You are on page 1of 45

MAOMBI NI JAMBO LA UMUHIMU SANA?

J. C. Ryle (1816-1900)
“Kisha Yesu akawapa wanafunzi wake mfano ili kuwaonyesha kuwa yawapasa
kuomba pasipo kukata tamaa” (Luka 18:1).

Maombi la jambo la muhimu sana katika maisha ya ukristo. Mambo


mengine yote kama, kusoma Biblia, kuiheshimu Siku ya Jumapili,
kusikiliza mahubiri, kuenda kanisani na hata kula meza ya Bwana, ni
mambo ambayo yanakuja baada ya maombi. Haya mambo yote ni ya
muhimu sana, lakini maombi ni ya muhimu Zaidi.

Kwanza, mtu lazima aombe ikiwa ataokoka.


Mtu yeyote asitarajie kuokoka bila kuomba. Ni ukweli kwamba
wokovu unapatikana kwa neema pekee na wala si kwa kuomba. Lakini
ili mtu apate kuokoka lazima aombe. Katika Biblia hatusomi mahali
popote ambapo mtu alipata kuokoka bila kuomba. Hakuna mtu ambaye
ataokoka bila kumwomba Yesu Kristo amuokoe. Ni ukweli kwamba
hakuna mtu ambaye ataokolewa kwa sababu ya maombi yake, lakini
hata hivyo hakuna yeyote ambaye ataokoka bila kuomba.
Siku ya mwisho wakristo wote watakusanywa kutoka pembe zote za
ulimwengu nao watakuwa kusanyiko moja kubwa sana ambalo hakuna
mtu awezaye kuhesabu (Ufunuo 7:9). Kusanyiko hili la watakatifu
litaimba nyimbo za kumsifu mwokozi. Nao watapaza sauti zao juu sana
zaidi ya sauti za maji mengi.Watakuwa wanaimba kwa sauti moja na
kwa moyo mmoja. Nao watakuwa wale ambao walimwamini Yesu
Kristo na kuoshwa katika damu Yake. Hao wote watakuwa wamezaliwa
mara ya pili na wote watakuwa watu ambao waliomba.
Ikiwa tunataka kuimba huko mbinguni pamoja na watakatifu
wengine, lazima tuombe wakati tuko hapa ulimwenguni. Ni lazima
tujifunze kuomba la sivyo, hatutawahi kuwa miongoni mwa wale ambao
watakuwa wakimsifu Mungu huku mbinguni. Kwa ufupi, ni kwamba
kukosa kuomba, ni kuwa bila Mungu, bila Kristo,bila neema,bila
tumaini na kuikosa mbingu. Inadhihirisha kwamba uko njiani
ukielekea Jehanamu.
2

Tabia ya maombi ni ishara kuu ya mtu ambaye ameokoka.


Watoto wa Mungu wote katika ulimwengu huu, wanafanana, kwa
sababu wao ni watu wa maombi. Wakati wao wanapata uhai wa kiroho,
wao huanza kuomba. Kama tu vile mtoto anapozaliwa katika
ulimwengu huu, ishara ya kuonyesha kwamba yuko hai, yeye hulia.
Vivyo hivyo mtoto wa Mungu ishara kuu katika maisha yake kwamba
yeye ni wa Mungu, ni kwamba yeye huomba.
Hii ni mojawapo wa ishara ya wale wote ambao wameokoka,
wanaomba mchana na usiku (Luka 18:7). Roho Mtakatifu ambaye
anatufanya kuwa viumbe vipya, hutudhihirishia kwamba sisi ni watoto
wa Mungu, na anatuwezesha kulia, “Abba, yaani Baba” (Warumi 8:15).
Wakati Bwana Yesu Kristo anatuokoa, yeye hutuambia kwamba,
“msiwe mabubu tena.” Watoto wa Mungu si mabubu. Maombi ni asili
yao mpya kama tu vile mtoto mdogo aliavyo. Wao huona haja yao ya
neema na huruma. Wao huhisi uovu wao na dhambi na kwa hivyo wao
wanaomba.
Nimesoma katika Biblia kuhusu watu wa Mungu wote, na sijaona
mtu ambaye hakuwa mtu wa maombi. Ilikuwa tabia yao kila wakati
kumwita Baba yao ambaye ni Mungu, na pia kwamba wao waliliita jina
la Kristo Yesu. Biblia inasema kwamba ni tabia ya wale ambao
hawajaokoka, kukosa kuomba (1 Petro 1:17; 1 wakorintho 1:2; Zaburi
14:4).
Nimesoma sana kuhusu maisha ya wakristo wengi ambao walikuwa
matajiri na wengine walikuwa maskini; wengine walikuwa watu ambao
wamesoma sana na wengine walikuwa hawajasoma; wao walitoka katika
madhehebu tofauti tofauti na walikuwa na jambo moja ambalo
lilifahamika miongoni mwao na hilo ni, wao walikuwa watu wa
maombi.
Pia tunapaswa kujua kwamba kuna wengi ambao wanaomba, lakini
maombi yao haitoki katika mioyo yao. Pia tunapaswa kujua kwamba
maombi hayamaanishi kwamba mtu huyu ni mtakatifu kwa sababu
kuna wengi ambao wanaomba lakini hawajaokoka, maombi yao ni
maneno matupu maskioni mwa Mungu.
Kukosa kuomba ni ishara kwamba mtu hajaokoka. Huyu ni mtu
ambaye hahisi dhambi zake na yeye hampendi Mungu. Yeye hawezi
kutamani utakatifu na yeye hana tamaa ya mbinguni, na yeye
hajazaliwa mara ya pili. Hata kama mtu huyu anaweza kudai kuelewa
mafundisho ya kweli ya Biblia. Kwa mfano, anaweza kuamini kwamba
Mungu ndiye aliwachagua wote ambao wanaokoka, wokovu ni kwa
Maombi ya wale ambao wameokoka 3

neema, ni kwa imani tu ndani ya Kristo mtu anaokolewa na anapata


tumaini la kweli la mbinguni. Ukweli ni kwamba ikiwa mtu huyu
haombi, haya yote anaamini hayamsaidii.
Ishara ya kazi ya Roho mtakatifu katika maisha ya mtu ni kwamba
mtu huyo anaomba. Mtu anaweza kufanya mambo mengi sana. Kwa
mfano mtu anaweza kuwa anajua kuzungumza vizuri sana, na pia
anaweza kuandika vitabu vizuri sana, lakini awe kama Yuda Iskariote
ambaye hakuwa ameokoka. Mtu hawezi kuomba kwa kweli ikiwa yeye
hajaokoka. Mojawapo wa ishara ambazo Mungu ameweka katika
maisha ya yule ambaye ameokoka ni kwamba mtu huyo, ni mtu wa
maombi. Wakati Mungu alipomtuma Anania kwa Sauli alimwambia,
“..kwa maana wakati huu anaomba” (Matendo 9:11). Ninajua kwamba
wale ambao wameokoka, ni wale ambao Mungu aliwachagua kabla ya
kuiweka misingi ya ulimwengu. Pia ninajua kwamba ni Roho Mtakatifu
ambaye anawaongoza kuja kwa Kristo Yesu. Hakuna mtu ambaye
anaweza kumfanya mwingine afanywe mwenye haki mbele za Mungu
ikiwa mtu huyu hataamini. Hakuna mtu ambaye anaamini, na awe
haombi. Ishara ya kwanza ya imani ni kuomba Mungu. Imani ndio
maisha ya nafsi. Maombi ni kudhihirishi imani kama tu vile pumzi
inadhihirisha uhai ndani ya mtu. Haiwezekani kwamba mtu ambaye
ameokoka, ni mtu ambaye haombi. Ikiwa umeokoka, lazima wewe
utakuwa mtu wa maombi, unapenda kuzungumza na Mungu, ambaye
ni Baba wako.

JE, MAOMBI YA KWELI NI MAOMBI YA


AINA GANI?
John Bunyan (1628-1688)

Maombi ni kuzungumza maneno ambayo yanaeleweka kwa Mungu


kutoka ndani ya mioyo yetu, tukikiri kwa imani ahadi zake ambazo
zinapatikana katika Neno Lake, kupitia kwa Yesu Kristo, tukiwa
tunaongozwa na Roho Mtakatifu. Maombi yanaombwa tu, kwa uzuri wa
kanisa la Mungu kwa unyenyekevu katika imani na kwa mapenzi ya
Mungu.

Katika ufafanuzi huu kuhusu maombi, kuna mambo saba.


4

a). Maombi ni jambo ambalo linatoka moyoni mwa mtu.


b). Maombi ni kuzungumza Kutoka ndani ya moyo wako
c). Maombi ni Kuzungumza na Mungu maneno ambayo yanaeleweka
kutoka ndani ya moyo wako.
d). Maombi ni kuzungumza na Mungu kutoka ndani ya moyo wako
kupitia kwa Kristo tukisaidiwa na Roho Mtakatifu.
e). Maombi ni kuzungumza na Mungu kulingana na neno Lake.
f). Maombi yanapaswa kuombwa kwa uzuri wa kanisa
g). Maombi yanaombwa kwa unyenyekevu kwa imani na kwa
mapenzi ya Mungu.

a). Maombi ni jambo ambalo linatoka moyoni mwa mtu.


Kufanya mambo kutoka katika moyo ni jambo ambalo
linamfurahisha Mungu sana. Ikiwa hatutafanya mambo ya Mungu kwa
mioyo yetu yote, basi ni wazi kwamba hatutamfurahisha Mungu
kamwe. Daudi anazungumza kuhusu jambo hili na kusema,
“Ninamlilia kwa kinywa changu, sifa zake zilikuwa katika ulimi
wangu” (Zaburi 66:17). Maombi ambayo yanaombwa na hayatoki katika
moyo wa mtu, Mungu hayakubali kamwe. Biblia inasema, “Ee Mungu,
uniweke salama kwa maana kwako nimekimbilia. Nilimwambia
BWANA, “Wewe ndiwe Bwana wangu; pasipo wewe sina jambo jema.”
Kwa habari ya watakatifu walioko duniani, ndio walio wa fahari ambao
ninapendezwa nao. Huzuni zitaongezeka kwa wale wanaokimbilia
miungu mingine. Sitazimimina sadaka zao za damu au kutaja majina
yao midomoni mwangu” (Zaburi 16:1-4). Mungu anaendelea kusema
katika neno lake kwamba, “Kisha mtaniita na mtakuja na kuniomba,
nami nitawasikiliza. Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa
moyo wenu wote” (Yeremia 29:12-13). Kwa sababu ya kutoomba kutoka
kwa mioyo yao, Mungu alikataa maombi ya wengi: “Hawanililii mimi
kutoka mioyoni mwao, bali wanaomboleza vitandani mwao.
Hukusanyika pamoja kwa ajili ya nafaka na divai mpya, lakini
hugeukia mbali nami” (Hosea 7:14). Ni unafiki kuonekana kwamba
mtu anaomba ilhali katika moyo wake haombi kabisa. Jambo la
kuzungumza kutoka katika mioyo yetu ni jambo ambalo Kristo aliliona
katika Nathanieli wakati alipokuwa chini ya mti: “Tazama ni mwisraeli
kweli kweli, hana hila ndani yake” (Yohana 1:47). Wale wote ambao
wanaomba kutoka katika mioyo yao, wao humpendeza Mungu sana:
“Bwana huchukia sana dhabihu za waovu, bali maombi ya wanyofu
humfurahisha Mungu” (Mithali 15:8).
Maombi ya wale ambao wameokoka 5

Je, ni kwa nini tunapaswa kuomba kutoka katika mioyo yetu? Ni kwa
sababu hali hii inawezesha moyo kumlilia Mungu bila unafiki wowote
na bila uoga wowote: “Hakika nimeyasikia maombolezo ya Efraimu:
Ulinirudi kama ndama mkaidi, nami nimekubali kutii” (Yeremia
31:18). Maombi ambayo yanatoka katika moyo, ni maombi ambayo
hayabadiliki katika hali yoyote. Mtu akiwa peke yake ataomba na hata
akiwa mbele za wengine pia ataomba. Mtu kama huyu haombi kwa
sababu ya kuwafurahisha watu au kwa sababu aonekane yeye ni mtu wa
maombi. Yeye huomba kwa sababu anapenda na anajua kwamba
Mungu wake anamsikia na atajibu. Mungu huwa anatazama ndani ya
moyo, na humo ndimo maombi ya kweli yanafaa kutoka.

b). Maombi ni kuzungumza na Mungu maneno ambayo yanaeleweka


kutoka ndani ya moyo wako.
Maombi si kuzungumza-zungumza tu maneno matupu kama wengi
wanavyowaza na kufanya. Maomba yanapaswa kueleweka kwa sababu
yule ambaye anaomba anajua ni mambo gani ambayo anayaombea.
Maombi ya aina hii, yanatambua dhambi, hushukuru kwa sababu ya
neema ya Mungu na kuomba msamaha kutoka kwa Mungu.
i). Mtu ambaye anaomba, yeye huomba ahurumiwe kwa sababu
anajua hatari ya dhambi zake.
Nafsi yake inahisi dhambi na kwa sababu hiyo, yeye anamlilia
Mungu kwa ajili ya huruma wake na msamaha wa dhambi zake. Mtu
anaomba kwa sababu anajua uzito na huzuni ambao umeletwa na
dhambi (Isaya 1:10 Zaburi 69:3). Daudi aliomba na akamlilia Mungu,
akadhofika na kupondwa kabisa, alisononeka kwa maumivu makuu
moyoni na moyo wake ulipigapiga (Zaburi 38:8-10). Hezekia alilia
kama korongo (Isaya 38:14). Efraimu aliomboleza (Yeremia 31:18).
Petro alilia sana (Mathayo 26:75). Yesu Kristo alilia kwa machozi
(Waebrania 5:7).
Hii yote inatokana na kujua kwamba Mungu ni mwenye haki, sisi ni
wenye hatia mbele za Mungu na tunastahili jahanum ni mahali pa
mateso na uangamizi. Daudi aliomba akisema, “Kamba za mauti
zilinizunguka, maumivu makuu ya kuzimu yalinipata, nikalemewa na
taabu na huzuni. Ndipo nikaliita jina la BWANA: “Ee BWANA,
niokoe”( Zaburi 116:3-4). Pia aliomba, “Nilipokuwa katika taabu,
nilimtafuta BWANA, usiku nilinyosha mikono bila kuchoka na nafsi
yangu ilikataa kufarijiwa” (Zaburi 77:2). Tena aliomba akisema,
“Nimeinamishwa chini na kushushwa sana, mchana kutwa nazunguka
6

nikiomboleza” (Zaburi 38:6). Katika hali hizi zote, unaona kwamba


maombi yanaombwa kwa njia ambayo inaeleweka. Yaani wanaomba
wakielewa kile wanaomba na hali ambayo wako ndani wakati wanakuja
katika maombi.
ii. Wale wanaomba wanahurumiwa, hufarijiwa, hupewa nguvu na
kuhimizwa.
Daudi anaomba akimbariki, kumsifu na kumtamani Mungu kwa ajili
ya rehema zake kwa wenye dhambi: “Ee nafsi yangu, umhimidi
BWANA, vyote vilivyomo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu. Ee
nafsi yangu, umhimidi BWANA, wala usisahau wema wake wote,
akusamehe dhambi zako zote, akuponya magonjwa yako yote,
aukomboa uhai wako na kaburi, akuvika taji ya upendo na huruma,
atosheleza mahitaji yako kwa vitu vyema, ili ujana wako uhuishwe
kama wa tai” (Zaburi 103:1-5). Haya ni maombi ya watu wa Mungu
ambayo kwa wakati mwingine huwa yanageuka na kuwa wimbo wa sifa
kwa Mungu. Biblia inasema kwamba, “Msijisumbue kwa jambo lolote,
bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru,
haja zenu na zijulikane na Mungu” (Wafilipi 4:6). Kumshukuru Mungu
kwa ajili ya huruma wake ni maombi ambayo yanamfurahisha Mungu
sana na yanafaa.
iii. Wale wanaomba, wao huomba wakitarajia kuhurumiwa.
Biblia inasema, “Ee BWANA mwenye nguvu zote, Mungu wa Israeli,
umelifunua hili kwa mtumishi wako, ukisema, ‘Nitakujengea nyumba’
Hivyo mtumishi wako amepata ujasiri kukuletea dua hii” (2 Samweli
7:27). Hili liliwafanya, Yakobo, Daudi, Danieli na wengine kumlilia
Mungu kwa sababu walijua Mungu alikuwa tayari kuwapa mahitaji yao.
Pia Mungu alikuwa tayari kuwasamehe dhambi (Mwanzo 32:10-11;
Danieli 9:3-4).

c). Maombi ni Kuzungumza na Mungu kutoka ndani ya moyo wako.


Katika maombi ya kweli, kuna nguvu, uzima na upendo: “Kama vile
paa aoneavyo shauku vijito vya maji, ndivyo nafsi yangu ikuoneavyo
shauku, Ee Mungu” (Zaburi 42:1); “Tazama jinsi ninavyoonea shauku
mausia yako! Hifadhi maisha yangu katika haki yako” (Zaburi 119:40);
“Ee BWANA, ninatamani wokovu wako, na sharia yako ni furaha
yangu” (Zaburi 119:174); ‘Nafsi yangu inatamani sana, naam, hata
kuona shauku, kwa ajili ya nyua za BWANA; moyo wangu na mwili
wangu vinamlilia Mungu Aliye Hai” (Zaburi 84:2); ‘Nafsi yangu
inataabika kwa shauku kubwa juu ya sharia zako wakati wote” (Zaburi
Maombi ya wale ambao wameokoka 7

119:20). Katika kitabu cha Danieli tunasoma, “Ee BWANA, sikiliza! Ee,
BWANA samehe! Ee, BWANA sikia na ukatende! Kwa ajili yako, Ee
Mungu wangu, usikawie, kwa sababu mji wako na watu wako wanaitwa
kwa Jina lako” (Danieli 9:19). Yakobo anaita maombi haya kuwa,
maombi yenye nguvu na yanafaa sana. Tunasoma katika Luka kwamba,
“Naye akiwa katika maumivu makuu, akaomba kwa bidii” (Luka
22:44). Yesu Kristo alijua kwamba ni Mungu pekee ambaye angempa
nguvu na uwezo wa kuvumilia msalaba. Wamebarikiwa sana na
wanabarikiwa sana wale wote ambao wanaomba maombi ya aina hii.
Lakini jambo la huzuni ni kwamba kuna wengi leo ambao
wanaomba, lakini maombi yao si yenye nguvu na kwamba pia hayafai.
Wengine wao wengi maombi yao hayatoki katika mioyo yao na
hayazingatii ukuu wa Mungu na huruma zake kwetu wenye dhambi.
Watu kama hawa wanatosheka tu na maneno machache ambayo
wanayarudia mara kwa mara. Ni wakati ambapo tunaomba kutoka kwa
mioyo yetu na kukizingatia ukuu wa Mungu na huruma zake kwetu,
ndipo nafsi zetu zitajengwa na Kristo kutukuzwa. Ni katika maombi
watakatifu wamemaliza muda wao mwingi wakihakikishwa kwamba
wanabarikiwa na Mungu (Zaburi 69:3; 38:10; Mwanzo 32:24,26).
Wengi hawaombi jinsi inanwapasa kwa sababu ya kupuuza na kukosa
tamaa ya utakatifu katika maisha yao. Wengi wao wako na tamaa ya
kufuata dini lakini si tamaa ya kuomba jinsi wanapaswa. Wengi wao pia
hawajui mtu ameokoka ni mtu wa aina gani. Pia hawajui kuwa na
ushirika na Mungu baba kupitia kwa Kristo Yesu na kuwa na nguvu za
utakaso katika moyo wa mtu inamaanisha nini. Hata kama wao
wanaomba, wao bado wanaishi maisha ambayo yamelaaniwa, maisha ya
ulevi, ya zinaa ambayo ni chukizo kwa Mungu. Maisha yao yamejawa
na chuki, wivu, masengenyo na kuwatesa watoto wa Mungu. Wao
hawajui hatari ambayo wako ndani yake. Hukumu ya Mungu inakuja
juu yao. Maombi yao yote ambayo wanaomba hayatawasadia wakati wa
hukumu ya Mungu.
Maombi ni kumsifu Mungu, kumlilia Mungu kwa ajili ya dhambi
zetu na kuleta mahitaji yetu yote mbele zake, kutoka kwa mioyo yetu.
Daudi anasema kwamba, “Ee BWANA, yote ninayoyaonea shauku yako
wazi mbele zako, kutamani kwangu sana hakufichiki mbele zako”
(Zaburi 38:9). Pia Daudi anaomba akisema kwamba, “Nafsi yangu
inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye Hai. Ni lini nitaweza kwenda
kukutana na Mungu?..Vitu hivi ninavikumbuka ninapoimimina nafsi
yangu: Jinsi nilivyokuwa nikienda na umati wa watu..” (Zaburi 42:2,4).
Daudi anasema, anaimimina nafsi yake. Hili ni dhihirisho kwamba,
8

kupitia kwa maombi, tunaunganishwa na nguvu za Mungu. Biblia


inasema kwamba, “Enyi watu, mtumainini yeye, wakati wote,
mmiminieni yeye mioyo yenu, kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu’
(Zaburi 62:8). Hili ndilo ombi ambalo Mungu ameahidi kwamba
atamwokoa yule ambaye amefanywa kuwa mtumwa na dhambi na
shetani: “Lakini kama mtamtafuta BWANA Mungu wenu, mtampata
kama mtamtafuta kwa moyo wenu wote na kwa roho yote”
(Kumbukumbu la Torati 4:29).
Tena tunaona kwamba maombi ni kuumimina moyo wako wote
mbele ya Mungu. Hii pia inatuonyesha umuhimu wa maombi. Maombi
ni kwa Mungu pekee. Biblia inasema kwamba, “Nafsi yangu
inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai. Ni lini nitaweza kwenda
kukutana na Mungu? (Zaburi 42:2). Ni ukweli kwamba mtu ambaye
anaomba kwa kweli kwa moyo wake wote, yeye huona vitu vya hapa
ulimwenguni vikiwa ni bure na ni katika Mungu pekee nafsi yake
inapata pumzisho la kweli na kutosheka. Biblia inasema, “Mwanamke
ambaye ni mjane kweli kweli, yaani, yeye aliyebaki peke yake, huweka
tumaini lake kwa Mungu naye hudumu katika maombi usiku na
mchana, akimwomba Mungu ili amsaidie” (1 Timotheo 5:5). Daudi
anasema naye, ‘Ee BWANA, nimekukimbilia Wewe, Usiniache
nikaaibika kamwe. Kwa haki uniponye na kuniokoa, unitegee sikio lako
uniokoe. Uwe mwamba wa kimbilio, mahali nitakapokimbilia kila
wakati; toa amri ya kuniokoa, kwa kuwa wewe, ni mwamba wangu na
ngome yangu. Ee Mungu wangu niokoe kutoka kwenye mkono wa
mwovu, kutoka kwenye makucha ya watu wabaya na wakatili. Ee
BWANA mwenyezi, kwa kuwa umekuwa tumaini langu, tegemeo langu
tangu ujana wangu” (Zaburi 71:1-5). Wengi huzungumza kumhusu
Mungu, lakini maombi ya kweli humfanya Mungu awe ndiye tumaini,
ngome na kila kitu katika kila hali. Maombi ya kweli huwa haizingatii
jambo jingine lolote isipokuwa utukufu wa Mungu. Hili ndilo ombi la
kweli ambalo lafaa.
Ikiwa maombi hayaombwi kupitia kwa Kristo Yesu, basi hayo si
maombi kwa Mungu. Kristo ndiye njia ambapo tunapata kuwa na kibali
mbele za Mungu. “nanyi mkiomba lo lote kwa jina Langu, hilo
nitalifanya, ili Baba apate kutukuzwa katika Mwana. Kama mkiomba lo
lote, kwa Jina Langu, nitalifanya” (Yohana 14:13-14). Hii ndio njia
ambayo Danieli alitumia wakati alikuwa anawaombea watu wa Mungu.
Yeye aliwaombea katika Jina la Kristo: “Basi Mungu wetu, sasa sikia
maombi na dua ya mtumishi wako. Ee Bwana, kwa ajili yako tuangalie
kwa huruma ukiwa ma mahali pako patakatifu” (Danieli 9:17). Daudi
Maombi ya wale ambao wameokoka 9

naye aliomba, “Ee BWANA,kwa ajili ya jina lako, unisamehe uovu


wangu, ijapokuwa ni mwingi” (Zaburi 25:11). Hii sasa haimaanishi
kwamba kila mtu ambaye analitaja jina la Kristo, anaomba kwa Mungu.
Kuja mbele za Mungu kupitia kwa Kristo ndilo jambo ambalo si rahisi
kwa kila mtu. Mtu anaweza kweli kuwa anaomba kwa moyo wake wote,
lakini awe haombi kupitia kwa jina la Kristo. Mtu ambaye anakuja kwa
Mungu kupitia kwa Kristo, lazima amtambue Kristo: “..kwa ye yote
anayemjia Mungu lazima aamini kwamba yeye yupo na kuwa huwapa
thawabu wale wamtafutao kwa bidii” (Waebrania 11:6). Kwa hivyo yule
ambaye anakuja kwa Mungu kupitia kwa Kristo ni lazima awe
amewezeshwa kumjua Kristo: “Ikiwa umependezwa nami, nifundishe
njia zako ili nipate kukujua, nami nizidi kupata kibali mbele zako”
(Kutoka 33:13).
Hakuna mtu ambaye anaweza kumjua Kristo asipofahamishwa na
Mungu Baba (Mathayo 11:27). Kuja kwa Mungu kupitia kwa Kristo ni
kuwezeshwa na Mungu Baba kuwa ndani ya Kristo (Mathayo 16:16).
Kwa sababu hiii, Daudi anamwita Kristo kuwa ngao yake, mwamba
wake imara na mnara wake (Zaburi 18:2; 27:1; 28:1). Daudi hasemi
hivyo kwa sababu ni kupitia kwa Kristo yeye aliwashinda adui wake,
bali pia ni kwa sababu kupitia kwa Kristo Yesu, yeye alipata kukubalika
na Mungu Baba. Mungu alimwambia Abraham, “Usiogope Abramu.
Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana” (Mwanzo 15:1). Kwa
hivyo mtu ambaye anakuja kwa Mungu kupitia kwa Kristo, lazima awe
amemwamini Kristo kwa ajili ya wokovu wake. Yule ambaye yuko na
Imani ndani ya Kristo, Biblia inasema kwamba yeye amezaliwa na
Mungu na sasa yeye ameunganishwa kwa Kristo na yuko ndani ya
Kristo (Yohana 3:5,7; 1:12). Kwa hivyo kwa sababu sasa yeye yuko ndani
ya Kristo, sasa anaweza kuja kwa Mungu, kwa sababu sasa Mungu
anamtazama mtu huyu akiwa na Kristo na katika Kristo. Yeye sasa ni
mmoja wa mwili wa Kristo, ambaye ameunganishwa kwa Kristo kwa
sababu Mungu alimchagua, akamwokoa na sasa yuko na Roho
Mtakatifu katika moyo wake ambaye Mungu amempa (Waefeso 5:30).
Wakati mtu huyu anakuja kwa Mungu, haji kwa nguvu zake, bali kwa
nguvu za Kristo, kazi ya Kristo ikiwa ndio msingi wa kukubalika kwake
mbele za Mungu (Waefeso 1:6). Anapokuja kwa Mungu katika maombi,
yeye husaidiwa na Roho Mtakatifu kuomba.

d). Maombi ni kuzungumza na Mungu kutoka ndani ya moyo wako


kupitia kwa Kristo tukisaidiwa na Roho Mtakatifu.
10

Mambo ambayo tunayataja hapa ni mambo ambayo yote lazima yawe


pamoja ikiwa maombi ambayo tutaomba yatakubalika na Mungu.
Haijalishi mtu anazungumza maneno ya aina gani na ni mangapi, ikiwa
maombi yake, si kupitia kwa Kristo na haongozwi na Roho Mtakatifu,
basi maombi yake hayatasikilizwa na Mungu. Wao watakuwa kama
watoto wa Haruni ambao walitumiwa moto mbaya na waliuawa na
Mungu (Walawi 10:1-2).
Maombi ambayo hayaongozwi na Roho Mtakatifu, hayo hayaombwi
kulingana na neno la Mungu (Warumi 8:26-27). Hakuna mtu au kanisa
ambalo linaweza kuja kwa Mungu kwa maombi bila usaidizi wa Roho
Mtakatifu. Biblia inasema kwamba, “Kwa maana kwa kupitia Kwake,
sisi sote tunaweza kumkaribia Baba katika Roho mmoja” (Waefeso
2:18). Pia Biblia inaendelea kusema kwamba, “Vivyo hivyo, Roho
hutusaidia katika udhaifu wetu, kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo.
Lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu usioweza kutamkwa.
Naye Mungu aichunguzaye mioyo, anaijua nia ya Roho, kwa sababu
Roho huwaombea watakatifu sawasawa na mapenzi ya Mungu”
(Warumi 8:26-27). Biblia inatuonyesha kwamba mwanadamu hawezi
akajileta peke yake mbele za Mungu. Lazima amtegemee Roho
Mtakatifu.
Mungu aliwatumia mitume kueneza ujumbe wa injili kwa watu wote
lakini hata katika maandishi ya Biblia, Paulo anaandika akisema
kwamba, hatujui kuomba ipasavyo, Paulo pia akiwa mmoja wa wale
ambao anasema kwamba hawajui kuomba. Mitume hawa pia walikuwa
wanadamu kama tu wanadamu wengine, na kwa hivyo walipungukiwa
katika mambo mengi kama tu wanadamu wengine. Njia za neema ya
Mungu katika maisha ya watu wake, ndizo njia ambazo Paulo na
mitume wengine walitumia. Wao walikuwa wamepewa karama za
kumtumikia kama tu Mungu amewapatia karamu wengine. Lakini hata
hivyo, wao pia walisaidiwa kuomba na Roho Mtakatifu.
Hatujui jinsi ya kuomba, mambo ambayo tunapaswa kuyaombea au
njia ambayo tunapaswa kutumia wakati tunaenda mbele za Mungu.
Wakati mwingi tunachanganyikiwa kama tuombe juu ya Imani au
neema au utakatifu. Huwa hatujui ni lipi tunafaa kuliombea. Lakini
kwa nguvu na uwezo Roho Mtakatifu, tunawezeshwa kuomba jinsi
tupasavyo. Biblia inasema kwamba, “Kwa maana ni nani anayejua
mawazo ya mtu isipokuwa roho iliyo ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo
hakuna mtu ajuaye mawazo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu” (1
Wakorintho 2:11). Mstari huu unazungumza juu ya mambo ya kiroho
ambayo ulimwengu hautambui kamwe (Isaya 29:11).
Maombi ya wale ambao wameokoka 11

Hatuwezi kuomba bila kusaidiwa na Roho Mtakatifu kwa sababu


hatujui hata jinsi tunapaswa kuomba. Biblia inasema, “hatujui kuomba
ipasavyo. Lakini Roho mwenywe hutuombea kwa uchungu usioweza
kutamkwa.” Mitume pia wao hawakuweza kutekeleza jukumu hili
kama tu vile leo pia hatuwezi kulitekeleza bila kusaidiwa na Roho
Mtakatifu. Wakati Roho Mtakatifu aliwasaidia mitume kuomba, wao
walitamka maneno kwa uchungu usioweza kutamkwa.
Pia tunasoma kwamba, “hatujui kuomba ipasavyo.” Wengi
hawajaelewa maana ya maneno haya na kwa sababu hii wametunga
mbinu tofauti tofauti za kuomba kama vile Yeroboamu alivyofanya (1
Wafalme 12:26-33). Ili tuweze kuomba jinsi inavyotupasa, hatuwezi
kubuni mbinu fulani fulani za wanadamu au za malaika jinsi wengi
wanavyodai. Bali tunapaswa kumtegemea tu Roho Mtakatifu. Kile
mwanadamu anaweza kubuni ni mawazo yake na wala si kile ambacho
ameambiwa afanye katika neno la Mungu.
Yakobo anasema, “Mnapoomba hampati kwa sababu mnaomba kwa
nia mbaya, ili mpate kuvitumia hivyo mtakavyopata kwa tamaa zenu”
(Yakobo 4:3). Si maneno mengi ambayo yatamfanya Mungu ajibu ombi
la mtu. Wakati tunapoomba, Mungu huchunguza nia ya maombi yetu
ambayo tunaleta mbele zake (1 Yohana 5:14). Biblia inasema kwamba,
“Naye Mungu aichunguzaye mioyo, anaijua nia ya Roho, kwa sababu
Roho huwaombea watakatifu sawasawa na mapenzi ya Mungu”
(Warumi 8:27). Mungu anasikiliza tu maombi ambayo yanaombwa
kulingana na mapenzi yake pekee. Ni Roho Mtakatifu pekee ambaye
anaweza kutusaidia kuomba kulingana na mapenzi ya Mungu.
Haijalishi tumejifundishwa kuomba kwa njia gani, au ni vitabu gani
ambavyo tumesoma kuhusu maombi, ikiwa hatutaomba tukiongozwa
na Roho Mtakatifu, basi ni wazi kwamba hatutaomba kulingana na
mapenzi ya Mungu. Kwa hivyo Mungu hatayasikia maombi yetu.

e). Maombi ni kuzungumza na Mungu kulingana na neno Lake.


Maombi yanakuwa ya kweli na ya hakika wakati mtu anapoomba
kulingana na neno la Mungu. Ikiwa mtu haombi kulingana na neno la
Mungu, basi yeye anapiga tu kelele. Daudi katika maombi yake kila
wakati alilikumbuka neno la Mungu: “Nimelazwa chini mavumbini,
yahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako” (Zaburi 119:25). Pia
unaweza soma mistari hii, 41-42,58,65,74,81-82, 107,147,154,169,170).
Pia Daudi aliomba kwamba, “Kumbuka neno lako kwa mtumishi wako,
kwa sababu umenipa tumaini” (Zaburi 119:49). Roho Mtakatifu hafanyi
kazi yake bila neno la Mungu. Yeye hutumia neno la Mungu
12

kumshawishi mkristo aende mbele za Mungu na kumlilia katika


maombi. Ni Roho Mtakatifu ambaye alimwezesha Danieli kukumbuka
kwamba siku za utumwa za Waisraeli zilikuwa zimefika mwisho na kwa
hivyo, aliomba, “..mimi Danieli, nilielewa kutokana na Maandiko,
kulingana na neno la BWANA alilopewa nabii Yeremia, kwamba ukiwa
wa Yerusalemu ungetimizwa kwa miaka sabini. Kwa hivyo
nikamgeukia BWANA Mungu na kumsihi katika maombi na dua,
katika kufunga, kuvaa nguo ya gunia na kujipaka majivu” (Danieli 9:2-
3).
Roho Mtakatifu anapotuongoza katika maombi yetu, huwa
anatuwezesha kuomba kulingana na neno la Mungu na ahadi za
Mungu. Bwana Yesu Kristo aliomba kulingana na neno la Mungu na
ahadi za Mungu: “Je, unadhani siwezi kumwomba Baba yangu naye
mara moja akaniletea Zaidi ya majeshi kumi na wawili ya malaika?
Lakini je, Maandiko yatatimiaje yale yasemayo kwamba ni lazima
itokee hivi?” (Mathayo 26:53-54). Ni ukweli kwamba yale Kristo
alisema mbeleni yalikuwa katika maandiko, lakini pia alizingatia
kukamilika kwa maandiko.
Roho Mtakatifu lazima atuongoza kulingana na neno la Mungu jinsi
tunapasavyo kuomba. Biblia inasema, “Nifanyeje basi? Nitaomba kwa
Roho lakini nitaomba kwa akili ya pia” (1 Wakorintho 14:15). Lakini
tufahamu kwamba hakuna kuelewa bila neno la Mungu. Kwa kuwa
neno la Mungu likikataliwa, basi hiyo hekima uliyo nayo itakuwa na
namna gani? (Yeremia 8:9).

f). Maombi yanapaswa kuombwa kwa uzuri wa kanisa.


Hii inadhihirisha kwamba maombi yanapaswa kuomba kwa utukufu
wa Mungu. Mungu, Kristo na watu wake wako pamoja. Kama tu vile
Kristo na Mungu Baba ni kitu kimoja, vivyo hivyo wale ambao
wameokoka wako ndani ya Kristo na yeyote ambaye anawatesa watu wa
Mungu, huwa anamtesa Kristo mwenyewe (Matendo 9:5). Kwa hivyo
Biblia inatuhimiza kwamba tuombee amani ya mji wa Yerusalemu,
yaani kanisa la Kristo wakati tunapokuwa unaombea chochote ambacho
unakihitaji. Kanisa halitawahi kuwa na amani kamili hadi lifike
mbinguni mahali ambapo Kristo anataka liwe. Mbinguni ndipo mahali
Mungu amekusudia kanisa lake liwe. Kwa hivyo ni lazima tuombe
kwamba kanisa litakuwa na amani na kwamba litaendelea kwa uzuri.
Wale wote ambao wanaliombea kanisa, wanaombea watu wake Kristo.
Yeyote ambaye anaombea kanisa, anapaswa kuomba kwamba neema ya
Mungu itaongezeka katika kanisa na kwamba kanisa litakua katika
Maombi ya wale ambao wameokoka 13

neema. Pia tunapaswa kuomba kwamba kanisa litashinda majaribu


yake yote na kwamba Mungu atalisaidia kanisa katika majukumu yake
hapa ulimwenguni. Pia tuombe kwamba kila kitu katika kanisa
kitafanyika kwa uzuri wa kanisa na watu wake. Tuombe kwamba
Mungu atatulinda katika utakatifu tunapoendelea kuishi miongoni
mwa watu waovu (Wafilipi 2:15). Hivi ndivyo Kristo alivyoomba katika
Yohana 17. Paulo pia aliomba hivi: “Haya ndio maombi yangu kwamba
upendo wenu uongezeke zaidi na zaidi katika maarifa na ufahamu wote,
ili mpate kutambua yale yaliyo mema, mkawe safi, wasio na hatia hadi
siku ya Kristo, mkiwa mmejawa na matunda ya haki yapatikanayo kwa
njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa za Mungu” (Wafilipi 1:9-11).
Hili ni ombi fupi sana. Lakini unapolisoma unaona kwamba limejawa
na shauku ya kuona kwamba kanisa linaendelea vyema kiroho hadi
kuja kwa Kristo Yesu (Waefeso 1:16-21; 3:14-19; Wakolosai 1:13).

g). Maombi yanapaswa kuombwa kwa unyenyekevu chini mapenzi ya


Mungu.
Maombi haya yanaombwa kwamba mapenzi ya Mungu yafanyike
jinsi Kristo ametufundisha katika Mathayo 6:10. Watu wote wa Mungu
tunapaswa kunyenyekea na kuomba kulingana na mapenzi ya Mungu.
Tunapaswa kila wakati kuwa tayari kufahamu na kukubali kwamba
Mungu atende jinsi inavyomfurahisha na kwa hekima yake. Hata
wakati tunanyenyekea hivyo, hatufai kuwa na shaka kwamba Mungu
hatayajibu maombi yetu. Bali tunapaswa kujua kwamba Mungu atajibu
kwa utukufu wake na kwa uzuri wetu. Kwa hivyo tusiwe na shaka juu
ya upendo na ukarimu wa Mungu kwetu. Tuwe waangalifu tusije
tukajaribiwa na shetani kuomba maombi ambayo hayamletei Mungu
utukufu wala kwa sababu ya uzuri wa kanisa lake. Biblia inasema
kwamba, “Huu ndio ujasiri tulio nao tunapomkaribia Mungu, kwamba
kama tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atatusikia. Na kama
tunajua ya kuwa atatusikia, lo lote tuombalo, tunajua ya kwamba
tumekwisha kupata zile haja tulizomwomba” (1 Yohana 5:14-15). Hivi
ikiwa tutaomba tukiongozwa na Roho Mtakatifu. Tunapaswa
kukumbuka kila wakati kwamba, chochote tunachokiomba, ikiwa
hatuongozwi na Roho Mtakatifu, basi tujue kwamba Mungu hatasikia
maombi yetu. Kwa sababu ni Roho Mtakatifu ambaye anatuongoza
kuomba kulingana na mapenzi ya Mungu. Biblia inasema kwamba,
“Kwa maana ni nani anayejua mawazo ya mtu isipokuwa roho iliyo
ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu ajuaye mawazo ya Mungu
isipokuwa Roho wa Mungu” (1 Wakorintho 2:11).
14

MAOMBI NI NGUVU ZA MAOMBI KWA


WATU WAKE
Eugene Bradford (1915-2010)
“Siku zote tunamshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo,
tunapowaombea ninyi, kwa sababu tumesikia juu ya Imani yenu katika Kristo
Yesu na juu ya upendo wenu mlio nao kwa watakatifu wote, Imani na upendo ule
utokao katika tumaini mlilowekewa akiba mbinguni na ambalo mmesikia habari
zake katika neno la kweli” (Wakolosai 1:3-5).

Ni kwa sababu ya kazi ya Yesu Kristo ya wokovu ambapo Paulo


anaomba kwa ajili ya kanisa. Wakristo katika kanisa la Kolose
walikuwa wamemwamini Kristo na Imani yao ilidhihirika kwa jinsi
walivyopendana. Kwa sababu hii Paulo anamshukuru Mungu na
anaendelea kuwaombea wakristo katika kanisa la Kolose. Kwa sababu
ya yale ambayo ameyasikia kwamba walikuwa wakiyafanya kwa ajili ya
Kristo, yeye anawaombea na anashukuru kwa sababu ya tumaini
walilowekewa akiba mbinguni. Tumaini hilo ni lao kwa sababu
walilisikia katika habari ambayo ni neno la Mungu la kweli. Paulo
hakuwa na sababu nyingine ambayo ilimfanya aombee wakristo wa
kanisa la Kolose. Ombi la Paulo kwa ajili ya kanisa hili la kolose msingi
wake ni kazi ya Kristo Yesu. Baada ya Paulo kuwaombea kwamba, wao
wawe na hekima, wakue katika utakatifu, waendelee kukua katika
kumfahamu Mungu, na pia wawe na uvumilivu, kiasi na furaha, Paulo
anamalizia maombi yake, “mkimshukuru Baba, ambaye
amewastahilisha kushiriki katika urithi wa watakatifu katika ufalme wa
nuru. Kwa maana ametuokoa kutoka katika ufalme wa giza na
kutuingiza katika ufalme wa Mwana Wake mpendwa, ambaye katika
Yeye tunao ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi kwa njia ya damu
yake” (Wakolosai 1:12-14). Kutokana na kifungu hiki, maombi ya Paulo
kwa kanisa hili ni kwamba, anatoa shukurani kwa ajili yao kwa sababu
wao walimwamini Kristo na kwa sababu ya kuamini kwao, wao
walisamehewa dhambi zao na kupewa ahadi ya kuurith Ufalme wa
mbinguni. Kwa sababu ya jambo hili, yeye aliomba Mungu kwamba,
wakristo wa kanisa la kolose wataendelea kukua na kufurahia neema ya
Bwana katika maisha yao.
Katika waraka kwa kanisa la Waefeso, Paulo alifundisha pia juu ya
umihimu wa kuombea kanisa. Katika maombi yake anasema kwamba
Maombi ya wale ambao wameokoka 15

yeye amesikia juu ya imani yao katika Kristo na upendo wao juu ya
watu wote amabo wameokoka. Yeye anaambia kanisa kwamba, hakomi
kuendelea kumshukuru Mungu kwa ajili yao na kwamba kila wakati
anawataja katika maombi yake kwa Mungu. Katika Waefeso 1:18-19,
anaandika akisema kwamba, “Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo
yenu yatiwe nuru ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, utajiri wa urithi
wa utukufu wake kwa watakatifu na uweza wake mkuu usiolinganishwa
kwa ajili yetu sisi tuaminio. Uweza huo unaofanya kazi ndani yetu, ni
sawa na ile nguvu kuu mno.” Tazama jinsi anavyozungumza kuhusu
nguvu hizo na jinsi zilifanya kazi katika kumfufua Kristo na
kumketisha kwa mkono wa kuume wa Mungu Baba. Anaomba, “..na
uweza wake mkuu usiolinganishwa kwa ajili yetu sisi tuaminio. Uweza
huo unaofanya kazi ndani yetu, ni sawa na ile nguvu kuu mno ambayo
aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamketisha mkono
wake wa kuume katika mbingu, juu sana kuliko falme zote na mamlaka,
enzi na milki na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu,
bali na katika ule ujao pia. Naye Mungu ameweka vitu vyote chini ya
miguu yake na amemfanya yeye awe kichwa cha vitu vyote kwa ajili ya
Kanisa, ambalo ndilo mwili Wake, ukamilifu wake yeye aliye yote
katika yote” (Waefeso 1:19-23). Kwa ufupi anawaambia kwamba,
ninaomba kwamba nguvu zile ambazo zilimfufua Kristo kutoka kwa
wafu, zifanye kazi katika maisha yenu na kwamba Kristo ambaye
ameinuliwa juu sana kuliko majina mengine, na ambaye ndiye kichwa
cha kanisa, atawala kanisa lake. Kwa sababu Kristo ameshinda nguvu
za giza ili aletee kanisa lake uzuri, ambalo ni mwili wake. Paulo
anaomba kwamba kila mshirika wa kanisa apate kutawaliwa na nguvu
ambazo zilimfufua Kristo kutoka kwa wafu. Kristo ambaye ndiye
kichwa cha kanisa hawezi kamwe kutenganishwa na mwili wake ambao
ndilo kanisa lake. Muungano huu wa Kristo na kanisa lake
umewezeshwa kwa nguvu za Mungu na ni kwa imani pekee wakristo
wote wanaamini. Kwa sababu ni nguvu za Mungu ambazo zimemfufua
Kristo na kumwinua juu sana kuliko viumbe vyote, pia washirika wa
kanisa wataishi kwa nguvu hizi za Mungu.
16

MAMBO AMBAYO YANAWEZA KUMZUIA


MAOMBI YA MKRISTO
Charles H. Spurgeon (1834-1892)
“Vivyo hivyo ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili, nanyi wapeni heshima
makitambua ya kuwa wao ni wenzi walio dhaifu na kama warithi pamoja nanyi
wa kipawa cha thamani cha uzima, ili kusiwepo na chochote cha kuzuia maombi
yenu” ( 1 Petero 3:7).

Kwa wale ambao huwa hawaombi, mafundisho hayatakuwa na


umuhimu wowote kwao. Pia kuna wale ambao huwa wanadai kuomba,
lakini maombi yao hayafai hata kidogo. Kwa sababu mtu anapiga
magoti au anazungumza maneno fulani fulani akidai kuomba, hiyo
haimaanishi kwamba mtu huyu anaomba. Kwa kufanya hivi, ni
kumkejeli Mungu. Kuna pia wengi ambao wanapoomba, wanarudia-
rudia maneno fulani wakiwaza kwamba wao watasikika zaidi na
Mungu.
Kwa wale ambao huwa hawaombi au kwamba wanaomba kwa njia
isiofaa, wanapaswa kujua kwamba Mungu hawafurahii hata kidogo na
gadhabu yake iko juu yao. Yeyote ambaye haombi kuhurumiwa, yeye
hatapata huruma. Wale wote ambao hawaombi, Mungu hatawapatia
chochote. Kumwomba Mungu lolote ni jukumu letu na ikiwa
hatumwombi, basi tusitarajie kupata kutoka kwake.
Maombi si jambo gumu kufanya, kwa sababu ni jukumu la
mwanadamu kutoka kwa muumba wake. Kwa hivyo hili ndilo jambo
rahisi ambalo kila mtu anaweza kulifanya na kumuomba Mungu
ambaye ameumba. Wale wote ambao hawaombi, siku moja watasikia
sauti ya Mungu kwao akisema, “Lakini kwa kuwa mlinikata nilipowaita
na hakuna yeyote aliyekubali niliponyosha mkono wangu” (Mithali
1:24). Ikiwa mwenye dhambi hataomba katika jina la Kristo Yesu
ambalo ndani mwake Mungu ameahidi msamaha wa dhambi,
halitakuwa jambo la kushangaza ikiwa yeye ataangamia katika
jahanum. Hakuna mtu ambaye atamlalamikia Mungu ikiwa yeye
atatupwa jahanum. Wewe ambaye hutaki kumwomba Mungu, siku
moja utasimama mbele yake na kutetemeka sana kwa sababu alikupatia
na nafasi ya kuomba, lakini ulikataa.
Maombi ya wale ambao wameokoka 17

Kwa wale wote ambao wanaomba, maombi ni jambo bora sana na


lafaa sana.Tukiomba, Mungu huwa anaachilia baraka zake kwetu. Kwa
njia ya maombi Mungu huwa anatosheleza mahitaji yetu. Kwa wale
wote ambao wameokoka, maombi ni njia ambayo tunapata nafsi zetu
zikihuishwa. Maombi kwa wale ambao tumeokoka, ni chombo ambacho
tunatumia kuwasiliana na nyumbani kwetu ambamo ni mbinguni.
Maombi ni jambo ambalo lafaa sana na kwa sababu hii, Petero
anaandika akisema kwamba ndoa na maisha ya nyumbani, furaha yake;
yatokana na jinsi wakristo tunavyoomba. Anawahimiza waume kwamba
wanapaswa kuwaheshimu wake wao ili maombi yao yasizuiliwe.
Chochote ambacho kinazuia maombi ni kitu kibaya sana. Ikiwa kuna
jambo lolote ambalo linafanya tukose kuomba, basi tunafaa kuliacha.
Mume na mke wanapaswa kuomba kwa pamoja kwa sababu ni warithi
wa ufalme moja na chochote ambacho kinazuia jambo hili, kinapaswa
kuachwa kabisa.

Kuna baadhi ya mambo ambayo yanafanya maombi yazuiliwe.

a). Maombi yazuiliwa ikiwa tutakuwa vuguvugu juu ya vitu vya


Mungu.
Mkristo ambaye maisha yake ni vuguvugu juu ya vitu vya Mungu,
utaona kwamba yeye hatajali maombi. Kwa kawaida mtu anapokuwa
mgonjwa sana, utaona kwamba sauti yake haitasikika sana kwa sababu
mapafu yake yameugua sana. Hivyo ndivyo ilivyo na mkristo ambaye
maisha yake ya kiroho ni mabaya, yeye huacha kuomba na hata kama
anaomba, maombi yake yanakuwa dhaifu sana. Maombi katika maisha
ya mkristo, yanadhihirisha maisha yake ya kiroho jinsi yanavyoendelea.
Kuacha kuomba ni jambo hatari sana katika maisha ya mkristo na
kutoomba kabisa ni hatari zaidi katika maisha ya yule ambaye
hajaokoka. Mkristo ambaye anachukua jambo la maombi kuwa jambo
la muhimu sana katika maisha yake na kwamba yeye analizingatia si
kwa sababu ya dini au unafiki bali kwa sababu ya kumtukuza Mungu,
mkristo huyu maisha yake ya kiroho yanaendelea vyema kabisa. Lakini
ikiwa kwamba maombi yako yanazuiliwa, basi ni kwamba kuna jambo
katika maisha yako ambalo unalipasa kulirekebisha kabisa. Maisha
yako ya kiroho hayako sawa.

b). Maombi yanazuiliwa kwa sababu ya kukosa wakati wa kuomba.


18

Hili ni jambo la kawaida kwa wengi. Unapotazama wengi utaona


kwamba wana kazi nyingi za kila siku za kufanya. Kwa sababu ya
majukumu ambayo kila jamii iko nayo, wengi wamejikuta kwamba
wakati wao wa kuomba ni mdogo mno. Kuna wachungaji wengi ambao
ni wazuri sana, lakini kwa sababu ya kujihusisha na biashara, wao sasa
ni watu ambao hawana hata muda wa kuomba na jambo hili limedhuru
sana maisha yao ya kiroho na huduma wao. Tunapaswa kuhakikisha
kwamba tunaweka muda katika maisha yetu wa kuomba. Wengi badala
ya kutumia muda kwa kumtukuza Mungu, wao wametumia muda wao
mwingi wakitafuta mali ya ulimwengu huu. Wengi wameingiwa na
tamaa ya ulimwengu na vitu vyake vyote.
Unaposoma kifungu cha Luka 12:20 kuendelea utaona kwamba yule
tajiri hakuwa na muda wa kuomba kwa sababu alimaliza muda wake
mwingi kwa kushughulika tu na biashara zake. “Lakini Mungu
akamwambia, Mpumbavu wewe! Usiku huu uhai wako unatakiwa. Sasa
hivyo vitu ulivyojiwekea akiba vitakuwa vya nani” (Luka 12:20) na pia
tunasoma kwamba, “lakini masumbufu ya maisha haya, udanganyifu
wa mali na tamaa ya mambo mengine huja na kulisonga lile neno na
kulifanya lisizae” (Marko 4:19). Ni tamaa ya mali ya ulimwengu na
kutotosheka na vile ambavyo wako navyo, ndio sababu ya wao kunaswa
na shetani. Hakikisha kwamba maombi yako hayazuiliwi.
Pia tunaweza kuwa na mengi ya kufanya katika kazi ya Mungu na pia
tukose muda wa kuomba, na hii itazuia maombi yetu kama vile Matha
alivyokuwa na muda mwingi wa kutumika. Si wengi ambao wanaomba
jinsi wanavyotumika. Tunapaswa kuahakikisha kwamba tunaomba sana
na pia tunamtumikia Mungu sana. Ni vyema kwamba tuhakikishe
kwamba tunaomba sana kuliko jinsi tunavyofanya kazi sana. Ninajua
kwamba kuna wengi ambao, wanahubiri sana, wanafundisha sana,
wanasoma Biblia sana, wanahudhuria mikutano mingi ya kanisa lakini
wao hawana muda wa kumaliza katika maombi. Haya mambo yote ni
mazuri, lakini tusipokuwa waangalifu, tutakuwa tunaumiza nafsi zetu
kwa kukosa kuwa na wakati mwafaka na Mungu wetu. Ni lazima
tuombe ikiwa kweli tutahubiri kwa utukufu wa Mungu. Ni jambo la
hatari ikiwa tutakosa kuomba kwa sababu tunahubiri.
c). Maombi pia yanazuiliwa kwa sabau ya kuwa wavivu au wazembe
katika majuku yetu.
Kuna uwekano mkubwa sana tufanye mengi ambayo yanatuzuia
kuomba lakini pia ni ukweli kwamba kuna wakristo wengi ambao
wamezembea katika majukumu yao mengi. Mungu amewapatia mali
nyingi na hawahitaji kujihusisha na mambo mengine mengi. Mara
Maombi ya wale ambao wameokoka 19

mingi hawa wako na muda, na mara mingi wanamaliza muda huu kwa
njia ambazo ni za kujifurahisha lakini hawajali mambo ya Mungu
kamwe. Wanasahau kwamba kuna wengi ambao wanahitaji
kufundishwa neno la Mungu, kuna wagonjwa ambao wanahitaji
kutembelewa na maskini ambao wanahitaji kusaidiwa. Watu hawa kwa
nini wanamaliza muda wao katika anasa na wala si katika kazi ya
Mungu. Kwa nini wao hawatumii muda wao katika kuomba? Ukweli ni
kwamba wengi wao wamezembea katika kazi ya Mungu na haswa katika
maombi. Ninatamani kwamba wao wangefanya maombi kuwa jambo la
muhimu sana katika maisha yao na kujitolea katika kumtumikia
Mungu.
d). Maombi pia yanazuiliwa kwa sababu ya kukosa mpangilio katika
maisha ya wengi.
Wengi huwa wanaamka wakiwa wamechelewa na wanaharakisha sana
kuenda kazini kwa sababu wamechelewa. Wengine wanapata kwamba
kwa sababu ya kukosa mpangilio, mambo ambayo hawajayapanga
yanajitokeza mara kwa mara na wanayashughulikia kwa haraka. Wao
hawana nafasi ya kuomba kwa sababu ya shughuli nyingi. Kila mara
mambo yanajitokeza na wanajipata kwamba hawezi kuomba
iwapasavyo. Na kama hata wataomba, utapata kwamba maombi yao
yatakuwa ya haraka-haraka, na maombi kama hayo Mungu hayasikii.
Ni jambo jema kwamba kila mkristo awe na mahali ambapo
ameandika majukumu yake ambayo anayapasa kufanya kila wakati.
Maombi linafaa kuwa jambo la kwanza katika mipangilio yake yote.
Ikiwa utafanya hivi, utapata kuona ni muda gani ambao unamaliza
katika maombi. Utapata kwamba muda wako mwingi uko katika
shughuli zako mwenyewe, unaumaliza na marafiki zako au katika
burudani na wala si na Mungu. Ikiwa utaona hivi, basi huenda
itakusaidia kujichunguza ili ujipatia muda wa kutosha katika maombi .
Hakikisha kwamba muda mwingi uwe ni ushirika na Mungu.

Tuwe waangalifu kwamba hatuzuiliwe katika maombi.


Ni kweli kwamba maombi yetu yanaweza kuzuiliwa kabisa. Kuna
mambo matatu ambayo ninataka tutazame ambayo yanaweza kufanya
maombi yetu yazuiliwe kabisa.
a). Maombi yetu yanaweza kuzuiliwa ikiwa tutakosa kumheshimu
Mungu Baba.
Tunaweza kukosa kumheshimu Mungu Baba kwa kukosa kutii neno
lake. Ikiwa tunakataa mapenzi ya Mungu Baba jinsi neno lake
20

linafundisha, basi tusishangae wakati tunapata kwamba ni vigumu sana


kwetu kuomba. Ikiwa hatutii neno la Mungu, tutapata kwamba hata
kutamka maneno ni jambo gumu sana. Litakuwa jambo gumu sana
kuomba kikamilifu ikiwa hatumwamini Mungu Baba. Ikiwa moyo wako
ni mugumu dhidi ya Mungu, ikiwa wewe huheshimu jina la Mungu,
ikiwa huamini kwamba Yeye ndiye huwabariki watu wake, ikiwa huna
upendo Kwake, na humwamini, kwa sababu ya mambo haya, wewe
maombi yako yatazuiliwa kabisa.
Wakati mkristo moyo wake unampenda Mungu, wakati yeye
anamwita Baba kutoka katika moyo wake, na nafsi yake kufurahia
katika mapenzi ya Mungu Baba, Mungu atasikia maombi yake. Mungu
hatasikia tu, bali pia atatimiza mapenzi yake katika maisha ya mtoto
wake.
b). Maombi yatazuiliwa ikiwa tutakosa kumheshimu Kristo ambaye
kupitia Yeye, si tunapaswa kuomba Mungu.
Ikiwa tunajiamini wenyewe badala ya kumwamini kristo, ikiwa
tunawaza kwamba tunaweza kuishi bila Kristo, na tuombe kama jinsi
Mfarisayo aliomba katika Luka 18, basi tujue kwamba maombi yetu
yatazuiliwa na Mungu. Ikiwa Kristo si mfano wetu na ikiwa
tunaendelea katika dhambi na kumwaibisha na pia ikiwa sisi hatuna
shukurani kwa yale ambayo anatufanyia katika maisha yetu, basi tujue
kwamba maombi yetu yatazuiliwa kabisa.
c). Maombi yetu yatazuiliwa ikiwa tutakosa kumheshimu Roho
Mtakatifu.
Maombi ambayo hayaongozwi na Roho Mtakatifu, si maombi
ambayo yanakubalika na Mungu. Maombi ya kweli, ni yale ambayo
Roho Mtakatifu anatuongoza kuomba wala si maneno matupu ambayo
tunayazungumza. Kwa hivyo ikiwa tutamhuzunisha Roho Mtakatifu,
basi ni wazi kwamba hatatusaidia kuomba. Ikiwa tutaomba kinyume na
mapenzi ya Roho Mtakatifu, basi hatatusaidia kuomba kulingana na
mapenzi ya Mungu. Kwa hivyo tuhakikishe kwamba hatumhuzunishi
Roho Mtakatifu haswa kwa kukosa kumtii wakati anatuonya, anatuita
na wakati anatuongoza. Ikiwa wewe hutamtii Roho Mtakatifu, basi jua
kwamba hatakuongoza katika maombi yako.
Mungu atayasikia maombi ya wale wote ambao wanataka
kuhurumiwa ikiwa wataomba kupitia kwa Bwana Yesu Kristo. Yeye
Mungu huwa hayakatai maombi ya wale ambao wananyenyekea. Yeye
ni Mungu ambaye yuko tayari kuyasikia maombi ya wale wote ambao
wanataka kusamehewa, ikiwa wao wataomba na kutubu kupitia kwa
Maombi ya wale ambao wameokoka 21

Kristo Yesu. Yeye hatasikia tu, bali atawasamehe wao dhambi zao zote.
Kwa wale ambao hawajaokoka, maombi yao yote ni makelele masikioni
mwa Mungu. Biblia inasema, “Tunajua ya kwamba Mungu hawasikilizi
wenye dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomcha na kumtii”
(Yohana 9:31). Mungu atasikia maombi ya watoto wake pekee na wala si
ya wale ambao si wake, yaani hawajaokoka. Pia ni vyema kufahamu
kwamba Mungu husikia maombi ya watoto wake wote, lakini kunao
miongoni mwa watoto wake ambao maombi yao ni dhaifu, yaani
hawatilii manani jambo la maombi. Wao wanaomba, lakini hawaombi
sana, hawamalizi muda wao mwingi katika maombi. Ikiwa mtoto wa
Mungu anapata kwamba maombi yake hayajibiwi, jambo zuri kufanya
ni kujichunguza jinsi anavyoomba na hali ya maisha yao. Ikiwa
tutajichunguza, tutapata jibu sahihi kwa nini maombi yetu hayajibiwi.

Maombi ambayo Mungu anayasikia na kuyajibu ni maombi ya aina


gani?
a). Mungu anayasikia na kujibu maombi ambayo ni ya wale wakristo
ambao wanaishi maisha matakatifu.
Yakobo anaandika akisema, “Kwa hiyo, ndugu zangu, vumilieni hadi
kuja kwake Bwana. Angalieni jinsi mkulima angojavyo ardhi itoe
mavuno yake yaliyo ya thamani na jinsi anavyovumilia kwa ajili ya
kupata mvua za kwanza na za mwisho…maombi ya mwenye haki yana
nguvu tena yanafaa sana” (Yakobo 5:7,16). Bwana Yesu Kristo anasema
kwamba, “Kaeni ndani yangu, name nikae ndani yenu” (Yohana 15:4)
Kristo anasema “kaeni.” Kristo hapa anamaanisha kwamba ikiwa
hatutafanya mapenzi yake, naye hatatufanyia yale ambayo
tunamwomba atufanyie. Kristo anasema kwamba kulitii neno lake
huleta Baraka. Mungu hawezi kamwe kumjibu yule ambaye
anajitegemea na hamtegemei Yeye mwenyewe. Yesu alipomponya yule
kipofu, kipofu alisema, “Tunajua ya kuwa Mungu hawasikilizi wenye
dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomcha na kumtii” (Nukuu
Yohana 9:31).
b). Mungu anayasikia na kuyajibu maombi ambayo yanaombwa kwa
Imani.
Biblia inasema kwamba, “lakini pasipo Imani haiwekezekani
kumpendeza Mungu” (Waebrania 11:6). “lakini anapoomba lazima
aamini wala asiwe na shaka” (Yakobo 1:6). Biblia inasema kwamba bila
imani, hakuna mtu ambaye anaweza kumfurahisha Mungu, hata katika
maombi. Imani ndio chombo ambacho kinatuleta kwa Mungu katika
22

maombi na kwa imani sisi huamini kwamba kile ambacho tunaomba


kulingana na neno la Mungu, Mungu atakifanya kwa utukufu wake
pekee.
c). Mungu anayasikia na kuyajibu maombi ambayo yamejawa na
hitaji takatifu.
Ikiwa mambo ambayo tunayahitaji au kuyaombea katika maombi
yetu ni mabaya, basi Mungu hatayajibu maombi yetu. Mahitaji yetu
lazima yawe yanaambatana na ahadi za Mungu katika neno lake kwetu.
Maombi kama haya ni yale ambao yanatuleta kwa Mungu tukifahamu
kwamba Yeye anafurahia na atajibu. Maombi haya, hayawezi kamwe
kukosa kufaulu, kwa sababu yanatoka mbinguni na yanarudi mbinguni.
d). Mungu anayasikia na kuyajibu maombi ambayo yanaombwa bila
kukata tamaa na yanatarajia kile ambacho kinaombwa.
Biblia inasema kwamba, “maombi ya mwenye haki yana nguvu tena
yanafaa sana” (Yakobo 5:17). Siyo maombi ya ambayo ni maneno
matupu tu. Si maombi ya wale ambao wanaomba bila kuratajia
chochote. Katika maombi yetu, lazima kuwa na kutarajia, kumtafuta
Mungu kwa ukweli na bila kukata tamaa. Ni lazima yawe maombi
ambayo yanatoka mioyoni mwetu kabisa na si maneno tu ambayo
hayajali kama Mungu atafanya au hapana. Ni maombi ambayo
yanasema, ‘mapenzi ya Mungu na yafanyike.’
e). Mungu anayajibu na kuyasikia maombi ambayo tamaa yake ni
utukufu wa Mungu.
Hili ndilo linafaa kuwa kusudi la kila ombi, na ikiwa hili si kusudi la
maombi yetu, basi tutakuwa hatuombi kamwe. Ni lazima tuombe
chochote na tuwe na imani kwamba Mungu atakileta ili atukuzwe
katika hicho. Ni lazima tufahamu kweli kwamba Mungu atatukuzwa
wakati anajibu maombi yetu. Ikiwa tunaishi maisha matakatifu ambayo
yanamletea Mungu utukufu, maombi yetu kila wakati yatakuwa
yanaambatana na mapenzi yake Mungu, na kwa hivyo Mungu
atayasikia kabisa na kuyajibu. “Jifurahishe katika Bwana naye atakupa
haja za moyo wako” (Zaburi 37:4).
f). Mungu anayasikia na kuyajibu maombi ambayo tarajio lake ni
takatifu.
Mtu ambaye anaomba, ni lazima atazame na kuona ni wapi ambapo
maombi yake yanaelekea. Ni lazima maombi yetu yawe ni kwa Mungu
pekee na tarajio letu liwe kwake tu. Ni lazima tutarajie Mungu kujibu
maombi yetu kutokana na kazi ya Kristo Yesu msalabani na wala si kwa
yale ambayo tumefanya sisi wenyewe. Ikiwa tunaamini kwamba
Maombi ya wale ambao wameokoka 23

anatusikia, tutaamini kwamba ataleta yale ambayo tumeweka mbele


zake.
Mungu hutupatia neema sisi wakristo ili tuweze kuenenda katika
nguvu za Roho Mtakatifu, tukimtumainia Kristo pekee. Ni Yeye
Mungu ambaye tunafaa kumtegemea ili atuwezeshe kuomba
itupasavyo. Mtu ambaye Mungu amemfundisha kuomba impasavyo,
yeye anaomba kulingana na mampenzi ya Mungu na mkono wa Mungu
uko pamoja naye popote anapokuwa. Yeye anapofanya jambo, Mungu
ndiye analifanya jambo hilo ndani mwake.

JUKUMU LA MCHUNGAJI KUWAOMBEA


WATU WAKE
Eugene Bradford (1915-2010)
Maombi ni jambo la muhimu sana katika maisha ya mchungaji. Ni
jukumu la mchungaji kwamba kila siku anamaliza muda katika
maombi kwa ajili ya nafsi yake na kwa ajili ya wale ambao
anawachungaji. Kwa sababu ya mambo mengi ambayo wachungaji
wanahusika nayo, ni rahisi kujipata kwamba mchungaji anakosa muda
wa kuomba. Wale wachungaji ambao wanapuuza jukumu hili, ni wale
ambao watajipata katika shida kubwa sana.
Wachungaji na wale wote wanataka kufanya kazi ya uchungaji
wanapaswa kuwa watu ambao wanaomba kwa ajili ya nafsi zao na kwa
ajili ya nafsi za wale ambao wanawachunga.
Maombi ndio uhai wa nafsi na bila maombi hatutafanikiwa katika
kazi ya huduma. Bila maombi, kazi zote ambazo tunazifanya ni bure.
Kabla hatujaanza kazi ya kuhudumu, lazima tuwe kama Musa ambaye
aliomba kwanza. Maombi hata ya yule ambaye anaonekana kwamba
anafanya kidogo ni ya nguvu sana kuliko ya yule ambaaye anaonekana
kufanya mengi lakini haombi. Ikiwa mchungaji si mtu wa maombi,
hata kama yeye anajulikana kuwa mhubiri mzuri, ukweli ni kwamba
yeye si mtumishi wa Mungu. Yeye ni mtumishi wa shetani ambaye
alichaguliwa na shetani kama tu yule nyoka aliye mwongoza Hawa
katika dhambi. Mchungaji wa aina hii ni adui mkubwa sana wa watu wa
Mungu.
24

Kwa sababu wachungaji wanamtumikia Mungu kuwapatanisha watu


na Naye, maombi ni jukumu letu kufanya. Kupitia kwa maombi ya
wachungaji Mungu huwa analeta baraka katika maisha ya kanisa. Kwa
hivyo mchungaji huwa tu hawaelezi watu maneno ya Mungu, bali huwa
anamweleza Mungu yale ambayo yanawahusu watu wake. Ni jukumu
letu wachungaji kwamba kila siku tunapaswa kuleta mahitaji yetu
mbele za Mungu kwa maombi na wakati huo huo kuleta ya wale ambao
tunawachunga pia. Ni jukumu kuomba kwamba Mungu atawasamehe
dhambi zao. Ni jukumu letu kuwaombea wale ambao hawajaokoka
kwamba wamwamini Kristo. Pia ni jukumu letu kuhakikisha kwamba
tunawahimiza wale ambao wameokoka na kuwaonya. Dhambi na
mahitaji ya wale ambao tunawaongoza zinapozidi, ndipo pia tunafaa
kuzidishi maombi yetu kwa ajili yao.
Kazi ya mchungaji itaendelea na kuwafaidi wengi ambao
anawahudumia ikiwa yeye mwenyewe anamtii Mungu katika
majukumu yake yote. Mchungaji wa kanisa ni mtumishi wa Mungu na
kwa hivyo anapaswa kumtii Mungu ambaye amemwita kumtumikia
miongoni mwa watu wake. Paulo katika Waraka wake kwa Warumi
anandika akisema, “Paulo mtumishi wa kristo Yesu, aliyeitwa kuwa
mtume na kutengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu” (Warumi 1:1). Yeye
Paulo ni mtumwa wa Kristo na wala hajitumikii yeye mwenyewe. Yeye
alikuwa ameitwa na kutengwa kwa sababu ya injili. Ni kwa kazi hii
ambayo ameitwa kufanya ambapo anapaswa kujitolea kabisa kwa
kuifanya. Yeye si mfanya kazi wa mtu mwingine au mwanabishara, yeye
ni mtumwa na ni balozi wa Kristo. Baada ya Paulo kujitambulisha kwa
Warumi yeye ni nani, anaendelea kuwaeleza kwamba haja yake na
kusudi ni watu ambao Mungu amemtuma kwao: “Kwanza kabisa
namshukuru Mungu wangu kwa nji ya Yesu Kristo kwa ajili yenu
nyote, kwa sababu Imani yenu inatangazwa duniani kote. Kwa maana
Mungu ninayemtumikia kwa moyo wangu wote katika kuhubiri injili ya
Mwanawe, ni shahidi wangu jinsi ninavyowakumbuka” (Warumi 1:8-9).
Yeye anasema kwamba hawezi kamwe kuwatumikia warumi ikiwa
haombi kwa Mungu. Paulo alionyesha uaminifu wake kwa Mungu
kwamba hata katika maombi yake, yeye anamwomba Mungu awe
shahidi. Yeye alijua kwamba kazi yake yote ya injili ilikuwa ni kazi ya
Mungu na kazi hii ilijumlisha kuwaombea watu wa Mungu. Yeye pia
anasema kwamba “Anamtumikia Mungu katika roho, yaani
akimaanisha uaminifu wake kwa Mungu. Yeye anaonyesha kwamba
anatekeleza majukumu yake, bali anahakikisha kwamba anamtii
Mungu ambaye amemwitia kufanya kazi hiyo. Lingekuwa jambo baya
sana ikiwa Paulo angesema maneno haya lakini awe hayafanyi.
Maombi ya wale ambao wameokoka 25

Unaposoma Maandishi ya Paulo utapata kwamba yeye alikuwa mtu


ambaye alijitolea kabisa katika kazi ambayo Mungu alikuwa amemwita
aifanye. Kwa ufupi ni kwamba, Kwa sababu Paulo alikuwa mtumishi
wa Mungu ambaye alikuwa ameitwa na Mungu kuihubiri injili ya
Kristo, kwa sababu hii, yeye aliomba kwa ajili ya kanisa la Kristo. Yeye
alihakikishia kanisa kwamba aliwaombea kila wakati. Lilikuwa jukumu
kubwa sana kwa Paulo kuwaombea wakristo . Yeye aliona kwamba kazi
ya mtume alijumlisha kuombea watu wa Mungu. Yeye aliona kwamba
maombi ni kuwa mwaminifu kwa yule ambaye alikuwa amemwita
kumtumikia, yaani Kristo Yesu.
Je, leo tuko kama Paulo ambaye alijitoa kila wakati kuomba kwa
sababu hili likuwa jukumu lake kama mtume wa Mungu? Ni ombi
langu kwamba tusije tuione kazi ya mchungaji kuwa kama kazi zingine
na kutazama ufanisi wake katika mambo ya nje tu na wala si katika
mambo ya kiroho. Tusije tukajaribiwa kuwaza kwamba tunaweza
kufanya kazi ya uchungaji kama tunavyofanya kazi nyingine nyingi.
Paulo anasema kwamba ni jukumu letu. Anasema, “Kwa maana
hatujihubiri sisi wenyewe ila tunamhubiri Kristo kuwa ni Bwana na sisi
ni watumishi kwa ajili ya Yesu” (2 Wakorintho 4:5). Katika
kuwahudumia wanadamu, tunajukumika kwa Mungu ambaye ametuita
katika Kristo kufanya kazi ya uchungaji. Paulo anaandika akisema
kwamba, “..tulinena kama watu tuliokubaliwa na Mungu
tukakabidhiwa Injili. Sisi hatujaribu kuwapendeza wanadamu bali
kumpendeza Mungu, Yeye ayachunguzaye mawazo ya ndani sana ya
mioyo yetu” (1 Wathesalonike 2:4). Ikiwa mchungaji katika mahubiri
yake hawalengi wasikilizaji wake, basi yeye pia hataweza kuwaombea
hawa wasikilizaji wake. Wengi wanaweza kumsifu mchungaji kwamba
mahubiri yake ni mazuri sana, Wengi wanaweza kuchukia mahubiri
yake na wengine kumsifu kwa jinsi anavyoonekana kuwa mtu ambaye
amesoma na anaelewa sana maandiko. Lakini ikiwa mchungaji huyu
haombi kwa ajili ya wale ambao anawachunga, yeye si mwaminifu kwa
Mungu ambaye amemwita katika kazi hiyo.
26

UMUHIMU WA MIKUTANO YA MAOMBI


Erroll Hulse (1931-2017)
Mikutano ya maombi ya kanisa ni ishara ya kuonyesha jinsi kanisa
linavyoendelea kiroho. Unaweza kujua jinsi kanisa linavyoendelea kwa
kuona jinsi kanisa linavyomba wakati limekutana pamoja. Je, kanisa
liko na lengo la kuwafikia wengi na ujumbe wa injili? Ikiwa lengo hili
lipo, utalisikia katika maombi ya kanisa hilo. Je, kuna tamaa ya
kuwaona wengi wakija kwa kristo? Pia ikiwa hili la kweli katika kanisa
hilo, utalisikia likiombwa. Je, kuna tamaa ya kuona ulimwengu ukikuja
kwa Kristo na kujihusisha katika kazi ya Mungu ulimwenguni kote?
Ikiwa kanisa liko na mzigo huu, pia utalisikia likiomba juu ya jambo
hili. Je, kuna tamaa ya kuona kwamba kuna amani katika ulimwengu ili
wale ambao vita na njaa vimewakumba wafikiwa na ujumbe wa Injili?
Katika mikutano ya maombi ya kanisa, hili utalisikia likiombwa. Jinsi
kanisa linavyoomba itadhihirisha upendo na kujali kwa kanisa juu ya
wale wote ambao wanateswa na dhambi na majaribu katika maisha yao.
Wale wote ambao wanapitia katika hali ngumu za maisha watapata
kwamba watafarijiwa katika mikutano ya maombi kwa sababu Roho
Mtakatifu atafanya kazi katika maisha na mioyo yao.

Mikutano ya kila siku ya maombi ya kanisa.


Katika nchi ya Korea kulitokea uvuvio kwa sababu ya mikutano ya
kila siku ya maombi. Huko, nilipouliza niliambiwa kwamba kila watu
wanakutana kwa kuomba saa kumi na moja ya asubuhi na wakati
mwingine saa kumi na mbili za asubuhi. Haya ndio maisha ya baadhi
ya wakristo huko.
Rafiki wangu mwingine, alinieleza kwamba baba yake alikuwa mtu
ambaye alijitolea kuomba kila siku na alikuwa akifanya kazi kuanzia
saa moja asubuhi hadi saa moja jioni. Lakini hata hivyo, yeye alitenga
muda wa kuomba kila siku saa kumi na mbili ya asubuhi.
Katika mwaka wa 1866, Mchungaji Spurgeon alianzisha mkutano wa
maombi kila siku saa moja asubuhi na saa moja na unusu jioni.
Mkutano mmoja wa kanisa lote ulifanyika siku ya Jumatatu kanisani
mwao na watu Zaidi ya 3000 walikuwa wakihudhuria.
Maombi ya wale ambao wameokoka 27

Mafundisho ya Biblia kuhusu maombi.


Maombi ni kuleta mahitaji yetu mbele za Mungu kulingana na neno
lake kupitia kwa Kristo Yesu tukisaidiwa na Roho Mtakatifu, pia
tukikiri dhambi zetu na kwa kumshukuru Mungu kwa huruma zake.
Tunafaa kukumbuka kwamba hatuwezi kamwe kuomba kulingana na
mapenzi ya Mungu ikiwa Roho Mtakatifu hatuongozi. Wakati Roho
Mtakatifu anatuongoza, basi ndipo tunaweza kuomba kulingana na
neno la Mungu na kumfurahisha Mungu katika maombi yetu. Bila
kusaidiwa na Roho Mtakatifu, basi hatuwezi kamwe kuomba na hata
kama tutaonekana kuomba, tutakuwa tunasema maneno matupu tu. Ni
katika maombi ambapo tunaweza kueleza yale ambayo Roho Mtakatifu
anatuongoza ndani. Ni Roho Mtakatifu ambaye huwa anatusaidia
katika udhaifu wetu. Biblia inasema, “Vivyo hivyo, Roho hutusaidia
katika udhaifu wetu, kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo. Lakini
Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu usiyoweza kutamkwa”
(Warumi 8:26).
Toba la kweli linatokana na Roho Mtakatifu. Daudi hangeweza
kamwe kutubu juu ya ile dhambi yake ya kumuua Uraya na ya kuzini
na Bethsheba ikiwa Roho Mtakatifu hangemdhibitishia dhambi yake.
Daudi aliandika Zaburi 51, kama matokeo ya toba lake. Kuomba kwa
ajili ya utukufu wa Kristo na kwa ajili ya ufalme wa Mungu uendelee
kupanuka, ni Roho Mtakatifu ambaye anatuwezesha tuombe hivyo.
Wakati huo huo lazima pia tujue kwamba huu ndio unafaa kuwa
upendo wetu katika mioyo yetu, yaani utukufu wa Kristo na ufanisi wa
Ufalme wake. Si kweli hata kidogo ikiwa tutasema kwamba,
hatutaomba hadi Roho aje atuongoze. Biblia inatuhimiza kwamba
tunafaa kuomba, wakati huo huo tukimtegemea Roho Mtakatifu
atuongoze katika maombi yetu.
Je, tunaweza pia kuwaza kwamba, ikiwa Mungu ameamua kufanya
jambo fulani, je, kuna haja ya sisi kuomba? Tunapaswa kujua kwamba
Mungu anatawala katika kila jambo na wakati huo huo, tunapawa
kujua kwamba Mungu ameweka mbele zetu majukumu ambayo tunafaa
kuyatekeleza kikamilifu. Ni lazima mambo haya mawili tuyafahamu
vyema kila wakati. Tunawajibika mbele za Mungu kwa kumtegemea
Yeye pekee kwa njia ya neno lake na kwa kuomba Kwake. Hivi ndivyo
tunavyoishi maisha yetu hapa ulimwenguni. Kufuata mapenzi ya
Mungu katika maisha yetu ndio njia ya amani, furaha na uaminifu.
Bwana Yesu alimtegemea Mungu Baba, na kwa hivyo Yeye aliomba
Kwake. Hata kama Kristo alikuwa Mungu kamili, Yeye aliomba. Biblia
inasema kwamba wakati wa ubatizo wake, Yeye alikuwa anaomba (Luka
28

3:21). Yeye aliamka mapema sana ili aombe (Marko 1:35). Yeye aliomba
usiku kucha kabla ya kuwachagua wanafunzi wake kumi na wawili
(Luka 6:12). Yeye alikuwa katika maombi wakati sura yake
ilipobadilishwa (Luka 9:29). Maombi ndio ilikuwa njia yake ya
kushinda alipokuwa katika bustani ya Gethsemane (Luka 22:44).
Tutumie muda wetu wa maombi katika mikutano ya maombi
kuombe mambo mbali mbali. Tukumbuke kuombea jamii, kanisa, kazi
ya uinjilisti, makanisa mengine na wachungaji wa makanisa hayo.
Tukumbuke pia kuyaombea mataifa yetu, kazi ya Mungu kote duniani,
Amani katika mataifa ambayo hayana Amani, maskini, na uaminifu
katika uongozi: “Awali ya yote, naishi, kwanza kabisa, naagiza kwamba
dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili watu wote: kwa ajili
ya wafalme na wale wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi kwa Amani
na utulivu, katika uchaji wote wa Mungu na utakatifu. Jambo hili ni
jema tena linapendeza machoni pa Mungu Mwokozi wetu anayetaka
watu wote waokolewa na wafikie kuijua kweli” (1 Timotheo 2:1-4).
Ikiwa siku moja katika juma haitoshi, basi kanisa linafaa kutenga
wakati mwingine wa kuomba pamoja. Muda huu unaweza kuwa hata
mapema siku ya jumapili kabla ibada zianze. Hii ni njia moja sana
nzuri ya kujitayarisha kwa ajili ya ibada za siku hiyo.
Je, katika makanisa ambamo kuna wengi ambao hawahudhurii siku
ya maombi nini inapaswa kufanyika? Ukweli ni kwamba hatuwezi
kamwe kuwalazimisha watu kukua, lakini tunaweza kuwaongoza kwa
njia nzuri kwa upole na ukarimu. Biblia inasema kwamba, “Mwanzi
uliopondeka hatauvunja na utambi ufukao moshi hatauzima” (Isaya
42:3).
Katika makanisa yetu, kuna wale ambao Mungu amewapa karama ya
kuhimiza wengine (Warumi 12:8). Ikiwa wao watatumia karama hii
vyema, watawasaidia wengi kuwa waaminifu katika kuhudhuria
mikutano ya maombi ya kanisa.
Katika mikutano ya maombi ya kanisa, kunahitajika kiongozi
ambaye anapaswa kuongoza na kuhimiza kutoka katika Biblia. Yeye
anastahili kuwahimiza wengine kuomba. Anapaswa kuwaeleza wengine
kwamba hafai kutumia muda mrefu sana kwa sababu hiyo pia inaweza
kuwazuia wengine wasiombe. Kunahitajika maelezo kabla ya kuomba
ili kuwa na mwelekezo mwema. Pia huenda kuwe na haja ya
kuyagawana mambo ambayo yanaombewa. Njia hii itawahimiza
wengine kuomba pia. Yule ambaye anaongoza anapaswa kuacha kuwe
na uhuru wa kuomba kwa wote.
Maombi ya wale ambao wameokoka 29

Umuhimu wa mkutano wa maombi wa kanisa kulingana na mafundisho


ya kitabu cha matendo ya mitume.
Katika sura za kwanza za kitabu cha Matendo ya Mitume, tunasoma
kuhusu mikutano ya maombi. Siku ya Pentekoste, tunasoma kwamba
wanafunzi wa Kristo Yesu walikuwa wakiomba kabla ya Roho
Mtakatifu kuja juu yao. Walikuwa wakiomba wakisubiri ahadi ya
Bwana Yesu Kristo kwao, yaanii Roho Mtakatifu. Je, ni wangapi leo
ambao wanaomba kwamba Mungu alete uvivio. Baada ya Pentekoste,
tunasoma kwamba kulitokea mateso makali sana kwa kanisa na mitume
walikatazwa kwamba wasihubiri tena katika jina la Kristo Yesu. Je,
katika hali hii, wao wangefanya nini? Jibu ni moja, wao walikutana na
kuomba kama kanisa. Walikutana na kumweleza Mungu juu yay ale
yote ambayo walikuwa wanapitia kama kanisa. Bwana aliwaongoza na
kuwahimiza katika mateso yao. Baada ya muda mfupi tena, Yakobo
alichinjwa. Petro naye alikamatwa na kuwekwa kwa jela. Je, wale
wanafunzi waliobaki walifanya nini? Wao walikusanyika na wakaomba.
Wao waliendelea kuomba kwa siku nane, hadi siku ile Petro alikuwa
auliwe. Mungu aliyajibhu maombi yao na akamtuma malaika ambaye
alimfungua nyororo Petro na kumwongoza nje ya jela.
Je, Petro alienda wapi wakati alipofunguliwa? Yeye alienda mahali
ambapo kanisa lilikuwa likiomba. Je, alijua aje kwamba walikuwa
huko? Ni kwa sababu yeye alijua maisha ya kanisa na kwa hivyo
alifahamu vyema kwamba walikuwa wakiomba, kwa sababu hii ilikuwa
tabia yao kila wakati. Wakati alipoingia, hata mitume walishangaa sana
kumwona kwa sababu kama sisi leo, waliomba lakini walikuwa na
shauku katika maombi yao.
Baadaye katika kitabu hiki cha matendo ya Mitume, tunasoma
kwamba kanisa lingine lilianzishwa katika mkutano wa maombi
(Matendo ya Mitume 16:13).

Uvivio na mabadiliko ambayo yanatokana na mikuna ya kanisa ya


maombi.
Katika maombi ya kanisa, ni lazima tuombe kwamba Mungu alete
uvuvio katika maisha yetu, katika kanisa letu, katika nchi yetu na
katika mataifa mengine ulimwenguni. Ndipo Mungu alete uvuvio,
Roho Mtakatifu atatupatia uwezo wa kuomba juu ya jambo hili
Mara kwa mara uvuvio hutokana na mikutano ya maombi ya
makanisa. Nikimalizia, ninakusihi ukitafute kitabu ambacho kinaitwa
nguvu za maombi (Power of Prayer) ambacho kimeandikwa na Samuel
30

Prime. Kitabu hiki kinafundisha jinsi kulikuwa na uvuvio mkubwa


ambao ulianza kwa mkutani mmoja wa maombi. Mkutano wa kila wiki
wa maombi ndio mahali pazuri sana pa kumwomba Mungu alete
uvuvio katika kazi yake na katika maisha ya watu wake na katika
kanisa. Biblia inasema, “Basi kwa Yeye awezaye kutenda mambo ya
ajabu yasiopimika kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo kwa kadiri ya
uweza wake ule utendao kazi ndani yetu” (Waefeso 3:20).

MCHUNGAJI AMBAYE HAOMBI


Andrew Murray (1828-1917)

Wachungaji wengi tuko na hatia ya kuwa watu ambao hatuombi. Hii ni


dhambi kubwa sana katika maisha ya mchungaji.
Je, kwa nini kukosa kuomba na mchungaji ni dhambi kubwa sana?
Kwanza ninajua kuna wengi ambao huwa wanasingizia kwa kusema
kwamba huu ni udhaifu tu. Kuna wengi pia ambao wanasema kwamba
hakuna wakati wa kuomba. Lakini hata kama tunavisababu hivi vyote,
ukweli ni kwamba kukosa kuomba na mchungaji ni dhambi kubwa sana
machoni pa Mungu.

Je, kwa nini hii ni dhambi kubwa sana?

Hii ni kwa sababu kukosa kuomba ni kinyume na mapenzi ya Mungu.


Mungu anakualika uje kwake ili uzungumze naye na umwombe vile
vitu ambavyo unavihitaji na upate baraka nyingi kutoka kwake, lakini
unakataa. Yeye anakuita ili uwe na ushirika naye lakini wewe bado
unakataa. Mungu ametuumba katika umbo lake na kutukomboa kwa
njia ya Mwanawe Yesu Kristo, ili katika kumwomba Yeye tuweze
kushiriki katika utukufu na wokovu wake.
Je, tunatumiaje hizi baraka zake kwetu? Wengi wanaomba kwa muda
mfupi na wansema kwamba wao hawana muda mwingi wa kuomba na
mioyo yao haina tamaa ya kuomba. Wao hawaelewi jinsi mtu anaweza
kumaliza hata nusu saa katika maombi. Shida si kwamba hawaombi,
bali wanapoomba kila siku wao hawana furaha ya kuomba. Wao
hawazungumzi na Mungu na kwa hivyo wanadhihirisha katika maisha
yao kwamba hawamtegemei Mungu kabisa.
Maombi ya wale ambao wameokoka 31

Wachungaji hawa, ikiwa rafiki yao anakuja kuwatembelea, wao


wanatenga muda mwingi hata kama inamaanisha kuacha kufanya
mambo fulani fulani ya muhimu katika maisha yao. Ukweli ni kwamba
wako na wakati wakufanya mambo ambayo wanayapenda sana lakini
hawana wakati kuwa na ushirika na Mungu na kumfurahia Mungu.
Wao wanapata muda wa kumalizana na viumbe lakini hawana muda wa
kumalizana na muumbaji wao.
Hii ni kutomheshimu Mungu na kumchukia Mungu ikiwa kweli
hatupati wakati wa kumaliza katika maombi tukiwa naye. Hii ni
dhambi ambayo tunapaswa kulia juu yake na kumlilia Mungu.

Hiki ndicho chanzo cha ugonjwa hatari wa kiroho.


Ni ukweli kwamba hata baada ya kuokoka, hali ya dhambi bado imo
ndani mwetu. Maombi ni uhai wa maisha, kupitia kwa maombi
tunaweza kujua hali ya moyo. Dhambi ya kutoomba ni ishara katika
maisha ya mkristo au ya mchungaji kwamba maisha ya Mungu katika
nafsi yamedhofika sana.
Mambo mengi yamesemwa juu ya udhaifu wa kanisa katika
kutekeleza majukumu yake, kushawishi washirika wake katika mema
na kuwakomboa kutoka katika nguvu za ulimwengu na vitu vyake na
kuwaleta katika maisha ya utakatifu ambayo inamletea Mungu
utukufu. Pia mengi yamesemwa juu ya ushawishi wa kanisa katika
maisha ya wale ambao hawajaokoka, ambao Kristo alilituma kwao
wakahubiri injili ya wokovu kwao. Je, ni kwa nini wengi wa wale ambao
wameokoka hawana ushawishi wowote katika maisha ya wale ambao
hawajaokoka? Jibu ni moja tu, wao si watu wa maombi. Kanisa
haliombi na wachungaji hawaombi iwapasavyo. Katika kazi zao zote
kwa Mungu, kanisa limepungukiwa na nguvu za Mungu kwa sababu
haliombi jinsi linapaswa kuomba. Ni dhambi ya kutoomba ambayo
imesababisha ukose wa nguvu za Mungu katika maisha ya kanisa.

Hatari kubwa sana ambayo kanisa limo kwa sababu ya dhambi ya


kukosa kuomba kwa mchungaji wake.
Ni kazi ya mchungaji kuhakikisha kwamba anawafundisha washirika
wake kuomba. Je, ikiwa yeye haombi, atawezaje kuwafundisha wengine?
Mchungaji hawezi kuelekeza kanisa zaidi ya jinsi yeye anavyofanya.
Hawezi kuwafundisha au kuwahubiria kwa hakika jambo ambalo yeye
mwenyewe hafanyi kwa sababu huo utakuwa unafiki.
32

Je, ni wakristo wangapi ambao wanafahamu vyema baraka ambazo


zinapatikana katika ushirika na Mungu kupitia kwa maombi? Kuna
wengi ambao wanapenda sana kuhimizwa katika jambo hili la maombi
lakini katika mahubiri ya mchungaji hawahimizwi kuvumilia na
kuendelea hadi wapokea baraka ya Mungu. Sababu ya hii ni kwamba
mchungaji mwenyewe hafahamu vyema inamaanisha nini kudumu
katika maombi kwa sababu yeye si mtu wa maombi na hajafahamu
baraka za Mungu ambazo zinaambatana kwa maombi. Ni ombi langu
kwamba wachungaji watafahamu hatari ya kutoomba na kwamba
watatubu dhambi hii na kuanza kuomba jinsi iwapasavyo.

Dhambi ya kutoomba husababisha ukosefu wa uwezo wa kuwafikia


wengi na ujumbe wa injili.
Hatutaweza kutekeleza majukumu yetu jinsi Kristo amesema ikiwa
tutaendelea katika dhambi hii ya kutoomba. Leo hitaji kubwa sana
katika huduma zetu, ni roho ya kuomba. Tunahitaji watu ambao
wanaomba na wanaomba iwapasavyo kwa Mungu, haswa kwamba wengi
wapate kuokoka. Wengi wamesema kwamba Mungu yuko tayari
kuwaokoa wengi leo ikiwa watu watamwomba na kumlilia kwa ajili ya
nafsi za waliopotea. Lakini swali ni je, hili litawezekanaje ikiwa tuna
wachungaji ambao hawaombi jinsi iwapasavyo. Ni lazima kwanza hawa
wachungaji watubu na wafanye jinsi Mungu amewaamuru, yaani
waombe jinsi wanapaswa kuomba kwa ajili yao na kanisa. Haitoshi tu
kuhubiri, au kuwatembelea wengi katika nyumba zao, au kufanya
zingine za kanisa, bali jambo la muhimu la kwanza katika maisha ya
mchungaji ni, ni kuwa na ushirika na Mungu kwa njia ya maombi ili
Mungu na kwa njia hii watapata nguvu za kufanya kazi yake.
Tunafaa kufahamu jambo hili la kutoomba kwamba ni dhambi
kubwa sana. Tuombe Mungu atusaidie na atuondoe katika dhambi hii.
Tuombe kwamba Mungu atatukomboa kutoka katika dhambi hii kwa
damu Kristo Yesu. Bwana nakuomba kwamba utatuondoa katika
dhambi ya kutoomba ili tuwe wachungaji ambao ni watu wa maombi
kabla tutekeleze lolote katika ufalme wako. Bwana tusaidie ili tupate
himizo, furaha, imani na uvumilivu mkubwa, tuwe watu wa kukuomba.
Tupe tamaa ya kuomba kila wakati.
Dhambi hii ya kutoomba ni mzigo mkubwa sana katika maisha ya
mchungaji na hatutapumzika hadi iondolewe kwa nguvu za Kristo
Yesu. Bwana tumwombe na atafanya na kutusamehe na kutupatia
nguvu za kuomba kila wakati.
Maombi ya wale ambao wameokoka 33

KUOMBA AU KUTOOMBA
J. C. Ryle (1816-1900)
“Nataka kila mahali wanaume wasali wakiinua mikono mitakatifu pasipo hasira
wala kugombana” (1 Timotheo 2:8).

Wacha nizungumze na wale wote ambao huwa hawaombi.


Ikiwa wewe huwa huombi, ninataka kuzungumza nawe sasa maneno
ya Mungu. Ninakuonya kwamba wewe uko katika hali ya hatari sana.
Ikiwa wewe utakufa sasa, nafsi yako itaelekea jahanum. Hata wakati
Kristo atarudi na kukufufua wewe, utafufuliwa ili uingie katika
jahanum milele. Ninakuonya kwamba wewe huna sababu yoyote ya
kusingizia ni kwa nini wewe huombi. Ninajua kwamba wewe
unavijisababu vingi sana ambavyo unavitoa kwa sababu ya ukosefu
wako wa kuomba. Ninakuambia kwamba vijisababu hivyo vyote ni
bure machoni pa Mungu.
Ninakuonya kwamba:
a). Haina maana yoyote ya kusema kwamba wewe hujui kuomba.
Kuomba ndilo jambo rahisi sana kufanya katika dini yoyote. Kuomba
ni kuzungumza na Mungu. Ili uombe, huhitaji kitabu cha kujifunza au
kuwa na hekima ya juu, unahitaji tu kuwa na moyo ambao unataka
kuomba. Mtoto mdogo ambaye anahisi njaa, yeye anahitaji tu kulia.
Maskini ambaye huomba-omba anahitaji tu kuweka mkono wake na
kuomba watu wamsaidie. Mtu yeyote anaweza kuzungumza na Mungu
ikiwa yeye ana akili.
b). Haina maana yoyote ya kusema kwamba huna mahali pazuri pa
kuombea.
Mtu yeyote anaweza kupata nafasi mahali popote na aombe. Bwana
Yesu Kristo aliomba akiwa mlimani, Petero aliomba akiwa juu ya
nyumba, Isaki aliomba akiwa shambani; Nathanieli aliomba akiwa
chini ya mti, Yona aliomba akiwa ndani ya samaki mkubwa. Mahali
popote ni mahali pazuri pa kumwomba Mungu.
c). Haina maana yoyote kusema kwamba huna wakati wa kuomba.
Kuna wakati mwingi sana wa kuomba ikiwa utatengwa wakati huo.
Wakati unaweza kuwa ni mfupi, lakini ukweli ni kwamba kila wakati
kuna wakati tosha wa kuomba. Danieli alikuwa na kazi nyingi ya
ufalme ya kufanya, lakini tusoma kwamba yeye aliomba mara tatu kila
34

siku. Daudi alikuwa mfalme wa Israeli, lakini tunasoma akisema,


“Jioni, asubuhi na adhuhuri ninalia kwa huzuni, naye husikia sauti
yangu” (Zaburi 55:17). Ikiwa kweli tunataka kuomba, wakati
utapatikana wa kuomba.
d). Haina maana yeyote kusema kwamba huwezi kuomba hadi wewe
uwe na Imani na moyo mpya.
Huwezi kusema kwamba wewe utakaa tu hadi wakati utapata imani
ndipo uweze kuomba. Ukifanya hivi, utakuwa unaongeza dhambi juu
ya dhambi. Ni jambo la hatari sana mtu akiwa hajaokoka, lakini ni
hatari sana kusema kwamba ninajua sijaokoka lakini sitaomba
msamaha wa dhambi zangu. Biblia inasema kwamba, “Mtafuteni
Bwana maadamu anapatikana; muiteni maadamu yu karibu” (Isaya
55:6); “Chukueni maneno pamoja nanyi, na mumrudie Bwana.
Mwambieni: Samehe dhambi zetu zote na utupokee kwa neema, ili
tuweze kutoa matunda yetu kama sadaka za mafahali” (Hosea 14:2);
“Kwa hiyo tubia huo uovu wako na umwombe Mungu, ili yamkini,
aweze kusamehe mawazo uliyo nayo moyoni mwako” (Matendo 8:22).
Ikiwa kweli unataka imani na moyo mpya, basi unapaswa kumwomba
Mungu akupatie haya mambo mawili.
Wewe ambaye huombi, je, kwa nini humwombi Mungu chochote? Je,
wewe uko tayari kuingia jahanum? Je, wewe huombi kwa sababu huna
dhambi za kusamehewa? Je, huogopi jahanum? Je, hutamani mbinguni?
Ninakusihi kwamba uanze kumwomba Mungu kwa sababu kuna siku
ambapo utatamani kuomba lakini litakuwa jambo gumu sana kwako.
Wengi siku moja wataomba, “Bwana, Bwana! Tufungulie mlango”
(Mathayo 25:11) lakini watakuwa wamechelewa sana. Wengi watalilia
milima iwangukie na vilima viwafunike kwa sababu wao walikataa
kuomba Mungu. Kwa hivyo ninakuonya kwamba huu usije ukawa ndio
mwisho wa nafsi yako. Wokovu uko karibu sana na usije ukakosa
mbinguni kwa sababu ulikataa kuomba.

Wacha nizungumze sasa na wale ambao wao huomba.


Kuna wale ambao wao wanajua umuhimu wa kuomba na wao
huomba kwa sababu wao ni wana wa Mungu. Kwa hawa wote, niko na
maneno ya kuwahimiza kama ndugu zangu. Mara nyingi ninajua
kwamba maombi yetu huwa ni madhaifu sana. Biblia inasema, “Hivyo
ninaona sharia ikitenda kazi. Ninapotaka kutenda jema, jambo baya
liko papo hapo” (Warumi 7:21). Wewe unafahamu vyema maneno ya
Daudi, “Ninachukia watu wa nia mbili, lakini ninapenda sheria yako”
Maombi ya wale ambao wameokoka 35

(Zaburi 119:113). Kila wakati unapoomba kwamba Mungu akuokoe


kutoka kwa maadui wako, pia unamwomba kwamba akuokoe kutoka
kwa hali yako ya dhambi ya kale. Kuna wakristo wachache sana ambao
huwa hawahuzuniki katika maombi yao. Shetani huwa anakasirika sana
wakati anatuona tukiomba. Ikiwa maombi yetu hayatugharimu, basi
huwa hatujayadhamini hata kidogo. Mara kwa mara utaona kwamba
yale maombi ambayo huwa tunayaona kwamba si kitu, hayo ndio huwa
yanamfurahisha Mungu.

Maneno machache ya kukuhimiza.


a). Ninataka kukuhimiza juu ya umuhimu wa heshima na
unyenyekevu kwa Mungu katika maombi.
Tukumbuke kila wakati kwamba sisi ni wanadamu na kwamba
tunapaswa kumheshimu Mungu wakati tunakuja kuzungumza naye
katika maombi. Tuhakikishe kwamba hatuji kwa Mungu kwa njia ya
haraka-haraka na kutojali. Tunapaswa kujua kwamba kila neno ambalo
tunalizungumza lazima liwe ni la kweli. Tukumbuke maneno ya
Suleimani: “Usiwe mwepesi kuzungumza, usiwe na haraka katika moyo
wako kuzungumza lolote mbele za Mungu. Mungu yuko mbinguni
nawe uko duniani, kwa hiyo maneno yako yawe machache” (Mhubiri
5:2). Wakati Abrahamu alizungumza na Mungu alisema, “Kwa kuwa
nimekuwa na ujasiri wa kuzungumza na Bwana, ingawa mimi si kitu
bali ni mavumbi na majivu” (Mwanzo 18:27; Ayubu 40:4). Hata sisi
tuwe kama hawa.
b). Ninataka kukuhimiza juu ya umuhimu wa Kuomba ukiongozwa
na Roho Mtakatifu.
Kile ninamaanisha hapa ni kwamba, tunafaa kuhakikisha kwamba
Roho Mtakatifu anatauongoza katika maombi yetu na wala
hatuongozwi na mambo mengine. Tuhakikishe kwamba tusije
tukaanguka katika dhambi ya kutamka tu maneno ambayo
hatuyamanishi. Ni rahisi kutumia maneno mazuri sana na hata
kunukuu maandiko lakini tuwe kweli hatuombi Mungu, kwa sababu
maneno hayo hayatoki mioyoni mwetu. Ninajua kwamba kuna mambo
ambayo kila siku tunayahitaji, na kuna njia ambayo tunaweza
kuyaomba mambo haya lakini jinsi tunavyoyaomba, iwe si kwa njia ya
kweli na hatuongozwi na Roho Mtakatifu. Ulimwengu, shetani na
mioyo yetu ni vitu vidanganyifu sana. Kwa hivyo tuhakikishe kwamba
maombi yetu si maneno mazuri matupu, bali kwamba tunaongozwa na
Roho Mtakatifu.
36

c). Ninataka kukuhimiza kwamba hakikisha maombi ni jambo la


maisha yako ya kila siku.
Tukumbuke kwamba Mungu wetu ni Mungu wa mipangilio. Masaa
ya asubuhi na jioni ya kuomba katika hekalu huko Yerusalemu,
yaliwekwa kwa mpangilio ambao Mungu alidhibitisha. Kukosa
mpangilio katika maisha ya mtu, ni tunda la dhambi. Ni jambo la
muhimu sana kuhakikisha kwamba unatenga muda kila siku katika
maisha yako kuomba. Kama tu vile unavyoweka muda wa kula, kulala,
na kufanya mambo mengine, hakikisha pia unaweka muda wa kuomba.
Wewe mwenyewe chagua muda ambao unajua ni mzuri kwako na
kwamba wakati huo hutasumbuliwa na mtu. Omba asubuhi kabla
hujaanza kufanya lolote na omba usiku baada ya kumaliza shughuli
zako zote. Katika haya yoyote kumbuka kwamba maombi ni jambo la
muhimu kufanywa kila siku. Hakikisha kwamba unaomba.
d). Ninataka kukuhimiza umuhimu wa kuvumilia katika maombi.
Kumbuka kwamba usiwahi acha tabia ya kuomba. Kuna wakati
ambapo moyo wako utakuambia kwamba, “nimeomba na familia
pamoja, je hakuna haja ya kuomba pekee yangu.” Wakati mwingine,
mwili wako utakuambia, “wewe umechoka sana na unafaa kupumzika.”
Pia mawazo yako, yatakuambia, “Una mambo mengi muhimu ya
kushughulika nayo, fupisha maombi yako.” Kumbuka kwamba haya
mambo yote yanatoka kwa shetani. Kile shetani anataka kutoka kwao,
ni uache kuomba kabisa. Ni ukweli kwamba mara kwa mara hatuombi
kwa muda sawa, lakini tuhakikishe kwamba huachi tabia ya kuomba.
Biblia inasema, “Dumuni katika maombi…ombeni pasipo kukoma”
(Wakolosai 4:2; 1 Wathesalonike 5:17). Hii haimanisha sasa kwamba
tunafaa kila wakati kuwa tunapiga magoti na kuomba kama jinsi wengi
wanafanya. Ikiwa tutafanya hivyo, basi ni wazi kwamba hatutawezi
kutekeleza majukumu mengine kama kufanya kazi ili tule na mambo
mengine ambayo pia Mungu ametuamuru tuyafanya. Kile Biblia
inamaanisha ni kwamba hatufai kuacha tabia ya kuomba kila wakati na
kila siku. Mioyo yetu inafaa kuwa mioyo ambayo kila wakati iko katika
hali ya mazungumzo na Mungu na kuwa na tamaa ya wakati ambapo
tunakuwa na Mungu pekee katika maombi. Pia hata wakati tunafanya
kazi, tunaweza kuwa tunaomba katika mioyo yetu. Usiwahi kuwaza
kwamba kuomba ni kumaliza muda wako bure. Hakuna hasara katika
kuvumilia katika maombi. Bali ni faida na baraka tele ambazo
zinapatikana katika jambo hili.
e). Ninataka kukuhimiza uwe mtu wa kuomba kutoka kwa moyo
wako.
Maombi ya wale ambao wameokoka 37

Kwa sababu mtu anaomba kwa sauti kubwa, hiyo haimanisha


kwamba kweli yeye anaomba kutoka kwa moyo. Ni vyema kama
tutaomba kwa moyo ambao ni mnnyenyekevu tukijua kwamba kile
ambacho tunakiomba tutakipata kweli. Biblia inasema kwamba
maombi ya mwenye haki yanafaa sana na wala si maombi ya yule
ambaye anapiga kelele sana. Biblia inafundisha kwamba maombi ni
kulia, ni kutafuta, ni kufanya kazi, kubisha na kujitahidi. Yakobo
alimwambia malaika, “Sitakuacha usende usiponibariki” (Mwanzo
32:26). “Ee bwana, sikiliza! Ee Bwana, samehe! Ee Bwana, sikia na
ukatende! (Danieli 9:19). Biblia inafundisha kwamba Bwana Yesu
Kristo, “alimtolea maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi,
yeye awezaye kumwokoa na mauti, naye Mungu akamsikia kwa sababu
ya kutii kwake kwa unyenyekevu” (Waebrania 5:7). Unaposoma
maombi haya yote, utapata kwamba, wengi leo wanaomba kinyume
kabisa. Wengi wanaomba wakipiga kelele sana na wengine ni vugu-
vugu katika maombi yao. Kulingana na jinsi wengi wanavyoomba, ni
ukweli kwamba wao hawataki kile ambacho wanachokiomba. Kwa
hivyo tuhakikishe kwamba maombi yetu tuyaomba kwa unyenyekevu
na kwa bidii tukijua kwamba kile ambacho tunachokiomba kweli
tutakipata. Tuombe bila kukoma. Pia tuombe tukijua kwamba ikiwa
yale ambayo tunayaombea hayatafanyika, basi maisha yetu yako
hatarini. Tufahamu kwamba maombi yetu ambayo ni vugu-vugu ni
kama sadaka bila moto mbele za Mungu.
f). Ninataka kukuhimiza kwamba unapaswa kuomba kwa Imani.
Tunafaa kuamini kwamba maombi yetu huwa Mungu anayasikia
ikiwa tutaomba kulingana na mapenzi yake na kwamba Yeye atatupatia
kile ambacho tumwomba Yeye. Hii ndio amri ambayo Kristo Yesu
alipeana: “Yoyote myaombayo mkisali, amini ya kwamba mmeyapokea
nayo yatakuwa yenu” (Marko 11:24). Kuomba bila imani, ni maombi
bure na hayafaulu katika lolote. Tujifundishe kuomba kulingana na
ahadi za Mungu katika maombi yetu. Tunafaa kuomba kama Samweli:
“Basi sasa Mungu ukaitimize ahadi uliyosema kuhusu mtumishi wako
na nyumba yake milele” (2 Samweli 7:25). Hivi ndivyo Yakobo, Musa
na Daudi walivyoomba. Ukisoma Zaburi 119, utaona jinsi Daudi
alivyoomba akinukuu ahadi za Mungu. Pia tujifundishe kutarajia jibu
kwa maombi yetu.
Tusitosheke hadi tumeona kwamba maombi yetu yamejibiwa.
Tukumbuke kwamba kanisa la Yerusalemu lilimwombea sana Petro
alipokuwa gerezani na wakati maombi yao yalijibiwa, wao walishangaa
38

sana (Matendo 12:15). Ni hatari sana kuomba bila kutarajia, kwa


sababu ukweli ni kwamba hutapata lolote.
g). Ninataka kukuhimiza kwamba lazima uwe na ujasiri katika
maombi yako.
Kuna wengi ambao huomba kwa bidii na uajasiri lakini ujasiri wao
hautokani na utakatifu. Ukweli ni kwamba kuna ujasiri ambao
unatokana na utakatifu, na huu ndio kila mtu anapaswa kuwa nao
wakati anaomba. Ninazungumza juu ya ujasiri kama ule wa Musa
wakati alipowaombea Waisraeli walipoanguka katika dhambi ya
kuabudu sanamu. Yeye aliomba na kusema, “Kwa nini wamisri waseme,
Ni kwa nia mbaya aliwatoa Misri, ili awaue milimani na kuwafuta usoni
mwa dunia” (Kutoka 32:12). Ujasiri kama ule wa Yoshua wakati
Waisreali waliposhindwa kule Ai: “Wakanani na watu wengine wa nchi
watasikia habari hii, nao watatuzunguka na kutufutilia jina letu
duniani. Utafanya nini basi kwa ajili ya jina lako mwenywe lililo kuu”
(Yoshua 7:9). Ujasiri kama wa Luther. Wale waliomsikia akiomba,
walisema, yeye alikuwa na ujasiri wa juu sana. Yeye aliomba Mungu
kwa unyenyekevu lakini wakati huo huo na tumaini na hakika kwa yale
alikuwa akiombea. Mara kwa mara, sisi huwa hatuombi hivi kwa
sababu huwa hatufahamu kabisa baraka ambazo sisi ambao tumeokoka
tuko nazo. Huwa hatuombi jinsi itupasavyo.
h). Ninataka kukuhimiza kwamba unapaswa kuleta haja zako zote
mbele ya Mungu.
Bwana Yesu Kristo alituonya juu ya kuwa kama Mafarisayo ambao
waliomba maombi marefu sana. Wao walikuwa wanafiki. Yeye
anatuonya kwamba tusiwe watu wa kurudia-rudia maombi. Biblia
inatuambia kwamba Yesu Kristo mwenyewe aliomba kwa Mungu Baba
kwa muda mrefu sana. Hii inatuonyesha umuhimu wa kuwa na muda
wa kutosha katika maombi. Hatufai kuomba tu maneno machache
machache na kuondoka. Tunapaswa kuwa na muda, lakini tuhakikishe
kwamba tusimalize tu muda kwa kurudia-rudia tu maneno fulani
fulani. Ikiwa hatumalizi muda katika maombi kwa kuleta mahitaji yetu
yote kwa Mungu, basi ni wazi kwamba tuko na machache tu ambayo
tunataka Mungu atufanyie. Kuna wengi leo ambao wanalalamika
kwamba wao hawasikilizani na wengine au kwamba wao wako na neema
kidogo. Haya malalamishi yao ni kwa sababu ya wao kutoomba jinsi
inawapasa. Wale ambao wanaomba mengi, Mungu huwapa mengi. Wale
wanaomba machache, Mungu huwapa machache. Yakobo anasema
kwamba, hamna kwa sababu hamwombi. Msomaji wangu, shida
ambayo uko nayo ni yako mwenyewe. Kristo anataka kukupatia mengi
Maombi ya wale ambao wameokoka 39

lakini wewe unaomba machache. Bwana Yesu anasema, “Kisha


akasema, Chukua mishale, naye mfalme akaichukua. Elisha
akamwambia, piga ardhi kwa hiyo mishale. Akapiga mara tatu, halafu
akaacha. Mtu wa Mungu akamkasirikia na kusema, ungepiga chini
mara tano au sita, ndipo ungeishinda Aramu na kuiangamiza kabisa.
Lakini sasa utaishinda mara tatu tu” (2 Wafalme 13:18-19).
i). Ninataka kukumihiza kwamba unafaa kutaja yale ambayo unataka
Mungu akufanyie katika maombi yako.
Hatufai tu kutosheka na kusema maneno mengi tu, lakini pia tunafaa
kuhakikisha kwamba tunayataja mahitaji yetu mbele za Mungu. Ni
vyema kukiri na kutubu dhambi zetu, lakini ni vyema pia kutaja
dhambi hizo ambazo tumezitenda na tunajua kwamba tuko na hatia
mbele za Mungu. Ni vyema kuomba Mungu ataongoze katika utakatifu,
lakini pia ni vyema zaidi kutaja hali ambazo katika maisha yetu
tunaona kwamba tunapungukiwa na neema. Pia haitoshi kumwambia
Mungu kwamba tuko katika hali hatari, bali pia tunafaa kutaja hatari
ambayo tuko ndani mwake. Hivi ndivyo Yakobo aliomba alipokuwa
anaenda kukutana na ndugu yake Esau. Alimwambia Mungu kile
ambacho haswa alikuwa anakiogopa (Mwanzo 32:11). Hivi ndivyo
Eliyaza alifanya wakati alitumwa na Abrahamu kumtafutia Isaka mke
(Mwanzo 24:12). Hivi ndivyo Paulo alifanya wakati alikuwa na mwiba
katika maisha yake (Wakorintho 12:8). Hii ndio imani ya kweli na
ujasiri katika yale ambayo tunayaomba mbele za Mungu. Hakuna kitu
kidogo ambacho hatufai kutaja mbele za Mungu. Tunapaswa
kukumbuka kwamba Kristo ndiye tabibu mkuu na Baba wa watu wake
wote. Tuonyeshe jambo hili kwa njia ya kumweleza kila kitu, kikubwa
na hata kile kidogo. Tusifiche siri yoyote kutoka kwake, bali tumweleze
yale yote yaliomo katika mioyo yetu.
j). Ninataka kukuhimiza juu ya umuhimu wa kuwaombea wengine.
Kawaida sisi sote ni wachoyo na hata baada ya kuokoka, tusipokuwa
waangalifu, choyo hii hubaki nasi. Kuna tabia katika maisha yetu,
kuwaza juu maisha yetu pekee na wala si ya wengine. Kwa sababu ya
hii, tunafaa sisi sote kuwa waangalifu sana kwa kuomba. Tumwombe
Mungu atupatie moyo wa kuwapenda wengine na kuwaza juu yao.
Tunafaa kujifundisha pia kuwaombea wengine katika maombi yetu.
Tunafaa kuwaombea wale wote ambao hawajaokoka, na wale ambao
wameokoka. Tunafaa kuwaombea washirika wenzetu katika kanisa,
nchi yetu, viongozi wetu na nyumbani mwetu na marafiki zetu.
Kufanya hivi ni kuonyesha ukarimu mkubwa sana katika maisha ya
wengine. Tunaonyesha upendo wetu kwa wengine ikiwa tutawaombea
40

wakati tunaomba. Jambo hili hutufanya tukue katika huruma na mioyo


yetu inajawa na upendo kwa wengine kila wakati. Ikiwa tutawaombea
wengine katika kanisa, kanisa litafaidika sana. Jambo ambalo linasaidia
sana katika kueneza injili ya Kristo, ni kwamba tunaomba kwa ajili ya
kazi hii. Bila maombi hatuwezi kamwe kuifanya. Kuombeana ni kuwa
katika Kristo Yesu ambaye kila wakati Yeye huwaombea watu wake
akiwa Kuhani Mkuu mbele za Mungu Baba. Kuombea wengine, ni
kuwa wa msaada mkubwa sana kwa watumishi wa Kristo. Wale ambao
wanaomba na kuombeana, hilo ndilo kanisa bora.
k). Ninataka kukuhimiza juu ya kuwa wenye kushukuru katika
maombi yako.
Ni jambo moja kuleta mahitaji yako mbele za Mungu na pia ni
jingine kuwa mtu mwenye kushukuru Mungu. Unaposoma Biblia,
utapata kwamba, kuombea mahitaji na kushukuru ni mambo mawili
ambayo huwa yanaambata katika maombi. Kwa hivyo ombi ambalo
halina shukurani, hilo si ombi kwa Mungu. Biblia inasema,
“Msijusumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na
kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu”
(Wafilipi 4:6). Ni kwa neema ya Mungu kwamba hatuko jahanum. Ni
kwa huruma ya Mungu kwamba tuko na tumaini la kuingia mbinguni.
Ni kwa neema ya Mungu kwamba tunaishi katika nchi ambamo
tunakubalika kuhubiri injili bila kutatizwa. Ni kwa neema ya Mungu
kwamba Roho Mtakatifu anatuongoza leo ili tufanye mapenzi ya
Mungu. Ni kwa neema ya Mungu kwamba tunaishi leo na kwamba tuko
na fursa za kuendelea kumletea Mungu utukufu kwa matendo yetu kwa
wengine na katika maisha yetu. Mambo haya yanapaswa kuwa katika
mioyo yetu wakati tunaomba. Kweli hatufai kukosa kumsifu na
kumshukuru Mungu kwa yale ambayo ametufanyia. Tumshukuru kwa
ajili ya neema ambayo ametupatia na ni ya milele. Wale watakatifu
wote ambao wameishi siku zote, wamekuwa watu wa shukurani kwa
Mungu. Katika nyaraka zote za Paulo, yeye hakosi kumshukuru
Mungu.
Ni lazima tuwe na moyo wa kushukuru Mungu katika kila jambo.
Wacha maombi yetu yawe ni maombi ya kushukuru.
l). Ninataka kukuhimiza kwamba unafaa kuwa mwangalifu sana juu
yay ale ambayo unayaomba.
Ni kupitia kwa maombi tunaanza ukristo wa kweli na ni kupitia kwa
maombi tunaendelea katika ukristo wa kweli. Ukristo wa kweli
unadhihirika kupitia kwa jinsi mtu anavyoomba. Kupitia kwa maombi,
tunajua jinsi tunavyoenedelea kiroho. Kwa hivyo ni lazima kila wakati
Maombi ya wale ambao wameokoka 41

tuwe waangalifu jinsi tunavyoomba. Hapa ndipo ukristo unadhihirika


katika maisha ya mtu. Mahubiri mazuri, vitabu, vijitabu vya kikristo,
marafiki ambao wameokoka, mikutano ya mafundisho ya Biblia, haya
yote ni mambo mazuri, lakini haiwezi kuchukua nafasi ya maombi.
Hakikisha kwamba hakuna kitu ambacho kinakuzuia ili ukose kuomba.
Jichunge sana kwamba usije ukapuuza jambo la kuomba. Ikiwa
hutapuuza maombi, nafsi yako intakuwa katika hali mzuri kiroho.
Nimetaja mambo haya yote kwa unyenyekevu sana kwa ajili
kujichunguza. Ninajua kwamba mimi ndiye mmoja ambaye ninapaswa
kukumbuka mambo haya sana. Lakini pia ninaamini kwamba huu ni
ukweli kutoka kwa Mungu na ni ombi langu kwamba tutasaidika wote.
Ninaomba kwamba siku ambazo tunaishi, zitakuwa siku za maombi.
Ninaomba kwamba wakristo wa sasa wawe wakristo wa kuomba.
Ninaomba kwamba kanisa letu la sasa liwe kanisa la kuomba. Nia
yangu ya maandishi haya ni kwamba niwasaidie wengi kuwa na moyo
wa kuomba katika maisha yao ya ukristo. Ninaomba kwamba wale
ambao hawajawahi kuomba, waanze kwa kuliita jina la Mungu;
ninaomba kwamba wale ambao wanaomba, waendelee kukua katika
maombi kila mwaka na kwamba wa hakikishe kwamba hawaombi bure.

KUDUMU KATIKA MAOMBI


Charles H. Spurgeon (1834-1892)

Katika kitabu cha Mwanzo tunasoma kwamba, na watu wakaanza


kuliitia Jina la Mungu (Mwanzo 4:26). Katika kitabu cha Ufunuo
tunasoma neno hili “Amen” (Ufunuo 22:21). Tuna mifano mingi katika
Biblia kuhusu watu wakiomba. Kwa mfano tunasoma kuhusu Yakobo
ambaye hakumwachilia malaika, hadi alipombariki, Danieli ambaye
aliomba mara tatu kwa siku, Daudi ambaye kwa moyo wake wote
alimwomba Mungu. Pia tunasoma kuhusu Paulo na Sila wakiwa
gerezani wakiomba. Kuna amri nyingi na ahadi nyingi ambazo
zinaambatana na maombi. Je, hizi zinatufundisha nini kuhusu
umuhimu wa maombi?
Chochote Mungu amesema katika neno lake, kinahusu maisha yetu.
Mungu amesema mengi katika neno lake kuhusu maombi. Hii
inamaanisha kwamba Yeye anajua kwamba tunahitaji mengi. Kwa
42

sababu hii hatufai kupuuza maombi. Je, wewe unawaza kwamba


huhitaji chochote? Ukweli ni kwamba ikiwa unawaza hivi, basi wewe
hujui kwamba wewe ni maskini wa kiroho sana. Je, wewe kwa nini
usimwombe Mungu akuhurumie? Ukweli ni kwamba ikiwa humwombi
Mungu akuhurumie, basi ni wazi kwamba wewe hujatambua huruma za
Mungu katika maisha yako. Nafsi ambayo haiombi, ni nafsi ambayo
Kristo hayumo ndani mwake. Maombi ndio maneno ya moyo ambao
unamwamini Mungu, kelele ya mkristo ambaye anaendelea kupigana
na dhambi na wimbo wa mkristo ambaye anakufa akiwa katika Kristo
Yesu. Maombi ni, pumzi, neno la kutulinda, faraja, nguvu na heshima
ya mkristo.
Ikiwa wewe ni mtoto wa Mungu, wewe utakuwa unaomba Mungu na
utaishi katika upendo wa Baba wako, ambaye ni Mungu.Omba kwamba
mwaka huu wewe utakua katika utakatifu, unyenyekevu, tamaa juu ya
vitu vya Mungu na utakua katika uvumilivu ndani ya Kristo. Hakikisha
kwamba kila siku unaishi maisha yako karibu sana na Kristo na
kwamba kila wakati unadumu katika upendo wake. Omba Mungu
kwamba atakusaidia uwe wa Baraka katika maisha ya wengine na
kwamba maisha yako utayaishi kwa utukufu wa Mungu pekee. Ombi
lako mwaka huu linafaa kuwa, “Kudumu katika maombi” (Wakolosai
4:2).

MAOMBI YA WALE AMBAO


WAMEOKOKA
Octavius Winslow (1808-1878)
“ Alipokwisha kukitwaa kile kitabu, wale viumbe wenye uhai wane pamoja na
wale wazee ishirini na wane wakaanguka mbele ya yule Mwana-Kondoo. Kila
mmoja wao alikuwa na kinubi, nao walikuwa wameshika mabakuli ya dhahabu
yaliyojaa uvumba, ambayo ni maombi ya watakatifu” (Ufunuo 5:8).

Wale ambao wameokoka ni watu ambao wanaomba, ni ishara katika


maisha yao kwamba wamemwamini Kristo. Wale ambao hawajaokoka,
huwa hawaombi kwa sababu wao wamekufa kiroho. Maombi ni ishara
kwamba Roho Mtakatifu anaisha ndani mwa mtu, kwa sababu ni Yeye
ambaye anamwezesha mtu huyu kuomba. Maombi ni maisha ya Kiroho
Maombi ya wale ambao wameokoka 43

ya wale ambao wameokoka.


Mtu anaweza kuwa haonekani kufanya mambo mengi ya huduma,
awe hajui mengi katika ukristo lakini ukweli ni kwamba ikiwa yeye
ameokoka, yeye atakuwa mtu wa maombi. Yeye huzungumza na Mungu
kwa sababu yeye ana maisha ya Mungu ndani mwake na maisha haya ni
ya milele. Ndani mwake kuna maisha ya kiroho ambayo inaendelea
kukua. Hata katika majaribu mengi na huzuni nyingi, yeye ni mtu
ambaye anaomba. Maombi ni jambo zuri ambalo Mungu anatuwezesha
kufanya kama watu.
Katika mstari ambao ni kichwa cha sura hii, tunasoma kuhusu
maombi ya wale ambao walikuwa wameokoka. Wao walikuwa
wamekombolewa na damu ya Kristo Yesu. Wao walikuwa miongoni
mwa wale ambao walijumwishwa kwenye kanisa lote la Kristo. Maono
haya ya Yohana yamekusdiwa kutufundisha kwamba kanisa la Kristo,
ni kanisa ambalo linaomba na kwamba maombi ya watu wa Mungu
humfikia Mungu kama uvumba mzuri. Maombi yao yanamfikia Mungu
kupitia kwa kazi ya Kristo Yesu.

Je, haya maombi ni ya kina nani?


a). Biblia inasema kwamba, haya maombi ni ya watakatifu.
Watakatifu ni kina nani? Hawa si watakatifu ambao wako mbinguni
kwa sababu wale ambao wako mbinguni tayari hawaombi. Wao
walipokuwa hapa ulimwenguni waliomba, na sasa wako mbinguni, na
kwa hivyo huko hawaombi. Sasa wao wako katika utukufu kamili. Sasa
wao wako mbinguni wakimsifu Mungu. Hapa ulimwenguni, tunaomba
Mungu na kumtumainia katika kila jambo kwa sababu bado hatujafika
katika utukufu kamili huko mbinguni.
Ukweli ni kwamba huko mbinguni hakuna kuomba. Biblia
inatuelezea kwamba Kuhani wetu mkuu ambaye ni Kristo Yeye
anaomba huko mbinguni. Kristo Yesu pekee ndiye mwombaji huko
mbinguni. Biblia inasema kwamba Yesu, “hakuingia kwa njia ya damu
ya mbuzi na ya ndama, lakini alingia Patakatifu pa Patakatifu mara
moja tu kwa damu yake mwenyewe, akiisha kupata ukombozi wa
milele” (Waebrania 9:12) na “kwa hivyo anaweza kuwaokoa kabisa wale
wanaomjia Mungu kupitia kwake, kwa sababu Yeye adumu daima
kuomba kwa ajili yao” (Waebrania 7:25). Bwana Yesu Kristo ndiye
mpatanishaji ambaye Mungu anayemsikia pekee huko mbinguni. Yesu
ndiye mwombezi wetu huko mbinguni, si malaika au watakatifu
44

walioko mbinguni. Maombi ya Kristo, Mungu atayasikia na kuyajibu


kila wakati.
Kristo huombea kanisa lake na kanisa lake huomba katika jina lake,
kwa sababu hakuna jina lingine ambalo limepatiwa kanisa kuomba
kwalo. Hii ni baraka kubwa sana kwa kanisa kwamba Kristo
anatuombea na kupitia Yeye Mungu anakubali maombi yetu. Hakuna
jambo la faraja kwa kanisa kama kufahamu kwamba Kristo anatuombea
kila siku na kwamba maombi yake yanakubalika na Mungu wakati
wowote.
b). Wale ambao wameokoka, ndio watu ambao wanaomba kwa kweli.
Kwa wale ambao wameokoka, maombi ni jambo la muhimu sana kwao.
Wao wanamaliza muda wao mwingi katika maombi na wao
wanafuarahia kuomba na pia wanabarikiwa wanapoomba. Maombi
huwaleta pamoja kama watu wa Mungu.
Ni Baraka kubwa sana kwa wale ambao tumeokoka kwa sababu sisi
ndio Mungu anatuita watakatifu wake. Ni baraka kubwa sana kwa
sababu hata kama tumezaliwa tukiwa wenye dhambi na kupungukiwa
na utukufu wa Mungu, kwa neema Mungu ametuinua katika Kristo.
Kwa sababu ya wokovu ambao Kristo alitununulia, wale wote ambao
wamemwaini Kristo wao wamependwa sana na Mungu kuliko viumbe
vyote ambavyo ameviumba, hata malaika. Kuvishwa haki ya Mungu
(Warumi 3:21-22), ni kupewa nafasi ya heshima na utukufu mkubwa
sana ambao hakuna kiumbe kitafikia, isipokuwa Mungu mwenyewe.
Tumebarikiwa sana sisi ambao tuna ushirika na Mungu na tuko karibu
sana Naye, Yeye mwenye utukufu wote, heshima yote na Yeye ambaye
ni wa milele.
c). Je, Uvumba ni nini? “..maombi ya watakatifu.”
Maombi ni jambo takatifu. Daudi anasema kwamba, “Maombi yangu
na yafike mbele zako kama uvumba; kuinua mikono yangu juu na kuwe
kama dhabihu ya jioni” (Zaburi 142:2).
Tumeona ukweli kwamba watakatifu wa Mungu ni watu ambao
wanaomba, na kwamba kuzungumza na Mungu wa Utatu ni jambo
ambalo kila mkristo anapaswa kufanya. Hakuna mtakatifu ambaye
haombi, na wakatifu wote wa Mungu ni watu wa maombi. Wao
wanaombea katika sehemu tofauti tofauti na kuomba kwa njia tofauti
tofauti, lakini wao ni watu wa maombi. Wao wanaomba katika jengo
ambamo kanisa hukutana, majumbani mwao na popote pale wapatapo
nafasi ya kuomba, wao huomba. Watakatifu wa Mungu huja kwa
Mungu katika jina la Yesu na kuwa na ushirika na Mungu ambaye
Maombi ya wale ambao wameokoka 45

haonekani kwa macho ya kiasili. Maombi situ jambo muhimu katika


maisha ya wale ambao wameokoka, bali maisha yake yote mkristo ni ya
maombi.
Msomaji wangu, ikiwa wewe umeokoka, unahitaji kuwa mtu wa
maombi. Maombi ni njia ambayo inatambua utawala wa Mungu katika
kila jambo, upendo wake kwetu, jinsi anavyotujali yeye, na jinsi
anavyotuongoza katika maisha yetu ya kila siku. Ni kutambua kwamba
Mungu ni Baba wetu na ni rafiki wetu wa dhati. Mkristo anapaswa
kuomba kwa sababu kila siku yeye anapitia mambo mengi sana
magumu. Yeye hupigana na dhambi katika maisha yake, yeye huona
kila wakati jinsi amepungukiwa na utukufu wa Mungu, dunia kila
wakati inamjaribu kumnasa katika dhambi na tamaa zake,; Yeye pia
kila wakati anahuzunika na kuhuzunishwa na wakati mwingine
anashushwa moyo. Haya yote hawezi kuyadhibiti bila kuwa mtu wa
maombi. Ni kupitia kwa maombi, Mungu atampa nguvu, faraja,
tumaini na uwezo wa kukumbana, kuvumilia na nguvu za kushinda
mambo haya yote.

You might also like