You are on page 1of 56

JUMA LA MAOMBI

Somo la 1

Je! Mungu Analipenda Jiji Lako?

Na: Dr. S. Yeury Ferreira


(Mathayo 9:36).

Utangulizi
Je! Mungu analipenda jiji lako? Leo tutajaribu kujibu swali hilo. Laki-
ni kabla hatujafanya hivyo, hebu na tuangalie mambo ya kuvutia kuhusi-
ana na majiji. Kulingana na baadhi ya tafiti, jiji ni eneo lenye watu wengi
na lililopangwa kwa mpangilio mzuri ambalo hutumika kama kitovu cha
kila kitu: fedha, tamaduni, siasa na zaidi ya hayo. Majiji yamejawa na
maghorofa, barabara, njia za chini ya barabara kwa ajili ya waenda kwa
miguu, na hudumu chungu nzima. Kwa kuongezea, kwenye majiji, kuna
watu kutoka maeneo na tamaduni zote na kuna maeneo ambayo mambo
ya kupendeza yanatokea, kama vile uvumbuzi, elimu na kazi.
Sasa, hebu na tuzungumze kuhusu majiji makubwa ulimwenguni:
• Tokyo, huko Japani ni moja ya majiji yenye watu wengi sana
kwenye sayari hii. Jiji hilo linajulikana kwa kuwa la kiteknolojia
na kuwa na utamaduni wa kisasa wa hali ya juu.
• New York, nchini Marekani ni kama kitovu cha kila kitu, ni jiji
lenye fedha nyingi, biashara na utamaduni unaopendwa sana.
• London, mji mkuu wa Uingereza na Ufalme wa Uingereza ni jiji la
kihistoria ambalo bado lina jukumu kubwa katika uchumi na siasa
za ulimwengu.
• Beijing ni mji mkuu wa China na mahali pa muhimu sana kwa
siasa na utamaduni.
1
• Sao Paulo, Brazil ni mahali ambapo kila kitu kinaweza kufanyika
katika Amerika ya Kusini. Kuna biashara nyingi na utamaduni wa
kufurahisha.
• Mumbai, India ni jiji linalokua na ni la muhimu sana kwa biashara.
• Lagos nchini Nigeria ni kituo kikuu cha kibiashara kwa Afrika
ambacho kimeelezwa kuwa mji mkuu wa kitamaduni, kifedha na
maburudisho barani Afrika.
Sasa, vipi kuhusu masuala ya kimhemko ya watu wanaoishi mijini?
Kuishi katika jiji sio kila wakati inatokea kuwa kama inavyooneshwa
kwenye sinema. Watu katika jiji wanaweza kuhisi msongo kwa sababu
kila kitu huenda haraka, na msongamano unaweza kuwa fujo. Licha ya
kuwa unazungukwa na watu wengi, baadhi wanaweza kuhisi kuwa wap-
weke kwa sababu wanakosa uhusiano wa karibu na wengine. Kuwa na
wasiwasi kunaweza kuwa tatizo, kwa kuwa mashindano na msukumo
wa kutafuta mafanikio unaweza kuwa mkali sana. Nyakati fulani, hali
ya mfadhaiko inaweza kuwa jambo la kawaida katika majiji kwa sababu
maisha yanaweza kuwa magumu.
Lakini kuna habari njema, Mungu anayapenda majiji! Na, hilo
linamaanisha kwamba anawapenda watu wanaoishi ndani yake,
pamoja na matatizo na mihemko yao. Mungu anao moyo mkuu na ana-
guswa pale anapoona watu wakipitia nyakati ngumu. Sasa, ni kwa namna
gani Mungu anaonesha upendo Wake kwenye majiji? Hebu na tuangalie
mambo matatu yanayoonesha upendo Wake kwa vitendo.

Maendeleo
1. Mungu Anatuma Wajumbe Kwenye Majiji
Je! Uliwahi kujua kwamba kutajwa kwa neno mji kwa mara ya kwan-
za kwenye Biblia ilikuwa ni mji ambao Kaini aliujenga na kuupatia jina
la mwanawe (Mwanzo 4:17)? Inaonesha kwamba Henoko alitoka kati-
ka familia yenye historia ya changamoto nzito. Wazao wake waliunda
miji ambapo mambo ya kijinga yalitokea, kama vile kuoa wenzi wen-
gi na mauaji, lakini pia walikuwa wabunifu wa muziki na sanaa. Baa-
da ya gharika kuu, mambo hayakubadilika kuwa mazuri. Wajukuu wa
Nuhu, hususani wana wa Hamu, walianza kujenga miji iliyojawa na uovu
(Mwanzo 10:6–12) na kubwa zaidi, ni pale walipojenga Mnara wa Babe-
li kwa wazo la kujitengenezea jina (Mwanzo 11:4).
Ndani ya Biblia kuna miji kadhaa, baadhi iliyo maarufu ni Babeli, Uru
wa Wakaldayo, Sodoma, Gomora, Ninawi na Yerusalemu. Mengi ya ma-
2
jiji haya yalikuwa kama kitovu cha uovu na dhambi. Lakini cha kushan-
gaza, ukiachilia mbali majanga/matatizo yao yote, Mungu hakuikatia
tamaa miji hiyo bali alituma wajumbe wakiwa na ujumbe wa huruma na
fursa ya kubadilishwa. Tunaweza kusoma mfano wa hili katika kisa cha
Yona. (Soma kitabu cha Yona).
Mungu alimwambia Yona aende katika mji wa Ninawi ili awape ma-
onyo. Sasa, Ninawi palikuwa mahali penye jeuri sana iliyojaa uovu (Na-
humu 3:1). Cha kusikitisha ni kwamba kuna gombo la kale linalosema
wafalme wa Ninawi walikuwa wakiwakamata adui zao na kuwateketeza
kiuhalisia baada ya kuwachuna ngozi zao. Ilikuwa ni mbaya mno!
Lakini licha ya jeuri na uovu wao wote, Mungu hakutaka kuwaacha
bila kuwapa nafasi ya kubadilika. Alimtuma Yona, nabii, ili kuwaonya.
Na unajua ni nini? Mji wa Ninawi uliitikia kwa kufanya toba ya kweli
(Yona 3:5–10).
Je, unajua kwamba Mungu pia anataka kuona mabadiliko na toba kati-
ka miji leo? Ndio maana anatuma wajumbe! Soma kile Mungu anachose-
ma kupitia kwa mmoja wa mitume wake: “Kama mimi niishivyo, asema
Bwana, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na
kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu
mbaya; mbona mnataka kufa, enyi nyumba ya Israeli?” (Ezekieli 33:11).
Hebu subiri, hili halikutokea tu kwa nyakati za kale! Mungu bado
anataka kuona mabadiliko katika miji leo. Ni kama vile anasema, “Halo,
sitaki kukosa mambo mazuri katika miji yenu. Nataka utubu na ubadilike
kuwa bora.”
Hebu fikiria kuhusu mji wako. Unaweza ukawa umejawa na mambo
mazuri, lakini pia inawezekana kuwa una mambo yake wenyewe, ma-
tatizo, uhalifu, nk. Lakini bado, Mungu anaendelea kutuma watu mjini
mwako ili kuonesha upendo na kusema, “halo, niko hapa! Hebu na tuba-
dilishe hili pamoja.”
Kwa hiyo, kama umewahi kujihoji ikiwa Mungu anaujali mji wako,
jibu ni ndiyo, Anaujali! Mungu anahitaji kila mji uwe mahali ambapo
watu wanaweza kuishi kwa amani, kwa mafanikio na kwa mapatano.
Yuko tayari kutumia watu kama wewe ili kufanya hilo liwezekane. Kwa
hiyo, changamka na kuwa sehemu ya mabadiliko katika mji wako!
Hivyo basi, vijana, Mungu anashughulika kubadilisha hata miji ili-
yoasi na kuchanganyikiwa.
2. Mungu Anaonesha Huruma kwa Majiji
Inaonesha kwamba sio tu kwamba anatuma wajumbe bali pia ana-
3
onesha huruma kwa ajili ya watu wanaoishi katika majiji hayo, hususani
pale yanapopitia nyakati ngumu. Hebu angalia aya hii katika Mathayo
9:35–36:

“Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, aki-


fundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme,
na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. Na alipowaona
makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kut-
awanyika kama kondoo wasio na mchungaji.”
Na inamaanisha nini kuwahurumia? Kwa kifupi, inamaanisha kuji-
weka mwenyewe kwenye kiatu cha mtu mwingine na kuelewa matatizo
na maumivu yao. Ndiyo, Mungu anawajali sana watu walioko kwenye
majiji, hasa wanapopitia nyakati ngumu!
Hebu fikiria hili: jiji lako linaweza kuwa eneo lililojaa machafuko, am-
bapo wakati mwingine huhisi kama kila mtu amepotea katika machafu-
ko. Watu wanaweza kujihisi wapweke, wenye msongo, wagonjwa au wa-
nahangaika na masuala mengine. Lakini Mungu yupo! Yesu mwenyewe
alizunguka kote kwenye majiji, akifundisha na kuponya watu. Alipoliona
kusanyiko, moyo Wake uliguswa. Ni kana kwamba alitaka kusema, “Ja-
mani, niko hapa kwa ajili yenu. Hamko peke yenu katika hili.”
Wakati mwingine unapohisi kulemewa na kila kitu kinachotokea kati-
ka jiji lako, kumbuka kwamba Mungu anakuelewa. Anahuzunika pamoja
na wewe na kila mtu mwingine. Haidhuru ulimwengu unaweza kuwa
umechafuka kiasi gani, Mungu yuko tayari kuwa hapo na kututunza. Huo
ni upendo kwa vitendo!

1. Mungu anayabadilisha Majiji


Mpaka hapa sasa, tumezungumza kuhusu jinsi Mungu anavyotuma
wajumbe katika miji na jinsi anavyowahurumia watu wanaoishi humo.
Lakini hiyo haijatosha! Mungu pia ni mtaalamu katika kuipatia miji
mabadiliko kamili. Je! Unakikumbuka kisa cha Sauli wa Tarso?
Siku moja, Sauli alikuwa katika utume wake wa kuwatesa Wakristo na
kuelekea Dameski kufanya mambo yake. Lakini hebu subiri, hapa kuna
sehemu ya kupendeza: Yesu Mwenyewe alimtokea akiwa njiani na kuba-
dilisha maisha yake kabisa! Kisa hiki kiko katika Matendo 9:1–6. Sauli
ambaye alikuwa amezoea kuwa adui mkubwa wa Wakristo, alibadilish-
wa na kuwa Paulo, mmoja kati ya mitume waliokuwa wa muhimu sana
kwa nyakati zote.Hebu fikiria hili: Sauli, mtesaji wa Wakristo, aligeuka
na kuwa mtu aliyesimika makanisa mengi kila mahali na kuwa mwalimu
4
mkuu wa injili. Mungu alimbadilisha Sauli na kuwa mtu wa tofauti ka-
bisa.
Je! Hili linatufundisha nini? Mungu anao uwezo mkubwa sana wa
kubadilisha si watu binafsi tu bali pia miji mizima. Neema Yake inapoku-
wa kazini, kila kitu kinaweza kubadilika. Ikiwa unadhani kabisa kuwa
mji wako unahitaji kubadilishwa, kumbuka kwamba Mungu ni mtaalamu
katika kubadilisha watu na vitu. Yeye ni Msanifu katika vitendo, akibad-
ilisha kila kitu kuwa bora!

Hitimisho
Mungu anao upendo maalum kwa majiji yetu. Kote katika Biblia,
tumeona jinsi anavyoonesha upendo Wake katika njia za ajabu sana:
Anatuma ujumbe, Yeye ni mwenye uelewa mkuu, na hata anabadilisha
majiji yaliyobobea kwa dhambi. Kama vijana wa wakubwa wa Mungu,
ni wajibu wetu kuyapenda majiji yetu na kuupanua ufalme wa Mungu
ndani yake. Daima kumbuka kwamba Mungu anafanya kazi sana katika
miji yetu, na tunaweza kuwa vyombo vya upendo na huruma Yake. Hebu
tuombe upendo wa Mungu uendelee kutiririka na kubadilisha miji yetu.

5
Ibada: Mtazamo Tofauti
Na: Maria Manderson
Fungu: “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwa-
na, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku
zenu za mwisho” (Yeremia 29:11).
Kutokana na www,wickipedia.org, Uislamu ni dini inayokuwa kwa
haraka sana ulimwenguni, na kwa mujibu wa idadi halisi, kutokuwa na
dini kunaonekana kuongezeka (pamoja na kufuata mambo ya kidunia
kwa ujumla). Na kwa kumalizia, Utafiti wa Utambulisho wa Kidini wa
Marekani unaipa Wicca (umizimu) wastani wa ukuaji wa kila mwaka wa
143% kwa kipindi cha 1990 hadi 2001.
Kwa hiyo, kijana Mkristo Mwadventista anafanya nini? Je, tunashirik-
ishaje injili kwa vikundi hivi na vingine? Hebu tuangalie matukio matatu
katika Biblia na watu wa vikundi vingine vya imani.

KUWA NA MAKUSUDI:
Mungu Anamwita Ibrahimu
Katika maagano yote la Kale na Jipya, tunamwona Mungu kwa maku-
sudi akiita watu, wanafunzi, ambao kupitia kwao atawafikia watu. Mungu
alipomwita Ibrahimu (ambaye hapo awali aliitwa Abramu) katika Mwan-
zo 12:1, Alimwambia atoke katika nchi yake, familia yake na nyumba
ya babaye. Alipaswa kuacha nyuma kila kitu alichokuwa amekizoea, na
hili Iilijumuisha dini yake. Naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe
kuwa mtumishi Wangu ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza watu
wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa,
upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia” (Isaya 49:6). Badiliko
la pekee sana, kutoka kuwa mwabudu sanamu, Abramu hadi kuwa Rafiki
wa Mungu, Ibrahimu. Soma Yoshua 24:2 na Isaya 41:8. Urafiki huu kati
ya Mungu na Ibrahimu haukutokana na kitu chochote alichokifanya Ibra-
himu; badala yake, ulitokana na Agano la Mungu la Milele na Ibrahimu
na imani ya Ibrahimu katika kulikubali.
Yesu na Mwanamke Msamaria
Katika mkutano na mwanamke pale kisimani, tunamwona Yesu akifa-
nya makusudi kumkaribia mwanamke na kushiriki pamoja naye Habari
Njema. Yesu alitumia fursa hiyo kuzungumza na mwanamke wakati wa-
nafunzi Wake walipokwenda kununua chakula (Yohana 4:8). Mwanamke
huyo alikuwa akitafuta kitu kingine kilichokuwa bora. Alitamani mai-
6
sha kamili ambayo hayawezi kupatikana kwa mtu mwingine (au kitu).
Yesu alitumia muda huo kuzungumza naye na kumshirikisha kwa upole
kwenye mazungumzo hayo. Sisi pia tunalazimika kuwafikia wengine
kwa makusudi kabisa. Hakumdhalilisha, badala yake kwa upole Yesu
alimwonesha dhambi yake, jambo ambalo lilifanya macho yake yafum-
buliwe kuona ukweli wa yeye ni nani. Na Yesu alifunuliwa. Soma Yoha-
na 4:18–26.
Dhambi zake hazikumshtua Yesu. Dhambi zetu wala hazimshtui Yesu.
Ni kwa njia ya Yesu tu ndipo tunaweza kuokolewa kutoka katika dhambi
zetu.
Siku zote Mungu alijali sana kupanua upendo na msamaha Wake
kwa MATAIFA YOTE na kwa WATU WA DUNIA. Na kama Yeremia
29:11 inavyosema, Mungu anajua mawazo anayokuwazia na KILA MTU
MWINGINE, pia. Na ni mawazo ya kutufanikisha, sio ya kutuangamiza.
Mawazo ya kutupatia tumaini na miisho myema. Hiyo inamaanisha sisi
sote. KILA MTU!

Ombi:
Mpendwa Mungu wetu, tunakushukuru sana kwamba ulikusudia kutu-
fikia. Tunakushukuru sana kwa kutupenda upeo kiasi kwamba unataka
sisi wote kukaa na Wewe milele. Tafadhali naomba unikumbushe kwam-
ba unaweza kumwokoa kila mtu, bila kujali hali tulizonazo. Tunaomba
utukumbushe, nikumbushe mimi kwamba hatuwezi kuzishinda dhambi
zinazotukabili sisi wenyewe, bali tunakuhitaji. Tafadhali fungua macho
yangu na unioneshe njia ambazo ungependa mimi kuweza kushiriki na
wengine upendo Wako, hususani wale ambao hawakubali kwamba wewe
u Mwokozi na ulikufa ili kutufanya sisi tuweze kuishi tena. Ninaomba
unisaidia kuwa jasiri na kushiriki na kila mtu ninayekutana naye Habari
Yako Njema, kwa kile ninachosema na kwa namna ninavyoishi. Amina.

7
Somo la 2

Kuyabadilisha Majiji: Kuufuata Mfano wa Yesu


Na: Dr. S. Yeury Ferreira
Mathayo 9:35

Utangulizi
Leo, tunasafiri katika safari ya kiroho iliyovuviwa na Yesu, tukichun-
guza namna tunavyoweza kufanya kwa uzuri kazi ya umisionari katika
miji mikubwa. Hebu fikiri juu ya mji mkubwa wenye shughuli na chan-
gamoto nyingi, sawa na ule Yesu aliokabiliana nao katika wakati Wake.
Lakini kabla hatujatumbukia katika mada hii, hebu nikusimulie kisa ki-
fupi.
Miaka michache iliyopita, katikati ya jiji kubwa, aliishi kijana mmoja
aitwaye Daudi. Katikati ya shamrashamra za kila mara za jiji hilo, Dau-
di alihisi kulemewa kwa ukosefu wa tumaini na kusudi aliloona katika
maisha ya watu wengi waliomzunguka. Hata hivyo, siku moja, Daudi
alikabili hali ambayo ingebadili maisha yake milele. Alikutana na mwa-
namume mzee anayeitwa Eliya, ambaye alimsimulia kisa cha huduma ya
Yesu katika majiji. Mzee huyo aliichukua Biblia yake na kusoma Injili
ya Mathayo 9:35:

“Naye Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, aki-


fundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme,
na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.”
Daudi alimsikiliza kwa makini kadiri Eliya alivyoeleza kuwa aya hii
ilikuwa ikiangazia matendo makuu matatu ambayo Yesu aliyafanya kwa
manufaa ya majiji, yanayowakilishwa na vitenzi vikuu vitatu katika aya
hiyo.

8
Ufafanuzi

1. Kitenzi cha Kwanza: Fundisha


Hebu tuanze na kitenzi cha kwanza cha muhimu mno: “fundisha.” Yesu
alitumia muda mwingi akishiriki hekima Yake na watu wengi mijini.
Katika Mathayo 9:35, inasema, “Naye Yesu alikuwa akizunguka katika
miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao.” Hata hivyo, ma-
fundisho Yake hayakuwa ya maneno matupu; yaliakisiwa pia kwa jin-
si alivyoishi maisha Yake. Maisha Yake yaliwasilisha somo la upendo,
huruma, haki na imani.
Sasa hebu na tuendelee na kisa cha Daudi. Baada ya kukutana na Eliya
na shauku yake mpya ya kufuata nyayo za Yesu, Daudi alihisi kulazimika
kufanya jambo la maana sana. Badala ya kufagiliwa mbali na shughuli za
kila siku za jiji hilo na vikwazo visivyo na msingi, aliamua kuchukua hat-
ua. Mchana mmoja, alipokuwa akitembea kwenye bustani ya jiji, Daudi
alikutana na kundi la vijana wakijadili mambo ya kiroho na kidini. Aki-
wa amevutiwa, akasogea na kuanza kusikiliza. Vijana hawa walikuwa
wakitamani kujifunza zaidi kuhusu Mungu na Biblia. Daudi aliguswa na
shauku yao ya kweli katika kuchunguza kwa kina imani yao.
Akiwa ametiwa hamasa na shauku ya kujifunza ya vijana hawa, Daudi
alijitolea kuwa mwalimu wao. Alishiriki kile alichojifunza na kuwasaidia
kukabiliana na changamoto za maisha ya jijini katika mtazamo wa kiro-
ho. Zaidi sana, alitoa nyenzo za mtandaoni kuhusiana na mada za kiroho
na kupendekeza vitabu na masomo ya kusikiliza mtandaoni ambavyo vi-
likuwa vimeimarisha ufahamu wake wa kiroho. Vijana Wamisionari wa
jiji, walipata msukumo kutoka kwa kile Yesu alichokifanya na uzoefu
wa Daudi. Ni wakati wa kuchukua hatua na kuleta mabadiliko katika jiji
lako! Vifuatavyo ni baadhi ya vidokezo:
• Unda Vikundi vya Kujifunza Biblia: Kusanya marafiki zako au hata
watu usiowafahamu na uunde Vikundi vya Kujifunza Biblia katika
maeneo pendwa kama vile sehemu ya kupata chakula au bustanini.
Siyo tu kuhusu kuisoma Biblia bali kuchunguza maana yake katika
maisha ya kila siku.
• Kuwa Washauri: Kuwa washauri kwa vijana ambao wanahitaji
uongozi wa kiroho. Wasaidie kukabiliana na vikwazo vya maisha,
washirikishe uzoefu wako, na mkue pamoja katika imani.
• Mpeane Nyenzo: Mpeane vitabu, mafundisho ya kusikiliza na zana za
mtandaoni ambazo zimekusaidia wewe na zinazomwelezea Mungu
na wokovu kwa njia inayofaa na jumuishi kwa vijana wa leo. Fikiria
9
kile ambacho ungekipenda na uwashirikishe bila hiyana.
Kumbuka kwamba kufundisha sio tu kuhusiana na kuwapatia
mawaidha; inahusiana na kuwa kielelezo kwa wengine! Waoneshe
upendo, huruma na imani katika maisha yako ya kila siku, na utaona
jinsi nuru yako inavyoangaza jijini. Je! Uko tayari kuacha alama ka-
tika jumuia yako? Wasaa ni sasa vijana wakubwa!

1. Kitenzi cha Pili: Hubiri


Hebu sasa na tukiangalie kitenzi kikuu cha pili: “Hubiri.” Mwangalie
Yesu, kwa kweli, alikuwa gwiji katika hili. Hakuwafunulia tu hekima
Yake bali pia kwa upendo mkuu alimwambia kila mtu habari ya kusi-
simua sana katika historia: Ufalme wa Mungu ulikuwa umefika, wenye
tumaini kamili, msamaha na upatanisho!
Je! Bado unamkumbuka rafiki yetu Daudi, kijana mdogo ambaye
wakati fulani alihisi kutokuwa na tumaini jijini na kutafuta kusudi mais-
hani? Baada ya kukutana kwake na Eliya na shauku yake mpya ya ku-
fuata nyayo za Yesu, Daudi alijisikia kubidishwa kufanya kitu ambacho
kilikuwa cha muhimu mno.
Siku moja, wakati Daudi akiwa shuleni kwake, alipata fursa nzuri ili
kukifanyia kazi kitenzi cha “hubiri.” Mwalimu wake ambaye ni mkana
-Mungu anayejulikana, alimwuliza Daudi kwa nini alimwamini Mungu.
Papo hapo, mbele ya wanadarasa wenzake wote, Daudi alizungumza kwa
ujasiri na usadiki kuhusiana na sababu zilizomfanya awe na imani katika
Mungu. Alieleza maajabu ya uumbaji na namna Biblia ilivyo na athari
zifanyazo mabadiliko katika maisha yake. Kundi la wanafunzi lilisikili-
za kila neno alilolisema Daudi kwa umakini mkubwa, na hata mwalimu
aliguswa na uthabiti wa imani yake!
Baada ya kuzungumza kwa takribani dakika kumi, Daudi alishusha
pumzi ndefu na kisha kusimulia hadithi ya ajabu ya Yesu na jinsi imani
yake Kwake ilivyokuwa imebadilisha maisha yake mwenyewe. Alizu-
ngumzia tumaini na msamaha unaopatikana kwa Mungu, na namna am-
bavyo upatanisho unaweza kubadili kila kitu.
Alifanya hivyo kwa ujasiri lakini pia kwa unyenyekevu na upendo.
Hakujaribu kulazimisha imani yake ipokelewe bali aliwashirikisha uk-
weli kwa njia thabiti na ya heshima. Shauku ya Daudi na upendo wa
kweli uling’aa kupitia maneno yake.
Kuhubiri kwa Daudi kulileta tumaini kwa wale vijana wadogo walio-
kuwa wakisikiliza. Kama vile Yesu, Daudi aliihubiri habari njema kwa
10
ujasiri na upendo, na katika saa hiyo, alileta tofauti katika shule jijini
hapo.Kwa hiyo, wasichana na wavulana, “Kuhubiri” sio tu kuzungumza
kutokea mimbarini bali kutafuta kila siku fursa za kuushirikisha upen-
do wa Mungu kwa wale wanaotuzunguka. Hebu na tufuate mfano wa
Yesu na wa Daudi na tuifanye habari njema ing’ae jijini mwetu. Ninyi
pia mnaweza kuwa wabeba tumaini na mabadiliko katika maisha ya kila
siku!
2. Kitenzi cha Tatu: Ponya
Kitenzi cha tatu cha muhimu katika safari yetu ya kiroho ni “kupon-
ya.” Yesu hakufundisha na kuhubiri tu; aliponya pia wagonjwa na kuwa-
fariji walioteswa! Katika Injili ya Mathayo 9:35, inatuambia kwamba,
“Aliponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.” Lakini kumbuka, sio
tu kuhusiana na uponyaji wa magonjwa ya kimwili; inarejea pia kupon-
ya majeraha ya kiroho na kimhemko. Hiyo ni sehemu muhimu sana ya
utume wetu jijini.
Hebu na turudi pamoja na Daudi. Baada ya kuwasikiliza vijana hao,
siku moja alipata kujua umuhimu wa uponyaji, baada ya kuzama katika
kujifunza Biblia. Daudi alihisi moyoni mwake kwamba Mungu alikuwa
akimwita sio tu ili kufundisha na kuhubiri, bali pia kuhudumu katika
namna ya mguso zaidi.
Daudi aligundua kuwa jijini kwake, kulikuwa na watu wengi wasio-
kuwa na makazi waliohitaji chakula na mavazi, na kulikuwa pia na wazee
ambao walipata wageni kwa nadra sana. Aliamua kuongea na mchungaji
wa kanisa lake na kumweleza shauku yake ya kujihusisha katika hudu-
ma ya kikundi. Mchungaji alimjulisha kuhusu kikundi cha washiriki wa
kanisa ambao walikuwa na huduma ya kutoa chakula kwa watu wasio na
makazi.
Daudi hakusita hata kidogo, alijiunga na kundi hilo. Kila siku ya Ju-
mamosi baada ya ibada, alijiunga na washiriki wenzake wachache katika
kuandaa vyakula takribani sahani mia mbili na kisha walienda kuvigawa
katika mitaa jijini humo. Kazi hii iliujaza moyo wa Daudi furaha, na hapa
ndipo alipoelewa moja ya njia tunazoweza kutumia ili kutimiza kitenzi
“kuponya.”
Uponyaji haumaanishi tu kutibu wagonjwa; humaanisha pia kuwa-
hudumia wale walio wahitaji. Kunahusiana na kugawa chakula, mavazi
na usaidizi kwa wasio na makazi, kuwatembelea wagonjwa hospitalini,
kutumia muda pamoja na wazee katika makazi ya kulelea wazee jijini,
kuwatembelea wajane, kuonesha upendo kwa yatima, kunahusiana na
11
kufanya kile uwezacho kwa wale waliodharauliwa jijini mwako.
Kama alivyofanya Yesu, Daudi alielewa kwamba uponyaji unaenda
zaidi ya kimwili; unahusu kugusa mioyo na kuwapunguzia mizigo wale
wanaoteseka. Na hivyo, kama ilivyo kwetu sote, Daudi alipata njia yenye
nguvu ya kutimiza kitenzi cha “kuponya” katika jiji lake.
Kwa hiyo, vijana Wamisionari wa Jiji, hebu tufuate mfano wa Yesu na
Daudi. Tutafute fursa za kuwahudumia wahitaji. Unaweza kuleta tofauti
jijini kwa njia ya matendo yako yaliyojawa na upendo na huruma!

Hitimisho
Daudi, kijana mdogo kwenye kisa chetu, aliufuata mfano wa Yesu katika
jiji lake. Alijifunza kufundisha, kuhubiri na kuponya, na kazi yake ya
umisionari ilileta mabadiliko kwenye maisha ya watu wengi. Leo, sisi
kama vijana wadogo katika majiji, tunayo fursa sawa ya kuwa mawakala
wa mabadiliko. Kumbuka kwamba kufuata mfano wa Yesu kunahusi-
sha kufundisha kwa hekima, kuhubiri kwa upendo na kuponya kwa
huruma. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kuwa vyombo vya kuleta maba-
diliko kwenye majiji yetu, tukileta tumaini na upendo wa Mungu kwa
wale wanaouhitaji zaidi. Hebu utume huu uwe shauku na kujisalimisha
kwetu. Katika jina la Yesu, Amina.

12
Kushinda Vikwazo Rika: Ibada ya Umoja katika
Jumuia Mbalimbali za Mijini
Na: Ivonne Omaña
Katika miji yenye shughuli nyingi na tofauti katika ulimwengu wetu,
watu wa rika zote huishi pamoja, kila mmoja akibeba uzoefu na hekima
yake ya pekee. Wito wetu kama wachungaji ni kuunganisha vizazi, kuen-
deleza maelewano na umoja. Leo hebu na tupate hamasa kutoka kwenye
Maandiko na takwimu za sasa, tukijifunza jinsi ya kuwahudumia vyema
vijana na wazee, kama Yesu alivyofanya.
Aya ya Maandiko: 1 Timotheo 4:12
“Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao
waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na
usafi.”
Katika mandhari ya mijini kwenye shughuli nyingi na mabadiliko ya
kila mara, ni muhimu kutambua aina mbalimbali za rika zinazounda ju-
muia zetu. Mafundisho ya Biblia, yaliyooneshwa na watu kutoka kati-
ka vizazi mbalimbali ambavyo Yesu aliwahudumia, yanatoa mwongozo
usio na kikomo wa kuwaunganisha vijana na wazee.
1. Kukumbatia Nguvu za Ujana:
Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa, vijana huleta uchangam-
fu na uvumbuzi katika mazingira ya mijini. Mara nyingi huwa mstari
wa mbele katika kuleta mabadiliko ya kijamii, wakitetea haki na usa-
wa. Kama vile Yesu alivyowakaribisha watoto na shauku yao (Mathayo
19:14), hebu na tukumbatie nguvu na shauku ya ujana katika jumuia zetu.
Tukiwahamasisha vijana kuweka kielelezo katika usemi wao, mwenen-
do, upendo, imani na usafi wao (1 Timotheo 4:12).
2. Kuthamini Hekima na Uzoefu:
Kwa upande mwingine wa wigo wa rika, watu wazima huleta uzoefu
wa thamani sana wa maisha na hekima. Kulingana na tafiti za sasa, mara
nyingi huwa na majukumu muhimu kama walezi na washauri katika fa-
milia na jamii. Kama vile Yesu alivyoshughulika na watu kama Nikode-
mo na Simoni, ambao walikuwa wazee lakini wenye nguvu kiroho, hebu
na tuthamini hekima ya kizazi cha wazee.
3.Nguvu ya Uhusiano Kati ya Rika Mbalimbali:
Utafiti unaonesha kuwa uhusiano baina ya kizazi cha kale na cha ki-
13
sasa unaweza kuchochea afya ya akili kuwa bora na ustawi wa jumla
kwa makundi ya rika zote. Pale vijana na wazee wanapokuwa na uhusia-
no mwema, mafanikio ni makubwa. Katika Luka 2:36–38, tunamwona
Ana, nabii mke ambaye alimwona mtoto Yesu. Uwepo wake unaangazia
umuhimu wa uhusiano wa muunganiko wa rika.
4.Kufuata Mfano wa Yesu:
Katika huduma Yake yote, Yesu alionesha ujumuishaji kwa kuwakub-
ali watu wa kila kizazi. Kutoka kwa watoto waliokusanyika kumzunguka
hadi kwa wazee waliotafuta ushauri Wake, ujumbe Wake ulikuwa wa
watu wote. Alionesha mfano wa nguvu ya upendo, huruma na uelewa,
akivuka mipaka ya vikwazo rika.
Katika jamii zetu za mijini, kushinda vikwazo rika si changamoto tu
bali pia ni fursa kwa ajili ya ukuaji na umoja. Kwa kuchota hekima ku-
toka kwenye Maandiko na takwimu za hivi karibuni tunaweza kuwa-
hudumia vyema vijana na wazee kwa pamoja. Hebu na tuthamini nguvu
za pekee zinazoletwa na kila kizazi na kukuza uhusiano ambao unaakisi
upendo wa Yesu. Pamoja, tunaweza kujenga jumuia zinazostawi mahali
ambapo kila mtu, bila kujali umri, anapata kusudi, anajisikia nyumbani
na safari ya pamoja ya imani.

Ombi
Tunakusanyika mbele Yako leo, tukishukuru kwa wingi wa utofauti ka-
tika jumuia zetu za mijini, ambapo vijana na wazee huishi pamoja.
Tunapotafakari hekima ya Neno Lako lisilo na ukomo kwa nyakati zetu,
tunatafuta uongozi Wako katika kushinda vikwazo rika. Bwana, tunaom-
ba utuwezeshe kukumbatia nguvu na shauku ya vijana, ukiwatia moyo
ili kuweka kielelezo katika upendo, imani na usafi. Tusaidie kuheshimu
hekima na uzoefu wa wazee wetu, tukitambua mchango wao wenye
thamani. Tunaomba kwamba mazungumzo yetu yaakisi upendo na uju-
muishaji Wako, kama vile Yesu alivyohudumu kwa vizazi vyote. Tuungan-
ishe pamoja katika upendo, tukijenga jumuia yenye makusudi, kujisikia
nyumbani; katika jina la Yesu.
Amina.

14
Somo La 3

Kukabiliana Na Upweke Kwenye Jiji Lako


Na: Dk. S Yeury Ferreira
(Yohana 16:32)

Utangulizi
Upweke kwenye miji mikubwa ni suala linaloongezeka zaidi duni-
ani kote. Kutokana na hali ya kukua kwa miji na mabadiliko kwenye
elimumwendo ya familia, watu wengi wanajisikia hali ya upweke sana.
Katika miongo ya hivi karibuni, wakazi wa mijini wameongezeka. Mwa-
ka 2020, kulingana na takwimu ya Umoja wa Mataifa, zaidi ya 55% ya
wakazi wa dunia waliishi kwenye miji mikubwa, na huu ni mwelekeo
unaoendelea. Kinyume chake, licha ya wingi wa watu kwenye miji mi-
kubwa, sehemu kubwa ya wakazi wanapitia uzoefu wa upweke. Utafiti
uliofanywa na Chama cha Msalaba Mwekundu uling’amua ya kwamba
zaidi ya 20% ya watu wazima nchini Marekani mara kwa mara au wakati
wote, wanajisikia kuwa wapweke.
Upweke hauwapati watu wote kwa usawa na huwa unaathiri makundi
fulani ya watu kwa uzito zaidi. Wazee, walio wageni kwenye miji mi-
kubwa wanaotafuta fursa, walio na uraibu wa kazi, na wale wenye kazi
zinazohitajiwa sana mara kwa mara wanapitia uzoefu huu wa upweke.
Upweke sio tu hali ya kutengwa kimwili; ni hali pia ya kujisikia kutoku-
wa na uhusiano na kutengwa na wengine, jambo liwezalo kusababisha
hali ngumu kama vile sonona, fadhaa na hali duni ya kujistahi.
Ufafanuzi
1. Tatizo la Upweke
Upweke ni hali ambayo sisi sote tumepata kuipitia wakati fulani, je,
15
sivyo? Ni ile hisia inayojikita ndani kabisa ya tumbo wakati mtu un-
ayemjali sana anapokuwa mbali au pale unapodhani kwamba hakuna
anayekujali. Lakini ni muhimu kuelewa kwamba kuwa peke yako siyo
sawa na kujisikia mpweke. Nyakati fulani, kuwa peke yako ni sawa ka-
bisa. Hata Yesu Mwenyewe alikuwa akiondoka na kwenda mahali pa-
lipotulia ili aombe au atulie na marafiki (Mathayo 14:13; Marko 1:35;
6:31). Baadhi ya watu wanatumia muda mwingi wakiwa peke yao lakini
hawajisikii kuwa wapweke. Kwa mfano, mwanasayansi akiwa amezama
katika utafiti au msanii anapokuwa akiandaa kazi iliyo bora huwa anawe-
za kuwa peke yake lakini huwa hajisikii kuwa mpweke.
Kuwa peke yetu ni zaidi ya hali ya kimwili, kama vile pale unapocha-
gua kuwa peke yako kwa muda fulani. Lakini kujisikia mpweke ni suala
la kihisia; ni pale unapojisikia kutokuwa katika uhusiano, kutengwa, au
kupungukiwa na uhusiano wa maana na mtu mwingine. Nyakati fulani,
kuwa peke yako kunaweza kuwa ni jambo zuri, kama vile pale unapohi-
taji muda wa kufikiria au kuomba katika ukimya.
Kwa upande mwingine, upweke, huleta hisia mbaya. Hii ni hisia in-
ayoweza kufuatana na matukio ya kusikitisha kama vile kufiwa na mpen-
zi, talaka, ugonjwa mzito, au matatizo kama vile kukosa ajira. Sisi sote
tunaweza kupitia uzoefu wa upweke wakati fulani wa maisha kwa sa-
babu sisi sote tunahitaji uhusiano na watu wengine, na nyakati fulani
uhusiano hayo hujeruhiwa na kuharibiwa. Tunapojisikia kuwa wapweke
baada ya uzoefu unaoumiza, hapo ndipo tunapohitaji kweli msaada wa
mtu tuwezaye kumwamini.
2. Tiba ya Upweke
Suala la upweke linazungumzwa kwa kurudiwa-rudiwa kwenye Bib-
lia. Je, ulijua kwamba neno “pekee/peke yake” linaonekana sio chini ya
mara 188 kwenye toleo la Biblia ya tafsiri ya Kiswahili Union, lakini ni
mara chache sana linahusiana na kujisikia “mpweke”? Hapa tunao ukwe-
li mwingine wa kuvutia: Neno “upweke” halikuwa na maana yake kama
ilivyo sasa hadi hivi karibuni, katika karne hii, na katika Kiingereza hali-
kuonekana kwenye kamusi yoyote kubwa hadi baada ya Vita Kuu ya II.
Kwa maneno mengine, dhana ya kujisikia mpweke kama hali ya kiakili
ni jambo jipya.
Tunapoisoma Biblia, tunaona hoja muhimu sana mwanzoni: kamwe
Mungu hakukusudia kuwa wanadamu waishi peke yao. Baada ya Mun-
gu kuiumba dunia kwa siku saba, Biblia inasema, “Mungu akaona kila
kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana…” (Mwanzo 1:31). Lak-
ini kuna kitu kimoja ambacho Mungu hakuona kuwa ni chema: “Bwa-
16
na Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia
msaidizi wa kufanana naye” (Mwanzo 2:18). Tukiangalia kwa makini
maelezo ya Mwanzo 1, tunatambua kwamba wanyama waliumbwa ka-
tika makundi: “ndege” (Mwanzo 1:20), “Samaki” (Mwanzo 1:21) na
“wanyama” (Mwanzo 1:24). Lakini mwanadamu, aliumbwa peke yake
(Mwanzo 1:26). Hata hivyo, haukuwa mpango wa Mungu kwamba tui-
shi hivyo milele. Mungu alijua kwamba upweke haukuwa mzuri kwetu,
hivyo aliamua kumuumba mwenzi afaaye kwa ajili ya mwanamume.
Hivyo, katika Mwanzo 2:22, Biblia inatuambia kwamba Mungu alim-
uumba mwanamke kutoka katika ubavu wa mwanamume. Kisha, Mungu
akawabariki na kuwapa agizo: “Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na
kuitiisha” (Mwanzo 1:27–28).
Kama unavyoweza kuona, upweke haukuwa sehemu ya mpango wa
awali kwa ajili ya mwanadamu. Sisi tu viumbe wenye asili ya kujihusisha
kijamii. Tuliumbwa ili tuweze kuwasiliana na Mungu na watu wengine.
Tulizaliwa tukiwa na uwezo wa ndani wa kuunda uhusiano wa kijamii…
uhusiano huu wa kijamii na Muumba wetu na wanadamu wenzetu ni
muhimu kwa ajili ya kuishi kwetu. Lakini dhambi iliharibu mpango
huo, na sasa tunajisikia kuwa wapweke na kutokuwa na kuwa na hali ya
kuachana na Mungu na watu wengine.
Hivyo, tunapozungumzia upweke, tunapaswa kuelewa kwamba unat-
uathiri katika viwango viwili vya msingi. Kwanza, kiroho. Kiwango
cha kwanza cha uzoefu wa upweke ambacho watu wanapitia ni upweke
wa kiroho. Kama ilivyotajwa hapo awali, Mungu alituumba kwa ajili
ya kuwa na uhusiano na Yeye. Lakini jambo la kusikitisha, watu wengi
waliishi katika hali ya kuwa mbali na Mungu na hivyo huwa wanajisikia
kuwa na upweke wa kiroho. Hiyo ndiyo sababu, licha ya kuzingirwa na
watu na kuwa kila kitu wanachohitaji, wanajisikia kuwa wapweke. Ha-
watambui kwamba iwe ni pesa au vitu hakuna kiwezacho kujazia ombwe
lililopo maishani mwao. Upweke wa kiroho unaweza kujazwa tu kupitia
kwa uhusiano binafsi na Mungu.
Ukiwa na uhusiano na Mungu, unaweza kuwa peke yako kimwili bila
kujisikia ukiwa. Tafakari juu ya suala la Yusufu: aliuzwa kama mtumwa,
akitenganishwa na familia yao na rafiki zake, akipelekwa hadi mahali asi-
popajua ambapo hakujua lugha yao wala kuelewa utamaduni wao. Kwa
ufupi, alikuwa peke yake katika mtazamo wa kibinadamu. Lakini Biblia
inasema, “Bwana akawa pamoja na Yusufu, naye akasitawi” (Mwanzo
39:2). Ingawa alikuwa peke yake, hakuwa mpweke.

17
Vivyo hivyo, Bwana Yesu, katika siku zake za mwisho za maisha
Yake ya duniani, aliachwa na rafiki zake. Kama ilivyokuwa kwa Yusufu,
Bwana Yesu aliuzwa kwa gharama ile ile. Karibu kila mmoja aliyemfuata
Yeye aliondoka. Wakati fulani Bwana Yesu alisema, “Tazama, saa yaja,
naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao,
na kuniacha mimi peke yangu” (Yohana 16:32). Ukweli mzito usiopen-
deza, sivyo? Lakini alisema pia “Tazama, saa yaja, naam, imekwisha
kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi
peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja
nami.”
Kisha mtume Paulo, ambaye, wakati wa uhitaji, pia alijiona peke yake.
Alisema, “Katika jawabu langu la kwanza hakuna mtu aliyesimama upa-
nde wangu, bali wote waliniacha” (2 Timotheo 4:16). Hebu fikiria jinsi
huyu bingwa wa kuitetea kweli alivyohisi! Yeye aliyefungua makanisa
mengi, akahubiri watu wengi, na kufundisha mengi. Katika saa yake ya
giza nene, alijisikia mpweke. Lakini aliweza kuandika, “Lakini Bwana
alisimama upande wangu na kunipa nguvu” (2 Timotheo 4:17). Ingawa
Paulo alikuwa peke yake kimwili, kamwe hakuwa mpweke.
Kama Yusufu, Bwana Yesu, na Paulo, wewe pia, unaweza kuwa na
uhusiano maalum na Mungu. Unaweza kuishi na kutembea kila siku ka-
tika kuwepo kwake. Ukiwa na uhusiano huo na Mungu, utafurahia ush-
irika wake kwa namna ambayo, hata ukijikuta uko peke yako, hutajisikia
mpweke.
Pili, upweke unahusiana na uhusiano wa kibinadamu. Tunauita “up-
weke wa kiuhusiano.” Licha ya Adamu hapo awali kuwa na uhusiano
mkamilifu na Mungu, bado alijisikia hitaji la kupata urafiki wa wanada-
mu wengine. Mungu hakupuuzia au kudharau hitaji hilo. Badala yake,
Alimuumba mtu wa kujazia hitaji hilo. Mungu anajua ya kwamba tukiwa
wanadamu, tunahitaji urafiki. Upweke ni kama ishara inayotupa onyo au
kutuamsha: kama vile njaa inavyokuambia kwamba unahitaji chakula,
upweke unakuambia kwamba unahitaji urafiki na wenzi.
“Upweke wa kiuhusiano” unaponywa tu pale tunapojenga uhusiano
wa msingi na wengine. Tena, je, wajua? Kuna mahali uwezapo kufan-
ya hivyo! Kwa kweli waweza kufanya hilo kwenye familia yako, kazini
mwako, shuleni mwako, au kwenye vikundi vinavyoweza kutoa misaa-
da. Lakini moja ya njia zilizo bora zaidi imo kanisani.
Hebu nieleze kitu kabla sijaendelea. Biblia inaponena juu ya kanisa,
haizungumzii jengo bali kundi la waumini ambao wameokolewa kwa
neema ya Yesu Kristo (1 Petro 2:9). Hivyo, tunapoangalia kile Biblia
18
inachosema juu ya kanisa katika Agano Jipya, tunatambua kwamba kina-
husu jumuia ya Wakristo waliokuwa wakijaliana, waliopendana, walio-
kirimiana, waliokaribishana, waliohudumiana, waliofundishana, walio-
sameheana, waliosaidiana na kujaliana kila mmoja na mwingine kwa njia
nyingi. Kwa ufupi, hawa ni timu ya watu waliokuwa tayari kila mmoja
kwa ajili ya mwingine.

Hitimisho
Kwa ufupi, Mungu hataki ujisikie kuwa mpweke. Unaweza kujenga
uhusiano na Yeye na wengine pia, na hivyo kamwe usijisikie mpweke.
Katika moja ya mikutano yetu, dada mmoja aliyekuwa akisumbuliwa
na sonona na fadhaa kwa miaka mingi aliingia. Dada huyu alikuwa na
marafiki wachache sana na alitumia muda wake mwingi akiwa peke yake
kwenye makazi alikopanga. Hakutoka, ila tu alipokuwa akienda kazini
na kwenye duka la karibu kwa ajili ya kununua mahitaji. Yeye alidai
kwamba maisha yalikuwa ni mzingile au kero, na upweke ulikuwa ni
mwenzi wake wa siku zote.
Lakini siku moja, kupitia kwa mfanyakazi mwenzake, alipokea mwa-
liko wa kuhudhuria kwenye moja ya ibada za makanisa. Mwanzoni, ali-
toa udhuru kila mara, lakini rafiki yake alimsisitizia sana kiasi cha yeye
kusema, “Basi nitaenda mara moja tu, ili kujaribu nione hali inakuwaje.”
Hivyo alikuja kanisani Jumamosi moja na akawa nasi karibu siku yote.
Alishiriki nasi kwenye chakula kitamu cha mchana, na baada ya hapo,
akaenda pamoja na kikosi husika cha washiriki kwa ajili ya kugawa
chakula kwa waliokuwa na mahitaji. Kulingana na alivyoeleza baadaye,
siku ile iligeuka kuwa jambo maalum sana kwake. Miaka kadhaa ilikuwa
imepita tangu alipowahi kujisikia kukaribishwa hivyo mahali popote.
Juma lililofuata, aliamua kurudi. Vijana walimkaribisha kwenye kundi
lao lililokutanika kwenye moja ya makazi yao, naye akakubali. Alichoki-
shuhudia kilimshangaza: watu walikuwa wakifurahia maisha kwa namna
nzuri, bila ya hitaji la pombe wala madawa ya kulevya. Hakuamini. Ali-
jisikia kukubalika na kuthaminiwa. Zaidi ya hapo, alianza kupokea ujum-
be uliokuwa ukimjia kila juma wenye aya ya Biblia iliyovuviwa. Kundi
la wasichana lilimhusisha kwenye maombi yao maalum. Kwa hakika,
hakuwa na muda wa kujisikia mpweke.
Miezi sita baada ya kuingia kwenye lile kanisa kwa mara ya kwanza,
aliamua kubatizwa. Mara kabla ya kubatizwa, alitoa ushuhuda wake na
kusema kwamba upendo aliokuwa ameupokea kutoka kwa watoto wa
kanisa, vijana na watu wazima ulimsaidia kushinda upweke. Leo, yuko
19
huru kabisa, ameacha kabisa mazoea ya uvutaji wa sigara na unywaji wa
pombe, lakini jambo la muhimu zaidi, anafurahia uhusiano maalum na
Mungu pamoja na wengine.
Hivyo, vijana, ninaeleza kisa hiki ili kukuambieni kwamba wapo watu
wengi kwenye miji mikubwa wanaojisikia kama huyu msichana alivyo-
jisikia kabla hajakutana na kanisa letu. Hawa wanaweza wakawa waki-
pambana na mambo kama vile sonona na fadhaa, lakini urafiki wa dhati
wa kweli unaweza kufanya tofauti kubwa maishani mwao.
Mwaliko ni kwa ajili ya kuwatafuta wale wanaojisikia kuwa wapweke,
kuwapa mkono wa msaada, na kuwaonesha upendo na furaha ambayo
umeipata katika Yesu. Huwezi kujua ni mguso mzito kiasi gani uwezao
kuwa nao maishani mwa mtu.
Je, upo tayari kuitwaa changamoto hii?
Hebu tufanye jiji letu kupunguza upweke kwa kila mtu. Kwa pamoja
tunaweza kuleta mabadiliko!

20
Kupata Uponyaji na Matumaini
Na Ivonne Omaña

“Walilia, naye Bwana akasikia, Akawaponya na taabu zao zote. Bwa-


na yu karibu nao waliovunjika moyo, na waliopondeka roho huwaokoa”
(Zaburi 34:17-18).
Katika pilikapilika za majiji ya dunia, katikati ya kelele na vurugu,
ipo mioyo ambayo imefanywa kuwa migumu kutokana na mapambano
yasiyoonekana – changamoto za kiafya ambazo mara kwa mara huto-
kea bila kutambulika. Wakati wa harakati za mijini, kuwepo kwa Mungu
kunang’aa kwa upevu zaidi maishani mwa wale wanaopambana na chan-
gamoto za afya ya akili. Biblia inadhihirisha ya kwamba hata wale walio
waaminifu kwa Mungu walikabiliana na nyakati za kukatisha tamaa, fad-
haa na mazingira ya kutisha.

Eliya: Kushinda Hali ya Kukaa Pweke na Kukata Tamaa


Eliya, nabii mwenye nguvu, nabii wa Mungu, alikabiliana na wakati
wa kutengwa na kuteseka kiakili. Kwenye 1 Wafalme 19, tunamwona
akikimbia vitisho na kuanguka kutokana na uzito wa mizigo yake. Hata
hivyo, katikati ya mapambano yake, Mungu alikutana naye katika sauti
ya utulivu, akimhakikishia kwamba hakuwa peke yake. Kama ambavyo
Mungu alimpa Eliya hifadhi, faraja na kusudi kwa ajili ya kazi yake,
huwa anatembea karibu nasi katika nyakati zetu za kiza, akileta faraja na
mwelekeo.

Daudi: Kupata Nguvu Katika Hatari ya Kudhuriwa


Mfalme Daudi, aliyeupendeza moyo wa Mungu, alimimina hisia zake
na hali zake za kujisikia hatarini kwenye Zaburi. Katika Zaburi 42, Daudi
alieleza hamu yake kwa ajili ya Mungu katikati ya tufani yake ya ndani.
Licha ya hivyo, uaminifu ulifungua njia kwa ajili ya hali mpya ya ku-
jisikia kuamini na kutumaini upendo wa Mungu usioshindwa. Sisi pia
tunaweza kuanika mioyo yetu mbele za Bwana, tukiwa na ujasiri kwam-
ba anasikia vilio vyetu na anatupatia nguvu ya kustahimili.

Paulo: Kubadilishwa na Neema


Mtume Paulo, aliyefahamika kwa imani yake isiyoyumba, pia aline-
na juu ya mwiba uliokuwa mwilini mwake – pambano lililomsababishia
dhiki nyingi. Katika 2 Wakorintho 12, Paulo anaelezea jinsi neema ya
Mungu ilivyomstahimilisha, ikimfundisha nguvu ya Kristo katika udhai-
21
fu. Kama neema ya Mungu ilivyombadilisha Paulo, inaendelea kutenda
kazi ndani yetu, ikitupatia faraja na nguvu tunapopitia changamoto am-
bazo afya ya akili inazileta.

Tunaweza Kutia Nanga Katika Matumaini


Mapambano yetu huwa hayatufanyi sisi tufasiliwe nayo; hayo ni sehemu
ya safari yetu. Kama jinsi mapambazuko yafuatavyo usiku wenye kiza
kabisa, matumaini hung’aa hata katikati ya matatizo yetu. Biblia imeshe-
heni ahadi za urejeshwaji, kufanywa upya na uponyaji. Yeremia 29:11
inatukumbusha kwamba Mungu anayo mipango kwa ajili ya wakati wetu
ujao, mipango iliyojazwa kwa matumaini. Hebu tung’ang’anie ahadi hizi
tunapoendelea kupita katika changamoto za afya ya akili.
Tunapoendelea kuwahudumia wale wanaokabiliwa na changamoto za
kiakili kwenye miji mikubwa ya dunia, hebu tukumbuke kwamba Biblia
ni agano la rehema ya Mungu na ufahamu wake. Kupitia katika visa vya;
Eliya, Daudi, Paulo na wengine wengi, tunashuhudia jinsi nuru ya Mun-
gu inavyong’aa kwa uangavu zaidi katika nyakati zetu za udhaifu. Hebu
jiulize, tunawezaje kunyoosha mkono wa huruma na kuwapa uhakika
wanaopambana na matatizo ya afya ya akili? Tunawezaje kuwaonesha
kwamba hawako peke yao?

Ombi:
Bwana, ninaomba kwamba upate kutuongoza katika njia ya rehema na
Subira. Hebu tusaidie kuwafikia wale wanaopambana na changamoto
zao wenyewe na kuwapatia hali ya upendo na matumaini. Kama Mungu
alivyokutana na waliovunjika na waliochoka kwa neema na matumaini,
hebu nasi tuwe mifereji ya upendo, tukileta uponyaji na urejeshwaji kwa
mioyo inayohitaji hilo zaidi. Tusaidie kuhisi kuwepo Kwako na uongozi
Wako popote tuendapo ili tupate kuwasaidia wale wanaokuhitaji.

22
Somo la 4:

Kukabiliana na Sonona Kwenye Jiji Lako


Na: Dk. S. Yeury Ferreira
(Zaburi 40:2)

Utangulizi
Hebu tumtazame Ana, binti ambaye ameishi maisha yake yote kwenye
mji mkubwa. Huyu dada anapenda kila kitu kinachosisimua na kinacho-
changamsha ambacho kinapatikana kwenye jiji hili: utamaduni wake,
chakula na fursa za kazi. Lakini hivi karibuni, kuna jambo ambalo hali-
kuwa sawa. Yale mambo yaliyokuwa yakimsisimua na kuridhisha uhu-
siano ya kijamii, sasa yalionekana kuwa ya kuchosha na kutokuwa na
maana.
Takribani mwaka mmoja uliopita, Ana alianza kujisikia huzuni isi-
yo ya kawaida iliyodumu. Alijikuta akiamka asubuhi akiwa amechoka,
hata ingawa alikuwa kitandani usiku mzima. Kazi ikageuka kuwa mzigo
usiobebeka, naye akawa akipambana kumakinika katika kazi alizokuwa
amezifurahia hapo awali. Rafiki zake wakatambua alikuwa akianza ku-
jitenga na hakuwa tena na shauku ya kutoka na wenzake kwa ajili ya
kuwa pamoja tu kijamii. Wazo tu la kutoka kukutana na magari akienda
kukutana na marafiki lilimjaza fadhaa.
Zaidi ya hapo, Ana aliona badiliko kwake mwenyewe katika hamu
ya chakula. Nyakati fulani, alikula kupita kiasi katika jitihada ya kuja-
za utupu wa kihisia, huku nyakati zingine, akijikuta hana hamu ya kula
kiasi cha kupoteza sana uzito wa mwili. Kulala likawa ni suala lingine
lililogeuka kuwa pambano kubwa, kutokana na kukosa usingizi na hivyo
kujikuta akiamka katikati ya usiku akiwa na mawazo hasi.
23
Hatimaye, baada ya miezi ya kubeba mzigo huu kimya kimya, Ana
aliamua kutafuta msaada. Alikwenda kwa tabibu ambapo alianza kum-
welezea juu ya hisia zake za huzuni, fadhaa, na kukosa matumaini. Tabi-
bu huyu alimpima na kutambua kuwa alikuwa na sonona kali na hivyo
akampendekezea mpango tiba.
1. Tatizo la Sonona
Sonona ni kama wingu jeusi ambalo halisambai kwa haraka nalo li-
naweza kumwathiri mtu yeyote, vijana kama wewe na mimi. Hali hiyo
inaweza kukufanya kuwa mgonjwa na kutokupendezwa na vitu ulivyoku-
wa ukivifurahia hapo awali, hali iwezayo kukufanya kujisikia kuwa na
hatia au kujisikia kutokuwa na thamani. Hali hiyo inaweza pia kuathiri
usingizi wako na hamu ya chakula, kwa namna hiyo kusababisha uwe
dhaifu.
Zipo aina tofauti tofauti za sonona, kama vile:
• Sonona ya Kimazingira: Hii huwa inatokea katika mazingira ya
msongo kama vile kufiwa na mtu umpendaye wa karibu sana au ma-
tatizo ya kifedha. Hii inaweza kupotea mara hali inapokuwa bora.
• Sonona ya Misimu: Baadhi ya watu huwa wanajisikia kuwa na
huzuni nyakati fulani za mwaka, kama vile wakati wa majira ya bari-
di kukiwa na upungufu wa mwanga wa jua.
• Sonona ya Haiba ya Ghamu: Hapa dalili zinakuwa nzito zaidi. Un-
aweza kujisikia kutopenda shughuli zote, kupoteza uzito mwingi, ku-
weza kukasirishwa, au kuwa mzito sana katika kufanya mambo, na
kujisikia hatia.
• Sonona ya kiwendawazimu (kuchanganyikiwa): Hii inakuwa ni
tata zaidi, ikiwa na hali ya kuona vitu visivyokuwepo au kuwa na
dhana zisizo za kweli na zinazoonekana kuaminika sana akilini mwa
mgonjwa. Hii huwa inaongezea kwenye utata wa ugonjwa.
• Hali Upungufu Mkubwa ya Kisonona: Hii ni ya kawaida zaidi,
pale ambapo huzuni ya kina zaidi, kutokupendezwa na vitu, maba-
diliko ya hamu ya chakula na kukosa usingizi, na dalili zingine zin-
apoathiri maisha ya kila siku.

Miji mikubwa inaweza kuwa maeneo yanayolea na kukuza sonona


kutokana na msongo, kutokuwa na namna ya moja kwa moja ya kuun-
ganika na viumbe vya asili kama uoto wa asili, kuwepo kwa uchafuzi wa
hali ya hewa, na sababu zingine, kama vile mada yetu ya jana ya upweke.
24
Mambo haya yanaweza kuathiri hali yetu ya afya ya kiakili.
Sonona inaathiri vijana na wazee. Kulingana na taarifa za kitakwimu,
zaidi ya 20% ya vijana duniani kote wanataabishwa na hali ya changamo-
to za kiakili.1
2. Sonona Kwenye Biblia
Ingawa mara kwa mara huwa tunahusisha sonona na sayansi ya kisasa
ya tiba, mizizi yake inapatikana katika nyakati za kale, hata katika taarifa
za kibiblia. Biblia ina visa vya watu walioheshimika waliokabiliana na
nyakati za huzuni na kukata tamaa. Kupitia katika visa hivi, tunaweza
kupeleleza jinsi imani, matumaini, na uhusiano na Mungu vinavyowe-
za kuwa raslimali za kukabiliana na sonona na kupata njia ya uponyaji.
Hebu tutazame baadhi ya mifano:
3. Daudi: Mtu Aliyeupendeza Moyo wa Mungu
Daudi, aliyejulikana kama “mtu aliyeupendeza moyo wa Mungu,” ali-
pitia vipindi vya huzuni sana na dhiki. Zaburi zake ni ushuhuda unaogusa
kuhusu mapambano yake ya kihisia. Kwenye Zaburi 42, Daudi anaandi-
ka, “Nafsi yangu, kwa nini kuinama, na kufadhaika ndani yangu? Umtu-
maini Mungu; kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu,
Na Mungu wangu” (Zaburi 42:11).
Kwenye ibara hii, Daudi anakiri juu ya dhiki yake lakini pia anapata
nguvu yake kwenye imani yake na kutafuta matumaini na msaada wa
Mungu. Hii inatufundisha kwamba hata tunapokuwa katika hali ya ku-
katisha tamaa, imani inaweza kuwa nuru inayoongoza kwa wale wanao-
pambana na sonona.
4. Yeremia: Nabii Aliaye
Yeremia, ajulikanaye kama “nabii aliaye,” ni mfano mwingine wa
kibiblia wa mtu aliyepitia uzoefu wa huzuni ya kutisha. Kitabu chake,
Kitabu cha Maombolezo, kimesheheni masomo ya maumivu na taabu
kuhusu maafa yaliyoshuhudiwa. Katikati ya mateso haya, Yeremia anaan-
dika, “Najikumbusha neno hili, Kwa hiyo nina matumaini. Ni huruma za
Bwana kwamba hatuangamii, kwa kuwa rehema zake hazikomi” (Yere-
mia 3:21, 22). Licha ya uharibifu uliomzunguka Yeremia, uwezo wake
wa kuakisi na kupata matumaini moyoni mwake ni kumbusho kwam-
ba hata katika nyakati za giza kabisa, kujitathmini binafsi na matumaini
kunaweza kusaidia kufikia uponyaji wa kiroho.
1.https://www.unicef.org/mexico/comunicados-prensa/m%C3%A1s-del-20-de-losadoles-
centes-de-todo-el-mundo-sufren-trastornos-mentales
25
5. Eliya: Nabii Aliyechoka
Nabii Eliya ni mtu mwingine katika Biblia aliyekabiliana na sonona.
Baada ya ushindi mkubwa dhidi ya manabii wa Baali, Eliya alijisikia
kuzidiwa na uchovu na hofu na akatamani kufa. Hata hivyo, katika hali
yake ya kufa moyo, alipata uzoefu wa uhusiano maalum na Mungu kupi-
tia katika mnong’ono wa utulivu (1 Wafalme 19:12).
Kisa cha Eliya kinatufundisha kwamba hata katika nyakati mbaya ka-
bisa za sonona, kuwepo kwa Mungu kunaweza kuwa chimbuko la nguvu
na kufanywa upya kiroho.
6. Njia Iendayo Katika Kushinda Sonona
Mpendwa kijana, mtu fulani unayemfahamu au hata wewe mwenyewe,
anaweza akawa anataabishwa na sonona kwenye mji wako. Vifuatavyo
ni baadhi ya vidokezo viwezavyo kusaidia katika hali kama hiyo:
• Maombi na kutafuta Uwepo Wake Mungu: Maombi yanaweza
kuwa njia ya kupata faraja, matumaini na nguvu nyakati za sonona.
• Msaada wa Kijamii na wa Kiroho: Mwingiliano na waumini
wengine na kuunga mkono jamii ya Kikristo linaweza kuwa jam-
bo kubwa. Kushiriki kwenye kusanyiko, makundi yanayosaidia, na
jumuia ya kiimani vinaweza kusaidia katika kuleta hali ya kujisikia
kuhusishwa na kuungwa mkono kihisia.
• Kusoma na kutafakari Maandiko: Kusoma Biblia na kutafakari
maaya yanayozungumzia matumaini, nguvu na kushinda changamo-
to yanaweza kuwa msaada mkubwa.
• Kutafuta Ushauri wa Kikristo: Mshauri wa Kikristo au mchunga-
ji aliyefunzwa katika ushauri nasihi anaweza kukupa mwongozo wa
kiroho na kihisia ambao unahusu moja kwa moja sonona kutokana na
mtazamo wa kibiblia.
• Kuweka katika vitendo Msamaha na Shukrani: Kujifunza kusame-
he wengine na kujisamehe mwenyewe kunaweza kuwa mchakato
mzuri wa kujikomboa.
• Kuepuka Hali ya Kukaa Pweke: Kudumu katika kutafuta ushiri-
ka wa marafiki na wapendwa katika imani kunaweza kuwa kwenye
manufaa.
• Kutafuta Msaada wa Kitaalamu Pale Inapokuwa Muhimu: Sono-
na ni ugonjwa halisi, na katika hali zilizo nyingi, tiba za kitaalamu
kama vile matibabu au dawa vinahitajika.

26
• Kukumbatia Neema na Upendo wa Mungu: Kukumbuka upendo
wa Mungu huasaidia katika kupunguza hatia au aibu inayohusiana na
sonona.

Hitimisho
Kuna maelfu ya vijana na watu wazima kwenye mji wako wanaopam-
bana na sonona. Huu ni wakati mwafaka wa kuwapatia matumaini. Huu
ndio wakati wa kuwaambia kwamba Mungu anao uwezo wa kuwainua
kutoka katika shimo la kukata tamaa. Mpendwa kijana, ikiwa wewe au
mtu fulani umjuaye anapambana na sonona, akihitaji msaada kiroho na
kitiba anaweza kuwa yuko katika mahali bora zaidi pa kumwambia hili.
Wapo wazee na mashemasi walio tayari kukusaidia na kukupatia nyenzo
za kumfikia mtaalamu wa afya ya akili. Mwovu hataki kingine isipokuwa
kuua, kuiba na kuharibu maisha yako, LAKINI Mungu amekuja ili upate
kuwa maisha kamili. Mungu anakutakia uzima, nasi pia tunakutakia uz-
ima. Omba msaada!
Uwe jasiri, na kwa pamoja, hebu tukabiliane na suala la sonona
kwenye mji wako.

27
Maskini Utajiri Wangu
Na Ivonne Omaña
Aya ya Biblia: Wanafunzi waliposikia, walishangaa mno, wakisema,
Ni nani basi awezaye kuokoka? Yesu akawakazia macho, akawaambia,
Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.
Mathayo 19:25-26.
Katika suala la kushiriki injili na watu wengine, lipo kundi la watu
linaloleta hofu na hali ya mashaka kwa wengi wetu na hawa ni wale
walio matajiri na wenye mali nyingi. Ukweli ni kwamba mtazamo huu
kwa kundi hili la watu umekuwepo tangu Yesu alipokuwa pamoja na wa-
nafunzi Wake wakitembea kwenye njia za Yuda. Mfano bora zaidi katika
kuelezea mtazamo huu ambao watu wanao kuhusu kueneza habari za
wokovu kwa wenye mali nyingi unaelezewa kwenye kisa kuhusu Tajiri
Kijana kwenye Mathayo 19:16-26. Huyu mtawala alikuwa tajiri, na Bib-
lia inasema kwamba Yesu alimwomba aache vyote alivyokuwa navyo
vya kidunia na ndipo amfuate Kristo, huyu mtawala kijana akaondoka
akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi. Mathayo
19:22.
Jambo linaloshangaza zaidi na mwitiko wa mtazamo wetu wa kisasa
juu ya kushiriki injili na watu walio matajiri ni mwitiko waliokuwa nawo
wanafunzi wale baada ya tajiri yule kijana kuondoka na kukataa mwaliko
wa Mwokozi. Walimuuliza Yesu: “Ni nani basi awezaye kuokoka?” Aya
ya 25 lakini Yesu alitoa jibu lifaalo kabisa kwa swali hilo ambalo haliku-
wa la imani, “Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote
yanawezekana” aya ya 26. Hili ndilo limo kama kiini cha kile kilichoku-
sudiwa kushirikishwa katika mkakati wa kiinjilisti wa kueneza injili kwa
matajiri hasa hasa katika jamii ya kisasa iliiyoendelea.
Kile tunachokiona kama kisichowezekana, Mungu hana mipaka
na kufikia kwa mafanikio kile ambacho sisi wanadamu tulikiona kama
kisichowezekana. Mungu anatusubiri tuanze tu katika kuwafikiria watu
hawa kama watu wanaoweza kuokolewa. Hivi karibuni niliangalia video
fupi sana kutokana na kisa kilichokuwa na wanandoa wawili waliofaniki-
wa sana na kuwa matajiri. Kutokana na kufanya kazi kwa bidii na ustadi,
walikuwa wamejenga kampuni kubwa ya kutengeneza vitu vya kuchezea
watoto yenye thamani ya mamilioni ya dola. Walikuwa na majumba kad-
haa ya fahari yaliyokuwa na kila kitu ambacho mtu angetamani kuwa
nacho. Walikuwa na familia nzuri sana na kwa kuangalia kwa nje mtu
angeweza kudhani kuwa hawakuwa na mahitaji yoyote. Kisha wakati

28
wanandoa hawa walipoketi kujadili mafanikio ya kampuni yao mwandi-
shi wa habari alimuuliza mwanamke juu ya hisia zake kuhusu maisha na
mafanikio, naye akaelezea kwamba tangu alipokuwa na umri wa miaka
5, alijisikia kuwa tupu moyoni mwake kiasi cha kujitenga na kila mtu
akiwemo mumewe na mfanya biashara mwenzake kwa zaidi ya miaka
40. Alijisikia kama vile maisha hayana maana tena. Hakujali juu ya mai-
sha yake yaliyokuwa yamezingirwa na vitu ambavyo alikuwa amevitafu-
ta ili kujaza ombwe moyoni mwake. Inatupasa tutambue kwamba kundi
hili la watu wana hitaji la Mwokozi.
Mtume Paulo alifurahia fursa ya kushiriki injili kwenye mahakama
ya Agripa na waheshimiwa wengine. Danieli na rafiki zake Wayahudi
walikuwa kielelezo cha imani na utii kwa Mungu kwenye nyua za Ne-
bukadneza. Yusufu alifanya jambo hilo hilo kwenye Misri ya kale ali-
pomtumikia Farao. Kwa sababu ya ujasiri wa mtumwa kijana nyumbani
mwa Naamani, aliweza kupona na akaja kumjua na kumpenda Mungu
wa Israeli. Katika kizazi hiki cha leo, lazima tutafute fursa za kueneza
injili kwa matajiri. Yesu alikuja kumwokoa yeyote anayemwamini. Kin-
achoweza kuonekana kuwa hakiwezekani kwa wanadamu, kwa kweli ki-
nawezekana kwa Mungu. Hebu tumwombe Mungu kwa moyo ulio wazi
kabisa kufikia watu hawa walio katika hali ya uhitaji zaidi wa Mwokozi.

Ombi:
Mpendwa Mungu, tunaomba tukiwa na mioyo iliyo waziKwako, tukion-
gozwa na somo kutoka katika Mathayo 19:25 – 26. Tunajua ya kwamba
kuishiriki injili kwa walio matajiri kunaweza kuwa na changamoto, la-
kini tunakumbuka kwamba tukiwa pamoja nawe, hakuna kisichoweze-
kana. Kama wale wanafunzi walivyoshangaa kwamba yeyote anaweza
kuokolewa, tunaweza kuwa na mashaka na uwezo wetu wa kuwafikia
wenye mali. Hata hivyo, historia inatuonesha kwamba wewe unaweza
kugusa maisha ya hata wale wanaoonekana kuwa hawawezi kufikiwa.
Kama vile Paulo, Danieli na Yusufu walivyofikisha ujumbe Wako kwa
viongozi wakuu wenye mamlaka, hebu tusaidie tupate fursa za kufikisha
upendo Wako kwa matajiri kwenye dunia yetu leo. Tuwezeshe kuwaona
kama watu ambao pia wanamhitaji Mwokozi. Tupatie ujasiri, hekima,
na wema ili tufikishe Neno Lako kwao, tukijua kwamba kile kionekana-
cho kuwa kigumu kwetu, ni rahisi tu Kwako. Katika jina la Yesu tunaom-
ba. Amina.

29
Somo la 5

Kukabiliana Na Maradhi Kwenye Jiji Lako


Na: Dk. S. Yeury Ferreira
(3 Yohana 2)

Utangulizi:
Katikati ya jiji maarufu lenye hekaheka, maisha ya mjini hayakusi-
mama. Daima mitaa ilijaza watu wakiwa katika kasi na majengo mare-
fu yalionekana kufikia anga kama minara ya malengo shauku ya kupata
makuu. Lakini chini ya starehe zote hizo na mwonekano kulikuwa na
hatari zisizoonekana.
Asubuhi moja ya wakati wa baridi, tetesi zilianza kuzagaa kuhusu
ugonjwa ambao hakuna aliyeuelewa. Watu walijisikia kama wenye ma-
fua makali, homa kali, upumuaji wa shida, na vikohozi visivyokoma.
Mwanzoni, hakuna aliyejali kwa sababu, kwa kweli, mafua na homa za
mafua yalikuwa ni matatizo ya kawaida kwenye jiji kubwa kiasi kile,
sivyo?
Hata hivyo, ugonjwa huu ulianza kusambaa kwa kasi ya kutisha. Hos-
pitali zilijaa kwa muda mfupi na madaktari wakawa na hekaheka kuliko
mtiririko wa mtandao. Mamlaka za afya zikatoa tangazo la hali ya hatari
na kuanza kuchunguza kama ni kitu gani kilikuwa kikiendelea na ugon-
jwa huu. Wataalamu wa afya jamii walitathmini jinsi ugonjwa ulivyoku-
wa ukisambaa na kugundua kwamba ugonjwa huu ulikuwa na uhusiano
na duka fulani la chakula la “kigeni” katikati ya jiji, ambapo waliuza
nyama ambazo hazikuwa za kawaida.
Hali ya taharuki ikalishikilia jiji walipothibitisha kwamba ugonjwa
ule ulikuwa aina mpya ya kirusi ambacho kilikuwa kikiweza kuruka ku-
toka kwa wanyama kuja kwa binadamu. Hivyo, wakachukua hatua na
30
kutangaza mazuio, hali iliyofanya jiji zima kuwa katika hali ya tahad-
hari”! Lile duka kubwa lilifungwa haraka sana, lakini tayari walikuwa
wamechelewa kukomesha kasi ya kusambaa kwa ugonjwa. Maelfu ya
watu walikuwa wameambukizwa, na idadi ya waliokufa ikaongezeka.
Jiji liliingia kwenye ghasia kabisa. Mitaa ile iliyokuwa na hekahe-
ka ikageuka kuwa kama eneo tupu linaloandaliwa kwa ajili ya uigizaji
wa filamu. Watu walibaki majumbani kwa sababu ya hofu, milango ya
kibiashara ilifungwa na uchumi ukapinduka kwa nyuzi 180. Hospitali zi-
likaribia kushindwa kabisa, na madaktari walifanya kazi kama vile hapa-
kuwa na siku nyingine ya kuishi kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa.
Ingawa inaonekana kama kisa hiki ni cha kubuni kabisa, tunajua ya
kwamba hii ni kweli. Maisha kwenye mji yanaweza kuwa rahisi sana ku-
haribika kuliko ionekanavyo, na ni muhimu kujiandaa na kushirikiana
tunapokabiliana na maradhi kwenye miji mikubwa.

Mwendelezo
I. Maradhi Kwenye Miji Mikubwa
Maradhi kwenye miji mikubwa ni tatizo tata linalohusiana na maisha ya
kimji na afya za watu. Hebu tutazame baadhi ya visababishi vikuu vya
tatizo hili:
• Uchafuzi wa Hali ya Hewa: Kwenye miji kadhaa, hewa tunayoivu-
ta ni tatizo kubwa kutokana na idadi kubwa ya magari, viwanda,
na vyanzo vingine vya uchafuzi wa hewa. Uchafuzi huu wa hewa
unaweza kusababisha matatizo ya mfumo wa upumuaji kama vile
pumu, mkamba, na hata matatizo ya moyo.
• Uchafuzi wa Maji: Maji ni muhimu sana kwenye miji mikubwa, la-
kini ni suala liwezalo kusababisha madhara yasiyopendeza kama ha-
yakudhibitiwa vizuri. Maradhi yasambazwayo kwa njia za maji kama
vile kipindupindu yanaweza kuenezwa ikiwa mabomba na mifumo
ya utakasaji haipo katika hali nzuri.
• Wingi wa Wakazi: Kwenye miji mikubwa, watu wako pamoja kama
samaki kwenye karai, hali inayofanya maambukizi ya maradhi kuwa
jambo la kawaida. Homa ya mafua, UVIKO – 19 na maradhi mengine
yanaweza kusambaa kwa urahisi kwenye maeneo yenye wakazi wen-
gi zaidi.
• Kutokuwa na Huduma za Kiafya za Kutosha: Ingawa miji mikub-
wa inazo hospitali na kliniki kila mahali, siku zote sio rahisi kwa kila
mmoja kupata na kupokea huduma. Baadhi ya watu wanapungukiwa
31
kiuchumi au wanaishi mbali na vituo hivi vya afya, jambo lifanyalo
iwe vigumu kushughulikia magonjwa.
• Masuala ya Afya ya Kiakili: Msongo, fadhaa na sonona ni mambo
mazito na ya kweli kwenye miji mikubwa. Maisha ya mijini yanawe-
za kuwa na msongo mkubwa kutokana na ushindani wa kikazi, usafi-
ri, hali ya kuwa katika utengo wa kijamii na masuala mengine, jambo
linalochangia katika matatizo ya kiafya.
• Adha ya Wadudu na Wanyama Wagugunaji kama Panya, nk:
Kwenye baadhi ya miji mikubwa, wadudu kama vile mbu na wanya-
ma wagugunaji wanaweza kupitisha maradhi kama hawakudhibiti-
wa kikamilifu. Kwa mfano, dengue na maradhi mengine yanaweza
kuenezwa kupitia katika kuumwa au kukutana na wadudu hawa.
• Mtindo wa Maisha wa Kuketi: Wakazi wengi wa mijini wanaende-
sha maisha ya kuketi kwa sababu ya kazi za ofisini na hata kuwa
na upungufu wa nafasi za mazoezi. Hili linaweza kusababisha chan-
gamoto za kiafya kama vile unene kupita kiasi na maradhi yahusian-
ayo na moyo.
• Uchafuzi Utokanao na Kelele: Kelele zisizokoma kwenye miji mi-
kubwa zinaweza kusababisha viwango vikubwa vya msongo na ku-
vuruga usingizi. Hii inaweza kuathiri shinikizo la damu na hata hitaji
la pumziko, hii inasababisha kuwa na matatizo ya kiafya.

II. Mungu na Afya


Mungu wa kwenye Biblia ni Mungu wa afya. Katika 3 Yohana 1:2 ,
tunapata ujumbe wenye nguvu sana: “Mpenzi naomba ufanikiwe katika
mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.”
Katika mpango wa awali wa Mungu kwa ajili ya wanadamu, magonjwa
hayakuwepo katika kusudio. Je, waweza kuwafikiria wazazi wetu wa
kwanza wakiwa katika hali ile nzuri ya mtindo wa afya? Hakuna ucha-
fuzi, mazingira yakiwa ya kiafya, wakila njugu, nafaka, na matunda asil-
ia, vyote vikiwa havina kemikali ambazo ni hatari.
Ellen G. White, aliyeandikia suala la afya kwa upana, alisema kwamba
wazazi wetu wa kwanza, waliishi katika afya timilifu. Walikuwa warefu
na wenye mwonekano mzuri kama vile waliochorwa. Adamu alikuwa
mrefu sana zaidi ya urefu wa watu leo, na Hawa alikuwa mfupi kidogo tu
lakini akiwa mrembo na wa madaha.2
2 EllenG.White,
P a t ria r c h s a n d P r o p h e t s (Washington,D.C.:ReviewandHeraldPublishing
Association,2018),p.45.
32
Adamu na Hawa walikuwa na afya timilifu. Walikuwa na afya ya kim-
wili, kiakili na kijamii. Bora kuliko yote, walikuwa na muunganiko wa
karibu sana na Mungu, jambo lililowapatia hali nzuri sana ya afya ya
kiroho iliyovutia. Hata hivyo, afya hii kamlifu iliingiliwa. Wakati Adamu
na Hawa walipochagua kutokumtegemea Mungu nao wakafukuzwa ku-
toka katika paradiso, kila kitu kilibadilika na maradhi yakaibuka sehemu
zote.
Mwanzo 3 inaeleza jinsi wana ndoa wa kwanza walivyoanguka kwa
adui wa Mungu na kwa namna hiyo kumpa mgongo Muumbaji wao. La-
kini licha ya uasi wa wazazi wetu wa awali, bado Mungu anajali sana
afya zetu.
Kutokana na upendo Wake usio na ukomo, Mungu alituachia ahadi
inayotupatia fursa ya kuishi maisha yenye afya. Mwanzoni, Mungu al-
itoa ahadi Yake kwa Wana wa Israeli walipokuwa wakisafiri wakipita
jangwani, lakini sisi pia tunaweza kuikumbatia ahadi hiyo, kama Warumi
15:4 inavyosema: “Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandik-
wa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa
na tumaini.”
Hebu tazama ahadi hii ambayo Mungu aliwapatia Israeli kupitia kwa
Musa kwenye Kutoka 15:26: “Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya
Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega
masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu
yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwa-
na nikuponyaye.”
Nyakati za kale, watu wa Israeli walikuwa wameendelea katika ka-
nuni za afya. Inaonekana kwamba kitabu cha kale kiitwacho “Ebers Pa-
pyrus,” kilichoandikwa na Wamisri takriban mwaka wa 1500 KK, wakati
wa Musa, kiligunduliwa na wachimbuzi wa mambo ya kale. Kitabu hiki
kilikuwa ni mwongozo kwa ajili ya afya ya Wamisri, ingawa baadhi ya
dhana zao hazikuwa za kawaida. Hebu tutazame baadhi ya ushauri wa
kitiba unaopatikana kwenye mafunzo haya, lakini kwa kweli usije jaribu
haya nyumbani!
Kwa mfano, ili kuzuia uwepo wa mvi kichwani, walipendekeza
kwamba usugue damu ya paka mweusi iliyochemshwa kwenye mafuta
au mafuta ya nyoka mchacharikaji kwenye nywele zako. Na kama hu-
kutaka kuwa na upaa, ilikupasa utumie aina sita za mafuta: ya farasi,
kiboko, mamba, paka, a nyoka na ya mbuzi. Ilikupasa uchanganye asali
na unga wa meno ya punda ili kuimarisha nywele. Hapo vipi?

33
Kama umechomwa na kibanzi, maelekezo ya tiba yalihusisha “damu
ya mnyoo na kinyesi cha punda.” Ushauri mwingine wa ajabu uliku-
wa “damu ya mjusi, meno ya nguruwe, nyama iliyooza, mvuke kutoka
kwenye masikio ya nguruwe na hata wanadamu, wanyama, na kinyesi
cha inzi.” Hebu fikiria kama daktari wako angekupa vidokezo vya nam-
na hiyo leo. Ni ukichaa! Hawa ndio waliokuwa “watalaamu” wakati wa
Musa.
Bila shaka, lazima Musa alikuwa anajua maandishi haya ya Eber Papy-
rus kwa sababu, kulingana na Maandiko, alikuwa amejifunza elimu yote
ya Wamisri. Lakini jambo la kupendeza ni kwamba hutapata mapende-
kezo haya ya ajabu kwenye Biblia. Kwa nini? Kama ambavyo tumesema
tayari, kanuni za afya ambazo Mungu alikuwa amewapatia watu Wake
zilikuwa bora zaidi kwa ajili ya wakati wao.
Kwa mfano, katika zama za kati, Ulaya ilipigwa kwa pigo la “Black
Death” (Mauti nyeusi). Pigo hili liliua mmoja kati ya kila watu wanne na
hakuna aliyejua namna ya kulikomesha kwa sababu hawakuelewa kabisa
mikrobiolojia kama tuielewavyo leo. Je, unajua kama ni nani aliyewa-
okoa? Biblia! Hatimaye waliyageukia Maandiko, hasa Mambo ya Wala-
wi 13:46 isemayo, “Siku zote ambazo pigo li ndani yake, yeye atakuwa
mwenye unajisi; yeye yu najisi; atakaa peke yake; makazi yake yatakuwa
nje ya marago.” Kutokea kwenye Biblia wakajifunza umuhimu wa kum-
tenga mgonjwa.
Biblia inatoa maelekezo bayana kabisa kuhusu namna ya kuhudumia
afya zetu, na siyo tu afya ya kimwili, bali pia ya kihisia na kijamii – ka-
tika tamaduni husika na hasa afya ya kiroho.
Je, unafikiria nini?

Hitimisho
Wapendwa vijana, Mungu anwatakieni afya njema na kuieneza afya
hiyo kwenye mji wenu. Je, ulijua ya kwamba tiba ya Mungu imejiki-
ta zaidi katika kulinda na kuzuia kuliko katika kuponya? Alituachia vi-
dokezo nane ambavyo vinaweza kukusaidia kuishi maisha yenye nguvu
na yenye ulinganifu mzuri. Je, ungependa kuzijua? Ziko hapa zikiwa na
kifupisho HEKIMAMALIMAJUPU
• HE ni kwa Hewa Safi: Anza kujisikia vizuri kwa kujaza miili yenu
kwa hewa safi, kwa kuvuta pumzi ndani wakati wa jua. Oksijeni
ni muhimu kwa ajili ya chembehai. Hewa ikiwa ni safi ya kuvuta,
ndivyo unavyozidi kuwa na nguvu.
34
• KI ni kwa Kiasi: Epuka kuzidi kiasi, rafiki. Tumbaku, pombe, ka-
feini na vitu vyote vinavyopelekea kwenye uraibu. Lakini kiasi na
ulinganifu katika vile vilivyo salama.
• MA ni kwa maji: Maji, maji na tena maji zaidi. Maji yaliyo bora
zaidi kwa ajili ya kusafisha na kudumisha chembe hai katika hali ya
kuwa na maji. Lenga kunywa glasi sita hadi nane kwa siku.
• MA ni kwa ajili ya Mazoezi: Unahitaji kufanya mwili wako uwe hai
katika utendaji wake kwa mazoezi ya kila siku, hasa ikiwa ni kwenye
mazingira ya nje kadiri iwezekanavyo. Kutembea kidogo, kama nusu
saa, ni mwanzo mzuri. Songeni mbele, rafiki!
• LI ni kwa Lishe: Kula chakula cha kiafya na chenye viinilishe vyote
muhimu na nyuzinyuzi. Ulinganifu sawia ni muhimu katika kutunza
miili yetu katika hali iliyo bora zaidi.
• MA ni kwa Mapenzi ya Mungu: Usisahau maisha yako ya kiroho.
Imani na tumaini katika Mungu huimarisha afya yako na kuleta fu-
raha. Tumia muda wako kanisani pamoja na familia yako, mkijenga
upendo na matumaini.
• JU ni kwa ajili ya Mwanga wa Jua: Mwanga wa jua kidogo unajen-
ga hisia na nguvu. Lakini huo ni kwa kiasi, sawa? Kujianika kwenye
jua kusiko na kiasi ni hatari. Ni bora zaidi kupata mwanga huo asu-
buhi.
• PU ni kwa Pumziko: kupata usingizi wa kutosha ni muhimu, hii
ikimaanisha saa saba hadi nane kwenye chumba chenye hewa ya ku-
tosha. Weka ulinganifu sawia kati ya kazi na pumziko.
Hivyo rafiki, songa mbele ukiwa na hivi vidokezo vya afya! Tunzeni mii-
li yenu katika afya njema.

35
Usiruhusu Mashaka Yakudanganye
Na: Maria Manderson

Aya ya Biblia: Yakobo 1:5,6


“Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa
Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. Ila
na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni
kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku
na huku.”
Ilikuwa jioni ya ufufuo. Rafiki kumi wa Yesu wa karibu sana waliku-
wa wamekusanyika pamoja katika chumba, wakiwa na hofu...Yuda aliku-
wa tayari amejiua, na Tomaso (aliyejulikana pia kama Pacha hakuwepo.
Biblia haisemi kwa nini Tomaso hakuwepo, bali tunajua kuwa walikuwa
kumi tu. Walikuwa wameweka makomeo mlangoni, kwa tahadhari kue-
puka endapo baadhi ya watu waliomwua Yesu wangekuja kuwaua pia.
Walikuwa wapweke, waliochanganyikiwa, wenye huzuni...na mashaka
yalianza kuingia mioyoni mwao. Ingekuwaje kama wangekuwa wame-
kosea? Ingekuwaje kama Yesu alikuwa wa uongo? Ndipo ghafla Yesu al-
ipotokea kati yao. Licha ya kuweka makomeo yote, haikutosha kumzuia
Yesu asiingie; hapo akawa amesimama mbele yao. Wakati fulani baa-
daye wanafunzi walimweleza Tomaso yaliyotukia, na Tomaso, mwenye
kushuku kwamba amekuwa, alisema angeamini ikiwa tu angeona alama
za misumari katika mikono ya Yesu na kuweka mikono yake kwenye
jeraha la ubavuni Mwake. Wakati fulani baadaye walikuwa pamoja tena
na Yesu akawatokea. Lakini safari hii, Yesu aliweka mtazamo Wake kwa
Tomaso. Yesu akamwambia kwa upole, “Chukua kidole chako na uchun-
guze mikono Yangu. Chukua mkono wako na uweke ubavuni Mwangu.
Usiwe asiyeamini. Amini.” Je, wewe ni Tomaso? Je, unahitaji kuona ush-
ahidi?
Wenye mashaka/wenye kushuku mara kwa mara huwa wanaogopa
kupotoshwa na kwa kawaida wako macho dhidi ya watu wasio waamin-
ifu… na hivyo wana wasiwasi na Wakristo. Katika kushiriki Biblia na
wale wasioamini, ni muhimu sana kuwa waaminifu na wakweli. Kwenye
tukio hilo hapo juu tumeona kwamba Tomaso alikuwa mkweli kuhusu
hisia zake.
Hebu tuangalie mfano mwingine katika Biblia, Yohana 6:42 “Je!
Huyu siye Yesu, mwana wa Yusufu, ambaye twamjua babaye na ma-
maye? Sasa asemaje huyu, Nimeshuka kutoka mbinguni?”

36
Hapa tunaona kwamba watu wanaouliza swali walikuwa na sababu
halali za kutilia shaka, lakini kama watu wengi wenye shaka na wenye
dukuduku, wanajibu swali lao wenyewe. Unapozungumza nao ni lazima
uwape majibu ya uhakika kwa sababu wana maoni na imani kali sana juu
ya Mungu na Biblia. Wanaamini kuwa wanajua ukweli. Mtazamo huu
wakati mwingine ni mgumu sana kuupenya.
Kwa kweli, hata wanafunzi na marafiki wa karibu wa Yesu walikuwa
na shaka fulani. Tunasoma kwamba hata baada ya Kristo kufufuka kuto-
ka kwa wafu na kukutana na wanafunzi Wake huko Galilaya “wengine
waliona shaka.” Ili kuwafikia watu hawa kwa injili utahitaji kuomba ili
Mungu akuoneshe kwa usahihi jinsi na nini cha kuwaambia. Wanahitaji
kuona ushahidi.

Ombi:
Mpendwa Baba wa mbinguni, tunakushukuru kwa wema Wako na
rehema. Tunakushukuru Bwana ya kwamba bado tunayo imani laki-
ni tunaomba utusaidie kukuamini na kukutumaini zaidi. Pale tulipo na
mashaka, tafadhali tusaidie katika kutokuamini kwetu.
“Wahurumieni wengine walio na shaka” Yuda 1:22.

37
Somo la 6

Kukabiliana na Hali ya Kutokuwa na Matumaini


Kwenye Mji Wako
Na: Dk. S. Yeury Ferreira
(Wakolosai 1:27)

Utangulizi:
Mfikirie John, kijana aliyelelewa katikati ya jiji kubwa. Kuanzia umri
wake mdogo, alipitia changamoto zilizokuja na maisha ya jiji. Wazazi
wake walifanya kazi kwa saa nyingi ili kupata riziki, lakini kwa sababu
ya kazi zao ngumu, hawakuweza kuwapo karibu naye kila wakati.
Kadiri muda ulivyosonga, John aliingia katika ujana na kuanza kuhisi
shinikizo la kikatili la jiji. Katika shule yake, ushindani wa kitaaluma uli-
kuwa mkali, na shinikizo la kupata alama za juu lilikuwa kwenye kilele
chake. Licha ya jitihada zake za kusoma, nyakati fulani alihisi kulemewa
na kazi nyingi na matarajio ya wazazi wake. Alijiuliza ikiwa kweli an-
gekuwa na mustakabali wake katika jiji hilo.
Katika jamii yake, masuala ya usalama yalikuwa jambo la kila siku.
Wizi na michoro ya ovyo ilikuwa ya kawaida, na John alilazimika kutem-
bea katika mitaa yenye giza na iliyoharibiwa kwa kiasi fulani alipokuwa
akirudi kutoka shuleni. Hakujisikia salama wala kuwa na uhusiano na
jirani zake, jambo ambalo lilimfanya ajihisi mpweke na kuvunjika moyo
zaidi.
John alipoendelea kukua, alitambua kwamba rafiki na wanafunzi
wenzake pia walikuwa wakikabilina na matatizo kama hayo. Wengi wali-
pambana na msongo wa shule, matatizo ya kiuchumi, na ukosefu wa mi-
pango iliyo wazi jijini. Walihoji kama wangewahi kuachana na mzungu-
ko wa mfadhaiko na kupata maisha bora zaidi.
38
Ufafanuzi:
Kutokuwepo kwa matumaini kwenye miji mikubwa kunaathiri watu
kote duniani. Kimsingi, inafikia hatua ya kuhisi kana kwamba hakuna
fursa au nafasi kwa ajili ya kuboresha mambo na hili linaweza kuhusish-
wa na mambo kadhaa.
• Kukosekana kwa Usawa Kiuchumi: Moja ya mambo yanayochan-
gia sana ukosefu wa matumaini katika miji ni ukosefu wa usawa wa
kiuchumi. Wakati kuna pengo kubwa kati ya utajiri na hali ya maisha
ya makundi tofauti jijini, wale walio chini wanahisi kuwa wana fursa
chache za kuboresha maisha.
• Upungufu wa ajira: Miji inavutia watu wanaotafuta kazi na hali in-
ayoahidi mustakabali bora, lakini kazi zikiwa hazitoshi, wengi huwa
wanaachwa katika mashaka ya kiuchumi, hiyo huongeza kupotea
kwa matumaini.
• Kutokuwa na Makazi: upungufu wa makazi yenye gharama nafuu
au makazi yaliyo salama katika hali nzuri, inaweza kuwa ni moja ya
mambo ya msingi katika kupoteza kwa matumaini. Usipokuwa na
mahali salama na pakudumu pa kuishi, utajisikia kama huna uwezo
wa kudhibiti maisha yako.
• Uhalifu na Hali ya Kutokuwa na Usalama: Kujisikia kutokuwa
salama kutokana na viwango vikubwa vya uhalifu au kuwepo kwa
ukatili katika mji, huchangia kwa kutokuwepo kwa matumaini.
Nyakati fulani, mtu huwa najisikia ukiwa umenaswa kwenye ujirani
wako na hivyo kujisikia kuogopa kutafuta fursa mpya.
Je, inawezekana kushinda hali ya ukosefu wa matumaini kwenye mji?
Tutapata wapi matumaini? Neno hili, “matumaini” linaonekana mara
nyingi kwenye Biblia na huwa ni mada inayojirudia rudia, ikikazia
umuhimu wake katika imani na uhusiano wetu na Mungu.
Hebu tazama baadhi yaaya za Biblia kuhusu matumaini:
• Warumi 15:13: “Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha
yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini,
katika nguvu za Roho Mtakatifu.”
• Waebrania 11:1: “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yataraji-
wayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.”
• Zaburi 42:11: “Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani
yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya
ya uso wangu, Na Mungu wangu.”

39
• Yeremia 29:11: “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, ase-
ma Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi
tumaini siku zenu za mwisho.”
• 1 Petro 1:3: “Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kris-
to, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate
tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu.”
Aya hii imetusaidia kuelewa kwa ubora zaidi juu ya matumaini. Yapo
kama nanga inayotusaidia kukaa kwa namna thabiti katikati ya dhoruba.
Kama vile merikebu inavyohitaji nanga ili kuepuka kupelekwa pasipoku-
sudiwa, tunahitaji kweli hizi tatu ili kudumu katika matumaini.

Ukweli #1: Biblia – Kitabu cha Matumaini:


Warumi 15:4 inatuambia kwamba “Kwa kuwa yote yaliyotangulia
kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya
maandiko tupate kuwa na tumaini.” Biblia ni hazina ya tumaini. Biblia
imejaa visa vya watu ambao walikabili changamoto na vikwazo lakini
pia walipata tumaini na ukombozi wa kimungu. Mungu anazungumza
nasi kupitia katika Biblia, akitupatia ahadi na maneno ya kutia moyo
ambayo yanatujaza tumaini katikati ya nyakati ngumu.
Ili kupata tumaini, mwongozo, na faraja katika Neno la Mungu ni laz-
ima uwe na msimamo thabiti. Huwezi kuisoma tu wakati mwingine, iki-
wa una muda kidogo wa ziada na wakati mwingine husomi. Unapaswa
kusoma na kujifunza Neno kwa maombi kila siku. Yapasa iwe tabia ya
kila siku. Zaidi ya hayo, shiriki visa vya matumaini kutoka kwa Biblia na
wengine ili kuwatia moyo na kuwapatia ujasiri wa kukabiliana na nyakati
ngumu.

Ukweli #2: Yesu - Tumaini la Utukufu:


Wakolosai 1:27 inatuambia; “ambao Mungu alipenda kuwajulisha
jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo
ndani yenu, tumaini la utukufu.” Yesu ndiye chanzo kikuu cha tumaini
na anawakilisha utukufu wa Mungu. Uhai, kifo, na ufufuoWke hutupatia
tumaini la kupatanishwa na Mungu na ahadi ya uzima wa milele. Imani
katika Yesu hubadilisha maisha yetu na kutujaza na tumaini la kupata
utukufu wa milele pamoja Naye.
Ili kudumisha tumaini, ni muhimu kukuza uhusiano wa binafsi na
Yesu kupitia sala na kutafakari, huku tukipata uzoefu tumaini Lake na
mabadiliko katika maisha yetu.

40
Ukweli #3: Ujio wa Pili wa Kristo - Tumaini Letu Lenye Baraka:
Tito 2:13 inasema, “tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo
ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;.” Ahadi
kwamba Yesu atarudi ni chanzo cha tumaini kwa waumini. Kujua kwam-
ba Yesu atarudi kusimika ufalme Wake wa milele hutujaza na matarajio
na hutuchochea kuishi katika utakatifu na utayari. Tumaini hili linatupa-
tia nguvu ya kukabiliana na matatizo ya sasa kwa uhakika wa wakati ujao
mtukufu.
Katika nyakati zenye changamoto, daima kumbuka ahadi ya ujio wa
pili wa Kristo ili kupata faraja na nguvu.

Hitimisho:
Kwa muhtasari, Biblia inatupatia chanzo kisicho na kikomo cha
tumaini. Yesu ndiye kielelezo cha tumaini la utukufu na ujio wa pili
wa Kristo ni tumaini letu lenye baraka. Kwa kuzipokea kwa furaha
kweli hizi na kuzitumia katika maisha yetu ya kila siku, tunaweza kuwa
na uzoefu wa matumaini yanayopita hali na kutuongoza kuelekea mus-
takabali wa milele na Mungu.
Unamkumbuka John? Siku moja, alipata fursa ya kuhudhuria mkuta-
no wa uinjilisti katika jiji lake. Mhubiri alizungumza kuhusu umuhimu
wa kuwa na nguvu, kutafuta fursa, kujenga mtandao wa usaidizi, na ku-
endeleza uhusiano wa kina na Yesu Kristo. Maneno ya msemaji yalimgu-
sa sana John, ambaye alianza kutafuta njia za kuboresha hali yake.
Ingawa jiji hilo bado lilikuwa na changamoto zake, John alianza kuona
mwanga wa matumaini kwa ajili ya maisha yake ya baadaye. Alitambua
kwamba, kwa jitihada na usaidizi ufaao, angeweza kushinda vizuizi na
kutengeneza njia kwa ajili ya maisha bora. Kisa cha John kinatukumbu-
sha kwamba hata katika miji migumu zaidi, matumaini na ukuaji wa bin-
afsi unawezekana unapotafuta msaada, fursa, na kufungua moyo wako
kwa Yesu, tumaini la utukufu.

41
Kumcha Bwana Ndilo Jambo Muhimu!!
Na: Dr. Pako Mokgwane
Mithali 2:1-6, 1 Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu, Na
kuyaweka akiba maagizo yangu; 2 Hata ukatega sikio lako kusikia heki-
ma, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu; 3 Naam, ukiita busara, Na
kupaza sauti yako upate ufahamu; 4 Ukiutafuta kama fedha, Na kuuta-
futia kama hazina iliyositirika; 5 Ndipo utakapofahamu kumcha Bwana,
Na kupata kumjua Mungu. 6 Kwa kuwa Bwana huwapa watu hekima;
Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;
Kimsingi, majiji huwa na watu wengi sana , huwa ni mkubwa kuliko
miji au vijiji. Kwa hivyo, ungetarajia kuona watu wengi, magari mengi,
taa angavu, majengo marefu na kusikia kelele nyingi na kutokuwepo kwa
shughuli za kilimo au chache sana za namna hiyo, lakini kilicho muhimu
zaidi kwa usomaji wa leo ni ukweli kwamba miji huwa ina watu. Mion-
goni mwa wenyeji wa miji ni wenye elimu. Hii ni kwa sababu mashirika
mengi yanaajiri watu waliosoma. Aidha, taasisi za elimu ya juu zinapa-
tikana katika miji. Kwa hivyo, jiji ni zaidi ya alama halisi kwenye rama-
ni. Ni mahali ambapo tunaona aina nyingi za watu, baadhi yao wakiwa
wamejaliwa sana maarifa, habari, dhana na ufahamu. Walakini, haya
yote haijalishi ikiwa mtu hamuogopi Mungu!
Wasomi huwa ni wanadamu wa kawaida wenye mielekeo ya asili
kama sisi. Ukweli kwamba wamefikia viwango vya juu vya elimu hau-
waondoi kutoka kwa hali halisi ya maisha chini ya jua. Mtu fulani hana
budi kuwafikia kwa sababu neno la Mungu halina upendeleo. Ni kama
upanga ukatao kuwili (Waebrania 4:12). Linakata na kupita katika taba-
ka zote za piramidi ya kijamii. Hakuna mwanadamu anayeweza kusema
kwa usalama kuwa hamhitaji Yesu au hahitaji kutiwa moyo kwa sababu
ya kile alichonacho. Licha ya hivyo, Yesu ametutuma na injili ya neema
kwa watu wote (Ufunuo 14:6-12). Mbinu ya Kristo kulingana na Ellen
White (Ministry of Healing, uk.143) inastahili kuigwa, “Mwokozi ali-
changamana na watu kama mtu aliyewatakia mema. Aliwahurumia, ali-
hudumia mahitaji yao, na akawafanya wamwamini. Kisha Akawaalika,
‘Nifuateni.’” Kwa kufuata njia hii, hapa chini kuna baadhi ya njia za
kivitendo za kuwafikia wenye elimu ya kutosha:
1.Uwe mshirika wa jumuia za wanazuoni ili uweze kuwafahamu na
kukutana nao.
2.Hudhuria makongamano ya utafiti (ya Kikristo na yasiyo ya Kikris-
to) ili kuchanganyika nao.
42
3.Onesha huruma kwa kushiriki katika huzuni zao katika nyakati zao
za huzuni.
4.Waalike kwenye maonesho ya afya au siku za furaha za familia ili
kuhudumia mahitaji yao.
5.Anzisha kituo cha ubora kwa ajili ya watoto ili kuwavuta wazazi wao.
6.Zungumza kutokana na uthibitisho wa kisayansi ambao haupingani
na ukweli wa Biblia ili kupata imani yao.
7.Mtangaze Kristo kwao kupitia kwa Neno la Mungu na mtindo wa
maisha halisi.
Fanya hivyo kwa sababu unamcha Bwana kwa maana ndilo jambo kuu
la maana. Fanya hivyo ili kutambulisha kicho kwa ajili ya Bwana na kwa
wengine kwa sababu ni wajibu wako.

Ombi
Mpendwa Yesu, Leo nimechagua kufurahia aina zote za watu katika jiji
langu. Tafadhali nipe ujasiri, mawazo yaliyonyooka, ukuu wa tabia na
utulivu wa makusudi ili niwe kila kitu kwa kaka na dada zangu walioe-
limika. Nataka kusimama kwenye pengo kwa ajili ya utukufu Wako. Ta-
fadhali fungua njia kwa ajili ya mvuto wangu. Ninahitaji hekima Yako
jinsi ya kuhusiana na watu, kuchanganyika nao, kuonesha huruma,
kuhudumia mahitaji yao, kupata kuaminiwa nao na hatimaye kuwaalika
wakufuate. Katika jina la Yesu, AMINA.

43
Ibada: Ibada kwa njia ya Ukarimu
Na: Mwenya Mpundu

Fungu: “Mpe kwa kweli, wala moyo wako usisikitike utakapompa;


kwa kuwa atakubarikia Bwana, Mungu wako, kwa neno hili katika kazi
yako yote, na katika kila utakalotia mkono wako.”—Torati 15:10
Somo la ibada ya leo litakuwa limejikita katika kitabu cha Kumbu-
kumbu la Torati 15:4 – 11. Ikiwa ungeweza kufupisha kitabu cha Kum-
bukumbu la torati kwa neno moja, neno hilo lingekuwa Agano. Kitabu
hiki kinaelezea kwa muhtasari agano au ahadi ambazo zinamwunganisha
Mungu na wana wa Israeli kwa njia ya viapo vya uaminifu na utii. Ka-
tika aya ya tatu na ya kwanza ya kitabu cha Kumbukumbu la torati,
tunajifunza kuhusu miaka saba ya maachilio. Huko Israeli wakati kama
huu, watu walikopa fedha wakiwa na uelewa kwamba katika mwaka wa
saba, kutakuwa na maachilio, maachilio ya Bwana. Hii ilikuwa ni njia
ya Mungu ya kusimika mfumo wa uchumi ambao usingemwacha mtu
yeyote kuwa masikini wa kudumu. Baadhi wangepitia kipindi kigumu
maishani lakini walikuwa na fursa ya kujijenga upya.
Sasa soma Kumbukumbu la torati 15:4 – 11.
Mawazo manne yaliibuka kwangu nilipokuwa nikisoma aya hii.
Utii na Baraka Aya ya 4:
Katika ulimwengu ambao umejawa na ubinafsi, ukosefu, na uhitaji,
Mungu anaahidi kusimama imara—hakutakuwa na ukosefu miongoni
mwa watu Wake. Nchi ya urithi wetu sio tu ya kushikika; ni ya kiroho na
kwa ajili ya watu wote. Sisi kama vijana wakubwa, tunalazimika kutam-
bua kwamba Baraka za Mungu zimekusudiwa kwa ajili ya kila mtu. Tuk-
iukumbatia ukarimu Wake, tunakuwa vyombo vya kubeba upendo Wake,
tukihakikisha kwamba Baraka Zake nyingi zinatiririka kupitia kwetu ili
kuwafikia wengine. Na kisha Mungu anaendelea kutubariki.
Msimamo wa Moyo Wako Aya ya 7:
Aya hii inatupatia changamoto ya kukuza moyo wa ukarimu, tukiene-
za wema na upendo kwa wale wanaotuzunguka, bila kujali hali zao.
Katika ulimwengu ambao mara kwa mara unasisitiza kujifikiria sisi
wenyewe, Mungu anatuita kuwa tofauti na kuwafikiria wengine. Kama
vijana wakubwa, tunayo fursa ya kukuza roho ya huruma, ambayo inao-
na masumbuko ya wengine na kuwafikia. Hebu na tuchague kuitikia kwa
huruma dhidi ya kutojali na kuonesha huruma dhidi ya hali ya kutojali.
Namna ya Kutoa: Aya ya 9 – 11
44
Aya hii inanasisitiza mtazamo uliopo nyuma ya utoaji wetu. Mungu
anamfurahia mtu atoaye kwa moyo wa ukunjufu ambaye hutoa kwa hiari,
pasipo uchungu. Matendo yetu yaanaakisi tabia ya Mungu pale tunapo-
toa kwa moyo mchangamfu. Tunakumbushwa pia kwamba tunapokuwa
navyo, LAZIMA tutoe. Ni amri, na kutofanya hivyo itakuwa ni dhambi.
Kama vijana wakubwa, tunashauriwa kukumbatia moyo wa uchangamfu
katika matendo yetu ya utoaji—ikiwa ni muda wetu, mali au talanta zetu.
Mtazamo huu haumnufaishi tu yeye anayepokea; unatubadilisha na kule-
ta Baraka katika kila eneo maishani mwetu.

Ombi:
Bwana, tunakushukuru kwa yale yote ambayo umetubariki kwayo.
Tupatie neema ya kutoa bila kusaza, sio tu kwa vitu tulivyonavyo bali
pia katika muda wetu, talanta na wema. Tunaomba utufundishe kutoa
kwa furaha, bila ya kuhesabu gharama, tukijua kuwa unaiona mioyo yetu
na unaahidi kutubariki kwa njia ambazo hatuwezi kuzifikiria. Tunatam-
bua kwamba kila wakati ulimwengu unaweza kuwa na mahitaji na bado
tunaitwa kukunjua mikono yetu usoni pao wenye mahitaji. Tunaomba ut-
upatie uwezo ili kuwa vyombo vya upendo Wako, tukishiriki na wengine
kwa ukarimu Baraka Zako na wale wanaotuzunguka.—Katika jina la
Yesu tunaomba, Amina.

45
Somo La 7

Kukabiliana na Hofu Kwenye Mji Wako


Na: Dk. S. Yeury Ferreira
(Waebrania 11:1)

Utangulizi
Wakati Franklin D. Roosevelt alipokuwa Rais wa Marekani Machi 4,
1933, nchi ilikuwa katika msukosuko kutokana na mgogoro, na ilihitaji
dozi ya matumaini baada ya zaidi ya miaka mitatu ya kushuka kiuchumi.
Siku hiyo, Roosevelt alitoa hotuba ambayo bado inazungumzwa na ku-
tajwa katika vitabu na makala, kwa maneno ambayo yanajitokeza sana:
“Kitu pekee tunachopaswa kuogopa ni hofu yenyewe.”
Kwa maneno hayo, Roosevelt aliweka wazi kuwa adui namba moja si
uchumi ulioyumba bali ni hofu yenyewe. Hofu, kama mwanasaikolojia
wa Kyuba Mira Y. López alivyosema, ni mnyama mbaya sana anayefan-
ya mtetemo kwenye uti wa mgongo wako. Hofu huiba mawazo yako na
inaweza kuteka nyara ndoto na utashi wako. Inakufanya usahau kile un-
achokijua na kupoteza hali ya kujiona wewe ni nani. Inakufanya ujisikie
kukosa udhibiti wa kile unachokijua na kukufanya kana kwamba huwezi
kurejea tena katika hali ile ya awali. Inakufanya usiwaamini watu wale
ambao unapaswa kuwaamini bila kusita. Inakufanya uwe mwenye ku-
dai sana badala ya kuwa mnyenyekevu na kutumikia. Inakufanya ufikiri
kwamba Mungu si kitu katika kukabiliana na matatizo na changamo-
to zako. Inakufanya utafute ndani ya watu kile unachoweza kupata kwa
Yesu Kristo pekee.

46
Ufafanuzi
1. Hofu katika Miji
Hofu katika miji ni jambo changamano ambalo huathiri vijana na wazee
na linaweza kuhusishwa na mambo kadhaa yanayochangia. Hapa kuna
baadhi ya sababu kuu:
• Ghasia na Ukatili wa mijini: Mtazamo wa ukosefu wa usalama ku-
tokana na uhalifu na vurugu katika miji ni mojawapo ya sababu kuu
zinazochangia hofu. Uhalifu kama vile ujambazi, mashambulizi, na
mauaji yanaweza kuleta hofu kwa watu, hasa katika maeneo yenye
viwango vya juu vya uhalifu.
• Matatizo ya usafiri: Ukosefu wa usalama katika vyombo vya usafiri
wa umma, kama vile wizi au unyanyasaji wa kijinsia kwenye treni au
mabasi, kunaweza kuongeza hofu katika miji. Hii inaweza kupungu-
za uhamaji wa watu na kuathiri ubora wa maisha yao.
• Shinikizo la kijamii na la vyombo vya habari: Kuenea kila mara
kwa habari kuhusu matukio ya vurugu na uhalifu katika vyombo vya
habari na kwenye mitandao ya kijamii kunaweza kuongeza hofu kati-
ka jamii. Kudumu kupata visa vya kutisha kunaweza kuchangia mta-
zamo potovu wa usalama katika jiji.
• Kutokuwa na imani na taasisi: Kutokuwa na imani na taasisi za
serikali zinazohusika na kudumisha usalama na utulivu wa umma
kunaweza kusababisha kuongezeka kwa hofu. Mtazamo wa rushwa
au uzembe unaweza kudhoofisha hali ya usalama katika jiji.
Tukiwa tunakabiliwa na wimbo la hofu lililomo kwenye miji mikubwa,
tunaweza kufanya nini?
2. Kuishinda Hofu kwa Njia ya Imani
Ingawa Biblia si kitabu cha mwongozo wa saikolojia au andiko kuhu-
su ubongo, lakini inachunguza kwa kina suala la woga. Kwa kweli, ma-
neno “usiogope” yanaonekana takribani mara 365 katika Maandiko, na
kuyafanya kuwa ujumbe unaorudiwa mara nyingi zaidi katika Biblia.
Zaidi ya hayo, maneno “hofu” na “utisho” yametajwa zaidi ya mara mia
mbili, wakati “hofu” yenyewe katika tafsiri ya kiingereza ikionekana
zaidi ya mara mia moja. Huenda ikawa jambo la kushangaza kwamba ki-
tabu kinachosimulia matendo ya watu wa kihistoria kinazungumza sana
juu ya woga, lakini Biblia inarekodi kwamba zaidi ya watu mia mbili wa
wahusika wake walipitia uzoefu wa jambo hilo!

47
Kwa hivyo, je, kuna suluhu ya jambo lenye kulemea kama woga? Je,
tunaweza kushinda woga wetu? Je, inawezekana kuishi bila hofu? Wengi
wametafuta majibu kupitia kwa wanasaikolojia na matibabu, wakijaribu
kubadili mawazo na tabia zao kimantiki. Wengine wamegeukia dawa,
wakiitazama hofu kama aina ya ugonjwa. Hata hivyo, baada ya muda,
wanagundua kwamba, ingawa tiba hizi na dawa zinaweza kusaidia, sio
chaguo pekee.
Ikiwa hatuwezi kuondoa au kupuuza hofu zetu, je, tunaweza kuz-
idhibiti kwa njia fulani? Jibu ni “ndiyo” yenye nguvu. Kulingana na
Biblia, tunaweza kukabili na kushinda woga kwa njia ya imani. Ndiyo,
kijana mpendwa, imani ndiyo dawa ya Mungu ya kuondoa woga wetu
wote, lakini imani ni nini? Biblia inafafanua imani kwa njia hii: “Imani
ni kusadiki yale tunayotumainia na kuwa na hakika ya yale tusiyoya-
ona” (Waebrania 11:1, Tafsiri ya NIV). Kwa maneno mengine, imani
ni kumtumaini Mungu. Biblia inatuambia hivi baadaye: “Lakini pasipo
imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu
lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale
wamtafutao” (Waebrania 11:6).
Ni muhimu kutambua kwamba sio tu aina yoyote ya imani inayoshin-
da woga. Imani ambayo kweli inashinda hofu inakubali kwanza ku-
wepo kwa Mungu. Kumwamini Mungu ni hatua ya kwanza kuelekea
kuishi maisha ya ushindi. Wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu wana
dira inayowaongoza katika matatizo ya dunia. Kwa upande mwingine,
kwa wale wasiomwamini Mungu, ulimwengu huu unaweza kuonekana
kuwa wa ajabu, wenye kutatanisha, na wenye kuvunja moyo. Maisha
yanakuwa magumu na yasiyo na mwelekeo.
Pili, imani inayoshinda woga haikubali tu kuwepo kwa Mungu
bali pia inatafuta kustawisha uhusiano wa pekee Naye. Haitoshi ku-
jua kwamba Mungu yupo; ni muhimu kuchukua hatua ya kumjua Yeye.
Mungu mwenyewe anatuhimiza katika Neno lake tusijisifu kwa hekima,
nguvu, au utajiri wetu bali tujisifu kumjua na kuelewa kwamba anatenda
duniani kwa upendo, hukumu(Yeremia 9:23-24). Kabla ya kuendelea, ni
muhimu kutambua kwamba tunapozungumza kuhusu kumjua Mungu,
haimaanishi kumwelewa kikamilifu. Kama wanadamu, hatuwezi kumfa-
hamu kikamilifu Yule asiye na kikomo kutokana na mapungufu yetu ya
kiakili, matatizo ya kimaadili, na mapungufu katika ufunuo wa Mungu.
Hata hivyo, tunapozungumza juu ya kumjua Mungu, tunarejelea kuanzi-
sha uhusiano Naye kwa njia ambayo Alivyo Yeye huathiri jinsi tulivyo.

48
Tatu na mwisho, imani inayoshinda hofu ni ile inayotuongoza
kumwamini Mungu kabisa. Mtu fulani alisema kwamba imani inahu-
sisha kutumaini kwamba Mungu atatufanyia yale ambayo hatuwezi ku-
jifanyia wenyewe. Kiini cha imani ya kweli kinahusisha kuchukua Neno
la Mungu na kuamini kwamba atatimiza ahadi zake. Tunapomtumaini
Mungu, mtazamo wetu juu ya maisha hubadilika kabisa. Kumtegemea
Mungu kunabadilisha kila kitu. Inatuweka huru kutokana na athari mbaya
za zamani na kutoka kwa hisia hasi. Kwa kuamini kwamba kila kitu kiko
mikononi mwa Muumba wetu, tunaishi bila woga, tukijua kwamba haku-
na kinachotokea bila ridhaa yake.

Hitimisho
Harriet Tubman alikuwa mwanamke wa ajabu ambaye aliishi katika
wakati ambapo utumwa ulikuwa ndoto mbaya nchini Marekani. Fikiria
kuwa umenaswa, bila uhuru, unaishi katika hofu ya kudumu. Harriet ali-
pata uzoefu huo tangu akiwa mtoto, lakini hakukata tamaa.
Kuanzia umri mdogo, Harriet alipitia ukatili wa utumwa. Lakini kadi-
ri alivyoendelea kukua, ndivyo pia azimio lake la kutoroka na kuwasaid-
ia wengine kufanya vivyo hivyo lilivyoongezeka. Siri yake: Imani yenye
nguvu katika Mungu ambayo ilimpa ujasiri.
Alipokuwa na umri wa miaka 27, Harriet alifanya uamuzi wa ujasiri.
Alitoroka kutoka kwenye shamba ambalo alikuwa mtumwa na kuelekea
kaskazini, akifuata nyota na akijiamini katika uwezo wa uelewa wake.
Katika safari yake, alikabili hatari kama vile wawindaji wa watumwa
na mbwa wafuatiliaji, lakini imani yake kwa Mungu haikuyumba. Kila
hatua kuelekea uhuru ilikuwa ni tendo la imani.
Lakini Harriet hakuacha, baada ya kupata uhuru wake mwenyewe. Li-
cha ya hatari ya kudumu ya kukamatwa na kurudishwa utumwani, alirudi
Kusini mara kadhaa kusaidia watumwa wengine kutoroka kupitia Njia
ya Reli ya chini ya ardhi, mtandao wa siri wa njia salama na mahali pa
kujificha. Imani yake kwa Mungu iliongezeka hata zaidi, akiamini kabisa
kwamba Mungu alikuwa akimwongoza na kumlinda katika misheni yake
hatari.
Safari moja, alipokuwa akiongoza kikundi cha watumwa waliotoro-
ka katikati ya usiku, walikutana na bango lilitangaza kutafutwa kwake
Harriet, lililokuwa na picha ya uso wake mwenyewe. Badala ya kukata
tamaa, Harriet alimwomba Mungu na kukaza mwendo, akimfikisha kila
mtu kwenye usalama. Imani na ujasiri wake ulishinda woga.

49
Harriet Tubman, anayejulikana kama “Musa wa watu wake,” alisaidia
watumwa zaidi ya mia tatu kupata uhuru. Alikuwa shujaa wa kweli ka-
tika vita dhidi ya utumwa. Kisa chake kinaonesha kwamba imani katika
Mungu inaweza kukusaidia kushinda woga na kutimiza mambo ya ajabu.
Leo, kijana mpendwa, unaweza kujikuta ukikabiliana na hofu kati-
ka jiji lako kwa sababu ya ukosefu wa usalama, shinikizo la kijamii, na
changamoto zingine. Lakini, kama Harriet Tubman, imani na azma vi-
naweza kuwa washirika wako katika kushinda hofu hizi.

50
Ni Nani Atakayeitikia?
Na: Mwenya Mpundu

Fungu: Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa


uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. Yohana 15:13
Mnamo Septemba 11, 2001, ulimwengu ulitazama kwa mshangao
msiba uliotokea katika Jiji la New York. Ingawa nilikuwa na umri wa
miaka sita tu nikiwa nchini Kenya wakati huo, nakumbuka mayowe nili-
yosikia kutoka nyumbani wakati nikicheza nje. Picha kwenye skrini ya
runinga zilionesha ghorofa zikiporomoka, huku kundi kubwa la watu
wakikimbilia kwenye machafuko – waitikiaji wa kwanza. Watu hawa
jasiri mara nyingi hawatambuliwi na huonesha upendo wa kina ambao
unakinzana na hatari na shida.
Wakati wa hatari, ni silika ya asili kwa wengi kutafuta usalama, kuon-
doka kwenye eneo la hatari. Lakini, katikati ya janga, wapo wale ambao
huwa wanasonga mbele kwa ujasiri kuelekea kiini cha zahama, sio kwa
umaarufu au kutambuliwa lakini kwa dhamira isiyoyumba ya kuokoa
maisha. Wazima-moto, Watumishi wa Tiba ya Dharura, Maafisa wa Poli-
si, na Wanajeshi, wanaojulikana kwa pamoja kama Waitikiaji wa Kwan-
za, huwa wanajitosa mahali ambapo wengine hawathubutu kukanyaga.
Utume wao? Ili kuokoa maisha aidhuru ya mtu mmoja.

1.Msaada kwa njia ya Maombi


Katikati ya machafuko na hatari wanayokabiliana nayo, Waitikiaji wa
Kwanza wanahitaji maombi yetu. Hebu tufanye hili kuwa zoezi la kudumu,
kuwainua katika kuwaombea. Wagalatia 6:2 inatuhimiza “ Mchukuliane
mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo.” Maombi yetu yanakuwa
nguvu kwao, yakiwapa nguvu na ulinzi wanapoitikia mwito wa wajibu.

2.Tambua Kujitoa Kwao


Ni muhimu kutambua na kuheshimu dhamira ya waitikiaji wa kwan-
za. Kwa kufanya hivyo, tunaakisi upendo wa Mungu. Tukumbuke Wae-
brania 6:10, “Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo
lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakat-
ifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia.” Kutoa shukrani zetu na
kutambua kujitoa kwao ni ukumbusho unaoonekana kwamba jitihada
hazipuuzwi.
51
3.Himiza Uelewa wa Afya ya Akili
Huku mara nyingi wakichukuliwa kuwa nguzo imara za jamii,
waitikiaji wa kwanza hawaepuki kiwewe kinachotokana na matukio wa-
nayoyashuhudia. Kama vile tuwezavyo “kuwakagua marafiki zetu wenye
nguvu,” ni lazima pia tuendeleze huduma zetu kwa mashujaa hawa. Wa-
himize kupata wataalamu wa afya ya akili ambao wanaweza kuwasaidia
kushughulikia uzito wa uzoefu wao. Kukubali mahitaji yao ya kihisia
hutoa nafasi ya uponyaji na upatikanaji wa msaada.

Maswali: Unaweza kuungaje mkono kwa vitendo na kuwashukuru wale


wanaohudumia jamii yetu bila ubinafsi?

Ombi:
Mpendwa Mungu, tunakujia tukiwa na mioyo iliyojaa shukrani kutokana
na ujasiri wa waitikiaji wa kwanza. Hebu waimarishe katika kazi yao,
wape ulinzi na kuwazingira kwa amani Yako. Hebu maombi yetu na ku-
waunga kwetu mkono kuziinua nyoyo zao. Katika jina la Yesu tumeomba,
Amina.

52
Somo la 8

Kuinua Walioanguka Kwenye Jiji Lako


NA: DK. S. Yeury Ferreira
(Mathayo 11:19)

Utangulizi
Je, ulijua ya kwamba miji mikubwa imejaa mioyo iliyovunjika?
Baadhi ya watu wanaopitia nyakati ngumu huwa wanajaza maisha yao
kwa namna ya kiza. Kwenye miji mikubwa, tunakutana na vijana am-
bao wamenaswa katika ulimwengu wa madawa ya kulevya, wengine
wakiwa katika mvuto wa makundi mabaya na baadhi wanaopambana na
kunyanyaswa na hali za kuonewa. Unaweza kuona watu walio vijana
kwa wazee ambao wanaonekana kuwa wamepotea kabisa, wakiwa ha-
wana hata wazo kuwa waende katika njia gani. Wamevunjika ndani na
wanatafuta kwa shauku fursa ya kubadilika.
Hebu tumzungumzie Maria, dada mwenye umri wa miaka ishirini na
tano ambaye aliishi katikati ya jiji kubwa. Alikulia kwenye mazingira
magumu, akiwa amezingirwa na matatizo ya kifamilia na mvuto hasi wa
rafiki zake. Alianza kujaribu kutumia madawa ya kulevya katika umri
mdogo na muda mfupi tu baadaye alijikuta akiwa amenaswa katika mzu-
nguko wa kuporomoka kiafya. Aliachishwa kazi, uhusiano wake ulihari-
bika na afya yake ikaharibika pia kwa kasi sana. Maria aliharibikiwa,
kimwili na kihisia pia.
Ufafanuzi
Ningependa kuanza tafakari hii kwa aya kutoka katika Biblia ambayo
daima imenivutia:
53
“Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na
mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulika-
na kuwa ina haki kwa kazi zake’” (Mathayo 11:19).
Vijana wapendwa, mmewahi kujiuliza jinsi walivyomsema Yesu? Walim-
wita “rafiki wa wenye dhambi”! Je, unaweza kuwazia Yesu akitembea
katika jiji lako? Angezungumza na nani? Angeonesha huruma zaidi
kwa nani? Bila shaka, ninaamini angewakaribia wale kama Maria, wale
walioanguka na kuvunjika mioyo.
Sasa, ina maana gani hasa kwa Yesu kuwa rafiki ya watenda-dhambi?
Ina maana kwamba Yeye ni rafiki yetu na anatungoja tutambue kuwepo
kwake na utayari Wake. Upendo wa Mungu kwetu unapita zaidi ya vile
tunavyoweza kuwazia.
Inashangaza kwamba sifa hii, “rafiki wa wenye dhambi” ilitolewa na vi-
ongozi wa kidini kwa Yesu katika ule wakati wa huduma Yake. Walim-
kosoa kwa kutumia muda na watu waliotengwa na “wasiokubalika katika
jamii,” na ndiyo maana walimwita “rafiki wa wenye dhambi!”
Kwa mfano, safari moja, Waandishi na Mafarisayo walimnung’unikia
Yesu. Unajua kwa nini? “Basi watoza ushuru wote na wenye dhambi
walikuwa wakimkaribia wamsikilize. Mafarisayo na waandishi waka-
nung’unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena
hula nao” (Luka 15:1-2).
Akikabiliana na shutuma hizo, Yesu hakujitetea bali alitoa mfano un-
aoonesha jinsi Mungu anavyowapenda wale walioanguka.“Akawaambia
mfano huu, akisema, Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na
mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute
yule aliyepotea hata amwone? Naye akiisha kumwona, humweka mabe-
gani pake akifurahi. Na afikapo nyumbani kwake, huwaita rafiki zake na
jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimekwisha
kumpata kondoo wangu aliyepotea. Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa
na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko
kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.”
Yesu anazungumza kuhusu mchungaji aliyekuwa na kondoo mia moja,
lakini mmoja wao alitanga mbali na kupotea. Kulingana na zuolojia, kon-
doo ni wanyama wanaotanga na kupotea kwa urahisi kutokana na ukose-
fu wao wa mwelekeo. Lakini mchungaji aliwaacha wale tisini na kenda
na kufanya kila jitihada kumtafuta kondoo mmoja aliyepotea, hata ku-
fikia kiasi cha kukabiliana na hali mbaya ya hewa. Hatimaye, kwa wema
na upendo, alimpata kondoo na kumrudisha kundini. Aliporudi nyumba-
ni, alisherehekea kwa furaha kupatikana kwake.
54
Mwandishi Mkristo Ellen G. White anasema kwamba Mungu, kama
mchungaji wa kidunia, anawajua kondoo Wake, waliotawanyika ulim-
wenguni pote.
“Kama mchungaji wa kidunia ajuavyo kondoo zake, ndivyo Mchungaji
wa Kimbingu ajuavyo kundi lake lililosambaa duniani kote. “Na ninyi,
kondoo zangu, kondoo za malisho yangu, ni wanadamu, na mimi ni Mun-
gu wenu, asema Bwana MUNGU.” Yesu anasema, “Nimekuita kwa jina
lako, wewe u wangu.” “Nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu”
(Eze. 34:41; Isa. 43:1; 49:16). Yesu anatujua kila mmoja binafsi, Naye
huguswa na hisia zetu za udhaifu wetu. Yeye anatujua sisi sote kwa ma-
jina yetu. Yeye anajua nyumba mahususi tunamoishi, jina la kila mkazi.
Nyakati fulani ametoa maelekezo kwa watumishi wake kwenda kwenye
mtaa fulani kwenye mji fulani, kwenye nyumba fulani, ili kumpata mmo-
ja wa kondoo Zake.”
Yesu, mchungaji aliye Mungu, anapita kwenye miji akitafuta waliopotea,
walioumizwa, na walioanguka, walio na mioyo iliyovunjika kwa sababu
ya mapigo ya maisha haya na viwewe.
Kwa nini ninaamini kwamba Yesu huwa anawainua walioanguka?
• Alimwinua mwanamke aliyekuwa mzinzi (Yohana 8:1-11): Alim-
pata mwanamke aliyekamatwa katika uzinzi na badala ya kum-
hukumu, Alisema, “Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na
awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.” Umati ule wa watu ukasam-
baa, naye Yesu mwenyewe akamwambia yule mwanamke kwam-
ba naye hakumhukumu na kwamba hapaswi kutenda dhambi tena.
• Alimwinua MtuAliyepooza Kwenye Kisima cha Bethzatha (Yohana
5:1-15): Katika tukio lingine,Yesu alikutana na mtu aliyekuwa mgonjwa
kitandani na aliyelazwa kitandani kwa miaka 38. Yesu akamwambia,
“Simama, jitwike godoro lako, uende,” na yule mtu alipona mara ile.
• Alimwinua Zakayo, mtoza ushuru (Luka 19:1-10): Zakayo
alidharauliwa kwa sababu ya ajira yake na sifa yake kama mwenye
dhambi. Wakati Yesu alipomtembelea, Zakayo aliguswa na kuamua
kutoa nusu ya mali yake kwa maskini na kuwarejeshea mara nne
wale aliowadhulumu.
Katika kila moja ya mifano hii, Yesu anaonesha uwezo Wake wa kui-
nua walioanguka na kuwapatia matumaini, bila kujali mazingira yao au
dhambi zao za wakati uliopita. Anatufundisha ya kwamba daima kuna
fursa kwa ajili ya msamaha, uponyaji na badiliko katika kuwepo kwake.

55
Hitimisho
Siku moja, wakati akipambana na tatizo lake la uraibu, Maria alikabil-
iana na kundi la watu waliojitolea kutoka katika Kanisa la Waadventista
wa Sabato waliokuwa wakisaidia vijana waliokuwa kwenye hali ngumu.
Mmoja wao, aliyeitwa Pablo, alimjia kwa upole na kwa ajili ya kusaidia.
Walimpatia kimbilio salama na msaada katika kukabiliana na tatizo lake.
Licha ya mashaka yake ya awali, Maria aliamua kuupa nafasi mkono huu
ulioamua kumsaidia.
Miezi kadhaa iliyofuata, Maria alianza kujenga upya maisha yake.
Alipokea mafundisho ya Biblia na msaada wa kihisia, ushauri nasihi na
msaada kwa ajili ya kushinda uraibu wake. Alipopata ujasiri na ustadi
mpya katika utendaji wake, alipata pia ajira na kujenga upya uhusiano
mzuri na familia yake na marafiki. Leo, Maria ni ushuhuda hai wa jinsi
nafasi nyingine na mkono wa msaada uwezavyo kubadilisha maisha ya
mtu; ni mfano kwamba Yesu anaendelea kuinua walioanguka kwenye
miji mikubwa. Mpendwa kijana, hebu uinuke na kutafuta walioanguka
kwenye mji wako nawe uwalete kwa Yesu, ambaye ni rafiki wa wenye
dhambi.

56

You might also like