Professional Documents
Culture Documents
Lesoni Somo La 7 Feb 18 2023
Lesoni Somo La 7 Feb 18 2023
Mifano ya Biblia:
Kuwahudumia maskini
Kuwahudumia wahitaji
MUNGU HUWAJALI WAHITAJI
HUDUMA YA YESU
“Ndipo alipojibu, akawaambia, ‘Nendeni mkamweleze Yohana mlioyaona na kuyasikia:
vipofu wanaona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia,
wafu wanafufuliwa, maskini wanahubiriwa habari njema.’” (Luka 7:22)
Yesu alisoma Isaya 61:1-2 kwenye Sinagogi Nazareti. Aya hii inaainisha
maana ya huduma ya Masihi.
Yesu aliwahudumia wahitaji kwa namna ambayo haikuwa ya kawaida siku
zile.
Watu walifikiri kuwa wahitaji walikuwa
wanaumia kutokana na dhambi zao, hivyo
walihudumiwa kama waliolaaniwa na
Mungu. Yesu aliwapenda na kuwaona
kama watu wanaoweza kuwa raia wa
Ufalme wa Mbinguni.
Alijaribu kukidhi mahitaji yao na
kuwapatia tumaini la Injili.
SHERIA ZA UBINADAMU
“Ikiwa kuna mtu maskini miongoni mwa ndugu zenu, katika mji wowote wa nchi hiyo
ambayo Bwana Mungu wenu anawapa, msiwe na moyo mgumu wala usimfumbie
mkono ndugu yako aliye maskini,” (Kumb 15:7)
Umaskini hautaondolewa kamwe (Kumb. 15:11; Mar. 14:7). Kwa
hiyo Mungu, aliwapa Israeli sheria za kuwalinda wahitaji