You are on page 1of 5

IMANI POTOFU

UTANGULIZI

Imani potofu ni swala la kimtazamo zaidi (subjective issue), ni vigumu kuonyesha


au kuthibitisha kuwa imani fulani ni imani potofu. Hii ni kwa sababu kila imani
huwa na msingi wake na zingine huamini katika vitabu (misahafu) ya aina tofauti.
Hata imani za kikristo nazo hutofautiana. Jambo zote msingi wake ni katika kufa
na kufufuka kwa Kristo. Kwa maana hiyo basi ngumu sana kuainisha kuwa imani
fulani ni imani potofu kwa sababu upotofu wa imani hupimwa kwa kuipima imani
kwenye maandiko na pia kuipima imani kwenye mafundisho ya misingi
yaliyowekwa na waasisi wa imani.

MAANA YA IMANI POTOFU

Imani potofu ni imani inayojihusisha na kuabudu chochote kisichokuwa Mungu,


Pia imani potofu ni imani inayoshindwa kuongoza watu kuwa waadilifu na kutenda
haki kwa utukufu wa Mungu. Yakobo 1:27 tunasoma hivi:

Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda
kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia
pasipo mawaa.

Iwapo imani ya mtu hamfanyi kuwaonea huruma wajane na yatima, haimwongozi


katika machafu ya dunia basi ni dhahiri kuwa imani hiyo ni potofu. Mtu akisema
anamwamini Mungu basi tunarajia kuona kumwona kuwa ni mtu anawajali yatima
na wajane katika dhiki yao, lakini atakuwa ni mtu wa kujiepusha na uovu
(dhambi).

DALILI AU VIASHIRIA VYA IMANI POTOFU

Katika ukristo ziko imani nyingi sana zilizo potofu. Zipo imani nyingine ndani
ukristo hudaiwa kuwa ni potofu ni kwa sababu hazifuati misingi ya imani fulani.
1
Kuna dalili/viashiria vingi sana vya imani potofu katika makala hii nitataja
viashiria vya jumla.

a. Imani Kukinzana na Neno. Imani ya kikristo inayokinzana na neno


la Mungu yaani Biblia Takatifu hiyo ni dhahiri kuwa ni imani potofu. Yapo
mambo ambayo Biblia imetoa mwongozo basi imani inayoruhusu mambo
hayo kufanyika basi imani hiyo dhahiri ni imani potofu. Mfano:

(1) Ibada za Sanamu.

(2) Ulevi.

(3) Ndoa za mitaala.

Soma. Wagalatia 1: 6

6
Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita
katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna
nyingine. 7Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na
kutaka kuigeuza injili ya Kristo. 8Lakini ijapokuwa sisi au malaika
wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo
tuliyowahubiri, na alaaniwe. 9Kama tulivyotangulia kusema, na
sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote
isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.

b. Kukosekana kwa Msimamo wa Imani (Lack of Consistency).


Imani isiyokuwa msimamo ambayo leo wanasimamia hili na kesho
wanakuwa na msimamo tofauti na jana hiyo ni imani potofu. Mungu wetu
tunayemwamini ni Yeye Yule jana na leo. Mungu wetu si kigeugeu
alivyotutaka miaka ya 1900 ndivyo anatutaka na leo. Malaki 3:6

2
Kwa kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu; ndio maana ninyi
hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.

c. Kutojali Wahitaji. Imani hizi kwa sababu hujikita kujilimbikizia mali


hata mafundisho yake hujikita katika mafanikio kuliko utakatifu.
Mafundisho ya mafanikio huwafanya waamini wa imani hizi kuwa na
shauku ya mali nyingi na hivyo hawana mzigo wa kujali wahitaji. Yakobo
1:27:

Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda
kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na
dunia pasipo mawaa.

CHANZO CHA IMANI POTOFU

Chanzo cha imani potofu ni Ibilisi ambaye kazi ya ni kufanya udanganyifu hapa
duniani. Amekuwa akifanya hivyo kwa kuleta manabii wa uongo. Bahati mbaya
sana watu wengi wamekuwa wakiingia katika udanganyifu wa shetani na kupotea.
Kwa upande mwingine watu kwa tama za mafanikio ya haraka hujikuta katika
utumwa wa imani potofu.

1 Yohana 4:1

1 Timotheo 4:1

2 Timotheo 4:3-4

NINI KIFANYIKE ILI KUZUIA IMANI POTOFU

Imani potofu hukua kwa kasi sana kupitia vyombo vya habari, na watu wengi
hufuata imani potofu kwa sababu hazina masharti magumu, lakini pia husisitiza

3
kwenye mafanikio ya mwili kama vile mali, ndoa na uponyaji ambavyo ndiyo
hitaji kuu la watu katika ulimwengu huu. Mambo ya kufanyika ili kuzuia imani
potofu ni yafuatayo:

a. Waamini Wafundishwe Neno kwa Undani. Watumishi wa Mungu


wa kweli lazima wafanye jitihada za kuhakikisha kuwa washirika wao
wanakuwa na uelewa wa kina kuhusu neno la Mungu. Uelewa wa neno la
Mungu kutawafanya waepuke udanganyifu wa shetani.

b. Injili ya Kweli Kuhubiriwa kwa Wote. Injili ya kweli imebaki


kuhubiriwa makanisani tu. Ukienda kwenye vyombo vya habari imani
potofu zimetamalaki. Watumishi wa Mungu katika imani ya kweli hawana
ujasiri wa kukemea kuhusu imani potofu katika vyombo vya habari.
Inatakiwa kufanya juhudi za kukemea kuhusu imani potofu, makanisani,
mashuleni, kwenye mitandao na kwenye vyombo vya habari ili ulimwengu
ujue imani ya kweli na uongo.

MADHARA YA IMANI POTOFU

Madhara ya imani potofu huwa ni makubwa ijapokuwa yanaweza yasiwe papo


kwa papo. Madhara hayo ni kama ifuatavyo:

a. Kiroho.

(1) Kuzoelea dhambi/uovu.

(2) Laana.

b. Kiuchumi. Umaskini kwa sababu ya kutegemea mafanikio ya


miujiza.

4
c. Kijamii. Vifo kwa sababu imani potofu nyingi huzuia watu kupata
matibabu kutoka hospitali. Pia maafa yanayoweza kutokana na makafara ya
imani potofu.

d. Kitaifa.

(1) Taifa kuwa duni kiuchumi kwa sababu watu wake kutojihusisha
na uzalishaji na kutegemea utajiri wa miujiza.

(2) Pia taifa laweza kuingia kwenye machafuko hasa imani potofu
zinapohusisha misimamo mikali (religious extremist).

MIFANO

You might also like