You are on page 1of 3

UJUMBE: CHAKULA CHA KICHAWI

2 Wafalme 4:38-40

“Elisha akafika Gilgali tena, na kulikuwa na njaa katika nchi, na hao wana wa manabii walikuwa
wakikaa mbele yake. Akamwambia mtumishi wake, teleka sufuria kubwa, uwapikie wana wa
manabii. Na mmoja wao akaenda nje kondeni ili kuchuma mboga, akaona mtango-mwitu,
akayachuma matango – mwitu, hata nguo yake ikawa imejaa, akaja akayapasuapasua sufuriani;
kwa maana hawakuyajua. Basi wakawapakulia hao watu ili wale, ikawa walipokuwa katika kula
chakula, wakapiga kelele, wakasema, mauti imo sufuriani, ee mtu wa Mungu, wala hawakuweza
kula. Lakini yeye akasema, leteni unga, naye akautupa ndani ya sufuria, akasema, wapakulie
watu, ili wale, wala hakikuwamo kitu kibaya sufuriani”.

Kuna njia mbalimbali ambazo shetani hutumia kuwanasa wanadamu ili wamfuate; wasipotaka
kumfuata kwa hiari yao atawaletea magonjwa, atawaletea mateso, atawafanya wawe maskini,
atazuia mafanikio yao. Akitaka umfuate, atamfanya mume wako awe cha pombe, kila wakati,
kila saa yeye ziko kichwani, akitaka akupate atamfanya mume wako awe Malaya, yaani yeye
kila mwanamke anayemwona ni chakula, hata kama ni kichaa! Ndiyo maana utaona kichaa
anamimba!
Shetani hutumia mapepo na majini. Mapepo yanaweza kukuingia kwa njia ya chakula. Wewe
unaona unakula chipsi kuku kumbe unakula jini mahaba, wewe unaona unakula biriani kumbe
unakula dawa ya kukufanya uwe kichaa, unaona unakula nyama choma kumbe unakula pepo
likae katika tumbo lako ili usizae.

Leo hii chakula chenye pepo, chakula chenye jinni ulicholishwa na wachawi utakitapika kwa
jina la Yesu. Haijalishi kimekaa kwenye mwili wako miaka 5 au kumi, leo ni siku yako,
utasafishwa na damu ya Yesu. Leo tutaflush tumbo lako! Sema, “Ninatapika kila chakula
nilichokula, chakula cha wachawi, majini na mapepo kwa Jina la Yesu”

Una magonjwa katika tumbo la uzazi kwa sababu ya chakula cha kipepo. Una uvimbe tumboni
sababu ya chakula cha kichawi, ukienda hospital wakufanyie operation utakufa, unasikia mwili
mzima kuna vitu vinatembea sababu ya chakula ulicholishwa, ukienda hospitali wakipima
hawaoni kitu. Mateso yote haya yanaletwa kwako ili umkufuru Mungu na kwenda kuzimu
kutafuta uzima; uende kupiga ramli, uende kwa waganga wa kishenzi; na ukienda huko
wanakuongea matatizo mengine.

Kama ulipewa jini mahaba ndiyo hushikiki, msichana unatamani hata kutembea uchi; unavaa
nguo fupi unaona haisaidii, siku inaisha hakuna mwanamume anayekuita, unaamua uachie matiti
kuwa wazi, unayashikilia kwa sindilia mbili, nakwambia hayo maparachichi yatalala tu na
hakuna atakayeyatamani tena. Ukiona maparachichi hayavutii wanaume unaamua kuanza kuvaa
kichwani nywele za watu waliokufa; mtu akikuangalia jini si jini, mzungu si mzungu, muhindi
sio muhindi, basi tu unatia kichefuchefu. Na kama utampata mwanaume lazima atakuwa mlevi
tu; maana mlevi akili yake imepofushwa, yeye ukimwekea hata mkojo wake kwenye kikombe
anakunywa, anaweza kumbaka hata mama yake!
hayo ni mateso hivyo ni vifungo; Njoo kwa Yesu yeye ataondoa kiu yako ya dhambi na
kukutoa kwenye mateso!

Hadithi ya Mama aliyepewa uji na mchawi ili ajifungue haraka


“Mama mmoja alifikia siku zake za kujifungua, lakini zikapitiliza, madaktari walimwekea maji
ya uchungu mpaka wakachoka, Bibi mmoja mchawi akaenda kumwona hospitali, akamwambia
kesho nitakuletea uji, ukinywa huo basi utajifungua mara moja. Kesho yake akampelekea uji,
Yule mama akanywa, uji mtamu wenye hiriki na maziwa, Yule mama hakujua kuwa katika ule
uji kulikuwa na mauti. Ni kweli akaanza kupata uchungu, nao ukazidi sana, lakini akaanza
kusikia mtoto anapanda kifuani, badala ya kutoka katika njia ya kawaida, mtoto akawa anakuja
shingoni, mwishowe akiishiwa na pumzi, madaktari hawakuweza kufanya kitu, akafariki”.
Lakini mama Yule alichukuliwa tu hakufa; watu wakazika, lakini yeye na mtoto wake wakaenda
kuishi kwa Yule bibi. Yule Mama aliyefariki alikuwa na Mama yake, sasa ikawa anamtokea
usiku, anamwambia Mama mjukuu wako tangu juzi hajanyonya, maziwa hayatoki kwa sababu
ya chakula ninachopewa. Ikawa ni maajabu maana Mama Yule alikwishazika mtoto wake na
mjukuu, akaenda kwa padre, padre eti anampa maji ya baraka majini yasimfuate! Siku ya tatu
alipomtokea akamwambia Mama kwa sababu umekataa kunisaidia kutunza mjukuu wako inabidi
na wewe uje huku niliko, kweli Yule mama akapata presha ya ghafla watu wakazika”

Yupo mtu hapa ambaye yeye huota anakula nyama, na hiyo ndoto ndiyo chanzo cha mateso yako
kutoka kuzima. Yupo binti hapa ambaye yeye huota anafanya mapenzi na mtu asiyemjua, hicho
ndicho chanzo cha mateso yako!

Yeremia 30:16 inasema, “Basi, watu wote wakulao wataliwa, na adui zako wote watakwenda
kufungwa; kila mmoja wao na hao waliokuteka nyara watatekwa; na hao waliokuwinda
nitawafanya kuwa mawindo”

Mika 3:3 inasema, “Naam, mnakula nyama ya watu wangu, na kuwachuna ngozi zao, na
kuivunja mifupa yao; naam kuwakata vipande vipande kama kwa kutiwa chunguni, na kama
nyama sufuriani”.

- wanaopanga kunifanya mateka, ninawateka kwa jina la Yesu


- wanaotafuta kula nyama yangu, ninawalisha nyama yao wenyewe
- wanaopanga kunywa damu yangu, ninawanywesha damu yao wenyewe

Wachawi wanakula nyama za watu; wanawakatakata vipande kama mishikaki ya nyama ya


ng’ombe. Ukiokoka leo wewe na wale unaowapenda hawataliwa na mchawi kama Bwana
aishivyo; kwa jina la Yesu. Kuna mtu hapa leo asipookoka wiki ijayo analiwa nyama.

Mateso mengi katika maisha yako huletwa na dhambi ya mtu; changu doa akiugua ukimwi ni
halali yake, wala asiseme ni wachawi, wala asiseme ni shetani. Unaumwa magonjwa sehemu za
siri, kaswende kisonono, kwa sababu wewe ni chupi mkononi, yaani kila wakati uko tayari,
kwenye majani sawa, kwenye vichaka twende, kwenye ukuta wa nyumba ruksa.
Kwa hiyo wewe kama hupati magonjwa mara kwa mara ni vizuri kutubu kuacha dhambi ili
kuepuka magonjwa kwa sababu ya hukumu ya Mungu dhidi ya dhambi.
Pepo wachafu wanavyofanya kazi.
Mapepo ni roho chafu ambao shetani anawatumia. Roho hizi chafu zinamajina tofauti; majini,
mashetani, mapepo, mizimu kutokana na kazi na muonekano. Majini ni roho chafu ambao
wamebadilika na kuchukua umbo linaloonekana; umbo la binadamu, umbo la nyoka, samba,
sungura, ng’ombe ili kuweza kutimiza kazi yake.
Kama kazi ya jini ni kuharibu ndoa basi roho chafu itajigeuza kuwa mwanamke mzuri sana
ambaye kila mwanaume akimwona atataka azini naye, yaani ukimwangalia hata kama
ukiambiwa utoe nyumba ili umpate unatoa!
Katika Luka 8:2 Yesu aliondoa pepo 7 kutoka kwa Mariam Magadalena ambaye alikuwa
Malaya.
Kama kusudi ni kusababisha ajali na kuua, roho chafu itajigeuza jini lenye umbo la ng’ombe;
dreva anaona ghafla ng’ombe inakatiza barabarani akijaribu kuikwepa gari linapinduka na watu
wanakufa.

Wapo watumishi wanaojiita manabii ambao wanatumia nguvu za mapepo; hivyo shetani hutumia
roho chafu ili awateke wanadamu na kuwapotosha. Ukienda kuabudu kwenye kanisa wanakupa
vitambaa na maji ya baraka, na chumvi ujue ni nguvu za giza na ukivitumia unajiunganisha na
kuzimu; maisha yako yanakuwa chini ya ibilisi shetani. 2 Wathesalonike 2:9-12. Shetani na pepo
zake wana nguvu ya kufanya miujiza ya udanganyifu.

“Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; Kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa
lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa;
wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya” (Marko 16:17-18).

Yohana 6:35, “Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima, yeye ajaye kwangu,
hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu milele”
Yohana 6:54, “Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami
nitamfufua siku ya mwisho”

MAOMBI YA KUFUNGA
Sema maneno haya; Ugonjwa huu sio wangu, Mateso haya sio yangu, Kansa hii sio ya kwangu,
Kisukari hiki sio changu, Umasikini huu sio wa kwangu
Nayakataa kwa jina la Yesu. Nayafuta kwa damu ya Yesu.

Ninakutapisha chakula cha kichawi ulichokula, mapepo yaliyoingia ndani yako kwa njia ya
chakula nayaamuru kwa jina la Yesu toka, uvimbe ulioota kwa kula chakula cha kichawi
inauyeyusha kwa damu ya Yesu.
Waliofungwa ninawatoa katika vifungo vya shetani kwa jina la Yesu njooooo
Walio ndani ya mashamba njooo, walio baharini njooo, walio shimoni njoo
walio ndani ya makabati, walio ndani ya vibuyu, walio ndani ya tunguri, walio ndani ya jangwa
ndani ya madaraja, ndani ya makorongo njooo, njoooo, rudi, rudi kwa Jina la Yesu.

You might also like