You are on page 1of 15

NAMNA YA KUOMBA INAFAA SANA KATIKA SALA BINAFSI

(PRIVATE PRAYER) INAFAA PIA KATIKA SALA ZA KIKUNDI

AINA TATU ZA SALA ZA MAOMBI

Aina hizi tatu zinatokana na aina kuu tatu za mahitaji yetu katika maombi. 1) Maombi ya
kawaida ya kila siku ya kuwasiliana na Mungu. 2) Tafakari ya kina ili kuisikia sauti ya
Mungu 3) kupambana na shetani ama shida iliyoletwa na shetani.

Aina zote tatu hufuata hatua zinazofanana. Si lazima mtu akafuata moja kwa moja kila
hatua lakini walau katika maombi yako ya kila siku mambo hayo ni muhimu ukiweza
kuyatumia karibu yote.

1. Maombi ya kawaida ya kila siku


i) Kutubu dhambi
ii) Kumwita Roho Mtakatifu
iii) Kumsifu, na kumwabudu Mungu
iv) Kutoa Ombi la Siku
v) Kumshukuru Mungu na kumalizia maombi

2. Tafakari ya kina
i) Kutubu dhambi
ii) Kumwita Roho Mtakatifu
iii) Kumsifu na kumwabudu Mungu
iv) Tafakari ya kina
v) Kumshukuru Mungu na kumalizia maombi

3. Kupambana na shetani
i) Kutubu dhambi
ii) Kumwita Roho Mtakatifu
iii) Kumsifu na kumwabudu Mungu
iv) Kufukuza nguvu za giza/mashetani
v) Kumshukuru Mungu na kumalizia maombi

1
Kabla ya kuanza sala yoyote, anza kwa kumshukuru Mungu kwa kukujalia nafasi hiyo
adimu, mshukuru kwa uhai na Neema zingine anazotujalia. Kisha waweza kuendelea na
mtiririko unaofuata.

i) Kutubu Dhambi (walao dakika 3)


Nguvu ya Mungu hufanya kazi vyema ndani ya mtu msafi ndani ya roho yake. Dhambi ni
kikwazo dhidi ya mawasiliano yetu na Mungu. “Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi,
na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwa faa sana, akiomba
kwa bidii” (Yakobo 5:16). Kipengele hiki kina beba ujumbe mahsusi hapa; hasa
anaposema mwenye haki akiomba kwa bidii kwa faa sana. “mwenye haki” katika kifungu
hiki Yakobo anasema ni mtu mwenye moyo wa toba, mtu mwenye moyo msafi. Kila
unapoanza maombi yako fanya toba kwa dhambi zako zote za siku na unazozikumbuka
walau kwa dakika hivi 3. Rejea matendo yako ya siku nzima utubu;
mfano hivi; sikuwahudumia watu kwa upendo ofisini leo, nisamehe maana
nilimkasirikia mwenzangu, leo niliwaza machafu, sikutimiza wajibu wangu wa kazi
ipasavyo, nioshe ee Yesu kwa Damu yako takatifu, nioshe ee Yesu nitakase kabisa,
nitakase kwa damu yako Takatifu, kwa neema zako ninanuia kuacha dhambi zanu, kwa
msaada wako sitarudia tena, ee Yesu mwenye huruma nihurumie nk. Nawasamehe wote
walionikosea siku ya leo (wataje kwa majina na makosa waliokufanyia, mwambie Mungu
kuwa umewasamehe) (hapa ni ukiwa peke yako kwenye sala zako binfsi).

ii) Kumwita Roho Mtakatifu (walau kwa dakika 3 hivi)


Yesu alituachia Roho Mtakatifu awe msaidizi wetu katika maombi na pia atuunganishe
na Mungu. (Waroma 8:26 – 27) “Hali kadhalika naye, Roho anatusaidia katika udhaifu
wetu. Maana hatujui inavyotupasa kuomba; lakini Roho mwenyewe anatuombea kwa
Mungu kwa mlio wa huzuni usioelezeka. Naye Mungu aonaye mpaka ndani ya mioyo ya
watu, anajua fikira ya huyo Roho; kwani huyu Roho huwaombea watu wa Mungu
kufuatanana na mapenzi ya Mungu.” Kuomba si lelemama kama wengi tunavyochukulia
kuwa ni jambo la kawaida tu. Kuna namna ya kuomba kulingana na hitaji na namna ya
kumwendea Mungu kwa jinsi alivyo Mungu ili hali sisi ni binadam. Tumtumie Roho
Mtakatifu atusaidie kuomba na aombe na sisi.
Mfano: Karibu Roho Mtakatifu, karibu Baba unifundishe kuomba, nisaidie kuomba ee
Roho Mtakatifu, naomba uombe na mimi ee Mungu wangu, bila wewe siwezi lolote,
wewe ndio msaada wangu na kila kitu katika sala zangu, karibu Baba ukae moyoni
mwangu uombe pamoja nami, niangazie mwanga wako ee Roho Mtakatifu ili niombe
vyema inavyotakiwa, nitie nguvu nisichoke ninapoomba, bila wewe mimi siwezi
chochote nk.

iii) Kumsifu na kumwabudu Mungu, kwa muda wa kutosha kwa dakika kadhaa
Kumsifu Mungu ni kukiri ukuu wake na uzuri wake na kumweleza hivyo. Mtu
anapotambua ufanisi wako na kukueleza unafurahi hata Mungu pia. Hata kama akili yako
haioni sawasawa hayo makuu ya Mungu, hata kama unapitia matatizo mengi katika
maisha yako wewe msifu tu, kwa sababu akili zetu za kibinadamu haziwezi kuelewa vya
kutosha makusudi ya Mungu katika tunayopitia. Mara zote Mungu huwa na nia njema juu
ya maisha yetu hata kama ni ndani ya mafumbo ya taabu na adha. Kumwabudu Mungu ni
2
kuumimina moyo wako kwa Mungu na kwa kutambua na kutamka ukuu wake kwa nia.
“Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana; na wakuhofiwa kuliko miungu
yote” (1Mambo ya nyakati 16:25). Maandiko matakatifu yanatufundisha kumsifu Mungu.
“Na tena enyi mataifa yote, msifuni Bwana; enyi watu wote mhimidini Bwana” (Warumi
15:11). Lazima tukumbuke kuwa sisi ni binadamu hata tukiwa wakuu kiasi gani, tujue pia
Mungu ndiye Mungu. Kumsifu na kumwabudu Mungu kunaambatana na heshima ya
dhati toka moyoni, kumkubali Mungu kuwa Mungu nawewe kushika nafasi yako ya
ubinadamu. Lusifer aliipoteza nafasi yake mbinguni kwa kutaka kufanana na Mungu.
Mungu ametuumba wenye hadhi kubwa, kiasi kwamba wakati mwingine sisi binadamu
tunajisahau na kupandisha kiburi na kudhani hatustahili kujishusha sana mbele za Mungu
na kumwabudu. Badala ya kumsifu na kumshukuru Mungu kutupatia hadhi kubwa kiasi
hicho, tunapandisha majivuno! Kumsifu Mungu kwa dhati kunaambatana na hali ya
kujishusha kwa ndani na kuruhusu neema nyingi za Mungu kutenda kazi ndani mwetu.
Jishushe kabisa mbele ya Mungu mithili ya mtoto mdogo, kama vile mtoto anavyodeka
mbele za wazazi wake, sisi kwa Mungu ni wadogo tu hata kama umekuwa mtu mzima
sana huwezi kujilinganisha na Mungu. Yesu mwenyewe alipenda kuwaita binadamu
watoto wadogo na ndivyo tulivyo kwake hata kama tunaitwa babu ama bibi. . “Enyi
watoto wadogo, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi,….” (Yohana 13:33),
Waweza kusema hivi; Mungu wangu nakusifu, nakupenda, nakuheshimu, wewe ni
mwema, hakuna mwingine kama wewe, ni wewe peke yako, nakusifu kwa moyo wangu
wote, nayatolea maisha yangu yote kwako maana ni wewe uliye Mungu wangu,
nakwabudu, nakuhimidi Bwana, nakutukuza Mungu wangu, bila wewe ee Mungu siwezi
chochote, nk. Waweza pia kusoma zaburi inayomsifu Mungu kwa heshima ukijiweka
katika hali ya sala maana ziko zaburi za kumsifu Mungu.

iv) Kutoa ombi la siku/tafakari ya kina/kufukuza nguzu za giza

Siku hiyo inategemea unataka kusali namna gani ama unataka kufanya vyote kwa wakati
mmoja pia yawezekana. Ni muhimu kuangalia uzito wa hitaji lako kwa wakati huo, kama
kuna jambo unamwomba sana Mungu kwa wakati huo kazana kuomba zaidi, tafakari
utafanya muda mwingine. Kama unasumbuliwa na roho za giza kemea tu zaidi siku hiyo
nk.

KUTOA OMBI LA SIKU

Kama siku hiyo unataka kutoa ombi lako kwa Mungu basi mweleze shida yako kwa kina.
Sio kwamba hajui shida yako, bali anataka aone ukikiri kwa kinywa chako mwenyewe
juu ya hitaji lako, hiyo ndiyo heshima ya kweli na unyenyekevu kwa Mungu.
(Wafilipi 4:6) “Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na
kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Kadiri utakavyoeleza
shida yako waziwazi kwa Mungu, ndio nguvu ya Mungu itakapofanya kazi vyema ndani
yako. Wengine husikia uzito hata kumweleza Mungu mambo yao, wanaona ugumu wa
kujifunua kwake wakati hujafichika chochote, hapo ndio unyenyekevu wako anataka.
Mweleze Mungu hisia zako yaani unavyojisikia ndani mwako, machungu yako, huzuni
zako, hofu zako, furaha yako, unayotamani akutendee nk. bila kuogopa wala kumficha
3
maana anakujua vyema sana kuliko hata unavyojitambua wewe mwenyewe, ila tu
anapenda ukiri kwa moyo wako unavyomhitaji na unayohitaji. Shusha picha ya Mungu
mbele yako jitahidi kufukuza mawazo mengine yote kadiri uwezavyo, usitawanye
mawazo, jikusanye kila unapoelekea kutoka kwenye maombi.
Kwa mfano; Kama wewe ni mtu mwenye hasira na unataka ziishe mweleze Mungu
kuwa, “mimi ni mtu mwenye hasira naomba unisaidie kuzimaliza, mweleze kuwa huwa
unakasirika hasa wakati gani” jieleze kwa kina kama vile unavyomweleza daktari ama
rafiki yako shida yako. Kama kuna mtu unamchukia kwa mfano, na unataka msaada wa
Mungu akusaidie umsamehe mweleze kuwa una uchungu na mtu fulani na mtajie kwa
jina, mweleze jinsi unavyojisikia juu ya mtu huyo na sababu ya tofauti zenu, mweleze
kuwa unataka kumsamehe na hivyo unaomba msaada wake aili akusaidie kusamehe,
mwambie akusaidie uweze kumsamehe kabisa mtu huyo. Mwombee mtu huyo mema
mara nyingi iwezekanavyo, hiyo ndiyo namna ya kujiponya mwenyewe. Mweleze
Mungu kwa maneno mengi na kwa namna tofauti tofauti shida yako. Kama unataka kazi
yako ama mpango wako ufanikiwe mweleze huo mpango kwa jina, na unapanga nini, na
unatamani akusaidie nini. Mweleze kama unavyomweleza mtu umpendaye na aliye na
msaada kwako. Wengi huwa tunadhani kuwa pengine Mungu huwa hatusikilizi ama
anajua shida yetu kwa hiyo hamna haja ya kueleza sana; hiyo sio sawa, Mungu anataka
uzungumze naye kwa kina. Yeye ni baba yetu halisi anayetupenda nasi ni watoto wake
halisi aliyetuumba na kutupulizia pumzi yake ya uhai. Yeye ni zaidi ya baba wa kimwili
maana yeye Mungu ametupa mwili na roho, anatujalia kuishi kwa pumzi yake na kwa
mvua, jua, vyakula nk.
Ukimaliza Sali sala zingine. Kanisa lina utajiri wa sala nyingi sana, laiti tungekuwa
tumetambua zilivyo na nguvu! Zina nguvu sana zikisaliwa kwa wingi na mara nyingi.
Tuna vitabu vya kila aina vya sala katika maduka ya vitabu vya kanisa. Tunazo novena
nyingi, rozari nyingi na sala zingine ndani ya vitabu hivyo. Sali sala za kutosha walau
nusu saa kwa kuanzia. Kwa wazoefu Sali zaidi ya lisaa. Wengine husali hata masaa
mawili mpaka matatu mtu huchoki bali unasikia amani ya pekee kusali hivyo.

TAFAKARI YA KINA

Kama siku hiyo unataka kufanya tafakari ya kina ni sawa pia. Tafakari maana yake ni
kumpa Mungu nafasi azungumze na nafsi yako, na kweli Mungu hutoa majibu dhidi ya
shida zetu kama tukimpa nafasi ya kweli. Tafakari ya kina ni mwendo wa kawaida wa
kuitafuta sauti ya Mungu ndani mwetu. Pia ni mwendo wa kawaida wa sehemu ya sala
kumwachia Mungu nafasi ya kusema na moyo wetu. Ni muhimu sana kuweza
kutofautisha kati ya mawazo yako binafsi na sauti ya Mungu. Wengine hutabiri ovyo hata
kudai kutoa unabii kwa kubuni mawazo yao wenyewe, hii ni hatari sana katika imani. Hii
ni sehemu inayohitaji ukomavu na utulivu wa kutosemasema ovyo kwa watu unayodhani
kuwa ni sauti ya Mungu. Mara nyingi hapa sauti ya Mungu huja kukupatia majibu ya
shida zako binafsi, na mara chache sana tena kwa nadra kabisa Mungu kuwapatia ujumbe
unaohusu watu wengine na hasa tu kwa waliokomaa vizuri katika mahusiano yao na
Mungu, kupewa ujumbe juu ya wengine huwa pia ni karama si kawaida sana isipokuwa
kama Mungu amekuteua kwa ajili hiyo. Ukiona unatumia nguvu kuelewa kama umesikia
ujumbe wa Mungu ama la; basi ujue bado hujasikia kitu katika tafakari yako. Mungu
4
akikujibu hutatumia nguvu kuelewa utaelewa mojakwa moja ujumbe wa Mungu moyoni
mwako. Na mara nyingi sauti ya Mungu huja kinyume kabisa na matarajio ya mtu
mwenyewe. Kwa mfano unaweza kudhani kuwa umelogwa kwa tabia yako ya kuwa mtu
wa hofu kila mara, ukatafakari kujua aliyekuloga ni nani, yeye akakujibu kuwa ulitenda
dhambi fulani miaka kumi iliyopita wakati wewe umesha sahau. ukashangaa tukio zima
la picha hiyo ya dhambi yako na mazingira yake yakakujia kwa ghafla na kwa nguvu
kabisa kichwani mwako na ukajisikia uzito mkubwa ukikuelemea moyoni juu ya jambo
hilo, akikujulisha kuwa hukutubu vizuri na hivi unapaswa kutubu vizuri kosa lako na
kujisamehe na kumwomba Mungu akuponye na majeraha ya dhambi hiyo. Ama
ukaonyeshwa dhambi uliyotendewa na mtu kumbe hukumsamehe vyema mtu huyo, na
hivyo Mungu akataka akutoe hapo. Ukifanya unalopaswa kufanya kadiri ya maandiko
matakatifu shida yako hiyo inaanza kutokomea kidogokidogo, wakati ukiendelea kuomba
kila siku msaada wa Mungu, mpaka shida yako inapoisha kabisa.
Waweza kutafakari hivi: kwenda mbele za Bwana na baada ya kufuata hatua hizo za
sala hapo juu; kisha chagua jambo moja lolote linalokusumbua kichwani lilete mbele za
Bwana kisha acha kichwa chako kiwaze mambo mengi kadiri iwezekanavyo lakini
yanayohusiana na jambo unalolileta kwa Mungu, acha akili itoe majibu mengi kadiri
iwezekanavyo bila kutumia nguvu kufikiria, kuwa huru mbele za Bwana, usihamishe
mawazo, ila waweza kutaja jina la Bwana kwa unyenyekevu na upendo moyoni
ukiendelea kuitazamia huruma yake na msaada wake katika tafakari yako, lazimisha
mawazo yako yasihame, ukifanya kwa nia utaweza kutuliza mawazo, ni vyema
ukachagua muda ambao hujachoka ili usilale na kichwa kitulie vizuri. Fanya tafakari hiyo
ukiwa eneo la ukimya na ukiwa peke yako .Wakati wa usiku wakati wengine wamelala ni
muda mzuri zaidi. Ni vizuri wakati wa tafakari ukawa unatembeatembea kidogokidogo
kama ni chumbani ama popote. Ukiketi ama kuegema kitandani ama kwenye ukuta ni
rahisi kusinzia, angalia mwenyewe namna inayokufaa hata kama ni kukaa kama
hutasinzia. Tafakari kwa muda mwingi hata dakika ishirini ama zaidi mpaka nafsi yako
iridhike kuwa umetoka na mawazo mapya. Fanya zoezi hilo kwa siku kadhaa mpaka
utakapojisikia wepesi moyoni mwako.

NGUVU ZA GIZA

Nguvu za giza ni eneo lingine ambalo lina utata mkubwa maana linamchnganyiko wa
mambo mengi ya kiroho, lakini ni halisi. Tunaweza kuelewa tatizo ni la nguvu za giza
hasa kutokana na dalili alizonazo mtu. Baada ya kuona baadhi ya dalili zake mara nyingi
hujitokeza zaidi ya dalili moja, inatusaidia kumuuliza mhusika kujua zaidi namna ya
maisha anayoishi. Kwamba mahusiano yake na Mungu na mambo anayofanya mtu.

Dalili za Nguvu za Giza


Hizi ni baadhi ya dalili za nguvu za giza ambazo ndizo zinazojidhihirisha zaidi, ziko na
nyingine zaidi ya hizo.
1. Kukabwa wakati umelala hasa usiku lakini wakati mwingine hata mchana. Mtu
hukabwa mara kadhaa kwa wiki ama kwa mwezi ama karibia kila siku.

5
2. Kuona vitu visivyo vya kawaida hasa usiku hata mchana, watu/wanyama wakiwa
ndani nk. Kuona mwanga na kuondoa amani ndani mwako ama maruwe ruwe
mengine.
3. Kusikia unaitwa ama sauti zingine zisizoelezeka na utasikia mwenyewe
4. Kuhamishwa ufahamu. Mf. Unajikuta uko eneo ambalo hujui umefikaje.
5. Kuota ndoto za kutisha za mashetani, ama zingine zisizo za kawaida.
6. Kuota nyoka mara nyingi ama panya ama wanyama wengine kma paka, samba
mbwa, nk kwa kawaida wanakusumbua huko kwenye ndoto ama kukdhuru.
7. Kuanguka hasa wakati wa maombi ama kuzubaa kusiko kwa kawaida na
hospitalini kutogundua tatizo hilo. Inaweza kuwa ni dalili za ugonjwa mwingine
ama nguvu za giza.
8. Kuota na kupiga makelele itokee zaidi ya mara moja au na mchanganyiko na tabia
zingine.
9. Kusikia mwili unawaka moto na hospitalini hawatambui tatizo.
10. Kusikia vitu vinatembea kwenye mwili wako ndani ama nje ya mwili lakini
havionekani.
11. Kujikuta mwili wako kama unafanyishwa mapenzi hasa wakati wa usiku lakini
uko mwenyewe tu.
12. Roho za utambuzi 1Samweli 28, 2Falme23:24-25, Matendo 16:16-18
13. Dalili nyingine ni kushtukashtuka kwa moyo na kuumwa kichwa ambapo hata
baada ya vipimo mpaka hospitali kuumbwa hawaoni tatizo. Na hata baada ya
vipimo vingi.
14. Nyingine ni kupiga miayo hovyo mara nyingi mno hasa wakati wa kusali (hii ni
kwa watu wanaotaka kupiga hatua ya kiroho kuvuka hali ya ukawaida ili kuingia
hatua ya juu zaidi na Mungu) shetani hufanya bidii ili uache kusali.
15. Kushikwa na kwikwi mno kusiko kwa kawaida na hasa wakati wa kusali (hii ni ya
watu wanaotaka kuvuka hatua ya kiroho pia)
16. Kuchoka hovyo pasipo homa na mara nyingi wakati wa sala zako binafsi. (shetani
hataki usali)
17. Kuona picha ya kutisha mara unapotaka kuanza kusali. Kwa kawaida inakuja
kama ndani ya fikra zako. Nayo hukatisha tamaa ya kuendelea kusali.
 Dalili hizo zingine zinaingiliana na matatizo ya kawaida ya afya kwa hiyo
mhusika ni lazima awe amekwenda hospitalini kuangalia tiba za hospitali
kwanza. Mhusika aone dalili nyingi sio moja, Hasa muunganiko na zile zisizo
za kawaida.
 Hata kama ni matatizo ya kawaida ya kiafya tumia dawa za hospitalini na
maombi na sala viende pamoja.
 Hizo ni baadhi tu ya dalili, zinaweza kuwepo dalili zingine zaidi maana
mambo ya rohoni ni mapana zaidi. Kama dalili ni mbaya na kuondoa amani
moyoni yaweza kuwa ya shetani.

MILANGO INAYOSABABISHA NGUVU ZA GIZA

1. Maisha ya Dhambi

6
Maisha yasiyokuwa na toba. Si lazima mashetani yakakushika kwa sababu ya dhambi, ila
mtu mwenye maisha ya toba na sala nyingi hawezi kutawaliwa na nguvu za giza. Luka
10:19 “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za Yule adui,
wala hakuna kitu kitakachowadhuru.”
2. Majeraha ya nafsi;
mfano mtu amejeruhiwa nafsi kwa kutendewa dhambi na akashindwa kusamehe vizuri,
jeraha hilo huacha msongo mkubwa wa mawazo na mfadhaiko kwa mtu, ama jeraha
lilosababishwa na dhambi mbayo mtu mwenyewe ametenda na akashindwa kuitubu
vizuri. Maumivu hayo ya ndani yataisha kupitia juhudi za mhusika kuingia kwenye
maombi ya kina pamoja na kupitia ushauri wa watu wazoefu wa kiroho na tafakari za
kina za mara kwa mara. Pia kusamehe ama kutubu kwa kina juu ya kosa alilotenda mtu.
3. Dhambi za uzinzi;
Baada ya kuzini kimwili, ama kwa kutazama ama kusikiliza ama kuwazawaza ovyo
mambo kama hayo ama kufanya jambo lolote linaloendana na hayo, roho mbaya ya
shetani humwingia mtu. Kutamani kimwili, kutazama picha chafu, kuzungumza na
kusikiliza kwa kina ovyo ovyo mambo kama hayo ni hatari sana kwa roho. Siku zingine
mtu huweza kuamka siku hiyo akiwa na tamaa mbaya ya uzinzi, ajichunguze kwa makini
utakuta kuwa kuna siku amejiingiza kwenye kati ya hayo mambo hata kama hakumbuki
kuwa ni lini. Tamaa mbaya pia huweza kusababishwa pia na hali ya kujisikia kukataliwa
na Mungu au na wanadamu, pengine mtu kujihisi kama vile Mungu amemwacha, ni
tatizo linalohitaji msaada wa sala, maombi na tafakari ya kina. Mungu hajatuumba
wadhaifu hivi kwamba tusiweze kujithibiti, ila huwa tunaruhusu milango hiyo ya ibilisi
ndani mwetu itukalie. Lakini hata baada ya kukosea Mungu anatupenda katubu.
4. Kushiriki madhehebu wanaojiita ya Kikristo kumbe wanatumia nguvu za giza.
Wako baadhi ya watu wanajificha kwa jina la Ukristo kumbe wanatumia nguvu zingine;
Kuombewa huko, Kupakwa mafuta ya upako huko, kunywa, kuruka mafuta, kuchukua
maji huko, asali nk. Madhehebu wanaotumia vitu hivyo unauhakika wa vyanzo vyake?

5. Kwenda kwa waganga wa kienyeji.


Kufuata dawa za bahati, biashara, ili kupata watoto, nk. Kutatua matatizo yako kupitia
njia hizo za kishirikina ni mbaya.
Hili ni eneo lingine hatari sana ni kumfuata shetani mwenyewe na kumkaribisha afanye
maskani moyoni mwako. Ukimkaribisha shetani maishani mwako atakuja kweli na
atakaa moyoni mwako na maishani mwako atakutawala na kukuelekeza kufanya mengi
zaidi maovu ili akuangamize roho na mwili.

6. Kupokea vitu vya masharti kwa wazazi ama babu ama bib nk.
Mfano mtu kabla ya kufariki anakupatia mkuki, ama ngoma, ama fimbo, au nguo Fulani
anakupa masharti namna ya kutumia ama kutunza kitu hicho, mwingine anaweza
kukuambia asishike mwingine ni wewe tu! Huenda mtu huyo kuna mikataba alifanya juu
7
ya kitu hicho na miungu. Mtu asikutishie kukulazimishia kukurithisha vitu vyake, kama
wewe umekombolewa na Kristu usiogope watu, mche Mungu.
7. Kulogwa
Kama maisha yako hayana Yesu kutosha wakikuloga unalogeka, Lazima tuwe watu wa
kuwa karibu na Mungu kwa juhudi. Kuna watu wengine humiliki uchawi na hutumia
kulogea. Ila ukiona umelogwa ukalogeka, maisha yako ya kiroho ni duni. Na usimdhanie
mtu yoyote ni vibaya sana. Wakati mwingine shetani hupenda kutumia ndoto ama maono
ama sauti ya mtu fulani ukaona suru ya ndugu yako ama jirani ama mtu mwingie
unaemfahamu akikutendea kitimbwi. Usizingatie, shetani hupenda kutumia sura za watu
ili akufanye ugombane na huyo mtu. Badala ya kugombana na shetani ukagombana na
watu shetani ataharibu maisha yako kupitia dhambi za chuki na uchonganishi. Ibilisi ni
mbaya sana.

8. Kutambika
Kutambika ni kuabudu miungu mingine kabisa hizo ni ibada za kuabudu mizimu
watajenga undugu na muunganiko wa mtu. Muunganiko mkubwa zaidi maana
umewatolea sadaka. Wakristo kafara yetu ya ukombozi ni Kristo.

9. Changamoto Zingine ni kulishwa sumu na watu wabaya kwenye chakula au


kinywaji (sio uchawi bali sumu ya kweli)
Baadhi ya watu wenye wivu ama chuki ama kinyongo huweza kutumia sumu kuangamiza
wengine ama kudhuru mifugo yaw engine. Sumu hizo zinaweza kuwa zimetengenezwa
kwa miti shamba, au kutoka kwa wanyama wenye sumu, ama vyanzo vingine. Hata shida
kama hiyo pia inapaswa kwenda hospitalini na pia iweke kwenye maombi. Vyote viende
pamoja. Maombi yawe endelevu ya muda mrefu hata zaidi ya mwaka na kuendelea.

Usiishi na hali inayokusumbua ya nguvu za giza, hujui shetani anataka nini zaidi na
maisha yako. Maana yeye kazi yake ni kuangamiza. Yohana 10:10 “Mwivi haji ila aibe
na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele”.
Usitatue shida zako kutumia shetani, chochote ambacho kimekatazwa na Mungu
ulichofundishwa kupitia kanisa, unapaswa utii ili kuepuka madhara ya shetani sasa na
baada ya maisha yajayo.
Namna ya kutoka kwenye nguvu mbaya za shetani

Hili ni eneo hatari zaidi linalohitaji maombi ya kina na toba ya uhakika. Tubu juu ya
dhambi iliyosababisha tatizo hilo, hata kama hujui chanzo halisi wewe tubu tu, tubu na
kwa ajili ya makosa ya kizazi chenu kilichopita, samehe waliohusika na jisamehe
mwenyewe kwa kuruhusu ama kusababisha shida hiyo kukupata maana kila nguvu
mbaya ya shetani ina mlango wa uovu nyuma yake. Ama ulijisababishia ama
ulisababishiwa na wengine. Nenda kwenye Sakramenti ya kitubio mara kwa mara na
dhamiria kwa dhati kuacha njia mbaya za uovu. Moyo msafi ni kinga dhidi ya shetani.
Ni lazima kuwa na sala nyingi uwe mtu wa sala; ni vyema kusali sala za ibada kwa Bikira

8
Maria na watakatifu. Njia nzuri ni kununua vitabu vya sala na kujifunza sala mbalimbali
za kanisa na sala zilizotolewa na Bwana Yesu kupitia watakatifu na sala zingine nyingi
zilizoko ndani ya vitabu vya Sala. Wengi tumekuwa hatujui uzuri na ufanisi wa sala
zilizopo ndani ya vitabu vya sala ndani ya kanisa Katoliki. Sala hizo zina ufanisi mkubwa
sana. Sala za mtu anaedhamiria kwa dhati, sala binafsi zinapaswa kuwa walau kuanzia
lisaa na kuendelea zikipungua sana walau dakika arobaini na kuendelea. Mathayo 26:40;
“Akawajia wale wanafunzi akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je hamkuweza
kukesha pamoja nami hata saa moja?”

Baada ya hatua hiyo muhimu inafuata hatua nyingine muhimu sana. Wakati wa
kupambana na shetani inakupasa utumie mamlaka ya Jina la Yesu. Binadamu
tumepewa mamlaka na Yesu, ni lazima itumike kama anavyotufundisha. “Tazama
nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna
kitu kitakachowadhuru” (Luka 10:19) Yesu anatuthibitishia kuwa amekwisha kutupa
mamlaka na nguvu na ulinzi kazi yetu sisi ni kuitumia vyema, usiishie kumwomba
Mungu tu kwa sala kikawaida, tumia mamlaka uliyopewa kemea roho hizo
zinazokusumbua maana nguvu za giza ni roho nazo zitatoka kiroho. Usisubiri Mungu
akuhurumie tu bila kuomba!, Lazima kuomba; “Angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa
na juu ya falme, ili kung’oa na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na
kupanda” (Yeremia 1:10). Yeremia anatuwakilisha sisi binadamu wenzake; unahitaji
kung’oa na kuangamiza kazi za ibilisi ndani mwako na katika maisha yako, na kisha
kujenga ufalme wa Mungu.

Unapoomba vuta picha ya hilo tatizo kana kwamba ni kitu kinachoonekana, kisha
ipige shida hiyo kwa maombi. Tatizo ni la kiroho kwa hiyo linapigika kiroho kwa
maombi ya kushambulia. Omba kama hivi: Kwa jina la Yesu nakuvunja, nakubomoa,
nakuharibu, nakung’oa. Nakuangamiza kwa Damu ya Yesu Kristo Mwana wa Mungu
aliye hai, kwa mamlaka niliyopewa na Mungu, nakuamuru shetani unitoke uniache, acha
kufuatilia maisha yangu, nakukataa kabisa, nakuangamiza kabisa, huna mamlaka ndani
yangu. Shuka ee Moto kutoka mbinguni angamiza ‘uovu huu’ (taja hiyo shida kwa jina),
wewe hasira nakuvunja kabisa, uzinzi uliyoko ndani yangu nakuvunja kabisa, kiburi,
tamaa chafu, uchawi, ugonjwa, utaje, uchungu usioisha, hali ya kutosamehe nk; wewe
shetani mbaya, nguvu zote za giza ndani yangu, pepo na mashetani yote ndani yangu
nawakemea katika Jina la Yesu, nakuamuru toka kwa jina la Yesu, toweka kwa jina la
Yesu na usirudi tena, nk. Hata Kristo alikemea pepo na wewe kemea. Luka 8:29, “Kwa
kuwa Yesu alikuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke yule mtu”.

v) Kumshukuru Mungu
Kila baada ya kusali ni lazima tumshukuru Mungu kwa wema wake mkuu kwetu.
“Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na
kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu” (Wafilipi 4:6). Kushukuru iwe ni sehemu
9
muhimu ya mawasiliano yetu na Mungu kila siku. Kwa jinsi ambavyo huwa tunajisikia
furaha watu wanapotushukuru, ndivyo ambavyo Mungu anavyofurahi tukimshukuru.
Wakati mwingine tunatazama fadhila za Mungu kama wajibu wake kwetu, si sawa
kamwe. Mbona hata sisi binadamu tunapeana shukrani sisi wenyewe kwa wenyewe,
mkubwa hata mdogo akitutendea jambo huwa tunapeana shukrani, na anayepewa
shukrani hujisikia furaha. Ukimpa mtoto hela za mahitaji ya shule anakushukuru hata
kama ulichokifanya ni wajibu wako. Je hatupaswi kumshukuru Mungu zaidi? Yeye ndiye
aliyetuumba tuwe tunasikia faraja wanapotushukuru watu, kumbe hali hiyo ya kufurahia
shukrani iko ndani ya Mungu mwenyewe, kumbe basi Mungu anahitaji shukrani mara
dufu.
Isitoshe sio wakati wote tunastahili mbele za Mungu, tunazo dhambi nyingi za
kumwudhi Mungu ila yeye huendelea kutuvumilia tu na kutupatia mahitaji yetu.
Mwambie Mungu kuwa unamshukuru kwa kukuumba, kwa afya hata kama ni
mbaya walau bado unaishi, kuishi ni nafasi nyingine tunayopewa na Mungu ya kuendelea
kujiandaa vyema tukiwa safarini kuelekea kwake, mshukuru kwa msamaha wa dhambi,
kwa kutujalia hewa na jua na vyakula vya kila siku, mshukuru kwa kukupatia mwenza,
watoto na wazazi na marafiki wala usiangalie sana madhaifu yao, mshukuru kwa
kufanikiwa mipango yako, mshukuru kwa kuruhusu mateso mbalimbali unayopitia, hayo
ni kwa ajili ya utakaso na malipizi ya dhambi zetu na wongofu wa watu walio mbali na
Mungu. nk. Siku nyingine mfano mwisho wa wiki waweza kutumia maombi binafsi
kumshukuru Mungu tu kwa wema wa wiki nzima, mwezi au shukrani nyingine maalumu.
Mshukuru na kwa mema usiyoyaona pia.
IMANI INAHITAJIKA KATIKA MAOMBI
Imani haiji baada ya tukio, imani ni kuona pato la maombi kabla ya kupata jambo
lenyewe. Yesu alipokuwa anamfufua Lazaro aliomba hivi “.......Baba nakushukuru kwa
kuwa umenisikia .... akalia kwa sauti kuu Lazaro njoo huku nje” Yohana 11:41,43.
“Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana”
(Waebrania 11:1). Ndani mwetu tunapoomba tunapaswa tujitahidi kuamini hivyo kama
tumeshapata. Yesu anasema nashukuru kwa kuwa umenisikia, hasemi kwa kuwa
utanisikia. Ukiomba kumbe jambo hufanyika tayari kiroho ndio lisubiri kutimia kwa nje.
Kuna siri ya ajabu katika ulimwengu wa roho, binadamu ni kati ya viumbe wa kiroho,
sisi tuna mwili na roho, wakati malaika na shetani wana roho pekee. Viumbe wa kiroho
tumepewa nguvu ya kuamrisha mambo na yakatokea jinsi tulivyoamrisha, lakinii sisi
tunaamuru mambo kutokea kwa jina la Mungu, watu waliopotea hutumia nguvu za giza
kutenda baadhi ya mambo, ambapo itawagharim wasipotubu. Mwili umekuwa ni tatizo
katika mwono wa kupokea ya kiroho, tunatathmini mambo kimwili halafu tunadhani
kama kimwili haliwezekani ati kiroho pia haliwezekani. Hilo ni kosa katika imani.
Ulimwengu wa kiroho na ulimwengu wa kimwili ni vitu viwili tofauti, roho inaweza
kupenya hata milango ikiwa imefungwa mwili hauwezi, tusichanganye uwezo wa kiroho
na wa kimwili hata kidogo. Kuomba sio kumsumbua Mungu, Yesu anapenda tuombe,
Yohana 14:13, “Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya ili Baba
10
atukukuzwe ndani ya Mwana”. Unapoomba ujue wewe ni mshindi, Yesu anatupenda,
ujue umeshapata ila tu muda wa kudhihirika kwa hicho ndio utatimia.

“Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana”


(Waebrania 11:1). “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza ‘Mungu’ kwa maana
mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa
thawabu wale wamtafutao” (Waebrania 11:6). Imani inaonekana kuwa sio jambo rahisi,
hata Mitume wa Yesu walimwambia Yesu “Bwana tuongezee imani” (Luka 17:5). Hii ni
baada ya Yesu kuwafundisha mambo waliyoyaona kuwa magumu. Ugumu wa kuamini
haujaanza kwako na kwangu tu hata Mitume wa Yesu walipata shida namna ya kuamini.
Lakini cha kushangaza wanafunzi haohao baadae waliponya wagonjwa na kutoa pepo
hata kufufua wafu. “Petro aliwatoa nje wote, akapiga magoti, akasali. Kisha akaigeukia
ile maiti, akasema, “Tabitha, amka”. Naye akafumbua macho yake na alipomwona Petro
akaketi.” (Matendo 9:40). Kumbe imani huanza taratibu na baadae hukua kulingana na
utakavyoendelea kuzoea mazoezi mbalimbali ya kiimani kama sala nk. Na hasa
utakapokuja kugundua kwamba kumbe kweli Mungu anashughulika na maisa yetu.
Ndipo utatiwa moyo zaidi na zaidi.

Kuomba kwa imani ni kuomba bila kukoma


Kuamini katika maombi maana yake ni kuanza kuomba na kuendelea kuomba bila
kutazama ukubwa wa tatizo. Wewe omba tu haijalishi unavyojisikia, ama unavyodhani
bali unavyozidi kuomba, haijalishi unajisikia mdhaifu namna gani bali wewe endelea
kumwomba Mungu. Usiisikilize akili yako wakati wa kuomba, unapoomba kuna mawazo
yatakujia “utapata kweli”, ‘wewe mkosefu hivi’ weka nia ya kutubu na endelea kuomba,
‘wewe mdogo hivi kwa Mungu’ omba tu, ‘hili jambo mbona kubwa sana’ wewe endelea
kuomba tu mpakaa uone majibu. Imani haimaanishi kuwa mashaka yote yataisha, imani
ni kupuuzia mawazo hayo madogo madogo yanayokuambia eti unaomba bure.
kuyapuuzia na kuendelea kuomba, hiyo ndio imani, ni kuomba bila kukoma. Ukiyapuuzia
na kuzidi kuomba sana hatimaye utapata unachoomba hata kama ni baada ya miezi
mingi, na mara nyingi majibu huja baada ya miezi kadhaa. Utaona mambo yanatokea
kama kwa kawaida lakini kumbe ni matokeo ya sala zako. Uwe unaendelea kujitakasa
kiroroho kwa bidii kadiri ya taratibu za kanisa, mpende Mungu acha kuelekea maovu
jibidiishe kuwa mwema zaidi.
Wengine hujiona wadogo mno ama wadhaifu mno mbele za Mungu kiasi kwamba
wanadhani Mungu hawajali, lakini kumbe sivyo. “Basi ikiwa Mungu huyavika hivi
majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika
ninyi, enyi wa imani haba?” (Mathayo 6:30). Omba kila siku na mara nyingi hata kama ni
mwaka mzima na zaidi usiache kuomba na kushukuru, maana Yesu alisema kesheni
mkiomba, fanya maombi na sala kuwa sehemu ya ratiba zako. Kumwamini Mungu kuna
faida kubwa; “Basi twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo
matendo ya sheria” (Warumi 3:28). Imani ni msingi wa mahusiano yetu na Mungu,
endelea kumwamini Mungu hata kama huelewi hali ya mambo inavyokwenda, kazi yako
ni kumwamini Mungu mpaka kufa, hata kama mambo yakawa magumu namna gani
endelea kumwamini Mungu mpaka mwisho kabisa. Mahusiano yetu na Mungu ni
11
mahusiano kama ya wenzi wanaotembea pamoja maisha yote. Sio mahusiano ya kwenda
kupata msaada na kutulia!
Nimeshuhudia jambo la pekee katika maombi, nimeona mara nyingi Mungu
hujibu ombi baada ya mtu kuomba mpaka kufikia mwisho kabisa na kukaribia kukata
tamaa, yaani baada ya kutumia akili yako yote na kujisikia mkiwa pasipo msaada wowote
kutoka kwako na ukaendelea kumwamini Mungu basi ndio unaona majibu. Pengine
Mungu anataka atufanye tujitambue kuwa bila yeye hatuwezi lolote na tukiri hivyo
moyoni. Wakati ukiomba kama ni ugonjwa endelea na matibabu yako kama kawaida,
maana Mungu ndiye aliyekusudia dawa ziwepo ili kutuponya. Mara nyingi Mungu hujibu
mapema ndani ya mwezi mpaka miezi mitatu hivi kama utaomba kila siku kwa muda wa
kutosha walau lisaa kila siku. Yatatokea kati ya mambo mawili tu kama utaomba kwa
bidii, Mungu kukupatia kile unachohitaji ama la, kukujibu kwa namna nyingine
akikujulisha pengine uvumilie shida hiyo kama sehemu ya mapenzi yake. Pengine mtu
angeuliza ni kwa namna gani Mungu hujibu; hakika Mungu ana njia nyingi mno, lakini
atahakikisha kuwa umeelewa jibu lako bila mashaka yotote.

Yesu alisema “Ombeni mtapewa” (Mathayo 7:7)


“Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni mlango, nanyi
mtafunguliwa. Maana yeyote aombaye hupewa, atafutaye hupata, na abishaye mlango
hufunguliwa” (Mathayo 7:7). Binadamu ni wa kiroho Mungu ameumba viumbe
anaoweza kuwasilianana nao bila mashaka yoyote. Wewe kazi yako ni kuomba na
kushukura tu kila siku, ujue kila unachopitia na kuwaza anaona tu vizuri sana. Mungu
anapokuondolea tatizo kwa mfano kama ni ugonjwa ziko njia mbili. Ya kwanza ni
kupona kwa ghafla ukiwa ndani ya maombi ama baadae kidogo baada ya maombi, kwa
kawaida huambatana na hisi kama joto likipita sehemu husika na hatimaye ugonjwa
kutokomea, lakini kadiri ya wataalamu wengine wa kiroho njia hii hufanyika mara
chache, ila pia Mungu hafungwi na namna moja tu. Njia nyingine ni tatizo lako ama
ugonjwa kuisha taratibu mithili ya mtu anayemaliza kichuguu polepole mpaka kwisha
kabisa njiaa hii ni mara nyingi zaidi. Pengiine kwa sababu Mungu anataka akufanye
udumu zaidi kwenye maombi ili akuokoe roho na mwili. Lakini hata kama usipopona
ama tatizo kwisha yeye atakujalia amani na faraja nyingi rohoni akikuandaa taratibu kwa
ajili ya kuupokea uzima wa milele. Wengine hukata tamaa wanapoona hawapati
wanachokiomba kumbe pengine tatizo lako limeshapunguzwa kama vile sehemu kidogo
ya mlima ama kipande cha mkate hivi kinavyokatwa, unapoachia katikati inakuwa
vigumu kusaidika tena maana huombi na hivi tatizo lako linarudia palepale. Ama pengine
changamoto unayopitia ni njia ya kukufikisha nyumbani kwa Baba salama zaidi, ukiishia
kulalamika na kukata tamaa, unapoteza bure neema za Mungu na bado kama ni kufa
utakufa tu bila kufaidika chochote na mateso yako. Mateso hayo mtolee Mungu kama
malipizi ya dhambi zako na kama sadaka ya kuongoa wakosefu ikiwepo wewe
mwenyewe na pia ombea roho za marehemu toharani kupitia mauimivu unayopitia
Mungu awasaidie.
Maombi katika Shida kubwa

12
Wakati mwingine unaweza usione majibu haraka hata baada ya kuomba kwa muda.
Inabidi uongeze mbinu mbalimbali kadiri unavyoongozwa na Roho Mtakatifu. Mfano:
Kufunga; Yesu alipojiandaa kuchagua mitume wake alifunga kwa muda wa siku arobaini,
kutoa sadaka kubwa; unaweza kutenga kiasi kikubwa toka sehemu ya kipato chako
ukatolea kanisani, ama ukatolea ujenzi wa kanisa, ama ukotolea kwa maskini, ama kwa
vituo vya kulelea watoto yatima nk. Ukaambatanisha sadaka yako na maombi yako kwa
Mungu, toa sadaka kubwa; elfu hamsini, laki, laki tano nk kulingana na kipato chako.
Kornelio alitoa sadaka na sala akajibiwa maombi yake (Matendo ya mitume 10:1-4).
Unaweza kufanya novena kwa muda wa siku tisa ama zaidi. Unaweza kufanya sala ndefu
ukasali hata rozari tano kwa mara moja hata zaidi kwa kipindi cha siku kadhaa, rozari ya
Bikira Maria, ya huruma ya Mungu ama zingine. Unaweza kujitolea kufanya kazi
kanisani ama kwa watoto yatima nk. Kwa kipindi cha muda fulani, unaweza kukesha
usiku ukiomba, ama ukajipatia masaa kadhaa ukiomba usiku mbele za Mungu kwa siku
kadhaa, unaweza kukaa mbele ya Ekaristi Takatifu kwa masaa kadhaa kila siku kwa siku
kadhaa ukiomba, ama unaweza kuunganisha mazoezi haya mawili, ama matatu hata zaidi
kwa mara moja kulingana na unavyojisika moyoni. Njia ziko nyingi kadiri
utakavyoongozwa na Roho Mtakatifu. Lakini pamoja na mazoezi yote hayo sala na
maombi ni lazima yaendelee kwa bidii. Mwishowe Mungu atakupatia haja ya moyo
wako. “Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si
zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?” (Mathayo
7:11).

Maombi ya Muungano

Hii ni mbinu nyingine katika shida ya kufanikisha maombi. Maombi ya Muungano ni


maombi shirikishi ya kuunganisha watu ili msaidiane, wanaweza kuwa watatu hata na
kuendelea. Lakini ni vizuri kufanya hivyo baada ya kuomba mwenyewe na kuona kuwa
hali haibadiliki, ama unapoona tatizo ni kubwa ni vizuri kuungana. Mnaweza kufanya
maombi ya familia ama ya kikundi mnsali kwa kipindi cha siku ama miezi kadhaa, ama
kwa muda mrefu kulingana na shida. “Tena nawaambia ya kwamba wawili wenu
watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba watafanyiwa na Baba yangu
aliye mbinguni.” (Mathayo 18:19). Hapo Yesu anatutia moyo wakufanya maombi ya
pamoja. “Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi
kwa ajili yake. Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule Petro alikuwa analala
katikikati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango
wakalinda gereza. Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle
chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, ondoka upesi. Minyororo
yake ikamwanguka mikononi.” (Matendo ya mitume 12:5-7). Petro anaombewa na watu
waliokusanyika tena wanaomba kwa bidii na hapo Mungu anamtuma malaika wake
kumtoa Petro gerezani ambapo Herode alikusudia kukutana naye kesho yake. Hapa
13
tunajifunza mambo mawili la kwanza ni nguvu ya maombi ya watu waliokubaliana kama
kundi, pili Mungu anakuja kumtoa Petro mwishoni kabisa ambapo kesho yake tu pengine
angeadhibiwa au kuuawa. Ukianza kuomba usiishie njiani mpaka Mungu atende.
Maombi ya muungano mnaomba watu kadhaa kama watatu hivi au zaidi lakini watu
wawe na bidii ya kuomba. Mnapanga muda wa kuanza maombi pengine saa nne za usiku
mpaka saa tano. Kila mmoja akiwa nyumbani kwake mnaanza kuomba kila mtu kivyake
lakini mkiombea shida moja, lakini pia mnaweza kuomba kila mmoja muda wake binafsi
kulingana na nafasi ya kila mtu. Mtaamua kuomba kwa muda wa siku kadhaa ama wiki
kadhaa nk. Maombi ya muungano yana nguvu kubwa. Mkiweza kukutana kwa maombi
pia ni jambo jema, lakini kila mtu akiwa mwenyewe yaweza kuwa nzuri zaidi maana kila
mmoja atatumia maneno anayotaka mwenyewe na kwa namna anavyojisikia kwa uhuru
bila kutawanywa mawazo na mwingine wa pembeni mwake. Kama ni maombi ya
kupambana na nguvu za mwovu mkiwa wote itapendeza zaidi pia.

Kusali sala Mchanganyiko kuna majibu mazuri


Sali sala nyingi na mchanganyiko; Sala rasmi za kanisa kama rozari mbalimbali, sala
za vitabu, njia ya msalaba, unganisha sala hizo na maombi yako mwenyewe moja kwa
moja. Hutajisikia kuchoka sala maana unasali sala mchanganyiko. sala Mfano rozari
waweza kusali hata tano, nne, tatu, mbili ama zaidi kwa mara moja na kwa miezi mingi
hata miaka nk. Yakobo 5:16 Ungameni dhambi zenu niyinyi kwa ninyi, na kuombeana,
mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii. Mtu
mwenye toba akiomba kwa bidii kwafaa sana. Sali kila siku hasa kwenye utulivu.
Ukiweza kuamka usiku usali inapendeza sana maana kuna utulivu mkubwa. Yesu
alipenda kusali usiku pia “Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba
akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu” (Luka 6:12). “Basi kila mchana
alikuwa akifundisha hekaluni na usiku huenda kulala katika mlima uitwao wa Mizeituni”
(Luka21:37-38). Na nyakati zetu watu wengi wanasali pia usiku, watu wamegundua
faraja ya kusali usiku, wengi hawasemi kwasababu ya unyenyekevu labda kama
umemuuliza. Sali lisaa limoja au zaidi kila siku kwa muda mrefu. Mwanzoni mtu
huchoka lakini ukizoea utafurahia zaidi muda wako wa kusali ukifika maana utakutana na
faraja mbalimbali za kiroho hasa baada ya kusali hasa kwenye ndoto utagundua kuwa
mara baada ya kusali wakati mwingine utoata vitu vya kiroho. Kusali ni sehumu ya
maisha, kusali isiwe mzigo ni sehemu ya muunganiko wetu na Mungu.
Vitabu vya sala vinapatikana maduka ya vitabu vya kanisa, vingine vina sala
mchanganyiko, sala nyingi rozari za aina mbalimbali na litania, kuna vingine ni sala za
watakatifu Fulani tu. Ni bora uwe na vitabu vyako vya sala.

Kusali sala hizo za vitabu, rozari nk pamoja na maombi ya kujisemea mwenyewe ni


muhim zaidi. Sala kwa muda mrefu, miezi hata miaka, utaona tatizo likiisha polepole
ama kwa ghafla, hata kama ni kubwa. Tunahitaji sala nyingi na za muda mrefu.
Tunahitaji kutoa sadaka ama majitoleo kama kufanya usafi kanisani, wakati mwingine na
mifungo kama hamna shida ya afya,kutoa sadaka kubwa, nk. (Yesu ana maana aliposema
“Basi kesheni ninyi kila wakati, mkiomba...........” Luka 21:36) Watu tunamahitaji mengi
14
kwa Mungu hatupaswi kuyaacha tu ama kupambana kibinadamu pekee, tunapaswa
kuomba.

15

You might also like