) Badala ya
kusimama imara na kuitetea ile imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu, sasa wao, kama
ilivyokuwa, wanaomba radhi kwa Roma kwa sababu ya maoni yao yasiyo ya upendo dhidi yake,
wanaomba msamaha kwa ushupavu.
Kundi kubwa, hata la wale wasioupenda Uroma, wanatambui kidogo sana hatari inayowakabili kutokana
na mamlaka yake na ushawishi wake. Wengi husema kwamba giza la kiufahamu na kimaadili
lililokuwepo katika kipindi kile cha Zama za Kati lilimnufaisha kueneza mafundisho yake ya kutunga,
ushirikina wake, na ukandamizaji wake, na kwamba maarifa makubwa ya nyakati hizi za sasa, kuenea
kwa maarifa kwa ujumla, na kuongezeka kwa uliberali katika mambo ya dini kunazuia kurejea kwa roho
ya kutovumilia imani na roho ya ukandamizaji. Wazo lenyewe kwamba hali kama hiyo ya mambo
itakuwepo tena katika kizazi hiki chenye maarifa mengi linabezwa. Ni kweli kwamba nuru kubwa,
kiakili, kimaadili na kidini, inaangaza kwenye kizazi hiki. Katika kurasa wazi za Neno Takatifu la Mungu,
nuru kutoka mbinguni imeangazwa juu ya ulimwengu. Lakini yapaswa kukumbukwa kwamba kadiri nuru
inayotolewa inavyozidi kuwa kubwa, ndivyo giza linavyokuwa nene zaidi kwa wale wanaoipotoa na
kuikataa nuru.
Kujifunza Biblia kwa maombi kungeweza kuwaonyesha Waprotestanti tabia halisi ya upapa na
kungewafanya kuuchukia na kuuepuka; lakini wengi wana hekima sana machoni pao wenyewe kiasi
kwamba hawaoni hitaji la kumtafuta Mungu kwa unyenyekevu ili wapate kuongozwa kwenda katika
ukweli. Ingawa wanajivuna kwa mafunuo ya maarifa, hawajui Maandiko wala uweza wa Mungu. Lazima
wanayo namna ya kunyamazisha dhamiri zao, na wanatafuta kile ambacho si cha kiroho sana au si cha
kunyenyekeza. Wanachotaka ni njia ya kuwawezesha kumsahau Mungu ambayo itaidhinishwa na kuitwa
njia ya kumkumbuka Mungu. Upapa umejiweka tayari kukidhi matakwa ya hawa wote. Umejiandaa kwa
ajili ya makundi mawili ya watu, yanayokusanya karibu ulimwengu wote - wale wanaotaka kuokolewa
kwa kustahili kwao, na wale wanaotaka kuokolewa wakiwa katika dhambi zao. Hapa ndipo pana siri ya
nguvu zake.
Siku ya giza kuu la kiakili imeonyeshwa kwamba inanufaisha mafanikio ya upapa. Lakini bado (573)
itaonekana kwamba siku ya nuru kuu ya kiakili pia inanufaisha mafanikio yake kwa kiasi kile kile. Katika
zama zilizopita, wakati watu walipokuwa hawana neno la Mungu na bila kuujua ukweli, macho yao
yalikuwa yamefungwa katika upofu, na maelfu walikuwa wamenaswa, wakiwa hawaoni wavu
uliotandazwa kwa ajili ya kunasa miguu yao. Katika kizazi hiki wako wengi ambao macho yao
yanashindwa kuona vizuri kwa sababu ya mwanga mkali wa mawazo ya wanadamu ya kufikirika,
“sayansi iitwayo hivyo kwa uongo;” hawaugundui wavu wa mtego, wanaingia ndani yake kwa urahisi
kana kwamba wamefungwa macho yao wasione. Mungu alikusudia kwamba nguvu za akili ya
mwanadamu ziwe kama kipawa kutoka kwa Mwumbaji wake na zitumike katika kazi ya ukweli na haki;

333
lakini pindi kiburi na hamu ya mafanikio ya duniani vinapoendekezwa, na watu wanapozitukuza
nadharia zao na kuziweka juu ya neno la Mungu, ndipo maarifa yanapoweza kuleta madhara makubwa
kuliko ujinga unavyoweza kufanya. Hivyo sayansi ya uongo ya siku hizi, ambayo inaihafifisha imani
katika Biblia, itaonekana kama inafanikiwa katika kutayarisha njia ya kuukubali upapa, na miundo yake
ya kupendeza, kama kule kuficha maarifa kulivyofanya katika kufungua njia ya kupanuka kwake mnamo
Zama za Giza.
Katika harakati zilizopo sasa nchini Marekani za kanisa kupata kuungwa mkono na kuwezeshwa na
serikali, Waprotestanti wanafuata nyayo za watu wa upapa. Naam, zaidi ya hapo, wanaufungulia mlango
upapa katika Amerika ya Kiprotestanti upate kushika tena hatamu za utawala zilizopotea katika
Ulimwengu wa Zamani. Na hali ambayo inazipatia harakati hizo umuhimu mkubwa ni ukweli kwamba
lengo kuu linalofikiriwa ni kuhimiza utunzaji wa Jumapili - desturi ambayo ilianzishwa na Roma, na
ambayo anadai kuwa ishara ya mamlaka yake. Ni roho ya upapa – roho ya kuafikiana na desturi za
ulimwengu, utukuzaji wa mapokeo ya wanadamu zaidi ya amri za Mungu – ambayo inajipenyeza katika
makanisa ya Kiprotestanti na kuwaelekeza kuzidi kufanya kazi ile ile ya kuitukuza Jumapili ambayo
imefanywa na upapa mbele yao.
Ikiwa msomaji angependa kujua njia zitakazotumika katika pambano linalokuja hivi punde, hana budi
kufuatilia tu kumbukumbu za njia zilizotumiwa na Roma kwa lengo lile lile (574) katika vizazi
vilivyopita. Kama anataka kujua jinsi watu wa upapa na Waprotestanti wakiwa wameungana
watakavyoshughulikia wale wanaokataa mafundisho yao, hebu aone roho iliyoonyeshwa na Roma dhidi
ya Sabato na wale walioitetea.
Amri za watawala, mabaraza makubwa, sheria au kanuni za makanisa zinazoungwa mkono na mamlaka
za kidunia ndivyo vilikuwa hatua zilizopitiwa katika kuipatia sikukuu hiyo ya kipagani nafasi ya heshima
katika ulimwengu wa Kikristo. Hatua ya kwanza ya kuhimiza rasmi utunzaji wa Jumapili ilikuwa ni sheria
iliyowekwa na Konstantino (321 B.K.) Amri hii iliwataka watu wa mjini wapumzike katika “siku ya
taadhima ya jua,” lakini iliwaruhusu watu wa mashambani kuendelea na shughuli zao za kilimo. Ingawa
ilikuwa karibia amri ya kipagani, ilihimizwa kutekelezwa na mtawala baada ya kuukubali Ukristo kwa
jina tu.
Kama vile amri hii ya kifalme ilionekana haitoshi kuwa mbadala wa amri ya Mungu, Eusebius, askofu
aliyetafuta kupendwa na wakuu wa nchi, na ambaye alikuwa rafiki maalum wa Konstantino na mwenye
kujipendekeza kwake, aliongeza madai kwamba Kristo alikuwa amehamisha Sabato kwenda Jumapili.
Hakuna ushuhudi wa Maandiko hata mmoja uliotolewa kuthibitisha fundisho hili jipya. Eusebius
mwenyewe pasipo kujua anakiri uongo wa madai hayo na anaonyesha waanzilishi halisi wa mabadiliko
hayo. “Mambo yote,” anasema, “yoyote ambayo yalikuwa wajibu kufanywa siku ya Sabato,
tumeyahamishia katika Siku ya Bwana.” 396 Lakini hoja kuhusu Jumapili, ikiwa haina msingi kama
ilivyokuwa, ilisaidia kuwatia ujasiri watu katika kuikanyaga Sabato ya Bwana. Wote waliopenda
kuheshimiwa na ulimwengu waliikubali sikukuu hii maarufu.
Kadiri upapa ulivyokuwa umeimarika, kazi ya kuitukuza Jumapili iliendelezwa. Kwa wakati fulani watu
waliokuwa hawahudhurii kanisani walishughulika na kilimo, na siku ya saba ilikuwa bado inatambuliwa
kama Sabato. Lakini polepole mabadiliko yakafanywa. Wale waliokuwa katika mahakama ya kanisa
walikatazwa kufanya mashauri yaliyohusu mambo yasiyo ya kidini siku ya Jumapili. Punde baada ya
pale, watu wote, wa ngazi yoyote, waliamriwa kuacha kufanya kazi za kawaida kwa tishio la kutozwa

396
Robert Cox, Sabbath Laws and Sabbath Duties, page 538

334
faini kwa wale waliokuwa raia huru na (575) viboko kwa wale waliokuwa watumwa. Baadaye amri
ilitolewa kwamba matajiri wangeadhibiwa kwa kupoteza nusu ya mashamba yao; na hatimaye, kwamba
endapo wangeendelea kukaidi, wangefanywa kuwa watumwa. Watu wale wa matabaka ya chini
wangefukuzwa moja kwa moja.
Miujiza pia ilitakiwa kutumika. Miongoni mwa maajabu mengine ilisimuliwa kwamba wakati mkulima
mmoja aliyekuwa anataka kulima shamba lake siku ya Jumapili aliposafisha jembe lake kwa chuma,
chuma kile kiling’ang’ania mkononi mwake, na kwa miaka miwili alienda nacho kila alikoenda, “akiwa
na maumivu makali na kwa aibu.” 397
Baadaye papa alitoa maelekezo kwamba padri wa parokia anapaswa kuwakemea wale wanaoivunja
Jumapili na kuwataka waende kanisani na kutoa sala zao, wasije wakaleta balaa kubwa kwao wenyewe
na jirani zao. Baraza la kanisa la kitume lilileta hoja, ambayo tangu hapo imetumika sana, imetumiwa
hata na Waprotestanti, kwamba kwa kuwa watu walikuwa wamepigwa na radi walipokuwa wakifanya
kazi siku ya Jumapili, bila shaka hiyo ni Sabato. “Ni dhahiri,” walisema maaskofu wakuu, “jinsi Mungu
alivyochukizwa sana na kitendo chao cha kutojali siku hii.” Ndipo wito ulitolewa kwamba makasisi na
viongozi wa kiroho, wafalme na wakuu wa nchi, na watu wote walio waaminifu “watumie juhudi zao
zote na hadhari kwamba siku hiyo irejeshwe katika heshima yake, na, kwa heshima ya Ukristo, itunzwe
kwa kicho zaidi kwa ajili ya wakati ujao.” 398
Wakati amri hizo za mabaraza zikidhihirisha kwamba hazitoshelezi, mamlaka za kidunia ziliombwa
kutoa amri ambayo ingeleta utisho katika mioyo ya watu na kuwalazimisha kuacha kufanya kazi siku ya
Jumapili. Katika baraza la sinodi lililofanyika Roma, maamuzi yote ya nyuma yalithibitishwa kwa nguvu
na mkazo mkubwa zaidi. Pia yaliingizwa katika sheria za kanisa na kutekelezwa na mamlaka za
serikalini karibu kote katika ulimwengu wa Kikristo. 399
(576) Bado kukosekana kwa mamlaka ya Kimaandiko kuunga mkono utunzaji wa Jumapili kulileta aibu
ambayo si ndogo. Watu walihoji uhalali wa walimu wao kuliweka kando tangazo jema la Yehova, “Siku
ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako,” wao wakataka kuiheshimu siku ya jua. Kujaza pengo la
ukosefu wa ushuhuda wa Biblia, hatua nyingine zilihitajika. Mtetezi mmoja shupavu wa Jumapili,
ambaye karibu na mwisho wa karne ya kumi na mbili alitembelea makanisa ya Uingereza, alipingwa na
mashahidi waaminifu wa ile kweli; na juhudi zake hazikuzaa matunda kabisa hata akaondoka katika nchi
ile kwa kipindi fulani na kutafuta kila njia ya kuyahimiza mafundisho yake. Wakati aliporudi, mapungufu
yaliondolewa, na baada ya kazi zake hizi za baadaye alipata mafanikio makubwa. Alileta gombo
lililodaiwa kutoka kwa Mungu mwenyewe, ambalo lilikuwa na amri iliyohitajika ya kutunza Jumapili,
ikiwa pamoja na vitisho vya kuogofya ili kuwatisha wale wasiotii. Hati hii ya thamani – ikiwa ya bandia
kama fundisho lenyewe lilivyokuwa - ilisemekana kwamba ilikuwa imedondoka kutoka mbinguni na ya
kwamba ilikuwa imeonekana kule Yerusalemu, kwenye altare ya St. Simeon, kule Golgotha. Lakini,
kiukweli, jumba la kifalme la papa la Roma ndilo chanzo mahali gombo lile lilikotoka. Udanganyifu na
vitu vya kughushi ili kuendeleza mamlaka na usitawi wa kanisa vimetambuliwa na muundo msonge wa
upapa katika vizazi vyote kama mambo halali.
Gombo lile lilikataza ufanyaji wa kazi kuanzia saa tisa, siku ya Jumamosi alasiri, mpaka kuchomoza kwa
jua siku ya Jumatatu; na mamlaka yake ilitangazwa kwamba ilikuwa imethibitishwa kwa miujiza mingi.
Taarifa ilitolewa kuwa watu waliokuwa wakiendelea kufanya kazi zaidi ya muda ule uliosemwa

397
Francis West, Historical and Practical Discourse on the Lord’s Day, page 174
398
Thomas Morer, Discourse in Six Dialogues on the Name, Notion, and Observation of the Lord’s Day, page 271
399
Angalia Heylyn, History of the Sabbath, pt. 2, ch. 5, sec. 7.
335
walipigwa na ugonjwa wa kupooza. Mtu mmoja anayesaga unga alipojaribu kusaga ngano yake, aliona,
badala ya kutoka unga, kutirirka kwa damu, na gurudumu la kinu cha kusagia likasimama lisizunguke,
licha ya maji yenye nguvu kupita. Mwanamke aliyeweka mkate mbichi katika jiko la kuokea aliukuta
mbichi alipoutoa, ingawa jiko la kuokea lilikuwa na moto sana. Mwingine aliyekuwa amekanda mkate
tayari kuuoka kuanzia saa tisa, lakini akaamua kuuweka kando mpaka Jumatatu, siku iliyofuata
aligundua kwamba ulikuwa umetengenezwa katika umbo la mkate na kuokwa kwa nguvu za mbinguni.
Mwanaume aliyeoka mkate baada ya kupita saa tisa (577) siku ya Jumamosi alikuta, alipoumega asubuhi
iliyofuata, kwamba damu inaanza kutoka mle. Kwa kutunga uongo na ushirikina wale walioitetea
Jumapili walijitahidi sana kuthibitisha utakatifu wake. 400
Katika nchi ya Scotland, kama ilivyokuwa Uingereza, kuikubali zaidi Jumapili kulipatikana kwa njia ya
kuiunganishia sehemu ya Sabato ile ya kale. Lakini muda uliowekwa wa kuitakasa ulitofautiana. Amri
toka kwa mfalme wa Scotland ilitangaza kwamba “Jumamosi kuanzia saa sita adhudhuri ingepaswa
kuhesabiwa kuwa ni takatifu,” na ya kwamba asiwepo mtu ye yote, kuanzia saa ile mpaka Jumatatu
alfajiri, atakayejishughulisha na kazi za kiulimwengu. 401
Lakini licha ya juhudi zote zilizofanyika ili kuuweka utakatifu wa Jumapili, watu wa upapa wenyewe
walikiri hadharani mamlaka ya Mungu ya Sabato, na chimbuko la kibinadamu la siku ile ambayo ilikuwa
imewekwa badala yake. Katika karne ya kumi na sita baraza la papa lilitangaza waziwazi: “Wakristo
wote na wakumbuke kwamba siku ya saba iliwekwa wakfu na Mungu, nayo imepokewa na kutunzwa, si
tu na Wayahudi, bali na wengine wote waliojifanya kumwabudu Mungu; ingawa sisi Wakristo
tumeibadilisha Sabato yao kwenda Siku ya Bwana [Jumapili].” 402 Wale waliokuwa wanaichezea sheria ya
Mungu hawakuwa wajinga kuhusu kazi yao waliyokuwa wanafanya. Kwa makusudi walikuwa wanajiweka
juu ya Mungu.
Kielelezo murua cha mbinu ya Roma kwa wale wasiokubaliana naye ilionekana katika mateso ya muda
mrefu na ya umwagaji wa damu ya Wawaldensi, ambao baadhi yao walikuwa wanaitunza Sabato.
Wengine waliteswa kwa njia kama hiyo kwa ajili ya uaminifu wao kwa amri ya nne. Historia ya makanisa
ya Ethiopia na Uhabeshi ni muhimu. Katikati ya utusitusi wa Zama za Giza, Wakristo wa Afrika ya Kati
hawakuonwa na walisahauliwa na ulimwengu, na kwa karne nyingi walifurahia uhuru katika
kushughulika na imani yao. Lakini hatimaye Roma aligundua kuwepo kwao, ndipo punde mfalme wa dola
ya Uhabeshi alidanganywa katika kumkiri papa kuwa yu mwakilishi wa Kristo. Maridhiano mengine
yakafuata.
(578) Amri ilitolewa ikikataza kutunza Sabato chini ya tishio la adhabu kali sana. 403 Lakini udikteta wa
kipapa mara ukawa kongwa zito la kuumiza kiasi kwamba wale Wahabeshi wakaazimu kulivunjilia mbali
kutoka katika shingo zao. Baada ya mapambano ya kutisha Warumi waliondoshwa katika maeneo yale,
na imani ya zamani ikrejeshwa. Makanisa yalifurahia tena ule uhuru wao, na kamwe hawakusahau
fundisho walilokuwa wamejifunza kuhusu madanganyo, ushupavu, na mamlaka ya ukandamizaji ya
Roma. Ndani ya dola yao iliyokuwa imejitenga mbali walikuwa wameridhika kusalia, wakiwa
hawajulikani kwa ulimwengu wa Kikristo uliobaki.

400
Roger de Hoveden, Annals, pages 528-530
401
Morer, pages 290, 291
402
Ibid., pages 281, 282
403
Angalia Michael Geddes, Church History of Ethiopia, pages 311,312

336
Makanisa ya Afrika yaliitunza Sabato kama ilivyotunzwa na kanisa la upapa kabla halijaasi sawasawa.
Wakati waliitunza siku ya saba kwa kuitii amri ya Mungu, waliacha kufanya kazi siku ya Jumapili ili
kuendana na desturi ya kanisa. Ilipojipatia mamlaka kuu, Roma ilikuwa imeikanyaga Sabato ya Mungu ili
kuitukuza ile ya kwake; lakini makanisa ya Afrika, yakiwa yamefichika kwa karibu miaka elfu moja,
hayakushiriki katika uasi huo. Yalipowekwa chini ya utawala wa Roma, yalishurutishwa kuiweka kando
sabato ya kweli na kuitukuza sabato ya uongo; lakini punde tu walipojipatia uhuru tena walirudi katika
utii kwa amri ya nne. 404
Kumbukumbu hizi za mambo yaliyopita huonyesha wazi uadui alio nao Roma dhidi ya Sabato ya kweli na
wale wanaoitetea, na njia anazo kuiheshimu siku ya kubuni aliyoanzisha. Neno la Mungu linafundisha
kwamba matukio hayo yatarudiwa tena wakati Wakatoliki wa Roma na Waprotestanti watakapoungana
kwa ajili ya kuitukuza Jumapili.
Unabii wa Ufunuo 13 unasema kwamba mamlaka inayoonyeshwa na mnyama mwenye pembe kama za
mwana-kondoo itaifanya “dunia na wote wakaao ndani yake” kuusujudia upapa - ambao umewakilishwa
kwa mfano wa mnyama “mfano wa chui.” Mnyama yule mwenye pembe mbili pia atawaambia “wakaao
juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama”, na, (579) zaidi ya hayo, ataamuru wote, “wadogo kwa
wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa,” kutiwa alama ya mnyama. Ufunuo
13:11-16. Imeonyeshwa kwamba Marekani ndiyo mamlaka iliyowakilishwa na mnyamna yule mwenye
pembe mbili kama mwana-kondoo, na ya kwamba unabii huu utatimizwa wakati Marekani itakapohimiza
utunzaji wa Jumapili, jambo ambalo linadaiwa na Roma kwamba ni kutambua ukuu wa mamlaka ya
Roma. Lakini katika huku kuupa upapa heshima Marekani hatakuwa peke yake. Ushawishi wa Roma
katika nchi zilizopata kutambua mamlaka yake bado hauko karibu na kutoweka. Na unabii unatabiri
kuhusu kurejeshwa kwa mamlaka yake. “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa
jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.” Fungu la 3.
Pigo lile la mauti linaonyesha anguko la upapa mwaka 1798. Baada ya hapo, nabii anasema, “jeraha
lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.” Paulo anasema wazi kwamba “yule
mtu wa dhambi” ataendelea kuwako hadi wakati wa kuja kwa Kristo mara ya pili. 2 Wathesalonike 2:3-
8. Kuelekea mwisho wenyewe wa wakati ataiendeleza kazi yake ya madanganyo. Na mwandishi wa
Ufunuo anasema, akirejea kwa upapa: “Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye
jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo”. Ufunuo 13:8. Kote katika
Ulimwengu wa Kale na Ulimwengu Mpya, upapa utapata kusujudiwa kwa heshima inayotolewa kwa
Jumapili uliyoianzisha, heshima ambayo kwa ujumla inastahili kwenda Roma.
Tangu katikati ya karne ya kumi na tisa, watu wajifunzao unabii kule Marekani wamehubiri ushuhuda
huu kwa ulimwengu. Katika matukio yanayotokea hivi sasa maendeleo ya kasi yanaonekana kuelekea
katika utimilizo wa utabiri huu. Kwa upande wa walimu wa Kiprotestanti kuna madai kama yale yale ya
kuwepo kwa mamlaka ya kimbingu katika utunzaji wa Jumapili, na ukosefu ule ule wa ushahidi wa
Maandiko, kama ilivyokuwa kwa viongozi wa upapa waliotunga miujiza ya uongo ili kuiweka katika
nafasi ya kuonyesha kwamba ni amri ya Mungu. Madai kwamba hukumu za Mungu zinawajilia watu kwa
kuinajisi (580) sabato ya Jumapili, yatarudiwa tena; na tayari yameanza kusemwa. Na harakati za
kuhimiza utunzaji wa Jumapili zinashika kasi haraka.
Werevu na mbinu za Kanisa la Roma ni za kushangaza. Ni kanisa linaloweza kusoma mapema kile
kitakachotokea. Linangoja wakati muafaka, likiona kwamba makanisa ya Kiprotestanti yanalisujudia

404
Maelezo ya nyongeza yametolewa mwishoni

337
kwa kuikubali sabato ya uongo na kwamba yanaandaa mazingira ya kuihimiza kwa kutumia njia zile zile
lilizotumia zamani. Wale wanaoikataa nuru ya kweli wataishia kutafuta msaada kutoka kwa mamlaka
hiyo inayojifanya kuwa haiwezi kukosea ili wapate kuitukuza siku hiyo iliyoiweka. Uharaka wa jinsi
kanisa hilo litakavyokuja kuwasaidia Waprotestanti katika kazi hiyo si jambo gumu kubashiri. Ni nani
aliye zaidi ya viongozi wa upapa katika kujua namna ya kushughulikia watu wasiolitii kanisa?
Kanisa Katoliki la Roma, pamoja na mtawanyiko wake ulimwenguni kote, huunda shirika moja kubwa
chini ya udhibiti wa upapa, na likiwa limeundwa kwa ajili ya maslahi ya upapa. Mamilioni ya watu
wanaokomunika, katika kila nchi katika dunia hii, wameelekezwa kujiona kama waliofungamanishwa
pamoja kumheshimu papa. Bila kujali utaifa wao au serikali yao, yawapasa kuchukulia mamlaka ya
kanisa kama mamlaka iliyo juu ya zote. Ingawa wanaweza wakala kiapo wakiahidi kuitii serikali ya nchi,
bado nyuma ya hili kuna nadhiri ya utii kwa Roma, inayoondosha viapo vyote vinavyopingana na
matakwa yake.
Historia inatoa ushuhuda kuhusu juhudi za Roma za ustadi na za kudumu za kujiingiza katika mambo ya
mataifa; na ikiisha kupata mahali pa kukita mguu wake, huyaendeleza malengo yake, hata kwa gharama
ya maangamizi ya wakuu wa nchi na watu. Katika mwaka wa 1204, Papa Innocent III alimlazimisha Peter
II, mfalme wa Araggon, kufanya kiapo kifuatacho kisicho cha kawaida: “Mimi, Petro, Mfalme wa watu
wa Araggon, nakiri na kuahidi kwamba daima nitakuwa mwaminifu na mtii kwa bwana wangu, Papa
Innocent, na kwa watu wa Kikatoliki watakaorithi baada yake, na kwa Kanisa la Roma, na kwa uaminifu
nitauhifadhi ufalme wangu katika hali ya utii kwake, nikiilinda imani ya Kikatoliki, na kutesa uzushi
uliopotoka.” - John Dowling, The History of Romanism, b. 5, ch. 6, sec. (581) 55. Hilo hupatana na
madai yahusuyo uwezo wa kasisi wa Roma “kwamba ni halali kwake kuwaondoa wafalme wafalme
mamlakani” na “kwamba anaweza kuwafanya watu kuacha kuwatii watawala wao wasio na haki.”
Mosheim, b. 3, cent. 11, pt. 2, ch. 2, sec. 9, note 17 405
Hebu na ikumbukwe ya kwamba Roma inajigamba kwamba huwa haibadiliki kamwe. Kanuni za Gregory
VII na Innocent III bado ndizo kanuni za Kanisa Katoliki la Roma. Laiti kama angekuwa tu na uwezo,
angeuweka katika vitendo kwa nguvu nyingi kama ilivyokuwa katika karne zilizopita. Waprotestanti
wanajua kidogo sana kuhusu wanachokifanya wanapopendekeza kukubali msaada wa Roma katika kazi
ya kuitukuza Jumapili. Wakati wamejielekeza kutimiza kusudi lao, Roma analenga kuimarisha tena
nguvu zake, kurejesha ukuu wake uliopotea. Hebu na ianzishwe mara moja kanuni ya kwamba kanisa
linaweza kutumia au kudhibiti nguvu ya dola nchini Marekani; kwamba maadhimisho ya kidini yanaweza
kuhimizwa na sheria za nchi; kwa kifupi, kwamba mamlaka ya kanisa na nchi itawale dhamiri ya mtu,
hapo ushindi wa Roma katika nchi hii utakuwa wa hakika.
Neno la Mungu limetoa onyo la hatari iliyo karibu sana; ngoja lisizingatiwe, ndipo ulimwengu wa
Kiprotestanti utakapojifunza kwamba makusudi ya Roma ni nini hasa, wakati ambapo watakuwa
wamechelewa kukwepa mtego wake. Kimya kimya mamlaka ya Roma inaongezeka. Mafundisho yake
yanatia ushawishi katika kumbi za vyombo vya kutunga sheria, katika makanisa, na katika mioyo ya
watu. Anapandisha majengo yake marefu na makubwa ya fahari sana katika maeneo ya siri yaliyofichika
ambamo mateso aliyofanya zamani yatarudiwa. Kimyakimya na pasipo kutiliwa shaka anaimarisha
majeshi yake kuendeleza makusudi yake wakati muda wa kupiga utakapowadia. Anachotamani ni kupata
uwanja muafaka, na huo umeshatolewa kwake tayari. Hivi karibuni tutajionea wenyewe na kuhisi kile

405
Mosheim, b. 3, cent. 11, pt. 2, ch. 2, sec. 9, note 17

338
ambacho ni kusudi la utawala wa Roma. Yeyote atakayeamini na kutii neno la Mungu atakutwa na
shutuma na mateso.

339
Sura ya 36
VITA INAYOKARIBIA
Tangu mwanzo wenyewe wa pambano kuu mbinguni kusudi la Shetani limekuwa ni kuipindua sheria ya
Mungu. Aliingia katika uasi dhidi ya Muumba kwa nia ya kutekeleza jambo hilo, na ingawa alitupwa nje
kutoka mbinguni ameendelea na vita ile duniani. Kuwadanganya watu, na hivyo kuwaongoza katika
kuivunja sheria ya Mungu, ndilo lengo ambalo amekuwa akilitekeleza kwa uthabiti. Iwe ni kulitekeleza
kwa kuitupa kando sheria yote, au kwa kukataa amri moja, hatimaye matokeo yatakuwa yale yale.
Anayekosea “katika neno moja,” anaonyesha kukataa sheria yote; mvuto wake na kielelezo chake viko
upande wa uasi; anakuwa “amekosa juu ya yote.” Yakobo 2:10.
Katika jitihada yake ya kuchukia amri za Mungu, Shetani amepotoa mafundisho ya Biblia, na mafundisho
potofu yameingizwa katika imani ya maelfu ya watu wanaodai kwamba wanayaamini Maandiko.
Pambano kuu la mwisho kati ya ukweli na uongo ni jitihada tu ya mwisho ya pambano la muda mrefu
kuhusu sheria ya Mungu. Ni katika vita hiyo ambamo sasa tunaingia - vita kati ya sheria za wanadamu na
amri za Yehova, kati ya dini ya Biblia na dini ya hadithi za uongo na mapokeo.
Nguvu zitakazoungana dhidi ya ile kweli na haki katika pambano hili zinafanya kazi sasa. Neno takatifu
la Mungu, ambalo limesafiri hadi kufika kwetu kwa gharama ya (583) mateso na damu kiasi hicho,
linathaminiwa kwa kiasi kidogo tu. Biblia iko mahali inapoweza kufikiwa na watu wote, lakini ni
wachache tu wanaoikubali kama mwongozo wa maisha. Ukafiri unaendelea kwa kiwango cha kuogofya
sana, si katika ulimwengu tu, bali katika kanisa. Wengi wamekuja kuyakataa mafundisho ambayo ndiyo
nguzo zenyewe za imani ya Kikristo. Mambo ya kweli yahusuyo uumbaji kama yalivyoelezwa na
waandishi waliovuviwa, anguko la mwanadamu, upatanisho, na kudumu kwa sheria ya Mungu,
yanakataliwa na sehemu kubwa ya wale waitwao ulimwengu wa Kikristo, ama yote au sehemu yake.
Maelfu wanaojivunia hekima yao na uhuru wanaona kama ni ushahidi wa dhaifu kuweka imani yao yote
katika Biblia; wanaona kama ni uthibitisho wa talanta ya juu na elimu kuhoji Maandiko na kuzitafsiri
kiroho na kupotoa kweli muhimu za Maandiko. Viongozi wa kiroho wengi wanafundisha watu wao, na
maprofesa na walimu wengi wanafundisha wanafunzi wao, kwamba sheria ya Mungu imebadilishwa au
kufutiliwa mbali; na wale wanaoyaona matakwa yake kuwa bado yanafaa, kwamba yanapaswa kutiiwa
kama yalivyo, wanafikiriwa kustahili dhihaka na kudharauliwa tu.
Katika kuukataa ukweli, wanadamu humkataa Mwasisi wake. Katika kuikanyaga sheria ya Mungu,
wanaikana mamlaka ya Mtoa-sheria. Ni rahisi kutengeneza sanamu ya mafundisho ya uongo na nadharia
za uongo kama ilivyo rahisi kuchonga sanamu ya mti au jiwe. Kwa kuzieleza vibaya sifa za Mungu,
Shetani anawashawishi watu kumfikiria katika tabia isiyo sahihi. Kwa wengi, sanamu ya falsafa
imetawazwa mahali pa Yehova; wakati Mungu aliye hai, kama anavyofunuliwa katika neno lake, katika
Kristo, na katika kazi za uumbaji, anaabudiwa na wachache tu. Maelfu wanatukuza vitu vya asili kuwa
mungu, huku wakimkana Mungu wa vitu vya asili. Ingawa katika mfumo tofauti, ibada ya sanamu ipo
katika ulimwengu wa Kikristo leo kama ilivyokuwemo miongoni mwa Israeli ya kale mnamo siku za Eliya.
Mungu wa wengi wanaojidai kuwa na hekima, mungu wa wanafalsafa, watungaji wa mashairi,
wanasiasa, waandishi wa habari - mungu wa jamii zilizotengenezwa na kunakshiwa kwa mitindo, ya
vyuo na vyuo vikuu vingi, na hata ya baadhi ya taasisi za kithiolojia - yu bora kidogo tu kuliko Baali, yule
mungu-jua wa Wafoenike.

340
(584) Hakuna fundisho la uongo lipokelewalo na Ulimwengu wa Kikristo linalopinga kwa nguvu zaidi
mamlaka ya Mbinguni, hakuna linalopingana moja kwa moja na sababu za kifikra zaidi, hakuna lililo na
athari za kudhuru kubwa zaidi, kuliko fundisho la siku hizi, linalojengeka kwa haraka mno, kwamba
sheria ya Mungu haiwafungi tena wanadamu. Kila taifa linazo sheria zake, ambazo zinawataka watu
kuheshimu na kutii; hakuna serikali ambayo ingeweza kudumu bila kuwa na sheria hizo; na je, inaweza
kufikiriwa kwamba Mwumbaji wa mbingu na nchi hana sheria inayowatawala viumbe aliowaumba?
Chukulia kwamba whubiri maarufu wanafundisha hadharani kwamba amri zinazoongoza nchi yao na
kulinda haki za raia hazikuwa lazima kushikwa - kwamba zilikuwa zinawanyima uhuru wananchi, na kwa
hiyo zilikuwa hazipaswi kutiiwa; watu kama hao wangevumiliwa katika mimbara zao kwa muda kiasi
gani? Lakini ni kosa kubwa sana kutozijali sheria za serikali na za mataifa kuliko kuzikanyaga amri za
Mungu ambazo ndizo msingi wa serikali zote.
Ingekuwa jambo linalowezekana zaidi sana kwa mataifa kuzikomesha sheria zao, na kuwaruhusu watu
kufanya kama wapendavyo, kuliko Mtawala wa malimwengu kuifuta sheria yake, na kuuacha ulimwengu
bila kuwa na kiwango cha kuwahukumu wenye hatia au kuwahesabia haki watiifu. Je, tunaweza kujua
matokeo ya kuibatilisha sheria ya Mungu? Jaribio limeshafanywa. Wakati kutokumwamini Mungu
kulipokuwa kama nguvu inayoongoza jamii, mambo yaliyofanywa katika nchi ya Ufaransa yalikuwa ya
kuogofya sana. Hapo ndipo ilipodhihirika kwa ulimwengu kwamba kutupilia mbali mipaka iliyowekwa na
Mungu ni kukubali utawala wa madikteta katili kuliko wote. Wakati kiwango cha haki kinapowekwa
kando, njia inawekwa wazi kwa kwa ajili ya mkuu wa uovu kuimarisha nguvu zake duniani.
Popote ambapo amri za Mungu zinakataliwa, dhambi inakoma kuonekana kama dhambi au haki kuwa
kitu kinachotakiwa. Wale wanaokataa kujiweka chini ya serikali ya Mungu hawafai kabisa kujitawala
wenyewe. Kupitia mafundisho yao ya kudhuru roho ya kutotii inapandikizwa katika mioyo ya watoto na
vijana, ambao kwa asili hawana subira ya kudhibitiwa; na jamii yenye hali ya uovu na kutokuwa na
sheria inatokea. Wakati wanapodhihaki wepesi wa kuamini wa wale wanaotii matakwa ya Mungu, (585)
makutano wengi huyakubali madanganyo ya Shetani. Wanaziacha tamaa za mwili kutawala na kutenda
dhambi ambazo zimeitisha hukumu kushuka chini kwa waovu.
Wale wanaowafundisha watu kuchukulia amri za Mungu kwa uzito mdogo wanapanda mbegu ya maasi ili
kuvuna maasi. Ngoja mipaka iliyowekwa na sheria ya Mungu iondoshwe kabisa ili ionekane jinsi ambavyo
watu hawatajali sheria za wanadamu. Kwa kuwa Mungu anakataza vitendo vya udanganyifu, kutamani,
kusema uongo, na ghiliba, watu wako tayari kuzikanyaga amri zake kama kipingamizi kwa usitawi wao
wa mambo ya kiulimwengu; lakini matokeo ya kuziacha amri hizo yangekuwa ya kiwango kile
wasichotarajia. Ikiwa sheria haiwafungi watu, kungekuwa na sababu gani kuzivunja? Mali isingekuwa
salama tena. Watu wangejipatia mali za jirani zao kwa nguvu, na aliye na nguvu kuliko wote angekuwa
tajiri kuliko wote. Maisha yenyewe yasingeweza kuheshimiwa. Kiapo cha ndoa kisingeweza tena kuwa
kama boma takatifu la kuilinda familia. Yule ambaye angekuwa na nguvu, kama angetaka, angechukua
mke wa jirani yake kwa mabavu. Amri ya tano ingewekwa kando pamoja na ile ya nne. Watoto
wasingesita kuondoa uhai wa wazazi wao kama kwa kufanya hivyo wangepata kile ambacho mioyo yao
iliyopotoka ingetaka. Ulimwengu wa kistaarabu ungegeuka kuwa genge la majambazi na wauaji; na
amani, utulivu, na furaha ingetoweshwa duniani.
Tayari fundisho kwamba watu wamewekwa huru mbali na kutii matakwa ya Mungu limehafifisha nguvu
ya wajibu wa kimaadili na kufungulia malango ya mafuriko ya uovu ulimwenguni. Kutofuata sheria,
uasherati, na ufisadi vinatufagia kama wimbi linalofunika. Katika familia, Shetani yuko kazini. Bendera
yake hupepea, hata katika nyumba zinazoitwa za Kikristo. Kuna wivu, kuwawazia wengine mabaya,
unafiki, mafarakano, kushindana, magomvi, kuyasaliti matumaini matakatifu, kujifurahisha katika
341
tamaa mbaya. Mfumo mzima wa kanuni na mafundisho ya dini, ambao unapaswa kujenga msingi na
muundo wa maisha ya kijamii, unaonekana kuwa kama vitu visivyo imara, ambavyo viko tayari
kuporomoka na kuwa magofu. Waovu waliopindukia, wanapotupwa gerezani kwa makosa yao, mara
nyingi wanafanywa kuwa watu wa kupokea zawadi na (586) uangalifu kama vile wamefanya jambo
lenye ubora wa hali ya juu. Habari za tabia zao na uhalifu wao zinatangazwa sana mbele ya watu.
Magazeti huchapisha maelezo ya kina kuhusu uovu wao, hivyo huwasukuma wengine kufanya matendo
yale ya udanganyifu, uporaji, na mauaji; na Shetani hushangilia mafanikio ya mbinu zake za kuzimu.
Kupenda maovu, kuuondoa uhai wa wengine, kuongezeka kwa namna ya kutisha kwa ulevi na maovu ya
kila namna na ya kila kiwango, yanapaswa kuwashtua wale wote wanaomcha Mungu, kuuliza kwamba ni
kitu gani hasa kinahitaji kufanywa ili kulizuia wimbi la maovu.
Mahakama za sheria zimejawa rushwa. Watawala wanasukumwa na tamaa ya kupata mali na kupenda
kujifurahisha katika tamaa za mwili. Ulevi umezitia giza fahamu za wengi kiasi kwamba karibu Shetani
anawadhibiti kabisa. Wataalam wa sheria wamepotoka, wanapewa rushwa, wanadanganyika. Ulevi na
karamu za ulevi na ulafi, tamaa mbaya za mwili, wivu, kukosa uaminifu kwa kila aina, mambo hayo
huonekana miongoni mwa wale wanaosimamia ulekelezaji wa sheria. “Haki inasimama mbali sana;
maana kweli imeanguka katika njia kuu, na unyofu hauwezi kuingia.” Isaya 59:14.
Uovu na giza la kiroho vilivyokuwepo wakati wa Roma kushika hatamu ni matokeo yasiyoepukika ya
Roma kuondosha Maandiko; lakini sasa, chini ya nuru kamili ya injili inayoangaza kikamilifu katika kizazi
hiki cha uhuru wa dini, ziko wapi sababu za kuenea kwa ukafiri, kuikataa sheria ya Mungu, na matokeo
yake ya ufisadi? Kwa kuwa sasa Shetani hawezi tena kuuweka ulimwengu chini ya udhibiti wake kwa
kuyazuia Maandiko, anatumia njia nyingine kutimiza kusudi lake lile lile. Kuharibu imani ya watu kwa
Biblia hutimiza kusudi lake kama ilivyo kwa kuiharibu Biblia yenyewe. Kwa kuingiz imani kwamba sheria
ya Mungu si ya lazima, anaongoza watu kuivunja kama vile hawazijui amri kabisa. Na kwa sasa, kama
ilivyokuwa katika zama zilizopita, amefanya kazi ya kuendeleza mipango yake kwa kulitumia kanisa.
Mashirika ya dini ya siku hizi yamekataa kuzisikiliza kweli zisizo maarufu ambazo zimefunuliwa wazi
katika Maandiko, na ili kupambana nazo wamekuwa na tafsiri zao na kuchukua misimano ambayo
imetapakaza mbegu za kutokuamini. Waking’ang’ania fundisho la uongo la upapa la kutokufa kabisa na
hali ya mwanadamu (587) kuwa na dhamiri anapokuwa katika kifo, wameikataa kinga pekee dhidi ya
madanganyo ya imani ya mizimu. Fundisho kuhusu mateso ya milele limewafanya wengi wasiamini
Biblia. Na wakati madai ya amri ya nne yanaposisitizwa kwa watu, inaonekana kama utunzaji wa Sabato
ya siku ya saba umeamriwa; na kama njia ya pekee ya wao kuondokana na jukumu hilo wasilotaka
kulitenda, walimu wengi walio maarufu wanasema kwamba sheria ya Mungu si ya lazima tena. Hivyo
wanaitupilia mbali sheria na Sabato pamoja. Kadiri kazi ya matengenezo ya Sabato inavyoenea,
kuikataa sheria ya Mungu ili kukwepa madai ya amri ya nne kutakuwa kumeenea karibu kila mahali.
Mafundisho ya viongozi wa dini yamefungua mlango ili kuingiza ukafiri, imani ya mizimu, na kukataa
sheria takatifu ya Mungu; na viongozi hawa wanawajibika kwa namna ya kuogofya kwa maovu yaliyopo
katika ulimwengu wa Kikristo.
Bado kundi lili hili liliweka madai kwamba kule kuenea kwa haraka kwa ufisadi kunahusiana kwa sehemu
kubwa na kunajisi kile kiitwacho “sabato ya Kikristo,” na ya kwamba uhimizaji wa utunzaji wa Jumapili
ungefanya kiwango cha maadili ya jamii kuwa bora. Dai hili linasisitizwa hasa katika nchi ya Amerika,
mahalo ambako fundisho la Sabato ya kweli limehubiriwa kwa kiasi kikubwa mahali pengi. Kazi ya
kufundisha kuhusu kutokutumia vileo hapa, moja ya matengenezo maarufu na muhimu ya kimaadili,
mara kwa mara inaunganishwa na harakati za kuitunza Jumapili, na watetezi wa hilo wanajionyesha
kama watu wanaofanya kazi ya kuendeleza matakwa ya kiwango cha juu ya jamii; na wale wanaokataa

342
kujiunga nao wanashutumiwa kwamba ni maadui wa mpango wa matengenezo na kuhimiza kutotumia
vileo. Lakini hali hii ya kwamba harakati ya kuanzisha fundisho potofu imefungamanishwa na kazi
ambayo kwa yenyewe ni nzuri, si hoja ya kuunga mkono fundisho hilo potofu. Tunaweza kuificha sumu
kwa kuichanganya na chakula chema kwa afya ya mwili, lakini kwa kufanya hivyo hatubadili hali ya
sumu. Kinyume chake, inafanywa kuwa ya hatari zaidi, kwa vile inaweza kuliwa pasipo kujulikana. Ni
mojawapo ya mbinu za Shetani kuweka pamoja uongo na ukweli wa kiasi cha kutosha kuufanya
uaminike. Viongozi wa harakati za Jumapili wanaweza kutetea matengenezo (588) yanayohitajiwa na
watu, kanuni ambazo zinapatana na Biblia; lakini kama ndani ya hayo kuna matakwa yaliyo kinyume na
sheria ya Mungu, watumishi wa Mungu hawawezi kuungana nao. Hakuna kinachoweza kuwahalalishia
kuweka kando amri za Mungu kwa ajili ya maagizo ya wanadamu.
Kupitia hayo mafundisho ya uongo makuu mawili, kutokufa kwa roho na utakatifu wa Jumapili, Shetani
atawaleta watu chini ya madanganyo yake. Wakati hilo la kwanza linaweka msingi wa imani ya
umizimu, hilo jingine linaunda mfungamano pamoja na Roma. Waprotestanti wa Marekani watakuwa
mstari wa mbele kuinyosha mikono yao kuvuka ghuba na kuupokea mkono wa umizimu; watanyosha
mikono kupita juu ya kilindi ili kushikana mikono na mamlaka ya Roma; na chini ya ushawishi wa
muungano wa vitu hivi vitatu, nchi hii itatembea katika nyayo za Roma kuzikanyaga chini ya miguu yake
haki za dhamiri.
Kadiri umizimu unavyoiga kwa karibu zaidi Ukristo ulio wa jina tu wa siku hizi, unakuwa na nguvu kubwa
zaidi ya kudanganya na kunasa mtegoni. Shetani mwenyewe ameongoka, kwa utaratibu wa kisasa wa
mambo. Atajitokeza katika mwonekano wa malaika wa nuru. Kupitia mbinu ya umizimu, miujiza
itatendwa, wagonjwa wataponywa, na maajabu mengi yasiyokanushika yatafanyika. Na kwa vile hizo
roho zitakiri kuwa na imani katika Biblia, na kuonyesha kuziheshimu kawaida zilizowekwa na kanisa,
kazi ya hizo itakubalika kama ishara ya mwonekano wa nguvu za Mungu.

Kwa sasa ni vigumu kubainisha mstari unaotofautisha kati ya wale wanaodaiwa kuwa Wakristo na wale
wasiomcha Mungu. Washiriki wa kanisa wanapenda mambo yale yale yanayopendwa na walimwengu na
wako tayari kujiunga nao, na Shetani amedhamiria kuwaunganisha pamoja katika shirika moja na kwa
njia hiyo kuimarisha kazi yake kwa kuwasukumia wote katika himaya ya umizimu. Watu wa upapa,
wanaojivunia miujiza kama ishara ya hakika ya kanisa la kweli, kwa urahisi watadanganywa na mamlaka
hii itendayo maajabu; na Waprotestanti, wakiwa wameitupa mbali ngao ya ukweli, watadanganyika pia.
Watu wa upapa, Waprotestanti, na kupenda mambo ya dunia kwa namna moja watapokea mfano wa
utauwa bila kuwa na nguvu, na wataona katika muungano huu harakati kuu (589) kwa ajili ya kuuongoa
ulimwengu na kuikaribisha ile milenia inayotarajiwa kwa muda mrefu.
Kwa njia ya umizimu, Shetani anaonekana kama mfadhili wa mashindano, akiponya magonjwa ya watu,
na kudai kuleta mfumo mpya na bora zaidi wa imani ya dini; lakini wakati huo huo anafanya kazi kama
mharibifu. Majaribu yake yanawapeleka watu wengi katika maangamizi. Ulevi huondoa busara; kufuata
hisia za kujifurahisha katika tamaa, magomvi, na umwagaji wa damu hufuata. Shetani anafurahia katika
vita, maana vita inachochea misukumo mibaya kupita kiasi ya moyoni na kuwafagilia waathirika wake
katika umilele wakiwa wamezama katika dhambi na damu. Ni lengo lake kuyachochea mataifa kupigana
vita baina yao, maana hivyo ndivyo awezavyo kupindisha mawazo ya watu kutoka katika kazi ya
kujiandaa kusimama katika siku ya Bwana.
Katika ajali na majanga ya baharini na nchi kavu, katika milipuko ya moto mkubwa, katika ukali wa
tufani (590) na dhoruba, mafuriko, pepo za kisulisuli, na matetemeko, Shetani anatumia nguvu zake.
343
Anafagilia mbali mavuno yaliyokomaa, na njaa na hali ngumu ya maisha hufuata. Anaweka hewani
uchafu wa kufisha, na maelfu wanaangamia kwa maradhi. Majanga haya yatakuwa ya mara kwa mara na
yenye kiasi kikubwa cha uharibifu. Uharibifu utakuwa kwa wote, mwanadamu na mnyama. “Dunia
inaomboleza, inazimia,” “watu wakuu wa dunia wanadhoofika. Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu
wanaoikaa; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele.” Isaya
24:4,5.
Halafu huyo mwongo mkuu atawaaminisha wanadamu kwamba wale wanaomtumikia Mungu
wanasababisha maovu hayo. Kundi lile lililoamsha ghadhabu ya Mbingu litaelekeza lawama zote za
taabu zitakazokuwepo kwa wale ambao utii wao kwa amri za Mungu ni kemeo la kudumu kwa wavunjaji
wa sheria. Itatangazwa kwamba watu wanamchukiza Mungu kwa kuihalifu sabato ya Jumapili; kwamba
dhambi hiyo imeleta misiba ambayo haitakoma mpaka utunzaji wa Jumapili utakapohimizwa kwa
lazima; na kwamba wale wanaoeleza matakwa ya kuitunza amri ya nne, kwa njia hiyo wakiiharibu
taadhima ya Jumapili, ni wataabishaji wa watu, wanaowazuia wasipate kurejeshwa katika upendeleo
wa Mungu na usitawi wa maisha haya. Kwa hiyo mashtaka yaliyotolewa zamani dhidi ya mtumishi wa
Mungu yatarudiwa tena kwa sababu za namna ile ile: “Ikawa, Ahabu alipomwona Eliya, Ahabu
akamwambia, Je! ni wewe, Ewe mtaabishaji wa Israeli? Naye akajibu, si mimi niliyewataabisha Israeli;
bali ni wewe, na nyumba ya baba yako, kwa kuwa mmeziacha amri za BWANA; nawe umewafuata
mabaali.” 1 Wafalme 18:17,18. Pindi ghadhabu ya watu itakapochochewa kwa mashtaka ya uongo,
watu watawachukulia mabalozi wa Mungu hatua zinazofanana kabisa na zile ambazo Israeli iliyoasi
ilichumchulia ya Eliya.
Nguvu itendayo miujiza idhihirishwayo kupitia imani ya umizimu (591) itashinikiza ushawishi wake dhidi
ya wale wanaochagua kumtii Mungu kuliko wanadamu. Ujumbe uletwao na roho za mapepo utaonyesha
kwamba Mungu amewatuma kuja kuwahakikishia wale wanaoikataa Jumapili kosa lao, wakithibitisha
kwamba lazima sheria za nchi zitiiwe kama sheria ya Mungu. Wataomboleza kwa ajili ya uovu mkuu
uliomo ulimwenguni duniani na kuongeza juu ya ushuhuda wa walimu wa dini kwamba hali ya
mmomonyoko wa maadili imesababishwa na kuinajisi Jumapili. Hasira kali itaelekezwa kwa wale wote
wanaokataa kukubali ushuhuda wao.
Mbinu ya Shetani katika vita hii ya mwisho ni ile ile aliyotumia wakati wa kulianzisha pambano kuu kule
mbinguni. Alidai kwamba alikuwa anatafuta kuimarisha serikali ya mbinguni, wakati kwa siri alikuwa
anaweka kila jitihada ili kupata kuipindua. Na anazitupa lawama za kazi ile ile aliyokuwa anajaribu
kuifanya kwa malaika waliobaki kuwa watiifu. Mbinu hiyo hiyo ya udanganyifu ndiyo inayoonekana
katika historia ya Kanisa la Kirumi. Limedai kuwa kama badala ya Mbingu, wakati likitafuta kujiinua juu
kuliko Mungu na kuibadili sheria yake. Chini ya utawala wa Roma, wale walioteswa hadi kufa kwa
sababu ya msimamo wao kwa injili walishutumiwa kama watenda maovu; walisemekana kwamba
walikuwa katika makubaliano ya kushirikiana na Shetani; na kila njia iliyowezekana ilitumika
kuwafunika kwa kuwapinga, kuwafanya waonekane machoni mwa watu na hata machoni pao wenyewe
kama wahalifu sugu. Hivyo ndivyo itakavyokuwa sasa. Wakati Shetani anatafuta kuwaharibu wale
wanaoiheshimu sheria ya Mungu; atasababisha washtakiwe kama wavunja-sheria, kama watu
wanaomkosea heshima Mungu na wanaozileta hukumu ulimwenguni.
Kamwe Mungu halazimishi nia au dhamiri ya mtu; lakini juhudi ya Shetani wakati wote – kupata
kuwadhibiti wale ambao hawezi isipokuwa kwa kuwapotosha - ni kuwalazimisha kwa ukatili. Kupitia
hofu au nguvu anatafuta kuzitawala dhamiri na kuwafanya wamwabudu yeye. Kutimiza hili, anafanya
kazi kupitia vyote viwili, mamlaka za kidini na mamlaka za kidunia, akizisukuma kuhimiza sheria za
wanadamu zinazopishana na sheria ya Mungu.
344
(592) Wale wanaoiheshimu Sabato ya Biblia watashutumiwa kuwa maadui wanaopingana na sheria na
utaratibu, kama watu wanaovunja mipaka ya maadili katika jamii, wakisababisha ufisadi na mfumo wa
maisha usio na utaratibu, na kuziita hukumu za Mungu zishuke juu ya dunia hii. Kujizuia kwao kwa
sababu ya dhamiri kutatangazwa kuwa ni kiburi, ukaidi, na dharau kwa wenye mamlaka. Watashtakiwa
kwa kutoheshimu serikali. Wahubiri wanaokana wajibu wa watu kwa sheria ya Mungu watahubiri
mimbarani kuhusu wajibu wa kutii mamlaka za kiraia kwamba zimewekwa na Mungu. Katika kumbi za
kutungia sheria na katika mahakama, wale wanaozishika amri wataelezwa vibaya na kuhukumiwa.
Maneno yao yatapakwa rangi ya uongo; mwonekano mbaya mno wa kutungwa utavishwa katika tabia
zao.
Kadiri makanisa ya Kiprotestanti yanavyokataa hoja za wazi za Maandiko zinazoitetea sheria ya Mungu,
watatafuta kuwanyamazisha wale ambao imani yao haiwezi kupinduliwa kwa kutumia Biblia. Ingawa
wanajifanya kuwa vipofu wasiuone ukweli huu, hivi sasa wanaifuata njia ile itakayowapeleka katika
kuwatesa wale ambao wanakataa kwa dhamiri zao kufanya kile ambacho kinafanywa na ulimwengu wa
Kikristo mwingine uliobaki, na kukataa kukubali madai ya sabato ya kipapa.
Viongozi wakuu wa kanisa na serikali wataungana pamoja ili kuhonga, kushawishi, au kulazimisha watu
wa tabaka zote ili wapate kuiheshimu Jumapili. Kule kukosekana kwa idhini ya Mungu kutafidiwa kwa
kutungwa kwa sheria za ukandamizaji. Rushwa ya kisiasa inaharibu hali ya kupenda haki na kuali ukweli;
na hata katika Amerika huru, watawala na wajumbe wa kutunga sheria, ili kujipatia kupendwa na watu,
watakubaliana na matakwa ya wengi ya kuhitaji sheria inayohimiza utunzaji wa Jumapili. Uhuru wa
dhamiri, ambao umegharimu sana watu kujitoa mhanga, hautaheshimiwa tena. Katika vita hilo
linalokuja hivi punde tutaona kutimia kwa maneno ya ya nabii: “Joka akamkasirikia yule mwanamke,
akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na
ushuhuda wa Yesu.” Ufunuo 12:17.

345
Sura ya 37
MAANDIKO KINGA SALAMA

“Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao
hapana asubuhi.” Isaya 8:20. Watu wa Mungu wanaelekezwa kwenye Maandiko kama kinga yao dhidi ya
ushawishi wa walimu wa uongo na nguvu idanganyayo ya roho za giza. Shetani anatumia kila njia
inayowezekana kuwazuia watu wasipate maarifa ya kuijua Biblia; maana maneno ya wazi yaliyomo
hufunua madanganyo yake. Katika kila uamsho wa kazi ya Mungu mkuu wa uovu anaamka na kufanya
juhudi kubwa zaidi; hivi sasa anatumia nguvu zake zote kwa ajili ya vita ya mwisho dhidi ya Kristo na
wafuasi wake. Punde udanganyifu mkuu wa mwisho utaonekana mbele yetu. Mpinga Kristo anataka
kufanya maajabu yake machoni petu. Kitu cha bandia kitafanana kwa karibu sana na kile cha kweli kiasi
kwamba haitawezekana kuvitofautisha isipokuwa kwa Maandiko Matakatifu. Lazima kila kauli na kila
mwujiza vipimwe kwa ushuhuda wa Maandiko Matakatifu.
Wale wanaodhamiria kutii amri za Mungu zote watapingwa na kudhihakiwa. Wanaweza kusimama tu
ndani ya Mungu. Ili kustahimili jaribu lililo mbele yao, lazima waelewe mapenzi ya Mungu kama
yanavyofunuliwa katika neno lake; wanaweza kumheshimu tu pale wanapokuwa na uelewa sahihi kuhusu
tabia yake, serikali yake, na makusudi yake, na kutenda kulingana na hayo. Hakuna watakaoweza
kusimama katika vita kuu ya mwisho isipokuwa wale tu walioimarisha akili zao kwa zile kweli za Biblia.
(594) Jaribio hili la uchunguzi litakuja kwa kila mtu: Je, nimtii Mungu kuliko wanadamu? Saa ya kuamua
hatima imewadia hata sasa. Je, miguu yetu imesimikwa kwenye mwamba wa neno la Mungu
lisilobadilika? Tuko tayari kusimama imara kutetea amri za Mungu na imani ya Yesu?
Kabla ya kusulibiwa kwake Mwokozi aliwaeleza wanafunzi wake kwamba ilikuwa imempasa kuuawa na
kufufuka kutoka kaburini, na malaika walikuwepo pale ili kuyafanya maneno yake yaeleweke katika akili
na mioyo yao. Lakini wanafunzi walikuwa wanatarajia ukombozi wa kidunia kuwatoa katika kongwa la
Kirumi, na hawakulivumilia wazo la kwamba yeye ambaye matumaini yao yote yalikuwa kwake
angepaswa kupatikana na kifo cha aibu. Maneno yale ambayo walihitaji kuyakumbuka yaliondoshwa
mawazoni mwao; na wakati wa kujaribiwa ulipokuja, uliwakuta wakiwa hawakujiandaa. Kifo cha Yesu
kilivunja matumaini yao kabisa kwa kiasi ambacho ni kana kwamba alikuwa hakuwaonya kabla. Katika
unabii wakati ujao umefunuliwa kwetu kwa uwazi kama ulivyofunuliwa kwa wanafunzi wa Kristo kwa
maneno yake. Matukio yanayounganishwa na kufungwa kwa rehema na kazi ya kujiandaa kwa ajili ya
wakati wa taabu, yameelezwa kwa uwazi. Lakini watu wengi sana hawana ufahamu wa kweli hizi
muhimu kuzidi vile ambavyo ingekuwa kama zisingekuwa zimepata kufunuliwa kabisa. Shetani yuko
macho ili kuondoa kila hisia ambazo zingewahekimisha kwa wokovu, na wakati wa taabu utawakuta
wakiwa hawajajiandaa.
Mungu anapopeleka kwa wanadamu maonyo muhimu sana kiasi kwamba yanaonyeshwa kama
yanatangazwa na malaika warukao katika mbingu, anataka kila mtu aliyejaaliwa uwezo wa akili
kuzingatia ujumbe huo. Hukumu za kuogofya zilizotajwa dhidi ya kumsujudu yule mnyama na sanamu
yake (Ufunuo 14:9-11), ingewafanya wote wajifunze kwa bidii unabii huo ili kujua alama ya mnyama ni
nini, na ni kwa jinsi gani wanaweza kuepuka kuipokea. Lakini makundi makubwa ya watu yanageuza
masikio yao wasisikie ukweli na wanazigeukia hadithi za uongo. Mtume Paulo alisema, akiangalia mbele
mnamo siku za mwisho: “Maana utakuja wakati (595) watakapoyakataa mafundisho yenye uzima.” 2

346
Timotheo 4:3. Wakati huo umefika sawasawa. Watu wengi hawataki ukweli wa Biblia, kwa sababu
unaingilia mapenzi ya moyo wa dhambi unaopenda dunia, na mahali pake Shetani anawapatia
madanganyo wanayopenda.
Lakini Mungu atakuwa na watu wake duniani watakaoidumisha Biblia, na Biblia pekee, kama kiwango
cha mafundisho yote na msingi wa matengenezo yote. Maoni ya wasomi, mahitimisho ya kisayansi,
mafundisho ya makanisa yatokanayo na maamuzi ya mabaraza ya kidini, kwa kadiri yalivyo tofauti na
yasivyokubaliana kama yalivyo makanisa yenyewe yanayowakilishwa nayo, au maamuzi ya sauti ya walio
wengi – moja kati ya hayo au yote hayo yasiwe ushahidi wa kukubali au kukataa jambo lolote linalohusu
imani ya dini. Kabla ya kukubali fundisho lolote au agizo lolote, lazima tudai kupata maneno ya wazi
kwamba “Hivi ndivyo asemavyo Bwana.”
Shetani anajitahidi daima kuyavuta mawazo ya watu kuelekea kwa mwanadamu badala ya kumwelekea
Mungu. Anawaongoza watu kuwaangalia maaskofu, wachungaji, maprofesa wa thiolojia, kama ndio
miongozo yao, badala ya wao kuyachunguza Maandiko ili wao wenyewe kujifunza wajibu wao. Halafu,
kwa kuyadhibiti mawazo ya viongozi hao, anaweza kuwashawishi watu wengi sana kwa namna
apendavyo.
Wakati Yesu alipokuja kusema maneno ya uzima, watu wa kawaida walimsikiliza kwa furaha; na wengi,
hata miongoni mwa makuhani na watawala, walimwamini. Lakini wakuu wa ukuhani na viongozi
wakubwa wa taifa walidhamiria kuyahukumu na kuyakataa mafundisho yake. Ingawa walishindwa
kupata mashtaka yoyote dhidi yake, ingawa hawakuweza kupata lolote isipokuwa ushawishi wa nguvu ya
Mungu na hekima vilivyoambatana na maneno yake, bado walijifungia wenyewe kwa chuki isiyo na
sababu; walikataa ushahidi wa wazi mno wa Umasihi wake, wasije wakalazimika kuwa wanafunzi wake.
Wapinzani hawa wa Yesu walikuwa watu wale ambao watu walikuwa wamefundishwa tangu utotoni
kuwaheshimu kwa kuwatukuza, ni watu waliokuwa na mamlaka ambayo watu walikuwa wamezoea
kuisujudia pasipo shaka. Walisema, “Inakuwaje kwamba watawala wetu na waandishi wenye elimu
hawamwamini Yesu? Je, watu hawa washika dini wasingempokea kama kweli angekuwa (596) Kristo?”
Ulikuwa ushawishi wa walimu wa namna hii ulioongoza taifa la Wayahudi kumkataa Mkombozi wao.
Roho ile iliyowasukuma makuhani na watawala wale bado inadhihirishwa na wengi wanaodai kuwa
wacha Mungu wakubwa. Wanakataa kuuchunguza ushuhuda wa Maandiko unaohusu kweli maalum za
wakati huu. Wanaonyesha idadi yao, utajiri wao, na umaarufu wao, na kwa dharau wanawaangalia
watetezi wa ukweli kama watu wachache, maskini, na watu wasio maarufu, wakiwa na imani
inayowatenganisha na ulimwengu.
Kristo aliona mbali kwamba hali ya kujitwalia mamlaka kupita kiasi iliyodaiwa na waandishi na
Mafarisayo isingekoma wakati wa kutawanyika kwa Wayahudi. Alikuwa na jicho la kinabii kuhusu kazi ya
kuinua juu mamlaka ya mwanadamu ili kutawala dhamiri za watu, hali ambayo imekuwa laana ya
kuogofya ya kanisa katika vizazi vyote. Na hukumu ya Yesu ya kuogofya dhidi ya waandishi na
Mafarisayo, na maonyo yake kwa watu akitaka wasifuate viongozi hawa vipofu, yameandikwa ili kuwa
onyo kwa vizazi vya wakati ujao.
Kanisa la Kirumi linazuia haki ya kufasiri Maandiko na kuiacha kwa viongozi wakuu wa kanisa. Kwa
msingi kwamba viongozi wa kanisa peke yao ndio wenye uwezo wa kufafanua neno la Mungu, neno hilo
linazuiliwa mbali na watu wa kawaida. 406 Ingawa Matengenezo yaliwapatia watu wote Maandiko, bado

406
Maelezo ya nyongeza yametolewa mwishoni

347
kanuni ile ile iliyoendelezwa na Roma inazuia watu wengi walio katika makanisa ya Kiprotestanti
kujisomea Biblia wao wenyewe. Wamefundishwa kukubali mafundisho ya Biblia vile yanavyofasiriwa na
kanisa; na kuna maelfu ya watu ambao hawathubutu kupokea neno lolote, hata kama limefunuliwa kwa
uwazi katika Maandiko, ambalo liko tofauti na agizo la kanisa lao au fundisho lililowekwa na kanisa lao.
Licha ya kwamba Biblia imejaa maonyo dhidi ya walimu wa uongo, wengi wako tayari kuikabidhi kazi ya
kuchunga roho zao kwa viongozi wa kanisa. Kuna maelfu ya watu leo wanaokiri kuwa na dini ambao
hawawezi kutoa sababu yoyote ya mambo ya imani waliyo nayo zaidi ya kusema kwamba hivyo ndivyo
walivyofundishwa na viongozi wao wa dini. Wanayapita mafundisho ya Mwokozi nusura ya (597)
kutoyajali kabisa, na huweka uhakika wa imani katika maneno ya wahubiri. Lakini viongozi wa dini
hawakosei? Kwa nini tunaweka roho zetu kama amana katika uongozi wao isipokuwa kama tunajua
kutokana na neno la Mungu kwamba wanaibeba nuru? Ukosefu wa ujasiri wa kimaadili wa kwenda nje ya
njia iliyowekwa na ulimwengu huwafanya wengi kufuata nyayo za wasomi; na kwa kuwa wagumu wa
kuchunguza wao wenyewe, wanakuwa watu wa kufungwa bila tumaini katika minyororo ya mafundisho
ya uongo. Wanaona kwamba ukweli wa wakati huu umefunuliwa wazi katika Biblia; na wanasikia nguvu
ya Roho Mtakatifu ikiambatana na kutangazwa kwa neno hilo la Biblia; lakini bado wanaruhusu upinzani
wa viongozi wa kanisa kuwageuzia mbali na nuru. Ingawa akili ya kawaida na dhamiri vimesadikishwa,
watu hao waliodanganyika hawathubutu kufikiri kwa namna inayotofautiana na ya viongozi wao; na
maamuzi yao binafsi, shauku yao kwa ajili ya mambo ya milele, hutolewa kama kafara kwa mtu
mwingine asiyeamini, mwenye kiburi na mwenye chuki.
Ni nyingi njia ambazo kwazo Shetani anafanya kazi ya kuwafunga mateka wake kupitia ushawishi wa
wanadamu. Analeta watu wengi katika upande wake kwa njia ya kutumia nyuzi laini za upendo
kuwafungamanisha watu na maadui wa msalaba wa Kristo. Vyovyote vile kufungamana huko kulivyo, iwe
ni ushawishi wa wazazi, watoto, wanandoa, au mahusiano katika jamii, matokeo yake ni yale yale;
wapinzani wa ile kweli wanatumia nguvu yao kuidhibiti dhamiri ya mtu, na watu walioshikiliwa katika
mwelekeo wa wapinzani hao hawana ujasiri au uhuru wa kutosha kutii wajibu ule wanaosadikishwa
moyoni.
Ukweli na utukufu wa Mungu havitenganishiki; ni jambo lisilowezekana kwetu kumheshimu Mungu kwa
kushikilia maoni potofu, na Biblia ikiwa mahali panapofikika kwetu. Wengi hudai kwamba haijalishi kile
mtu anachokiamini, alimradi tu maisha yake yawe sawasawa. Lakini maisha huundwa na imani. Ikiwa
nuru na kweli iko mahali tunapoweza kuifikia, sisi tunapuuza kutumia vizuri nafasi ya kuisikia na kuiona,
basi tunaikataa; tuko tunachagua giza kuliko nuru.
“Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; lakini mwisho wake ni njia za mauti.” Mithali 16:25.
Kutojua si udhuru wa kupotoka au kutenda dhambi, wakati ambapo kuna kila fursa (598) ya kuyajua
mapenzi ya Mungu. Mtu anasafiri na kufika mahali penye barabara kadhaa na kibao kinachoonyesha
mahali kila barabara inakokwenda. Ikiwa hajali kile kibao, bali afuata barabara yoyote inayoonekana
kuwa sahihi kwake, anaweza kuendelea kuwa mwaminifu hivyo, lakini atakuta uelekeo wake uko katika
barabara ya makosa.
Mungu ametupatia neno lake ili tufahamu mafundisho yaliyomo na kujua kwa ajili yetu wenyewe
anachotaka kwetu. Mwanasheria yule alipomjia Yesu na kumwuliza, “Nifanye nini ili niurithi uzima wa
milele?” Mwokozi alimrejesha kwenye Maandiko, akisema, “Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?
Kutojua hakutampa udhuru kijana wala mzee, wala kuwaachilia wasipatwe na adhabu ambayo ipo kwa
sababu ya kuivunja sheria ya Mungu; kwa sababu mikononi mwao kuna maelezo ya kuaminika ya sheria
hiyo pamoja na kanuni na matakwa yake. Haitoshi tu kuwa na dhamira njema; haitoshi kufanya kile

348
ambacho mtu anafikiri kuwa ni sahihi au kile ambacho mhubiri anamwambia kuwa ni sahihi. Wokovu wa
roho yake unahusika hapa, hivyo yampasa kuyachunguza Maandiko kwa ajili yake mwenyewe. Hata awe
amesadikishwa kiasi gani, hata awe na imani kiasi gani kwamba mhubiri anajua ukweli ulivyo, huu si
msingi wake yeye. Anayo ramani inayoonyesha kila alama ya njiani katika safari ya kwenda mbinguni,
hivyo haimpasi kukisia kuhusu jambo lolote.
Ni jukumu la kwanza na la kiwango cha juu kwa kila kiumbe mwenye akili kujifunza mwenyewe ukweli
kutoka katika Maandiko, halafu kutembea katika nuru hiyo na kuwatia moyo wengine kufuata mfano
wake. Yatupasa kujifunza Biblia kwa bidii siku kwa siku, tukipima kila wazo na kulinganisha andiko na
andiko. Kwa msaada wa kimbingu tupate mitazamo yetu kwa ajili yetu wenyewe maana tutajibu
wenyewe mbele za Mungu.
Kweli zilizofunuliwa wazi kabisa katika Biblia zimewekwa katika mashaka na giza na wasomi, ambao,
kwa kujifanya kuwa na hekima kuu, wanafundisha watu kwamba Maandiko yana maana ya fumbo la
kiroho isiyoweza kueleweka kwa wanadamu, na ya siri, ambayo haionekani wazi katika lugha
iliyotumika. Watu hawa ni walimu wa uongo. Kwa (599) kundi la watu kama hao Yesu alisema:
“Hamyajui Maandiko wala uweza wa Mungu.” Marko 12:24. Lazima lugha ya Biblia ifafanuliwe kwa
maana yake hiyo hiyo iliyopo, isipokuwa kama lugha ya alama au ya kielelezo imetumika. Kristo ametoa
ahadi: “Mtu akipenda kuyatenda mapenzi ya Mungu, atajua habari ya yale mafundisho kwamba yatoka
kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu.” Yohana 7:17. Laiti watu wangeichukulia
Biblia kama inavyosomeka, kama kusingekuwa na walimu wa uongo wa kupotosha na kuchanganya
mawazo yao, kazi ambayo ingeleta furaha kwa malaika na ambayo ingeleta katika zizi la Kristo maelfu
kwa maelfu ambao sasa wanatangatanga katika mafundisho ya uongo ingefanyika.
Yatupasa kutumia nguvu zetu zote za akili katika kujifunza Maandiko na yatupasa kushughulisha fahamu
zetu kuelewa, kwa kadiri ya uwezo wa wanadamu mwenye ukomo, mambo ya kina ya Mungu; hata hivyo
haitupasi kusahau kwamba utayari wa kuongozwa na unyenyekevu wa mtoto ndiyo roho ya kweli ya mtu
anayejifunza. Kamwe ugumu wa Kimaandiko hauwezi kushughulikiwa kwa kutumia njia zile zile
zinazotumika katika kupambana na matatizo ya kifalsafa. Tusijishughulishe katika kujifunza Biblia
tukiwa na hali ya kujitegemea wenyewe kama ile waliyo nayo wengi wanaoingia katika nyanja za
sayansi, bali tukiwa katika kumtegemea Mungu kwa maombi na nia ya kweli ya kujifunza mapenzi yake.
Lazima tuje na roho ya unyenyekevu na ya kufundishika ili kuweza kupata maarifa kutoka kwa MIMI
NIKO mkuu. Vinginevyo, malaika waovu watayapofusha mawazo yetu na kuifanya migumu mioyo yetu
kiasi kwamba hatutaweza kuguswa na ukweli.

Mara nyingi sehemu ya Maandiko inayotajwa na wasomi kwamba ni fumbo, au inayopitwa kwamba si
muhimu, imejaa faraja na mafundisho kwa mtu yule ambaye amejifunza katika shule ya Kristo. Sababu
moja inayowafanya wanathiolojia wengi kukosa kuwa na ufahamu ulio wazi zaidi wa neno la Mungu ni
kwamba, wanafumbia macho ule ukweli ambao hawataki kuuweka katika maisha yao halisi. Ufahamu wa
ukweli wa Biblia hautegemei sana nguvu ya akili inayotumika katika kuuchunguza bali uelekevu wa nia,
hamu ya kutafuta kwa dhati kuwa mwenye haki.
Kamwe Biblia isisomwe pasipo maombi. Roho Mtakatifu pekee ndiye anayeweza kutufanya tuone
umuhimu wa (600) mambo yale yaliyo rahisi kueleweka, au kutuzuia tusizipotoshe kweli zile zilizo
ngumu kueleweka. Ni kazi ya malaika wa mbinguni kuutayarisha moyo kwa njia ya kuelewa neno la
Mungu hata tuweze kuvutwa na uzuri wake, kuonywa na maonyo yake, au kutiwa nguvu na kuimarishwa
na ahadi zake. Yatupasa tuifanye dua ya mwimba zaburi kuwa yetu: “Unifumbue macho yangu
349
niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako.” Zaburi 119:18. Mara kwa mara majaribu
yanaonekana kama yasiyowezekana kupingwa kwa sababu, kwa njia ya kupuuza maombi na kujifunza
Biblia, mtu anayejaribiwa hawezi kuzikumbuka kwa haraka ahadi za Mungu na kupambana na Shetani
kwa kutumia silaha za Maandiko. Lakini malaika wanawazunguka pande zote wale wenye nia ya
kufundishwa mambo ya kimbingu; na wakati watakapokuwa katika ulazima mkubwa wataweza
kuzikumbuka kweli zile zile zinazohitajika. Hivyo “adui atakapokuja kama mkondo wa mto ufurikao,
Roho wa BWANA atainua bendera juu na kumpinga.” Isaya 59:19.
Yesu aliwaahidi wanafunzi wake: “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka
kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.” Yohana 14:26. Lakini
lazima mafundisho hayo ya Kristo yawe yamehifadhiwa kabla moyoni ili Roho wa Mungu aweze kuyaleta
katika kumbukumbu zetu wakati wa hatari. “Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda
dhambi.” Zaburi 119:11.
Wote wanaothamini mambo ya milele wanapaswa kuwa macho kulinda njia ziletazo ndani yao hali ya
kutokukubali ukweli. Nguzo za ukweli zitashambuliwa. Haiwezekani kuwa mbali na mahali panafikiwa na
kejeli, hoja potofu, mafundisho yenye hila na ya kuharibu, ya ukafiri wa kisasa. Shetani analeta
majaribu yake kulingana na mazingira ya matabaka yote ya watu. Anashambulia watu wasio na elimu
kupitia kufanya utani au mzaha, wakati anawakabili wasomi kwa kutumia vitu vigumu vya kisayansi na
hoja za kifalsafa, kwa namna moja yakiwa yamekadiriwa ili kuamsha mashaka au dharau kwa Maandiko.
Hata vijana walio na uzoefu kidogo wanathubutu kuonyesha mashaka juu ya kanuni kuu (601) za
Ukristo. Na ukafiri huu wa vijana, japo usio wa kina, una ushawishi wake. Kwa njia hiyo wengi
wanashawishiwa kuifanyia mzaha imani ya baba zao na kutenda kinyume na Roho wa neema. Waebrania
10:29. Kwa wengi maisha yaliyoahidiwa kuwa heshima kwa Mungu na mbaraka kwa ulimwengu
yamepotoshwa na maisha machafu ya ukafiri. Wote wanaotegemea maamuzi ya majivuno yatolewayo na
hekima ya wanadamu na kufikiri kwamba wanaweza kufafanua siri za kimbingu na kuufikia ukweli
pasipo msaada wa hekima ya Mungu wanajitatiza wenyewe katika mtego wa Shetani.
Tunaishi katika kipindi muhimu sana katika historia ya ulimwengu huu. Hatima ya watu walioijaza dunia
inaelekea kuamuliwa. Mafanikio yetu ya baadaye na pia wokovu wa watu wengine hutegemea njia
tunayoifuata sasa. Tunahitaji kuongozwa na Roho wa kweli. Yapasa kila mfuasi wa Kristo aulize kwa
dhati: “Bwana, unanitaka nifanye nini?” Tunahitaji kujinyenyekeza mbele za Bwana, kwa kufunga na
kuomba, na kulitafakari sana neno lake, hasa matukio yanayohusiana na hukumu. Yatupasa sasa
kutafuta uzoefu wa wa kina na ulio hai katika mambo ya Mungu. Hatuna muda wa kupoteza. Matukio
yenye umuhimu mkubwa yanatokea pande zetu zote; tuko katika uwanja unaomfaa Shetani. Msilale,
walinzi wa upande wa Mungu; adui anawanyemelea kwa karibu, akiwa tayari wakati wowote, mkufanya
uzembe na kusinzia, awarukie na kuwafanya mawindo yake.
Wengi wamedanganyika kuhusu jinsi hali yao halisi ilivyo mbele za Mungu. Wanajipongeza kwa matendo
mabaya ambayo hawafanyi, na kusahau kuorodhesha matendo mema na tabia njema ambayo Mungu
anaitaka kwao, lakini ambayo wamepuuza kufanya. Haitoshi kwamba wao ni miti katika shamba la
Mungu. Wanapaswa kutimiza matarajio yake kwa kuzaa matunda. Anawataka wawajibike kwa
kushindwa kwao kufanaya mema yote ambayo wangekuwa wamefanya, kupitia kwa neema yake
inayowatia nguvu. Katika vitabu vya mbinguni wameandikwa kama watu wanaoiharibu wa ardhi. Lakini
bado hoja kundi hata hili si ya kukata tamaa kabisa. Kwa wale walioidharau rehema ya Mungu na
kuitumia vibaya neema yake, bado moyo ule wa (602) upendo wenye uvumilivu unawasihi. “Hivyo
husema, Amka, wewe usinziaye, ufufuke katika wafu, na Kristo atakuangaza. Basi angalieni sana jinsi
mnavyoenenda,… mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.” Waefeso 5:14-16.
350
Wakati ule wa kujaribiwa utakapokuja, wale ambao wamelifanya neno la Mungu kuwa kiongozi cha
utaratibu wao wa maisha watadhihirishwa. Wakati wa majira ya joto hakuna tofauti iliyo bayana kati ya
miti isiyopukutisha majani wakati wote na miti mingine; lakini wakati mfumuko wa baridi kali ya majira
ya kiangazi unapokuja, ile miti isiyopukutisha majani inabaki vile vile bila kubadilika, wakati miti
mingine inapoteza majani. Hivyo ndivyo ambavyo wanaodai kwa uongo kuwa ni Wakristo wasivyoweza
kutofautishwa kwa sasa na Wakristo wa kweli, lakini wakati umewadia ambapo tofauti hiyo itakuwa
wazi. Ngoja upinzani uinuke, ngoja ushupavu wa dini na kukosa uvumilivu wa imani ya wengine uvume
tena, ngoja moto wa mateso uwashwe, wenye imani nusu-nusu na wanafiki watayumba na kusalimu
amri kwa kuiacha imani yao; lakini Mkristo wa kweli atasimama imara kama mwamba, imani yake
itakuwa na nguvu zaidi, na tumaini lake liking’aa zaidi, kuliko katika siku zile za usitawi.
Mwimba zaburi anasema: “Shuhuda zako ndizo nizifikirizo.” “Kwa mausia yako najipatia ufahamu, ndiyo
maana naichukia kila njia ya uongo.” Zaburi 119:99,104.
“Heri mtu yule aonaye hekima.” “Atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, uenezao mizizi yake
karibu na mto; hautaona hofu wakati wa hari ujapo, bali jani lake litakuwa bichi; wala hautahangaika
mwaka wa uchache wa mvua, wala hautaacha kuzaa matunda.” Mithali 3:13; Yeremia 17:8.

351
Sura ya 38
ONYO LA MWISHO

“Naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa
utukufu wake. Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa
maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye
kuchukiza.” “Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu,
msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” Ufunuo 18:1, 2, 4.
Andiko hili linaelekeza kwa kipindi cha mbele wakati tangazo la kuanguka kwa Babeli, kama
lilivyotolewa na malaika wa pili wa Ufunuo 14 (fungu la 8), litakaporudiwa, likiwa na nyongeza ya
kutajwa kwa mapotofu ambayo yamekuwa yakiingia katika mashirika mbalimbali yanayounda Babeli,
tangu ujumbe huo ulipotolewa kwa mara ya kwanza katika majira ya joto ya mwaka wa 1844. Hali ya
kuogofya ya ulimwengu wa kidini inaelezwa hapa. Kila mara ukweli unapokataliwa akili za watu zinazidi
kutiwa giza, mioyo yao inazidi kuwa sugu, mpaka wanapokuwa wamejizungushia boma katika ugumu wa
ukafiri. Kwa kukiuka maonyo yaliyotolewa na Mungu, wataendelea kuikanyaga moja ya Amri Kumi, hadi
watakapofikishwa hatua ya kuwatesa wale wanaoishikilia amri hiyo kama takatifu. Kristo anawekwa
mahali ambapo si kitu katika dharau inayofanywa juu ya neno lake na watu wake. Kadiri mafundisho ya
umizimu yanavyopokelewa na makanisa, (604) kizuizi kilichowekwa kwenye moyo huondolewa, na
kuitangaza dini kutafanywa kama vazi la bandia la kusitiri maovu makubwa. Imani katika ishara za roho
hufungua mlango kwa ajili ya roho zile zidanganyazo na mafundisho ya mashetani, na hivyo ushawishi
wa malaika hao wabaya utakuwepo katika makanisa hayo.
Kwa habari za Babeli, wakati ule ulioonyeshwa katika unabii huu, inatangazwa: “Kwa maana dhambi
zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.” Ufunuo 18:5. Amekijaza kikombe
cha maovu yake, na maangamizi yako karibu kuanguka juu yake. Lakini bado Mungu anao watu katika
Babeli; na kabla ya kupatilizwa kwa hukumu zake, waaminifu hao hawana budi kuitwa ili watoke kwake,
wasishiriki dhambi zake, wala wasipokee mapigo yake. Hivyo harakati iliyoonyeshwa kwa kutumia
malaika ashukaye kutoka mbinguni, akiiangaza nchi kwa utukufu na kulia kwa sauti kuu, anazitangaza
dhambi za Babeli. Kwa mwunganiko na ujumbe wake wito unasikika: “Tokeni kwake, enyi watu wangu.”
Matangazo haya, yakiungana na ujumbe wa malaika wa tatu, yana onyo la mwisho la kutolewa kwa
wakazi wa dunia hii.
Mahali ambapo ulimwengu utafikishwa ni katika suala la kuogofya. Mamlaka za dunia, zikiungana
kufanya vita dhidi ya amri za Mungu, zitatoa amri kwamba “wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri
kwa maskini, na walio huru kwa watumwa,” (Ufunuo 13:16), wafuate desturi za kanisa kwa kuishika
sabato ya uongo. Wote wanaokataa kutii watafikwa na adhabu kwa mujibu wa sheria, na hatimaye
itatangazwa kwamba wanastahili kifo. Kwa upande mwingine, sheria ya Mungu yenye siku ya pumziko ya
Mwumbaji inadai kutiiwa na itishia ghadhabu dhidi ya wote wanaozivunja amri zilizomo.
Kwa jambo kama hilo linaloletwa wazi hivyo mbele yake, yeyote atakayeikanyaga sheria ya Mungu ili
kuitii sheria iliyotungwa na wanadamu anapokea alama ya mnyama; anakubali ishara ya heshima yake
kwa mamlaka anayochagua kuitii badala ya kumtii Mungu. Onyo kutoka mbinguni ni: “Mtu awaye yote
akimsujudu huyo mnyama (605) na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, yeye
naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji,
katika kikombe cha hasira yake.” Ufunuo 14:9,10.

352
Lakini hakuna hata mmoja anayepaswa kupatwa na ghadhabu ya Mungu bali mpaka ukweli utakapokuwa
umeleletwa hadi mawazoni mwake na katika dhamiri yake, na ukawa umekataliwa. Wako wengi ambao
hawajapata fursa ya kuzisikia kweli maalum za wakati huu. Wajibu kwa amri ya nne haujapata kamwe
kuwekwa mbele yao katika nuru yake halisi. Yeye anayesoma kila moyo na kulipima kila dhamira ya
moyoni hatamwacha mtu yeyote anayetamani kuijua kweli yake, hata adanganyike kwa habari ya
mambo yanayohusu pambano hilo. Amri ile haitahimizwa kwa watu katika upofu. Kila mmoja atakuwa
na nuru ya kutosha ili afanye uamuzi kwa kufikiri.
Sabato itakuwa jaribio kuu la utii, maana ndiyo kweli moja inayobishaniwa hasa. Wakati jaribio la
mwisho litakapoletwa juu ya wanadamu, ndipo mstari utakapochorwa kutenganisha kati ya wale
wamtumikiao Mungu na wale wasiomtumikia. Wakati utunzaji wa sabato ya uongo kama utii kwa sheria
ya serikali, kinyume na amri ya nne, utakuwa ni kiapo cha utii kwa mamlaka ile inayopingana na Mungu,
utunzaji wa Sabato ya kweli, kama utii wa sheria ya Mungu, ni ushahidi wa utii kwa Mwumbaji. Wakati
kundi moja, kwa kuipokea ishara ya utii kwa mamlaka za dunia, linapokea alama ya mnyama, kundi
jingine linalochgua ishara ya utii kwa mamlaka ya mbinguni, linapokea muhuri wa Mungu.
Mpaka sasa wale waliozihubiri kweli za ujumbe wa malaika wa tatu wamefikiriwa mara nyingi kuwa
wavumishaji wa mambo. Utabiri wao kwamba hali ya kukosa uvumilivu wa kidini ingejitawala katika
nchi ya Marekani, kwamba kanisa na serikali vingeungana kuwatesa wale wanaozishika amri za Mungu,
umetangazwa kuwa hauna msingi na ni upuuzi tu. Imetangazwa kwa ujasiri kwamba kamwe nchi hii
isingeweza kuwa tofauti na vile ambavyo imekuwa - mlinzi wa uhuru wa kidini. Lakini (606) kadiri suala
la kuhimiza utunzaji wa Jumapili linavyozidi kusisitizwa sana, tukio lile lililotiliwa mashaka kwa muda
mrefu na kutosadikiwa linaonekana kukaribia, na ujumbe ule wa tatu utaleta matokeo ambayo
usingeweza kuwa ulikuwa nayo kabla.
Katika kila kizazi Mungu ametuma watumishi wake kukemea dhambi, ulimwengu na kanisani. Lakini
watu wanapenda kuambiwa mambo laini, na ukweli ulio safi, usiopakwa mafuta ili kulainishwa
haukubaliki. Wanamatengenezo wengi, wakati wa kuingia katika kuanza kazi yao, walidhamiria kuwa
makini sana katika kushambulia dhambi za kanisa na za taifa. Walitumaini, kwa kielelezo cha maisha
safi ya Kikristo, kuwarejesha watu katika mafundisho ya Biblia. Lakini Roho wa Mungu alikuja juu yao
kama alivyokuja kwa Eliya, akamsukuma akemee dhambi za mfalme mwovu na watu walioasi;
hawakuweza kujizuia kuhubiri maneno yaliyo wazi ya Biblia - mafundisho ambayo walikuwa wanasita
kuyatoa. Walisukumwa kuutangaza ukweli kwa bidii na hatari iliyotishia watu. Walitamka maneno
waliyopewa na Bwana, bila kujali madhara, na watu walisukumwa kulisikia onyo.
Hivyo ndivyo ujumbe wa malaika wa tatu utakavyotangazwa. Wakati muda wa kutoa ujumbe huo kwa
nguvu kubwa sana utakapofika, Bwana atafanya kazi kupitia vyombo vyake vya hali ya chini, akiongoza
mawazo ya wale wanaojitoa kwa kazi yake. Watendakazi wa Mungu watapata sifa za kazi kwa
kustahilishwa na Roho wake wala si kwa mafunzo yanayotolewa katika taasisi za kawaida za mafunzo.
Watu wenye imani na wa maombi, watabidishwa kusonga mbele kwa msukumo mtakatifu, wakitangaza
maneno wanayopewa na Mungu. Dhambi za Babeli zitawekwa wazi. Matokeo ya kuogofya ya mamlaka ya
kiraia kulazimisha utunzaji wa maadhimisho ya kanisa, kuingia kwa imani ya umizimu, maendeleo ya
kificho lakini ya haraka ya nguvu za upapa - yote yatafichuliwa. Kwa maonyo hayo ya kutisha watu
wataamshwa. Maelfu kwa maelfu ambao hawajapata kamwe kusikia maneno kama hayo watasikiliza.
Kwa mshangao wanasikia (607) ushuhuda kwamba Babeli ni kanisa, lililoanguka kwa sababu ya
mafundisho yake potofu na dhambi zake, kwa sababu ya kukataa ukweli uliotumwa kwake kutoka
mbinguni. Kadiri watu wanavyowaendea walimu wao wa siku za nyuma wakiuliza kwa hamu, Je, mambo
haya ndivyo yalivyo? wahubiri wanawaambia hadithi za uongo, wanatabiri mambo laini, ili kutuliza hofu
353
yao na kunyamazisha dhamiri zao zilizoamshwa. Lakini kwa kuwa wengi wanakataa kuridhika na
mamlaka ya wanadamu tu na kudai kwa dhahiri uthibitisho kwamba “Hivi ndivyo asemavyo Bwana,”
hapo ndipo wahubiri hawa maarufu, kama Mafarisayo wale wa zamani, wakijawa na hasira kali kwa
kuwa mamlaka yao inatiliwa mashaka, wataukataa ujumbe wakisema ni wa Shetani na kuwaamsha watu
wengi walio wapenda dhambi wawalaani na kuwatesa wale wanaotangaza ujumbe huo.
Kadiri pambano linavyoenea katika maeneo mapya na akili za watu zikaitwa kuelekea kwa sheria ya
Mungu iliyokanyagwa, shetani atachachamaa. Nguvu zinazousukuma ujumbe huo zitawapumbaza wale
wanaoupinga. Viongozi wa kanisa watatumia juhudi iliyo takriban zaidi ya uwezo wa kibinadamu
kuzuilia mbali nuru hiyo isiangazie makundi yao ya waumini. Kwa kutumia kila njia iliyo katika uwezo
wao watajitahidi kuondosha mazungumzo ya kujadiliana kuhusu mambo haya nyeti. Kanisa linaomba
msaada kutoka kwa mkono wenye nguvu wa mamlaka ya dola, na, katika kazi hii, watu wa upapa na
Waprotestanti wanaungana. Kadiri harakati za kuihimiza Jumapili zinavyozidi kuwa na nguvu na za
kudhamiria, sheria itahitajika kuwekwa dhidi ya hao wazishikao amri. Watatishiwa kwa kutozwa faini na
kufungwa gerezani, na baadhi yao wataahidiwa vyeo vyenye ushawishi, pamoja na thawabu na
marupurupu mengine, kama vivutio ili waikane imani yao. Lakini jibu lao lilio thabiti litakuwa ni:
“Tuonyesheni makosa yetu kulingana na neno la Mungu” - sababu ile ile iliyotolewa na Martin Luther
akiwa katika mazingira kama hayo. Wale wanaoshtakiwa mahakamani wanasimama kwa nguvu
kuuthibitisha ukweli, na baadhi ya wale wanaowasia wanaongozwa kuchukua msimamo wao katika
kuzishika amri za Mungu zote. Kwa njia hiyo nuru italetwa mbele ya maelfu ambao vinginevyo
wasingejua lolote katika kweli hizo.
(608) Utii wa neno la Mungu unaotokana na dhamiri utachukuliwa kama uasi. Akiwa amepofushwa
macho na Shetani, mzazi atafanya ukatili na ukali kwa mtoto wake aaminiye; bwana au bibi mwajiri
atamkandamiza mtumishi wake azishikaye amri za Mungu. Hisia za upendo zitatoweka; watoto
watanyang’anywa haki ya urithi wao na kufukuzwa kutoka nyumbani. Maneno ya Paulo yatatimizwa
kama yalivyo: “Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.” 2
Timotheo 3:12. Kadiri wale wanotetea ukweli wanavyokataa kuiheshimu sabato ya Jumapili, baadhi yao
watatupwa gerezani, wengine watafanywa kuishi uhamishoni, wengine watafanywa kuwa watumwa.
Kwa hekima ya mwanadamu mambo haya yote kwa sasa yanaonekana yasiyowezekana; lakini wakati
Roho wa Mungu azuiaye atakapoondolewa kwa wanadamu, na watakapokuwa chini ya udhibiti wa
Shetani, ambaye anazichukia amri za Mungu, mambo mageni yatajitokeza. Moyo unaweza kuwa katili
sana pindi hofu ya Mungu na upendo vinapoondolewa.
Kadiri dhoruba inavyokaribia, kundi kubwa la wale ambao wamekuwa wakiitangaza imani katika ujumbe
wa malaika wa tatu, lakini hawakutakaswa kwa kutii ukweli, wanaiacha nafasi yao na kujiunga na jeshi
la upinzani. Kwa kuungana na ulimwengu na kushiriki mambo ya roho ya ulimwengu, wameelekea
kuyaangalia mambo kwa mtazamo wa nuru karibu ile ile ya ulimwengu; na jaribio linapoletwa,
wamejiandaa kuchagua upande ulio rahisi, unaopendwa na wengi. Watu wenye vipaji na hotuba nzuri,
ambao wakati fulani walifurahia katika ukweli, sasa wanatumia uwezo wao huo kuwadanganya na
kuwapotosha watu. Wanakuwa maadui wachungu zaidi kwa ndugu zao wa zamani. Pindi watunza-sabato
wanapoletwa mbele za mahakama kujibu kwa ajili ya imani yao, waasi hawa ndio mawakala mahiri sana
wa Shetani katika kuwaeleza vibaya na kuwashtaki, na kwa kutoa taarifa za uongo na masingizio
wanawachochea watawala dhidi ya watu hawa.
Katika kipindi hiki cha mateso imani ya watumishi wa Bwana itajaribiwa. Wametoa onyo kwa uaminifu,
wakimtazama Mungu na neno lake tu. Roho wa Mungu, akiwa katika mioyo yao, amewabidisha kunena.
Wakiwa wamechochewa (609) na ari takatifu, na mguso wa mbinguni ukiwa na nguvu juu yao, waliingia
354
katika kutekeleza majukumu pasipo kufikiria matokeo ya kuwaambia watu neno ambalo walikuwa
wamepewa na Bwana. Hawakuyaangalia mambo yao ya maisha, wala hawakutafuta kulinda bafasi zao
au maisha yao. Lakini pindi dhoruba ya upinzani na mashutumu vinapolipuka juu yao, baadhi, wakiwa
wameelemewa na kushtushwa, watakuwa tayari kushangaa, wakisema: “Laiti kama tungejua mapema
matokeo ya maneno yetu, tungenyamaza kimya.” Wamezingirwa na mambo magumu. Shetani
anawashambulia kwa majaribu makali. Kazi ambayo wameingia kuifanya inaonekana kuwa mbali juu ya
uwezo wao kuikamilisha. Wanatishwa na maangamizi. Shauku ile iliyowachochea inatoweka; lakini bado
hawawezi kurudi nyuma. Halafu wanapojisikia ya kuwa hawana uwezo kabisa, wanamwendea yeye
Mwenye Uweza ili awatie nguvu. Wanakumbuka kwamba maneno yale ambayo wamesema hayakuwa
yao, bali yake yeye aliyewaamuru kutoa onyo lile. Mungu anaweka ukweli mioyoni mwao, na
wasingeweza kujizuia kuutangaza.
Maonjo kama hayo yamewapata watu wa Mungu katika vizazi vilivyopita. Wycliffe, Huss, Luther,
Tyndale, Baxter, Wesley, walisisitiza kwamba sharti mafundisho yote ya dini yapimwe kwa Biblia na
walitangaza kwamba wangeachana na kila kitu kilichokatazwa na Biblia. Mateso yalilipuka dhidi yao kwa
ukali mkubwa; hata hivyo hawakukoma kuutangaza ukweli. Vipindi tofauti katika historia ya kanisa
vimekuwa na uendelezaji wa ukweli fulani maalum, uliochukuliwa kukidhi mahitaji ya watu wa Mungu
kwa kipindi husika. Kila ukweli mpya umepitia katika njia ya chuki na upinzani; wale waliobarikiwa na
nuru ya ukweli huo walijaribiwa na kupimwa. Bwana huwapa watu ukweli maalum katika wakati
maalum. Nani atathubutu kukataa usitangazwe? Anawaamuru watumishi wake kutoa mwaliko wa
mwisho wa rehema kwa ulimwengu. Hawawezi kubaki kimya, isipokuwa kwa hasara ya nafsi zao.
Mabalozi wa Kristo (610) hawashughuliki na matokeo. Lazima wafanye wajibu wao na kuacha matokeo
mikononi mwa Mungu.
Kadiri upinzani unavyoongezeka ukali kuelekea kwenye kilele chake, watumishi wa Mungu wanafadhaika
tena; maana inaonekana kwao kama wameleta hali ya hatari. Lakini dhamiri na neno la Mungu
vinawahakikishia kwamba njia yao ni sahihi; na japokuwa maonjo yanaendelea, wanatiwa nguvu
kuyastahimili. Vita inazidi kuja karibu zaidi na kuwa kali zaidi, lakini imani yao na ujasiri wao
huongezeka kulingana na hali inayojitokeza. Ushuhuda wao n: “Hatuwezi kuthubutu kucheza na neno la
Mungu, kugawa sheria yake takatifu; kuiona sehemu moja muhimu na nyingine kuwa si umuhimu, ili
kupata kupendwa na ulimwengu. Mungu tunayemtumikia anaweza kutuokoa. Kristo amezishinda nguvu
za dunia; sisi tuogope ulimwengu ambao umekwisha kushindwa tayari?”
Mateso katika aina zake mbalimbali ni maendeleo ya kanuni itakayoendelea kuwako kadiri Shetani
anakavyoendelea kuwepo na Ukristo kuwa na nguvu nyingi. Hakuna mtu awezaye kumtumikia Mungu bila
kujiorodhesha kuwa dhidi ya upinzani wa majeshi ya giza. Malaika waovu watamshambulia, wakitiwa
hofu kwamba ushawishi wake unapora mawindo yao toka mikononi mwao. Watu waovu, ambao
wanakemewa na kielelezo cha maisha yake, wataungana na hao malaika waovu katika kutafuta
kumtenga mbali na Mungu kwa kumletea vishawishi. Hivyo visipofanikiwa, ndipo nguvu hutumika
kuilazimisha dhamiri yake.
Lakini kadiri Yesu anavyoendelea kuwa mwombezi wa mwanadamu katika patakatifu huko juu, uwezo
ule uzuiao wa Roho Mtakatifu unazidi kuigusa mioyo ya watawala na watu. Bado uwezo huo unadhibiti
kwa kiasi fulani sheria za nchi. Kama isingekuwa sheria hizo, hali ya ulimwengu ingekuwa mbaya zaidi
kwa mbali kuliko ilivyo sasa. Wakati wengi miongoni mwa watawala wetu ni mawakala hai wa Shetani,
Mungu pia anao mawakala wake miongoni mwa wakuu wa taifa. Adui anawachochea watumishi wake
kupendekeza hatua ambazo zingeweza kuikwamisha kazi ya Mungu; lakini viongozi wa kisiasa wamchao
Mungu hushawishiwa na malaika watakatifu kuyapinga mapendekezo hayo kwa hoja zisizopingika. Kwa
355
njia hiyo watu wachache (611) watazuia mkondo wenye nguvu wa uovu. Upinzani wa maadui wa ile
kweli utazuiwa ili ujumbe wa malaika wa tatu ufanye kazi yake. Wakati onyo la mwisho litakapotolewa,
litayakamata usikivu wa viongozi hawa ambao kupitia wao Bwana anafanya kazi yake hivi sasa, na
baadhi yao watalikubali onyo hilo, na watasimama pamoja na watu wa Mungu mnamo wakati wa taabu.
Malaika anayejiunga katika kuutangaza ujumbe wa malaika wa tatu ataiangaza dunia yote kwa utukufu
wake. Kazi yenye kuenea ulimwenguni na yenye nguvu isiyo ya kawaida inatabiriwa hapa. Harakati za
marejeo za miaka ya 1840-1844 zilikuwa udhihirisho mtukufu wa nguvu za Mungu; ujumbe wa malaika
wa kwanza ulipelekwa katika kila kituo cha umishonari ulimwenguni, na katika baadhi ya nchi kulikuwa
na mwamko mkubwa wa mambo ya kiroho ambao haujapata kushuhudiwa katika nchi yoyote tangu siku
zile za Matengenezo ya karne ya kumi na sita; lakini harakati hizi zitapitwa na harakati zenye nguvu
nyingi zitakazofanyika chini ya onyo la mwisho la malaika wa tatu.
Kazi hii itafanana na ile ya Siku ya Pentekoste. Kama vile “mvua ya awali” ilivyotolewa, katika
kumwagwa kwa Roho Mtakatifu wakati wa kuifungua injili, kuifanya mbegu ile ya thamani ipate
kuchipua, ndivyo “mvua ya masika” itakavyotolewa wakati wa kuifunga kazi hiyo ili kuyakomaza
mavuno. “Ndipo tutajua, tukiendelea kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi: naye
atatujilia kama mvua, mvua ya masika na ya vuli iinyweshayo nchi.” Hosea 6:3. “Furahini, basi, enyi
wana wa Sayuni, mkamfurahie BWANA, Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa ninyi mvua ya masika, kwa
kipimo cha haki, naye huwanyeshea mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli, kama kwanza.” Yoeli 2:23.
“Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu.” “Na itakuwa kila
atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa.” Matendo 2:17,21.
Kazi kuu ya injili haitafungwa kwa udhihirisho wa nguvu za Mungu ulio mdogo kuliko ule uliokuwepo
wakati wa kuanza kwake. Unabii ule uliotimizwa kwa kumwagwa kwa (612) mvua ya vuli wakati wa
kuanza kwa kazi ya injili utatimizwa tena katika mvua ya masika wakati kazi itakapokuwa inafungwa.
Hapa ndipo penye “nyakati za kuburudishwa” ambazo mtume Petro alizitarajia aliposema: “Tubuni basi,
mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; apate
kumtuma Kristo Yesu.” Matendo 3:19,20.
Watumishi wa Mungu, wakiwa na nyuso zinazoangazwa na kung’aa kwa kujitoa wakfu kwa utakatifu,
wataharakisha huku na huko kuutangaza ujumbe uliotoka mbinguni. Kwa maelfu ya sauti, ulimwenguni
kote, onyo hilo litatolewa. Miujiza itafanyika, wagonjwa wataponywa, na ishara na maajabu vitafuatana
na wale waaminio. Shetani naye afanya kazi, kwa ishara za uongo, hata kufanya moto kushuka kutoka
mbinguni uje mbele ya watu. Ufunuo 13:13. Hivyo ndivyo wakazi wa dunia watakavyofikishwa mahali pa
kuwa na msimamo.
Ujumbe huo hautapelekwa kwa nguvu ya hoja sana bali kwa mguso wa kusadikisha wa kina ufanywao na
Roho wa Mungu. Hoja zimekwisha kutolewa. Mbegu imekwisha kupandwa, na sasa itachipua na kuzaa
matunda. Machapisho yaliyotawanywa na watendakazi wamishonari yamefanya ushawishi wake, lakini
wengi ambao mioyo yao ilikuwa imeguswa wamezuiwa wasiweze kuuelewa kikamilifu ukweli huo au
wamezuiwa kuutii. Sasa miale ya nuru inapenya kila mahali, kweli inaonekana katika uwazi wake, na
watoto wa Mungu walio waaminifu wanakata kamba zilizowafunga na kuwashikilia. Miunganiko ya
familia, mahusiano ya kikanisa, havina nguvu ya kuwazuia sasa. Ukweli una thamani sana kuliko mambo
mengine yote. Licha ya mamlaka zote zilizojikusanya pamoja dhidi ya ukweli, watu wengi wanachagua
kusimama upande wa Bwana.

356
Sura ya 39
WAKATI WA TAABU

“Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na
kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo
huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu
kile.” Danieli 12:1.
Wakati ujumbe wa malaika wa tatu ufungwapo, rehema haipo tena kwa wakazi wa dunia wenye hatia.
Watu wa Mungu wamemaliza kazi yao. Wamepokea “mvua ya masika,” “kuburudishwa kwa kuwako
kwake Bwana,” na wako tayari kukabiliana na ile saa ya kujaribiwa iliyo mbele yao. Malaika
wanaharakisha kwenda huku na huko mbinguni. Malaika anayerudi kutoka duniani anatangaza kwamba
kazi yake imekamilika; jaribio la mwisho limeletwa juu ya ulimwengu, na wote waliojithibitisha kuwa
watiifu kwa amri za kimbingu wamepokea “muhuri wa Mungu aliye hai.” Hapo ndipo Yesu anapokoma
kufanya maombezi yake katika patakatifu huko juu. Anainua mikono yake na kusema kwa sauti kuu,
“Imekamilika;” na majeshi yote ya malaika wanavua taji zao wakati anapotoa tamko: “Mwenye
kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi
kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.” Ufunuo 22:11. Kila shauri limekatwa kwa uzima au
mauti. Kristo amefanya upatanisho kwa ajili ya watu wake na (614) kuzifuta dhambi zao. Idadi ya watu
walio katika himaya yake imekamilika; “Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme chini ya mbingu
zote,” uko karibu kukabidhiwa kwa hao warithi wa wokovu, na Yesu anaelekea kutawala kama Mfalme
wa wafalme na Bwana wa mabwana.
Yesu anapoondoka katika patakatifu, giza linawafunika wakazi wa dunia. Katika kipindi hicho cha
kuogofya watakatifu hawana budi kuishi mbele za Mungu mtakatifu bila kuwa na mwombezi. Kizuizi
kilichokuwa juu ya waovu kimeondolewa kwao, na Shetani anakuwa na udhibiti mpana kwa wale ambao
hatimaye hawakutubu. Uvumilivu wa Mungu umefika mwisho. Ulimwengu umeikataa rehema yake,
umedharau upendo wake, na kuikanyaga sheria yake. Waovu wamevuka mpaka wa muda wao wa
rehema; Roho wa Mungu, aliyepingwa muda wote, hatimaye ameondolewa kwao. Wakiwa hawana kinga
ya neema ya Mungu, watakuwa hawana ulinzi wo wote dhidi ya yule mwovu. Ndipo Shetani
atakapowatumbukiza wakazi wa dunia katika taabu moja kuu ya mwisho. Pindi malaika wa Mungu
wanapoacha kuzuia pepo kali za hisia ya mwanadamu, mambo yote yanayohusiana na vurugu
yataachiliwa. Ulimwengu wote utawekwa kataika maangamizi ya kutisha sana kuliko yale yaliyokuja juu
ya Yerusalemu ya zamani.
Malaika mmoja tu aliangamiza wazaliwa wa kwanza wote wa Wamisri na kujaza maombolezo katika
nchi. Pindi Daudi alipomkosea Mungu kwa kuwahesabu watu, malaika mmoja tu alisababisha
maangamizi yale ya kutisha ambayo kwayo dhambi yake ilipatilizwa. Uwezo ule ule wa kuangamiza
unaotumiwa na malaika watakatifu pindi Mungu anapoamuru, utatumiwa na malaika waovu wakati
Mungu atakaporuhusu. Kwa sasa kuna majeshi ambayo yako tayari, na yakingojea tu ruhusa kutoka
mbingu, kueneza maangamizi kila mahali.
Wale wanaoiheshimu sheria ya Mungu wameshtakiwa kwamba ndio walioleta hukumu za Mungu
ulimwenguni, na watachukuliwa kama ndio wanaosababisha misukosuko ya maumbile ya asili na
mapigano na umwagaji wa damu miongoni mwa watu, vitu vinavyojaza maafa duniani. Nguvu isukumayo

357
lile onyo la mwisho umewakasirisha waovu; hasira yao imewashwa dhidi ya wote (615) waliopokea
ujumbe huo, na Shetani bado atachochea kwa kiwango kikubwa zaidi roho ya kuchukia na kutesa watu.
Wakati hatimaye kuwepo kwa Mungu kulipoondolewa katika taifa la Kiyahudi, makuhani na watu
hawakujua. Ingawa walikuwa chini ya udhibiti wa Shetani, na kutawaliwa na hasira ya kutisha na
mwelekeo wa kuwadhuru wengine, bado wao walijiona kama watu waliochaguliwa na Mungu. Huduma
katika hekalu ziliendelea; dhabihu zilitolewa kwenye madhabahu zile zilizonajisiwa, na waliomba
baraka ya Mungu kila siku iwe juu yao wao waliokuwa na hatia ya damu ya Mwana mpendwa wa Mungu
na ambao walikuwa wanatafuta kuwaua watumishi na mitume wake. Kwa hiyo wakati hukumu ya
patakatifu isiyobatilishika itakapokuwa imetamkwa na hatima ya ulimwengu kuamuliwa milele, wakazi
wa dunia hawatajua. Taratibu za dini zitaendelea kufanywa na watu ambao kwao Roho wa Mungu
atakuwa hatimaye ameondolewa; na juhudi ya kishetani ambayo mkuu wa uovu atawavuvia ili
watekeleze mipango yake ya kudhuru, itakuwa kama vile ni juhudi kwa ajili ya Mungu.
Kwa kuwa Sabato imekuwa hoja maalum inayobishaniwa katika ulimwengu wote wa Kikristo, na
mamlaka za kidini na za dola zimeungana kulazimisha utunzaji wa Jumapili, kitendo cha watu walio
wachache sana kuendelea kukataa kufuata matakwa ya watu wengi kitawafanya wawe wahanga wa
chuki. Itasisitizwa kwamba lazima wale wachache wanaopinga jambo lililoanzishwa na kanisa na sheria
ya nchi wasivumiliwe; kwamba ni heri waumie kuliko mataifa yote kutumbukizwa katika machafuko na
maasi. Hoja hiyo hiyo ililetwa na “watawala wa watu.” dhidi ya Kristo miaka elfu na mia nane iliyopita.
Kayafa yule mwerevu alisema, “Yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima.”
Yohana 11:50. Sababu hiyo itaonekana kufaa kuhitimishia mambo; na hatimaye amri itatolewa dhidi ya
wale wanaoitakasa Sabato ya amri ya nne, ikiwashutumu kwamba ni watu wanaostahili adhabu kali sana
na itawapa (616) watu uhuru, baada ya muda fulani, kuwaua. Uroma katika Ulimwengu wa Kale na
Uprotestanti uliosi katika Ulimwengu Mpya utafuata njia hiyo hiyo dhidi ya wale wanaoziheshimu amri
zote za Mungu.
Hapo ndipo watu wa Mungu watakapotumbukizwa katika hali ya mateso na dhiki inayoelezwa na nabii
kuwa ni wakati wa taabu ya Yakobo. “Maana BWANA asema hivi, Tumesikia sauti ya kutetemeka, na ya
hofu, wala si ya amani…. Nyuso zote zimegeuka rangi. Ole! maana siku ile ni kuu, hata hapana
inayofanana nayo; maana ni wakati wa taabu yake Yakobo; lakini ataokolewa nayo.” Yeremia 30:5-7.
Usiku ule wa utungu wa Yakobo, alipopambana katika maombi ili apate kuokolewa na mkono wa Esau
(Mwanzo 32:24-30), huwakilisha uzoefu wa watu wa Mungu mnamo wakati wa taabu. Kwa sababu ya
udanganyifu aliofanya ili kujipatia mbaraka toka kwa baba yake uliokusudiwa kutolewa kwa Esau,
Yakobo alikimbia ili kuokoa maisha yake, akiogofywa na vitisho vya kaka yake kutaka kumwangamiza.
Baada ya kukaa uhamishoni kwa miaka mingi, alikuwa ameanza kuondoka kule, kwa agizo la Mungu,
kurudi katika nchi yake akiwa na wake zake na watoto wake, kondoo wake na ng’ombe wake. Alipofika
katika mipaka ya nchi yake, alijawa na hofu kuu kufuatia habari kwamba Esau anakaribia akiongoza
kundi la watu wa vita, bila shaka akiazimia kulipiza kisasi. Kundi la Yakobo, likiwa halina silaha na
pasipo kinga yoyote, lilionekana kana kwamba linakaribia kuwa wahanga wa ukatili na upanga wasio na
msaada wowote. Na juu ya mzigo ule wa wasiwasi na hofu kuliongezeka uzito wa kujilaumu mwenyewe,
maana ni dhambi yake mwenyewe iliyokuwa imeleta hatari hii. Tumaini lake pekee lilikuwa katika
rehema ya Mungu; kinga yake pekee ilikuwa ni maombi. Lakini yeye haachi kufanya kila kitu
kilichopaswa kufanywa kwa upande wake ili kufanya upatanisho kwa kosa alilomfanyia ndugu yake na ili
kuiepusha hatari ile iliyomkabili. Hivyo ndivyo wafuasi wa Kristo, kadiri wanavyoukaribia wakati wa
taabu, wanavyopaswa kufanya bidii kujiweka katika nuru inayofaa mbele ya watu, kupoza chuki na
hasira za watu, na kuepusha hatari inayotishia uhuru wa dhamiri.
358
Akiwa ameipeleka familia yake mbali, ili isishuhudie dhiki yake, Yakobo anabaki peke yake ili kumsihi
Mungu. Anaiungama (617) dhambi yake na kwa shukrani anaikubali rehema ya Mungu kwake wakati kwa
unyenyekevu wa kina anaomba agano lililofanywa na baba zake na ahadi zilizotolewa kwake katika
maono ya usiku kule Betheli na katika nchi yake ya ugeni. Zahama imekuja katika maisha yake; kila kitu
kiko hatarini. Katika giza na upweke, anaendelea kuomba na kujinyenyekeza mbele za Mungu. Ghafla
mkono unamshika kwenye bega lake. Yeye anadhani ni adui anayetaka roho yake, na kwa nguvu zote
kama za mtu asiye na msaada wowote anapambana na mshambuliaji wake. Siku inapoanza
kupambazuka, mtu yule aliye mgeni anatumia nguvu yake isiyo ya kibinadamu; anamgusa, na mtu huyu
mwenye nguvu anaonekana kupooza, na anaanguka shingoni mwa mshindani wake asiye wa kawaida,
akiwa hana msaada, na akilia kwa dua. Sasa Yakobo anajua kwamba yule ambaye amekuwa akipigana
naye ni Malaika wa agano. Ingawa amelemazwa na ana maumivu makali, haachani na kusudi lake. Muda
mrefu amestahimili mfadhaiko, majuto, na masumbuko kwa ajili ya dhambi yake, sasa lazima apate
uthibitisho kwamba imesamehewa. Mgeni yule wa kimbingu anaonekana kama anataka kuondoka; lakini
Yakobo anamng’ang’ania, akimsihi ambariki. Malaika anasema, “Niache, niende, maana
kunapambazuka.” Lakini yule mzee anasema, “Sikuachi, usiponibariki.” Ni ujasiri ulioje, ni uthabiti na
uvumilivu wa namna gani, vinavyoonyeshwa hapa! Kama hapa kungekuwa na madai ya majivuno na
kiburi, Yakobo angekuwa ameangamizwa mara moja; lakini madai yake yalikuwa hakikisho la mtu
aungamaye udhaifu wake na kutostahili kwake, lakini akitumiania rehema ya Mungu atunzaye agano.
“Naam, alikuwa na uwezo juu ya malaika akashinda.” Hosea 12:4. Kwa njia ya kujidhili, toba, na
kujisalimisha binafsi, mwanadamu wa dhambi alimshinda Mfalme wa mbinguni. Alikuwa ameshikilia kwa
kutetemeka ahadi za Mungu, na moyo wake yeye Mwenye Upendo haukuweza kugeuzia mbali ombi la
mwenye dhambi. Kama ushahidi wa ushindi wake na kielelezo cha kutia moyo wengine ili wapate kuiga
mfano wake, jina lake likabadilishwa kutoka lile lililokuwa linakumbusha dhambi yake, na kuwa jina la
kumbukumbu ya ushindi wake. Na ukweli kwamba Yakobo (618) alikuwa amemshinda Mungu ulikuwa ni
hakikisho kwamba angewashinda wanadamu. Hakuogopa tena kukutana na hasira ya ndugu yake, kwa
kuwa Bwana alikuwa kinga yake.
Shetani alikuwa amemshtaki Yakobo kwa malaika za Mungu, akidai haki ya kumwangamiza kwa sababu
ya dhambi yake; alikuwa amemshawishi Esau ili kwenda kumpiga; na katika usiku ule mrefu wa
mapambano ya yule mzee, Shetani alijitahidi kumwingizia hisia ya hatia yake ili kumkatisha tamaa na
kuvunja nia yake ya kumshikilia Mungu. Yakobo alipelekwa katika hali ya kukosa tumaini; lakini alijua
kwamba bila kupata msaada kutoka mbinguni lazima ataangamia. Alikuwa ametubu dhambi yake kuu
kwa moyo mnyofu, na aliomba rehema toka kwa Mungu. Hkuweza kugeuzwa mbali na kusudi lake, bali
alimshikilia Malaika kwa nguvu na kutoa dua yake kwa kilio cha dhati na uchungu mpaka akashinda.
Kama vile Shetani alivyomshawishi Esau kwenda kumpiga Yakobo, ndivyo atakavyowachochea waovu
kuwaangamiza watu wa Mungu mnamo wakati wa taabu. Na kama vile alivyomshtaki Yakobo, ndivyo
atakavyoshinikiza mashtaka yake dhidi ya watu wa Mungu. Anahesabu ulimwengu wote kuwa ni raia
zake; lakini kundi dogo la watu wanaozishika amri za Mungu linapinga ukuu wake duniani. Laiti kama
angewafutilia mbali kutoka duniani, ushindi wake ungekuwa umekamilika. Anaona kwamba malaika
watakatifu wanawalinda, na anahisi kwamba dhambi zao zimesamehewa; lakini hajui kama kesi zao
zimekwisha kukatwa katika patakatifu huko juu. Anajua kwa usahihi dhambi ambazo alizowahimiza
kuzitenda, na anazionyesha mbele za Mungu katika mwonekano uliokuzwa sana, akionyesha kwamba
watu hawa wanastahili kutengwa mbali na Mungu kama yeye alivyo. Anadai kwamba kwa haki Bwana
hawezi kuwasamehe dhambi zao na wakati huohuo amwangamize yeye na malaika zake. Anadai kwamba
wao ni mateka wake na anataka wakabidhiwe mikononi mwake ili awaangamize.

359
Kadiri Shetani anavyowashtaki watu wa Mungu kwa sababu ya dhambi zao, Bwana anamruhusu
kuwajaribu hadi upeo. Ujasiri wao katika Mungu, imani yao na uthabiti wao, vitajaribiwa vikali.
Wanapoangalia mambo ya nyuma, matumaini yao yanazama; (619) maana katika maisha yao yote
wanaona wema kidogo sana. Wanatambua kwa ukamilifu udhaifu wao na kutokufaa kwao. Shetani
anajitahidi kuwatisha kwa mawazo kwamba kesi zao hazina matumaini, kwamba waa la uchafu wao
halitaoshwa kamwe. Anatumaini kwa njia hiyo kuharibu imani yao ili wapate kuanguka katika majaribu
yake na kugeuka na kuachana na utiifu kwa Mungu.
Ingawa watu wa Mungu watakuwa wamezingirwa na maadui waliopania kuwaangamiza, bado utungu ule
watakaoupata hausababishwi na utisho wa mateso watakayopata kwa ajili ya ile kweli; wanaogopa
kwamba kila dhambi haijatubiwa, na kwamba kutokana na kosa fulani lililo ndani yao watashindwa
kutimiziwa ahadi ya Mwokozi isemayo: Mimi “nami nitakulinda, utoke katika saa ya kujaribiwa iliyo
tayari kuujilia ulimwengu wote.” Ufunuo 3:10. Kama wangeweza kupata uthibitisho wa kusamehewa
dhambi wasingeogopa mateso au kifo; lakini kama wangeonekana kuwa hawafai, na kupoteza uhai wao
kwa sababu ya kasoro katika tabia zao, jina takatifu la Mungu lingetukanwa.
Kila upande wanasikia njama za usaliti na kuona utendaji wa kazi ya maasi; na ndani yao inaamshwa
shauku kubwa, hamu ya dhati ya roho, kwamba uasi huo mkuu uweze kukomeshwa na uovu wa hao
waovu ufike mwisho. Lakini wakati wanamsihi Mungu kusimamisha kazi ya maasi, kuna hisia za
kujilaumu wenyewe kiasi kwamba wao wenyewe hawana uwezo zaidi wa kupinga na kuzuia wimbi hilo
kubwa la uovu. Wanahisi kwamba laiti sikuzote wangekuwa wametumia uwezo wao wote katika kazi ya
Kristo, wakisonga mbele toka nguvu hadi nguvu, majeshi ya Shetani yangekuwa na nguvu kidogo kiasi
cha kutoweza kuwashinda.
Wanajitesa nafsi zao mbele za Mungu, wakionyesha toba ya siku za nyuma ya dhambi zao nyingi, na
kudai ahadi ya Mwokozi: “Hebu na azishike nguvu zangu, ili afanye amani nami, naye atafanya amani
nami.” Isaya 27:5. Imani yao haiondoki kwa sababu maombi yao (620) hayajibiwi wakati huo. Ingawa
wanaumia kwa mfadhaiko, hofu kuu, na dhiki, hawakomi kutoa dua zao. Wanazishikilia nguvu za Mungu
kama Yakobo alivyomshikilia Malaika; na lugha iliyo katika roho zao ni: “Sitakuacha, usiponibariki.”
Ingekuwa kwamba Yakobo hakuwa ametubia kabla dhambi yake ya kujipatia haki ya mzaliwa wa kwanza
kwa udanganyifu, Mungu asingesikia maombi yake na kwa rehema kuyahifadhi maisha yake. Kwa hiyo,
mnamo wakati wa taabu, ikiwa watu wa Mungu wangekuwa na dhambi zisizoungamwa ambazo
zitaonekana mbele yao wakati wakiteseka kwa hofu na utungu, wangeshindwa kabisa; kukosa tumaini
kungekatilia mbali imani yao, wala wasingeweza kuwa na ujasiri wa kumwomba Mungu ili waokolewe.
Lakini wakati wakiwa na hisia ya kina ya kutokufaa kwao, hawana makosa yoyote waliyoficha ambayo
wanatakiwa kuyaweka wazi. Dhambi zao zimetangulia kwenda hukumuni na zimekwisha kufutwa, wala
hawawezi kuzikumbuka tena.
Shetani anawashawishi wengi kuamini kwamba Mungu hatatilia maanani kutokuamini kwao katika
mambo madogo sana ya maisha yao; lakini Bwana anatuonyesha katika kushughulika kwake na Yakobo
kwamba kwa vyovyote vile hatakubali au kuvumilia uovu. Wote wanaojitahidi kutoa udhuru au kuficha
dhambi, na kuziacha ziendelee kubaki katika vitabu vya mbinguni, paipo kuungamwa na kusamehewa,
watashindwa na Shetani. Kadiri wanavyokuwa na kazi zenye kutukuzwa zaidi na kadiri nyadhifa walizo
nazo zinavyozidi kuheshimiwa, ndivyo njia yao inavyokuwa ngumu zaidi machoni pa Mungu, na ndivyo
ushindi wa yule adui yao mkuu unavyokuwa wa hakika zaidi. Wale wanaochelewesha kujiandaa kwa ajili
ya siku ya Mungu hawawezi kupata nafasi ya kujianda mnamo wakati wa taabu au wakati mwingine wa
baada ya hapo. Hali ya watu wote kama hao haina matumaini kabisa.

360
Watu waitwao Wakristo ambao wanaelekea katika pambano lile la kuogofya la mwisho wakiwa
hawajajiandaa wataungama dhambi zao, pasipo matumaini, kwa maneno yenye mwako wa utungu,
wakati waovu wanashangilia dhiki yao. Maungamo hayo yana tabia kama ile aliyokuwa nayo Esau au
Yuda. Wale wanaoyafanya, wanaombolezea matokeo ya kutenda dhambi, lakini si kuhisi hatia ya
dhambi. Hawahisi (621) mguso wa toba ya kweli, hakuna kuchukia uovu. Wanakiri kutenda dhambi,
ingawa ni kwa kuogopa adhabu; lakini, kama alivyokuwa Farao wa zamani, wangerudi katika kuasi dhidi
ya Mbingu ikiwa hukumu ingeondolewa.
Historia ya Yakobo ni hakikisho pia kwamba Mungu hatawatupa nje wale waliodanganywa na kujaribiwa
na kuingizwa katika dhambi, lakini ambao wamerudi kwake Mungu kwa toba ya kweli. Wakati Shetani
anatafuta kuwaangamiza watu hawa, Mungu atatuma malaika zake kuwafariji na kuwalinda katika
wakati wa hatari. Mashambulizi ya Shetani ni makali na ya kudhamiria, madanganyo yake yanatisha;
lakini jicho la Bwana li juu ya watu wake, na sikio lake hukisikia kilio chao. Mateso yao ni makubwa,
ndimi za moto wa tanuru zinaonekana kuwa tayari kuwateketeza; lakini Msafishaji wa dhahabu
atawatoa wakiwa kama dhahabu iliyojaribiwa kwa moto. Upendo wa Mungu kwa watoto wake katika
kipindi cha majaribu makali mno una nguvu na huruma kama katika siku nuru kubwa ya jua la usitawi
wao; lakini kuna hitaji la wao kuwekwa katika tanuru la moto; lazima mambo yao ya kiulimwengu
yateketezwe, kusudi sura halisi ya Kristo ipate kuakisiwa kwa usahihi.
Kipindi cha dhiki na utungu kilicho mbele yetu kitahitaji tuwe na imani inayoweza kustahimili uchovu,
ucheleweshaji, na njaa - imani isiyoweza kuzimia japo ijaribiwe vikali kiasi gani. Muda wa majaribio
umetolewa kwa wote ili wapate kujiandaa kwa ajili ya wakati huo. Yakobo alishinda kwa sababu
alikuwa mwenye kuvumilia na mwenye nia thabiti. Ushindi wake ni ushahidi wa nguvu ya maombi
yasiyochoka. Wote watakaozishikilia ahadi za Mungu, kama alivyofanya, na kuwa na bidii na ustahimilivu
kama alivyokuwa, watafanikiwa kama alivyofanikiwa. Wale ambao hawapendi kukana nafsi zao, kuugua
mbele za Mungu, kuomba sana na kwa bidii kutaka baraka zake, hawatapata. Kushindana mwereka na
Mungu - ni wachache kiasi gani wanaojua maana yake! Ni wachache kiasi gani waliopata kuifungua
mioyo yao kwa Mungu wakiwa na hamu kubwa kiasi cha kuvuta nguvu zote hadi mwisho wa upeo wake!
Wakati mawimbi ya kukosa tumaini yasiyoelezeka kwa lugha yanaposukuma juu ya mwombaji, ni
wachache kiasi gani wanaong’ang’ania ahadi za Mungu kwa imani isiyochoka!
(622) Wale ambao wanatumia imani ndogo sasa, wako katika hatari kubwa sana ya kuanguka katika
uwezo wa madanganyo ya Shetani na chini ya amri ya kulazimisha dhamiri. Na hata kama watastahimili
jaribio hilo, watatumbukizwa katika dhiki na utungu mkubwa zaidi katika wakati wa taabu, kwa sababu
hawakujiweka katika hali ya kuwa na tabia ya kumtumaini Mungu. Mafundisho yale ya imani ambayo
wameyapuuza, watalazimika kujifunza wakiwa katika shinikizo la kutisha la kukata tamaa.
Yatupasa sasa kujifahamisha kuhusu Mungu kwa kuhakikisha ahadi zake. Malaika wanaweka katika
kumbukumbu kila ombi la dhati na la moyoni. Heri tuachane kujifurahisha binafsi kuliko kuacha kuwa
katika ushirika na Mungu. Umaskini uliopitiliza, kujinyima kwa hali ya juu sana, pamoja na kukubaliwa
naye, ni bora kuliko utajiri, heshima, raha, na urafiki na watu pasipo kukubaliwa naye. Lazima tutumie
muda kuomba. Kama tunaruhusu mawazo yetu kuvutwa na mahitaji ya kiulimwengu, Bwana aweza
kutupatia muda mzuri kwa kutuondolea sanamu za dhahabu yetu, sanamu za nyumba zetu, au sanamu
za mashamba yetu yenye rutuba.
Vijana wasingeshawishika kuingia dhambini kama wangekataa kuingia katika njia yoyote isipokuwa ile
ambayo kwayo wangeweza kuomba mbaraka wa Mungu. Ikiwa wajumbe wanaolipeleka onyo la mwisho
kwa ulimwengu wangeomba mbaraka wa Mungu katika hali isiyo ya ubaridi, uchovu, uvivu, bali kwa bidii

361
na kwa imani, kama vile alivyofanya Yakobo, wangepata mahali pengi ambapo wangeweza kusema:
“Nimeonana na Mungu uso kwa uso, na nafsi yangu imeokoka.” Mwanzo 32:30. Wangehesabiwa na
mbingu kama wana wa kifalme, wakiwa na nguvu ya kumshinda Mungu na kuwashinda wanadamu.
“Wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo,” inakaribia kufunguliwa juu yetu; na tutahitaji kuwa na
uzoefu ambao kwa sasa hatuna na wengi ni wavivu mno kiasi kwamba hawawezi kuupata. Mara nyingi ni
kawaida kwamba taabu inaonekana kubwa sana katika matarajio kuliko uhalisia; lakini jambo hilo si la
kweli kuhusu hatari iliyo mbele yetu. Maelezo yanayoeleweka wazi kuliko yote hayawezi kufikia ukubwa
wa uhalisia wa mateso hayo. Katika kipindi hicho cha kujaribiwa, lazima kila mtu asimame peke yake
mbele za Mungu. “Wajapokuwamo ndani yake Nuhu, na Danieli, na Ayubu, kama mimi niishivyo, asema
Bwana MUNGU, hawataokoa wana (623) wala binti; watajiokoa nafsi zao tu kwa haki yao.” Ezekieli
14:20.
Hivi sasa, wakati Kuhani Mkuu wetu anafanya upatanisho kwa ajili yetu, tungejitahidi sana kuwa
wakamilifu ndani ya Kristo. Hata kwa wazo tu Mwokozi wetu hakuweza kuletwa mahali pa kushindwa na
majaribu. Shetani hutafuta jambo fulani ndani ya mioyo ya wanadamu mahali anapoweza kupata pa
kuweka mguu wake, tamaa fulani ya dhambi inaendelezwa, kwa njia ambayo majaribu yanawekeza
nguvu yake. Lakini Kristo alisema kwa habari yake: “Kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala
hana kitu kwangu.” Yohana 14:30. Shetani hakuweza kupata kitu ndani ya Mwana wa Mungu ambacho
kingemwezesha kupata ushindi. Alikuwa amezishika amri za Baba yake, na ndani yake haikuonekana
dhambi yoyote ambayo Shetani angeweza kuitumia kwa manufaa yake. Hii ndiyo hali ambayo
wanapaswa kuwa nayo wale watakaosimama katika wakati ule wa taabu.
Ni katika maisha haya haya tuliyo nayo ambapo tunapaswa kuitenga dhambi mbali nasi, kwa njia ya
imani katika damu ya upatanisho ya Kristo. Mwokozo wetu wa thamani anatualika ili tupate
kuunganishwa naye, kuunganisha udhaifu wetu na nguvu zake, ujinga wetu na hekima yake, kutofaa
kwetu na wema wake. Maongozi ya Mungu ndiyo shule yetu ambapo ndani yake tunatakiwa kujifunza
upole na kujishusha kama Yesu. Daima Bwana anaweka mbele yetu malengo ya kweli ya maisha, si njia
ambayo tungependa kuchagua, ambayo inaonekana rahisi na ya kupendeza kwetu. Ni juu yetu kuamua
kushirikiana na njia hizo ambazo Mbingu inatumia katika kazi ya kuzifanya tabia zetu zifanane na mfano
wa Mungu. Hakuna wanaoweza kuipuuza au kuiacha kazi hiyo isipokuwa kwa hatari ya kuogofya sana ya
roho zao.
Mtume Yohana katika maono alisikia sauti kuu mbinguni ikisema: “Ole wa nchi na bahari! Kwa maana
yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.” Ufunuo
12:12. Matukio yanayohusu kutolewa kwa sauti hiyo kutoka mbinguni ni ya kuogofya mno. Ghadhabu ya
Shetani inazidi kuongezeka kadiri wakati wake unavyozidi kuwa mfupi, na kazi yake ya kudanganya na
kuangamiza itafikia kilele chake katika wakati wa taabu.
(624) Mwonekano wa kuogofya wa hali isiyo ya kawaida utaonekana muda si mrefu katika mbingu,
katika mwonekano wa uweza wa mapepo yafanyayo miujiza. Roho za mashetani zitatoka na kuwaendea
wafalme wa dunia na kwa ulimwenguni wote, ili kuwafunga katika madanganyo, na kuwashawishi
waungana na Shetani katika pambano lake lake la mwisho dhidi ya serikali ya mbinguni. Kwa njia hizi,
watawala na raia watadanganyika kwa hali moja. Watu watatokea wakijifanya kuwa Kristo mwenyewe,
na kudai heshima na kusujudiwa ambavyo ni ya Mkombozi wa ulimwengu. Watafanya miujiza ya ajabu
ya kuponya kisha watatangaza kuwa na mafunuo kutoka mbinguni ambayo yanapingana na ushuhuda wa
Maandiko.

362
Kama tendo lake la juu kabisa katika mfululizo wa matukio ya udanganyifu, Shetani mwenyewe
atajiweka katika mwonekano wa Kristo. Kwa muda mrefu kanisa limetangaza kwamba linatazamia
kumwona Mwokozi akija mara ya pili kuja kutimiliza matumaini yake. Sasa mwongo mkuu atafanya
ionekane kwamba Kristo amekuja. Katika sehemu tofauti za dunia, Shetani atajionyesha mwenyewe
miongoni mwa wanadamu kama kiumbe mwenye ukuu na utukufu mwenye mng’ao wa mwangaza,
akifanana na maelezo yaliyotolewa na Yohana kuhusu Mwana wa Mungu katika Ufunuo 1:13-15. Utukufu
unaomzunguka unazidi kitu chochote ambacho macho ya mwanadamu yamepata kuona. Kelele za
shangwe zinavuma angani: “Kristo amekuja! Kristo amekuja!” Watu wanaanguka kifudifudi mbele yake
na kumsujudia, wakati yeye anainua mikono yake juu na kutamka baraka kwao, kama Kristo
alivyowabariki wanafunzi wake alipokuwa hapa duniani. Sauti yake ni nyororo na tulivu, na tamu sana
iliyopangiliwa. Kwa sauti ya upole, yenye huruma, anazihubiri baadhi ya kweli za thamani za mbinguni
ambazo Mwokozi alizisema; anaponya magonjwa ya watu, halafu, katika tabia ya kuigiza ya Kristo,
anadai kwamba ameibadili Sabato kuwa Jumapili, na kuwaamuru wote kuitakasa siku hiyo ambayo
ameibariki. Anatangaza kwamba wale wanaoendelea kuitakasa siku ya saba wanalikufuru jina lake kwa
kukataa kuwasikiliza malaika zake waliotumwa kwao kuleta nuru na kweli. Huu ni udanganyifu wenye
nguvu, karibu mkubwa kuliko wote. Kama ilivyokuwa kwa wale Wasamaria ambao (625) walidanganywa
na Simoni mchawi, watu wengi, kuanzia aliye wa chini kuliko wote hadi aliye mkuu kuliko wote,
wanazingatia uchawi huu, wakisema: Huu ni “uweza mkuu wa Mungu.” Matendo 8:10.
Lakini watu wa Mungu hawatapotoshwa. Mafundisho ya kristo huyu wa uongo hayapatani na Maandiko.
Baraka yake inatamkwa juu ya wale wanaomsujudia mnyama na sanamu yake, kundi la watu wale wale
ambao Biblia inasema kwamba ghadhabu ya Mungu isiyochanganywa na maji itamwagwa juu yao.
Na, zaidi ya hayo, Shetani haruhusiwi kuigiza namna Kristo atakavyokuja mara ya pili. Mwokozi
amewaonya watu wake dhidi ya udanganyifu katika jambo hilI, tena ametabiri waziwazi jinsi kuja
kwake mara ya pili kutakavyokuwa. “Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo,
nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule…. Basi,
wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; Yumo nyumbani, msisadiki. Kwa maana kama vile umeme
utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa
Adamu.” Mathayo 24:24-27,31; 25:31; Ufunuo 1:7; 1 Wathesalonike 4:16, 17. Hakuna uwezekano
wowote wa kuigiza kuja huko. Kutajulikana ulimwenguni kote - kukishuhudiwa na ulimwengu wote.
Wale tu waliokuwa wanafunzi makini wa Maandiko na waliopokea hali ya kupenda ukweli ndio
watalindwa na nguvu ya madanganyo inayouteka ulimwengu. Kwa ushuhuda wa Biblia watu hawa
watamng’amua mdanganyaji huyo katika kujificha kwake. Wakati wa kujaribiwa utawajia watu wote.
Kwa kupepetwa kwa njia ya majaribu Mkristo wa kweli atadhihirika. Je, watu wa Mungu wa sasa
wamejiimarisha vyema juu ya neno lake kiasi kwamba hawawezi kusalimu amri katika maoni yao? Je,
katika wakati wa hatari kama huo, wangeweza kuing’ang’ania Biblia na Biblia peke yake? Shetani
atawazuia, ikiwezekana, wasiweze kujitayarisha kusimama katika siku ile. Atayapanga mambo kwa njia
ambayo itaifanya njia yao itingwe, atawashughulisha sana na utajiri wa dunia, atawafanya kubeba
mzigo mzito ulemeao, ili kwamba (626) mioyo yao ilemewe na masumbufu ya maisha haya na siku ya
kujaribiwa iweze kuwajia kama mwivi.
Wakati amri iliyotolewa na watawala mbalimbali wa ulimwengu wa Kikristo dhidi ya wale wanaozishika
amri itakapoondoa ulinzi wa serikali na kuwaacha mikononi mwa wale wanaotaka kuwaangamiza, watu
wa Mungu watakimbia kutoka katika miji na vijiji na kuungana pamoja makundi makundi, wakiishi
mahali pa ukiwa na upweke mno. Wengi watapata kimbilio katika ngome za milima. Kama wale
Wakristo wa mabonde ya Piedmont, watafanya mahali pa nchi palipoinuka kuwa maskani yao, na
363
watamshukuru Mungu kwa “majabali yatakuwa ngome yao.” Isaya 33:16. Lakini watu wengi kutoka
katika mataifa yote na matabaka yote, wenye hadhi ya juu na wale wa hali ya chini, matajiri na
maskini, weusi na weupe, watatupwa katika utumwa wa ukatili na kutokuwa na haki. Wapenzi wa
Mungu wako katika siku zinazowaacha wakiwa na uchovu, wakiwa wamefungwa minyororo, wakiwa
wamefungiwa ndani ya vyumba vya magereza, wakiwa wamehukumiwa kuuawa, wengine wakiwa
wameachwa wafe kwa njaa katika magereza ya chini ya ardhi yenye giza na kukera mno. Hakuna sikio
lolote la mwanadamu lililo tayari kusikia kilio chao cha maumivu; hakuna mkono wowote wa
mwanadamu ambao uko tayari kuwasaidia.
Je, Bwana atasahau watu wake katika saa hii ya kujaribiwa? Je, alimsahau Nuhu mwaminifu wakati
hukumu zake zilipopatilizwa juu ya ulimwengu wa kabla ya Gharika? Je, alimsahau Lutu wakati moto
uliposhuka kutoka mbinguni kuja kuiteketeza miji ile iliyokuwa katika tambarare? Je, alimsahau Yusufu
alipokuwa amezungukwa na waabudu sanamu wa Misri? Je, alimsahau Eliya wakati kiapo cha Yezebeli
kilipotishia maisha yake kwa sababu ya hatima ya manabii wa Baali? Je, alimsahau Yeremia katika shimo
lile la giza na la kukatisha tamaa la nyumba yake ya kifungo? Je, aliwasahau wale vijana wema watatu
katika tanuru la moto? au Danieli katika tundu la simba?
“Bali Sayuni alisema, YEHOVA ameniacha, Bwana amenisahau. Je! mwanamke aweza kumsahau mtoto
wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi
sitakusahau wewe. Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu.” Isaya 49:14-16. Bwana wa
majeshi amesema: “Maana yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho lake.” Zekaria 2:8. (627)
Ingawa maadui wanaweza kuwatupa gerezani, bado kuta za gereza la chini ya ardhi haziwezi kukata
mawasiliano kati ya roho zao na Kristo. Yeye aonaye kila udhaifu walio nao, alijuaye kila jaribu, yu juu
ya mamlaka zote za dunia; na malaika watawajia katika vyumba vile vya upweke, wakileta nuru na
amani kutoka mbinguni. Gereza litakuwa kama jumba la kifalme; kwa maana walio matajiri wa imani
wanaishi pale, na kuta zile za giza zitaangazwa kwa nuru ya mbinguni kama vile ilivyokuwa wakati Paulo
na Sila walipokuwa wakiomba na kuimba nyimbo za sifa usiku wa manane katika gereza la chini ya ardhi
kule Filipi.
Hukumu za Mungu zitapatilizwa juu ya wale wanaotafuta kuwatesa na kuwaangamiza watu wake.
Uvumilivu wake wa muda mrefu dhidi ya waovu unawatia nguvu wanadamu kuendelea na dhambi zao,
lakini adhabu yao, hata hivyo, ni ya hakika na ya kutisha kwa sababu imecheleweshwa sana. “Maana
BWANA ataondoka kama vile katika mlima Perasimu, ataghadhabika kama vile katika bonde la Gibeoni;
apate kufanya kazi yake, kazi yake ya ajabu.” Isaya 38:21. Kwa Mungu wetu mwenye rehema tendo la
kuadhibu ni tendo geni kwake. “Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu
mwovu.” Ezekieli 33:11. Bwana ni “mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi
wa rehema na kweli;… mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi.” Lakini yeye hata“mhesabia mtu
mwovu kuwa hana hatia kamwe.” “Bwana si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia
mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe.” Kutoka 34:6,7; Nahumu 1:3. Kwa mambo ya kutisha katika haki
ataithibitisha mamlaka ya sheria yake iliyokanyagwa. Ukali wa kisasi kinachomngojea mtu aliyeasi
unaweza kufahamika kwa kuangalia jinsi Bwana anavyosita kutekeleza haki. Taifa lile analolivumilia
kwa muda mrefu, na ambalo hatalipiga mpaka limekijaza kikombe chake cha maovu katika hesabu ya
Mungu, hatimaye litakinywea kikombe cha ghadhabu yake kisichochanganywa na huruma.
Wakati Kristo atakapokoma kufanya kazi yake ya maombezi katika patakatifu, ndipo itamwagwa
ghadhabu isiyochanganywa iliyowekwa dhidi ya wale wote wanaomsujudu yule mnyama na sanamu yake
na kuipokea chapa yake (Ufunuo 14:9,10). Mapigo yale yaliyoanguka juu ya Misri wakati Mungu

364
alipokuwa anakaribia kuwaokoa Israeli yanafanana na zile (628) hukumu za kutisha na pana zaidi
ambazo zitaanguka juu ya ulimwengu punde tu kabla ya wokovu wa mwisho wa watu wa Mungu.
Mwandishi wa Ufunuo anasema, akiyaelezea mapigo yale ya kuogofya: “Pakawa na jipu baya, bovu, juu
ya wale watu wenye chapa ya huyo mnyama, na wale wenye kuisujudia sanamu yake.” Bahari “ikawa
damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.” Na “mito na
chemchemi za maji; zikawa damu.” Japo ni ya kutisha mapigo hayo, kama jinsi yalivyo, haki ya Mungu
inathibitishwa kikamilifu. Malaika wa Bwana anatangaza, akisema: “Wewe u mwenye haki,… kwa kuwa
umehukumu hivi; kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu
wainywe; nao wamestahili.” Ufunuo 16:2-6. Kwa kuwakumu watu wa Mungu kufa, hakika wamejipatia
hatia ya damu yao kana kwamba ilikuwa imemwagwa kwa mikono yao. Kwa namna kama hiyo, Kristo
aliwatangazia Wayahudi wa siku zake kwamba walikuwa na hatia ya damu yote ya watakatifu iliyokuwa
imemwagwa tangu siku za Habili; kwa kuwa walikuwa na roho ile ile na walitafuta kufanya yale yale
kama ya wauaji wa manabii.
Katika pigo linalofuata, jua linapewa uwezo ili lipate “kuwaunguza wanadamu kwa moto. Wanadamu
wakaunguzwa maunguzo makubwa.” Fungu la 8 na la 9. Hivi ndivyo manabii wanavyoeleza hali ya dunia
katika wakati huo wa kuogofya sana: “Nchi inaomboleza; maana nafaka imeharibika,… miti yote ya
mashamba imekauka; maana furaha imekauka katika wanadamu.” “Mbegu zinaoza chini ya udongo
wake; ghala zimeachwa ukiwa;… Jinsi wanyama wanavyougua! makundi ya ng’ombe yamefadhaika, kwa
sababu hawana malisho;… Vijito vya maji vimekauka, na moto umeyateketeza malisho ya nyikani.”
“Tena nyimbo za hekaluni zitakuwa vilio siku ile, asema Bwana MUNGU; mizoga itakuwa mingi; kila
mahali wataitupa, wakinyamaza kimya.” Yoeli 1:10-12,17-20; Amosi 8:3.
Mapigo hayo hayaji mahali pote, la wakazi wa dunia wangekatiliwa mbali kabisa. Hata hivyo, yatakuwa
mapigo ya (629) kuumiza mno kiasi ambacho hakipata kujulikana kwa wanadamu. Hukumu zote
zilizowajilia wanadamu, kabla ya kufungwa kwa mlango wa rehema, zimekuwa zimechanganywa na
rehema. Damu ya Kristo inayosihi imemkinga mwenye dhambi asipate kipimo kamili cha hatia yake;
lakini katika hukumu ya mwisho, ghadhabu inamiminwa pasipo kuchanganywa na rehema.
Katika siku ile, watu wengi watatamani kupata kinga ya rehema ya Mungu ambayo kwa muda mrefu
wameidharau. “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa
ya kukosa chakula wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya BWANA. Nao watatanga-
tanga toka bahari hata bahari; na toka upande wa kaskazi hata upande wa mashariki; watapiga mbio,
wakienda huko na huko, kulitafuta neno la BWANA, wasilione.” Amosi 8:11,12.
Watu wa Mungu hawatakuwa huru na maumivu; lakini wakiwa wanateswa na kupata dhiki, wakiwa
wanastahimili umaskini na kuteseka kwa kukosa chakula, hawataachwa waangamie. Mungu yule
aliyemtunza Eliya hatampita mmojawapo wa watoto wake aliyejitoa. Yeye azihesabuye hata nywele za
kichwa chao atawatunza, na wakati wa njaa watashibishwa. Wakati waovu wanakufa kwa njaa na tauni,
malaika watawalinda wenye haki na kuwapatia mahitaji yao. Kwake yeye “aendaye kwa haki” ahadi
imetolewa: “Atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma.” “Maskini na wahitaji wanatafuta maji,
wala hapana; ndimi zao zimekauka kwa kiu, mimi BWANA, nitawasikia, mimi, Mungu wa Israeli,
sitawaacha.” Isaya 33;15,16; 41:17.
Ingawa “mtini hautachanua maua, wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; taabu ya mzeituni itakuwa
bure, na mashamba hayatatoa chakula; zizini hamtakuwa na kundi, wala vibandani hamtakuwa na kundi
la ng’ombe;” hata hivyo, wale wamchao watamfurahia BWANA, nao watamshangilia Mungu wa wokovu
wao. Habakuki 3:17,18.

365
“BWANA ndiye mlinzi wako; BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume. Jua halitakupiga mchana, wala
mwezi wakati wa usiku. BWANA atakulinda na mabaya yote, (630) atakulinda nafsi yako.” “Maana Yeye
atakuokoa na mtego wa mwindaji, na katika tauni iharibuyo. Kwa manyoya yake atakufunika, chini ya
mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao Hutaogopa hofu ya usiku, wala mshale
urukao mchana, wala tauni ipitayo gizani, wala uwele uharibuo adhuhuri, Ijapo watu elfu waanguka
ubavuni pako, naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe. Ila kwa macho
yako utatazama, na kuyaona malipo ya wasio haki. Kwa kuwa Wewe BWANA ndiwe kimbilio langu;
Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako. Mabaya hayatakupata wewe, wala tauni haitaikaribia hema
yako.” Zaburi 121:5-7; 91:3-10.
Lakini kwa macho ya kibinadamu itaonekana kama lazima watu wa Mungu watie muhuri ushuhuda wao
kwa damu yao kama walivyofanya wafia-dini kabla yao. Wao wenyewe wanaanza kuogopa kwamba
Bwana amewaacha ili wapate kuanguka kwa mkono wa adui zao. Ni wakati wa utungu wa kuogofya.
Mchana na usiku wanamlilia Mungu ili awaokoe. Waovu wanashangilia, na makelele ya kuzomea
yanasikika: “Imani yenu i wapi sasa? Mbona Mungu hawaokoi na mikono yetu ikiwa kweli ninyi ni watu
wake?” Lakini wale wanaongojea wanamkumbuka Yesu alipokuwa akifa kwenye msalaba wa Kalvari na
wakuu wa makuhani na watawala walivyopiga makelele kwa dhihaka: “Aliokoa wengine, hawezi
kujiokoa mwenyewe. Kama yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini.”
Mathayo 27:42. Kama Yakobo, wote wanashindana na Mungu. Nyuso zao zinaonyesha pambano lililo
ndani yao. Uso wa kila mmoja umebadilika rangi. Lakini hawaachi kutoa dua kwa bidii.
Laiti kama wanadamu wangeweza kuona kwa muono wa mbinguni, wangeweza kuyaona makundi kwa
makundi ya malaika walio hodari sana wakifanya kituo kuwazunguka wale waliolitunza neno la subira
yake Kristo. Kwa upole uliojaa huruma, malaika wameshuhudia dhiki yao na kuyasikia maombi yao.
Wanangoja amri ya Kamanda wao ili wawanyakue kutoka katika hatari inayowakabili. Lakini hawana
budi kusubiri kitambo kidogo zaidi. Lazima watu wa Mungu wakinywee (631) kikombe kile na kubatizwa
kwa ubatizo ule. Kule kuchelewa kule, kunakowaumiza sana, ndilo jibu bora la dua zao. Kadiri
wanavyojitahidi kungoja kwa imani ili Bwana apate kufanya kazi yake, wanaongozwa kutumia imani,
tumaini, na saburi, mambo ambayo wameyatumia kwa kiwango kidogo mno katika uzoefu wao wa dini.
Lakini kwa ajili ya hao wateule wakati wa taabu utafupishwa. “Na Mungu, je! hatawapatia haki wateule
wake wanaomlilia mchana na usiku?… Nawaambia, atawapatia haki upesi.” Luka 18:7,8. Mwisho utakuja
kwa haraka sana kuliko vile watu wanavyotarajia. Ngano itakusanywa na kufungwa katika matita tayari
kuwekwa katika ghala ya Mungu; magugu yatafungwa matita-matita kwa ajili ya moto uharibuo.
Walinzi wale wa kimbingu, walio waaminifu, wanaendelea kukesha. Ingawa amri ya jumla imeweka
muda maalum ambapo wale wazishikao amri watauawa, adui zao katika mazingira fulani watatarajia
amri hiyo, na kabla ya muda uliowekwa, watataka kuwaua. Lakini hakuna awezaye kuwapita walinzi
wale hodari waliofanya kituo kumzunguka kila mtu aliye mwaminifu. Wengine wanashambuliwa katika
kukimbia kwao toka mijini na vijijini; lakini mapanga yaliyoinuliwa ili kuwakata yatavunjika na
kuanguka chini yakiwa hayana nguvu kama vile nyasi. Wengine wanalindwa na malaika wakiwa katika
maumbile ya watu wa vita.
Katika vizazi vyote, Mungu amewatumia malaika zake watakatifu kuwasaidia na kuwaokoa watu wake.
Viumbe hao wa mbinguni wamekuwa na sehemu ya utendaji katika mambo ya wanadamu.
Wameonekana wakiwa wamevaa mavazi yaliyong’aa kama umeme; wamekuja kama wanadamu katika
mwonekano wa wasafiri. Malaika wametokea kwa watu wa Mungu wakiwa katika umbile la mwanadamu.
Wamepumzika chini ya mialoni kama waliochoka wakati wa adhuhuri. Wamekubali ukarimu waliopewa
katika nyumba za watu. Wamefanya kazi ya kuwaongoza njiani wasafiri waliokutwa na usiku. Kwa
366
mikono yao wenyewe, wamewasha moto katika madhabahu. Wamefungua milango ya gereza na
kuwaweka huru watumishi wa Bwana. Wakiwa wamevaa utukufu wa mbinguni, walikuja na kulivingirisha
jiwe kutoka katika kaburi la Mwokozi.
Wakiwa katika umbo la wanadamu, mara kwa mara malaika wanakuwa katika mikutano ya (632) wenye
haki; na wanaitembelea mikutano ya waovu, kama vile walivyokwenda Sodoma, ili kuandika
kumbukumbu ya matendo, kuona kama wamevuka mpaka wa uvumilivu wa Mungu. Mungu anavutwa na
huruma; na kwa ajili ya wachache ambao wanamtumikia kweli kweli, anazuia misiba na kurefusha hali
ya utulivu miongoni mwa watu wengi. Wale wanaotenda dhambi dhidi ya Mungu hutambua kidogo mno
kwamba wanawiwa uhai walio nao kwa wale wachache ambao wao wanafurahia kuwadhihaki na
kuwatesa.
Ingawa watawala wa dunia hii hawajui, lakini katika mabaraza yao malaika wamekuwa wasemaji mara
kwa mara. Macho ya wanadamu yamewatazama; masikio ya wanadamu yamesikia wito wao; midomo ya
wanadamu imeyapinga mapendekezo yao na kudhihaki mashauri yao; mikono ya wanadamu
imekabiliana kwa kuwafedhehesha na kuwadhalilisha. Katika ukumbi wa baraza na mahakama ya kutoa
wajumbe hao wa mbinguni wameonyesha uelewa mkubwa wa historia ya mwanadamu; wamejionyesha
wenyewe kuwa wanao uwezo bora wa kutetea hoja ya wale wanaoonewa kuliko walivyo mawakili wao
walio na uwezo mkubwa kuliko wote. Wameyashinda makusudi mabaya na kuyazuia maovu ambayo
yangeweza kuichelewesha sana kazi ya Mungu na kusababisha maumivu makubwa kwa watu wake.
Katika saa ya hatari kubwa na adha “Malaika wa BWANA hufanya kituo, akiwazungukia wamchao na
kuwaokoa.” Zaburi 34:7.
Kwa subira kubwa, watu wa Mungu wanazingojea dalili za Mfalme wao anayekuja. Walinzi
wanaposalimiwa kwa kuulizwa, “Habari gani za usiku?” jibu linatolewa bila kusita, “Mchana unakuja na
usiku pia.” Isaya 21:11,12. Nuru inamulika mawinguni juu ya vilele vya milima. Punde utukufu wake
utadhihirika. Jua la Haki karibu litaangaza. Asubuhi na usiku vi karibu - mwanzo wa mchana usio na
mwisho kwa wenye haki, na kuja kwa usiku wa milele kwa waovu.”
Kadiri wale wanaoshindana mwereka wanavyosihi mbele za Mungu, pazia lile linalowatenganisha na yale
yasiyoonekana linaonekana kama limeondolewa. Mbingu zinaangazwa na kupambazuka kwa siku ya
milele, na kama sauti tamu nyimbo za malaika maneno haya yanadondoka (633) sikioni: “Simameni
imara katika utii wenu. Msaada uko njiani.” Kristo, Mshindi hodari, anawaonyesha taji ya utukufu wa
milele askari wake waliochoka; na sauti yake inatoka katika milango iliyoachwa wazi, ikisema:
“Tazama, mimi ni pamoja nanyi. Msiogope. Nazijua huzuni zenu zote; nimebeba huzuni zenu.
Hampigani vita dhidi ya adui ambao hawajapata kupimwa. Nimepigana vita hiyo kwa niaba yenu, na
katika jina langu ninyi ni zaidi ya washindi.”
Mwokozi wa thamani atatuma msaada wakati tunapouhitaji. Njia ya kwenda mbinguni imewekwa wakfu
kwa nyayo zake. Kila mwiba unaochoma nyayo zetu umekwisha kuzichoma nyayo zake. Kila msalaba
tunaoagizwa kubeba yeye ameubeba kabla yetu. Bwana anaruhusu mapambano ili kuutayarisha moyo
kwa ajili ya amani. Wakati wa taabu ni uzoefu mgumu kwa watu wa Mungu; lakini ni wakati wa kila
muumini wa kweli kutazama juu, na kwa imani anaweza kuuona upinde wa mvua wa ahadi
ukimzungushia duara.
“Nao waliokombolewa na BWANA watarejea, watafika Sayuni, wakiimba; furaha ya milele itakuwa juu
ya vichwa vyao; watapata shangwe na furaha; huzuni na kuugua zitakimbia. Mimi, naam, mimi, ndimi
niwafarijiye; wewe u nani hata ukamwogopa mtu atakayekufa, na mwanadamu atakayefanywa kuwa
kama majani? Ukamsahau BWANA, Muumba wako,… nawe unaogopa daima mchana kutwa kwa sababu ya
367
ghadhabu yake aoneaye, hapo afanyapo tayari kuharibu; nayo i wapi ghadhabu yake aoneaye? Yeye
aliyehamishwa na kufungwa atafunguliwa kwa haraka; wala hatakufa na kushuka shimoni wala chakula
chake hakitapunguka. Maana mimi ni BWANA, Mungu wako, niichafuaye bahari, mawimbi yake
yakavuma. BWANA wa majeshi ndilo jina lake. Nami nimetia maneno yangu kinywani mwako, nami
nimekusitiri katika kivuli cha mkono wangu.” Isaya 51:11-16.
“Basi, kwa sababu ya hayo, ulisikilize neno hili, ewe uliyeteswa, na kulewa, lakini si kwa mvinyo;
BWANA, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi
mwako kikombe cha kulevya-levya, hilo bakuli la kikombe cha hasira yangu; hutakinywea tena; nami
nitakitia mikononi mwao wakutesao; waliokuambia (634) nafsi yako, Inama, tupate kupita; nawe
uliufanya mgongo wako kuwa kama nchi, na kama njia, kwa hao wapitao juu yake.” Mafungu ya 21-23.
Glorious will be the deliverance of those who have patiently waited for His coming and whose names
are written in the book of life.
Jicho la Mungu, likiangalia kupitia katika vizazi vingi, lilikazwa juu ya hatari kubwa ambayo watu wake
watapaswa kukabiliana nayo, wakati ule mataifa yatakapojipanga dhidi yao. Kama mfungwa aliye
uhamishoni, watakuwa katika hali ya kuogopa kufa kwa njaa au kwa kuuawa kikatili. Lakini Yeye Aliye
Mtakatifu aliyeigawa Bahari ya Shamu mbele ya Israeli, ataonyesha uweza wake mkuu na kuwaweka
huru. “Nao watakuwa wangu, asema BWANA wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa
hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe
amtumikiaye.” Malaki 3:17. Kama damu ya mashahidi wa Kristo hao waaminifu ingemwagwa wakati huu,
isingeweza kuwa mbegu iliyopandwa itakayotoa mavuno kwa ajili ya Mungu, kama ilivyokuwa ile damu
ya wafia-dini. Msimamo thabiti usingekuwa ushuhuda ambao ungeweza kuwavuta wengine kuiamini ile
kweli; maana moyo ulio mkaidi umeyarudisha nyuma mawimbi ya rehema mpaka hayaji tena kwake.
Kama wenye haki wangeachwa sasa kuwa mateka wa maadui zao, ungekuwa ushindi mkubwa kwa yule
mkuu wa giza. Mtunga Zaburi anasemai: “Mradi atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya, atanisitiri
katika sitara [maficho] ya hema yake.” Zaburi 27:5. Kristo amesema: “Njoni watu wangu, ingia wewe
ndani ya vyumba vyako, ukafunge mlango nyuma yako ujifiche kitambo kidogo, mpaka ghadhabu hii
itakapopita. Kwa maana, tazama, BWANA anakuja, kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani,
kwa sababu ya uovu wao.” Isaya 26:20,21. Ukombozi na utukufu vitakuwa kwa wale ambao
wamekungojea kuja kwake kwa saburi na ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima.

368
Sura ya 40
WATU WA MUNGU WAOKOLEWA

Wakati ulinzi wa sheria za wanadamu utakapoondolewa kwa wale wanaoiheshimu sheria ya Mungu,
kutakuwa na harakati za kuwaangamiza ambazo zitatekelezwa kwa wakati huo huo katika maeneo
mbalimbali. Kadiri muda uliowekwa katika amri itakayotolewa utakavyokuwa unakaribia, watu
watafanya njama za kung’oa kabisa kundi la dini linalochukiwa. Itapangwa kwamba kipigo
kilichoamuliwa kitolewe katika usiku mmoja, ambacho kitainyamazisha kabisa sauti ya wapingaji na
wakosoaji hao.
Watu wa Mungu - wengine wakiwa katika vyumba vya magerezani, wengine wakiwa wamejificha katika
mahali upweke katika misitu na milima – lakini bado wakiendelea kumlilia Mungu wakiomba ulinzi wake,
wakati katika kila mtaa makundi ya watu wenye silaha, wakisukumwa na majeshi ya malaika waovu,
wanajiandaa kufanya kazi yao kuleta vifo. Ni katika wakati huu, katika saa ya hatari kabisa, ambapo
Mungu wa Israeli wa Israeli ataingilia kati kwa ajili ya wokovu wa wateule wake. Asema Bwana;
“Mtakuwa na wimbo kama vile wakati wa usiku, ishikwapo sikukuu takatifu, mtakuwa na furaha ya moyo
kama vile mtu aendapo … katika mlima wa BWANA, aliye Mwamba wa Israeli. Naye BWANA
atawasikizisha watu sauti yake ya utukufu, naye atawaonyesha jinsi mkono wake ushukavyo, na
ghadhabu ya hasira yake, na mwako wa moto ulao, pamoja na dhoruba, na tufani, na mvua ya mawe ya
barafu.” Isaya 30:29,30.
Kwa kelele za ushindi, dhihaka, na kulaani, msongamano wa watu waovu uko tayari kurukia mawindo
yao, wakati ambapo, lo, (636) giza zito, nene kuliko giza la usiku, linaifunika dunia. Kisha upinde wa
mvua, uking’aa kwa utukufu utokao kwenye kiti cha enzi cha Mungu, unatanda mbinguni, na
unaonekana kuzunguka kila kundi linaloomba. Ghafla wale watu wengi wenye hasira wanazuiwa.
Makelele yao ya dhihaka yanapotelea mbali. Wahanga wa ghadhabu yao ya mauaji wanasahauliwa. Kwa
hofu ya kinachoenda kutokea wanaiangalia ile ishara ya agano la Mungu na kutafuta kusitiriwa kutokana
na mng’ao ule mkali unaowashinda nguvu.
Kwa watu wa Mungu sauti iliyo wazi na tamu inasikika, ikisema, “Tazameni juu,” nao wakiinua macho
yao mbinguni, wanauona ule upinde wa mvua wa ahadi. Mawingu meusi, yenye ghadhabu, yaliyofunika
anga yanatawanyika, kama Stefano wanakaza macho juu mbinguni na kuuona utukufu wa Mungu na
Mwana wa Adamu akiwa ameketi katika kiti chake cha enzi. Katika umbile lake la kiungu,
wanazitambua alama za kudhalilishwa kwake; na kutoka katika midomo yake wanasikia ombi likitolewa
mbele za Baba yake na malaika zake watakatifu, akisema: “Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja
nami po pote nilipo.” Yohana 17:24. Na tena sauti, ya muziki na ya ushindi, inasikika ikisema: “Hao
wanakuja! Hao wanakuja! Ni watakatifu, hawana madhara yo yote, wala hawajanajisiwa. Wamelitunza
neno la subira yangu; watatembea miongoni mwa malaika;” na midomo ile iliyogeuka rangi, yenye
mitetemo, ya wale walioishikilia imani yao, inapiga kelele ya ushindi.
Ni wakati wa usiku wa manane ambapo Mungu anaonyesha uweza wake katika kuwaokoa watu wake.
Jua linatoka, likiwaka kwa nguvu yake yote. Ishara na maajabu vinafuata kwa mfuatano wa haraka.
Waovu wanaangalia mandhari hii kwa hofu kuu na mshangao mkubwa, wakati wenye haki wanaziangalia
kwa furaha kuu ishara za ukombozi wao. Kila kitu katika maumbile ya asili kinaonekana kugeuka kutoka
katika njia yake ya kawaida. Mito inakoma kutitirika. Mawingu meusi mazito yanatokea na kugongana.

369
Katikati ya anga hilo lililoghadhabika kuna nafasi moja wazi yenye utukufu usioelezeka, ambamo
kunatokea sauti ya Mungu kama sauti ya maji mengi, ikisema: “Imekwisha kuwa.” Ufunuo 16:17.
Sauti ile inazitikisa mbingu na dunia. Kuna (637) tetemeko kubwa la nchi, “ambalo tangu wanadamu
kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo.” Mafungu ya 17 na 18.
Anga linaonekana kana kwamba linafunguka na kujifunga. Utukufu kutoka katika kiti cha enzi cha Mungu
unaonekana kumulika kupitia katika anga hilo. Milima inatikisika kama unyasi katika upepo, na miamba
iliyopasuka inatawanyika kila upande. Kuna ngurumo kama ya tufani inayokuja. Bahari inachafuka na
kupiga huko na huko. Inasikika sauti kubwa ya kimbunga kama sauti ya mapepo yanayokwenda
kuangamiza. Dunia yote inainuka na kupanda kama mawimbi ya bahari. Uso wa dunia unavunjika-
vunjika. Misingi yenyewe ya dunia inaonekana kana kwamba inavunjika. Safu za milima zinazama.
Visiwa vilivyokaliwa na watu vinatoweka. Bandari ambazo zimekuwa kama Sodoma kwa uovu zinazama
katika maji yenye hasira. Babeli ule Mkuu umekumbukwa mbele za Mungu, “kupewa kikombe cha
mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.” Mvua ya mawe makubwa, kila moja “likiwa na uzito kama wa
talanta,” yanafanya kazi yake ya uharibifu. Mafungu ya 19 na 21. Miji ya dunia yenye kiburi mno
inashushwa chini. Majumba ya kifalme, ambayo kwayo wakuu wametapanya mali zao nyingi ili
kujitukuza wenyewe, yanaporomoka na kuwa magofu mbele ya macho yao. Kuta za magereza
zinapasuka vipande vipande, na watu wa Mungu, waliokuwa wameshikiliwa humo kama wafungwa kwa
ajili ya imani yao, wanawekwa huru.
Makaburi yanafunguka, na “wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate
uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.” Danieli 12:2. Wale wote waliokufa wakiwa
katika imani ya ujumbe wa malaika wa tatu wanatoka kaburini wakiwa na utukufu, kuja kusikia agano la
Mungu la amani analofanya na wale walioishika sheria yake. “Na hao waliomchoma” (Ufunuo 1:7), wale
waliodhihaki na kudharau maumivu ya kifo cha Kristo, na wapinzani wakubwa mno wenye ukatili dhidi
ya kweli yake na watu wake, wanafufuliwa ili wapate kumwona katika utukufu wake na kuiona heshima
wanayopewa waaminifu na watiifu.
Mawingu manene bado yanalifunika anga; lakini wakati fulani fulani jua linaonekana, likiwa na
mwonekano kama wa jicho la kuadhibu la Yehova. (638 Umeme mkali wa radi unaruka kutoka
mbinguni, ukiifunika dunia kwa tabaka la mwali wake. Juu ya ngurumo ya radi ya kuogofya, sauti, za
ajabu na za kuogofya, zinatangaza hukumu ya waovu. Maneno yanayosemwa hayaeleweki kwa wote; ila
yanaeleweka wazi zaidi kwa wale walimu wa uongo tu. Wale ambao kitambo kidogo tu kilichopita
walikuwa hawajali kabisa, walikuwa wanajidai na kujigamba katika upotofu, ambao walikuwa
wanajitukuza katika ukatili wao dhidi ya watu wazishikao amri za Mungu, sasa wametekewa na
kushangazwa katika hofu. Mayowe yao yanasikika ziadi kuliko makelele ya matukio yanayotokea.
Mapepo yanakiri uungu wa Kristo na kutetemeka mbele ya uweza wake, wakati huo wanadamu
wanaomba rehema yake na wakionyesha unyenyekevu wa uongo kwa sababu ya hofu.
Manabii wa zamani walisema walipoiona siku ya Mungu katika maono: “Pigeni kelele za hofu; maana
siku ya BWANA i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu.” Isaya 13:6. “Ingia
ndani ya jabali; ukajifiche mavumbini mbele za utisho wa BWANA, mbele ya utukufu wa enzi yake.
Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, kiburi cha mwanadamu kitainamishwa.” “Siku
hiyo kila mtu atazitupilia mbali sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu, walizojifanyia ili
kuziabudu, kwa fuko na popo; ili aingie ndani ya pango za majabali, na ndani ya tundu za miamba
iliyopasuka, mbele za utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno
dunia.” Isaya 2:10-12,20,21.

370
Kupitia katika nafasi iliyo wazi katika mawingu kunaonekana nyota ambayo mng’ao wake unaongezeka
hadi mara nne ukilinganisha na giza lililopo. Inasema maneno yenye matumaini na furaha kwa
waaminifu, lakini inasema mambo ya ukali na ghadhabu kwa wale wavunja sheria ya Mungu. Wale
waliojikana kwa kuacha vyote kwa ajili ya Kristo wako salama sasa, wakiwa wamefichwa kama mahali
pa siri ndani ya Bwana. Wamepimwa, na mbele ya ulimwengu na mbele ya wale wanaodharau ukweli
wameudhihirisha msimamo wao kwake yeye (639) aliyewafia. Badiliko la ajabu limekuja kwa wale
waliokuwa wameushikilia uaminifu wao katika kukabiliana ana kwa ana na kifo. Ghafla wameokolewa
kutoka katika ukatili wa giza na wa kutisha wa watu waliogeuka kuwa mapepo. Nyuso zao, ambazo
muda mfupi zilikuwa zimegeuka rangi, na kuwa na wasiwasi, na kudhoofika, sasa zinang’aa kwa
mshangao, imani, na upendo. Wanazipaza sauti zao katika wimbo huu wa ushindi: “Mungu kwetu sisi ni
kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika
nchi, ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, ijapopepesuka
milima kwa kiburi chake.” Zaburi 46:1-3.
Wakati maneno haya ya tumaini takatifu yanapanda juu kwenda kwa Mungu, mawingu yanarudi nyuma,
kisha anga lenye nyota linaonekana, likiwa tukufu kuliko inavyoweza kuelezwa ikilinganishwa na lile
anga jeusi lenye ghadhabu, linaloonekana katika pande mbili nyingine za anga. Utukufu wa mji ule wa
mbinguni unatoka kama mkondo katika malango yaliyoachwa wazi. halafu unaonekana mkono angani
ukiwa umezishika mbao mbili za mawe ambazo zimekunjwa pamoja. Nabii anasema: “Na mbingu
zitatangaza haki yake, kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu.” Zaburi 50:6. Sheria ile takatifu, haki ya
Mungu, ile iliyotangazwa katikati ya ngurumo na moto kutokea Sinai kama mwongozo wa maisha yetu,
sasa inaonyeshwa kwa wanadamu kama kipimo kinachotumika katika hukumu. Ule mkono unazifungua
mbao zile, kisha zinaonekana kanuni za Amri Kumi, zikiwa zimeandikwa kama kwa kalamu ya moto.
Maneno yale yako wazi kiasi kwamba watu wote wanaweza kuyasoma. Kumbukumbu inaamshwa, giza la
upotofu na uzushi linafagiliwa kutoka katika akili ya kila mtu, na maneno yale kumi ya Mungu, mafupi,
yanayoeleweka, na yenye mamlaka, yanaonyeshwa kwa wakazi wote wa dunia.
Haiwezekani kuieleza hofu kuu na kukosa tumaini kutakakowapata wale waliozikanyaga amri takatifu za
Mungu. Bwana aliwapa sheria yake; wangepaswa wawe wamelinganisha tabia zao na sheria hiyo na
kuzijua kasoro zao wakati ule ilipokuwapo bado nafasi ya kutubu na kufanya matengenezo; lakini ili
kujipatia kupendwa na ulimwengu, waliziweka kando amri zile na kuwafundisha wengine kuzikiuka.
Wamejitahidi sana kuwalazimisha (640) watu wa Mungu kuidharau Sabato yake. Sasa wanahukumiwa na
sheria ile ambayo wameidharau. Kwa utambuzi maalum wa kuogofya wanaona kwamba hawana udhuru.
Walichagua yule ambaye wangemtumikia na kumwabudu. “Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati
ya wenye haki, na waovu, na kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.” Malaki 3:18.
Maadui wa sheria ya Mungu, kuanzia kwa viongozi wa kiroho kushuka chini mpaka kwa yule aliye mdogo
kabisa miongoni mwao, wana mawazo mapya juu ya ile kweli na wajibu wao. Wakiwa wamechelewa
wanagundua kwamba Sabato ya amri ya nne, ndiyo Muhuri wa Mungu aliye hai. Wakiwa wamechelewa
wanaiona tabia halisi ya sabato yao ya uongo na msingi wa mchanga mahali ambapo wamekuwa
wakijenga. Wanagundua kwamba wamekuwa wakipigana dhidi ya Mungu. Walimu wa kidini wameongoza
watu kwenda kwenye uharibifu huku wakidai kuwaongoza kwenda katika malango ya Paradiso. Mpaka
siku ile ya kutoa hesabu ndipo itajulikana kwamba wale walio katika ofisi takatifu wanawajibika kwa
ukubwa kiasi gani, na kwamba matokeo ya wao kukosa uaminifu yanatisha kiasi gani. Ni katika umilele
tu ndipo tunapoweza kukadiria kwa usahihi hasara ya kupotea kwa nafsi hata moja. Ya kuogofya ni
hukumu atakayopata yeye atakayeambiwa na Mungu kwamba: Ondoka kwangu, ewe mtumishi mwovu.

371
Sauti ya Mungu inasikika kutoka mbinguni, ikitangaza siku na saa ya kuja kwa Yesu, na kuwapatia watu
wake agano lake la milele. Kama ngurumo ya radi kali sana maneno yake yanavuma katika dunia yote.
Israeli wa Mungu wanasimama na kusikiliza, macho yao yakiwa yamekazwa juu. Nyuso zao zinaangazwa
kwa utukufu wake, na zinang’aa kama ulivyong’aa uso wa Musa aliposhuka kutoka Sinai. Waovu
hawawezi kuwatazama. Na wakati mbaraka ule unapotamkwa kwa wale ambao wamemheshimu Mungu
kwa kuitakasa Sabato yake, kunakuwa na kelele kuu ya ushindi.
Punde kunaonekana upande wa mashariki wingu dogo jeusi, kama nusu ya kiganja cha mkono wa mtu.
Ni wingu linalomzunguka Mwokozi na ambalo kwa mbali linaonekana kama limefunikwa katika giza.
Watu wa Mungu wanaijua hii kuwa ishara ya Mwana wa Adamu. Kwa ukimya wa kicho wanalikazia macho
linapozidi (641) kuikaribia dunia zaidi na zaidi, likizidi kuwa jepesi na tukufu zaidi, mpaka linakuwa
wingu kubwa jeupe, kwa chini likiwa tukufu kama moto ulao, na juu yake kuna ule upinde wa mvua wa
agano. Yesu anakuja juu ya lile wingu akiwa kama mshindi mwenye nguvu. Wakati huu si kama yule
“Mtu wa huzuni nyingi,” aendaye kukinywea kikombe kichungu cha aibu na majonzi, bali anakuja kama
mshindi wa mbinguni na duniani, akija kuwakuhumu walio hai na waliokufa. “Mwaminifu na Kweli,”
“kwa haki ahukumu na kufanya vita.” Na “majeshi yaliyo mbinguni” (Ufunuo 19:11,14) yanamfuata. Kwa
nyimbo tamu za mbinguni malaika watakatifu, wakiwa kundi kubwa lisilohesabika, wanamsindikiza
katika njia yake. Anga linaonekana kujawa na viumbe wanaong’aa kama miale ya mwanga - “elfu kumi
mara elfu kumi na maelfu ya maelfu.” Hakuna kalamu ya mwanadamu iwezayo kuiandika picha ile;
hakuna akili ya binadamu inayoweza kuuelewa mwonekano wa mandhari ile. “Utukufu wake ukazifunika
mbingu, nayo dunia ikajaa sifa yake. Mwangaza wake ulikuwa kama nuru.” Habakuki 3:3,4. Kadiri wingu
lile hai linavyozidi kukaribia zaidi, kila jicho linamwona Mkuu wa uzima. Hakuna taji ya miiba sasa
inayoharibu kichwa kile kitakatifu; bali taji tukufu ya kifalme iko juu ya paji la kichwa chake kitakatifu.
Uso wake unang’aa sana kupita mng’ao wa jua la adhuhuri. “Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake
na paja lake, Mfalme wa wafalme, na Bwana wa mabwana.” Ufunuo 19:16.
Mbele zake “nyuso zote zinageuka rangi;” juu ya wale walioikataa rehema ya Mungu kunaanguka hofu
kuu inayowakatisha tamaa milele. “Hata moyo unayeyuka, na magoti yanagongana-gongana;… na nyuso
za wote zimekuwa nyeusi kwa hofu.” Yeremia 30:6; Nahumu 2:10. Wenye haki wanapiga kelele na
kutetemeka, wanasema: “Ni nani awezaye kusimama?” Wimbo wa malaika unanyamazishwa, halafu
kuna kipindi cha ukimya wa kuogofya sana. Kisha sauti ya Yesu inasikika, ikisema: “Neema yangu
yakutosha.” Nyuso za wenye haki zinachangamka, na furaha inaujaza kila moyo. Kisha malaika wanapiga
noti kwa sauti ya juu zaidi na kuimba tena wanapozidi kukaribia duniani.
Mfalme wa wafalme anashuka akiwa juu ya wingu, likizungukwa na miale ya moto. Mbingu zinakunjwa
pamoja kama karatasi, nchi inatetemeka mbele zake, na kila mlima na kila kisiwa (642) kinaondolewa
mahali pake. “Mungu wetu atakuja wala hatanyamaza, moto utakula mbele zake, na tufani yavuma
sana ikimzunguka pande zote. Ataziita mbingu zilizo juu, na nchi pia awahukumu watu wake.” Zaburi
50:3,4.
"And the kings of the earth, and the great men, and the rich men, and the chief captains, and the
mighty men, and every bondman, and every freeman, hid themselves in the dens and in the rocks of the
mountains; and said to the mountains and rocks, Fall on us, and hide us from the face of Him that
sitteth on the throne, and from the wrath of the Lamb: for the great day of His wrath is come; and who
shall be able to stand?" Revelation 6:15-17.
“Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na
mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, wakiiambia milima na miamba,

372
Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-
Kondoo. Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?” Ufunuo
6:15-17.
Dhihaka za mizaha zimekoma. Midomo inayosema uongo inazimwa katika ukimya. Mapigo ya silaha,
ghasia za vita, “na makelele yaliyojaa ghasia, na mavazi yaliyofingirishwa katika damu” (Isaya 9:5),
vinazimwa. Sasa hakuna kinachosikika isipokuwa sauti ya maombi na mlio wa vilio na maombolezo. Kilio
hiki kinalipua kutoka katika ile midomo iliyokuwa inafanya dhihaka muda mfupi uliopita kwamba: “Siku
iliyo kuu ya hasira yake, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?” Waovu wanaomba wazikwe chini ya
miamba ya milima ili wasikutane uso kwa uso na yeye ambaye wamemdharau na kumkataa.
Sauti ile inayopenya hata sikio la watu waliokufa, wanaijua. Ni mara ngapi sauti hiyo ya kusihi, sauti ya
upole, imewaita ili wapate kutubu. Ni mara ngapi imesikika katika kusihi kwa rafiki, ndugu, Mkombozi.
Kwa wale walioikataa neema yake hakuna sauti nyingine ambayo ingewagusa, ingewaonyesha kuwa na
mzigo wa kuhukumu, kama sauti ile iliyowasihi kwa muda mrefu, ikisema: “Ghairini, ghairini, mkaache
njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa?” Ezekieli 33:11. Oh, kwao ilikuwa kama sauti ya mgeni
wasiyemjua! Yesu anasema: “Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa; nimeunyosha mkono wangu,
asiangalie mtu; bali mmebatilisha shauri langu,wala hamkutaka maonyo yangu.” Mithali 1:24,25. Sauti
ile inaziamsha kumbukumbu zao ambazo wangetamani zifutiliwe mbali - maonyo yaliyodharauliwa, wito
uliokataliwa, na fursa zilizochezewa.
(643) Wapo wale waliomdhihaki Kristo wakti wa kudhalilishwa kwake. Kwa nguvu ya kutisha yanawajia
mawazoni maneno ya Mtesekaji, wakati alipokuwa akiapizwa na kuhani mkuu, aliposema kwa utulivu:
“Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya
mbinguni.” Mathayo 26:64. Sasa wanamwona katika utukufu wake, na bado hawajamwona akiketi
mkono wa kuume wa nguvu.
Wale waliodhihaki madai yake kuwa ni Mwana wa Mungu hawana la kusema sasa. Yupo yule Herode
mwenye majivuno makuu aliyekejeli ufalme wa Yesu na kuwaagiza askari wamvike taji ya kifalme kwa
dhihaka. Wapo wale watu ambao kwa mikono yao miovu waliuvika mwili wake vazi la zambarau, na juu
ya kichwa chake taji ya miiba, na katika mkono wake usio na upinzani wakaweka fimbo ya bandia ya
kifalme, na kusujudu mbele yake kwa dhihaka ya makufuru. Wale watu waliompiga na kumtemea mate
Mkuu wa uzima sasa wanageukia mbali na macho yake yanakozwa na kupenya mpaka ndani yao huku
wakitafuta kukimbia mbali na utukufu wa nguvu wa kuwapo kwake. Wale waliopigilia misumari katika
mikono yake na miguu yake, askari yule aliyemchoma kwa mkuki ubavuni, wanaziangalia alama za
makovu kwa hofu kuu na majuto.
Kwa umahususi wa kuogofya makuhani na watawala wanayakumbuka matukio ya Kalvari. Kwa hofu kuu
ya kutetemesha wanakumbuka jinsi, wakiwa wanatikisa vichwa vyao kwa masimango ya kishetani,
walivyosema: “Aliokoa wengine, hawezi kujiokoa mwenyewe. Kama yeye ni mfalme wa Israeli; na
ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini. Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama anamtaka.”
Mathayo 27:41-43.
Kwa uwazi kabisa wanaukumbuka mfano alioutoa Mwokozi wa wakulima waliokataa kumpa bwana wao
matunda ya shamba lake la mizabibu, waliowatenda vibaya watumishi wake na kumwua mwanawe. Pia,
wanakumbuka hukumu waliyoitamka wenyewe, wakisema: Bwana wa shamba la mizabibu
“atawaangamiza vibaya wale wabaya.” Katika dhambi na adhabu ya watu wale wasio waaminifu
makuhani na wazee wanaona njia yao waliyoipitia na hatima yao ya kuangamizwa ambayo ni ya haki. Na
sasa kinapanda juu kilio cha utungu wa mwanadamu. Ni kilio kikubwa kuliko makelele yale yaliyosema,
373
“Msulibishe! Msulibishe!” ambayo yalivuma katika mitaa ya Yerusalemu, kikiongeza kilio cha kukata
tamaa na (644) kukosa tumaini, wakisema, “Huyu ni Mwana wa Mungu! Huyu ndiye Masihi wa kweli!”
Wanatafuta kukimbia kutoka mbele za Mfalme wa wafalme. Katika mashimo marefu ya nchi,
yaliyotokea kwa kupasuka kwa ardhi kutokana na mgongano wa matukio yale ya mwisho, wanajaribu
kujificha humo pasipo mafanikio.
Katika maisha ya wote wanaoukataa ukweli kuna nyakati ambapo dhamiri inaamshwa, wakati ambapo
kumbukumbu zinaonyesha mkusanyiko unaosumbua wa maisha ya kinafiki na moyo huteswa na majuto
yasiyo na msaada tena. Lakini haya ni kitu gani ukilinganisha na majuto makubwa ya siku ile, wakati
“hofu ifikapo kama tufani,” na “msiba ufikapo kama kisulisuli”! Mithali 1:27. Wale ambao
wangemwangamiza Kristo na watu wake waaminifu sasa wanashuhudia utukufu ulio juu yao. Katikati ya
shida zao wanasikia sauti za watakatifu wakiimba nyimbo za furaha, wakisema: “Tazama, huyu ndiye
Mungu wetu, ndiye tuliyemngoja, naye atatuokoa.” Isaya 25:9.
Katikati ya kusukwasukwa kwa dunia, kumulika kwa umeme wa radi, na kunguruma kwa radi, sauti ya
Mwana wa Mungu inawaita watakatifu waliolala watoke. Anayaangalia makaburi ya wenye haki, kisha,
akiinua mikono yake kuelekea mbinguni, anasema: “Amkeni, amkeni, ninyi mlalao mavumbini, nasema
tena, amkeni!” Kila mahali kwa mapana na marefu ya dunia hii, wafu wataisikia sauti ile, na wale
watakaoisikia watakuwa hai. Na dunia yote itavuma kwa vishindo vya jeshi kubwa sana lile litokalo kila
taifa, lugha, na jamaa. Kutoka katika nyumba ya gereza la mauti, wanatoka, wakiwa wamevikwa
utukufu wa miili isiyokufa, wakisema: “U wapi, Ewe mauti uchungu wako? Ku wapi, Ewe mauti kushinda
kwako?” 1 Wakorintho 15:55. Na wenye haki walio hai wanaunganisha sauti zao humo kupiga kelele
ndefu, za furaha, za ushindi.
Wote wanatoka makaburini mwao wakiwa na kimo kile kile walichokuwa nacho walipoingia kaburini.
Adamu, anayesimama miongoni mwa kundi la waliofufuliwa, ana kimo kirefu sana na umbile kubwa,
umbo lake likiwa chini kidogo ya Mwana wa Mungu. Anaonyesha tofauti kubwa na watu wa vizazi
vilivyofuata baadaye; katika jambo hilo moja yanaonekana mapungufu ya kunyong’onyea kwa jamii ya
wanadamu. Lakini wote wanafufuka wakiwa na mwonekano mzuri wa afya na nguvu za ujana wa milele.
Hapo mwanzo, mwanadamu (645) aliumbwa kwa mfano wa Mungu, si kwa tabia tu, bali kwa umbo na
sura. Dhambi iliondosha sura na karibu ifutilie mbali kabisa kufanana na Mungu; lakini Kristo alikuja
kurejesha kile kilichokuwa kimepotea. Atabadilisha miili yetu hii ya unyonge na kuifanya kuwa kama
mwili wake wa utukufu. Umbile hili linalokufa, linaloharibika, lisilokuwa na mwonekano mzuri, ambalo
wakati fulani lilichafuliwa na dhambi, linageuka kuwa lenye ukamilifu, la kupendeza, na lisikufa.
Mapungufu na vilema vyote vinaachwa kaburini. Wakiwa wamerejeshwa kwa ule mti wa uzima uliokuwa
katika Edeni ile iliyopotea zamani, wale waliokombolewa watakua (Malaki 4:2) mpaka watakapofikia
ukubwa wa umbo la mwanadamu katika utukufu ule wa asili. Alama za mwisho za laana zitakazokuwa
bado zimesalia zitaondolewa, na waaminifu wa Kristo wataonekana katika “uzuri wa Bwana Mungu
wetu,” wakiaksi mfano wa Bwana wao katika akili, roho, na mwili. Lo! ukombozi wa ajabu! uliosemwa
kwa muda mrefu, uliotarajiwa kwa kwa muda mrefu, uliotafakariwa kwa shauku kubwa, lakini ambao
kamwe haukueleweka kwa ukamilifu wake.
Wenye haki walio hai wanabadilika “kwa dakika moja, kufumba na kufumbua.” Wakati wa ile sauti ya
Mungu, walipata utukufu; sasa wanapewa kutokufa na pamoja na watakatifu waliofufuliwa
wananyakuliwa na kumlaki Bwana hewani. Malaika wanawakusanya “wateule wake toka pepo nne, toka
mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.” Watoto wachanga wanabebwa na malaika watakatifu na
kupelekwa mikononi mwa mama zao. Marafiki waliotengwa na mauti kwa muda mrefu wanakutanishwa,
wasiweze kuachana tena, na wakiimba nyimbo za furaha wanapaa pamoja kwenda katika Jiji la Mungu.
374
Kila upande wa gari lile la wingu kuna mabawa, na chini yake yako magurudumu yaliyo hai; na kadiri
gari lile linavyotembea kwenda juu, magurudumu yale yanatoa sauti, yakilia, “Mtakatifu,” na mabawa
yale, yanaposogea, yanalia, “Mtakatifu,” na msafara wa malaika unaimba, “Mtakatifu, Mtakatifu,
Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi.” Na wale waliokombolewa wanapaza sauti wakisema, “Haleluya!”
kadiri gari linavyoendelea kusonga mbele kuelekea kule Yerusalemu Mpya.
Kabla ya kuingia katika Jiji la Mungu, Mwokozi anawawekea wafuasi wake nembo za ushindi na
kuwatunuku nembo za ufalme. Mipangilio yao ya kumeremeta imepangwa katika mzunguko wa umbo la
mraba kumzunguka Mfalme wao, ambaye umbo lake limepanda juu zaidi ya mtakatifu na malaika, (646)
ambaye mwonekano wake unawasambazia miale ya upendo. Kila jicho katika jeshi lile lisilohesabika
limekazwa kwake, kila jicho linatazama utukufu wake yeye ambaye “uso wake ulikuwa umeharibiwa
sana zaidi ya mtu ye yote, na umbo lake zaidi ya wanadamu.” Yesu kwa mkono wake wa kulia anaweka
taji ya utukufu juu ya vichwa vya washindi wale. Kuna taji kwa ajili ya kila mmoja, ikiwa na “jina jipya”
la kwake (Ufunuo 2:17), na maneno haya yameandikwa juu ya taji hiyo, “Utakatifu kwa Bwana.” Katika
kila mkono linawekwa tawi la mtende la mshindi na kinubi kinachometameta. Halafu, pindi malaika
wanaoongoza wanapoanza kupiga, kila mkono unacharaza nyuzi za kinubi kwa ustadi, ukitokea muziki
mtamu , wimbo mtamu. Furaha kuu isiyoneneka inausisimua kila moyo, na kila sauti inapazwa kutoa
shukrani pamoja na sifa kwa kusema: “Kwake yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu
yake, na kutufanya kuwa wafalme na makuhani kwa Mungu na kwa Baba yake; kwake na uwe utukufu na
mamlaka milele hata milele.” Ufunuo 1:5,6.
Mbele ya msafara wa waliokombolewa kuna lile Jiji Takatifu. Yesu anayafungua wazi malango yale ya
lulu, na mataifa yale yaliyoishika kweli yake yanaingia ndani. Wanaiona pale ile Paradiso ya Mungu,
makazi yale ya Adamu wakati akiwa hana hatia. Ndipo sauti ile, tamu sana kuliko muziki wa aina yoyote
ambayo masikio ya mwanadamu yamepata kusikia, inasikika ikisema: “Mapambano yenu yamekwisha.”
“Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu.”
Sasa limetimizwa lile ombi la Mwokozi kwa ajili ya wanafunzi wake: “Baba, hao ulionipa nataka wawe
pamoja nami po pote nilipo.” “Kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu”
(Yuda 24), Kristo anawaweka mbele ya Baba yake wale aliowanunua kwa damu yake, akisema: “Mimi
hapa, na watoto ulionipa mimi.” “Wote ulionipa nimewatunza.” Lo! maajabu ya upendo unaokomboao!
Furaha kuu ya saa ile wakati Baba wa milele, akiwaangalia wale waliokombolewa, atakapowatazama
wao ambao ni sura yake, uchafu wa dhambi ukiwa umekomeshwa, waa la dhambi likiwa limekwisha
kuondolewa, na mwanadamu akiwa tena katika upatanifu na Mungu!
(647) Kwa upendo usiotamkika, Yesu anawakaribisha waaminifu wake katika furaha ya Bwana wao.
Furaha ya Mwokozi ni kuona, katika ufalme wa utukufu, watu ambao wameokolewa kwa maumivu yake
na kudhalilishwa kwake. Na wale waliokombolewa watakuwa washiriki katika furaha yake, kadiri
wanapowaona, miongoni mwa wabarikiwa, wale walioongoka na kuletwa kwa Kristo kupitia maombi
yao, juhudi zao, na kujitoa kwao kwa upendo. Wanapokusanyika kukizunguka kile kiti cha enzi cheupe,
kikubwa, furaha isiyosemekana itaijaza mioyo yao, wakati watakapowaona wale ambao wamewaongoa
kuwaleta kwa Kristo, na kuona kwamba mmoja wao ameongoa na wengine, na hao wengine wakapata
wengine, wote wakiwa wameletwa kwenye makazi salama ya kupumzikia, wanazitupa taji zao miguuni
pa Yesu na kumsifu yeye kwa kurudia-rudia milele na milele.
Wakati wale waliokombolewa wanapokaribishwa katika lile Jiji la Mungu, kelele za shangwe na kuabudu
zinasikika hewani. Akina Adamu wawili wanaenda kukutana. Mwana wa Mungu anasimama akiwa
amenyoosha mikono yake mbele ili kumpokea baba wa jamii yote ya wanadamu - kiumbe yule

375
aliyemwumba, aliyemtenda dhambi Muumba wake, na ambaye kwa dhambi yake alama za kusulibiwa
zimebebwa katika mwili wa Mwokozi. Pindi Adamu anapozitambua alama za misumari ya kikatili,
haanguki kifuani pa Bwana wake, bali kwa kujidhili anajitupa chini ya miguu yake, akilia: “Astahili,
astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa!” Kwa upole Mwokozi anamwinua juu na kumtaka ayatazame tena
makazi yake ya Edeni ambamo kwa muda mrefu alikuwa amefukuzwa.
Baada ya kufukuzwa kwake kutoka Edeni, maisha ya Adamu hapa duniani yalijaa huzuni. Kila jani
lililokuwa linanyauka, kila kiumbe aliyetolewa kama kafara, kila baka lililo kwenye uso wa maumbile ya
asili, kila waa juu ya usafi wa maisha ya mwanadamu, vilikuwa ni kumbukumbu mpya ya dhambi yake.
Cha kutisha kilikuwa ni maumivu ya hatia alipoona uovu ukizidi kuongezeka, na, kama majibu kwa
maonyo yake aliyotoa, alikabiliwa na shutuma nyingi alizotupiwa kwamba yeye ndiye chanzo cha
dhambi. Kwa uvumilivu wa unyenyekevu unaostahimili alibeba adhabu ya uasi wake kwa karibu miaka
elfu moja. Kwa imani alitubu dhambi yake na kutumainia wema wa Mwokozi aliyeahidiwa, na alikufa
katika tumaini la ufufuo. Mwana wa Mungu alikomboa kushindwa na kuanguka kwa mwanadamu, na
(648) sasa, kupitia ya kazi ya upatanisho, Adamu anarejeshwa katika mamlaka yake ya kwanza.
Akiwa amechukuliwa na furaha, anaiangalia miti ile ambayo wakati fulani ilikuwa furaha yake - miti ile
ile ambayo alichuma matunda yake yeye mwenyewe katika siku zake zile zisizo za hatia na za furaha.
Anaiona mizabibu ile ambayo mikono yake mwenyewe iliihudumia, maua yale yale ambayo zamani
alipenda kuyatunza. Akili yake inatambua hali halisi ya mwonekano ule; anaelewa kwamba kweli hii ni
Edeni iliyorejeshwa, ikiwa nzuri zaidi kuliko vile ilivyokuwa alipofukuzwa kutoka humo. Mwokozi
anampeleka kwenye mti wa uzima na kuchuma tunda lake tukufu na kumwambia ale. Anaangalia pande
zote kuona kundi kubwa la jamaa yake iliyokombolewa, wakisimama katika Paradiso ya Mungu. Anatupa
taji yake inayomeremeta miguuni pa Yesu na, akianguka kifuani pake, anamkumbatia Mkombozi wake.
Anakigusa kinubi cha dhahabu, na anga lote la mbinguni linavuma kwa wimbo wa ushindi usemao:
“Astahili, astahili, astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, na aliye hai tena!” Jamaa ile ya Adamu
wanaitikia wimbo huo na kuzitupa taji zao miguuni pa Mwokozi wakisujudu mbele zake na kumwabudu.
Kurudiana huku kunashuhudiwa na malaika waliolia pindi Adamu alipoanguka na kushangilia wakati
Yesu, baada ya kufufuka kwake, alipopaa mbinguni, akiwa amefungua kaburi kwa ajili ya wote
watakaoliamini jina lake. Sasa wanaiona kazi yake ya ukombozi ikiwa imekamilika, nao wanaunganisha
sauti zao katika wimbo ule wa sifa.
Penye bahari ya kioo mbele ya kiti cha enzi, that bahari ya kioo iliyochanganyika na moto, - ikiwa
inametameta kwa utukufu wa Mungu, - limekusanyika kundi la wale waliopata “ushindi dhidi ya
mnyama, na dhidi ya sanamu yake, na dhidi ya chapa yake, na dhidi ya hesabu ya jina lake.” Wakiwa
pamoja na Mwana-Kondoo kwenye Mlima Sayuni, wanasimama wale “wenye vinubi vya Mungu,”
wanasimama, mia na arobaini na nne elfu waliokombolewa kutoka miongoni mwa watu; kisha inasikika
sauti kama ya maji mengi, na kama sauti ya radi kuu, “sauti ya wapiga vinubi, wakivipiga vinubi vyao.”
Nao wanaimba “wimbo (649) mpya” mbele ya kiti cha enzi, wimbo ambao hapana mtu awezaye
kujifunza, ila wale mia na arobaini na nne elfu. Huo ni wimbo wa Musa na Mwana-Kondoo - wimbo wa
ukombozi. Hakuna awezaye kujifunza wimbo huo ila wale mia na arobaini na nne elfu; maana ni wimbo
wa uzoefu wao waliopitia - uzoefu ambao hakuna kundi jingine liwalo lote lililopata kuupitia. “Hawa
ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako.” Hawa, wakiwa wamenyakuliwa kutoka duniani, kutokana
miongoni mwa walio hai, wanahesabika kama “malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.” Ufunuo
15:2,3; 14:1-5. “Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu,” wamepita katika wakati wa taabu ambao
mfano wake haujapata kuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa; wamestahimili uchungu wa wakati wa
taabu ya Yakobo; wamesimama pasipokuwa na mwombezi katika kipindi kile cha kumwagwa kwa
376
mwisho kwa hukumu za Mungu. Lakini wameokolewa, kwa kuwa “wamefua mavazi yao, na kuyafanya
meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.” “Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana
mawaa” mbele zake Mungu. “Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia
mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao.”
Wameiona dunia ikiharibiwa na njaa na tauni, jua likiwa na nguvu ya kuwaunguza wanadamu kwa joto
kubwa, na wao wenyewe wamestahimili maumivu, njaa, na kiu. Lakini “hawataona njaa tena, wala
hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala joto kali. Kwa maana huyo Mwana-Kondoo aliye
katikati ya kiti cha enzi atawalisha, naye atawapeleka kwenye chemchemi ya maji yaliyo hai, naye
Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.” Ufunuo 7:14-17.
Katika vizazi vyote wateule wa Mwokozi wamefunzwa na kulelewa katika shule majaribu. Walitembea
katika njia nyembamba duniani; walitakaswa katika tanuru la mateso. Kwa ajili ya Kristo walistahimili
upinzani, kuchukiwa, na kusingiziwa. Walimfuata Kristo kupitia maumivu ya mapambano makali;
walistahimili kujikana nafsi na walistahimili fadhaa. Kutokana na (650) uzoefu wao mchungu,
walijifunza ubaya wa dhambi, nguvu ya dhambi, hatia ya dhambi, na majonzi yaletwayo na dhambi; na
wanaiangalia dhambi kwa kuikataa. Kutambua kwao kafara isiyo na kifani ambayo ilitolewa kama tiba
ya dhambi huwafanya wajinyenyekeze machoni pao wenyewe na kunaijaza mioyo yao shukrani na sifa
kwa kiasi ambacho wale ambao hawakupata kuanguka dhambini hawawezi kutambua. Wanapenda sana
kwa sababu wamesamehewa sana. Wakiwa wamekuwa washirika wa mateso ya Kristo, wametayarishwa
kushiriki pamoja naye katika utukufu wake.
Warithi wa Mungu wametoka katika vyumba vilivyojificha juu ya dari, kutoka katika vibanda vibaya vya
kimaskini, kutoka katika magereza ya chini ya ardhi, kutoka kwenye majukwaa ya kunyongea, kutoka
milimani, kutoka katika majangwa, kutoka katika matundu na mashimo ya nchi, kutoka katika mapango
ya bahari. Duniani walikuwa “wahitaji, wakiteswa, wakitendwa mabaya.” Mamilioni miongoni mwao
walishuka kaburini wakiwa wamebebeshwa mzigo mzito wa shutuma kwa sababu walikataa kwa uthabiti
kuyakubali madai ya uongo ya Shetani. Katika mahakama za wanadamu watu hawa walihukumiwa kuwa
wahalifu wabaya kupitiliza. Lakini sasa “Mungu ndiye aliye hakimu.” Zaburi 50:6. Sasa maamuzi kuhusu
kila mmoja yanapinduliwa na kuwa kinyume. “Na aibu ya watu wake ataiondoa.” Isaya 25:8. “Nao
watawaita, Watu watakatifu, waliokombolewa na BWANA.” Yeye amepanga kwamba wao “wapewe taji
ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito.”
Isaya 62:12; 61:3. Wao si watu wanyonge, waliotawanyika, na wanaoteswa tena. Tangu sasa watakuwa
pamoja na Bwana. Wanasimama mbele ya kiti cha enzi wakiwa wamevikwa mavazi mazuri mno kuliko
yale waliyopata kuvaa waheshimiwa sana wa duniani. Wamevikwa taji za kifalme zenye utukufu mwingi
kuliko zile zilizopata kuwekwa juu ya vichwa vya watawala wenye nguvu kuliko wote duniani. Siku za
maumivu na maombolezo zimekoma milele. Mfalme wa utukufu ameyafuta machozi kutoka katika nyuso
zote; kila sababu ya majonzi imeondolewa. Katikati ya kupepewa kwa matawi ya mitende wanapaza
sauti zao na kuimba wimbo wa sifa, msafi, mtamu, na sauti zake zinakubaliana vizuri; kila sauti
inauitikia wimbo huo, mpaka wimbo huo unaongezeka sauti na kuvuma katika anga la mbinguni,
wakisema: “Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo.” Na wakazi wote
wa mbinguni wanaitikia sifa hizo kwa kusema: “Amina; Baraka na utukufu na hekima na shukrani na
heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele.” Ufunuo 7:10,12.
Katika maisha haya tunaweza kuanza tu kulielewa somo la ajabu la ukombozi. Kwa ufahamu wetu finyu
wa kibinadamu tunaweza kuona jinsi aibu na utukufu, uzima na mauti, haki na rehema, vinavyokutana
kwenye msalaba; lakini hata tukitanua uwezo wetu wa akili mpaka mwisho hatuwezi kuelewa maana
yake kwa ukamilifu. Urefu na upana, kina na kimo, cha upendo unaokomboa hueleweka kwa kiwango

377
hafifu tu. Mpango wa ukombozi hautafahamika kwa ukamilifu, hata wakati wale waliokombolewa
watakapoona kama wanavyoonwa na kufahamu kama wanavyofahamika; bali kupitia vizazi na vizazi
milele ukweli mpya utazidi kufunuka daima katika akili zinazoshangaa na zenye furaha. Ingawa majonzi
na maumivu na majaribu ya dunia yamefika mwisho na sababu zake zimeondolewa, watu wa Mungu
wataendelea daima kuwa na ufahamu maalum wa kile ambacho wokovu wao umegharimu.
Msalaba wa Kristo utakuwa ndiyo sayansi na wimbo wa waliokombolewa milele zote. Katika Kristo
aliyetukuzwa watamwona Kristo aliyesulibiwa. Kamwe haitasahaulika kwamba yeye ambaye uweza
wake uliyaumba na kuyategemeza malimwengu yasiyohesabika katika milki kubwa ya anga la
malimwengu, Mpendwa wa Mungu, Mfalme wa Mbinguni, yeye ambaye makerubi na maserafi wenye
kung’aa walipendezwa kumheshimu - alijinyenyekeza ili apate kumwinua mwanadamu aliyeanguka; hata
akaibeba hatia na aibu ya dhambi, na kule kufichwa kwa uso wa Baba yake, mpaka msiba ule wa
ulimwengu uliopotea ukaupasua moyo wake na kuyaponda maisha yake kwenye msalaba wa Kalvari.
Kwamba Mwumbaji wa malimwengu yote, Mwasisi wa hatima zote, anaweka kando utukufu wake na
kujidhili kutokana na upendo wake kwa mwanadamu ni jambo ambalo litaendelea daima kuamsha
mshangao na heshima kuu ya malimwengu yote. Kadiri mataifa ya waliookolewa wanavyomtazama
Mkombozi wao na kuuona utukufu wa milele wa Baba uking’aa katika uso wake; kadiri wanavyokiona kiti
chake cha enzi, ambacho kipo tangu milele hata milele, na kujua kwamba ufalme wake hautakuwa na
mwisho, wanalipuka katika wimbo wa shangwe, wakisema: “Astahili, astahili Mwana-Kondoo (652)
aliyechinjwa, naye ametukomboa sisi kwa damu yake ya thamani sana!”
Fumbo la msalaba linafumbua mafumbo mengine yote. Katika nuru inayotiririka kutoka Kalvari, sifa za
tabia ya Mungu ambazo zilikuwa zimetujaza woga na hofu zinaonekana kuwa za kupendeza na kuvutia.
Rehema, upole, na upendo kama wa mzazi vinaonekana kuunganika na utakatifu, haki, na uweza.
Wakati tunapotazama ukuu wa kiti chake cha enzi, kilicho juu na kilichoinuliwa, tunaiona tabia yake
katika mwonekano wake mtukufu, na kuelewa vema, kuliko ilivyokuwa kabla, maana ya kile cheo chake
cha kupendeza, yaani, “Baba Yetu.”
Itadhihirika kwamba yeye ambaye hekima yake haina kikomo asingeweza kubuni mpango mwingine
wowote kwa ajili ya wokovu wetu zaidi ya ule wa kumtoa Mwana wake kafara. Fidia ya kafara hiyo ni ile
furaha ya kuijaza dunia kwa viumbe waliokombolewa, watakatifu, wenye furaha, na wenye miili
isiyokufa. Matokeo ya pambano la Mwokozi wetu dhidi ya nguvu za giza ni furaha kwa ajili
waliokombolewa, inayojitokeza katika utukufu wa Mungu milele zote. Na hiyo ndiyo thamani ya mtu
kiasi kwamba Baba anaridhishwa na gharama iliyolipwa; na Kristo mwenyewe, anapoyaona matunda ya
kafara yake kuu, anaridhika.

378
Sura ya 41
DUNIA KUFANYWA UKIWA

“Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake…. Katika
kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni maradufu. Kwa kadiri alivyojitukuza na kufanya
anasa, mpeni maumivu na huzuni kadiri iyo hiyo. Kwa kuwa husema moyoni mwake, Nimeketi malkia,
wala si mjane, wala sitaona huzuni kamwe. Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja,
mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu
aliyemhukumu ni mwenye nguvu. Na hao wafalme wa nchi waliozini naye na kufanya anasa pamoja
naye, watalia na kumwombolezea;… wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na
nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.” Ufunuo 18:5-10.
“Nao wafanya biashara wa nchi,” ambao “walipata “mali kwa nguvu za kiburi chake,” “watasimama
mbali, kwa hofu ya maumivu yake; wakilia na kuomboleza, wakisema, Ole, ole, mji ule mkuu! Uliovikwa
kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na nguo nyekundu, na kupambwa kwa dhahabu, na kito cha
thamani, na lulu! Kwa kuwa katika saa moja utajiri mwingi namna hii umekuwa ukiwa.” Ufunuo
18:11,3,15-17.
Hizo ndizo hukumu zinazomwangukia Babeli katika siku ya kupatilizwa kwa ghadhabu ya Mungu kwake.
Amekijaza kikombe cha maovu yake; wakati wake umefika; amefika katika wakati unaofaa kwa ajili ya
kuangamizwa.
(654) Wakati sauti ya Mungu inapobadilisha wake wake walio mateka, kuna hali ya kutisha ya kuamsha
wale waliopoteza kila kitu katika pambano kuu la maisha. Wakati muda wa rehema uliendelea kuwapo
wao walipofushwa na madanganyo ya Shetani, na waliihalalisha njia yao ya dhambi. Matajiri walijivunia
kuwa juu ya wale waliokuwa wamejaliwa kidogo; lakini walikuwa wamepata utajiri wao kwa kuivunja
sheria ya Mungu. Walikuwa wamepuuza kuwalisha wenye njaa, kuwavika nguo walio uchi, kutenda kwa
haki, na kupenda kuwa na huruma. Walikuwa wamejitahidi kujitukuza wenyewe na kutafuta kutukuzwa
na viumbe wenzao. Sasa wameondoshewa vitu vyote vilivyowafanya wawe wakubwa na wameachwa
wasio na kitu wala kinga. Wanatazama kwa hofu kuu kuangamizwa kwa sanamu ambazo walipenda zaidi
kuliko Mwumbaji wao. Wameuza nafsi zao kwa kubadilishana na utajiri na anasa za dunia, wala
hawakutafuta kuwa matajiri kwa Mungu. Matokeo yake ni maisha yao kushindwa; anasa zao zimegeuka
sasa na kuwa uchungu, hazina zao zimekuwa kuwa uharibifu. Faida yote iliyopatikana kwa muda wa
maisha yote imefagiliwa kwa muda mfupi. Matajiri wanaombolezea kuharibiwa kwa majumba yao ya
fahari, kutawanywa kwa dhahabu na fedha yao. Lakini maombolezo yao hayo yananyamazishwa na woga
kwamba kwamba wao wenyewe hawana budi kuangamizwa pamoja na sanamu zao hizo.
Waovu wamejawa na majuto, si kwa sababu ya dhambi yao ya kumpuuza Mungu na wanadamu wenzao,
bali kwa sababu Mungu ameshinda. Wanaomboleza kwa kuwa matokeo yako hivyo yalivyo; lakini
hawatubii uovu wao. Wasingeacha kutumia mbinu yoyote inayoweza kutumiwa ili kushinda kama
wangeweza.
Ulimwengu unaliona kundi lile lile walilodhihaki na kudharau, na kutaka kuliangamiza kabisa, likipita
katika tauni, tufani, na tetemeko la nchi, bila kupatikana na madhara yoyote. Yeye ambaye ni moto
ulao kwa wavunjaji wa sheria yake, ni hifadhi salama kwa watu wake.

379
Mtumishi wa dini aliyepotosha ukweli ili apate kupendwa na watu sasa anatambua uhalisia na matokeo
ya mafundisho yake. Inakuwa dhahiri kwamba jicho lile linalojua yote lilikuwa linamfuata wakati
aliposimama mimbarani, wakati alipokuwa akitembea mitaani, wakati alipojichanganya na watu katika
matukio mbalimbali ya maisha. Kila (655) wazo la moyoni, kila mstari ulioandikwa, kila neno
lililotamkwa, kila tendo lililowaongoza watu kupumzika katika hifadhi ya uongo, yamekuwa yakitawanya
mbegu; na sasa, katika hali mbaya, akiwa amezungukwa pande zote na watu hao waliopotea, anayaona
mavuno ya kazi yake.
Bwana asema hivi: “Kwa maana wameiponya jeraha ya binti ya watu wangu kwa juu-juu tu, wakisema,
Amani, Amani, wala hapana amani.” “Kwa kuwa ninyi mmemhuzunisha mwenye haki kwa uongo,
ambaye mimi sikumhuzunisha; na kuitia nguvu mikono ya mtu mbaya, hata asigeuke, na kuiacha njia
yake mbaya, na kumwahidia uzima.” Yeremia 8:11; Ezekieli 13:22.
Ole “wao wachungaji, wanaoharibu kondoo za malisho yangu na kuwatawanya!… Angalieni,
nitawapatiliza uovu wa matendo yenu.” “Pigeni yowe, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika
majivu, enyi mlio wakuu katika kundi; maana siku za kuuawa kwenu zimetimia kabisa,… Nao wachungaji
watakuwa hawana njia ya kukimbia, wala walio wakuu katika kundi hawataokoka.” Yeremia 23:1,2;
25:34,35.
Viongozi wa kiroho na watu wanagundua kwamba hawajawa na uhusiano sahihi na Mungu. Wanaona
kwamba wamemwasi Mwasisi wa sheria yote iliyo adilifu na ya haki. Kule kuziweka kando amri za Mungu
kulifanya zitokee maelfu ya chemchemi za uovu, vita, chuki, udhalimu, mpaka dunia yote ikawa uwanja
mmoja mkubwa wa mapambano, shimo moja la taka za ufisadi. Hiyo ndiyo picha inayoonekana sasa kwa
wale walioikataa kweli na kuchagua kuendelea na uongo. Hakuna lugha inayoweza kueleza maumivu
ambayo wasio watiifu wanaipata kwa ajili ya kile ambacho wamepoteza milele – uzima wa milele. Watu
wale walioabudiwa na ulimwengu kwa talanta zao na ufasaha wao, sasa wanayaona mambo hayo katika
nuru yake ya kweli. Wanatambua kile walichokipoteza kwa uasi wao, na wanaanguka miguuni mwa watu
wale wenye msimamo thabiti ambao wao wameudharau na kuudhihaki, na wanakiri kwamba Mungu
amewapenda hao.
Watu hawa wanaona kwamba wamedanganywa. Wanalaumiana wao kwa wao kwamba wameelekezwa
katika uharibifu; lakini wote wanaungana pamoja kuwarudikia lawama viongozi wa dini. Wachungaji
wasio waaminifu wametabiri mambo laini; wamewaongoza wasikilizaji kutojali sheria ya Mungu na (656)
kuwatesa wale ambao wangetaka kutunza utakatifu wake. Sasa, katika kukata tamaa kwao, walimu hao
wanakiri mbele ya ulimwengu kwamba kazi yao ilikuwa ya udanganyifu. Makundi ya watu yanashikwa na
ghadhabu kali. Wanalia na kuwageukia wachungaji wa uongo, wakisema, “Tumepotea! na ninyi ndio
sababu ya maangamizi yetu;” Watu wale wale ambao waliwapenda sana zamani watatamka laana za
kutisha sana juu yao. Mikono ile ile ambayo zamani iliwavalisha tuzo za heshima itainuliwa ili
kuwaangamiza. Mapanga yale ambayo yalikuwa yatumike kuwaua watu wa Mungu sasa yanatumika
kuharibu maadui hawa. Kila mahali ni vita na kumwaga damu.
“Kelele zitafika hata mwisho wa dunia; maana BWANA ana mashindano na mataifa, atateta na watu
wote wenye mwili; na waovu atawatoa wauawe kwa upanga.” Yeremia 25:31. Kwa miaka elfu sita
pambano kuu limekuwa likiendelea; Mwana wa Mungu na wajumbe wa mbinguni wamekuwa wakipigana
na nguvu za yule mwovu, katika kuwaonya, kuwatia nuru, na kuwaokoa wana wa wanadamu. Sasa wote
wamekwisha kufanya maamuzi yao; waovu wameungana kikamilifu na Shetani katika vita yake dhidi ya
Mungu. Wakati umewadia wa Mungu kuithibitisha mamlaka ya sheria yake iliyokanyagwa. Sasa pambano

380
hilo si dhidi ya Shetani peke yake, bali na wanadamu. “BWANA ana mapambano na mataifa.” “Waovu
atawatoa wauawe kwa upanga.”
Alama ya ukombozi imekwisha kuwekwa juu ya wale “wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo
yote yanayofanyika kati yake.” Sasa malaika wa kifo anatokea, aliyewakilishwa katika maono ya Ezekieli
na watu wenye silaha za kuua, ambao walipewa amri isemayo: “Waueni kabisa, mzee, na kijana, na
msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama;
tena anzeni katika patakatifu pangu.” Nabii huyo anasema: “Basi, wakaanza kwa wazee waliokuwa
mbele ya nyumba.” Ezekieli 9:1-6. Kazi hiyo ya maangamizi inaanzia miongoni mwa wale waliojidai
kuwa ni walinzi wa kiroho wa watu. Walinzi hao wa uongo ndio wa kwanza kufyekwa na kuanguka chini.
Hakuna wanaohurumiwa au kuachwa. Wanaume, wanawake, wasichana, na watoto wadogo
wanaangamizwa kwa pamoja.
“Kwa maana, tazama, BWANA anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao (657) duniani, kwa
sababu ya uovu wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunika tena watu wake waliouawa.”
Isaya 26:21. “Na hii ndiyo tauni, ambayo BWANA atawapiga watu wote waliofanya vita juu ya
Yerusalemu; nyama ya mwili wao itaharibika, wasimamapo juu ya miguu yao, na macho yao
yataharibika ndani ya vichwa vyao, na ndimi zao zitaharibika vinywani mwao. Tena itakuwa siku hiyo,
ya kwamba machafuko makubwa yatokayo kwa BWANA yatakuwa kati yao; na kila mmoja wao
atakamata mkono wa jirani yake, na mkono wake utainuliwa ili kushindana na mkono wa jirani yake.”
Zekaria 14:12,13. Katika vita ile ya fujo ya hasira zao kali, na kwa kumiminwa kwa ile ghadhabu ya
Mungu isiyochanganywa na maji, wakazi waovu wa dunia wanaanguka - makasisi, watawala, na watu,
matajiri kwa maskini, wenye vyeo kwa wasio na vyeo. “Na waliouawa na BWANA siku ile watakuwapo,
toka upande mmoja wa dunia hata upande wa pili; hawataliliwa, wala kukusanywa, wala kuzikwa.”
Yeremia 25:33.
Wakati wa kuja kwa Kristo waovu wanafutiliwa mbali kutoka katika uso wa dunia - watauawa kwa pumzi
ya kinywa chake na kuangamizwa kwa mwanga mkali wa utukufu wake. Kristo anawachukua watu wake
kwenda nao katika Jiji la Mungu, na dunia hii inabaki ukiwa bila wakazi wake. “Tazama, BWANA
ameifanya dunia kuwa tupu, aifanya ukiwa, aipindua, na kuwatawanya wakaao ndani yake.” “Dunia hii
itafanywa tupu kabisa, na kuharibiwa kabisa; maana BWANA amenena neno hilo.” “Kwa maana
wameziasi sheria, wamelivunja agano la milele. Ndiyo sababu laana imeila dunia hii, na hao wanaoikaa
wametelekezwa [wameachwa peke yao]; ndiyo sababu watu wanaoikaa dunia wameteketezwa.” Isaya
24:1,3,5,6.
Dunia yote inaonekana kama jangwa la ukiwa. Magofu ya majumba ya majiji na vijiji yaliyoharibiwa na
tetemeko la nchi, miti iliyong’olewa, miamba iliyopasuka kwa kutupwa na bahari juu ya nchi kavu au
iliyomeguka kutoka katika nchi yenyewe, ikiwa imetawanyika juu ya uso wa dunia, wakati mashimo
makubwa yanaonyesha mahali milima ilipong’olewa toka katika misingi yake. (658)
Sasa linatokea tukio lile lililoonyeshwa kwa mfano katika huduma ile ya Siku ya Upatanisho. Wakati
huduma katika patakatifu pa patakatifu ilipokamilika, na dhambi za Israeli zilipokuwa zimekwisha
kuondolewa kutoka katika patakatifu pale kwa njia ya damu ya sadaka ya dhambi, ndipo yule mbuzi wa
Azazeli alipoletwa akiwa hai mbele za Bwana; na mbele ya mkutano ule kuhani mkuu aliungama juu
yake “uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao yote, naam, dhambi zao zote; naye aliziweka juu
ya kichwa chake yule mbuzi.” Mambo ya Walawi 16:21. Kwa namna ile ile, kazi ya upatanisho kule
mbinguni itakapokuwa imekamilika, ndipo dhambi za watu wa Mungu zitakapowekwa juu ya Shetani
mbele za Mungu na mbele ya malaika wa mbinguni na mbele ya majeshi ya wale waliokombolewa;

381
atatangazwa kuwa ana hatia ya uovu wote aliowasababisha kuutenda. Na kama yule mbuzi wa Azazeli
alivyopelekwa katika nchi isiyokaliwa na watu, ndivyo Shetani atakavyotengwa na kuachwa katika dunia
iliyobaki ukiwa, jangwa baya lisilokaliwa na watu.
Mwandishi wa Ufunuo anatabiri kuhusu kutengwa kwa Shetani na jinsi ambavyo dunia itapunguzwa hali
yake hadi kuwa ya kero na ukiwa, na anatangaza kwamba hali hiyo itaendelea kuwa hivyo kwa miaka
elfu moja. Baada ya kuelezea matukio ya marejeo ya Bwana na kuangamizwa kwa waovu, unabii huo
unaendelea: “Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na
mnyororo mkubwa mkononi mwake. Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na
Shetani, akamfunga miaka elfu; akamtupa katika kuzimu akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate
kuwadanganya mataifa tena hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda
mchache. Ufunuo 20:1-3.
Kwamba usemi huu “kuzimu” unaiwakilisha dunia hii katika hali yake ya kuvurugika na giza ni dhahiri
kutokana na maandiko mengine. Kuhusu hali ya dunia hii “hapo mwanzo” maandiko ya Biblia yanasema
kwamba “ilikuwa ukiwa tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji.” Mwanzo 1:1,2. 407
(659) Unabii unafundisha kwamba hali hiyo itarudishwa tena, walau kwa sehemu. Akiangalia mbele
kwenye siku kuu ya Mungu, nabii Yeremia anatangaza hivi: “Naliiangalia nchi, na tazama ilikuwa ukiwa,
haina watu; naliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru. Naliiangalia milima, na tazama,
ilitetemeka, na milima yote ilisogea huko na huko. Nikaangalia, na tazama, hapakuwa na mtu hata
mmoja, na ndege wote wa angani wamekwenda zao. Nikaangalia, na tazama, shamba lililozaa sana
limekuwa ukiwa, na miji yake yote ilikuwa imebomoka.” Yeramia 4:23-26.
Hapa ndipo patakuwa makazi ya Shetani na malaika zake waovu kwa miaka elfu moja. Akiwa
amezuiliwa duniani, hatakuwa na uwezo wa kuyafikia malimwengu mengine kuwajaribu na kuwasumbua
wale ambao hawajapata kuanguka dhambini. Ni kwa mtazamo huu anaposemekana kuwa amefungwa:
hakuna watu waliosalia kwa ajili ya yeye kuonyesha uwezo wake. Ametengwa kabisa na kazi ya
udanganyifu na maangamizi ambayo kwa karne nyingi ameifanya kuwa furaha yake.
Nabii Isaya, akiangalia mbele katika wakati ule Shetani atakapoangamizwa, anasema kwa mshangao:
“Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa
kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni,
nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu;… Nitafanana na yeye Aliye juu. Lakini utashushwa
mpaka kuzimu; mpaka pande za mwisho za shimo. Wao wakuonao watakukazia macho, watakuangalia
sana, wakisema, Je! huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, huyu ndiye aliyetikisa falme; aliyeufanya
ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?” Isaya 14:12-17.
Kwa miaka elfu sita, kazi ya Shetani ya maasi imeitetemesha dunia. Alikuwa ameufanya “ulimwengu
ukiwa, akaipindua miji yake.” Na hawafungui “wafungwa wake waende kwao.” Kwa miaka elfu sita
nyumba yake ya gereza imepokea watu wa Mungu, naye angekuwa amewashikilia mateka humo milele;
lakini Kristo alikuwa amevivunja vifungo vyake na kuwaweka huru wafungwa. (660)
Hata waovu sasa wamewekwa nje ya uwezo wa Shetani, na yeye pamoja na malaika zake tu wamebaki
na kutambua matokeo ya laana iliyoletwa na dhambi. “Wafalme wote wa mataifa wamezikwa wote kwa
heshima, kila mmoja ndani ya nyumba yake mwenyewe. Bali wewe umetupwa mbali na kaburi lako,

407
Neno la Kiebrania lilitafsiriwa hapa kama “kuzimu” limetolewa katika tafsiri ya Septuaginta (Kigiriki) ya Agano la Kale kwa
neno lile lile linalotafisiriwa "shimo lefu sana" katika Ufunuo 20:1-3.

382
kama chipukizi lililochukiza kabisa;… Hutaunganishwa pamoja nao katika mazishi, kwa maana
umeiharibu nchi yako, umewaua watu wako.” Isaya 14:18-20.
Kwa miaka elfu moja, Shetani atatangatanga huku na huko katika dunia iliyobaki ukiwa ili kuona
matokeo ya maasi yake dhidi ya sheria ya Mungu. Katika kipindi hiki maumivu yake ni makubwa sana.
Tangu alipoanguka maisha yake yaliyojaa shughuli zake zisizokoma yalikuwa yamemwondolea mawazo
ya kutafakari; lakini sasa amenyang’anywa uwezo wake na kuachwa kutafakari nafasi aliyofanya tangu
alipofanya maasi kwa mara ya kwanza dhidi ya serikali ya mbinguni, na aangalie mbele kwa kutetemeka
na hofu ili aone hatima yake ya kutisha wakati atakapoumia kwa uovu wote alioutenda na kuadhibiwa
kwa dhambi alizosababisha kutendwa.
Kwa watu wa Mungu kufungwa kwa Shetani kutawaletea furaha na kushangilia. Nabii anasema: “Tena
itakuwa katika siku ile, ambayo BWANA atakupa raha baada ya huzuni yako, na baada ya taabu yako, na
baada ya utumishi ule mgumu uliotumikishwa; utatunga mithali hii juu ya mfalme wa Babeli, na
kusema, Jinsi alivyokoma mwenye kuonea!… BWANA amelivunja gongo la wabaya, fimbo ya enzi yao
wenye kutawala. Yeye aliyewapiga mataifa kwa ghadhabu, kwa mapigo yasiyokoma; aliyetawala
mataifa kwa hasira, kwa mateso ambayo hakuna mtu aliyeweza kuyazuia.” Fungu la 3 hadi la 6.
Katika kipindi cha miaka elfu moja kilicho katikati ya ufufuo wa kwanza na ule wa pili hukumu ya waovu
inafanyika. Mtume Paulo anaelekeza kwenye hukumu hiyo kama tukio linalofuata marejeo ya Kristo.
“Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha
yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya (661) mioyo.” 1 Wakorintho 4:5. Danieli anasema
kwamba wakati yule Mzee wa Siku alipokuja, “watakatifu wake Aliye juu wakapewa hukumu.” Danieli
7:22. Wakati huu wenye haki wanatawala kama wafalme na makuhani kwa Mungu. Yohana katika
Ufunuo anasema: “Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu.” “Watakuwa
makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.” Ufunuo 20:4,6. Ni
wakati huo, kama alivyotabiri Paulo, ambapo “watakatifu watauhukumu ulimwengu.” 1 Wakorintho 6:2.
Wakiwa wameungana na Kristo wanawahukumu waovu, wakiyalinganisha matendo yao na kitabu cha
sheria, Biblia, na kuamua kila kesi kadiri ya matendo yaliyotendwa katika mwili. Ndipo kiwango
wanachopaswa kuteswa wale waovu kinakadiriwa kulingana na matendo yao; na kinaandikwa mbele ya
majina yao katika kitabu cha mauti.
Shetani pia pamoja na malaika zake waovu wanahukumiwa na Kristo na watu wake. Paulo anasema:
“Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika.” Fungu la 3. Naye Yuda anatangaza kwamba wale “Malaika
wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo
vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu."” Yuda 6.
Mwishoni mwa miaka ile elfu moja ufufuo wa pili unatokea. Halafu waovu watafufuka kutoka kwa wafu
na kusimama mbele za Mungu kwa utekelezaji wa ile “hukumu iliyoandikwa.” Hivyo mwandishi wa
Ufunuo, baada ya kueleza habari ya ufufuo wa wenye haki, anasema: “Hao wafu waliosalia hawakuwa
hai, hata itimie ile miaka elfu.” Ufunuo 20:5. Na Isaya anatangaza, kuhusu waovu hao: “Nao
watakusanywa pamoja kama vile wakusanywavyo wafungwa katika shimo nao watafungwa katika
gereza; na baada ya muda wa siku nyingi watajiliwa.” Isaya 24:22.

383
Sura ya 42
PAMBANO LIKIWA LIMEKWISHA

Mwishoni mwa ile miaka elfu moja, Kristo anarudi tena duniani. Anakuja akiwa pamoja na jeshi la
waliokombolewa na kufuatana na msafara wa malaika. Anaposhuka katika utukufu wa kuogofya na ukuu
anawaamuru waovu waliokufa kufufuka na kupokea hukumu yao. Mara wanafufuka, jeshi kubwa,
wasiohesabika kama mchanga wa bahari. Ni tofauti kubwa iliyoje kati ya hawa na wale walifufuliwa
katika ule ufufuo wa kwanza! Wenye haki walifufuka wakiwa wamevikwa mwili wa ujana na uzuri
usiokufa. Waovu wana alama za magonjwa na kifo.
Kila jicho katika umati ule mkubwa wa watu limegeuka kuutazama utukufu wa Mwana wa Mungu. Kwa
sauti moja watu walio katika jeshi lile la waovu wanasema kwa mshangao, “Amebarikiwa yeye ajaye
kwa jina la Bwana!” Si upendo wao kwa Yesu unaowasukuma kutamka maneno haya. Nguvu ya ukweli
inalazimisha maneno hayo yatoke katika midomo isiyopenda kuyatoa. Kama vile waovu walivyoingia
makaburini mwao, ndivyo wanavyotoka wakiwa na uadui ule ule dhidi ya Kristo na roho ile ile ya uasi.
Hawatakuwa na muda mwingine wa rehema ambamo wanaweza kurekebisha kasoro za maisha yao
yaliyopita. Hakuna manufaa yoyote ambayo yangepatikana kwa sasa kwa jambo hilo. Muda wa maisha
ya uasi umeshindwa kulainisha mioyo yao. Nafasi ya pili ya rehema, hata kama ingetolewa kwao,
ingetumiwa vile muda ule wa kwanza ulivyotumika katika kuyakwepa matakwa ya Mungu na kuchochea
maasi dhidi yake.
Kristo anashuka kwenye Mlima wa Mizeituni, mahali ambapo, baada ya kufufuka kwake, alipaa kwenda
mbinguni, na mahali ambapo malaika waliirudia ile ahadi ya kurudi kwake. Nabii anasema: “BWANA,
Mungu wangu, (663) atakuja, na watakatifu wote pamoja naye.” “Na siku hiyo miguu yake itasimama
juu ya Mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao Mlima wa Mizeituni
utapasuka katikati yake,… litakuwako huko bonde kubwa sana.” “Naye BWANA atakuwa mfalme juu ya
nchi yote; siku hiyo BWANA atakuwa mmoja, na jina lake moja.” Zekaria 14:5,4,9. Wakati Yerusalemu
Mpya, katika fahari yake ya kumetameta, unaposhuka kutoka mbinguni, unatua mahali palipotakaswa na
kutayarishwa kuupokea, naye Kristo, pamoja na watu wake na malaika zake, wanaingia katika Jiji
Takatifu.
Sasa Shetani anajiandaa kwa pambano kubwa la mwisho ili kupata utawala. Wakati alipokuwa
amenyang’anywa uwezo wake na kuzuiwa kabisa kufanya kazi yake ya udanganyifu, huyo mkuu wa uovu
alikuwa mnyonge na asiye na furaha; lakini waovu waliokufa wanapofufuliwa na anapoona kundi lile
kubwa likiwa upande wake, matumaini yake yanajea, na anaazimu kwamba hatashindwa katika
pambano kuu hilo. Atayapanga majeshi yote ya wale waliopotea chini ya bendera yake na kwa
kuwatumia hao atajitahidi kutekeleza mipango yake. Waovu ni mateka wa Shetani. Kwa kumkataa
Kristo wameukubali utawala wa kiongozi huyo mwasi. Wako tayari kupokea mapendekezo yake na
kufanya matakwa yake. Hata hivyo, akiwa mwaminifu kwa hila zake za tangu awali, hakiri kwamba yeye
ni Shetani. Anadai kwamba yeye ni mkuu ambaye na mmiliki wa haki wa ulimwengu na ambaye urithi
wake huo wa kutawala umenyang’anywa kutoka kwake isivyo halali. Anajionyesha kwa watu hao walio
chini yake na waliodanganyika kuwa yeye ndiye mkombozi, akiwahakikishia kwamba uwezo wake
umewafufua kutoka makaburini mwao na ya kwamba yuko tayari kuwaepusha na utawala katili wa
384
kikandamizaji. Uwepo wa Kristo ukiwa umeondolewa, Shetani anafanya miujiza kuyatia nguvu madai
yake. Anawafanya walio dhaifu kupata nguvu na kuwavuvia wote roho yake na nguvu zake.
Anapendekeza kuwaongoza kupigana na kambi ile ya watakatifu na kulitwaa lile Jiji la Mungu. Kwa
furaha ya kishetani anaonyesha mamilioni yasiyohesabika ya wale waliofufuliwa kutoka kwa wafu na
kutangaza kwamba yeye kama kiongozi wao anaweza kabisa kulipindua jiji lile na kutwaa kwa mara
nyingine kiti chake cha enzi pamoja na ufalme wake.
(664) Katika msongamano ule mkubwa wamo watu wengi wa jamii ya wanadamu walioishi kabla ya
Gharika; watu wenye maumbo makubwa na akili nyingi, ambao, wakikubali kuongozwa na malaika
walioanguka, walitumia ujuzi wao wote na maarifa yao yote katika kujitukuza wenyewe; watu ambao
kazi zao za ajabu za ustadi ziliufanya ulimwengu kuuona ujuzi wao mkubwa kama sanamu yao; lakini
watu ambao ukatili wao na mavumbuzi yao maovu, yakiinajisi dunia na kuondoa sura ya Mungu,
yalisababisha Mungu kuwafutilia mbali na uso uumbaji wake. Hapo wapo wafalme na majemadari
waliopigana na kuyashinda mataifa, wapo mashujaa ambao kamwe hawakupata kushindwa katika vita
yoyote, wapo wapiganaji ambao kukaribia kwao kulitetemesha falme. Katika umauti hawa hawakupata
badiliko lolote. Wanapotoka kaburini, wanaendelea na mkondo wa mawazo mahali pale pale
ulipokomea wakati walipokufa. Wanasukumwa na shauku ile ile ya kushinda katika vita iliyowatawala
wakati walipoanguka chini na kufa.
Shetani anashauriana na malaika zake, kisha anashauriana na hawa wafalme na washindi wa vita na
watu hodari. Wanaangalia nguvu na idadi iliyo upande wao, na kusema kwamba jeshi lililo ndani ya jiji
ni dogo likilinganishwa na lao, na kwamba inawezekana kulishinda. Wanaweka mipango yao ya kujipatia
utajiri na utukufu uliomo ndani ya Yerusalemu Mpya. Mara wote wanaanza kujiandaa kwa vita. Wafundi
stadi wanaunda silaha za vita. Viongozi wa majeshi, wenye kusifiwa sana kwa ushindi wao, wanapanga
makundi ya watu kama wa vita katika vikosi.
Hatimaye amri ya kusonga mbele vitani inatolewa, na jeshi lile la watu wasiohesabika linasonga mbele -
jeshi ambalo halijapata kamwe kuongozwa na washindi wa vita duniani, ambalo muungano wa majeshi
ya vizazi vyote tangu vita vilipoanza kupiganwa duniani lisingeweza kulingana nalo. Shetani, hodari wa
vita kuliko wote, anaongoza jeshi lile, na malaika zake wanaunganisha ngguvu zao tayari kwa pambano
hilo la mwisho. Wafalme na wapiganaji wako katika safu yake, kisha watu wengi wanafuata nyuma
katika vikosi vikubwa, kila moja chini ya kiongozi wake aliyeteuliwa. Kwa kufuata taratibu za kijeshi
safu zile zinasonga mbele juu ya uso wa dunia uliovunjika-vunjika na mbaya zikielekea kwenye Jiji la
Mungu. Kwa amri ya Yesu, malango ya Yerusalemu Mpya yanafungwa, na majeshi ya Shetani yanazingira
Jiji lile na kujitayarisha kufanya shambulio.
(665) Sasa Kristo anajitokeza tena mbele ya macho ya adui zake. Juu sana ya lile jiji, kwenye msingi wa
dhahabu iliyong’arishwa, kuna kiti cha enzi, kirefu kwenda juu na kikiwa kimeinuliwa juu. Kwenye kiti
hicho cha enzi ameketi Mwana wa Mungu, na wanaomzunguka pande zote ni wale raia wa ufalme wake.
Hakuna lugha inayoweza kueleza uweza na ukuu alio nao Kristo, hakuna kalamu iwezayo kuufafanua.
Utukufu wa Baba wa Milele unamfunika Mwana wake. Mng’ao wa uwepo wake unalijaza nuru Jiji la
Mungu, na unatirirka hadi mbali nje malango, ukiijaza dunia yote kwa mng’ao wake.
Karibu sana na kile kiti cha enzi wapo wale ambao wakati fulani walikuwa shupavu katika kazi ya
Shetani, lakini ambao, kwa kuopolewa kama kutoka motoni, wamemfuata Bwana wao kwa kujitoa kwa
bidii na kina. Wanaofuata ni wale walioonyesha tabia kamilifu za Kikristo katikati ya uongo na ukafiri,
wale walioiheshimu sheria ya Mungu wakati ambapo ulimwengu wa Kikristo ulikuwa unatangaza kwamba
haipo, na wale mamilioni, wa vizazi vyote, waliouawa kama wafia-dini kwa ajili ya imani yao. Na baada

385
ya hapo kuna ule “mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa,
na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo,
wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao.” Ufunuo 7:9. Vita yao imekwisha,
ushindi wao umepatikana. Wamepiga mbio na kupata thawabu. Tawi la mtende lililo mikononi mwao ni
ishara ya ushindi wao, vazi jeupe ni nembo ya haki ya Kristo isiyo na waa ambayo sasa ni yao.
Waliokombolewa wanapaza sauti zao na kuimba wimbo wa sifa ambao unatoa mwangwi tena na tena
katika anga la mbinguni, wakisema: “Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-
Kondoo.” Fungu 1a 10. Kisha malaika na maserafi wanaunganisha sauti zao katika kuabudu. Kwa kuwa
wale waliokombolewa wameuona uwezo na uovu wa Shetani, wameona, kwa namna ambavyo
hawajawahi kuona, ya kuwa hakuna uwezo wowote ambao ungeweza kuwafanya kuwa washindi
isipokuwa ule wa Kristo. Katika mkutano mkubwa ule unaong’aa hakuna wanaodhani kwamba wokovu
wao umetokana na uwezo wao wenyewe, kana kwamba walikuwa wameshinda kwa uwezo na wema wao
wenyewe. Hakuna kinachosemwa kuhusu yale waliyotenda au walivyoteseka; bali mzigo wa kila wimbo,
wazo kuu linalojitokeza katika kila wimbo, ni: Wokovu una Mungu wetu na Mwana-Kondoo.
(666) Mbele ya mkutano wa wakazi wa duniani na wa mbinguni kutawazwa kwa mwisho kwa Mwana wa
Mungu kunafanyika. Na sasa, yeye akiwa amepewa fahari kuu na uweza mkuu, Mfalme wa wafalme
anatamka hukumu juu ya waasi dhidi ya serikali yake na kutekeleza haki yake juu ya wale walioivunja
sheria yake na kuwakandamiza watu wake. Nabii wa Mungu anasema: “Kisha nikaona kiti cha enzi,
kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali
pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha
enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu
wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.”
Ufunuo 20:11,12.
Mara tu vitabu vya kumbukumbu vinapofunguliwa, na jicho la Yesu linapowatazama waovu, wanapata
ufahamu kuhusu kila dhambi waliyopata kuitenda. Wanaona mahali ambapo miguu yao iligeukia kando
na kuiacha njia ya usafi wa maisha na utakatifu, wanaona kiasi gani kiburi chao na uasi wao
vimewapeleka mbali katika kuivunja sheria ya Mungu. Vishawishi vya majaribu ambavyo walihamasisha
kwa kujifurahisha katika dhambi, mibaraka iliyopotoshwa, wajumbe wa Mungu waliodharauliwa,
maonyo yaliyokataliwa, mawimbi ya rehema yaliyosukumwa na kurudishwa nyuma kwa usumbufu, moyo
ambao haukutubu - yote yanaonekana kama yameandikwa kwa moto.
Juu ya kile kiti cha enzi unadhihirishwa msalaba; na kama mwonekano wa senema yanajitokeza matukio
ya kujaribiwa na kuanguka kwa Adamu, na hatua zilizofuata katika mpango mkuu wa ukombozi.
Kuzaliwa kwa Yesu katika hali ya chini sana; maisha yake ya awali mepesi na ya utii; ubatizo wake
katika Yordani; kufunga na kujaribiwa nyikani; huduma yake ya hadhara, akiwafunulia wanadamu
mibaraka ya thamani ya mbinguni; siku zile zilizojaa matendo ya upendo na huruma, zile nyakati za
usiku za maombi na kukesha katika sehemu za upweke milimani; mipango ile ya hila, wivu, chuki, na nia
mbaya ambavyo alilipwa kwa wema wake; maumivu ya ajabu ya kutisha katika Gethsemane akiwa chini
ya mkandamizo wa uzito wa mzigo wa dhambi za ulimwengu wote; kusalitiwa kwake mikononi mwa
kundi la wauaji (667) wenye ghasia; matukio ya kuogofya ya usiku ule wa kutisha - mfungwa asiyetoa
upinzani, aliyeachwa na wanafunzi wake aliowapenda sana, akisukumwa kikatili kupitia katika mitaa ile
ya Yerusalemu; Mwana wa Mungu akifanywa kama maonyesho ya kufurahisha mbele ya Anasi,
akishtakiwa katika ukumbi wa kuhani mkuu, katika ukumbi wa hukumu wa Pilato, mbele ya Herode yule
mwoga na katili, akidhihakiwa, akitukanwa, akiteswa, na kuhukumiwa kufa - yote hayo yanaonyeshwa
waziwazi.
386
Na sasa mbele ya mwonekano wa watu wale yanaonyeshwa matukio yale ya mwisho – mvumilivu
Anayeteswa akitembea njiani kuelekea Kalvari; Mfalme wa mbinguni akiwa ananing’inia kwenye
msalaba; makuhani wenye majivuno na mkusanyiko wa watu wenye vurugu, wakimdhihaki katika
maumivu yake makali ya kukata roho; giza lisilo la kawaida; tetemeko la nchi, miamba iliyopasuka,
makaburi yaliyofunguka, vyote vikikamilisha wakati ambao Mkombozi wa ulimwengu aliyatoa maisha
yake.
Maonyesho hayo ya kuogofya yanaonekana kama vile yalivyokuwa. Shetani, malaika zake, na wale walio
chini yao wanageuza nyuso kuangalia kwingine ili wasiione picha ile ya kazi yao. Kila mhusika
anakumbuka sehemu yake aliyofanya katika matukio yale. Herode, aliyewachinja watoto wasio na hatia
wa Bethlehemu ili kumwangamiza Mfalme wa Israeli; Herodia asiye na uadilifu, ambaye damu ya Yohana
Mbatizaji iko juu ya nafsi yake yenye hatia; Pilato aliyekuwa dhaifu na mwepesi kuokoa muda; askari
wale waliomdhihaki; makuhani na wakuu pamoja na mkusanyiko wa watu waliokuwa kama vichaa,
waliopiga kelele, wakisema, “Damu yake na iwe juu yetu, na juu ya watoto wetu!” - wote wanaona
ukubwa wa hatia yao. Wanajitahidi pasipo mafanikio kujificha mbali na mwonekano wa ukuu wake wa
uungu, ukiangaza utukufu wa jua, wakati wale waliokombolewa wakizitupa taji zao miguuni pa
Mwokozi, na kusema kwa mshangao: “Alikufa kwa ajili yangu mimi!”
Miongoni mwa umati ule wa waliokombolewa wamo mitume wa Kristo, Paulo mwenye ushujaa, Petro
aliyekuwa mwenye usikivu, Yohana aliyependwa kupenda sana, pamoja na ndugu zao waliokuwa na
moyo wa kweli, na pamoja nao likiwepo jeshi kubwa la wafia-dini; wakati nje ya kuta, wakiwa na kila
hali ya unyonge na kuchukiza, wapo wale waliowatesa, waliowafunga, na kuwaua. Yupo Nero, jitu la
ukatili na uovu mkubwa, akiitazama furaha na utukufu wa wale aliowatesa wakati fulani, na ambao
katika mateso yao makubwa yeye alipata furaha ya kishetani. Mama yake yupo pale kushuhudia
matokeo ya (668) kazi yake huyo mama; kuona jinsi tabia yake mbaya ilivyohamia kwa mwanawe,
hasira kali alizohimiza na kuendeleza kwa ushawishi wake na kielelezo chake, zimezaa matunda katika
uhalifu uliosababisha dunia kutetemeka.
Wapo makasisi wa upapa na viongozi wa juu wa kanisa, waliojidai kwamba ni mabalozi wa Kristo,
wakati walitumia kitanda cha kutesea watu, magereza ya chini ya ardhi, na nguzo ya kuchomea watu
moto ili wapate kudhibiti dhamiri za watu wake Kristo. Wapo wale mapapa wenye majivuno waliojiinua
juu kuliko Mungu na kujidai kuibadili sheria yake yeye Aliye Juu. Wale waliojifanya kuwa mababa wa
kanisa wana hesabu ya kutoa kwa Mungu ambayo wangetamani kusamehewa wasiitoe. Wakiwa
wamechelewa wanawezeshwa kutambua kwamba yeye Ajuaye Yote anaona wivu kwa sheria yake na ya
kwamba kwa vyovyote vile hawezi kuifuta hatia. Sasa wanajifunza kwamba Kristo anaonyesha mapenzi
yake miongoni mwa watu wake wanaoteswa; na wanahisi nguvu ya maneno yake aliyosema kwamba:
“Kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.” Mathayo
25:40.
Ulimwengu wote wa waovu unasimama ukishtakiwa katika kizimba cha Mungu kwa mashtaka ya usaliti
dhidi ya serikali ya mbinguni. Hawana mtu wa kuwatetea katika kesi yao hiyo; hawana udhuru; na
hukumu ya mauti ya milele inatamkwa juu yao.
Sasa imedhihirika kwa wote kwamba mshahara wa dhambi sio uhuru na uzima wa milele, bali utumwa,
uharibifu, na mauti. Waovu wanaona kile walichokipoteza kutokana na maisha yao ya uasi. Utukufu wa
milele uzidio kuwa mwingi sana ulidharauliwa ulipotolewa kwao; lakini unaonekana kwa kutamanika
kiasi gani sasa. Mtu huyo aliyepotea analia, akisema: “Ningeweza kuyapata yote haya; lakini nilichagua
kuyaweka haya mbali nami. Lo! kupumbazika kwa ajabu! Nimebadilishana nikitoa amani, furaha, na

387
heshima kwa kupata taabu, aibu, na kukosa tumaini.” Wote wanaona kwamba kuzuiwa kwao kuingia
mbinguni ni kwa haki. Kwa maisha yao wametangaza kwamba: “Hatutaki kuwa na mtu huyu [Yesu]
atutawale.”
Kana kwamba wamevutiwa, waovu wameangalia kutawazwa kwa Mwana wa Mungu. Wanaona mikononi
mwake zile mbao mbili za sheria ya Mungu, amri zile ambazo (669) wao wamezidharau na kuzivunja.
Wanashuhudia mlipuko wa mshangao, furaha, na kuabudu zinazotoka kwa waliookolewa; na wimbi la
auti za wimbo zinapovuma juu ya umati ule mkubwa ulio nje ya jiji, wote kwa pamoja wanasema kwa
nguvu, “Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli njia
zako, Ee Mfalme wa mataifa” (Ufunuo 15:3); kisha, wanaanguka kifudifudi, na kumwabudu huyo Mfalme
wa uzima.
Shetani anaonekana kupooza kadiri anavyouona utukufu na ukuu wa Kristo. Yeye ambaye hapo zamani
alikuwa kerubi afunikaye anakumbuka mahali alikoanguka. Serafi ang’aaye, “mwana wa asubuhi,” jinsi
alivyobadilika, jinsi alivyoshushwa! Kutoka katika baraza lile ambamo wakati fulani alikuwa
anaheshimiwa, ametengwa nalo milele. Anamwona mwingine sasa akisimama karibu na Baba, akifunika
utukufu wa Baba. Ameona malaika yule mrefu, mwenye utukufu akiweka taji ya kifalme kwenye kichwa
cha Kristo, na anajua kwamba nafasi ile ya malaika iliyotukuzwa ingeweza kuwa yake.
Kumbukumbu zake zinarejea katika makao yake wakati akiwa msafi na asiye na hatia, amani na
kutosheka vilikuwa vyake hadi alipojiingiza katika manung’uniko dhidi ya Mungu, na kuwa na wivu dhidi
ya Kristo. Mashtaka yake, uasi wake, madanganyo yake ili kutaka kuhurumiwa na kuungwa mkono na
malaika, ukaidi wake wa kudumu katika kutofanya juhudi ya kubadili msimamo wake na kujirejesha
wakati ambapo bado Mungu angempatia msamaha - yote yanakuja mbele yake wazi wazi. Anatathmini
kazi yake miongoni mwa wanadamu na matokeo yake, - uadui wa mtu kwa mtu mwenzake, maangamizi
ya kutisha ya maisha, kuinuka na kuanguka kwa falme, mapindunzi ya utawala, mfululizo mrefu wa
machafuko, mapigano, na mapinduzi ya serikali. Anakumbuka juhudi zake za wakati wote katika
kuipinga kazi ya Kristo na kumzamisha mwanadamu chini zaidi na zaidi. Anaona kwamba mipango yake
ya hila za kuzimu imekuwa isiyo na nguvu kuwaharibu wale walioweka tumaini lao kwa Yesu. Kadiri
Shetani anavyangalia ufalme wake, matunda ya kazi yake, anaona kushindwa na uharibifu tu.
Amewafanya watu wengi kuamini kwamba Jiji la Mungu lingetekwa kwa urahisi; lakini anajua kwamba
huo ni uongo. Tena na tena, katika maendeleo ya pambano kuu, ameshindwa na kulazimishwa kusalimu
amri. Anaujua vema uweza na ukuu wa yule wa Milele.
(670) Lengo la mwasi mkuu daima limekuwa ni kujihalalisha mwenyewe na kuthibitisha kuhusika kwa
serikali ya Mungu kwa maasi yale. Amejitahidi kufikia lengo hili kwa kuelekeza nguvu zake zote za akili
yake nyingi hapo. Amefanya kazi kwa makusudi ya dhati na kwa utaratibu uliopangiliwa, na kwa
mafanikio makubwa ya kushangaza, akiwafanya watu wengi sana kukubali mwelekeo wake wa pambano
kuu ambalo limeendelea kwa kwa muda mrefu. Kwa maelfu ya miaka kiongozi huyu wa mipango miovu
ameendeleza uongo kama ukweli. Lakini sasa wakati umefika kwa maasi hayo hatimaye kushindwa na
historia na tabia yake Shetani kufichuliwa. Katika juhudi yake kubwa ya mwisho kutafuta kumwondoa
Kristo kwenye kiti cha enzi, kuwaangamiza watu wake, na kulitwaa Jiji la Mungu, mdanganyifu mkuu
huyo amewekwa amewekwa wazi. Wale waliojiunga naye wanaona kushindwa kwa kazi yake kwa
ujumla. Wafuasi wa Kristo na malaika watiifu wanaona kwa ukamilifu njama zake dhidi ya serikali ya
Mungu. Yeye ndiye wa kuchukiwa kwa ujumla.
Shetani anaona kwamba maasi yake ya kujitakia yamemfanya asiyefaa kukaa mbinguni. Ameziongoza
nguvu zake kupigana vita dhidi ya Mungu; usafi, amani, na utulivu wa mbinguni vitakuwa mateso

388
makubwa sana kwake. Mashtaka yake dhidi ya rehema na haki ya Mungu sasa yamenyamazishwa.
Shutuma alizojitahidi kuelekeza kwa Yehova kwa ujumla zinamkalia yeye mwenyewe. Na sasa Shetani
anainama na kukiri kwamba hukumu aliyopewa ni ya haki.
“Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa
maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha
kufunuliwa.” Fungu la 4. Kila hoja ya kweli na uongo katika pambano hilo lililodumu kwa muda mrefu
sasa imefunuliwa wazi. Matokeo ya maasi, matunda ya kuziweka kando amri za Mungu, yamewekwa
wazi mbele ya macho ya viumbe wote. Utendaji wa utawala wa Shetani kama unavyotofautiana na ule
wa serikali ya Mungu umeonyeshwa kwa malimwengu yote. Shetani amehukumiwa na kazi zake
mwenyewe. Hekima ya Mungu, haki yake, na wema wake vinasimama vikiwa vimethibitika. Inaonekana
kwamba namna Mungu alivyoshughulikia mambo katika pambano kuu ni (671) kwa kuzingatia usitawi wa
milele wa watu wake na usitawi wa malimwengu yote aliyoyaumba. “Ee BWANA, kazi zako zote
zitakushukuru, na wacha Mungu wako watakuhimidi.” Zaburi 145:10. Historia ya dhambi itadumu
kusimama milele zote kama ushahidi kwamba furaha ya viumbe vyote alivyoviumba Mungu
imefungamana na kuwapo kwa sheria yake. Kwa kuonekana kwa matukio yote ya pambano kuu,
malimwengu yote, ya wale walio watiifu na wa wale walioasi, wanatangaza kwa kauli moja: “Ni za haki,
na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.”
Mbele ya macho ya malimwengu imeonyeshwa wazi ile kafara kuu iliyotolewa na Baba na Mwana kwa
ajili ya mwanadamu. Saa imefika kwa Kristo kuweza kukaa katika nafasi yake halali na anatukuzwa juu
ya falme na mamlaka zote na kila jina linalotajwa. Ilikuwa kwa furaha iliyowekwa mbele yake – ya
kwamba apate kuwaleta wana wengi kwenye utukufu - kwamba aliustahimili ule msalaba na kuidharau
aibu. Na ingwa huzuni na aibu ile ilikuwa kubwa isivyowezekana kufikiri, furaha na utukufu wake ni
mkubwa zaidi. Anawatazama wale waliokombolewa, wakiwa wamefanywa upya katika sura yake, kila
moyo ukiwa na chapa ya kamilifu ya uungu, kila uso ukiakisi mfanano wa Mfalme wao. Anaona ndani yao
taabu ya nafsi yake, na anaridhika. Kisha, kwa sauti inayoufikia mkutano mkubwa sana uliokusanyika
pale wa wenye haki na wa waovu, anasema: “Tazameni hao walionunuliwa kwa damu yangu! Kwa ajili
ya hao mimi niliteswa, kwa ajili yao mimi nilikufa, ili wapate kukaa mbele zangu milele hata milele.”
Na wimbo wa sifa unapaa juu kutoka kwa wale waliovikwa mavazi meupe ambao wamekizunguka kile
kiti cha enzi, wakisema: “Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na hekima na
nguvu na heshima na utukufu na baraka.” Ufunuo 5:12.
Licha ya kwamba Shetani amelazimishwa kukiri haki ya Mungu na kuuinamia ukuu wa Kristo, tabia yake
inabaki bila kubadilika. Roho ya uasi, kama bubujiko la maji yenye nguvu, inalipuka tena. Akiwa
amejazwa na roho isiyojitawala, anadhamiria kutokukubali kushindwa katika pambano kuu. Wakati
umefika wa kufanya pambano muhimu la mwisho dhidi ya Mfalme wa mbinguni. Anakimbia kwenda
katikati ya wale waovu na kujitahidi sana kuwaambukiza ghadhabu yake na kuwamsha kwa ajili ya vita
ya haraka. Lakini miongoni mwa mamilioni wale wasiyohesabika ambao alikuwa amewadanganya kuingia
katika maasi, hakuna hata mmoja sasa anayekiri ukuu wake. Nguvu zake ziko mwishoni. Waovu
wamejawa na chuki ile ile inayochochewa na Shetani dhidi ya Mungu; lakini wanatambua kwamba suala
lao halina matumaini, kwamba hawawezi kumshinda Yehova. Ghadhabu yao inawaka dhidi ya Shetani na
wale waliokuwa mawakala wake katika udanganyifu, na wakiwa na hasira ya mapepo wanawarukia.
Bwana anasema: “Kwa kuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu; basi, tazama, nitaleta wageni
juu yako, watu wa mataifa wenye kutisha; nao watafuta panga zao juu ya uzuri wa hekima yako, nao
watautia uchafu mwangaza wako. Watakushusha hata shimoni.” “Nami nimekuangamiza, Ewe kerubi
ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto…. Nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme,
389
wapate kukutazama…. Umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele.” Ezekieli 28:6-
8,16-19.
“Maana kila pambano la askari wa vita lina makelele yaliyojaa ghasia, na mavazi yaliyofingirishwa
katika damu; lakini hayo yatakuwa tayari kuteketezwa, yatakuwa kuni za kutiwa motoni.” “Maana
BWANA ana ghadhabu juu ya mataifa yote, na hasira kali juu ya jeshi lao lote; amewaangamiza kabisa,
amewatoa waende kuchinjwa.” “Juu ya waovu atawanyeshea makaa ya moto yanayowaka upesi, moto
na kiberiti na upepo mkali wa kutisha; hilo ndilo fungu la kikombe chao.” Isaya 9:5; 34:2; Zaburi 11:6.
Moto unashuka chini kutoka mbinguni kwa Mungu. Dunia inapasuka-pasuka. Silaha za vita zilizofichwa
chini ya ardhi zinatupwa juu. Ndimi za moto zinazoteketeza kila kitu zinalipuka kutoka katika kila uwazi
wa mpasuko wa ardhi. Miamba inawaka moto. Siku ile inayowaka kama tanuru imekuja. Viumbe vya asili
vinaunguzwa kwa moto mkali, na nchi pia, na kazi zote zilizomo ndani yake zinateketezwa kabisa.
Malaki 4:2; 2 Petro 3:10. Uso wa dunia unaonekana kama bonge lililoyeyuka - ziwa kubwa (673) sana la
moto linalochemka. Huu ni wakati wa hukumu na maangamizi ya waovu - “Siku ya kisasi cha BWANA,
mwaka wa malipo, ili kushindania Sayuni.” Isaya 34:8.
Waovu wanapata malipo yao hapa hapa duniani. Mithali 11:31. Watakuwa “makapi; na siku ile inayokuja
itawateketeza, asema BWANA wa majeshi.” Malaki 4:1. Wengine wanateketea kama kwa muda mfupi,
wakati wengine wanaumia kwa siku nyingi. Wote wanapata adhabu yao kwa “kadiri ya matendo yao.”
Dhambi zile za wenye haki zikiwa zimekwisha kuhamishiwa kwa Shetani, atapewa maumivu ambayo si
uasi wake tu, bali pia kwa dhambi zote alizowafanya watu wa Mungu kuzitenda. Adhabu yake itakuwa
kwa mbali kubwa sana kuliko ya wale aliowadanganya. Baada ya kuteketezwa wote walioangukia
dhambini kutokana na madanganyo yake, yeye ataendelea kuwa hai na kuumia. Katika miale ile
inayosafisha uchafu wote, hatimaye waovu wote watateketezwa, mzizi na tawi - Shetani ndiye mzizi,
wafuasi wake ndio matawi. Adhabu kamili ya kuivunja sheria imepatilizwa; matakwa ya haki yatakuwa
yametimizwa; na mbingu na nchi, zinazotazama, zitatangaza haki ya Yehova.
Kazi ya Shetani ya maangamizi imekomeshwa milele. Kwa miaka elfu sita amefanya mapenzi yake,
akiijaza dunia kwa misiba na kusababisha huzuni kubwa katika malimwengu yote. Uumbaji wote
umeugua na kuteseka kwa maumivu makali. Sasa viumbe vya Mungu vimekombolewa milele na kuwekwa
mbali na uwepo wake na majaribu yake. “Dunia yote inastarehe na kutulia; hata huanzilisha kuimba.”
Isaya 14:7. Na kelele za sifa na ushindi zinapanda juu kutoka kwa malimwengu yote yaliyo na utiifu.
“Sauti ya makutano mengi,” “kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu,” inasikika,
ikisema: “Haleluya; kwa kua Bwana Mungu wetu, Mwenyezi,amemiliki.” Ufunuo 19:6.
Wakati dunia ilipokuwa imefunikwa na moto wa maangamizi, watakatifu walikaa salama katika lile Jiji
Takatifu. Juu ya wale waliokuwa na sehemu katika ufufuo ule wa kwanza, mauti ya pili haina nguvu.
Wakati Mungu ni moto ulao kwa waovu, kwa watu wake yeye ni jua na ngao. Ufunuo 20:6; Zaburi 84:11.
(674) “Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza
zimekwisha kupita.” Ufunuo 21:1. Moto ule unaowateketeza waovu unaitakasa dunia. Kila dalili ya laana
inafagiliwa mbali. Hakuna moto wa jehanum ya milele utakaoendelea kuwaka mbele ya
waliokombolewa ukileta kumbukumbu ya kuogofya ya matokeo ya dhambi.
Kumbukumbu moja tu ndiyo inasalia: Mwokozi wetu atabaki na alama za kusulibiwa kwake milele. Juu
ya kichwa chake kilichojeruhiwa, ubavuni pake, katika mikono na miguu yake, kuna ishara za kazi ya
kikatili iliyofanywa na dhambi. Nabii anasema, akimwangalia Kristo katika utukufu wake: “Mwangaza
wake ulikuwa kama nuru; Alikuwa na mishale ya nuru ubavuni pake; ndipo ulipofichwa uweza wake.”
Habakuki 3:4. Katika ubavu uliochomwa kwa mkuki mahali pale ilipobubujika chemchemi ambayo
390
ilimpatanisha mwanadamu na Mungu - kuna utukufu wa Mwokozi, pale “ndipo ulipofichwa uweza wake.”
“Hodari wa kuokoa,” kwa njia ya kafara yake ile ya ukombozi, kwa sababu hiyo, yeye alikuwa na uwezo
wa kutekeleza haki juu ya wale walioidharau rehema ya Mungu. Na alama za kudhalilishwa kwake ndizo
heshima yake ya juu sana; katika zama zote milele majeraha ya Kalvari yataonyesha sifa zake na
kutangaza uweza wake.
“Na wewe, Ee mnara wa kundi, kilima cha binti Sayuni, utajiliwa; naam, mamlaka ya kwanza yatakuja.”
Mika 4:8. Wakati umefika ambao watakatifu waliutazamia kwa shauku nyingi tangu upanga uwakao
moto ulipowazuia kuingia Edeni watu wale mume na mke wa kwanza, ni wakati wa “ukombozi wa milki
yake.” Waefeso 1:14. Dunia mwanzoni ikiwa ilikabidhiwa kwa mwanadamu ili iwe ufalme wake, na kwa
kukosa uaminifu kwake ikaangukia mikononi mwa Shetani, na kushikiliwa na adui huyo kwa muda mrefu
sana, imerejeshwa kwa njia ya mpango mkuu wa Ukombozi. Kila kilichopotezwa na dhambi,
kimerejeshwa. “Maana BWANA, aliyeziumba mbingu, asema hivi … aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye
aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ikaliwe na watu.” Isaya 45:18. Kusudi la Mungu la tangu
mwanzo katika kuiumba dunia hii limetimizwa wakati inapofanywa kuwa makao ya milele ya
waliokombolewa. “Wenye haki watairithi nchi, nao watakaa humo milele.” Zaburi 37:29.
Hofu ya kuufanya urithi wa baadaye kuonekana sana kama kitu halisi kinachoshikika (675) imewafanya
wengi kuzifikiria kama za kiroho zaidi zile kweli zenyewe zinazotufanya kuuangalia urithi huo kama
makao yetu. Kristo aliwahakikishia wanafunzi wake kwamba alikwenda kuwaandalia makao katika
nyumba ya Baba yake. Wale wanaoyakubali mafundisho ya neno la Mungu hawatakuwa wajinga kabisa
kuhusu makao yao ya mbinguni. Na tena, “mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia,
wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.” 1
Wakorintho 2:9. Lugha ya mwanadamu haitoshi kuelezea thawabu ile ya wenye haki. Itajulikana tu kwa
wale waionao. Hakuna akili finyu ya kibinadamu iwezayo kuelewa utukufu wa ile Paradiso ya Mungu.
Katika Biblia urithi wa waliookolewa unaitwa “nchi.” Waebrania 11:14-16. Mle Mchungaji wa mbinguni
anawaongoza kondoo zake kwenye chemchemi za maji yaliyo hai. Mti wa uzima unazaa matunda yake
kila mwezi, na majani yake ni ya kuwaponya mataifa. Kuna mito inayodumu kutiririka, yenye maji safi
kama kioo, na kando yake iko miti inayopepea ikivitupa vivuli vyake kwenye njia zake zilizoandaliwa
kwa ajili ya waliokombolewa na Bwana. Mle tambarare pana zinazoinuka na kuwa vilima vizuri, na
milima ya Mungu ina vilele vyake vilivyoinuka juu sana. Katika mbuga zile za amani, kando ya mito ile
ya maji yaliyo hai, watu wa Mungu, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wasafiri na wapitaji, watapata
makao yao.
“Na watu wangu watakaa katika kao la amani; na katika maskani zilizo salama, na katika mahali pa
kupumzikia penye utulivu.” “Jeuri haitasikiwa tena katika nchi yako, ukiwa na uharibifu hazitakuwa
mipakani mwako; bali utaziita kuta zako, Wokovu, na malango yako, Sifa.” “Nao watajenga nyumba, na
kukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake. Hawatajenga akakaa mtu mwingine
ndani yake; hawatapanda, akala mtu mwingine,… na wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao.”
Isaya 32:18; 60:18; 65:21,22.
Pale “nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi.”
“Badala ya michongoma utamea msunobari, na badala ya mibigili, mhadesi.” “Mbwa-mwitu atakaa
pamoja na mwana-kondoo, na chui (676) atalala pamoja na mwanambuzi;… na mtoto mdogo
atawaongoza.” “Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu,” asema Bwana.
Isaya 35:1; 55:13; 11:6,9.

391
Maumivu hayawezi kuweepo katika mazingira ya mbinguni. Machozi hayatakuwapo tena, wala misafara
ya mazishi, wala nguo za matanga. “Wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio;… kwa
kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.” “Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa;
watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.” Ufunuo 21:4; Isaya 33:24.
Kuna Yerusalemu Mpya, mji mkubwa wa nchi mpya, uliojaa utukufu mwingi, “taji ya uzuri katika mkono
wa BWANA, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako.” “Na mwangaza wake ulikuwa mfano
wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi.” “Na mataifa ya wale waliookolewa watatembea
katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.” Asema hivi Bwana: “Nami
nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu.” “Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na
wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu
mwenyewe atakuwa pamoja nao, na kuwa Mungu wao.” Isaya 62:3; Ufunuo 21:11,24; Isaya 65:19;
Ufunuo 21:3.
Katika Jiji la Mungu “hapatakuwa na usiku tena.” Hakuna yeyote atakayehitaji au atakayetamani
kupumzika. Hapatakuwa na uchovu kule katika kufanya yaliyo mapenzi ya Mungu na kulisifu jina lake.
Daima tutajisikia kuwa na nguvu mpya za asubuhi, na daima tutakuwa mbali na kuishiwa nguvu kama
mwishoni mwa siku. “Wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia
nuru.” Ufunuo 22:5. Nuru ya jua itazidiwa na nuru ile inayometameta bila kuumiza macho, lakini
ambayo inang’aa sana kuliko nuru ya adhuhuri. Utukufu wa Mungu na wa Mwana-Kondoo unaligharikisha
Jiji la Mungu kwa nuru isiyofifia. Wale waliokombolewa wanatembea katika utukufu usio wa jua wa
mchana usiokoma.
“Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu
lake.” Ufunuo 21:22. Watu wa Mungu wanajaliwa fursa ya kuongea moja kwa moja na Baba na Mwana.
“Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo, kwa jinsi ya fumbo.” (677) 1 Wakorintho 13:12. Tunaiona
sura ya Mungu ikiakisiwa, kama katika kioo, katika kazi zake za uumbaji na katika kushughulika kwake
na wanadamu; lakini wakati ule tutamwona uso kwa uso, bila kuwepo pazia la kupunguza nuru kati yake
na sisi. Tutasimama mbele zake na kuuona utukufu wa uso wake.
Kule waliokombolewa watajua, kama vile ambavyo wanajulikanaa. Upendo na hisia zao za huruma
ambazo Mungu mwenyewe amezipandikiza moyoni vitapata nafasi ya kuwekwa katika matendo ya kweli
na matamu kule. Ushirikiano safi na viumbe watakatifu, maisha ya kijamii mazuri pamoja na malaika
wabarikiwa, na waaminifu wote wa vizazi vyote walioyafua mavazi yao na kuyafanya meupe katika
damu ya Mwana-Kondoo, vifungo vile vitakatifu vinavyowafunga pamoja watu wa “familia yote ya
mbinguni na ya duniani” (Waefeso 3:15) - hivi vinachangia kufanya furaha ya waliokombolewa.
Kule, watu wenye akili zisizo na ukomo watatafakari kwa furaha isiyokoma maajabu ya uweza wa
uumbaji, siri za upendo ukomboao. Kule hatakuwako adui katili, na mdanganyifu atakayewajaribu ili
wamsahau Mungu. Kila akili itakuzwa, kila uwezo utaongezeka. Kupata maarifa hakutachosha akili wala
kupunguza nguvu za mwili. Kule kazi kubwa mno zinaweza kufanywa, malengo makubwa kufikiwa, nia
ya kufanya mambo makubwa kutimizwa; lakini bado vitainuka vilele vipya vya kupita, maajabu mapya
ya kushangaa, kweli mpya za kuelewa, vitu vipya vitakavyohitaji nguvu za akili, roho na mwili.
Hazina zote za malimwengu zitakuwa wazi ili kuchunguzwa na waliokombolewa wa Mungu. Wakiwa
hawafungwi na mwili huu unaokufa, wataruka kwa mabawa bila kuchoka kwenda kwenye malimwengu
ya mbali – malimwengu yale yaliyotetemeka kwa huzuni yalipoiona misiba iliyowapata wanadamu, na
waliopiga kelele kwa nyimbo za furaha walipopata habari ya kukombolewa kwa mtu. Kwa furaha
isiyotamkika wana wa dunia wanaingia katika furaha na hekima ya viumbe wale ambao hawakuanguka
392
dhambini. Wanashiriki katika maarifa na ufahamu wao uliopatikana katika vizazi na vizazi kwa
kuitafakari kazi ya mikono ya Mungu. Wakiwa na macho yasiyo na mipaka ya uhafifu wanaangalia wa
uumbaji - majua, nyota na mifumo ya nyota, vyote vikienda katika mpangilio viliowekewa kukizunguka
kiti cha enzi (678) cha Mungu. Juu ya vitu vyote, kuanzia kidogo sana hadi kikubwa sana, jina la
Mwumbaji limeandikwa, na ndani ya vyote unaonekana utajiri wa uweza wake.
Na ile miaka ya milele, kadiri inavyopita, bado italeta mafunuo mengi zaidi na utukufu mwingi zaidi
kuhusu Mungu na Kristo. Kadiri maarifa yanavyozidi kuongezeka, ndivyo upendo, kicho kwa Mungu, na
furaha vinavyoongezeka. Kadiri wanadamu wanavyojifunza zaidi kuhusu Mungu, ndivyo watakavyozidi
kushangaa kwa kupendezwa kuhusu tabia yake. Kadiri Yesu anavyowafunulia utajiri wa ukombozi na
mafanikio ya ajabu sana yaliyopatikana katika pambano kuu dhidi ya Shetani, mioyo ya waliokombolewa
inasisimka na kujitoa kwake zaidi, na kwa furaha nyingi sana wanacharaza vinubi vyao vya dhahabu; na
elfu kumi mara elfu kumi, na maelfu ya maelfu ya sauti zitaungana pamoja kwa nguvu kuvumisha
kibwagizo cha sifa.
“Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi na juu ya bahari, na vitu vyote
vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye
juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.” Ufunuo 5:13.
Pambano kuu limefika mwisho. Dhambi na wenye dhambi hawapo tena. Malimwengu yote yako safi.
Pigo la aina moja la amani na furaha linapiga katika uumbaji wote. Kutoka kwake yeye aliyeumba
vyote, hububujika uzima na nuru na furaha, katika ufalme wake wote katika maanga yasiyo na mpaka.
Kutoka katika chembe ndogo kabisa ya atomu hadi kwenye ulimwengu mkubwa kuliko yote, vitu vyote,
vyenye uhai na vile visivyokuwa na uhai, katika uzuri usiofunikwa na kivuli chochote na furaha kamilifu,
vinatangaza kwamba Mungu ni upendo.

393
KIAMBATANISHO
Maelezo ya Jumla
Masahihisho au maelezo yaliyofanywa na Wadhamini wa E. G. White Mnamo Novemba 19, 1956, na
Desemba 6, 1979
Uk 50. Majina ya Vyeo. - Katika aya zilizo katika Kanuni za Kanisa Katoliki (Catholic Canon Law, au,
Corpus Juris Canonici), Papa Innocent III anatangaza kwamba Papa wa Roma ni “msaidizi atawalaye
duniani mahali pa Mungu, yeye si mwanadamu tu, bali Mungu halisi;” na katika ufafanuzi wa kifungu
hicho inaelezwa kwamba hiyo ni kwa sababu yeye ni msaidisi atawalaye badala ya Kristo, tena kwamba
yeye ni “Mungu halisi na mwanadamu halisi.” Angalia katika Decretales Domini Gregorii Papae IX
(Decretals of the Lord Pope Gregory IX), Title 7, Ch. 3; Corpus Juris Canonici (2d Leipzig Ed., 1881),
Col. 99; (Paris, 1612), Tom. 2, Decretales, Col. 205. Hati zilizounda Amri hizo zilikusanywa na Gratiani,
aliyekuwa anafundisha katika Chuo Kikuu cha Bolgna kadiri ya mwaka 1140. Kazi yake iliongezewa na
kuhaririwa tena na Papa Gregory IX katika toleo lililotoka mwaka 1234. Hati nyingine zilionekana katika
miaka iliyofuata toka wakati hata wakati ikiwa ni pamoja na Extravagantes, zilizoongezwa karibu na
mwisho wa karne ya kumi na tano. Zote hizo, pamoja na Decretum zilizokusanywa na Gratian,
zilichapishwa kama Corpus Juris Canonici (Kanuni za Kanisa Katoliki) za mwaka wa 1582. Papa Pius X
aliidhinisha kuwekwa kwa amri hizo za mapapa katika Kanuni za Kanisa katika mwaka wa 1904, na
kanuni ile iliyotengenezwa ilianza kutumika rasmi mwaka 1918.
Kuhusu cheo hiki cha “Lord God the Pope” (Bwana Mungu Papa) angalia maelezo ya Extravagantes of
Pope John XXII, Title 14, Ch. 4. (Kuna vitabu vingine pia vimetajwa.)
680
Uk. 50 - Kutoweza Kukosea Kamwe (Infallibility). -Kuhusu fundisho hili la kutoweza kukosea kamwe
kama lilivyotangazwa katika kikao cha Baraza la Vatikani cha mwaka 1870-71, angalia Philip Schaff, The
Creeds of Christendom, Vol. 2, Dogmatic Decrees of the Vatican Council, pp 234-271, ambazo ndani
yake, maandishi ya Kilatini na ya Kiingereza yametumika. Kwa mjadala ajili ya mjadala angalia, kwa
mtazamo wa Kanisa Katoliki, katika The Catholic Encyclopedia, Vol 7, Art. “Infallibity,” iliyoandikwa na
Patrick J. Toner, p. 790. (Kuna rejea nyingine nyingi zemewekwa)
Uk. 52 - IBADA YA SANAMU. -“Ibada ya Sanamu … ilikuwa ni mojawapo ya mambo yaupotofu katika
Ukristo yaliyoingia kwa kunyatia na kama pasipo kuonekana. Upotofu huu haukujitokeza mara moja,
kama ulivyofanya uzushi mwingine, la sivyo ungekosolewa na kukemewa kwa nguvu: lakini ukiwa
umeanza kwa kujificha vilivyo, desturi moja baada ya nyingine iliingizwa taratibu kuhusianishwa na
ibada, mpaka kanisa likawa limezama katika ibada ya sanamu, sio tu kwamba bila kukabiliwa na
upinzani wenye nguvu, bali pia hata pasipo kulalamikiwa kwa namna yoyote yenye nguvu ya kulipinga
jambo hilo; na hatimaye jitihada ilipofanywa kuung’oa, uovu huo ulionekana ya kuwa ulikuwa
umeshaotesha mizizi sana kiasi cha kutoweza kuondolewa…. Jambo hilo linaweza kufuatiwa kwa
kuangalia mwelekeo wa ibada ya sanamu uliomo ndani ya moyo wa mwanadamu, na mwelekeo wake wa
kukitumikia kiumbe kuliko Muumbaji…
“Sanamu na picha ziliingizwa kanisani kwa mara ya kwanza, si kwa kusudi la kuziabudu, lakini kuwa
kama vitabu katika kuwafundishia wale waliokuwa hawawezi kusoma, au kuamsha moyo wa kumcha

394
Mungu ndani ya wengine. Ni kwa kiasi gani zilikidhi kusudi hilo ni jambo la kutiliwa mashaka; lakini,
hata tukikubali kwamba jambo hilo lilikuwa hivyo kwa muda fulani, mara moja lilikoma kuwa hivyo,
tena iligunduliwa kwamba picha zile na sanamu zilizoingizwa kanisani zilitia giza ndani ya mioyo ya
wale waliokuwa wajinga kuliko nuru na ziliidhalilisha kuliko kuiinua juu ibada ya yule aabuduye. Kwa
hali yoyote ile wakati zilikuwa zimekusudiwa kuyaelekeza mawazo ya watu kwa Mungu, ziliishia
kuwageuzia mbali naye na kuwafanya waabudu vitu vilivyotengenezwa.” - J. Mendham, The Seventh
General Council, the Second of Nicaea, Introduction, Pages iii-vi. (Kumbukumbu za maandishi
zimeonyeshwa hapa kwa wingi).
Uk. 53 - AMRI YA JUMAPILI YA KONSTANTINO. - Amri ile iliyotolewa na mfalme wa dola Konstantino
(Constantine) tarehe 7 Machi, 321 B.K., kuhusu siku ya kupumzika na kuacha kufanya kazi, inasomeka
hivi:
“Mahakimu na watu na mafundi-stadi wote wanaokaa mijini watalazimika kupumzika katika Siku Tukufu
ya Jua. Watu wale wa mashambani, hata hivyo, wanaweza kuendelea kwa uhuru kushughulika na kazi
zao za kulima mashamba, kwa sababu inatokea mara kwa mara kwamba hakuna siku nyingine zaidi
zinazofaa kwa upandaji wa mbegu za nafaka au kupanda mizabibu. Ili kwamba manufaa yale
yanayotolewa na Mungu wa mbinguni yasije yakapotea bure kwa kukosa nafasi ya muda huo mfupi.” -
Joseph Cullen Ayer, A Source Book for Ancient Church History (New York: Charles Scribner’s Sons,
1913), Div. 2, Per. 1, Ch. 1, Sec. 59, G, Pp. 284, 285. (Rejea nyingine zimetolewa hapa) (681)
Uk. 54 – SIKU ZA KIUNABII. - Kanuni muhimu katika kutafsiri unabii unaohusu wakati ni kanuni ile ya
mwaka mmoja-siku moja, ambayo katika hiyo siku moja ya wakati wa unabii inahesabika kama mwaka
mmoja wa kawaida. Kabla wana wa Israeli hawajaingia katika nchi ile Kanaani waliwatuma wapelelezi
12 kuichunguza. Wapelelezi wale walikuwa kule kwa siku arobaini, nao waliporudi Waebrania, wakiwa
wameingiwa na hofu kuu kutokana na taarifa yao, walikataa kupanda na kwenda kuikalia ile nchi ya
ahadi. Matokeo yake yalikuwa ni hukumu ambayo Bwana aliitoa kwao: “Kwa hesabu ya hizo siku
mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu,
ndiyo miaka arobaini.” Hesabu 14:34. Njia inayofanana na hiyo ya kuhesabu wakati ulio mbele
imedokezwa kupitia kwa nabii Ezekieli. Miaka arobaini ya adhabu kwa makosa yao iliungojea ufalme ule
wa Yuda. Bwana alisema hivi kupitia kwa nabii huyo: “Tena utakapozitimiza hizo, utalala kwa ubavu
wako wa kuume, nawe utauchukua uovu wa nyumba ya Yuda; siku arobaini, siku moja kwa mwaka
mmoja, nimekuagizia.” Ezekieli 4:6. Kanuni hiyo ya mwaka mmoja kwa siku moja ina matumizi yake ya
maana katika kutafsiri wakati wa unabii wa “nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu” (Danieli
8:14), pamoja na kipindi kile cha siku 1260, kilichoonyeshwa kwa njia mbalimbali kama “wakati, na
nyakati mbili, na nusu wakati” (Danieli 7:25;, tena kama “miezi arobaini na miwili” (Ufunuo 11:2; 13:5),
tena kama “siku elfu na mia mbili na sitini” (Ufunuo 11:3; 12:6).
Uk. 56 – MAANDIKO YA KUGHUSHI. - Miongoni mwa hati ambazo kwa wakati huu wa sasa zinakubaliwa na
watu wote kuwa ni za kughushi au za bandia, “Donation of Contantine (Mchango wa Konstantino)
pamoja na zile za Pseudo-Isdorian Decretals (Mkusanyo wa Amri za Mapapa wa Isidori wa Uongo).
“Mchango wa Konstantino” ni jina linalotumika kimapokeo, kuanzia sehemu ya mwisho ya Zama za Kati,
kwa hati inayosemekana kwamba ilipelekwa na Konstantino Mkuu kwa Papa Sylvester I, ambayo
inapatikana kwanza katika hati ya mkono ya Paris (Codex lat. 2777), ambayo huenda iliandikwa mwanzo
wa karne ya tisa. Tangu karne ya kumi na moja hati hiyo imetumika kama hoja yenye nguvu
inayoyaunga mkono madai ya kipapa, na matokeo yake ni kwamba kuanzia karne ya kumi na mbili
imekuwa kiini cha mabishano makali sana. Kwa wakati huo, kwa kuufanya upapa ufikiriwe kuwa ni kitu
cha hivi karibuni kilichoingia katikati ya Dola Asilia ya Roma na Dola ya Roma ya Zama za Kati, na kwa
395
njia hiyo kuweka msingi wa kinadharia wa kuviunganisha vipindi hivyo viwili bila kukatika kwa
kuendelea kuzipokea sheria za serikali ya Kirumi katika Zama zile za Kati, ushawishi wake si mdogo
katika historia ya ulimwengu.” -The New (682) Schaff-Herzog Encyclopedia of Religious Knowledge, Vol.
3, Art. "Donation of Constantine," pp. 484, 485.
Nadharia hiyo ya kihistoria iliyokuzwa kwa njia ya huo “Mchango” imejadiliwa kikamilifu katika kitabu
cha Henry E. Cardinal Manning, kiitwacho The Temporal Power of the Vicar of Jesus Christ, London,
1862. Hoja kuhusu huo “Mchango” zilikuwa ni za aina ya kisomi na uwezekano wa kughushi haukutajwa
mpaka ulipotokea uhakiki wa historia katika karne ile ya kumi na tano. Nicholas of Cusa alikuwa mtu wa
kwanza aliyetoa hitimisho lake kwamba Konstantino hakuwa amepata kamwe kutoa mchango kama ule.
Lorenzo Valla wa Italia alionyesha kwa wazi kabisa uongo wa hati ile katika mwaka 1450. Angalia kitabu
cha Christopher B. Coleman cha Treatise of Lorenzo Valla on the Donation of Constantine (New York,
1927). Walakini, kwa karne moja zaidi imani juu ya uhalali wa ule “Mchango wa Konstantino” pamoja na
False Decretals ilidumishwa. Kwa mfano, Martin Luther mara ya kwanza alizikubali amri zile za mapapa,
lakini katika muda ule mfupi alimwambia Eck: “Mimi nazikana amri hizo za mapapa;” na kwa Spalatini,
alisema: “Papa katika amri zake anamnajisi na kumsulibisha Kristo, anaisulibisha ile kweli.”
Inasadikiwa ya kuwa imekwisha kuthibitishwa kwamba ule “Mchango” ni (1) hati ya kughushi, (2) kazi ya
mtu fulani mmoja au ya kipindi fulani kimoja, (3) yule aliyeghushi maandiko hayo ametumia hati za
zamani mno, (4) kughushi huko kulitokea karibu na mwaka wa 752 na 778. Kwa upande wa Wakatoliki,
wao walikwisha kuachilia mbali kutetea uhalali wa hati hiyo pamoja na Baronius katika kitabu chake cha
Ecclesiastical Annals, katika mwaka wa 1592. (Vitabu na nyaraka za rejea zimetajwa hapa).
“Maandiko ya Uongo” yaliyotajwa katika maandiko haya yanajumuisha pia Pseudo-Isdorian Decretals,
pamoja na maandiko mengine ya kughushi. Maandishi hayo ni nyaraka za uongo zinazosemekana
kwamba zilitolewa na mapapa wale wa mwanzo kuanzia kwa Clement (mwaka 100 B.K.), zilizoingizwa
katika mkusanyo wa amri wa karne ya tisa unaodaiwa kwamba ulifanywa na “Isdore Mercator.” Jina hilo
la Pseudo-Isdorian Decretals limetumika tangu kuzuka kwa hali ya kuhoji maandiko katika karne ya kumi
na tano.
Huyo Isdore-wa-Uongo alichukua kama msingi wa maandiko yake ya kughushi mkusanyo wa kanuni halali
za kanisa zilizoitwa Hispana Gallica Augustodunensis, kwa njia hiyo akipunguza kugunduliwa kwake, kwa
sababu mkusanyo ule wa kanuni za kanisa ulifanywa na watu wengi kwa kuongeza mambo mapya kwa
yale ya zamani. Kwa njia hiyo kughushi kwake maandiko yale hakukuweza kuonekana wazi zaidi
kulipoingizwa katika maandiko yale halisi. Uongo wa maandiko yale ya kubuni tu ya yule Pse-Isdore sasa
unakubalika bila kupingwa, ukihakikishwa kutokana na ushahidi ule uliomo ndani yake, uchunguzi wa
vyanzo vyake, mbinu zilizotumika, na ukweli kwamba maandiko hayo yalikuwa hayajulikani kabisa kabla
ya mwaka ule wa 852. Wanahistoria wanaafikiana kwamba mwaka 850 au 851 ulikuwa ndio mwaka
unaowezekana kukamilisha kazi ya mkusanyo huo wa maandiko, kwa sababu hati hiyo inanukuliwa kwa
mara ya kwanza katika kitabu cha Admonitio cha mkusanyo wa sheria kilichotolewa na Baraza la
makasisi wa kanisa la Quiercy, katika mwaka wa 857.
Mwandishi wa hati hizo za kughushi hajulikani. Uwezekano upo kwamba (683) zilitoka kwenye chama
kipya cha kanisa cha wakereketwa kilichoundwa Rheims, Ufaransa katika karne ya tisa. Inakubalika
kwamba Askofu Hincmar wa Rheims aliutumia mkusanyo huo wa amri za mapapa wakati wa
kumthibitisha kwa kiapo yule Rothad Soissons, ambaye aliupeleka Roma mkusanyo ule wa amri za
mapapa katika mwaka ule wa 864 na kuuweka mbele ya Papa Nicolas I.
(Hapa yametolewa maandiko ya waandishi wengi waliopinga maandiko hayo ya kughushi)
396
Uk. 57 - AMRI YA HILDEBRAND (GREGORY VII). – (Hapa zinatolewa rejea tele zinazoonyesha amri hiyo na
waandishi waliojadili amri hiyo).
Uk. 59 - TOHARANI (PURGATORY). -Dk. Joseph Faa Di Bruno anafafanua maana ya toharani kwa maneno
haya: Toharani ni hali ya mateso baada ya maisha haya, ambapo zinashikiliwa pale kwa muda roho
zinazoachana na maisha haya baada ya dhambi zao za mauti kuondolewa mawaa na hatia yake, na
kusamehewa mateso yale ya milele ambayo zilistahili kuyapata; lakini kuhusiana na zile dhambi zao
bado zinalo deni la kulipa kwa kuteswa kimwili; sawasawa na roho zile zinazoachana na maisha haya
zikiwa zina hatia ya kutenda dhambi ndogo.” -Catholic Belief (1884 Ed.; Imprimatur Archbishop of New
York), Page 196.
(Hapa zinatolewa rejea nyingine tatu kuhusu Purgatory)
Uk. 59 - MSAMAHA WA DHAMBI (INDULGENCES). – (Hapa zimetolewa rejea na mbalimbali zinazoeleza
kuhusu historia na utendaji wa namna kanisa linavyosamehe dhambi na kupunguza muda na kiasi cha
mateso ya toharani kwa mtu) (684)
Uk. 59 – MISA (THE MASS) - (Hapa zinatolewa rejea kuhusu fundisho la misa kama lilivyoamriwa na
Baraza la Trent; na rejea kuhusu mjadala wa fundisho hilo).
Uk. 65. SABATO MIONGONI MWA WAWALDENSI – Kuna waandishi ambao wanaendelea kushikilia kwamba
Wawaldensi walikuwa na kawaida ya kuitunza Sabato. Mgongano umekuwepo kwa sababu tangu wakati
wa Matengenezo maneno “Siku ya Bwana” yalikuwa yamehusianishwa na “Jumapili” na hiyo ndiyo
ilikuwa imeitwa Sabato.
Lakini upo ushahidi wa kihistoria kwamba kulikuwa na utunzaji wa Sabato ya siku ya saba miongoni mwa
Wawaldensi. Taarifa inayotokana na maelezo ya mmoja wa Wawaldensi aliyeletwa kuhojiwa barazani
yanaonyesha kwamba Wawaldensi walikuwa wanaitunza (685) pamoja na Wayahudi. Hii ni kulingana na
Johann Joseph Ignaz von Dollinger, Beitrage zur Sektengeschichte des Mittelalters (Reports on the
History of the Sects of the Middle Ages), Munich, 1890, 2d Pt., P. 661.
Uk. 65. - TOLEO LA BIBLIA YA WAWALDENSI. – (Hapa kuna rejea hapa zinazoonyesha kuhusu
kuvumbuliwa kwa maandishi ya Wawaldensi; na nyingine zinazoonyesha historian a maisha ya
Wawaldensi).
Uk. 77. AMRI DHIDI YA WAWALDENSI. – (Hapa inatolewa sehemu ya tamko la kipapa lililotolewa na
Innocent VIII mwaka 1487 dhidi ya Wawaldensi, likiwa katika rejea kadhaa za maandishi yaliyo katika
maktaba).
Uk. 85. - WYCLIFFE. – Mwanahistoria anagundua kwamba jila la Wycliffe linaandikwa kwa namna
tofauti-tofauti. (Zinaonyeshwa rejea kwa ajili ya hilo).
Uk. 86. - HALI YA KUTOKOSEA (INFALLIBILITY. – (Hapa zinatolewa rejea za maandishi na matamko ya
kanisa kuhusu jambo hili). (686)
Uk. 104. BARAZA LA CONSTANCE. – (Hapa vinatolewa vyanzo mbalimbali vinavyotoa habari za baraza
hilo, na watu waliotoa maoni kuhusu baraza hilo).
Uk. 234. MAJESUITI. – (Hapa vinatajwa vitabu vinachoeleza kuhusu chimbuko, misingi, na malengo ya
cha hiki kinachoitwa “Chama cha Yesu” Moja ya nukuu zinazotoka humo ni hii:
Msukumo mkuu wa chama hicho ni roho ya kuwa na utii mkamilifu: ‘Hebu kila mmoja,’ anaandika Mt.
Ignatius, ‘na ashawishike kwamba wale wanaoishi chini ya utii wanapaswa kujiachia wenyewe

397
kusukumwa na kuongozwa na maongozi ya Mungu kupitia kwa wakuu wao, kama vile kwa maiti
inayojiachia kuchukuliwa na kupelekwa kokote na kutendewa vyovyote, au kama gongo la mzee
linalomsaidia yule anayelishika mkononi mwake kwa njia yo yote ile atakayo yeye.’
(Halafu zinatolewa rejea nyingine tele kuhusu jamii hii ya Majesuiti).
Uk. 235. MAHAKAMA YA KANISA. – (Hapa kunatolewa vyanzo mbalimbali vya rejea kuhusu mahakama
hii).
Uk. 265. SABABU ZA MAPINDUZI YA UFARANSA. - Kuhusu matokeo yenye athari nyingi ya kuikataa Biblia
na dini ya Biblia yaliyowapata watu wa Ufaransa (zinatolewa rejea hapa).
Uk. 267. JUHUDI ZA KUONDOSHA NA KUHARIBU BIBLIA – (Vinatolewa vyanzo mbalimbali vinavyoeleza
kuhusu juhudi za mamlaka na mabaraza mbalimbali katika kuzuia na kupiga marufuku watu wa kawaida
kuwa na Biblia). (688)
Uk 276. UTAWALA WA KITISHO. - (Vinatolewa vyanzo mbalimbali vinavyoeleza kuhusu Mapinduzi ya
Ufaransa) (689)
Uk. 280. – WATU WA KAWAIDA NA MATABAKA YA JUU – (Kuna kitabu kinatajwa kinachohusu hali ya
maisha ya kijamii ya watu wa Ufaransa kabla ya Mapinduzi).
Uk. 283. – KULIPIZA KISASI. – (Kinatolewa chanzo kinachoonyesha kwamba Mapinduzi ya Ufaransa
yalikuwa kama ya kulipiza kisasi).
Uk. 284. – UKATILI MBAYA WA UTAWALA WA KITISHO. – (Vinatajwa vitabu vitatu vinavyotoa habari hizo).
Uk. KUTAWANYWA KWA MAANDIKO. - Katika mwaka wa 1804, kwa mujibu wa William Canton wa Chama
cha Biblia cha Uingereza na Nchi za Kigeni, “Biblia zote zilizopo sasa ulimwenguni, katika mwandiko wa
mkono au zilizochapishwa, ukihesabu kila toleo katika kila nchi, zilihesabiwa kwa kiwango kisichozidi
milioni nne…. lugha mbalimbali ambazo milioni hizo nne ziliandikwa, pamoja na lugha za zamani za
Moeso-Gothic za Ulfilas na Kianglo-Saksoni cha Bede, zimeandikwa katika kumbukumbu kuwa zinafikia
takriban hamsini.” -What is the Bible Society? Rev. Ed., 1904, p. 23.
Chama cha Biblia cha Amerika kilitoa taarifa ya Biblia zilizotawanywa 481,149,365 kwa kipindi
kinachoanzia 1816 hadi 1955, ukijumuisha Maagano na sehemu za Maagano katika ulimwengu wote.
Maandiko, kamili au kwa sehemu sehemu, yamechapishwa katika lugha 1,092 kufikia Desemba, 1955; na
lugha mpya zinazidi kuongezeka daima. (690)
Uk. 288. – MISHENI KATIKA NCHI ZA NG’AMBO. - Shughuli za Kimishonari za Kanisa la mwanzo la Kikristo
hazijarudiwa mpaka siku za sasa kama zilivyokuwa. Zilikuwa zimekufa kabisa kufikia mwaka wa 1000,
tena zilifuatiwa na mapambano ya kijeshi katika Vita Takatifu (Crusades). Kipindi cha Matengenezo
kilifanya kazi kidogo mno za umishonari katika nchi za kigeni, isipokuwa kwa upande wa Majesuiti wa
mwanzo. Uamsho wa utauwa ulitoa baadhi ya wamishonari. Kazi ya Kanisa la Moravian katika karne ya
kumi na nane ilikuwa ni ya kusifika, na palikuwa na vyama fulani vya Kimishonari vilivyoundwa na
Waingereza kufanya kazi katika makoloni yao kule Amerika Kaskazini. Lakini kufufuka tena kukubwa
kwa shughuli za kimishonari kunaanzia mwaka 1800, “wakati wa mwisho.” Danieli 12:4. Katika mwaka
wa 1792 kiliundwa Chama cha Kimishonari cha Kibaptisti, ambacho kilimtuma Carey kwenda India.
Katika mwaka wa 1795 Chama cha Kimishonari cha London kilianzishwa, na chama kingine katika mwaka
wa 1799 ambacho katika mwaka wa 1812 kiligeuka na kuwa Chama cha Kimishonari cha Kanisa (CMS).
Muda mfupi baadaye Chama cha Kimishonari cha Wesley kiliundwa. Katika nchi ya Marekani Bodi ya
Makamishna wa Amerika wa Misheni katika Nchi za Kigeni iliundwa mwaka wa 1812, na Adoniram Judson
398
alitumwa katika mwaka ule kwenda Calcutta. Alijiimarisha kule Burma mwaka uliofuata. Katika mwaka
wa 1814 Umoja wa Misheni wa Kibaptisti wa Amerika uliundwa. Bodi ya Presibiteri ya Misheni katika
Nchi za Mbali iliundwa mwaka 1837.
“Katika mwaka wa 1800 B.K.,… idadi kubwa mno ya Wakristo ilikuwa ya wazawa wa wale waliokuwa
wameongolewa kabla ya mwaka wa 1500 B.K….. Sasa, katika karne ile ya kumi na tisa, Ukristo
ukaongezeka kupanuka tena. Si makontinenti mengi au nchi kubwa ambazo zilikuwa zimeingiwa kwa
mara ya kwanza katika karne tatu zile zilizotangulia. Jambo hilo lingekuwa haliwezekani, kwa sababu
katika nchi zile kubwa zaidi za dunia, ukiacha Australia na miongoni mwa maeneo yote yenye ustaarabu
wa Kikristo wa hali ya juu, Ukristo ulikuwa umeanzishwa kabla ya mwaka wa 1800. Kilichotokea sasa
ilikuwa ni kule kujipatia maeneo mapya ya kuotesha mizizi, na miongoni mwa watu waliokuwa tayari
wamefikiwa, upanuzi wenye eneo kubwa lisilowahi kutokea kutoka katika maeneo mapya na yale ya
zamani zaidi, na kuingia kwa Ukristo kwa watu wengi katika nchi kubwa kama hizo, na visiwa, pamoja
na mataifa na makabila yaliyokuwa hayajapata kuguswa kabla ya hapo….
“Kuenea kwa Ukristo katika karne ile ya kumi na tisa, kimsingi kulitokana na mbubujiko mpya wa
maisha ya kidini utokanao na msukumo wa Kikristo…. Kamwe haujapata kuwako wakati wo wote
unaolingana na huo, ambao msukumo huo wa Kikristo ulipata kuanzisha harakati nyingi mno. Ulikuwa
haujapata kamwe kuleta mabadiliko makubwa mno juu ya watu wale wa Ulaya Magharibi. Ilikuwa ni
kutokana na nguvu hiyo tele viliweza kutokea Vyama vya Kimishonari ambavyo katika karne ile ya kumi
na tisa vilizidisha sana nguvu yake kwa kuongeza wingi wa watu walioamini pamoja na mvuto wa
Ukristo.” -Kenneth Scott Latourette, A History of the Expansion of Christianity, vol IV, The Great
Century A..D. 1800A..D.1914 (New York:Harper & Brothers, 1941), pp 2-4.
Uk. 327, 329. – SIKU ZA KINABII. - Kulingana na hesabu za Kiyahudi, mwezi wa tano (Ab) wa mwaka wa
saba wa utawala wa Artashasta ulianzia Julai 23 hadi Agosti 21, 457 K.K. Baada ya kufika kwa Ezra kule
Yerusalemu katika majira ya kupukutisha (autumn) ya mwaka ule, amri ya mfalme huyo ilianza
kutekelezwa. Kwa uhakika wa mwaka huo wa 457 K.K. kwamba ulikuwa ni mwaka wa saba wa
Artashasta, angalia kitabu cha S. H. Horn and L. H. Wood, The (691) Chronology of Ezra 7 (Washington,
D.C.: Review and Herald Publishing Assn., 1953); E. G. Kraeling, The Brooklyn Museum Aramaic Papyri
(New Haven or London, 1953), pp 191-193; The Seventh-day Adventist Bible Commentary (Washington,
D.C.: Review and Herald Publishing Assn., 1954)), vol 3, pp 97-110.
Uk. 335. – KUANGUKA KWA HIMAYA YA OTTOMAN. – (Hapa kunatokelewa maelezo mafupi ya matokeo ya
Uturuki ya Kiislam baada ya anguko la Constantinople mwaka 1453, yakifuatiwa na maelezo na rejea
mbalimbali zinazohusu kuanguka kwa himaya ya Ottoman).
Uk. 340. KUZUIA WATU KUWA NA BIBLIA – (Hapa kunatolewa habari na vyanzo mbalimbali
vinavyoonyesha kwamba Kanisa Katoliki lilikuwa halipendezwi na hali ya kuchapisha Biblia katika lugha
za watu).
Uk. 373. MAVAZI YA WAKATI WA KUPAA (ASCENSION ROBES). - Kisa kisemacho kwamba Wanamarejeo
walishona mavazi ya kuvaa wakati wa kupaa “kumlaki Bwana hewani,” kilibuniwa na wale waliotaka
kuyashutumu mahubiri ya Wanamarejeo. Kisa hicho kilienezwa kwa bidii sana kiasi kwamba wengi
walikisadiki, lakini uchunguzi wa makini ulithibitisha uongo wa kisa kile. Kwa miaka mingi zawadi nono
ilitolewa kwa yule atakayetoa ushahidi kuonyesha mfano mmoja uliopata kutokea, lakini hakuna
ushahidi wo wote uliotolewa. Hakuna hata mmoja miongoni mwa wale waliopenda kuona kuja kwake
Mwokozi, ambao wangekuwa wajinga mno wa mafundisho ya Maandiko kiasi cha kudhani kwamba

399
mavazi ambayo wangeweza kuyashona yangehitajika kwa tukio lile. Vazi pekee ambalo watakatifu
watalihitaji ili kumlaki Bwana ni vazi la haki ya Kristo. Angalia pia Isaya 61:10; Ufunuo 19:8.
Kwa ukanushaji kamili wa kisa hicho kisichokuwa cha kweli kuhusu mavazi ya kuvaa wakati wa kupaa,
angalia kitabu cha Francis D. Nichol, Midnight Cry (Washington, D.C.: Review and Herald Publishing
Assn., 1944), pp 25-27, Froom, Prophetic Faith of Our Fathers (Washington, D.C.: Review and Herald
Publishing Assn., 1954), vol 4, pp 822-826.
Uk 374. MPANGILIO WA MIAKA YA UNABII. -Dk. George Bush, profesa wa Kiebrania na maandiko ya
Mashariki katika Chuo Kikuu cha Mji wa New York, katika barua aliyomwandikia William Miller, ambayo
ilichapishwa katika magazeti ya Advent Herald na Signs of the Times Reporter , Boston, Machi 6 and 13,
1844, alitoa maelezo fulani ya maana kukiri usahihi wa mahesabu yake aliyoyafanya kuhusu kipindi cha
unabii. Dk. Bush aliandika hivi:
“Wala ubishi hauwezi kutolewa kwako, wewe mwenyewe au kwa rafiki zako, kama ninavyoona mimi,
kwamba mmetumia wakati mwingi na fikra zenu kujifunza mfuatano wa miaka ya unabii, tena
mmejitahidi sana kuweka tarehe za mwanzo na za mwisho za vipindi vyake vikuu. Kama vipindi hivyo
vimetolewa hasa na Roho Mtakatifu katika vitabu vya unabii, basi, bila shaka, ilikuwa kwa kusudi
kwamba (693) vipate kuchunguzwa, na labda, mwisho wake, vipate kueleweka kikamilifu; wala hakuna
mtu ye yote atakayeshtakiwa kuwa na upumbavu wa makusudi ambaye kwa kicho anajitahidi kufanya
hivyo…. Kwa kuchukua siku moja kama neno linalotumika kiunabii kwa mwaka mmoja, mimi naamini
mmeungwa mkono kwa uchambuzi wa mafungu ulio wa busara kabisa, tena mmeimarishwa kwa majina
yenye sifa ya Mede, Sir Isaac Newton, Askofu Newton, Kirby, Scott, Keith, na jeshi la wengine ambao
kwa muda mrefu uliopita wamefikia hitimisho la msingi kama lenu juu ya kichwa hiki. Wote hao
wanakubaliana kwamba vipindi vile vikuu vilivyotajwa na Danieli na Yohana, ni kweli vinafikia mwisho
wake mnamo kizazi hiki cha ulimwengu, na ingekuwa ni mantiki ya ajabu ambayo ingekuhukumu wewe
kuwa mzushi kwa kuyashikilia maoni yale yale yanayojitokeza yenyewe kwa wazi mno katika matangazo
ya wajuzi hao mashuhuri wa mambo ya Mungu.” “Matokeo yako uliyoyapata katika nyanja hii ya
uchunguzi hayanishangazi mimi kuwa yako nje ya njia yenyewe kiasi cha kuathiri mambo yo yote ya
maana ya ile kweli au wajibu.” “Kosa lako, ninavyofahamu mimi, linaelekea upande mwingine zaidi ya
ule wa mpangilio wa miaka. “Umekosea kabisa kwa habari ya aina ya mambo yenyewe yanayopaswa
kutokea wakati vipindi vile vitakapokuwa vimekwisha. Hiki ndicho kichwa na uso wa kosa la ufafanuzi
wako.” Angalia pia kitabu cha Leroy Edwin Froom, Prophetic Faith of Our Fathers (Washington, D.C.:
Review and Herald Publishing Assn., 1950), vol 1, ch. 1,2.
Uk. 435. UJUMBE WA NAMNA TATU. - Ufunuo 14:6,7 huhubiri juu ya tangazo la ujumbe wa malaika wa
kwanza. Kisha nabii huyo anaendelea kusema: “Kisha akafuata malaika mwingine, akisema, Umeanguka,
umeanguka Babeli,… na malaika wa tatu akawafuata.” Neno lililotumika hapa lisemalo “akawafuata”
lina maana ya “kwenda pamoja nao,” “kumfuata mmoja,” “kwenda pamoja naye.” Tazama kitabu cha
Henry George Liddell and Robert Scott, Greek English Lexicon (Oxford: Clarendon Press, 1940), vol 1, p.
52. Pia linamaanisha “kusindikiza/kufuatana na.” Angalia kitabu cha George Abbot-Smith, A Manual of
Greek Lexicon of the New Testament (Edinburgh: T. and T. Clark, 1950), p. 17. Ni neno lile lile
lililotumika katika Marko 5:24, “Yesu akaenda pamoja naye; mkutano mkuu wakamfuata,
wakimsongasonga.” Pia limetumika kuhusiana na wale mia na arobaini na nne elfu waliokombolewa,
Ufunuo 14:4, inaposemekana kwamba, “Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako.” Mahali
pote hapo pawili ni dhahiri kwamba wazo lililokusudiwa kueleweka hapo ni lile la “kwenda pamoja,”
“kufuatana na.” Kwa hiyo katika 1 Wakorintho 10:4 tusomapo habari za wana wa Israeli kuwa
“waliunywea Mwamba wa kiroho uliowafuata,” neno hilo “uliowafuata” limetafsiriwa kutokana na neno
400
lile lile la Kigiriki, na pambizoni kuna maneno haya “uliokwenda pamoja nao.” Kutokana na maneno
hayo twajifunza kwamba wazo lililo katika Ufunuo 14:8,9 sio tu kwamba malaika wa pili na yule wa tatu
walimfuata yule wa kwanza kwa kufuata wakati, bali kwamba walikwenda pamoja naye. Ujumbe huo
wa aina tatu ni ujumbe mmoja tu wa aina tatu. Ni ujumbe wa aina tatu tu kwa utaratibu wa kutokea
kwao. Lakini baada ya kutokea kwao, wanaendelea kwa pamoja, wala hawatenganishiki.
Uk. 447. UKUU WA MAASKOFU WA ROMA. – (Hapa vinatolewa vyanzo mbalimbali vya rejea kuhusu mada
hiyo) (694)
Uk. 565. KUWANYIMA WATU BIBLIA. – Angalia maelezo kwa ajili ya Uk. 340.
Uk. 578. KANISA LA ETHIOPIA NA SABATO. - Mpaka karibu na miaka ya karibuni sana Kanisa la Kikoptiki
la Ethiopia lilikuwa likiitunza Sabato ya siku ya saba. Waethiopia pia walitunza Jumapili, siku ya kwanza
ya juma, katika historia yao yote kama Wakristo. Siku hizo mbili ziliadhimishwa kwa huduma maalum
katika makanisa yao. Lakini, utunzaji wa Sabato ya siku ya saba umekoma kabisa katika Ethiopia ya leo.
Kwa taarifa ya mashahidi walioona kwa macho siku hizo mbili za kidini zikitunzwa katika Ethiopia,
angalia kitabu cha Pero Gomes de Teixeira, The Discovery of Abyssinia by the Portuguese in 1520
London: British Museum, 1938), p. 79; kitabu cha Father Francisco Alvarez, Narrative of the Portuguese
Embassy to Abyssinia During the Years 1520-1527 katika kumbukumbu za Hakluyt Society (London,
1881), vol 64, kurasa 22-49; kitabu cha Michael Russell, Nubia and Abyssinia (New York: Harper &
Brothers, 1837), pp 226229; kitabu cha S. Giacomo Baratti, Late Travels into the Remote Countries of
Abyssinia (London: Benjamin Billingsley, 1670), pp 134-137; kitabu cha Job Ludolphus, (London: S.
Smith, 1682), pp. 234-357; kitabu cha Samuel Gobat, Journal of Three Years’ Residence in Abyssinia
(New York: toleo la 1850), kurasa 55-58,83-98. (Na vitabu vingine vimetolewa kuonyesha hilo.

401
MAELEZO YA MANENO
Fafanuzi za Maneno Mageni Zinazotolewa na Mtafsiri
Belial – (Ukurasa ulio katika mabano (191)): Hili ni neno linamaanisha uovu au limetumika kuwakilisha
shetani katika Biblia ya tafsiri ya King James. Katika tafsiri nyingine, neno hilo limetafsiriwa kama
baradhuli au mtu asiyefaa kitu. Neno hilo limetumika katika Kumbukumbu 13:13; Waamuzi 19:22; 1
Samweli sura ya 1 na ya 2.
Duke – (Ukurasa ulio katika mabano (149)): Hiki ni cheo cha mtawala wa eneo dogo la kiutawala katika
jimbo au jimbo dogo. Linatumika pia kuonyesha mtu mkubwa mweye hadhi ya juu.
Jesuit – (Ukurasa ulio katika mabano (234)): Mwanachama wa chama cha Majesuiti (chama au taasisi
katika Kanisa Katoliki unaojihusisha na umishonari na kazi za kielimu duniani kote; inasemekana kuwa
kilianzishwa na mtu anayeitwa Mtakatifu Ignatius Loyola mwaka 1534 kwa lengo la kulinda na kutetea
Ukatoliki dhidi ya Matengenezo (Microsoft Encarta 2009. © 1993-2008 Microsoft Corporation)
Mamlaka takatifu - (Ukurasa ulio katika mabano (237 na 248)): Haya ni maneno yaliyotafsiriwa kutoka
maneno ya Kingereza ‘holy see’ ambayo katika Kanisa Katoliki yana maana ya mamlaka ya papa au
mfumo wa kitaasisi wa mamlaka ya papa au eneo la makao makuu ya kanisa kule Roma.
Mzushi (Ukurasa ulio katika mabano (114)): Mzushi (heretic) ni mtu ambaye anaonyesha imani au
mafundisho yaliyo tofauti au yanayopingana na imani au mafundisho ya dini iliyopo au dini
inayokubaliwa na mamlaka zilizopo. Nyakati za zamani, uzushi (herecy) ulihesabika kama makosa ya
kupingana na mamlaka; ilikuwa kama uhaini wa kutaka kupindua mfumo wa dini na adhabu yake ilikuwa
kubwa.
Protestant – (Ukurasa wa mabano (197)): maana yake ni kupinga, kukataa au kuonyesha kutokukubali
kukandamizwa, kunyanyaswa au kufanyiwa jambo lisilo jema. Dhana hiyo ndiyo iliyoleta kikundi cha
watu wanaoitwa Waprotestanti, yaani, madhehebu yale yanayopinga mamlaka ya upapa na mafundisho
ya kanisa la Roma.
Uadventisti - (Ukurasa wa mabano (357)): Uadventisti ni neno linalotafsiriwa kutokana na neno la
Kingereza Adventism; likiwa na maana ya hali ya mwamko wa kutangaza habari za kurudi au kurejea
kwa Yesu. Watu wanaohubiri au kuamini habari hizo za marejeo wameitwa Adventists, yaani
Waadventisti. Katika kitabu hiki, mahali pengi, neno Adventists limetafsiriwa kama Wanamarejeo.

402

You might also like