You are on page 1of 5

Upendo miongoni mwa Wakristo

1 Mar

Neno la Mungu katika Yohana 13:34-35 linasema hivi: Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. Je! Hali ya upendo/kupendana miongoni mwa wakristo ikoje? Share this:

Facebook Twitter Email Print

Like this:
Like Be the first to like this post.

Comments 9 Comments Categories MIJADALA

Ukweli kuhusu Watumishi Militants kill Christian minister in Pakistan

9 Responses to Upendo miongoni mwa Wakristo

1. Samuel Tuesday, March 1, 2011 at 7:36 pm #

Biblia inasema Mbingu na Nchi zitapita, lakini Neno halitapita lazima yote, sasa Biblia inasema nini kuhusu upendo? Math 24;12 Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. Ndugu yangu huu ni wakati mbaya kabisa, maasi yameongezeka, upendo wa wengi( Kwa Mungu umepoa, kwa wanadamu umepoa) Suala la kufanya kama wakristo wenye akili ni kuangalia maandiko yasitutimilie, unajua hata Yesu aliposema kuwa mmoja wenu atanisaliti, hakusema YUDA alisema mmoja wenu, sasa ikuwa ni juu ya kila mmoja kukaa chonjo, unaona Petro kwa kuwa hakuwa karibu na Bwana Yesu, alimuuliza yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda(Yohana) Alimuuliza kuwa amesema kuna mtu anamsaliti, ebu muulize ni nani? Yohana akamuuliza Bwana unasema kuna mtu anakusaliti ni nani? Bwana akamwambia yule nitakayemtoelea tonge, unaona, mara moja Yohana akambonyeza Petro kuwa ndugu yangu kwepa tonge! Na mwanafunzi mwingine yeyote aliyesikia tahadhari hiyo alikwepa tonge. Lakini Yuda mawazo yake yote yalikuwa ni kwenye pesa, hata hakusikia, alichoona ni tonge linakaribia mdomoni mwake akalibugia kumbe lilikuwa chambo, alipokwisha kulibugia unajua kilichotokea kuwa shetani akamwingia. Kwa huu ni wakati maandiko yanatimia kasi, lakini mwenye busara hayatamtimilia. Asante na Ubarikiwe.

2. kamala Lutatinisibwa Wednesday, March 2, 2011 at 2:54 pm # labda kwanza define upendo. elezea maana ya upendo, twapaswa kupenda nini na kumpenda nani. wengi twajichukia ni vigumu kuwapenda wengine. twataka kupendwa badala ya kupenda twapaswa kuipenda hata hali ya hewa maana ni Mungu katupatia! lakini upendo ni kitu gani tofauti na nukuu fulani fulani? upendo au kumpenda mtu/kitu ni kumchukulia/kukichukulia kama kilivyo bila kulazimisha kuki/kumbadilisha!

3. Mubelwa T Bandio Wednesday, March 2, 2011 at 8:42 pm # AMANI HESHIMA NA UPENDO. Naamini nyote mu-wema. Kwanza nishukuru kwa swali. Kisha niulize swali kabla sijajibu nifahamuvyo.

Naamini NUKUU hiyo ya AMRI MPYA ni kutoka kwa YESU. Kama nipo sahihi, naamini pia kuwa YESU ALIKUJA KUOKOA WENYE DHAMBI. Na kama hapoo pia nipo sahihi, nawaza KWANINI TUZUNGUMZIE UPENDO MIONGONI MWA WAKRISTO WAKATI TUNAJADILI UPENDO ULIOLETWA KWETU NA MTU MWANA WA MUNGU KWETU WATENDA DHAMBI? Nadhani ni vema kujadili zaidi upendo kwa wahitaji wa upendo huo ambao ni wale waaminio visivyo ama kutoiamini. Kupendana sisi kwa sisi na kuwapuuza wengine kutatufanya tujitenge nao na HATUTAKUWA MSAADA KWAO Baraka kwenu

4. muzaffar Durrani Thursday, March 3, 2011 at 7:29 am # Jamani! sioni popote.

5. Christopher Makunzo Thursday, March 3, 2011 at 8:00 pm # Swali linasema Je! Hali ya upendo/kupendana miongoni mwa wakristo ikoje? Jibu ni hili kwa mawazo yangu, Upendo upo lakini sio mia kwa mia. Upendo wa watu wa Mungu leo umegawanyika katika makundi makundi yafuatayo: Kwanza, Upendo wa kawaida: Upendo huu ni wa kumuona mwenzie kama mtu wa kawaida. Ameokoka sawa, amejazwa roho mtakatifu sawa, lakini kwa kuwa hasali ibada za kanisani kwenu kuwa ni mtu wa kawaida, sana sana ataambulia salamu yetu ya Bwana asifiwe Amen Basi. Pili, Upendo wa udini (Dhehebu): Upendo huu hufanya watu wa kanisa moja au dhehebu moja kupendana zaidi kuliko wa kanisa (dhahebu) jingine, unadharau wengine hata kama wameokoka. Upendo huu una tabia ya kusema sisi kwetu Bwana.. tuna wengine hawako kama sisi. Tatu, Upendo wa kiuwezo au kielimu: Upendo huu unawaweka watu wenye uwezo fulani fulani katika Kanisa kuwa pamoja kutokana na uwezo wao kifedha au kiuchumi na hata kielimu, wakiacha wengine wasio na uwezo kiuchumi, kifedha na kielimu kuwa na kundi lao la ufukara, umaskini na ujinga kuwa kundi lao.

Nne, Upendo wa unafiki: Upendo huu una tabia ya kuficha kilichomo moyoni. Yaani kwa sura ya nje unaonyesha unampenda mtu, lakini moyoni upo mbali nae kabisa. Upendo huu ni hatari sana katika Kanisa la Kristo kwa kuwa unaficha uhalisia wa mtu moyoni wake yaani kwa hali ya nje lakini ndani tofauti kabisa. Tano, Upendo wa Kikabila: Upendo huu ni ule wa watu wa kabila moja kupendana zaidi kuliko watu wa kabila au makabila mengine makanisani. Upendo huu unatabia ya kuchagua wakwetu na wakule wa hapa na wale. Upendo huu huwafanya watu wakuulize wewe umeoa/ kuolewa na mtu wa kabila letu au? Mchungaji au Askofu huyu ni kabila letu au? Mtu huyu anajua mila zetu? au lazima tuchague wa kwetu awe nk. Sita, Upendo Halisi wa Kristo: Upendo huu ni ule unaompenda Mungu, na Watoto wote wa Mungu popote walipo, bila kujali hali waliyonayo, Upendo wa mtu kukubali, kujitoa kwa ajili ya kazi ya Mungu. Makanisani kwetu wapo watu wa aina hii lakini sio wengi sana. Watu hawa ndiyo wenye jibu zuri kumwambia Bwana Yesu Neno la Amri mpya uliyotupa, twapendana. Kama vile ulivyotupenda sisi, nasi twapendana vivyo hivyo. Na watu wote wanatutambua ya kuwa sisi tumekuwa wanafunzi wako kweli tukiwa na upendo sisi kwa sisi. Amen

6. willy mshila Thursday, March 3, 2011 at 8:46 pm # upendo umepungua sana. sababu mojawapo ya kupungua ni kutokupambanua mwili wa Kristo, 1 wakorintho 11:29. Mstari huu unaongea kushiriki meza ya Bwana huku tukipambanua mwili. Mara nyingi huwa tunawaza tu mwili wa Yesu pale msalabani. ni vyema tukajua kuna upande mkubwa wa kupambanua Mwili, Kanisa la Kristo. ni vyema tukawa na ufunuo kuwa walio Kanisa ni nani. kila aliyetakaswa na damu ya Yesu ni sehemu ya mwili. kama inavyosema kwa wana ndoa kuwa amchukiae mke au mume wake ajichukia mwenyewe, achukuie mwenzake katika mwili ajichukia mwenye. tukishajua hilo mtu ataomba apate roho ya ufahamu ili ajue ndugu zake ni nani na kuwapa upendo wa upendeleo kabisa. watumishi na wapendwa wote tufanye bidii kuondoa udhehebu na kutafutana ili kujengana zaidi. kwamba maandiko yanasema upendo wa wengi utapoa, isiwe hivyo na kupokea kirahisi eti tukubali tu kutimiza maandiko kwa kinyume. kama mtume(wa upendo) Yohana alivyosisitiza, tupendane. kumbuka amchukiae ndugu yake ni kama muuaji kwa mujibu wa Maandiko. Mchungaji Willy Mshila.

7. JOSHUA PHILEMON Thursday, March 3, 2011 at 9:38 pm #

UPENDO UNAKUJA KWA KUKUBALI KAZI YA MSALABA KAMA YESU BILA KUJALI MWILI UNASEMAJE.

8. dada anayempenda yesu Friday, July 8, 2011 at 4:54 pm # Mimi naona upendo upo ila sio mwingi sana,naamini neno linaanza kutimia taratibu kwamba siku za mwisho upendo mmiongoni mwa watu utapoa,baadhi ya wakisto kwa kweli tunapendana,na pia kuwapenda hata wale walio wakristo,sema siku hizi wanadamu tumegeuka,unawezakujitoa kumsaidia mtu baadaye huruma yako ,inakujakuwa jeraha kwako. upendo upo ndio maana siku hizi watu wengi hukimbilia sehemu yeyote yenye kanisa anapokuwa na shida nasema haya wapo wengi ,wakristo na ambao sio wakristo wamefika kanisani kwetu wakiamini watasaidiwa ,kihali,chochote kile ,wakisema sehemu nyingine ili usaidiwe ni lazima utii masharti na sehemu zingine kama huitwi asha au omary hauruhusiwi kupita mlangoni ,Kwa kweli hakuna kitu bora kama upendo ,maana ukimpenda mwenzio kama unavyojipenda hautamfanyia kitu kibaya,wakristo tupendane ,na pia tuwapende hata wale wanaotuita makafri .sisi tuwapende maana mungu wetu,ndio anavyosema

9. Daniel magendo Wednesday, September 21, 2011 at 12:49 am # Jamani wapendwa ktk kristo mimi sijambo. Yesu aliposema upendo wa wengi utapoa alimaanisha kwamba siku za mwisho watu watakumbwa na changamoto mbalimbali za maisha (k.v watu kupenda pesa,majanga i.e ukimwi njaa e.t.c) hivyo kusababisha watu kumpenda kristo kupungue. Ndo maana sasa mtu anaenda kanisani kwa sababu tu ya janga alilonalo kama ni mgonjwa akishakupona analiacha tena kanisa na hii inadhihirisha kwamba huyu mtu kumpenda Yesu hakukuwemo ndani ya moyo wake. Ahsanteni.

You might also like