You are on page 1of 10

MPENDE JIRANI YAKO

Luka 10:25 – 37
UTANGULIZI
Katika siku za leo tunazoishi zilitabiriwa na Kristo kwamba ni siku ambazo
upendo wa wengi utapoa kwa sababu ya kuongezeka maasi kama
tunavyoweza kusoma katika Mathayo 24:12 ambapo tunasoma:
12
Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa.
13
Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho ndiyo atakayeokoka.
Hali kadhalika Mtume Paulo katika waraka wake 2 Timotheo 3: 1 – 5
inasomeka hivi:
1
Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako
nyakati za hatari. 2Maana watu watakuwa wenye kujipenda
wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi,
wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
3
wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji,
wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, 4wasaliti, wakaidi, wenye
kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; 5wenye mfano
wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
Ni kawaida kwa siku za leo kuona ndugu waliozaliwa pamoja
wamefarakana wala hawataki suluhu. Mambo haya yapo hata kanisa la
Mungu. Ndani ya kanisa la Mungu watu wamegawanyika na pia wamekuwa
ni watu wasiojali uhitaji wa wenzao. Pamoja na hali zote zilizoainishwa
hapo juu, bado neno la Mungu linatutaka kujiepusha na maovu yote.
Asubuhi ya leo imempendeza BWANA tujikumbushe kuhusu upendo,
katika ujumbe usemao MPENDE JIRANI YAKO. Na katika kufanya

1
hivyo tutakwenda kuangalia maandiko matakatifu katika Luka 10: 25 – 37
yanayohusu habari ya Msamaria Mwema.
HABARI YA MSAMARIA MWEMA
Habari hii ya msamaria tunaisoma katika Luka 10:25 – 37
25
Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema,
Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele? 26Akamwambia,
Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje? 27Akajibu akasema,
Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho
yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani
yako kama nafsi yako. 28Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi
nawe utaishi. 29Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na
jirani yangu ni nani? 30Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka
toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang'anyi;
wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha
karibu ya kufa. 31Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile;
na alipomwona alipita kando. 32Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika
pale akamwona, akapita kando. 33Lakini, Msamaria mmoja katika
kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia,
34
akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai;
akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya
wageni, akamtunza. 35Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa
mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote
utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa. 36Waonaje
wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule
aliyeangukia kati ya wanyang'anyi? 37
Akasema, Ni huyo
aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe
ukafanye vivyo hivyo.

2
Ukisoma maandiko kwa makini utabaini kwamba mtu mmoja mwanasheria
(mtaalamu yaani mtu aliyebobea katika sheria za Musa, torati) alimkabili
Yesu ili amjaribu. Mtu huyu hakwenda kumuuliza Yesu ili kujifunza bali
alikwenda kumuuliza kwa nia mbili:
a. Kwanza, ili kupima uelewa wa Yesu kuhusiana na sheria za
Mungu, kama Yesu angeweza kubabaika basi angekuwa amepata
ushindi kwa kuudhibitishia umma kwamba Yesu ni mpotoshaji
wala hapaswi kufuatwa.
b. Pili, alimuulizaYesu ili kumtega, iwapo Yesu angetoa maelezo
yanayopingana na sheria za Musa basi angekuwa amefanikiwa
kumuingiza Yesu kwenye mtego na hivyo viongozi wa kiyahudi
waliokuwa wakimpinga Yesu wangekuwa na sababu ya
kumshtaki Yesu kwenye Baraza la wayahudi kwa kupotosha
neno la Mungu.
Mwanasheria huyu aliuliza swali zuri; ila kwa mtazamo mbaya, lakini si
kwamba alikuwa na mtazamo mbaya tu; bali hakuwa akihitaji majibu ya
swali lake.
Mtu huyu alimuuliza Yesu, “Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa
milele?” Ukiliangalia swali hili ni la msingi kabisa kwa sababu linagusa
tumaini tuliloitiwa. Bila shaka kila mmoja wetu angependa kusikia majibu
ya swali hili. Lakini Bwana Yesu anatuonyesha kwamba mtu huyu alikosea
kuuliza swali hili.
Katika kulikabili swali Yesu hakumjibu moja kwa moja badala akamuuliza
swali Yule mwanasheria, akamwambia, Imeandikwa nini katika torati?
Wasomaje? Yesu hakutaka mabishano na mtu yule, na kama siku za leo ni
sawa na kuuliza je neno la Mungu linasemaje?

3
Hapa tunajifunza hekima ya ajabu, kwamba kitu cha kwanza unapokumbana
na swali ni kujiuliza, je neno la Mungu linasemaje? Ukiwa na utaratibu wa
kukabili maswali kwa mtazamo huu hutopata shida wala ugumu wowote.
Mtu huyu alikuwa akijaribu kumtega Yesu na si kwamba alikuwa hajui
maandiko. Aliyajua maandiko vizuri na alipoulizwa imeandikwa nini katika
torati aliweza kutoa jibu mujarabu.
Mtu huyu alijibu hivi
Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako
27

wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili
zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.

Katika kujibu mtu yule alinukuu vifungu vya torati kama ambavyo unaweza
kusoma katika Kumbu 6:5 na Walawi 19:18.
Baada ya mtu kumjibu Yesu, Yesu akamwambia Umejibu vema; fanya hivi
nawe utaishi. Jinsi alivyomalizana na swali hili hakuna aliyetarajia. Mtego
wa jamaa ukawa haufai tena.
Kwanza kwa mwanasheria yule; alitarajia Yesu angeeleza kwa namna
ambavyo amekuwa akifundisha kwa mamlaka. Watu hawa walikuwa na
uzoefu na jinsi Yesu alivyokuwa akifundisha. Mara nyingi Yesu alifundisha
kwa mamlaka. Katika kufundisha kwake Yesu hakuwa anasema
imeandikwa au neno la Bwana linasema bali alikuwa anawaambia amini
amini nawaambia. Kuna mahali alikuwa anawaambia imeandikwa hivi.....
lakini mimi nawaambia.
Kuna wakati wakuu wa makuhani, waandishi pamoja na wazee wa
kiyahudi waliwahi kumuuliza Yesu kwamba anafundisha kwa mamlaka
gani? Soma katika Luka 20:1 – 8

4
Kwa hiyo watu hawa kwa kuwa walikuwa na uzoefu wa mafundisho ya
Yesu walikuwa na uhakika Yesu katika kujibu swali hilo lazima angetoa
maelezo tofauti na waliyokuwa wanayajua wao katika torati ya Musa. Na
hapo ndipo wangeweza kuwa na uhalali wa kumshitaki. Kinyume na
matarajio yao Yesu akamrudishia swali yule mtu akawa amemaliza kazi.
Pili kwa upande sisi, ni hakika tusingelikabili swali kama Yesu alivyofanya,
bila shaka tungesema ili mtu aweze kuurithi uzima wa milele sharti
unapaswa uokoke ili usamehe dhambi zako kisha uendelee kuishi katika
neema ya Mungu.
Lakini ili tuurithi uzima wa milele Yesu anasema tufanye hivi Mpende
Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na
kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi
yako.
Yule mwanasheria baada kuwaambiwa vile hakutaka kuona jambo lake
limemalizwa kirahisi vile. Maandiko yanasema hivi Naye akitaka kujidai
haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani? Hapo ndipo Yesu
anaeleza habari ya msamaria mwema. Na kwa kupitia habari ya Msamaria
tunajifunza kweli kuu nne zinazohusu upendo.
I. UPENDO WETU UWE KWA KILA MHITAJI PASIPO KUJALI
KUWA NI NDUGU, RAFIKI AU ADUI
Katika kumjibu mwanasheria kuwa jirani yake ni nani? Yesu alimwambia
habari ya msamaria. Unaweza kujiuliza kwa nini Yesu anatumia mfano
huu?
Wayahudi na Wasamaria walikuwa ni watu wasiopatana ijapokuwa wote ni
uzao wa Yakobo. Wayahudi walikuwa ni watu wa makabila mawili ya Yuda
na Benyamini waliounda ufalme wa Yuda na Wasamaria walikuwa ni watu

5
kabila za kumi za Yakobo zilizounda ufalme wa Kaskazini uliojulikana kwa
jina la Israeli.
Wasamaria waliacha kufuata maagizo ya Musa (torati) watu hawa walioana
na watu wa mataifa waliyokuwa wamekatazwa lakini pia waliamua kuwa
watu wa kuabudu miungu ya sanamu. Kwa hiyo Wayahudi waliwaona
Wasamaria kuwa ni wapagani na watu waliopotoka wasiofaa hata
kuchangamana nao. Kibaya zaidi Wasamaria walikuwa wanajua jinsi
ambavyo wayahudi walivyokuwa wanawachukulia. Hii inadhihirika katika
Yohana 4: 9
9
Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe
Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria?
(Maana Wayahudi hawachangamani na wasamaria)
Kwa maelezo haya nahisi kwamba yule Myahudi iwapo angekuwa katika
hali ya kujitambua angelikataa asisaidiwe na Msamaria.
Lakini yule Msamaria hakujali mahusiano mabaya yaliyopo baina ya
Wayahudi na Wasamaria, alichofanya ni kumpatia huduma ya kwanza yule
majeruhi, akampandisha katika punda wake, akampeleka katika nyumba ya
wageni, akamtunza pia akaahidi kubeba gharama zote za matunzo ya
Myahudi yule.
Hapa Yesu anatufundisha kwamba upendo wetu uwe juu ya kila mhitaji
pasipo kujali kuwa ni rafiki, ndugu au ni adui. Tunapaswa kuwaonyesha
upendo watu wote pasipo kujali mahusiano yaliyopo baina yetu. Upendo
wetu unapaswa kudhihirika hata kwa adui zetu.
II. KATIKA KUONYESHA HAUHITAJI UWE NA VITU VYA
ZIADA ONYESHA UPENDO KWA VICHACHE ULIVYONAVYO
Yule Msamaria alikuwa na punda mmoja lakini alimpakia yule majeruhi na
bila shaka yeye akatembea. Ukisoma kwa makini utaona yule Msamaria

6
akatumia pesa zake na bila shaka alipungukiwa kiasi kwamba aliacha
huduma zingine atakazopewa yule Myahudi ziwe deni lake na atalipa
atakaporudi.
Katika hili tunajifunza kwamba ili kuonyesha upendo kwa wengine haihitaji
kuwa na vitu vya ziada, unapaswa kutumia vile vichache ulivyonavyo.
Na hapo ndipo maandiko yanatuelekeza kwamba mpende jirani yako kama
nafsi yako yaani maana yake ni kwamba uhitaji wa jirani yako unapaswa
kuupa kipaumbele kama vile ambavyo ungeupa kipaumbele uhitaji wako
binafsi.
Mfano
Jirani yako mtoto wake ni mgonjwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji
naye amepungukiwa fedha ili kuwezesha matibabu ya mtoto wake na
amekukabili na wewe unayo fedha uliyoiandaa kwa ajili ya ada ya
mwanao ambapo usipolipa mwanao atasimamishwa na masomo. Je
utafanya lipi? Upendo unataka ule uhitaji wa mtoto wa jirani yako
uchukulie kama uhitaji wa mwanao. Je unaweza kuacha kulipia
matibabu ya mwanao ukalipia ada ya shule?
Kumbuka yule Msamaria alikuwa na punda mmoja, hakuona shida ya yeye
kutembea kwa miguu ili majeruhi abebwe juu ya punda wake.
III. KATIKA KUONYESHA UPENDO USIANGALIE GHARAMA
AU HASARA UNAYOWEZA KUIPATA
Maandiko yanatuambia kwamba mahali pale alipita Kuhani na Mlawi katika
eneo lile lakini hawakutoa msaada wowote. Binafsi nashindwa kuelewa
kuwa kwa nini watu hawa hawakutoa msaada?
Pamoja na lawama tunazoweza kuwatupia watu hawa bila shaka walikuwa
na sababu za msingi za kupita bila kutoa msaada kwa majeruhi:

7
 Pengine walikuwa wanawahi kwenye jukumu au huduma
maalumu kama vile ibada.
 Pengine walikuwa wanahofia usalama wao katika eneo hilo.
Eneo hilo huwa ni eneo la wanyang’anyi kwa hiyo kusimama
kwao kutoa msaada kwa eneo hilo bila shaka kungepelekea na
wao kushambuliwa.
Ushuhuda:
Mwaka 2016 tukiwa Dodoma siku moja usiku tulikuwa
tunatoka mahali fulani na ilikuwa usiku umeendelea sana,
tukiwa mimi na mke wangu tunaelekea nyumbani mimi nikiwa
naendesha gari tukapita sehemu tulikuta mwendesha pikipiki
amepata ajali na hana msaada nilimkwepa nikaendelea na
safari. Mke wangu akaniambia mbona hutaki kutoa msaada
kwa huyo mtu, mimi nikamwambia ogopa sana kusimama
maeneo haya usiku unaweza kuta ni vibaka au la unaweza
simama wakati unamsaidia wanaibuka waendesha pikipiki
wanaweza kuzusha vurugu bila kujua hauhusiku kwenye ajali
hiyo bali unatoa msaada tu. Maelezo haya yalimridhisha mke
wangu lakini si Mungu maana siku zote ninapokumbuka tukio
hilo ninakosa amani. Nina sikia hukumu ndani yangu.
Hata hivyo kulingana na jinsi Yesu alivyohitimisha katika habari hii ya
Msamaria hakuna sababu inayowahalalisha yule kuhani na mlawi kutokutoa
msaada kwa majeruhi yule.
Kumbuka yule Msamaria hakujali iwapo anahatarisha maisha yake, wala
hakujali hata kama atachelewa kwenye shughuli zake.
Katika kuonyesha upendo hatupaswi kuhesabu gharama au hasara
tunayoweza kuipata.

8
Mfano wa Yonathani na Daudi 1 Samweli sura ya 19 na 20
IV KATIKA KUONYESHA UPENDO USITARAJIE KUPOKEA
CHOCHOTE TOKA KWA MTU BALI TARAJIA KUPOKEA TOKA
KWA BWANA
Yule Msamaria hakuwa anatarajia chochote toka kwa Myahudi. Kuna
wakati tunashindwa kuwasaidia watu kisa hawana shukrani.
Usisaidie mtu ili akusifu, wala msisaidie mtu kwa sababu kuna jambo
utapata toka kwake. Mtendee mema kila mtu kwa sababu ni wajibu wa
kikristo. Warumi 12:14 – 21.
Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani. 15Furahini
14

pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao. 16Mpatane nia


zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali
kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia
akili. 17Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni
pa watu wote. 18Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika
amani na watu wote. 19Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni
ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu
mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. 20Lakini, Adui yako akiwa na
njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo,
utampalia makaa ya moto kichwani pake. 21Usishindwe na ubaya,
bali uushinde ubaya kwa wema.
Upendo wa kikristo haupaswi kuwa wa nipe nikupe bali ni upendo unaotoa
tu.
HITIMISHO
Wapendwa bila shaka kila mmoja wetu hapa ameshaelewa jinsi ya
kumpenda jirani yako. Jirani yako ni mtu yoyote anaguswa na mwenendo
wa maisha yako. Jirani yako anaweza kuwa ni ndugu. Rafiki au adui.

9
Vyovyote atakavyokuwa unapaswa kumpenda kama ambavyo unajipenda
mwenyewe. Kwa maana nyingine uhitaji wa rafiki yako uchukulie kuwa
kama uhitaji wako.
Katika habari ya Msamaria Mwema tulijifunza leo kuna kweli kuu nne
ambazo tunapaswa kuzitendea kazi ili kudhihirisha upendo wetu kwa
wengine:
a. Upendo wetu uwe kwa kila mhitaji pasipo kujali kuwa ni ndugu,
rafiki au adui.
b. Katika kuonyesha hauhitaji uwe na vitu vya ziada onyesha
upendo kwa vichache ulivyonavyo.
c. Katika kuonyesha upendo usiangalia gharama au hasara
unayoweza kuipata.
d. katika kuonyesha upendo usitarajie kupokea chochote toka kwa
mtu bali tarajia kupokea toka kwa Bwana.

Mungu awabariki sana


Mpelenja Bernard Mongella
Mtumwa asiye na faida

10

You might also like